51
Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli ya Tatu Taasisi ya Elimu Tanzania Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 1 25/04/2019 12:50

Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

  • Upload
    others

  • View
    49

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali

Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini

Moduli ya Tatu

Taasisi ya Elimu Tanzania

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 1 25/04/2019 12:50

Page 2: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

ii

© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2018

Toleo la Kwanza, 2018

ISBN: 978 - 9976 - 61 - 801 - 3

Taasisi ya Elimu TanzaniaS.L.P. 35094Dar es Salaam

Simu : +255 22 2773005 / +255 22 277 1358Faksi: +255 22 2774420Baruapepe: [email protected]: www.tie.go.tz

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa, kurudufu au kutoa andiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 2 25/04/2019 12:50

Page 3: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

iii

Yaliyomo

Ukurasa

Utangulizi ...................................................................................................... iv

Shukurani....................................................................................................... ix

Vifupisho........................................................................................................... x

Sura ya Kwanza Elimu ya mazingira ………………………....……...................................….. 1

Sura ya Pili Virusi vya UKIMWI na UKIMWI……………........................…........……… 8

Sura ya Tatu Haki na wajibu wa mtoto…………….......................…………........……….. 13

Sura ya Nne Elimu ya jinsia ………………...........................……………..........…………. 18

Sura ya Tano Afya na lishe ……………….............................……………......……………. 25

Sura ya Sita Ushauri na unasihi ………............................................................…………… 31

Sura ya Saba Ulinzi kwa mtoto…………………..................................….......……………. 35

Faharasa …………………………………….……………………………….. 40

Marejeleo …………………………………….………………………………. 41

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 3 25/04/2019 12:50

Page 4: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

iv

UtanguliziUsuliMafunzo kazini kwa mwalimu ni jambo la msingi sana ili kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji kufanyika kwa ufanisi. Mafunzo humuongezea mwalimu maarifa na stadi kulingana na mabadiliko yanayotokea siku hadi siku. Hivyo, ni muhimu kwako mwalimu wa elimu ya awali kupata mafunzo uwapo kazini. Mafunzo hayo yatakusaidia kujenga umahiri katika kutekeleza mtaala wa elimu ya awali kwa ufanisi na hivyo kuboresha kiwango cha elimu katika ngazi husika na ngazi nyingine zinazofuata. Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) 2012- 2016, vimebainisha kuwa Elimu ya Awali ni moja kati ya vipaumbele vya serikali. Aidha, kila shule ya msingi inatakiwa kuwa na darasa la elimu ya awali. Mwaka 2016, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) iliboresha mtaala wa elimu ya awali. Mtaala huo ulianza kutumika rasmi mwaka 2017. Baada ya uboreshaji, baadhi ya walimu wa elimu ya awali walipata mafunzo ya namna ya kutekeleza mtaala huo.

Hata hivyo, imeonekana kuwa kuna haja ya kuwajengea uwezo walimu wote wa elimu ya awali katika ufundishaji na ujifunzaji wa mtoto. Hivyo, TET kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Aga Khan Foundation (AKF) na Shirika la Umoja wa Mafaifa la Kuhudumia Watoto “UNICEF “ waliandaa moduli za mafunzo kazini kwa walimu wa elimu ya awali kwa kuzingatia mtaala wa elimu ya awali wa mwaka 2016.

Lengo la moduliLengo la moduli hii ni kukuwezesha kujenga uelewa wa namna ya kuchopeka masuala mtambuka katika kutekeleza mtaala wa elimu ya awali.

Mlengwa Mlengwa mkuu wa moduli hii ni mwalimu wa elimu ya awali aliye kazini. Moduli hii inaweza pia kutumiwa na walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule, maafisa elimu wa wilaya na wadau wengine wa elimu.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 4 25/04/2019 12:50

Page 5: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

v

Jinsi ya kutumia moduliMwalimu unatakiwa kuisoma moduli hii na kufanya kazi mbalimbali zilizoainishwa. Utashirikiana na wenzako kama itakavyokuwa imeelekezwa. Aidha, unatakiwa kuwashirikisha walimu wenzako katika changamoto mbalimbali ulizokumbana nazo katika ufundishaji na ujifunzaji ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kuzitatua. Muundo wa moduliModuli hii imegawanyika katika sura saba. Sura ya kwanza ni Elimu ya mazingira, Sura ya pili ni Virusi vya UKIMWI na UKIMWI na Sura ya tatu ni Haki na wajibu wa mtoto, Sura ya nne ni Elimu ya jinsia, Sura ya tano ni Afya na lishe, Sura ya sita ni Ushauri na unasihi na Sura ya saba ni Ulinzi kwa mtoto.

Kila sura ina utangulizi, umahiri wa kujifunza na jaribio la awali ambalo mwalimu utafanya ili kujipima uelewa wako kabla ya kuanza kusoma sura inayohusika. Vilevile, kila sura ina maudhui utakayojifunza, shughuli, tafakuri na jaribio baada ya kujifunza ambalo utalifanya ili kupima ulichojifunza katika sura inayohusika. Aidha, katika vipindi tofauti, utafanya shughuli mbalimbali zilizopo mwishoni mwa moduli katika jumuiya za ujifunzaji.

Utaratibu wa utoaji mafunzoMuda wa mafunzo kwa kutumia moduli hii pamoja na moduli nyingine zilizomo katika mpango huu ni mwaka mmoja. Mwalimu unatarajiwa kukamilisha moduli zote nne (4) za mafunzo husika. Moduli hizo ni Utoaji wa elimu ya awali, Ukuaji na ujifunzaji wa mtoto, Uchopekaji wa masuala mtambuka katika mtaala wa elimu ya awali na Utekelezaji wa mtaala wa elimu ya awali. Pamoja na kujifunza maudhui yaliyomo katika moduli hizi, unapaswa kutumia maarifa na ujuzi unaopata katika muda wote unapokuwa kazini ili kuboresha ufundishaji wa ujifunzaji wa mtoto.

Mwalimu, utakabidhiwa moduli husika na utajifunza mwenyewe katika kituo chako cha kazi. Unapaswa kusoma na kufanya kazi zote zilizoainishwa katika kila moduli. Unatakiwa pia kujipangia utaratibu wa kuzisoma moduli hizo kwa ukamilifu kwa kuzingatia muda wa mafunzo uliopangwa. Sambamba na hilo, kutakuwa na jumuiya za ujifunzaji katika ngazi ya shule na vituo vya ujifunzaji ndani ya kata ambapo mtakutana kwa ajili kubadilishana uzoefu, mafanikio na changamoto mlizokutana

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 5 25/04/2019 12:50

Page 6: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

vi

nazo katika ujifunzaji. Ujifunzaji katika jumuiya utaongozwa na shughuli zilizoainishwa mwishoni mwa kila moduli.

Aidha, ili kuhakikisha kwamba jumuiya za ujifunzaji zinafanyika kwa ufanisi, mnapaswa kukutana angalau mara moja kwa wiki katika ngazi ya shule, mara moja kwa mwezi katika ngazi ya kata na mara mbili kwa mwaka katika vituo vya walimu vya ujifunzaji ngazi ya kata.

Kabla hujaanza kusoma sura, unapaswa kufanya jaribio ambalo linaakisi maudhui ya sura husika. Baada ya kujifunza maudhui ya sura hiyo utafanya tena jaribio lile lile ili kupima uelewa wako baada ya kusoma sura husika ya moduli. Vilevile, utapewa kazimradi za kufanya ambazo zitajumuishwa katika upimaji utakaofanyiwa.

Upimaji wa mafunzoUpimaji wa mafunzo utafanyika ili kubaini kama umejenga umahiri kama ilivyokusudiwa na utahusisha mambo yafutatayo:

i. Mkoba wa kazi ambao utajumuisha vitu mbalimbali kama vile kazi za vikundi, zana za kufundishia na kujifunzia, machapisho mbalimbali uliyotumia katika kujifunza na majibu ya shughuli mbalimbali ambazo umezifanya katika moduli husika.

ii. Kazimradi itahusisha zana zinazogusa umahiri sita zilizopo katika mtaala na muhtasari wa elimu ya awali ambazo zitahakikiwa mwisho wa mafunzo.

iii. Uangalizi wa ufundishaji ndani na nje ya darasa utafanyika mara tatu (3) kwa muda wote wa mafunzo. Uangalizi utafanywa na mwalimu mkuu, afisa elimu kata na mthibiti ubora wa shule. Zana itakayotumika katika uangalizi itatoka kwenye kiongozi cha mthibiti ubora wa shule.

Upimaji wa mafunzo utafanywa na mwalimu mkuu katika ngazi ya shule na afisa elimu kata katika ngazi ya kata. Aidha, wathibiti ubora wa shule ngazi ya wilaya na kanda na maafisa elimu wa wilaya na mkoa watasimamia zoezi zima la ujifunzaji na upimaji ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yana ubora uliokusudiwa. Mwalimu unapaswa kusoma na kupimwa katika moduli zote nne na kufaulu kwa kiwango kisichopungua alama C ili kuweza kutunukiwa cheti cha kukutambua kama

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 6 25/04/2019 12:50

Page 7: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

vii

mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali la 1 na la 2.

Jedwali 1: Mwongozo wa upimaji

Mkoba wa kazi KazimradiUangalizi wa

ufundishajiJumla

20 20 60 100

Jedwali 2: Viwango vya ufauluAlama Daraja Kiashirio75 – 100 A Bora64 – 74 B Vizuri sana44 – 63 C Vizuri35 – 43 D Inaridhisha0 – 34 F Dhaifu

Ufuatiliaji na tathmini ya mafunzo Kwa kuwa mafunzo yatafanyika katika ngazi ya shule na vituo vya ujifunzaji ndani ya kata, walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu wa wilaya ndio watakaokuwa wafuatiliaji wakuu wa mafunzo haya. Kutakuwa pia na ufuatiliaji katika ngazi ya taifa ikijumuisha TET, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kitengo cha elimu ya ualimu na idara ya usimamizi wa elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI).

Tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo Kazini kwa walimu wa elimu ya awali itafanyika baada ya kumaliza mafunzo. Lengo la tathmini hii ni kuona kama mafunzo yametekelezwa kama yalivyopangwa na kubaini changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji kwa ajili ya kuboresha. Tathmini hii itahusisha wadau mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi taifa. Zana za kufanyia tathmini zitaandaliwa na TET kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali. Baada ya tathmini kukamilika, maboresho yatafanyika katika maeneo yanayohusika na mafunzo yataendelea. Tathmini zitafanyika pale inapobidi kulingana na mahitaji.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 7 25/04/2019 12:50

Page 8: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

viii

Tafsiri ya alama Katika moduli hii kuna alama mbalimbali zinazokuwezesha kutambua shughuli zinazotakiwa kufanyika wakati wa usomaji.

Alama Maelezo

Lengo au malengo yanayopaswa kufikiwa na msomaji wa programu hii katika sura.

Maswali ya kujiuliza kabla au hata wakati wa kuendelea kusoma.

Muhtasari uliotolewa kuhusu sura inayohusika.

Marejeleo yaliyotumika ambayo yanapendekezwa uyasome ili kuelewa zaidi.

Tafakuri ambayo utaifanya katika sura inayohusika.

Kazi ya kufanya.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 8 25/04/2019 12:50

Page 9: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

ix

Shukurani

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatambua na kuthamini mchango muhimu wa washiriki waliofanikisha uandishi wa moduli hii ya Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali.

TET inatoa shukurani za dhati kwa mchango uliotolewa na wataalamu wafuatao walioshiriki kutayarisha moduli hii:

Waandishi: Deborah Llewellyn, Vida Ngowi, Masumbuko Mpoli, Sharifa Majid, Sauda Hamis, Hanifa Mponji, Mathias Suyi, Flora Henjewele, Manjula Jogy, Christina Kamamba, Dkt. Richard Shukia, Davis Gisuka, Dkt. Daphina Mabagala, Rehema Mwawa, Nestory Mgimwa, Eric Kilala, Sister Cecilia Boniface, Wesket Mlagulwa, Dkt. Tandika Pambas, Edith Mdoe na Lomitu Mollel

Wahariri: Prof. Elinami Swai na Ambrose F. Mghanga

Msanifu: Rehema H. Maganga

Wachoraji: Alama Art and Media Production

Mratibu: Mwanahamisi A. Jokolo

Aidha, TET inatoa shukrani za pekee kwa Shirikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ‘UNICEF’ na Aga Khan Foundation (AKF) kwa kufadhili uandishi na ujaribishaji wa moduli hii.

Mwisho, TET inatoa shukurani kwa Global Partnership for Education (GPE) chini ya mpango wa kuboresha ufundishaji wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaojulikana kama Literacy and Numeracy Education Support (LANES) kwa kufadhili uhakiki na uchapaji wa moduli hii.

...................................Dkt. Aneth A. Komba Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 9 25/04/2019 12:50

Page 10: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

x

Vifupisho

AKF - Aga Khan Foundation

GPE - Global Partnership for Education

KKK - Kusoma, Kuandika na Kuhesabu

LANES - Literacy and Numeracy Education Support

MMEM - Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

TET - Taasisi ya Elimu Tanzania

OR-TAMISEMI - Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

UNICEF - United Nations Chidren's Fund

UKIMWI - Upungufu wa Kinga Mwilini

VVU - Virusi Vya UKIMWI

WyEST - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 10 25/04/2019 12:50

Page 11: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

1

Sura ya Kwanza

Elimu ya mazingira

Karibu katika sura ya kwanza ya moduli hii. Katika sura hii utajifunza kuhusu mazingira, namna ya kutunza mazingira na uharibifu wa mazingira. Sura hii inalenga kukusaidia kujenga umahiri utakaokuwezesha kufundisha elimu ya mazingira kwa ufanisi zaidi.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza dhana ya mazingiraii. kufafanua namna ya kutunza mazingiraiii. kueleza njia za uharibifu wa mazingiraiv. kuchopeka elimu ya mazingira katika ufundishaji na ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Neno mazingira lina maana gani?

2. Eleza umuhimu wa kufundisha elimu ya mazingira katika elimu ya awali.

3. Mambo gani yanasababisha uharibifu wa mazingira?

1.1 Dhana ya mazingira

Je, unafahamu nini juu ya dhana ya mazingira?

Pamoja na majibu uliyonayo, mazingira ni kila kitu kinachotuzunguka na kinachoweza kuathiri maisha yetu. Mazingira yanahusisha vitu vingi vikiwemo vyenye uhai kama wanyama na mimea. Vilevile, kwenye mazingira kuna vitu visivyo

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 1 25/04/2019 12:50

Page 12: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

2

na uhai kama hewa, udongo, miamba, mito, maziwa, bahari, milima, jua, mwezi, na nyota. Kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa mazingira ni kila kitu kilichopo karibu yako ambacho unaweza kukiona, kukigusa, kukihisi, kukinusa, au kukisikia.

Mazingira yana umuhimu kwa mwanadamu kama ifuatavyo:i. Mimea hutupatia chakula na hewa ya oksijeni. Kwa kupitia mimea, tunapata

hewa safi na pia tunapata malighafi za kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya binadamu.

ii. Kwa upande mwingine, wanyama hutupatia chakula kama vile nyama na maziwa, usafiri kama vile punda na ngamia, ngozi kama malighafi ya kutengeneza vitu mbalimbali na pia wanyama wa porini kwa ajili ya kuvutia utalii.

iii. Viumbe visivyo hai, navyo vina umuhimu katika maisha yetu na mazingira kwa ujumla. Kwa mfano, udongo unasaidia mimea kujishikiza na pia ni makazi kwa ajili ya baadhi ya wanyama na wadudu. Maji yanasaidia maisha ya viumbe hai na ni makazi ya baadhi ya mimea na wanyama. Vilevile, maji yanatunza hewa kwa ajili ya ustawi wa mimea na wanyama hao.

Ufundishaji wa elimu ya mazingira kwa watoto wa elimu ya awali ni muhimu kwao ili waweze kushiriki katika juhudi za nchi na dunia katika kuhakikisha kuwa wanatunza rasilimali zilizomo katika mazingira yanayowazunguka. Hivyo, ni vema ukatambua kuwa unao wajibu wa kuifikisha elimu ya mazingira kwa watoto wa elimu ya awali na kuwajengea tabia ya kuwa rafiki wa mazingira na rasilimali zake. Katika ngazi ya shule na darasa la elimu ya awali, mazingira ya ujifunzaji yanapaswa kuwa rafiki kwa watoto. Mazingira rafiki yanahusisha upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, vifaa stahiki vya usafi wa mazingira na uhimizaji wa elimu ya afya. Shule zenye madarasa ya elimu ya awali zinapaswa kutoa fursa ya kupata maji safi na salama ya kunywa na kuwahimiza watoto wanywe maji kila wakati.

Elimu ya mazingira katika ustawi wa jamii yoyote ni muhimu. Hivyo, utoaji wa elimu ya mazingira kwa watoto, utasaidia katika kufahamu dhana ya mazingira, vitu vilivyomo katika mazingira na kuwajengea watoto mtazamo chanya juu ya matumizi sahihi, na uhifadhi wa rasilimali zinazopatikana katika mazingira.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 2 25/04/2019 12:50

Page 13: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

3

Utunzaji wa mazingira ni suala linalomhusu kila mmoja katika jamii. Mazingira yanapaswa kutunzwa kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadaye. Desturi za utunzaji wa mazingira zinahusisha kutumia njia bora za kilimo kama vile matuta, kupanda miti na kutumia mbolea inayotokana na wanyama badala ya mbolea za viwandani. Njia nyingine ni kuacha shamba bila kulilima wala kupanda chochote ili lijirutubishe lenyewe, kupanda mimea jamii ya kunde ambayo hurutubisha udongo na kutumia zaidi viuatilifu salama. Aidha, kufuga idadi ndogo ya mifugo ni njia mojawapo ya kuzuia mmomonyoko wa udongo na kulinda vyanzo vya maji.

Unapaswa kujua njia mbalimbali za utunzaji wa mazingira ambazo zinaweza kufanywa na watoto kulingana na uwezo wao. Shughuli hizo ni kama vile kupanda miti, maua na nyasi, kufanya usafi wa mazingira na kutotupa takataka hovyo. Vilevile, unapaswa kuwasaidia watoto kujenga tabia ya kuthamini mazingira yanayowazunguka.

Fafanua mbinu utakazotumia kuwasaidia watoto kujenga tabia ya kutunza mazingira?

1.3 Uharibifu wa mazingira

Unaelewa nini kuhusu uharibifu wa mazingira?

Ujifunzaji wa kipengele hiki, utakuwezesha mwalimu, kutambua kuwa uharibifu wa mazingira ni hatarishi kwa maisha ya watu na viumbe vingine. Kiwango cha uharibifu wa mazingira kinatofautiana kutegemeana na chanzo kinachohusika. Uharibifu wa mazingira unahusisha ukataji wa miti hovyo, mmomonyoko wa udongo na umwagaji au utupaji hovyo wa vitu visivyofaa kwa matumizi ya binadamu na wanyama katika mazingira.

1.2 Utunzaji wa mazingira

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 3 25/04/2019 12:50

Page 14: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

4

Kielelezo namba 1: Mazingira machafu ya shule

Baada ya kujifunza maana na aina za uharibifu wa mazingira, je mwalimu, unafikiri ni mambo gani yanayosababisha uharibifu wa mazingira?

Bila shaka, kuna vyanzo vingi vya uharibifu wa mazingira. Vyanzo hivyo ni pamoja na utiririshaji wa majitaka na utupaji hovyo wa takataka kutoka viwandani na majumbani. Utumiaji wa dawa mbalimbali kwa ajili ya kuulia wadudu waharibifu wa mazao, huchafua maji, udongo na hewa. Ukataji wa miti na vichaka unasababisha ardhi iwe wazi na kuwa katika hatari ya kumomonyoka kwa udongo kwa njia ya upepo na maji. Hali hii inaweza kusababisha jangwa na uharibifu wa mazingira.

