Upload
hamzatemba
View
252
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
1/8
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHESHIMIWA
JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA
TAREHE 16 MEI, 2013.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,S.L.P 128, Sumbawanga,RUKWA.Simu. Na. 025 - 2802137/2802138Nukushi: 2802117/2802318
Baruapepe: [email protected] MEI 16, 2013
mailto:[email protected]:[email protected]7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
2/8
1.0. UTANGULIZI.
Mheshimiwa Jaji Mkuu, Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kwa
Niaba ya Wananchi na Viongozi wa Mkoa wa Rukwa kukukaribisha wewe
na Viongozi ulioambatana nao hapa Mkoani Rukwa. Ni matumaini ya
Uongozi wa Mkoa wa Rukwa na wananchi wake kuwa, ziara hii italeta Tija
katika Utumishi wetu kwa Umma kutokana na ukweli kwamba tunajua
tutapata ushauri, maelekezo na maagizo kwa ajili ya kuboresha utendaji
wetu wa kazi.
Mheshimiwa Jaji Mkuu, Baada ya Serikali kuridhia kumega sehemu ya
Mkoa wa Rukwa na kuanzishwa Mkoa mpya wa Katavi, kuna mabadiliko
ya eneo la jiografia la Mkoa na maeneo ya Utawala. Kwa sasa Mkoa wa
Rukwa unaundwa na Wilaya tatu ambazo ni:- Sumbawanga, Nkasi na
Kalambo. Mkoa una Halmashauri nne, Halmashauri za Wilaya ya
Sumbawanga, Nkasi, Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga.
Kwa kuzingatia mgawanyo huo sasa Mkoa wa Rukwa una eneo la
kilometa za mraba 27,713 wakati kilometa za mraba 22,792 ni la ardhi
na kilometa za mraba 4,921 ni eneo la maji. Mipaka ya sasa ya Mkoa wa
Rukwa upande wa Kusini - Magharibi Mkoa unapakana na nchi ya
Zambia, upande wa Kaskazini - Mashariki Mkoa wa Katavi, upande wa
Kusini - Mashariki Mkoa wa Mbeya, na upande Magharibi nchi ya
Kidemokrasi ya Kongo (DRC). Mkoa wa Rukwa uko Kusini-Magharibi
mwa Tanzania kwenye Latitudo 050 na 090 Kusini na Longitudo 30 - 330
Mashariki.
2.0. SENSA YA WATU NA MAKAZI
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Mkoa wa
Rukwa una Jumla ya Watu 1,004,539 kwa mchanganuo wa Wanaume
487,311 na Wanawake 517,228
Na
.
Jina la Wilaya ME KE JUMLA
1 Kalambo 100,474 107,226 207,7002 Sumbawanga DC 149,062 156,784 305,846
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
3/8
3 Nkasi DC 137,041 144,159 281,2004 Sumbawanga MC 100,734 109,059 209,793
JUMLA 487,31
1
517,22
8
1,004,53
9
3.0. SHUGHULI ZA UCHUMI ZA WAKAZI WA MKOA WA RUKWA
Shughuli kuu za kiuchumi za Wakazi wa Mkoa wa Rukwa ni kilimo,
ufugaji na Uvuvi.
3.1. Kilimo
Wakazi wengi wa Mkoa wa Rukwa hujishughulisha na Kilimo takribani
70% ya wakulima wa Mkoa wa Rukwa wanatumia kilimo cha jembe la
kukokotwa na Ngombe
Katika msimu wa kilimo wa 2012/2013 Mkoa umelenga kulima jumla ya
hekta 401,837.0 za mazao ya chakula na hekta 93,103.0 za mazao ya
biashara ambazo tunatarajia kutupatia kiasi cha tani 1,357,836.0 za
mazao ya chakula na tani 184,731.4 za mazao ya biashara.
