89

Sayyid wa Vijana wa Peponi - shia-maktab.info

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

SAYYID WA VIJANA WA

PEPONI

Kimepangwa na:

Sayyid Murtaza Rizvi

Kimetolewa na Kimechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P. 20033 Dar es Salaam - Tanzania

Haki za kunakili imehifadhiwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 10 8

Toleo la Kwanza: April, 1999 Nakala 4,000 Toleo la Pili: Juni, 1999 Nakala 2,000

Kimetolewa na Kimechapishwa na::BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P. 20033DAR ES SALAAM - TANZANIA

DIBAJI

Makala haya yaliyoandikwa na waandishi mbali mbali mashuhuri, yalikusanywa na kuchapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania kama “Toleo Maalum la Muharram” la Sauti ya Bilal (Na. 2/3) Machi - Mei 1999 (Muharram 1420).

Nakala zake zilisambazwa hapa Dar-es-Salaam, Morogoro, Mombasa na Zanzibar. Lakini matilaba yake ni makubwa na yenye kuendelea.

Sasa Toleo hili linachapishwa tena kama kitabu kwa jina la “Sayyid wa Vijana wa Peponi”. Mtungaji na Watoaji wanamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Ta’ala kuikubali kazi yao hii ya kiroho na awape wasomaji wake Tawfeeq ya kupata faida kutokana na kijitabu hiki.

Kwa hiyo, tunamuomba Subhanahu wa Ta’ala atuhesabu miongoni mwa wafuasi wema wa Imam Husayn (as.) katika Siku ya Mwisho.

Wa Ma Tawfiqi Illa Billah,

Bilal Muslim Mission of TanzaniaS.L.P. 20033,

Dar-es-Salaam.

MIUJIZA ILIYOTOKEA ZANZlBARMIAKA 55 ILIYOPITA

Machozi ya Damu yasiyotoka kwa binadamu wa kawaida.

Tangu asubuhi ya Mwezi 11 Muharram alama za damu zimekuwa zikionekana juu ya mimbar ya Azaa (kumbukumbu ya maombolezo kuadhimisha kuuawa kishahidi Imam Husayn na Ahl-al-Bait).

Sehemu zingine ambapo Maombolezo haya hufanyika, damu hii ilionekana katika karatasi iliyozingwa kwa kioo ambayo juu yake majina matano1 (rehema na amani ya Allah iwe juu yao) yameandikwa kwa maji ya fedha. Damu ilikuwa juu ya kila herufi kama machozi yabubujikayo na ambayo mchoraji au msanii yeyote asingeweza kumathilisha angalau alama ya damu.

Mwenyezi Mungu amrehemu yule asikiaye na apokeaye uongofu.

Nimethibitisha haya kwa macho yangu mwenyewe.

Mimi Mwandishi:Mohamed Al-Fazaari 1365 A.H.

(Tumepokea Bayana hii kwa hisani ya:Sheikh Suleiman Abdullah Al-Shaybani wa MUSCAT).

1 Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Imam Ali (a.s.), Bibi Fatima (s.a.), Imam Hassan (a.s.) na Imam Husein (a.s.).

SAUTI YA BILALJUZUU 33 Na. 2/3

ZILQAD/MUHARRAM MACHI/MEI, 1999

TOLEO MAALUM LA MUHHARAM

1. Aza ya Mashahidi wa Karbala hapa Tanzania Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi . . . . . . . . . . . . . . . . . .

2. Hussein Mrithi wa Miongozo ya Mungu Hujjatul lslam Sayyid Muhammad Rizvi . . . . . . . . . . . . ..

3. Ushirikiano katika Kujitolea Muhanga Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi . . . . . . . . . . . . . . . . .

4. Maana ya Azadari Bw. Azadar . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

5. Muharram Allamah Sayyid Ali Naqi Naqavi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

6. Dhulma dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s.) Shaykh Musabaha Shabaan Mapinda . . . . . . . . . . . . . . .

7. Mashahidi waliouawa Karbala Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi . . . . . . . . . . . . . . . ..

8. Utenzi: Kwa Mwezi wa Muhharam . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

9. Waafrika waliojitolea Karbala Khwaja Muhammad Latif Ansari . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

1

4

11

17

22

29

35

40

41

10. Nauha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

11. Ua la Mwisho la Imam Hussein (a.s.) . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12. Hazrat Abbas (a.s.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

13. Kisa cha kichwa cha Imam Husain (a.s.) Sayyid Mahdi Shuja’ii . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

14. Wafuasi wa Yazidi ni Nani? Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi . . . . . . . . . . . . . . . ..

15. Nafasi ya Wanawake katika Historia ya Ashura Syed Muhammad Ridha Shushtary . . . . . . . . . . . . . . . . .

16. Njia aliopita Imam Hussein (a.s.) kutoka Makka hadi Karbala

Hujjatul lslam Sayyid Muhammad Rizvi . . . . . . . . . . . ..

17. Kujenga Makaburi na kumlilia Imam Husain (a.s.) Allamah Sayyid Murtaza Askariy . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

18. Historia fupi ya Makbarah ya Imam Husain (a.s.) . . . . . ..

19. Amali za Ashura . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

20. Ziyarate Waaritha Maalim Kassamali Chandoo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

21. Vitabu vya Kiswahili Juu ya Imam Husain Sayyid Murtaza Rizvi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

43

44

47

56

61

63

66

67

70

73

76

80

1

‘AZÃ (MAOMBOLEZO) YAMASHAHIDI WA KARBALA

HAPA TANZANIA

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Imetafsiriwa na:AI-Hajj Jumanne J. Kiambu

Waislamu wa Kiafrika hapa Tanzania, kama walivyo Waislamu wa nchi zingine za Afrika, walikuwa hawafahamu hata kidogo ni kwa nini Imamu Husayn (a.s.) aliuliwa, pia ni nanialiyemua yeye (Imam Husain)pamoja na Wafuasi wake na kwa nini Mashia wenye asili ya Bara Hindi walikumbuka na kuadhimisha masaibu ya Karbalamwaka baada ya mwaka.

Wanavyuo/Ulema wao walijazwa vichwa na itikadi mbaya ya wenye choyo na Wageuzaji wa mambo ili waeneze “Imani’’ kwamba ni wao wenyewe Mashia waliomua Imamu Husayo (a.s.) huko Karbala, na eti ni kwa sababu hii wanapiga vifua vyao kila mwaka kujutia na kutubia kwa dhambi hiyo nzito waliotenda.!!!

Baadaye mwaka 1965 ilianzishwa Bilal Muslim Mission. Mwaka 1967, tulifikiria kuendesha Majlis ya ‘Aza’ (Maombolezo) ya ‘Sayyid -ush-Shuhada’ katika mwezi wa Muharram kwenye nyumba ya Shaykh Mohamed Ali Ngongabure, Temeke, (ambayo hapo awali ilitumika kama kituo cha Bilal). Kwa bahati nzuri Marhum Muallim Seif kutoka Arusha alikubali kuja Dar-es-Salaam kusoma Majlis hizi. Yeye alikuwa ni Shia mwenye ujuzi kutoka Bahrayn, ambaye alikuwa anaweza kusoma majlis kwa lugha za Kiarabu na Kiswahlli (pamoja). Sauti ya na mbinu zake za usomaji zilikuwa zenye kuathiri mioyo, na kwa Hotuba zake wasikilizaji wa Kiafrika waliweza kujua kwa kina Masaibu ya Karbala.

2

Mwaka 1969 tulijenga Msikiti wetu na Madrasa ya vyumba viwili Temeke, na Majlis za mwaka 1970 zilifanyika Msikitini. Baada ya miaka michache hali ya kiafya ya Muallim Seif ilimzuia kuja Dar-es-Salaam. Muda huo tayari baadhi ya Wafrika waliokubali Ushia waliweza kuchukuwa nafasi na kuendeleza majlisi hizi.

Sasa baada ya miaka kama thelathini, tunafuraha kutangaza kuwa ‘aza’ (‘Maombolezo’) ya Imam Husain (a.s.) na Mashahidi wengine wa Karbala yanapangwa na kuendeshwa na Mashia wa Kiafrika katika vituo 14 (kumi na vinne) hapa Dar-esSalaam. Kati ya vituo hivyo, 4 (vinne) vipo moja kwa moja chini ya Bilal Muslim Mission na 10 ni vituo vinginevyo. Orodha yake ni kama ifuatavyo:1. Kwenye ukumbi wa Bilal

Husainiyah Haidariyah (Temeke): Usiku (Wanawake na Wanaume). (Nyaz) chakula huandaliwa kwa wote waliohudhuria. (Hii ni Majlis yetu yake awwali iliyotajwa hapajuu).

2. Kwenye ukumbi ule ule wa

Husainiyah, saa 4.00 asububi kwa wanawake (chini ya usimamizi wa Mama Batul Chatoo).

3. Kwenye Fatimiyah Madrassa iliyopo kwenye Nyumba za Makazi za Bilal (Chang’ombe). chini ya uongozi wa Mama Shufaa Hilal.

4. Masjid Ahlul Bayt, Tabata (Dsm) (Bilal Mission, kupitia kwa Shaykh Haroon R. Pingili).

Vituo vingine (pamoja na majina ya Wasimamizi katika mabano) ni kama ifuatavyo:-5. Al-Baqir Foundation

Magomeni (Shaykh Omari Juma Mayunga)

6. Imam Husayn Foundation, Bunju, Kinondoni (Shariff Saggaf).

7. Thaqalayn Seminary, Charambe, Mbagala (Shaykh Mohamed Ali Ngongabure).

8. Tanzania Ithna-‘ashari Community, Tandika (Shaykh Dhikiri O. M. Kiondo).

Kuanzia mwaka huu (Muharram 1420) vituo vifuatavyo

3

vitaendesha majlis, Insha-Allah:-9. Masjid Ahlul-Bayt Mbande,

(Shaykh Ramadhani Idrissa Kwezi).

10. Madrasa Al-Muntazar, Mbagala (Shaykh Ramadhani Idrissa Kwezi).

11. Masjidi Amirul Muuminiin, Magomeni (Shaykh Musabaha Shaaban).

12. Madrasa Fatimiyah, Mbagala (Shaykh Hassan A. Ndimbo).

13. Masjidi Quba, Kijitonyama (Sheikh Abdul Majid Nassoro).

14. Madrasa Askariyah, Mikocheni (Shaykh Is’haq Pingili).

Baadaye tutaandika taarifu za Majlis za Muharram zitakazofanyika nje ya Dar-es-Salaam, “Insha-Allah”.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) azikubali juhudi za kaka na dada zetu wote wanaojihusisha na Majlis hizi, na awalipe malipo yao hapa Duniani na Akhera. Amen.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)ASEMA:

(1) “Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia.”

(2) “ .... Allah hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain yu adui wa wale walio maadui zake.”

*****

4

HUSEIN MRITHI WAMIONGOZO YA MUNGU

Imeandikwa na:Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Rizvi

Imetafsiriwa na:Dr. Mohamed S. Kanju

Husein, mtoto wa Ali na Fatimah; mjukuu wa Muhammad, ndugu yake Hasani; mrithi wa tatu wa haki wa Mtume wa Uislamu.

Husein, mrithi wa Adam, Nuh, Ibrahim, Musa, Isa, Muhammad na Ali. Muimarishaji nguvu za jeshi la Mungu dhidi ya majeshi ya Shetani.1 Husein kiigizo cha kweli cha Mtumishi wa Allah.

Huseini na ndugu yake Hasani wametambulishwa na Mtume wa Uislamu kama wafuasi wa Mtume, Maimamu na viongozi wa Waislamu, wawe wanapigana au wanafanya amani (na maadui), na viongozi wa vijana wa Peponi. Mtume wa Allah alisema: “Huseini anatokana na mimi na mimi natokana na Huseini.”

Alifanya Nini?

Husein alikataa kula kiapo cha utii kwa Yazid.

Aliondoka Madina, sehemu yake aliyozaliwa, aridhi ambayo ina makaburi ya babu yake, mama na kaka; mji ambao aliishi karibu maisha yake yote; mji ambao umefungamanishwa siku zake kumbukumbu za furaha na huzuni.

Alikwenda Makka. Lakini kule nako vile vile hakupata hifadhi na ilimbidi aondoke siku ya maadhimisho ya hija.

Lakini kwa nini?! Kwa nini aondoke Makka katikati ya maadhimisho makubwa ya hija?! Makka haikuwa salama

5

tena kwa Huseini. Lakini nani anayethubutu kumdhuru mtu yeyote katika mji wa Makka?! Je, si kweli kwamba Allah anasema: “Yeyote atakaeingia humo atakuwa salama?”2 Ndio, Yazidi alithubutu kufanya hivyo. Yazid alipeleka mamluki kama mahujaji na maagizo (amri) ya kumuua Imam Husein hata kama wakimkuta ndani ya msikiti Mtukufu. Mamluki walificha silaha ndani ya Ihram zao. Kwa ajili ya utukufu wa nyumba ya Allah, Imam Huseini hakutaka damu yake imwagwe pale; hivyo aliondoka Makka.

Alikwenda Karbala -- Karbala uwanja wa mapambano kati ya mtu ambaye alikuwa akiwakilisha Mitume wote wa Allah na mtu ambaye alikuwa akimuakilisha Shetani na jeshi lake.

Katika siku ya Ashura, Husein alipendelea kufa Shahidi kuliko kuishi chini ya dhalimu; alipendelea kifo cha heshima kuliko uhai ambao kwayo angepata cheo kikubwa cha kidunia kama angelikula kiapo cha utii kwa Yazid.

Lini?

Aliondoka Madina siku ya mwezi 28 Rajab 60 A.H.

Alifika Makka siku ya mwezi 3 Shabani 60 A.H.

Aliondoka Makka siku ya mwezi 8 Dhil-hijja 60 A.H. - 10 Sept. 680M.

Aliwasili Karbala siku ya mwezi 2 Muharram 61 A.H. - 2 Oct. 680M.

Alipanda kwenye daraja ya juu zaidi ya ukamilifu kwa kupata shabada katika siku ya Ashura, mwezi 10 Muharram 61 A.H. - 10 Oct. 680M

Dhidi ya Nani?

Dhidi ya Yazid. Hapana, sio Yazid tu. Yazid alikuwa mrithi wa Kaini, mrithi wa Nimrod, mrithi wa Firauni, mrithi wa mawakala wa Shetani ambao walimkataa Isa, mrithi wa Abu Sufyani, mrithi wa Muawiya. Yazid alikuwa akiwakilisha jeshi la Shetani.

Yazid mtoto wa Muawiya, mjukuu wa Abu Sufyan na Hind.

6

Abu Sufyan, alikuwa mkubwa wa majeshi ya Makafiri wa Makka ambao siku zote walijaribu kuhujumu ujumbe na dini iliyoletwa na Muhammad (s.a.w.w.). Ni baada tu ya ushindi wa Makka ambapo Abu Sufyan kwa dhahiri alikubali, na kusalimu amri kwenye Uislamu. Hata baada ya kuukubali Uislamu aliendelea kuudhoofisha Uislamu kutoka ndani. Hili linaweza kuonekana kwa uwazi kwa yale aliyosema wakati Uthman alipopata Ukhalifa. Alisema: “Enyi watoto wa Umayya! Kwa vile sasa Ufalme huu umekuja kwenu, chezeni nao kama vile watoto wanavyocheza na mpira na peaneni wenyewe kwa wenyewe katika ukoo wenu.Ufalme huu ni wa hakika; na hatujui iwapo kweli au sikweli kama kuna pepo au moto.”3 Kisha alikwenda Uhud na kulipiga teke Kaburi la Hamza, ami yake Mtume, na akasema: “Ewe Abu Ya-la! elewa kwamba Ufalme ambao ulikuwa unapigania dhidi yetu hatimae sasa umerudi kwetu.”4

Bibi yake Yazid, Hind, alikuwa malaya anayejulikana wa zama za kabla ya Uislamu; ni mashuhuri

katika historia ya Uislamu kwa Ushenzi wake: Katika vita vya Uhud aliahidi kumpa zawadi mtumwa wake, Wahshi, kama angemuua Muhammad au Hamza au Ali. Wahshi alimuua Hamza. Wakati Hind alipojua kwamba Hamza ameuawa, alikwenda kwenye mwili wa Hamza alipasua tumbo lake akatoa ini na akalitafuna na akazima kiu yake kwa ajili ya kulipa kisasi cha baba yake ambaye aliuawa na Hamza katika vita iliyopita ijulikanayo kama vita vya Badir. Vile vile alichana chana mwili wa Hamza kwa kukata masikio yake na pua.

Yazid kwa jeuri kabisa alikataa kuamini Utume. Alielezea imani yake kwa uwazi kabisa katika shairi lake kama ifuatavyo: “Bani Hashim walibuni mchezo (ili) kupata Ufalme, kwa hakika kulikuwa hakuna habari zozote kutoka kwa Mungu wala ufunuo (wahai) wowote.”5 Wala hakuamini siku ya hukumu kama alivyosema katika shairi: “Enyi wapenzi wangu! Msiamini katika kukutana na mimi baada ya kifo, kwa sababu walichokuambieni kuhusu kufufuliwa baada ya kifo ni ngano tu (hadithi za watu wa

7

zamani) ambazo hufanya moyo usahau starehe za ulimwengu huu wa kweli.”6

Kwa wazi kabisa alidhihaki sala za Kiislamu; alionyesha kutoheshimu dini kwa kuwavisha mbwa na ngedele (tumbiri) Majoho ya wanachuo wa dini. Kamari na kucheza na mbwa ilikuwa ndio burudani yake ya kupitisha muda. Alitumia muda wake wote kwa kunywa pombe popote na kila mahali bila kusitasita kokote; hana heshima kwa mwanamke yeyote. Hata waliokatazwa (Mahirim) kama mkwe, dada shangazi na binti walikuwa sawa sawa na mwanamke yeyote machoni kwake.

Na Nani?

Husein alikwenda Karbala na wake zake, watoto, ndugu, dada, na wapwaze; na marafiki wengi, baadhi na familia zao, waliungana naye njiani akitokea Makka kwenda Karbala. Walikuepo takriban wanaume 120, kuanzia watoto wa miezi sita mpaka wazee Mujahid wa miaka themanini, katika msafara wa Huseini. Wote hao walitoa

mhanga maisha yao kwa ajili ya Uislamu.

Lakini kwa nini kuchukuwa wanawake katika hali kama hii? Kwa sababu walikuwa ni dada wa Imamu Huseini na wanawake wengine wa familia yake ambao walichukuwa ujumbe kuupeleka kwenye miji yote na vijiji kati ya Kufa na Damascus. Walichukuliwa kutoka Karbala mpaka Kufa na kutoka pale mpaka Damascus kama wafungwa na jeshi la Yazid. Kama isingelikuwa kwa sababu ya Zainab na Umm Kulthum na wengine, ujumbe wa Imamu Huseini na mwenendo wake vyote vingezikwa Karbala, au angalau ungevurugika kwa muda mrefu, na hatimae kuchelewesha matokeo ya mhanga huu mkubwa.

Kwa Nini?

Yewezekana mtu kama Huseini akala kiapo cha utii kwa mtu kama Yazid?! Hapana! Kamwe! Ingawa kila mtu katika nchi za Kiislamu wamekwisha kula kiapo cha utii kwa Yazid, bado kukataa kwa Huseini ilikuwa ni jambo kubwa la muhimu hata katika

8

macho ya Yazid. Kukubali kwa umma wote wa Uislamu hakuna thamani yoyote bila kukubali kwa Huseini. Sio tu kwa kuwa Huseini alikuwa mjukuu wa Mtume, lakini kwa sababu yeye, kama makamu wa Allah katika ardhi hii, akimuakilisha Hasani, Ali, Mtume Muhammad, Isa, Musa, Ibrabim, Nuh, na Adam. Kutoa mkono wake katika mkono wa Yazid, yaani kula kiapo cha utii kwake, itakuwa kama Ali alikula kiapo cha utii kwa Muawiya, Muhammad kula kiapo cha utii kwa Abu Sufyan, Isa kula kiapo cha utii kwa makasisi wa Kiyahudi, Musa kula kiapo cha utii kwa Firauni, Ibrahim kula kiapo cha utii kwa Nimrod ..... ingekuwa kama Uislamu kusalimu amri kwenye ukafiri na kana kwamba jeshi la Mungu linasalimu amri kwenye jeshi la Shetani.

Kwa mhanga wake mkubwa katika Karbala, Imam Huseini aliamsha moyo wa umma wa Uislamu, aliweka wazi kwamba Yazid na wengine kama yeye hawastahiki, wala hawana haki yoyote yakuwa Makhalifa, viongozi na watawala wa Waislamu. Aliandika kwa damu

yake katika uwanga wa Karbala kwamba mtu haimpasi kujitoa yeye mwenyewe kwa yeyote ila kwa Allah au kwa mtu ambaye amechaguliwa na Allah. Husein alikuwa muimarishaji wa nguvu ya nuru, kweli, haki, uadilifu, na kwame nuru haiwezi kujitoa (kunyenyekea) kwenye giza, au haki kwenye dhulma, au uadilifu kwenye uonevu,

Alisema Nini?