Madhara ya uharibifu wa mazingira Kuna madhara mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira. Madhara hayo ni pamoja na uchafuzi wa hali ya hewa na kuenea kwa magonjwa kama vile kuhara, kipindupindu, kichocho, homa ya matumbo na kuhara damu.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 4 25/04/2019 12:50

Page 15: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

5

Aidha, kupungua kwa tabaka la juu kabisa la hewa linaloitwa ozoni na ongezeko la hewa ya ukaa na joto duniani kunasababishwa na uchafuzi wa mazingira. Madhara mengine ni kuathirika kwa shughuli za kilimo kutokana na mmomonyoko wa udongo na hivyo kusababisha baa la njaa, kuathiri shughuli za utalii kutokana na wanyama kutoweka kwa kukosa malisho na hivyo uchumi wa nchi kuathirika.

Je, ni njia zipi zinaweza kutumika kuzuia uharibifu wa mazingira katika jamii yako?

Bila shaka, shughuli zifuatazo zinaweza kuzuia uharibifu huo na kuwezesha utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya viumbe hai:

i. Kupunguza matumizi holela ya viuatilifu katika shughuli za kilimo

ii. Kutibu majitaka kabla hayajaanza kutiririshwa kwenye mito, maziwa na bahari

iii. Kuacha kuchoma misitu ili kuepuka uchafuzi wa hali ya hewa

iv. Kupanda miti na kuacha kukata miti hovyo

v. Kuacha kufuga mifugo mingi katika eneo dogo

vi. Kutumia kilimo cha matuta yanayokinga mteremko.

1.4 Namna ya kuchopeka elimu ya mazingira katika ufundishaji

Elimu ya mazingira inajitokeza katika umahiri mbalimbali kwenye muhtasari wa Elimu ya Awali. Hivyo, mtoto atajifunza elimu hii kupitia shughuli mbalimbali zilizoainishwa katika muhtasari. Unapaswa kubaini shughuli hizo na kutumia mbinu na zana stahiki kuhakikisha kuwa mtoto anajenga umahiri wa kutunza mazingira. Kwa mfano, namna utakavyowasidia watoto kutambua njia za kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kutumia picha na michoro au namna utakavyotumia igizodhima katika ujifunzaji wa watoto kukabiliana na vitendo vinavyoharibu mazingira kama vile utupaji sahihi wa takataka, kupanda miti na nyasi katika maeneo ya shule na kuihudumia.

Ufuatao ni mfano unaoonesha namna utakavyochopeka elimu ya mazingira kupitia shughuli zilizoainishwa katika muhtasari wa elimu ya awali. Kumbuka kuwa, huu

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 5 25/04/2019 12:50

Page 16: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

6

ni mfano mmoja wa shughuli ya kuchopeka elimu ya mazingira katika kila umahiri. Zipo shughuli nyingine nyingi unazoweza kufundisha elimu ya mazingira.

Jedwali la 3: Uchopekaji wa elimu ya mazingira katika ujifunzaji

Umahiri mkuu

Kuhusiana Kuwasiliana Kutunza afya

Kutunza mazingira

Kumudu stadi za kisanii

Kutumia dhana za kihisabati

Umahiri mahsusi

Kujali Kusikiliza Kubaini magonjwa

mbali-

mbali

Kusafisha mazingira

Kumudu stadi za ubunifu wa sauti

Kujenga dhana ya wakati

Shughuli kuu

Kuwawezesha watoto kushiriki katika shughuli mbalimbali

Kusimulia hadithi mbalimbali

Kuelezea jinsi ya kujikinga na magonjwa

Kubainisha matendo yanayosa-babisha uchafuzi wa mazingira

Kuimba nyimbo mbalimbali

Kubainisha matendo yanayo-fanywa kulingana na wakati

Shughuli ndogo

Kushiriki katika shughuli za upandaji miti, maua na majani

Kusimulia hadithi zinazohusu utunzajimazingira

Kufanya usafi wa mazingira

Kuokota takataka katika mazingira yao

Kuimba nyimbo kuhusu utunzaji wa mazingira

Kumwagilia miti na maua asubuhi na jioni

Je ni mbinu gani inafaa zaidi kufundisha elimu ya mazingira kwa watoto wa elimu ya awali?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 6 25/04/2019 12:50

Page 17: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

7

Mazingira safi na bora ni muhimu katika maisha tunayoishi. Hivyo, watoto wana jukumu la kutunza mazingira ya shuleni na nyumbani. Kwa mfano, watoto waelimishwe umuhimu wa kukata nyasi ili kujikinga na ugonjwa hatari wa malaria pamoja na magonjwa mengine ya mlipuko. Pia, watoto waelimishwe kuhusu umuhimu wa kupanda miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuleta hewa safi. Elimu hii ni muhimu katika umri wao ili waweze kuthamini na kutunza vema mazingira yao na hata baadaye wawe mabalozi wazuri.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Neno mazingira lina maana gani? 2. Eleza umuhimu wa kufundisha elimu ya mazingira katika elimu ya

awali.

3. Ni mambo gani yanasababisha uharibifu wa mazingira?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 7 25/04/2019 12:50

Page 18: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

8

Sura ya Pili

Virusi vya UKIMWI na UKIMWI

Karibu katika sura ya pili ya moduli hii. Katika sura hii utajifunza kuhusu Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI, uambukizwaji, dalili zake na jinsi ya kujikinga na maambukizi. Lengo la sura hii ni kukuongezea maarifa juu ya swala hili mtambuka na namna unavyoweza kulichopeka wakati wa ufundishaji na ujifunzaji.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza maana ya VVU na UKIMWI ii. kufafanua namna UKIMWI unavyoambukizwaiii. kufafanua namna ya kujikinga na maambukizi ya VVUiv. kuchopeka elimu ya VVU na UKIMWI katika ufundishaji na

ujifunzaji.

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Fafanua tofauti iliyopo kati ya VVU na UKIMWI.

2. Taja njia zinazosababisha maambukizi ya VVU.

3. Eleza njia zinazoweza kutumika katika kujikinga na maambukizi ya VVU.

2.1 Maana ya VVU na UKIMWI

Katika kujifunza kuhusu VVU na UKIMWI, inakupasa mwalimu kujiuliza kwanza maana ya maneno haya. UKIMWI ni kifupisho cha Upungufu wa Kinga Mwilini. Upungufu huo wa kinga mwilini unasababishwa na mashambulizi ya virusi vinavyoitwa Virusi vya UKIMWI (VVU). UKIMWI ni miongoni mwa magonjwa yanayoathiri maendeleo ya ukuaji wa mtoto kwa ujumla. Baadhi ya watoto wameambukizwa VVU na wengine ni yatima, kwa sababu wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa UKIMWI. Kuondokewa na wazazi kunasababisha

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 8 25/04/2019 12:50

Page 19: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

9

baadhi ya watoto kulelewa na ndugu ambao huwajibika kwa kiwango kidogo katika maendeleo yao. Baadhi ya watoto hawaandikishwi katika madarasa ya elimu ya awali kutokana na kuwa waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Mtoto au familia iliyoathiriwa na ugonjwa wa UKIMWI, wakati mwingine, hutengwa na jamii, hali inayosababisha mtoto aathirike kisaikolojia awapo shuleni.

Shule zihakikishe kuwa watoto wote walioathirika na VVU na UKIMWI wanaandikishwa kujiunga na elimu ya awali. Pamoja na hayo, shule zina wajibu wa kuandaa mazingira mazuri yaliyo rafiki kwa watoto wote wakiwemo wale walioathirika ili waweze kujifunza. Wataalamu wanashauri kuwa shule kama taasisi zina nafasi nzuri ya kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu. Hivyo ziwajibike vya kutosha kuwatambua na kuwahudumia watoto wenye maambukizo ya VVU na kuwapatia mahitaji yao.

2.2 Maambukizi ya VVU

Waelekeze watoto kuwa wanaweza kuambukizwa VVU wakiwa shuleni au katika mazingira ya nje ya shule. Maambukizi haya yanaweza kutokea wakiwa katika shughuli mbalimbali kama vile michezo. Njia zinazoweza kusababisha maambukizi ni pamoja na:

i. Kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama vile nyembe na sindanoii. Kuchangia miswakiiii. Kung’atana na mtoto mwenye maambukiziiv. Kugusana hasa kunakohusisha vidonda v. Kula vyakula mbalimbali ambavyo vilishawekwa mdomoni mwa

muathirika (Hapa mtoto anaweza kuambukizwa iwapo ana mchubuko mdomoni)

vi. Kuwekewa damu yenye maambukizi.

2.3 Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya VVU

Ili kuwakinga watoto na maambukizi ya VVU, watoto waelimishwe kupitia shughuli mbalimbali kama vile kuwasomea au kuwasimulia hadithi, kisa mafunzo na kufanya igizo dhima. Kupitia shughuli mbalimbali, watoto wanaweza kujifunza njia za kuzuia

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 9 25/04/2019 12:50

Page 20: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

10

maambukizi ya VVU. Kumbuka kuwa mwangalifu wakati wa utendaji wa shughuli hizo ili kutomnyanyapaa mtoto yeyote kisaikolojia au kihisia. Ni vema mwalimu ukawabaini watoto wenye maambukizi ya VVU na kuwa karibu na wazazi/walezi wao. Hii itakuwezesha kuwasaidia watoto hao katika ukuaji na ujifunzaji wao.

Je, ni njia zipi unazozifahamu ambazo zinazoweza kusaidia kujikinga na maambukizi ya VVU?

Pamoja na majibu yako, baadhi ya njia zinazosaidia kujikinga na maambukizi ya VVU ni pamoja na kutokuchangia vitu vyenye ncha kali, kutumia glovu unapomhudumia mtu anayetokwa na damu, kutokufanya ngono na kuzuia maambukizi ya mama kwa mtoto kwa kupata dawa kutoka kwa wataalamu wa afya. Unapaswa kuwafundisha watoto namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU kulingana na umri wao.

Kielelezo namba 1: Mwalimu akimhudumia mtoto aliyeumia

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 10 25/04/2019 12:50

Page 21: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

11

Elezea kwa kifupi namna utakavyoweza kumsaidia mtoto ambaye ana maambukizi ya VVU ili kuboresha ujifunzaji wake.

