59
1 SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi 1 “00” na 2”45” kusini mwa Ikweta na kati ya Iongitudo 30”25” na 32”40” mashariki mwa ‘Greenwich’. Makao makuu ya mkoa yapo mjini Bukoba, uliopo umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam. Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa upande wa kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi, mikoa ya Kigoma na Mwanza kwa upande wa kusini na Ziwa Victoria kwa upande wa mashariki. Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168. Kati ya hizo, kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 10,655 (sawa na 27%) ni eneo la maji. Sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga, isipokuwa kwa wilaya za Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare. Mkoa katika upande wa magharibi una mito mingi ambayo inamwaga maji yake katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria. Kabla ya mwaka 1979, mkoa huu wa Kagera ulikuwa unaitwa “Ziwa Magharibi”. Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera” (Orodha ya Wakuu na Makatibu Tawala wa Mkoa wa Kagera tangu Uhuru ipo katika Kiambatanisho Na 1 na 2). Pendekezo la kuubadlisha jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Kagera lilitokana na Mto Kagera kugusa sehemu kubwa ya wilaya zote zinazounda mkoa huu ukiwa unatiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika Ziwa Victoria. 1.2. Historia ya Mkoa kabla ya Uhuru Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliounda jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba.

SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

1

SURA YA KWANZA

1. UTANGULIZI

1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo

Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi 1 “00” na 2”45” kusini mwa Ikweta na kati ya Iongitudo 30”25” na 32”40” mashariki mwa ‘Greenwich’. Makao makuu ya mkoa yapo mjini Bukoba, uliopo umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam. Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa upande wa kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi, mikoa ya Kigoma na Mwanza kwa upande wa kusini na Ziwa Victoria kwa upande wa mashariki.

Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168. Kati ya hizo, kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 10,655 (sawa na 27%) ni eneo la maji. Sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga, isipokuwa kwa wilaya za Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare. Mkoa katika upande wa magharibi una mito mingi ambayo inamwaga maji yake katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.

Kabla ya mwaka 1979, mkoa huu wa Kagera ulikuwa unaitwa “Ziwa Magharibi”. Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera” (Orodha ya Wakuu na Makatibu Tawala wa Mkoa wa Kagera tangu Uhuru ipo katika Kiambatanisho Na 1 na 2). Pendekezo la kuubadlisha jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Kagera lilitokana na Mto Kagera kugusa sehemu kubwa ya wilaya zote zinazounda mkoa huu ukiwa unatiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika Ziwa Victoria.

1.2. Historia ya Mkoa kabla ya Uhuru

Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliounda jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba.

Page 2: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

2

Ramani ya Mkoa wa Kagera

Uchumi wa wenyeji wa mkoa wa Kagera ulijikita katika mashamba ya migomba na kahawa. Chakula chao kikuu ni ndizi katika aina zake mbalimbali. Katika mashamba yao hulima mazao mengine kufuatana na msimu. Mazao hayo ni pamoja na maharage, mihogo, mahindi na mboga. Baada ya kuja kwa wazungu waliongeza ulimaji wa kahawa kama zao la biashara lililowasaidia kujiongezea kipato.

Wakazi wa asili ya Kagera ni wabantu na wengi wao wana asili ya Bunyoro. Wanaongea lugha sawa na ile ya Wanyoro, Wanyankole, Watoro na Wakiga. Busubi na Bugufi wana lugha na desturi sawa na Watusi, Wahutu na Waha. Lakini makabila hayo ni ya Wabantu wa Ziwa (Interlacustrine Bantu) na yanafanana mila na desturi. Makundi hayo yaligawanyika kati ya wachungaji (Bahima) ambao walitawala na wakulima (Bairu) ambao walitawaliwa na mara nyingi kudharauliwa. Bahima (Balangira) walikuwa na koo chache zipatazo 20 na walitawaliwa na Wahinda, Wabito na Wankango.

Page 3: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

3

Bairu walikuwa na koo kama 130 zenye mashina 24 ambayo kiasili walikuwa Bairu lakini kwa kuoa katika Bahima au kufanya kazi kwa Watemi walipandishwa hadhi na kuwa Bahima (Batware). Kila ukoo uliitwa jina la Baba mwanzilishi wake na kina ukoo ulikuwa na kitu walichokatazwa kula (Omuziro) na mnyama walioshirikishwa nae (Ekyerumono).

Kabla na baada ya kuja kwa wakoloni mkoa wa Kagera ulikuwa na utawala wa Kimila (Chiefdoms) uliogawanyika katika himaya 8. Himaya hizo ni pamoja na Kyamutwara, Kihanja (Kanazi), Kiziba, Ihangiro, Bugabo, Karagwe, Biharamulo (Rusubi) na Maruku (Bukara).

Moja ya nyumba za asili aina mshonge mkoani Kagera

Baadhi ya Watemi waliotawala himaya hizo ni pamoja na Emmanuel Rukamba (Kyamtwara), Rumanyika (Karagwe), Kasusura (Biharamulo), Lugomola (Bukara), Rutinwa (Kiziba), Kayoza (Bugabo), Kahigi (Kihanja) na Nyarubamba (Ihangiro). Kila mtemi alikuwa na walinzi wake walioitwa Warugaruga.

Makabila yanayopatikana hivi sasa katika mkoa wa Kagera ni pamoja na Wahaya ambao wanapatikana zaidi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Missenyi. Makabila mengine ni Wanyambo, wanaopatikana katika Wilaya ya Karagwe, Wasubi katika wilaya ya Biharamulo, Wasukuma katika

Page 4: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

4

Wilaya ya Chato na Wahangaza wanaopatikana katika Wilaya ya Ngara. Pia kuna Waha, Wazinza and Warongo. 1.3. Hali ya Hewa

Hali ya hewa ya mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa

26C. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800 – 1,100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwa uoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhimu kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

1.4. Utawala

Kiutawala Mkoa wa Kagera una Wilaya saba (7) na Mamlaka nane (8) za Serikali za Mitaa. Wilaya hizo ni Biharamulo, Bukoba, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. Mkoa una Tarafa 25, Kata 203, Vijiji 748, Vitongoji 4236 na Mitaa 66. Tarafa na Kata za kila Wilaya zimeonyeshwa katika Kiambatanisho Na 3. Kisiasa mkoa una majimbo 10 ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Biharamulo Magharibi (katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo), Jimbo la Bukoba Mjini (katika Manispaa ya Bukoba), Jimbo la Bukoba Vijijini (katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba), Jimbo la Chato (katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato), Majimbo ya Karagwe na Kyerwa (katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Jimbo la Nkenge (katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi), Majimbo ya Muleba Kaskazini na Muleba Kusini (katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba), na Jimbo la Ngara (katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara).

1.5. Idadi ya Watu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 mkoa ulikuwa na watu 2,028,157, wakiwa wanaongeza kwa wastani asilimia 3.1 kwa mwaka. Kutokana na wastani huo wa ongezeko la watu, mkoa sasa (Agosti 2011) unakadiriwa kuwa na watu 2,739,492 (ambapo wanaume wanakadiriwa kuwa 1,353,123 na wanawake wanakadiriwa kuwa 1,386,369.

Page 5: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

5

Idadi ya watu kwa kila Halmashauri kama ifuatavyo:-

Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba 153,016 Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo 252,218 Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba 325,808 Halmashauri ya Wilaya ya Chato 376,596 Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe 542,517 Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi 174,889 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba 492,404 Halmashauri ya Wilaya ya Ngara 422,044

1.6. Hali ya Uchumi

1.6.1. Shughuli za Kiuchumi

Uchumi wa Mkoa unategemea zaidi kilimo ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wake hutegemea kilimo kukidhi mahitaji yao ya chakula na pia kama chanzo cha mapato. Shughuli kuu nyingine za kiuchumi ni uvuvi, na ufugaji. Shughuli nyingine ni pamoja na viwanda, madini na biashara za kati na ndogondogo.

Kwa upande wa kilimo, wastani wa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula ni tani 2,800,000 na uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara ni tani 125,000. Mazao makuu ya chakula yanayozalishwa ni ndizi, maharage, mahindi na muhogo ambapo mazao makuu ya biashara ni kahawa, pamba, miwa, chai na vanilla. Kutokana na kuwapo kwa fursa za kuendesha shughuli za ufugaji kama vile upatikanaji wa malisho na maji ya mifugo, mkoa una kaya zipatazo 1,600 au wafugaji wapatao 113,000 zinazojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe (hasa wa asili), mbuzi na kondoo. Kwa hivi sasa mkoa unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 537,511 wanaofugwa ambapo ng’ombe wa asili ni 517,292 na ng’ombe wa maziwa ni 20,115. mbuzi wafugwao ni 642,969 ambapo mbuzi wa asili ni 633,037 na mbuzi wa maziwa ni 9,932. wanyama wengine ni kondoo 67,660, nguruwe; 11,243 na wanyama kazi kama vile punda 236 na farasi 18. wengine ni bata; 640,087; sungura; 13,201 na mbwa; 31,304.

Hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2011 mkoa ulikuwa na jumla ya wavuvi wapatao 30,500 wanajishughulisha na uvuvi katika Ziwa Victoria. Wavuvi wengine huendesha shughuli zao katika mito na mabwawa. Hata hivyo, kiujumla, hali ya uvuvi katika ziwa Victoria sio nzuri sana kwa sasa

Page 6: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

6

kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu na mabadiliko ya tabia nchi. Kipato cha wavuvi kimeshuka kutoka Kg 150 mwaka 2006/2007 kwa mtumbwi mmoja hadi Kg 15 mwaka 2011 kwa mtumbwi mmoja.

Kwa upande wa viwanda, mkoa haujawa na viwanda vingi au vikubwa Kwa takwimu za mwaka 2010, mkoa wa Kagera una jumla ya viwanda vikubwa na vya kati saba (7) tu ambavyo ni Kiwanda cha Sukari cha Kagera, viwanda vya kuchakata samaki vya Vic-fish na Kagera Fish, Kiwanda cha Kusindika Kahawa TANICA, Kiwanda cha Chai, Kiwanda cha Kahawa BUKOP na Kiwanda cha Kahawa cha Amir Hamza (T) Ltd. Pia kuna viwanda vidogo vidogo ishirini na mbili (22) na viwanda vidogo vinavyoendelezwa na SIDO 2,347.

1.6.2. Wastani wa Pato la mwananchi

Wastani wa pato la mkazi wa mkoa wa Kagera ni shilingi 453,253 kwa makadirio ya mwaka 2009. Wastani wa pato la mwananchi katika kila mamlaka ya serikali za mitaa ni kama ifuatavyo:-

Na Halmashauri Wastani wa Pato

1 Manispaa ya Bukoba 385,000

2 Wilaya ya Bukoba 386,000

3 Wilaya ya Biharamulo 429,000

4 Wilaya ya Chato 380,000

5 Wilaya ya Karagwe 425,000

6 Wilaya ya Missenyi 430,000

7 Wilaya ya Muleba 150,000

8 Wilaya ya Ngara 245,000

Kutokana na juhudi zinazoendelea za kuimarisha miundombinu na kuongeza uwekezaji katika kilimo hususan zao la kahawa, chai, miwa,na maharagwe, wastani wa pato la mwananchi wa mkoa wa Kagera linatarajiwa kukua mwaka hata mwaka.

Page 7: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

7

1.7. Huduma za Kijamii

Huduma za kijamii zinazopatikana katika mkoa wa Kagera ni pamoja na elimu, afya na maji. Mkoa una shule za msingi 1,050 zenye jumla ya wanafunzi 533,987 (wavulana 264,915 na wasichana 269,072) na walimu 9,896 mwaka 2011. Idadi ya shule za sekondari zilizopo mkoani Kagera 235 ambapo shule za serikali ni 199 na shule 36 ni za binafsi. Shule zenye kidato cha tano na sita ni 24, kati ya hizo 14 za serikali na 10 za binafsi. Kuna vyuo vya ualimu vitano (5) kimoja ni cha serikali na ufundi stadi 13 na Tawi la Chuo Kikuu Huria.

Kwa upande wa huduma za afya, mkoa una hospitali 15 (03 za serikali); vituo vya Afya 30 (25 vya serikali); na zahanati 244 (207 za serikali). Changamoto iliyopo katika utoaji wa huduma za afya ni uhaba wa watumishi.

Kiwango cha upatikananji wa huduma ya maji vijijini hivi sasa ni asilimia 55.3, kiwango katika maeneo ya makao makuu ya wilaya ni asilimia 65.8 na kiwango katika Manispaa ya Bukoba ni asilimia 76.5.

1.8. Hali ya Miundombinu ya Usafiri na Mawasiliano

Mkoa wa Kagera una mtandao wa barabara zenye urefu wa Km. 7,498 zinazohudumiwa na wakala wa barabara (TANROADS) na Halmashauri za Wilaya/Manispaa. Kati ya hizo jumla ya km. 563 ni za kiwango cha lami.

Mbali ya barabara njia nyingine muhimu ya ysafiri kwa Mkoa wa Kagera ni njia ya majini. Meli kadhaa na boti zinatoa huduma za usafiri wa abiria na mizigo kati ya mji wa Bukoba na Mwanza na pia kwenda kwenye visiwa vilivyomo katika Ziwa Victoria.

Hivi sasa hali ya usafiri wa anga katika mkoa wa Kagera nao umekuwa ukiimarika kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji kuwa mazuri zaidi kufuatia juhudi za serikali ambapo mashirika ya ndege ya Precision Air, Auric Air yamekuwa yakitoa huduma hii ya usafiri wa anga. Pia kuna huduma za ndege za kukodi.

Mkoa una viwanja vinne vya kutua ndege. Kuna kiwanja cha ndege cha Bukoba ambacho mwaka 2010 kimefanyiwa ukarabati mkubwa wa upanuzi wa njia ya ndege (run away) kutoka urefu wa kilomita 1.2 hadi kilomita 1.6.

Page 8: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

8

Viwanja vingine ni vidogo vya Ngara, Ihanda (wilayani Karagwe), Katoke (wilayani Biharamulo) na Rubya (wilayani Muleba), Hata hivyo viwanja hivi hutumiwa na ndege ndogo za serikali na mashirika yasiyo ya serikali. Wastani wa wasifiri wa anga kwa mkoa wa Kagera kwa mwaka ni abiria 24,865.

