T4 - Ushindi Book

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    1/16

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    2/16

    Ushahidi

    Kimeandaliwa na:

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

    © LHRC

    Septemba, 2013

    ii

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    3/16

    iiiUshahidi

    Yaliyomo

    SHUKURANI..........................................................v

    UTAMBULISHO WA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU....................................v

    MAONO...................................................................v

    TAMKO LA LENGO MAHUSUSI.........................vLENGO KUU..........................................................vi

    DIBAJI...................................................................vii

    1.0 UTANGULIZI.............................................. 1

    2.0 TAFSIRI/MAANA YA USHAHIDI............. 12.1 Aina za Ushahidi............................. 12.1.1 Ushahidi wa Matamshi.................... 12.1.2 Ushahidi wa Maandishi................... 22.1.3 Ushahidi wa Uhalisi......................... 22.1.4 Ushahidi wa Kimazingira................ 3

    3.0 KUTHIBITISHA TUHUMA,MASHITAKA, SHAURI AUUSHAHIDI MAHAKAMANI.....................3

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    4/16

    iv Ushahidi

    4.0 KUKANUSHA TUHUMA, MASHITAKA, SHAURI AU USHAHIDI

    MAHAKAMANI......................................... 3

    5.0 AINA ZA MASHAHIDI.............................. 45.1 Shahidi ni Nani?................................... 45.2 Nani Anaweza kuwa Shahidi?.............. 4

    5.3 Mume na Mke....................................... 55.4 Shahidi wa utaalamu maalum au fani... 55.5 Mtu mwenye Matatizo ya Akili

    (Mwenye Mtindio wa Ubongo)............ 6

    6.0 KUHOJI NA KUULIZA MASWALIMASHAHIDI............................................... 66.1 Upande wa Mashitaka au Mlalamikaji. 66.2 Upande wa Utetezi au Mdaiwa............. 76.3 Mahakama............................................. 7

    7.0 KUPOKELEWA NA KUKUBALIWAKWA USHAHIDI MAHAKAMANI........... 7

    8.0 HITIMISHO................................................. 8

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    5/16

    vUshahidi

    SHUKURANI

    T unatoa shukurani kwa wanasheria wetu nawale wa kujitolea katika uandaaji wa vijaridahivi. Pia tunawashukuru kwa dhati wale wotewalioshiriki kwenye kukirejea kijitabu hiki ilikuandaa toleo hili la tatu hususan Wakili HaroldSungusia, Wakili Fulgence Massawe, WakiliJeremiah Mtobesya, Bw. Rodrick Maro na Bw.Evans Sichalwe, pamoja na wafanyakazi wote waKituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    6/16

    vi Ushahidi

    UTAMBULISHO WA KITUO CHA SHERIANA HAKI ZA BINADAMU

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamuni shirika binafsi la kujitolea na la hiariambalo si la kisiasa wala kibiashara. Kituokimeandikishwa na kusajiliwa kwa mujibu washeria za Tanzania mnamo Septemba, 1995.

    Kabla ya kusajiliwa kama chombo huru, Kituocha Sheria na Haki za Binadamu kilikuwani mradi wa haki za binadamu wa Mfukowa Kuendeleza Elimu ya Sheria Tanzania(TANLET). Makao makuu ya Kituo ni Dar esSalaam na Arusha kuna o si ndogo.

    MAONO

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatamani jamii yenye haki na usawa.

    TAMKO LA LENGO MAHUSUSI

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nishirika lisilo la kiserikali wala kibiasharalinalojibidisha kukuza uwezo wa jamii iliiweze kukuza, kuendeleza na kulinda haki za

    binadamu na utawala bora nchini Tanzania.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    7/16

    viiUshahidi

    LENGO KUU

    Lengo kuu la Kituo cha Sheria na Haki zaBinadamu ni kukuza uelewa wa sheria nahaki za binadamu kwa jamii kwa ujumlana hasa wale wanajamii ambao kwa sababumoja au nyingine wameachwa nyuma. Uelewautakuzwa kwa njia ya elimu ya uraia na msaada

    wa sheria.

    DIBAJI

    K ituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaazma ya kusaidia jamii ya watanzania kuwana uwezo wa kufahamu sheria za nchi pamojana kufahamu haki zao ili kuzilinda na kuzitetea

    pamoja na kuheshimu haki za wengine ilihatimaye tuwe na jamii yenye utamaduni wakuheshimu haki za binadamu pamoja na nchiinayoheshimu utawala wa sheria.

