1
KUCHAGUA KUKU WA MBEGU (BREEDING STOCK) Kabla ya kuanza mradi wa kuku, ni vizuri uchague mbegu inayofaa kwa kuangalia yafuatayo; Chagua jogoo mwenye afya na mwenye umbile kubwa na mwenye nguvu. Chagua kuku jike (Temba) ambae hana tabia ya kususa mayai wakati wa kuatamia na anaewalea watoto wake vizuri. NB: Kama utatumia kifaa cha kutotoreshea mayai (Incubator) au mama kuku au kuku mwingine (broody hen), tumia mayai yaliyotagwa si zaidi ya siku 14 (wiki 2) SABABU ZINAZOPUNGUZA UZALISHAJI WA KUKU WA KIENYEJI Changamoto kubwa ya kuku hawa wa kienyeji ni kiwango kidogo cha kutaga mayai chini ya asilimia 60% na maranyingi hufika hatima ya kutaga haraka sana tofauti na kuku wa kisasa ambao utagaji mayai hufikia hadi asilimia 80%. Kufuga kuku hawa kwa njia ya kisasa ni gharama sana na mara nyingine unakuta unashindwa kurudisha gharama za uzalishaji. Lakini kama mfugaji atajipanga vizuri kimkakati anaweza akapunguza hasara na kuongeza faida. Ugonjwa wa Kideli (New castle disease) husababisha kuku wengi kufa kwa wakati mmoja, hivyo kuathiri kipato cha mfugaji kwa kiwango kikubwa Ndui ya kuku (Fowl Pox/pimple head) husababisha uzalishaji kupungua. Chawa, kupe na utitiri ambao jhusababishwa na uchafu bandani hupunguza uzalishaji wa kuku. Minyoo inayosababishwa na majeraha yaliyotokana na ndege wengine Damu inayoonekana kwenye kinyesi inayotokana na Muharo mwekundu (Coccidiosis), homa ya matumbo (Fowl typhoid) au homa ya kipindupindu (Fowl cholera) husababisha kuku kukua taratibu sana na kudumaa na kuwa dhaifu. Utotoaji wa kiwango kidogo unaotokana na kuhifadhi mayai machafu (yenye damu au uchafu), pia kutumia mayai yenye umri zaidi ya siku 14 kutoka kwa kuku wenye mbegu za ubora wa chini. UZURI WA KUKU WA KIENYEJI 1. Ladha ya Nyama na mayai yake ni tamu sana na hupendelewa na watu wengi kulinganisha na kuku wa kisasa. 2. Mtaji wa kuanzia kufuga kuku hawa wa kienyeji ni kidogo sana kulinganisha na kuku wa kisasa. 3. Wanavumilia sana mazingira hatarishi ikiwa ni pamoja na magonjwa 4. Wanalishwa vyakula vya gharama ya chini vinavyopatikana kwenye mazingira ya mfugaji 5. Wakiachiwa wajitafutie wenyewe, gharama za chakula zinakua ndogo kwa mfugaji. 6. Maranyingi Wanawake na watoto, wanajipatia kipato chao kutokana na ufugaji wa kuku. 7. Soko la kuku na mayai ya kienyeji linapatikana kwa kiasi kikubwa. 8. Kinyesi chao ni mbolea nzuri sana kwa mazao ya bustani na mazao mengine. KWA NINI UNATAKIWA KUBOLESHA UFUGAJI WA KUKU HAWA? 1. Hali ya kuku kufa kutokana na magonjwa itapungua kwa kiasi kikubwa. 2. Ukifikia hatua ya kuangua mayai na kuuza vifaranga, mapato yako yataongezeka sana (mara 7 zaidi) kuliko kuuza mayai. 3. Kuangua mayai mengi kwa wakati mmoja hupelekea vifranga wengi kupatikana kwa wakati mmoja hivyo kusaidia taratibu za chanjo kufanyika vizuri na kwa ufanisi. 4. Utaweza kushirikiana na wafugaji wenzako, hivyo kwa wafugaji wenye kuku wachache wataweza kupata chanjo kwa bei ndogo ya kuchangiana. 5. Unaweza kupanga uzalishaji wa kuku wako ili kuteka soko hususani wakati wa sikukuu kubwa kama Christmas, Pasaka (Easter), Iddi na sherehe mbalimbali, utaratibu huu utakuongezea kipato kwa kiasi kikubwa. JINSI YA KUANZA KUFUGA Kabla ya kuanza ufugaji jitahidi uwe na mahitaji yafuatayo; 1. Uwiano wa kuku jike na jogoo uwe 10:1, yaani kila kuku jike (tetea) 10 jogoo awe mmoja. Ina maana kwamba kama una kuku jike 30, jogoo wawe watatu (3). 2. Maji na vifaa vya kulishia & kunywea maji 3. Banda la kuku la kutosha. 4. Sehemu ya kutagia mayai 5. Maranda ya mbao au mapumba ya mpunga kwa ajili ya kuweka juu ya sakafu la banda, ili kuongeza joto bandani. 6. Madawa ya kutibu na kukinga magonjwa (Drugs and Vaccines) KUCHAGUA KUKU WA MBEGU (BREEDING STOCK) 1. Chagua kuku jike mwenye afya, umbile zuri na mkubwa, pia ambaye hasusi mayai wakati wa kuatamia, pia anayetunza vizuri vifaranga wake. 2. Chagua jogoo mwenye afya, mkubwa na mwenye nguvu. SIFA ZA BANDA Banda kubwa na lenye hewa ya kutosha ndilo linalofaa kwa ufugaji bora wa kuku wa kienyeji. Sifa nyingine nyingi za banda bora nimezieleza kwa undani kwenye Sehemu ya kwanza ya makala hii, bofya hapa kuona sifa hizo. Bofya hapa kurejea sehemu ya kwanza ya Makala hii. MABORESHO YA UFUGAJI BORA 1. Chakula, Chanjo na Matibabu mara tu Wanapougua Andaa chakula chenye lishe mbali mbali (Balanced diet), kwa mfano Pumba, Mashudu, kiasi kidogo cha dagaa waliosagwa na mboga za majani, pia kuku watajiongezea virutubisho wakila wadudu waliopo kwenye mazingira yao. Wapatie maji ya kutosha wakati wote. Wapatie chanjo za kuwakinga na Magonjwa Watibu mara tu wanapougua. 2. Usafi wa Banda Hakikisha banda linakua safi wakati wote, ili kuwakinga kuku wasipatwe na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko. 3. Kukusanya mayai Sehemu ya kutagia mayai lazima iwe salama, kavu na yenye kiza kidogo. Kusanya mayai kila siku andika tarehe ya kutagwa yai hilo juu ya yai kwa kutumia penseli. Hakikisha unahifadhi mayai kwenye trei, sehemu pana ya yai iangalie juu na sehemu nyembamba iliyochongoka iangalie chini, kwa sababu sehemu hiyo pana ina kimfuko cha hewa ambacho husaidia kifaranga kukua kikiwa ndani ya yai. Tunza mayai yako sehemu ya chini ndani ya nyumba, kwa sababu sehemu ya chini ndani ya nyumba kuna joto la kadri tofauti na sehemu ya juu. Joto linalotakiwa ili kutunza uhai wa yai ni sentigredi 10 hadi sentigredi 21 (10°C - 21°C) Usioshe mayai na maji, “chonde chonde usioshe mayai na maji” kwa sababu ukiosha na maji bacteria wanaweza wakaingia ndani ya yai kupitia gamba la yai. Kama mayai yako yana udongo, yafute kwa karatasi kavu au kitambaa kikavu au tauro kavu. Kama limechafuka sana halifai kwa kuanguliwa. Chunguza mayai yako kama yamevunjika au yana kreki au yaliyokua na shepu mbaya, mayai ya namna hiyo hayafai kuanguliwa au kuatamiwa. Wakati wa kuweka alama au tarehe za kutagwa kwenye mayai, tumia penseli. Usithubutu kutumia kalamu ya wino au mark pen au kuweka alama ya kudumu ya wino, kwa sababu baadhi ya wino huwa na sumu inayoweza kuharibu kiini cha ndani cha yai. Kuandika tarehe ya kutagwa kwenye yai ni jambo la msingi sana kwa sababu utaweza kujua umri wa yai tangu kutagwa. NB: * Mayai yanayofaa kuanguliwa ni yale yenye umri wa siku 7 hadi 10, mayai yenye umri zaidi ya siku 10 hayafai kuanguliwa kwa sababu uwezo wake unakua mdogo sana. * 4. Kuangua mayai / Kuatamia Tumia mayai yaliyotagwa si zaidi ya wiki mbili zilizopita Angua vifaranga kwa kutumia mama kuku, au kuku wengine wanaoatamia, au bata au mashine ya kutotoreshea (incubator). Kwa kuku na bata hakikisha unawapa idadi ya mayai kulingana na ukubwa wa maumbile yao, yaani lazima mayai yatoshe chini ya matumbo yao wakati wa kuatamia. Baada ya kuangua mayai safisha maeneo ya kutagia pamoja na kutupa maganda ya mayai yaliyoanguliwa. Kama unatumia mashine ya kuangulia mayai, hakikisha unageuza mayai angalau kwa siku mara 3, isipokua siku tatu za mwisho kuelekea kuangua vifaranga (Siku ya 1 hadi 18: Geuza mayai, Siku ya 19 hadi 21: Usigeuze mayai) KULEA VIFARANGA Wapatie maji safi na salama wakati wote Wapatie vyakula laini kama unga wa nafaka au mazao ya mizizi. Waruhusu vifaranga watembee kwa uhuru, wakifikia wiki 3 au 4. Wapatie vifaranga wako chanjo ya KIDELI wakiwa na umri wa siku 4 tangu kuzaliwa. KUWEKA KUMBUKUMBU Mfugaji anapaswa aweke kumbukumbu kimaandishi kwa kila anachokifanya kwenye mradi wake, hii itamsaidia kumpa dira mfugaji kama anafuga kwa hasara au kwa faida. Mfano wa kumbukumbu anazoweza kuandaa ni pamoja na Gharama za kuanzisha mradi, gharama za kendeshea mradi kama chakula na usafiri, idadi ya kuku jike, Majogoo, vifaranga, idadi ya mayai yanayokusanywa kwa siku au wiki au mwezi, Idadi ya mayai yaliyoanguliwa na taarifa nyingine muhimu. MAGONJWA YA KUKU Udhibiti wa magonjwa mbalimbali ya kuku ni muhimu sana kwa mfugaji, udhibiti huo ni pamoja na Kukinga kuku wako dhidi ya magonjwa ambukizi kwa kuwapa Chanjo mbalimbali pamoja na kuzingatia usafi wa banda na chakula. Pia udhibiti wa magonjwa ni pamoja na kuwatibu kuku mara wanapoumwa. Asilimia kubwa magonjwa yanayoathiri wa kuku ni yale yanayodhibitiwa na Chanjo, Kwa hiyo ukizingatia utoaji wa chanjo kwa kuku wako kama inavyofaa kitaalamu, utaweza kidhibiti vifo vya kuku kutokana na magonjwa kwa asilimia kubwa. Mambo Muhimu ya kuzingatia ili Kufanikisha chanjo bora Chanjo mbalimbali za kukinga magonjwa zina utaratibu wake kitaalamu, kama namna ya utunzaji na namna kuwapa kuku. Zifuatazo ni dondoo muhimu za kufahamu ili chanjo yako ifanikiwe; 1. Ukihifadhi chanjo yako hovyo hovyo bila kufwata maelekezo ya kitaalamu, chanjo hiyo inakua Sumu badala ya kuwa kinga na tiba. Chanjo iliyohifadhiwa vibaya haiwezi kufanikisha matibabu. Chupa za chanjo huwa zinakuwa na lebo au karatasi yenye maelekezo ya jinsi ya kutumia pamoja na tarehe ya mwisho ya matumizi (Expire date). Usipochanja kuku wako vizuri, ugonjwa unaweza kuenea zaidi. 2. Vifaranga vilivyoanguliwa huweza kuwa na magonjwa mbalimbali yaliyotoka kwa Mama kuku, kupitia yai. Kwa hiyo kuwachanja kuku walio na umri chini ya siku kumi (10) ni muhimu sana, kwa sababu itazuia magonjwa ambukizi kwa vifaranga kadri wanavyokua. 3. Kila chanjo imetengenezwa kwa kuwekwa mahali sahihi kwenye mwili wa kuku, kuna baadhi huwekwa kwenye macho, baadhi kwenye maji na baadhi huchomwa kwa sindano kwenye mabawa. Kwa hiyo usibadilishe matumizi ya chanjo. 4. Usiwape chanjo kuku Waliokwisha kuugua [Isipokua kama kuna mlipuko wa ugonjwa wa Laryngotracheitis au Fowl pox] 5. Hifadhi chanjo mahali salama pasipokua na joto & mwanga wa jua wa moja kwa moja. 6. Chanjo zilizo nyingi ni viumbe hai visivyoonekana kwa macho (Living micro-organisms) au chembe chembe zinazotengeneza magonjwa (disease-producing agents), Kwa hiyo hifadhi chanjo zako kwa Uangalifu. 7. Kama unatumia maji ya kunywa kuku kama njia ya kuwapa chanjo, hakikisha Unatumia maji yasiyokua na chumvi na Chlorine, kwa sababu chembechembe au viumbe waliopo kwenye chanjo huharibiwa na hizo kemikali. 8. Baada ya kutoa chanjo hakikisha unachoma au unavitibu (Kuosha na Kemikali inayoua vimelea vya magonjwa, Disinfect) vifaa vyote ulivyotumia wakati wa kutoa chanjo. Ukifanya hivi utazuia kueneza magonjwa kwa kuku wazima wasiokua magonjwa. MAGONJWA YA KUKU NA UDHIBITI WAKE 1. MUHARO MWEKUNDU (COCCIDIOSIS) Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Coccidian, vimelea hivi huzaliana haraka sana kwenye utumbo mwembamba wa kuku. Mara nyingi ugonjwa huu huwakumba kuku walio na umri wa wiki 8 hadi 10, mara nyingi ugonjwa huu unaweza ukaua kuku kwa muda mfupi wa siku 5 hadi 7 (Acute type) au unaweza ukaua Kuku baada ya muda mrefu kupita (Chronic type). Dalili za Ugonjwa Kuku wanakua dhaifu, wanazubaa na kuinamisha kichwa chini Kuku wanakua na manyoya yaliyovurugika Kuku wanapauka mdomo na miguu Kuku wanatoa kinyesi cha damu, hii hutokea endapo vimelea vya ugonjwa huu vikizaliana kwenye utumbo mpana wa kuku. Kuku wanakufa wengi kwa muda mfupi. Namna ya kudhibiti Tumia dawa za Salfa (Sulphur drugs) kwa matibabu Tumia dawa za kuzuia kuzaliana kwa vimelea wa ugonjwa huu (Coccidiostat) kwa kuweka kwenye Chakula. Hakisha banda linakuwa kavu wakati wote, kama unatumia mapumba ya mpunga au malanda ya mbao kwa kuweka chini, basi zingatia usafi yaani badilisha mapumba hayo au malanda yaliyoloana na kuweka Makavu. 