Pia mkoa una huduma bora za mawasiliano na upashanaji habari kama vile simu, ambayo hupatikana kwenye miji yote ya makao makuu ya wilaya na katika maeneo mengi ya vijijini, huduma za Posta, radio, televisheni, magazeti na intaneti.

Page 9: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

9

SURA YA PILI

2. MAFANIKIO YA MKOA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

2.1. Shughuli za Kiuchumi

2.1.1. Kilimo

Mwaka 1961 wakati tunapata UHURU, karibu asilimia 95 ya wakazi wa mkoa wa Kagera walikuwa wanajishughulisha na kilimo. Kwa kiasi kikubwa kilimo hicho kilikuwa cha jembe la mkono.

Kutokana na hali nzuri ya hewa mkoa wa Kagera ulikuwa ni miongoni mwa mikoa iliyokuwa inajitosheleza kwa chakula ambapo mazao kama ndizi, maharage, mahindi, mihogo na mtama yalikuwa yanazalishwa kwa wingi. Mazao makuu ya biashara yalikuwa ni chai na kahawa, pamba, chai na tumbaku.

Miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini, wakulima wa mkoa wa Kagera walihimizwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara ya kahawa na chai ili waweze kuinua vipato vyao.

Moja ya mashamba ya migomba mkoani Kagera

Kwa takwimu zilizopo, mwaka1988 wananchi wa mkoa wa Kagera walilima na kutunza jumla ya hekta zipatazo 226,192, eneo hili lilikuwa asilimia 11 ya eneo lote linalofaa kwa ajili ya kilimo.

Page 10: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

10

Mwaka 1994 wananchi walilima na kutunza jumla ya hekta zipatazo 358,528, eneo hili lilikuwa asilimia 19 ya eneo lote linalofaa kwa ajili ya kilimo ambalo lilikuwa hekta 1,868,750.

Katika msimu wa kilimo 2010/2011 mkoa umelima na kutunza jumla ya hekta 546,296 za mazao mbalimbali ya chakula ambazo zinatarajiwa kuzalisha jumla ya tani 1,298,890 za ndizi, tani 277,490 za nafaka, tani 145,335 za mikunde, tani 1,004,550 za mazao ya mizizi. Aidha,

Mkoa umelenga kulima na kutunza jumla ya hekta 67,920 za mazao mbalimbali ya biashara ambazo zinatarajiwa kuzalisha tani 61,837 za kahawa, tani 956 za tumbaku, tani 14,719 za pamba mbegu na tani 4,300 za majani mabichi ya chai.

Uzalishaji wa mazao ya chakula kuanzia mwaka 2007/08 – 2010/11

Mwaka Uzalishaji wa mazao (tani)

Mahindi Mchele Ndizi Mihogo Maharagwe Mtama Viazi Mengine

2007/08 218,996 1,539 621,708 119,540 7,095 1,201 30,800 698

2008/09 220,888 1,581 638,400 119,556 8,299 1,115 31,920 723

2009/10 240,103 2,943 1,056,401 121,132 8,919 1,172 31,914 738

2010/11 161,000 1,896 - - - - - -

JUMLA 840,987 7,959 2,316,509 306,228 24,313 3,488 94,634 2,159

2.1.2. Ufugaji

Mkoa wa Kagera ulikuwa ni miongoni mwa mikoa ya wafugaji wakati nchi yetu inapata Uhuru. Wakati huo mkoa ulikadiriwa kuwa na ng’ombe wa asili wanaokisiwa kufikia 184,236.

Kutokana na hali nzuri ya hewa na kutokuwepo kwa magonjwa ya mifugo ya mara kwa mara, idadi ya mifugo imekuwa ikiongezeka kadiri miaka

Page 11: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

11

ilivyokwenda. Kwa mfano, hadi kufikia mwaka 1984, mkoa ulikuwa na ng’ombe 364,866 (wa maziwa 6,417 na wa asili 358,449) na kuku 460,816 na bata 113,438. Hadi mwaka 1994 familia 20,549 kati ya familia 271,375 mkoani Kagera zilikuwa zikijishughulisha na ufugaji wa wanyama mbalimbali.

Hivi sasa mkoa unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 537,511 wanaofugwa ambapo ng’ombe wa asili ni 517,292 na ng’ombe wa maziwa ni 20,115. Mbuzi wafugwao ni 642,969 ambapo mbuzi wa asili ni 633,037 na mbuzi wa maziwa ni 9,932. Wanyama wengine ni kondoo 67,660, nguruwe; 11,243 na wanyama kazi kama vile punda 236 na farasi 18. Wengine ni bata; 640,087; Sungura; 13,201 na mbwa; 31,304. Kaya zipatazo 16,000 za wafugaji ambazo hufuga makundi makubwa ya ng’ombe.

Pamoja na watu binafsi, taasisi kama Kampuni ya Huria ya Taifa (NARCO), Jeshi la Magereza na taasisi nyingine mbalimbali zimekuwa zikijishughulisha na ufugaji wa kisasa. Ranchi za Kitengule, Mabale, Kagoma, Kikulula na Missenyi ndizo zinazoongoza kwa kufuga ng’ombe wengi na wa kisasa na wenye ubora zikifuatiwa na ranchi za Jeshi la Magereza za Kitengule na Rusumo.

Moja ya makundi makubwa ya ng’ombe aina ya Ankole mkoani Kagera

Uzalishaji wa maziwa katika mkoa wa Kagera umekuwa ukiongezeka kila mwaka na hivyo kuchangia kipato cha mwananchi na kuboresha lishe

Page 12: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

12

kwenye kaya za mkoa wa Kagera. Kwenye mwanzoni mwa miaka ya 1980 uzalishaji wa maziwa ulikuwa lita 1,488,900 na kuongezeka hadi lita 1,860,000 mwaka 1987 (sawa na ongezeko la asilimia 25). Aidha, mwaka 2002 zilizalishwa lita 5,000,000, mwaka 2005 zilizalishwa lita 15,000,000 na mwaka 2010 jumla ya lita 18,000,000 zilizalishwa.

2.1.3. Uvuvi

Tangu enzi za Uhuru, shughuli za uvuvi zimekuwa miongoni mwa vyanzo muhimu vya mapato na lishe kwa wakazi wa mkoa wa Kagera. Shughuli za uvuvi hufanyika kwa kiasi kikubwa katika ziwa Victoria.

Katika miaka ya 1970 uvuvi katika Ziwa Victoria uliendelea kukua kwa kasi. Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwaka 1986 jumla ya tani 39,468 za samaki zilivuliwa zikiwa na thamani ya shilingi 983 milioni. Mwaka 1988 samaki tani 50,756 (zenye thamani ya shilingi 1,118,991,200) walivuliwa na kilo 14,640 za dagaa ziliuzwa nje ya nchi na kuingiza pato la $7,320.

Baadhi ya mitumbwi ya kuvulia samaki kwenye kituo cha wavuvi eneo la Kemondo halmashauri ya wilaya Bukoba

Katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kumekuwa na mapinduzi makubwa katika sekta ya uvuvi. Viwanda vya kuchakata samaki vimeanzishwa na biashara ya samaki nje ya nchi imeendelea kukua. Hivi sasa mkoa wa Kagera una viwanda vikubwa viwili vya samaki (Kagera Fish na Vic Fish) ambavyo husafirisha samaki nje ya nchi na kuipatia nchi yetu fedha za kigeni. Jumla ya shilingi 2,258,539,408.06 zimekusanywa na

Page 13: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

13

serikali zikiwa ni mrahaba wa mazao ya uvuvi kati ya mwaka 2006/7 na mwaka 2009/10.

2.1.4. Viwanda

Hali ya viwanda mkoani Kagera wakati wa Uhuru haikuwa nzuri sana kwani kulikuwa na kiwanda kimoja tu cha kusindika chai cha “Kagera Tea Company”. Mwaka 1967 kiliongezeka kiwanda kingine, cha TANICA, ambacho ni cha kusindika kahawa. Hadi kufikia mwaka 1977, mkoa wa Kagera ulikuwa na viwanda vya kati vitano (5). Viwanda vilivyoongezeka vilikuwa kiwanda cha kukoboa Kahawa cha BUKOP, kiwanda cha kusindika Pamba na kukamua mafuta ya Pamba BCU, na kiwanda cha sukari cha KAGERA.

Kiwanda cha sita kiliongezeka mwaka 1990 ambacho ni cha kutengeneza soda “West Lake Bottlers”. Pia kulikuwa na viwanda vidogo vidogo 270 vilivyotengeneza aina tofauti ya bidhaa.

Kiwanda cha TANICA kilichopo Manispaa ya Bukoba. Kiwanda hiki kilifunguliwa rasmi na Mwl. J.K Nyerere tarehe 18 Julai, 1967

Kwa takwimu za mwaka 2010, mkoa wa Kagera una jumla ya viwanda vikubwa na vya kati saba (7) ambavyo ni Kagera Sugar, Vic-fish, Kagera Fish, kiwanda cha kusindika kahawa TANICA, kiwanda cha chai, kiwanda cha kahawa BUKOP na kiwanda cha kahawa kijulikanacho kama Amir

Page 14: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

14

Hamza (T) Ltd. Vile vile kuna viwanda vidogo vidogo ishirini na mbili (22) na viwanda vidogo jamii ya SIDO 2,347.

Kutokana na uwepo wa viwanda vikubwa 7 katika mkoa kumekuwepo na ongezeko la ukuaji wa ajira ambao pia umechangia ongezeko la pato la mkazi. Mwaka 1975 ajira katika viwanda zilikuwa 250, mwaka 1995 ajira katika viwanda hivyo zilikuwa 1,337, mwaka 1996 zilikuwa 1,323, mwaka 1997 zilikuwa 1,350, mwaka 1998 zilikuwa 1,403, mwaka 1999 zilikuwa 1,480 na mwaka 2000 ajira zilikuwa 1,576. Hadi mwaka 2010 ajira viwandani zilikuwa zimefikia 4,856.

Ongezeko la viwanda limetokana na upatikanaji wa malighafi, umeme wa uhakika, teknolojia na nguvukazi/wataalam.

2.1.5. Ushirika

Ushirika katika mkoa wa Kagera una historia ndefu. Hadi nchi hii inapata Uhuru, ushirika katika mkoa huu ulikuwa wenye nguvu kuliko maeneo mengi ya Tanzania Bara. Ushirika ulikuwa umeanza tangu katikati mwa miaka ya 1930 ambapo mwaka 1935 chama cha kwanza cha ushirika (Bugufi Coffee Cooperative Union) kilianzishwa katika Wilaya ya Ngara.

Mwaka 1939 chama kingine cha Ushirika cha Buhaya (BCU) kilianzishwa ambapo kilihudumia wilaya za Bukoba, Muleba, Karagwe na Biharamulo. Chama hiki kilikua na hatimaye kusajiliwa kama chama kikuu cha ushirika cha Bukoba (Native Coffee Cooperative Union (BNCU Ltd)) katika mwaka 1950. Mwaka 1960 BNCU na vyama vya ushirika vya msingi 74 vilinunua kiwanda cha kukoboa Kahawa cha BUKOP kutoka kwa Kampuni ya BCCCO Ltd iliyokuwa inamilikiwa na wafanyabiashara wa Kihindi.

Mara baada ya uhuru kulikuwa na ongezeko kubwa la vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) katika maeneo ya Ibwera, Izigo, Bugandika, Itawa, Kanyigo na Kamachumu. Ongezeko la vyama hivi vya kuweka na kukopa lilitokana pia na uhamasishaji wa Mhashamu Kardinali Laurian Rugambwa, alioufanya mara baada ya kurudi nchini kutoka Canada mwaka 1961. Kiujumla wakati wa Uhuru mkoa ulikuwa na jumla ya vyama vya ushirika 89 na chama kikuu kimoja cha BNCU Ltd.

Mwaka mmoja baada ya Uhuru, yaani mwaka 1962, chama kingine cha usambazaji cha ushirika-Tanganyika (COSATA) kilianzishwa ambacho kilikuwa ndiyo muuzaji mkuu na msambazaji wa bidhaa kwa wanachama wake na wananchi kwa jumla.

Page 15: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

15

Kutungwa kwa sheria ya kwanza ya vyama vya ushirika mwaka 1968 kuliimarisha zaidi harakati za ushirika katika mkoa huu ambapo pamoja na matukio mengine ya kukua kwa ushirika kiwanda cha Kahawa cha TANICA kilianza uzalishaji. Kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya ushirika katika Tanzania Bara, vyama vya ushirika vya mkoa wa Kagera vilivunjwa na Serikali mwaka 1976 ambapo wakulima wa kahawa, pamba na mazao mengine ya biashara walihudumiwa na bodi za mazao ambazo zilianzishwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya vyama vya ushirika. Hata hivyo miaka miwili baadae, mwaka 1978 jumuiya ya wanaushirika nchini (UCS) ilianzishwa na mwaka 1979 WASHIRIKA (UCS) walitambuliwa kama Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi (C.C.M). Baadae, kufuatia mapendekezo ya Tume iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya kumshauri juu ya kuanzishwa upya kwa vyama vya ushirika nchini, kulitungwa sheria mpya ya vyama vya ushirika nchini mwaka 1982. Kufuatia kutungwa na kuanza kutumika kwa sheria hiyo Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Kagera (Kagera Co-operative Union, KCU-1984- Ltd), kilianzishwa mwaka 1984. Chama cha Ushirika cha mkoa wa Kagera KCU (1984) Ltd kilivunjiaka miaka miwili tu baadae. Vyama vipya viwili viundwa: Biharamulo Cooperative Union (BCU 1986 Ltd) kilichoundwa baada ya Wilaya ya Biharamulo kujitenga, na Kagera Cooperative Union (KCU 1986 Ltd) ambacho kilihusisha wilaya za Bukoba, Muleba, Karagwe na Ngara. Matukio zaidi katika sekta ya ushirika mkoani Kagera yalitokea mwaka 1990 ambapo chama kikuu cha KCU (1986) Ltd kilivunjika na kufilisika. Hata Serikali iliposaidia kufufua ushirika KCU (1990) Ltd ilifufuka ikiwa na na vyama vya msingi 125 tu vya wilaya za Bukoba na Muleba. Pia katika mwaka huo huo wa 1986, vyama vya ushirika vya msingi 76 vya wilaya ya Karagwe vilijiondoa kutoka KCU (1986) Ltd na kuanzisha muungano wa Karagwe Development Coperative Union (KDCU Ltd).

