Upload
others
View
76
Download
4
Embed Size (px)
Citation preview
i
UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA
WASIKILIZAJI
Johanes Sylivester
Tasinifu ya M.A. Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Septemba, 2011
ii
UBADILISHAJI MSIMBO BUNGENI NA ATHARI ZAKE KWA
WASIKILIZAJI
Na
Johanes Sylivester
Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha masharti ya Digirii ya M.A.
Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Septemba, 2011
i
UTHIBITISHO
Aliyetia saini hapa chini anathibitisha kuwa amesoma tasinifu hii inayoitwa:
“Ubadilishaji Msimbo Bungeni na Athari Zake Kwa Wasikilizaji” na anapendekeza
ikubaliwe na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha Masharti ya
Digirii ya M.A. Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
………………………….………
Dkt E. K. F. CHIDUO
(Msimamizi)
Tarehe: ……………………
ii
IKIRARI
NA
HAKIMILIKI
Mimi, Johanes Sylivester, nathibitisha kwamba tasinifu hii ni kazi yangu halisi na
haijawahi kuwasilishwa na haitawasilishwa katika Chuo Kikuu kingine kwa ajili ya
kutunukiwa Digirii nyingine yoyote.
Saini: …………………………………
Haki ya kunakili tasinifu hii inalindwa na Mkataba wa Berne, Sheria ya Haki ya
Kunakili ya mwaka 1999 na mikataba mingine ya Sheria za Kitaifa na Kimataifa
zinazolinda mali za Kitaaluma. Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga au
kunakili kwa njia yoyote ile, iwe ama yote au sehemu ya tasinifu hii, isipokuwa kwa
shughuli halali, kwa ajili ya utafiti, kujisomea au kufanya marejeo ya kitaaluma bila ya
kibali cha maandishi cha Mkuu wa Kurugenzi ya Taaluma za Uzamili kwa niaba ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
iii
SHUKURANI
Kazi hii imekamilika kutokana na michango ya watu mbalimbali walioshirikiana nami
bega kwa bega kuhakikisha inafanyika kama ilivyopangwa. Sina budi kutoa shukurani
zangu za dhati na upendo kwa watu hao. Kwa kuwa ni wengi mno, ni vigumu kuwataja
wote ila itanilazimu kuwataja wachache tu kwa niaba ya wote kama ifuatavyo:-
Kwanza kabisa, napenda kumshukuru msimamizi wangu Dkt E. K. F. Chiduo ambaye
amekuwa nami bega kwa bega ili kuhakikisha kazi hii inakuwa katika kiwango hiki.
Licha ya kazi zake nyingi hakusita kunipa miongozo ya kuboresha kazi hii.
Pili, niwashukuru Prof. Y. P. Msanjila na Dkt. P. S. Malangwa kwa kupitia kazi hii
kuanzia hatua za awali za uandishi wa pendekezo la utafiti hadi hatua za mwisho za
kazi hii na kunipa mchango na changamoto ambavyo vimesaidia katika kuiboresha na
kuifikisha katika kiwango hiki.
Bila shaka nisingeruhusiwa kufanya utafiti kama nisingekuwa nimekamilisha tamrini.
Hivyo, niwashukuru wahadhiri wangu ambao ni; Prof. D. P. B. Massamba, Prof. D. J.
Mkude, Prof. Y. M. Kihore, Prof. Y. P. Msanjila, Prof. Y. I. Rubanza, Prof. H. J. M.
Mwansoko, Prof. J. G. Kiango, Prof. M. M. Mulokozi, Prof. E. Kezilahabi, Prof. F. E.
M. K. Senkoro, Dkt. E. K. F. Chiduo, Dkt. S. S. Sewangi, Dkt P. S. Malangwa, Dkt A.
Mutembei, Dkt G. Mrikaria, Dkt S. E. Mrikaria na Dkt S. Omari kwa mchango wao
mkubwa darasani na wakati wa uwasilishaji wa mada ya tasnifu hii ambao
nimeuzingatia katika uandishi wa mwisho wa tasnifu hii.
iv
Pia niwashukuru wanafunzi wenzangu wa M.A. Kiswahili kwa ushirikiano na upendo
walionionesha wakati wa kukamilisha tamrini na kwa kuhudhuria siku ya uwasilishaji
wa mada hii pamoja na mchango wao mkubwa ambao nimeuzingatia. Lakini nitakuwa
mchoyo wa fadhira iwapo sitowataja N. Mbiling’i, Ngowo Asnath, E. Mbogela, F.
Mwendamseke, na A. Gawasike ambao tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega
darasani na hata katika uandishi wa tasnifu hii.
Tatu, shukurani zangu za dhati ziwaendee dada yangu mpendwa Beatrice Balige na
mume wake Yesse Kanyuma kwa kunipatia kila lililohitajika katika harakati zangu za
masomo kuanzia sekondari hadi ninapomaliza tasnifu hii. Mchango wenu wa hali na
mali umekuwa msaada ambao kamwe sitausahau maishani mwangu.
Pia namshukuru mama yangu mpendwa Emelensiana Kokubanza kwa kunilea katika
hali iliyoniwezesha kupenda masomo na pia kwa kunitia moyo katika hatua zangu zote
za masomo. Nimshukuru pia baba yangu mpendwa Sylivester Mugyabuso Balige, japo
ulitangulia mbele ya haki nikiwa nasubiri kujiunga shahada ya awali lakini uliacha
changamoto kichwani mwangu ya nami siku moja kuwa mtu mwenye mchango chanya
katika familia na jamii kwa ujumla. Mungu ailaze roho yako maali pema peponi;
Amina. Nakushukuru pia marehemu bibi yangu mpendwa Maria Masela kwa upendo
ulionionesha katika hatua zangu za awali za utoto. Bibi nitakuenzi kwa kuonesha
upendo kwa wengine.
Nne, niwashukuru wanafunzi na walimu walionisadia katika ukusanyaji wa data. Kwa
kuwa nafasi haitoshi niishie tu kutaja shule watokazo ambazo ni shule ya Sekondari
v
Lubugu, Mkolani na Sekondari ya Mwanza. Nawashukuru sana, jitiada zenu
ziliniwezesha kupata data halisi. Pia, niwashukuru watafitiwa wote waliohusika katika
kutoa data, hakika mmekuwa mchango wa kunipa cha kuandika.
Pamoja na hayo, bila Mungu kuniwezesha michango ya hawa niliowataja isingezaa
matunda haya, hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha maana
“Nayaweza yote katika wewe unitiaye nguvu”.
vi
TABARUKU
Kwa dada yangu mpendwa Beatrice Balige na mume wake Yesse Kanyuma ambao
jitihada zao zilinifanya kupata kila nyenzo ya kuniwezesha kusonga mbele katika hatua
zangu zote za masomo. Nawapenda sana na Mungu awabariki.
vii
IKISIRI
Wakati takribani 5% ya watanzania ndio wanaofahamu Kiingereza (Msanjila 2004:45
akimnukuu Schmied 1989), hali halisi inaonesha kuwa mijadala ya Bunge inaendeshwa
kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kutokana na hali hii utafiti huu ulihusu
ubadilishaji msimbo Bungeni na athari zake kwa wasikilizaji na uliongozwa na modeli ya
Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji” na mkabala wa Fishman (1971)
“Mkabala wa Mawanda”.
Kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na kwa usampulishaji
nasibu tabakishi tuliweza kuwatafiti wasikilizaji 775 kutoka Wilaya za Nyamagana na
Magu mkoani Mwanza. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, wastani wa 08.90% tu ya
wasikilizaji ndio wanaoelewa kwa kiwango kilichokusudiwa mijadala inayohusisha
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Pili, kwa wasioelewa takribani 59.23% hawatafuti
mbinu mbadala za kuelewa mijadala hiyo. Tatu, 81.68% ya watafitiwa hawafurahishwi na
uzungumzaji wa namna hii kwani hawapati ujumbe uliokusudiwa na kubadilisha Kiswahili
na Kiingereza ni kutokithamini Kiswahili na utamaduni wake. Ili kuondoa athari hasi
zinazosababishwa na ubadilishaji msimbo Bungeni, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza
kuwa Kiswahili kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa
wanatoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa; kinaeleweka kwa watanzania wengi na
hivyo kitawezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake; ni lugha ya taifa na
inafungamana na utamaduni wa watanzania; kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi;
kinaepusha utumwa wa kifikra; ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na itasaidia kukilinda na
kukikuza Kiswahili. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla ambayo kimsingi yanalenga
kukiimarisha Kiswahili kidhima.
viii
YALIYOMO Ukurasa
Uthibitisho .............................................................................................
Ikirari na Hakimiliki …..........................................................................
Shukurani ..............................................................................................
Tabaruku ...............................................................................................
Ikisiri .....................................................................................................
Yaliyomo ……………………………………………………………...
Orodha ya Majedwali ………………………………………………...
Vifupisho ……………………………………………………………..
i
ii
iii
vi
vii
viii
xii
xiii
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI 1
1.0
1.1
1.2
1.3
1.3.1
1.3.2
1.4
1.5
1.6
1.7
1.7.1
1.7.2
1.8
Utangulizi wa Jumla........................................................
Usuli wa Tatizo................................................................
Tatizo la Utafiti................................................................
Malengo ya Utafiti...........................................................
Lengo la Jumla.................................................................
Malengo Mahususi...........................................................
Maswali ya Utafiti............................................................
Umuhimu wa Utafiti........................................................
Mawanda ya Utafiti..........................................................
Kiunzi cha Kinadharia …………………………………
Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji …………………..
Mkabala wa Mawanda …………………………………
Vikwazo vya Utafiti ……………………………………
1
2
7
7
8
8
8
9
9
10
10
11
12
ix
1.9 Hitimisho.......................................................................... 13
SURA YA PILI: MAPITIO YA MACHAPISHO 14
2.0
2.1
2.2
2.2.1
2.2.2
2.3
2.4
2.5
2.6
2.7
2.8
Utangulizi............................................................................
Maana ya Ubadilishaji Msimbo..........................................
Aina za Ubadilishaji Msimbo…………………………….
Ubadilishaji Msimbo Ndani ……………………………
Ubadilishaji Msimbo Kati ………………………………..
Tofauti Kati ya Ubadilishaji Msimbo na Ukopaji ………..
Sababu za Ubadilishaji Msimbo …………………………
Uelewekaji wa Maongezi Yanayohusisha Ubadilishaji
Msimbo…………………………………………………...
Mbinu za Kuelewa Matini zenye Ubadilishaji Msimbo …
Mtazamo wa Wasikilizaji Kuhusu Ubadilishaji Msimbo ..
Hitimisho …………………………………………………
14
14
18
18
23
25
29
32
36
36
39
SURA YA TATU: MBINU ZA UTAFITI 40
3.0
3.1
3.2
3.3
3.3.1
3.3.2
3.3.2.1
Utangulizi ............................................................................
Eneo la Utafiti .....................................................................
Populesheni Lengwa ya Utafiti ...........................................
Sampuli na Usampulishaji ..................................................
Sampuli...............................................................................
Usampulishaji......................................................................
Aina ya Usampulishaji........................................................
40
40
41
42
42
42
42
x
3.4
3.4.1
3.4.2
3.4.3
3.5
3.6
Mbinu za Ukusanyaji wa Data............................................
Hojaji...................................................................................
Usaili...................................................................................
Mijadala ya Vikundi Lengani.............................................
Uchanganuzi wa Data.........................................................
Hitimisho …………………………………………………
45
46
46
47
48
49
SURA YA NNE: UWASILISHAJI, UCHANGANUZI NA
UFASIRI WA DATA
50
4.0
4.1
4.2
4.3
4.4
4.5
4.5.1
4.5.1.1
4.5.1.2
4.5.1.3
4.5.1.4
4.5.1.5
4.5.1.6
Utangulizi.............................................................................
Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge….................................
Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala…...………………..
Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni:
Mtazamo wa Wasikilizaji…………………………………
Ufuatiliaji wa Mijadala ya Bunge ……………………......
Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Maoni
ya Wasikilizaji …………………………………………...
Lugha ya Shughuli za Bunge na Kufaa kwa Kiswahili ….
Kiswahili Kinaeleweka kwa Watanzania Wengi ………...
Lugha ya Taifa na Utambulisho wa Watanzania …………
Lugha ya Umoja…………………………………..... …….
Kinawaepusha Watanzania na Utumwa wa Kifikra ………
Kukilinda na Kukikuza Kiswahili ………………………...
Kiswahili ni Lugha Rasmi ya Bunge la Afrika …………...
50
51
55
59
62
64
65
70
73
75
76
77
78
xi
4.6
4.7
4.8
4.9
Mbinu za Kukifanya Kiswahili kuwa Lugha Pekee ya
Shughuli za Bunge………………………………………..
Kufaa kwa Kiingereza kuwa Lugha Rasmi ya Shughuli za
Bunge ……...……..............................................................
Kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza ……………………..
Hitimisho …………………………………………………
79
81
82
82
SURA YA TANO: MUHTASARI NA MAPENDEKEZO
85
5.1
5.2
5.3
5.4
Utangulizi............................................................................
Muhtasari............................................................................
Mapendekezo......................................................................
Hitimisho …………………………………………………
85
85
87
88
Marejeo.................................................................................................
Viambatanisho.....................................................................................
Kiambatanisho I: Hojaji ……………………………………………...
Kiambanisho II: Maswali ya Usaili …………………………………
Kiambanisho III: Maswali ya Vikundi Lengani …………………
Kiambatanisho IV: Mijadala ya Bunge ………………………………
Matini A: ……………………………………….
Matini B: ………………………………………....
Matini C: ………………………………………
Matini D: ………………………………………
89
97
97
100
101
102
102
102
102
103
xii
ORODHA YA MAJEDWALI UKURASA
Jedwali la 1: Sampuli ya Utafiti Kutoka katika Wilaya za
Nyamagana na Magu ……………………………...
Jedwali la 2: Sampuli ya Utafiti Kutoka Kata tatu za Wilaya ya
Nyamagana ………………………………………..
Jedwali la 3: Sampuli kutoka Kata tatu za Wilaya ya Magu ……..
Jedwali la 4: Sampuli ya Utafiti …………………………………..
Jedwali la 5: Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge. ………………..
Jedwali la 6: Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala ……………
Jedwali la 7: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza: Mtazamo
wa Wasikilizaji……………………………………....
Jedwali la 8: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Unasababisha Wasikilizaji Wasifuatilie Mijadala ya
Bunge? ………………………………………………
Jedwali la 9: Mapendekezo ya Lugha ya Shughuli za Bunge …….
Jedwali la 10: Sababu za Kutetea Kiswahili Kuendeshea Shughuli
za Bunge….…………………………………………
Jedwali la 11: Ongezeko la Idadi ya Watumiaji wa Kiswahili
Tanzania……………………………………………
Jedwali la12: Sababu za Wasikilizaji Kutetea kuwa Kiingereza
Kinafaa kwa shughuli za Bunge …………………..
Jedwali la 13: Sababu za Wasikilizaji Kutetea Kiswahili na Kiingereza
Kufaa Kuendeshea Shughuli za Bunge………………….
43
44
44
45
52
56
60
62
67
69
71
81
82
xiii
VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA
Kifupisho Maana
BAKITA Baraza la Kiswahili Tanzania
BAKIZA Baraza la Kiswahili Zanzibar
TATAKI Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Me Wanaume
Ke Wanawake
Nfs1u Nafsi ya kwanza umoja
Nsf1w Nafsi ya kwanza wingi
Nsf2u Nafsi ya pili umoja
Nsf2w Nafsi ya pili wingi
Nsf3u Nafsi ya tatu umoja
Nsf3w Nafsi ya tatu wingi
K/kiso Kitenzi kiso na ukomo
Ki/ng Kipatanishi ngeli
Lejico “Legico” legislative council (Baraza la Kutunga Sheria)
Nj Njeo
Rej Rejeshi
MOMWA Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji
MKAMA Mkabala wa Mawanda
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.0 Utangulizi wa Jumla
Utafiti huu unahusu ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni na athari zake
kwa wasikilizaji. Utafiti unaongozwa na modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo
wa Wasikilizaji” na Mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda”. Katika
kufanya utafiti huu: kwanza, tumejikita kwa wasikilizaji tukitaka kubainisha uelewa wa
mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
miongoni mwa wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu. Uchanganuzi wa data
unaonesha kuwa 8.9% ya wasikilizaji ndio wanaoelewa, 14.58% wanaelewa baadhi ya
sentensi, 34.84% baadhi ya maneno na 41.68% hawaelewi mijadala yenye kuhusisha
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Uchanganuzi zaidi unaonesha kuwa kiwango
cha kuelewa au kutoelewa mijadala hii kinahusiana moja kwa moja na kiwango cha
elimu cha msikilizaji.
Pili, tulitaka kufafanua mbinu wazitumiazo wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya
elimu kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza. Data inaonesha kuwa, 85.04% ya wasikilizaji wasiojua kusoma na
kuandika na 70.86% wa kiwango cha elimu ya msingi hawatafuti mbinu mbadala za
kuwafanya waelewe mijadala hiyo. Kwa upande mwingine, asilimia kubwa ya
wasikilizaji wasomi (wa viwango vya sekondari na chuo) hupata maana ya mijadala ya
Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo kupitia vyombo vya habari na/au kuulizia
kwa wenzao. Pia, data inaonesha kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali
ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza katika mijadala ya Bungeni. Hata hivyo,
2
pamoja na kutofurahishwa na namna hii ya uzungumzaji, katika sehemu ya nne tunaona
kuwa hali hii sio sababu pekee inayosababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya
Bunge.
Nne, kwa kuzingatia maoni ya wasikilizaji tumetoa mapendekezo ya kupunguza athari
hasi za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni. Katika sehemu ya tano
tumeona kuwa 85.55% ya watafitiwa wanapendekeza kuwa Kiswahili kiwe lugha rasmi
na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu wazitoazo ni kuwa; mosi,
kinaeleweka kwa watanzania wengi; pili, ni lugha ya taifa na inafungamana na
utamaduni wa watanzania; tatu, ni lugha ya umoja; nne, kinawaepusha na utumwa wa
kifikra; tano, ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na sita, ni lugha rasmi ya Bunge la
Afrika. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla kuhusu nini kifanyike kukifanya
Kiswahili kuwa lugha kidhi ya mijadala ya Bunge.
Katika utafiti huu, tumetumia istilahi ubadilishaji msimbo kama anavyoitumia Cromdal
(2000:2), anayetumia istilahi hii kumaanisha hali ya utumizi wa lugha mbili au zaidi
katika tamko moja, au mfuatano wa matamko kati ya wazungumzaji wawili au zaidi.
Hivyo, katika utafiti huu ubadilishaji msimbo unaainishwa kuwili: (i) ubadilishaji lugha
ndani ya sentensi moja ambao umerejelewa na baadhi ya wataalamu kama
uchanganyaji msimbo (Salimu-Sawe 2008) na (ii) ubadilishaji lugha baina ya sentensi
na sentensi.
1.1 Usuli wa Tatizo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni chombo cha uwakilishi wa watu,
chenye misingi ya kikatiba kama inavyoainishwa katika sura ya tatu ya Katiba ya
3
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Mathalani, katika ibara ya 62.-(1)
Katiba inaeleza kuwa;
kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na
sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.
Uwakilishi wa wananchi katika chombo maaalumu, chenye msingi wa kikatiba
uliasisiwa na wakoloni wa Kiingereza mwaka 1926 (Nsekela 1965:166). Enzi hizo
kilijulikana kama “Baraza la Kutunga Sheria” au kwa kifupi Legico “lejiko”, jina
lililotokana na uhulutishaji wa “legislative council” (Mwansoko na Tumbo-Masabo
(1996:3).
Utumizi wa Kiswahili kwenye lejiko wakati huo ulichochewa na kuwapo kwa Waafrika
kwani wajumbe wa Kizungu wa lejiko walitosheka na mawasiliano kwa lugha ya
Kiingereza. Wawakilishi wa kwanza wa Kiafrika waliteuliwa mwaka 1945, ambao
walikuwa machifu A.S. Mkwawa, K. Makwaia na A.Shangali (Legere 1987:158).
Kipindi hiki Kiswahili kilitumika sana kama lugha ya ukombozi wa Waafrika na chama
kilichokuwa kikitetea maslahi ya wafanyakazi wa Kiafrika yaani Tanganyika African
Association (TAA), kilichoanzishwa mwaka 1929. Kudhibitisha hili, mwaka 1946
mkutano mkuu wa TAA uliazimia kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano
yake1.
Kutokana na mwamko huu wa kukithamini Kiswahili nchini, wawakilishi wa Afrika
kwenye lejiko walidai Kiswahili kitumike sambamba na Kiingereza katika mawasiliano
1 Legere 1987 uk. 153.
4
ya lejiko muda mfupi baada ya wao kujiunga na Baraza la Kutunga Sheria, wazo
lililoungwa mkono na wakereketwa wa Kiswahili (Mwansoko na mwenzake 1996:3).
Tofauti na ilivyotarajiwa, hoja hii ilipingwa vikali na wajumbe wa Kiingereza wa lejiko
kwa visingizio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:-
I. Kwamba hali ilikuwa hairuhusu kwa lejiko kutumia lugha mbili
II. Kwamba Kiswahili kilikuwa hakijitoshelezi kisarufi na kimsamiati
III. Kwamba Kiswahili kingeshusha hadhi ya lejiko kwani hata Watanzania wa
tabaka la chini (yaani wasio machifu) ambao hawakusomeshwa kwa mfumo
wa elimu ya kikoloni wangeweza kuwa wajumbe wa lejiko.
Kutokana na pingamizi hili, iliwalazimu wana-lejiko wa Kiafrika kupunguza makali ya
madai yao. Sasa walidai hoja muhimu za lejiko zifasiliwe kwa Kiswahili na usambazwa
kwa maofisa wa Kiafrika wa serikali. Katika kikao cha 25 cha lejiko cha mwaka 1950
Chifu A. Shangali aliwasilisha rasmi hoja hii ya kutaka kufasiri hati zote za lejiko kwa
Kiswahili. Hoja hii pamoja na kuungwa mkono na wakuu wa majimbo (ma-PC),
wajumbe wa lejiko Waingereza pamoja na serikali yao walipinga.
Baada ya kuanzishwa chama cha TANU, mnamo tarehe 7/7/1954, pamoja na mambo
mengine kiliamua kwamba Kiswahili kitumike kama lugha ya pili kwenye lejiko.
Mwaka 1958 mkutano mkuu wa TANU uliazimia kukifanya Kiswahili lugha rasmi ya
taifa la Tanganyika pindi tu litakapojipatia uhuru wake. Baada ya kupata uhuru
(9/12/1961), wazalendo wakiongozwa na Rais wa TANU na serikali, Hayati Mwalimu
J. K. Nyerere walitambua vema dhima ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa
5
nchi hii na hivyo hawakusita kukikuza na kukienzi ipasavyo. Kudhibitisha hili, mnamo
tarehe 10/12/1962 Hayati Rais J.K.Nyerere alihutubia Bunge kwa kutumia Kiswahili
kwa mara ya kwanza, hotuba ambayo ilipokelewa na Wabunge kwa shangwe kubwa2 .
Kutokana na hotuba hii iliyosisitiza kuwa na Kiswahili sanifu na kinachoeleweka, ilitoa
changamoto kwa wabunge hasa kuhusu lugha ya mawasiliano Bungeni. Ilidhihirika
kuwa Kiswahili kilikuwa na uwezo wa kukidhi mawasiliano ya Bungeni bila kuathiri
hadhi wala ufanisi wa Bunge. Kwa kuzingatia kuwa nchi ilikuwa imeishapata uhuru,
Wabunge wengi wazalendo walihamasika kukitumia na hivyo kuongeza shinikizo la
kutaka Kiswahili kiruhusiwe Bungeni.
Tarehe 12/2/1963 takribani miezi miwili tu baada ya hotuba ya kihistoria ya aliyekuwa
Rais, Hayati Julius Kambarage Nyerere, serikali ilikitangaza Kiswahili kuwa lugha ya
taifa. Kwa kuwa, kwa muda mrefu wabunge wazalendo walikuwa na shauku kubwa ya
kutumia Kiswahili Bungeni, kutangazwa kwake kuwa lugha ya taifa kulitoa fursa nzuri
ya kuingiza lugha hiyo Bungeni. Mara tu baada ya kutangazwa kuwa lugha ya taifa,
wabunge mashabiki wa Kiswahili walianza kukitumia rasmi kwenye mijadala ya
Bunge, yaani kuanzia kwenye mkutano wa 5, kikao cha 2, cha Februari 12, 19633.
Kwa kuzingatia hili, tunaweza kusema bila wasi wasi kuwa, matumizi ya Kiswahili
katika mijadala ya Bunge yalianza mapema mwaka 1963. Kwa kuwa Bunge lilikuwa na
wabunge wazalendo pamoja na wazungu (Waingereza), basi kulijitokeza matumizi ya
lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza. Wabunge wazalendo walitumia Kiswahili
2 Mwansoko na Tumbo-Masabo (wameshatajwa, ukurasa 5)
3 Mwansoko na Tumbo-Masabo, wakinukuu Hansard, 5
th session, 1963
6
huku wabunge wazungu wakitumia Kiingereza. Hivyo basi, kutokana na sababu za
kihistoria, hadi leo Kiswahili na Kiingereza zinaendelea kuwa lugha rasmi za Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2004
kanuni ya 118(1) inavyoelekeza;-
Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili
au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo kutolewa.
