RAI -Zitto Kabwe: Bado Sijamuona mtu mwenye sifa za urais

Embed Size (px)

DESCRIPTION

ZITTO KABWE: Bado Sijamuona mtumwenye sifa za uraisRai /AlhamisiOktoba 2-8, 2014

Citation preview

  • 5/19/2018 RAI -Zitto Kabwe: Bado Sijamuona mtu mwenye sifa za urais

    1/1

    Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 2014Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 201416 17

    Inaendelea uk. 21

    NA GABRIEL MUSHI

    Rai /AlhamisiOktoba 2-8, 2014

    >>Ronaldo mtoto wa familia mas-kini anayezidi kutikisa medani yasokaKwenye mbio hizo, Ronaldo alimzidi Lionel Messi wa Barcelona.Aidha tuzo hiyo ilimfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanzaMreno kuchukua baada ya Luis Figo mwaka 2001.

    Adha yamichangona maisha

    magumu yakujitakiauk19

    MAHOJIANO

    Watanzaniahawajatambuafalsafa ya Sitta

    uk20

    Naibu wazirihana mamlaka ya

    kuamuauk24

    Hong Kongkuivuruga

    China?uk28

    uk31

    NA GABRIEL MUSHI

    ZIITO Kabwe ni mmoja wawanasiasa vijana wenye majinamakubwa nchini kwa sasa,

    amefanikiwa kupenya na nyotayake kungaa kisiasa kutokana nauwezo wake wa kuibua hoja nzito nakuzisimamia.

    Mara zote hoja zake alizowahikuziibua iwe ndani ya Bungeama kwenye majukwaa ya kisiasazimekuwa mwiba mkali kwa Serikaliama makundi yaliyoelekezewamakombora hayo.

    Zitto amekuwa akiendesha siasaza kimkakati endelevu ambazo marazote zimekuwa na tija kwake, chamachake na nchi kwa ujumla.

    Anabainisha kuwa amekuwamuumini wa siasa safi zenye tijakwa pande zote na ndio sababu ya

    kupendezwa na siasa za aliyekuwaWaziri Mkuu wa Malaysia, MahathirMohamed ambaye hufunga safari yakwenda kuonana naye kila ufikapomwezi Oktoba.

    Anaamini Mahathir ni mwanasiasawa mrengo wake kwani mamboanayokabiliana nayo yanamuelekeo nayale aliyokabiliana nayo mpambanajihuyo wa Malaysia ambaye alishawahikufukuzwa kwenye chama chakeakiwa mbunge, lakini kutokana nakukabiliana na changamoto za siasaalifanikiwa kushika wadhifa waWaziri Mkuu.

    Hata hivyo akiwa kwenye safari yakuelekea kwenye kilele cha mafanikiokisiasa, alikumbana na ajali mbaya yakisasa ambaye imetajwa kumrudisha

    nyuma kwa kiwango kikubwa, ingawa mara zoteamekuwa akiamini kwamba ajali hiyo ya kisiasaimemkomaza zaidi.

    Alijikuta akivuliwa nyadhifa zake zote ndani yaChama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kutokana na kutwisha zigo la shutuma za usaliti,aidha alinusurika kuvuliwa uanachama kutokana nakukimbilia mahakamani.

    Lakini pia ajali hiyo imekuwa ikitajwa kamamtaji kwa wapinzani wake kisiasa kama pigokwake, ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanyaziara rasmi na zisizo rasmi kwenye jimbo lake namkoani Kigoma kwa ujumla ili kuimarisha mizizi yakupambana nae kwenye chaguzi zijazo.

    Hali hiyo imelisukuma RAI kufanya mahojianomaalumu na Zitto ili kueleza changamotoanazokumbana nazo jimboni kwake pamoja na

    masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wakekisiasa pamoja na hali ya kisiasa nchini.

    RAI: Kuna taarifa kuwa wapo baadhiya wapinzani wako kisiasa wanakwendajimboni kwako kwa lengo la kukita mizizi ilikuhakikisha unapoteza mvuto kwa wapigakura wako, je unawazungumziaje?

    ZITTO: Kwanza hakuna mtu ambaye anawezakuwavuruga watu wa Kigoma Kaskazini kuhusianana Zitto, sio Kigoma kaskazini tu hata Kigomayote, watu wa kule hawaambiwi maneno matupu,wanaona utendaji wa kazi, katika kipindi ambachonimekuwa mbunge na heshima niliyowapakwa ujumla sina mashaka hata kidogo, mtuyeyote ambaye anakwenda Kigoma kwa lengo lakumshughulikia Zitto atashindwa.

    Zitto Kabwe:Bado Sijamuona mtumwenye sifa za urais

    Sina hofu na yeyote, mimi ndiyo nembo ya Kigoma

    Lakini pia ajalihiyo imekuwa

    ikitajwa kamamtaji kwawapinzani wakekisiasa kamapigo kwake,ambapo baadhiyao wamekuwawakifanya ziararasmi na zisizorasmi kwenyejimbo lake namkoani Kigomakwa ujumlaili kuimarishamizizi yakupambana naekwenye chaguzizijazo.

