64
Tunatumaini kwamba utafurahia toleo hili kubwa la MATENDO! Tafadhali angalia uk. 63 kwa maelezo jinsi ya kuendelea kupokea matoleo ya MATENDO kwa njia ya posta - na kwa haraka zaidi kwa njia ya barua pepe ('email'). TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 Mwandishi Mch. Frank R. Parrish MATENDO “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu, asema Bwana wa Majeshi” (Zekaria 4:6) UPAKO WA ROHO MTAKATIFU

TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Tunatumaini kwamba utafurahia toleo hili kubwa la MATENDO! Tafadhali angalia uk. 63 kwa maelezo jinsi yakuendelea kupokea matoleo ya MATENDO kwa njia ya posta - na kwa haraka zaidi kwa njia ya barua pepe ('email').

TOLEO LA KISWAHILI

Nakala 16 / Nambari 1

Mwandishi Mch. Frank R. Parrish

MATENDO

“Si kwa uwezo,wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho

Yangu, asema Bwana wa

Majeshi” (Zekaria 4:6)

UPAKO WA ROHO

MTAKATIFU

Page 2: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mpendwa Kiongozi Mwenzangu wa Kanisa:Toleo hili la Gazeti la MATENDO juu ya

“Upako” limeandaliwa liwe somo la ndani nala ki-Biblia kuhusu hoja hii. Ili upate ufahamubora wa hoja hiyo nyeti, itakubidi utafakarikwa makini, ujifunze na kujibidisha kikamilifu.

Itakupasa utumie muda mrefu katikakujifunza somo hili. Huenda ujifunze kurasambili au tatu tu kwa siku. Lakininakuhamasisha sana ujitoe katika sala na bidii yakujifunza. Ukifanya hivyo, maisha yako na utumishiwako vitabadilishwa!

Mimi nilikuwa mtumishi kwa muda mrefu kablasijatambua hamu ya Mungu kwamba upako wa RohoWake uwepo katika maisha yangu na utumishi wangu.Nilipofungua moyo wangu na kumruhusu Mungu“afungue macho ya ufahamu wangu” (taz. Waefeso1:18), nilibadilishwa! Utumishi wangu ulibadilishwa!Uwepo na uweza wa Roho Mtakatifu ulidhihirika nakutendeka zaidi sana ndani yangu, na kupitia kwamaisha yangu na utumishi wangu.

Matunda mengi zaidi yalionekana katika utumishiwangu. Nilitambua uwepo wa Mungu kwa ndani zaidikabisa kuliko zamani zote. Maisha yangu hayakuwarahisi zaidi; lakini niliona uwezo wa kuwa zaidi yamshindi kwa Kristo anipendaye (taz. Warumi 8:37).

Ninataka kukutia moyo sana ujibidishe kamamfanyakazi mwaminifu na madhubuti katika kujifunzasomo hili. Yafuatayo ni maagizo ya kimatendoyatakayokusaidia kufanya hivyo:

Kwanza, nimetaja mistari mingi ya Biblia katikamafunzo haya yote. Tafadhali tumia muda wa kutafutana kusoma kila mstari wa Maandiko uliotajwa.Kufanya hivyo kutakusaidia katika malengo kadhaayaliyo muhimu sana: 1) Wewe kama kiongozi wakanisa, wakati wowote usipokee hivi hivi kila fundishounalosoma au kulisikia, haidhuru limetokea wapi.Wakati wote uchunguze Maandiko mwenyewe(Matendo 17:11); 2) Kama kiongozi wa kanisa, nimuhimu kwako kuongeza ujuzi, uzoefu na ufahamuwako wa Maandiko (2Timotheo 2:15-18). Kufanyahivyo kutakulinda mwenyewe na wale unaowaongozaili msidanganyike, na pia kutakufanya uwe mstadikatika Neno la Mungu; 3) Neno la Mungu peke yakelimethibitishwa na uweza wa Mungu (2Timotheo 3:16- 17;Waebrania 4:12-13; 2Petro 1:20-21). Ni utendaji wa

pamoja tu wa Roho Mtakatifu na Neno laMungu unaobadilisha moyo wa mwanadamu.

Pili, ukae na daftari na kalamu uandikekumbukumbu, maswali au mistari ya Biblia yakuchunguza baadaye. Mungu ataongea nawewe akikufunulia ukweli unapojifunza NenoLake. Mafunzo haya yawe safari ya kukuakwako binafsi, yenye kukusaidia zaidi sanakuliko kupokea mafundisho mazuri tu.

Mwisho, mtenda kazi mwenzangu mpendwa,nataka kukutia moyo uambatanishe na kujifunzakwako, kumwomba na kumngojea Bwana kwa wingi.Maana ni Roho Mtakatifu anayefunua ukweli, na asilina tabia ya Kristo (Yohana 14:17,26). Usiache mafunzohaya yahusiane na akili yako tu, kwa sababu ukifanyahivyo utafungia mengine ambayo ungaliwezakuyapokea. Ni kweli akili zetu ni karama ya Mungu,lakini bado zina mipaka (taz. 1Wakorintho sura ya 3na 4). Ufungue moyo wako, ukamruhusu RohoMtakatifu akufundishe wewe na kukutengeneza wewe.Unaweza kuwaongoza wengine mahali pale tu ambapowewe, mwenyewe, umekwisha fika. Kwa hiyo uombe,ujifunze na kufurahia mafunzo haya – nawe ukuekatika uweza wa upako wa Mungu hata katika kusomakwako!

Tafadhali pia uangalie jambo maalum tuliloongezakatika toleo hili la MATENDO. Kila mara kwa marakatika mafunzo yote, kutakuwa na viangalizo maalumkutoka kwangu kwa ajili yako. Hivi vimeandaliwa iliwewe kama kiongozi wa kanisa upate mtazamo wandani zaidi kuhusu kanuni fulani muhimu ya ki-Bibliakuhusu utumishi au kukua kwako binafsi. Viangalizohivyo hutambulika kwa kichwa “Mchungaji kwaMchungaji” navyo vimewekewa rangi ya kijivu nyumakusudi vionekane kwa urahisi zaidi.

Mchungaji, mimi ninakupenda katika Kristo, tenanaamini makusudi ya Mungu kwa ajili yako. Wewe uchombo kilichochaguliwa na Mungu, ili Yeye akutumiekwa ajili ya Ufalme na utukufu Wake, na katikakubariki Kanisa Lake. Ubarikiwe katika Jina la BwanaYesu Kristo. Mungu sasa akubariki, akupe uwezo naukuzi unapojifunza na kupokea kutoka kwa Neno Lakena Roho Wake!

Ndugu yako,Mch. Frank R. Parrish

Mkurugenzi, World MAP

2 • MATENDO

Upako wa Roho Mtakatifu

BARUA YA MWANDISHI – MUHIMU!Mwandishi Rev. Frank R. Parrish

REV.FRANK

PARRISH

Nakala 16 / Nambari 1

Page 3: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Kabla hatujaweza kuanza mafunzo haya kuhusu

“Upako”, yaliyo ya ki-Biblia na yenye ufanisi wake,

inatubidi tuweke msingi wa kanuni fulani muhimu.

Kanuni hizi zitatujengea jukwaa la kusimamia ambapo

tutaweza kupata mandhari au picha ifaayo ya upako.

Mafungu ya kwanza ya mafunzo hayo yatahusiana na

kanuni hizo za kimsingi. Huenda ni mapya kwako, au

pengine umekwisha kuyazoea. Lakini ni muhimu sana tuwe

na msingi wa pamoja wa kujengea mafunzo hayo. Nakuomba

ujifunze kanuni zifuatazo kwa makini. Umruhusu Roho

Mtakatifu apate muda wa kutosha ili afunue, kuthibitisha,

kupima na kuyakinisha kiasi gani kanuni hizo zimejengwa na

kujulikana katika maisha yako na utumishi wako.

Kiongozi mwenzangu, haya si mafunzo ya kupevuka

“kimkato”. Pia hayakupatii utaratibu mwepesi wala ufundi

maridadi utakaokufanya “maarufu”.

Kinyume chake, mafunzo hayo ni ya ki-Biblia yahusuyo

jinsi inavyotubidi sisi kama viongozi wa kanisa tukue na

kutenda kazi katika Ufalme wa Mungu. Njia ya upevu ni

mafuatano ya lazima ili tuwe na matunda halisi, na utumishi

unaodumu na kumletea Mungu utukufu mwingi!

Kwa hiyo, tujishughulishe kwa bidii tunapojifunza

kuhusu hoja hii ya upako. Mungu aweza kubariki yale tu

aliyoyaweka kama njia na mapenzi Yake. Kwa hiyo ni lazima

tuweke msingi imara wa kanuni zinazotokana na Neno Lake

kabla ya kuendelea na hoja zinazofuatana za upako (Isaya

28:10).

Utumishi Usio Na MipakaHoja ya UPAKO ni muhimu sana kwa kila mwamini wa

Yesu Kristo. Lakini ufahamu wa UPAKO – u nini,

unafanyaje, na jinsi tunavyoweza kukua na kutenda ndani

yake – ni wa lazima, hasa kwa wale walioitiwa utumishi wa

muda wote.

“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali nikwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.”

(Zekaria 4:6)

Mwandishi Rev. Frank R. Parrish

MATENDO • 3

UTANGULIZI

Upako wa RohoMtakatifu

Nakala 16 / Nambari 1

Page 4: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Inasikitisha kwamba UPAKO mara nyingi haufahamiki

vema au ni hoja ambayo viongozi wengine hata

wanajiepusha nayo. Ingawa ni karama ambayo Mungu

anataka kutupatia, viongozi wengi hawajui upako ni nini

wala jinsi ya kuupokea. Kwa hiyo, wanajaribu kuvipatia vitu

vingine nafasi ya upako wa Roho Mtakatifu.

Viongozi fulani huwa na ustadi katika utawala au

utaratibu. Huenda wanajiongezea elimu, wakiweka cheo, jina

au digrii katika majina yao. Wanahudhuria mikutano mingi

na kuhuishwa na wahutubu wakuu. Pengine wanakuza

vipawa vyao binafsi vya kuhutubu au kuimba ili

wawaongoze au kuwahamasisha watu kwa ufanisi zaidi.

Mambo yaliyotajwa hapo huenda si mabaya yenyewe,

tena yanaweza yasaidie au yasisaidie katika utumishi.

LAKINI HAYA SI UPAKO! Wala hayawezi kuwepo badala

ya upako halisi wa Roho Mtakatifu katika maisha ya

mtumishi.

Elimu na ustadi katika utawala huweza kufaa na

kusaidia. Lakini huwa na mipaka katika kumsaidia kiongozi.

Tunapotegemea elimu yetu, matokeo bora tunayoweza

kutumainia hulingana na upeo wa elimu yetu.

Tunapotegemea ubora wetu wa kuhutubu au ustadi

mwingine, tunafungiwa mipaka ya uwezo wake.

Lakini, tunapomtegemea Roho Mtakatifu,

tunawekewa mipaka ya uweza wa Roho Mtakatifu tu!

Tunayochagua kutegemea, au kuamini, ili tutekeleze

wito wetu wa utumishi – ndiyo yatakayoweka mipaka ya

uwezo wetu. Je, unataka mipaka kiasi gani katika utumishi

wako?

Kwa Mungu, hakuna mipaka (taz. Luka 18:27)! Kwa

hiyo, nikimwamini na kumtegemea Mungu katika uweza

Wake, mipaka yangu peke yake katika utumishi ni mapenzi

ya Mungu na makusudi Yake kwa ajili yangu (Wafilipi 4:13).

Ni mapenzi ya Mungu kwa ajili ya kila mwamini

aliyezaliwa mara ya pili kwamba adhihirishe matunda ya

Roho (Wagalatia 5:16-26) katika mwenendo na matendo

yake. Matunda ya Roho ni tabia ya Kristo. Aina hii hii ya

tabia hutakiwa hasa kwao walioitwa wawaongoze wengine

katika Mwili wa Kristo. Ni kazi ya kiongozi kuwa mfano wa

mwenendo wa kiuchaji kwao anaowaongoza (1Wakorintho

11:1; Wafilipi 3:17; 1Timotheo 4:12). Hakuna karama, ustadi

wa kutawala, wala ujuzi wa kuhubiri au kufundisha

vinavyoweza kuwepo badala ya unyofu na tabia ya kufanana

na Kristo.

Ni mapenzi ya Mungu pia – hasa kwao wanaoitwa ili

waongoze – kwamba tuwe na uweza upitao akili zetu wa

ki-Mungu wa Roho Mtakatifu. Yesu aliwaambia wanafunzi

Wake: “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni miminiliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazaematunda; na matunda yenu yapate kukaa” (Yohana 15:16).

Kutokana na mstari huu tunaona kwamba Yesu anataka

matunda ya maisha yetu yadumu. Yatawezaje kufanya hivyo?

Utumishi wetu unapojaa uweza wa upako wa Mungu –

uweza wa Roho Mtakatifu – uweza Wake kupitia kwetuunatuwezesha kuongoza maisha ya watu kwa njia yenye

matunda yanayodumu.

Haidhuru kiongozi ana vipawa, talanta au akili kiasi

gani. Pasipo kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, kiongozi

hawezi kutimiza mapenzi ya Mungu kwa njia ya Mungu

katika utumishi. Ni baraka kwetu kwamba Mungu anajua

4 • MATENDO

TOLEO LA KISWAHILITOLEO 16 / NAMBARI 1

Limetolewa na World MAP

CHENNAI, INDIA

YALIYOMO

UPAKO WA ROHO MTAKATIFU“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho

Yangu, asema Bwana wa Majeshi” (Zekaria 4:6)

Mwandishi Mch. Frank R. Parrish

Barua Ya Mwandishi – Muhimu! .................................2Utangulizi ........................................................................3

SEHEMU YA IUtangulizi Wa Ki-Historia Na Ki-Biblia Wa Upako ...9

SEHEMU YA IIAsili, Kusudi Na Matumizi Ya Upako ........................11

SEHEMU YA IIIKutembea Katika Apako .............................................35Kutazama Kwa Kifupi Ishara Na Maajabu...............54

Wahariri.........................................Frank & Wendy Parrish

Wahariri Kimataifa .........................................Gayla Dease

Mfasiri wa Kiswahili..................................Judie Mwarabu

Wahairi wa Kiswahili...........................................Sig Feser

Mhakiki wa Kiswahili: ................................Ndelilio Nnko

Gharama za Posta zimelipwa Chennai - 600 010 India

MAONO NA UTUME WA GAZETI LA MATENDO

Kuwapatia bure mafundisho ya Bibliana mafunzo yahuduma viongozi wa makanisa wa nchi za Asia, Afrika, naLatini Amerika ambao wanafundisha au kuhubiri neon laMungu (Biblia) kwa kundi la watu 20 au zaidi angalaumara moja kwa wiki.

MATENDO (ISSN 0744-1789) hutolewa mara nne kwamwaka na World MAP ACTS INDIA, 67 Beracah Road,Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA. Head office andcopyright: World MAP, 1419 North San Fernando Blvd.,Burbank, CA 91504-4194, U.S.A. Gharama za Posta zagazeti zimelipwa kule Arcadia, California na katika ofisinyingine za Posta. Maswali hupokelewa kwa anwani yahapo juu pamoja na Box 4142, Manila, Philippines; Box942, White River 1240, South Africa.

MKUU WA POSTA: Tafadhali utume mabadiliko yaanwani kwa World MAP ACTS INDIA, 67 Beracah Road,Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA. World MAP, 1419North San Fernando Blvd., Burbank CA 91504-4194,U.S.A. MATENDO ni gazeti linalotolewa bure, ambalohuchapishwa na kutumwa kwa viongozi wa makanisa.

MATENDO

Nakala 16 / Nambari 1

Page 5: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

mahitaji yetu vizuri sana kuliko sisi tujuavyo wenyewe. Na

Yeye amekwisha kutupatia uweza Wake utusaidie katika

kutimiza wito Wake ulio tukufu.

Sura Pasipo UwezaKuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo

ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu

umefungiwa mipaka. Huduma hizi huenda zinavuta umati

mkubwa wa watu, tena zina vituo na vifaa vya hali ya juu na

tamasha za kusisimua. Lakini kama uwepo na uweza halisi

wa Roho Mtakatifu hauonekani wala kukaribishwa,

mikutano yake huenda itakuwa sherehe za kidini zisizo na

uhai wowote.

Ukumbi au uwanja mkubwa hujaa umati mkubwa sana

wa watu, huwa na vifaa vya kisasa na ratiba ya kusisimua

kwa ajili ya mechi ya kandanda tu. Lakini mambo haya ya

kimwili au ya nje hayana uhusiano wa maana na kuwafanya

watu wawe wanafunzi wanaomfuata Yesu Kristo kwa bidii!

Katika historia ya Kanisa, kuna maeneo mengi duniani

ambapo Mungu alitenda miujiza na mambo mengine makuu

akitumia wanadamu waliojitolea kama vyombo Vyake.

Makanisa mengi ya maeneo haya na hata maeneo yenyewe

makubwa, zamani yalijulikana kwa ajili ya uwepo wa

Ukristo wenye uhai na uwezo. Inasikitisha kwamba leo

maeneo hayo yamo ndani ya giza ya kiroho. Pale Kanisa la

zamani lilipositawi na kuwa na uongozi mkubwa, sasa ni

patupu pasipo nuru ya Injili.

Kati ya makanisa ya aina hii yanayojulikana zaidi katika

historia ya Agano Jipya ni yale ya Asia Ndogo (sasa taifa la

Uturuki). Habari za makanisa haya hupatikana katika kitabu

cha Ufunuo. Kwa kawaida hujulikana kama “Makanisa Saba

ya Ufunuo”.

Makanisa hayo yalisifiwa kuwa ngome kuu zenye uwezo

kwa kazi ya ukombozi ya Kristo katika mioyo ya watu.

Miujiza mingi ilitendeka hapo (soma Kitabu cha Matendo).

Lakini leo, watalii wanatoa fedha ili watembee kati ya

magofu ambapo mitume wale wakuu walipohubiri Neno la

Uzima. Sehemu hizi sasa hazina uhai wala uwezo wowote wa

Injili.

Ilitokeaje basi kwa hayo makanisa na hizi huduma

ambavyo zamani vilikuwa vikuu? Magofu haya matupu,

yanayotumiwa sasa na ndege wa angani tu, yamesimama

kama onyo na mafundisho kwetu sisi sote.

Haya ndiyo tunayoweza kujifunza: Wakati wowoteambapo viongozi wa kanisa wanaanza kutegemea uwezowao, au mapokeo, vyeo, siasa za kikanisa, au hata elimu naujuzi wa kimasomo – badala ya kumtegemea RohoMtakatifu wa Mungu na kweli za milele za Neno Lake –ndipo uhai na uweza wa Mungu unapoanza kutoweka kwetusisi kama viongozi, na pia kwenye huduma au makanisaambayo Mungu ameweka chini ya uongozi wetu.

Kanisa Ni Nini?Roho Mtakatifu alimwezesha Paulo ashughulikie hali ya

kanisa (taz. 1Wakorintho sura ya 3). Kanisa la Korintho

lilikemewa kwa ajili ya kugombana kwao katika hali ya

kimwili, kitoto na kibinafsi. Watu walikuwa wakigawanyika

katika vikundi kwa ajili ya kujipatia nafasi ya kutawala

wengine kana kwamba ni wakubwa wao (3:1-4). Hali hii

ilikuwa, na hata leo bado ndiyo, kiburi cha kujisifu – yaani

dhambi ya ibilisi (1Timotheo 3:6). Huu mwenendo wa kiburina hii bidii ya kujitegemea ya kibinadamu bado huzuia

ufanisi wa kuzaa matunda katika Kanisa leo.

Paulo anaendelea kutamka wazi kwamba Mungu ndiye

Peke Yake anayewezesha Kanisa likue kikweli. “Hivyo,apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye”

(1Wakorintho 3:7).

Kuna MSINGI MMOJA tu ambao Kanisa linaweza

kujengwa juu yake: Yesu Kristo aliye Jiwe Kuu la Pembeni

(1Wakorintho 3:10-11; taz. pia Waefeso 2:20-22). Hili ndilo

Jiwe letu Kuu la Pembeni kwa Kanisa la leo, vile vile kama

lilivyokuwa wakati Kanisa lilipozaliwa zaidi ya miaka elfu

mbili iliyopita!

Kiini Cha KanisaMatumizi ya jiwe kuu la pembeni katika ulimwengu wa

zamani yalikuwa ya kipekee kabisa, nayo yatatusaidia

tufahamu vizuri zaidi sababu ya Yesu kuitwa “jiwe kuu lapembeni” (Mathayo 21:42).

Katika Mashariki ya Kati wakati wa zamani, nyumba na

majengo mengine yote yalijengwa kwa njia ile ile. Jiwe moja

liliwekwa kwa vipimo vilivyofuatwa kwa uangalifu, nalo

lilikuwa jiwe kuu la pembeni. Halafu jengo lote liliendelea

kupimiwa ukubwa, ramani na uwekaji, kufuatana na

kulingana na jiwe kuu lile pekee la pembeni.Huu ndio mfano uliotumiwa na Roho Mtakatifu kupitia

kwa Paulo akionesha ukuu wa Kristo kwa ajili ya kujengwa

kwa Kanisa lililo hai. Ni la mawe yaliyo hai, yanayokua na

kuhuishwa kiroho, ambayo yamejengwa kulingana na Jiwe

Kuu la Pembeni la wokovu katika Yesu Kristo (1Petro

2:4-10). Hakuna sehemu nyingine yoyote itakayokaa sawa

wala kunyoka pasipo Jiwe hili likaalo kama kiini cha Kanisa.

Sisi kama viongozi wa kanisa tumeitwa tuwe washirika

wa Kristo katika kutii makusudi na mipango Yake tukisaidia

kujenga Kanisa la Mungu lililo hai. Kanisa la Agano Jipya –

Kanisa la Kristo – ni kundi la watu waliopata ufahamu wa

wokovu katika kumwamini Yesu Kristo. Neno “kanisa”

katika Agano Jipya halimaanishi utaratibu wa kiutawala,

vyeo, majengo wala madhehebu. “Kanisa” ni watuwaliookolewa na kuhesabiwa haki kwa imani katika Kristo,

na ambao wanaendelea kuwa wanafunzi wanaopevushwa.

MATENDO • 5

Kutangaza Neno la Uzima

Nakala 16 / Nambari 1

Page 6: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Uzao Halisi Wa MatundaMajina mengine ya Agano Jipya yanayofafanua Kanisa

ni pamoja na: “Mawe yaliyo hai” (1Petro 2:5); “Mwili waKristo” (1Wakorintho 12:27); “shamba”, “jengo” au

“hekalu” la Mungu (1Wakorintho 3:9,16-17). Majina haya

yote yana uhusiano mmoja: yote yanawahusu watu ambao ni

waamini wa kweli wa Yesu Kristo.

Ni muhimu kabisa kuyaelewa haya. Sisi kama viongozi

wa kanisa, tumeitiwa zaidi ya kufuata utaratibu wa kutawala

kanisa, kusimamia majengo mapya, au kuandaa matamasha

na matukio ya kikanisa. Sisi tumeitwa tuwe washiriki wa

Mungu katika kuwafunza na kuwajenga watu.

Tumeitwa na Mungu tulichunge na kulilea Kanisa lililo

hai la Mungu aliye hai, yaani watu wanaoamini –

tukiwasaidia wawe wanafunzi wanaokua wa Yesu Kristo.

Hatuwezi kutekeleza wito huu wa kuwa mawakili bila

msaada na uweza wa Mungu (taz. Zaburi 127:1).

Mungu atatuwajibisha kuhusu jinsi tulivyojenga juu ya

Msingi Mmoja yaani wokovu kwa njia ya Kristo

(1Wakorintho 3:12-23). Je, sisi tunavuta umati wa watu

kutokana na ubunifu wetu, nguvu na akili zetu? Njia hii

inaweza kuonekana kuwa na ufanisi kwa muda, lakini

haitaleta matunda ya kudumu ambayo Mungu anayatafuta

(Yohana 15:5,8,16).

Au badala ya haya, je, sisi tunajitoa kwa Roho wa

Mungu kila siku na kujisalimisha kwa mapenzi Yake? Je,

tunaongozwa na Yeye kama wana wa kweli wa Mungu

(Warumi 8:14), tukimtegemea kwa ajili ya kila dakika ya

utumishi ambayo anatukubalia? Kama ndivyo, basi kwa

uweza na msaada Wake, tunaweza kuwa na matunda ya

kweli, na matunda yetu yatakaa milele (Yohana 15:16).

Tafadhali ufahamu kwamba matunda na uzazi wakehavikuainishwa na Mungu jinsi akili ya kibinadamu awezavyo

kuviainisha. Wanadamu huenda wasema kwamba uzazi wa

matunda ni kuwa na wafuasi wengi, au kupata kuwa tajiri na

mwenye kusikilizwa. Hekima ya kibinadamu huweza

kuuainisha kama umashuhuri, uwezo wa kutawala au ufanisi.

Lakini uzazi wa kweli wa matunda kwa maoni ya Mungu

huainishwa na kupimwa kufuatana na kipimo kimoja tu:

maisha ya watu wanaogeuzwa katika mfano na tabia yaKristo jinsi wanavyopevuka kama wanafunzi Wake.Kufahamu kanuni zifuatazo kutakusaidia kushikamana na

ukweli wa kuainishwa huku.

Kurejezwa Upya Katika Mfano WakeBinadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu (Mwanzo

1:26-27). Mfano huu si wa kimwili hasa, bali ni mfano katika

uwezo na ustadi. “Mfano” katika maana hii ya ki-Biblia

huhusiana na akili na kutafakari, hisia na ubunifu, na uwezo

wa kuchagua. Tuliumbwa na uwezo wa kupenda, kujitolea na

kutambua yaliyo mema, ya kweli na ya haki.

Kwa nini Mungu alituumba hivi? Mungu alituumba kwa

kusudi moja: kwa ajili Yake Mwenyewe, ili tuwe na uhusiano

na Yeye. Ndio wito wetu mkuu kabisa! Kama Mungu

angalihitaji au kutamani kuwa na malaika wengi zaidi,

angaliwaumba wengine. Lakini badala yake, tunaona katika

Biblia nzima kwamba Mungu alitaka wana wa kiume na wa

kike ambao wangekuwa na uhusiano wa karibu katika

kupendana na Yeye.

Lakini uwezekano wa uhusiano huu na Mungu

uliharibika wakati dhambi ilipoingia ulimwenguni kutokana

na uasi wa kimakusudi wa Adamu na Hawa. Uasi wao

uliwaletea dhambi wanadamu wote (Warumi 5:12-21).

Lakini wakati ule, mpango wa ajabu wa Mungu kwa ajili ya

kukomboa uhusiano Wake na binadamu ulianzishwa

(Mwanzo 3:15: “Uzao wake” unamaanisha hatimaye

kufanywa mwili na kuzaliwa kwa Mungu Mwana, yaani

Yesu).

Ulipowadia utimilifu wa wakati (Wagalatia 4:4-5),

Kristo alikuja duniani akafa kwa ajili ya dhambi zetu. Tendo

Lake la kujitoa dhabihu lilifungua uwezekano wa kurejeza

uhusiano wetu na Mungu Mwumbaji wetu, uliokuwa

umeharibiwa na dhambi. Tunapopokea kazi ya Kristo ya

wokovu na kwa njia ya kumwamini Yeye, dhambi zetu

zinaweza kusamehewa, nasi tunaweza kumjua Mungu na

kushirikiana na Yeye.

Kazi Ya KubadilishwaLakini zaidi ya haya, Mungu anataka pia kutuweka huru

na matokeo ya dhambi, na uharibifu wake katika maisha yetu.

Kwa hiyo, matokeo ya moja kwa moja ya wokovu wetu

katika Kristo ni kwamba Mungu anaanza kufanya kazi katika

maisha yetu akitugeuza na kuturejeza katika “mfano” ule

ambao alituumba nao.

“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tanguasili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye [Yesu

Kristo] awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa nduguwengi” (Warumi 8:29). Mstari huu unafunua kwamba ni

mapenzi yalioamriwa awali ya Mungu kuwa sisi tunaomjia

Kristo katika wokovu tubadilishwe ili “[tu]fananishwe namfano wa Mwana wake”.

Kazi hii ya kugeuzwa inaanza na wokovu na kuendelea

katika maisha yetu yote. Mungu ni mwenye hekima

isiyokoma. Aliunda Ufalme Wake ufuate njia fulani kwa

sababu maalum. Tunapogeuzwa zaidi katika “mfano” wa

uumbaji wetu wa asili (mfano wa Mwana Wake), mambo

mawili maalum yatatendeka:

6 • MATENDO

Kufanya wawe wanafunzi na kuimarisha imani yao.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 7: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

1) Tutaweza kutembea katika uhusiano na Mungu usio

na vizuizi, unaoingia ndani zaidi wakati wote. Ni dhambi

iliyoharibu na inayoendelea kuharibu uhusiano wetu na

Mungu. Kwa hiyo, tunapowekwa huru na dhambi na

matokeo yake, tunapata uwezo zaidi wa kushiriki uhusiano

na Mwumbaji wetu ulio na upendo na undani zaidi.

2) Tutarejezwa katika nafasi na lengo vilivyokusudiwa

na Mungu kwa ajili yetu. Binadamu hakuumbwa katika

dhambi wala kwa ajili ya dhambi. Tuliumbwa katika

utakatifu, usafi na utakaso. Uumbaji wote wa asili wa Mungu

ulikuwa mema. “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, natazama, ni chema sana” (Mwanzo 1:31).

Hatukuumbwa na mapungufu yoyote, lakini dhambi

iliharibu uzuri wa ule mfano wa kwanza. Kwa hiyo,

tunapowekwa huru na dhambi na kugeuzwa ili tuwe pia huru

zaidi na matokeo ya dhambi, hatima yake itakuwa furaha,

amani na uhuru zaidi katika maisha yetu. Pia tutakuwa

tumeandaliwa vizuri zaidi kabisa kutimiza mapenzi na

makusudi ya Mungu.

Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba

mageuzi binafsi ni kipaumbele cha Mungu kwa ajili ya

kila mtu pekee. Tunaweza kuainisha maana ya mageuzi

hapa hivi, “kufananishwa zaidi na Yesu katika mawazo,

mapenzi na matendo yetu”.

Kubadilishwa Kwa Uwezo Wa Roho MtakatifuTunapookolewa, maisha yetu ya zamani yamepita.

Tunaanza mafuatano ya mambo yote yakigeuzwa yawe

mapya (2Wakorintho 5:17). Kwa uweza wa Roho Mtakatifu

na Neno la Mungu tunabadilishwa katika “mfano wa Mwanawake” (Warumi 8:29).

Kazi hii ya kimwujiza ya mabadiliko haiwezi kutimizwa

kwa nguvu yetu wala bidii zetu binafsi (Yeremia 13:23).

Tunaweza kujirekebisha katika mambo madogo, ambayo kwa

kawaida ni ya nje tu. Tunaweza kufanya kazi kwa bidii

tukijaribu kubadilisha maisha yetu na kuendeleza tabia njema.

Lakini kuna kazi ya ndani zaidi sana tunayohitaji kabisa,

kama vile: uponyaji wa kuvunjika na kuumia; ukombozi

katika kukataliwa na aina nyingine za utumwa; uhuru kutoka

katika mienendo yetu ya ubinafsi na dhambi. Aina hii ya

mabadiliko huwezekana kwa uweza wa Roho Mtakatifu peke

yake (Warumi 8:1-11; taz. pia Mathayo 19:23-26; Waefeso

2:1-10; Waebrania 9:13-14).

Mungu anatutakia tukue na kupevuka baada ya kumjia

Kristo kama Mwokozi wetu. Ingawa neema Yake na

msamaha Wake ni kweli kwa wakati wote (1Yohana 1:9), si

kisingizio cha kuendelea katika dhambi au mwenendo wa

kibinafsi. Mungu anasamehe kujikwaa au kuanguka kwetu

mara kwa mara; lakini lazima tusiendelee katika dhambi ile,

bali tusogee mbele katika kutembea kwetu na Mungu

(Luka 9:23-26).

Ukweli ni kwamba watu wanaokataa kubadilishwa au

wanaopinga kazi ya Roho Mtakatifu ya kuwabadilisha

wamemwasi Mungu (Yakobo 1:21-25). Hukumu ya Mungu

juu ya maasi ni kali sana (Mithali 29:1; Waebrania 3:8-11).

Matunda Ambayo Mungu AnatakaMaana ya kuwa mtumishi wa Injili anayezaa matunda

ni kwamba maisha ya wale watu unaowahudumia

yanageuzwa kufuatana zaidi na mfano wa Yesu. Ukumbuke

kwamba kuzaa matunda hakuhusiani na umati wa watu wala

takwimu. Ni rahisi kuingiza watu wengi katika kanisa lako.

Uwape chakula, nguo au fedha pasipo malipo nawe utapata

umati! Au uwape tamasha, ukiwaambia mambo

yanayofurahisha “masikio ya utafiti” (2Timotheo 4:3-4)

wapate kujisikia vizuri.

Lakini umati si usharika, kundi wala jamii. Mkusanyiko

mkubwa wa watu si uthibitisho kwamba una kanisa la Agano

Jipya lenye afya, wala kwamba wewe unafanya wanafunzi!

Swali tunalopaswa kujiuliza kila wakati kuhusu utumishi

wetu ni hili: “Je, maisha ya watu ninaowatumikia

yanabadilishwa wafanane zaidi na Yesu?” Je, lengo lako ni

kuwa na watu wengi zaidi katika kanisa lako tu, au ni kupata

wanafunzi wa kweli wanaopevuka na kukua katika Kristo?

Haidhuru wakiwepo watu kumi au watu elfu moja – wewe

unazaa matunda ikiwa watu wako wanazidi kufanana na

Yesu!

Aina Ya Udhaifu InayofaaTumethibitisha kwamba kugeuzwa katika mfano wa

Kristo ni mapenzi ya Mungu kwa wafuasi wote wa Kristo.

Tunajua kwamba hali hii haiwezi kutimizwa kwa bidii za

kibinadamu, ila tu kwa uweza na uwepo wa Roho Mtakatifu.

Hali hiyo inatufundisha nini basi kuhusu uendeshaji wa

utumishi tuliopewa na Mungu?

Kwa urahisi, tufahamu hili: Uweza unaoonekana wazi

wa Roho Mtakatifu, akifanya kazi na kuongoza pasipo

kuzuiwa ndani ya mwanadamu aliyejitoa, ndio

utakaoleta mageuzi makuu katika maisha ya mtu

mwingine.

Huenda ukweli huu unaonekana kuwa dhahiri mno!

Lakini je, mara ngapi bidii zetu binafsi zenye nia njema

zinachukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu kati yetu?

Tukiwa wanyofu kama viongozi na kujichunguza kwa

makini, inatubidi tukiri kwamba mara nyingi sisi ndio tatizo.

Hatuendelei muda mrefu katika utumishi pasipo kutambua

kwamba hatuna uwezo wa kutimiza kazi. Kwa hiyo

tunajishughulisha na mipango, elimu na njia nyingine

MATENDO • 7

Roho Mtakatifu atagusa mwinginekupita kwako.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 8: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

zinazotakiwa zilete ushindi au ufanisi. Lakini ukweli ni

kwamba ndani yetu sisi hatuna uwezo wa kutimiza yote

Mungu anayotaka kufanya! Je, unaweza kukiri hali hii juu

yako binafsi?

Kama viongozi, tunataka tufikie upeo wa uwezo wetu

wakati wote. Lakini bidii zetu za juu kabisa za kibinadamu

hazitoshi kwa ajili ya kutimiza mapenzi na makusudi ya

Mungu.

Haya huenda yanaonekana kuwa habari mbaya. Lakini

hali halisi – kama tu tayari kuikubali na kuipokea – ni

kwamba upungufu wetu ni chanzo cha habari njema! Angalia

yale mtume mmoja mkuu kabisa aliyoandika kuhusu

kitendawili hiki:

“Kwa ajili ya kitu hicho [“mwiba katika mwili” wa

Paulo, ms. 7] nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uwezawangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifuwangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juuyangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, namisiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maananiwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu” (2Wakorintho

12:8-10).

Paulo hakukubali mwelekeo wa kushindwa, wala

hakufikiri kwamba alikuwa akiadhibiwa na Mungu. Bali,

Paulo alifurahia mafunuo yake na utendaji wa neema ya

Mungu yenye ushindi katika maisha yake binafsi!

Ni kwa neema ya Mungu kwamba tuna uhai na ushindi

wa washindaji (Warumi 8:37). Lakini kujitoa kabisa na kukiri

wazi haja yake ndiko kulikomfungulia Paulo njia na kuachia

uweza wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yake na kupitia

kwake.

Paulo hakujaribu kuficha au kufunika udhaifu wake, bali

alisema: “nitajisifia udhaifu wangu” (ms. 9) na “napendezwana udhaifu” (ms. 10). Maana katika hali hii hasa Paulo

alitegemea kabisa uweza na utoshelevu wa Mungu – naye

aliweza kuishia uweza huo uliomtegemeza na kumwezesha!

(Taz. pia 2Wakorintho 3:1-6.)

Mchungaji kwa Mchungaji: Hatujui “mwibakatika mwili” wa Paulo ulikuwa nini hasa. Lakinitunajua kwa uhakika kwamba haikuwa dhambi auukosefu wa maadili kwa upande wa Paulo. Mungukamwe haachilii dhambi yetu, bali anatuhukumu nakutuadhibu ili atufikishe kwenye toba ya kweli (Mithali3:11-12; 2Wakorintho 7:9-10; 1Yohana 1:9). Hakunainayofichwa kwa Mungu. Ingawa neema Yakeinaweza kumpa mtu muda wa kufikia toba, Yeyehadanganyiki tunapojaribu kuficha dhambi. Hatimayedhambi yetu itafunuliwa (Hesabu 32:23; Wagalatia6:7; 1Timotheo 5:24).

Mungu Anawatumia Watu WanyenyekevuKwa ajili ya mafunzo haya, tuainishe udhaifu kuwa:

• kutambua kushindwa kwetu katika kutimiza mapenzi ya

Mungu peke yetu;

• kutoa mioyo yetu na kutegemea kabisa uweza wa Roho

Mtakatifu;

• kumruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi kupitia kwetu ili

atimize mambo yenye thamani ya milele katika utumishi

– maisha ya watu yaliyobadilishwa – kwa uweza Wake

na si wetu.

Viongozi wa kanisa mara nyingi wanasikia msukumo

mkubwa wa kuwa na “ufanisi” katika utumishi. Inasikitisha

kwamba mawazo yetu kuhusu ufanisi mara nyingi hufuatana

na vipimo vya dunia au hata vya kujiona kwetu. Tunataka

kuwa maarufu machoni pa wengine. Tunataka kuwa “wakuu”

katika Ufalme wa Mungu ili Mungu atutumie katika mambo

makuu!

Lakini ukweli ndio, nao wakati wote umekuwa, kwamba

hakuna watu wakuu wa Mungu – waliopo tu ni watuwanyenyekevu waliotumiwa na Mungu katika mambomakuu! (Taz. Mathayo 20:20-28.)

Tena, hoja ya kimsingi kwa ajili ya utumishi wenye

matunda ni uwepo wa Roho Mtakatifu na kazi anayofanyaYeye! Mungu hawapingi watu wenye elimu, vipawa vya

utawala au talanta nyingi. Lakini hakuna yoyote kati yake

ambayo yanafaa badala ya uweza wa upako wa Roho

Mtakatifu katika utumishi.

Mungu anaweza kutumia vipawa na karama zetu katika

kuongeza ufanisi wetu. Lakini amefunua wazi katika Neno

Lake kwamba “Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yohana 15:5) na “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu,bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi” (Zekaria

4:6).

Mungu anayajua haja zetu, tena amekwisha andaa

kikamilifu mahitaji yetu yote. Ametuandalia Upako wa

Roho Mtakatifu ili tuzae matunda wakati wa kutimiza wito

wake wa utumishi.

Kwa hiyo, sasa tujifunze pamoja ili tupate ufahamu

imara wa ki-Biblia wa Upako wa Roho Mtakatifu.

Lengo la masomo haya ni: 1) kuainisha upako, kama

ulivyo na usivyo; 2) kufafanua jinsi upako unavyotenda kazi

katika na kupitia kwa maisha ya mtumishi; na, 3) kufunua jinsi

tunavyoweza kupokea upako huo na kukua ndani yake.

8 • MATENDO

Kukaza mwendo ilikufikia ufahamu

imara wa ki-Biblia waupako....

Upako

Nakala 16 / Nambari 1

Page 9: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

A. UPAKO KATIKA AGANO LA KALE

Ili tuweze kufahamu Agano la Kale kikamilifu, ni lazima

tutumie Agano Jipya pia. Maandiko ya Agano Jipya ni kama

“vioo” au “miwani” ambavyo mara nyingi husaidia kulenga

na kuongeza uwazi katika kuangalia maandiko ya Agano laKale.

Agano Jipya linafafanua kwamba Agano la Kale (au

Mapatano ya Kale) la Torati au Sheria ni Neno la Mungu

(Mathayo 5:17-18; 2Petro 1:20-21). Lakini sisi sasa tunaishi

chini ya Agano Jipya (Mapatano) ya neema na wokovu

katika Yesu Kristo aliye Mwokozi. Hatuishi tena chini ya

Agano la Kale la Sheria na hatuwezi kupata wokovu kwanjia ya matendo yetu binafsi (Wagalatia 3:21-25).

Agano Jipya limebatilisha Agano la Kale (taz.

Waebrania sura 7-8). Agano hili Jipya linatimiza Agano la

Kale (Mathayo 5:17-18; Luka 24:25-27) na kuweka msingi

ulio “njia mpya, iliyo hai” (Waebrania 10:20) kwa ajili ya

uhusiano wa binadamu na Mungu.

Hata hivyo, maandiko ya Agano la Kale bado ni sehemu

ya Neno la Mungu la milele (Isaya 40:8). Tunaposoma Agano

la Kale, bado tunaweza kujifunza kanuni nyingi muhimu

ambazo zinahusiana na maisha yetu chini ya utawala wa

Agano Jipya.

Paulo akiwaandikia Wakorintho (1Wakorintho 10:1-13)

alieleza kwamba historia, matukio na mambo ya kujifunza

yaliyoandikwa katika Agano la Kale yafaa kujifunzwa,

kueleweka na kutumiwa katika maisha yetu kama waamini

wa Agano Jipya. “Mambo hayo yalikuwa mifano kwetu…”

(1Wakorintho 10:6).

Kwa hiyo tunaweza kupokea maarifa ya thamani kuhusu

upako wa Roho Mtakatifu ambao sasa hupatikana kwa

waamini wa Agano Jipya tukichunguza picha au “mifano” ya

upako iliyotolewa katika Agano la Kale.

1. Asili ya neno “upako”

Neno la Kiebrania katika Agano la Kale lenye maana ya

“upako” ni masah, nalo hutumika mara 69. Neno

linamaanisha kuwekea mafuta kwa kumimina, kupaka au

kutia kwa kusukuma na kueneza kwenye kitu au mtu

mwenye kupakwa.

Mazoea ya kupaka mafuta yalikuwepo kati ya tamaduni

na makabila mengi ya Mashariki ya Kati ya awali. Mazoea

haya yalikuwa na matumizi ya kawaida na pia matakatifu.

Kwa mfano, kumpaka mgeni mafuta kama tendo la ukarimu

kulifanyika hata wakati wa Yesu (Zaburi 23:5; Luka 7:46;

Yohana 12:3).

Lakini mazoea ya kupaka mafuta yalikuwa na maana

mazito zaidi sana kwa watu wa Israeli katika Agano la Kale.

Tunaona kupakwa kwa kitu mara ya kwanza Yakobo

alipoweka kumbukumbu ya kukutana kwake na Mungu mara

ya kwanza. Yakobo alimimina mafuta juu ya jiwe alilokuwa

amewekea kichwa chake akilala na kuota ndoto (Mwanzo

28:10-18).

Badaye, mafuta yalipakwa kwenye madhabahu na vitu

vingine vilivyotumiwa katika ibada za Hema ya Kukutania

(Kutoka 30:26-29; Walawi 8:10-11). Makuhani pia walitiwa

mafuta (Kutoka 28:41; 30:30; Walawi 8:12). (Pia kulikuwa

na upako wa makuhani kwa kutiwa damu ya kondoo, ambao

tutauangalia baadaye katika mafundisho haya wakati wa

kuchunguza mifano ya upako katika Agano la Kale.)

Mazoea ya kutia mafuta yalipanuliwa kwa wafalme

(1Samweli 9:16; 15:1; 16:3,12) na mara chache kwa manabii

(1Wafalme 19:16).

Upako ulitumiwa kwa makusudi matatu muhimu katika

Agano la Kale. Kwanza, ulitumiwa katika kuweka wakfu:kutenga, kwa mfano vifaa fulani, kwa ajili ya matumizi

matakatifu. Haya ni pamoja na kuruhusu kitu fulani kwa ajili

ya huduma ya Mungu (k.m. vifaa vilivyotumiwa katika ibada

ya Hema ya Kukutania, Kutoka 30:26-29).

Pili, tendo la upako, ingawa lilifanywa na mwakilishi

mwanadamu, lilieleweka kuwa limetoka kwa Mungu. Mfano

ulio wazi ni wakati Samweli alipowatia mafuta Sauli na pia

Daudi kuwa wafalme juu ya Israeli (1Samweli 10:1;

16:12-13; 2Samweli 12:7). Upako huu wa Mungu

uliwakilisha kuchaguliwa na kuitwa kwa mtu binafsi awe

mtumishi Wake aliyewekwa rasmi.

Tatu, upako huu mara fulani ulifuatana na uwezo

maalum wa ki-Mungu. Huu ulitoka kwa Mungu na kuhusiana

moja kwa moja na kukamilishwa kwa kazi ambayo Mungu

alikuwa amemwagizia yule aliyetiwa mafuta (taz. 1Samweli

16:1-13; 2Wafalme 2:9-15).

2. Asili la neno “masihi”

Neno hili limetoka moja kwa moja katika neno la

kimzizi masah likiwa katika Kiebrania masiah, na

kutafsiriwa masihi kwa maana ya “aliyetiwa mafuta”. Neno

hili limetumika mara 39 katika Agano la Kale kwa ajili ya

watu wengi mbalimbali. Matumizi yake ya wazi kabisa ni

MATENDO • 9

SEHEMU YA I

UTANGULIZI WA KI-HISTORIA NA KI-BIBLIA WA UPAKO

Upako wa

Roho Mtakatifu

Nakala 16 / Nambari 1

Page 10: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

kwa Masihi mwenyewe – Yesu, Mwana wa Mungu (Isaya

9:7; 11:1-5; sura ya 53). Lakini neno hili limetumiwa pia kwa

ajili ya wafalme wa Israeli katika 1Samweli na 2Samweli na

Zaburi. Linatumiwa hasa kumaanisha uzao katika ukoo wa

kifalme wa Daudi (Zaburi 2:2; 18:50; 84:9; n.k.).

B. UPAKO KATIKA AGANO JIPYA

Maneno matatu tofauti ya Kiyunani hutumiwa katika

Agano Jipya kwa maana ya “upako”. Kila neno

linadhihirisha namna tofauti ya upako.

1. Aleipho (limetumiwa mara 8): kupaka na kusugua

mafuta mwilini (taz. Marko 6:13; Luka 7:38,46; Yakobo

5:14). Katika Yakobo 5:14, upako haukuhusu uponyaji wa

ugonjwa. Ila upako huu ulikuwa ishara ya uwepo wa Roho

Mtakatifu na kumweka wakfu mtu aliyekuwa mgonjwa ili

amwombe Mungu uponyaji katika imani.

Ifahamike kwamba si kosa kutafuta matibabu ya

hospitali au daktari. Mungu aliumba vitu vinavyotumiwa

kutengeneza madawa na amewapa madaktari hekima ya

kuyatumia ifaavyo. Lakini Wakristo wanapaswa kuishi kwa

imani katika maamuzi yote ya maisha yao. Tusione maombi

kama njia ya mwisho baada ya nyingine zote kushindikana.

Kulipo na ugonjwa au majeruhi, umwombe Mungu kwanzakwa ajili ya uponyaji. Mungu akifanya mwujiza wa uponyaji,

usifu Jina Lake! Mungu akichagua kutumia madawa na

madaktari katika kuponya, usifu Jina Lake! Kusipokuwa na

uponyaji wowote, bado usifu Jina Lake – maana, uponyaji

wetu wa mwisho na nyumba yetu ya milele ni Kwake

ambapo tutamwona uso kwa uso (1Wathesalonike 4:16-18).

Mungu wetu wakati wote ni mwaminifu na mnyofu!

2. Chrio (limetumiwa mara 5): humaanisha wito au

utume maalum wa Mungu unaomtenga mtu (au watu) peke

yake atimize kazi fulani aliyopewa (taz. Luka 4:18; Matendo

10:38; 2Wakorintho 1:21; Waebrania 1:9).

3. Chrisma (limetumiwa mara 3): kupewa uweza na

Roho Mtakatifu kwa ajili ya kujua yaliyo kweli na haki;

uweza wa Roho Mtakatifu akishirikiana na Neno la Mungu

katika moyo wa mwamini.

Waraka wa kwanza wa Yohana 2:20 na 2:27 hutaja

huduma ya Roho Mtakatifu katika kufunulia ukweli moyo wa

mfuasi wa Kristo (taz. pia Yohana 14:16-17,26; 1Wakorintho

2:10-16; Waefeso 1:17-18).

Mtume Yohana alikuwa akiandika barua hii (1Yohana)

apinge uzushi wa kikundi cha watu waliojidai kuwa na

ufahamu maalum wa Mungu. Hao walimu wa uwongo

walikataa kwamba Mwana wa Mungu alikuwa amekuja

katika mwili (1Yohana 2:18-23). Walidai kwamba wao peke

yao ndio waliokuwa na ufahamu halisi wa Mungu na

kwamba iliwabidi wote wawafuate.

Lakini Yohana aliwatuliza moyo Wakristo kwamba wale

walikuwa wakifanya kazi chini ya mwongozo wa kishetani

wa roho wa Mpinga Kristo (ms. 18). Yohana anapinga

mafunzo haya ya uwongo kwa kuwakumbusha waamini

kwamba wao tayari wamempokea Roho Mtakatifu ambaye

“mafuta yake yana-wafundisha habari za mambo yote”

(ms. 27).

Yohana hapunguzi wala kuzuia huduma ya kufundisha (taz.

Warumi 12:7 na Waefeso 4:11); badala yake, Yohana anatilia

mkazo huduma ya Roho Mtakatifu, anayetuongoza katika

ufahamu wa Ukweli katika Neno la Mungu (Yohana 16:13).

Masihi – Mwenye UpakoTumejifunza kwamba maana ya neno “Masihi” ni

“aliyepakwa mafuta” au “mwenye upako”. Injili za Agano

Jipya zinathibitisha kabisa kwamba Yesu wa Nazareti

alikuwa (na ndiye) Masihi PEKEE, Mwenye Upako PEKEE!

Yesu alikuwa (na ndiye) mwenye upako kwa ajili ya utume

au kusudi maalum.

Katika lugha ya asili ya Kiyunani ya Agano Jipya, Yesu

aitwa “Kristo” au “Yesu Kristo”. Lakini “Kristo” pia ni jina la

cheo linalomaanisha “mwenye upako”. Agano Jipya lote

linafunua wazi kwamba Yesu ndiye Mwenye Upako (Yohana

1:41; 4:25-26).

Wayahudi walikuwa wakimsubiri masihi (Kiebrania

“mwenye upako”), mfalme katika ukoo wa kifalme wa

Daudi, ambaye angerejesha taifa la Israeli katika utukufu

wake wa zamani kama wakati wa Sulemani. Kwa sababu ya

matazamio yao, Wayahudi wengi walimkataa Yesu.

Hakulingana na mawazo yao mapungufu na yasiyo sahihi

kuhusu Masihi aliyeahidiwa (Mathayo 11:1-19; Yohana

6:26-29).

Wayahudi hawakuona kwamba Mungu alikuwa na

mpango mkuu zaidi kabisa ulioenea mbali na taifa lao (Isaya

42:5-9; 49:5-6; Matendo 4:8-12; 13:44-49). Mungu aliwapa

wao (na sisi) lililo kuu kabisa kuliko mfalme wa muda wa

kidunia. Aliupatia ulimwengu Mfalme wa wafalme,

Mwokozi wa kweli wa wote, hata milele – Yesu, Masihi,

utukufu kwa jina Lake!

MuhtasariUpako katika Agano la Kale ulikuwa tendo lenye maana

kuu kabisa. Upako wa vifaa, makuhani, manabii na wafalme

uliwaweka wakfu kwa ajili ya makusudi ya Mungu. Lakini

tuelewe kwamba upako huo wa Agano la Kale ulikuwa

mfano au fumbo wa yale ambayo Mungu angeyatimiza chini

ya utawala wa Agano Jipya.

