26
SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA LENGO LA SERA: Kutumia rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi ili kuchangia mafanikio ya awali ya kuondoa umasikini na kujenga thamani ya kudumu katika jamii. TAFSIRI MAARUFU APRIL 2014 WIZARA YA KAWI (NISHATI) NA USTAWISHAJI WA MADINI JAMHURI YA UGANDA

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDApau.go.ug/uploads/Popular_NOGP_Swahili.pdf · (wale ambao wameiandaa nakala maarufu ya sera ya taifa ya mafuta na gesi). Ni matumaini yangu aminifu

  • Upload
    others

  • View
    18

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

LENGO LA SERA:Kutumia rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi ili kuchangia

mafanikio ya awali ya kuondoa umasikini na kujenga thamani ya kudumu katika jamii.

TAFSIRI MAARUFU

APRIL 2014

WIZARA YA KAWI (NISHATI) NA USTAWISHAJI WA MADINI

JAMHURI YA UGANDA

For more information please contactMinistry of Energy and Mineral Development

Amber House, Plot 29/33, Kampala Road,P. O. Box 7270, Kampala, Uganda

Tel: +256 (0)414 341494www.energyandminerals.go.ug

www.petroleum.go.ug

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

1

JAMHURI YA UGANDA

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

LENGO LA SERA :

Kutumia rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi ili kuchangia mafanikio ya awali ya kuondoa umasikini na kujenga thamani ya

kudumu katika jamii.

TAFSIRI MAARUFU

APRILI 2014

WIZARA YA KAWI (NISHATI) NA USTAWISHAJI WA MADINI UTANGULIZI

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

2

UTANGULIZI

Wizara ya Kawi na Ustawishaji wa Madini ((Ministry of Energy and Mineral Development) inafuraha kuwakilisha sera maarufuya gesi na mafuta Uganda. Sera ilipitishwa mwaka wa 2008 na kwa sasa iko chini ya utekelezaji. Ukuzaji wa nakala hii ulisukumwana haja ya kutambulisha mipango ya serekali ya kuendeleza ustawishaji

ahsiafunuk ili itibahd an arob aijn awk iseg an atufamay atkes awwananchi wote wa Uganda.Nakala hii itafikishwa kwa wahusika wote ikiwimo Wizara, idara na wakala waserikali, serikali za wilaya, vyombo vya habari, vyama vya kijamii) (civil society organisations), vikundi vya utamaduni, kampuni za mafuta na raia kwa ujumla ikiwa ni njia moja ya kuifanya serikali iwajibike huku tukiendeleza sekta. Kukamilika kwa nakala hii kunadhihirisha juhudi zetu kuweka wazi habari katika sekta kwa njia bora ili kuleta majadiliano kamilifu, uhusikaji na kufanya uamuzi.Ningependa kupongeza timu kutoka kwa wizara ikiongozwa na BW.F.A.Kabagambe Kaliisa, Katibu mkuu, wizara ya kawi na usitawishaji wa madini, pamoja na BW.Ernest Rubondo, Kamishna, idara ya uchimbaji na uzalishaji wa mafuta), BW Clovice Irumba, Jiokemia (Geochemist) na Bi. Gloria Sebikari, a�iisa wa mawasiliano (wale ambao wameiandaa nakala maarufu ya sera ya taifa ya mafuta na gesi). Ni matumaini yangu aminifu ya kwamba, kando na juhudi zingine, uchangiaji na ustawishaji wa sekta ya gesi ambayo itaangazia tamaa na taswira ya watu wote wa Uganda.

Inginia Irene N. Muloni (Mbunge) MPWaziriwa kawi na ustawishaji wa madini.

Aprili 2014

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

3

YALIOMO:

1.1 Sehemu Ya Rasilimali Ya Mafuta 61.1.1 Je’ mafuta na gesi inapatikana Uganda? 61.1.2 Ni wapi ambapo gesi na mafuta vinapatikana? 61.1.3 Ni nani ambao wanaimiliki rasilimali ya mafuta na

gesi?6

1.2 Sera ya kitaifa ya mafuta na gesi ya Uganda 61.2.1 Sera ni nini? 61.2.2 Je, Sera ya kitaifa ya mafuta na gesi Uganda ina

husu nini?7

1.2.3 Ni kwa nini serikali inatakikana iwe na Sera ya sekta ya mafuta na gesi?

7

1.2.4 Je! ni mfululizo gani wa faida wa mafuta na gesi na unahusishwaji na Sera ya mafuta na gesi Uganda (NOGP)?

7

81.2.5 Ni sera gani iliokuwepo na mfumo wa kisheria wa sekta ya mafuta na gesi na sera gani ilioongoza sekta kabla ya kupitishwa kwa NOGP.

1.2.6 Ni vipengele vipi viliangaziwa kwa utungaji wa sera hizi?

9

1.2.71.3

Je! ni miongozo ipi mwafaka ya sera hizi?Lengo ya sera.

1011

2.0 MASWALA NA MALENGO YA SERA 112.1 Ustawishaji wa taasisi 112.2 Upana wa maeneo na usimamiaji wa rasilimali 122.3 Usimamiaji wa mapato ya mafuta na gesi 132.4 Matokeo ya shughuli za mafuta na gesi 132.5 Mchango wa rasilimali ya mafuta na gesi kwa kawi 142.6 kuimarisha uwekezaji 152.7 Uhusikaji wa kitaifa 15

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

4

2.8 Wasiwasi wa raia na matarajio 162.9 Vipengele muhimu 163.0 MFUMO WA KITAASISI 173.1 Majukumu ya serikali 173.2 Majukumu ya kampuni za mafuta 213.3 Majukumu ya vyama vya kijamii na vikundi vya

utamaduni21

4.0 KUFUATILIA NA KUKAGUA SERA 215.0 HITIMISHO 21

SHABAHA

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

5

MIKATO

BOPD Mapipa ya mafuta kwa kila siku

CSO Vyama vya kijamii

EA Maeneo ya uchimbaji

DWRM Idara ya uimarishaji wa rasilimali ya maji

EIA Azimio lamatokeo ya mazingira

EITI Uwazi wa utendakazi wa makampuni yanayochimba

EPS Ratiba ya uzalishaji wa mwanzo

FRD Idara la rasilimali za samaki

HSE Afya Usalama na Mazigira.