Mjini Madina, alisema: “Sisi ni jamaa wa nyumba ya Utume chanzo cha ujumbe, sehemu ya mashukio ya malaika, kupitia kwetu Allah alianza kuonyesha neema zake, na kwetu sisi Alikamilisha neema zake. Ambapo Yazid ni mtu mwenye Madhambi, mlevi, muuaji wa watu wasio na hatia na mtu ambaye kwa wazi alijitumbukiza katika matendo maovu. Mtu kama mimi siwezi kamwe kula kiapo cha utii kwa mtu kama yeye...”7

Kabla ya kuondoka Madina, aliandika: “Nimesimama dhidi ya Yazid kwa vile nataka kuutengeneza umma wa babu yangu. Napenda kuamrisha

9

mema na kukataza maovu, na kufuata mwendo wa babu yangu na baba yangu, Ali bin Abi Talib.”8

Mjini Makka, kwa majibu kwa watu wa Kufa aliandika: “..... Kwa ajili ya maisha yangu, anachotazamia kuona Imamu ni mtu ambaye anahukumu kwa Kitabu (cha Allah), mtu anayetekeleza haki, mtu mwenye kuhubiri dini ya kweli, na mtu aliyejitoa mwenyewe katika njia ya Allah.”9

Akiwa njiani kuelekea Karbala alisema kuliambia jeshi la Hurr: “(Hali iko kama hivi) Muumin wa haki yampasa kutamani kukutana na Mola wake (kwa kutoa mhanga maisha yake) - Kwani sioni kifo

ila raha ya milele; na maisha na madhalimu ni kitu chenye kutia kichefuchefu.”10

Akiwa Karbala, akikabili jeshi la Yazid, alisema: “Enyi watu hakika Mtume wa Allah alisema: ‘Mtu yeyote ambaye anamuona Mfalme katili ambaye anaruhusu vitu vile ambavyo vimekatazwa na Allah, ambaye anapuuza jukumu lake, ambaye anapinga mwendo wa Mtume wa Allah, na anayewatendea maovu na ukatili watumishi wa Allah - na mtu yule hafanyi chochote, kwa matendo au kwa kusema, kubadilisha ile hali, basi itakuwa haki kwa Allah kumuweka sambamba na mtawala yule dhalimu katika siku ya hukumu’.”11

1. Dhana ya Imamu Husein kuwa mrithi wa viongozi wote wa Ki-Mungu imechukuliwa kutoka Ziyarat Waritha aliyoifundisha Imam Ja’far (a.s.) kwa Safwan. Tazama Mafatihu ’l-Jinan ya Sheikh Abbas Qummi.

2. Qu’ran Tukufu (3:97)

3. Ibn Abi ’l-Barr, al-Isti’ab fi ma’rifati-s-Sahabah, Juz.4. Cairo (katika juzuu nne) n.d., uk.1679.

4. Ibn Abi ’l-Hadid, Sharh Nahju ’l-Balagha, J.16 Cairo 1959. uk 136

10

5. Sibt lbna ’l-Jauzi, Tadhkirah Khawasil-Ummah, Tehran n.d., uk.261, at-Tabari, Ibn Janriri; Tarikhu ’l-Umma wa ’l-Muluki, Juz.13, Laden 1890 uk.2174,

6. Sibt lbna ’l-Jauzi, op. cit., uk. 291.

7. Sayyid ibn Ta’us, Maqtalu ’l-Husayn, 10-11.

8. Al-Khatib al-Khawarazmi, Maqtalu ’l-Husayn Juz.1 uk.88.

9. Shaykh al-Mufid, Kitabu ’l-Irshad, (kilichotafsiriwa na Dr. I. K. Howard), uk. 305.

10. Sayyid ibn Ta’us, op. cit .. uk. 32033.

11. Ibnu ’l-Kathir, al-Kamil fi ’t-Tarikh. Juz.4. 1385 A.H.

*****

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)ASEMA:

1. Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain.

2. Hao (Hassan na Husain) ni maua yangu katika dunia.

11

USHIRIKIANO KATIKA KUJITOLEAMUHANGA

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Imetafsiriwa na:Bw. Mohsin M. R. Alidina

Hafla hii ya siku ya leo inaadhimisha tukio adhimu la kujitolea muhanga kwa kundi la mawalii wa Mwenyezi Mungu takriban miaka arubatashara elfu iliyopita katika jangwa la Karbala kandoni mwa mto wa Furati katika nchi ambayo leo inajulikana kwa jina la Iraq. Tendo la kundi hila ni la pekee katika tarehe ya mwanadamu tangu kuumbwa kwake. Ufaridi wa tendo hila utawadhirika iwapo tutazingatia historia ya dini. Tukizingatia historia ya dini tutaona kuwa kabla ya enzi ya Mtume Ibrahim (a.s.) watu hawakuwa wanaelewa dhana ya kujitolea muhanga kijumla kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mfano unaojitokeza wa kundi lililohirimia kuvumilia mashaka na misiba ili kuendeleza ujumbe wa Mungu, kundi lililoazimia kutoa muhanga

kila raha na faraja za dunia waliokuwa nazo ili kulinda na kutangaza ukweli, kundi lililohiari kustahamili madhila na mateso ili kuhakikisha kuwa beramu ya dini imesimama imara. Dhana hizi zilikuwa ngeni kwa mitume wa sabiki.

Nia ya utoaji muhanga wa roho ya Mtume Ismail ilikuwa ndiyo mara ya kwanza ambapo watu wa familia ya Mtume mmoja walipokuwa tayari kwa hiari yao kujitolea maisha yao ili kukamilisha mipango ya Mtume aliyehusika. Kabla ya Nabii Ibrahim mitume watatu wanajulikana sana: nao ni Nabii Adam, Nabii Idris na Nabii Nuh. Miongoni mwa hirimu wa Nabii Ibrahim (a.s.) linapatikana jina la Nabii Lut.

Nabii Adam hakuwa na haja ya kutoa muhanga katika njia

12

ya Mwenyezi Mungu. Kazi yake ilikuwa kulea wanae na kuwafanya wawe waja watiifu wa Mwenyezi Mungu. Lakini tunaona kuwa alikuwa peke yake katika juhudi hizi. Jamii alimoishi Mtume Adam (a.s.) haikuwa na utata na mazingira yalikuwa hayana uovu. Nabii Adam alikuwa na matumaini kuwa wanae watamhami katika kutekeleza kazi yake. Lakini, Qabil kavunja miiko kwa kumwua ndugu yake Habil. Hata Bibi Hawwa haonekani kuwa alichangia katika juhudi hizo za Nabii Adam. Kadhalika, hakuna ushahidi uonyeshao kuwa familia ya Nabii Idris ilishirikiana naye katika kutekeleza kazi yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Baadaye akafuata Nabii Nuh (a.s.). Nabii huyo alikabidhiwa wadhifa wa kuwarejesha kwenye haki na wema watu waliopotoka. Kwa muda wa miaka 950, Nabii Nuhu alisarifu nguvu zake katika kuwafahamisha watu ya kuwa jaha zao za kimali na kiroho zilitegemea jinsi walivyofuata njia ya haki iliyoteuliwa na Mwenyezi Mungu. Lakini juhudi zake hazikufana. Mwito wake kwa watu wake kutenda wema

ulijibiwa na utwezo na utani na ujira wa juhudi zake ulikuwa kupigwa mawe na magongo.

Nabii Nuhu (a.s.) alivumilia mashaka na mateso peke yake. Familia yake na marafiki zake wakamtupa mkono. Licha ya hayo, mwanae akaasi na kukata uhusiano na familia yake. Huyu ni mwana yule ambaye Mwenyezi Mungu katika Suratul Hud aya ya 46 alimwasa Nabii Nuhu asimwingilie kati wala kumwoombea shufaa kwa Mwenyezi Mungu. Pia tuwaangalie wanae ambao walimwamini. Sam, Ham na Yafeth walimwamini Nabii Nuhu kama walivyofanya watu themanini wengine. Hawa kufanya la ziada wala la upungufu. Hatuna ushahidi wowote wa kuthibitisha dai lolote la kuwa wana hao watatu walimsaidia baba yao katika jitihada zake za kuendeleza dini ya Mwenyezi Mungu. Mkewe Nabii Nuhu akatokea kuwa jasusi wa maadui wa Nabii Nuhu na kuwafichulia siri za Nabii huyo. Hayo ya thibitishwa na aya ya 10 ya Suratul Tahrim.

Katika hali kama hii hatuna budi kumwongezea Nabii Ibrahim

13

sifa moja nyingine mbali na kuwa alikuwa Mtume Khalili wa Mwenyezi Mungu. Sifa hii ni kuwa alipata msaada kamili wenye ikhlasi kutoka kwa familia yake katika kutimiza wajibu aliopewa na Mwenyezi Mungu. Tukio la nia yake ya kutoa muhanga roho ya mwanae lsmail lilikuwa mfano wa kwanza wa dhana hii ambayo tunaizungumzia usiku huu wa leo, yaani utoaji muhanga wa pamoja. Katika Qur’ani Takatifu, Mwenyezi Mungu asema:“Na Ismail alipofika umri wa kufanya kazi naye, yeye (yaani Nabii Ibrahim) akasema: “Ee mwanangu! Bila shaka nimeona katika ndoto yangu kuwa ninakutoa muhanga; fikiria hilo kisha (nieleze) nini uamuzi wako?” Hapo (Ismail) akasema: “Ee baba yangu! Fanya lile uliloamrishwa Mungu akipenda, utaniona kuwa nikiwa miongoni mwenye subira.” (Surah Al-Saffat: 102).

Kwa kushauriana na Ismail na kumpa fursa ya kuamua Nabii Ibrahim akalibadilisha tukio liwela mafanikio ya pamoja. Iwapo Nabii Ibrahim angetekeleza amri hiyo pasi kumshauri Ismail, basi tukio hilo lingekuwa la mafanikio

yake binafsi bila ya Ismail kuwa na hisa yoyote ile. Lakini sasa tukio hili limedhihirisha uimara, ubora wa khulka. subira na ustahamilivu wa Ismail, sawa na imani na uchaji Mungu wa Ibrahim (a.s.).

Katika zama za Nabii Musa, ushirikiano huu ulipita hadi ya familia na kuingiza kabila zima la wanae Ismail wakiungana chini ya kiongozi mmoja, kama tujuavyo kutokana na historia na maelezo ya Qur’ani Takatifu. Hivyo daira ya ushirikiano ilipanuka kuanzia ukoo kufikia hadi kabila. Lakini inafaa kukumbuka hapa kuwa ushirikiano wa Bani Israil ulikuwa wa kigeugeu na daima kulikuwa na hatari ya kuondolewa ghafla.

Nabil Isa alitumwa kazi ya kuendeleza juhudi za Nabii Musa miongoni mwa wana wa Israeli kama vile alivyotamka yeye mwenyewe kuwa aliletwa kuja kuwaokoa Bani Israel waliopotea. Taba’an, wasaidizi wake walikuwa wana wa Israeli na daira ya ushirikiano ikabaki vile alivyoacha Nabii Musa, pasi kuongezeka.

14

Hapo ikafuata zama adhimu za Mtume Muhammad (s.a.w.). Kutokana na uongozi wake, ushirikiano katika kuimarisha dini ya Mwenyezi Mungu uliongezeka na kutanda katika eneo kubwa ukikiuka tofauti za kikabila, rangi, utaifa na lugha.

Wafuasi wake Mtume (s.a.w.) waliunda udugu wa kiulimwengu. Baada ya hapo hapajawa na nafasi tena ya upanuzi ama katika eneo au masafa.

Hata hivyo bado kulikuwa na fursa ya kuongeza sifa ya ushirikiiano huo kwa kuimarisha na kuijadidi imani ya mfuasi kufikia daraja lile ambalo lingefanya kundi zima liwe limezama katika huba ya Mola Mwenyezi Mungu. Hivyo, hali ilikuwa haijafika bado ambayo rifaa ya kiroho ingewafanya Waislamu wawe nafsi moja. Kimwili wangekuwa wengi, bali nafsi zao zingeungana chini ya beramu moja ya Uislamu. Maoni yao, hamasa zao na fikra zao zingeungana kuwa moja. Hali ilifika nusu karne baada ya kufariki Mtume (s.a.w.). Naam, hali hii ilifika huko

katika jangwa la Karbala chini ya uongozi wa Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.). Kama walivyoeleza wanazuoni wengi, miongoni mwao wakiwa Imam Bukhari, Imam Muslim, Ibne Maja’a na Imam Ahmad Ibne Hanbal.

Mtume Muhammad alisema: “Husain ametokana nami na mimi nimetokana na Husain.”

Hapa inafaa tuelewe maana ya usemi huu wa Mtume (s.a.w.). Usemi huu una maana kuwa Mtume (s.a.w.) atueleza kuwa urithi wangu, ujumbe wangu na kazi yangu haitakamilika bila ya Husain. Hivyo, Imam Husain ndiye aliyelinda, kuihami na kuiokoa dini ya Mwenyezi Mungu ambayo aliteremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w.).

Juhidi, jasho na damu ya Mtume vingepotea iwapo mjukuwe asingejitolea muhanga na kupambana dhidi ya uonevu, udhalimu, mateso, maovu, hila, njama na juhudi za kuufuta Uislamu zilizofanywa na Yazid ibne Muawiya ambaye wanahistoria kwa kauli moja wameeleza kuwa alikuwa Sharibul Khamri na mwenye

15

kusema kuwa hapakuteremshwa wahyi wala Qur’ani bali Banu Hashimu walibuni habari zote. Kauli yake ilikuwa kauli ya kutaka kukadhibisha na kuangamiza kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na kuwarejesha Waislamu kwenye zama za Jahiliyah.

Hatimaye, ukawaida wakati ambapo sura ya “Utoaji Muhanga wa Pamoja” ikadhihirika uliwenguni; Imam Hussein akaja Karbala akifuatana na kundi la mchanganyiko wa wanawake na wanaume, vijana barobaro na vijana wadogo, wazee na vijana shababi. Pamoja nao alikuwa na mtoto mmoja mchanga pia. Kundi hili lilikuwa la watoto, wake, ndugu, jamaa, marafiki na masahaba.

Kadhalika, katika kundi hilo walikuwemo Waarabu, Waajemi, Wahindi na Waafrika, Walikuwemo baba na mama, wana, wajomba, wapwa, mashangazi, ami, waume na wake zao, alimuradi kila aina ya uhusiano wa ukoo uliwakilishwa. Ukoo, kabila, rangi na dini zilikusanyika mahala pamoja. Wote hao wakaja na azma ile ile moja ambayo alikuja nayo

Imam Hussein (a.s.). Nyoyo zao ziliakisi moyo wa Hussein, fikra na hisia zao ni zile za Hussein. Vitendo vyao vikaiga vile vya Hussein na mwenendo wao ulithibitishwa na muhuri wa ukabilifu wa Hussein (a.s.).

Hapo mwanzoni tulitaja ya kuwa Nabii Ibrahim akampa mwanae fursa ya kujiamulia. Vile vile, Imam Hussein (a.s.) akawapa jamaa na marafiki fursa ya kujiamulia huko Karbala. Usiku ule wakuamikia Siku ya Ashura, tarehe 10 Muharram. Imam Hussein akawakusanya wote na kuwaeleza kuwa wangeamikia kifo na kuwapa fursa ya kuondoka ili kuokoa maisha yao. Hebu turudie Jibu la Ismail kwa baba yake: “Ee baba yangu! Fanya ulivyoamrishwa. Mungu Akipenda, utanikuta miongoni mwa wenye subira.” Kauli hii ya Ismail inaonyesha kuwa alichukulia amri hiyo kuwa ni maafa ambayo angeyakabili kwa subira. Lakini majibu aliyopewa Imam Hussein na wafuasi wake ni tofauti.

Mwanae Imamu aitwaye Ali Akber akamwambia baba yake: “Kwa vile tuko kwenye njia ya Haki basi sijali mauti.”

16

Mpwa wake aitwaye Kassim alipoulizwa na ami yake, Imam Hussein (a.s.) jinsi aliivyofikiria mauti, akasema: “Ee Ami yangu, kwangu miye mauti ni tamu kuliko asali.” Mtoto mchanga wa Imam Hussein, mtoto wa miezi sita, Ali Asgher alipokuwa anakata roho baada ya kupigwa mshale wa Hurumala akatabasamu, kana kwamba alikuwa anamhakikishia baba yake kuwa furaha yake ilikuwa katika kuingia midomoni mwa mauti kwa ajili ya Huba ya Mwenyezi Mungu.

Hivyo, usiku huu wa leo tunapoadhimisha ukumbusho

huu wa Karbala tunapaswa kuwapongeza mashahidi wa Karbala na kuwashukuru kuwa wametuokolea Uislamu na kuuhuisha mti wa Uislamu aliopanda Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa taabu na mashaka ya miaka ishirini na mitatu. Usiku huu wa leo kila mwanadamu anapaswa aelewe ihsani aliyofanyiwa na Sayyidu Shuhadaa na wafuasi wake huko Karbala. La sivyo, tungekuwa na sura na umbo la wanadamu lakini khulka, mienendo, tabia na sira zingekuwa za kiwahshi.

Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuhu.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)ASEMA:

(EWE HUSAIN), WEWE U SAYYID, MWANA WA SAYYID, NA NDUGU WA SAYYID; WEWE UTHIBITISHO (WA MWENYEZI MUNGU) NA MWANA WA UTHIBITISHO (WA MWENYEZI MUNGU) NA NDUGU WA UTHIBITISHO (WA MWENYEZI MUNGU); NA BABA WA UTHIBITISHO TISA AMBAO WA TISA WAO NI QAIM WAO: AMBAYE ATAKUWA AL-MAHDI

*****

17

MAANA YA AZADARI

Imeandikwa na:Bw. Azadar

Imetafsiriwa na:Maallim Dhikiri U. M. Kiondo

UTANGULIZI

Mara kwa mara Mubaligh wetu wamewahi kuulizwa maswali kuhusu Azadari (maombolezo) kwa ajili ya Masaibu yaliyomfika Imamu Husaini (a.s.) Mjukuu wake Mtukufu Mtume (s.a.w.) huko Karbala (nchini Iraq) kama hili:-“Kwa nini ninyi Mashia lthna-asharia mnapiga vifua vyenu kwa ngumi na kujikata miili yenu katika siku ya Ashura?”

Ili kutoajibu kamili kwa swali kama hili, tunaona afadhali tutafsiri makala iliyoandikwa na ndugu yetu Azadar wa Dar-es-Salaam, Tanzania, ambaye amelielezea vizuri jambo hili kufuatana na misingi ya kiakili ya mwanadamu.

Sina shaka mtu yeyote yule mwenye swali kama hili aisomapo makala hii hatabakiwa na shaka yoyote ile tena juu ya uzuri na falsafa iliyomo katika tendo hili - Insha-Allah.

*****Katika makala hii, ambayo naiandika hasa kwa ajili ya vijana wa Jamaat yangu, sitaki kujitia katika kazi ya kulielezea jambo linalojulikana sana. Kila Shia Ithna-asharia, mume, mke au mtoto anayafahamu masaibu ya Karbala kwa kirefu na athari zake katika Historia ya Kiislamu. Kusudi langu hasa ni kuelezea umuhimu wa kuuadhimisha Msiba wa Karbala kila mwaka na maana ya Azadari.

Katika jamii yetu tumelelewa kuamini kuwa siku 12 za mwanzoni za mwezi wa

18

Muharram ni siku za “Majlis” (Hotuba) na “Matam” (Huzuni kwa ajili ya Masaibu yaliyomsihu Imamu Husain a.s.), na kuonyeshwa kwa ujumla kwa huzuni zetu nyingi kwa kifo cha Kishahidi cha Imamu Husain (a.s.). Itakuwa ni kutofikiria, kwa mtu yeyote yule miongoni mwetu kujitia katika mambo yoyote ya raha katika siku hizi. Tunaona kama vile ambavyo kwa hakika ni lazima tuone, kuwa ni wajibu kuomboleza kwa ajili ya kifo cha mpenzi Imamu wetu, na kwa kufanya hivyo tunaendelea kuiwasha ile tochi waliyoiwasha Mashahidi wa Karbala kwa kuyatoa maisha yao, tochi inayoimulika njia ya kwendea kwenye haki, utu, mapenzi na ukarimu, vitu ambayo ndio msingi unamosimamia jengo la Ustarabu wa Kiislamu.

Tunaona fahari kuwa, ingawa zimekwishapita karne kumi na nne, bado hatujakosa nia wala hamu ya kuomboleza kwa ajili ya masaibu ya Karbala. Hakika itakuwa ni siku ya huzuni kwa Uislamu kama tukiziruhusu fikara za kuwa Azadari haina maana. Wakati huo huo Azadari inaweza kutoa mafanikio

kidogo sana kama maana yake isipofahamika vizuri, kama ikichukuliwa kama desturi tu, na kama ikiadhimishwa kama jambo la kawaida tu.

Hakuna kitu kiwezacho kuwa hatari kubwa kwa imani zetu na dini yetu kuliko zile fikara za kuwa kile tukifanyacho, na kile tukiadhimishacho ni mapokeo tulioyarithi bila ya kuyafikiria maana yake na faida yake.

Imamu Husain (a.s.) aliyatoa maisha yake kwa nia moja katika hali ya kimasaibu ili kuusimamisha Uislamu. Tunaidumisha kumbukumbu ya masaibu ya Karbala kwa machozi na kwa kujitia kabisa katika huzuni. Kwa jinsi hii, tunajikumbusha sisi wenyewe na ulimwengu mzima kuwa ile misingi lilimojengewa jengo la dini yetu ina faida zaidi kuliko maisha yetu, na kuwa kama misingi hii inakuwa katika hatari ya Kuharibiwa ni lazima tusimame kuihami misingi hiyo, hata kama ikiwa ni kwa kuyatoa maisha yetu.