3.1.1. Kilimo cha Umwagiliaji
Kutokana na Mpango kabambe wa Umwagiliaji Taifa wa mwaka 2002,
ilibainika kuwa Mkoa wa Rukwa una jumla ya Hekta 527,721 zenye
uwezo wa kumwagiliwa. Kati ya eneo hilo kekta 14,310 zina uwezo wa
juu, hekta 42,294 zina uwezo wa kati na hekta 471,117 uwezo wake ni
wa chini. Kwa sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 14,382.08 sawa na
25.41% ya eneo lenye uwezo wa juu na kati wa kumwagiliwa.
Mkoa una jumla ya Miradi ya Umwagiliaji 10 ambayo inaendelezwa kwa
njia ya kisasa na Miradi ya Umwagiliaji 16 ambayo haijaendelezwa
inamwagilia kwa kutumia njia za asili (Traditional Irrigation).
Kwa mwaka 2011/2012 Mkoa ulipangiwa jumla ya Sh. Bilioni
1,322,000,000/=kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF).
Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
4/8
Sumbawanga TShs. 1,072, 000,000/= na Wilaya ya Nkasi TShs. 250,
000,000/= .
Aidha, kwa mwaka 2012/2013 Mkoa umepangiwa jumla ya
Sh.1,031,250,000/= kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF).
Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya
Sumbawanga TShs. 515,625,000/= na Wilaya ya Nkasi TShs.
515,625,000/=. Kazi za utekelezaji wa miradi hiyo zinaendelea.
3.2. Hali ya ufugaji
Kulingana na sensa ya sampuli ya kilimo ya mwaka 2002/2003 Mkoa wa
Rukwa ni moja kati ya mikoa yenye idadi ya wastani (moderate) ya
mifugo.
Kufuatana na Sensa hiyo, Daftari la Mkulima na Taarifa za maendeleo ya
mifugo za kila mwaka kutoka katika Halmashauri Idadi ya mifugo
(mwaka 2011) inakisiwa kufikia ngombe 438,555, mbuzi 152,899,
kondoo 22,867, nguruwe 49989, punda 6,171, kuku 470,595. Takwimu
hizi, hususan za ngombe zinatiliwa mashaka na baadhi ya wadau ambao
wanaamini idadi ya ngombe ni kubwa zaidi. Mikakati ya mkoa ya
kuendeleza ufugaji ni pamoja na kuhakiki takwimu za mifugo.
3.2.1. Mfumo wa ufugaji
Ufugaji katika Mkoa wa Rukwa huendeshwa chini ya mifumo ya aina
mbili kubwa, ufugaji huria (extensive) na ufugaji shadidi (intensive).
Ufugaji shadidi ni mdogo sana; chini ya 1% na hufanyika katika ranchi ya
Kampuni za Ranchi za Taifa (KARATA) iliyoko Kalambo pamoja na
kwenye mashamba ya mifugo yaliyobinafsishwa ya Nkundi na Malonje.
Ranchi ya Kalambo na shamba la mifugo la Nkundi huzalisha ngombe
wa nyama wakati shamba la Malonje ni la ngombe wa maziwa. Kwa
kiwango kidogo pia, ufugaji wa ngombe wa maziwa upo, hasa katika
eneo la Manispaa ya Sumbawanga. Mkoani Rukwa kuna ngombe wa
maziwa 5,760, na mbuzi wa maziwa 496 (Taarifa za maendeleo ya
mifugo toka Halmashauri 2012).
3.3. Uvuvi.
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
5/8
Kutokana na sensa ya mwaka 1999 uzalishaji wa samaki toka Ziwa
Rukwa unakadiriwa kuwa ni tani 7,000 na Ziwa Tanganyika linakadiriwa
kuzalisha samaki kiasi cha tani 165,000 hadi tani 200,000 kwa mwaka
wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 80 hadi milioni 100.
Kuna aina mbali mbali ya samaki wanaopatikana katika maziwa na mito
iliyopo katika Mkoa wetu. Ziwa Tanganyika linatupatia samaki aina ya
dagaa, migebuka, sangara, kuhe, kambale na samaki wa mapambo.