Chini ya Agano Jipya, kuliingia njia mpya iliyo hai ya

uhusiano kati ya Mungu na binadamu. Njia hii ilionekana

kwanza katika kutumwa kwa Yesu (Yohana 7:28-29), Mwana

wa Mungu, Masihi, Mwenye Upako, ili atimize makusudi na

maagizo ya Mungu (Yohana 3:14-17). Yesu alikamilisha kazi

hii alipokufa Msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kwa njia

hiyo alifungua mlango wa wokovu kwa wote wamwaminio

(Warumi 10:9-13; Waefeso 2:1-10; Waebrania 7:11-25;

9:11-15).

Sehemu moja ya mpango wa Mungu Baba kwa ajili ya

wokovu wa binadamu ilikuwa kuwapatia msaada wa

ki-Mungu wale ambao wangemwamini Mwana Wake.

Waamini wangepata msaada na uwezo wote wahitajio ili

watimize mapenzi ya Mungu kwao.

Kwa hiyo, Yesu alipomaliza kazi Yake aliyopewa na

Mungu duniani (Yohana 17:4; 19:30), aliahidi kututumia

“Msaidizi” (Yohana 7:37-39; 15:26; 16:5-15). Huyu

Msaidizi (Mfariji) ni Roho Mtakatifu – Mungu Roho.

Yaliyoonekana katika fumbo au mfano katika Agano la

Kale katika kumimina au kupaka mafuta (upako) sasa

yalipata kuwa ya kweli halisi kwa waamini wa Yesu Kristo

katika Agano Jipya. Haya yalianza wakati Mungu Roho

alipomiminwa katika Siku ya Pentekoste (Yoeli 2:28-32;

Luka 24:29-32; Matendo 2:1-39).

10 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 11: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

A. ASILI YA UPAKO

Maoni ya watu wengi yamechanganyikiwa kuhusu

upako, kwa sababu ya ukosefu wa mafunzo na masomo halisi

ya ki-Biblia kuhusu hoja hii. Katika sehemu hii, tutaainisha

upako unavyodhihirishwa kwetu katika Maandiko.

Baadaye katika sehemu hii, tutaainisha upako jinsi

ulivyo; lakini kwanza, tudhihirishe ule USIO upako.

1. Mambo Ambayo Upako Siyo

a. Upako SI nguvu isiyo na uhai, wala uwezo wa

kifumbo. Upako si kama umeme (nguvu isiyo na uhai), wala

aina fulani ya nguvu ya kishirikina au uchawi. Simoni

mchawi (Matendo 8:9-25) alikuwa na aina ya nguvu (ya

kishetani); lakini alitambua haraka kwamba nguvu ile

haikulingana kabisa na uwezo uliokuwemo ndani ya mitume.

Upako wa Mungu si wa kimaumbile, ni wa kiroho.

b. Upako, jinsi unavyoelezwa katika Maandiko, SI

miitikio ya kihisia tu, yanayoonesha ama nafsi yenye

nguvu kubwa ama mtindo fulani wa kuhubiri. Mara

nyingi Mungu anagusa hisia zetu tunapotembea katika uwezo

wa upako Wake. Lakini kuonesha hisia zenye nguvu si

kuthibitisha uwepo wa upako Wake Mungu. Watu wanaweza

kuonesha hisia zenye nguvu katika michezo ya kuigiza,

uimbaji au michezo. Lakini bila shaka si uthibitisho wa

kuwepo kwa upako wa Mungu!

Watu fulani wanafikiri kwamba mhubiri akipaza sauti au

kusisimka na kurukaruka, anao upako. Lakini upako wa

kweli kutoka kwa Mungu unaweza uonekane au usionekane

katika matendo ya kimwili.

Vile vile, mtu hawezi “kustahili” kuwepo kwa upako wa

Mungu kwa njia ya elimu, ujuzi au utaratibu. Vipawa au

talanta za asili zenye uwezo pia si alama ya upako wa

Mungu. Ingawa talanta zetu za asili yetu ya kibinadamu ni

vipawa kutoka kwa Mungu, hata mtu asiyeokolewa anaweza

kuwa navyo na kuvitumia. Tusichanganye kuwepo kwa

talanta na vipawa, na upako.

Ni kweli kwamba Mungu anaweza kupatia vipawa vyetu

uwezo wa upako Wake ili vifanye kazi katika eneo kubwa

zaidi kuliko tuliloweza kufikia kwa nguvu yetu, kama

alivyofanya kwa Sulemani (1Wafalme 4:29-34). Lakini

talanta na vipawa vyetu kamwe visichukue nafasi yetu ya

kumtegemea Mungu kwa ajili ya uweza Wake wa ki-Mungu.

Upako unaotoka kwa Mungu ni wa ki-Mungu, si wa

kimaumbile, nao hutokana na nguvu na uweza Wake!c. Upako SI wokovu. Kila mtu aliyetubu dhambi zake

na kumjia Kristo kwa wokovu anaye Roho Mtakatifu!

Lakini hali hii ni tofauti na upako wa Roho Mtakatifu.Tuangalie kazi za Roho Mtakatifu wakati mtu

anapookolewa:

• Mtu anaweza kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya kazi na

uweza wa Roho Mtakatifu peke Yake (Yohana 3:3-8;

Warumi 8:9,16).

• Mtu anaungwa na Mwili wa Kristo uliopo mahali pote,

wakati wa kuokolewa kwa njia isiyo ya kimaumbile;

Mwili wa Kristo ukiwa watu wote wanaomwamini Yeye

kwa ajili ya wokovu (1Wakorintho 12:13).

MATENDO • 11

SEHEMU YA II

ASILI, KUSUDI NA

MATUMIZI YA UPAKO

Upako wa Roho

Mtakatifu

Nakala 16 / Nambari 1

Page 12: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

• Mtu “hutiwa muhuri” na Roho Mtakatifu wakati wa

kuokolewa (2Wakorintho 1:22; 5:5; Waefeso 1:13-14).

Neno la Kiyunani lililotafsiriwa “kutiwa muhuri” ni

arrabon, maana yake arabuni au dhamana. Lakini zaidi

ya kuainisha kwa juujuu hivi, kuna maana ya ndani.

Kwanza “kutiwa muhuri” ni kuwekewa alama ya kuwa

mali ya Mungu. Ni ishara iliyo hai kwamba Mungu

amepokea fidia kwa ajili yetu. Fidia hiyo ni dhabihu ya

damu ya Mwana wa Mungu kwa ajili ya dhambi zetu

(Waefeso 1:7). Pili, tunapomjia Kristo katika imani kwa

ajili ya wokovu (Warumi 10:9-10) tunapewa Roho

Mtakatifu kama “arabuni” au “fungu ya kwanza ya

malipo” ya uwekaji wa Mungu ndani yetu. Uwekaji huu

ni dhamana (au ahadi) kwamba tunaweza kuongezeka

kila siku katika uhai, furaha, baraka na uweza wa Roho

Mtakatifu mpaka siku ambapo Mungu atatupokea kabisa

Kwake kule mbinguni (Wafilipi 1:6; 2Petro 1:5-11)!

Kazi na huduma ya Roho Mtakatifu huanza ndani yetu na

kupitia kwetu wakati tunapookolewa. Yale tunayopokea

wakati huo ni hatua ya kwanza tu katika mfuatano wa

kupevuka kwetu. Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya waamini

wote ni kwamba wafikie kuwa wanafunzi waliopevuka kama

wana Wake wa kiume na kike. Ili tufikie hapo inatubidi tujitoe

kikamilifu katika kukua na kugeuzwa kwetu binafsi. Lazima

tujitoe kila siku kwa Roho Mtakatifu katika maisha yetu

anapotuhukumu, kutuadhibu, kutuhamasisha na kutuwezesha!

Mchungaji kwa Mchungaji: Wewe kamamchungaji na kiongozi wa kanisa, umeitwa na Munguuwe mfano kwa wengine wa kundi lako wa kujitoa iliuendelee kukua katika mambo ya Mungu.Tunashawishika tufikiri kwamba, kama viongozi,hatuna haja tena kuwekea kipaumbele kukua kwetubinafsi katika Kristo. Lakini ukweli halisi ni kinyumechake! (Taz. 1Petro 5:2-3.)

Kwa sababu sisi ni viongozi, tunapaswa tuwemifano hai zaidi wa maneno ya Yesu: “Mtu ye yoteakitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwikemsalaba wake kila siku, anifuate” (Luka 9:23). Kilamwamini amepewa Roho Mtakatifu wakati wakuokolewa; tujinyenyekeze, basi, kwa kazi yake namwongozo Wake katika maisha yetu kila siku!

d. Upako SI sawasawa na Ubatizo wa Roho

Mtakatifu. Ubatizo huu ni tukio maalum, inayopatikana kwa

waamini wote wa Kristo (Mathayo 3:11). Ubatizo wa Roho

Mtakatifu pia si sawasawa na kuja kwa Roho Mtakatifu ili

akae ndani ya mwamini wakati wa kuokolewa kwake.

Karama ya Roho Mtakatifu ilitabiriwa na nabii Yoeli

zaidi ya miaka mia nane kabla ya karama hiyo kumiminwa

siku ya Pentekoste (taz. Yoeli 2:28-32 na Matendo 2:1-39).

Ubatizo wa Roho Mtakatifu umeandaliwa ili

kumwezesha kila mfuasi wa Kristo awe na ufanisi na uwezo

zaidi kwa ajili ya kazi ya Bwana! Ubatizo huu utamwongoza

mwamini wa Kristo katika:

• kushughulikia zaidi roho za watu;

• uwezo mkubwa zaidi katika sala na hamu kubwa

zaidi ya kuomba;

• upendo wa ndani zaidi kwa Kristo na Mwili Wake;

• kuandaliwa kwa ajili ya mapambano ya kiroho;

• ufahamu unaoongezeka wa Neno la Mungu.

Waamini wote wa Kristo hupokea karama ya moyoni ya

Roho Mtakatifu wakati wa kuokolewa (Yohana 3:5-6;

Warumi 8:15-16). Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili

ya kujazwa na kufurikiwa na Roho wa Mungu. Ubatizo huo

haukupatii wokovu zaidi wala upendo mwingi zaidi wa

Mungu. Lakini utakuandaa uweze kuwa na maisha ya ufanisi

na ushindi zaidi katika Kristo!

Kama umepokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu,

ukumbuke kwamba si tukio la mara moja la kupata; ila zaidi

ni mwenendo wa maisha wa kudumisha. Tunapaswa

tuendelee kujazwa wakati wote! [Angalia Sehemu Ya III,

C.1, “Mjazwe!”, kwa ajili ya mafunzo zaidi kuhusu hoja hii.]

Mchungaji kwa Mchungaji: Tunapojifunza kuhusuRoho Mtakatifu, ni lazima tutambue kuwepo kwa rohonyingine katika dunia yetu. Kuna aina tatu za rohozinazofanya kazi duniani siku hizi:

1) MashetaniWapo mapepo waovu (mashetani) leo hapa

duniani. Wameagizwa na Shetani (Ibilisi)wawadanganye wanadamu wote (Ufunuo 12:7-9) nakuwapofusha wasione ukweli kwamba Yesu ndiye nani(2Wakorintho 4:4; 1Yohana 2:22; 4:1-3). Ufalme waowa kishetani hufanya kazi zaidi kwa njia ya dini zauwongo. Wanatumia udanganyifu kama silaha yaokubwa, wakishirikiana na Ibilisi ambaye ni “mwongo, nababa wa huo” (Yohana 8:44).

Mapepo waovu huwatawala kwa nguvu watu wasiowaamini (2Wakorintho 4:3-4). Lakini pia wanajaribukuwalenga waamini wa kweli wa Kristo, ambao kwaonuru tukufu ya Injili inahubiriwa (Waefeso 6:10-12;2Wakorintho 10:3-5; 11:3). Ufalme wa kishetani, kamadhambi, hauna mamlaka juu ya Wakristo – isipokuwaMkristo akichagua kwa hiari kushirikiana nao katika hilazao au majaribu yao.

Shetani atatumia wanadamu kama vyombo vyake(hata wengine wanaojidai kuwa ni Wakristo) akijaribukuwapotosha watu (Mathayo 24:24; 2Wakorintho11:13-15; 2Petro sura ya 2). Mapepo waovu hatawanaweza kusema nusu-ukweli mara nyingine(Mathayo 4:1-11; Marko 5:1-8; Matendo 16:16-19), lakinihawatamtukuza Mungu wala kufanya mapenzi Yake.

Roho hizi za kishetani hujua kwamba Mungu ni wakweli na halisi:

12 • MATENDO

Roho Mtakatifuanahudumia ndani yetu

na kupitia kwetu.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 13: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

“Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja;watenda vema. Mashetani nao waamini nakutetemeka” (Yakobo 2:19). Lakini mashetanihawatubu kamwe. Wanafanya kazi kwa bidii wapatekudanganya wanadamu, kwa sababu wanajua kwambahukumu yao inawajia (Ufunuo 12:12).

2) Roho za kibinadamuKila mwanadamu ana roho tangu mama yake

alipotunga mimba. Binadamu ana sehemu muhimutatu: mwili, nafsi na roho (1Wathesalonike 5:23;Waebrania 4:12). Lakini roho yetu ni mfu ndani yetumpaka inapohuishwa kwa imani katika Kristo (Waefeso2:1-8).

Biblia inafundisha kwamba mwanadamu akishakufa kimwili, roho yake huondoka mwilini. Walio katikaKristo wanakwenda kukaa pamoja na Bwana(2Wakorintho 5:6,8). Wanaokufa pasipo Kristowanawekwa hadi siku ya hukumu (Waebrania 9:27;Ufunuo 20:11-15). Roho za wanadamu waliokufahaziruhusiwi kutembea duniani! Wala haziingii tenakatika mwanadamu mwingine, mnyama wala kiumbechochote. Kila mtu ana maisha MOJA tu, na baada yakufa hukumu (Waebrania 9:27).

Zipo dini nyingi zinazoabudu roho za ainambalimbali. Watu wengine huamini kwamba wanawezakuwasiliana na roho za mababu zao au mizimumingine. Lakini watu hao hawawasiliani na wanadamuwaliokufa; ukweli ni kwamba wanawasiliana namapepo wanaowaigiza waliokufa.

Usidanganywe na roho hizi za uwongo! Bibliainatufundisha kwamba Shetani na mapepo yakewanaweza kujifanya mifano ya “malaika wa nuru”wakijaribu kuiga mambo ya ki-Mungu (2Wakorintho11:14). Wakiweza kufanya hivyo, si vigumu kwao kuigasauti ya mtu aliyekufa na kujua historia yake. Usijaribukamwe kuwasiliana na watu waliokufa, wala kushirikikatika aina yoyote ya ibada au sherehe inayojaribukuwaabudu au kuwaomba mababu au mizimu.Ukifanya hivyo, unawakaribisha mapepo wa kishetanikwako!

3) Roho MtakatifuRoho Mtakatifu ni Roho wa Mungu, naye ndiye

Roho pekee anayestahili kuitwa mtakatifu (Warumi1:4). Roho Mtakatifu ni Mungu mkamilifu, kamaBaba ni Mungu na Yesu ni Mungu (Mathayo 28:19;2Wakorintho 13:14).

Katika Maandiko, Roho Mtakatifu ana sifa zifuatazo:

• Anaitwa Mungu (Yohana 4:24; Matendo 5:3-4; • 1Wakorintho 3:16; 2Wakorintho 3:17)• Yeye ni wa milele (Waebrania 9:14)• Yeye anajua mambo yote (Yohana 14:26;

1Wakorintho 2:10)• Yeye yupo kila mahali (Zaburi 139:7)• Yeye ana uweza wote (Luka 1:35; katika uumbaji,

Mwanzo 1:2)• Anajua mambo yote kabla hayajatokea (Matendo

1:16; 11:27-28)• Ana upendo (Warumi 15:30)• Aliongoza kuandikwa kwa Biblia kwa pumzi ya

Mungu (2Petro 1:21; 2Timotheo 3:16)• Yeye ni Mtendaji katika uongozi wa ki-Mungu (Marko

13:11; Warumi 8:14)

• Yeye ni Mtu, kama Yesu na Baba ni Watu (Yohana

14:16-17,26)

• Yeye anaweza kuhuzunishwa (Waefeso 4:30)

Masomo kamili kuhusu Roho Mtakatifu yana upana

mkubwa usioweza kufikiwa katika mafunzo haya.

Lakini Agano la Kale na Agano Jipya pia hufunua

kwamba Roho ni wa kweli naye ni Mungu; anaishi

pamoja na Baba na Mwana akiwa na usawa na umilele

pamoja nao; ndiye Nafsi ya tatu katika Utatu.

e. Upako SI sawasawa na utakaso. Tuainishe utakasona kuuchunguza kwa kifupi ili tupate kufahamu mfuatano

huu vizuri zaidi.

Kuainisha UtakasoUtakaso una maana mbili muhimu. Maana ya kwanza ni

kuwekwa wakfu – kutengwa kwa mtu au kitu fulani kwa ajili

ya matumizi maalum matakatifu.

Tumejifunza kutoka Agano la Kale kwamba kuwekwa

wakfu kulihusiana na vitu vya kimwili kama vile: nyumba

(Walawi 27:14), shamba (Walawi 27:16), vyombo

vilivyotumiwa katika Hekalu (2Nyakati 29:18-19). Vitu hivi

vyote viliwekwa wakfu na kutengwa kwa ajili ya matumizi

maalum.

Watu pia walitengwa kwa ajili ya matumizi maalum: kila

mtoto wa kiume wa kwanza wa Waisraeli (Kutoka 13:2),

makuhani (2Nyakati 29:4-5,15), nabii Yeremia (Yeremia

1:5), Yesu Mwenyewe, kama Mwana wa Mungu asiye na

dhambi (Yohana 10:36; 17:19).

Maana ya pili ya utakaso ni kusafishwa – kuondolewa au

kutakaswa na uchafu wa kimaadili. Kwa mfano, Paulo

alipowaombea waamini kwa ajili ya maisha yao yote

(1Wathesalonike 5:23) au kusafishwa kwa dhamiri ya

mwamini (Waebrania 9:13-14), n.k.

MATENDO • 13

Utakaso: kutengwa kwa ajiliya matumizi matakatifu

Nakala 16 / Nambari 1

Page 14: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mchungaji kwa Mchungaji: Aina hizi mbili zautakaso husaidia kudhihirisha tofauti ya maoni yaAgano la Kale na ya Agano Jipya kuhusu utakaso.

Katika Agano la Kale, kitu cha kawaidakilihesabiwa kuwa kitakatifu na chenye utakasokilipotengwa kwa ajili ya matumizi au utumishi waMungu.

Katika Agano Jipya, kitu cha kawaida kilijazwaRoho wa Mungu na kugeuzwa kiwe chombo kilichofaakwa matumizi au utumishi wa Bwana (2Timotheo2:19-21).

Sisi kama viongozi katika Mwili wa Kristo, tumeitwakatika mwito mtakatifu (2Timotheo 1:9). Mwito huounatutenga kwa ajili ya utumishi wa Kristo. LakiniMungu hajamaliza hapo. Anaanza kazi ya “kututakasa”ndani yetu, akiendelea kutugeuza kwa Roho Wake naNeno Lake. Tunaposhirikiana na Yeye katika kazi hii nakutii Neno, Yeye anatugeuza tupate kuwa aina ya watuambao mawazo, maneno na matendo yao katikamaisha ya kila siku yanamfunua Yeye aliye Bwanandani yetu.

2. Pande Tatu Za Utakaso

a. Kuchaguliwa Na Kuwekwa Katika Utakaso – Kazi

Iliyotimilizwa. Alipokuwa hapa duniani, Yesu alikuwa

mkamilifu kabisa kimaadili naye hakuwa na dhambi yoyote.

Alitumwa hapa na Baba Yake atimilize kusudi la kujia

ulimwengu wetu ulioanguka akijitoa dhabihu kwa ajili ya adhabu

ya dhambi zetu. Katika Yeye, tena katika Yeye peke Yake,

tunaweza kupata msamaha, wokovu na ukombozi kwa Mungu.

Mtu anapofikia imani katika Kristo na kujisalimisha kwa

Ubwana wa Kristo, mtu huyu anaunganishwa kiufalme na

Mwili wa Kristo, yaani Kanisa (1Wakorintho 12:13). Neno la

Kiyunani lililotafsiriwa “kanisa” ni ekklesia, maana yake

“walioitwa nje”. Tukiainisha kanisa hivi tunaona jinsi kilamwamini wa Kristo anapaswa aitwe nje au kutengwa kwa

ajili ya matumizi ya Mungu.

Aina hii ya utakaso – kutengwa kwa ajili ya matumizi

matakatifu – tunaweza kuita pia kuchaguliwa na kuwekwakatika utakaso (taz. 1Wakorintho 1:30; 6:11; 2Wathesalonike

2:13). Huku kuchaguliwa na kuwekwa katika utakaso ni kazi

ambayo Mungu amekwisha timiliza na kumpatia kila mtu

binafsi wakati anapookolewa (Matendo 26:18; Warumi

15:16; 1Wakorintho 6:11).

Kristo alimwaga damu Yake Mwenyewe na kutoa uhai

Wake kwa ajili ya dhambi zetu. Kazi mojawapo

iliyotimilizwa ni utakaso wa wale wanaomwamini. “Katikamapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili waYesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10); “Bali kwayeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywakwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu[utakaso], na ukombozi” (1Wakorintho 1:30).

Kule “kutakaswa” ni asili ya waamini wa Kanisa la awali

kuitwa “watakatifu” (1Wakorintho 1:2; Waefeso 1:1).

Utakaso huo unatolewa bure kwetu kwa sababu ya kazi

iliyotimilizwa na Kristo pale msalabani. Hatuwezi kamwe

kufanya matendo mema wala ya dini ya kutosha ili tuustahili.

Hatuwezi kamwe kuwa “wema kiasi cha kutosha” ili tustahili

kukubaliwa na Mungu au kupata wokovu kwa ustahili wetu

binafsi.

Baba yetu wa Mbinguni asiye na dhambi yoyote, aliye

mkamilifu kabisa kimaadili, anapotuangalia sisi, anatambua

kila aina ya kupungukiwa na kushindwa. Lakini pia anatuona

kupitia damu ya Yesu, Mwana Wake, ambayo imetufunika

(imetutakasa) kabisa. “Kufunikwa” huku kwa dhambi zetu ni

njia pekee inayotuwezesha tukubalike mbele za Mungu aliye

mtakatifu na mwenye haki (Waefeso 1:6-7). Hii kweli ni

Habari Njema!

Kwa njia ya damu ya milele ya Mwana-Kondoo Asiye na

dhambi, waamini wametakaswa (Waebrania 10:11-14;

13:12). Sadaka ya Kristo ya damu Yake iliyomwagika ni kazi

ya utakaso ya mara-moja-kwa-wakati-wote, (Waebrania

9:28; 10:12). Hatuhitaji “kazi ya pili ya neema” (kama

wengine wanavyofundisha) ili tukubaliwe na Mungu. Dakika

ile ile ambapo tunamwamini Kristo na dhabihu Yake kwa ajili

ya dhambi zetu (Warumi 10:9-10), Mungu anatuhesabia

utakatifu wa Kristo na kututangazia kuwa “watakatifu”

(1Wakorintho 1:30).

b. Utakaso Unaoendelea – Mfuatano wa Kimatendo.

Upande wa pili wa pande tatu za utakaso ni mfuatano

wa utakaso unaoendelea katika maisha yote ya mwamini.

Mara nyingi huitwa utakaso unaoendelea.Tumekwisha jifunza kwamba utakaso wa kuchaguliwa

na kuwekwa ni tendo la kifalme la Mungu linalotupatia

utakatifu unaotokana na dhabihu ya Kristo peke yake.

Hatuwezi kuupata kwa bidii yoyote ya kibinadamu, kwa

sababu wanadamu wote wamepotea kabisa chini ya dhambi

(Warumi 3:9-26).

Lakini mtu akiisha kufikia imani katika Kristo kwa

wokovu, kazi kuu ya Mungu inayofuata ni mfuatano wa

“[ku]badilishwa tufanane na mfano uo huo [wa Kristo], tokautukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwaBwana, aliye Roho” (2Wakorintho 3:18). Maana ni mapenzi

ya Mungu sisi “[tu]fananishwe na mfano wa Mwana wake,ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa nduguwengi” (Warumi 8:29).

Mfuatano huu (au maendeleo) wa utakaso ni tofauti na

aina ile ya kuchaguliwa na kuwekwa. Utakaso wa

kuchaguliwa na kuwekwa ni tendo la kifalme la mara moja la

Mungu wakati tunapopokea kazi ya Kristo ya wokovu.

Lakini utakaso wa mfuatano unahusiana na maendeleo ya

mapenzi, hamu na bidii zetu kwa muda mrefu.

Tendo hili la kujitoa kwa ajili ya “kugeuzwa” ni

ushirikiano wa ki-Mungu na kibinadamu. Inawabidi waamini

washirikiane na Mungu kwenye kazi yake ya ki-Mungu ya

kuleta mageuzi katika maisha yao.

Biblia inafunua wazi kwamba inawabidi wafuasi wote

wa Kristo wakazane kabisa katika kufanana zaidi na Kristo,

wakiishi maisha yenye utakatifu na utakaso. “Basi, wapenziwangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu nauchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifukatika kumcha Mungu” (2Wakorintho 7:1).

Tumeambiwa: “Mvue kwa habari ya mwenendo wakwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaazenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya niazenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungukatika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:22-24).

Tafadhali tumia muda sasa hivi kusoma mistari ifuatayo,

ambayo ni michache kati ya mingi iliyopo yenye

14 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 15: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

kutuhamasisha kuhusu hoja hii: Warumi 6:11-13; 12:1-2;

13:14; 2Timotheo 2:20-21; 1Petro 1:13-19; 1Yohana 3:3.

Hoja hiyo ni muhimu sana katika imani yetu ya Kikristo.

Lakini pia ni eneo ambapo waamini wengi wanashindwa

kufikia hali ambayo Mungu amekusudia kwa ajili yao.

Wanaendelea kufungwa na hasira, dhambi, utumwa au hofu,

badala ya kumruhusu Mungu awaweke huru na mambo haya.

Ingawa wanajaribu kwa nguvu yao binafsi kujiweka huru na

tabia au matendo yasiyowafaa kama wacha Mungu,

hawafahamu kuwa wanahitaji msaada wa Mungu ili wapate

kuwa na uhuru kamili.

Ni wazi kufuatana na Maandiko kwamba haiwezekanikuwa mtakatifu na safi kimaadili pasipo uweza wa Mungu

ukitusaidia (Yeremia 13:23; 17:9-10; Warumi 3:20,23; 7:18).

Ni kweli kwamba damu ya Kristo huweka msingi wa utakaso

wetu wa kwanza (Waebrania 10:29), lakini ni ushirikiano wa

Roho Mtakatifu na Neno la Mungu la milele (Waefeso 5:26)

vikifanya kazi pamoja, vinavyoendelea kutugeuza zaidi

katika mfano wa Kristo (Warumi 8:29-30; 2Wakorintho 3:18;

Wafilipi 1:6; 1Petro 5:10). Kazi hiyo ni ya maisha yote,

itaendelea mpaka tutakapoonana na Yeye “uso kwa uso”

(1Wakorintho 13:12; 1Yohana 3:2).

Mungu anataka kufanya kazi ya kufululiza ndani yetu ili

atutengeneze. Lakini ni lazima pia awe na ushirikiano wetu

na bidii yetu kamili kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu na

Neno la Mungu. Lazima tuchague kusikia na kutii, kusikiliza

na kuitikia maagizo ya Neno la Mungu na ya Roho

Mtakatifu.

Huo utakaso unaoendelea ni mageuzi ya muda wote wa

maisha yetu. Hatutakamilika wala kuwa huru kabisa na

dhambi katika maisha haya (1Yohana 1:8), lakini tunaweza

kuendelea kukua katika upevu wa kiroho, na inatubidi tukue

hivyo.

c. Utakaso Kamili Au Wa Mwisho. Ukamilifu wetu wa

kutokuwa na dhambi yoyote husubiri kurudi kwa Bwana

Yesu Kristo au dakika ile ambapo, katika kifo, tunaondoka

maisha haya na kwenda kwa Bwana. Ndipo tutawekwa huru

na mwili huu wa uharibifu na “kufumba na kufumbua, wakatiwa parapanda ya mwisho” (1Wakorintho 15:52)

tutabadilishwa tuwe viumbe visivyokufa wala kuwa na

uharibifu (1Wakorintho 15:45-47; taz. pia Wafilipi 3:20-21;

1Yohana 3:2).

Kristo alipokufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi

zetu, tuliokolewa na adhabu ya dhambi. Tunavyokua katika

imani na utakatifu, tunawekwa huru zaidi na zaidi na nguvu

ya dhambi. Na wakati Kristo atakaporudi (au tunapokufa

katika Bwana) tutaokolewa na uwepo wa dhambi!

Utakaso si upako. Lakini utakaso (hasa utakasounaoendelea) ni muhimu sana kwa ajili ya upako. Kuishi

maisha matakatifu na yenye kujitoa huhusiana kabisa na

kufurika kwa upako katika maisha yetu na utumishi wetu.

[Hoja hii itazungumzwa zaidi katika Sehemu Ya III, A.

“Kuhifadhi Upako”.]

3. Njia ya Kukua

Wakristo wanapaswa wakue wakati wote. Biblia

inatuhamasisha: “Kueni katika neema, na katika kumjuaBwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2Petro 3:18; taz. pia

2Petro 1:5-11).

Utakaso unaoendelea ni mfuatano unaohitaji

ushirikiano kati ya Mungu na kila mtu binafsi (Wafilipi

2:12-13). Mungu anatenda kazi kwa ajili yetu, kwa sababu

hatuna budi tupokee msaada Wake ili tupate kufanana na

Kristo katika tabia zetu. Lakini nafasi yetu katika mfuatano

huu ni ipi?

Ni lazima:

a. Tumwamini Kristo. Pasipo imani, hatuwezi kupokea

karama ya wokovu, wala karama inayofuata ya Kristo ya

kuchaguliwa na kuwekwa katika utakaso. Tunapookolewa,

Kristo anakuwa utakaso wetu (1Wakorintho 1:30).

Tunapokea karama hii kutoka Kwake kwa kumwamini Yeye

(Matendo 26:18).

b. Tumtolee Mungu maisha yetu. Ndivyo tunavyoanza

maisha yetu kama Wakristo; ndivyo tunavyopaswa kuishi

siku kwa siku pia. Mfululizo wa kujitoa au kujisalimisha kwa

Mungu ni muhimu kabisa. Yeye ndiye anayejua yaliyo ya

lazima kwetu ili tufanane zaidi na Kristo. (Taz. Warumi

6:13,19-21; 12:1-2; 2Timotheo 2:21.) Kujisalimisha kwa

Mungu kila siku ni lazima pia ili imani yetu ikue na kuongeza

nguvu, tunapochagua kumtegemea na kumwamini Yeye

(Waebrania 11:6).

c. Tutii Neno la Mungu. Maandiko Matakatifu ni

kipimo chetu cha mwisho kwa ajili ya imani na matendo

yetu. “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake: Kwa kutii,akilifuata neno lako” (Zaburi 119:9). Roho Mtakatifu

atatumia Neno la Mungu aseme nasi na kutengeneza tabia

zetu (Yohana 14:26). Neno la Mungu litatuandaa na

kutufanya zana zifaazo kwa ajili ya utukufu wa Mungu

(2Timotheo 3:16-17). Neno la Mungu litatusafisha (Waefeso

5:26). Biblia inafunua pia mawazo na makusudi yetu ya

ndani kabisa (Waebrania 4:12). Inatupasa tusome Biblia kila

siku; na halafu lazima tuitii (Yakobo 1:22). Mungu anatoa

yote yanayohitajika ili tuishi na kukua katika uchaji (2Petro

1:3-4). Lakini ni lazima sisi tushiriki na kutii kwa hiari yetu!

d. Tuweke ahadi yetu binafsi ya kufuata utakatifu.

“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huoutakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwanaasipokuwa nao” (Waebrania 12:14; taz. pia Mathayo 5:8).

Petro anawahamasisha waamini wawe na kiasi na

kutumaini kwa utimilifu neema ya Mungu. Tunapaswa tumtii

Mungu na tusifanane na tamaa zilizotutawala zamani.

Matazamio haya ya ki-Mungu ya utakatifu wetu ni kwa

sababu Mungu ni mtakatifu katika asili Yake na mwenye haki

katika hukumu Zake zote (1Petro 1:13-21). Lengo la maisha

yetu na hatima yetu si kuishi katika furaha au starehe, bali ni

utakatifu.

Kutafuta mwenendo wa maisha ulio mtakatifu – katika

matendo, mawazo, mahusiano na maneno yetu – si hiari kwa

mfuasi wa Kristo. Tusiridhiane na lolote lisilokubaliana na

Mungu mtakatifu! Mfano na kielelezo kwetu si

wanavyofanya watu wengine (Wakristo ama sivyo), wala

maridhia ya mienendo tunayopata kushuhudia, hata katika

viongozi wengine. Mwongozo halisi wa maisha si utamaduni

au ukoo wetu wala jamaa yetu. Sisi kama raia wa Ufalme wa

Kristo (Wafilipi 3:17-20) tunawajibika kufuata kwanza na

hasa yale ambayo Mungu ametufunulia katika Neno Lake

kwa njia ya Roho Mtakatifu; ndiyo tunayopaswa kukazana

kuyatii (Luka 9:23-26)!

Kama tutakuwa na juhudi na uangalifu katika kuishi

MATENDO • 15Nakala 16 / Nambari 1

Page 16: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

maisha yetu kufuatana na kipimo cha tabia ya Mungu na

Neno vilivyofunuliwa, tumehakikishiwa kukua katika

utakaso. Na tunapokua katika utakaso, tunapata kuwa

“chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaachoBwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema”

(2Timotheo 2:21).

B. KUSUDI LA UPAKO

Kwa sababu watu wengine wamechanganyikiwa kuhusu

upako, tulitumia nafasi katika sehemu iliyotangulia kuainisha

yale yasiyo upako. Sasa turejee kwa kifupi yale tuliyojifunza:

• Upako si nguvu ya kifumbo wala nguvu isiyo ya uhai.

• Upako si karama, kipawa, talanta, hisia wala nafsi

yenye kuvutia.

• Upako si wokovu.

• Upako si Ubatizo wa Roho Mtakatifu.

• Upako si kutakaswa kwa mwamini.

1. Maana ya Upako

Hivyo basi, upako ni nini?

Njia bora ya kuainisha upako ni hii:

Upako si tofauti na Roho Mtakatifu Mwenyewe katikakuwepo Kwake, akileta pamoja naye uwezo, mamlaka nakarama vinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenzi yaMungu kwa muda au dakika fulani ya utumishi au agizofulani.

Ieleweke wazi kwamba Roho Mtakatifu anahusika

kimatendo katika mambo yote matano mengine

yaliyoorodheshwa hapo juu. Pasipo kuwepo na kutenda kwa

Mungu Roho, mambo hayo matano ya lazima katika maisha

ya kila mwamini yasingekuwepo.

Hata hivyo, sehemu hii ya kazi ya Roho Mtakatifu

inayoitwa upako ina kusudi maalum lisilo na kifani.

2. Uweza Wenye Kusudi

a. Uwezo wa Ki-Mungu. Kusudi la kimsingi la upako

wa Roho Mtakatifu ni kumpa mwamini uwezo usio wa

kimaumbile.

Mungu anampa mtu yeyote anayependa Yeye uwezo

huu, ili kumsaidia afanye yale yanayotakiwa na Mungu.

Huenda ni kwa ajili ya kusema au kuhubiri, kufanya kazi

fulani, kuimba au kutumia chombo cha muziki. Au pengine

ni kwa ajili ya kuwawekea wagonjwa mikono kwa uponyaji

au ishara na miujiza mingine ambayo hutendwa na Mungu.

Unamwezesha mtu pia asali na kuombea watu kwa ufanisi

zaidi.

Ni muhimu kuona pia kwamba Mungu anaweza kumpa

mtu fulani upako kwa ajili ya kuongoza au kuwa na ustadi

hata katika biashara au kazi ya mikono (taz. Kutoka 31:3).

Mungu anataka kuwapa watu Wake upako kwa ajili ya

nafasi za utumishi ndani na nje ya Kanisa Lake – lakini

kumbuka, ni kwa ajili ya makusudi YAKE na utukufu

WAKE, si yetu au wetu!

Kumbuka upako ni nini: Ni Mungu kwa Roho Wakeakipatia chombo cha kibinadamu kilichojitoa, uwezo,mamlaka na karama vyovyote vinavyohitajika kwa ajili yakutimiza mapenzi ya Baba katika dakika fulani ya utumishiau agizo fulani.

Ni muhimu kufahamu kwamba upako ni Roho

Mtakatifu Mwenyewe! Uweza wa Mungu haupo mbali na

Yeye Mwenyewe na kuwepo Kwake. Tunaposema kuwa mtu

fulani anao upako, maana yetu ni kwamba Roho Mtakatifu

Mwenyewe yumo ndani ya maisha yake kwa njia ya pekee ili

atimize mapenzi ya Mungu kupitia kwake.

b. Nani anaweza kupokea upako huu? Unaposoma

Agano la Kale, ni rahisi kutambua wakati ambapo Roho

Mtakatifu alimjia nabii, mwamuzi, mfalme, kuhani n.k.

Lakini mgawo wa Roho Mtakatifu ulikuwa tofauti katika

Agano la Kale na Agano Jipya. Mtume Yohana aliandika:

“Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye walewamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Rohoalikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”

(Yohana 7:39).

Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mkamilifu,

amekuwepo tangu milele yote. Alihusika katika uumbaji

(Mwanzo 1:2) na katika Agano la Kale lote. Lakini MunguBaba alikuwa hajapatia maumbile Yake Mungu Roho kwa

ukamilifu mpaka Mungu Mwana alipokuwa amefungua njia

ya wokovu katika kifo Chake kama dhabihu msalabani

(Yohana 14:16-17; 16:7).

Mchungaji kwa Mchungaji: Sisi kama Wakristowanaoamini Biblia, hatuabudu miungu mitatu. Balitunamwabudu Mungu Mmoja anayejifunua katika Nafsitatu. Katika Mungu, kuna “nafsi” tatu ambazo si miungumitatu wala sehemu tatu. Nafsi hizi tatu ni Mmoja, nakila moja ni Mungu katika usawa na umilele. Akili zetuzinapata shida kubwa kufahamu asili ya Mungu aliye“tatu”-katika-mmoja. Lakini Maandiko yamefunuaukweli huu juu Yake.

Kuna tofauti moja ya kimsingi kati ya mgawo wa Roho

Mtakatifu katika Agano la Kale na mgawo katika Agano

Jipya. Katika Agano la Kale, Roho Mtakatifu alimjia juu yakemtu aliyechaguliwa kuwa chombo kwa muda. Roho

Mtakatifu alimwezesha mtu fulani binafsi (nabii, kuhani,

mwamuzi, n.k.) afanye mapenzi ya Mungu kwa dakika ile.

Ndipo Roho Mtakatifu alimwondokea mpaka dakika

nyingine ya kufanya kazi ya utumishi.

16 • MATENDO

Upako unaweza kuongeza

ufanisi wa vipawa,kwa mfano

muziki.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 17: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Lakini katika Agano Jipya, Roho Mtakatifu alitolewa ili

aingie na kukaa ndani ya mioyo ya wanadamu na kuishi

katika uhusiano unaoendelea pamoja nao. Tuangalie mifano

kadhaa ya upako wa Roho Mtakatifu katika Agano Jipya:

YesuMtu wa kwanza katika Agano Jipya aliyepokea upako

wa Roho Mtakatifu ni – Yesu! Yesu alipokea upako uliomtilia

uweza wa Roho Mtakatifu wakati wa ubatizo Wake katika

maji (Mathayo 3:16). Baada ya kujaribiwa kwake Yesu

jangwani, tendo Lake la kwanza la huduma ya hadharani

lilikuwa kusoma Isaya 61:1-2 ndani ya sinagogi. Ndipo

alipotangaza kwamba maandiko haya ya ki-Masihi yalikuwa

yametimia (Luka 4:14-21).

Unaona kwamba upako wa Roho Mtakatifu uliotajwa

katika Isaya 61:1-2 ulikuwa kwa ajili ya kuwezesha mapenzi

ya Baba yatimizwe katika huduma ya miaka ya kwanza ya

Yesu.

Yesu alikuwa Mungu mkamilifu na mwanadamu

mkamilifu wakati alipokuwa katika mwili Wake hapa duniani

(Wafilipi 2:5-8). Lakini alihitaji uweza wa Roho Mtakatifu ili

atimize mapenzi ya Baba. Ikiwa Yesu, Mwana wa Mungu,

alimhitaji Roho Mtakatifu, je, haja yetu sisi ni zaidi kiasi

gani? (Taz. pia Matendo 10:38.)

Kanisa La AwaliViongozi wa Kanisa la Awali

Siku ile ya Pentekoste (Matendo 1:12 – 2:4), viongozi

wa Kanisa la awali na wanafunzi wengine walikuwa wakisali

katika chumba kikubwa orofani. Waliokuwepo ni pamoja na

wanafunzi wa kwanza kumi na mmoja (Yuda akiwa ameisha

kufa), mtume mpya aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda

kwa kupiga kura, na kundi la wanafunzi wengine (kama watu

120 hivi). Ghafla, Roho Mtakatifu aliyeahidiwa (Yoeli

2:28-32) alimiminwa juu yao (Matendo 2:2-4).

Mtume Paulo aliongoka na kumwamini Kristo baadaye.

Yeye pia alipokea Roho Mtakatifu akaanza kuhubiri Injili ya

Yesu Kristo kwa bidii kubwa (Matendo 9:1-22).

Wainjilisti kama Filipo walijazwa na Roho Mtakatifu na

pia kuongozwa na Yeye (Matendo 8:29). Waliopewa karama

ya kufundisha, kama Apolo, wasingaliweza kufundisha kwa

ujasiri pasipo upako wa Roho Mtakatifu (Matendo 18:24-28;

taz. pia 1Wakorintho 3:5-7). Walioitwa watumikie Mwili wa

Kristo uliokuwa ukikua haraka walijaa Roho, kwa mfano

Stefano (Matendo 6:1-10). Kuna mafungu mengine ya Agano

Jipya pia yanayohusu hoja hii (yaani Matendo 4:13,33;

11:27-28; 21:10-11).

Wanafunzi wa Kanisa la AwaliWaliojazwa katika chumba cha orofani Siku ya

Pentekoste walikuwa wa kwanza tu kati ya waamini wengi

zaidi waliojazwa na kupewa upako wa Roho Mtakatifu

(Matendo 4:31; 5:32; 13:52; n.k.).

Uwezo Kwa Ajili Ya UinjilistiJinsi mwako wa Injili ulivyoenea, ndivyo miminiko

mkuu wa Roho Mtakatifu ulivyoongezeka pia. Haya

yalitimiza maneno ya Yesu mara kabla ya kupaa Kwake:

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu RohoMtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katikaYerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hatamwisho wa nchi” (Matendo 1:8).

Yesu alipoorodhesha maeneo haya ya kijiografia hakuwa

akibuni kilugha. Kitabu cha Matendo kinafunua kutimizwa

kwa ahadi hii ya kumiminwa kwa Roho Mtakatifu juu ya

wale wote ambao wangemwamini, pamoja na kuanzishwa

kwa uinjilisti kwa dunia nzima.

Katika Yerusalemu… (ilitimizwa Siku ya Pentekoste –

Matendo sura ya 2). Ilionekana kama kundi hili ya waamini

Wayahudi wangehubiri kule Yerusalemu tu. Kufanya hivyo

kungaliweza kuzuia kusudi la Kristo na utume wa Injili

kutolewa kwa watu wote, nyakati zote, mahali pote.Lakini waamini walianza kuteswa karibu mara baada ya

Injili kuanza kuhubiriwa. Mungu alitumia mateso yale

kulazimisha Kanisa la awali litawanywe mbali kuanzia

Yerusalemu, ili watimize mapenzi ya Baba ya kufikisha

ujumbe wa wokovu kwa kila mtu.

Ndipo katika Matendo sura ya 8 tunakutana na mtesi

mkubwa wa Kanisa – Sauli. Mashambulio haya yangeonekana

kuwa habari mbaya, kabla hatujasoma katika Maandiko:

“Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na hukowakilihubiri neno [Injili]” (Matendo 8:4). Maeneo waliyofikia

ni pamoja na Uyahudi na Samaria (Matendo 8:1-25).

Kusonga Mbele Na Mbali Kwa InjiliAngalia kwamba Roho Mtakatifu alikuwa akimiminwa

juu ya wale waliopokea Injili (Matendo 8:16-17). Kulikuwa

na ishara na miujiza pia iliyofuatana na kuhubiriwa kwa Injili

(Matendo 8:6,13).

Lakini kazi kubwa zaidi ilikuwa ifunuliwe katika Kanisa

la awali. Mungu alitaka Injili ihubiriwe pote duniani. Yesu

aliwaamuru waamini “Enendeni ulimwenguni mwote,mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Neno

linalofanana na hili limeandikwa katika Matendo 1:8: “hatamwisho wa nchi”.

Kusonga mbele na nje zaidi kulianza wakati Filipo

alipokutana na towashi wa Kushi, ambaye aliongoka

mapema akawa Mkristo (Matendo 8:26-40). Mtu huyu wa

MATENDO • 17

Mtummojammoja,

kujazwa nakupakwamafuta...

Nakala 16 / Nambari 1

Page 18: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Kushi katika mapokeo ya Kanisa anasifiwa kuwa mtu wa

kwanza kuleta Injili barani Afrika!

Mapema baadaye, Sauli alibadilishwa kabisa kwa ajili ya

kukutana na Yesu (Matendo 9:1-19), naye aliitwa awe mtume

kwa Mataifa (Matendo 9:15). Lakini lengo la sehemu kubwa

ya mahubiri ya Injili bado lilikuwa Wayahudi – mpaka

Mungu alipofanya badiliko kubwa kabisa!

Tunasoma katika Matendo kuhusu Kornelio, Mrumi

(Matendo 10:1-48). Petro alitumwa kwa Kornelio aanze

kuwashirikisha Injili watu wa Mataifa. Tendo hili lilikuwa

gumu kwa Petro kufanya kama Myahudi (Matendo 10:9-16).

Lakini wakati Petro alipokuwa akihubiri, Roho

Mtakatifu aliwashukia Kornelio na watu wote wa nyumba

yake – katikati ya mahubiri ya Petro (Matendo 10:44)! Hata

hivyo, ndugu wa Kiyahudi waliokuwepo walionea ugumu

ukweli kwamba watu wa Mataifa walikuwa wakipewa Injili

na Roho Mtakatifu (Matendo 10:45-48).

Mwisho, kulikuwa na mkutano mkuu muhimu wa

mitume pale Yerusalemu, ambapo Petro aliitwa atoe

ushuhuda wake (Matendo 11:1-15). Hatimaye waliweza

kufahamu na kukubali yale ambayo Yesu alikuwa

amewaambia wazi: Injili ihubiriwe kwa kila mtu – “hatamwisho wa nchi” (Matendo 1:8).

Mpango Wa Mungu UmefunuliwaNi muhimu kabisa kutambua jambo fulani kuhusu Kitabu

cha Matendo. Injili ya Yesu Kristo SI dini mpya wala

mafundisho mapya ya dini ya Kiyahudi. Mambo yote

yaliyokuwa yametokea katika uhusiano uliopo kati ya binadamu

na Mungu tangu Bustani ya Edeni – historia nzima ya Agano la

Kale – yalikuwa yakiendea kilele chake katika wakati huu.

Mungu alikuwa na mkakati Wake ulioanza baada ya

binadamu kuchagua dhambi (Mwanzo 3:15). Mpango huu

ulikuwa kumwokoa katika adhabu ya kifo kwa ajili ya

dhambi, kwa neema kupitia imani (si kwa matendo) katika

Yesu Kristo. Mpango huo uliwezekana tu kutokana na

dhabihu ya kifo iliyofuatwa na ufufuo wa Yesu. Tunasoma

kuhusu mkakati huo wa Mungu katika Injili (Mathayo,

Marko, Luka na Yohana).

Lakini kusudi la Mungu lilikuwa zaidi ya imani mpya na

uhusiano na Yeye uliorudishwa. Mungu alitaka (na bado

anataka) kuishi ndani yetu, kutupa uhakika na uwezo

tunaohitaji ili tuishi katika ushindi na kutimiza mapenzi Yake

katika maisha yetu hapa.

Kwa hiyo, katika hekima Yake na upendo Wake visivyo na

mwisho, Mungu alimimina Roho Mtakatifu, ambaye angeishi

ndani ya kila mwamini (Yoeli 2:28-29). Kristo hakuja ili alete

dini au theolojia mpya. Bali alikuja ili atimize yote ambayo

Mungu alikuwa ameahidi kwa ajili ya wokovu wa binadamu!

Kwa kweli, dhabihu ya Kristo inatuwezesha turudishwe

katika ushirikiano wa karibu sana na Mungu. Lakini Mungu

anakusudia pia kwamba uweza wa Mungu Mwenyezi ukaendani yetu katika Roho Mtakatifu. Ulimwengu hauwezi

kupuuza wala kugeuzia maana uweza huu. Watu wanaweza

kudhihaki, kukemea au kuhukumu, kama walivyofanya Siku

ile ya Pentekoste (Matendo 2:5-13), lakini hawawezi kuzuia

kazi na uweza wa Roho Mtakatifu kupitia kwa maisha ya

mwamini yaliyotolewa Kwake!

Tunayoona katika Kitabu cha Matendo kuhusu ishara,

maajabu, miujiza, wokovu, uponyaji, n.k. yanawezekana

nayo yanahusiana na sisi leo, kama yalivyokuwa kwa Kanisa

la awali (Yoeli sura ya 2; Matendo 2:33,38-39). Tunahitaji

uwepo na uweza wa Roho Mtakatifu leo kama miaka 2000

iliyopita! Tumshukuru Mungu kwamba “Yesu Kristo [na

Roho Mtakatifu] ni yeye yule, jana na leo na hata milele”

(Waebrania 13:8).

Waamini Wote Wa Kristo Kwa Nyakati ZotePetro, akiongozwa na Roho Mtakatifu, alitangaza

kwamba karama iliyoahidiwa ya Roho Mtakatifu akaaye

ndani yetu ni “kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwawatu wote walio mbali, watakaoitwa na Bwana Mungu wetuwamjie” (taz. Matendo 2:33,38-39).

Walioainishwa kuwa “watu wote walio mbali” kwa

hakika ni pamoja na vizazi (vya Wayahudi) vilivyozaliwa na

vitakavyozaliwa, lakini pia makabila ya Mataifa na kila

kabila, lugha na ukoo duniani (Waefeso 2:11-19; Wagalatia

3:28; Wakolosai 3:11).

18 • MATENDO

Kila kabila... ...kila kizazi

Nakala 16 / Nambari 1

Page 19: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Uhusiano Wa Maisha YoteKarama ya uwepo wa Roho Mtakatifu katika upako

huingia ndani ya moyo wa kila mfuasi wa Kristo. Huu ni

upako wa kawaida ambao kila mwamini anapokea wakati wa

kuokolewa.

Mtume Yohana anatupa maoni ya ndani kuhusu upako

huu wa kawaida katika barua yake ya kwanza. Yohana

aliwakumbusha wafuasi wa awali wa Kristo jambo muhimu:

“Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyimnajua yote” (1Yohana 2:20).

Kufuatana na sarufi ya lugha ya Kiyunani ya asili katika

mstari huu, ni wazi kwamba Yohana hakumaanisha ibada ya

kidini ambapo walipakwa mafuta au kitu kingine. Bali upako

huu ulitoka kwa “Yeye aliye Mtakatifu”, ambaye ni Yesu

Kristo, Mwana wa Mungu (Yohana 6:69; Matendo 3:14; 4:27).

Kwa maneno mengine, “YULE Aliyepakwa Mafuta”

(Yesu Kristo) anawapa wafuasi Wake karama kutoka Kwake;

karama hii ni Roho Mtakatifu, aishi ndani yetu na kukaa

pamoja nasi (Mathayo 3:11; Matendo 1:5; Yohana

14:16-17,26; 16:7). Upako huo ni kwa ajili ya kila mwamini

anayemtegemea Kristo kwa ajili ya wokovu kwa neema

katika imani.

Ndipo Yohana, kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu,

anaendelea: “Nanyi, mafuta [ya kiroho, si ya kimwili] yalemliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja yamtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yakeyanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweliwala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndaniyake” (1Yohana 2:27).