Wale miongoni mwetu wanaojifanya kuwa wanajua zaidi

19

mambo ya kisayansi huwa mara nyingi wanauliza, “Nini maana ya Azadari, kisayansi? Kwa nini tusikumbuke na kuifuata misingi ya Uislamu tu? Kwi nini tuzieleze huzuni zetu na masikitiko yetu namna hiyo kwa mambo yaliopita karne nyingi zilizopita?” Ninalo jibu moja tu kwa watu hao, Karbala, mahali Uislamu uliposimamia kama “Phoenix” (Ndege wa hadithi) umeziathiri sana fikara za mwanadamu, unayadhihirisha sana matokeo ya maovu, kiasi ambacho ile kumbukumbu ya Masaibu ya Karbala yanayo nguvu ya kutosha kuzisafisha akili za mwanadamu kutokana na athari mbaya.

Mwanadamu, kwa vyovyote vile awavyo na elimu, kwa kadri yoyote ile elimu yake iwavyo kubwa, yu kiumbe asiye na nguvu ya kitabia imtoshayo kujiepusha na athari za nguvu za uovu. Hii inauonyesha waziwazi ukweli uliopo kuwa si kweli kuwa wale walioshiriki katika kuwawa kikatili kwa wayahudi wakati vita ya Pili ya Ulimwengu walikuwa watu waliozoea kupigana na kuleta ghasia nchini. Watu waliosawiri,

waliotengeneza na waliofanya kazi katika mitungi ya hewa, madaktari waliowafanyia upasuaji usio wa kiutu, wanawake wasio na makosa, watu waliosawiri na kutengeneza mitungi ya taa kutokana na ngozi ya mwanadamu, wote hao walikuwa wale watu tuwezao kuwaita watu wenye akili nchini. Hawakufanya ukatili huu katika Zama za Mawe, wala si katika zama ambazo dunia ilikaliwa na wale watu tunaopendelea kuwaita, “washenzi”, bali ni katika kame hii hii ya utaalamu wa kisayansi na ustaarabu.

Mpaka leo, maisha ya mwanadamu bado yangali jinamizi lile lile la uovu, kunyonywa anakofanyiwa maskini na tajiri, vita, mauwaji ya kutokusudia na mauawaji ya kukusudia.

Bila ya athari ziimarishazo hisia mwanadamu hawezi kuishi kwa furaha, kwa fikara zake tu.

Bwana T. N. Rabbit, Profesa wa Elimu ya Saikolojia kwenye chuo fulani mjini London ameandika katika kitabu chake kiitwacho, “Psychology of Emotions” kuwa:-

20

“Hali ya kihisia inatokea kwanza na baadaye huja hali ya kiakili”.

Na usisahau kuwa kila kizazi ni lazima kipitie hali hii ya kihisia kabla ya kufikia utu uzima wa kiakili. Hivyo basi, haja ya kuomboleza kihisia haiwezi kupotea.

Pia huzuni humuongoza mwanadamu kwa Mola wake. Furaha hujaribu kumtenga mwanadamu mbali na Mwenyezi Mungu, lakini huzuni na kuionyesha huzuni hiyo kwa vitendo siku zote humsogeza karibu zaidi na Muumha na Msaidizi wake.

Tena, kuwa na moyo mgumu kumelaumiwa katika kila kitabu kilichofunuliwa na katika kila falsafa ya maisha kwa sababu ni moja ya chanzo kikubwa cha dhambi na dhulma. Azadari (kumuombolezea Imamu Husain a.s.) ndio dawa halisi ya maradhi haya ya kiroho.

Azadari ndio roho ya hisia zenye afya nzuri ambayo hutuambatanisha na Uislamu na misingi yake. Ni roho ya Masaibu ya Karabala ambayo huimarisha

roho ya Uislamu. Kwa kila tone la machozi lidondokalo kutoka machoni petu tunaahidi kuzitii amri za Mwenyezi Mungu. Roho zetu za dunia hii zinapokataa kufunga katika mwezi wa Ramadhani, Masaibu ya Karbala yatatukumbusha kiu ya Bwana Ali Asghar. Utii wetu kwa Uislamu unapodhoofika, Masaibu ya Karbala yatatukumbusha utii wa Bwana Abbas. Tunapokabiliwa na uchaguzi baina ya mema na maovu, Masaibu ya Karbala yanatukumbusha uchaguzi wa Bwana Hur (aliyechagua kulitoka jeshi la Yazid na kuacha Uamiri Jeshi wa Jeshi hilo na kujiunga na Imam Husain (a.s.) bila ya kujali matokeo ya Uchaguzi wake huo). Masaibu yanapoyashinda maisha yetu, Masaibu ya Karbala yanatukumbusha uvumilivu na ushupavu wa Imamu Husain (a.s.) wakati alipouchomoa mkuki uliovunjika kutoka kifuani mwa Bwana Ali Akbar.

Imamu Husain (a.s.) alipoku-wa safarini kwenda Karbala alisema: “Kama dini ya (Mtume) Muhammad (s.a.w) haiwezi kuendelea ila kwa kukitoa mhanga kichwa changu, basi

21

upanga nauje ukichukue”.

Shairi hili la lmamu Husain (a.s.) linatukumbusha tusirudi nyuma katika kujitoa mhanga wowote ule katika kuutangazia Uislamu wakweli miongoni mwa wale ambao bado hawajaufahamu vizuri.

Hivyo Azadari ni jambo muhimu na tusizidhanie faida zake kuwa ni kidogo. Wakati huo huo tusizifikirie zile siku kumi na mbili za mwezi wa Muharram kuwa ni wakati wetu wa kuburudishwa kwa ufasaha wa lugha (uliotumika katika tenzi za huzuni). Majlis (Hotuba) ndio njia ya kufundishia na “matum” ni njia yetu ya kudhihirishia

mapenzi yetu ya kweli kwa wale waliojitoa kuangamia iii tuweze kufaidika kutokana na Ustarabu wa Kiislamu. Siwezi hata kuliwazia kosa baya zaidi dhidi ya kumbukumbu ya Imamu Husain (a.s.) kuliko ile fikara ya kuwa tunahudhuria katika majlis si kwa kupata maelezo ya kielimu bali kuburudishwa na ufasaha wa lugha (wa hizi tenzi na majlisi). Yeyote yule awaye na mawazo kama haya hawezi kudai kuwa Azadar ya Imamu Husain (a.s.).

Mwenyezi Mungu na atupe hekima ya kuielewa maana halisi ya Azadari na uwezo wa kuifanya Azadari katika miaka ijayo kwa nguvu kubwa zaidi kuliko ile ya miaka iliyopita --Amin.

IMAM SHAFII (A.R.)ASEMA:

1. IKIWA DHAMBI ZANGU NI KUWAPENDA WATOTO WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.)BASI NI DHAMBI AMBAZO SITATUBIYA.

2. NI NANI ATAKAYEMFIKISHIA HUSSEIN UJUMBE WANGU NA HATA KAMA NYOYO ZATUKIA?

*****

22

MUHHARAM

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Ali Naqi Naqavi

Imetafsiriwa na:Maallim Dhikiri U. M. Kiondo

Bismillahir Rahmaanir RahimAllahumma Swalli Alaa Muhammadin Wa Aali

Muhammad

“HUSAYN, HUSAYN” “HUSAIN, HUSAYN”.Ni nani miongoni mwetu amaye bado hawahi kuzisikia kelele za huzuni na vilio vya maombolezo kwenye miezi ya Muharram? Vilio hivi vinatupiliwa hewani na kikundi cha watu, wakimwombholezea Imamu Husayn (a.s.) na Mashahidi wengine wa Karbala. Watu hawa hutembea kwenye maandamano, wakienda pole pole, wakisimama kwenye sehemu mbali mbali, wakipiga vifua vyao na wakisoma tenzi mbalimbali.

Watu hawa wanayatenda yote haya kwa kumwombolezea Imamu Husayn (a.s.) ambaye, mnamo tarehe 10 ya mwezi wa Muharram, mwaka 61 Hijiriya aliitoa “Dhibihul Adhiim” (Dhabihu Kuu) kwa ajili ya

kuuhami ukweli, akizipinga nguvu za jeuri zilizokuwemo kwenye Serikali ya zama zile.

Hawa wenye kumwombalezea Imamu Husayn (a.s.) wanaitwa “Azadar” (nena litokanala na nena “Aza” lenye maana ya kuomboleza) na matendo yote yatendwayo kuhusiana na maombolezo haya, kwa pamoja yanaitwa “Azadari.”

Hii kumbukumbu isiyopotea ya kuwakumbuka hawa Mashahidi Watukufu na ombi la kuibakisha hai kumbukumbu hii, lililomo nyoyoni mwao wale wote wenye kuuamini uhuru na haki ya dhamira ni alama ya msingi isioonekana lakini lio bora zaidi na ulio kamili ambao, Mashahidi kama vile Imamu

23

Husayn (a.s.) na Wafuasi wake waoapozimulika kurasa za historia zenye kufifia, sauti wanayoitoa si sauti ya watu wachache bali ni sauti ya wanadamu wote iliyodhamiriwa kuyadumisha mapinduzi ya Serikali, na zitaendelea milele kutoa mwanga nyoyoni mwao wale wenye kuamini utu wema.

KWA NINITUNAOMBOLEZA?

Hebu ifikirie bali aliyokuwamo yule mtu mwenye cheo kikuu zaidi cha kiroho (Imamu Husayna.s), akipigania lengo tukufu la ukweli, akizungukwa na majeshi ya watu wagomvi na jeuri; wafuasi wake ni wachache, na maadui wake ni wengi mno. Maadui hao wamewakingia watukufu hawa maji, hivyo wakadhamiria kuwaua kwa kiu, lakini vivyo wapoiganaji hawa wasiotishika wanaendelea kuyatoa mhanga maisha yao kwa ajili ya lengo lao tukufu. Na Amiri-jeshi wa hawa waumini na askari wachache waliojitoa mhanga (askari waliouawa na jeshi la hawa watu jeuri na wagomvi, ikiwa ni pamoja na mtoto mdogo wa umri wa miezi sita na watoto wengine wengi wasio na hatia) ikabidi

kuwatazama wakifa mmoja baada ya mwingine, huku midomo yao ikikosa japo tone moja tu la maji, na hizo koo zao zilizokauka zikikatwa na kuchomwa kwa panga zenye sumu; wake wakiwa wajane na watoto wakiwa yatima.

Kutokana na hali hii, Je, nyoyo za kibinadamu na za kiroho zitahisi vipi kutokana na hisia za kiroho na ukamilifu wa ukweli wake mtu? Kwa kawaida, iwapo mtu atakuwa na uwezo wa kumsaidia Shahidi yule atajitoa mhanga yeye mwenyewe kulipigania lengo hili. Kisha basi, kule kutoshika kutokanako na kuutimiza wajibu wake, kunaweza kukawaka kwenye midomo yake. Lakini kama kutokana na sababu fulani fulani hawezi kufanya hivyo, moyo wake utamuuwa na kule kukosa kwake msaada kutatoa, kutoka kwenye moyo wake unaoungua, vilio na machozi.

Kukata tamaa mbele ya matatizo, ni dalili ya moyo dhaifu, lakini kama huna hofu yoyote juu ya maisha yako, na ukaiombolezea hasara iliyokupata kutokana na kukosa uwezo wa kuwasaidia na ukatiririkwa na machozi

24

mkakipiga kifua chako, itakuwa ni dalili ya hisia madhubuti kwamba unauona muhimu wa lengo walilolipigania, ili mradi tu onyesho hili la huzuni haliwi desturi isiyo na uhai ndani yake, bali badala yake, inasimamia kwenye msingi wa thamani ya huduma waliyoitoa watu hawa katika lengo la ubinadamu na uhuru.

MAJLIS:

Mkutano ambao twayakumbuka malukio ya kufa kishahidi, kwa Imamu Husayn (a.s.) pamoja na wafuasi wake na matatizo na taabu nyinginezo walizozikabili watu wa nyumba (familia) yake waliobakia hai kwenye Mhanga wa Karbala, unaitwa “Majlis”.

Baada ya Mhanga wa Karbala, mikutano hii ilikuwa ikifanyika pasi na matayarisho ya kabla na kila alipokaa mteswa Majlisi iliundwa. Majlisi zilizofunywa na Maimamu (a.s.) waliofuatia baada ya Imamu Husayn (a.s.) zilikuwa za aina hii. Marafiki na Wafuasi wa Imamu (a.s.) walikusanyika na kumsikiliza Imamu (a.s.) akiyahadihtia matukio hayo yenye kuhuzunisha, na hiyo ilikuwa ni “Majlis”. Wakati

mwingine washairi waliwajia Maimamu na tenzi ambazo walizisoma mbele ya Maimamu hao na wafuasi wao, na hiyo nayo iliitwa “Majlis”. Wakati mwingine Imamu (a.s.) aliwatayarisha wanawake wa Nyumha yake kukaa nyuma ya pazia kuzisikiliza tenzi hizo. Kwenye Majlisi za aina hiyo yalikuwako maombolezo tu. Baadaye zilipopatikana zana za kutosha za kufundishia dini, na mafunzo ya kidini yalipokuwa yakitolewa misikitini, na kisha shule zikafunguliwa, mtindo wa Majlis nao ukapata aina fulani ya mabadiliko na maendeleo. Sasa mikutano ikaanza kukua, ikiwa inafanyika hadharani, hata tarehe sasa zikaanza kutajwa kabla yake, na taarifa zikaanza kutolewa kabla ya mikutano hiyo kufanyika ili kuweza kuwakusanya wasikilizaji wengi kiasi walivyoweza kupatikana. Zaidi ya ile desturi ya kawaida (ya kumwombolezea Imam Husayn a.s. tu), mambo mengineyo vile vile yaliongezewa kwenye hotuba zilizotolewa kwenye mikutano hiyo. Hadi hivi sasa, maombolezo hayo yamekuwa kawaida iliyo zana muhimu zaidi katika kufundishia mafunzo ya kidini na kiroho.

25

TA’ZIAH:

Ta’ziah ni nakala (mfano) ya Kaburi la Imamu Husayn (a.s.) iliyotengenezwa kwa dhahabu, fedha, shaba nyeupe au mbao. Nakala hii, kwa sababu za kiuchumi na wepesi, yaweza kutengenezwa kwa miawa, karatasi ya rangi na jaribosi (namna ya karatasi yenye rangi ya fedha, dhahabu, n.k.). Desturi ya kuwa na Ta’ziah kwenye Majlisi hizi imeanzia India na inafahamika kuwa ilianzishwa na Mfalme Tamerlane wa huko. Hiki ni chombo cha faraja cha kuizimishia, kwa kiasi fulani, kiu ya wenye kuabudu, ya kutaka kulifika kaburi la Imamu Husayn (a.s.), inaheshimiwa kwenye kumbukumbu hii ya kiuchamungu.

ALAM:

Neno “Alam” lina maana ya bendera ya jeshi linalopigana. Mshika bendera wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ni binamu na Mrithi wake, Saidina Ali bin Abi Talib (a.s.). Kwenye vita ya Karbala, mwana aliye bora wa Baba aliya bora, Saidina Abbas Ali bin Abi Talib (kumbukumbu yake na idumu milele) ndiye aliyekuwa

mshika bendera wa Imamu Husayn (a.s.). Kutokana na kazi yake hii, Saidina Abbas (a.s.) alikuwa mtu wa mwisho kuruhusiwa na huyu Amiri-jeshi mpweke (Imamu Husayn (a.s.)) kuuingia uwanja wa vita kwenda kupigana. Jinsi Saidina Abbas (a.s.), alivyoyaendea maneno ya “Alam” (bendera ya vita) na “Alamdar” (mshika bendera ya vita) ni moja ya Tochi za Karbala, na katu Historia, haitaweza kusahsu jinsi Saidina Abbas alivyoinua juu bendera ya ukweli mbele ya maelfu ya maadui. Mkono wake wa kulia ulipokatwa, aliishika bendera hiyo kwa mkono wa kushoto; ulipokatwa nao, aliishikilia bendera hiyo nzito kwa kuibabatizia moyoni pake kwa vigutu vya hiyo mikono yake iliyokatwa na akaishikilia hivyo hadi alipoanguka chini kutoka mgongoni mwa farasi wake mwaminifu. Hii ndio sababu inayoifanya “Alam”, kuwa sehemu muhimu kiasi hicho kwenye “Aza”. Ni kwa sababu ni alama ya ombi kwamba, watu wa Imamu Husayn wanawajibika kuiinua bendera ya ukweli juu zaidi. “Alama” inazielezea hisia za majuto kwa kutoweza kwetu kufa kifo cha Mashahidi pamoja

26

na kundi lile lililobarikiwa na inazipaka rangi ya kiuanaume zile safu za waombolezaji na daima kuwaitia wawe tayari kulipigania lengo lile.

MASHK:

Wakati mwingine humo kwenye “Alam” huning’inizwa kiriba (mfuko wa ngozi wa kuchukulia maji) kilichokitwa mkuki. Kiriba hiki ndicho kinachoitwa “Mashk”, nacho ni kwa ajili ya kulikumbuka tukio lililofanyika kwenye siku ile ya Ashura. Kwenye siku hiyo, Saidina Abbas (a.s.) alikwenda mtoni Furati kuwachotea maji watoto wa Imamu Husayn (a.s.) waliokuwa wakifa kiu, baada ya kukatiwa maji kwa zaidi ya siku tatu. Pamoja na taabu zote za Mshika bendera, alifaulu kuipata njia kupitia katikati ya kundi kubwa sana la maadui zake na akakijaza kiriba hicho maji. Lakini kama tulivyoeleza hapo juu, hakuweza kuyafikia mahema ya watoto hao, kwa kuwa, alipokuwa akirudi, alishambuliwa na maadui hadi wakamkata mikono yote miwili, na huku akiwa damu inamtiririka kutoka kwenye majeraha yake hayo, kile kiriba nacho walikipiga mshale na maji

yakawa yanatiririka nayo. Hapo Saidina Abbas (a.s.) akavunjikwa na moyo na akaanguka chini pamoja na ile bendera yake na kile kiriba chake katu ile “Alam” na ile “Mashk” havikutengana na hadi hivi leo vinaonekana vikiwa vimeshikana vile vile.

TABUT:

“Tabut” ni aina ya tusi au jeneza anamochukulia maiti kwenda kuzikwa. Nchini Iraq na Iran, kwa kawaida kitu hiki kinatumika kwenye “Aza”, na vile vile kinatumika huko nchini India, kwenye jimbo la Uttar Pradesh, hasa huko Lucknow na miongoni mwa jumuiya ya Kishia wa duniani kote. Kwenye historia ya Kiislamu, jeneza lilitumika kwa mara ya kwanza kwenye maziko ya Binti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) --- Bibi Fatima (s.a.) kufuatana na mapenzi na usia wake yeye mwenyewe. Ikiwa ni sehemu ya “Azadari” jeneza hutolewa likiwa ni ishara ya kwamba, kwenye tukio la Mhanga wa Karbala, maiti ya Imamu Husayn (a.s.) na Mashahidi wengine ziliachwa na watu wa jeshi la Yazid bila ya kuzikwa. Kwenye siku ya tatu baada ya Mhanga huo watu wa kabila la Asad walizizika maiti

27

za Mashahidi hao. “Tabut” ni njia fulani ya kuonyesha huzuni zetu na masikitiko yetu kwamba hatukuweza hata kuyaona maziko ya Imamu Husayn (a.s.).

DHUL-JANAH:

“Dhul-Janah” ni jina la farasi wa Imamu Husayn (a.s.) aliyetumiwa kwenye Mhanga wa Karbala. Vile vile farasi huyu anaitwa “Duldul”. Pengine kwenye maandamano ya Muharram, na pengine mwishoni mwa Majlisi, hutolewa farasi aliyefunikwa shuka nyeupe iliyonyunyiziwa matone ya rangi nyekundu huku akiwa amevikwa hatamu za vita na akiwa na upanga, ngao na pengine na mishale pia. Farasi huyu ni yule “Dhul-Janah” au “Duldul”. Kitendo hiki hufanywa kwa kumbukumbu ya yule farasi mtiifu wa Imam Husayn (a.s.) aliyembeba kwenye uwanja huo wa vita, na baada ya Imamu (a.s.) kukatwa kichwa, farasi huyu akiwa ametapakawa na damu hii tukufu kichwani mwake, aliyarudia mahema ya Imamu Husayn (a.s.) kwenda kuwaeleza wanawake wa Nyumba Tukufu ya Imamu (a.s.) kile kilichotokea huko uwanjani.

SUSU:

“Gahwarah”, ambayo vile vile huitwa “Jhula” ni pembea la mtoto susu, kitanda cha mtoto mdogo au mehdi. Kitanda hiki kinatumika kwenye Azadari ili kiwe kumbukumbu la mmoja wa Mashahidi wa Karbala aliyekuwa muhimu sana, lakini aliyekuwa na umri mdogo zaidi. Huyu ni Saidina Ali Asghar (a.s.), mwana wa Imamu Husayn (a.s.) aliyekuwa na umri wa miezi sita tu. Mtoto huyu aliukabili ukosefu wa maji ule ule walioukabili watu wakubwa wa Nyumba ya Imamu Husayn (a.s.) waliokuwapo pale Karbala, pamoja na wafuasi wao. Kutokana na kiu kali mno, Mama wa mtoto huyu hakuwa na maziwa kifuani mwake, hivyo hakuweza kumpa kitu chochote mtoto wake. Hali ya mtoto huyu ilipozidi kuwa mbaya sana na kukaribia kufa, Imam Husayn (a.s.) alimpakata mikononi mwake, akakipanda kichunguu cha mchanga wa jangwani hapo Karbala, na akalionyesha jeshi la maadui, mtoto yule na hali aliyokuwamo. Wengi wa askari hao walipouona ulimi mkavu wa mtoto yule ukigeuka geuka juu ya midomo iliyokuwa ikichomwa

28

na joto kali na kiu, walizigeuza nyuma nyuso zao na wakaanza kulia. Amiri-jeshi wa jeshi la maadui hao alipoona athari ya kuwapo kwa mtoto yule pale, kwa upande wa jeshi lake, alimwamrisha askari wake mmoja aliyekuwa katili sana, aliyeitwa Hurmulah kukiondoshea mbali kizuizi kile kilichoweza kuzaa mfarakano miongoni mwa askari wa jeshi lake. Hurmulah akachukua mshale wenye vichwa vitatu akailenga shingo nyororo ya mtoto Ali Asghar, ule mshale ukamchinja mtoto hadi ukaingia mkono wa Imamu Husayn (a.s.), kutokezea upande wa pili na mtoto akafa kishahidi. Kutokana na tukio hili “Gahwarah” au “Jhula” inakuwa miongoni mwa kitu, muhimu mno kwenye “Azadari”.