Ziwa Rukwa linatupatia kambale, gege na mamba. Dagaa na migebuka
wanaopatikana ziwa Tanganyina na gege toka ziwa Rukwa mara nyingi
hukaushwa na kupelekwa kuuzwa kweye masoko makubwa ndani na nje
ya nchi mfano Zambia, Kongo na Burundi.
4.0. HALI YA ULINZI NA USALAMA.
Mheshimiwa Jaji Mkuu, Kwa upande wa Kisiasa viko vyama tisa (9)
vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2010 wa Rais, Wabunge na
Madiwani. Chama Cha Mapinduzi, ndicho chama chenye nguvu kisiasa
katika Mkoa wa Rukwa. Kati ya Waheshimiwa Wabunge 7, wote
wanatoka Chama Cha Mapinduzi na kati ya Wahe. Madiwani 86 wa
kuchaguliwa, 78 wanatoka Chama Cha Mapinduzi, 6 kutoka CHADEMA, 1
kutoka CUF na 1 kutoka UDP.
Taarifa ya Waheshimiwa Wabunge hao saba inajumlisha matokeo ya
kurejesha kiti cha ubunge kwa Mhe. Aeshi Khalifan Hilaly baada ya
mchakato wa kisheria kufanyika.
Kwa ujumla hali ya Ulinzi na Usalama katika Mkoa ni shwari japo kuwa
kuna changamoto mbalimbali za uhalifu ambazo Mkoa umeendelea
kudhibiti na kuzishughulikia kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa
na Wilaya.
4.1. MATUKIO YASIYO YA KAWAIDA NDANI YA MKOA
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
6/8
Ndani ya mwezi Februari, 2013 Mkoa umekubwa na matukio makubwa
mawili mabaya, ambayo Serikali ya Mkoa kupitia vyombo vya Ulinzi na
Usalama tulijitahidi kuhakikisha wale wote waliohusika wanawajibishwa
kwa mujibu wa Sheria.
4.1.1. Tukio la kukatwa Mkono Albino Mwanamke Miangalua
Mnamo tarehe 14/02/2013 Albino Bibi. Maria Chambanenge miaka 39
Mkazi wa Kata ya Miangalua Wilaya ya Sumbawanga alikatwa mkono
kwa kile kinachosadikika ni imani za kishirikina. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, ilitoa msaada wa
haraka ili kuokoa maisha ya Bibi Maria Chambanenge kwa kumuwahisha
Hospitali ya Mkoa kwa ajili ya matibabu na aliweza kuhudumiwa.
Kupitia vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkono wa Bibi. Maria
Chambanenge uliweza kupatikana na kuhifadhiwa katika chumba cha
maiti Hospitali ya Mkoa.
Katika tukio hilo wahusika wa uhalifu huo wanne (4) walikamatwa na
suala hilo lipo katika vyombo vya sheria hadi sasa.
4.1.2. Tukio la kukatwa Mkono kwa Albino Mtoto - Milepa
Mnamo siku ya tarehe 15/02/2013 Majira ya Mchana katika Kijiji cha Msia
huko Milepa Wilaya ya Sumbawanga Mtoto wa kiume Mwigulu
Mwasonange miaka 12 akiwa na mtoto mwenzake wakioga mtoni ghafla
walivamiwa, na Mtoto Mwigulu Mwasonange alikatwa mkono na watu
wasiojulikana na kuweza kutokomea nao kusikojulikana na kuacha mtoto
akipoteza fahamu kutokana na maumivu makali na kuvuja damu kwa
wingi.
Mtoto Mwigulu Mwasonange alipatiwa matibabu na hali yake kiafya
iliweza kuimarika. Kwa sasa Mtoto Mwigulu Mwasonange alipata ufadhili
wa kusomeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Under the Same Sun
nanaendelea na Masomo yake Jijini Dar es Salaam.
