146
Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu muongoza wa somo Muandishi: Tammie Friberg Mchora Picha: Beutyani Mimi Cheung Mfasiri: Alfred Mtawali Wahariri: David Sikolia

Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

  • Upload
    others

  • View
    31

  • Download
    4

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Uanafunzi UnaozingatiaJinsi Watu Wanavyouona

Ulimwengumuongoza wa somo

Muandishi: Tammie FribergMchora Picha: Beutyani Mimi Cheung

Mfasiri: Alfred Mtawali Wahariri: David Sikolia

Page 2: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Maandishi ya Bibilia yote yametolewa kwa Manukuu yafuatayo:UBS Habari NjemaNeno, International Bible Society

Hakimiliki © 2007 Tammie Friberg and Beutyani Mimi CheungCopyright © 2007 Tammie Friberg and Beutyani Mimi Cheung. All rights reserved. Permission is freely granted to copy and use the text of this curriculum or the pictures without alteration for the purpose of evangelism and discipleship to further the Kingdom of God, as long as any copies are disseminated freely in a not-for-profit manner and are not part of any endeavor intended for commercial gain.

Page 3: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Yaliyomo

Utangulizi

Masomo Ya Uanafunzi:

1 Mungu Na Uumbaji Wake Wa Kiroho

2 Mungu Na Uumbaji Wake Wa Vitu Vionekanavyo

3 Jinsi Mungu Anavyowasiliana Na Watu

4 Sheria Za Mungu Kwa Ajili Ya Maisha: Amri Kumi

5 Sifa Za Dini Za Uongo

6 Kupima Kila Kitu Katika Mizani Ya Neno La Mungu

7 Falme Mbili

8 Kuhamishwa Kutoka Katika Ufalme Mmoja Hadi Mwingine

9 Upatanisho

10Kukua Kiroho Na Vita Vya Kiroho

11Uwakili

12Mambo Yajayo

Page 4: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

UtanguliziIkiwa maisha yako yangefananishwa na jengo fulani, je ungeweza kuyaelezeaje maisha yako? Hebu jiulize swali hili: Umejenga nyumba yako wapi?—umeijenga katika njia gain na kwa msingi gain? Je, umeijenga vipi? Umeijenga itumike kwa njia gain? Je, umeijenga kwa kuzingatia vigezo gain? Je, umeijenga impendeze nani? Je, umeijenga kwa kutumia nyenzo gani? Je, ulizitoa wapi nyenzo hizo ulizotumia kujengea nyumba? Je, nyenzo hizo zilikuwa na sifa gani, na zilikuwa za aina gani? Katika kujenga nyumba hiyo, ni kina nani waliokusaidia? Ni wazazi, viongozi wa kanisa, marafiki, jamaa, watu usiowajua, Mungu, Yesu, au Roho Mtakatifu? Je, kwa sasa bado unajenga nyumba hiyo, au unawasaidia wengine kujenga nyumba zao? Unaona itakuchukua muda gani kumaliza nyumba unayoijenga? Je, itakubidi kufanya ukarabati fulani au kujenga mahali pengine? Maswali haya yanaweza kuonekana kuwa ya kidunia, lakini katika hali ya kiroho, maswali haya yote yanahusiana na maswala ya uanafunzi.

Kwa mfano, Siku moja Yesu alitoa fumbo juu ya wajenzi wawili; mwenye busara na mjinga. Katika fumbo hilo, yule mjenzi mwenye busara alijenga nyumba yake juu ya mwamba hivi kwamba upepo mkali ulipopiga nyumba hiyo na mafuriko yalipoikumba, iliweza kusimama imara. Lakini yule mjenzi mjinga hakujenga nyumba yake kwenye mwamba. Kwa hiyo upepo na mvua vilipoipiga ile nyumba, ilianguka kwa kishindo kikubwa. Yesu alitumia fumbo hili ili kufundisha umuhimu wa kuyajenga maisha yako juu ya msingi wa Ukweli Wa Neno La Mungu-ambaye ni Yesu. Yesu anasema kwamba nyumba hii ilijengwa kwa kuzingatia msingi uliopo kati ya binadamu na yeye; na ilistahili kujengwa kwa kufuata mafundisho ya Yesu. Je, wewe umeijenga nyumba yako ya kiroho kwa njia gani?

Katika fumbo hili Yesu alikuwa anazungumzia swala la uanafunzi. Uanafunzi unajumuisha kujifunza kibinafsi/kujenga kiroho; na kujifunza kwa kushirikiana na wengine/kujenga pamoja. Hebu tuchukue muda na kuangalia familia zetu, vikundi vya kujifunza Biblia, makanisa, makanisa, miji, nchi, na ulimwengu kwa jumla. Yesu alipokuwa akiwapa wanafunzi wake wito mkuu, alisema hivi, “Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.” (Mathayo 28:18-20). Yesu hakutuachia jukumu la kujenga maisha yetu juu ya msingi wa mafundisho yake, bali pia jukumu la kuujenga ufalme wa Mungu kwa kuwafundisha wengine yote ambayo ametuagiza.

Hebu angalia maneno aliyosema Mtume Paulo kwa waamini, “Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Katika kuungana naye, nyinyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.” (Waefeso 2:19-22). Sisi hatujengi maisha yetu juu ya mafundisho ya Yesu tu, bali pia tunakuwa sehemu ya jengo kubwa linalojengwa ulimwengu mzima. Kwa hiyo sharti tuende na kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu...na kuwafundisha yote tuliyofunzwa na Yesu. Kila tunapoenda tunajenga ufalme wa Mungu. Tambua kwamba katika fumbo la wajenzi wawili na katika Wito Mkuu, kanuni zinazowaongoza watu ni mafundisho ya Yesu.

Swala la Uanafunzi sio kwamba lililetwa na Yesu kwa mara ya kwanza, bali lilikuwa sehemu ya mpango wa Mungu katika uumbaji wake. Nabii Malaki anawapa changamoto wazai kwa kusema, “Je, Mungu hakuwafanya nyote wawili muwe mwili mmoja na roho moja? Je, alikusudia nini alipofanya hayo? Yamkini alikusudia tuzae watoto ambao watamcha yeye. Kwa hiyo, hakikisheni kuwa hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”(Malaki 2:15). Je, tunawezaje kupata kizazi kinachomcha Mungu?Jibu ni kwa kuishi maisha yanayompendeza Mungu na yaendayo sawa na Injili, kwa kujifunza kila wakati na kwa kuwafundisha wengine, huku tukiwa na shauku ya kuzifuata njia zake Mungu. Mungu alimuumba wanadamu, mke na mume waonyeshe mfano wake. Kwa hiyo wanapoketi, wanapotembea na kulala, wanastahili kuwafundisha wale waliowekwa mikononi mwao. Musa alilizungumzia swala hili kwa njia hii, “Basi sikilizeni enyi Waisraeli! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni Mwenyezi-Mungu mmoja. Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu yenu yote. Wekeni moyoni mwenu maneno hayo ninayowaamuru leo na kuwafundisha kwa uangalifu watoto wenu. Mtawasimulia mwapo mnakaa nyumbani au mlipo safarini au mnapolala au

Copyright © 2007 Tammie Friberg 1

Page 5: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mnapoamka. Yafungeni katika mikono yenu na kuyavaa katika paji za nyuso zenu kama ukumbusho. Yaandikeni kwenye miimo ya milango yenu na malango ya miji yenu.” (Kumbukumbu 6:4-9). Uanafunzi ni sehemu ya maisha ya waamini. Sisi ni walimu wakati wote, uwe wakati wa shida au wakati wa raha. Tujue tusijue, sisi tunawafunza watoto wetu na wengine juu ya uaminifu, kumtegemea Mungu, upendo, ukweli, kiasi na mambo mengine mengi. Hii hufanyika wakati tunapoishi maisha ya kiungu mbele zao.

Katika Biblia kuna maneno maalum ya Kiebrania ambayo hutumiwa kwa maana ya kufundisha. Mojawapo ya maneno hayo ni lamed. Neno hili maana yake ni kuwafundisha wengine kutambua yale yanayompendeza Mungu, au kutambua mapenzi ya Mungu maishani mwao. Neno lingine ni Yirah. Maana ya Yirah ni kuwafundisha watu jinsi ya kuishi katika hali zote. Katika Agano Jipya neon lililotumiwa ni paideo. Neno hili limetumika kwa maana ya kuwafundisha watoto au kuwapa elimu. Neno mwanafunzi maana yake ni “kujifunza, au kutia nidhamu.” Lakini huenda mojawapo ya maneno maalum ni hili la Theodidasktos. Neno hili maana yake ni “Kufundishwa na Mungu” (1 Wathesalonike 4:9). Maneno haya yote yakiwekwa pamoja, yanaweza kutusaidia kuelewa jukumu letu la kuwafunza wengine mambo ya kiroho. Neno Theodidasktos linatukumbusha kwamba Mungu ndiye mwalimu mkuu. Watoto au watu wengine katika jamii zetu huwa wanatuona jinsi tunavyoishi kila siku. Watu hawa waliokwisha tajwa wana nafasi ya kipekee ya kuona iwapo tunaifuata imani au la. Maisha yetu ya kila siku hukumbwa na changamoto nyingi, lakini uhusiano tulionao na Mungu na muda tunaotumia kulisoma neno lake hutupa hekima na nguvu za kila siku za kutusaidia kukabiliana na hali hizo na kuibuka washindi. Vilevile wale tuliopewa na Mungu ili tuwafundishe, sharti pia wazingatie kanuni hiyo. Watu hawa wanaweza kuwa watoto wetu, mke au mme wako, familia inayojumuisha babu na nyanya zetu, marafiki, majirani au hata washirika wenzetu kanisani.

Wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Mungu aliwaruhusu kuona njaa ili aweze kuona kilekilichokuwa mioyoni mwao. Alitaka kuona iwapo wangezitii sheria zake. Mungu alifanya hivi iliwaweze kujifunza kwamba mwanadamu hawezi kuishi kwa mkate tu, “bali kwa kila asemaloMwenyezi-Mung” (Kumbukumbu 8:3). Tunahitaji chakula cha kimwili na cha kiroho ili tuwezekuishi maisha ya utakatifu hata tunapokumbwa na hali ngumu za maisha. Hebu tazama mfano waAyubu, yeye alikuwa mcha Mungu, lakini pamoja na hayo alikumbwa na hali ngumu sana ya maisha. Shetani alitaka kumthibitishia Mungu kwamba Ayubu alimcha kwa sababu ya baraka zamali nyingi na pamoja na watoto aliokuwa nao. Kwa hiyo Shetani alimpiga Ayubu kwa mambomengi, yakiwemo majanga ya asili, kufiwa na watumishi wake na watoto wake, jeshi la adui,kupoteza mifugo wake, makao na hata magonjwa ya mwili. Ndipo Ayubu akachanganyikiwa. Hakuweza kuelewa alichokuwa akikifanya Mungu au pale alipokuwa Mungu. Ayubu alisema, “Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati, narudi nyuma, lakini siwezi kumwona. Namtafutaupande wa kushoto lakini simwoni; nageukia kulia, lakini siwezi kumwona. Lakini yeye anajua njia ninayofuata; atakapomaliza kunijaribu nitatoka humo safi kama dhahabu.Nafuata nyayo zake kwa uaminifu njia yake nimeishikilia wala sikupinda. Kamwe sijaacha kushika amri yake, maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.” (Ayubu 23:8-12). Tambua kwamba Mungu alikuwa akimwangalia Ayubu, akitaka kuona jinsi angelivyokabiliana na majaribu yaliyompata. Vilevile Mungu anatazama njia zetu. Anataka kuona watu wake wakilipenda Neno lake kuliko hata chakula chetu cha kila siku.

Jinsi Ya Kutumia Kitabu Hiki:Kitabu hiki kimeandikwa kwa lengo la kuwasaidia waamini kujenga msingi imara kwa ajili ya maisha yao nay a wale walio chini ya uangalizi wao. Hakikuandikwa ili kichukue mahali pa Biblia, bali kimsadie msomaji katika kujifunza Neno La Mungu. Mafundisho mbalimbali ya Kimsingi kutoka katika Biblia yamegawanywa katika masomo 12. Kila somo linaweza kufundishwa kwa kuzingatia uwezo, ukomavu na umri wa wanafunzi wenyewe. Kila sura ya ina picha, maelezo mafupi, mwongozo wa mafundisho na orodha ya marejeo ya Biblia. Katika kuwafunza watu, utatumia sehemu mbalimbali za kitabu kulingana na uwezo wa mwanafunzi. Ukitazama hapa chini utaona viwango fulani vilivyoorodheshwa na jinsi ya kutumia viwango hivyo. Lengo hasa ni kuhakikisha kwamba katika akili na mioyo ya waamini wana picha halisi ya kuwawezesha kukua katika kumjua Mungu, kumpendeza, na kutumia kitabu hiki kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 2

Page 6: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Viwango Vya Kufundishia:1. Kiwango Cha Kimsingi—Fundisha tu mambo yaliyo katika picha kwa kila somo. Maelezo ya kila

picha yamewekwa katika kila sehemu yenye Maelezo Mafupi Ya Somo. Itakubidi kusoma kila sehemu ya Maelezo Mafupi ili kuweza kutambua ni mafundisho gani yatakayowafaa watu wako. Unaweza kuchukua siku moja, wiki, au mwezi mzima kumaliza kupitia kila somo. Wasikilizaji au wanafunzi sharti waweze kueleza yale waliyojifunza kwa kutazama picha na kuelezea walichokiona.

2. Kiwango Cha Kati—Fundisha somo hili kwa kina zaidi kama ilivyoandikwa katika Maelezo Mafupi Ya Somo. Baadhi ya sehemu hazitawakilishwa kikamilifu na picha zilizowekwa. Unaweza kuamua kutumia Muhtasari Wa Mafundisho mwishoni mwa Maelezo Mafupi Ya Somo kukusaidia katika kufundisha kwako.

3. Kiwango Cha Juu—Baada ya masomo kufundishwa katika kiwango cha Kimsingi Na Cha Kati, Marejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto wa chati kuna Hadithi Za Biblia ambazo zinafunza mambo yaliyoonyeshwa kwenye picha. Unaposoma kila hadithi, fuata muhtasari uliopo hapo chini na ujadili na kujifunza kutokana na matini hiyo. Maandiko yanayofunza mambo fulani yameorodheshwa upande wa kulia. Hakikisha kwamba unayasoma Maandiko haya pamoja na hadithi za Biblia, ili uweze kukua kiroho na kujifunza mengi zaidi. Masomo mengine yana mafundisho ya ziada yaliyoorodheshwa chini yake. Mafundisho haya yanaweza kutumiwa kujifunza zaidi juu ya mada au kichwa cha somo.

Lengo: Lengo la mafundisho haya ni kujenga jamii thabiti zilizojitoa kuhakikisha kwamba usafi wa Neno La Mungu unadumishwa, kueneza Habari Njema ya Wokovu kupitia kwa Yesu Kristo, na kuwafanya watu wa mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu kwa kuanzia na familia zetu. Mpango: Mungu alituweka katika jamii ili kuweza kudhihirisha mfano wake katika ndoa zetu, na kulea watoto wanaomcha Mungu. Kwa kuwa watoto wanatuona kila wakati, iwe ni wakati wa raha au wa tabu, tuna nafasi ya kipekee ya kuweza kuwafundisha watoto wetu njia za Mungu huku sisi wenyewe tukijifunza kumtegemea Mungu na kumtii. Sisi sote ni wanafunzi, na tunawafanya wengine kuwa wanafunzi wakati wote-usiku na mchana.

Unashauriwa kutumia kitabu hiki pamoja na masomo ya Biblia Ya Kila siku. Vipengele vifuatavyo ni sehemu ya kuhakikisha kwamba unatenga wakati wa kusoma Biblia wewe pamoja na familia yako au pamoja na kikundi chako cha kujifunza Biblia.

1. Kusoma na Kujifunza Biblia Kila Siku2. Kuabudu3. Kutoa ushuhuda na Kuomba Pamoja

Kila moja ya mambo haya yanaweza kutekelezwa kwa njia nyingi tofauti:Kusoma Biblia Na Kujifunza Biblia Kila Siku.

1 Masomo Ya BibliaSoma hadithi fulani katika Biblia kila siku.Soma takriban sura tatu za Biblia kila siku, kwa njia hii utaweza kusoma Biblia nzima kwa mwaka mmoja.Soma sura moja kutoka katika Agano la Kale na sura moja kutoka katika Agano Jipya kila siku.Soma Zaburi moja na Sura moja ya Mithali kila siku.Waombe watu kusoma Biblia kwa sauti. Hii itawafundisha watoto wako au watu wa kikundi chako cha kujifunza Biblia kuweza kusoma Biblia na kuwaongoza wengine hadharani.

2. Mafundisho Ya BibliaBaada ya kusoma aya za Biblia, uliza maswali yaliyo hapa chini ambayo yanahusiana na matini ya Biblia uliyosoma. Maswali haya yatakusaidia kujibu maswali ya nani, nini, kwa nini, wapi, na maandiko haya yanaweza kutasaidiaje katika maisha yetu ya kila siku?

A. Maswali Yanayohitaji Majibu Ya Maelezo:Habari hizi zilizo katika hadithi hii zilifanyika wapi, au habari hizi ziliandikwa katika hali gani ya kihistoria?Je, habari hizi, au barua, zaburi, au unabii huu uliandikiwa nani?

Copyright © 2007 Tammie Friberg 3

Page 7: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Je, wahusika gani walio katika kisa hiki? Je, wahusika hao ni sehemu ya jamii ya Mungu, au ni watu wasiomjua Mungu?Je, ni mambo gani yanayotendeka katika kisa hiki? Ni matatizo gani yanayochipuka katika kisa hiki?Je, wahusika wanakabiliana na tatizo kwa njia gani au wahusika wanapata suluhisho kwa njia gani?Je, wahusika walifuata njia ya Bwana au njia yao wenyewe katika kutatua tatizo lao?Je, matokeo ya matendo yao yalikuwa nini?Je, maandiko haya yanatufunza nini kuhusu ulimwengu wa kiroho, shetani, au dini za uongo?Je, ni funzo gani linalofunzwa na kisa hiki ulichosoma?B. Maswali Ya Kitheologia:Je, maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu Mungu, Yesu, malaika, au mbinguni?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya watu?Je, maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu dhambi?What does this passage teach about good community relationships?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya jinsi mke na mume wanavyoweza kuchukuliana?Je, maandiko yanatufundisha nini juu ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya jinsi Mungu anavyotawala uumbaji wake?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya jamii ya Mungu?Je, maandiko yanatufundisha nini juu ya msamaha?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu kuwapenda maadui zetu?Je, unaweza kupata hekima gani kutokana na maandiko haya?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya kumtafuta Mungu na kuomba?Je, maandiko haya yanatufundisha nini juu ya wokovu?Je, maandiko haya yanaingilianaje na Maandiko mengine na Mpango wa Mungu wa wokovu kwa jumla?C. Maswali Ya Kutusaidia Kuyatumia Maandiko kwa Maisha Ya Kila siku:Baada ya kujifunza ujumbe wa maandiko haya na maana yake wakati ulipoandikwa, je, ninawezaje kuutumia katika maisha yangu ya kila siku?Je, mafundisho ya maandiko haya niliyosoma yanatofautianaje na mila za kabila langu?Je, kwa kulingana na mafundisho niliyopokea, ni mambo gani ninayostahili kuyabadilisha katika maisha yangu kama mwana, mume, mke, rafiki, au mwamini?

3. Mafundisho, Majadiliano, Ushuhuda: Mafundisho haya yanaweza kuwa yalikuwa katika taratibu yako ya kujisomea Biblia, au yanaweza kuwa hayakuwepo, lakini hata hivyo sharti yajumuishwe kila wakati unapopata nafasi ya kufundisha watu wa jamii yako.Mafundisho haya ndiyo yanayopatikana katika kitabu hiki. Kila jioni sharti watoto wake au watu wa kikundi chako cha kujifunza Biblia wapitie muhtasari wa somo, au wajizoeze kufuata mafundisho ya somo lenyewe. Mambo mengine mapya yanaweza kuongezwa wakati unaposoma na kujifunza Biblia.

Kila somo limewekewa picha; Maelezo Mafupi Ya picha hiyo; Muhtasari wa Maelezo unaoweza kutumiwa kwa marejeo ya haraka; na habari za Biblia pamoja na marejeo ya Biblia kwa ajili ya mafunzo ya ziada ya kila sehemu. Hapa chini kuna muhtasari wa jinsi unavyoweza kutumia Habari/hadithi na Marejeo Ya Maandiko yaliyowekwa.

1. Chagua Habari/hadithi kutoka katika Biblia katika sehemu ya Habari Zinazoambatana Na Somo.2. Soma Hadithi hiyo, huku ukizingatia mkutadha wa kisa chenyewe. Zingatia habari zilizotangulia na

zinazofuata na vilevile somo linalofundishwa na hadithi hiyo.3. Linganisha hadithi hiyo na mambo uliyojifunza kutoka katika somo hilo, na utumie Maandiko

Yanayoambatana na Somo kukusaidia kuelewa zaidi mada ya somo.4. Sasa andika kauli moja ambayo ni muhtasari wa yale yote uliyojifunza.5. Sasa yahusishe mambo uliyojifunza katika maisha yako ya kila siku. Je, tunaweza kujifunza nini leo hii

kutokana na maandiko tuliyosoma?

Kwa mfano:Chagua Somo: Somo La 4: Amri Kumi Za Mungu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 4

Page 8: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Chagua Habari/Hadithi Inayoambatana na Somo: Waisraeli Watengeneza Ndama Wa Dhahabu- Kutoka 32; na Stefano Asimulia Historia Ya Israeli- Matendo 7.Changua Andiko Linaloambatana na Somo: Ezekieli 20.

1. Soma maandiko uliyoyachagua hapo juu kutoka katika Marejeo Ya Mafundisho Ya Biblia.2. Kwa kutumia maswali ya Biblia hapo juu, jiulize maswali yanayohitaji majibu ya maelezo, maswali ya

kitheologia, na maswali ya kukusaidia kutumia maandiko katika maisha yako ya kila siku.1 Maswali Yanayohitaji Majibu Ya Maelezo:

2 Je, hali ya kiroho nay a kimwili ya Waisraeli huko Misri ilikuwa vipi?3 Je, Mungu alifanya nini kutatua shida yao ya kimwili?4 Je, Mungu alifanya nini kutatua shida yao ya kiroho?5 Je, Waisraeli waliyapokeaje matendo na maagizo ya Mungu?

6 Maswali Ya Kitheologia:7 Je, habari/hadithi hizi zinatufunza nini juu ya Mungu?8 Je, habari/hadithi hizi zinatufunza nini juu ya watu?9 Je, watu walistahili kufanya nini?

10 Maswali Ya Kutusaidia kutumia maandiko katika maisha yetu ya kila siku:11 Je, hali yetu ya kimwili ni gani?12 Je, hali yetu ya kiroho ni gani?13 Je, Mungu anafanya kazi gani katika maisha yetu?14 Je, tunapokeaje kazi hiyo ya Mungu?15 Je, ni changamoto gani kutoka katika habari tulizosoma zinahusiana nasi leo?16 Je, kuna dhambi zozote tunazostahili kuzitubu?

2. Kumsifu Na Kuwabudu MunguKila wakati wa familia kuomba pamoja au wakati wa kikundi cha kujifunza Biblia kukutana sharti kuwe na kipindi kumwimbia Mungu nyimbo za sifa. 3. MaombiMwombe kila mtu katika familia yako kuomba, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Waombe watoe mambo yanayostahili kuombewa. Iwapo mmetembelewa na wageni nyumbani kwenu, waombe watoe mambo ya kuyaombea ili watu wa familia yako waweze kuwaombea. Wale walio wadogo zaidi, waweza kuwapatia mistari au mambo ya kuyaombea. Vilevile wafundishe kuomba.Sehemu Muhimu Katika Maombi:

Sifa.Kushukuru.Kuungama Dhambi na Kuomba Msamaha.Kuombea Mahitaji.

Kuombea ukuaji wa kiroho, kupanuliwa kwa ufalme wa Mungu.Kuwaombea Wakristo.Kuwaombea Watu Wasiokuwa Wakristo.

Kuyaombea mahitaji maalum kutoka kwa watu wa familia yako au kutoka kwa marafiki.Kuiombea nchi yako na viongozi wake.Kuombea matatizo ya kiafya au mazoea mabaya ya dhambi.

Maoni Juu ya Mafundisho/Wakati Wa kuabudu:Hakikisha kwamba unakuwa mbunifu kila wakati unapoendesha kipindi cha kujifunza Biblia. Usiwe na taratibu moja ja kufanyia vitu.Wakati unapokuwa na wageni nyumbani, hakikisha kwamba unaendelea na mafundisho yako ya uanafunzi na uwaalike kujumuika nanyi.Hakikisha kwamba wakati wote unajitengea muda wa kuwa na Mungu, usiivunje taratibu hii kamwe. Uwe tayari kukabiliana na mtazamo mbaya unaweza kukumba au kuwakumba wenzako.Tambua kazi njema anayoifanya Mungu katika maisha ya watu wa jamii yako wakati unapotekeleza haya.Jitahidi uwafundishe watu wa familia nyingine kutekeleza mafundisho haya katika eneo lako na kanisa lako.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 5

Page 9: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Noti Zuhusuzo Mafundisho ya Biblia:Biblia ndio Msingi wetu wa Ukweli.Kuelewa hadithi kwa misingi ya kihistoria na kujua maana ya hadithi yenyewe ni muhimu sana katika kujifunza kanuni tunazoweza kuzitumia leo katika maisha yetu.Tuwe waangalifu tusiingize imani zetu na asilia zetu katika mafundishu ya Biblia. Badala yake tunahitaji kuchunguza kujua Biblia inasema nini, na sio vinginevyo.Mambo tuliyoyapitia katika maisha au yale ambayo tumewahi kuyasikia yasiwe ndio mwongozo wetu katika kufafanua Maandiko.Lazima tufafanue maandiko kwa kuzingatia ujumbe wote wa Biblia ili tuweze kuelewa maana ya matini tunayoisoma. Maandiko yaliyo magumu kuelewa sharti yasitumiwe kufundishia mafundisho makuu ya Biblia.Pima kila kitu katika mizani ya Neno La Mungu. Kujifunza Biblia huwasaidia watu wa mila zote kushikilia itikadi nzuri za utamaduni wao, na kutupilia mbali mambo yale ambayo Shetani ameyaingiza katika tamaduni zote duniani, mambo ambayo yako kinyume na mapenzi ya Mungu.

‘“Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu, na kuyathamini maagizo yangu; ukitega sikio lako kusikiliza hekima,cccvna kuuelekeza moyo wako upate ufahamu; naam, ukiomba upewe busara, ukisihi upewe ufahamu; ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu,utafahamu maana ya kumjua Mungu. Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu.Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki, utajua jambo lililo sawa na jema. Maana hekima itaingia moyoni mwako, na maarifa yataipendeza nafsi yako. Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi; vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu; watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; watu wafurahiao kutenda maovu,na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.Utaepukana na mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu; mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera. Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai. Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema, na kuzingatia mienendo ya waadilifu. Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watang'olewa humo.(Mithali 2:2-22).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 6

Page 10: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 7

Page 11: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 1: Mungu na Uumbaji Wake wa Kiroho

Maandiko: Mbingu ni zako na dunia ni yako pia; ulimwengu na vitu vyote vilivyomo wewe uliviumna. Wewe uliumba kaskazini na kusini; milima Tabari na Hermoni inakusifu kwa furaha. Mkono wako una nguvu na umeshinda! Uadilifu na haki ni msingi wa utawala wako; fadhili na uaminifu vyakutangulia! Heri watu wanaojua kukushangilia, wanaoishi katika mwanga wa wema wako ee Mwenyezi-Mungu. Wanaofurahi mchana kutwa kwa sababu yako, na kukusifu kwa ajili ya uadilifu wako.” (Zaburi 89:11-16).

Maelezo mafupi

Mungu anayeishi milele na milele na tena ni MkuuMchoro ulioko katika ukurasa uliotangulia ni mfano au kielelezo (mfano wa 1) juu ya Mungu na uumbaji wake. Juu ya picha hiyo ni Kiti Cha Enzi. Hiki ndicho Kiti Cha Enzi cha Mungu huko mbinguni. Kiti hicho cha enzi kinatukumbusha kwamba Mungu ndiye anayetawala kila kitu alichokiumba. Aliumba vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana. Kwa hiyo Mungu ana uwezo na mamlaka ya kuvitawala viumbe vyote kama Mfalme. Nguvu zote, uwezo, falme, na mamlaka yote, yawe mamlaka ya kiroho au ya kibinadamu, vyote viko chini ya ukuu wake. Mungu alikuweko hata kabla hajaumba chochote. Yeye amekuwepo siku zote, hana mwanzo wala mwisho. Mungu ni mfalme anayeishi milele na milele.

Mungu ni Mkombozi na tena ni MwokoziIjapokuwa Mungu ni roho, hapa anaonyeshwa akiwa amenyoosha mkono. Biblia inatufunza kwamba Mungu aliwakomboa watu wake kutoka katika nira ya utumwa huko nchini Misri kwa mkono wake mwenyewe. Mkono wake huo ni wa kuwakomboa na kuwaokoa watu. Mkono hapa unawakilisha jinsi Mungu anavyoshuka chini duniani ili kuwatunza watu wake, kuwakomboa, kuwahukumu waovu, na kuwatia nguvu watu wake ili wamtumikie na mioyo yao yote. Mara nyingi katika Biblia kunao watu waliotoa ushuhuda kwa kusema kwamba tunaweza kupata ulinzi na usalama katika mikono ya Mungu. Yeye ndiye Mungu anayeokoa.

Mungu ni Mungu aliye na silika za mtu na asili ya uadilifuMungu ni Mungu aliye na silika za mtu na asili ya uadilifu. Yeye anawapenda watu na anapenda sana kuwa na ushirika nao. Mungu anachukia dhambi pamoja na athari mbaya zinazosababishwa na dhambi duniani. Yeye anajua mambo yote, hata mawazo ya wanadamu. Watu wakitudanganya na kututendea mabaya, Mungu huwa anasikia na kuona kila kitu kinachoendelea. Ndiposa anaweza kuwahukumu watu kwa njia ya haki na ya sawa. Mungu ametenga siku maalum ambapo atakuja kuwahukumu watu wote. Mungu huwapa haki wale walioonewa. Yeye anawapenda watu, na kwa sababu hiyo yeye huwahurumia wale wanaotubu dhambi zao na kuziacha. Mungu si kama mwanadamu. Yeye ni mtakatifu na mwenye haki. Hajawahi kutenda dhambi na hawezi kumdanganya mtu. Dhambi haiwezi kamwe kukaa katika uwepo wake. Lakini yeye huwapenda kwa dhati wale wote wanaomwamini Yesu kama mwokozi wao.

Mungu ni mmoja, hata ingawa yuko katika utatu, Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho MtakatifuKutoka katika Biblia tunajua kwamba Mungu ni mmoja, hata ingawa yuko katika utatu, Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Katika mchoro uliotangulia, ukiutazama utaona kwamba kuna picha nyingine mbili katika Kiti Cha Enzi. Picha moja inamwakilisha Mungu Mwana, ambaye ni Yesu. Katika picha hiyo ameonyeshwa kama Mwanakondoo. Yeye ndiye Mwanakondoo aliyechinjwa, lakini anaishi. Yesu ameonyeshwa kwa mfano wa Mwanakondoo kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa dhabihu ya kuondoa dhambi zetu. Alikufa kwa ajili yetu ili tuweze kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu. Aidha ameonyeshwa akiwa katika kiti cha enzi kwa sababu Mungu alimfufua kutoka katika wafu na kumketisha katika kiti cha enzi, juu ya watawala na mamlaka ya kila aina. Kwa hiyo Yesu ana uwezo juu ya nguvu zote za kiroho na za kibinadamu duniani. Yeye ni Bwana na Mwokozi wetu. Alikufa kwa ajili yetu; tunaishi kwa ajili yake. Yeye ndiye anayewapatanisha watu na Mungu.

Picha ya pili ni ile ya njiwa. Njiwa ni mfano wa Roho Mtakatifu. Yeye ndiye ambaye hutufariji wakati tunapopitia hali ngumu katika maisha. Roho hutuwezesha kuziona na kuzitubu dhambi zetu. Tunapolisoma neno la Mungu na

Copyright © 2007 Tammie Friberg 8

Page 12: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kulihubiri, Roho Mtakatifu huwa ndiye mwalimu wetu. Aidha hutuongoza tunaposhirikiana na wengine katika kuujenga ufalme wa Mungu. Yeye hukaa ndani yetu na kutupa vipawa tunavyohitaji katika kazi ya kumtumikia Mungu. Pia Roho Mtakatifu hutuombea wakati tunapokuwa na mahitaji. Watu hao wote watatu katika uungu huitwa Utatu. Nasi tunawaabudu wote pamoja kama Mungu Mmoja.

Utengano wa Mungu na uumbaji wakeChini ya Kiti Cha Enzi cha Mungu katika hiyo picha kuna msitari unaowakilisha utengano wa Mungu na uumbaji wake. Mungu aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kwa Maneno ya Kinywa chake. Ule mchoro wa duara unawakilisha ulimwengu. Ile sehemu ya ulimwengu iliyoonyeshwa hapo pichani ni bara la Afrika na sehemu moja ya Mashariki Ya Kati (Middle East).

Uumbaji wa viumbe vya kirohoBiblia inasema kwamba kabla ulimwengu haujaumbwa, Mungu aliumba jeshi la malaika, ambao ni viumbe vya kiroho. Basi siku moja kukawa na vurugu huko juu mbinguni. Mmoja wa wale viumbe wa kiroho akaingiwa na kiburi na akataka kujiinua kumshinda Mungu. Naye akafukuzwa kutoka huko juu mbinguni, akachukua thuluthi moja ya malaika akaja nao duniani. Malaika huyu aliyeasi anaitwa Shetani, Joka, Baba wa Uongo, na Mdanganyifu mkuu. Wafuasi wake wa kiroho huitwa pepo wachafu. Katika picha ya somo hili Shetani ameonyeshwa kama kiumbe chenye mkia, na mabaragumu, na mkuki mkononi. Huyo huyo Shetani ndiye aliyewajaribu Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni.

Vyeo mbalimbali na jukumu za shetani na mapepoPepo wale wanaomfuata Shetani wameonyeshwa katika picha hii kama viumbe vidogo vyenye mabaragumu na mikia na vyeo vyao ni jini ya shetani kulingana na (Waefeso 6:12-24). Biblia humtaja kiongozi wa pepo hao kama kiongozi mkuu (Shetani). Chini yake kuna watawala/mamlaka. Halafu kinachofuatia ni falme za duniani katika ulimwengu wa sasa. Pepo hawa wachafu hudhibiti maeneo fulani hapa duniani. Pepo hawa huwa na ushawishi mkubwa katika mafundisho ya uongo. Huzifanya serikali kuwakandamiza watu, huwafanya watu kubuni dini za uongo, kuwa na tabia potofu kwa kupitia kwa mila na desturi zao. Pepo ndio chanzo cha dini za uongo na ibada za sanamu. Katika picha yetu pepo wanaonyeshwa kama pepo wenye uwezo mkubwa juu ya sehemu mbalimbali duniani. Pepo hao ndio ambao wakati mwingine huwatokea manabii fulani na viongozi na kuwapa mafundisho ya uongo. Mfano wa jambo hilo ni kile kisa cha Mohammed kutokewa na malaika (pepo) na kumfunulia mafundisho ya Kurani. Uongo huu wa kipepo ndio uliokuwa chanzo ya dini ya uongo ya Uislamu. Mfano mwingine ni ule wa bwana mmoja kutoka Amerika kwa jina Joseph Smith. Joseph Smith alitokewa na pepo na hatima yake ikawa kuanzisha dini ya uongo ya Momoni. Vilevile kuna pepo ambao kazi yao maalum ni kuanzisha hadithi na mapokeo fulani ambayo huenda sambamba na ibada za miungu mingi.

Hatimaye, zipo zile nguvu za giza za kiroho. Hawa ni wale pepo ambao hufanya kazi kwa karibu miongoni mwa watu. Pepo hawa ndio vigogo vya mambo ya uchawi na uganga wa kienyeji. Huwafumba macho watu wasioamini, na pia kusababisha mafarakano kati ya Wakristo. Vilevile huwafundisha watu ili waweze kuwatumia, na matokeo yake ni kwamba watu hufungwa nira na kuwaogopa hao badala ya kumwogopa Mungu. Pepo hawa wote hufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba wanawapotosha watu wasimwabudu Mungu aliyewaumba na anayewapenda. Kusema kweli ni waharibifu mno. Fahamu kwamba pepo sio roho za mababu waliokufa zamani. Pepo ni nguvu mbaya za kiroho zinazofanya kazi katika uchawi na dini za uongo. Pepo wanaweza kuwapagaa watu, sanamu na hata wanyama. Pia wanaweza kusababisha maradhi au kifo, na hata wanaweza hata kuwaponya watu kutokana na magonjwa waliyoyasababisha wao wenyewe (pepo). Ni wadanganyifu na wakati mwingine husabisha vita kati ya watu na wakauana wenyewe kwa wenyewe. Itakapofika siku ya kiyama, pepo wote watatupwa katika ziwa la moto pamoja na mkuu wao Shetani na wafuasi wake wote. Vyeo mbalimbali na jukumu za MalaikaUpande mwingine wa picha yetu, kuna malaika wengi. Malaika humwabudu Mungu jinsi alivyo. Wao hufanya kazi kama wajumbe wa Mungu na pia hufanya shughuli za uokozi, hukumu, na ulinzi. Kama vile pepo walivyo na vyeo mbalimbali, malaika pia huunda jeshi kubwa la Mungu lenye malaika wenye vyeo mbalimbali. Mikaeli na Gabrieli ndio malaika wawili walio na vyeo vikuu katika Biblia. Malaika hutusaidia katika uenezaji wa Injili kwa watu ambao hawajamjua Yesu. Malaika hawana jukumu la kutuombea sisi, na wala sisi hatustahili kuwaomba wao, kuwatolea dhabihu/sadaka, au hata kuwaabudu. Lakini tunaweza kumwomba Mungu atume malaika watulinde. Malaika si roho za mababu waliokufa zamani. Malaika ni viumbe vilivyoumbwa na kwa ajili ya kumtumikia yeye na kuwahudumia watu wake. Nyingi ya kazi wanazofanya malaika huwa zimesitirika machoni mwa watu, kwa sababu hatuwezi kuwaona kwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 9

Page 13: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

macho wakifanya kazi zao. Lakini hata hivyo wakati mwingine tunaweza kujua kwamba malaika wanatusaidia. Yesu alisema kwamba watoto wadogo wana malaika wanaowalinda. Malaika hawa husikizwa na Mungu huko juu mbinguni, kwa hiyo sharti watu wawe waangalifu katika yale wanayowatendea watoto. Utakapofika mwisho wa dunia, Wakristo watawahukumu malaika. Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu viko chini ya udbibiti wake mkuu na vina uwezo ulio na mpaka.

Muhtasari Wa Somo La 11.a. Mungu. 1.b. Ulimwengu wa Kiroho.Sifa Za Mungu.Mungu ndiye Muumba wa Vitu vyote, vionekanavyo na Visivyoonekana.Mungu anaishi Milele.Mungu ni Mwenye-Enzi/Mwenye Uwezo wote.Mungu yuko Kila Mahali.Mungu Anajua Kila kitu.Mungu ni Roho.Mungu Ana NafsiMungu Ni Mkamilifu.Mungu Ni Mtakatifu na Msafi; Ni mwenye Haki.Mungu ni mwenye Upendo na Huruma.Mungu ndiye Mkombozi wetu wa Kimwili na Kiroho.Mungu ni Mwaminifu Milele.Mungu Habadiliki.Hali ya Mungu.Mungu ni Utatu.Mungu Baba.Mungu Mwana, Yesu.Mungu Roho Mtakatifu.

Mungu Aliumba Ulimwengu wa KirohoShetani na Pepo.Shetani, Yule Adui.Ngazi za Pepo.Pepo Wanapigana na Waamini.Hatima Ya Pepo.Mikaeli, Gabrieli na Malaika.Malaika ni Wajumbe wa Mungu.Malaika Huwalinda Waamini.Malaika Hutenda Kazi ya Mungu Duniani.Malaika Husaidia Uenezaji wa Injili.

Marejeo ya Kujifunza Biblia Ya Somo La 1

1a. Mungu

Mungu Ndiye Muumbaji wa Kila Kitu, Kionekanacho na KisichoonekanaMaandiko: “Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli; Mungu aliye hai, mfalme wa milele. Akikasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake. "Basi, utawaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.” Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alitandaza mbingu. Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzunisha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake” (Yeremia 10:10-13).“Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu. Wala hatumikiwi na mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na kuwapa kila kitu. Kutokana na mtu mmoja aliumba mataifa yote na kuyawezesha kuishi duniani kote. Aliamua na kupanga kabla kabisa lini wapi mataifa hayo yangeishi. Alifanya hivyo, ili mataifa hayo yapate kumfuata, na kama vile kwa kupapasapapasa, yapate kumfikia. Hata hivyo lakini, Mungu hayuko mbali na kila mmoja wetu. Kama alivyosema mtu mmoja: ‘Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, na tuko!’ Ni kama washairi wenu wengine walivyosema: ‘Sisi ni watoto wake.’ Ikiwa basi, sisi ni watoto wa Mungu, haifai kumfikiria Mungu kuwa kama dhahabu, fedha au hata jiwe lililochongwa na kutiwa nakshi na binadamu. Mungu alifanya kana kwamba haoni nyakati zile watu walipokuwa wajinga. Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahali watubu. Kwa maana amekwishaweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki kwa njia ya mtu mmoja aliyemteua. Mungu amewathibitishia wote jambo hili kwa kumfufua mtu huyo kutoka wafu!” (Matendo 17:24-31).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Habari za Uumbaji- Mwanzo 1-2.*Kurudi Kutoka Uhamishoni- Nehemia. 9:6-21.*Mungu ndiye Muumbaji, Sanamu Hutengenezwa kwa Mikono- Matendo 17.*Daudi Analeta Sanduku La Agano ndani Ya Hema- 1 Mambo Ya Nyakati 15:26; Zaburi 95:6.*Mfalme wa Shamu Anakabiliana na Hezekia - 2 Wafalme

*Miungu Ambayo Haikuumba Mbingu na Nchi Itaangamizwa...Mungu ameiumba dunia kwa Uwezo wake, Hekima na kuwa Ufahamu wake – Yeremia 10:10-13.*Mungu Analeta Giza kuu Katika Nuru na Usiku kutoka kwa Mchana - Amosi 5:8; Yeremia 31:35.*Mungu anadhibiti Mvua- Ayubu 37:11-12.*Mungu Huleta Mvua- Amosi 9:6.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 10

Page 14: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo18-19. *Bwana Anajibu- Ayubu 38.*Kazi Ya Yesu ya Uumbaji- Yohana 1:1-14.

*Mungu ndiye Aliyejenga Kila Kitu -Waebrania 3:4.*Mungu ndiye aliyewaumba Wafinyanzi, na Mharibufu – Isaya 54:16.

Mungu ni wa Milele Maandiko:“Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli; Mungu aliye ahi, mfalme wa milele. Akikasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake. Basi, utaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.” Mwenyezi-Mungu aliumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu. Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake” (Yeremia 10:10-13).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Hotuba ya Mwisho ya Musa- Kumbukumbu 33:26-29.*Mungu Anamfunulia Musa Jina Lake- Kutoka 3:15.*Chumba Chenye Kiti Cha Enzi Mbinguni - Ufunuo 4:8-11.*Maono Ya Danieli Alipokuwa Uhamishoni- Danieli 7:27.

*Kiti Chako Cha Enzi Kiliwekwa Kuanzia Zamani; Wewe Umekuwapo Tangu Milele- Zaburi 93:2.*Miaka Yako Haitafikia Mwisho- Zaburi 102:26-27.*Tangu Milele na Milele, Wewe ni Mungu- wa Musa Zaburi 90:1-2.*Bwana Atatawala Milele na Milele- Kutoka 15:18; Kumbukumbu 32:37-40.*"Mungu Aliumba Vizazi Kutokea Mwanzo 'Mimi, BWANA, Ndimi Mwanzo na Mwisho. Mimi Ndiye- Isaya 41:4.*Huutangaza Mwisho kutoka Mwanzo - Isaya 46:10.*Mungu tangu Siku Za Milele- Mika 5:2.*Nguvu Za Mungu Za Milele Zajulikana kutoka katika Uumbaji wake Warumi 1:20.*Nuguv za Mungu Za Milele Zajulikana Kupitia kwa Maandiko – Warumi, 16:26.

Mungu ni Mwenye EnziMaandiko: “Hukumu haitoki mashariki au magharibi; wala haitoki nyikani au mlimani. Mungu mwenyewe ndiye hakimu; humshusha mmoja na kumkweza mwingine” (Zaburi 75:6-7).“Mwenyezi-Mungu ameweka kiti chake cha enzi mbinguni; yeye anatawala juu ya vitu vyote” (Zaburi103:19)."Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, Wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru. 37 "Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapouliza watu wake, ‘Iko wapi ile miungu yenu, mwamba mlioukimbilia usalama? 38 'Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenu na kunywa divai na dhabihu zenu za kinywaji? Basi na iinuke, iwasaidieni; acheni hiyo iwe kinga yenu sasa! 39 'Oneni kuwa mimi ndimi Mungu na wala hakuna mwingine ila mimi; Mimi huua na kuweka hai; hujeruhi na kuponya, na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu” ( Kumbukumbu 32: 36-39 ).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Kutoka Misri- Kutoka 1-20.*Kisa Cha Ayubu- Ayubu 1-3.*Ushuda wa Mfalme Daudi, Mikononi Mwake Mna Uwezo, Nguvu, Anawatia Nguvu- 1 Mambo Ya Nyakati 29:12.*Bwana Ndiye Anayemiliki Dunia- Mwanzo 14:9 na kuendelea.*Mungu Anatofautisha Kati ya Watu Wake na Waabudu Sanamu- Kutoka 8:22-24.*Mungu juu Mbinguni na Chini Duniani– Kumbukumbu 4:39.*Ombi la Hana la Shukrani- 1 Samueli 1-10 (vs. 6-10)*Sauli Anamwasi Mungu- 1 Samueli 15.*Hakuna Kigumu Kwa Mungu- Yeremia 32 (v.17, 27).*Danieli Anatafsiri Ndoto- Danieli 2:21-22.

*Mauti na Uzima, Kuumizwa na Kuponywa- Kumbukumbu 32:36, 39. *Mungu Akiumba Nuru na Giza, Uhai na Majanga- Isaya 45:7.*Ukubwa Kwa Wale Wanaoamini- Waefeso 1:19-22. *Kiti Cha Enzi Mbinguni, Ukuu Wake Watawala Vyote- Zaburi 103:19.

Mungu Yuko Kila Mahali Maandiko:“Nikimbilie wapi ambapo Roho yako haipo? Niende wapi ambapo wewe hupo? Nikipanda juu mbinguni, wewe upo;nikijilaza chini kuzimu, wewe upo. Nikiruka hadi mawio ya jua, au hata mipakani mwa bahari, hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidigo, na usiku wang’ara kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja” (Zaburi139:7-12).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 11

Page 15: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

“Macho ya Mwenyezi- Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya” (Methali 15:3).“Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu” (Zaburi 46:1).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Mungu Anayeniona- Mwanzo 16:13.*Kuwekwa wakfu Kwa Hekalu La Sulemani- 1 Wafalme 8:27.*Yesu Yuko Pamoja Nasi Hadi Ukamilifu wa Dahari- Mathayo28:20.

*Je Mwanadamu Anaweza Kujificha Mungu Asimwone?– Yeremia 23:9-40. *Hakuna Kiumbe Kilichofichika Machoni Mwake, Lakini Kila Kitu Kinaonekana Wazi– Waebrania 4:13.*Mungu Yuko Karibu Nasi Tumwombapo- Kumbukumbu 4:7.

Mungu Anajua Kila KituMaandiko:“Aliyefanya sikio, je, hawezi kusikia? Aliyeumba jicho, je, hawezi kuona” (Zaburi 94:9)?"Hufunua siri na mafumbo, ajua kilichoko gizani, mwanga wakaa kwake” (Danieli 2:22). “Utajiri,hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichungiziki, na njia zake hazieleweki! NANI ALIYEPATA KUYAJUA MAWAZO YA BWANA? NANI AWEZAYE KUWA MSHAURI WAKE? AU, NANI ALIYEMPA YEYE KITU KWANZA HATA AWEZE TENA KULIPWA KITU HICHO? Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele. Amina” (Warumi 11:33-36).“Mungu ni mkuu kuliko dhamiri yetu, na kwamba yeye ajua kila kitu” (1 Yohana 3:20).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Sara na Abimeleki, Mfalme wa Gerari- Mwanzo 20.*Mungu alijua mateso ya Waisraeli huko Misri- Kutoka 3:7.*Mungu alijua kuwa Farao hangewaachilia watu Waende- Kutoka 3:19-20; 6:1.*Mungu alijua vile watu walivyozunguka na akawatunza- Kumbukumbu 2:7.*Mungu alijua mioyo ya watu kabla hawajaingia nchi ya ahadi Kumb. 31:21.*Ombi la Hana, Mungu ni Mungu mwenye Ufahamu- 1 Samueli 2:3.*Mungu alivyomchagua Daudi, Mungu huujua Moyo wa mtu- 1 Samueli 16:7.*Mungu anajua shughuli zetu zote, na mipango yetu mibaya dhidi yake- 2 Wafalme19:27; Isaya 37:28.*Yesu anajua vile watu fulani katika maeneo fulani wanavyoupokea ujumbe wake- Mathayo11:21.*Mungu huwapa zawadi wale wanaotoa, wanaofunga, wamwombao, katika siri- Mathayo 6:1-8; 6:17-18.*Baraza la Yerusalemu, Watu wa mataifa waamini Matendo15:7-20.*Upumbavu wa kuwaaibisha Wenye Hekima- 1 Wakorintho 1:23-31.

*Mungu aelewa matendo yetu yote- Zaburi 33:15.*Mungu anajua Mawazo Yetu, Maneno yetu kabla hatujasema; mienendo yetu, Kuishi kwetu- Zaburi 139:1-4.*Ufahamu wake hauna mpaka- Zaburi 147:4-5.*Mungu Pekee ndiye anayejua mioyo yetu- 1 Wafalme 8:39; 1 Nyakati. 28:9.*Mungu anajua aibu na fedheha zangu, Maadui wangu wote anawajua- Zaburi 69:19. *Hakuna anayeweza kuuelewa ufahamu wake- Isaya 40:28.*Wanadamu hawawezi kumficha BWANA siri kwani mioyo yao i wazi mbele zake- Methali 15:11.*Ole wao wale wanaomficha BWANA mipango yao, na kufanya mambo yao gizani na kusema, “Hakuna anayetuona wala kutujua”- Isaya 29:15.* Wao husema, 'BWANA ameitupa nchi, Naam BWANA haoni!'- Zaburi 94:7.

Mungu ni RohoMaandiko: "Mungu ni Roho, na wale wamwabuduo lazima wamwabudu kwa Roho na Ukweli” (John 4:24).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Mwanamke Msamaria Kisimani- Yohana 4.*Mungu si kama Sanamu- Matendo 17:29.*Musa alimtumikia Mungu asiyeonekana kama Anaonekana- Waebrania 11:24-29.

*Bwana ni Roho- 1 Wakorintho 3:17-18.*Mungu haonekani- Wakolosai 1:15; 1 Timotheo 1:17.*Yeye aishiye katika mwanga usioweza kukaribiwa na mtu, na Hakuna mtu aliyepata kumwona- 1 Timotheo 6:16.

Mungu ni Nafsi

Maandiko: “Je, nyinyi bado hamjui? Je, hamjapata kusikia? Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele; yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani. Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu. Maarifa yake hayachunguziki. Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu. Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea” (Isaya 40:28-31).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 12

Page 16: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Mungu hufanya Jina lake lijulikane- Kutoka 3 (v.14).*Mungu ni Mungu Mwenye Wivu- Kutoka 34 (v.14).*Muumba ndiye Mutunzi wetu- Zaburi 121.*Mungu huzungumza na watu- Zaburi 57:1-11.

*Mungu huwainua maskini na wahitaji kutoka mavumbini, na kuwafanya wakae na Wafalme- 1 Samueli 2:8. *Wema na Fadhili za Muumba- Zaburi 136.*Huwapatia watu haki, Chakula, Hufungua Wafungwa, Hufungua Macho ya Vipofu, Huwainua wanyenyekevu, Hulinda, Husaidia, Huzuia ubaya- Zaburi 146:5-10.*Miungu ya watu ni sanamu, Lakini BWANA aliumba mbingu- Zaburi 96:5.*Baba na Mama Wameniacha, Bali BWANA atanisaidia- Zaburi 27:10.Mungu ni Kimbilio Letu- Zaburi 32:7; Yeremia 16:19-21.*Wema na Huruma zangu, Ngome yangu, Boma langu, Mwokozi wangu, Ngao yangu, Kwake hukimbilia, Anayewatiisha watu chini yangu- Zaburi 144:2.

Mungu ni Mwokozi wa Mili yetu na Roho zetuMaandiko: “Maana hawa ni watu na urithi wako, watu ambao uliwatoa kwa nguvu na uwezo wako mkuu” (Kumbukumbu 9:29).“Waadilifu wakimlilia Mwenyezi- Mungu yeye huwasikia, na kuwaokoa katika taabu zao zote. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa. Mateso ya mwadilifu ni mengi lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote. Huvilinda viungo vya mwili wake wote hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa” (Zaburi 34:17-20).“Mwenyezi-Mungu aliwaumba enyi watu wa Yakobo, yeye aliyewafanya enyi watu wa Israeli, asema: "Msiogope maana mimi nimewakomboa, nimewaita kwa jina nanyi ni wangu! "Mkipita katika mafuriko mimi nitakuwa pamoja nanyi; Mkipita katika mito haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto hamtaunguzwa, mwali wa moto hautawaunguza. "Maana mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, Mungu Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wenu; Nitaito nchi ya Misri iwe fidia yenu, nitaitoa Kushi na Seba ili mwachwe huru. "Kwa vile mna thamani mbele yangu, kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda, mimi nawaacha watu kusudi niwapate nyinyi nayaachilia mataifa badala ya maisha yenu. "Msiogope, maana mimi nipo pamoja nanyi; Nitawarudisha wazawa wenu toka mashariki, Nitawakusanyeni toka magharibi. "Nitaiambia Kaskazini, 'Waache waondoke!' Na kusini 'Usiwazuie.' Warudisheni watu kutoka mbali, kutoka kila mahali duniani, Kila mmoja hujulikana kwa jina langu, niliwaumba wote na kuwafanya kwa ajili ya utukufu wangu. Waleteni mbele watu hao ambao wana macho lakini hawaoni, wanamasikio lakini hawasikii. Mataifa yote na yakusanyike watu wote nawakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonyesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema “Ilikuwa kweli." "Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu,niliwachagua muwe watumishi wangu, mpate kunijua na kuniamini kwamba ndimi peke yangu Mungu. Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine,wala hatakuwapo mungu mwingine. "Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu hakuna mkombozi mwingine ila mimi. "Nilitangaza yale ambayo yangetukia kisha nikaja na kuwakombo Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo, nanyi ni mashahidi wangu. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima. Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu. Hakuna awezaye kupinga ninayofanya?” (Isaya 43:1-13).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Kukombolewa kwa Waisraeli kutoka Misri- Kutoka 1-10.*Kuvuka Mto Yorodani- Kumbukumbu 9 (v.29).*Samsoni anavunja hekalu la Wafilisti-Waamuzi 16.Bwana anawaletea Waisraeli Wakombozi- Waamuzi 3:9, 15; 2 Wafalme 13:5; Nehamia 9:27.*Jua linasimama- Yoshua 10.*Watu wanamkataa Mungu Mkombozi wao- 1 Samueli 10:18.*Mungu anamwokoa Daudi kutoka kwa Sauli- 2 Samueli 22.*Mungu atatenda jambo jipya- Isaya 43.*Mungu anamwokoa Danieli katika tundu la simba- Danieli 6.*Kisa cha Shedraki, Meshaki, na Abedinego- Danieli 3.*Mungu ametuumba kwa utukufu wake- Isaya 40:1-21.*Yesu anamfufua Lazaro- Yohana 11 (v.25).*Yesu anakufa kwa ajili ya dhambi zetu- Mathayo 26-27; Mariko 14-15; Luka 22-23; Yohana 17-19; Warumi 5-6; *Yesu anafufuka kutoka kwa wafu- Mathayo 28; Mariko 16; Luka 24; Yohana 20-21.*Siri juu ya Kristo- Warumi 11 (v.26).

*Mungu ni Mungu anayeokoa watu kutoka kwa kifo- Zaburi 68:20.*Mungu hutuokoa na maadui- Zaburi 18:48.*Huokoa walioumizwa kutoka kwa watesi wao, Na wahitaji kutoka kwa wanyang’anyi- Zaburi 35:10; 37:40.*Hukuokoa wewe na wanaokutega ... Hukuokoa na ugonjwa mbaya- Zaburi 91:3.*Huwaokoa kutoka kwa mikono ya waovu- Zaburi 91:10; Kutoka 18:8-10).*Alituokoa na hatari kubwa ya kifo, na atatuokoa- 2 Wakorintho 1:10.* Urithi wetu, NA Wokovu wetu wafunuliwa wakati wa mwisho- 1 Petero 1:3-12.*Kristo alijitoa mara moja ili azichukue dhambi za watu wengi, Atafunuliwa mara ya pili kuwaokoa wote wanaomngojea kwa hamu, hatafunuliwa ili aondoe dhambi-Waebrania 9:28.*Kutoionea haya Injili/Habari Njema- Warumi 1:16.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 13

Page 17: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Wimbo wa Maryamu, Mungu ni Mwokozi- Luka 2.*Kumshinda Shetani- Ufunuo 12.

Mungu ni MkamilifuMaandiko: "Mungu si mtu,wala si binadamu, abadili nia yake; Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?” (Hesabu 23:19)."Mwenyezi-Mungu ni mwamba wa usalama, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni za haki. Yeye ni Mungu mwaminifu asiye na kosa Yeye hufanya mambo ya uadilifu na ya haki” (Kumbukumbu 32:4).“Mwenyezi-Mungu ni mwenye haki katika njia zake zote, ni mwema katika matendo yake yote. Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu. Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa. Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wanaompenda, lakini atawaangamiza waovu wote.” (Zaburi 145:17-20).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Balamu anapokea ujumbe kutoka kwa Mungu- Hesabu 23 (v.19).*Mungu ni Mkamilifu. 32.*Wimbo wa Daudi kuhusu alivyookolewa- 1 Samueli 22 (v. 31).

*Njia yake ni kamilifu- Zaburi 18:30.*Iweni wakamilifu, kama baba yenu wa mbinguni, Mathayo 5:48.*Mungu habadiliki wala kuwa kigeugeu- Yakobo 1:17.

Mungu ni Mtakatifu, na Mwenye Haki

Maandiko: “Basi usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.' "Naam,wote waliokuwakia hasira, wataaibishwa na kupata fedheha. Wote wanopingana nawe, watakuwa si kitu na kuangamia. "Utawatafuta hao wanaopingana nawe, lakini watakuwa wameangamia. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: 'Usiogope, nitakusaidia” (Isaya 41:10-13).“Iambie jumuiya yote ya watu wa Israeli hivi: Ni lazima muwe watakatifu kwani mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ni mtakatifu. Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Msizigeukie sanamu za miungu, wala msijitengenezee sanamu za kusubu za miungu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.“Utakapovuna mavuno ya nchi yako, usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. Msirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini; utawaachia maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.“Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo. Msiape uongo kwa jina langu hata kulikufuru jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.“Usimdhulumu jirani yako wala kumwibia. Mshahara wa mtu aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi. Usimlaani kiziwi wala kuweka kizuizi mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Unapotoa hukumu amueni kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki. Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Usimwekee kisasi ndugu yako moyoni mwako, bali upatane daima na jirani yako ili usije ukatenda dhambi. Usijilipize kisasi au kuwa na kinyongo dhidi ya wazawa wa watu wako bali umpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Usimchafue binti yako kwa kumfanya kahaba, nchi nzima isije ikaangukia katika ukahaba na hivyo kujaa uovu. Mtazishika Sabato zangu na kupaheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. “Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. “Kama kuna mgeni katika nchi yako usimtendee vibaya. Huyo mgeni anayekaa nawe atakuwa kwako kama mwenyeji nawe utampenda kama unavyojipenda mwenyewe, kwa kuwa nawe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Ni lazima mtumie mizani halali, na vipimo vilivyo halali. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu” (Walawi 19:2-4, 9-18, 26, 28-37).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Musa na Kichaka cha Kuwaka- Kutoka 3.*Wimbo wa Musa- Kutoka 15.*Wenye Dhambi hawawezi kukaa Mungu alipo-Walawi 16; 10:1-2.*Sheria za Usafi na Unajisi/Uchafu- Wasawe. 11:44-47.*Mwito wa Isaiya- Isaya 6.*Amuri kumi zaonyesha mwongozo mwema- Kutoka 20.*Haki inaonekana katika vile Sheria zinavyowatazamia

*Utakatifu na Haki ndio msingi wa Utawala wake- Zaburi 97:2.*Ni lazima muwe watakatifu kwangu, Maana Mimi Mwenyezi-Mungu ni Mtakatifu; nami nimewatenga na watu ili muwe wangu- Walawi 20:26.*Ndani yake hamna uchafu- Zaburi 92:15.*Mungu ni Mtakatifu- Zaburi 99:9; 1 Petero 1:16.*Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu- Warumi 3:23.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 14

Page 18: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo viongozi wafanye- 2 Nyakati 19:5-9.*Tujitoe kwake Yeye anayehukumu kwa Haki- 1 Petero 2:18-25.*Tafuta Utakatifu wake, Mahitaji ya kimwili- Mathayo 6:25-34.

*Wewe ni Mnyofu, Naam, Sisi wakosaji tuko mbele zako, Kwa sababu hii hakuna anayeweza kusimama hakuna awezaye kusimama mbele yako- Ezira 19:15.*Niongoze katika unyofu wako kwa sabau ya Adui zangu- Zaburi 5:8.*Mungu huhukumu kwa Haki- Kumbukumbu 32:4; 2 Nyakati 19:7; Zaburi 19:7-9; Yeremia 9:24a; Kumbukumbu 10:17; Kumbukumbu 32:4; Warumi 2:11.*Mwenyezi-Mungu hupima nia za watu- Methali 6:2.*Upatano mwema kati ya Unyofu na Rehema- Zaburi 116:5.*Nihuishe kwa Unyofu wako- Zaburi 119:40.*Unyofu wake ni wa milele- Isaya 51:8.

Mungu ni mwenye Upendo na mwenye Rehema/HurumaMaandiko:“Hatakuacha uanguke;mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali. Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;yuko upande wako wa kulia kukukinga. Mchana jua halitakuumiza,wala mwezi wakati wa usiku Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele” (Zaburi 121:3)."Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:38-39).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Mungu aliwachagua Waisraeli wawe watu wake wa thamani si kwa sababu ati walikuwa wengi, au wadogo, bali ni kwa sababu aliwapenda- Kumbukumbu 7:6-13.*Bwana hamsikizi Balamu- Kumbukumbu 23:5.*Musa Awabariki Waisraeli- Kumbukumbu 33 (v.3).*Mungu aliwapenda Waisraeli, Akamweka Sulemani awe mfalme ili kuwe na haki ndani ya nchi- 1 Wafalme 10:1-9 (v.9); 2 Nyakati 9:8; Nehamiai 13:23-31.*Mtoto Mpotevu/Baba wa Upendo- Luka 15.*Kupendwa na Baba- Yohana 14:21, 23; 16:27.

*Mungu anatupenda- Yohana 3:16; Zaburi 103:17; Waefeso 2:4-5; 1 Yohana 4:8, 10.*Bwana ni Mwenye Upendo, Rehema, si mwepesi wa hasira, anaupendo mwingi, Anawapenda wote aliowaumba- Zaburi 145:8, 17.*Upendo wake hutuokoa na shimo la uharibifu- Isaya 38:17.*Mungu anatupenda na huacha kutuletea majanga- Yoeli 2:13.*Yesu alitufia tulipokuwa tungali wenye dhambi- Warumi 5:8; Waefeso 2:4-5.*Alituokoa kwa sababu ya huruma zake kupitia kwa Roho Mtakatifu, na kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, na sio kwa sababu ya matendo yetu.- Tito 3:5-6.*Mungu huwatia adabu wale awapendao- Waebrania 12:5-15.*Sisi Tunaitwa Wana wa Mungu- 1 Yohana 3:1.*Tunapenda kwa sababu Alitupenda kwanza- 1 Yohana 4:19.*Anatupenda, kwa hiyo ni lazima tupendane- 1 Yohana 4:11.*Yeye Hataacha Upendo na Wema wake- Zaburi 89:33-37.*Hakuna kitu kinachoweza kututenga na Upendo wa Mungu- Warumi 8: 38-39.*Upendo na Wema kuwazunguka Wale wanao mtumaini Bwana- Zaburi 32:10.

Mungu ni Mwaminifu MileleMaandiko: “Hakuna hata ahadi yoyote njema ambayo Mwenyezi-Mungu aliiahidi Israeli ambayo haikutimia. Ahadi zote zilitimia” (Yoshua 21:45).“Yeye anayewaita nyinyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu” (1 Wathesalonike 5:24)."Muwe imara na hodari, wala msiwaogope au kutishwa nao, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu ndiye anayekwenda pamoja nanyi. Yeye hataacha kuwasaidia na hatawatupa” (Kumbukumbu 31:6).“Wimbo wa wanaoenda juus. Natazama huko juu milimani; msaada wangu watoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,aliyeumba mbingu na dunia. Hatakuacha uanguke;mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Mchana jua halitakuumiza,wala mwezi wakati wa usiku. Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele” (Zaburi 121).“Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama. Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu” (1 Wakorintho 10:13-14).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 15

Page 19: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Sara Anapata mimba- Mwanzo 21.*Mke wa Isaka - Mwanzo 24 (v.27).*Ndoto ya Yakobo- Mwanzo 28 (v.15).*Malipo ya Kutotii- Wal. 26:15-46 (v.42-46).*Mungu anamwambia Musa jina lake- Kutoka 34:6. *Mungu aliwachagua Waisraeli- Kumbukumbu 7:1-11.*Matayarisho ya Kuingia Nchi ya ahadi- Kumbukumbu 31.*Ahadi ya Kisiki- Mwanzo 9.*Kumkimbilia Mungu Mwaminifu- Zaburi 91.*Kujenga Yerusalemu Upya- Ezira 9 (v.9).

*Tukiwa waaminifu yeye anabaki kuwa Mwaminifu- 2 Timotheo 2:13.*Mungu ni Mwaminifu Hadanganyi- Zaburi 89:33.*Mwenyezi-Mungu Hatawaacha watu wake- Zaburi 94:14.*Natushikilie ungamo la tumaini letu bila kuacha, Kwani yeye aliyetuahidi ni Mwaminifu- Waebrania 10:23.*Wale ambao huteseka kwa mapenzi ya Mungu watamkabidhi Muumba Mwaminifu Roho zao kwa kutenda haki- 1 Petero 4:19.*Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na mwenye haki naye atatuondolea dhambi zetu na kutusafisha na uovu wote- 1 Yohana 1:9.

Mungu Habadiliki

Maandiko: “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, mimi sibadiliki. Lakini nyinyi, nyinyi wazawa wa Yakobo hamjatoweka bado” (Malaki 3:6).“ Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu” (Yakobo 1:17).“Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake. Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu” (Waebrania 6:17-18).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Ujumbe wa Bwana kwa Balaki- Hesabu 23:13-23.*Mungu anamkataa Mfalme Sauli- 1 Samueli 15 (v.29).*Sulemani anamsifu Bwana- 1 Wafalme 8:54-60.

*Dunia inaweza Kubadilika lakini Mungu habadiliki- Zaburi 102:25-27.*Wewe hugeuki, na Huna Mwisho- Zaburi 102:27.*Mipango na Malengo yako hudumu milele- Zaburi 33:11.

Asili ya Mungu

Mungu ni Mmoja katika nafsi Tatu Mungu Baba

Maandiko:“Hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu; Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake” (1 Wakorintho 8:6)."Nyinyi mlijaliwa kuyaona mambo hayo, ili mpate kutambua kwamba Mwenyezi-Mungu, ndiye peke yake Mungu na wala hakuna mwingine. "Basi, kumbukeni leo na kuweka mioyoni mwenu, kwamba Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani; hakuna mwingine” (Kumbukumbu 4:35, 39).“Kwake yeye aliye Mfalme wa milele, asiyekufa, asiyeonekana na aliye Mungu pekee - kwake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina” (1 Timotheo 1:17)."“Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine;hakuna Mungu mwingine ila mimi. Ninakuimarisha ingawa wewe hunijui, ili watu wote, toka mashariki hadi magharibi,wajue kwamba hakuna Mungu mwingine ila mimi;mimi ni Mwenyezi-Mungu na hakuna mwingine. Mimi hufanya mwanga na kuumba giza;huleta fanaka na kusababisha balaa. Mimi Mwenyezi-Mungu hutenda vitu hivi vyote. Enyi mbingu, nyesheni kutoka huko juu, mawingu na yadondoshe uadilifu; dunia na ifunuke, ichipushe wokovu,na kuchanusha uadilifu pia! Mimi, Mwenyezi-Mungu nimefanya hayo” (Isaya 45:5-8).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Kuumbwa kwa mke na mume katika mfano wa Mungu-Mwanzo 1:26.*Sasa Mwanadamu amekuwa kama sisi- Mwanzo 3 (v.22).*Natuivuruge Lugha yao- Mwanzo 11 (v.7).* Maneno ya Mwisho ya Daudi- 2 Samueli 23 (v.2-3).*Sikia e Israeli, Mungu wetu ni Mmoja- Kumbukumbu 6:4.*Ubatizo wa Yesu (Baba, Mwana, Roho Pamoja)- Mathayo 3.*Bwana alimtuma Isaya kwa Roho Wake- Isaya 63:8-11.*Kula nyama zilizotolewa kwa miungu ya sanamu- 1 Wakorintho 8:4-6.

*Sasa mpatanishi si wa upande mmoja tu; ila Mungu ni mmoja- Wagalatia 3:20.*Jina lake ni nani, na Mwanawe anaitwaje- Mith. 30:4.*Bwana Mmoja, Imani moja, Ubatizo mmoja; Mungu mmoja na Baba wa wote- Waefeso 4:5.*Jina Elohimu- Wingi wa Utukufu ('im' Kiebrania ni wingi, na inatafusiriwa, “Mungu”). Imetumiwa katika Mwanzo 1:26 (Natuumbe Mtu kwa mfano wetu); na pia katika Kumbukumbu 6:4 (”Sikia ewe Israeli, Bwana Wetu (jina la Mungu la Agano, tunalitafsiri Bwana]) ni Elohimu [wingi wa utukufu]. Bwana Wetu ni mmoja (umoja, peke yake-tunamwabudu kama Mmoja).” Pia wakati kutolewa kwa amuri

Copyright © 2007 Tammie Friberg 16

Page 20: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo kumi Kutoka 20:2-4a (“mimi ni Bwana Elohimu [Mungu] wako, Nilikutoa katika utumwa. Usiwe na miungu mingine. Usijifanyie miungu ya sanamu”).

Mungu, Mwana (Yesu)Maandiko: “Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu. Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu. Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini. Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote. Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua. Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, ambao walizaliwa si kutokana na uwezo wa kibinadamu wala nguvu za kimwili wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe. Naye Neno akawa mwanaadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli” (Yohana 1:1-14).“Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu. Mwana ni mkuu kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu kuliko jina lao. Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:“WEWE NI MWANANGU; MIMI LEO NIMEKUWA BABA YAKO.”Wala hakusema juu ya malaika yeyote:“MIMI NITAKUWA BABA YAKE,NAYE ATAKUWA MWANANGU.” Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae, mzaliwa wa kwanza, ulimwenguni alisema:“MALAIKA WOTE WA MUNGU NA WAMWABUDU.” Lakini kuhusu malaika, alisema:“AMEWAFANYA MALAIKA WAKE KUWA UPEPO,NA WAHUDUMU WAKE NDIMI ZA MOTO.” Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema:“KITI CHAKO CHA ENZI, EE MUNGU, CHADUMU MILELE NA MILELE! WEWE WAWATAWALA WATU WAKO KWA HAKI. WEWE WAPENDA UADILIFU NA KUCHUKIA UOVU. NDIYO MAANA MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUWEKA WAKFUNA KUKUMIMINIA FURAHA KUBWA KULIKO WENZAKO.” Na tena:“BWANA, WEWE ULIUMBA DUNIA HAPO MWANZO, MBINGU NI KAZI YA MIKONO YAKO. HIZO ZITATOWEKA, LAKINI WEWE WABAKI DAIMA,ZOTE ZITACHAKAA KAMA VAZI. UTAZIKUNJAKUNJA KAMA KOTI, NAZO ZITABADILISHWA KAMA VAZI.LAKINI WEWE NI YULEYULE DAIMA, NA MAISHA YAKO HAYATAKOMA.” Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:“KETI UPANDE WANGU WA KULIA, MPAKA NIWAWEKE ADUI ZAKO CHINI YA MIGUU YAKO?”(Waebrania 1:3-13; Zaburi 110:1).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo Katika Agano la Kale anajulikana kama Malaika wa Bwana.*Mgeni wa Ibrahimu- Mwanzo 18:1-33; 19:24.Mahali Malaika wa Bwana anapopatikana-*Ndoto ya Yakobo: Mwanzo 31:11-13.*Yakobo anambariki Yusufu- Mwanzo 48:15-16.*Jina la Mungu katika Malaika- Kutoka 23:20.*Malaika Anaokoa watu watatu katika moto- Danieli 3:25-28.*Malaika anayekaambele zake aliwaokoa- Isaya 63:8-11; Waamuzi 2:1-6.*Mtoto wa Ibrahimu anaokolewa Mwanzo 22:11-18.*Musa na kichaka cha kuwaka- Kutoka 3:2-6.*Kondoo wa Pasaka -Kutoka 12:3-6, 46; Hesabu 9:12; Zaburi 34:20; Yohana 19:36; 1 Wakorintho 5:7.*Jiwe la Horebu- Kutoka 17:6; 1 Wakorintho 10:3-4.*Anamtokea Gideoni- Waamuzi 6:11-24.*Malaika anatangaza- Luka 2.*Yesu ni Chakula cha Uzima- Yohana 6:31-58.Mtoto wa Mariamu kuitwa Imanueli-yaani Mungu pamoja nasi- Mathayo 1:23.*Filipo na Afisaa wa Ethiopia, Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu- Matendo 8:30-35.*Yesu alisema, Kama umeniona mimi, umemwona Baba- Yohana 14:6-11.

*Ufalme wako Ee Mungu ni wa milele- Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8-9.*Nguvu za milee- Warumi 1:20.*Yesu ni mfano hasa wa vile Alivyo-Waebrania1:3.*Yeye ni Mungu wa kweli na Uzima wa milele- 1 Yohana 5:20.*Shetani amepofusha akili za watu wasioamini ili wasiuone mwanga wa Habari Njema ya Utukufu wa Kristo, ambaye ndiye mfano kamili wa Mungu- 2 Wakorintho 4:4.*Yeye ni mfano wa Mungu ambaye hatumuoni, mzaliwa wa kwanza wa vitu vyote vilivyoumbwa- Wakolosai 1:15.*Pia Mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, Mwanadamu Kristo Yesu- 1 Timotheo 2:5-6; Warumi 8:34; Waebrania 7:25.*Jina lake ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani- Isaya 9:6-7.*Yesu alikuwako kabla kuzaliwa kwake hapa duniani- Yohana 8:58; 16:28.*Yesu ni Nabii- Kumbukumbu 18:15-19; Mathayo 21:11; Luka 24:19; Yohana 4:19; Matendo 3:22; 7:37.*Yesu ni Kuhani- Zaburi 110:4; Isaya 53:12; Zeka. 6:12-13; Luka 23:34; Warumi 8:34; Waebrania 5:5-10; 6:19-20; 7:15-28; 9:11-14; 9:24; 1 Yohana 2:1.*Yesu ni Mfalme- Zaburi 2:6; 132:11; Yeremia 23:5-6; Eze. 37:24-25; Mathayo 2:5-6; Luka 1:32-33; Yohana 1:49; 18:33-37.*Yesu Mwokozi- Zaburi 2:2; Danieli 9:24-25; Mariko 8:27-29; Matendo 2:36; 18:28.*Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu- Isaya 53:5-12; Danieli 9:26;

Copyright © 2007 Tammie Friberg 17

Page 21: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo Mathayo 27:50; Matendo 8:30-35; 1 Wakorintho 15:3; Wagalatia 1:3; 1 Petero 2:23-24.*Kufufuka kwa Yesu- Mathayo 28:5-7; Mariko 6:6-7; Luka 24:5-7; Yohana 20:26-27; Matendo 1:3; 2:24; Warumi 1:4; 6:4; 1 Wakorintho 15:20; Waebrania 13:20; Ufunuo 1:5.*Kuinuliwa kwa Yesu- Zaburi 110:1-7; 118:22;Matendo 2:32; 5:31; 7:55-56; Waefeso 1:20; Wafilipi 2:9-11; Wakolosai 3:1; Waebrania 1:3; 8:1; 10:12; 1 Petero 3:22; Ufunuo 3:21; 5:13.*Kurudi kwa Yesu- Mathayo 25:31; Mariko 8:38; Luka 12:40; Yohana 14:3; Matendo 1:11; 1 Wakorintho 1:8; Wafilipi 1:6; 1 Wathesalonike 3:13; 4:13-17; 5:2; 2 Wathesalonike 1:7; Tito 2:13; 2 Petero 3:10; Ufunuo 19:11-21.

Mungu, Roho Mtakatifu Maandiko: "Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele. Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu..” "Lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni” (Yohana 14:16-17, 26).“Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu” (Matendo 9:31).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Roho Mtakatifu ni Mungu, Anania alimdanganya Roho Mtakatifu/Mungu- Matendo 5:3-4.*Hadithi ya Nikodemo- Yohana 3:3-5.*Roho wa Mungu ndani ya Yusufu- Mwanzo 41:38.*Kuja kwa Roho Mtakatifu/Mfariji/Mtulizi- John 14.*Kanisa linakua kwa kutulizwa na Roho Mtakatifu- Matendo 9:31.*Pepo husaidia kupinga- Luka 11:37-12:12.*Alimfunza Paulo mambo ya kufundisha- 1 Wakorintho 2:6-16.*Roho Mtakatifu ni Kiongozi katika kuifanya kazi ya Mungu- Matendo 16:6-7.*Hutufanya tuamini kuwa sisi ni wenye dhambi, au ni wenye haki, au tutahukumiwa.*Siku ya Pentekote- Yohana 16:7-11; Matendo 2.*Roho Mtakatifu hutu hutufanya watakatifu-1 Wakorintho 6:11.*Roho Mtakatifu hupatia zawadi- Kutoka 31:3; 1 Wakorintho 12:7-11.*Roho alimwongoza Yesu kwenda nyika ili akajaribiwe - Mathayo 4.*Yesu alitoa mapepo kwa nguvu za Roho wa Mungu- Mathayo 12:22-32.