SABIIL:

“Sabiil” ni matayarisho yafanywayo kwenye sehemu mbali mbali ya kuwapatia maji ya kunywa wale wote wabahatikao kuzipitia sehemu hizo. Mwezi wa Muharram ili kuyaadhimisha mapigano ya kishujaa waliyopigana mashahidi

wa Karbala na kwamba walipigana hivyo huku wakiwa wamenyimwa maji, maji yanawekwa kwenye sehemu mbali mbali, kwenye mitungi ya udongo ili watu wanywe. Kila mwenye kunywa humo anakumbushwa taabu kali mno aliyoikabili Imamu Husayn (a.s.) pamoja na wafuasi wake na watoto ambao hawakuweza kupata hata tone moja la maji kwa muda wa siku tatu mfululizo, na ambaa walilazimika kulivumilia kwa taabu kubwa mno joto kali la jangwa hili la Uarabuni.

Hivyo tunaona kuwa wenyeji wa nchi mbali mbali humwombolezea Imamu Husayn (a.s.) kufuatana na desturi zao za kuomboleza, lakini lengo lililomo kwenye desturi zote hizi ni lile lile la kuzidhihirisha na kuzidumisha fikara za Imamu Husayn (a.s.) na kuyachukua maneno ya Imamu Husayn (a.s.) kuwa hamasa (motto) yetu na kuwaelezea watu maombolezo halisi ya:

“Kufa kwenye utukufu ni bora zaidi kuliko kuishi kwenye fedheha”.

*****

29

DHULMADHIDI YA AHLUL-BAYT (A.S.)

Imeandikwa na:Shaykh Musabaha S. Mapinda

BISMILLAHIR RAHMAANIR RAHIM

Mema na mambo matukufu ya nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.) ni mengi mno. Kuyataja kikamilifu itachukua muda mrefu, na kwa kweli siyo rahisi kukamilisha utajo wa sifa za kikazi hiki kitukufu.

Hebu na itoshleze kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na Akutakaseni sana sana.” (Al-Ahzab. 33:33)

Iliposhuka aya hii Bwana Mtume (s.a.w.) akiwa ndiye mfasiri bora wa maana na tafsiri ya Qur’an, alitambulisha makusudio ya kushuka aya hii; licha ya kusema, alionyesha tendo la kuifasiri bayana.

Mama Ummu Salama mkewe Bwana Mtume (s.a.w.) anaeleza namna ilivyokuwa kama walivyopokea wanachuoni wa Hadith, mabwana Tirmidhi,

Ibnu Jariri, al-Hakim, al-Baihaqii na wengineo. Anasema: “Ndani ya nyumbu yangu ilishuka (Aya isemayo): ‘INNAMAA YURIIDULLAHU LIYUDHIIDBA ANKUMU RIJSA AHLAL-BAIT’, hali yakuwa Fatima yupo nyumbani humo na Ali na Hasan na Husein.” Anaendelea Ummu Salama: “Mtume wa Mwenyezi Mungu akawafunika wote hawa kwa nguo (Kisaa) aliyokuwa nayo kisha akasema, ‘Hawa ndiyo watu wa nyumba yangu, basi (Ewe Mola) waondolae uchafu na uwatabse sana sana’.”

Nao mabwana Al-Khatib na Ibnu Mar-Dawaih wamepokea kutoka kwa Abu Said Al-Khudriy kama ifuatavyo: “Mtume aliposema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndiyo watu wa nyumba yangu, Ewe Mwenyezi Mungu! Waondolee uchafu na uwatakase sana sana’, Mama Ummu Salama alisema

30

kumwambia Mtume, ‘Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu! Basi nami ni katika wao,’ Mtume akasema; ‘Wewe una mahali pako nawe umo katika wema’.”

Kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Bwana Mtume (s.a.w.) kama tulivyoashiria hivi punde, ni wazi kabisa kwamba Bibi Fatima (s.a.), Imamu Ali (a.s.) na watoto wao Hasan na Husein (a.s.) pamoja na Bwana Mtume (s.a.w.) ndiyo Ahlul-Bait (nyumba ya Mtume) walioondolewa uchafu na kutakaswa sana sana.

AHLUL-BAIT NDIOVIONGOZI WA UMMAT

WA MUHAMMAD

Sahaba, Bwana Ibnu Abbas anasema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) mwenye kufurahishwa kuishi kama maisha yangu na kufa kama kifo changu, na ili apate kuishi katika Bustani ya milele aliyoiandaa Mola wangu, basi na amtawalishe Ali baada yangu, na pia afuate uongozi wa watu wa nyumba yangu, baada yangu, kwani wao ni kizazi changu, wameumbwa kutokana na umbile langu, na wamepewa fahamu zangu na Elimu yangu, basi ole wao wenye kukanusha

ubora wa (Ahlul-Bait) katika umma wangu, wenye kuyakata ndani yao mahusiano yangu, Mwenyezi Mungu asiwape maombezi yangu (siku ya Qiyama)’.” Taz. Kanzul Ummal. Hadith Na. 3819.,

Kwa mujibu wa Hadithi hii Bwana Mtume ametuonyesha ubora wa watu wa nyumba yake, na kututaka tufuate uongozi wao baada yake, na ametuonya dhidi ya kuwa wapinzani wa fadhila na heshima walizotunukiwa watu wa nyumba ya Mtume. Isitoshe, Bwana Mtume (s.a.w.) ameonya wazi kwamba kwa kuwaendea kinyume hao Ahlul-Bait Mwenyezi Mungu asiwafikishie uombezi wake wote watakaojishughulisha na upinzani kwa nyumba yake.

Kwa kuongezea zaidi hadhi ya kizazi cha Mtume (s.a.w.) mabwana Ahmad bin Hanbal na An-Nasaiy wamepokea kama ifuatavyo:-Kutoka kwa Zaid Bin Arqam amesema, Bwana Mtume alitoa hotuba akasema, “Hakika mimi ninaacha ndani yenu vitu vizito viwili. Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, watu wa nyumba yangu, na hakika hivi vitu viwili havitaachana

31

mpaka vinifikie kwenye Haudh. Basi tazameni ni vipi mtanifuata katika viwili hivyo.”

NYUMBA YA MTUMEMASHAKANI

Baada ya kuisoma aya ya 33:33 na kuona tafsiri yake kama alivyoifasiri Mwenyewe Bwana Mtume (s.a.w.) na pia Hadithi zilizoonyesha Utukufu wa nyumba hiyo, na wajibu wa kuiandama ili ituongezee, inahuzunisha sana kuona kwamba baada tu ya Mtume (s.a.w.) kufariki Waislamu wa zama hizo walianza kuitia mashaka na msukosuko Nyumba ya Mtume wetu (s.a.w.).

Baadhi ya misukosuko hiyo ni pamoja na kuuawa kwa mashujaa hao kutoka kizazi cha Nyumba ya Mtume (s.a.w.), mapema kabisa aliuawa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) ambaye ndiye Mrithi wa kwanza wa Bwana Mtume (s.a.w.).

Ujasiri gani uliowafanya watu hao kushika silaha na kumwua Imamu Ali (a.s.) ambaye Mtume (s.a.w.) amesema, “Mimi ndiye Mji wa Elimu na Ali ndiye mlango wake, basi yeyote atakaye na aje mlangoni.”

Pia ziko riwaya zisemazo kuwa, hapana sahaba yeyote wa Mtume aliyekuwa akithubutu kusema niulizeni, ila Ali (a.s.) peke yake.

Kama kwamba Waislamu hao hawakuwa na haja ya Elimu kutoka kwa Imamu Ali (a.s.) wakamwuua. Hakika wametudhulumu, tunaamini kabisa ya kuwa alikuwa na mengi ya kutufundisha.

Na ukitazama tena unawakuta ni hao hao Waislamu waliomsikia Mtume akisema “Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa Peponi.”

Lakini Muawiya anafanya njama za kumwua Imamu Hasan bin Ali bin Abi Talib (a.s.) kwa kumtilia sumu ndani ya chakula, na anafanikisha azma hiyo kwa kumtumia mkewe Imamu Hasan (a.s.) baada ya kumuahidi chungu ya mapesa na kwamba angemuoza kwa mwanawe aliyekuwa akiitwa Yazid.

Katika ukatili usio na mfano Waislamu hao, kwa jina la Uislamu, mwaka wa sitini na moja Hijiriya wanamwua mauaji ya kinyama bila huruma mjukuu wa Mtume Imamu Husein (a.s.).

32

Ni miaka isiyopungua hamsini tu tangu Bwana Mtume kufariki, tendo lao hili wanalitenda dhidi ya Mtume na kizazi chake. Ni wazi kabisa mauaji haya yalipangwa, kwa sababu inaonekana kana kwamba, walikuwa wakipeana usia wa kukiangamiza kizazi cha Mtume (s.a.w,) wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu (na Mwenyezi Mungu anakataa mpaka aitimize Nuru yake).

IMAMU HUSEIN (A.S.)NA YAZID

Hapo kabla tumesema kwamba, “Yaonekana wazi jinsi kizazi cha Mtume kilivyoandamwa kuwa ni usia uliowekwa baina ya wauaji na wanyanyaaaji hao.”

Jambo hili ni kutokana na jinsi ambavyo Muawiya alivyokuwa kajizatiti dhidi ya Imamu Ali na Imamu Hasan (a.s.).

Baadaye tunamuona Yazid bin Muawiya alivyo muandama Imamu Husein (a.s.), na wanawe pamoja na nduguze ambapo baadae kawaua kikatili hapo Karbala.

Yazid hana aina yoyote ya historia katika Uislamu

inayoweza kupigiwa mfano wa kuigwa, bali hata kwa huyo baba yake Muawiya hatukuti chochote cha maana ndani ya Uislamu kinachoweza kuwa ni mfano wa kurejea.

Sana kuhusu Muawiya ni uasi dhidi ya Mtume hata mpaka Mtume alipata kumwombea Dua baya kutokana na uasi wake akasema “Ewe Mola! Usilishibishe tumbo lake.”

Hivyo basi, Yazid alifuata uasi wa baba yake aliyejitwalia madaraka kwa nguvu na baadaye kumuachia madaraka hayo mwanawe kwa nguvu na vitisho dhidi ya Waislamu.

Kutokana na sifa zisizostahili kwa Yazidi kuwa kiongozi wa Waislamu licha ya kuwa siyo haki yake, Imam Husein (a.s.) alikataa kumpa Yazid mkono wa baia (kiapo cha utii), pale Yazid alipomtaka afanye hivyo.

Kukataa kwa Imamu Husein kutoa baia kwa Yazid kulikuwa na maana ya kupinga Dhulma nakupinga kuwa chini ya watawala wasiyo waatilifu. Lau Imamu Husein (a.s.) angelikubali kutoa baia kwa Yazid angesalimisha maisha yake na Dini

33

ingepotoshwa, jambo ambalo Imamu Husein (a.s.) hakutaka kulishuhudia linafanyika machoni pake. Ndio maana aliona kufa ni bora kuliko namna nyingine yoyote, akasema Imamu Husein (a.s.): “Iwapo Dini ya babu yangu haitasimama ila kwa kuuawa mimi, basi enyi panga nichukueni.”

Akasema tena Imamu Husein (a.s.) “Siyaoni mauti (kuwa ni chochote) isipokuwa ni mafanikio na kuishi na wadhalimu sioni ila ni Fedheha.”

Hivyo basi, Imam Husein alikataa kata kata kuwa chini ya Yazid na walio mfano wa Yazid. Nao kina Yazid na wenziwe waliona kwamba bila kupata baia ya Imamu Husein (a.s.) watakuwa hawakubaliki mbele ya Umma wa Kiislamu.

Uamuzi waliouana kuwa unafaa, ni kumwua Imamu Husain (a.s.).

MTUME KASHUHUDIAKUUAWA KWA IMAMU

HUSEIN (A.S.).

Mauaji ya kikatili yaliyofanywa dhidi ya Imamu Husein (a.s.) hapo Karbala, yanahuzunisha sana. Yazid na majeshi yake

licha ya kumchinja Imamu Husein (a.s.) na kukitundika kichwa chake juu ya Mkuki, walikiponda ponda kiwiliwili chake kwa miguu ya farasi, bila kukumbuka kuwa, wanayemfanyia hayo ni Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.).

Amesema Mtume (s.a.w.): “Husein anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husein.”

Usemi huu una maana kuwa, Mtume (s.a.w.) ndiye Husein (a.s.) na Husein (a.s.) ndiye Mtume (s.a.w.), damu yao ni moja.

Ni vigumu kuipima huzuni ya Bwana Mtume (s.a.w.) ilikuwa ya kiasi gani kutokana na matendo aliyotendewa Imamu Husein (a.s.), lakini yatosha kusema kwamba Mtume wetu (s.a.w.) alishuhudia yote hayo wakati yakifanyika.

Imepokewa kwamba, katika kipindi hicho cha mauaji hayo, Ummu Salama mkewe Bwana Mtume (s.a.w.) usingizini alimwona Mtume hali ya kuwa ameenea vumbi na nywele zake na ndevu zake zimevurugika. Ummu Salama alimwuliza Mtume (s.a.w.) sababu ya kuwa

34

katika hali hiyo naye alijibu, “Natoka kuchimba kaburi la mwanangu Husein.”

Ikiwa Bwana Mtume (s.a.w.) alishiriki kuchimba kaburi la mwanawe huyo, basi ni wazi anayafahamu hayo aliyotendewa mwanawe. Basi, Ole wao waliomwulia Mtume wetu kizazi chake na sahaba zake waaminifu. Ole wao waliorusha mikuki dhidi yakizazi cha Mtume (s.a.w.). Ole wao waliomkata mikono Abbas Bin Ali aliyekuwa kafuata maji aje aipoze kiu ya watoto wa Mtume (s.a.w.) waliokuwa

wakipiga kelele za kuomba maji. Ole wake aliyetupa mshale kumwua Abdillahi akiwa mikononi mwa Imamu Husein.

Ameangamia aliyeikata shingo ya Imamu Husein (a.s.) kwa kutaraji kupata zawadi za kina Yazid na Ibnu Ziyad.

Ole wao waliosikia dhulma hii na wakaridhia.

Je, wanatarajia kupata uombezi wa Mtume (s.a.w.) siku ya Qiyama hao watu waliomwua Imamu Husein (a.s)?

*****

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W)ASEMA:

1. EWE MWANANGU (HUSAIN! MWILI WAKO NI MWILI WANGU NA DAMU YAKO NI DAMU YANGU;

2. EWE MOLA WANGU! MPENDE YULE AMPENDAE HUSAIN.

3. HASSAN NA HUSAIN NI MASAYYID WA VIJANA WA PEPONI

35

MASHAHIDI WALIOUAWAKARBALA

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Orodha hii ya mashahidi imenukuliwa KutokaTh e Martyrs of Karbala cha

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Iliochapishwa Katika Jarida ya Th e Light Vol.11, No.6, 1977.

Makala halisi zina maelezo mengi zaidi kuhusu Mashahidi, uhusiano wa wao wanyewe kwa wanyewe na vipi na lini Waliuwawa Shahidi;

I. Mashahid kutoka kwa Banu Hashim(A) Watoto wa Imam Ali bin Abi Talib: 1. Imam Husayn 2. ‘Abbas 3. ‘Uthman 4. Ja’far 5. ‘Abdullah 6. Ibrahim 7. ‘Umar 8. Muhammad al-Asghar

(B) Watoto wa Imam Hasan bin Ali: 9. Ahmad (Abu Bakr) 10. ‘Abdullah 11. Qasim

36

(C) Watoto wa Imam Husayn bin Ali: 12. ‘Ali al-Akbar 13. ‘Ali al-Asghar (pia anajulikana kama Abdullah ar-Radi’)

(D) Watoto na Wajukuu wa ‘Aqil bin Abi Talib: 14. Muslim bin ‘Aqil (Allia uwawa Kufa) 15. Ja’far bin ‘Aqil 16. ‘Abdu ‘r-Rahman bin ‘Aqil 17. Muhammad (Au Abu ‘Ubaydullah) bin Muslim bin ‘Aqil 18. ‘Abdullah bin Muslim 19. Ja’far bin Muhammad bin ‘Aqil 20. Muhammad bin Abi Sa’id bin ‘Aqil

(E) Wajukuu wa Ja’far at-Tayyar bin Abi Talib: 21. ‘Awn bin ‘Abdullah bin Ja’far 22. Muhammad bin ‘Abdullah bin Ja’far 23. ‘Ubaydullah bin ‘Abdullah bin Ja’far

II. Masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) 24. Anas bin Harth al-Kahlili 25. Habib bin Muzahir 26. Muslim bin ‘Awsajah 27. Hani bin ‘Urwah al-Muradi - (Allia uwawa Kufa) 28. ‘Abdullah bin Yaqtur - (Allia uwawa Kufa)

III. Waumini na Wafuasi 29. Nasr bin Abi Naizar 30. Sa’d bin Harth31. Munjih bin Sahm32. Aslam bin ‘Amr

37

33. Qarib bin ‘Abdullah Du’ali34. Harth bin Nabhan35. John bin Huwai36. Sa’id au Sa’d37. Nafi’ au Rafi’38. Salim39. Salim40. Shawdhab41. Shabib42. Wadih43. Sulayman44. Zahir bin ‘Amr45. Abu ‘l-Hatuf bin Harth al-Ansari46. Adham bin Umayyah47. Aslam bin Kuthayr al-Azdi48. ‘Abis bin Abi Shabib ash-Shakiri49. ‘Amir bin Muslim50. ‘Abdu ‘r-Rahman bin ‘Abdullah bin al-Kudar al-Arhabi51. ‘Abdu ‘r-Rahman bin Mas’ud bin Hajjaj52. ‘Abdu ‘r-Rahman bin ‘Urwah bin Hiraq al-Ghifari53. ‘Abdullah bin ‘Aidhi54. ‘Abdullah bin Bishr55. ‘Abdullah bin ‘Urwah bin Hiraq al-Ghifari56. ‘Abdullah bin ‘Urnayr al-Kalbi57. ‘Abdullah bin Zayd al-Qaysi al-Basri58. ‘Ammar bin Abi Salamah al-Hamdani59. ‘Ammar bin Hassan bin Shurayh at-Ta’i60. ‘Amr bin Dubai’ah Dubu’i61. ‘Amr bin Junadah bin Harth62. ‘Amr bin Qarazah al-Ansari

38

63. ‘Amr bin Khalid as-Saydawi64. Bakr bin Hai at-Taymi65. Bishr bin ‘Umar al-Hadrami66. Dirghamah bin Malik67. Hubab bin Harith as-Salmani al-Azdi68. Hajjaj bin Badr Basri69. Hajjaj bin Masruq al-Ju’fi70. Hajjaj bin Zayd Sa’di71. Hur bin Yazid ar-Riyahi72. Handalah bin Sa’d (au As’ad) ash-Shabami (au ash-Syabani)73. Huwai bin Malik ad-Dabu’i74. ‘Imran bin Ka’b bin Harith al-Ashja’i75. Jabalah bin ‘Ali ash-Shaybani76. Junadah bin Harth Salmani77. Jundab bin Hijr al-Khawlani78. Julas bin ‘Amr ar-Rasibi79. Karsh (au Kurdus) bin Zahir at-Taghlibi80. Kananah bin ‘Atiq81. Khalid bin ‘Amr bin Khalid as-Saydawi82. Malik al-Jabiri83. Malik bin ‘Abd bin Sari’84. Mas’ud bin Hajjaj85. Mujamma’ bin ‘Abdullah86. Masqit bin Zahir at-Taghlibi87. Nafi’ bin Hilal bin Nafi’ al-Bajalli (au al-Jamali)88. Nu’man bin ‘Ajlan al-Ansari89. Nu’man bin ‘Amr ar-Rasibi90. Qasim bin Habib al-Azdi91. Qasit bin Zahir at-Taghlibi92. Qa’nab bin ‘Amr at-Tamri

39

93. Qays bin Musahhar as-Saydawi94. Sa’d bin’ Abdullah al-Hanafi95. Sa’d bin Harth al-Ansari96. Sayf al-Jabiri97. Sayf bin ‘Abdullah bin Malik98. Sayf bin ‘Abdullah al-‘Abdi99. Shabib bin al-Harith bin Sari’

100. Shabib bin ‘Abdullah an-Nahshali101. ‘Ulaydullah bin al-Qaysi al-Basri102. ‘Umar bin Junadab al-Hadrami103. ‘Umar (Abu thamamah) bin ‘Abdullah as-Sa’idi (as-Saydawi)104. Umayyah bin Sa’d a-Ta’i105. Wahab bin ‘Abdullah al-Kalbi106. Mke wa Wahab al-Kalbi107. Yazid bin Hasin al-Hamdani108. Yazid bin Ziyad bin Muhasir al-Kindi109. Zayd bin Ma’qil al-Juf ’fi110. Zayd bin Thubayt al-Qaysi al-Basri111. Zuhayr bin Bishr al-Khath’ami112. Zuhayr bin Sulaym al-Azdi113. Zuhayr bin Qayn al-Bajalli

IV. Waliouawa baada ya Imam Hussein114. Suway bin ‘Amr bin Abi ’l-Muta’115. Sa’d bin Harth116. ‘Abdu ‘l-Hatuff bin Harth117- 118. Watoto wawili wa Muslim bin Aqil waliuawa huko Kufa

V. Waliojeruhiwa na Kufa baadae119. Sawwar bin Mun’im Abi ‘Umayr an-Nahm

40

120. Muwaqqa’ bin Thamamah121. ‘Amr bin ‘Abdullah al-Hamadani al-Jundu’iy

*****

KWA MWEZI WA MUHHARAM

Naanziliza kauliNa Swalawati Rasul

Kwa jina lake JalaliNa-ali zake pamoja

Mswiba ulo adhimuDhuriya zake Hashimu

Kwa mwezi wa MuhharamuKarbala wakingiya

Hadithi imetuwambiyaWapendwa wake dhuriya

Rasuli ameuswiyaKinyume wakatumiya

Umati walibadiliIkawa ni kuwadhili

Mahabba yao kwa AliNa maji kuwaziwiya

Yasitoshe walofanyaDhuluma wakamuonya

Ya Mtume kuyakanyaVijana kumuuliya

Hawakujali hishimaVijana waliye wema

Ya Sayyidati FatimaWa Haidari Aliya

Sina budi nitaliaIwe kwetu mazoweya

Kukosa kuwateteaAshura ikingiliya

Hadithi walisahauWakawauwa na kiu

Mapenzi wakadharauFurati wakangaliya

Walikuwa KauthariPamoja na Answari

Maji mema ya fakhariDini waloitetea

Yalopita tayakidhiNa kwa Mungu ni fawidhi

Kwa Tumwa nipate radhiNa Aya kiisomeya.