Kiswahili kilipotangazwa kuwa lugha ya taifa, ilidhaniwa kuwa kiuhalisia Bunge
lingekuwa miongoni mwa taasisi za umma ambazo wanasiasa wangezungumza
Kiswahili ili kuonesha utaifa wao au wangeelewa kuwa wasikilizaji walio wengi
hawawezi kuongea wala kuelewa Kiingereza. Hata hivyo, wanafanya hivyo lakini
katika namna ya kipekee, yaani ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza maarufu kama
Swaenglish4.
Katika jamiilugha ulumbi yoyote, ni jambo la kawaida mtu kuongea lugha fulani na
ghafla kubadilisha lugha au kuchanganya vipashio vya lugha mbili au zaidi ili kueleza
jambo (Rajabu 1991:24). Huu ndiyo huitwa ubadilishaji msimbo. Hata hivyo,
kinachofanya namna hii ya uzungumzaji kuonekana ya kipekee katika Bunge ni kuwa
taasisi hii ni rasmi na yenye hadhi kubwa. Urasmi wake unahitaji matumizi ya lugha
sanifu na fasaha, yenye kueleweka mara moja na isiyo na uvulivuli.
4 Kwa lugha ya mtaani lugha yenye mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza huitwa Swaenglish
7
1.2 Tatizo la Utafiti
Bunge la Tanzania linatoa maamuzi ya mambo mabalimbali kwa njia ya vikao au
mikutano yake. Kwa hiyo, jambo lolote linalohitaji uamuzi wa Bunge, huamuliwa
katika mikutano rasmi ya Bunge. Ili kumudu jukumu hili, lazima kuwepo na lugha
inayofaa kuwezesha mawasiliano kati ya wabunge na serikali na kati ya wabunge na
wananchi na pia kati ya serikali na wananchi kupitia kwa wabunge. Kanuni za kudumu
za Bunge zinabainisha kuwa; “Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya
Kiswahili au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo kutolewa” (toleo la 2004 kanuni
ya 118(1)). Hata hivyo, mapitio ya taarifa rasmi za Bunge yanadhihirisha kuwa, wakati
wa mijadala wabunge wanatumia ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.
Tafiti zilizofanyika kuhusu ubadilishaji msimbo Bungeni ni pamoja na tafiti za
MacWilliam na Chuwa (1990) na Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996). Tafiti hizi
zimejikita katika kuainisha sababu za ubadilishaji msimbo Bungeni. Hakuna tafiti
zinazoonesha athari kwa wasikilizaji na watazamaji kwa kuzingatia matabaka yao
kielimu. Pia, maoni ya wasikilizaji juu ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
hayajabainishwa. Kwa kuzingatia hili, utafiti huu ulikuwa muhimu kufanyika ili
kufahamu athari kwa wasikilizaji zinazotokana na ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza Bungeni.
1.3 Malengo ya Utafiti
Sehemu hii inabainisha madhumuni ya utafiti huu ambayo yamegawanyika katika
sehemu mbili, yaani lengo la jumla na malengo mahususi.
8
1.3.1 Lengo la Jumla
Utafiti huu unalenga kutathmini athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Bungeni kwa wasikilizaji na mtazamo wao kuhusu kaida hii ya utumizi wa lugha.
1.3.2 Malengo Mahususi
I. Kubainisha uelewa wa mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji
wa Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wasikilizaji wa viwango
mbalimbali vya elimu.
II. Kufafanua mbinu wazitumiazo wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya
elimu kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza.
III. Kubainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza Bungeni.
IV. Kutoa mapendekezo ya kuondoa athari hasi kwa wasikilizaji zinazotokana
na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni.
1.4 Maswali ya Utafiti
I. Uelewa wa mijadala inayoendeshwa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili
na Kiingereza miongoni mwa wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya
elimu ukoje?
II. Wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wanatumia mbinu gani ili
kupata ujumbe unaotolewa Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza?
9
III. Wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wana mtazamo gani kuhusu
tabia ya Wabunge ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni?
IV. Nini kifanyike ili kuondoa athari hasi kwa wasikilizaji zinazotokana na
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni?
1.5 Umuhimu wa Utafiti
Kwa kuwa utafiti huu unabainisha athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Bungeni kwa wasikilizaji, utawasaidia wabunge pamoja na wadau wa sera ya lugha
kuelewa athari za kiisimu za uzungumzaji wa namna hii. Hii itasaidia katika upangaji
lugha hasa kuhusu lugha inayofaa kutumika katika mijadala Bungeni.
Kutokana na kiwango cha ubadilishaji msimbo Bungeni kuongezeka mwaka hadi
mwaka, utafiti huu utaongezea katika uelewa kuhusu athari za kiisimu na kijamii
zinazosababishwa na ubadilishaji lugha Bungeni. Pia utawawezesha wadau (wabunge)
kuelewa mtazamo na kiwango cha wasikilizaji katika kuelewa mijadala
inayoendeshwa. Kwa wataalamu wa isimujamii, utafiti huu utakuwa chanzo kingine
cha habari na data kuhusu ubadilishaji msimbo na vipengele vingine vya jamiiilugha
ulumbi. Kwa kupata habari na data ya utafiti huu, tunapata data kuhusu ubadilishaji
msimbo na jamii lugha ulumbi. Mwisho utafiti huu unatarajiwa kutia chachu katika
tafiti zinazohusu ubadilishaji na ubadilishaji lugha hasa katika muktadha wa Bungeni.
1.6 Mawanda ya Utafiti
Kutokana na mapitio ya kumbukumbu za Bunge, imebainika kuwa wabunge mara
nyingi hubadilisha Kiswahili na Kingereza. Hata hivyo, kuna sehemu chache ambapo
10
huchanganya na lugha za asili au Kiarabu lakini kwa kutoa maana zake katika
Kiswahili. Kwa kuzingatia hili, utafiti huu umejikita katika ubadilishaji wa Kiswahili
na Kingereza tu. Pili, utafiti haujashughulikia kubainisha sababu za ubadilishaji wa
Kiswahili na Kingereza kwa sababu tafiti zilizotangulia (rejea 2.4) zinaonesha sababu
mbalimbali za ubadilishaji msimbo. Kwa kuzingatia hili, tumejikita katika kubainisha
athari za ubadilishaji wa Kiswahili na Kingereza kwa wasikilizaji.
1.7 Kiunzi cha Kinadharia
Katika kutafuta nadharia za kutumika kama kiolezo cha utafiti huu, nadharia
mbalimbali zimepitiwa. Japokuwa zipo nadharia nyingine ambazo zingetumika kama
kiolezo katika utafiti huu, modeli ya Bell (1984) “Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji”
na Mkabala wa Fishman (1971) “Mkabala wa Mawanda” zimeonekana kuwa mahususi
zaidi.
1.7.1 Modeli ya Mtazamo wa Wasikilizaji (MOMWA)5
Hii ni modeli ya kiisimujamii iliyoasisiwa na Allan Bell mwaka 1984, inayozingatia
kuwa namna ya uzungumzaji inazingatia mtazamo wa wasikilizaji. Kwa modeli hii
wazungumzaji wanateua namna ya uzungumzaji kwa kutilia maanani wasikilizaji ili
kuleta umoja au ukaribu na wasikilizaji au kuzungumza tofauti na matakwa ya
wasikilizaji ili kuelezea kuwa kuna utofauti kati ya mzungumzaji na hadhira yake.
Modeli hii ilianzishwa kutokana na utafiti alioufanya Bell kuhusu utangazaji redioni
nchini Newsland. Utafiti wake ulijikita katika redio mbili ambazo zilitumia studio moja
5 Kwa Kiingereza inaitwa Audience-Design Model
11
na baadhi ya watangazaji wale wale. Redio moja, redio ya taifa iliwavutia sana
wasikilizaji wa hali ya juu kiuchumi. Redio ya pili, redio ya jamii iliwavutia
wasikilizaji wengi ikiwa ni pamoja na wale wa tabaka la chini kiuchumi.
Katika kuchanganua data, Bell anabainisha kuwa watangazaji walizungumza kwa
namna tofauti tofauti kwa kuzingatia wasikilizaji wa redio husika. Kutokana na hali hii
anasema kuwa, kwa sababu mada, wazungumzaji na jambo la kuzungumzia vilikuwa
vile vile, jambo lililosababisha utofauti lilikuwa ni kwamba watangazaji walizungumza
kwa namna ya kutambua kuwa wasikilizaji walitarajia nini. Hivyo basi, mtazamo wa
wasikilizaji kuhusu namna ya uzungumzaji wa mzungumzaji ndio hutawala uteuzi wa
jinsi ya kuzungumza. Kwa mantiki hii, iwapo mzungumzaji atateua namna fulani ya
uzungumzaji ambayo wasikilizaji wake wana mtazamo hasi kwayo, basi
hawatamsikiliza na watakuwa na mtazamo hasi kwa huyo mzungumzaji. Hivyo basi,
modeli hii inasisitiza kuwa wasikilizaji ndio huongoza uteuzi wa namna au lugha ya
kuongea. Modeli hii ni muhimu katika utafiti huu hasa katika kipengele kinacholenga
kubainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu kaida ya ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza Bungeni.
1.7.2 Mkabala wa Mawanda (MKAMA)6
Mkabala huu unachukulia lugha au lahaja za lugha husika kuwa zimepewa dhima
maalumu katika jamii. Uliasisiwa na wanaisimujamii katika jitihada za kumaliza tatizo
la uteuzi wa lugha kwa kuzingatia muundojamii. Fishman (1971) ni miongoni mwa
watetezi wa mkabala huu. Anapendekeza kuwa kuna mazingira ya kitaasisi, yahusuyo
6 Kwa Kiingereza unaitwa The Domain Analytic Aproach
12
mawanda ambapo kwayo lugha moja au lahaja ya lugha inafaa zaidi ya nyingine.
Mkabala huu unachukulia mawanda kujumuisha sehemu, mada na wahusika. Kwa
kuzingatia mtazamo huu wa kisosholojia, mkabala huu unachukulia kuwa muundojamii
ndio huongoza tabia ya watu kuhusu utumizi wa lugha. Hii inamaanisha kuwa, kwa kila
mazungumzo kuna kanuni maalumu ikiwa ni pamoja na kanuni zinazobainisha ni lugha
gani itumike.
Mkabala huu unachukulia kuwa, kwa kila taasisi kama vile Bunge iainishwe ni lugha
gani rasmi itatumika katika shughuli zake zote. Iwapo mkabala huu utazingatiwa katika
taasisi za serikali inategemewa kuwa Kiswahili na Kiingereza kila mojawapo itatumika
katika mawanda mahususi yanayozingatia sehemu/mahali, tukio, mada au wahusika.
Hivyo basi, utumizi wa lugha zote mbili Bungeni yaani Kiswahili na Kiingereza
unapingana na mkabala huu. Kwa ufupi mkabala huu unachukulia ubadilishaji msimbo
kama tabia ya uzungumzaji isiyokubalika katika jamii na hivyo wanajamii wana
mtazamo hasi kwa kaida hii ya uzungumzaji. Kwa kuwa mkabala huu unajihusisha na
mambo ya sera ya lugha na upangaji lugha, hivyo basi ni muhimu katika utafiti huu
hasa katika kipengele kinachohusu nini kifanyike kuondoa/kupunguza ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza (kama una athari hasi kwa wasikilizaji).
1.8 Vikwazo vya Utafiti
Kwa kuwa utafiti huu uligusia mambo ya Bunge watafitiwa wengine walitoa maoni
ambayo yalikuwa ya kisiasa zaidi kuliko kiisimu. Wengine walitoa kero zao kama
upungufu wa walimu, ukosefu wa huduma za jamii na kadhalika. Hii ilimpa kazi mtafiti
kuwarudisha katika mstari kuhusu nini kinahitajika katika utafiti huu. Ili kuweka
13
mazingira ya kirafiki na watafitiwa, mara nyingine ilimpasa mtafiti kumwacha mtoa
data kuongea ananachohitaji huku mtafiti akichukua hoja zinazohusu mada ya utafiti.
Hii ilisaidia kuweka upamoja kati ya mtafiti na watafitiwa kwani kinyume na hapo
mtafiti angenasibishwa na walalamikiwa (serikali na Wabunge) na hivyo kuathiri
upatikanaji wa data. Hata hivyo, hali hii ilimlazimu mtafiti kuchukua muda zaidi ya
uliolengwa awali. Jambo jingine lililochangia hali hii ni kwamba mtafiti alikusanya
data kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu ambapo harakati za kisiasa zilikuwa katika
kiwango cha juu ambapo watu walikuwa tayari kuchangia katika mambo ya kisiasa
zaidi ya yale ya kiisimu.
1.9 Hitimisho
Sura hii imeanza kwa utangulizi wa jumla na kujadili usuli wa tatizo na baadaye
kubainisha tatizo la utafiti. Malengo na maswali ya utafiti yameainishwa kabla ya
kuelezea umuhimu na mawanda ya utafiti. Pia modeli na mkabala vitakavyoongoza
utafiti huu vimejadiliwa. Hivi ni modeli ya Bell (1984) “MOMWA” na mkabala wa
Fishman (1971) “MKAMA” vimejadiliwa. Mjadala huu unatupa mwanzo mzuri wa
kupitia machapisho na tafiti mbalimbali kuhusu ubadilishaji msimbo. Kwa mantiki hii,
sura inayofuata inajikita katika kupitia machapiosho mbalimbali kuhusu ubadilishaji
msimbo.
14
SURA YA PILI
MAPITIO YA MACHAPISHO
2.0 Utangulizi
Sura hii inahusika na upitiaji wa machapisho mbalimbali yanayohusu ubadilishaji
msimbo. Katika sura hii tumeanza kwa kuelezea maana ya ubadilishaji msimbo na
baadaye kuainisha aina zake na kiwango cha utokeaji wake katika matini kabla ya
kutofautisha ubadilishaji msimbo na ukopaji. Baada ya hapo machapisho kuhusu
sababu za wabunge kubadilisha msimbo zimebainishwa na baadaye ni machapisho
kuhusu uelewekaji wa maongezi yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Pia,
machapisho kuhusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini zenye kuhusisha
ubadilishaji msimbo yamepitiwa. Mwisho ni mapitio ya machapisho kuhusu mtazamo
wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji msimbo.
2.1 Maana ya Ubadilishaji Msimbo
Istilahi hii imeelezwa na wataalamu wengi lakini wafuatao ndio watakaohusishwa
katika utafiti huu. Cromdal (2000:2) anasema kuwa, ubadilishaji msimbo ni utumizi wa
lugha mbili au zaidi katika sentensi moja au mfuatano wa sentensi nyingi kati ya watu
wawili au zaidi. Hii inamaanisha kwamba, ubadilishaji msimbo hutokea pale tu zaidi ya
lugha moja zinapotumiwa katika mazungumzo.
Wataalamu wengine wanasema kuwa, ubadilishaji msimbo ni utumizi wa mbadilishano
wa lugha mbili katika jamiilugha uwili ndani ya mada ile ile (Grosjean 1982:145,
Mirloy na Muysken 1995:7). Wataalamu hawa wanatumia istilahi ubadilishaji msimbo
kama istilahi jumuishi ambapo aina tofauti tofauti za jamiilugha uwili zimejuishwa.
15
Wanatumia istilahi ubadilishaji msimbo ndani kumaanisha kubadilisha msimbo ndani
ya sentensi na ubadilishaji msimbo kati kumaanisha ubadilishaji msimbo kati ya
sentensi na sentensi.
Myers-Scotton (1993:1) pia anatumia istilahi ubadilishaji msimbo kama istilahi
jumuishi kwa kuielezea kama utumizi wa lahaja katika mada moja. Wataalamu
wengine kama vile Gardnne-Chloros (1991) pia wanasisitiza kuwa ubadilishaji msimbo
unaweza kutokea sio tu kati ya lugha na lugha bali kati ya lahaja moja na nyingine, na
pia kati ya namna ya uzungumzaji wa lugha moja.
Minloy na Muysken (1995:07) kama wanavyofasiliwa na Cromdal (2000:02), Grosjean
na (1982:145) nao wanasema kuwa ubadilishaji msimbo ni utumizi wa mbadilishano
wa lugha mbili au zaidi katika semo ile ile. Maana hii inahusu lugha moja au zaidi ya
moja zilizo tofauti. Kwa upande mwingine Muysken (1995:189) amepanua maana ya
ubadilishaji msimbo kwa kuhusisha vijenzi vya semo ambapo anasema kuwa ni utumizi
wa lugha mbili katika semo moja au kirai.
Badala ya kujikita katika kirai au semo, Eastman (1992) anatoa msingi mwingine
ambapo anasema kuwa ubadilishaji msimbo ni utumizi wa lugha mbili au zaidi au
lahaja za lugha moja kwa kuzingatia uchocheo unaotegemea hali na muktadha wa
mazungumzo. Maana hii ni nzuri (tukiachilia mbali dhana ya lahaja za lugha moja)
katika utafiti huu kwani modeli na mkabala vinavyoongoza utafiti huu vinachukulia
kuwa utumizi wa lugha lazima uzingatie muktadha na hali ya mazunguzo. Hii
inamaanisha kuwa, uwezo wa mzungumzaji kuwa na umilisi wa lugha mbili unamfanya
16
kuwa na uteuzi wa lugha katika mazungumzo (Kadeghe 2000). Hata hivyo, uteuzi wa
lugha lazima uzingatie: (1) sifa na uhusiano wa msemaji na msikilizaji; (2) muktadha
wa mazungumzo (baa, kanisani, Bungeni n.k); (3) aina ya kilongo (majibizano,
mahojiano, usaili, hotuba n.k); na (4) mada. Jambo hili linabainishwa na Rubin (1968)
anayedai kuwa nchini Paragwai ambapo Kihispania na Kiguarani ni lugha rasmi, watu
hutumia lugha hizi kwa kuzingatia muktadha wa kijamii.
Dhana ya utumizi wa lahaja mbili au zaidi katika semo moja kama inavyojitokeza
katika maelezo ya Myers-Scotton (1993), Gardnne-Chloros (1991) na Eastman (1992)
kuhusu maana ya ubadilishaji msimbo na pia dhana ya ubadilishaji wa namna ya
uzungumzaji kama anavyobainisha Gardnne-Chloros (1991), zinaleta mkanganyiko
fulani zinapojumuishwa katika utafiti huu. Dhana hizi zinapanua wigo wa ubadilishaji
msimbo zaidi ya ilivyolengwa katika utafiti huu. Hii ni kwa sababu zinaingiza dhana
za; ubadilishaji wa namna ya uzungumzaji, ubadilishaji wa vipashio vya kiisimu (kama
vile lafudhi, toni, mkazo, kiimbo na kadhalika) vya lugha mbili tofauti, au hata
ubadilishaji msimbo unaohusisha lahaja za lugha moja. Kwa kuzingatia hili utafiti huu
unajikita tu katika ubadilishaji msimbo katika daraja la lugha.
Katika utafiti huu, tutatumia istilahi ubadilishaji msimbo kama anavyoitumia Cromdal
(2000:2). Anatumia istilahi hii kumaanisha hali ya utumizi wa lugha mbili au zaidi
katika tamko moja, au mfuatano wa matamko kati ya wazungumzaji wawili au zaidi.
Hii ni maana nzuri ya ubadilishaji msimbo kwa sababu inachukulia ubadilishaji
msimbo katika ngazi ya lugha, tofauti na maana nyingine ambazo kama ilivyodokezwa
awali zinaangalia ubadilishaji msimbo kati ya lahaja za lugha moja au namna ya
17
uzungumzaji. Kwa kuzingatia maana hii ubadilishaji msimbo ni istilahi jumuishi
ambapo inaweza kutokea katika ngazi ya mofimu, neno, kirai, kishazi, sentensi na hata
katika ngazi ya kilongo. Jambo la kuzingatia ni kwamba, japo ubadilishaji msimbo
uhusisha lugha mbili au zaidi lakini lugha husika hazipotezi sifa zake za kiisimu
(Mochiwa 1979). Hii inamaanisha kuwa, mifumo ya lugha husika inaweza kuainishwa
kirahisi katika kilongo (Maggati 2004). Hili linaweza kudhihirishwa katika mfano
ufuatao:-
Mfano wa 2 (a)
.… zipo advantage za kutumia long term bonds na advantage ya kwanza ni
non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia internal source of finance
lakini rahisi ku-meet our development goals ….
(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge tarehe 12 Julai, 2007:32)
Tafsiri:
…… Zipo faida za kutumia mikataba ya mda mrefu na faida ya kwanza ni kuwa
haisababishi mfumko wa bei lakini faida ya pili tunatumia chanzo cha ndani cha
fedha lakini rahisi kufikia malengo yetu ya maendeleo…..
Katika matini hii mbunge alikuwa akibadilisha Kiingereza (maneno ya hati za italiki)
na Kiswahili. Mzungumzaji ameanza na neno la Kiswahili “zipo” na baadaye
akabadilisha kwenda Kiingereza “advantage” tena akarudi Kiswahili “za kutumia” na
tena Kiingereza “long term bonds” akaweka kiunganishi “na” (Kiswahili) na kufuatisha
neno la Kiingereza “advantages” . Mwendelezo wa maneno mengine katika matini hii
unaweza kuainishwa kama ifuatavyo “ya kwanza ni” (Kiswahili), “non inflationary”
(Kiingereza), “lakini” (Kiswahili) “advantage” (Kiingereza), “ya pili tunatumia”
18
(Kiswahili), “internal source of finance” (Kiingereza), “lakini rahisi ku-” (Kiswahili),
“-meet our development goals” (Kiingereza). Pamoja na ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza, mfumo wa kileksika wa lugha ni rahisi kubainishwa kwa sababu kila
mfumo unajitegemea. Uzungumzaji wa namna hii ndio huitwa ubadilishaji msimbo.
Pamoja na kukumbwa na changamoto, maana zote za ubadilishaji msimbo kama
zilivyojadiliwa hapo juu zinatupa usuli kuwa, ubadilishaji msimbo huusisha walau
lugha mbili. Inahusisha ubadilishaji kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine wakati
wa mazungumzo. Sehemu ifuatayo inaainisha aina za ubadilishaji msimbo na kiwango
cha utokeaji wake katika matini kama zinavyobainishwa na wataalamu mbalimbali na
kama zinavyojitokeza katika mijadala ya Bunge.
2.2 Aina za Ubadilishaji Msimbo
Ubadilishaji msimbo hugawanywa katika aina kuu mbili ambazo ni ubadilshaji msimbo
ndani, ambao ni ubadilishaji lugha ndani ya sentensi na ubadilishaji msimbo kati,
ambao ni ubadilishaji kutoka lugha moja kwenda nyingine kati ya sentensi moja na
nyingine (Poplack 1981; 1982; Heller 1992; na Kamwangamalu 1992). Pamoja na
wataalamu mbalimbali kutofautiana katika kuelezea ubadilishaji msimbo jambo la
msingi katika mijadala kuhusu maana na aina zake ni kuwa, lazima lugha mbili au zaidi
au lahaja zihusike katika semo moja au tukio la kiusemaji.
2.2.1 Ubadilishaji Msimbo Ndani
Istilahi ubadilishaji msimbo ndani hutumika kumaanisha kubadilisha lugha ndani ya
sentensi moja (Stephens 2000). Hapa vipashio katika kiwango cha mofimu, maneno,
19
virai, vishazi na ua sentensi kutoka lugha moja, mbili au zaidi vinapatikana ndani au
kati ya sentensi (Brice n.d, Muysken 2000 na Scotton 1990). Kwa mujibu wa Myers-
Scotton (1990), ubadilishaji msimbo ndani ni ubadilishaji wa lugha katika kiwango cha
mofimu, neno, kirai au kishazi. Muysken (2000:1) anabainisha vizuri zaidi kwa kudai
kuwa ubadilishaji msimbo ndani ni utumizi wa lugha ambapo vipashio vya kileksika na
kisarufi kutoka lugha mbili hujitokeza katika sentensi moja. Katika machapisho
mengine aina hii ya ubadilishaji msimbo huitwa uchanganyaji msimbo (Kalong
2008:11). Mfano ufuatao unaonesha aina hii ya ubadilishaji msimbo.
Mfano wa 2 (b)
Matini (a)
I. Mheshimiwa spika, India is one of the best country katika Railway network,
tukachukua ma-expert waje watusaidie lakini iwe chini yetu. ……….
Tutasafirisha abiria na mizigo na bidhaa at the end of the day hatuna kitu.
Halafu unampa contract ya 25 years is not a joke……
(Matini kutoka kumbukumbu rasmi za Bunge 12 Julai, 2007:83).
