4
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI OKTOBA, 2015 Ndugu Waandishi wa Habari, napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha kwa mara nyingine tena katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kuwashukuru kwa kuitikia mwito wa kuhudhuria mkutano huu. Naomba niwakumbushe kwamba, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka ya kukusanya, kuchambua na kutoa takwimu rasmi za nchi kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351. Lengo kuu la mkutano huu ni kuwafahamisha kuhusu Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015. Nitazungumzia pia uwezo wa Shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Oktoba, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 na mwenendo wa Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Ndugu Waandishi wa Habari, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015 kutoka 149.70 mwezi Oktoba, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi 1

Taarifa Kwa Vyomba Vya Hbr - Cpi-oct2015

Embed Size (px)

DESCRIPTION

TAARIFA KWA VYOMBA VYA HBR - CPI-OCT2015

Citation preview

Page 1: Taarifa Kwa Vyomba Vya Hbr - Cpi-oct2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI OKTOBA, 2015

Ndugu Waandishi wa Habari, napenda kutumia fursa hii

kuwakaribisha kwa mara nyingine tena katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu

na kuwashukuru kwa kuitikia mwito wa kuhudhuria mkutano huu.

Naomba niwakumbushe kwamba, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye

mamlaka ya kukusanya, kuchambua na kutoa takwimu rasmi za nchi

kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351.

Lengo kuu la mkutano huu ni kuwafahamisha kuhusu Mfumuko wa Bei

wa mwezi Oktoba, 2015. Nitazungumzia pia uwezo wa Shilingi ya

Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Oktoba,

2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 na mwenendo wa Mfumuko wa Bei

kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki.

Ndugu Waandishi wa Habari, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015 kutoka 149.70 mwezi Oktoba, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 9.6 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015.

Ndugu Waandishi wa Habari, Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Septemba, 2015 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2014. Mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kuongezeka mwezi Oktoba, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi

1

Page 2: Taarifa Kwa Vyomba Vya Hbr - Cpi-oct2015

Oktoba, 2014 ni pamoja na bei za mchele kwa asilimia 28.3, mihogo mibichi kwa asilimia 19.0, viazi mviringo kwa asilimia 18.9, samaki kwa asilimia 15.9, mbogamboga kwa asilimia 13.0, viazi vitamu kwa asilimia 10.5, mahindi kwa asilimia 9.6, ndizi za kupika kwa asilimia 7.8, nyama kwa asilimia 5.7, unga wa mahindi kwa asilimia 4.9 na unga wa muhogo kwa asilimia 4.6. Kwa upande mwingine, baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kuongezeka mwezi Oktoba, 2015 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2014 ni pamoja na kitambaa kwa ajili ya suruali ya kiume kwa asilimia 12.7, nguo za kiume na nguo za kike kwa asilimia 5.6, nguo za watoto kwa asilimia 4.5, viatu vya kiume kwa asilimia 7.0 na mkaa kwa asilimia 15.2.

MFUMUKO WA BEI KWA KIPIMO CHA MWEZI

Ndugu Waandishi wa Habari, Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 159.17 mwezi Oktoba, 2015 kutoka 159.04 mwezi Septemba, 2015. Kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 0.8, unga wa muhogo kwa asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika kwa asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia 0.9. Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na vitambaa kwa ajili ya nguo za kike kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume kwa asilimia 1.1, mkaa kwa asilimia 1.4 na gharama za kupata ushauri wa daktari kwenye hospitali binafsi kwa asilimia 1.4.

THAMANI YA SHILINGI YA TANZANIA MWEZI OKTOBA, 2015 IKILINGANISHWA NA MWEZI SEPTEMBA, 2010

2

Page 3: Taarifa Kwa Vyomba Vya Hbr - Cpi-oct2015

Ndugu Waandishi wa Habari, uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 62 na senti 82 mwezi Oktoba, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na Shilingi 62 na senti 88 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2015.

HALI YA MFUMUKO WA BEI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Ndugu Waandishi wa Habari, Mfumuko wa Bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mfano; Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 nchini Kenya umeongezeka hadi asilimia 6.72 kutoka asilimia 5.97 mwezi Septemba, 2015 na Uganda umeongezeka hadi asilimia 8.8 kutoka asilimia 7.2 mwezi Septemba, 2015.

Ndugu Waandishi wa Habari, napenda kuwashukuru kwa mara

nyingine tena kwa kuhudhuria kikao hiki na natoa wito kwenu kuhusu

umuhimu wa kuwaelimisha Watunga Sera na Wananchi wote kwa

ujumla juu ya umuhimu wa matumizi ya takwimu hizi za bei pamoja na

nyinginezo zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Pia, ninawaomba sana Wananchi wote kwa ujumla kutoa ushirikiano wa

dhati kwa Ofisi za Takwimu za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu

mbali mbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya

maendeleo ya nchi yetu.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

3