41

WAAFRIKA WALIOJITOLEA KERBALA

Imeandikwa na:Khwaja Mohamed Latiff Ansari

Dini ya Kiislamu haina ubaguzi wowote wa taifa au wa ngozi; weusi au weupe; wenye kumiliki au wenye kumilikiwa. Mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu wanadamu wote ni sawa na Dini ya Kiislamu yakubali udugu wa wanadamu, si kwa Sheria tu, bali na kwa vitendo.

Kisa cha kusikitisha kilichotukia Kerbala kinatupa kielelezo chenye kustahili cha jinsi ulivyo Udugu wa Kiislamu. Pengine itaonekana kuwa ajabu, lakini ni hakika jambo hili. Miongoni mwa wafuasi wa Imam Husein katika uwanja wa Kerbala, walikuwako mashujaa kumi na mbili wa Nabii Muhammad (s.a.w.) kwa ajili ya kuitetea Dini ya Kiislamu. Mbali na taifa la Kiarabu, taifa lililokuwa na watu wengi waliojitolea katika hawa mashujaa wa Kerbala lilikuwa ni taifa la Kiafrika.

Wengi wao mashujaa hawa wa Kiafrika ni watu ambao kwamba asili yao walikuwa watumwa

Bara Arabu enzi za zamani za ushenzi. Kwa rehema ya Nabii Muhammad (s.a.w.) watu hawa wakapatiwa njia ya kuwa huru, licha ya kuwa huru tuu, lakini wakajipatia na vyeo heshima katika historia ya Kiislamu. Vyeo hivyo walivyovipata vimewafanya wao wawe ni watu wenye kuheshimika katika Dini ya Kiislamu ulimwengu mzima.

Tangu kisa cha Kerbala yapata karne kumi na tatu, lakini kisa hiki hata hivi leo kingali chenye kuumiza nyoyo za watu kama vile kimetukia hivi jana. Ushujaa na uthabiti wa hao waliopoteza roho zao unazidi kuwatia nguvu watu wote ambao ni watafutaji wa kweli.

Ingawa Imam Husein, mjukuu wake Mtume Muhammad (s.a.w.) ndiye mwenye kuiokoa Dini ya Kiislamu tena ndiye kichwa cha Waislamu, pamoja na hayo yeye anatuonyesha jinsi inavyopasa kutenda haki na kuonyesha huruma pasi na kujali kabila

42

au dini. Funzo atupalo, si kwa Waislamu tu, bali anaupa ulimwengu mzima. Wakati huu ambapo kuna mambo mengi ya ubishani, Imam Hussein amekuwa kielelezo cha kila jambo la haki.

Yeye alipigana vita vya Kerbala, wala si kwa kupigania nchi yoyote au dini yoyote. Alipiganana Waislamu wenziwe ambao walizoea tabia ya mambo maovu na dhambi, kuonea wenziwao, mambo ambayo yapingana na kila jambo lililo safi.

Imam Husein, kwa maisha yake alijaribu kuonyesha kuwa nikielelezo cha mtu mwenye kuamini Mwenyezi Mungu. Watu wenye roho za uovu walipoona hivi wakaungana pamoja wakiongozana chini ya bendera ya Yazid wapate kuyakashifu na kuyapinga mafundisho ya Mtume. Imam Husein aliwapinga, ndipo wakataka kumwangamiza. Katika vita hivyo yeye na wafuasi wake wachache waliuawa. Waliopona ni mmoja tu alikuwa mwanawe Ali (II), ambave alikuwa mgonjwa. Mtoto huyu wa Imam katika miaka yake ya baadaye

alipewa jina la “Zainul Aabedeen” (Pambo la Wateule) na kwa kupona kwake kizazi chenye utuwaa cha Mlango wa Mtume kikasimama. Ku-uliwa huku katika vita kulikuwa ni kama ushindi wa roho uliobuni njia ya kumwonyesha mwanadamu kuwa yeye yu juu ya kila jambo lililo la ulimwengu huu au kila majeshi ya binadamu, na kwa kuandama mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.), ushindi juu ukaonyesha jinsi ya kujiweka katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Ni jambo la kukumbukwa kuwa katika taabu na dhiki aliyoipata Imam Hussein aliungwa mkono na mataifa mengi ya ulimwenguni. Mbali na watu wa jamaa ya Mtume Muhammad (s.a.w.) walikuwako Waarabu wa kabila mbali mbali, pamoja na “Ashabe Rasool” (Masababa wa Mtume). Alikuwako Mturuki mmoja kutoka kwa kabila la Aryan na mashujaa kumi na mbili kutoka Bara la Afrika.

Historia imehifadhi kwa kutunza sana majina ya mashujaa kumi na mbili waafrika waliosimama Kerbala pamoja na mjukuu wa Mtume na kuyatoa maisha yao

43

kwa ajili ya kuifufua dini ya Kiislamu Majina yenyewe ni haya:1. Qarib Abdulla2. Manjih Sahim3. Saad4. Haria Nabham5. Saleem6. Shabib7. Salim8. John

9. Salim Amer10. Shouzab11. Saad Haris12. Zahir

Pamoja na majina ya watu hawa, historia imehifadhi majina ya wanawake mashujaa Waafrika waliojitilea kusaidia kukua kwa dini ya Kiislamu.

NAUHATunasikitika sana kwa kifo chako HusainEwe Husain ya shahida Karbala x 2

Mal-uni alofika kukuua ya HusainNa Mungu atayaweka makazi yake motoniEwe Husain ya shahida Karbala x 2

Mbingu zilitikisika kwa kifo chako HusainMajabali kupasuka kwa khofu na kwa huzuniEwe Husain ya shahida Karbala x 2

Upanga uliushika ili kutetea diniKuchezewa yetu dini Husain hukuridhikaEwe Husain ya shahida Karbala x 2

Tarehe zatuonyesha kwa kifo chako HusainHusain umeondoka umeacha pengo kubwaEwe Husain ya shahida Karbala x 2

Tunamuomba Manani amlani mal-uniAmlani hayawani Yazidi na jeshi lakeEwe Husain ya shahida Karbala x 2

*****

44

UA LA MWISHO LAIMAM HUSEIN (A.S.)

Mwaka wa 61 wa Al-Hijra, mwezi kumi Muharramu, wakati wa adhuhuri, joto kupita kiasi, katika mji wa Iraqi mahala paitwapo Karbala mtazamaji mmoja anaeleza namna alivyoona.

Jua lilikuwa kali mno, upepo mkali wa moto ukivuma hata miti na majani ya mahala hapo kwa joto ilibadilika rangi kuwa meusi. Upande mmoja jeshi lisilo na kiasi kwa wingi wake, utafikiri upando huo umeingia kiza ya usiku, makelele na vigeregere vya furaha ya kushinda vinasikika.

Nyuma ya jeshi hilo kumesimamishwa mahema yasiyo na idadi na kati ya hema hizo, kuna mahala pamepambwa na bendera za Serikali ya Bani Umayyah kuonesha adhama na ukubwa wa utawala wao.

Upande mwingine wapo baadhi ya viumbo vya Mungu waliojeruhiwa na kuuawa, miliyo yao imetupwa hapo, na nuru kama mbaramwezi kutoka nyusoni mwao yameremeta.

Kwa kupiga makelele ya kutaka msaada jinsi ilivyokuwa ya kuhuzunisha hata ikaathiri miili ya hao mashahidi waliouawa hapo, na kila rotu akaanza kusema (LAB-BAYK, LAB-BAYK na tayari kukusaidia mara, tukifanywa lena wazima). Upande mwingine makelele ya kutaka msaada yaliathiri sana kwenye hema za watu wa nyumbani kwake mtukufu huyo, nao wakaanza kuulizana kwa sauti.

Mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) Imam Husein (a.s.) aliposikia sauti ya watu wa nyumbani kwake, akaondoka mahala hapo akaenda kwenye hema, akaingia ndani. Akamwuliza dada yake, Bibi Zainab sababu za vilio, akajibu yule Bibi Ewe kaka uliponyanyua sauti yako kutaka msaada kwa maadui, ilituathiri sana hata mwanao mchanga Bw. Ali Asghar akajitupa nje ya susu yake nasi tukalia.

Imam (a.s.) akasema, mleteni mwanangu mchanga kwangu nipate kumchukua mbele ya

45

hawa maadui kumtakia maji. Bibi Zainab alipopata hukumu hiyo, akaenda akamleta huyo mtoto mchanga Ali Asghar. Imam (a.s.) akampakata mwanawe akatoka naye nje.

Kuja kwa Mtoto mchangakwenye uwanja wa Vita

Kwa vile jua lilikuwa kali mno akamfunika mwanawe kwa joho (aba) yake hata akafika mbele ya jeshi la maadui. Wanajeshi wakasemezana kwa kufikiria kuwa Imam (a.s.) ameleta msahafu kutuapisha sisi! Mara tu aliposogeza joho lake wakaona mtoto mchanga kabisa wa miezi sita Ali Asghar ameletwa.

Mtoto huyo kwa njaa na kiu alidhoofika mno hata hawezi kukamata shingo yake. Imam (a.s.) akaanza kumbusu mtoto yule huku anamwambia, “Ewe mwanagu hadi leo baba yako hakupata kunyosha mkono kutaka msaada kwa yeyote ila kwa Mwenyezi Mungu. Lakini nifanyeje ninavyoona hali yako ilivyo kwa kiu siwezi kustahimili, ijapokuwa nina hakika nyoyo ngumu za hawa maadui hazitathiri kitu kwa maneno yangu lakini inanibidi

kufanya hivyo ili nitimize hoja zangu kwao, wasiwe na hoja yeyote kesho mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya babu yangu mtukufu Mtume (s.a.w.).” Imam mwenye harara na wivu (ghera) akaangalia kwenye majeshi ya adui namna ya kuomba lakini asiseme kitu kwa haya, jasho lamtoka kwenye kipaji chake kitukufu, mwishowe macho na kichwa kainamisha chini akawahutubia kusema, “Enyi mnaosoma kalima na kumkubali Mtukufu Mtume. Enyi wenye watoto! huyu, mwanangu mchanga asiyeweza kusema, mwana wa Mtume wenu, na mtoto mdogo kabisa wangu mwenye umri wa miezi sita tu! maziwa ya mama yake yamekauka kwa masaibu na ukosefu wa chakula na maji, roho mikononi amekuja kusema nanyi. Enyi wafuasi wa Yazid, wadai wa Uislamu, ikiwa nyinyi mwafikiria mimi nina makosa (dbambi) kwa kosa la kumkubali Yazidi, basi huyu mtoto mchanga asiyeweza hata kusema amekosa nini? Mnywesheni asife kiu!”

Imam asipate jibu lolote, mwishowe Imam akasema: “ikiwa mnadhani kwamba kwa

46

kumsingizia na kumtakia mtoto maji, mimi pia nitakunywa maji! Basi na aje mtu yeyote kwenu amchukuwe kwangu!” Imam asipate majibu kwa jinsi roho za maadui zilivyo ngumu kuliko jiwe. Basi Imam (a.s.) akasema: “ikiwa mnaniogopa kuja kwangu kumchukua mtoto, basi ninamweka chini na ninasogea mbali na aje mtu kumywesha maji!” Jii, hata mtu asijibu wala kusogea.

Baadaye Imam akamwambia mwanawe “Ewe mwanangu, wewe mtoto wa Imam, mjuku wa Mtukufu Mtume, sasa wewe pia onyesha hoja yako kwa maadui,” basi kusikia hivyo, yule mtoto mtukufu akatoa ulimi wake nje na kuuzungusha nje ya mdomo kuonyesha kiu aliyonayo. Kufanya hivyo yule mtoto, wale wenye watoto (waliozaa) katika jeshi la adui wakaanza kulia na safu za jeshi zikaparaganyika! Kuona hivyo Jamadari wa jeshi Umar bin Saadi akampigia kelele HARMALA maluni (mpiga mshale mashuhuri) kumwambia “Kata maneno ya Husein.” Basi yule maluni Harmala akatumia mshale mkubwa wenye sehemu tatu, akamrushia yule mtoto mchanga wa Imam (Ali Asghar)

aliyekuwa mikononi mwa baba yake mtukufu. Ule mshale mkubwa ukaja na ukamkata shingo yule mtoto na kumchomba mkononi baba yake.

Mtoto akapinduka kugeuka kwa nguvu ya ule mshale mikononi mwa baba yake na kutoka damu kwa wingi, mtoto papa hapo mikononi mwa baba yake akafariki. Imam akachukua akakinga damu ya yule masoom (mtoto asiyekuwa na hatia) na akapakaa usoni na kwenye ndevu, huku anasema, “nitaonana na babu yangu Mtukufu Mtume vivyo hivi.”

Sasa tena siwezi kwenda mbele kueleza masaibu haya, mikono yanitetemeka na machozi yanichururika. Kwa ufupi ninawauliza wasomaji wenzangu:hebu fikirini na mwaze vipi ilikuwa hali ya mama yake na jamaa zake walipomwona amechinjwa namna ile!

Msiba huu mkuu hautasahaulika kamwe hadi mwisho wa dunia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilia sana kabla ya kupita mambo haya alipohubiriwa na Jabrilu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na masaibu yatayowapata wajukuze Mtukufu.

47

HAZRAT ABBAS BIN ALI (A.S.)Makala hii ilichapishwa Katika Jarida la

“The Muslim Review”, Lucknow, India, July, 1996.Dr. Mohammed Simba ameitafasiri kwa

Lugha ya Kiswahili

UTANGULIZI

Hazrat Abbas alikuwa mtoto wa kiume wa Hazrat Imam Ali bin Abi Talib. Jina la mama yake lilikuwa Bibi Fatima Binti Hazam bin Khalid. Alikuwa pia anajulikana kama Ummul Baneen. Alikuwa wa ukoo wa Banu Kilah. Miongoni mwa Wahashimu, ukoo wake ulikuwa wa jamaa ya watu wenye heshima kubwa baada ya ule wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), na walijulikana kwa uhodari na ujasiri wa wapiganaji wake.

Fatima Binti Hazam alikuwa mtimilifu, mwenye maarifa, aliyelelewa vizuri na mstaarabu, akazaa watoto wanaume wanne wa Hazrat Ali: Abbas, Abdullah, Jafar na Usman. ‘Ummul Baneen’ maana yake ni “Mama wa Watoto Wakiume”. Watoto wake wote walikufa kifo cha kishahidi pamoja na Imamu Husain (a.s). Baada ya kifo chao cha kishahidi, mama yao

aliwaomba watu wasimwite tena ‘Ummul Baneen’.

Siku aliyoingia ndani ya nyumba ya Hazrat Ali, Ummul Baneen aliweka wazi kwa Imamu Hasan na Imamu Husain (a.s.) kuwa alijiona kuwa ni mtumwa wao, na alitumaini na kuomba kuwa wangekubali kama mmoja wa watumwa wao. Heshima na upendo wake kwao ulikubalika mara mojo na ndusu hawa wawili, na hata baada ya kuzaliwa watoto wake, Imamu Hasan na Imamu Husain (a.s.) walichukua nafasi kubwa ya mbele katika moyo wake.

Mmoja wa wafuasi hodari mno wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alikuwa Ja’far Tayyar, kaka yake Hazrat Ali (a.s.). Katika vita vya Mura, Ja’far Tayyar alichukuwa Bendera ya Uislamu na katika vita vile alizidiwa na maadui na kuuawa. Habari zilipomfikia Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), alilia na kusali kwa ajali ya

48

roha ya Ja’far na malaika Gabrieli alishuka chini na kumfariji Mtume, akisema “Ja’far alikuwa askari hodari na mwaminifu. Mungu amempa maisha ya milele, na mahali pa mikono yake miwili iliyokatwa vitani, Mola amempa mabawa mawili”.

Hazrat Ali aliyekuwa amekaa karibu na Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) wakati ule, alisema, “Tafadhali mwombe Mungu kwamba nife nikipigana katika njia ya Uislamu na kuwa shahidi.” “Ewe Ali, kifo chako tayari kimeamriwa. Utakufa ukiwa msikitini wakati wa sala zako, lakini Mwenyezi Mungu atakupa mtoto mwanamume atakaye kufa vitani siku ya Ashura”. Toka wakati ule Ali alisubiri kwa hamu kuzaliwa kwa mtoto huyo mwanamume.

(Unabii huu ulifanyika mnamo mwaka wa 8 A.H wakati Imam Hasan (a.s.) akiwa na umri wa miaka 5 na Imamu Husain (a.s.) miaka 4).

KUZALIWA KWAKE

Hazrat Abbas alizaliwa Medina tarehe 4 Shaban 26 A.H. (sawa na 645 (A.D.) wakati wetu wa

kawaida). Wakati habari za kuzaliwa kwake zilipomfikia Hazrat Ali, alisujudu hadi ardhi kama zawadi yake ya shukrani ya unyenyekevu kwa Mungu. Imamu Husain (a.s.) alimchukua mtoto mikonani mwake na kusoma Azana na Iqama (wito kwa sala) katika sikio la kulia na kushoto kwa zamu, yaani, Azana katika sikio la kulia na Iqama, sikio la kushoto, kisha huyo mtoto akafumbua macho yake kuuona uso wa upendo wa Imamu Husein (a.s.). Mna-mo siku ya saba ya kuzali-wa kwake sherehe ya Aqeeqa ilifanywa ambayo ni sunnah ya kuzingatiwa, na Hazrat Ali alimpa mtoto jina la ‘Abbas.’

Tukio la aina hii lilifanyika katika wakati wa kuzaliwa kwa Hazrat Ali (a.s.). Alifumbua macho yake tu wakati Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alipomchukua mikononi mwake.

KULELEWA KWAKE

Hazrat Ali alitaka, kwamba mtu huyu aliyempa jina la ‘Abbas’ (maana yake Simba Asiyehofu) angetimiza matendo yale yale ya jasiri na angefuata mafundisho yake bila woga wa kuishi na kifo. Vilevile alitamani kuwa Abbas

49

angekuwa rafiki wa kudumu wa Imamu Husain (a.s.) na kuwa mchukuaji wa Bendera pale Kerbala.

Hazrat Ali, ambaye yeye mwenyewe alijulikana kama ‘Simba wa Mungu’ na ‘Lango la Elimu’ alimlea Hazrat Abbas ana kuweza kumwongoza mpaka alipofikia umri wa miaka 14, Miaka kumi (10) iliyofuata ilitumika akiwa katika uangalizi makini wa Imamu Hasan (a.s.) na miaka kumi (10) ya mwisho alikuwa pamoja na Imamu Husain (a.s.). Hiyo haikushangaza kwamba Hazrat Abbas alipata ukamilifu wa karibu katika maneno mengi ya maisha. Umahiri wake, ujasiri, umbile la kishupavu na ufundi wa kupigana na uaskari, vilikuwa vimerithiwa toka kwa Hazrat Ali (a.s.), na hili alilithibitisha vizuri sana katika vita vya Jamal, Siffin, Nahrwan. Imamu Hasan (a.s.) alimfundisha subira na uvumilivu; uaminifu wake wa Moyo wa Simba na kujitoa kwake muhanga yalikuwa matokeo ya ushirikiano wake na Imamu Husain, Janab-e-Zainab. Kimwili, kiakili, kimaadili na kiroho alikuwa amekomaa kabisa, licha ya kuwa mwanazuoni

aliyehitimu.

