RAI- Zitto -Ripoti Ya IPTL Kuiangusha Serikali

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Zitto: Ripoti ya IPTL kuiangusha SerikaliRai /Alhamisi Oktoba 2-8, 2014

Citation preview

  • Rai /Alhamisi Oktoba 2-8, 20142 HABARI

    NA MWANDISHI WETU

    MOJA ya kashfa inayotajwa kulitesa Taifa kwa sasa na huenda ikaitingisha kwa kiasi kikubwa Serikali, ni ile ya ukwapuaji wa kiasi cha Sh. bilioni 200 kutoka kwenye akaunti ya Escrow iliyoihusisha kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco).

    Kashfa hiyo ambayo ilijadiliwa kwa kiasi kikubwa kwenye Bunge la Bajeti la mwaka huu, iliibua mjadala mzito uliosababisha pande zinazosigana kufikishana mahakani, huku Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akipewa jukumu la kuchunguza saka-ta hilo.

    Madai ya ukwapuaji wa fedha hizo ya-naelekezwa moja kwa moja kwa baadhi ya watendaji wa juu serikalini ambao wanata-jwa kushirikiana na mwekezaji ambaye ina-daiwa umiliki wake wa IPTL umejaa utata.

    Utetezi na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na baadhi ya watendaji wa Serikali juu ya wabunge waliokuwa wakilipigia kelele su-

    ala hilo unatajwa kuuaminisha umma kuwa wakubwa hao wamehusika na kwamba wana-fanya jitihada za kuuficha ukweli wa jambo hilo ambalo hivi karibuni liliingia kwenye vichwa vya habari vya gazeti la African Confi-dential la Uingereza.

    Pamoja na jitihada hizo za kutaka ukweli kufichwa, mambo yanaonekana kwenda kombo kwani hivi karibuni ukweli utabaini-ka.

    Ukweli huo utabainika kutokana na ri-poti uchunguzi ya CAG kukamilika, ambapo inatajwa kubaini madudu ya hatari ambayo yanatishia uimara wa Serikali ya awamu ya nne.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesa-bu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, ameliam-bia RAI kuwa ripoti hiyo itaingia mikononi mwake wiki hii.

    Hatua ya Zitto kukabidhiwa ripoti hiyo inakuja kufuatia agizo la Kamati yake Machi 20, mwaka huu kumtaka CAG kufanya uchunguzi wa kina wa sakata hilo.

    PAC ilimtaka CAG kuchunguza kama akaunti hiyo iliihusisha Kampuni ya Mech-mar iliyokuwa na hisa za umiliki katika Kam-puni ya IPTL.

    Aidha alitakiwa kuthibitisha kama Mech-mar ilikuwa imehamisha umiliki wake kwen-da kampuni ya Pan African Power Solution (PAP) kabla ya kufilisiwa.

    Pia CAG alitakiwa kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa kuwapo kwenye akaunti ya Escrow wakati Benki Kuu ina-hamisha fedha hizo kwenda IPTL.

    Pamoja na mambo mengine lakini pia, CAG alipewa jukumu la kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu kiasi cha fedha kilichowekwa na kila mhusika hadi siku uamuzi wa Ma-hakama Kuu kuhusu kesi hiyo ulipotolewa.

    Jukumu jingine lilikuwa ni kuchunguza madai ya Benki ya Standard Chartered (Hong kong) kwa IPTL na madai mengine ya kuzali-sha umeme wa IPTL na kama Serikali iliji-hadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa dhidi yake na wadai mbalimbali.

    Pia CAG alitakiwa kuchunguza uadilifu wa Wizara ya Nishati na Madini ambayo iliingia mkataba na IPTL kufungua akaunti hiyo na kuweka uangalizi kabla ya kutoa fedha zi-lizokuwapo kwenye akaunti hiyo.

    Katika kuusaka ukweli wa jambo hilo CAG alitakiwa kufanya uchunguzi kuhusu hisa za Mechmar iliyotajwa kufilisika huku ikidaiwa kuwa na hisa nyingi za IPTL.