Hadi mwaka 2007 jumla ya vyama vya ushirika vilivyoandikishwa mkoani Kagera ni 513 vikiwa ni pamoja na vyama vikuu vitatu (3) na Benki ya ushirika ya KFCB Ltd.

Page 16: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

16

Hadi kufikia sasa, mwaka 2011, mkoa una jumla ya vyama vilivyoandikishwa 675, SACCOS (352), AMCO (250), vyama vikuu (3) na ushirika wa aina nyingine (70). Aidha, idadi ya wanachama katika vyama vya ushirika imeongezeka kutoka wanachama 23,500 mwaka 1965 hadi wanachama 160,252 Juni, 2011.

2.1.6. Taasisi za Fedha

Mwaka 1961, mkoa ulikuwa unapata huduma za kibenki kutoka taasisi moja tu, Benki ya Posta, wakati huo ikijulikana kama Shirika la Posta na Simu. Benki ya National Bank of Commerce tawi la Kagera lilianzishwa mwaka 1971 na benki ya CRDB ilifungua tawi lake Mkoani Kagera mwaka 1987.

Hadi kufikia sasa kuna jumla ya taasisi za fedha tano (5 ambazo ni CRDB (1996) Ltd, National Microfinance Bank (NMB), Benki ya Posta, National Bank of Commerce (NBC) na Kagera Farmers Co-operative Bank (KFCB) katika mkoa huu. Aidha, zipo pia taasisi za fedha ambazo hutoa huduma za kukopa, taasisi hizo ni PRIDE, FINCA, BAYPORT na NUFAIKA.

2.1.7. Uchimbaji Madini

Tangu Uhuru mkoa wa Kagera umekuwa na shughuli chache sana za madini zikiwahusisha wachimbaji wadogo wadogo katika maeneo mbalimbali mkoani. Madini yanayochimbwa na wachimbaji wadogowadogo ni dhahabu Biharamulo na Chato, bati Karagwe.

Kwa upande wa uchimbaji mkubwa hadi sasa kuna kampuni moja tu kubwa wilaya ya Biharamulo inayochimba madini ya dhahabu, inayoitwa Tulawaka Gold Mine. Pia wilayani Ngara kunafanyika utafiti wa madini ya nikeli kampuni moja ya Kabanga Nikel Company.

2.2. Ujenzi wa Miundombinu

2.2.1. Barabara

Hadi kufikia mwaka 1973 mtandao wa barabara ulikuwa umefikia jumla ya kilometa 1,643. Kati ya barabara hizo za mkoa zilikuwa 818, na barabara zilizokuwa chini ya mamlaka za serikali za mitaa zilikuwa 825. Urefu wa mtandao huo uliongezeka hadi kilomita 3,015 mwaka 1988, kilomita 3,951

Page 17: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

17

mwaka mwaka 1996 na kilomita 4,258 mwaka 2002. Hivyo kati ya mwaka 1996 na mwaka 2002 kulikuwa na ongezeko la kilomita 1,307.8 sawa na asilimia 33.

Hivi sasa mkoa una mtandao wa barabara zenye urefu wa Km. 7,498 zinazohudumiwa na wakala wa barabara (TANROADS) na Halmashauri za Wilaya/Manispaa. Kati ya hizo jumla ya km. 563 ni za kiwango cha lami.

2.2.2. Usafiri wa Majini

Wakati tunapata UHURU mwaka 1961, wakazi wa mkoa wa Kagera walitegemea sana usafiri wa majini. Usafiri wa majini ulisaidia sana kusafirisha mizigo na abiria kati ya miji ya Bukoba, Kemondo, Musoma, Mwanza na hata Jinja.

Wakati tunapata UHURU mwaka 1961, huduma hii ya usafiri wa majini ilikuwa inatolewa na meli za MV. Victoria, Kabilondo, Nyangumi, Umoja, Ng’ombe, Subili na Usoga.

Mwaka 1978 meli ya MV Bukoba ilianza kufanya kazi na ambapo miaka miwili baadae, yaani mwaka 1980, meli nyingine ya MV. Butiama nayo ilianza kufanya kazi baada ya kutengenezwa na Wabelgiji. Aidha, mwaka 1988 meli ya MV Serengeti ilianza kufanya kazi zake kati ya Bukoba na Mwanza.

Hadi sasa, meli ya MV. Victoria, Nyangumi na Umoja ndizo zinazoendelea kutoa huduma za usafiri wa abiria na mizigo kati ya Bukoba, Mwanza na nchi jirani ya Uganda. Meli ya MV Kabilondo, Ng’ombe, Subili na Usoga kwa sasa haifanyi kazi katika ziwa Victoria.

Page 18: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

18

Bandari ya Bukoba mkoani Kagera

Hali kadhalika, katika kipindi hiki cha miaka hamsini ya Uhuru kumekuwa na ongezeko la meli na boti za watu binafsi ambazo zinafanya kazi ya usafirishaji abiria na mizigo kati ya Bukoba, Mwanza na visiwa ndani ya ziwa Victoria.

2.2.3. Mawasiliano

2.2.3.1. Simu

Upatikanaji wa huduma ya simu katika miaka ya 1960 ulikuwa mgumu hasa katika maeneo ya vijijini. Simu zilipatikana mjini ama maeneo maalumu yaliyokuwa yakikaliwa na wamisionari na vikundi vya kiulinzi. Kufuatia upanuzi wa mawasiliano ya simu kwa kujenga mitambo mipya ya STD hapa mkoani, kumekuwa na ongezeko la wateja wapatao 3,344.

Hivi sasa mawasiliano kwa njia ya simu yameendelea kuimarika hasa kupitia mitandao ya simu za mkononi. Makampuni ya Tigo, Vodacom, Zain na Zantel yanatoa huduma miji yote ya makao makuu ya wilaya na katika maeneo mengi ya vijijini.

2.2.3.2. Huduma za Posta

Taasisi ya kuendesha huduma za posta mkoani Kagera ilianzishwa na serikali ya kikoloni ya Ujerumani mwaka, 1880. Kabla ya uhuru huduma za

Page 19: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

19

posta zilikuwa zinatolewa na Wajeurumani katika jengo la mkuu wa wilaya. Wakati huo watu walikuwa wakipeleka barua kwa miguu kwa kukabidhiana baina ya watu wawili kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Baada ya uhuru huduma za posta na simu kwa pamoja zilihamia katika jengo linalotumika hadi sasa likiwa linamilikiwa na watanzania wenye asili ya kiasia ambapo serikali kupitia shirika la posta iliweza kulinunua. Kuanzia mwaka 1967 hadi 1977 shirika hili lilikuwa likiendeshwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1977 uendeshaji huo wa pamoja ulifikia ukomo baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika. Serikali ya Tanzania iliunda shirika la posta na simu Tanzania (TP & TC). Mnamo mwaka 1993 serikali ililivunja lililokuwa shirika la posta na simu na kuanzisha shirika la posta la Tanzania (TPC) ili liweze kuendesha shughuli za posta nchini, baada ya serikali kuligawanya shirika katika taasisi tatu zinazojitegemea za TPC, Benki ya Posta Tanzania na Kampuni ya simu Tanzania (TTCL)

Hadi kufikia mwaka 2011 kampuni ya DHL imefungua tawi lake mkoani Kagera na hivyo kufanya makampuni yenye kutoa huduma za kubeba vifurusi kufikia mawili.

2.2.3.3. Mkongo wa Taifa na Intaneti

Mwaka 1961 hakukuwa na mawasiliano kwa njia ya intaneti, hadi mwaka 2011 mawasiliano kwa njia ya intaneti yameimarika mkoani Kagera kupitia mkongo wa taifa na makampuni binafsi yanatoa huduma hiyo.

2.2.3.4. Redio

Kama ilivyokuwa katika mikoa mingine yote ya Tanzania Bara, wakati wa UHURU mkoa wa Kagera ulikuwa unategemea radio moja tu ya Taifa (Radio Tanzania Dar es Salaam) katika kupata habari, burudani na hata elimu ya mambo mbalimbali. Kutokana na mabadilko ya sera za habari na mawasiliano ambapo vituo binafsi vya radio vimeruhusiwa kuanzishwa, mkoa wa Kagera sasa una vituo vitano (5) vya radio. Aidha, kuna jumla ya vituo vya redio kumi kutoka nje ya mkoa vinavyosikika mkoani Kagera.

2.2.3.5. Magazeti

Wakati tunapata UHURU mwaka 1961, mkoa wa Kagera ulikuwa na magazeti matatu (3) ya Rumuli, Ijawebonele na Kagera Leo. Hadi kufikia Juni mwaka 2011 mkoa una jumla ya magazeti mawili (2) ambayo ni

Page 20: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

20

Rumuli na Ijawebonele. Magazeti mengine hupatikana kutoka nje ya mkoa wa Kagera.

2.2.3.6. Televisheni

Tangu UHURU hadi sasa mkoa hauna kituo chochote cha televisheni. Aidha, mawimbi ya televisheni kutoka nje ya mkoa yameweza kufika mkoani na hivyo kurahisisha upatikanaji wa habari na mawasiliano.

2.2.4. Usafiri wa Anga

Katika miaka ya 1970 huduma ya usafiri wa anga ilikuwa ikitolewa na Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (East Africa Airways). Baada ya shirika la EAA kusitisha huduma zake, huduma hiyo ilitolewa na shirika la ndege la Air Tanzania hadi mwaka 2003 liliposimamisha huduma hiyo.

Hivi sasa hali ya usafiri wa anga katika mkoa wa Kagera imekuwa ikiimarika kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji kuwa mazuri zaidi kufuatia juhudi za serikali ambapo mashirika ya ndege ya Precision Air, Auric Air yamekuwa yakitoa huduma hii ya usafiri wa anga. Pia kuna huduma za ndege za kukodi.

Mkoa una viwanja vinne. Mbali na kiwanja cha ndege cha Bukoba kuna viwanja vingine vidogo vya Ngara, Ihanda (wilayani Karagwe), Katoke (wilayani Biharamulo) na Rubya (wilayani Muleba), Hata hivyo viwanja hivi hutumiwa na ndege ndogo za serikali na mashirika yasiyo ya serikali.

Hivi sasa uwanja wa ndege wa Bukoba umefanyiwa ukarabati mkubwa wa upanuzi wa njia ya ndege (run away) kutoka urefu wa kilomita 1.2 hadi kilomita 1.6 ili kuwezesha ndege kubwa aina ya ATR 42 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 kutua.

Page 21: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

21

Eneo la uwanja wa ndege wa Bukoba uliopo Manispaa ya Bukoba

Kulingana na takwimu zilizopo kumekuwa na ongezeko la wasafiri wa anga kadiri miundombinu ya usafiri huo inavyoimarika. Mwaka 1967 kulikuwa na wasafiri 750, mwaka 1977 kulikuwa na wasafiri 2,378, mwaka 1988 kulikuwa na wasafiri 4,560, mwaka 1998 kulikuwa na wasafiri 10,855, mwaka 1990 wasafiri 10,185, mwaka 2000 kulikuwa na wasafiri 11,278 na mwaka 2010 kulikuwa na jumla ya wasafiri 24,865. Idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga imeongezeka kutoka abiria 750 mwaka 1967 hadi 24,865 mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia 1,404.

taarifa ya wasafiri

0

5000

10000

15000

20000

25000

30000

1967 1977 1988 1998 1990 2000 2010

mwaka

wa

sa

firi

Page 22: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

22

2.3. Huduma za Jamii

2.3.1. Elimu

2.3.1.1. Elimu ya Msingi

Mkoani Kagera kumetokea mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu ya msingi kuanzia uhuru wa nchi hii. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa mwaka 1975, kutokana na mpango wa Elimu kwa Wote (UPE) kulikuwa na shule za msingi 592 za serikali. Idadi ya shule imekuwa ikiongezeka na kufikia shule 619 mwaka 1985 na shule 677 mwaka 1990. Hadi kufikia mwaka mwaka 2011 kumekuwa na shule 1,050 zenye jumla ya wanafunzi 533,987 kati ya hawa 269,072 wasichana na 264,915 wavulana.

Walimu pia wamekuwa wakiongezeka kutoka walimu 5,503 mwaka 1985 hadi walimu 6,361 mwaka 1996. Mwaka 2002 kulikuwa na walimu 6,521 na idadi kufikia walimu 9,896 mwaka 2011.

2.3.1.2. Elimu ya Sekondari

Mkoa umepata maendeleo makubwa katika sehemu ya elimu ya sekondari kuanzia nchi yetu ipate uhuru mwaka 1961. Mwaka 1963 kulikuwa na shule za sekondari nne ambazo ni Kahororo, Ihungo, Bukoba (Grewal) na Nyakato. Idadi ya shule za sekondari ziliongeka hadi kufikia shule 36 katika mwaka 1996 ambapo shule 9 kati ya hizo zilikuwa za serikali na 27 za binafsi,

Idadi ya shule za sekondari za sasa ni 235. Shule za serikali ni 199 na shule 36 ni za binafsi. Shule za kidato cha tano na sita zimefikia 24, kati ya hizo 14 za serikali na 10 za binafsi.

2.3.1.3. Vyuo na Ufundi Stadi

Wakati tunapata UHURU mwaka 1961, mkoa ulikuwa na chuo kimoja cha ualimu cha Katoke ambacho kilimilikiwa na dhehebu la Anglikana. Chuo hiki kilianza kama ‘middle school’ mwaka 1933 na baadae kuwa chuo cha ualimu mwaka 1937. Mwaka 1967 chuo hiki kilitaifishwa na kuwa chuo cha ualimu cha serikali na mkuu wa chuo hicho wa kwanza ambaye alikuwa Mtanzania aliitwa Harun Sembuche ambaye yuko hai hadi sasa. Chuo hiki kinatoa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti.

Hadi mwaka 2010 mkoa una jumla ya vyuo vya ualimu vitano (5) kati yake kimoja ni cha serikali; Chuo cha Ualimu Katoke, na vyuo 4 ni vya

Page 23: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

23

binafsi/mashirika ya Dini. Vyuo hivi vinawaandaa walimu wa daraja la IIIA na Elimu ya Awali.

Kwa upande wa ufundi stadi, mkoa wa Kagera haukuwa na chuo chochote cha ufundi wakati wa UHURU. Hivi sasa mkoa una jumla ya vituo vya ufundi stadi 13. Fani zinazofundishwa ni useremala, uashi na sayansi kimu.