2.4 Uchopekaji wa elimu ya VVU na UKIMWI katika ufundishaji na Ujifunzaji

Elimu ya VVU na UKIMWI inajitokeza katika umahiri mbalimbali kwenye muhtasari wa elimu ya awali. Hivyo mtoto atajifunza elimu hii kupitia shughuli mbalimbali zilizoainishwa katika muhtasari. Mwalimu unapaswa kubaini shughuli hizo na kutumia mbinu na zana stahiki kuhakikisha kuwa mtoto anajenga umahiri kuhusu VVU na UKIMWI na namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU. Kwa mfano, namna utakavyowasaidia watoto kutambua njia za kujikinga na VVU kwa kutumia picha na michoro au namna utakavyotumia igizodhima katika ujifunzaji wa watoto kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU.

Ufuatao ni mfano unaoonesha namna utakavyochopeka elimu ya VVU na UKIMWI kupitia shughuli zilizoainishwa katika muhtasari wa elimu ya awali. Kumbuka kuwa, huu ni mfano mmoja wa shughuli ya kuchopeka elimu ya VVU na UKIMWI katika kila umahiri. Zipo shughuli nyingine nyingi unazoweza kufundishia elimu ya VVU na UKIMWI.

Jedwali la 4: Elimu ya VVU na UKIMWIUmahiri mkuu

Kuhusiana Kuwasiliana Kutunza afya

Kutunza mazingira

Kumudu stadi za kisanii

Kutumia dhana za kihisabati

Umahiri mahsusi

Kujali Kuzungumza Kubaini magonjwa

mbalimbali

Kusafisha Mazingira

Kumudu stadi za ubunifu wa sauti

Shughuli kuu

Kushirikiana katika shughuli mbalimbali

Kuimba nyimbo mbalimbali

Kubaini vyanzo vya magonjwa

Kutenda matendo yanayohusisha kuchukua tahadhari

Kutamba ngonjera

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 11 25/04/2019 12:50

Page 22: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

12

Shughuli ndogo

Kuchangia na kutumia vitu pamoja

Kuimba nyimbo zinazohusu kujikinga na maambukizi ya VVU

Kuigiza namna mtoto anavyoweza kuambukizwa VVU

Kufanya igizo dhima la namna ya kujikinga na maambu-kizi ya VVU

Kutamba ngonjera kuhusu ugonjwa hatari wa UKIMWI

Je, unafundishaje elimu ya VVU na UKIMWI kwa watoto wa elimu ya awali?

Ni muhimu kuwakumbusha watoto mara kwa mara namna ya kujikinga na maambukizo ya VVU. Waeleze watoto kuwa wanapaswa kuchukua tahadhari ya kutoshiriki katika matendo yatakayoweza kuwasababishia maambukizo ya VVU. Tahadhari ichukuliwe katika kuchangia vitu kama mswaki, wembe, sindano na kugusana kwa vidonda.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Fafanua tofauti iliyopo kati ya VVU na UKIMWI.

2. Eleza njia zinazosababisha maambukizo ya VVU.

3. Eleza njia zinazoweza kutumika katika kujikinga na maambukizo ya VVU.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 12 25/04/2019 12:50

Page 23: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

13

Sura ya Tatu

Haki na wajibu wa mtoto

Mwalimu, karibu katika sura hii inayoelezea haki na wajibu wa mtoto. Katika sura hii, utajifunza dhana ya haki na wajibu wa mtoto na umuhimu wa mtoto kutambua haki zake na kutimiza wajibu wake. Baada ya kukamilisha sura hii, utaweza kuzingatia haki za mtoto katika ufundishaji wako.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza maana ya mtoto, haki na wajibu wa mtotoii. kufafanua haki na wajibu mbalimbali wa mtotoiii. kuchopeka elimu ya haki na wajibu wa mtoto wakati wa

ufundishaji na ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:

1. Nini maana ya haki ya mtoto?

2. Eleza kwa kifupi haki za mtoto.

3. Je, kuna umuhimu gani wa mtoto kujua haki zake?

4. Fafanua wajibu wa mtoto nyumbani na shuleni.

3.1 Haki za mtoto

Je, mwalimu, unaelewa nini kuhusu mtoto?

Pamoja na majibu yako, Sera ya Maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008 na Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inatoa tafsiri ya mtoto kama mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18. Tafsiri hii ni ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa ambao Tanzania ni mwanachama wake. Mtoto ana haki mbalimbali ambazo anatakiwa kupewa ili aweze kukua katika ujumla wake.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 13 25/04/2019 12:50

Page 24: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

14

Je, mwalimu, unaelewa nini kuhusu haki za mtoto?

Pamoja na majibu uliyonayo, haki za mtoto ni vigezo vya msingi vya utu wa mtoto na utambulisho wake. Haki hizi na utambulisho wake vinajikita katika kila utamaduni, dini na desturi. Mfano wa haki za mtoto ni kama vile haki ya kuishi, kulindwa, kutoa maoni na faragha.

Mtoto anapaswa kuzielewa haki zake za msingi ambazo ni pamoja na: i. usajili baada ya kuzaliwa, jina na utaifaii. kushiriki katika kutoa maamuziiii. kutoa maoni na kusikilizwaiv. kutotengwav. kuishi na wazazi/walezivi. kulindwavii. kuishi bila ubaguziviii. kupata huduma (mavazi, malazi, chakula, elimu, afya na dawa)ix. kushiriki katika michezo na shughuli za kiutamaduni.x. kusikilizwaxi. kuheshimiwa

Kielelezo namba 1: Watoto wanaaga kwenda shuleni

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 14 25/04/2019 12:50

Page 25: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

15

Je, kuna umuhimu wa mtoto kujua haki zake?

Ufuatao ni umuhimu wa mtoto kujua haki zake:i. Hujiamini katika kutoa maamuziii. Hulinda na kutetea haki zakeiii. Hujijengea uvumilivu, heshima na kuthamini watu wengine katika jamiiiv. Hukuza uwajibikaji, ushirikiano, udadisi na ujasiri

3.2 Wajibu wa mtoto

Je, wajibu wa mtoto ni upi?

Kwa kifupi, wajibu ni jambo linalomlazimu mtoto kulifanya kulingana na sheria, kanuni, taratibu, mila na desturi za jamii anamoishi. Mara nyingi haki huenda na wajibu. Hivyo basi wajibu wa mtoto ni pamoja na:

i. kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa zake na watu wazima muda wote na kuwasaidia pale inapohitajika;

ii. kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kwa kutumia nguvu na akili kulingana na umri wake;

iii. kudumisha mambo mema katika utamaduni wa jamii na taifa kwa ujumla;iv. kuhudhuria shuleni bila kukosa na kujifunza kwa bidii;v. kufuata na kutii kanuni na taratibu zote zinazokubalika katika jamii.

Eleza namna unavyozingatia haki za mtoto katika ufundishaji wako

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 15 25/04/2019 12:50

Page 26: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

16

3.3 Uchopekaji wa elimu ya haki na wajibu wa mtoto katika ufundishaji na ujifunzaji

Elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoto inajitokeza katika umahiri mbalimbali kwenye muhtasari wa elimu ya awali. Hivyo, mtoto atajifunza elimu hii kupitia shughuli mbalimbali zilizoainishwa katika muhtasari. Unapaswa kubaini shughuli hizo na kutumia mbinu na zana stahiki kuhakikisha kuwa mtoto anajenga umahiri kuhusu haki na wajibu wake. Kwa mfano, namna utakavyowasaidia watoto kutambua haki na wajibu wao kwa kutumia picha na michoro au namna utakavyotumia igizodhima katika ujifunzaji wa watoto kuhusu haki na wajibu wao katika jamii.

Ufuatao ni mfano unaoonesha namna utakavyochopeka elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoto kupitia shughuli zilizoainishwa katika muhtasari wa elimu ya awali. Kumbuka kuwa, huu ni mfano mmoja wa shughuli ya kuchopeka elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoto katika kila umahiri. Zipo shughuli nyingine nyingi unazoweza kuzitumia katika ufundishaji kuhusu haki na wajibu wa mtoto.

Jedwali la 5: Uchopekaji wa elimu ya haki na wajibu wa utoto

Umahiri mkuu

Kuhusiana Kuwasiliana Kutunza afya

Kutunza mazingira

Kumudu stadi za kisanii

Kutumia dhana za kihisabati

Umahiri mahsusi

Kujitawala Kuzungumza Kutunza mwili

Kuchukua tahadhari

Kumudu stadi za ubunifu zinazo-husisha utendaji wa mwili

Kujenga dhana ya wakati

Shughuli kuu

Kufanya shughuli zinazohusiana na utunzaji wa vitu

Kuelezea shughuli za kila siku

Kusafisha mwili

Kubainisha vitu na maeneo hatarishi katika mazingira

Kucheza michezo mbalimbali

Kutofautisha siku katika juma

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 16 25/04/2019 12:50

Page 27: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

17

Shughuli ndogo

Kutunza vitu vyake mahala sahihi(wajibu)

Kutaja matendo anayofanya kila siku kulingana na wakati (wajibu)

Kufanya vitendo vya kusafisha mwili(wajibu)

Kuigiza namna ya kujikinga na maeneo hatarishi(haki ya kulindwa)

Kucheza michezo mbalimbali kwa kushiri-kiana na wenzake (haki ya kucheza)

Kutaja siku za kwenda shule(haki ya kupata elimu)

Je, unawasidiaje watoto kutambua haki zao na kutimiza wajibu wao?

Ikumbukwe kuwa mtoto anatakiwa kujua haki na wajibu wake katika jamii anayoishi. Unatakiwa kuwakumbusha watoto juu ya haki zao za msingi na wajibu wao wanapokuwa nyumbani na shuleni. Hivyo, wasisitize kutoa malalamiko yao pindi watakapokuwa hawatendewi haki katika jamii inayowazunguka au shuleni ili waweze kupata msaada unaotakiwa.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Nini maana ya haki ya mtoto?

