Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    1/11

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    OFISI YA RAIS

    SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

    Kumb. Na EA.7/96/01/H/34 23 Januari, 2015

    TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa

    mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa

    na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,

    pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea

    katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

    Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa

    Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 121 za kazi kwa ajili ya Wizara,

    Idara zinazojitegemea, Wakala wa serikali na Mamlaka za serikali za mitaa

    NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

    i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

    ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

    iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia

    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za

    kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

    iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili

    kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

    v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye

    anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.

    vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato

    cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu

    mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe

    sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

    - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

    - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

    - Computer Certificate

    - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

    - Picha moja Passport size ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    2/11

    vii. Testmonials, Provisional Results, Statement of results, hati matokeo za

    kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

    HAVITAKUBALIWA.

    viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

    kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

    ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa

    kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

    x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika

    Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika

    Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

    xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za

    kisheria.

    xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 Febuari, 2015

    xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira

    HAURUHUSIWI.xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe

    kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

    Katibu, AU Secretary,

    Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment

    Utumishi wa Umma, Secretariat,

    SLP.63100, P.O.Box 63100

    Dar es Salaam. Dar es Salaam.

    1.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FOREST OFFICER GRADE II)NAFAS 5

    1.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.

    Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili

    isiyozidi hekta 10,000.

    Kufanya utafiti wa misitu.

    Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.

    Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.

    Kukusanya takwimu za misitu.

    Kufanya ukaguzi wa misitu.

    Kupanga na kupima madaraja ya mbao.

    Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.

    Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu

    ya miti na kwa wananchi.

    Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.

    Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.

    1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine auVyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    3/11

    1.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.

    2.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA IIINAFASI 72.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi

    Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi

    Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha

    Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori

    Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali

    Kufanya usafi na ulinzi wa kambi

    Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi

    Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani

    Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na

    kukusanya takwimu zao

    Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi

    Kudhibiti wanyamapori waharibifu

    Kudhibiti moto kwenye hifadhi

    Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

    2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada au

    Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Technician or BasicTechnician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya

    Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

    2.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi

    3.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER

    GRADE III)NAFASI 30

    3.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika

    kata na atashughulikia masuala yote ya kata

    Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,

    mali, kuondoa njaa na Umasikini.

    Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.

    Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na

    vitongoji.

    Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata

    yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika

    Kata.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    4/11

    Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo

    lake.

    Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya

    Kata.

    Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na

    nakala kwa Katibu Tarafa.

    Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji

    wa vjiji, na NGOS katika kata yake.

    Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,

    vitongoji, na kata yake.

    3.2 SIFA ZA MWOMBAJI.

    Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na mwenye cheti cha Mafunzo ya

    Stashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Maendeleo

    ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango kutoka chuo cha Serikali zaMitaa Hombolo Dodoma au chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

    3.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.

    4.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGROOFFICERS)NAFASI 10

    4.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,

    Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,

    Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,

    Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,

    Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,

    Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,

    Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,

    Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,

    Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,

    Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao

    mengine,

    Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora, Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,

    Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,

    Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya

    kupitishwa,

    Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,

    Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,

    Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya

    kilimo cha umwagiliaji,

    Kufanya utafiti wa udongo, Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    5/11

    Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,

    Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi

    maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

    4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya

    sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo

    Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

    4.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS DKwa mwezi.

    5.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)

    NAFASI 12

    5.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,

    Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,

    Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,

    Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,

    Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,

    pembejeo za kilimo,

    Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka

    ngazi ya halmashauri,

    Kukusanya takwimu za mvua,

    Kushiriki katika savei za kilimo, Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za

    kutumia,

    Kupanga mipango ya uzalishaji,

    Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,

    Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhifadhi,

    Kutunza miti mizazi,

    Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,

    Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,

    Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu, Kusimamia taratibu za ukaguzi,

    Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,

    Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,

    Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,

    Kutoa ushauri wa kilimo mseto,

    Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na

    Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.

    5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    6/11

    Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne au Sita (VI) wenye stashahada (Diploma)

    ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

    5.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS CKwa mwezi.

    6.0 MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II)NAFASI 5

    6.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu

    Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua

    takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)

    Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.

    6.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati au sifazinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye

    ujuzi wa kutumia Kompyuta.