2.3.1.4. Elimu ya Juu

Mwaka 1961 wakati wa UHURU mkoa wa Kagera haukuwa na chuo chochote cha elimu ya juu. Aidha, hadi kufikia Juni 2011 mkoa una chuo kikuu kimoja ambacho ni Tawi la chuo kikuu huria cha Tanzania.

2.3.1.5. Elimu ya Watu Wazima

Kuanzia mwaka 1961 elimu ya watu wazima mkoani Kagera iliendeshwa katika vituo vya maendeleo (social community centers) na kiwango cha watu wasiojua kusoma na kuandika kilikuwa 75%. Kufuatia kutangazwa kwa harakati za kupambana na adui ujinga katika nchi yetu ambazo zilitangazwa na Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere katika hotuba yake ya mkesha wa mwaka mpya tarehe 31/12/1969, watu wazima waliandikishwa katika kisomo chenye manufaa (KCM) na kisomo cha kujiendeleza (KCK). Aidha, program zaidi za elimu ya watu wazima (EWW) zilitolewa kwenye magazeti, vijijini, redio, elimu kwa njia ya filamu, maktaba na magazeti ya kanda. Gazeti la kanda linajulikana kama Jalida la Elimu Tanzania-kanda ya ziwa. Upimaji ulifanyika miaka ya 1975 na 1983 na utafiti wa mwaka 1992 na 2002 ambao ulibaini watu wazima 200,000 walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu mkoani Kagera. Mwaka 2002 ujinga ulifikia asilimia 28, mwaka 2004 asilimia 31 na mwaka 2010 ujinga umefikia asilimia 43.

2.3.2. Sekta ya Afya

2.3.2.1. Huduma za Afya wakati wa Uhuru

Wakati nchi inapata Uhuru, Serikali mkoani Kagera ilikuwa inamiliki hospitali moja tu (ambayo ni hospitali ya mkoa kwa sasa). Hospitali hii ilijengwa mwaka1923 ikiwa kama kituo cha afya cha kambi ya jeshi. Baadaye ilipanuliwa na kuwa hospitali ya eneo la Buhaya katika Jimbo la Ziwa (mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara na Shinyanga). Baada tu ya Uhuru

Page 24: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

24

hospitali hii ilitangazwa rasmi kuwa hospitali ya mkoa wa Ziwa Magharibi kama mkoa ulivyokuwa ukiitwa wakati huo.

Kiasi kikubwa cha huduma za tiba zilipatikana kwenye hospitali za mashirika ya dini kama vile Hospitali za Kagondo (iliyofunguliwa mwaka 1912) na Hospitali ya Ndolage (ya mwaka 1929), zote wilayani Muleba. Pia kulikuwa na Hospitali za Murgwanza (ya mwaka 1953) na Rulenge (ya mwaka 1954) wilayani Ngara.

Wakati wa Uhuru kulikuwa na kituo kimoja tu cha afya kimoja, cha Kaigara na zahanati chache tu.

2.3.2.2. Upanuzi wa Huduma za Afya baada ya Uhuru

Mara baada ya Uhuru, serikali katika kupigana na adui maradhi ilitoa kipaumbele katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanati. Katika miaka 50 ya uhuru serikali imejenga hospitali mbili, za Chato ambayo ilifunguliwa mwaka 2004 na Nyamiaga ambayo ilifunguliwa mwaka 2009. Pia imejenga, vituo vya Afya 25 na zahanati 186. Vituo vya Afya vilivyojengwa na serikali katika miaka 50 ya Uhuru ni kama ifuatavyo:-

Na. Jina la Halmashauri

Jina la Kituo Mwaka wa kujengwa Kituo

1 Manispaa ya Bukoba

Zamzam 1979

Rwamishenye 1987

2 Bukoba DC Katoro 1972

Kanazi 2008

Kishanje 2008

Rubale 2008

3 Missenyi Bunazi 1970

4 Muleba Kaigara 1958

Kimeya 1976

Kamachumu 2004

Izigo 2004

Page 25: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

25

Nshamba 2011

5 Karagwe Murongo 1972

Nkwenda 1974

Kayanga 2002

6

Ngara Mabawe 1974

Bukiriro 1974

Murusagamba 2002

Rukole 2010

7 Biharamulo Nyakahura 2002

Rukaragata 2008

Nyabusozi 2008

8 Chato Bwanga 2005

Kachwamba 2010

Butarama 2010

Hivi sasa baada ya miaka hamsini, serikali mkoani Kagera inamiliki hospitali 3, vituo vya afya 25 na zahanati 207. Aidha Hospitali ya mkoa ina sura mpya na majengo ya kupendeza ilikingamishwa na majengo yaliyokuwepo wakati wa Uhuru baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ambao ulikamilika mwaka 2002. Pia majengo mengine mengi ya enzi ya ukoloni yalibomolewa na kujengwa mapya.

2.3.2.3. Mchango wa wadau katika Hudumza za Afya

Katika kipindi hiki cha miaka hamsini wadau wengine hasa mashirika ya dini wamekuwa na mchango mkubwa katika upanuzi wa huduma za afya. Mashirika ya dini mkoani Kagera yaliongeza au kupanua hospitali na vituo vya afya. Mathalan, Hospitali za Mugana na Nyakahanga zilifunguliwa mwaka 1962. Hospitali nyingine ni pamoja na Rubya, mwaka 1963, Biharamulo, mwaka 1969, Isingiro, mwaka 1984, Nyakaiga, mwaka 1996 na Izimbya, mwaka 2008. Baadhi ya hospitali hizo kwa sasa ni hospitali

Page 26: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

26

kuu za wilaya kutokana na makubaliano kati ya serikali na mashirika hayo ya dini.

Mashirika ya dini pia yalianzisha vyuo vya mafunzo ya watumishi wa sekta ya afya. Kuna vyuo vya wauguzi katika hospitali za Rubya, Ndolange, Murgwanza na Mugana. Hospitali ya Biharamulo ina chuo cha wateknolojia wasaidizi wa maabara. Vyuo hivyo vimechangia sana na vinaendelea kuelimisha watumishi wa afya, hususan wauguzi, ambao wanahudumia wananchi ndani na nje ya mkoa.

Kutokana na ushirikiano baina ya serikali na wadau wengine, wananchi wa mkoa huu hivi sasa wanapata huduma za afya kupitia vituo vya kutolea huduma 289 ambavyo ni:-

Hospitali 15 (03 za serikali); Vituo vya Afya 30 (25 vya serikali); na Zahanati 244 (207 za serikali)

2.3.3. Huduma za Maji

2.3.3.1. Huduma za Maji wakati wa Uhuru

Tangu mwaka 1961 sehemu kubwa ya huduma ya maji katika mkoa wa Kagera ilikuwa ikitolewa bure na serikali kupitia idara ya Maji. Serikali, kupitia Mhandisi wa Maji wa Mkoa (RWE), ilikuwa ikigharamia shughuli zote za matengenezo, uendeshaji na ukarabati wa miundombinu ya maji. Kufikia mwaka 1969 kulikuwa na miradi ya bomba (msukumo na bubujiko) 17 iliyokuwa ikifanya kazi na kuongezeka kufikia miradi ya bomba (msukumo na bubujiko) 30 mwaka 1980. Miradi zaidi yenye tekinolojia ya bomba 30 (ya msukumo na bubujiko) ilijengwa na kufanya jumla miradi 77 mwaka 1995. Aidha, visima vifupi (shallow wells) 384 pia vilikuwa vimechimbwa na hivyo kufanya idadi ya wakazi wa Mkoa wa Kagera waliokuwa wanapata maji safi na salama kufikia mwaka 1995 kuwa asilimia 20. Tangu Uhuru Huduma za jamii zikiwemo maji, Afya na Elimu zilikuwa zikitolewa bure na serikali. Serikali kuu ilikuwa na jukumu la kuibua, kupanga, kutekeleza na kuendesha miradi ya maji katika maeneo ya mijini na vijijini.

Page 27: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

27

Mwaka 1988 Sera ikabadilika kwa kurudisha baadhi ya majukumu ya uendeshaji na matengenezo wa miradi ya maji kwa wananchi. Hata hivyo badiliko hayo hayakuleta matunda kwani miradi mingi iliendelea kuharibika na kuhujumiwa na wananchi wenyewe ndipo mwaka 1991 ilipoundwa sera mpya. Katika sera hii wananchi walipewa jukumu la kupanga, kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maji na kupewa baadhi ya shughuli za uendeshaji na matengenezo wa miradi hiyo kupitia kwenye Halmashauri za Wilaya. Mwaka 2002 baada ya kuona sera ya mwaka 1991 kutozaa matunda yaliyokusudiwa serikali iliamua kupitia upya na kubadili sera ya maji. Sera ya mwaka 2002 ilihamishia shughuli zote kwa wananchi zikiwemo za kuibua, kupanga, kuchangia baadhi ya fedha za utekelezaji, kuendesha miradi yao ikiwa ni pamoja na kufanya matengeneo kupitia kamati za maji. Sera pia inasisitiza kuundwa kwa vyombo huru vya watumiaji maji na kuanzisha mifuko ya maji kwa ajili uendeshaji na matengenezo, kushirikisha sekta binafsi katika kutekeleza na kuendesha miradi ya maji. Sera hii ndiyo bado inatumika hadi sasa. Mwaka 1997 ilitungwa sheria ya kuanzisha Mamlaka za maji safi na maji taka mijini ikiwa la lengo la kuziruhusu mamlaka hizi zijiendeshe kibiashara badala ya kutegemea kila kitu kutoka serikali kuu, pia kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji na uondoaji wa maji taka mijini. 2.3.3.2. Hali ya sasa ya Upatikanaji wa Maji

Kiwango cha upatikananji wa huduma ya maji vijijini hivi sasa ni asilimia 55.3, kiwango katika maeneo ya makao makuu ya wilaya ni asilimia 65.8 na kiwango katika Manispaa ya Bukoba ni asilimia 76.5. Upatikanaji huo wa maji unatokana na vyanzo vifuatavyo:-

Miradi ya maji ya bomba (msukumo na bubujiko) 127 Visima vifupi 1,291 Visima virefu 281 Vyanzo vya maji vilivyoboreshwa 842 Matanki ya uvunaji wa maji ya mvua 777 Malambo/mabwawa 35

Page 28: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

28

2.4. Uhifadhi wa Maliasili na Utunzaji wa Mazingira

2.4.1. Misitu

Kuanzia Uhuru hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980, misitu katika mkoa wa Kagera ilikuwa haijaharibiwa kwa kiwango kikubwa. Miti mingi ya asili, matingatinga na mapori ya asili yaliufanya mkoa kupata mvua nyingi sana kwa mwaka. Hadi kufikia mwaka 1993 mkoa wa Kagera ulikuwa na eneo la misitu lililohifadhiwa kisheria kiasi cha kilomita za mraba 3,539 sawa na asilimia 12% ya eneo la nchi kavu. Sehemu kubwa ya misitu ipo katika wilaya za Biharamulo, Bukoba na Muleba.

Katika kuendelea kuhifadhi maliasili na uoto katika mkoa juhudi za kupanda miti zimekuwa zikiendelea katika wilaya zote. Hadi kufikia mwaka 2010 mkoa umepanda jumla ya miti 32,913,765 kati ya lengo la kupanda miti 33,000,000. Kutokana na juhudi hizi mkoa wa Kagera, kupitia wilaya ya Chato na kata ya Kigongo katika wilaya ya Chato, ulishinda tuzo ya kombe, cheti na fedha taslimu shilingi 9,000,000 katika mashindano ya uhifadhi wa mazingira kitaifa kwa mwaka 2009/10. Biharamulo 134,000 Ha, Minziro 25,000Ha, Ruiga 98,337Ha, Nyantakara 26,000Ha,

2.4.2. Ufugaji Nyuki

Ufugaji nyuki wakati tunapata UHURU na hadi miaka ya mwishoni mwa 1970, umekuwa ukiendeshwa kwa kutumia mbinu za kiasili. Wafugaji walitengeneza mizinga ya asili na kuifunga porini ambapo nyuki walitengeneza asali. Shughuli za uvunaji asali zilifanywa katika mazingira magumu kutokana na uhaba na uduni wa vitendea kazi. Moshi wa nyasi ulitumika kufukuza nyuki kabla ya kulina asali.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980 mkoa ulianzisha mizinga ya kisasa ya kuvuga nyuki. Kufikia mwaka 1988 mkoa ulikuwa na jumla ya mizinga ya nyuki 3,078 kati ya maliasili hiyo 226 ilikuwa chini ya uangalizi wa idara ya maliasili na 2,852 ilimilikiwa na vikundi vya ufugaji nyuki. Aidha, kati ya mizinga 226 ya idara 186 ilikuwa ya asili na 40 ilikuwa ya kisasa. Matumizi ya mizinga ya kisasa katika mkoa yameongezeka kutoka mizinga 151,860 mwaka 2005/6 hadi mizinga 212,250 mwaka 2010.

Page 29: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

29

2.4.3. Utalii

Katika utalii jitihada zimekuwapo tangu Uhuru za kuutangaza mkoa huu kiutalii hasa katika utalii wenye kuhusisha utamaduni, mazingira, makumbusho (historia). Ingawaje mafanikio ya shughuli za utalii katika mkoa wa Kagera si makubwa sana, mkoa unaendelea na juhudi za kutangaza fursa za kitalii zilizoko mkoani kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa utalii kama Kiroyera Tours Company, Walkguard na wengineo. Kisiwa cha musila, nyumba ya asili (msonge) iliyopo Kamachumu yenye zaidi ya miaka mia moja, maporomoko ya Rusumo yako kwenye mpaka kati ya Rwanda na Tanzania, Ziwa Viktoria kwa sababu ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani, chemchem ya maji moto (Karagwe) pori la Burigi, msitu wa Minziro. 2.4.4. Hifadhi ya Mazingira

Mkoa wa Kagera unaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kitaifa yenye lengo la kuhimiza hifadhi ya mazingira na kuibua shughuli endelevu za kiuchumu ili kuwapatia wananchi kipato na lishe. Program mbalimbali zinendeshwa na mkoa katika usimamizi wa mazingira kama vile Kampeni ya upandaji miti kimkoa na kiwilaya, mkakati wa kuhifadhi ardhi na vyanzo vya maji, miradi ya usimamizi shirikishi wa misitu na kuendesha operesheni na doria za mara kwa katika misitu ya hifadhi na mapori ya akiba.