Tafsiri:
Mheshimiwa spika, India ni miongoni mwa nchi mashuhuri katika mtandao wa reli,
tukachukua wataalamu waje watusaidie lakini iwe chini yetu. ….. Tutasafirisha
abiria na mizigo na bidhaa mwisho wa siku hatuna kitu. Halafu unampa mkataba
wa miaka 25 sio utani ……
II. Je serikali haioni kwamba ni vyema tukajitahidi tukahakikisha kwamba the
only suppliers and the only producer wa zao hili kwa sababu tusipoingia
kwenye ku-monopolize hii product itafikia mahali suppliers wengine ndio
20
watapata faida kuliko sisi ambao Mwenyezi Mungu ametujalia kuvipata vitu
hivi.
(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 30 Julai, 2007:14).
Tafsiri:
Je serikali haioni kwamba ni vyema tukajitahidi tukahakikisha kwamba
tunakuwa wazalishaji na wauzaji peke wa zao hili kwa sababu tusipoingia
kwenye kumiriki hii bidhaa itafikia mahali wauzaji wengine ndio watapata
faida kuliko sisi ambao Mwenyezi Mungu ametujalia kuvipata vitu hivi.
Matini (b)
1. …Possessive individualism ya ku-grab mali una-acquire au unazaliwa
nayo?
2. … hapa kila mtu anamwona na anaweza aji-reform zaidi kuliko hata
yule….. wengine wameji-reform wengine wanaendelea……
3. …..kwa mfano, katika nchi kama USA niliwaambia mwaka 1998 ambao
wame-import kitu kile halafu waka-export kitu kile kile……
4. …. huyu agent NDC anaji-commit kwa niaba ya serikali, inayoitwa
National Development Corporation sasa leo National Development inataka
kufanya biashara lakini inaingia in a wrong way inaji-commit kabisa………
(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge mkutano wa saba Aprili 2002:54)
Tafsiri:
1. ……. Umiriki binafsi wa kunyakua mali unauamili au unazaliwa nayo?
2. …….. hapa kila mtu anamwona na anaweza ajirekebishe zaidi kuliko hata
yule….. wengine wamejirekebisha wengine wanaendelea……
21
3. …..kwa mfano, katika nchi kama USA niliwaambia mwaka 1998 ambao
waliingiza kitu kile kutoka nchi za nje halafu wakasafirisha nje kitu kile
kile……
4. …. huyu wakala NDC anajifunga kwa niaba ya serikali, inayoitwa National
Development Corporation sasa leo National Development inataka kufanya
biashara lakini inaingia in a wrong way inajifunga kabisa………
Mifano kutoka matini hizi inaonesha jinsi wazungumzaji wanavyobadilisha kutoka
lugha moja kwenda nyingine lakini ndani ya sentensi ile ile. Katika matini hizi kuna
ubadilishaji ulio ndani ya neno yaani kati ya mofimu na mofimu na ulio ndani ya kirai
na pia ndani ya kishazi ambapo viambajengo hivi kwa pamoja vianaunda sentensi.
Mathalani, ubadilishaji msimbo ulio ndani ya neno yaani kati ya mofimu na mofimu
upo katika maneno ma-expert, ku-monopolize, ku-grab, anaji-reform, wameji-reform,
wame-eport, waka-export, anaji-commit, na inaji-commit. Kimsigi maneno haya
yamekamilika na yanajitegemea kimaana na kimuundo japo yameundwa na mofimu za
lugha mbili tofauti ambapo mofimu zilizokolezwa ni za lugha ya Kiswahili na ambazo
zimeambikwa kwenye mzizi wa neno/maneno ya Kiingereza. Huu ndio huitwa
ubadilishaji msimbo ndani ya neno. Mchanganua wa mofimu katika maneno haya
unaweza kuwa kama ifuatavyo:-
22
1. Ma - expert “wataalamu”
Nfs3w mz
2. A - na - ji - reform “anajirekebisha”
Nfs2u nj rej mz
3. Wa - me - ji - reform “wamejirekebisha”
Nfs3w nj rej mz
4. Ku - grab “kunyakua/chopoa”
K/kiso mz
5. I - na - ji - commit “inajifunga”
Ki/ng nj rej mz
Mnyambulisho wa maneno hapa juu unaonesha jinsi maneno hayo yalivyoundwa na
mofimu mbalimbali za lugha mbili ambapo mzizi ni wa lugha ya Kiingereza na wakati
viambishi awali vyake ni vya Kiswahili.
23
Baada ya kupitia taarifa rasmi za Bunge imeonekana kuwa ubadilishaji msimbo ndani
ndio hujitokeza sana katika majadiliano ya Bunge. Hii inamaanisha kuwa wabunge
hawapendelei au hawawezi kuongea semo ndefu kwa lugha ya Kiingereza bila
kuchanganya na Kiswahili japo kinyume chake inawezekana.
Hoja ya ubadilishaji msimbo ndani kujitokeza zaidi inaungana na utafiti wa Kadeghe
(2000) na Kanyuma (2005), ambapo Kadeghe anaainisha kuwa walimu na wanafunzi
hupendelea ubadilishaji msimbo ndani ambapo ni takribani 65% ya ubadilishaji
msimbo unaojitokeza katika data za utafiti huo.
Naye Kanyuma (uk. 83) katika utafiti uliohusu ubadilishaji msimbo miongoni mwa
walimu na wanafunzi wa shule za msingi, data yake inabainisha kuwa 38% ni
ubadilishaji msimbo kati na wakati ubadilishaji msimbo ndani ni 62%.
2.2.2 Ubadilishaji Msimbo Kati
Ubadilishaji msimbo kati humaanisha kubadilisha lugha nje ya mipaka ya sentensi. Hii
inamaanisha kuwa matini nzima ya sentensi hutolewa katika lugha moja kabla ya
kubadilisha kwenda lugha nyingine katika semo ile ile (Myers-Scotton 1993).
Mfano 2 (c)
Matini (a)
Mheshimiwa Spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa
yeye, mtondogoo wao. I better warn you today comrades, you will not afford.
Hatutavumilia matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya watu
wachache. (Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 14 Julai, 2004:82).
24
Tafsiri:
Mheshimiwa Spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa
yeye, mtondogoo wao. Ndugu zangu ni vizuri leo niwatahadharishe,
hamtaweza. Hatutavumilia matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya
watu wachache.
Matini (b)
Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu Minister ni nani, ni wale
wengine nisioongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe
hujui nani aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
nikamwambia uliteuliwa wewe. But you don’t seem to be. Why do you
understand me when we talk here together and when you go to your office you
are powerless, what is wrong?
(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 14 Julai, 2004:83).
Tafsiri:
Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu waziri ni nani ni wale wengine
nisiongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe hujui nani
aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikamwambia
uliteuliwa wewe. Lakini huonekani hivyo. Mbona tunapokuwa pamoja
tunaelewana lakini uendapo ofisini kwako unapoteza mamlaka, kuna tatizo
gani?
Katika matini hizi ((a) na (b)) sentensi “I better warn you today comrades, you will not
afford” kutoka matini (a) na “Why do you understand me when we talk here together
and when you go to your office you are powerless, what is wrong”?, kutoka matini (b)
25
zinaonesha ubadilishaji msimbo kati. Hii ni kwa sababu tungo za Kiswahili zilizopo
awali na/au baada yake zinaonekana kuwa nje ya mipaka ya sentensi hizi na
zinajitegemea kimuundo na kimaana. Kwa mantiki hii tungo hizi sio sehemu ya
sentensi za Kiswahili zilizo karibu nazo. Hivyo basi, huu ndio ubadilishaji msimbo nje
ya mipaka ya sentensi uitwao ubadilishaji msimbo kati. Kinyume na utafiti wa Wu
(1985) na Grice (2000) wanaodai kuwa ubadilishaji msimbo kati ndio hutokea sana
katika maongezi, aina hii ya ubadilishaji msimbo inatokea mara chache katika
maongezi ya wabunge.
2.3 Tofauti Kati ya Ubadilishaji Msimbo na Ukopaji
Ubadilishaji msimbo ndani umeibua mjadala mkubwa katika tafiti za ubadilishaji
msimbo pamoja na makutano ya lugha kwa ujumla kwa sababu hakuna makubaliano
kati ya watafiti kuhusu jinsi ya kuutofautisha na ukopaji (Kibogoya 1998:03). Pamoja
na kuwa kumekuwepo na makubaliano kuwa dhana hizi inabidi zitofautishwe bado
hakuna makubaliano kuhusu ni vigezo gani vitumike kutofautisha dhana hizi. Kutokana
na hoja hii ndio maana sio rahisi kuelezea dhana mojawapo bila kudokeza tofauti zake
za msingi.
Miongoni mwa tofauti zilizopendekezwa na wataalamu mbalimbali ni pamoja na mosi,
urefu wa semo ambapo neno moja katika tungo lilichukuliwa kama ukopaji na sio
ubadilishaji msimbo (Clyne 1967; Grosjean 1982). Hoja ya msingi ni kuwa utumizi wa
neno moja au maneno ambatani yanayowakilisha neno moja yanamotishwa na uhitaji
wa kuziba mwanya wa kileksika ambayo hii ni motisha ya msingi ya ukopaji (Poplack,
Sankoff na Miller (1988), Bentahila na Davies (1983) na Bokamba (1988). Hii haiwezi
26
kuwa tofauti ya msingi kwani mzungumzaji anaweza kubadilisha msimbo kwa
kuchanganya neno moja tu katika sentensi.
Mfano wa 2 (d)
1. Mimi nafikiri nalo hili tungeliangalia kwa sababu experience ndiyo inaweza
kutusaidia sana katika kujenga taasisi hii ya madini.
2. Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu Minister ni nani ni wale
wengine nisioongea nao au ni wewe tunayeongea wote…….
Katika matini hizi neno “experience” kama linavyojitokeza katika (1) na neno
“minister” kama linavyojitokeza katika (2) hayawezi kuchukuliwa kama maneno ya
mkopo kwani yana visawe vyake katika Kiswahili. Neno “experience” ni uzoefu na
“minister” ni waziri. Pia, maneno haya hayaendani na mofofonolojia ya Kiswahili.
Pili, ni kuwa iwapo neno au tungo imetoholewa katika lugha husika kimofolojia na
kifonolojia hivyo huo ni ukopaji. Hoja ya msingi ni kuwa usilimishaji wa kifonolojia na
kimofolojia wa neno husika ni kigezo cha kutofautisha ukopaji na ubadilishaji msimbo
ndani (Haugen 1973). Changamoto ya kutumia kigezo hiki ni kuwa utohoaji wa
kifonolojia ni vigumu kuubainishwa hasa pale utamkaji wa lugha fulani unapokuwa
umeathiriwa na lugha nyingine.
Kigezo kingine kinachopendekezwa na Shaffer (1975) ni cha kimtindo ambapo anadai
kuwa ubadilishaji msimbo hutokea katika mazungumzo yasiyo rasmi na wakati ukopaji
27
hutokea katika mazungunzo rasmi. Katika utafiti huu hoja hii inakosa mashiko kwani
mazungumzo ya Bungeni ni rasmi lakini ubadilishaji msimbo hutokea.
Hoja nyingine inayopendekezwa kutofautisha dhana hizi na wataalamu kama Pfaff
(1979), Sridhar na Sridhar (1980), Kachru (1982), na Bentahila (1983) ni kuwa
ubadilishaji msimbo hutokea tu kwenye mazungumzo yenye kuhusisha lugha mbili
(jamiilugha uwili) ukopaji hutokea katika mazungumzo yenye kuhusisha lugha moja.
Kigezo hiki kinaibua changamoto kwani hata katika mazungumzo yenye kuhusisha
lugha mbili ukopaji unaweza kujitokeza. Mathalani, kulingana na kanuni za Bunge,
Mbunge anaruhusiwa kuchangia hoja kwa Kiswahili au Kiingereza. Lakini katika
mijadala Wabunge huweza kuhusisha maneno ya mkopo kama vile spika, kompyuta,
redio, data, ripoti na kadhalika.
Naye Berk-Seligson (1986) anaongezea tofauti nyingine kuwa maneno ya lugha moja
yanayotumiwa katika lugha nyingine lakini yakiwa na visawe katika lugha hiyo basi
ichukuliwa kuwa huu ni ubadilishaji msimbo. Changamoto katika hoja hii ni kuwa kuna
ukopaji unaosababisha uongezekaji wa visawe katika lugha husika. Kwa mfano,
maneno “shule” na “skuli” ni visawe na ni maneno ya mkopo.
Naye Myers-Scotton (1983:192) anatoa tofauti ya msingi kuwa msamiati unaotokana
na ukopaji huingia katika msamiati wa akilini mwa mzungumzaji na wakati ule
unaotokana na ubadilishaji msimbo hauwi katika mfumo wa kamusi ya akilini ya
mzungumzaji. Pia anaongezea kuwa msamiati wa ukopaji unatabirika na wakati ule wa
28
ubadilishaji msimbo hautabiriki (uk. 207). Kimsingi japo hoja hii ni ya kinadharia kama
itakavyobainishwa baadaye inatupa usuli wa kutofautisha dhana hizi.
Katika utafiti huu dhana hizi ni muhimu zibainishwe utofauti wake pamoja na kuwa
wanaisimu wanaojihusisha na uchunguzi wa michakato ya uundaji wa maneno katika
lugha hasa wakijikita katika njia za ubadilishaji msimbo na ukopaji wameshindwa
kutoa tofauti za msingi za dhana hizi. Kinadharia tofauti kati yake iko wazi kwamba
ubadilishaji msimbo unajumuhisha utumizi wa vipashio kunjiano7 katika lugha lengwa.
Kiujumla inachukuliwa kuwa ubadilishaji msimbo ni ubadilishaji wa lugha wa
mzungumzaji katika muktadha fulani. Lakini ieleweke kuwa ubadilishaji kutoka lugha
moja kwenda lugha nyingine unahitaji umilisi wa lugha zote zinazohusika na hivyo
inamlazimu mzungumzaji kuelewa lugha husika. Tofauti na hili ukopaji hauhitaji
mhusika kuwa mmilisi wa lugha husika (lengwa na chanzi) bali ni matokeo ya
makutano ya lugha hizo. Kwa mantiki hii, ukopaji unaweza kutokea bila hata mzawa
wa lugha lengwa kujua au hata kuwahi kuongea lugha chanzi. Kwa mfano; Mswahili
ambaye hajui wala hajawai kusikia lugha ya Kiingereza anatumia maneno kama shati,
benki, data, baa, bia, kompyuta, redio na kadhalika ambayo kimsingi yamekopwa
kutoka lugha ya Kiingereza.
Kwa uelewa wetu ukopaji hutokea pale wazungumzaji wa lugha wanapoanza kutumia
maneno kutoka lugha mkopo bila kuwa na uelewa kuwa maneno hayo si msamiati
asilia wa lugha yao. Hata hivyo kwa vyovyote vile ukopaji na ubadilishaji msimbo ni
7 Imetafsiriwa kutoka dhana ya Kiingereza “Embedded elements”
29
matokeo ya makutano ya lugha husika. Kwa mantiki hii hali ya kijamii ya dhana hizi
haiwezi kutupiliwa mbali.
Tofauti nyingine tunaungana na Scotton (keshatajwa) kuwa moja ya sababu nyingi
inayodokezwa katika machapisho mengi ni kuwa katika ubadilishaji msimbo maneno
yake hayawi msamiati wa akilini mwa mzungumzaji wakati ukopaji huongezea
msamiati katika kamusi ya akilini. Tofauti nyingine inabainishwa na Heller`s (1988:11)
kuwa ubadilishaji msimbo ni mbinu ya kimawasiliano ambayo wazungumzaji huitumia
katika hali ya utambuzi na wakati ukopaji kwa sababu umechukuliwa kama mfumo wa
lugha husika basi hutokea katika hali ya ung’amuzi bwete.
2.4 Sababu za Ubadilishaji Msimbo
Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusu ubadilishaji msimbo na sababu zake kwa ujumla.
Hizi ni pamoja na tafiti za Blommaert 1992; Myers-Scotton 1993; Romaine 1996,
Rajabu 1981 na Kanyuma 2005. Tafiti hizi kwa ujumla zimejikita katika ubadilishaji
msimbo katika mfumo wa elimu kwa mtazamo wa ufundishaji na mbinu za
kufundishia.
Katika muktadha wa matumizi ya lugha Bungeni na ubadilishaji msimbo kwa ujumla
wataalamu MacWilliam na Chuwa 1990; na Mwansoko na Tumbo-Masabo 1996
wameainisha sababu za ubadilishaji msimbo katika muktadha wa Tanzania. Kwa
kutumia data kutoka vipindi vya redio na taarifa za magazetini MacWilliam na Chuwa
(1990) pamoja na mambo mengine waliweza kuainisha sababu za ubadilishaji msimbo.
Hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la utafiti huu. Kwa kutumia sababu zilizopendekezwa
30
na Grosjean (1982), waliweza kuainisha sababu zinazopelekea wabunge wachanganye
Kiingereza na Kiswahihili. Sababu hizo ni:-
a) Kujaza pengo lilipo katika msamiati ama wa mzungumzaji mwenyewe
ama wa lugha.
b) Kurejea usemi halisi wa mzungumzaji mwingine, au nahau ya lugha
nyingine.
c) Kusisitiza jambo au kutia chumvi/nguvu habari fulani.
d) Kujitambulisha na habari anazozitoa
e) Kujionyesha na kusisitiza umoja wa kundi fulani
f) Kumtenga mwingine
g) Kujishaua, kujiongezea wadhifa, kuonesha ujuzi
h) Kuwa na uvivu/kutojali
Nao utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) kwa kiasi kikubwa ulipata msingi
wake kutoka utafiti wa MacWilliam na Chuwa. Tofauti na utafiti wa awali, watafiti
hawa walifanya utafiti ambao uliwahusisha moja kwa moja wabunge na maofisa wa
Bunge.
Pamoja na mambo mengine watafiti waliwatafiti wabunge na maofisa wa Bunge
kuhusu sababu za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza wakati wa mjadala. Baada
ya kuchanganua hojaji sababu zifuatazo zilibainishwa.
a) Kutaka kueleweka/kufahamika
31
b) Mazoea, ya kwamba Wabunge/wawakilishi wengi wamesoma kwa
kutumia Kiingereza na wamekuwa wakikitumia kazini kabla ya kuingia
Bungeni/Baraza la Wawakilishi
c) Kuwepo kwa neno moja la Kiingereza ambalo ni kuntu wakati hakuna
neno moja la Kiswahili na hivyo kulazimika kutumia maneno mengi ya
Kiswahili.
d) Upungufu na uchache wa neno/maneno ya Kiswahili kutotoa dhana
inayotakiwa
e) Kulemaa/ulemavu au kujionyesha
f) Kupata maana kamili ya fikra
g) Ufafanuzi wa haraka
h) Kufikiri kwa Kiingereza
i) Miswada na maandiko mengine Bungeni kutolewa katika Kiingereza
wakati majadiliano huweza kuwa katika lugha ya Kiingereza au
Kiswahili
j) Jazba (kwamba mzungumzaji anapokuwa na mori basi hajali lugha
anayotumia)
k) Kutoa mifano ambayo hueleweka vizuri zaidi kwa Kiingereza.
l) Kutojua Kiswahili barabara
m) Ugumu wa kupata maneno
n) Kanuni za Bunge hazimfungi mbunge asichanganye lugha, yaani
zinamruhusu mbunge kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
o) Kufupisha majadiliano (wabunge hupewa muda maalumu wa kutoa hoja
zao)
32
Katika kipengele hiki, kama ilivyodokezwa katika utangulizi wao, wameweza
kupunguza kama si kumaliza mapungufu yaliyojitokeza katika utafiti wa MacWilliam
na Chuwa (1990) hasa katika kipengele cha sababu zinazomfanya mbunge kutumia
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni. Hii ni kwa sababu wamepata sababu
hizi kutoka kwa wabunge wenyewe. Kwa kuzingatia hili, inaonekana hakuna haja ya
kufanya utafiti tena kuhusu sababu za ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Bungeni. Kwa kuwa kipengele hiki hakimo katika malengo ya utafiti huu, tuseme tu
kwamba inatosha kuzitaja sababu hizi bila kuzijadili kwa undani.
2.5 Uelewekaji wa Maongezi Yanayohusisha Ubadilishaji Msimbo.
Pamoja na kutofautiana katika kuelezea dhana ya lugha, wanaisimu wengi wakiwemo
Trudgil (1974), Sapir (1921) na Weber (1985) wanakubaliana katika dhana moja
muhimu kwamba dhima kuu ya lugha yoyote ni kuwezesha mawasiliano. Kwa
kuzingatia hoja hii, tafiti zimefanyika kubainisha kama ubadilishaji msimbo
unasababisha walengwa wa mazungumzo/maandishi kuelewa ujumbe uliolengwa na
mwandishi/mzungumzaji. Miongoni mwa watafiti hawa ni pamoja na Leung (2010),
Hammink (2000), Chung (2006), Adendorff (1996), MacWilliam na Chuwa (1990) na
Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996).
Adendorff (1996) alifanya utafiti wake nchini Afrika kusini. Utafiti huu unahusu
ubadilishaji msimbo kati ya Kiingereza na Kizulu katika muktadha wa darasani yaani
katika mijadala kati ya walimu na wanafunzi. Utafiti huu unabainisha kuwa,
ubadilishaji msimbo ni mbinu ya kimawasiliano inayowezesha walimu na wanafunzi
kuwasiliana vizuri.
33
Utafiti wa Chung (2006) uliolenga kuangalia kama ubadilishaji msimbo unawezesha
mawasiliano miongoni mwa wanajamii wenye umahiri tofauti wa lugha husika. Ufafiti
uliwahusisha wanafamilia (baba, mama na watoto wao wawili) ambao walikuwa na
umahiri tofauti wa lugha za Kikorea na Kiingereza na ambao waliishi Marekani. Kwa
kuwa wanafamilia walikuwa na umahiri tofauti wa Kiingereza na Kikorea, mtafiti
anabainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unatumika kuwezesha mawasiliano miongoni
mwa wanafamilia. Utafiti huu unabainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unasaidia
kuepusha vikwazo vya kiisimu na tofauti za kiutamaduni miongoni mwa wanajamii.
Anaongeza kuwa ubadilishaji msimbo unawezesha utoaji wa maelezo ya ziada na
kusisitiza hoja. Hivyo basi, mtafiti anahitimisha kuwa, ubadilishaji msimbo ni mbinu
itumikayo kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wanajamiilugha uwili.
Tafiti hizi zinaungana na hoja ya Tay (1989) na Myers-Scotton (1995) kuwa,
ubadilishaji msimbo hutumika kama mbinu ya kimawasiliano miongoni mwa
wazungumzaji kwa kuzingatia lengo la mzungumzaji kubadili msimbo.
Utafiti mwingine ni utafiti wa MacWilliam na Chuwa (1990) ambao unajikita katika
ubadilishaji msimbo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Utafiti huu
unabainisha kuwa, maneno ya lugha ya kigeni yaliyotumiwa katika sentensi za
Kiswahili siyo maneno rahisi yanayoweza kubuniwa na mwenye kiwango kidogo cha
Kiingereza. Matokeo yake ni sentensi kutoeleweka kwa msikilizaji na hivyo kumnyima
fursa ya kufuata majadiliano ya wabunge.
34
Athari nyingine iliyobainishwa katika utafiti wao ni ile ya upotoshaji wa ufasaha wa
lugha yenyewe. Ikiwa unatumia lugha mbili ambazo kimsingi ziko tofauti kabisa kuna
hatari ya kuathiri sarufi na maumbo mengine ya lugha. Hoja hii haitashughulikiwa
katika utafiti huu.
Utafiti huu kwa ujumla bado una mapengo yanayotakiwa kuzibwa. Kwanza, utafiti huu
haukuwashirikisha wazungumzaji ambao ni wabunge wala wasikilizaji yaani wananchi.
Hitimisho hili lilifikiwa kwa kusoma taarifa rasmi za Bunge, magazeti na kusikiliza
mijadala ya Wabunge redioni kama wanavyosema:-
….tulifuatilia kwa makini majadiliano ya Bunge la 1987 kwa kusikiliza
vipindi vya “LEO KATIKA BUNGE” vilivyotolewa redioni. Tulipata
pia fursa ya kuazima na kusoma nakala za majadiliano hayo kutoka
ofisi ya Bunge wakati wa kufanya utafiti huu….
Kwa kuzingatia hili, ni vigumu kubainisha kama wasikilizaji wanaelewa au hawaelewi
mijadala iendeshwayo Bungeni kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza bila
kuwahusisha wasikilizaji wenyewe. Kwa mantiki hii, utafiti huu unalenga kubainisha
kama wasikilizaji wa matabaka mbalimbali wanaelewa mijadala ya Bunge inayohusisha
ubadilishaji msimbo ambapo wasikilizaji ndio chanzo cha data.
Utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) kwa kiasi kikubwa ulipata msingi
wake kutoka utafiti wa MacWilliam na Chuwa. Tofauti na utafiti wa awali, watafiti
hawa walifanya utafiti ambao uliwahusisha moja kwa moja wabunge na maofisa wa
Bunge. Nia hasa ya utafiti huu ilikuwa kusikia kutoka kwa wabunge, wawakilishi na
35
maofisa walengwa wa majadiliano Bungeni kwa kuzingatia kuwa hadhira anayotarajia
mzungumzaji huathiri sana matumizi ya lugha.