Aliwasaidia maskini na wenye uhitaji, na kufanya wajibu wake kwa binadamu wenzake kulingana, na mafundisho ya Kiislamu. Alikuwa sifa katika mawazo yake, maneno na matendo, lisije lolote la haya likamkasirisha Mwenyezi Mungu kwa kutolitimiza. Aliishi kwa kuzingatia mafundisho ya Qur’an Tukufu na maneno ya hekima ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.).

Kama vile Hazrat Ali (a.s.) alivyokua akiwa chini ya uangalizi wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), Hazrat Abbas alilelewa na Hazrat Ali (a.s.), aliyekuwa anajua vema mafumbo ya maisha na kifo, na Abbas alikuwa ameitumia roho ya kweli ya Uislamu. Mtu aliyelelewa na kukaa, kusomeshwa na kumfundishwa na Hazrat Ali asingeweza kwa namna yoyote kufungamana na maisha ya ulimwengu huu, wala kuogopa kifo, na Abbas alionyesha hili kikamilifu kwa matendo yake.

Hazrat Abbas alimuoa Lubaba, binti wa Obaidullah Ibn Abbas Ibne Abdul Muttalib, na alikuwa

50

na watoto wanaume wawili Fazl na Muhammad. Vyanzo vingine vinasema kuwa Lubaba alikuwapo Kerbala na mtoto wao Muhammad alikufa kifo cha kishahidi hapa ya kafara ya hali ya juu, ushujaa mkubwa na ujitoaji katika njia ya haki na kweli.

Katika vita vya Kerbala Hazrat Abbas (a.s.) alikuwa amiri-jeshi mkuu wa Imamu Husain (a.s.). Aliyapiga majeshi ya uovu ya Yazid kishujaa akiwa anayakumbuka maneno ya mwisho wa baba yake. Hadithi ya muhanga wa uhai wake katika kujaribu kupata maji kwa ajili ya watoto wa Imam Husain (a.s.) katika uwanja wa vita ni yenye kugusa mioyo sana na ya kipekee katika historia ya Kiislamu.

Maisha ya Hazrat Abbas ni mfano wa uaminifu na upendo kwa ndugu. Pia ni hadithi ya mpiganaji shujaa aliyeyatoa maisha yake kwa ajili ya Uislamu. ambayo kulingana na Hazrat Abbas, ilikuwa sabahu ya haki.

UPENDO WAKE KWAIMAMU HUSAIN

(A.S.) PALE KERBALA

Tangu walipotoka Madina,

Hazrat Abbas alikuwa karibu sana na Imamu Husain (a.s.), na alipendwa sana na watu wa jamaa ya Imamu Husain (a.s.). Alikuwa mwaminifu sana kwa Imamu Huaain (a.s.), kwamba, Jemedari msaidizi wa Jeshi la Yazid alipokuwa anakuja kuelekea kambi ya Imamu Husain (a.s.) na kuita, “Wako wapi wapwa zangu Abbas, Abdullah, Jafar na Usman?” Hazrat Abbas alikataa kujibu. Alikuwa kimya tu mpaka Imamu Husain (a.s.) alipomwambia: “Mjibu, kwa sababu, licha ya ukweli kwamba amegeuzwa, ni mmoja wa ndugu zako pia”, ndipo Hazrat Abbas alipomwuliza Shimr Ibne Ziljashan kile alichokuwa anataka. Shimr alijibu: “Enyi wapwa zangu nimemwomba Obaidullah Ibne Ziad mahsusi kwa ajili ya usalama wenu nyote. Kwa nini basi mnataka kujiua wenyewe ajili ya Husain? Kwa nini hamkiungi na jeshi la Yazid mwenye nguvu?”

Hazrat Abbas alimtazama kwa dharau na alimjibu kwa ukali: “Ghadhabu ya Mungu iwe juu yako na juu ya kusudi lako, Ewe adui wa Mungu! Unathubutuje wewe kutushauri sisi kumwacha Bwana wetu, Imam Husain (a.s.)

51

na kujifungamanisha wenyewe na Mlarushwa, aliyepotoshwa, Yazid?” Shimr aligeuka nyuma na kuondoka mwenye hasira.

Katika mkesha wa Alshura, Hazrat Abbas akiwa amekaa akinoa upanga wake ndani ya hema lake, dada yake Umme Kulsum alikuja kwake, na akiwa na machozi machoni mwake, alisema, “Siwezi kufanya kafara yoyote kwa kaka yengu Imamu Husain (a.s.), aliyezungukwa na maadui, Zainab ana watoto wawili atakaowatoa kafara kwa Imamu Husain (a.s.); Umme Lailah atampeleka mwanae Ali Akbar katika uwanja wa vita; hata Rubab atatoa kafara kichanga chake cha kiume, Ali Ashgari; lakini mimi sina watoto, na nikiwa mwanamke, siruhusiwi kupigana vita. Watu watawakumbuka akina mama hawa Shujaa wote, na kuimba sifa zao, lakini mimi sina wa kumtoa kafara kwa niaba yangu.”

“Usiwe na wasi wasi dada yangu, umenilea tangu utoto wangu mpaka nimekua, na umenipenda kama mama. Nitajitoa kafara mimi mwenyewe kwa niaba yako.”

Asubuhi Umme Kulsum alimchukua Abbas kaka yake hadi kwa Imamu Husain (a.s.) na kusema “Acha kaka yangu Abbas apigano kwa ajili yako kwa niaba yangu na yeye ni kafara kwako na Uislamu.”

Mwishowe, baada ya kumsihi sana, Imamu Husain alimpa ruksa kwenda kuteka maji kwa ajili ya watoto wenye kiu. Hazrat Abbas aliondoka na mfuko wa ngozi wa maji na beramu (bendera).

ALIPIGANA KIJASIRI

Akiwa na mfuko wa maji uliojaa aliruka juu ya mgongo wa farasi akiwa na wazo moja tu la juu zaidi katika akili yake - kufikisha maji kwa watoto kusubiri wanaosubiri kwa hamu kubwa, haraka iwezekanavyo. Wakimwona anakwenda shoti kuelekea kambi la Husain (a.s.), adui walimgeukia. Mtu fulani alipiga kelele toka katika safu za adui kwamba kama Husain (a.s.) na watu wake watapata maji ingekuwa vigumu kupigana nao kwenye uwanja wa vita.

Ingawa lilikuwa pambano la upande mmoja, alipigana kwa

52

ujasiri na ushujaa tabia aliyorithi kwa baba yake.

Walipoona kuwa shambulio la uso kwa uso kwa mtu hodari kiasi kile lisingewezekana, walitumia kizuizi cha mishale. Abbas alikuwa na wazo moja tu katika akili yake - jinsi gani aulinde vizurimfuko wa maji? Kwake mfuko huo ulionekana kuwa kitu muhimu sana na kuulinda, kuliko kuulinda uhai wake. Kuona Abbas anajishughulisha hivyo, adui mmoja mjanja aliyejificha nyuma ya fungo la mchanga alifumka na kumpiga moja na kukata mkono wake wa kulia. Kwa kasi ya ajabu Abbas alibadilisha upanga mkono wa kushoto na bendera aliyokuwa amechukua, aliikumbatia kifuani. Sasa kwa kuwa Simba wa Ali (a.s.) alikuwa kiwete, maadui walipata ujasiri kumzunguka. Pigo la upanga toka kwa adui lilikata kabisa mkono wake wa kushoto. Alishikilia mfuko wa maji mwno yake na kuilinda bendera kwa kifua chake kukuegemesha juu ya mgongo wa farasi.

Sasa wazo la juu zaidi katika akili zaka lilikuwa kufika kambini kwa njia yoyote. Lakini

hilo lisingewezekana. Mshale ulitoboa mfuko wa maji na maji yakaanza kutoka katika mfuko kwa nguvu. Jitihada zake zote zilikuwa bure tu. Maadui waliokuwa wamepata ujasiri kumzunguka, sasa walimsonga kwa wingi. Mmoja wao alikuja karibu yake na kumpija dharabu ya kuua kwa rungu la chuma. Aliyumba na kuanguka toka katika farasi wake.

BWANA NJOO KWANGU

Alianguka juu ya mchanga wenye kuunguza kwa uchungu wa kuumiza. Aliweza kuuona uhai wake ukiondoka kwa haraka kama mkondo wa bahari, lakini tamaa yake kumwona bwana wake ilibaki bila kutimizwa. Pamoja na jitihada ya mwisho, aliitaka kwa nguvu: “Ewe Bwana wangu, njoo kwangu kabla sijafa.” Kana kwamba katika jibu la maombi yake, alihisi hatua za mtu alimjia karibu. Ndiyo, akili yake ilimwambia kuwa alikuwa ni Bwana wake.

Alihisi Bwana wake anapiga magoti kando yake, akiinua kichwa chake na kukiweka katika mapaja yake. Kwa nukta chache hapana mtu aliyesema

53

neno, kwa sababu wote wawili walishikwa nafadhaa. Hatimaye Abbas alisikia sauti ya Husain (a.s.) (ambaye ndiye Bwana wake aliyepiga magoti kando yake), nusu akilia kwa kwikwi na nusu kama aliyezuiliwa kwa kitambaa ili sauti yake isitoke, sauti yenye kukwama: “Abbas kaka yanju (ndugu yangu), wa mwaka kufanya nini?”

Abbas sasa alihisi mguso wa upendo wa mkono wa Bwana wake, kwa jitihada kubwa alisema maneno yasiyosikika: “Mwishowe umekuja Bwana wangu. Nilifikiri sitaweza kukuona kwa mara ya mwisho lakini Mungu ashukuriwa, upo hapa.”

Husain (a.s.) alibubujikwa na machozi. Hali ya ndugu yake, mwenye jina ambalo lingekuwa lenye kuvuma kwa ajili ya upendo na uaminifu thabit, usioshindwa, akilaza uhai wake wa thamani mikoni mwake ilikuwa yenye kuumiza moyo.

Abbas alisikika akinong’ona taratibu. “Bwana wangu, Nina, matakwa ya mwisho kueleza. Nilipozaliwa, nilitazama kwanza uso wako na tamaa yangu ya

mwisho kwamba ninapokufa, macho yangu ya utazame uso wako. Jicho lango moja limetobolewa utalisafisha jicho lenye damu ninaweza kukoona na kutimiza takwa langu la mwisho la kifo. Takwa langu la pili kwamba nitakapokufa, usichukie mwili wangu kambini. Niliahidi kumletea maji Sakina na kwa vile nimeshindwa katika jitihada za kuleta maji kwake, siwezi kumwona hata kama katika kifo. Hata hivyo, ninajua, kuwa mapigo ambayo umeyapata tangu asubuhi, yamekutesa na kukuvunja nguvu na kuuchukua mwili wangu hadi kambini itakuwa kazi ya kuvunja mgongo kwako. Na ombi langu la tatu ni kwamba Sakina asiletwe hapa kuona hali yangu mbaya. Najua ni upendo namahaba kiasi gani aliyokuwa nayo kwangu! Tamasha la mwili wangu uliokufa ukiwa umelala hapa utamwua.”

KAKA YANGUI KAKAYANGU!

Katika hali ya kulia, Husain (a.s.) alimuhakikishia kuwa atatimiza matakwa yake ya mwisho na kuongeza “Abbas, Mimi pia nina takwa la kunitimizia. Tangu utoto siku zote umekuwa unaniita

54

Bwana. Kwa mara moja angalau, niite kaka kwa pumzi yako ya kifo.” Damu ilikuwa imesafishwa katika jicho, ndugu mmoja alimtazama mwingine kwa mtazamo wa kuendelea. Abbas alisikika akinong’ona; “Kaka yangu!” na kwa maneno haya alisalimu roho yake kwa Muumba wake; Kwa kilio Husain (a.s.) alianguka amezimia juu ya mwili uliokufa wa Abbas.

Maji ya Mto Furati yalikuwa giza kama wakti wa kurudi kali na sauti za chini-chini zilitoka katika maji yaliyokuwa yanateremka kuelekea baharini kama kwamba yalikuwa yanapinga mauaji ya mwenye kiu mchukua maji kwenye kingo zake, mpendwa - “Mwezi wa Wahashim”.

‘Ole’ mpendwa Hazrat Abbas aliuawa kishahidi kati umri wake mdogo wa miaka 35, mnamo 10 Muharram, 61 A.H. (sawa na AD 680).

“Assalaam Alaykum ya Abul Fazlil Abbas Ibn Amirul Momeneen wa Rahmatulahey wa Barakatoh”(“Amani iwe juu yaka Ewe Abul Fazlil Abbas mwana wa Hazrat Ali, Jemedari wa Wenye kuamini,

na mwenyezi Mungu amwage baraka zake juu yake”)

KUZURU KABURI LAKE

Ni karibu miaka elfu moja mia tatu tukio hili la kutisha lilipotokwa kule kerbala na bado makumi ya maelfu ya mahitaji wanaendelea kuja hapa mwaka baada ya mwaka kutoka sehemu zote za ulimwengu ilikutoa heshima zao kwa shujaa “mwezi wa Wahashim” kwenye kaburi lake lenye utukufu.

Wanatoa salaam na kuomba kwa Mungu kwa ajili ya mahitaji yao wakiomba maombezi yake, kwani hapa ndipo mahali ambapo nadhiri nyingi zimetimizwa na ambapo miujiza mingi imetokea.

Wengi wa waaminifu wametamani kwamba wangezikwa mahali hapa patakatifu na mara nyingi limeonekana jeneza limechukuliwa na kuzungushwa mara kadhaa kwenye kaburi la Hazrat Abbas na kisha kupelekwa kwenye eneo la kawaida la maziko na kuzikwa huko.

Quran Tukufu inasema:

55

“Msidhani kuwa wale waliouawa katika njia ya Mungu wamekufa. hapana, wanaishi wakipata riziki zao mbele ya Mola wao.”

Wakati wa majlisi za Muharram, kwa kawaida mnamo 8 Muharram, imekuwa kama namna ya mazoea kusoma matukio yaliyopelekea mauti ya shahidi Hazrat Abbas, na wakati “Alam” - (nakala ya Beramu (bendera) ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), na Maimamu Watakatifu) inatolewa nje vikiwa vimeambatana na upigaji wa vifua na vichwa na waombolezaji, utagundua ipo

mashk (mfuko wa maji wa ngozi) kwa kawaida umefanyizwa kwa chuma, kwa kumbukumbu ya Hazrat Abbas aliyetoa mhanga uhai wake akijaribu kuleta maji kwa watoto wa Imamu Hussain (a.s.) waliokuwa wankufa kwa kiu.

Wakati Hazrat Abbas alipobingilika chini toka kwenye farasi wake - baada ya dharuba la kuua la rungu juu ya kichwa chake, Alam (Bendera) na mfuko wa maji wa ngozi vilikuwa pamoja naye, na wakati mwingine unaona mahale pia pamoja na mfuko.

ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI ASEMA:

Imam Hassan na Imam Husain (a.s.) wameuhurishaUislamu kutokana na utumwa wa Wafalme na hivyo basi, wameuhifadhi kutokana na uharibifu daima. Wafalme watakuja na Wafalme watakwenda, lakini Uislamu utadumu milele. Kwa Uislamu, majina matakatifu ya Hassan na Husain yataangaza milele.

*****

56

KISA CHA KICHWA CHAIMAM HUSAIN (A.S.)

Imeandikwa na:Sayyid Mahdi Shuja’ii

Imetafsiriwa na:Sayyid Muhammad Ridha Shushtary

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kichwa kilichokatwa cha Imam Husain (a.s.) kiliwekwa katika chombo kimoja, na kikaletwa mbele ya Yazid bin Muawiyah huko Sham.

Yazid akiwa amelewa chakari, alikuwa alikipiga kwa fimbo aliyoishika mkononi, kichwa, uso, mdomo na meno ya Imam Husain (a.s.), huku akicheka.

Watu wengine pia walikuwa wakicheka. Watu waliokuwepo katika baraza la Yazid walikuwa wakimshangilia kwa vicheko na makofi.

Kati ya watu waliokuwa wameketi pamoja na Yazid, alikuwepo Balozi wa Mfalme wa Roma. Wote walikuwa wakijua kwamba alikuwa Mkristo;

Lakini yeye hakufurahia kitendo hicho cha Yazid. Alikuwa akitazama kwa mshangao mkubwa kichwa kilichokatwa cha Imam Husain (a.s.), mwendo wa Yazid, vicheko vya watu wa baraza la Yazid, na hata kiti, taji na baraza la Yazid.

Balozi alipomwuliza Yazid: “Hiki kichwa ni cha nani?”

Yazidi katika hali ambayo macho yake yalikuwa yakiwaka kwa kiburi, alijibu: “Sisi tumewaua baadhi ya waasi ambao walipigana dhidi yangu kunipinga kama Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

meno yake na kusema:“Hapana! Ngojea nikuambie

57

umemwua nani! Hiki ni kichwa cha nani! Nawe unapiga fimbo kwenye mdomo na meno ya nani?”

Kwa maneno hayo, Yazid akatokwa na nishai. Watu waliokuwepo walipigwa na bumbuazi. Wote walikuwa wakimtazama Mrumi kwa mshangao, na kujiuliza:“Anataka kusema nini Mkristo huyu!”

Balozi wa Roma akasema:“Mimi zamani nilikuwa mfanya biashara Mkristo. Nilikuwa nikisafiri kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine, na kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Nilikuwa nikinunua na nikiuza vitu, na njia hiyo nikiendesha maisha yangu.

“Makumi ya miaka iliyopita nilipita katika mji wa Madina. Ilikuwa katika miaka ambayo Mtukufu Muhammad (s.a.w.) alitangaza Utume wake.

“Mimi nilikuwa nimesoma katika vitabu vya Kikristo kwamba: ‘Mtume mwenye jina la Muhammad atatumwa na

Mwenyezi Mungu, ambaye atakuwa ni Mtume wa Mwisho. Na ni lazima mfuasi wa dini yoyote ile amwamini Mtume huyo.’

“Mimi nilikuwa na hamu kubwa ya kumwona Mtume wa Mwisho. Kwa sababu hiyo, nilipoingia mjini Madina tu, kabla ya kufanya jambo lolote, nilikwenda kumwona. Nilipomwona akiwa na sura iliyojaa nuru na utukufu, nikafahamu kwamba alikuwa ndiye huyohuyo Mtume wa Mwisho, ambaye Isa alibashiri kuja kwake.

“Wakati huohuo nikasilimu mbele ya Mtume Mtukufu (s.a.w.), na tangu siku hizo niliuficha Uislamu wangu nchini mwangu. Mimi nina watoto wa kiume watano na wa kike wanne. Wote ni Waislamu, na hakuna mtu yeyote anayejua hayo.”

Maneno ya Mrumi yaliwashangaza watu wote. Kimya kizito kilitawala katika baraza.

Balozi wa Roma aliendelea kusema:

58

“Nilipokuwa Mwislamu, moyo wangu haukupenda niondoke Madina na nimwache Mtume (s.a.w.). Nikakaa mjini Madina kwa muda fulani kupata mahufaa kutoka kwake. Siku moja, wakati nilipokuwepo msikitini karibu na Mtume, niliwaona watoto wawili kama mashada mawili ya maua, kama miezi miwili na kama malaika wawili, wakiingia msikitini.

“Walikuwa ni Hasan na Husain, wana wawili wa Fatima Zahra, wajukuu wawili wa Bwana Mtume (s.a.w.), na wapenzi wawili wa Ali (a.s.).

“Mtume Mtukufu (s.a.w.) mbali na kuwa na utukufu wote huo, aliondoka mahali pake, na akaenda mpaka kwenye mlango wa Msikiti kuwapokea watoto hao wawili. Akawakumbatia, kisha akawakalisha ubavuni mwake. Akabusu kichwa, uso, mdomo na meno ya Husain, na akamwambia:‘Mwenyezi Mungu amlaani yule atakayekuua, na yule atakayesaidia katika kuuliwa kwako.’

“Mtume Mtukufu (s.a.w.) alipokuwa akimwambia Husain (a.s.) maneno haye, machozi yalikuwa yakimtiririka, na alikuwa akimbusu mara kwa mara.

“Hakika watoto hao wawili walikuwa wazuri nmo!

“Hasan na Husain wakasema: ‘Babu! Sisi tumeshindana mwereka, lakini hatuna aliyeshinda. Tumekuja kukuuliza, ni nani mwenye nguvu zaidi.’

“Mtume akawaambia kwa tabasamu tamu.‘Wapenzi wangu! Mwereka si laiki yenu. Nendeni mkaandike hati, kisha nileteebu. Kila atakayeandika hati nzuri, ndiye mwenye nguvu zaidi.’

“Hasan na Husain wakarukaruka kama njiwa wawili na wakaenda zao. Baada ya muda, wakarejea na mbao (loho) mbili ziliwandikwa kwa hati nzuri. Wakauliza!‘Hati ipi ni nzuri, ewe Mtume? Ni nani mwenye nguvu zaidi, Babu?’

59

“Mtume alizitazama hati zote mbili. Ni wazi kuwa hakutaka kuvunja moyo wa yeyote kati yao.

“Kama angesema hati ya Hasan ni nzuri zaidi, huenda Husain angevunjika moyo. Na kama angesema hati ya Husain ni nzuri zaidi, huenda Hasan angehuzunika.

“Mtume akawakumbatia na kuwabusu wote wawili, huku akicheka, akawaambia: ‘Hati zote mbili ni nzuri, lakini mimi siamui.

‘Sote twende zetu kwa baba yenu Ali bin Abu Talib ili yeye aamue.’”

Balozi wa Roma aliendelea kuhadithia:“Nilikuwa nikipenda sana kujua jambo hilo litamalizikia vipi. Vipi Ali (a.s.) ataamua, na yupi atamtangaza kuwa ni mshindi!

