9
Na Augustino Chengula UJENZI WA BANDA AU NYUMBA YA NGURUWE 1. Uchaguzi wa eneo la ku jenga banda Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unapendekeza eneo la kujenga banda au nyumba ya nguruwe i. Liwe ni en eo l ilil o kwenye mwin uko japo kid ogo kias i ch a kut otu amis ha ma ji y a mvua ii. Ni v izur i eneo lika wa n a kiv uli c ha mit i ya asil i au k upan dwa na li we n a uwezo wa kupitisha hewa ya kutosha iii. Ni vizuri likawa mbali kid ogo na makaz i ya watu h asa kama una tak a kufu ga nguruwe wengi. iv. Pia kama una taka k ufu ga ngu ruwe wengi , ni vizuri eneo likawa karibu na barabara au liwe linafikika kwa gari ili iwe rahisi kusafirisha nguruwe wako wakati wa kufanya biashara. v. Upa tik anaji wa maji na umeme uwe wa uhakika 2. Mpan go wa uj enzi wa band a au ny umba nzuri wa ngur uwe Mambo ya muhimu kwenye nyumba ya nguruwe ni kama ifuatavyo; i. Saka fu y a ny umba lazi ma i we ya mita 3 kwa 3 ii. Saka fu y a ny umba lazima iinuke sen timita 6 0 ju u ya ardhi iii. Paa la zima liwe na uwezo wa kuz uia mvua k wa as ilimia 100 iv. Upan de mmo ja wa paa l azima uinuke zaid i ya mwin gine , ule up ande mrefu zaidi uta zame mwe lek eo usi o wa jua ili kuk ing a mwa nga mak li wa jua . Laki ni hakikisha kuwa mwan ga wa wa jua unaing ia ndani ya banda na kivuri kipo upande mmojawapo. v. Band a au ny umba i jen gwe k wa uimara wa k utos ha, l akin i ni vi zuri k utumia vif aa vinavyopatikana katika eneo husika kwa bei rahisi. Banda au nyumba ijengwe kwa kuzingatia aina ya ufugaji na hali ya hewa ya mahali husika. vi. Banda au nyumba ya nguruwe ni vema ikawa yeny e kulet a furah a kwa ngur uwe na si mateso; iwe na hewa nzuri, kivuri cha kutosha, isiyo na unyevunyevu, joto kali, harufu mbaya wala matope. vii . Band a au jingo lije ngwe kwa urefu unaotazama Mashariki-Ma ghar ibi ili kuk inga  jua na mv ua. viii. Banda au ny umba ya ngu ruwe igawan ywe katika maeneo mad ogo madog o (pens) yatakay oweka nguruw e kulinga na umri wao wa kuzaliwa. Namba na idad i na ukub wa wa vyumba utat egemea na namb a ya ngur uwe ina yota rajiw a kuwekwa au kuzaliwa katika uzazi husika.

Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 1/9

Na Augustino Chengula

UJENZI WA BANDA AU NYUMBA YA NGURUWE

1. Uchaguzi wa eneo la kujenga bandaMambo muhimu ya kuzingatia wakati unapendekeza eneo la kujenga banda au nyumba

ya nguruwe

i. Liwe ni eneo lililo kwenye mwinuko japo kidogo kiasi cha kutotuamisha maji ya

mvua

ii. Ni vizuri eneo likawa na kivuli cha miti ya asili au kupandwa na liwe na uwezo

wa kupitisha hewa ya kutosha

iii. Ni vizuri likawa mbali kidogo na makazi ya watu hasa kama unataka kufuga

nguruwe wengi.

iv. Pia kama unataka kufuga nguruwe wengi, ni vizuri eneo likawa karibu na

barabara au liwe linafikika kwa gari ili iwe rahisi kusafirisha nguruwe wako

wakati wa kufanya biashara.

v. Upatikanaji wa maji na umeme uwe wa uhakika

2. Mpango wa ujenzi wa banda au nyumba nzuri wa nguruwe

Mambo ya muhimu kwenye nyumba ya nguruwe ni kama ifuatavyo;

i. Sakafu ya nyumba lazima iwe ya mita 3 kwa 3

ii. Sakafu ya nyumba lazima iinuke sentimita 60 juu ya ardhi

iii. Paa lazima liwe na uwezo wa kuzuia mvua kwa asilimia 100

iv. Upande mmoja wa paa lazima uinuke zaidi ya mwingine, ule upande mrefu zaidi

utazame mwelekeo usio wa jua ili kukinga mwanga makli wa jua. Lakini

hakikisha kuwa mwanga wa wa jua unaingia ndani ya banda na kivuri kipo

upande mmojawapo.

