of 140/140
1 Programu kuhusu msaada wa sera kwa ajira vijijini na kazi yenye heshima kwa uhimizaji maisha sawa endelevu vijijini kulingana na mabadiliko ya tabia nchi Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania Kiongozi Cha Mwezeshaji Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle Kwa kushireikiana na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) na Muungano wa Vyama vya Ushirika Zanzibar (CUZA). Kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Kazi

Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana

 • View
  554

 • Download
  6

Embed Size (px)

Text of Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana

 • 1

  Programu kuhusu msaada wa sera kwa ajira vijijini na kazi yenye heshima kwa uhimizaji maisha sawa

  endelevu vijijini kulingana na mabadiliko ya tabia nchi

  Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV) Tanzania

  Kiongozi Cha Mwezeshaji

  Jaap Van Pol na Francesca Dalla Valle

  Kwa kushireikiana na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) na Muungano wa

  Vyama vya Ushirika Zanzibar (CUZA).

  Kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Kazi

  In collaboration with the Ministry of Agriculture, Food Security and Cooperatives and Ministry of Labour

 • 2

  Juzuu ya 1

  Mtaala wa Mada za Kilimo za SDSMV

 • 3

  Yaliyomo

  Mada/zoezi Ukurasa

  Utangulizi wa ufundishaji

  0.1. Zoezi: Kutambulishana na SDSMV

  Mada za Kilimo

  A.1.1. Zoezi: Kujua shamba la kujifunzia na kufanya majaribio

  A.1.2. Zoezi: Sifa za shamba la Kilimo

  A.1.3. Zoezi: Jaribio la Utepe

  A.1.4. Zoezi: Kupanga shughuli zako za Kilimo

  A.1.5. Zoezi: Hatua za maisha ya mazao

  A.1.6. Zoezi: Kuandaa kalenda za mazao

  A.2.1. Zoezi: Kuchagua mbegu bora

  A.3.1. Zoezi: Jaribio la utoaji wa mbegu

  A.4.1. Zoezi: Kuandaa mpangilio wa shamba darasa

  A.4.2. Zoezi: Maandalizi ya Ardhi

  A.4.3. Zoezi: Kwa nini tunahitaji vitalu

  A.4.4. Zoezi: Kuandaa Kitalu

  A.5.1. Zoezi: Kuacha nafasi baina ya mimea

  A.6.2. Zoezi: Kuelewa mifumi ikolijoa ya shmamba

  A.6.1. Zoezi: Kuotesha mazao yanayostawi kwa IPM

  A.6.3. Zoezi: Desturi mbalimbali za kudhibiti visumbufu vya mimea

  A.6.4. Zoezi: Kanuni za Kiasili za Kudhibiti visumbufu vy mimea

  A.6.5. Zoezi: Kulinda mazao dhidi ya wadudu shambani shambani na taratibu za Udhibiti

  Husishi wa Visumbufu vya Mimea (IPM)

  A.6.6. Zoezi: Kupata maarifa zaidi kuhusu wadudu na visumbufu vya mimea

  1

  3

  5

  6

  7

  8

  9

  10

  12

  12

  13

  14

  14

  15

  16

  18

  18

  19

  20

  20

 • 4

  vilivyochunguzwa katika shamba darasa

  A.6.7. Zoezi: Utayarishaji wa dawa kutoka mti wa mwarubaini kwa kudhibiti visumbufu

  A.6.8. Zoezi: Kuepuka madhara ya dawa na Kemikali za Kilimo

  A.7.1. Zoezi: Kutambulisha AESA.

  A.7.2. Zoezi: Ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa Kutumia AESA.

  A.8.1. Zoezi: Palizi, Kwa nini, lini na namna ya kupalilia

  A.9.1. Zoezi: Upandikizaji wa miche (mboga za majani)

  A.10.1. Zoezi: Kuzitambua njia mbalimbali za umwagiliaji na unyevu kwenye udongo

  A.11.1. Zoezi: Urutubishaji wa Udongo

  A.11.2. Zoezi: Urutubishaji wa pili

  A.11.3. Zoezi: Udhibiti wa Rutuba ya Ardhi katika Kilimo Kisichotumia Mbolea za Kemikali

  A.11.4. Zoezi: Rundo la mboji ni nini na tunaweza kutumia vitu gani

  A.11.5. Zoezi: Kutayarisha Mboji

  A.11.6. Zoezi: Kuchagua, kugeuza na kutumia mboji

  A.12.1. Zoezi: Kulinda Shamba letu

  A.12.2. Zoezi: Kujenga uzio

  A.13.1. Zoezi: Wakati na namna ya Kuvuna

  A.14.1. Zoezi: Namna ya Kupunguza Hasara ya Mazao baada ya kuvuna

  A.14.2. Zoezi: Usindikaji/Uhifadhi wa vyakula

  A.14.3. Zoezi: Ghala/Stoo bora

  A.14.4. Zoezi: Kuuza bidhaa/mazao yetu

  Kiambatisho: Mtaala wa Shamba Darasa na Stadi za Maisha kwa Vijana (SDSMV)

  21

  21

  22

  23

  25

  27

  27

  29

  30

  31

  31

  32

  32

  34

  35

  35

  36

  36

  37

  38

  39

  41

 • 5

  Utangulizi wa Ufundishaji SDSMV

  Ufundishaji wa SDSMV

  Mwezeshaji anajaribu kutumia kwa ukamilifu kujifunza kwa (vijana) watu wazima kwa njia ya ugunduzi.

  Vijana watajifunza kadiri iwezekanavyo kwa vitendo, kufanya mazoezi ya kanuni zote za kilimo kwenye

  mashamba darasa yao, kugundua njia mbalimbali kwa kufanya majaribio, kuiga hali za maisha kwa njia

  ya igizo kifani au mchezo wa kuigiza, majadiliano katika vikundi vidogo vidogo na michezo na mbinu za

  kikundi.

  Maana ya mwezeshaji

  Mtu anayeongoza na kuelekeza mchakato. Mtu anayehakikisha mtiririko unaofaa wa taarifa

  ndani ya kikundi ili washiriki washirikiane taarifa na kufikia uamuzi

  Kiongozi/msimamizi wa mchakato wa kujifunza kwa mbinu shirikishi.

  Anayesaidia katika kushirikiana taarifa kwa njia shirikishi

  Kiwango chakukumbuka ni kama ifuatavyo

  20% wakati wanaposikia

  40% wakati wanapoona

  80% wakati wanapogundua

  Uzoefu unaonyesha kuwa

  Unaposikia,unasahau

  Unapoona, unakumbuka

  Unapogundua unamiliki maishani

 • 6

  Jedwali: Tofauti kati ya kuwezesha na kufundisha

  Kuwezesha Kufundisha

  1. Kunahusisha majadiliano Majadiliano kidogo

  2. Ushiriki kwa ukamilifu Ushiriki mdogo

  3. Kunahimiza mawazo yaliyopo na mapya Hutambulisha mawazo mapya tu

  4. Mawasiliano miongoni mwa washiriki Mawasiliano kutoka kwa mwalimu

  5. Kujifunza kusiko rasmi Kujifunza rasmi

  6. Utoaji uamuzi wa pamoja Utoaji uamuzi kiasi

  7. Kushirikiana mawazo Kuelekeza

  8. Kuanzia chini kwenda juu Huanzia juu kwenda chini

  9. Mtaala umetayarishwa kutokana na tathmini ya mahitaji

  Mtaala umetayarishwa na wizara

  10. Vifaa vya kujifunza vinatokanana mshiriki Vifaa vya kujifunzia vinatokana na mwalimu

  K azi na Wajibu wa Mwezeshaji wa SDSMV

  Msaada mkubwa wa kiufundi

  Huongoza katika mchakato wa kujifunza

  Huwa kiungo cha mawasilianona watendaji wa nje na wataalamu

  Husaidia kikundi kufikia malengo yao

  Husaidia udhibiti wa migogoro

  Husaidia kuanzishwa kwa SDSMV mpya.

  Huelezamalengo na mchakato wa SDSMV

  Lazima asaidie uchaguzi na uchanganuzi

  Hufanya majadiliano yawe ya kusisimua

  Hudadisi ili kuwasaidia washiriki kufikia mahitimisho yanayofaa

  Husaidia kutanzua matukio ya kukandamiza mawazo na hisia za washiriki wengine.

  Husaidia washiriki kufikia mwafaka unaofaa

  Usimamizi wa muda

  Huwaheshimu washiriki wote na mawazo yao

  Huwasaidia washiriki kubainisha fursa na na uwezekano kwenye mazingira yao.

  Somo la SDSMV (saa 3 4).

  1. Kuanza /kufungua ( dakika 5)

  2. Muhtasari wa somo lililopita ( dakika 5)

  3. Programu ya leo ( dakika 5)

 • 7

  4. Uchunguzi wa mfumo wa kilimo na Ikolojia (AESA) au mada ya maisha ( saa 1 - 2)

  5. Mapumziko ( dakika 5)

  6. Vichangamsho au group dynamics ( dakika 10)

  7. Mada mahususi (kilimo au mada ya maisha ) ( dakika 50)

  8. Muhtasari ( dakika 5)

  9. Tathmini ( dakika 5)

  10. Kufunga ( dakika 5)

  Mazoezi ya SDSMV

  Mazoezimbalimbali ya SDSMV yaliyochaguliwa yamekusanywa na kuwasilishwa kwenye kiongozi hiki

  kutokana na moduli za mwezeshaji wa SDSMV zilizotayarishwa na kuchapishwa na (ambazo

  hazijachapishwa) FAO.

  Mazoezi haya yamechaguliwa kutokana na mitaala ya SDSMV iliyotayarishwa wakati wa mafunzo ya

  wawezeshaji wa SDSMV yaliyofanyika Kibaha Conference Centre, Tanzania, mwezi Juni, 2011, angalia

  kiambatisho kwa ajili ya nakala za Mitaala ya SDSMV, mazoezi yamepangwa kulingana na mazoezi

  yanayohusu kilimo (Juzuu ya 1) na; mazoezi ya stadi za kazi na kutengeneza ajira (Juzuu ya 2)

 • 8

  Mada ndogo: Utangulizi wa SDSMV

  0.1. Zoezi: Kutambulishana na SDSMV

  Muda: Karibu saa 2

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  1. Wakaribishe vijana wote na washiriki wengine waliohudhuria kwenye somo lakwanza la SDSMV

  2. Jitambulishe pamoja na wawezeshaji wengine. Mwambie kila kijana ajitambulishe kwa kikundi (jina,

  umri, mahali wanakotoka)

  3. Wagawe vijana katika vikundi vidogo vya watu watano au sita. Waambie vijana wajadili kile

  wanachotarajia kujifunza na kufanya wakati wa SDSMV na waandike matarajio yao kwenye karatasi

  kubwa . jadili kwa muhtasari matarajio waliyoorodhesha

  4. Wasilisha mchezo wa vidoti tisana waambie vikundi kama wanaweza kuunganisha vidoti vyote tisa

  kwa kutumia mistari minne iliyonyooka bila ya kuondoakalamu. Vipatie vikundi dakika 10 kufanya

  hivyo

  5. Viulize vikundi vimefanya nini kutatua tatizo hili. Kamakikundi kimeweza kutatua tatizo, waambie

  waeleze ufumbuzi. Kama hakuna aliyepata ufumbuzi, kwanza jadili kwanini hakuna aliyepata jibu na

  halafu onyesha namna ya kufanya.

  6. Waeleze vijana kuwa SDSMV itawasiaidia kwenda zaidi ya njia za kujifunza na kutafuta ufumbuzi

  zinazotumika.

  7. Tambulisha moduli mbalimbali za mtaala wa SDSMV na eleza aina tofauti za shughuli

  wanazotarajiwa vijana wafanye wakati wa masomo ya SDSMV kwa mfano, shughuli kwenye

  shamba darasa, kujifunza kwa vitendo na majaribio, majadiliano na shughuli za vikundi vidogo,

  mchezo wa kuigiza na igizo dhima.

 • 9

  8. Waulize vijana ni aina gani ya sheria na kanuni ambazo SDSMV wafuate kujenga mazingira yenye

  mafanikio kwa vijana kufanya kazi na kujifunza pamoja. Orodhesha kwenye karatasi kubwa sheria

  na kanuni zote walizotaja - kwa mfano, kuwahi, kushiriki kwaukamilifu, kuheshimu mawazo ya kila

  mmoja, kumsikiliza kila mmoja, kuzungumza mmoja mmoja kwa zamu, kutopigana,

  9. Ongeza kanuni na sheria zilizokosekana kwenye orodha.

  10. Waulize vijana kama wako tayari kushiriki kwa ukamilifu katika masomo yote ya SDSMV, wako tayari

  kufanya kazi katika vikundi vidogo, kujifunza kwa vitendo na kuheshimu orodha ya sheria na kanuni

  za SDSMV zilizotayarishwa.

  11. Toa muhtasari wa majadiliano.

  Maelezo kwa wawezeshaji

  Je, unatoka wapi?

  Je, umekuwa unaishi katika eneo hili kila mara?

  Je, unamfahamu kijana mwingine?

  Je, una jamaana ndugu katika kikundi cha vijana wanaoshiriki?

  Je, unasoma shule?

  Wakati wa SDSMV unataka kujifunza nini?

  Je, unapenda kujifunza zaidi kuhusu kilimo?

  Je, ungetaka kujifunza zaidi kuhusu aina gani za mazao au wanyama?

  Je, unataka kujifunza zaidi kuhusu afya, lishe au kuhusu uanzishaji wa biashara

  ndogondogo?

  Je, unapenda kujifunza kwa vitendo?

  Je, umezoea kufanya kazi katika vikundi?

  Je,kufanya kazi na kujifunza katika vikundi kuna maanagani?