“Lakini sikuweza. Niliona haya kumwambia Mtume anichukue pamoja naye.

“Nilikaa tu. Nilikaa pamoja na Masahaba wengine humo Msikitini. Salman alifuatana

nao. Salman alikuwa karibu sana na Mtume. Mtume alikuwa akimhesabu kuwa ni miongoni mwa Ahli Bait yake.

“Kisa kilichobakia nilikisikia kutoku kwa Salman.”

Bolozi wa Roma alipofika hapo, akamnukuu Salman akiendelea kusimulia kisa chenyewe: “Mtume, Hasan na Husain wakazichukua lobo mbili na wakampa Ali (a.s.), na kusema: ‘Hati zote mbili ni nzuri. Pelekeni kwa mama yenu aamue.’

“Mtukufu Fatima - amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake - alimtazama Hasan, alimtazama Husain; kisha akazitazama hati mbili.

“Hati zote mbili zilikuwa nzuri na zilipendeza, ingawa zilitofautiana. Hati hizo hazikuwa tofauti sana hata kuweza kusema kwamba: mmoja ameshinda, mwingine ameshindwa. Vile vile Bibi Fatima (a.s.) hakuwa tayari kuvunja moyo wa mtoto yeyote.

“Bibi Fatima (a.s.) aliwakumbatia wate wawili na kuwaambia:

60

‘Mimi ninayo njia moja ya kuamua. Mkufu wangu una shanga saba. Nitaukata mbele yenu. Kila atakayekusanya shanga zaidi atakuwa mshindi.’

“Ulikuwa utatuzi mzuri. Watoto wote wawili walikubali kwa hamu kushiriki katika mashindano haya. Shanga zilipotawanyishwa mbele yao, kila mmoja alifanya haraka kutafuta shanga zaidi.

“Lakini hakuna aliyepata zaidi ya shanga tatu. Ushanga wa saba ulipotea! Kila walivyozidi kutafuta, hawakuweza kuupata ushanga wa saba. Ajabu! Kana kwamba Mwenyezi Mungu pia hakutaka kuuvunja moyo wa mtoto yeyote.

“Hasan na Husain waliwatazama mama, baba na Mtume wao. Hakuna aliyesema kitu. Wote walikuwa wakitazama tu na kungojea kuona Mwenyezi Mungu anaamua vipi

“Hasan na Husain waliendelea kutafuta. Uko wapi huo ushanga wa saba ambao hakuna aliyeupata!? Kwa ghafla, watoto wawili walipiga kelele kwa

furaha. Kila mmoja amepata.

“Kila mmoja amepata nusu moja ya ushanga wa saba. Wote walifurahi mno. Mashindano hayakuwa na mshindwa. Wote kwa furaha. Kila mmoja amepata.

“Kila mmoja amepata nusu moja ya ushanga wa saba. Wote walifurahi mno. Mashindano hayakuwa na mshindwa. Wote wawili walishinda.”

Balozi wa Roma alimpokonya Yazid fimbo yake, akaivunja na kusema: “Ewe Yazid! Huyu mtu uliyemwua na kichwa chake ukakiweka mbele yako, na unaupiga mdomo na meno yake, ndiye huyo huyo Husain!

“Huyu ndiye Husain ambaye Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na binti wa Mtume Wake, na Wasii wa Mtume Wake, hawakuwa tayari kumvunja moya wake hata katika mchezo wa watata!

“Ukatike mkono wako, Ewe Yazid! umejipachika Ukhalifa waMtume hali unamtendea hivi mwana wa Mtume!?”

61

WAFUASI WA YAZID NI NANI?

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Imetafsiriwa na:Maalim Dhikiri U. M. Kiondo

Makala hii ni sehemu ya mwisho ya Kitabu kiitwachoMawahhabiyah na Wauaji wa Imam Husain (a.s.) cha

Allamah Sayyid Saeed Akhtar RizviNdugu wasomaji, kwa maelezo zaidi juu ya wauaji wa Imam Husain (a.s.) soma kitabu kilichotajwa hapo juu.

Kwenye mwaka wa 1954 watawala wa Raisi ya Uarabuni (ambao kwa makosa huitwa Saudi Arabia) walikuwa bado hawajatiwa kiburi na dola ya petroli. Hivyo, hawakuhisi kuwa walikuwa mashujaa mno kiasi cha kuyatangaza mapatano na mapenzi yao kwa Yazid. Hii ndio maana ilinibidi nizipange thibitisho za kiuandishi hizo hapo juu, ili kuonyesha uhusiano wao na wauaji wa Imamu Husayn (a.s.).

Kwenye miaka ya 1960 Mwarabu mmoja (ambaye nadhani ni Mwahhabiya), hapa mjini Dar es Salaam aliniambia: “Nyie watu mlimwua Imamu Husayn”. Nikamjibu: “Sawa! Lakini hebu,

yasikilize haya ninayotaka kukueleza.” Mimi nikasema:(La’ana Allahu ummat qatalat al-HusaynWa la’ana Allahu ummat dhala-mat al-HusaynWa la’ana Allahu ummat sami’at bi dhaalika faradhiyat bihi)

“(Laana ya Allah na iwe juu ya watu waliomwua Imamu Husayn; na laana ya Allah na iwe juu ya watu waliomdhulumu Husayn; na laana ya Allah na iwe juu ya watu walioyasikia hayo (maovu aliyotendewa Husayn) na wakayaridhia).”

Kisha nikamwambia ayatamke maneno haya iwapo yu mkweli kwenye hilo dai lake.

62

Yeye alikataa.

Kwenye mwaka 1973 bei ya petroli ilipanda kwa kiwango ambacho hakikuweza kutegemewa kabla yake. Sasa Mawahhabiya wa Saudia wakawa na uwezo wa kukodi kalamu na vinywa, kila mahali ulimwenguni na sasa wakaanza kuionyesha rangi yao halisi. Wizara yao ya Elimu, kwa ujasiri mkubwa ikachapisha na kuwatawanyia bure Mahujaji, kitabu kiitwacho:

Haqaiq ‘an Amir al-Mu’minin, Yazid ibn Mu’awiyah(Ukweli juu ya Amirul Muminin, Yazid ibn Mu’awiyah).

Mnamo tarehe 6 Aprili 1989, nilisimama kwenye soko kuu la mjini Karachi (Pakistan) nikiutazama msikiti mpya, mkubwa na wenye mnara mrefu sana. Kwenye kitako cha mnara huo ilikuwako sentensi ya Kiurdu iliyoandikwa kwa

maandishi makubwa na yenye kuvutia machoni. Sentensi hiyo ilidai hivi: “Hadhrat Amiirul Muuminiin Yazid - Allah na Amwie Radhi - yu miongoni mwa watu wa Peponi.”

Hivyo, mwuaji wa Seyyid wa vijana wa Peponi ataingia Peponi! Inashangaza, au sivyo?

Lakini linaloshangaza zaidi ya hayo ni ule ufedhuli wao wa kuendelea kuwashutumu Mashia kuhusiana na mauaji ya Imamu Husayn (a.s.) kama ilivyofanywa na Mawahhabiya wa mjini Dar es Salaam mwaka uliopita na kumhimiza Al-Haj Muhsin Alidina kuitafsiri makala yangu ya Kiurdu.

Mawahhabiya waelekea kuielewa vizuri sana methali ya Kiarabu isemayo: “Kama huna haya basi fanya lolote lile upendalo.”

IMAMU HUSAYN (A.S.)ASEMA:

KUFA KWA HESHIMA NI BORAKULIKO KUISHI KWA AIBU

*****

63

NAFASI YA WANAWAKEKATIKA HISTORIA YA

ASHURA

Imetafsiriwa na:Sayyid Muhammad Ridha Shushtary

Tukio la Karbala ni dhihirisho la ukakamavu wa haki mbele ya uzukaji wa upotofu na bidaa. Upotofu ambao ulikuwa ukihatarisha msingi wa Uislamu na kufanya uamuzi wa mambo ya Waislamu uamuliwe na watu wasiofaa na kuhosika. Katika hali kama hiyo, mbali na Imam Husain (a.s.) na wafuasi wake ambao walitambua hatari ya kupotoshwa Uislamu, wanawake pia walifuatana naye ambao walilelewa katika chuo cha Kiislamu, na kutokana na kujifunza mafunzo yake matukufu, walipata shakhsia na uhuru halisi. Kwa jumla, dini ya Kiislamu imebadilisha mawazo yasiyokuwa ya kiutu kuhusiana na wanawake, na kutokana na nafasi ya kimsingi waliyonayo wanawake katika jamii, inatambua kwamba ni lazima zifanywe juhudi kukuza fi kra na maarifa yao.

Kwa upande mwingine, Uislamu unatambua kwamba nafasi ya ulezi wa mwanamke unathamani sawa na jihadi. Kwa wakati huo huo, mafundisho ya Kiislamu yanatanabahisha jambo hili kwamba wanawake wanapaswa kushiriki kwa hima na kutoa mchango wa maana katika jamii katika nyakati muhimu. Katika tukio la mwaka 61 Hijria, wanawake walichukua nafasi muhimu sana. Wanawake walitumia uwezo wao wote wakiwa pamoja na Imam Husain (a.s.) kuhifadhi thamani za kimaanawi, kiroho na kibinadamu.

Wanafi kra wanaamini kwamba nafasi ya wanawake katika kuandika historia ya tukio la Ashura haiwezi kukataliwa.

Katika tukio hilo, mfungamano wa mapenzi na akili, sura ya kupendeza kabisa ya kutoa

64

mhanga, uaminifu na imani, vimedhihirishwa; na historia haikurekodi hata katika zama hizi nafasi kama hiyo iliyochukuliwa na mwanamke.

Kuhamasisha naKupambana

Nafasi ya mwanamke katika Ashura ilidhihirika katika sura mbili. Kwa upande mmoja ilidhihirika wakati wa mapambano kutokana na kuwahamasisha na kuwashujaisha wanaume katika kulihami jeshi la haki. Na kwa upande wa pili, baada ya kuuawa shahidi Imam Husayn (a.s.) na masahaba zake kwa kuchukua jukumu la kufikisha ujumbe wa mapambano hayo.

Miongoni mwa wanawake hao alikuwepo mama yake Wahab ambaye alimpeleka mwanawe kumsaidia Imam Husain (a.s.). Mama wa Wahab alipokuwa katika uwanja wa vita na kukiona kichwa kilichokatwa cha mwanawe, alikibusu, kisha akamshukuru Mwenyezi Mungu - kwa kusema kwamba mwanawe ameweka utukufu wa Uislamu.

Baada ya tukio la Karbala, sehemu kubwa ya matokeo mazuri ya mapambano ya Imam Husain (a.s.) yalitokana na ukakamavu na juhudi za wanawake kama vile Bibi Zaynab, dadake mpenzi Imam Husayn, na wanawake pamoja na mabinti wengineo ambao walikuwepo katika tukio la Karbala, na ambao walichukuliwa mateka. Wao licha ya kuwa na uchungu mkubwa kutokana na kuuawa shahidi Husayn bin Ali (a.s.), na waume pamoja na wana wao, walijitahidi kufikisha ujumbe mtakatifu wa mapambano hayo ambayo maadui walikuwa wakidhani kwamba yalimalizika adhuhuri ya Ashura.

Bibi Zaynab ni mtu aliyechomoza kuliko watu wote baada ya Ashura. Dk. Bint ash-Shaatwi amesema: “Zaynab alichukua wajibu mkubwa na mgumu kabisa baada ya tukio la Ashura, naye akautekeleza vizuri sana.”

Mateka

Baada ya ushahidi wa Imam Husain (a.s.). Yazid alitoa amri

65

kwamba watu wa nyumba ya Imam Husain wachukuliwe mateka na wazungushwe mjini Kufa kama ni maadui. Mji ulipambwa na watu waliokuwa wakisherehekea. Ni watu wachacha tu waliweza kuamini kwamba wangeliwaona watu wa nyumba ya Mtume Mtukufu (s.a.w.) kama ni mateka. Lakini baada ya muda mdogo tu waliwaona wanawake mateka, lakini waliokuwa wasemaji hodari na mashujaa. Waliwashuhudia wanawake watukufu na wahifadhi wa Qur’ani, na ingawa walifikwa na msiba, lakini nyoyo zao zilikuwa zikiwaka, na bila kulegea hata kidogo walikuwa wakiwajulisha

Ahli Bait wa Mtume Mtukufu (s.a.w.), na shakhsiya tukufu ya Imam Husain (a.s.) furaha za watu wa mji wa Kufa ziligeuka kuwahuzuni na majonzi, na Bibi Zaynab akaitumia fursa hiyo kutangaza ujumbe wa Imam Husain (a.s.). Na kwa ushujaa na ufasaha usio na kifani akasema:“Enyi Watu! Je, ni kweli kwamba mnalilia masaibu yetu? Je, mnajua vipi mlivyoupasua moya wa Mtume Mtukufu (s.a.w.), na namna mlivyowavua hijabu wanawake wa kizazi cha Mtume? Jueini kwamba adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa wale wasiothubutu kuchukua hatua yoyote na wakashiriki katika dhulma ya madhalimu ni kali.”

KHWAJAMUIENUDDIN CHISHTI AJMERI

ASEMA:

HUSAIN NI MFALME (NI BWANA); HUSAIN NI MFALME WA WAFALME (NI BWANA

WA MABWANA) HUSAIN NI DINI, HUSAIN NDIYEMHIFADHI WA DINI.

KICHWA ALIKITOA, BALI HAKUTOA MKONO WAKEJUU YA MKONO WA YAZID

HAKIKA HUSAIN NDIYE MSINGI WALAILAHA ILLALLAH.

*****

66

NJIA ALIOPITA IMAM HUSAIN (a.s.)KUTOKA MAKKAH HADI KARBALA

Imenukuliwa kutoka kitabu ChaHujjatul lslam Sayyid Muhammad Rizvi

“IMAM HUSAIN THE SAVIOR OF ISLAM”

67

KUJENGA MAKABURI NA KUMLILIAIMAM HUSAIN (A.S.)

Imeandikwa na:Allamah Sayyid Murtadha ‘Askariy’

Kujenga Makaburi:

Kujenga msikiti mahali walipozikwa mawalii wa Mwenyezi Mungu kumetajwa katika Qur’ani Tukufu. Tunasoma katika kisa cha As’hahul Kahf kwamba wale waliowatambua As’hahul Kahf walisema: “Hakika tutajenga msikiti juu yao.” (18:21).

Kwa hiyo, kujenga msikiti, mahali pa ibada, karibu na makaburi ya mawalii kumetajwa katika Qur’an.

Qur’ani Tukufu inasema pia: “Na pafanyeni mahali pa Ibrahim kuwa mahali pa kusali.” (2:125).

Mahali alipokanyaga Nabii Ibrahim (a.s.) ambapo panaitwa Maqamu Ibrahim (katika Masjidul Haram) ni mabali pa kupata tabaruku, na mahujaji wanatakiwa wasali hapo rakaa

mbili. Kwa hivyo, tabaruku za kizama na kimahali asili yake zinatokana na kuteremshwa baraka kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu katika zama na mahali maalum, na baraka hizo hudumu daima dawamu katika mahali na zama hizo. Na huko kuabudu kwetu katika mahali hapo na kumwomba Mwenyezi Mungu hutokana na sababu hiyo hiyo ya kuwepo baraka hizo.

Waislamu wa madhehebu zote, wawe na madhehebu ya Ahli Bait au wa madhehebu ya Makhalifa wanakubaliana juu ya jambo hili.

Katika zama za lbn Taymiyya ambaya alifariki karibu katika mwaka 700 Hijiria, kulikuwepo mijadala mingi. Miongoni mwa mijadala hiyo, ni suala la kutufu kaburi au kutabaruku kwa Maimam watoharifu (a.s.) au Mtume Mtukufu (s.a.w.) lilikuwa likichukuliwa kuwa ni shiriki.

68

Ikiwa kutufu au kulizunguuka kaburi ni shiriki, basi Waislamu wote, Mitume, Mtume Muhammad (s.a.w.) na masahaba ambao walikuwa wakiizunguuka Hajr Ismail watakuwa ni washirikina, kwa sababu Hajr Ismail (iliyopo kandoni mwa Kaaba) ni makaburi ya Nabii Ismail (a.s.), Hajar na wana wa Ismail. Hayo yote yanathibitisha kwamba maneno hayo ni ya upinzani (ya Wahabii) na kinyume na Qur’ani Tukufu na sunna za Mtume Mtukufu (s.a.w.).

Kumlilia Imam Husayn (a.s.)

Jambo jingine ambalo limapaswa kujadiliwa ni suala la kumlilia Bwana wa Mashahidi, Imam Husayn (a.s.), katika siku ya Ashura. Suala hili aghlabu huzungumziwa na wafuasi wa Ibn Taymiyya wanaojiita Wasalafi, ambaye Muhammad bin Abdul Wahhab (mwasisi wa Uwahabi) amejenga itikadi zake kutokana na ‘madhehebu’ ya Ibn Taymiyya. Sisi tunajibu hivi kwamba: Tunasoma katika sira ya Mtume Mtukufu (s.a.w.) kwamba wakati Hamza alipouawa shahidi, Mtume

Mtukufu (s.a.w.) alimlilia sana. Vile vile Waislamu waliporejea Madina baada ya vita vya Uhud, wanawake wa Kiansari waliwalilia sana mashahidi wao.

Mtume Mtukufu (s.a.w.) akasema: “Hamza hana watu wa kumlilia.” Waansari waliposikia maneno hayo, wakawapeleka wanawake wao kwenye nyumba ya Hamza ili kwanza waomboleze na walie huko.

Mtume Mtukufu (s.a.w.) aliposikia sauti ya vilio vya wanawake, akasema: “Mwenyezi awarehemu Waansari, wanaume na wanawake wao.”

Vile vile wakati Ibrahim mwana wa Mtume Mtukufu (s.a.w.) alipofariki, Mtume alilia kwenye kaburi lake. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba kumlilia mtu mkubwa ni muhimu zaidi kuliko mtu kujililia mwenyewe. Hata kabla ya Wahabi kuuteka mji wa Madina, watu wa Madina walikuwa wakiendelea kufuata desturi hiyo hiyo iliyokuwa ikifuatwa katika zama za Mtume Mtukufu (s.a.w.), kwamba ikiwa mtu amekufa, basi watu walikuwa kwanza wakiomboleza ushahidi

69

wa Hamza na kumlilia, kisha wakimlilia maiti wao. Hiyo ilikuwa sunna ya Mtume Mtukufu (s.a.w.).

Katika juzuu ya tatu ya kitabu changu kiitwacho Ma’alimu ’l-Madrasatayn, nimeelezea kuhusu Sayidu’sh-Shuhadaa (Bwana wa Mashahidi), Imam Huseyn (a.s.). Nimenukuu humo hadith kutoka vitabu vinavyotegemewa vya madbehebu ya Makhalifa (Sunni) kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.) alikuwa akilia mara kwa mara baada ya kupewa habari kutoka kwa Jibrail na malaika wengine juu ya kuuawa shahidi Imam Husayn (a.s.). Mtume Mtukufu mwenyewe alikuwa akiwasimulia

Umm Salma na wengine kisa cha masaibu ya Imam Husayn (a.s.) na alikuwa akilia. Kwa hiyo, kumlilia Imam Husayn (a.s.) ni sunna ya Mtume pia, na hasa kwa kuzingatia kwamba Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s,) wameusia mno kumlilia Imam Husayn (a.s.).

Jambo hili nilizozungumzia, haliwahusu wafuasi wa Ahli Bait peke yao, bali linawahusu Waislamu wote, isipokuwa Wahabi. Waislamu wote wanaafikiana kikamilifu juu ya mambo haya (ya kutabaruku na kumlilia shahidi) kwa kuwa ni katika nususi ya Qur’ani na sunna.

IMAM SHAFII (A.R.)ASEMA:

1. HUSSEIN! ALIULIWA SHAHIDI PASI NA MAKOSA YOYOTE NA KANZU YAKE IKATAPAKAZWA WEKUNDU

2. KWA SABABU YA AHLIL-BEIT WA MTUME (S.A.W.W.), ULIMWENGU MZIMA ULITETEMA NA MAJABALI NA MILIMA ILIKARIBIA KUYEYUKA.

*****

70

HISTORIA FUPI YAMAKBARAH YA IMAMHUSAIN (A.S.) HUKOKARBALA (IRAQ)

A.H. A. D. TUKIO61 1.10.680 Imam Husain (a.s.) alizikwa patakatifu hapa.

65 18.8.684 Mukhtar Ibn Abu ‘Obaidah Thaqafi alijenga uzio wa kaburi katika sura ya msikiti na kujengea Quba kwa matofali na kuwekea sakafu juu ya kaburi. Kulikuwa na milango miwili ya kuingilia.

132 12.8.749 Kulijengwa paa juu la msikiti huo na kuongezewa milango miwili katika zama za As-Saffah.

140 31.3.763 Katika zama za al-Mansur paa lilibomolewa.

158 11.11.774 Paa lilijengwa tena katika zama za al-Mahdi.

171 22.6.787 Katika zama za Al-Rashid paa na Quba vilibomolewa na mti uliokuwa karibu la msikiti uliokatwa.

193 25.10.808 Katika zama za Al-Amin jengo zima lilijengwa tena.

236 15.7.850 Mutawakkil alilibomoa tena jengo hila na kuamrisha kuwa ardhi nzima itifuliwe.

247 17.3.861 Muntasir alijenga tena paa juu ya kaburi na kuweka nguzo ya chuma kuonyesha nishani ya hapo.