2. KIPINDUPINDU CHA KUKU (FOWL CHOLERA) Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Pasteurella avicida na vimelea vingine vinavyozaliana kwa kasi sana ndani ya damu na kusababisha sumu. Kuku wagonjwa, Ndege wa mwituni, binadamu, wanyama na vifaaa mbalimbali husambaza ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa. Dalili za Ugonjwa Kuku wanatoa majimaji au udenda wa rangi ya manjano Kuku wanaharisha uhalo wa njano au wa kijani Kuku wananyong’onyea kama wamemwagiwa maji Kuku wanapatwa na homa na wanalala kila wakati Kuku wanakaa wakiwa wameinamisha kichwa chini au wanageuza kichwa uelekeo wa mkia au wanalaza kichwa juu ya mabawa uelekeo wa mkia. Picha: Kinyesi cha kuku mgonjwa Namna ya kudhibiti Teketeza au choma moto kuku wote waliokufa ghafra Hakikisha banda la kuku linakua safi wakati wote Tumia dawa za Salfa (Sulphur drugs) kuwatibu kuku waliougua Hakikisha hakuna unyevuunyevu ndani ya banda kwa kubadilisha mapumba ya mpunga au malanda ya mbao yaliyoloana, kwa sababu unyevu unyevu ndani ya banda husababisha kuzaliana kwa vimelea (Coccidian) vya ugonjwa huu. 3. KIDELI/MDONDO (NEW CASTLE DISEASE) Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huathiri mfumo wa upumuaji na neva za fahamu. Vifo vya vifaranga na kuku wakubwa huanzia asilimia 0 hadi 100%, itategemeana na kasi ya mashambulizi ya virusi hao. Dalili za Ugonjwa Uzalishaji wa mayai hupungua kwa kasi kubwa hadi kufikia sifuri (0) ndani ya siku nne. Kuku wanapalalaizi shingo na kupinda Kuku wanakohoa na kupumua kwa shida na wakati mwingine hutokwa na majimaji puani. Kuku wanaharisha muharo wa majimaji wenye rangi ya kijani mpauko. Kuku wakianza kutaga tena, mayai yao huwa na sura isiyokua ya kawaida au sura iliyopindapinda. Kuku wanakohoa na kupiga chafya Kuku wanakaa wakiwa wamenyong’onyea viungo vya miguu na mara nyingine wanatembea kinyumenyume. Kuku wanatembea kwa kuzunguka mduara au wanainamisha vichwa vyao katikati ya miguu. Kuku wanakosa hamu ya kula, hali ikiwa mbaya sana wanakaa chini na kupoteza fahamu na baadae hufa. Picha: Kuku mwenye kideli aliyepalalaizi shingo Namna Ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa, maji maji ya kuku kama udenda au kinyesi. Pia husambazwa kupitia vifaa mbalimbali vilivyochafuliwa na majimaji yaliyotoka kwa kuku kama udenda au kinyesi. Pia Virusi vya kideli husambazwa kupitia mayai yaliyotagwa na kuku muathirika wa ugonjwa huu, Uzuri ni kwamba kiini cha yai lenye vimelea vya kideli hufa na yai kushindwa kuanguliwa. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba, bali hukingwa kwa chanjo. Wapatie chanjo ya kideli kuku wako wenye umri wa wiki 3 hadi 4, pia rudia tena chanjo wakiwa na umri wa wiki 16 na wakifikia wiki 24. Baada ya hapo uwapatie tena chanjo mara uonapo kuna mlipuko wa ugonjwa kwenye eneo lako. 4. HOMA YA MATUMBO (FOWL TYPHOID) Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa gallinarum au shigella gallinarum. Dalili za ugonjwa huonekana siku 3 hadi 4 baada kuku kuingiliwa na vimelea, pia vifo huonekana ndani ya wiki 2 tangu kuona dalili. Ugonjwa huu husambazwa kupitia kuku walioathilika, vifaa mbalimbali ikiwemo vya kuku, viatu, unyevu unyevu ndani ya banda (hususani kwenye sakafu ya banda kama mapumba ya mpunga au malanda ya mbao), n.k Dalili za Ugonjwa Kuku wanazubaa na manyoya yao yanakua hovyo hovyo tofauti na kuku wasiougua. Kichwa chake hupauka, na upanga wa kichwani hulegea na kulala Wanakosa hamu ya kula Wanaharisha kinyesi cha rangi ya chungwa Namna ya kudhibiti Wape chanjo ya ugonjwa huu kwa kuku wenye umri wa wiki saba (7) Teketeza kuku wote waliokufa kwa kuchoma moto Usiruhusu watu mbali mbali kutembelea mazingira ya banda lako bila kuondosha vimelea (Disinfection) kwa kukanyaga sehemu yenye maji ya dawa (Footbath) kila wanapoingia au wanapotoka bandani. Tumia dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu. 5. PULLURUM DISEASE (MUHARO MWEUPE) Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Salmonella Pullurum, vimelea hivi huathiri mfuko wa mayai wa kuku jike (Ovary). Vimelea hivi pia hukaa kwenye utumbo mwembamba wa kuku. Ugonjwa huu husambaa kwa kupitia mayai yaliyotagwa na kuku aliyeathirika na ugonjwa huu pia vifaranga walioanguliwa kutokana na mayai hayo huwa na vimelea vya ugonjwa huu. Dalili za Ugonjwa Vifaranga wanalia kwa kutoa sauti kali Manyoya yanavurugika Sehemu ya hajakubwa ya vifaranga hulowana kinyesi Kuku wakubwa hawaonyeshi dalili zozote. Kwa vifaranga dalili huonekana kuanzia siku 4 hadi 10, na vifo hutokea baada ya wiki 3 tangu kuanza ugonjwa. Kuku wanaharisha muharo mweupe. Namna ya kudhibiti Teketeza Kuku wote wenye ugonjwa huu Safisha vifaa vyote bandani kwa kutumia kemikali (Disinfectant) itakayoua vimelea wa magonjwa, pia safisha vifaa vya kuangulia mayai (Incubators). Nunua kuku au vifaranga wasiokua na magonjwa kutoka kwa wauzaji wanaodhibiti vizuri magonjwa ya kuku. 6. NDUI YA KUKU (FOWL POX) Ugonjwa husababishwa na virusi, huathiri ngozi ya kuku. Kuku wanakua na mabaka mabaka usoni hususani upanga wa juu na wa chini. Ugonjwa huu umegawanyika makundi mawili; Hali ya ukavu (dry form) na Hali ya unyevu (Wet form). Hali ya ukavu huwa na muonekano wa vivimbe vigumu vidogovidogo kwenye maeneo ya mwili wa kuku yasiyo na manyoya kama Kichwa, miguu, sehemu ya hajakubwa n.k). Hali ya unyevu huwa na uwepo wa vidonda visivyopona maeneo ya mdomoni, koo la chakula na koo la hewa. Hali hii husababisha kuku kutopumua vizuri, Kuku wanaweza kupata mojawapo ya kundi la ugonjwa huu au yote makundi mawili. Dalili za ugonjwa Vivimbe vigumu vidogovidogo kwenye maeneo ya mwili wa kuku yasiyo na manyoya kama Kichwa, miguu, sehemu ya hajakubwa n.k). Kuku kupumua kwa taabu. Namna Ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kwa kugusana moja kwa moja kati ya kuku mgonjwa na kuku asiyeumwa au kupitia Mbu. Pia ukurutu uliotoka kwa kuku mgonjwa huwa ni mojawapo ya chanzo cha kusambaza ugonjwa. Virusi wa ugonjwa huu huingia kwenye mishipa ya damu ya kuku kupitia Macho, Ngozi, vidonda, au kupitia koo la hewa. Mbu wanabeba virusi hivi baada ya kufyonza damu ya kuku mwenye ugonjwa huu. Ushahidi wa kisayansi unasema kwamba Mbu aliyebeba virusi hivi huathirika kwa maisha yake yote. Mbu ndio wasambazaji wa kwanza wa ugonjwa huu. Mbu wa aina nyingi husambaza ugonjwa huu mara nyingi wakati wa kipindi cha baridi. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba, hivyo unazuiwa kwa chanjo. Ugonjwa huu unasambaa polepole kwahiyo ukipiga chanjo unazuia maambukizi haraka sana. Chanjo hii inawekwa kwenye mabawa ya kuku kwa sindano. Pia unaweza kudhibiti ugonjwa huu kwa kuua na kuangamiza mazalia ya Mbu. Ingawaje kama ugonjwa umesambaa kwa kiasi kikubwa ni muhimu kupiga chanjo. Weka maji ya kuosha viatu (Footbath), ili kuzuia vimelea vya nje kuingizwa ndani ya banda. Punguza idadi ya watu wanaotembelea bandani Kila unapotembelea bandani au kufanya kazi, hakikisha unaanzia kwenye kuku wadogo au vifaranga halafu unamalizia kwenye kuku wakubwa. Hii itasaidia kupunguza vimelea vya magonjwa kusambaa kutoka kwa kuku wakubwa kwenda kwa wadogo. Safisha vifaa vyote bandani kwa kutumia kemikali (Disinfectants) ya kuzuia ukuaji wa vimelea. Kitu cha msingi kwa ugonjwa huu ni kwamba Usiwape chanjo kuku wako kama ugonjwa haujaingia kwenye eneo lako au kwenye banda lako, kwa hiyo hakikisha unapiga chanjo baada ya ugonjwa kuingia. 7. MAHEPE (MAREK’S DISEASE) Majina mengine ya ugonjwa huu ni kama Acute leukosis, Neural leukosis, Range paralysis na Gray eye (Kama macho yameathirika). Ugonjwa huu hufanana na ugonjwa unaoitwa Lymphoid Leukosis, lakini tofauti ni kwamba; Ugonjwa wa Marek’s hutokea kwa kuku wenye umri wa wiki 12 hadi 25, wakati ugonjwa wa Leukosis huwapata kuku wakiwa na umri wa wiki 16. Ugonjwa wa Marek’s ni aina ya Kansa ya ndege (Kuku), Husababishwa na virusi wanaoleta uvimbe ndani ya mishipa ya neva za fahamu, hatimae kuku wanapalalaizi viungo na kulemaa. Vilevile uvimbe hutokea kwenye macho na kusababisha mboni za jicho kubadilika hatimae macho kupofuka. Uvimbe uliopo kwenye viungo mbalimbali vya mwili kama Ini, Figo, Nyongo, Kongosho, Mapafu, Misuli, Ngozi na viungo vingine, husababisha mwili wa kuku kutofanya kazi vizuri na kudhoofu. Kwa hali hiyo kuku wenye ugonjwa huu huwa na dalili zifuatazo; Dalili za ugonjwa Kupumua kwa shida Sehemu za nyama zilizoshika manyoya huvimba Wanaharisha kinyesi cha kijani Hali ikiwa mbaya sana, kuku wanadhoofu na kukonda sana pia upanga wa juu na chini wa kichwa hupauka na kuwa na magamba. Wanapalalaizi viungo hususani miguu Mboni ya macho hubadilika isivyokawaida hatimae kuku hushindwa kuona kabisa Namna Ugonjwa Unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa ndani ya banda. Virusi wa ugonjwa huu hutoka kwa kuku wagonjwa kutoka kwenye manyoya ya kuku yaliyonyofoka, vumbi ndani ya banda, kinyesi na Mate au majimaji ya kuku. Kuku walioathirika hubeba virusi ndani ya damu kwa maisha yao yote na ndio chanzo cha kuambukiza kuku wengine wenye afya. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba, kwa hiyo kinachotakiwa ni kuwapatia kuku wako chanjo. Chanjo ya Ugonjwa huu inazuia utengenezaji wa uvimbe (Kansa) kwenye viungo mbalimbali vya mwili wa kuku. 8. MATATIZO YA MFUMO WA UPUMUAJI (INFECTIOUS BRONCHITIS) Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na IB, Brionchitis, cold. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huathiri mfumo wa upumuaji wa kuku. Athari za ugonjwa huu hutegemeana na umri na kinga ya kuku aliyonayo, mazingira ya kuku na uwepo wa magonjwa mengine ya kuku. Pia ugonjwa huu huathiri tishu mbalimbali za mwili ikiwemo mfumo wa uzazi wa kuku jike (Reproductive tract). Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu; Dalili za Ugonjwa Kuku wanakosa hamu ya kula na kunywa maji Kuku wanalia kwa sauti kali, hutokwa machozi machoni na puani. Kuku wadogo hupumua kwa shida kwa kukoroma. Kuku wanapumua kwa kukoroma wakati wa Usiku. Uzalishaji wa mayai hupungua kadiri siku zinavyokwenda, unaweza ukaona uzalishaji wa mayai ukaongezeka baada ya wiki 5 au 6 lakini kwa kiwango kidogo sana. Gamba la yai huwa rafu na majimaji ya yai huwa maji kabisa. Picha: Kuku akikoroma na kupumua kwa shida, mdomo upo wazi anajaribu kuvuta hewa kwa mdomo Picha: Magamba ya mayai yapo rafu Picha: Magamba ya mayai yapo rafu na baadhi hupasuka Namna ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa, mifuko ya chakula, mizoga ya kuku iliyokwisha kufa kwa ugonjwa huu, banda la kuku lenye virusi vya ugonjwa huu na panya. Virusi vya ugonjwa huu hupenyeza kwenye mayai yaliyotagwa, Uzuri ni kwamba kiini cha yai hilo hufa na yai hushindwa kuanguliwa. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba, bali unakingwa kwa chanjo. Dawa za Antibayotiki kwa siku 3 hadi 5 zinaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huu kwa kutibu magonjwa nyemerezi yanayosababishwa na bacteria. Dawa hizo za Antibayotiki hazitibu ugonjwa huu bali zinapunguza kasi ya ugonjwa. 