Kuhusu walengwa wa mawasiliano ya wabunge na wawakilishi, utafiti unaonesha kuwa
90% ya wabunge walitambua kuwa hadhira yao ni wasikilizaji ambao ni wananchi na
umma unaowakilishwa na mbunge. Wakimnukuu mmoja wa wabunge wanasema:-
Mbunge kama mwakilishi wa wananchi na umma kwa ujumla hueleza ujumbe
wake kwa serikali kupitia spika ingawa umma wote unategemewa kumuelewa.
Katika kipengele hiki inaonesha watafiti walilenga kufahamu tu kama wabunge
wanafahamu hadhira yao ambayo ingekuwa na athari katika utumizi wao wa lugha
Bungeni. Kwa kuzingatia hili, bado kuna pengo linalotakiwa kuzibwa. Suala la msingi
si kufahamu tu hadhira yake bali ni kwenda mbali zaidi na kufahamu kama wasikilizaji
wanaelewa mijadala inayoendeshwa kwa ubadiloishaji wa Kiswahili na Kiingereza.
Ikumbukwe kuwa wabunge ndio hutumia ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Bungeni, hivyo kimantiki kuwauliza wao kuhusu athari za uzungumzaji na namna hii
kwa kiasi fulani inakosa mashiko, bali ni vizuri kuwahoji wasikilizaji ambao kwa kiasi
kikubwa ndio wanapata athari hizo. Kwa mantiki hii, utafiti huu unalenga kujaza pengo
lililoachwa katika utafiti huu.
2.6 Mbinu za Kuelewa Matini zenye Ubadilishaji Msimbo.
Dhima kuu ya lugha ni mawasiliano na ili mawasiliano yawepo ni lazima msikilizaji
aelewe nini msemaji amesema. Katika muktadha wa Bungeni, mbunge ni mtetezi
anayepaswa kuzungumzia matatizo ya wananchi Bungeni na wananchi wana shauku na
36
haki ya kumsikia (na kumuelewa) mbunge wao akiwatetea (Msekwa 2000:58). Kwa
kuwa imedhihirika kuwa wabunge huchangia hoja kwa ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza na kwa kuwa Kiingereza hakieleweki vizuri kwa watanzania walio wengi,
baada ya kupitia tafiti mbalimbali imeonekana kuwa tafiti hizi hazioneshi ni kwa
namna gani wasikilizaji huelewa mijadala ya Bunge.
Utafiti wa Mwansoko na Tumbo-Masabo (1996) pamoja na mambo mengine ulijikita
katika kuelewa ni njia gani wazitumiazo wabunge na wawakilishi katika kutatua
matatizo yao ya lugha. Utafiti unabainisha kuwa, wabunge na wawakilishi hutumia njia
kadhaa ikiwa ni pamoja na kuangalia kwenye kamusi, marejeo katika maktaba ya
Bunge na hasa vitabu vya BAKITA, kuulizana, na kuunda neno linalohitajika.
Kutokana na majibu haya, bado kuna swali la msingi ambalo halijajibiwa. Kama
wabunge wanatumia njia hizi kutatua tatizo la lugha, je, wasikilizaji wanatumia njia
gani? Hivyo basi, utafiti huu unalenga kubaini mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa
mijadala ya wabunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.
2.7 Mtazamo wa Wasikilizaji Kuhusu Ubadilishaji Msimbo
Katika jamiilugha yoyote ile watu wanakuwa na mtazamo tofauti kuhusu tabia ya
ubadilishaji msimbo. Wapo wanaoichukulia kama mbinu ya kimawasiliano, huku
wengine wakiichukulia kama uzungumzaji usio na hadhi wala staha, mbaya au ukosefu
wa umahiri wa lugha husika (a). Pamoja na mitazamo hii tafiti zinaonesha kuwa
ubadilishaji msimbo ni sifa mojawapo ya jamiilugha uwili au ulumbi.
37
Kutokana na hali hii tafiti kadhaa zimefanyika ili kubainisha mtazamo wa wasikilizaji
na au wazungumzaji kuhusu ubadilishaji msimbo. Miongoni mwa tafiti hizi ni pamoja
na Hammink (2000), Leung (2010), Rajabu (1991) na Kanyuma (2005).
Hammink (2000) amefanya utafiti wake nchini Meksiko kwenye jimbo la EI Paso
liliko mpakani mwa Marekani. Katika jimbo hili wanajamii wanatumia lugha za
Kiingereza na Kihispania japo katika viwango tofauti vya umilisi wa lugha husika. Kwa
mantiki hii, lugha zinazohusika katika ubadilishaji msimbo ni Kihispania na
Kiingereza. Katika utafiti huu, mtafiti amebainisha kuwa watafitiwa wanaonesha
mtazamo chanya kuhusu tabia ya ubadilishaji msimbo. Anaendelea kuelezea kuwa,
vijana (wanafunzi) ndio wanaopendelea zaidi namna hii ya uzungumzaji ambapo
69.23% ya wanafunzi wenye uwezo wa kuzungumza lugha mbili wana mtazamo
chanya kuhusu ubadilishaji msimbo. Hata hivyo, mtafiti anabainisha kuwa hali ni
tofauti kwa upande wa watu wazima ambapo wenye mtazamo chanya kuhusu
ubadilishaji msimbo ni takribani 50%.
Utafiti mwingine ni wa Leung (2010) uliofanyika nchini Hong Kong ambao pamoja na
mambo mengine amebainisha mtazamo wa wasikilizaji kuhusu ubadilishaji msimbo.
Utafiti huu ulijikita katika ubadilishaji msimbo kwenye matangazo ya kibiashara
unaohusisha Kichina na Kiingereza. Mtafiti anabainisha kuwa, watafitiwa wengi
walijibu kuwa wanajisikia vizuri na kawaida kusikia matangazo ya bidhaa yenye
kutumia mchanganyiko wa lugha hizi. Katika uchanganuzi wa data mtafiti
anahitimisha kwa kusema kuwa, ubadilishaji msimbo ni tabia ya utumizi wa lugha
iliyozoeleka nchini Hong Kong hivyo utokeaji wake katika matangazo ya biashara
38
unaendana na hali ya maisha, utamaduni pamoja na utambulisho wa wanunuzi wa
bidhaa na hivyo ubadilishaji msimbo unakubalika miongoni mwa wanajamii hawa.
Katika utafiti huu watu wachache ndio waliokuwa na mtazamo hasi kuhusu ubadilishaji
msimbo. Hata hivyo, kuna bidhaa maalumu ambazo takribani 80% hawakupenda
zitangazwe kwa ubadilishaji wa lugha.
Kuhusu utafiti wa Rajabu (1991) alioufanya katika vyuo vikuu nchini Tanzania
alibainisha kuwa, watafitiwa walikuwa na mtazamo chanya kuhusu tabia ya ubadilishaji
msimbo. Anabainisha kuwa, 50% wanapendezwa na ubadilishaji msimbo na hujisikia
kawaida; 16% walidai kuwa hawafurahishwi na hali hii ya utumizi wa lugha. Kwa
upande mwingine 34% walidai kuwa mtu akibadilisha msimbo nao hubadilisha pia.
Kimsingi utafiti huu hauwezi kutoa jibu sahihi kuhusu mtazamo wa wasikiliaji kuhusu
ubadilishaji msimbo Bungeni katika muktadha wa Bunge la Tanzania. Hii ni kwa
sababu muktadha wa utumizi wa lugha vyuoni ni tofauti na ule wa Bungeni. Pili utafiti
huu unaonesha kuwa watafitiwa wanahusika katika uzungumzaji wa namna hii na
wanaelewa lugha zote husika yaani Kiswahili na Kiingereza. Hivyo basi kwa kuwa
walengwa wa mazungumzo na muktadha wa mazungumzo ni tofauti bado kuna
mwanya unaotakiwa kuzibwa.
Naye Kanyuma (2005) katika utafiti wake anabainisha kuwa, walimu na wanafunzi
wana mtazamo chanya kuhusu kaida ya ubadilishaji msimbo. Anabainisha kuwa 94%
ya walimu wanapendezwa na tabia ya ubadilishaji msimbo. Kwa upande wa wanafunzi
anadai kuwa 84% wanapendezwa na tabia hii ya uzungumzaji. Kimsingi kama ilivyo
39
katika utafiti wa Rajabu (keshatajwa), muktadha na wahusika wa mazungumzo ni
tofauti na ya utafiti huu.
2.8 Hitimisho
Sura hii imejikita katika upitiaji wa machapisho mbalimbali yanayohusu ubadilishaji
msimbo. Katika sura hii tumeanza kwa kuelezea maana ya ubadilishaji msimbo na
baadaye kuainisha aina zake na kiwango cha utokeaji wake katika matini kabla ya
kutofautisha ubadilishaji msimbo na ukopaji. Baada ya hapo machapisho kuhusu
sababu za wabunge kubadilisha msimbo yamepitiwa na baadaye ni machapisho kuhusu
uelewekaji wa maongezi yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Pia, machapisho
kuhusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini zenye kuhusisha ubadilishaji
msimbo yamepitiwa. Mwisho, tumepitia machapisho kuhusu mtazamo wa wasikilizaji
kuhusu ubadilishaji msimbo. Upitiaji wa machapisho unatupa usuli wa kuelezea mbinu
zilizotumika katika utafiti huu. Hivyo basi, sura ifuatayo inaelezea mbinu za utafiti.
40
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.0 Utangulizi
Sehemu hii inahusu mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data na usampulishaji wa
populesheni. Mambo muhimu yaliyobainishwa ni eneo la utafiti, populesheni lengwa,
sampuli na usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data na uchanganuzi wa data.
Katika mjadala aina ya data iliyokusanywa imeainishwa ikiwa ni pamoja na mbinu
zilizotumika kukusanya data.
3.1 Eneo la Utafiti
Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mwanza. Mkoa huu umeteuliwa kuwa eneo la
utafiti kwa kuzingatia vigezo vingi ambavyo ni pamoja na, mosi; jamii ya wakazi wake
imeundwa na watu wa sifa mbalimbali kielimu, kiuchumi (Wakulima, Wafugaji,
Wavuvi, Wafanyabiashara na hata Wachimbaji wadogo na wakubwa). Kwa mantiki hii,
data iliyopatikana imetoka katika matabaka mbalimbali. Pili, mtafiti ameishi na
kufanya kazi mkoa huu, hii imerahisisha ukusanyaji wa data kwani mtafiti kwa kiasi
fulani anaelewa jiografia ya mkoa pamoja na mila na desturi za watafitiwa. Wilaya za
Nyamagana na Magu ndizo zilizohusika katika utafiti huu. Wilaya ya Nyamagana ni
moja kati ya wilaya mbili zinazounda jiji la Mwanza na wakati Magu ipo nje ya jiji na
hivyo inawakilisha maeneo ya vijijini.
Katika wilaya ya Nyamagana mtafiti aliteua kata za Mkolani, Pamba na Igoma. Kigezo
cha uteuzi wa kata hizi ni kwamba katika kata ya Mkolani ndipo kuna Chuo Kikuu cha
Mt. Augustini hivyo mtafiti aliweza kupata watu wa kiwango cha elimu ya chuo na
41
chuo kikuu. Kata ya Pamba ni kata iliyo katikati ya jiji na hivyo inawakilisha maeneo
yenye msongamano wa watu wa aina na shughuli mbalimbali. Kata ya Igoma
inawakilisha maeneno ya pembezoni mwa jiji.
Kwa upande wa Wilaya ya Magu mtafiti aliteua kata tatu ambazo ni Lubugu, Ngasamo,
na Sukuma. Hata hivyo, mtafiti hakuwahoji watu katika eneo zima la kata husika bali
aliteua kinasibu baadhi ya vijiji. Vijiji vilivyoteuliwa ni Bubinza na Nsolla kutoka kata
ya Lubugu, Imalamate na Jiseka kutoka kata ya Ngasamo na Kitongo na Nyang’hanga
kutoka kata ya Sukuma. Hii ni kwa sababu kijiografia kata hizi zilionekana kuwa
kubwa na ingechukua muda mrefu na rasilimali kubwa kutafiti vijiji vyote vya kata
hizi.
3.2 Populesheni Lengwa ya Utafiti
Populesheni ni vitu au watu ambao kwao mtafiti anatarajia au amepata data ya utafiti
(Enon 199:13, Kanyuma 2005:63). Kwa mujibu wa Cooper (1989) na Vans (1990)
populesheni lengwa ya utafiti inahusisha jamii nzima, makundi ya watu, au vitu vingine
ambavyo kwavyo mtafiti amevihusisha kama chanzo cha data. Katika utafiti huu
populasheni imejumuisha watu kutoka matabaka mbalimbali, yaani wanaume,
wanawake, vijana, wazee, wasomi na wasio wasomi, wafanyakazi na wanafunzi, wa
vijijini na mjini, wakulima, wavuvi na wafanyabiashara.
42
3.3 Sampuli na Usampulishaji
3.3.1 Sampuli
Sampuli ni kundi dogo la watafitiwa kutoka kundi kubwa ambalo humpa mtafiti data
zinazomsaidia kutoa hitimisho (Enon 1998:13). Sampuli hupatikana kwa mchakato wa
usampulishaji.
3.3.2 Usampulishaji
Usampulishaji ni mchakato wa uteuzi wa watafitiwa kutoka katika populesheni lengwa
ya utafiti ili wawe sampuli ya utafiti (Kothari 1990). Kutoka katika jamii ya watu wengi
watu wachache wanaweza kuteuliwa ili kuwa sampuli ya utafiti. Data inayopatikana
kutoka katika sampuli hiyo inatakiwa kutoa majibu ambayo yangepatikana iwapo
populasheni nzima ingehusika. Hii ni mbinu ya kupunguza gharama, muda na nguvu.
3.3.2.1 Aina ya Usampulishaji
Aina ya usampulishaji iliyotumika katika utafiti huu ni usampulishaji nasibu tabakishi.
Hii ni aina ya usampulishaji ambayo inahusisha usampulishaji tabakishi na nasibu
(Kothari 2004:16). Kwa kutumia njia hii mtafiti amepanga populasheni katika makundi
madogo madogo yaani matabaka. Matabaka yaliyopatikana ni ya makundi ya wakazi
wa mjini na wale wa vijijini, wakulima, wafanyakazi, wasomi (elimu ya msingi,
sekondari na chuo/chuo kikuu), wasiojua kusoma wala kuandika, wafanyabiashara na
pia wanaume na wanawake. Hata hivyo, kutokana na aina na malengo ya utafiti huu,
kigezo cha kiwango cha elimu ndicho kimetiliwa mkazo katika uchanganuzi na ufasiri
43
wa data (itaainishwa katika sura ya nne)8. Baada ya kuainisha matabaka mtafiti
ametumia njia ya usampulishaji nasibu ili kupata idadi ya watafitiwa kutoka katika kila
tabaka. Hapa kila mtu katika tabaka husika alikuwa na nafasi sawa ya kujumuishwa.
Pia fursa na utayari wa mtafitiwa katika tabaka husika vilizingatiwa. Muainisho wa
sampuli ya utafiti huu umefupishwa katika majedwali yafuatayo:-
Jedwali la 1: Sampuli ya Utafiti kutoka katika Wilaya za Nyamagana na Magu
WILAYA
NYAMAGANA
MAGU
Jumla KIWANGO CHA
ELIMU
Me Ke Jumla Me Ke Jumla
Wasiojua Kusoma 13 16 29 41 57 98 127
Elimu ya Msingi 99 104 203 128 122 250 453
Elimu ya Sekondari 48 41 89 21 20 41 130
Chuo/Chuo Kikuu 31 25 56 06 03 09 65
Jumla 191 186 377 196 202 398 775
Jedwali hili linaonesha sampuli nzima ya utafiti kutoka katika wilaya za Nyamagana na
Magu ambayo ni watafitiwa 775 ambao ni; wanaume 387 (49.94%) na wanawake 388
(50.06%). Katika wilaya ya Nyamagana jumla ya watafitiwa ni 377 ambao ni wanaume
191 na wanawake 186. Kwa upande wa Magu jumla ya watafitiwa ni 398 ambao ni
wanaume 196 na wanawake 202.
8 Populesheni na sampuli ya utafiti inaoneshwa kwa kuzingatia kiwango cha elimu. Hata hivyo mtafiti
alihakikisha kuwa sampuli hiyo inajumuhisha watu wa tabaka mbalimbali yaani wakulima, wafugaji,
wafanyabiashara, wafanyakazi, wanafunzi/wanachuo, wakazi wa mjini na wakazi wa vijijini. Pia watu
wa rika na jinsia zote walijuishwa.
44
Jedwali la 2: Sampuli ya Utafiti kutoka Kata Tatu za Wilaya ya Nyamagana
KATA MKOLANI PAMBA IGOMA
Jumla
KIWANGO
CHA ELIMU
Me Ke Jumla Me Ke Jumla Me Ke Jumla
Wasiojua Kusoma 4 6 10 3 4 7 6 6 12 29
Elimu ya Msingi 31 34 65 31 37 68 37 33 70 203
Elimu ya
Sekondari
18 15 33 16 13 29 14 13 27 89
Chuo/Chuo Kikuu 19 17 36 7 4 11 5 4 09 56
Jumla 72 72 144 57 58 115 62 56 118 377
Jedwali hili linaonesha sampuli ya utafiti katika kata tatu za wilaya ya Nyamagana
ambazo ni Mkolani, Pamba na Igoma. Katika kata ya Mkolani jumla ya watafitiwa ni
144 ambao ni wanaume 72 na wanawake 72; kata ya Pamba ni watafitiwa 155 ambao ni
wanaume 57 na wanawake 58 na kata ya Igoma ni watafitiwa 118 ambao ni wanaume
62 na wanawake 56.
Jedwali la 3: Sampuli kutoka katika Kata tatu za Wilaya ya Magu
KATA LUBUGU NGASAMO SUKUMA
KIWANGO CHA
ELIMU
Me Ke Jumla Me Ke Jumla Me Ke Jumla
Wasiojua kusoma 14 18 32 12 21 33 15 18 33
Elimu ya Msingi 42 42 84 43 39 82 43 41 84
Elimu ya
Sekondari
09 08 17 05 07 12 07 05 10
Chuo/Chuo kikuu 03 01 04 02 01 03 01 01 03
Jumla 68 69 137 62 68 130 66 65 131
Jedwali hili linaonesha sampuli ya utafiti kutoka kata tatu za Wilaya ya Magu.
Muanisho wa sampuli ni; kata ya Lubugu 137 (wanaume 68 na wanawake 69),
Ngasamo 130 (wanaume 62 na wanawake 68) na Sukuma 131 (wanaume 66 na
wanawake 65).
45
Jedwali la 4: Sampuli ya Utafiti
KIWANGO CHA
ELIMU
IDADI YA WATAFITIWA
Me
%
Ke
%
Jum
la
%
Wasiojua kusoma na
kuandika
54
42.52
73
57.48
127
16.39
Elimu ya msingi 227 50.11 226 49.89 453 58.45
Sekondari 69 53.08 61 46.92 130 16.77
Chuo/Chuo kikuu 37 56.92 28 43.08 65 8.39
Jumla 387 49.94 388 50.06 775 100
Jedwali hili linaonesha sampuli nzima ya utafiti ambayo ni jumla ya watafitiwa 775.
Kwa kuzingatia kigezo cha elimu sampuli ya utafiti huu ina watafitiwa wasiojua
kusoma na kuandika 127 (16.39%) ambao ni wanaume 54 (42.52%) na wanawake 73
(57.48%); elimu ya msingi 453 (58.45%) ambao ni wanaume 227 (50.11%) na
wanawake 226 (49.89%); sekondari 130 (16.77%) ambao ni wanaume 69 (53.08%) na
wanawake 61 (46.92%); na chuo/chuo kikuu 65 (8.39%) ambao ni wanaume 37
(56.92%) na wanawake 28 (43.08%).
3.4 Mbinu za Ukusanyaji wa Data
Wataalamu mbalimbali akiwemo Cohen (2000) wanathibitisha kuwa, katika ukusanyaji
wa data za utafiti hakuna mbinu moja inayojitosheleza na hivyo kupendekeza
matumizi ya mbinu zaidi ya moja ili kupata taarifa sahihi katika sayansi ya jamii. Kwa
mantiki hii, utafiti huu umetumia mbinu kuu tatu za ukusanyaji data ambazo ni usaili,
hojaji na mijadala ya vikundi lengani. Sababu za uteuzi wa mbinu hizi zimeelezwa
katika 3.4.1, 3.4.2 na 3.4.3.
46
3.4.1 Hojaji
Hii ni mbinu ya kutumia orodha ya maswali (yaliyoandikwa/kuchapwa) inayotakiwa
kujibiwa na kuelezewa na wanaotafitiwa. Mbinu hii ambayo inatumiwa sana na watafiti
wengi imetumika kwa sababu inaokoa muda na inawezesha kuwatafiti watu wengi kwa
wakati mmoja. Katika hojaji, maswali mengi yalikuwa funge ambapo watafitiwa
walitakiwa kuweka alama ya vema au kujaza sehemu zilizo wazi. Kwa kusaidiwa na
baadhi ya wanafunzi wa sekondari zilizomo katika maeneo husika watafitiwa kutoka
matabaka mbalimbali walipewa hojaji. Waliokuwa tayari walizijaza na kumrejeshea
mtafiti papo kwa papo. Kwa waliochelewa kukamilisha, mtafiti alizifuata baadae au
siku nyingine kulingana na makubaliano na mtafitiwa. Kwa zile zilizosambazwa na
wanafunzi zilirejeshwa kwa kiongozi wao aliyehakikisha zinamfikia mtafiti haraka
iwezekanavyo. Kwa kutumia njia hii hojaji 300 zilisambazwa na kila mtu aliyekuwa
tayari alipewa hojaji moja. Jumla ya hojaji 277 sawa na 92.33% zilirejeshwa na hivyo
kuwezesha kuwatafiti watu 277 ambao ni watu 194 wa elimu ya msingi, sekondari 55
na chuo/chuo kikuu 28. Katika utafiti huu mbinu hii imekuwa ya muhimu na msingi
kwa sababu imesaidia kuwahoji watafitiwa wengi kwa muda mfupi.
3.4.2 Usaili
Haya ni majibizano ya ana kwa ana (au simu, barua pepe n.k), kati ya watu wawili au
zaidi kwa lengo la kukusanya data au maoni kuhusu suala la kiutafiti (Kothari
2004:97). Katika utafiti huu watafitiwa waliulizwa maswali ya ana kwa ana ambayo
mtafiti aliyaandaa awali ili kuhakikisha kuwa mtu anatoa hoja na maoni yaliyo ndani ya
malengo ya utafiti. Mahojiano yalianza kwa mtafiti kwanza, kumsomea au kuwasomea
watafitiwa matini kutoka kumbukumbu za Bunge zinazoonesha jinsi Wabunge
47
wanavyobadilisha Kiswahili na Kiingereza. Baadaye alielezea mada na malengo ya
utafiti na mwisho watafitiwa waliombwa kutoa hoja zao kwa kuzingatia maswali
yaliyoulizwa. Wakati wa mahojiano mtafiti alinakili majibu katika shajara na wakati
mwingine kinasa sauti kilitumika kurekodi (japo mara chache kwani watu wengi
hawakuwa tayari kurekodiwa) na baadaye majibu yaliwekwa katika maandishi.
Kutokana na utumizi wa mbinu hii mtafiti ameweza kuwahoji watu 227 ambao
muainisho wao ni wasiojua kusoma wala kuandika 57, elimu ya msingi 121, sekondari
33 na chuo/chuo kikuu 16. Mtafiti alihakikisha kuwa kila tabaka la watu linatoa maoni
na mchango wao kuhusu mada lengwa. Mbinu hii imesaidia sana hasa kwa watafitiwa
wasiojua kusoma na kuandika ambao hawangeweza kusoma na kujibu hojaji. Pia,
ilimpa nafasi mtafiti kufafanua maswali yaliyoonekana kuleta utata na wakati
mwingine kutoa maelekezo zaidi kwa watafitiwa. Mbinu hii pia imeepusha majibu ya
sijui au sina uhakika yaliyojitokeza katika hojaji.
3.4.3 Mijadala ya Vikundi Lengani
Vikundi lengani kwa kawaida hujumuisha kati ya watu watano na kumi na wawili
(Grbich 1999) kama alivyonukuliwa na Mutembei (2001). Jumla ya makundi 30 yenye
watu kati ya saba na kumi na mmoja yalitafitiwa ambapo makundi 16 yalitoka wilaya
ya Magu na 14 yalitoka wilaya ya Nyamagana. Mtafiti alihakikisha kuwa watu wa kila
tabaka wanahusika katika mjadala. Ilipojitokeza kuwa watu kutoka tabaka fulani
hawajapatikana katika eneo husika, mtafiti alihakikisha anatafuta watu hao katika kundi
linalofuata. Mathalani, ilikuwa kazi ngumu kuwapata watu wenye kiwango cha elimu
ya chuo au chuo kikuu katika maeneo ya vijini. Hawa mtafiti aliwapata maeneno ya
48
mjini hasa mitaa ya karibu na chuo cha Mt. Augustini au walimu wa shule za sekondari.