4.2. Mgogoro wa Uchinjaji wa Kitoweo
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
7/8
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Mhandisi Stella Martin Manyanya (Mb)
aliandaa Mkutano wa pamoja baina yake na Viongozi wa Madhehebu ya
Dini ya Waislamu na Wakristo, tarehe 23 Machi, 2013. katika Mkutano
ambao ulihudhuriwa na Viongozi Waandamizi wa Serikali.
Mkuu wa Mkoa aliitisha mkutano huo, akiwa na malengo ya kuwasihi
Viongozi hao wa madhehebu ya Dini kuvumiliana, kwa kila mtu kuabudu
kulingana na imani yake. Pamoja na kuhubiri Amani kufuatia Viongozi wa
pande zote mbili kutoa Matamko mbalimbali. Hali iliyokuwa ikitishia
Amani na Usalama wa Mkoa.
5.0 MIGOGORO YA ARDHI
Migogoro ya ardhi ipo Mkoani kwetu, katika sura tatu.
(i) Mgogoro unaotokana na pande mbili kuuziana viwanja na
kugombania mipaka au kukosa nyaaka muhimu za kuhalarisha
umiliki . Ambapo sehemu kubwa migogoro hii uamuliwa na
Baraza la Ardhi na Nyumba la Sumbawanga.
(ii) Mgogoro wa pili ni baina ya Wakulima na Wafugaji. Mkoa
umeuhisha TAMKO LA MTOWISA kwa kuzitaka Wilaya kuwa na
Master plan ambazo zitaonesha matumizi bora ya ardhi. Pia
Halmashauri zote zimeagizwa kuwa Vyama vya Wafugaji kama
kile cha Wilayani Nkasi ambacho kinawaunganisha wafugaji na
kuwataka kuwa na mifugo kulinana na maeneo ya malisho
(iii) Eneo la tatu la mgogoro ni baina ya Wawekezaji wakubwa wa
mashamba na Vijiji jirani. Ili kutatua matatizo kama haya Mkoa
huunda Kamati ya uchunguzi ili kubaini ukweli na baadaye suala
husika huwasilishwa OWM TAMISEMI na Wizara ya Ardhi kwa
maamuzi.
6.0. MSONGAMANO WA MAHABUSU
Mheshimiwa Jaji, Tunakabiliwa na msongamano mkubwa wa
mahabusu katika Gereza la Mahabusu la Sumbawanga mara tatu zaidi
ya uwezo wake; hii inatokana na kwamba Wilaya ya Nkasi na Kalambo
hazina mahabusu wala Mahakama za Wilaya hivyo kupelekea mashauri
7/30/2019 TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA MHE. JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN
8/8
yote kutoka Wilaya zote za mkoa huu kutajwa katika Wilaya ya
Sumbawanga pekee.
Katika kukabiliana na hili Mkoa ulifanya mawasiliano kwa njia ya barua
na kwa njia ya ana kwa ana na Wizara ya Katiba ya Sheria kuhusu
mpango wa Mkoa kujenga Mahakama za Wilaya na Wizara ifanye
umaliziaji wa majengo hayo. Tunashukuru ramani za majengo ya
Mahakama za Wilaya tumeshapokea na tuliahidiwa maombi yetu
yatawekwa katika bajeti ya mwaka 2013/2014. Ni matumaini yetu suala
hilo litafanyika kama tulivyoahidiwa.
7.0. HITIMISHO
Mheshimiwa Jaji Mkuu,Tumewasilisha Taarifa ya Mkoa kwa Muhtasari
ili uweze kupata mwanga kuhusu Mkoa wetu, kwa niaba ya Wananchi wa
Mkoa wa Rukwa na Wananchi napenda kutumia fursa hii kukukaribisha
tena Mkoani kwetu wewe na msafara wako ulioambatana nao, tupo
tayari kuufanyia kazi maagizo, ushauri, maoni au maelekezo
utakayotupatia kwa ajili ya Ustawi na Maendeleo ya Taifa letu.
Karibu sana Mkoani Rukwa Mheshimiwa Jaji.
Salum Mohamed Chima (Alhaj)
Katibu Tawala wa Mkoa Rukwa