9. MAFUA YA NDEGE (AVIAN INFLUENZA) Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na AI, Flu, Influenza, Fowl plague. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huathiri mfumo wa upumuaji wa kuku. Ugonjwa huu huwakumba kuku na jamii zote za ndege. Virusi wa Mafua ya ndege huishi muda mrefu kwenye mazingira tofauti tofauti bila kupoteza uhai wake. Virusi hawa wanaweza kuishi kwenye mazingira ya joto la kadiri au baridi kali, pia wanaishi vizuri kwenye mazingira ya barafu iliyoganda. Hii hupelekea ugonjwa huu kusambazwa kupitia kinyesi na mizoga ambayo haikuteketezwa vizuri. Dalili za Ugonjwa Kuku wanakosa hamu ya kula. Kuku wanapata matatizo ya mfumo wa upumuaji kama kupiga chafya, kukohoa n.k Kuku wanaharisha sana Uzalishaji wa mayai hupungua kwa kasi sana Kuku wanavimba upanga wa juu na chini wa kichwa. Kuku wanakua na madoa mekundu au meupe kwenye miguu na upanga wa kichwani. Kunaweza kukawa na matone ya damu yayotoka puani Vifo huweza kuanzia asilimia chache hadi kukaribia asilimia 100%. Namna ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kupitia vifaa mbalimbali vilivyochafuliwa na majimaji au kinyesi cha kuku Mwenye ugonjwa kama viatu, nguo, trei za mayai, vifaa vya kulia na kunywea maji na vifaa vingine. Wadudu mbalimbali na panya wanaweza kusambaza ugonjwa huu kwa kubeba virusi kutoka weye mzoga wa kuku aliyekufa kwa ugonjwa huu. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba, bali unachanjo. Pia dawa za Antibayotiki mbalimbali huweza kutumika kupunguza kasi ya ugonjwa kwa kuua bakteria wa magonjwa nyemerezi. Kuku wakipata nafuu kidogo huendelea kupunguza kasi ya virusi, lakini dawa hizi za Antibayotiki haziui virusi. Chanjo ya ugonjwa huu isitumike bila ruhusa maalum kutoka kwa wataalamu wa mifugo na serikali kwa ujumla. Udhibiti wa uingizwaji wa kuku na jamii nyingine za ndege ndani ya eneo husika hususani mipakani. Ugonjwa huu huathiri maeneo makubwa kama nchi nzima, mikoa au wilaya, hivyo taratibu za kuzuia uingizwaji au kutoa jamii ya ndege mbalimbali kwa eneo husika (Quarantine) hufanywa na taasisi mbalimbali za serikali hususani Wizara ya mifugo (kama Wizara ya mifugo na uvuvi nchini Tanzania) Teketeza kwa kuchoma moto mizoga ya kuku wote wenye ugonjwa huu (Hii ndio njia bora zaidi ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huu, ikifuatiwa na chanjo pamoja na kuzuia uingizwaji na utoaji wa jamii zote za ndege kwa eneo husika) Muhimu* Kama umegundua kwamba shamba lako au banda lako la kuku lina ugonjwa huu, toa ripoti kwenye mamlaka husika hususani Maafisa mifugo wa vijiji au Kata, kama maafisa hawapo kwenye maeneo yako toa taarifa wilayani kwenye Idara ya mifugo. 10. INFECTIOUS CORYZA Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na Roup, cold, coryza. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya Bakteria vinavyoitwa Haemophilus paragallinarum. Kuku ambao hawahudumiwi vizuri kiasi kwamba wakawa wanaishi kwenye mazingira machafu yasiyofaa, wako hatarini sana kukumbwa na ugonjwa huu. Dalili za ugonjwa Kuku wanavimba usoni Wanapumua kwa shida Wanatoa harufu mbaya Wanatoa majimaji puani na machoni Macho yanatoa majimaji na kushikamana Wanaweza kuharisha Kuku wadogo wanadumaa Vifo vinanzia asilimia 20% hadi 50% Ugonjwa unaweza ukadumu siku chache au miezi michache inategemeana na kiwango cha magonjwa nyemelezi yaliyopo Namna ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya mgusano baina ya kuku na kuku. Pia kuku wanaweza kuambukizwa kupitia hewa, kwa kuvuta hewa yenye vimelea vya ugonjwa huu Vile vile kuku wanapata ugonjwa huu kwa kula vyakula na maji yaliyochafuliwa na uchafu wenye bakteria wa ugonjwa huu. Pia ugonjwa unaweza ukasambazwa endapo mizoga ya kuku wenye ugonjwa kuwekwa ndani ya banda la kuku. Pia kuku waliopona wanakua bado na vimelea hivi kwa maisha yao yote. Namna ya kudhibiti Fuga kuku wako katika mazingira ya usafi, kwa sababu uchafu ndio chanzo cha mlipuko na kusambaa kwa vimelea hivi. Tumia dawa mbalimbli za antibayotiki kutibu ugonjwa huu, dawa hizi hufanya kazi vizuri kama utatibu mapema kuku wako, wakati maambukizi ndo yameanza. Dawa hizo ni zenye viua sumu vya erthyromycin, streptomycin na sulfonamides. Mfano wa dawa hizo kwa majina ya kibiashara ni kama Sulfadimethoxine (Albon®, Di-Methox™) hii dawa ndio inayopendekezwa sana. Kama dawa hii haipo au haifanyi kazi vizuri jaribu dawa hizi=> sulfamethazine (Sulfa-Max®, SulfaSure™), au erythromycin (gallimycin®), au tetracycline (Aureomycin®). Punguza msongamano wa kuku ndani ya banda, hii itasaidia kuruhusu hewa ya kutosha bandani. Kama kuna mlipuko mkubwa wa ugonjwa huu kwenye eneo lako, piga chanjo. 11. ASPERGILLOSIS Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na Brooder pneumonia, mycotic pneumonia, Aspergillus. Ugonjwa huu husababishwa na fangasi. Kama chanzo cha vimelea ni viwanda vya kutotoreshea vifaranga ugonjwa huu utaitwa brooder pneumonia. Ugonjwa huu ukiwapata kuku wakubwa unaitwa Aspergillosis. Dalili za Ugonjwa Ugonjwa huu huanza kuwa mkali sana kwa kuku wadogo na hukomaa sana kwa kuku wakubwa. Kuku wadogo hupumua kwa shida Wakati wa usiku au mchana kuku hawakoromi kama magonjwa mengine. Kuku wanakosa hamu ya kula kuku wanapalalaizi viungo na kulemaa kwa sababu ya sumu ya fangasi hao. Vifo vinaanzia asilimia 5% hadi 50% Kuku wakubwa wanapata matatizo ya kupumua na kukosa hamu ya kula. Kuku wanakua na rangi ya bluu na nyeusi kwenye ngozi (cyanosis) Kuku wanakua na matatizo ya neva za fahamu kama kupinda shingo. Vifo kwa kuku wakubwa huwa ni chini ya asilimia 5%. Namna ugonjwa unavyosambazwa Vimelea vya fangasi huzaliana kwa kasi kwenye joto la kawaida la bandani Vimelea hivi husambazwa kupitia masalia ya mimea yaliyowekwa juu ya sakafu la banda kama mapumba ya mpunga, malanda ya mbao na masalia mengine. Pia Kuku wanaambukizwa kupitia vyakula na maji yaliyochafuliwa na uchafu wenye vimelea hivi. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba kwa kuku waliathirika Ugonjwa huu unazuiwa kwa kuhakikisha usafi wa banda kila wakati na kuruhusu hewa ya kutosha bandani. Ili kuondoa chanzo cha maambukizi, weka dawa za kuua hao fangasi kwenye chakula kama Mycostatin, Mold curb, Sodium, Calcium Propionate na Gentian violet), pia weka Copper sulfate au Acidified copper kwenye maji ya kunywa kwa siku tatu. Pulizia mapumba ya mpunga au malanda dawa ya kudhibiti vumbi na usambazaji wa vimelea vya fangasi, dawa hiyo inaitwa Germicide yenye mafuta (Oil-base germicide) Osha vifaa vya kulia na kunywea maji na kemikali zinazoua vimelea vya fangasi (Disinfectant). 12. GUMBORO (INFECTIOUS BURSAL DISEASE) Majina mengine ya Ugonjwa huu ni kama IBD, Infectious bursitis na infectious avian nephrosis. Gumboro ni Ugonjwa unaosababishwa na virusi, pia dalili za ugonjwa huu huonekana kwa kuku wenye umri wa Zaidi ya wiki 3. Pia manyoya yanayozunguka sehemu ya hajakubwa huwa yametapakaa kinyesi chenye muonekano wa chumvi chumvi. Dalili za Ugonjwa Manyoya ya kuku huwa rafu Kuku wenye umri chini ya wiki tatu hawaonyeshi dalili zozote Kuku wanaishiwa nguvu halafu wanakaa mkao wa kubinua mgongo Kuku wanakosa hamu ya kula Wanatembea kwa shida Kuku wanaharisha muharo wa maji maji Wanakua ni kama wanajificha Namna Ugonjwa unavyosambazwa Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusana baina ya kuku na kuku, pia kupitia mgusano baina ya kuku na mtu au vifaa. Pia ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa kupitia vumbi iliyochafuliwa na majimaji ya kuku mgonjwa Mizoga ya kuku wenye virusi ndio chanzo kingine cha kusambaza ugonjwa huu, hakikisha unateketeza kuku wote waliokufa na ugonjwa huu. Namna ya kudhibiti Ugonjwa huu hauna tiba hivyo huzibitiwa kwa chanjo, ila unaweza ukatumia antibayotiki mbalimbali kupunguza makali ya ugonjwa huu au tumia dawa za salfa kama Sulfonamides, au tumia dawa zingine kama Nitrofurans n.k Teketeza kwa moto kuku wote waliokufa kwa ugonjwa huu. 1. CHAWA, VIROBOTO NA UTITIRI WA KUKU Wadudu hawa huathiri ustawi wa kuku kwa asilimia kubwa, humfanya kuku kutotulia bandani na afya yake hudhoofu. Pia hushambulia vifaranga na kusababisha vifo vingi, Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani sana lakini nao huathiriwa sana. Dalili za kuwa na wadudu hawa Kuku kutochangamka Ukuaji mdogo wa kuku Kuku kutotaga na kutoatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto (Kuku hatulii kwenye kiota chake) Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu Namna ya kudhibiti Hakikisha banda la kuku linakua safi wakati wote Tumia dawa mbalimbali za kudhibiti wadudu hawa kama za Unga au za maji, pia hakikisha unatumia dozi sahihi kama inavyotakiwa kitaalamu. Badilisha mapumba ya mpunga au malanda kila yanapolowana. Kama viriboto wamewakumba kuku maeneo ya usoni, wapake mafuta ya taa kwa kutumia kitambaa laini, ukifanya hivyo viroboto hao watakufa baada ya muda mfupi. Usafi wa banda ni muhimu sana kudhibiti wadudu hawa. Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao. TAZAMA PICHA ZIFUATAZO KUWAFAHAMU WADUDU HAWA A: CHAWA Picha: Muonekano wa chawa kwa kutumia Hadubini (Microscope) Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku B: VIROBOTO Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope) Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope) Picha: Viroboto wakiwa kwenye mwili wa kuku C: UTITILI Picha: Muonekano wa Utitili kwa kutumia Hadubini (Microscope) Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku 2. MINYOO YA KUKU Viumbe hawa hukaa ndani ya mwili wa kuku hususani kwenye mfumo wa chakula wa kuku, minyoo hao ni kama Roundworms, Tapeworms, gapeworms n.k Dalili za minyoo Kuku hukonda Kuku huarisha Kuku hukohoa Kuku hupunguza utagaji Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri Kuku hupungua uzito Namna ya kudhibiti Hakikisha unawapa chakula na maji katika nazingira ya usafi Wapatie dawa za minyoo kama inavyotakiwa kitaalamu kila baada ya miezi mitatu Picha: Kinyesi cha kuku chenye minyoo Picha: Utumbo wa kuku wenye minyoo 3. UKOSEFU WA VITAMINI A Huathiri sana kuku wadogo, kuku hao huwa na dalili zifuatazo; Dalili za ukosefu wa vitamini Kuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowana. Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi Namna ya kudhibiti Wapatie kuku wote dawa za vitamini za kuku zinazouzwa kwenye maduka ya madawa ya mifugo Wapatie majani mabichi ya aina mbalimbali au mboga za majani kama mchicha, chainizi n.k., Fanya hivi mara kwa mara hii itasaidia kuwakinga kuku wako na tatizo hili. 4. TABIA MBAYA ZA KUKU Kuku huwa na tabia mbaya bandani kama kudonoa wenzake mpaka kuwasababishia majeraha, kupasua na kula mayai yake au ya kuku wengine n.k Namna ya kudhibiti tabia hizi Wapatie kuku majani ili waendelee kudonoa majani badala ya kudonoana wenyewe. Watenge kuku wenye tabia hiyo na wengine, kwa sababu ukiwaacha wataambuza tabia hiyo kuku wengine Kama tabia hiyo itaendelea, wapunguze midomo (De-beaking) kwa kutumia kifaa cha moto kama kisu au kifaa kingine. Picha: Kuku wakila yai Picha: Usawa wa kupunguza mdomo(De-beaking), Photo Credit: Wikihow.com