2.5. Maendeleo ya Kijamii

2.5.1. Asasi Zisizo za Kiserikali (NGOs)

Wakati nchi inapata uhuru Mkoa wa Kagera haukuwa na asasi zisizo za Serikali ila kulikuwa na vikundi vya kijamii ambavyo vilijishughulisha na kusaidiana wakati wa matukio mbalimbali kama misiba, harusi na sherehe. Asasi zisizo za Serikali kwenye Mkoa wa Kagera zilienea kuanzia miaka ya themanini baada ya mabadiliko ya kijamii hasa janga la UKIMWI kuathiri sana mkoa wa Kagera. Asasi ziliendelea kuongezeka katika miaka ya tisini baada ya ujio wa wakimbizi kutoka nchi za Rwanda na Burundi. Mkoa una asasi zisizo za Serikali 125 zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI, mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, zinazotoa huduma kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira

Page 30: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

30

hatarishi,wajane, wazee,watu wenye ulemavu na asasi zinazojishughulisha na mazingira. Asasi za Kidini Wakati tunapata UHURU mwaka 1961, mkoa ulikuwa na taasisi mbalimbali za kidini za Kanisa katoliki, Kanisa la Anglikana, Kanisa la AICT, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Kanisa la Waadventista Wasabato na dini ya Kiislamu.

Kanisa lililojengwa na Wakatoliki mwaka 1910, Bunena, Manispaa ya Bukoba, ambalo linaendelea kutoa huduma za kiroho kwa kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru

Katika miaka ya 1980 na 1990 madhehebu mengine ya kidini yalianzishwa mkoani. Mashirika haya ya dini yamekuwa na mchango mkubwa sana katika kutoa huduma za kiroho na kijamii. Katika kipindi cha kuanzia Uhuru hadi sasa taasisi hizi za dini/binafsi zimejenga shule 35, vituo vya afya vitano (5), hospitali kumi na mbili (12), zahanati ishirini na saba (27) na vyuo vinne (4) mkoani Kagera.

Page 31: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

31

SURA YA TATU

3. MATUKIO NA MABADILIKO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA HAMSINI (1961- 2011)

3.1. Mabadilko ya Muundo wa Mkoa

3.1.1. Mabadiliko katika muundo wa Serikali Kuu

Wakati nchi inapata UHURU mwaka 1961, muundo wa utawala kimkoa ulikuwa ni ule wa Majimbo. Utawala wa kijimbo (Provinces) ulidumu kwa miaka minne zaidi baada ya Uhuru ambapo mwaka 1965 mkoa wa Ziwa Magharibi (West Lake) ulianzishwa. Mkoa wa Ziwa Magharibi ulikuwa na wilaya nne (4) tu za kiutawala. Wilaya hizo ni Ngara, ambayo ilianzishwa tangu mwaka 1947, Biharamulo, Bukoba, na Karagwe (ambayo ilizinduliwa rasmi na Gavana wa Kiingereza, Sir Richard Turnbul, mwaka 1958). Mnamo mwaka 1975 wilaya mpya ya Muleba ilianzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Bukoba. Mkuu wa Wilaya wa kwanza alikuwa Bw. Joseph Kasubi (Orodha ya Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huu tangu Uhuru hadi sasa ni kama inavyoonekana katika Kiambatanisho 4 - 10). Wilaya nyingine mpya za Chato na Missenyi zilianzishwa mwaka 2007. Wilaya ya Chato ilianzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Biharamulo na wilaya mpya ya Missenyi ilianzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Bukoba. Mabadiliko haya yakaufanya mkoa wa Kagera kuwa na wilaya saba zilizopo hivi sasa. Kiutendaji, baada ya mabadiliko makubwa ya mwaka 1972 ya kufutwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuanzishwa kwa mfumo wa Madaraka Mikoani, mabadiliko mengine ni ya kuanzishwa Sekretarieti za Mikoa mwaka 1997. Sekretarieti ya Mkoa ilianzishwa kwa Sheria Na. 19 ya mwaka 1997 ambapo Mkuu wa Mkoa (Regional Commissioner) aliendelea kuwa kiongozi mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za serikali katika Mkoa. Cheo cha Katibu Tawala Mkoa (Regional Administrative Secretary) kilianzishwa kuchukua nafasi ya Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (Regional Development Director).

3.1.2. Mabadiliko katika muundo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

Kuanzia mwaka 1961-1972 mkoa ulisimamia shughuli za kiutawala na maendeleo katika wilaya kwa kutumia mamlaka za serikali za mitaa. Katika

Page 32: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

32

kipindi hiki kulikuwa na malalamiko ya wananchi ya kutoridhika na huduma mbalimbali zilizotolewa katika maeneo yao ya vijiji na miji. Kutokana na hali hiyo serikali ilivunja mfumo wa Serikali za Mitaa mwaka 1972. Utawala wa Madaraka Mikoani (Centralization) ukaanzishwa na kufanya madaraka yote yabaki mikononi mwa serikali kuu na hivyo katika kipindi hiki hapakuwa na Serikali za Mitaa. Idara zote na vitengo vilivyohusika na maendeleo ya vijiji na miji vilikuwa chini ya Kurugenzi za Mkoa na za Wilaya.

Hata hivyo mfumo huo wa “Madaraka Mikoani” (1972 – 1984) haukuleta ufanisi uliotarajiwa. Udhaifu mkubwa wa mfumo huu ulikuwa ni uamuzi kufanyika ngazi za juu (Mkoa na Wilaya) na utendaji na utekelezaji kufanyika ngazi za chini (vijiji). Udhaifu mwingine ulikuwa ni maamuzi kuhusu maendeleo katika ngazi za chini kufanywa na watumishi wa serikali kuu na sio wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa njia ya demokrasia.

Mwaka 1978 Serikali ilirejesha mamlaka za umma kwa kuanzia na mamlaka za miji baada ya kubaini kuwa huduma za mijini ziliendelea kuharibika. Mwaka 1982 Bunge lilitunga sheria mbalimbali za kuanzishwa upya kwa Serikali za Mitaa nchini, ambazo zilianza kutekelezwa mwaka 1984. uanzishwaji wa mamlaka za serikali za mitaa ulienda sambamba na kuanzishwa kwa taasisi nyingine zilizohusika na Serikali za Mitaa ambazo ni Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa (TUMITAA), Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB), Mfuko wa Akiba wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT).

Wakati mamlaka za serikali za mitaa zinaanzishwa tena mwaka 1984, Mkoa wa Kagera ulikuwa na halmashauri tano za wilaya: Bukoba, Biharamulo, Karagwe, Muleba na Ngara.

Halmashauri ya Mji wa Bukoba ilipewa hadhi ya kuwa Manispaa mwezi Julai mwaka 2005. Mwaka 2006 Halmashauri za Missenyi na Chato zilianzishwa. Kwa sasa mkoa una jumla ya Halmashauri za wilaya saba (7) na Manispaa moja.

3.2. Ukuaji wa Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 1967 mkoa ulikuwa na watu 658,712, mwaka 1978 watu 1,009,379, mwaka 1988 mkoa ulikuwa na watu 1,326,183 na mwaka 2002 watu 2,033,888. Ongezeko la idadi ya watu lilikuwa kwa wastani wa asilimia 2.7. Aidha, mwaka 2011 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 mkoa unakadiriwa kuwa na idadi ya watu 2,746,058.

Page 33: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

33

Jedwali Na. 1: Idadi ya watu 1967 – 2011

NA WILAYA/ HALMASHAURI

MWAKA

1967 1978 1988 2002 Maoteo 2011

1. Bukoba (V) 374,988 296,462 343,956 395,130 325,808

2. Bukoba (M) 8,141 36,914 47,009 81,221 153,016

3. Biharamulo 81,854 165,580 209,524 410,794 252,218

4. Chato - - - - 383,162

5. Muleba - 217,493 274,447 386,328 492,404

6. Missenyi - - - - 174,889

7. Ngara 96,322 107,917 158,658 334,939 422,044

8. Karagwe 97,407 185,013 292,589 425,476 542,517

JUMLA 658,712 1,009,379 1,326,183 2,033,888 2,746,058

3.3. Matukio makuu 1961 – 2011

Katika kipindi cha miaka hamsini tangu tupate uhuru yapo matukio mengi ya kihistoria ambayo yametokea katika mkoa wa Kagera. Mtiririko wa matukio hayo ni kama yanavyoainishwa hapa chini.

Mwaka 1961

Uhuru wa Tanganyika: tarehe 09 Desemba 1961 Mkoa wa Kagera uliungana na mikoa mingine kusherehekea kupatikana kwa Uhuru. Sherehe hizo zilifanyika katika Uwanja wa Uhuru uliopo katika Manispaa ya Bukoba. Uwanja huo ulipewa jina hilo la Uhuru kwa kuwa ndio uliotumika kufanyia mikutano ya kisiasa katika harakati za kudai Uhuru. Maadhimisho makubwa yalifanyika kitaifa mkoani Dar es Salaam na mkoa uliwakilishwa na watu wanne ambao ni Ndugu Samweli Luangisa (Assistant Province Commissioner), Mzee Ziadi alikuwa Mwenyekiti wa TANU, ndugu Abdulsued Kahasheki aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba na Ndugu Masabala aliwakilisha umoja wa vijana wa TANU.

Mwaka 1962

Mafuriko: Mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kutokea sehemu kubwa ya Mkoa, ambapo wananchi waliipa jina la “Mvua ya Uhuru” kwa sababu mvua kubwa ya masika ilinyesha baada ya Tanganyika kupata Uhuru.

Page 34: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

34

Mwaka 1963

TANICA Yaanzishwa: Kampuni ya Kukoboa Kahawa ya TANICA ilianzishwa. Kampuni hii imechangia kukua kwa pato la mwananchi wa mkoa wa Kagera. Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa kampuni hii imetoa ajira nyingi sana kwa wakazi wa mkoa wa Kagera.

Kufutwa kwa Tawala za Kichifu (Kitemi): Tawala za kichifu za Ntare, Nyarubanja, Ruhinda na Rumanyika zilifutwa kutoka na serikali kufuta mfumo huo wa utawala kote nchini.

Mwaka 1965

Kuanzishwa kwa Mkoa wa Kagera: Mkoa wa Ziwa Magharibi ambao sasa ni “Kagera” ulianzishwa.

Uchaguzi Mkuu: Uchaguzi Mkuu ulifanyika ambapo ulihusisha watemi na Wakama. Watemi na Wakama waliotawala kuanzia mwaka 1965-1970 katika Mkoa wa Kagera ni wafuatao:

Bakampenja - alitawala sehemu ya Ihangiro;

Kaneno - aliongoza sehemu ya Karagwe;

Kasusura – aliongoza sehemu ya Biharamulo;

Kasano - aliongoza sehemu ya Kiziba na Missenyi;

J. Kibogoyo – aliongoza sehemu ya Kiyanja; na

Kami – aliongoza sehemu ya Bugabo na Kyamutwara. Orodha ya Wabunge tangu Uhuru ipo kuanzia Kiambatanisho Na 11

Mwaka 1966

Ukame: Ukame mkubwa uliodumu hadi mwaka 1970 watokea na kusababisha njaa kali katika wilaya ya Karagwe. Hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu kupoteza maisha, kupungua kwa nguvukazi, baadhi ya familia kukosa matunzo kwa ukaribu baada ya wanaume kwenda maeneo ya mbali kutafuta chakula.

Mwaka 1970

Uchaguzi Mkuu: Uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge ulifanyika katika majimbo matano ya Uchaguzi ya Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Muleba na Ngara. Waliochaguliwa kuwakilisha majimbo

Page 35: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

35

hayo ni Ndugu Kasusura (Biharamulo), Ndugu Ishungisa (Karagwe), Ndugu Zimbihire (Muleba) na Ndugu Niboye (Ngara). Kwa Wilaya ya Bukoba ambayo ilikuwa kubwa na ilikuwa ikiendeleza utawala wa watemi na wakama, iliwakilishwa na wawakilishi watatu kwa kupigiwa kura na wananchi wa Wilaya hiyo. Waliowakilisha wilaya hiyo walikuwa Ndugu Kibogoyo, Ndugu Kasano na Ndugu Rutagwerela.

Mwaka 1975

Kuanzishwa kwa Wilaya ya Muleba: Wilaya ya Muleba ilianzishwa kwa kuunganisha Tarafa ya Ihangiro, Kimwani na baadhi ya kata za Tarafa ya Kihanja.

Mwaka 1976

Kuanzishwa kwa kijiji cha Kyamnyorwa katika wilaya ya Muleba kutokana na operesheni ya vijiji. Katika kijiji cha Kyamyorwa kulikua na ardhi yenye rutuba, na huduma nyingine muhimu kama maji. karibu na huduma stahili ambapo waliishi kwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja

Mwaka 1977

Kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi: sherehe za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi zilifanyika mkaoni kwenye uwanja wa uhuru.

Mwaka 1978

Vita kati ya Tanzania na Uganda: Mwezi Oktoba 1978 kulitokea vita kati ya nchi ya Tanzania na nchi ya Uganda. Vita hii ilijulikana kwa jina maarufu la “vita ya Kagera” iliitwa jina hilo kutokana kwamba ilipiganiwa katika ardhi ya Tanzania mkoani Kagera.

Page 36: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

36

Mnara wa kumbukumbu ya mahali ambapo mabomu yaliyokuwa katika gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania yalilipuka katika eneo la Mutukula,

Wilaya ya Misenyi, na kuua wanajeshi wote waliokuwamo garini wakielekea kwenye uwanja wa mapambano

Vita hii ilisababishwa na kitendo cha Majeshi ya Uganda, chini ya Nduli Idd Amin Dada, kuvamia ardhi ya Tanzania katika eneo la Missenyi na kudai kuwa eneo lote lililo kaskazini mwa Mto Kagera ni ardhi ya nchi ya Uganda. Vita hivyo vilimalizika mwezi April, 1979 kwa Majeshi ya Tanzania kushinda vita na kumuondoa madarakani Nduli Idd Amin.