2. Eleza kwa kifupi haki za mtoto.

3. Je, kuna umuhimu gani wa mtoto kujua haki zake?

4. Fafanua wajibu wa mtoto nyumbani na shuleni.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 17 25/04/2019 12:50

Page 28: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

18

Sura ya Nne

Elimu ya jinsia

Karibu mwalimu, katika sura ya nne inayohusu elimu ya jinsia. Katika sura hii, utajifunza majukumu mbalimbali ya kijinsia na namna unavyoweza kuzingatia jinsia katika ufundishaji na ujifunzaji. Unashauriwa kuzingatia usawa wa kijinsia katika shughuli zako zote za ufundishaji ili kuwashirikisha watoto wote katika tendo zima la ujifunzaji.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza dhana ya jinsiaii. kufafanua majukumu ya kijinsia katika jamiiiii. kueleza dhana ya shule rafiki kijinsia iv. kueleza namna ya kuzingatia jinsia katika ufundishaji na

ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Unaelewa nini kuhusu jinsia?

2. Je, kuna tofauti gani kati ya jinsi na jinsia?

3. Unaelewa nini kuhusu shule rafiki kijinsia?

4.1 Dhana za jinsia

Sehemu hii itakusaida wewe mwalimu kuelewa dhana mbalimbali zinazotumika katika elimu ya jinsia na majukumu mbalimbali ya kijinsia katika jamii. Ni muhimu kuzifahamu dhana hizi kwa sababu zitakusaidia katika ufundishaji wa watoto ili kuwajengea uelewa katika masuala mbalimbali ya jinsia.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 18 25/04/2019 12:50

Page 29: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

19

Mwalimu, hebu jiulize jinsia maana yake nini?

Bila shaka utaona kwamba jinsia ni uhusiano wa kijamii kati ya mwanamke/msichana na mwanaume/mvulana. Uhusiano huu upo katika wajibu na mgawanyo wa majukumu kwa wanawake/wasichana na wanaume/wavulana katika jamii.

Katika kujifunza dhana ya jinsia, utaona pia kuna maneno mbalimbali yanayohusiana na dhana hiyo kama vile jinsi, upendeleo wa kijinsia, ubaguzi wa kijinsia, usawa wa kijinsia, fikra mgando za kijinsia na ukatili wa kijinsia. Yafuatayo ni maelezo kuhusu maneno hayo:

Jedwali la 6: Dhana ya elimu ya jinsi

Jinsi Ni tofauti za kibaiolojia na kimaumbile zinazowatofautisha wanaume au wavulana na wanawake au wasichana.

Jinsia Ni uhusiano wa kijamii kati ya mwanamke au msichana na mwanaume au mvulana. Mahusiano hayo yapo katika wajibu na mgawanyo wa majukumu kwa wanawake au wasichana na wanaume au wavulana katika jamii.

Upendeleo wa kijinsia Ni kitendo cha kumpa mtu fursa na haki anayostahili kutokana na jinsi yake.

Ubaguzi wa kijinsia Ni kitendo cha kumnyima mtu fursa na haki kwa sababu ya jinsi yake.

Usawa wa kijinsia Ni hali inayoruhusu wasichana au wanawake, wavulana au wanaume kuwa na fursa na haki sawa.

Fikra mgando za kijinsia Ni taswira iliyojengeka kuwa wanaume wana thamani kuliko wanawake katika jamii na kuwa wanastahili fursa na haki zaidi.

Ukatili wa kijinsia Ni tendo la kumuumiza mtu kimwili, kiakili na kisaikolojia kwa sababu ya jinsi yake.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 19 25/04/2019 12:50

Page 30: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

20

4.2 Majukumu ya kijinsia yaliyomo katika jamii

Baada ya kueleza maana ya jinsia na dhana mbalimbali zitumikazo katika elimu ya jinsia, mwalimu unapaswa kuwaelezea watoto jinsi majukumu ya kijinsia yanavyotekelezwa nyumbani na shuleni.

4.2.1 NyumbaniMgawanyo wa majukumu, haki na fursa kati ya watoto wa kiume na wa kike hutofautiana. Watoto wa kike hupewa kazi za kupika, kuchota maji, kulea watoto, kuandaa chakula na shughuli nyingine za nyumbani. Watoto wa kiume wao hupewa kazi ambazo hazihusiki na shughuli za jikoni. Mgawanyo huu wa kazi huanza tangu watoto wakiwa wadogo na kuendelea hivyo katika ukuaji wao na kujenga taswira hiyo katika vizazi vyao. Hivyo, mwalimu unapaswa kuwafundisha watoto kuwa shughuli hizo zinapaswa kufanywa na watoto wote bila kubagua kama ni wa kike au wa kiume, na hii itawasaidia kujua kuwa wanapaswa kufanya kazi za aina zote bila ubaguzi.

Kielelezo Namba 1: Mtoto akimsaidia mama kupika

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 20 25/04/2019 12:50

Page 31: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

21

4.2.2 Shuleni

Katika mazingira ya shule, walimu wanaweza kuwa kichocheo cha utofauti kati ya wasichana na wavulana. Kwa mfano, katika uchaguzi wa viongozi shuleni, wavulana hupewa nafasi za juu za uongozi na wasichana hupewa nafasi za chini. Hata katika kuuliza maswali darasani, uulizaji wa maswali haupo sawa kwani wavulana huuliza zaidi kuliko kwa wasichana. Mwalimu, unapaswa kuhakikisha kuwa unawashirikisha watoto wote kwa usawa bila kujali jinsi zao.

i. Fanya uchunguzi mdogo wa namna wavulana na wasichana wanavyocheza na kushirikiana, chunguza na andika aina za michezo na mafunzo katika michezo ya wavulana na wasichana.

ii. Andaa taarifa fupi ya uchunguzi huo.iii. Jadiliana na wenzako taarifa hiyo inayoonesha haki ya

mgawanyo wa majukumu kwa wanawake na wanaume.iv. Nini athari za michezo kwa mvulana na wasichana katika

ujifunzaji na ukuaji wa watoto?

4.3 Kuzingatia usawa wa kijinsia katika ujifunzaji na ufundishaji

Unelewa nini unaposikia usawa wa kijinsia katika ujifunzaji na ufundishaji?

Usawa wa kijinsia katika ujifunzaji na ufundishaji ni hali ambayo mwalimu na watoto wanashiriki katika shughuli za ujifunzaji bila kujali jinsi zao. Mwalimu, ukiwa mwezeshaji unatakiwa ujiepushe na viashiria vya upendeleo wa kijinsia. Unatakiwa ujenge mazingira ya shule yenye misingi rafiki kijinsia kwa wasichana na wavulana. Pia, uwawezeshe watoto kutekeleza usawa wa kijinsia na kulinda demokrasia na haki za binadamu kwa jinsi zote. Mazingira ya shule yaani majengo, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinatakiwa viwe rafiki kwa jinsi zote.

Zifuatazo ni mbinu zinazopendekezwa kutumiwa kwa watoto ili kutekeleza usawa wa kijinsia katika kufanya kazi pamoja, kuheshimiana na kupunguza fikra mgando za ubaguzi wa kijinsia.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 21 25/04/2019 12:50

Page 32: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

22

i. Andaa mazingira rafiki kwa ajili ya watoto (wasichana na wavulana), mahali ambapo watacheza au kuimba pamoja, watashirikiana katika shughuli mbalimbali ili kujenga uhusiano wa kijamii na kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe.

ii. Wape nafasi watoto wachague shughuli tofauti wanazotaka kuzifanya. Tumia shughuli hizo kuwafundisha watoto jinsi wanavyoweza kuzifanya bila kubagua jinsi. Onesha mifano ya baba na mama wakishirikiana katika shughuli mbalimbali mfano, kupika, kulea, kulima na kufuga.

iii. Waongoze watoto kusema wanachokiona ili kujenga dhana sahihi za jinsia.

iv. Fafanua ili kuonesha pale ambapo kuna mgawanyo wa kazi unaozingatia usawa wa kijinsia.

4.4 Namna ya kuzingatia jinsia katika ujifunzaji na ufundishaji

Unaelewa nini mwalimu kuhusu ujifunzaji na ufundishaji unaozingatia usawa wa kijinsia?

Pendekeza mbinu za kufundishia na kujifunzia zinazofaa kutumika katika ufundishaji unaozingatia usawa wa kijinsia.

Ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia usawa wa kijinsia ni ule unaojali mahitaji ya ujifunzaji kwa wasichana na wavulana, kusikilizana na kufanya mambo ya msingi kwa ushirikiano na kuheshimiana. Ufundishaji huu unamtaka mwalimu kuzingatia jinsia katika uandaaji wa shughuli na kutawala darasa. Vilevile, katika matumizi ya lugha na zana na wakati wa kufanya tathimini.