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI - farmersmarket.co.tzfarmersmarket.co.tz/wp-content/uploads/2018/08/Ufugaji-wa-kuku-wa-kienyeji.pdf · Kuku wa kienyeji wanafugwa na wananchi waliowengi

  • Upload
    vukhanh

  • View
    303

  • Download
    8

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI - farmersmarket.co.tzfarmersmarket.co.tz/wp-content/uploads/2018/08/Ufugaji-wa-kuku-wa-kienyeji.pdf · Kuku wa kienyeji wanafugwa na wananchi waliowengi

Kuku wa kienyeji wanafugwa na wananchi waliowengi nchini Tanzania, hii inatokana na urahisi wa kufuga pia hawaitaji miundombinu ya ghali sana. Mara nyingi kwenye mazingira yetu kuku hawa hufugwa kwa kuwaachia watafute chakula chao wenyewe (Free-range-system). Katika makala hii nitakueleza namna ya kufuga vizuri kuku wa kienyeji kwa njia za kisasa, ili uongeze uzalishaji na kukuza kipato chako.

KUANDAA BANDAKwa mazingira yetu ya Afrika mashariki, ambapo maeneo mengi ni joto unatakiwa ujenge banda lenye uwazi upande mmoja ili kuruhusu hewa kupita ndani ya banda. Kitu kingine cha msingi inatakiwa banda la kuku liwe uelekeo wa Mashariki-Magharibi, hii itapunguza mwangaza wa jua unaoingia ndani ya banda na kuweka hali ya ubaridi bandani. Kuku hawali chakula vizuri kwenye banda lenye joto kwa hiyo hali hii ikiwepo inatashusha uzalishaji.

