Upload
others
View
78
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1 | P a g e
TAARIFA YA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA
UTENDAJI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA LISHE
ULIOFANYIKA TAREHE 28 AGOSTI, 2018 JIJINI DODOMA.
1.0 UTANGULIZI;
Katika Mkuatano wa Kitaifa wa Urutubishaji Chakula (National Summit
on Food Fortification) uliofanyika tarehe 23-24 mwezi Agosti, 2017 katika
ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan
alikuwa ni Mgeni Rasmi. Katika hotuba yake aliagiza kuwepo kwa
mkataba wa utendaji na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara ili
wasimamie utekelezaji wa shughuli za lishe katika Mikoa yao ili kuondoa
tatizo la utapiamlo nchini. Kwa kuwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI ina jukumu
la kusimamia utekelezaji katika ngazi za Mikoa na Halmashauri, iliandaa
mkataba huo wenye viashiria vya upimaji vipatavyo 11. Aidha, tathimini
ya kwanza ilipangwa kufanyika baada ya miezi sita ili kujenga uelewa wa
pamoja juu ya viashiria vya Mkataba vitakavyokuwa vikipimwa na pia
kubaini maeneo ya kuboresha.
1.1. Malengo ya kuwa na Mkataba wa Lishe:
1.1.1. Lengo Kuu,
Ni kusimamia masuala ya lishe ili kupunguza athari za utapiamlo katika
Mikoa na Taifa kwa ujumla.
2 | P a g e
1.1.2. Malengo mahsusi;
2. Kuhakikisha kuwa Mikoa inasimamia ipasavyo utekelezaji wa afua
za lishe katika maeneo yao.
3. Kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hali duni ya lishe katika
Mikoa husika
4. Kutenga na kutumia fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe
katika mipango ya Mikoa na Halmashauri.
5. Kusimamia na kuratibu shughuli za wadau mbalimbali
wanaotekeleza na kufadhili shughuli za lishe katika maeneo yao.
2.0. Hatua za Utekelezaji;
2.1 Timu ya kusimamia utekelezaji wa Agizo,
OR TAMISEMI iliteua jumla ya wataalam tisa (9) waliounda timu
iliyosimamia utekelezaji wa agizo la kuandaa mkataba wa kusimamia
shughuli za lishe uliosainiwa baina Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
TAMISEMI na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara. Timu
hii ilitekeleza agizo hili chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu na Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
3 | P a g e
Jedwali 1. Timu ya usimamizi wa agizo la kuandaa mkataba
Na. Jina Cheo Idara
1 Dkt. Ntuli A.Kapologwe Mkurugenzi DHS
2 Steven J. Motambi Mkurugenzi
msaidizi
DHS
3 Ibrahim Minja Mkurugenzi
msaidizi
DRA
4 Suleiman Lukanga Mwanasheria DLS
5 Mwita J.M. Waibe Afisa Lishe DHS
6 Rose Lugendo Afisa Utawala DAHRM
7 Jeremiah H. Mwambange Afisa Lishe DHS
8 Mariam Nakuwa Afisa Lishe DHS
9 Magesa Japhari Afisa Lishe DHS
Nyenzo ya kukusanyia taarifa iliandaliwa kulingana na vigezo
vilivyoainishwa kwenye Mkataba na kusambazwa katika Mikoa yote ya
Tanzania Bara.
2.2 Viashiria na vigezo vilivyotumika kupima utekelezaji wa Mkataba;
Vigezo viliandaliwa na sehemu ya huduma za Lishe katika Idara ya Afya
Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI. Jumla ya Viashiria 11
viliandaliwa na kujumuishwa katika Mkataba ili kuwawezesha
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa kusimamia utekelezaji wa mkataba
husika. Aidha, viashiria hivyo vilivyotumika wakati wa tathmini ni kama
vifuatavyo: -
4 | P a g e
1. ASILIMIA YA KIASI CHA FEDHA KILICHOTENGWA KATIKA BAJETI KWA AJILI
YA AFUA ZA LISHE KULINGANA NA IDADI YA WATOTO WALIO NA UMRI
CHINI YA MIAKA MITANO KATIKA MKOA KWA MUJIBU WA MWONGOZO WA
MWAKA HUSIKA. 2. ASILIMIA YA KIASI CHA FEDHA KILICHOTENGWA KATIKA BAJETI KWA
AJILI YA URATIBU WA HUDUMA ZA LISHE KATIKA NGAZI YA MKOA KWA
MUJIBU WA MWONGOZO.