Mabaki ya Kanisa la Kyaka ambalo lilibomolewa na Majeshi ya Idd Amin wakati wa vita. Kwa sasa hii ni sehemu ya utalii katika Mkoa wa Kagera

Vita hivi vya Kagera vilikuwa na athari kubwa kwa mkoa wa Kagera. Athari hizo ni pamoja na vifo, wananchi kunyang’anywa mali zao na uharibifu wa miundombinu ya majengo na barabara.

Page 37: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

37

Mwaka 1979

Mkoa wa Ziwa Magharibi wabadilishwa Jina: Baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda Mkoa wa Ziwa Magharibi (West Lake) ulibadilishwa jina na kuitwa Kagera.

Uwanja wa Uhuru wabadilishwa Jina: Uwanja wa Uhuru uliopo mjini Bukoba ambao ulitumika mwaka 1961 kusherehekea Uhuru ulibadilishwa jina na kuitwa “Uwanja wa Jenerali Mayunga” kwa kumbukumbu ya vita ya Kagera na heshima ya shujaa na kiongozi wa vita hivyo.

Sanamu ya Marehemu Jenerali Silas P. Mayunga kwenye Uwanja wa Uhuru (ambao sasa unaitwa Uwanja wa Jenerali Mayunga)

Mwaka 1983

Operesheni Uhujumu Uchumi: Kutokana na kukosekana kwa bidhaa muhimu katika jamii na kupungua kwa uwianao wa kipato kati ya walio nacho na wasio nacho serikali iliendesha operesheni dhidi ya wahujumu uchumi nchi nzima. Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitupa bidhaa zao kwenye Ziwa Victoria na mto Ngono ili kuhofia kukamatwa na Serikali.

Page 38: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

38

Kugunduliwa kwa Mgonjwa wa UKIMWI: Ugonjwa ambao unadhoofisha kinga za mwili za kujikinga na maradhi ambao baadae ulikuja kujulikana zaidi kama UKIMWI (Ukosefu wa Kinga Mwilini) uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mkoani Kagera. Mgojwa wa kwanza aligundulika kuwa na virusi vya UKIMWI alitoka katika Kijijini cha Kanyigo Wilaya ya Missenyi. Ugonjwa huu uligunduliwa katika hospitali ya Ndolage iliyoko wilaya ya Muleba na inayo milikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Hospitali hii ilikuwa ya kwanza kutoa huduma ya kupima UKIMWI kwenye mkoa wa Kagera ambapo baada ya mtu wa kwanza kuugua ugonjwa huo alipelekwa kupimwa kwenye hospitali hiyo.

Mwanzoni wananchi wa Mkoa wa Kagera waliuita ugonjwa huo “Juliana” au “Slim”. Uliitwa Juliana kwa sababu iliaminika kuwa ugonjwa huo uliingizwa nchini na vijana waliokuwa wakitokea Uganda wakiwa wamevaa mashati ya Juliana. Pia uliitwa ‘slim’ kwa sababu waathirika wa ugonjwa huo walikuwa wanakonda hadi kufa. Ugonjwa huu baadae ulienea Tanzania nzima na kuleta athari kubwa katika jamii. Mkoa wa Kagera ulikuwa wa kwanza kuathirika. Ugonjwa huu uliwakumba zaidi vijana, wanajamii ambao wanaotegemewa sana katika uzalishaji mali. Vijana wengi wakaangamia kwa UKIMWI na kufanya familia nyingi kubaki na wazee wakibeba mzigo wa kutunza watoto yatima. Pia muda mwingi wa kuzalisha mali ulipotea katika kuhudhuria mazishi na matanga ya ndugu na jamaa, kuuguza wagonjwa na kutunza yatima. Ugonjwa wa UKIMWI bado upo mpaka sasa katika mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla ambapo kiwango cha maambukizi mkoani Kagera ni asilimia 3.4.

Mwaka 1985

Uchaguzi Mkuu: Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, na Tanzania ilipata Rais wa awamu ya pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.

Mwaka 1990

KDCU na KCU Vyaanzishwa: Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe na Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera (KCU) vyaanishwa.

Page 39: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

39

Mwaka 1992

Mfumo wa Vyama Vingi: Mfumo wa vyama vingi vya siasa waanzishwa nchini na kuingia mkoani Kagera kwa kufunguliwa matawi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), United Democratic Party (UDP), NCCR-Mageuzi, United Movement for Democracy (UMD) na Tanzania Labour Party (TLP).

Mwaka 1994

Kuingia kwa Wakimbizi wa Rwanda na Burundi: Kutokana na mapigano ya kikabila nchini Burundi na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, inakadiriwa kuwa Wanyarandwa na Warundi laki sita (600,000) waliingia mkoani Kagera wakikimbia mapigano hayo. Ujio wa wakimbizi ulisababisha madhara makubwa kwa mkoa wa Kagera yakiwemo uharibifu wa mazingira na kushamili kwa uhalifu mwingiliano wa utamaduni, kuzaliana Hadi kufikia Juni, 2011 wakimbizi wote walikuwa wamerudi katika nchi zao.

Mwaka 1995

Mvua kubwa: Mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko na uharibifu wa mazao na miundombinu. Mafuriko yaliathiri sana Wilaya yote ya Bukoba na Missenyi. Madaraja yalisombwa na maji hivyo kuathiri watumiaji na baadhi ya nyumba za watu ziliharibiwa.

Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Vyama Vingi: Kutokana na

kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 uchaguzi mkuu ulifanyika ukihusisha vyma vingi. Vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo mkoani Kagera ni Chama cha Mapinduzi (CCM), United Democratic Party (UDP), NCCR-Mageuzi, United Movement for Democracy (UMD) na Tanzania Labour Party (TLP).

Mwaka 1996

Kuzama kwa MV Bukoba: MV Bukoba ikiwa safirini kutoka Bukoba kwenda Mwanza, ilizama katika Ziwa Victoria kilomita nane kabla ya kufika bandari ya Mwanza. Inakadiriwa kuwa watu mia nane (800), wengi wao walikuwa wakazi wa mkoa wa Kagera, walipoteza maisha huku mali yenye thamani ya mamilioni ya shilingi ilipotea. Sababu za

Page 40: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

40

kuzama kwa meli hiyo kulisababishwa na ujazaji wa abiria na miziko kupita uwezo wake.

MV Bukoba ikiwa inazama katika Ziwa Victoria

Mwaka 1997

Mradi wa KAEMP waanzishwa: Katika kukabiliana na athari za wakimbizi, mkoani Kagera mradi mkubwa wa Kilimo na Usimamizi wa Mazingira, uliojukana zaidi kwa jina la KAEMP (Kagera Agricultural and Environmental Management Program) ulianzishwa. Programu hii ilileta mapinduzi makubwa katika maendeleo ya kilimo, mazingira, afya, maji na barabara.

Mvua za El – Nino: Mvua kubwa za El Nino zilinyesha na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu ya wakazi wa Kagera

Mwaka 2000

Uchaguzi Mkuu: Uchaguzi mkuu wa pili katika mfumo wa vyama vingi wafanyika huku kukiwa na ongezeko la majimbo ya uchaguzi. Majimbo hayo mapya yalitokana na kugawanywa kwa Jimbo la Muleba na kuwa na majimbo ya Muleba Kaskazini na Muleba Kusini na kugawanywa ka Jimbo la Biharamulo na majimbo ya Biharamulo Mashariki na Biharamulo Magharibi. Jimbo la Bukoba pia liligawanywa na kuwa na majimbo ya Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini na

Page 41: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

41

Nkenge. Jimbo la Karagwe nalo liligawanywa na kuwa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.

Mwaka 2002

Benki ya Wakulima (KFCB) Yaanzishwa: Benki ya wakulima ambayo inamilikiwa na kusimamiwa na vyama vya ushirika vya msingi, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa, mfuko wa mazao na chama kikuu cha ushirika KCU ilianzishwa. Makao makuu ya benki hii yapo Manispaa ya Bukoba

Mwaka 2004

Kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru: Mwenge wa Uhuru wawashwa kwenye uwanja wa Kaitaba na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Ali Mohamed Shein. Mwenge ulikimbizwa katika Wilaya zote za mkoa wa Kagera na baadaye kukabidhiwa Mkoa wa Kigoma.

Mwaka 2006

Kuanzishwa kwa Wilaya ya Chato: Wilaya ya Chato yaanzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Biharamulo. Eneo la wilaya mpya ya Chato ni eneo lote la liliokuwa Jimbo la Uchaguzi la Biharamulo Mashariki likiwa na Tarafa 3, Kata 14 na Vijiji 74. Bw. Said Mkumbo ndiye alikuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya hiyo.

Kuanzishwa kwa Wilaya ya Missenyi: Wilaya ya Missenyi yaanzishwa kwa kuigawa Wilaya ya Bukoba. Wilaya ya Missenyi ina ukubwa wa hekta 270,875, na inaundwa na tarafa 2, kata 20, vijiji 74 na vitongoji 350. Ina jimbo moja la uchaguzi liitwalo Nkenge, madiwani 20 wa kuchaguliwa na 8 viti maalum. Bw. Elias Maarugu ndiye alikuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya hiyo.

Mwaka 2008

Kagera Day: Kagera Day Fund rising” kwa ajili kuchangia maendeleo ya elimu mkoani Kagera. Mfuko huu uliweza kufadhili ujenzi wa vyumba vya madarasa. Shule ya sekondari za Ijuganyondo imejengewa madarasa 3, shule ya sekondari ya Bugene iliyopo wilayani Karagwe imejengewa madarasa 3.

Page 42: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

42

Shule sita kutoka halmashauri za Muleba (Kagondo), Ngara (Shyunga), Biharamulo (Rubondo), Chato (Makurugusi), Bukoba Vijijini (Izimbya) na Missenyi (Bunazi) zimepata ufadhili wa kujengewa maabara.

Mfuko wa Kagera Day umeweza kupata wafadhili ambao wameleta kompyuta 51 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari.

Mfuko umeweza kutoa mabati 600 ambayo yamegawiwa kwa halmashauri zote kwa uwiano wa mabati 75 kwa kila moja.

Mwaka 2009

Mafuriko Chato: Mvua kubwa yanyesha wilayani Chato na kusababisha mafuriko makubwa yaliyoharibu mazao mashambani na miundombinu mbalimbali.

Page 43: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

43

SURA YA NNE

4. CHANGAMOTO NA MATARAJIO YA MIAKA HAMSINI IJAYO

4.1. Changamoto katika miaka hamsini ya Uhuru

Katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita Mkoa wa Kagera umepitia mabadiliko mengi kama ilivyoelezwa katika sura zilizotangulia. Mkoa unajivuna kwa kuweza, kwa kiasi kikubwa, kufanikiwa kutekeleza majukumu yake makuu katika kufikia malengo ya mkoa na ya kitaifa na hatimaye kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa huu.

Hata hivyo kumekuwa na changamoto nyingi ambazo mkoa ulikabiliana nazo katika kipindi hiki cha miaka hamsini iliyopita.

(a) Changamoto za kiutawala

Katika kipindi cha miaka hamsini ya Uhuru mkoa umekuwa na changamoto nyingi za kiutawala na kisiasa. Baadhi ya changamoto hizo ni:-

(i) Changamoto kwenye mpaka na nchi jirani: Ingawa hali ya mipaka yetu ni shwari, kuna changamoto mbalimbali zinazotokana na hali ya mpaka wetu na nchi jirani za Burundi, Rwanda na Uganda. Changamoto hizo ni pamoja na:-

Uhamiaji haramu ambapo wananchi kutoka nchi jirani huingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria za Uhamiaji. Kutokana na uhamiaji haramu mkoa umekuwa ukikabiliwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu, kuenea kwa magonjwa ya binadamu (kama vile Surua, T.B nk) kunasababishwa na wahamiaji hao kutopata chanjo katika nchi wanazotoka, uvunaji holela wa miti katika misitu ya hifadhi ya Minziro, Burigi na Biharamulo,

Wizi wa mifugo unaoshamiri kutokana na upande wa nchi jirani hasa Uganda kuwa na minada mingi bubu karibu na mpaka. Mifugo mingi toka Tanzania kuibiwa na kuuzwa nchini Uganda. Wimbi la wizi wa mifugo ni tishio na tatizo kubwa kwa maendeleo ya wananchi husasan wafugaji na wawekezaji wa vitalu vya huria za Taifa na mashamba ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO); na

Biashara ya magendo ya kahawa, nafaka na maharage kwenda nchi jirani kwa kutumia nija za panya au vivuko visivyo rasmi;

Page 44: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

44

(b) Changamoto za kiuchumi

(i) Kilimo duni: Kilimo, shughuli ambayo inategemewa na wananchi wengi (zaidi ya asilimia 80) katika kuendesha maisha yao, kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi. Chngamoto hizo nipamoja na utegemezi wa mvua, uzalishaji wenye tija ndogo kutoka na utumiaji wa zana hafifu ya zana, kutotumika kwa pembejeo za kutosha, magonjwa hatari ya mazao kama vile unyanjano wa migomba (Banana bacterial wilt BBW), kahawia kakamavu ya matunda ya ndizi (Banana Fruits Fungal disease), Mnyauko Fuzari wa Kahawa (Coffee Wilt disease) Batobato kali ya Muhogo (Cassava Masaic disease). Pia kilimo kimekuwa kikikabiliwa na kuyumba mara kwa mara kwa bei ya mazao ya biashara katika masomo ya kimataifa;

(ii) Changamoto zinazohusiana na Mifugo kama vile magonjwa ya milipuko husasan Black quarter, Foot and Mouth disease (Ugonjwa wa Miguu na Midomo), CBPP (Homa ya Mapafu); ongezeko la mifugo kutoka nchi jirani wanaofuata hali nzuri ya malisho na maji ya kutosha kwa mifugo, uharibifu wa mazingira na migogoro baina ya wakulima na wafugaji;

(iii) Uvuvi haramu katika Ziwa Victoria unaohusisha utumiaji wa sumu, zana haramu kama makokoro na nyavu zisizoruhusiwa. Sehemu kubwa ya eneo la Tanzania katika Ziwa Victoria kama vile Bugabo, Malehe na Igabilo katika wilaya ya Missenyi, huvamiwa mara kwa mara na wavuvi haramu kutoka Uganda ambao pia huwanyang’anya wananchi mitumbwi, injini na nyavu;

(iv) Uharibifu wa Mazingira na maliasili: Katika mapori ya akiba, lipo tatizo kubwa la uwindaji haramu, uchomaji mkaa, ukataji wa mbao pamoja na uchungaji wa mifugo unaofanywa na wananchi na watu kutoka nchi jirani.