Kuna mbinu mbalimbali za kujifunzia na kufundishia ambazo hazina dosari kwa mwitikio wa kijinsia. Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na vitendo, kazi mradi, ziara, maswali na majibu na igizo. Ufundishaji kwa kutumia mbinu hizi unaweza kuwashirikisha watoto wote darasani na hivyo kuibua vipaji vya aina mbalimbali na kuwajengea ushirikiano baina yao. Haya yote yanahitaji umakini wa mwalimu ili asiwabague wasichana na wavulana katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 22 25/04/2019 12:50

Page 33: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

23

Mambo ya kuzingatia katika ufundishaji na ujifunzaji unaojali usawa wa kijinsiai. Vifaa na zana za kujifunzia na kufundishia Mwalimu, wakati unaandaa zana, unatakiwa kuhakikisha kwamba zana hizo

zimezingatia suala la kijinsia. Utumiaji wa zana zinazozingatia usawa wa kijinsia utawahamasisha watoto katika ujifunzaji. Kwa mfano, utakapotumia picha baba anafua nguo wakati mama analisha ng'ombe. Zana hii italeta maswali mengi kwa mtoto. Mwalimu, jadiliana na watoto kwa kuwauliza maswali kuhusu masuala ya kijinsia. Wakati wote wa kipindi kuwa makini, rejea wajibu wa kijinsia na lugha iliyotumika katika zana za kufundishia na kujifunzia. Hakikisha zana zinagawanywa sawa kwa wasichana na wavulana hasa pale zinapokuwa pungufu.

ii. Mpangilio wa darasa na mwingiliano Mpangilio wa darasa unapaswa uwe na mchangamano wa watoto katika

ushiriki ulio sawa. Mwalimu, katika utekelezaji wa shughuli uliyoiandaa, uliza maswali huru kwa watoto wa kike na wa kiume. Liweke darasa katika vikundi vidogovidogo vyenye mchanganyiko wa wasichana na wavulana, ili washiriki vizuri katika kujifunza. Pia, fikiria ni sehemu gani nzuri kwako kusimama, kukaa au kutembea wakati ukiwa darasani.

iii. Mbinu/njia za kufundishia na kujifunzia Chagua njia za kufundishia ambazo zitakuhakikishia ushirikishwaji sawa

wa wasichana na wavulana. Baadhi ya njia/mbinu za kufundishia kama vile majadiliano katika vikundi, uchunguzi, igizodhima, zinaweza kuwa njia nzuri sana katika kuwashirikisha watoto na kuwatia moyo. Hakikisha unawapa watoto wote fursa ya kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji. Unapotumia vitendo vya ujifunzaji uwe makini usiruhusu mtoto mmoja kumiliki na kuwaacha wengine. Wagawie majukumu katika vikundi kwa usawa ili wote washiriki tendo la ujifunzaji kwa ufanisi.

iv. Shughuli za ujifunzaji Hakikisha watoto wote wanashirikiana vema katika shughuli za ujifunzaji

wanapofanya kazi kwa vitendo darasani. Hakikisha kuwa wasichana na wavulana wote wana nafasi sawa za kushiriki katika shughuli za kuwasilisha kazi zao. Vilevile, unapotoa kazi hakikisha kuwa wasichana na wavulana wanapewa nafasi za uongozi na majukumu sawa katika vikundi.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 23 25/04/2019 12:50

Page 34: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

24

v. Mrejesho na tathimini Toa muda wa kupata mrejesho kutoka kwa wasichana na wavulana kuhakikisha

kuwa wasichana na wavulana wote wameelewa na wanashiriki kufanya tathmini.

vi. Matumizi ya lugha na jinsia Matumizi ya lugha darasani yanatakiwa yawachukulie wasichana na wavulana

kwa usawa ili kuweka mazingira tulivu ya ujifunzaji kwa wote. Unatakiwa kutathmini lugha unayotumia kuhakikisha kuwa inaakisi usawa wa kijinsia. Lugha ya ishara kama vile kukonyeza inaweza kuendelea bila kujulikana na wengine kwa muda mrefu na hivyo kuchangia kuathiri ushiriki wa mtoto anayefanyiwa hivyo darasani.

Andaa shughuli itakayomwezesha mtoto kujifunza masuala ya kijinsia. Kisha uielezee ni kwa namna gani imemsaidia mtoto kujifunza suala la kijinsia.

Ni kwa namna gani unazingatia usawa wa kijinsia?

Suala la usawa wa kijinsia ni muhimu kusisitizwa kwa watoto wa elimu ya awali. Watoto wanapaswa kukua huku wakijua kuwa kazi zote zinapaswa kufanywa na wote bila kujali jinsia ili kujiletea maendeleo. Hivyo, wawapo darasani au nje ya darasa wanapaswa kufanya kazi zote wakishirikiana bila kubaguana.

Jaribio baada ya kujifunza Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii:

1. Unaelewa nini kuhusu jinsia? 2. Je, kuna tofauti gani kati ya jinsi na jinsia? 3. Nini maana ya shule rafiki kijinsia?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 24 25/04/2019 12:50

Page 35: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

25

Sura ya Tano

Afya na lishe

Mwalimu, katika sura hii utajifunza kuhusu afya na lishe kwa mtoto. Maarifa haya yatakusaidia kujenga umahiri utakaokuwezesha kuwaelekeza watoto namna ya kutunza afya zao kwa kufanya usafi wa mwili na kula chakula bora.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza maana ya afya ya mtotoii. kufafanua matendo muhimu ya afya kwa mtotoiii. kuchopeka elimu ya afya na lishe katika ufundishaji na

ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Nini maana ya afya ya mtoto?

2. Ni matendo gani yanadumisha afya ya mtoto?

3. Ni kwa namna gani utaboresha afya ya mtoto shuleni?

5.1 Afya ya mtoto

Mwalimu, unafahamu nini juu ya afya ya mtoto? Ni Matendo gani yakifanyika mara kwa mara yanadumisha afya njema kwa mtoto?

Afya ni hali ya uzima wa mwili na akili ambayo inamwezesha mtoto kutekeleza shughuli mbalimbali za kila siku na kuonesha uwezo wake kama binadamu. Kufanya usafi wa mwili ni moja ya matendo muhimu yanayotendeka ili kulinda afya ya mwili na ustawi. Unapaswa kuwaeleza watoto umuhimu wa usafi wa mwili kwa ustawi wao.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 25 25/04/2019 12:50

Page 36: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

26

Zipo faida mbalimbali za kufanya usafi wa mwili ambazo ni pamoja na kuzuia magonjwa, kuondoa harufu mbaya mwilini na kuonekana safi na wenye kuvutia.

Kielelezo namba 1: Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wa mwili

Kwa kutumia uzoefu wako na maarifa uliyoyapata, utawawezesha watoto kuvifahamu na kuvitumia vifaa mbalimbali vinavyotumika kufanya usafi wa mwili.Vifaa hivi ni kama vile sabuni, dawa ya meno, mswaki na maji. Kumbuka kuwa usafi wa mwili (kuoga kunakojumuisha sehemu muhimu za mwili yaani masikio, macho, pua, meno, na kucha) na utunzaji wa vyoo vinahitaji matumizi ya maji safi na salama.

Pia, inatarajiwa kuwa maarifa haya yatakuwezesha kuwaongoza watoto kufahamu na kutenda matendo mbalimbali kwa ustawi wa afya zao wawapo shuleni na nyumbani. Matendo hayo ni kama vile:

i. Kupatikana kwa maji ya kunywa yaliyo safi na salama

ii. Kudumisha usafi wa vyoo

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 26 25/04/2019 12:50

Page 37: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

27

iii. Kudumisha usafi wa mwili ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa

yanayosababishwa na uchafu wa mwili ama mazingira

iv. Kunawa mikono kwa maji safi na salama mara baada ya kutoka chooni, kabla ya kula na wakati wa kuandaa chakula

v. Kuhifadhi chakula mahali safi na salama ili kuzuia wadudu kama nzi na mende wanaosambaza uchafu wasikifikie

vi. Kuvaa viatu

vii. Kuhifadhi maji mahali salama na sahihi

5.2 Matendo muhimu kwa afya ya mtoto

Je, ni matendo gani muhimu yanayoimarisha afya ya mtoto?

Matendo muhimu kwa afya ya mtoto ni kama yafuatayo:-i. Uhusiano mwema kati ya mzazi/mlezi na mtoto, humjenga mtoto kuwa

na ustawi wa kihisia na kijamii

ii. Lishe bora hupunguza utapiamlo. Lishe duni na njaa ni tatizo kubwa hasa kwa nchi maskini na zilizo na janga la vita ama ukame na mambo haya huathiri zaidi ukuaji wa watoto. Hivyo unapswa kutambua watoto wenye matatizo ya ukuaji na utapiamlo mapema kadiri iwezekanavyo

iii. Kubaini watoto wenye matatizo yanayohusiana na ukosefu wa lishe bora na usalama na kuchukua hatua stahiki za mapema ili kuwanusuru na matatizo hayo

iv. Kubaini viashiria ama vitu vinavyoweza kuathiri ustawi katika familia.

Vilevile, ni vema ukumbuke kuwa lishe humpatia mtoto nguvu na kumsaidia kujifunza, kufikiri vizuri na humlinda dhidi ya maambukizi ya magonjwa na kuimarisha misuli na viungo vya mwili wake. Watoto walio chini ya miaka mitano wanahitaji chakula chenye lishe bora (kinachojumuisha makundi yote ya vyakula) ili kusaidia ujenzi na ukuaji wa viungo vya mwili vitakavyosaidia katika ukuaji na ujifunzaji bora.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 27 25/04/2019 12:50

Page 38: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

28

Kielelezo namba 2: Makundi ya chakula bora

5.3 Namna ya kuchopeka elimu ya afya na lishe katika ufundishaji na ujifunzaji

Elimu ya afya na lishe inajitokeza katika umahiri mbalimbali kwenye muhtasari wa elimu ya awali. Hivyo, mtoto atajifunza elimu hii kupitia shughuli mbalimbali zilizoainishwa katika muhtasari. Mwalimu, unapaswa kubaini shughuli hizo na kutumia mbinu na zana stahiki kuhakikisha kuwa mtoto anajenga umahiri kuhusu utunzaji wa afya yake. Kwa mfano, namna utakavyowasaidia watoto kufanya usafi wa miili yao na kula vyakula bora kwa kutumia picha na michoro au namna utakavyotumia igizo dhima au kufanya matendo halisi ya kutunza afya zao.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 28 25/04/2019 12:50

Page 39: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

29

Ufuatao ni mfano unaoonesha namna utakavyochopeka elimu kuhusu afya na lishe ya mtoto kupitia shughuli zilizoainishwa katika muhtasari wa elimu ya awali. Kumbuka kuwa, huu ni mfano mmoja wa shughuli ya kuchopeka elimu kuhusu afya na lishe ya mtoto katika umahiri.