3. ASILIMIA YA KIASI CHA FEDHA KILICHOTUMIKA KUTEKELEZA AFUA ZA
LISHE UKILINGANISHA NA KIASI CHA FEDHA KILICHOTENGWA KATIKA
BAJETI KATIKA NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI.
4. UWEPO WA MPANGO MKAKATI WA LISHE WA MKOA.
5. IDADI YA WATOTO WENYE UMRI WA MIEZI 6 HADI MIAKA 5 WALIOPATIWA
NYONGEZA YA MATONE YA VITAMINI A UKILINGANISHA NA IDADI YA
WATOTO WENYE UMRI HUO KATIKA MKOA.
6. IDADI YA WANAWAKE WAJAWAZITO WALIOPATIWA VIDONGE VYA MADINI
YA CHUMA NA ASIDI YA FOLIKI UKILINGANISHA NA IDADI YA WAJAWAZITO
WOTE WANAOTARAJIWA KATIKA MKOA.
7. IDADI YA AKINAMAMA WENYE WATOTO WALIO NA UMRI CHINI YA MIEZI
6 WALIOPATIWA ELIMU YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA PEKEE
UKILINGANISHA NA IDADI YA AKINAMAMA WOTE WENYE WATOTO WALIO
NA UMRI CHINI YA MIEZI SITA KATIKA MKOA.
8. IDADI YA AKINAMAMA WENYE WATOTO WENYE UMRI WA KUANZIA MIEZI 6
HADI MIAKA 2 WALIOPATIWA ELIMU YA ULISHAJI WA VYAKULA VYA
NYONGEZA KWA WATOTO UKILINGANISHA NA IDADI YA AKINAMAMA
WOTE WENYE WATOTO WENYE UMRI HUO KATIKA MKOA.
9. IDADI YA WATOTO WENYE UTAPIAMLO WALIOPATIWA MATIBABU
UKILINGANISHA NA IDADI YA WATOTO WOTE WALIOGUNDULIWA KUWA NA
UTAPIAMLO.
10. IDADI YA VIKAO VYA KAMATI YA LISHE VILIVYOFANYIKA UKILINGANISHA
NA IDADI YA VIKAO 4 VINAVYOTAKIWA KUFANYIKA KWA MWAKA HUSIKA
KATIKA MKOA NA HALMASHAURI.
11. IDADI YA KAGUZI ZA CHAKULA NA DAWA ZILIZOFANYIKA
KULINGANISHA NA KAGUZI ZILIZOTAKIWA KUFANYIKA KWA MWAKA
HUSIKA KATIKA MKOA NA HALMASHAURI.
5 | P a g e
2.3 Kusaini mkataba wa usimamizi wa afua za lishe,
Mkataba wa utekelezaji wa masuala ya Lishe ulisainiwa baina ya Mhe. WN
OR - TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Desemba,
2017 na kuanza utekelezaji wa Mkataba huu mwezi Januari, 2018.
2.4. Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe,
Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ulifanyika ukilenga mambo
yafuatayo: -
Mikoa kuwasilisha utekelezaji wa viashiria vilivyo kwenye Mkataba
wa Makubaliano wa Masuala ya Lishe baada ya miezi sita ya
utekelezaji.
Kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa viashiria vilivyoko
katika Mkataba wa Lishe.
Kuongeza msukumo wa usimamizi na uelewa wa masuala ya Lishe
ili kupunguza kiwango cha utapiamlo nchini.
Kufafanua madhara na hasara ya utapiamlo katika uchumi na
maendeleo ya nchi.
