24
UHAKIKI WA MAUDHUI TAMTHILIYA YA ORODHA (Steve Reynolds) Mussa Shekinyashi +255 743 98 98 29 +255 714 80 75 65 [email protected]

UHAKIKI WA MAUDHUI TAMTHILIYA YA ORODHA · Tamthiliya ya Orodha ni tamthiliya inayohusu suala zima la ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika jamii. Mwandishi anaweka wazi kuhusu

  • Upload
    others

  • View
    553

  • Download
    93

Embed Size (px)

Citation preview

UHAKIKI WA MAUDHUI TAMTHILIYA

YA

ORODHA (Steve

Reynolds)

Mussa Shekinyashi

+255 743 98 98 29

+255 714 80 75 65

[email protected]

Utangulizi

Tamthiliya ya Orodha ni tamthiliya inayohusu suala zima la ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika jamii.

Mwandishi anaweka wazi kuhusu gonjwa hili. Mhusika mkuu Furaha anaathirika na gonjwa hili na kufariki dunia.

Kimaudhui tamthiliya hii imesawiri maisha ya sasa ya jamii ya Watanzania kwani ugonjwa huu bado ni tishio.

Kwa upande wa fani, mwandishi amewaumba vyema wahusika wake, muundo wake ni unaomvutia msomaji kujua ni nini kingeendelea mbeleni, ameteua lugha nzuri ya kisanaa. Haya yote yanajielekeza katika uchambuzi tutaoenda kuufanya.

Maudhui

Kipengelecha

Dhamira

Maambukizi ya VVU na UKIMWI

UKIMWI ni kifupi cha Upungufu wa Kinga Mwilini. Hili ni gonjwa lilitingisha jamii na kutangazwa kama janga la Taifa mwanzoni mwa miaka ya tisini mpaka sasa.

Mwandishi anaiangalia jamii ya mtanzania na kuona kuwa kunauhitaji mkubwa wa elimu juu ya ugonjwa huu.

Mwandishi ameonesha jinsi maambukizi ya UKIMWI yanavyoweza kutokea katika jamii. Kupitia mhusika Furaha, Bwana Ecko, Padri James, Kitunda na Salim mwandishi anaonesha jinsi gonjwa hili hatari linavyoweza kuathiri jamii nzima kwa muda mfupi.

Dhamira hii inajitokeza katika jamii yetu.

Athari za makundirika

Vijana wa rika moja (marafiki) hushawishiana kufanya mambo pamoja. Katika hali kama hiyo kuna uwezekano wakafundishana na kushawishiana kufanya mambo mabaya.

Mwandishi anamtumia mhusika Mary anayemshawishi Furaha na kumpeleka Baa kwa bwana Ecko. Huko anamuingiza katika ulevi na kumshawishi kufanya ngono na watu wazima.

Tatizo la makundirika lipo kwenye jamii yetu. Vijana wengi hutumbukia katika mambo mabaya kwa kufuata mkumbo wa marafiki.

Vishawishi

Hii ni hali ya kumfanya mtu kutenda jambo fulani.

Mwandishi ameonesha udhaifu wa binadamu katika ushawishi.

Anamtumia mhusika Padri James anayeshawishika kwa Furaha na kujikuta akiingia katika dhambi ya ngono.

Pia mhusika Mary anamshawishi Furaha kumkubali Bwana Ecko na kumuahidi kuwa atapata vitu vizuri.

Mwisho mhusika Kitunda anamshawishi Furaha kuvuta bangi na kumshawishi wafanye ngono.

Hofu

Hofu ni hali ya kuwa na woga. Wahusika wanaonekana wakisongwa na hofu juu ya orodha inayokwenda kusomwa.

Wanakijiji wote walikuwa na hofu kwa kuwa hawakuwa na taarifa za kutosha juu ya ugonjwa wa UKIMWI. Mwandishi anaonesha jinsi hofu inavyoweza kuathiri maisha ya mwanadamu.

Anaonesha jinsi Bwana Ecko, Juma, Padri James na Kitunda wanavyopata shida kutafuta orodha.

Mwisho wa yote orodha hiyo haikuwa kama walivyofikiri wao.