Upako huu si wa mara moja tu; unatakiwa uwe uhusiano

na Roho Mtakatifu wa maisha yote unaoendelea kukua. Ni

Roho Mtakatifu anayetutia kwenye kweli yote, kutufundisha

mambo yote na kutukumbusha yale ambayo Yesu alifundisha

(Yohana 14:26). Roho Mtakatifu anatusaidia tufahamu

ukweli na kumtukuza Yesu (Yohana 16:13-14).

Ni wazi kwamba Yohana hasemi kwamba huduma za

kufundisha hazihitajiki (Mungu anatupa walimu – tazama

Warumi 12:7; Waefeso 4:11). Lakini hapa Yohana

anamaanisha mafunuo na ufahamu ambavyo Roho Mtakatifu

atampatia mtu binafsi anapomwitikia Yeye katika maisha

yake (1Wakorintho 2:10-16; Waefeso 1:17-18).

Kwa hiyo tunaona kutokana na Neno la Mungu kwamba

upo upako ambao kila mfuasi wa Kristo anaupokea wakati

anapookolewa.

Mchungaji kwa Mchungaji: Yale ambayo RohoMtakatifu anatilia mwangaza au anayofunua kuhusuukweli yatakubaliana wakati wote na yale ambayoamekwisha funua katika Neno la Mungu lililoandikwa(Yohana 16:13-14).

C. KAZI YA UPAKO

Tunapojifunza kuhusu kazi na hamasa ya Roho

Mtakatifu inatubidi tukiri kuwepo kwa siri za kifumbo

zisizoeleweka. Kuna sehemu ya ukuu wa Mungu katika

upako ambayo hatuwezi kuielewa (Yohana 3:8). Itikio letu

pekee kwa ukuu wa Mungu lazima liwe kujitolea kwa wazi

na ukamilifu kwa Ubwana Wake na mapenzi Yake.

Katika hekima Yake Mungu amependa kuacha sehemu

isiyoeleweka katika njia Zake, ikitubidi tuishi kwa imani

(2Wakorintho 5:7; Waebrania 11:6). Kuna mengi katika

maisha haya ambayo tunayaona na kuyafahamu “kwasehemu” (1Wakorintho 13:12). Mwelekeo wetu kwa Bwana

lazima sikuzote uwe wa kuamini, kutii na kunyenyekea Neno

Lake zima.

Kanuni Za Kimatendo Za UpakoTukiendelea na mafunzo haya, turejee tena kuainishwa

kwa upako:

Upako ni Roho Mtakatifu Mwenyewe katika kuwepoKwake, akileta pamoja naye uwezo, mamlaka na karamavinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu kwamuda au dakika fulani ya utumishi au agizo fulani.

Tukiwa tumeyafahamu haya kikamilifu, tuangalie

kanuni kadhaa kuhusu jinsi upako wa Roho Mtakatifu

unavyotenda kazi.

1. Upako unahusiana moja kwa moja na wito wa mtu

binafsi kutimiza kazi ya huduma aliyopewa na Mungu.

Kwa maneno mengine, Mungu anapompa mtu fulani

kazi au wito wa kihuduma, Yeye anampatia pia mahitaji yoteya uwezo, mamlaka, vipawa, mafunuo, utambuzi, n.k.

yanayotakiwa kwa ajili ya kutimiza kazi ile. Haleluya!

Mungu anapokuamuru au kukuongoza ufanye mapenzi

Yake, yote unayohitaji ili uweze kutimiza mapenzi Yake kwa

ufanisi yamepatikana kwa uweza na upako wa Roho

Mtakatifu. Yale ambayo Mungu anamwamuru mtu ayatende,

anampatia uwezo wa kuyatenda!

Bila shaka, sikuzote kuna kusoma, kujifunza na

kubadilishwa kibinafsi kunavyohitaji kufanyika njiani.

Tunapokazana - hali tunakua katika uwezo wetu, vipawa

vyetu na ujuzi wetu katika Neno la Mungu - ndipo Mungu

atatupatia hata zaidi.

Kanuni hii ya kuwa waaminifu kwa yale tuliyo nayo na

Mungu kutupatia zaidi (Luka 16:10a; 19:17) ni kanuni ya

lazima kwa ajili ya kukua katika upako wa Mungu.

Kutenda Katika UpakoMungu anataka kutupatia upako ili tutimize mapenzi

Yake na wito Wake. Tunasoma kuhusu kanuni inayofananakatika maelezo ya Paulo kuhusu imani.

Warumi 12:3: “kama Mungu alivyomgawia kila mtukiasi cha imani.” Kiasi hiki cha imani (kama ilivyo kwa

upako) ni uweza wa Mungu unaolingana na kipawa

alichotupatia.

“Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiriya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri yaimani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenyekufundisha, katika kufundisha kwake” (Warumi 12:6-7).

Paulo anatamka kanuni hiyo hiyo kwa njia tofauti kidogo

katika barua yake kwa Waefeso: “Lakini kila mmoja wetualipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chakeKristo” (Waefeso 4:7). Kwa maneno mengine, kipawa hiki

kilichopimwa cha uweza wa ki-Mungu kinahusiana moja

kwa moja na kule kuweza kutenda katika kipawa ambacho

Mungu amempatia mtu fulani binafsi kwa ajili ya kutoa

huduma.

Mchungaji kwa Mchungaji: Mstari wa Waefeso4:7 unahusiana moja kwa moja na vipawa vya kirohovinavyotajwa chini katika Waefeso 4:11. Mstari huu

MATENDO • 19Nakala 16 / Nambari 1

Page 20: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

(4:7) HAUHUSU kipimo cha neema kwa ajili yawokovu jinsi wengine wanavyofundisha kwa makosa.Neema ya Mungu kwa ajili ya wokovu hutolewasawasawa kwa watu WOTE, kwa sababu Yeye anatakamtu yeyote asipotee, bali wote waokolewe (Matendo2:21; 17:30-31; Warumi 3:22-23; 11:32; 1Timotheo 2:4;4:10; Tito 2:11; 2Petro 3:9). Mungu anataka watu wotewapokee karama Yake ya wokovu inayotolewa kwaimani katika Kristo tu (Waefeso 2:8). Inasikitisha hatahivyo kwamba wengi wamekataa na wataendeleakukataa karama hii - na lililo baya zaidi, mamilioni yawatu leo hawajasikia kamwe ujumbe wa Injili wawokovu kwa njia ya Yesu Kristo.

Mchungaji kwa Mchungaji: Ingawa huu si wakatiwa kujifunza kwa ukamilifu kuhusu vipawa vya kiroho,nikupatie kanuni moja muhimu kuhusu vipawa vyakiroho.

Vipawa vyote vya kiroho - kama ni vipawa vyamafunuo (1Wakorintho 12:1-11); vipawa vyamadhumuni (Warumi 12:3-8) au vipawa vya huduma(Waefeso 4:11) - hutolewa kwa uchaguzi wa Mungu.Si juu yetu kuchagua au kudai kipawa tunachotaka auambacho tunaona kinahitajika zaidi hasa. Munguanatoa vipawa Vyake kufuatana na ujuzi Wake usio namipaka na utakatifu Wake ulio kamilifu kabisa (taz.1Wakorintho 12:11).

Ingawa kila mwamini ana nafasi ya kihudumakatika mwili wa Kristo, na katika dunia ambamotunaishi, kuna tofauti kubwa za wito na vipawa. Katikakila moja, Mungu anatoa uweza, imani, neema naupako vinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenziYake na kusudi Lake.

Ingawa inatubidi tusijaribu kamwe kutawala aukufanyiza upako (Roho Mtakatifu) tunaweza kukuakatika upako. Tunapokuwa waaminifu kwa yaleambayo Mungu ametupatia, anaachia zaidi (Mathayo25:21). Tunaweza pia kujifunza kutenda kwa ufanisizaidi katika huduma, na kufuatana na mapenzi yaMungu kwa ukaribu zaidi [Haya yanajadiliwa zaidikatika Sehemu Ya III, B, “Kukua katika Upako”.]

“Kuhamisha” UpakoMafunzo fulani hudai kwamba mtu aliyepewa upako na

kuwa na uwezo katika huduma anaweza kumwekea mikono

mtu mwingine na kumpatia “sehemu ya upako wake” - hata

sehemu maradufu! Tendo hili limeitwa “kuhamisha upako”

nalo linahusiana kwa mbali na matukio katika Maandiko

kuhusu Eliya na mfuasi wake Elisha (taz. 1Wafalme

19:16,19; 2Wafalme 2:1-13).

Lakini maandiko yenyewe hayathibitishi mafunzo haya.

Eliya alimtupia Elisha vazi lake (joho) (1Wafalme 19:19).

Lakini tendo hili lilikuwa alama ya uthibitisho tu la yale

ambayo Bwana alikuwa amekwisha tamka kuhusu wito wa

Mungu kwa Elisha kuwa mrithi wa Eliya (1Wafalme 19:16).

Katika tendo hili, Eliya hakumwita Elisha, wala hakuweza

kumpa upako wa kuthibitisha wito wake. Ilikuwa kazi ya

Mungu. Eliya alitii Neno la Mungu tu, na kuwasilisha yale

ambayo Mungu alikuwa amemwagiza amwambie Elisha

(1Wafalme 19:19).

Elisha alitambua wazi kwamba yeye hakuwa na uwezo

wa kuendeleza huduma ya kinabii ya Eliya kama Mungu

alivyokuwa amemwita yeye (Eliya). Elisha alijua kwamba

alihitaji uwezo wa Mungu (upako), unaotajwa katika

Maandiko kama roho ya Eliya (2Wafalme 2:9,15). Kwa hiyo

Elisha alimwomba Eliya “sehemu maradufu” ya roho yake

(2Wafalme 2:10).

Kwa sababu Eliya alikuwa nabii aliyepakwa mafuta na

Mungu, itiko yake kwa ombi la Elisha ili apate maradufu

ilikuwa maneno ya unabii tu: “Umeomba neno gumu; lakini,ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona,hulipati” (2Wafalme 2:10).

Tunaposoma sehemu hii ya Maandiko ni wazi kwamba

Eliya alijua kwamba hakuweza kumpa Elisha lolote la

kiroho. Aliweza kukiri wito wa Mungu kwa Elisha, lakini

hakuweza kumtia mafuta (upako) kwa ajili ya kuthibitisha

wito huu.

Ni wazi kwamba Mungu, katika ukuu Wake, alimruhusu

Elisha amwone Eliya akinyakuliwa kwenda mbinguni. Kwa

hiyo Elisha aliokota vazi la Eliya kufuatana na mapenzi yaMungu, kama ilivyotabiriwa. Kutoka wakati huu, upako wa

Mungu ulionekana kwa wazi katika huduma ya Elisha

(2Wafalme 2:15).

Mtoaji wa wito, vipawa na upako ni Mungu Mwenyewe,

kwa sababu Mungu peke Yake anaweza kutoa Roho

Mtakatifu! Sisi hatuwezi kumtawala Mungu wala Roho Wake;

hatuwezi kuamua nani atapewa upako, au kiasi cha upako

atakachopokea. Wala hatutawali vipawa na wito kutoka kwa

Mungu. Kama Mungu ametupa upako kwa ajili ya huduma,

hatuwezi kuamua kumpatia mtu mwingine upako huo.

Mungu Anaita - Sisi TunathibitishaHata Musa, aliyekuwa mmojawapo wa watumishi

wakuu wa Mungu, hakuweza kuwapa wengine upako ambao

Mungu alikuwa amempa yeye. Lakini, Bwana Mwenyewe

alitwaa sehemu katika upako aliokuwa amempa Musa, naye

Bwana aliwawekea wazee (Hesabu 11:16-17).

Musa aliamriwa na Mungu ampe Yoshua sehemu ya

mamlaka yake (Hesabu 27:20) na kumpa mausia (Hesabu

27:23). Lakini haya yalitendeka baada ya Mungu kumteua

Yoshua kuwa mrithi wa Musa (27:18). Pia, Yoshua alikuwepo

wakati Bwana alipowapa wazee upako (11:16-17,28), ndiyo

sababu Yoshua anaelezwa kuwa “mtu mwenye roho ndaniyake” kama kiongozi kati ya Waisraeli (27:18).

Bwana ndiye aliyemwita Yoshua na kumpa upako. Musa

alithibitisha wito wa Yoshua, na kumpa mausia ya kuendelea

baada ya kuondoka kwake.

Ni Roho Mtakatifu aliyewapa Eliya na baadaye Elisha

kipawa cha unabii na upako wake, pamoja na ishara na

miujiza (taz. pia Hesabu 11:25-29; 1Samweli 10:6,10;

1Wafalme 18:46).

Mchungaji kwa Mchungaji: Si kosa kutaka kutokakwa Mungu “sehemu maradufu” ya Roho Wake. Wala sikosa kuomba kipawa fulani maalum ili tufanye huduma.Tunapaswa tuombe; halafu inatubidi tumtegemeeMungu kwa yale atakayotupatia, na lini atakapotupatia.

Lakini tazama pia kwamba Elisha alikuwa mtiifukatika kutimiza yote ambayo Mungu alikuwa amemwitaayatende - katika kuitikia wito wa awali, na pia katikakujiandaa kwa ajili ya kupokea upako wa Mungu(1Wafalme 19:20-21; 2Wafalme 2:1-11). Wito waMungu na upako Wake havitatimizwa moja kwa moja

20 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 21: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

katika maisha yetu. Bali utiifu na unyenyekevu wetu, nakushiriki kwetu, huhitajika katika kila hatua ya njia -wakati wa maandalizi, na utendaji, wa kazi ya hudumatuliyopewa.

MgawanyoWazo la mtu mmoja “kumhamishia” mwingine upako

wake si sahihi. Lakini Maandiko hutupatia mifano mingi ya

tendo linaloitwa mgawanyo. Hufuatana hasa na uwekaji wa

mikono (Waebrania 6:2) na maombi, kwa mwongozo wa

Roho Mtakatifu. (Taz. Matendo 13:1-3; 1Timotheo 4:14;

2Timotheo 1:6.)

Ninafahamu habari za wanaume na wanawake wa

Mungu wenye uwezo ambao huwaombea wengine wapokee

mgawanyo wa Roho Mtakatifu. Tumekwisha jifunza

kwamba hao hawawezi kumpatia mtu mwingine kipawa chao

wala upako wao. Lakini inaonekana kwamba sehemu fulani

ya yale ambayo Mungu anatenda kwa Roho Wake kwa njia

ya huduma fulani, au kwa msimu maalum ambapo Mungu

anatenda kwa njia thabiti na ya kifalme, inaweza kuamshwa

ndani ya wengine, au kugawanywa kwao. Mara kwa mara,

watu walioombewa katika mkutano maalum huonekana

wakitenda katika mamlaka na uweza wa Roho Mtakatifu vya

juu zaidi baada ya kuombewa.

Mimi binafsi mara kadhaa nimepokea mgawanyo wa

Roho Mtakatifu ulio na nguvu kubwa. Matukio haya

yalibadilisha maisha yangu binafsi pamoja na mwelekeo

wangu katika huduma baada ya kuombewa. Lakini hii ni kazi

ya kifalme ya Roho Mtakatifu akileta mgawanyo mpya wa

upako katika maisha yangu, si matendo ya wanadamu.

Mgawanyo UnaothibitishaMfano wa ki-Biblia ulio wazi hasa wa aina hii ya

mgawanyo huonekana katika kukua kwa huduma ya

Timotheo.

Paulo anamkumbusha Timotheo kuhusu tukio fulani

mapema katika huduma yake ambapo Paulo na wazee wa

makanisa ya Ikonio na Listra walimwekea Timotheo mikono

yao na kumwombea: “Usiache kuitumia karama ile iliyomondani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikonoya wazee” (1Timotheo 4:14).

Tukio hilo hilo limetajwa tena katika barua ya Paulo ya

pili kwa Timotheo: “Kwa sababu hiyo nakukumbusha,uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwakuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho yawoga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”(2Timotheo 1:6-7; taz. pia 1Timotheo 1:18).

Neno la asili lililotafsiriwa ‘karama’ katika mistari hii ni

charisma. Neno hili linaashiria kwamba mafunuo ya Roho

Mtakatifu yalitolewa kwa Timotheo wakati Paulo na wale

wazee walipomwombea.

Paulo hakuwa chanzo cha karama ya Timotheo wala cha

wito wake. Ila, wakati Paulo na wale wazee walipomwekea

Timotheo mikono na kumwombea, Roho Mtakatifu alifunua

mapenzi ya Mungu kwa Timotheo na kutamka kiunabii

kupitia kwao katika kuthibitisha wito wa Mungu na mapenzi

Yake kwa ajili ya maisha ya Timotheo. Walipomsimika

Timotheo katika utume wa Bwana, Roho Mtakatifu ndiye

aliyempa Timotheo upako wa kutimiza wito wake kutoka

kwa Mungu.

Mchungaji kwa Mchungaji: Ni kwa njia yamatukio haya ya maombi na kuwekewa mikonokwamba Roho Mtakatifu mara nyingi atafunua kiasifulani cha mapenzi na makusudi ya Mungu. MapenziYake yanaweza kufunuliwa kama picha akilini, neno lakinabii, andiko linalothibitisha, au maono ya yaleambayo Roho Mtakatifu yanamtakia mtu fulani au haliyake.

Katika hali hii, inatubidi tumsubiri Bwana kwautulivu na kusikiliza kwa ajili ya yule ambayeunamwombea. Lakini kama hatujasikia neno rasmikutoka kwa Bwana, inatupasa tusitamke.

Thamani ya nafasi yetu kama wachungajiinatokana na kuwa waaminifu na watiifu kwa Mungu naNeno Lake. Huenda tutashawishika kuwapendezawatu, au tutajisikia kusukumwa tuwe viongozi “wakiroho” wenye neno la kuwapa watu. Ndiyo Bibliainayoita “kuwaogopa wanadamu”. Ni mtego unaowezakusababisha kuridhiana kubaya zaidi sana pamoja namiitikio ya kimwili (Mithali 29:25).

Tumeitwa tuwe waaminifu: kwa Mungu, kwa NenoLake, na kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu. Kamaunamwombea mtu fulani, na Bwana hasemi na wewejuu yake, hali hii ni sawa. Huenda Bwana anatakakusema naye moja kwa moja, au kwa wakati mwingine,au kwa njia nyingine. Mungu akinyamaza, sisitunyamaze pia. Mungu akisema nasi kuhusu mtumwingine, lazima tuwe waaminifu na waangalifu katikakusema yale tu ambayo Mungu amesema au kufunua- si kuongeza wala kupunguza.

Si nafasi yetu kamwe kumwambia mtu afanye nini,aende wapi, na kadhalika. Sisi tunamwambia yule mtuyale tunayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maranyingi sana, yanapaswa yathibitishe jambo fulanikwake ambalo Bwana amekwisha weka moyonimwake. Ndipo hoja inabaki kati yake na Mungu kwa ajiliya kutimizwa.

MATENDO • 21

Kusimikwa kwa ajili ya utumishiwa Bwana

Nakala 16 / Nambari 1

Page 22: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mwisho, hoja muhimu: Neno la kinabii kutoka kwaMungu SIKUZOTE litakubaliana na yale ambayoMungu amekwisha kutufunulia katika Biblia, Neno Laketakatifu lililoandikwa! Yote tunayofanya maishanimwetu lazima yafuatane na kupatana na Neno laMungu, na kanuni zilizofunuliwa ndani yake.

Kufuata Mwongozo Wa Roho MtakatifuMifano mingine ya mgawanyo inaonekana katika

Matendo 6:1-7 na 13:1-3. Matukio haya katika Kanisa la

awali hayakuwa tu ibada ya dini. Katika masimulizi haya,

viongozi katika Mwili wa Kristo walitafuta mwongozo wa

Roho Mtakatifu wakaufuata kinaganaga. Ndipo kwa imani

thabiti, waliomba kwa kutii mwongozo huo. Katika kuitikia,

Mungu aliwaandaa, kuwabariki na kuwapa upako wale

walioombewa ili atimize yale aliyokuwa amewaagizia.

Jambo lililo muhimu kabisa ni hili: Mwongozo wa Roho

Mtakatifu ni kwa ajili ya kufunua makusudi na mapenzi

rasmi ya Mungu. Yesu Mwenyewe alikiri kwamba huduma

Yake ya duniani iliwezekana kwa sababu ile tu kwamba

alikuwa akifanya mapenzi ya Mungu Baba (Yohana 5:19,30;

6:38; 8:29). Tunaweza na inatubidi tufanye sawasawa.

Tunapofuata mwongozo wa Mungu Roho, Yeye

atatutumia katika kutimiza mapenzi Yake. Sehemu ya haya

inaweza kuwa kuthibitisha wito wake katika wengine; na

halafu kuwaombea ili wapewe upako na karama kwa ajili ya

yote ambayo Mungu amekusudia kwa ajili yao, kwa utukufu

Wake na kwa kujenga Mwili Wake (Waefeso 4:12-16).

Uhuru ZaidiKatika semina nyingi za World MAP za wachungaji,

nimefundisha kuhusu upako au kuhusu ubatizo wa Roho

Mtakatifu. Katika mikutano hii, wachungaji wasiohesabika

wamejazwa Roho Mtakatifu kwa upya; wengine walibatizwa

na Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza. Mimi binafsi

sikuwapa chochote, zaidi ya mafundisho kutoka katika

Maandiko kuhusu mambo haya. Huenda mimi niliwaombea,

lakini ni Roho Mtakatifu aliyewagusa na kuwajaza (Luka

3:16; Yohana 16:7) - kwa sababu waliona njaa ya kumpokeaYeye zaidi!

Tunapokea taarifa nyingi sana kutoka kwa wachungaji

hao hao kuhusu mabadiliko ya ajabu katika huduma zao.

Wameona nyongeza ya ishara, maajabu na miujiza katika

mikutano yao; wana bidii mpya kwa ajili ya Mungu na kwa

uinjilisti; wanawaongoza watu wengi kwenye wokovu au

ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Imekuwaje?

Kwanza, kumekuwa na mafundisho kutoka katika Neno

la Mungu, linaloleta mwangaza kuhusu hoja fulani. Mtu

anayesikia mafundisho anaamua kupokea kwa imani yale

aliyojifunza - na kuyatendea kazi!

Lakini yanayotokea ni zaidi. Roho Mtakatifu yupo naye

anatenda kwa njia pekee, akishuhudia ukweli wa Neno la

Mungu lililoelezwa. Kwa hiyo, watu wanapoitikia kwa moyo

wa wazi na kwa imani - na, katika njaa yao kwa Mungu,

wakiomba wapokee yote ambayo Yeye amewaandalia - Yeye

anaitikia njaa yao kwa njia maalum na nzito (Mathayo

5:6; Yohana 6:35). Wanapokea kweli! Upako zaidi wa Mungu

kwa ajili ya huduma unafunguliwa kwao.

Tafadhali ufahamu kwamba Mungu hawekewi mipaka

ya uwanja wa mkutano au ya tukio fulani. Mungu Roho yupo

kila mahali, naye atawaitikia wale wanaomtafuta kwa moyo

wao wote (Yeremia 29:12-13).

Mungu atakutana na wewe popote ulipo, unapomtafuta

kwa moyo wako wote. Haleluya!

Ninataka kusema tena kwamba hakuna mtu

anayefahamu kikamilifu jinsi Roho wa Mungu awezavyo

kutenda na atakavyofanya kazi. Lakini tunajua kwamba

Mungu kwa Roho Wake ataitikia njaa yetu Kwake.Roho Mtakatifu anawajaza watu kwa upya akiitikia

maombi yao (Luka 11:9-13). Imani yao inapohuishwa,

wanaanza kuomba kwa imani wakiamini kutoka hapo walipo

(Waebrania 11:6).

Maombi BoraKama tulivyojifunza, mitume waliwekeana mikono na

pia kuwawekea watenda kazi wengine, wakiwaombea na

kuwasimika katika huduma (Matendo 13:2-3; 6:1-6). Mungu

aliwaongoza wafanye hivyo, kwa hiyo tendo la lazima na

lenye nguvu lilikuwa likitokea.

Huenda hatufahamu njia zote za Roho Mtakatifu. Lakini

hili tunalijua: Wakati Roho Mtakatifu anapotuongoza

tuwaombee wengine - na wakati tunapowaruhusu watu

wengine wa Mungu, wanaume kwa wanawake, watuombee

sisi - upako, karama, hekima na mengine zaidi vya Mungu

hugawanywa.

Ingawa sisi hatuwezi kuamua wakina nani wapokee

karama za Mungu na upako Wake, kwa hakika tunaweza

kuwaombea wengine wawe zana zenye nguvu na kutumika

kwa ufanisi katika huduma ya Mungu kwa uweza wa Roho

Mtakatifu (2Timotheo 1:6-7).

Lazima sikuzote tutii na kupokea mapenzi makuu ya

Mungu kwa maisha yetu katika mambo haya. Huenda

maombi bora tunayoweza kumletea Mungu ni: “Je, ni vipi

vipawa, na kazi, ulivyoniandalia? Je, umeniita nivitumieje?

Unataka kunipa nini ili nitimize mapenzi Yako?”

Mungu ana makusudi pekee ya maagizo, wito na

huduma kwa ajili ya kila mwanamume na mwanamke.

Pamoja navyo, Yeye atatupa kwa utele “mambo ya ajabu mnokuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu[Roho Mtakatifu] itendayo kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20)

ili kutuwezesha tutimize mapenzi Yake tunapomtolea

kikamilifu maisha na mapenzi yetu.

2. Upako hautolewi ili kukaliwa, kutawaliwa wala

kufichwa ndani yetu.

Kusudi la msingi la upako ni kutuwezesha tuwe na

ufanisi katika huduma au katika kazi yetu. Hili ni pamoja na

kuwatolea wengine kwa hiari katika huduma yale ambayo

sisi tumepewa na Roho Mtakatifu.

Yesu Mwenyewe, mwanzoni mwa huduma Yake,

alisema: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maanaamenitia mafuta...” (Luka 4:16-21).

Utaona unaposoma mistari hii kwamba Yesu aliendelea

kusoma orodha ya mambo ambayo Yeye alitiliwa mafuta

(upako) kwa ajili ya watu wengine.

Upako ni heshima takatifu. Haitupasi tuutamani ili

tuonekane kuwa watu wa kiroho zaidi au wazuri kuliko

wengine. Upako ni maandalizi ya Roho Mtakatifu,

unaotolewa ili tuzae matunda mengi zaidi na kuwa na ufanisi

22 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 23: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

mkubwa zaidi katika huduma yetu na wito wetu. Maana yake

hasa ni kwamba tutapata kuwa watumishi bora kwa watu

wote (Yohana 13:12-17). Mwenendo wa maisha pamoja na

msimamo wa kutoa, katika kila kiwango cha maisha, ndiyo

amri ya Biblia kwa kila mwamini (Mathayo 10:8; Luka 6:38;

Matendo 20:35).

Mungu anawatakia watu Wake wajitolee wakati wote

katika mali yao na vipawa vyao kwa ajili ya kuwasaidia

wengine. Pasipo mwenendo wa maisha wa kutoa, hatutakuwa

na afya ya kiroho, na Mwili wa Kristo pia utapungukiwa.

Mungu ametupa mfano wa ndani katika jiografia ya nchi ya

Israeli utakaosaidia kufafanua kanuni hii.

Uhai Au MautiNchi ya Israeli ina maziwa makubwa mawili. Moja ni

Bahari ya Galilaya, la pili ni Bahari ya Chumvi. Bahari ya

Galilaya ni ziwa la maji baridi linalopendeza sana na kujaa

viumbe hai. Bahari ya Chumvi kwa Kiingereza huitwa

Bahari ya Mauti, kwa sababu imejaa chumvi na madini

mengine hadi haiwezekani kiumbe chochote kiishi ndani

yake. Maji yake hayafai kabisa kunywa, pia yanaweza

kuunguza ngozi ya mtu, kusababisha upofu na hata kukuua!

Bahari ya Galilaya huongezewa maji ya mito yenye maji

matamu mazuri. Upande wake wa chini, maji haya hutoka

katika Mto Yordani, ambao unaingia moja kwa moja katika

Bahari ya Chumvi. Inawezekanaje basi, maji mazuri yenye

uhai ya Bahari ya Galilaya yapate kuwa maji ya sumu na kifo

ya Bahari ya Chumvi?

Kuna tofauti kuu kati ya maziwa haya mawili: Maji

mazuri huingia katika yote mawili, lakini yanatoka katika

Bahari ya Galilaya tu. Bahari ya Chumvi haina pa kutolea.

Katika Bahari ya Chumvi maji yanakaa na kukauka (kugeuka

hewa), yakibakisha nyongeza ya chumvi na madini mengine.

Maji yanazidi kuwa na sumu inayoua.

Kwa njia hiyo hiyo, kusudi la upako wa Roho Mtakatifu

katika maisha ya mtumishi ni kuzalisha uhai wa Yesu katika

wengine. Utaongeza uhai wa Mungu ndani yetu, na kutiririka

kutoka kwetu kuwaendea wengine. Sisi tunapaswa wakati

wote tuwatolee wengine katika huduma na utumishi vyenye

nguvu na vinavyoleta uhai.

Tunapowaombea wengine, kuhubiri, kufundisha Neno

na kuwashirikisha maneno ya kuwajenga chini ya upako wa

Roho Mtakatifu, sisi ni watumishi tunaotoa uhai, ambao

tutabariki na kuadilisha wengine. Tukiwa na ubinafsi kwa

ajili ya muda wetu au bidii zetu - na kuchagua kutokutoa

‘mtiririko’ wa uhai wa Roho Mtakatifu katika utumishi na

huduma kwa wengine - basi upako wa Roho Mtakatifu

utaoza ndani yetu. Tunakusudiwa tupokee wakati wote kwa

upya kutoka kwa Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18-19) na

halafu tutoe “maji hai” tuliyopokea, katika utumishi na

huduma kwa wengine (Yohana 7:37-39).

Unaweza kusoma kuhusu kanuni hii katika Mathayo

25:14-30. Ilimtokeaje yule mtumishi asiyetendea kazi yoyote

vipawa na upako alivyopewa na Mungu?

3. Upako unaweza kuzuiwa au kusimamishwa.

Tumejifunza kwamba upako ni Nafsi na uwepo wa

Mungu Roho. Roho Mtakatifu si nguvu isiyo na uhai na

nafsi. Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Mungu.

Maandiko yamefunua kwamba Roho Mtakatifu anaweza

“kuhuzunishwa” (Waefeso 4:30). Maana yake ni kwamba

anasikia huzuni, anajeruhiwa au kuumizwa. Roho Mtakatifu

anaweza pia “kuzimishwa” (1Wathesalonike 5:19). Neno hili

lina maana ya kubanwa au kusongwa, au ya moto

ukizimishwa na maji.

a. Kuzimisha Roho Mtakatifu. Tunazimishaje Roho

Mtakatifu? Hutokea mara nyingi watu wanapopinga kazi ya

Roho Mtakatifu, au wasipojali kazi Yake. Kama watu

hawataki kuitikia misukumo ya Roho Mtakatifu au hamu

Yake ya kutenda kazi kati yao, wanaweza kuzuia (kuzimisha)

kazi Yake kati yao.

Kwa upande mwingine, Roho Mtakatifu anaweza

kuzimishwa pia wakati bidii zetu au misisimko yetu ya

kibinadamu vinapotenda kazi badala ya Roho Mtakatifu.

Kuna makanisa ambapo watu wanapendelea kufuata taratibu

zao kila juma, pasipo hamu yoyote ya kupokea kazi mpya ya

Roho Mtakatifu katika ibada zao. Katika hali hii, Yeye hana

uhuru wa kutenda kazi; kwa hiyo Roho “anazimishwa”.

Kuna sehemu nyingine pia ambapo watu wanataka

“kuigiza” kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Huenda

wanarukaruka, kupiga kelele, kutetemeka au mengine. Ni

kweli kwamba wakati Roho Mtakatifu anapofanya kazi, mara

kwa mara kuna matendo kama haya.

Lakini kama yanafanyika kama igizo, na si kama itikio la

kazi halisi ya Roho Mtakatifu, matendo kama haya yanaweza

kuzimisha kazi yenyewe ambayo Roho Mtakatifu anataka

kutenda kwa wakati ule.

Wakati wowote ambapo watu wanachagua utaratibubadala ya uwepo wenyewe wa Roho Mtakatifu na kazi Yake,

Yeye hana nafasi ya kutenda anavyotaka. Kwa hiyo, Yeye

“anazimishwa”.

Je, mifano hii yote inafananaje? Yote yanafunua

majaribu ya wanadamu kutawala au kuiga kazi ya Mungu.

Huenda watu wameamua kwamba wameridhika na aina

fulani ya utaratibu au mtindo ambao wanataka kufuata. Kila

juma, utaratibu wa ibada yao ni ule ule.

Inasikitisha kwamba hali hii inaweza kumzuia Roho

Mtakatifu asitende kazi halisi katika ibada zao kwa

kuwapatia watu uhai, uweza, uponyaji na upako Wake.

Hakuna nafasi wala ukaribisho Kwake kwamba aje na

kutenda kazi. Katika hali hii, nia ya mwanadamu imepinga

nia ya Roho Mtakatifu - na ndipo Roho Mtakatifu

“anapozimishwa” yaani hana uhuru wa kutenda kazi.

Biblia imetaja kipekee bidii za kibinadamu za kuchukua

nafasi ya uweza na uwepo wa Roho Mtakatifu: “Si kwauwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asemaBwana wa majeshi” (Zekaria 4:6).

Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,hata utaratibu au mtindo wako unaweza kuzuia kazi yaRoho Mtakatifu. Kila mara kundi la waaminilinapokusanyika, lazima tuwe wasikivu kwa yaleambayo Roho Mtakatifu anataka kutenda.

Pengine anataka kufanya kazi kwa upole na utulivuna kuwaponya watu. Roho Mtakatifu anaweza pia kujakwa nguvu na kuwaweka huru wafungwa! Anawezakuleta hali ya kusherehekea ushindi katika kuabudu,kujenga imani na matazamio ya waamini. Au anawezakuleta hukumu kali, na pamoja nayo hamu ya kutubu,kati ya waliohudhuria, kwa ajili ya makosa yao mbeleza Mungu.

MATENDO • 23Nakala 16 / Nambari 1

Page 24: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

24 • MATENDO

Hoja ni kwamba, inatupasa sikuzote tukaribishe nakuwekea nafasi kazi ya Roho Mtakatifu katika ibadazetu. Tunahitaji kuomba, kusikiliza, na kutii misukumona maneno ya kinabii ambavyo vinaweza kuja. Ndipo“mtindo” wetu wa utumishi au kuhubiri unapaswaufuatane na yale ambayo Roho Mtakatifu anayatendakwa wakati huo.

Kwa mfano, kama tutarukaruka au kupiga kelelewakati Roho Mtakatifu anapotaka kuleta amani auutulivu – “utege sikio lako“ (Zaburi 46:10) tutazimishakazi Yake ya dakika ile. Tukikataa msisimko wakusherehekea unaotokea katika kuabudu, tunawezakuzuia ushindi usitokee kati ya watu. Huenda itatubiditutulie katikati ya ibada, na kumruhusu kila mtuamsubiri Bwana ili yeye binafsi asikie kutoka Kwake.

Kutembea Katika Roho MtakatifuNi muhimu kabisa kwetu, kama viongozi wa kanisa,

kusitawisha uwezo wetu wa kupambanua na kumsikiaRoho Mtakatifu. Njia bora ya kufanya hivyo ni kutumiavipindi virefu vya maombi katika siku zinazotanguliakabla ya kukusanyika kwa waamini. Vipindi hivi vyamaombi visiwe tu vya kumwomba Mungu abariki yaleambayo umekwisha panga kufanya. Bali ni nafasi yakunyenyekeza moyo wako na kukabidhi mipango yakokwa Mungu, ukimsubiri hadi upokee maono ya yaleYEYE anayotaka kufanya! Utumie muda wakati wamkutano pia, wa kusubiri, kusikiliza na kupambanua.

Uamue kuwa mtu anayefuatana na yoyote ambayoMungu anataka kufanya. Kumbuka, hili ni Kanisa Lakena hao ni watu Wake. Wewe upo kwa ajili yakuwasimamia, kuwatunza na kuwafanya wawewanafunzi. Lakini iliyo muhimu kabisa, nafasi yako nikuwaelekeza watu kwa Mungu na kuwafundisha jinsiya kumwitikia Roho Wake Mtakatifu katika mamboyote!

Roho Mtakatifu anaweza kufanya tendo lakumweka huru, kumkuza au kumponya mtu kwaharaka sana wakati wa ibada. Kazi kama hii ingewezakutumia miezi, au hata kutokutendeka kamwe, pasipohuduma ya Roho Mtakatifu kwao kwa dakika ile. Kwahiyo sisi tufanye kazi pamoja na Roho Mtakatifu, nakushiriki katika kazi Yake kila mara tunapokusanyika!

b. Kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Maandiko

yanaeleza pia kuhusu kumhuzunisha Roho Mtakatifu

(Waefeso 4:30). Maana ya “kuhuzunisha” ni kumfanya

asikitike au kuumia. Roho Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa

na lolote tunaloruhusu au kutunza mioyoni mwetu

lisilofanana na Yesu.

Tunaweza kuwa na misimamo, tabia, mawazo, maneno

au matendo - lolote lisilofanana na Kristo litamhuzunisha

Roho Mtakatifu.

“Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu;ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukanoyaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweniwafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheanekama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi”(Waefeso 4:30-32).

Hamasa ya Paulo kwa Waefeso huwasaidia kufahamu

kwamba wao ni hekalu la Roho Mtakatifu, kama watu binafsi

(1Wakorintho 6:19) na kama kundi (1Wakorintho 3:9-17)

kama Mwili wa Kristo.

Kwa sababu Roho wa Mungu anaishi ndani yetu,

tunaweza kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yeye. Roho

Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa kwa sababu Yeye

anatupenda (Warumi 5:5). Tuachane na wazo au tendo lolote

linaloweza kumpa huzuni na majonzi huyo Roho wa Mungu

anayeishi ndani yetu.

Roho Na NenoHuenda wapo viongozi ambao wangesema kwamba

wanakaribisha kazi ya Roho Mtakatifu kati yao. Lakini

wanaweza kupata kuwa washupavu kwa kuacha kujifunza

Neno la Mungu kwa bidii na kufanya maandalizi

yanayohitajika kwa ajili ya kuwafundisha na kuwafunza

wengine katika njia za Bwana. Hao “wanamwachia Roho

Mtakatifu afanye kazi”. Mwelekeo huu wa akili haufai,

unaweza kusababisha matatizo mazito katika maisha ya

kiongozi na katika kanisa. Msimamo huu unaweza kuwa

kisingizio cha uvivu au utovu wa nidhamu, kitu ambacho

Mungu hatakibariki.

Biblia inasema wazi kabisa kwa viongozi kuhusu hoja

hii. “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwahalali neno la kweli” (2Timotheo 2:15-16).

Kama viongozi, lazima tuandae mioyo yetu kwa sala

nyingi, na kujaza akili zetu na Neno la Mungu. Lazima

tujifunze Maandiko na kuandaa mafundisho kutoka katika

Neno la Mungu ambayo yatawasaidia wale tunaowaongoza

wapate kuwa wanafunzi wenye upevu wa Yesu Kristo.

Lazima tusifundishe kamwe mambo yasiyo sahihi, imani ya

uwongo au mawazo ya kimwili kutokana na kutokujifunza na

kuzoea ukweli wa Neno la Mungu. Sisi tutahukumiwa

kufuatana na yale tunayowafundisha wengine (Yakobo 3:1).

Tunapokuwa tumeandaliwa kutokana na Neno la

Mungu, tunaweza kabisa kutazamia upako wa Roho

Mtakatifu utoe uwezo wa kuhubiri Neno la kweli la Mungu.

Tunaweza kumtazamia Roho Mtakatifu atutumie kama zana

kwa dakika ile ya huduma, na pia kutazamia uweza Wake

katika ishara na maajabu yatakayofuata.

Lakini tusipokuwa na bidii katika kujifunza Biblia na

kusali, ni rahisi zaidi kabisa kutoa huduma kutokana na

mawazo yetu au maelekeo yetu ya kimwili. Je, Roho

Mtakatifu atawezaje kutupa upako wakati hatufundishi Neno

la Mungu wala kumwakilisha Kristo kikamilifu katika

maisha yetu na huduma zetu?

Upako UsiotazamiwaBiblia inafundisha pia kwamba zipo nyakati ambapo

Roho Mtakatifu anaweza kutia maneno yafaayo midomoni

mwetu: “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsimtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema”

(Mathayo 10:19; taz. pia Marko 13:11 na Luka 12:11-12).

Lakini mistari hii inahusiana na hali za kufukuzwa na

kuteswa au matukio maalum, si ibada ya kawaida ya juma ya

kundi lako! Kwa hiyo mistari hii ya Maandiko isitumiwe

kama kisingizio cha kutokujifunza Neno la Mungu kwa bidii

na kuandaa mafundisho yafaayo.

Huenda nyakati zitatokea ambapo tunaitwa tuhubiri,

kusali au kutoa huduma pasipo maandalizi. Ninaamini

Nakala 16 / Nambari 1

Page 25: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

kwamba katika nyakati hizi msaada maalum wa upakousiotazamiwa huletwa na Roho Mtakatifu. Kumbuka, Yeye

ndiye anayetaka kumdhihirisha Yesu, na kuwaleta watu

katika wokovu kwa njia ya Kristo! Atatutumia katika hali

yoyote ili afanye hivyo. Lakini zaidi tunavyojiandaa katika

Neno la Mungu na sala, ndivyo tutakavyokuwa tayari zaidi ili

Mungu atutumie kwa ufanisi.Mungu anawataka viongozi Wake wawe waangalifu na

waaminifu kwa Neno Lake. Hii ni kwa ajili ya manufaa ya

kiongozi mwenyewe, pamoja na manufaa ya wale ambao

wanaoongozwa. Mazoea ya kusoma Biblia na kusali kila siku

yanajenga ndani yetu “akiba ya kiroho” ambamo Roho

Mtakatifu anaweza kuchota. Ndipo Roho Mtakatifu

anapoongeza uweza, hekima na utambuzi wa ki-Mungu

kutoka Kwake, katika yale tunayosema. Mchangamano huu

unaweza kubadilisha maisha ya msikilizaji!

Neno la Mungu linatuhimiza tuwe tayari wakati wote ili

Roho Mtakatifu atutumie katika hali yoyote (2Timotheo 4:2;

1Petro 3:15). Hali hii inatendeka kwa njia ya kujifunza Neno

la Mungu na kusali kwa bidii!

4. Upako unaweza kudhulumiwa au kutumiwa

vibaya.

Ipo mifano kadhaa katika Maandiko ya wanaume na

wanawake waliodhulumu au kutumia vibaya uwezo wa Roho

Mtakatifu. Walipofanya hivyo, Mungu aliwahukumu na

kuwaadhibu.

a. Waamuzi Sura za 13-16 - Samsoni. Karama ya

Mungu kwa Samsoni ilikuwa nguvu ya ajabu ya kimwili.

Roho Mtakatifu alipomjia (Waamuzi 13:24-25; 14:6,19;

15:14), Samsoni alifanya matendo makuu dhidi ya Wafilisti

waliowatesa Waisraeli. Lakini, ingawa Samsoni alikuwa na

karama kuu maalum, udhaifu wake wa kimaadili

ulimwangusha na kufupisha maisha yake na huduma yake

kwa Israeli (taz. Waamuzi sura ya 16).

Samsoni alifikiri kwamba angeweza kuishi maisha yake

kufuatana na mapenzi yake, na bado amtazamie Mungu ampe

upako. Hali hii ilikuwa ushupavu mkuu, nao ulisababisha

kushindwa kwake kama mtumishi wa Mungu. Ingawa

baadaye alitubu na Mungu alimtumia mara nyingine moja,

inaelekea kuwa maisha na huduma ya Samsoni havikufikia

makusudi ya Mungu.

[Tutaangalia kwa makini zaidi jinsi tabia inavyogusa

upako wa kiongozi wa kanisa katika Sehemu Ya III.B.1,

“Tabia na Upako”.]

b. Walawi 10:1-3 - Nadabu na Abihu. Hao wana

wawili wa Haruni (Kuhani Mkuu) walitiwa mafuta watoe

huduma kama makuhani kwa watu wa Israeli. Biblia

inafunua kwamba walitoa “moto wa kigeni mbele ya Bwana,ambao yeye hakuwaagiza” (Walawi 10:1). Tendo hili liliasi

amri ya awali ya Mungu (Kutoka 30:9).

Mungu alikuwa ameweka nyakati na njia rasmi kwa ajili

ya dhabihu na sadaka za makuhani. Kumtii Bwana na njia

Zake ni kipaumbele kikuu. Hali ya Nadabu na Abihu kuwa

watiwa mafuta au upako wa Bwana haikuwa udhuru kwa ajili

ya kutokutii kwao. Hukumu ya Mungu ilikuwa ya haraka na

ukali juu ya wana hao wawili wa Haruni ambao walitoa

huduma yao kwa Mungu kwa njia zao binafsi (Walawi 10:2).

Sisi kama viongozi wa kanisa, lazima tutii wakati wote

mwongozo wa Roho Mtakatifu pamoja na kanuni na amri za

Neno la Mungu. Tusianguke katika mtego wa kufikiri

kwamba sisi tunaweza kuchagua jinsi sisi tunavyotaka

kumfuata Mungu na kutoa huduma katika Kanisa Lake.

Lazima tupokee YOTE ambayo Yeye anataka kutufunulia

katika Neno Lake kuhusu huduma yenye ufanisi, na kufanya

huduma hiyo kwa uwezo wetu wote!

Mchungaji kwa Mchungaji: Ni rahisi kwa viongoziwa kanisa ambao Mungu amewapa upako - hasa waleambao Mungu anawatumia sana - kufikiri kuwa amri zakimsingi za Maandiko haziwahusu wao tena.Wanasahau kwamba yote wanayofanya hufanyikambele za macho ya Mungu aliye mtakatifu (Walawi10:3).

Sote tumesikia habari za wanaume na wanawakeambao Mungu amewatumia sana nao wameangukakatika kushindwa kimaadili, makosa kuhusu mali nafedha, na dhambi nyingine. Kuanguka kwao kwakawaida hakutokei kwa dakika moja. Huanza kwakuridhiana na kutoa udhuru “kidogo”, njiainayowafikisha katika kutokutii Neno na hatimayekuanguka kabisa (Yakobo 1:14-15).

Lazima tusisahau kwamba Mungu ni mtakatifu, naYeye ametuita sisi pia tuwe watakatifu (Walawi 11:44;1Petro 1:16). Neno la Mungu, amri Zake, kanuni Zake,ni kwa ajili ya kila mwamini na mfuasi wa Kristo - hasaviongozi Wake walioitwa na kupewa upako!

c. Hesabu 11:16-30 – Wazee. Biblia inaelezea tukio

moja wakati wa kusafiri kwa Waisraeli ambapo Mungu

aliwapa wazee sabini Roho Wake nao walitabiri (ms. 25).

Walikuwepo wanaume wengine wawili ambao

hawakuhudhuria pamoja na wenzao kwenye Hema ya

Kukutania, bali walibaki kambini. Roho aliwajia wao pia,

wakaanza kutabiri (ms. 26).

Joshua, ambaye kwa wakati ule alikuwa msaidizi wa

Musa, aliomba wale wawili wazuiliwe na kukatazwa

wasitabiri (ms. 28). Lakini Musa alimkemea Yoshua, na

kueleza hamu yake ya kinabii kwamba Bwana angewatia

watu wote roho Yake (ms. 29; taz. pia Yoeli 2:28-29;

Matendo 2:14-21).

Huenda Yoshua alikuwa na nia njema, akiona mashaka

kuwa wale wawili walitabiri visivyofaa kwa sababu

hawakuhudhuria pamoja na wazee wengine. Lakini alikosa

kwa kufikiri ilikuwa wajibu wake kuamua Mungu atamke lini

na kwa njia ya nani.

Mchungaji kwa Mchungaji: Viongozi wanapojaribukutawala au kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu, wanakosa.Mara nyingi, tuna hamu inayotokana na nia njema yakuwa “mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwautaratibu” (1Wakorintho 14:40). Lakini njia zetu si njia zaMungu (Isaya 55:8-9). Vipimo vyetu au maoni yetu yakibinadamu kuhusu mambo tunayofurahia huendahavihusiani kamwe na yale ambayo Mungu anatakakutenda kwa wakati fulani maalum.

Mungu anaweza kutenda kwa njia zisizo zakawaida, kutokana na vyanzo visivyotazamiwa, na kwamatendo yasiyo ya kawaida pia. Fikiria punda wakeBalaamu (Hesabu 22:22-40), au Yesu akitumia udongona mate alipomponya kipofu (Yohana 9:1-6).

MATENDO • 25Nakala 16 / Nambari 1

Page 26: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Tunaishi katika siku za Mavuno makuu nakumiminwa kwa Roho wa Mungu. Matukio ya ajabu,miujiza, matamko ya kinabii na mafunuo mengine yaRoho wa Mungu vinaongezeka kote duniani. Ni lazimatutumie karama ya kupambanua, naam, tusikubali nakuamini mambo yote yanayofanyika kwa jina la Mungu(Mathayo 7:21-23). Lakini ni lazima pia tujifunzekushirikiana na kutenda pamoja na Roho Mtakatifu kwawakati wowote maalum.

Si juu yetu sisi kumwamulia Roho Mtakatifu atendekazi lini, kwa njia gani na kupitia kwa nani. Chomboambacho Mungu anakitumia kwa hakika kitakuwa naupungufu na hitilafu. Hakuna yeyote kati yetu aliyemkamilifu, lakini Mungu ameamua kufanya kazi kupitiakwetu!

Hata hivyo, inatubidi tuangalie kuwa Maandikohueleza wazi kwamba tusishirikiane na watu wanaoishikatika dhambi au kufundisha uwongo (1Timotheo6:3-5; 2Timotheo 3:1-5). Lazima pia tuwe waangalifukatika kupima unabii kwa usahihi (1Wakorintho 14:29).Tena tusitumie vipimo vya nje vya dunia katikakutathmini au kutambua hali ya ndugu au dada katikaKristo (2Wakorintho 5:16-17).

Kama wachungaji, katika hamu yetu ya kuongoza,tunaweza kushawishika tujaribu kutawala. Hapo tumokatika hatari ya kuzuia, au kukataza, kazi ya RohoMtakatifu kati yetu (kama Yoshua alivyokaribiakufanya).

Inatupasa tutumie muda wa kuwafunza waletunaowahudumia kuhusu lini na jinsi ya kutoa unabii.Lakini ni lazima baada ya haya tuwe tayari kumruhusuRoho Mtakatifu atende kazi kupitia kwaowanapoendelea kujifunza na kukua.

Kumbuka, nafasi yetu kama wachungaji nikuwaongoza watu ili wakue kama wanafunzi. Maanayake, pamoja na mengine, ni kwamba tunawafundisha- na kuwaweka huru - wapokee na kuitikia mwongozowa Roho Mtakatifu.

d. Matendo 5:1-11; 8:9-24 - Anania na Safira; Simoni

Mchawi. Kitabu cha Matendo kinasimulia majaribu mawili

wakati wa Kanisa la awali ya kutumia vibaya uwezo wa

Roho Mtakatifu.

1) Jaribu la kwanza lilikuwa la Anania na Safira

(Matendo 5:1-11). Walijaribu kudanganya uongozi wa

Kanisa la awali kuhusu mauzo ya mali yao. Lakini Petro

alipowakabili, aliita kosa lao kuwa “kumwambia uongo RohoMtakatifu” (ms. 3).

Inaeleweka kwamba hoja haikuwa kiasi cha fedha

walichotoa. Bali walihukumiwa kwa sababu ya unafiki wao.

Mungu alikabili aina ya unafiki na roho ya kidini iliyokuwa

alama ya Waandishi na Mafarisayo (Mathayo 23:1-36; 6:1-6;

Marko 12:38-40; n.k.).

Watu wanaomfuata Kristo hupaswa wawe na haki

inayozidi ile ya Mafarisayo (Mathayo 5:20). Haki yao iwe

haki ya moyo, si hali ya nje au sura inayoonekana kuwa ya

haki. Ieleweke pia kwamba ikiwa mtu kweli anayo haki hii ya

ndani, itajidhihirisha katika matendo ya nje ambayo pia ni ya

haki kamili (Mathayo 23:25-26).

Inaonekana kuwa Anania na Safira walitumia kazi pekee na

nzito ya Roho Mtakatifu katika Kanisa la awali kwa ajili ya

kujifaidi wenyewe. Walijionesha kama wameshiriki katika kazi,

lakini ni wazi kwamba walikuwa na nia ya kibinafsi iliyofichwa.

Matendo yao yanafunua kwamba hawakuheshimu

mamlaka ya mitume ambao Mungu alikuwa amewaweka

kuwa viongozi - na hatimaye hawakumheshimu wala

kumstahi Roho Mtakatifu ambaye alikuwa amewapa mitume

mamlaka yao.

Mungu aliona mioyo ya Anania na Safira, na

kuwahukumu kwa haraka na ukali (Matendo 5:5,9-10).