MEMD Wizara ya kawi na ustawishaji wa madini

NATOIL Kampuni ya kitaifa ya mafuta

NEMA Idhara ya kitaifa ya usimamiaji wa mazingira

NOGP Sera ya taifa ya mafuta na gesi.

PAU Idhara ya mafuta ya Uganda

PEPD Uchimbaji wa mafuta na idara ya uzalishaji

PSA Mkataba wa ugavi nauzalishaji

RBP Mwongozo bora wa huduma

UWA Idhara ya wanyamapori la Uganda

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

6

1.0 UTANGULIZI

1.1 Sehemu Ya Rasilimali Ya Mafuta 1.1.1 Je’ mafuta na gesi inapatikana Uganda?

Utafutaji wa kina katika eneo la ziwa Albert (Albertine Graben) ulileta kuakikisha kuwepo kwa visima vya mafuta ya kibiashara nchini mwaka wa 2006. Ilikadiriwa ya kwamba mapipa milioni mia tatu (300) ya mafuta ya tapatikana mwanzo wa mwaka wa 2008. Ku�ikia mwisho wa mwaka wa2012, rasilimali ya mafuta ilikadiriwa kuzidi mapipa bilioni 3.5 katika eneo, (pipa 1 ni sawa na lita 159).Ijapokuwa kiasi cha gesi kimegunduliwa kiwango cha hiyo gesi kinachohifadhiwa nchini akijabainishwa kabla ya mipango madhubuti ya matumizi.

1.1.2 Ni wapiambapo gesi na mafuta vinapatikana?Juhudi zinazoendelea za uchimbaji katika eneo la ziwa Albert (Albertine Graben). Sehemu ambayo inapatikana katika eneo la magharibi ya nchi kutokea mpaka wa Uganda na Sudan kusini upande wa kaskazini mwa maziwa ya George na Edward kusini magharibu mwa Uganda.

1.1.3 Ni nani ambao wanaimiliki rasilimali ya mafuta na gesi?Kipengele cha 244 cha kitabu ya Uganda kinatambua uimilikaji na usimamizi wa madini na mafuta katika nchi na serikali kwa niaba ya watu (wananchi). Kwa hivyo serikali inamiliki rasilimali yote kwa niaba yawananchi. Pia katiba inaipa nguvu bunge kutungasheria ya kuongoza uchimbaji na mautumizi yamadini na mafuta.

1.2 Seraya kitaifa ya mafuta na gesi ya Uganda 1.2.1 Serani nini?

Serani mpango wautekelezaji unao pitishwa na shirika kama serikali kwa ku�ikia lengo la muda mrefu. Sera

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

7

hizihua zinachapishwa kwenye vijitabu au njia nyingine zinazopatikana kwa wingi. Sera inaambatana na mikakati ya buni na kuongoza maamuzi na juhudi ambazo zinafanyika katika sekta. Katika nchi ya Uganda, serani lazima iidhinishwe na ikubaliwe na Baraza la mawaziri.

1.2.2 Je, Seraya kitaifa ya mafuta na gesi Uganda inahusu nini?Seraya kitaifa ya mafuta na gesi ya Uganda iliindhinishwa na baraza la mawaziri mnamo tarehe 31/1/2008 ili kuongoza ustawishaji wa sekta ya ujimbajiwa mafuta na gesi ya nchi kufuatia ugunduzi wa rasilimali ya mafuta katika mwaka wa 2006. Serahii inaangazia uchimbaji, ustawishaji, utoaji matumizi warasilimali ya mafuta na gesi.

1.2.3 Ni kwa nini serikali inatakikana iwe na Seraya sektaya mafuta na gesi?Ugunduzi na udhibitishaji wa rasilimali ya mafuta katika eneo la ziwa Albert (Albertine Graben) unaibua nafasi mpya na changamoto kwa nchi. Rasilimali ya mafuta, iwapo itasimamiwa vizuri ina uwezo wa kubadilisha uchumi wa nchi. Serainatarajiwa kuakikisha sekta ya gesi na mafuta inasitawishwa kwa gharama bora na ya ufanisi naya kwamba rasilimali itatumika kuchangia kupunguza umasikini na kubuni faida bora ya nchi ya kudumu.

1.2.4 Je! ni mfululizo gani wa faida wa mafuta na gesi na unahusishwajina Sera ya mafuta na gesi Uganda (NOGP)?Mufululizo wa mafuta na gesi umegawanywa kwa upeo wa juu ,upeo wa kati na upeo wa chini. a) Upeo wa juu unajumuisha upandishaji, kupeana

leseni, uchimbaji na ukuzaji, ustawishaji na Uzalishaji. Uchimbaji unamaanisha kutafuta kuwepo kwa mafuta na kuraisisha na kuendeleza usambasaji wa mafuta ardhini. Ustawishaji unajumuisha maandalizi ya utoaji kwa kuweka vyombo vya ukusanyaji na usafishaji

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

8

wa mafuta gha�i. Uzalishaji ni utoaji wa mafuta yanayopatikana chini ya ardhi hadi kwenye uso wa ardhi, na kutayarisha mafuta kwa usa�irishaji na usa�ishaji.

b) upeo wa kati unahusisha kusa�irisha kwa ukubwa bidhaazamafuta (mafuta gha�i na gesi ya kiasili) namavuno, unahusu kubadilisha mafuta na gesi kuwabidhaa muhimu sokoni na kemikali.

a) Upeo wa chini unahusu usambazaji, kuweka soko na kuuza bidhaaza mafuta.