    6.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwe

    7.0 AFISA UGAVI MKUU DARAJA LA I - NAFASI 1(INARUDIWA)

    Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)

    7.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kushauri juu ya Sera ya Ununuzi na Ugavi katika Wakala; Kushauri juu ya Mfumo wa Mtandao wa Ununuzi na Ugavi kwa kutumia kompyuta,

    e-procurement;

    Kutathmini taarifa ya vifaa vinavyotumika na Wakala ili kujua aina ya kasi ya vifaa

    husika kwa hatua zaidi;

    Kusimamia utayarishaji wa Mpango wa manunuzi wa Wakala;

    Kusimamia utayarishaji wa makisio ya vifaa vinavyohitajika katika Wakala;

    Kusimamia upimaji wa utendaji wa Maafisa Ugavi walio chini yake;

    Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora kutekeleza majukumu yanayohusu

    ununuzi, utunzaji na ugavi katika Wakala;

    7.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye Shahada ya Ugavi na Shahada/Stashahada ya Uzamili katika fani

    za Biashara au Ugavi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya

    Usimamizi wa Vifaa, na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi na mbili (12).

    7.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7kwa mwezi

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    7/11

    8.0 AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 1 (INARUDIWA)

    Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA)

    1.1.2 MAJUKUMU YA KAZI

    Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;

    Kutunza na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;

    Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;

    Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo;

    Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;

    1.1.3 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Legal Metrology au Legal

    and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au

    Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sanyansi ambao wamepata

    crash programme in Legal and Industrial Metrology isiyopungua miezi mine (4)

    kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au

    Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sayansi ambao wamehitimu

    Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka Chuo

    kinachotambuliwa na Serikali.

    Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu katika fani ya Legal Metrology / Legal and

    Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

    1.1.4 MSHAHARA Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS3kwa mwezi.

    9.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI)WATER RESOURCE ENGINEER

    NAFASI 6 (INARUDIWA)

    Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mamlaka za Serikali za

    Mitaa.

    9.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo

    ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za

    upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu

    mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.

    Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu

    ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.

    Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa

    miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya

    kupata ubora unaokusudiwa.

    Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi

    (project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.

    Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokezawakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    8/11

    Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.

    Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo

    ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.

    Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta

    ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya

    Wahandisi.

    9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water

    Resource Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

    9.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Ekwa mwezi.

    10.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) NAFASI 15(INARUDIWA)

    Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

    10.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili

    aweze;

    Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya

    miradi ya maji na usafi wa mazingira;

    Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji

    na usafi wa mazingira;

    Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umemevya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu

    wa pampu na kuzuia uharibifu;

    Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;

    Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye

    mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya

    uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.

    Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji

    na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa

    mazingira; Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

    10.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya

    mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na

    Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).

    10.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Akwa mwezi.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    9/11

    11.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT TECHNICIAN - WATER) NAFASI

    24 (INARUDIWA)

    Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

    11.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kupima uwingi wa maji mtoni

    Kusoma kituo cha hali ya hewa

    Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

    11.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka

    mmoja kutoka kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na

    Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III katika fani ya maji.

    11.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS Akwa mwezi.

    12.0 MHANDISI KILIMO II (IRRIGATION) - 1

    12.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.

    Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.

    Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.

    Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za

    umwagiliaji.

    Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji. Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji

    pamoja na matumizi ya maji.

    Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.

    Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na

    wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.

    Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.

    Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji

    ipasavyo.

    12.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya

    kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali.

    12.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    10/11

    13.0 MHANDISI KILIMO II (MECHANIZATION)1

    13.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.

    Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.

    Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.

    Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za

    umwagiliaji.

    Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.

    Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji

    pamoja na matumizi ya maji.

    Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.

    Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na

    wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.

    Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.

    Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezajiipasavyo.

    13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya

    zana za kilimo kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali.

    13.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaaniTGS Ekwa mwezi

    14.0 MHANDISI KILIMO II (LAND USE PLANNING)1

    14.1 MAJUKUMU YA KAZI

    Kuandaa programu za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo.

    Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.

    Kushiri katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji.

    Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za

    umwagiliaji.

    Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji.

    Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji

    pamoja na matumizi ya maji.

    Kuandaa mafunzo/maonesha ya matumizi ya zana za kilimo.

    Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na

    wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta.

    Kuwafundisha wakulima jinsi ya ujenzi wa vihenge bora.

  • 8/9/2019 Tangazo Nafasi Za Kazi - Utumishi.

    11/11

    Kushughurikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji

    ipasavyo.

    14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wenye shahada ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya

    matumizi bora ya ardhi (land use planning) kutoka chuo kikuu kinachotambuliwana serikali.

    14.3 MSHAHARA

    Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E wa mwezi

    X.M. DAUDISecretary

    Public Service Recruitment Secretariat