Mungu anatamani Kanisa lililo safi na takatifu (Waefeso

5:27). Ili lipate kuwa hivyo, Bwana wa Kanisa anafanya kazi

isiyokoma ili abadilishe na kutakasa Bibi Arusi Wake

(Waefeso 5:26-27). Anatupenda kiasi cha kutuadilisha na

kutuadhibu (1Petro 4:17; Waebrania 12:3-11).

2) Jaribu la pili la kutumia vibaya upako wa Roho

Mtakatifu katika Kanisa la awali linaonekana katika Matendo

8:9-24. Hapa tunamwona Simoni mchawi, aliyekuwa

ameongoka na kuwa Mkristo muda mfupi kabla ya hapo

(ms. 13). Wakati Simoni alipokuwa akimfuata Filipo,

alishangazwa na matendo makuu na miujiza ambavyo

alimwona Roho Mtakatifu akiyatenda!

Simoni alipowaona mitume wakiwahudumia wengine

katika uweza wa Roho Mtakatifu, alitamani uwezo ule kwa

ajili yake binafsi. Katika mawazo yake machanga na bado ya

kidunia, Simoni alitaka kuwapa mitume fedha ili apate uweza

ule (ms. 18-19).

Petro, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, alitambua nia za

moyo wa Simoni:

“Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo,na tena u katika kifungo cha uovu” (ms. 23). Ilikuwa wazi

kwamba Simoni alikuwa na nia ya kibinafsi. Moyo wake

ulikuwa umefungwa na dhambi, naye hakutaka Roho

Mtakatifu ili amtukuze Mungu na kuwatumikia wengine.

“Uchungu” katika mstari huu ni kama wivu wa

kimashindano (Yakobo 3:14). Simoni alitaka awe mtu

26 • MATENDO

Utiifu kwa Bwana: Kipaumbelechetu cha kwanza

Nakala 16 / Nambari 1

Page 27: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

muhimu aliyewashangaza wengine, labda kama alivyokuwa

wakati wa kuwa mchawi (Matendo 8:9-11). Alitaka uweza

wa Mungu kwa ajili ya faida yake binafsi.

Mchungaji kwa Mchungaji: Hata leo, tunakutanana viongozi wenye vipawa na upako halisi ambaohutumiwa na Mungu. Lakini kinachosikitika ni kwambawanaweza kuanza kujiona kuliko iwapasavyo.Wanaanza kutenda kana kwamba uwezo unatokakwao, na si kutoka kwa Mungu mwenye rehema(2Wakorintho 4:5-7). Wanatumia huduma ili wafanyemajina yao yasifiwe, wapate utajiri, au wawavutewengine wawafuate.

Viongozi wengi hawaanzi hivi. Viongozi wemawanatamani kumwona Mungu akitenda kazi nakupokea utukufu wakati maisha ya watuyanapobadilishwa kwa uweza Wake. Lakini tusipokuwawaangalifu na wenye juhudi ya kulinda mioyo yetu(Mithali 4:23), tunaweza kudanganywa na kupotea.

Ibilisi hawezi kukana, kuzuia, kushambulia walakushinda uweza wa Mungu (Yohana 1:5). Kwa hiyobadala yake, Shetani anajaribu kumdanganya kiongozina kupotosha moyo wake (2Wakorintho 2:11;11:13-15), amfanye chombo kinachojitumikiamwenyewe, asimtumikie Mungu na makusudi Yaketena.

Kushikilia Kwa UaminifuKwa upande wa Anania na Safira, na kwa Simoni pia,

tunapewa mafunzo ya kutuangaliza na kutuonya. Lazima

tukumbuke kwamba Shetani ana nguvu ya kuvuta mawazo na

matendo yetu tukimruhusu (Matendo 5:3). Lazima tusimpe

nafasi (Waefeso 4:27).

Lakini, wakati viongozi wanapoanguka - wakichagua

dhambi badala ya haki - ni tatizo kubwa sana. Kwanza, kwa

sababu Mungu wetu ni mtakatifu, dhambi inavunja uhusiano

wetu na Mungu. Wafuasi wote wa Kristo wameitwa na

kuamriwa utakatifu wa binafsi na usafi wa kimaadili (1Petro

1:13-19).

Pili, tumeitwa tuwe viongozi wenye amana kwa ajili ya

kuwatunza watu wa Mungu. Sisi tunapokubali dhambi,

tunavunja amana ile na kuwa mifano mibaya kwa wale

tunaowaongoza. Pia tunawaacha kondoo washambuliwe na

pepo wachafu (1Petro 5:2-4; Matendo 20:28-30; Waebrania

13:7,17; Yakobo 3:1). Kama Shetani anaweza

kumwangamiza kiongozi, kondoo watatawanyika na

kukamatwa kwa urahisi (Marko 14:27).

Kushindwa kwetu kunawaudhi pia familia zetu na

kuharibu sifa zetu. Tunaumiza jamii ya Mungu pia, na

kuathiri sifa za viongozi wengine wa kanisa walio

waaminifu. Kwa sababu ya kosa letu, watu hata wa viongozi

waaminifu wangeweza kuwadharau viongozi wao na

kutowaamini (tazama maagizo ya Paulo kuhusu uchaguzi wa

wazee katika 1Timotheo 3:1-7). Shetani anawalenga

viongozi wa kanisa kwa kusudi katika hila zake za

uangamizi. Lakini kumbuka, hawezi kukufanya utende

dhambi usipochagua kufuata vishawishi vyake. Umpinge

Shetani, naye atakukimbia (Yakobo 4:7).

Nafasi yako kama kiongozi na upako wako ni heshima;

pia ni jukumu zito na muhimu sana. Biblia inatuhimiza sana

kuhusu kuendelea kuwa waaminifu na kumaliza mashindano

(Mathayo 24:13; Wafilipi 3:17-18; 2Timotheo 4:6-8).

Tushikamane na tumaini letu na imani yetu katika Kristo

mpaka mwisho, tukiwa mifano ya uaminifu kwa kundi letu,

kwa ajili ya Yesu na utukufu Wake (1Petro 5:2-3).

D. UTANGULIZI WA UPAKO

KATIKA AGANO LA KALE

Tukiwa tunaendelea na mafunzo yetu, tuchunguze

utangulizi fulani wa Agano la Kale wa upako. Kama

ilivyotajwa juu, Agano la Kale lilitolewa kwa ajili ya

mafunzo na mifano kwetu (Warumi 15:4; 1Wakorintho

10:11). Itatusaidia tupate picha kamili zaidi ya upako kama

ahadi iliyotolewa ambayo ilitimizwa mara ya kwanza

mwanzoni mwa awamu ya Kanisa la Agano Jipya (taz.

Matendo sura ya 2).

1. Alama au Ishara za Kiutangulizi

Zipo alama au ishara nyingi za kiutangulizi katika Agano

la Kale za Roho Mtakatifu na kazi Yake.

a. Moto - Katika Hema ya Kukutania na kwenye

madhabahu ya ubani, sadaka za kuteketezwa zilikuwa na

moto uliowaka daima ambao uliwashwa na Mungu (Walawi

9:24; 2Nyakati 7:1-3). Moto huu ulitakiwa uwake hata milele

(Walawi 6:13). Alama hii hii ya moto, inayoashiria uwepo hai

wa Roho wa Mungu, inaonekana pia katika Agano Jipya

(Mathayo 3:11; Matendo 2:3).

b. Maji - Maji ni alama inayotumiwa katika Agano la

Kale kuashiria Roho Mtakatifu katika kuleta burudisho na

baraka ya kiroho kutoka kwa Mungu. Katika eneo la dunia

ambapo maji yalipatikana kwa shida, matumizi ya maji kama

alama ya Roho wa Mungu yalieleweka wazi kwa watu

(Zaburi 23:2; Isaya 35:6-7).

Ezekieli alipewa maono ya mto mkuu uliotoka katika

makao ya Mungu ya hekalu Lake (Ezekieli 47:1-12). Haya

yalifuatana na kutiririka kwa Roho wa Mungu juu ya watu

Wake pasipo kuzuiliwa.

Yeremia anatumia “chemchemi ya maji ya uzima”

(Yeremia 2:13; 17:13) kufunua uwepo wa Mungu kwa Roho

Wake. Yesu pia aliongea kuhusu maji yaliyo hai: “...mito yamaji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisemakatika habari ya Roho...” (Yohana 7:37-39). Wakati ule, Yesu

alikuwa akitabiri rasmi kumiminwa kwa Roho Mtakatifu

ambako kungetokea (Yohana 14:16-17; Matendo sura ya 2).

c. Damu - Tunasoma katika Agano la Kale kuhusu upako

maalum kwa ajili ya makuhani, uliohusiana na damu (Kutoka

29:19-21).

d. Mafuta - Matumizi ya mafuta yalikuwa ya kawaida

katika muda wote wa Agano la Kale. Kuanzia matumizi ya

kila siku katika kupika, kwenye taa na kupaka mwilini,

mpaka matumizi maalum katika matendo makuu ya hekaluni,

mafuta yalikuwa na nafasi muhimu.

Mafuta yalikuwa alama maalum ya uwepo na uweza wa

Roho Mtakatifu wa kuweka watu au vitu wakfu. Tunaona

haya kuhusu wafalme (1Samweli 10:1), makuhani (Kutoka

29:1-9) na kutakaswa rasmi kwa watu wenye ukoma (Walawi

14:10-18).

Pia mafuta yaliashiria furaha (Isaya 61:3), na

kukosekana kwake kuliashiria huzuni au kutwezwa (Yoeli

1:10). Mafuta yalikuwa alama ya ufanisi wa maisha

(Kumbukumbu 33:24), faraja (Ayubu 29:6) na chakula cha

kiroho (Zaburi 45:7).

MATENDO • 27Nakala 16 / Nambari 1

Page 28: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Picha ya Kiishara Yenye NguvuKutokana na kuangalia Agano la Kale kwa kifupi tu,

tumeona akiba tele ya ishara, picha na alama

vinavyotufunulia mengi kuhusu upako wa Roho Mtakatifu na

kazi Yake katika maisha yetu. Kiutangulizi, vinawasilisha

upako wa Roho Mtakatifu na kazi Yake ambavyo

vinapatikana kwetu sisi leo! Upako huu ni ahadi iliyotimizwa

ya Baba yetu wa mbinguni (Yoeli 2:28-32) kumimina Roho

Yake juu ya watu Wake (Matendo 2:33-39).

Picha mojawapo yenye maana na nguvu kubwa kiishara

ya upako wa Roho Mtakatifu ni kutengenezwa na kutumiwakwa mafuta takatifu ya upako.

Tukisoma maelezo yafuatayo tutaona kwa ndani asili ya

upako wa Roho Mtakatifu pamoja na utendaji wake.

“Kisha Bwana akasema na Musa, na kumwambia,Jitwalie manukato yaliyo bora, manemane mbichi shekeli miatano, na mdalasini wenye harufu nzuri nusu ya kiasi hicho,yaani, shekeli mia mbili na hamsini, na kane shekeli mia mbilina hamsini, na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeliya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibabavitano; nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu,marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengenezajimanukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa. Naweutaipaka hema ya kukutania kwa mafuta hayo, na hilo sandukula ushuhuda, na hiyo meza, na vyombo vyake vyote, na kinaracha taa, na vyombo vyake, na madhabahu ya kufukiziauvumba, na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja navyombo vyake vyote, na birika, na tako lake. Nawe utavitakasavitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusachovyombo vile kitakuwa kitakatifu. Nawe utawatia mafutaHaruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kaziya ukuhani. Nawe utanena na wana wa Israeli na kuwaambia,Haya yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa kwa ajili yangumimi katika vizazi vyenu vyote. Hayatamiminwa katikakiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wahaya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, nakwenu ninyi yatakuwa matakatifu. Mtu awaye yoteatakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yoteatakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakatiliwambali na watu wake” (Kutoka 30:22-33).

Mafuta haya ya upako yalikuwa wakfu na matakatifu

kwa Bwana. Waisraeli walipaswa waone mafuta ya upako

katika hali hii. Mchanganyiko wake ulikuwa tofauti na

maalum kwa ajili ya matendo matakatifu tu (ms. 31-33).

Mungu alitoa maagizo Yake kwa ajili ya mchanganyiko

wa mafuta hayo ya upako (ms. 22-25). Yalikataliwa matumizi

mengine yoyote. Mtu yeyote wa nje ya watu wa Israeli wa

agano hakuruhusiwa kuyatumia (ms. 33).

Uteuzi Wa Mungu Kwa sababu mafuta haya yalikuwa ishara ya kiutangulizi

ya upako wa Roho Mtakatifu, masharti makali kuhusu

mafuta hayo maalum yanatufunulia kanuni tatu zilizo

muhimu sana.

Kwanza, Mungu ana mapenzi makuu ya kifalme kwa

ajili ya upako wa Roho Wake. Kama vile alivyoagiza

mchanganyiko wa mafuta ya upako (Kutoka 30:22-25),

Mungu peke Yake anaongoza upako Wake (1Samweli 10:1)

na pia jinsi upako huu utakavyotendewa kazi katika maisha

ya mtu fulani (1Wakorintho 12:7,11).

Pili, mafuta ya upako yalitakiwa kwa ajili ya makuhani

waliotumika ndani ya Hema ya Kukutania (Kutoka 30:30).

Yasitumiwe kwa kumpaka mtu mwilini (30:32). Waamini

wote wa kweli wa Yesu Kristo, kama “ukuhani mtakatifu” wa

Mungu, (1Petro 2:9-10; Ufunuo 1:6) wana upako wa Roho

Mtakatifu (1Yohana 2:20-27).

Upako huo haupo kwa ajili ya asiyeamini. Roho wa

Mungu anaishi ndani ya wale tu waliookolewa na ambao

wanatembea katika kumtii Mungu (Yohana 3:5-6; Warumi

8:14-16; 1Wakorintho 12:3).

Mchungaji kwa Mchungaji: Katika Agano la Kale,Kuhani Mkuu aliingia ndani ya mahali Patakatifu sanamara moja kwa mwaka afanye upatanisho kwa ajili yawatu (taz. Walawi sura ya 16). Yeye peke yake aliwezakuingia mbele za Mungu kila mwaka.

Wakati wa kifo cha Kristo msalabani, pazia zitokama zulia lililofunika mahali patakatifu sana ndani yahekalu lilipasuka vipande viwili toka juu hata chini(Marko 15:38; taz. pia Kutoka 26:31-33). Tukio hilipekee linafunua kwamba Mungu sasa aliweza kujiwamoja kwa moja na watu wote. Kristo alipofuta deni ladhambi ya binadamu msalabani, wokovu kutokana nakumwamini Yeye ulipatikana kwa wote waliokubalikumpokea (Warumi 10:9-10).

Watu wote watakaoliitia jina la Bwana wataokoka(Warumi 10:12-13). Nao wote waliookolewa kwa imanikatika Yesu Kristo wanaweza kufika mbele ya “kiti chaneema” (Waefeso 3:12; Waebrania 4:16; 10:19), yaanimbele za Mungu Mwenyewe! Haleluya!

Wakristo hawahitaji tena kuwakilishwa na kuhaniwala mtu yeyote mwingine ambaye anamwendeaMungu kwa niaba yao. Kila mwamini anaweza naanapaswa kuwa na uhusiano wake binafsi na Mungukwa njia ya sala, ibada na ushirikiano. Tunawezakuongea na Yeye, kumwomba na kusikia kutokaKwake.

Uwezekano huu wa kumfikia Mungu kwa watuwote wanaomwamini Mwana Wake kwa ajili ya wokovuni sababu waamini wote huitwa ukuhani mtakatifu.“Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwenyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu zaroho [yaani, ibada, sala, matendo ya huduma, zaka nasadaka] zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya YesuKristo” (1Petro 2:5; taz. pia Ufunuo 1:6).

“Dhabihu za roho” tunazoitiwa hazitufanyitukubaliwe na Mungu. Tumekwisha kubaliwa na Mungukwa sababu ya dhabihu ya Yesu msalabani. Wokovuwetu unatokana na imani katika Yesu, si kutokana namatendo yetu yoyote (Waefeso 2:8-9).

Ndiyo sababu lile pazia lililofunika mahali patakatifusana hekaluni lilipasuka toka juu hata chini. Tukio hilililithibitisha kiishara kwamba wokovu wetuulisababishwa na Mungu. Maana yake ni kwambaMungu alitufikia kwa neema tusiyoweza kustahili yaKristo alipokufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.

Bidii zetu za kuwa na haki hazina mafanikio yoyotewala haziwezi kutupatia wokovu (Warumi 3:9-20;Wagalatia 2:16). Lakini tunaishia na kutendea imaniyetu katika dhabihu za kiroho tunapotembea kwa kumtiiMungu na kutumikia Mwili Wake na pia watu wotewanaoishi duniani (Yakobo 2:14-26).

Mchungaji, ni lazima ufundishe kweli hizi za msingikuhusu msalaba mara nyingi. Wale unaowaongoza

28 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 29: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

lazima wafahamu wokovu ambao wameupokea bure;na halafu wao waweze kuuwasilisha kwa uwazi kwawatu wanaojaribu kwa mahangaiko “kustahili” wokovuwao kwa njia yoyote badala ya ile iliyotolewa na Kristo(1Petro 3:15).

Tatu, mafuta ya upako usitengenezwe kwa ajili ya kazi

nyingine, wala yasighushiwe (Kutoka 30:32-33).

Kupakwa kwa mafuta katika Agano la Kale ni ishara ya

mtu au chombo fulani kuteuliwa na Mungu. Uteuzi huu

uliweka mtu huyu au chombo hiki wakfu kwa ajili ya

mahali au kazi pekee katika makusudi ya Mungu. Pamoja

na uteuzi huu wa kifalme kulikuwa na mamlaka na uwezo

vilivyohitajika ili mtu binafsi aweze kutimiza yale Mungu

aliyoagiza (1Samweli 16:13; Isaya 61:1). Kanuni hii

inamhusu mwamini wa Agano Jipya pia, haidhuru nafasi ya

huduma ambayo Mungu amempatia ndani au nje ya

shughuli za ibada za Kanisa. Ni kweli pia kwa ajili ya wale

ambao Mungu amewaita hasa kwa ajili ya huduma ya

wakati wote (2Wakorintho 1:21; 1Wathesalonike 5:24).

Mungu anatupatia yote tunayohitaji siyo tu ili tuwe

watumishi wenye kumzalia matunda, bali pia washindi

katika maisha na huduma yetu!

Tatizo La KughushiwaKupatikana kwa upako wa Mungu kwetu ni habari nzuri

kabisa! Lakini ni lazima tusisahau maonyo katika Kutoka

sura ya 30 kuhusu kughushi mafuta ya upako. Mungu aliona

tendo hili kuwa kosa zito, hata la jinai (Kutoka 30:32-33).

Mtu aliyetenda dhambi ya aina hii “alitengwa” na watu wa

Israeli. Wasomi wa Biblia wameona mara nyingi kuwa

maana hasa ya neno hili ni kuuawa.

Mfano huu wa kughushi una maana gani kwetu sisi kama

watumishi wa Agano Jipya? Tumekwisha chunguza dhambi

ya kutumia upako wa Mungu kwa ajili ya faida yetu (Wafilipi

1:15-16). Kuna njia nyingine ambapo upako wa Mungu

unaghushiwa katika utumishi wa leo.

Watu wengine katika utumishi wanafikiri kwa makosa

kwamba lengo la mahubiri yao ni kuwafanya watu

wasisimke. Kwa hiyo wanaghushi upako katika mtindo wao

wa kuhubiri au kufundisha kwa vituko. Mara nyingine

wanasema maneno ambayo watu wanataka kuyasikia, hata

kama yanapinga Biblia; wanaweza kusimulia hadithi

zilizotiwa chumvi; au wanatumia njia nyingine za kuvuta

umati wa watu kwa hila.

Wengine katika utumishi wanataka kujulikana na

kujipatia wafuasi wao binafsi. Wanaweza kughushi upako

kwa kujifanya kwamba wamefahamu “siri za ndani” ambazo

wengine hawazijui (2Wakorintho 11:3-4); wanadai vyeo au

nafasi ili watu wawaheshimu; au wanatumia vyeo au

mamlaka katika kuwahimiza wengine watende mambo

yasiyo ya haki au yanayomfaidi kiongozi mwenyewe.

Zipo njia nyingine nyingi ambamo watu

wanashawishiwa waghushi upako au kuutumia vibaya.

Lakini hoja ni hii: Kughushi au kutumia vibaya Roho

Mtakatifu ni dhambi kubwa mbele za Mungu. Pia ni aina ya

udanganyifu ambayo, ikiendelezwa, itapatia ufalme wa

Shetani nafasi katika maisha ya kiongozi wa kanisa.

Hatimaye hali hii italeta hukumu ya Mungu juu ya maisha ya

mtu huyo pia.

Kughushi upako wa Roho Mtakatifu kumesimuliwa

katika Agano Jipya. Mfano wa wazi hasa ni wa Paulo

akiwahukumu “mitume wa uongo”. Paulo anawafananisha na

jaribu la Shetani la kuwaiga malaika wa Mungu ili

awadanganye waamini (taz. 2Wakorintho sura ya 11).

Wapo watu leo wanaoonekana kuwa ni wajumbe

waliotiwa mafuta na Mungu, lakini sivyo walivyo. Agano

Jipya limetoa maonyo mengi juu yao (Mathayo 7:15-20;

Matendo 20:27-30; 2Wakorintho 11:1-15; Wagalatia 1:6-10;

Wakolosai 2:18-23; 1Timotheo 4:1-3; 2Timotheo 3:1-9;

2Petro 2:1-22; 1Yohana 4:1-6; Yuda 3-19).

Baadaye katika toleo hili, tutajifunza tabia saba

zinazopatikana katika wale wanaotenda katika upako halisi

wa Roho Mtakatifu. Orodha hii itasaidia katika kuchunguza

utumishi wako, pamoja na kutambua uwepo wa kweli wa

Roho Mtakatifu katika watumishi au viongozi wengine wa

kanisa.

Mchungaji kwa Mchungaji: Si kosa kutaka kuwana ufanisi katika utumishi na kutamani uwezo wa RohoMtakatifu wenye upako. Lakini ni kosa kujifanyatusivyo, pamoja na kujaribu kufanya kana kwambatumepokea upako.

Kwa nini tujibidishe kujifanya kuwa na upako,wakati ambapo tunaweza kupata upako halisi - kamatutaupokea kwa masharti ya Mungu na si yetu.

Tunaweza kulinda maisha yetu na dhambi naudanganyifu kuhusu upako - na kuingia katika upakohalisi wa Roho unaoongezeka kila wakati - kwa njiambalimbali:

• Ukubali karama na wito ambao Mungu amekupawewe; na usiwaonee wivu wala kukosoa yale waliyonayo wengine wala kujaribu kuwaiga.

• Uombe kila siku uweze kujua mapenzi ya Mungukwa ajili yako binafsi pamoja na utumishi wako.

• Ukubali na kuridhika pale ulipoitiwa na Mungu,na yale ambayo Yeye amekuagiza uyatende.

• Umwombe Mungu wakati wote msaada nauwezo ili uweze kufanya mapenzi Yake.

• Ujikumbushe kila siku kwamba umo katikautumishi kwa ajili ya kutumikia Mungu na watuwengine, na si kujitumikia wala kujiendeleza.

Ukumbuke pia kwamba hakuna mtindo maalum wakuhubiri au kuongoza ulio na “upako” kuliko mtindomwingine. Nimewaona viongozi wenye upakowanaoongea kwa upole na utulivu. WalipofundishaNeno la Mungu, watu waliponywa au kuguswa na RohoMtakatifu. Viongozi wengine huenda wanafanyamatendo au kuongeza sauti zaidi wakati RohoMtakatifu anapohudumu kupitia kwao. Hakuna mtindoufaao au usiofaa.

Jambo muhimu ni kusitawisha usikivu kwa RohoMtakatifu kila mara unapotoa huduma. Tulia, sikiliza, nakuitikia yale ambayo Yeye anasema na kutenda katikamkutano fulani. Ndipo wewe ulinganishe mtindo wakona yale ambayo Roho Mtakatifu anataka kuyatendakwa dakika moja moja.

Ukumbushwe kwamba Mungu amekuita vile ulivyo.Amekupa vipawa maalum kwa sababu maalum.Anataka kukutumia kama ulivyo pamoja na vipawaulivyo navyo - ukishirikiana na kazi ya Roho WakeMtakatifu ya upako na mabadiliko - kwa ajili yakuwahudumia wengine.

MATENDO • 29Nakala 16 / Nambari 1

Page 30: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

2. Mafunzo Yanayotokana Na Mafuta Ya Upako

Sasa tuangalie kwa makini zaidi vitu vilivyotumika

katika kutengeneza mafuta ya upako, na yale ambayo

vinadhihirisha kuhusu upako wa Roho Mtakatifu.

Mchanganyiko wa mafuta ya upako, yaani manukato,

ulikuwa na vifuatavyo hasa: manemane, mdalasini, kane,

kida na mafuta ya zeituni (Kutoka 30:23-24).

a. Manemane. Manemane ilikuwa aina ya dawa ya

usingizi na kupunguza maumivu. Ikijulikana kwa harufu

yake tamu, ilitumiwa pia katika kutengeneza marashi na

vipodozi.

Manemane ni kati ya tunu ambazo wale mamajusi

walimletea Yesu (Mathayo 2:11). Pale msalabani, watu fulani

walijaribu kumpa Yesu manemane kwa ajili ya kupunguza

maumivu Yake, lakini aliikataa (Marko 15:23). Kwa kukataa

dawa hii ya maumivu, Kristo Yesu alishikamana na utume

Wake kwamba “Aionje mauti kwa ajili ya kila mtu”

(Waebrania 2:9). Kwa sababu ya harufu yake tamu,

manemane ni kati ya viungo vya manukato ambavyo

vilitumiwa katika kumzika Yesu (Yohana 19:39).

Matumizi ya manemane kwa kupunguza maumivu yana

maana maalum ya kinabii kwa upande wetu. Yesu Kristo,

Masihi (aliyetiwa mafuta) alikuja ili achukue mizigo yetu

pale msalabani. Pale mahali pa dhabihu Yesu alitimiza kusudi

Lake la kuwa Mponyaji wetu (1Petro 2:24) na aliyetuweka

huru na utumwa wa dhambi na mauti (Waebrania 2:9; 14-18).

Kama ishara ya kinabii katika manukato ya upako,

manemane hutufunua jinsi Roho Mtakatifu anavyowaleta

watu katika uponyaji na ukombozi kutoka kuvunjika kwao,

mafungo yao ya dhambi, na magonjwa yao. Nabii Isaya

anatamka kinabii kuhusu uwezo wa upako: “...nayo niraitaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta” (Isaya 10:27).

Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “kuharibiwa” ni zaidi ya

kuvunjwa au kuharibika; maana yake ni kuangamizwakabisa.

Nguvu ya Roho Mtakatifu inaweza kuwaweka watu huru

na kuwaponya kabisa. Mungu anatutakia tuwahudumie

wengine kwa njia hii kwa upako wa Roho Mtakatifu.

b. Mdalasini. Wakati wa Biblia, mdalasini ulikuwa

adimu, ghali na kuthaminiwa sana (Wimbo ulio Bora 4:14).

Mdalasini una harufu tamu, lakini hujulikana kwa ukali wake

katika vyakula fulani. Kwa hiyo kuwepo kwa kiungo hiki

katika manukato ya upako kunatufunulia moto au juhudiinayofuatana na upako wa Roho Mtakatifu.

Yohana Mbatizaji alimwelezea Yesu Masihi kuwa ndiye

Yeye atakayetubatiza kwa Roho Mtakatifu na moto (Mathayo

3:11). Neno “moto” katika mstari huu hutafsiriwa na wengine

kuwa kwa ajili ya utakaso katika moyo wa mwamini. Tafsiri

hii ina ukweli kiasi, lakini maana yake ni zaidi. Moto huwa

na uwako mkali na nguvu, tena unakula. Maandiko husimulia

jinsi Yesu alivyoliwa na wivu kwa ajili ya nyumba ya Baba

Yake (Yohana 2:13-17).

Ujasiri Usio Wa KimaumbileKuna mfano wa ujasiri huu wenye moto wa Roho

Mtakatifu katika Agano Jipya. Kabla ya Siku ya Pentekoste,

wanafunzi na waamini wachache waliobaki walikuwemo

pamoja katika chumba kimoja kule Yerusalemu (Matendo

1:12-24). Walikuwa wamekwisha agizwa na Yesu wahubiri

injili katika duniani kote (Matendo 1:8). Kazi hii kubwa

kabisa ingefanywaje na watu wale wachache? Hawakuwa

wahutubu, wasomi wala hata wenye elimu ya juu. Walikuwa

watu wa kawaida, waliozungukwa na utamaduni

uliowachukia ambao ulikuwa umemsulibisha kiongozi wao.

Wanaume na wanawake hao hawakuwa waoga, lakini

walichanganyikiwa, hawakuwa na uhakika wala mwelekeo

wa kutenda nini na kwa njia gani. Lakini walisubiri kwa

hekima, wakiendelea na maombi na kutunza umoja na

kuhamasishana. Ingawa hawakuielewa, walishikamana na

ahadi ambayo Yesu alikuwa amewapa, ya uwezo ujao kutoka

kwa Roho Mtakatifu (Matendo 1:5,8). Kwa hiyo

walisubiri...

“Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi waupepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yotewaliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimizilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kilammoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanzakusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajaliakutamka” (Matendo 2:2-4).

Kwa dakika moja, maisha ya wale watu wapatao 120

yalibadilishwa walipojazwa Roho Mtakatifu! Mara moja,

tukio hili lilijulikana (Matendo 2:5-13). Petro, mvuvi wa

samaki asiye na elimu ambaye alikuwa amemkana Kristo

kwa ajili ya woga, ghafula anasimama na kutoa mahubiri

yake ya kwanza chini ya upako wa Roho Mtakatifu

(2:14-39). Matokeo yake, zaidi ya watu 3000 waliungwa na

Ufalme wa Mungu siku ile ile (2:41).

Wanafunzi walitoka kuwa kondoo wenye hofu na

wasiwasi, wapate kuwa wachungaji wenye ujasiri, ushuhuda

na utendaji wa miujiza! Walitangaza Injili pasipo aibu, hata

kwenye mateso na kifo. Ndiyo juhudi yenye moto

inayotokana na upako wa Roho Mtakatifu (Matendo

4:23-31).

Juhudi hii si hisia ya kibinadamu inayopita na

kutoweka. Ni nguvu na ujasiri inayowaka kama moto kutoka

ndani yetu tunapokuwa na upako wa Roho Mtakatifu. Ni

imani yenye uhakika katika ukweli wa Neno la Mungu na

Injili ya Yesu Kristo ambayo inatuhamasisha tutende,

tuombe, tuhubiri, tuamini mwujiza - yote kwa uwezo wa

Roho Mtakatifu!

c. Kane (calamus). Huu ni mmea unaofanana na muwa,

ambao mzizi wake ulipendwa sana na watengeneza marashi.

Harufu yake tamu ilitolewa kwa kuponda mzizi wa mmea.

Vile vile, kuna aina ya kupondwa kwa maisha ya

mwamini ambayo ni ya lazima kwa ajili ya kuachia harufu

tamu ya kuwepo kwa Mungu ndani yetu.

Tafadhali angalia kwamba aina hii ya kupondwa si sawa

na aina ile ya kuvunjwa na kuharibiwa inayotokana na

kufanya uchaguzi wa dhambi na uasi. Badala yake, aina hiyo

ni kuvunjwa kutakatifu kunakotoka katika mkono wa Mungu

peke yake.

Huku kupondwa kiroho, ingawa mara nyingine

kunaumiza, kunazalisha matunda mawili:

Kwanza, kunafisha mwili wetu - tamaa zetu za kibinafsi

na kujitegemea kwetu (Luka 9:23-26; Warumi 12:1-2; 13:14;

Wagalatia 5:16-26).

Pili, huku “kuvunjwa wazi” kwa maisha yetu

kunaruhusu neema na uwezo zaidi ya Mungu kudhihirishwa

ndani yetu na kupitia kwetu. Paulo ameandika kuhusu hali hii

katika barua yake kwa Wakorintho (2Wakorintho 12:7-10).

30 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 31: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mchungaji kwa Mchungaji: Kama viongozi wakanisa, tunaona haja ya kuwa na nguvu, ujasiri naustadi. Matokeo yake yanaweza kuwa hatumwachiiRoho Mtakatifu nafasi ya kuwa na uweza kupitia kwetu.Kuna aina ya udhaifu inayofaa ambayo inatufanyatumwegemee Roho Mtakatifu itupasavyo nakutegemea upako Wake katika maisha yetu. Ndipohuduma inatolewa kwa uweza Wake na si kwa nguvuyetu.

Kuna msingi wa ki-Maandiko kwa aina yakupondwa inayofuatana na upako wa Roho Mtakatifu.Hatuwezi kuepuka kupondwa huku, tena haitupasitukuepuke. Ni sehemu ya lazima ya kupevuka katikamfano wa Kristo - kukituongoza katika maisha yakujitoa, kutegemea na kutii kuliko hali nyingine yoyote.

Tafadhali tumia dakika chache katika kusomamifano ifuatayo ya Maandiko, ukitafakari ukweli uliomokatika kila moja:

• Yesu - Isaya 53:1-6; Matendo 3:18; Waebrania5:9; 12:2

• Paulo (na wengine) - Matendo 9:15-16; Warumi8:18; 2Wakorintho 1:3-7; 4:7-18; 6:4-10; 11:22-30;12:7-10

• Waamini wote - 1Wathesalonike 2:14-16;2Timotheo 3:12; 1Petro 4:1-19

Kujikana Kunakoleta UhaiKanuni iliyo na nguvu kubwa ya kuvunjwa na kupondwa

inaonekana katika ishara nyingine za ki-Maandiko pia. Kwa

mfano, katika Ushirika Mtakatifu kuvunjwa na kupondwa

ni lazima katika utengenezaji wa mkate na divai (Luka

22:14-20; 1Wakorintho 11:23-26). Yesu alitumia mkate

(ngano iliyovunjwa na kupondwa) na divai (zabibu

zilizopondwa) kama ishara ya yale ambayo alikuwa atende

kwa ajili ya wanadamu wote katika kusulibiwa Kwake.

Yesu Kristo alibeba hukumu ya Mungu juu Yake kama

adhabu ya haki ya dhambi zetu zote. Kifo Chake kwenye

msalaba kinafunua kupondwa kutoka kwa Mungu kwa mara

ya mwisho kwa ajili ya kufungua uzima (Matendo 2:23-24) -

uzima wa milele wa wokovu kwa kumwamini Yesu.

Tumshukuru Mungu kwamba hatulazimiki sisi tupitie mateso

haya, ingawa ndiyo adhabu ya haki ya dhambi yetu na uasi

wetu!

Lakini kuna kufia ubinafsi wetu ambako ni lazima ili

uzima na uweza wa Mungu ndani yetu ufunguliwe kupitia

kwetu. Hii SI aina ya kujitoa mhanga au kujitesa ili

“kuthibitisha” hali yetu ya juu ya kiroho. Lakini sharti la

kutembea na Kristo na kumtumikia kikamilifu linadai uhiari

wa kuishi maisha ya kujikana na kunyenyekea mapenzi ya

Mungu hata kujitolea kama dhabihu (2Samweli 24:18-24;

Luka 9:23-26).

Kupata Kuwa Vyombo VinavyoaminikaMsimamo wa Yesu katikati ya mateso ni mfano wetu

bora: “...ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yakealiustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketimkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania

12:2). Yesu alikubali kikamilifu makusudi ya Mungu Baba

katika mateso na dhabihu Yake.

Bila shaka, Yesu hakufurahia mateso (Luka 22:42-44).

Lakini alitambua ulazima wa msalaba (Luka 24:46-49).

Uhiari wake wa kuteseka na kufa kwa niaba yetu

haukufungua tu wokovu wetu, bali pia ulikuwa tendo la kutii

ili atimize mapenzi ya Baba Yake (Mathayo 26:39,42,44).

Mateso yetu na dhabihu zetu ni vidogo kulingana na yale

ambayo Yesu alitoa kwa ajili yetu, lakini hata hivyo ni

vigumu. Lakini tunayo baraka ya ahadi ya ajabu ya Mungu

kwamba anatumia mateso yetu kwa utukufu Wake pamoja na

ufanisi wetu kwa wakati mmoja (Yakobo 1:2-5,12). Mungu

ameahidi kuchukua mateso na dhiki yetu katika maisha haya

na kuvibadilisha viwe na hatima yenye baraka (Warumi

5:1-5; 8:18; 2Wakorintho 4:17).

Ahadi ya Baba yetu kwetu imetamkwa wazi: “Nasitwajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazipamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani,wale walioitwa kwa kusudi lake” (Warumi 8:28). Na “kusudi”

la Mungu kwa ajili ya walioamini ni nini? Limetajwa wazi

kabisa katika mstari unaofuata: “...wafananishwe na mfanowa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongonimwa ndugu wengi” (Warumi 8:29).

Mungu anataka kutumia mambo yote katika maisha yetu

akitutengeneza katika mfano wa Kristo, vyombo vinavyofaa

kwa matumizi ya Bwana (2Timotheo 2:19-21). Mara

nyingine mateso yetu hutokana na kuharibika kwa dunia hii

na asili ya dhambi ya watu waliomo ndani yake. Wakati

mwingine Mungu anaweza kutumia matukio ya maisha yetu

kwa ajili ya matumizi na makusudi Yake. Kwa pande zote,

Mungu ameahidi kuyatumia kwa manufaa yetu.

Mungu atatubadilisha kwa njia itakayotufanya tuwe

vyombo safi na vinavyoaminika vya mapenzi na makusudi

Yake, vikiruhusu upako wa Roho Mtakatifu utiririke kupitia

kwetu pasipo kuzuiliwa. Lakini ni lazima tushirikiane na

kutii kazi Yake katika maisha yetu!

Harufu Tamu Ya KristoKila mwamini wa Kristo, na hasa kila kiongozi wa kanisa,

ameitwa “adhihirishe harufu ya kumjua yeye kila mahali kwakazi yetu. Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele zaMungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea”

(2Wakorintho 2:14-15). Nukato hii ya uhalisi wa kuwepo kwa

Mungu itatolewa kwa njia ya maisha yetu tunapokubali

“kupondwa” na Yeye katika kazi Yake ya kutubadilisha.

Katika Maandiko yote, na hata leo, Mungu amewatumia

wanaume na wanawake wa kawaida kwa njia za uwezo

mkuu. Mara nyingi, wanavumilia kusongwa na kupondwa

katika maandalizi yao na wakati wa huduma yao. Lakini kwa

sababu yake, makusudi ya Mungu yanatimizwa na harufu

tamu ya Mungu inatolewa kwa njia ya maisha yao. Ni vema

kukumbushwa tena kwamba hakuna wanaume na wanawake

wakuu wa Mungu - waliopo tu ni wanaume na wanawake

wanyenyekevu (waliovunjika, waliojitoa) ambao

wanatumiwa na Mungu katika mambo makuu!

d. Kida. Kida ni ganda la mmea unaofanana na

mdalasini. Kida ilitumiwa kama dawa ya kuharisha wakati

wa Biblia. Kama ishara katika mafuta matakatifu ya upako,

kida huwakilisha kazi ya kutakasa katika upako wa Roho

Mtakatifu.

Ni kweli kwamba upako wa Roho Mtakatifu unatupatia

nguvu, karama na uwezo wa ki-Mungu. Lakini pamoja na

haya, kazi ya Roho Mtakatifu ni kubadilisha maisha ya wale

anaowatia mafuta.

MATENDO • 31Nakala 16 / Nambari 1

Page 32: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Tunaweza kujifunza mfano wazi kabisa wa umuhimu wa

kazi hii katika maisha ya Mfalme Sauli. Samweli alimtia

mafuta Sauli awe mfalme juu ya Israeli (1Samweli 10:1).

Sauli alitengwa kwa ajili ya kusudi rasmi la Mungu kwamba

awe mfalme. Upako ulimpa Sauli mamlaka, karama na

uwezo wa kutendea kazi yake aliyopewa na Mungu.

Maandiko yanafunua mengi zaidi ambayo Sauli

aliyapokea pamoja na upako wake: “Na roho ya Bwanaitakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, naweutageuzwa kuwa mtu mwingine” (1Samweli 10:6). Ndipo

baadaye kidogo: “Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli,Mungu akambadilisha moyo” (ms. 9).

Tunaweza kuona kwamba upako haukumwandaa tu

Sauli na yale aliyohitaji, bali pia ulimbadilisha. Haya

yalimfanya astahili na awe chombo kilichofaa zaidi sana

mkononi mwa Mungu. Hii ni picha nzuri ya kutia moyo ya

yale ambayo upako wa Roho Mtakatifu unaweza kutupatia

sisi pia kama vyombo au zana za Mungu.

Inasikitisha kwamba Sauli (kama wengine) alivipa

kisogo vile vyote ambavyo Mungu alimpatia, kwa kukataa

Neno la Mungu na amri Zake na kufuata mapenzi yake

binafsi (1Samweli 15:22-33). Ni huzuni kubwa kwamba

ufalme ulioanza kwa fahari juu ya Israeli uliishia katika aibu

kwa Mfalme Sauli na familia yake.

Mchungaji kwa Mchungaji: Mungu alimpaMfalme Sauli vyote alivyohitaji ili atimize wajibu wakena awe mfalme mwenye ufanisi. Sauli alifanya hivyokwa muda, akafanikiwa. Lakini inasikitisha kwambabaadaye Sauli alichagua kufanya mapenzi yake binafsibadala ya kutii maagizo ya Mungu, na mwisho wakeulikuwa kushindwa.

Mungu anapotuita, anatupatia vile tunavyohitaji ilitutimize mapenzi Yake. Lakini usisahau kamwekwamba yale ambayo Baba anatutengeneza tuwe nimuhimu kama yale anayotuita tutende. Munguanataka tubadilishwe, tupate kufanana na Kristo katikatabia zetu na matendo yetu.

Baba yetu anatutakia tutii Neno Lake nakumwamini katika mambo yote. Hatutapevuka hadimahali ambapo hatutahitaji tena kukua na kuitikia kaziya kubadilishwa kwetu na Roho Mtakatifu! Ni mfuatanowa maisha yetu yote.

Roho Mtakatifu atatusahihisha, kutuonya nakututhibitishia. Mungu hatuhukumu (Warumi 8:1) lakinianatudai kwamba tumtii na kukubali kazi Yake yakutubadilisha. Mara nyingine tunaweza kujikwaa aukuanguka; lakini ni lazima tutubu haraka na kurudikatika mfuatano wetu na kujitoa kwetu kwa Mungu namapenzi Yake.

Mungu anatenda kazi ya kutubadilisha:• Kwa utukufu Wake;• Kwa furaha, amani na baraka yetu; na• Kutufanya tuzae matunda na kuwa na ufanisi

zaidi kama mabalozi na watumishi Wake kwa wenginekatika huduma.

Kuitikia Kazi Ya Roho MtakatifuKatika kuangalia kida, tumejifunza kuhusu kazi ya

kimsingi ya Roho Mtakatifu. Anakuja kuondoa na kusafisha

yale yasiyofuatana na maisha, tabia na Nafsi ya Kristo. Ishara

hai ya mtu mwenye upako halisi ni kwamba anazidi kufanana

na Kristo katika tabia yake - si lazima aoneshe uwezo,

karama wala huduma maalum.

Kama viongozi wa kanisa, ni lazima tumruhusu Roho

Mtakatifu aendelee wakati wote kushughulikia madhaifu

yetu ya kimwili, majaribu yetu na kushindwa kwetu. Lazima

tusimhuzunishe Roho Mtakatifu kwa kupinga kazi Yake ya

kuleta mabadiliko ndani yetu (Waefeso 4:30).

Tutavuna tulizopanda, kama ni mbegu za haki na baraka,

au za uozi (Wagalatia 6:7-8). Mungu atatuwekea kipimo

kikali zaidi kama viongozi (Yakobo 3:1). Usidanganyike;

Mungu hadanganyiki. Ukiendelea katika dhambi, hatimaye

itadhihirika wazi kwa wote (Hesabu 32:23).

Kwa hiyo uchague haki! Uitikie kazi ya Roho Mtakatifu!

Umtii na kumwamini Mungu! Upokee upako Wake juu ya

maisha yako na utumishi wako! Uwe mfano kwa wengine wa

chombo chenye kuitikia, kufundishika na kujitolea kwa kazi

ya Roho Mtakatifu. Umruhusu Yeye atende kazi ndani yako,

ili apate kutukuzwa hata zaidi kupitia kwako! Amina!

e. Mafuta Ya Mzeituni. Mafuta ni ishara inayotumika

mara nyingi kabisa katika kumwashiria Roho Mtakatifu

katika Agano la Kale na Agano Jipya. Mafuta ya mzeituni

kama sehemu ya mafuta matakatifu ya upako yana maana

mazito sana. Huwa na sifa za sehemu zile nne zote nyingine,

nao unaongeza sifa nyingine pekee.

Katika wakati wa Biblia, mafuta ya mzeituni:

• yalitumiwa kama dawa, kuponya magonjwa na maumivu

(kama manemane);

• yalitumiwa katika taa, na kuhusiana na moto (kama

mdalasini);

• yalitengenezwa kwa kupondwa na kusongwa, yakitoa

harufu tamu (kama kane);

• yalitumiwa kwa kusafisha na kutakasa kwa nje na kwa

ndani (kama kida).

Lakini mafuta ya mzeituni yana sifa maalum iliyo ya

lazima katika Mwili wa Kristo. Yanalainisha. Yanapowekwa

katikati ya vitu viwili, yanapunguza kusuguana na kuleta

utelezi.

Ishara hii inatufunulia ulazima wa umoja kati ya watu

wa Mungu. Maandiko yanatufunulia hoja hii ya kuhusisha

upako na umoja kwa njia inayopendeza sana: “Tazama, jinsiilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwaumoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni,ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, naam, uzima hatamilele” (Zaburi 133).

Umoja kati ya watu wa Mungu ni chanzo cha furaha na

amani. Mungu anapendezwa wakati watu Wake

wanapotembea pamoja katika mahusiano sahihi. Baraka Yake

inafunguliwa na upako wa Roho Mtakatifu unatiririka kwa

uhuru zaidi.

Uhusiano Wa WanamuzikiMaana ya umoja katika Biblia hayaeleweki vizuri mara

nyingi. Katika Maandiko, umoja ni tofauti na ufanani. Ufanani maana yake ni kwamba vyote vifanane, kama

vile nguo za sare, pasipo tofauti yoyote.

Lakini maana ya umoja katika Maandiko ni kama kundi

la wanamuziki wanaotumia vyombo mbalimbali kwa

ulinganifu. Kila chombo kina kazi yake tofauti. Lakini

32 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 33: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

vinapotumika pamoja chini ya kiongozi mkuu, vinafanya

kazi moja. Kwa hiyo muziki inayotokea inapendeza sana.

Ndiyo hali halisi pia katika Mwili wa Kristo. Kuna

vipawa, wito, mitindo, watu na uwezo tofauti. Lakini sisi sote

tumeitiwa uhusiano wa ulinganifu (Yohana 17:20-21).

Hakuna mtu yeyote anayefanana kikamilifu na mwingine;

lakini kila mmoja ameitwa afanye kazi katika nafasi yake.

Ndipo Mungu anaongoza washiriki wote katika muziki

inayopendeza - katika Mwili Wake, wakipendana kama

ushuhuda kwa ulimwengu (Yohana 13:34-35).

Paulo anaongea kuhusu haya anapoeleza kuhusu karamaza mafunuo za Roho katika 1Wakorintho sura ya 12 (taz. pia

1Wakorintho 14:26-40). Kanisa la awali lilikuwa mfano wa

umoja huu, uliositawishwa kwa uwepo wa Roho Mtakatifu

mwenye kuleta upako (Matendo 2:42,44-47).

Hatari Za Ukosefu Wa UmojaUkosefu wa umoja kati ya viungo vya Mwili wa Kristo

una madhara yake mapana sana. Paulo aliwakemea

Wakorintho kuhusu kugawanyika au kutengana kwao

(1Wakorintho 3:1-23). Aliwaita watu wa mwilini na

wasiopevuka: “Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabiaya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! si

watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi yakibinadamu?” (ms. 3).

Ukosefu wa umoja na mgawanyiko kati ya ndugu ni kosa

zito. Siyo tu kwamba huleta uharibifu; huzuia pia wepesi na

ufanisi wa kazi ya Ufalme wa Mungu. Maelezo ya Paulo

kuhusu karama za mafunuo yaliyotajwa hapo juu

yalisababishwa na ukosefu wa utaratibu na hali ya

mgawanyiko iliyosababishwa na kiburi na ubinafsi wa watu.

Inayosikitisha zaidi ni ukweli kwamba watu ambao ni

viungo vya Mwili wa Kristo wasipopendana na kutumikia

makusudi ya Bwana kwa umoja, ushuhuda wetu mbele ya

ulimwengu inazuiwa sana. Biblia inatukumbusha kwa bidii

kwamba ulimwengu utajua kuwa sisi ni Wakristo kutokana

na upendo uliopo kati yetu (Yohana 13:35). Kama

ulimwengu hauoni uwepo wa upendo kati yetu, ushuhuda

wetu kwa ulimwengu hauna uhakika wowote.

Tunaweza kufanya matendo makuu katika jina la Kristo;

kuwa mhubiri wa ajabu; kupanga mikutano ya hadharani; na

mengi zaidi. Hata hivyo, kama sisi hatupendi ndugu zetu

Wakristo, matendo hayo hayataleta tukio lililotakiwa

(1Wakorintho sura ya 13).

Kuna hamasa nyingi katika Maandiko kuhusu hatari ya

misimamo inayovunja au kuzuia umoja katika Mwili wa

Kristo. Tafadhali utumie dakika chache katika kusoma

mistari ifuatayo:

• Warumi 13:13-14

• Wagalatia 5:13-23

• Waefeso 4:20-29

• 1Timotheo 6:3-5

• Tito 3:9-11

• Yakobo 3:14-16

• 1Yohana 2:9-11; 3:10-18

Mistari hiyo inaonesha wazi kwamba palipo na

mgawanyo, magomvi, chuki, uchungu, wivu, mashindano,MATENDO • 33

Kanisa: umoja unaokubaliana kama kwaya au kundi la wanamuziki...kila mtu na kila chombo ni muhimu

Ukosefu wa umoja na

mgawanyiko kati ya ndugu ni kosa

zito. Siyo tu kwamba huleta

uharibifu; huzuia pia wepesi na

ufanisi wa kazi ya Ufalme wa

Mungu.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 34: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

hasira, n.k., umoja unazuiwa na hata kuvunjwa. Hali hii

inamhuzunisha Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30) nayo

inaweza kuzimisha uwepo Wake uletao upako

(1Wathesalonike 5:19).

Ni wazi kwamba palipo na misimamo ya kimwili kama

hii, ibilisi anafanya kazi yake ya siri alete mgawanyo na

kuzuia kazi ya Mungu (Yakobo 3:13-16). “Gawanya na

kushinda” ni mkakati wa zamani kama ibilisi mwenyewe -

mkakati ambao amejifunza kuutumia kwa ufanisi katika

kuzuia na kujaribu kuangamiza Mwili wa Kristo. Lakini

mikakati yake inafanikiwa ikiwa tu sisi tunashirikiana nayo!

Mahusiano: Yanathaminiwa Na MunguUpako wa Roho Mtakatifu utaleta uponyaji na

upatanisho wa mahusiano ndani ya Mwili. Hali hii iwe ya

kweli hasa kati ya viongozi. Mungu anatutazamia sisi tuishi

katika uhusiano ufaao - kwanza kwa Yeye, halafu kwa

wenzetu (Waefeso 2:14-17). Ni kiburi, wivu na ubinafsi

wenye uchungu, vyote vya kibinadamu, ambavyo vinamzuia.

Misimamo hii ndiyo ibilisi atakayoitumia akipanda

mgawanyo, chuki na kutosameheana katika Mwili.

Ukiona kuwa ndugu yako ana neno juu yako, nenda

ukajaribu kupatana naye (Mathayo 5:23-24). Ukiwa na neno

juu ya mtu mwingine, uwe mwepesi KUTUBU! (Mathayo

5:21-22). Utubu kuchukizwa na kuruhusu hasira, chuki na

misimamo ya kuhukumu viweke mizizi moyoni mwako.

Uwasamehe wengine, ili hukumu ya Mungu isikuangukie

wewe (Mathayo 6:14-15; taz. pia Mathayo 18:21-35).

Mungu anatilia mkazo mkuu mahusiano - mpaka

alimtuma Mwana Wake ateseke na kufa ili uhusiano wetu na

Yeye uliovunjwa na dhambi yetu uweze kurejeshwa. Kwa

njia hii hii, upendo na msamaha Wake kwetu unawezesha

mahusiano yafaayo kati yetu sisi kwa sisi.

Tumejifunza kwamba yale ambayo

Mungu anayaamuru, wakati wote

anayawezesha pia. Naye ametuamuru tuwe

na mahusiano yafaayo kati yetu (Yohana

13:34-35).

Lazima tuthamini na kuwekea

dhamana uhusiano wetu na Mungu. Na ni

lazima pia tufanye hivyo katika uhusiano

wetu na ndugu na dada zetu katika Kristo.

Utumishi wote wa kudumu na

kubadilisha maisha hutokana na

mahusiano yenye afya bora. Mfuatano

huu unaanza na yale tunayopokea kutoka

kwa Mungu katika uhusiano wetu na Yeye.

Ndipo, kutokana na upendo na huruma na

yale tuliyopokea kutoka kwa Mungu,

tunawatolea na kuwatumikia wengine.

Ndio mtindo wa Mungu kwa ajili ya

utumishi. Maisha ya Yesu hapa duniani ni

mfano wa kudumu wa aina hii ya mtindo

wa utumishi kwa ajili yetu.

Umoja, Tofauti, UpendoKuna tofauti za kuelezana au

mawasiliano katika Mwili wa Kristo.

Lakini si lazima tofauti hizi zilete vikwazo

kwa umoja na uhusiano (Warumi 14:13).

Kumbuka, umoja si ufanani. Umoja ni

uhusiano wa ulinganifu tunapoitikia kazi ya ndani ya upako

wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Roho Mtakatifu

wakati wote atatuthibitishia, kutusaidia na kutuongoza katika

uhusiano unaofaa pamoja na wengine - kama tutamwitikia.

Mwongozo rahisi kwa ajili ya umoja umeelezwa hivi:

“Katika mambo ya lazima ya msingi - umoja; katika yasiyo

ya lazima ya msingi - tofauti; katika yote - upendo.”

Tunapokua na kuishi katika upako wa Roho Mtakatifu,

tuwe na neema na upendo sisi kwa sisi. Tukifanya hivyo,

upako wa Roho Mtakatifu na ushuhuda wa Kristo

vitafunguliwa zaidi ndani yetu na kupitia kwetu!

Kupata UfahamuMafunzo haya mafupi kuhusu mafuta matakatifu ya

upako (Kutoka 30:22-33) yametufunulia kwamba Mungu

ametupatia picha na ishara ya ajabu ya utangulizi wa kazi ya

Roho Wake Mtakatifu. Kwa hakika, masomo yetu ya

Maandiko hutupatia ufahamu, hekima na tumaini (Warumi

15:4).

Katika mafunzo haya hadi hapa, huenda wewe una

maswali, kwa mfano:

• Je, ninaweza kukua katika upako? Kama ndiyo, kwa njia

gani?

• Je, kuna “upako wa uwongo”? Kama ndiyo, ninawezaje

kutambua upako wa kweli?

• Nini inaweza kudhuru au kuzimisha upako katika maisha

yangu?

• Je, ninaweza kuendelea wakati wote kujaa upako wa

Roho Mtakatifu?

Tutajadili maswali haya na mengine katika sehemu

ifuatayo, “Kutembea Katika Upako”.

34 • MATENDO

Roho Mtakatifuatatuongoza

katika mahusianoyanayofaa.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 35: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Tunapoanza kujifunza kuishi siku kwa siku katika upako

wa Roho Mtakatifu, turejee kwa kifupi kanuni za kimsingi

zilizo muhimu sana.

Upako wa Roho Mtakatifu si “nishani ya kiroho” ya

kujitafutia. Wala si uzoefu kwa maneno na matamshi ya

kidini. Bali ni uhusiano na Roho Mtakatifu wenye uhai

ambao unaendelea kukua.

Kumbuka, Roho Mtakatifu ni Nafsi, kama vile Yesu na

Baba ni Nafsi. Kwa hiyo tunaweza - na inatubidi - tujifunze

kutembea katika uhusiano ulio hai wa siku kwa siku pamoja

na Roho Mtakatifu.

Tumejifunza kwamba upako si aina fulani ya nguvu ya

kifumbo isiyoeleweka, ambayo tunapewa ili tuitumie kwa

ajili ya makusudi yetu binafsi. Bali upako ni uwezo wa

ki-Mungu, upaji unaohusiana moja kwa moja na Nafsi ya

Roho Mtakatifu na kuwepo Kwake katika maisha yetu.

Uwezo unaotokana na kuwepo kwa Roho Mtakatifu unapitia

uhusiano wetu binafsi na Yeye.

Upako ni Nafsi ya Roho Mtakatifu na kuwepo

Kwake, vikileta pamoja na kuwepo Kwake uwezo,

karama na mamlaka vyote vinavyohitajika kwa ajili ya

kutimiza mapenzi ya Baba kwa muda fulani maalum ya

utumishi au kazi.

Wajibu Wetu Wa KwanzaTumejifunza kwamba wakati wa Agano la Kale, Roho

Mtakatifu wa Mungu “aliwajia” manabii, makuhani,

waamuzi na watumishi Wake wengine.

Wakati wa Agano Jipya na baadaye - kipindi kiitwacho

pia Kipindi cha Kanisa - Roho Mtakatifu amekuwa

akimiminwa (Matendo sura ya 2). Mungu Roho anaishi

ndani ya kila mwamini wa kweli, amwongoze na kumfariji,

na kuwahudumia wengine kupitia kwake (Yohana 7:37-39;

14:16-17,26).

Waamini wote wa Yesu Kristo wamepewa Roho

Mtakatifu kwa kipimo fulani (1Yohana 2:20,27). Hali hii ni

lazima kwa sababu kila mwamini ameitiwa aina fulani ya

huduma kama kiungo cha Mwili wa Kristo (Waefeso 4:12).

Sisi sote tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu kila siku!

Lakini kwa watu wanaoitiwa utumishi maalum, kuna

upako maalum na mzito unaopatikana. Upako huu unatolewa

na Mungu katika ufalme Wake. Mtu anaweza ama kuupokeana kukua ndani yake, ama aamue kuukataa au kutoujali.

Aina hii ya upako (kuwezeshwa ki-Mungu na Roho

Mtakatifu) inahusiana moja kwa moja na vipawa vyako na

wito wako. Kwa mfano, mtu aliyeitwa atumie kipawa cha

uinjilisti (Waefeso 4:11) huenda hana upako wa kipawa cha

kimtume. Atafanya vema na kuzaa matunda zaidi ndani ya

uwezo, karama na mamlaka ambavyo amepewa upako kwa

ajili yake - katika mfano huu, kama mwinjilisti.

Lakini katika utendaji wa kila siku, inawezekana si rahisi

namna hii. Ingawa mtu fulani ameitiwa na kupewa upako

kwa ajili ya kazi fulani ya utumishi, kila mmoja wetu bado

ana wito wa kawaida kama mwamini wa Kristo, wa kuishi na

kufanya kazi kila siku kama mshirika wa Mwili wa Kristo.

Kwa mfano, kufuatana na yale tunayoona katika

Maandiko, Timotheo aliitwa afundishe na kuwa mchungaji

katika kanisa. Lakini pia aliagizwa na Paulo: “Fanya kazi yamhubiri wa Injili” (2Timotheo 4:5) - si kwamba awemwinjilisti, ila mara nyingine afanye kazi iliyohitajika kwa

ajili ya kuwapatia wengine habari njema ya Injili.

Kwa hiyo, tunaona kwamba sisi kama watumishi wa

Kristo, tuna wajibu wa kawaida na kazi ambazo huenda

hazihusiani na wito wetu pekee. Lakini hata hivyo ni za

lazima na muhimu kwa ajili ya ufanisi na afya katika Mwili

wa Kristo.

Wajibu wetu wa kwanza na wa msingi kama waamini wa

Yesu Kristo, na kama viongozi wa kanisa, ni utii kwa Kristo.

Lazima tumtii Bwana na kuishi kufuatana na kanuni ambazo

Yeye ametupatia katika Neno la Mungu.

MATENDO • 35

SEHEMU YA III

KUTEMBEA KATIKA APAKO

Upako wa Roho

Mtakatifu

Nakala 16 / Nambari 1

Page 36: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Katika Maandiko, tunaona kwamba waamini wamepewa

wajibu nyingi: kuwahudumia wengine, kuwapa maskini

chakula, kutunza yatima, kuwaandaa watakatifu, kuwafikia

waliopotea - orodha inaendelea. Kutakuwa na nyakati na

misimu katika maisha yako pamoja na Kristo ambapo

utahitaji kutumia wakati na bidii katika aina hizi za huduma

ya kuwafikia watu, pamoja na wito wako au kazi yako pekee.

Mwongozo mzuri wa kufuata katika kutambua yale

ambayo wewe unapaswa uyafanye katika huduma ni huu:

“Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwanguvu zako” (Mhubiri 9:10; taz. pia Wakolosai 3:23).

Uombee kila nafasi inayotokea, na halafu uwe mwepesi

kumtii Bwana anapokuita uwahudumie wengine. Haidhuru

kama kazi iliyo mbele yako ni kubwa au ndogo - iliyomuhimu ni kwamba Bwana anapokuagiza ufanye kazi fulani,

umtii Yeye!

Mchungaji kwa Mchungaji: Nafasi yangu yakwanza ya “kikazi” kama mtumishi aliyehitimu Shule yaBiblia na kupata leseni yangu, ilikuwa kama mlinzi wakanisa fulani kubwa. Nilikaa miaka miwili nikisafishavyoo, kutupa takataka, kufagia vyumba vya mikutano,kuokota takataka kwenye bustani na kufanya kazinyingine zisizochangamsha lakini zilizo za lazima.

Sikufurahia kazi hii. Haikuwa rahisi. Tena iliaibisha.Lakini nilijua kwamba Mungu aliniagiza nifanye kazihiyo, nayo ilikuwa maandalizi bora kabisa kwa ajili yakutumikia Mwili wa Kristo. Kwa hakika ilikuwa mtihanikwa uaminifu wangu.

Utiifu wangu kwa kazi hii na bidii yangu katikakuitekeleza vilinifungulia mlango wa kazi nyingine, nandivyo nilivyoendelea katika kila kazi ya utumishiniliyofanya katika miaka yote. Nimeanzisha makanisa,kufundisha vijana, kuwa mchungaji wa usharika,kuhutubia mikutano, kuongoza timu za misioni, namengine mengi. Na kwa neema ya Mungu, katikamuda ule wa miaka 30, Bwana aliniandaa nakunifikisha hapo nilipo sasa katika nafasi ya kuongozahuduma ya ulimwengu mzima.

Naamini kabisa kwamba nisingekuwa nikiongozaWorld MAP leo kama nisingalikuwa tayari kumtii Bwanakwa uwezo wangu wote katika njia ile yote - hatua kwahatua, nikitimiza kila kazi - haidhuru aliniomba nifanyenini katika jina Lake. Sikutii kikamilifu kila wakati, pianimefanya makosa mara kwa mara. Lakini kwa jumla,nilifanya nilivyoweza katika kufuata njia ya utiifuambayo Mungu alikuwa ameweka mbele yangu.

Mungu ana mpango kwa ajili ya maisha yako. Yeyeanajua njia bora ya kukuwezesha kutimiza mpangohuu. Utiifu wetu kwa Mungu na Neno Lake si hiari yetu- ni ya lazima!

Wito Wetu Wa KwanzaHaidhuru cheo chetu cha uongozi au utawala, wito wetu

wa kwanza sikuzote ni kwa uhusiano wetu na Kristo.

Uhusiano huu ni katika utiifu, uaminifu, huduma, utakaso

binafsi, unyenyekevu, matunda yote ya Roho (Wagalatia

5:22-23) na kuendelea kukua. Tabia hizi zinaweka msingi wa

uhusiano na Yesu Kristo ulio wa thamani na usitawi. Tokeo

moja la msingi huu imara wa uhusiano binafsi ni

kufunguliwa kwa huduma kupitia kwako, na upako

utakaohitaji ili utimize kazi zako za utumishi. Tukikumbuka

marejeo haya ya msingi ya kanuni muhimu, tuangalie sasa

kwa makini zaidi maana ya Kutembea Katika Upako.

A. KULINDA UPAKO

Roho Mtakatifu anapotutia mafuta kwa ajili ya huduma,

ni heshima takatifu. Ni hali ambayo inatubidi tuikuze na

kuilinda katika maisha yetu.

Bila shaka, maana yangu si kwamba Roho Mtakatifu

(anayetutia mafuta) anahitaji ulinzi wetu. Bali inatubidi

tulinde moyo wetu na maisha yetu kwa ajili ya uchafu wa

kiroho na kimaadili wa dunia hii (2Petro 1:2-4; 1Yohana

2:15-17).

Sulemani, mwandishi wa Kitabu cha Mithali,

anatuhimiza: “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” (Mithali 4:23).

Ni kupitia maisha yetu kwamba upako wa Roho Mtakatifu

utatiririka katika huduma kwa wengine. Kwa hiyo ni lazima

maisha yetu, moyo wetu, vilindwe katika utakaso.

1. Panya Katika Kisima

Paulo alisema kuwa kila mwamini wa Kristo ni “hekalula Roho Mtakatifu” (1Wakorintho 6:19-20). Kwa hiyo,

tunahimizwa tusiruhusu “hekalu” letu lichafuliwe kwa

kushiriki dhambi (taz. pia Warumi sura ya 6).

Biblia ina hamasa nyingi kuhusu kuendelea katika usafi

wa mwili, nafsi na roho (1Yohana 3:2-3). Maelezo haya ni

kwa ajili ya kila mwamini, na hasa viongozi katika Mwili

wa Kristo!

Kwa nini usafi (utakaso) wetu binafsi ni muhimu sana?

Kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu - kila mmoja

wetu aliyekombolewa “kwa damu ya thamani, kama yamwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo“

(1Petro 1:19), si kwa damu ya fahali na mbuzi (Waebrania

9:13-14). Tunaposhiriki matendo au misimamo ya dhambi,

mahali ambapo Roho Mtakatifu anataka kukaa huchafuliwa

na kunajisiwa.

Kuhifadhi UsafiTuseme kuna shamba au kijiji chenye kisima kimoja tu

cha maji. Watu wote wanatumia kisima hiki na kutegemea

maji yake. Maji hutumiwa kwa kuoga, kupika, kufua na

kunywa. Je, unaweza kubuni hali ya kuhitaji kutumia maji

haya, ukaona panya mfu walioelea juu yake?

Huu ni mfano wa wazi jinsi uchaguzi wetu unavyoweza

kugusa hekalu la Roho Mtakatifu ndani yetu. Yeye ni

chemchemi yetu kwa ajili ya mahitaji yote ya maisha ya kila

siku. Lakini si maisha yetu tu. Roho wa Mungu ndani yetu,

kama viongozi wa kanisa, anatusaidia tuwe chemchemi ya

ki-Mungu kwa ajili ya wengine.

Kwa hakika, katika utumishi tunawapatia wengine

kutokana na tulivyo wenyewe na yale tuliyopokea (Mathayo

10:8; taz. pia mfano wa Bahari ya Galilaya na Bahari ya

Chumvi katika Sehemu Ya II, C 2). Lakini itakuwaje kama

tumeruhusu “panya” kuingia katika maisha yetu? Kwa

hakika kuwepo kwa tabia na misimamo ya dhambi kutatutia

sumu na uchafu, kukigusa utumishi wetu, uhusiano wetu,

familia yetu, kazi yetu na yote tunayogusa.

Kwa kawaida “panya katika kisima” ni wa aina gani?

Agano Jipya linatupatia aina mbalimbali, halafu

linaorodhesha vilivyomo katika kila aina:

36 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 37: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

• Matunda ya mwili (Wagalatia 5:19-21).

• Matendo yasiyofaa yenye msingi katika udanganyifu wa

dhambi (Waefeso 4:17-32).

• Kufuata sheria, au roho ya dini (Wagalatia 5:1-6;

Wakolosai 2:11-23).

• Kugombea nafasi, cheo, nguvu (Mathayo 6:1-2,5,16;

23:2-12).

• Kutumia huduma kwa kujipatia utajiri na mali (Mathayo

6:19-21,24; 1Timotheo 6:3-10; 2Timotheo 4:10).

• Kuhukumu, kuwa na uchungu, kutosamehe (Mathayo

7:1-6; 18:21-35; Wakolosai 3:12-19; Waebrania 12:15;

Yakobo 3:13-18).

• Mafundisho ya uwongo, uzushi (Mathayo

24:4-5,11,23-27; Wagalatia 1:8; 2Wakorintho 11:13-15;

1Timotheo 4:1-5; 2Timotheo 2:14-18; 2Petro 2:1-22;

Yuda 7-19).

Haya ni maelezo mafupi tu ya “panya” wanaoweza

kuharibu “kisima” binafsi cha moyo wako, na pia

kuwachafua wengine wanaoguswa na maisha yako na

utumishi wako.

Kama kiongozi katika Mwili wa Kristo, umeitiwa

maisha ya utakaso na utakatifu (Mathayo 5:8; 1Wakorintho

9:24-27; Waebrania 12:14; 1Petro 1:13-19). Upako ambao

Mungu anawapa watumishi Wake walioitwa ni wa thamani

na uwakfu zaidi kabisa kuliko mafuta ya Hema ya Kukutania

ya Agano la Kale - kwa sababu ni kuwepo kwa Roho

Mtakatifu Mwenyewe!

Wito wetu wa juu kabisa ni wa kuishi katika uhusiano

bora na Mungu. Maana yake ni kwamba tuishi maisha yenye

utakaso, pasipo uchafu, kama “hekalu” linalomfaa

(1Wakorintho 6:19-20), mahali pa kuishi pa Roho Mtakatifu.

Maisha ya utakaso humtukuza na kumpendeza Mungu Baba

yetu, na kutufanya tuwe waaminifu zaidi sana na wenye

kuweza kutumiwa zaidi mikononi mwa Bwana.

Ni wewe peke yako unayeweza kuhifadhi usafi wa

kisima chako. Uamue sasa uwe chombo safi ambacho Roho

wa Mungu na Neno la Mungu lisiloghushiwa hutiririka

kutoka ndani yake. Uwe zana ya utumishi iliyotakata, mtu

ambaye Mungu anaweza kumtia mafuta katika kazi kubwa

kwa ajili ya utukufu Wake na makusudi Yake (1Wakorintho

10:31; 2Timotheo 2:19-21)!

Kujifunza Kutokana Na KushindwaSulemani alikuwa mfalme aliyeinuliwa na Mungu na

kupewa karama za pekee (1Wafalme 3:5-14; 4:29-34).

Bwana alimtembelea mara mbili kimwujiza (taz. 1Wafalme

sura ya 3 na 9). Sulemani aliamriwa afuate njia zote za

Mungu na kutii kanuni na amri Zake zote (3:14; 6:11-13;

9:4-9). Na ndivyo alivyofanya - kwa muda.

Lakini baadaye tunasoma kwamba utawala wa Sulemani

uliishia katika uharibifu kwake na kwa ufalme wake mzima

(tazama 1Wafalme sura ya 11).

Sulemani, kama viongozi wengi mno, alianza vizuri

lakini aliishia vibaya. Ilikuwaje? Kwa kifupi jibu ni neno

moja tu: kutokutii.Tukichunguza Kitabu cha 1Wafalme kwa makini zaidi,

tunaona kuwa Sulemani alikuwa mtu maarufu sana, “alikuwana hekima kuliko watu wote” (4:31). Alikusanya utajiri usio

na kifani (10:11-29) na sifa na heshima ya watu (10:1-9).

Lakini ndipo Sulemani alipoanza kuvunja amri za Mungu

zilizo wazi (11:1-2). Na pole pole, kwa kuchagua na

kuridhiana, alianza kujiangalia katika ubinafsi, pamoja na

baraka na heshima zote alizokusanya kutokana na upako wa

Mungu na karama Zake. Njia hii iliishia katika kuangamia

kwa utawala wake Sulemani.

Sisi basi, tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya

Sulemani na utawala wake?

a. Vishawishi vinasababisha uzembe (ukosefu wa

nidhamu na bidii). Sulemani aliandikia kwamba ni

“mbweha wadogo waiharibuo mizabibu” (Wimbo Ulio Bora

2:15). Jumba la Sulemani lilijaa utajiri na nafasi, na watu

wengi waliokuwa tayari kufanya lolote ili wakae karibu na

yeye.

Je, unafikiri kwamba Mungu anafahamu uwezo wa

moyo wa binadamu kushawishika, hata na furaha

zisizoonekana kuwa mbaya - na halafu kuingia katika

ukosefu wa nidhamu na hatimaye kutotii? Nina hakika

Mungu anaufahamu. Akijua haya, alimwambia Sulemani kila

mara kwamba atii amri Zake zote (1Wafalme 6:12; 9:4).

Lakini Sulemani hakumsikiliza Bwana, hasa alipopata

“ufanisi” mkuu.

MATENDO • 37

Kumbuka Sulemani: vishawishi....vilimwangamiza

WITOWA

MUNGU

Vishawishi

Nakala 16 / Nambari 1

Page 38: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,hata utumishi wako unaweza kuwa kishawishi ukipatakukuvuta kuliko mambo yote - ukikuondoa katika mudawa kukaa pamoja na Mungu kwa sababu ya kuwa nashughuli nyingi mno, au msukumo wa mahitaji ya watuwengine. Yesu alipokuwa hapa duniani alitupa mfanokwa ajili ya haja ya kutumia muda wa kumsikiliza BabaYake na kuburudishwa kiroho (Marko 1:35-39; Luka5:16; 6:12).

Lazima tusisahau kamwe kwamba Bwana ndiyechanzo na chemchemi kwa upako wa Roho Wake nakwa ufahamu wetu wa Neno Lake (Yohana 1:33;6:63,68). Hutoka KWAKE! Utumishi wenye kuzaamatunda halisi ni matokeo ya yale tunayopokeamiguuni pa Yesu katika kusali, kumsubiri na kusomaNeno Lake (Luka 10:41-42; Yohana 15:16). Wengi katiyetu tunatambua ukweli huu rahisi wa kimsingi. Shidainatokea tunaposhindwa kutekeleza kila siku kanuni hiiya msingi kwa ajili ya maisha yajaayo uwezo nahuduma.

Tujilinde na aina za vishawishi vinavyotuchosha,au kutuelekeza katika kuridhiana na kutenda dhambi.Moyo wa Sulemani ulivutwa mbali na Mungu na yalealiyoyaruhusu katika maisha yake (1Wafalme 11:1-4,9).Uaminifu na utiifu wake kwa Mungu vilighushiwa namambo ya dunia, hadi alipoangamia mwenyewe nakuleta uharibifu kwa vyote ambavyo Mungu alikuwaamempa avitawale.

Maswali mema ya kujiuliza kuhusu matendoYOYOTE katika maisha yako ni haya: “Je, tendo hili aumsimamo huu hunileta karibu zaidi na Mungu namakusudi Yake kwa maisha yangu? Au je, hunipelekambali na Yeye?

b. Sifa ya wanadamu ni mtego uletao mauti.

Kufundisha au kuhubiri kwa ajili ya kusifiwa na wanadamu

ni mtego unaodanganya. Ni Mungu peke Yake awezaye

kutenda mambo yenye thamani ya milele (Zekaria 4:6).

Ndiyo, Mungu anataka kututumia kama vyombo

anavyoweza kutendea kazi. Lakini uweza na utukufu ni wa

Mungu peke Yake kwa ajili ya lolote linalotendeka kupitia

kwetu. Maana pasipo Yeye, sisi hatuwezi kufanya lolote

(Yohana 15:5).

Mungu amefunua katika Neno Lake kwamba hatampa

mwingine utukufu Wake (Isaya 42:8; 48:11). Ni lazima

tusitafute utukufu au sifa kutoka kwa watu kwa ajili ya kazi

ya huduma (Yohana 7:18).

Yesu aliwakosoa waandishi na Mafarisayo kwa ukali

kuliko wote. Aliwakemea kwa ajili ya kupenda sifa za

wanadamu na walijaa kiburi (Mathayo 23:5-12; Yohana

5:41-44). Ingawa walifahamu Maandiko na kujua njia za

Mungu, kiburi chao kiliwafanya wakatae kumkubali wala

kumwamini Yesu kama Masihi wao (Yohana 5:39-40).

Kufuata Nyayo ZakeYesu alipewa upako wa Roho Mtakatifu pasipo kipimo

(Yohana 3:34-35). Yeye alikuwa, tena ndiye, Mfalme wa

wafalme wote, na Bwana wa mabwana wote. Lakini, kwa

ajili yetu, alijifanya Mtumishi mnyenyekevu (Mathayo

20:28; Wafilipi 2:3-11).

Kwa kweli, sisi kama viongozi katika Mwili wa Kristo,

tufanye kama Paulo asemavyo: “Iweni na nia iyo hiyo ndaniyenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu...”(Wafilipi 2:5). Sisi hatukupewa Roho Mtakatifu pasipo

kipimo kama Yesu alivyopewa. Lakini tunaweza kuwa na

msaada Wake wote tunapoishi katika uhusiano wa utiifu

Kwake na kwa Roho Mtakatifu (2Petro 1:2-4).

Bila shaka, hata tukiwa na karama hizi, sisi si wakubwa

wala wema kumzidi Bwana wetu. Badala yake, tunatakiwa

tufanane na Yeye (Yohana 13:12-17), tukitumia yale

ambayo Mungu anatupatia katika kuwatumikia wengine.

Kwa hiyo, tusijione au kujisifu wakati Mungu anapotutumia

katika huduma. Tujilinde na kiburi - dhambi ya ibilisi

(1Timotheo 3:6).

Dhambi Ya Hatari Kuliko ZoteKiburi ni dhambi iletayo kifo ambayo inaweza kumwua

kwa sumu hata kiongozi aliyejitoa kabisa, na kuziba

mtiririko wa upako wa Roho Mtakatifu. Kiongozi wa kanisa

anaweza kuwa na ustadi, hekima au ujuzi mwingi. Lakini ni

upumbavu kujisifu kwa ajili ya mambo haya. Kwanza, kwa

sababu vyote tulivyo navyo vimetoka kwa Mungu. Pili, kwa

sababu hekima, ustadi na uwezo wetu wote si kitu kabisa

kulingana na upako wa Roho wa Mungu na pia kulingana na

yale ambayo Mungu anaweza kufanya Mwenyewe peke

Yake (Mathayo 7:21-23; 1Wakorintho 3:18-21; 4:20;

8:1-3)!

Huenda kiburi ni dhambi ya hatari kuliko zote. Ilikuwa

dhambi ya kimsingi ya Shetani (Isaya 14:12-14). Kiburi

kinaweza kutufanya tufikiri kwamba tunaweza kutenda

mambo fulani vizuri kuliko Mungu anavyoweza, na hatimaye

kitatuongoza mpaka tumwasi Mungu.

Tunapoanza kufanya mipango yetu binafsi mbali na

kumtii Mungu, tumekwisha kumwasi Yeye. Kama

hatukujitoa Kwake kikamilifu, tunatengwa na Yeye, maana

“Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemawanyenyekevu” (Yakobo 4:6).

Kiburi kinatufanya tujione kuwa tunaweza kujitunza na

kujitegemea. Kwa hiyo, hatuamini tena kwamba tunahitaji

kufundishwa wala na Mungu wala na mwanadamu. Tunazuia

hisia kwamba tunahitaji lolote kutoka kwa Mungu, na

tunaacha kumwomba; kwa hiyo tunaacha pia kupokea

(Yakobo 4:1-2). Imani yenye unyenyekevu kama ya mtoto

inahitajika ili kumwomba Baba yetu wa Mbinguni au

kujifunza kutoka Kwake (Mathayo 18:3-4).

Mungu ndiye anayetupatia mahitaji yetu yote. Lazima

tutambue kwa unyenyekevu kwamba tunamhitaji Yeye

pamoja na vile alivyotupatia, la sivyo hatutapokea lolote.

Kiburi kinatuzuia tusiwe na unyenyekevu kama huu, na kwa

hiyo inatunyang’anya baraka za Ufalme wa Mungu,

ukiwemo upako.

Mwamini Bwana Peke YakeFikiria mara moja sarafu. Upande mmoja imepigwa neno

“kiburi”. Upande wa pili imepigwa “kuogopa au hofu ya

binadamu”. Dhambi hizi mbili za kimwili hudhihirishwa

pamoja mara nyingi katika maisha ya mtu.

“Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Baliamtumainiye Bwana atakuwa salama” (Mithali 29:25).

“Kuogopa wanadamu” kuna sura nyingi. Njia za kawaida

zinazowatega wachungaji ni kama hizi:

38 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 39: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

• Hofu ya kuwachukiza au kuwakasirisha watu katika

kundi (mpaka kuachilia dhambi zao).

• Kuwapendekeza watu wanaotoa fedha au wenye uwezo

wa kushawishi.

• Kusema au kutenda mambo ili kupendwa na (au

kuonekana mwema kuliko) wachungaji wenzi au

waamini wengine.

Zipo njia nyingine nyingi za kunaswa na hofu ya

wanadamu. Lakini haidhuru ni kwa njia gani, unapokubali

kuwaogopa watu unanaswa katika kufanya mapenzi ya watuwengine. Unanaswa na maoni na maamuzi yao. Unawezaje

basi kumtumikia Bwana kwa moyo wote, ukiwa unahangaika

kutumikia maoni ya watu? Mtu yeyote hawezi kutumikia

mabwana wawili (Mathayo 6:24), wala hawezi kusimama

hali moyo umegawanyika (Zaburi 86:11; Marko 3:24-25).

Yesu pia alikabili tatizo hili, kutokana na tamaa za

kibinafsi za watu (Marko 1:35-39; Yohana 6:15,22-40);

hukumu ya Mafarisayo (Mathayo 22:15-22; Luka 7:36-50);

au hata matakwa ya familia Yake ya kibinadamu (Mathayo

12:46-50; Yohana 7:1-9).

Katika hoja hizi zote na nyingine, Yesu hakufuata maoni

ya watu. Badala yake Yesu alilenga kufanya mapenzi ya

Mungu kuliko yote, pasipo kujali kamwe gharama yake.

Hata watu walipomwamini Yesu na kuonekana kuwa

walimfuata, Yeye alijua kigeugeu cha mioyo ya wanadamu

(Yohana 2:23-25). Yesu aliwaonya wafuasi Wake

wasiwaamini wanadamu wala kutafuta sifa zao (Luka 6:26).

Maana kama ni heshima ya watu tunayotafuta, mioyo yetu

haitaelekea kumtumikia Bwana peke Yake.

Bwana anawatafuta watu walio waaminifu Kwake

kabisa na pekee katika mioyo yao. Yeye atafanya mambo

makuu kupitia watu kama hao (2Nyakati 16:9) na ndio

ambao atawamiminia upako Wake hasa!

Angalia ni nini itakayotulinda na hofu ya wanadamu: ni

kumtumaini Bwana (Mithali 29:25). Tunapomjua Bwana,

tukiwa tumemtafuta kwa ajili ya mapenzi Yake, tunapotenda

kwa kutii yale aliyosema kwa sababu tunamwamini Yeye

kabisa - haidhuru wanadamu wafikiri nini.

c. Maridhiano makubwa huanza na “mbweha

wadogo” wa maridhiano madogo (Wimbo Ulio Bora

2:15). Kuna tatizo la kawaida kati ya viongozi ambao Mungu

anawatumia katika kazi ya maana. Huanza kujiona kuwa

muhimu mpaka wasihitaji kutii amri na kanuni zote za

Mungu. Huenda wanazifahamu na kuweza kuzifundisha;

lakini hawaamini tena kwamba wao binafsi wanahitaji

kuziishia kwa kuzitii.

Hali hii nimeita “Kanuni ya Udhuru wa Kiongozi”.

Yaani viongozi wanaona kwamba wao ni muhimu sana

mpaka wasihitaji tena kuwa wanyenyekevu, wala kutumika,

wala kuwavumilia wengine, wala kujitoa, n.k. Katika akili

zao, wao wamepata kuwa na “udhuru” kwa ajili ya kanuni za

Mungu; wanaona kufuata njia zao za ubinafsi na mwili kuwa

na udhuru kwa sababu ya “umuhimu” au “ufanisi” wao.

Wanakubaliana na njia ya kuwaza ya kidunia, kwamba

ufanisi wao katika huduma umesababishwa na uwezo wao na

vipawa vyao vikuu - nao wanaanza kuishi kana kwamba wao

ni wasanii wakuu!

Kwa sababu Mungu ni mwaminifu katika kuendelea

kuhudumia wengine kupitia kwao (Warumi 11:29), viongozi

hao wanaanza kufanyia fidhuli wema wa Mungu. Polepole

wanaanza kuwa na misimamo na mienendo ambayo

hatimaye itawaingiza katika dhambi halisi. Hali hii

itasababisha kuanguka kwao katika huduma, mpaka hata

kuangamiza imani yao (1Timotheo 1:19) au kuchoma

dhamiri zao (1Timotheo 4:2).

Hali hiyo itasababisha pia kumhuzunisha (Waefeso 4:30)

na kumzimisha (1Wathesalonike 5:19) Roho Mtakatifu wa

Mungu. Na hatimaye itafunga kabisa mtiririko wa upako wa

Mungu.

Sisi kama viongozi wa kanisa, tumeitwa tuwe mfano wa

tabia ya Kristo kwa Mwili wa Kristo. Lazima tufahamu Neno

la Mungu na kuliishia, kwa uwezo wetu wote. Kama

tutashindwa, lazima tuwe wepesi wa kutubu (2Wakorintho

7:10; Ufunuo 3:19).

Kila mmoja wetu atie maanani maonyo ya Maandiko:

“dhambi yenu itawapata hapana budi” (Hesabu 32:23; taz.

pia Wagalatia 6:7-8; 1Timotheo 5:24-25).

Kulinda Moyo WakoBiblia inahimiza: “Linda moyo wako kuliko yote

uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”

(Mithali 4:23). Sulemani aliandika mstari huu, pengine baada

ya kuharibu uhusiano wake na Mungu na kuangamiza ufalme

wake. Hatujui kwa uhakika. Lakini ukweli wa yale ambayo

Sulemani aliandika kwa Roho wa Mungu bado unasema wazi

na sisi leo.

Ibilisi ana “panya” wengi ambao anapenda kutumia

katika kutujaribu. Mwili wetu pia una tamaa nyingi za

dhambi na zisizofaa. Lakini mambo haya yanaweza kuingia

na kuchafua kisima cha maisha yetu ikiwa tu tutayafungulia

mlango. Yanaweza kuozesha nyumba ya moyo wetu - makao

ya Roho Mtakatifu - ikiwa tu tutayaingiza na kupatia dhambi

nafasi.

Kwa hiyo tunaweza kufanya nini ili tulinde “kisima”

chetu katika usafi? Kwa kuwa sisi ni hekalu ya Roho

Mtakatifu (1Wakorintho 6:19-20) kuna hatua za kiutendaji

ambazo tunaweza kuzichukua. Tuziangalie sasa.

MATENDO • 39

Hata watu walipomwamini Yesu

na kuonekana kuwa

walimfuata, Yeye alijua

kigeugeu cha mioyo ya

wanadamu (Yohana 2:23-25).

Yesu aliwaonya wafuasi Wake

wasiwaamini wanadamu wala

kutafuta sifa zao (Luka 6:26).

Maana kama ni heshima ya

watu tunayotafuta, mioyo yetu

haitaelekea kumtumikia Bwana

peke Yake.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 40: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

2. Njia Ya Utakaso

a. Kuishi kwa kanuni za Neno la Mungu. Mtunga

Zaburi aliuliza swali la maana sana, na kulijibu. “Jinsi ganikijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”

(Zaburi 119:9).

Katika barua za Paulo kwa Timotheo na Tito, Roho

Mtakatifu ametoa maagizo ya wazi kwa wachungaji wote.

Barua hizi tatu “za Kiuchungaji” (1 & 2Timotheo na Tito)

ziliandikwa kwa wachungaji (Timotheo na Tito) kuhusu

mambo ya kiuchungaji.

Ni katika barua kwa Timotheo kwamba tunasoma kuwa

Neno la Mungu - na si maoni ya wanadamu - ni mwongozo

wetu kwa yote tunayofanya, kusema, kuwa na kufanyia

huduma (1Timotheo 4:12-16; 2Timotheo 2:15-18; 3:16-17).

Yesu anaongea kwamba Neno la Mungu ni kipimo chetu

cha maisha. Anasema kuwa kutokutenda yote yaliyomo

katika Neno la Mungu ni kushindwa kunakoleta hukumu

(Mathayo 5:17-20). Neno la Mungu lina upuzio wa Roho

Mtakatifu (2Timotheo 3:16; 2Petro 1:19-21) nalo

limethibitishwa na Roho Mtakatifu (Yohana 14:26;

Waebrania 4:12-13).

Maoni na mawazo ya wanadamu, hata kama yana

makusudi mema na yanapendeza, si mwongozo wa maisha

yetu. Pia si ambayo tunapaswa kufundisha washarika wetu

kuhusu maisha katika Ufalme wa Mungu. Lazima tuwe

waangalifu sana kuhusu maoni ya watu (1Wakorintho

2:1-16) - hata kama tunakubaliana nayo. Kwa sababu

wanadamu, hata wale tunaowaheshimu na kuwaamini,

ndivyo walivyo: wanadamu tu.Ni kweli kwamba watu fulani wanaweza kutusaidia.

Wanaweza kutufundisha yale waliyojifunza. Ujuzi wao

katika Neno la Mungu na ustadi wao huweza kutufaidi.

Lakini ni sehemu, inayosaidia pale tu inapokubaliana na

Neno la Mungu!

Haiwezekani maisha yetu kutakaswa kwa maoni ya watu

wala kwa mbinu mpya ya utumishi. Tunaweza kutembea kwa

haki mbele za Bwana wakati ule tu ambapo tunamfuata Yeye

na kutii Neno Lake.

Kuna Roho Mtakatifu mmoja na chanzo kimoja tu cha

Neno la Mungu la milele - yaani Biblia! Kwa hiyo usome

Biblia, kutafakari, kujifunza, kukariri, kutii, kuishia, kuhubiri

na kufundisha Biblia! Amina!

b. Roho Mtakatifu anatenda kazi katika sala na

maombi. “Pumzi [roho] ya mwanadamu ni taa ya Bwana;hupeleleza yote yaliyomo ndani yake” (Mithali 20:27).

Nyakati zetu za kusali ni chanzo cha baraka na mafunzo,

na mahali pa mawasiliano na Mungu. Pia sala inaweza

kuwa silaha yenye nguvu inapoongozwa na Roho

Mtakatifu.

Inasikitisha kwamba katika shughuli nyingi za maisha ya

kila siku, viongozi wa kanisa kama wewe na mimi mara

nyingi tunaacha nafasi zetu muhimu kabisa za kukaa na

Bwana. Lakini ni pale tu ambapo tunatoa nafasi ya kutulia na

kusikiliza ndipo Roho Mtakatifu anapoweza kweli kufanya

kazi ndani ya mioyo yetu.

Kila mmoja wetu anahitaji “kupimwa kwa moyo” kwa

utaratibu na uangalifu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Yeye

aweza kufunua nia na makusudi ya siri, sehemu zenye uchafu

au udhaifu. Katika upendo Wake kwetu na kwa Mwili wa

Kristo, Roho Mtakatifu anataka pia kututhibitishia na

kututengeneza, ili sisi tutunze kwa uangalifu mambo yale

ambayo vinginevyo yatazuia au hata kuharibu maisha na

huduma yetu.

Ulinzi Dhidi Ya KujidanganyaUkweli kwamba tunafanya bidii katika huduma,

kufahamu Biblia na kuweza kuwafundisha wengine,

haumaanishi kwamba sisi tumekamilika. Kinyume chake,

mambo haya yangetufanya tutambue zaidi uwezo wa moyo

wa binadamu kudanganywa na kutoa udhuru kwa ajili ya

dhambi!

Tafadhali tumia muda hata sasa wa kusoma mistari

ifuatayo:

• Mithali 16:2,25; 28:26

• Yeremia 17:9-10

• 1Wakorintho 10:12-13

Kuna mistari mingine mingi inayofunua wazi haja yetu

ya kufungua mioyo yetu mbele za Roho Mtakatifu. Bwana

amekwisha jua maeneo yetu ya mapambano, hatuwezi

kuyaficha Kwake. Lakini tunaweza kujidanganya wenyewe

na kuruhusu dhambi, tamaa za mwili au kuvunjika kutokana

na mwenendo wa dhambi viendelee mpaka vizae matunda ya

udhalimu katika maisha yetu.

Bwana anatafuta mioyo inayosafishiwa dhambi. Anataka

lisiwepo lolote la kuzuia upako Wake, wala ufanisi wa

maisha yetu na huduma zetu. Unapoonekana kuwa

mwaminifu katika kulinda moyo wako na dhambi na

kumruhusu Roho Mtakatifu akusafishe kwa ndani, upako wa

Mungu unaweza kumiminwa pasipo kizuio.

Mchungaji kwa Mchungaji: Zaidi tunapotembea pamoja naBwana, ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kutokutambua haja ya kaziya Roho Mtakatifu ya kutengeneza maisha yetu.

Inasikitisha kwamba kwa upande wa viongozi wa kanisa halihii ni kweli hasa. Tulivyo na shughuli nyingi za kujifunza nakufundisha Neno la Mungu, tunaanza kufikiri kwamba tunalitendeakazi pia katika maisha yetu ya kila siku. Tunavyokazana katikakuombea huduma yetu pamoja na wengine, hatutoi nafasi yakutosha katika kukaa tu na Bwana ili tusikie kutoka Kwake kwa ajiliyetu sisi wenyewe. Tunajifunza kuendelea kuchekelea na kutendakana kwamba yote ni sawasawa, hata kama tunapambana nadhambi na kuvunjika kwa ndani. Je, unaweza kukiri kwamba hii nihali yako mara kwa mara?

Yesu alitamka kwamba haki yetu lazima iwe haki ya moyo.Lazima izidi haki ya Mafarisayo iliyo ya nje na yenye mipaka(Mathayo 5:20).

Tafadhali kumbuka kwamba Yesu hakufia wanadamu iliaanzishe dini mpya. Alitoa uhai Wake ili sisi tuweze kurudishwa kwaMungu, na halafu kuendelea kubadilishwa zaidi na zaidi katikamfano ambao binadamu aliumbwa nao mwanzoni kabla dhambihaijatuharibu (Mathayo 15:10-20; 23:23-28; Warumi 12:1-2;2Wakorintho 3:18; 1Yohana 3:1-3). Tumekwisha jifunza kwambamabadiliko haya yanaendelea katika maisha yetu yote, hata kwetusisi viongozi.

Tukizembea hali ya ndani ya moyo wetu, huwa rahisi mnokunaswa na dhambi. Matatizo yanaweza kuanza yakiwa madogo,lakini maridhiano madogo sikuzote huendea yaliyo makubwa nayenye kuangamiza. Ndiyo sababu ni muhimu kabisa tumruhusuRoho Mtakatifu afanye kazi ndani ya mioyo yetu kila siku,akituthibitishia na kushinda matatizo kabla hayajatuingiza katikadhambi.

40 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 41: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

“Ee Mungu, Unichunguze!”Tunamhitaji sana Roho Mtakatifu awe taa inayomulika

ndani ya nafsi na roho zetu. Tunamhitaji afunue hali halisi ya

mioyo yetu, ili tutakaswe, kuhuishwa na kubadilishwa.

Ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu (Wafilipi

1:6; 2Wakorintho 3:18; Warumi 8:29)!

Tunaposhiriki katika kazi hii ya Roho kwa sala,

tutakuzwa tuwe “vyombo vya heshima” (2Timotheo

2:20-21). Ndipo Mungu anapoweza kumimina upako wa

Roho Wake Mtakatifu kwa wingi na uhuru, akiachia zaidi

Yake ndani yetu na kupitia kwetu kwa wengine katika

huduma.

Sala yetu ya kila siku iwe ile ya Daudi: “Ee Mungu,unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazoyangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu,Ukaniongoze katika njia ya milele” (Zaburi 139:23-24).

c. Tembea katika kutii. “Na sisi tu mashahidi wamambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Munguamewapa wote wamtiio” (Matendo 5:32).

Tumekwisha zungumzia nafasi ya Neno la Mungu na

kazi inayobadilisha ya Roho Mtakatifu katika maisha binafsi

ya mchungaji. Hizi ni funguo za lazima kwa ajili ya kuishi

maisha ya utakaso.

Lakini, zinaweza kutokufanya kazi katika maisha yetu -

kama tunakataa kutii.

Hatutii tunapokataa amri za Mungu au kutojali kufuata

yale ambayo Roho Mtakatifu ameyafunua mioyoni mwetu

(Yakobo 1:21-25). Sauli ni mfano dhahiri wa kuanguka kwa

namna hii (taz. 1Samweli 15:1-35). Daudi alijifunza vema

kutokana na kushindwa kwa Sauli, akaandika kuhusu kanuni

hii iliyo muhimu sana (taz. Zaburi 40:6-8).

Mara nyingi viongozi wa kanisa wapo tayari kutumika

na hata kujitoa kama dhabihu kwa ajili ya huduma. Hali hii si

mbaya. Lakini Mungu anataka zaidi ya dhabihu; anadai kutii

kwetu kwa unyenyekevu na hiari (1Samweli 15:22-23).

Tumekwisha jifunza umuhimu wa utiifu kwa Bwana na

Neno Lake katika mambo ya nia zetu za ndani, misimamo na

mienendo yetu ya kila siku. Lakini kazi ya Roho inahitaji pia

utiifu wetu katika mambo ya kazi ya Bwana - katika yale

tunayotenda, na katika jinsi tunavyoyatenda.

Kuwekwa Sawa Katika KutiiMusa alijifunza jambo gumu kabisa kuhusu kutii

mwongozo wa Mungu (Hesabu 20:7-13). Musa aliamriwa na

Mungu “Ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe majiyake” (ms. 8). Lakini badala yake, Musa alipiga mwamba ule

(ms. 11). Matokeo yake yalikuwa kwamba Musa

hakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi (ms. 12; taz. pia

Kumbukumbu 31:1-2; 32:48-52). Kwa nini Musa asitii amri

hii ya wazi ya Bwana? Wana wa Israeli walikuwa tayari

wamekabiliana na ukame na kiu jangwani mara mbili kabla

ya hapo (Kutoka 15:22-26; 17:1-7). Mara ya kwanza, Mungu

alimwongoza Musa atupe mti fulani katika maji yaliyokuwa

machungu hadi yasinyweke, na maji yale yalipata kuwa

matamu. Mara ya pili, Mungu alikuwa amemwambia Musa

apige mwamba fulani, na maji matamu yalitoka.

Lakini mara hii ya tatu, Mungu alimwambia Musa

afanye tendo jingine. Alimwambia aambie mwamba. Lakini

badala yake, Musa alirudia mtindo wa awali, akaupiga

mwamba. Labda Musa hakuwa wazi kwa njia hii mpya

mbayo Mungu alitaka kutendea kazi. Labda Musa alikuwa

amewakasirikia wana wa Israeli wenye kunung’unika.

Hatujui kwa uhakika. Lakini tunayojua ni hii: Kule kutotii

kwa Musa kulimwudhi Bwana (Hesabu 20:12).

Jambo muhimu la kujifunza hapa ni hili: tokeo katika

hali ile halikuwa muhimu kama mtindo! Wana wa Israeli

walipata maji waliyotamani. Lakini kipimo cha Mungu kwa

ajili ya utiifu hakikuwa katika tokeo; kilikuwa kwamba

mtumishi wake atii na kufuata kikamilifu njia ya Mungu

ya kutimiza kusudi Lake. Ndiyo maana hasa ya utiifu!

Tunatakiwa tufuate Neno la Mungu na mwongozo wa

Roho Mtakatifu, hata kama hatuoni sababu kwa akili zetu

zenye mipaka (taz. Isaya 55:8-9; 1Wakorintho 1:18-25).

Mungu ametupa Roho Wake Mtakatifu atuongoze. Sisi kama

watoto wa Mungu, tumeitwa tumwamini na kumtii (Warumi

8:14).

Tafadhali ufahamu kwamba kutii si jambo la kustahili

baraka ya Mungu wala upako Wake. Lakini tunapotembea

katika kutii, tunajiweka sawa na Bwana na kanuni za Neno

Lake. Tunapofanya hivyo, tuko tayari kupokea zaidi katika

uwezo wa upako wa Mungu.

Paulo alifafanua kanuni hii: “Bali nautesa mwili wanguna kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wenginemwenyewe niwe mtu wa kukataliwa” (1Wakorintho 9:27).

Paulo alitambua kabisa kwamba mwenendo wake binafsi

ulihusiana moja kwa moja na huduma ambayo Mungu

alikuwa amempatia.

Vipimo Vya Agano JipyaKila mchungaji ana sehemu mbili katika maisha yake:

maisha yake binafsi na maisha yake ya huduma mbele ya

watu. Matazamio ya Mungu kwa ajili ya utiifu yanahusiana

na sehemu zote mbili. Ni lazima maisha binafsi na maisha ya

kazi ya mchungaji yawe chini ya marudi na maendeleo ya

Roho Mtakatifu na Neno la Mungu.

Kama kiongozi wa kanisa amejitoa kwa utiifu katika

maeneo yote ya maisha yake, upako wa Roho Mtakatifu

utatiririka katika maeneo yote pia.

Ni kosa kuamini kwamba upako ni kwa ajili ya huduma

yetu mbele ya watu tu. Bwana anajali ufanisi wako vile vile

katika maisha ya familia yako na nafsi yako, pamoja na jinsi

anavyoweza pengine akutumie katika kazi ya kawaida au

nafasi yoyote nyingine.

Masharti ya Agano Jipya kwa ajili ya viongozi wa kanisa

(soma 1Timotheo 3:1-7) ni vipimo vyetu pia kama

wachungaji. Wazee wa Kanisa la awali ndio waliokuwawachungaji wa makanisa ya kila mahali. Kwa hiyo,

mwongozo na vipimo kwa ajili ya maisha yao binafsi na

katika huduma ndivyo vinavyofaa wachungaji leo.

Utaratibu Wa Ki-BibliaWachungaji wengi mno hawajali vipimo hivi, hasa jinsi

vinavyohusiana na mahitaji ya wake na watoto wao.

Wanafikiri ni aina ya utauwa kutowajali familia zao ili

wajitoe katika huduma wakati wote. Neno la Mungu

limethibitisha wazi kwamba SIVYO Mungu alivyowaagiza

wachungaji!

Mume (akiwemo mchungaji) ameagizwa ampende mke

wake kama Kristo anavyopenda Kanisa, kwa ukarimu na

utoaji kifedha. Mchungaji na mke wake hupaswa

MATENDO • 41Nakala 16 / Nambari 1

Page 42: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

kuheshimiana na kupendana, wakiombeana na kuhudumiana.

Watoto wasidekezwe, wala kutendewa kama watumishi. Bali

walelewe, kuthaminiwa, kuelimishwa katika utaratibu wa

ki-Mungu na wa upendo. Sisi tuwe mifano kwa watoto wetu

ya tabia ya Kristo na ya Baba yao wa mbinguni

anayewapenda. (Taz. Waefeso 5:22-33; 6:1-4; Wakolosai

3:18-21; 1Petro 3:7.)

Familia zetu zipewe kipaumbele, na kuwatunza ni

wajibu ambao hatuwezi kuacha: “Lakini mtu ye yoteasiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwakehasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”(1Timotheo 5:8). Utaratibu wa ki-Biblia ni: kwanza -

uhusiano wetu na Mungu; pili - familia yetu; tatu - huduma

na wajibu nyingine baada ya hayo mawili ya kwanza.

Uwakili wa mchungaji kwa upande wa fedha pia

uongozwe na kanuni za Neno la Mungu na Roho Mtakatifu.

Malipo ambayo mchungaji anapokea binafsi yatumiwe katika:

• kumbariki Bwana katika zaka na sadaka;

• kubariki familia yetu kwa kuwatunza;

• kuwabariki wengine tunapowagawia katika yale ambayo

Mungu ametupatia.

Msaada Wote TunaohitajiHuduma ya mchungaji itekelezwe pia katika kutii Neno

la Mungu na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Roho

Mtakatifu atatusaidia na mara nyingi kutuongoza kuhusu yale

ambayo Yeye anapenda tufanye katika hali halisi za huduma

yetu.

Tunapojitoa na kujiadilisha, kusikiliza ushauri wa

ki-Mungu, kujifunza Neno la Mungu, kusali kila mara

pamoja na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, tutakua

na kupevuka kama viongozi wa ki-Kristo. Tunapofanya

hivyo, tunaweza kutazamia ongezeko la kutiririka kwa upako

wa Mungu juu ya maisha yetu na kupitia huduma yetu

(tazama hamasa za Paulo kwa Timotheo: 1Timotheo 4:12-16;

6:11-12,20; 2Timotheo 1:6-7,13-14; 2:1,15-16,22-25; 4:1-5).

Ndiyo hamu ya Mungu kwa ajili yetu! Anatupatia msaada

wote tunaohitaji ili tumtumikie kwa uaminifu, na kuishi

kufuatana na njia Zake. Lakini ni lazima tuchague kutii!

Mchungaji kwa Mchungaji: Kama mchungaji aukiongozi wa kanisa anavunja au kuendelea kudharaukanuni hizi za msingi kuhusu maisha yake binafsi na yahuduma, upako wa Mungu utazimishwa. Kutakuwa naukosefu wa matunda nyumbani mwake na katikahuduma yake.

Pasipo toba halisi na kujitoa kwa upya na kweli kwamakusudi ya Mungu, kiongozi yumo katika hatari yakuangamia binafsi na katika huduma. Uangamizi huuunaweza kutumia muda, lakini tuwe na hakika kwambasisi sote tunavuna yale tuliyopanda (Wagalatia 6:7-8).

Inasikitisha kwamba wapo viongozi katika Kanisaleo wenye karama na upako wenye nguvu, ambaowanaanza kuishi maisha ya unafiki. Kwa manenomengine, wanafundisha jambo fulani, lakini wameanzakuishia njia nyingine.

Sisi sote tutashindwa mara kwa mara, na hakunahata mmoja wetu aliye mkamilifu pasipo dhambi. Lakinisiongei kuhusu kuanguka kwa mara moja, na baadayake kutubu haraka. Bali ninaongea kuhusu kuvunjakwa mfululizo na makusudi kanuni za Neno la Mungukatika maisha binafsi ya kiongozi.

Mungu Baba yetu na jina la Yesu Kristohutahayarishwa katika haya. Unafiki huu unawafukuzawatu wa dunia mbali na wokovu katika Kristo. Waliondani ya Kanisa pamoja na familia zetu pia huchukizwana mambo ya Mungu kwa sababu ya ukosefu huu waunyofu katika maisha binafsi ya viongozi wa kanisa.

Hali hii ni uovu, na ikiwa mwenendo wakounamsababishia mwingine ajikwae, Yesu ameonyakuhusu hukumu ya hakika (Luka 17:1-2). Hukumu yaMungu juu ya kazi zetu ni ya uhakika (1Wakorintho3:11-15).

Bwana Wa Maisha Yetu YoteRoho Mtakatifu anakaa ndani yetu sisi kama waamini;

anatutia mafuta ya upako ili makusudi ya Mungu yatendeke.

Yeye anataka kujaza maisha yetu kikamilifu, si kwa upande

wa huduma tu. Yesu awe Bwana wa maisha yetu yote - wa

moyo wetu wote, si sehemu tu (1Petro 3:15). Lazima tumtii

Bwana na Neno Lake katika maeneo yote ya maisha yetu, ili

Yeye apokee utukufu nasi tuwe zana zenye ufanisi kwa ajili

ya makusudi Yake!

d. Tunahitaji mahusiano ya kimwenzi. Wachungaji na

viongozi mara nyingi hawataki kufunua mambo ya ndani ya

maisha yao. Hofu yao inaweza kuamsha wivu au mashindano

kati yao. Shetani anatumia madhaifu haya katika kugawanya

Mwili wa Kristo, na hasa kuwafanya viongozi watengane na

kuogopana.

Sehemu kubwa ya ufanisi wetu kama viongozi wa kanisa

itapotea pasipokuwa na mahusiano yenye afya kati yetu na

viongozi wengine. Tunategemeana, huenda zaidi kuliko

tunavyotambua au kutaka kukiri. Waamini, wakiwemo

wachungaji, ni familia (ndugu na dada). Uhusiano huu ni

muhimu zaidi kabisa kuliko vyeo, nafasi, uanachama katika

dhehebu au ukubwa/udogo wa kanisa lako.

Karama na nafasi mbalimbali katika Mwili wa Kristo

hutolewa ili tufanye kazi pamoja kwa ufanisi (Warumi 12:3-8;

1Wakorintho sura ya 12). Hakuna yeyote kati yetu aliye na yote

yanayohitajika ili awe na ufanisi katika huduma pasipo

ushirikiano pamoja na waamini na viongozi wengine. Lakini aina

hii ya umoja inahitaji upevu, upendo, utumishi na unyenyekevu.

KuegemezanaWachungaji hasa wanahitaji kuegemezana. Lazima tutoe

nafasi ya mahusiano na kuyasitawisha pamoja na wachungaji

na viongozi wengine wachaji. Kusudi la msingi la kufanya

hivyo ni kudirikiana. Lazima tufanye hivyo kwa ajili ya

kulinda afya yetu ya kiroho tusipate kushindwa.

Mahusiano kama haya yawe na uwazi halisi, nafasi ya

kushirikishana hamasa zetu, matatizo yetu na ushindi wetu

katika maisha na huduma. Katika kundi hili la urafiki na

uhusiano, sisi tunaweza kuhudumiwa wenyewe, tukiombewa

na kupokea ushauri wa ki-Biblia.

Mungu anakusudia aina hii ya uhusiano kwa ajili ya

kukua na kupevuka kwetu: “Chuma hunoa chuma; ndivyomtu aunoavyo uso wa rafiki yake” (Mithali 27:17).

Mahusiano haya ya kuaminiana yanatupatia nafasi yenye

usalama pa kushirikishana hofu zetu, mahangaiko yetu, na

majaribu na vishawishi vyetu. Tunaweza kuungama makosa

yetu na dhambi zetu (Yakobo 5:16) na kupokea huduma

pamoja na kutiwa moyo.

42 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 43: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Kila mtu katika utumishi anahitaji kutiwa moyo. Ibilisi

anakazana kuwashawishi viongozi waanguke katika

kushindwa binafsi au kuacha utumishi. Mara nyingine watu -

hata katika sharika zetu - wanatufahamu vibaya, kutupinga,

au hata kutudhulumu. Tunahitaji kuegemezwa na marafiki

waaminifu wenye nguvu ya kiroho watusaidie kupitia nyakati

kama hizi, ili tutoke kama washindi katika Kristo!

Mchungaji kwa Mchungaji: Usiamini uwongokwamba ni “kiroho” zaidi kutohitaji watu wengine katikamaisha yako. Bali, zaidi tunavyopevuka ndivyotutakavyotambua zaidi haja yetu ya mahusianomatakatifu katika Mwili wa Kristo. Paulo anatuambiakwamba sisi kwa pamoja ndio hekalu la Mungu, naRoho Mtakatifu anakaa ndani yetu (1Wakorintho3:16-17).

Vikundi hivi vya urafiki vya kushirikiana viteuliwekwa maombi na kwa uangalifu. Si kila mtuunayemfahamu atakayefaa kwa ajili ya kushirikianakatika maombi, tena si kila mtu atakayekuwa na upevuwa kutosha ili aaminike. Utafute wale unaowaheshimuna kuwaamini - wenye upevu, hekima na uwazi kwaRoho Mtakatifu, waweze kutamka ukweli kwa unyofuna upendo.

Lengo kuu la muda wa kukutana liwe maombi. Piavikundi hivi viwe na watu wa jinsia moja - wanaumekwa wanaume, wanawake kwa wanawake.

Mahusiano haya “yatatunoa” na kutuimarishakatika kukua, kutakaswa na kupokea upako mwingizaidi!

3. Alama Saba Za Upako Halisi

Mara nyingi watu wanachanganywa kuhusu asili ya

upako na kusudi lake kutokana na kukutana nao mara moja

au kwa muda mfupi katika tukio fulani. Huenda ni mahubiri

yenye nguvu, sala yenye msisimko, au kuwepo kwa ishara na

miujiza katika mkutano.

Maoni ya muda mfupi kama haya yanaweza kusababisha

kutoelewa kwa njia mbili. Kwanza, ni rahisi kuelewa upako

vibaya kama msisimko, kipawa, karama, mtindo au mbinu

katika utumishi. Pili, tunaweza kufikiri kwamba dakika ya

kilele ya mafunuo yasiyo ya kiasili ndilo kusudi lenyewe la

upako.

Ingawa matukio haya ya kimwujiza au msisimko

yanaweza kweli kuwa matokeo ya upako wa Roho Mtakatifu,

lazima tukumbuke kuwa upako ni zaidi ya hayo.

Ni muhimu tuendeleze maoni ya muda mrefu juu ya

upako. Huu ni ufahamu kwamba upako halisi utasababisha

maisha ya watu yaliyogeuzwa (Warumi 12:1-2).

Maana yangu ya maisha yaliyogeuzwa ni maisha yenye

msingi imara katika Neno la Mungu na sala. Watu wanaoishi

maisha yaliyogeuzwa wanafikia ulimwengu uliowazunguka

kwa ushuhuda na huduma ya upendo. Wanapinga dhambi na

matendo ya mwili, wakitembea kwa unyenyekevu na toba.

Wana utendaji katika Mwili wa Kristo; baada ya kutambua

vipawa vyao vya kiroho, wanavitumia katika huduma.

Wanazidi kufanana na Kristo wakati wote!

Mambo haya yawe ya kweli katika kiongozi aliyegeuzwa,pamoja na wale ambao kiongozi wa kanisa aliye na upako

anawahudumia.

Huduma yenye upako wa kweli itakuwa na matunda, na

matokeo yake yataendelea katika maisha ya watu

waliookolewa na kufunzwa ili wawe wafuasi wa Kristo.

Huduma yenye upako si njia ya kupata heshima, utajiri

au starehe. Mtume Paulo alikuwa na upako wa hali ya juu

kabisa, na kutumiwa sana na Mungu. Lakini aliteswa kupita

kiasi, alikuwa maskini, kufukuzwa, kutiwa gerezani mara

kwa mara, na hata kudharauliwa na kanisa ambalo alijaribu

kulitumikia (2Wakorintho 4:8-15; 7:2-6; 11:23-33). Mwisho

wa maisha ya Paulo ulikuwa kukatwa kichwa na shoka ya

mwuaji wa serikali pale Roma.

Lakini muda mfupi kabla ya kifo chake, Paulo alitamka

kwamba thawabu yake yote ilikuwa “taji ya haki, ambayoBwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala simimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwakwake” (2Timotheo 4:8).

Maisha ya Paulo haikuwa ya maana kufuatana na vipimo

vya dunia vya “ufanisi”. Pengine hata Wakristo fulani leo

wasingeona kuwa Paulo alikuwa mtume mwenye ufanisi.

Lakini sifa ya Paulo ilikuwa kwamba alitangaza Injili ya

Yesu Kristo kwa ujasiri (Matendo 17:1-6). Alijulikana kuwa

mtu mwenye mamlaka na uwezo, hata katika ufalme wa

mapepo (Matendo 19:15). Aliwafundisha na kuwafunza watu

wengine, na kuanzisha makanisa. Paulo akiwa na upuzio wa

Roho Mtakatifu aliandika sehemu ya theluthi moja ya Agano

Jipya letu (hasa wakati alipokuwa gerezani kwa ajili ya imani

yake). Na mtume Paulo alikuwa mtendaji mkuu wa kueneza

Injili katika ulimwengu wote uliojulikana wakati ule. Paulo

alikuwa kweli amepokea upako wa Mungu, akijaa uweza wa

Roho Mtakatifu (Wakolosai 1:24-29)!

Ni lazima tuelewe kikamilifu kusudi la upako wa

Mungu. Hatupewi upako wa Mungu kwa ajili ya manufaa

yetu wala kwa kuwapendeza watu wengine. Ni kwa ajili ya

kutimiza makusudi ya Mungu! Ni ya kutoa huduma kwa njia

inayogeuza maisha ya watu kwa Neno na uweza wa Mungu!

KujipimaNi lazima tutumie upambanuzi siku hizi, ili tutambue

nini ni ya Mungu na nini ni ya binadamu. Lazima

tupambanue yaliyotoka kwa Roho wa Mungu, na yaliotoka

kwa roho mwingine (2Wakorintho 11:4). Biblia hutuambia

kwamba, wakati unapoendelea, ufalme wa mapepo utazidi

kujaribu kuwapotosha watu. Hata Wakristo watadanganyika

na kupotoshwa, wakikataa mambo ya kweli yaliyotoka kwa

Mungu (2Timotheo 3:1-9; 4:3-4).

Ni lazima “kujaribu roho” (1Yohana 4:1-6), kwa sababu

ibilisi hufanya kazi kwa bidii akijaribu kuwadanganya watu

na kuwaangamiza (2Wakorintho 2:11; 10:1-5; 11:14; 1Petro

5:8). Pia, watu waovu watajaribu kumtumia Mungu na

mambo ya kiroho kwa kujifanikisha wenyewe (2Wakorintho

11:13-15; Wafilipi 1:15-16; 2Petro sura ya 2).

Tunawezaje basi kufahamu upako halisi wa Roho

Mtakatifu?

Na tunaweza kutumia vipimo gani katika kujipima

wenyewe ili kuhakikisha kwamba tunatembea kwa uaminifu

na utii kwa Kristo kwa ajili ya upako?

Hizi ni alama saba zitakazodhihirika kuhusu upako wa

Roho Mtakatifu.

Upako halisi wa Roho Mtakatifu:

1) utamtukuza Yesu Kristo wakati wote (Yohana 16:14),

si hasa kuwatukuza watu wala hata huduma yenyewe;

2) utafuatana na kulingana na mashauri yote ya msingi

MATENDO • 43Nakala 16 / Nambari 1

Page 44: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

ya Neno la Mungu (Yohana 14:26), kwa sababu Roho

Mtakatifu kamwe hatakwenda kinyume cha Neno la Mungu

lililoandikwa;

3) utasababisha uhai wa kiroho katika wale wanaokutana

na huduma au kuipokea (Yohana 6:63) - watu watajitoa kwa

Yesu, Neno Lake na njia Zake kwa ukamilifu zaidi;

4) utawaelekeza watu kwa Yesu na wokovu Wake, si kwa

mtu mwingine wala kwa ishara na maajabu tu (Yohana

15:26);

5) utajaribu kuendeleza amani na umoja katika Mwili wa

Kristo (1Wakorintho 12:1-14) kati ya watu wanaompenda

Bwana na Kanisa Lake kuliko msimamo wao;

6) utakuwa na uwezo unaogeuza maisha (1Wakorintho

2:4-5; 4:20; 1Wathesalonike 1:5), ambao ni matunda ya

huduma yenye upako;

7) utazalisha tabia ya Kristo ndani ya watu (Wagalatia

5:16-24; 2Wakorintho 3:18) - ndiyo mapenzi ya Mungu kwa

ajili ya kila mfuasi wa Kristo!

Kuwepo kwa alama hizi saba za upako halisi kutakuwa

uthibitisho wa watu wanaotoa huduma katika upako wa Roho

Mtakatifu. Alama hizi pia zinatusaidia tuone haja ya kuwa na

maono ya muda mrefu ya upako.

Upako wa mara moja unaweza uwepo kwa dakika fulani

ya huduma. Lakini sisi kama wachungaji wa Mwili wa

Kristo, tumepewa upako ili tufanye watu wawe wanafunzi nakuwaandaa watu wa Mungu - kazi ya muda mrefu – si tu

kwa ajili ya dakika za huduma yenye msisimko za mara kwa

mara.

Utumie orodha ya hapo juu katika kuchunguza huduma

yako. Kama kiongozi wa kanisa, una wito wenye thamani na

umuhimu wa kuchunga watu wa Mwili wa Kristo. Kristo ndiye

Mchungaji wetu Mkuu. Yeye amekuita uwe mchungaji

msaidizi. Utawajibika kumtolea Yeye ripoti ya jinsi

ulivyotimiza agizo Lake la kuwachunga kondoo Zake (1Petro

5:1-4).

Je, Tunaweza Kupokea Zaidi?Nafasi yetu ni ya kumfuata Kristo kwa bidii na uaminifu.

Lazima tutumie vipimo na kanuni ya Neno la Mungu katika

maisha yetu, na kukua kila wakati katika uwezo wetu wa

kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Wito wa huduma uliopewa na Mungu si huduma yako.

Ni huduma YAKE ambayo Yeye anataka kutenda kupitia

kwako! Huduma inayotendeka kwa kufuata njia ya Mungu

itazaa matunda mengi (Yohana 15:14-16) nao utafuatana na

upako Wake.

Tumethibitisha kwamba upako wa Roho Mtakatifu

umeandaliwa na Mungu aliye mfalme. Hufuatana na wito

wetu na vipawa vyetu. Upako huu hautii mapenzi ya

mwanadamu, isipokuwa tu kwamba tunaweza kuupokea au

kuukataa.Kama wewe unafanana na mimi, unataka zaidi ya upako

wa Mungu katika maisha na huduma yako. Kilio cha moyo

wako ni kuwa chombo kifaacho kwa kutimiza makusudi ya

Ufalme wa Mungu.

Kwa hiyo je, inawezekana siyo tu kupokea upako wa

Mungu, bali pia kukua katika upako ambao Mungu

anatupatia?

Je, tunaweza kupokea zaidi kuliko tunaopokea sasa?

Tuangalie maswali haya kwa kifupi.

B. KUKUA KATIKA UPAKO

Bwana anataka upokee upako wa Roho Mtakatifu.

Anataka pia ukue katika uwezo wako wa kuishi na kutoa

huduma katika upako wa Roho Mtakatifu.

Hakuna njia za mkato za kukua katika upako wa Mungu.

Wala upako si wetu wa kukamata na kutumia ili tuwe na

nguvu katika huduma kwa ufanisi wetu. Kumbuka kwamba

uweza wa Mungu hautengani na nafsi Yake. Upako ndiouwepo wa Roho Mtakatifu - nao daima utakuwa chini ya

mapenzi na makusudi ya Mungu, si yetu.

1. Tabia Na Upako

Ni muhimu kutambua kwamba jinsi unavyokua katika

tabia ya Kristo, ndivyo utakavyokua katika upako. Tabia yetu

ama italingana na upako na kuufungua, ama itaziba na kuzuia

kazi ya Roho Mtakatifu kupitia kwetu (taz. Waefeso 4:30;

1Wathesalonike 5:19).

Kumbuka kwamba sisi kwanza na hasa ni wana wa

Mungu wa kiume na kike. Kazi ya dhabihu ya Kristo

ilituwezesha turejeshwe katika uhusiano pamoja na Baba

yetu wa Mbinguni.

Yesu Kristo, kama Kichwa cha Kanisa (Wakolosai 1:18;

2:19) ametuita na kutupatia karama za kiroho - ili sisi, kama

wana wa Mungu, tuweze kutumikia Mwili wa Kristo

(Waefeso 4:11-16; 2Timotheo 1:9). Karama na wito hizi za

kiroho zitafanya kazi kikamilifu na kwa usahihi pale tu

ambapo zimetiwa nguvu na kuongozwa na Roho Mtakatifu

(1Wakorintho 12:7 - karama zote zinafanya kazi kufuatana na

kanuni hii).

Ndiyo sababu tunaweza kusema kwamba huduma yoteyenye upako wa kweli inatokana na uhusiano. Uhusiano wetu

na Kristo wa kujitolea na kukua ndio msingi ambamo

huduma inayogeuza maisha hutenda kazi.

Haidhuru kiwango chako cha upevu au ujuzi kwa

Bwana, hali hii ni ya kweli. Usisahau kamwe kwamba

huduma yenye ufanisi hutokana na kuendeleza uhusiano hai

unaozidi kuwa wa ndani pamoja na Yesu Kristo!

44 • MATENDO

Hakuna njia za mkato za kukua

katika upako wa Mungu. Wala

upako si wetu wa kukamata na

kutumia ili tuwe na nguvu katika

huduma kwa ufanisi wetu.

Kumbuka kwamba uweza wa

Mungu hautengani na nafsi Yake.

Upako ndio uwepo wa Roho

Mtakatifu nao daima utakuwa

chini ya mapenzi na makusudi ya

Mungu, si yetu.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 45: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mchungaji kwa Mchungaji: Ni rahisi mno katikahuduma kuzembea uhusiano wetu na Bwana. Huendatunaanza kufikiri kwamba “mana” ya jana kutokaKwake inatosha kwa ajili ya leo. Haitoshi!

Yesu ametoa maonyo makali yanayodhihirishatatizo hili. Soma Mathayo 7:21-23. Watu wanaoelezwahapa ni watu walio ndani ya Kanisa - watu wenyehuduma za unabii, wanaotoa mapepo, wanaotoahuduma katika ishara na maajabu, n.k.

Lakini viongozi hao kwa wakati fulani njiani,wameacha “upendo wa kwanza” (Ufunuo 2:1-5).Wamedanganyika, wakifikiri kwamba kuendeleza suraya ufanisi katika huduma (kuonekana kwa nje)kunatosha. Huenda wanaweza kukariri mistari yaMaandiko na kutumia mamlaka ya jina la Yesu. Lakinihawatembei katika uhusiano wa ukweli, utiifu na uhaipamoja na Bwana. Hawamjui, wala Yeye hawajui wao.Hatima yao ni ya kutisha (Mathayo 7:23).

Mkakati Wa ShetaniKama tulivyojifunza, kazi moja ya Roho katika maisha

yetu baada ya kuokolewa ni kubadilishwa kwetu binafsi

(Warumi 8:29; 2Wakorintho 3:18). Ni kushirikiana kwetu

katika maisha yetu yote - pamoja na kutii kwetu kila siku kwa

Neno la Mungu, na kuwa na muda wa kukaa pamoja na Yeye

- kunakositawisha tabia ya uchaji ndani yetu.

Shetani anapinga kwa bidii kukua kwa tabia ya uchaji

katika viongozi wa kanisa. Ibilisi hawezi kupotosha au

kutuibia upako wa Roho Mtakatifu wala karama Zake.

Ukweli ni kinyume chake: “Kwa kusudi hili Mwana waMungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi” (1Yohana

3:8), taz. pia Luka 10:17-20; Warumi 8:37-39; 2Wakorintho

10:3-5; Wakolosai 2:14-15; Waebrania 2:14).

Kwa sababu ibilisi hana uwezo wa kudhuru wala

kupotosha upako wa Roho Mtakatifu na karama Zake, lengo

lake kuu ni wewe! Shetani anajaribu kwa bidii

kuwanyang’anya, kuwaua na kuwaangamiza watakatifu

(Yohana 10:10). Njia yake moja ya kufanya hivyo ni kujaribu

kubomoa tabia ya uchaji, hasa katika viongozi wa kanisa.

Ibilisi anajaribu kupotosha viongozi wa kanisa wasifae

kwa ajili ya makusudi ya Mungu (1Wakorintho 9:24-27;

2Timotheo 2:19-22). Anafanya hivyo kwa njia ya vishawishi,

kudanganya, kutisha, kuogofya, kugawanya, kiburi, ubinafsi

- dhambi yoyote ile, Shetani atakuwa chanzo chake!

Kwa kawaida majaribu ya Shetani huanza katika mambo

madogo. Anaanza kuvuta tamaa zetu za kimwili na asili yetu

ya ubinafsi. Ibilisi amekuwa na karne nyingi za kuchunguza

mienendo ya wanadamu, na kutengeneza njia za kujaribu

kutuangusha. Hatuhitaji kumwogopa - lakini kwa hakika

tunahitaji kuwa waangalifu na kujilinda wakati wote (1Petro

5:8-9)!

Uangalie kwamba tunakuwa wazi zaidi kwa hila za

ibilisi tunapozembea uhusiano wetu unaoendelea na kukua

pamoja na Yesu Kristo (1Timotheo 4:1-2; 2Timotheo 1:1-9;

Waebrania 2:1-3). Pasipo ukaribu na Kristo, tutajaribiwa

zaidi sana kujipatia udhuru, kusingizia maanguko ya

mwenendo, kukubali mawazo ya tamaa - mambo ambayo

yatatuongoza katika dhambi, udanganyifu na kushindwa

(Yakobo 1:13-15).

Mungu anataka upako Wake upenyee tabia yetu. Tabia

ya uchaji (au ukosefu wake) huhusiana moja kwa moja na

uzalishaji na ufanisi wetu katika huduma. Mungu anataka

upako Wake utiririke na kutokea ndani ya maisha yetu,

pasipo kizuizi cha ukosefu wa uchaji. Si ‘kutia chumvi’

kusema kwamba upako unahusiana na tabia (yetu) sawasawa

na uweza (wa Mungu).

Tutumie muda kidogo sasa kujifunza kutoka katika mtu

aliyekuwa na upako kuliko mwingine yeyote aliyewahi

kuishi.

2. Nyayo Za Bwana

Kwa kweli Yesu Kristo alikuwa mtu aliyekuwa na upako

kuliko mwingine yeyote aliyetembea hapa duniani. Yeye

alikuwa na Roho Mtakatifu pasipo kipimo (Yohana 3:33-35).

Upako Wake usio na kifani ulitabiriwa karne nyingi kabla ya

kuzaliwa Kwake (Isaya 61:1-3). Yesu alithibitisha unabii huu

mwanzoni mwa huduma Yake (Luka 4:17-20).

Huduma ya Yesu duniani ilithibitisha kwamba Yeye

alikuwa kweli Mwenye Upako HASA. Tukiangalia Injili ya

Luka sura ya 4 na 5, tunaona mara moja uweza Wake mkuu

tangu mwanzo wa huduma Yake. Yesu alitiwa mafuta ili:

• Atoe mapepo (4:33-37,41);

• Afundishe kwa mamlaka (4:22,32);

• Aponye wagonjwa (4:38-40; 5:15);

• Awaite watu watubu (5:17-26,31-32);

• Atende ishara na maajabu (5:4-9);

• Awaite watu katika huduma kinabii (5:10,27);

• Aanzishe kundi la uongozi (5:11);

• Amponye mtu mwenye ukoma, tendo la ajabu wakati ule

(5:12-15).

Hii ni mifano tu kati ya mengine, jinsi Yesu alivyoanzahuduma Yake hapa duniani. Alifanya zaidi nyingi sanakuliko haya. Kuna Mwana wa Mungu mmoja tu aliyekuja

duniani, aliyekufa kwa ajili yetu, na halafu aliyefufuka ili

athibitishe kwamba Yeye alikuwa Mungu wa kweli!

Yesu Ndiye aliyetuita (1Wakorintho 1:26-31). Yeye

ametupa karama zote tunazohitaji (Waefeso 4:11-16) na

uwezo (Yohana 16:7) ili tutimize mapenzi Yake (Yohana

15:16).

MATENDO • 45

Shetani: Mpelelezi wa

tabia za binadamu tangu awali

Nakala 16 / Nambari 1

Page 46: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Kristo alituma Kanisa Lake liendeleze kazi Yake

(Matendo 1:4-8). Ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu peke

Yake kwamba sisi tunaweza kufanya hivyo kikamilifu. Roho

yule yule aliyemtia Yesu mafuta sasa amemiminwa hapa

duniani, akipatikana kwao wote wanaomwamini Yesu Kristo

kwa ajili ya wokovu (Warumi 8:14-17). Haleluya!

Kufuata Nyayo Za YesuMungu anawatafuta watu walio waaminifu Kwake

(2Nyakati 16:9). Yesu alijithibitisha kuwa mwaminifu kwa

Mungu na kumpendeza (Mathayo 3:17). Yesu alitii mapenzi

ya Baba katika mambo yote (Waebrania 10:5-7). Ingawa

Yesu alikuwa na uwezo wa kutenda dhambi, hakutenda

dhambi hata mara moja (Waebrania 4:15).

Kwa kuwa Yeye ni mfano wetu katika mambo yote,

tunaweza kujifunza nini kutoka katika maisha ya Yesu Kristo

kuhusu kukua katika upako? Tufuate nyayo Zake mara moja

tupate mafunzo yatakayotukuza katika tabia zetu na katika

mambo ya kiroho.

a. Yesu alikuwa chini ya mamlaka. Yesu alichagua

kutii mamlaka iliyokuwa juu yake. Hata kama kijana, alitii

wazazi Wake na mamlaka nyingine katika jamii Yake (Luka

2:41-51). Na wakati wote wa huduma yake ya duniani, Yesu

aliendelea kumtii Baba Yake wa Mbinguni.

Biblia inatufundisha kwamba sisi kama viongozi

tumewekwa chini ya taratibu za mamlaka katika maisha yetu.

Kuna serikali, madhehebu, makanisa (sharika), kazi - hivi

vyote vina taratibu za utawala au mamlaka.

Tunaweza kuona usalama na faraja kwamba mamlaka

hizi zipo juu yetu. Lakini mara nyingine, tunaweza

tusikubaliane nazo. Pengine tutajikuta chini ya watu wasio

wachaji, wenye ubinafsi au ukatili.

Inawezekana kabisa kwamba katika maisha yetu

tutatumika chini ya mamlaka yenye ufanisi kwetu na

mamlaka inayoonekana haina maana. Lakini haidhuru hali ya

mamlaka hizo, Neno la Mungu limetuagiza kuhusu umuhimu

wa kutii kama mfano wa maisha. Haya ni pamoja na kutii:

• Mungu (Yakobo 4:7);

• Mamlaka za serikali (Warumi 13:1-7; 1Petro 2:13-17;

taz. pia angalizo hapo chini);

• Uongozi katika Mwili wa Kristo (1Wakorintho

16:15-16; 1Wathesalonike 5:12-13; Waebrania 13:7,17);

• Kunyenyekeana sisi kwa sisi katika Mwili wa Kristo

(Waefeso 5:21; 1Petro 5:5);

• Waume, na wake zao (Waefeso 5:22; Wakolosai 3:18);

• Wazazi, na watoto wao (Waefeso 6:1-3; Wakolosai

3:20);

• Waajiri, na waajiriwa wao (Waefeso 6:5-9; Wakolosai

3:22 - 4:1; 1Petro 2:18-21).

ANGALIZO: Sisi kama Wakristo, tunapaswa kuvumilia

serikali yetu kila iwezekanapo. Yesu hakutafuta njia ya

kupindua serikali ya Rumi, ingawa wakati ule iliwatesa

Waisraeli vibaya sana. Lakini kama serikali au kiongozi

anawakataza watu uhuru wa kumwabudu Mungu na kumtii,

ni lazima tuendelee kumtumikia Mungu - hata kama tutapata

mateso (1Petro 4:12-19).

Wakati pekee ambapo unaweza kufikiria kukataa kutii

mamlaka iliyo juu yako ni kama wamekuamuru uvunje amri

ya Maandiko, au kanuni ya kimaadili (yaani, kwa kusema

uwongo, kuiba, kufanya zinaa, n.k.).

Kwa mfano, kama mamlaka ya serikali inakuamuru

uache kuhubiri Injili au kutamka kwa jina la Yesu, amri kuu

ya Kristo inakulazimisha uendelee kutamka. Mitume

waliendelea kuhubiri namna hii (Matendo 4:1-31; 5:17-42;

8:1-4). Ukikabiliwa na hali kama hii, utahitaji uangalifu,

hekima na ujasiri kwa wingi. Uongozwe na Roho Mtakatifu,

na Mungu atatukuzwa (Marko 13:9-13)!

Kanuni Ya KunyenyekeaKunyenyekea ni kanuni ya kimsingi katika maisha ya

mwamini, na hasa maisha ya kiongozi wa kanisa. Kwanza

ni lazima kabisa tumnyenyekee Mungu katika mambo yote.

Halafu inatubidi tuchague kuwanyenyekea walio na

mamlaka juu yetu - katika jamii, dhehebu, kazi au hali

yoyote nyingine.

Hata kama hatukubaliani nao, kuwapenda wala

kuwaheshimu, bado inatubidi tuendelee kuwanyenyekea

katika mwelekeo wetu na matendo yetu.

Sababu pekee kabisa ya kinyume ni ikiwa, katika nafasi

yao ya mamlaka, wamekuamuru uvunje Neno la Mungu au

kama wanawaongoza wengine wafanye hivyo.

46 • MATENDO

Uruhusu mfano wa Yesu uongoze kukua kwako.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 47: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Mchungaji kwa Mchungaji: Kuna wakati ambapotunaweza kupata shida na mtu mwenye mamlaka.Huenda tunaona kuwa tunanyanyaswa au hatupewiheshima inayotuhusu.

Mfano wa Yesu kwetu katika hali hizi ni kwambaYeye “alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna yamtumwa” (Wafilipi 2:7). Kristo hakutafuta kibali chawatu wala sifa yao, kwa upande mmoja kwa sababualijua havina maana yoyote; watu wanabadilisha maoniyao haraka sana (Yohana 2:23-25; 6:15,26,60-66).

Badala yake, Yesu Kristo alitafuta furaha ya BabaYake wa Mbinguni. Pia alichagua nafasi ya mtumishi(Mathayo 20:28). Kutoka katika moyo Wake wakunyenyekea na kutumika kulikuja wokovu kwetu nautukufu mkuu kwa Mungu (Wafilipi 2:7-11).

Sisi kama viongozi wa kanisa, tutawekwa katikanafasi za mamlaka mara kwa mara. Ili tuongoze kwaufanisi tukitumia mamlaka, inatubidi kwanza tujifunzekuishi na kutembea chini ya mamlaka! Maana yake nikwamba hatuna budi tufahamu jinsi ya kuishi kufuatanana kanuni ya kunyenyekea.

Ikiwa wewe unapata shida na kiongozi fulanimwenye mamlaka, kuna njia za kiutendaji za kufuata.Kwanza, umwombee mhusika kila siku. Kufanyahivyo kutakusaidia kumwona kwa upande wa Mungu.Halafu, umtafute Bwana kuhusu ufumbuzi Wake washida yako. Uchunguze Maandiko, na kumsubiri Bwanaakupe jibu Lake.

Huenda itakubidi umwendee huyu mtu nakumshirikisha shida yako kwa unyenyekevu (Mathayo5:23-24). Unaweza pia kutafuta ushauri wa watu wenyehekima na wasiopendelea upande wowote, ambaowatakusaidia kutatua tatizo na siyo tu kushikamana nawewe.

Mwisho ulinde moyo wako mwenyewe (pamoja nakutokulalamika wala kusengenya) na kumwaminiMungu akutetee (Zaburi 5:1; 7:10; 31:2; 59:16-17; n.k.).Mfano mkuu unapatikana katika maisha ya Daudi,aliyechagua kumheshimu Mungu na kusubiri wakatiWake ingawa matendo ya Sauli yalikuwa magumu namara nyingine pasipo uchaji (soma 1Samweli suraya 16 mpaka 24).

Huenda Mungu si chanzo cha jaribu au tatizo fulani

katika maisha yetu. Lakini ameahidi kutumia kila hali katika

maisha yetu kwa wema; “wema” huu ni kututengeneza sisi

katika mfano wa Kristo (Warumi 8:28-29).

Mara kwa mara Mungu atatumia mambo magumu

yanayotukabili katika kupima mioyo yetu (Kutoka 20:20;

1Nyakati 29:17). Wakati mwingine, uhusiano fulani wenye

magumu utatulazimisha tupevuke. Kuchagua miitikio ya

kiuchaji katikati ya matatizo wakati wote kutatukuza katika

tabia.

Tukichagua kuwa na msimamo wa Kristo na moyo Wake

katikati ya majaribu, mara nyingi matokeo yake ni kwamba

Mungu atatukabidhi zaidi ya mamlaka Yake, na uwezo na

upako Wake.

b. Yesu alikua katika kupevuka. Yesu alijitoa katika

utaratibu wa kukua wenye uimara na uwiano (Luka 2:52).

Ingawa mstari huu unaelekea kuhusiana na ujana wa Yesu,

bado ni mfano kwetu wa utaratibu wenye afya wa kukua na

kupevuka kwetu binafsi.

1) “kuendelea katika hekima” - chanzo kikuu cha hekima

ni Neno la Mungu. Unapolisoma na kulijifunza, umwombe

Roho Mtakatifu akufungulie ufahamu wako na kusema nawe

kuhusu ukweli (2Timotheo 2:15).

Yesu alisema kuwa Roho Mtakatifu “atawafundishayote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana

14:26). Roho wa Mungu atahuisha (kufanya hai na yenye

kuhusika) maneno ya Yesu.

Roho Mtakatifu atatoa katika Neno la Mungu ambalo

sisi tumeweka kama akiba ya maisha yetu. Tunaweka akiba

hii tunaposoma Biblia, pamoja na kusikiliza au kujifunza

mafundisho na mahubiri imara ya ki-Biblia.

Kama viongozi wa kanisa, inatubidi tujitoe kikamilifu

katika kujifunza, kukariri na kutendea kazi Maandiko ili

tukue katika hekima. Lakini huku kusoma na kujifunza si

kwa ajili ya kutunga mahubiri! Ni kwa ajili ya kukua kwetu

binafsi. Ndipo, kutoka katika kisima hiki kinachoongeza

urefu kila wakati, tunaweza kuchota kweli zile ambazo

Bwana anazihuisha mioyoni mwetu wakati wa kuwahudumia

wengine. Hali hii itatupa sisi baraka kubwa sana, pamoja na

wale tunaowahudumia (1Timotheo 4:12-16).

2) “kuendelea... na kimo” - Tumejifunza kwamba miili

yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:12-20;

1Wathesalonike 4:1-8). Kwa hiyo, tunapaswa tuwe wakili

wema wa miili ambayo Mungu ametupatia. Afya yetu ya

kimwili inahusiana moja kwa moja na uwezo wetu wa

kutumiwa na Mungu kwa ufanisi katika huduma.

Sote tunafahamu matumizi mabaya ya mwili wetu

ambayo ni ya kuepuka: ulevi au matumizi ya madawa

(Waefeso 5:18); zinaa na uasherati (1Wathesalonike 4:3-5);

ulafi (1Wakorintho 6:12-13; 9:24-27). Badala ya haya,

tutumie miili yetu katika kumtumikia Bwana!

Biblia inatuambia kuwa mazoezi ya mwili yana thamani

ndogo kuliko uchaji (1Timotheo 4:8); lakini mazoezi yana

thamani fulani. Hata hivyo, tuweke vipaumbele vyetu,

tusihangaikie zaidi hali yetu ya kimwili kuliko hali yetu ya

kiroho.

Mazoezi kiasi ya mwili ya kila siku ni mazuri kwa afya

yetu. Ni muhimu pia kujaribu kula vyakula vinavyofaa kwa

afya. Tuangalie ratiba zetu kuhakikisha kwamba tunapata

usingizi wa kutosha. Mambo haya yanaweza kuongeza muda

wetu wa kuishi na ufanisi wetu wa kazi, kwa kuongeza idadi

ya miaka ambapo Mungu anaweza kututumia na kupokea

utukufu kutokana na huduma yetu Kwake!

3) “akimpendeza Mungu” - Yesu alitembea katika kutiimapenzi ya Baba. Huduma Yake yote ilikuwa kutenda

mapenzi ya Baba Kwake (Yohana 5:19,30). Yesu alitamka

yale ambayo Baba alikuwa akiyasema (Yohana 8:26,28) na

kufanya matendo ya Mungu (Yohana 5:17; 9:4; 14:10).

Yesu alitii mapenzi ya Baba kikamilifu, hadi aweze

kusema, “[Baba] hakuniacha peke yangu; kwa sababunafanya sikuzote yale yampendezayo” (Yohana 8:29; taz. pia

Yohana 4:34; 6:38).

Lakini zaidi ya utiifu, Yesu pia alitembea katika

uhusiano wa karibu na wa ushirikiano na Baba kwa Roho.

Mara nyingi Yesu alikwenda kusali peke Yake (Luka 5:16).

Neno la Kiyunani lilitafsiriwa hapa “alikuwa akijiepua”

linaonesha kuwa kwenda kusali peke Yake kulikuwa mazoea

ya kawaida kwa Yesu.

Utiifu wa Yesu haukumfanya astahili upendo na baraka

MATENDO • 47Nakala 16 / Nambari 1

Page 48: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

ya Mungu. Lakini ulihakikisha kwamba wala dhambi wala

kuridhiana yoyote havikuweza kuvunja uhusiano Wake na

Baba. Hali hii ni muhimu sana kwetu, kwa sababu Yesu

ametupatia sisi ahadi hiyo hiyo ya uhusiano wa karibu na

Yeye!

Yesu ameahidi “kujidhihirisha” kwetu tunapotembea

katika kutii amri Zake (Yohana 14:21-24). Utiifu wetu kwa

Kristo na Neno Lake, katika mambo makubwa na madogo,

utatusaidia kuwepo panapofaa kwa ajili ya kutembea kwa

ukaribu zaidi pamoja na Bwana wetu. Utiifu wetu haustahiliupendo wa Bwana. Lakini unasaidia kuwepo kwa uhusiano

na ushirika wa ndani zaidi pamoja na Baba, Mwana na Roho

Mtakatifu. Na kutoka mahali hapo pa uhusiano wa karibu

sana, upako wa Roho Mtakatifu utatiririka ndani yetu na

kupitia kwetu zaidi na zaidi.

4) “akimpendeza... na wanadamu” - Maana yake si

kwamba Yesu alitafuta sifa ya wanadamu wala kupata kibali

chao. Lakini Yesu alichagua kutokutenda kwa kiburi, ingawa

kweli Yeye alikuwa mkuu kuliko watu wote! Badala yake,

Yesu alisema na kutenda kwa upendo.

Neema Na UkweliYesu alikuwa mfano kwetu wa uwiano kamili wa tabia

ya Mungu: “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasitukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekeeatokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14);

“Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema nakweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo” (ms. 17).

Yesu alikaa pamoja na wenye dhambi (Mathayo 9:9-13)

na pamoja na watu wa dini (Luka 7:36-50). Aliongea kuhusu

upendo wa Mungu na makusudi Yake kwa wote waliokubali

kusikiliza. Yesu hakutafuta kibali cha watu wala sifa yao, bali

alitafuta njia ya kufunua moyo wa Mungu Baba na Neno

Lake katika kila hali.

Yesu alifundisha kwamba Mungu anatutazamia tutunze

mahusiano kati yetu yaliyo safi na pasipo unajisi. Biblia

inafunua wazi matendo mengi sana ya kimwili na dhambi

ambayo hayakubaliki kwa Mungu katika mahusiano yetu,

yakiwemo: kutosamehe, uchungu, hasira, wivu, kuonea,

ugomvi, masengenyo, kuhukumu, n.k. (Mathayo

5:21-24,43-48; 6:12,14-15; 7:1-6; 18:21-35; Warumi

12:9-21; Wagalatia 5:13-15,19-21; 1Yohana 2:9-10; 3:10-18

- hii ni mistari kadhaa tu kati ya mingi inayoonesha mkazo

wa Mungu kwa ajili ya kuwa na mahusiano yafaayo kati

yetu).

Hatuwezi kutawala misimamo na mienendo ya wengine;

lakini tunaweza kuamua juu ya misimamo na mienendo yetu

binafsi. Na mara nyingi, msimamo wetu wa “neema na

ukweli” utafungua njia kwa upatanisho na amani pamoja na

wengine.

Tunapofanya kazi ya kuleta mahusiano mema, yajaayo

“neema na ukweli” ya Mungu, tunasitawisha umoja. Umoja

mkubwa zaidi katika Mwili wa Kristo ni kufungulia uwepo

wenye upako wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu,

makanisa yetu na jamii zetu. Pia ni ushuhuda kwa dunia wa

ukweli halisi wa Injili (Yohana 17:20-21).

c. Yesu alitembea kwa unyenyekevu. Kwa hakika,

Mungu Mwana alikuwa mwanadamu mnyenyekevu kuliko

wote. Yesu alikuwa Mungu hasa, lakini alitwaa namna ya

mtumwa na mfano wa mwanadamu, ili atoe uhai Wake kwa

ajili yetu sisi sote (Wafilipi 2:7-8). Kama sisi tutafuata nyayo

Zake, lazima tutembee kwa unyenyekevu.

Yesu alianza huduma Yake kwa kujinyenyekeza, hata

wakati ambapo haikuonekana kuwa ni lazima afanye hivyo.

Tunaona hali hii Yesu alipofika kwa Yohana Mbatizaji wakati

alipokuwa akiwabatiza watu kwa ajili ya kutubu dhambi

(Mathayo 3:13-17).

Ni wazi kwamba Yesu hakuhitaji kutubu, kwa sababu

Yeye hakuwa na dhambi (Waebrania 4:15). Hata Yohana

alijaribu kumzuia Yesu, akijua kwamba Yesu hakuwa na

dhambi tena alikuwa mkuu kuliko yeye (Mathayo 3:14).

Lakini Yesu bado aliomba abatizwe na Yohana: “Kubali hivisasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote”

(ms. 15).

Kwa nini Yesu alitaka abatizwe? Tukio hili lilianzisha

huduma ya Yesu. Kwa hiyo, Yesu alichagua tendo hili la

kujinyenyekeza katika ubatizo wa maji ili afungamane nawatu wenye dhambi - watu kama wewe na mimi.

Yesu, Mwana wa Mungu asiye na dhambi yoyote,

alichagua kujiweka sawa na wanadamu wenye dhambi katika

utume Wake wa kuleta tumaini la wokovu kwa wanadamu

wote. Ili “kuitimiza haki yote” Yesu alikiri mapenzi ya

Mungu kwamba Yeye achukue mzigo wa dhambi zote za

wanadamu, awe Mkombozi na Mwokozi wao.

Mtumishi Wa WatumishiYesu alijua kwamba utume Wake kutoka kwa Mungu

ulikuwa kama mtumishi mnyenyekevu kwa wanadamu wote

(Mathayo 20:28). Alitambua hali hii alipokuwa na miaka

kumi na miwili tu (Luka 2:41-50). Ilithibitishwa tena na yale

yaliyotokea mara baada ya kubatizwa Kwake kwa maji.

“Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapandakutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwonaRoho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; natazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (Mathayo 3:16-17).

Mambo matatu yalimtukia Yesu alipotii mapenzi ya

Baba Yake kwa unyenyekevu katika ubatizo:

1) “mbingu zikamfunukia” (ms. 16b) - Hii ni alama ya

Mungu akijifunua pamoja na makusudi Yake kwa njia mpya

yenye nguvu kupitia kwa Mwana Wake. Yesu alikuwa na

Ndiye Mungu (Wakolosai 1:15-16,19; Waebrania 1:3).

Kumwona, kumsikia na kumjua Yeye ni kumjua Mungu

kikamilifu. Katika Yesu, Mungu alikuwa amejidhihirisha

kwa binadamu mwenye dhambi kwa uwazi zaidi kuliko

wakati wowote uliotangulia.

2) “Roho wa Mungu akishuka” (ms. 16c) - Yesu alipokea

upako wenye uweza usio na kipimo wa Roho Mtakatifu. Huu

ulimwezesha kutimiza makusudi na mapenzi ya Mungu,

akifunua moyo wa Mungu kwa ukamilifu zaidi na kufungua

njia ya wokovu kwa watu wote. Katika kupokea upako wa

Roho Mtakatifu, Yesu amepata kuwa Yeye anayembatiza

mwamini na Roho Mtakatifu (Luka 3:16).

3) “Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwanaye” (ms. 17). Kwa hakika, Mungu alitamka kwa ufunuo wa

ndani sana katika kuthibitisha asili ya Kristo. Lakini tamko

hili lina maana yenye uzito hata zaidi.

Kuna sehemu mbili za tamko hilo zinazotokana na

maneno ya unabii ya Agano la Kale kuhusu Masihi. “Huyu niMwanangu, mpendwa wangu” hutoka Zaburi 2:7. Wayahudi

48 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 49: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

walikubali Zaburi hii nzima kama maelezo ya kinabii kuhusu

Masihi ajaye.

Sehemu ya pili, “ninayependezwa naye” hutoka Isaya

42:1. Sura hii nzima ya Isaya, pamoja na sura ya 43, ni unabii

kuhusu Masihi kama Mtumishi anayeteswa, Mkombozi

atakayeleta haki, rehema na wokovu wa Mungu kwa

wanadamu wote.

Mungu alipotamka maneno haya, alithibitisha kwamba

Yesu kweli ndiye Masihi aliyesubiriwa na kutabiriwa kwa

muda mrefu. Yeye ni Mteuliwa wa Mungu awe Mwokozi,

Mfalme wa wafalme wote na Bwana wa mabwana wote.

Alithibitisha pia kwamba njia ya kufikia taji ya milele ya

ki-Mungu ni kupitia msalabani. Mfalme wa wafalme

alipaswa kwanza awe Mtumishi wa wote (Wafilipi 2:5-11).

Njia yake ya kufikia kiti cha enzi ilikuwa utiifu kwa Baba

(Waebrania 5:8). Yesu angetimiza utume uliohamasishwa na

upendo (Yohana 3:16).

Yesu Alilenga Kuwafikia WoteKutokana na matukio haya katika ubatizo wa Yesu,

tunaweza kujifunza mambo muhimu kuhusu upako.

Kwanza, utiifu wa hiari wa Yesu katika kujinyenyekeza,

hata wakati pasipokuwa lazima, ulifungua zaidi ya yale

ambayo Mungu alikusudia kwa ajili Yake na kupitia Kwake.

Yesu aliwafikia wote, pasipo kuwahukumu, akawapatia

upendo, msamaha na wokovu wa Mungu (Yohana 8:1-11).

Aliongoza kwa kuwa mfano katika unyenyekevu (Yohana

13:1-17), akifunua kikamilifu kabisa moyo wa Mungu wa

upendo pale msalabani (1Yohana 4:9-10).

Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,sisi pia lazima tutembee katika kumtii Mungu kwaunyenyekevu. Lazima tuwapelekee wote Injili kwaunyenyekevu. Huenda kweli hizi zinaeleweka wazi.Lakini haina maana kuwa tunazitendea kazi! Maranyingi kujinyenyekeza ni hamasa kubwa sana.Unyenyekevu unahusiana na tabia yetu moja kwamoja. Na tabia yetu ni muhimu kabisa kwa ajili ya kukuana kuzaa matunda kwa kutenda kazi katika upako waRoho Mtakatifu.

Mungu anawapinga wenye kiburi; lakini anawapawanyenyekevu neema. Nani kati yetu hahitaji zaidi yaneema ya Mungu katika maisha yake? Inatolewa kwetukupitia unyenyekevu wetu.

Unyenyekevu huu si kujidhili au kujichukiakunavyokusudia kuwaonesha wengine jinsi sisi tulivyo“wa kiroho”. Mtu mwenye unyenyekevu wa kweli hanahaja ya kuuonesha kwa watu. Mtu anapojifanya kuwamnyenyekevu, matokeo yanachukiza sawasawa namaonesho ya kiburi. Unyenyekevu wa kweli ni wamoyoni. Ni mwelekeo wa kujali wengine bila ubinafsi.Ni kutokuwa na kujiona wala kujivuna kabisa.

Nikupendekezee mielekeo na matendo ambayohuweza kutusaidia tutembee katika unyenyekevu wakutii. Ni busara kuwa na mazoea haya kila siku:

• Tuwaombe wale tuliowaumiza au kuwaudhi

watusamehe.

• Tutoe msamaha kutoka moyoni, hata kama

haujaombwa.

• Tumpende mtu anayeonekana kwamba hapendeki

wala kustahili.

• Tuombe msaada, na kuupokea.

• Tukatae cheo, nafasi na heshima ambavyo faida

yake ni kutuweka “juu ya” wengine tu.

• Tuchague aina ya kazi isiyoonekana, kusifiwa,

kuheshimiwa wala kuleta faida au thawabu kwa

wakati huu.

• Tuwaachie wengine wapokee sifa ambayo huenda

ingalikuwa yetu kwa haki.

Yesu alifundisha mara nyingi kuhusu unyenyekevu,

akifahamu mwelekeo wetu wa kibinadamu wa kiburi

(Mathayo 6:1-15; 18:1-4; 20:20-28). Kama tunataka kupokea

upako halisi wa Roho Mtakatifu - ambayo huleta maisha

yaliyobadilishwa na kuzaa matunda - ni lazima tutembee

kama Yesu alivyotembea.

Ni njia ya kutii kwa unyenyekevu na uaminifu kwa

mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika Neno Lake; ni

kutembea kufuatana na mwongozo wa Roho Mtakatifu kila

siku (Mika 6:8).

d. Yesu alifahamu majaribu. Mara baada ya kubatizwa

Kwake, Yesu “akaongozwa na Roho” kwenda nyikani

afunge, kusali na kupambana na Shetani (Luka 4:1-12).

Tungeweza kutazamia kwamba baada ya tukio kuu la

kubatizwa na kutiwa mafuta ya upako wa Roho Mtakatifu,

Yesu angalitumwa moja kwa moja katika huduma ya wazi

yenye nguvu.

Lakini hekima ya Mungu imezidi yetu kabisa (Isaya

55:8-9) na makusudi Yake yameandaliwa kwa upeo wa

umilele. Ni wazi kwamba kujaribiwa kwa Yesu kulifuatana

na mpango wa Mungu (Mathayo 4:1; Marko 1:12-13; Luka

4:1).

Tunaweza kujifunza mengi kutokana na mielekeo ya

Yesu katika muda Wake wa kujaribiwa na kupimwa.

Hakulalamika wala kunung’unika. Hakushindwa na hofu

wala mashaka. Kupitia majaribu yote na katika ushindi wa

mwisho, Yesu alimtegemea kabisa Mungu Baba Yake.

Mchungaji kwa Mchungaji: Kama viongozi wakanisa, tunakabiliwa na majaribu, mateso na vishawishikwa wingi. Kuwa kiongozi katika Kanisa kunawezakututoa katika kilele cha furaha kuu mpaka kwenyebonde la ubatilisho na kukatishwa tamaa - na maranyingi, kati ya Jumapili moja na nyingine!

Mchungaji mwenzangu, kama kiongozi katikakanisa, wewe ni shabaha ya mashambulizi ya ibilisi.Unaweza kujisikia kuwa peke yako katika mapambanoyako, ukifikiri hakuna mtu anayefahamu. Kuna jaribu lakufikiri kwamba kama ungekuwa na upevu au tabia yakiroho zaidi, usingepitia vipindi vigumu hivi. Huendautashawishiwa ukate tamaa na kuacha utumishi.Uwongo huu wa ibilisi unalenga kukuvunja moyo -usiuamini!

Ukweli ni kwamba yeyote anayejaribu kumtumikiaBwana atakabiliwa na mateso, majaribu na vishawishi(2Timotheo 3:12) - hata Yesu. Maisha Yake ni mfanokwetu jinsi tunavyoweza kukabili na kuvumilia majaributukiwa na uhakika wa ushindi na tukimwamini Mungu.

Yesu alijua kwamba Mungu asingemwacha walakumsahau. Alijua kwamba Mungu ni mwaminifu naahadi Zake ni za kweli. Alijua kuwa angeweza kutimizamapenzi ya Baba yake, kwa uweza wa Roho Mtakatifuna msaada wa Mungu: “Yeye ni mwaminifu ambayeawaita, naye atafanya” (1Wathesalonike 5:24).

MATENDO • 49Nakala 16 / Nambari 1

Page 50: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Nakushauri ukariri mstari huu wa Maandiko, nakuutafakari unapokabiliwa na hamasa au jambo gumu.Pia uchukue muda wa kusoma maoni na kanunikutokana na maisha ya Yesu (Sehemu Ya III, B.2); hivipia vitakusaidia katika vipindi vya mambo magumu.

Yesu hakuuliza kwa nini haya yalimtokea. Bali

alistahimili majaribu, akiamini kuwa sehemu ya makusudi ya

Mungu ilitendeka kupitia katika maisha Yake na ndani yake

pia. Yesu alipata amani na uwezo katika kumnyenyekea

Mungu, na katika imani Yake kwa uwezo usiobadilika wa

Neno la Mungu.

Mavazi Ya Vita YafaayoWakati ambapo Mungu anatufikisha katika eneo jipya la

wajibu au kufungua upako mpya katika maisha yetu, mara

nyingi anaruhusu kipindi cha kujaribiwa kifuate. Tuangalie

sababu kadhaa za kipindi hiki kuwa muhimu sana:

Tunahitaji “kukua katika” upako tunaopewa na

Mungu. Mungu atatunyosha kiroho kwa ajili ya ufanisi wetu.

Lakini kukua kunaweza kuumiza; huenda tutataka kuchukia

au kuzuia kukua kwetu. Lakini kwa sababu Mungu anajua

yaliyo mbele yetu, anataka kutuandaa kwa ajili ya kushinda

na si kushindwa. Kwa hiyo tunatakiwa tuwe na nguvu na

upevu, na pia tukubali yanayotendeka.

Tunaweza kuona mfano wa awali wa kanuni hii katika

Agano la Kale (1Samweli 17:38-39). Daudi anakwenda

kumkabili jitu Goliathi. Sauli anamtakia Daudi avae mavazi

yake ya vita. Lakini Daudi anakataa mavazi ya Sauli,

akisema, “Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu”

(ms. 39).

Daudi hakuweza kutumia kwa ufanisi mavazi

yasiyolingana na mwili wake na ambayo alikuwa hajazoea

kuyavaa. Ingawa mavazi haya yalimfaa Sauli, yalikuwa

mageni na yasiyoaminika kwa Daudi.

Vile vile, upako na karama ambavyo sisi tunatakiwa

tutembee navyo viwe vyetu - si wa mtu mwingine. Ni rahisi

mno kutegemea na kuamini karama na upako vya mtu

mwingine. Huenda tunajaribu hata kumwiga, tukihubiri

mahubiri yake au kuiga mtindo wake. Tunajaribu kutembea

katika “mavazi” yasiyo yetu!

Kule kujaribu kutembea katika upako wa mtu mwingine

ni tatizo, kwa sababu Mungu amekuita wewe. Anataka

akutumie wewe. Upako aliokupatia umetolewa kwa ajili

yako. Wewe ni chombo pekee ambacho Mungu anataka

kutumia kwa njia maalum. Kazi anayotoa ni kwa ajili yako,

na upako atakaokupa utalingana kikamilifu na kazi

unayotakiwa ufanye.

Lakini mara nyingi inachukua muda mpaka ufahamu na

“kukua katika” wito wako, kazi yako na upako wako. Mara

nyingine, Mungu atatumia kipindi cha kujaribiwa au

kuteswa, kwa kukusaidia ukue ili upate kuwa na nguvu na

kuweza kufanya katika “mavazi” yako mwenyewe - upako

ambao amekupa wewe - uwe na ushindi na kuzaa matunda

katika wito Wake.

Ni lazima tujifunze kutumia yale ambayo Yeye

ametupatia. Mara nyingi majaribu yatafunua upungufu

wetu. Katika vipindi vigumu, tunatambua hata zaidi jinsi

tunavyomhitaji Bwana na yale ambayo Yeye peke Yake

anaweza kutupatia.

Tumekwisha jifunza umuhimu wa kuwa na aina ya

udhaifu wa kiuchaji, unaotuongezea kumtegemea Mungu

(2Wakorintho 12:7-10). Aina hii ya udhaifu inatuwezesha

kuwa vyombo ambavyo upako wa Roho Mtakatifu unaweza

kutiririka kupitia kwake.

Haja Yetu Ya Mungu IsiyokwishaTunapojazwa upako wa Mungu, na kutenda kwa uhakika

na imani (vinavyotegemea utii), bado kuna hatari ambayo

inatubidi tuitambue. Hatari hii ni kwamba, polepole,

tunaanza kujitegemea wenyewe pamoja na ujuzi na ustadi

wetu tuliojiongezea. Hapo tunapunguza kumtegemea Bwana

na uweza wa Roho Mtakatifu. Si kwamba hali hii haina budiitokee; lakini inaweza kutokea tusipokuwa waangalifu.

Yesu alisema, “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi;akaaye [kubaki, kuishi] ndani yangu nami ndani yake, huyohuzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya nenolo lote” (Yohana 15:5).

Nikaze hapa kwamba upako wa Roho Mtakatifuunamhusu Yesu tu. Hauhusu karama, uwezo wala utumishi.

Hauhusu hata wale tunaowahudumia - unamhusu Yesu! Tabia

saba za upako halisi [zilizoorodheshwa katika Sehemu Ya III,

A.3] zilifanana katika jambo moja: ZOTE zilimwashiria Yesu.

Ni katika Yeye tu, kwa Roho wa Mungu, kwamba sisi

“tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu” (Matendo

17:28). Haidhuru Mungu anatutumia kiasi gani, wala

tunapata ujuzi kiasi gani, inatubidi daima tutunze imani

yenye unyofu kama ya mtoto. Imani ya aina hii inahitaji

kumtumaini Bwana kwa unyenyekevu na kuongeza undani

wetu wa kumtegemea Yeye.

Asili yetu ya kibinadamu inaweza kutuelekeza katika

ubinafsi na hisia ya kujitegemea mbali na Mungu. Lakini

majaribu na mateso yatatukumbusha jinsi tunavyomhitaji

wakati wote, pamoja na neema Yake na uwepo Wake katika

maisha yetu.

Tunahitaji kutakaswa ili tuwekwe huru kwa ajili ya

kupokea upako Wake zaidi. Yesu alisema, “Roho ndiyoitiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambiani roho, tena ni uzima” (Yohana 6:63).

Uwepo wa Roho wa Mungu katika maisha yetu utafanya

asili yetu ya dhambi kutokuona raha - ndiyo hali

inayotakiwa! Kwa sababu Roho na mwili (asili ya dhambi)

hupigana, au “kushindana” (Wagalatia 5:16-17; taz. pia

Yakobo 4:1-10; 1Petro 2:11).

Mungu anayajua yaliyo ndani ya mioyo, akili na nafsi

zetu ambayo yatazuia au kuziba upako wa Roho Wake

Mtakatifu. Majaribu na mateso mara nyingi hutusafisha,

yakisogeza madhaifu nje yaonekane na kushughulikiwa.

Kusafishwa Na UchafuWatu kama sonara wanaofua madini ya fedha na

dhahabu watakuambia kuwa mawe yanapochimbwa hujaa

uchafu. Inabidi kuyachemsha mpaka yayeyuke ili uchafu

uelee juu.

Ndipo uchafu (uitwao mavi ya madini) unaenguliwa kwa

ustadi juu ya madini yaliyoyeyuka (Mithali 25:4). Utaratibu

huu unarudiwa mara nyingi mpaka madini yawe safi kabisa

na kufaa kutumiwa. Watu wanaotia moto katika mawe

wanajua dakika halisi ya kuondoa madini kwenye moto ili

yasiungue.

50 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 51: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Kwa njia kama hii, Mungu atatumia majaribu

yanayoweza kuingia katika maisha yetu kufanya uchafu

uliopo katika maisha yetu “uelee juu” na kuonekana. Ndipo

unaweza kutambuliwa - na kuondolewa kwa njia ya toba,

uponyaji na ukombozi, viletavyo uhuru kutoka katika

vifungo vya asili yetu ya dhambi.

Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,nini inaelea juu katika maisha yako wakati mazingira“inachemka” (inazidi) au unapojisikia kuzidiwa nashughuli? Unaitikiaje, unatafuta msaada wapi? Je,yanayojitokeza yanafunua mwelekeo au mwenendoambao Mungu anataka kusafisha, kuponya au kuondoamaishani mwako? Je, kuna jambo fulani ambalo Yeyeanataka kukufundisha katika jaribu au tatizo lako?

Vipindi hivi vya kukabiliwa na madhaifu yetu nauchafu wetu si vya kuogopa. Mungu, katika upendoWake, atatumia majaribu, mateso na dhiki katikakututakasa na kututengeneza. Pia atatupa mafunuo,ufahamu, kutugusa na upendo Wake na kutufunuliayaliyomo ndani ya Neno Lake. Anatumia nafasi hizikupanua imani yetu na kubadili tabia yetu ili tuwevyombo vyenye kufaa na kutumika zaidi.

Hekima Katika MajaribuMungu anatumia majaribu kututakasa na kutuongezea

nguvu. Mungu hatujaribu ili atufanye tujisikie tumeshindwa

au kwa sababu sisi “hatuna wema wa kutosha”. Hasha!

Mungu anaruhusu majaribu na mateso katika maisha yetu ili

atuongezee nguvu; kwa sababu Yeye hataki sisi tuwe

wadhaifu wakati tunapohitaji kuwa na nguvu (Mithali 24:10;

Yeremia 12:5). Mungu anatumia majaribu kutuandaa ili

tuweze kupokea, na kutumia kwa uaminifu, zaidi ya upako

Wake!

Ndiyo sababu Yakobo anatuhimiza: “Hesabuni ya kuwani furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali”(Yakobo 1:2). Maandiko yanaendelea kututia moyo tuvumilie

majaribu (ms. 3 na 4), tukijua na kuamini kwamba Mungu

wetu mwaminifu atayatumia kwa ufanisi wetu na utukufu

Wake. Ndiyo ahadi Yake kwetu (Warumi 8:28-29).

Yakobo anaendelea kutushauri tuombe pia hekima

(Yakobo 1:5-8) - na, kwa imani, kutazamia kusikia kutoka

kwa Mungu. Kwa nini tunahitaji hekima hii? Kwa ajili ya

kutoroka majaribu tu? Sivyo, ila ni kutuwezesha

kupambanua na kufahamu ili tujue tufanye nini wakati

Mungu anapotenda kazi ndani yetu - haidhuru chanzo cha

jaribu ni nini.

Hitaji La Historia IliyothibitikaMungu anataka kutupa zaidi ya Roho Wake. Lakini mara

nyingi maana yake ni kwamba tuwe na nguvu ya kitabia na

upevu ili tusipoteze au kuchezea karama Zake. Usingempa

mtoto wa miaka mitano gari, hata kama yeye ameona yu

tayari kuliendesha, sivyo? Asingekuwa na upevu wa kutosha

ili awajibike juu yake. Anahitaji kwanza kukua kimwili,

kiakili na kihisia.

Kanuni hii ni kweli pia katika Ufalme wa Mungu.

Angalia maagizo ya Paulo kwa Timotheo kuhusu kuwateua

wazee (maaskofu) na mashemasi (1Timotheo 3:1-13). Ni

vema mtu akipenda kuwa kiongozi, maana atamani kazi

njema. Lakini lazima awe na historia iliyothibitika ya

mwenendo na tabia ya uchaji, na upevu katika maisha. Paulo

alimwagiza Timotheo hasa kwamba mtu aliyeongoka karibu

asiteuliwe kama mzee wa kanisa, kwa sababu waongofu

wapya bado hawajawa na historia kama hii.

Kusimama Wima Wakati Wa MajaribuMungu wetu ni mkamilifu katika utakatifu. Yeye

hatatenda uovu kamwe, wala Mungu hatatujaribu sisi -

ambao Yeye anatupenda - tufanye uovu au dhambi (Ayubu

34:10-12; Yakobo 1:13-18).

Ni Shetani aliye mwanzilishi wa uovu wote, anayetafuta

kuiba, kuua na kuangamiza (Yohana 10:10). Ibilisi hawezikuharibu au kuzuia karama zetu au upako wetu moja kwa

moja. Hivi vipo chini ya mamlaka ya Mungu peke Yake.

Lakini Shetani atajaribu kutushawishi katika eneo la tabia

yetu. Atajaribu kutushambulia, kutudanganya, kutuchafua au

kutuondolea haki kama vyombo vya Mungu. Akiweza

kutushawishi tuchague mwenendo au msimamo wa dhambi,

kazi ya Mungu kupitia maisha yetu inaweza kuzuiwa au

kuharibiwa kutokana na kushindwa kwetu binafsi.

Tufanyeje basi kwa kuwa “mshtaki [wetu] ibilisi, kamasimba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtuammeze” (1Petro 5:8)?

Tupambane na majaribu kama Yesu alivyofanya pale

nyikani (Luka 4:3-12). Njia za kupinga kazi za ibilisi

zimeorodheshwa pia katika Yakobo 4:7-10. Usome sehemu

hii ya Maandiko, na tuiangalie hapa sasa.

“Mtiini Mungu” - tumtii na kumtegemea Mungu. Kutii

Neno Lake kutatuweka mbali na mahali na nafasi za

vishawishi. Pia, umkimbilie Yeye kwanza katika sala

unapopata majaribu au vishawishi; usijaribu kupinga

majaribu pasipo msaada wa Mungu.

“Mpingeni Shetani” - tumia Neno la Mungu na lugha

yako ya kiroho ya kusali (1Wakorintho sura ya 12 na 14);

uungane na mtu unayemwamini katika sala.

“Mkaribieni Mungu” - umletee Mungu hali yako kamili

katika sala ukimruhusu aangaze ndani ya moyo wako kwa

nuru ya Roho Yake na Neno Lake. Uwe mvumilivu na

kumsubiri atende yale ambayo Yeye peke Yake anaweza

kuyatenda. Upinge jaribu la kushughulika mwenyewe na

kujaribu kubadili au kutengeneza hali wewe mwenyewe.

“Itakaseni mikono yenu”, “na kuisafisha mioyo yenu”,“Jidhilini mbele za Bwana” - wakati Roho Mtakatifu

anapofunua au kukuthibitishia maeneo ya utumwa, dhambi

na udhaifu katika maisha yako, uyalete kwa Mungu katika

sala kwa moyo wa unyenyekevu na toba; ungama makosa

yako na haja yako ya kazi ya utakaso ya Mungu, msamaha,

uponyaji na ukombozi Wake.

Neema Ya Kuwa WashindiZaidi yake, kuna orodha nyingine ya maagizo yenye

nguvu ya kutusaidia kupambana katika vita vya kiroho. Soma

Waefeso 6:10-18. Mistari hii inatuagiza tuvae silaha, kushika

upanga wa Roho (Neno la Mungu) na “kuloweshwa” sala.

Ndipo baada ya kufanya yote uwezayo, simama imara katika

imani, tumaini na utiifu kwa Mungu. Unaweza kumpinga

ibilisi na kazi zake, naye lazima akimbie! Mungu atakupa

ushindi leo!

Adui hakati tamaa. Atajaribu tena, kwa sababu lengo

lake ni kukuangamiza. Hali hii ilikuwa ya kweli hata kwa

MATENDO • 51Nakala 16 / Nambari 1

Page 52: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Yesu. Ingawa alikabili jaribu kuu nyikani - na kupata ushindi

mkuu - haikuwa mara Yake ya mwisho ya kukutana na adui

(tazama Luka 4:13; taz. pia Mathayo 16:23; Luka 22:1-6).

Lakini katika kila jaribu, Yesu hakukubali dhambi.

Kumbuka kwamba Mungu yu upande wako kabisa

(Warumi 8:31). Ameahidi kwamba hataruhusu ujaribiwe

kuzidi uwezo wako; daima Yeye atakupatia mlango wa

kutoka (1Wakorintho 10:13; 2Petro 2:9).

Tushangilie, basi, kwamba sisi tunaye Mfalme anayejua

na kufahamu mapambano yetu kwa ndani. Mwokozi huyu

mwenye haki na upendo ametukaribisha kwa hiari kupokea

uwezo, nguvu na neema Yake ili tuwe washindi kama Yeye

(Waebrania 4:14-16).

Lazima tufuate utaratibu wa maisha yote wa

kutegemea uweza wa Roho Mtakatifu.

Yesu aliporudi kutoka siku zile arobaini nyikani, Biblia

inasema hivi: “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaendaGalilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote zakandokando” (Luka 4:14).

Yesu aliendea mji wake wa nyumbani, Nazareti. Ndipo

alipokulia na alipokwenda katika sinagogi siku ya Sabato

(Luka 4:16-30). Ndipo aliposimama asome, akichagua

kutoka katika Maandiko mistari hii kutoka Isaya 61:1-2:

“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafutakuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangaziawafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kuona tena,kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwanauliokubaliwa” (Luka 4:18-19).

Yesu alitangaza kwamba kazi Yake ya Masihi

ingefanywa na “Roho wa Bwana”. Yesu alitiwa mafuta na

kupewa uwezo na Roho Mtakatifu. Ilikuwa kutokana na

upako huu tu kwamba aliweza kufanya yote aliyotangaza

kinabii kuhusu huduma Yake.

Kumtegemea Bwana KikamilifuKatika mistari hii, Yesu ameweka utaratibu kamili jinsi

tunavyoweza kufanya mapenzi ya Baba. Kama tunavyojua,

Yesu alikuja ili afanye mapenzi ya Baba, si ya Kwake. Vile

vile, wewe na mimi tumeitwa tufanye mapenzi ya Baba na si

yetu. Hatujaitwa tufuate “mpango wetu” hata kama tunauona

ni mzuri kabisa. Bali tumeitwa, kupewa mamlaka na

kuwezeshwa tufanye mapenzi ya Mtu Mmoja - Mungu. Na ili

tufanye mapenzi ya Mungu, tunahitaji uwezo wa Mungu!

Kama tulivyojifunza, hamasa yetu kuu tunapopevuka

katika mambo ya Mungu ni jinsi ya kutegemea Mungu na

uwezo wa Roho Mtakatifu zaidi na zaidi. Ni rahisi mno

kuanza kutegemea karama na nguvu zetu zinazoongezeka.

Tumepata ufanisi kiasi, kwa hiyo tunapunguza kusali kwa

bidii na kujifunza Biblia. Njaa yetu ya kiroho, au hamu yetu

ya kumwona Mungu akifanya kazi katika maisha ya watu au

katika jamii yetu, vinapungua. Ndipo tunapoanza kutegemea

zaidi ujuzi na ustadi wetu wa muda mrefu, kuliko uwezo wa

upako wa Roho wa Mungu.

Katika hali kama hizi, matatizo na majaribu yanaweza

kuturudisha kwenye kupiga magoti na kusali, penye nafasi

yetu ya kumtegemea Bwana kwa ajili ya yote tunayohitaji

katika maisha na huduma.

Tunaweza kuona, katika maisha ya Yesu, vipindi vya

miujiza mikuu na huduma kubwa, na vipindi vya majaribu

makuu na upinzani mkubwa. Lakini kwa pande zote, Mwana

wa Mungu asiye na dhambi alitegemea kabisa uwezo wa

Roho wa Mungu.

Yesu alichagua kupokea vizuizi au mipaka ya mwili wa

kibinadamu na kujifanya kuwa hana utukufu (Wafilipi 2:7).

Kwa sababu ya hali hii, Yesu alijiachia ategemee kabisa

mapenzi ya Baba na uwezo wa Roho Mtakatifu. Ndivyo

vilivyompitisha katika maisha ya hapa duniani, huduma

Yake, na hata kupitia kifo Chake na kufufuka Kwake kwa

utukufu kulikofuata!

Kama Yesu, Mwana wa Mungu, alihitaji nguvu ya upako

ya Roho Mtakatifu ili atimize mapenzi ya Baba - je, si zaidisana basi kwetu wewe na mimi?

Majaribu: Silaha Za Mungu Za KututengenezaMungu atatumia majaribu katika maisha yetu. Si

kwamba anatuadhibu katika vipindi hivi. Ukweli ni kinyume.

Kwa sababu Mungu anatupenda, anaturudi (Waebrania

12:3-11). Kwa sababu sisi kweli ni wana wake wa kiume na

kike (Warumi 8:14-16), Yeye anafanya yote yaliyo lazima

kututengeneza na kutuwezesha kukua katika mfano Wake

(2Wakorintho 3:18). Kwa sababu sisi ni warithi pamoja na

Kristo (Warumi 8:17), na hatima yetu ni kutawala pamoja na

Yeye (2Timotheo 2:12; Ufunuo 5:10), tutapitia majaribu ya

kutuandaa kwa ajili ya mambo yajayo (Warumi 8:18;

2Wakorintho 4:17).

Tusiogope wala kutoroka majaribu na matatizo

yatakayotujia sisi sote. Lakini badala yake, kama Yakobo

anavyoandika, “hesabuni kuwa ni furaha tupu, mkiangukiakatika majaribu mbalimbali” (Yakobo 1:2). Maana ndiyo

silaha hasa ambazo Mungu atazitumia katika kutuumba,

kutugeuza na kutuandaa kwa matumizi Yake na utukufu

Wake!

52 • MATENDO

Majaribu si tishio.

KIBURI

HASIRA

HOFU

Nakala 16 / Nambari 1

Page 53: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

3. Kufuata Nafsi Ya Mungu

Kama tulivyoona, kuna kanuni nyingi na masomo mengi

ya kujifunza katika maisha na huduma ya Yesu. Kwa hakika,

hakuna mtu aliyefundisha kama Yeye (Luka 4:32). Yesu

alifanya ishara, maajabu na miujiza katika muda wote wa

huduma Yake - kiasi ambacho mtume Yohana alisema

kwamba ni vingi mno kabisa visiweze kuandikwa (Yohana

21:25)!

Kwa kuwa Yesu Kristo ni Yeye yule jana, leo na hata

milele (Waebrania 13:8), mambo aliyofanya wakati wa

huduma Yake hapa duniani yanaendelea kufanyika hata

leo. Matendo makuu na miujiza bado hufanywa na Roho

Mtakatifu, kwa njia ya viungo vya Mwili wa Kristo. Maana

yake ni kwamba huduma ambayo Yesu alianzisha alipokuwa

duniani, amewapa wafuasi Wake sasa waiendeleze (Matendo

1:1-8).

Bila shaka sisi hatukupewa utume Wake wa kufa

msalabani kwa ajili ya dhambi za binadamu. Ule ulikuwa

utume wa Kristo peke Yake. Wokovu wa milele unatokana na

dhabihu Yake tu (Matendo 4:12). Hakuna tunachoweza

kuongeza katika kazi ile kuu iliyokwisha timiziwa kabisa.

Sisi tunatakiwa tuipokee tu!

Mchungaji kwa Mchungaji: Tafadhali ufahamukwamba huduma ya Yesu haikukatishwa kutokana nakusulibiwa Kwake. Lengo kuu la utume wa Yesu hapaduniani lilikuwa kifo Chake msalabani kwa ajili yawokovu wa wanadamu wote. Wokovu huu ulitimizwakwa utukufu katika kifo Chake na kufufuka Kwakekulikofuata (Yohana 19:30; Waefeso 1:17-23; Wafilipi2:5-11; Waebrania 9:11-15).

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa uhakika kwambahakuna mtu aliyemwua Yesu kinyume cha mapenziYake. Bali, kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi zetukilikuwa sehemu ya makusudi ya Munguyaliyoandaliwa kwa ajili Yake (Yohana 1:29; 12:27;19:5-11; Matendo 2:22-24,33). Yesu alikubali nakutimiza kabisa utume huu.

Kazi Kubwa ZaidiSisi tuliopokea wokovu kwa Yesu Kristo tumepewa

huduma ya Yesu tuiendeleze, hata “mpaka mwisho wa nchi”(Matendo 1:8). Tumepewa Roho Mtakatifu atuwezeshe

tutimize amri hii yenye baraka.

Yesu alisema pia, “Amin, amin, nawaambieni, Yeyeaniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye nayeatazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwamimi naenda kwa Baba” (Yohana 14:12). Katika mstari huu,

tunaona wazi kabisa kwamba Yesu ametuita tuendeleze kazi

Zake.

Lakini ni lazima tufahamu kwamba maana yake si

kwamba kazi zetu kwa aina fulani zitakuwa kuu kuliko kazi ya

Kristo. Wala hatuwezi kamwe kupata kuwa sawasawa na Kristo

kwa njia yoyote (Mathayo 10:24-25; Yohana 13:16). Maana

Yesu peke Yake alikuwa na ndiye Mungu; na Yesu ni Mmoja

pamoja na Mungu Baba na Roho Mtakatifu (Yohana 10:30).

Yesu aliposema “kazi kubwa zaidi” alimaanisha kwamba

sisi tutafanya kazi yenye upana zaidi au matendo mengi zaidi.Muda wa huduma ya Yesu ulikuwa kama miaka mitatu na

nusu. Huduma yetu inaweza kuendelea katika maisha yetu

yote.

Huduma ya Yesu duniani ilifungiwa katika eneo dogo na

kati ya watu wachache. Ni ndogo kulingana na mamilioni ya

wafuasi wa Kristo tulioitwa tuende “mpaka mwisho wa nchi”(Matendo 1:8). Tumeagizwa “kuihubiri injili kwa kilakiumbe” (Marko 16:15) na “kuwafanya mataifa yote kuwawanafunzi” (Mathayo 28:19). Ndizo “kazi kubwa zaidi”

ambazo tutazifanya!

Habari Njema Kwa WoteImekuwa mpango wa moyo wa Mungu Baba kufikisha

wokovu kwa watu wote. Kwa njia ya kufa na kufufuka kwa

Yesu, mpango huu sasa unawezekana. Lakini hii Habari

Njema ya ajabu lazima itangazwe kwa mataifa yote

(Mathayo 24:14; Yohana 4:35). Watajuaje pasipo mtu wa

kuwaambia (Warumi 10:14-15)?

Ni wajibu wa kila mwamini kutangaza Habari Njema ya

wokovu katika Kristo kwa watu wote. Lakini ili tufanye

hivyo, tunahitaji nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu wa

Mungu!

Kwa uweza wa Roho Mtakatifu, “Atauhakikishaulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu”

(Yohana 16:8, usome ms. 7-11). Ni kwa njia ya Roho

Mtakatifu pia kwamba ishara na miujiza vilifanywa na

mitume wa kwanza (Matendo 2:43; 5:12; n.k.) Ishara hizi

hizi na miujiza hiyo hiyo vimeendelea kupitia kipindi kizima

cha Kanisa, navyo hupatikana kwetu leo (1Wakorintho

12:9-10).

Wachungaji na viongozi wa kanisa walio wengi leo wana

njaa ya kuona zaidi ya nguvu ya Mungu kwa wazi katika

huduma zao. Tunatamani kuwaona wagonjwa wakiponywa,

mapepo yakiondolewa, wafu wakifufuliwa - na zaidi - yote

kwa utukufu wa Yesu!

Matendo haya kwa hakika yanapatikana kwetu sisi kwa

uweza wa Roho Mtakatifu. Yesu alifanya matendo hayo

katika huduma Yake kwa Roho Mtakatifu (Matendo 2:22).

Naye ameahidi kwamba sisi pia tutazifanya (Yohana 14:12)

kwa Roho Mtakatifu yule yule (1Wakorintho 12:11).

Tunaweza na tunapaswa kutazamia - na kuaminia kwa

imani - kwamba Mungu atathibitisha mahubiri ya Injili kwa

nguvu ya kimwujiza katika huduma zetu (Marko 16:19-20).

Ndivyo atakavyofanya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,

kufuatana na mapenzi Yake. Haleluya!

Ishara Zinamwashiria MunguHapa inatubidi tuweke utaratibu wenye uwiano na

uangalifu. Lengo au shabaha ya huduma yetu isiwe kamwemiujiza, ishara na maajabu. Na mambo hayo yasije yawe

tamaa ya moyo wetu.

Ni kweli kwamba Mungu anafanya mambo mengi na

miujiza ya ajabu hapa duniani leo. Lakini je, kusudi la ishara

hizi, maajabu na miujiza vyote hivi vikuu?

“Ishara” au “ajabu” ni tukio lisilo la kawaida (tafadhali

soma zaidi kuhusu ishara na maajabu katika sehemu maalum

hapa chini). Mungu anatoa ishara kwa ajili ya kuvuta akili

zetu. Kwa mfano, kijiti kinachowaka moto nyikani huenda si

jambo la ajabu sana. Lakini kijiti kinapoendelea kuwaka

moto kwa muda mrefu pasipo kuteketea, bila shaka kinavuta

macho na akili yetu (taz. Kutoka 3:1-3)!

Lakini ishara ni zaidi ya tukio lisilo la kawaida. Kusudi

hasa la ishara na maajabu ni kwamba zinaashiria jambo

MATENDO • 53Nakala 16 / Nambari 1

Page 54: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

fulani. Lile lililoashiriwa na ishara au ajabu ndilo

linalothibitisha uhalisi wake.

Ishara na maajabu yote yanayofanywa na Roho

Mtakatifu daima na kila mara zitawaelekeza watu kwa

Mungu Baba au Mungu Mwana - Yesu. Ishara yenyewe si

“hatima” au lengo. Badala yake, ishara inatakiwa imwongoze

mtu afikie hatima.Mungu alivuta akili ya Musa kwa kutumia kijiti

kisichoteketea. Lakini alipokuwa amekwisha kuvuta akili

yake, Mungu alianza kujidhihirisha (Kutoka 3:4-6) pamoja

na kusudi Lake kwa ajili ya watu Wake (Kutoka 3:7 - 4:17).

Je, lipi lilikuwa muhimu zaidi? Kwamba Mungu alifanya

kijiti kisiteketee, au yale aliyofunua juu Yake Mwenyewe

pamoja na kusudi Lake?

Je, Injili Inahubiriwa Kwa Udhahiri?Msingi wa kupima ishara na maajabu, maneno ya

kinabii, maono, na matukio mengine ya kiroho kama haya, si

kwamba ni tofauti, isiyo kawaida au nje ya utaratibu wa

kimaumbile. Hata ibilisi anaweza kutumia hila afanye ishara

na maajabu yasiyo ya kimaumbile kiasi fulani (2Wakorintho

11:14). Kazi za Shetani za aina hii zitaongezeka tunapoingia

zaidi katika nyakati za mwisho (Mathayo 24:23-25;

2Wathesalonike 2:8-10; Ufunuo 13:13-14; 16:14; 19:20).

Ufalme wa mapepo utajaribu kufanya miujiza ya

uwongo ili kuwadanganya watu, ikiwavuta mbali na ukweli

wa Injili na Yesu akiwa njia pekee ya wokovu. Lakini hata

mfano huu wa kikano unaonesha kwamba ishara na maajabu

huweza kuvuta akili za watu.

Kwa hiyo, msingi wa kupima ishara na maajabu kwa

Roho Mtakatifu ni hii: Je, tukio hili linamtukuza Yesu? Je,

linawaelekeza watu Kwake? Je, linawaongoza wamwitikie

Yeye - kumpenda, kumwabudu, kumtii na kumfuata Yesu

Kristo? Je, Injili inahubiriwa kwa uwazi, ili wasiookolewa

wapate nafasi ya kutubu? Je, jina la Yesu linainuliwa kuliko

majina mengine yote? Ndiyo maswali tunayopaswa tuulize

tunapotafuta kupambanua na kufahamu hoja hii ya ishara na

maajabu.

54 • MATENDO

ISHARA, MAAJABU NA

MIUJIZA KUTOKA KWA MUNGU

NI VIZURI, NA TUTAZAMIE

KUVIONA LEO. Havikukoma wakati

wa kifo cha mitume wa kwanza (kama

100 b.K. hivi). Wala havikukoma

wakati Maandiko ya Agano Jipya

yalipothibitishwa (kutambuliwa rasmi

na uongozi wa Kanisa kwamba ni

maandiko ya mitume yaliyo na upuzio

wa Mungu kama 300 b.K.).

Roho Mtakatifu bado anatenda leo

kazi ambazo Yesu alianza kufanya

karibu miaka 2,000 iliyopita! “Yesu

Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata

milele” (Waebrania 13:8). Naye ndiye

aliyetuita sisi tuendeleze kazi Zake

(Yohana 14:12), kwa uweza wa Roho

Mtakatifu.

Lakini, pamoja na kwamba ishara,

maajabu na miujiza ni mambo ya

kusisimua sana, kuna mipaka kwa

utendaji wake. Tumekwisha ona

kwamba ishara zipo kwa ajili ya kuvuta

akili za watu. Nazo daima ziwaelekeze

watu kwa Yesu.

Hoja hii ni muhimu, kwa sababu

ishara na maajabu havisababishi “imani

iokoayo” ikue katika moyo wa mtu.

Imani inayotegemea ishara au mwujiza

tu itakuwa hafifu na haitadumu. (Kwa

kuona mfano wake, soma Yohana sura

ya 6, hasa mistari 14-15,26-35,60-64).

Hatimaye, ili aingie katika

wokovu, inambidi mtu achague

kuitikia ukweli wa Yesu Kristo

kwamba Yeye ni nani, na jinsi

alivyotenda msalabani kwa ajili yake.

Lazima amwamini Yeye, azitubu

dhambi zake binafsi, na ampokee Yesu

kama Bwana na Mwokozi wake.

Nafasi Ya Kwanza Ni Ya Yesu

Yesu, mapema katika huduma

Yake, alifahamu asili ya uovu na

uhafifu katika moyo wa binadamu

(Yeremia 17:9). Yesu hakujiachia au

"kujitoa" kwa watu waliomfuata

(Yohana 2:23-25). Alitambua kwamba

walikuwa na imani hafifu ya juujuu tu

iliyotokea “walipoziona ishara zake

alizozifanya” (ms. 23).

Miujiza, ishara na maajabu

zinazofanywa kwa uwezo wa Roho

Mtakatifu ni sahihi na zinakubalika.

Mungu anazitumia kuvuta akili za

watu. Lakini imani ya kudumu lazima

iwekwe juu ya msingi imara zaidi na

wa milele: Yesu Kristo!

Imani ambayo mtu ameweka juu

ya Yesu Kristo na dhabihu Yake kwa

ajili ya dhambi zake ni imani iliyo

imara, ya kudumu na ya kuokoa. Ndiyo

aina ya imani inayobadilisha maisha

ambayo itaendelea kuwa na nguvu na

kukua, ijapokuwa mapambano na

majaribu. Ndiyo aina ya imani

inayodumu katika maisha yote na

mpaka milele!

Roho Mtakatifu anatumia ishara,

maajabu na miujiza ili avute akili za

watu. Lakini anafanya hivyo ili

awafikishe kwenye nafasi ya kuchagua

kumwamini Kristo kwa wokovu.

Tuangalie mifano miwili ya hali hii.

Katika mfano wa kwanza (Yohana

9:1-41) Yesu alimponya mtu

aliyezaliwa kipofu. Mtu huyu

aliponywa, lakini ndipo Yesu

alipompatia nafasi ya kumwamini Yeye

(9:35-38).

Katika mfano wa pili (Matendo

13:4-12) Paulo alimkabili mchawi

mwovu. Chini ya upako wa Roho

Mtakatifu, Paulo alitamka hukumu ya

kinabii juu ya mchawi huyu (ms. 9-11).

Liwali (mtumishi wa juu katika

serikali) aliona tendo lile la uweza na

kuamini kwamba yale ambayo Paulo

alimfundisha kuhusu Kristo ni kweli

(ms. 12).

Utaona kwamba katika mifano

yote miwili, imani katika Kristo

haikutegemea ishara yenyewe. Msingi

wa imani ulikuwa kama walimwamini

Yesu Kristo ama sivyo (Yohana 9:35-38;

Matendo 13:12). Ishara zilisaidia tu

katika kuthibitisha ukweli na uwezo wa

Injili ya Yesu Kristo.

Kiongozi wa kanisa, ishara na

maajabu ziwe na nafasi katika huduma

yako. Lakini nafasi ya kwanza katika

mambo yote ni ya Yesu; mengine yote

yawaelekeze watu Kwake kwa urahisi

na uwazi mkubwa.

Yesu ndiye Mwokozi wao! Yesu ni

Bwana wao! Sifa na utukufu yote yawe

Kwake!

KUTAZAMA KWA KIFUPI ISHARA NA MAAJABU

Nakala 16 / Nambari 1

Page 55: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Hakuna Miungu MingineHapa tumefikia kanuni ya msingi mojawapo kwa ajili ya

kutembea, kutoa huduma, na kukua katika upako wa Roho

Mtakatifu:

Je, tunamtafuta Mungu kwa ajili ya yale

atakayotutendea? Au je, tunamtafuta kwa ajili Yake

Mwenyewe, na kwa hamu yetu ya kuwa na uhusiano na

Yeye - tukitaka tu kumjua na kumtambulisha kwa

wengine?

Tumethibitisha kwamba uweza wa Mungu hautengani na

nafsi ya Mungu. Upako wa Mungu ndiye Roho Mtakatifu

akifanya kazi ndani ya, na kupitia kwa, chombo cha

kibinadamu kilichojitoa Kwake.

Lakini inatokeaje wakati mtu fulani anapopoteza lengo

lake kwa Mungu, au kugeuza hamu yake ya mambo ya

kiroho mbali na Yeye? Tunaweza kuona matokeo yake kati ya

viongozi wa Wayahudi wakati wa Yesu.

Yesu aliwakabili viongozi hao waliotaka kumwua

(Yohana 5:16-18). Walikuwa watu wenye elimu ya hali ya

juu, lakini walikuwa wamepoteza njia yao ijapokuwa ujuzi

wao.

Yesu aliwakemea kwa ajili ya kupoteza lengo lenyewe la

masomo yao yote: “Mwayachunguza maandiko, kwa sababumnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; nahayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangumpate kuwa na uzima” (Yohana 5:39-40).

Viongozi hao wa Wayahudi walijua Maandiko. Lakini

walikuwa wamepoteza Neno Lililo Hai - Yesu, aliyekuwa

amesimama pale pale mbele yao (Yohana 1:1-5,14)!

Baadaye, Yesu aliwakemea tena viongozi wa dini kwa

ajili ya kutafuta ishara kila wakati, ingawa walikuwa

wamekwisha ona ishara nyingi (Mathayo 12:38-39). Na Yesu

aliwakemea mara ya tatu alipolenga upofu wa Mafarisayo,

waandishi na wanasheria waliokuwa wakidai hata ishara

nyingine (Mathayo 16:1-4).

Ndipo karibu na mwisho wa huduma ya Yesu, upofu wa

makusudi wa Mafarisayo uliokuwapo haujabadilika, Yesu

alitamka hukumu juu yao (Mathayo 23:37-39).

Hoja ya Yesu hapa ilikuwa nini? Kuna mambo mengi

tunayoweza kujifunza kutokana na makabiliano kati ya Yesu

na viongozi wa dini wa wakati Wake. Lakini hasa, Yesu

alikuwa akifunua kwamba Wayahudi walikuwa wakitafuta

yale ambayo walimtaka Mungu awatendee - lakini

hawakuwa wakimtafuta Mungu Mwenyewe!

Ndiyo sababu yao moja ya kumkataa Yesu kama Masihi.

Hakuwapa lile walilolitaka, yaani kwamba Yeye aanzishe

Ufalme wa duniani wakati ule ule ambamo Mafarisayo,

waandishi na wanasheria wangekuwemo kati ya viongozi

wenye heshima. Walitamani nguvu, utawala na utajiri.

Walikuwa wameridhia nafasi zao, vyeo vya heshima na

daraja ya juu katika jamii (Mathayo 6:2,5-6,16-18; 23:2-7;

Yohana 12:42-43; n.k.). Walikuwa wamepoteza lengo kabisa,

wakijifikiria wenyewe tu. Yesu, bila shaka, alihukumu

msimamo huu wa kujiendeleza na kiburi cha kidini.

Viongozi wa dini walikuwa wamesahau ukweli wa

kimsingi kuhusu Mungu ambaye walidai walimtumikia.

“Usiwe na miungu mingine ila mimi... kwa kuwa mimi,Bwana, Mungu wako , ni Mungu mwenye wivu” (Kutoka

20:3,5).

Mungu ana wivu wa haki kwa ajili ya upendo na uchaji

wetu. Kwanza, kwa sababu Yeye peke Yake katika maumbile

yote anastahili upendo wetu na ibada yetu. Pili, kwa sababu

Mungu ni mwumbaji wetu na kuwepo kwetu kama

wanadamu hutokana na Yeye (Mwanzo 1:26-28; 2:18-25;

Yohana 1:3). Tatu, kwa sababu alimtoa Mwana Wake

atukomboe - sisi ambao Yeye alitupenda kwa ukamilifu wote

- kutoka katika dhambi na mauti (Wakolosai 2:11-15;

1Yohana 4:9-10).

Ukweli huu umethibitishwa tena katika Agano Jipya:

“Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuonawivu” (Yakobo 4:5). Neno hili limetamkwa kwa Wakristo wa

awali waliojaribu kumtumia Mungu atimize tamaa zao

binafsi (Yakobo 4:1-4).

Hao wameitwa “wazinzi... adui wa Mungu” (ms. 4) kwa

sababu walikuwa wakiasi uhusiano wao takatifu wa kujitoa

kwa Mwokozi wao ili wafuate starehe za mwili zinazopita

haraka za dunia.

Lakini hata hapo Mungu hakuwatupa. Bali aliwatamani

kwa wivu, kwa sababu Yeye peke Yake aliwapenda katika

ukweli. Mungu atampokea tena mzinzi anayetubu kwa kweli

(Yakobo 4:6-10).

Ni wazi, basi, kwamba ni lazima tusivunje upendo wetu

na huduma yetu kwa Mungu kwa kupendezwa na mambo

yoyote mengine.

Ujiepushe Na MivutoKatika nafasi yetu kama wachungaji na viongozi katika

Mwili wa Kristo, awepo Mmoja tu anayepokea uaminifu,

utiifu, hamu na tumaini kutoka kwetu - Yesu!

• Si ishara, maajabu wala miujiza

• Si huduma kubwa, au watu walio nayo

• Si karama, wito, ujuzi, nafasi au cheo

• Si hata baraka Zake

Imesemwa kwamba mara nyingi vizuizi vikuu kwa

waamini ni baraka ambazo Mungu anawapatia watu wake.

Kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu usikivu wetu na hamu zetu

zinaweza kusogezwa mbali na Mungu kwa urahisi, na

kulenga baraka Zake badala ya Yeye Mwenyewe. Mioyo yetu

ina ubinafsi wa kudanganya (Yeremia 17:9). Hata kama

tumeokolewa, bado tuna mwelekeo kuendea dhambi

(1Yohana 1:8).

Mchungaji kwa Mchungaji: Rafiki na kiongozi wakanisa, tafadhali uelewe kwamba si kosa kutaka uwepowa upako wa Roho Mtakatifu umiminwe juu yako na juuya huduma yako. Ni hamu kuu ya Mungu kwamba uwenao!

Lakini tusipokuwa na hekima na uangalifu, mioyoyetu inaweza kupotoshwa. Katika hamu yetu yaufanisi katika huduma, tunaweza kuanza kulenga yaleambayo Mungu anaweza kututendea, badala yaupendo wetu Kwake kwa ajili Yake Mwenyewe.

Polepole na kwa ndani, tunaweza kuvutwa mbali,na badala ya kutafuta uwepo wa Mungu kuliko sahihi,kuonea njaa yale anayoweza kututendea. Ndivyoilivyokuwa kwa Mafarisayo. Walishikilia ujuzi waokuhusu Mungu badala ya kuwa na uhusiano halisi wakutii pamoja na Mungu. Walijua mengi kuhusuMaandiko na mambo ya dini, lakini hawakumjua Yeye.Hawakumtamani Mungu Mwenyewe, bali walitafutayale aliyoweza kuwatendea.

MATENDO • 55Nakala 16 / Nambari 1

Page 56: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Viongozi fulani leo, badala ya kuvutwa kwa Mungu,wanavutwa kwa matukio yasiyo ya kimaumbile ambayomara nyingi hufuatana na kazi ya Roho Mtakatifu. Haoni kama mtu anayetaka kuoa (au kuolewa na) mtu tajirikwa sababu ya utajiri wake. Wanatamani utajiri wahuyu mtu na mambo ambayo utawatendea kulikokumtamani yule mtu. Huu ni mwelekeo wa kutisha waubinafsi mtupu!

Tunapotamani maajabu, upendo wetu kwa MunguMwenyewe unaweza kunajisiwa - na hata kupoa kamabarafu (Mathayo 24:12). Hali hii inafanana namsimamo wa yule Simoni mchawi, aliyetafuta uwezowa miujiza wa Roho Mtakatifu kwa faida yake binafsi(Matendo 8:9-24).

Mungu wetu anatuonea wivu sisi. Anatamaniuaminifu, upendo na uchaji wetu kwa sababu Yeyeanatupenda kwa upendo wa milele (Warumi 5:5;1Yohana 3:1). Yeye anawatafuta watu waliotoa moyowao wote Kwake Yeye Bwana. Ni kwa kuwapitia watotoWake wanaompenda kwamba anaweza kujidhihirishakwa njia za nguvu (Danieli 11:32).

Wito Wetu Wa KwanzaMara nyingi katika Maandiko, tunahimizwa tutafute

“uso” wa Bwana (2Nyakati 7:14; Hosea 5:15; Zaburi 27:8;

n.k.). Uso wa Mungu unavyotajwa katika Maandiko

humaanisha Nafsi ya Mungu, moyo Wake, uwepo Wake.

Lakini hakuna popote katika Maandiko ambapo

tunahimizwa tutafute “mkono” wa Mungu. “Mkono” wa

Mungu, au “Mkono wa Bwana”, humaanisha kazi Zake,

matendo Yake, baraka Zake. Tunaona matokeo ya kazi ya

Bwana (mkono Wake) katika mambo anayotenda. Na si kosa

kutaka kuona matokeo haya katika huduma yetu na kuipitia.

Lakini tafadhali ufahamu:

Tunapotafuta uso wa Mungu (moyo Wake, Yeye

Mwenyewe) ndipo tunapotambua mapenzi ya Mungu na yale

anayotaka kufanya.

Tunapofuata na kutii mapenzi Yake, ndipo tutaonamkono mkuu wa Mungu kwa Roho atendaye kazi!

Kumtafuta Mungu, na uhusiano wetu na Yeye, lazima kuwe

kipaumbele chetu cha kwanza. Kutoka hapa ndipo mambo

yote ya thamani yatakapotokea.

Wana Wa Kweli, Watumishi Wa KweliYesu alisema, “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami

nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtuakinitumikia, Baba atamheshimu” (Yohana 12:26).

Angalia kwamba katika mstari huu, Yesu ana nafasi ya

kwanza. Yesu ndiye Bwana wa Kanisa (Waefeso 1:22); sisi

tunatakiwa tumfuate Yeye. Si kwamba Yeye anatufuata katika

huduma abariki yale tunayomwomba ayabariki.

Wito wetu wa kwanza kama viongozi wa kanisa ni

uhusiano wa kila siku wa kumtafuta Bwana - kumjua,

kumpenda, kumwabudu, kuongea na Yeye (Zaburi 63:1-8).

Ni kutoka mahali hapo ndipo tutakapotambua mapenzi Yake

ya kweli na mipango Yake kwa ajili ya maisha yetu, huduma

zetu na mambo mengine yote.

Mungu anataka kumimina baraka Yake, upako Wake,

ishara na maajabu Zake juu ya Kanisa Lake, na juu yako

wewe kama kiongozi Wake uliyeitwa.

Lakini je, anaweza kukuamini na haya? Je, una upevu,

uthabiti wa tabia na hekima, uwe mwaminifu kwa Yeye peke

Yake?

Mungu ameahidi kutoa zaidi ya “mkono Wake” kama

mioyo yetu ni mali Yake peke Yake. “Kwa maana macho yaBwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshemwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyokuelekea kwake” (2Nyakati 16:9).

Yeye anataka mioyo yetu kwa wivu wa haki, kwa sababu

anatupenda kwa upendo Wake wa milele (Warumi 8:31-39).

Mchungaji kwa Mchungaji: Mungu anakupendakabisa na pasipo masharti yoyote! Haidhuru upungufuwako, anakupenda kwa ndani, katika nafsi yako na kwamilele. Wewe hukuumbwa kwa ajili ya utumishi nahuduma tu.

Kama Mungu angalitaka watumishi wengi zaidi,angaliumba malaika wengi zaidi. Lakini alikuumbawewe kwa sababu alitaka wana wa kiume na wa kikewanaotembea katika uhusiano na Yeye. Malaikahawawezi kuwa na uhusiano huu pamoja na Mwumbajiwao - sisi wanadamu peke yetu tunaweza kuwa nauhusiano huu (Waebrania 2:14-18; 1Petro 1:12).

Kristo hakutoa uhai Wake ili uwe katika huduma.Alikufa awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zako, ili uwezekurejeshwa katika uhusiano na Mungu.

Sisi si watumishi tu wa Bwana. Sisi ni rafiki waKristo (Yohana 15:15) na warithi pamoja na Yeye(Warumi 8:17). Sisi ni wana wa Mungu aliye Hai(Warumi 8:15-16). Tuna heshima na nafasi yakumtumikia Bwana na Mwili Wake kutokana na upendowetu na shukrani yetu Kwake.

Mbele Zake Kila SikuUpako wa Roho Mtakatifu unahusiana moja kwa moja

na kipaumbele chetu cha kutafuta Uwepo wa Mungu kila

wakati. Mfalme Daudi ambaye Bwana alimtaja kuwa “mtuanayeupendeza moyo wangu” (Matendo 13:22), anatupatia

maelekezo kwa ajili ya uhusiano wetu na Mungu:

“Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wanguumekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta” (Zaburi 27:8).

Maana ya “kutafuta” ni kufanya bidii pasipo kuchoka wala

kuachia mpaka tuone lile tunalotafuta. Yesu aliongea kuhusu

kanuni hii pia (Mathayo 6:33; 13:44-46; Luka 11:9-13).

Kumtafuta Mungu kunahitaji muda na bidii. Huenda

itatupasa tuache starehe, heshima au shughuli fulani. Lakini

ni kwa kumtafuta Mungu kwamba tunapata kumfahamu.

Kutokana na uhusiano huu wa karibu na Yeye, tunaanza

kutambua mapenzi Yake kwa ajili ya maisha yetu na huduma

zetu. Tunapotembea katika kutii mapenzi Yake, anafungua

upako Wake juu yetu na kupitia kwetu.

Tuweke kipaumbele chetu cha kwanza kabisa katika

nafasi ya kila siku ya kukaa mbele za Bwana. Ndipo

tunapopokea yale yaliyo ya milele hasa, ambayo

hayatapungua wala kuchakaa (Luka 10:38-42). Uamue leo,

na kila siku: “Uso wako, Bwana, nitautafuta.”

MarejeoTukimaliza sehemu hii, “Kukua Katika Upako”,

tafadhali kumbuka kwamba kila mmoja wetu anaweza na

anapaswa akue katika uwezo wa upako wa Roho Mtakatifu.

Waliomo ni pamoja na wewe (kama mchungaji na kiongozi)

- na watu unaowaongoza!56 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 57: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Wewe una wajibu kama mchungaji msaidizi (1Petro

5:2-4) wa watu wa Mungu. Hizi ni pamoja na kuhakikisha

kwamba kila mtu unayemwongoza anakua katika ufahamu

wake wa Neno la Mungu na kukua pia katika uwezo wake wa

kutoa huduma katika upako wa Roho Mtakatifu. Ndio

utaratibu wa ki-Maandiko kwa ajili ya kukua kwa afya katika

Mwili wa Kristo (taz. Waefeso 4:11-16, hasa ms. 12).