Kuku wa Kienyeji wanapenda sana kuzunguka zungunga, na kuparua kwenye udongo, unapojenga banda ni vizuri kuacha eneo nje ya banda kwa ajili ya kuku kujitawala zaidi. Kwa usalama zaidi unaweza ukajenga wavu kuzunguka banda ili iwe sehemu kushinda kuku wakati wa mchana. Tazama picha za mabanda bora utakayoweza kujenga ili uboreshe mradi wako wa kuku.

KUCHAGUA KUKU WA MBEGU (BREEDING STOCK)Kabla ya kuanza mradi wa kuku, ni vizuri uchague mbegu inayofaa kwa kuangalia yafuatayo;• Chagua jogoo mwenye afya na mwenye umbile kubwa na mwenye nguvu.• Chagua kuku jike (Temba) ambae hana tabia ya kususa mayai wakati wa kuatamia na anaewalea

watoto wake vizuri.

NB:Kama utatumia kifaa cha kutotoreshea mayai (Incubator) au mama kuku au kuku mwingine (broody hen), tumia mayai yaliyotagwa si zaidi ya siku 14 (wiki 2)

SABABU ZINAZOPUNGUZA UZALISHAJI WA KUKU WA KIENYEJI• Changamoto kubwa ya kuku hawa wa kienyeji ni kiwango kidogo cha kutaga mayai chini ya asilimia

60% na maranyingi hufika hatima ya kutaga haraka sana tofauti na kuku wa kisasa ambao utagaji mayai hufikia hadi asilimia 80%.

• Kufuga kuku hawa kwa njia ya kisasa ni gharama sana na mara nyingine unakuta unashindwa kurudisha gharama za uzalishaji. Lakini kama mfugaji atajipanga vizuri kimkakati anaweza akapunguza hasara na kuongeza faida.

• Ugonjwa wa Kideli (New castle disease) husababisha kuku wengi kufa kwa wakati mmoja, hivyo kuathiri kipato cha mfugaji kwa kiwango kikubwa

• Ndui ya kuku (Fowl Pox/pimple head) husababisha uzalishaji kupungua.• Chawa, kupe na utitiri ambao jhusababishwa na uchafu bandani hupunguza uzalishaji wa kuku.• Minyoo inayosababishwa na majeraha yaliyotokana na ndege wengine• Damu inayoonekana kwenye kinyesi inayotokana na Muharo mwekundu (Coccidiosis), homa ya

matumbo (Fowl typhoid) au homa ya kipindupindu (Fowl cholera) husababisha kuku kukua taratibu sana na kudumaa na kuwa dhaifu.

• Utotoaji wa kiwango kidogo unaotokana na kuhifadhi mayai machafu (yenye damu au uchafu), pia kutumia mayai yenye umri zaidi ya siku 14 kutoka kwa kuku wenye mbegu za ubora wa chini.

UZURI WA KUKU WA KIENYEJI1. Ladha ya Nyama na mayai yake ni tamu sana na hupendelewa na watu wengi kulinganisha na kuku wa kisasa.2. Mtaji wa kuanzia kufuga kuku hawa wa kienyeji ni kidogo sana kulinganisha na kuku wa kisasa.3. Wanavumilia sana mazingira hatarishi ikiwa ni pamoja na magonjwa4. Wanalishwa vyakula vya gharama ya chini vinavyopatikana kwenye mazingira ya mfugaji5. Wakiachiwa wajitafutie wenyewe, gharama za chakula zinakua ndogo kwa mfugaji.6. Maranyingi Wanawake na watoto, wanajipatia kipato chao kutokana na ufugaji wa kuku.7. Soko la kuku na mayai ya kienyeji linapatikana kwa kiasi kikubwa.8. Kinyesi chao ni mbolea nzuri sana kwa mazao ya bustani na mazao mengine.

KWA NINI UNATAKIWA KUBOLESHA UFUGAJI WA KUKU HAWA?1. Hali ya kuku kufa kutokana na magonjwa itapungua kwa kiasi kikubwa.2. Ukifikia hatua ya kuangua mayai na kuuza vifaranga, mapato yako yataongezeka sana (mara 7 zaidi) kuliko kuuza mayai.3. Kuangua mayai mengi kwa wakati mmoja hupelekea vifranga wengi kupatikana kwa wakati mmoja hivyo kusaidia taratibu za chanjo kufanyika vizuri na kwa ufanisi.4. Utaweza kushirikiana na wafugaji wenzako, hivyo kwa wafugaji wenye kuku wachache wataweza kupata chanjo kwa bei ndogo ya kuchangiana.5. Unaweza kupanga uzalishaji wa kuku wako ili kuteka soko hususani wakati wa sikukuu kubwa kama Christmas, Pasaka (Easter), Iddi na sherehe mbalimbali, utaratibu huu utakuongezea kipato kwa kiasi kikubwa.

JINSI YA KUANZA KUFUGAKabla ya kuanza ufugaji jitahidi uwe na mahitaji yafuatayo;1. Uwiano wa kuku jike na jogoo uwe 10:1, yaani kila kuku jike (tetea) 10 jogoo awe mmoja. Ina maana kwamba kama una kuku jike 30, jogoo wawe watatu (3).2. Maji na vifaa vya kulishia & kunywea maji3. Banda la kuku la kutosha.4. Sehemu ya kutagia mayai5. Maranda ya mbao au mapumba ya mpunga kwa ajili ya kuweka juu ya sakafu la banda, ili kuongeza joto bandani.6. Madawa ya kutibu na kukinga magonjwa (Drugs and Vaccines)

KUCHAGUA KUKU WA MBEGU (BREEDING STOCK)1. Chagua kuku jike mwenye afya, umbile zuri na mkubwa, pia ambaye hasusi mayai wakati wa kuatamia, pia anayetunza vizuri vifaranga wake.2. Chagua jogoo mwenye afya, mkubwa na mwenye nguvu.

SIFA ZA BANDABanda kubwa na lenye hewa ya kutosha ndilo linalofaa kwa ufugaji bora wa kuku wa kienyeji. Sifa nyingine nyingi za banda bora nimezieleza kwa undani kwenye Sehemu ya kwanza ya makala hii, bofya hapa kuona sifa hizo. Bofya hapa kurejea sehemu ya kwanza ya Makala hii.

MABORESHO YA UFUGAJI BORA1. Chakula, Chanjo na Matibabu mara tu Wanapougua• Andaa chakula chenye lishe mbali mbali (Balanced diet), kwa mfano Pumba, Mashudu, kiasi kidogo

cha dagaa waliosagwa na mboga za majani, pia kuku watajiongezea virutubisho wakila wadudu waliopo kwenye mazingira yao.

• Wapatie maji ya kutosha wakati wote.• Wapatie chanjo za kuwakinga na Magonjwa• Watibu mara tu wanapougua.

2. Usafi wa BandaHakikisha banda linakua safi wakati wote, ili kuwakinga kuku wasipatwe na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko.

3. Kukusanya mayai• Sehemu ya kutagia mayai lazima iwe salama, kavu na yenye kiza kidogo.• Kusanya mayai kila siku andika tarehe ya kutagwa yai hilo juu ya yai kwa kutumia penseli. Hakikisha

unahifadhi mayai kwenye trei, sehemu pana ya yai iangalie juu na sehemu nyembamba iliyochongoka iangalie chini, kwa sababu sehemu hiyo pana ina kimfuko cha hewa ambacho husaidia kifaranga kukua kikiwa ndani ya yai.

• Tunza mayai yako sehemu ya chini ndani ya nyumba, kwa sababu sehemu ya chini ndani ya nyumba kuna joto la kadri tofauti na sehemu ya juu. Joto linalotakiwa ili kutunza uhai wa yai ni sentigredi 10 hadi sentigredi 21 (10°C - 21°C)

• Usioshe mayai na maji, “chonde chonde usioshe mayai na maji” kwa sababu ukiosha na maji bacteria wanaweza wakaingia ndani ya yai kupitia gamba la yai. Kama mayai yako yana udongo, yafute kwa karatasi kavu au kitambaa kikavu au tauro kavu. Kama limechafuka sana halifai kwa kuanguliwa.

• Chunguza mayai yako kama yamevunjika au yana kreki au yaliyokua na shepu mbaya, mayai ya namna hiyo hayafai kuanguliwa au kuatamiwa.

• Wakati wa kuweka alama au tarehe za kutagwa kwenye mayai, tumia penseli. Usithubutu kutumia kalamu ya wino au mark pen au kuweka alama ya kudumu ya wino, kwa sababu baadhi ya wino huwa na sumu inayoweza kuharibu kiini cha ndani cha yai.

• Kuandika tarehe ya kutagwa kwenye yai ni jambo la msingi sana kwa sababu utaweza kujua umri wa yai tangu kutagwa.

NB:* Mayai yanayofaa kuanguliwa ni yale yenye umri wa siku 7 hadi 10, mayai yenye umri zaidi ya siku 10 hayafai kuanguliwa kwa sababu uwezo wake unakua mdogo sana. *

4. Kuangua mayai / Kuatamia• Tumia mayai yaliyotagwa si zaidi ya wiki mbili zilizopita• Angua vifaranga kwa kutumia mama kuku, au kuku wengine wanaoatamia, au bata au mashine ya

kutotoreshea (incubator).• Kwa kuku na bata hakikisha unawapa idadi ya mayai kulingana na ukubwa wa maumbile yao, yaani

lazima mayai yatoshe chini ya matumbo yao wakati wa kuatamia.• Baada ya kuangua mayai safisha maeneo ya kutagia pamoja na kutupa maganda ya mayai

yaliyoanguliwa.• Kama unatumia mashine ya kuangulia mayai, hakikisha unageuza mayai angalau kwa siku mara 3,

isipokua siku tatu za mwisho kuelekea kuangua vifaranga (Siku ya 1 hadi 18: Geuza mayai, Siku ya 19 hadi 21: Usigeuze mayai)

KULEA VIFARANGA• Wapatie maji safi na salama wakati wote• Wapatie vyakula laini kama unga wa nafaka au mazao ya mizizi.• Waruhusu vifaranga watembee kwa uhuru, wakifikia wiki 3 au 4.• Wapatie vifaranga wako chanjo ya KIDELI wakiwa na umri wa siku 4 tangu kuzaliwa.

KUWEKA KUMBUKUMBUMfugaji anapaswa aweke kumbukumbu kimaandishi kwa kila anachokifanya kwenye mradi wake, hii itamsaidia kumpa dira mfugaji kama anafuga kwa hasara au kwa faida. Mfano wa kumbukumbu anazoweza kuandaa ni pamoja na Gharama za kuanzisha mradi, gharama za kendeshea mradi kama chakula na usafiri, idadi ya kuku jike, Majogoo, vifaranga, idadi ya mayai yanayokusanywa kwa siku au wiki au mwezi, Idadi ya mayai yaliyoanguliwa na taarifa nyingine muhimu.