    Tunafahamu kuwa kwa raia wa kawaida si rahisikuzifahamu sheria zetu zote, na hata baadhi tuya sheria zinazomgusa kutokana na mfumo tulionao, ambao hautoi nafasi kwa watu wote kujua

    sheria. Hali hii inasababisha watu wengi kujikuta

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    8/16

    viii Ushahidi

    katika matatizo ya kisheria ambayo yangewezakuepukika kama angejua sheria. Ndio maana

    basi Kituo kimeamua kutoa machapisho haya namengine, kwa lengo la kutoa msaada wa kisheriakwa raia.

    Huu ni usaidizi kisheria unaotoa maelezo mafupina ya msingi ya kisheria ili kukusaidia ndugu

    msomaji uweze kupata ufumbuzi au maelekezo yatatizo linalokusibu. Ni lengo letu kuwa, katikavijitabu hivi tunatoa usaidizi wa moja kwamoja kwako wewe pale utakapokuwa na tatizoau mmoja wa ndugu au jamaa zako wanapopatamatatizo ya namna hii.

    Tunachokuomba ni wewe kusoma kwa makini;na pale suala lako linapokwenda mbali zaidi yamaelezo haya, basi utafute msaada wa kisheriaau uende kwa mwanasheria aliye karibu na weweili aweze kukusaidia. Tunaamini utapata usaidizihuu kiurahisi zaidi na maelezo yaliyomo humuyatakusaidia kwa karibu. Umalizapo, tafadhaliumsaidie na mwenzako kupata usaidizi huu.

    Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    9/16

    1Ushahidi

    1.0 UTANGULIZI

    Masuala yanayohusu ushahidi nchiniyanasimamiwa na Sheria ya Ushahidi, Sura

    ya 6 ya Sheria za Tanzania, ya mwaka 1967. Sheriahii inaweka masharti ya jumla ya sheria ya ushahidinchini Tanzania japo sheria nyingine zinaweza piakuweka vipengele maalum kuhusiana na mazingirana mahitaji maalum ya sheria husika.

    2.0 TAFSIRI/MAANA YA USHAHIDIUshahidi ni njia ambayo hutumika kuthibitisha aukukanusha masuala au tuhuma iliyopo au jambolinalobishaniwa.

    2.1 Aina za Ushahidi

    Kuna aina kuu nne za ushahidi nazo ni:-1. Ushahidi wa matamshi;2. Ushahidi wa maandishi;3. Ushahidi wa uhalisia; na4. Ushahidi wa kimazingira.

    2.1.1 Ushahidi wa MatamshiHuu ni ushahidi usio wa maandishi ambao unatolewamoja kwa moja kwa mdomo wa shahidi. Misingi yakukubalika ushahidi huu ni kama ifuatavyo:-(a) Iwapo unahusisha suala la kuona, ushahidi

    huo unatolewa na shahidi aliyeshuhudia kuona

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    10/16

    2 Ushahidi

    kitendo hicho;(b) Iwapo unahusisha kusikia, ni lazima utolewe na

    shahidi aliyesikia;(c) Iwapo unahusisha hisia nyinginezo tofauti na

    kusikia pamoja na kuona ni lazima ushahidi huoutolewe na shahidi aliyepata hisia hizo mfano,kuguswa, kuonja au kunusa.

    2.1.2 Ushahidi wa Maandishi

    Ushahidi wa maandishi ni ushahidi wowoteunaotolewa kwa maandishi mahakamani. Ushahidihuu unaweza kuwa katika nyaraka, picha, alamayoyote, kanda ya video au radio au katika haliyoyote, ambayo ni imara, ya kudumu na kusomekaau kutambulika.

    Ushahidi wa maandishi unatakiwa uwe katika haliya asilia isipokuwa pale sheria inaporuhusu unawezakutolewa kwa nakala.

    2.1.3 Ushahidi wa UhalisiUshahidi wa uhalisia, ni ushahidi ule ambaounatolewa kwa kuonyesha kitu, mfano kisukilichotumika kuulia, au mikanda ya video, au picha,au kutembelea eneo la tukio mfano pale panapotokeamgogoro wa shamba.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    11/16

    3Ushahidi

    2.1.4 Ushahidi wa KimazingiraUshahidi wa kimazingira, ni ushahidi unaopatikana

    baada ya kuunganisha matukio sehemu tukiolilipotokea na maelezo yanayotoa tafsiri ya mazingiramaalum yanayothibitisha jambo au tukio.