*Roho katika Agano la Kale- Mwanzo 1:26; Kumbukumbu 6:4.*Hututuliza na kututia nguvu/moyo- Warumi 12:8; 1 Wakorintho 12:4,7.*Roho Mtakatifu ni kama muhuri kuonyesha kwamba sisi ni wa Mungu- 2 Wakorintho 1:22; Waefeso 1:13-14; 4:30. *Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu- 1 Wakorintho 3:16; Warumi 8:9-11; Wagalatia 4:6; 1 Yohana 3:24; Yohana 14:1.* Roho Mtakatifu hutusafisha na kutufanya wapya- Tito 3:5; Yohana 3:5-6. *Roho Mtakatifu hutuombea- Warumi 8:26.*Roho Mtakatifu akija juu yenu mtapokea nguvu nanyi mtakuwa mashahidi wangu- Matendo 1:8.*Roho Mtakatifu Hushuhudia Ukweli mioyoni mwetu- Warumi 9:1.*Hututia Nguvu za kufanya kazi ya Mungu- 1 Wakorintho 2:4; Warumi 8:13; Wagalatia 5:17-18, 22-23.*Hutufundisha- Yohana 16:12-14; 1 Wakorintho 2:13.*Yeye hujulikana kama Roho wa Hekima na Maarifa- 1 Timotheo 1:17.

1b. Masomo Maalumu Kuhusu viumbe wa Kiroho

Mungu aliumba Viumbe wa KirohoMaandiko: “Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo.” (Mwanzo 2:1)."“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,dunia na vyote vilivyomo,bahari na vyote vilivyomo;nawe ndiwe unayevihifadhi hai, na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe” (Nehamia 9:6).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Kuumbwa- Mwanzo 1-2 (2:1). *Mungu aliumba Jeshi la Mbinguni- Nehamia 9:6.

Shetani na Mapepo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 18

Page 22: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Maandiko: “Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara” (Waefeso 6:12-13)."Nyinyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na hali yake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wa uongo” (Yohana 8:44).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Mfalme wa Tiro Kuanguka, Kama Shetani- Ezekieli 28:1-19.*Mfalme wa Babeli Kuanguka kama Shetani- Isaya 14:3-23.*Theluthi moja ya malaika walianguka na kumfuata Shetani- Luka 10:18; Ufunuo 12:7-9; 14.*Shetani alimjaribu Adamu na Hawa- Mwanzo 3; Ufunuo 12:9.*Shetani ni Baba wa uongo na Mwuaji- Yohana 8:44; Ufunuo 12:3, 9; 1 Petero 5:8.*Shetani anajulikana kama Joka, humpinga Kristo na wa wanaomwamini- Ufunuo 12:3-9.*Huleta magonjwa- Ayubu 2:7; Luka 13:16.*Mfano wa mpanzi, Shetani huiba kazi ya neno kutoka mioyoni mwa watu- Mathayo 13.Ngazi za Madaraka katika Ulimwengu wa Kiroho (Waefeso 6:12):*Shetani ndiye Mtawala au Mfalme- Waefeso 2:2; Yohana 12:31.*Mamlaka- Waefeso 6:12; 1 Wakorintho 15:24; Wakolosai 2:15; 1 Petero 3:22.*Nguvu za Ulimwengu wa giza- Danieli 10:12-13, 20; Warumi 8:38; 1 Wakorintho 15:24; Wakolosai 2:15; 1 Petero 3:22 (Mapepo wanaofunza elimu na dini za uongo, Huingia ndani ya mila, Serikali, mfumo wa jamii).*Nguvu mbaya/mbovu za Kiroho- Matendo 8:9-24 (Mapepo wanaowapa nguvu Waganga na Wachawi, na wajuzi wa mitishamba).Waumini na Shetani:*Shetani alimtokea Adamu na Hawa, na Yesu ili awajaribu. Hakuwatokea Ayubu ama Petero alipowakandamiza- Mathayo 16:21-23; Ayubu 1-3. *Ni lazima waumini wamwendee Mungu ili wapate ukombozi kutoka kwa Shetani- Mathayo 6:13; Warumi 16:20; 2 Wathesalonike 3:3; 1 Yohana 3:8-10; Yuda 1:8-9.*Ni lazima waumini wapinge majaribu ya Shetani- Waefeso 4:27; Waefeso 6:11-18; Yakobo 4:7; 1 Petero 5:8-9.*Mungu humtumia Shetani kuwatia adabu waumini- Luka 22:31-32; 1 Wakorintho 5:5; 2 Wakorintho 12:7; 1 Timotheo 1:20.*Paulo alijaribu kwenda Thesalonike lakini akampinga (1 Wathesalonike 2:18). *Yeye ndiye chanzo cha mapigano kati ya waumini - Yakobo 4:1-7.*Shetani anatumia kutosameheana katikati ya waumini ili alete tabu- 2 Wakorintho 2:10-11.*Mungu anawakataza waumini wasitumie aina yoyote ya uganga, uchawe, au kupiga ramli/mburuga au ubashiri- Kumbukumbu 18:9-14.*Yesu amewapokonya silaha mapepo- Wakolosai 2:15; 1 Wakorintho 15:24.

*Shetani ni adui yetu- 1 Petero 5:8.*Shetani ndiye Atujaribuye- Mathayo 4:3; 1 Wathesalonike 3:5.*Shetani hujigeuza/hujifanya Malaika wa Nuru- 2 Wakorintho 11:13-14.*Hufanya kazi ndani ya watu wasiotii- Waefeso 2:2.*mungu wa ulimwengu huu(Shetani) huwaziba macho watu wasioamini- 2 Wakorintho 4:4; Yohana 12:31.*Shetani hana mamlaka yote- 2 Wathesalonike 2:9.*Hufunza mafundisho ya uongo- 1 Timotheo 4:1-3.*Siku moja Shetani atatupwa katika ziwa la moto- Mathayo 25:41; Yohana 12:31; 16:11; Wakolosai 2:15; Ufunuo 20:10.*Malaika waliacha mahali pao pa sawa- Yuda 1:6-7.

Malaika ni Wajumbe wa MunguMaandiko: “ Enyi malaika wakuu, msifuni Mwenyezi-Mungu;mnaotimiza amri zake na kutekeleza neno lake!Enyi jeshi lote la mbinguni, msifuni Mwenyezi-Mungu;enyi watumishi wake mnaotekeleza matakwa yake!Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote;msifuni popote mlipo katika milki yake. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! ” (Zaburi 103:20-22).“Maana Mungu atawaamuru malaika wake,wakulinde popote uendapo” (Zaburi 91:11).“Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao,na kuwaokoa katika hatari” (Zaburi 34:7).“Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe hai wanne na wale wazee; wakasema kwa sauti kuu:“Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa.” Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini — viumbe vyote ulimwenguni — vikisema:“Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo iwe sifa na heshima na utukufu na enzi,milele na milele.”Na wale viumbe hai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu” ( Ufunuo. 5: 11 -14).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 19

Page 23: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo *Malaika wanawalinda Waisraeli katika vita vyao na Waaramu- 2 Wafalme 6:8-23.*Malaika anamwonya Yusufu akimbilie Misri- Mathayo 2:3-15.*Malaika huwachunga watoto kwa njia ya kipekee- Mathayo 18:10.Malaika huwasaidia waumini waepukane na hatari- Matendo 12:6-11.*Malaika hutekeleza hukumu, kama walivyofanya Sodoma na Gomora- Mwanzo 19:1-29; Kufa kwa mfalme Herode- Matendo 12:23; Nyakati za Mwisho- Ufunuo 16:1; 19:17-18.*Malaika wanaweza kuwaongoza wale wanaomtafuta Mungu wampate yule anayeweza kuwahubiri- Matendo 8:26; 10:3-32.*Malaika watawakusanya waumini wakati wa mwisho- Mathayo 24:31.*Malaika aliwapatia habari Mariamu na Yusufu- Luka 1-2; Mathayo 2:19-20.*Malaika analeta habari za kuzaliwa kwa Yesu- Luka 2:8-15.*Malaika anamtia nguvu Yesu kabla hajashikwa- Luka 22:39-43.*Malaika wanatangaza habari za kufufuka kwa Yesu kutoka kwa wafu- Mathayo 28:1-7; Mariko 16:2-7; Luka 24:1-7; Yohana 20:10-11; Matendo 1:10-11.

*Alimpatia Musa amuri/sheria- Matendo 7:53; Wagalatia 3:19.*Haifai kuwaabudu Malaika- Wakolosai 2:18.*Sisi tutawahukumu malaika- 1 Wakorintho 6:3.*Malaika wanajua hekima ya Mungu kupitia kwa Kanisa- Waefeso 3:8-12.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 20

Page 24: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 21

Page 25: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 2: Mungu na Uumbaji wake wa Vitu Vionekanavyo kwa Macho

Maandiko: Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipokuwa natungwa ndani ya tumbo la mamangu. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika” (Zaburi 139:13-17).

Maelezo MafupiMfano wa 2, ni picha ya sehemu ya uumbaji wa Mungu wa vitu vionekanavyo. Mungu ameonyeshwa akiwa katika Kiti chake cha Enzi, kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kuna msitari unaomtenganisha Mungu na uumbaji wake. Msitari huu haumaanishi kwamba Mungu yuko mbali nasi, lakini lengo lake hasa ni kutuonyesha tofauti iliyoko kati ya Muumbaji na viumbe. Chini ya msitari kuna sehemu ya dunia.

Tumejifunza kwamba Mungu aliumba kila kitu tukionacho kwa macho na tusichokiona kwa macho. Je, Mungu aliviumbaje vitu vyote hivi? Katika Biblia tunajifunza kwamba Mungu aliuumba ulimwengu kwa Maneno ya kinywa chake. Alisema, “Mwanga uwe,” na mwanga ukawa. Aliviumba vitu vyote kutoka kwa utupu kwa kufanya kusema tu. Kinyume chake wanadamu hutengeneza vitu kutokana na rasilimali zilizoko duniani.

Mpango wa uumbaji wa Mungu waonyesha lengo maalumKwa hiyo tukiangalia jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu, tunaweza kuona kwamba aliuumba kwa lengo maalum na kwa mpangilio fulani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa muda wa siku sita. Siku hizi sita zinaonyesha mpangilio wa uumbaji, kuanzia vitu visivyo muhimu sana mpaka kuumbwa kwa vitu muhimu zaidi. Ukitazama mchoro, unaweza kufuatilia mpangilio wa uumbaji kuanzia juu hadi chini na upande wa kulia. Katika kuumba kwake, Mungu alianza na mwanga na giza. Kisha kutokea hapo akaziumba mbingu, maji, na nchi; ikiwemo mimea, na miti ya matunda; jua, mwezi, nyota; samaki, na ndege; wanyama wa porini na wa kufugwa; na hatimaye akawaumba binadamu; mke na mume. Pamoja na kuumba vitu vyote hivi, Mungu aliumba majira na wakati wa mavuno. Vilevile aliwafunza ndege jinsi ya kutengeneza viota vyao na akawafunza mafundi stadi jinsi ya kubuni mitindo. Aliumba kina cha dunia na kina cha moyo wa mwanadamu. Mungu aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Mwanamume na Mwanamke, kilele cha uumbaji wa MunguKatikati ya picha yetu kuna mwanamume na mwanamke. Watu hawa wawili wameonyeshwa hapa kwa sababu hao ndio kilele cha uumbaji wa Mungu. Tunajua hivyo sio tu kutokana na mpangilio wa uumbaji, bali pia kutokana na ujumbe mzima wa Biblia. Biblia inasema kwamba Mungu alipokuwa akiumba vilindi vya dunia, aliona jinsi tulivyokuwa bila umbo lolote. Hii ina maana kwamba Mungu alituona mimi na wewe, wakati alipokuwa akiumba ulimwengu. Alijua jinsi mimi na wewe tungalivyoumbwa katika wakati ujao. Biblia pia inasema kwamba ameziandika siku zetu zote katika kitabu. Hajaiacha nje hata moja. Kwa hivyo uwe ukijua kwamba Mungu alipokuumba alikuwa na lengo fulani! Yeye hakufanya hivyo kwa viumbe vyake vingine, bali kwa mwanadamu pekee. Ukiangalia tena mchoro, upande wa kushoto, utaona sehemu tofauti tofauti hapa duniani. Kunayo milima, majangwa, nchi tambarare zenye maua, na misitu iletayo mvua. Hizo ni baadhi tu ya sehemu nyingi zilizoumbwa na Mungu. Mungu alijiwekea ushahidi katika mioyo yetu kupitia kwa vitu alivyoviumba duniani. Vitu hivi vyote tunavichukulia kuwa ushahidi, au Ufuno wa Jumla. Mungu amejifunua kwa watu wote kupitia kwa asili ya uumbaji wake. Unaweza kuona rehema zake kupitia kwa mvua ambayo huwapa maji binadamu, mimea na wanyama. Mungu hunyeshea mvua yake kwa watu waovu na wema. Kupitia kwa milima, tunaweza kuona ukuu wa Mungu. Katika enzi za Biblia, milima hii ilikuwa ikitumiwa na watu kama mahali pa kukimbilia usalama na pia pa kujisitiri. Jinsi jua linavyochomoza na kutua kila siku, ndivyo tunavyoona uaminifu wake katika kazi anazozifanya ulimwengu mzima. Uaminifu huu wa Mungu unaleta matumaini ya kutarajia mambo mapya kila siku. Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kujifunza juu ya

Copyright © 2007 Tammie Friberg 22

Page 26: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mungu kwa kutazama uumbaji wake. Biblia inasema kwamba Mungu amejiwekea ushahidi unaomhusu hapa duniani, hivyo sharti sote tumjue yeye kama Bwana na mwokozi wetu.

Mungu aliwapanga watu duniani kama alivyopenda yeye mwenyeweVilevile Biblia inasema kwamba Mungu aliwapanga watu duniani kama alivyopenda yeye mwenyewe. Watu wengine aliwaweka katika sehemu zenye milima, na wengine aliwaweka katika maeneo yenye majangwa. Mungu alifanya hivyo ili watu waweze kumfuata na kumfikia (Matendo 17:26-27). Ukiutazama mchoro wa somo hili, utaona kwamba kuna mipaka iliyowekwa na Mungu katika ya sehemu moja hadi nyingine. Kwa hiyo sasa unaweza kuelewa kwamba lengo la Mungu kuwaweka watu wengine katika maeneo yenye jangwa, ni kwamba watu hao waweze kumtegemea yeye kwa mahitaji yao ya chakula na mengineyo ya kimaisha. Familia ni shauri ya MunguSasa tukiangalia sehemu ya katikati ya picha tutaona kwamba kuna familia au jamii. Kuna duara linalozunguka familia. Hii inaonyesha kwamba kila familia ni kipengele kinachoundwa na mume na mke. Kitengo hiki cha cha mume na mke ndicho kinachounda familia, huku watoto wakiwa ni wa watu hao wawili waliooana. Familia inaweza kuishi na kuchangama na watu wengine katika jamii, lakini familia ni kipengee cha kipekee au kilichotofauti na vipengee vingine.

Mungu aliwaumba Mme na Mke kwa mfano wake mwenyeweKitu muhimu kabisa ambacho tunastahili kujifunza juu ya uumbaji wa Mungu wa mume na mke ni hiki: Mungu aliwaumba kwa mfano wake mwenyewe. Mungu ni Roho, kwa hiyo Biblia inaposema kwamba wanadamu wameumbwa kwa mafano wa Mungu, mfano huo sio wa kimwili bali unarejea hali ya Mungu pamoja na asili yake ya uadilifu. Ukuu wa Mungu na asili yake ya udilifu ni wa kina sana hivi kwamba wanadamu walioumbwa, yaani mke na mume walikuwa hawana budi kuudhihirisha mfano huo wa Mungu. Mungu ni Roho, na hana jinsia, yeye sio mke wala mume. Lakini kwa kuwaumba watu wawili; mke na mume na wote kudhirihisha mfano wake, Mungu aliweka mpango mahsusi wa uhusiano kati ya mke na mume.

Kulingana na Mungu: Ndoa sharti iwe ya watu wawili wa jinsia tofauti; mke na mumeJambo la kwanza tunalostahili kujua juu ya mpango wa Mungu ni kwamba ndoa sharti iwe ya watu wawili wa jinsia tofauti; mke na mume. Ndoa yoyote nyingine ni kinyume cha mfano wa Mungu na mpango wake juu ya ndoa. Kwa hiyo basi mwanamume hana ruhusa ya kuoana au kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine; vivyo hivyo mwanamke hana ruhusa ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine. Ni vyema na muhimu kutambua kwamba mpango wa Mungu kuhusu jamii ni mwanamume aoe mwanamke mmoja tu. Lakini cha kusikitisha ni kwamba amri hii haikufuatwa kikamilifu na watu wa enzi ya Biblia na hata leo vilevile haifuatwi na watu wa sasa. Mpango wa Mungu katika ndoa ya mke na mume ni kumdhihirisha yeye, asili yake ya uadilifu, hali yake ya kibinafsi na ile ya uhusiano, na upendo wake udumuo hadi milele. Uhusiano kati ya mtu na mumewe hautaki kamwe kutatizwa na watu wengine wa nje, kama ilivyo pia na uhusiano wetu na Mungu. Mungu hapendi watu wake waabudu miungu mingine. Kwa hiyo katika maswala ya ndoa na mahusiano, hakustahili kuingia uzinzi kabla ya ndoa na hata baada ya ndoa. Ngono sharti iwe kati ya watu wawili wa jinsia tofauti waliooana kwa njia inayostahili. Ndoa kati ya mme mmoja na mke mmoja yaonyesha uaminifu wa Mungu.

Mpango wa Mungu wa jukumu la wazazi kuwafundisha watoto wao kumjua MunguJambo la pili katika mpango wa Mungu juu ya ndoa ni hili: Mungu aliwaagiza Adamu na mkewe kuzaana na kuongezeka katika dunia. Wawili hao walikuwa na jukumu la kuwalea watoto watakaowazaa katika njia za kiungu. Katika mchoro huo huo, ukiutazama utaona kwamba kuna picha ya Biblia, imewazunguka Bwana na Bibi, kando yao kuna watoto wao, biblia yawafundusha jinsi ya kuishi. Kazi kubwa inayowakabili wazazi ni ile ya kuhakikisha kwamba watoto wao wanamjua Mungu na kumwamini kama mwokozi wao. Hii ina maana kwamba kabla watoto wetu hawajaenda kulala, ni vyema kuwafunza mambo yanayomhusu Mungu na mapenzi yake. Vivyo hivyo mafunzo hayo yanastahili kuendelea wakati wanapoamka asubuhi, wanapokaa chini kula chakula, na hata wanapoziendea shughuli zao za kila siku. Nyumbani ndipo mahali ambapo watoto wanaweza kujifunza mengi juu ya Mungu kwa kuwatazama jinsi wazazi wao wanavyohusiana na Mungu na kuhusiana wao wenyewe wakati wa raha na wa shida. Watoto wakiyaona haya wataweza kujifanyia maamuzi bora. Wataweza kuchagua na kufuata njia bora na kwa kufanya hivyo wataepuka kufuata njia iendayo upotevuni na kuabudu miungu ya uongo. Kusoma Biblia kila siku, kujadiliana, kuomba, na kumwabudu Mungu ni sehemu ya kila siku katika kujifunza kuwa mwanafunzi bora wa Yesu. Biblia ni neno la Mungu na kila tunapolisoma huwa na athari nzuri za kiroho katika maisha yetu. Kwa hiyo ni lazima kila siku tujitengee muda wa kulisoma neno la Mungu. Zoezi hili ni zuri na linafaa kuanzishwa kama desturi katika familia na kupokezwa watu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 23

Page 27: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

wa vizazi vijavyo. Ukifanya hivyo utaweza kumzalia Mungu matunda hata baada ya kuaga dunia, kwa sababu utakuwa umeanzisha desturi ya kukuza maisha ya kiroho katika familia yako.

Mke na mume wote huunda familia mpyaMke na mume wote huunda familia mpya. Biblia inasema kwamba wakati watu wawili; mke na mume wanapooana, yule mwanamume huacha jamaa zake na huungana na mkewe na wote huwa mwili mmoja. Kunao watu wengine ambao bado wanafuata utamaduni wao kwa kushikamana na mababu zao waliokufa. Watu hao huona kwamba uhusiano kati yao na mababu zao ndio muhimu zaidi kuliko uhusiano katika yao na familia zao za karibu; yaani mke na mume. Lakini huu si mfano mzuri wa kufuata. Wakati mume na mke wanapounganishwa, huwa mwili mmoja. Uhusiano huu wa kuwa mwili mmoja ni uhusiano wa uaminifu, una gusa kila sehemu ya maisha-kihisia, kimwili, kiroho, na kiuhusiano. Hii haimaanishi kwamba kila mshika dau katika uhusiano huo atapata mahitaji yake yote. Mahitaji mengine hupatikana tu kwa mtu kuwa na uhusiano na Mungu. Hii haimaanishi kwamba watu wa ukoo hawana maana.

Ndoa ni uhusiano wa mwili mmojaKatika mfano wetu utaona kwamba mume na mke wanaheshimiana kwa kufuata uongozi wa Kristo. Uhusiano wa kuwa mwili mmoja unaonekana pia katika waraka wa Paulo kwa Waefeso sura ya 5. Paulo anaonyesha wazi jinsi uhusiano wa mume na mke unavyostahili kuwa. Anasema katika waraka huo kwamba mke ni amtii mume kama kumtii Bwana ; na mume ampende mke wake kama Kristo alivyolipenda kanisa na kujitoa sadaka kwa ajili yake. Matokeo kamili ya uhusiano wa jinsi hiyo ni kuwa watu hao wawili watakuwa mwili mmoja, kila mmoja akimtii mwenzake(Waefeso sura ya 5:21, 31). Yesu Kristo atakuwa Bwana wa familia au nyumba hiyo. Ukiangalia mchoro utaona kwamba mume na mke wake wametazama mbinguni kama ishara ya kuwa tiyari kumtii Mungu. Tunapomtii Mungu, kuwa watakatifu, na kupokea hekima kutoka kwake, basi huwa tunamheshimu Mungu. Kwa hiyo uhusiano wa mwili mmoja hufanya kazi pale tu Kristo anaporuhusiwa kuwa Bwana wa maisha ya wanandoa hao.

Jukumu la MmeMume ndiye kichwa au shina(mwanzo,asili) wa familia. Yeye hukidhi mahitaji ya familia yake, na pia ndiye mlinzi na nguzo ya jamii yake. Biblia inasema kwamba mtu yeyote ambaye hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani wake, basi mtu huyo ameikana imani na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini (1 Timotheo 5:8). Kwa hiyo mume sharti awe mwangalifu na kutumia pesa zake kwa hekima na kwa ukarimu. Jinsi mume anavyoishi na kufanya kazi katika jamii ndivyo familia yake inavyotambuliwa na watu. Ikiwa atafanya makosa, atakosa kuwa mwaminifu, atakuwa na ubinafsi, au kumchukiza mkewe na watoto wake, au jamii kwa jumla, basi atakuwa akiikosea heshima familia yake. Mume akiuwakilisha upendo wa Mungu na utunzaji wake, na kweli yake, basi atakuwa anaiheshimu familia yake. Kwa hiyo ni muhimu mume akimwomba Mungu kila wakati ampe hekima na mwongozo kwa mambo ya kimaisha na ya kifamilia, ili Bwana Yesu aweze kujulikana na kuheshimiwa katika jamii zetu. Kina baba hawastahili kuwaudhi watoto wao au kuwaadhibu kupita kiasi. Katika kitabu cha Mithali, ni wazi kwamba waume na pia wake hushiriki katika kuwafundisha watoto njia za Bwana. Jukumu la BibiKina mama hawastahili kuwa wasengenyaji. Badala yake wanastahili kutunza familia zao, kwa maana Mungu amewapa ujuzi na uwezo wa kuwalea na kuwatunza watoto wao. Vilevile kina mama wana ushawishi mkubwa katika maisha ya kiroho ya watoto wao kwa kuwaonyesha mfano wa uaminifu kwa Bwana. Wanaweza kufanya kazi hiyo ya kuwafundisha watoto njia za Mungu kwa kushirikiana na waume zao. Wakati mwingine jukumu la kina mama katika kuwalea watoto limepita lile la kina baba, kwa sababu mara nyingi kina mama wanakuwa na watoto kwa muda mwingi katika siku moja. Wanawake wameumbwa na asili ya ulezi. Hivyo basi kina mama wanapokuwa wakimtumikia Mungu kwa vipawa vyao sharti wawe waangalifu kutunza familia zao kila siku, hususan watoto wao. Aidha wanaweza kufanya kazi kwa mikono yao na kupata fedha za kusaidia kukidhi mahitaji ya familia zao. Hawastahili kutumia pesa vibaya. Kina mama ndio mameneja wa nyumba zao. Kwa hiyo ni sharti wawe waangalifu wasizibomoe nyumba zao kwa manung’uniko, uvivu, na maneno yasiyojenga.

Jukumu la watotoWatoto sharti wawatii wazazi wao ili waweze kuishi maisha marefu duniani. Katika Biblia kuwaheshimu wazazi lilikuwa jambo muhimu sana, kwa maana kulikuwa kumekaribiana na kutii. Watoto huwaheshimu wazazi wao kwa kuwatii nyumbani au hata wakiwa mbali na nyumbani, kwa kufanya kazi wapewazo na wazazi wao, kufanya kazi za shule kwa uaminifu na kwa kuwaheshimu watu wote katika jamii. Kitabu cha Mithali kinatoa maagizo kwamba watoto wawatii na kuwaheshimu wazazi wao. Mungu amewapa watoto wazazi, ili wazazi hao waweze kuwafundisha watoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 24

Page 28: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

wao kuishi kwa kuzifuata sheria za Mungu. Wakizifuata njia za Mungu, watakuwa na busara, na wataepuka kuzifuata njia potofu. Watoto sharti wawe waangalifu wakati wanaposhikana na watoto wengine. Ni vyema kuepuka marafiki wabaya. Vilevile watoto niwaonyeshe uaminifu wao kwa kuzifuata njia za Mungu, wawapo nyumbani au nje na marafiki zao.

Kuwatunza watu wa ukooPia ni muhimu kuwatunza wazazi wetu wakati wanapokuwa wazee. Tukifanya hivyo tutakuwa tunawalipa kwa kazi ile waliyotufanyia wakati walipokuwa wakitulea tukiwa wadogo. Mungu pia hufurahi wakati tunapowaheshimu na kuwatunza wajane na wazee katika jamii zetu. Kumbuka kwamba vitu vyote viliumbwa na Yesu na aliviumba kwa ajili yake. Mtume Yohana anasema kwamba vitu vyote viliumbwa kwa Neno la Mungu (Yesu). Neno hilo lilifanyika mwili na kuishi kati yetu.

Mafundisho Ya Somo La 2Uumbaji wa Mungu Kuumbwa kwa wanadamu:

Mpango maalumu aliouweka Mungu juu ya familiaMungu aliumba ulimwengu kwa lengoMwanamume na mwanamke walikuwa kilele cha uumbaji wa MunguMungu aliwaweka wanadamu duniani kama alivyopendaFamilia ni mpango wa MunguMungu aliumba mwanamme na mwanamke kwa mfano wakeMungu alipanga kwamba ndoa iwe baina ya Mume mmoja na mke mmoja

Mungu alipanga kwamba nyumba iwe mahali pa mafundishoMungu alipanga kwamba mume, mke, na watoto wawe ndio familia Ndoa iwe uhusiano wa kimwili wa mmoja kwa mmojaWajibu wa mumeWajibu wa mkeWajibu wa watoto Kutunza jamaa moja

Marejeo Ya Mafundisho Ya Somo La 2

Uumbaji wa MunguMaandiko: "Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mimi, naam mimi, ndimi ninayekufariji. Kwa nini wewe unamwogopa mtu ambaye hufa, binadamu ambaye hutoweka kama nyasi? Wewe umenisahau mimi Mwenyezi-Mungu Muumba wako,niliyezitandaza mbingu,na kuiweka misingi ya dunia! Wewe waendelea kuogopa siku zote,kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu wako,kwamba yuko tayari kukuangamiza! Lakini hasira yake itafika wapi? Wanaodhulumiwa watafunguliwa hima,hawatakufa na kushuka shimoni,wala hawatatindikiwa chakula. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; nivurugaye bahari, mawimbi yake yakanguruma;Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina langu! Nimeyaweka maneno yangu mdomoni mwako; nimekuficha katika kivuli cha mkono wangu. Mimi nilizitandaza mbingu,nikaiweka misingi ya dunia.Mimi nawaambieni enyi watu wa Siyoni: ‘Nyinyi ni watu wangu” (Isa. 51:12-16).“Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli;Mungu aliye hai, mfalme wa milele.Akikasirika, dunia hutetemeka,mataifa hayawezi kustahimili hasira yake. Basi, utawaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.” Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake;kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu” (Yer. 10:10-12).” Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari. Umejizungushia mwanga kama vazi,umezitandaza mbingu kama hema;umejenga makao yako juu ya maji ya mbingu.Umeyafanya mawingu kuwa gari lako;waruka juu ya mabawa ya upepo,waufanya upepo kuwa mjumbe wako,moto na miali yake kuwa watumishi wako. Dunia umeiweka imara juu ya misingi yake,ili isitikisike milele. Uliifunika dunia kwa bahari kama vazi,na maji yakaimeza milima mirefu. Ulipoyakaripia, maji yalikimbia, yaliposikia ngurumo yako yalitimka mbio. Yaliporomoka toka milimani hadi mabondeni,mpaka pale mahali ulipoyatengenezea. Uliyawekea hayo maji mipaka,yasije yakaifunika tena dunia. Umetokeza chemchemi mabondeni,na mikondo yake ipite kati ya vilima. Hizo zawapatia maji wanyama wote porini. Humo pundamwitu huzima kiu yao. Ndege hujenga viota vyao katika miti ya hapo,hutua katika matawi yake na kuimba. Toka juu angani wainyeshea milima mvua,nayo dunia waitosheleza kwa baraka yako. Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo,na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: divai ya kumchangamsha,mafuta ya zeituni ya kumfurahisha,na mkate wa kumpa nguvu. Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha;naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha. Humo, ndege hujenga viota vyao;korongo hufanya maskani yao katika misunobari. Milima mirefu ni makao ya mbuzimwitu; na pelele hupata maficho yao miambani. Umeuumba mwezi utupimie majira;jua nalo lajua wakati wa kutua. Waleta giza, usiku waingia;nao wanyama wote wa porini wanatoka: wanasimba hunguruma wapate mawindo,humngojea Mungu awape chakula chao. Jua lichomozapo hurudi makwao,na kujipumzisha mapangoni mwao. Hapo naye binadamu huenda kwenye shughuli zake;na kufanya kazi zake mpaka jioni. Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari — kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visiohesabika, viumbe

Copyright © 2007 Tammie Friberg 25

Page 29: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli,na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo. Wote wanakungojea wewe, uwapatie chakula chao kwa wakati wake. Wanaokota chochote kile unachowapa;ukifumbua mkono wako wanashiba vinono. Ukiwapa kisogo, wanaogopa;ukiondoa pumzi yao, wanakufa,na kurudi mavumbini walimotoka. Ukiwapulizia pumzi yako, wanaishi tena;wewe waipa dunia sura mpya. Utukufu wa Mwenyezi-Mungu udumu milele;Mwenyezi-Mungu apendezwe na matendo yake mwenyewe. Huitazama dunia nayo hutetemeka,huigusa milima nayo hutoa moshi! Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote;nitamsifu Mungu wangu muda wote niishipo. Upendezwe, ee Mwenyezi-Mungu, na mawazo haya yangu;maana furaha yangu naipata kwako. Wenye dhambi waondolewe duniani, pasiwe na waovu wowote tena! Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Msifuni Mwenyezi-Mungu! ” (Zaburi 104).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Hadithi ya uumbaji- Mwanzo 1-2.*Nafasi ya Hekima katika uumbaji- Methali 8:22-31.*Mungu aliweka wakati na mahali ambapo kila mtu angeshi- Matendo 17.*Zaburi iliandikwa ili iwe ushahidi kwa mataifa mengine- Zab. 48, 82, na 104.*Mungu anamjibu Ayubu- Ayubu 38-41.*Ayubu anamjibu Bwana- Ayubu 42.*Ushahidi wa Yona- Yona 1-4 (1:9).*Mungu ataumba Mbingu mpya na Nchi mpya- Isa. 65:17-25.*Mungu anafanya kazi katika uumbaji wake siku zote- Zab. 145; Yohana 5:17; Ebr. 1:2-3.Soma Zaburi 104 huku ukilinganisha na nyimbo za kipagani za Ugaritic wakati huo. Mwandishi anachukua kifungu cha mziki wa kuimbiwa Baali ili aonyeshe kwamba Mungu wa Israeli ndiye Mungu wa mkuu na wa kweli.

Zab. 104:3- Mungu ameyafanya mawingu kuwa gari lake.

Ugaritic- Baali ni dereva wa mawingu.

Zab. 104:4- Watumishi au malaika wa Bwana wanaweza kugeuka wakawa moto na ndimi za moto.

Ugaritic-moto na ndimi zake hutumiwa kutayarishia dhahabu na fedha za hekalu la Baali.

Zaburi 104:7- Ngurumo za radi ndiyo sauti ya Bwana.

Ugaritic- ngurumo za radi ni sauti ya Baali.

Zaburi 104:16- Mungu ndiye aliyepanda mierezi ya Lebanoni.

Ugaritic- Miti kutoka Lebanoni hutumika kujengea hekalu la Baali.

Zaburi 104:13- Bwana humwagia maji milima kutoka juu.

Ugaritic- Kufungua dirisha la Baali ili amwagie maji dunia.

Zaburi 104- Zaidi ya hayo, Mungu ndiye anayewapatia watu maji na chakula kwa viumbe vyote. Yeye hufanya majira. Yeye anatunza kila jambo duniani.

*Mungu anajionyesha wazi kupitia kwa uumbaji- Waroma 1:20.*Mungu hujionyesha kwa mioyo ya wanadamu- 2 Wakorintho 4:6.*Kwa nini tuogope watu ambao ni kama nyasi, na tumsahau Mungu aliyetuumba?- Isa. 51:12-13, 16.*Mungu aliumba watu, akaona mili yao ndani ya mchanga kabla hajawaumba- Zaburi 139:14-15.*Mungu aliumba vitu vyote, vionekanavyo na visivyoonekana- Mwanzo 1-3; Wakolosai. 1:16.*Mungu aliumba kwa kutumia neno- Zab. 33:6, 9; Ebr. 11:3; Yohana 1.*Mungu alifanya usiku na mchana, mwaka na vuli, na mipaka- Zab. 74:16-17.*Mungu aliumba kuzimu na vilele vya milima-Zab. 95:4-7.*Vitu vyote viliumbwa kwa mapenzi ya Mungu -Ufunuo 4:11.*Ulimwengu uliumbwa kwa hekima na ujuzi- Yer. 51:15.*Kuna kitabu ambacho Mungu ameandika siku za kila mtu- Zaburi 139:14-16.*Mungu huwanyeshea mvua wazuri na wabaya- Mathayo 5:45.*Msaada wetu hutoka kwa Muumba wetu- Zab. 121.*Yeye aliumba nguvu za upepo, akaumba maji, akatengeneza njia ya radi, na kukadiria hekima ya uumbaji- Ayubu 28:24-27.*Kwa hekima aliweka misingi ya dunia, Kwa maarifa akaweka mbingu pahali pake. Na kwa ujuzi vilindi viligawanywa mawingu yakatoa umande - Meth. 3:19.*Uumbaji unaonyesha utukufu wa Mungu-Zab. 19:1-4.*Yeye hushikilia viumbe vyote duniani- Wakolosai. 1:15-17.

Kuumbwa kwa wanadamu: Mungu alikuwa na mpango maalumu kwa familiaMaandiko:“Watoto ni riziki kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; watoto ni tuzo lake kwetu sisi. Watoto walio na nguvu,ni kama mishale mikononi mwa askari. Heri mtu aliye na mishale hiyo kwa wingi. Hatashindwa atakapokabiliana na adui mahakamani” (Zab. 127:3-5).“Aliwapa wazawa wa Yakobo masharti,aliweka sheria katika Israeli,ambayo aliwaamuru wazee wetuwawafundishe watoto wao; ili watu wa kizazi kijacho,watoto watakaozaliwa baadaye, wazijue, nao pia wawajulishe watoto wao, ili wamwekee Mungu tumaini lao,wasije wakasahau matendo ya Mungu,bali wazingatie amri zake. Wasiwe kama walivyokuwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 26

Page 30: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

wazee wao,watu wakaidi na waasi;kizazi ambacho hakikuwa na msimamo thabiti,ambacho hakikuwa na uaminifu kwa Mungu” (Zab. 78:5-8).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Watu waliumbwa kwa mfano wa Mungu- Mwanzo 1:26-28; 5:1; 9:6 (Usiue, Mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu); Waefeso 4:22-23 (Aliumbwa awe kama Mungu katika haki na utakatifu); Wakolosai. 3:9-10; Yakobo 3:9-10.*Mbele za Mungu wanawake wako sawa na wanaume- Wagalatia 3:28.*Wanadamu ni wakuu wa wanyama- Mwanzo 1:28; 2:19-20.*Watoto ni zawadi kutoka kwa Bwana- Zab. 127:3-5.*Watu wanajua mema na mabaya mioyoni mwao- Mwanzo 3:6-11; 4:8-12); Ndugu zake Yusufu- Mwanzo 42:21.*Watu wana hiari ya kuchagua kumtumikia na kumtii Mungu- Mwanzo 2:16-19.*Ndoa ni uhusiano wa kimwili wa mmoja kwa mmoja- Mwanzo 2:21-25; Waefeso 5:21-33 (kuhusiana na ndoa); Mathayo 19:3-9; Mariko 10:1-12 (Yesu anajibu swali kuhusu talaka); 1 Wakorintho 6:12-20 (Paulo anaongea juu ya umalaya).

*Mungu alituumba katika tumbo za mama zetu- Zab. 139:13.*Tulivyoumbwa ni vya kutisha na kuajabisha- Zab. 139:14.*Mungu aliumba matajiri na maskini sawasawa- Meth. 22:2.*Mungu akaweka siku za watu- Zaburi 139:16.*Mungu ni Mfinyanzi, sisi ni udongo, Malengo yake kwetu yanaweza kubadilika, na sisi tunaweza kutii ama tukakataa kutii Isa. 64:8; Yer. 18:1-11.*Mungu alituita katika haki, na tuwe mashahidi- Isa. 42:5-6.*Mwanadamu aliumbwa ampatie Mungu utukufu- Isa. 43:7.*Watu watawale viumbe- Zab. 8:3-8.*Uumbaji mpya na mfano mpya wa Mungu, Mume, mke, na watoto- 2 Wakorintho 3:18; Wakolosai. 3:5-19.Waume na wake zao:*Kila mmoja naajitoe kwa mwenzake katika kumheshimu Kristo- Waefeso 5:21.*Wake watii kama wanavyomtii Bwana- Waefeso 5:22-24.*Wanawake wapevu wawafunze wanawake wachanga kuwapenda waume zao na watoto wao, na sio kusengenya watu- Tito 2:3-5.*Waume, wapendeni wake zenu kama mnavyojependa, huku mkiwaza vile Kristo alivyomwokoa- Waefeso 5:25-31.*Ishini katika uhusiano wa kimwili wa mmoja kwa mmoja- Waefeso 5:31.*Waume msiwe wakali kwa wake zenu- Wakolosai. 3:19.*Maagizo maalumu kwa wale wenye waume ambao si waumini- 1 Petro 3:1-6.*Watoto watiini wazazi wenu, Akina baba msiwachokoze na kuwakasirisha watoto- Waefeso 6:1-4.*Mungu anataka tuzae na tulee watoto wa kimungu- Mal. 2:15.*Baba na mama wana wajibu wa kuwalea watoto katika njia za Mungu- Kumbukumbu 31:12-13; Meth. 1:8; 6:20-23; 22:6.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 27

Page 31: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 28

Page 32: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 3: Jinsi Mungu Anavyowasiliana na Wanadamu.

Maandiko: “Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii, lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanawe. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu, akamteua avimiliki vitu vyote.” “Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na mafuta. Neno hili huchambua nia na fikira za mioyo ya watu” (Waebrania 1:1; 4:12).

Maelezo MafupiKatika mfano huu kuna jengo moja lenye orofa tatu. Kila orofa ina picha zake maalum. Jengo hili limejengwa katika maeneo yenye nyumba nyingi na limezungukwa na nyumba nyingi ndogondogo. Ikiwa mtu anataka kuona kinachowazunguka, itawalazimu kupanda jengo na kwenda katika orofa ya juu kabisa na kutazama nje. Picha hii ni mfano wa viwango vitatu vya kusikia kutoka kwa Mungu. Orofa ya juu kabisa inawakilisha kiwango cha juu na hapo ndipo mtu alipo karibu kabisa na Mungu, kwa hiyo akiwa hapo anaweza kumwona na kumsikia Mungu anapowasiliana naye. Kama ilivyo rahisi kuona mandhari ya ulimwengu kutoka mahali pa juu, vivyo hivyo ni rahisi na wazi kumsikia Mungu kutoka katika kiwango hicho kama ilivyoonyeshwa pichani. Unaposhuka hadi orofa za chini, sharti uwe mwangalifu usikivu wako wa Mungu usikatizwe na jambo lolote. Ni lazima wakati wote urejee yale uliyoyasikia kutoka kwa Mungu katika orofa ya juu zaidi. Unapokuwa katika orofa cha chini, sharti uwe mwangalifu kwa maana jinsi unavyoshuka chini ndivyo mawasiliano yako na Mungu yanavyoweza kukatizwa na mawazo yako mwenyewe, imani zitokanazo na utamaduni wako, na hata vitu vya bandia vya Shetani. Katika orofa ya juu, Mungu huzungumza nasi kwa uwazi kwa kupitia kwa Biblia, Yesu, na Roho Mtakatifu. Njia hizi tatu za mawasiliano kati yetu na Mungu zinaitwa Ufunuo Maalum. Katika orofa ya pili, utaona kuna mtu anaomba, mwingine anaota ndoto au kuona maono, na waaumini wanatiana moyo. Njia hizi za kuisikia sauti ya Mungu zinaitwa Mawasiliano ya Kibinafsi kutoka kwa Mungu. Katika orofa ya chini kabisa au ya kwanza kuna picha za watu, milima, na mvua. Mungu hutumia vitu alivyoviumba ili kutoa ujumbe fulani unaohusu tabia au hulka yake. Njia hii ya mawasiliano inaitwa Ufunuo wa Jumla.

Kiwango cha kwanza: Mungu huwaziliana nazi kupitia ufunuo maalum: Biblia, Yesu na Roho MtakatifuSasa turudie ile orofa ya tatu ambapo kuna picha ya Yesu, Biblia, na Roho Mtakatifu. Katika njia zote za mawasiliano, njia muhimu zaidi ni ile ya mawasiliano kupitia kwa Yesu, Biblia na Roho Mtakatifu. Kifungu cha kwanza cha Maandiko kutoka katika Waebrania 1:1 kinatuonenyesha kwamba Mungu amenena nasi katika Agano Jipya kupitia kwa Mwanawe Yesu. Yesu alitufundisha kuhusu Ufalme wa Mungu na jinsi tunavyostahili kuishi kama wana wa Ufalme huo. Kifungu cha pili kutoka katika Waebrania 4:12 kinatufundisha kwamba Neno la Mungu li hai, lina nguvu na linaweza kupenya hadi ndani katika kilindi cha mioyo yetu. Tunaweza kuyatia nguvu masikio yetu ya kiroho ili yaweze kusikia ujumbe wa Mungu kwa kulisoma na kujifunza Biblia. Biblia ina habari zinazohusu matendo ya Mungu na mipango yake katika historia. Habari hizo zinamfunua yeye na wokovu wake. Roho Mtakatifu ameonyeshwa hapa kwa sababu yeye ndiye kiongozi na mshauri wetu. Yeye hutufundisha kile cha kusema wakati tunapokuwa mbele ya watu kutoa ushahidi juu ya Mungu. Roho Mtakatifu huzungumza nasi na kutoonyesha dhambi zetu ili tuweze kuzitubu. Ukiangalia picha ya somo hili utakuta kwamba kilele cha jengo hili kinamwelekea Mungu. Kwa hiyo Yesu, Biblia, na Roho Mtakatifu ndizo njia za moja kwa moja anazotumia Mungu kuwasiliana nasi. Njia hii ya mawasiliano inawalenga waumini wote, sio tu kwa viongozi wa kanisa. Neno la Mungu ndilo chanzo cha Ukweli wote. Kupitia kwalo tunaweza kusikia kutoka kwa Mungu. Njia hizi tatu za mawasiliano ya moja kwa moja; yaani za kupitia kwa Yesu, Biblia na Roho Mtakatifu zinaitwa Ufunuo Maalum.

Kiwango cha pili- Mungu hunena nasi kupitia Mawasiliano ya KibinafsiKatika orofa ya pili utaona watu wanaomba, wakiota ndoto, wakiona maono na kutiwa moyo na waumini wenzao au viongozi. Kiwango hii cha mawasiliano inaitwa Mawasiliano ya Kibinafsi, hata ijapokuwa vile viwango vingine viwili ni vya kibinafsi pia. Watu wengine hufikiria kwamba kiwango cha pili cha mawasiliano ndicho muhimu zaidi. Viongozi

Copyright © 2007 Tammie Friberg 29

Page 33: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

wanaojivunia mawasiliano kama hayo wanaweza kuwa na wafuasi wengi sana. Lakini cha kusikitisha ni kwamba watu wanaweza kudanganywa katika mawasiliano ya aina hii, hii ni kwa sababu Shetani pia hutumia njia hii kuwasiliana na watu. Isitoshe, wakati mwingine sisi huingiza mawazo na ufasiri wetu wenyewe katika kuuelewa ujumbe wa Mungu. Vilevile marafiki au viongozi wetu wanaweza kutupa ushauri ambao unahitilafiana na mafundisho ya Yesu. Manabii na walimu wa uongo ambao lengo lao ni kijipatia pesa wanaweza kuwadanganya watu kwa kudai kwamba wamepokea ujumbe moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Mbali na kasoro hizi katika mawasiliano ya aina hii, bado njia hii ni muhimu katika kupokea mawasiliano kutoka kwa Mungu. Lakini ni lazima kila Mawasiliano ya Kibinafsi tunayoyapokea au mtu mwingine anyoyapokea, yapimwe katika mizani ya Biblia. Katika Maandiko, manabii wote, wahubiri, na walimu walipimwa kwa ukweli wa Biblia na kwa matokeo ya maneno yao. Mungu hawezi kamwe kwenda kinyume cha Neno lake. Waumini walionyeshwa katika picha ya somo hili wanaonekana wakitiana moyo. Kumbuka kwamba lengo la Mungu ni kuona Wakristo wakitiana moyo na kuhimizana! Aidha ni mpango wake kuujenga mwili wake na kuhakikisha kwamba unakomaa. Kwa hiyo, sio jambo jema kuhukumiana kwa njia ya unafiki. Kuna wakati fulani katika maisha yetu sisi binadamu huwa tunahitaji kutiwa moyo ili tuendelee kumtumikia Mungu hata katika hali ngumu. Wakati mwingine sisi huweza kukengeuka au kupotoshwa na matendo ya wengine, lakini pamoja na hayo sharti tupime kila kitu tunachowasilisha na kusikia kutoka kwa watu kwa kukipima katika mizani ya Biblia.

Maombi ni njia mojawapo inayoweza kutusaidia kupata mwongozo kutoka kwa Mungu. Ni vyema tunapokuwa tunaomba kufungua masikio yetu ya ndani kumsikiza Mungu ili anene nasi kwa hekima na ufahamu. Mara nyingi maombi hugeuzwa na kuwa chombo cha kumwambia Mungu kukidhi mahitaji yetu, badala ya kusikiza yale asemayo na kuyashika. Wakati mwingine mahitaji na matarajio yetu hukita katika mawazo yetu mpaka tukaanza kufikiria kwamba mambo hayo yanaweza kumfanya Mungu kujibu maombi yetu. Lakini Mungu anaweza kutujibu kwa kusema, “Hapana,” au “Subiri jibu.” Mungu huongea na mioyo yetu kwa njia ya kimya, au kwa kuweka wazo lenye uzito katika mioyo yetu. Maombi sio kumwambia Mungu jambo analostahili kufanya, badala yake maombi yanastahili kuwa na sifa hizi tatu; kusikiza sauti ya Mungu, kuwaombea wengine na hatimaye kumwomba Mungu kutupa mahitaji yetu. Sharti tuwe waangalifu tusilitumie Biblia kama chombo cha kumshinikiza Mungu kujibu maombi yetu. Mungu hajibu maombi yetu kwa kuzingatia aya za Biblia tunazozinukuu au ahadi tunazofikiria zinatulenga sisi. Mungu wetu anaitwa “NDIMI NILIYE.” Yeye hutenda kulingana na mapenzi na asili yake mwenyewe na wala sio kwa kushurutishwa na mtu yeyote. Mungu ametuweka hapa duniani ili tuweze kumtumikia. Kunao uwezekano mkubwa wa Mungu kuyajibu maombi yetu kwa kuangalia nia tuliyo nayo, jinsi tunavyoishi, na iwapo mahitaji tuliyoyaomba yanakubaliana na asili yake na mapenzi yake, na wala sio kwa ufasaha wa maneno katika maombi. Katika picha ya somo hili kuna mtu anayeonekana amelala kitandani na huku akiona maono au kuota ndoto. Wakati mwingine Mungu huchagua kuwasiliana na watu kwa kupitia ndoto. Hii hufanyika hasa katika maeneo ambayo watu hawajazisikia habari za Yesu au hawana Biblia katika lugha zao. Mtu anaweza kuona maono ikiwa mtu huyo ana lengo la kumjua Mungu kibinafsi, kama ilivyokuwa kwa Kornelio katika Matendo ya Mitume. Aidha mtu anaweza kuona maono ya kumwezesha kujua mwelekeo wa huduma yake au jinsi ya kuwafikia watu. Ndoto ni njia moja wapo anayotumia Mungu kuwasiliana nasi. Hata hivyo, lazima tuwe waangalifu juu ya ndoto na maono kwa sababu inawezekana mambo hayo yakatoka katika akili zetu au kwa Shetani. Wakati mwingine tunapokuwa na shughuli nyingi mchana, Shetani anaweza kutumia hali hiyo katika ndoto na kututia wasiwasi mwingi. Vilevile wakati mwingine tunaweza kutafsiri vibaya ndoto zetu, na kuziona kuwa ufunuo kutoka kwa Mungu, ilhali sivyo. Viongozi nao wanaweza kuwa na mazoea ya kutumia ndoto kama njia ya kujiongezea mamlaka juu ya wengine, pia wanaweza kutumia ndoto kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe. Watu wanaweza kumfuata kiongozi fulani aotaye ndoto kwa sababu wanatafuta uhusiano wa karibu na Mungu au neno kutoka kwake. Kumbuka kwamba tunaweza kumkaribia Mungu tu kwa kumwamini yeye kama mwokozi wetu, bidii katika maombi, kusoma Biblia, kuwatangazia wengine habari njema, kutumia vipawa vyetu kwa ajili yake, kuishi maisha ya utaua, na kwa kumwabudu yeye. Kuna hatari iwapo watu watawafuata viongozi wanaotegemea sana mfumo huu wa mawasiliano, kwa sababu watu hao wataupuzilia mbali uhusiano wa kibinafsi walio nao na Mungu na kutegemea mwongozo wa ndoto za kiongozi wao. Ndoto zinazotoka kwa Shetani zitawapotosha watu kwa njia moja au nyingine wasimfuate Mungu. Shetani anaweza hata kuwapa ndoto “viongozi wa Kikristo” na kuwafanya kuwa na tabia za ajabu ajabu au litujia ya kushangaza. Viongozi kama hawa hulifanya kanisa kuwa dhaifu na kuwakengeusha watu kutoka katika njia ya Mungu. Ndoto zote

Copyright © 2007 Tammie Friberg 30

Page 34: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

sharti zipimwe katika mizani ya Maandiko. Sharti Maandiko yawe chanzo cha kweli yote, ambayo kupitia kwayo tunaweza kupima kila aina ya mafundisho. Katika Biblia, Mungu hakuwapa watu ndoto ili wamfuate nabii fulani au kiongozi, bali lengo la ndoto ni kuwafanya watu wamjue Mungu na kuokoka.

Ijapokuwa ishara na miujiza havijawekwa katika mchoro wetu, wakati mwingine vimetajwa katika Biblia kama njia ya mawasiliano. Kunazo aina tofauti za ishara na miujiza. Ishara nyingine huwa ni mawasiliano yanayomlenga mtu binafsi, ilhali miujiza na maajabu mengine hulenga kundi la watu. Katika Biblia kuna kisa cha mtu mmoja aliyeitwa Gideoni ambaye alitaka kuona ishara kutoka kwa Mungu itakayomhakikishia ushindi katika vita (Waamuzi 6). Hata ijapokuwa Mungu alimjibu Gideoni kwa kumpa ishara, msingi wa ombi lake haukuwa imani, bali aliomba ishara kwa sababu hakufikiria kwamba Mungu angetimiza ahadi yake. Gideoni hakuwa na imani na pia alikuwa mtu mwenye hofu nyingi. Kwa hiyo Gideoni hawezi kutumiwa kama mfano wa kuigwa, kwa maana alitegemea ishara zaidi kuliko kumwamini Mungu. Yesu alisema, “Hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza.” Yesu alipokuwa akisema haya, hakuwa na maana ya kuwapongeza watu kwa kupenda ishara, bali alikuwa akiwakaripia. Vivyo hivyo, Yesu alimwambia Tomaso, mtu aliyekuwa na mashaka, “Heri wale ambao huamini pasipo kuona kwa macho.” Mbele za Mungu imani ya ukweli na imani dhaifu hutofautishwa kwa kuamini kwa kutoona na kuamini kwa kuona. Kumbuka kwamba Shetani pia huwapa watu ishara na miujiza, kwa sababu watu ni wepesi kukubali kitu wanachokiona kwa macho, na kutilia shaka kitu wasichokiona. Manabii wa uongo na Mpinga Kristo watatumia ishara na miujiza kuwapotosha watu kutoka katika njia ya Mungu. Kwa hiyo sharti watu wawe waangalifu wanapokuwa wakitafuta ishara. Mara nyingi tunaweza kumwomba Mungu atupe “ishara” kwa jambo ambalo halikuhitaji ishara kamwe. Inapokuwa hivyo, basi huwa ile ishara sio ishara halisi. Imani thabiti na iliyokomaa msingi wake ni kumtegemea Mungu, badala ya kuzitegemea ishara na miujiza.

Kiwango cha tatu – Mungu hunena nasi kupitia Ufunuo wa JumlaKatika orofa ya chini kuna picha ya milima, mvua, na wanadamu. Katika somo la 2 tulijifunza kwamba Mungu ameweka habari zinazomhusu yeye katika ulimwengu alioumba, na katika mioyo ya watu. Njia hii ya mawasiliano huitwa Ufunuo wa Jumla. Mfumo huu wa mawasiliano ndio ufunuo au mawasiliano ya kimsingi zaidi ambayo Mungu hutumia kuwasiliana na watu. Jambo la kipekee katika mawasiliano ya kiwango hiki ni kwamba, kila mtu anaweza kutumia njia hii. Lakini kuna sehemu nyingi duniani ambako hawana nafasi hii ya Ufunuo wa Jumla, kwa hiyo ufahamu walio nao juu ya Mungu ni duni. Kwa mengi zaidi juu ya Ufunuo wa Jumla, tazama Somo la 2.

Kwa kutamatisha, tunaweza kusema kwamba, Ufunuo wa Jumla ndiyo njia ya uhakika ya kupokea mawasiliano kutoka kwa Mungu. Tunahitaji kuzitia moyo familia zetu, jamii, na waumini, kuupa mfumo huu wa mawasiliano kipau mbele. Ikiwa tutafanya makosa na kuupa umuhimu mfumo wa Mawasiliano wa Kibinafsi, tunaweza kuwategemea watu au viongozi wetu badala ya kumtegemea Mungu. Kila Mkristo anastahili kujifunza jinsi ya kuutafuta Ukweli kutoka katika Biblia na jinsi ya Kumsikiza Roho Mtakatifu. Tunaposoma Biblia, Mungu huzungumza nasi moja kwa moja na kufanya kazi yake mioyoni mwetu. Kumbuka kwamba ni lazima tupime kila kitu katika mizani ya Maandiko matakatifu.

Muhtasari wa Somo La 3

Ufunuo maalumu wa Mungu kama mawasiliano

Mawasiliano ya Mungu kibinafsi Ufunuo wa Mungu kwa jumla kama mawasiliano

BibliaYesuRoho Mtakatifu

MaombiNdoto na maonoWaumini kama sisi

MilimaMvuaMoyo wa mwanadamu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 31

Page 35: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Marejo Ya Mafundisho Ya Somo La 3

Ufunuo maalumu wa Mungu kama mawasilianoMaandiko: "Kama vile mvua na theluji ishukavyo toka mbinguni,wala hairudi huko bali huinywesha ardhi,ikaifanya ichipue mimea ikakua,ikampatia mpanzi mbegu na kuwapa watu chakula, vivyohivyo na neno langu mimi:halitanirudia bila mafanikio,bali litatekeleza matakwa yangu,litafanikiwa lengo nililoliweke” (Isaya 55:10-11).Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na SomoNeno la Mungu:*Mfano wa Mpanzi- Mathayo 13; Luka 8.*Yesu atarudi na Neno la Mungu- Ufunuo 19:15-21.

Neno la Mungu:*Neno la Mungu li hai na lina nguvu, ni kali kuliko upanga ukatao kuwili, hukata roho zetu na mioyo yetu- Waebrania 4:12.*Tumezaliwa mara ya pili kupitia kwa Neno la Mungu (Yesu)- 1 Petero 1:23.*Mbingu ziko kwa sababu ya Neno la Mungu (Yesu), Dunia ya sasa na mbingu ya sasa zimewekewa moto, Watu wasiomjua Mungu wataangamizwa- 2 Petero 3:5-16; Waebrania 11:3.*Neno la Mungu hukaa ndani yetu- 1 Yohana 2:14.*Wakati mwingine Wakristo wanauawa kwa sababu ya kujitolea kwao kuhubiri na kufunza Neno la Mungu- Ufunuo 6:9; 19:13: 20:4.*Sisi tunaweza kufungwa jela lakini neno la Mungu haliwezi- 2 Timotheo 2:9.*Neno la Mungu hufanya kazi katika maisha yetu- 1 Wathesalonike 2:13.*Neno nalikae ndani yenu kwa wingi pamoja na Zaburi , na nyimbo za kiroho- Wakolosai 3:16.*Neno ni sehemu ya Silaha ya kiroho (angslia somo la 10)- Waefeso 6:7; 2 Wakorintho 6:7.*Kwa ulimwengu Neno ni upuzi, lakini ni nguvu ya Mungu- 1 Wakorintho 1:18.*Amuri za Bwana huelimisha macho- Zaburi 19:7-8.

Yesu:*Juu ya mlima Yesu alipogeuka sura, Msikizani Yesu- Mathayo 17 (v.5).*Mfano wa Wakulima wa mizabibu- Mariko 12:1-12 (v. 6).*Hakuna mtu aliyemwona Mungu, ila Yesu ndiye mfano wake- Yohana 1:14-18; 15:1-16.*Mamlaka yote yalipewa Yesu- Mathayo 28: 18-20.*Maombi ya Yesu kabla kusalitiwa- Yohana 17 (v. 2,8).*Yesu anawaeleza wanafunzi namna maandiko yalivyotabiri kuja kwake- Luka 24.

Yesu:*Katika siku za mwisho Mungu alisema kupitia kwa Yesu- Waebrania 1:1-2.

Roho Mtakatifu:*Siku ya Pentekote- Matendo 2; Yoeli 2:28.*Yesu anafundisha ya kwamba Roho hutufunza mambo yote- Yohana 14:26; 16:13; 1 Yohana 2:20, 27.*Musa anamwachia Yoshua uongozi- Kumbukumbu 34:9-12; Yoshua 1.*Danieli anasoma maandishi juu ya ukuta- Dan. 5.

Roho Mtakatifu:*Majina ya Roho Mtakatifu, Roho wa Hekima, Utambuzi; Ushauri; Maarifa; Roho huyatafuta mambo ya ndani ya Mungu- 1 Wakorintho 2:10-13; 12:8.*Yesu alijazwa na Roho wa Hekima- Isaya 11:2-5.*Roho hutoa ufunuo, kumjua yeye, huelimisha watu, Tumaini la kuitwa, Utukufu kwa wingi- Waefeso 1:17-23.*Roho hupeana vipawa/zawadi na ujuzi- Kutoka 28:3; 31:3; 35:31.

Mawasiliano ya Mungu Ya kibinafsiMaandiko: " Mimi nimeyasikia maneno waliyosema hao manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, ‘Nimeota ndoto, nimeota ndoto!’ Itakuwa hivyo mpaka lini? Hao manabii wataendelea mpaka lini kupotoka moyo; kutabiri uongo na udanganyifu wa mioyo yao wenyewe? Kwa ndoto hizo zao wanapanga kuwafanya watu wangu wanisahau mimi kama baba zao walivyonisahau, wakamwendea Baali! Nabii aliyeota ndoto, na aitangaze ndoto yake, lakini yeye aliye na neno langu, na alitangaze kwa uaminifu. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema, makapi si sawa na ngano! Neno langu ni kama moto; ni kama nyundo ipasuayo miamba vipandevipande. Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nitawashambulia manabii ambao wanaibiana maneno yangu. Kweli mimi Mwenyezi-Mungu nasema, nitawashambulia manabii wanaoropoka maneno yao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi-Mungu asema’. Naam, mimi Mwenyezi-Mungu nasema kuwa nitawashambulia manabii wanaotabiri ndoto zao za uongo kwa watu wangu, na

Copyright © 2007 Tammie Friberg 32

Page 36: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kuwapotosha kwa uongo wao na kuropoka kwao. Mimi sikuwatuma wala kuwaamuru waende; kwa hiyo hawatawafaa watu hao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” (Yeremia 23:25-32).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na SomoMaombi:*Mungu atatwambia, Hii ndio njia tembeeni katika hiyo- Isaya 30:19-36.*Daudi aliomba kwamba Mungu amthibitishie Neno lake- 1 Wafalme 8.*Mungu hatawaangalia wa wauaji. Tunatakikana tujifunze kutenda mema, Wacha uovu- Isaya 1:15-17. *Mungu alisema na Eliya wakati kukiwa kumetulia- 1 Wafalme 19.*Musiombe kama watu wasiomjua Mungu, Yesu anatufunza kuomba- Mathayo 6.*Yesu anaomba Usiku mzima ili ajue ni akina nani atakaowachagua kuwa wanafunzi wake- Luka 6:12-16.*Yesu Anawafukuza wabadilishaji wa pesa kutoka Nyumba ya maombi (Hekaluni)- Luka 19:45-48; Isaya 56:7.*Utiifu wa Yesu katika maombi, Ombeni ili musiingie katika majaribu- Luka 22:39-46.*Waumini wanamwombea Petero atolewe jela- Matendo 12.*Mungu anajibu maombi ya Korinelio- Matendo 10.*Kanisa la Kwanza linaombea uongozi- Matendo 6.*Kanisa la Kwanza linajitoa kuwa na ushirika wa kumega mkate na kuomba pamoja, Watu wengi waliokolewa- Matendo 2:42-47.*Mwandishi wa Zaburi anamwomba Mungu ampeleleze wakati anapoomba- Zaburi 17.*Mwandishi wa Zaburi anawaombea wale wanaopingana na yeye, Na anatenda haki katika kufunga na kuomba- Zaburi 35; 109.*Mwandishi wa Zaburi anaomba wakati unaokubalika wa Mungu kujibu maombi yake- Zaburi 69:13.*Mungu husikia maombi ya wale wanaoteseka- Zaburi 102.*Mungu anaweza kukataa kujibu maombi unayoombea watu wanajihusisha na dini za uongo- Yeremia 7:16-20.*Bwana hawezi kukataa milele- Maomb. 3.*Mungu anayasikia maombi ya Danieli- Dan. 9.

Maombi*Ungameni dhambi na kuombeana ili magonjwa yaliyoletwa na dhambi yapate kupona; Warudisheni watu waliotenda dhambi kwenye imani- Yakobo 5:15-20.*Kueni macho na muombe- 1 Petero 4:7.*Kile alichokiumba Mungu ni kizuri, kimesafishwa kwa maombi- 1 Timotheo 4:1-7.*Jitoeni kwa maombi- Wakolosai 4:2; Rom. 12:12.*Ombeeni kila kitu, Amani ya Mungu naitawale mioyo yenu- Wafilipi 4:6.*Mtu aombaye kwa nia mbaya, maombi yake hayawezi kujibiwa Yakobo 4:3.*Ombeni ili mpate kujua mapenzi ya Mungu ni nini - Waefeso 1:18-23; Wakolosai 1:9.* Ombeni ili Neno la Mungu lisambae kwa haraka - 2 Wathesalonike 3:1-2.*Ombeni kulingana na vile Mungu anavyotaka (Namna inavyompendeza Mungu)- 1 Yohana 5:14.

Waumini wenzetu:*Paulo anamkemea Kefa- Wagalatia 2.*Mkutano wa Jerusalemu- Matendo 15.*Barinaba alitoa ushauri mzuri- Matendo 11:22-23.*Waumini wa Efeso walitoa ushauri mzuri- Matendo 18:24-27.*Yuda na Sila walitoa ushauri mzuri- Matendo 15:32.*Paulo alitoa ushauri mzuri- Matendo 16:40, 20:1-2; 2 Wakorintho 13:2; Wakolosai 1:28; 1 Wathesalonike 2:11-12; 4:6.*Timotheo alitoa ushauri mzuri- 1 Wathesalonike 3:2-3.*Tukiko alitoa ushauri mzuri- Waefeso 6:21-22; Wakolosai 4:7-9.*Onesiforo anawaburudisha wengine- 2 Timotheo 1:16-18.

Waumini wenzetu:*Waigizeni viongozi wanaohubiri Neno la Mungu, Biblia- Waebrania 13:7.*Kueni waangalifu ili mpate Kutumia na kutafasiri neno la Mungu sawasawa- 2 Timotheo 2:15.*Jitahidini ili ujumbe wa neno la Mungu uwe msafi bila Kasoro- 1 Wathesalonike 1:8-10.*Musichanganye Neno la Mungu na mambo mengine, bali Onyesheni ukweli- 2 Wakorintho 4:2.*Musitumie Neno la Mungu wa kujinufaisha wenyewe- 2 Wakorintho 2:17.*Waumini wengine wanapofanya dhambi- Mathayo 18:15-17; Luka 17:3-4; Wagalatia 6:1-2; Yakobo 5:16.*Ugumu wa kutiana Nguvu- Rom. 14:19.*Viongozi na waumini wengine watiane moyo- Rom. 1:11-12.*Waonyeni watu wavivu, Watieni moyo watu wadogo, Wasaidieni wanyonge, Vumilianeni- 1 Wathesalonike 5:14.*Tianeni moyo ili kusiweko na mtu yeyote ambaye dhambi imemfanya kuwa sugu au mkaidi- Waebrania 10:24-25.*Hubiri Neno, Kosoa, Kemea, Tia moyo kwa uangalifu kwa mafundisho kamili- 2 Timotheo 4:2.

Ndoto na Maono: Ndoto na Maono:

Copyright © 2007 Tammie Friberg 33

Page 37: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Yusufu na ndoto zake- Mwanzo 37; 41-46.*Mungu anamtokea Yakobo katika maono- Mwanzo 46:2-7.*Watu waasi hupenda kusikia maneno matamu - Isaya 30:9-26; Maomb. 2:14.*Mungu anawalaumu manabii walevi, wanaoambia watu maono ya uongo- Isaya 30:7-8.*Mungu anakataa kumjibu Sauli- 1 Samueli 28.*Wanawake, maono, hirizi, Kupiga ramli- Ezekieli 13:17-23; Wanaume- Ezekieli 13:9-16; Zakaria 10:2.*Danieli anamsaidia Mfalme Nebukadineza kufasiri ndoto- Dan. 2; 4.*Mungu anasema na Petero na Korinelio- Matendo 10.*Maono ya Paulo- 2 Wakorintho 12:1-10.

*Kipimo cha ndoto- Kumbukumbu 13 [Kumbuka: Sheria kuhusu ndoto za uongo, kuwashawishi watu wafuate miungu ya uongo, pamoja na adhabu yake iliishia kwa Waisraeli katika Agano la kale, haikuletwa kwenye Agano Jipya na kuendelea].*Kwani kuna ndoto nyingi ambazo hazina maana, na pia kuna maneno mengi ambayo hayana maana. Bali mcheni Mungu- Mhubiri 5:7.

Ufunuo wa Mungu kwa jumla kama mawasilianoMaandiko: “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu;anga ladhihirisha kazi ya mikono yake. Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Hamna msemo au maneno yanayotumika;wala hakuna sauti inayosikika;hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote, na maneno yao yafika kingo za ulimwengu. Mungu ameliwekea jua makao yake angani; nalo hutoka kama bwana arusi chumbani mwake,lafurahi kama shujaa aliye tayari kushindana. Lachomoza toka upande mmoja,na kuzunguka hadi upande mwingine;hakuna kiwezacho kuliepa joto lake” (Zaburi 19:1-6).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Mungu hujionyesha wazi kupitia kwa Historia na ulimwengu- Matendo 14:15-17.*Mshairi asiyemjua Mungu hupokea maarifa ya kiroho lakini hayampatii wokovu- Matendo 17:22-31.

*Mbingu zinaonyesha- Zaburi 19:1-6.*Mungu amejionyesha wazi kupitia kwa vitu alivyoviumba- Warumi. 1:18-22.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 34

Page 38: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 35

Page 39: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 4: Amri Kumi za Mungu

Maandiko:“Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja. Mmoja wao mwanasheria akamwuliza Yesu kwa kumjaribu, “Mwalimu, ni amri ipi iliyokuu katika sheria?" Yesu akamjibu, "MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE NA KWA AKILI YAKO YOTE.' Hii ndiyo amri kuu ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo, ‘MPENDE JIRANI YAKO KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE MWENYEWE’ Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili” (Mathayo 22:34-40).

Maelezo MafupiMfano ulioko katika ukurasa uliotangulia una picha inayowakilisha Amri 10 za Mungu. Mungu alimpa Musa Amri hizi kumi wakati alipokuwa katika mlima wa Sinai. Vile vibao vyenye hizo amri vimegawanywa katika sehemu mbili. Katika sehemu ya kwanza upande wa kushoto, juu, kuna picha ya Mungu akinyoosha mkono wake. Amri nne za kwanza zilizoorodheshwa chini ya mkono wa Mungu, hutupa mwongozo wa jinsi ya kumwabudu na kumtumikia Mungu. Kundi la pili la Amri za Mungu limeorodheshwa upande wa kulia, chini ya jamii ya watu. Amri hizi sita hutoa mwongozo wa jinsi tunavyostahili kuishi katika jamii. Mungu ni mwadilifu na hana kasoro hata kidogo. Asili yetu katika uadilifu ina kasoro kwa sababu ya dhambi. Mungu alipotupa Sheria, lengo la sheria hiyo lilikuwa ni kutuonyesha matarajio ya Mungu kwetu, na pia kutuonyesha kwamba tunahitaji msamaha. Sadaka na matambiko ya enzi za Agano la Kale hayakutosha kuwaondolea watu wa wakati huo hatia iletwayo na dhambi. Kwa hiyo, ni wazi kwamba tunahitaji Mwokozi anayeweza kutusafisha mioyo yetu na kutuunganisha na Mungu, ili tuweze kuwa na ushirka naye. Tunahitaji sadaka ya kutosha na kuhani wa mbinguni. Kwa hiyo Sheria inatusaidia kutambua kwamba tunahitaji Mwokozi.

Mungu alipotoa amri hizi kumi, wana wa Israeli walikuwa njiani kuelekea katika Nchi ya Ahadi, kwa hiyo walihitaji mwongozo ili waweze kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Walipokuwa karibu kuingia katika Nchi ya Ahadi Mungu aliwapa ushauri mzuri sana. Aliwashauri wasiige tabia za kule walikotoka yaani Misri, vilevile wasiige tabia za ile nchi waliyokuwa wakielekea yaani Kanaani (Mambo ya Walawi 18:3). Kutokana na agizo hili tunaweza kujifunza kanuni fulani. Katika kila utamaduni duniani kuna tabia fulani au vitu fulani visivyompendeza Mungu. Kwa hiyo ni vyema kushika na kuzitii sheria za Mungu, badala ya kushika au kuendelea kuishi sawa na tabia za kule tulikotoka au kule tuendako. Sheria za Mungu hazibadiliki hata tuende wapi! Hazibadiliki kamwe. Sheria hizi za Mungu ndizo kigezo cha tabia na matendo yetu. Tunapozitii tunaonyesha wazi uaminifu wetu kwa Mungu na kwa kufanya hivyo tunamtangaza Kristo kwa wengine. Ili kuweza kuwafunza watu kwamba amri za Mungu ndizo vigezo vinavyostahili kufuatwa, ni vyema kutumia picha hizi kila siku katika marudio ya somo. Wakati wazazi wanapowafunza watoto wao Sheria za Mungu, sharti wawaeleze waziwazi kwamba uasi sio tu kwa kuwakosea wazazi bali pia kwa kumkosea Mungu. Kila amri katika somo hili imewekewa picha ili kusaidia kufunza amri hizi.

Amri ya 1- katika amri hii kuna picha ya mkono wa Mungu ulionyooshwa. Amri ya kwanza yasema kwamba Mungu ni mmoja na twastahili kumwabudu yeye.

Amri ya 2- kuna picha ya sanamu. Amri inasema kwamba tusiiabudu miungu mingine wala sanamu, pamoja na kumwabudu Mungu wa kweli. Vilevile tusiabudu sanamu au miungu mingine mahali pa Mungu wa kweli.

Amri ya 3- kuna picha ya mtu anayeongea. Amri hii inasema kwamba tusilitaje bure jina la Mungu (BWANA) wetu.

Amri ya 4- kuna picha ya watu wanaomwabudu Mungu. Amri hii inasema kwamba tusisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato. Katika enzi hii ya Agano Jipya tunamwabudu Mungu ifikapo Siku ya Bwana (Jumapili, siku aliyofufuka Yesu. Vilevile tunaamriwa kumwabudu Mungu kwa kushirikana na wengine wanaomwamini Mungu.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 36

Page 40: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Amri ya 5- kuna picha ya mume na mkewe, na watoto wanaotarajia kuwaheshimu wazazi wao. Amri hii inasema kwamba watoto sharti wawatii na kuwaheshimu wazazi wao.Amri ya 6- kuna picha ya kisu na ya mtu aliyeuawa. Amri hii inasema kwamba ni hatia kuwaua watu.

Amri ya 7- kuna picha ya mtu na mabibi wengi, mwanamme mwingine amekaa kwenya baa akitaka uhusiano na malaya. Amri hii inasema kwamba wake na waume sharti wawe waaminifu katika mambo ya ngono. Mtu atachukuliwa kuwa mzinzi iwapo atakuwa na uhusiano wa kingono nje ya ndoa( kwa bwana au bibi mmoja), au kabla hajafunga ndoa.

Amrit 8- kuna picha anayekimbia mbio huku akiwa na mkoba wa mtu mwingine. Amrii hii inasema kwamba tusiibian.

Amri 9- kuna picha ya mtu anayemsingizia makosa mwenzake. Amri hii inasema kwamba hatustahili kutoa ushahidi wa uongo.

Amri ya 10- kuna picha ya vitu ambavyo wengine wanaweza kuona wivu kwa kumwona mwenzake navyo. Amrii hii inasema kwamba tusitamani mali za wenzetu.

Yesu alisema kwamba sheria yote ya Musa inategemea Sheria hizi mbili: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote.” Ya pili: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe”(Mathayo 22:27-29). Upendo ndio unaotamatisha Sheria yote. Siku zote inakuwa vigumu kwetu kuwapenda wengine na kumpenda Mungu kama inavyotakiwa. Ndiposa Mtume Paulo alimwomba Mungu ili upendo wetu uongezeke na tumjue Mungu na tupendane sisi kwa sisi. Vilevile alisema kwamba upendo wetu kwa wengine unaweza kuongezeka iwapo tutakuwa watiifu na kupendana sisi kwa sisi. Kwa hiyo tunapowapenda wengine kwa upendo wa Kristo, Mungu huikuza imani yetu. Hata ijapokuwa tunaombeana ili tuweze kufaulu kwa mambo ya kimwili, ni vyema kuombeana ili tuweze kukua kiroho katika kumpenda Mungu na watu. Tukimtii Mungu kwa kufuata amri zake , tutaweza kuwapenda wengine zaidi kama alivyotupenda yeye mwenyewe.

Muhtasari wa Somo La 4

Amuri Zinazohusu Uhusiano wetu na Mungu Amuri Zinazohusu Uhusiano wetu na watu wengineKuna Mungu mmoja Mwabudu yeye Waheshimu na Kuwatii Wazazi wakoUsiwe na miungu mingine UsiueUsilitaje bure Jina la Bwana Mungu Wako UsiziniIkumbuke Siku ya Sabato Uitakase Usiibe

- Usimshuhudie Jirani yako Uongo- Usitamani

Marejeo Ya Mafundisho Ya Somo La 4

Amuri Zinazohusu Uhusiano wetu na MunguMaandiko: Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu;niliwachagua muwe watumishi wangu,mpate kunijua na kuniamini,kwamba ndimi peke yangu Mungu. Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine,wala hatakuwapo mungu mwingine. “Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu,hakuna mkombozi mwingine ila mimi. Nilitangaza yale ambayo yangetukia, kisha nikaja na kuwakomboa. Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo,nanyi ni mashahidi wangu. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima. Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu;hakuna awezaye kupinga ninayofanya?” (Isaya 43:10-13).“Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule milimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana, msipotoke kwa kujifanyia sanamu yoyote ya kuchonga, au ya umbo au mfano wowote, mfano wa kiume au wa kike,wa mnyama yeyote duniani au ndege au mfano wa mnyama atambaaye ardhini au wa samaki majini. Jihadharini ili wakati mtakapoangalia na kutazama nyota, vitu vyote vya mbinguni, msije mkavutwa kuviabudu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 37

Page 41: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

na kuvitumikia. Vitu hivyo Mwenyezi-Mungu amewaachia watu wengine waviabudu. Lakini nyinyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika tanuri la chuma. Aliwatoeni huko ili muwe watu wake kama vile mlivyo hivi leo” (Kumbukumbu 4:15-20).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na SomoKuna Mungu mmoja Mwabudu yeye:*Mungu anasema Kuna Mungu mmoja Mwabudu yeye- Kutoka 20:3; Kumbukumbu 5:7.*Yoshua, Chagueni leo Mtakayemtumikia- Yoshua 24.

Kuna Mungu mmoja Mwabudu yeye:*Mimi ndimi MWENYEZI-MUNGU, Hilo ndilo jina langu; Sitampa mwingine Utukufu wangu, Wala Sifa zangu kwa Sanamu za Kuchonga- Isaya 42:8; 46:9.

Usiabudu miungu mingine:*Watu wanatengeneza Sanamu ya Ndama- Kutoka 32.*Stefano aeleza historia ya Israeli – Matendo 7*Yeroboamu Anawekea watu Sanamu mbili za Ndama ili waabudu- 1 Wafame 12-13.*Manase Anaweka Sanamu ndani ya Hekalu- 2 Nya. 33.*Mfalme Yosia Anaondoa Sanamu- 2 Nya. 34-35.*Watu wanaoishi Israeli wakati Waisraeli walipokuwa Uhamishoni wanamwabudu Mungu wa kweli pamoja na miungu mingine- 2 Wafalme 17:29-35.*Yesu Anajaribiwa Amwabudu Shetani- Mathayo 4:1-12.*Kula nyama zilizotolewa Sanamu- 1 Wakorintho 8:4-13; 10.*Kundi kubwa la watu linamkasirikia Paulo kwa kusema miungu ya kutengenezwa na wanadamu si miungu hata kidogo- Matendo 19:22-41.