  Je,unadhani nini muhimu wakati unapotakiwa kufanya kazi katika kikundi?

  Je, kuna majukumu ya aina gani unayotakiwakuyatimiza ili uweze kufanyakazi katika

  kikundi kwa mafanikio na ipasavyo?

  Je, ni kanuni na taratibu gani zinazotakiwa kuheshimiwa wakati wa kufanya kazi katika

  kikundi?

 • 10

  Mada za Kilimo

  1. Mada ndogo: Kupanga katika kilimo

  Malengo:

  Kuelewa namna ya kuchagua mazaobora zaidi ya kupanda.

  Kuelewa namna ya kuanza kupanga shughuli za kilimo

  Wakati vijana wanapopanga shamba lao, ni lazima wafikirie kuhusu mambo mbalimbali kwa wakati

  mmoja. Je, wanataka kuzalisha nini, aina ya ardhi na udongo waliyonayo, aina ya mbegu na zana zilizopo

  kwa ajili yao, watakuwa namuda kiasi gani (na lini ) wa kuhudumia shamba lao, ni watu wengine gani

  watakaowasaidia shambani, n.k.

  A. 1.1. Zoezi. Kujua shamba la kujifunza na kufanya majaribio.

  Mada: Karibu saa 2

  Vifaa: karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Mahali muhimu katika mafunzoya SDSMV ni eneo la uwandani la kujifunza. Kwa kuwa kanuni muhimu

  ya SDSMV ni kujifunza kwa kufanya majaribio, mahali pa kujifunza ni pale ambapo washiriki watajifunza

  taratibu na stadi za usimamizi wa kilimo. Washiriki watagundua wenyewe njia bora zaidi ya kulima aina

  fulani ya mazao na kupambana na matatizoya mmomonyoko wa udongo au masuala mengine ya kilimo.

  Katika zoezi hili, vijana watatambulishwa malengo na shughuli za aina mbalimbali watakazofanya katika

  shamba darasa.

  1. Anzisha mada ya shamba darasa. Waulize vijana kwanini SDSMV ina eneo la uwandani la

  kujifunzia na wanafikiri watafanya nini katika eneo la uwandani la kujifunzia wakati wavipindi

  vya SDSMV

  2. Eleza kuwa shamba darasa litatumika kujifunza kuhusu taratibu bora na stadi za usimamizi wa

  kilimo kwa kufanya mazoezi kwa vitendo. Hakikisha kuwa wanaelewa uzalishaji wa kilimo si

  lengo kuu.

  3. Waulize vijana kama wanaruhusiwa kufanya makosa katika shamba darasa yanayoweza kuathiri

  uzalishaji. Waeleze kuwa wanaruhusiwa kufanya makosa wakati wa kujifunza kwa kuwa

  kujifunza kunatokana na makosa na kuyaelewa ni njia bora ya kuwaongezea maarifa alimradi

  makosa hayo hayafanywi makusudi.

  4. Nenda na vijana kwenye shamba darasa. Waulize wanapenda kupanda mazao gani na kwanini.

 • 11

  5. Eleza kuwa kwanza wanahitaji kuandaa mpango kuonyesha wanaopenda kupanda nini, wapi,

  lakini kwanamna gani katika shamba darasa na kuwa mpango ujumuishe majaribio madogo na

  mbinu mbalimbali zakilimo

  6. Waulize washiriki kwa nini wanatakiwa kuingiza majaribio katika mpango

  7. Eleza kuwa kuna njia nyingi za kulima mazao kulingana na hali ya shamba na ujuzi wa mkulima,

  kila mkulima anatakiwa kufuata njia bora zaidi ya kulima kulingana na hali yake. Njia bora zaidi

  kutekeleza hili ni kwakujaribu njia mbalimbali za katika maeneo madogo ya ardhi

  8. Eleza kuwa katika wiki zijazo wataanza kupanga shughuli mbalimbali watakazotaka kufanya

  katika shamba darasa kwa kufanya mazoezi kadhaa.

  A.1.2. Zoezi : Sifa za shamba la Kilimo

  Muda: Karibu dakika 20

  Vifaa : Shamba darasa, karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Anzisha mada ya uchunguzi wa hali ya shambani. Waulize vijana kwanini wanafikiri ni muhimu

  kuchunguza hali ya shamba kabla ya kupanga mazao watakayopanda

  Waambie vijana wataje sifa zote muhimu za shamba la kilimo, ambazo mkulima anatakiwa kuzijua

  anapoanza kulima. Orodhesha sifa zote zilizotajwa kwenye karatasi kubwa. Iwapo unafikiri kuwa kuna

  kitu walichokisahau, kitaje na kujadili na vijana

  Sifa muhimu za shamba lakilimo

  Aina ya udongo (umbile: mwepesi mzito, muundo: ulioshikamana - kichanga , mbolea: nyingi

  kidogo)

  Kina chaudongo (kina kirefu cha kutosha kuwezesha ukuaji wa mizizi)

  Mteremko wa ardhi (hatari ya mmomonyoko, maji hutiririka, haufai kulima kwa kutumia

  mashine)

  Hali ya mtiririko wa maji (mabonde shambani, sehemu iliyo chini zaidi shambani)

  Kuwapo kwa vyanzo vya maji (kama kuna haja ya kumwagilia)

 • 12

  Mimea (je, kunamimea mingi? je, kunamajani?)

  Historia (kujua kilicholimwa katika shamba hilo siku za nyuma kunatoa habari kuhusu hali ya

  shamba)

  Mambo gani yanayofanyika katika mashamba jirani (nyasi, wadudunamagonjwa,mara nyingi

  huingia kutoka katika mashamba jirani)

  Toa muhtasari wa orodha ya sifa muhimu kwa ajili ya shamba darasa na waombe vijana wanakili

  orodha kwenye daftari zao.

  A.1.3. Kuchunguza Hali ya Udongo

  Majaribio rahisi yanayoweza kufanywa pamoja na vijana yametayarishwa kwa ajili ya kutambua umbile

  la udongo, muundo nahali ya aina mbalimbali ya udongo

  Muda: Saa 1 dakika 30

  Vifaa na matayarisho: karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  1. Anzisha mada ya kuchunguza hali ya udongo (umbile, muundo na aina za udongo na sifa zake)

  2. Nenda na vijana kwenye shamba darasa halafu waulizevijanahao maana yaumbile namuundo

  wa udongo. Eleza maana ya rangi ya udongo, muundo wa udongona umbile la udongo

  3. Chukua sampuli za udongo kutoka kwenye shamba darasa halafu waambie vijana waeleze rangi

  ya udongo na tunavyoweza kutambua umbile la sampuli ya udongo.

  4. Waonyeshe vijana namna ya kutambua umbile la udongo kwa kutumia ribbon test (angalia hapo

  chini)

  5. Waambie vijana wakusanye viganja vya udongo na warudie ribbon test

  6. Toa muhtasariwa matokeo ya uchunguzi waliofanya kuhusu udongo na jadili matokeo yahaliya

  udongo uliyochunguzwa kwa ukuaji wa mazao

  7. Toa muhtasari na hitimisha somo

 • 13

  Je, rangi ya udongo ina maana ganikwetu?

  Rangi nyeusi Udongo mweusi wa tabakala juu la ardhi, unaonyesha kiwango kikubwa cha mbolea,

  ikiwa na maana kwamba maji yanapenye kwa urahisi sana, virutubisho vingi na udongo wenye muundo

  mzuri.

  Rangi nyekundu - kahawia na rangi ya chungwa maji hutiririka na kupenye vizuri , mzunguko mzuri wa

  hewana maji. Kwa kuwa na maji ya kutosha ina maana rutuba pia ni ya kutosha. Hata hivyo tindikali

  (acidity) inaweza kuwa tatizo.

  Rangi ya manjano na buluu isiyokoza una matatizo la utiririshaji maji katika baadhi ya misimu

  (kufurika maji ) ambapo hewa hukosekana katika udongo, hasa wakati wa mvua.

  Rangi ya kijivu - huwa haupitishi maji vizuri, maji mengi na hakuna hewa ya kutosha.

  Chanzo: ABSA 1997

  Jaribio la utoaji wa mbegu

  Vifaa

  Chupa ya maji

  Udongo kutoka tabaka na aina mbalimbali

  Uso laini wa kitu kigumu kamavile plywood au metali au kipande cha kadibodi

  Namna ya Kufunga (chanzo: FAO 2000b)

  Udongo lazima uwe na unyevunyevu ili kutambua umbile lake kwa kuugusa. Ongeza maji kidogo kidogo

  mpaka udongo uwe laini. Pitisha udongo kati ya kidole gumba na kidole cha shahada. Vunja

  chembechembe ngumu na ondoa mawe au mizizi yoyote itakayokuwemo. Utaweza kupata sifa ya

  mguso wa udongo: wenye chembechembe za mchanga huachana, wamfinyanzi hunata, udongo wa

  kitope/mchanga tope ni laini sana. Sokota vidole kati ya vidole gumba na na kidole cha shahada

  kutengeneza utepe. Kadiri utepe unavyokuwa mrefu ndivyo unavyoonyesha kuwa sampuli hiyo ina

  udongo mwingi wa mfinyanzi. Udongo wenye mchanga mwingi utaachana, udongo wenye udongo

  mwingi wa mfinyanzi unaweza kusokotwa kutengeneza utepe mzuri wenye urefu wa zaidi ya sentimita

  5. Udongo wa kitope/mchangatope ni laini sana. Udongo tifutifu ni laini japo unanata na unahali ya

 • 14

  kichanga kidogo. Mwishowe baada ya kufanya mazoezi zaidi nitaweza kutathmini kwa usahihi aina ya

  udongo kwa kutumia mbinu hii.

  1. Kama udongo una chembechembe za mchanga huwa unaachana (yaani haushikamani).

  Umbile la udongo ni mwepesi sana (mchanga mchanga)

  2. Viringa udongo wa unyevunyevu kuwa gololi au mpira mdogo halafu bonyeza mpira huo

  kwakidole gumba na kuunda umbo la kikombe. Kama udongo huo hauwezi kuviringwa au kama

  kikombe kinamongonyoka , umbile la udongo ni . Mwepesi sana

  Kama mpira hauwezi kuviringwa lakini kikombe kinabaki na sura yake, endelea hatua ya 3.

  3. Viringa bonge au mpira wa udongo kati ya viganja vyako, halafu kwenye kitu kigumu ili kuunda

  utepe mnene kama penseli wenye urefu wa shadi entimeta 20 25. Kama

  hakunautepeuliotengenezwa au ulikuwa mfupi zaidi, umbile la udongo ni .mwepesi

  (mchanga tifutifu)

  Kama utepe mrefu haukutengenezwa endeleahatua ya 4

  4. Finyanga udongo kutengeneza utepe wa duara. Kama mduara huo utakuwa na nyufa umbile la

  udongo ni . Wastani (mfinyanzi mwepesi)

  Kama umefinyangwa mduara bila nyufa,na udongo unanata sana,umbile la udongo ni

  .. mzito (mfinyanzi mzito).

  A.1.4. Zoezi: Kupanga shughuli za kilimo

  Muda: Karibu saa 2

  Vifaa: Karatasi ya chatipindu na kalamu ya kuchorea.

  Mkiwa shambani, waulize vijana maswali yafuatayo na orodhesha majibuyao kwenye chatipindu:

  Shamba darasa letu lina ukubwa gani?

  Wakati gani unafaa zaidi kulima mazao kwa kuangalia hali ya hewa na masoko?

  Ni mbinu za kilimo za aina gani zinazoweza kutumika kupanda mazao?

  Je, tutapanda namna gani mazao manne yaliyochaguliwa kwa shamba darasa? (moja kwa

  moja au kwanza kitalu na baadaye kupandikiza miche?)

 • 15

  Waambie vijana katika vikundi vidogo vinne, kila kikundi kipatie mojawapo ya mazao manne

  yaliyochaguliwa na waambie watayarishe mpango utakaoonyesha mawazo ya hatua kwa hatua

  wanachopaswa kufanya ili kuzalisha zaohilo kwenye shamba darasa.

  Warejeshe washiriki pamoja na wape fursa wawasilishe mipango yao. Hitimisha somo kwa kuuliza

  maswali yafuatayo:

  Je,ilikuwa rahisi au vigumu kupanga mipango katika kikundi?

  Hatua gani za msingi tunahitaji kuzifuata ili kupanga mipango?

  Je, kupanga mipango ni wazo linalofaa? Kwa nini ndiyo na kwa nini hapana?

  A.1.5. Zoezi: Hatua za maisha ya mazao

  Muda: Saa 1 dakika 30

  Vifaa na matayarisho: Karatasi ya chatipindu, kalamu za kuchorea na mifano ya mimea

  (mazao katika hatua mbalimbali iliyokusanywa na mwezeshaji kabla ya somo)

  1. Waeleze washiriki mimea,kama kilivyo kiumbe kingine chochote kinachoishi, hupitia hatua

  mbalimbali

  2. Waulize vijana wanafikiri zao moja linapitia hatua zipi mbalimbali za ukuaji,kwa mfano mahindi,

  ambayo wangependa kupanda kwenye shamba darasa?

  3. Duria hatua ya 2 kwa zao moja au mawili ambayo vijana wangependa kuyapanda kwenye

  shamba darasa

  4. Eleza hatua nne tofauti zinazotumika zaidi katika vitabu: hatua ya awali, hatua ya ukuaji wa

  mazao, hatua ya katikati ya msimu na hatua ya mwisho wa msimu. Fafanua hatua hizo

  mbalimbali na waonyeshe washiriki mifano ya hatua mbalimbali.

  5. Waombe vijana wataje mahitaji ya mimea/mazaoili yaweze kukua kwa afya. Yaorodheshe

  kwenye karatasi kubwa na ikibidi ongeza vitu vilivyokosekana.