Sera ya kitaifa ya mafuta na Gesi (NOGP) inahusika na majukumu ya upeo wa juu na wa kati na mfululizo wa mafuta.

1.2.5Ni sera gani iliokuwepo na mfumo wa kisheria wa sekta ya mafuta na gesi na sera gani ilioongoza sekta kabla ya kupitishwa kwa NOGP.

Sekta ya mafuta ya Uganda inaongozwa na;a) Kipengele cha mafuta sura ya 150,)cha sheria za

Uganda mwaka wa1985, na kurudiwa mwaka wa 2000. b) Mafuta (uchimbaji na usalishaji) (mienendo ya shughuli

za uchimbaji) kanuni, mwaka wa 1993. c) Sheria za mazingira, wanyama pori, maji, ushuru,

na ardhina miongozo.d) aotemi awukili oyabma 2002 aw akawm ,iwak ayareS

muongozo miongoni mwa mambo mengine kuhusu upeo wa sekta ya chini.

Kabla ya kubuniwa kwa NOGP sera ya kawi ya mwaka wa 2002 ilitoa muongozo wa mfululizo wa ubora wa mafuta. NOGP inatoa sera ya utawala na usimamisi wa mafuta wa upeo wa juu na inatoa msingi wa kusimamia na kuwekeza katika sekta ndogo. NOGP inapendekeza uzalishaji wa mfumo wa juu wa kisheria.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

9

1.2.6 Ni vipengele vipi viliangaziwa kwa utungaji wa serahizi?a) Seraya kawi mwaka wa 2002 ilikuwa na taswira

kuhusiana na uwanda wa mafuta na gesi, lengo kuu ilikuwa ni kuboresha, kuvutia wawekezaji ,kusimamia kampuni za mafuta na jopo la wafanyakazi. Kwa hivyo, kulikuwepo na haja yasera ya kujumuisha viwango vyote vya upeo wa juu na upeo wa kati.Hivyo ikiwa ni kuboresha na kuidhinishwa, uchimbaji, ustawishaji, utoaji na kuongeza thamani.

b) Kufuatia ugunduzi wa rasilimali ya mafuta mwaka wa 2006, ilibainika wazi kuwa shughuli za mafuta na gesi ziliwajibika kupelekea kubuniwa kwa mikakati mipya ambayo inaagazia changamoto za rasilimali zinazoinuka, utunzaji wa mazingira, hisia za wa wananchi, usimamizi wa ushuru na mengineyo.

c) Mafuta na gesi ni rasilimali isiyofanywa upya kwa hivyo ugunduzi na matumizi yake ni lazima yaendeshwe kwa njia inayofaa ili kuhakikisha kuna manufaa ya hali ya juu kuzidi maisha ya rasilimali.

d) d) Rasilimali hii ina uwezo wa kupeana faida madhubuti kwa nchi kupitia ubunifu wa kazi, kuzalisha ushuru ili kuinua sekta zingine, ustawishaji wa miundo msingi na pia kukua kwa kasi na kubadilisha umma katika nchi kwa hivyo kuchangia kupunguza umasikini na kuimarika kwa maendeleo yanayostahili.

e) Ikiwa haitasimamiwa vizuri, rasilimali ya mafuta na gesi pia na ukusanyaji wa ushuru unaweza kuchangia kuanguka kwa uchumi, kwa hivyo kuna haja ya sheria inayolenga usimamizi wa ushuru kama swala linalofaa kushughulikiwa.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

10

1.2.7 Je! ni miongozo ipi mwafaka ya serahizi?Seraya kiserekali inayohusiana na sekta ya mafuta na gesi imewekwa katika misingi ifuatayo:- a) Kutumia rasilimali iliyopo kubuni faida ya kudumu

katika jamii: Rasilimali ya mafuta na gesiaiwezi kufanya upya na inaweza kumalizika,kwa hivyo ushuru unaotoka kwa rasilimali hii unaitajika kuekezwa kwa sehemu kama vile kustawisha ujuzi, miundo msingi, teknolojia na afya ambayo itafaidi kizazi kijacho.

b) Usimamizi bora wa rasilimali: Sera hii inapigania kuakikisha kuwa rasilimali ya mafuta na gesi inasimamiwa ifaavyo kupunguza gharama ya utekelezaji, kuimarisha uzalishaji wa hali ya juu na matumizi ya kubuni miundo msingi ili kuimarisha maendeleo ya kibiashara nchini.

c) Uwazi na uwajibikaji: Uwazi na habari kuwa�ikia wahusika na wasimamizi katika sekta ni muhimu .Ni zoezi bora kuhusisha wahusika katika shughuli za ubunifu wa sheria, ku�ichua wazi malipo na kunadi shughuli za kuidhinisha na vile kukadiri bidhaa za huduma katika kiwanda.

d) Mashidanona uzalishaji: Sareinaunga mkono mashindano yasio na mapendeleo ikiwa na wazola kuinua ubora na uzalishaji wa operesheni ya mafuta na gesi ili kuimarisha faida kamilifu kwa wawekezaji na jamii kwa kizazi cha leo na kesho.

e) Utunzaji wa mazingira na uifadhi wa viumbe: Shughuli za mafuta na gesi zinawezakusababisha hatari ya mazingira iwapo hazitatumiwa vizuri. Kwa hivyosheria inahakikisha utunzaji bora wa mazingira unatekelezwa.

f) Roho ya ushirikiano: Ili kubuni sekta ya kudumu ya mafuta na gesi. Ni muhimu kuwa na roho ya ushirikianona sheria ya kitaifa ya mafuta na gesi nchini

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

11

Uganda. Ushirikiano uko kwa viwango vinne: (i) Kati ya serikali na kampuni za mafuta, (ii) kati ya jamii zinazoishi pamoja, (iii)baina ya kampuni za mafuta, (iv) na kati ya serikali na mataifa jirani kwa kuchimba na kuzalisha visima vya mafuta kufikia baharini.

g) Uwezo na ujenzi wataasisi: Kampuni ya mafuta na gesi inahitaji ujuzi madhubuti ili kuimarisha faida kutunzamazingira na kubuni utajiri wa kudumu. Kufuatana na hayo sera ina haja ya kuboresha uwezo wa kibinadamu na kujenga taasisi dhabiti katika nchi.

1.3 LENGO LA SERA: KUAFIKIANA NA MAAGIZO YALIYOELEZWA PALE JUU, LENGO LA SERA HIZI NI “KUTUMIA RASILIMALI YA MAFUTA NA GESI YA NCHI ILI KUCHANGIA MAFANIKIO YA AWALI YA KUONDOA UMASIKINI NA KUJENGA THAMANI YA KUDUMU KATIKA JAMII”.

2.0 MASWALA NA MALENGO YA SERASeraya kitaifa ya mafuta na gesi inaeleza maswala ambayo yanaibuka kuhusiana na dhibitisho ya vipimo vya mali ya mafuta na gesi ya Uganda. Maswala haya yanatokeza vipengele kumi muhimu vya sheria na mikakati yake na matendo. Ufuatao ni muktasari wa jinsi ya sheria inavyoangazia maswala fulani.

2.1 Ustawishaji wa taasisiSera inatambua haja ya kuweka mikakati ya kusimamia na kudhibiti sekta mpya ya kimaendeleo. Hii itahusisha utunzi wa sheria mpya na ubunifu wa taasisina vile vile kuimarisha taasisi zilizopona mafunzo maalum na uwezo wa ustawishaji. Kwa mjibu wa lengo hili la sera ni kuweka msingi na usimamizi bora wa rasilimali ya mafuta na gesi nchini. Taasisi mpya zitabuniwa, kwa mfano, idara ya mafuta,

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

12

kudhibiti sekta ya kampuni ya kitaifa ya mafuta ili kuelekeza serikali katika sekta ya kibiashara. Taasisi hizi zitaongezwa kwa wizara ambayo itaongoza ubunifu wa sheria kupitia miongozo ya mafuta. Ubadilishaji huu utaleta matengano kati ya udhabiti na matendo ya sheria ya kibiashara kutokana na sheria zilizowekwa kwa hivyo kuondoa mizozo ya masilahi na kukuza ufanisi.Benki ya rasilimali ya mafuta na gesi pia itaazishwa. Kuimanirishwa kwa utaratibu wa uchimbaji na utekelezaji wa sheria ya sekta pia utatiliwa mkazo.

2.2 Upana wa maeneo na usimamiaji wa rasilimaliHili kuwa na usimamishi bora wa rasilimali ya mafuta na gesi, ni muhimu kujua ukubwa wa visima kupitia ugunduzi na uchunguzi uliofanywa. Hii ni muhimukujua jinsi rasilimali itakavyotumika.Kwa kuidhinishwa kwa maeneo mapya yenye uwezo wa uzalishaji wa mafuta na kuidhinishwa upya maeneo ambayo yamekabidhiwa serikali, yataitaji ubunifu ulio wazi, bora na mipango madhubuti yakuidhinishwa.Kwa hivyo sera inalenga kuakikisha uborakatika kuidhinisha maeneo ya uchimbaji na utoaji wa mafuta. Serikali itaweka wazi mnada ikiwa ni lengo kuu ya kuidhinisha upya wa maeneo mapya. Serikali pia itaepukana na soko kiritimba kwa kuidhinisha na kuboresha kampuni kadhaa za mafuta zilizo hitimu nchini. Ili kuvutia uwekezaji, juhudi za uboreshaji pia zitaendelea kuangaziwa.Kwa kuongezea, sera huboresha uwazi katika usalishaji wa rasilimali ya gesi nchini, kwa kupendekeza mipango ya kimaendeleo ya kimaeneo iliyokabidhiwa na kampuni za mafuta itaangaliwa kimakini kabla ya kuidhinishwa na serikali.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

13

2.3 Usimamiaji wa mafuta na gesiUshuru muhimu utapatikana kutokana na sekta ya mafuta na gesi, ule ambao huenda utachangia kukua na kustawi kwa nchi, ama unaweza kuangusha uchumi ikiwa hautapangwa kimakinifu kwa kupitia njia bora na ya kujitolea. Juhudi hizi ni pamoja na kuakikisha nchi inadumisha mfumo wa uchumi na inapokea ushuru mwafaka na ushuru huu unatumiwa kuchipua maendeleo ya kitaifa kwa kizazi cha leo na kesho.Malengo ya serikali kwa mjibu wa usimamizi wa ushuru ni kuakikisha ukusanyaji wa ushuru na kuutumia kujenga thamani inayodumu kwa taifa letu. Mapato kutoka kwa mafuta na gesi nikama mpato yenye ushuru na yasiokuwa na ushuru kama vile miliki, uwekaji sahihi, mafunzo na ada ya maeneo miongoni mwa mengine. Kutakuwepo na usawa na uwazi kwa matumizi yamapato, ikizingatia matakwa ya serikali za wilaya na wahusika wengine wakati wa ugavi wa miliki kwa mjibu wa katiba. Mapato haya yatatumika kuimarisha maeneo muhimu ya uchumi kama vile elimu, afya na ustawishaji wa miundo msingi kulingana na uwezo wa kiuchumi.Kuakikisha kuwa vizazi vijavyo vitanufaika kutokona na mapato, hazina ya mafuta itabuniwa kuweka mapato ambayo hayatatumiwa. Sera inapendekeza kwamba mikakati mipya ya udhibiti wa malipo, kugawana, matumizi na usimamizi kutokana na shughuli za mafuta na gesi imeimarishwa. Kama njia moja ya kuendeleza uwazi na uwajibikaji, serikali itakuwa mwanachama na kushiriki katika jitihada wazi za viwanda vya uchimbaji (EITI).

2.4 Matokeo ya shughuli za mafuta na gesiSekta ya mafuta na gesi inauwezo wa kuhusika bayana na serikali, uchumi, mazingira na maendeleo ya kibinadamu. Hata hivyo, inaweza pia kuleta hali mbovu ya kiuchumi kwa umma ikiwa haitasimamiwa vizuri. Kutambuliwa

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

14

kunahitajika ili kuleta uwiano kati ya maendeleo ya rasilimali ya mafuta na gesi nchini na kutunza utajiri wa viumbe.Kwa hivyo ni muhimu kuakikisha kua shughuli za mafuta na gesi zinaendeshwa kwa njia ambayo inatunza mazingira na viumbe vilivyomo. Matokeo ya shughuli zagesi na mafuta katika mazingira na viumbe vilivyomo zitaangaliwa kwa karibu na mashirika kama NEMA, UWA, FRD, na DWRM, Ikiwa na uwezo wa kusimamia shughuli za mafuta na gesi katika mazingira na viumbe vitatiwa nguvu.Sheria ya mazingira na viumbe itawekwa kuangazia shughuli za mafuta na gesi na kuakikisha zoezi bora kama vile mipango ya kimaeneo,ramani ya hisia ya mazingira na mipango ya utapakaji wa mafuta katika maeneo yanayotoa mafuta na gesi na kila njia yote ya usafirishaji itaimarishwa.

2.5 Mchango wa rasilimali ya mafuta na gesi kwa kawiUganda inakabidhiwa na changamoto ya usalama wa usambazaji wa bidhaa za mafuta na kuongezeka kwa mahitaji ya kawi kwa ujumla. Rasilimali ya mafuta na gesi inaweza kutumika kuangazia changamoto kwa kupitia uzalishaji wa nguvu za umeme kutokana na mafuta na pia kuchangia bidhaa za mafuta zinazoagiziwa kutoka nchi za nje.Kwa hivyo ni muhimu ya kuwa sera hizo zitaendeleza matumizi ya rasilimali zamafuta kwa njia ambayo italeta thamani kwa taifa. Hii itaafikiwa kwa kutumia kikamilifu mafuta na gesi ya kiasiri nakupiga marufuka kuchoma katika viwango vyote vya mfululizo, mafuta ghafi na gesi kwa viwango vya mapema vinaweza kutumiwa kuzalisha umeme. Kwa Kuongezea, serikali itatia mipango ya kutekeleza katika nchi shughuli za usafishaji wa mafuta ili kubadilisha iwe bidhaa ya mafuta ili kuakikisha usambasaji salama wa bidhaa za mafuta katika soko za nyumbani.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

15

2.6 Kuimarisha uwekezajiUwekezaji madhubuti unaitajika kukuza rasilimali ya mafuta na gesi na kustawisha visima. Uwekezaji mkubwa utahitajika kustawisha rasilimali ya visima vyote vya gesi na mafuta kwa kujenga miundo msingi ya kusafirisha,kuhifadhi na kutengeneza (kusafisha na kubadilisha) mafuta na gesi. Kwa hivyo juhudi inahitajika ili kuvutia waekezaji ambao watashughulika.Serikali itaimarisha na kuunga mkono maendeleo ya usafirishaji bora na uhifadhi ambao utatia thamani kwa rasilimali ya mafuta na gesi ya serikali. Hii itahusisha,lakini bila kupunguza,mabomba ya mafuta, barabara na reli iliyoimarishwa, viwanda na vituo vyake.Hii miundo msingi yote inahitajika kukuza uzalishaji.Kwa hivyo serikali itatengeneza mikakati ya kukuza uekezaji katika utafutaji wa mafuta na kuweka miundo msingi ya kusaidia uzalishaji.

2.7 Uhusikaji wa kitaifa Ustawishaji wa sekta ya mafuta na gesi utaafikia kubuni nafasi za kazi kwa sekta zingine. Ni muhimu kutumia nafasi hizi za uekezaji kuinua kiwango cha nchi kupitia uhusikaji wa kitaifa. Hii inaweza kupitia kumiliki leseni na kuwakilisha bidhaana huduma ya nchi na biashara ya jamii. Kwa hivyo ni muhimu kwa sekta binafasi ya serikali kupata na kukuza ujuzi muhimu wa kuhusika na sekta.Sera hii inakusudia kuhusisha taifa kikamilifu kwa shughuli za mafuta na gesi. Hii itaafikiwa kupitia ujihusishaji wa taifa na uimarishaji wa mali ghafi ya hapa nchini, bidhaa na shughuli za huduma ya sekta mafuta na gesi, kuajiri wananchi wa uganda katika sekta ya mafuta na gesi na kusambaza ujuzi na teknologia kwa nchi. Kwa ujumla, wahusika wote wanaoshiriki watakua muhimu kwakuhakikisha uhusikaji wa kitaifa. Mapendekezo ya taasisi na kisheria yatatoa mfumo wa kushiriki katika leseni kwa kutambua uhusikaji wa raija katika sekta.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

16

Uhusikaji wa taifa pia unahitaji uungwaji mkono wa usitawishaji na utaalamu wa kitaifa.. Kuna haja ya mipango ya maendeleo yao kupitia njia na mafunzo ya viwandani. Serikali itaangali upya na Kupanua mwongozo wa elimu nchini ikiwa na lengo la kuzalisha wafanyikazi watakao shughulika kwa mafuta na gesi ya kitaifa. Kampuni za mafuta zilizoidhinishwa zitaitajika kuwafunza raia wa Uganda.

2.8 Wasiwasi waraia na matarajioMatarajio makubwa kutokana na faida kutoka kwa mafuta na gesi na ustawishaji yameimarishwa katika ummana pia wasi wasi juu ya usimamizi mbaya katika mataifa kama vile ya Afrika. Habari iliyotolewa kwa wakati mwafaka ni muhimu kuangazia kwa kina matakwa ya raia pia ni muhimu katika jamhuri, kampuni za mafuta na wahusika wengine kuhusishwa kwa majadiliano dhabiti na kujenga uhusiano bora wa uishirikiano ili kuangazia shauku na matarajio ya wasimamizi.Kwa hivyo, lengo la Sera nikuakikisha faida sawa ya uhusiano kati ya wahusika wote wa kimaendeleo ya sekta ya mafuta na gesi inayohitajika nchini. Hii itaafikiwa kwakuweka msingi dhabiti wamawasiliano bora ya sekta ya mafuta na gesi na kufanya upelelezi wa kutosha na wahusika kama vile maeneo ya uzalishaji wa mafuta na gesi pamoja na shughuli nyinginezo.

2.9 Vipengele muhimuMatokeo mazuri na mabaya katika sekta ya mafuta na gesi kwenye sekta zingine za uchumi kwa mfano, matumizi yaardhi, mipango ya kiramani, ukaguzi wa fedha, viwanda, kilimo, uvuvi, idadi ya watu, uwepo wa kawi, nafasi za kazi, afya, elimu, utafiti na ushusiano bora na mataifa jirani, na mengineyo yanatambuliwa na sera. Sera itaboresha matokeo mazuri katika sekta ya uchumi na kupunguza matokeo mabaya. Sheria ya kitaifa ya mafuta na gesi

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

17

inapendekeza kwamba matokeo hayo yaangazie sera ya sekta husika na hivyo kuelezea majukumu na kazi ya wizara zingine za serikali, idhaa na vitengo vigine kuhusiana na mafuta na gesi katika taasisi za kisheria zinazopendekezwa hapa chini.

3.0 MFUMO WA KITAASISIUmuhimu wa mfumo wa kitaasisi uko katika mngawanyo wa majukumu kwa wahusika mbalimbali. Mngawanyiko huu unaazia katika viwango tofauti vya vitengo vya serikali, kwa mfano, vituo vya uongozi kama serikali, bunge na mahakama. Sera inalenga kujenga tofauti kati ya majukumuya vitengo mbalimbali vya serikali, makampuni ya mafuta na washusika wengine. Majukumu haya yanaelezwa ifwatavyo;

3.1 Majukumu ya serikalia) Baraza la mawaziri linaamrisha na kuidhinisha

kipengele kinachohitajika na bunge; linaidhinisha wasimamiza wa mafuta na kuwapa ruhusa PSAS kupeana leseni.

b) Bunge linatengeneza sheria ya mafuta ikiwemo uongozi katika pato la mafuta na kuchunguza utendakazi katika sekta ya mafuta kupitia ripoti ya mwaka na shughuli za kidhinisha bajeti.

c) Wizara inayohusika na uongozi wa gesi na mafuta, inapeana miongozo ya sera na inasimamia kazi za mashirika ya mafuta na gesi chini yake,kwa mfano;idhara ya mafuta ya Uganda na kampuni ya kitaifa ya mafuta.Sera inapendekeza kubuni vitengo vitatu vikiwa na majukumu yafwatayo:-i. Shirika la mafuta kwa wizara husika nasera ,

usimamizi na kutathmini na kuunganisha maendeleo katika sekta pia kupeana leseni na ujenzi wa taifa .

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

18

ii. Idara ya mafuta ya Uganda itashikilia uongozi wa vipengele ikiwemo kusimamia shughuli za kampuni.

iii. Kampuni ya kitaifa ya mafuta kama taasisi ya kipekee itakuwa na majukumu yanayohusu ushiriki wa taifa kupeana leseni na shughuli zingine kama hizo.

d) Wizara inayohusika na haki na maswala ya kikatiba inaongoza kubuni na kutengeneza sera, kupeana leseni na kuandaa maongezi na utawala wa PSAS.

e) Wizara inayohusika na fedha, mipango na ustawi wa kiuchumi inahakikisha maendeleo madogo ya kiuchumi istaawishwe, inayohusika na usimamizi wa kimakini na kuhakikisha usambazaji dhabiti wa pesa za serikali. Kuendesha sawa sawa na kutoa huduma kwa njia bora.

f) Wizara inayohusika na serikali ya wilaya inafanya shuguli muhimu za kubuni, kusimamia kustaawisha mipango na ratiba kwa serikali za wilaya ambayo inachukua maelewano ya shughuli za mafuta na gesi.

g) Wizara inayohusika na ujenzi na usafiri inapanga na kuongoza huduma za usafiri, kupeana uongozi wa kiufundi kwa utaalamu wa mashine na pia kushiriki kuhalalisha miundo msingi ya mafuta.

h) Wizara inayohusika na maji pamoja na mazingira, inahakikisha uwiano wa sera na kuafikiana na viwango bora vya uhifadhi na matumizi ya mazingira.

i) Wizara inayohusika na misitu na chemichemi itahakikisha uwianowa sera za mafuta na gesi na vipengele vya ustawishaji na matumizi yarasilimali ya misitu na vile vile kuhifadhi misitu na chemichemi.

j) Wizara inayohusika na utalii na wanyamapori itahakikisha kuwa sera za mafuta na gesi ziko na uwianona sera na shughuli za uhifadhi wa wanyampori na ustawi wa utalii, na kusimamia shughuli za matokeo

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

19

ya gesi na mafuta kuhusu uhifadhi wa wanyama,utalii, uhusiano bora baina ya utalii wa mazingira na mambo ya kale. Wizara ya wafanyikazi itafanya zoezi la kukagua kuhakikisha afya na usalama na uzingativu wa kutekeleza sera za kitaifa za wafanyikazi,miongozo na viwango, inabuni na kuihimiza miongozo ya usalama,inawakilisha matakwa ya wafanyikazi na mizozo na kuchunguza �idia.

k) Wizara inayohushika na elimu itaboresha ustawi wa elimu na kuandaa mafunzo,uta�iti sambamba wa mafunzo ili kubuni nguvu ya kitaifa na ujuzi wa sekta ya mafuta na gesi pamoja na hatua za kurekebisha madhara katika sekta ya elimu.

l) Wizara inayohushika na elimu itaboresha ustawi wa elimu na kuandaa mafunzo,uta�iti sambamba na mafunzo ili kubuni nguvu ya kitaifa na ujuzi wa sekta ya mafuta na gesi pamoja na hatua za kurekebisha madhara katika sekta ya elimu.

m) Wizara inayohusika na mipango itahakikisha uwianowa sera za gesi na mafuta na sera ya viwanda. Kuboresha miongozo ya ustawi wa viwanda pamoja na kutumia mafutana bidhaa za gesi kuimarisha ustawi wa kiviwanda.

n) Wizara inayohusika na maswala ya kigeni itahakikisha uhusiano bora wa mataifa jirani na kupigania utafutaji wa pamoja na uchimbaji wa rasilimali ya mafuta na gesi inayopatikani mipakani.

o) Wizara inayohusika na usalama italinda shughuli za ujenzi wa mashine ya mafuta na gesi dhidi ya uvamizi wowote wa ndani au nje.

p) Wizara inayohusika na habari na teknologia itabuni na kutekeleza sheria za habari na kusimamia usambazaji wa habari na shughuli za uhifadhi wa gesi

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

20

na mafuta, inaboresha, inasadia na kutoa mwelekeo kwa matumizi ya ICT (Teknologia ya kupeana habari kupitia taraklishi) na kuakikisha ya kwamba miundo msingi ya teknologia na habari inajengwa.

q) Banki kuu itasimamia matokeo yote ya mafuta na gesi kwa ajili ya uchumi wa taifa na kuipa mawaidha serikali, pia kuendesha na kusimamia hazina ya mafuta.

r) Idara ya ukusanyaji wa ushuru Uganda itasimamia ukusanyaji wa ushuru, kuchunguza na kubaini mapato kutoka kwa mafuta na gesi kwa uchumi na kubuni hatua bora ya ukusanyaji wa ushuru.

s) Idara ya kitaifa ya mipango itaelekeza mipango dhabiti ya kushirikisha shughuli za mafuta na gesi kukuza uchumi wa kitaifa na kuchunguza uhusiano baina ya vitengo mbalimbali vya almashauri ya usimamizi wa mafuta.

t) Idara ya kitaifa ya usimamizi wa mazingira itahakikisha na kufuatilia shughuli za gesi na mafuta zinaambatana pamoja na miongozo ya viwango vya kimataifa na kuuinganisha matokeo ya kimazingira na ukaguzi.

u) Idara ya wanyama pori ya Uganda (UWA) inafatilia utekelezi wa miongozo na viwango vya kimataifa vinavyosimamia operesheni ya utunzaji wa maeneo ya wanyama pori, ukubali harakati ya utunzaji wa maeneo ya wanyama pori na kufuatilia matokeo, pamoja na kushiriki kwa ukaguzi wa mazingira.

v) Mkakuzi mkuu atapeana upeo wa kibinafasi wa usimamizi wa operesheni ya mafuta ya serikali kupitia fedha na wasimamizi wengine wa ukaguzi na kuhakikisha uzingatifu wa viwango vya taifa na kimataifa vya hesabu.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

21

3.2 Majukumu ya kampuni za mafutaa) Uchimbaji bora wa mafuta, kuzalisha, kustawisha

rasilimali ya mafuta na gesi. b) Kuwa mwananchi mwema na mengineyo, kuheshimu

sera na sheria za nchi vile vile kusimamia maswala yanayoibuka kutokana na shughuli za gesi na mafuta.

3.3 Majukumu ya vyama vya kijamii na vikundi vya utamaduni

Vyama vya kijamii na vikundi vya kitamaduni vinaweza kuchangia kutetea, kuhamasisha na kufanya majadiliano na jamii, kuchangia uwajibikaji kuhusiana na maswala ya mafuta na gesi, kushiriki kukusanya sauti ya wanyonge ionekane, kufuatilia na kutekeleza mipango katika sekta ya mafuta na gesi. CSO’s pia inaweza kupewa kandarasi ya uwasilishaji wa huduma, hasa hasa jamii zinazoishi mahali ambapo shughuli za uchimbaji mafuta na gesi zinaendelea.

4.0 KUFUATILIA NA KUKAGUA SERAKuweka na kuondoa mipango, kukagua na kubaini na kufuatilia viwango tofauti vya kutekeleza sera. Sera inapendekeza kwamba, njia ya matokeo na majibu inayokagua na kufuatilia ikubalike kisera kwa viwango vya miongozo vilivya azishwa na ofisi ya waziri mkuu chini ya usimamiaji, ukakaguzi na tathmini (NIMES), ili kuchunguza mipango ya serikali.

5.0 HITIMISHOMafanikio mbalimbali yamefanywa kufikia kutekeleza sera hizi. Ili kubaini uwezo wa kufikia sasa wakutekeleza sera, wizara iko inastawisha ukaguzi na zoezi la kutekeleza sera za kitaifa za mafuta na gesi Uganda.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

22

Serikali ya Uganda imejitolea vilivyo ustawishaji sekta ya mafuta na gesi kupitia njia ya kutengeneza sera .Wizara ya kawi na ustawishaji wa madini inaalika wahusika wanaoitajika ili kuunga mkono sekta ya maendeleo nchini kupitia kuhusika katika kutengeneza sera ili kuchangia ku�ikia malengo.

MUKHTASARI WA DONDOO MUHIMU KUHUSIANA NA SERA ZA MAFUTA NA GESI UGANDA MASWALAKufuatia uvumbuzi wa rasilimali ya mafuta na gesi Uganda mwaka wa 2006 uliibua maswala yafuatayo:-

1. Haja ya kustaawisha taasisi kurekebisha sheria zilizopo na kukuza nguvu za ustawishaji ili kusimamia na kuongoza sekta kikamilifu

2. Kuboresha usambazaji wa shughuli za rasilimali ya mafuta na gesi na kufadhili mipango ya karibuni, ya kadri na ya baadaye ya sekta.

3. Usimamizi wa rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi,pamoja na ushuru wake kwa njia ambayo itafadhili ustawi wa kujitosheleza ili kuzuia upotokaji na uaribifu wa uchumi wa nchi.

4. Kukuza rasilimali ya gesi na mafuta katika sekta ya nchi ya kiutawala, uchumi na mazingira na mengineyo.

5. Haja ya kuendeleza rasilimali ya mafuta na gesi ili kuchangia kawi ya nchi.Kuakikisha ya kwamba nchi inaweka mazingira bora ya kuwavutia wawekezaji katika viwango vyote vinavyoitajika kwa rasilimali ya nchi na kufadhi maendeleo yake.

6. Kuhusika kwa sekta binafsi ya serikali na wafanya biashara katika sekta ya mafuta na gesi.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

23

7. Usimamizi wa matarajio, unoibuka kutokana na faida yashughuli za gesi na mafuta, pamoja na wasiwasi unoinuka kutokana na ujuzi wa baadhi ya usimamizi mbaya wa sekta zingine kama hizo kutoka sehemu nyingine za dunia.

KANUNI ZA MIONGOZOSera hizo zinaongozwa na kanuni zifuatazo:-

1. Kutumia rasilimali ili kubuni faida za kudumu katika jamii.2. Usimamizi bora wa rasilimali.3. Uwazi na uwajibikaji. 4. Ushindani na Uzalishaji.5. Utunziji wa mazingira na uhifadhi wa viumbe vilivyomo.6. Roho ya ushirikiano.

7. Uwezo na ujenzi wa taasisi. LENGO LA SERA :Kutumia rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi ili

kuchangia mafanikio ya awali yakuondoa umasikini na kujenga

thamani ya kudumu katika jamii.SHABAHA,

• Shabaha 1: Kuakikisha ufanisi katika kuidhinisha maeneo yanye uwezo wa kuzalisha mafuta na gesi nchini.

• Shabaha 2: Kuweka misingi na usimamiaji bora wa rasilimali ya gesi na mafuta.

• Shabaha 3: kuzalisha kwa ufanisi rasilimali ya mafuta na gesi.

• Shabaha. 4: Kuboresha matumizi bora ya rasilimali ya mafuta na gesi .

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

24

• Shabaha 5: Kuboresha maendeleo ya usafiri na uhifadhi ambayo yatapeana matokeo bora ya rasilimali ya mafuta na gesi.

• Shabaha 6 : Kuhakisha ukusanyaji wa mapata ya ushuru na kuyatumia kujenga uwezo wa kudumu wanchi.

• Shabaha 7: Kuhakikisha kushiriki kwa taifa kithabiti katika shughuli za mafuta na gesi .

• Shabaha 8: Kuunga mkono ukuzaji na uimarishwaji na ujuzi wa taifa.

• Shabaha 9: Kuhakisha shughuli ya utoaji wa mafuta na gesi unaendeshwa kwa njia ambayo itahifadhi mazingira na viumbe vilivyomo.

• Shabaha 10: Kuhakikisha kunufaika kwa uhusiono baina ya wahusika wote katika maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi nchini.

Tafadhali tembelea www.petroleum.go.ug ili kupata naka ya sera ya taifa ya mafuta na gesi na hali ya utekelezaji wake.

SERA YA TAIFA YA MAFUTA NA GESI UGANDA

LENGO LA SERA:Kutumia rasilimali ya mafuta na gesi ya nchi ili kuchangia

mafanikio ya awali ya kuondoa umasikini na kujenga thamani ya kudumu katika jamii.

TAFSIRI MAARUFU

APRIL 2014

WIZARA YA KAWI (NISHATI) NA USTAWISHAJI WA MADINI

JAMHURI YA UGANDA

For more information please contactMinistry of Energy and Mineral Development

Amber House, Plot 29/33, Kampala Road,P. O. Box 7270, Kampala, Uganda

Tel: +256 (0)414 341494www.energyandminerals.go.ug

www.petroleum.go.ug