Usiabudu miungu mingine:*Mtume aeleza kukombolewa kutoka Misri – Ezekieli 20*Hutafuata miungu mingine yoyote katika ile inayoabudiwa na watu wanaomzunguka- Kumbukumbu 6:14.*Usitengeneze Sanamu yoyote, yenye mfano wowote, wa watu, wanyama, ndege, wadudu, samaki, Mbingu, Jua, na Mwezi- Kutoka 34:17; Walawi. 19:4; 26:1; Kumbukumbu 4:15-20.*Wanakosa kuona udanganyifu wa Sanamu, ili wapate Kuaibishwa- Isaya 44:9; 45:16.*Mtu yeyeto Atakayeabudu miungu mingine hatakuwa na urithi pamoja na watu wa Mungu- Waefeso 5:5-12.*Mungu wa uongo anawezakuwa ulafi wako- Wafilipi 3:19.*Jiepusheni na miungu ya sanamu- 1 Yohana 5:21.*Watu wanaotaka kufuata raha zao hugeukia miungu ya sanamu- Waroma 1:18-32.*Magonjwa yalitumwa kwa wale waabuduo mapepo- Ufunuo 9:20-21.*Mvunjaji wa Sheria atakuja kujiinua kama Mungu, akitenda ishara na miujiza- 2 Wathesalonike 2:3-12.*Watu wanatakikana wachome miungu yote katika nchi. Usiilete nyumbani usije ukaangamizwa- Kumbukumbu 7:25-26.

Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako:*Mvulana anapigwa mawe kukufuru jina la Mungu- Walawi 24:11-23.

Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako:*Msilikufuru Jina la Mungu; Msiape uongo- Walawi 19:12.*Mungu Atawaadhibu wale wanaolikufuru Jina lake- Kumbukumbu 5:11.*Ombi la kutaka kuwa na mali ya kiasi, asiwe tajiri wala maskini asije akamkufuru Bwana- Methali. 30:9.*Maagizo Kuhusu kuweka nadhiri- Mathayo 5:33-37; 23:16-22; Yakobo 5:12.

Ikumbuke Siku ya Sabato na Uitakase:*Mungu aliagiza kwamba Sabato iwe siku ya kupumzika kulingana na siku za uumbaji- Mwanzo 2:3; Walawi 19:3; 23:3.*Waisraeli wanapewa maagizo kuhusu kula Mana siku ya Sabato- Kutoka 16:23-30.

Ikumbuke Siku ya Sabato na Uitakase:*Sabato ni Ishara kati yenu na mimi katika vizazi vyenu vyote, ili mpate kutambua kwamba Mimi ndimi MWENYEZI-MUNGU ninaye watakasa- Kutoka 31:13-14.*Maagizo juu ya wageni na juu ya Sabato- Isaya 56:4-6.

Amuri Zinazohusu Uhusiano wetu na watu wengineMaandiko: “Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako?Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu?Ni mtu aishiye bila lawama, atendaye daima yaliyo mema,asemaye ukweli kutoka moyoni; ni mtu asiyesengenya watu,asiyemtendea uovu rafiki yake,wala kumfitini jirani yake;ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu;ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara ;asiyekopesha fedha yake kwa riba,wala kupokea rushwa kumdhulumu asiye na hatia. Mtu atendaye hayo, kamwe hatatikisika” (Zaburi 15).“Je, waweza kuweka moto kifuani na nguo zako zisiungue? Je, waweza kukanyaga makaa ya moto na nyayo zako zisiungue? Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake;yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa. Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa; lakini akipatikana lazima alipe mara saba;tena atatoa mali yote aliyo nayo. Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa; huyo hujiangamiza yeye mwenyewe. Atapata majeraha na madharau;fedheha atakayopata haitamtoka. Maana wivu wa mume humfanya kuwa mkali kabisa;wakati atakapolipiza kisasi hana cha kuhurumia” (Methali. 6:27-34).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na SomoHeshimu na Kuwatii Wazazi wako:*Yesu Anafundisha juu ya kuapa uongo- Mathayo15:4-6.*Kijana Tajiri na Kiongozi- Luka 18:18-27.*Mfano wa Wavulana wawili- Mathayo 21:28-31.

Heshimu na Kuwatii Wazazi wako:*Sheria kuhusu Kuheshimu Wazazi- Kutoka 21:15-17; Walawi. 19:3, 32.*Usiache Mafundisho ya babako na mamako- Methali.1:8.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 38

Page 42: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Mpumbavu hukataa mafundisho ya baba yake- Methali. 15:5.*Kumwibia babako na mamako ni dhambi- Methali. 28:24.*Ni makosa kumlaani Baba au Mama- Methali. 20:20; 30:17.*Watoto watiini wazazi wenu ili mpate kuishi maisha marefu hapa duniani- Waefeso 6:1-4.*Watoto watiini wazazi wenu katika kila jambo- Wakolosai 3:20.

Usiue:*Kaini anamwua Abeli- Mwanzo 4:8-23; Waebrania 11:4; Yuda; 1 Yohana 3:12-15.*Sauli Anataka kumwua Daudi- 1 Samueli 18-31.*Daudi Anakataa kumwua Sauli- 1 Samueli 24; 26.* Anamwua Uria na Kuchukua mke wake- 2 Samueli 12.*Yezebeli na Mfalme Ahabu wanamwua Nabothi ili wachukue shamba lake la mizabibu- 1 Wafalme 21.*Yeremia Anatabiri katika sebule ya Hekalu la Bwana- Yeremia 26.*Paulo Anawaua Wakristo- Matendo 7.*Baadaye Paulo Anaambiwa kwamba ni Mwuaji; wakati alipoumwa na nyoka- Matendo 28.

Usiue:*Mtu aliyeua makusudi hata akikimbilia madhabahuni kisha atolewe huko- Kutoka 21:14.*Mungu Mtu akiuwa naye auawe; Mwanadamu ni kiumbe wa maana kwani aliumbwa kwa mfano wa Mungu- Mwanzo 9:5-6; Walawi 21:24; Hesabu 35:16-34; Kumbukumbu. 5:17.*Sheria kuhusu wale wanaovizia watu wawaue- Kumbukumbu. 19:11-13; Zaburi 10:8-11; Methali. 1:11-12.*Kila mtu anayejifaidisha kwa ukatili; Wakatili huangamizwa na Ukatili wao- Methali. 1:19.*Usiue, na Usimkasirikie ndugu yako, Pataneni- Mathayo 5:21-26.*Sheria imejumlishwa ikawa mpende mwenzi kama unavyojipenda mwenyewe- Waroma 13:9.*Sheria ilitengenezewa Wauaji, wazinzi na kadhalika- 1 Timotheo. 1:9-11.*Kila anayemchukia ndugu yake ni Mwuaji- 1 Yohana 3:12-15.

Usizini:*Daudi na Bathisheba- 2 Samueli 11-12.*Yusufu Asingiziwa na mke wa Potifa kwamba alitaka kumnajisi- Mwanzo 39:1-20.*Kutafuta Hekima, Kuenda katika njia za wenye Hekima, Kujiepusha na njia za Wazinzi- Methali 2; 5:3-5. *Mafundisho ya Baba na Mama ya kuwazuia vijana wasiende katika njia za Wazinzi- Methali 6:20-35.*Amri za Mungu, Hekima huwaepusha watu wanyofu na njia za Wazinzi; Ujanja na mvuto wa dhambi- Methali. 7.*Yesu anamsamehe Malaya dhambi zake- Yohana 8:1-11.

Usizini:*Taabu ya Uzinzi katika siku za Manabii- Yeremia. 5:6-9; 29:22-23.*Yesu anasema kwamba, Kila amwangaliaye mwanamke na kutamani, ameshazini naye katika moyo wake [Kumbuka kwamba Yesu anaipevusha Sheria ya Agano la Kale. Yeye anawajumuisha hata wanaume wanaotamani wanawake wengine, na kufanya uzinzi katika fikira zao bila kuwa na uhusiano wowote nao. Mwanamme kama hawa hata akiwa mwaminifu kwa mke wake mmoja bado ni mzinzi- Mathayo 5:27-28.*Yesu alisema kila anayempa talaka mkewe na kuoa mke mwingine anafanya uzinzi; Na mwanamke naye akimpa talaka mumewe na kuolewa na mwanamme mwingine, yeye naye anafanya uzinzi - Mariko 10:11-12.*Mungu anachukia talaka- Malaki 2:16; Talaka iliruhusiwa kwa sababu ya mioyo migumu- Mathayo 19:3-9.*Talaka inaruhusiwa kama mmoja ni mzinifu- Mathayo 5:31-32.*Ndoa naiheshimiwe na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu; kwani Mungu ata wahukumu waasherati na wazinzi- Waebrania 13:4.*Maagizo kwa wale ambao waume, au wake zao hawajaamini- 1 Wakorintho 7:12-15; 1 Petero. 3:1-6.*Maagizo juu ya wale waliotengana kwamba wadumishe amani- 1 Wakorintho 7:10-11.*Mume akifa na mke akiolewa na mume mwingine, yeye hafanyi uzinzi. Lakini mke akiolewa na mume mwingine huku mumewe yuhai, atakuwa anafanya uzinzi- Waroma 7:2-3; Maagizo kuhusu wajane- 1 Wakorintho 7:8-9.*Tukitawaliwa na tamaa zetu mbaya tunafanya dhambi- Yakobo 1:13-16.*Uzinzi, ama uchafu wowote, ama choyo usisikike kati yenu, kama watu wa Mungu inavyowastahili kuwa- Waefeso 5:3.*Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, 5 na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu. 6 Basi, mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili. Tulikwisha waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu wanaofanya mambo hayo- 1 Wathesalonike 4:1-6.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 39

Page 43: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na SomoUsiibe:*Yesu anawafukuza Wanyang’anyi kutoka Hekaluni- Mathayo 21:12-13.*Yuda alikuwa mwizi- Yohana 12:1-8.*Msamaria Mwema- Luka 10:25-42.*Mfano wa Mlango, Mwizi huja ili aibe, aue, na aharibu basi; Mimi nilikuja ili wapate uzima, na wawe nao teletele- Yohana 10:1-18.*Wezi wawili wanasulubishwa pamoja na Yesu- Mathayo 27:28-44; Luka 23:39-43.

Usiibe:*Sheria za kumlipiza Mwizi- Walawi 6:1-7; 19:11, 13.*Sheria kuhusu kuteka nyara- Kumbukumbu 24:7.*Utumiaji wa vipimo visivyo sahihi, Kudanganya watu- Kumbukumbu 25:13-16; Methali 11:1; Mika 6:10-16.*Kuwaonea maskini, Kuwapokonya nyumba au vitu vyao- Ayubu 20:15-22; Amosi 8:4-7; Ezekieli 22:29.*Wizi watoka moyoni- Mathayo 15:19; Hosea 4:1-2.*Mwizi naaache kuiba, bali afanye kazi nzuri kwa bidii na kwa mikono yake mwenyewe ili awe na kitu cha kumgawia anayehitaji- Waefeso 4:28.*Watu humwibia Mungu sadaka na mafungu ya kumi- Malaki 3:8-10.*Hakikisheni kwamba hakuna mtu kati yenu atakayepata taabu kwa sababu ni mwuaji, au mwizi…lakini mtu asisikie aibu akiwa anapata taabu kwa sababu yeye ni Mkristo, bali naamtukuze Mungu katika jina hilo- 1 Petero 4:15-16.

Usimshuhudie Jirani yako uongo*Watu humsingizia Mungu- Kumbukumbu 1:27-28; Kutoka 16:3; Adhabu ya Mungu- Hesabu 14.*Ahabu na Yezebeli wakodisha Mashahidi wa uongo- 1 Wafalme 21.*Mashahidi wa uongo dhidi ya Wajenzi wa ukuta wa Yerusalemu- Ezira 4.*Uongo wa Sanbalati, TobiaThe Deception of Sanballat, Tobiah, waliomwambia Geshemu- Neh. 6.*Mashahidi wa uongo wakati Yesu alipokuwa anahukumiwa- Mathayo 26:57-75; Mathayo 27:41-42.*Mashahidi wa uongo dhidi ya Stefano- Matendo 6.*Barua kwa Timotheo juu ya tabia nzuri na mbaya- 2 Timotheo 3.*Yesu anaambiwa kwamba anatoa pepo kwa uwezo wa shetani- Mathayo 12:22-24.*Paulo anashitakiwa kwa kusingiziwa- Matendo 24.*Diotrefe anatumia maneno maovu- 3 Yohana.*Anania na Safira- Matendo 5:1-9.

Usimshuhudie Jirani yako uongo: *Usipotoshe haki anayohitaji ndugu yako katika kesi yake- Kutoka 23:6.*Usizunguke kukashifu watu katika jamaa yako, Mimi ni Mwenyezi-Mungu- Walawi 19:16.*Haki halisi katika kesi ya ushahidi wa uongo- Kumbukumbu 19:15-21.*Wanaokashifu watu kisiri wataadhibiwa- Zaburi 101:5-7.*Mafundisho dhidi ya Kukashifu- Methali 10:18;11:13.*Acha na uzushi na Kashifa- Waefeso 4:31.*Yule anayesema vibaya juu ya mwenzake anaihukumu Sheria- Yakobo 4:11-17.*Kuendelea kuwa watumishi wa Mungu katikati ya masingizio- 2 Wakorintho 6.*Mazungumzo yako nayawe ya heshima ili watu wapate kumtukuza Mungu wakati wa kurudi kwake kwa sababu ya yale unayosingiziwa - 1 Petero. 2:19.*Yesu anafundisha kuwa tumebarikiwa wakati watu wanaposema kila aina ya mambo mabaya juu yetu kwa ajili yake- Mathayo 5:11-12.

Usitamani:*Hawa anatamani tunda- Mwanzo 3.*Kuanguka kwa Yeriko, Usitamani vitu vilivyokatazwa- Yoshua 6.*Kutamani katika nyakati za Manabii, Watamani mashamba na kuyanyakua, wanatamani nyumba na kuzichukua. Wanamnyang’anya mtu na nyumba yake pamoja na urithi wake- Mika. 2:2.*Dhambi ya Akani- Yoshua 7.*Mfano mzuri wa Paulo wa kuzingatia huduma kisawasawa- Matendo 20:17-38.*Mfano wa Mpanzi- Mathayo 13.*Mfano wa Tajiri- Luka 12:15-40.

Usitamani:*Chomeni sanamu za miungu yao; Musitamani dhahabu wala fedha iliyo juu yao, wala msiichukue mkaifanya yenu, msije mkanaswa kwenye mtego, Kwani hiyo ni machukizo kwa MWENYEZI-MUNGU Mungu wenu- Kumbukumbu 7:25.*Maana kupenda pesa ndio chanzo cha kila uovu. Kwa kupenda pesa wengine wameenda kando na imani na kujiumiza kwa masikitiko mengi- 1 Timotheo 6:10-12; Waebrania 13:5.*Watu wengine wanatumia Uchaji wa Mungu kuwa njia ya kujinufaisha- 1 Timotheo 6:3-21; 1 Petero. 5:2.*Methali juu ya Kutamani na kujinufaisha- Methali 21:26; 22:16; 23:4-5; 30:8; Mhubiri 4:8.*Manabii wanapinga kutamani- Isaya 56:11; 57:17; Yeremia 6:13; 8:10; Ezekieli 33:3; Mika 2:2.*Kupata faida isiyo haki kwa kuua- Ezekieli 22:12-13.*Usijiwekee hazina yako hapa duniani. Weka hazina yako mbinguni- Mathayo 6:19-34.*Itamfaidi nini mtu akipata ulimwengu wote na aipoteze roho yake- Mathayo 16:26.*Kutamani kunatoka ndani ya moyo- Mariko 7:21-22.*Mungu huwaachilia wale wanaoabudu miungu ya sanamu waende katika upotovu- Waroma 1:29.*Msishirikiane na Mkristo mwenye kutamani vitu vya watu- 1 Wakorintho 5:9-13; 6:10.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 40

Page 44: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo*Msiwaze juu ya vitu vya hapa duniani, bali mawazo yenu nayawe juu ya vitu vilivyo juu mbinguni- Wakolosai 3:2.*Mwatamani lakini hamna; Kwa hiyo mwaua. Mnatamani vitu na hamwezi kuvipata; Ndiposa mnagombana na kuteta- Yakobo 4:2. *Tabia za Manabii wa uongo- 2 Petero 2:1-3.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 41

Page 45: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 42

Page 46: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 5: Sifa Za Dini ya Uongo

Maandiko: Yesu alisema, “Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho." Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji,waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ja mji” (Ufunuo 22:13-15 ).

Maelezo MafupiKatika mfano wa 5, utaona mfululizo wa picha mbili zilizoonyeshwa katika mistari miwili ya kwenda chini. Kila moja ya picha hizo inawakilisha vitu fulani vinavyoonyesha sifa za dini za uongo. Msitari ulioko upande wa kushoto unaonyesha dini za uongo zinazochipuka kwa sababu ya kukataa Ufunuo wa Jumla wa Mungu. Safu iliyoko upande wa kulia inawakilisha vitu vinavyoonyesha sifa za dini za uongo zinazochipuka kwa sababu ya kukataa Ufunuo Maalum wa Mungu. Baadhi ya sifa za dini za uongo zinapatikana katika sehemu zote mbili. Ni jambo la busara ikiwa mtu atajua vitu hivi vinavyochangia kuwepo kwa dini za uongo katika utamaduni wetu mbalimbali, kwa sababu hivyo huchangia katika kuwachanganya na kuwapotosha watu.

Sifa za watu wanaokataa Ufunuo wa Jumla wa MunguIkiwa unataka kuelewa vyema yale yanayotukia wakati watu wanapoukataa Ufunuo wa Jumla wa Mungu, soma Warumi 1:18-32. Mtume Paulo katika kujifunza Maandiko na katika kuwafunza watu na kuchangamana nao, aligundua kwamba watu wanaoabudu sanamu huwa na tabia fulani zilizokita katika maisha yao. Katika kisanduku, sehemu ya juu upande wa kushoto kuna picha ya ulimwengu na watu kadhaa. Picha hizi zinawakilisha ushahidi wa ndani na wa nje ambao Mungu ametupatia kwa kupitia kwa Ufunuo wake wa Jumla. Kuna msitari unaopitia ndani ya kisanduku, kama ishara ya kukataa kwa sababu wanaoigekia miungu mingine, huwa wameukataa Ufunuo wa Jumla wa Mungu. Watu huona uumbaji wa Mungu na katika mioyo yao huwa wana ushahidi juu ya Mungu muumbaji. Lakini kwa sababu ya kuzifuata tamaa za miili yao na pia kwa kufanya makisio juu ya Mungu, wanamkataa Mungu Mmoja na aliye wa kweli, na pia kuzikataa sheria zake. Tamaa zao za mwili huwafanya kumkisia Mungu. Mtume Paulo anasema hivi katika barua yake kwa Warumi, “Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane. Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maana Mungu mwenyewe ameyadhihirisha. Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea! Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili, wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao tupu zimejaa giza” (Warumi. 1:18-21).

Watu wajitengenezea sanamu( zinazo fanana na watu, pepo, wanyama, miti au viumbe mbali mbali)Katika kisanduku kinachofuata kinaonyesha picha za aina za sanamu au vitu wanavyowezakutengeneza wanadamu wakati wanapomwacha Mungu na kugeukia miungu ya uongo. Mtume Paulo aligundua kwamba watu wanaomwacha Mungu wa Kweli na kuasi sheria zake, hujiundia miungu yao wenyewe inayofanana na makisio yao juu ya Mungu na inayokubaliana na mtindo wao wa kimaisha. Kwa kawaida watu hupenda kudhibiti hali zao, afya zao, mimea yao, mafanikio yao na maadui zao. Watu hupenda kupata majibu ya haraka na uwezo wa kugeuza hali zao. Kwa hiyo hujitengenezea miungu yao kutokana na mbao au mawe, au hujitengea sehemu fulani au miti fulani na kufanya maeneo hayo kuwa “matakatifu.” Miungu hii yaweza kuwa na mfano wa wanyama, au binadamu, viumbe vya kiroho, au mseto wa vitu hivyo vyote. Biblia katika kulezea miungu hii inasema kwamba ni, “Miungu yao ni ya fedha na dhahabu; imetengenezwa kwa mikono ya wanaadamu. Ina vinywa lakini haisemi. Ina macho lakini haioni. Ina masikio lakini haisikii. Ina pua lakini hainusi. Ina mikono lakini haipapasi. Ina miguu lakini haitembei. Haiwezi kamwe kutoa sauti. Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo, kadhalika na wote wanaoitumainia” (Zaburi 115:4-8).

Miungu hii ya sanamu huundwa tu na wanadamu, lakini pia ina nguvu za kipepo ndani yao. Kwanza neno hasa la Kigiriki linalomaanisha sanamu, lina maana mbili. Ya kwanza ni mfano wa kitu na ya pili ni zimwi. Mtume Paulo alisema, “tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi mwe na ushirika na pepo” (1 Wakorintho 10:20). Kwa hiyo kama tulivyosema awali ni kwamba pepo hufanya kazi katika

Copyright © 2007 Tammie Friberg 43

Page 47: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ulimwengu kuwavuta watu wajiabudu wao wenyewe, badala ya kumwabudu Mungu. Watu wanachangia kwa kiwango fulani, kudanganywa kwao na Shetani, lakini matokeo yake ni kwamba watu hujiingiza katika ibada za pepo kupitia kwa sanamu wanazozitengeneza. Paulo pia alisema kwamba watu hujidai kuwa na hekima kumbe ni wapumbavu (Warumi 1:18-21). Wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe. Katika enzi ya Agano la Kale, Mfalme Daudi alisema miungu yote ya mataifa mengine si kitu (1 Mambo ya Nyakati 16:26).

Kuabudu miungu ya uongo huwafanya watu kujiingiza katika uchawi na ulozi Kuabudu miungu ya uongo huwafanya watu kujiingiza katika uchawi na ulozi. Watu wanapojitengenezea miungu hii (pepo) huwashawishi watu na kuwafumba macho wasiijue Kweli, watu huzigeukia nguvu za giza ili kudhibiti hali zao za kimaisha. Uchawi kwa kawaida huhusisha wachawi wa kike na wa kiume, wapiga ramli na waganga wa mitishamba. Vilevile uchawi hutumia roho zikandamizazo, matambiko ya wanyama na mitishamba, kugonga misumari katika vitu fulani, na kujigeuza umbo kama vile la popo. Watu hutumia uchawi kujilinda, kutafuta mafanikio, kufungua kizazi na kuiletea nchi rotuba, kuwaponya wagonjwa, au kuwaloga wengine. Mungu ameukataza uchawi. Pepo ndio wahusika wakuu katika maswala ya uchawi, uwe ni uchawi wa kuroga au wa kufanya matambiko yanoonekana kuwa mazuri.

Kuabudu miungu ya uongo huwafanya watu kuwa wazinzi na wachafu kupindukiaSasa tukiangalia katika kisanduku kinachofuata, Mtume Paulo anasema kwamba kuabudu sanamu huwafanya watu kuwa wazinzi na wachafu kupindukia. Mungu huwaruhusu watu hawa kufuata matendo ya ngono yasiyo ya kawaida, na kwa kufanya hivi huitia najisi miili yao. Kuabudu sanamu kuna madhara makubwa sana kwa watu. Kutokuwa waaminifu kwa Mungu wakati mwingine hufananishwa na uzinzi katika lugha ya kiroho. Wakati mwingine watu hujiingiza katika ngono kupitia kwa ushawishi wa pepo. Pepo hawa huwadanganya watu kwa kuwaambia kwamba wakifanya ngono na wanawake fulani au watu wa kabila fulani watapona magonjwa yao. Imani hizi huwa ni uongo unaoenezwa na pepo ili kuleta uharibifu mkubwa zaidi na magonjwa. Pepo pia huwashawishi watu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wa jinsia moja, wa familia moja, na wapenzi wengi, au makahaba. Kwa hiyo ni wazi kabisa kwamba pepo huzigeuza sheria za Mungu na kuwaangamiza watu.

Kuabudu miungu ya uongo huwafanya watu kuwa na akili zilizopotoshwaKisanduku cha nne kiwakilisha akili zilizopotoshwa. Paulo anasema kwamba jambo ambalo hutendeka katika jamii zinazotumikia pepo, ni kwamba Mungu huwaachilia kufuata akili zao potofu. Inapofanyika hivyo, watu huanza kutenda maovu na mambo yatakayowaangamiza. Picha zilizo katika kisanduku hiki ni mfano wa wanadamu waliopotoka. Picha ya kwanza katika kisanduku hiki ni mauaji. Wakati mwingine kumwua mtu au kundi la watu huwa tambiko kwa mashetani ili watu hao waweze kupokea kibali fulani. Picha ndogo inayofuata inaonyesha wanaume wengi wakimnajisi mwanamke. Picha inayofuata hiyo ya unajisi ni ile inayoonyesha ubaguzi miongoni mwa watu kwa kupitia masengenyo, kuwakashifu watu, na matusi. Ulevi na utumiaji wa dawa za kulevya umeonyeshwa katika picha inayofuata. Mambo haya yote huleta uharibifu katika jamii na pia kuharibu maisha ambayo Mungu anataka tuishi. Sio watu wote wanaotenda maovu na mambo maharibifu yaliyotajwa hapo mbeleni. Kunao Wakristo wengine ambao wanateseka kwa sababu ya dhambi za hao wanaoabudu sanamu. Mambo haya yameandikwa ili Wakristo waweze kuchanganua utamaduni wa kabila lao na kwa kufanya hivyo wajue jinsi ya kukabiliana na vipengele vilivyo kinyume na neno la Mungu.

Dini danganyifu hufunza kwamba kuishi kihaki ni kibali kwa yeyote ya maaisha mema peponiKatika kisanduku kifuatacho utaona watu wakifanya kazi pamoja kwa lengo la kusaidiana. Haya ni matendo mema na ya ukarimu ambayo wanadamu hutendeana. Mambo yaliyoonyeshwa katika kisanduku hiki sio maendelezo ya mambo ya Mtume Paulo, kwa hiyo utaona kwamba kuna msitari kati ya kisanduku hiki na kile kilichotangulia. Nyingi ya jamii zinazoendekeza kuabudu sanamu huamini kwamba mtu akimtendea mema jirani yake na pia akitenda mambo yanayochangia amani katika jamii, basi watakapokufa wataenda mahali pazuri. Hata ingawa ni jambo zuri sana kuchangia amani katika jamii, ni lazima ifahamike kwamba kutenda matendo mema hakuwezi kusafisha mioyo ya watu kutokana na hatia iletwayo na dhambi. Hatuwezi kumpendeza au kumridhisha Mungu kwa bidii zetu wenyewe. Maisha yetu ya baadaye baada ya kuaga dunia yanategemea uhusiano tulio nao na Yesu Kristo (Tazama Somo La 1, 7, 8, na la 12).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 44

Page 48: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuchanganya dini changanyifu na Ukristo haikubaliwi na MunguKisanduku cha mwisho upande wa kushoto hakina orodha ya mambo ya Mtume Paulo. Lakini tunaweza kuyagundua kwa kutazama tamaduni za watu na pia kwa kusoma hadhithi nyingine katika Biblia. Siku hizi kuna mazoea ya kuchanganya mafunzo ya dini za uongo pamoja na ukweli wa Biblia wakati watu wanapomwamini Yesu kama mwokozi wao. Hivi ndivyo ilivyokuwa hata katika enzi ya Biblia, watu walichanganya ukweli na uongo. Inawezekana kuna hali fulani zinazochangia kutokea kwa jambo hili. Lakini ni bayana kabisa kwamba tangu zamani katika enzi za manabii wa Agano la Kale hadi enzi ya maandiko na huduma ya Mtume Paulo, Mungu anataka tuache kuabudu sanamu na badala yake tumwabudu Mungu wa kweli na aliye hai. Kuchanganya imani za kitamaduni na za Biblia huufanya ujumbe kuwa dhaifu, ushuhuda kukosa nguvu, na kwa jumla moto wa kanisa kupungua (Tazama Somo La 1 na La 6). Kumbuka kwamba Shetani huwa na ushawishi mkubwa katika tamaduni zote duniani. Suluhisho la tatizo hili ni kanisa kuwa na kipawa cha utambuzi wa roho zidanganyazo, na pia kufanya kazi pamoja kutambua na kukabiliana na tatizo hili. Athari za mafundisho ya uongo kutoka kwa Shetani na desturi potofu zahitaji kuvuliwa kutoka katika kila mila na desturi kama mtu avuavyo nguo mwilini mwake. Badala yake tamaduni na mila za watu zipambwe kwa mafundisho ya kweli kutoka kwa Mungu, na kwa njia hiyo tamadani hizo zitapendeza zaidi kama mtu aliyevaa vizuri apendezavyo.

Sifa za watu waliokataa Ufunuo Maalum wa MunguKwa kuwa tumeshajadili sifa za dini za uongo ambazo chanzo chake ni kukataa Ufunuo wa Jumla wa Mungu, sasa tutajadili sifa za watu waliokataa Ufunuo Maalum wa Mungu. Kumbuka katika Somo La 3 tulijifunza kwamba kuna aina tatu za Ufunuo Maalum, yaani Yesu, Biblia na Roho Mtakatifu. Watu hawa watatu wameonyeshwa katika kisanduku cha kwanza, juu, upande wa kulia. Kisanduku hiki kimepewa alama ya hasi au kuondoa kuonyesha kwamba tunazungumzia watu waliokataa Ufunuo Maalum wa Mungu kwa njia moja au nyingine.

Dini danganyifu hukataa kuamini kwamba Yesu ni Mungu; wao husema kwamba Yesu ni mmoja wa miungu mingi, au ya kwamba binadamu aweza kuwa mungu(Wamomoni)Kisanduku kilicho chini ya hiki kinaonyesha picha ya Yesu (Mwanakondoo), akiwa na alama ya hasi au ya kuondoa inayopitia kati yake. Watu wanaokataa Ufunuo Maalum wa Mungu wanaweza pia kukataa kuamini kwamba Yesu ni Mungu, na pia kukataa kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Mfano mmoja wa kukataa kwa jinsi hii ni kule kunakofanywa na Waislamu. Wengine walio katika kipengele hiki wanaweza kufunza kwamba wanadamu wanaweza kuwa miungu. Vilevile katika picha hii unaweza kuona mtu aliyekaa katika Kiti Cha Enzi cha Mungu. Baadhi ya mifano ya dini za aina hii zinazochukua nafasi ya Mungu ni ile ya Wamomoni na wa Wabudha.

Dini danganyifu inazo vitabu vingine au mafunzo ya ziadaKatika kisanduku kinachofuata kuna Biblia, alama ya msalaba au ya chanya (+) na kitabu kingine au mafunzo ya ziada. Wale wanaokataa Ufunuo Maalum wa Mungu upatikanao katika Biblia, bado hutumia baadhi ya Maandiko ya Biblia, lakini pia huongeza mafunzo mengine juu ya yale ya Biblia. Mfano wa dini zinazofanya hivi ni Wamomoni: Dini hii hutumia Kitabu Cha Wamomoni na vitabu kadhaa vingine, pamoja na Biblia kama vyanzo vyao vya Ukweli. Uislamu: Dini hii hutumia Biblia, lakini haswa hutumia Kurani. Dini nyingine ni ile ya Mashahidi wa Yehova. Hawa hutumia Biblia, pamoja na maandiko mengine kufasiri na kuelezea maana ya ujumbe wa Biblia. Dini nyingine za uongo hukataa ujumbe wa Biblia kabisa.

Dini nyingine hufundisha kwamba kuna njia nyingi ziendazo kwa Mungu au matendo mazuri kama njia inayoweza kumfanya mtu kwenda peponi atakapokufa Katika kisanduku kifuatacho kuna picha inayoonyesha injili bandia ambayo inavuruga njia kamili iletayo wokovu au maisha mema baada ya kufa. Biblia inasema kwamba Yesu pekee ndiye njia iendayo kwa Mungu (Matendo 4:12; Yohana 14:6). Lakini kama ilivyoonyeshwa katika picha hii, dini nyingine hufundisha kwamba kuna njia nyingi ziendazo kwa Mungu. Ukiangalia utaona kwamba upande wa kushoto wa kisanduku kuna njia nyingi zinazoelekea mahali pamoja hapo juu. Watu hudhani kwamba njia hizi zote zinaelekea katika kiti cha Enzi cha Mungu. Mfano wa dini kama hizi ni Imani ya Wabahai na Kihindu. Picha iliyoko upande wa kulia wa kisanduku inaonyesha matendo mazuri kama njia inayoweza kumfanya mtu kwenda peponi atakapokufa. Dini nyingi za uongo huwafunza watu kwamba mtu akitenda mema ataenda mbinguni. Mfano wa dini hizi ni Uislamu, Dini ya Budha, na Kihindu.

Dini danganyifu hudai kwamba “malaika” alionekana kwa kiongozi na kufunua dini mpyaKisanduku kinachofuata kinaonyesha picha ya pepo, anayeonekana kama malaika, akimtokea mtu. Dini zinazokataa Ufunuo Maalum wa Mungu mara nyingi huwa na uhusiano na kiumbe cha kiroho kama malaika (ambaye sio malaika bali pepo) anayemfunulia mwanadamu mafundisho fulani ya uongo. Biblia inasema kwamba hata malaika akija kutoka

Copyright © 2007 Tammie Friberg 45

Page 49: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mbinguni na kufunza watu mafundisho yanayohitilafiana na ufunuo wa Mungu, malaika huyo ni alaniwe. Roho yoyote inayofunza kwamba Yesu si Mungu, ni ya Mpinga Kristo. Roho Mtakatifu hutufundisha mambo yaliyo ya kweli na sawa. Biblia inasema kwamba pepo huwafunza watu mafundisho ya uongo (1 Timotheo 4:1). Mfano wa mafundisho potofu kama haya ni kama yale mafunzo aliyopewa Mohamed, mwanzilishi wa dini ya Kiislamu na malaika, na yale aliyopewa Joseph Smith na malaika. Joseph Smith ndiye mwanzilishi wa dini ya Wamomoni (ambalo kwa kimombo huitwa kanisa la Later Day Saints). Pia kuna pepo ambao huwatokea manabii au viongozi wa kiroho wa dini za uongo, na kuwafunulia mafundisho ya uongo na matambiko ya uchawi.

Dini danganyifu huongozwa na wapinga Kristo wengiHatimaye kisanduku cha mwisho kinawakilisha kuwepo kwa wapinga Kristo wengi. Hapa wameonyeshwa kama kondoo weusi. Watu wa jinsi hii hujiona kuwa Mungu au kusema wao ndio Yesu. Aidha wanaweza kufanya ishara na miujiza kwa kutumia nguvu za pepo ili waweze kujipatia wafuasi. Mara nyingi wapinga Kristo kugeuza maana iliyomo katika Biblia na kufundisha mafundisho yanayohitilafiana na ujumbe halisi wa Maandiko hayo. Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo amejipatia kwa damu ya Mwanae. “Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo. Hata kutoka miongoni mwenu wata-tokea watu ambao watasema mambo ya uongo ili kuwapotosha watu na kuwafanya wawafuate wao tu. Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi” (Matendo ya Watume 20:29-31). Mtume Yohana alisema katika Biblia kwamba wapinga Kristo wengi tayari walikuwa wamejitokeza duniani. Hawa ndio wale wanaopinga kuja kwa Yesu kama mwanadamu. Lakini hata hivyo waandishi wa Agano Jipya wana waonya watu juu ya Mpinga Kristo atakayekuja katika siku za usoni. Mpinga Kristo huyo atawapotosha watu wengi, hasa waiache imani.

Visanduku vyote katika ukurasa huu vimewekwa kwa lengo la kutoa sifa za dini za uongo, ili sisi kama Wakristo tuwafundishe wengine walio chini ya utunzaji wetu juu ya udanganyifu unaotumiwa na pepo kugeuza Ukweli wa Mungu. Tambua kwamba dini hizi zote za uongo lengo lake ni kuupinga ukweli wa Mungu alioufunua kwetu. Katika mafundisho yatakayofuata, kuna mengi zaidi yatakayomulikwa juu ya dini za uongo. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakisha kwamba waumini wanaelewa na imani yao inaepuka kutiwa dosari na dini hizi za uongo.

Mafundisho Juu Ya Somo La 5

Sifa Za Wale Wanaoukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu

Sifa Za Wale Wanaoukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu

1. Kukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu Kupitia Kwa Uumbaji Wake

1. Kukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu

2. Watu Hutengeneza Miungu Yao Inayofanana Na Viumbe: Sanamu zinazofanana na wanyama, watu, pepo. Mambo Haya Huelekeza kwenye Uchawi.

2. Watu Hukataa Uungu, na Historia Ya Yesu; Wanaamini Kwamba Yesu Ni Mmoja Wa Miungu wengi, au wanaamini Watu Wanaweza Kukifikia Kilele Cha Uungu.

3. Mungu Aliwaacha Wafanye Uzinzi Na Kuikosea Heshima Miili Yao.

3. Watu Hutumia Biblia Pamoja Na Kitabu Kingine Kinachochukuliwa Kama “Kitakatifu”.

4. Mungu Aliwaacha Wafuate Nia Zao Potofu 4. Huamini Kwamba Kuna Njia Nyingi Ziendazo Kwa Mungu. Huku ni Kukataa Kwamba Njia Ya Wokovu Ni Yesu Pekee.

5. Watu Huamini Kwamba Matendo Mazuri Yatawasaidia Katika Maisha Yajayo. Hii Pia Ni Sifa ya Wale Walioukataa Ufunuo Wa Mungu Wa Jumla.

5. Mara Kwa Mara Mambo Yanayotendwa Na Dini Za Uongo Huwa Yametoka Kwa Pepo. Pepo Huwa Amemtokea Mtu.

6. Watu Huchanganya Ukristo Na Upagani 6. Wapinga Kristo Ni Wale Ambao Wanapinga Kwamba Yesu Ndiye Kristo. Kunao Wapinga Kristo Wengi Ambao Tayari Wamejitokeza, lakini Kunaye Mmoja Atakayekuja Siku Za Mwisho.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 46

Page 50: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Marejeo ya Kujifunza Biblia Ya Somo La 5Sifa Za Wale Wanaukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu

Maandiko: “Nani asiyekuogopa wewe, ee mfalme wa mataifa? Wewe wastahili kuheshimiwa. Miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika falme zao zote, hakuna hata mmoja aliye kama wewe. Wote ni wajinga na wapumbavu, mafunzo ya vinyago ni upuuzi mtupu! Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ofiri; kazi ya mafundi staid na wafua dhahabu; Zimevishwa nguo za samawi na zambarau, zilizofumwa na wafumaji staid. Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli’ Mungu aliye hai, mfalme wa milele. Akikasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake. Basi utawaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.” Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu. Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake. Binadamu ni mjinga na mpumbavu; kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake; maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu. Havina uhai wowote ndani yao. Havina thamani, na ni udanganyifu mtupu; wakati vitakapoadhibiwa vyote vitaangamia (Yeremia 10:7-15)."Kwako wamo wanaowasingizia wengine ili wauawe. Wakazi wako hushiriki chakula kilichotolewa miungu milimani. Watu wako wanatenda ufisadi. "Kwako wamo watu ambao hulala na wake za baba zao. Huwanajisi wanawake katika siku zao za hedhi. "Wengine hufanya machukizo kwa kulala na wake za jirani zao. Wengine hulala na wake za watoto wao, na wengine hulala na dada zao. Huko kwako kuna watu ambao huua kwa malipo. Umepokea riba na kuwalangua wenzako ili kujitajirisha, na kunisahau mimi kabisa! Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. "Nimekunja ngumi yangu dhidi yako kwa sababu ya hiyo faida uliyopata kwa njia isiyo halali na kwa mauaji yaliyofanyika kwako. "Je, utaweza kustahimili kuwa hodari siku nitakapopambana nawe? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesea na nitayatekeleza hayo” (Ezekieli 22:9-14).

Kuukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu Ulio Katika Uumbaji Habari Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo

Watu Hujitengenezea Miungu Iliyofanana Na Viumbe: Sanamu Zinazofanana Na Wanyama, Watu, Na Pepo. Mambo Haya Huelekeza Kwenye Uchawi*Mataifa Ya Kigeni Hayataacha Kuabudu Miungu Yao Wakati wakiwa Samaria - 2 Wafalme 17.*Mfalme Yosia Aitii Sheria- 2 Wafalme 22-23.*Mungu Ajibu Maombi Ya Hezekia- 2 Wafalme 19.*Madhababu ya Mungu Asiyejulikana- Matendo 17.*Sanamu Ya Dagoni Yaanguka-1 Samueli 5:3-5.*Mungu ni Mungu wa Milima Na Mabonde- 1 Wafalme 20.*Kuingia Katika Nchi Ya Ahadi- Kutoka 34:11-17.*Mungu Anawaadhibu Watu Kwa Kuabudu Sanamu- Kumbukumbu 32.*Paulo na Barinaba Wanadhiwa Kuwa Miungu- Matendo 4:15-18.*Nebukadneza Ajitangaza Kuwa Mungu- Danieli 6.*Mfalme Yehoshafati- 2 Mambo Ya Nyakati 17; 19.*Mfalme Manase- 2 Nyakati 33:15.*Mfalme Ahabu: “Maadamu miungu ya Shamu iliwasaidia wafalme wa Shamu, nikiitolea dhabihu huenda ikanisaidia nami pia.” Lakini hiyo ilisababisha kuangamia kwake na taifa lote la Israeli - 2 Mambo Ya Nyakati 28:23.

Watu Hujitengenezea Miungu Iliyofanana Na Viumbe: Sanamu Zinazofanana Na Wanyama, Watu, Na Pepo. Mambo Haya Huelekeza Kwenye Uchawi*mila za dini za watu hawa ni za uongo, Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege katika shamba la matango, havina uwezo wa kuongea; ni lazima vibebwe maana haviwezi kutembea- Yeremia 10:3-6.*Vinyago Haviwezi Kujibu Hata Tukivililia; Haviwezi Kututoa Katika Shida - Isaya 46:5-11.*Miungu yote husujudu mbele yake (Bwana)- Zaburi 97:7.*Msiige Tabia Za Mataifa- Kutoka 34:11-17.*Kuabudu Sanamu Ni Kama Kuingia Katika Mtego- Kumbukumbu 7:16, 25-26; Kumbukumbu 17:2-3.*Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu- Zaburi 19:1. *Mtu Anayetengeneza Vinyago Ni Mpumbavu- Yeremia 51:17-19.*Waabudu Sanamu Huabudi Kazi Za Mikono Yao Wenyewe- Isaya 44:10-20; Yeremia 1:16; Hosea 13.2; Habakuki 2:18.*Vyakula Viliyotolewa Miungu- 1 Wakorintho 8:4-6; 1 Wakorintho 10:20.*Wanaotengeneza Vinyago, Watafanana Navyo- Zaburi 115: 4-8.*Miungu Ya Sanamu Haiwezi Kukomboa- Isaya 46:7-9.*Wanaobudu Miungu Mingine Watapata Majonzi Mengi- Zaburi 16:4. *Vinyago Humchukiza Mungu- Yeremia 11:17; 32:29; Yeremia 44.

Mungu Anawaacha Wafuate Uzinzi Na Waikosee Heshima Miili Yao*Sodomu Na Gomora- Mwanzo 18-19.*Yuda Na Kahaba Wa Hekaluni- Mwanzo 38.*Eliya Anakabiliana na Baali (mungu wa rutuba)- 1 Wafalme 18.*Ezekieli Akemea Uzinzi- Ezekieli 22:9-11.*Eliya Anakabiliana Na Manabii Wa Baali (mungu wa rutuba na dhoruba)-1 Wafalme 18.*Waisraeli Walishikamana na Baalil of Peori-Hesabu 25:1-9.*Kuabudu Sanamu Kwafananishwa Na Kufanya Makahaba Na Mataifa- Ezekieli 16, 23; Isaya 57.*Watu Wanaendelea Kufanya Ukahaba- Hosea 4.

Mungu Anawaacha Wafuate Uzinzi Na Waikosee Heshima Miili Yao*Kujamiiana Kwa Maharimu Katika Kanisa La Korintho- 1 Wakorintho 5:1,11. *Watu Wakifanya Uzinzi- Yeremia 5:7-8; 13:27.*Baba Na Mama Wakizini Na Mwanamke Mmoja- Amosi 2:7.*Kuabudu Sanamu Ni Sawa Na Kuzini Na Mawe Na Mbao-Yeremia 3:9; Yeremia 5:7-8.*Mungu Aliwaacha Wafuate Tamaa Zao- Warumi 1:24, 26-27. *Orodha Ya Dhambi Za Kuzini Na Sanamu-1 Wakorintho 6:9. *Kufanya Ushoga Na Kulala Na Wanyama ni Chukuzo Kwa Mungu- Mambo Ya Walawi 18:22-24.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 47

Page 51: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu Ulio Katika Uumbaji *Makahaba Wa Kiume Katika Yuda- 1 Wafalme 14.*Asa Awaondoa Makahaba Na Sanamu Kutoka Katika Nchi- 1 Wafalme 15.*Nabii Ezekieli Akemea Uasherati- Ezekieli 23:1-44.*Kahaba Mkuu Katika Ufunuo Wa Yohana- Ufunuo 17.

*Kuzini Na Mke Wa Jirani Yako, Mkaza Mwanao, Au Dada Yako- Ezekieli 22:9-11; Ezekieli 16:17-*Hatima Ya Miungu Ya Uongo - Yeremia 10:10-15. *Uasherati Unahusiana Na Kubudu Sanamu- Kutoka 32:6, 25; Hesabu 25:1-3; 1 Wafalme 14:24; 15:12; 2 Wafalme 17:30; 23:7; Ezekieli 16:17; Hosea 4:12-14; Amosi 2:8; 1 Cor. 10:7,8; Rev. 2:14, 20-22; 9:20-21; 14:8; 17:1-6.

Mungu Anaawacha Wafuate Nia Zao PotofuUchawi:*Mfalme Manase Ajiingiza Katika Mambo Ya Uchawi -2 Wafalme 21.*Waisraeli Wanafanya Machukizo Kwa Siri- Wanajiingiza katika Uchawi- 2 Wafalme 17.*Mungu Anahukumu Mji Wa Ninawi Kwa Kujiingiza Katika Uchawi- Nahumu 3:1-19.*Mfalme Sauli Anamwasi Mungu: Uasi Ni Sawa Na Dhambi Ya Kupiga Ramli- 1 Samueli 15:1-23.*Wale Wote Wanaotenda Mambo Ya Uchawi Wanatupwa Katika Ziwa La Moto- Ufunuo 21:8.Ulevi:*Ulevi Wa Kufanya Ukahaba- Ufunuo 17; 18:3; Yeremia 51:7.*Aroni Atangaza Karamu Kwa Ajili Ya Ndama Wa Dhahabu- Kutoka 32.*Kulewa Na Maandishi Ukutani- Danieli 5.Uuaji:*Ahabu Na Yezebeli- 1 Wafalme 21.*Farao- Kutoka 1.*Mlawi Na Suria- Waamuzi 19.Sherehe Na Matambiko Yawakalisha Dini Ya Uongo:*Aroni Atangaza Karamu Kwa Ajili Ya Ndama Wa Dhahabu- Kutoka 32:5-*Waisraeli Wafanya Sherehe Na Wamoabu- Hesabu 25:1-9.*Paulo Anajadili Swala Hili Kwa Ajili Ya Waamini- 1 Wakorintho 8-10.*Kanisa La Pergamoni-Ufunuo 2:14.*Kwa Kanisa La Thuatira- Ufunuo 2:20.*Mfalme Yeroboamu Afanya Karamu Kwa Ajili Ya Ndama Wawili Wa Dhahabu Aliowatengeneza ili Waabudiwe -1 Wafalme 12:25-*Mfalme Hezekia Na Sherehe Ya Pasaka- 2 Mambo Ya Nyakati 30.*Mfalme Yosia Na Sherehe Ya Pasaka- 2 Wafalme 23; 2 Mambo Ya Nyakati 35.

Mungu Anaawacha Wafuate Nia Zao PotofuUchawi:*Amri Ya Mungu Juu Ya Uchawi- Kumbukumbu 18:9-18; Kutoka 22:18.*Kuabudu Sanamu Kukiambatana Na Uchawi- 2 Wafalme 21; Nahumu 3:1-19.*Uchawi/Uganga Ni Matendo Ya Mwili- Wagalatia 5:20.Ulevi:*Divai Huleta Dhihaka- Mithali 20:1.*Sifa Za Mlevi- Mithali 23:29-35.Uuaji:*Moleki- Walawi 18:21.*Kuwaua Wasio Na Hatia, Bonde La Machinjo- Yeremia 19.*Mtu mwadilifu akifa, hakuna mtu anayejali; Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa- Isaya 57:1-2.Sherehe Na Matambiko Yawakalisha Dini Ya Uongo:*Waabudu Sanamu Walikaa, Wakanywa Na kusimama Kucheza - 1 Wakorintho 10:7; Kutoka 32:5-6.*Petro Awasihi Watu Wasijiingize Katika Mambo Hayo- 1 Petro 4:3-5.*Jua Na Mwezi Viliumbwa Viwe Ishara Ya Sherehe, Siku Na Miaka- Mwanzo 1:14.*Waisraeli Waanzisha Sherehe Zao Wenyewe Kwa Kuzingatia Yale Waliyotendewa Na Mungu- Kumbukumbu 6:1-25; Kutoka 12:1-51; 13:1-22; Mathayo 26:17-30; 1 Wakorintho 11:23-34.

Watu Huamini Kwamba Matendo Mazuri Yatawasaidia Katika Maisha Yajayo. Hii Pia Ni Sifa ya Wale Walioukataa Ufunuo Maalum Wa Mungu.*Ibrahimu, Mtu Huhesabiwa Haki Kwa Imani- Mwanzo 15; Wagalatia 3:6-29; Warumi 4:3; Yakobo 2:23.

Watu Huamini Kwamba Matendo Mazuri Yatawasaidia Katika Maisha Yajayo. Hii Pia Ni Sifa ya Wale Walioukataa Ufunuo Maalum Wa Mungu.*Hatuwezi Kwenda Mbinguni Kwa Matendo Yetu Wenyewe- Waefeso 2:8-9.*Wote Wametenda Dhambi- Warumi 3:23.*Wokovu Ni Karama Ya Bure Ya Mungu Tunayoipokea Kupitia Kwa Yesu- Warumi 6:23. *Ikiwa Wokovu Unaweza Kupatikana Kupitia Kwa Sheria, Basi Kristo Alikufa Bure- Wagalatia 2:16-21.

Watu Huchanganya Ukristo Na Upagani *Msiongeze Wala Kupunguza Sheria Za Mungu - Kumbukumbu 12:32.*Waisraeli Waabudu Sanamu Misri- Ezekieli 20:6-10.*Waisraeli Watengeneza Ndama Wa Dhahabu- Kutoka 32.

Watu Huchanganya Ukristo Na Upagani *Kuabudu Sanamu Ni Kitambulisho cha Mpinga Kristo- 1 Yohana 5:21; Wakolosai 3:5-7.*Mungu Aliihukumu Miungu Ya Misri Kwa- Hesabu 33:4. *Waamini Waacha Kuabudu Sanamu Na Kuanza Kumwabudu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 48

Page 52: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuukataa Ufunuo Wa Jumla Wa Mungu Ulio Katika Uumbaji *Yakobo Aiondolea Mbali Miungu Ya Kigeni- Mwanzo 35.*Kutokuwa Na Msimamo Kwa Yehu- 2 Wafalme 9.*Stefano Ajitetea- Matendo 7:41-43.*Sulemani Apotoshwa Na Wake Zake Wa Kigeni- 1 Wafalme 11:1-11.*Changamoto Ya Mwisho Ya Yoshua, Mimi Na Nyumba Yangu Tutamtumikia Bwana- Yoshua 24:14-17.*Mfalme Yosia Ampendeza Bwana- 2 Wafalme 22-23.*Safari Ya Ezekieli Kwenda Hekaluni Mlimojaa Sanamu - Ezekieli 8-9.*Kujenga Sanamu Moyoni- Ezekieli 14.*Hosea Aoa Kahaba- Hosea 1:1-8

Mungu-1 Wathesalonike 1:9

Sifa Za Watu Wanaoukataa Ufunuo Maalum Wa MunguMaandiko: “Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Kristo. Mtu wa namna hiyo ni mpinzani wa Kristo-anamkana Baba na Mwana. Maana yeyote anayemkana Mwana , anamkana Baba pia; na yeyote anayemkubali Mwana, anampata Baba pia. Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae ndani yenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtakaa ndani yake Mwana na Baba. Na Ahadi aliyotuahidi sisi ndiyo hii: uhai wa milele. Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha nyinyi” (1 Yohana 2:22-26).“Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye niw a mpinzani wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni! Lakini nyinyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabiiwa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu. Wao husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani wao ni wa ulimwengu. Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa kweli bar oho wa uongo” (1 Yohana 4:3-6).

Kuukataa Ufunuo Maalum Wa MunguHabari Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Watu Hukataa Uungu, na Historia Ya Yesu; Wanaamini Kwamba Yesu Ni Mmoja Wa Miungu wengi, au wanaamini Watu Wanaweza Kukifikia Kilele Cha Uungu. *Nebukadneza Anajitangaza Kwua Mungu- Danieli 6.*Petro Anajitetea, Yesu Ndiye Njia Ya Pekee- Matendo 4:1-12.*Yesu Afikishwa Mbele Ya Baraza, na Mbele Ya Pilato- Mathayo 26-27; Luka 22-23.*Stefano Mbele Ya Baraza- Matendo 7.*Kurudi Kwa Yesu- Ufunuo 19:13-21.

Watu Hukataa Uungu, na Historia Ya Yesu; Wanaamini Kwamba Yesu Ni Mmoja Wa Miungu wengi, au wanaamini Watu Wanaweza Kukifikia Kilele Cha Uungu.*Yesu Ndiye Njia, Kweli Na Uzima- Yohana 14:6.*Yesu Pekee Ndiye Njia Iendayo Kwa Baba- Matendo 4:12.*Usimkufuru Roho Mtakatifu- Mathayo 12:31-32.

Watu Hutumia Biblia Pamoja Na Kitabu Kingine Kinachochukuliwa Kama “Kitakatifu.”*Watu wa Efeso Wachoma Vitabu Vyao Vya Kufanyia Uchawi- Matendo 19.*Paulo Awahutubia Watu Wa Kolosai: Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo ba kukombolewa katika nguvu za utawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa nasharti: “Msishike hiki,” “Msionje kile,” “Msiguse kile!” Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu. Kweli, masharti hayo yanaonekana kuwa ya hekima kwa namna ya ibada wanayojishurutishia, unyenyekevu, na kuutendea mwili kwa ukali; lakini hayafai chochote kuzuia tama za mwili- Wakolosai 2:20-23.*Mimi na Nyumba Yangu (Kufuata Neno Au Amri)- Yoshua 24:14-17.

Watu Hutumia Biblia Pamoja Na Kitabu Kingine Kinachochukuliwa Kama “Kitakatifu.”*Usiongeze Neno Katika Maneno yake, Asije Akakukemea, nawe ukaonekana mwongo- Mithali 30:6.*Msiongeze chochote Katika Amri Ninazowapeni, wala Msipunguze Kitu; zingatieni Amri Za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo Ninawapeni - Kumbukumbu 4:2.*Mimi Yohane Nawapa Onyo Wotw Wanaosikia Maneno Ya Unabii Yaliyomo Katika Kitabu Hiki: Mtu Yeyote Akiongeza chochote Katika Mambo Haya, Mungu Atamwongezea Mabaya Yaliyoandikwa Katika Kitabu Hiki. NA Mtu yeyote Akipunguza chochote Katika Maneno Unabii Yaliyomo Katika Hiki, Mungu Atamnyang’anya Sehemu Yake Katika Mji Mtakatifu, ambavyo Vimeelezwa Katika Kitabu Hiki - Ufunuo 22: 18-19.*Msilichafue Neno La Mungu- 2 Wakorintho 4:1-7.*Ufundishe Sawa Ule Ujumbe Wa Mungu- 2 Timotheo 2:15.

Huamini Kwamba Kuna Njia Nyingi Ziendazo Kwa Mungu. Huku ni Kukataa Kwamba Njia Ya Wokovu Ni Yesu Pekee.

Huamini Kwamba Kuna Njia Nyingi Ziendazo Kwa Mungu. Huku ni Kukataa Kwamba Njia Ya Wokovu Ni Yesu Pekee. *Msiwakaribishe Walimu Wa Uongo- 2 Yohan 7-11.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 49

Page 53: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuukataa Ufunuo Maalum Wa Mungu*Watu Wa Kidini wa Athene-Matendo 17:15-34. *Njia Ionekanayo Kuwa Sawa, Lakini Mwisho wake Ni Mauti -

Mithali 14:12.*Wokovu Unapatikana Kupitia Kwa Yesu tu - Matendo 4:12.

Mara Kwa Mara Mafundisho Ya Dini Za Uongo Hutoka Kwa Pepo. Pepo Humtokea Mtu.*Pepo Huwafunza Watu Mafundisho Ya Uongo- 1 Timotheo 4:1.

Mara Kwa Mara Mafundisho Ya Dini Za Uongo Hutoka Kwa Pepo. Pepo Humtokea Mtu.*Malaika Yeyote Akija Kuhubiri Injili Nyingine, Ni Alaniwe - Wagalatia 1:7-8; 2 Wakorintho 11:4.

Wapinga Kristo Ni Wale Wanaokana Kwamba Yesu Ndiye Kristo. Tayari Kunao Wapinga Kristo Ambao Wameshakwisha Kuja Duniani, Lakini Kuna Mmoja Atakayekuja Siku Za Mwisho.*Watu Watajitokeza Hata Makanisani Kuwapotosha Wengine Ili Wawe Wanafunzi Wao - Matendo 20:28.*Yesu Anawakemea Wapinga Kristo Na Manabii Wa Uongo-Mathayo 24:1-27; Marko 13; Luka 21.*Simoni Mchawi, Nguvu Kuu Ya -Matendo 8:5-12.

Wapinga Kristo Ni Wale Wanaokana Kwamba Yesu Ndiye Kristo. Tayari Kunao Wapinga Kristo Ambao Wameshakwisha Kuja Duniani, Lakini Kuna Mmoja Atakayekuja Siku Za Mwisho.*Mtu Anayemkana Kristo ni Mwongo Na Mpinga Kristo - 1 Yohana 2:22-23; 1 Yohana 4:2-6; 2 Yohana 1:7.*Mpinga Kristo- 2 Wathesalonike 2:3-11.*Mpinga Kristo Atatupwa Katika Ziwa La Moto- Ufunuo 19-20.*Kunao Wapinga Kristo Wengi- 1 Yohana 2:18.*Nafasi Ya Kutoa- Luka 21:13.

Mafundisho Ya ZiadaHabari Za Biblia Zinazoonyesha Kwamba Wakristo Hawastahili Kujiingiza Katika UchawiSimoni Mchawi Alitaka Kununua Nguvu Za Mungu, lakini hakuweza na badala yake akaitwa adui wa haki Matendo 8:9-24.Wakazi Wa Efeso walivichoma vitabu vyao vya kufanyia. Matendo 19:11-20.Roho wa utambuzi akemewa na kumtoka msichana fualni. Matendo 16:16-18.Paulo anamkemea Bari-yesu yule mchawi. Matendo 13:6-12.Katika Agano La Kale Mchawi Yeyote Aliuawa. Kutoka 22:18Habari Za Biblia Zinazoonyesha Kwamba Nguvu Za Mungu Ni Kuu Kuliko Nguvu az.Mungu anaweza kuziangusha nguvu za wachawi- Isaya. 44:24-26.Gideoni abomoa madhabahu za Baali- Waamuzi 6.Uwezo wa Yusufu Wa Kutafsiri Ndoto- Mwanzo 41:8.Kisa Cha Musa na Waganga/wachawi wa Misri- Kutoka 9:11.Mapigo Ya Misri Yaliilenga Miungu Yao-Kutoka 12:12.Uwezo wa Danieli wa kutafsiri ndoto- Danieli 1:20; 2:2, 10-11.Yesu anatoa pepo- Luka 11:15-20.Mfalme Ahazi abadili miungu akifikiri kwamba itamsaidia- 2 Mambo Ya Nyakati 28:9-27.Simoni Mchawi anadhani kwamba anaweza kuzinunua nguvu za Roho Mtakatifu kwa fedha zake- Matendo 8:9-25.Barnaba na Sauli Wanakabiliana na nabii wa uongo wa Kiyahudi- Matendo 13:6ff.Je, Biblia Inauzungumziaje Uchawi?Ni sawa na dhambi ya uasi. 1 Samueli 15:23.NI upotofuw wa imani Wagalatia 3:1.Umechanganyika na ibada ya sanamu. 2 Mambo Ya Nyakati 33:6; 2 Wafalme 9:22.Ni kazi ya mwili. Wagalatia 5:20.Waoendekeza uchawi watatupwa katika ziwa la moto. Ufunuo 21:8Je, tuna uwezo gani dhidi ya pepo?Yesu alikuja kuziharibu kazi za Shetani. 1 Yohana 3:8 Yesu alikufa msalabani ili kuwapokonya nguvu pepo. Wakolosai 2:15 Yesu yuko juu ya nguvu zote. Waefeso 1:20 Mungu ametuketisha pamoja na Yesu na anatupa nguvu kupitia kwake. Waefeso 2:6 Hatustahili kuongea na pepo moja kwa moja. Yuda 9-10. Lakini tunastahili kumwomba Yesu awafunge na kuwatoa. Sisi ni muhimu kuliko pepo. Lakini wao wana nguvu kutushinda sisi. Ni vyema tusiwachukulie juu juu tu. Mruhusu Yesu awatoe pepo.Je, tunawezaje Kuvunja Nira Ya Mambo Yaliyopita?Kwa kuchoma hirizi, sanamu, na kila aina ya vitu vyake.Usiende kutafuta ushauri kwa waganga na wapiga ramli.Mtegemee Mungu tu.Anzisha desturi mpya.Yale yaliyo mazuri katika utamaduni wako waweza kuyaendeleza, lakini mabaya yote ni lazima uyatupilie.Wakati wote shirikiana na waamini wenzako kama jamii moja ya Mungu, ili mtiane moyo mwendelee kuwa waaminifu wka Mungu.Jitenge na dini za uongo na matambiko potofu.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 50

Page 54: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 51

Page 55: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 6: Kupima Mafundisho kwa Neno la Mungu

Maandiko: Usiku, wale ndugu waliwahimiza Paulo na Sila waende Berea. Mara tu walipofika huko, walikwenda katika sinagogi la Wayahudi. Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wake wa Thesalonike. Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila yalikuwa kweli. Wengi wao waliamini na pia wanawake wa Kigiriki wa tabaka la juu na wanaume pia” (Matendo 17:10-12).“Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yafaa katika kufundisha ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili, ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila kazi njema” (2Timotheo 3:16-17).

Maelezo mafupi

Ni lazima kuchunguza kila kitu vizuri ili kuhakikisha kwamba hatumchukizi au kumkosea heshima Mungu, hii ni kwa sababu Shetani anafanya kazi katika tamaduni na imani za watu wa kila kabila na rangi duniani. Shetani hujaribu kupenyeza mafundisho yake ya uongo na yanayokandamiza watu katika tamaduni na sherehe za watu duniani. Matendo yenye uhusiano na kuabudu sanamu, mawazo yaziyo bora na kutoheshimu uhai wa binadamu. Biblia inasema,“Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema, na kuepuka kila aina ya uovu.” (1 Wathesalonike 5:21-22).

Waumini hulichanganua kila jambo kulingana na neno la MunguMfano uliopo hapo juu unaonyesha kundi la waamini wakibeba Biblia katika mikono yao ya kulia. Kundi hili la watu tutaliita Waberea, kwa sababu katika Biblia kundi hili ndilo lililochunguza kila neno lililosemwa na Mtume Paulo na Sila kwa kutumia Maandiko kuhakikisha kwamba kila kilichosemwa kilikuwa kweli (Matendo 17:10-11). Katika picha hii wanaonekana wakibeba vikapu juu ya vichwa vyao na wakitembea katika barabara yenye mambo mengi. Upande wao wa kushoto kuna jalala kubwa la taka. Watu hawa ni wafuasi wa Yesu na wanachunguza yale mambo tofauti wanayoyasikia, kuyaona, na kuyatenda duniani ili wajue iwapo mambo hayo yanampendeza Mungu au la. Njia wanayoitumia kupima wanayoyasikia ni kwa kuchukua yale yote waliyoyasikia na kuyachanganua vizuri halafu kuyaweka katika mizani ya Neno la Mungu. Chochote kinachoonekana kuhitilafiana na Biblia au kutompendeza Mungu, kinatupiliwa mbali katika jalala la taka. Chochote kinachoonekana kutofungamana na upande wowote, au hakihitalifiani na Neno la Mungu na njia zake wanakiweka katika vikapu vilivyo kichwani mwao ili kuvihifadhi. Waumini wote hufanya kazi pamoja kufasiri Maandiko kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Waumini hujenga imani yao kwa msingi imaraKila mmoja wa waamini hawa huishi katika nyumba inayofanana na ile iliyoko katika picha hii, sehemu ya chini, upande wa mkono wa kulia. Nyumba hii wanamoishi waamini hawa ina msingi imara na hata mvua na dhoruba kali vijapo haitasambaratika. Msingi walioutumia kujengea nyumba hii ni Neno la Mungu. Kinyume chake ni kwamba kunao watu ambao msingi wa maisha yao ni mila na tamaduni za maeneo wanayoishi. Watu wa jinsi hii wakati wanapokumbwa na “mvua”(matatizo), nyumba zao huporomoka na kusongwa na maji kwa sababu hazijajengwa katika msingi wa KWELI. Ili tuweze kutumia kanuni zilizo katika somo hili, lazima kwanza usimame kidete na kujenga msingi wa maisha yako kwa kutumia Neno la Mungu. Hata ingawa tamaduni zote duniani zina itikadi na imani ambazo ni za maana, imani hizi sio msingi wa kutegemewa. Usisahau kwamba Shetani hupenyeza mafundisho ya uongo katika tamaduni za watu. Kwa hiyo basi itatubidi kuyaondoa mafundisho ya uongo kutoka kwa Shetani na mahali pake kujaza kwa ukweli wa Neno la Mungu. Kila kabila la watu linastahili kujinasua kutokana na kongwa hili la mafundisho ya uongo kutoka kwa Shetani. Hata hivyo kunayo mambo mazuri katika tamaduni za watu, mambo hayo yanaweza kudumishwa katika tamaduni hizo. Tukifanya hivyo Mungu atatujaza furaha na kuyapa maisha yetu maana mpya inayoshinda ile itokayo kwa tamaduni za awali zilizotufunga. Watu kwa kawaida huwa katika hali ya hatari iwapo hawana Neno la Mungu kama msingi wao, hii ni kwa sababu hufungwa na mila na itikadi zao. Maandiko yanapokuwa msingi, basi kila kitu huwa hakina budi kufuata mwongozo wa Maandiko hayo. Maandiko ndio msingi wa Ukweli. Maandiko yanapochukua sehemu ya kwanza, mabadiliko huja pasipo shida yoyote. Waumini huchanganua mambo ya kimila kulingana na neno la MunguSasa baada ya misingi yote kuwekwa vizuri, waamini hawa huanza safari yao ya maisha ya kila siku. Katika mfano huu utaona vitu vingi njiani ambavyo hawa watu wenye busara huwa hawana budi kukubaliana navyo. Baadhi ya mambo wanayokumbana nayo njiani ni tamaduni za makabila yao. Wanaweza kukumbwa na itikadi zinazojitokeza wakati mtoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 52

Page 56: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

anapozaliwa, sherehe za tohara zinapoandaliwa, au mtu anapokufa na mpango wa mazishi kupangwa. Wakati mwingine mambo haya ya mila huchipuka wakati wa majira ya kupanda au kuvuna. Mambo haya yote sharti yapimwe katika mizani ya Neno la Mungu. Iwapo kuna kipengele fulani katika sherehe hizo ambacho ni sehemu ya ibada za miungu ya uongo au mababu, basi kipengele hicho cha sherehe kinastahili kutupwa katika jalala la taka. Lakini iwapo kuna mambo muhimu yanayoweza kudumishwa kama vile sherehe za kuzaliwa mtoto, basi jambo hilo linawekwa katika vikapu walivyojitwika. Kwa njia hii itikadi mpya zitaweza kuchukua sehemu ya zile za zamani, na zile nzuri zitaendelea kudumishwa na kusherehekewa. Mungu alipowakomboa Waisraeli kutoka utumwani, aliwapa watu itikadi mpya ambazo lengo lake lilikuwa ni kazi yake na ukombozi wake wa wanadamu duniani. Walizitupilia mbali sherehe au matambiko yaliyokuwa na uhusiano na miungu wa uongo. Sasa swali ambalo hatuna budi kujiuliza ni hili: Je, tutafanyaje iwapo tutaalikwa kuhudhuria sherehe Fulani ambazo zitaambatana na mambo yasiyompendeza Mungu? Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuomba. Halafu kujaribu kuungana na waamini wengine. Mtume Paulo aliulizwa swali juu ya sherehe Fulani ambapo watu walikula nyama iliyotolewa kama sadaka kwa sanamu (1 Wakorintho 8-10). Naye aliwapa jibu la ajabu. Jambo la kwanza alilosema ni kwamba sisi kama Wakristo tusithubutu kufanya jambo litakalowakwaza Wakristo wengine. Ikiwa Mkristo mwenzetu atatuona tukijiingiza katika sherehe kama hizo, basi huenda hata naye akazirudia njia zake za zamani. Vilevile Mtume Paulo alisema kwamba wale Wakristo ambao ni wadhaifu kiimani na ambao bado wanaabudu sanamu hawaoni kwamba wanafanya makosa kwa sababu, hata Wakristo waliokomaa bado wanajiingiza katika sherehe hizo zao. Hatimaye Paulo, anasema kwamba hata ijapokuwa hakuna miungu/sanamu duniani, wale watu wasiomjua Mungu huwatolea sadaka pepo walio katika sanamu hizo. Sisi kama Wakristo haturusiwi hujiingiza hata kwa kiasi kidogo katika sherehe za kitamaduni zinazohusisha dini za uongo, kwa sababu tukifanya hivyo tutakuwa tunashirikiana na pepo. Tambua kwamba katika picha yetu, Wakristo wanatembea pamoja. Wanasaidiana na kushirikiana katika kila jambo katika jamii. Ikiwa Wakristo watakuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto, au kuhudhuria matanga, basi wataandaa kila kipengele cha sherehe hizo katika njia ya Kikristo. Watajitengenezea itikadi na njia mpya za kufanya mambo zisizotegemea mila zao, bali zinazotegemea uenyeji wao wa Mbinguni. Wakristo sharti waungane mapema na kujadiliana pamoja juu ya kukabiliana na hali zinazoweza kuwafanya kukubaliana na tamaduni mbaya, na pia kuweka mikakati ya kusherehekea sherehe zao kwa njia ya Kikristo. Swala hili la Wakristo kujiingiza katika maswala ya kijamii, ni moja wapo ya maswala magumu yanayolikabili kanisa.

Waumini huchanganua ujumbe, ndoto, unabii wa WaKristo wenzao na ile yao binafsiMambo mengine ambayo wanaweza kukumbana nayo katika safari yao ni watu wanaohubiri, au kutoa unabii, au mtu aliyeota ndoto au kuona maono fulani. Hata ijapokuwa baadhi ya watu hawa wanaweza kuwa Wakristo wa kweli, ni muhimu kuyajaribu maneno yao, lutugia yao, na matendo yao kwa Neno la Mungu. Tena, ikiwa katika jumbe zao kuna dalili ya uhusiano wowote na ibada ya miungu ya uongo, basi sharti jumbe zao zitupwe katika jalala la taka. Lazima sisi kama Wakristo tufuate viongozi ambao wanahubiri Neno la Mungu kweli. Kila kitu kinachowahusu viongozi hawa kinastahili kupimwa katika mizani ya Neno la Mungu, sio tu mafundisho yao na jinsi wanavyofanya kazi ya Mungu. Ikiwa wanawahudumia watu kwa tamaa ya kupata fedha, au mamlaka, basi huduma hiyo yao itakuwa inastahili kuchunguzwa vyema. Viongozi wengi huongeza itikadi na imani zao za kitamaduni katika Biblia. Hivi ndivyo walivyofanya Waisraeli, waliingiza miungu ya uongo katika hekalu la Mungu wa kweli. Aidha waliiabudu miungu ya bandia katika sehemu zilizoinuka, na pia chini ya miti waliyoiona mitakatifu pamoja na kumwabudu Mungu wa kweli. Mambo haya hayakumpendeza Mungu. Watu katika picha hii wanachunguza itikadi zao za Kristo ili kuona iwapo kuna yoyote iliyoathiriwa na imani za kitamaduni. Ikiwa kuna mseto wa aina yoyote ile, basi utatupwa katika jalala la taka. Mungu anatafuta viongozi watakaomtumikia kwa mioyo yao yote.

Wakristo hawa hawazitupilii mbali desturi zilizoingizwa katika Maandiko tu, bali pia hutupilia mbali desturi zote ambazo hutumia Biblia au mambo fulani ya Kikristo vibaya au kwa njia ya kipagani. Kwa mfano, mtu anaweza kutumia Biblia kama sanamu/hirizi ya kutulinda nyumbani. Biblia sio hirizi wala kitu cha kuabudiwa. Mungu pekee ndiye anayeweza kutulinda na kukabiliana na pepo. Pia Biblia sio chombo kinachoweza kutumiwa kumlazimisha Mungu kutenda jambo lolote tunalomtaka atutendee. Lazima tujihadhari tusitumie Biblia kumlazimisha Mungu kufanya yale tunayoyataka sisi. WaKristo hutembea kwenye njia nyembambaTambua kwamba watu wote walio katika mchoro huu wanatembea katika njia, na wanatembea wakilenga mahali fulani. Kitabu cha Mithali kina marejeo mengi yahusuyo kutembea katika njia fulani. Njia hii wameichagua wenyewe, ni njia nzuri na iliyojaa hekima, na sheria za Mungu. Wakati mwingine tunapokumbwa na matatizo, au kujaribiwa kwa mambo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 53

Page 57: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ya ulimwengu, tunaweza kutoka katika njia nzuri na badala yake kufuata njia za kipumbavu. Kandoni mwa njia hii kunazo njia nyingine, lakini njia hizi sharti tuziepuke kwa sababu zinatuelekeza upotevuni na kwenye uchafu. Njia hizo zinapopimwa katika mizani ya Neno la Mungu, huonekana kutokuwa na maana yoyote. Yesu anapenda tuifuate njia nyembamba hata ikiwa kwa kufanya hivyo tutakumbwa na shida nyingi. Wakati Ayubu alipokumbwa na dhiki huu, Mungu alimwona kuwa mwaminifu na aliyebaki katika njia ifaayo na akalipenda Neno la Mungu kuliko hata chakula chake cha kila siku. Yesu anapenda tuchague kuifuata njia ile nyembamba. Njia hii inaelekea mahali pazuri. Lengo la kuifuata njia hii ni kwamba mtu aweze kuwa kama Yesu. Kila siku watu wanaifuata njia hujiuliza maswali mengi kama, je mambo ninayofikiria, kupanga, kusema, na kufanya yanaenda sawa na lengo la mimi kuwa kama Yesu? Kwa hiyo watu hawa hawayapimi mambo yanayotukia nje tu, mbali hata yaliyo mioyoni mwao wenyewe. Watu hawa huyatiisha mawazo yao, matendo yao na maneno yao kwa Yesu. Wanapofanya hivyo huwa wameanza kuzivunja ngome za Shetani katika maisha yao.

Njia pana ya uovu, utumwa na upotevuKatika picha hii utaona katika ile njia pana kuna jumba la kufanyia ukahaba (danguro) na baa inayouzwa pombe. Njia hii ni ya kukubaliana na uovu, utumwa na inayoelekea upotevuni. Watu wanaoifuata njia hii, huanza kukubaliana na mambo mabaya na kuacha kufuata vigezo vilivyo katika Biblia katika njia moja au nyingine. Wakianza kufanya hivyo mwishowe hujikuta wamejiingiza katika upotevu huo na kushindwa kujinasua kutoka katika utumwa huo. Matendo haya ni kama ngono nje ya ndoa, picha za ngono, na utumiaji wa dawa za kulevya. Watu wangine wanaishi kwa kuvutwa kotekote. Hii ina maana kwamba ifikapo wakati wa kuchangamana na watu wa jamii zao kama sehemu ya jamii hiyo, hufuata yale yanayotendwa na watu hawa hata kama ni maovu. Sisi kama wazazi au watu wazima, tunahitaji kuwa na msimamo thabiti kutofuata mambo haya sisi wenyewe, na hata watoto wetu. Mambo haya yanaweza kuuharibu mwili wa mtu pamoja na familia yake. Vijana wakati mwingine hujikuta wakifuata njia hizi potofu kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa marafiki zao au kwa sababu ndio mtindo wa maisha ya vijana wakati huo. Wazazi wengine ambao wamefungwa nira katika utumwa fulani wanaweza kujikuta wakitumia pesa kwa pombe badala ya kuzitumia kwa kuwaelimisha watoto wao. Wanaume wengine hutafuta wanawake nje ya ndoa zao kwa ajili ya kufanya ngono nao. Ni jambo la kushangaza kuona kwamba katika Biblia neno lililotumiwa mahali pa uzinzi ni pornea (Mathayo 5:32), ambalo vilevile ndilo ambalo hutumiwa mahali pa picha za ngono kwa kiingireza pornography. Kwa hiyo kutokuwa waaminifu katika ndoa hakumaanishi tu kufanya tendo la ngono na watu wasio waume au wake zetu, bali pia kutazama picha za ngono katika mtandao au katika majarida. Watu wengi huifuata njia hii kwa sababu ndio njia inayofuatwa na wengi na ndiposa njia hii ni pana. Kitu muhimu cha kukumbuka katika mambo haya ni kwamba yanaweza kumvuta mtu polepole na hatimaye kumfanya mtu huyo kuzoea tabia hizo kabisa. Mara kwa mara watu huifuata njia hii kwa lengo la kufunika uchungu ulioko mioyoni mwao au kujaribu kuondoa uchungu huo. Katika kitabu cha Mithali sura ya 2, mwandishi anaelezea kahaba au Malaya kuwa mtu anayesimama nje ya nyumba yake na kuwabembeleza vijana wa kiume kuingia ndani na kufanya ngono naye. Ukiwa nje ya nyumba hiyo, starehe hizo zinaonekana kuwa za kupendeza mno, lakini mara tu uingiapo ndani unakuta ni mauti. Biblia inasema kwamba ukiutafuta ufahamu au hekima ya Mungu, “vitakuepusha na njia ya uovu, na watu wa maneno mapotovu; watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki. Utaepukana na mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu; mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera. Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai.”(Mithali 2:12-19). Lazima wakati wote kupima matendo yetu katika mizani ya Biblia, na wala sio kwa kutumia utamaduni. Tunastahili kuwafunza watoto wetu na watu wazima katika makanisa yetu jinsi ya kusimama katika ukweli, hata kuwapo na shinikizo za kijamii. Tukifanya hivyo, huo utakuwa mwanzo wa kuyafuatisha maisha yetu kulingana na njia au sheria za Mungu. Njia pana ya fujo na chukiNjia nyingine iliyoonyeshwa hapa ni ile ya fujo na chuki. Hii ni njia moja wapo inayoweza kuwapoteza watu binafsi na hata jamii nzima kwa kusababisha umwagikaji wa damu. Fujo au vita ni njia ambayo watu huitumia ili kidhibiti hali fulani, mali, rasilimali au kuyafikia matamanio yao mabaya. Hii sio njia ya Mungu. Yesu alituamuru kuwapenda majirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe. Uhusiano mzuri sharti uanze nyumbani na halafu kuenea katika jamii yote na hatimaye dunia nzima. Uhusiano wa kuwa mwili mmoja tulioujadili katika Somo La 2 unaweza kutumiwa kama mfano mzuri wa chanzo cha kuleta amani. Lazima tusitishe kuwatesa wanawake, watoto, na watu wasio na hatia.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 54

Page 58: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Tunahitaji kuwafunza watu kwamba vita na fujo huwa chanjo cha mapigano ya kulipiza kisasi na chuki. Mwisho wa vitu hivyo ni kuangamiza familia zetu pamoja na jamii kwa jumla. Tunaweza kuweka mfano mzuri wa tabia kwa kujizuia kutoanzisha fujo au vita. Lakini hata hivyo sharti wakati wote tuwe tayari kulinda familia zetu zinapovamiwa.“Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga.Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.” (Warumi12:12-14).