MAGONJWA YA KUKUUdhibiti wa magonjwa mbalimbali ya kuku ni muhimu sana kwa mfugaji, udhibiti huo ni pamoja na Kukinga kuku wako dhidi ya magonjwa ambukizi kwa kuwapa Chanjo mbalimbali pamoja na kuzingatia usafi wa banda na chakula. Pia udhibiti wa magonjwa ni pamoja na kuwatibu kuku mara wanapoumwa. Asilimia kubwa magonjwa yanayoathiri wa kuku ni yale yanayodhibitiwa na Chanjo, Kwa hiyo ukizingatia utoaji wa chanjo kwa kuku wako kama inavyofaa kitaalamu, utaweza kidhibiti vifo vya kuku kutokana na magonjwa kwa asilimia kubwa.

Mambo Muhimu ya kuzingatia ili Kufanikisha chanjo boraChanjo mbalimbali za kukinga magonjwa zina utaratibu wake kitaalamu, kama namna ya utunzaji na namna kuwapa kuku. Zifuatazo ni dondoo muhimu za kufahamu ili chanjo yako ifanikiwe;

1. Ukihifadhi chanjo yako hovyo hovyo bila kufwata maelekezo ya kitaalamu, chanjo hiyo inakua Sumu badala ya kuwa kinga na tiba. Chanjo iliyohifadhiwa vibaya haiwezi kufanikisha matibabu. Chupa za chanjo huwa zinakuwa na lebo au karatasi yenye maelekezo ya jinsi ya kutumia pamoja na tarehe ya mwisho ya matumizi (Expire date). Usipochanja kuku wako vizuri, ugonjwa unaweza kuenea zaidi.

2. Vifaranga vilivyoanguliwa huweza kuwa na magonjwa mbalimbali yaliyotoka kwa Mama kuku, kupitia yai. Kwa hiyo kuwachanja kuku walio na umri chini ya siku kumi (10) ni muhimu sana, kwa sababu itazuia magonjwa ambukizi kwa vifaranga kadri wanavyokua.

3. Kila chanjo imetengenezwa kwa kuwekwa mahali sahihi kwenye mwili wa kuku, kuna baadhi huwekwa kwenye macho, baadhi kwenye maji na baadhi huchomwa kwa sindano kwenye mabawa. Kwa hiyo usibadilishe matumizi ya chanjo.

4. Usiwape chanjo kuku Waliokwisha kuugua [Isipokua kama kuna mlipuko wa ugonjwa wa Laryngotracheitis au Fowl pox]

5. Hifadhi chanjo mahali salama pasipokua na joto & mwanga wa jua wa moja kwa moja.

6. Chanjo zilizo nyingi ni viumbe hai visivyoonekana kwa macho (Living micro-organisms) au chembe chembe zinazotengeneza magonjwa (disease-producing agents), Kwa hiyo hifadhi chanjo zako kwa Uangalifu.

7. Kama unatumia maji ya kunywa kuku kama njia ya kuwapa chanjo, hakikisha Unatumia maji yasiyokua na chumvi na Chlorine, kwa sababu chembechembe au viumbe waliopo kwenye chanjo huharibiwa na hizo kemikali.

8. Baada ya kutoa chanjo hakikisha unachoma au unavitibu (Kuosha na Kemikali inayoua vimelea vya magonjwa, Disinfect) vifaa vyote ulivyotumia wakati wa kutoa chanjo. Ukifanya hivi utazuia kueneza magonjwa kwa kuku wazima wasiokua magonjwa.

MAGONJWA YA KUKU NA UDHIBITI WAKE1. MUHARO MWEKUNDU (COCCIDIOSIS)Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Coccidian, vimelea hivi huzaliana haraka sana kwenye utumbo mwembamba wa kuku. Mara nyingi ugonjwa huu huwakumba kuku walio na umri wa wiki 8 hadi 10, mara nyingi ugonjwa huu unaweza ukaua kuku kwa muda mfupi wa siku 5 hadi 7 (Acute type) au unaweza ukaua Kuku baada ya muda mrefu kupita (Chronic type).

Dalili za Ugonjwa• Kuku wanakua dhaifu, wanazubaa na kuinamisha kichwa chini• Kuku wanakua na manyoya yaliyovurugika• Kuku wanapauka mdomo na miguu• Kuku wanatoa kinyesi cha damu, hii hutokea endapo vimelea vya ugonjwa huu vikizaliana kwenye

utumbo mpana wa kuku.• Kuku wanakufa wengi kwa muda mfupi.

Namna ya kudhibiti• Tumia dawa za Salfa (Sulphur drugs) kwa matibabu• Tumia dawa za kuzuia kuzaliana kwa vimelea wa ugonjwa huu (Coccidiostat) kwa kuweka kwenye

Chakula.• Hakisha banda linakuwa kavu wakati wote, kama unatumia mapumba ya mpunga au malanda ya

mbao kwa kuweka chini, basi zingatia usafi yaani badilisha mapumba hayo au malanda yaliyoloana na kuweka Makavu.

2. KIPINDUPINDU CHA KUKU (FOWL CHOLERA)Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Pasteurella avicida na vimelea vingine vinavyozaliana kwa kasi sana ndani ya damu na kusababisha sumu. Kuku wagonjwa, Ndege wa mwituni, binadamu, wanyama na vifaaa mbalimbali husambaza ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa.

Dalili za Ugonjwa• Kuku wanatoa majimaji au udenda wa rangi ya manjano• Kuku wanaharisha uhalo wa njano au wa kijani• Kuku wananyong’onyea kama wamemwagiwa maji• Kuku wanapatwa na homa na wanalala kila wakati• Kuku wanakaa wakiwa wameinamisha kichwa chini au wanageuza kichwa uelekeo wa mkia au

wanalaza kichwa juu ya mabawa uelekeo wa mkia.

Picha: Kinyesi cha kuku mgonjwa

Namna ya kudhibiti• Teketeza au choma moto kuku wote waliokufa ghafra• Hakikisha banda la kuku linakua safi wakati wote• Tumia dawa za Salfa (Sulphur drugs) kuwatibu kuku waliougua• Hakikisha hakuna unyevuunyevu ndani ya banda kwa kubadilisha mapumba ya mpunga au malanda

ya mbao yaliyoloana, kwa sababu unyevu unyevu ndani ya banda husababisha kuzaliana kwa vimelea (Coccidian) vya ugonjwa huu.

3. KIDELI/MDONDO (NEW CASTLE DISEASE)Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huathiri mfumo wa upumuaji na neva za fahamu. Vifo vya vifaranga na kuku wakubwa huanzia asilimia 0 hadi 100%, itategemeana na kasi ya mashambulizi ya virusi hao.

Dalili za Ugonjwa• Uzalishaji wa mayai hupungua kwa kasi kubwa hadi kufikia sifuri (0) ndani ya siku nne.• Kuku wanapalalaizi shingo na kupinda• Kuku wanakohoa na kupumua kwa shida na wakati mwingine hutokwa na majimaji puani.• Kuku wanaharisha muharo wa majimaji wenye rangi ya kijani mpauko.• Kuku wakianza kutaga tena, mayai yao huwa na sura isiyokua ya kawaida au sura iliyopindapinda.• Kuku wanakohoa na kupiga chafya• Kuku wanakaa wakiwa wamenyong’onyea viungo vya miguu na mara nyingine wanatembea

kinyumenyume.• Kuku wanatembea kwa kuzunguka mduara au wanainamisha vichwa vyao katikati ya miguu.• Kuku wanakosa hamu ya kula, hali ikiwa mbaya sana wanakaa chini na kupoteza fahamu na baadae

hufa.

Picha: Kuku mwenye kideli aliyepalalaizi shingo

Namna Ugonjwa unavyosambazwaUgonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa, maji maji ya kuku kama udenda au kinyesi. Pia husambazwa kupitia vifaa mbalimbali vilivyochafuliwa na majimaji yaliyotoka kwa kuku kama udenda au kinyesi.Pia Virusi vya kideli husambazwa kupitia mayai yaliyotagwa na kuku muathirika wa ugonjwa huu, Uzuri ni kwamba kiini cha yai lenye vimelea vya kideli hufa na yai kushindwa kuanguliwa.

Namna ya kudhibiti• Ugonjwa huu hauna tiba, bali hukingwa kwa chanjo.• Wapatie chanjo ya kideli kuku wako wenye umri wa wiki 3 hadi 4, pia rudia tena chanjo wakiwa na umri

wa wiki 16 na wakifikia wiki 24. Baada ya hapo uwapatie tena chanjo mara uonapo kuna mlipuko wa ugonjwa kwenye eneo lako.

4. HOMA YA MATUMBO (FOWL TYPHOID)Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa gallinarum au shigella gallinarum. Dalili za ugonjwa huonekana siku 3 hadi 4 baada kuku kuingiliwa na vimelea, pia vifo huonekana ndani ya wiki 2 tangu kuona dalili. Ugonjwa huu husambazwa kupitia kuku walioathilika, vifaa mbalimbali ikiwemo vya kuku, viatu, unyevu unyevu ndani ya banda (hususani kwenye sakafu ya banda kama mapumba ya mpunga au malanda ya mbao), n.k

Dalili za Ugonjwa• Kuku wanazubaa na manyoya yao yanakua hovyo hovyo tofauti na kuku wasiougua.• Kichwa chake hupauka, na upanga wa kichwani hulegea na kulala• Wanakosa hamu ya kula• Wanaharisha kinyesi cha rangi ya chungwa

Namna ya kudhibiti• Wape chanjo ya ugonjwa huu kwa kuku wenye umri wa wiki saba (7)• Teketeza kuku wote waliokufa kwa kuchoma moto• Usiruhusu watu mbali mbali kutembelea mazingira ya banda lako bila kuondosha vimelea

(Disinfection) kwa kukanyaga sehemu yenye maji ya dawa (Footbath) kila wanapoingia au wanapotoka bandani.

• Tumia dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

5. PULLURUM DISEASE (MUHARO MWEUPE)Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vinavyoitwa Salmonella Pullurum, vimelea hivi huathiri mfuko wa mayai wa kuku jike (Ovary). Vimelea hivi pia hukaa kwenye utumbo mwembamba wa kuku. Ugonjwa huu husambaa kwa kupitia mayai yaliyotagwa na kuku aliyeathirika na ugonjwa huu pia vifaranga walioanguliwa kutokana na mayai hayo huwa na vimelea vya ugonjwa huu.

Dalili za Ugonjwa• Vifaranga wanalia kwa kutoa sauti kali• Manyoya yanavurugika• Sehemu ya hajakubwa ya vifaranga hulowana kinyesi• Kuku wakubwa hawaonyeshi dalili zozote.• Kwa vifaranga dalili huonekana kuanzia siku 4 hadi 10, na vifo hutokea baada ya wiki 3 tangu kuanza

ugonjwa.• Kuku wanaharisha muharo mweupe.

Namna ya kudhibiti• Teketeza Kuku wote wenye ugonjwa huu• Safisha vifaa vyote bandani kwa kutumia kemikali (Disinfectant) itakayoua vimelea wa magonjwa, pia

safisha vifaa vya kuangulia mayai (Incubators).• Nunua kuku au vifaranga wasiokua na magonjwa kutoka kwa wauzaji wanaodhibiti vizuri magonjwa ya

kuku.