    Watu wanawezak u j i f u r a h i s h awakawachukulia wenzaofomu za kugombeanawapa changamotokwamba waende, waitishemkutano waone kama

    wananchi watahudhuria.Sina wasiwasi wowote jimbolipo sawa, wanachokifanyasasa ni kutekeleza siasa zakujifurahisha.

    Wanafanya kitu chamaudhi ili wajifurahishe,mimi ndiye nembo yaKigoma.

    RAI: Unazunguziajemisukosuko uliyopitiakisiasa?

    ZITTO: Katika hali yakawaida kama nisingekuwaimara ningeanguka,naamini wengi walitegemeaningeanguka, lakini nikoimara zaidi ya nilivyokuwaawali.

    Wanashangaa mimibado nafanya kazi zangu,nina kazi nyingi za kufanya,sijali nini wanachokifanya,juhudi zozote wanazozifanyakwa ajili ya kunishughulikia

    katika jimbo langu au katikamkoa wangu watashindwa,naaimini nimeingia kwenyemioyo ya watu wa Kigoma,kwa sababu mimi ni alamayao, hivyo wanajifurahisha.

    Mimi kuna kazi nafanya,siwezi kuhangaika nawatu wasiokuwa na kaziza kufanya, wasiokuwa nakazi ya kufanya wao ndiyowanadili na Zitto, mimi hiyosiyo aina yangu ya siasa,nafanya mambo mazitokwenye siasa.

    Kamati ya Bungeimenipa kazi kubwa ya

    kufanya, nalitumikia taifa, tayaritumeshaliita Jeshi lije kuelezamatumizi na mapato yao, hili nijambo zito ambalo halijawahikufanyika, kama ilivyo kwa polisina Usalama wa Taifa.

    RAI: Imekuwajeumeamua kubadili muelekeo

    wa majimbo, kutoka KigomaKaskazini hadi kulipigiamahesabu jimbo la KigomaMjini?

    ZITTO: Uamuzi wangu nikugombea urais, hiyo ndiyodhamira yangu kuu na mimi ndiyemtu wa kwanza kutangaza wazikwamba nitagombea urais.

    Kama vigezo vitaruhusunitagombea urais, nilishawaelezawapiga kura wangu kuwanitaongoza awamu mbili tu,kwa sababu vitu ambavyonimeshindwa kuvifanya ndaniya miaka 10 sitaweza kuvifanyandani ya miaka 30, kwa hiyonilichofanya ni kutoa nafasi kwamwingine aje aliongoze jimbo hiloili tuende mbele zaidi.

    Kama sitapata nafasi yakugombea urais, nitahamishianguvu Kigoma Mjini, lengo languni kusambaza maendeleo mkoaniKigoma.

    RAI: Utawania kwa tiketiya chama gani?

    ZITTO: Kabla ya mwisho wamwaka huu wananchi watakuwawamejua chama nitakachojiunganacho.

    Kwa sasa kuna kazi nazifanya,lazima nizimalize, lakini piaitategemea uamuzi wa kesi yangudhidi ya Chadema.

    RAI: Kuna taarifa kuwaunajiandaa kuhamia

    ACT iwapo mustakabaliwako ndani ya Chademahautotengamaa?

    ZITTO:Sijasema mahali popotekwamba nakwenda ACT, siku zotenasema nina kesi, nikimalizanitajua mwelekeo wangu wakisiasa ukoje, sasa hivi akili na

    nguvu zangu nimezielekeza PAC,natakiwa kutoa taarifa ya mwaka,kusimamia uwajibika katikanchi na kuhakikisha fedha zawananchi zinatumika sawasawa.

    Hilo ndilo jukumu kubwanililopewa kwa sasa nanitahakikisha nalitimiza.

    Wakati kuna watu ambaowanaweweseka na Zitto miminimeshapiga mstari, naangaliambele nafanya mambo menginesiangalii kabisa nini kilitokeahuko nyuma, watu ambaowanaweweseka na Zitto ndiowanaongalia nyuma, vitendovinatamka zaidi kuliko maneno.

    RAI: Uchunguzi wa

    ripoti ya IPTL umefikiawapi, je, Kamati yakoimeshakabidhiwa ripotihiyo?

    ZITTO: Machi mwaka huunilimwagiza CAG afanye ukaguzimaalum kuhusu sakata la

    IPTL, amefanya, atanikabidhiripoti hiyo wiki ijayo (wiki hii),tutaishughulikia kwenye Kamatina kuiwasilisha kwenye vikao vyaBunge la mwezi Novemba mwakahuu.

    Sasa hivi nimeshapokearipoti maalum ya jengo la wagenimaarufu kwenye uwanja wa ndegeKimataifa wa Dar es Salaam.