2.4.1 Ukusanyaji na uchakataji wa taarifa;
Taarifa za utekelezaji wa mkataba zilikusanywa kutoka Mikoa na
kuchakatwa kulingana na viashiria na vigezo vilivyowekwa ambapo kila
Mkoa ulipangwa kulingana na utekelezaji wa kila kiashiria. Baada ya hapo
6 | P a g e
taarifa ilitumwa katika Mikoa kabla ya kuwasilishwa katika Mkutano wa
tathmini uliofanyika tarehe 28 Agosti, 2018 Jijini Dodoma na kuhudhuriwa
na: -
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
Katibu Mkuu OR – TAMISEMI,
Manaibu Katibu Wakuu Afya na Elimu- OR – TAMISEMI,
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara,
Makatibu Tawala wa Mikoa yote ya Tanzania Bara,
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Wawakilishi kutoka Wizara Mbalimbali ambazo ni Wizara ya Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika,
Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Wizara ya Mifungo na Uvuvi,
Wakurugenzi na wataalamu kutoka OR TAMISEMI,
Wawakilishi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC)
Wadau wa Lishe nchini (USAID, UNICEF, DFID, WFP na PANITA)
Wawakilishi wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri
Wawakilishi wa Maafisa Lishe wa Mikoa na Halmashauri
2.4.2 Matokeo ya utekelezaji wa viashiria;
Hali ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha miezi sita tangu
kusainiwa kwa mkataba huo ni kama inavyoonekana kwenye jedwali:
7 | P a g e
2.4.2.1 Kiasi cha fedha zilizotumika kutekeleza shughuli za lishe
kulinganisha na fedha iliyotengwa,
Mkoa 1 tu wa Kilimanjaro kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara ndio
umefanikiwa kutumia zaidi ya 50% ya fedha walizopanga.
COMPACT indicator % of Gov.
fund
expended
against
budgeted
Gov. budget
spent per
under-five
child (THS.)
Availability
of regional
nutrition
strategic
plan
Completion
rate of
nutrition
quarterly
steering
committee
against
Completion
rate of
nutrition
quarterly
supportive
supervision
against
# of
quarterly
food
inspection
conducted
in the
region
% of
expected
cases of
SAM
amongst
children 0-
59 months
% of
mothers/car
egivers of
children 0-
23 months
who have
received
% of
children
aged 6-59
months
supplement
ed with
Vit.A
% of
pregnant
women who
received IFA
among
attended
casesARUSHA 14% 186 - 41% 31% 0 36% 3% 92% 61%
DAR ES SALAAM 32% 135 - 33% 63% 0 3% 0% 92% 71%
DODOMA 17% 120 - 39% 39% 0 9% 52% 101% 70%
GEITA 48% 252 - 0% 75% 0 8% 50% 97% 63%
IRINGA 18% 64 - 71% 63% 0 98% 68% 96% 59%
KAGERA 25% 62 - 67% 61% 0 17% 38% 91% 72%
KATAVI 11% 192 - 25% 25% 0 13% 39% 97% 40%
KIGOMA 3% 6 - 22% 31% 0 11% 26% 98% 48%
KILIMANJARO 58% 178 - 16% 56% 4 2% 35% 97% 69%
LINDI 31% 321 - 25% 57% 4 35% 19% 96% 55%
MANYARA 38% 439 1 63% 69% 0 2% 47% 100% 61%
MARA 18% 418 - 4% 11% 0 2% 5% 91% 51%
MBEYA 11% 119 1 43% 64% 4 78% 64% 92% 70%
MOROGORO 37% 523 - 25% 45% 4 11% 53% 96% 61%
MTWARA 21% 225 - 80% 68% 4 26% 13% 100% 53%
MWANZA 12% 89 - 47% 53% 4 5% 45% 98% 58%
NJOMBE 37% 181 - 50% 61% 4 65% 60% 113% 44%
PWANI 13% 391 - 14% 36% 4 4% 32% 99% 56%
RUKWA 24% 335 1 25% 35% 0 1% 44% 98% 51%
RUVUMA 10% 445 - 9% 31% 0 31% 24% 92% 45%
SHINYANGA 13% 98 - 86% 71% 0 21% 49% 98% 68%
SIMIYU 14% 86 - 14% 64% 4 14% 57% 96% 39%
SINGIDA 25% 377 - 33% 66% 0 17% 38% 105% 54%
SONGWE 15% 18 - 50% 58% 0 61% 64% 92% 58%
TABORA 19% 240 - 47% 28% 4 4% 29% 96% 38%
TANGA 5% 33 - 2% 11% 0 12% 17% 97% 53%
8 | P a g e
Chanzo cha Taarifa: Taarifa za Mkoa
COMPACT indicator % of Gov.