Kwa kutumia mbinu hii mtafiti ameweza kuwatafiti watu 271 kutoka matabaka
mbalimbali ambao ni watu 70 wasiojua kusoma wala kuandika, 138 wa kiwango cha
elimu ya msingi, 42 sekondari na 21 chuo/chuo kikuu. Kabla ya kuanza kwa mjadala
mtafiti alijitambulisha na watafitiwa pia. Katika utangulizi mtafiti alielezea mada na
malengo ya utafiti. Pia mtafiti aliwasomea baadhi ya matini za kutoka kumbukumbu za
Bunge ili kuwajengea watafitiwa picha halisi ya utumizi wa lugha Bungeni. Kwa
upande wa watafitiwa walijitambulisha kwa kutaja jina (haikuwa lazima), umri,
kiwango cha elimu, kazi na mahali wanakoishi. Baada ya hapo mjadala uliodumu kwa
takribani kati ya dakika arobaini na tano na saa moja na nusu uliendeshwa ukijikita
katika maswali yaliyoulizwa na mtafiti ambayo yaliandaliwa awali. Ili kurahisisha
utunzaji wa kumbukumbu za majadiliano mbinu ya kurekodi (kutumia kinasa sauti)
ilitumika wakati wa mjadala japo si mara zote kwani watafitiwa wengine hawakuwa
tayari kurekodiwa.
3.5 Uchanganuzi wa Data
Utafiti huu umetumia mkabala wa utafiti usio wa kiidadi. Kwa mujibu wa Enon
(1998:24) huu ni mkabala wa utafiti ambao data zinazopatikana hazielezewi au
kuwakilishwa kitakwimu. Hii haimaanishi kuwa takwimu hazihusiki bali maelezo
ndiyo hutiliwa mkazo. Hata hivyo katika kuchanganua na kusasanyua data njia za
kitakwimu kama vile ujedwalishaji na utumizi wa asilimia zimetumika. Majedwali
yametumika hasa katika kuainisha majibu ya watafitiwa kiidadi na kwa kuzingatia
kiwango cha elimu. Utumizi wa asilimia umetumika kubainisha kiwango cha
kitakwimu cha waliotoa jibu husika ili kutoa ulinganifu wa data husika. Kwa kuzingatia
49
jedwali husika na asilimia za data husika imewezesha kutoa uchanganuzi wa kimaelezo
unaothibitishwa na data katika idadi na asilimia ya data husika.
3.6 Hitimisho
Sura hii imebainisha na kujadili mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Mambo
muhimu yaliyobainishwa ni eneo la utafiti, populasheni lengwa, sampuli na
usampulishaji, mbinu za ukusanyaji wa data na uchanganuzi wa data. Katika mjadala
aina ya data iliyokusanywa imeainishwa ikiwa ni pamoja na njia zilizotumika
kukusanya data. Sura inayofuata inahusu uwasilishaji na uchambuzi wa matokeo ya
utafiti.
50
SURA YA NNE
UWASILISHAJI, UCHANGANUZI NA UFASIRI WA DATA
4.0 Utangulizi
Sura hii inahusu uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data zilizokusanywa kutoka
uwandani. Kama tulivyoona katika sura ya tatu (kipengele cha 3.4) data zilikusanywa
kwa njia kuu tatu ambazo ni hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani. Uchanganuzi
wa data umefanywa kwa maelezo isipokuwa data zilizohitaji hesabu ndogondogo kama
vile kukokotoa asilimia, kikokotozi kilitumika. Majedwali na maelezo kuntu
vimetumika kuwasilisha matokeo ya utafiti.
Sura hii ina sehemu kuu tano. Sehemu ya kwanza ni mawasilisho kuhusu uelewekaji
wa mijadala ya wabunge kwa wasikilizaji yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo.
Sehemu ya pili inahusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa mijadala ya Bunge
yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Sehemu ya tatu ni mawasilisho ya mjadala
kuhusu mtazamo wa wasikilizaji kuhusu tabia ya wabunge ya ubadilishaji msimbo.
Sehemu ya nne, ni mjadala kuhusu kama ubadilishaji msimbo Bungeni unasababisha
wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge. Sehemu ya tano, ni mjadala wa maoni ya
wasikilizaji kuhusu mapendekezo ya kupunguza athari hasi za ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza Bungeni na lugha gani itumike kama lugha rasmi ya shughuli
za Bunge. Hii imegawanyika katika vijisehemu vidogo ambavyo ni lugha inayofaa
kuendesha shughuli za Bunge na mbinu za kuifanya lugha hiyo kutekeleza dhima hiyo.
51
4.1 Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge
Sehemu hii inaonesha kiwango cha kueleweka kwa mijadala ya Bunge yenye kuhusisha
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Kama tulivyoona katika sura ya pili
(kipengele 2.5), dhima kuu ya lugha yoyote ile ni kuwezesha mawasiliano miongoni
mwa wanajamii. Jambo muhimu la kuzingatia ni kuwa, wabunge wanapokuwa Bungeni
majadiliano yao yanavuka mipaka ya jengo kwa kutangazwa na vyombo vya habari na
hivyo kusikika kwa watu wengine wasiokuwepo Bungeni. Kwa mantiki hii, walengwa
wa majadiliano ya Bungeni sio tu wabunge bali pia ni wale wote wanaofuatilia
majadiliano hayo popote pale walipo. Hivyo basi, kwa kuongozwa na dhana hii tulitaka
kujua ni kwa kiwango gani wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu wanaelewa
mijadala ya Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza.
Kwa kutumia mbinu zilizoainishwa katika 3.4 tumeweza kupata data inayoonesha
viwango vya wasikilizaji wa viwango mbalimbali vya elimu kuelewa mijadala
inayoendeshwa Bungeni. Ili kujiridhisha na kuhakikisha kuwa majibu yanayopatikana
yanaaminika, tulijumuisha katika hojaji matini kutoka taarifa rasmi za Bunge zenye
mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza na kuwataka watafitiwa kueleza
wameelewa nini. Pia katika usaili na mijadala tuliwasomea matini hizo na kuwataka
kueleza walichokielewa kwa ufupi. Hili lilisaidia sana kwani iliepusha udanganyifu na
iligeuza zoezi zima kuwa la kivitendo. Matokeo kuhusu kiwango cha wasikilizaji
kuelewa mijadala ya Bungeni yameainishwa katika jedwali lifuatalo:-
52
Jedwali la 5: Kueleweka kwa Mijadala ya Bunge
KIWANGO
CHA ELIMU
Jum
la
%
Wan
aoel
ewa
%
Baa
dh
i y
a S
ente
nsi
%
Baa
dh
i y
a M
anen
o
%
Was
ioel
ewa
%
Wasiojua
Kusoma
127
16.39 00 00 15 11.81 35 27.56 77 60.63
Elimu ya Msingi 453
58.45 03 0.66 53 11.70 167 36.87 230 50.77
Sekondari 130 16.77 24 18.46 32 24.62 60 46.15 14 10.77
Chuo/Chuo
Kikuu
65 8.39 42 64.62 13 20
08
12.31
02 3.08
Jumla 775 100 69 8.9 113 14.58 270 34.84 323 41.68
Jedwali la 5 linaonesha viwango vya uelewekaji wa mijadala ya Bunge yenye
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Data inaonesha kuwa, wasikilizaji 77
(60.63%) wasiojua kusoma na kuandika, 230 (50.77%) wa kiwango cha elimu ya
msingi, 14 (10.77%) wa kiwango cha sekondari na 02 (3.08%) wa kiwango cha
chuo/chuo kikuu hawaelewi mijadala ya Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza. Kwa upande wa wasikilizaji wanaoelewa mijadala ni 00
(00%) wasiojua kusoma wala kuandika, 03 (0.66%) elimu ya msingi, 24 (18.46%)
sekondari na 42 (64.62%) chuo/chuo kikuu.
Wasikilizaji wengi wa kiwango cha elimu ya sekondari wakifuatiwa na wa elimu ya
msingi wanaonekana kuelewa baadhi ya maneno au baadhi ya sentensi. Mathalani,
wasikiliizaji 60 (46.15%) wa kiwango cha elimu ya sekondari wanaelewa baadhi ya
maneno, huku 32 (24.62%) wakielewa baadhi ya sentensi. Kwa upande wa wasikilizaji
wa kiwango cha elimu ya msingi data inaonesha kuwa 167 (36.87%) wanaelewa baadhi
ya maneno huku 53 (11.70%) wakielewa baadhi ya sentensi. Katika usaili na mijadala
53
ya vikundi lengani pamoja na mambo mengine tulilenga kufahamu wanaoelewa baadhi
ya maneno au sentensi kama ni ya Kiswahili, Kiingereza au lugha zote mbili. Jumla ya
watafitiwa 89 waliulizwa swali hili na kati ya hao 14 (16.18%) walidai kuwa
wanaelewa maneno ya lugha zote mbili yaani Kiswahili na Kiingereza, huku 75
(84.27%) wakidai kuwa wanaelewa maneno ya Kiswahili tu. Kutokana na hali hii ni
idadi ndogo tu (16.18%) wanaoelewa sentensi au maneno ya Kiingereza. Kuelewa
baadhi ya maneno tu katika sentensi kunaweza kusababisha msikilizaji asifahamu
kinachozungumzwa. Hebu tuangalie mfano ufuatao:-
Mfano wa 4 (a)
….… nianze kwa kuelezea umuhimu wa infrastructure katika maendeleo ya
nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa sana, bahati yetu ni ambako
Mungu aliamua nchi hii iwe hapa iliko leo na maana yake ni geographical
position ya nchi yetu. Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie
advantage ya jiografia yetu kwa sababu engine ya maendeleo ni infrastructure,
mimi sijui nchi yoyote iliyoendelea duniani bila kuwa na infrastructure ……..
(Matini kutoka taarifa rasmi za Bunge 12 Julai, 2007:30).
Tafsiri;
…….. nianze kwa kuelezea umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya
nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa sana, bahati yetu ni ambako
Mungu alimua iwe hapa ilipo na maana yake ni eneo la kijiografia la nchi yetu.
Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie faida ya jiografia yetu kwa
sababu injini ya maendeleo ni miundombinu, mimi sijui nchi yoyote
iliyoendelea duniani bila kuwa na miundombinu…………
54
Iwapo msikilizaji hataelewa maana ya maneno infrastructure, geographical position,
advantage na engine itakuwa vigumu kuelewa matini nzima. Pamoja na hayo, hata
asipoelewa neno moja tu “infrastructure” bado itakuwa kazi ngumu kuelewa matini
nzima kwani hili ndilo neno la msingi katika matini hii na limerudiwarudiwa. Hii ndiyo
hali tuliyobaini kuwa inawakumba wasikilizaji. Mathalani, wapo waliotumia neno
“barabara” kama kibadala cha neno “infrastructure”. Kimsingi kibadala cha neno hili
ni “miundo mbinu” na japo barabara ni mojawapo ya miundombinu lakini ipo
miundombinu nyingine kama vile reli, viwanja vya ndege, bandari, minara ya simu na
kadhalika.
Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa wasikilizaji wa kiwango cha elimu ya
chuo au chuo kikuu 42 (64.62%) wanaelewa mijadala yenye kuhusisha ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza. Hii ni kwa sababu Kiingereza ndiyo lugha inayotumika
kufundishia kuanzia ngazi ya sekondari hadi chuo kikuu. Hata hivyo, pamoja na kuwa
wanachuo wanasoma kwa Kiingereza bado umahiri wao wa lugha hii si wa kiwango
cha kuridhisha. Hili lilijidihirisha tulipowataka kuelezea kwa ufupi wameelewa nini
kutoka matini zilizokuwa na mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza. Baadhi yao
walitoa maana zenye uvulivuli, utata na wengine kupotosha maana kabisa.
Kimsingi, data hii inaonesha kuwa wasikilizaji (hasa wa kiwango cha elimu ya chini)
hawaelewi mijadala ya Bungeni inayoendeshwa kwa kubadilisha Kiswahili na
Kiingereza. Kwa ujumla data inaonesha kuwa, 8.9% tu ya wasikilizaji wanaelewa
mijadala hii huku 41.68% wakiwa hawaelewi, 14.58% wakielewa baadhi ya sentensi
55
wakati 34.84% wakielewa baadhi ya maneno. Majumuhisho ya data hii yanaonesha
kuwa, kiwango cha uelewaji wa mijadala ya Bungeni yenye kuhusisha ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza kinapanda kadri ya kiwango cha elimu kinavyopanda na
kinyume chake pia.
Matokeo ya utafiti huu yanapingana na tafiti za Adendorff (1996) na Chung (2000)
zinazobainisha kuwa, ubadilishaji msimbo unawezesha mawasiliano miongoni mwa
watu wenye umahiri tofauti wa lugha. Pia, matokeo yanapingana na hoja ya Tay (1989)
na Myers-Scotton (1995) wanaodai kuwa, ubadilishaji msimbo hutumika kama mbinu
ya kimawasiliano miongoni mwa wazungumzaji kwa kuzingatia lengo la mzungumzaji.
Kwa upande mwingine matokeo ya utafiti huu yanaungana na hoja ya MacWilliam na
Chuwa (1990) inayodai kuwa, maneno ya lugha ya Kiingereza yanayotumiwa katika
sentensi za Kiswahili siyo maneno rahisi yanayoweza kubuniwa na mwenye kiwango
kidogo cha Kiingereza. Matokeo yake ni sentensi kutoeleweka kwa msikilizaji na hivyo
kumnyima fursa ya kufuatilia majadiliano ya wabunge. Hata hivyo, utafiti huu
umesogea mbele zaidi kwa kuainisha uelewekaji wa mijadala ya Bunge yenye
kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza kwa kuzingatia matabaka
mbalimbali ya viwango vya elimu.
4.2 Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala.
Kama ilivyoelezwa awali, dhima kuu ya lugha ni mawasiliano. Kwa kuwa ilibainika
kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji hawaelewi mijadala ya Bunge yenye kuhusisha
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza (rejea 4.1) na hivyo kuwa na vizuizi vya
56
mawasiliano, tulitaka kujua mbinu wazitumiazo wasikilizaji hao kufahamu
yaliyojadiliwa katika vikao vya Bunge. Katika kipengele hiki tuliongozwa na dhana
kuwa, mbunge anachangia hoja ili aweze kueleweka si na wabunge wenzake tu bali pia
na wananchi na hivyo wasikilizaji huwa na haki na shauku ya kumsikia na kumuelewa.
Majibu ya swali hili yamefupishwa katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali la 6: Mbinu Zitumikazo Kuelewa Mijadala.
KIWANGO
CHA ELEIMU
Jum
la
%
Kam
usi
%
Ku
uli
za
kw
a W
atu
%
Vy
om
bo
vy
a
Hab
ari
%
Was
iofu
atil
ia
%
Wasiojua
Kusoma
127
16.39
00
00 07 5.51 12 9.45 108 85.04
Elimu ya
Msingi
453 58.45 13 02.87 33 7.28 86 18.98 321 70.86
Sekondari 130 16.77 08 6.15 38 29.23 61 46.92 23 17.16
Chuo/Chuo
Kikuu
65
8.39 05
7.69
20
30.77
33
50.77
07
10.77
Jumla 775 100 26 0.03 98 12.65 192 24.77 459 59.23
Data inaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wasikilizaji wasiojua kusoma na kuandika na
wale wa kiwango cha elimu ya msingi hawatafuti mbinu mbadala za kuwafanya
waelewe mijadala ambayo hawakuielewa kutokana na kiwango cha juu cha ubadilishaji
wa Kiswahili na Kiingereza. Data inadokeza kuwa, wasikilizaji wasiofuatilia au
wasiotafuta mbinu mbadala za kuelewa mijadala ya Bunge ni; wasiojua kusoma na
kuandika 108 (85.04%), kiwango cha elimu ya msingi 321 (70.86%), sekondari 23
(17.69%) na chuo au chuo kikuu 07 (10.77%). Hii ni sawa na 59.23% ya watafitiwa
wote. Data hii inapingana na Mekacha (2000:36) anayesisitiza kuwa, katika
mawasiliano msikilizaji au msomaji huwa anafanya jitihada ya kuelewa
kinachokusudiwa.
57
Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji wasomi
(wa viwango vya sekondari na vyuo) hupata maana ya mijadala ya Bunge yenye
kuhusisha ubadilishaji msimbo kupitia vyombo vya habari na au kuulizia kwa wenzao.
Mathalani, data inaonesha kuwa, 29.23% ya wasikilizaji wa viwanga vya sekondari
huulizia kwa wenzao huku 46.92% wakifuatilia kwenye vyombo vya habari. Kwa
upande wa wasikilizaji wa elimu ya vyuo na vyuo vikuu ni 30.77% wanaouliza kwa
wenzao na 50.77% wanaofuatilia kwenye vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu
kwanza, asilimia kubwa ya wasomi wanaishi mijini ambako vyombo vya habari kama
vile magazeti, runinga, redio na mitandao hupatikana kwa uhakika. Kadri ya kiwango
cha elimu kinavyopanda, uwezekano wa kutumia vyombo vya habari unaongezeka pia.
Sababu za msingi ni kuwa, wasomi wa ngazi ya juu ndio huishi mijini na pia wana
uwezo wa kununua magazeti, kutumia mtandao na hata kumiliki redio na runinga. Pia
sio rahisi kupata vyombo vya habari kama vile magazeti, runinga na mitandao katika
maeneo ya vijijini ambapo asilimia kubwa ya watanzania hasa wa viwango vya chini
vya elimu huishi. Redio ndizo hupatikana katika maeneo mengi ya vijijini lakini
kutokana na ukosefu wa umeme na umaskini, watu walio wengi hawazisikilizi mara
kwa mara na kwa wale wanaozisikiliza (hasa vijana) hutafuta vituo vinavyopiga
muziki.
Pili, wasomi wanaweza kuulizana wao kwa wao kwani kwa kiasi fulani wana uelewa
wa lugha ya Kiingereza. Hii inadhihirishwa na data kwani kadri kiwango cha elimu
kinavyoongezeka, asilimia ya wanaouliza kwa wenzao inazidi kupanda. Mathalani, data
inaonesha kuwa katika sampuli ya wasiojua kusoma na kuandika wanaotumia mbinu hii
58
ni 07 (5.51%), elimu ya msingi ni 33 (7.28%), sekondari ni 38 (29.23%), na wasikilizaji
wa kiwango cha chuo/chuo kikuu ni 20 (30.77%). Jambo muhimu la kuzingatia katika
hoja hii ni kwamba, wasomi na wenye kujua Kiingereza ni takribani asilimia tano
(Msanjila 2004:45 akimnukuu Schmied 1989). Kwa mantiki hii Watanzania
wanaoelewa mijadala yenye kuhusiha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni
takribani asilimia tano9. Pia kama anavyodai Rubanza (2005:4) ndani ya lugha kuna
vionjo ambavyo havihamishiki kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Hata kama
tafsiri zitafanyika lazima maudhui ya yale yazungumzwayo katika lugha moja
hayajipambanui kikamilifu katika lugha nyingine. Kwa hoja hii, (kama tutakavyoona
katika 4.5.1) ili kuwezesha usemezano uliosawa kati ya Bunge na wadau wake ni vema
lugha ya Kiswahili ikatumika wakati wote hasa pale ambapo hakuna hitaji la
kubadilisha lugha.
Kwa upande mwingine, data inaonesha kuwa watanzania hawana tabia na hulka ya
kurejea vitabu maalumu kama kamusi ili kutafuta kuelewa jambo fulani. Data
inaonesha kuwa, watafitiwa 13 (2.87%) wa kiwango cha elimu ya msingi, 8 (6.15%)
sekondari na 5 (7.69%) wa chuo/chuo kikuu ikiwa ni 0.03% ya watafitiwa ndio hutumia
kamusi kuelewa maneno ambayo hayakueleweka. Jambo hili linadhihirisha kuwa sio tu
kuwa watanzania walio wengi hawana kamusi bali pia na wale wenye nazo
hawazitumii kutatua matatizo ya kiisimu kama vile kutafuta maana za maneno. Pia,
katika ukusanyaji wa data neno “kamusi’ lilionekana kuwa geni kwa watafitiwa wa
kiwango cha elimu ya msingi na wale wasiojua kusoma na kuandika na baadhi ya
9 Kwa mujibu wa data ya utafiti huu (rejea 4.1) wanaoelewa mijadala yenye kuhusisha ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza ni 8.9% ya watafitiwa wote.
59
watafitiwa wa sekondari. Hii inadhihirisha kuwa, shule nyingi hazina maktaba wala
vitabu muhimu vya rejea kwa wanafunzi ikiwemo kamusi.
Kimsingi katika kipengele hiki tulilenga kubainisha kama kuna mbinu mbadala
zitumiwazo na wasikilizaji kupunguza vikwazo vya kimawasiliano vinavyosababishwa
na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Data inabainisha wazi kuwa, asilimia
kubwa ya watanzania wa viwango vya chini vya elimu hawana mbinu mbadala na
hivyo hawapati ujumbe kama ulivyokusudiwa na mzungumzaji yaani mbunge.
Mathalani, data inaonesha kuwa wasikilizaji 108 (85.04%) wasiojua kusoma wala
kuandika, na 321 (70.86%) wa kiwango cha elimu ya msingi hawana mbinu mbadala za
kuelewa mijadala inayohusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Ikumbukwe
kuwa, kitakwimu watanzania wenye kiwango cha elimu ya msingi/kati na wale
wasiojua kusoma na kuandika ni zaidi ya 85% ya populesheni nzima ya watanzania.
Kwa mantiki hii, zaidi ya 85% ya watanzania hawaelewi mijadala ya Bungeni yenye
kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza na mbaya zaidi hawana mbinu
mbadala za kuwafanya waelewe mijadala hii. Kiisimu hii ni kinyume cha dhima kuu ya
lugha kwani maongezi yoyote lazima yafikishe ujumbe kwa mlengwa wa mawasiliano.
4.3 Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Mtazamo wa Wasikilizaji
Kama ilivyoelezwa katika 2.7 katika jamiilugha yoyote watu wanakuwa na mitazamo
tofauti kuhusu tabia ya ubadilishaji msimbo pamoja na kuwa ni sifa mojawapo ya
jamiilugha ulumbi. Wapo wanaoichukulia kama mbinu ya kimawasiliano huku wengine
wakiichukulia kama uzungumzaji usio na hadhi wala staha au ukosefu wa umahiri wa
lugha husika. Kwa mantiki hii, kuna kambi mbili kuhusu hili. Kambi ya kwanza
60
inayochukulia ubadilishaji msimbo kama mbinu ya kuwezesha mawasiliano ina
mtazamo chanya huku kambi ya pili inayochukulia ubadilishaji msimbo kama ukosefu
wa umahiri wa lugha husika ina mtazamo hasi.
Kutokana na mjadala huu tumeonelea ni vema kubainisha mtazamo wa wasikilizaji
kuhusu tabia ya wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Hivyo basi, watafitiwa
waliulizwa kama hawafurahishwi, hawajali, wanajisikia kawaida au wanapendezwa na
namna hii ya uzungumzaji wa wabunge. Majibu ya maswali hayo yamefupishwa katika
jedwali lifuatalo ambapo muainisho wake umezingatia viwango vya elimu.
Jedwali la 7: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza: Mtazamo wa Wasikilizaji
KIWANGO
CHA ELIMU
JUM
LA
%
Was
iofu
rah
i-
shw
a
%
Was
ioja
li
%
Kaw
aid
a
%
Wan
aop
end
e-
zwa
%
Wasiojua
Kusoma
127 16.39 112 88.19 09 07.09 02 1.57 4 3.15
Elimu ya Msingi 453 58.45 394 86.98 19 4.19 18 3.97 22 4.86
Sekondari 130 16.77 90 69.23 4 3.08 25 19.23 11 8.46
Chuo/Chuo
Kikuu
65
8.39 37
56.92
01
1.54
20
30.77
07
10.77
Jumla 775 100 633 81.68 33 4.26 65 8.39 44 5.68
Jedwali la 7 hapo juu linaonesha kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali
ya wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Kwa maneno mengine tunaweza
kusema kuwa, wana mtazamo hasi kuhusu namna hii ya ubadilishaji msimbo. Data
inaonesha kuwa, wasikilizaji 112 (88.19%) wasiojua kusoma na kuandika, 394
(86.98%) wenye elimu ya msingi, 90 (69.23%) sekondari na 37 (56.92%) wa kiwango
61
cha chuo/chuo kikuu hawafurahishwi na ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza
Bungeni.
Hata hivyo, tofauti na wanaisimu kama vile Bloomfield 1927; Weinreich 1953;1968 na
Becker 1997 ambao wanauchukulia ubadilishaji msimbo kama ukosefu wa umahiri wa
mzungumzaji wa lugha husika na hivyo wana mtazamo hasi, watafitiwa wana mtazamo
hasi kwa sababu zilizoainishwa katika 2.5. Miongoni mwa sababu hizi ni pamoja na:-
a) Wasikilizaji hawaelewi mijadala na hivyo kutopata ujumbe uliokusudiwa
b) Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni kutoithamini lugha ya taifa yaani
Kiswahili na utamaduni wake
c) Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza ni kuwatenga wasikilizaji wasioelewa
mojawapo ya lugha hizo.