  6. Jadiliana na vijana kuhusu mahitaji yaliyotajwa kwa kila mmea/zao moja hadi jingine

  7. Wagawe vijana katika vikundi vidogo vidogo na waombe kila kikundi wachague zao moja na

  kujadili katika kikundi jinsi mahitaji mbalimbali ya mazao yanavyotofautiana kutoka hatua moja

  ya zao hadi nyingine.Waambie kilakikundi waandike maelezo kwenye karatasi.

 • 16

  8. Waambie kila kikundi wawasilishe matokeo ya majadiliano yao

  9. Toa muhtasari wa majadiliano.

  Maelezo kwa Mwezeshaji: Tumia maswali yafuatayo ya mwongozo

  Je, kuna hatua ambayo zao linahitaji maji kidogo?

  Je, kuna hatua ambayo zao haliwezi kustawi kwa maji kidogo?

  Je, kuna hatua za mazao ambapo mazao yanahitaji kuchukuliwa hatua maalumu za

  kuyalinda?

  Je, mahitaji ya mbolea yanatofautiana kutoka hatua moja ya zao hadi nyingine?

  Usuli:

  Kwa kawaida kipindi cha ukuaji wa mazao kimegawanyika katika hatua 4 za ukuaji (tazama mchoro hapa

  chini)

  1. Hatua ya awali: hiki ni kipindi kuanzia wakati wakusia mbegu au kupandikiza, hadi mazao

  yanapofunika karibu asilimia 10 ya ardhi

  2. Hatua ya ukuaji wa mazao: hiki ni kipindi cha kuanzia mwishoni mwa hatua ya awali

  nakuendelea hadi itakapofikia kufunika ardhi yote (ardhi inaweza kufunikwa 70-80%)

  3. Hatua ya katikati ya msimu: kipindi hiki kinaanza mwishoni mwa hatua ya ukuaji wa mazao

  nakuendelea hadi kukomaa, kinajumuisha kutoa maua na kutoa punje

  4. Hatua ya mwisho wa msimu: kipindi hiki kinaanza mwishoni mwa hatua ya katikati ya msimu

  na kuendelea hadi siku ya mwisho ya kuvuna; kinajumuisha kuvuna.

 • 17

  Crop

  needs\stages

  Initial stage Crop development Mid-season Late season

  Water ++ ++ +++ +

  Fertilizer ++ +++ +++ -

  Protection* ++++ +++ ++ +

 • 18

  A.1.6. Zoezi: Kuandaa Kalenda za Mazao

  Muda: Karibu saa 2

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Mwambie kijana ajitolee kueleza awamu mbalimbali za mzunguko wa maisha ya mimea.

  Chagua mojawapo ya mazao yaliyochaguliwa kwa ajili ya SDSMV (kwa mfano nyanya)

  namwambie kijana aeleze mzunguko wa maisha wa zao hili, hasa katika miezi ipi zao hili

  linalimwa, kupandwa na kuvunwa

  Onyesha kalenda tupu ya mazao kama hii iliyo hapa chini

  Nyanya

  Mwezi Shughuli za Kilimo Pembejeo/Vifaa gani

  vinahitajika

  Januari

  Februari

  Machi

  Aprili

  Mei

  Wagawe vijana katika vikundi vinne na kiambie kila kikundi kikamilishe kalenda ya mazao kwa zao

  walilopewa kushughulikia (nyanya, bamia,(ladies sugar), tango, boga)

  Wahimize washiriki kujaza jedwali kwa kutumia maswali kama vile:-

  Zao hili tunalipanda lini?

  Zaohili tunalivuna lini?

  Shughuli gani za kilimo zinafanyika katika kila awamu/hatua?

 • 19

  Wakusanye vikundi wote pamoja na waambie wawasilishe kazi yao ya kikundi. Hakikisha kuwa

  wamejumuisha shughuli muhimu zaidi (matayarisho ya shamba, utiaji mbolea wa kwanza, kupalilia,

  umwagiliaji maji, kupandikiza miche (nyanya), kupalilia mara ya pili, top dressing, IPM, kuvuna, baada ya

  kuvuna) na pembejeo/vifaa (mbegu (mboji) mbole, dawa za kuulia wadudu, wa mimea, zana za kilimo

  na kupalilia)

  A.2. Mada Ndogo: Uchaguzi wa mazao na mbegu

  Lengo:

  1. Kuelewa umuhimu wa kuchagua mbegu bora

  Wakati wa SDSMV vijana watapanda aina nne za mazao (nyanya, tango, bamia na boga (boga)) ambayo

  hulimwana wakulimakatika kipindi hicho cha mwaka. Ni muhimu kwa kila zao kutumia mbegu bora. Ni

  muhimu kuelewa pia kwa nini tunapanda mboga na sifa za mbegu bora ni zipi

  A.2.1. Zoezi: Kuchagua mbegu bora

  Muda: Saa moja na dakika 30

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  1. Wagawe vijana katika vikundi vidogo vidogo na waulize nini wanadhani nisifa za mbegu bora na

  waorodheshe sifa hizo kwenye karatasi kubwa

  2. Waambie kila kikundi kiwasilishe orodha yao

 • 20

  3. Jadili orodha zilizowasilishwa na hitimisha zile sifa muhimu zaidi za mbegu bora (hutoa mazao

  mengi, hufaa zaidi kwamazingira na hali ya mahali (hali ya hewa), safi hazina virusi, n.k.)

  4. Jadiliana na vijana kuhusu mahali watakapopata mbegu bora.

  A.3. Muda Mdogo: Kuelewa uwezo wa kutoa wa mbegu

  Lengo: kuelewa namna mbegu zinavyoota

  Vijana wanahitaji kujifunza kuwa mbegu zitakuwa tu kama kiini kina afya, wakati kinapokuwa na viini

  lishe vya kutosha na wakati kunapokuwa na maji na hewa ya oksijeni ya kutosha.

  A.3.1. Zoezi: Jaribio la uotaji wa mbegu

  Muda: Nusu siku nakaribu wiki moja ya ufuatiliji

  Vifaa: Karatasi laini (au njia nyingine mbadala kama vile majani au magomeya miti); mbegu

  zamazaombalimbali ya chakula/miti (mbegu za kutosha kwa kila kikundi cha vijana )

  mifuko ya plastiki na maji safi

  1. Wagawe vijana katika vikundi na waambie kila kikundi wahesabu mbegu 100 kutoka aina

  mbalimbali zambegu.

  2. Waambie waandae matabaka mawili ya karatasi laini na kunyunyiza maji safi kwa makini hadi

  ziwe na unyevu zisilowe

  3. Waambie vijana waweke mbegu 100 juu ya karatasi laini katika safu 10 zenye mbegu 10 (umbali

  kati ya mbegu na mbegu iwe karibu sm 2)

  4. Waambie vijana wafunike mbegu na tabaka jingine la karatasi laini, nyunyuzia maji kwenye

  karatasi laini na zungushia karatasi laini lenye mbegu kwenye aina nyingine ya karatasi.

  5. Waambie vijana waweke karatasi hiyo kwenye mfuko wa plastiki ili kutunza unyevu wa karatasi

  yenye mbegu (mbegu nyingi humea vizuri zaidi katika sehemu yenye giza, hivyo mfuko wa

  plastiki mweusi ni bora zaidi kutumiwa)

  6. Waambie vijana waandike jina la kikundi kwenye mfuko, herufi ya bechi ya mbegu zilizomo

  ndani yake, na tarehe mbegu ziliposiwa.

  7. Hakikisha kuwa unahifadhi mahali penye giza.

 • 21

  Kutegemea na zao, mchakato wa uotaji unaweza kuonekana baada ya siku 1, 2 au zaidi. Andika idadi ya

  mbegu zilizokwisha ota kwa kipindi hiki cha kwanza cha kuchunguza.

  Mara baada ya kuangalia na kuandika idadi (na kuondoa mbegu zilizoota ) zungushia tena karatasi laini

  na rudisha kwenye mfuko wa plastiki kwa ajili ya uchunguzi mwingine wa kila siku

  Wakati vijana wanapochunguza na kufuatilia mbegu waulize maswali yafuatayo:

  Imechukua muda gani kwa mbegukumea?

  Mbegu ngapi zimemea? Je, idadi ilikuwa ndogo au kubwa?

  Kwa nini ni muhimu kujua uwezo wa mbegu kumea?

  A.4. Mada Ndogo: Kuandaa shamba darasa

  Baada ya kuandaa mpango wa kuhusu kile watakacholima vijana kwenye shamba darasa lao itakubidi

  kuanza kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo chenyewe

  A.4.1. Zoezi: Kuanda mpangilio wa shamba darasa.

  Vijana hawana budi kwanza kuamua kuhusu mpangilio wa shamba darasa ili kuelewa mahali pa kupanda

  na aina ya mazao

  Mada: Karibu saa 1

  Vifaa : Chatipindu na kalamu za kuchorea

  1. Nenda na vijana katika shamba darasa na waambie wakumbuke sifa zote za shamba darasa

  ambazo ni muhimu kwa kuandaa mpangilio wa shamba (mteremko, tofauti za rutuba ya udongo,

  njia ya kuingilia shamba, chanzocha maji n.k)

  2. Waambie wanafunzi wabainishe maeneo mbalimbali ya shamba, mahali pa kitalu na njia

  zitakazojumuishwa kwenye mpangiliohuo

  Zingatia kwamba kila zao litapandwa kwenye eneo moja litakalolimwa kulingana na kanuni

  za IPM na wenyeji wanavyolima, ili mwishoni kuweza kuchunguza athari ya IPM.

 • 22

  3. Waambie vijana kwenye vikundi vyao vidogo waandae mipangilio ya shamba darasa zikiwemo

  sehemu zote, kitalu na njia. Waambie wazingatie mahali pa kupitishia maji na umwagiliaji

  shamba na mwelekeo wa matuta ya vitalu na safu/mistari

  4. Waambie vikundi wawasilishe mipangilio yao na kuamua kuhusu mpangilio wa mwisho

  watakaotumia.

  A.4.2. Zoezi: Maandalizi ya Ardhi

  Kabla ya kupanda mbegu, ardhi haina budi kuandaliwa kwanza

  Muda: Karibu saa 1

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Bungua bongo na vijana kuhusu kinachotakiwa kufanywa shambani kabla ya kuanza upandaji wa mbegu

  (kusafisha ardhi, kuondoa mabaki yote ya mimea, kusawazisha ardhi inapohitajiwa, kutumia mboji,

  kutifua na kuandaa vitalu vya mbegu).

  Jadili shughuli zote zilizotajwa, kwa nini lazima zifanywe na zifanywe namna gani. Panga shughuli

  mbalimbali kwa mfuatano unaofaa.

  Tayarisha mpango na vijana kuhusu lini kifanyike nini. Njia bora zaidi ya kueleza namna ya kufanya

  shughuli mbalimbali ni kwa kufanya kwa vitendo shughuli hizo na vijana. Kazi kubwa (kusafisha shamba

  na kulima na kutifua) lazima ifanywe na watu wazima.

  Mada Ndogo: Kuandaa kitalu na kupandikiza.

  Malengo:

  Kuelewa umuhimu wa vitalu

  Kujua namna ya kuandaa kitalu

  Kujua namna ya kupandikiza miche

 • 23

  Mazao mengi ambayo tunataka kuyapanda shambani, yanahitaji kupandwa kwenye vitalu kwanza, na

  kisha kuhamishiwa shambani baada ya wiki chache. Ni muhimu kwa washiriki kuelewa jinsi ya kuandaa

  kitalu, kupanda mbegu, kutunza miche na jinsi ya kuhamisha miche kwenda shamba darasa kwa wakati

  mwafaka. Hapa kuna baadhi ya mazoezi ya mfano ambayo unaweza kuhitaji kuyatumia.

  A.4.3. Zoezi: Kwanini tunahitaji vitalu?

  Muda: Karibu saa moja na dakika 30

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Waulize vijana maswali yafuatayo na andika majibu yao kwenye chatipindu

  Kwa nini wakulima mara nyingi hupanda mazao ya mbogamboga kwenye vitalu kwanza na

  baadaye kwenye shamba?

  Kutokana na majibu yako, unatakiwa kuandaa vipina wapi kitalu chako?

  Kisha wapeleke vijana mahali ambako umeamua kuandaa kitalu

  Waulize vijana maswali yafuatayo:

  Je, mbegu zilizosiwa kwenye kitalu zinahitaji kukingwa kutokana na vitu gani mbalimbali?

  Je, tutawezaje kutoa kinga inayotakiwa?

  Je, tunahitaji kutunza miche namna gani?

  Je, tutaandaa vipi vitalu ili visaidiae kukinga na kutunza vizuri miche?

  A.4.4. Zoezi: Kuandaa kitalu

  Muda: Karibu saa 2

  Vifaa: Hakuna.

  Sasa vijana wataandaa kitalu kwa vitendo. Wapitishe katika hatua zifuatazo kwa kuzingatia kuwa kila

  mmoja anashiriki kwenye kazi hiyo. Kulingana na idadi ya vitalu mnavyoandaa, unawezakuwagawa

  washiriki katika vikundi vidogovidogo zaidi.

 • 24

  Sehemu ya 1.10

  1. Tafuta udongo kwenye., vunja mabonge ya udongo naondoa mabaki ya mizizi na mashina ya

  majani

  2. Tifua udongo na pandisha udongo toka pande zote ili kitalu kiwe kimeinuka na kuachaaaaa njia

  pande zote ili kuruhusu kupalilia bila kukanyaga juu yake. (upana wa mita 1)

  3. Ongeza mbolea ya samadi/mboji na mchanga wa mtoni, changa vizuri. Mchanga unaweza

  kusaidia kulainisha udongo ili kuwe na mtiririko mzuri wa maji na kungoa mizizi ya miche kwa

  urahisi.