fund
expended
against
budgeted
ARUSHA 14%
DAR ES SALAAM 32%
DODOMA 17%
GEITA 48%
IRINGA 18%
KAGERA 25%
KATAVI 11%
KIGOMA 3%
KILIMANJARO 58%
LINDI 31%
MANYARA 38%
MARA 18%
MBEYA 11%
MOROGORO 37%
MTWARA 21%
MWANZA 12%
NJOMBE 37%
PWANI 13%
RUKWA 24%
RUVUMA 10%
SHINYANGA 13%
SIMIYU 14%
SINGIDA 25%
SONGWE 15%
TABORA 19%
TANGA 5%
9 | P a g e
2.4.2.2 Mikoa kuwa na mpango mkakati wa lishe.
Ni Mikoa mitatu tu ambayo imeshaandaa mpango mkakati wa lishe
kufikia tarehe ya kikao. Mikoa mingine ipo katika hatua mbalimbali za
uandaaji wa mpango mkakati wa lishe.
Chanzo: Taarifa ya mkoa
2.4.2.3 Ufanisi wa kutoa nyongeza ya Vitamin A
Watoto walio na umri wa miezi 6-59 waliopatiwa nyongeza ya matone ya
Vitamin A ambapo wastani wa kitaifa ni asilimia 96. Mikoa 19 ilitoa
nyongeza ya matone ya vitamin A zaidi ya wastani wa kitaifa wakati
Mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Kagera na
Mara hawakuweza kufikia wastani huo wa kitaifa.
10 | P a g e
Chanzo: CHNM campaign report June, 2018
2.4.2.4 Vidonge vya kuongeza wekundu wa damu (madini ya chuma na
asidi ya foliki).
Wastani wa wajawazito waliopatiwa vidonge vya kuongeza wekundu wa
damu (FeFo) ambapo wastani wa Kitaifa ni asilimia 76. Mikoa yaTabora,
Simiyu, Katavi, Njombe, Ruvuma na Kigoma ipo chini ya wastani wa
Kitaifa katika utoaji wa Madini Chuma na asidi ya foliki kwa Wanawake
wajawazito wanaohudhuria kliniki katika vituo vya kutolea huduma za
afya.
11 | P a g e
Chanzo: DHIS 2
Matokeo ya ufanisi wa utoaji wa Madini ya Chuma na Asidi ya Foliki kwa
Mikoa yote (FeFO)
12 | P a g e
Chanzo: DHIS 2
2.4.2.6 Elimu ya ulishaji wa vyakula vya nyongeza kwa watoto;
Katika utoaji wa elimu hii ni Mikoa 8 tu ya Iringa, Songwe, Mbeya,
Njombe, Simiyu, Morogoro, Dodoma na Geita imefikia zaidi ya asilimia 50
ya utoaji wa elimu hii kwa wazazi na walezi. Aidha, Mikoa mingine yote
imetekeleza kwa kiwango chini ya asilimia 50.
Chanzo: Taarifa za Mikoa
13 | P a g e
2.4.2.7 Matibabu ya utapiamlo mkali katika vituo vya kutolea huduma za
afya;
Katika huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali ni Mikoa 4 ya Iringa,
Mbeya, Njombe, Songwe ndio imefikia zaidi ya asilimia 50. Aidha Mikoa
iliyobaki imetekeleza kwa kiwango chini ya asilimia 50.