Data inaonesha kuwa, idadi ya wasikilizaji wasiofurahishwa na ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza inapungua kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka na
kinyume chake kwa wale wanaopendezwa. Pia idadi na kiwango cha wasiojali
kinapungua kadri ya kiwango cha elimu kinavyoongezeka huku wanaojisikia kawaida
idadi yao ikiongezeka kadri ya kiwango cha elimu kinavyoongezeka. Data hii
inadokeza jambo muhimu kuwa, kuna sababu tofauti tofauti zinazofanya watu wawe na
mtazamo hasi. Tunaweza kusema kuwa, idadi inakuwa kubwa kwa wale wa viwango
vya chini vya elimu kwa sababu pamoja na sababu walizonazo wale wa viwango vya
juu vya elimu, inaongezeka sababu ya kutoelewa Kiingereza, huku wale wa viwango
vya juu vya elimu wakiwa na sababu za kukithamini Kiswahili na utamaduni wake,
kuiheshimu hadhi ya Bunge na kadhalika.
62
4.4 Ufuatiliaji wa Mijadala ya Bunge.
Kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya wasikilizaji wana mtazamo hasi
kuhusu wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza, tulitaka kujua kama hali hii
inaweza kusababisha wasikilizaji waamue kutofuatilia mijadala ya Bunge inayorushwa
kupitia vyombo vya habari kama vile redio na runinga. Kwa mujibu wa Bell (1984)
mtazamo wa wasikilizaji kuhusu namna ya uzungumzaji wa mzungumzaji ndio
hutawala uteuzi wa jinsi ya kuzungumza. Kwa mantiki hii, iwapo mzungumzaji atateua
namna fulani ya uzungumzaji ambayo kwayo wasikilizaji wake wana mtazamo hasi,
basi hawatamsikiliza na watakuwa na mtazamo hasi kwa huyo mzungumzaji. Kwa
kuongozwa na hoja hii, tuliwahoji wasikilizaji ili kujua kama ubadilishaji msimbo
unasababisha wasifuatilie mijadala ya Bunge. Majibu ya swali hili yamefupishwa
katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali la 8: Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Unasababisha Wasikilizaji
Wasifuatilie Mijadala ya Bunge?
KIWANGO
CHA ELIMU
Jum
la
% Nd
iyo
%
Kw
a K
iasi
Fu
lan
i
%
Hap
ana
%
Wasiojua Kusoma 127 16.39 28 22.05 35 27.56
64
50.39
Elimu ya Msingi 453 58.45 91 20.09 104 22.96 258 56.95
Sekondari 130 16.77 07 5.38 31 23.85 92 70.77
Chuo/Chuo Kikuu 65 8.39 01 1.54 08 12.31 56 86.15
Jumla 775 100 127 16.39 178 22.97 470 60.65
Data inaonesha kuwa, ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza una asilimia ndogo
(16.39%) ya kusababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge. Mathalani,
wasikilizaji 28 (22.05%) wasiojua kusoma na kuandika, 91 (20.09%) elimu ya msingi,
63
07 (5.38%) sekondari na 01 (1.54%) chuo/chuo kikuu, wote walidai kuwa ubadilishaji
wa Kiswahili na Kiingereza hausababishi washindwe kufuatilia mijadala ya Bunge.
Wakati huo, watafitiwa 178 (22.97%) walidai kuwa kwa kiasi fulani unasababisha
wasifuatilie mijadala ya Bunge. Kwa upande mwingine, wasikilizaji 470 (60.65%)
walidai kuwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza hauwasababishii waamue
kutofuatilia mijadala ya Bunge. Mathalani, wasikilizaji 64 (50.59%) wasiojua kusoma
na kuandika, 258 (56.95%) elimu ya msingi, 92 (70.77%) sekondari na 56 (86.15)
chuo/chuo kikuu walisema kuwa ubadilishaji msimbo hausababishi waache kufuatilia
mijadala ya Bunge.
Pia data inaonesha kuwa, kiwango cha kufuatilia mijadala ya Bunge kinapanda kadri
kiwango cha elimu cha wasikilizaji kinavyopanda. Kama ilivyoainishwa katika 4.2 hii
ni kwa sababu wasomi ndio wako mijini na wana uwezo wa kupata vyombo vya habari
kama vile redio, rununga, magazeti na mtandao.
Kimsingi, data hii kwa ujumla inapingana na mawazo ya Bell (keshatajwa) kwani kama
tulivyoona katika kipengele 4.3 wasikilizaji wana mtazamo hasi kuhusu hali ya
wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza lakini bado wanaweza kufuatilia
mijadala yenye kuhusisha uzungumzaji wa namna hii. Jambo hili linadhihirisha
umuhimu wa Bunge kwa wasikilizaji kwani japokuwa hawapati ujumbe kama
ilivyokusudiwa (rejea 4.1) na japokuwa wana mtazamo hasi kuhusu tabia ya wabunge
kubadilisha Kiswahili na Kiingereza (rejea 4.3) bado wanaweza kufuatilia mijadala ya
Bunge.
64
Hata hivyo, katika mijadala na mahojiano ilibainika kuwa wasikilizaji walio wengi hasa
wa vijijini hawafuatilii mijadala ya Bungeni mara kwa mara. Walipodadisiwa kama
kuna sababu nyingine zinazowafanya wafuatilie mijadala mara chache, miongoni mwa
sababu zilizotajwa ni: (1) kukosa muda wa kuangalia au kusikiliza kutokana na kuwa
na shughuli nyingi, (2) umaskini unaosababisha wakose redio au runinga, (3) ukosefu
wa umeme, (4) wabunge kutochangia hoja muhimu zenye kutia hamasa ya kusikiliza na
(5) kutokuwa na hobi ya kusikiliza mijadala ya Bunge.
4.5 Ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni: Maoni ya Wasikilizaji
Kutokana na uchanganuzi wa data, imebainika kuna makundi makuu mawili ya maoni
yaliyotolewa na wasikilizaji. Haya yote yanalenga kuondoa athari za ubadilishaji
msimbo Bungeni kwa kupendekeza mbinu zitakazowafanya wabunge wasichangie hoja
kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Sehemu ya kwanza inahusisha maoni
kuhusu ni lugha gani inayofaa kuendeshea shughuli za Bunge ambapo tumepata
makundi madogo matatu ya wasikilizaji, yaani wanaopendekeza Kiswahili tu,
wanaopendekeza Kiingereza tu na wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza. Bila
shaka, kila kundi limetoa sababu zake kuhusu sababu za kupendekeza lugha mojawapo.
Kama tutakavyoona data inaonesha kuwa, asilimia 85.55% ya watafitiwa
wanapendekeza Kiswahili tu. Hawa wanaongozwa na dhana kuwa, iwapo Kiswahili tu
kitateuliwa kuwa lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge, pamoja na mambo
mengine kutakuwa na uwezekano wa wabunge kutochanganya Kiswahili na Kiingereza
na hivyo wasikilizaji kupata ujumbe kama ulivyokusudiwa. Kundi la pili la maoni ni
maoni ya jumla yanayolenga kuhakikisha kuwa ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza unakomeshwa au kupunguza athari zake kwa wasikilizaji. Kimsingi
65
tukichanganua kwa undani maoni ya kundi hili yanalenga kukifanya Kiswahili kuwa
lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge.
4.5.1 Lugha ya Shughuli za Bunge
Bunge ni chombo cha uwakilishi wa watu. Chombo hiki kimeundwa kwa mujibu wa
Katiba ya nchi, na muundo wake, pamoja na baadhi ya majukumu yake, vile vile
yameelezwa katika katiba hiyo. Majukumu ya Bunge yametamkwa katika ibara ya
63(2) ya katiba ya nchi kwamba:
Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho
kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, ya kusimamia na kuishauri
Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji
wa majukumu yake.
Bunge linatekeleza majukumu yake yote kwa njia ya vikao vyake. Kwa hiyo jambo
lolote linalohitaji uamuzi wa Bunge, huamuliwa katika mikutano rasmi ya Bunge. Bila
shaka, ili kumudu jukumu hili lazima kuwepo na lugha inayofaa kuwezesha
mawasiliano kati ya wabunge na serikali na kati ya wabunge na wasikilizaji yaani
wananchi na pia kati ya serikali na wananchi kupitia kwa wabunge. Lugha inayofaa
kwa mujibu wa Sewangi (2004:87-88) kama anavyowanukuu wanaisimu Rubagumya
(1986) na Massamba (1993), ni ile inayofikisha ujumbe au inayoeleweka kwa watu
wanaohusika. Kanuni za kudumu za Bunge zinadai kuwa; “Shughuli za Bunge
zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili au ya Kiingereza, bila tafsiri ya lugha hizo
kutolewa” (toleo la 2004 kanuni ya 118(1)).
66
Kimsingi tuseme tu kwamba, suala la ni lugha gani inafaa kuendeshea shughuli za
Bunge linahusiana moja kwa moja na dhana ya upangaji lugha. Huu ni mchakato
unaohusu uamuzi wa makusudi kabisa wa kuchagua lugha mojawapo, kati ya lugha
zilizopo, na kuiendeleza na kuikuza kwa ajili ya matumizi maalumu (Msanjila
2009:76). Ikumbukwe kuwa, uamuzi wa lugha gani itumike, wapi, kwa matumizi gani
na kwa kiwango gani ni uamuzi wa kisera; na kama tujuavyo utungaji wa sera ni wajibu
wa serikali baada ya kuidhinishwa na Bunge.
Pamoja na hayo, ili serikali ifikie uamuzi huo ni lazima iwahusishe wataalamu wa
masuala hayo ili kujiridhisha kuwa maamuzi hayo yanaendana na hali halisi ya jamii
husika na makusudi ya uteuzi wa lugha hiyo. Bila shaka, wataalamu hukamilisha kazi
hii kwa kufanya tafiti zenye kuihusisha jamii. Kwa kuongozwa na dhana hii, tuliwataka
wasikilizaji kutoa maoni yao kuhusu nini kifanyike kwa upande wa lugha ya kutumia
Bungeni au kwa maneno mengine ni lugha gani inayofaa/zinazofaa kuwa lugha rasmi
ya/za kuendeshea shughuli za Bunge.
Maoni ya wasikilizaji kuhusu swali hili yalijitokeza katika makundi makuu matatu
yaani wanaopendekeza Kiswahili tu, wanaopendekeza Kiingereza tu na
wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza. Bila shaka, kila kundi lilitoa sababu za
kupendekeza lugha hiyo au hizo ambazo zitabainishwa baadaye. Baada ya kuchanganua
data matokeo yake yamewasilishwa katika jedwali lifuatalo:-
67
Jedwali la 9: Mapendekezo ya Lugha ya Shughuli za Bunge
KIWANGO
CHA ELIMU Jum
la
%
Kis
wah
ili
tu
%
Kii
ng
erez
a tu
%
Kis
wah
ili
na
Kii
ng
erza
%
Wasiojua Kusoma 127 16.39 118 92.91 00 00 09 7.09
Elimu ya Msingi 453 58.45 403 88.96 05 1.10 45 9.93
Sekondari 130 16.77 101 77.69 04 3.08 25 19.23
Chuo/Chuo Kikuu 65 8.39 41 63.08 4 6.15 20 30.77
Jumla 775 100 663 85.55 13 1.68 99 12.77
Mchanganuo wa data unaonesha kuwa, wasikilizaji 663 (85.55%) wanapendekeza
kuwa Kiswahili kinafaa zaidi, 99 (12.77%) wanapendekeza Kiingereza na 13 (1.68%)
wanapendekeza Kiswahili na Kiingereza kuendelea kutumika kwa pamoja.
Muainisho zaidi kwa kuzingatia matabaka mbalimbali ya kielimu unaonesha
wanaopendekeza Kiswahili tu ni: wasiojua kusoma na kuandika 118 (92.91%), elimu
ya msingi 403 (88.96%), sekondari 101 (77.69%), na elimu ya chuo/chuo kikuu 41
(63.08%). Wanaopendekeza Kiingereza tu ni: wasiojua kusoma na kuandika 00 (00%),
elimu ya msingi 05 (1.10%), sekondari 04 (3.08%), na elimu ya chuo/chuo kikuu 04
(6.15%). Kwa upande wa wanaopendekeza Kiswahili na Kiingereza ni: wasiojua
kusoma na kuandika 09 (7.09%), elimu ya msingi 45 (9.93%), sekondari 25 (19.23%),
na elimu ya chuo/chuo kikuu 20 (30.77%).
Kwa ujumla data inaonesha kuwa, idadi kubwa ya wasikilizaji wanapendekeza
Kiswahili tu. Mathalani, data inaonesha kuwa watafitiwa 663 ambao ni sawa na 85.55%
ya sampuli nzima ya utafiti wanapendekeza kuwa Kiswahili kinafaa kuwa lugha rasmi
na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hii inaungana na mkabala unaoongoza
68
utafiti huu “MKAMA” kama ulivyoasisiwa na Fishman (1971) unaodai kuwa, lugha au
lahaja za lugha husika zipewe dhima maalumu katika jamii. Kama matokeo ya utafiti
yanavyobainisha, mkabala huu unatetea kuwa kuna mazingira ya kitaasisi yahusuyo
mawanda (mada, sehemu na wahusika) ambapo kwayo lugha moja inafaa zaidi ya
nyingine. Hivyo basi, kadri ya mkabala huu inatakiwa ianishwe ni lugha gani rasmi ya
kutumika katika shughuli zake zote. Kwa mantiki hii, data inaungana na mkabala huu
kwamba lazima lugha moja yaani Kiswahili katika muktadha wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania iwe lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge kwani
kinaendana na muktadha (mahali, matukio, mada na wahusika) wa sehemu hii.
Ikumbukwe kuwa, muundojamii ndio huongoza uteuzi wa lugha husika kwa kuzingatia
sababu maalumu. Kwa kuzingatia hili watafitiwa, walitoa sababu kadhaa kutetea kuwa
Kiswahili kinafaa zaidi ya lugha nyingine ambapo sababu hizo zimewasilishwa katika
jedwali lifuatalo:-
69
Jedwali la 10: Sababu za Kutetea Kiswahili Kuendeshea Shughuli za Bunge
Sababu za kufaa kwa Kiswahili tu
Idadiya wasikilizaji
%
Kinaeleweka kwa Watanzania wengi 643 96.98
Ni lugha ya taifa 617 93.06
Kinatambulisha utaifa wa Watanzania 570 85.97
Kimefungamana na utamaduni na jadi ya Watanzania 557 84.01
Kinawaunganisha Watanzania kama kilivyowaunganisha katika
kudai uhuru kutoka kwa mkoloni
555 83.71
Kinaendana na jamii ya Watanzania 530 79.94
Hakijinasibishi na tabaka au kabila lolote hivyo kuondoa ubaguzi 477 71.95
Sio Wabunge wote wanaofahamu Kiingereza 470 70.89
Kinawaepusha Watanzania na utumwa wa kifikra 456 68.78
Ni rahisi kueleweka kwani kinaendana na lugha za kibantu 444 66.97
Ili kukilinda na kukikuza Kiswahili 411 61.99
Ili kuondokana na kero ya ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza 332 50.08
Kimeruhusiwa kutumika katika Bunge la Afrika 192 28.96
Jedwali la 10 hapa juu linaonesha sababu za kutetea kufaa kwa Kiswahili kuendeshea
shughuli za Bunge kama zilizotolewa na watafitiwa. Baadhi ya sababu zilitolewa na
watafitiwa walio wengi10
wakati baadhi zikitajwa na wachache. Hata hivyo, hoja hizi
zinaonesha kuingiliana na hivyo tunaweza kuzichanganua zaidi na kupata sababu
zifuatazo:-
I. Kiswahili kinaeleweka kwa Watanzania wengi
II. Ni lugha ya taifa na inafungamana na utamaduni wa Watanzania
10
Watafitiwa walikuwa huru kutaja sababu nyingi kadri wawezavyo, hivyo kuna sababu ambazo pamoja
na kutaja sababu nyingine zilikuwa zikitajwa mara kwa mara
70
III. Ni lugha ya umoja
IV. Kinawaepusha na utumwa wa kifikra
V. Ili kukilinda na kukikuza Kiswahili
VI. Ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika
4.5.1.1 Kiswahili Kinaeleweka kwa Watanzania Wengi
Hoja hii inaunganisha sababu tatu kama zinavyojitokeza katika jedwali la 10 ambazo
ni: mosi, kwamba Kiswahili kinafahamika kwa watanzania wengi; pili, kwamba sio
wabunge wote wanafahamu Kiingereza; na tatu ni kwamba ni rahisi kueleweka kwani
kinaendana na lugha za kibantu. Katika muktadha huu watafitiwa wanatetea kuwa sifa
hizi zinatosha kukifanya Kiswahili kufaa kuwa lugha rasmi na pekee ya kuendeshea
shughuli za Bunge. Kama tulivyoona katika 4.5.1 lugha inayofaa ni ile inayofikisha
ujumbe au inayoeleweka na kufahamika kwa watu wanaohusika. Kwa mujibu wa
Mekacha (2000:85) wanaisimu na watu wengine wote wanakubaliana kuwa, hadi
mwaka 2001 watanzania takribani wote (100%) wanafahamu na kutumia Kiswahili
kwa namna moja au nyingine. Ongezeko la idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini
Tanzania kuanzia mwaka 1870 hadi 2000 linaainishwa katika jedwali lifuatalo:-
71
Jedwali la 11: Ongezeko la Idadi ya Watumiaji wa Kiswahili Tanzania
Mwaka Idadi ya watu wote
(milioni)
Watumiaji wa Kiswahili
(milioni)
Asilimia
(%)
1870 4 0.08 2
1900 6 1 17
1940 9 3 33
1960 12 6 50
1978 15 11 74
1985 22 20 90
2000 30 30 100
Chanzo: Mekacha (2000:86)
Jedwali hili linaonesha jinsi kunavyokuwepo na ongezeko la watumiaji wa Kiswahili
kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya lugha hii katika kipindi chote cha historia ya
kuenea kwake. Kwa mantiki hii, kama kigezo cha kueleweka na kufahamika kwa
wasikilizaji kikizingatiwa, tunategemea Kiswahili kupewa hadhi ya kuwa lugha rasmi
na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.
Pia, izingatiwe kuwa Kiswahili kinaendana na lugha za kibantu ambazo kimsingi
zinaunda idadi kubwa ya lugha zinazopatikana Tanzania. Ni kutokana na hoja hii
watafitiwa walipendekeza kuwa kiruhusiwe kutumika kama lugha rasmi ya kuendeshea
shughuli za Bunge kwani itakuwa rahisi kwa mtanzania anayefahamu lugha mojawapo
ya kibantu kuelewa kinachozungumzwa Bungeni. Wakati wa kukusanya data mtafiti
alilishuhudia hili kivitendo kwani kuna watafitiwa waliokuwa hawawezi kuongea
Kiswahili kabisa (waliongea Kisukuma) lakini kwa kuwa mtafiti aliongozana na mtu
aliyefahamu Kiswahili na Kisukuma, ilimlazimu mtu huyo awe mkalimani. Hata hivyo,
72
mkalimani alikuwa na kazi ya kutafsiri katika Kiswahili kinachosemwa na mtafitiwa
(aliyetumia Kisukuma) huku maswali yaliyoulizwa na mtafiti kutohitaji kutafsiriwa
kwani watafitiwa walielewa Kiswahili japo wanashindwa kukiongea. Pia kuna maneno
mengine ya Kisukuma ambayo mtafiti aliyaelewa bila kutafsiriwa na mkalimani (japo
mtafiti hafahamu Kisukuma) kwani yaliendana na Kiswahili. Kwa ushahidi huu,
inatosha tu kusema kwamba, kwa kuwa Kiswahili kinaendana na lugha za Kibantu
(Chachage 2004:12) na jamii ya watanzania walio wengi ni wabantu ni vema kikawa
lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.
Hoja nyingine iliyodokezwa ni kwamba, si wabunge wote wanafahamu na kukielewa
Kiingereza. Katika mijadala ya vikundi lengani mtafitiwa mmoja alikuwa na haya ya
kusema:-
Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (akiinukuu ibara
ya 67 (a) japo hakuitaja katika mjadala) mojawapo ya sifa ya mtu kuwa mbunge
ni kuwa awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza. Kwa
mantiki hii mtu anayeelewa kusoma na kuandika Kiswahili tu ana sifa ya kuwa
Mbunge. Hivyo basi, Kiswahili kiwe lugha pekee ya Bunge ili kuwafanya
wabunge wenye sifa hii kuelewa na kuwa katika nafasi nzuri ya kujenga hoja.
Pointi ya msingi inayopatikana katika hoja hii ni kuwa, suala la kutoelewa Kiingereza
haliwakumbi wasikilizaji tu bali pia na wabunge wenyewe. Hatusemi kuwa wabunge
wote hawaelewi Kiingereza vizuri, la hasha; wapo wataalamu na mahiri wa lugha hii ila
uzuri ni kuwa wanaelewa na Kiswahili pia kwani ndiyo lugha wanayoitumia katika
harakati za kuomba ridhaa kwa wananchi. Hivyo basi, Kiswahili kinafaa kutumika
73
kwani kitaondoa tatizo la kiisimu kwa wasikilizaji na wabunge pia kwa sababu umahiri
katika lugha ni msingi wa ufikishaji ujumbe kwa usahihi zaidi bila ya upotoshaji (Shoo
2004:80). Kama tutakavyoona baadaye mojawapo ya njia ya kuwezesha hili ni
kuhakikisha kuwa miswada na nyaraka muhimu za Bunge zinakuwa katika lugha ya
Kiswahili.
4.5.1.2 Lugha ya Taifa na Utambulisho wa Watanzania
Hoja hii inaunganisha sababu nne kama zinavyoainishwa katika jedwali la 4.6, ambazo
ni: mosi, Kiswahili ni lugha ya taifa; pili, kinautambulisha utaifa wa watanzania; tatu,
kimefungamana na utamaduni na jadi ya watanzania; na nne, kinaendana na jamii ya
watanzania.
Tukianza na hoja kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa, lugha hii ilipewa hadhi hii mwaka
1963. Kutokana na hadhi hii watafitiwa wanadai kuwa, kwa kuwa Bunge ni taasisi na
mhimili mmojawapo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vema
Kiswahili kikawa lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Wanadai kuwa
kukifanya Kiswahili kuwa na hadhi hii kunaashiria uzalendo wa kukithamini kilicho
chao yaani lugha ya taifa na kuachana na lugha ya kigeni (Kiingereza).
Hoja hii inafungamana na sababu ya pili kuwa Kiswahili kinautambulisha utaifa wa
watanzania. Utambulisho kwa mujibu wa Msanjila (2009:46) ni jumla ya vigezo
maalumu vinavyotumiwa kumtambulisha mtu, kundi la watu, jamii au taifa fulani ili
kuonesha kuwa liko tofauti na taifa jingine, jamii fulani iko tofauti na jamii nyingine,
kundi fulani liko tofauti na kundi jingine au mtu fulani yuko tofauti na kundi jingine au
74
mtu fulani yuko tofauti na mtu wa kundi jingine, jamii nyingine au taifa jingine. Kwa
mujibu wa Tabouret-Keller (1989) kama anavyonukuliwa na Msanjila (Keshatajwa)
utambulisho wa mtu umefungamana na mambo mengi ya kijamii kama vile lugha,
utamaduni, mila na desturi, mavazi, chakula, dini (imani mbalimbali), historia ya jamii,
siasa na uchumi. Hoja za wataalamu hawa zinaungana na maoni ya wasikilizaji kuhusu
ni lugha gani inayofaa kuwa lugha rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Ili kubaini
utambulisho wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, watafitiwa wanasema
kuwa ni vema kutumia Kiswahili sanifu na kisichohusisha ubadilishaji wake na lugha
nyingine kama vile Kiingereza. Huu utakuwa utambulisho wa Watanzania kwani
matamshi ya mzungumzaji yeyote ni matamshi ya utambulisho wake.
Sababu nyingine ni kuwa Kiswahili kimefungamana na utamaduni na jadi ya
watanzania. Jambo la kuzingatia ni kuwa lugha ni mojawapo ya nguzo muhimu za
utamaduni. Bila shaka hii ndiyo ilikuwa sababu ya msingi ya wasikilizaji
kukipendekeza Kiswahili kuwa lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za
Bunge. Watafitiwa wanadai kuwa Kiswahili kupewa hadhi hii ni kuuinua na kuuenzi
utamaduni wa nchi yetu kwani nchi yeyote huru lazima ijivunie utamaduni wake na iwe
na itikadi na vitu vya kuitambulisha kama vile lugha, bendera ya taifa, wimbo wa taifa,
vazi la taifa na kadhalika. Katika hoja hii tunahitimsha kuwa, ni vema kuyaenzi maneno
ya Hayati mwalimu Julius K. Nyerere (1974:91) kuwa nchi isiyo na utamaduni wake
haina tofauti na mkusanyiko wa watu ambao hawana roho iwawezeshayo kuwa taifa.
Katika muktadha huu, Bunge lisilouenzi utamaduni wa nchi yake yaani kwa kutumia
lugha yenye kutambulisha taifa lake halina tofauti na mkusanyiko wa watu ambao
hawana roho iwawezeshayo kuwa Bunge la taifa.