Njia ya uvivu na uturufuWakati mwingine, waKristo wanapo anza kufa moyo, hao hupoteza hamu ya kusimama imara na kisha kuanza kuwa wavivu. Hili laweza kuwa jambo kuhusiana na watoto, bibi au bwana, au uhusiano na mungu. Wakati mwingine watu huanza kuwa wavivu bila kutarajia. Wanaweza wacha jambo la muhimu maana waanza kusinzia. Wakati mwingine yawaza kuwa ni kwa sababu ya kujishugilisha na mambo mengi mengi.

Njia pana ya kupotoka kimaadiliNjia ya mwisho tutakayoijadili ni ile ya kupotoka kimaadili. Kivutio cha njia hii ni ulafi. Hata katika enzi ya Biblia, kulikuwa na tatizo kubwa la watu kuwatoza wenzao riba kubwa. Vilevile kulikuwa na udanganyifu wa mizani katika kupima vitu, kubadilisha mipaka iliyowekwa, na pia kutumia mbinu nyingi kuwadaganya na kuwaibia watu. Mungu alimpa Musa sheria za kukataza ufisadi wa aina hiyo; na pia Mithali nyingi ziliandikwa kupinga tabia kama hiyo ya kuwapunja wengine. Lakini hata hivyo kufikia enzi za manabii bado kulikuwa na watu wengi waliowadhulumu wenzao kwa kutofuata maagizo ya Mungu juu ya kuwatendea haki wengine. Bibilia ya sema hivi kuhusu hili Jambo: “Ole kwao wanaosema ubaya ni uzuri na uzuri ni ubaya. Wanasema giza ni mwangaza na mwangaza ni giza. Wanasema kichungu ni kitamu na kitamu ni kichungu. 21 Ole kwao wanaojiona kuwa wenye hekima na akili. Ole kwao wanaokuwa wafundi wa kunywa divai,wanaokuwa hodari sana wa kuchanganya vinywaji vya kulewesha. Kwa ajili ya kituliro kidogo wanawaachilia wenye kosa na kuwanyima wasiokuwa na kosa haki yao. Kwa hiyo, kama vile moto unavyoteketeza nyasi,kama vile majani yanavyotoweka ndani ya moto,ndivyo mizizi yao itakavyooza,na maua yao yatakavyopeperushwa juu kama mavumbi. Maana wameacha sheria ya Yawe wa majeshi,wamezarau neno la yule Mutakatifu wa Israeli” (Isaya 5:20-24). “Unapotoa hukumu uamue kwa haki, usimupendelee masikini wala kumwogopa mwenye cheo. Lakini hukumu mwenzako kwa haki. Usipitepite hata kidogo ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usitie maisha ya mwenzako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ni Yawe. Usimuchukie ndugu yako ndani ya moyo wako, lakini upatane siku zote na mwenzako kusudi usitende zambi. Usijilipize kisasi au kuwa na kinyongo juu ya wazao wa watu wako lakini umupende mwenzako kama vile unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ni Yawe. Unapaswa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandiwe na nyama wa aina nyingine. Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. Usivae nguo iliyofumwa kwa aina mbili za nguo. Mwanaume akilala na mwanamuke mujakazi ambaye amechumbiwa na mwanaume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamuke huyo hakukuwa bado huru. Mwanaume huyo ataleta mbele ya hema la mukutano sadaka yake ya kondoo dume kwa ajili ya kosa na kunitolea mimi Yawe. Kuhani atamufanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Yawe kwa ajili ya zambi aliyotenda, naye atasamehewa zambi hiyo aliyotenda. Mutakapofika katika inchi ya Kanana na kupanda aina zote za miti ya matunda, matunda hayo hamutayakula. Hamutaruhusiwa kuyakula kwa muda wa miaka mitatu. Katika mwaka wa ine matunda yake yote yatakuwa matakatifu, yatatolewa kuwa sadaka ya sifa,b kwa Yawe. Lakini matunda ya kuanzia mwaka wa tano hayo munaweza kuyakula na mavuno yenu yataongezeka. Mimi ni Yawe, Mungu wenu. Musikule nyama yoyote pamoja na damu. Musifanye ulozi wala kuaguza. * 27 Musikate kwa kiviringo nywele za pembeni ya kichwa wala kunyoa pembe za ndevu zenu. Musijitie chanjo juu ya mwili wenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata chanjo yoyote juu ya mwili. Mimi ni Yawe. Usimuchafue binti yako kwa kumufanya kahaba, inchi nzima isipate kuangukia katika ukahaba na hivyo kujaa uovu. Mutashika Sabato zangu na kuheshimu Pahali pangu Patakatifu. Mimi ni Yawe. Musiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi kwa kuwaomba wawaaguzie. Mukifanya hivi, mutajichafua. Mimi ni Yawe, Mungu wenu. Unapokuwa mbele ya muzee unapaswa kusimama kwa kumupa heshima yake, nawe umwogope Mungu wako. Mimi ni Yawe. Kama kuna mugeni katika inchi yako usimutendee vibaya. Huyo mugeni anayekaa nawe atakuwa kwako kama vile mwenyeji nawe utamupenda kama vile unavyojipenda mwenyewe, kwa sababu nawe ulikuwa mugeni katika inchi ya Misri. Mimi ni Yawe, Mungu wenu. Usikose kuamua kwa haki juu ya vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Munapaswa kutumia mizani ya kweli na vipimo vinavyokuwa vya kweli. Mimi ni Yawe, Mungu wenu, niliyewatoa katika inchi ya Misri. Munapaswa kushika na kutimiza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ni Yawe” (Mambo ya Walawi 19: 15-37).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 55

Page 59: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

“Wandugu zangu, kufuatana na vile munavyomwamini Bwana wetu Yesu Kristo mwenye utukufu, musikuwe vilevile na upendeleo na watu. Kwa mufano: tajiri mumoja anayevaa pete ya zahabu na nguo nzuri anaingia katika nyumba yenu ya kuabudia. Na kisha kunaingia vilevile masikini anayevaa nguo zinazopasukapasuka. Halafu munaonyesha heshima kwa yule anayevaa vizuri na kumwambia: Ikaa hapa kwenye nafasi nzuri. Lakini munamwambia yule masikini: We! Simama pale, au uikae hapa chini kwenye nafasi ya kuwekea miguu yangu. Jambo hilo halionyeshi kwamba munafanya ubaguzi, na kwamba kwa kuamua vile munaongozwa na mawazo mabaya? Wandugu zangu wapenzi, musikilize: Mungu amewachagua wamasikini wa dunia hii kusudi wakuwe watajiri katika imani, nao wapokee Ufalme ule aliowaahidi wale wanaomupenda. Lakini ninyi munawazarau wamasikini! Watajiri si ndio wale wanaowagandamiza ninyi na kuwashitaki kwenye tribinali? Vilevile si wao ndio wanaotukana jina lile nzuri mulilopewa? Munafanya vizuri kama mukitimiza sheria hii ya kifalme inayopatikana katika Maandiko Matakatifu: Umupende mwenzako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Lakini kama mukifanya upendeleo, munafanya zambi, nanyi munahukumiwa na Sheria kwa sababu mumeivunja” (Yakobo 2: 1-9).

Watu hao waliwakandamiza masikini na badala yake kuwapa mali matajiri. Katika shughuli zetu zote za kibiashara, tusiwadanganye au kuwapunja watu. Njia inayoweza kuleta amani na Injili katika nchi, ni watu kuwa wakweli na kufanya kazi zao kwa uaminifu. Waumini hupelekea Yesu mawazo yao ya kindaniMoja wapo wa mafundisho muhimu ya Biblia ni ule ushauri unaotolewa na Maandiko hayo kwamba tunastahili kuhakikisha kwamba mawazo yetu yanamtii Bwana Yesu. Maisha yetu katika kufuata Yesu hayategemei matendo ya nje tu, bali pia mawazo yetu ya ndani. Mawazo yanaweza kutupotosha njia. Tukisoma vitabu vyenye ujumbe ulio kinyume na mapenzi ya Mungu au kujaza akili zetu kwa propaganda mbaya, nia zetu zinaweza kutiwa utumwani na vitu hivyo. Mawazo yetu ndiyo ambayo huzaa dhambi, kwa sababu kuwafikiria wengine vibaya kunaweza kutuchochea kutenda dhambi ya kihisia. Kutosamehe, usaliti na hila huanza katika mawazo yetu kwanza kabla hatujatenda. Mambo haya yote sharti yapelekwe kwa Yesu, ambaye atatutakasa mioyo yetu pamoja na nia zetu. Pia tuna jukumu la kusafisha mawazo yetu sisi wenyewe kwa kumtii Kristo. Biblia katika 1 Petro 1:22-23 inasema, “Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote. Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.”

Waumini ni chumvi ya duniaKatika picha ya somo hili utaona Wakristo wakimwaga chumvi njiani. Yesu alisema kwamba sisi ni chumvi ya dunia. Chumvi ni kiungo kinachoweza kuhifadhi kitu kisiharibike, kuongeza ladha, na kusafishia mejeraha au vidonda. Kwa hiyo Yesu aliposema sisi ni chumvi, alikuwa na maana kwamba tunastahili kuhifadhi mafundisho aliyotupa katika Biblia. Tunastahili pia kuongeza ladha katika tamaduni zetu na katika uliwemwengu wetu kwa jumla kwa kuzifuata sheria za Mungu. Vilevile tunastahili kusafisha mioyo yetu na kuponya kila aina ya majeraha ya kihisia na ya kiroho.

Waumini hujifunza kwamba Neno la Mungu ni taa ya kutuongoza na mwanga katika njia zetuKatika Zaburi 119:105, tunajifunza kwamba Neno la Mungu ni taa ya kutuongoza na mwanga katika njia zetu. Tukiishi kwa kuufuata ukweli wa Neno la Mungu, basi tutakuwa na umoja sisi kwa sisi (1 Yohana 1:7). Kwa hiyo uruhusu mwanga wa Mungu kuangaza njia zako kwa kulitumia Neno la Mungu kama mwongozo wako.

Mafundisho Ya Somo La 6

Waamini Njia za KupotoshaWaamini Hupima Kila Kitu Katika Mizani ya Neno La Mungu Njia za Kushawishi na Kuleta Mazoea MabayaWaamini Hujenga Nyumba/Maisha Yao Juu ya Neno La Mungu Njia za Fujo na ChukiWaamini Huzipima Mila na Desturi Zao Katika Mizani ya Neno la Mungu Njia za Uvivu na KutowajibikaWaamini Huupima Unabii, Maono, na Mafundisho Yao na Ya Wengine, Katika Mizani ya Neno La Mungu

Njia za Kupotoka Kimaadili

Waamini Huendelea Kuzifuata Njia Nyembama -Waamini Huyapeleka Mawazo Yao Ya Ndani, Kwa Yesu -Waamini Sharti Wawe Kama Chumvi, Wakihifadhi, Wakitia Ladha, na Kutakasa.

-

Waamini Hutumia Neno La Mungu Kama Taa Ya Kuangaza Njia Zao. -

Copyright © 2007 Tammie Friberg 56

Page 60: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Marejeo Ya Mafundisho Ya Somo La 6

Jukumu La Mwamini Katika Kukaa Katika Njia IfaayoMaandiko: “Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na mafuta. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.” (Waebrania 4:12).“Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa, kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali. Tangu manabii hadi makuhani, kila mmoja wao ni mdanganyifu. "Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu, wanasema; ‘Amani, amani’, kumbe hakuna amani yoyote! “Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo? Labb! Hawakuonaaibu hata kidogo. Hawakujua hata namna ya kuona aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao; wakati nitakapowaadhibu, wataangamizwa kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Simameni katika njia panda, mtazame. Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani. Tafuteni mahali ilipo njia nzuri mwifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu. Lakini wakasema: ‘Hatutafuata njia hiyo.’ Kisha nikawawekea walinzi, nikawaambia: ‘Sikizeni ishara ya tarumbeta.’ Lakini wao wakasema ‘Hatutasikiliza’ (Yeremia 6:13-17).“Mkienda kulia au kushoto, mtasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Njia ni hii; ifuateni.” Mtavifanya haramu vinyago vyenu vya miungu vilivyopakwa fedha na sanamu zenu zilizopakwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitu najisi, mkisema, “Poteleeni mbali!” Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi. Mafahali na punda wenu wa kulimia watapata malisho yaliyochambuliwa vizuri na kutiwa chumvi. Wakati utakapofika ambapo maadui watauawa na ngome zao kubomolewa, vijito vya maji vitatiririka kutoka kila mlima na kilima. Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake” (Isaya 30:21-26).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Zinazoambatana na SomoWaamini Hupima Kila Kitu Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Paulo na Sila Wazuru Berea- Matendo 17:10-14.*Filipo anamshuhudia Nathanaeli- John 1:45-51.*Yesu Anazungumzia Juu Yake kama Ilivyo Katika Torati na Manabii- Luka 24:44-53.*Paulo Anaupima Utiifu wa Waamini Katika Mambo Yote- 2 Wakorintho 2.

Waamini Hupima Kila Kitu Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Kuyathamini Maagizo ya Mungu- Mithali 2:1.*Nyumba hujengwa kwa Hekima, na kuimarishwa kwa Busara; Kwa maarifa Vyumba Vyake Hujazwa Vitu Vya thamani na vya kupendeza- Mithali 24:3-4.*Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tendeni mambo ya haki na uadilifu. Mwokoeni mikononi mwa mdhalimu mtu yeyote aliyenyang'anywa mali zake. Msiwatendee vibaya au ukatili wageni, yatima na wajane wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa - Yeremia 22:3.*Jichunguzeni nyinyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani- 2 Wakorintho 13:5.*Kumwomba Mungu aijaribu akili na moyo-Zaburi 26:2.

Waamini Hujenga Maisha Yao juu ya Neno La Mungu*Fumbo La Tajiri Na Lazaro- Luka 16:13-31.*Fumbo La Nyumba Iliyojengwa Juu Ya Mwamba- Mathayo 7:24-29.

Waamini Hujenga Maisha Yao Juu Ya Neno La Mungu*Waamini Wanaipokea Biblia Kama Neno La Mungu - 1 Wathesalonike 2:13.*Pokea Neno Lililopandwa Ndani Yako, Linafanya Kazi Nafsini Mwenu-Yakobo 1:21.*Tamanini Maziwa Halisi Ya Neno, Kueni Katika Wokovu Wenu- 1 Petro 2:2.*bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, - Zaburi 1:2-3.*Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako-Zaburi 119:148.

Waamini Hupima Mila na Desturi Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Nadabu na Abihu Wanamtolea Bwana Sadaka Ya Moto Bandia- Mambo Ya Walawi 10.*Paulo Anajadili Swala La Kula Nyama Iliyotolewa Dhabihu Kwa Miungu- I Wakorintho 8-10.*Kipimo Cha Nabii Wa Kweli- KumbuKumbu 13.

Waamini Hupima Mila na Desturi Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe. Lakini mwenye kuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu - Yohana 3:20-21.*Yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni wao vivyo hivyo. Hii ndiyo maana ya sheria ya Mose na mafundisho ya manabii- Mathayo 7:12.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 57

Page 61: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Zinazoambatana na Somo*Pepo Hufundisha Mafundisho Ya Uongo- 1 Timotheo 4:1-8.*Usiongeze Maagizo Ya Mungu au Kuyapunguza- Kumbukumbu 12:32.*Tusiige Mitindo Ya Watu wa Mataifa, Mungu Ametukataza Kufanya Hivyo- Kumbukumbu 18:9-15.

Waamini Hupima Unabii, Maono Na Mafundisho Yao na Ya Wengine Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Isaya Anatabiri Gadhabu Ya Mungu Kwa Israeli- Isaya 34.*Yesu Aongea Na Wayahudi- Yohana 5:18-47.*Manabii Walitutumikia Sisi Kwa Kutoa Unabii Juu Ya Yesu 1Petro 1:10-25.*Yesu Anafundisha Juu Ya Manabii Wa Uongo- Mathayo 7:15-23.*Paulo Anazunngumzia Juu Ya Wana Filosofia Wa Athene Waitwao Epikuro Na Stoiki – Matendo 17:15-34.*Yesu Anatufundisha Tusiache Sheria Za Mungu Kwa Kufuata Mapokeo Ya Wanadamu - Mathayo 15:1-9; Mariko 7:3-13.*Yeremia Anazungumzia Mahubiri Potofu- Yeremia 6:13-17. *Yeremia Anazungumzia Waotaji Wa Uongo- Yeremia 23:25-40; 27:9; 29:8.*Zekaria Anapinga Manabii Wa Uongo- Zekaria 10:2*Ezekieli Anapinga Manabii Wa Uongo Wanaofuata Na Kuzungumza Yaliyo Moyoni Mwao tu, Kuliko Kutoka Kwa Mungu - Ezekieli 13. *Yeremia Anampinga Shemaya Wa Nehelamu Kwa Kutoa Unabii Wa Uongo - Yeremia 29:24-32.*Yesu Anatufundisha Kwamba Manabii Wa Uongo Watakuja Katika Ngozi Ya Kondoo, Lakini Ni Mbwa Mwitu. Tutawatambua Kwa Matunda Yao- Mathayo 7:15-20.

Waamini Hupima Unabii, Maono Na Mafundisho Yao na Ya Wengine Katika Mizani Ya Neno La Mungu*Unabii Wa Maandiko Hautegemei Ufasiri Wa Mtu Binafsi - 2 Petro 1:19-21.*Angalieni, basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu na ya pepo watawala, na wala si Kristo mwenyewe! Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu- Wakolosai 2:8-9.* Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Msikubali kudanganywa na manabii wenu na waaguzi waliomo miongoni mwenu, wala msisikilize ndoto wanazoota. Maana wanawatabiria uongo kwa kutumia jina langu. Mimi sikuwatuma. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema - Yeremia 29:8-9.*Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao, maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu. Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya furaha yangu. Nawatakeni mwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya. Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi- Warumi 16:17-20.* Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu- Waebrania 13:9.

Waamini Wanaendelea Kuifuata Njia Nyembamba*Yesu Anafundisha Juu Ya Njia Nyembamba - Luka 13:2-30; Mathayo 7:13-14.*Sheria Inatolewa- Kumbukumbu 5.*Njia Ya Wenye Haki Dhidi Ya Njia Ya Watenda Maovu- Zaburi 1.*Baraka Na Laana- Kumbukumbu 11:26-28; 30:15-20; Yeremia 21:8.

Waamini Wanaendelea Kuifuata Njia Nyembamba*Lakini nyinyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, mwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara. Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo- 2 Petro 3:17-18.*Njia ya wanyofu huepukana na uovu; anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake- Mithali 16:17.*Mungu Hutuongeza Katika Njia Za Haki- Zaburi 23:3.*Mungu Anatupa Ushauri Kuhusu Njia Tunayostahili Kuifuata - Zaburi 50:23.*Njia Ya Uzima Hutuelekeza Juu- Mithali 15:24.*Heri Watu Wanaoishi Bila Kosa- Zaburi 119:1.*Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili- Mithali 4:26.*Tembea Kwa Unyenyekevu na Mungu- Mika 6:8.*Usizifuate Njia Za Mataifa- Yeremia 10:2.*Njia Ya Wokovu- Isaya 40:3.*Yesu Alisema Mimi Ndimi Njia Kweli Na Uzima- Yohana 14:6. *Ishi Katika Ukweli Wa Mungu- Zaburi 86:11; 2 Yohana 4; 3 Yohana 3-4.*Ishi Kama Yesu Alivyoishi- 1 Yohana 2:6.*Ishi Katika Upya Wa Maisha- Warumi 6:4.

Waamini Huyapeleka Mawazo Yao Ya Ndani Kwa Yesu*Ndoto Ya Nebukadneza- Danieli 4.*Kuokolewa Kwa Sauli- Matendo 9; Wafilipi 3:4-9.*Ahadi Kwa Nuhu, Moyo Wa Mwanadamu Ni Mwovu Tangu

Waamini Huyapeleka Mawazo Yao Ya Ndani Kwa Yesu*Waamini Hutiisha Mawazo Yote Kwa Kristo- 2 Wakorintho 10:5.*Kufuata Mambo Yasiyo na Maana Hututenganisha na Mungu-Warumi 1:21.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 58

Page 62: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Zinazoambatana na SomoKuzaliwa Kwake- Mwanzo 8:21. *Mungu Aliyachagua Mambo Yale Ambayo Ulimwengu Huyaona Ni

Upumbavu, Ili Awaaibishe Wenye Hekima- 1 Wakorintho 1:27; 3:19.*Kiburi chote cha watu kitakomeshwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa. Na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo. Vinyago vyote vya miungu vitatoweka kabisa- Isaya 2:17-18.*Tunaishi Katika Nuru Ya Uwepo Wa Mungu- Zaburi 89:15.*Ishi Kwa Kumcha Bwana- Nehemia 5:9.*Fuata Njia Ya Akili- Mithali 9:6.

Waamini Sharti Wawe Kama Chumvi, Wakihifadhi, Kuongeza Ladha, Na Kutakasa.*Yosia Josia Atawazwa Kuwa Mfalme- 2 Wafalme 22.*Paulo Akiwa Efeso- Matendo 20:17-38.*Paulo Aliyachunguza Maandiko Na Kuutafuta Uso Wa Bwana Kabla Hayakwenda Kufanya Huduma - Wagalatia 1-2.*Paulo Anamkemea Petro Kwa Mafundisho Yake Potofu- Wagalatia 2.*Huduma Ya Paulo Ilikuwa Kuwatia Moyo Waamini Wote- Wakolosai 1:28.*Msifuate Hadithi- Tito 1:14; 1 Timotheo 1:4; 2 Timotheo 4:4.*Paulo Anasimama Kidete Wakati Anaposongwa na Mateso- 2 Timotheo 4:16; 2 Timotheo 4:10.

Waamini Sharti Wawe Kama Chumvi, Wakihifadhi, Kuongeza Ladha, Na Kutakasa.*Endeleeni Kufuata Yale Mliyojifunza- 2 Timotheo 3:13-15.*Sisi Ni Chumvi Ya Dunia- Mathayo 5:13.*Mwe na Chumvi Ndani Yenu, Na Mwe na Amani Kati Yenu- Marko 9:50.*Utoeni Uovu Kati Yenu- Kumbukumbu 19:18-19; 22:21-24; 24:7.*Nyinyi wenyewe mmejaa wema, Ufahamu Na Mnaweza Kutiana Moyo - Warumi 15:14.*Ukweli Na Wema Wa Mungu Utaendelea Kutuhifadhi Siku Zote- Zaburi 40:11; 61:7.*Tendeni Haki na Mwe Wataua- Isaya 56:1.* Ni wajibu wa makuhani kuwafundisha watu maarifa ya kweli juu ya Mungu - Malaki 2:7.* Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu - Waefeso 4:3.* Faida ya maarifa ni kwamba hekima hulinda maisha ya mtu aliye nayo- Mhubiri 7:12.*Usimwache Yesu- Wagalatia 1:6-10.*Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima, lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara- Mithali 13:20.*Maneno Yetu Yakolee Chumvi- Wakolosai 4:6.

Waamini Hutumia Neno La Mungu Kama Nuru Ya Kuangaza Njia Zao*Nuhu Alitenda Yote Aliyoagizwa na Mungu- Mwanzo 6:22.*Maneno Ya Mungu Kwa Yoshua- Yoshua 1.*Naamani Anatii Maagizo Ya Mungu- 2 Wafalme 5:14.*Yesu Anajaribiwa na Shetani Nyikani- Mathayo 4.*Biblia Ikijulikana Kama Sheria- Zaburi 1:2.*Mitume Walimtii Mungu Badala Ya Wanadamu- Matendo 5:28-29.*Watu Wanapewa Changamoto Kubadilisha Mwenendo Wao na Kufuata Neno Na Njia Za Mungu- Isaya 1:15-17.

Waamini Hutumia Neno La Mungu Kama Nuru Ya Kuangaza Njia Zao*Neno La Mungu Laangaza Njia Zetu Na Miguu Yetu- Zaburi 119:105; 2 Petro 1:19.*Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili- 2 Timotheo 3:16-17.*Mbona mwaniita “Bwana, Bwana,” na huku hamtimizi yale ninayosema? - Luka 6:46-47.*Biblia Ndio Mwongozo Wetu, Tunapotafakari Mafundisho Yake- Zaburi 1:2.*Maandiko Ndio Mwongozo Wetu Wa Wokovu- 1 Timotheo 3:15.*Tunastahili Kuyatii Maandiko- Luka 11:28; 2 Mambo Ya Nyakati 34:21; Zaburi 119:67; Yohana 14:23.*Biblia Ndio Mwongozo Wetu Tunapolisikia Na Kulipokea- Yeremia 31:10; Efeso 1:13; 1 Wathesalonike 2:13.*Tunastahili Kukaa Katika Neno La Mungu- Efeso 3:17.*Neno Linakaa Ndani Yetu- Yohana 5:38; 1 Yohana 2:14; Yakobo 1:21.*Tunastahili Kuenenda Katika Nuru Na sio Katika Giza- Yohana 8:12; 11:9; 1 Yohana 1:7, 16; 2 Yohana 11.

Njia Za DhambiMaandiko: “Makuhani wao wanavunja sheria zangu, na kukufuru vyombo vyangu vitakatifu. Hawapambanui kati ya vitu vitakatifu na vitu visivyo vitakatifu, wala hawafundishi watu tofauti kati ya mambo yaliyo najisi na yaliyo safi. Wameacha kuzishika sabato zangu, na kunifanya nidharauliwe kati yao. Viongozi wake waliomo mjini ni kama mbwamwitu wararuao mawindo yao; wanaua ili kujitajirisha visivyo halali. Manabii wake wanaficha maovu hayo kama mtu anapotia chokaa kwenye

Copyright © 2007 Tammie Friberg 59

Page 63: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ukuta mbovu. Wanaona maono ya uongo na kutabiri udanganyifu mtupu, wakisema, ‘Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi,’ wakati mimi mwenyewe sijawaambia chochote. Kila mahali nchini ni dhuluma na unyanganyi. Wanawadhulumu maskini na wanyonge, na kuwaonea wageni bila kujali. Nilitafuta miongoni mwao mtu mmoja atengeneze ukuta na kusimama juu ya mahali palipobomoka mbele yangu, ili ailinde nchi na kunizuia nisiiharibu, lakini sikumpata hata mmoja. 31 Kwa hiyo nimewamwagia ghadhabu yangu na kwa moto wa hasira yangu nimewateketeza kulingana na matendo yao. Ndivyo nisemavyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu” (Ezekieli 22:26-31).“Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao, maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu. Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya furaha yangu. Nawatakieni mwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya. Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi” (Warumi 16:17-20).

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana Na SomoNjia Za Ushawishi Na Mazoea Mabaya*Jinsi Ya Kuepuka Njia Ya Uzinzi- Mithali 1-2.*Kushawishiwa Kisiri Kuifuata Miungu Ya Uongo- Kumbukumbu 13.*Binti Za Lutu Wapata Mimba- Mwanzo 19:36.*Samsoni Atoa Kitendawili- Waamuzi 14.*Samsoni Na Delila- Waamuzi 16.*Roho Idanganyayo Yamshawishi Ahabu- 1 Wafalme 22:20-38; 2 Mamba Ya Nyakati 18:18-34.*Nadhiri Ya Mnaziri- Hesabu 6.*Samsoni- Waamuzi 13.*Manabii Wa Uongo Nyakati Za Petro- 2 Petro 2.*Kujamiiana Kwa Maharimu- 2 Samueli 13:12-13; 1 Wakorintho 5:1; Mwanzo 19:36.*(Tazama Mafundisho Ya Biblia Juu Ya Uzinzi Katika Somo La 4).

Njia Za Ushawishi Na Mazoea Mabaya* Ole wao mabingwa wa kunywa divai, hodari sana wa kuchanganya vileo- Isaya 5:22.* Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya. Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo- Yakobo 1:14-15.*Askofu Asiwe Mlevi- 1 Timotheo 3:3, 8; Tito 1:7.* Mnapoingia ndani ya hema la mkutano, wewe na wanao msinywe divai wala kileo chochote, la sivyo mtakufa– Mambo Ya Walawi 10:9.*Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; yeyote anayevutiwa navyo hana hekima- Mithali 20:1.* Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema wapate kukimbilia kunywa kileo; wanaokesha hata usiku, mpaka divai iwaleweshe! Katika karamu zao, hapakosekani vinubi, zeze, matari, filimbi na divai. Lakini hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu, wala kuzitambua kazi za mikono yake- Isaya 5:11-12.* Makuhani na manabii wamelewa mvinyo, wamevurugika kwa divai. Wanayumbayumba kwa pombe kali; maono yao yamepotoka, wanakosea katika kutoa hukumu- Isaya 28:7.* Tangu sasa, basi, maisha yaliyowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, sio na tamaa za kibinadamu. Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi, kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu. Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo wanawatukaneni. Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa! - 1 Petro 4:2-5.*Ishini Kwa Kuwa na Kiasi- Warumi 13:13.

Njia Za Vita Na Chuki*Nuhu Na Gharika- Mwanzo 6-9.*Fumbo La Mwana Kondoo Wa Kike- 2 Samueli 12.*Vita Katika Nchi- Hosea 4.*Sauli Alikuwa Adui Wa Kudumu Wa Daudi; Lakini Daudi Hakumwua Sauli - 1 Samueli 18:28-29; 1 Samueli 24; 26.*Paulo Anaacha Maisha Ya Fujo Na Badala Yake Aanza Kumtumikia Mungu- 1 Timotheo 1; Matendo 9:1-2.*Vita Vya Kizazi Hadi Kizazi- Mathayo 23:31-33.*Fujo Dhidi Ya Watu Wanaomwanini Mungu- Waebrania 11.*Mambo Anayochukia Mungu- Mithali 6:16-19.*Esau Anamchukia Ndugu Yake Kwa Kumwibia Haki Yake Ya Mzaliwa Wa Kwanza; Lakini Baadaye Wanapatana- Mwanzo 27, 33.*Hamani Amchukia Modekai- Esta 3:5-6.

Njia Za Vita Na Chuki*Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu- 2 Timotheo 2:19.* Mwenyezi-Mungu huwapima waadilifu na waovu; huwachukia kabisa watu wakatili-Zaburi 11:5*Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Anayekonyeza jicho kwa hila amepanga maovu; anayekaza midomo amekwisha nuia mabaya- Mithali 16:29-30.*Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali, maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki- Mithali 21:7.*Uhalifu wa Sheria Kwa Nguvu- Sefania 3:4.*Kuhusu matendo watendayo watu; mimi nimeitii amri yako, nimeepa njia ya wadhalimu. Nimefuata daima njia yako; wala sijateleza kamwe- Zaburi 17:4-5.*Dhuluma- Mika 3:10.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 60

Page 64: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo*Ahabu Anamchukia Nabii Anayetabiri Mabaya Dhidi Yake- 1 Wafalme 22:8.*Herodia Anaghadhabishwa Na Yohana- Marko 6:18-19.

*Wananilipa uovu kwa wema wangu, na chuki kwa mapendo yangu- Zaburi 109:5.*Mtu Amchukiaye Ndugu Yake Hawezi Kumpenda Mungu- 1 Yohana 2:9; 4:20.*Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanawe; watoto nao watawashambulia wazazi wao na kuwaua - Marko 13:12.*Watenda Maovu Huichukia Nuru- Yohana 3:20-21.*Ulimwengu Utawachukia Wakristo- Yohana 15:18-19.*Maangamizi Yanawasubiri Maadui Wa Msalaba- Wafilipi 3:18-19.*Adui yetu akiwa na njaa, tumpe chakula, Akiwa Na Kiu Tumpe Maji Ya Kunywa- Mithali 25:21-22.*Wapende Adui Zako, Watendee Mema, Na Uwabariki- Mathayo 5:43-44.*Usichague Njia Za Fujo- Mithali 3:31.

Njia Za Uvivu Na Kutowajibika*Mafunzo Kutoka Kwa Sisimizi- Mithali 6:6-11.*Muokaji Mikate Anasahau Kumsaidia Yusufu- Mwanzo 40:23.*Paulo Anawashauri Wathesalonike Juu Ya Uvivu- 2 Wathesalonike 3:10-13.*Fumbo La Mtu Mwenye Busara Na Mpumbavu- Mathayo 7:26-27.*Fumbo La Talanta- Mathayo 25:14-30.Fumbo La Wanawali Kumi- Mathayo 25:1-12.*Kupuuzwa Kwa Nyumba Ya Mungu- Hagai 1:2-6.*Kupuuzwa Kwa Habari Njema- Mathayo 22:4-5.*Kupuuzwa Kwa Njia Za Mungu- Mathayo 23:23-24.*Kupuuzwa Kwa Maskini- Mathayo 25:44-46.*Kupuuzwa Kwa Matayarisho Ya Kurudi Kwa Bwana Yesu- Mathayo 22:12-13.*Kutokuwa Shahidi Wa Kweli- Mambo Ya Walawi 5:1.*Hesabu Gharama Za Ujenzi Ndio Ujenge- Luka 14:28-30.*Paulo Anawashauri Warumi Kufanya Kazi Ya Mungu Kwa Bidii- Warumi 12:4-21.*Fumbo La Msamaria Mwema- Luka 10.*(Tazama Somo La 11 Juu Ya Uwakili).

Njia Za Uvivu Na Kutowajibika*Uzembe ni kama usingizi mzito; mtu mvivu atateseka kwa njaa- Mithali 19:15.*Uvivu husababisha umaskini, lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha. Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno, kulala wakati wa kuvuna ni aibu- Mithali 10:4-5.*Njia ya mvivu imesambaa miiba, njia ya mwaminifu ni wazi kama barabara kuu - Mithali 15:19.*Mtu mvivu kazini mwake ni ndugu yake mharibifu- Mithali 18:9.*Mvivu hufa kwa kutokutimizwa tamaa zake, maana mikono yake milegevu haitaki kufanya kazi. Mchana kutwa mwovu hutamani kupata kitu, lakini mwadilifu hutoa, tena kwa ukarimu - Mithali 21:25-26.*Mungu Hatasahau Kazi Tuliyomfanyia- Waebrania 6:10-20.*Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo- Mithali 3:27-28.

Njia Ya Ufisadi Wa Kimaadili*Joka Ladanganya- Mwanzo 3.*Mungu Anauona Uovu Wa Wanadamu- Mwanzo 65-6.*Yakobo Amdanganya Ndugu Yake- Mwanzo 27.*Maelezo Ya Njia Ya Ufisadi- Mithali 1:13-15.*Vipimo Na Mizani Ya Haki- Ezekieli 45.*Nabii Mwongo- 1 Wafalme 13:11-18.*Uasi Wa Sauli- 1 Samueli 15.*Ufisadi Katika Haki- Habakuki 1.*Akani Aiba Vitu- Yoshua 7.*Ufisadi Wa Waandishi Na Mafarisayo- Mathayo 23:23; Luka 11:44.*Askari Wanahongwa- Mathayo 28:12-13.*Usaliti Wa Yuda- Mathayo 26.*Anania Na Safira- Matendo 5.*Kanisa La Laodikea- Ufunuo 3:17-18.*Mafarisayo Wanajaribu Kumtega Yesu- Mathayo 22:15-17.*Wabadilishaji Pesa Katika Hekalu- Yohana 2:14-16.

Njia Ya Ufisadi Wa Kimaadili*Tulikuwa Tukiishi Katika Njia Za Dhambi Kwa Kumfuata Shetani, Sasa Tunaishi Kwa Kutenda Matendo Mema Kwa Sababu Ya Yesu - Waefeso 2:1-10.*Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu. Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu. Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu. Kwa hiyo, acheni uongo. KILA MMOJA ANAPASWA KUMWAMBIA MWENZAKE UKWELI, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo- Waefeso 4:22-25.*Ole wao wanaosema uovu ni wema na wema ni uovu. Giza wanasema ni mwanga na mwanga wanasema ni giza. Kichungu wanasema ni kitamu na kitamu wanakiona kuwa kichungu. Kwa hongo kidogo wanawaachilia wenye hatia na kuwanyima wasio na hatia haki yao- Isaya 5:20, 23.*Moyoni Ndimo Mwenye Uovu- Mathayo 15:19-20.*Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu, lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani - Mithali 20:17.*Ole wao wanaosema uovu ni wema na wema ni uovu- Isaya 5:20.*Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha

Copyright © 2007 Tammie Friberg 61

Page 65: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Hadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somomafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao - Warumi 16:17-20.* Watu waovu na wadanganyifu wataendelea kuwa wabaya, wakidanganya wengine, na wao wenyewe wakidanganywa. Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa ukaukubali kabisa. Wawajua wale waliokuwa waalimu wako- 2 Timotheo 3:13-14.

Njia Za Dini Za Uongo/Mila Na Desturi*Aroni Anatengeneza Ndama Wa Dhahabu- Kutoka 32.*Itupilieni Mbali Miungu Ya Kigeni- Yoshua 24.*Amazia- 2 Mambo Ya Nyakati 25.*Yeroboamu Atengeneza Ndama Wawili wa Dhahabu- 1 Wafalme 12:28-29.*Manase Anaweka Sanamu Katika Hekalu La Mungu- 1 Wafalme 21.*Wake Wa Sulemani Wampotosha- 1 Wafalme 11:1-8.*Paulo Azungumzia Swala La Kula Nyama Iliyotolewa kama Dhabihu Kwa Miungu - 1 Wakorintho 8-10.*Waamini Efeso Wanayapima Maneno Ya Manabii- Ufunuo. 2:1-7.

Njia Za Dini Za Uongo/Mila Na Desturi *Mimi huzivuruga ishara za watabiri waongo na kuwapumbaza waaguzi. Mimi huyakanusha maneno ya wenye hekima na kufanya ujuzi wao kuwa upumbavu. Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni- Isaya 44:24-28.*Katika Siku Za Mwisho Watu Watasikiza Mafundisho Ya Pepo - 1 Timotheo 4:1-2.*Kimbieni Uabudu Sanamu- 1 Wakorintho 10:14.*Bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni - 1 Yohana 4:1.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 62

Page 66: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 63

Page 67: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 7: Falme Mbili

Maandiko: "WATU WALIOKAA GIZANI WAMEONA MWANGA MKUBWA, NAO WALIOSHI KATIKA NCHI YA GIZA NA KIVULI CHA KIFO, MWANGA UMEWAANGAZIA" (Mathayo 4:16).“Utayafumbua macho yao na kwuawezesha watoke gizani na kuingia katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukie Mungu; ili kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu” (Matendo 26:18).

Maelezo MafupiMfano wa 7 unaoneysha bara la Afrika likiwa na falme mbili zinazofanya kazi katika bara hilo. Falme hizi mbili si za kibinadamu. Badala yake ni falme za kiroho ambazo Biblia huziita Ufalme wa Giza na Ufalme wa Nuru. Falme hizi zinafanya kazi katika kila pembe ya dunia hii, sio tu katika bara la Afrika. Hata ijapokuwa watu hawatambui ni wafuasi wa ufalme gani, bado ni wafuasi wa falme hizi mbili. Katika picha ya somo hili utaona kwamba Shetani ndiye mungu wa dunia hii. Katika Biblia, ufalme wa Shetani huitwa Ufalme wa Giza. Ufalme ule mwingine unawakilisha Ufalme wa Mungu. Mungu anaonekana akiwa katika Kiti chake Enzi. Ufalme wake si wa dunia hii, bali unafanya kazi na kutawala katika mioyo ya Wakristo. Ufalme wa Mungu huitwa Ufalme wa Nuru. Falme hizi mbili hazina mamlaka sawa. Mungu ni mwenye nguvu zote, na anatawala kila kitu duniani na mbinguni. Lakini kwa sababu ya dhambi, na kazi ya Shetani duniani, sasa kuna falme zinazotawala duniani. Siku moja Mungu atausitisha au kuuharibu ule Ufalme wa Giza. Lakini kabla wakati huo haujafika, wale walio katika Ufalme wa Nuru jukumu lao kubwa ni kufanya kazi kuupanua Ufalme wa Mungu katika maisha ya watu. Ikiangalia picha ya ulimwengu hapa, utaona kwamba mioyo mingine ya watu duniani imejaa giza na mingine ni misafi. Macho mengine yamefumbwa na macho mengine yanaweza kuona. Hata ingawa watu wengine wameonyeshwa kuwa vipofu kimwili, ukweli ni kwamba wamegubikwa na upofu wa kiroho. Aina hizi mbili za watu ni wanachama wa falme mbili tofauti. Utakuta kwamba ijapokuwa watu hawa ni wanachama wa falme tofauti, bado wanaishi pamoja katika ulimwengu mmoja.

Tatizo ya wale walioko katika ufalme wa gizaKwanza kabisa natuzungumzie juu ya Ufalme wa Giza. Sote tumezaliwa katika ufalme huu wa giza. Shetani ndiye mungu wa ufalme huu(1 Yohana 5:19; 2 Wakorintho 4:4). Watu walio katika ufalme huu wameonyeshwa hapa kama watu walio na mioyo iliyojaa giza na macho yaliyofumbwa. Mioyo iliyojaa giza inawakilisha doa litokanalo na dhambi tunapokosa kutenda mambo yaliyo sawa katika uhusiano wetu na watu pamoja na Mungu. Zile Amri Kumi tulizojifunza hapo awali zinatusaidia kuelewa ni kitu gani kinachotia mioyo yetu doa wakati tunapokosa kuzitii Amri hizo. Macho yaliyopofushwa yako katika hali hiyo kwa sababu Shetani huyafumba macho ya wasioamini ili wasimwone Mungu na wokovu wake.

Watu hawa pasipo kujua au kwa kujua wamefanywa kuwa watumwa wa kumtumikia mfalme asiyefaa. Vilevile watu waishio katika ufalme huu hufikiria kwamba kwa kutenda mema wanaweza kuelekea mahali pazuri watakapokufa. Lakini Biblia inasema kwamba mshara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Mauti hii ni ya kimwili na kiroho.

Baadhi ya watu walio katika ufalme huu wamejikuta katika hali ya uadui kati yao na wanadamu wenzao na pia kati yao na Mungu. Ufalme huu pia wakati mwingine huwa na sifa za uadui kati ya makabila ya watu, kati ya watu wa rangi mbalimbali au hata kati ya watu wenye hadhi tofauti kiuchumi. Uchungu ule unaosababishwa na dhambi wanazotenda na dhambi watendewazo, huwavuta na kuwafanya kupigana vita isiyoisha. Vita hii huchochewa na hamu ya kulipiza kisasi na ya kuwakandamiza wengine. Maisha yao yanatawalwa na tamaa za mwili, anasa, na kiburi cha uzima. Ukiangalia chini ya ukurasa utaona mahali penye moto uwakao. Wale ambao bado wanaishi katika Ufalme wa Giza, watakapokufa watatupwa katika ziwa la moto liitwalo jehenamu. Lakini kwanza watasimama mbele ya Kiti Cha Enzi cha Mungu na kuhukumiwa. Baada ya kuhukumiwa watatupwa katika Ziwa la Moto.

Baraka za wale waliomo katika Ufalme wa Nuru

Copyright © 2007 Tammie Friberg 64

Page 68: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Ufalme wa Pili ni ule Ufalme wa Nuru. Watu walio katika ufalme huu wamehamishwa kutoka katika Ufalme wa Giza hadi katika Ufalme wa Nuru kupitia kwa uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Kuwa na sehemu katika jamii ya Mungu kuna maana ya kuzaliwa mara ya pili, yaani kuzaliwa kiroho. Uzazi huu wa kiroho, haufanyiki baada ya mtu kufa, lakini kabla hatujafa. Uzazi huu ni wa hiari (Kwa mengi zaidi tazama Somo La 8). Ufalme huu wa Nuru unawakilishwa na watu wenye mioyo safi. Yesu amewasafisha mioyo yao kutokana na hatia iletwayo na dhambi. Watu wote walio katika Ufalme wa Nuru ni sehemu ya jamii kubwa ya waamini dunia nzima. Katika ufalme huu hakuna ukabila, ubaguzi wa rangi, na chuki ya kikabila, kwa sababu wote wamejiunga na jamii moja ya Mungu. Wote walio katika jamii ya Mungu lengo lao kubwa ni kuwapatanisha watu wote kwa Mungu na hatimaye kuleta amani katika dunia nzima kupitia kwa Yesu Kristo. Watu walio katika Ufalme wa Nuru hawajagawanyika katika makundi kama ilivyo kwa wale walio katika Ufalme wa Giza. Wale walio katika Ufalme wa Nuru wakati wote wanahudumiana na pia kuwafikia wale wa Ufalme wa Giza ili ikiwezekana wawalete katika Ufalme wa Mungu. Hata ijapokuwa Wakristo wanatoka katika makabila na mataifa tofauti, wote wana baba mmoja, ambaye ni Ibrahimu.

Ili tuweze kuelewa habari za kimsingi za ufalme huu ujao, tunahitaji kurejea hadithi ya Ibrahimu katika Agano la Kale. Mungu alimwahidi Abramu ahadi ambayo msingi wake ulikuwa imani. Alimwahidi kwamba angepata mtoto wa kiume na pia angemfanya kuwa baba wa ukoo mkubwa. Mungu alimwahidi kwamba kizazi chake kingekuwa cha watu wengi kushinda nyota za angani. Mungu aliahidi kubariki mataifa yote ulimwenguni kwa kupitia Ibrahimu. Uzao wa Ibrahimu ni uzao wa kiroho na umeshinda ule wa kimwili. Biblia inasema kwamba tunapomwamini Yesu tunafanyika uzao wa Ibrahimu. Basi jambo hili linatimiza ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu; ahadi iliyoonyeshwa wazi katika Agano la Kale. Kwa hiyo hata ijapokuwa tunatoka katika makabila mbalimbali, rangi tofauti na wa mbari tofauti, sote kama waamini tumeunganishwa pamoja katika jamii ya imani chini ya baba yetu Ibrahimu. Mtume Paulo anasema kwamba sisi sote ni wenyeji wa nchi moja, tukitegemea msingi mmoja, na tukiwa tumejengwa pamoja na kuwa makazi matakatifu ya Mungu (Waefeso 2:18-22).

Kwa kuelezea haya zaidi katika Waebrania 11 kuna orodha ya watu walioishi kwa imani katika Enzi za Agano la Kale. Waebrania 12 inaendelea kutufunza kwamba watu hawa wote wamekuwa kama wingu la mashahidi Mbinguni na wanatutazama kuona jinsi tunavyomwishia Yesu. Katika Maandiko haya kuna changamoto, kwamba tuondoe au kuyaweka kando mambo yanayotuzinga kwa upesi na kujaribu kututatiza tusiwe kama Yesu. Huku wingu la mashahidi likiwa linatutazama, Yesu ndiye tunayemtazama ili tumpendeze yeye (Waebrania 12:1-2).

Kwa kuwa watu hawa wamejiunga na Ufalme wa Nuru, Yesu huwapa uwezo juu ya pepo waliowakandamiza wakati walipokuwa washirika katika Ufalme wa Giza (Tazama Somo la 8, 11, na 12 kwa maelezo ya ziada). Vilevile tunajua kwamba watu hawa wakifa wataenda mbinguni kuwa na Yesu. Kuna watu wa kila aina wanaojiunga na Ufalme wa Nuru, kuna watoto, watu wazima, na waume kwa wake. Biblia hata inasema kwamba kuna familia kadhaa zilizomwamini Yesu kwa wakati mmoja. Mara kwa mara waandishi wa Agano Jipya waliwakumbusha Wakristo kuishi maisha yanayofanana na mwito wa Injili kwa kuacha kuzifuata njia zao za awali. Hatustahili kurudia dhambi tulizokuwa tukifanya kabla hatujamwamini Yesu katika Ufalme wa Giza (Tazama Somo la 11).

Kwa hiyo mioyo unayoiona katika picha hii ni misafi. Watu wa Ufalme huu wameungana pamoja kutoka katika makabila mbalimbali, rangi, na mbari tofauti. Wote hao wana baba mmoja yaani Kristo-Ibrahimu. Sasa hakuna tofauti yoyote kati ya Myahudi na mtu wa mataifa, mke na mume, mtumwa au mtu aliye huru. Wote wamekuwa kitu kimoja katika Kristo. Watu wa Ufalme wa Nuru wanaishi kwa kufuata tabia na mwenendo wa maisha wa Yesu, kwa hiyo wanaitwa “Wakristo.” Hawaishi kwa kufuata tamaa zao wenyewe au kwa kujifurahisha wenyewe, bali wanaishi wakiwa na lengo la kumpendeza Mfalme wa maisha yao-Yesu Kristo.

Mafundisho Ya Somo La 7Ufalme Wa Giza Ufalme Wa Nuru

Shetani ndiye mungu wa ufalme huu Mungu Ni Bwana Wa VyoteWatu Huzaliwa Katika Ufalme huu Watu Sharti Wazaliwe Kiroho Kupitia Kwa Yesu Ndipi Waweze Kujiunga na

Ufalme HuuMioyo Ya Watu Imechafuliwa Na Dhambi Mioyo Ya Watu Imeoshwa Dhambi Zake Kwa Kumwamini YesuWatu Wamefumbwa Macho Wasiweze Kuelewa Ukweli wa Habari Njema!

Watu Hawajapofushwa Na Shetani Tena

Watu Huishi Kwa Ukatili, Ukabila, Ubaguzi Wa Rangi, Kutegemea Watu Sasa Ni Wana Wa Ibrahimu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 65

Page 69: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Ukubwa wa Kabila Lako, na Uhasama wa Mbari n.k.Watu Bado Wamekandamizwa Na Pepo Kupitia Kwa Yesu, Watu Wana Uwezo Dhidi Ya PepoHatima Ya Watu wa Ufalme Huu ni Ziwa La Moto Hatima Ya Watu Wa Ufalme Huu Ni Kuishi Mbinguni Na Yesu

Marejeo ya Kujifunza Biblia Ya Somo La 7

Ufalme Wa GizaHadithi Zinasoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Shetani Ndiye Mungu Wa Ufalme Huu*Kujaribiwa Kwa Yesu- Mathayo 4:1-11.*Baba Wa Uongo na Mwuaji - Yohana 8:13-59.

Shetani Ndiye Mungu Wa Ufalme Huu* Shetani Ndiye Mungu Wa Ufalme Huu-2 Wakorintho 4:4.*Mtawala Wa Dunia Hii Atatupwa- Yohana 12:31.*Mtawala Wa Dunia Hii Hana Uhusiano Wowote Na Yesu- Yohana 14:30.*Mtawala Wa Dunia Hii Amehukumiwa- Yohana 16:11.

Watu Huzaliwa Katika Ufalme huu *Nikodemu Ajifunza Juu Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili- Yohana 3.*Kutimia Kwa Unabii: Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwakwa njia ya nabii Isaya: “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng’ambo yam to Yordani, Galilaya, nchi ya watu wa mataifa! Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!” Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!”- Mathayo 4:14-17.*Yohana Mbatizaji Atoa Ushahidi wa Kuthibitisha Kwamba Yesu Ndiye Nuru- Yohana 1.*Maana giza linatoweka, na mwanga wa ukweli umekwisha anza kuangaza- 1 Yohana 2:8 (kiroho); Mwanzo 1:2-3 (Kimwili); Mungu ambaye alisema, “Mwanga na uangaze kutoka gizani,” ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa- 2 Wakorintho 4:6.

Watu Huzaliwa Katika Ufalme huu *Watu Walio Katika Ufalme wa Giza, Fikira Zao Zimekuwa upuuzi mtupu, na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao. Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu- Waefeso 4:17-19.*Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu. Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo matendo yake maovu yamulikwe- Yohana 3:19-20.*Kwa maana mlikuwa giza, lakini sana ni nuru; enendeni kama watoto wa nuru – Waefeso 5:1-21.

Mioyo Ya Watu Imechafuliwa Na Dhambi *Hakuna Mwenye Haki- Warumi 3:9-31.*Yesu Awakemea Viongozi Wanafiki- Mathayo 23.

Mioyo Ya Watu Imechafuliwa Na Dhambi *Nyinyi mlikuwa mmekufa wka sababu ya makosa na dhambi zenu. Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. Na hata sisi tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kudunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu- Eph. 2:1-3.

Watu Wamefumbwa Macho Wasiweze Kuelewa Ukweli wa Habari Njema!*Mafarisayo Ni Viongozi Vipofu- Mathayo 15, 23.*Fumbo La Mpanzi- Mathayo 13; Isaya 6:10.*Paulo Akiwa Rumi- Matendo 28:11-31.*Mfarisayo ni Vipofu- Mathayo 23.*Yesu Anaponya Kipofu- Yohana 9.

Watu Wamefumbwa Macho Wasiweze Kuelewa Ukweli wa Habari Njema!*Yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu- 2 Wakorintho 4:4.

Watu Huishi Kwa Ukatili, Ukabila, Ubaguzi Wa Rangi, Kutegemea Ukubwa wa Kabila Lako, na Uhasama wa Mbari n.k.*Wamisri Wawaua Watoto Wachanga- Kutoka 1.*Mafarisayo Wampangia Yesu Njama Mbaya- Marko 3:5-6.*Miriamu Na Aroni Wamsema Vibaya Mk e Wa Musa Mkushi- Hesabu 12:1.*Yesu Azungumzia Siku Ya Hukumu Inayokaribia Na Apia Azungumzia Siku Za Mwisho- Mathayo 24; Luka 21; Marko 13.*Sifa Za Ufalme Wa Giza Ni Chuki, Hila, Wivu, Uasi- Tito

Watu Huishi Kwa Ukatili, Ukabila, Ubaguzi Wa Rangi, Kutegemea Ukubwa wa Kabila Lako, na Uhasama wa Mbari n.k.*Anayetenda Dhambi Ni Wa Ibilisi- 1 Yohana 3:8.*Katika Siku Za Mwisho, Mapigo Yatawajia Wale Wanaoabudu Pepo na Kuua - Ufunuo 9.*Wauaji Watupwa Katika Ziwa La Moto- Ufunuo 21:8.*Ukatili Dhidi Ya Mungu- Mambo Ya Walawi 26; Warumi 8:7; Wakolosai 1:21.*Ukatili Dhidi Ya Ndugu- Deut. 15:9.*Watu Wengine Ni Wakatili Na Wanaizuia Habari Njema Isihubiriwe - 1 Wathesalonike 2.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 66

Page 70: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

3:3.*Siku Inakuja Ambapo Mataifa Hayatapigana Tena- Mika 4.*Yesu Azungumza Na Mwanamke- Yohana 4.Watu Bado Wamekandamizwa Na Pepo *Ibilisi Afanya Vita Na Wafuasi Wa Yesu- Ufunuo 12.*Makazi Na Kazi ZA Shetani Hapa Duniani- Ufunuo 16, 18.*Nyakati Za Mwisho Watu Watayafuata Mafundisho Ya Mashetani - 1 Timotheo 4:1.*Mataifa Hutoa Kafara Kwa Mashetani-1 Wakorintho10:20.*Yesu Aliwatoa Pepo- Luka 11.*Watu Wanaozungumza Na Mashetani- 2 Petro 2:9-22.

Watu Bado Wamekandamizwa Na Pepo *Vita Vyetu Si Dhidi Ya Wanadamu, Bali Dhidi Ya Nguvu Za Kiroho - Waefeso 6:12.*Dunia Yote Iko Chini Ya Utawala Wa Mwovu Shetani- 1 Yohana 5:19.*Mwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama samba angurumaye akitafuta mawindo. Mwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo. Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushirki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara - 1 Petro 5:8-10.

Hatima Ya Watu wa Ufalme Huu ni Ziwa La Moto *Fumbo La Tajiri La -Luka 16:19-31.*Yesu Amponya Mtumishi Wa Jemedari Mrumi- Mathayo 8:1-13.*Fumbo La Magugu Na Ngano- Mathayo 13.*Fumbo La Karamu Ya Harusi- Mathayo 22:1-14.*Fumbo La Mtini- Mathayo 24:32-51.*Fumbo La Wanawali Kumi Na La Talanta- Mathayo 25.*Yesu Anawapa Changamoto Mafarisayo- Luka 13:17-35.

Hatima Ya Watu wa Ufalme Huu ni Ziwa La Moto *Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto - Ufunuo 20:10-15.*Kwa hiyo, basi bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu- 2 Petro 2:9.*Kila mtu hufa mara moja tu, kasha husimama mbele ya hukumu ya Mungu - Waebrania 9:27.

Ufalme Wa NuruHadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Mungu Ni Bwana Wa Vyote* (Tazama Somo La 1, Mungu Ni Mwenye Nguvu Na Muumba)

Mungu Ni Bwana Wa Vyote*Kumkiri Yesu Kama Bwana- Warumi 10:9.*Lazima Tuyaweke kando Matendo Ya Giza, Hasira, Hila, Chuki, Na Tusameheane – Waefeso 4:17-32.*Yatafuteni Mambo Yaliyo Juu Mbinguni, Uvueni Utu Wenu Wa Kale, Sameheaneni- Wakolosai 3:1-17.

Watu Sharti Wazaliwe Kiroho Kupitia Kwa Yesu Ndipi Waweze Kujiunga na Ufalme Huu *Paulo Atoa Ushahidi Wake Mbele Ya Mfalme Agripa- Matendo 26.

Watu Sharti Wazaliwe Kiroho Kupitia Kwa Yesu Ndipi Waweze Kujiunga na Ufalme Huu *Yesu alipozungumza nao tena aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai”- Yohana 8:12.*Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga.” - Yohana 12:36.*Msikubali tena kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga. Iweni watakatifu katika mambo yote, pendaneni nyinyi kwa nyinyi kwa sababu mmezaliwa mara ya pili - 1 Petro 1:14-25.*Basi akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo”- Yohana 10:7.*Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; Mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu – Zaburi 112:4.*Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu. Wakati mmoja nyinyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa hurumua ya Mungu, lakini sasa mmepokea huruma-1 Petro 2:9-10.

Mioyo Ya Watu Imeoshwa Dhambi Zake Kwa Kumwamini Yesu *Kisa Cha Zakayo Kupanda Mkuyu- Luka 19:1-10.*Yesu Aponya Mtu Aliyepooza- Mathayo 9:1-8; Luka 5:17-26.

Mioyo Ya Watu Imeoshwa Dhambi Zake Kwa Kumwamini Yesu *Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu. Lakini yeyote asiyetenda mambo ya mambo maadilifu, au asiyempenda ndugu yake , huyo si mtoto wa Mungu. Hiyo ndiyo tofauti iliyoko kati ya watoto wa Mungu na watoto wa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 67

Page 71: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Ibilisi- 1 Yohana 3:9-10.*Tumezifia Dhambi- Warumi 6:6-8.*Yesu Ametusamehe Dhambi Zetu Zote- Wakolosai 2:13-14.*Lakini tukiziungama dhambi zetu,basi, Mungu ni mwaminifu an mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zatu na kututakasa uovu wote - 1 Yohana 1:9.

Watu Hawajapofushwa Na Shetani Tena*Ushuhuda wa Paulo- Wagalatia 1:13-24.*Huduma Ya Paulo Kama Inavyohusiana na Mfalme Agripa: Kuyafumbua Macho Yao na Kuwawezesha watoke gizani na kuingia katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani wamgeukie Mungu, ili kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu- Matendo 26.*Yesu Ndiye Nuru Ya Ulimwengi- Yohana 8:1-12.

Watu Hawajapofushwa Na Shetani Tena*Jicho ni taa ya mwili. Kama basi jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa katika giza. Basi, ikiwa mwanga uliomo ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza la kutisha mno! - Mathayo 6:22-23; Luka 11:34-36.

Watu Sasa Ni Wana Wa Ibrahimu *Paulo Anafundisha Kwamba Tu Wana Wa Ibrahimu Kupitia Kwa Imani- Wagalatia 3, Warumi 4.*Ahadi Ya Mungu Kwa Ibrahimu- Mwanzo 12, 15.*Maono Ya Petro- Matendo 10:28-29.

Watu Sasa Ni Wana Wa Ibrahimu *Mungu Huwasaidia Wana Wa Ibrahimu - Waebrania 2:16.*Kuhubiriwa Kwa Yesu Ulimwengu Mzima- Matendo 1:8.*Nyinyi ni raia pamoja na watu wa, mmejengwa juu ya msingi mmoja, mmejengwa kama hekalu takatifu la Mungu- Waefeso 2:18-22.*Imani, Bwana Mmoja, Ubatizo Mmoja, Mungu mmoja Na Baba wa Vyote- Waefeso 4:4-5.

Kupitia Kwa Yesu, Watu Wana Uwezo Dhidi Ya Pepo *Mikaeli Malaika Mkuu Anakabiliana Shetani - Yuda 1:9.*Yesu Anatoa Pepo Kutoka Kwa Mtu Katika Sinagogi- Luka 4:33-44.

Kupitia Kwa Yesu, Watu Wana Uwezo Dhidi Ya Pepo *Vita Vya Kiroho- Waefeso 6:10-18.*Yesu Alikuja Kuziharibu Kazi Za Shetani- 1 Yohana 3:8.*Yesu Ameinuliwa Juu Ya Nguvu Zote- Waefeso 1:20-23.*Yesu Ametufufua Pamoja Naye Mbinguni- Waefeso 2:1-7.

Hatima Ya Watu Wa Ufalme Huu Ni Kuishi Mbinguni Na Yesu *Fumbo La Maskini Na Lazaro- Luka 16:19-31.*Imani Ya Waamini Juu Ya Maisha Yajayo, Mji, Mbinguni - Waebrania 11:8-10; 14-16.*Paulo Anazungumzia Hamu Yake Ya Kwenda Mbinguni Kuwa Na Yesu- Wafilipi 1:19-30.*Mji Mtakatifu Wa Yerusalemu- Ufunuo 21.

Hatima Ya Watu Wa Ufalme Huu Ni Kuishi Mbinguni Na Yesu *Yesu Ameenda Kutuandalia Makao Ya Kuishi Naye- Yohana 14:1-4.*Ikiwa Makazi Yetu Ya Duniani Yanaharibika, Tuna Makazi Mema Zaidi Mbinguni- 2 Wakorintho 5:1-9.*Msihuzunike Kama Watu Wa Ulimwengu Wasiomjua Mungu, Tutaishi Na Yesu Milele- 1 Wathesalonike 4:13-18.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 68

Page 72: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 69

Page 73: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 8: Kuingia Katika Ufalme wa Nuru.

Maandiko: “Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi. Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa” (Wakolosai 1:13-14)."Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu aliyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema, yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo, yeye awapaye watu waliomo pumzi, na kuwajalia uhai wote waishio humo. ‘Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki, nimekushika mkono na kukulinda. Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwanga wa mataifa. Utayafumbua macho ya vipofu, uwatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru” (Isaya 42:5-7).

Maelezo Mafupi

Yesu ndiye Njia PekeeKatika Somo La 7, tulijifunza kuwamba kuna falme mbili zisizoonekana kwa macho zinazofanya kazi duniani. Ufalme wa Giza ni ufalme wa Shetani. Sote tumezaliwa katika ufalme huu. Vilevile tulijifunza kwamba Shetani anafanya kazi duniani kwa lengo la kuharibu na kuwafanya wanadamu kuwa watumwa wake. Ufalme mwingine ni ule wa wa Nuru. Huu ndio Ufalme wa Mungu. Ili tuweze kuingia katika ufalme huu sharti tuzaliwe mara ya pili. Mtu hazaliwi kiroho wakati anapoaga dunia, bali wakati akiwa yu ngali hai! Uzazi huu hufanyika ndani yetu kupitia kwa Yesu Kristo. Tunapompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wetu, huwa tunazifia dhambi na kuishi upya katika maisha mapya ya wokovu. Biblia inasema kwamba tukimpokea Yesu, “mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.” Kwa kupitia kazi ya Yesu msalabani, tunaweza kuingia katika Ufalme wa Nuru.

Lakini kabla hatujazungumzia juu ya Yesu, lazima kwanza turudie habari za uumbaji wa Mungu ili tuweze kuelewa Yesu ni nani na kwa nini alikuja duniani. Katika mfano huu, kuna picha kadhaa zinazotukumbusha visa na mafundisho fulani kutoka katika Biblia. Mengi ya maswali tuliyo nayo kama wanadamu yanaweza kujibiwa kwa kuelewa vizuri kule tulikotoka na jinsi Mungu alivyoanza kufanya kazi hadi sasa. Aya zifuatazo zimepangwa katika taratibu fulani inayofuata jinsi mambo yalivyotukia kulengana na wakati, kuanzia Agano La Kale hadi Agano Jipya. Lengo la Maandiko hayo ni kutufundisha kwamba Yesu alikuja duniani kutimiza unabii wa Agano La Kale na kwamba yeye ndiye suluhisho la tabu za maisha yetu. Pili, ni kutufundisha kwamba kifo cha Yesu msalabani na kufufuka kwake hututengenezea njia ili tuweze kumfikia Mungu na kuwa na ushirika naye milele. Picha hizi zinatupa habari za msingi zinazoweza kutusaidia kuelewa jinsi Mungu alivyotuandalia njia ya kuingia katika Ufalme wa Nuru. Picha ya 1: Kuwa na Uhusiano wa Kibinafsi na MunguHapo mwanzo, Mungu alikuwa na uhusiano wa kibinafsi na wanadamu. Tunaweza kujua haya kwa kupitia hadithi ya kwanza katika kitabu cha Mwanzo Bibliani. Picha ya kwanza, juu kushoto inaonyesha Mungu akiwa amenyoosha mkono na kuwashikilia Adamu na Hawa. Picha hii inatukumbusha kwamba, hapo mwanzo kabisa, Mungu alikuwa na uhusiano wa kibinafsi na Adamu na Hawa. Alikuwa akizungumza na wawili hao mara kwa mara katika Bustani ya Edeni. Mungu aliwapa Adamu na Hawa sheria za kuwaongoza. Vilevile aliweza kujua wakati jambo fulani lilipokuwa kombo. Hata hivyo bado Mungu anataka kuwa na uhusiano wa kibinafsi na watu wake.

Picha ya 2: Kifo, Maradhi, Uovu, Uzindzi, na MatesoLakini uhusiano aliokuwa nao Mungu na Adamu na Hawa uliingia dosari. Dosari iliyoingia katika uhusiano huo ina uhusiano wa karibu na maswali magumu tuliyo nayo sisi kama wanadamu: Moja ya maswali hayo ni, “Kwa nini kuna kifo, maradhi, uovu, uzindzi, na mateso duniani?” Ni muhimu kufahamu kwamba mambo haya ni sehemu ya maisha ya duniani kwa sababu watu wote wamemwasi Mungu (Warumi 3:23). Uasi huu ndio ambao huitwa dhambi. Uasi huu ulianza zamani wakati Adamu na Hawa walipokiuka maagizo ya Mungu na kula tunda lililokatazwa katika Bustani ya Edeni. Katika Somo La 1 tulijifunza kwamba Mungu ni mtakatifu. Yeye hawezi kuangalia watu wakitenda dhambi pasipo kufanya kitu, na isitoshe wenye dhambi hawawezi kukaa mbele yake. Dhambi ni kule kuwa na utengano kati ya Mungu na wanadamu.

Mfano wa pili unaonyesha moyo uliojaa giza la dhambi. Kando ya moyo huo kuna kaburi. Dhambi ilichafua mioyo yetu kwa hatia ambayo hakuna mwanadamu anayeweza kuiondoa. Dhambi haikututenganisha na Mungu tu, bali pia ilikuwa chanzo cha shida nyinginezo. Athari ya kwanza ya dhambi, ni kwamba iliwafanya watu kufa kimwili na kiroho.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 70

Page 74: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Adamu na Hawa walipofanya dhambi, hawakuruhusiwa tena kula matunda kutoka katika Mti wa Uzima, mti huu uliweza kuwapa uzima wa milele. Matokeo yake yalikuwa ni kufurushwa kutoka katika Bustani hiyo na kuvishwa ngozi za wanyama. Ngozi hizo za wanyama zilikuwa dhabihu ya kwanza ya kuondoa dhambi ambayo Mungu aliianzisha. Kifo kilianza kuwakumba watu kwa sababu walijichafua kwa dhambi. Matokeo yake ikawa ni Mungu kuwaondolea maisha ya milele katika miili yao. Hali ya dhambi na madhara yake viliiendelea kupokezwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi nyingine. Athari ya pili, ni kwamba dhambi iliuvuruga uhusiano uliokuwepo kati ya wanadamu. Watu huwatendea vibaya wanadamu wenzao. Tunaumizana na kupigana wenyewe kwa wenyewe. Wakati tunapofanyiana maovu sisi kwa sisi, huwa ni kwa sababu tumejaa hasira na ukatili. Ukatili hujitokeza katika kulipiza kisasi na mapigano ya kimwili au kihisia. Ukatili mwingine baina ya watu huweza kudumu kizazi hadi kizazi. Dhambi huleta mateso, mauti, vita, na uhasama baina ya watu. Hali hii huwafanya watu kuwa mbali na Mungu na kutohusiana na wengine vizuri, na kuwa katika hali ya kumhitaji mwokozi. Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe aliyeleta dhambi; lakini adamu wa mwisho (Yesu) ni Roho awapaye watu uzima. Picha ya 3: Ukandamizaji wa KirohoDhambi haikuingia duniani tu kwa sababu ya Adamu na Hawa peke yake; Shetani pia alichangia kiasi kikubwa kuwashawishi Adamu na Hawa kutenda dhambi (Tazama Somo La 1 na La 5). Kuanzia wakati huo Shetani alipowajaribu Adamu na Hawa katika bustani, yeye na pepo wake wanaomfuata wamekuwa wakifanya kazi duniani kuwakandamiza watu, kuwafanya watumwa, kuwajaribu, na kuwafanya kuabudu sanamu. Yesu ndiye suluhisho dhidi ya kazi za Shetani na pepo duniani. Katika picha ya tatu kuna nyoka na msitari wa kuondoa uliopitia katikati yake. Kumbuka Mungu alipomlaani nyoka katika Bustani ya Edeni, alimwambia kwamba kuna mtu atakayekuja na kumponda kichwa (Mwanzo 3:15). Huu ndio uliokuwa unabii wa kwanza juu ya ushindi wa Yesu dhidi ya Shetani wakati atakapokuja duniani. Katika Agani Jipya, tunasoma kwamba Yesu alikuja kuziharibu kazi za mwovu (1 Yohana 3:8). Yesu aliweza kuwapokonya nguvu pepo kwa kifo chake msalabani (Wakolosai 2:15; WaHebrania 2:14-15).

Kazi ya Yesu msalabani inatusaidia katika vita vyetu vya kila siku vya kiroho. Mtume Paulo anasema kwamba nguvu za Mungu ni kwa ajili yetu. Vilevile anasema kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka kifoni ili aweze kuzitawala nguvu za kiroho na za duniani, na kwamba sisi pia tuweze kufufuliwa pamoja naye na kuketi pamoja naye mbinguni. Uwezo wa Yesu na utawala wake ndivyo vinavyotupa sisi mamlaka juu ya ulimwengu wa kiroho. Hebu soma matini ifuatayo, “mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu ni sawa na nguvu ile kuu mno. Mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu ni sawa na nguvu ile kuu mno aliyomfufua nayo Kristo kutoka wafu, akamketisha upande wake wa kulia mbinguni. Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote…Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni” (Waefeso 1:19-22; 2:6).

Kwa hiyo, jinsi Mungu alivyomfufua Yesu kutoka kwa watu kwa uwezo wake, vivyo hivyo uwezo wake kwa wale wamwaminio ni mkuu. Yeye huwatia nguvu na kuwasaidia kupigana vita vya kila siku katika maisha (tazama Somo La 1, 5, na La 10 kwa habari za kina zaidi juu ya vita vya kiroho). Sababu moja inayoweza kuwafanya Wakristo kutokuwa huru kutokana na ukandamizaji wa pepo, ni kwamba wao wenyewe huruhusu pepo kuwakandamiza kutokana na matendo yao ya kila siku (Tazama Somo La 6 na La 9). Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, tunaona kwamba mwishowe Shetani atatupwa katika Ziwa La Moto, na kwa njia hiyo atakuwa ameshindwa kabisa. Katika Somo la 10, utajifunza juu ya vita vya kiroho na njia zile ambazo Mungu ametupa ili kuweza kukabiliana na ukandamizaji wa Shetani dhidi ya Wakristo.

Picha ya 4: JamiiVizazi kadhaa baada ya kizazi cha Adamu na Hawa, Mungu alianza kutenda kazi yake kwa kumtumia mtu mmoja aliyeitwa Ibrahimu. Katika mfano unaofuata, kuna picha ya mwezi na nyota. Picha hii inatukumbusha ile ahadi tuliyozungumzia katika Somo la 6 juu ya Ibrahimu. Mungu alipomwahidi Ibrahimu kwamba angepata mtoto katika uzee wake, Ibrahimu alimwamini Mungu. Basi kwa sababu ya imani yake hiyo kubwa Ibrahimu alihesabiwa haki. Kupitia kwa ungamo hili la imani Mungu angeongeza uzao wa Ibrahimu. Mungu alisema kwamba kizazi cha Ibrahimu kingekuwa kingi kama nyota za angani.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 71

Page 75: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mtume Paulo alisema kwamba wale wanaomwamini Yesu, wanafanywa kuwa wana wa Ibrahimu kwa kupitia imani yao(Wagalatia 3:29). Hata kulikuwa na unabii uliosema kwamba Masihi mwenyewe angetoka katika nyumba ya Ibrahimu, Isaka, na Yakobo . Chanzo cha amani duniani ni kwamba Wakristo wote duniani wameunganishwa na kuwa jamii moja kupitia kwa imani.

Yesu alileta umoja kati yetu. Umoja huu unavunja kila aina ya utengano, uwe wa kikabila, kimbari, kirangi, au kitaifa. Wakristo wote duniani wameunganishwa kama jamii moja kwa kupitia kwa Yesu Kristo. Mtume Paulo anasema kwamba, “Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Katika kuungana naye, nyinyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, mwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake” (Waefeso 2:19-22). Kile kinachosemwa katika aya hizi juu ya Wakristo wote ni kwamba sote tumejengwa katika mwamba mmoja. Tumejengwa pamoja na kuwa hekalu takatifu la Bwana—tuwe nyumba ya Mungu!

Sharti kuwe na amani kati yetu na wala sio mafarakano na ukabila. Udumishaji huu wa amani kunastahili kufanyika kwa kila kabila, mbari, rangi, na kila taifa. Watu huletwa pamoja kama jamii na kifo cha Yesu, kuzikwa kwake na kufufuka kwake. Yesu anapotusamehe sisi, tunastahili pia kuwasamehe wengine. Hakuna mwanadamu hata mmoja aliyestahili msamaha wa Mungu, wala hakuna anayestahili kusamehewa na mwanadamu mwenzake. Lakini uzuri wa msamaha ni kwamba ni kipawa cha bure ambacho huleta amani. Sisi sote tuko katika chombo kimoja, kwa kuwa sote tumetenda dhambi na Yesu alitufia sote. Yesu anapenda tuwasamehe wengine kama yeye anavyotusamehe, kwa sababu alitulipia gharama kubwa ya damu yake. Hapo ndipo kila aina ya vizuizi vilivyotutenganisha vinapobomolewa, na watu wote wanafanywa kuwa familia moja. Kuvunjwa kwa vikwazo vya kikabila au dhambi au ukatili kuna kamilishwa na kazi ya Yesu msalabani. Yesu alitufia ili tuweze kupatanishwa na Mungu na pia tupatanishwe sisi kwa sisi. Kile tunachostahili kutambua ni kwamba Yesu amefanya haya kwa ajili yetu, na vivyo hivyo sisi nasi tunastahili kufanya hivyo kwa wenzetu. Sisi sote ni watu wa jamii moja, yaani wana wa Ibrahimu!

Picha ya 5: WokovuKatika picha inayofuata, utaona chakula cha Pasaka. Baada ya Ibrahimu, tukio lingine muhimu lililowahi kutokea katika historia ya Waisraeli ni kule kukombolewa kwa Israeli kutoka utumwani huko Misri. Kama tunavyojifunza katika Agano Jipya, kukombolewa kwa wana wa Israeli kulikuwa mfano wa wokovu tunaoupokea kupitia kwa Yesu Kristo. Katika enzi za Agano la Kale, ukombozi wa Mungu ulihusu tu kukombolewa kutoka katika utumwa wa kibinadamu au kutoka kwa maadui. Lakini Katika Agano Jipya ukombozi unachukua mwelekeo mpya na kumaanisha ukombozi wa kiroho. Mungu aliwakomboa Waisraeli kutoka Misri ili watu waweze kutambua kwamba Mungu ni Mungu. Katika Agano lote la Kale, hakuna tukio kubwa lililotendeka isipokuwa hili la kukombolewa kwa wana wa Israeli kutoka Misri. Tukio hilo linakumbukwa na kutajwa katika sherehe zao, Zaburi, na katika vitabu vya Unabii. Katika kisa cha Kutoka, Waisraeli walichukua damu ya Mwanakondoo wa Pasaka na kuipaka juu ya vizingiti vya milango yao ili kuepuka mauti ya malaika wa kifo aliyekuwa atakuja na kuwaua wana wa kwanza wa Wamisri. Kila aliyepaka damu hii juu ya vizingiti vya mlango wake hakuuawa. Baada ya tukio hilo Mungu aliwaagiza Waisraeli kuadhimisha siku hii katika siku zijazo. Katika Agano Jipya tunafahamishwa kwamba Yesu alisherehekea Pasaka pamoja na wanafunzi wake usiku ule aliposalitiwa. Yesu aliwaeleza wanafunzi wake maana ya mkate na divai ya pasaka. Mkate uliwakilisha mwili wake alioutoa kwa ajili yetu, ilhali divai iliwakilisha damu yake iliyomwagika kwa ondoleo la dhambi zetu. Tukio kuu katika Agano Jipya ni kufufuka kwa Yesu, ambako kwetu sisi kulituletea tumaini la uzima wa milele. Yesu basi ndiye Pasaka yetu.