Mmomonyoko wa Maadili Maadili ni jumla ya taratibu jamii ilizojiweke ili watu wake wawe na

mwenendo mwema. Mwandishi anaiakosoa jamii kwa kuionesha jinsi ilivyokengeuka kutoka katika maadili iliyojiwekea.

Anamtumia mhusika Furaha ambaye hukutoroka nyumbani na kwenda kwenye sehemu za starehe. Kwa desturi za jmii yetu msichana wa rika la Furaha haruhusiwi kwenda sehemu hizo. Pia, Furaha anajihusisha na vitendo vya kihuni na kuidharirisha familia yake.

Vitendo vingine vinavyoashiria mmomonyoko wa maadili ni pale;

Bwana Ecko na Juma ni wakubwa kiumri lakini wanajihusisha kimapenzi na wasichana wadogo (Furaha na Mary).

Padri James anaitumia nafasi yake kama kiongozi wa dini kufanya ngono na Furaha.

Furaha anapokutana na Salimu nyumba ya nyumba yao.

Matukio yote haya yaashiria kumomonyoka kwa maadili ya jamii.

Mapenzi ya kweli

Mapenzi ya kweli yamejidhihirisha kupitia mhusika Furaha kwa jamii yake. Upendo huo umedhihirika pale alipoamua kuandikia jamii yake barua yenye orodha ya mambo ya msingi ambayo yangeisaidia jamii kujiepusha na maambukizi ya UKIMWI.

Mama Furaha anaonesha kuwa na upendo wa dhati na binti yake. Alimuangalia kwa ukaribu na kumtunza hata pale alipogundua kuwa alikuwa ameathirika na VVU. Alimpa tumaini mpaka siku yake ya mwisho.

Mama furaha alionesha kuwa na upendo wa kweli na jamii yake.

Furaha alionesha kuwa na upendo wa ukweli na jamii yake.

Umbeya na masengenyo

Umbeya ni tabia ya kutoa habari bila ya kutumwa.

Mwandishi anaonesha tabia hiyo kupitia wanakijiji, wanakijiji wanatabia za umbea na masengenyo sana. Mfano katika Uk 18 Mwanakijiji wa 3 anampasha habari Mama Furaha juu ya umbea uliozagaa kijijini kwao kuhusu Furaha.

Pia, baada ya kuugua kwa Furaha habari zilizagaa kijijini kuwa ameandaa orodha itakayosomwa kwa sauti siku ya mazishi yake.

Tabia za namna hii zipo miongoni mwa wanajamii wenzetu.

Kukata Tamaa

Kukata tamaa ni kitendo cha kuacha kuwa na shauku ya kufanya jambo Fulani zaidi. Kitendo cha Furaha kuandika orodha baada ya kujua kuwa anaugua UKIMWI kinaonesha kuwa alikuwa amekata tamaa.

Hakuona tumaini la maisha tena baada ya kugunduliwa ameathirika na virusi vya UKIMWI.

Watu wengi kwenye jamii yetu hujikuta wakikata tamaa wanapogundulika kuwa wameathirika na UKIMWI.

Tamaa

Kila binadamu huwa na matarajio ya kupata kitu fulani.

Furaha alijiingiza katika vitendo vya ngono na bwana Ecko kwa kutamani pesa zake.

Pia, Furaha alijikuta yumo kwenye mtego wa Kitunda kwa kutamani vitu alivyonavyo; kama sterio na vinginevyo.

Mwandishi anaikemea tabia hii na kubainisha kuwa ni moja ya chanzo cha maambukizi kwa vijana.

Umalaya (Ukahaba)

Hii ni tabia ya baadhi ya watu wanaoshiriki vitendo vya ngono na watu wengi kwa dhumuni la kulipwa pesa au starehe.

Mhusika mkuu, Furaha anajihusisha na vitendo vya ngono na watu wengi kijijini kwao.

Pia, Bwana Ecko anajihusisha na vitendo vya ngono na wasichana wengi hapo kwa kijijini.

Wapo vijana wanaojihusisha na tabia za kikahaba katika jamii zetu

Unyanyapaa

Kunyanyapaa ni kumuepuka mtu na kumuona kinyaa.