75
Sababu ya nne ni kuwa Kiswahili kinaendana na jamii ya watanzania. Kimsingi sababu
hii ni jumuishi kwani inaunganisha sababu tatu zilizojadiliwa awali katika kipengele
hiki. Kiswahili kuendana na jamii ya watanzania kunanasibishwa na kuwa lugha ya
taifa, kuwa lugha ya utambulisho na kufungamana na utamaduni na jadi ya watanzania.
Katika hoja hii inatosha tu kusema kwamba, maoni ya watafitiwa yanaungana na hoja
ya Kiango (2004:70) kama anavyowanukuu Sapir (1958) na Worf (1958) kuwa lugha
ina dhima kubwa katika utamaduni wa jamii. Ni mfumo wa mawasiliano na ni njia ya
kuongoza fikra za wazungumzaji. Kwa vile lugha hutofautiana, tunatarajia kuwepo kwa
mikwamo katika mawasiliano ya watu wa tamaduni tofauti. Hivyo basi, kwa kuwa
Kiswahili kimefungamana na kinaendana na utamaduni wa watanzania ni vema kikawa
lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge.
4.5.1.3 Lugha ya Umoja
Hoja hii inajumuisha sababu mbili ambazo ni kwamba; mosi, Kiswahili
kinawaunganisha watanzania kama kilivyowaunganisha katika harakati za kudai uhuru
kutoka kwa mkoloni; pili, ni kwamba hakijinasibishi na tabaka au kabila lolote hivyo
kuondoa ubaguzi. Jambo lililoonekana kusisitizwa na watafitiwa ni kuwa hakuna jamii
au tabaka linaloweza kudai kuwa Kiswahili ni lugha yake binafsi. Kwa mantiki hii
wanadai kuwa, kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya watanzania wote na hakijinasibishi na
jamii au tabaka lolote ni vema kikapewa hadhi ya kuwa lugha pekee ya kuendeshea
shughuli za Bunge. Tofauti na hili watafitiwa wanadai kuwa kuruhusu Kiingereza kuwa
lugha mojawapo au lugha pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge ni kuleta ubaguzi
miongoni mwa watanzania kwani lugha hii ni ya matabaka maalumu hasa wasomi.
76
Wakirejea historia watafitiwa wanadai kuwa Kiswahili ni lugha iliyotumika
kuwaunganisha watanzania wa kabila na itikadi tofauti katika harakati za kudai uhuru.
Kwa mfano, katika mahojiano mtafitiwa mmoja alisema:-
...…. Hakuna lugha yoyote iliyotetea maslahi ya taifa letu kama Kiswahili.
Ni Kiswahili kilichotumika katika harakati za kudai uhuru na hatimaye
kutuletea uhuru na umoja wa kitaifa ambao matokeo yake ni utulivu. Utulivu na
amani ndivyo vilivyowawezesha wasomi kusoma, na kupata madigrii
yanayowapa kiburi na kukidharau Kiswahili hivi leo. Napenda kukiri kuwa si
wote, lakini wapo watu wa namna hiyo na wengine ni viongozi tena wenye
dhamana kubwa waliyopewa ama na Rais au wananchi. ………
Hapa mtafitiwa anazinadi sifa zinazokipa sifa Kiswahili kufaa kuwa lugha pekee ya
Bunge. Pia mtafitiwa anaonekana kuwalaumu wasomi kuwa ndio wanaotumia fursa ya
kufahamu Kiingereza kukidharau Kiswahili. Hivyo basi, watafitiwa wanadai kuwa
Kiswahili ni lugha inayotetea maslahi ya kitaifa kwani inaleta umoja wa kitaifa na
kuwezesha harakati za kimaendeleo. Kwa kuwa Bunge ni taasisi ya watanzania wote, ni
vema lugha inayopewa hadhi ya kuwa lugha pekee ya Bunge iwe lugha
inayowaunganisha watanzania wote na isijinasibishe na tabaka au jamii yoyote.
4.5.1.4 Kinawaepusha Watanzania na Utumwa wa Kifikra.
Katika hoja hii watafitiwa wanadai kuwa kukikumbatia Kiingereza ni kujiingiza au
kuendeleza utumwa wa kifikra. Hawa wanaongozwa na dhana kuwa Kiingereza ni
lugha ya mkoloni na kwa kuwa Tanzania ilishajipatia uhuru wake ni vema ikawa na
uhuru wa kutumia lugha yake katika shughuli zote za kiserikali. Wanachotetea ni kuwa,
77
uhuru haupaswi kuwa wa bendera tu bali uwe wa nyanja zote ikiwa ni pamoja na
utamaduni ambapo nguzo mojawapo ya utamaduni ni lugha. Hivyo basi, kwa hoja hii
watetezi wa Kiingereza kuwa mojawapo ya lugha za Bunge wananekana watumwa wa
kifikra.
4.5.1.5 Kukilinda na Kukikuza Kiswahili.
Hii ni hoja iliyotolewa na watafitiwa katika kutetea kuwa Kiswahili kinafaa kuwa lugha
pekee ya kuendesha shughuli za Bunge. Hii inabeba sababu mbili kuu ambazo ni; mosi,
ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na pili, ili kuondokana na ubadilishaji wa
Kiswahili na Kiingereza. Kimsingi watafitiwa walionesha kutambua kuwa lugha
yoyote ile inafaa kukuzwa na kulindwa. Watafitiwa wanadai kuwa ili Kiswahili kiwe na
msamiati wa kutosha kuelezea mambo muhimu yanayoendana na maendeleo ya sayansi
na teknolojia na pia kuweza kuendana na kasi ya utandawazi ni vema kikapewa hadhi
ya kuendeshea shughuli za Bunge kama lugha pekee ya mawasiliano. Wanaendelea
kudai kuwa si kwamba Kiswahili hakina istilahi na msamiati wa kutosha kuwezesha
mawasiliano ya Bunge, ila tatizo ni kuwa, kwa kuwa kunakuwepo na mbadala wake
(Kiingereza) wabunge hawajishughulishi kutafuta msamiati wa kuelezea dhana fulani.
Kutokana na hili ndio maana mbunge akikwama kupata msamiati wa Kiswahili
huchanganya Kiingereza na kinyume chake pia. Kutokana na hali hii ndio maana
kunajitokeza uzungumzaji wa kubadilisha Kiswahili na Kiingereza.
Kimsingi hoja hii ililenga kujibu hoja zinazotolewa na watetezi wa Kiingereza kuwa ni
lugha ya utandawazi, kilaalamu na kitaaluma na ina istilahi zinazokidhi haja za
kuelezea dhana mbalimbali (rejea 4.7). Hizi haziwezi kuwa sababu muafaka na kuntu
78
za kutushawishi kukubali kuwa Kiingereza kiwe mojawapo au lugha pekee ya
kuendeshea shughuli za Bunge. Tukubaliane kuwa Kiswahili kinakidhi dhima yake
yaani kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wanajamii (rejea 4.5.1) na hivyo hakuna
haja ya kuendelea kukikumbatia na kukitetea Kiingereza.
Tuseme tu kwamba, serikali haina budi kuunga mkono kikamilifu juhudi za kukuza
Kiswahili ikitilia maanani kuwa, kama asemavyo Broomfield (1931) hata lugha ya
Kiingereza ambayo kwa sasa hivi ina uwezo mkubwa sana ilipokuwa katika hatua zake
za mwanzo za maendeleo, ilidharauliwa na kutazamwa kama lugha ambayo haikuwa na
uwezo wa kufafanua dhana za sayansi na teknolojia. Hivyo basi kama asemavyo
Mulokozi (2009:82) jukumu letu sisi wakuzaji wa Kiswahili ni kuufanya utandawazi
utandawaze Kiswahili.
4.5.1.6 Kiswahili ni Lugha Rasmi ya Bunge la Afrika
Hii ni hoja iliyotolewa na watafitiwa katika kutetea kuwa Kiingereza kisipewe hadhi ya
kuwa lugha ya kuendeshea shughuli za Bunge kwa kigezo kuwa ni lugha ya kimataifa.
Katika kujenga hoja mtafitiwa mmoja alikuwa na haya ya kusema:
….. ni lazima tutambue kuwa Kiswahili tayari ni lugha ya kimataifa kwani
tangu mwaka 2004 kimekubaliwa kutumika rasmi katika vikao vya umoja wa
Afrika…. Bunge la Afrika Mashariki tayari lipo, na shughuli za kisiasa ndani ya
Afrika Mashariki zinatumia sana Kiswahili na dalili zinaonesha kuwa Kiswahli
kitakuwa ndiyo lugha kuu ya umoja wa Afrika Mashariki……
79
Nukuu hii inaonesha ni jinsi gani watafitiwa wanavyokithamini na kukitetea Kiswahili.
Pamoja na hayo inaonekana Kiswahili kinaweza kuongezwa katika lugha za umoja wa
mataifa na hivyo kuwa lugha ya kimataifa (Gikambi 2010). Katika hoja hii tuhitimishe
kwa kusema kuwa, Kiswahili katu hakitastawi na kuchanua katika ukanda huu kama
kitabakia kuwa lugha ya sokoni tu bila kupewa hadhi ya kuendesha shughuli zote za
serikali na taasisi zake na bila kuingizwa na kutumiwa katika ngazi za juu za elimu na
teknolojia.
4.6 Mbinu za Kukifanya Kiswahili kuwa Lugha Pekee ya Shughuli za Bunge.
Kama tulivyoona katika kipengele 4.5.1 wasikilizaji wanapendekeza kuwa Kiswahili
kiwe lugha pekee na rasmi ya kuendeshea shughuli za Bunge. Hata hivyo, hawakuishia
hili tu bali walikwenda mbali zaidi kwa kutoe mbinu mbadala za kuwezesha lengo hili.
Yafuatayo ni maoni yao:-
1. Kanuni za kudumu za Bunge zifanyiwe marekebisho na kuweka vipengele
vifuatavyo:-
(a) Kwamba wakati wa mijadala mbunge yoyote asichanganye Kiswahili na
Kiingereza au lugha iwayo yote bali atumie Kiswahili fasaha.
(b) Kama itakuwa ni lazima kuchanganya lugha kwa sababu maalumu,
mbunge alazimike kuelezea au kufasiri alichomaanisha kwa Kiswahili
fasaha.
2. Miswada yote inayowasilishwa Bungeni iandaliwe katika lugha ya Kiswahili ili iwe
rahisi kwa wabunge wote na pia isiwalazimu wabunge kutumia Kiingereza
wanaporejelea au kunukuu kwenye kifungu fulani katika muswada husika. Pia
80
sheria zote ziandikwe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri zilizoandikwa
kwa lugha za kigeni.
3. Sera na miongozo yote ya serikali itolewe kwa Kiswahili ili kukipa hadhi yake. Pia,
taarifa za mikutano, semina na warsha nchini zitolewe kwa Kiswahili kwa manufaa
ya wananchi.
4. Bunge liwe na kitengo maalumu cha tafsiri ambacho kitahusika na ufasiri wa
kumbukumbu na nyaraka mbalimbali, sheria na miswada ya Bunge viliyoandikwa
kwa lugha ya Kiingereza. Pia, wabunge wakitumie kitengo hiki kupata fasiri sahihi
za nyaraka wazipatazo kutoka vyanzo mbalimbali zilizoandikwa kwa lugha
nyingine.
5. Lugha ya kufundishia iwe Kiswahili kwa ngazi zote za elimu ili kuwafanya
watanzania kuwa na istilahi na msamiati wa kutosha wa lugha hii. Hii itasaidia
wahitimu na wabunge wa baadaye kuwa mahiri wa Kiswahili kwa kuwa na istilahi
za taaluma mbalimbali.
6. Serikali ihakikishe kwamba kunakuwepo machapisho ya kutosha yanayoorodhesha
istilahi muhimu zinazoendana na mazingira ya Bungeni. Haya yaandaliwe kwa
ushirikiano na taasisi maalumu zenye jukumu la kulinda na kukuza Kiswahili kama
vile BAKITA, TATAKI na BAKIZA.
81
4.7 Kufaa kwa Kiingereza kuwa Lugha Rasmi ya Shughuli za Bunge.
Kama tulivyodekeza awali, kulijitokeza watafitiwa wanaotetea kuwa Kiingereza tu
kinafaa kuendeshea shughuli za Bunge. Hawa walikuwa watafitiwa 13 (1.68%) kati ya
sampuli nzima ya utafiti. Sababu za kukitetea Kiingereza zimeainishwa katika jedwali
lifuatalo:-
Jedwali la 12: Sababu za Wasikilizaji Kutetea Kuwa Kiingereza Kinafaa kwa
Shughuli za Bunge
Sababu za kufaa kwa Kiingereza tu
Idadi ya wasikilizaji
%
Ni lugha ya utandawazi 13 100
Inaeleweka kwa wanajuiya ya Afrika Mashariki 11 84.62
Wabunge ni wasomi na wanakielewa Kiingereza vizuri 10 76.92
Ni lugha ya kitaalamu na kitaaluma 9 69.23
Ina istilahi muhimu zisizopatikana katika Kiswahili 9 69.23
Miswada huandikwa kwa Kiingereza 8 61.54
Nyaraka nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza 6 46.15
Tuseme tu kwamba baadhi ya watafitiwa wa viwango vya juu vya elimu (ngazi ya chuo
kikuu na baadhi sekondari) ndio walionekana kupendekeza lugha hii (rejea jedwali la
4.5). Sababu ya msingi inaweza kuwa ni kwa sababu wanaelewa Kiingereza na hivyo
maamuzi haya hayana athari hasi kwao. Hata hivyo, sababu za uteuzi wa Kiingereza tu
zinaonekana kukosa mashiko kwani sababu zinazotolewa na watetezi wa Kiswahili tu
(rejea 4.5) zinaonekana kutoa majibu yake.
82
4.8 Kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza.
Kundi hili lilikuwa na watetezi wachache ambao ni watafitiwa 99 (12.77%) katika
sampuli nzima ya utafiti. Kundi hili pia lilihusisha watafitiwa wenye kuelewa
Kiingereza na Kiswahili kwa namna moja au nyingine. Hoja zao zimewasilishwa katika
jedwali lifuatalo:-
Jedwali la 13: Sababu za Kutetea Kuwa Kiswahili na Kiingereza Zinafaa.
Sababu za kufaa kwa Kiswahili na Kiingereza
Idadi ya
wasikilizaji
%
Kumpa Mbunge uhuru wa kujieleza kwa lugha anayoimudu zaidi
ili mjadala unoge
90
90.91
Wabunge ni wasomi wanaoweza kujieleza kwa lugha hizi 85 85.86
Zote zinatumika katika ngazi zote za elimu kama somo au lugha ya
mawasiliano
81
81.82
Ili kuwamotisha watoto kujifunza lugha hizi 76 76.77
Bunge hupata wageni wasiojua Kiswahili, hivyo wakiwepo
Kiingereza kitumike zaidi.
62
62.63
Nchi imekuwa na wasomi wengi wanaofahamu Kiswahili na
Kiingereza
49
49.49
Itoshe kusema tu kwamba mjadala wa 4.5 unatoa majibu ya hoja hizi. Kwa mantiki hii
hoja hizi hazitajengewa mjadala.
4.9 Hitimisho
Sura hii ilihusu uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data zilizokusanywa kutoka
uwandani. Mjadala umewasilishwa katika sehemu kuu tano. Sehemu ya kwanza ilihusu
uelewekaji wa mijadala ya wabunge yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Katika
83
sehemu hii tumeona kuwa, 8.9% ya wasikilizaji ndio wanaoelewa mijadala yenye
kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza huku 41.68% wakiwa hawaelewi,
14.58% wakielewa baadhi ya sentensi, na 34.84% wakielewa baadhi ya maneno.
Uchanganuzi zaidi unaonesha kuwa kiwango cha kuelewa au kutoelewa mijadala hii
kinahusiana moja kwa moja na kiwango cha elimu.
Sehemu ya pili ilihusu mbinu wazitumiazo wasikilizaji kuelewa mijadala ya Bunge
yenye kuhusisha ubadilishaji msimbo. Tumeona kuwa 59.23% ya wasikilizaji
hawatafuti mbinu mbadala za kuwafanya waelewe mijadala ya Bunge yenye kuhusisha
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo, imeonekana kuwa kwa kiasi
fulani wasomi wanatumia mbinu mbadala kama vile kuuliza kwa wenzao, vyombo vya
habari na hata kusoma kamusi.
Katika sehemu ya tatu tumeona kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na hali ya
wabunge kubadilisha Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo, pamoja na kutofurahishwa
na namna hii ya uzungumzaji, katika sehemu ya nne tumeona kuwa hali hii sio sababu
pekee inayosababisha wasikilizaji kutofuatilia mijadala ya Bunge.
Katika sehemu ya tano tumeona kuwa 85.55% ya watafitiwa wanapendekeza kuwa
Kiswahili kiwe lugha rasmi na pekee ya kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu
wazitoazo ni kuwa; mosi, kinaeleweka kwa Watanzania wengi; pili, ni lugha ya taifa na
inafungamana na utamaduni wa Watanzania; tatu, kinawaunganisha Watanzania kama
kilivyowaunganisha kudai uhuru na hivyo kuondoa ubaguzi; nne, Kinawaepusha na
utumwa wa kifikra; tano, ili kukilinda na kukikuza Kiswahili; na sita, ni lugha rasmi ya
84
Bunge la Afrika. Pia, watafitiwa wametoa maoni ya jumla kuhusu nini kifanyike
kukifanya Kiswahili kuwa lugha kidhi ya mijadala ya Bunge na shughuli nyingine za
kiserikali.
Kimsingi mawasilisho ya mjadala ya matokeo ya utafiti yanatupa mwanzo mzuri wa
sura inayofuata. Sura hii inahusu hitimisho na mapendekezo kuhusu tafiti nyingine.
85
SURA YA TANO
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii inahitimisha sura za awali za tasnifu hii kwa kudokeza vipengele muhimu
katika kila sura. Kuna sehemu ambayo inatoa muhtasari wa mambo muhimu katika sura
za awali ambayo yanaendana na malengo ya utafiti huu. Baada ya hapo ni sehemu
inayotoa mapendekezo ya utafiti mwingine na mwisho hitimisho.
5.2 Muhtasari
Kama ilivyoelezwa awali utafiti huu ulihusu ubadilishaji msimbo Bungeni na athari
zake kwa wasikilizaji. Sura ya kwanza inajumuisha utangulizi, usuli wa tatizo, tatizo la
utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mawanda ya utafiti,
kiunzi cha kinadharia na vikwazo vya utafiti.
Sura ya pili ilihusika na mapitio ya machapisho yanayohusiana na maana na aina za
ubadilishaji msimbo, tofauti kati ya ubadilishaji msimbo na ukopaji, sababu za
ubadilishaji msimbo, kueleweka kwa maongezi yenye ubadilishaji msimbo, mbinu
wazitumiazo wasikilizaji kuelewa matini za mchanganyiko wa lugha, na mtazamo wa
wasikilizaji kuhusu hali ya ubadilishaji msimbo. Katika sura hii tumeona kuwa hakuna
tafiti zilizojadili athari za ubadilishaji msimbo Bungeni kwa wasikilizaji. Kutokana na
hili utafiti huu umelenga kuziba pengo hili la kiutafiti.
Sura ya tatu inajadili mbinu zilizotumika katika utafiti huu. Vipengele vilivyojadiliwa
ni eneo la utafiti, populesheni lengwa ya utafiti, sampuli na usampulishaji
86
kinachojumuisha sampuli, usamulishaji na aina ya usampulishaji, mbinu za ukusanyaji
wa data ambazo ni hojaji, usaili na mijadala ya vikundi lengani na mwisho ni kipengele
cha uchanganuzi wa data.
Sura ya nne ilijikita katika uwasilishaji, uchanganuzi na ufasiri wa data ya utafiti.
Matokeo yanaonesha kuwa, kwanza; 8.9% tu ya wasikilizaji ndio wanaoelewa mijadala
ya Bunge inayoendeshwa kwa ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza, 41.68%
hawaelewi, 14.58% wanaelewa baadhi ya sentensi na 34.84% wanaelewa baadhi ya
maneno. Majumuisho yanaonesha kuwa, kiwango cha uelewekaji wa mijadala ya
Bunge yenye kuhusisha ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza kinapanda kadri ya
kiwango cha elimu kinavyopanda na kinyume chake pia. Pili; matokeo yanaonesha
kuwa 81.68% ya wasikilizaji hawafurahishwi na ubadilishaji wa Kiswahili na
Kiingereza Bungeni. Hata hivyo idadi ya wasiofurahishwa inapungua kadri ya kiwango
cha elimu kinavyoongezeka. Pia, tumeona kuwa pamoja na kutofurahishwa na namna
hii ya uzungumzaji Bungeni siyo sababu pekee inayosababisha wananchi kutofuatilia
mijadala ya Bungeni inayorushwa kupitia vyombo vya habari. Sababu nyingine ni
pamoja na; (1) kukosa muda wa kuangalia au kusikiliza kutokana na kuwa na shughuli
nyingi, (2) umaskini unaosababisha kukosa redio au runinga, (3) ukosefu wa umeme,
(4) Wabunge kutochangia hoja muhimu zenye kutia hamasa ya kusikiliza na (5)
kutokuwa na mazoea ya kusikiliza mijadala ya Bunge.
Tatu, matokeo yanaonesha kuwa, ili kuondoa athari za ubadilishaji msimbo kwa
wasikilizaji, 85.55% ya wasikilizaji wanapendekeza Kiswahili kuwa lugha pekee ya
kuendeshea shughuli za Bunge. Sababu zinazotolewa kutetea hoja hii ni pamoja na
87
kuwa; (1) Kiswahili kinaeleweka kwa watanzania wengi, (2) ni lugha ya taifa na
inafungamana na utamaduni wa watanzania, (3) kinaleta umoja na kuondoa ubaguzi,
(4) kinaepusha utumwa wa kifikra, (5) ni lugha rasmi ya Bunge la Afrika na (6)
itasaidia kukilinda na kukikuza Kiswahili.
Sura ya tano inahusu hitimisho na mapendekezo. Sura hii imejikita katika kuelezea kwa
mhitasari mambo yaliyojadiliwa katika sura za awali. Pia katika kipengele cha
mapendekezo pendekezo la utafiti mwingine linatolewa.
5.3 Mapendekezo
Kwa kawaida matokeo ya utafiti huanzisha tatizo la utafiti mwingine. Utafiti huu
ulijikita katika ubadilishaji msimbo na athari zake kwa wasikilizaji. Wasikilizaji katika
utafiti huu walimaanisha wananchi walio nje ya Bunge wanaofuatilia Bunge kupitia
vyombo vya habari hasa redio na runinga. Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania ibara ya 67 (a) mojawapo ya sifa ya mtu kuwa mbunge ni kuwa
awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza. Kwa kuzingatia hili
upo uwezekano wa kuwepo wabunge wanaofahamu kusoma na kuandika Kiswahili tu
na wasiofahamu Kiingereza.
Pamoja na hayo kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2004 kanuni ya 118(1) inaeleza
kuwa Shughuli za Bunge zitaendeshwa katika lugha ya Kiswahili au ya Kiingereza, bila
tafsiri ya lugha hizo kutolewa. Kutokana na hali hii wabunge wenye kuelewa
Kiingereza kwa namna moja au nyingine huchangia hoja kwa kubadilisha Kiswahili na
Kiingereza na wakati mwingine Kiingereza pekee. Pia miswada mingi ya Bunge
88
huandikwa katika Kiingereza tu. Kwa mantiki hii kuna haja ya kufanya utafiti
unaoendana na huu utakaojikita katika kubainisha matumizi ya Kiingereza Bungeni na
athari zake kwa wabunge. Katika utafiti huu kwa kuzingatia viwango mbalimbali vya
elimu vya wabunge, ulenge:-
I. kubainisha kama wabunge wanaelewa mijadala inayoendeshwa kwa
Kiingereza au kubadilisha Kiswahili na Kiingereza na pia kama wanaelewa
miswada inayoandikwa kwa Kiingereza.
II. ubainishe mtazamo wa wabunge kuhusu namna ya uzungumzaji ya
ubadilishaji wa Kiswahili na Kiingereza Bungeni.
III. ubainishe maoni ya wabunge kuhusu lugha inayofaa kuendeshea shughuli za
Bunge na kuandikia miswada na sheria za nchi na kwa namna gani lugha hiyo
iwezeshwe kukidhi dhima hiyo.
5.4 Hitimisho
Sura hii ilihusu hitimisho na mapendekezo ambapo kwanza inaanza kwa utangulizi
unaodokeza vipengele muhimu katika sura nzima. Sehemu iliyofuatia ni muhitasari
unaodokeza kwa ufupi lakini kwa undani mambo muhimu yaliyojadilwa katika sura za
awali za tasnifu hii. Baada ya hapo ni sehemu inayotoa mapendekezo ya utafiti
mwingine na kisha hitimisho.