    Aidha alitakiwa kuangalia kama hisa hizo sasa zinamilikiwa na PAP, ambapo alipewa jukumu la kutoa mapendekezo ya njia sa-hihi za kisheria zinazoweza kutumika kwa ajili ya kulinda Serikali isipate hasara katika utekelezaji mkataba wa IPTL.

    PAC ilimtaka CAG kufanya ukaguzi kwe-nye shughuli zote za uhamishaji fedha zi-lizofanyika Julai Mosi, 2006 hadi Machi 31, mwaka huu.

    Akizungumzia majukumu hayo aliyopewa CAG, Zitto alisema yametekelezwa kwa ufani-si mkubwa na kwamba ripoti hiyo ikiwekwa hadharani haitaiacha salama Serikali.

    Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema kutokana na unyeti wa sakata lenyewe na ripoti ya CAG, hali inaonesha kuwa mbaya kwa serikali ku-tokana na vielelezo vilivyokusanywa na CAG.

    Kazi hii tayari CAG ameifanya na atani-kabidhi ripoti hiyo wiki ijayo (wiki hii), sisi tutaishughulikia kwenye Kamati na kuiwasil-isha kwenye vikao vya Bunge la mwezi No-vemba mwaka huu.

    Tayari nimeshapokea ripoti maalum ya jengo la wageni maarufu kwenye uwanja wa ndege Kimataifa wa Dar es Salaam. Ujenzi wake umegharimu Sh. bilioni 12, ambazo ni sawa dola za Marekani milioni nane, kati ya hizo dola milioni tano ni msaada kutoka kwe-nye shirika moja la China na dola milioni tatu zilitoka Serikalini.

    Tunapokea ripoti nyingi, lakini hii ya IPTL ni nzito zaidi. Oktoba 20, mwaka huu tumemuita Gavana wa Benki Kuu kwenye Kamati, naamini hii ripoti itawashangaza wengi, niliagiza ukaguzi wa vyama vya siasa kwenye upande wa ruzuku, tunatarajia pia kupokea taarifa hiyo na tutamwita msajili wa vyama vya siasa.

    Pia kuna tatizo la mifuko ya hifadhi ya jamii, tumemwita mjumbe wa SSRA wote watakuja, nawahakikishia Watanzania ripoti hii ya IPTL inaweza kuiangusha serikali, alisema.

    Tayari sakata hilo limemuibua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye amekiri kupokea kiasi cha Sh. bilioni moja ambazo amedai kuwa alipe-wa kama mchango kwa ajili ya shule ya se-kondari Babro.

    Wadadisi wa mambo wanaamini kuwa ripoti ya CAG ambayo inamfanano mkubwa na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) hazitawaacha salama baadhi ya vigogo serikalini na kwenye taasisi kubwa za fedha nchini kutokana na kuguswa kwao moja kwa moja.

    Spika wa Bunge Anne Makinda ni mmoja wa wanasiasa wanaoamini kuwa ripoti ya CAG, Ludovick Utouh ambaye ametajwa kustaafu hivi karibuni haiwezi kuwaacha salama baadhi ya mawaziri.

    Makinda aliweka wazi kuwa ripoti za Ut-ouh zimekuwa zikiandikwa kwa umakini mkubwa na kwamba kilichowaokoa mawaziri walioguswa na ripoti hiyo kwa sasa ni Bunge Maalum la Katiba.

    Ripoti nyingi za Utouh zimekuwa zikiwangoa mawaziri, naamini hata hii ya IPTL itaondoka na watu, kwa sasa baadhi ya mawaziri wameokolewa na Bunge Maalum la Katiba,alinukuliwa Makinda wakati wa hafla ya kumuaga Utouh.

    Zitto: Ripoti ya IPTL kuiangusha Serikali

    Jukumu jingine lilikuwa ni kuchunguza madai ya Benki ya Standard Chartered (Hong kong) kwa IPTL na madai mengine ya kuzalisha umeme wa IPTL na kama Serikali ilijihadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa dhidi yake na wadai mbalimbali.

    Pia CAG alitakiwa kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa kuwapo kwenye akaunti ya Escrow wakati Benki Kuu inahamisha fedha hizo kwenda IPTL.