280 23.3.893 Kizazi cha Ali (a.s.) walijenga Quba katikati na paa lote pamoja na uzio na milango miwili ya kuingilia.

307 19.8.977 Adad ibn Boweih alijenga tena Quba na sehemu zizungukazo na kujenga Zarih ya mbao kuzunguka kaburi takatifu. Yeye pia alijenga majumba kuzunguka msikiti huo na kujenga kuta za mipaka ya mji. Wakati huo huo Imran bin Shahin alijenga msikiti karibu na makbarah hayo takatifu.

71

407 10.6.1016 Majengo yote yaliteketezwa kwa mote na Waziri Al-Hassan ibn al-Fadhl alijenga tena upya.

620 4.2.1223 Nasir ud-Din alijenga uzio wa kaburi.

757 18.9.1365 Sultan Owais ibn Hasan Jalairi alichongesha makbarah upya na kuinua kuta zake.

780 24.2.1384 Ahmad ibn Owais alijenga minara miwili ambayo aliivika kwa dhahabu na kupanua Baraza.

920 26.2.1514 Wakati Shah Ismail Safavi alipoizuru makbarah alijengesha juu ya kaburi.

1032 15.11.1622 Shah Abbas Safavi alijenga Zarih za shaba na fedha na kutengeneza nakshi kwa vigae vya Kashi.

1048 15.5.1638 Sultsn Murad IV alipoizuru kaburi takatifu aliipakaa chokaa.

1155 8.3.1742 Nadir Shah alipoizuru kuburi takatifu aliirembesha na kutoa zawadi ya vito vya thamani kwa hazina ya makbarah.

1211 7.7.1796 Shah Mohammad Qachar aliivika Quba nzima kwa dhahabu.

1216 14.5.1801 Mawahhabi waliishambulia Karbala wakaharibu uzio wa kaburi tukufu na kupora mali na vito vyote vya thamani vilivyokuwapo.

1232 21.11.1866 Fatah Ali Shah Qachar alifanya matengenezo tena na kuvisha fedha na dhahabu sehemu ya kati na kukarabati kasoro zote zilizotokana na uporaji wa Mawahhabi.

1283 16.5.1866 Nasiruddin Shah Qachar aliipanua Baraza la Makbarah takatifu.

72

1358 21.2.1939 Mulla Tahir Saifuddin, Imam wa Jumuiya ya Mabohora alitoa uzio wa fedha kwa ajili ya Kaburi tukufu ambalo lipo limejengewa katikati.

1360 29.1.1941 Mulla Tahir Saifuddin alijenga tena mnara wa upande wa magharibi.

1367 20.12.1948 Sayyid Abdul Rasul Khalsi, Afisa tawala wa Karbala alinunua majumba kwa thamani iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kujenga barabara na kupanua Baraza.

1411 15.3.1991 Saddam alipiga mizinga 35 aina ya Scud Karbala kuwafagia Mashia.

1411 28.3.1991 Mkwe wa Saddam akiongozwa na vifaru alielekea Makbarah tukufu kwa ajili ya kuangamiza. Makbarah tukufu ilishambuliwa na Mashia 16,000 waliuawa.

1411 3.4.1991 Makbarah tukufu ilifungwa na Mashia wote walipigiwa marufuku kuzuru, vile vile Adhaan pia ilipigwa marufuku. Kuliwekwa maberamu yasemayo: Hakuna Mashia kuanzia leo ..... Hali ya mji wa Karbala inalinganishwa na Beirut ambayo ilikumbwa na vita vya wao kwa wao kwa muda wa miaka 16 ambapo uasi dhidi ya Saddam ulidumu kwa muda wa majuma mawili tu! Inasadikiwa kuwa Saddam amewaua Mashia milioni moja na nusu (1,500,000). Saddam alipora vito vya thamani, dbahabu n.k. na kuteketeza majumba yaliyozunguuka Makbarah tukufu.

73

AMALI ZA ASHURA

Mwezi wa Muharram kama ilivyo miezi mingine ya Kiislamu, unaza ibada nyingi ambazo utazikuta kwenye vitabu vya dua na Ibada kama vile “Mafaatihul Jinnan”, lakini iliyo maarufu sana ni ile inayohusiana na Masaibu ya Imamu Hussayn (a.s.) au Masaibu ya Karbala yaliyotukia mnamo tarehe 10 Muharram, mwaka wa 61 Hijiriya.

Kuanzia usiku wa siku ya kuandama kwa mwezi huu hadi mnamo tarehe 10 au 12 ya mwezi huwa zinaendeshwa Majlisi za kuelezea asili ma matukio ya Mhanga wa Karabala.

Kwenye usiku wa kuamkia tarehe 10, na kwenye mchana wa hiyo tarehe 10 yenyewe kuna Ibada maalum kama ifuatavyo:-

AMALI ZA USIKU WAASHURA

Usiku wa kuamkia tarehe 10 Muharram ni usiku wa huzuni zaidi kwa Mashia. Kwenye usiku huu Ahlul Bayt

(a.s.) walizungukwa na jeshi la askari wapatao 100,000 hivi wa Yazid, wakiwa wamekatiwa maji kwa muda wa siku tatu. Huku watoto wakilia kwa kiu, Imamu Husayn (a.s.) na familia yake na Wafuasi wake waliutumia usiku huu kwa Ibada.

Ahadith za Maasumiin (a.s.) wetu zatueleza kuwa, kukesha usiku huu kuna thawabu nyingi, na kufanya Ibada kwenye usiku huu kuna thawabu za kufanya Ibada kwenye miaka 70. Kukesha kwenye kaburi la Imamu Husayn (a.s.) huko Karbala humfanya mtu kufufuliwa kesho huko Akhera na Damu ya Shahidi (mtu aifiaye Dini yake).

Katika usiku huo fanya hivi:-1. Soma: “Allahumma Swalli

Alaa Muhammadin wa Aali Muhammad” kwa wingi kiasi uwezavyo.

2. Soma maneno: “Allahumal A’n Qatalatal Husayn Wa Awlaadihee Wa Ashaabihee” -- kwa wingi kiasi uwezavyo.

74

3. Sali Rakaa 100 kwa Rakka mbilimbili (kama katika Sala ya al-Fajiri) ukisoma Sura ya Qul Huwallahu-Ahad mara 3 baada ya Alhamdu.

4. Soma Dua ifuatayo: “Allahumma Swalli Alaa Muhammadin wa Aali Muhammad”.

“Subhanallahi Walhamdulil-lahi wa laa ilaha illal Laahu Wallahu Akbar, wa laa hawla walaa Quwwata illa Billahil ‘Aliyil, Adhim.”

“Allahumma Swalli ‘Alaa Muhammadin wa Aali Muhammad.”

5. Imehimizwa sana kusali Rakaa 4 (kwa Rakaa mbilimbili kama katika Sala ya al-Fajiri) na kwenye kila Rakaa, baada ya Sura ya Alhamdu, usome Ayatul Kursi 10, Qul-Huwallahu 10, Qul-Audbu birabil Falaq 10, na Qul-Audbu Birabbin-Nas 10.

6. Vile vile imehimizwa kusali Rakaa 4 (kwa Rakaa mbilimbili kama katika Sala

ya al-Fajiri) na kwenye kila Rakaa, baada ya Alhamdu usome Qul-huwallahu Ahad mara 25.

7. Usiku huu ni muhimu kwa marafiki wa Ahlul Bayt (a.s.) kuutumia muda mrefu kiasi iwezekanavyo katika Ibada, Dua, Sala, na kusoma Qur’ani Tukufu.

SIKU YA ASHURAKatika siku hii kuwa mwenye huzuni kama uliyepoteza nduguyo mpenzi na fanya Ibada zifuatazo:-

1. Jinyime kula chakula na kunywa maji bila ya Nia ya kufunga tangu al-Fajiri ya kweli hadi wakati wa alasiri.

2. Soma Sura ya Qulhuwallahu Ahad mara 1,000

3. Soma “Allahumal A’n Qatalatal Husayn Wa Awlaadihee Wa Ashaabihee” --- mara 1,000.

4. Sali Sala ya Rakaa 4 (kwa Rakaa mbilimbili kama katika Sala ya al-Fajiri) kwa utaratibu huu:-

75

(a) Katika Rakaa 2 za Kwanza:Katika Rakaa ya 1 baada ya “Alhamdu” soma “Qul-yaa Ayyu-hal Kafiruun”, na kwenye Rakaa ya 2, baada ya “Alhamdu” soma Qul-huwallahu Ahad”.

(b) Katika Rakaa 2 za Pili:Katika Rakaa ya 1 baada ya “Alhamdu” soma Al-Ahzab (Sura ya 33), na katika Rakaa ya 2 baada ya “Al-hamdu”, soma Sura ya Al-Munafiquun (Sura ya 63).

5. Soma “Laana” 100 na “Swalawaat” 100.

6. Soma “Ziyaratul-Ashura.”

7. Soma Ziyaratul-Waritha.

8. Sali Sala ya Rakaa 2 kwa Nia ya Sala ya Ziyarat.

9. Soma Dua Al-Qamah.

10. Soma Dua kutoka “Zaadul-Maad.”

11. Tembea mara 7 kimbele mbele na kinyume nyume ukisoma hivi:-“Ina Lillahi wa inna ilaihi Raaj’uun, Ridhan biqadhaihi wa tasliman li Amrihi.”

12. Unapowadia wakati wa Alasiri soma “Ziyaratul-Taaziyah”.

13. Fungua kwa kunywa maji kisha ikumbuke kiu ya Imamu Husayn (a.s.) na uwatakie “laana” wauaji wake.

14. Kula chakula chepesi na bila ya kushiba sana.

IMAM HUSSEIN (A.S.)ASEMA:

IMAM HUSAIN (A.S.) ALIPOKUWA SAFARINI KWENDA KARBALA ALISEMA:

“KAMA DINI YA (MTUME) MUHAMMAD (S.A.W.W.) HAIWEZI KUENDELEA ILA KWA KUKITOA MHANGA KICHWA CHANGU, BASI UPANGA NA UJE UKICHUKUE”

*****

76

ZIYARATE WAARITHA(Ziyara ya Mrithi)

Imeandikwa na:Maalim Kassamali Chandoo,

ZanzibarKusoma Ziyarate Waaritha maana yake kumtolea salamu Imam Hussein (Imam wa tatu katika ma-Imamu 12). Inaitwa Ziyarate Waaritha (Ziyara ya Mrithi) kwa sahabu Imam Hussein ni Mrithi wa Watume wa Mwenyezi Mungu, kuanzia Adam mpaka Mtume wa Mwisho Muhammad (amani na rehema za Mungu juu yao). Vile vile kamrithi baba yake Imam Ali, Imam wa Kwanza wa Waislamu. Imam Hussein karithi kwao hekima, elimu, subran, ucha-Mungu, ushujaa na vitendo, tabia na sifa zote nzuri. Yeye ndiye miongoni mwa waliyoiokoa Dini ya Ki-Islamu. Dini ya Mwenyezi Mungu, Dini iliyoanzishwa na Mtume Adam na kukamilishwa na Mtume Muhammad. Baada ya kufariki dunia Mtume Muhammad (632 A.D.), ulifi kia wakati jahazi la Uislamu lilikuwa linapigwa na mawimbiya unafi ki na ukafi ri, na

lilifi kia kuzamishwa na nahodha wake Yazidi, mtoto wa Muawiya.

Huyu Yazid alikamata kwa nguvu Usukani wa jahazi la Uislamu ili apate kulizamisha. Katika mwaka 680 A.D. Imam Hussein akamwaga damu yake, ya ndugu zake, ya watoto wake na masababa zake kuyatuliza yale mawimbi makali yaliyokuwa yanakaribia kulizamisha jahazi la Uislamu. Akakubali ukoo wake mzima upotee, lakini Dini ya Mwenyezi Mungu ibakie. Basi katika Ziyarate Waaritha twamtolea salamu Imam Hussein kwa kumwita yeye mrithi wa Watume. Tunasema:“Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi wa Adam, Aliyechaguliwa na Mungu. Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi wa Nuh, Nabii wa Mungu. Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi wa Ibrahim, Mpenzi wa Mungu. Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi

77

wa Musa, Aliyeongea na Mungu.Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi wa Isa, Roho wa Mungu.Amani iwe juu yako, Ewe Mrithi wa Muhammad, Kipenzi cha Mungu. Amani iwe juu Yake, Ewe Mrithi wa Kiongozi wa Walioamini (Ali), Rafiki wa Mungu. Amani iwe juu yako, Ewe mtoto wa Muhammad, Aliyechaguliwa. Amani iwe juu yako, Ewe mtoto wa Ali, Aliyeridhiwa. Amani iwe juu yake, Ewe mwana wa Fatima, Mwenye Nuru. Amani iwe juu yako, Ewe mwana wa Khadija Mkubwa. Amani iwe juu yako, Ewe mwenye kulipizwa kisasi na Mungu, na Mtoto wa mwenye kulipizwa kisasi na Mungu; Mwenye kupotezewa watoto wake. Mimi nashuhudia kwamba wewe (Imam Hussein) umeimarisha sala, na umetoa zaka, umeamrisha mema, umekataza mabaya na umemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake mpaka ulipouawa. Basi laana ya Mwenyezi Mungu iteremshwe juu ya wale watu waliokuua wewe, na laana ya Mwenyezi Mungu iteremshwe juu ya wale watu waliofanya dhulma juu yaka na laana ya

Mwenyezi Mungu iteremshwe juu ya wale waliosikia hayo na kufurahia.

Ewe Kiongozi wangu, Ewe baba wa Abdulla (Ali Asghar), Mimi ninashuhudia kwamba wewe ulikuwa Mwangaza tangu asili ya wazee wako watakatifu. Wewe umetakasika na uchafu wa zama za ujinga, wala hukuvishwa nguo chafu za zama hizo. Mimi nashuhudia kwamba wewe ni kutoka nguzo ya dini, na viongozi wa Walioamini.Nashuhudia kwamba wewe ni Kiongozi mwema, Mcha-Mungu.Mimi nashuhudia kwamba ma-Imamu (9) katika vizazi vyako ni Viongozi wa ucha-Mungu Mabingwa wa Uongozi, kamba madhubiti na Alama juu ya watu wa dunia. Na mimi namweka Mwenyezi Mungu shuhuda, na Malaika wake, kwamba mimi naleta imani juu yenu, na ninaya yakini juu ya kurejea kwenu (Imam Mehdi kurejea), juu ya Sheria ya dini yangu, na matokeo ya vitendo vyangu. Moyo wangu umesalim amri kwenu nyinyi, na mambo yangu yatakuwa yanakwenda kwa mujibu ya mwendo wenu.

78

Rehema na Barka ya Mungu iwe juu yenu, juu ya roho zenu, na viwiliwili vyenu; waliokuwepo na wasiokuwepo katika nyinyi, waliodhirika na waliofichika katika nyinyi.”

Tusisahau kwamba katika hii Ziyarate Waaritha, tunampa ahadi Imam Hussein kwamba mwendo wetu tutaoenda utakuwa kwa mujibu wa mwendo wake. Na mwendo wake, kama tulivyoshuhdudia ni:Kuimarisha sala, kutoa zaka, kuamrisha mema na kukataza mabaya, kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake mpaka yatapafika mauti.

Basi mapenzi ya kweli juu ya Imam Hussein ni kujitahidi siku zote kumfuata yeye kwa vitendo. Kwa mfano, Imam Hussein Kaimarisha sala ya Jamaa na masahaba zake wakati wa adhuhuri siku ya Ashura, ingawa walikuwa wamezungukwa na maadui na walikuwa na njaa na kiu ya siku tatu. Wamesali kwa wakati wake na sala ya Jamaa. Na Dini ya Kiislamu, nguvu yake ipo katika kusali juu ya wakati na kusali msikitini sala ya Jamaa. Wengi katika sisi hatuamki

asubuhi kusali sala ya asubuhi kwa wakati wake, na kusoma Qur’an, na katika sala zingine vile vile tunalegea. Tujikaze sisi na watoto wetu katika kutimiza hii ahadi tunayompa Imam Hussein. Vile vile katika chochote Mwenyezi Mungu atupacho, na sisi tutuoe Zaka, Na tusiache kuamrisha mema na kukataza mabaya. Tukumbuke kila wakati kwamba Uislamu umesimama kwa kumwagwa damu ya watu wengi watukufu; hata mtoto wa miezi sita (Ali Asghar) katoa sehemu yake katika Dini hii tukufu. Basi tusimkasiri Imam Hussein kwa kuelekea upande wa maasi na ukafiri, yaani upande wa mawimbi ya Yazid; bali tuelekee upande wa mila za Kiislamu, kwa kumtii Mwenyezl Mungu na Mtume wake Muhammad. Na kwa kufanya hivyo ndio salama na kheri yetu wenyewe, hapa duniani na kesho Akhera.

Namaliza kwa kuandika mashairi juu ya Imam Hussein. Amesema Chisti katika lugha ya Farsi:Shahast HusseinBadshahst HusseinDinast HusseinDipanahast Hussein

79

Sar dad.Na dad dast dar daste YazidHakkake Binae La ilahastHussein.

Maana yake:“Hussein ni Mfalme (ni Bwana)Hussein ni Mfalme wa Wafalme, (ni Bwana wa Mabwana)Hussein ndiye Mhifadhi waDini,

Kichwa alikiwa, bali Hakutoamkono kuuweka juu yamkono wa Yazidi.Hakika Hussein ndiye msingiwaLa ilaha illallah.

Wassalamu AlalkumWarahmatullahiWabarakatuh.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)ASEMA:

1. Ewe Mola wangu! Mpende yule ampendae Husain.

2. Adhabu atakayoipewa yule mwuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayoipewa wenye dhambi waulimwengu.

3. Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia.

*****

80

VITABU VYA KISWAHILI JUU YAIMAM HUSAIN (A.S.) NA MASAIBU YA KARBALA

Imekusanywa na:Sayyid Murtaza Rizvi

1. CHEMCHEM YA UHURUToleo la kwanza lilichapishwa mwaka 1976.

Maisha ya Imam Husain (a.s.)kwa ufupi. Kiliandikwa na Allamah Sayyid Ali Naqi Naqvi, na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Bw. L. W. Hamisi Kitomboy.

Kitabu hiki kina milango minne kama ifuatavyo: Nasaba, Kuzaliwa kwake, kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.), Tabia yake, Masaibu ya Karbala, na Hadithi chache za Imam Husain (a.s.).

Imetolewa zaidi ya toleo tatu na Bilal Muslim Mission of Tanzania, S.L.P. 20033, Dar es Salaam.

2. SHUJAA BAADA YA KARBALAMaisha ya Imam Zainul Abidiin bin Husain (a.s.) kwa ufupi. Kiliandikwa na Allamah Sayyid Ali Naqi Naqvi, na

kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Bw. L. W. Hamisi Kitomboy.

Kitabu hiki kina milango sita kama ifuatavyo. Nasaba, kuzaliwa kwake, kulelewa kwake, ndoa yake, Masaibu ya Karbala.

Kimetolewa zaidi ya toleo mbili na Bilal Muslim Mission of Tanzania, S.L.P. 20033, Dar es Salaam.

3. MAWAHHABIYAH NA WAUAJI WA IMAM HUSAIN (AS.)Toleo la kwanza lilichapishwa mwaka 1996.

Kitabu hiki kina eleza kuhusu wauaji wa Imam Husain (a.s.) walikuwa ni nani; na nani hadi sasa wanawafuata. Kimeandikwa na Allama Sayyid Saeed Akhtar Rizvi na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Maalim Dhikiri Omari Kiondo.

81

Kina milango Mitano kama ifuatavyo: Swali la kwanza, Swali la pili, Swali la tatu, Mwishilizo na hati ya nyongeza.

Kimetolewa mara mbili na Bilal Muslim Mission of Tanzania, S.L.P. 20033, Dar es Salaam.

4. MAOMBOLEZO YA KlFO CHA IMAM HUSAIN (A.S.)Toleo la kwanza 1998.

Kimeandikwa na Allamah Sayyid Abdul Husain Sharafuddin al-Musawi, na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Shaykh Musabah Shaban Mapinda.

Kitabu hiki kimetolewa na Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly of Tanzania, S.L.P . 75215, Dar es Salaam.

Hiki ni kitabu cha Majlisi, kuna Majlisi kumi na mbili za Maudhui mbali mbali juu ya Imam Husain (a.s.) na Karbala.

5. MASHAIRI YA MASAIBU YA KARBALAToleo la kwanza 1999.

Kimekusanywa na Sayyid Murtaza Rizvi na Sheikh Abdul Majid Nassor.

Hiki ni kitabu cha Nauha na Utenzi (Mashairi); kuna Nauha na Matam Saba na Utenzi kumi na moja.

Kitabu hiki kimetolewa na Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly of Tanzania, S.L.P . 75215, Dar es Salaam.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ASEMA:Naapa kwa Yule ambaye Roho yangu i Mikononi Mwake (yaani Mwenyezi Mungu), hakuna hata mtu mmoja atakayasogea mbele (japo) hatua moja katika Siku ya Kiyama mpaka atakapoulizwa kuhusu: 1. Jinsi alivyoyatumia maisha yake;2. Vipi alijipatia mahitaji yake ya maisha; 3. Ameutumia utajiri wake kwa ajili ya kufikia lengo gani,

na4. Kama alikuwa na mapenzi kwetu sisi, Watu wa Nyumba

(Ahlul-Bait wa Mtume s.a.w.w.)

*****

Kimetolewa na Kuchapishwa na:Bilal Muslim Mission of Tanzania

S.L.P 20033Dar es Salaam

ISBN: 9987 620 10 8