89
MAREJEO
Becker, K.R. (1997) “Spanish/English Bilingual Code-Switching Asyncretic
Model”, in Bilingual Review, Volume 22 pp 1, 3 – 28
Bell, A. (1984) “Language Style as Audience Design”, in Coupland, N. and Jaworski
(1997, eds.) Sociolinguistics, a Reader and Coursebook, pp. 240-50
Bentahila, A. and Davies E. (1983) “The Syntax of Arabic-French Code-switching” in
Lingua 59, pp 301-330
Berk-Seligson, S. (1986) “Linguistic Contraints on Intra-sentential Code-switching:
A Study of Spanish/Hebrew Bilingualism” in Language in Society Volume
15 (3), pp 313-348
Bloomfield, J. (1927) “Literate and Illiterate Speech”, in American Speech, Volume 2,
pp 432 – 439
Bokamba, E. G (1988) “Code Switching, Language Variation and Linguistic Theory”
Evidence from Bantu Languages” in Lingua Volume 76
Brice, A (2000) “Code Switching and Code Mixing in the ESL Classroom, A Study of
Pragmatic and Syntactic Features, Advances in Speech Language
Pathology”, in Journal of the Speech Pathology Association of Australia,
Volume 1, No. 20, pp. 19-28
Broomfield, G.W. (1931) Sarufi ya Kiswahili, London, The Sheldon Press
Chachage, S.L.C. (2004) “Kiswahili Katika Muktadha wa Utandawazi” katika
Kiswahili na Utandawazi, Dar es Salaam, Baraza la Kiswahili la Taifa, Uk.
1-17
90
Chung, H.H. (2006) “Code Switching as a Communicative Stratey: A Case Study of
Korean-English Bilingual”, in Bilingual Research Journal, Defence
Language Institute, pp 293-307
Clyne, M. (1967) Transference and Triggering Martinus Nijhof, The Hague.
Cooper, H.M (1989) Personal Management and Practise, Eastlagh
Hampshire, DP Publishing House
Cohen, L (2000) Research Methodology in Education, 5th
ed, London, Ruttedge Farmer
Cromdal, J. (2000) Code Switching for All Practical Purposes, Bilingual
Organization of Children’s Play, Linkoping Universilet, New York. St
Mattin’s Press Inc.
Enon, J. C. (1998) Education Research, Statistics and Measurements, Kampala,
Makerere University
Fishman, J. (1971) “The sociology of Language: An Interdisciplianary Approach to
Language and Society”, in J. Fishman (ed) Advances in the Sociology of
Language, The Hague, Mouton, pp 217-404
Gardnne-Chloros, P. (1991) Social Development of Linguistic Change in Bilingual
Austria, New York, Academic Press
Gikambi H. (2010) Kiswahili: a UN Working Language?
http://www.azaniansea.com/2010/06/kiswahili-un-working-language.html
retrieved on Monday, 27th
June, 2011
Grosjean, F (1982) Life With Two Languages, An Introduction to Bilingualism,
Cambridge Mass and London, Harvard University Press
Habwe, J. na Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili, Nairobi, Phoenix
Publishers Ltd
91
Hammink, J.E (2000) A Comparison of the Code Switching Behavior an Knowledge of
Adults and Children, http://hamminkj.tripod.com/hamminkCS.pdf retrieved
on Wednesday, 15th
December, 2010
Haugen, E. (1973) “Bilingualism, Language Contact and Immigrant Languages in the
United States”, A Research Report 1956-1970 in Sebeok, T.A. (Ed) Current
Trends in Linguistics, The Hague, Mouton de Gruyter
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (2005) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya Mwaka 1977, Dar es Salaam, Mpigachapa Mkuu wa Serikali
Kachru, B.B (1982) “The Bilingual’s Linguistic Reportoire” in Valdman, A et al (Eds)
Issues in International Bilingual Education, New York, Plenum Press
Kadeghe, M. (2000), The Implication of Bilingualism in Learning and Teaching: The
Case of Tanzania Sekondary Schools, Dar es Salaam, University of Dar es
Salaam, Unpublished Doctorial Thesis
Kalong, R.I.A.S. (2008) Code Switching in Informal Among a Group of 4th
Year TESL
Students of UTM, Univesiti Teknoloji Malaysia, Unpublished Bachelor
Degree Project
Kanyuma, Y. (2005) Social Motivations for Code-Switching Among Members of
Primary School Communities: A Case Study of Rubour Ward, Tarime
District, University of Dar es Salaam, Unpublished M.A Dissertation
Kiango, J.G. (2004) “Ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na
Moja” katika Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na Moja, Dar es Salaam,
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Kibogoya, M. A (1998) “Single Word Switches in Kiswahili/English Codeswitching”
in Journal of Linguistics and Language in Education Volume 4, pp 1-23
92
Kothari, C. J. (2004) Research Methodology, Methods and Technique, New Delhi
India: International (P)
Legele, K. (1987) “Kiswahili na Lugha Nyingine katika Harakati za Kudai Uhuru
Tanganyika (1945-1961)”, katika Kiswahili, Juzuu la 54/1 na 54/2, Dar es
Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, uk.152-166
Leung, C.H. (2010) An Empirical Study on Code Mixing in Print Advertisements in
Hong Kong, http://www.scialert.net/fulltext/?doi=ajm.2010.49.61&org=10,
retrieved on Friday, 10th
December, 2010
MacWilliam, A. na Chuwa, A. (1990) “Kubadili Msimbo Bungeni” katika Kiswahili
Juzuu 57, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Uk. 33-45
Maggati, C. (2004) The Influence of Kiswahili on Non-Bantu Languages: The Case of
Dholuo in Tarime, University of Dar es Salaam, Unpublished M.A
Dissertation
Massamba, D.D.P. (1993) “The Role of Language in Education and Research” in
Preceedings African/Japanese Scholars Conference for Cooperation in
Educational, Cultural and Environmenatal Spheres in Africa, Tokyo
Meeuwis, M. na Blommaert, J.(1998) “A Monolectal View of Code-Switching,
Layered codeswitching among Zairians in Belgium”, in Peter Auer (ed.),
Code-switching in Conversation, New York, Routledge, pp 76-98
Mekacha, R.D.K. (2000) Isimujamii: Nadharia na Muktadha wa Kiswahili, Minoo city,
Osaka, Japan Osaka, University of Foreign Studies
Mirloy, L. na Muysken, P. (1995) One Speaker, Two Languages, Cross Disciplinary
Perspective on Code Switching, Cambridge University Press, Cambridge
93
Mochiwa, Z.S.M (1979) The Impact of Kiswahili Language on Ethnic Languages: A
Case Study From Handeni Disrict. Unpublished M.A Dissertation,
University of Dar es Salaam
Msanjila Y.P (2004) “Kiswahili Kitumike Kufundishia Shule za Sekondari na Elimu
ya Juu Tanzania” katika Kiswahili katika Karne ya Ishirini na Moja, Dar
es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Msekwa, P. (2000) Bunge la Kwanza Katika Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa
Tanzania: 1995-2000, Dar es Salaaam Tanzania, DUP {1996} LTD
Mulokozi M.M.(2009) “Mustakabali wa Kiswahili Katika Ukanda wa Maziwa Makuu”
katika Mulika Na. 28, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Mutembei, A (2001) Poetry and Aids in Tanzania: Changing Metaphor and
Metonymies in Haya Oral Tradition, Research School of Asian, African
and Amerindian Studies, Netherlands, Laiden University, Unpublished
Doctorial Thesis
Muysken, P (2000) Bilingual Speech, A Typology of Code-mixing, Cambridge,
Cambridge University Press
Mwansoko, H.J.M. na Tumbo-Masabo, Z.N.Z (1996), Matumizi ya Kiswahili Bungeni,
Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Myers-Scotton, C (1983) “The Negation of Identities in Conversation: A Theory of
Markedness and Code Choice”, in International Journal of the Sociology of
Language, Volume 44
__________, (1993) Duelling Languages: Grammatical Structure in Code Switching,
Oxford, Clarendan Press
94
Nsekela, A.J. (1965) Minara ya Historia ya Tanganyika: Tanganyika Hadi Tanzania,
Dar es Salaam, Longman Tanzania
Nyerere, J.K. (1974) Binadamu na Maendeleo, Naorobi, Oxford University Press
Pandit, Ira (1986) Hindi English Code Switching: Mixed Hindi English, Dheli:
detta Book Center
Pfaff, C. (1979) “Contraints on Language-mixing: Intrasentential Code-switching and
Borrowing in Spanish/English Language” in Journal of the Linguistic
Society of America 55(2), pp 291-318
Poplack, S. Sankoff, D. and Miller C. (1988) “The social Correlates and Linguistic
Processes of Lexical Borrowing and Assimilation”, in Linguistics 26, pp 47-
104
Rubagumya, C.M. (1986) “Planning in the Tanzania Education System: The Problems
and Prospects”, Journal of Multilingual and Multicultural Development,
Volume 7, No. 4, pp 289-300
Rubanza, Y.I. (2006) “Utandawazi bila Lugha Miliki? Nafasi ya Kiswahili” katika
Makala ya Kongamano la Kimataifa la Jubilee ya TUKI-2005 (2), Dar es
Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Salimu-Sawe, K (2008) “Ubadilishaji Msimbo wa Wanautatu-lugha: Uchunguzi wa
Kisarufi” katika Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za
Kiafrika, Nairobi, Moi University Press
Sapir, E. (1958) Selected Writings in Language Culture and Personality, Berkely,
University of Califonia Press
_________, (1921) Language, New York, Harcourt Brace
95
Shaffer, D. (1975) “The Place of Code-switching in Linguistic Contact” Second Annual
Forum, Linguistic Association of Canada
Sewangi, S.S. (2004) “Nafasi ya Lugha katika Maendeleo ya Uchum: Mfano wa
Kiswahili katika Tanzania” katika Kiswahili katika Karne ya Ishirini na
Moja, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Uk. 87-93
Shoo, G (2004) “Nafasi ya Kiswahili Katika Vyombo vya Habari Wakati huu wa
Utandawazi” katika Kiswahili na Utandawazi, Dar es Salaam, Baraza la
Kiswahili la Taifa, Uk. 79-87
Sridhar, S. and Shridhar K. (1980) “The Syntax and Psycholinguistics of Bilingual
Code-mixing” in Studies in the Linguistic Sciences, Volume 10, No. 1
Swigart, L. (1992) “ Two Codes or One? The insiders’ View and the Description of
Codeswitching in Dakar”, Journal of Multilingual and Multicultural
Development, pp 13:83-102
Tabouret-Keller, A. (1989) “Seminar danthropologie du langage”, MSH Informations,
Bulletin de la Fondation des Sciences de I’Homme NO. 59, pp 15-17
Tabouret-Keller, A. and Le Page R.B. (1986) “The Mother-Tongue Metaphor”, Grazer
Linguistische Studien, Volume 27, pp 249-259
Tay, W.W. (1989) “Code Switching and Code-mixing as a Communicative
Strategy in Multilingual Discourse”, Journal of World Englishes, Volume 8,
pp 407-417
Vans, V. (1990) Introduction to Social Research, mcgraw-Hill, Unwin Hyman
Weber, H. (1985) A Dictionary of Phonetics and Linguistics, Longman, Harlow
Weinreich, U. (1953) Languages in Contact, The Hague, Mouton
96
Whorf, B.L. (1958) Language, Thought and Reality, New York, MIT & John Wiley &
Sons Ltd
Wu, Y. (1985) “Code-Mixing by English-Chinese Bilingual Teachers of the People’s
Republic of China”, Journal of World Englishes, Volume 4(3), pp.303-317
97
VIAMBATANISHO
KIAMBATANISHO I: HOJAJI KWA WASIKILIZAJI
MAELEKEZO: Weka tiki katika kisanduku unachoona kina jibu sawa kwa swali la 2
hadi 5 na 7 hadi 11 (a) na 12 hadi 15. Kwa swali la 6, 11 (b) na 15 hadi 18 andika
maelezo mafupi katika sehemu zilizo wazi. Unaombwa kutomuuliza mtu wala kusoma
kokote bali toa maoni yako kwa kuzingatia uelewa wako tu.
1. Jina …………………………………………………(si lazima)
2. Mahali unapoishi:- vijijini [ ] mjini [ ]
3. Jinsia: mme [ ] mke [ ]
4. Umri: 18-27 [ ] 58-67 [ ]
28-37 [ ] 68-77 [ ]
38- 47 [ ] 78…. [ ]
48-57 [ ]
5. Kiwango cha elimu:-
Shule ya msingi/kati [ ]
Shule ya sekondari [ ]
Chuo/chuo kikuu [ ]
6. Kazi…………………………………………………..
7. Unaweza kuzungumza na au kuelewa lugha gani?
a) Kiswahili [ ]
b) Kiingereza [ ]
c) Nyinginezo [ ]
d) (itaje/zitataje)…………………………………
8. Wabunge wamekuwa na kawaida ya kuchangia hoja bungeni kwa kuchanganya
Kiswahili na Kiingereza. Unalifahamu hili?
a) Ndiyo [ ]
b) Sijui [ ]
c) Sina uhakika [ ]
9. Je, wabunge wanapochanganya Kiswahili na Kiingereza huwa unaelewa
kinachozunguzwa?
a) Ndiyo [ ]
b) Kwa baadhi ya sentensi [ ]
c) Naelewa neno moja moja [ ]
d) Sielewi kabisa [ ]
98
10. Pale ambapo Mbunge anachangia hoja kwa kuchanganya Kiswahili na
Kiingereza na hivyo kusababisha usimuelewe. Huwa unatimia mbinu gani
kuwamuelewa?
a) Nafuatilia kwenye kamusi [ ]
b) Nauliza kwa watu wengine [ ]
c) Nafuatilia magazetini na kwenye taarifa za habari (redio/TV) [ ]
d) Sifuatilii na hivyo kutoelewa chochote kuhusu kilichosemwa [ ]
11. Soma sentensi ifuatayo; -
“zipo advantage za kutumia long term bonds na advantage ya kwanza ni
non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia internal source of
finance lakini rahisi ku-meet our development goals….” (12 Julai, 2007)
a) Je umeelewa kinachozungumzwa?
I. Ndiyo [ ]
II. Nimeelewa baadhi ya sentensi [ ]
III. Nimeelewa baadhi ya maneno [ ]
IV. Sijaelewa kabisa [ ]
b) Kama umeelewa kwa maneno yako eleza kwa ufupi umeelewa
nini………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………
…………………………………………………………
12. Je, huwa unafuatilia majadiliano ya Bunge kupitia redio, luninga/TV na ua
magazeti?
a) Ndiyo [ ]
b) Mara chache [ ]
c) Sifuatilii kabisa [ ]
d) Sina uhakika [ ]
13. Je, uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza unakusababisha ushindwe
kufuatilia mijadala ya bungeni?
a) Ndiyo [ ]
b) Kwa kiasi fulani [ ]
c) Hapana [ ]
14. Inasemekana ni jambo la kawaida kusikia watu wakichanganya lugha kama vile
Kiswahili, Kiingereza na hata lugha za asili katika mazingira yasiyo rasmi (
kama vile vijiweni, kwenye daladala, virabu vya pombe, sokoni n.k). Je,
unajisikiaje namna hiyo hiyo ya uzungumzaji inapojitokeza bungeni?
a) Sifurahishwi [ ]
b) Sijali [ ]
c) Ninajisikia kawaida [ ]
d) Napendezwa [ ]
99
15. Unashauri ni lugha gani itumike kuendeshea shughuli za Bunge.
a) Kiswahili na Kiingereza [ ]
b) Kiswahili tu [ ]
c) Kiingereza tu [ ]
d) Nyingine [ ] Itaje/zitaje…………………….
16. Kwa nini umechagua hiyo/hizo lugha hapo juu? (eleza kwa ufupi)
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
17. Unaishauri nini Serikali kuhusu lugha rasmi ya/za kutumia katika shughuli za
Bunge.
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………
18. Ukikutana na Mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali yake au ya wenzake ya
kuchanganya Kiswahili na Kiingereza
Bungeni………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
………………………………………………………..
Ahsante sana kwa ushirikiano wako!
100
KIAMBATANISHO II: MASWALI YA MWONGOZO WAKATI WA USAILI11
1. Baadhi ya wabunge wamekuwa na tabia ya kuchanganya Kiswahili na
Kiingereza wakati wa mijadala Bungeni. Je, una habari kuwa aina hii ya
uzungumzaji inatokea katika vikao rasmi vya Bunge?
2. wabunge wanazungumza Bungeni kwa niaba ya wananchi (wasikilizaji) na
wasikilizaji wanapaswa kufahamu wanachozungumza. Je, wabunge
wanapozungumza kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza huwa unaelewa
kinachozungumzwa? (Baada ya hapo mtafiti alisoma sentensi kwenye matini
kutoka kumbukumbu za Bunge na kumtaka mtafitiwa kutoa maana yake kwa
Kiswahili).
3. Pale ambapo mbunge anachangia hoja kwa kuchanganya Kiswahili na
Kiingereza na hivyo kusababisha usielewe. Je, huwa unatumia mbinu gani
kuelewa au kupata ujumbe uliokusudiwa?
4. Ni jambo la kawaida kusikia watu wakichanganya Kiswahili, Kiingereza na
wakati mwingine lugha za asili (k.v. Kisukuma, Kikerewe, Kihaya n.k) katika
mazungumzo yasiyo rasmi (k.v. baa, kwenye daladala n.k ). Je, unadhani inafaa
aina hiyo ya uzungumzaji ijitokeze katika mijadala rasmi ya Bunge?
5. Huwa unafuatilia mijadala ya Bunge kupitia vyombo vya habari?
6. Je, uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza huwa unakufanya kutopendelea
kufuatilia mijadala ya Bunge? Kama kuna sababu nyingine zitaje.
7. Wewe kama mdau na mlengwa wa mijadala iendeshwayo Bungeni, ni athari
gani unazozipata kutokana na wabunge kuchanganya Kiswahili na Kiingereza?
8. Kanuni za kudumu za Bunge zinamruhusu mbunge kuchangia mjadala kwa
Kiswahili au Kiingereza bila tafsiri kutolewa. Je, hii inafaa? Kama haifai kama
mdau unaishauri nini serikali kuhusu ni lugha gani inayofaa/zinazofaa
kuendeshea shughuli za Bunge?
9. Kwa nini umechagua lugha hiyo/hizo kuwa lugha rasmi ya/za kuendeshea
mijadala Bungeni?
10. Ukikutana na mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali ya wabunge
kuchanganya Kiswahili na Kiingereza Bungeni?
11
Kabla ya kuanza kwa maojiano mtafiti alimsomea mtafitiwa matini kutoka kumbukumbu rasmi za
Bunge zinazoonesha ni jinsi gani wabunge wanavyochanganya Kiswahili na Kiingereza. Hii ilisaidia
kumjengea uelewa mtafitiwa.
101
KIAMBATANISHO III: MASWALI YA KUONGOZA MIJADALA KATIKA
VIKUNDI LENGANI12
1. Je, huwa unafuatilia mijadala ya Bunge kupitia vyombo vya habari?
Vitaje/kitaje?
2. Kwa nini unapendelea/haupendelei kufuatilia majadiliano ya Bunge?
3. Wakati wa mijadala baadhi ya wabunge wamekuwa na kasumba ya
kuchanganya Kiswahili na Kiingereza. Je, una mtazamo gani kuhusu namna
hiyo ya uzungumzaji Bungeni?
4. Je, wabunge wanapozungumza Bungeni kwa kuchanganya Kiswahili na
Kiingereza huwa unaelewa wanachozungumza?
5. Sikiliza kwa makini sentensi hizi kutoka kumbukumbu za Bunge na kisha
uelezee ulichoelewa kwa Kiswahili (rejea kiambatanisho III).
6. Je, namna hii ya uzungumzaji Bungeni inakusababishia usipendelee kufuatilia
mijadala ya Bunge?
7. Ikitokea kwamba hujaelewa huwa unatumia njia na mbinu gani kuelewa
alichomaaanisha mbunge?
8. Kikanuni Kiswahili na Kiingereza zote zinaruhusiwa kutumika kuendeshea
mijadala ya Bunge. Je, hii ni sawa? Unatoa ushauri gani kwa serikali kuhusu
lugha ya kutumika Bungeni?
9. Ukikutana na mbunge wako utamshauri nini kuhusu hali ya wabunge
kuchanganya Kiswahili na Kiingereza Bungeni?
12
Kama ilivyokuwa katika usaili watafitiwa walisomewa matini kutoka kumbukumbu za bunge zenye
mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza.
102
KIAMBATANISHO IV: MATINI KUTOKA KUMBUKUMBU ZA BUNGE
MATINI: A
12 JULAI, 2007 Uk. 30
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nilitaka nianze na kuelezea umuhimu wa wa
infrastructure katika maendeleo ya nchi yetu, sisi Tanzania tumepata bahati kubwa
sana, bahati yetu ni ambako Mungu aliamua nchi hii iwe hapa iliko leo na maana yake
ni ni geography position ya nchi yetu. Sasa tunapopanga mipango yetu lazima tutumie
advantage ya jeografia yetu kwa sababu engine ya maendeleo ni infrastructure, mimi
sijui nchi yoyote iliyoendelea Duniani bila kuwa na infrastructure. Kwa hiyo
tunapokuwa tunapanga barabara zetu, tunapanga resources zetu lazima tujenge
barabara hizi kule ambako tunaamini tukipeleka pesa zetu zitarudi, kuna barabara
ambazo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu barabara ya kwanza ni Manyoni,
Itigi, Tabora na Kigoma. Siyasemi haya kwa sababu labda natoka Kigoma lakini
niwaambie advantage tukijenga barabara hii Kongo ya Mashariki kuna mzigo wa tani
miliono nne, tunao mzigo Burundi, tunao mzigo Rwanda ukijenga ile transit business
peke yake itatuingizia pesa nyingi sana kwenye nchi yetu kwa hiyo lazima maamuzi
yetu yaende haraka tuweze kufanya vizuri kwenye area hiyo. Tunayo barabara ya
Tunduma, Sumbawanga, Mpanda mpaka Kanyani tunayo barabara Kigoma Nyakanazi,
Mwandiga, Manyovu, Mpanda, Tabora, Sumbawanga mpaka Kasanga Port. (Makofi)
MATINI B.
12 JULAI, 2007 Uk. 32-33
Mheshimiwa Spika, lakini nilitaka niongezea pia jambo lingine, jana rafiki yangu
Kaboyonga aliliongea hapa, ujenzi wa barabara unahitaji pesa nyingi sana na mimi
nakubali lakini liko suala la kutumia long term bonds, long term bonds ni sources of
finance ni govern papers hizi tunaziuza, ziko advantage za kutumia hizi long term
bonds na advantage ya kwanza ni non inflationary lakini advantage ya pili tunatumia
internal source of finance lakini rahisi ku-meet our development goals tumepanga
kufanya jambo hili hatuna pesa government inauza zile government bonds kwa hivi
financial institutions miaka 15 inapofika miaka 10 hujaweza kulipa zile pesa ni rahisi
una-issue nyingine ili pesa imlipe huyu unaenda mbele. Halafu tutumie load fund board
yetu iwe inatenga fedha kidogo kwa ajili ya kulipia hizo interest kwenye hizo long term
bonds zetu, nawaambieni tukifanya jambo hili nchi hii tutawashangaza Mataifa,
tutajenga nchi hii na tutaenda kwa kasi kubwa kweli kweli.
MATINI C.
12 JULAI, 2007:83
Mheshimiwa Spika, India is one of the best country katika Railway netwok,
tukachukue ma-expert waje watusaidie lakini liwe chini yetu. Tutakuja kupakiwa rangi
haya mabehewa tushindwe kuleta pamba Dar es Salaam kusafirishwa. Tutasafirisha
abiria na mizigo na bidhaa at the end of the day hatuna kitu. Halafu unampa contract ya
25 years is not a joke. (Makofi)
103
MATINI D.
14 JULAI, 2004 Uk. 82-83
Mimi kama mwanataaluma nawaachieni sina tatizo kama nchi hii inaingia kwenye
southern grid. Bora mradi iingie ikiwa na umeme wa kutosha siku nyingine tukiwa na
matatizo watuuzie na siku nyingine tuwauzie wao. Lakini Wizaara ya Nishati na
Madini inaendeshwa na watu utadhani ni mamluki kumbe ni Watanzania. Mimi
nashindwa hata kuwaelewa. (Makofi)
Ninajua ni wasomi najua kila ninaloelewa wanalielewa, najua yako mengine
wanaelewa kuliko mimi, sasa ni nguvu ipi inayowasukuma waihujumu Tanzania. Mimi
najua arrogance ya Wizara hii niwaambie tu inawezekana wana-rub shoulders na press
and bosses tutawaadhibu baadaye. You wili answer there is no way nchi hii itaendelea
kuteseka sababu mtu mmoja analeta maamuzi yanayoua wananchi.
Mheshimiwa spika, uongozi tunapokezana, leo mimi kesho wewe, kesho kutwa yeye,
mtondogoo wao. I better worn you today comrades, you will not afford. Hatutavumilia
matendo batili ya makusudi kwa ajili ya starehe ya watu wachache. (Makofi)
Siku moja nilimwuliza Yona hivi ofisini kwenu minister ni nani ni wale wengine
nisiongea nao au ni wewe tunayeongea wote. Alisema kwani wewe hujui nani
aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nikamwambia uliteuliwa
wewe. But you don’t seem to be. Why don’t you understand me when we talk here
together and when you to your office you are powerless. What is wrong? (Makofi)