6. NDUI YA KUKU (FOWL POX)Ugonjwa husababishwa na virusi, huathiri ngozi ya kuku. Kuku wanakua na mabaka mabaka usoni hususani upanga wa juu na wa chini.

Ugonjwa huu umegawanyika makundi mawili; Hali ya ukavu (dry form) na Hali ya unyevu (Wet form). Hali ya ukavu huwa na muonekano wa vivimbe vigumu vidogovidogo kwenye maeneo ya mwili wa kuku yasiyo na manyoya kama Kichwa, miguu, sehemu ya hajakubwa n.k). Hali ya unyevu huwa na uwepo wa vidonda visivyopona maeneo ya mdomoni, koo la chakula na koo la hewa. Hali hii husababisha kuku kutopumua vizuri, Kuku wanaweza kupata mojawapo ya kundi la ugonjwa huu au yote makundi mawili.

Dalili za ugonjwa• Vivimbe vigumu vidogovidogo kwenye maeneo ya mwili wa kuku yasiyo na manyoya kama Kichwa,

miguu, sehemu ya hajakubwa n.k).• Kuku kupumua kwa taabu.

Namna Ugonjwa unavyosambazwa• Ugonjwa huu husambazwa kwa kugusana moja kwa moja kati ya kuku mgonjwa na kuku asiyeumwa

au kupitia Mbu. Pia ukurutu uliotoka kwa kuku mgonjwa huwa ni mojawapo ya chanzo cha kusambaza ugonjwa.

• Virusi wa ugonjwa huu huingia kwenye mishipa ya damu ya kuku kupitia Macho, Ngozi, vidonda, au kupitia koo la hewa. Mbu wanabeba virusi hivi baada ya kufyonza damu ya kuku mwenye ugonjwa huu. Ushahidi wa kisayansi unasema kwamba Mbu aliyebeba virusi hivi huathirika kwa maisha yake yote. Mbu ndio wasambazaji wa kwanza wa ugonjwa huu. Mbu wa aina nyingi husambaza ugonjwa huu mara nyingi wakati wa kipindi cha baridi.

Namna ya kudhibiti• Ugonjwa huu hauna tiba, hivyo unazuiwa kwa chanjo. Ugonjwa huu unasambaa polepole kwahiyo

ukipiga chanjo unazuia maambukizi haraka sana. Chanjo hii inawekwa kwenye mabawa ya kuku kwa sindano.

• Pia unaweza kudhibiti ugonjwa huu kwa kuua na kuangamiza mazalia ya Mbu. Ingawaje kama ugonjwa umesambaa kwa kiasi kikubwa ni muhimu kupiga chanjo.

• Weka maji ya kuosha viatu (Footbath), ili kuzuia vimelea vya nje kuingizwa ndani ya banda.• Punguza idadi ya watu wanaotembelea bandani• Kila unapotembelea bandani au kufanya kazi, hakikisha unaanzia kwenye kuku wadogo au vifaranga

halafu unamalizia kwenye kuku wakubwa. Hii itasaidia kupunguza vimelea vya magonjwa kusambaa kutoka kwa kuku wakubwa kwenda kwa wadogo.

• Safisha vifaa vyote bandani kwa kutumia kemikali (Disinfectants) ya kuzuia ukuaji wa vimelea.• Kitu cha msingi kwa ugonjwa huu ni kwamba Usiwape chanjo kuku wako kama ugonjwa haujaingia

kwenye eneo lako au kwenye banda lako, kwa hiyo hakikisha unapiga chanjo baada ya ugonjwa kuingia.

7. MAHEPE (MAREK’S DISEASE)Majina mengine ya ugonjwa huu ni kama Acute leukosis, Neural leukosis, Range paralysis na Gray eye (Kama macho yameathirika).Ugonjwa huu hufanana na ugonjwa unaoitwa Lymphoid Leukosis, lakini tofauti ni kwamba; Ugonjwa wa Marek’s hutokea kwa kuku wenye umri wa wiki 12 hadi 25, wakati ugonjwa wa Leukosis huwapata kuku wakiwa na umri wa wiki 16.

Ugonjwa wa Marek’s ni aina ya Kansa ya ndege (Kuku), Husababishwa na virusi wanaoleta uvimbe ndani ya mishipa ya neva za fahamu, hatimae kuku wanapalalaizi viungo na kulemaa. Vilevile uvimbe hutokea kwenye macho na kusababisha mboni za jicho kubadilika hatimae macho kupofuka.

Uvimbe uliopo kwenye viungo mbalimbali vya mwili kama Ini, Figo, Nyongo, Kongosho, Mapafu, Misuli, Ngozi na viungo vingine, husababisha mwili wa kuku kutofanya kazi vizuri na kudhoofu. Kwa hali hiyo kuku wenye ugonjwa huu huwa na dalili zifuatazo;

Dalili za ugonjwa• Kupumua kwa shida• Sehemu za nyama zilizoshika manyoya huvimba• Wanaharisha kinyesi cha kijani• Hali ikiwa mbaya sana, kuku wanadhoofu na kukonda sana pia upanga wa juu na chini wa kichwa

hupauka na kuwa na magamba.• Wanapalalaizi viungo hususani miguu• Mboni ya macho hubadilika isivyokawaida hatimae kuku hushindwa kuona kabisa

Namna Ugonjwa UnavyosambazwaUgonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa ndani ya banda. Virusi wa ugonjwa huu hutoka kwa kuku wagonjwa kutoka kwenye manyoya ya kuku yaliyonyofoka, vumbi ndani ya banda, kinyesi na Mate au majimaji ya kuku. Kuku walioathirika hubeba virusi ndani ya damu kwa maisha yao yote na ndio chanzo cha kuambukiza kuku wengine wenye afya.

Namna ya kudhibitiUgonjwa huu hauna tiba, kwa hiyo kinachotakiwa ni kuwapatia kuku wako chanjo. Chanjo ya Ugonjwa huu inazuia utengenezaji wa uvimbe (Kansa) kwenye viungo mbalimbali vya mwili wa kuku.

8. MATATIZO YA MFUMO WA UPUMUAJI (INFECTIOUS BRONCHITIS)Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na IB, Brionchitis, cold. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huathiri mfumo wa upumuaji wa kuku. Athari za ugonjwa huu hutegemeana na umri na kinga ya kuku aliyonayo, mazingira ya kuku na uwepo wa magonjwa mengine ya kuku.

Pia ugonjwa huu huathiri tishu mbalimbali za mwili ikiwemo mfumo wa uzazi wa kuku jike (Reproductive tract). Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu;

Dalili za Ugonjwa• Kuku wanakosa hamu ya kula na kunywa maji• Kuku wanalia kwa sauti kali, hutokwa machozi machoni na puani. Kuku wadogo hupumua kwa shida

kwa kukoroma.• Kuku wanapumua kwa kukoroma wakati wa Usiku.• Uzalishaji wa mayai hupungua kadiri siku zinavyokwenda, unaweza ukaona uzalishaji wa mayai

ukaongezeka baada ya wiki 5 au 6 lakini kwa kiwango kidogo sana.• Gamba la yai huwa rafu na majimaji ya yai huwa maji kabisa.

Picha: Kuku akikoroma na kupumua kwa shida, mdomo upo wazi anajaribu kuvuta hewa kwa mdomo

Picha: Magamba ya mayai yapo rafu

Picha: Magamba ya mayai yapo rafu na baadhi hupasuka

Namna ugonjwa unavyosambazwaUgonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa, mifuko ya chakula, mizoga ya kuku iliyokwisha kufa kwa ugonjwa huu, banda la kuku lenye virusi vya ugonjwa huu na panya. Virusi vya ugonjwa huu hupenyeza kwenye mayai yaliyotagwa, Uzuri ni kwamba kiini cha yai hilo hufa na yai hushindwa kuanguliwa.

Namna ya kudhibitiUgonjwa huu hauna tiba, bali unakingwa kwa chanjo. Dawa za Antibayotiki kwa siku 3 hadi 5 zinaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huu kwa kutibu magonjwa nyemerezi yanayosababishwa na bacteria. Dawa hizo za Antibayotiki hazitibu ugonjwa huu bali zinapunguza kasi ya ugonjwa.

9. MAFUA YA NDEGE (AVIAN INFLUENZA)Majina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na AI, Flu, Influenza, Fowl plague. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huathiri mfumo wa upumuaji wa kuku. Ugonjwa huu huwakumba kuku na jamii zote za ndege.

Virusi wa Mafua ya ndege huishi muda mrefu kwenye mazingira tofauti tofauti bila kupoteza uhai wake. Virusi hawa wanaweza kuishi kwenye mazingira ya joto la kadiri au baridi kali, pia wanaishi vizuri kwenye mazingira ya barafu iliyoganda. Hii hupelekea ugonjwa huu kusambazwa kupitia kinyesi na mizoga ambayo haikuteketezwa vizuri.

Dalili za Ugonjwa• Kuku wanakosa hamu ya kula.• Kuku wanapata matatizo ya mfumo wa upumuaji kama kupiga chafya, kukohoa n.k• Kuku wanaharisha sana• Uzalishaji wa mayai hupungua kwa kasi sana• Kuku wanavimba upanga wa juu na chini wa kichwa.• Kuku wanakua na madoa mekundu au meupe kwenye miguu na upanga wa kichwani.• Kunaweza kukawa na matone ya damu yayotoka puani• Vifo huweza kuanzia asilimia chache hadi kukaribia asilimia 100%.

Namna ugonjwa unavyosambazwaUgonjwa huu husambazwa kupitia vifaa mbalimbali vilivyochafuliwa na majimaji au kinyesi cha kuku Mwenye ugonjwa kama viatu, nguo, trei za mayai, vifaa vya kulia na kunywea maji na vifaa vingine.Wadudu mbalimbali na panya wanaweza kusambaza ugonjwa huu kwa kubeba virusi kutoka weye mzoga wa kuku aliyekufa kwa ugonjwa huu.

Namna ya kudhibitiUgonjwa huu hauna tiba, bali unachanjo. Pia dawa za Antibayotiki mbalimbali huweza kutumika kupunguza kasi ya ugonjwa kwa kuua bakteria wa magonjwa nyemerezi. Kuku wakipata nafuu kidogo huendelea kupunguza kasi ya virusi, lakini dawa hizi za Antibayotiki haziui virusi. Chanjo ya ugonjwa huu isitumike bila ruhusa maalum kutoka kwa wataalamu wa mifugo na serikali kwa ujumla.Udhibiti wa uingizwaji wa kuku na jamii nyingine za ndege ndani ya eneo husika hususani mipakani. Ugonjwa huu huathiri maeneo makubwa kama nchi nzima, mikoa au wilaya, hivyo taratibu za kuzuia uingizwaji au kutoa jamii ya ndege mbalimbali kwa eneo husika (Quarantine) hufanywa na taasisi mbalimbali za serikali hususani Wizara ya mifugo (kama Wizara ya mifugo na uvuvi nchini Tanzania)Teketeza kwa kuchoma moto mizoga ya kuku wote wenye ugonjwa huu (Hii ndio njia bora zaidi ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huu, ikifuatiwa na chanjo pamoja na kuzuia uingizwaji na utoaji wa jamii zote za ndege kwa eneo husika)

Muhimu*Kama umegundua kwamba shamba lako au banda lako la kuku lina ugonjwa huu, toa ripoti kwenye mamlaka husika hususani Maafisa mifugo wa vijiji au Kata, kama maafisa hawapo kwenye maeneo yako toa taarifa wilayani kwenye Idara ya mifugo.