Picha ya 6: Ukuu wa YesuMiaka mingi baada ya tukio la Mungu kuongea na Ibrahimu na pia kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri, Israeli walipata mfalme ambaye alisifiwa kwa kumpenda Mungu. Mfalme huyu aliitwa Daudi. Picha inayofuata inaonyesha kiti cha enzi cha Daudi. Unabii uliotolewa katika Agano la Kale ulitabiri kuja kwa mfalme kutoka katika ukoo wa Daudi. Mfalme huyu alikuwa ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi na kutawala milele. “Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema, UFALME WAKO EE MUNGU, WADUMU MILELE NA MILELE,WEWE WATAWALA WATU WAKO KWA HAKI. WEWE WAPENDA UADILIFU NA KUCHUKIA UOVU; NDIYO MAANA MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUWEKA WAKFU NA KUKUMININIA FURAHA KUBWA KULIKO WENZAKO. NA TENA, "BWANA, WEWE ULIUMBA DUNIA HAPO MWANZO, MBINGU NI KAZI YA MIKONO YAKO; HIZO ZITATOWEKA, LAKINI WEWE WABAKI DAIMA; ZOTE ZITACHAKAA KAMA VAZI. UTAZIKUNJAKUNJA KAMA KOTI, NAZO ZITABADILISHWA KAMA VAZI. LAKINI WEWE NI YULEYULE DAIMA, NA MAISHA YAKO HAYATAKOMA DAIMA" (Waebrania 1:8-

Copyright © 2007 Tammie Friberg 72

Page 76: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

12; Zaburi 45: 6-7). Watu wengi katika enzi hizo walifikiria kwamba ufalme huu ungekuwa wa kimwili na ungekuwa huko Israeli. Lakini ukweli ni kwamba ufalme huu ni wa kiroho, hasa ikizingatiwa kwamba neno lililotumiwa ni “daima.”

Kwa hiyo utawala huu hauko katika mji fulani, bali katika mioyo ya watu wanaomwamini Yesu. Yesu ndiye utimilifu wa unabii huu. Yeye alitoka katika ukoo wa Daudi, na anatawala kutoka mbinguni, na katika mioyo ya watu. Katika huduma yote ya Yesu duniani, alihubiri juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu. Moja ya mafumbo aliyotumia Yesu kufundisha juu ya ufalme huu ni lile ya Lulu ya Thamani kubwa iliyokuwa katika shamba la mtu fulani. Katika mfano huo, kuna mtu mmoja aliyepata lulu ya thamani kubwa, naye akaenda kuuza mali zake ili aweze kuipata lulu hiyo. Fumbo hili linahusu thamani ya kumruhusu Mungu kutawala mioyo yetu. Kulingana na fumbo hili, kumruhusu Mungu kutawala mioyo yetu kuna thamani na pia kunahitaji kujitoa mhanga. Biblia inasema kwamba ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuaminbi moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka”(Warumi 10:9). Kumwamini Yesu kama Bwana, kumwamini kama alivyo, na kuzitubu dhambi zetu ndiyo njia inayoweza kutuingiza katika Ufalme wa Nuru. Ukuu wa Yesu ndicho kigezo kinacholifanya kanisa kuwapenda wengine na kumtii Mungu na sheria zake. Watu wanapomfuata Yesu kama mwokozi wa maisha yao, basi uhusiano huo huweza kuathiri jinsi wanavyowatendea wengine, na jinsi wanavyoishi katika jamii. Hata ingawa Yesu atukabidhi haki yake na kutusafisha( WaKorintho wa Pili 5: 21; WaKorintho wa Kwanza 1: 30-31), inabidi tuweke bidii kumfwata Yesu kama Bwana wa maisha yetu. Picha ya 7: Mungu aliyekuja duniani kama mwanadamuBaada ya utawala wa Daudi, walifuata wafalme kadhaa ambao hawakuzifuata sheria za Bwana. Mungu aliwatuma manabii kwenda kuwarudisha wafalme hawa waasi katika njia zake Mungu. Manabii hao pia walitoa unabii juu ya kuja kwa Masihi duniani. Masihi huyu angeweka agano jipya na wanadamu. Katika kisanduki kinachofuata, upande wa chini, kuna picha ya Mungu akiwa amenyoosha mkono huku akiwa na Mwanakondoo mkononi mwake. Unabii mwingi uliotolewa na manabii unaonyesha wazi kwamba Masihi ambaye alikuwa akitarajiwa angekuwa Mungu mwenyewe. Mungu ambaye ni roho, alishuka chini na kuja kwa wanadamu katika mwili. Yesu alikuwa Mungu aliyekuja katika umbo la mwanadamu (Mungu mwanadamu). Yesu alikuwa mfano wa Mungu asiyeonekana. Yeye alikuwa Neno aliyefanyika mwili. Yeye alikuwa mfano halisi wa Mungu Baba. Nabii Isaya alitabiri kwamba Masihi mtarajiwa angeitwa “Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenyezi, Baba wa Milele, na Mfalme wa Amani (Isaya 9:6). Jina lingine alilopewa Yesu wakati alipokuja duniani ni Emanueli. Jina Emanueli maana yake ni Mungu pamoja nasi. Hilo ndilo jina alilofunuliwa Mariamu wakati alipotembelewa na malaika kumpa habari kwamba atamzaa Yesu (Isaya 7:14; Mathayo 1:23).

Picha ya 8: Dhabihu ya kuondoa DhambiHii ni picha ya msalaba. Unabii mwingine uliotolewa ulionyesha kwamba Mungu angeleta suluhisho la kuurejesha upya uhusiano uliovunjika kati ya Mungu na wanadamu. Dhabihu hii ilikuwa sawa na ile ya Mwanakondoo wa Pasaka, lakini wakati huu ilikuwa inawakilisha mtu. Nabii Isaya alitabiri kuja kwa Mwokozi ambaye angetoka katika ukoo wa Mfalme Daudi. Mtu huyu wa uzao wa Daudi angekuwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, kuteswa kwa ajili ya dhambi zetu. Wayahudi wengi waliona vigumu kuelewa jinsi Masihi angalivyokuwa mfalme milele na vilevile kufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Lakini manabii walionyesha kwamba sisi tungeponywa kwa kupitia kwa kupigwa kwake (Isaya 53:4-5). Pia katika kitabu hicho cha Isaya tunasoma kwamba katika kifo chake angeweza kuona uzao wake wa kiroho (Isaya 53:10). Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili tuweze kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu. Yeye ndiye anayeweza kutusaidia kuondoa hatia ya dhambi katika mioyo yetu. Katika enzi za Agano la Kale, watu walikuwa wakitoa dhabihu ya wanyama ili kusafisha mioyo yao kutokana na dhambi na hatia. Lakini hata hivyo dhabihu hizo hazikuweza kuondoa dhambi kabisa kabisa. Mfalme Daudi na manabii walitarajia kwa hamu kuona dhabihu ile ambayo Mungu angeitumia kuondoa hatia ya dhambi kabisa. Yesu alikuja duniani kama dhabihu ya mwisho ya kuondoa na kusamehe dhambi ulimwenguni. Ni vyema kutambua kwamba Yesu alikuwa dhabihu na Kuhani Mkuu mbinguni aliyekuja duniani kututakasa na kutusamehe dhambi zetu. Makuhani wa duniani hawakuweza kumaliza kazi yao, lakini Yesu yeye aliingia mbinguni na kukaa mkono wa kuume wa Mungu. Hii ilionyesha kwamba kazi ya kuondoa dhambi ilikuwa imefanywa mara moja na kukamilishwa kabisa kwa kifo chake.Kwa kufa msalabani, Yesu alilipa deni letu la dhambi mbele ya Mungu Baba( WaKolosai 2:8, 13-14; WaHebrania 10: 14,18; WaHebrania 1:3). Hakuna haja ya watu kuenda kwa padre kuomba msamaha. Biblia yasema, “ Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.”( Yohana wa Kwanza 1:9). Yesu alitulipia kamili deni letu la dhambi.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 73

Page 77: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Picha ya 9: Kurejeshwa upyaHii ni picha ya moyo uliofungwa kwa bendeji, na mikono iliyofungwa nyororo zilizokatika. Unabii mwingine uliohusu kuja kwa Masihi ulikuwa kwamba Masihi angelikuja kuwahuisha upya wale walioteswa na kuumizwa. Nabii Isaya alitangaza kazi ya Masihi ya kuwarudisha watu kati hali zao nzuri. Alisema hivi: “… niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa.” (Isaya 61:1). Vilevile Isaya alitumia tashbihi kuelezea watu waliokandamizwa na jinsi Yesu alivyowajali na kwamba angewapa haki yao. Alisema kwamba Masihi, "Mwanzi uliochubuka hatauvunja, utambi ufukao moshi hatauzima;ataleta haki kwa uaminifu” (Isaya 42.3). Wakati Yesu alipokuwa duniani, aliwaponya watu ili kuwaonyesha yeye ni nani na pia kuwajulisha kwamba yeye ndiye anayeweza kuwapatia uzima wa milele mbinguni. Yesu alikuja duniani kuwarejesha upya, kuwapa nguvu mpya, na kuwaponya kihisia, kiroho na kimwili. Aidha alikuja kuwafunulia wanadamu kwamba katika yeye kuna suluhisho la huzuni, na mateso, na wafungwa watafunguliwa, na waliovunjika moyo watatiwa moyo. Yesu aliposulubishwa msalabani, alitupatanisha na Mungu na vilevile alitupatanisha na wanadamu wenzetu. Biblia inasema kwamba Yesu alikivunja kiambaza kilichowatenganisha watu, kiwe kiambaza cha ukabila, utaifa, jinsia, utumwa au uhuru. Alikuja kuwarudisha wanadamu kwa Mungu na kurudisha tena uhusiano mwema kati yao. Yeye ndiye Muumbaji na kwa hiyo ana uwezo na nguvu juu ya viumbe vyote. Wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu, yeye anaweza kuyarejesha upya, anaweza kutupatia haki yetu na kuigeuza upya mioyo yetu iliyopondeka. Yesu anataka tumtegemee yeye ili aweze kutubadilisha. Na vilevile lazima tuwe tayari kuzifuata sheria zake. Wale waliokuwa na imani kubwa wameorodheshwa katika Waebrania 11, ili kutuonyesha kwamba imani ni kuamini kwamba Mungu atatimiza yale aliyoyaahidi hata ikiwa hakutakuwa na ishara za kuonekana kwa macho kuthibitisha jambo hilo.

Kuelewa na Kuitikia mwito wa InjiliSasa zipitie zile picha tena. Kwa kifupi, Yesu alikuja duniani kusuluhisha shida tunazokumbana nazo. Yeye ndiye anayeweza kuurudisha upya uhusiano wetu na Mungu (angalia picha ya 1). Yeye ndiye anayeweza kuisafisha mioyo yetu kutokana na dhambi (angalia picha ya 2). Vilevile yeye ndiye anayeweza kuziharibu nguvu za Shetani duniani. Yesu alimshinda Shetani na kifo wakati alipofufuka kutoka kwa wafu. Sasa amewafufua Wakristo na kuwapa uwezo wake juu ya roho zote za giza (picha ya 3). Pia Yesu ndiye anayetupa amani, kwa kuwaunganisha Wakristo wote kutoka katika kabila, rangi, taifa, na kuwa watu wa jamii moja chini ya baba mmoja Ibrahimu. “Nyinyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa Kristo. Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. Ikiwa nyinyi ni wa Kristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, na mtapokea yale aliyoahidi Mungu” (Wagalatia 3:27-29; angalia picha ya 4). Yesu hutukomboa kiroho kutoka katika Ufalme Wa Giza, kama alivyowakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani huko Misri. Siku moja tutakuwa naye kule mbinguni. Wokovu wake in kamili na tunao uhakikisho kuwa tunao maisha ya milele (Yohana 6:37,39; Yohana wa Kwanza 5:13; angalia picha ya 5). Yeye ndiye Bwana anayetawala maisha yetu. Ni lazima tumkiri yeye kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Ukitazama picha utaona kwamba Kiti Chake Cha Enzi kiko katika moyo wa mwanadamu (angalia picha 6). Yesu ni Mungu aliyekuja duniani kama mwanadamu. Alipokuja duniani, alituonyesha yeye ni nani kupitia kwa matendo yake na mafundisho yake. Yesu alikuwa na uwezo juu ya uumbaji (asili), magonjwa, pepo, na hata mauti. Vilevile ana nguvu na uwezo wa kutusamehe dhambi zetu. Yesu alituonyesha uwezo huu sio tu kwa kupitia kwa miujiza aliyotenda, bali pia alipozibeba dhambi zetu mwilini mwake na kusulubiwa msalabani. Yeye ana ufunguo wa mauti na wa kaburi. Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, alituahidi kwamba wale watakaomwamini watafufuliwa kama yeye alivyofufuliwa. Tutaishi milele na milele (angalia picha ya 7). Yeye ndiye suluhisho kwa watu waliopondeka, wagonjwa, wadhaifu, na wale waliokandamizwa. Sio kwamba anaweza tu kutuponya au kuwaweka huru wafungwa, bali katika yeye tuna tumaini la uzima wa milele mbinguni. Yesu anaweza kutuponya majeraja yetu na kutukomboa kutoka katika utumwa wa Ufalme wa Giza. Yeye amevunja kila aina ya kuta zinazowatenganisha watu (tazama picha ya 8). Yesu anaweza kututendea mambo haya yote lakini kila mmoja wetu sharti amwalike moyoni mwake, amwamini, na kuzitubu dhambi zake, na kumfuata yeye kama Bwana wa maisha yake.

Pengine tunaweza kusema kwamba tofauti kubwa iliyoko kati ya Ukristo na dini zilizoanzishwa na wanadamu ni kwamba dini za wanadamu hufunza watu kwamba wakitenda matendo mazuri na kufanya matambiko yafaayo, wataenda mbinguni. Lakini sio kweli. Ukristo hutupa nguvu na pia kuisafisha mioyo yetu kutokana na dhambi zote. Biblia inasema kwamba tumeokolewa kwa Neema yake. Neema hiyo ni kipawa cha bure kwa hao wanaokipokea, na wala sio kwa matendo yetu, isije mtu akajivunia kitu kingine isipokuwa Yesu (Waefeso 2:8-9). Neema yatoka kwake Bwana Mungu, sio dini wala mambo ya kidini.(Wagalatia 1:3; Waefeso 1:2) Hatuwezi kamwe kuingia mbinguni kwa juhudi zetu sisi wenyewe. Yesu ndiye ambaye ametuandalia njia kupitia kwa kifo chake msalabani.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 74

Page 78: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Waebrania sura ya 2:14-18 imeyaweka mambo haya katika muhtasari vizuri. Biblia inasema, “Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo, na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwa maisha yao yote kwa sababu ya hofu yao ya kifo. Maana ni wazi kwamba yeye hakuja kwa ajili ya kuwasaidia malaika, bali kama yasemavyo Maandiko: “Anawasaidia wazawa wa Abrahamu.” Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe. Na, anaweza sasa kuwasaidia wale wanaojaribiwa na kuteswa.”

Yesu Anawaita Watu wote Wazaliwe UpyaMara kwa mara katika kufundisha kwake, Yesu alirudia fungu hili la maneno, “Aliye na masikio, naasikie.” Alitumia kirai hii wakati alipokuwa akizungumzia Ufalme wa Nuru. Moyo wakati wote huonyeshwa ukiwa umeshikana na sikia. Ikiwa moyo wa mtu hauna nguvu ya kulisoma na kulitii neno la Mungu, na badala yake umesongwa na mahangaiko ya maisha, kuwachukia watu, anasa za maisha, au Shetani kuliiba Neno kutoka katika mioyo ya watu, basi ujumbe wa Injili katika mtu huyo huwa umetatizwa (Mathayo 13, Fumbo la Mpanzi). “Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: “KAMA MKISIKIA SAUTI YAKE LEO, MSIWE WAKAIDI KAMA WAKATI ULE WALIPONIASI KAMA WAKATI ULE WA MAJARIBIO KULE JANGWANI. HUKO WAZEE WENU WALINIJARIBU NA KUNICHUNGUZA, INGAWA WALISHUHUDIA MATENDO YANGU KWA MIAKA ARUBAINI! KWA SABABU HIYO NILIWAKASIRIKIA WATU HAO NIKASEMA, ‘FIKIRA ZA WATU HAWA ZIMEPOTOKA, HAWAJAPATA KAMWE KUZIJUA NJIA ZANGU’. BASI, NILIKASIRIKA, NIKAAPA: ‘HAWATAINGIA MAHALI PANGU PA PUMZIKO’” (Waebrania 3:7-11). Picha ya 10: Mwite Bwana wa WokovuHii ndiyo picha kubwa zaidi katika ukurasa. Siku moja mtu mmoja kwa jina Nekodemu alimwuliza Yesu, “Nifanye nini ili nipate kuokoka?” Yesu akamjibu na kusema kwamba sharti azaliwe mara ya pili. Kuna njia MOJA tu inayoelekea katika Ufalme wa Nuru-njia hiyo ni Yesu (Matendo 4:12; Matayo 11:5; Marko 1:14; Luka 4 :14-21; 8:1). Mtume Paulo anatushauri jinsi tunavyoweza kuingia katika Ufalme wa Nuru. Anasema, “KILA MTU ATAKAYEOMBA KWA JINA LA BWANA ATAOKOLEWA”(Warumi 10:13). Kwa hiyo mwite kwa maombi, naye atakuokoa. Tazama jinsi familia inavyomwomba Yesu awaokoe. Wamesimama pale panapoanzia njia ile nyembamba, na kando yao kuna lile jalala la taka. Watu hawa wako karibu kujiunga na wale wengine wanaoifuata njia nyembamba ili kuwa sehemu ya jamii moja ya imani. Wameyatupia kisogo maisha yao ya zamani na kupokea maisha mapya. Unaweza kuingia katika Ufalme wa Nuru kwa moyo wako na kwa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako (Warumi 10:9-10). Kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako kunamaanisha kuanza kumtii yeye katika maisha yako ya kila siku na kwa matendo yako, na maneno yako. Pia ina maana kwamba tutaacha kuabudu miungu ya sanamu na dhambi nyingizo zilizotuzinga. Wakati mwingine kumruhusu Yesu kuyatawala maisha yetu huchukua muda, kwa sababu tunaweza kumhuzunisha Mungu pasipo kujua. Katika picha utaona kwamba kila mtu amemruhusu Yesu kukaa katika kiti cha enzi cha moyo wake. Jambo la pili tunalostahili kufanya ni kuamini Yesu ni nani na alikuja duniani kutufanyia nini. Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili ya dhambi zetu, kwa hiyo hakuna haja tena kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. Yesu ndiye mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Yesu ndiye anayetupatia uwezo wa kushinda pepo na ndiye anayetupatanisha na Mungu, kwa sababu hiyo tunaweza kumwamini au kumtegemea yeye. Ukiangalia picha utaona chini ya msalaba, kuna pepo walioshindwa. Na juu mbinguni unaweza kumwona Yesu amekaa katika kiti cha enzi. Jambo la tatu, ni sharti tukiri dhambi zetu kwa Mungu, naye atatusamehe (1 Yohana 1:9). Kukiri dhambi zetu maana yake ni kukubali kwamba katika maisha yetu tumefanya mambo yasiyompendeza Mungu. Katika ungamo hili, lazima tutubu, na kuyatupia kisogo maisha ya nyumani ya dhambi. Ukiangalia picha utamwona Yesu akizichukua dhambi za wanadamu. Hatua hizi zinaweza kufanywa na mtu pasipo kuzingatia ipi ya kwanza, ipi ya pili, bora tu hatua zote zitekelezwe. Picha 11: Ubatizo na Meza ya Bwana Picha hii ndogo inaonyesha mtu akibatizwa, na vilevile inaonyesha kikombe na mkate wa Meza ya Bwana. Kuna matambiko mawili katika Biblia ambayo Wakristo wanastahili kuyatekeleza. Matambiko haya ni ishara ya kazi aliyoifanya Yesu msalabani. Tambiko la kwanza ni ubatizo. Ubatizo hauwezi kutuokoa (Luka 23:43 -Mwizi msalabani; Matendo 18-19- hadithi ya Apollo), bali ni ishara au picha ya kufa au kufia dhambi na kufufuka katika maisha mapya. Vilevile ni ishara ya ile kazi aliyofanya Yesu kwa ajili yetu. Yesu anaamuru kila Mkristo abatizwe kuonyesha utiifu wa agizo hilo. Watu wanstahili kubatizwa baada ya kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 75

Page 79: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Tambiko la pili muhimu ni Meza ya Bwana, au Ushirika Mtakatifu. Mkesha wa kusulubiwa kwake, Yesu alisherehekea Pasaka pamoja na wanafunzi wake. Ni katika wakati huo ndipo alipowaeleza wanafunzi wake maana halisi ya divai na mkate usiochachwa. Yesu alisema kwamba divai iliwakilisha damu yake inayoondoa dhambi, na mkate uliwakilisha mwili wake uliotolewa kwa ajili yao (wanafunzi). Baadaye Wakristo walikuja kuliita tambiko hili “Meza ya Bwana.” Kanisa la kwanza lilikuwa na mazoea ya kula Meza ya Bwana mara kwa mara. Kabla ya kula Meza ya Bwana, Wakristo walihitaji kwanza kuzitubu dhambi zao kwa Mungu na kuhakikisha kwamba hakuna uhasama wowote kati yao na wanadamu wenzao. Kwa njia hii, watakuwa wanaiheshimu kazi ya upatanisho aliyofanya Yesu msalabani. Picha 12: Mikononi Mwa MunguPicha hii inaonyesha watu waliookolewa wakipumzika mikononi mwa Mungu. Kuna mambo kadhaa ambayo hufanyika wakati tunapookolewa. Tunahamishwa kutoka katika Ufalme wa Giza hadi katika Ufalme wa Nuru. Tazama kwamba watu hawa wanayo mioyo iliyo safi. Tunapatanishwa na Mungu kupitia kwa Yesu. Kila kizuizi cha kuwagawanya watu kinavunnjwa. Yesu hutufufua pamoja naye, na kutupatia nguvu dhidi ya pepo. Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu. Roho hutuongoza, kutuonyesha dhambi zetu, na kutufariji. Tunapewa mioyo mipya na Roho Mtakatifu, na tunazaliwa mara ya pili kiroho. Tunatiwa muhuri katika Kristo. Muhuri huu unaonyesha kwamba hakuna yeyote anayeweza kututoa katika mkono wa Mungu wa usalama juu ya ufalme ujao. Tunafanywa kuwa wana wa Ibrahimu kwa imani. Kwa hiyo, tunajiunga na jamii mpya ya imani. Jamii hii imeshinda mipaka ya kikabila, kitaifa, na kirangi. Tunapewa uzima wa milele. Sasa tunapewa jukumu la kuwapatanisha watu na Mungu kwa kuwaambia Habari Njema watu wa familia zetu, jamii, nchi, na ulimwengu kwa jumla.

Kunayo mambo kadhaa yanayoweza kutusaidia sisi kama Wakristo kuishi kitakatifu. Mambo haya yatajadiliwa kwa kina katika masomo matatu yatakayofuata.

Mafundisho Ya Somo La 8Yesu Ndiye Jibu Jinsi Ya Kuhama Kutoka Katika Ufalme Wa Giza hadi Wa Nuru

Hapo mwanzo watu walikuwa na ushirika na Mungu Hatuwezi Kujipeleka Mbinguni Sisi wenyewe, Wokovu NI Kwa NeamaAdamu na Hawa Walitenda Dhambi na wakawa chanzo cha wanadamu kutenganishwa na Mungu

Yesu Anatimiza Unabii wote wa Agano La Kale

Unabii: Kuna Mtu Atakayekuja Kumwangamiza Shetani Lazima Tuusikie Ujumbe Wa Mungu Na TuuaminiAhadi Ya Mungu Kwa Ibrahimu Yesu Alituonyesha yeye ni nani: Ana uwezo juu ya uumbaji, pepo.

Magonjwa, na kifo.Mwanakondoo Wa Pasaka Lazima tuziungame dhambi zetu kwa Mungu, naye atatusameheMtu Atatawala Katika Kiti Cha Daudi Milele Lazima Tumwamini YesuMungu mwanadamu, Mwana wa Mariamu, Majina Ya Yesu Lazima Tumkiri Yesu Kama Bwana Na Mwokozi wa Maisha YetuAjaye Atakuwa Dhabihu Ya Mwisho Ya Dhambi Roho Mtakatifu Huisafisha Mioyo YetuAjaye Atawaponya Watu Na kuwarejesha Katika hali yao Tunafanyika Wana Wa Ibrahimu

Yesu Anatufufua pamoja naye na kutupa nguvu dhidi ya pepoTumeamriwa kubatizwa; Tunastahili Kushiriki Meza Ya BwanaHakuna Anayeweza Kututoa Kutoka Katika Mkono Wa Mungu

Marejeo ya Kujifunza Biblia Ya Somo La 8

Yesu Ndiye JibuHadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

1. Hapo mwanzo watu walikuwa na ushirika na Mungu *Adamu Na Hawa Walikuwa Na Ushirika Na Mungu- Mwanzo 2.

1. Hapo mwanzo watu walikuwa na ushirika na Mungu

2. Adamu na Hawa Walitenda Dhambi na wakawa chanzo cha wanadamu kutenganishwa na Mungu *Adamu Na Hawa Walitenda Dhambi Kwa Mungu- Mwanzo 3.*Adamu Alileta Kifo, Yesu Alileta Uzima- 1 Wakorintho 15:21-58.

2. Adamu na Hawa Walitenda Dhambi na wakawa chanzo cha wanadamu kutenganishwa na Mungu *Wote Wametenda Dhambi Na Kupungukiwa Na Utukufu Wa Mungu- Warumi 3:23.*Dhambi Ni Nini?- Wagalatia 5:19-21; Kutoka 20:1-17.*Mshahara Wa Dhambi ni Mauti- Warumi 6:23.*Dhambi Hututenganisha Na Mungu- Isaya 59:2.*Tulizaliwa Katika Dhambi- Zaburi 51:5.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 76

Page 80: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Tamaa Kuzaa Dhambi Ndani Yetu- Yakobo 1:15.3. Kuna Mtu Atakayekuja Kumwangamiza Shetani *Kuna Mtu Atakayekuja Kumwangamiza Shetani Kwa Kumponda Kichwa- Mwanzo 3:14-15.*Hatima Ya Shetani Ni Ziwa La Moto- Ufunuo 20:10.*Yesu Ana Uwezo Juu Ya Pepo-Mathayo 8:16; 9:32-38; 17:14-21; Marko 7:26-37; Luka 4:33-44.*Yesu Anamponya Mtu Aliyepagawa Na Jeshi La Pepo- Marko 5.

3. Kuna Mtu Atakayekuja Kumwangamiza Shetani *Yesu Alikuja Duniani Kuharibu Kazi Za Shetani- 1 Yohana 3:8.*Yesu Alikufa Msalabani Kuwapokonya Uwezo Pepo- Wakolosai 2:15; Waebrania 2:14-15.*Yesu Ameinuliwa Juu Ya Nguvu Zote Duniani Na mbinguni- Waefeso 1:20; 2:6.*Ameketi mkono wa kuume wa Mungu, Yuko juu ya Nguvu Zote, malaika, mamlaka na uwezo - 1 Petro 3:22.

4. Ahadi Ya Mungu Kwa Ibrahimu*Kizazi Cha Ibrahimu Kitakuwa na watu wengi kama nyota za angani, hakitaweza kuhesabika- Mwanzo 15:5-6.

4. Ahadi Ya Mungu Kwa Ibrahimu*Paulo Anatufundisha Kwamba Sisi ni Kizazi Cha Ibrahimu Kwa Imani- Wagalatia 3, Warumi 4.*Mungu Anawasaidia Watu wa Kizazi Cha Ibrahimu- Waebrania 2:16.

5. Mwanakondoo Wa Pasaka*Pasaka Ya Kwanza- Kutoka 12-13; Kumbukumbu 6:1-25.*Chakula Cha Mwisho Cha Yesu- Mathayo 26:17-30.*Kifo Cha Yesu- Yohana 19-20; Luka 22; Mathayo 28.

5. Mwanakondoo Wa Pasaka*Yesu Kama Pasaka- 1 Wakorintho 5:6-8.

6. Mtu Atatawala Katika Kiti Cha Daudi Milele *Ufalme Wake Wadumu Hata Milele- Zaburi 45:6-7; 89:29, 36; 145:13; Waebrania 1:8-9.Malaika akamwambia Maraimu, "Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho- Luka 1:32-33.

6. Mtu Atatawala Katika Kiti Cha Daudi Milele *Wakati wa wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao kamwe hautaangamizwa. Watu wengine hawataushinda na kuutawala ufalme huo, bali ufalme huo utaziponda na kuzikomesha falme zilizotangulia, nao utadumu milele- Danieli 2:44.*Maana Mtoto amezaliwa kwa ajli yetu., tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa, “Mshauri wa Ajabu”. Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba Wa Milele”, “Mfalme Wa Amani”. Utawala wake utastawi daima, amani ya ufalme wake haitakoma. Atachukua wadhifa wa mfalme Daudi na kutawala juu ya ufalme wake; ataustawisha na kuuimarisha, kwa haki na udailifu, tangu sasa na hata milele. Hayo atayafanya Mwenyezi-Mungu wa majeshi- Isaya 9:6-7.*Tazama, siku zaja nitakapomchipushia Daudi chipukizi adili. Huyo atatawala kama mfalme, na atatenda kwa busara, haki na uadilifu katika nchi. Katika siku za utawala wake, Yuda ataokolewa na Israeli ataishi kwa usalama. Naye ataitwa, Mwenyezi-Mungu ni uadilifu wetu- Yeremia 23:5-6.

7. Mungu mwanadamu, Mwana wa Mariamu, Majina Ya Yesu *Malaika Anamwambia Mariamu Kwamba Atamzaa Mwokozi - Luka 1.*Yesu Anajiita “MIMI NIKO”- Yohana 8:58; Kutoka 3:14.*Yesu Anajiweka Sawa Na Mungu-Yohana 5:18-19.*Ungamo La Tomaso- Yohana 20:28.

7. Mungu mwanadamu, Mwana wa Mariamu, Majina Ya Yesu * Maana Mtoto amezaliwa kwa ajli yetu., tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa, “Mshauri wa Ajabu”. Mungu Mwenye Nguvu”, “Baba Wa Milele”, “Mfalme Wa Amani”- Isaya 9:6.*Mwenyezi-Mungu ni uadilifu wetu- Yeremia 23:5-6.*Emanueli, Mungu Yuko Nasi- Isaya 7:14; Mathayo. 1:23.*Yesu ni Mungu, Aliyefanyika Mwanadamu; Muumbaji- Yohana 1:1-14.*Yesu Ndiye Mfano wa Mungu Asiyeoonekana; Na Aliumba Vitu Vyote Kwa Ajili Yake mwenyew (Falme zote, Uwezo, n.k.)- Wakolosai 1:15-16.*Yeye ni Mng’ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu- Waebrania 1:1-3.*Yesu Anaitaw Mungu Na Mwokozi- Tito 2:13.

8. Ajaye Atakuwa Dhabihu Ya Mwisho Ya Dhambi*Mtumishi Anayeteseka- Isaya 53.*Malaika Gabraeli Anampatia Danieli Maarifa- Danieli 9 (Tambua Kwamba Kihistoria Wakati huu Ndio Unawakilisha Mwaka Aliosulubishwa Yesu.*Yesu Ndiye Kuhani Wetu Na Dhabihu Yetu - Waebrania 7:27; Waebrania 9-10.*Kufa na Kufufuka Kwa Yesu- Yohana 19-20; Luka 22; Mathayo. 28.

8. Ajaye Atakuwa Dhabihu Ya Mwisho Ya Dhambi *Kwa maana Kristo mwenyewe, alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwena kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho; na kwa maisha yake ya kiroho alikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwa kifungoni. Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Nuhu alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji - 1 Petro 3:18-20.*Hivyo, kwa kuwa alikufa-mara moja tu-dhambi haina nguvu tena juu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 77

Page 81: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu. Hali kadhalika nanyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusu dhambi, lakini kama mnaoishi katika umoja na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu. Kwa hiyo, dhambi isitawale tena miili yenu ambayo hufa, na hivyo kuzitii tama zake. Wala msitoe hata sehemu moja ya miili yenu iwe chombo cha kutenda uovu na dhambi. Badala yake, jitoleeni nyinyi wenyewe kwa Mungu kama watu waliofufuliwa kutoka wafu; toeni nafsi zenu zote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu – Warumi 6:10-13.

9. Ajaye Atawaponya Watu Na kuwarejesha Katika hali yao *Hezekia Anaponywa na Mungu- Isaya 38:9-32.*Yesu Anaponya Mtu mwenye ukoma- Mathayo. 8:2; Marko 1:40; Luka 5:12.*Yesu Anamponya Mtu Kwa Mbali- Mathayo. 8:5; Luka 7:1.*Yesu Anamponya Mama Mkwe Wa Petro- Mathayo. 8:14; Marko 1:30; Luka 4:38.*Yesu Anawaponya Watu wawili vipofu- Mathayo. 9:27.*Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono- Mathayo. 12:9; Luka 6:6.*Yesu Anamponya Mwanamke Aliyevimba Mwili- Luka 14:1.*Yesu Anawaponya Watu Kumi Wenye Ukoma Kumi- Luka 22:51.*Yesu Anatimiza Unabii wa Kuwaponya Watu- Mathayo. 8:17; Isaya 53.

9. Ajaye Atawaponya Watu Na kuwarejesha Katika hali yao *Mwenyezi-Mungu amenijza roho yake, maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa- Isaya 61:1-3.

Kuingia Katika Ufalme Wa NuruHadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Hatuwezi Kujipeleka Mbinguni Sisi wenyewe, Wokovu ni Kwa Neama *Petro Anajitetea Kwa Kueleza Ni Kwa nini Anaihubiri Habari Njema: Yesu Ndiye Njia Pekee Ya Kwenda Mbinguni- Matendo 4:1-12 (aya 12).

Hatuwezi Kujipeleka Mbinguni Sisi wenyewe, Wokovu ni Kwa Neama *Twaokolewa Kwa Neema, Na sio Kwa matendo yetu- Waefeso 2:8-9.*Utakatifu Wetu ni kama matambara machafu- Isaya 64:6.*Matendo mema Hayawezi kutuokoa- Tito 3:5-7.*Hatuwezi Kujivuna- Warumi 3:27-28.*Kuna Njia Ionekanayo Sawa Kwa Mwanadamu, Lakini Mwisho Wake ni Mauti- Mithali 14:12.

Yesu Anatimiza Unabii wote wa Agano La Kale (TAZAMA CHATI HAPO JUU)

Yesu Anatimiza Unabii wote wa Agano La Kale (TAZAMA CHATI HAPO JUU)

Lazima Tuusikie Ujumbe Wa Mungu Na Tuuamini *Yohana Anamwuliza Yesu Ikiwa Ndiye Masihi- Mathayo. 11:1-15.*Fumbo La Mpanzi- Marko 4:1-23; Luka 8.*Yesu Anafundisha Juu Ya Uanafunzi- Luka 14:25-45.

Lazima Tuusikie Ujumbe Wa Mungu Na Tuuamini *Leo Ukiisikia Sauti Yake, Usiufanye Moyo Wako Kuwa Mgumu- Waebrania 3:7-11.

Yesu Alituonyesha yeye ni nani: Ana uwezo juu ya uumbaji, pepo. Magonjwa, na kifo.*Yesu Ana Uwezo Juu Ya Asili:*Jukumu La Yesu Katika Uumbaji- Yohana 1.*Yesu Anatuliza Dhoruba- Mathayo. 8:23-27.*Yesu Anawalisha Watu Zaidi Ya 5,000- Mathayo. 14:13; Marko 6:30; Luka 9:10; Yohana 6:1.*Yesu Anawalisha Watu 4,000- Mathayo. 15:32; Marko 8:1.*Yesu Anatembea Juu Ya Maji- Mathayo. 14:25; Marko 6:48; Yohana 6:19.*Samaki Aliyekuwa Na Pesa Tumboni- Mathayo. 17:24.*Yesu Anageuza Maji Kuwa Divai- Yohana 2:1.*Muujiza Wa Samaki Wengi- Luka 5:1; Yohana 21:1.Uwezo Juu Ya Pepo- (Tazama Noti Ya 3 Katika Chati Iliyojuu).

Yesu Alituonyesha yeye ni nani: Ana uwezo juu ya uumbaji, pepo. Magonjwa, na kifo.*Yesu Anakuja Kukishinda Kifo- 1 Yohana 3:5; 1 Wakorintho 15:24-28.*Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu nay ale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema - Yohana 2:22.*Umuhimu Wa Ufufuo- 1 Wakorintho 15.*Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa pia pamoja naye kwa kuamini katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu- Wakolosai 2:12.*Ufufuo Ulikuwa wa mwili, Hakufufuliwa Kama Roho- Yohana 20:28.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 78

Page 82: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Yesu Ana Uwezo Juu Ya Magonjwa:*Yesu Anaponya Mtu Mwenye Ukoma; Mtumishi Wa Akida; Mama Mkwe Wa Petro; Na Wagonjwa Wengine- Mathayo. 8; Marko 1; Luka 5:12; 7:1; 4:38-40.*Yesu Anaponya Mtu Aliyepooza- Mathayo. 9:2; Marko 2:3; Luka 5:18.*Yesu Anaponya Mwanamke Aliyevuja Damu- Mathayo. 9:20; Marko 5:25; Luka 8:43.*Yesu Anaponya Watu Waliokuwa Vipofu- Marko 7:31.*Yesu Anaponya Watu 10 wenye ukoma- Luka 22:51.Yesu Ana Uwezo Juu Ya Kifo:*Adamu Na Hawa Walaaniwa, Hawataishi Milele- Mwanzo 3.*Yesu Anamponya Binti Wa Mkuu Fulani - Mathayo. 9:18, 23; Marko 5:22, 35; Luka 8:40, 49.*Yesu Anamfufua Mwana Wa Kiume Wa Mama Mjane- Luka 7:11.*Yesu Anamfufua Lazaro- Yohana 11-12.*Yesu Anazungumza Na Petro Baada Ya Kufufuka Kwake- Yohana 21:14-25.*Yesu Anazungumza Na Viongozi Wa Kidini Juu Ya ufufuo- Mathayo. 22:23-33.*Paulo Anawahutubia Watu Juu Ya Ufufuo- Matendo 13:13-41.*Watakatifu Wafufuka Wakati Wa Kifo Cha Yesu- Mathayo. 27:52-54.*Yesu Alijifufua Mwenyewe Kutoka Kwa wafu-Yohana 2:19-21.*Petro Atiwa Gerezani- Matendo 4.*Paulo Akiwa Athene- Matendo 17.Lazima tuziungame dhambi zetu kwa Mungu, naye atatusamehe *Mungu Husamehe Dhambi- Danieli 6.*Sala Ya Bwana- Mathayo. 6:1-15; Marko 11:25-26.*Ungamo La Daudi- Zaburi 51.*Ombi La Danieli La Kuungama- Danieli 9.*Ubatizo wa Yohana- Mathayo. 3.*Paulo Akiwa Athene- Matendo 19.

Lazima tuziungame dhambi zetu kwa Mungu, naye atatusamehe *Tukiungama Dhambi Zetu…- 1 Yohana 1:9.*Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu nyinyi mlikuwa watuw a mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa nyinyi uhai pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote; alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani. Huko Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake- Wakolosai 2:13-15.*Kisha nilikiri makosa yangu kwako; wala sikuuficha uovu wangu. Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu, ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote. Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi-Zaburi 32:5-6.*Afichaye makosa yake hatafanikiwa; lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema- Mithali. 28:13.

Lazima Tumwamini Yesu*Tukimwamini Tutakuwa Na Haki Ya Kufanyika Wana wa Mungu- Yohana 1:1-13.*Nikodemo Aokolewa- Yohana 3.*Heri Wale Waaminio Pasipo Kuona Kwa Macho- Yohana 4:47-48.*Yesu Anahubiri Injili- Marko 1.*Yesu Anawatokea Wale Mitume Kumi Na Wawili: Luka 24.*Waisraeli Na Kutoamini Kwao- Zaburi 78.*Yesu Anafundisha Juu Ya Kutoamini Na Juu Ya Hukumu- Yohana 3:18-21. *Yesu Ndiye Mkate Uliotoka Mbinguni: "Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uhai wa milele. Mimi ni Mkate wa uhai. Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa. Lakini huu ni mkate unaoshuka kutoka

Lazima Tumwamini Yesu*Tukiamini Mioyoni Mwetu ya Kwamba Mungu Alimfufua Yesu Kutoka Kwa Wafu, Tutaokoka- Warumi 10:9.*Nyinyi mnapenda, ingawaje hamjamwona,na mnamwamini, ingawa hammwoni sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka, kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu -1 Petro 1:8-9.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 79

Page 83: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mbinguni ili yeyote atakayekula asife. Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili ya uhai wa ulimwengu- Yohana 6:47-51.*Yesu Anazungumza Na Mafarisayo Juu Ya Kuamini: “Kama msipoamini kwamba, ‘Mimi Ndimi,’ mtakufa katika dhambi zenu”- Yohana 8:24.*Kipofu Anamwamini Yesu- Yohana 9.*Yesu Anawaandaa Wanafunzi Wake Juu Ya Kifo Chake- Yohana 14.*Ombi La Kikuhani La Yesu- Yohana 17.*Ushuhuda Wa Paulo: Usemi huu ni wa kuaminika, na tena unafaa kukubaliwa kabisa: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Nami ni mkosefu zaidi kuliko hao wote, lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aonyeshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uhai wa milele-1 Timotheo 1:15-16.Lazima Tumkiri Yesu Kama Bwana Na Mwokozi wa Maisha Yetu *Kila goti litapigwa- Isaya 45:16-25.*Kuokolewa Kwa Paulo- Matendo 26.*Watu Wanastahili Kuwa Kama Watoto- Mathayo. 18:1-14.*Ushuhuda Kutoka Thesalonike: Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si huko Makedonia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena hatuhitaji kusema zaidi. Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli, na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja- 1 Wathesalonike 1:8-10.*Mahubiri Ya Petro Siku Ya Pentekote- Matendo 2.*Petro Atiwa Gerezani- Matendo 4.*Yesu alisema, “Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. Lakini yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni-Mathayo. 10:32-33.*Watawala Wengi Wamkiri Yesu- Yohana 12:42-50.*Ungamo La Tomaso- Yohana 20:26-29.

Lazima Tumkiri Yesu Kama Bwana Na Mwokozi wa Maisha Yetu *Mkiri Yesu Kama Bwana- Warumi 10:9.*Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tama mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga. Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. Maandiko yasema: “MWE WATAKATIFU, KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.” Mnapomtaja Mungu, nyinyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakait wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu. Maana mnajua kwamba nyinyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu. Lakini hamkukombolewa kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu; bali kwa damu tukufu ya Kristo, asiye na doasari wala doa. Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabka ya ulimwengu kuumbwa, akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. Kwa njia yake, mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu. Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote. Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele -1 Petro 1:14-23.*Maana Maandiko yanasema: "KAMA NIISHIVYO, ASEMA BWANA, KILA MTU ATANIPIGIA MAGOTI, NA KILA MMOJA ATAKIRI KWAMBA MIMI NI MUNGU.” Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu- Warumi 14:11-12.*Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanaadamu. Akajinyenyekeza kwa kutii mpaka kufa, hata kufa msalabani. Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa, akampa jina lililo kuu kuliko majina yote. Ili kwa heshima ya jina la Yesu, VIUMBE VYOTE MBINGUNI, DUNIANI NA KUZIMU, VIPIGE MAGOTI MBELE YAKE, na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba - Wafilipi 2:7-11.

Roho Mtakatifu Na Dhabihu Ya Yesu Husafisha Mioyo Yetu *Baraza La Yerusalemu- Matendo 15.

Roho Mtakatifu Na Dhabihu Ya Yesu Husafisha Mioyo Yetu *Yeye Hutuokoa Kwa Kutusafisha Kwa Roho Wake- Tito 3:5.*Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti, wezi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang’anyi, hao wote hawatashiriki ufalme wa Mungu. Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa,

Copyright © 2007 Tammie Friberg 80

Page 84: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mkafanywa watakatifu, na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu- 1 Wakorintho 6:9-11.*Watu waliokuwa najisi kidini waliweza kutakasika na kuwa safi waliponyunyiziwa damu ya mbuzi na ng’ombe pamoja na majivu ya ndama. Lakini, kwa damu ya Kristo mambo makuu zaidi hufanyika! Kwa nguvu ya Roho wa milele, Kristo alijitolea mwenyewe dhabihu kamilifu kwa Mungu. Damu yake itatutakasa dhamiri zetu kutokana na na matendo yaletayo kifo, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai- Waebrania 9:13-14; Mambo Ya Walawi 6:14-16; Hesabu 19.

Tunafanyika Wana Wa Ibrahimu (TAZAMA CHATI HAPO JUU)

Tunafanyika Wana Wa Ibrahimu (TAZAMA CHATI HAPO JUU)

Yesu Anatufufua pamoja naye na kutupa nguvu dhidi ya pepo *Yesu Anatupa Uzima Wa Milele- Yohana 6:37-40; 17:1-8.

Yesu Anatufufua pamoja naye na kutupa nguvu dhidi ya pepo *Ambaye Alilkwenda mbinguni na sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, anatawala juu ya malaika, wakuu na wenye enzi- 1 Petro 3:22.*Vitu Vyote Viko Chini Ya Miguu Yake- 1 Wakorintho 15:24-28.*Yesu Alikuja Kuziharibu Kazi Za Shetani- 1 Yohana 3:8.*Yesu Alikufa Msalabani il kuzitwaa nguvu za pepo- Wakolosai 2:15; Waebrania 2:14-15.*Yesu ameinuliwa juu ya Nguvu zote mbinguni na duniani- Waefeso 1:20; 2:6.*Anayemwamini mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae. Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai. Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uhai wa milele nyinyi mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu- 1 Yohana 5:10-13.

Tumeamriwa kubatizwa; Tunastahili Kushiriki Meza Ya Bwana *Mwito Mkuu- Mathayo. 28:16-20.*Wanaoitumia Meza Ya Bwana Vibaya- 1 Wakorintho 11:21.*Yesu Anabatizwa- Mathayo. 3; Marko 1:1-11; Luka 3.*Filipo Alimbatiza Towashi Mwethiopia- Matendo 8: 26-38.*Petro Anambatiza Kornelio- Matendo 10.*Ludia Anabatizwa- Matendo 16:9-15.*Askari wa Gereza Aokolewa (Kuamini Huleta Wokovu, Sio Ubatizo)- Matendo 16:16-40.*Apolo Anajua Maandiko Vizuri, Lakini Alibatizwa Baadaye (Akiwa Tayari Ameokolewa)- Matendo 18:24-28.* Mwizi Msalabani Hakubatizwa, Lakini Alikwenda Paradiso Na Yesu- Luka 23:43.

Tumeamriwa kubatizwa; Tunastahili Kushiriki Meza Ya Bwana *Paulo Azungumzia Swala La Ubatizo- Warumi 6; Warumi 8.

Hakuna Anayeweza Kututoa Kutoka Katika Mkono Wa Mungu *Hakuna Anayeweza Kututoa Kutoka Mkononi Wa Baba- Yohana 10:24-30.*Mungu Huwahifadhi Wale Wanaomwamini Yesu- Yohana 17:1-13.

Hakuna Anayeweza Kututoa Kutoka Katika Mkono Wa Mungu *Tumewekwa Muhuri Na Roho Mtakatifu- Waefeso 1:13; 4:30.*Hakuna Kitu Kinachoweza Kututenganisha na Upendo wa Mungu- Warumi 8:35-39.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 81

Page 85: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 82

Page 86: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 9: Huduma Ya UpatanishoMaelezo Mafupi

Maandiko: “..mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetarajiwa na asiyetarajiwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, yumo katika yote.” “Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui. Aliindoa ile sheria pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani. Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu. “Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jingo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Katika kuungana naye, nyinyi pia mmejengwa pamoja na wote wengine, mwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake” (Wakolosai 3:10-11; Waefeso 2:14-16, 19-22).

Mfano huu ni picha ya kiroho ya huduma ya Upatanisho ambayo Mungu amewapa Wakristo hapa duniani. Yesu alipokufa msalabani na kufufuka kutoka kwa wafu, aliuvunja ule ukuta ulijengwa na dhambi, ukuta huo uliwatenganisha wanadamu na Mungu. Kwa njia hiyo aliweza kutupatanisha na Mungu. Upatanisho huu sio tu kati yetu na Mungu, bali pia ni kati yetu na watu wengine. Tunastahili kupatana na watu tunaoishi nao katika jamii, vilevile tunastahili kuwasamehe wengine kama Mungu alivyotusamehe. Tunastahili kufanya hivyo kwa sababu Mungu ametusamehe dhambi na kutupatanisha naye mwenyewe. Kuwapatanisha watu ni tendo linaloonyesha upendo mkuu na hali ya kujitoa. Pia tendo hili linaonyesha jinsi Mungu anavyotupenda. Tunapowapatanisha watu, tunaujenga ufalme wa Mungu na wala sio ufalme wetu. Tukifanya juhudi kuleta amani duniani, basi tunafanya kazi inayomletea Mungu heshima. Upatanisho maana yake ni hali ya kusuluhisha pande mbili au zaidi zilizo na ugomvi. Baada ya upatanisho, pande zinazozozana hurudi kuwa marafiki tena. Lakini hata hivyo upatanisho ni kipawa na jukumu la wanadamu. Mungu tayari amekwisha tufanyia kazi hiyo, lakini lazima turuhusu kazi hiyo ya Mungu kuleta amani katika vilindi vya mioyo yetu. Ni jambo la kushangaza kuona kwamba neno la upatanisho halikuwepo katika dini za kipagani. Upatanisho ni moja yapo ya sifa muhimu za Ukristo. Upatanisho unadhihirisha shauku ya Mungu. Yesu alisema, "Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.” (Yohana 13:35). Swali tunalopaswa kujiuliza ni hili: Je, tunawezaje kufanya huduma hii ya upatanisho katika siku hizi za chuki, uhasama, hasira, vita na kulipiza kisasi? Ili kuweza kupata jibu la swali hili, tunastahili kuangalia kile kinachosemwa na Biblia kuhusu msamaha. Katika mfano wa somo hili kuna picha za falme zote mbili zikifanya kazi katika ulimwengu wetu. Kulingana na Maandiko yaliyo katika kisanduku hapo juu, kuna picha katika sehemu ya chini, upande wa kulia wa ukurasa yenye hekalu na kuta za Wakristo wakiungana pamoja kumwabudu Mungu. Watu wa kutoka kila kabila, taifa, na rangi wameungana pamoja na kuwa kuta za Hekalu takatifu. Waumini hawa wamejengwa katika msingi wa mafundisho ya mitume na manabii kama ilivyo katika Biblia. Kanisa hili huongezeka kila siku kwa sababu waamini wanawafikia wengine na habari njema ya msamaha wa Kristo. Watu hawa ni wale ambao bado wako katika Ufalme wa Giza. Vilevile Wakristo wanaonyesha msamaha wa Yesu kati yao hao walio katika Ufalme wa Nuru, kwa kupendana na kusameheana. Wakristo sharti kwanza wapendane na kusameheana, ndipo waweze kuwafikia wengine ulimwenguni na ujumbe wa Kristo. Pia ujumbe wao kwa wale walio katika Ufalme wa Giza unatiwa nguvu na jinsi wanavyopendana na kusameheana wenyewe kwa wenyewe. Kuwapenda na kuwasamehe watu sio jambo rahisi kamwe. Lakini iwapo imani yetu haiambatani na matendo yetu basi ujumbe wetu kwa wenye dhambi utakuwa dhaifu. Yesu alisema kwamba kuabudu kwetu kunategemea uhusiano tulio nao na Wakristo wengine. Uhasama kati yetu huwa kikwazo cha ibada inayompendeza Mungu. Katika kifundisha kwake, Yesu alisema kwamba kabla hatujatoa sadaka au dhabihu ni vyema kuhakikisha kwamba tumepatana na ndugu zetu. Tukifanya hivyo tutakuwa tunafuata huduma hii ya upatanisho tuliyopewa na Mungu. Katikati ya hekalu kuna mkono wa Mungu ulionyooshwa. Mkono huu unawakilisha uwepo wa Mungu. Wakristo wote pamoja huunda mwili wa Kristo, huku uwepo wa Mungu ukiwa kati yetu. Katika vilindi vya mioyo ya Wakristo hakuna hasira au chuku, lakini kumejaa upendo na hali ya kuwajali wengine. Chini upande wa kushoto wa ukurasa huu, kuna picha ya watu wanaoishi katika Ufalme wa Giza. Kundi la kwanza la watu, lililoko upande wa kushoto linaonekana kumkasirikia Mungu, kwa sababu sheria zake zinapinga matendo yao.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 83

Page 87: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Watu hawa hawako tayari kuruhusu sheria ya Mungu kutawala maisha yao, badala yake wanaishi kama watakavyo. Vilevile watu hawa wakati mwingine huwa wanatawalwa na uchungu, hasira, na mfundo, ikiwa sio mambo hayo basi wanatawalwa na tamaa ya mali, mamlaka, anasa, na upendo usio wa kiungu. Biblia inasema kwamba, “Maana, wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya mwili, hutawaliwa na fikira za mwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya Roho Mtakatifu, hutawaliwa na fikira za Roho. Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uhai na amani. Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii. Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.” (Warumi 8:5-8). Maandiko haya yanatufunza kwamba tamaa za kibinadamu huwafanya watu kumchukia Mungu, hii ni kwa sababu yeye ametupa Sheria za kutujulisha lipi linalostahili kutendwa na lipi halifai kutendwa. Kwa upande mwingine watu hawa wamemuasi Mungu kwa kutofuata sheria zake katika Biblia na katika uumbaji wake. Matokeo yake ni kwamba watu hupenda kuasi na uadui kati ya Mungu na wanadamu huongezeka. Katika kuonyesha sifa au tabia ya Mungu, tumemwonyesha Mungu katika picha zote akiwa amenyoosha mkono wake. Hata ingawa wanadamu wamemuasi Mungu, bado amenyoosha mkono wake kupatana na watu. Biblia inasema kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, hata ingawa bado tulikuwa maadui wa Mungu (Warumi 5:8). Kifo chake kina maana kwa wanadamu wote hata ijapokuwa kila mtu ametenda dhambi katika wakati tofauti. Watu walio katika Ufalme wa Giza huwa na uadui kati yao na Mungu, na kati yao wenyewe. Hili ni moja wapo ya maswala tuliyoyajadili katika Somo la 6. Tulijifunza kwamba watu walio katika Ufalme wa Giza hupenda kujitambua kwa kutegemea kabila, rangi, mbari, taifa wanalotoka na hata kwa misingi ya jinsia zao. Sehemu ya picha inaonyesha kundi la watu likipigana na kundi lingine. Vita hivyo vinaonyesha jinsi makundi hayo yalivyojaa chuki na uhasama. Sehemu nyingine ya picha inaonyesha hasira baridi inayodhihirishwa na kuwadunisha wengine. Hasira hii imetanda kote na inasababisha hali ya watu kutoaminiana, ubaguzi, kesengenyana na kuwaharibia majina wengine. Hata ijapokuwa kuna mambo mengine yasiyozungumzwa kwa maneno, kuna lugha ya mwili au ishara na hata mawazo yanayowatenganisha watu na wenzao. Vita na mafarakano hutokea wakati watu wanaposengenyana na kuharibiana majina; kwa sababu ya kuwadunisha au hata kwa njia ya fujo au vita. Mifano hii yote sio mizuri, kwa sababu mambo haya maovu husambaa kama sumu au ugonjwa wa saratani miongoni mwa watu.

Chanzo cha uhasama na chuki baina ya watu ni dhambi. Vita na chuki hutokea kati ya watu wakati wanapozivunja sheria za Mungu kama jamii au kama mtu binafsi. Mtu anapomtenda dhambi mtu mwingine, uadui na ukatili huingina kati ya watu hao. Ikiwa hali hii haitasuluhishwa, watu hawa huanza kuwa maadui, na shina la uchungu huchipuka na kuenea kwa watu na hatimaye watu hao huanza kupigana. Katika lugha ya Kiebrania neno linalowakilisha uadui lina uhusiano wa karibu na neno lenye maana ya adui. Uadui maana yake ni kutuoaminiana, kutengana, au uhasama. Watu huwatendea wengine maovu kwa sababu kadhaa mbalimbali. Kwa mfano wanaweza kuchochewa na ubinafsi, faida ya kibinafsi, ubaguzi, hamu ya kulipiza kisasi, anasa, wivu, ulafi na tamaa au hata hamu ya mamlaka. Ubinafsi ndicho chanzo hasa cha kila aina ya uhasama. Hasira yaweza kuwafanya watu kuwaangalia wengine kwa mtazamo fulani mbaya, halafu wakaanza kuwafanyia vibaya wakifikiria kwamba kwa kufanya hivyo wanafanya jambo lililo sawa na la haki.

Ukatili au asili yake vyaweza kumalizika iwapo mtu atakuwa na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Swali tunalostahili kujiuliza ni hili: Wakristo walio pichani wanaweza kuwasamehe wengine kwa njia gani? Msamaha ni jambo gumu kwa sababu ya dhambi iliyokita mioyoni mwetu na pia kwa sababu ya hamu ya kutaka kuona haki ikitendeka. Mungu amejaa huruma. Yeye ametoa njia ya kuwasaidia watu kupokea amani na uponyaji kutoka kwake.

Yesu anatuhimiza tuwapende watu na kuwasamehe kama yeye alivyowapenda na kuwasamehe. Juu ya ukurasa kuna picha inayoonyesha jinsi msamaha na upatanisho ulivyokuwa ukipokewa katika Agano la Kale na Agano Jipya. Haya ndiyo mambo ambayo waamini walioonyeshwa kwenye picha huyatafakari na kuyakumbuka kadri wanavyoishi hapa duniani. Waamini hawa kila siku hukabiliana na watu waliojaa uchungu, wasiosamehe wenzao, wenye chuki, na hasira. Wakati mwingine ni rahisi sana kufanya mambo yale yale yanayofanywa na watu walio katika Ufalme wa Giza. Lakini sisi kama Wakristo waliosamehewa na Mungu, lazima tujitahidi kuishi sawa na vigezo vya Mungu. Hasira ile ambayo waamini wanastahili kuionyesha ni ile hasira nzuri ambayo lengo lake nikubadilisha hali ya dhambi duniani au miongoni mwa watu. Ukiangalia picha, kwanza kabisa utaona madhabahu upande wa juu kushoto. Madhabahu hii ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na wana wa Israeli kumtolea Mungu dhabihu. Katika enzi hizo msamaha ulihitaji dhabihu ya damu. Dhabihu hiyo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 84

Page 88: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ilitolewa ili kufunika na kuwasafisha watu kutokana na dhambi zao. Tendo hili la kutoa dhabihu liliitwa kufanya upatanisho. Dhambi au sababu ya mtu kutenda kosa ilipoondolewa kwa tendo la upatanisho, hakukuwa na uadui tena kati ya Mungu na mtu huyo. Kutoa dhabihu safi kwa ajili ya kitu kisicho kisafi kulionyesha jinsi kutoa dhabihu ya msamaha kulivyokuwa kugumu. Dhabihu sio kitu cha rahisi. Vilevile dhabihu ya kuondoa dhambi sio kitu rahisi! Dhabihu ilikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Wakati mwingine lazima tukabiliane na ugumu huo sisi wenyewe kwa sababu itatubidi ile hali ya kutaka kulipiza kisasi tuitoe kama dhabihu kwa Mungu ili tuwapende wengine kama Yesu alivyowapenda. Kwa kweli hili si jambo rahisi kamwe. Lazima tuamini kwamba Mungu atatenda haki katika kila hali na kwa wakati ufaao, na sisi sharti tufanye lile linalostahili. Mara nyingi, tunalipiza kisasi na kwa kufanya hivyo mzunguko wa chuki na kisasi huanza kuenea na kuwaathiri wengine vibaya mpaka nao wakatamani kulipiza kisasi. Kulipiza kisasi kunaweza kuleta migawanyiko mingi kanisani. Watu husameheana wakati kila mmoja wao anapoziweka madhabahuni hamu zao za kutaka kulipiza kisasi. Njia moja wapo ambayo Mungu aliwaagiza watu wa enzi za Biblia kufanya ili kusamehewa dhambi ni ile ya kumtumia mbuzi au beberu kubeba dhambi za watu. Ukitazama picha hii utaona kundi la watu likimwekea mikono beberu. Watu walipomwekea mikono huyo beberu, iliashiria kuondolewa kwa dhambi zao na kupakaziwa yule beberu. Baada ya kila mtu kumwekea mikono, mbuzi huyo aliachiwa huru kuyoyoma nyikani kwenda kufa. Tendo hili lilikuwa ishara ya kuziondoa dhambi, na kwa sababu hiyo uhasama baina ya watu na Mungu, na watu na watu uliweza kuondolewa. Mbuzi huyu alipewa jina na kuitwa beberu aondoaye dhambi, kwa sababu beberu huyo asiye na hatia ndiye aliyebeba adhabu ya wanadamu ya dhambi. Neno msamaha lina uhusiano wa karibu na tendo hili. Linamaanisha kufunika au kuondoa kabisa. Hii ni njia nzuri za kutusaidia kufikiria juu ya msamaha wakati kunapotokea uhasama kati ya watu au kati ya makabila. Vivyo hivyo sisi sharti tuitupilie mbali dhambi ili kusiweko na uhasama wa aina yoyote. Sisi kama waamini tunaweza pia kuyaondoa makosa ya watu kutoka akilini mwetu na mioyoni mwetu, tukifanya hivyo tutakuwa tumewasamehe. Tukianza kuwachukulia wengine kama watu waliosamehewa, basi wazo la kutaka kulipiza kisasi litaondoka. Njia moja ya kuweza kupoza hasira ni kuchukua mawazo yetu na kuyaelekeza kwingine pindi tunapokasirika. Unaweza kwa mfano kuwazia picha ya mvua inayonyesha na kuzima moto wa hasira, badala ya kufikiria juu ya kosa tulilotendewa. Wakati tunayaondoa mawazo ya kosa tulilofanyiwa, basi tunaweza sasa kuwasamehe wengine. Wakati mwingine kumsamehe mtu ni sawa na kufunga safari ndefu. Hii ni kwa sababu inachukua muda kwa hasira ya mtu aliyekosewa kupoa na kuweza kumsamehe mkosaji. Hata hivyo wakati mwingine inabidi watu walipe fidia iwapo kosa linahusu uharibifu wa kitu fulani cha mtu huyo. Katika Biblia kuna tofauti ya jinsi watu wa Agano la Kale walivyokabiliana na maadui na jinsi watu wa Agano Jipya walivokabiliana nao. Katika enzi za Agano la Kale, maadui wa Israeli vilevile walikuwa maadui wa Mungu. Maadui wa Israeli walitumikia miungu wengine. Kwa hiyo maadui wa aina hii walikuwa wa kidini, wala sio tu maadui wa kisiasa. Lakini katika Agano Jipya, Yesu alitufundisha kwamba, badala ya kuwapenda marafiki zetu na kuwachukia maadui zetu, tunastahili kuwapenda maadui zetu na kuwaombea kama tuwaombeavyo marafiki zetu. Yesu alitupa changamoto tuwe wakamilifu, au tukomae, kama Mungu alivyo mkamilifu katika uwezo wake wa kuwapenda maadui wa kibinadamu. Yesu alitumia mifano ya mambo ya asili, kwamba Mungu hunyeshea mvua watu wabaya na wazuri. Tunastahili basi kuwaonea huruma watu wengine kama Mungu atuoneavyo huruma. Wakati umefika wa kanisa kuinuka na kutoa viongozi waliokomaa katika jamii zetu. Kuwaleta watu katika Ufalme wa Nuru, ndiyo njia bora zaidi ya kukabiliana na uadui na ukatili wa wanadamu.

Kitu cha mwisho kilichoonyeshwa katika picha hii ni msalaba. Yesu ndiye mfano wetu wa kuiga kwa sababu tuko chini ya Agano Jipya. Yesu alipokufa msalabani, alifanyika kuwa dhabihu ya kutuondolea dhambi zetu. Yeye alitimiza matakwa ya Sheria kwa kujitoa yeye mwenyewe kama Mwanakondoo wa Mungu asiye na ila, ili kuondoa dhambi za wanadamu wote. Sheria haikuweza kutosha kuondoa hatia au dhambi moyoni kabisa. Lakini dhabihu ya Yesu ilikuwa kamilifu na ilitosha kuondoa dhambi zote kabisa. Yesu aliteseka nje ya mji kama vile beberu wa kuondoa dhambi alivyoachwa kuteseka na kufia nyikani. Kifo cha Yesu nje ya mji ilikuwa ishara ya kuzitupa dhambi zetu mbali kabisa, kama beberu wa kuondoa dhambi alivyoachwa kwenda nyikani.

Changamoto tuliyonayo kama Wakristo ni kwamba jinsi Yesu alivyotufia msalabani sisi watu tuliokuwa hatustahili, vivyo hivyo tunastahili kusameheana sisi kwa sisi. Unakumbuka maneno ya Yesu wakati alipopigwa vibaya na kusulubiwa msalabani? Yesu alisema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya” (Luka 23:34). Je, unajua kwamba kuna viongozi wawili katika Biblia waliofuata mfano wa Yesu wa kusamehe kwa njia hii? Stefano alipokuwa akipigwa mawe kwa sababu ya ushahidi wake, alimwomba Mungu kutowaalaumu kwa sababu ya dhambi hiyo (Matendo 7:60). Naye Paulo ambaye alikuwepo wakati Stefano akipigwa mawe (baadaye alikuja kuwa Mkristo), alikuja

Copyright © 2007 Tammie Friberg 85

Page 89: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kuwasamehe Wakristo waliomwacha kwa sababu ya hofu (2 Timotheo. 4:16). Msamaha wa aina hii hutekelezwa na waamini waliokomaa kiroho, waamini ambao wanauona ulimwengu kwa mtazamo wa Mungu. Shauku ya Mungu ni kwamba watu wote waingie katika Ufalme wake. Yeye alimtuma Mwanawe awe dhabihu ili watu waingie katika Ufalme wake. Jambo hili sio rahisi. Vilevile Mungu ametupa kazi ya kuhubiri Habari Njema ya Wokovu kwa ajili ya wale walio katika Ufalme wa Giza. Hii haimanishi kwamba sio muhimu kwa watu kupewa haki yao kwa njia ya mahakama. Bado kuna hukumu ikiwa tutatenda dhambi za kuwakandamiza wanadamu. Hata hivyo katika ulimwengu wa kiroho lazima tujifunze kusamehe kama Mungu anavyowasamehe wale wamwombao. Tunaweza kumwomba Mungu ili haki itendeke duniani, na kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu ataleta haki kwa wakati wake.

Mtume Paulo anaelezea vizuri swala hili anaposema kwamba kwa Yesu, “… vitu vyote vilipatanishwa na Mungu: na kwa damu yake msalabani akafanya amani na vitu vyote duniani na mbinguni. Hapo kwanza nyinyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu. Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.” (Wakolosai 1:20-22). Tambua kwamba Paulo anasema vitu vyote duniani na mbinguni! Yesu alitupatanisha ili tuwe watakatifu na wakamilifu mbele ya Mungu, na pasipo lawama yoyote! Shauku yake ni kwamba tuishi maisha matakatifu na makamilifu hapa duniani kwa kuwapenda maadui zetu. Lakini pamoja na hayo lazima tuwe tayari kufunika dhambi za wengine ili tuweze kumpendeza Mungu. Watu wanaweza kuwa hawastahili kusamehewa, lakini kwa sababu ya kutaka kukomaa katika Kristo na kudhihirisha kazi aliyoifanya msalabani, lazima tuwasamehe wengine kama njia moja ya kumtii Mungu. Tusitegemee kuwasamehe watu wengine kwa kutarajia kwamba nao watatusamehe, bali tuwasamehe bila masharti yoyote. Kwa njia hii upatanisho unaweza kuwa rahisi kwa sababu hautegemei matendo ya mtu, bali shauku ya kutaka kumpendeza Mungu kwa kumtii. Mtume Petro alisema kwamba tunasafisha mioyo yetu na kuwapenda wengine kwa sababu ya kumtii Mungu.

Siku moja Mtume Petro alimwuliza Yesu iwapo mtu alistahili kumsamehe mwingine mara ngapi. Yesu alimjibu kwa kusema, “Msamehe mara sabini mara saba.” Yesu aliposema hivyo, hakuwa na maana ya kutoa idadi kamili ya mara ngapi tumsamehe mtu, badala yake alitaka kuanzisha mazoea ya kusameheana kati ya wanafunzi wake. Yesu alitoa uhai wake bure, vivyo hivyo pia sisi tunastahili kuwasamehe wengine kwa msamaha ule unaowiana na kifo cha Yesu msalabani. Lazima tukumbuke kwamba kile Mungu anachotaka kukiharibu, hatustahili kukihifadhi kwa vyovyote vile. Ukatili kwa kawaida hudumu katika mioyo ya watu wale wasiotaka kuwasamehe wengine inavyotakiwa. Ukatili wa watu hao huzidi kadri wanavyoendelea kutofuata sheria za Mungu kuhusu jamii. Msamaha unaweza kutatizwa na watu ambao hawako tayari kubadilisha tabia zao mbaya, au wasio tayari kuwasamehe wengine. Watu wengine ni kama wakusanyaji taka, hii ni kwa sababu hurundika pamoja yale yote waliyotendewa na watu, na hawasahau au kuyatupilia mbali mabaya waliyotendewa. Ni vyema tuwe tayari kuwasamehe watu watakaokuja kwetu kuungama makosa yao na kuomba msamaha. Vilevile ni vyema kuwaacha wengine kukomaa kwa kutoyakumbuka makosa yao. Kuna sababu mbalimbali zinazotufanya tuteseke duniani. Wakati mwingine tunateseka kwa kupenda wenyewe. Hii ina maana kwamba tumejiletea dhiki wenyewe kwa kufanya makosa fulani au kutokuwa na busara. Hata hivyo wakati mwingine tunateseka bila sababu yoyote. Inawezekana tukateseka kutokana na makosa ya watu wengine au hata kwa kusingiziwa mambo fulani. Lakini kile tunachostahili kukumbuka ni kwamba mateso yote yanaweza kuleta ukombozi wa aina fulani. Mateso yaletayo ukombozi yanaweza kuwafaidi wengine au hata sisi wenyewe kwa njia moja au nyingine. Mateso yanaweza kusafisha njia zetu ili tuweze kumpendeza Mungu na kuwa watu wazuri nyumbani na katika jamii kwa jumla. Kwa wale wanaompenda Mungu kwa dhati, Mungu anaweza kugeuza mateso yao, yakaleta faida katika maisha yao. Sisi kama Wakristo tunaweza kuishi kwa kutegemea ahadi hiyo ya Mungu pamoja na tumaini lake.

Chini ya msalaba katika mchoro wetu, utaona picha ya pete na pesa. Sababu moja wapo inayotufanya sisi Wakristo tusipokee uponyaji kama inavyostahili ni kwamba tumepoteza maana ya kusameheana na kulipana mema. Tunaruhusu kuta ziendelee kudumu kwa sababu hatujakomaa kiiamani hadi kufikia kiwango cha kuzivunja, au kiburi chetu kinatufanya kutoona kuta hizo kuwa tatizo. Lazima tung’oe magugu pamoja na mizizi yale, vinginevyo yatachipuka tena. Hebu sasa tulingalishe visa viwili kutoka katika Biblia. Kisa cha kwanza ni kile cha Mwana Mpotevu. Mwana Mpotevu alirudi kwa babaye baada ya kuponda mali zake zote kwa anasa na kila aina ya starehe. Wakati alipokuwa akirudi nyumbani, babake alimwona kwa mbali, akaenda mbio na kumkumbatia. Mwana huyu alikiri kwa babaye makosa aliyoyatenda. Kurudi kwake nyumbani kulikuwa ishara ya kutubu kwake. Baba mtu kwa upande wake alimrejesha katika hadhi aliyoistahili. Ikiwa hata wewe umekuwa ukitamani kurejeshwa upya, basi bila shaka unajua

Copyright © 2007 Tammie Friberg 86

Page 90: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

shauku inayoletwa na jambo hilo. Watu wengine wanaweza kushindwa kabisa kumsamehe mtu, na badala yake wakaendelea kuishi na uchungu mioyoni mwao kwa muda mrefu, au hata kwa miaka mingi. Hawawezi kamwe kumrudishia mtu aliyewakosea hadhi yake kama zamani. Jambo la kwanza kwao ni kuwaadhibu hao waliowakosea. Lakini katika kisa hiki baba mtu alimsamehe mwanawe na kumrejesha katika hadhi yake kama zamani. Alimkaribisha nyumbani, na vilevile akampa heshima ya uana. Alimpa hadhi yake kwa kumvisha pete. Pia alimwandalia karamu kubwa sana. Pete ile iliyoonyeshwa katika picha inaonyesha jinsi tunavyostahili kuwarudishia watu hadhi yao. Ni baraka iliyoje ikiwa tutafuata mfano wa Yesu kwa kuwarudisha watu katika hadhi yao hata ikiwa wamefanya makosa kiasi gani! Kukataa kuwapatanisha watu na kuwarudisha katika heshima waliyokuwa nayo zamani, kunadumisha kuta na ukatili baina ya watu.

Jambo la pili ambalo sisi husahau kulitekeleza ni kuwalipa fidia watu tuliowadhulumu. Ile picha ya pesa inatukumbusha jinsi tunavyostahili kuwalipa watu tuliowadhulumu. Pengine tunaweza kujifunza kwa mfano wa Zakayo mtoza ushuru. Yeye alikuwa mtoza ushuru katika enzi za Yesu. Watoza ushuru walichukiwa sana enzi hizo kwa sababu walikuwa wakiwatoza watu zaidi ya kiwango kilichowekwa. Jambo hili liliwafanya watu kuwa maskini sana. Lakini siku moja Zakayo alimwona Yesu akija na akakimbia mbele na kupanda mkuyu ili aweze kumwona. Yesu alipopitia njia hiyo alimwambia Zakayo ashuke chini, na baadaye Yesu akaenda kula karamu nyumbani kwa Zakayo. Zakayo alifurahi kusamehewa na Yesu, na akaahidi kuwalipa fidia wale wote aliowadhulumu kwa kuwatoza ushuru uliozidi kiwango kilichowekwa. Aliwalipa mara nne zaidi ya zile pesa alizowaibia kwa sababu alisikitika sana kwa kuwadhulumu watu jinsi hiyo. Kwa hiyo tunapowadhulumu watu , tunahitaji kuwalipa fidia! Wakati mwingine kama watu wangeacha kubishana juu ya nani mwenye makosa na nani hana makosa, na badala yake kuwalipa fidia au kurudisha uhusiano, basi tungeponya mambo mengi kati ya watu. Hata hivyo kuna mambo mengi ambayo hatuwezi kuwafidia watu, lakini ni lazima tujitahidi tuwezavyo kuwafidia. Watu wengine wamejaa uchungu na chuki nyingi hivi kwamba mtu yoyote anayewakumbusha mtu aliyewakosea, basi mtu huyo anaweza kuchukuliwa vibaya kwa sababu ya kumbukumbu hiyo. Watu wa jinsi hiyo bado hawajaielewa kazi ya Yesu ya upatanisho pale msalabani. Hawaitilii maanani kazi aliyoifanya Yesu kwa ajili yao. Yamkini ndiposa Yesu alisema, “Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia. Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu” (Mathayo 6:14-15).

Kama Yesu alivyotusamehe bure na kuturudisha upya, sisi pia tunastahili kuwasamehe wengine na kuwarudisha upya. Lazima tuwafanyie watu vitu bila malipo yoyote. Katika Biblia Yesu alisimulia kisa cha mtumwa mmoja ambaye hakumsamehe deni mwenziwe. Basi mfalme alimsamehe deni lake, lakini yule mtumwa hakuwa tayari naye kumsamehe mdeni wake. Badala yake alienda kumshika koo na kumwamrisha kumlipa. Mfalme alipoyasikia hayo, alimwita yule mtumwa na kumwadhibu vibaya. Yesu alinukuu maneno ya yule mfalme na kusema, “Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia? Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote”(Mathayo 18:33-35). Yesu alijitoa kama sadaka sana ili sisi tuweze kupatanishwa na Mungu na wanadamu wenzetu! Tendo hili lilikuwa la gharama kubwa mno! Kwa hiyo tusichukulie jambo hili kwa juujuu au kwa njia ya unafiki kwa kutowasamehe wengine kama sisi wenyewe tulivyokwisha samehewa na Mungu. Mtume Paulo alijua wazi kwamba kanisa la kwanza lilikuwa na shida katika swala zima la kupendana. Naye aliwaombea mara kwa mara wale waliokuwa chini ya ulinzi wake, kwamba upendo wao uzidi kukua zaidi na zaidi. Katika 1 Wathesalonike 3:12-13, anasema hivi, “Bwana awawezeshe nyinyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda nyinyi. Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake. Lazima tumwombe Mungu ili tukomae katika kuwapenda wengine kwa upendo wa Mungu, vilevile upendo huu ukue katika watu wa jamii yetu na ulimwenguni kwa jumla. Kwa hiyo ikiwa kuna uhasama kati ya waamini kanisani, watu wanahitajika kuungama, kumwomba Mungu, na kutubu, vilevile wanastahili kuwalipa fidia watu waliowadhulumu na pia kuwarejesha upya katika hali zao. Yakobo alisema katika Biblia kwamba tunahitaji kuungamaniana dhambi zetu na kuombeana ili tupate kuponywa (Yakobo 5:16). Ikiwa moja ya mambo haya yameachwa nje, basi linabaki shina la uchungu lisiloweza kupona vizuri. Viongozi sharti wahamasishe watu kuwasiliana wao kwa wao. Watu sharti wawahukumu watu kulingana na ukweli uliopo na wala sio kwa kutegemea uvumi. Uvumi huzidisha chuki na mafarakano kati ya watu. Kwa kawaida pande zote mbili huwa zina makosa, kwa hiyo kila mtu sharti azingatie na kupitia hatua hizi. Wakati mwingine itabidi kuwe na mwombezi wa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 87

Page 91: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mambo hayo. Viongozi pia kama watu wengine wanastahili kupatanishwa na wengine. Kila kiongozi sharti afuate mwongozo ule ule wanaowafundisha wengine kanisani. Wasihubiri mambo wasiyoyatenda wao wenyewe.

Ukitazama picha utaona jinsi waamini wanavyotiana moyo, huku wakiwa wameshikana mikono. Wote wanasalimiana, hakuna yoyote aliyeachwa nje. Watu hawa wote wanabebeana mizigo. Wanafuata upendo ule ule ulio katika Kristo Yesu. Wanajali maslahi ya wengine na wala sio tu kujitakia mazuri wao wenyewe. Matendo haya yote ya upendo huleta uponyaji na kuhuishwa upya katika kanisa. Kumbuka kwamba huduma ya upatanisho maana yake ni kutenda au kuwatendea wengine yale ambayo Yesu amewatendea watu wote. Hili ndilo linalostahili kuwa ombi letu kwa makanisa na kwa Wakristo ulimwenguni kote. Njia rahisi ya kuweza kusitisha hali ya kulipizana kisasi ni kuchagua kutenda yale yaliyo sawa hata ikiwa wengine wote wanatenda yale yaliyo kinyume. Ukifanya hivyo Mungu atauona uaminifu wako katika kuzitii sheria zake. Yeye tu ndiye anayeweza kuyageuza mambo mabaya au hali mbaya na kuwa nzuri na kutupatia matumaini ya kuingia mbinguni, ambalo ndilo jambo muhimu kushinda hali zote zinazotukumba. Sharti tujitoe kuwapenda na kuwasamehe wengine kama Yesu alivyotupenda na kutusamehe. Kwa njia hii tutaweza kuishi maisha bora katika jamii. Ushinde uovu kwa kutenda mema (Warumi 12:18-21).