Chanzo: BNA for FY 2017/2018
2.4.2.8 Utendaji wa kamati za lishe;
Mikoa 2 ya Shinyanga na Mtwara ndiyo pekee iliweza kukaa wastani wa
vikao 3 kati ya 4 vilivyotakiwa, hii ikiwa ni asilimia 75%. Mikoa mingine
haikutekeleza kiashiria hiki kama ilivyotakiwa.
14 | P a g e
Chanzo: Taarifa za Miko
Ufanisi wa Kamati za Lishe
COMPACT indicator Completion
rate of
nutrition
quarterly
steering
committee
against ARUSHA 41%
DAR ES SALAAM 33%
DODOMA 39%
GEITA 0%
IRINGA 71%
KAGERA 67%
KATAVI 25%
KIGOMA 22%
KILIMANJARO 16%
LINDI 25%
MANYARA 63%
MARA 4%
MBEYA 43%
MOROGORO 25%
MTWARA 80%
MWANZA 47%
NJOMBE 50%
PWANI 14%
RUKWA 25%
RUVUMA 9%
SHINYANGA 86%
SIMIYU 14%
SINGIDA 33%
SONGWE 50%
TABORA 47%
TANGA 2%
15 | P a g e
2.4.2.10 Usimamizi Shirikishi uliofanyika;
Mkoa mmoja tu wa Geita ndio umefanya usimamizi shirikishi wa shughuli
za Lishe kwa zaidi ya 75%. Mikoa mingine imefanya usimamizi kwa chini
ya asilimia 75.
Chanzo: taarifa za Mikoa
2.4.2.11 Ukaguzi wa usafi na usalama wa vyakula;
Mikoa 10 ya Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza,
Njombe, Pwani, Simiyu na Tabora imeripoti kufanya ukaguzi wa vyakula
angalau mara moja katika kipindi cha mwaka 2017/18. Mikoa 16 iliyobaki
haijafanya kabisa.
16 | P a g e
2.4.3 Maazimio na Mapendekezo;
Baada ya mawasilisho yaliyoonyesha hali halisi ya utekelezaji wa afua za
Lishe washiriki wa Mkutano walipata wasaa wa kufanya majadiliano na
kuweka maazimio kadhaa ya kuhakikisha usimamizi na utekelezaji wa
shughuli za lishe unafikia kiwango cha kuridhisha na hatimaye
kupunguza tatizo la utapiamlo nchini.
Jedwali lifuatalo limeanisha maazimio yaliyofikiwa katika majadiliano ya
kutathmini utekelezaji wa Mkataba wa Lishe nchini:
17 | P a g e
Na. HOJA MAELEKEZO MUHUSIKA MUDA WA
MWISHO WA
UTEKELEZAJI
1 Kutosimamiwa kwa
karibu utekelezaji wa
Afua za Lishe kwenye
Mikoa na
Halmashauri.
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa
Mikoa waingie Mikataba ya usimamizi wa
afua za Lishe wenye viashiria 11 na Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa
Majiji/Manispaa/Miji/Halmashauri.
Katibu Tawala
wa Mkoa
30 Septemba,
2018
2 Kutoingizwa kwa
shughuli za lishe za
wadau kwenye
Mipango ya Mikoa na
Halmashauri. Pamoja
na kutenga fedha
kutoka vyanzo vya
ndani na kuzitoa ili
kutekeleza afua za
lishe.
Wadau wote wanaotekeleza afua za lishe
wasimamiwe na kuhakikisha shughuli zao
zinaingizwa kwenye mipango ya Mikoa na
Halmashauri wakati wa kufanya mapitio ya
mipango mwezi Disemba 2018. Aidha, kila
mwaka wa fedha mipango yote ya wadau
iwe sehemu ya MTEF’s za Mikoa na
Halmashauri na fedha zinazopangwa
zitolewe kama zilivyowekwa kwenye bajeti.
Kutenga na kutoa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa afua za lishe. Kamati za fedha
zisimamie na kutoa taarifa ya utekelezaji wa
afua za lishe na matumizi ya fedha
Katibu Tawala
wa Mkoa na
Wakurugenzi
Watendaji wa
MSM
31 Januari,
2019
Katika kutenga
fedha ni kila
mwaka wa
mpango na
bajeti
18 | P a g e
zilizotumika katika kutekeleza afua hizo
Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa wakati
Kwa kamati za
fedha ni kila
robo ya
utekelezaji
3 Wadau wanaofanya
shughuli za Afya na
Lishe kutotambulika.