(v) Bei za bidhaa: Kutokana na mkoa kuwapo pembezoni mwa nchi na umbali uliopo toka bandari kuu ya Dar es Salaam, mkoa unakabiliwa na ongezeko la mara kwa mara la bei za bidhaa mbalimbali zikiwemo za ujenzi na mafuta ya magarina mitambo. Ongezeko la bidhaa hizi siyo tu limemwathiri mwananchiwa kawaida bali pia hata miradi ya maendeleo iliyokuwa inatarajiwa kutekelezwa;

(vi) Ukosefu wa mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara na miradi ya uzalishaji. Hii inatokana na kutokuwa na dhamana mbalimbali zinazohitajika na taasisi za kifedha kama masharti ya uombaji mikopo;

Page 45: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

45

(vii) Vyama Vikuu vya Ushirika (Unions) kushindwa kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa mazao kutokana na uwepo wa biashara ya magendo ya kahawa katika maeneo ya mpakani. Pia vyama hivyo vinakabiliwa na ukosefu wa mitaji, ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, wizi na ubadhilifu wa mali za vyama vya ushirika na viongozi wasio waadilifu.

(c) Changamoto za Kijamii

(i) Ongezeko la idadi ya watu ambalo husababisha ongezeko la mahitaji ya huduma za kijamii kama vile afya, elimu na maji. Ongezeko la watu pia huongeza kasi ya uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchomaji wa misitu ya asili, ukataji miti ovyo na uchungaji haramu wa mifugo hasa ng’ombe katika misitu na mapori ya akiba;

(ii) Uhaba au upungufu wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kama vile vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, madawati na hata matundu ya vyoo. Kwa mfano hivi sasa kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 1,582 sawa na asilimia 60 ya mahitaji’

(iii) Ugonjwa wa UKIMWI umeendelea kupunguza/kuathiri upatikanaji wa nguvukazi na kusababisha vifo;

(iv) Upungufu wa watumishi katika Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za wilaya unaotokana na mazingira ya mkoa kuwa pembezoni ambayo hayavutii watumishi kuja kufanya kazi;

4.2. Jinsi Mkoa unavyokabiliana na Changamoto

Pamoja na kuwapo kwa changamoto hizo, mkoa umethubutu, na kwa kiasi kikubwa umeweza kukabiliana na changamoto hizo na unazidi kusonga mbele. Hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kwa ushirikiano wa viongozi na wananchi kama ifuatavyo:-

(a) Kukabiliana na changamoto za kiutawala

(i) Kuwa na mikutano ya ujirani mwema na mkoa na wilaya za mpakani. Kupitia mikutano hii ya ujirani mwema mambo mbalimbali hujadiliwa na maazimio kadhaa yanayohusu udhibiti wa uhamiaji haramu, uharibifu wa mazingira na uingizaji haramu wa mifugo hufikiwa na kutekelezwa;

(ii) Kutoa elimu kwa wananchi juu ya dhana ya ulinzi shirikishi na Polisi jamii pamoja na kuhimiza vijiji na vitongoji kutunza rejista za wakaaji ili kubaini wageni wanaoingia na kutoka;

Page 46: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

46

(b) Kukabiliana na changamoto za kiuchumi

(i) Kuhamasisha wananchi kupitia vikao na mikutano mbalimbali kuchangia katika maendeleo yao;

(ii) Kuendeleza na kupanua kilimo cha umwagiliaji kwa kuongeza eneo lenye miundo mbinu ya umwagiliaji;

(iii) Kuendelea kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa na huduma za ugani kwa wakulima na wafugaji;

(iv) Kuongeza kiwango cha matumizi ya zana za kisasa kama vile matrekta, power tiller na wanyamakzai;

(v) Kupambana na magonjwa na mifuko hadi kuufanya Mkoa wa Kagera kuwa huru kwa magonjwa ya mifugo (Disease Free Zone);

(vi) Kuendelea kupambana na uvuvi haramu mkoani kwa kushirikia na jamii pamoja na vikundi ya ulinzi wa maeneo ya mialo (Beach Management Unit-BMUs); na

(vii) Kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika kulinda na kutunza mazingira yao pamoja na kuwafichua wale ambao wanafanya matendo yanayosababisha uharibifu wa mazingira;

(c) Kukabiliana na changamoto za kijamii

(i) Utoaji wa huduma za uzazi wa mpango sambamba na kampeni za kujenga uelewa wa jamii juu ya athari za ongezeko la idadi ya watu.

(ii) Kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo na ununuzi wa samani ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza Mpango wa Elimu kwa Shule za Msingi (MMEM) na Mpango wa Elimu kwa Shule za Sekondari (MMES).

(iii) Kuimarisha huduma ya afya kwa wagonjwa wa UKIMWI pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI na kuhamasisha wananchi kupima afya zao.

(iv) Katika kukabiliana upungufu wa watumishi mkoa umekuwa ukitumia motisha mbalimbali kama vile ujenzi wa nyumba za watumishi, mikopo ya vifaa vya ujenzi na usafiri, zawadi kwa wafanyakazi bora, malipo kwa muda wa kazi wa ziada, ulipaji wa mishahara kwa wakati na hata utoaji wa misaada kwa watumishi wakati wa matatizo.

Page 47: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

47

4.3. Matarajio ya miaka 50 ijayo

Katika miaka hamsini iliyopita Mkoa umepata mafanikio makubwa pamoja na kuwapo kwa changamoto mbalimbali kama zilivyoainishwa katika sura zilizotangulia. Kiujumla, matarajio ya Mkoa katika miaka hamsini ijayo ni pamoja na kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kiutawala na usimamizi wa shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikisha matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Katika miaka hamsini ijayo mkoa unatarajia yafuatayo:- (a) Mkoa kuendelea kuwa na Amani na Utulivu: Uongozi mkoani Kagera, kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine, utaendelea kudumisha amani na utulivu mkubwa pamoja na kuishi vyema na mikoa ya nchi jirani. Ili kufikia lengo hili mkoa:-

(i) Utadumisha utawala wa kisheria kwa njia mbalimbali ikiwemo kuelimisha wananchi juu ya dhana ya ulinzi shirikishi na Polisi jamii;

(ii) Utaendelea kuimarisha ujirani mwema na nchi za jirani ili kuweza kudhibiti vitendo vya wahamiaji haramu.Pia mkoa utaendelea kuweka mazingira ya kuvutia watumishi kuja kufanya kazi mkoani.Majengo na ofisi za Serikali yataendelea kujengwa na kuboreshwa iliyawe katika hadhi inayostahili;

(iii) Utaendelea kushirikiana na taasisi za ulinzi kama vile Jeshi la Kujenga Taifa ili kuimarisha ulinzi wa mpaka kwa kulitengea eneo (Blocks) katika katika ranchi ya Missenyi. Uwepo wao mpakani utasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu mpakani; na

(iv) Utaendelea kuhimiza vijiji na vitongoji kutunza rejista za wakaaji ili kubaini wageni wanaoingia na kutoka.

(b) Uchumi wa mkoa kuwa imara na wenye ushindani Katika kuongeza pato la wananchi wa mkoa wa Kagera, na hatimaye kuwa na maisha bora na mazuri mkoa utaendelea kusimamia mamlaka za serikali za mitaa na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo taasisi zisizo za kiserikali, madhehebu ya dini na watu binafsi, katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo inayolenga kuboresha hali ya maisha ya wananchi. Mipango hiyo ni pamoja na:-

(i) Ukuzaji wa kilimo kwa kuimarisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, mbegu bora za mazao, ufugaji wa ng’ombe kwa njia za kisasa, ufugaji wa samaki na ufugaji wa nyuki;

(ii) Kuimarisha miundombinu kama vile kuongeza urefu wa mtandao wa barabara za lami kutoka km. 563 za sasa km. 2,035, kujenga

Page 48: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

48

kiwanja cha ndege cha kimataifa kwa ajili ya usafirisahji nje wa mazao ya kilimo na uvuvi, kuongeza ukubwa wa bandari ya Bukoba;

(iii) Kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji wa ndani na nje katika Ziwa Victoria, viwanda, madini, usafirishaji na utalii wa ndani na nje na kuufanya mkoa upande kutoka nafasi ya 13 kitaifa ukiwa na asilimia 12 kuwa hadi kuwa miongoni mwa mikoa sita bora kwa kuwa na wastani wa asilimia 42; na

(iv) Kuimarisha ushirika ili kuwaongezea wananchi nguvu ya uwekezaji na ushindani wa kibiashara.

(c) Wananchi kuwa na maisha bora na mazuri: Katika kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa wa Kagera, mamlaka za serikali za mitaa zitaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii chini ya uangalizi na ushauri wa Sekretarieti ya Mkoa kwa:-

(i) Kuimarisha huduma ya afya kwa kujenga hospitali ya rufaa, kuboresha hospitali ya mkoa iliyopo, kujenga hospitali za wilaya za serikali, kuongeza vituo vya afya kila kata na zahanati katika kila mtaa/kijiji. Mkoa utaendelea kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 108/100,000 mwaka 2010 hadi 20/100,000 ifikapo mwaka 2061. Mkoa utaendelea kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 254/100,000 hadi 97/100,000 ifikapo mwaka 2061. Kuongeza kiwango cha chanjo DPT-HB3 toka 88.8% hadi 98% na chanjo ya surua toka 89.9% hadi 98% kufikia 2061. Kuongeza kiwango cha wajawazito wanaojifungulia vituoni toka 53% hadi 85% mwishoni mwa 2061. Mkoa utaendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI kwa wananchi ili kiwango cha maambukizi kipungue kutoka 3.4% hadi kufikia 0.01% mwaka 2061. Lengo ni kuhakikisha ugonjwa huu unakuwa historia katika mkoa wa Kagera; na

(ii) Kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama na kutunza vyanzo vya maji kwa kuzuia shughuli zote za binadamu karibu na vyanzo hivyo;

(d) Mkoa kuwa na Jamii iliyoelimika vema Hadi kufikia mwaka 2061 mkoa unalenga kuboresha kiwango cha elimu kwa kuimarisha maeneo yafuatayo; mafunzo kwa walimu, vifaa vya kufundishia, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara katika kila shule ya sekondari, nyumba za walimu, ujenzi wa vyuo mbalimbali vya ualimu na elimu ya juu

Page 49: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

49

(e) Kuendelea kuimarisha utawala bora (i) kupambana na rushwa; na (ii) kuziba mianya ya ukwepaji wa kulipa kodi.

(f) Mkoa kujitosheleza kwa watumishi wa umma Ili kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita mkoa unahitaji kuwa na watumishi wa kutosha na wenye ujuzi unaohitajika. Mkoa utaendelea kujenga mazingira mazuri ya utendaji na kuongeza juhudi katika kuvutia na kuwabakiza (attract and retain) watumishi kwa kuwa na mpango maalum wa utoaji motisha kwa watumishi (incentive scheme). Aidha katika kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu, juhudi zitaelekezwa katika kujenga utumishi katika mkoa wenye kuzingatia:- (i) Maadili ya utumishi wa umma (ikiwemo heshima, utu, uaminifu, utiifu,

na uadilifu kwa umma); (ii) Maslahi ya umma; na (iii) Dhana ya uwajibikaji na usikivu kwa umma na wenye kujali wateja.

4.4. Hitimisho

Uongozi wa Mkoa unatoa shukrani za pekee kwa wananchi wote na wadau wote wa maendeleo wa mkoa wa Kagera kwa ushirikiano waliotoa katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika Mkoa wa kagera. Kutokana na ushirikiano huo, mkoa katika miaka hamsini ya Uhuru, umeweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Katika kipindi cha miaka hamsini ijayo mkoa uyahitaji kupata ushirikiano zaidi kutoka kwa kila mdau ili uweze kufanikiwa zaidi. Kwa upande wake uongozi wa mkoa utaendelea kujenga uwezo wa jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuzingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA II), mipango ya maendeleo ya miaka mitano na Dira ya Taifa ya mwaka 2025.

MIAKA HAMSINI YA UHURU MKOANI KAGERA, TUMETHUBUTU,

TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!

Page 50: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

50

Kiambatanisho 1: Wakuu wa Mkoa wa Kagera tangu Uhuru Wakuu wa Mkoa wa Kagera tangu mwaka 1961 ni hawa wafuatao:- 1. Bw. Samuel N. Luangisa (1961 – 1964), 2. Bw. Oswald Marwa (1964 – 1966), 3. Bw. P. C. Walwa (1966 – 1967), 4. Bw. S. S. Semshanga (1967 – 1970), 5. Bw. L. N Sijaona (1970 – 1972), 6. Maj. Gen. Twalipo (1972 – 1974), 7. Brig. M. M Marwa (1974 – 1975), 8. Col.T. A Simba (1975 – 1977), 9. Bw. Mohamed Kisoki (1977 – 1978), 10. Capt. Peter Kafanabo (1978 – 1981), 11. LT.Col. Nsa Kaisi (1981 – 1987), 12. Bw. Horace Kolimba (1987 – 1989), 13. Bw. Paul Kimiti (1989 – 1991), 14. Capt. A. M Kiwanuka (1991 – 1993), 15. Bw. Philip J. Mangula (1993 – 1996), 16. Bw. Mohamed A. Babu (1996 – 1999), 17. Gen. T. N. Kiwelu (1999 – 2006), 18. Col. E. Mfuru (2006 – 2009), 19. Bw. Mohamed A. Babu (2009 - 2011), 20. Col Fabian I. Massawe (2011 hadi sasa

Page 51: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

51

Kiambatanisho 2: Makatibu Tawala wa Mkoa tangu Uhuru Makatibu Tawala wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera tangu mwaka 1961 ni hawa wafuatao:- 1. Bw. Khatibu 2. Bw. P. V. Tesha 3. Bw. J. A. Mwambungu 4. Bw. Urassa Tengea 5. Bw. Msambichaka (1972 – 1975) 6. Bw. E. J. Malamia (1975 – 1978) 7. Bw. Edward Oluoch (1978 – 1983) 8. Bw. Godwin M. Mugendi (1983 - 1985) 9. Bw. C. T. Kisanji (1985 – 1986) 10. Bw. S. Kanyasi Masinde (1986 – 1993) 11. Bw. M.O. Nicolao (1993 – 1995) 12. Bw. Matiko T. Nyitambe (1995 – 1997) 13. Bw. Rajabu B. Kiravu (1997 – 1999) 14. Bw. Hussein H. Seif (2001 – 2006) 15. Bw. Peter B Barie (2006 – 2007) 16. Bibi Maria Bilia (2007 – 2010) 17. Bw. Nassor Mnambila (2010 hadi sasa