Jedwali la 7: Uchopekaji wa masuala ya afya na lishe katika ufundishaji na ujifunzaji

Umahiri mkuu

Kuhusiana Kuwasiliana Kutunza afya

Kutunza mazingira

Kumudu stadi za kisanii

Kutumia dhana za kihisabati

Umahiri mahsusi

Kujitawala Kumudu stadi za awali za kusoma

Kutunza mwili

Kusafisha mazingira

Kumudu stadi za ubunifu zinazohusisha utendaji wa mwili

Kujenga dhana ya wakati

Shughuli kuu

Kufanya vitendo vya kujitegemea

Kusoma picha

Kusafisha mwili

Kubainisha matendo yanayosababisha uchafuzi wa mazingira

Kucheza

michezo mbalimbali

Kubainisha matendo yanayofanywa kulingana na wakati

Shughuli ndogo

Kunawa mikono kwa usahihi

Kubainisha chakula bora kwa kutumia vyakula halisi au picha

Kuigiza namna ya kuoga kwa usahihi

Kueleza madhara ya mazingira machafu kwa afya

Kucheza michezo ya kuruka kamba

Kufanya igizo dhima kuhusu shughuli za mtoto tangu anapoamka mpaka anapolala.

Andaa taarifa fupi inayoonesha namna unavyowapatia watoto lishe bora kwa ajili ya afya yao ili kuimarisha ujifunzaji.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 29 25/04/2019 12:50

Page 40: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

30

Je, kwa namna gani unadumisha afya ya mtoto katika shule yako?

Mtoto wa Elimu ya Awali anatakiwa kupata chakula bora chenye mchanganyiko wa wanga, protini na vitamini kwa wingi kila siku ili kumsaidia katika kuujenga mwili na kuukinga dhidi ya magonjwa. Mwalimu, unatakiwa kuwasisitiza watoto kula mchanganyiko wa vyakula kama vile ugali, wali, nyama, samaki, dagaa, ndizi, machungwa, maembe, tikitimaji, parachichi, mboga za majani, jibini na maharagwe. Pia, mwalimu unapaswa kuwakumbusha wazazi/walezi kuwapa watoto lishe bora ili wakue na kujifunza vema.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii:1. Nini maana ya afya ya mtoto?

2. Ni matendo gani yanadumisha afya ya mtoto?

3. Je, ni kwa namna gani utaboresha afya ya mtoto shuleni?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 30 25/04/2019 12:50

Page 41: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

31

Sura ya Sita

Ushauri na unasihi

Karibu katika sura ya sita kuhusu elimu ya ushauri na unasihi. Katika sura hii utajifunza namna unavyoweza kutoa ushauri na unasihi kwa watoto katika tendo zima la ufundishaji na ujifunzaji. Mwalimu, unashauriwa kuwa karibu na watoto ili uweze kuwashauri na kuwanasihi pale inapobidi ili kuongeza ufanisi katika tendo zima la ufundishaji na ujifunzaji.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza dhana ya ushauri na unasihi ii. kufafanua changamoto zinazoweza kuhitaji ushauri na unasihiiii. kueleza namna ya kutoa ushauri na unasihi katika ufundishaji

na ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Kuna tofauti gani kati ya ushauri na unasihi? 2. Ni mambo gani ya watoto unafikiri yanahitaji ushauri?3. Ni mambo gani ya watoto unafikiri yanahitaji unasihi? 4. Taja changamoto mbili zinazohitaji ushauri na mbili zinazohitaji

unasihi?

6.1 Dhana ya ushauri na unasihi

Je, unaelewa nini kuhusu dhana ya ushauri na unasihi?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 31 25/04/2019 12:50

Page 42: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

32

Ushauri na unasihi ni moja ya masuala muhimu yanayopewa kipaumbele katika kuwezesha ujifunzaji na ufundishaji fanisi katika ngazi mbalimbali za elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya awali.

Ushauri na unasihi ni huduma na maelekezo yanayotolewa katika kuwezesha ukuaji chanya wa mtoto. Huduma na maelekezo haya hutolewa na mtaalamu aliyesomea ama mtu mwenye uzoefu na ujuzi wa kutosha. Ushauri unalenga kutoa mwongozo au maelekezo kwa mhitaji ili atatue changamoto inayomkabili. Unasihi kwa upande mwingine unalenga kumjengea mtu uwezo wa kutatua tatizo linaloweza kuathiri utendaji na mwenendo wake wa kila siku. Tatizo linalomsababisha mtu ama mtoto kuhitaji huduma ya unasihi linaweza kuwa la kihisia, la kitaaluma/ujifunzaji, ama la kutendewa matendo na mtu mwingine kiasi ambacho linafedhehesha utu wake. Hivyo, ni vema kubaini matatizo yanayoathiri ukuaji na ujifunzaji na kufifisha kiwango cha mtoto kuchangamana na mwalimu au watoto wenzake ili uweze kuchukua hatua stahiki za kumsaidia kukabiliana nayo.

Unasihi una umuhimu mkubwa kwa mtoto wa elimu ya awali kwani:i. humsaidia kuwa na mtazamo chanya wa maisha ii. humsaidia kutambua uwezo wake na kuutumia vizuri katika ujifunzajiiii. humwezesha kubaini njia sahihi ya kutumia katika kufanya uamuziiv. humjengea kujiamini

6.2 Changamoto zinazohitaji ushauri na unasihi

Unaweza kutumia mbinu mbalimbali kuwasaidia watoto kueleza changamoto walizonazo na kuwasaidia kujadili hisia zao. Mbinu hizi ni pamoja na kutumia hadithi na kuelezea hisia za matukio katika hadithi, kutumia michoro, upakaji wa rangi na ngoma. Mbinu hizi za kufanya unasihi pia zinampa mnasihi taarifa muhimu za watoto ambazo zisingeweza kupatikana kwa urahisi kwa kutumia njia zisizogusa na kuibua hisia zao. Zifuatazo ni changamoto zinazoweza kuhitaji unasihi:

i. unyanyaswaji wa kijinsia, kimwili na kisaikolojiaii. msongo wa mawazo unaotokana na hali duni za maisha ya familiaiii. kufiwa na mzazi/mlezi iv. kukosa stadi za kutatua matatizo mbalimbaliv. matatizo ya ukuaji wa mtoto

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 32 25/04/2019 12:50

Page 43: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

33

vi. matatizo ya ujifunzaji mfano, uoni hafifu, usikivu hafifu au maumbile ya mwili yanayoweza kukwaza ujifunzaji wa mtoto

vii. vurugu shuleni

Majadiliano na watoto yanaweza kusaidia pia kujijengea uwezo wa kufahamu hatua na mwelekeo unaofaa kufuatwa ili kukabiliana na changamoto za kila siku. Changamoto kama ya kukosa fursa ya kwenda shuleni ama kukosa mtu wa kumwamini kwa ajili ya kueleza matatizo yake zinatatuliwa kwa ushauri wa namna mbadala inayofaa kuchukuliwa na mtoto kuzikabili changamoto zinazohusika.Changamoto zinazohitaji ushauri zinaweza kuwa:

i. kukosa fursa ya kwenda shuleii. kukosa mtu wa kumwamini kwa ajili ya kueleza matatizo yakeiii. kutopenda shuleiv. kutotumia lishe borav. afya na usafivi. hali ya kutojali

Fafanua ni mbinu zipi utakazotumia kuwashauri na kuwanasihi watoto?

6.3 Namna ya kutoa ushauri na unasihi katika ufundishaji na ujifunzaji

Ushauri na unasihi ni muhimu sana katika ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto wa elimu ya awali.

Hivyo, mwalimu unashauriwa kuwaonesha watoto upendo wa hali ya juu ili waweze kuelezea changamoto zinazowakabili katika kujifunza darasani na nje ya darasa. Mtoto anahitaji kutiwa moyo pale anapokosea kwa sababu yupo katika hatua za awali za ujifunzaji. Hivyo ni vyema usimkatishe tamaa pale anaposhindwa kufanya sawa sawa kile anachofundishwa hivyo hujikuta akikasirika au kuchukia kile anachofundishwa. Mwalimu, unapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufundishia

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 33 25/04/2019 12:50

Page 44: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

34

kama vile kuimba, kucheza, kuchora, kusoma kuandika na kuwanasihi watoto namna bora ya kujifunza kutokana na mbinu hizo.

Mtoto anaweza kuwa na matatizo ambayo yanasababisha ashindwe kujifunza.Hivyo, mwalimu unapaswa kuwatambua watoto hao na kutoa ushauri au unasihi kwa kuwashirikisha wazazi/walezi wao na walimu wengine.

Je, ni kwa namna gani utamshauri mzazi/mlezi wa mtoto wa elimu ya awali kuhusu maendeleo ya mtoto wake?

Mara nyingi tunafikiri ushauri na unasihi ni kwa watoto waliopo shule za msingi na sekondari tu. Mawazo haya ni potofu kwani ushauri na unasihi ni kwa watu wote hata kwa watoto wa elimu ya awali ili kuwawezesha kumudu na kutatua changamoto zao. Watoto wengi hawapewi ushauri na nasaha hivyo kujikuta wakikaa kimya na kushindwa kutoa dukuduku zao kwa kuhofia kuchapwa au kugombezwa. Ni vyema kuwa karibu na watoto hawa kila wakati kuwashauri na kuwanasihi kwa mambo yote wanayokumbana nayo shuleni au katika jamii inayowazunguka.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii:1. Kuna tofauti gani kati ya ushauri na unasihi?

2. Ni mambo gani ya watoto unayofikiri kuwa yanahitaji ushauri?

3. Ni mambo gani ya watoto unayofikiri yanahitaji unasihi?

4. Taja changamoto mbili za kushauri na mbili za kunasihi.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 34 25/04/2019 12:50

Page 45: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

35

Sura ya Saba

Ulinzi kwa mtoto

Karibu katika sura ya saba. Katika sura hii utajifunza kuhusu ulinzi kwa mtoto. Baada ya kujifunza sura hii utapata uelewa kuhusu mazingira salama kwa mtoto kujifunza na namna ya kuboresha ulinzi kwa mtoto wakati wote wa ufundishaji na ujifunzaji wa mtoto.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza dhana ya ulinzi kwa mtotoii. kufafanua namna ya kuboresha ulinzi kwa mtotoiii. kueleza namna ya kuzingatia ulinzi kwa mtoto wakati wa

ufundishaji na ujifunzaji

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Nini maana ya ulinzi kwa mtoto?

2. Eleza namna utakavyoboresha ulinzi kwa mtoto.

3. Utawezaje kuzingatia ulinzi kwa mtoto wakati wa ufundishaji na ujifunzaji?

7.1 Dhana ya ulinzi kwa mtoto

Je, unaelewa nini kuhusu ulinzi kwa mtoto?