v. Banda au nyumba ijengwe kwa uimara wa kutosha, lakini ni vizuri kutumia vifaa

vinavyopatikana katika eneo husika kwa bei rahisi. Banda au nyumba ijengwe

kwa kuzingatia aina ya ufugaji na hali ya hewa ya mahali husika.

vi. Banda au nyumba ya nguruwe ni vema ikawa yenye kuleta furaha kwa nguruwe

na si mateso; iwe na hewa nzuri, kivuri cha kutosha, isiyo na unyevunyevu, joto

kali, harufu mbaya wala matope.vii. Banda au jingo lijengwe kwa urefu unaotazama Mashariki-Magharibi ili kukinga

 jua na mvua.

viii. Banda au nyumba ya nguruwe igawanywe katika maeneo madogo madogo

(pens) yatakayoweka nguruwe kulinga na umri wao wa kuzaliwa. Namba na

idadi na ukubwa wa vyumba utategemea na namba ya nguruwe inayotarajiwa

kuwekwa au kuzaliwa katika uzazi husika.

Page 2: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 2/9

ix. Gharama za ujenzi wa banda au nyumba ya nguruwe zitegemeane sana na

aina ya uzalishaji unaotarajia kuufanya ili uzalishaji uweze kuwa wenye tija.

3. Aina za sakafu

Kimsingi, kuna aina kuu tatu za sakafu zinazotumiwa na wafugaji wa nguruwe sehemumbalimbali duniani kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini:

4. Mahitaji ya nafasi kwa nguruwe

Mahitaji ya nafasi katika ya nguruwe katika banda au nyumba ya nguruwe inategemeana aina ya nguwruwe walioko kwenye nyumba ya nguruwe.

i . Ng uruwe wad og o  

Hawa ni nguruwe walioachishwa kunyonya, wana hitaji mita za eneo la mraba kuanzia

0.3 hadi 0.5 kwa kila kitoto kimoja cha nguruwe. Hivyo ili kujua ukubwa wa chumba

(pen) cha kukaa vitoto hivyo zidisha hiyo namba na idadi ya vitoto vya nguruwe

unaotaka kuwaweka.

Page 3: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 3/9

Picha: Mfano mzuri wa banda la vitoto vya nguruwe lenye nafasi ya kukidhi mahitaji wa

nguruwe.

-Sakafu ya banda au nyumba ya nguruwe ijengwe kwa simenti au kwa udongo mgumu

lakini isiwe ya kuteleza. Sakafu pia iwe na mteremko mdogo kurahisha usafishaji na

maji na kuruhu sakafu kukauka kwa haraka na isiwe na mibonyeo yeyote.

i i . Ng uru we d ume:  

Nguruwe dume kwa ajili ya kuzalisha wanahitaji nafasi ya eneo la mraba kati ya mita 6

hadi 8.

-Uangalizi mkubwa kwa nguwe dume unahitajika maana anaweza kutoka ndani ya

banda na kufuata majike hasa yaliyoko kwenye joto (majike yaliyotayari kwa

kupandwa).

Page 4: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 4/9

i ii . Ngu ruwe wenye m imba 

Nguruwe wenye mimba wanahitaji nafasi kati ya mita 1.5 hadi 2.0 za eneo la mraba

kwa kila nguruwe mmoja.

Nguruwe wenye mimba wanahitaji mazingira yenye utulivu sana. Wakati mwingine

nguruwe mwenye mimba anahitaji chumba cha peke yake. Katika mazingira ya joto ni

vizuri kuweka angalau nguruwe wasiozidi watatu kwa chumba kimoja.

i v. Nguruwe wanaonyonyesha 

Nguruwe wanaonyonyesha wanahitaji nafasi kati ya mita 4 hadi 6 za eneo la mraba kwa

kila nguruwe.