Wanakijiji wanogopa kukutana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya UKIMWI kwa kuwa wanaamini wataambukizwa.

Salim anapomtembelea Furaha anaogopa kukaa naye karibu au kumshika mkono kwa kuwa anahofia kuwa ataambukizwa VVU.

Hivyo mwandishi ameona tatizo hili la unyanyapaa katika jamii yetu na kuliweka bayana.

Imani Potofu

Hizi ni imani zisizo za ukweli. Jamii mara nyingine hujijengea imani juu ya jambo Fulani bila kuwa na uhakika au uthibitisho juu yake.

Mhusika mwanakijiji wa kwanza anapendekeza kuwa Furaha alipata ugonjwa kwa kurogwa.

Bwana Juma anaamini ukifanya mapenzi na msichana bikira ni dawa ya UKIMWI.

Hii inaonesha kuwa watu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya ugonjwa wa UKIMWI.

Kukosekana kwa elimu Juu ya ugonjwa wa UKIMWI

Gonjwa la UKIMWI ni gonjwa jipya kwenye jamii ya waafrika. Hivyo watu wengi hawajui mambo mengi kuhusu ugonjwa huu.

Mwandishi anaonesha kuwa wanakijiji hawajui masuala mengi yanayohusiana na ugonjwa wa UKIMWI; ikiwemo namna unavyoenezwa, tiba na namna ya kujikinga.

Wanatoa mawazo mengi ambayo si ya kweli juu ya ugonjwa huu hatari.

Tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania.

Vipengele vinginevya

Maudhui

Migogoro

Mgogoro kati ya Furaha na Dada Mdogo

Mgogoro huu umejitokeza pale Furaha alipokuwa anatoroka usiku kwenda baa.

Mgogoro kati ya Baba Furaha na furaha

Mgogoro huu umetokea baada ya baba kugundua kuwa furaha huwa anatoroka usiku.

Mgogoro kati ya Furaha na Salim

Mgogoro huu unajitokeza pale Salimu anapoenda kuulizia orodha kwa Furaha.

Mgogoro kati ya bwana Juma na Mary

Mgogoro kati ya Salim na Mama Furaha

Baada ya Salim kuchana barua iliyokuwa imeshikwa na mama Furaha.

Ujumbe

Tamaa mbele mauti nyuma

UKIMWI huathiri watu wa rika zote

Mapenzi ya utotoni si mazuri katika jamii

Tunatakiwa tuwatii wazazi na kufanya kazi kwa bidi

Marafiki wabaya hutupeleka katika njia isiyofaa

Matumizi ya kondomu hupunguza maambukizi ya UKIMWI

Dhana potofu hupelekea unyanyapaa

Falsafa

Mwandishi anaamini kuwa Binadamu ni kiumbe dhaifu sana kisichoweza kupingana na vishawishi. Anamtumia mhusika furaha na Padre James ambao wanashindwa kupambana na tamaa za miili yao na kujikuta wakiingia katika vitendo vya ngono. Matokeo yake ni kuongezeka kwa maambukizi ya UKIMWI.

Pia mwandishi anaamini kuwa watu wakipata elimu juu ya ugonjwa wa UKIMWI tunaweza kupunguza mambukizi mapya. Anatoa mapendekezo yatakayoiokoa jamii yake kwa kutumia orodha ya mambo ya msingi ya kuzingatiwa.

Mtazamo

Mwandishi anamtazamo yakinifu. Anaiangalia jamii yake katika mtazamo dhahiri wenye uthibitisho.

Anabainisha changamoto zinazoikumba jamii yake na kuonesha suluhisho la matatizo hayo.

Mfano anaonesha tatizo la jamii kukosa elimu ya ugonjwa wa UKIMWI na kutoa namna ya kuliepuka janga hilo.

Mwandishi anamtazama Padri James kwa jicho la kibinadamu. Anamuona kama binadamu mwingine na kwamba anaweza kuathiriwa na tamaa za kibinadamu.

Swali

“Mwandishi ni mwanga wa jamii, unaomulika katika kiza kinene cha ouvu.” Jadili kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma darasani.