Ulinzi kwa mtoto ni kumweka mtoto katika hali ya usalama dhidi ya madhara yanayotarajiwa na yasiyotarajiwa. Moja ya mahali panapofaa kumlea mtoto katika hali ya usalama ni Darasa la elimu ya awali. Mwalimu, ujifunzaji katika elimu ya awali ufanyike katika mazingira salama kwa watoto, katika kucheza na kuchunguza

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 35 25/04/2019 12:50

Page 46: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

36

vitu bila hofu. Pia, walimu wana mchango mkubwa katika kumweka mtoto katika hali ya usalama awapo shuleni na nyumbani kwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usalama wa mtoto. Kwa kuzingatia umuhimu wa elimu ya awali, umakini wa kuwalinda watoto unahitajika ili wasipate madhara yoyote wawapo shuleni au hata njiani wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani. Suala hili linahitaji ushirikiano mzuri kati ya mwalimu, watoto na wazazi/walezi wa watoto.

Miaka ya mwanzo ya ukuaji wa mtoto ni muda ambao watoto wanaweza kudhuriwa kwa sababu hawawezi kujilinda wenyewe kwa kuwa wanategemea watu wazima wawalinde. Ni vema walimu wa elimu ya awali wawe karibu na kufuatilia usalama wa watoto kwa kujenga uhusiano chanya na watoto pamoja na familia zao.

7.2 Kuimarisha ulinzi kwa mtoto

Ulinzi na usalama ni kitu muhimu sana kwa mtoto awapo shuleni ama nyumbani. Hii inachangia katika ukuaji na ujifunzaji wa mtoto. Hivyo, shule inapaswa kuwa ni sehemu ambapo:

i. Ni salama kisaikolojia. Mtoto hataumizwa kimwili au kihisia

ii. Ni salama kimwili. Vifaa na midoli inayotumiwa na watoto kujifunzia na kuchezea vinapaswa kuwa safi na salama na vinavyoendana na umri wao. Vifaa katika viwanja vya kuchezea, visiwe vyenye kumuumiza mtoto. Shule ya awali isiwe karibu na maeneo hatarishi kama barabarani au maeneo yenye maji hasa madimbwi au mito. Aidha, watu wazima wahakikishe mazingira wanayotumia watoto kujifunzia na kucheza ni salama.

iii. Ni rafiki kwa mtoto. Mazingira ya shule yawe rafiki kwa watoto ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli wanazozifurahia watoto hujifunza kupitia michezo na shughuli mbalimbali na kuchangamana na vitu salama na vyenye kufurahisha. Michezo na shughuli wanazofanya watoto ziwasaidie kuchangamana na watoto wenzao pamoja na mwalimu wao.

iv. Ni wezeshi. Mazingira wezeshi humpatia mtoto uhuru wa kuzungumza na walimu, watoto wenzao na wazazi/walezi wao juu ya matatizo wanayoyapata shuleni na nyumbani. Watu wazima wanapaswa wawasaidie, wawalinde na kuwahusisha watoto katika njia na vitendo ambavyo vinawasaidia kujenga akili, miili, stadi za kijamii na tabia zao.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 36 25/04/2019 12:50

Page 47: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

37

v. Panamjengea kila mtoto hali ya kujistahi. Maendeleo ya mtoto kijamii na kihisia yapewe kipaumbele katika shule ya awali. Katika kujifunza, watoto hujenga stadi za mawasiliano kwa ajili ya kutoa mawazo yao, na kuwasilisha mahitaji yao na kuona fahari.

vi. Pana usawa. Wavulana na wasichana wanaangaliwa, wanapewa heshima na kupatiwa fursa sawa katika kupata vifaa vya kujifunzia. Kwa kupitia vitendo mbalimbali darasani, wanajifunza kujithamini wenyewe na kuona kuwa wako sawa. Watoto wenye ulemavu na wale wanaotoka katika familia masikini waheshimiwe na walezi, walimu, watoto wenzao, na washiriki kikamilifu katika mpango mzima wa elimu ya awali.

vii. Panawafundisha watoto stadi za kujilinda wenyewe. Watoto na walimu wajadiliane njia mbalimbali wanazoweza kuzitumia kujiweka katika hali ya usalama kama vile kujua jina, namba ya simu, mahali ambapo anaishi, na jinsi ya kujihadhari na watu wasiowajua. Aidha, kujua jinsi ya kutembea barabarani na alama za barabarani ni jambo muhimu kwa usalama wa watoto.

viii. Panaongozwa vizuri. Jamii iliyoko jirani na shule ya awali inapaswa kujua na kuujali mpango wa elimu ya awali, kuwaheshimu walimu na kamati tendaji na kuutegemeza mpango wa ujifunzaji.

Jamii iwe na mpango wa kukutana mara kwa mara kwa kupitia kamati yao ya shule ili kujenga uelewa kuhusu ulinzi kwa mtoto. Wakati wa mkutano na jamii, mjadala ufanyike kuweka utaratibu unaofaa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

i. Jinsi ya kubaini na kutoa taarifa kuhusu unyanyasaji na utelekezwaji wa mtoto

ii. Kukuza mawasiliano ya kuwaangalia watoto katika masuala ya ulinzi kwa mtoto

iii. Kujenga uelewa juu ya ulinzi kwa mtoto

Aidha, wazazi/walezi na walimu wanaweza kufanya kazi pamoja kuboresha malezi ya watoto na kuondoa unyanyasaji na utelekezaji wa watoto.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 37 25/04/2019 12:50

Page 48: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

38

7.3 Namna ya kukuza ulinzi kwa mtoto katika ufundishaji

Watoto wa elimu ya awali wanahitaji sana ulinzi katika eneo la ujifunzaji, hivyo mwalimu unapaswa kuwa na umakini wa hali ya juu kwa watoto hawa kwa kuwakumbusha mara kwa mara kutokufanya matendo yatakayowaumiza. Matendo hayo ni kama vile kuchukua kalamu na kuweka machoni na kuingiza punje ya mbegu puani au masikioni. Hata wakati mwingine kuwaonya kwa upole kutopenda kupigana darasani au nje ya darasa kwani wataweza kuumizana. Hapa watoto wataweza kulindana wenyewe kwa wenyewe kwa kutoa taarifa kwa mwalimu juu ya vitendo vibaya watakavyokuwa wakifanyiwa au vikifanywa na wenzao darasani au nje ya darasa.

Mwalimu, unapaswa pia kuhakikisha kuwa mazingira yanayowazunguka watoto katika shule yako ni salama ili kuepuka watoto kupata madhara wanapojifunza au kucheza.

Je, ni changamoto gani zinazohusu ulinzi kwa mtoto zilizopo katika jamii inayokuzunguka?

Mara nyingi watoto wa elimu ya awali kulingana na umri wao huwaamini watu wote. Hivyo ni muhimu kuwaelimisha juu ya namna ya kujilinda. Ili kuepuka kuibwa au hata kufanyiwa vitendo vibaya kwa kurubuniwa kwa kupewa zawadi. Mwalimu ni vyema kuwakumbusha watoto mara kwa mara kutopokea zawadi au kitu chochote kwa watu wasiowafahamu. Vilevile, mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa mazingira ya shule ni salama wakati wote. Hivyo, ni jukumu letu sote kuwalinda watoto wetu wawapo shuleni na nyumbani.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 38 25/04/2019 12:50

Page 49: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

39

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kujifunza maudhui ya sura hii: 1. Nini maana ya ulinzi kwa mtoto?

2. Eleza namna utakavyotayarisha ulinzi kwa mtoto.

3. Utawezaje kuzingatia ulinzi kwa mtoto wakati wa ufundishaji na ujifunzaji?

Jumuiya za ujifunzaji

Maswali yafuatayo yataongoza majadiliano katika jumuiya za ujifunzaji:1. Ni kitu gani ulichojifunza katika moduli hii ambacho kimekusaidia katika

kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa watoto wa elimu ya awali?2. Ni changamoto gani ulikutana nazo wakati wa ujifunzaji wa maudhui ya

moduli hii?3. Ni mbinu gani ulizotumia katika kutatua changamoto hizo?4. Unadhani nini kifanyike ili kuimarisha ulinzi kwa mtoto katika shule ya

awali?

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 39 25/04/2019 12:50

Page 50: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

40

Faharasa

Huduma Ni jumla ya mambo yote anayopatiwa mtoto kama haki zake za msingi na yakamwezesha kukua vizuri.

Mazingira rafiki Ni maeneo yenye kuvutia, salama na safi yenye kukidhi shughuli ya ujifunzaji wa mtoto ndani na nje ya darasa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto wote.

Mkoba wa kazi Ni jalada au kifaa kinachotumika kuhifadhia kazi za mwalimu alizozifanya hatua kwa hatua katika nyakati tofauti za ujifunzaji ambazo zitatumika katika upimaji ili kutathimini maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji.

Tafakuri Ni ile hali ya kufikiri kwa kina juu ya ubora au udhaifu wa jambo fulani ili kujua kipi kilifanikiwa na kipi hakikufanikiwa na wapi panahitaji maboresho ili kuleta ufanisi.

Umahiri Ni uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ufanisi mkubwa.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 40 25/04/2019 12:50

Page 51: Uchopekaji wa Masuala Mtambuka katika Mtaala wa Elimu ya Awali 3... · mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali

41

Heward, W. L., Alber- Morgan, S.R., and Konrad, M. (2016). Exceptional Children: An intoroduction to Special Education. Peason. Columbus, Ohio. USA.

Ministry of the Education and Vocational Training (2013). National Strategy on Inclusive Education, 2009-17, Ministry of Education and Vocational Training.

Ministry of Education and Culture (2004). Guidelines for Implementing HIV/ AIDS/STDs and Life Skills Education in Schools and Teachers' Colleges Ministry of Education and Culture.

Taasisi ya Elimu Tanzania (2018). Afya na Mazingira. Darasa la Kwanza. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Moduli 3 - Uchopekaji Masuala Mtambuka-icon 9.indd 41 25/04/2019 12:50