Mafundisho Ya Somo La 9Ufalme wa Giza/Ulimwengu Ufalme wa Nuru/Kanisa

Uadui, Migawanyiko, Ukatili, Hasira Huduma Ya Upatanisho-Kuwafanya Kuwa na Uhusiano MzuriUkatili Dhidi Ya Mungu Au Watakatifu wake Waamini Huungana Pamoja Na Kuwa Makao Ya Mungu

- Ondoleo La Dhambi Katika Agano La Kale (Kulipa fidia); Ukombozi (Kununua tena); Msamaha (Kutupilia Mbali)

- Dhabihu

Kazi YetuHuduma Ya Upatanisho Kuwatoa Watu Kutoka Katika Ufalme wa Giza Hadi Katika Ufalme Wa Nuru, Kuwapatanisha Watu Na Mungu.

Within the Church:

Mbuzi Azibebaye Dhambi

Ondoleo La Dhambi Katika Agano Jipya

Dhabihu Ya Yesu

Taratibu Iliyopuziliwa Mbali

Kuungama Makosa Yetu Kwa wale Tuliowaumiza

Kumrejesha Mwenye Dhambi Katika Hali Yake Ya Zamani

Mwenye Dhambi Kulipa Fidia Kwa Wale Aliowaumiza

Marejeo Ya Mafundisho Ya Biblia Kwa Somo La 9

Ufalme Wa Giza/UlimwenguHadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Uadui, Migawanyiko, Ukatili, Hasira *Stefano Apigwa Mawe- Matendo 7.*Elihu Akasirishwa Na Ayubu- Ayubu 32:2-3.*Kisa cha Mwana Mpotevu- Luka 15:27-28.*Naamani Akasirika Kwa Yale Aliyotumwa Kufanya- 2 Wafalme 5.*Kisa Cha Esau Na Yakobo- Mwanzo 27:41.*Bwana Akasirishwa Na Kuabudu Sanamu Kwa Waisraeli- Waamuzi 10:6-7.*Mungu Akasirishwa Na Jinsi Sulemani Alivyokuwa Na Moyo Uliopenda Kotekote- 1 Wafalme 11:9.*Mungu Akasirishwa Na Manung’uniko- Hesabu 11.*Mungu Akasirishwa Na Watu Wenye Mioyo Migumu- Marko 3.*Musa Anawaombea Watu- Kutoka 32.*Yonathani Akasirishwa Na Kisasi Cha Babake Kutaka

Uadui, Migawanyiko, Ukatili, Hasira *Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawataupata ufalme wa Mungu uwe wao- Wagalatia 5:19-21.*Hapo kwanza nyinyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu. Lakini sasa, wka kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa wakatifu, safi na bila lawama- Wakolosai 1:21-22.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 88

Page 92: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kumwua Daudi- 1 Samueli 20:33-34.*Mungu Akasirishwa Na Uuzaji Wa Watoto- Nehemia 5.*Yeremia Azungumzia Juu Ya Gadhabu Ya Mungu Dhidi Ya Dhambi- Yeremia 32.*Yusufu Anachukiwa na Ndugu Zake- Mwanzo 37.*Chuki Ya Amnoni- 2 Samueli 13.Kumchukia Mungu Na Kuwachukia Wenye Haki *Yona Amkasirikia Mungu- Yona 3-4.*Nebukadneza Agadhabishwa na Vijana Watatu Wenye Haki- Danieli 3:18-19.*Hasira Ya Hamani- Esta 3:5-6.*King Herod- Mathayo 2:16.*Herodia Akasirishwa Na Yohana Mbatizaji- Marko 6:18-19.*Maisha Ya Nyumani Ya Sauli- Matendo 26:11.*Yoshua Na Kalebu Wasimama Upande wa Mungu- Hesabu 14:10.*Mafarisayo Wamtendea Ukatili Yesu- Luka 11:53-54.*Yesu Anatufunza Kuwapenda Maadui Zetu- Mathayo 5:43-48.

Kumchukia Mungu Na Kuwachukia Wenye Haki *Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe. Lakini mwenye kuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu- Yohana 3:20-21.*"Kama ulimwengu ukiwachukia nyinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi. Kama mngalikuwa watuw a ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda nyinyi kama watu wake. Lakini kwa vile nyinyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, wka sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niliyowaambieni: mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia- Yohana 15:18-20.*Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kwua rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu. Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: “Roho ambaye Mungu ameweka ndani yetu ana wivu mkubwa”- Yakobo 4:4-5.*Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii. Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu- Warumi 8:7-8.*…ambao walimwua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!- 1 Wathesalonike 2:15.*Mwovu hula njama dhidi ya mwadilifu, na kumsagia meno kwa chuki. Lakini Mwenyezi-Mungu humcheka mwovu kwani ajua mwisho wake u karibu. Waovu huchomoa panga na kuvuta pinde zao, wapate kuwaua maskini na fukara; wawachinje watu waishio kwa unyofu. Lakini panga zao zitawapenya wao wenyewe, na pinde zao zitavunjwavunjwa- Zaburi 37:12-15.*Watu wote watawachukieni nyinyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka- Mathayo 10:22; Marko 13:13.*Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo wala msikate- Waebrania 12:3.

Ufalme Wa Nuru / KanisaHadithi Zinazoambatana na Somo Maandiko Yanayoambatana na Somo

Huduma Ya Upatanisho-Kuwafanya Kuwa na Uhusiano Mzuri *Mwana Mpotevu- Luka 15.*Yusufu Anawasamehe Ndugu Zake- Mwanzo 45-50.*Yakobo Na Ndugu Yake Esau Wapatana tena- Mwanzo 32-33.

Huduma Ya Upatanisho-Kuwafanya Kuwa na Uhusiano Mzuri *Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye. Ndiyo kusema: Mungu, amekuwa akiupatanisha ulimwengu naye kwa njia ya Kristo, bila kutia maanani dhambi dhambi zao binadamu. Yeye ametupa ujumbe kuhusu kuwapatanisha watu naye. Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi nyinyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu- 2 Wakorintho 5:18-20.*Maana, tulipokuwa bado adui zake, Mungu alitupatanisha naye kwa kifo cha Mwanae. Na kwa vile sasa tumepatanishwa naye, ni dhahiri zaidi kwamba tutaokolewa kwa uhai wa Kristo. Wala si hayo tu, ila tunafurahi pia katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 89

Page 93: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ambaye ametupatanisha na Mungu- Warumi 5:10-11.*Yesu Amevunja kila kizuizi kilichowatenganisha wanadamu na Mungu- Waefeso 2.*Kwa sababu hiyo, tulimsihi Tito aliyeianza kazi hiyo awasaidieni pia mwitekeleze huduma hii ya upendo. Nyinyi mna kila kitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia mwe wakarimu katika huduma hii ya upendo. Siwapi nyinyi amri, lakini nataka kuonyesha jinsi wengine walivyo na bidii ya kusaidia ili nipate kujua jinsi upendo wenu ulivyo wa kweli. Maana, nyinyi mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo: yeye, ingawa alikuwa na kila kitu, alijifanya maskini kwa ajili yenu, ili kutokana na umaskini wake, awatajirishe- 2 Wakorintho 8:6-9.

Waamini Huungana Pamoja Na Kuwa Makao Ya Mungu *Miili Yetu Ndiyo Hekalu La Mungu- 1 Wakorintho 3:16-17; 6:19-20.*Mungu Na Mwanakondoo (Yesu) Ndio Hekalu Mbinguni- Ufunuo 21:22.

Waamini Huungana Pamoja Na Kuwa Makao Ya Mungu*Kwa maana yeye ndiye amani yetu; yeye aliyetufanya tuwe jamii moja, akavunjavunja ule ukuta wa uadui uliotutenga kwa kuifuta ile sheria na amri zake na kanuni zake alipoutoa mwili wake. Alifanya hivyo ili aumbe taifa jipya kutokana na jamii mbili: Wayahudi na watu wa mataifa, na hivyo alete amani. Kwa kutoa mwili wake pale msalabani, ali patanisha jamii zote mbili na Mungu; na kwa njia hiyo akaua ule uadui uliokuwepo kati yao. Alikuja akahubiri amani KWENU NINYI WATU WA MATAIFA AMBAO MLIKUWA MBALI NA MUNGU, NA PIA KWA WALE WALIOKUWA KARIBU NA MUNGU. Kwa maana, kwa kupitia kwake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa, tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. Ndani yake yeye, jengo lote limeunganishwa pamoja na kusimamishwa kuwa Hekalu takatifu la Mungu. Katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaishi kwa njia ya Roho wake- Waefeso 2:14-22.

*Kama mkipendana hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu- Yohana 13:35.

*Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu ambao hakuna mtu awezaye kuwahesabu: watu wa kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakisema kwa sauti kuu, “Ukombozi hutoka kwa Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo!'”- Ufunuo 7:9-10.

Upatanisho Katika Agano La KaleOndoleo La Dhambi (Kulipa Kufidia) *Dhabihu Za Kuondoa Dhambi- Kutoka 29-30; Mambo Ya Walawi 1-17; 26:41-43.*Musa Anatoa Dhabihu Ya Ondoleo La Dhambi Kwa watu- Kutoka. 32.*Fidia/Kurejeshwa- Mambo Ya Walawi 6:4.*Mungu Anaahidi Kuwarejesha Upya Wenye Dhambi- Kumbukumbu 30; Yeremia 15:16; 27:22; 29:14.

Ondoleo La Dhambi (Kulipa Kufidia*Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu Wa Israeli, asema hivi: Rekebisheni mienendo yenu yenu na matendo yenu, nami nitawaacha mwendelee kukaa mahali hapa. Msitumainie maneno maneno haya ya uongo: “Hili ni hekalu la Mwenyezi-Mungu, hekalu la Mwenyezi-Mungu, naam hekalu la Mwenyezi-Mungu.” Ila kama mkibadili mienendo yenu na matendo yenu, mkitendeana haki kwa dhati; kama mkiacha kuwadhulumu wageni, yatima au wajane au kuwaua watu wasio na hatia katika nchi hii; kama mkiacha kuabudu miungu mingine na kujiangamiza wenyewe, basi mimi nitawaacha daima make mahali hapa, katika nchi niliyowapa wazee wenu tangu zamani- Yeremia 7:3-7.*Unifanye nifurahi tena kwa kuniokoa, utegemeze ndani yangu moyo wa utii. Hapo nitawafunza wakosefu njia yako, nao wenye dhambi watarudi kwako- Zaburi 51:12-13.*Zaburi Ya Urejesho- Zaburi 80.*..na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani- Zaburi 23:3.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 90

Page 94: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Dhabihu Ya Ukombozi (Kununua tena)*Sheria Za Ukombozi- Mambo Ya Walawi 25.*Boazi Amkomboa Ruthu- Ruthu 4.*Yeremia Akomboa Shamba- Yeremia 32.

Dhabihu Ya Ukombozi (Kununua tena)*Ee, Israeli umtumainie Mwenyezi-Mungu, maana kwake Mwenyezi-Mungu kuna fadhili, kwake kuna nguvu kubwa ua kutukomboa - Zaburi 130:7.

Mbuzi Azibebaye Dhambi (Kuzitupilia Mbali)*Dhabihu Ya Kuondoa Dhambi Hutolewa Nje Ya Kambi- Kutoka 29:14; Mambo Ya Walawi 4:12.*Mbuzi Abebaye Dhambi Kwenda Kuzitupilia Mbali- Mambo Ya Walawi 16.

Mbuzi Azibebaye Dhambi (Kuzitupilia Mbali)*Nyama za hao wanyama ambao damu yao huletwa na kuhani mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu kama dhabihu ya dhambi, huchomwa nje ya kambi. Kwa hiyo Yesu naye aliteswa nje ya mlango wa mji ili awatakase watu kwa damu yake. Kwa hiyo tum wendee nje ya kambi, tukashiriki aibu aliyostahimili - Waebrania 13:11-13.*Wewe, ee Bwana, u mwema na mwenye kusamehe; mwingi wa fadhili kwa wote wakuombao- Zaburi 86:5.

Upatanisho Katika Agano Jipya

Dhabihu Ya Yesu*Yesu Ndiye Mfalme wa Amani- Isaya 9:6.*Kisa Cha Ibrahimu na Isaka, Mungu Ampa Ibrahimu Kondoo wa Sadaka- Mwanzo 22.*Habari za Dhabihu Ya Yesu- Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19.

Dhabihu Ya Yesu*Kila mfanyalo kifanyike kwa upendo- 1 Wakorintho 16:14.*Mafundisho Juu Ya Dhabihu Ya Yesu- Waebrania 7-10.*Hakika katika sheria, karibu kila kitu hutakaswa kwa damu; na pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi- Waebrania 9:22.

Ondoleo La Dhambi (Kulipa Fidia) *Abigaili Alipa Fidia- 1 Waebrania 25:18.*Yesu Ndiye Ondoleo La Dhambi- Waebrania 7-10.

Ondoleo La Dhambi (Kulipa Fidia) *Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo, akatufanya tukae pamoja naye katika makao ya mbinguni tukiwa ndani yake Kristo; ili katika vizazi vijavyo aonyeshe wingi wa neema yake isiyo na mfano, ambayo imedhihirishwa kwa wema wake kwetu sisi tunaoishi ndani ya Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote- Waefeso 2:4-9.

Dhabihu Ya Ukombozi (Kununua tena) *Unabii Wa Zekaria- Luka 1:67-80. *Yesu Kama Fidia: …kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi-Mathayo 20:28.*Paulo awaasa Wazee wa Efeso: Jilindeni nafsi zenu, na mlinde kundi lote la kondoo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka chini ya uongozi wenu; mtunze kanisa la Mungu ambalo amelinunua kwa damu ya Mwa nae. Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate. Kwa hiyo muwe macho; mkumbuke jinsi nilivyomwonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu- Matendo 20:28-31.*Yesu Ndiye Anayefaa Kukifungua Kitabu Cha Uzima- Ufunuo 5.

Dhabihu Ya Ukombozi (Kununua tena) *Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua, kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani. Pia alifanya hivi ili kuonyesha kwa wakati huu kuwa yeye ni wa haki na kwamba yeye ndiye anayewahesabia haki watu wote wamwaminio Yesu - Warumi 3:22-26.*Upendo wa Yesu Hutudhibiti- 2 Wakorintho 5:14.*Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi- Wagalatia 4:4-7.*Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji- 1 Petro 3:18-20.

Mbuzi Azibebaye Dhambi (Kuzitupilia mbali) Mbuzi Azibebaye Dhambi (Kuzitupilia mbali)

Copyright © 2007 Tammie Friberg 91

Page 95: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Yesu kama Dhabihu Ya Dhambi Nje ya kambi- Luka 23; Mathayo 24-27; Marko 15; Yohana 19.*Sala Ya Bwana- Mathayo 6.

*Mpende Jirani Yako Kama Unavyojipenda- Wagalatia 5:14.

Kuishi Maisha Ya UpatanishoKuungama Dhambi Zetu Kwa wale tuliowaumiza/msamaha/upatanisho*Kisa Cha Yusufu- Mwanzo 37-50.*Yesu Anawasamehe Wale Wanaomwua- Luka 23:34.*Stefano Anawasamehe wale wanaompiga mawe, “Usiwahesabie dhambi hii”- Matendo 7.*Paulo Anasamehe Kama Stefano na Yesu, “Naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo”- 2 Timotheo 4:16.*Yesu Amsamehe kahaba- Luka 7:37-50.*Yesu Anatuamuru Tuwapende wengine Kama Anavyowapenda yeye- Yohana 15:12.

Kuungama Dhambi Zetu Kwa wale tuliowaumiza/msamaha/upatanisho*”Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako. Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa” - Mathayo 5:23-26.*Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini”- Mathayo 18:21-22.* Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mtu mwenye haki yana nguvu na huleta matokeo- Yakobo 5:16.*…na kwamba kwa njia ya mwanae vitu vyote vilivyoko duniani na vilivyoko mbinguni vipatanishwe na Mungu, kwa ajili ya damu yake iliyomwagwa msala bani kuleta amani. Hapo kwanza ninyi mlikuwa mmefarakana na Mungu na mlikuwa maadui zake kwa sababu ya mawazo na matendo yenu maovu. Lakini sasa Mungu amewapatanisha naye kwa njia ya mwili wa Kristo katika kifo, ili awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, bila doa wala lawama- Wakolosai 1:20-22.*Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote- Warumi 12:18.

Kumrejesha Mwenye Dhambi Katika Hali Yake Ya Zamani *Wasio Haki Kuzawadiwa- Mathayo 18:23-35.*Kisa Cha Mwana Mpotevu- Luka 15.*Yesu Amsamehe Mwanamke Aliyeshikwa Akizini- Yohana 8.*Yesu Amrejesha Petro Katika Uhusiano Naye Baada Ya Petro Kumkana Yesu Mara Tatu- Yohana 21:15-25.

Kumrejesha Mwenye Dhambi Katika Hali Yake Ya Zamani *Na tujishughulishe kutafuta jinsi ya kuhimizana katika kuonyeshana upendo na kutenda mema- Waebrania 10:24.*Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu-Wakolosai 3:14.*Kuwapenda Wengine Kunaonyesha Jinsi Tunavyompenda Mungu- 1 Yohana 5:2. *Kuwapenda Wengine Kama Alivyofanya Yesu Ni Kuwa Tayari Kufa Kwa Ajili Ya wengine- Yohana 15:13; 1 Yohana 3:16.*upendo wetu usiwe wa maneno matupu, bali upendo wetu udhihirishwe kwa vitendo na kweli- 1 Yohana 3:18.*Upendo Wetu Kwa Mungu Unakamilishwa Tunapopendana- 1 Yohana 4.*Hatuwezi Kumpenda Mungu Iwapo Tunawachukia Ndugu Zetu- 1 Yohana 4:20-21.*Dumisheni Upendo huo huo- Wafilipi 2:2.*Vumilianeni- Waefeso 4:2-3.*Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe-Warumi 12:10.*Hatimaye ndugu zangu, kwaherini. Sahihisheni mwenendo wenu, pokeeni ushauri wangu; sikilizaneni ninyi kwa ninyi; kaeni kwa amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu-2 Wakorintho13:11-12.

Mwenye Dhambi Kulipa Fidia Kwa Wale Aliowaumiza *Kisa Cha Zakayo Mtoza Ushuru- Luka 19.*Paulo Anampa Yohana Marko Nafasi Nyingine Katika Huduma- Matendo 15:37-39; 2 Timotheo 4:11.

Mwenye Dhambi Kulipa Fidia Kwa Wale Aliowaumiza *Upendo Huadilisha- 1 Wakorintho 8:1.*Upendo Hauwezi Kumkosea Jirani- Warumi 13:10.*Upendo Na Uwe Bila Unafiki- Warumi 12:9.

Kukabiliana Na Dhambi Kukabiliana Na Dhambi

Copyright © 2007 Tammie Friberg 92

Page 96: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Paulo Anamkabili Mwenye Dhambi: Kama vile tunavyoshiriki mateso ya Kristo yaliyo mengi, ndivyo na far aja yetu inavyomiminika kwa wengine. Kama tunateseka ni kwa faraja yenu na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa faraja yenu, ambayo mnapata wakati mkivumilia kwa subira mateso hayo hayo tunayopata sisi. Matumaini yetu kwenu ni imara; kwa maana tunajua ya kuwa kama mnavyoshiriki katika mateso yetu, tashiriki pia katika faraja yetu- 2 Wakorintho 1:5-7.*Mafundhisho Juu Ya Upendo wa Mungu-1 Wakorintho 13.

*Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi WAWEPO MASHAHIDI WAWILI AU WATATU WA KUTHI BITISHA JAMBO HILO. Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpa gani au mtoza ushuru- Mathayo 18:15-17.*Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa-Wagalatia 6:1.*Ambienani Ukweli Kwa Upendo- Waefeso 4:15.

Mafundisho Ya Ziada Kwa Ajili Ya KanisaMigawanyiko:*Wakati mwingine Yesu Alileta Migawanyiko-Luka 12:51; Yohana 7:43; 9:16; 10:19.*Paulo Aandika Juu Ya Migawanyiko Kanisani- 1 Wakorintho 1.*Migawanyiko Katika Kanisa La Kwanza- 1 Wakorintho 11:18.*Yakobo Na Yohana Wazua Sintofahamu Miongoni Mwa Wanafunzi- Marko 10:35-52.*Roho Huwaganyia watu vipawa ili kusiwe na mgawanyiko Katika Mwili Wake- 1 Wakorintho 12:25.*Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,” je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu? Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa: je, Mungu hakuwachagua wale walio fukara hapa duniani kuwa matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidi wale wampendao? Lakini ninyi mmemvunjia heshima aliye fukara. Je, si matajiri ndio wanaowagandamiza na kuwapelekeni mahakamani? Je, si wao wanaolikufuru jina lile jema mliloitiwa? Kama kweli mnatimiza ile sheria ya kifalme iliyomo katika Maandiko, “MPENDE JIRANI YAKO KAMA UNAVYOJIPENDA MWENYEWE,” mnafanya vema. Lakini kama mnafanya ubaguzi, mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji- Yakobo 2:1-9.

Mambo Yahusuyo Hasira:*Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha- Zaburi 30:5.*Jinsi Mungu alivyowatendea watu wake- Zaburi 78.*Epuka hasira wala usiwe na ghadhabu; usihangaike maana hiyo huzidisha ubaya. Watu watendao mabaya wataangamizwa, bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu watamiliki nchi. Bado kitambo kidogo, naye mwovu atatoweka; utamtafuta pale alipokuwa, wala hutamwona. Lakini wapole wataimiliki nchi, hao watafurahia wingi wa fanaka - Zaburi 37:8-11.*”Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu, wakati ule tuliposhambuliwa na adui, hakika tungalimezwa tukiwa hai, wakati hasira zao zilipotuwakia. Tungalikumbwa na gharika, tungalifunikwa na mto wa maji, mkondo wa maji ungalituchukua.” Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, ambaye hakutuacha makuchani mwao. Tumeponyoka kama ndege mtegoni; mtego umeteguliwa, nasi tukaokoka. Msaada wetu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia- Zaburi 124:2-8.*Mtu asiye mwepesi wa hasira ana busara kubwa, lakini akasirikaye upesi hukuza upumbavu- Mithali 14:29.*Mtu wa hasira mbaya husababisha ugomvi, lakini asiye mwepese wa hasira hutuliza ugomvi- Mithali 15:18.*Asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwenye nguvu; Aitawalaye nafsi yake ni bora kuliko autekaye mji - Mithali 16:32. *Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari yake- Mithali 19:11.*Ni jambo la hekima kuepa ugomvi; wapumbavu ndio wanaogombana- Mithali 20:3.*Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu- Mithali 29:8.*Usiwe mwepesi wa hasira, maana, hasira hukaa ndani ya wapumbavu- Mhubiri 7:9.*Ondoa mahangaiko moyoni mwako, jikinge, usipate maumivu mwilini kwa sababu ujana na mwisho wa maisha ni bure kabis - Mhubiri 11:10.

*MKIKASIRIKA, MSITENDE DHAMBI; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima na kumpa she tani nafasi-

Waefeso 4:26-27. *Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo-Waefeso 4:31-32.

*Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu. Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake- Wakolosai 3:8-9.

*Ndugu wapendwa, fahamuni jambo hili: kila mtu awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema wala kukasirika. Maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu- Yakobo 1:19-20.*Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi. “Naam! Wote waliokuwakia hasira, wataaibishwa na kupata fedheha. Wote wanaopingana nawe, watakuwa si kitu na kuangamia. Utawatafuta hao wanaopingana nawe, lakini watakuwa wameangamia. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: ‘Usiogope, nitakusaidia.’ ”- Isaya 41:10-13.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 93

Page 97: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 94

Page 98: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 10: Kukua Kiroho na Vita vya Kiroho.

Maandiko: “Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga. Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha” (Warumi13:12-14).“Hatimaye, nawatakeni mwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara” (Waefeso 6:10-13).

Maelezo MafupiMfano huu unahusu ukuaji wa kiroho na jinsi unavyoweza kututia nguvu kwa ajili ya vita vya kiroho. Kitu cha kwanza kilicho katika picha hii ni jalala kubwa. Jalala hili ni lile tulilojifunza katika Somo La 6. Jalala hili lina vitu vyote vinavyohusiana na maisha ya Ufalme wa Giza. Watu wengi wanapofikiri juu ya vita vya kiroho, huwa hawafikirii juu ya jalala. Jalala hilo limewekwa nyuma ya picha kwa sababu linawakilisha mambo yale tunayoyaacha nyuma tunapokomaa kiroho tayari kupiga vita vya kiroho. Vilevile katika picha hii utaona watu. Baadhi ya watu hawa wamevaa mavazi ya kivita na ilhali wengine wamebeba silaha. Wengine wanaonekana kuwa na silaha chache tu, na wengine hawana silaha zozote miilini mwao. Silaha na mavazi ya kivita katika picha hii vinawakilisha hali ya sasa ya kiroho ya watu, yaani, ukomavu wao wa kiroho na utiifu wao kwa Mungu.

Jinsi Ulimwengu Unavyopiga Vita Vya KirohoLazima tuelewe kwamba jinsi watu wa ulimwengu wanavyopiga vita vya kiroho ni tofauti na jinsi Wakristo wanavyopiga vita ni tofauti kabisa! Watu walio katika Ufalme wa Giza wanapotaka kupiga vita vya kiroho, kwa kawaida huenda kwa waganga wa kienyeji au waganga wa mitishamba. Mganga huyo wa kienyeji atawapatia njia za kuweza kuudhibiti ulimwengu wa kiroho. Watafanyiwa matambiko, na watatoa dhabihu, na kusemewa maneno ya kichawi ili waweze kuzidhibiti roho za giza ziwafanyie kazi fulani. Katika kufanya hivyo wanaweza kutumia vifaa ndani na nje ya nyumba zao kuweza kufukuza mashetani. Vifaa hivi ni kama hirizi, mifupa, au vifaa fulani ving’aavyo vilivyoangikwa mitini, au hata makombe yaliyojazwa mitishamba. Wakati mwingine wanaweza kutengeneza madhabahu katika maeneo yenye njia panda. Vilevile wanaweza kutengeneza sanamu ndogo. Sanamu hiyo yaweza kuwa na tundu ndogo tumboni ya kuwekea mchanganyiko wa mitishamba, na mwilini mwa sanamu hiyo hugongwa misumari ili kudhibiti mashetani, au kuweka maagano kati ya watu. Pia wanaweza kupitia tambiko fulani au kutoa dhabihu kuwatuliza mababu waliokufa zamani, au kufanya mashetani kurutubisha ardhi yao, au kutambua ni nani aliyewaroga na kuwalipiza pia kwa kuwaroga.

Hatua Ya Kwanza Ya Kumwezesha Mtu kupiga vita Vya kiroho Vizuri: Yaweke Kando Matendo Ya GizaJambo tunalotakiwa kuelewa ni kwamba mambo haya ndiyo yanayofanya watu walio katika Ufalme wa Giza kudhibiti mashetani na kuyatumia kama wapendavyo. Watu walio katika Ufalme huu wamefunzwa kwamba ili waweze kupata mahitaji yao sharti wapitie kwa maombezi au pepo fulani. Wanaamini kwamba Mungu yuko mbali yao na hawezi kuwasikia kamwe. Lakini ukweli ni kwamba mambo haya yote yanahusu uchawi. Mungu amewakataza watu kujihusisha katika uchawi. Kwa hiyo ikiwa mchungaji au mshirika bado anajiingiza katika mambo ya uchawi, lazima tuwahimize kuyatumbukiza mambo hayo katika jaa la taka. Mtu akijiingiza katika mambo yaliyokatazwa na Mungu, basi mtu huyo atakosa uwezo na nguvu ambazo Mungu angependa kumpa kwa ajili ya vita vya kiroho. Kwa kuwa mtu anatumia nguvu za uchawi, basi nguvu hizo si za Mungu, bali ni za Shetani. Kwa hiyo mtu akitumia uchawi, atakuwa anawakaribisha pepo katika maisha yake badala ya kuyafukuza. Wale waamini katika mji wa Efeso walifikia kiwango cha kutambua kwamba matendo yao ya uchawi yalikuwa yamekatazwa na Mungu, kwa hiyo wakaleta vitabu vyao vyenye maneno ya kichawi na kuvichoma (Matendo 19:19). Kwa hiyo jambo la kwanza la kufanya katika vita vya kiroho ni kuvitupilia mbali vitu vinavyotumiwa katika Ufalme wa Giza.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 95

Page 99: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Jambo la kusikitisha ni kwamba, Wakristo wengi bado hujihusisha na mambo ya uchawi kisiri. Kwa kutumia maneno mengine, Wakristo hao huwa wanajua kwamba uchawi ni kinyume cha Ukristo, kwa hiyo wanajiingiza katika uchawi kisiri. Lakini Mungu anajua wanayotenda na matendo hayo huathiri ukuaji na ukomavu wao wa kiroho. Watu wengi wameishi katika dhambi hizi kwa muda mrefu hivi kwamba wanapojaribu kuchunguza kwa nini hawana nguvu na uwezo wa Mungu maishani mwao, hupuuza uhusiano wao na mambo ya uchawi. Maandiko yaliyoko katika kisanduku yanatufundisha kwamba jambo la kwanza tunalostahili kufanya kama tunataka kufaulu katika vita vya kiroho, ni kuyatupilia mbali matendo ya giza. Mambo mengine yaliyoorodheshwa katika kisanduku chenye maandiko ni yale yale ambayo yatari yametajwa katika Somo la 6 na la 7. Mambo haya yanaonyesha ukengeufu na ni sehemu ya Ufalme wa Giza. Mambo haya yanajumuisha: njia ya udanganyifu; njia ya mazoea mabaya; njia ya fujo; njia ya kuhisi kutosheka au uvivu; na njia ya ufisadi. Ikiwa Wakristo watakuwa na mguu mmoja au miguu yote miwili katika njia zisizofaa, hawataweza kupata ushindi katika vita vyao vya kiroho na vile vile ukuaji wao wa kiroho utatizwa. Kwa Wakristo wengi, kuzichukua sehemu fulani za maisha yao na kuziweka chini ya utawala wa Kristo huwachukua muda mrefu. Kuna mambo mengine ambayo hatujui iwapo ni makosa kuyatenda, lakini jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi maishani mwetu na pia jinsi Mungu anavyowasiliana nasi kwa njia mbalimbali (tazama Somo la 3) ndivyo tunavyoweza kusaidika na maisha yetu kubadilika. Hata hivyo watu wengine huweza kukwama mahali pamoja na kwa sababu hiyo hawakui kiroho kamwe. Katika picha ya somo hili unaweza kuona kwamba baadhi ya watu walioko hawana zana za kutosha za kupigia vita vya kiroho. Hawana vifaa vyote vinavyoweza kuwapa ushindi katika vita vya kiroho. Pepo hawakemewi au kutolewa kwa sababu watu wanaishi maisha yanayowafanya pepo kuendelea kudumu ndani yao. Moja ya maswali tuliyonayo kama waamini ni hili: tunawezaje kupigana na pepo tunaokumbana nao katika maisha yetu ya kila siku? Tumejifunza katika Somo la 1 kwamba Mungu ndiye aliyeumba vitu vionekanavyo na visivyoonekana. Yeye ana uwezo juu ya viumbe vyake vyote, vikiwemo vile vilivyo katika ulimwengu wa kiroho. Pia tumejifunza katika Somo la 8 kwamba Wakristo wamefufuliwa pamoja na Kristo mbinguni hivi kwamba wana nguvu za Mungu za kuwasaidia kupiga vita vya kiroho. Lakini nguvu za Mungu hufanya kazi kwa njia gani katika maisha yetu?

Wakristo Hupata Ushindi Katika Vita Vya Kiroho Kwa Kukua kwao KirohoJibu la swali lililo katika aya iliyotangulia linapatikana katika Waefeso 6. Jibu lenyewe ni kukua kiroho. Kiwango cha ufanisi katika vita vya kiroho kwa waamini hakitegemei ujanja wa nje wa kutumia nguvu za uchawi, bali unategemea ukuaji na ukomavu wa kiroho! Mambo tutakayoyajadili hapa sio matambiko tunayostahili kufanya ndipo Mungu atujibu, la! Badala yake mambo haya ni ya kutuhimiza tuweze kukua katika sehemu fulani za Ukristo ili kwa kufanya hivyo tuweze kupokea nguvu kutoka kwa Mungu za kutusaidia kupiga vita vya kiroho. Baadhi ya vipengele vya Ukristo ni: kulisoma neno la Mungu kila siku; kuomba bila kukoma; kuhubiri Habari Njema ya wokovu na ya Ufalme wa Mungu; kuishi maisha matakatifu na ya utaua; na kukua katika imani kwa kumtegemea Mungu katika kila sehemu ya maisha yetu. Katika picha ya somo hili mambo haya yamewakilishwa na silaha pamoja na zana za kivita wanazovaa Wakristo. Ukanda wa UkweliJambo la pili litakalotusaidia kukua kiroho ni kuvaa silaha za kiroho. Ukiangalia vizuri utakuta kwamba wale walio na silaha zote wamejifunga ukanda viunoni mwao. Ukanda huu unaitwa Ukanda wa Ukweli. Ukanda huu hushikanisha vitu pamoja katika mwili wa mtu. Wakati askari alipokwenda vitani, kwa kawaida angechukua sehemu ya nyuma ya mavazi yake na kuitia katika sehemu ya mbele ya ukanda. Katika enzi za Biblia ukanda ndio uliokuwa kitu cha kwanza ambacho mtu angekivaa. Hii ndiyo maana ukisoma Biblia utakuta maneno yasemayo walijifunga ukanda kwenda vitani. Ukweli ni kiungo muhimu ambacho hushikanisha vitu vyote pamoja. Ikiwa hatuishi na kuvaa Ukweli, basi hatuwakilishi Ukweli duniani. Shetani ndiye Baba wa uongo, kwa hiyo tunastahili kutumia kanuni zote tulizojifunza katika Somo la 5 na la 6 kujihami kwa ajili ya vita vya kiroho. Tunastahili kujitenga na uongo. Biblia hata inasema, “Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu” (Wakolosai 3:9-10). Ukweli ni sifa muhimu kwa Wakristo. Ulimwenguni tunamoishi mmejaa uongo. Watu hudanganyana kwa minajili ya faida za kibinafsi, kupata umaarufu au hata kwa nia ya kuepuka majukumu fulani. Lakini sharti tukue kufikia kiwango cha kusikia vibaya wakati tunaposema uongo. Uongo umeruhusiwa tu iwapo lengo lake ni kuokoa maisha, kama ilivyo katika kisa cha Musa wakati wakunga walipodanganya juu ya wanawake wa Kiebrania kujifungua haraka hivi kwamba hawawezi kufika wakati ufaao kuweza kuwaua watoto wao. Mungu aliwabariki wakunga hao kwa kazi waliyofanya ya kuwalinda watoto. Mungu aliwabariki wakunga kwa kuwafanikisha na kuwapa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 96

Page 100: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

jamii (Kutoka 1). Kipande kingine cha mavazi ya kivita kilichotajwa ni Vazi la Uadilifu au Dirii ya Haki kifuani. Dirii ya haki huufunika moyo. Dirii inakinga viungo vyetu muhimu. Mioyo yetu ni mitakatifu. Tusiwe tu watakatifu kwa nje bali pia kwa ndani. Hata ingawa Yesu anatusafisha mioyo yetu, lazima tuhakikishe kwamba mioyo yetu ni misafi kwa kutenda yale yaliyo sawa katika familia zetu, kazini, makanisani mwetu, na katika jamii kwa jumla. Haki na utakatifu vina uhusiano wa karibu kama tulivyoona katika Somo la 1. Sharti tutende yale ambayo ni sawa machoni mwa Mungu na mwa wanadamu. Kwa hiyo sharti tuwe watu wanaosimama katika ukweli.

Viatu vya Utayari wa Kuitangaza Habari NjemaKitu cha tatu kilichotajwa katika msururu wa zana za kivita kinawakilisha kazi yote ya Mungu na kazi ya watu wake ya kuupanua Ufalme wake kwa kuhubiri Injili ili watu waokoke na wamjue yeye. Aya ya Waefeso inasema, “na HAMU YA KUTANGAZA HABARI NJEMA YA AMANI IWE KAMA VIATU MIGUUNI MWENU” (Waefeso 6:15). Njia moja inayodhihirisha ushindi katika vita vya kiroho ni wakati ule watu wengine wanapompokea Yesu na kuhamishwa kutoka katika Ufalme wa Giza hadi katika Ufalme wa Nuru na Wakristo wanaochukua jukumu la kuutangaza ujumbe wa Mungu ulimwenguni kote. Kwa namna nyingine, tunayachukua maeneo ambayo yalimilikiwa na adui Shetani. Tunatenda hivyo kwa kuufikisha ujumbe wa Habari Njema kwa watu. Maeneo yanayostahili kutekwa nyara yako katika mioyo ya watu, na yanatekwa nyara kwa ujumbe wa Amani, na wala sio vita au fujo. Kwa Biblia kutumia ishara ya viatu kuzungumzia hamu ya kutangaza Habari Njema, kunamaanisha kwamba sisi ni wajumbe au mitume. “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!”(Isaya 52:7; Warumi 10:15). Tambua kwamba hata ijapo Wakristo wanaenda na kuteka nyara maeneo ya adui, ni Injili tu ndiyo inayoweza kufanya hivyo! Tunastahili kupeleka amani kila mahali tuendapo. Vilevile tunastahili kuonyesha upendo na msamaha wa Yesu, sio tu kwa maneno, bali pia kwa matendo. Katika mafunzo haya kuna mwongozo wa kukusaidia kuwahuburia watu habari za Yesu na kutoa ushuhuda wako. Yesu alihubiri Habari Njema ya Wokovu na Habari Njema ya Ufalme. Njia nzuri inayoweza kutusaidia kuelewa maana ya Habari Njema ya Ufalme ni kwa kukumbuka kwamba neno “ufalme” linamaanisha uwezo wote na mamlaka aliyo nayo mfalme. Tunaweza kutafsiri neno Ufalme kama “hali ya kutawala.” Luka anazungumzia kazi aliyofanya Yesu pamoja na wanafunzi wake. Anasema, “Baada ya hayo, Yesu alipitia mijini na vijijini akitangaza Habari Njema za ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye. Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba” (Luka 8:1-2). Hata ijapokuwa inawezekana hatutasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mara kwa mara, kuna mfano mzuri unaonyesha uendelevu wa kuhubiri Habari Njema na wa kuwa mfano mzuri machoni pa watu. Wewe ni mfano na mwalimu kwa watu unaochangamana nao katika maisha yako ya kila siku. Unawafunza kwa njia ya unyamavu juu ya Mungu, na pia unawafunza kwa matendo yako. Njia nzuri ya kuweza kukusaidia kuelewa maana ya Habari Njema ya Ufalme ni kukumbuka kwamba habari hiyo inahusu utawala wa Kristo (Tazama mafumbo aliyotoa Yesu katika vitabu vya Injili). Katika ule Mwito Mkuu, Yesu aliwatuma wanafunzi wake kwenda ulimwenguni kote kuhubiri Injili na kuwafanya watu kuwa wanafunzi, halafu mwisho wa aya hiyo anasema, “Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni.” Kwa hiyo mafundisho yote ya Yesu ndiyo Habari Njema ya Ufalme. Yesu alizuru miji mingi akihubiri mambo haya. Kwanza, mafundisho yake mengi na mafumbo yake yanahusu mada hii ya Ufalme. Filipo katika Matendo ya Mitume 8:12, alienda akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na juu ya Yesu. Ikiwa tutahubiri tu Habari Njema ya Wokovu duniani, tutakuwa hatutimizi kikamilifu kazi yetu tuliyopewa katika Mwito Mkuu. Mwito huo Mkuu si tu kutangaza ujumbe wa Yesu wa wokovu, bali pia ujumbe unaohusu utawala wake na jinsi watu wanavyoweza kuwa wanafunzi wake. Moja ya maswali tunayostahili kujiuliza ni hili: Je, mimi ni mwanafunzi wa Yesu wakati fulani tu, au wakati wote? Kila wakati, tunastahili kuwafundisha watu kupitia kwa maisha yetu, matendo yetu, na maneno yetu wajue Utawala wa Mungu unahusu nini. Watu wengi hufikiria kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni kuhudhuria mafundisho ya Biblia tu. Lakini ukweli ni kwamba tunastahili kuwa wanafunzi wa Yesu wakati wote, usiku na mchana. Ngao Ya Imani Katika mkono mmoja tumebeba Ngao Ya Imani. Hii ndiyo ngao inayotukinga kutokana na mishale ya moto ya mwovu Shetani. Katika picha hii unaweza kuona pepo wakiwarushia Wakristo mishale ya moto. Pepo hurusha mishale ya moto katika akili zetu, mioyoni, na miguuni mwetu. Lengo lao ni kudhoofisha akili na hisia zetu kwa kutunong’onezea mawazo machafu, kutufanya tuwashuku wenzetu, kutujaza woga, na kwa kutwambia kwamba hatuna faida yoyote na kamwe hatutafaulu katika maisha. Wanataka kutuvunja moyo na kutulegeza mwendo kwa kututwika mizigo mizito. Lakini tukiamini kwamba Mungu ana uwezo wa kutenda kazi maishani mwetu na mioyoni mwetu na kutupa uwezo wa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 97

Page 101: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kuizima mishale ya Shetani, tutaweza kupata ushindi. Imani maana yake ni kuamini kwamba Mungu atatimiza yote aliyoahidi hata ikiwa hakuna ishara zozote za nje za kuthibitisha kwamba ahadi hizo zitatimia. Mfano mmoja wa imani katika Biblia ni wakati ule wana wa Israeli walipotembea katika nchi kavu wakati Mungu alipoitenganisha bahari ya Shamu (Waebrania 11:29). Katika enzi za Agano Jipya Petro alipomwona Yesu akitembea juu ya maji, alitamani na yeye kutembea juu ya maji. Ndipo Yesu akamwita atembee juu ya maji. Basi Petro akatoka ndani ya mashua na kuanza kutembea juu ya maji. Lakini mara akaingiwa na woga na kuanza kuzama (Mathayo 14:29-31). Wakati mwingine Mungu hutuamuru kutoka mahali tulipopazoea na tutembee naye. Mambo yale tunayoyategemea hayana budi kubaki nyuma. Ngao ya Imani ni kumtegemea Mungu kabisa na kuamini kwamba yeye atatutunza vyema. Yeye Mungu ametushika kwa mikono yake. “Hata nikikumbana na taabu, wewe wanilinda; waunyosha mkono wako dhidi ya adui zangu wakali, kwa nguvu yako kuu wanisalimisha. Ee Mwenyezi-Mungu, utatimiza yote uliyoniahidi. Fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, zadumu milele. Usisahau kazi ya mkono wako mwenyewe” (Zaburi 138:7-8). Kuwa na shaka na Mungu ni kule kugeukia vitu au watu wasiostahili na kuwategemea kutusadia. Chepeo (Kofia) Ya WokovuChepeo ya Wokovu ndicho chombo kingine cha kujikingia. Wokovu una vipengele vitatu. Cha kwanza ni wakati ule tunapompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Tunapofanya hivyo huwa tumeingia katika wokovu aliotuandalia Yesu pale msalabani. Huu huwa ndio mwanzo wa kuifuata njia nyembamba huku tukiwa na Yesu. Kipengele cha pili, ni kufanya kazi kwa hofu na tetemeko kwa ajili ya ukombozi wetu (Wafilipi 2:12). Huku ndiko kunakoitwa “kutakaswa.” Neno hili maana yake ni “kuwa mtakatifu au kutengwa kwa ajili ya Mungu.” Vile vile lina maana ya kuishi maisha masafi na matakatifu. Kwa hiyo Chepeo ya Wokovu ndiyo inayotukumbusha kuishi tukijua kwamba tumetengwa na mambo ya Ufalme wa Giza. Chapeo hiyo vilevile inatukinga kutokana na kuzifuata njia zisizostahili au hata kupotoshwa njia. Watu wengine katika picha ya somo hili wamekaa mahali pamoja. Wanakaa hapo wakati wote. Watu hawa hawajavaa kofia zao. Sisi kama Wakristo tunastahili kukua katika kumjua Mungu. Ikiwa tutafikia mahali tujisikie tumetosheka jinsi tulivyo, basi hilo litadhihirisha kwamba tumevua kofia yetu! Kipengele cha tatu, ni kwamba wokovu wetu uko katika wakati ujao. Tuna tumaini la wokovu, kwa sababu majina yetu yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo. Kwa hiyo tutakapokufa, tutaenda kuwa na Yesu mbinguni. Tunaweza kukabiliana na hali ngumu za kimaisha kwa sababu ya tumaini hili, huku tukijua kwamba tutapata maisha mema zaidi. Wakatu huo hakutakuwa na kilio tena, kifo wala kutengwa na Mungu. Tuna tumaini la kwenda mbinguni na kuwa na Yesu milele na milele. Haijalishi tunapitia nini kwa wakati huu hapa duniani, tunachojua ni kwamba tuna ulinzi wa milele katika Yesu. Kuwa na tumaini ni sehemu moja ya vita vya kiroho. Tumaini hili hutusaidia kukaza mwendo wakati tunahisi kama kwamba mambo yote yanatuendea mrama. Tumaini la maisha yajayo limeshinda mateso yote tunayopitia sasa. Tumaini ni kama mafuta katika gari, linatusadia kumtumikia Mungu katikati ya masaibu ya maisha. Upanga Wa Roho-Neno La MunguHatimaye silaha ya mwisho ni Upanga Wa Roho ambalo ni Biblia. Biblia ndiyo silaha tunayoweza kuitumia kumpigia Shetani. Biblia ni Neno la Mungu lililohai. Tunapolitangaza neno la Mungu kwa ulimwengu, huwa kwa kawaida halirudi bure. Yesu alipoongozwa na Roho kwenda nyikani kujaribiwa na Shetani, silaha yake ilikuwa Neno la Mungu. Kuliweka Neno la Mungu katika kumbukumbu zetu na kulitafakari kunaweza kututia nguvu kutenda yale yaliyo sawa na vilevile ya kupiga vita vya kiroho. Lazima tujitengee muda wa kulisoma Neno la Mungu, na kuliweka katika mioyo yetu. Tukifanya hivyo tutaweza kupata nguvu za kuweza kukataa njia mbaya (Mithali 2). Kila siku tunapowafunza watoto wetu Neno la Mungu, Neno hilo hukita mizizi katika mioyo yao na kuwapa sababu ya kuchagua kufuata njia zifaazo. Kazi yetu si tu kuwakataza watoto wetu kutenda mabaya, bali pia ni kuwafundisha Kibiblia kwa kuwaeleza kwa nini hawastahili kufanya mambo fulani. Ikiwa watoto wetu hawana sababu yoyote mioyoni mwao ya kuwazuia kutenda mabaya, basi kuna uwezekano mkubwa wa wao kutenda dhambi wakati wanapojaribiwa. Wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani, Mungu hakuwapa chakula ili aweze kuijaribu mioyo yao. Alitaka kuona iwapo wangemfuata yeye kwa mioyo yao yote hata ijapokuwa walikuwa wakikumbwa na pigo la njaa (Kumbukumbu La Torati 8). Wakati mwingine tunapitia hali ngumu katika maisha. Ufikapo wakati wa shida kama huo hatustahili kumwacha Mungu. Lazima wakati wote tumkimbilie Mungu, na kukaa katika njia yake. Maandiko vilevile yanasema kwamba Mungu aliwaacha na njaa ili waweze kutambua kwamba wanahitaji zaidi ya chakula cha kimwili. Wanahitaji chakula cha kiroho kutoka katika Neno la Mungu. Hii ndiyo maana Mungu aliwalisha mana. Katika Agano Jipya, tunasoma kwamba Yesu ndiye Mkate wa Uzima na pia ndiye Neno la Mungu (Yohana 1 na 6). Yeye ndiye mana iliyoshuka chini kutoka mbinguni. Yesu ndiye chakula tunachohitaji kwa ajili ya maisha ya kila siku. Katika nyakati za ukame wa kiroho katika maisha yetu, na wakati tunapopitia mambo magumu ya kimwili au njaa, tunahitaji kulisoma

Copyright © 2007 Tammie Friberg 98

Page 102: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Neno la Mungu kila siku. Dhiki zaweza kututia nguvu au kutufanya kushindwa kiroho. Lazima tushinde dhiki zote za maisha na tumtumikie yule anayetukomboa. Neno la Mungu liko kiroho na linaishi. Hupenya katika mioyo yetu na kuturekebisha makosa yetu.

Maombi Maombi ndilo jambo la mwisho lililotajwa katika aya hizi za Maandiko. Tambua kwamba baadhi ya watu katika picha wanaomba. Ni vyema kuomba pamoja na familia yako kila siku. Pia ni lazima tuwafunze watoto wetu jinsi ya kuomba kwa kuwaonyesha mfano, kuwaambia maneno ya kusema, na pia kuwaomba kuwaombea watu wengine. Wakati mwingine tunahitaji kuwafunza watoto wetu kukaa chini, wayamaze na wamsikize Mungu. Tunapoomba, Mungu hutupa mwongozo. Katika maombi lazima tuwe waangalifu tusiongozwe na hisia zetu. Twahitaji kupima hisia zetu katika mizani za Maandiko. Hana alimwomba Mungu na kumtegemea yeye hata ijapokuwa alikuwa tasa. Naye Mungu aliyasikia maombi yake na kumjalia mtoto wa kiume. Hana alikuwa mwanamke mwenye imani kubwa. Yeye hakwenda kwa waganga kutafuta usaidizi ili apate mtoto, hakusema kwamba alikuwa amerogwa na mtu, hakutaka kulipiza kisasi, kutoa sadaka kwa mizimu au kutafuta tiba iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu, badala yake alimwendea Mungu na kumkabidhi shida zake. Mungu aliyajibu maombi ya Hana kwa sababu, alikuwa anamwamini Mungu.

Maombi ni huduma kwa ajili ya familia yako na jamii kwa jumla. Pia maombi ni ushuhuda kwa wale wasiomjua Mungu. Wakati tunapomwomba Mungu, sharti tumsifu, tumshukuru, tuwaombee wengine ili wabarikiwe kimwili, kihisia na kiroho. Wakati mwingine tunajikuta kwamba tunaombea mahitaji yetu wenyewe hivi kwamba hatuombeani kiroho. Lakini Paulo na mitume wengine mara kwa mara waliyaombea mahitaji ya kiroho ya watu wengine. Hebu soma mfano ufuatao, “ Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina” (Waebrania 13:20-21). “Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu. Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili mweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu. Na kwa furaha mshukuruni Baba, aliyewawezesha nyinyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale aliyowawekea watu wake katika ufalme wa mwanga. Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi. Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa (Wakolosai 1:10-14). “Sala yangu ni hii: naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna, ili mweze kuchagua jambo lililo bora. Hapo ndipo mtakuwa safi na bila lawama yoyote ile katika siku ile ya Kristo” (Wafilipi 1:9-10).

Rafiki mmoja wa Paulo kwa jina Epafra aliliombea kanisa kwa bidii (Wakolosai 4:12). Mara nyingi tunapomwomba Mungu, tunaruhusu mahitaji yetu ya kimwili kumeza yale ya kiroho. Ifundishe familia yako jinsi ya kuomba na hususan jinsi ya kuomba mahitaji ya kiroho kutoka kwa Mungu. Uwanja wa Vita-Maisha HalisiKatika picha yetu kuna baadhi ya waamini wanaonekana wakiwatendea mabaya wale waamini waliovaa silaha za kiroho. Paulo anasema kwamba silaha za kiroho si tu kwa kurejea roho, bali pia kwa kurejea shida za maisha tunazopitia. Tambua kwamba katika aya ya Maandiko ifuatayo, katikati ya dhiki alizoziorodhesha, Paulo anatukumbusha kuchukua Neno la Ukweli kwa uwezo wa Mungu, na tutumie silaha za haki. Anatuonyesha lengo jipya ambalo tunastahili kulilenga hata tunapokuwa tumesongwa na dhiki na uonevu. Maandiko haya yanatuonyesha jinsi tunavyostahili kukabiliana na uonevu. Anasema, “…tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuio chochote. Badala yake, tunajionyesha kuwa kweliwatumishi wa Mungu kwa kila kitu: kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu. Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula. Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki, kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia na upande wa kushoto. Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli; kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote; kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni hai kabisa. Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu” (2 Wakorintho 6: 3-10). Yesu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 99

Page 103: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

anatukumbusha kwamba tuna heri iwapo tutateswa kwa ajili yake. Anasema kwamba thawabu yetu mbinguni itakuwa kubwa (Mathayo 5:10-12).

Tunateseka kwa sababu ya dhambi za watu wengine, na kwa mateso hayo tunajifunza kumtii Mungu na imani yetu inakomaa zaidi. Hata watu wakijaribu kukusingizia mabaya, wakati unajaribu kutenda mema, usife moyo endelea kudumu katika imani na umtumkie Mungu. Tunapopitia dhiki katika maisha yetu, sharti tutumie imani yetu na tulitegemee Neno la Mungu kutupa hekima na mwongozo wa kustahimili dhiki hizo. Kushiriki katika mateso ya Yesu hutufanya tufanane naye. Wakati mwingine itatubidi tuteseke kwa sababu ya dhambi za watu wengine, kama yeye alivyoteseka kwa ajili ya dhambi zetu. Mateso hutufanya tumtii Mungu na vilevile hututakasa. Hebu angalia jinsi alivyokabiliana na mateso katika njia ya ukomavu. Anasema, “ Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa” (Wakolosai 1:24). “…nipate walau kusikia kwamba mnasimama imara mkiwa na lengo moja, na kwamba mnapigana vita kwa pamoja na mnayo nia moja kwa ajili ya imani ya injili. Msiwaogope adui zenu, bali mwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi. Maana nyinyi mmepewa fadhili ya kumtumikia Kristo si tu kwa kumwamini bali pia kwa kuteswa kwa ajili yake. Sasa mwaweza kushirikiana nami katika kupigana vita. Vita hivi ni vile mlivyoona nikipigana pale awali na ambavyo bado napigana sasa kama mnavyosikia” (Wafilipi 1:27-30). Hii ndiyo sababu yule mtu aliyevaa silaha zote za kivita amebeba msalaba mabegani mwake. Msalaba huo ni wa kutukumbusha kwamba mara nyingine tunateseka kwa sababu ya dhambi za watu wengine. Hata hivyo ubebaji huu wa msalaba waweza kuleta ukombozi (Tazama Somo la 8). “...tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini. Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia” (Warumi 5:3-5). Mateso huleta nidhamu (yaani utiifu wa kudumu) na pia huleta utakaso (utakatifu, kutengwa kwa ajili ya Mungu, na usafi) katika maisha yetu.

Kuyapitia Mateso Ya YesuMtume Paulo alisema kwamba tunapoteseka, basi maisha na kazi ya Yesu hudhihirishwa zaidi katika maisha yetu. Hii ni kwa sababu huwa tunashiriki mateso ya Yesu. Wakati mwingine tunaweza kusalitiwa, kuteswa na viongozi wa kidini, kuchekwa kwa sababu tuwafuasi wa Yesu, kuachwa, na kupakaziwa makosa yasiyokuwa yetu. Watu wanaweza kufanya bidii zote kukataa uadilifu au ushawishi wetu wa kidini. Wanaweza kututesa kwa sababu ya kutoshiriki katika matendo ambayo ni sehemu ya Ufalme wa Giza. Kwa hiyo sharti tutazame mbele kuliko na uzima wa milele kuliko kuyaangazia mateso tunayopitia sasa. “Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe. Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa; twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa chini, hatukuangamizwa. Kila wakati tumekuwa tukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo, ili uhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu. Naam, muda tuishipo tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa. Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanya kazi. Maandiko Matakatifu yasema: “Niliamini, ndiyo maana nilinena.” Nasi pia, tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini, na kwa sababu hiyo twanena. Tunajua kwamba yule aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka mbele yake pamoja nanyi. Yote haya ni kwa faida yenu, hata neema ya Mungu inapowafikia watu wengi zaidi na zaidi, shukrani nazo ziongezeke zaidi, kwa utukufu wa Mungu. Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku. Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu; lakini itatupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho. Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vile visivyoonekana ni vya milele” (2 Wakorintho 4:7-18). Tusichoke, kwa maana Mungu atatupatia nguvu mpya kila siku! Wakati wote fikiria mambo yahusuyo maisha ya milele.

Wakati tunapoteseka kwa sababu ya kuwa Wakristo, lazima tukumbuke kujiweka mikononi mwa Mungu ambaye siku moja atawahukumu watu wote. “Wapenzi wangu, msishangae kuhusu majaribio makali mnayopata kana kwamba mnapatwa na kitu kisicho cha kawaida. Ila furahini kwamba mnashiriki mateso ya Kristo ili mweze kuwa na furaha tele wakati utukufu wake utakapofunuliwa. Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa nanyi. Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni mwuaji, mwizi, mhalifu au mwovu. Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi, asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo. Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi,

Copyright © 2007 Tammie Friberg 100

Page 104: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “NI VIGUMU KWA WATU WAADILIFU KUOKOLEWA; ITAKUWAJE BASI, KWA WASIOMCHA MUNGU NA WENYE DHAMBI?” Kwa hiyo, wale wanaoteseka kufuatana na matakwa ya Mungu, wanapaswa, kwa matendo yao mema, kujiweka chini ya Muumba wao ambaye ni wa kuaminika kabisa” (1 Petro 4:12-19).

Amri Mbili KuuMbele ya waumini kuna picha ya amri mbili za Mungu. Kila mtu anayepiga vita vya kiroho sharti akomae katika kuzitii amri za Mungu. Yesu alipoulizwa ni amri gani iliyo kuu, alijibu kwa kusema ni: Kumpenda Mungu kwa Moyo wako wote, nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa uwezo wako wote. Halafu akaongeza kwa kusema kwamba amri ya pili ni kumpenda jirani yako kama ujipendavyo mwenyewe. Amri hizi mbili ni muhtasari wa Amri Kumi za Mungu tulizojifunza katika Somo la 4. Amri hizi mbili ndizo zinazostahili kuwa mwongozo kamili wa Wakristo wote. Tukizifuata amri hizi tutaweza kuishi maisha yanayompendeza Mungu na vilevile tutaweza kufanya maamuzi yaliyo sawa na mapenzi ya Mungu.

Mungu Hutuadhibu ili Tuweze Kukua KirohoUpande wa kulia wa picha, kuna mchungaji anayetumia fimbo yake kumrudisha kondoo mahali pake, na kumwepusha na madhara yangaliyoweza kumpata. Huu ni mfano wa nidhamu ambayo wakati mwingine sisi huipokea kutoka kwa Mungu. Wakati waamini wanapokwama mahali pamoja na kutozaa matunda, Mungu anaweza kuleta shida fulani katika maisha yetu ili aweze kututia nidhamu au kututia nguvu. Biblia inasema, “Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi” (Mithali 3:11-12). Mwandishi wa Waebrania naye anatwambia hivi,“Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili. Mafundisho na maonyo. Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu. Endeleeni kutembea katika njia iliyonyoka, ili kile kilicholemaa kisiumizwe, bali kiponywe. Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama hayo (Waebrania 12:11-14).

Njia moja ya inayoweza kutusaidia kumwangalia Yesu na kutufanya kuwa na nidhamu katika maisha yetu ni kufunga na kuomba. Kufunga ni kule kususia chakula au aina fulani ya chakula kwa muda wa siku nzima au hata zaidi. Tunaweza kususia chakula au aina fulani ya chakula kwa kipindi fulani. Chakula cha mwili mahali pake hujazwa na kulisoma Neno la Mungu, na kwa kuomba. Tunaweza kufunga wakati tunapokuwa katika harakati kali za kupiga vita vya kiroho ili kuzivunja ngome za adui au ngome zilizo katika maisha yetu. Ngome hizi zaweza kuwa imani potofu, au mazoea mabaya kama vile uzinzi, kuwalaani watu, kutumia lugha chafu, ulevi wa pombe au dawa za kulevya. Pia tunaweza kufunga na kuomba ili mtu fulani tunayempenda aweze kuokolewa. Vilevile tunaweza kufunga na kuomba wakati tunapokuwa tunahitaji mwongozo wa Mungu juu ya maisha yetu, au kwa ajili ya kufanya maamuzi fulani.

Kuishi Kwa Kuongozwa na Roho Mtakatifu Ndani ya moyo wa kila Mkristo kuna vita vikali vinavyoendelea. Vita hivi ni baina ya mwili na roho. Mtume Paulo alikumbana na aina hii ya mvutano wa mwili na roho katika maisha yake, ndiposa akasema, “Tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia, mimi nimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi. Sielewi nifanyacho, maana kile ninachotaka sikifanyi, bali kile ninachochukia ndicho nikifanyacho. Ikiwa basi, ninatenda kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba nakubali kuwa ile sheria ni nzuri. Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, bali ile dhambi iliyo ndani yangu. Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza. Yaani, badala ya kufanya lile jambo jema ninalotaka, nafanya lile baya nisilotaka. Basi, kama ninafanya kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha kwamba si mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambi iliyo ndani yangu. Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua. Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahia sheria ya Mungu. Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu. Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini mwangu. Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka mwili huu unaonipeleka kifoni? Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo! Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu ninaitumikia sheria ya dhambi” (Warumi 7:14-25). Mara nyingi tunajaribu kutenda mema, lakini akili zetu za kibinadamu, mapenzi yetu, hisia na miili yetu huchukua hatamu na tukatumbukia katika dhambi. Tunajua wazi wakati haya yanapotendeka kwa sababu tunapojaribu kumpendeza Mungu kwa maisha yetu, tunahisi vibaya tunapotenda kinyume cha mapenzi ya Mungu. Tukiendelea kutenda maovu mara kwa mara, wakati mwingine hujikuta tumekuwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 101

Page 105: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

sugu hivi kwamba hatusikii sauti ya Roho Mtakatifu, na dhamiri zetu hopoteza usikivu wake. Watu wengine huiita hali hii ya dhamira kupoteza usikivu kama “kuchomwa kwa dhamira.” Tunaweza kuyaanza maisha ya Ukristo huku tukiwa na dhamira iliyokwisha kufa ganzi kwa sababu ya mambo tuliyokwishapitia katika maisha. Kwa hiyo sasa swali ni hili: Tunawezaje kushinda vita hivi vya kiroho?

Jibu la swali hilo ni kwamba tunastahili kumruhusu Roho wa Mungu kutawala mawazo yetu, hisia, na miili yetu. Sababu inayofanya mpaka tushindwe katika vita hivi ni kwamba tunaruhusu moja ya sehemu hizo sumbufu kuchukua nafasi ya Roho Mtakatifu. Sisi tuna akili zetu wenyewe, tuna hisia zinazohusu mambo tunayopitia, na tuna malengo fulani katika maisha, malengo ambayo tunataka kuyatimiza. Wakati tunapokabiliana na majaribu ya aina mbalimbali mbele yetu, au watu wanapotutendea mabaya na kututesa, au tunapoona kwamba kuna njia fulani tunayoweza kuitumia, ni rahisi sana kujikuta tunatumia nguvu zetu kukabiliana na hali hiyo, kwa njia hiyo tunashindwa.

Njia ya kutuletea ushindi katika vita vya kiroho ni wakati wote kuongeza usikivu wa sauti ya Roho Mtakatifu. Tunaweza kufanya hivi kwa kujitengea muda wa kulisoma Neno la Mungu na kwa kuomba. Mara nyingi sababu ya kwanza inayotufanya kupoteza ushindi wetu ni kutoombea hali inayotukabili kwanza. Sababu ya pili, ni kutokaa kwa makini kumsikiza Mungu aongee nasi na kutupa hekima yake. Sababu ya tatu, ni kuruhusu hisia na shauku zetu kuchukua hatamu ya mawazo yetu na kwa njia hiyo kutufanya kufanya maamuzi kwa kutegemea hisia au shauku zetu badala ya kumtafuta Mungu kwanza. “Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada” (Mathayo 6:33). Mungu anataka tukomae katika kumjua Kristo! Tunastahili kufanya maamuzi ya ukomavu na yanayompendeza Mungu. Sasa andika chini mambo yale magumu unayopitia, au uyanakili tu katika akili yako. Baada ya kuyaandika mpelekee Mungu mambo hayo katika maombi, halafu umsikize atasema nini. Mungu anaweza kukujibu na kukwambia la kufanya wakati ukiwa katika shughuli zako, au ukiwa umelala, mchana, au ukiwa unachangamana na waumini wenzako. Liandike jibu la Mungu au uliweke katika akili yako. Sasa lipime jibu hilo katika mizani ya Maandiko. Halafu ukishakuwa na uhakika, unaweza kulifuata jibu hilo kwa moyo wako wote. Nyingi ya shida tulizojikuta ndani yake, chanzo chake huwa ni utovu wa usikivu wetu, na ukosefu wa uadilifu. Kwa hiyo tukitega masikio kwa makini na kuweza kuisikia sauti ya Roho Mtakatifu juu ya tabia zetu, hisia au kuchangamana kwetu na watu, basi tutapokea hekima ya kutusaidia katika maisha. Lakini tukiendelea kuyaziba masikio yetu, tutajikuta tunafanya makosa mengi zaidi katika maisha. Yesu mara kwa mara alipokuwa akifundisha alisema, “Mwenye masikio, naasikie!” Mtu akisikiza kwa makini asemayo Mungu, basi mtu huyo ataweza kutenda matendo yanayoenda sambamba na usikivu wake. Mtume Paulo anasema kwamba mvutano ulioko ndani yake juu ya kumtii Mungu, ni sawa na kuupiga mwili wake na kuufanya umtii Mungu (1 Wakorintho 9:27). Paulo hakuwa na maana ya juujuu aliposema maneno haya, bali alimaanisha kwamba ilimbidi kufuata yale Roho wa Mungu aliyokuwa akimwambia. Tunaposikiza na kutii sauti ya Roho Mtakatifu, tunamruhusu Roho Mtakatifu awe na uhuru zaidi wa kufanya kazi ndani yetu. Naye Roho anapofanya kazi katika maisha yetu, hutufanya kuzaa tunda linaloitwa kiasi. Sisi sote tumejifunza kusikiza hisia zetu, kusikiza tamaa zetu, akili zetu, au kumsikiza Roho Mtakatifu. Ikiwa tutazifuata hisia, tamaa, na akili zetu kwanza, tutaishi maisha yasiyokuwa na msimamo thabiti.

Mahali mambo ya kusikiza yanapoanzia ni masikioni mwetu, halafu moyo huyapokea yale yaliyosikizwa, na hatimaye mambo hayo hujidhihirisha katika jinsi tunavyomwishia Kristo kila siku. Mtume Paulo aliyasema hayo namna hii, “Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. 17 Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe” (Wagalatia 5:16-17).

Katika picha ya somo hili, utaona Roho wa Mungu akimwongoza yule mtu aliyevaa silaha za kiroho. Jinsi Roho anavyomwongoza huyo mtu, ndivyo jinsi mtu huyo anavyomruhusu Roho kutawala akili na hisia zake.

MuhtasariKitu cha muhimu juu ya ukurasa wa Waefeso 6 unazozungumzia silaha za kiroho, ni zile sifa za ndani, zilivyowakilishwa kwa nje na silaa za kiroho. Imani iko katika sehemu ya ndani, pamoja na wokovu wetu, haki, na Ukweli wa Mungu. Lakini mambo haya yote sharti yaweze kudhihirishwa kwa nje kwa jinsi tunavyoishi. Haya yote ni ushuhuda wa nje wa uwezo wa Mungu uletao wokovu. Hii ndiyo njia bora ya kupiga vita vya kiroho, yaani kuwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 102

Page 106: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

mashahidi kwa kudhihirisha kazi ya Mungu kwa ulimwengu: Kudhihirisha Wokovu, Imani, Haki, Ukweli, Injili, na maombi.

Mambo ambayo yatatusaidia kukua katika Kristo ni kama yafuatayo: Kusoma na kujifunza Biblia; kuomba kwa bidii zaidi; kuhudhuria ibada katika kanisa linalofuata mafundisho ya Biblia vizuri; kumwabudu Mungu na kumtumikia kwa vipawa vyetu; kushiriki imani yetu na wengine; kuishi maisha matakatifu; kumtegemea Mungu; na kuwa na matarajio ya kwenda mbinguni.

Lazima tukue kiroho kwa kupata lishe bora ya kiroho na kwa kuwasiliana na Mungu kila siku, vilevile lazima tuitangaze Habari Njema ya Amani katika Yesu Kristo kwa watu wa ulimwengu. Kukua kiroho, kuwa na ushirika na Mungu, na kuwatangazia wengine ujumbe wa wokovu, kunahusiana na nguvu za kupiga vita vya kiroho. Elewa kwamba kiwango cha nguvu za kiroho tunachohitaji ili kupiga vita vya kiroho kinategemea uhusiano wetu na Mungu ulivyo. Mwe hodari katika Bwana na uweza wa nguvu zake…uwezo wa Mungu na nguvu zake unategemea jinsi tunavyoendelea kudumu ndani ya uwezo huo. Jambo hili linajumuisha mambo mawili muhimu, ambayo ni kuhusika na kuwajibika. “Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama dhabihu iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu” (Warumi 12:1-2).

Mafundisho Ya Somo La 10

Kukua Kiroho Ni Muhimu Katika Vita Vya Kiroho Kukua na Kutayarishwa Yawekeni Kando Matendo Ya Giza Kutumia Silaha Katika Vita Vyetu Vya Kila SikuKuvaa Ukanda Wa Kweli Kushiriki Mateso Ya KristoKuvaa Dirii Ya Haki Kifuani Kuzitii Amri Mbili KuuKuvaa Viatu Vya Habari Njema Kumbuka Mungu Huwaadhibu Wale Anaowapenda

Kuchukua Ngao Ya Imani

Kuikumbuka Kuchukua Kofia Ya Wokovu

Kuchukua Upanga Wa Roho, Yanni Neno La Mungu

Kudumu Katika Maombi

Marejeo Ya Biblia Kwa Mafundisho Ya Somo La 10

Kukua Kiroho Ni Muhimu Katika Vita Vya KirohoHadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na SomoYawekeni Kando Matendo Ya Giza*Unabii Wa Isaya Juu Ya Yuda Na Yerusalemu- Isaya 2; 30:22.*Wathesalonike Waacha Kuabudu Sanamu Na Kumtumikia Mungu Aliye Hai- 1 Wathesalonike 1:9.*Paulo Na Barnaba Wawahimiza Watu Huko Lustra Kuacha Kuabudu Sanamu Na Badala Yake Wamtumikie Mungu- Matendo 14:6-19.*Paulo Aelezea Huduma Yake Kwa Mfalme Agripa- Matendo 26 (Tazama Aya ya 18).*Paulo Awakaripia Wagalatia Kwa Kurudia Mambo Yaliyofunga Awali-

Yawekeni Kando Matendo Ya Giza*Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Kwa hiyo tutupe kando matendo ya giza, tuvae silaha za nuru. Tuishi maisha ya heshima kama inavyopasa wakati wamchana: si kwa ulafi na ulevi; si kwa ufisadi na uasherati; si kwa ugomvi na wivu. Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, na msitoe nafasi kwa miili yenu yenye asili ya dhambi, kutimiza tamaa zake- Warumi 13:12-14.

*Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane- Waefeso 5:11-13.

*Tupilieni mbali dhambi mlizonitendea; jipatieni moyo na roho mpya. Enyi Waisraeli, ya nini mfe? Sifurahii kifo cha mtu yeyote. Hivyo tubuni ili mpate kuishi. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.” - Ezekieli 18:31-32.

*Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na

Copyright © 2007 Tammie Friberg 103

Page 107: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Wagalatia 4: 8-9. *Bwana Avaa Silaha Za Kiroho Dhidi Ya Waisraeli Watenda Dhambi- Isaya 59.

tamaa potovu. Nia zenu zifanywe upya na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na AMWAMBIE NDUGU YAKE UKWELI, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmo-ja. MKIKASIRIKA, MSITENDE DHAMBI; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima na kumpa she tani nafasi. Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. Msiruhusu maneno machafu ya-toke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika- Waefeso 4:22-29.

*Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu. Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake. Katika hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru. Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. Vumilianeni na kusameheana kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha kuwasame-he. Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu. Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani-Wakolosai 3:8-15.

*Kwa hiyo epukeni uchafu wote na uovu ambao umeenea, mkapokee kwa unyenyekevu lile neno lililopandwa mioyoni mwenu ambalo linaweza kuokoa nafsi zenu. Basi muwe watendaji wa neno na wala msiwe wasikilizaji tu, ambao wanajidanganya wenyewe- Yakobo 1:21-22.

Kuvaa Ukanda Wa Kweli *Musa Anachagua Wazee Wa Kumsaidia- Kutoka 18:13-27.*Mtumikie Mungu Katika Kweli- Yoshua 24.*Samueli Awahimiza Watu Kumtumikia Mungu Katika Kweli- 1 Samueli 12 (Aya ya 24).*Wafalme Wanastahili Kuifuata Kweli- 1 Wafalme 2:1-4; 1 Wafalme 3:6; 2 Wafalme 20:3.*Eliya Na Mama mjane wa Sarefathi- 1 Wafalme. 17:10-24, (Aya 24).

Kuvaa Ukanda Wa Ukweli *Fadhili zako ziko mbele ya macho yangu, ninaishi kutokana na uaminifu wako. Sijumuiki naw atu wapotovu; sishirikiani na watu wanafiki. Nachukia mikutano ya wabaya; wala sitajumuika na waovu- Zaburi 26:3-5.*Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu, nipate kuwa kuaw mwaminifu kwako; uongoze moyo wangu nikuheshimu- Zaburi 86:11.*Matendo yake ni ya haki nay a kuaminika; kanunizake zote ni za kutegemewa. Amri zake zadumu daima na milele; zimetolewa kwa haki na uadilifu-Zaburi 111:7-8.*Kitovu na neno lako ni ukweli, maagizo yako yote adili, yadumu milele- Zaburi 119:160.*Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako. Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu- Mithali 3:3-4.*Ukweli umekosekana, naye anayeacha uovu hunyanyaswa. Mungu aliona mambo hayo akachukizwa kwamba hakuna haki- Isaya 59:15.

Vaeni Dirii Ya Haki Kifuani*Kuhani na dirii kifuani- Kutoka 28; 39; Walawi 8:8.*Sadaka Ya Haki Ya Abeli- Mwanzo 4.*Kisa Cha Ayubu- Ayubu.*Yesu Na Haki (utakatifu) Ya Mafarisayo- Mathayo 5; 23:2-5, 23-28; Luka 11:39-54.*Farisayo Na Mtoza Ushuru Mmoja- Luka 18:10-14.

Vaeni Dirii Ya Haki Kifuani*Tukisema tuna ushirika naye huku tunaendelea kuishi gizani tunasema uongo, wala hatutendi yaliyo ya kweli. Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote- 1 Yohana 1:6-7.

*Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma- 1 Wathesa-lonike 5:8.

*Haki Itokanayo na Imani- Warumi 10.*Msiambatane pamoja na watu wasioamini. Kwa maana kuna uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? Kuna kuelewana gani kati ya Kristo na shetani? Mwamini ana uhusiano gani na asiyeamini? Kuna uelewano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema, ``NITAISHI NDANI YAO NA KUTEMBEA KATI YAO, NAMI NITAKUWA MUNGU WAO, NAO WATAKUWA WATU WANGU. KWA HIYO, TOKENI KATI YAO, MKAJITENGE NAO, ASEMA BWANA. MSIGUSE CHO CHOTE KISICHO SAFI; NDIPO NITAWAKARIBISHA KWANGU. Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa vijana wangu na binti zangu, asema Bwana- 2 Wakorintho 6:14-18.

*Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa na faida kubwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 104

Page 108: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu. Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; na nikiwa kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa imani. Nataka nimjue Kristo na nguvu ya ufufuo wake na nishi riki mateso yake, niwe kama yeye katika kifo chake; na hivyo, kama ikiwezekana, niufikie ufufuo kutoka kwa wafu- Wafilipi 3:8-11.

Kuvaa Viatu Vya Habari Njema Miguuni Mwetu*Yesu Anawatuma Mashahidi 70 - Luka 10.*Kitabu Cha Matendo Ya Mitume.*Mikakati Ya Paulo Kuwafikia Watu Waliopotea- 1 Wakorintho 9:16-27.*Walihubiri Habari Njema Kila Siku- Matendo 5:42.*Msihubiri Kupita Kiwango Tulichopewa- Matendo 26:22-23.*Hatuhitaji Ufasaha wa maneno au Ujuzi Fulani wa Kuhubiri- 1 Wakorintho 2:1.*Paulo Aliwahubiria Watu Waweze Kutubu, Na kumgeukia Mungu, Na Kuthibitisha Toba Kwa Matendo - Matendo 10:39-42; 26:19-20.*Paulo Aliwahubiria Watu Bila Malipo- 1 Wakorintho 19:16-18.

Kuvaa Viatu Vya Habari Njema Miguuni Mwetu*hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. Bali wewe uwe imara, katika mambo yote, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako- 2 Timotheo 4:1-5.*Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung'aao katika uso wa Kristo- 2 Wakorintho 4:5-6.*Kinyume chake, tunahubiri kama watu tuliopata kibali cha Mungu tukakabidhiwa Habari Njema. Nia yetu si kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu anayejua mawazo ya mioyo yetu. Mnafahamu kuwa hatukutumia maneno matamu ya kujipendekeza kwenu, wala hatukutumia hila kuficha tamaa ya kujipatia fedha, kwa maana Mungu ni shahidi yetu. Hatukutafuta kupata sifa kutoka kwa mwanadamu ye yote, kwenu au kwa mtu mwin gine. Kama mitume wa Kristo tungaliweza kudai heshima kutoka kwenu, lakini tulikuwa wapole kwenu kama mama anayetunza watoto wake wadogo- 1 Wathesalonike 2:4-7.*Bwana Hututia nguvu Za Kuweza Kuwahubiria Wengine Na Za Kutuokoa Kutoka Katika Vinywa Vya Simba- 2 Timotheo 4:17.*Habari Njema: Yesu Alikufa Kwa Ajili Ya Dhambi Zetu. Alizikwa, Akafufuka, Akawatokea Watu Kadhaa- 1 Wakorintho 15:1-5.*Habari Njema Si Ya Mwanadamu Bali Ni Ya Mungu- Wagalatia 1:11-12.*Wahubirieni Watu Wenye Hekima Na Wasio Na Hekima, Watu Wa Kabila Lako Na watu Wasio Wa Kabila Lako- Warumi 1:14-16.

Kuchuka Ngao Ya Imani *Yesu Anafundisha Juu Ya Vizuizi Vya Imani- Mathayo 6:25-34.*Yoshua Na Kalebu Wamwamini Mungu- Hesabu 14.*Msifadhaike- Luka 12:27-28.*Watu Wenye Imani Kuu- Waebrania 11.*Imani Ya Ibrahimu- Mwanzo 22.*Yesu Anamtokea Tomaso - Yohana 20.*Bwana Anamsaidia Asa Dhidi Ya Kundi La Watu- 2 Mambo Ya Nyakati 14.*Imani Ya Hezekia- 2 Wafalme 18.*Daudi Anakabiliana Na Goliathi- 1 Samueli 17.*Shadraki, Meshaki na Abednego- Danieli 3.*Yesu Amwombea Petro- Luka 22:31-34.

Kuchuka Ngao Ya Imani *Waangalie wenye kiburi, hao wataangamia; lakini waadilifu wataishi kwa kumwamini Mungu- Habakuki 2:4.*Naamini nutauona wema wake Mwenyezi-Mungu katika makao ya walio hai. Mtegemee Mwenyezi-Mungu! Uwe na moyo, usikate tama! Naam, mtegemee- Zaburi 27:13-14.*Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako- Mithali 3:5-6.*Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada, ole wao wanaotegemea farasi, wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita, na nguvu za askari wao wapanda farasi, nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!- Isaya 31:1.