  4. Sawazisha kitalu na ikibidi weka mipaka. Pasua mipaka kwa kutumia kijiti.

  5. Sia mbegu (zilizowekwa dawa ya kukinga ikibidi) kwenye mistari kwa kina kilichopendekezwa.

  Acha nafasi ya kutosha kwa ajili ya ukuaji wa miche.

  6. Funika mistari hiyo kwa udongo kidogo usiozidi mara 2-3 ya unene wa mbegu

  7. Kama kuna tatizo la mchwa na konokono, tawanya majivu kwenye kitalu chote.

  8. Tandaza majani, nyasi, mabua ya mpunga, mbolea ya samadi/mboji nakiasi fulani cha tabia za

  msituni kuzuia mbegu za udongo usisombwe na mvua kubwa nakuzuia magugu na kutunza

  unyegu wa udongo wakati wote

  9. Ikibidi, jengea vivuli, kama paa dogo

  Sehemu ya 1.02. Mpangilio wa vitalu kupanga mbegu kujenga kivuli

 • 25

  MAMBO MUHIMU Kabla ya kuandaa kitalu

  Chagua mahali pazuri: Mahali panapofaa patakuwa sehemu ya karibu na shamba darasa (ili

  kitalu kitembelewe mara kwa mara nakutunzwa vizuri) yenye ardhi nzuri na yenye

  rutuba,karibu nachanzo cha maji kinachoaminika na ambapo maji hayatuami au kukusanyika.

  Epuka kuweka kitalu mahali ambapo mimea iliyopoya jamii moja na ile unayosia ina tatizo la

  wadudu waharibifu na magonjwa

  Safisha eneo: Ondoa visiki, mizizi na mawe katika eneo hilo. Majani na mabakimengine ya vitu

  visivyokuwa vya miti, yanaweza kutengenishwa na kufanywa mbolea ya mboji.

  Mpangilio wa vitalu: Ulalo, kamainawezekana vielekee (jua) mashariki kwenda magharibi,

  upana wa mita moja na nafasi kati ya kitalu na kitalu iwe nusu mita.

  A.5. Mada ndogo: Kupanda: Kuelewa umuhimu wa kuacha nafasi baina ya mimea

  Malengo:

  Kuelewa umuhimu wa kuacha nafasi baina ya mimea

  Kuelewa umuhimu wa uzazi wa mpango

  Ili kuotesha mazao yaliyostawi vizuri, kila mmea unahitaji kuwa nanafasi ya kutosha. Kuipa mimea nafasi

  ya kutosha ni sawa na kuupa kila mmea viini lishe na maji ya kutosha kutoka kwenye udongo

  uliyozunguka. Inakuwa rahisi vilevile kuondoa magugu na kupunguza mimea wakati utakapowadia.

  Wakati huo huo mkulima huwa anapenda kupanda mimea mingi kadiri iwezekanavyo. Ni muhimu

  kuelewa namna ya kupata mavuno mengi wakati huo huo kuhakikisha kuwa mazao yamestawi vizuri.

  Kuacha nafasibaina ya mimeani muhimu sana katika kuamua ni mazao gani ya kupanda na wakati gani

  wa kupanda mazao hayo.

  A.5.1. Zoezi: Kuacha nafasi baina ya mimea.

  Muda: Karibu saa 1 na dakika 30

  Vifaa: Karatasi ya chatipindu na kalamu za kuchorea, tepu ya kupimia

  Andaa ziara ya kwendakwenye shambalenye mazao yaliyo komaa ili kila mtu aweze kuona nafasi baina

  ya mimea mbalimbali shambani hapo.

 • 26

  Wakati unapowasili shambani, waambie vijana waangalie nafasi kati ya mimeana wajaribu kufikiria jinsi

  ilivyopandwa (kwenye msatari, kwenye kitalu,bila mpangilio maalumu). Vijana mbalimbali wapime

  nafasi baina ya mimea ya mazao ya aina mbalimbali (nafasi baina ya mstari na baina ya kila mmea).

  Waambie waandike mambo waliyoona kwenye jedwali , wapange kulingana na mazao ya aina

  mbalimbali shambani.

  Waulize vijana maswali yafuatayo:-

  Je, wingi wa mazao una maana gani?

  Kwa nini ni muhimu kufuata nafasi fulani baina ya mimea au mbegu wakati wa kupanda

  mazao?

  Kuna faida au hasara gani kupanda mbegu kwenye mstari au bila mpangilio maalumu?

  Unafikiri kutatokea nini kwenye mimea kama itapandwa karibu karibu?

  Waeleze kwamba kupata wingi mzuri wa mimea, ni muhimu kupanda mbegu nyingi wakati wa msimu

  wa kupanda ili kuepuka baadhi ya mimea kutoota au mingine inaweza kufa ikiwa michanga kutokana na

  wadudu waharibifu au maginjwa.

  A.6. Mada Ngogo: Kupanda Mazao Yenye Afya

  Kupitia Kanuni za Udhibiti Husishi wa Wadudu Waharibifu (IPM) Utangulizi.

  Malengo:

  Kuelewa Kanuni Kuu za Udhibiti Husishi wa Wadudu Waharibifu wa Mimea

  Kuelewa maana ya mfumo wa kiikolojia

  Kuelewa umuhimu wa usafi na afya, mazingira shambani kama njia ya kukinga wqadudu

  waharibifu na maginjwa ya mimea

  Kupanda mazao yanayostawi ni ufunguo wa kilimo bora. Mazao yaliyostawi ni imara zaidi na

  yanawezakujilinda vizuri zaidi dhidi ya wadudu waharibifu na magonjwa. Njia mbalimbali ambazo

  tunatumia katika mashamba yetu zinaleta athari kwa ustawi wa mazao na zinaweza kutumika pia

  kudhibiti matatizo yoyote ya wadudu waharibifu.

  Kulima mazao yenye afya na yanayostawi ni kanuni ya kwanza ya Udhibiti Husishi wa Visumbufu vya

  Mimea (IPM). IPM inahusu wadudu waharibifu lakini ni zaidi ya udhibiti wa wadudu waharibifu. IPM si

 • 27

  kuhusu kuwaangamiza wadudu wote waharibifu. Baadhi ya wadudu waharibifu huhitajika kwa ajili ya

  kuwaondoa maadui shambani. IPM inahusu kuwapunguza wale wadudu waharibifu ambao husababisha

  uharibifu wa mazao na kuleta hasara.

  Mara nyingi IPM inaweza kulenga matumizi madogo ya dawa za kuulia wadudu waharibifu kadiri

  iwezekanavyo. Lakini msingi wa maamuzi ya udhibiti mzuri wa mazao ni kuelewa kwa ukamilifu mfumo

  wa ikolojia ya mazao, pamoja na yale ya wadudu waharibifu, maadui wao wa asili na mazingira ya

  mahali. Ufuatiliaji wa mazao ni hatua ya kwanza katika kuelewa mfumo wa ikolojia.

  Ifuatayo ni baadhi ya mifumo ya shughuli unayoweza kutumia kuanza kuwafundisha vijana Mada

  Maalumu ya Kilimo: Udhibiti Husishi wa Visumbufu vya Mimea.

  A.6.1. Zoezi: Kupanda mazao yanayostawi kwa kutumia IPM

  Muda: Saa 1 na dakika 30

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Hatua:

  1. Taja kanuni nne za Vdhibiti Husishi wa Visumbufu vya Mimea:

  Kupanda mazao yanayostawi

  Kuelewa na kuhifadhi wadudu wanaolinda

  Kutembelea shamba mara kwa mara

  Kuwa mtaalamu katika kusimamia mazao yako

  2. Waulize vijana wanafikiri kila moja ya kanuni hizo ina maana gani.

  3. Wagawe vijana katika vikundi na waambie kila kikundi waandike taratibu mbalimbali za

  usimamizi wa mazao ambazo wanafikiri zinaleta athari katika ustawi wa mazao

  4. Mwambie mwakilishi mmoja kutoka katika kila kikundi awasilishe matokeo yao darasani.

 • 28

  A.6.2. Zoezi: Kuelewa mifumo ya ikolojia ya shamba

  Ili kukinga mazao dhidi ya wadudu waharibifu na magonjwa, vijana kwanza wanahitaji kuelewa mfumo

  wa ikolojia wa shamba darasa. Mfumo waikolojia ni mimea, wanyama na viumbe wadogo wote katika

  eneo fulani na namna wanavyoishi na kushirikiana na kutegemeana. Vijana watachunguza mfumo wa

  ikolojia wa shamba na nafasi ya wadudu wa asili katika kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa ya

  mimea.

  Mada: Saa 1 dakika 30

  Vifaa na matayarisho: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea, mifuko ya plastiki, alkoholi na gundi.

  Hatua:

  1. Anzisha mada ya kukinga mazao dhidi ya wadudu waharibifu na magonjwa

  2. Waambie vijana wataje kanuni nne za IPM na kujadili kanuni hizo nne kuhusiana na kulinda

  mazao dhidi ya wadudu waharibifu na magonjwa ya mimea.

  3. Waulize vijana wanafikiri mfumo wa ikolojia una maana gani.

  4. Nenda na vijana kwenye shamba darasa na wagawe katika vikundi vidogo vidogo na waambie

  vikundi wakusanye aina mbalimbali za viumbe shambani (mfumo wa ikolojia) kadiri

  iwezekanavyo, ikiwemo mimea, mimea yenye magonjwa, wadudu, buibui, panya, nyoka n.k.

  5. Waambie wanakikundi waende mahali penye kivuli. Miminia alkoholi kwenye mfuko waplastiki

  na uutikise ili wadudu na buibui wafe.

  6. Jadili na tengenisha pamoja na vijana viumbe waliyokusanywa kulingana na kazi zao kwenye

  mfumo wa ikolojia. Waambie vijana wawapange katika matabaka mbalimbali; mimea chini, wala

  mimea katika tabaka la 2, maadui wa asili katika tabaka la 3, na waozeshaji katika tabaka la 4.

  Wagundishe kwenye karatasi. Kama hawana uhakika na kazi, wawekee kiumbe hicho lebo

  hawana uhakika

  7. Waulize vijana kama mimea yote waliyoipata ni magugu. Kwanini ndiyo au kwanini hapana?

  Halafu waulize pia kama wadudu wote ni wadudu waharibifu. Kwa nini ndiyo au kwanini ni

  hapana?

  8. Jadiliana na vijana namna maadui wa asili (walinzi) wanavyomsaidia mkulima katika kudhibiti

  wadudu waharibifu na magonjwa ya mimea shambani.

 • 29

  9. Toa muhtasari wa majadiliano na mambo mliyoyaona shambani.

  Maelezo kwa Mwezeshaji: Maswali ya Kuongoza.

  Je, wadudu wote ni wadudu waharibifu?

  Je, wadudu wote waharibifu waliyopo shambani husababisha matatizo?

  Je, tunahitaji maadui wa asili wangapi kudhibiti wadudu waharibifu?

  Je, mdudu mharibifu ni tatizo wakati wote wa hatua za ukuaji wake au wakati wa hatua moja

  au mbili tu?

  Je, nini hatua za ukuaji wa mmoja wa wadudu aliyechaguliwa?

  A.6.3. Zoezi: Desturi mbalimbali za kudhibiti visumbufu vya mimea

  Muda: Karibu saa 1

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Eleza kuwa kwa kutumia desturi mbalimbali za kilimo, mkulima anaweza kupunguza hatari ya

  mashambulizi ya wadudu waharibifu kwenye mazao yake. Waulize vijana kama wanaelewa baadhi ya

  desturi hizo. Ziorodheshe kwenye karatasi kubwa.

  Panga desturi hizo kwa makundi kulingana na zile za kiutamaduni, za kiutendaji na za kibiolojia na jaribu

  kukamilisha orodha pamoja na vijana

  Desturi za Kiutamaduni: Muda wa kulima/kupanda, kulima kwa kwa mzunguko wa mazao/kubadilisha

  mazao (crop rotation), kuchanganya mazao, kutumia mitego na kutandaza majani.

  Desturi za kiutendaji: Utumiaji jua/utashishaji, kupalilia, uondoaji wadudu waharibifu na/au mimea

  inayoambukiza

  Desturi za Kibiolojia: Wadudu wenye manufaa (adui wa asili) dawa za kuulia wadudu za viumbe (bio

  pesticides) na /au dawa za kunyunyizia mimea, mitego (pheromone traps).

  Jadiliana na vijana desturi zote zilizotajwa.

 • 30

  A.6.4. Zoezi : Desturi za kijadi za kudhibiti wadudu waaribifu wa mazao

  Matumizi ya dawa za kuulia wadudu waharibifu (vinatilifu) na kemikali yamezoeleka sana katika kipindi

  kilichopita cha miaka 30-40 kwenye nchi nyingi za tropiki na hasa kwakilimo cha biashara. Bado kuna

  maarifa mengi kuhusu namna ya kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa kwa kutumia dawa za

  mimeana mbinu za kijadi. Mara nyingi mbinu hizi wanazo wazee katika jamii

  Muda: Karibu saa 1

  Vifaa: Mwenyeji mwenye maarifa ya kilimo.

  Mwalike( mzee) mtu kutoka kwenye jamii ambaye anafahamika kuwa ana maarifa mengi kuhusu

  matumizi ya dawa za mimea na mbinu za kijadi katika kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa katika

  kilimo.

  Waambie vijana watunge baadhi ya maswali katika vikundividogo vidogo na kumwuliza mwenyeji

  mwenye maarifa ya kilimo.

  Kama ikiwezekana kwa kushirikiana na mwenyeji huyo mwenye maarifa ya kilimo, kusanya baadhi ya

  mimea inayotumika na tayarisha dawa.