Page 5: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 5/9

Nguruwe wanaonyonyesha pia wanahitaji mazingira tulivu, hivyo wanapaswa wapewechumba cha peke yao. Chumba chao kinahitaji kiwe na vitu vifuatavyo; sehemu ya

kuzalia, vifaa vya kutoa na kupunguza joto, kiota/chumba cha nguruwe wadogo,

chombo cha chakula cha watoto na chakula cha mwanzo cha watoto.

Banda la kuzalia Taa ya kuongeza joto

Chombo cha chakula cha watoto Kiota/chumba cha watoto

v . Ng uruwe wa Kun en ep es hwa  

Page 6: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 6/9

Nguruwe wa kunenepeshwa wanahitaji nafasi kati ya mita 0.5 hadi 1.0 eneo la mraba

kwa kila nguruwe.

-Sakafu ya banda au nyumba ya nguruwe ijengwe kwa simenti au kwa udongo mgumu

lakini isiwe ya kuteleza. Sakafu pia iwe na mteremko mdogo kurahisha usafishaji na

maji na kuruhu sakafu kukauka kwa haraka na isiwe na mibonyeo yeyote

5. Aina mbalimbali za nyumba na au mabanda ya nguruwe

Zipo aina mbalimbali za nyumba na au mabanda ya nguruwe yanayotumika sehemu

mbalimbali duniani na hasa maeneo ya vijijini. Mifano ya nyumba au mabanda

unazoweza kujenga ni kama inavyoonyesha kwenye michoro hapa chini:

Page 7: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 7/9

Page 8: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 8/9

6. Vyombo vya chakula

Chombo cha chakula lazima kishikiliwe vizuri kwenye sakafu ili nguruwe

wasikiyumbishe na kumwaga chakula. Ukubwa wa chombo cha chakula utategemea

sana umri wa nguruwe unaotaka kuanza nao kufuga au ulio nao. Jedwali hapa chinikitakusaidia sana kutengeneza chombo kitakachokidhi mahitaji ya nguruwe wako.

Umri wa nguruwe Urefu wa chombo Upana wachombo

Kimo chachombo

Nguruwe wanaonyonya Sm 15-20 kwanguruwe

Sm 20 Sm 10

Nguruwewanaonenepeshwa

Sm 30-35 kwanguruwe

Sm 20 Sm 15-20

Nguruwe wenye mimba Sm 40-50 kwanguruwe

Sm 35-40 Sm 15-20

Nguruwewanaonyonyesha

Sm 40-50 kwanguruwe

Sm 35-40 Sm 15-20

Nguruwe Dume Sm 40-50 kwanguruwe

Sm 35-40 Sm 15-20

Vyombo vya chakula visafishwe kila siku ili kuweka chakula safi kitakacho mvutia

nguruwe kula chakula. Na view na umbali wa kutosha kati ya chombo na chombo

kumruhusu nguruwe kuchagua chakula anachotaka.

7. Vyombo vya maji

Vyombo vinavyotumika kwa chakula vyaweza pia kutumika kuwekea maji ya

kunywesha nguruwe kama inavyoonekana hapa chini hasa kwa mashamba madogo.

Page 9: Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

7/21/2019 Ufugaji Wa Nguruwe, Ujenzi Wa Banda

http://slidepdf.com/reader/full/ufugaji-wa-nguruwe-ujenzi-wa-banda 9/9

Kwa mashamba makubwa mfumo wa bomba unaweza kutumika kwa kuingiza

mabomba ya maji ndani ya nyumba ya nguruwe (automatic drinkers) na nguruwe

wakanywa maji kwa muda wanaotaka wao (tazama kielelezo hapa chini).

Nguruwe wanahitaji maji safi nay a kutosha kwa siku, na mahitaji yao kulingana na umri

wa nguruwe ni kama yalivyo kwenye jedwali hapa chini. Maji yanapaswa yawepo muda

wote ili kumruhusu nguruwe kunywa maji kwa kadri na muda atakao yeye.

 Aina/umri ya nguruwe Kiasi cha maji kwa siku (Lita)

Nguruwe wanao kua 6 hadi 8

Nguruwe dume 12 hadi 15

Nguruwe wenye mimba 10 hadi 12

Nguruwe wanaonyonyesha 20 hadi 30

REFERENCE:

Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO). Farmer's Hand Book on

Pig Production (For the small holders at village level).