*Kwa hakika tulijisikia kana kwamba tumehukumiwa kifo. Lakini hii ilitokea ili tusijitege-mee wenyewe bali tumtege mee Mungu ambaye anawafufua wafu. Alituokoa katika hatari hiyo ya kifo, na atatuokoa. Tumeweka tumaini letu juu yake kwamba ataendelea ku-tuokoa- 2 Wakorintho 1:9-10.

*Nijapopita katika bonde la giza kuu, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako la fimbo yako vyanilinda. Umeniandalia karamu mbele ya adui zangu; umenipaka mafuta kichwani pangu; kikombe changu umekijaza mpaka kufurika. Kweli wema wako na fadhili zitakuwa pamoja nami, siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi- Mungu milele- Zaburi 23:4-6.*Mungu aniue akitaka, sina la kupoteza, hata hivyo nitautetea mwenendo wangu mbele yake- Ayubu 13:15.*Wanaomtegemea Mwenyezi- Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara daima- Zaburi 125:1.*Msiwaoge Wanaoweza Kuua Mwili tu- Mathayo 10:28-33.

Kuikumbuka Kuchukua Kofia Ya Kuikumbuka Kuchukua Kofia Ya Wokovu

Copyright © 2007 Tammie Friberg 105

Page 109: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Wokovu *Ibrahimu Ana Matumaini Ya Ufufuo- Mwanzo 22; Waebrania 1:17-19.*Yesu anafundisha Juu Ya Wokovu- Yohana 5-7.*Kijana Aliyekuwa Tajiri- Mathayo 19:16-30; Marko 10; Luka 18:18-30.*Mwanamke Msamaria Kisimani- Yohana 4.

*Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. Maana Mungu hakutuchagua ili tupate ghadhabu yake bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo - 1 Wathesalonike 5:8-9.

*Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele . ‘Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele- Yohana 3:14-16.

Kuchukua Upanga Wa Roho, Yanni Neno La Mungu*Kujaribiwa Kwa Yesu- Mathayo 4.*Paulo Amkemea Petro Kuhusu Kufundisha Mafundisho Yasiyo sahihi- Wagalatia 2.*Waberea Wachunguza Maandiko- Matendo 17:10-13.*Kurudi Kwa Yesu- Ufunuo 1:12- 2:20; 19:15-21.*Kanisa La Pergamo- Ufunuo 2:12-17.

Kuchukua Upanga Wa Roho, Yanni Neno La Mungu *Basi, acheni kabisa uovu wote, hila yote, unafiki, wivu na masingizio yote. Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu wenu, kwa maana mmekwisha kuonja fadhili za Bwana- 1 Petro 2:1-3.*Kwa maana neno la Mungu ni hai tena lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, linachoma kabisa na kutenganisha nafsi na roho, viungo vya mwili na mafuta yaliyomo ndani yake; na kutambua nia na mawazo ya mioyo ya watu- Waebrania 4:12.

*Andiko zima lina pumzi ya Mungu nalo lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki 17ili mtu wa Mungu awe kamili akiwa na nyenzo zote za kutenda kila jambo jema- 2 Timotheo 3:16-17.

*..hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo- 2 Timotheo 4:2-4.

Kuomba Kwa Bidii*Bwana Anatufundisha Jinsi Ya Kuomba- Mathayo 6:5-15.*Jesus In Garden Of Gethsemane- Mathayo 26:36-56.*Yesu Anageuka Sura- Luka 9:28-36.*Mua Aweka Mikono Yake Juu Kwa Ajili ya Ushindi- Kutoka 17.*Daudi Aliomba Asubuhi, Mchana Na Usiku- Zaburi 55:16-17.*Ombi La Hana- 1 Samueli 1.*Maombi Ya Paulo Juu Ya Mwiba Wake- 2 Wakorintho 12:1-10.*Eliya Aombea Mvua- 1 Wafalme 18:42-44.*Manabii Wa Baali Waomba Bila Mafanikio- 1 Wafalem 18.*Epafra, ambaye ni mtu wa kwenu, na mtumishi wa Kristo Yesu , anawasalimu. Yeye anawaombea kwa bidii kila wakati kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu mkiwa mmekomaa na mkiwa thabiti. Ninashuhudia kwamba anaomba kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na Hierapoli- Wakolosai 4:12-13.*Musa Awaombea Waisraeli- Kutoka 32.*Waisraeli Waomba Mambo Ya Kinafiki- Hosea 7:14.*Mungu Anatuma Mjumbe Kwa Kornelio Kwa sababu ya maombi- Matendo 10.*Tunaweza Kumwendea Mungu Moja Kwa Moja Katika Maombi- Waebrania 4:15-16.

Kuomba Kwa Bidii*Ila mara kwa mara alitoka peke yake akaenda pasipo na watu akaomba- Luka 5:16.

*Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza- Luka 6:28.

*Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo- Waefeso 1:18-21.*Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo- Waefeso 6:18-20.*Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa- Wafilipi 1:9-11.

*Kwa sababu hii, tangu tuliposikia habari zenu, hatujaacha kuwaombea. Tunamsihi Mungu awape kwa wingi, maarifa ya kujua mapenzi yake, kwa njia ya hekima ya kiroho na ufahamu. Ili mpate kuishi maisha yanayomtukuza Bwana na kumpendeza kabisa: mk-izaa matunda kwa kila kazi njema na kukua katika kumjua Mungu. Tunawaombea pia muimarishwe na nguvu zote kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake; mpate kuwa na subira na uvumilivu, huku mkimshukuru kwa furaha Baba aliyewafanya mustahili kuwa na fungu katika urithi wa watakatifu, katika ufalme wa nuru- Wakolosai 1:9-12.

*ombeni pasipo kukoma, 18shu kuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu- 1 Wathesalonike 5:17-28.

*Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnas-tahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo-2 Wathesalonike 1:11-12.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 106

Page 110: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu - 2 Wathesalonike 3:1-3.

*Kwa hiyo, nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono iliyotakaswa pasipo hasira wala mabishano - 1 Timotheo 2:8.

*Ninakuombea kwamba unaposhirikiana na wengine juu ya imani yako upate kuelewa kikamilifu kila jambo jema ambalo tunapata ndani ya Kristo. Ndugu yangu, upendo wako umenipa furaha kubwa na faraja, kwa maana wewe umechangamsha mioyo ya watakatifu- Filemoni 1:6-7.

*Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima- Waebrania 13:18.

*Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo muwe na akili timamu na wenye kiasi ili mweze kuomba- 1 Petro 4:7.

*Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru. Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu- Wafilipi 4:6-7.

Kukua Na Kutayarishwa Hadithi Zinazoamatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Kutumia Silaha Katika Vita Vyetu Vya Kila Siku

(Tazama Sehemu Zilizo Hapo Juu)

Kutumia Silaha Katika Vita Vyetu Vya Kila Siku(Tazama Sehemu Zilizo Hapo Juu)

Kushiriki Mateso Ya Yesu*Maono Ya Anania Juu Ya Paulo- Matendo 9.*Paulo Afundisha Juu Ya Faida Za Mateso- 2 Wakorintho 1.*Paulo Anateseka Kwa Sababu Ya Ushuhuda Wake Juu Ya Yesu- Matendo 16.*Mateso Ya Paulo Yaorodheshwa- 2 Wakorintho 11.*Mateso Ya Mitume- 1 Wakorintho 4:8-13.

Kushiriki Mateso Ya Yesu*Yesu Alikamilishwa Katika Mateso- Waebrania 2:10.

*Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu- Yohana 16:2.

*Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kub-wa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi- Mathayo 5:10-12.

*Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

Nayahesabu mateso tunayopata sasa kuwa si kitu yakilinganishwa na utukufu utakaodhihirishwa kwetu- Warumi 8:17-18.

*Kwa ajili ya Kristo sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima ndani ya Kristo. Sisi ni dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa. Mpaka wakati huu tuna njaa na kiu, tumevaa matambara, tumeteswa, hatuna makao. Tunafanya kazi ngumu kwa mikono yetu. Tunapolaaniwa, tunabar iki; tunapoteswa tunavumilia. Tu-naposingiziwa tunajibu kwa maneno ya upole. Tumekuwa kama takataka ya dunia hii, na uchafu wa ulimwengu mpaka leo hii- 1 Wakorintho 4:10-13.

*Kwa maana sisi tunaoishi, maisha yetu yako katika hatari ya kifo wakati wote kwa ajili ya Yesu ili uhai wake uweze kuonekana katika miili yetu ya mauti. Kwa hiyo, mauti inat-uandama wakati wote, bali uzima unafanya kazi ndani yenu- 2 Wakorintho 4:11-12.

*Kwa maana mmepewa heshima kwa ajili ya Kristo, sio tu kumwamini, bali pia kuteswa kwa ajili yake- Wafilipi 1:29.

*Nataka nimjue Kristo na nguvu ya ufufuo wake na nishi riki mateso yake, niwe kama yeye katika kifo chake; na hivyo, kama ikiwezekana, niufikie ufufuo kutoka kwa wafu – Wafilipi 3:10-11.

*Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu na kwa mateso yangu ninakamilisha kile ambacho kimepungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake- Wakolosai 1:24.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 107

Page 111: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tuna-jivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mna-zopata. Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake. 6Mungu ni wa haki: atawalipa kwa mateso wale wanaowatesa ninyi na kuwapeni ninyi mnaoteseka nafuu pamoja na sisi pia. Haya yatatokea wakati Bwana Yesu atakapodhi-hirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabi-wa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu- 2 Wathesalonike 1:4-10.

*Ndugu zangu, kama mfano wa subira wakati wa mateso, waangalieni manabii walionena katika jina la Bwana. Kama mnavyojua tunawahesabu kuwa wamebarikiwa wale ambao wamevumilia. Mmek wisha kusikia habari za ustahimilivu wa Ayubu na mmeona shabaha ya Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma na rehema- Yakobo 5:10-11.

*Bali furahini kwamba mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi na kushangilia wakati utukufu wake utakapofunuliwa. Kama mkilau miwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa Utukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu yenu. Lakini asiwepo mtu ye yote kati yenu ambaye atateswa kwa kuwa ni mwuaji, au mwizi, au mhalifu au anayejiingiza katika mambo ya watu wengine. Lakini kama mtu akiteseka kwa kuwa ni mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu kwa jina hilo. Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya watu wa Mungu; na kama itaanza na sisi, mwisho wa hao ambao hawatii Injili ya Mungu utakuwaje? Na, “KAMA NI VIGUMU KWA MTU WA HAKI KUOKOLEWA, ITAKUWAJE KWA MTU ASIYEMCHA MUNGU NA MWENYE DHAMBI?” Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu- 1 Petro 4:13-19.

*Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu- 1 Petro 5:10.

Kuzitii Amri Mbili Kuu*Mwanasheria Amwuliza Yesu, “Ni ipi amri iliyo kuu zaidi?”- Luka 10:25-42.*Kisa Cha Msamaria Mwema- Luka 10:30-42.*Yesu Ampa Petro Changamoto- Yohana 21:17.*Jinsi Paulo Anavyowapenda Watu Wan chi yake- Warumi 9:3.*Yesu Anatufundisha Kuwapenda Adui Zetu- Mathayo 5:43-44.*Yesu Anatufundisha Kuwapenda Ndugu Zetu- 1 Yohana 3:16-17.*Kumpenda Mungu Kunaambatana na Kumtii- 1 Yohana 2:3-6; 5:2-3.

Kuzitii Amri Mbili Kuu*Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hu-fanyiana hivyo. Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”- Mathayo 5:46-48.

*Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu yenu yote. Wekeni moyoni mwenu maneno hayo ninayowaamuru leo na kuwafundisha kwa uangalifu watoto wenu. Mtawasimulia mwapo mnakaa nyumbani au mlipo safarini au mnapolala au mnapoamka. Yafungeni katika mikono yenu na kuyavaa katika paji za nyuso zenu kama ukumbusho. Yaandikeni kwenye miimo ya milango yenu na malango ya miji yenu- Kumbukumbu. 6:5-9.

Kumbuka Mungu Huwaadhibu Wale Anaowapenda *Mwana Wa Mfalme Daudi Afariki- 2 Samueli 12.*Mungu Anawafundisha Waisraeli Juu Ya Nidhamu- Deut. 11.*Paulo Anajitia Nidhamu- 1 Wakorintho 9:24-27.*Paulo Akemea Wazinzi- 1 Wakorintho 5.*Mungu Anaweza Kutumia waamini Katika Nidhamu- 2 Wakorintho 2; 7:8-16;

Kumbuka Mungu Huwaadhibu Wale Anaowapenda *Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike lwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi- Mithali 3:11-12.*Adhabu yo yote huonekana kuwa kitu cha kuumiza na kisichofu rahisha wakati ule inapotolewa. Lakini baadaye, matunda yake kwa wale waliofundishwa kwa nidhamu hiyo, ni haki na amani. Kwa hiyo imarisheni mikono yenu iliyolegea na magoti yenu yaliyo dhaifu. Nyosheni njia za miguu yenu ili mguu ulioumia usilemae, bali upone- Waebrania 12:11-14.*Mungu Huipima Mioyo Na Akili Za Wenye Haki- Zaburi 7:9.*Wewe wachukia kuwa na nidhamu, na maneno yangu hupendi kuyafuata. Ukimwona

Copyright © 2007 Tammie Friberg 108

Page 112: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Tito 1:10-16.*Mungu Anawatia Nidhamu Humenayo Na Aleksanda - Timotheo 1:18-20.*Wanaohitaji Nidhamu- Tito 2.

mwizi unaandamana naye, na wazinzi unashirikiana nao. Uko tayari daima kunena mabaya; kazi ya ulimi wako ni kutunga uongo. Wakaa kitako kumsengenya binadamu mwenzako, naam, kumchongea ndugu yako mwenyew. Umefanya hayo yote nami nimenyamaa. Je, wadhani kweli mimi ni kama wewe? Lakini sasa ninakuripia, ninakugombeza wazi wazi. “Fikirini vizuri jambo hili, enyi msionijali, la sivyo nitawaangamizeni, wala hapatakuwa na wa kuwaokoeni. Anayenipa shukrani kama dhahabu yake, huyo ndiye anayeniheshimu; yeyote anayedumu katika njia yangu huyo ndiye mmi nitakayemwokoa- Zaburi 50: 17-23.*Maonyo hayo na nidhamu yataweka njiani mwa uzima. Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya, yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni- Mithali 6:23-24.*Apendaye nidhamu hupenda maarifa, bali asiyependa kuonywa ni mjinga- Mithali 12:1.*Mtoto mwenye hekima husikia maagizo ya baba yake, lakini mwenye dharau hasikilizi maonyo- Mithali 13:1.*Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo- Mithali 19:20.*Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako- Ufunuo 3:19.*Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa- Wagalatia 6:1.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 109

Page 113: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 110

Page 114: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 11: Uwakili

Maelezo Mafupi

Maandiko: “ Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine kama wakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu” (1 Petro 4:10). “Ndiye aliyewapa watu zawadi: Wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Injili, wengine wachungaji na walimu. Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe. Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila. Kama tukiuzingatia ukwei kwa moyo wa mapendo tutazidi katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo. Basi, kwa jina la Bwana, nawaonyeni: msiishi tena kama watu wasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwa upuuzi mtupu, na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao. Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu. Lakini nyinyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo. Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu. Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu. Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu. Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu” (Waefeso 4:11-24).“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako” (Mathayo 6:19-21).

Picha iliyo hapo juu inaonyesha vipawa alivyotupa Mungu na majukumu tuliyonayo juu ya vipawa hivyo. Ukitazama juu ya ukurasa utaona picha ya Kiti Cha Enzi cha Mungu pamoja na Utatu mtakatifu, yaani Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Mishale inayotoka juu mbinguni inaonyesha jinsi Mungu wanavyowajalia wanadamu na vipawa vya kila aina. Baadhi ya mambo anayotupa Mungu ni mahitaji yetu ya kimwili ya kila siku. Mambo mengine anayotupa yana lengo la kiroho hapa duniani. Mahitaji ya kimwili ni kama vile kazi, pesa, chakula, nguo, na makazi. Mahitaji haya yote hutoka katika uumbaji wake wa vitu vionekanavyo kwa macho. Zaidi ya hayo Mungu ametupa aina mbili za vipawa vya kiroho. Aina ya kwanza ni vile vipawa vya neema anavyotoa Roho Mtakatifu kwa kanisa (kuhubiri, kufundisha, huduma ya umisionari, n.k.) Aina ya pili ya vipawa ni ule ujumbe wa Habari Njema, yaani huduma ya upatanisho. Lakini mahitaji yawe ya kimwili au kiroho, bado mahitaji hayo ya aina mbili yanahitaji uwakili mzuri kutoka kwetu. Je, tunawezaje kuwa mawakili wazuri wa vile vipawa alivyotupa Mungu? Uwakili mzuri huanza kwa kushukuru na kwa kupanga. Katika Biblia kuna neno moja ambalo hutumiwa kuelezea vipawa alivyotupa Mungu. Neno hilo ni Neema. Neema ni neno la ajabu sana, kwa sababu linagusia pande mbili. Hii inamaanisha kwamba neno Neema lina sehemu mbili zinazoenda katika mzunguko. Sehemu ya kwanza ni hicho kipawa chenyewe kutoka kwa Mungu. Sehemu ya pili, ni ile shukrani inayotolewa kwa ajili ya kipawa hicho. Katika picha ya somo hili sehemu hiyo imeonyeshwa kwa mishale inayotoka juu kuja chini, na mingine kutoka chini kwenda juu. Lugha nyingi duniani zina maneno mawili tofauti. Maneno haya ni kipawa na shukrani, haya yote hutumiwa kuelezea kitendo hiki cha Neema. Lakini neno neema linajumuisha vitendo vya mtoaji na mpokeaji. Katika kujifunza kwetu vipawa vya Mungu vya kimwili na vya kiroho, tutakuwa tukirejea hali hii ya neno ili neema kuwa na dhana mbili. Tunachotaka kufanya ni kuona kwamba tunakua katika Bwana ili hata tukumbwe na dhiki za aina gani, tuendelea kumshukuru Mungu kwa neema yake.

Ukitazama picha utaona kwamba Mungu anatupatia mahitaji yetu ya kiroho na ya kimwili, huku Shetani akijitahidi awezavyo kuwapotosha waamini ili wasiwe mawakili wazuri na vilevile wasimtumikie Mungu. Unaweza kuona pepo wakirusha mishale yao kanisani, majumbani, na hata ndani ya hisia na mitazamo ya watu. Pia ukiangalia utaona kwamba chini kuna mashimo. Mashimo haya yanawakilisha mambo ya mwili kama vile ulafi, kiburi, choyo, na tamaa mbaya. Shetani na miili yetu ni maadui wakuu wanaopinga uwakili mzuri na wenye faida.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 111

Page 115: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mpinzani mwingine wa uwakili mzuri ni masumbufu ya maisha. Masumbufu haya huleta hali ya kuvunjika moyo na kukata tamaa. Sote tunaweza kukubali kwamba kuna kipindi fulani tumewahi kuvunjika moyo. Kuvunjika moyo au kukata tamaa ndilo shimo kubwa zaidi ambalo Shetani angependa tutumbukie humo. Jambo gumu kabisa juu ya hali ya kuvunjika moyo ni kwamba hali hiyo hutokea ndani yetu na wala sio kwa nje. Kuvunjika moyo huletwa na jinsi sisi wenyewe tunavyojitathmini, tunavyotathminiwa na watu, na pia yale wanayotutendea. Kuvunjika moyo msingi wake ni kupima uwezo wetu kwa kuulinganisha na vigezo vya ulimwengu huu uliopotoka. Kuvunjika moyo kunaweza kuathiri mtazamo wetu juu ya utunzaji wa Mungu kwa ajili yetu, na pia kuathiri umuhimu tulio nao kwa Mungu, hasa wakati tunapokumbwa na mateso ya dunia hii. Tunaweza kuvunjika moyo sana hivi kwamba tukakosa kuona umuhimu wa Mungu kututumia sisi katika Ufalme wake. Tunaweza kufikiri kwamba hakuna chochote kikubwa kinachoweza kufanyika kupitia kwa juhudi zetu, kwa sababu tuna shida nyingi na ni wadhaifu. Inawezekana tukawa tuna ulemavu fulani, ugonjwa, tulitenda dhambi au makosa fulani awali, au tuna udhaifu fulani ambao ni kama mwiba wa mtume Paulo katika maisha yetu, na kwa sababu hiyo tukaona ni vigumu Mungu kututumia kwa kazi yake. Wakristo wenzetu wanaweza kutuvunja moyo kwa sababu ya wivu, au kwa sababu ya kutaka kushindana nasi, au hata kwa kututazama kwa mtazamo uliopotoka. Hali ya kuvunjika moyo inaweza kutudhoofisha kihisia na kimwili hivi kwamba tukashindwa kuwa mawakili wazuri nyumbani au makanisani mwetu. Kuvunjika moyo kunaweza hata kutufanya tukate tamaa kabisa.

Lakini sharti tujue kwamba Shetani hapendi kabisa tusisimke katika kazi ya Bwana na vilevile hapendi waamini watiane moyo na kujengana katika imani. Atajaribu kutumia masumbufu ya kila aina kudhoofisha kanisa pamoja na Wakristo. Ikiwa Shetani anaweza kuwashawishi baadhi ya watu kuishi kwa kujitegemea wao wenyewe na ikiwa anaweza kutumia ukandamizaji wa wengine ili kuwavunja moyo wakristo wasimfanyie kazi Mungu, basi vilevile anaweza kuwazuia Wakristo wasiyatimize malengo ya Mungu duniani. Hii ndiyo sababu inayofanya uwakili kuwa muhimu sana! Lazima tuendelee kumtumikia Mungu pasipo kuogopa uvamizi wa Shetani, au matendo ya watu wengine. Ili tuweze kukabiliana na hali ya kuvunjika moyo, lazima tujaze akili zetu na Ukweli wa Mungu na kujichunguza iwapo tuko katika njia yake. Sasa hebu tuangalie Maandiko machache tuone jinsi Wakristo wenzetu walivyodumu kuwa mawakili wa Mungu na jinsi walivyokabiliana na hali za kimaisha zinazovunja moyo.

Jinsi Ya Kumtumikia Mungu Wakati Tunapokumbwa na Hali Ngumu na Masumbufu ya Kutukatisha TamaaKubali kwamba Shida Zipo na Ujizatiti Kumtumikia Mungu Katika Hali Hiyo NgumuKabla hatujaanza maajadiliano ya kina juu ya uwakili, kwanza tuanze kuzungumzia jinsi tunavyoweza kuendelea kuwa na mwelekeo tunapopitia mateso. Katika waraka wa pili kwa Wakorintho tunaona jinsi Mtume Paulo alivyopitia shida za kila aina. “Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi -- nanena hayo kiwazimu -- ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi. Mara tano nilichapwa vile viboko arubaini kasoro moja vya Wayahudi. Nilipigwa fimbo mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa. Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo. Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote” (2 Wakorintho 11:23-28). Licha ya mambo haya yote, mtume Paulo alikuwa na uwezo wa ajabu wa kukabiliana na hali ngumu na kumtumikia Mungu kiasi kwamba katika historia ya Ukristo, makanisa yamekuwa yakifaidika sana na uwakili wa Paulo. Paulo aliweza kudumu katika mwelekeo wake na wala hakuzitazama shida zilizomkabili. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaelezea jinsi watu walioishi kwa imani walivyokuwa. Anasema, “Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele (Waebrania 10:34). Kuna mambo mengine ambayo hakuna mwanadamu, hali za maisha, magonjwa, au kipigo, kinachoweza kututenganisha nayo. Mambo hayo ni yetu hata iweje! Mambo haya ni: Upendo wa Mungu kwetu, urithi wetu mbinguni na wokovu wetu, hivyo vyote ni vyetu.

Mtume Paulo hakuishi huku akijaribu kujilinda asipatwe na shida hizo, la hasha! Badala yake, aliishi huku akijua kwamba kunazo shida ambazo zingemkumba na shida hizo ningemletea Mungu heshima na utukufu. Lengo lake hasa lilikuwa ni kuwa shahidi wa Yesu na kuwajenga waamini kiimani. Lengo la Yesu lilikuwa ni kuwa shahidi na kutuletea wokovu kupitia kwa mateso yake. Kuna mambo mengine ambayo hayapatikani kwa njia yoyote nyingine isipokuwa kwa mateso. Wakati tunapopitia mateso na kuendelea kuwa waaminifu kwa Mungu, tunaufanya ujumbe wa Injili kuwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 112

Page 116: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

na nguvu. Tunastahili kuomba kwa ajili ya shida zinazotukumba, lakini hatustahili kutumia njia zilizokatazwa na Mungu, kama vile kwenda kwa waganga kutatulia shida hizo. Tukimwangalia Bwana Yesu na kumtegemea yeye, basi haijalishi tutapitia shida gani, tutaweza kuwa na nguvu zaidi za kuweza kuwashuhudia walimwengu habari zake. Tukikaa ndani ya Yesu—hata tupitie shida kiasi gani-imani yetu itathibitika kuwa ya kweli. Mtume Petro aliyajua haya vizuri wakati alipokuwa akiwatia moyo Wakristo kwa maneno haya, “Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka, majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa” (1 Petro 1:6-7).

Mtegemee Mungu na Usiwe na Shaka Hebu sasa tusome moja ya maelezo ya mtume Paulo juu ya mateso na tuone jinsi alivyotumia mateso kuieneza Habari Njema. “Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi. Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe. Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena, nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu”(2 Wakorintho 1:8-11). Ukitazama juu ya picha, utauona mkono wa Mungu wa ukombozi upande wa kushoto kabisa. Tumejifunza jinsi Mungu alivyowakomboa kimwili wana wa Israeli kutoka Misri na jinsi tulivyokombolewa kiroho na Yesu kupitia kwa kifo chake na kufufuka kwake, yaani kwa kifupi tumejifunza kwamba Mungu ndiye mkombozi wetu. Ikiwa Mungu anaweza kutukomboa kutokana na mambo haya, vivyo hivyo anaweza kutusaidia katika dhiki tunazopitia kila siku katika kumtumikia yeye. Mkono ulio katika picha unawakilisha jinsi Paulo alivyoamua kumtegemea Mungu, hata katika mateso aliyokuwa akiyapitia. Yeye hakujali iwapo mateso hayo yangeweza kumletea mauti. Paulo alijifunza kumtegemea Mungu, ambaye yeye pekee ndiye aliye na uwezo wa kuwafufua wafu. Wakati mwingine tutajikuta tuko katika hatari inayoweza kutuua, au pengine tunaweza kuteswa na mambo ya kijamii, kisiasa, au hata kutengwa kidini. Hata ijapokuwa ni rahisi sana kusongwa na mambo hayo, tunaweza kujifunza kumtegemea Mungu. Yesu alipitia mateso hayo hayo ya kijamii, kidini, na kutengwa kisiasa, na hata aliuawa kabisa. Lakini mpango wa Mungu u zaidi ya mateso haya yote. Kumtegemea Mungu, ndilo jibu hasa la kukabiliana na hali ngumu na wala sio kuwa na shaka. Tunapokaribia kufa kwa sababu tumeokoka, na badala ya kufa moyo, tuendelee kumtegemea Mungu, imani yetu huongezeka. Tafuta Watu wa KukuombeaKuna jambo la pili ambalo tunaweza kuliona katika maisha ya Paulo. Jambo hilo ni hili. Paulo alijua umuhimu wa kuwa na watu waliokuwa wakimwombea katika huduma yake. Kuwa na watu wanaokuombea huongeza uzito wa shukrani wakati Mungu anapojibu maombi hayo. Lengo kuu la Paulo lilikuwa ni kumpa sifa na utukufu Mungu. Jambo kubwa lilikuwa ni yale Mungu aliyotaka kuyatenda duniani na wala sio yale aliyoweza au kutoweza kuyafanya Paulo. Picha ya pili hapo juu ya ukurasa inaonyesha watu wakiombeana. Shauku ya Mungu ni kuona watu wakiomba na pia kuombeana wao kwa wao. Tunapoombeana, huwa tunashikana mikono pamoja kwa ajili ya kazi ya Mungu! Heshima iliyoje! Tunapoombeana, huwa pia tunakomaa katika kuutunza mwili wa Kristo. Mungu angependa kutuona sote tukifanya kazi pamoja kwa ajili ya Ufalme wake. Kwa hiyo basi natutiane moyo na tuombeane. Roho haziwezi kutuombea mbele za Mungu, bali Wakristo ndio wanaoweza kuombeana! Yesu ndiye mpatanishi na Roho Mtakatifu ndiye mtetezi au mwombezi wetu, kama tulivyojifunza katika Somo la 1.

Yaone Mateso Kuwa Nafasi Nzuri ya Kufanya HudumaHatimaye, Paulo alijifunza kutumia faraja aliyoipokea kutoka kwa Mungu na kuitumia katika huduma yake ya kueneza Habari Njema. Alisema, “Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu. Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye. Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi. Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu” (2 Wakorintho 1:3-7). Huu ni ufahamu mzuri sana wa uwakili! Mwandishi wa Waebrania anasema hivi, “ Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele. Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tbbuzo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 113

Page 117: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kubwa. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili mweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi. Maana kama yasemavyo Maandiko: “BADO KIDOGO TU, NA YULE ANAYEKUJA, ATAKUJA, WALA HATAKAWIA. LAKINI MTU WANGU ALIYE MWADILIFU ATAAMINI NA KUISHI; WALAKINI AKIRUDI NYUMA, MIMI SITAPENDEZWA NAYE.” Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa” (Waebrania 10:34-39). Katika mfano huu, utaona mtu ameweka mkono wake begani mwa mwenzake. Picha hii inawakilisha nafasi za kuwahudumia watu zinazojitokeza wakati tunapofarijiwa na kuwafariji wengine. Usiruhusu hali za maisha na hali za kukatisha tamaa kuwa kikwazo cha kumtumikia Mungu. Tumia hali hizo ngumu kumpa sifa na heshima Mungu unapoendelea kukua katika imani yako isiyotikisika. Wakusanye pamoja waamini wenzio waweze kukuombea. Hii inafaa zaidi nyumbani, kwa sababu kwa kufanya hivyo utakuwa unawaonyesha mfano mwema watoto wako. Pia hakikisha kwamba unawahudumia wengine kwa kutumia yale uliyojifunza juu ya Mungu wakati ulipokuwa unapitia dhiki. Wajenge kiimani na uwatie moyo. Mfalme Daudi ni mmoja wa wale waliotumia mateso waliyopata kumpa utukufu Mungu. Daudi aliandika nyimbo kwa kuzingatia shida zilizompata. Nyimbo hizo zilihusu imani na ukombozi wa Mungu kwa taifa la Israeli.! Mfalme Daudi na Mtume Paulo yamkini hawakujua kwamba mambo yale waliyojifunza katika dhiki yangekuja kuwa msaada kwa wengine katika maelfu ya miaka iliyokuwa mbele yake! Huenda Mungu alikuwa na mpango mzuri zaidi kwako kwa kukabiliana na dhiki kwa ujasiri wakati ulipokuwa ukimtumikia! Kumbuka Nguvu Za Mungu Hudhihirishwa Wakati tunapokuwa Wadhaifu Ukitazama picha utaona mwiba na uwezo uliowakilishwa kama mwanga ukiuangazia mwiba huo. Picha hii ni mfano wa nguvu za Mungu zinazodhihirishwa kwa kupitia kwa udhaifu wetu. Sababu inayowafanya watu kutomtumikia Mungu haiko kwa nje mbali iko ndani yao. Paulo anayachukulia mambo ya kibinafsi sawa na jinsi anavyoyachukulia mambo ya nje. Usisahau kwamba Paulo alipewa mwiba mwilini mwake na Shetani. Ijapokuwa hatujui mwiba huo ulikuwa wa aina gani, tunachojua ni kwamba uliwakilisha udhaifu fulani ambao ungemzuia Paulo kumtumikia Mungu vizuri na kuleta faida katika Ufalme wa Mungu. Kwa mtazamo wa kibinadamu tunaweza kuruhusu udhaifu wetu wa kibinafsi kutuvunja moyo sawa na mazingira ya nje yanavyoweza kutuvunja moyo. Tunaweza hata kutumia udhaifu wetu kama sababu ya kutomtumikia Mungu. Haya hapa ni maneno ya mtume Paulo juu ya udhaifu wake binafsi. Anasema, “Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga, nisijivune kupita kiasi. Nilimsihi Bwana mara tatu kuhusu jambo hili ili linitoke. Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo nakubali kwa radhi udhaifu, dharau, taabu, udhalimu na mateso, kwa ajili ya Kristo; maana ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa na nguvu” (2 Wakorintho 12:7-10). Neno la Kigiriki lililotumiwa kumaanisha udhaifu katika 2 Wakorintho 12:7-11 linaweza kutafsiriwa vizuri kama, “duni.” Kwa hiyo chochote kinachoweza “kutudunisha” ndicho ambacho Mungu anaweza kukitumia kudhihirisha uwezo wake ndani yetu! Shetani atatunong’onezea uongo na kusema kwamba hatuwezi kumtumikia Mungu kwa sababu ya udhaifu fulani katika maisha yetu. Lakini jambo la kupendeza kuhusu uwezo wa Mungu ni kwamba hauwezi kuzuiwa na udhaifu wetu! Mtume Paulo anasema kwamba uwezo wa Mungu unadhihirishwa katika udhaifu wetu. Mungu anataka tumtegemee yeye wakati tunapomtumikia. Ikiwa tutajitegemea sisi wenyewe, basi huenda tusimsikize Mungu au kumtegemea yeye katika kumtumikia kwetu. Kwa hiyo usifikirie kwamba udhaifu wako unaweza kuwa sababu ya wewe kutomtumikia Mungu. Jambo tu linaloweza kuwa sababu ya wewe kutomtumikia Mungu ni kudumu katika dhambi pasipo toba au kufuata mafundisho ya uongo. Usiuangalie udhaifu wako, bali mwangalie Mungu na uwezo wake. Pia usitumie udhaifu kama sababu ya kutomtumikia Mungu kwa maisha yako. Tambua katika aya ya mwisho Paulo anarejea yale mambo aliyoyaorodhesha mbeleni katika kitabu chake na kuyaita dhiki za nje—yaani udhaifu, matukano, dhiki, mateso, na masumbufu yanayowapata watu kwa ajili ya Kristo. Lengo la Paulo katika shida zote zilizomkumba lilikuwa ni kumtegemea Mungu amtie nguvu kwa kupitia kwa mateso hayo na mwisho wake uwe mzuri zaidi kupita ingalivyokuwa iwapo angetumia nguvu za kibinadamu. Kudumu Kuwa Watumishi wa MunguSiri kuu ya kutusaidia kukabiliana na mateso ni kudumu kuwa watumishi wa Mungu. Katika 2 Wakorintho 6:3-10 Biblia inasema, “Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuio chochote. Badala yake, tunajionyesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu. Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula. Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki, kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia na upande wa kushoto. Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli; kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote; kama waliokufa,

Copyright © 2007 Tammie Friberg 114

Page 118: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

lakini mwonavyo, sisi ni hai kabisa. Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu” Kitu cha ajabu kuhusu orodha hii ni kwamba mambo haya yote yako kinyume na yale tunayoyatarajia kutoka kwa wengine baada ya kuwatendea mema na kwa kuyatumia maisha yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Lakini ukweli ni kwamba hata Wakristo wenzetu wanaweza kutupakazia maneno ya uongo, kutukosea heshima, na kutuita waongo. Ufikapo wakati kama huo, lazima tumwombe Mungu atuchunguze iwapo tuna dhambi fulani iliyofichika, na pia tuyafungue macho yetu ya kiroho tuone jinsi Mungu anavyotusaidia, kutuhifadhi ili tusishindwe. Wakati Wote Ikuze Nafsi Yako Kwa Kulisoma Neno la MunguWakati mwingine Mungu huijaribu imani yetu ili aweze kuona iwapo tutaendelea kuzifuata njia zake hata wakati tunapokuwa na njaa, "Kumbukeni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyowaongoza katika safari ndefu kupitia jangwani kwa muda wa miaka hiyo arubaini, ili awatweze na kuwajaribu ili ajue mliyokuwa mnawaza mioyoni mwenu, na kama mngezishika amri zake au la. Aliwadharau akawaacha mwone njaa na baadaye akawapeni mana mle, chakula ambacho hamkukijua, wala babu zenu hawajapata kukijua. Alifanya hivyo ili apate kuwafundisha kuwa binadamu haishi kwa mkate tu, bali kwa kila asemalo Mwenyezi-Mungu” (Deut. 8:2-3). Wakati tunapojaribiwa kwa umaskini, tunajifunza thamani ya chakula cha kila siku cha kiroho. Usife moyo wakati unapokosa mahitaji yako ya kiroho. Badala yake zifuate sheria za Mungu, na uhakikishe kila siku unapata lishe bora ya kiroho. 1. Jinsi Mungu Anavyokutana na Mahitaji Yetu kwa Kutumia Mali asili:Katika picha yetu, utaona milima, mvua, miti, na ziwa lililo upande wa nyuma wa picha hiyo. Vitu hivi vyote vinawakilisha mahitaji ya asili ambayo Mungu huwapa wanadamu. Kwa kupitia rasilimali hizi tunaweza kujenga nyumba zetu, kushona nguo, na kupata chakula. Mungu ametupa vitu hivi ili viweze kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku, kwa hiyo kuna uhitaji wa kuwa mawakili wazuri wa mali asili na sio kuharibu rasilimali hizo. Lazima tuzitumie rasilimali za Mungu kwa njia ya busara na kwa uangalifu. Njia moja ya kutunza mali asili ni kwa kupanda miti kila tukatapo miti kwa ajili ya kuni, mbao au kwa kujengea nyumba. Njia ya pili ya kuwa mawakili wazuri ni kwa kukusanya taka zote au kwa kutoyachafua maji. Kutunza miili yetu ni njia moja yapo ya kuwa mawakili wazuri wa vyote alivyoumba Mungu. Mungu alituumba na ana mpango mzuri juu ya maisha yetu, tuwe wanaume, wanawake au watoto. Mtume Paulo anasema, “Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni nyinyi wenyewe”(1 Wakorintho 3:16-17). Miili yetu ni hekalu la Mungu. Mungu anaishi ndani yetu kwa hiyo sharti tuwe waangalifu wakati tunapoitia miili yetu vitu. Sharti tumtukuze Mungu kwa miili yetu. Tusimkosee Mungu kwa kutumia miili yetu vibaya kwa kuihusisha na uzinzi, ulevi, au hata kwa ulafi. Kumheshimu Mungu kwa miili yetu pia kunamaanisha kutojaza akili zetu kwa mambo machafu, au kutumia macho yetu kuangalia mambo maovu. Kwa kuongezea, hatufai kuitumia vibaya miili ya wengine, iwe ni kwa kiakili, kihisia, kimwili, au kiroho. Hii ni kwa sababu sisi ni kazi ya Mungu. Pia hatufai kuitendea vibaya miili ya watoto na ya wanawake. Huu ndio msingi wa uwakili mzuri.

2. Jinsi Mungu Anavyokidhi Mahitaji Ya Watu Binafsi:Mungu hukidhi Mahitaji ya FamiliaHebu sasa tuzungumzie kila moja ya picha kubwa zilizo katika mfano wa somo hili. Upande wa kushoto kuna nyumba ya Mkristo. Nyumba hii imejengwa kwenye msingi wa Maandiko. Ndani ya nyumba hiyo mna familia. Watu wa familia hii walitumia pesa walizopewa na Mungu kupitia kwa kazi ngumu kununua nyumba na kuifanya kuwa makazi yao, vilevile wametumia fedha hizo kununua chakula kwa ajili ya lishe bora, kununua nguo wanazohitaji, na pia kuweka akiba kwa ajili ya watoto wao, kutoa sadaka kanisani, na pia kuwasaidia maskini. Hata ijapokuwa familia moja inaweza kuwa na kipato kidogo cha pesa, bado wao ni mawakili wazuri wa mapato yao. Wakati kila familia inapopokea mapato yao, sharti wapange bajeti yao vizuri. Kiasi fulani cha fedha kitatumiwa kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku, asilimia fulani itatengwa kando kwa ajili ya matumizi ya kielimu au kujiwekea akiba ya wakati wa kustaafu, na asilimia nyingine kutengwa kwa ajili ya kanisa na maskini. Katika Agano la Kale watu walitoa asilimia 10% ya mapato yao kwa kazi ya Mungu. Huu unaonekana kuwa mfano mzuri kwetu, hata ijapokuwa kuna watu wengine ambao hutoa zaidi ya asilimia 10% ya mapato yao kwa kazi ya Mungu. Familia hii katika picha hii imeandika chini kanuni fulani za kuwaongoza katika matumizi yao ya pesa wapatazo, wanafanya hivi ili waweze kuwa mawakili wazuri wa Mungu. Tukizifuata kanuni hizi, tutakuwa tunamheshimu Mungu na vilevile tutakuwa tunampa shukrani anazostahili kupewa. Kutoa Sadaka Kanisani

Copyright © 2007 Tammie Friberg 115

Page 119: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Njia moja tunayoweza kuitumia kumwonyesha Mungu kwamba tunamshukuru ni kwa kuzidhibiti fedha zetu vizuri ili tuweze kutoa sadaka kanisani. Tunapotoa pesa kanisani pamoja kama Wakristo, tunaweza kuchangia upanuzi wa Ufalme wa Mungu na pia tunaweza kukidhi mahitaji ya wahudumu wetu kanisani. Tukitegemea rasilimali kutoka nje, hatuweza kukua kama kanisa. Mpango wa matumizi ya pesa unahitajika nyumbani na hata kanisani. Kanisa lazima liamue ni jinsi gani litakavyogawanya pesa kwa matumizi mbalimbali kama vile kumlipa mchungaji, mradi wa ujenzi, huduma za kanisani na kwa huduma za umisionari. Mipango hii ya bajeti ya pesa sharti uhusishe wazee wa kanisa, ambao hukutana pamoja na kuomba na kupanga jinsi pesa zitakavyotumiwa. Wale watu wanaotoa pesa zao kwa ajili ya kanisa, sharti nao wawe na hamu ya kuona uwakili mzuri katika maswala ya kifedha, na pia sharti wawaombee wazee wa kanisa ili waweze kupanga mipango itakayompa Mungu utukufu.

Huduma moja ambayo kanisa linaweza kuianzisha ni kutoa pesa kwa ajili ya kusaidia familia zinazofanya kazi ya umisionari. Pesa hizi zinaweza kutumika kama kianzio cha biashara, ili wamisionari hao waweze kujikimu kimaisha popote watakapotumwa na kanisa. Baadhi ya biashara ambazo zinaweza kuleta faida ni kama ufugaji wa kuku, kufungua duka dogo, au hoteli ndogo. Kuwatunza MaskiniKuwatunza maskini ni huduma muhimu sana kwa watu binafsi, kwa kanisa, na kwa jamii kwa jumla. Tunaweza kuwaleta wengi katika Ufalme wa Nuru iwapo kanisa litaanzisha huduma za kuwafikia maskini na watu wasio na makao. Yesu anataka tuwafikie wale watu walio na shida mbalimbali. Yesu siku moja alisimulia kisa kimoja cha bwana aliyeandaa karamu kubwa. Wakati wa kuhudhburia karamu hiyo ulipofika, wote walioalikwa walitoa udhuru. Kwa hiyo yule bwana mwenye karamu akawatuma watumishi wake akisema, “Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: ‘Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na wale waliolemaa.’ Baadaye, mtumishi huyo akasema: ‘Bwana, mambo yamefanyika kama ulivyoamuru, lakini bado iko nafasi.’ Yule bwana akamwambia mtumishi: ‘Nenda katika barabara na vichochoro vya mji uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae. Kwa maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeonja karamu yangu.’” (Luka 14:21-24). Yesu alisema kwamba wale wanaowaalika maskini watapata thawabu wakati wa ufufuo wa watakatifu (Luka 14:14). Yesu anapenda tukidhi mahitaji ya maskini wanaoishi miongoni mwetu. Tutakapowajali, tutakuwa pia tunamjali Yesu. Kuwahudumia wengine ni njia moja wapo ya kudhihirisha imani yetu katika Kristo. Hebu soma maneno ya Yesu juu ya kuwasadia wengine, “Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha; nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.’ Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme ‘Bwana, ni lini tulikuona mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha maji? Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo nasi tukakuvika? Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja kukutazama?’ Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’ “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake. Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi hamkunipa maji. Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.’ “Hapo nao watajibu, ‘Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukukuhudumia?’Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uhai wa milele” (Mathayo 25:35-46). Jinsi tunavyopewa changamoto na masumbufu ya dunia, ndivyo tunavyoweza kupata wasaa wa kuwasaidia wengine katika jina la Yesu. Wakristo makanisani wanaweza kutumia vipawa vyao kuanzisha huduma mpya zinazolenga kuwasaidia wengine. Wahimize washirika wako kanisani waweze kujitoa na kuwafikia maskini katika jamii. Hatari Zilizoko Katika Uwakili wa NyumbaniTunaweza kujikuta katika hatari iwapo lengo letu katika maisha ni kufanikiwa au kujipatia fedha nyingi. Ikiwa lengo letu kuu litakuwa ni kujitafutia mafanikio ya ulimwengu, basi tutajikuta tumeacha kumtumikia Mungu na kuanza kujitumikia sisi wenyewe. Lazima tuelewe kwamba kila utamaduni wa watu, huwa una lengo la kuwaangazia watu fulani maalum. Kwa hiyo ikiwa tuna lengo lisilokuwa sawa tunaweza kujikuta tunatumia pesa zetu kwa kununua nguo za ghali, kwa anasa kama vile ulevi au uzinzi. Kukosa kuwa na mwelekeo mzuri kwaweza pia kutufanya tukajiingiza katika biashara zisizofaa, au kuwahadaa watu kibiashara, kuwaibia wengine, au kuuza bidhaa ambazo zinawakilisha itikadi za Ufalme Wa Giza. Tukifanya mambo haya tutakuwa bado tunaishi kwa kujitegemea wenyewe na wala sio kwa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 116

Page 120: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kumtegemea Mungu. Badala yakei, tunastahili kuungama dhambi zetu, na kumwomba Mungu atusaidie kutumia pesa kulingana na mpango wake, vilevile kutupa mapato kwa njia takatifu. Tutakapoanza kuwa na mwelekeo mzuri na kutenda yale yanayostahili, huku tukisubiri Mungu akutane na mahitaji yetu, Mungu atatubariki.

Mahitaji ya kimsingi ya wanadamu kama vile ulinzi kutokana na maadui zetu, ulinzi kutokana na pepo, matamanio ya kutaka kuoa au kuolewa, au shauku ya kupata mtoto, ulinzi safarini, ufanisi wa mazao ya shambani, au mahitaji ya uponyaji, haya yote yanaweza kumfanya mtu kujiingiza katika matambiko ya kipagani. Lengo kuu la dini za kipagani ni kuweza kudhibiti au kuwa na uwezo dhidi ya pepo walio na uwezo juu ya matatizo yaliyokwishatajwa hapo juu. Watu hutumia matambiko, dhabihu au kafara, kunena maneno yenye uwezo, au kutumia mitishamba kuwafanya pepo wawatumikie au kuwa watetezi wao katika hali ngumu zinazowakumba. Mahitaji ya aina hiyo yanaweza pia kuwafanya watu kutumia Maandiko fulani, Zaburi na maombi yaliyochanganywa na matambiko ili kuweza kudhibiti hali wanazopitia au kuweza kumshawishi Mungu kuwatendea watakavyo. Lakini lazima tukumbuke kwamba, sisi kama Wakristo hatustahili kuwaiga wapagani! Biblia inasema katika Kumbukumu La Torati 18: 9-14, “Mtakapofika katika ile nchi awapayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, msifuate zile tabia za kuchukiza za mataifa ya huko. Pasiwe mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye motoni mwanawe wa kiume au wa kike kuwa tambiko, wala mtu apigaye ramli, wala mwaguzi, wala mpiga bao, wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu. Maana yeyote atendaye mambo haya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; na kwa ajili ya mambo haya ya kuchukiza Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawafukuza watu wa namna hiyo mbele yenu. Mwe wakamilifu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. “Mataifa haya ambayo mtaimiliki nchi yao hufuata maongozi ya waaguzi na wapiga ramli; lakini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu hawaruhusu nyinyi kufanya hivyo.” Ni wazi kutoka katika aya hizi za Maandiko kwamba matendo ya aina hiyo ni machukizo kwa Mungu, na wale wanaoyatenda wanakuwa chukizo kwa Mungu. Kujaribu kudhibiti pepo au roho kwa kutumia mazingaombwe na matambiko, ni sehemu ya itikadi za dini za kipagani (Tazama Somo La5). Mungu kwa upande wake, huwasikiza wale wanaozifuata njia na Sheria zake. “Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu, na kusikiliza malalamiko yao; lakini huwapinga watu watendao maovu, awafutilie mbali kutoka duniani. Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia, na kuwaokoa katika taabu zao zote. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa. Mateso ya mwadilifu ni mengi, lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote” (Zaburi 34:15-19).

Watu wanapoanza kujiona kuwa wao ndio mambo yote, huwa wanapotoka njia na kufuata njia ziletazo mazoea mabaya, ushawishi mbaya, ulafi na ufisadi, uchawi, uvivu, na fujo. Shetani hufurahi akiwaona watu wakijitegemea wao wenyewe badala ya kumtegemea Mungu na kumtumikia yeye. Jinsi Mungu Anavyokidhi Mahitaji Yetu Ya Kiroho1. Vipawa Vya Kiroho:Sasa hebu tuzungumzie picha ya kanisa. Ukitazama upande wa kulia wa ukurasa, utaona, jengo moja la kanisa lenye picha ndogo juu yake. Picha hizi zinawakilisha vipengee vya jumla vya vipawa vya Roho ambavyo Mungu huvipa kanisa. Ukiangalia kwa makini utaona kwamba Maandiko yanasema vipawa hivi ni vya kuwahudumia watu, na hata wakati mwingine huitwa “vipawa vya neema.” Kumbuka kwamba neno neema lina maana inayohusisha pande mbili. Mungu hutupa vipawa vya kiroho na talanta. Tunastahili kuviendelea hivyo vipawa na kuvitumia kwa ajili ya Mungu. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunaonyesha shukrani zetu kwa Mungu na vilevile tutakuwa tunaujenga Ufalme wake duniani. Yesu alisema, “Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi” (Luka 12:48). Hata ijapokuwa tumepewa vipawa hivi bure, tunahitaji kuviendeleza na kuvitumia kwa njia nzuri.

Jinsi Ya Kutumia Kipawa Chako Cha RohoMungu anataka kukutumia wewe katika Ufalme wake! Kumbuka tuliyojifunza katika Somo la 2, kwamba Mungu ana mpango na kila mmoja wetu! Mungu aliweza kuiona miili ya wanadamu katika vilindi vya dunia wakati alipokuwa akitekeleza uumbaji wake. Kabla kila mtu hajazaliwa, tayari Mungu alikuwa ameziandika siku zake duniani katika kitabu chake (Zaburi 139). Kwa hiyo Mungu ana sehemu maalum aliyokutengea ili uweze kumtumikia yeye kanisani. Watu hawawezi kujichagulia vipawa kutoka kwa Mungu. Badala yake, Roho Mtakatifu huwapa watu vipawa kama apendavyo.

Je, ni vipawa gani vya kimsingi ambavyo Mungu amelipa kanisa? Ile picha ya mdomo iliyo kwenye kanisa inaashiria vipawa vya usemi. Vipawa hivi ni kama vile kuhubiri, kufundisha, uinjilisti, unabii (kurejesha watu katika njia za Mungu), na pia kipawa cha utume au umisionari. Wakati mwingine vipawa vya usemi vinaweza kujumuisha kipawa cha kuongea kwa ndimi au lugha. Kipawa hiki cha kunena kwa lugha katika Biblia kilihusisha mtu kuongea kwa lugha

Copyright © 2007 Tammie Friberg 117

Page 121: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

ya duniani ambayo atakuwa hajajifunza kamwe, na kutumia lugha hiyo kumwambia mwenyeji wa lugha hiyo habari za Yesu. Maandiko yanasema kwamba lengo la kipawa hicho ni kuhakikisha kwamba yule mtu asiyemwamini Mungu anafikia mahali pa kumwamini Mungu. Yule mtu aliyeweka mkono juu ya bega la mwenziwe, anawakilisha vipawa vya kutia moyo, kuponya, na kuwahimiza wengine. Vipawa hivi huwafanya wale wanaopitia dhiki kuponywa, kujengwa na kutiwa nguvu. Vipawa hivi vya kuwahimiza watu, huweza kuwafanya watu wakamtumikia Mungu tena, na kutiwa nguvu katika maisha yao ya Ukristo. Pia vipawa hivi vinajumuisha wale walio na kipawa cha rehema na ukarimu kwa wengine. Picha ya pesa pamoja na kisanduku cha kuwekea pesa, vinawakilisha wale walio na kipawa cha utawala, na wale walio na kipawa cha kutoa. Wale watawala ndio ambao hupanga jinsi kazi ya Mungu itakavyofanywa kanisani. Kipawa cha kutoa kinajumuisha watu wale ambao huweza hujitoa wao wenyewe kwa kazi ya Mungu na pia kutoa mali zao kusaidia kazi za kanisani au kuwasaidia wengine. Ule mkono uliobeba nyundo, unawakilisha vipawa vya utumishi. Watu walio na kipawa hiki huwa mara nyingi hufanya kazi zao pasipo kuonekana na watu. Watu hawa hushughulikia mambo yanayotaka kutendwa, na kuhakikisha kwamba yametendwa. Kazi za watu kama hawa ni ujenzi au ukarabati wa majengo, kusafisha kanisa, kuwapikia watu, kuwasaidia wengine katika kazi zao, au kazi nyinginezo. Mkono ule uliobeba gita, unawakilisha vipawa vya utumishi vinavyohusu ujuzi maalum kama vile muziki, kushona nguo, au ufundi.

Kila kipawa kina utunzaji au uwakili wake wa kipekee. Baadhi ya mambo muhimu ya uwakili yanayostahili kutekelezwa ni kama haya yafuatayo: Walimu, wanahitajika kufunza Neno la Mungu kwa njia ya usahihi. “Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli” (2 Timotheo 2:15). Mungu atawapa walimu hukumu kubwa zaidi, kwa sababu wana jukumu la kuwafunza wengine. “Ndugu zangu, wengi wenu msiwe waalimu. Kama mjuavyo, sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine. Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, na anaweza kutawala nafsi yake yote” (Yakobo 3:1-2). Katika Warumi 12:6-8, Paulo anawashauri watu jinsi ya kutumia vipawa vyao. Anasema, “Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake. Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe. Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.” Maandiko yafuatayo ni kwa ajili ya wale walio na kipawa cha kuhubiri, “Basi, wewe unawafundisha wengine; kwa nini hujifundishi wewe mwenyewe? Unawahubiria wengine wasiibe, lakini kumbe wewe mwenyewe unaiba. Unasema: “Msizini,” na huku wewe unazini; unachukia sanamu za miungu hali wewe unajitajirisha kwa kuiba katika nyumba za miungu” (Warumi 2:21-22)? “Maana hatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiri Yesu Kristo aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwa watumishi wenu kwa ajili ya Yesu (2 Wakorintho 4:5). “Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni injili tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe! Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni injili ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe! Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo. Paulo alivyopata wito wake Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile injili niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu. Wala mimi sikuipokea kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia” (Wagalatia 1:8-12). Kile tunachoweza kujifunza kutoka katika ushauri huu ni kwamba, tunastahili kufanya ile kazi tuliyopewa na Bwana, kwa bidii na kwa njia ya uadilifu, huku tukikitunza kile tulichopewa na Mungu. Waruhusu Wengine Kutumia Vipawa Vyao Vya KirohoKwa kuwa kanisa huwa na washiriki wengi. Roho huwapa watu kadhaa vipawa vinavyofanana. Kila mtu ana silika yake tofauti na ana uhuru wa kutumia kipawa chake kanisani kwa kuzingatia vigezo vya Maandiko. Wakati mwingine wazee wa kanisa, au washirika wa muda mrefu kanisani hawawapi nafasi watu wenye vipawa kama vyao kufanya kazi ya Mungu pamoja nao kanisani. Hali ya kushindana huingia kanisani kwa sababu ya kung’ang’ania vyeo. Katika kitabu cha 3 Yohana, tunasoma habari za mtu mmoja aliyeitwa Diotrefe. Mtu huyu anaelezewa kuwa mtu “aliyependa kuwa wa kwanza.” Yeye alikuwa kiongozi katika kanisa fulani. Katika kanisa hilo mlikuwa na marafiki wa Mtume Yohana. Bwana huyu alikuwa akiyapinga mafundisho ya Yohana, na pia aliwakataza wamisionari kupitia kanisani kwake na kuhubiri. Ikiwa mtu yeyote angejitokeza kumpinga, basi mtu huyo angefukuzwa kanisani. Tunaweza kujifunza mambo fulani kutokana na hadithi hii ya Diotrefe. Jambo la kwanza ni kwamba tunastahili kuwa wanyenyekevu kama viongozi na kuruhusu vipawa vya Mungu kufanya kazi kanisani kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. Mungu hakumpa vipawa mtu mmoja pekee kuujenga mwili wote wa Kristo. Ikiwa mtu anang’ang’nia cheo kanisani, ni vyema kumtuma mtu anayeheshimiwa ili kwenda kujaribu kuzungumza na mtu huyo. Huenda kwa kufanya hivyo shida ya tamaa ya uongozi ikatatuliwa. Katika waraka huo wa tatu wa Yohana tunasoma kwamba Yohana alikuwa na mpango wa kwenda

Copyright © 2007 Tammie Friberg 118

Page 122: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

kulitembelea kanisa hilo na kuongea na Diotrefe ana kwa ana. Asili yetu kama wanadamu ni kufikiria kwamba Mungu yuko kwa ajili yetu tu, na pia ya kwamba kanisa liko kwa ajili yetu tu…ili kupitia kwa Mungu na kanisa tuweze kujipatia umaarufu, tuwe watu wakubwa, matajiri na wenye uwezo mkubwa. Lakini ukweli ni kwamba Mungu amewapa watu vipawa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo na kwa ajili ya utumishi katika Ufalme wa Mungu.

Mtume Paulo alizungumzia swala hili la vipawa vya kiroho. Alisema kwamba vipawa vimegawanywa kwa watu ili kuwe na usawa na heshimwa kwa kila mshirika wa mwili wa Kristo. Usawa huu unaweza kutatizwa ikiwa mtu mwenye kipawa kimoja atamkataa yule mwenye kipawa cha aina nyingine kwa kumwambia, “Sikuhitaji wewe” (1 Wakorintho 12:19-31). Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii. Lakini hali hii ikitokea, mwili wa Kristo hudhoofika na kuumizwa kwa kupungua kwa kipawa fulani. Mungu ameliunda kanisa kwa njia ambayo, washiriki wote hufanya kazi pamoja kutimiza lengo la kuwaandaa watu kwa ajili ya huduma za Ufalme wa mbinguni. Hakuna kipawa ambacho ni muhimu kuliko kingine katika mwili wa Kristo. Tofauti za kitabia au kisilika hazistahili kuwazuia watu kutumia vipawa vyao. Mungu ndiye aliyeumba kila mmoja wetu. Wakati Mungu anapowapa watu vipawa, tofauti za kitabia na vipawa, vyote hutumiwa ili kuhakikisha kwamba mwili wa Kristo uko thabiti na katika hali nzuri. Kama binadamu wote wangekuwa sawa katika kila kitu, basi kungekuwa na upungufu fulani katika matokeo ya matumizi ya vipawa vya watu hao. Jambo la muhimu tunalopaswa kuzingatia katika kutumia vipawa vyetu, ni kuhakikisha kwamba tunatumia vipawa vyetu kulingana na Maandiko.

Baada ya Paulo kujadili matumizi ya vipawa katika mwili wa Kristo, anaendelea na kutuonyesha kwamba kiungo muhimu katika kutumia vipawa vya kiroho ni upendo. Anatufundisha kwamba upendo ndiyo kanuni muhimu zaidi katika utumiaji wa vipawa vya roho. Paulo anaendelea kusema kwamba pasipo upendo kutuongoza katika matumizi yetu ya vipawa na katika kuchangamana na Wakristo wenzetu, basi sisi ni kama tu debe tupu au upatu uvumao. Kwa maneno mengine, upendo unathibitisha na kuwasilisha kwa walimwengu ujumbe ulioko katika vipawa vyetu. Ikiwa hatupendani, basi lengo la kuwafikia wengine na ujumbe wa Ufalme wa Mungu halitaweza kufikiwa, hii ni kwa sababu maisha yetu yatakuwa yanahitilafiana na Injili ya Kristo. Tambua Kwamba Mungu Amewapa Watu Vipawa Vya Kiroho Kwa Lengo La Kulijenga Kanisa ili Liweze Kuwahudumia WatuJambo la muhimu zaidi tunalostahili kulijua kuhusu vipawa vya kiroho ni kwamba vimetolewa kwa lengo la kulitayarisha kanisa ili liweze kufanya kazi ya Mungu! Huu unaweza kuonekana kuwa ukweli wa kawaida kwa wengi, lakini makanisa mengi hayazingatii matumizi haya ya vipawa vya roho. Kwa bahati mbaya, uongozi wa Kanisa Katoliki umeathiri utawala wa makanisa ya kiprotestanti na hata jinsi yanavyofanya kazi ya umisionari. Hata ijapokuwa mchunguji wa kanisa lengo lake kubwa ni kutoa mwongozo wa kiuchungaji, kufundisha waamini, na mhubiri wa Neno la Mungu, wengi hawaoni umuhimu wa kazi yao kuwa ni kuwahudumia watu kiroho. Badala yake lengo kuu la viongozzi hawa ni kujipatia wafuasi wengi. Kazi hii ya uchungaji mara nyingi inatumiwa kujenga ufalme wa mtu binafsi badala ya kuujenga ufalme wa Mungu. Mchungaji anastahili kuwajenga waamini wenzake kiroho ili waweze kuchukua majukumu ya uongozi na wamtumikie Mungu. Wahubiri wengi na manabii wa siku hizi wanajilisha wenyewe badala ya kuwalisha kondoo wa Mungu. Mfumo huu unazingatia sana kuwaachia wale walioitwa kumtumikia Mungu kufanya kazi zote za kuwahudumia watu kiroho. Hii hufanya Ufalme wa Mungu kutoenea, na vilevile huleta mgawanyiko kati ya wachungaji na wafanyakazi wa kawaida kanisani. Mungu aliwagawanyia vipawa watu wote, ili mwili wa Kristo uweze kujengwa na uweze kufanya kazi ya kuwahudumia wengine. Ikiwa tutaiachia kazi yote wachungaji, basi kazi ya Mungu haiwezi kukamilishwa, kwa maana ni kubwa mno! Wachungaji wamepewa kazi hiyo ili waweze kutuongoza kwa kuwa mfano bora kwetu, ili tuweze kukua kufikia kiwango cha kumtumikia Mungu kwa vipawa vyetu. “Ndiye aliyewapa watu zawadi: wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza injili, wengine wachungaji na waalimu. Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe. Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila. Kama tukiuzingatia ukweli kwa moyo wa mapendo tutazidi katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo” (Waefeso 4:11-16). Neno lililotumiwa kutafsiri huduma katika Maandiko haya ni lilelile tunalolitumia kwa maana ya shemasi. Mara nyingi linatafsiriwa kama, “kufanya huduma.” Hebu sasa tutumie chati kuelezea yale anayosema mtume Paulo juu ya vipawa vya kiroho.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 119

Page 123: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kwa hiyo lengo kuu la vipawa vya kiroho ni kutusaidia sisi waamini kufikia ukomavu wa kiroho katika Kristo, kwa kutumia vipawa hivyo kwa njia ya upendo. Mamlaka na UongoziPaulo alitazama mamlaka aliyo nayo sawa na alivyotazama ugawaji wa vipawa mbalimbali. Katika barua zake kwa Wakorintho na Kwa Wathesalonike, Paulo anatoa kauli kadhaa juu ya jinsi alivyotumia vipawa vyake vya uongozi katika huduma yake ya kueneza Injili Anasema kwamba badala ya kutumia ukali, yeye alitumia mamlaka yake kulijenga kanisa, na wala sio kulibomoa (2 Wakorintho 1:10). Paulo hakutaka kuwapendeza watu kwa faida za kibinafsi, bali alichukua jukumu la mzazi katika kuwaasa watu kuishi maisha yanayomletea utukufu Mungu. “Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote, ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake. Tuliwapenda nyinyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu! Ndugu, nyinyi mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu. Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama. Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe. Tuliwapeni moyo, tuliwafarijini na kuwahimiza ili mpate kuishi maisha yampendezayo Mungu ambaye anawaiteni mshiriki ufalme na utukufu wake” (1 Wathesalonike 2:5-12). Jukumu linaloenda pamoja na uongozi ni kule kufanya huduma kwa nia moja na lengo moja-ili kuwasadia waamini wakomae kiimani. Lengo la uongozi sio kumletea mtu umaarufu. Hata katika Biblia kuna mahali Paulo anawasihi waamini kutopigana juu ya kumfuata kiongozi fulani, badala yake watambue kwamba Mungu ndiye anayekuza kanisa kupitia kwa kazi za watu wake (1 Wakorintho 3). Jambo la muhimu la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba wanajenga juu ya msingi wa Yesu na sio juu ya misingi yao wenyewe. Mfano anaouweka Paulo kwa viongozi ni sawa na ule wa wazazi wa kiroho wanavyoweza kuwalea wana wao wa kiroho kwa njia ya upole na utakatifu.

Usiipuze FamiliaLazima tukumbuke kwamba kuiimarisha familia ni muhimu zaidi hata kuliko kuendeleza kazi ya Mungu. Wachungaji wanastahili kutunza familia zao katika mambo ya kiroho, kihisia, na kimahitaji ya kimwili. Ni makosa kwa mchungaji kuitelekeza familia yake. Familia ya mchungaji sharti iwe mfano mwema katika uaminifu na katika uanafunzi wake wa Yesu. Ikiwa mhubiri au mchungaji atatumia muda wake mwingi kwenda hapa na pale kuhubiri na kuwahudumia watu wengine, familia yake inaweza kuteseka, na matokeo yake ikawa ni kupotoka kwa watu wa familia hiyo, maana itabidi watumie mbinu zozote kukidhi mahitaji yao. Kwa upande mwingine, ikiwa viongozi wa kanisa watatumia muda wa kutosha kuwa nyumbani na watoto wao na kuwalea katika njia za Mungu, basi matunda ya kufanya hivyo yataonekana pia katika jamii nzima. Kuwasaidia Wakristo Wachanga na Wadhaifu KukuaSifa nyingine ambayo viongozi wanastahili kuwa nayo ni kujifunza kutochoshwa na watu. Viongozi sharti wawe watu wenye subira huku wakijua kwamba mpango wa Mungu juu ya maisha ya kila mmoja wa washirika wao bado unaendelea kutekelezwa. Lengo kuu la viongozi ni kuona kwamba kila mtu anakomaa kiroho, na sio huwapuzilia mbali wale walio wadhaifu, wakaidi au waliovunjia moyo. “Ndugu, tunawahimizeni mwaonye watu walio wavivu, mwatie moyo watu wanyonge, mwasaidie watu dhaifu, mwe na subira kwa wote ( 1 Wathesalonike 5:14). Manabii waliwakemea viongozi waliokuwa hawalisaidii kundi lililowekwa chini yao. “Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu! Toa unabii dhidi ya wachungaji wa Israeli. Waambie hao wachungaji kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ole wenu nyinyi wachungaji wa Israeli, mnaojilisha nyinyi wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? Mnakunywa maziwa,mnavaa mavazi ya manyoya yao na kondoo wanono mnawachinja na kula. Lakini hamwalishi hao kondoo. Walio dhaifu hamkuwapatia nguvu, wagonjwa hamkuwaponya, waliojeruhiwa hamkuwafungia dawa, waliotangatanga hamkuwarudisha na waliopotea hamkuwatafuta. Lakini mmetumia mabavu na ukatili kuwatawala. Basi, kwa kuwa hao kondoo hawakuwa na mchungaji walitawanywa, wakawa mawindo ya wanyama wakali” (Ezekieli 34:1-5). Wakati mwingine viongozi wa kanisa huwaangalia sana wale wenye pesa nyingi kanisani, wanaovaa vizuri, na walio maarufu katika kanisa au katika jamii. Lakini watu hawa, wanaweza kuwa sio wale ambao Mungu anataka kuwatumia kwa kazi yake muhimu. Mungu alimwagiza nabii Samweli kuhusu kuwabagua watu kwa njia hii wakati alipokuwa akitafuta ni nani wa kumpaka mafuta awe mfalme wa Israeli. “Lakini Mwenyezi-Mungu alimwambia, “Usiangalie sura yake na urefu wa kimo chake. Mimi nimemkataa kwa siangalii mambo kama wanavyoangalia binadamu wenye kufa. Binadamu huangalia uzuri wa nje, lakini mimi naangalia moyoni.” ( 1 Samueli

Copyright © 2007 Tammie Friberg 120

Page 124: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

16:7 ). Kanisa halistahili kuwaangalia watu kama ulimwengu ufanyavyo, hii ni kwa sababu malengo ya watu wa ulimwengu na ya kanisa ni tofauti kabisa. Kanisa lastahili kuzingatia maneno ya Mtume Paulo, aliposema, “Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo. Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu” (Wakolosai 1:28-29).

Usikatae Maonyo Madogo Kama tulivyokwisha ona hapo mbeleni, kuna wakati tunahitajika kuonyana na kukosoana. Kuonyana ni kiungo muhimu katika uwakili na utendaji kazi wa pamoja wa kanisa. Tunapoonyana, huwa tunausaidia mwili wa Kristo udumu katika hali njema na uwe na mwelekeo. Mtume Paulo aliwatia moyo Wakristo wa Kirumi waliokuwa wamekomaa kiimani kiasi cha kuweza kuonyana wenyewe kwa wenyewe. Alisema, “Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba nyinyi pia mmejaa wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana nyinyi kwa nyinyi (Warumo 15:14 ). Tusikose kutofautisha kati ya kuonyana au kushauriana na kuwahukumu wengine kwa njia ya kinafiki, kwa kutumia mtazamo wetu au shida zetu, na kuanza kusema waamini wenzetu wako hivi au vile. Pia tusitegemee maneno ya kusikia kutoka kwa watu, au kuwawekea wengine sheria sisizo kuwa za Mungu. Vipawa vyote lengo lake ni kuujenga mwili wa Kristo, kwa sababu hiyo, sote tunastahili kulindana kiimani Mhubiri sharti awe tayari kukosolewa matendo yake, au mafundisho anayohubiri. Hakuna mtenda kazi kanisani ambaye hastahili kufuata sheria, au kwa maneno mengine, anayejiona kuwa yeye tayari ndiye sheria. Viongozi wa kanisa sharti waishi kwa kufuata yale yale wanayoyahubiri wao wenyewe. Lazima pia tumruhusu Mungu kutuchunguza kwa undani iwapo tuna dhambi za siri au dhambi tunazozifanya kwa hairi . Huenda tumeruhusu hali ya uvivu kutukumba kwa kuwaiga watu wa ulimwengu wasiozifuata sheria za Mungu. Katika kuchangamana kwetu na watu wa ulimwengu, huwa kwa kiasi fulani tunaathiriwa na kuiga tabia zao, na kwa njia hiyo dhamira zetu kuchomwa na kufa ganzi kabisa. Mfalme Daudi aliandika maneno haya, “Lakini nani anonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi, usikubali hayo yanitawale. Hapo nitakuwa mkamilifu, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu” (Zaburi19:12-14). Kama Daudi alivyomruhusu Mungu kuyachunguza mawazo yake, ndivyo tunavyostahili kunyenyekea na kumruhusu Mungu kutuchunguza. Kutumia Vipawa Vya Kiroho Kwa Njia IpasayoKatika kanisa kuna shida zinazotokana na matumizi mabaya ya vipawa vya kiroho. Kwa hiyo sharti tuwe waangalifu kuhakikisha kwamba matumizi ya vipawa vya kiroho hayafanani au kufuata mfumo wa kipagani. Vipawa vya kiroho vinastahili kutumiwa kwa kufuata kanuni za Maandiko. Kwa mfano, tusichanganye matambiko ya waganga wa kienyeji na huduma ya leo ya kuhubiri au kutoa unabii. Matambiko yoyote yanayofanana na matambiko ya kipagani, yamekatazwa na Mungu katika Biblia. Mungu anapenda tutumie vipawa vyetu kulingana na mwongozo wake. Mkristo hastahili kutumia matambiko ya kupunga pepo au kuleta uponyaji, kwa sababu kwa kufanya hivyo, mtu huyo atakuwa hazitegemei nguvu za ufufuo wa Yesu dhidi ya mamlaka, falme na uwezo wa Shetani. Nguvu hizi zinapatikana kwa Yesu pekee. Sharti tumwombe yeye wakati tunapotaka usaidizi wowote. Sio vibaya kwenda kutafuta matibabu, almradi matibabu hayo yasiambatane na matambiko, dhabihu, au maneno ya kichawi au kiganga. Ikiwa mtu anataka kuwa wakili mzuri wa vipawa vya kiroho, sharti kwanza ayatupie kisogo mambo yote ya Ufalme wa Giza, na badala yake atumie vipawa vyake sawa na maagizo ya Mungu katika Neno lake (Tazama Somo la 6, Kupima Kila Kitu katika mizani ya Neno la Mungu; na Somo la 3, Jinsi Mungu Anavyowasiliana Nasi). Ukiangalia chini ya picha utaona jaa la taka kama ilivyo katika masomo yaliyotangulia. Katika kutumia vipawa vya kiroho, sharti tuweke kando mambo ya kidunia yanayotufunga. Tukiweka kando mambo ya kale tulipokuwa katika Ufalme wa Giza, basi mwili wa Kristo, utaendelea kukua na kukamilika (Tazama kisanduku chenye Maandiko kilicho mwanzoni wa somo hili).

Kila Mtu Sharti Awe Mwaminifu Katika Majukumu MadogoSasa baada ya kutazama uwakili wa viongozi, hebu sasa tujiulize: Je, jukumu la kondoo katika mambo ya uwakili ni gani? Kwa kujibu swahili hebu tuangalia kisa kimoja alichokisimulia Yesu juu ya bwana mmoja aliyekuwa anakwenda safari. Naye kabla hajaondoka akachukua mali yake na kuwakabidhi watumishi au mawakili kadhaa. Kisa chenyewe kinasema hivi, “Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja fedha talanta tano, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri. Mara yule aliyekabidhiwa fedha talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano. Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili. Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaenda, akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake. “Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake. Mtumishi

Copyright © 2007 Tammie Friberg 121

Page 125: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

aliyekabidhiwa fedha talanta tano akaja amechukua talanta tano faida, akamwambia, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.’Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’ “Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.’ Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’“Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya. Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.’ “Bwana wake akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya. Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake! Basi, mnyang'anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi. Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno’” (Mathayo 25:15-30). Yesu ametupa uwezo na talanta za kutumia kwa ajili ya Ufalme wake. Wakati mwingine tunatamani cheo kikubwa kitakachotufanya kuwa watu wenye ushawishi mkubwa na pia kuwa na watu walio chini ya mamlaka yetu. Lakini kulingana na kanuni hii ya Mungu inavyofanya kazi, lazima tuwe waaminifu katika mambo madogo kwanza. Tunapokuwa waaminifu na wenye bidii, tunadhihirisha kwamba sisi ni waaminifu na wakutegemeeka. Tunakua kwa kujifunza kanuni za Mungu. Tukifanya hivyo Mungu atatuongezea majukumu mengine. Kiongozi kuwa na wafuasi wengi haimaanishi kwamba kiongozi huyo amebarikiwa na Mungu, na vilevile haimaanishi kwamba wafuasi hao wamejitoa kufuata mafundisho ya kweli. Makundi ya watu kwa kawaida hugeukageuka, na mara nyingi watu hutaka kusikia yale wanayotaka kusikia. Yesu alifanya kazi na mitume kumi na wawili tu, lakini pamoja na hayo watu hao kumi na wawili waliweza kuibadilisha dunia! Mtume Paulo alikuwa ni mtu mmoja, lakini ushawishi wa mafundisho yake umeweza kutufikia hata sisi leo! Kwa hiyo kuwa mwaminifu, uone kazi ile Mungu atakayokukabidhi umfanyie. Inaweza kuwa kazi kubwa au ndogo. Hakikisha unakuwa mwaminifu katika mambo madogo, na hatimaye mambo yanaweza kuwa makubwa zaidi ya unavyofikiria, na yakamletea Mungu sifa na utukufu. 2. Habari Njema:Picha ya msalaba chini ya ukurasa inawakilisha aina mbalimbali za uwakili. Uwakili huu ni ule wa ujumbe wa Mungu. Je, unajua kwamba kila mmoja wetu amepewa ujumbe fulani kwa ajili ya ulimwengu? Ujumbe huu ni ujumbe wa Upatanisho. Ni ile Habari Njema Ya Wokovu na Habari Njema ya Ufalme wa Mungu. Mtume Paulo alionyesha uwakili wa aina hii wakati Mungu alipomfunulia kwamba Habari Njema haikuwa kwa ajili ya Wayahudi tu, bali pia kwa ajili ya Mataifa (Waefeso 3:2-6). Paulo alitimiza uwakili huu kwa kusafiri na kueneza Injili katika miji na vijiji kila mahali. Ujumbe tuliokabidhiwa ni muhimu sana, kwa sababu katika Ufalme wa Giza, upatanisho ni tendo lisilokuwa kamilifu. Upatanisho unaweza kukamilishwa tu iwapo mtu atakuwa na uhusiano na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo. “Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za Mungu” ( 1 Wakorintho 4:1).

Uwakili Wa Kimisionari Ukiitazama milima iliyoko katika picha, utaweza kuona makanisa madogo yaliyoenea vijijini kote. Vitu hivi vinawakilisha uwakili wa kimisionari tuliopewa na Mungu, ili tuweze kwenda maeneo yaliyo mbali na kwetu na kuieneza Injili huko. Matendo 1:8 inasema, “Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.” Tambua kwamba kuna sehemu tatu zilizotajwa katika Andiko hili. Sehemu ya kwanza ni Yerusalemu. Yerusalemu unaweza kulinganishwa na watu wa kabila lako, nyumbani kwako, kijijini kwako, au mjini kwako. Jimbo la Judea linaweza kuwakilisha sehemu zilizo katika nchi zetu, lakini ziko mbali na mji wetu. Jimbo la Samaria linawakilisha changamoto ya kuwafikia watu walio nchini mwetu, na tunaowabagua kwa njia moja au nyingine. Hatimaye mwisho wa dunia, ni mwito kwa kanisa kuweza kupeleka Habari Njema katika sehemu zilizo nje ya nchi. Kanisa litakapotenda kazi yake kwa misingi ya Biblia, litafikia kiwango cha kuwatuma watu walio na vipawa vya utume, watu waliofunzwa na kuhitimu, katika kazi ya kuanzisha makanisa, kuhubiri, nao wataondoka na kwenda kuanzisha makanisa mapya. Kanisa lililowatuma litakuwa sasa ndilo mama, na makanisa mengine yatakayoanzishwa yatakuwa kama watoto wa lile kanisa “mama.” Hapa kuna habari zinazohusu wamisionari wa kwanza waliowahi kutumwa kwenda kuhubiri Habari Njema, “Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia” (Matendo 13:2). Paulo alikuwa na wamisionari wenzake walioambatana naye kila alipokwenda. Paulo alisafiri na kuanzisha makanisa, kuwafundisha viongozi na kuendelea kuwa na uhusiano wa karibu na makanisa yale aliyoyaanzisha kama baba wa kiroho. Kwa njia hii, Habari Njema iliweza kuwafikia watu wa Mataifa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 122

Page 126: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

miaka ya mwanzo mwanzo ya Ukristo. Sisi tumepewa uwakili wa ujumbe wa Wokovu! Ili uwakilii huu uweze kufanya kazi vizuri, sharti kama kanisa tufanye kazi ya umisionari kanisani.