  A.6.5. Zoezi: Kulinda mazao dhidi ya wadudu na magonjwa katika shamba darasa (IPM)

  Muda: Karibu saa 2

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea.

  1. Waambie vijana wakae kwenye vikundi vyao vidogo vidogo na kugawa mazao yanayokuwa

  katika shamba darasa miongoni mwa vikundi vidogo, kwa mfano kila kikundi mazao mawili na

  kila zao lishughulikiwe na angalao vikundi viwili. Kila kikundi kichore safu mbili kwenye karatasi

  kubwa.

  2. Kiambie kila kikundi kihorodheshe wadudu waharibifu na magonjwa ya mazao waliopangiwa

  kwa msingi wa walichochunguza katika shamba darasa wakati wa uchunguzi wa mfumo wa

  Ikolojia ya Kilimo (AESA) pamoja na kutokana na uzoefu katika safu ya kwanza

  3. Kiambie kila kikundi kihorodheshe kwenye safu ya pili desturi za kulinda na kudhibiti wadudu

  waharibifu na magonjwa waliyotajiwa.

  4. Kiambie kila kikundi kiwasilishe matokeo ya majadiliano yao ya kulinganisha mawasiliano

  yanayohusu wadudu waharibifu na magonjwa na desturi za kulinda za mazao hayo.

 • 31

  5. Jadili na kukubaliana kuhusu njia bora zaidi za kulinda wadudu waharibifu na magonjwa

  yaliyobainishwa kwa mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye shamba darasa.

  6. Kama bado kuna maswali yasiyohitaji kukatiwa shauri kuhusu baadhi ya wadudu waharibifu na

  magonjwa na namna ya kulinda, mwalike kwenye somo la SDSMV mkulima mwenyeji mwenye

  uzoefu na jadili maswali haya pamoja naye

  A.6.6. Zoezi: Kupata maarifa zaidi kuhusu wadudu waharibifu na magonjwa katika shamba darasa

  Kama matatizo au maswali yanayohusiana na kudhibiti baadhi ya magonjwa na wadudu katika shamba

  darasa hayawezi kutanzuliwa na vijana na mwezeshaji wa SDSMV, Shamba Darasa na Stadi za Maisha

  kwa Vijana , italazimika kuanzisha shughuli za ziada kupata taarifa inayotakiwa kutanzulia matatizo

  yaliyobainishwa.

  Njia ya a) Kumwalika mkulima mwenyeji mwenye uzoefu au mtaalamu (afisa kilimo wa ugani) kwenye

  somo la SDSMV na kuwapa fursa vijana kujadiliana naye matatizo hayo

  Njia ya b) Kama ufumbuzi unawezekana unafahamika, fanya jaribio dogo , kupima ufumbuzi

  mbalimbali. Kwa mfano, mimea michache au u2 moja imetiwa dawa ya aina moja na mimea michache au

  m2 moja imetiwa dawa nyingine .

  Njia ya c) Anzisha bustani ya wadudu

  Kwa maelezo zaidi kuhusu matumizi

  Kwa maelezo zaidi kuhusu matumizi na matayarisho ya bustani ya wadudu, tafadhali angalia

  kiambatisho cha 2

  A.6.7.Zoezi : Kutayarisha dawa ya Mwarubaini kwa ajili ya kudhibiti wadudu waharibifu

  Mwarubaini ni dawa ya kuulia wadudu ya kiasili au ya mimea. Mwarubaini una uwezo mkubwa wa

  kudhibiti wadudu wa aina mbalimbali waharibifu. Ina kiwango kidogo sana cha sumu kwa binadamu na

  haiharibu mazingira. Miti ya mwarubaini inapatikana katika nchinyingi za tropiki hasa katika maeneo ya

  ukame. Sehemu nyingi za mmea huo zinaweza kutumika kwa utayarishaji wa dawa ya kudhibiti wadudu

  waharibifu lakini sehemu zinazotumika mara kwa mara ni mbegu na majani ya mti

  Njia raisi zaidi ya kueleza matayarisho ya dawa ya mwarubaini ni kwa kufanya kwa vitendo na watoto

  Muda: Karibu matayarisho ya saa 1, siku inayofuata, umaliziaji wa nusu saa.

 • 32

  Vifaa: Mbegu za mwarubaini, majani ya mwarubaini, kinu, kitambaa chepesina safi, ndoo,

  kipulizia dawa cha kubeba mgongoni

  1. Kusanya mbegu za mwarubaini zilizoiva, hasa zile zilizoanguka kutoka mtini, menya maganda na

  zianike kivulini (ukaushaji kwa hewa). Kama ni lazima, hifadhi mbegu hizo kwenye magunia kwa

  matumizi ya baadaye.

  Inakadiriwa kwamba kilo 12 za mbegu za mwarubaini zisizomenywa zinatosha kutia dawa hekta

  1 au eka 2.5 ya mazao yaliyoshambuliwa na wadudu waharibifu. Ili kupata uzito unaofaa wa

  dawa, gramu 50 za mbegu zisizomenywa hazina budi kulowekwa kwenye lita 1 ya maji. Mkulima

  anahitaji gramu 750 za mbegu za mwarubaini kama anataka kunyunyizia kwa klutumia kipuliza

  dawa cha kubeba mgongoni cha ujazo wa lita 15.

  2. Weka kinuni kiasi kinachotakiwa cha mbegu za mwarubaini zisizomenywa na twanga mbegu kwa

  ukamilifu mpaka ziwe rojo.

  3. Changanya rojo na maji na acha kwa usiku kucha

  4. Itakapofika mchana, chuja maji ya mbegu kwa kitambaa safi na chepesi. Chujua/zimua

  mchanganyiko huo kwa uwiano wa 1:2 halafu nyunyizia mazao yaliyoshambuliwa na wadudu

  kwa kutumia kipulizia dawa cha kubeba mgongoni.

  5. Changanya mabaki ya chembechembe ngumu za mbegu iliyochujwa na udongo wa kitalu ili

  kudhibiti wadudu wa kwenye udongo wa kitalu.

  Namna ya kutayarisha dawa ya majani ya mwarubaini.

  1. Kusanya majani ya mwarubaini kabla mti haujaalika maua

  2. Twanga kiasi cha kilo moja ya majani , changanya na maji kiasi cha gramu 100 (kiasi cha kiganja

  kilichojaa) cha pilipili hoho mbichi kwenye kinu. Pilipili hoho zinaongeza ufanisi wa dawa ya

  majani ya mwarubaini.

  3. Loweka rojo la majani ya mwarubaini kwenye lita 5 za maji usiku kucha.

  4. Chuja mchanganyiko kwa kitambaa safi na chepesi naongeza lita 1 ya sabuni ya maji. Sabuni ya

  maji itakuwa haina kiambata.

  5. Chujua/zimua mchanganyiko huo kwa uwiano wa 1:2 kwa kunyunyizia moja kwa moja kwenye

  mazao ili kudhibiti wadudu.

 • 33

  A.6.8. Zoezi: Punguza matumizi ya kemikali za kilimo

  Wakulima wengi hutumia kemikali za kilimo katika urutubishaji na /au udhibiti wa wadudu waharibifu na

  magonjwa. Kemikali nyingi ni hatari sana na wakulima hawana budi kuzisambaza na kuzitumia kwa

  makini.

  Muda: Kiasi cha saa 2

  Vifaa: Karatasi kubwana kalamu za kuchorea

  1. Waambie vijana wataje aina mbalimbali za kemikali zinazotumiwa na wakulimakatika katika

  na waziorodheshe kwenye karatasi kubwa

  2. Jadiliana na vijana hatari mbalimbali zilizopo katika kutumia kemikali hizi na namna mkulima

  anavyoweza kupunguza hatari. Orodhesha kwenye karatasi kubwa namna bora za kushughulikia

  kemikali hizo.

  3. Waambie vijana wataje mifano ya ajali zilizotokea katika jamii zao na kiambie kikundi kimoja

  kifanye mchezo wa kugiza kuhusu mfano wa ajali

  4. Jadili makosa yaliyofanywa katika kushughulikia kemikali kwenye mchezo wa kuigiza. Kaimbie

  kikundi kingine kiigize tena mchezo lakini safari hii huonyesha namna bora za kushughulikia

  5. Hitimisha kuhusu namna bora za kushughulikia kemikali za kilimo

  Zingatia: Namna bora za kushughulikia kemikali za kilimo ni

  Chagua dawa za wadudu zilizo salama zaidi na tumia kiasi kidogo sana

  Tunza dawa za wadudu, kemikali za kulima na vifaa vya kupulizia dawa mahali salama na

  palipotengwa

  Andika majina/lebo kwenye dawa za wadudu na kemikali za kilimo (kwa kutumia Kiswahili)

  Weka njia salama za kushughulikia chupa na makopo ya dawa za wadudu na kemikali

  Kusanya taarifa za afya na usalama kwa mfano matumizi salama ya kemikali za kilimo na

  eneza taarifa hizo kwa jamii

 • 34

  A.7. Mada ndogo: Uchunguzi wa mfumo wa kilimo na ikolojia (AESA ) Zana ya ufuatiliaji na kufanya

  maamuzi katika kilimo

  Malengo: Kuelewa namna ya kuchanganua mara kwa mara jinsi mashamba yao yanavyoendelea

  Wakati wakupanga shughuli zaoza shamba, vijana hawana budi kujifunza kuchanganua hali ya

  mashamba yao kwanza kabla ya kufanya uamuzi kuhusu namna ya kusimamia mazao yao. AESA ni zana

  inayofaa kwa ajili ya kufanya shughuli hii, pamoja na kubadilishana maarifa. AESA inahusisha uchunguzi

  na uchanganuzi wa mara kwa mara wa mazao wakati wa hatua mbalimbali za ukuaji. Pia inahimiza

  kujifunza kwa kugundua. Vipengele vya msingi vya uchanganuzi ni:-

  Hakikisha mimea ina afya katika hatua mbalimbali za ukuaji wao

  Wadudu na wanyama wanaokula wenzao

  Hali ya udongo na maji

  Hali ya hewa

  A.7.1. Zoezi: Kutambulisha AESA

  MUDA: Karibu saa 2

  VIFAA: Karatasi kubwa ya chatipindu, kalamu za kuchorea, tepu na shamba lenye mazao.

  1. Eleza kwamba ni muhimu kuchunguza mazao mara kwa mara ili kuyatunza

  2. Nenda na vijana kwenye shamba lenye zao maalumu, wagawe vujana katika vikundi vya vijana

  6-7 na kila kikundi kiandae orodha ya mambo muhimu wanayotaka kuyaona kuhusu mazao.

  Wasaidie vijana kubaini mambo yafuatayo

  Idadi ya mimea iliyopo

  Idadi ya wadudu wanaoruka (wadudu waharibifu na wanyama wa asili wanaokula

  mazao), kwenye mimea na eneo la jirani

  Wadudu, wanyama wanaokula wenzao waliyopo kwenye eneo la udongo na kwenye

  mimea

  Mabaka, madoa na kuchujuka rangi kunakoonyesha kuwapo kwa magonjwa

  Madhara yanayosababishwa na wadudu na aina mbalimbali za magonjwa

 • 35

  Aina za nyasi,ukubwa na wingi ikilinganishwa na mazao

  Hali ya udongo

  Hali ya hewa siku hiyo (kwa mfano joto, mawingu kidogo, mvua, unyevunyevu/mavunde

  mavunde)

  3. Chagua mmea wa mfano na waambie vijana wachunguze mambo yafuatayo

  Idadi ya majani

  Urefu wa mimea

  Sehemu za uzazi za mmea uliyochaguliwa

  Sifa nyingine zozote zitakazokusaidia kutoa uamuzi kuhusu mmea huo wiki

  zitakazofuata.

  4. Waonyeshe vijana muundo watakao wasilishia data zao. Mfano umeonyeshwa hapa chini

  5. Kwa kushirikiana kwa vikundi vyao, waambie vijana wajaribu kufanya AESA ya sehemu ya

  shamba

  6. Waambie vijana wawasilishe kazi yao, na jadili tofauti zozote zilizojitokeza

  7. Hitimisha somo kwa kuwauliza vijana, Je, AESA inawasaidiaje kufanya uamuzi?

 • 36

  Mfano wa Muundo wa Uwasilishaji wa Data - AESA

  AESA No.

  Jina la kikundi

  Tarehe

  HALI YA HEWA

  Taarifa ya

  jumla

  Aina ya mimea

  Je, umetumia

  mbolea(ya

  kemikali)

  Tarehe ya

  kupanda

  Muda wa

  kuchunguza

  (tarehe, saa

  n.k.)

  (

  Wanyama

  walioonekan

  a

  Wadudu

 • 37

  Uchunguzi

  kuhusu mmea

  Upana wa jani

  Urefu wa

  mmea

  Idadi ya majani

  Idadi ya vifuko

  vinavyoonekan

  a

  Magonjwa

  yaliyoonekana

  Taarifa kuhusu udongo na maji

  Wanyama

  wanaokula

  mazao wa

  asili

  Uchunguzi wa jumla wa hali ya mmea na

  shamba

  MAPENDEKEZO

 • 38

  A.7.2. Zoezi: Ufuatiliaji wa Mara kwa Mara kwa kutumia AESA.

  AESA ilielezwa kwenye moduli iliyotangulia, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa AESA inatakiwa kufanya

  mara kwa mara ili vijana waelewe kwa ukamilifu na kudhibiti ukuaji wa mazao yao. Alimradi mazao yako

  kwenye shamba darasa, washiriki wafanye AESA mara moja kila wiki.