    3.0 KUTHIBITISHA TUHUMA, MASHITAKA,SHAURI AU USHAHIDI MAHAKAMANI

    Mtu yeyote ambaye anashitaki, amefungua shauri,anaiomba au kuitaka mahakama itoe uamuzi auhukumu katika mashitaka au shauri kwa manufaayake analazimika kuwasilisha mahakamani ushahidiunaojenga hoja kuthibitisha madai au tuhumaanazozitoa dhidi ya mtuhumiwa, mshitakiwa au

    mdaiwa. Kiwango cha uthibitishaji wa tuhuma, daiau hoja katika kesi ya jinai ni kutoacha shaka yoyote,na katika kesi ya daawa ni ukweli kwa kiwangokikubwa au cha kusadikika.

    4.0 KUKANUSHA TUHUMA, MASHITAKA,SHAURI AU USHAHIDI MAHAKAMANI

    Niwajibu wa mtu yeyote ambaye anatuhumiwa,anashitakiwa au ushahidi umetolewa dhidi yakekatika shauri kujitetea, kukanusha tuhuma, shitakaau ushahidi uliotolewa dhidi yake kwani asipofanyahivyo mahakama inaweza kutoa uamuzi dhidi yake.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    12/16

    4 Ushahidi

    5.0 AINA ZA MASHAHIDI

    5.1 Shahidi ni Nani?

    Shahidi ni mtu yeyote ambaye anatoa maelezokuthibitisha tuhuma, shitaka au tukio fulani mbele yaMahakama.

    5.2 Nani Anaweza kuwa Shahidi?Kutokana na sheria ya ushahidi ya mwaka 1967,watu wote wanaweza kuwa mashahidi isipokuwa

    pale mahakama inapoona kuwa hawaelewi kilewanachokisema au kuulizwa na pia hawatoi majibuya kueleweka labda kwa sababu ya umri mdogo,uzee, magonjwa au kitu kingine chochote.

    Mfano mtoto mdogo wa chini ya umri wa miaka(14) anaweza kutoa ushahidi juu ya jambo fulani naushahidi wake unapokelewa kwa kiapo ikiwa mtotohuyo ataonekana kuelewa maana ya kiapo. Ikiwamahakama itaona mtoto haelewi maana ya kiapo,ushahidi wake utachukuliwa kwa kuangalia kuwa

    mtoto ni muelewa na anaelewa kwamba anatakiwakuongea ukweli mtupu mbele ya mahakama.

    Kwa kawaida mahakama inatakiwa kujitahadharishayenyewe wakati inapopokea na kutumia ushahidi wamtoto.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    13/16

    5Ushahidi

    5.3 Mume na MkeSheria inaeleza kuwa mume au mke ni mashahidiambao wanaweza kutoa ushahidi lakini hawawezikulazimishwa kutoa ushahidi dhidi ya mwenzi wakeisipokuwa kwenye mashitaka yanayohusu makosa yakujamiiana na yaliyo kwenye sheria ya ndoa au kosaanaloshitakiwa nalo linamhusu mke, mume au mtotoau mali zao.

    Mwendesha mashitaka anapotaka kumuita mumeau mke kama shahidi wake kwa namna yoyoteile mfano, kwa maandishi au kutoa ishara mradiushahidi wake utaeleweka na ni lazima ushahidi huuutolewe katika mahakama ya wazi. Ushahidi wa ainahii unachukuliwa kama ushahidi wa matamshi.

    5.4 Shahidi wa utaalamu maalum au faniUshahidi wa mtaalamu juu ya jambo fulani piahukubalika. Mfano daktari anaweza kutoa ushahidikuhusu sababu ya kifo cha mtu ambaye alimtibu aukufanya uchunguzi wa sababu ya kifo chake.

    MuhimuMahakama haifungwi na ushahidi wa utaalamumaalum au fani bali inaupima kama ushahidimwingine na inaweza kuukataa au kutouzingatiakatika kutoa maamuzi yake.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    14/16

    6 Ushahidi

    5.5 Mtu mwenye Matatizo ya Akili (MwenyeMtindio wa Ubongo)

    Mtu mwenye matatizo ya akili anaweza kutoa ushahidikwa kitu anachokielewa isipokuwa pale mahakamaitakapoona kwamba haelewi anachosema au kuulizwana hivyo ushahidi wake kutokuaminika na hajui maanaya kiapo.