Watu wengine hushindwa kutofautisha kati ya misaada ya kibinadamu na kazi ya umisionari. Kama tulivyojifunza, kuwatunza maskini ni baadhi ya kazi alizotukabidhi Yesu. Lakini kuwapa watu misaada ya kibinadamu, bila kuwatangazia Habari Njema hakuwezi kuwapatanisha na Mungu. Habari Njema ni ujumbe wa kusema, unaothibitishwa na ujumbe wa vitendo kama vile kuwapenda watu kwa upendo wa Kristo. Katika makanisa yetu tunahitaji kuwa na sehemu zote mbili. Ujumbe wa Injili sharti utangazwe kwa wanadamu.

MuhtasariMsingi wa uhusiano wetu na Mungu ni neema. Mungu alituumba, na kutokomboa, kwa hiyo tunastahili kumwishia yeye. Yeye ndiye anayekidhi mahitaji yetu. Vilevile ametupa uzima wa milele kupitia kwa Yesu Kristo. Yesu hutupa vipawa vya kiroho ili tuweze kivitumia kuujenga Ufalme wake. Pia alitukabidhi jukumu la kuwapatanisha watu kwa Mungu. Nasi kwa kuonyesha shukrani zetu tunastahili kutunza na kuvitumia vipawa vyote alivyotupatia. Watu sio kiini cha kuwepo kwetu, bali Mungu ndiye kiini na chanzo cha kuishi kwetu. Hii ndiyo sababu tunastahili kuwa mawakili wazuri wa vipawa vyake. Mungu amekuumba wewe ili uwe na sehemu muhimu katika Ufalme wake. “Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu” (1 Wakorintho 4:2). Tumia vipawa ulivyopewa na Mungu, na Ufalme wa Mungu utaenea kwa njia ya ajabu. Wakristo wote ni watimize majukumu waliyopewa ya uwakili na kuitangaza Habari Njema, na Ufalme utakua na kuenea ulimwengu mzima.

Mahtasari Wa Mafundisho Ya Somo La 11Vizuizi Vya UwakiliShetaniWatu WengineSisi WenyeweNguvu Za Mungu Huimarishwa Katika Udhaifu Wetu

Mungu Anavyokutana na mahitaji yetu ya kimwili Jinsi Mungu Anavyokutana na mahitaji yetu ya kirohoKwa watu binafsi Kwa kila Mtu Vipawa Kwa Kanisa Habari

Makazi/Nyumba *Kutunza Uumbaji Wa Mungu *Lengo Ni Kujengana Kwa Ajili Ya Huduma

Habari Njema Za Wokovu

Chakula *Kutunza Miili Yetu Vipawa Vya Kusema, Vipawa Vya kutangaza Habari Njema

Habari Njema Za Ufalme Wa Mungu

Mahitaji Ya Nguo Vipawa Vya Kutia Moyo, Kuhimiza Na Kuponya

Elimu Ya Watoto Rehema, UkarimuKutoa Kanisani UtumishiKutoa kwa maskini Utawala

Kutoa Karama Maalum*Hupewa Watu Kulingana Na Apendavyo Roho*Waruhusu Watu Kutumia Vipawa Vyao *Waimarisheni Wadhaifu *Iweni Waaminifu Katika Mambo Madogo

Marejeo Ya Biblia Kwa Mafundisho Ya Somo La 11

Kuwa Mawakili Wa Uumbaji Wa MunguHadithi Zinazoamatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Tunza Uumbaji Wa Mungu Wa Vitu Vya Nje*Agizo La Mungu Kwa Adamu Na Hawa- Mwanzo 1:26-30; 2:15.*Mungu Alimweka Mwanadamu Awe Mwangalizi Wa Uumbaji Wake- Zaburi 8:5-8; 115:16.*Yesu Anafundisha Juu Ya Jinsi Mungu Anavyokutana na

Tunza Uumbaji Wa Mungu Wa Vitu Vya Nje*Je miungu ya uongo ya mataifayaweza kuleta mvua?Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote- Yeremia 14:22.*Mungu Hukutana Na Mahitaji Ya Mimea Na Miti Ili Iweze Kuzaa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 123

Page 127: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mahitaji Yetu- Luka 12:22-34; Mathayo 6:25-34.*Barnaba Na Paulo Wadhaniwa Kuwa Miungu. Wanawasihi Watu Watambue Kwamba Mungu Ndiye Anayeleta Mvua- Matendo 14:16-17*Yeremia Anaelezea Kwa Nini Mungu Amezuia Baraka Zake Kwa Waisraeli-kwa sababu hawakumcha Bwana Anayewapa Mvua Na Mavuno Mazuri- Yeremia 5:19-31.

Matunda- Mambo Ya Walawi 26:4-5.*Mungu Huwapa Mifugo Nyasi- Kumbu 11:14-15.*Mungu Hukutana Na Mahitaji Ya Wale Wanaomcha- Zaburi 136:25.*Mungu Hukutana Na Mahitaji Ya Mimea, Wanyama, na Watu- Zaburi 65:9-13; Zaburi 19; Zaburi 104.

*Kutunza Miili Yetu*Paulo Anafundisha Kwamba Miili Yetu Ni Ya Bwana- 1 Wakorintho 3:16-17; 6:11-20.*Watu Wameumbwa Kwa Mfano Wa Mungu- Mwanzo 1:26-31.

Kutunza Miili Yetu *Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabIsaya Umbo langu halikufichika kwako nilipokuwa natungwa ndani ya tumbo la mamangu. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga,hata kabla ya kuweko ile ya kwanza - Zaburi 139:14-16.

Kuwa Mawakili Majumbani MwetuHadithi Zinazoamatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Kazi/Nyumba/Makazi/Chakula/Nguo*Umaskini Na Shamba La Mtu Mvivu- Mithali 24:30-34.*Fumbo La Mjenzi Mwenye Busara Na Mjenzi Mpumbavu- Mathayo 7:24-27.*Yesu Anafundisha Juu Ya Mahitaji Ya Kijamii Anayotupa Mungu- Mathayo 6:25-34.

Kazi/Nyumba/Makazi/Chakula/Nguo*Kutokana na uvivu wa mtu, paa hubonyea; kwa sababu ya uzembe, nyumba huvuja - Mhubiri 10:18.*Kuwa na bidii kutampa mtu cheo, lakini uvivu utamfanya mtumwa- Mithali 12:24.*Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe- Mithali 14:1.*Mvivu halimi wakati wa kulima; wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote- Mithali 20:4.*Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie mambo yake mwenyewe na afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama tulivyowaagiza pale awali. Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu- 1 Wathesalonike 4:11-12.

Kuweka Akiba Kwa Ajili Ya Siku Zijazo-Elimu Ya Watoto, Mambo Ya Dharura, Kustaafu*Mwana Mpotevu- Luka 15.*Utajiri Wa Ibrahimu- Mwanzo 13; 24:35.*Ibrahimu Anunua Pango la Kuwazikia Wafu- Mwanzo 23.*Kisa Cha Yusufu, Farao Na Ndoto Yake- Mwanzo 41-50.*Israeli Yanunua Chakula Na Maji Kutoka Katika Nchi Ya Seiri- Kumbukumbu 2:1-8.*Yeremia Anunua Shamba- Yeremia 32.

Kuweka Akiba Kwa Ajili Ya Siku Zijazo-Elimu Ya Watoto, Mambo Ya Dharura, Kustaafu*Kulindwa na hekima ni kama kulindwa na fedha. Faida ya maarifa ni kwamba hekima hulinda maisha ya mtu aliye nayo- Mhubiri 7:12.*Haya! Kila mwenye kiu na aje kwenye maji! Njoni, nyote hata msio na fedha; nunueni ngano mkale, nunueni divai na maziwa. Bila fedha, bila gharama! Mbona mnatumia fedha yenu kwa ajili ya kitu kisicho chakula? Ya nini kutoa jasho lenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni mimi kwa makini, nanyi mtakula vilivyo bora, na kufurahia vinono. “Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu; nisikilizeni, ili mpate kuishi. Nami nitafanya nanyi agano la milele; nitawapeni fadhili nilizomwaminisha Daudi - Isaya 55:1-3.*Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini- 1 Timotheo 5:8.

Kutoa Kanisani*Watu Wanaishi Vizuri, Kanisa Laachwa Ukiwa- Hagai 1.*Yoashi Arekebisha Hekalu- 2 Wafalme 12; 2 Mambo Ya Nyakati 24.*Mfalme Yosia Arekebisha Hekalu- 2 Wafalme 22; 2 Mambo Ya Nyakati 34.*Cha Kaisari Mpeni`Kaisari, Na Cha Mungu Mpeni Mungu- Mathayo 22:17-22.*Ezra Akusanya Fedha ZA Kujengea Hekalu- Ezra 3; 7-8.*Mamajusi Wa Mashariki Wamletea

Kutoa Kanisani*Kumbukeni: “Apandaye kidogo huvuna kidogo; apandaye kwa wingi huvuna kwa wingi.” Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha. Mungu anaweza kuwapeni nyinyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “YEYE HUTOA KWA UKARIMU, HUWAPA MASKINI; WEMA WAKE WADUMU MILELE.” Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa nyinyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, zikue na kuwapa mavuno mengi ya ukarimu wenu. Yeye atawatajirisha nyinyi daima kwa kila kitu, ili watu wapate kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi zenu wanazozipokea kwa mikono yetu- 2 Wakorintho 9:6-11.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 124

Page 128: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Yesu Zawadi- Mathayo 2.*Wanafunzi Wa Yesu Walitoa Kulingana Na Uwezo Wao- Matendo 11:29.*Waamini Wote Walikuwa Na Nia Moja Na Waligawanyiana Mali Zao - Matendo 4:32-35.*Waamini Wa Akaya Na Makedonia Walitoa Mchango Wao Kuwasadia Maskini- Warumi 15:25-27; 2 Wakorintho 8:1-15; 2 Wakorintho 9:1-13.Kuwasaidia Maskini*Yesu Anafundisha Juu Ya Kuwatunza Walio Na Njaa, Au Wageni, Wasio Na Nguo, Wagonjwa, au Waliofungwa, Kama tungalivyomtendea yeye - Mathayo 25:31-46.*Sheria Zanazohusu Majirani Zetu- Kumbukumbu 23:19-25.

Kuwasaidia Maskini*Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu- Warumi 12:11-13.*Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma, anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu? Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo- 1 Yohana 3:17-18.*Endeleeni kupendana kindugu. Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua. Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao- Waebrania 13:1-3.*Mnafunga, na kugombana na kupigana ngumi. Mkifunga namna hiyo maombi yenu hayatafika kwangu juu. Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu.Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami? “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote! Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu. “Mkifanya hivyo mtang'ara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka.Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu. Ndipo mtakapoomba,nami Mwenyezi- Mungu nitawaitikia; mtalia kwa sauti kuomba msaada, nami nitajibu, ‘Niko hapa!’ “Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu, mkiacha kudharau wengine na kusema maovu, mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana. Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe. Magofu yenu ya kale yatajengwa; mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena- Isaya 58:4-12.*Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe? Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka? Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale anaomwomba. “Yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo. Hii ndiyo maana ya sheria ya Mose na mafundisho ya manabii- Mathayo 7:9-12; Luka 11:11-13.*Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu- Wagalatia 6:10.*Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini-Waefeso 4:28.*Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. Yafaa kitu gani nyinyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?- Yakobo 2:15-16.*Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma, anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu? Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo- 1 Yohana 3:17-18.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 125

Page 129: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuwa Mawakili Wa Yesu KanisaniHadithi Zinazoamatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Lengo Ni Kujengana Kwa Ajili Ya Huduma*Malaki Azungumzia Juu Ya Dhuluma Katika Huduma- Malaki 2:7-17.*Ezekieli Azungumzia Dhuluma Katika Huduma- Ezekieli 22:23-31.*Wanawake Na Uwakili Katika Huduma- Hesabu 31:13-18.*Sulemani Apewa Karama Ya Hekima- 1 Wafalme 3.

Lengo Ni Kujengana Kwa Ajili Ya Huduma*Mungu Ana Mpango Mzuri Kwa Kila Mmoja Wetu- Zaburi 139:14-16.*Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, husema na watu kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji na kuwatia moyo. Hali kadhalika na nyinyi, maadamu mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa- 1 Wakorintho 14:3, 12.*Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa- 1 Wathesalonike 5:11.*Basi sikilizeni enyi Waisraeli! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni Mwenyezi-Mungu mmoja. Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu yenu yote. Wekeni moyoni mwenu maneno hayo inayowaamuru leo na kuwafundisha kwa uangalifu watoto wenu. Mtawasimulia mwapo mnakaa nyumbani au mlipo safarini au mnapolala au mnapoamka. Yafungeni katika mikono yenu na kuyavaa katika paji za nyuso zenu kama ukumbusho.Yaandikeni kwenye miimo ya milango yenu na malango ya miji yenu- Kumbukumbu 6:4-9.

Karama Za Kusema, Karama Za Kutangaza Habari Njema[Utume (mmisionari), Kuhubiri, Kufundisha, Uinjilisti, Na Unabii (Kuwarejesha Watu Katika Njia ZA Mungu). Vipawa Au Karama Zinazohusiana Na Kusema Ni Kama Utambuzi, Ufahamu, Na Uongozi. Karama Za Miujiza Zinazohusiana Na Kusema au Uinjilisti ni: Kusema Kwa Lugha, Kutafsiri Lugha, Na Kazi Za Miujiza.]*Viongozi Na Walawi Wanawafundisha Watu Katika Kila Mji- 2 Mambo Ya Nyakati 17:7-9.*Ezra Ajitoa Kimasomaso Katika Mafundisho Ya Bwana- Ezra 7:10.*Wakristo Wa Kanisa La Kwanza walikuwa Na Juhudi Katika mafundisho Na Maombi- Matendo 5:42.*Bwana Anamfundisha Daudi Ili Na Yeye Aweze Kuwa na Ufahamu Zaidi Kuliko walimu wake- Zaburi 119:99-104.*Paulo Ana Hakika Kwamba Watu Wanaweza Kutiana Moyo Na Kufundishana-Warumi 15:14.*Unabii Hutumika Kuwatia Moyo Na Kuwafundisha Watu- 1 Wakorintho 14:31.*Jinsi Ya Kumjua Nabii Wa Kweli- Kumbukumbu 13; 18:22.*Debora Alikuwa Nabii Na Vilevile Mwamuzi- Waamuzi 4.*Miriamu, Nabii Wa Kike- Kutoka 15:20.*Hulda, Nabii Wa Kike- 2 Wafalme 22; 2 Mambo Ya Nyakati 34.*Ana, Nabii Wa Kike- Luka 2:36-52.*Binti Za Filipo- Matendo 21.*Eldadi Na Medadi Walikuwa Manabii Enzi Za Musa; Musa Anatamani Kila Mtu Angelikuwa Nabii- Hesabu 11.*Eliya Akabiliana Vikali Na Manabii Wa Baali- 1 Wafalme 18.*Maonyo Juu Ya Manabii Wa Uongo- 2 Petro 2; 1 Yohana 4.*Farao Anamtafuta Mtu Mwenye Uwezo Wa Kutafsiri Ndoto- Mwanzo 41.

Karama Za Kusema, Karama Za Kutangaza Habari Njema[Utume (mmisionari), Kuhubiri, Kufundisha, Uinjilisti, Na Unabii (Kuwarejesha Watu Katika Njia ZA Mungu). Vipawa Au Karama Zinazohusiana Na Kusema Ni Kama Utambuzi, Ufahamu, Na Uongozi. Karama Za Miujiza Zinazohusiana Na Kusema au Uinjilisti ni: Kusema Kwa Lugha, Kutafsiri Lugha, Na Kazi Za Miujiza.]*Ni wajibu wa makuhani kuwafundisha watu maarifa ya kweli juu ya Mungu. Watu wawaendee kujifunza matakwa yangu kwao, kwani makuhani ni wajumbe wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi- Malaki 2:7.*Hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote. Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia. Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako- 2 Timotheo 4:2-5.*Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote. Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani. Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi! Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote, ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake. Tuliwapenda nyinyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu! Ndugu, nyinyi mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu. Nyinyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, kwamba mwenendo wetu kati yenu nyinyi mnaoamini ulikuwa mzuri, mwadilifu na bila lawama. Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe. Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza ili mpate kuishi maisha yampendezayo Mungu ambaye anawaiteni mshiriki ufalme na utukufu wake. Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, nyinyi mliusikia, mkaupokea, si kama vile ujumbe wa

Copyright © 2007 Tammie Friberg 126

Page 130: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Danieli Na Uwezo Wake Wa Utambuzi- Danieli 6.

Kusema Kwa Lugha:Watu Waliongea Kwa Lugha Katika Sehemu Ambazo Injili Ilikuwa Inahubiriwa Kwa Mara Ya Kwanza Kabisa:*Siku Ya Pentekote (Wayahudi)- Matendo 2.*Kujumuishwa Kwa Watu Wa Mataifa Katika Imani- Matendo 10:45-46; 11:16-18.*Wanafunzi Wa Yohana (Walijua Ubatizo Wa Yohana Pekee)- Matendo 19:6.*Yamkini Watu Walisema Kwa Lugha, Lakini Biblia Haisemi Wazi Wazi (Wasamaria)- Matendo 8:4-8; 14-17.Sehemu Zinazoonyesha Kuwa Watu Waliokoka Hata Bila Kusema Kwa Lugha:*Watu 3,000 Waokolewa- Matendo 2:41.*Katika Tukio La Uponyaji Yerusalemu, Watu 2,000 Walimpokea Yesu Kama Mwokozi Wao- Matendo 4:4.*Kuokolewa Kwa Paulo- Matendo 9.*Towashi Mwethiopia- Matendo 8:26-40.*Watu Waliitwa Wakristo Kwa Mara Ya Kwanza Antioki- Matendo 11:19-21; 13:1-3.*Ludia Na Familia Yake- Matendo 16:14-15.*Askari Wa Magereza Aokoka Na Familia Yake Huko Filipi- Matendo 16:29-34.*Wayahudi, Watu Wa Mataifa Wanaomcha Mungu, Wanawake Wenye Hadhi Kubwa Kutoka Thesalonike Waokolewa- Matendo 17:1-4.*WaBerea Wenye Busara- Matendo 17:10-12.*Hotuba Ya Paulo Huko Athene- Matendo 17:32-34.*Waamini Wa Kwanza Huko Korintho Akiwemo Mkuu mmoja Wa Sinagogi Na Jamii Yak- Matendo 18:7-8.

Maagizo Juu Ya Kusema Kwa Lugha:[Lugha Zilizotajwa katika Biblia Zilikuwa Lugha Halisi Zilizofahamika kwa Watu Waliozisikia, Lakini Sio Kwa Wale Waliozisema. Lugha Zilikuwa Ishara Kwa Wale Wasiomwamini Mungu, hususan Katika Sehemu Ambazo Ukristo Ulikuwa Ndio Waanza]Malengo Ya Lugha Nje Ya Kanisa*Utangulizi wa Uinjilisti- Matendo 2:11, 14-41.*Kama Ishara Ya Wokovu Au Laana- 1 Wakorintho 14:20-22; Isaya 28:11-na kuendelea.Malengo Ya Lugha Kanisani*Sharti Lengo Liwe Ni Kulitia moyo Kanisa- 1 Wakorintho 14:26-28.*Lazima Lugha Zitafsiriwe- 1 Wakorintho 12:28-29.*Sio Kila Mtu Ana Kipawa Cha Kusema Kwa Lugha- 1 Wakorintho 12:30.*Wanaosema Kwa Lugha Sharti Wawe Wawili Au Watatu tu- 1 Wakorintho 14:27-28.*Mtu Anayesema Kwa Lugha Hujijenga Yeye mwenyewe- 1 Wakorintho 14:4.*Mafundisho Ni Muhimu Zaidi Kuliko Kusema Kwa Lugha- 1 Wakorintho 14:19.Lugha Hutumiwa Wakati Wa Maombi*Maandiko Yanayotumiwa Kuunga Mkono Kusema

binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu nyinyi mnaoamini- 1 Wathesalonike 2:3-13.*Ndugu zangu, wengi wenu msiwe waalimu. Kama mjuavyo, sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine-Yakobo 3:1.*Kwa wakati huu nyinyi mngalipaswa kuwa waalimu tayari, lakini mnahitaji bado mtu wa kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo juu ya neno la Mungu. Mnahitaji maziwa badala ya chakula kigumu. Kila anayepaswa kunywa maziwa ni mtoto bado, hajui uadilifu ni nini. Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, waliofunzwa kwa vitendo kubainisha mema na mabaya- Waebrania 5:12-14.*Ndiye aliyewapa watu zawadi: wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza injili, wengine wachungaji na waalimu. Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo- Waefeso 4:11-12.*Kuhusu wale wenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, waseme wawili au watatu, na wengine wayapime maneno yao. Ikiwa mmoja anaposema na mwingine wa wasikilizaji amepata ufunuo kutoka kwa Mungu, basi, yule anayesema anyamaze. Maana nyote mwaweza kutangaza ujumbe wa Mungu, mmoja baada ya mwingine, ili nyote mpate kujifunza na kutiwa moyo. Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni lazima kitawaliwe na huyo mwenye hicho kipaji. Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani. Kuhusu wale wenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, waseme wawili au watatu, na wengine wayapime maneno yao- 1 Wakorintho 14:29-33.*Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana- Yakobo 5:10.*humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua. Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe- 1 Wakorintho 12:10-11.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 127

Page 131: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kwa Lugha Ni Maandiko Yaliyo Na Muktadha Wa Kanisani- Warumi 8:26; 1 Wakorintho 14:15.*Lugha Za Malaika,” Kama Ilivyo Katika- 1 Wakorintho 13:1; Job 1-2; 2 Wakorintho 12: na kuendelea, huchukuliwa na Wengi Kuwa Mbalagha Au Lugha Ya kutia Chumvi.*Maombi Ya Yesu- Mathayo 6:9-13; Yohana 17; Luka 22:41-46.Vipawa Vya Kuwatia Moyo Watu, Kuwakaripia/kuwahimiza, Watu, Na Kuponya*Yonathani Amtia Moyo Daudi- 1 Samueli 23:16.*Maombi Ya Yesu Kwa Petro- Luka 22:32.*Petro Anamwomba Mungu Kumponya Mgonjwa Badala Ya Kumpa Pesa- Matendo 3.*Musa Anamtia Moyo Yoshua- Kumbukumbu 3.*Barnaba Anawatia Moyo Waamini Wadumu Katika Imani-Matendo 11:21-24.*Viongozi Wa Kanisa Wawatia Moyo Waamini Wa Kolosai- Wakolosai 4:7-18.*Timotheo Atumwa Kwenda Kuwatia Moyo Wathesalonike- 1 Wathesalonike 3:2.*Daudi Ajitia Moyo Katika Bwana- 1 Samueli 30:3-6.*Yesu Amtia Moyo Mariamu- Luka 10:40-42.*Paulo Anamkaripia Petro- Wagalatia 2.

Vipawa Vya Kuwatia Moyo Watu, Kuwakaripia/kuwahimiza, Watu, Na Kuponya*Imarisheni mikono yenu dhaifu, kazeni magoti yenu manyonge. Waambieni waliokufa moyo: “Jipeni moyo, msiogope! Tazameni Mungu wenu atakuja kulipiza kisasi, atakuja kuwaadhibu adui zenu; atakuja yeye mwenyewe kuwaokoeni.” Hapo vipofu wataona tena, na viziwi watasikia tena. Walemavu watarukaruka kama paa, na bubuwataimba kwa furaha. Maji yatabubujika nyikani na vijito vya maji jangwani- Isaya 35:3-6.*Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa- 1 Wathesalonike 5:11.*Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, mwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote- 1 Wathesalonike 5:14.*Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji wa Mungu; wasiwe wachongezi au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha mambo mema, ili wawazoeze kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto, wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa- Tito 2:3-5.*Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi-Waebrania 3:13.*Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini, mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi-Mungu nitamshangilia Mungu anayeniokoa. Bwana, Mwenyezi- Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani- Habakuki 3:17-19.*Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, muonye; akitubu, msamehe. Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema, ‘Nimetubu,’ lazima umsamehe- Luka 17:3-4.

Huruma/Rehema, Ukarimu*Kisa Cha Msamaria Mwema- Luka 10.*Yesu Awaonea Huruma Watu Wa Yerusalemu- Mathayo 23:37.*Fumbo La Mtumishi Asiyesamehe- Mathayo 18.*Mungu Anawahurumia Watu Wa Ninawi- Yona*Mungu Anamhrumia Paulo- 1 Timotheo 1:13.*Daudi Anamhurumia Sauli- 1 Samueli 26; 28.*Ayubu Awatendea Ukarimu Watu Wengine- Ayubu 29:15-17.

Huruma/Rehema, Ukarimu*Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Hakuna sheria inayoweza kupinga mambo hayo-Wagalatia 5:22-23.*Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate, wakiwa wamekauka koo kwa kiu, mimi Mwenyezi- Mungu nitawajibu; mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha. Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu, na chemchemi katika mabonde. Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji, na nchi kame kuwa chemchemi za maji. Nitapanda miti huko nyikani: mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni;nitaweka huko jangwani: miberoshi, mivinje na misunobari. Watu wataona jambo hilo, nao watatambua na kuelewa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo, mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo - Isaya 41:17-20.

Utumishi*Simoni Mkurene Anamtumikia Yesu- Marko 15:21-22.*Watumwa Wa Haki/Uadilifu- Warumi 6.*Nyumba Ya Stefana Ilijitolea Kuwatumikia Watu Wa Mungu- 1 Wakorintho 16:15-16.*Kanisa La Thuatira Lamtumikia Bwana- Ufunuo

Utumishi*Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi-Mathayo 20:28.*Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi. Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata

Copyright © 2007 Tammie Friberg 128

Page 132: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

2:18-19. hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi- Luka 22:26-27.*Nyinyi ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo. Maana sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: “MPENDE JIRANI YAKO KAMA UNAVYOJIPENDA MWENYEWE.” Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe- Wagalatia 5:13-15.*Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za Mungu. Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa waminifu- 1 Wakorintho 4:1-2.*Ishinikama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu. Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme- 1 Petro 2:16-17.

Utawala*Musa Ateua Viongozi- Kutoka 18.*Danieli Na Wenzake Wateuliwa Kama Watawala- Danieli 2:49; 3:12.*Utawala Katika Kanisa La Kwanza- 2 Wakorintho 8; 1 Timotheo 1.

Utawala*Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni- 1 Wakorintho 12:28.

Kutoa*Waamini Wa Yerusalemu Waligawanyiana Vitu Vyao- Matendo 2:44-45; 4:32-35.*Ukarimu Wa Kanisa La Antiokia- Matendo 11:27-30.*Barnaba Ni Mkarimu- Matendo 4:36.*Waamini Wa Makedonia Na Akaya Walikuwa Wakarimu- Warumi 15:25-28; 2 Wakorintho 8:1-5.*Wafilipi Walitoa Mali Zao Kusaidia Kazi Ya Mungu- Wafilipi 1:10, 14-19.*Wakorintho Ndio Waliokuwa Baadhi Ya Watu Wa Kwanza Kutoa- 1 Wakorintho 16:3; 2 Wakorintho 8:10.*Kisa Cha Mwanamke Mjane aliyekuwa Maskini- Marko 12:38-44.*Wanaume Kwa Wanawake Watoa Kwa Ajili Ya Kujenga Hema La Mkutano- Kutoka 35:22.*Paulo Ni Mtumishi Wa Kuwavuta Watu Kwa Kristo- 1 Wakorintho 9:19-20.

Kutoa*Ndugu, tunapenda kuwapa habari juu ya neema ambazo Mungu ameyajalia makanisa ya Makedonia. Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana. Naweza kushuhudia kwamba walikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao na hata zaidi. Kwa hiari yao wenyewe, walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu. Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia, kufuatana na mapenzi ya Mungu- 2 Wakorintho 8:1-5.*Mtu yeyote atakayewapeni kikombe cha maji ya kunywa, kwa sababu nyinyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake. “Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali kwa mtu huyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa la kusagia na kutupwa baharini - Marko 9:41-42.*Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima. Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria- Warumi 13:7-8.*Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na astahiliye heshima, heshima-Warumi 13:7.*Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme- 1 Petro 2:17.*Je, ni sawa mtu kumdanganya Mungu? La! Lakini nyinyi mnanidanganya! Walakini nyinyi mwauliza: ‘Tunakudanganya kwa namna gani?’ Naam! Mnanidanganya kuhusu zaka na dhabihu zenu. Nyinyi na taifa lenu lote mmelaaniwa kwa sababu ya kunidanganya. Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele- Malaki 3:8-10.

Karama/Talanta Maalum*Fumbo La Talanta- Mathayo 25.*Mungu Huwapa Watu Ujuzi Wa Sanaa- Kutoka 31:1-11.*Hiramu Kutoka Tiro- 1 Wafalme 7.

Karama/Talanta Maalum*Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine kama wakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina- 1 Petro 4:10-11.

Vipawa Hutolewa Kulingana Na Apendavyo Roho*Paulo Anafundisha Juu Ya Matumizi Ya Vipawa Vya

Vipawa Hutolewa Kulingana Na Apendavyo Roho*Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 129

Page 133: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Roho- Warumi 12:6-8. Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja. Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote. Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu, apendavyo Roho huyohuyo. Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya; humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua. Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe- 1 Wakorintho 12:4-11.

Waruhusu Watu Kutumia Vipawa Vyao*Paulo Anafundisha Juu Ya Matumizi Ya Vipawa Kanisani- 1 Wakorintho 12:14-31.*Diotrefe- 3 Yohana.*Kupanda Na Kuvuna- 1 Wakorintho 1; 3.

Waruhusu Watu Kutumia Vipawa Vyao *Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi. Tumia wakati wako na juhudi yako katika kusoma hadharani Maandiko Matakatifu, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja. Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee. Fikiri kwa makini juu ya hayo yotena kuyatekeleza kusudi maendeleo yako yaonekane na wote. Angalia sana mambo yako mwenyewe na mafundisho yako. Endelea kufanya hayo, maana ukifanya hivyo, utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza- 1 Timotheo 4:12-16.

Uwe Mwaminifu Katika Mambo Madogo*Fumbo La Talanta- Luka 19.

Uwe Mwaminifu Katika Mambo Madogo*Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake. Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia. Hivyo msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu, wakapokea yale aliyoahidi Mungu- Waebrania 6:10-12.*Kwa sababu hiyo, fanyeni bidii ya kuongeza imani yenu kwa fadhila, fadhila yenu kwa elimu, elimu yenu kwa kuwa na kiasi, kuwa na kiasi kwa uvumilivu, uvumilivu wenu kwa uchaji, uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani. Kwa hiyo basi, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuufanya huo wito wenu mlioitiwa na Mungu uwe jambo la kudumu katika maisha yenu; kama mkiishi namna hiyo hamtaanguka kamwe- 2 Petro 1:5-10.* Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unayopewa na Mungu. Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya mastahili ya matendo yetu, bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo kwa ajili ya Kristo Yesu kabla ya wakati, lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo. Mimi nimechaguliwa niwe mtume na mwalimu kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema, nami nateseka mambo haya kwa sababu hiyo. Lakini niko bado timamu kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina hakika kwamba yeye atakilinda salama kile alichonikabidhi, mpaka siku ile. Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu. Jambo lile bora ulilokabidhiwa lilinde kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu- 2 Timotheo 1:8-14.

Kuwa Mawakili Wazuri Wa Habari NjemaHabari Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Somo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 130

Page 134: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Habari Njema Ya Wokovu*Filipo Aenda Samaria- Matendo 8:5.*Makanisa Yanatuma Wamisionari- Matendo 13.*Ludia Ampokea Yesu Kama Mwokozi Wake; Askari Wa Magereza Ampokea Yesu Kama Mwokozi Wake- Matendo 16.*Mahubiri Ya Petro- Matendo 2.*Yesu Anapaa Kwenda Mbinguni- Matendo 1:1-11.*Wakristo Wa Kwanza Walihubiri Habari Njema Kila Siku- Matendo 5:42.

Habari Njema Ya Wokovu*Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati”- Mathayo 28:19-20.*Hubiri Kwa Nia Safi- Wafilipi 1:15-18.*Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishi katika ukweli.Mpenzi wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu, hata kama ni wageni. Ndugu hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali uwasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu. Maana wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. Basi, sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushiriki katika kazi yao kwa ajili ya ukweli- 3 Yohana 1:4-8.*Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni jukumu lao kwa hao. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki baraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi katika mahitaji yao ya kidunia- Warumi 15:27.*Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki,nimekushika mkono na kukulinda. Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwanga wa mataifa. Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu. Tazama, mambo niliyotabiri yametukia; na sasa natangaza mambo mapya, nakueleza hayo kabla hayajatukia”- Isaya 42:6-8.*Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe. “Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu. Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu. Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe. Lakini mwenye kuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu-Yohana 3:16-21.

Habari Njema Ya Ufalme Wa Mungu*Yesu Awatuma Wanafunzi Sabini- Mathayo 10; Marko 6:1-13.*Wafilipi Walihubiri Habari Njema Ya Ufalme- Matendo 8:12.*Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili Kuhubiri Ufalme Wa Mungu- Luka 9.*Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu. Basi, akawatuma wajumbe wamtangulie, nao wakaenda wakaingia kijiji kimoja cha Wasamaria ili amtayarishie mahali. Lakini wenyeji wa hapo hawakutaka kumpokea kwa sababu alikuwa anaelekea Yerusalemu. Basi, wanafunziwake, kina Yohane na Yakobo, walipoona hayo, wakasema, “Bwana, wataka tuamuru moto ushuke kutoka mbinguni uwateketeze?” Lakini yeye akawageukia, akawakemea. “Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo; kwa maana Mwana wa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya watu, bali kuyaokoa.” Wakatoka, wakaenda kijiji kingine- Luka 9:51-56.

Habari Njema Ya Ufalme Wa Mungu*Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati- Mathayo 28:19-20.*Wengi waliyakubali maneno yake, wakabatizwa. Watu wapatao elfu tatu wakaongezeka katika kile kikundi siku hiyo. Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali- Matendo 2:41-42.* Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni mekaribia!- Mathayo 4:17.*Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu- Mathayo 4:23.* Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na waalimu wa sheria, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni- Mathayo 5:19-20.*Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada- Mathayo 6:33.*Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ONDOKENI MBELE YANGU, ENYI WATENDA MAOVU- Mathayo 7:21-

Copyright © 2007 Tammie Friberg 131

Page 135: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Ufalme Wa Mungu Ni Wa watoto Wadogo- Mathayo 19:13-15; Marko 10.*Mafumbo Ya Ufalme Wa Mungu- Mathayo 13; 20; 23; 25; Marko 4.*Paulo Anawasihi Watu Juu Juu ya Ufalme Wa Mungu- Matendo 19.*Kiwango Cha Kuhubiri Ufalme Wa Mungu-Matendo 28.

23.*Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”-Mathayo 19:23-24.*Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote- Mathayo 24:14.* Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu. Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii. Basi, msishirikiane nao. Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga, maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni. Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja- Waefeso 5:5-12.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 132

Page 136: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Copyright © 2007 Tammie Friberg 133

Page 137: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Somo La 12: Ufalme Ujao

Maelezo Mafupi

Maandiko: “Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, nyinyi mlistahimili. Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo. Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang’anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele. Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili mweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi. Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia. Lakini mtu wangu aliye mwaminifu ataamini na kuishi; walakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye.” Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa” (Waebrania 10:32-39)."Ndiyo maana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungu mchana na usiku katika hekalu lake; naye aketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yao kuwalinda. “Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena, kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uhai. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao” (Ufunuo 7: 15-17).“Ufalme, utawala na ukuu wa falme zote duniani watapewa watu watakatifu wa Mungu Mkuu. Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele, na tawala zote zitawatumikia na kuwati” (Danieli 7:27).

Mfano huu unaonyesha jinsi mambo yalivyo Mbinguni na katika Ziwa la Moto (picha ya 1 na ya 2). Mambo mengine ya kina juu ya nyakati za mwisho yameachwa nje kwa sababu ya mgawanyiko ulioko katika kutafsiri mambo ya nyakati za mwisho. Kila kanisa na dhehebu linafuata nadharia fulani katika kutafsiri Maandiko ya siku za mwisho. Mengi ya yale yaliyoandikwa kuhusu siku za mwisho, yaliandikwa kwa lengo la kuwatia moyo Wakristo waliokuwa wakipitia mateso makali. Uchanganuzi wa Maandiko hayo umejumuishwa katika mafunzo haya ili kuwahimiza na kuwatia moyo waamini. Yesu aliahidi kwamba siku moja atarudi duniani, na kwamba wakati huo kila jicho litamwona mawinguni. Msururu wa katikati wa picha ni marudio ya yale tuliyokwisha jifunza katika mfululizo huu wa mafundisho, yaani mambo tunayostahili kuyatenda hadi Yesu arudi duniani.

Picha ya 1: Mandhari ya MbinguniPicha ya juu inaonyesha mandhari yalivyo mbele za Kiti Cha Enzi cha Mungu huko mbinguni. Maelezo yaliyoelezwa katika picha yanapatikana katika Ufunuo 21:10-23; na 22:1-5. Kumbuka kwamba Yesu ameonyeshwa kama Mwanakondoo kwa sababu ya dhabihu yake ya kutuondolea dhambi zetu (Ufunuo 5:6). Ukiangalia pembe nne za picha, utaona malango matatu ya lulu katika kila moja ya pembe hizo. Mji wenyewe umejengwa kwa dhahabu safi, na una makao katika kuta zake zote. Makao haya yanawakilisha yale makao ambayo Yesu aliahidi kutuandalia (Yohana14:2,3). Katikati ya picha kuna kile Kiti Cha Enzi. Hakuna hekalu, kwa sababu Mungu ndiye hekalu. Malaika wamekizunguka Kiti Cha Enzi, wakimsifu na kumtukuza Mungu. Kutoka katika Kiti Cha Enzi kuna tiririka mto wa maji safi. Maji ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, kwa hiyo katika Maandiko maji yametumiwa kurejelea kipawa cha Mungu cha uzima wa milele. Ile hali ya maji kutiririka kutoka katika Kiti Cha Enzi inaonyesha kwamba Mungu ndiye chanzo cha uzima wa milele na ndiye anayetunza maisha huko mbinguni. Katika kitabu cha Yeremia, Mungu anarejelewa kwa jina la Chemchemi Ya Maji ya Uhai (Yeremia 2:13; 17:13); na Yesu pia alimpa yule mwanamke Msamaria maji ya uzima yanayoondoa kiu milele (Yohana 4:10-15). Kitu kingine cha kupendeza kinachoonekana katika maelezo ya mbinguni ni Ule Mti wa Uzima. Mti huu pia umetajwa katika Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:9; 3:17). Huko mbinguni, Mti Wa Uzima unamea pande zote za mto na kuzaa matunda. Majani ya mti huu ni dawa za kuwaponya watu wa mataifa. Watu walio pichani wamevalia kanzu nyeupe. Rangi nyeupe inawakilisha usafi na utakaso kutoka katika dhambi. Yesu anawafuta machozi, na kuwaambia kwamba hakutakuwa na kilio, maumivu, huzuni, mauti, wala kuombolezai tena (Ufunuo 21:4). Yeye anafanya kila kitu upya. Yesu anastahili sifa, heshima na utukuftu wote, kwa sababu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Ikiwa Tutaenda Mbinguni, Twastahili Kufanya Kazi Gani Sasa Hivi?Msitari wa katikati (A) katika picha ni muhtasari wa yale mambo yote tunayostahili kufanya hadi tuage dunia au hadi Yesu arudi kutuchukua. Ukitazama utaona picha ya wazazi wakiwafundisha watoto wao Neno la Mungu. Zile Amri Kumi zimewekwa kwenye picha ili zitukumbushe vigezo vya Mungu vya kumpenda yeye, na kumpenda jirani yetu.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 134

Page 138: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Kuna mtu anayeonekana akitembea kwenye njia nyembamba huku akipima kila kitu katika mizani ya Neno la Mungu, na kumwaga chumvi njiani. Pia unaweza kuona mioyo iliyosafishwa ya watu walioingia katika Ufalme wa Nuru, na Yesu akiwa katika Kiti Cha Enzi cha mioyo yao. Kuna msalaba wa kutukumbusha huduma ya upatanisho na jengo la kanisa linaloundwa na jumuia ya waamini dunia nzima, wakijaribu kuwafikia wengine na Habari Njema. Halafu kuna mtu aliyevaa silaha za kiroho. Imani ya mtu huyu inakua kila siku. Vilevile unaweza kuona uwakili wa waamini. Wanatumia vipawa vyao kwa ajili ya kumtumikia Mungu na kulijenga kanisa na kulitayarisha kufanya huduma. Mafundisho ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu ni ya kila dakika, wala sio mara moja kwa juma zima. Kaa chini na ujifunze Biblia pamoja na jirani zako. Hatustahili kujifunza Biblia peke yetu, bali kwa kushirikiana na wenzetu, tunaweza kumruhusu Mungu kutawala maisha yetu, na ya wenzetu. Tunastahili kuendelea kuwa ndani ya Mzabibu (Yesu), kulisoma Neno la Mungu, na kumruhusu Roho Mtakatifu kutuongoza na kutupa nyenzo tunazohitaji katika huduma. Tunastahili kumpenda na kumtii Mungu. Endelea mbele kumjua Bwana!

Kuelewa mambo yaliyofunzwa katika masomo yaliyotangulia, kunaweza kutusaidia kuelewa jinsi maisha yetu yanavyostahili kuwa wakati tunapotarajia kurudi kwa Yesu. Mtume Paulo alisema, “ Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu nyakati na majira ya mambo haya yatakapotukia. Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku. Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa” (1 Wathesalonike 5:1-11). Tukitumia Maandiko hayo kwa kufanyia marudio, tunastahili kuishi na kutenda kama watu wa Ufalme wa Nuru, sio kama wale wanaoishi gizani. Tunastahili kuziweka kando tabia za kale na mazoea mabaya yanayotendwa na watu waliopotoka njia. Sisi ni watu wa mchana, kwa hiyo tunastahili kuvaa silaha zote za vita vya kiroho. Hatimaye tunapaswa kuwa mawakili wazuri kwa kutiana moyo na kujengana kiimani. Neno la Kigiriki lenye maana ya kutia moyo ni parakaleo. Neno hili linahusiana kwa karibu na neno la Kigiriki lenye maana ya Roho Mtakatifu (paraklete), ambalo maana yake ni kwenda bega kwa bega. Tunapotiana moyo, tunaenda bega kwa bega na ndugu zetu wanaohitaji msaada wetu. Neno hili linamaanisha kwenda bega kwa bega,kusaidia, kuagizia msaada, au kutia moyo au kuhimiza. Katika matini hii ya Maandiko, tunashauriwa kutiana moyo na kujengana kiimani. Kujengana kunatokana na neno lenye maana ya kujenga nyumba. Kujenga nyumba huanza na kuweka msingi thabiti, hali thabiti ya ndani, halafu kupata nyenzo muhimu za kuweza kuijenga nyumba hadi iwe jengo moja. Sote tukitumia vipawa vyetu vizuri, tutakuwa tunajengana na kusaidia kuenea kwa Ufalme wa Mungu.

Sharti Tuwe na BidiiMara kwa mara tunajaribika kuishi maisha yetu kwa kuangalia ya leo tu. Hatufikirii juu ya maisha yajayo, kwa sababu tumeathiriwa na dhana za kidunia zinazozingatia mambo ya leo tu. Lakini Mungu anapenda tuishi maisha yetu hapa duniani huku tukiwazia juu ya maisha yajayo. Kuna sababu kadhaa zinazotufanya tuwe na mtazamo huu, nazo ni kama zifuatazo. Sababu ya kwanza na ya kimsingi ni kwamba, maisha yajayo yanaweza kuwa kichocheo cha kutufanya tukue, tujifunze, na tumtumkie Mungu kwa bidii. Tukiishi pasipo kuzingatia maisha yajayo, tunaweza kusahau lengo letu la kufanana na Yesu, kukua katika imani yetu na katika utumishi wetu kwake. Mara kwa mara Yesu alitumia mafumbo kufundisha juu ya wakati ujao na jinsi waamini wanavyostahili kuwa tayari kungojea kurudi kwake. Kwa sababu tuna tumaini hili la uzima wa milele mbinguni, tunaweza kuishi hapa duniani kwa kuvumilia, kuboreshwa na kukomazwa. Lakini tukiishi kwa kuyaangalia ya leo tu, tutakosa mambo haya muhimu katika maisha yetu. Ni vyema pia kutambua kwamba katika ombi ambalo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake liiitwalo Sala Ya Bwana (Mathayo 6:9-13), Yesu alisema, “Utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni” (Mathayo 6:10). Katika Biblia ya Kigiriki mpangilio wa maneno ni tofauti, neno mbinguni ndilo lijalo kwanza halafu ndio duniani. Hii ni kauli muhimu juu ya Ufalme wa Mungu. Hii ina maana kwamba mambo yale yakayofanyika mbinguni, yafanyike pia duniani. Hii ni changamoto kubwa sana kwetu! Tutakapofika mbinguni, uhusiano wetu na wengine hautakuwa na dosari au uadui kama ilivyo duniani. Kuabudu na kumtumikia Mungu kwetu mbinguni kutakuwa kwa hali ya juu zaidi kuliko tunavyoabudu duniani. Changamoto kwetu ni kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kuwatendea wengine sawa na itakavyokuwa mbinguni! Vilevile kuna changamoto ya kumtumikia Mungu kwa nguvu zetu zote, na sio kwa udhaifu wetu.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 135

Page 139: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Basi tunawezaje kuitumia kanuni hii? Kwanza kabisa tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu hatasahau kazi tunayomfanyia yeye. Maisha yanapokuwa magumu na hatumwoni Mungu akitenda kazi, tunaweza kujaribika kuzembea katika kumtumkia Bwana, au hata kuacha kumtumikia kabisa. Lakini Mungu hawezi kusahau kazi yetu. Kwa hiyo natuendelee kutia bidii na kuiga imani ya wale ambao wameonyesha bidii katika maisha yao yote. Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anatuhimiza kukumbuka haya, “Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonyesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake. Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia. Hivyo msiwe wavivu, bali mwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu, wakapokea yale aliyoahidi Mungu” (Waebrania 6:10-12). Hata watu waliozeeka wanaweza kuendelea kutia bidii kiroho, huku wakiwafunza watu wa kizazi kipya njia za Mungu. Lazima Tumtumikie Mungu Kwa Nguvu Zetu Zote Ikiwa tunajua kwamba kazi tunayomfanyia Bwana itajaribiwa kwa moto, basi tunastahili kutiwa motisha kuwa makini katika kumtumikia Mungu. Sharti tumfanyie Bwana kazi nzuri. Katika Somo la 11, tulijadili juu ya uwakili wa vipawa vya kiroho tulivyopewa na Mungu. Tutakapofika mbinguni, kazi ile tukayokuwa tumemfanyia Yesu duniani itajaribiwa. “Juu ya msingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha au mawe ya thamani; anaweza kutumia miti, majani au nyasi. Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonyesha ubora wake. Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; 15 lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni” (1 Wakorintho 3:12-15). Kwa hiyo tunapomtumikia Mungu pamoja, sharti tuhakikishe kuwa tunajenga juu ya msingi wa Yesu na sio juu ya msingi wetu wenyewe. Pia lazima tuwe waangalifu na kutenda kazi njema. Je, unakumbuka maelezo marefu juu ya Hema kule jangwani? Mungu alitoa maagizo mwafaka kuhusu utengenezaji wa hema hilo na jinsi watu watakavyotumika ndani ya hema (Mambo Ya Walawi). Hata ijapokuwa maelezo hayatupi mwongozo wa jinsi ya kutumia vipawa vyetu vya kiroho, yanatuonyesha jinsi utengenezaji wa hema ulivyokuwa wa hali ya juu, na jinsi ulivyohusishwa na kumwabudu Mungu aliye Mtakatifu. Kwa hiyo natumtumikie Mungu vizuri sana na kutumia vipawa kwa ajili ya kumletea utukufu Mungu! “Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu” (Wafilipi 1:6).

Sharti Tuvumilie na Kuwa Waaminifu, Ndipo Mungu Atatupa ThawabuYesu anasema kwamba wakati atakaporudi atakuwa na thawabu mikononi mwake. Atawapa Taji Ya Uzima wale ambao watakuwa wamedumu kuwa waaminifu na kuvumilia mateso duniani, au hata kuawa kwa ajili ya Yesu. (Yakobo 1:12; Ufunuo 2:10). Taji Ya Utukufu itapewa wale viongozi watakaokuwa wameongoza kwa upole na kwa kuwa mfano bora (1 Petro 5:4). Itakuwa heshima kubwa kupewa taji kwa sababu ulikuwa mfano mwema kwa wengine! Mtume Paulo aliwaona wale watu aliowahuburia Habari Njema na kuokoka na kuwafudisha, kama furaha yake na taji yake (1 Wathesalonike 2:19; Wafilipi 4:1). Pia alizungumzia juu ya Taji Ya Haki ambayo itapewa wale ambao watakuwa hawakupotoshwa na mafundisho au hadithi za uongo (2 Timotheo 4:8). Tunaweza kupata faraja kwa kujua kwamba Mungu atatupa zawadi kwa kazi ile tunayomtendea. Tunachotakiwa kufanya ni kuwa na subira, huku tukijua kwamba siku moja tukapofika mbinguni tutapewa thawabu. Hapa duniani tunaweza kutoelewa kwa nini wanaotenda maovu huonekana kufaulu, au kwa nini manabii wa uongo hufanikiwa. Lakini lazima tuendelee kudumu katika Ukweli Wa Imani Yetu, kwa sababu siku moja tutapokea thawabu! Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana! ( Wakolosai 3:23 -24).

Sharti Tuendelee Kufanana na YesuKwa KujitasaMtume Yohana anatuhimiza kuendelea kujitakasa huku tukijua kwamba siku moja tutamwona Yesu ana kwa ana. “Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa, lakini bado haijadhihirishwa wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba wakati Kristo atakapodhihirishwa, tutafanana naye kwani tutamwona vile alivyo. Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa” (1 Yohana 3:2-3). Ikiwa tutafika mahali pa kujiona kwamba tumetosheka kiroho na hatuhiji kukua tena, basi tutakuwa tunakosa mambo muhimu ya kuweza kutusaidia kukua kiimani na kitakatifu, kama Mungu anavyotaka. Tutakuwa kama maji yaliyochafuliwa na yaliyotulia mahali pamoja, maji yaliyojaa magonjwa na uvundo. Tukitaka kuishi maisha matakatifu itatubidi kuwa na nidhamu ya hali ya juu, na kumtii Mungu ili aweze kutufunulia mambo yale tunayostahili kuyabadilisha katika maisha yetu. Huenda Mungu amekuwa akifanya kazi katika sehemu fulani ya maisha yako ili uweze kufanana naye. Pengine watu wengine

Copyright © 2007 Tammie Friberg 136

Page 140: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

wamekuwa wakikushauri kuyarekebisha maisha yako ili uhusiano wako na Mungu uweze kuwa bora zaidi. Au pengine watu fulani wamejaribu kukuonyesha makosa yako. Lakini cha muhimu ni kulenga kufuata hatua hizo za utakatifu, ili hatimaye uweze kupokea thawabu mbinguni. Kwa Kujifunza Kuwapenda Wengine Kama Yesu AlivyowapendaLazima tufikie kiwango cha kuwapenda wengine kama Yesu alivyowapenda. Hatua ya kwanza katika kuwapenda wengine ni kumtii Mungu. Mungu ametuamuru kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe. Ikiwa tunaona vigumu kuwapenda watu fulani, tunaweza kulenga kumtii Mungu na kwa kufanya hivyo tutajikuta tunaweza kuwapenda wengine kwa uwezo wa Mungu na sio kwa kutegemea hisia zetu. Hisia zetu za kibinadamu hubadilika badilika. Kutowasemehe watu, kuwa na uchungu, hasira, na chuki ndivyo vizuizi vikubwa vinavyotuzuia kutoifuata amri ya Mungu. Wakati mwingine tunaweza kujaribika kuwatenga watu kwa sababu ya hasira zetu. Lakini ili tuweze kuwapenda wengine, sharti tusafishe mioyo kutokana na hisia potofu. “Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote. Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi. Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili. Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena mwe na shukrani!” (Wakolosai 3:8-15). Tunapoendelea kumtii Mungu, lazima pia tuweze kuvumiliana na kusameheana. Lazima upendo uwe kama vazi letu, lionekane na watu wote. “Sala yangu ni hii: naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna, ili mweze kuchagua jambo lililo bora. Hapo ndipo mtakuwa safi na bila lawama yoyote ile katika siku ile ya Kristo. Maisha yenu yatajazwa mambo yote yaliyo kweli bora, ambayo Yesu Kristo mwenyewe anaweza kuwajalieni, kwa ajili ya utukufu na sifa ya Mungu” (Wafilipi 1:9-11).

Kwa Kukua Katika Ufahamu na Uwezo wa KupambanuaKufanana na Yesu kunamaanisha pia kujifunza zaidi juu yake. Tunaweza kufanya hivi kupitia kwa nidhamu ya kusoma Neno la Mungu na kwa kulishiriki Neno hilo na wengine. Kujifunza juu ya Yesu ni mazoea yanayostahili kuendelea katika maisha yetu yote. Katika waraka kwa Waebrania, mwandishi anatufafanulia aina nne za mafunzo ya kimsingi. Lakini mwandishi hawaachi waamini katika hatua ya kwanza. Badala yake, anawahimiza kula chakula kigumu. Mwandishi anasema kwamba watu wengi hubaki katika hatua ya watoto wachanga kwa sababu hawakomai kupita mafundisho ya kimsingi ya Biblia (5:11-6:2). Mwandishi anaendelea kusema kwamba chakula kigumu, au mafundisho ya kina zaidi ya Biblia ni kwa wale ambao wamezifunza hisia zao za kiroho kuweza kutambua ukweli na uongo (5:14). Sisi kama wanadamu tuna hisia za kimwili kama vile kuona, kusikia, kugusa, na kuonja. Vilevile kuna hisia nyingi za kiroho. Tunahitaji kusikiza kwa kutumia masikio yetu ya kiroho, kuona kwa macho ya kiroho, kuonja kwa midomo ya kiroho, na kugusa kwa mikono ya kiroho. Tunastahili kufanya hivi katika mambo yote tunayokumbana nayo kila siku. Ikiwa tutahisi kwamba kitu fulani sio sawa, au hakina ladha nzuri, inawezekana Roho Mtakatifu ndiye anayeweka shani hiyo katika mioyo yetu. Tukiweza kufuata mwongozo wa hisia zetu vizuri, tutafikia kiwango cha kuweza kutambua ukweli na uongo, au kitu kilicho sawa na kilicho makosa. Wakati mwingine tunaweza kukosa sababu yoyote ya nje ya kutufanya kukataa jambo fulani, na hata tunaweza kushindwa kueleza kwa nini tumekataa jambo fulani. Hali ya kuweza kuhisi ukweli na uongo katika Roho huja wakati tunapomtegemea Roho wa Mungu. Tunapokua na kuchunguza vizuri, tunaweza kukuta kwamba kuna sababu zilizomfanya Roho Mtakatifu kutushawishi jinsi alivyofanya. Hatuwezi kukua hadi kukifikia kiwango cha ukomavu kiroho iwapo tutapuzilia mbali hisia zetu za kiroho. Katika Biblia, kupuuza mawasiliano ya Roho Mtakatifu, huitwa kumpinga Roho (1 Wathesalonike 5:19).

Je, Watu Watafikaje Mbinguni au Katika Ziwa La Moto?Hukumu Ya Kiti Cha EnziSwali tunaloweza kujiuluza ni hili: Ni kitu gani kilichowatenganisha watu walio katika picha ya 1 na wale walio katika picha ya 2? Watu walio katika picha ya kwanza ni wale ambao wamempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao hapa duniani. Wao sasa ni wenyeji wa Ufalme wa Nuru, na sasa wameingia mbinguni. Watu walio katika picha ya 2 ni wale ambao waliukataa ujumbe wa Yesu Kristo. Waliishi katika Ufalme wa Giza wakati walipokuwa duniani. Hatima ya watu hawa wote itajulikana katika Hukumu Ya Kiti cha Enzi.

Copyright © 2007 Tammie Friberg 137

Page 141: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Huenda kitu cha kutisha zaidi kwa watu wasiomjua Mungu ni Hukumu Ya Kiti Cha Enzi. Hukumu hii itafanyika wakati wa mwisho. Katika hukumu hii, Kitabu Cha Uzima cha Mwanakondoo kitafunguliwa. Kitabu hiki kitakuwa na majina ya wale watakaoruhusiwa kuingia mbinguni. Yeyote ambaye amempokea Yesu kweli kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, ataingia mbinguni. Majina ya watu hawa yamo katika Kitabu Cha Uzima. Wale ambao majina yao hayataonekana katika Kitabu Cha Uzima, watatupwa katika Ziwa La Moto. Huu ndio utakuwa wakati ambao pia Shetani na jeshi lake lote watashindwa kabisa. Shetani, Mpinga Kristo, pepo, pamoja na “wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili” wote watatupwa katika ziwa moto (Ufunuo 21:8; Mathayo 25:41,46; 2 Wathesalonike 1:8-10).

Yesu alitoa fumbo la tajiri na Lazaro (Luka 16:19-31). Katika fumbo hili, yule tajiri aliaga dunia na akaenda mahali pa mateso, na Lazaro naye akafa, lakini yeye akaenda mbinguni (kifuani mwa Ibrahimu). Yule tajiri akamwomba maji Lazaro, lakini akawa hawezi kuvuka na kumfikia Lazaro. Pia yule tajiri akaomba kutumwe wajumbe kuja duniani kuwaonya ndugu zake wasiende mahali aliko yeye. Lakini Ibrahimu akamjibu kwamba kama ndugu zake hawatawasikiza manabii, basi hata kukatoka mtu kutoka kuzimu tena hawatasikia. Mengi ya mafumbo ya Yesu yaliwaonya watu juu ya kwenda mahali palipo na kilio na kusaga meno. Watu wanapokufa, hawawezi kupata nafasi nyingine na kugeuza msimamo wao juu ya Yesu. Mwandishi wa Waebrania anasema, “Basi, kama vile mtu kufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu” (Waebrania 9:27). Watu wanapokufa, hawageuki na kuwa roho za mababu, au waombezi wetu. Uwe Tayari Kwa Kuja Kwa YesuJuu ya watu wasioamini, Yesu, alitoa fumbo la wanawali watano wajinga, ambao hawakubeba mafuta ya kutosha katika taa zao kwa kuwa bwana harusi alichelewa kufika (Mathayo 25:1-13). Basi bwana harusi alipofika, sawa na Yesu atakavyorudi, wale wanawali hawakuonekana. Hatimaye walifungiwa nje. Wakati unakuja ambapo kutakuwa hakuna wakati tena wa kumwamini Yesu. Kumwamini Yesu ni tendo la imani. Kila mtu sharti apitie mlango huo, kwa wakati unaofaa, kwa maana hakuna wokovu katika mtu yeyote mwingine isipokuwa Yesu (Matendo 4:12; Yohana 14:6).

Kwa waamini, “Basi, ndugu zangu, mwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli. Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia. Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia. Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana. Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema ” (Yakobo 5:7-11).

Umuhimu wa Kuwafanya Watu Kuwa WanafunziLazima tufanye kazi ya Bwana hapa duniani kwa sababu ya yale yanayoweza kuwapata watu wasiomjua Yesu. Yesu alipoondoka duniani, aliwaambia wanafunzi wake maneno haya, “Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.” (Mathayo 28:19-20). Ukiangalia kwa makini kiini cha agizo hili utakuta kwamba lengo hasa ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu. Hii ni kazi ngumu zaidi kuliko hata kuwatangazia watu Habari Njema Ya Wokovu, kwa sababu inahusisha kuwafunza watu yale yote tuliyoagizwa na Yesu. Huduma ya Paulo ni mfano mzuri wa jinsi mtu anavyoweza kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu. Paulo alijua wazi kwamba lengo lake kuu lilikuwa ni kuwashuhudia watu wa Mataifa juu ya imani yake katika Kristo. Lakini unaposoma nyaraka zake alizoandika katika Agano Jipya, utakuta kwamba zimejaa ujumbe wa kuwahimiza watu na kuwasaidia kukomaa kiroho. Paulo aliandika barua, alichagua viongozi, alisafiri na kuyatembelea makanisa, na vilevile aliwaombea wale waliokuwa mikononi mwake. Hii ni kazi inayochukua nguvu na wakati mwingi. Paulo anaelezea lengo lake katika Wakolosai 1:28-29 “Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo. Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu.” Kuwasaidia watu kufikia kiwango cha kukomaa katika Kristo ni kazi kubwa sana. Sisi kama wazazi, viongozi wa kanisa, na wanafunzi wa Yesu, tunastahili kushirikiana kutekeleza jukumu hili. Tupige mbio kwa saburi kwa lengo la kushinda mbio hizo tulizowekewa!

Copyright © 2007 Tammie Friberg 138

Page 142: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Mara baada ya Yesu kupaa mbinguni, wanafunzi wake walisimama mahali hapo kutazama mbinguni. Inaonekana kwamba hata sisi tungeweza kutenda hivyo iwapo tungemwona Yesu akipaa mbinguni siku hiyo. Lakini baadaye kulitokea watu wawili waliovalia mavazi meupe. Wakawaambia wale wanafunzi, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). Mbona mnasimama kutazama angani?

Muhtasari Wa Mafundisho Ya Somo La 12Mbinguni Ziwa La Moto

Kuta Za Mji Zenye Malango 12 Ya Lulu Katika Pande Nne Limeandaliwa Kwa Ajili Ya Shetani, Malaika Zake, Wapinga Kristo, Na Wasioamini...Wachawi, Waganga, Wapiga Ramli, Wazinzi, Waabuduo Sanamu, Waongo, Wauaji.

Mji Umetengenezwa Kwa Dhahabu Safi, Makao Ya Waamini Mahali Pa Mateso Ya MileleKiti Cha Enzi Katikati Mwa Hekalu Onyo Juu Ya Kujiandaa Kwa Kurudi Kwa YesuMto Ung’aao Ukitiririka Kutoka Katika Kiti Cha Enzi Kiti Cha Enzi Cheupe Cha HukumuMti Wa Uzima Pande Zote Mbili Za MtoWatu Waliovalia Mavazi Meupe Wakikizunguka Kiti Cha EnziYesu Anawafuta Machozi Watu WakeThawabu:Taji Ya UzimaTaji Ya UtukufuTaji Ya Haki/UadilifuWatu Waliompokea Yesu Ni Taji

Jinsi Ya Kuishi Kwa Kuyawazia Mambo Ya MbinguniMwe Na BidiiMtumikie Bwana VizuriJitahidi Ufanane Na Yesu Siku Hadi Siku*Kwa Kukomaa Katika Upendo*Kwa Kukomaa Katika Kumjua Mungu*Kwa Kukomaa Katika UtambuziKazi Iliyoko Kabla Yesu Hajarudi: Uanafunzi!

Marejeo Ya Biblia Kwa Mafundisho Ya Somo La 12

MbinguniHabari/Hadithi Zinazoambatana Na Somo Maandiko Yanayoambatana Na Somo

Maelezo*Ibada Mbinguni- Ufunuo 7:7-17.*Nani Anayestahili Kukifungua Kitabu Cha Uzima?- Ufunuo 5:1-14.*Mto Na Mti Wa Uzima- Ufunuo 22:1-5; Mwanzo 2:9; 3:17.*Mungu Wa Haki- Isaya 60:14-22.*Yesu Anatuandalia Makao- Yohana14:2,3.*Mwanamke Msamaria Kisimani, Yesu Ndiye Maji Ya Uzima- John 4:10-15.*Yesu Na Mwizi- Luka 23:43.

Maelezo*Kuna mto ambao maji yake hufurahisha mji wa Mungu, makao matakatifu ya Mungu Mkuu. Mungu yumo mjini humo, nao hauwezi kutikiswa; Mungu ataupa msaada alfajiri na mapema- Zaburi 46:4-5.*Basi, kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu- Waebrania 9:27.*Mungu Ndiye Chemichemi Ya Maji Ya Uzima- Yeremia 2:13; 17:13.*Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapong'olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono. Na sasa, katika hali hii, tunaugua tukitazamia kwa hamu kubwa kuvikwa makao yetu yaliyo mbinguni. Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya Mungu bila vazi. Tukiwa bado katika hema hii ya duniani, tunalia kwa kukandamizwa; si kwamba tunataka kuuvua mwili huu wa kufa, ila tuna hamu ya kuvalishwa ule usiokufa, ili kile chenye kufa kimezwe kabisa na uhai. Mungu mwenyewe alitutayarishia mabadiliko hayo, naye ametupa Roho wake awe dhamana ya yote aliyotuwekea.Tuko imara daima. Tunajua kwamba kuishi katika mwili huu tu ni kukaa mbali na Bwana. Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona. Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana- 2 Wakorintho 5:1-8.

Thawabu*Thawabu Katika Karamu Ya Harusi Mbinguni- Luka 14.

Thawabu*Juu ya msingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha au mawe ya thamani; anaweza kutumia miti, majani au nyasi. Iwe iwavyo, ubora wa kazi

Copyright © 2007 Tammie Friberg 139

Page 143: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

*Taji Ya Uzima- Yakobo 1:12; Ufunuo 2:10.*Taji Ya Utukufu- 1 Petro 5:4.*Watu Waliompokea Yesu Ndio Taji- 1 Wathesalonike 2:19; Wafilipi 4:1.*Taji Ya Haki/Uadilifu- 2 Timotheo 4:8.*Thawabu Ya Urithi- Wakolosai 3:23-24.*Hotuba Ya Mlimani- Mathayo 5.*Ujasiri Wenu Una Thawabu Kubwa- Waebrania 10:35-36.

ya kila mmoja utaonekana wakati siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonesha ubora wake. Ikiwaalichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni- 1 Wakorintho 3:12-15.*Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hakika hatakosa kamwe kupata tuzo lake- Mathayo 10:42.

Ziwa La MotoHabari/Hadithi Zinazoambatana Na

SomoMaandiko Yanayoambatana Na Somo

Maelezo*Yesu Anafundisha Juu Ya Kushindwa Kwa Shetani Mara Ya Mwisho- Mathayo 25:41, 46.*Yuda Anafundisha Juu Ya Hatima Ya Shetani- Yuda 1:6-7.

Maelezo*Shetani, Pepo, Wapinga Kristo, Wauaji, Wachawi, Na Wazinzi Wote Watatupwa Katika Ziwa La Moto- Ufunuo 20:10; 21:8; Ufunuo 21:8; Mathayo 25:41,46; 2 Wathesalonike 1:8-10.

Changamoto*Fumbo La Wanawali Kumi- Mathayo 25:1-13-10.*Fumbo La Tajiri Na Lazaro- Luka 16:19-31.*Ngano Na Magugu- Mathayo 13:24-30.*Je, Yesu Ni Bwana Wa Maisha Yako?- Mathayo 7:21-29.*Mbuzi Na Kondoo- Mathayo 25:31-46.

Changamoto*Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uhai wa- Wagalatia 6:8.*Ndugu, tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana. Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata. Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka. Mungu atafanya jambo la haki: atawalipa mateso wale wanaowatesa nyinyi na kuwapeni nafuu nyinyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake wenye nguvu na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu, wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea- 2 Wathesalonike 1:3-10.*Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake. Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu- 1 Yohana 3:15-16.

Jinsi Ya Kuishi Kwa Kuyawazia Ya MbinguniHabari/Hadithi Zinazoambatana

Na SomoMaandiko Yanayoambatana Na Somo

Mwe Na Bidii*Maisha Ya Waamini Hubaki Kuwa Ya Bidii- Waebrania 11.*Lakini Atakayevumilia Mpaka Mwisho, Ataokoka- Mathayo 24:13; Marko 13:13; Ufunuo 2:10.*Zaburi Zihusuzo Bidii- Zaburi 37; 73.*Shetani Anaomba Apewe Ruhusa Ya Kumpepeta Petro Kama Ngano- Luka 22:31-32.*Wanafunzi Wa Kweli Hudumu Katika Neno- Yohana 8:31.*Watu Wa Kupro Na Kurene

Mwe Na Bidii*Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira ya mambo haya yatakapotukia. Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku. Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. Kwa hiyo

Copyright © 2007 Tammie Friberg 140

Page 144: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

Wahubiri Juu Ya Yesu- Matendo 11:20-30.Paulo Na Barnaba Wawatia Moyo Wanafunzi Kuendelea Kuwa Waaminifu Kwa Bwana- Matendo 13:43-44; 14:19-28; 1 Wakorintho 15; 2 Wathesalonike 2:15.*Yohana Anawafundisha Wakristo Kuvumilia Mateso- Kitabu Cha Ufunuo.

farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa- 1 Wathesalonike 5:1-11.*Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake. Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia. Hivyo msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu, wakapokea yale aliyoahidi Mungu- Waebrania 6:10-12.*Roho asema waziwazi kwamba siku za baadaye watu wengine wataitupilia mbali imani; watazitii roho danganyifu na kufuata mafundisho ya pepo. Mafundisho ya namna hiyo yanaenezwa na watu waongo wadanganyifu, ambao dhamiri zao ziko kama zimechomwa kwa chuma cha moto- 1 Timotheo 4:1-2.*Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi. Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, upendo, subira na unyenyekevu. Piga mbio kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani, ukajipatie tuzo la uhai wa milele uliloitiwa wakati ulipokiri imani yako mbele ya mashahidi wengi- 1 Timotheo 6:10-12.*Tulia mbele ya Mwenyezi- Mungu, mngojee kwa saburi; usihangaike juu ya wale wanaofanikiwa, watu wanaofaulu katika mipango yao mibaya. Epuka hasira wala usiwe na ghadhabu; usihangaike maana hiyo huzidisha ubaya. Watu watendao mabaya wataangamizwa, bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi. Bado kitambo kidogo, naye mwovu atatoweka; utamtafuta pale alipokuwa, wala hutamwona. Lakini wapole wataimiliki nchi, hao watafurahia wingi wa fanaka. Mwovu hula njama dhidi ya mwadilifu, na kumsagia meno kwa chuki. Lakini Mwenyezi-Mungu humcheka mwovu, kwani ajua mwisho wake u karibu. Waovu huchomoa panga na kuvuta pinde zao, wapate kuwaua maskini na fukara; wawachinje watu waishio kwa unyofu. Lakini panga zao zitawapenya wao wenyewe, na pinde zao zitavunjwavunjwa- Zaburi 37:7-15.*Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake- Wagalatia 6:9.*Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama. Mnapaswa, lakini kuendelea na msingi imara katika imani, wala msikubali kutikiswa kutoka katika tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia injili. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo injili ambayo imekwisha hubiriwa kila mtu duniani- Wakol. 1:22-23.*Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye.Tukimkana, naye pia atatukana- 2 Timotheo 2:12.

Mtumikie Bwana Vizuri*Viongozi Wazuri- Kutoka 18:20-21.*Fumbo La Talanta- Mathayo 25:14-46.

Mtumikie Bwana Vizuri*Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu- Wafilipi. 1:6.*Basi, jambo muhimu ni kwamba mwenendo wenu uambatane na matakwa ya injili ya Kristo, ili kama nikiweza kuja kwenu au nisipoweza, nipate walau kusikia kwamba mnasimamaimara mkiwa na lengo moja, na kwamba mnapigana vita kwa pamoja na mnayo nia moja kwa ajili ya imani ya injili- Wafilipi. 1:27.*Kwa vyovyote, tusonge mbele katika njia hiyohiyo ambayo tumeifuata mpaka hivi sasa. Nduguzangu, fuateni mfano wangu. Tumewapeni mfano mwema, na hivyo wasikilizeni wale wanaofuata mfano huo. Nimekwisha waambieni jambo hili mara nyingi, na sasa narudia tena kwa machozi: watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo. Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia. Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi aje kutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo. Yeye ataibadili miili yetu dhaifu na kuifanya ifanane na mwili wake mtukufu, kwa nguvu ile ambayo kwayo anaweza kuviweka vitu vyote chini ya utawala wake- Wafilipi. 3:16-21.*Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu- Wakolosai 1:10.*Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu. Jambo lile bora ulilokabidhiwa lilinde kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu- 2 Timotheo 1:13-14.*Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu,

Copyright © 2007 Tammie Friberg 141

Page 145: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

bila kupungukiwa chochote- Yakobo 1:2-4.Jitahidi Ufanane Na Yesu Siku Hadi Siku*Petro Na Paulo Huko Antiokia- Matendo 11.

Jitahidi Ufanane Na Yesu Siku Hadi Siku*Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa, lakini bado haijaonekana wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba, wakati Kristo atakapotokea, tutafanana naye kwani tutamwona vile alivyo. Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa- 1 Yohana 3:2-3.

* Kwa Kukomaa Katika Upendo *Mpende Mwenzako Kama Unavyojipenda- Mambo Ya Walawi 19:18.*Mpendeni Mgeni Aliye Kati Yenu- Mambo Ya Walawi 19:34; Kumbukumbu 10:19.*Yesu Anatufundisha Jinsi Ya Kuwapenda Adui Zetu- Mathayo 5:41-48.*Yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo- Mathayo 7:12.*Fumbo La Msamaria Mwema- Luka 10:30-42.*Amri Mpya Ya Yesu- Yohana 13:34-35; 15:12-18; Waefeso 5:2.*Paulo Anafundisha Jinsi Ya Watu Kupendana- Warumi 12; 1 Wakorintho 13.*Paulo Anawahamasisha Watu Wapendane- 2 Wakorintho 8:7.*Paulo Anaomba Upendo Udumu Makanisani Zaidi Na Zaidi- Wafilipi. 1:9-11.*Tukiwapenda Wengine, Tutakuwa Tunajitambulisha Na Yesu- Wafilipi. 2.*Kuwa Na Mioyo Isiyo Na Kasoro Wakati Yesu Atakaporudi- 1 Wathesalonike 3:12-13.*Yakobo Anatufundisha Tusiwabague Watu- Yakobo 2.*Yohana Anatufundisha Jinsi Ya Kujua Kama Kweli Tunampenda Mungu Na Wanadamu- 1 Yohana.

* Kwa Kukomaa Katika Upendo *Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli. Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia. Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia. Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso, fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana. Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema. Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na Mungu- Yakobo 5:7-12.*Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote. Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi. Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili. Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!- Wakolosai 3:9-15.*Sala yangu ni hii: naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna, ili muweze kuchagua jambo lililo bora. Hapo ndipo mtakuwa safi na bila lawama yoyote ile katika siku ile ya Kristo. Maisha yenu yatajazwa mambo yote yaliyo kweli bora, ambayo Yesu Kristo mwenyewe anaweza kuwajalieni, kwa ajili ya utukufu na sifa ya Mungu- Wafilipi 1:9-11.*Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo- 1 Wakorintho 16:14.*Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema- Waebrania 10:24.

*Kwa Kukua Katika Kumjua Mungu*Kornelio- Matendo 10.*Apolo- Matendo 18:24-28.*Yesu Anawafafanulia wanafunzi wake maandiko- Luka 24:27.

*Kwa Kukua Katika Kumjua Mungu*Kukua katika kumjua Mungu- Waebrania 5:11-6:2.*Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo- Mithali 1:5.*Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu; mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele- Waebrania 6:1-2.*Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina- 2 Petro 3:8.*Kama tukiuzingatia ukweli kwa moyo wa mapendo tutazidi katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo- Waefeso 4:15-16.*Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu. Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu. Na kwa furaha mshukuruni Baba, aliyewawezesha

Copyright © 2007 Tammie Friberg 142

Page 146: Uanafunzi Unaozingatia Jinsi Watu Wanavyouona Ulimwengu - Swahili3.pdfMarejeo Ya Mafundisho Ya Biblia yanaweza kutumiwa kwa kufundishia kila somo kwa kina zaidi. Upande wa kushoto

nyinyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale aliyowawekea watu wake katika ufalme wa mwanga- Wakolosai 1:10-12.*Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema- 1 Petro 2:2-3.*Naam, wala si hayo tu; ila naona kila kitu kuwa ni hasara tupu, kwa ajili ya jambo bora zaidi, yaani kumjua Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimekubali kutupilia mbali kila kitu; nimeyaona hayo yote kuwa ni takataka, ili nimpate Kristo- Wafilipi. 3:8.*Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote- Mithali 10:12.

* Kwa Kukomaa Katika Utambuzi *Petro akiri kwamba Yesu Ndiye Masihi- Mathayo 16:13-28.*Mwanamke Mkanaani Azungumza na Yesu- Mathayo 15:21-28.*Mwanamke Mwenye Busara Wa Tekoa- 2 Samueli 14.*Sulemani Amwomba Mungu Kumpa Kipawa Cha utambuzi- 1 Wafalme 3; 4:29-31.*Jukumu La Kuhani Mlawi- Ezekieli 44:15-31.*Yesu Afundisha Juu Ya Kutambua Nyakati Za Kiroho- Mathayo 16.*Samueli Apata Kibali Mbele Za Mungu Na wanadamu- 1 Samueli 2:26.*Kukua Katika Hekima- Mithali 8.

* Kwa Kukomaa Katika Utambuzi *Msimhuzunishe Roho- 1 Wathesalonike 5:19.* Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, waliofunzwa kwa vitendo kubainisha mema na mabaya - Waebrania 5:14.

Kazi Iliyoko Kabla Yesu Hajarudi: Uanafunzi!*Wito Mkuu- Mathayo 28:19-20.*Yesu Anafundisa Juu Ya Uanafunzi- Luka 14:26-45.*Lisha Wanakondo Zangu- Yohana 21:15-25.*Yesu Awaombea Wanafunzi wake- Yohana 17.*Mungu awapa changamoto Waisraeli- Kumbukumbu 6.*Watu Wapatana Upya Na Mungu- Nehemia 8.

Kazi Iliyoko Kabla Yesu Hajarudi: Uanafunzi!*Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo. Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu -Wakolosai 1:28-29.* Lakini nyinyi ni UKOO MTEULE, MAKUHANI WA MFALME, TAIFA TAKATIFU; WATU WAKE MUNGU MWENYEWE, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu. Wakati mmoja nyinyi HAMKUWA WATU WA MUNGU, lakini sasa nyinyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa MMEPOKEA HURUMA- 1 Petro 2.9-10.*Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, nyinyi mlistahimili. Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo. Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwambamnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele. Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa. Mnahitaji kuwa na uvumilivu ili muweze kutimiza matakwa ya Mungu na kupokea kile alichoahidi. Maana kama yasemavyo Maandiko: “BADO KIDOGO TU, NA YULE ANAYEKUJA, ATAKUJA, WALA HATAKAWIA. LAKINI MTU WANGU ALIYE MWADILIFU ATAAMINI NA KUISHI; WALAKINI AKIRUDI NYUMA, MIMI SITAPENDEZWA NAYE.” Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa-Waebrania 10:32-39.

"Sikiza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. "Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza naw a mwisho, mwisho na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.”Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, "Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo. (Ufunuo 22:12-17).

Copyright © 2007 Tammie Friberg 143