  Muda: Wastani saa 2

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea, tepu na kijiti

  1. Endesha majadiliano ya kukumbuka na vijana kuhusu AESA

  2. Nenda na vijana kwenye shamba darasa na wagawe katika vikundi vidogo vidogo

  3. Panga eneo kwenye shamba darasa kwa kila kikundi kuchunguza ukubwa wa eneo lililochaguliwa au

  idadi ya mimea (kulingana na zao)

  4. Viambie vikundi waandae orodha ya mambo muhimu waliyoona kuhusu ukuaji wa mazao

  5. Waambie kila kikundi wajadili habari walizoandika na kupendekeza taratibu za udhibiti ili kutatua

  matatizo yoyote yatakayojitokeza. Kwa mfano, kama magugu mengi yameonekana, inawezekana

  kupendekeza palizi kama pendekezo la usimamizi

  6. Toa muhtasari wa matokeo kwenye karatasi ambayo inaweza kutumika kama karatasi ya ufuatiliaji

  na kutunzia kumbukumbu: Michoro iwe rahisi na inayoonyesha hali/matokeo ya shamba.

  7. Kila kikundi kidogo kiwasilishe matokeo yao. Hakikisha watu tofauti wanawasilisha matokeo kila

  wakati.

  8. Jadili mawasiliano ya vikundi na njia za udhibiti zilizopendekezwa, na amueni pamoja kuhusu hatua

  gani zinatakiwa kuchukuliwa na nani watazichukua.

  Maelezo kwa Mwezeshaji: Maswali kwa ajili ya majadiliano katika hatua ya miche.

  Je, mimea imestawi vizuri (hatua ya miche)?

  Je, kwa jumla mazao yamestawi na yenye afya?

  Je, kuna hali ya majani kuwa njano? Kama ni hivyo ni kitu gani kinaweza kusababisha hali hiyo?

  Hali ya hewa ina athari gani katika ukuaji wa mimea?

  Je, unawaona aina gani ya wadudu waharibifu na wako wangapi?

 • 39

  Je, kuna mayai mengi ya wadudu rafiki?

  Je, uharibifu wa aina gani unafanywa na wadudu waharibifu katika hatua hii ya mazao?

  Je, kuna njia yoyote ya kuzuia wadudu hawa wasiongezeke?

  Je, hali ya wadudu waharibifu katika kashamba mengine kwenye eneo ikoje?

  Je, mashamba mengine yanaweza kuathiri shamba lako?

  Je, kuna aina gani ya maadui wa asili shambani?

  Je,wako wangapi? Unafikiri wanaweza kuwa wametoka wapi?

  Je, wanakula nini? Na walikuwa wanakila nini kabla hawajawa wadudu waharibifu?

  Je kuna wadudu ambao si waharibifu wala wadudu wa asili?

  Je, kuna wadudu waozeshaji ambao hula vitu vilivyokufa ndani ya udongo?

  Je, idadi ya wadudu waharibifu namaadui wa asili inaongezeka au kupungua ikilinganishwa na

  wiki zilizopita?

  Je, unatarajia kutatokea nini wiki ijayo?

  Je, kuna wadudu waharibifu maalumu wa kufuatilia kwa makini zaidi?

  Je,unafikiri kuna haja ya kutumia dawa ya kuulia wadudu waharibifu? Kama hapana,je kuna njia

  mbadala?

  Je, mimea imepata nafuu kutokana na uharibifu wa wadudu katika hatua iliyopita?

  Je, kuna ugonjwa wowote shambani? Unawezaje kudhibitiwa au kutibiwa?

  Je, mimea inakuwa kama ilivyotarajiwa (majani mangapi, kimo, n.k.)

  Je, kuna magugu kwa wingi? Ni wakati gani unafaa kufanya palizi?

  Je, kuna mpango gani waudhibiti kwa wiki ijayo?

  Je, uamuzi wa wiki iliyopita ullikuwa na ufanisi?

 • 40

  A.8.1. Zoezi: Palizi, Kwa nini, Wakati gani na namna gani

  Muda: Saa mbili

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Zingatia: Shughuli hii ni lazima ifanywe kwenye shamba la karibu ambapo mazao tayari

  yanakuwa na magugu yamekuwa ni tatizo

  Hatua:

  1. Wakiwa shambani, waambie vijana waketi katika mduara. Waulize wanafikiri mkulima atafanya

  nini kukinga mazao yasipatwe na magonjwa. Orodhesha mawazo yao yote

  2. Himiza majadiliano kuhusu umuhimu wa kuzingatia usafi wamazingira katika shamba kupunguza

  hatari za wadudu waharibifu namagonjwa. Waambie vijana wataje shughuli nyingi ambazo

  mkulima anaweza kufanya kuweka usafi wa mazingira unaofaa shambani kwao. Orodhesha

  shughuli hizo (palizi, kuondoa magugu na sehemu za mimea zilizoathiriwa shambani)

  3. Wagawe vijana katika vikundi vidogo vidogo na kiambie kila kikundi kichunguze sehemu moja ya

  shamba. Waulize vikundi kile kinachotakiwa kufanya

  4. Jaribu kuhitimisha ni wakati gani mkulima anatakiwa aanze palizi na anatakiwa aondoshe nini na

  abakishe nini shambani.

  A.9.1. Zoezi: Kupandikiza miche (mboga za majani n.k.)

  Muda: Wastani wa saa 2

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Upandikizaji huifanya mimea iwe minyonge. Kama upandikizaji haufanywi kwa makini, mimea haiwezi

  kukua vizuri. Kabla ya kwenda kwenye shamba darasa, waulize vijana maswali yafuatayo na orodhesha

  majibu yao kwenye chatipindu.

  Je, unadhani kupandikiza miche kuna hatua gani mbalimbali?

  Je, unafikiri ni mambo gani muhimu zaidi kufanya wakati unapopandikiza miche?

  Kwa nini unadhani ni muhimu kupandikiza miche jioni?

  Kwa nini unadhani mkulima lazima apandikize miche imara na si ile yenye afya ambayo

  imeambukizwa magonjwa?

 • 41

  Kwa nini ni muhimu kupandikiza miche ikifikia umri unaofaa, yaani si michanga sana wala si

  mikubwa sana?

  Je, unadhani mkulima atafanya nini kuipunguzia miche unyonge baada ya

  kupandikiza?(kutandaza nyasi na majani)

  Sasa unaweza kwenda na vijana kwenye shamba litakalopandikizwa miche inayotoka kwenye

  kitalu/vitalu. Waulize vijana maswali yafuatayo:

  Je,shamba limeandaliwa tayari kwa ajili ya kupandikiza miche? Kama ndiyo, kwanini unadhani

  liko tayari? Kama bado, unadhani kunahitajika kufanywa kitu gani ili kuanza kupandikiza miche?

  Sasa unaweza kuwaambia vijana washiriki katikakupandikiza miche.

  1. Jadili hatua mbalimbali za kupandikiza miche

  2. Mwagilia maji kitalu cha mbegu na onyesha namna ya kungoa miche kutoka kwenye kitalu

  3. Waambie vijana wote wangoe miche mingi kutoaka kwenye kitalu

  4. Onyesha namna ya kusafirisha miche mapaka shambani

  5. Waambie vijana wakusnaye miche yote iliyongolewa kutoka kwenye kitalu na waipeleke

  shambani

  6. Jadili na waonyeshe vijana namna ya kupandikiza miche kwenye shamba darasa

  7. Waambie vijana wapandikize miche yote iliyobaki

  8. Waambie vijana wamwagilie miche iliyipandikizwa

  Ukishamaliza, toa muhtasari wa hatua zote za kupandikiza miche.

  Taarifa ya msingi.

  Hatua za upandikizaji miche Vipengele muhimu

  1. Kutayarisha shamba darasa Udongo uliolimwa na kutiwa mbolea vizuri, hakuna magugu

  2. Kumwagilia kitalu chamnegu

  3. Kungoa miche Jioni, chagua miche imara na yenye afya kwa ajili ya

  kupandikiza, bakisha udongo kwenye mizizi na uwe mwangalifu

 • 42

  usiharibi mizizi

  4. Kusafirisha miche Muda mfupi,hakikisha kuwa imelowa na iwe kivulini. Miche

  iliyongolewa iondolewe kwenye udongo kwa muda mfupi tu (<

  saa moja).

  5. Kupandikiza miche Jioni, kuwa mwangalifu usiharibu wala kupinda mizizi

  6. Kumwagilia shamba darasa Mimea isikose maji baada ya kupandikizwa - isinyauke

  A.10. Mada ndogo: Umwagiliaji maji

  Malengo: Kuelewa maana ua umwagiliaji maji

  Kuelewa njia mbalimbali za umwagiliaji

  Kama ilivyotajwa hapo awali, kudhibiti maji shambani ni muhimu sana kwa ajili ya kulima mazao

  yanayostawi. Mvuainapokuwa kidogo sana, mhulima anatakiwa kutafuta njia ya kuyapatia mazao maji.

  Kuna njia mbalimbali za kumwagilia mazao. Ni muhimu kwa vijana kujua njia mbalimbali za umwagiliaji

  zinazotumika katika eneo hili. Pia wanahitaji kuelewa kuwa udongo unanyonya maji kwa haraka kiasi

  gani (kiasi cha udongo kupitisha maji)na kwa kiasi gani unavyoweza kuhifadhi maji (kiasi cha udongo

  kuhifadhi maji). Kwa kujua mambo haya mawili kutawasaidia kumwagilia mashamba yao kwa njia bora

  zaidi

  A.10.1. Zoezi: Kuelewa aina ya umwagiliaji na upitishaji maji

  Muda : Wastani wa saa2

  Vifaa: Kiasi cha chupa 20 za maji ( lita 15 05), kisu kikali. Kilo 1ya udongo wa mchanga, kilo 1 ya

  udongo wa mfinyanzi na maji

 • 43

  HATUA:

  Majadiliano ya Kikundi (Dakika 30)

  1. Waulize vijana kama yuko anayefahamu umwagiliaji ni nini. Mara baada ya maana ya

  umwagiliaji kueleweka kwa kila mmoja,waulize vijana kwanini wanafikiria ni muhimu kumwagilia

  mimea wakati wa ukame.

  2. Waulize vijana kama wanafahamu njia mbalimbali za umwagiliaji mazao shambani

  kwaonahalafu wabainishe njia zinazotumika na wakulima kwenye eneo/kijiji chao

  3. Waulize vijana wanafikiri kuna umuhimu gani katika kumwagilia mazao yao na katika kuchagua

  njia inayofaa kumwagilia

  4. Toa muhtasari wa matokeoya majadiliano: aina ya mazao, hatua ya mazao (kitalu au shambani),

  ukubwa wa shamba, mteremko na aina ya udongo

  5. Pitia pamoja na vijana aina ya udongo uliyojadiliwa kwenye moduli iliyopita. Anza kueleza

  wazola sifa za udongo na namna zinavyoathiri kiwango cha upitishaji maji na uwezo ya

  kuhifadhi maji

  Kuonyesha na kufanya majaribio (saa 1 dakika 30)

  1. Kata sehemu ya juu ya chupa (sehemu nyembemba) za chupa nnekwa kisu halafu toboa

  matundu sehemu ya kitako cha chupa mbili zamaji. Jaza udongo kwenye theluthi moja ya

  udongo kwenye chupa zenye matundu chupa moja udongo wa mchanga na chupa nyingine

  kiasi sawa cha udongo wa mfinyanzi. Tayarisha kiasi cha maji cha kutosha kwenye chupa

  nyingine (1/4 ya chupa) na weka alama kiwango cha maji.

  2. Mwambie kijana mmoja aangalie saa. Mimina maji kwa uangalifu kwenye udongo uliyomo

  kwenye mojawapo ya chupa na anza kupima muda utakaochukua kwamaji kunywea kwenye

  udongo hadi kwenye chupa iliyowekwa chini ya udongo (inapoanza kudoda juu ya chupa na

  inapoacha kudoda)

  3. Tayarisha kiasi sawa cha maji na mwambie klijana mwingine kufuatilia muda. Mimina maji kwa

  uangalifu juu ya udongo na kwenye chupa ya pili halafu pima muda utakaochukua kwa maji

  kunywea kwenye udongo

  4. Jadili tofauti za muda uliotumika kwa maji kunywea katika aina mbalimbali za udongo (kiwango

  cha upitishaji maji)

  5. Linganisha kiasi cha maji kilichoweza kunywea kwenye udongo na jadili kulitokea nini kwamaji

  yaliyobaki kwenye udongo(uwezo wakuhifadhi maji)

 • 44

  6. Wagawe vijana katika vikundi vya vijana watatu watatu au wanne na waambie warudie zoezi.

  Waambie kila kikundi kikusanye aina mbili tofauti za udongo karibu na wanapolutania kwa ajili

  ya SDSMV au kutumia kiasi sawa cha udongo kama uliotumiwa kwa zoezi. Wasaidie vijana

  wakati wa zoezi hilo na hakikisha kuchukua vipimo vyote vya majaribio

  Majadiliano ya Kikundi (Dakika 15)

  Jadili matokeo ya majadiliano kuhusiana na umwagiliaji. Udongo wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi

  maji unaweza kumwagiliwa mara chache zaidi ingawa kwa kutumia kiasi kikubwa cha maji. Kuhusu

  udongo wenye kiwango kikubwa cha upitishaji maji, maji yatatiririka haraka sana juu ya usawa wa bonde

  au mtaro kwa hiyo nilazima vijengwe kwamwinuko mkali . Toa muhtasari wa mambo yaliyoonekana

  katika jaribiona majadiliano.

  Maswali ya kuongoza majadiliano

  Tutajuaje kuwa tumemwagilia maji ya kutosgha?

  Je, tunatakiwa kumwagilia kila siku au mara moja kila baada ya siku mbili au tatu?

  Je, uwezo wa udongo kuhifadhi maji unaathari gani katika umwagiliaji

  Tutawezaje kukagua kama mmea/zao linahitaji kumwagiliwa?

  Je, ni dalili gani zinazoonyesha upungufu wa maji katika mmea/zao?