Page 52: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

52

Kiambatanisho 3: Wakuu wa Wilaya wa Wilaya za Mkoa wa Kagera tangu Uhuru

Wilaya ya Biharamulo 1. Bw. Talawa (1961 – 1962), 2. Bw. Mushote (1962 – 1962) 3. Bw. S. R. Kasusura (1962 – 1964) 4. Bw. Philipo Mbogo (1965 – 1966) 5. Bw. D. Semuguruka (1967 – 1970) 6. Bw. Gustav M. Bundara (1971 – 1972) 7. Bw. T. A. K. Musonge (1973 – 1976) 8. Bw. J. B. R. Mhagama (1977 – 1977) 9. Bw. Jacob K Mujule (1977 – 1979) 10. Cpt. J. R. Barongo (1979 – 1983) 11. Lt Col. Peter madaha (1983 – 1988) 12. Col. L. Makunenge (1988 – 1990) 13. Bw. F Saria (1990 – 1994) 14. Bw. S. Siwale (1994 – 1996) 15. Cpt S. A. Mpembenwe (1996 – 2000) 16. Bw. Moses Sanga (2000 – 2003) 17. Lt Col. S. M. Mrengo (2003 – 2006) 18. Bw. Ernest N. Kahindi (2006 hadi sasa Wilaya ya Bukoba 1. Bw.John Tayari (1987 – 1990), 2. Bibi Rhoda Kahatano (1990 – 1993) 3. Bw. William Lukuvi (1993 – 1995) 4. Bw. Chemo Mtani (1995 – 1997) 5. Bw. Michael Mlowe (1997 – 1998) 6. Bw. Moses Chang’a (1998 – 2000) 7. Bw. John Tupa (2000 – 2004) 8. Bw. Abeid Mwinyimusa (2004 – 2008) 9. Bibi Amina Mrisho Said (2008 – 2008) 10. Bw. Albert Mnari (2008 – 2009) 11. Bw. Samwel J. Kamote (2009 hadi sasa) NB Orodha ya Wakuu wa Wilaya kuanzia Uhuru hadi mwaka 1987 haikupatikana

Page 53: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

53

Wilaya ya Chato (Ilianzishwa mwaka 2006) 1. Bw. Said Mkumbo (2006 – 2009), 2. Mwl Hadija Nyembo (2009 hadi sasa Wilaya ya Karagwe 1. Bw. Peter N. Kafanabo (1961 – 1965), 2. Bw. Enos Ryangaro (1965 – 1969) 3. Bw. Losa Liyemba (1969 – 1973) 4. Bw. Thomas Msonge (1973 – 1977) 5. Bw. Ruhasi (1977 – 1978) 6. Bw. F. X. Itala (1978 – 1980) 7. Bw. Rafael Chayeka (1980 – 1984) 8. Bw. Mohamed Chamsala (1984 – 1989) 9. Bw. Luhozya E. Siwale (1989 – 1994) 10. Capt Joseph E. Nditi (1994 – 1997) 11. Bw. Gerald J. Ghachoch (1997 – 1999) 12. Bw. Peter Kangwa (1999 – 2000) 13. Bw. Saning’o Ole Telele (2000 – 2004) 14. Bw. David J. Daud (2004 – 2006) 15. Bw. Frank Uhahula (2006 – 2009) 16. Col (mst) Fabian I Massawe (2009 hadi sasa

Wilaya ya Missenyi (Ilianzishwa mwaka 2006) 1. Bw. Elias Maarugu (2006 – 2009), 2. Col. Issa Njiku (2009 hadi sasa Wilaya ya Muleba (Ilianzishwa mwaka 1975) 1. Bw. Joseph Kasubi (1975 – 1977), 2. Bw. Said Ng’wanang’walu (1977 – 1979) 3. Bw. Jasper Mbonde (1979 – 1983) 4. Bw. Joseph Nditi (1983 – 1988) 5. Bw. Abdon Achileka (1988 – 1990) 6. Bw. Musobi Mageni (1990 – 1991) 7. Bibi Jalia Katetemela (1991 – 1998) 8. Alhaj Ahmed Lugusha (1998 – 2003) 9. Bw. John G. Tupa (2003 – 2006) 10. Bw. Desdedit Mtambalike (2006 – 2009) 11. Bw. Fabian Massawe (8/4/2009) 12. Bibi Angelina Mabula (2009 hadi sasa

Page 54: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

54

Wilaya ya Ngara 1. Bw.Edwin Aran K. Nyamubi (1962 – 1963), 2. Bw. Ibrahim Bakampenja (1963 – 1965) 3. Bw. Mbuta M. Mirando (1965 – 1967) 4. Bw. Waziri Tuma Waziri (1967 – 1969) 5. Bw. Ibrahim Kajembo (1969 – 1972) 6. Bw. Pius Mikongoti (1972 – 1973 7. Bw. Losa Kamba Yemba (1973 – 1975) 8. Bw. Enock Lyangalo (1975 – 1976) 9. Bw. Paul Ghamela (1976 – 1979) 10. Bw. Faustine Katoyo ( 1979 – 1983) 11. Bw. Hohn Peter Tayari (1983 – 1987) 12. Bw. Anthony T. Nderumaki (1987 – 1990) 13. Lt. Evans Balama (1990 – 1992) 14. Bw. John Mwakisyomba (1992 – 1994) 15. Brig. Gen Sylivester Hemed (1994 – 1996) 16. Lt. Evans Balama ( 1996 – 1999) 17. Bw. Deusdedith Mtambalike (1999 – 2001) 18. Col. Samwel A. Ndomba (2001 – 2006) 19. Col (mst) S. W. Nyakonji (2006 hadi sasa

Page 55: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

55

Kiambatanisho 4: Wabunge wa Majimbo ya Uchaguzi na wa Viti Maalum, 1965 – 1970

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Kiziba & Misenyi Mhe. Kasano TANU

Bukoba Bugabo & Kyamutwara Mhe. Kami TANU

Karagwe Karagwe Mhe. Kaneno TANU

Muleba Ihangiro Mhe.Bakampenja TANU

Muleba Kiyanja Mhe. J. Kibogoyo TANU

Biharamulo Biharamulo Mhe. Kasusura TANU

1990 – 1995

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Mhe. CCM

Biharamulo Biharamulo Mhe. Fares Kabuye CCM

Karagwe Mhe. CCM

Muleba Mhe. CCM

Ngara Mhe. Gerald Ghachocha CCM

1995 – 2000

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Bukoba Mjini Mhe. Mujuni Kataraia CCM

Bukoba vijijini Mhe. Sebastian Kinyondo CCM

Biharamulo Biharamulo Magharibi Mhe. John Pombe Magufuli CCM

Biharamulo Mashariki Mh. Antony K. Kashazi CCM

Karagwe Karagwe Mhe. Sir. George Kahama CCM

Kyerwa Mhe. Eustace katagira CCM

Muleba Muleba Kusini Mhe. Wilson masilingi CCM

Muleba Kaskazini Mhe. Ndimara Tegambwage CCM

Missenyi Nkenge Mhe. Joseph Rwegasira CCM

Ngara Ngara Mhe. Pius Ngeze CCM

Viti maalum Mhe. Elizabeth Batenga CCM

2005

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Bukoba Mjini Mhe. Wilfred Rwakatare CUF

Bukoba Vijijini Mhe. Nazir Karamagi CCM

Biharamulo Biharamulo Magharibi Mhe. John Pombe Magufuli CCM

Biharamulo Mashariki Mh. Anatory Choya CCM

Page 56: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

56

Karagwe Karagwe Mhe. Gosbert Blandes CCM

Kyerwa Mhe. Eustace katagira CCM

Muleba Muleba Kusini Mhe. Wilson Masilingi CCM

Muleba kaskazini Mhe. Ruth Msafiri CCM

Missenyi Nkenge Mhe. Deodarus Kamala CCM

Ngara Ngara Mhe. Angasi Sebabili CCM

Viti Maalum Mhe. Elizabeth Batenga CCM

Viti Maalum Mhe. Savelina mwijage CUF

2005 – 2010

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Bukoba Mjini Mhe. Hamis Sued Kagasheki CCM

Bukoba Vijijini Mhe. Nazir karamagi CCM

Biharamulo Biharamulo Magharibi Mhe. John Pombe Magufuli CCM

Biharamulo Mashariki Mh. Fares Kabuye

Oscar Mukasa

TLP

CCM

Karagwe Karagwe Mhe. Gosbert Blandes CCM

Kagera Kyerwa Mhe. Eustace Katagira CCM

Muleba Muleba kusini Mhe. Wilson Masilingi CCM

Muleba Muleba Kaskazini Mhe. Luth Msafiri CCM

Missenyi Nkenge Mhe.Deodorus Kamala CCM

Ngara Ngara Mhe. Prof. Banyikwa CCM

Viti Maalum Mhe. Bernadetha Mushashu CCM

Viti Maalum Mhe. Elizabeth Batenga CCM

Viti Maalum Mhe. Savelina Mwijage CUF

2010 – 2015

Wilaya Jimbo Mbunge Chama Bukoba Bukoba Mjini Mhe. Hamis Sued Kagasheki CCM

Bukoba Vijijini Mhe. Jason Samson Rweikiza CCM

Biharamulo Biharamulo Magharibi Mhe. Dk Antony Mbasa CHADEMA

Chato Chato Mhe. John Pombe Magufuli CCM

Karagwe Karagwe Mhe. Gosbert Blandes CCM

Kyerwa Mhe. Eustace Katagira CCM

Missenyi Nkenge Mhe.Asumpta Nshunju Mushama CCM

Muleba Muleba Kaskazini Mhe. Anna Tibaijuka CCM

Muleba Kusini Mhe. Charles Mwijage CCM

Ngara Ngara Mhe. Deogratius Ntukamazina CCM

Viti Maalum Mhe. Bernadetha Mushashu CCM

Mhe. Elizabeth Batenga CCM

Mhe. Conjester Rwamulaza CHADEMA

Page 57: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

57

Kiambatanisho 5: Tarafa na Kata mkoani Kagera

HALMASHAURI TARAFA MAJINA YA KATA

Manispaa ya Bukoba

Rwamishenye Bukoba, Ijuganyondo, Rwamishenye, Bilele, Nshambya, Buhembe, Kahororo, Kitendaguro, Kibeta, Nyanga, Hamugembe, Miembeni, Kagondo, Kashai.

Biharamulo Biharamulo, Nyakahura

Biharamulo Mjini, Bisibo, Ruziba, Nyamahanga, Nyarubungo, Lusahunga, Nyakahura, Nyantakara, Kahina, Kalenge, Nemba, Nyabusuzi, Kabindi, Runazi, Nyamigogo

Bukoba Bugabo, Kyamutwara, Katerero, Rubale

Kanyangereko, Maruku, Karabagaine, Katoma, Nyakato, Buhendangabo, Kaagya, Kishanje, Rubafu, Kyamulaile, Katoro, Kaibanja, Kasharu, Nyakibimbili, Mikoni, Katerero, Bujugo, Kishogo, Kemondo, Ibwera, Butelankuzi, Rubale, Rukoma, Kikomelo, Izimbya, Butulage, Kibirizi, Ruhunga, Mugajwale.

Chato Buseresere, Bwanga, Kachwamba, Nyamirembe

Chato, Bwina, Muungano, Ilemela, Bukome, Katende, Ilyamchele, Muganza, Bwongera, Kachwamba, Kasenga, Ichwankima, Kigongo, Nyamirembe, Buseresere, Bwanga, Nyarutembo, Buziku, Iparamasa, Makurugusi, Butengo Rumasa.

Page 58: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

58

Karagwe Bugene Nyaishozi, Kintuntu Mabira, Nyabiyonza, Kaisho murongo

Kayanga, Bugene, Ndama, Rugela, Kihanga, Nyakahanga, Nyaishozi, Ihembe, Rugu, Nyakasimbi, Nyakakika, Nyakabanga, Kibondo, Bweranyange, Nyabiyonza, Kiruruma, Rwabwere, Nkwenda, Songambele, Rukulaijo, Kyerwa, Isingiro, Kaisho, Rutunguru, Kibingo, Murongo, Bugomora, Kibale, Kamuli, Kimuli, Kikukuru, Mabira, Businde, Igurwa, Kanoni, Kituntu, Chanika, Ihanda, Chonyonyo, Nyakatuntu.

Missenyi

Kiziba, Missenyi

Kashenye, Kanyigo, Bwanjai, Bugandika, Ishozi, Ishunju, Gera, Buyango, Kitobo, Bugolora, Mushasha, Kyaka, Kilimilile, Kassambya, Minziro, Mabale, Nsunga, Mutukula, Kakunyu, Ruzinga

Muleba Nshamba, Izigo, Kamachumu, Muleba, Kimwani

Muleba Mjini, Rushwa, Nyakatanga, Ngenge, Rutoro, Izigo, Katoke, Muhutwe, Mayondwe, Bumbire, Kagoma, Kikuku, Goziba, Kerebe, Kamachumu, Bulyakashaju, Ruhanga, Mafumbo, Ibuga, Burungura, Kibanga, Ikondo, Buhangaza, Magatalarutanga, Gwanseli, Bureza, Mazinga, Ikuza, Nshamba, Kishanda, Biirabo, Ijumbi, Buganguzi, Kashasha, Kabirizi, Kimwani,

Page 59: SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa … SURA YA KWANZA 1. UTANGULIZI 1.1. Mkoa wa Kagera: Mahali Ulipo Mkoa wa Kagera upo kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania, kati ya latitudi

59

Nyakabango, Karambi, Kasharunga, Rulanda, Mubunda, Bisheke, Kyebitembe

Ngara Nyamiaga, Kanazi, Murusagamba, Rulenge

Ngara Mjini, Nyamiaga, Mulukutazo, Ntobeye, Kirushya, Mabawe, Mugoma, Kabanga, Kanazi, Kidimba, Rusumo, Kasulo,Nyakisasa, Rulenge, Keza, Mbuba, Bukiriro,Bugarama,Muganza, Murusagamba