    6.0 KUHOJI NA KUULIZA MASWALI MASHAHIDIShahidi anayetoa ushahidi mbele ya mahakamaanaulizwa maswali na pande tatu;(i) Upande wa mashitaka, mdai au mlalamikaji

    anaouunga mkono katika ushahidi;(ii) Upande wa utetezi, mlalamikiwa au mdaiwa;(iii) Mahakama.

    6.1 Upande wa Mashitaka au MlalamikajiMtu yoyote ambaye analalamika au kushitaki, anahaki ya kuita mashahidi ambao atawauliza maswalikwa lengo la kuthibitisha madai au mashitaka yake.Hawa mashahidi wanatakiwa kuunga mkono yaleanayoyasema/anayolalamikia ili kuweza kuyathibitisha

    na hivyo kuweza kujenga kesi au shauri lake hatimayekushinda.

    Maswali anayotakiwa kuwauliza mashahidi wake yasiweya kuwaongoza shahidi bali ya kuwawezesha kuelezaukweli wanaofahamu kuhusu jambo linalobishaniwa.Upande wa mdaiwa au mshitakiwa una haki yakuwauliza maswali mashahidi wa upande wa utetezi

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    15/16

    7Ushahidi

    kwa lengo la kudhoo sha, kanusha au kupima ukwelina uzito wa ushahidi uliotolewa na mdai au mshitaki.

    6.2 Upande wa Utetezi au MdaiwaUpande wa utetezi una haki ya kuita mashahidi wakena kuwauliza maswali kwa lengo la kujenga uteteziwake. Maswali hayo yasiwe ya kumuongoza shahidikusema ambayo mdaiwa anataka aseme. Ushahidiuwe ni wa kujenga kesi ya utetezi kwa kueleza ukweliunaomwondolea mdaiwa au mshitakiwa hatia aulawama.

    Vile vile upande wa mdai au mshitaki una haki yakuuliza maswali mashahidi wa mdaiwa au mshitakiwawa mashitaka kwa lengo la kukanusha, kudhoo shaau kupima ukweli na uzito wa ushahidi uliotolewa naupande wa mdaiwa au mshitakiwa.

    6.3 MahakamaMahakama ina haki ya kuuliza maswali pande zotekatika shitaka au shauri ili kupata ufafanuzi au ukweliwa jambo linalobishaniwa.

    7.0 KUPOKELEWA NA KUKUBALIWA KWAUSHAHIDI MAHAKAMANI

    Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kukubali aukukataa kupokea shahidi. Mahakama inafanya hivyokwa kuzingatia kanuni za kutolewa kwa ushahidi huona kama unahusu suala linalobishaniwa.

  • 8/15/2019 T4 - Ushindi Book

    16/16

    8 Ushahidi

    8.0 HITIMISHO

    Ni muhimu kuzingatia na kufuata kanuni za kutoa

    ushahidi ili ukubalike mahakamani kwa ajili yakukanusha au kuthibitisha jambo linalobishaniwa ilimtu aweze kupata haki yake.

    Mashahidi wa upande mmoja, mfano mdai, mashitaka aumlalamikaji wanatakiwa kutoa ushahidi unaoshabihianaambao haupingani ili kuweza kuthibitisha jambo

    linalobishaniwa, vilevile kwa upande wa utetezi.Idadi ya mashahidi si hoja bali kinachotakiwa ni ukweli,uzito na kushabihiana kwa ushahidi unaotolewa. Hivyoshahidi mmoja anaweza kuwa na ushahidi mzuri nakuthibitisha jambo linalobishaniwa vizuri zaidi kulikomashahidi wengi ambao hawajui wayasemayo na

    ushahidi wao unapingana au hauna mtiririko.Hivyo kabla mtu hajafungua shauri au mashitakamahakamani, lazima ajiulize kama ana ushahidi wakutosha au kabla hajajitetea au kukanusha mashitaka,tuhuma au madai lazima ajiulize kama ana ushahidi.

    Ndugu msomaji, umepata elimu ya kutosha kuhusuushahidi, pamoja na kanuni za kutoa ushahidimahakamani. Ni ombi letu kuwa elimu hii uliyoipatausikae nayo mwenyewe uitoe kwa jamii nzima ili tuwena jamii ya ufahamu wa kutosha kuhusu sheria za nchi.