  Je, tutawezaje kutumia mteremko wa shamba kusambaza maji kwa usawa?

  Je,zao linahitaji kiasi gani cha maji kinacholingana kila siku?

  Mkulima afanyaje ili kupunguza mtiririko wa maji kwenye mtaro (umwagiliaji wa mtaro)?

  Kwa nini inatubidi kufikiria kuhusu mifereji ya kutoa maji mashambani vilevile

  tunapopanga umwagiliaji?

 • 45

  A.11.1. Zoezi: Urutubishaji Ardhi.

  Muda: Wastani wa saa 1

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  1. Waulize vijana kama wanafahamu mbolea ni nini na kwa nini wakulima wengi wanatumia

  mbolea kwenye mazao yao.

  2. Waambie vijana wataje aina mbalimbali za mbolea wanazozifahamu ambazo mkulima anaweza

  kutumia na waziorodheshe (mbolea za asili: mboji, samadi,mabakiya mimea nambolea za

  kemikali: urea, DAS, TSP, Potasium Kompaundi (NPK)).

  3. Viambie vikundi vijadiliane kwa vikundi vidogo tofauti kati ya aina mbalimbali za mbolea,

  madhumuni yake na namna zinavyotakiwa kutumika.

  4. Amua na vijana ni aina gani za mbolea zitumike kwenye shamba darasa na kiasi kinachotakiwa

  A.11.2. Zoezi: Utiaji mbolea wa mara ya pili

  Muda: Wastani wa saa moja

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  1. Mazao mengi hayahitaji utiaji mbolea wa mara ya pili. Waulize vijana kwa nini wanafikiri kuwa

  wanahitaji (mbolea za naitrojeni zinachujisha au vukiza kwa urahisi udongo wa juu na kuhitaji

  kuongezwa baada ya miezi 2-3)

  2. Jadili ni mazao gani katiya manne yaliyolimwa yanahitaji utiaji mbolea wa mara ya pili na

  zinahitajika mbolea za aina gani na zitumiwe lini (mazao ambayo hayajafikia hatua ya uzazi,

  baada ya miezi miwili,mbolea za naitrijeni, wiki chache kabla mazao hayajafikia hatua ya uzazi).

  Jadili njia bora zaidi ya kutia mbolea. Waambie vijana wafanye kwa vitendo shambani.

 • 46

  A.11.3. Zoezi: Ulindaji wa Rutuba ya udongo katika kilimo cha kutumia mbolea ya asili/kimaumbile

  Muda: Wastani wa dakika 20

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea

  Katika kilimo cha kutumia mbolea ya asili/kimaumbile wakulima wanatumia njia mbalimbali za kutunza

  na kuboresha rutuba ya udongo wao

  Bungua bongo na wanafunzi kuhusu njia mbalimbali mkulima anazoweza kulinda rutuba ya ardhi yake

  (mbolea za kemikali, samadi kutoka kwa wanyama, matumizi ya mazao jamii ya kunde katika kilimo cha

  kubadili mazao ya mizizi mifupi na mirefu, kutumia mboji).

  Jadiliana na wanafunzi, iwapo mbolea za kemikali/chumvichumvi haziwezi kutumika, tutatumiaje

  ainanyingine za kilimo kwenye shamba darasa letu. Tumia matokeo ya majadiliano katika kupanga

  shughuli za shamba darasa

  Kutegemea mboji

  Mboji ni mbolea ya takataka zilizoozeshwa na bakteria na viumbe hai vingine aghalabu za kikaboni kwa

  kipindi fulani. Mboji ni nafuu na rahisi kwa kutengeneza. Aina mbalimbali za vitu vya kikaboni ambavyo

  mara nyingi vinaonekana kuwa ni takataka katika mashamba na nyumbani kama vile maganda ya

  mboga, maagugu, matunda, majani na takataka za jikoni vinaweza kutumika.

  Kutumia mboji kunaongeza rutuba ya udongo kwa uongezaji watija na mavuno shambani. Mkulima

  anaweza kutengeneza mboji yeye mwenyewe ili kuokoa fedha. Ni njia salama katika kilimo na hivyo

  kuhifadhi ardhi kwa vizazi vijavyo

  A.11.4. Zoezi: Je, kutengeneza mboji ni nini na tunaweza kutumia vitu gani?

  Muda: Wastani wa dakika 40

  Vifaa: Karatasi kubwa na kalamu za kuchorea.

  Ili kulinda rutuba ya udongo katika kilimo cha kutumia mbolea ya asili, mkulima anawezakutumia mboji

  anayoweza kuitengeneza yeye mwenyewe. Waulize vijana kama kuna mtu wanayemfahamu katika jamii

  yao anayetengeneza mboji. Kama wanamfahamu, waulize vijana iwapo wanajua mtu huyo anavyofanya.

  Eleza kwa muhtasari kutengeneza mboji ni nini na kwamba tunawezakutumia aina zote za vitu vya

  kikaboni vinavyoonekana kuwa ni takataka mashambani na nyumbani. Bungua bongo kuhusu aina

  mbalimbali za vitu vya kikaboni vilivyopo katika jamii vinavyoweza kutumika kwa kutengenezea mboji.

 • 47

  Waambie vijana wakusanye kwenye gunia kwa jumla moja takataka za kikaboni zilizoorodheshwa na

  kuzileta kwenye somo lijalo kwa ajili ya kutengeneza mboji

  A.11.5. Zoezi: Kutengeneza Mboji

  Muda: Wastani wa dakika 60

  Vifaa: Ardhi, kasha, takataka za kikaboni, samadi, panga, sepeto, magunia, ndoo ya

  kumwagilia

  Eleza kuwa kuna njia mbalimbali za kutengeneza mboji. Mboji inawezakutengenezwa kwenye kasha,

  rundo, shimo, na kwenye rundo lililofukiwa kidogo (nusu mita), kutegemea hali ya mtiririko wa maji

  machafu mahali hapo. Jadiliana mfumo wa maji machafu na vijana na chagua namna ya kutayarisha

  mboji.

  Kama ni mboji ya shimo, mashimo matatu ya mboji yatachimbwa ubavuni kwa mfuatano. Mashimo hayo

  yatakuwa na kina cha sentimita 50, upana wa sentimita 150, na urefu kulingana na nafasi, kama

  inavyoonyeshwa kwenye Mchoro wa 1. Vitu vitakavyotumiwa, vinarundikwa kwa mpango maalumu

  kama ifuatavyo.

  1. Tabia ya udongo wa mfinyanzi (a) inatandazwa chini ya shimo kuzuia upotevu wa maji

  yatakayomwagiliwa kwenye rundo

  2. Tabaka ya matawi ya mti au mabua ya nafaka ya sentimita 15 (b) chini ya vitu vya kutengenezea

  mboji, husaidia kuzuia mmomonyoko

 • 48

  3. Tabaka ya vitu vya sentimita 15-30 (c ) kama vile mabaki ya mazao yaliyovunwa, nyasi, takataka

  za jikoni, n.k. huwa ndilo rundo kuu

  4. Juu kuna samadi ya kina cha sentimeta 10 20 (d) ambayo hurutubisha mboji nakuharakisha

  kuoza

  5. Katika hatua hii, umwagiliaji maji wa kutosha (lita 600-800 za maji kwa kila mita ya ujazo ya

  mboji) hufanywa.

  6. Tabaka nyembamba ya udongo (e) huziba tabaka zilizotangulia ili kuhakikisha joto linabaki ndani

  7. Rundo huongezeka kwa kurudia tabaka (c ) , (d), umwagiliaji wa maji na tabaka (e)

  8. Mwisho rundo linaezekwa tabaka la nyasi au mabua ya mimea sentimeta 20 (f)

  Rundo lililokamilika linaachwa lioze kwa siku 15 20 ambapo litageuzwa kutoka shimo 1 hadi la 2

  ambapo litakaa kwa siku nyingine zaidi 15 20 kabla ya kugeuzwa na kuingizwakwenye shimo la 3.

  Mboji bora ya mwisho itakuwa tayari kutumiwa baadaya siku nyingine 15 20.

  Zingatia: Chomeka mti mrefu kwenye rundo tangu mwanzoili kuhakikisha hali joto. Kama mti una joto,

  inaonyesha kwamba mboji inaoza na ikiwa baridi inaonyesha kupungua kwa uozaji wa mboji.

 • 49

  A.11.6. Zoezi: Kukagua, Kugeuza na Kutumia Mboji.

  Vitu vyote vilivyotumika kutengenezea mboji ni lazima vioze kwa ukamilifu kabla ya kutumiwa shambani.

  Kwa hiyo vijana ni lazima wajifunze kukagua hali mara kwa mara. Watakagua kwa mti au kwa kuingiza

  mkono kwenye mboji.

  Kama vitu vya kutengenezea mboji vinaoza kwa ukamilifu, halijoto itakaribia 80 0C. mti wakukagulia

  utakuwa na joto kali na mvuke kidogo utaonekana kwenye mti. Kama watakagua kwamkono,

  watumbukizemkono kwenye mboji kwa sekunde chache sana.

  Wakati halijoto inapoanza kupungua, (baada ya wiki mbili) mboji inahitaji kugeuzwa na kuchanganywa

  kwenye rundo jingine au shimo, na vitu ambavyo havijaoza kwa ukamilifu viwekwe katikati kadiri

  iwezekanavyo. Lazima igeuzwe mara mbili.

  Baada ya siku 45 60 mboji itakuwa tayari na inaweza kutumiwa shambani. Matumizi yake yataanza na

  ile mimea inayohitaji virutubisho vingi zaidi,mimea jamii ya kunde na hata mazao ya kwenye ardhi

  iliyorutubishwa kwa mboji msimu uliyopita, haihitaji mboji. Kiasi cha matumizi kitategemea aina ya

  mazao, hata hivyo kwa kawaida mboga za majani zinahitaji mboji kiasi cha kg/m2 4-6.

  Mboji ni lazima ichanganywe kwenye udongo kabla ya kupanda mazao

  A.12. Mada ndogo: Kulinda shamba la Kilimo

  Malengo:

  Kuelewa umuhimu wa kulinda shamba la kilimo

  Kubainisha na kuorodhesha njia mbalimbali za kulinda mimea shambani

  Kueleza mbinu mbalimbali za kulinda shamba.

  Shamba darasa ni miongoni mwa sehemu muhimu za maisha ya vijana ambazo wanahitaji kulinda.

  Kuhakikisha kwamba, shamba darasa linalindwa ipasavyo, ni vizuri kwa vijana kushirikiana na jamii na

  kuomba msaada wao. Kama wakiridhishwa kuhusu umuhimu wa mradi, ulinzi wa shamba/bustani

  utafanikiwa. Matatizo kama ya kuingiliwa na wezi na wanyama yataepukwa kwa urahisi.

  Kama matatizo ya usalama yatatokea kuhusiana na shamba darasa/bustani ya SDSMV, omba kufanya

  mkutano na viongozi wa jamii kujadili tatizo hilo na kuomba kusaidiakushughulikia matatizo ya usalama.

 • 50

  A.12.1. Zoezi: Kulinda Shamba Letu

  Muda: Wastani wa saa 2

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Mifano ya matatizo kwenye mashamba yasiyolindwa

  mbuzi huingia na kuharibu, na kula mazao

  ng'ombe huingia na kula kila kitu

  sungura huingia na kula saladi na kabichi changa

  panya huingia na kula mbegu za alizeti

  mavuno yanaweza kuibwa wakati wa usiku

  mazao hufa kutokana na ukame, wadudu au wadudu waharibifu

  1. Endeshs majadiliano mafupi na vijana kupitia vipengele vyote walivyokwishapitia kabla kuhusu

  wanataka kuyalinda mashamba yao kutokana na nini? Ili kuwasaidia kukumbuka, unaweza

  kutaka kuuliza maswali yafuatayo

  Kwa nini inatubidi kulinda shamba letu?

  Kutatokea nini kama hatutalinda vizuri mashamba?

  Tutafanyaje kuboresha hali hii?

  2. Wagawe vijana katika makundi manne. Waambie kila kikundi waandike au kuchora:

  Njia mbili za kulinda shamba dhidi ya wanyama wanaokula mimea.

  Njia moja ya kulinda dhidi ya ukame

  Njia mbili za kushughulikia wadudu waharibifu

  Njia mbili za kulinda dhidi ya wezi

  3. Waambie watu wawili kutoka kila kikundi wawasilishe na kueleza hatua walizopanga kuchukua

  pamoja

 • 51

  A.12.2. Zoezi: Kujenga uzio na uzio zaidi.

  Muda: wastani wa saa 1

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea, karatasina penseli

  1. Wapeleke vijana kwenye matembezi katika jamii na waambie wachague aina mbalimbali za uzio

  na maboma wanayoona

  2. Waambie wawadadisi baadhi ya wakulima ambao wanakutana nao wakati wa matembezi yao.

  Baadhi ya maswali wanayoweza kuwauliza wakulima ni:-

  Kwa nini mlichagua aina hiyo ya uzio?

  Kuna faida na hasara gani za uzio mlionao?

  Vifaa gani mmetumia kujenga uzio wenu?

  Je, uliujengaje?

  Ilichukuwa muda gani kujenga?

  Je, umeridhika na uzio huo?

  Je, ungependelea kuwa na aina mbalimbali za uzio? Kwa nini au kwa nini hapana?

  3. Baada ya matembezi na usaili, tafuta mahali penye kivuli kukaa na kufanya majadiliano ya

  jumla kuhusu wamejifunza nini. Wakati wa majadiliano, andaa mpango wa jinsi ya kupata vifaa

  ambavyo mtahitaji kwa ajili ya kujenga uzio na waambie vijana walete vifaa vya kujenga uzio

  kutoka nyumbani kwao kwa ajili ya somo linalofuata

  A.13. Mada ndogo: Kuvuna

  A.13.1. Zoezi: Wakati na mbinu za kuvuna

  Mazao mbalimbali katika shamba darasa yanahitaji kuvunwa siku chache kabla au wakati yamekwisha

  komaa kabisa, kutegemea aina ya mazao na matumizi ya mazao yaliyovunwa. Kila zao lina njia yake ya

  kuvuna.