Njia ya kukua katika upako huenda ni tofauti na

ulivyotazamia. Turudie kanuni za msingi zilizo lazima kwa

ajili ya kukua katika upako:

• Utakaso

• Udhaifu wa ki-Mungu

• Unyenyekevu

• Utiifu kwa mamlaka

• Miitikio sahihi kwa majaribu

• Moyo kwa ajili ya Mungu peke Yake

• Kutembea na kukua katika uhusiano wetu na Mungu kila

siku

Yesu alikuwa mfano wetu wa tabia au kanuni hizi zote.

Yeye alikuwa Mtu mwenye upako zaidi ya wote wengine

waliotembea duniani. Anatukaribisha tufuate nyayo zake

kwenye njia ya upako wa Mungu. Tunapofanya hivyo,

tutapokea fungu litoshalo kabisa la vyote tunavyohitaji ili

tutimize wito mkuu wa Bwana kwetu!

C. KUPOKEA UPAKO WAKE

Nilikuwa mmoja wa timu ya viongozi wahudumu katika

Mkutano wa Wachungaji nchini Cuba. Karibu na mwisho wa

Mkutano, nafasi ilitolewa ya kusikia shuhuda za watu

waliohudhuria. Bwana mmoja mzee, mdhaifu na kipofu,

alisaidiwa alipokuja polepole mpaka kwenye jukwaa.

Ndugu huyu mzee alianza kutoa ushuhuda wake kwa

kueleza kwamba alikuwa amemtumikia Bwana kwa maisha

yake yote; ndugu zake pia walikuwa wakimtumikia Bwana.

Aliambia umati wa watu kuhusu makanisa mengi aliyokuwa

ameanzisha katika maisha yake, yakiwemo makanisa sita

mapya aliyoanzisha katika mwaka ule!

Aliongea kuhusu kuwa kipofu na jinsi ilivyokuwa

vigumu, hasa alipomhitaji mtu mwingine amsomee Biblia

kila siku.

Ndipo alitulia kwa dakika moja na kuinamisha kichwa

chake. Kundi la wachungaji zaidi ya 1,000 lilinyamaza.

Ghafla, yule mzee aliinua mikono yake katika ishara ya

ushindi na kupaza sauti yake: “Nimepoteza macho yangu,

lakini sijapoteza moto!” Kundi lile zima lilishangilia na

kumtukuza Mungu.

Je, nini ingemwezesha mzee wa miaka 76 aendelee kuwa

na “moto” - aendelee kuhubiri, kufundisha, kufanya uinjilisti

na kuanzisha makanisa? Upako wa Roho Mtakatifu tu,

pamoja na kujitoa kwa yule mzee atumiwe na Mungu kwa

ajili ya makusudi Yake na utukufu Wake!

Hazina Katika Chombo Cha UdongoNi tumaini langu kwamba Mungu atanitumia kwa ufanisi

kila siku mpaka atakaponichukua katika nyumba ya

mbinguni. Lakini hatuhitaji muda mrefu katika huduma

kutambua kwamba kule kutumika kunaweza kuchosha na

kutaabisha katika maeneo yote - kimwili, kiakili, kihisia na

kiroho.

Hali hii si ubaya mtupu, kwa sababu tunatakiwa tusiwe

na ubinafsi katika karama, nguvu na upako wa Mungu.

Tunatakiwa tutoe wakati wote yale ambayo Mungu

ametupatia. Tena tunatakiwa tusiwe wavivu au wazembe

katika huduma (Luka 9:62; Mhubiri 9:10; Wakolosai 3:23),

bali tunatakiwa tufanye bidii zote kwa ajili ya Kristo.

Lakini tukichoka kupita kiasi, “kuungua” au kutaabika

mno, matatizo makubwa yaweza kutokea. Mungu anajua

kwamba sisi tuna mipaka kwa nguvu yetu. Kwa hiyo anataka

kutupa nguvu, hekima, neema, vipawa na uwezo ili tuweze

kufanya mapenzi Yake - nasi tunahitaji sana hivi vyote.

Maana pasipo Yeye hatuwezi kufanya lolote (Yohana 15:5).

Paulo alifahamu haja hii alipoandika: “Lakini tunahazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu yauwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu” (2Wakorintho

4:7). Akiwa mtume mwenye mazoea mengi na ujuzi mwingi,

Paulo alijua kuwa nguvu na bidii ya kufanya mapenzi ya

Mungu havimo katika maumbile ya binadamu. Bali “hazinahii” ndani ya “vyombo vya udongo” vya maisha yetu -

ambayo inatupa mahitaji yetu yote - ni upako wa Roho

Mtakatifu! (Soma 2Wakorintho 3:1-4:18.)

Yeye Anatujazia Kila TunachohitajiMadai ya huduma (au hata kuishi tu kama Wakristo

katika dunia ya leo) yanaweza kutuondolea uwezo na nguvu

ya Mungu. Yesu Mwenyewe alihitaji kuburudishwa kiroho,

akihudumiwa na Roho wa Mungu.

Tukisoma Injili kwa makini tutaona mara nyingi ambapo

Yesu aliondoka akaenda kusali katika mahali peke Yake (kwa

mfano, Luka 4:42; 5:16; 6:12). Baada ya vipindi hivi vya

sala, Yesu alifanya kazi kwa nguvu, kufikia maamuzi

muhimu katika huduma Yake, kuandaliwa kwa ajili ya

kustahimili majaribu, n.k.

Tunafunuliwa nini katika mfano wa Yesu? Ili tujibu

swali hili, tuangalie sehemu mbili za Maandiko.

1. Mjazwe!

“Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; balimjazwe Roho” (Waefeso 5:18).

Kuna hoja tatu muhimu zinazotokana na lugha ya asili ya

Kiyunani katika maneno haya “Mjazwe Roho”.a. Neno lipo katika wakati wa sasa. Maana yake ni

tendo linalofanyika sasa na kuendelea kufanyika. Kwa hiyo

maana ya “Mjazwe Roho” ni kwamba tuendelee kujazwa

wakati wote na Roho Mtakatifu. Hii ni habari njema kweli!

Kuendelea kujazwa ni kwamba hatujazwi mara moja tu, bali

tena na tena!

Tunampokea Roho Mtakatifu tunapookolewa (Warumi

8:15-16; Waefeso 1:13-15). Huu ni upako wa kawaida

unaotolewa kwa waamini wote (1Yohana 2:20,27).

Tunapoitwa kifalme kwa ajili ya kazi za huduma, Mungu

anatuongezea upako wa mara kwa mara utakaotusaidia

kufanikiwa katika kazi ile.

Mungu anatupatia katika Nafsi Yake, uweza Wake na

karama Zake. Lakini tunavyovitoa hivi katika huduma,

tunaweza kufikia utupu au upungufu wa kiroho. Kwa hiyo

Mungu amewezesha kujazwa kwetu na Roho Wake

Mtakatifu tena na tena, kila mara tunapohitaji!

Kujazwa tena na tena kunaonekana wazi katika huduma

ya watu Kanisani kwa awali. Kitabu cha Matendo ni

kumbukumbu za matokeo yale:

MATENDO • 57Nakala 16 / Nambari 1

Page 58: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

• Petro alijazwa ahubiri Injili na kutetea imani (Matendo

4:8).

• Wanafunzi walipokea ujasiri na nguvu kuhubiri Injili,

ingawa waliteswa (Matendo 4:31).

• Paulo alijazwa na Roho Mtakatifu mara ya kwanza

(Matendo 9:17) na kujazwa tena alipokuwa akabiliane na

nguvu za mapepo (Matendo 13:9).

• Baada ya kupambana na viongozi wa dini, wanafunzi

walijazwa tena na Roho Mtakatifu (Matendo 13:42-52).

• Stefano alijazwa, na kujazwa tena (Matendo 6:5; 7:55).

• Barnaba pia alijazwa mara ya pili (Matendo 13:52).

Kurudia kujazwa na Roho Mtakatifu kulileta nguvu

kubwa kwa mahubiri na mafundisho ya wanafunzi hao.

Kutangaza Injili kwao kwa ujasiri kulifuatana na ishara na

maajabu (Matendo 5:12).

Huenda watu wengine wanaamini kwamba miujiza hii

ilitokea kupitia kwa mitume wa awali tu. Lakini Kitabu cha

Matendo kinatufunulia kwamba ishara na maajabu za Roho

Mtakatifu zilitolewa kupitia mtu yeyote aliyechaguliwa na

Yeye.

Kwa mfano, Stefano, aliyepewa kazi ya kuhudumu

mezani (Matendo 6:8) na “ndugu” (Matendo 14:1-7) waliona

miujiza katika huduma zao. Paulo anaandika kwamba Roho

Mtakatifu anaweza kufanya kazi kupitia yeyote ambaye Yeye

amemteua ili ampe uwezo na kumwongoza (taz.

1Wakorintho 12:1-11).

Kuongezewa Kwa KutoaKuna baraka ya nyongeza ya kujazwa kila wakati na

Roho Mtakatifu. Tunavyopata bure, tunatoa bure (Mathayo

10:8) na uwezo wetu wa kupokea upako Wake kwa wingi

zaidi unaongezwa! Kanuni hii ya Ufalme wa Mungu ni ya

kweli katika mambo ya fedha, muda, huduma na maeneo

mengine - zaidi tunayotoa, ndivyo tunavyopewa zaidi.

Tunakua kila mara tunapotoa huduma, tukiwatolea

wengine uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu. Ndipo sisi

tunaweza kupokea zaidi, na kuwa na zaidi tena ya kutoa.Mtindo huu uliobarikiwa wa kupokea na kutoa,

kupokea na kutoa tena, ni baraka kwa wote wanaohusika.

Mungu anabarikiwa na kutukuzwa kwa sababu mapenzi

Yake yanatimizwa. Viungo vya Mwili wa Kristo

hubarikiwa, na kukua katika kuwa wanafunzi wenye nguvu

(Waefeso 6:12-16). Wewe, kama mhudumu, unabarikiwa -

ukiwa mtumishi wa Bwana uliye na nguvu na uaminifu,

ukitimiza wito Wake na kukua katika uwezo wako wa kutoa

katika huduma na kupokea zaidi kutoka kwa Roho

Mtakatifu!

Haya yote yanategemea kujazwa na Roho Mtakatifu -

mfululizo. Utaratibu huu ni tofauti na ule wa kupokea karama

ya kifalme ya Roho Mtakatifu wakati wa kuokolewa, au

baadaye kubatizwa na Roho Mtakatifu (Matendo 8:14-17;

19:1-7). Tunapaswa tuishi katika hali ya kuendelea kujazwa

na Roho Mtakatifu, tena na tena!

b. Maneno yale “Mjazwe Roho” (Waefeso 5:18) ni ya

kiamri. Maana yake ni kwamba ni amri, si pendekezo!

Mungu anajua vizuri zaidi sana kuliko sisi jinsi tunavyohitaji

nguvu na uwezo Wake. Kwa hakika tunamhitaji Roho

Mtakatifu ili tuishi kama washindi katika maisha ya kila siku.

Lakini hata zaidi, tunahitaji uwepo unaofurika wa Roho

Mtakatifu ili tuzae matunda na kufanikiwa katika huduma.

Mungu anapotoa amri, daima ni:

• ya haki na maana;

• kwa ajili ya utukufu Wake;

• kwa ajili ya ufanisi wetu;

• yenye kuwezekana kwa utoaji Wake!

Mungu, kwa mapenzi Yake ya kifalme, ametuwezesha

kuwa na ukarimu wa Roho Mtakatifu usio na kipimo. Naye

ameamuru kwamba tuendelee kujazwa na utoaji Wake wa

Roho Mtakatifu. Haleluya!

Hii ni amri ambayo tunapaswa kukimbilia kuitii kila

siku, na katika kila dakika ya haja.

c. Maneno haya pia ni katika hali ya kutendewa.

Maana yake ni kwamba kule kujazwa kila wakati kwa upya

na Roho Mtakatifu si tendo tunalofanya sisi. Hatuwezi

kustahili wala kufanya kazi ili tujazwe. Ni karama ya Mungu

kwetu. Sisi tunaweza kufungua mioyo yetu tu na kupokeayote anayotaka kutukirimia.

Hata hivyo, inatubidi tuwe katika nafasi ya kupokea!

Huu ni ufunguo wa msingi wa kuishi maisha ya kujazwa

Roho na kuwa na huduma ya kujazwa Roho.

Je, umewahi kujiuliza kwa nini watu fulani wanaonekana

kujazwa Roho Mtakatifu wakati wote, wakitumia karama,

hekima, uwezo, n.k. - wakati watu wengine hawafanyi

hivyo?

Njia ya kujiweka katika nafasi ya kujazwa mfululizo na

Roho Mtakatifu wa Mungu ni kujisalimisha. Maana yake ni

kwamba mambo yote katika maisha yako yametolewa na

kusalimishwa kwa Mungu - mapenzi yako, mipango yako,

madhaifu yako na hasa, nguvu zako. Ukifanya hivyo,

umejitoa kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na mapenzi Yake

kwa ajili yako.

Kusalimisha maisha yetu kwa Roho Mtakatifu

kunatuweka katika nafasi ya kiroho ya kupokea kwa uhiari na

uhuru zaidi yale anayotaka kutupatia.

Lakini tafadhali ieleweke kwamba kusalimisha maisha

yetu kwa Roho Mtakatifu si sawa na kupagawa. Ni mapepo

na mashetani tu wanaojaribu kutawala mapenzi na nafsi ya

mtu katika kumpagaa (Luka 8:29-38a). Viongozi wa

madhehebu ya dini za uwongo huenda pia wanajaribu

kutawala au kutiisha watu wengine, kwa sababu wanatenda

katika udanganyifu wa kishetani.

Sisi hatukuitwa tuwe “wanasesere” wanaoongozwa kwa

kamba pasipo akili wala uwezo wowote wa kuchagua. Bali

sisi tumeitiwa uhusiano wa upendo, kuaminiana na

kushirikiana na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Yeye

amekuja afanye kazi ndani yetu, kutubadilisha na kututakasa;

na kufanya kazi kupitia kwetu kama vyombo vya huduma

vya Bwana Mungu. Tunapotoa maisha yetu kwa Mungu na

kazi Yake kwa njia hii, tutakaa katika nafasi ya kupokea

ujazo mpya wa kufululiza wa upako.

Mchungaji kwa Mchungaji: Sisi kama wana waBaba yetu wa mbinguni, tuongozwe na Roho Mtakatifu(Warumi 8:14). Neno “kuongozwa” katika mstari huu nila wakati wa sasa wa kuendelea. Kwa hiyo tunapaswatuongozwe mfululizo.

Huku kuongozwa mfululizo na Roho Mtakatifu nipamoja na kufahamu kimasomo amri na kanuni zaMaandiko - na utiifu wetu kwazo - ingawa si hivi tu. Hiini njia ya msingi ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, kwakuwa Mungu amekwisha kutufunulia katika Neno Lake

58 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1

Page 59: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

jinsi tunavyopaswa kuishi siku kwa siku.Lakini kuongozwa mfululizo na Roho Mtakatifu

humaanisha pia kusitawisha usikivu wetu kwamaelekezo Yake, yanayoweza kutujia saa yoyote.Roho Mtakatifu anaweza kukuelekeza kuhusu hudumayako, maisha yako binafsi, hitaji fulani la mtu mwingine,au mambo mengine mengi. Yeye yupo wakati wotepamoja nawe ili akuongoze katika maisha haya. RohoMtakatifu atakusaidia pia ujue jinsi ya kushirikiana naYeye katika kuhudumia mahitaji ya watu wengine.

Ikiwa elekezo fulani limetoka kwa Roho Mtakatifu,litakuongoza daima kutii amri na kanuni za maadili zaNeno la Mungu lililoandikwa. Ukijisikia kuongozwa naRoho Mtakatifu kufanya badiliko kubwa au kufanyatendo lisilo la kawaida kwako; ni bora kufuata maagizoya Maandiko na kuwatafuta washauri wa kirohowaliopevuka (Mithali 11:14; 24:6). Wao wanawezakusaidia kuthibitisha kwamba lile unalosikia kwelilimetoka kwa Roho Mtakatifu - au kushauri kwambasivyo. Kufanya hivyo kutakusaidia kujilinda na kupotokaau kudanganyika.

MuhtasariTumejifunza kanuni tatu muhimu kuhusu maneno ya

Biblia: “Mjazwe Roho” (Waefeso 5:18).

• Tunaweza kujazwa mfululizo, zaidi ya kujazwa mara ya

kwanza.

• Inatubidi tujazwe, kwa sababu Mungu ametuamuru

hivyo.

• Tunaweza kupokea ujazo na upako wa Roho Mtakatifu

kupitia Kwake tu - ni karama kutoka Kwake ambayo

tunajiweka katika nafasi ya kuipokea kwa kusalimisha

maisha yetu Kwake.

2. Umtafute Mungu!

Huenda unajiuliza sasa, “Nifanyeje ili nipokee ujazo huu

mpya (upako) wa Roho Mtakatifu wa Mungu? Niende mahali

fulani maalum? Niseme maneno maalum? Nimtafute mtu wa

kuniombea? Je, inanibidi nihudhurie mikutano maalum?”

Mistari ifuatayo ya Maandiko inatuonesha jinsi na lini

tunaweza kupokea upako zaidi wa Roho Mtakatifu. Yesu

alisema hivi: “Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwakuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; nayeabishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba,ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe ausamaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwombayai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuakuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbingunihatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”

(Luka 11:9-13).

Katika mistari hii, Yesu ametupatia maelekezo rahisi

sana jinsi tunavyoweza kujazwa kwa upya, tena na tena, na

Roho Mtakatifu.

a. Tunatakiwa tuombe, tutafute na tubishe. Mungu

ndiye Mtoaji wa Roho Mtakatifu (ms. 13). Agizo katika

mstari huu la kumfuata Bwana - kuomba, kutafuta, kubisha -

limeandikwa katika wakati wa sasa katika lugha ya

Kiyunani.

Maneno haya maana yake ni kuendelea kufanya hivyo,

hata sasa. Tunatakiwa tuendelee kuomba, tuendelee kutafuta,

tuendelee kubisha - mpaka tunapopokea jibu kutoka kwa

Bwana anayetupenda.

Tumeahidiwa, “Kila aombaye hupokea; naye atafutayehuona; naye abishaye atafunguliwa” (ms. 10). Haleluya!

Mungu anafurahia kumimina Roho Wake juu yetu; kwetu si

zaidi ya kumwomba Yeye.

Yesu alitoa mifano mitatu ya kumfuata Roho Mtakatifu -

kuomba, kutafuta, kubisha. Siyo kwamba anatufunulia njia

au mitindo mitatu tofauti. Bali anatuhimiza tumfuate Mungu

kwa bidii na kwa unyofu.

Unaona kwamba hakuna kuombaomba wala kujaribu

kuthibitisha ustahili wako wa kupokea. Bidii hizi hazihitajiki;

tena ni mielekeo inayoweza kuziba njia yetu ya kupokea kwa

imani kama wana wa Mungu wapendwao.

b. Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya wana (wa kiume

na wa kike). Watu ambao ni wana wa Mungu, waliofanywa

hivyo kwa kuzaliwa upya (Yohana 1:12-13; 3:5-8)

hawalazimiki kuombaomba kwa Baba yao wa mbinguni

anayewapenda, kwa ajili ya baraka Zake alizowaahidi.

Yesu amefunua ukweli huu mkuu katika mfano wa jinsi

sisi kama wazazi tungeitikia watoto wetu (ms. 11 na 12).

Ndipo Yesu anaendelea kulinganisha nafasi yetu kama

wazazi na nafasi ya Mungu kama Baba yetu wa mbinguni

(ms. 13).

Halafu Yesu anatofautisha asili yetu yenye dhambi na

mipaka, na ukamilifu na upendo wa Mungu usio na mipaka.

Ikiwa sisi tulio wazazi “waovu” (wenye dhambi)

tusingewanyima watoto wetu vipawa vizuri, kwa nini tuwaze

kwamba Baba yetu wa mbinguni aliye mkamilifu na

mtakatifu angewatendea watoto Wake namna hii? (Kwa zaidi

kuhusu moyo wa Mungu kwetu, soma Warumi 5:6-10;

8:31-39; 1Yohana 3:1; 4:10,12-19.)

Sisi si waombaomba wanaolazimika kumsihi na

kumbembeleza Mungu asiyetaka kusikia. Sisi ni wana wa

Mungu Aliye Juu, naye anafurahia kutujaza Roho Wake

Mtakatifu.

Kwa kweli inatupasa tuombe kwa unyenyekevu na kwa

kutoa maisha yetu kabisa. Lakini sisi, kama watoto Wake,

tunaweza “kukaribia kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewerehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”(Waebrania 4:16; taz. pia Waefeso 3:12; Waebrania

10:19-22).

c. Kuna nini inayoweza kutuzuia tusipokee? Yapo

matatizo yanayoweza kutuzuia tusijazwe Roho Mtakatifu

mfululizo.

1) Kuwepo kwa dhambi au kuridhiana katika maisha

yetu (Warumi 6:12-14; 1Wakorintho 5:6-7). Biblia

inafundisha kwamba hatutakuwa huru kabisa na dhambi kwa

wakati wa maisha haya (1Yohana 1:8). Sisi sote tutakuwa na

vipindi vya kushindwa, ambavyo inatubidi tuvitubu kwa

haraka na kupokea msamaha wa Mungu.

Lakini ni lazima tusijiruhusu kuridhiana mfululizo na

dunia, mwili, na ibilisi. Biblia huwaita watu wenye

mwenendo huu “watendao” dhambi kama kawaida au wakati

wote (Wagalatia 5:21). Maana yake ni kufanya dhambi kama

mazoea au kwa kurudiarudia.

Dhambi ya kufululiza kama hii itatufanya tusifae kama

vyombo vya matumizi ya Bwana (1Wakorintho 9:24-27;

2Timotheo 2:19-21). Mungu wetu ni Mungu Mtakatifu

anayetuita sisi pia tuwe watakatifu, kwa uweza wa Roho

MATENDO • 59Nakala 16 / Nambari 1

Page 60: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Wake na neema Yake vikifanya kazi ndani yetu (1Petro

1:13-19).

Roho, ambaye ni mtakatifu (Warumi 1:4), hutaka

kutumia vyombo vitakatifu kwa kazi Yake.

2) Kuwepo kwa nia au motisha za kujitumikia, kama

ubinafsi au kiburi (Mathayo 7:21-23; Wafilipi 2:3-4;

1Timotheo 6:3-5). Tumekwisha jifunza kuhusu dhambi ya

kiburi na hatari zake. Kama viongozi wa kanisa, tunapaswa

tufanane na Yesu, aliye “mpole” na “mnyenyekevu”

(Mathayo 11:29).

Mungu hatawatia upako watu wanaotoa huduma kwa

motisha au nia zisizo halali (Yakobo 4:6). Lazima turuhusu

mioyo yetu ichunguzwe na Roho Mtakatifu (Mithali 16:2) na

kusafishiwa tamaa yetu ya kutukuzwa wenyewe. Ifuatayo ni

mistari fulani ya Biblia ambayo usome na kutafakari:

2Nyakati 16:9; Mithali 13:10; 16:5,18; Mathayo 23:8-14;

Wagalatia 5:20; Wafilipi 1:15-16; 1Timotheo 3:6; Yakobo

3:14 - 4:4.

3) Kutokusalimisha maisha yako yote (Warumi

12:1-2; Wagalatia 2:20). Nimekwisha andika kuhusu

umuhimu wa kusalimisha maisha yako yote kwa Mungu.

Lakini nitilie mkazo kwamba upako wa Roho Mtakatifu

unatolewa ili mtumishi wa Mungu aliyejisalimisha awe na

uwezo katika utumishi na kwa ajili ya utumishi. Kama

tunatamani uwezo wa Mungu kwa sababu yoyote nyingine

ila tu kumtumikia Yeye na watu, hatuwezi kutazamia upako

Wake katika maisha yetu.

Utumishi wetu uliosalimishwa uongozwe na Mungu,

kwa sababu Yeye anajua jinsi ya kututumia kwa ubora katika

Mwili wa Kristo. Huenda sisi hatutapewa nafasi ya kuchagua

yale tutakayomfanyia Mungu kazi. Mioyo yetu hupaswa

itamani kutenda lolote ambalo Yeye atatuagiza.

Nafasi yetu ya kujisalimisha kikamilifu ni ya lazima ili

tupokee uwezo kutoka kwa Mungu na pia tufahamu mapenzi

Yake. Ndipo inapotubidi tuchague kumtii Yeye. Ndivyo

tunavyoweza kuzaa matunda halisi katika utumishi.

4) Imani dhaifu au inayokosekana (Waebrania 11:6;

Yakobo 1:6). “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikiahuja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Lazima tujifunze

kutoka Maandiko yale ambayo Mungu ametuandalia, ama

sivyo imani yetu itakuwa dhaifu.

Ulipofuata masomo haya ya ki-Biblia ya upako,

umejifunza kwamba uwezo wa Roho Mtakatifu unapatikana

leo kwa ajili yako. Wala si kidogo tu, kama tone la maji

jangwani. Roho Mtakatifu atatiririka kupitia kwako kama

MITO (Yohana 7:37-39)!

Mungu ni Baba mwenye upendo, anayefurahi kuwapa

watoto Wake uzima na uwezo. Lakini inatubidi tuombe kwaimani, tukimtegemea aitikie kilio cha mioyo yetu (Zaburi

138:3).

Kama una mashaka kwamba imani yako ni dhaifu au

ndogo, kumbuka Yesu alivyosema kuhusu imani: “...Mkiwana imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu,Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwakoneno lisilowezekana kwenu” (Mathayo 17:20b).

Yesu alieleza kwamba imani yetu inaweza kuwa ndogo,

lakini bado ina ufanisi - KAMA imeelekezwa kwa Mungu!

Inatubidi tusijiamini wenyewe, wala kutegemea kiasi cha

imani tulicho nacho. Tunapaswa kuweka imani yetu katikaMungu na Neno Lake. Maana Yeye anayoahidi, atatenda!

Tunaweza kutegemea kwamba Yeye atatimiza Neno Lake, na

kwa hiyo tunaweza kumwekea kikamilifu imani yetu.

Kwa hiyo, uimarishe imani yako katika Neno la Mungu.

Uamini yale yaliyofunuliwa katika Neno kuhusu Yeye aliye

Mwumbaji, Mwokozi na Mfalme wako! Umwendee mara

nyingi, tafuta uso Wake - naye atakuitikia (Yeremia

29:11-13).

5) Ukosefu wa njaa ya kiroho (Zaburi 63:1-2; 84:1-2;

Mathayo 5:6; Yohana 6:35,48; 7:37-39). Mungu daima

anaitikia njaa ya kiroho ya kupata zaidi ya Yeye.

Ukosefu wa njaa ya kiroho unaweza kusababishwa na

mambo mengi, kwa mfano:

• Msiba, huzuni au mauti (kama ya ndugu wa karibu)

inayosababisha uzito wa kihisia au kiroho

• Kuvunjika moyo, kushindwa au kuchoka,

kunavyokufanya ukate tamaa au kupoteza motisha ya

kumtafuta Bwana

• Hasira, uchungu au kutokusamehe wengine - akiwemo

Mungu na hata wewe mwenyewe - vinavyozimisha

hamu yako ya Mungu

• Raha na starehe za dunia hii, au uvivu na kinaya,

vinavyoziba au hata kuangamiza njaa yenye haki kwa

ajili ya kupata zaidi ya Mungu

Maisha ya hapa duniani huweza kuwa na ugumu na

hamasa nyingi za kushinda. Lakini tunaweza kutiwa moyo

kwamba Mungu ameandaa njia za kuvuka huzuni, maumivu

moyoni, kushindwa au vingine vyovyote ambavyo

tumeviona. Uponyaji na ukombozi wa Mungu, upendo na

msamaha Wake, rehema na neema Yake - na upako Wake -

vyote ni vyetu kama tutamjia Yeye Mwenyewe tu.

Mtume Paulo ametufunulia jinsi yeye alivyovuka

mambo ya dunia ambayo vingaliweza kumzuia asimtafute

Mungu wala kumwonea njaa ya kiroho. Aliwaandikia

Wafilipi (3:12-14): “Si kwamba nimekwisha kufika, aunimekwisha kuwa mkamilifu...” (ms. 12a). Paulo alitambua

kwa unyenyekevu udhaifu wake na kushindwa kwake.

60 • MATENDO

KizuiziKinachoua

UKAMILIFU WA MUNGU

DHAMBI

Nakala 16 / Nambari 1

Page 61: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

“...la! bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lileambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Yesu Kristo...”(ms. 12b). Paulo alijua kwamba ilikuwa lazima asikate

tamaa; ilimbidi aendelee, kwa ajili ya Injili.

“Ndugu, sijidhanii kwamba nimekwisha kushika...”(ms. 13a). Paulo hakufahamu mambo yote, yakiwemo yote

yaliyokuwa yamemtokea yeye.

“...ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyonyuma...” (ms. 13b). Paulo alifanya uamuzi wa kuachia

maumivu au maudhi, kushinda au kushindwa - yote

yaliyokuwa yamekwisha pita.

“...nikiyachuchumilia yaliyo mbele...” (ms. 13c). Paulo

alichagua kuachia mambo ya zamani, na badala yale

kuchuchumilia makusudi ya Mungu kwa ajili yake.

“Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwitomkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (ms. 14). Paulo aliamua

kuendelea kumtafuta Mungu, na mapenzi Yake, haidhuru nini

ingemtokea.

Kupitia kila aina ya upinzani na mateso, kila furaha na

ushindi, Paulo alimfuata Bwana kwa moyo wake wote.

Kuchimba udongo usiozaa wa mioyo yetu (Hosea 10:12) si

kazi fupi au rahisi. Lakini kama tutajitoa kwa wazi kwa

Mungu - Yeye aliyetuumba, aliyetuokoa, na anayetupenda -

tunaweza kupokea moyo mpya na njaa mpya kwa ajili ya

Bwana (Ezekieli 36:26-27).

d. Lazima tumngojee Bwana. Maandiko yanatuhimiza

mara nyingi “kumngoj(e)a Bwana” (Zaburi 25:5; 27:14;

37:7,9,34; Isaya 30:18; 40:31; Maombolezo 3:25-26; n.k.).

Hii ni kanuni muhimu kwa maisha ya Kikristo. Kuna baraka

daima zinazotokana na kumngoja Bwana.

Lakini mara nyingi si asili yetu kungoja. Tunahamaki,

kuogopa au kusahau. Maisha yetu ya shughuli nyingi, kazi ya

huduma, mkazo tunaotiliwa kufikia uamuzi - mambo mengi

yanatukandamiza na kuchukua nafasi yetu.

Lakini kuna ukweli wa wazi, ingawa unaumiza, katika

maisha yetu: utayapatia yale yaliyo muhimu kwako nafasisikuzote. Inasikitisha kwamba mara nyingine hatutambui nini

ni muhimu hasa mpaka tumekwisha chelewa.

Mchungaji kwa Mchungaji: Ni muhimu kuchukuamuda mara kwa mara kutathmini vipaumbele vyetu,kuchunguza maisha yetu na kutafakari shughuli zetuzote. Halafu tuviweke hivi vyote mbele za Bwana,kutafakari Neno Lake, na kuamua kama vipaumbelevyetu vinalingana na Vyake.

Ikiwa hamasa ya Maandiko ya kuchukua muda wa“kumngojea Bwana” haina nafasi ya juu katika orodhayetu, inabidi ipatiwe nafasi hii. Maana mara nyingindiyo njia pekee ambayo kwayo tutamsikia Yeyeakisema nasi.

Kumkaribia MunguIli tupokee zaidi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu,

lazima tuiombe. Na halafu lazima tumngojee Bwana.

Wakati tunapongoja, ni rahisi zaidi sana kusikia “sautindogo, ya utulivu” (1Wafalme 19:12). Kungoja kunampatia

Roho Mtakatifu nafasi ya kushughulikia mioyo na maisha

yetu, akituandaa ili tupokee zaidi ya uwepo na uwezo Wake.

Huenda atafunua kizuizi au kipingamizi cha kupokea kwetu;

anaweza atuthibitishie (dhambi); anaweza kutufundisha au

kutuelekeza; na zaidi.

Mara nyingi wakati wa kusubiri kwa uvumilivu ndipo

kazi ya kubadilishwa inapotendeka katika maisha yetu.

Tunavyobadilishwa, tutapokea; tunavyopokea zaidi ya

Roho Wake, bila shaka tutazaa matunda zaidi katika

huduma yetu.

Faida nyingine kubwa ya kumngojea Bwana ni kwamba

vipindi vya kukaa pamoja na Yeye vinatufikisha karibu na

Yeye Mwenyewe zaidi na zaidi. Tunapata kumfahamu kwa

ndani zaidi na kinafsi zaidi sana.

Unapomngojea Bwana, huenda utataka kunyamaza

(Zaburi 46:10). Au unaweza kusali kwa utulivu katika lugha

yako ya kiroho, au kuabudu kwa sauti ndogo (1Wakorintho

14:2,15). Lakini kumbuka, kusudi kuu la kungoja ni

kusikiliza na kupokea. Mara nyingi njia bora ya kufanya

hivyo ni katika hali ya utulivu na ukimya.

Katika njaa yako ya zaidi ya Mungu, huenda sala zako

zitaongeza sauti. Si lazima hali hii ni mbaya. Lakini

ukumbuke kwamba huna haja ya kuthibitisha hamu yako

wala ustahili wako kwa sauti kubwa ya sala zako; wala huna

haja ya kumpigia Mungu kelele ili aweze kukusikia na

kukujibu.

Badala yake, uamini ahadi Yake: “Je! Baba aliyembinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu haowamwombao” (Luka 11:13).

UsiogopeWengine huenda wataogopa kwamba kumngoja Bwana

kwa ajili ya kupokea zaidi ya Roho Mtakatifu kungeleta pepo

mchafu badala ya Yeye. Hii haiwezekani! Kwanza, mapepo

wanaweza kuingia mahali walipokaribishwa tu, au kwa

sababu ya mtu kushiriki mambo ya ushirikina au uchawi.

Kama unamwomba Bwana na hamu yako ni kwa ajili ya

Yeye peke Yake, hakuna pepo mchafu anayeweza “kupenya”

ndani yako. Usiogope hili kamwe!

Ufalme wa mapepo unatambua kwamba jinsi

unavyopokea zaidi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyozidi

kutembea katika uwezo wa Mungu. Maana yake ni kwamba

ujasiri wako na mamlaka yako katika mambo ya kiroho

vitaongezeka kama mfuatano. Kwa hiyo ibilisi huenda

atakazana kukujaribu au kukugeuza mbali na nafasi ya

kumtafuta Bwana.

Lakini ukumbuke: Wewe ni mtakatifu uliyenunuliwa na

kutakaswa na damu ya Yesu Kristo. Shetani na mapepo yake

hawana nguvu juu yako ambayo wewe hukuwapatia

mwenyewe. Ibilisi alishindwa msalabani (Wakolosai

2:14-15). Kwa hiyo chukua silaha zako na upanga wako

(Waefeso 6:10-18) na kusimama imara katika Roho

unapomkaribia Mungu (Yakobo 4:7-8).

e. Upokee upako wa Roho Mtakatifu kwa imani. Sisi

ni wana wa Mungu na warithi wa ahadi Zake (Warumi 8:17;

2Wakorintho 1:20; Wagalatia 3:26). Hii ni pamoja na ahadi

ya kuja kwake Roho Mtakatifu (Matendo 2:38-39).

Tumejifunza kwamba si hoja ya kujazwa mara moja tu, bali

ni kujazwa mfululizo na uwepo na uwezo Wake katika

maisha yetu (Waefeso 5:18). Yale ambayo Mungu ameahidi,

atatimiza - kwa hiyo wewe umwombe tu!

Kwa hiyo tuombe - na kuendelea kuomba, kutafuta na

kubisha mpaka tuwe tumekwisha pokea (Luka 11:9-10).

Mungu anakutakia uwe na Roho Mtakatifu kwa ukamilifu

(Luka 11:13). Ufungue moyo wako na kumwamini Yeye

MATENDO • 61Nakala 16 / Nambari 1

Page 62: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

pamoja na hamu Yake ya kukujaza - wakati unapomngojea

kwa subira (Waebrania 11:6).

Kuomba tujazwe kwa upya kunaweza kufanyika kila

siku, kwa sababu tunapaswa tujazwe mfululizo! Tunahitaji

uwezo na uwepo Wake, dakika kwa dakika, katika mambo

yote tunayofanya.

Pokea TuTunapokea kwa imani, si kwa hisia. Tunatafuta

mgawanyo wa Roho Mtakatifu, si tukio la kihisia.

Unapoomba, unaweza kukalisha mwili katika hali yoyote

inayokusaidia kutulia - kuketi, kusimama, au kulala chini.

Unaweza kuwa ndani ya mahali pako pa kusali, au jikoni,

katika chumba cha kulala, kanisani au nje. Hali ya mwili na

mahali ulipo si muhimu kama uwazi wa moyo wako na hamu

yako ya kupokea.

Unapoomba kujazwa Roho Mtakatifu kwa upya, utumie

maneno yaliyo moyoni mwako. Hakuna njia ifaayo au

isiyofaa ya kumwomba Mungu. Anataka kusikia kutoka

kwako, hivi ulivyo.

Huenda ungeomba namna hii: “Njoo Roho Mtakatifu,

ninafungua moyo wangu nipokee zaidi ya Wewe.

Ninasalimisha moyo wangu na maisha yangu Kwako.

Nakuomba unijaze kwa upya. Jaza maisha yangu na uwepo

Wako. Jaza kinywa changu na sifa kwa Mungu. Jaza huduma

yangu na uwezo Wako, ili niwe chombo kinachomfaa

Mungu....” Tumia maneno yako na kufungua moyo wako

kwa Mungu. Omba upokee! Ujazwe, katika Jina la Yesu!

Haleluya!

MwishoNdugu na dada zangu, watenda kazi wenzangu katika

mashamba ya Mungu, na washiriki wenzangu katika huduma

ya kiutumishi kwa ajili ya Injili - sisi tuna wito wa hali ya juu

kabisa! Tunayo heshima ya kutumikia Mwili mpendwa wa

Kristo (Kanisa Lake), sisi ambao Petro atuambia

“mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha audhahabu... bali kwa damu ya thamani, kama yamwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa” (1Petro 1:18-19).

Huu ni wito ambao hatuwezi kujaribu kutimiza kwa

uwezo wetu binafsi, tena ni lazima tusijaribu kufanya hivyo.

Tumshukuru Mungu, Yeye ametupatia yote tunayohitaji ili

tuzae matunda kamili, tuwe na ufanisi kamili, na tumtukuzeYeye kikamilifu!

Tulianza masomo haya kwa Neno la Mungu:

“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi”

(Zekaria 4:6)

Mungu, katika karne zote, amekwisha tenda mambo

makuu ya ajabu sana. Lakini bado kuna mengi zaidi kabisa

ambayo ameahidi kutenda, yatakayotendeka!

Kuna “kazi kubwa zaidi” za kufanywa - miujiza, ishara

na maajabu kwa ajili ya utukufu wa Yesu (Yohana 14:12). Na

Mungu anataka kuyafanya kupitia Kwako! Bwana anataka

utangazaji wa ujasiri wa Injili, kuongoka kwa waliopotea

kwa Kristo na kujengwa kwa Kanisa Lake. Anatamani haya

kwa ajili ya kanisa LAKO, jiji LAKO, taifa LAKO! Utukufu

kwa Mungu!

Mungu daima anawatafuta watakaosalimisha maisha yao

yote kwa mapenzi Yake. Anawatafuta ambao mioyo yao ina

uaminifu Kwake, ambao anaweza kuonesha nguvu Yake

kupitia kwao. Anawaitikia wale wanaomtamani kuliko yote

mengine, na ambao wanaruhusu njaa yao Kwake iongezeke -

wale watakaosema kwa ujasiri “Mimi hapa! Nitume mimi”(Isaya 6:8)!

Kuna njia moja pekee ya kutimiza wito wa Mungu na

mapenzi Yake kwa ajili ya maisha na huduma yako - kwa

upako wa Roho Mtakatifu! Ni kwa uweza wa Roho

Mtakatifu kwamba utapokea mabadiliko, karama na vipawa

vilivyo lazima ili uwe na utende yote ambayo Mungu

anatamani kwako. Na haya yote ni yako kwa kuyaomba tu!

Mungu atakupa Roho Wake kwa wingi kabisa; uamini

hili, upokee upako Wake, utembee na kutoa huduma ndani

yake. Unapotoa uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu katika

kuwahudumia wengine, Yeye atakuwa na zaidi ya kumimina

ndani yako na kupitia kwako.

Bwana akubariki na kukufungulia macho yako ya kiroho

ufahamu ukweli Wake. Upokee neema Yake na msaada Wake

ili umtii katika mambo yote. Akutie mafuta ya upako Wake

kwa wingi mwenyewe na katika huduma yako, ili maisha ya

wengine yabadilishwe na kuwa utukufu Kwake Yeye

aliyekufa ili awaokoe. Na Mungu apokee sifa yote, utukufu

wote, heshima yote anayostahili kutokana na maisha na

huduma yako unapotembea na kukua katika upako wa Roho

Wake Mtakatifu. Ninaomba haya mbele za Baba, katika jina

lenye nguvu na uweza la Yesu Kristo Mwokozi wetu. Amina!

62 • MATENDO

Kuna njia moja pekee ya kutimiza

wito wa Mungu na mapenzi Yake kwa

ajili ya maisha na huduma yako - kwa

upako wa Roho Mtakatifu! Ni kwa

uweza wa Roho Mtakatifu kwamba

utapokea mabadiliko, karama na

vipawa vilivyo lazima ili uwe na

utende yote ambayo Mungu anatamani

kwako. Na haya yote ni yako kwa

kuyaomba tu! Mungu atakupa Roho

Wake kwa wingi kabisa; uamini hili,

upokee upako Wake, utembee na

kutoa huduma ndani yake. Unapotoa

uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu

katika kuwahudumia wengine, Yeye

atakuwa na zaidi ya kumimina ndaniyako na kupitia kwako.

Angalizo la Mhariri: Tafadhali angalia ukurasa ufuatao kwaajili ya maelezo jinsi unavyoweza kupata toleo lijalo ya Gazetila MATENDO kwa haraka zaidi katika mtandao wa Internet,kwa anwani ya www.world-map.com.

Nakala 16 / Nambari 1

Page 63: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

MATENDO • 63

1. Je, wakati umefika kwamba unapaswa kujiandikisha upya? Angalia tarehe kwenye kibandiko chako cha anwaniambayo ni tarehe ya mwisho wa kuandikishwa kwako.

2. Kama tarehe hii ni CHINI YA MIEZI SITA kutoka sasa huu ni wakati wa kujiandikisha kwa upya!3. HUTAKIWI kujiandikisha baada ya kupokea kila toleo la MATENDO: unapaswa kujiandikisha kwa upya ikiwa TU muda

wa miaka mitatu umekwisha pita au muda huu utakwisha katika miezi sita ijayo.

UNAWEZA KUJIANDIKISHA UPYA KWA "INTERNET ONLINE" AU KWA KUTUMA BARUA YA POSTA YA KAWAIDA.• Kwa kujiandikisha upya online, utume email kwa: [email protected] na kufuata maelekezo haya:1. Kuharakisha kazi, andika "Ufanye upya kibali changu cha MATENDO" kwenye “Subject Line” ya barua pepe yako.2. Utume jina lako la kwanza na jina la mwisho, na utume pia namba yako ya kutumiwa MATENDO kutoka kwenye

kibandiko chako cha anwani yako. Ukifanya hivyo utaharakisha sana utekelezaji wa kukuandikisha upya. Kuna watuwengine ambao majina yao yanafanana. Ukitupatia namba yako ya kibandiko, tutaweza kuona na kushughulikia habarizako kwa haraka na usahihi.

3. Kama unabadilisha anwani yako, ututumie jina lako, namba ya kibandiko, anwani YA ZAMANI na anwani MPYA.Ukiandika anwani mpya utumie utaratibu wa kawaida wa nchi yako, kama vile sanduku la posta, mji, mkoa, na nchi.

4. Ingiza maelezo mengine yanayotakiwa kwenye fomu hapa chini. Tafadhali ujibu maswali yote. (Tafadhali usitume"Attachment" yoyote. Hatufungui “Attachments”.)

5. Ili upewe kiungo cha barua pepe cha kuweza kupokea MATENDO kwa njia ya Internet, utupatie pia anwani yako yabarua pepe. Hakikisha imeandikwa kwa usahihi. (Hata hivyo utapokea nakala yako ya MATENDO kwa njia ya Postapia, baadaye.)

• Kwa kujiandikisha kwa njia ya posta, kata fomu hapa chini au inakilishe kwenye karatasi nyingine.1. Fuata maagizo YOTE kwenye fomu hii (chora mviringo kwa Ndiyo au kwa Hapana).2. Ujibu KILA swali kwenye fomu hii tumia herufi kubwa zinazosomeka vizuri.3. Ili upewe kiungo cha barua pepe cha kuweza kupokea MATENDO kwa njia ya internet, andika anwani yako ya barua

pepe kwa usahihi ukitumia HERUFI KUBWA. 4. Tuma fomu hii kwa: WORLD MAP ACTS INDIA, P.O. Box 1037 Kilpauk Chennai, 600010 T.N. India; au World MAP,

P.O. Box 721, Arusha, Tanzania; au kwa makao makuu ya Marekani; au kwa tawi lililo karibu na wewe (tazama orodhaya anwani hapo chini).

ANGALIZO: Gazeti la Matendo linatolewa pasipo malipo kwa viongozi wa kanisa katika Asia, Afrika naMarekani Kusini (ambao wanawafundisha au kuwahubiria watu wasiopungua 20 kila juma) ambaowameomba walipokee. Kiongozi wa kanisa angalia: Utapokea MATENDO kwa miaka mitatu; ndipo utahitajikujiandikisha upya ili ulipokee tena kwa miaka mitatu mingine. Gazeti la MATENDO si “Masomo kwa njiaya posta”. Hutapokea “cheti” au “diploma” baada ya kusoma MATENDO. Ni tumaini letu na sala yetukwamba utapokea kilicho na thamani kubwa zaidi sana: Mafundisho yenye msingi katika Biblia namafunzo kwa ajili ya utendaji wa huduma yako! Hivyo vitakuandaa uwe na ufanisi mwingi zaidi katikakuwafundisha, kuwahudumia na kuwashuhudia watu wengine.

1. Kwa kuwa muda wangu wa kupokea Gazeti la MATENDO utakwisha katika miezi sita ijayo, ninahitajikujiandikisha upya. NDIYO HAPANA

2. Namba yangu ya kibandiko cha MATENDO ni ___________ Tarehe ya mwisho wake ni ______ / ______3. Mimi ni mtenda kazi wa kanisa katika Asia, Afrika au Marekani Kusini, na ninahubiri au kufundisha watu wa-

siopungua 20 kutoka katika Biblia kila juma (Ni LAZIMA hoja hii iwe ya kweli ili uweze kupokea maandikoyetu.) NDIYO HAPANA

4. Je, unayo nakala ya kitabu cha Fimbo ya Mchungaji? NDIYO HAPANA5. Je, unaomba nakala ya kitabu cha Fimbo ya Mchungaji sasa? NDIYO HAPANA6. Je, unataka kupewa kiungo cha barua pepe cha kupokea toleo lijalo la MATENDO litakapokuwa tayari?

NDIYO HAPANA7. TAFADHALI ANDIKA MAJINA YAKO YOTE KWA HERUFI KUBWA PAMOJA NA ANWANI YAKO HAPO

CHINI. JE, ANWANI HII NI MPYA? NDIYO HAPANA

Jina langu la Ukoo (la mwisho): ___________________ Jina la ubatizo (la kwanza):____________________Anwani yangu ya posta: ___________________________________________________________________Mji/Jiji _______________________________________ Mkoa (kama inahitajika)______________________Nchi yangu ___________________________________ (Namba ya jiji kama ipo)_______________________Nafasi, madaraka au cheo changu katika kanisa ________________________________________________Sahihi yangu _____________________ Anwani yangu ya barua pepe: ____________________________8. Je, mafunzo ya toleo hili la MATENDO yamekuwa: _______ rahisi kuelewa _____magumu kuelewa

_______ yamenisaidia _____hayakunisaidiaUkitumia karatasi nyingine au kwa barua pepe kwa [email protected], unaweza kutushirikisha ushuhuda wako au maoni yako

kuhusu jinsi mafundisho ya MATENDO au Fimbo Ya Mchungaji yanavyokusaidia.

UTUME FOMU HII KWA: WORLD MAP ACTS INDIA, P.O. Box 1037 Kilpauk Chennai, 600010 T.N. India;

POST BOX 721 ARUSHA, TANZANIA (au kwa anwani nyingine hapa chini kama ni karibu zaidi na kwako): au World MAP Head Office, at World MAP, 1419 N. San Fernando Boulevard, Burbank CA 91504 USA

KUJIANDIKISHA UPYA / KUOMBA KITABU CHA FIMBO YA MCHUNGAJI (Viringisha Ndiyo au Hapana kwenye maswali hapo chini)

SW 0108

* *

TU

MIA

HE

RU

FI K

UB

WA

ZIN

AZ

OS

OM

EK

A V

IZU

RI

* *

MUHIMU • UJIANDIKISHE KWA UPYA KWA NJIA YA MTANDAO NA BARUA PEPE! • MUHIMU

Uwe kati ya viongozi wa kwanza watakaopokea toleo lijalo la MATENDO - online!Fuata maelekezo hapa chini kwa "kujiandikisha" ili uweze kupokea Gazeti la Matendo kwa njia ya "internet".

Nakala 16 / Nambari 1

Page 64: TOLEO LA KISWAHILI Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO · 2018-10-05 · Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu umefungiwa mipaka

Fimbo Ya Mchungaji hujulikana kwa

wengine kama "Shule ya Biblia katika

Kitabu" iliyo kamili kabisa. Kina kurasa 1000

na kimeandaliwa kwa ajili ya kuwafunza na

kuwaandaa viongozi wa kanisa. Ndani yake

kuna maandiko yenye upako wa Roho na

msingi wa ki Biblia, ya waandishi wengi.

Kitabu hiki kiliandaliwa kwa ajili ya

mahitaji maalum ya viongozi wa

kanisa wanaofanya kazi katika

Asia, Afrika na Marekani Kusini.

Kama wewe ni msomaji mpya

wa MATENDO na hujapokea nakala ya

Fimbo Ya Mchungaji, uombe nakala

yako sasa.Yaliyomo ndani ya “Fimbo Ya Mchungaji”:[1] Kitabu Kidogo cha Malezi ya Waamini Wapya chenye masomo yote unayohitaji ili uwafundishe

waongofu wapya.[2] Mwandani Wa Biblia yenye orodha ya maelfu ya mistari ya Biblia inayohusiana na hoja 200

kubwa za Biblia.[3] Mwongozo Wa Kufunza Viongozi wenye masomo bora yote yaliyokusanywa na World MAP kwa

muda wa miaka thelathini iliyopita.Yote haya na mengine yamo katika kitabu kimoja kiitwacho Fimbo Ya Mchungaji.Ili upokee nakala yako ya kitabu hiki chenye nguvu kubwa, Fimbo Ya Mchungaji, unahitaji kuiombakwa njia ya INTERNET kwa kutumia anwani www.world-map.com au ujaze kwa makini fomu yamaombi nyuma ya ukurasa huu (au unaweza kuandika maelezo yote kwa HERUFI KUBWA kwenyekaratasi nyingine kama hutaki kukata gazeti lako). Ukiwa umejibu maswali yote na kuandika maelezoyako kwa usahihi, utume fomu kwa Ofisi ya World MAP iliyo karibu na wewe. (Anwani zipo chini yafomu yenyewe.) Kama unaweza kutumia INTERNET, hutahitaji kununua stempu! Utapokea nakalayako ya Fimbo Ya Mchungaji mapema iwezekanavyo (lakini kwa kuwa vifurushi na barua za postahuchukua muda mrefu mara nyingi, tafadhali uache miezi sita au hata zaidi kwa ajili ya kupokea nakalayako ya Fimbo Ya Mchungaji). Asante.

For private circulation • Kwa wahusika binafsi tu

Tafadhali u

ombe

kitabu cha

Fimbo

Ya Mchung

aji

kama tu

hujakipoke

a.

ANGALIZO KWA VIONGOZI WA KANISA:

Je, unachimba ndani zaidi katika Maandiko kwa

kutumia Fimbo Ya Mchungaji, zana ya World MAP

ya kufanya wanafunzi iliyo na nguvu kubwa?

Fimbo Ya

Mchungaji

Biblia