Mikoa kusimamia na kutambua (Mapping)
wadau wote wanaotekeleza afua za Afya na
Lishe kwenye Mikoa yao.
Katibu Tawala na
Wakurugenzi
Watendaji wa
MSM
1 Disemba,
2018
4 Kutofanyika kwa
vikao vya kamati za
lishe katika Mikoa na
Halmashauri kwa
mujibu wa miongozo
Vikao vya kila robo vya kamati ya lishe
viwekwe kwenye Kalenda ya vikao ya
Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na
vifanyike kwa mujibu wa ratiba hiyo.
Aidha, vikao vya kamati ya lishe vijadili
taarifa za lishe kabla hazijawasilishwa katika
ngazi inayofuata na pia mikutano
mbalimbali itumike katika kujenga uelewa
wa pamoja kuhusu masuala ya Lishe nchini
KatibuTawala wa
Mkoa na
Wakurugenzi wa
MSM
30 Septemba,
2018
19 | P a g e
5 Kutokufanyika kwa
usimamizi shirikishi
katika afua za Lishe
Ngazi zote (Mikoa na Halmashauri) kufanya
usimamizi shirikishi kwa kila robo ya
mwaka kwa mujibu wa miongozo.
Katibu Tawala
wa Mkoa na
Mkurugenzi wa
MSM
Kila robo
mwaka.
6 Wadau kutowasilisha
taarifa ya utekelezaji
ya afua za lishe
kwenye Mikoa na
Halmashauri
Taarifa za utekelezaji wa afua za lishe
zinazofanywa na wadau ziwasilishwe
kwenye Mikoa na Halmashauri kila robo
kwa ajili ya tathimini na ufuatiliaji.
Makatibu Tawala
na Wakurugenzi
Watendaji wa
MSM
Kila robo
mwaka.
7 Vikao mbalimbali
kutojadili masuala ya
lishe.
Lishe iwe Ajenda ya kudumu katika vikao
vya RCC, DCC, CMT na vikao vingine
tendaji. Aidha, vikao hivyo vitumike katika
kuwawezesha viongozi wa ngazi mbalimbali
kupata uelewa wa pamoja katika utekelezaji
wa afua za Lishe.
Mkuu wa Mkoa
na Mkuu wa
Wilaya
Endelevu
20 | P a g e
2.5 Changamoto katika uchakataji wa taarifa za mkataba;
Taarifa zilizopokelewa kuwa na mapungufu ya kitakwimu hivyo
kukosa ubora
Ucheleweshaji wa taarifa kufikia Wizara kwa wakati kwa mujibu wa
taratibu.
Taarifa kutojadiliwa katika mamlaka husika za Mikoa na
Halmashauri.
Kutotekelezwa kwa ufanisi kwa baadhi ya viashiria ndani ya
Mkataba wa Lishe.
2.6 Maeneo ya kuboresha;
1. Mipango na bajeti kuzingatia matatizo yaliyopo katika Halmashauri
na Mkoa husika.
2. Kuendelea kuwajengea uwezo Maafisa Lishe na watoa huduma juu
ya ubora katika ukusanyaji na utoaji wa taarifa.
3. Kutumia mifumo iliyopo kupata taarifa sahihi mf. Epicor, DHIS n.k
HITIMISHO;
Kwa ujumla baada ya tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa kusimamia
shughuli za Lishe kulingana na viashiria pamoja na vigezo vilivyowekwa
matokeo yake si ya kuridhisha japo kuna baadhi ya Mikoa imeonyesha
mwelekeo mzuri kwenye utekelezaji. Hivyo, OR TAMISEMI itaendelea
kusimamia kwa ukaribu utekelezaji na itaendelea kufanya tathmini ndani
ya miezi sita ili kupima mafanikio yanayofikiwa.