 • 52

  Muda: Wastani wa dakika 30

  Vifaa: Hakuna

  Waulize vijana kama wanajua namna ya kuvuna mazao mbalimbali yaliyolimwa kwenye shamba darasa.

  Je, wanawajua wakulima wowote wanaotumia mbinu mbalimbali na kwa nini wanavuna tofauti?

  Jadili namna ya kuvuna mazao mbalimbali kwenye shamba darasa. Waulize vijana ni wakati gani wa siku

  unaofaa zaidi kuvuna mahindi na mbogamboga

  Nyanya wakati mwingine zinavunwa zikiwa bado mbichi na wakati mwingine zikiiva. Jadili kwa nini na

  kwa nini ni muhimu kila mara kufikiria unachopanga kufanya na mavuno kuhusu lini na namna

  inavyokubidi kuvuna zao hilo.

  A.14. Baada ya Kuvuna

  A.14.1. Zoezi: Namna ya kupunguza hasara baada ya kuvuna.

  Mkulima bado anapoteza asilimia kubwa ya mazao yake kati ya kuvuna na utumiaji au kuvuna mazao

  yake. Kama mambo mengi ambayo mkulima anaweza kufanya kupunguza hasara ya baada ya kilimo,

  kuanzia wakati wa kuvuna, na kufuatiwa na usafirishaji kutoka shambani, uhifadhi na ufungashaji. Vijana

  watajadili mkulima anachotakiwa kufanya kupunguza hasara baada ya mavuno wakati wa shughuli

  mbalimbali za baada ya kuvuna.

  Lengo: Kujifunza kuhusu mkulima anapaswa kufanya nini kupunguza hasara baada ya kuvuna

  Muda: Wastani wa saa 1

  Vifaa: Chatipindu na kalamu za kuchorea

  Hatua:

  Kubungua bongo (Dakika 20)

  1. Anza mada ya namna ya kupunguza hasara baada ya kuvuna. Waeleze vijana kuwa hasara baada

  ya kuvuna inaweza kugawanyika katika hasara ya kiasi (kg) na ubora. Aina mbili zote zinafanya

  hasara ya kiuchumi ya mazao.

 • 53

  2. Waulize vijana kuwa mkulima atafanya nini kupunguza hasara ya baada ya kuvuna. Andika hoja

  mbalimbali za hatua za uzingatiaji uliotajwa kwenye karatasi kubwa

  3. Jadili hoja mbali za hatua atakazozingatia mkulima zilizotajwa na zipange kwenye shughuli

  mbalimbali za shughuli za baada ya kuvuna (kuvuna, usafirishaji wa mazao, uhifadhi, usafirishaji,

  ufungashaji na uuzaji)

  Majadiliano ya vikundi vidogo vidogo(Dakika 40)

  4. Wagawe vijana katika vikundi vidogo na kiambie kila kikundi kichague mojawapo ya mazao

  yanayolimwa katika eneo

  5. Kwa zao walilolichagua, kiambie kila kikundi kijadili hoja za hatua za uzingatiaji ambazo mkulima

  hana budi kuchukua kwa shughuli mbalimbali za baada ya kuvuna ili kupunguza hasara ya

  mazao. Waambie kikundi watoe taarifa ya matokeo ya mazungumzo yao kwenye karatasi kubwa

  6. Kiambie kila kikundi kiwasilishe matokeo ya majadiliano yao

  7. Jadili mawasiliano mbalimbali

  8. Toa muhtasari wa hoja za hatua za uzingatiaji ambazo mkulima hana budi kuchukua wakati wa

  shughuli mbalimbali za baada ya kuvuna ili kupunguza hasara ya mazao.

  Maelezo kwa Mwezeshaji: Swali lakuongoza

  Je, kufanyike nini kuhifadhi ubora wa mazao yaliyovunwa

  Taarifa ya Awali/Usuli: Hoja za kuzingatia wakati wa kuvuna kupunguza hasara baada ya kuvuna.

  Muda unaofaa wa kuvuna (mazao yasiive sana)

  Zuia kuharibika kwa mazao

  Kutenganisha mazao yaliyoathiriwa na yenye magonjwa.

  Matumizi ya aina safi ya kuvuna.

  Uvunaji wa rejareja unapunguza haja ya kuhifadhina hasara ya uhifadhi

  Punguza kuharibika kwa mazao wakati wa usafirishaji

 • 54

  A.14.1. Zoezi: Utayarishaji/Uhifadhi wa mazao

  Mazao mapya ya kilimo yaliyovunwa (aina ya mizizi, mbogamboga na/au matunda) mara nyingi

  yanaweza kusindikwa ili kuongeza muda wa kutunza/uhifadhi wa mazao. Kutegemea aina ya mazao,

  kunahitajika kusafishwa kwa maji, kukatwakatwa silesi, kuchemshwa, kukaushwa (kwa jua), kusagwa

  na/au kufungashwa kabla ya kuhifadhiwa mahali salama na pa kavu. Kwa wenyeji, njia mbalimbali za

  kusindika huwa zinafahamika. Vijana watajadili na kufanya kwa vitendo na mwezeshaji mwenyeji njia

  mbalimbali za kusindika mazao ya kilimo

  Muda: Saa 1 na dakika 30

  Vifaa na matayarisho: Bainisha mwezeshaji mwenyeji anayefahamu usindikaji wa mazao ya

  kilimo ya chakula, mazao mapya, visu na sufuria.

  Majadiliano ya wote (Dakika 20)

  1. Anza mada ya usindikaji/ na utunzaji wa chakula. Jadili na vijana madhumuni ya

  usindikaji/utunzaji wa chakula

  2. Waulize vijana kama wanajua mifano mbalimbali ya utunzaji wa mazao ya kilimo (chakula)

  inayofanywa na watu katika eneo

  Vitendo (saa 1)

  3. Mtambulishe mwezeshaji mwenyeji na mwombe aonyeshe na/au kufanya kwa vitendo na

  vijana baadhi ya desturi za wenyeji za utunzaji wa chakula

  4. Jadili njia mbalimbali za utunzaji wa chakula na kuna mahitaji gani muhimu na maeneo

  yanayohitaji uzingativu maalumu katika utunzaji wa chakula (usafi, unyevunyevu na uhifadhi

  ghalani/ufungashaji)

  Majadiliano ya wote: (Dakika 10)

  Toa muhtasari wa somo

  A.14.3. Zoezi: Ghala bora

  Hasara inayotokana na uhifadhi ni tatizo kubwa. Wadudu waharibifu na magonjwa yanaweza kuharibu

  sehemu ya akiba kama mazao hayakuhifadhiwa mahali safi, pakavu na palipolindwa kwa ukamilifu.

  Vijana watajifunza aina mbalimbali za ghala za kuhifadhia zinazotumiwa katika eneo lao kuhifadhi aina

  mbalimbali za mazao ya kilimo

 • 55

  Lengo: Kujifunza kuhusu sifa muhimu za ghala bora

  Muda: Saa 1 dakika 30

  Vifaa na matayarisho: Kabla ya somo bainisha idadi ya ghala zilizopo karibu na fanya

  mpango vijana waweze kuruhusiwa kuzitembelea

  Bungua bongo (Dakika 15)

  1. Anza mada ya ghala bora

  2. Waulize vijana masharti muhimu zaidi ya uhifadhi na maghala ya kuhifadhia ni yapi kwamazao

  ya kilimo kwa kipindi cha miezi kadhaa. Andika masharti hayo kwenye karatasi kubwa. Ongeza

  masharti yaliyoachwa kwenye orodha kama inahitajika

  3. Jadili masharti ya uhifadhi

  Ziara (dakika 50)

  4. Nenda na vijana kwenye ghala za kuhifadhia zilizopo karibu na jadili na vijana hali/masharti ya

  ghala hizo. Kama ikiwezekana zungumza na wamiliki na waulize faida na hasara za ghala zao.

  5. Jadiliana na vijana ni ghala gani bora zaidi waliyoioana na kwa nini ni bora.

  Majadiliano ya wote: (dakika 15)

  6. Toa muhtasari wa sifa muhimu za ghala ya kuhifadhia mazao

  7. Jadili uwezekano wa kujenga ghala na SDSMV ya kuhifadhia mazao ya shamba darasa. Kama

  ikiwezekana andaa mpango wa kazi

  Maelezo kwa mwezeshaji: Maswali ya Kuongoza

  Ni kiasi gani cha mazao kinapotea wakati wa uvunaji, usafirishaji na uhifadhi wa mavuno?

  Je, kuna sababu gani kuu za hasara hiyo?

  Je, tutawezaje kupunguza hasara hii wakati wa uhifadhi wa mavuno?

  Je, tunawezaje kuzuia wadudu waharibifu na magonjwa visiingie kwenye ghala ya

  kuhifadhia?

 • 56

  Je, tunawezaje kudhibiti/ kukagua ubora wa mazao yaliyohifadhiwa?

  Je, aina mbalimbali ya mazao ya kilimo yanaweza kuhifadhiwa ghalani kwa muda gani?

  (mapya, yasiyosindikwa)

  Je, mkulima atafanya nini kuongeza muda wa kuhifadhi mazao ya kilimo?

  Je, ni njia zipi zinazotumiwa zaidi katika eneo kutunza mazao ya kilimo?

  Taarifa ya Awali/Usuli: Sifa muhimu za ghala2. Ghala bora haina budi kutunza mazao katika hali ya

  baridi na kavu. Lazima pia iweze kulinda mazao dhidi ya panya, ndege, wanyama wa shambani na wezi.

  Ghala nyingi ( isipokuwa baadhi ya ghala zenye ukuta imara za zege zinaweza kuzibwa) hazizuii kuingia

  kwa wadudu

  Ghala lazima ijengwe mahali pakavu, mbali na matawi ya miti, vinginevyo panya wanaweza kuruka

  kutoka kwenye matawi ya miti na kuingia ghalani. Ghala lazima liwe na paa linalomwaga maji ya mvua

  na lenye kivuli. Ghala hainabudi kuinuliwa juu ya usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasinywee ghalani na

  kuzuia panya na wanyama wa shambani wasifikie mazao yaliyohifadhiwa. Kama zitatumiwa nguzo za

  miti/mbao kuinulia jengo la ghala ni lazima vikingwe dhidi ya mashambulizi ya mchwa, mara nyingi oili

  chafu ya magari hutumiwa kuipaka miti/mbao.

  Kinga dhidi ya panya lazima zifungwe kwenye miguu ya ghala kuzuia panya wasipande ghalani. Kinga

  dhidi ya panya zitafanya kazi tu kama ghala itainuliwa angalau mita moja kutoka ardhini na hakuna

  mimea au nguzo karibu na ghala zitakazowawezesha panya na panya buku kupanda. Ghala haina budi

  kujengwa angalau umbali wa mita 1 kutoka kwenye mgongo na miti. Paka na mbwa husaidia

  kuwafukuza panya

  2. Chanzo: T., Namanda, S., Mwanga, R.O.M., Khisa, G., Kapinga, R. (2205) Manual for Sweetpotato Integrated Production and

  Pest Management Farmer Field Schools in sub-Saharan Africa. International Potato Center, Kampala, Uganda

 • 57

  A.14.4. Zoezi: Kuuza Mazao

  Muda: Saa nyingi katika masaa mbalimbali

  Vifaa: Vifaa vinavyotakiwa kwa ufungashaji, utangazaji na usafiri wa mazao

  Hatua:

  1. Kutegemea mikakati ya soko iliyotayarishwa, saidia vikundi mbalimbali matayarisho yao kwa ajili

  ya uuzaji wa mazao waliyovuna

  2. Warahisishie vijana kuuza mazao yao. Waambie vijana watunze kumbukumbu zao vizuri na kiasi

  cha mazao walichouza, bei waliyopata, gharama walizotumia, muda waliotumia kutayarisha na

  kuuza mazao yao na faida waliyopata

  3. Baada ya kuuza mazao yao, waambie vikundi wawasilishe matokeo yao ya shughuli za mauzo,

  wakieleza uzoefu wote waliopata, gharama na faida waliyopata

  4. Jaribu kuhitimisha masomo muhimu zaidi waliyojifunza

 • 58

  Juzuu ya 2

  Mtaala wa SDSMV Mada za Stadi za Maisha na

  Uanzishaji Shughuli

 • 59

  Yaliyomo:

  Mada/Zoezi uk

  Mazoezi ya Stadi za Maisha na Uanzishaji Shughuli

  J.1.1. Zoezi: Kupanga kwa ajili ya Baadaye

  J.2.1. Zoezi: Utunzaji Kumbukumbu

  J.3.1. Zoezi: Kutoa maamuzi

  J.4.1. Zoezi: Umuhimu wa Usafi bora

  J.4.2. Zoezi: Maandalizi Bora na Usafi wa Mtu

  J.5.1. Zoezi: Maji ni Uhai Ina maana gani?

  J.6.1. Zoezi: Desturi za Lishe Bora

  J.7.1. Zoezi: Utunzaji wa Kumbukumbu za Ushughulikiaji Mazao

  J.8.1. Zoezi: Mambo yanayolingana kuhusu kupanga biashara na kupanga katika kilimo

  J.9.1. Zoezi: Kuugua na kupata nafuu

  J.9.2. Zoezi: Magonjwa katika Maisha

  J.9.3. Zoezi: Jaribio la Kupiga Mpira wa VVU

  J.9.4. Zoezi: Mchezo wa Ugonjw