    Ujenzi wake umegharimu Sh.bilioni 12, ambazo ni sawa dolaza Marekani milioni nane, kati yahizo dola milioni tano ni msaadakutoka kwenye shirika moja laChina na dola milioni tatu zilitokaSerikalini.

    Niliagiza ukaguzi wa vyamavya siasa kwenye upande waruzuku, tunapokea taarifa hiyo natutamwita msajili wa vyama vyasiasa.

    Kuna tatizo la mifuko yahifadhi ya jamii, tumemwitaGavana wa Benki Kuu kwenyeKamati. Na mjumbe wa SSRAwote watakuja Oktoba 20 mwakahuu, tunataka kumaliza matatizoya wafanyakazi, hivyo nina kaziza kufanya siwezi kusumbuka nasiasa ndogondogo.

    Kiujumla ripoti hizi zotehususani ile ya IPTL inawezakuiangusha serikali.

    RAI: Hivi karibuniProfesa Abdalah Safariameteuliwa kuwa MakamuMwenyekiti wa Chadema, piaalizungumzia kutokuwapokwako ndani ya chama hichohakuna kilichoharibika, jeunamzungumziaje?

    ZITTO: Nimesikitishwa sanana maneno ya Profesa Safarinaomba aweke akiba ya manenoyake, asiongee sana atakujakuyameza hayo amaneo baadaye,yeye siyo wa kwanza kushika

    nafasi hiyo aliyo nayo.RAI: Lakini pia Profesa

    Safari amesema iwapoutakuwa tayari kuomba radhi

    wao wako tayari kumalizatofauti, je utakuwa tayarikwa hilo?

    ZITTO: Nikiomba radhiwatanisamehe!! Mimi sina kosawao ndio wanapaswa kuniombaradhi, sio mimi kuwaomba waoradhi, sina kosa hata moja,hakuna tuhuma yoyote ndani yaChadema ambayo mtu anawezakudhibitisha.

    RAI: Chadema wapokwenye mkakati wa

    kutekeleza maandamanonchi nzima kwa lengo lakupinga Bunge la Katibalinaloendelea, je, unadhanimaandamano ndio njiasahihi?

    ZITTO: Nikizungumzia

    suala hilo, nitaingilia uamuziya Chadema, sitaki kuendelezaugomvi, huo ni uamuzi waMkutano Mkuu, maswali yamsingi ya kujiuliza ni kwambaje, wanamiliki chama chawafanyakazi?

    Ni kwanini waseme watakuwana migomo isiyokwisha nchinzima ile hali migomo ya namnahiyo inatakiwa kutekelezwa navyama vya wafanyakazi? Hakunachama cha wafanyakazi kilichopondani ya Chadema, kwa maanahiyo si rahisi kwa suala hilokufanikiwa.

    Lakini ndio uamuzi wao,watu wengi walitarajia baada yaMkutano Mkuu chama kingetokana matangazo ya kisera kwa ajiliya Uchaguzi Mkuu, badala yaketunatangaziwa maandamano, je,hizo ndio sera za chama katikakuwasaidia wananchi?

    Chama kilipaswa kuibuka namipango ya kuwaboreshea maishawananchi kwa kuzungumziamasuala ya maji, afya na mambomengine ya maendeleo.

    Kwangu kilichofanywa nawatu hawa ni upotevu wa nafasi,duniani kote mikutano mikuuya vyama ndiyo mahala ambapochama kinajitanabaisha kwa serambalimbali za mabadiliko kwenyenchi.

    Hata hivyo siwezi kujuamkakati wao kwa sababusikuwapo kwenye mkutano huohivyo siwezi kuzungumza zaidi.

    Lakini pia si jambo bayakufanya maandamano kwasababu Watanzania wanatakasuluhisho la mambo ya Katiba.Lakini pia ni vema tukajiuliza hajaya maandamano inatoka wapi,wanataka Bunge liahirishwe sasa,kwa madai ya kuokoa fedha zawalipa kodi, lakini mbona hatuoni

    wakifanya maandamano yakupambana na wezi wa fedha zaEscrow ambazo ni Sh. biloni 200.

    Sijasikia watu wakitoa kauli zakupinga wizi uliofanyika na BenkiKuu ambao unakwenda kuingoaserikali, sijasikia mambo kamahaya, wananchi wanataka kusikiakuhusu mali zao na uwajibikaji.

    Lakini si jambo baya piakupigania fedha za walipa kodihata kama ni ndogo kiujumla niza umma.

    Kwa sababu maandamanoni haki ya kila raia, ingawa sijuikama yatatufanya tupate kileambacho tunataka kukipata.

    Jambo la msingi nikuhakikisha wananchi wanapata

    ZITTO:Nimesikitishwasana na manenoya Profesa Safarinaomba awekeakiba ya manenoyake, asiongeesana atakujakuyamezahayo amaneobaadaye, yeyesiyo wa kwanzakushika nafasihiyo aliyo nayo.

    Zitto Kabwe akiwa na viongozi wa Chadema