10. INFECTIOUS CORYZAMajina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na Roup, cold, coryza. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya Bakteria vinavyoitwa Haemophilus paragallinarum. Kuku ambao hawahudumiwi vizuri kiasi kwamba wakawa wanaishi kwenye mazingira machafu yasiyofaa, wako hatarini sana kukumbwa na ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa• Kuku wanavimba usoni• Wanapumua kwa shida• Wanatoa harufu mbaya• Wanatoa majimaji puani na machoni• Macho yanatoa majimaji na kushikamana• Wanaweza kuharisha• Kuku wadogo wanadumaa• Vifo vinanzia asilimia 20% hadi 50%• Ugonjwa unaweza ukadumu siku chache au miezi michache inategemeana na kiwango cha magonjwa

nyemelezi yaliyopo

Namna ugonjwa unavyosambazwa• Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya mgusano baina ya kuku na kuku. Pia kuku wanaweza

kuambukizwa kupitia hewa, kwa kuvuta hewa yenye vimelea vya ugonjwa huu• Vile vile kuku wanapata ugonjwa huu kwa kula vyakula na maji yaliyochafuliwa na uchafu wenye

bakteria wa ugonjwa huu.• Pia ugonjwa unaweza ukasambazwa endapo mizoga ya kuku wenye ugonjwa kuwekwa ndani ya banda

la kuku. Pia kuku waliopona wanakua bado na vimelea hivi kwa maisha yao yote.

Namna ya kudhibitiFuga kuku wako katika mazingira ya usafi, kwa sababu uchafu ndio chanzo cha mlipuko na kusambaa kwa vimelea hivi.Tumia dawa mbalimbli za antibayotiki kutibu ugonjwa huu, dawa hizi hufanya kazi vizuri kama utatibu mapema kuku wako, wakati maambukizi ndo yameanza. Dawa hizo ni zenye viua sumu vya erthyromycin, streptomycin na sulfonamides. Mfano wa dawa hizo kwa majina ya kibiashara ni kama Sulfadimethoxine (Albon®, Di-Methox™) hii dawa ndio inayopendekezwa sana. Kama dawa hii haipo au haifanyi kazi vizuri jaribu dawa hizi=> sulfamethazine (Sulfa-Max®, SulfaSure™), au erythromycin (gallimycin®), au tetracycline (Aureomycin®).Punguza msongamano wa kuku ndani ya banda, hii itasaidia kuruhusu hewa ya kutosha bandani.Kama kuna mlipuko mkubwa wa ugonjwa huu kwenye eneo lako, piga chanjo.

11. ASPERGILLOSISMajina mengine ya ugonjwa huu ni pamoja na Brooder pneumonia, mycotic pneumonia, Aspergillus. Ugonjwa huu husababishwa na fangasi. Kama chanzo cha vimelea ni viwanda vya kutotoreshea vifaranga ugonjwa huu utaitwa brooder pneumonia. Ugonjwa huu ukiwapata kuku wakubwa unaitwa Aspergillosis.

Dalili za Ugonjwa• Ugonjwa huu huanza kuwa mkali sana kwa kuku wadogo na hukomaa sana kwa kuku wakubwa.• Kuku wadogo hupumua kwa shida• Wakati wa usiku au mchana kuku hawakoromi kama magonjwa mengine.• Kuku wanakosa hamu ya kula• kuku wanapalalaizi viungo na kulemaa kwa sababu ya sumu ya fangasi hao.• Vifo vinaanzia asilimia 5% hadi 50%• Kuku wakubwa wanapata matatizo ya kupumua na kukosa hamu ya kula.• Kuku wanakua na rangi ya bluu na nyeusi kwenye ngozi (cyanosis)• Kuku wanakua na matatizo ya neva za fahamu kama kupinda shingo.• Vifo kwa kuku wakubwa huwa ni chini ya asilimia 5%.

Namna ugonjwa unavyosambazwa• Vimelea vya fangasi huzaliana kwa kasi kwenye joto la kawaida la bandani• Vimelea hivi husambazwa kupitia masalia ya mimea yaliyowekwa juu ya sakafu la banda kama

mapumba ya mpunga, malanda ya mbao na masalia mengine.• Pia Kuku wanaambukizwa kupitia vyakula na maji yaliyochafuliwa na uchafu wenye vimelea hivi.• Namna ya kudhibiti• Ugonjwa huu hauna tiba kwa kuku waliathirika• Ugonjwa huu unazuiwa kwa kuhakikisha usafi wa banda kila wakati na kuruhusu hewa ya kutosha

bandani.• Ili kuondoa chanzo cha maambukizi, weka dawa za kuua hao fangasi kwenye chakula kama

Mycostatin, Mold curb, Sodium, Calcium Propionate na Gentian violet), pia weka Copper sulfate au Acidified copper kwenye maji ya kunywa kwa siku tatu.

• Pulizia mapumba ya mpunga au malanda dawa ya kudhibiti vumbi na usambazaji wa vimelea vya fangasi, dawa hiyo inaitwa Germicide yenye mafuta (Oil-base germicide)

• Osha vifaa vya kulia na kunywea maji na kemikali zinazoua vimelea vya fangasi (Disinfectant).

12. GUMBORO (INFECTIOUS BURSAL DISEASE)Majina mengine ya Ugonjwa huu ni kama IBD, Infectious bursitis na infectious avian nephrosis. Gumboro ni Ugonjwa unaosababishwa na virusi, pia dalili za ugonjwa huu huonekana kwa kuku wenye umri wa Zaidi ya wiki 3. Pia manyoya yanayozunguka sehemu ya hajakubwa huwa yametapakaa kinyesi chenye muonekano wa chumvi chumvi.

Dalili za Ugonjwa• Manyoya ya kuku huwa rafu• Kuku wenye umri chini ya wiki tatu hawaonyeshi dalili zozote• Kuku wanaishiwa nguvu halafu wanakaa mkao wa kubinua mgongo• Kuku wanakosa hamu ya kula• Wanatembea kwa shida• Kuku wanaharisha muharo wa maji maji• Wanakua ni kama wanajificha

Namna Ugonjwa unavyosambazwaUgonjwa huu huenezwa kwa kugusana baina ya kuku na kuku, pia kupitia mgusano baina ya kuku na mtu au vifaa.Pia ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa kupitia vumbi iliyochafuliwa na majimaji ya kuku mgonjwaMizoga ya kuku wenye virusi ndio chanzo kingine cha kusambaza ugonjwa huu, hakikisha unateketeza kuku wote waliokufa na ugonjwa huu.

Namna ya kudhibiti• Ugonjwa huu hauna tiba hivyo huzibitiwa kwa chanjo, ila unaweza ukatumia antibayotiki mbalimbali

kupunguza makali ya ugonjwa huu au tumia dawa za salfa kama Sulfonamides, au tumia dawa zingine kama Nitrofurans n.k

• Teketeza kwa moto kuku wote waliokufa kwa ugonjwa huu.

1. CHAWA, VIROBOTO NA UTITIRI WA KUKUWadudu hawa huathiri ustawi wa kuku kwa asilimia kubwa, humfanya kuku kutotulia bandani na afya yake hudhoofu. Pia hushambulia vifaranga na kusababisha vifo vingi, Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani sana lakini nao huathiriwa sana.

Dalili za kuwa na wadudu hawa• Kuku kutochangamka• Ukuaji mdogo wa kuku• Kuku kutotaga na kutoatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au viroboto (Kuku

hatulii kwenye kiota chake)• Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu

Namna ya kudhibiti• Hakikisha banda la kuku linakua safi wakati wote• Tumia dawa mbalimbali za kudhibiti wadudu hawa kama za Unga au za maji, pia hakikisha unatumia

dozi sahihi kama inavyotakiwa kitaalamu.• Badilisha mapumba ya mpunga au malanda kila yanapolowana.• Kama viriboto wamewakumba kuku maeneo ya usoni, wapake mafuta ya taa kwa kutumia kitambaa

laini, ukifanya hivyo viroboto hao watakufa baada ya muda mfupi. Usafi wa banda ni muhimu sana kudhibiti wadudu hawa.

• Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.

TAZAMA PICHA ZIFUATAZO KUWAFAHAMU WADUDU HAWA

A: CHAWA

Picha: Muonekano wa chawa kwa kutumia Hadubini (Microscope)

Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

Picha: Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

B: VIROBOTO

Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope)

Picha: Muonekano wa Kiroboto kwa kutumia Hadubini (Microscope)

Picha: Viroboto wakiwa kwenye mwili wa kuku

C: UTITILI

Picha: Muonekano wa Utitili kwa kutumia Hadubini (Microscope)

Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

Picha: Utitili na Chawa wakiwa kwenye mwili wa kuku

2. MINYOO YA KUKUViumbe hawa hukaa ndani ya mwili wa kuku hususani kwenye mfumo wa chakula wa kuku, minyoo hao ni kama Roundworms, Tapeworms, gapeworms n.k

Dalili za minyoo• Kuku hukonda• Kuku huarisha• Kuku hukohoa• Kuku hupunguza utagaji• Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri• Kuku hupungua uzito

Namna ya kudhibitiHakikisha unawapa chakula na maji katika nazingira ya usafiWapatie dawa za minyoo kama inavyotakiwa kitaalamu kila baada ya miezi mitatu

Picha: Kinyesi cha kuku chenye minyoo

Picha: Utumbo wa kuku wenye minyoo

3. UKOSEFU WA VITAMINI AHuathiri sana kuku wadogo, kuku hao huwa na dalili zifuatazo;

Dalili za ukosefu wa vitaminiKuku huvimba macho na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowana.Mara nyingi ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangaziNamna ya kudhibitiWapatie kuku wote dawa za vitamini za kuku zinazouzwa kwenye maduka ya madawa ya mifugoWapatie majani mabichi ya aina mbalimbali au mboga za majani kama mchicha, chainizi n.k., Fanya hivi mara kwa mara hii itasaidia kuwakinga kuku wako na tatizo hili.

4. TABIA MBAYA ZA KUKUKuku huwa na tabia mbaya bandani kama kudonoa wenzake mpaka kuwasababishia majeraha, kupasua na kula mayai yake au ya kuku wengine n.k

Namna ya kudhibiti tabia hiziWapatie kuku majani ili waendelee kudonoa majani badala ya kudonoana wenyewe.Watenge kuku wenye tabia hiyo na wengine, kwa sababu ukiwaacha wataambuza tabia hiyo kuku wengineKama tabia hiyo itaendelea, wapunguze midomo (De-beaking) kwa kutumia kifaa cha moto kama kisu au kifaa kingine.

Picha: Kuku wakila yai

Picha: Usawa wa kupunguza mdomo(De-beaking), Photo Credit: Wikihow.com

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI