Upload
x-paster
View
2.234
Download
5
Tags:
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Uislamu kamwe haujawahi kuwa na uadui dhidi ya Ukristo. Bali, tangu mwanzo wa kudhihiri kwake ulifungua milango ya majadiliano: “Na utawaona walio karibu zaidi (kwa mapenzi) na waumini ni wale wanaosema: Sisi ni Wakristo. Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao wanachuoni na wamchao Mwenyezi Mungu, na kwamba wao hawatakabari”Heshima kubwa kwa Yesu Kristo na kwa mama yake Mariam Mtakatifu ni sehemu ya kanuni za mafundisho ya Uislam: “Na (kumbukeni) malaika waliposema: Ewe Mariam, Hakika Mwenyezi-Enzi-Mungu amekuchagua na amekutakasa, na amekuchagua kuliko wanawake wate ulimwenguni”.Kufungua milango ya majadiliano ni kitu kinachopewa umuhimu mkubwa katika Uislam, kwa sababu kwa upande mmoja mazungumzo na majadiliano haya hufanywa kwa ustahamilivu na utulivu, na kwa upande mwingine ni kitu cha kimataifa “Sema: Enyi watu wa kitabu, njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, tusimwabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa ni waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakikataa, waambieni: Shuhudieni kwamba sisi ni wenye kunyenyekea (kwa Mwenyezi Mungu)”Kama Wakristo wasingekuwa na chuki wangefanya juhudi makhsusi na ya makusudi ya kuichapisha Qur‟an pembezoni mwa Injili zao. badala ya Torati ya Agano la Kale ambalo halikumtaja Kristo wala mama yake hata mara moja. Theluthi nzima ya Qur‟an inaelezea maisha ya Kristo na mamaye Mariam. Hivyo, wangelifahamu mengi ndani ya Qur‟an kwani imejitosheleza kwa hilo.
Citation preview
1
UISLAMU MAHAKAMANI
Mtunzi
Shawki Abu Khaleel Ph.D.
Mfasiri
Ibrahimu H. Kabuga
Islamic Centre for Research (ICR)
2
YALIYOMO
UKURASA
UTANGULIZI 5
KESI YA KWANZA - Chanzo cha Qur‟an. 12
KESI YA PILI - Qur‟an na Watawa. 18
KESI YA TATU - Hitilafu ndani ya Qur‟an. 21
KESI YA NNE - Uislam kwa Watu Wote. 28
KESI YA TANO - Barua zilizobuniwa. 33
KESI YA SITA - Muhammad na Ubashiri Wake. 40
KESI YA SABA - Kuenea kwa Uislam. 44
1. Maquraish. 45
2. Mapambano ya Muhammad dhidi ya Wayahudi. 47
3. Vita dhidi ya Waghassani na Watawala wao Wabyzantine. 50
Jihadi Maana yake, Misingi yake, Maadili yake, Malengo na Faida zake. 51
Maadili na Sheria za Jihadi. 54
1. Maeneo ya Syria 60
2. Hispania 62
3. Ulaya ya Mashariki 63
4. Fursi (Irani) na ng‟ambo ya Mto. 65
5. Wamongolia na Watartar 66
KESI YA NANE - Wasiokuwa Waislam na kodi ya Ushuru (Jizyah) 74
1. Qur‟an Tukufu 75
2. Hadithi za Muhammad (S.A.W.) na Matendo yake 76
3. Waislam na Matendo yao 77
4. Maoni ya Wakristo kuhusu muamala wao na wanaharakati wa Kiislam 78
Kwa nini wasiokuwa Waislam walipe Kodi? 78
Kiwango chake. 79
Haki za kijamii za watu wa Kitabu. 79
1. Ulinzi wa Nafsi 80
2. Sheria za Uhalifu 80
3. Sheria za Kiraia 80
4. Utunzaji wa Heshima 80
3
5. Kudumisha Makubaliano 80
6. Sheria za Kibinafsi 81
7. Taratibu na Ibada za Kidini 81
8. Uvumilivu katika kuchukua Kodi 81
KESI YA TISA - Uislam na Ukoloni 84
1. Historia ya harakati mbalimbali za uvamizi wa Nchi 85
2. Ukoloni wa Makazi 89
3. Ukoloni wa Kijeshi 89
4. Hadhi ya Nchi iliyo chini ya Himaya ya Nchi nyingine 89
5. Kukabizi madaraka ya Nchi kwa Nchi nyingine (Mandate) 89
Madhara yatokanayo na Ukoloni 90
LAKINI KUHUSU UISLAM 94
KESI YA KUMI - Uislam na Utumwa 98
Waarabu na Utumwa 101
Uislam na Utumwa 102
1. Kupunguza vyanzo mbalimbali vya Utumwa 102
2. Kufungua njia ya kuwaokoa Watumwa 103
KESI YA KUMI NA MOJA - Ngawira ndio Lengo 111
KESI YA KUMI NA MBILI - Uislam na Sayansi 117
Maktaba Wa Alexandria 120
KESI YA KUMI NA TATU - Uislam na Mwanamke 125
Wanawake hapo Zamani 125
Msimamo wa Uislam kwa Mwanamke 127
Ndoa za Wake wengi 127
Talaka 129
Udhibiti katika Ndoa 131
Adhabu katika Ndoa 132
Mirathi 133
KESI YA KUMI NA NNE - Wake wa Muhammad 139
1. Khadija bint Khuwailed 140
2. Sawda bint Zuma 141
3. Aisha bint Abu Bakr 142
4. Hafsa bint Omar 143
4
5. Zainab bint Khuzaima 144
6. Um Salama (Hind bint Abi Umayya Ibn Al-Mughira) 144
7. Zainab bint Jahsh 145
8. Juwairiya bint Al-Hareth 146
9. Safiya bint Huyay 147
10. Um Habiba „Ramla bint Abu Sufian‟ 147
11. Maria 148
12. Maymouna bint Al-Harith 149
KESI YA KUMI NA TANO - Chembechembe za Upagani 152
KESI YA KUMI NA SITA - Kikao cha Mwisho 157
Swali la Kwanza 157
Swali la Pili 159
Swali la Tatu 161
Swali la Nne 163
Swali la Tano 167
Swali la Sita 169
RUSHDI NA AYA ZA KISHETANI 175
5
UTANGULIZI
Uislamu kamwe haujawahi kuwa na uadui dhidi ya Ukristo. Bali, tangu mwanzo wa kudhihiri
kwake ulifungua milango ya majadiliano: “Na utawaona walio karibu zaidi (kwa mapenzi) na
waumini ni wale wanaosema: Sisi ni Wakristo. Hayo ni kwa sababu wako miongoni mwao
wanachuoni na wamchao Mwenyezi Mungu, na kwamba wao hawatakabari” (1)
Heshima kubwa kwa Yesu Kristo na kwa mama yake Mariam Mtakatifu ni sehemu ya kanuni za
mafundisho ya Uislam: “Na (kumbukeni) malaika waliposema: Ewe Mariam, Hakika Mwenyezi-
Enzi-Mungu amekuchagua na amekutakasa, na amekuchagua kuliko wanawake wate
ulimwenguni”.(2)
Kufungua milango ya majadiliano ni kitu kinachopewa umuhimu mkubwa katika Uislam, kwa
sababu kwa upande mmoja mazungumzo na majadiliano haya hufanywa kwa ustahamilivu na
utulivu, na kwa upande mwingine ni kitu cha kimataifa “Sema: Enyi watu wa kitabu, njooni katika
neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, tusimwabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala
tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa ni waungu badala ya
Mwenyezi Mungu. Basi wakikataa, waambieni: Shuhudieni kwamba sisi ni wenye kunyenyekea
(kwa Mwenyezi Mungu)”(3)
Kama Wakristo wasingekuwa na chuki wangefanya juhudi makhsusi na ya makusudi ya
kuichapisha Qur‟an pembezoni mwa Injili zao. badala ya Torati ya Agano la Kale ambalo
halikumtaja Kristo wala mama yake hata mara moja. Theluthi nzima ya Qur‟an inaelezea maisha
ya Kristo na mamaye Mariam. Hivyo, wangelifahamu mengi ndani ya Qur‟an kwani imejitosheleza
kwa hilo.
Kuna sura nzima ya Qur‟an iliyopewa jina la familia ya Kristo: Al Imran (familia ya Imran). Neno
“Al” hupewa familia maalumu zenye hadhi,utukufu na daraja ya juu.
Aidha, katika Qur‟an Tukufu kuna Sura nyingi sana zinazoelezea masuala ya Yesu „Masih‟. Jinsi
gani alivyokuwa akifikisha ujumbe aliotumwa na jinsi alivyoweza kudhihirisha miujiza aliyopewa
na Mola wake ili awathibitishie wafuasi wake „Mayahudi. Mfano wa Sura hizo ni Suratul Maidah
„meza‟, ndani ya sura hii kuna miujiza mitatu, ambayo haikutajwa katika kitabu chochote cha Injili,
isipokuwa Qur‟an pekee. Nayo ni kama ifuatayo.
1. Uteremshwaji wa chakula kutoka mbinguni: “Akasema Isa bin Mariam:
Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu, tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe sikukuu
kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe dalili itokayo kwako, na
turuzuku, na wewe ni mbora wa wanaoruzuku. Mwenyezi Mungu akasema: Bila shaka
mimi nitakiteremsha juu yenu, lakini miongoni mwenu atakayekataa mafundisho yangu
baada ya haya, basi mimi nitamuadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yeyote katika
walimwengu” (4)
6
2. Kuwapa ndege uhai: “….. na ulipotengeneza udongo sura ya ndege
ukampulizia akawa ndege kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha vipofu na wakoma kwa
idhini yangu” (5)
3. Kuzungumza na watu katika utoto: “(kumbuka) Mwenyezi Mungu
atakaposema: Ewe Isa bin Mariam; kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama
yako, nilipokutia nguvu kwa roho mtakatifu, ukazungumza na watu katika utoto na katika
utu uzima wako” (6)
Kuna Sura ndani ya Qur‟an iliyopewa jina la Mariam, mama wa Kristo: “Na mtaje Mariam
kitabuni alipojitenga na jamaa zake, (akaenda) mahala upande wa mashariki. Na akaweka
pazia kujikinga nao, kisha tukampeleka malaika wetu aliyejimithilisha kwake kama mtu kamili.
(Mariam) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ikiwa
unamuogopa Mwenyezi Mungu, (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako,
nimetumwa ili nikubashirie kupata mtoto mtakatifu. Akasema: Ninawezaje kupata mtoto hali
hajanigusa mwanaume yeyote wala mimi si asherati? (Malaika) akasema: Ni kama hivyo, Mola
wako amesema; haya ni rahisi kwangu, na ili tuufanye muujiza kwa watu na rehma itokayo
kwetu, na ni jambo ambalo limekwisha hukumiwa litokee”(7)
Vile vile kuna Sura nyingine iliyopewa jina la watu wa pangoni: Al Kahf: “Hakika wao ni vijana
waliomwamini Mola wao, nasi tukawazidisha katika muongozo”(8)
Hizi sura tatu, Al-Maidah, Mariam na Al Kahf, ni miongoni mwa sura ndefu katika Qur‟an.
Hata hivyo, pamoja na hayo yote, Mustashriqiina (orientists) na wamishionari wanaunyima Uislam
na Mtume wake kila aina ya sifa bora na hawana imani naye. Wanataka kuwambia Wakristo kabla
ya kuudurusu na kuustaajabia Uislam ambao ni dini na ustaarabu katika historia, kwamba Uislam ni
mchanganyiko usio lingana wala kuafikiana na Uyahudi, Ukristo na Upagani. Tatizo walilo nalo ni
ujinga mkubwa au ushabiki wa upofu uliopindukia, chuki na inda kubwa au yote kwa pamoja.
Ukosefu wa mtazamo sahihi umewapelekea kufika kwenye maamuzi potofu katika uhakiki na
utafiti wao.
Huwezi kukosa kuona kitu hata kimoja kinachoaminiwa na dini zote tatu. Ni ajabu kutokuta itikadi
moja iliyonadiwa na mitume wote, ijapokuwa dini zipo nyingi. Nabii Mussa (A.S.) alikuja baada
ya Ibrahim (A.S.) na Mussa (A.S.) aliyaamini mafundisho aliyokuja nayo Ibrahim; Issa (A.S.)
„Yesu‟ vilevile aliyekuja baada ya hao wote aliyaamini mafundisho yao kuwa ni ya kweli, na
hatimaye Muhammad (S.A.W.) ambaye ndiye wa mwisho kabisa, naye amefuata njia hiyo hiyo ya
kuyaamini mafundisho ya mitume waliotangulia. (9)
Uislam haujafahamika au kutafitiwa kikamilifu katika vyuo vikuu vingi vya Kimagharibi.
Nasikitika kusema kuwa huenda jambo hili lilifanywa kwa madhumuni maalum; hata hivyo
kumekuwepo na baadhi ya waliokwenda kinyume na mtazamo na mwelekeo huo: Wasomi kadhaa
wa kimataifa hawakuwa na itikadi za upendeleo. Wasomi hao ni kama vile Carlyle, Tolstory, Lord
7
Headley, Bernard Shaw, Edward Gibbon, Etienne Dinet, Count Henry de Castry, Renet Ginout, Dr.
Griniet, na Roger Garody. Ni jambo zuri mno kama Wamagharibi wataachana na chuki za
kimapokeo dhidi ya Uislam ambazo zimekuwa zikiongezwa bila ya ukweli wowote na mabeberu
wa kisiasa na viongozi wao wa kidini wenye ushabiki na inda nyoyoni mwao, na badala yake
wausome na kuudurusu Uislam bila upendeleo wowote, kama walivyofanya watu waliotajwa hapo
juu. Uongo na uzushi wa Mustashriqiina na wamishionari hujirudia mwanzoni mwa kila kizazi.
Hawajapata mambo mapya kwa karne nyingi sasa. Hung‟ang‟ania kuzusha mambo yafuatayo bila
uthibitisho:-
- Muhammad hakuwa Mtume kwa sababu alijifunza Qur‟an au aliipokea kutoka kwa
mtawa aliyeitwa Bahira au kutoka kwa Waraqah bin Nawfal. (10)
- Uislam ulienezwa kwa nguvu ya upanga: Watu walilazimishwa kuingia katika Uislam la
sivyo wauawe, wakati ambapo Wahubiri wa Kikristo walipata wafuasi wengi kwa
kutumia huruma na ukweli.
- Uislam uliwakandamiza wanawake na kutangaza ndoa ya mitala.
Kashfa nyingi zilizotolewa na Mustashriqiina na wamishionari ni upotoshaji mkubwa. Ni vizuri
wakafuata njia ya utafiti wa kisayansi unaowataka wasomi waadilifu na makini kuusoma Uislam
katika namna ambayo Waislam huitumia kuusoma, yaani kuepukana na chuki za kupangwa,
kuondokana na madhumuni yasiyokuwa ya kisayansi au mawazo ya ajabu ajabu yasiyotabirika
ambayo hupotosha na kutoa mahitimisho yaliyoandaliwa na hivyo kuwa mbali na ukweli.
Mbali na hilo, uzushi huu unaowadhihaki Waislam, unaweza kukanushwa kirahisi kwa ushahidi na
uthibitisho. Wale wanaoushutumu Uislam tunawakumbusha aibu na mapungufu yao wenyewe
kwamba, mkutano wa Nicea uliofanyika mwaka 325 A.D. uliamuru kuchomwa moto kwa vitabu
vyote visivyoafikiana na mafundisho ya Kanisa na kupiga marufuku kila kitu kilicho kinyume na
imani za Kanisa. Kwa njia hii Kanisa linajaribu kudhibiti nyoyo na kuzizuia roho za watu ambao
zililazimishwa kuamini kile tu kilichoafikiwa katika mkutano huo.
Mkutano huo wa wakuu wa Kanisa ulifanya dhuluma kwa kuweka marufuku hiyo na ulifanya
dhambi kwa uchomaji wa vitabu vya dini. Vikao vilivyofuata baadaye vilirekebisha matendo hayo
ya kijinga na kuondosha marufuku iliyowekwa juu ya vitabu vilivyo na elimu sawa ya dini.
Wanahistoria wa Kikristo wanasema kuwa kulikuwepo na Injili nyingi. Lakini mwishoni mwa
karne ya 2 na mwanzoni mwa karne ya tatu kanisa liliamua kubaki na Injili ambazo liliamini kuwa
zilikuwa sahihi na hivyo likachagua Injili nne zilizopo leo hii na kuwalazimisha Wakristo kuzifuata
sambamba na kuweka udhibiti na ukaguzi mkali na wa hali ya juu ili kuzifuta kabisa zile Injili
nyingine. Je, watu wa Ulaya wamewahi kujali au kujiuliza kwamba Injili zilizofutwa zilikuwa na
nini na kwa nini zilipigwa marufuku na nani aliyekuwa na haki ya kuzifuata? Hata hivyo pamoja
na kufanya marekebisho na kuvibakisha vitabu walivyoamini kuwa vilikuwa na mafundisho
8
mazuri, Injili hizo sasa zimeingizwa mikono ya watu na kuufanya ukweli wa mafundisho yake
kuwa wa kutia shaka kubwa, isipokuwa Injili aliyoiacha Yesu tu.
Wanaushambulia Usilam kwamba ulienea kwa nguvu ya upanga! Kuna tofauti kubwa sana kati ya
harakati iliyostaarabika ya kueneza mafundisho, na kulazimisha mafundisho na imani kwa njia ya
upanga, kama Charlemagne alivyofanya katika zama za kati, na kama wamishionari waliosuhubiana
na utafiti wa kijiografia katika zama za leo, walivyofanya huko Afrika na Amerika. (Wamishionari
hao) waliwaangamiza watu, waliingia katika biashara ya utumwa na kuwachukua mamia kwa
maelfu ya watu hao kama mateka na kupora maliasili za maeneo husika. Yote hayo yakifanywa
kwa jina la Yesu na kwa baraka za Papa. Lakini Uislam ulitoa fursa huru kwa mwenye kuamua
kuyafuata mafundisho yake.
Qur‟an Tukufu inasema:-
“Hakuna kulazimishwa (kuingia) katika dini, hakika uongofu umekwisha pambanuka na
upotovu umedhihirishwa” (11)
“Na sema: Huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi anayependa akubali, na anayependa
basi akatae, kwa hakika tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguuka” (12)
“Lakini wakikataa, basi hakika juu yako ni kufikisha tu ujumbe ulio wazi” (13)
Injili ya Mathayo 10:34 inasema:-
“Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja
kuleta amani, bali upanga”
Bado wanadai kwamba Uislam ni dini ya upanga lakini Ukristo ni dini ya upendo, itawezekanaje?
Kutokana na ushahidi wa {10:34} Mathayo?
Kanisa liliposhusha jina la mwanamke na kumdhalilisha kwa kumuona kuwa ndiye chanzo cha
uovu na dhambi, Uislam ulikuja na kuinyanyua daraja ya mwanamke na kuiweka juu. Muhammad
(S.A.W.) alisema:-
“Wanawake ni sawa na wanaume”.
Uislam umemfanya mwanamke kuwa „Mnara‟ wa wema na huruma; taji linalopamba kichwa cha
kila mwanamke wa Kiislam ni upendo na huruma. Ndoa ya wake wengi ilienea sana na ikakubalika
kwa watu wote wakiwemo hata watumishi wa Kanisa wenyewe. Mtawala wa Kirumi aitwaye
Jastinian, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufikiri juu ya kuweka sheria ya kuweka kikomo cha idadi
ya wake na kuoa mmoja lakini Kanisa lilipinga fikra yake hiyo.
9
Uislam ulipokuja ulijaribu kuiwekea udhibiti ndoa ya wake wengi. Ilikuwa ni kazi ngumu kuzuia
mtazamo wao huu. Bali Uislam ukaingiza utaratibu wa mwanaume mmoja kuruhusiwa kuoa wake
hadi wanne. Hii ilikuwa kama njia (ponyo) kwa watu wasiendeleze uchafu wa uzinzi. Hakuna
dhambi kwa asiyeweza kutekeleza utaratibu huo na wala haivunji sheria za Uislam, ijapokuwa ni
bora sana kwa wenye kuweza „kufanya uadilifu‟. Kuna faida nyingi sana katika hili kwa pande zote
mbili „mke na mume‟
“Ndoa ya mitala ni tiba dhidi ya uchafu wa uzinzi na sio matendo ya mazoea”
Nani anayesema kuwa Wamagharibi wamefungwa kuwa na mke mmoja tu? Je, siku hizi hakuna
ndoa za mitala katika nchi za Kikristo?
Kwa hakika ndoa ni mkataba unaowekwa baina ya mwanaume na mwanamke. Lakini kwa kuwa
mkataba huo unahusika kwa kiasi kikubwa na mustakabali wa vizazi vya baadaye na kwa kuwa
uthabiti wa kweli wa nasaba za wahenga unapatikana kupitia ndoa, Uislam unachukulia muungano
huu kuwa ni kitu kitukufu. Kama tukiiangalia ndoa kama ndoa tunakuta kuwa Wakristo huko
Magharibi wana mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengi kuliko hata Waislam, ambapo
Wakristo hao huwa na wanawake wengi bila haya wala aibu. Kile anachokifanya Muislam kwa
kikomo kwa kuthibitishwa na madhumuni yaliyohalalishwa huchukuliwa kuwa ni aibu au kosa na
kuitwa mitala, wakati ambapo Mkristo hufanya ufedhuli bila kuona haya na bila kizuizi.
Haadhibiwi na sheria! Ni uzinzi!
Maadui wa Uislam wanatambua vyema kuwa lau wangetumia sehemu ya juhudi zao katika
kukashifu na kusingizia mafundisho yoyote kinyume na Uislam mafundisho hayo yangekanushwa.
Lakini ni jambo la kawaida kwamba siku zote Uislam husimama imara, kwa utukufu, hupanda
milima na hatimaye kushinda vita vyote vinavyoanzishwa na kupiganwa dhidi yake. Kwamba
Uislam ni dini ambayo siku zote inakwenda mbele na kuendelea kwa rehma, ulinzi na msaada wa
Allah:-
“Hakika sisi tumeiteremsha Qur‟an, na hakika sisi ndio wenye
kuilinda” (14)
Ndani ya kitabu hiki tutajadili juu ya imani na mafundisho halisi ya Uislam badala ya matendo
yenye makosa yanayofanywa na baadhi ya wanaofuata dini hii kwa jina tu. Maisha na matendo ya
kweli ya baadhi ya Waislam wa siku hizi yanatofautiana na mtazamo wa Uislam wa kweli. Uislam
sio yale wayaonayo Wamagharibi katika matendo ya mtalii wa Kiarabu ambaye huenda mbio
akiyakanyaga maadili yote wakati akikimbia kwa kutwetatweta kwenda kuridhisha matamanio
yake, kwani sio kila Mwarabu ni Muislam na hivyo mitazamo wanayotumia kuhukumu Uislam
wanakosea.
Katika kurasa zijazo tutaweka mahakama. Katika kila kesi au kikao cha mahakama Uislam utaitwa
kusimama kama mshitakiwa. Mwendesha mashtaka ataleta mashtaka dhidi ya Uislam. Huyu
mwendesha mashtaka atakuwa ni Mustashriqiina au mmishionari. Tutataja jina la kitabu chake
10
ambacho ndani yake tuhuma zimetokea. Hakimu atauita Uislam kuja kujitetea. Huyu hakimu ni
akili yenye busara, yenye umakini na hekima inayopenda kudhihirisha ukweli, ikaacha
upendeleo na ambayo haina ushabiki.
Uislam utasimama kutii amri ya hakimu na hautahitaji mwanasheria kuutetea kwani kesi iko wazi
na dhahiri na Uislam unajiamini utasimama na kutoa hoja zake kwa sauti kupinga mashtaka.
Utetezi wake utaandikwa na ushahidi wake utadokezwa kwa uwazi katika vitabu rejea ili wale
wanaohudhuria mahakamani waweze kupata ushahidi huo kwa urahisi. Kesi itahitimishwa na
hakimu ambaye, hatatoa hukumu ya kuuachia huru au kuutia hatiani Uislamu, kwani wasomaji au
wasikilizaji wana tabia tofauti za akili na fikra. Sitataja hukumu ya kila mashtaka kulazimisha
mtazamo wangu ambao, nina hakika kwamba Uislam hauna dosari na hauna hatia ya mashtaka
yanayotolewa na mustashriqiina na wamishionari. Uislamu ni mkamilifu, hauna dosari wala kasoro
zozote, lakini nataka msomaji agundue jambo hili yeye mwenyewe.
Mwisho ninapenda kuwatanabahisha wale ambao wamejichagulia kashfa dhidi ya Uislam kama
kazi yao na kujitolea kuuvunjia heshima, kwamba ukweli na nguvu ya haki ni vyenye kushinda na
kwamba hisia za chuki katika maamuzi siku zote humpeleka mtu kwenye hitimisho lenye makosa.
Vile vile tunawakumbusha kuwa shutuma zao na mazungumzo yao ya bure yanafahamika vyema na
hurudiwarudiwa mara kwa mara, na kwamba Uislam unapotoshwa katika akili zao si katika uhalisia
wake.
Ninapenda kuwaambia wasomaji kuwa mazungumzo au majadiliano yapo wazi kwa watu wote,
kwa utulivu, bila wasiwasi, kwa uadilifu, bila upendeleo, bila chuki, uongo na fujo ambazo kamwe
hazipelekei kwenye matokeo yoyote mazuri.
Basi majadiliano baina ya ustaarabu mbali mbali na yaanze katika ulimwengu huu ambapo masafa
na umbali vimeondoshwa. Mtu anaweza kuwa Damascus, muda wa asubuhi na jioni akawa London
au New York, au jioni anaweza kutembelea Paris au Rome na asubuhi akazuru Karachi au Tokyo.
Majadiliano ni njia nzuri ya kudhihirisha ukweli.
Zama mpya au mwanzo wa historia mpya baada ya kufunga mlango wa karne ya ishirini zinapaswa
kuanza kwa mtu kutafuta mambo mema popote yalipo hata kama yamo katika Uislam ambao
ushabiki wa Kanisa unafanya njama ya kuiharibu sura yake kwa makusudi machoni mwa
Wamagharibi ili kuwazuia wasiukaribie.
Ni wakati mwafaka kwa wapenda elimu na ukweli, kwa kutumia majadiliano ya busara na maarifa,
waondokane na picha ya uongo dhidi ya Uislam iliyochorwa na ushabiki wenye chuki wa wabebaji
wa msalaba. Uzayuni una nafasi kubwa katika kutangaza propaganda hizo kwa kutumia uwezo wa
kila aina ya vyombo vya habari inavyovimiliki.
Katika maisha ya kila siku mtu hufanya juhudi kujua iwapo habari alizosikia ni za kweli au sio za
kweli. Huenda likawa tukio la kawaida linalorudiwarudiwa mahali popote ulimwenguni. Katika
11
kutafuta ukweli wa habari au ripoti aliyoisikia binadamu, hujiheshimu yeye na huiheshimu akili
yake, basi itakuwaje iwapo ukweli anaoutafuta unahusu dini yenye mabilioni ya wafuasi na
waumini. Je, hapaswi kuiandaa akili yake katika kutaka kujua misingi na mafundisho yake ya
kweli? Je, wakati haujafika wa kuudurusu Uislam kwa busara na bila ya ushabiki na upendeleo
katika namna ile ile inayofanywa na mtu mwenye akili kudurusu jambo lolote popote pale
ulimwenguni katika maisha yake ya kila siku? Ninatambua kuwa jibu sahihi la mtu makini ni
„Ndiyo‟.
Rejea:
1. Qur‟an Tukufu, Sura Maidah: 82
2. Al Imran: 43
3. Al Imran: 64
4. Al-Maidah: 114- 115.
5 -6. Al-Maidah: 110.
1. Surah Mariam: 15- 21.
8. Al-Kahf: 13.
9. Rejea (Sura 2:285), (2:130), (2:285):
“Mtume (S.A.W.) ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa
Mola wake, na Waislam wote wamemwamini Mwenyezi Mungu
(S.W.), na malaika wake na vitabu vyake, na mitume yake „yote‟.
Wanasema “Hatutofautishi baina ya yeyote katika mitume yake.
Na husema tumesikia na tumetii …”
10. Wanaozua uwongo kwa kusema kuwa Muhammad amefundishwa Qur‟an na huyo „Mrumi‟ ni wale wasio
ziamini aya za Mwenyezi Mungu na hao ndio waongo.
{16:105}
11. Al-Baqarah: 256.
12. Al-Kahf: 29.
13. An-Nahl: 82.
14. Al- Hijr: 9.
12
KESI YA KWANZA
Chanzo cha Qur‟an (1)
Hakimu anamuamuru bawabu wa mahakama kuuita Uislamu.
Bawabu anaita kwa sauti: “Islam”
Uislam unaingia kortini. Mwendesha Mashtaka anakuja kusoma mashtaka. Mshitakiwa anaendelea
kusimama kizimbani akiwa ni mwenye shauku ya kusikiliza mashtaka yanayoletwa dhidi yake.
Mwendesha Mshataka: Qur‟an ni ya Muhammad: Muhammad ndiye aliyeitunga (2)
. Je,
unawezaje kudai kuwa ni neno la Mungu? Unaweza kuthibitisha ---- kwa busara na elimu bila
kutumia maandiko ya kidini ----- kwamba chanzo chake cha asili ni Mungu na wala sio
Muhammad?
Hakimu (akiuambia Uislam): Una chochote cha kusema?
Uislam: Msheshimiwa Hakimu! Kuhusu chanzo cha asili cha kitabu hiki, kuna uwezekano
wa aina tatu. Uwezekano:-
a) Ni kama anavyosema mwendesha mashtaka kwamba imetungwa na
Muhammad. Au
b) Imetungwa na Waarabu. Au
c) Inatoka kwa mwingine , chanzo kisichojulikana, ambacho tunaweza kukipa
jina la X, na ambacho tunatakiwa kukitafuta na kukigundua. Naomba
uniruhusu nirudi kulitazama kila jambo moja katika swala hili.
Uwezekano (a): Kwamba imetungwa na Muhammad. Ninaweza kukanusha hili kwa
vielelezo vinane.
(1) Suala la mtindo. Kama kila mmoja ajuavyo, kuna tofauti
kubwa sana kati ya mtindo wa maneno ya Qur‟an na mtindo
wa maneno ya Muhammad (S.A.W.) mwenyewe.
Ukilinganisha Qur‟an na maneno ya Muhammad –--- yaliyokusanywa
katika Vitabu vya hadithi –--- tofauti huonekana dhahiri katika mtindo
na maudhui ya vitu hivyo viwili. Maneno ya Muhammad ni aina ya
mazungumzo, maelezo ya kina, ya kuadilisha na fasaha ambayo
tayari yalikuwa yamezoeleka kwa Waarabu.
Kinyume na muundo wa Qur‟an, ambao haukuwa ukijulikana
kwa Waarabu, uliokuwa unakosoa kila ovu na kuweka sheria
ya mambo mbali mbali.
13
(2) Taathira inayotokea kwa msomaji. Wakati wa kusoma vitabu vya
hadithi, mtu hujihisi kuwa yuko mbele ya mwanadamu mwenye kila
aina ya udhaifu na udhalili.
Tofauti iliyoje wakati wa kusoma Qur‟an! Msomaji huona kuwa yupo mbele
ya Mungu, muumba wa vitu vyote, mwenye nguvu, haki, hekima na rehma
ambayo haina hata chembe ya udhaifu ndani yake. Kama Qur‟an ingekuwa
imetungwa na Muhammad, basi muundo wake ungaliafikiana na ule wa hadithi
zake. Kwani siyo jambo la kawaida katika elimu ya uandishi kuwa mtu mmoja
akaweza kuwa na mitindo miwili, ambayo yote ina tofauti sana ya asili?
(3) Muhammad (S.A.W.) hakuwahi kusoma wala kuandika (3)
.
Mtume hakwenda shule au kuwa na mwalimu, kamwe hakuwahi kusoma chini
ya mkufunzi wa aina yoyote. Je inaingia akilini, kufikiria kuwa mtu kama
huyo alieweza kuwa na haya maandiko ya sheria ya ajabu, yenye kukubalika
sana na yasiyokuwa na hitilafu yoyote, yenye ukuu wenye kutambulika sana.
Ukuu unaotambulika kwa Waislam na wasiokuwa Waislam na ambayo
imepitishwa kama chanzo kikuu cha sheria za ulaya? Mtu asiyejua kuandika
aliwezaje kubuni Qur‟an, pamoja na upekee wa mtindo wake, na sheria zake za
kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini?
(4) Maudhui ya kielimu yaliyomo ndani ya Qur‟an. Mtazamo juu ya
ulimwengu, maisha, fikra, shughuli za kifedha, vita, ndoa, ibada, biashara na
mengine yaliyomo ndani ya Qur‟an ni kamili, yote yanapatikana,
hayatofautiani. Kama yote haya yangetoka kwa Muhammad, isingewezekana
tena kumchukulia kama mwanadamu. Kwa sababu hata kama kundi la kamati
zote duniani, zenye wajumbe wanaounda tamaduni zote za kimataifa pamoja
na wenye elimu kubwa, wangelikusanyika kutengeneza kanuni hizo za
kimaadili na za kisheria wangekabiliwa na ugumu wa hali ya juu, hata kama
wangepewa rejea na tafiti nyingi kiasi gani, na hata kama wangepewa muda
mwingi kiasi gani wa kuandaa sheria kama hizo wangeshindwa. Hakuna mtu
yeyote, mwenye kipaji cha aina gani na elimu pana kiasi gani, ambaye
angeweza kutunga suluhisho hata moja la tatizo lolote miongoni mwa utitiri wa
matatizo yanayomkabili mwanadamu; sasa tutasema nini tutakapofikiria utata
wa matatizo hayo na tofauti zake nyingi? Iliwezekanaje kwa mtu asiyesoma
awe ndiye mwanzilishi wa ufumbuzi wa yote haya?
(5) Suala la ufahari binafsi wa mtunzi. Sababu gani ambayo
ingemfanya Muhammad (S.A.W.) aandike Qur‟an kisha
akaihusisha na mtunzi mwingine? Sifa hii ingekuwa kubwa sana kama
angekuwa ametengeneza kazi yake mwenyewe na kuushangaza ulimwengu
mzima kwa kitu ambacho wao walimwengu binafsi hawakuwa na uwezo hata
kidogo wa kukitengeneza. Jambo hili bila shaka lingemwinua kwenye daraja
14
ya juu zaidi ya wanadamu wengine. Faida au manufaa gani ambayo
Muhammad (S.A.W.) angeyapata kwa kutunga Qur‟an na kisha akawapa sifa
ya utungaji huu wengine?
(6) Mambo ya kweli yaliyomo ndani ya Qur‟an. Ndani ya Qur‟an
kuna ukweli mbalimbali kuhusu mambo ya kale ambayo hayakuwa
yakijulikana kwa watu wa rika na zama za Muhammad (S.A.W.). Katika Aya
mbalimbali tunakuta rejea ya maajabu ya kisayansi yanayohusu ulimwengu na
uhai, madawa, hisabati, n.k. Je, mtu asiyesoma aliwezaje kuhusika na
utambuzi wa mambo hayo ya kielimu na kitaalamu? Muhammad aliwezaje
kusema kuwa dunia ipo katika muundo wa yai(4)
? Aliwezaje kuijua nadharia
ya upanukaji wa ulimwengu(5)
? Angewezaje kudai kuwa „element‟ za mada
inayounda ulimwengu zote ni za aina moja(6)
? Kwamba msongamano wa hewa
huongezeka kadiri mtu aendavyo juu na hivyo kupumua huwa taabu(7)
, na jinsi
jua na mwezi vinavyoelea angani(8)
? Qur‟an imejaa mifano kama hiyo.
Muhammad asiyesoma aliwezaje kujua mambo ya kisayansi ambayo yamekuja
kujulikana hivi karibuni tu kwa msaada wa maabara na satelaiti
zilizogunduliwa hivi karibuni tu?
(7) Makemeo kwa Muhammad. Kuna Aya nyingi za Qur‟an ambazo ndani
yake Mtume amekemewa. Sura iitwayo “Abasa” yaweza kuwa mfano
unaojulikana vyema:-
“Alikunja uso na akageuza mgongo. Kwa sababu alimjia kipofu”(9)
.
Siku moja kipofu mmoja aliyejulikana kwa jina la Abdullah Ibn Umm
Maktum, alimkatiza Muhammad (S.A.W.) wakati akizungumza na Walid na
wakubwa wengine wa Kikuraishi. Mtume akionesha kutomtambua, kipofu
huyo aliinua sauti yake kwa ari na kuomba maelekezo ya kidini, lakini
Muhammad akiudhika na uingiliaji kati huo, alikunja uso na kugeuza mgongo.
Aya hiyo ni lawama kwa Mtume kwa kitendo chake kwenye tukio hilo.
Vile vile kuna idadi ya mifano mingine kama hiyo ndani ya Qur‟an(10)
Je,
inaingia akilini kufikiri kuwa Muhammad ndiye aliyetunga kitabu ambacho
ndani yake yeye mtunzi mwenyewe analaumiwa? Kuna matukio mengi
ambapo Muhammad (S.A.W.) alionesha tabia fulani, lakini Qur‟an kwa uwazi
kabisa ikailaumu hali hiyo na kuonesha kosa alilotenda(11)
. Muhammad
hakujisikia vibaya kunukuu matukio hayo. Kama angekuwa ndiye mtunzi wa
Qur‟an je asingebadilisha rekodi hizo kwa kuzifuta au kwa kuzirekebisha ili
kuakisi mapendeleo yake mwenyewe?
15
(8) Kipindi cha muda baina ya tamaa ya Muhammad ya kuongea
na ufunuo uliokuwa ukimfikia. Wakati fulani Muhammad (S.A.W.) alihisi
udharura wa kuzungumzia mambo fulani au kutoa maelekezo kuhusu namna
ya kuyatenda. Lakini bado alisubiri usiku na mchana mpaka agizo limfikie
kabla ya kufanya vitu hivyo kujulikana kwa watu wengine.
Mheshimiwa Hakimu! Kitabu kilichotengenezwa na binadamu kiliwezaje
kutangaza umoja wa Mungu katika mtindo na mfumo adilifu ambao haukupatikana katika
maandiko matakatifu yaliyotangulia? Je, akili yenye busara na nguvu haitoshi kupinga moja kwa
moja hoja ya kwamba Qur‟an imetungwa na Muhammad?
Sasa nakwenda kwenye Uwezekano (b); kwamba kitabu hiki sio kazi ya mtu mmoja, bali watu
wengi, Waarabu. Kama inavyofahamika vyema, Waarabu walikuwa na mapenzi ya asili ya kupenda
ushairi na fasihi ya ufasaha wa kuzungumza. Hafla na matamasha ya mara kwa mara yalifanyika,
ambapo washairi na wasemaji wao walishindana. Katika medani ya vita, wapiganaji wao walitiwa
ujasiri wa ajabu uliotokana na ufasaha wa tenzi na hotuba zilizosifu makabila yao na kuwamiminia
dharau na kuwavunja nguvu maadui zao.
Sasa, miujiza iliyofanywa na Mitume wa Mungu ni matukio yaliyokuwa na kikomo cha muda na
mahali, na yalikuwa na faida kwa wale waliokuwa mahali hapo na kuyashuhudia. Na miongoni
mwa mambo yaliyokubalika kuwa, katika miujiza aliyopewa Musa (A.S.) ilikuwemo ya namna ya
uchawi, kwa sababu uchawi ulikuwa ukifanywa sana zama hizo. Hivyo, Musa aliweza kuwashinda
wachawi wa zama zake katika uwanda wa fani yao wenyewe, na hivyo kuweza kufikisha ujumbe.
Vivyo hivyo, miujiza iliyofanywa na Masih “Issa” ilikuwa katika mazingira ya tiba, hivyo
changamoto iliyokuwa ikimkabili ni kuwashinda matabibu wa zama hizo ndani ya fani yao
wenyewe.
Vile vile, Qur‟an ni tukio la kimiujiza lililoteremshwa kwa watu waliokuwa na desturi ya kujivunia
uwezo wao katika medani ya fasihi, lakini ambao walitakiwa kuzidiwa katika medani
waliyoichagua wenyewe. Sasa basi, iliwezekanaje Qur‟an iwe ni kazi ya Waarabu? Hususani pale
kitabu hiki kinapowapa changamoto kabambe na ya kweli kwa kuwaambia walete mfano wake
kwa kutunga sura moja au hata Aya moja inayolingana nayo. Lau kama Waarabu wangekuwa na
uwezo wa kuandika Qur‟an yao wenyewe, wasingesita kufanya hivyo ili kulinda ibada ya
masanamu yao ambayo imekatazwa na kushutumiwa vikali ndani ya Qur‟an. Hakuna shaka hata
kidogo kuwa Qur‟an haikutoka kwa Waarabu kwa sababu wao wenyewe walistaajabishwa na
mtindo, ufasaha na sheria yake iliyoitangaza rasmi, kiasi ambacho walisalimu amri mbele yake na
kuingia katika dini ya Mwenyezi Mungu. Walifanya hivyo kwa sababu wao wenyewe hawakuwa
na uwezo wa kuiga mfano wa Qur‟an(12)
.
Hivyo, changamoto iliyotolewa ndani ya Qur‟an ni ya milele; hali ya kushindwa kutunga Qur‟an ni
ushahidi tosha kuwa Qur‟an haiwezi kuwa imetungwa na Waarabu ambao ni wanadamu kama
sisi(13)
.
16
Nikirudi kwenye uwezekano wa tatu ambao ni wa mwisho, Uwezekano C, ule wa chanzo
kisichojulikana. Ikiwa Waarabu (ambao ndio wazungumzaji wa asili wa lugha hii) hawakuwa na
uwezo wa kujibu changamoto nilizozieleza, je, inaingia akilini hata kidogo kudhani kuwa Qur‟an
iliandikwa na watu wengine wenye lugha tofauti na hii ambao walikuwa hawajui Kiarabu? Je,
itakuwa imetungwa na Wafursi (Waajemi), Warumi, Wahabeshi? Kama haikutokea kwa Waarabu,
wala majirani zao, ilitokea wapi? Kama Waarabu walikaa kimya wakashindwa kuijibu Qur‟an, bila
shaka itakuwa imetoka kwa chanzo kilicho juu zaidi ya uwezo wa mwanadamu.
Mheshimiwa Hakimu! Wewe ndiye mwakilishi wa akili na fikra; hivyo wewe ndiye unayestahiki
zaidi kutoa hukumu ya kesi hii. Hoja juu ya upekee wa kitabu hiki ni nyingi sana. Miongoni
mwake ni kama vile: ufasaha wa matamshi, kutokuwa na hali ya kutofautiana au makosa, wingi wa
maana, utabiri na miujiza, mfumo wa sheria uliokusanya kila kitu na uliokamilika …. Haya yote
yametoka wapi?
Rejea: 1. “Je, wanasema ameitunga? Sema: Basi leteni sura moja mfano wake
na muwaite muwezao wasaidie asiyekuwa Mwenyezi Mungu ikiwa
nyinyi mnasema kweli”. (Yunus 10:38)
2. The Reader‟s Companion to World Literature, Hornstein, Persy, Brown,
ukurasa 298 “Mohammed au Muhammad, kiongozi wa dini na mtunzi wa Qur‟an”.
3. “Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hakuandika kwa mkono wako wa
kulia”. (Ankabuut 29:48)
4. “Na ardhi baada ya hapo akaitandaza”
(Naazia‟at 79:30)
5. “Na mbingu tumeifanya kwa uwezo na hakika sisi ndio wapanuao”
(Dhariyaat 51:47)
6. “…. Mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana kisha tukaviambua”
(Anbiyaa 21:30)
7. “….. hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana kama kwamba anapanda
mbinguni”. (An’aam 6:125)
8. “….. na amevitiisha jua na mwezi vyote hupita mpaka wakati uliowekwa”
(Luqmaan 31:29)
9. Qur’an (80: 1 – 2)
10. “Haiwi kwa Mtume na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina ijapokuwa ni jamaa,
baada ya kuwabainikia kuwa wao ni watu wa moto wa Jahannam” (Tawbah 9:113)
“Wala usiseme kabisa juu ya jambo lolote. Hakika mimi nitalifanya kesho, isipokuwa
Mungu akipenda na mkumbuke Mola wako unaposahau, na sema: Hakika Mola wangu ataniongoza
njia iliyo karibu zaidi na muongozo kuliko hii” (Al-Kahf 18:23 – 24)
“Ewe Nabii; mbona unaharamisha alichokuhalalishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta radhi ya wake
zako, na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu” (Tahriim 66:1)
17
11. “Na ikiwa mnashaka kwa hayo tuliyomteremshia Mja wetu, basi leteni sura
iliyo mfano wa hii, na muwaite wasaidizi wenu badala ya Mwenye-Enzi-
Mungu, ikwa mnasema kweli. Lakini kama hamtafanya basi, uogopeni Moto ambao
kuni zake ni watu na mawe, ulioandaliwa kwa makafiri”. (2:23 – 24)
“Sema: Hata wakijikusanya watu wote na majini wote ili kuleta mfano wa hii Qur‟an hawataweza
kuleta mfano wake hata kama watasaidiana wao kwa wao” (17:88)
12. katika kitabu chake kiitwacho “The Inimitability of the Qur‟an” Al-Rafeie anasema:-
“Wakati huo, Waarabu hawakuweza kukabiliana na changamoto ya Qur‟an kwa ufasaha waliokuwa
wakijivunia. Kwa miaka mingi changamoto hii imeendelea kuwaita kwenye ushindani wasemaji
wote wazuri na watu wenye ufasaha, na hivyo kutoacha nafasi ya wakosoaji kudai kwamba Waarabu
walikuwa na uwezo wa kutengeneza kitu kinachofanana nayo, au kwamba Qur‟an inaweza kuigwa na
mtu yeyote” (Uk. 218)
13 “Taha Hussein, katika kitabu chake kiitwacho “The Discourse of
the Poetry and Prose” anasema: “Qur‟an sio nathari wala ushairi kwa sababu haiendani na kanuni
za hiyo ya kwanza wala ile ya pili. Qur‟an ni ya amaumbile yake yenyewe”
(Uk. 25)
18
KESI YA PILI
Qur‟an na Watawa
Uislam unaingia mahakamani, kichwa juu na mwendo wa kujiamini. Mwendesha mashtaka
anainuka.
Mwendesha Mashtaka: Qur‟an yote ilitungwa na Mtawa aliyeitwa Bahira aliyempatia
Muhammad jirani na eneo la Busra nchini Syria pindi Muhammad alipopita kwenye nyumba ya
Mtawa huyu wa Kikristo alipokuwa akisafiri pamoja na Ami yake(1)
.
Hakimu: Utajibu vipi hoja hii?
Uislam: Mheshimiwa Hakimu! Kabla ya kuendelea na utetezi wangu kamili, kuna jambo moja
dogo ambalo ni muhimu niliseme, nalo ni utambulisho wa Mtawa husika. Kwani
tunaona kuwa jina halisi la mtu huyu anayedaiwa kumpa Muhammad visa vya Qur‟an
jina lake sio jambo lenye maafikiano hata kidogo, bali hutofautiana kutoka chanzo
kimoja hadi kingine. Hivyo, katika vyanzo vya Kikristo wakati fulani anajitokeza
kama Sergius au Bahira, wakati mwingine anajitokeza kamaWaraqa bin Nawfal,
ambapo tukirudi kwenye vyanzo vya Kiyahudi kama vile Bidrodi Alphonso, mtunzi
huyo wa Qur‟an anakuwa ni Myahudi asiyejulikana.
Mheshimiwa Hakimu! Sasa niruhusu nitoe nukta kadhaa zinazotakiwa kuzingatiwa:-
1. Khitilafu zilizopo baina ya visa vinavyohusu walimu wa Muhammad, inatosha kukanusha
mashtaka haya.
2. Muhammad aliposuhubiana na Ami yake, Abu Talib, kwenda Syria hakuwa na zaidi ya umri
wa miaka tisa. Je, inaingia akilini kufikiri kwamba mtoto huyo mdogo angeweza kuelewa
yale anayosomewa? Katika safari yake ya pili kwenda Syria, akiwa na umri wa miaka
Ishirini na tano, hakuna visa vyovyote vinavyohusu makabiliano yoyote na Mtawa au
mwalimu. Katika tukio hili alikuwa katika mradi wa biashara kwa niaba ya Bi Khadija
(R.A.), ambaye mtumishi wake alisuhubiana na Mtume, na ambaye alisimulia matukio
Mengi aliyoyashuhudia yanayohusu msaada na ulinzi ambao Mwenyezi Mungu
alimjaalia Muhammad wakati wa safari na ziara hiyo. Sasa basi, kwanini rehma ambazo
Mwenyezi Mungu alimjaalia Muhammad (S.A.W.) wakati wa safari hii zilionekana,
wakati ambapo visa vya makutano yake na Watawa vilibuniwa ili tu kuthibitisha kwamba
Watawa hao ndio walimsimulia Qur‟an? Kwa nini pahitajike kitu kama vile safari ya
kibiashara ili itumike kama mbinu ya kuficha lengo la kweli ambalo ni kujifunza Qur‟an
kutoka kwa Bahira? Kulikuwa na kiunganishi gani baina ya Bahira na Muhammad
(S.A.W.)? [ Bahira na Muhammad walikutanaje mahali pa kwanza?]
19
Kwa nini Bahira amchague Muhammad, asiyejua kusoma, kijana mwenye miaka tisa au
ishirini na tano, awe mpokeaji wa kitabu hicho cha sheria? Kwa nini asimchague mwanaye
mwenyewe, au ndugu yake, au hata mwananchi mwenzake kwa ajili ya kazi hii?
Mwisho, kwa nini akubali kuachia fahari na sifa yote, nguvu na umaarufu wa kudumu,
pamoja na mema yote ambayo angewaletea binadamu, viende tu kwa kijana asiyejulikana
huku akivikataa yeye binafsi? Je, si bora sifa hizo zingeenda kwa Bahira kuliko Muhammad,
yatima aliyelelewa na Abu Talib?
3. Makutano ya Muhammad (S.A.W.) na Bahira yalikuwa ya muda mfupi na yalitokea mbele
ya idadi kubwa ya watu wa kabila lake. Hivyo, suala la muda ni muhimu sana. Ilikuwaje kijana
wa miaka tisa ambaye hajui kusoma aielewe Qur‟an ya Bahira, hata sehemu yake, achilia mbali
Qur‟an yote, ndani ya kipindi kifupi sana? Na zaidi, kama kweli angekuwa ameichukua Qur‟an
kutoka kwa Bahira, kabila lake Maquraish wangemtuhumu kwa jambo hili punde tu
alipotangaza utume wake. Hiyo ingekuwa turufu mikononi mwa Maquraishi katika vita vyao
dhidi yake. Muhammad angethubutu vipi kukataa kwamba hakuichukua hiyo Qur‟an kwa
Bahira pindi watu wa kabila lake wangeamua kuitumia kama ushahidi dhidi ya madai yake?
Lakini jambo hili halikutajwa hata kidogo na Maquraishi katika kampeni yao kali ya propaganda
dhidi ya Muhammad na Qur‟an, ingawa hawakuacha hata kitu chochote katika harakati zao za
kumfedhehesha Muhammad na kitabu chake.
4. Hapo awali, katika kumbukumbu hizi, tulikanusha moja kwa moja ---- kwa misingi ya
busara na elimu ---- dhana hiyo kwa kusema kuwa kamwe Qur‟an kama ilivyo isingeweza
kutungwa na binadamu. Hivyo, hakuna uwezekano wa Bahira, Waraqah au Myahudi wa
Alphonso, ambao walikuwa wanadamu, kuwa wawe wameweza kuitunga Qur‟an, hata kama
Muhammad angeishi nao kwa maelfu ya miaka.
5. Si Bahira wala wengine waliokuwa mashahidi wa mlolongo wa matukio yaliyosimuliwa
ndani ya Qur‟an kwa kuwa walikuwepo miaka kadhaa kabla ya matukio hayo. Sasa waliwezaje
kujibu maswali aliyoulizwa Muhammad miongo kadhaa baadaye? Hata kama wangekuwa
wamejaaliwa au kuzawadiwa uwezo wa kuona mbele na kutabiri mambo ya baadaye, sio wao
wala mtu yeyote ambaye angeweza kutabiri matukio hayo na kumwelekeza Muhammad jinsi ya
kuyakabili muda wote wa baadaye.
6. Katika Qur‟an kuna Aya kadhaa zinazolingania imani halisi ya umoja wa Mungu, na hili
linapingana na mafundisho ya Kikristo ya utatu. Tunaweza kuhoji, Bahira au Waraqah
waliwezaje kumfanya Muhammad aje na kitu kinachopingana sana na imani yao wenyewe ya
utatu?(2)
Hali kadhalika kuna Aya zinazodokezea kuhusu matendo mabaya ya Wayahudi; Je, Aya
hizo zinaweza kuwa zimeandikwa na Myahudi?(3)
7. Je, watawa Bahira na Waraqah ni waongo? Tunawezaje kukubali kuwa mtu wa dini
ambaye ameutumia umri wa maisha yake yote kama mtawa akimuabudu Mungu na kufuata
Mafundisho yake, atamke uongo ambao ungemshusha hadhi na kuwa mtu wa kawaida, achilia
20
mbali mtu wa Mungu? Mmoja wao aliwezaje kumfanya Muhammad aseme kuwa Qur‟an ni
ufunuo wa Mungu kwa Muhammad, wakati muda wote huo ni kazi yake mwenyewe Bahira au
Waraqah? Je, Norman Daniel, mchochezi wa madai haya, anakubali kwamba mtu wa dini kama
Bahira anaweza kuitwa mwongo? Ni wema gani anaoifanyia nafsi yake kwa kutunga tuhuma
kama hizo?
8. Mheshimiwa Hakimu; Baadhi ya tafsiri za Qur‟an ambazo zimekuwa zikitumika kama
vyanzo vya kunukuu, zimepotoshwa sana na kutumika vibaya kwa kiasi kwamba zinapingana na
Qur‟an, si tu katika ufasaha na uzuri wake, bali pia uwazi na ukweli wake. Wakati fulani
tunakutana na visa vya ajabu, kwa mfano; visa vya mapenzi vinavyomzungumzia Muhammad,
ambavyo mtu hawezi kuamini kuwa vimetendwa na watu wa kawaida, achilia mbali Muhammad
aliyejulikana sana katika Arabia nzima kwa wema, utukufu na usafi wa moyo. Kwa kutoa mfano
mmoja hapa kuna kisa kimoja kilichozushwa na Padri Fidenzio kilichoelezwa katika muundo wa
hadithi maarufu za mapenzi:-
„Kuna mtu mmoja aliyeitwa Sidos (Zaid) ambaye mkewe Zabib (Zainab) alikuwa mwanamke
mrembo zaidi katika enzi zake. Muhammad aliposikia kuhusu urembo wake alijihisi kumtamani
sana. Ili apate kumuona, alisubiri mpaka mume wake alipotoka, kisha naye akaenda nyumbani kwa
mwanamke huyo na kumuulizia mumewe. Sidos aliporudi Zainab alimweleza kuwa Muhammad,
Mtume wa Mungu, alikwenda kumuulizia. Alipouliza kama Muhammad aliweza kuona uso wake,
Zainab alikubali na kuongeza kuwa alimkodolea macho kwa kumtazama usoni kwa muda mrefu.
Zaid aliposikia hivyo alimpa talaka mkewe”. Kisha Padri huyu ( msema kweli) akaendeleza kisa
chake kwa kunukuu Aya ndani ya Qur‟an zinazohitimisha mapenzi haya ya siri kwa Muhammad
kumuona Zabib.
Kwa hakika anayezusha uzushi kama huo ambao haukubaliki na mtu yeyote mwenye akili atakuwa
na uwezo wa kueneza uvumi kwamba Qur‟an ilitungwa na Padri?.
Rejea:
1. Madai haya yalitoka kwa Norman Daniel (Deen of Queen‟s College Oxford) katika kitabu chake kinachoitwa
“Islam and the West 1100 – 1350 AD”.
2. “Kwa hakika wamekufuru waliosema: Mwenyezi Mungu ni Masihi Isa bin Mariam”
{5:17}
“Na kumbukeni Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Mariam Je, wewe uliwambia watu:
„Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu baadala ya Mwenyezi Mungu‟? Aseme: “Wewe umetakasika na
kuwa huna mshirika. Hainipasi mimi kusema ambayo sina haki kuyasema, kama ningelisema bila shaka ungelijua.
Unajua yaliyomo katika nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo kwako, hakika wewe ndiye ujuaye sana mambo ya
siri”.
{5:116}
3. “Mfano wa wale weliopewa Taurati kisha hawakuichukua, ni kama mfano
wa punda abebeshwae vitabu vikubwa vikubwa (bila kunufaika kwavyo), ni mfano mbaya mno wa watu
waliozikadhibisha Aya za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu
madhalimu”. (62:5)
21
KESI YA TATU
Hitilafu ndani ya Qur‟an (1)
Mwendesha Mashtaka: Ndani ya Qur‟an yenyewe ni vigumu kupata mafundisho thabiti na ya
wazi yenye kueleweka na yasiyopingana. Katika masuala ya kidini, ambayo ni muhimu sana kwetu
kuyafahamu, tumepata tu maelezo yenye makosa, ambayo kama tukiyapima kwa undani wakati
fulani huthibitika kuwa yanajipinga. Kwa mfano, Qur‟an inasema kwamba Mwenyezi Mungu
aliumba viumbe vyote kutokana na maji, na katika Aya saba imesimulia kuwa mwanadamu
aliumbwa na Mwenyezi Mungu, wakati huo huo inajipinga yenyewe mara saba kwa kusema, katika
Aya husika kwamba mwanadamu aliumbwa kutokana na ardhi, tope, udongo, udongo utoao sauti,
udongo wa mfinyanzi, udongo mweusi na mwisho kutokana na maji. Hitilafu hizi na nyingine
zinathibitisha kwamba Qur‟an haikuandikwa katika kipindi kimoja wala haikuandikwa na
mwandishi mmoja (2)
.
Mwendesha mashtaka anarudi kukaa katika kiti chake akiwa ameridhika na hoja yake.
Hakimu anauita Uislam kuja kujitetea mbele ya shutuma hii mpya na yenye nguvu.
Uislam: Mheshimiwa Hakimu! Kitu kinachonishangaza mimi zaidi kuliko mambo yote ni
pale ushereheshaji na ufafanuzi wa Qur‟an unapofanywa na watu wasiokuwa na maarifa yoyote ya
lugha ya Kiarabu ----- lugha pekee ya Qur‟an ----- na pale ambapo vijana wetu mara nyingi
huchukuliwa na tafsiri hizo za Mustashriqiin, wanaoonekana kuwa na aidha ujinga au uovu na
ushabiki wa kidini. Swali ninalouliza hapa ni: jambo gani kati ya haya mambo mawili
linalokubalika zaidi kiakili: tafsiri za wasomi wa Kiarabu ambao ndio mabwana wa lugha hiyo na
wanaoienzi sana, au tafsiri za baadhi ya Mustashriqiin ambao wao hawawezi hata kutamka baadhi
ya maneno ya Kiarabu? Nani anayeweza kuitafsiri Qur‟an kwa namna bora; ni yule mzungumzaji
wa asili wa lugha hii ya Qur‟an au yule anayeitafsiri kimakosa, iwe kwa kutojua au kwa kusudi la
maslahi yake binafsi, mtu anayeongozwa na uovu, ushabiki wa kidini na chuki iliyo moyoni mwake
dhidi ya Waarabu na Waislam?
Hitilafu hiyo (aliyoizzungumza) ambayo haipo ndani ya Qur‟an, ipo katika akili za washabiki hao
wenye msimamo mkali wa kidini, inapatikana katika fikra na maneno yao ya kiburi. Hitilafu hii ipo
katika maneno ya Goldziher mwenyewe, pale anapoieleza Qur‟an kuwa ni: Kitabu kitakatifu cha
Uislam na katiba yake iliyofunuliwa na Mungu. Hivyo, anakubali kuwa ni kitabu cha Mungu na
kwamba hakiwezi kuwa ni ubunifu wa Muhammad au mtu yeyote yule, kwa sababu kipo nje ya
uwezo wa ubunifu wa mwanadamu. Lakini baadaye Goldziher anakuja kujichanganya na kukubali
kuwa chini ya taathira ya watu wengine, anavitelekeza viwango vyake vya usomi na kuiruhusu
nafsi yake kuikubali chuki yao dhidi ya Qur‟an.
22
Sasa katika kukanusha mashtaka yanayohusu uumbaji wa binadamu, maandiko hayo yanaeleza
kuwa kuna michakato miwili tofauti ya uumbaji: Uumbaji wa binadamu kutokana na maji unahusu
uzalianaji wa watoto kupitia mwanaume na mwanamke katika uendelezaji wa jamii ya binadamu;
wakati ambapo uumbaji wa mwanadamu kutokana na udongo unahusu uumbwaji wa mtu wa
kwanza, yaani Adam. „Maji‟ haya ni mbegu ya uzazi, ambayo mahali fulani katika Qur‟an
imeelezewa kama „hafifu‟ na mahali pengine kama „Maji yanayotoka kwa nguvu‟. Lakini
uumbaji wa asili, yaani wa Adam, kutokana na ardhi au udongo au kitu kingine, sio jambo lenye
kujikanganya wala kujipinga, kwani hakuna Aya hata moja inayosema kuwa wakati mmoja
uumbwaji huu wa Adamu ulitokana na ardhi, wakati mwingine ulitokana na chuma, na kisha maji.
Vitu vilivyotajwa katika mchakato ule wa uumbaji kutokana na ardhi na udongo na vinginevyo sio
tu kwamba vyote vina uhusiano wa karibu na ardhi, bali pia vinahusiana na hatua za baadaye katika
utengenezaji wa chombo kutokana na ardhi. Sasa iko wapi hii hitilafu inayomfanya Klimovitch
adai kwamba Qur‟an haikuandikwa katika kipindi kimoja, wala haikuandikwa na mtu mmoja?
Mwendesha Mashtaka: Sasa nitatoa jozi nne za Aya kutoka ndani ya Qur‟an, ambazo kila moja
inapingana waziwazi na nyingine, huo ukiwa ni uthibitisho kuwa Qur‟an sio kitabu cha Mungu.
Jozi ya kwanza: Katika sura inayoitwa Tuur; Aya ya 25, tunasoma: “Wataelekeana wao kwa
wao wakiulizana”
Wakati huo huo katika sura Muuminuun; Aya ya 101, tunakuta:- “Hapo hautakuwapo ujamaa
baina yao siku hiyo, wala hawataulizana” Angalia! Kuuliza kunathibitishwa katika Aya ya kwanza, wakati Aya ya pili inakataa, huku ni
kupingana kwa wazi kabisa.
Jozi ya pili: Katika suratul-Hijr; Aya ya 92 tunasoma:- “Na kwa haki ya Mola wako lazima sisi
tutawauliza wote” Lakini Aya ya 39 ya sura Rahaman inasema:- “Na siku hiyo hataulizwa kwa dhambi yake mtu
wala jinni” Hii tena ni hitilafu ya wazi katika hizi Aya mbili.
Jozi ya tatu: Aya ya 33 ya sura Anfal inasema:- “Wala Mwenyezi Mungu hakuwa wa
kuwaadhibu hali wanaomba msamaha” Hii inapingana moja kwa moja na Aya ya mbele yake inayosema:- “Na wana udhuru gani ili
Mwenyezi Mungu asiwaadhibu?”
Jozi ya mwisho: Aya ya 46 ya Suratul-Kahf inapingana na Aya ya 14 ya sura Taghabun,
halikadhalika Aya ya 28 ya Suratul-Anfaal, ambayo maana ya kila moja ina mtazamo tofauti kabisa
na ule wa zile Aya mbili. Aya hizo zinasema:-
“Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia”
“Enyi mlioamini, Kwa hakika baadhi ya wake zenu Na watoto wenu Ni maadui zenu”, Na
23
“Jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni mtihani”
Uislam: Mheshimiwa hakimu! Kabla sijaanza kukunjua ukweli dhidi ya haya yote yanayoitwa
„hitilafu‟ niruhusu nisimulie kisa kifuatacho:-
Siku moja shetani alimtokea mchamungu fulani. Baada ya mazungumzo yao ya muda mfupi,
Mcha-Mungu alimuuliza shetani kama alikuwa amehifadhi Aya zozote za Qur‟an, ambapo alijibu
kwa ukali, “Kwa nini nisihifadhi? Ni kitabu cha Mwenyezi Mungu. Sikiliza:-
“Enyi mlioamini msikaribie swala”
“Basi ole wao wanaoswali”
Mchamungu huyo aliyeshikwa na mshangao alibainisha kuwa Aya ya kwanza inatakiwa kusomwa:-
“Enyi mlio amini, msikaribie swala hali ya kuwa mmelewa”
{4:43}
Na Aya ya pili:-
“Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanapuuza swala zao”
{107:4 – 5}
Akamuuliza shetani kwanini hakusoma Aya kwa ukamilifu, na badala yake akasoma nusu? Shetani
akajibu kuwa hakuwa na ulazima wa kuhifadhi Qur‟an yote.
Mheshimiwa hakimu! Kwa ufupi hii ndio hali ya wale Mustashriqiina wanaotafsiri vitu kulingana
na mawazo yao, na kuacha nusu ya hadithi bila kusimuliwa. Sasa acha nielezee kuhusu mifano
minne ambayo mwendesha mashtaka anadai kuwa ina hitilafu.
Mfano wa kwanza: Parapanda litakapolizwa siku ya Kiyama, ujamaa wa ulimwengu huu
utatoweka na ndugu watatengana, kwa sababu kila mmoja atakuwa ameshughulishwa na majaaliwa
yake mwenyewe, na hakuna atakayekuwa katika nafasi ya kuwaulizia wengine. Wale waliopo
mbinguni na ardhini watazimia. Parapanda litakapopulizwa kwa mara nyingine wataamka na
kujitazama, kisha watakaribiana wakiulizana kuhusu kilichowapata, wakisema:-
“Nani ametufufua malaloni petu? Haya ndiyo aliyoahidi Mwenye- Enzi-Mungu Mwingi wa
Rehma, na Mitume walisema kweli” (3)
Hivyo, tunaona kuwa mustashriqiina walioibuka na tuhuma za kuwepo hitilafu bila shaka
hawakuona tofauti iliyopo baina ya mazingira haya ya aina mbili: kukaa kimya katika mfano wa
kwanza kutokana na matokeo ya kuzimia, na katika mfano wa pili kuulizana pale watakapoelekeana
baada ya kufufuliwa kutoka katika mapumziko yao.
Katika kujibu hitilafu ya pili iliyozushwa, kuhusu „kuulizwa‟ na „kutoulizwa‟ siku ya malipo,
tunaweza kueleza kwamba hapa pia pako dhahiri na wazi kwamba hizi ni hatua mbili. Hatua ya
24
kwanza itakuwa ni ile mtu kuitwa kwenda kuhesabiwa matendo aliyoyafanya duniani, hatua
itakayohitimishwa na kutolewa hukumu ya kuwa katika watu waliorehemewa au waliolaaniwa.
Katika hatua ya pili, tayari watu wameshatenganishwa, kila mmoja ameshajuwa majaaliwa yake,
hapo hapawezi kuwa na suala la kuulizwa zaidi, kwani kila kitu sasa kimekwisha.
Katika suala la tatu: Maquraishi, kabla ya kuingia katika Uislam, walimuomba Mwenyezi Mungu
awateremshie mvua ya mawe iwaangamize na kuwahilikisha watu wote akiwemo Muhammad
ambaye alikuwa nao akiwalingania kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. Imeelezwa wazi kuwa, kwa
kuwa walikuwepo waumini miongoni mwao, maombi hayo yasingetekelezwa. Aya zinasema hivi:-
“Ewe Mwenyezi Mungu kama hii ni haki itokayo kwako, basi tupige kwa mvua ya
mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu nyingine iumizayo!”
Lakini Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu madamu wewe umo pamoja nao, wala
Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali wanaomba msamaha” (4)
Lakini Muhammad, alielezea kuwa kama wasingeingia katika Uislam wangeadhibiwa kwa matendo
yao. Sasa hitilafu iko wapi hapa?
Na mwisho kabisa: Kwa kweli hakuna hitilafu au kujichanganya hata kidogo katika Aya mbali
mbali zinazoelezea kuwa mali na watoto ni mapambo ya maisha ya duniani, ni maadui zetu, na ni
mtihani kwetu.
Katika sehemu ya kwanza, vitu hivyo huwa pambo la maisha ya dunia pale muumini wa kweli
anaposhikamana na Mola wake na akawa hajavutwa na majaribu yoyote. Lakini yule mwenye
imani dhaifu, mali na watoto vitamkokota kumtoa kwa Mola wake, kwani vitamfanya kuwa
mwenye kushughulishwa sana kiasi kwamba hatorudi tena kwa Muumba wake. Hivyo, ni jambo la
busara kumpa tahadhari kwamba kila kilichoambatana na moyo wake ndio adui wake wa kweli,
hata kama ni mali na watoto wake. Anapaswa kuweka uwiano, kuwa na fungu katika maisha ya
Dunia na kutosahau fungu lake katika maisha ya Akhera.
Katika muktadha huu mali na watoto ni mtihani; na Mwenyezi Mungu atamlipa kwa wingi yule
awekaye ibada ya Mwenyezi Mungu mbele ya ibada ya mali na watoto.
Mwendesha Mashtaka: Uislam unadai kuwa Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa. Lakini
tunasoma ndani ya Qur‟an kwamba Malaika walimsujudia Adamu. Je, hii sio hali ya kupingana
dhahiri?
Nukta nyingine: Tutazielewa vipi sifa za Mwenyezi Mungu pale tunaposoma sehemu moja
ndani ya Qur‟an kwamba yeye ni :-
“Mwingi wa rehma na mwenye kurehemu” na mahali pengine
25
“Mwenye nguvu na muweza” na sehemu ya tatu
“Mwenye kusamehe na mwenye huruma” na mahali pengine kuwa
“Yeye ni mkali wa kuadhibu”
Je, hapa si tunakabiliwa tena na utata mkubwa usiosuluhishika?
Kisha tunaelezwa kuwa Mwenyezi Mungu ni:-
“Mola wa mashariki na magharibi” (5)
“Mola wa mashariki mbili na magharibi mbili” (6)
, na
“Mola wa mashariki zote na magharibi zote” (7)
Kwa hakika ni sehemu ndogo tu ya uthibitisho usiokanushika wa hoja yetu. Tungetaka tungetoa
ushahidi mwingine mwingi unaoonesha hali ya hitilafu na kujichanganya inavyoonekana ndani ya
Qur‟an.
Uislam: Kwanza nitashughulika na suala la kusujudu. Kusujudu ni kitendo kinachoashiria
utukufu na ukuu. Lakini katika kadhia hii, kinaonesha utiifu wa Malaika kwa Mwenyezi Mungu,
ambaye hutoa amri nasi tukazitii. Hivyo, sijda hii sio sijda ya kawaida tu iliyomlenga Adam. Aidha,
sijda hii ilifanywa na Malaika kwa Adamu na wala sio sisi kama wanadamu, tuliofanya sijda kwa
Adam. Kuna tofuauti kubwa sana kati ya hali hizi mbili. Kwa namna hiyo hapa kuna hitilafu gani?
Tukienda kwenye sifa za Mwenyezi Mungu: ni kweli kabisa kuwa Yeye ni Mwingi wa rehma na ni
Mwenye kurehemu kwa wale walioamini, lakini pia ni mwenye nguvu na uwezo pale nguvu na
uwezo huu vinapooneshwa dhidi ya wale wasioamini na wakaasi. Ni Mwingi wa kusamehe kwa
wale wanaotubia na kurudi kwake, lakini ni mkali wa kuadhibu kwa wale wanaoendelea katika
madhambi yao na wakawa hawajarudi kwake. Tunasoma: - “Na wale waliofanya mabaya, kisha
wakatubu baada yake na kuamini, hakika Mola wako baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe,
Mwenye kurehemu” (8)
Baada yake utakuta:
“Ni kama desturi ya watu wa Firaun na wale waliokuwa kabla yao. Walizikadhibisha Aya zetu,
Mwenyezi Mungu akawashika kwa sababu ya madhambi yao, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa
kuadhibu” (9)
Je, badala yake huu si ushuhuda kamili kuwa hitilafu hiyo inapatikana katika akili za hao
mustashriqiina waliopotoka?
26
Mwisho, turudi kwenye mkanganyiko wa hakika unaohusu mashariki na magharibi. Bila shaka
mashariki na magharibi zinafahamika vyema. Mashariki ni: sehemu ambayo siku zote jua
huchomoza na magharibi ni ile ambayo siku zote jua huzama.
Tukienda kwenye „mashariki mbili na magharibi mbili‟ inaonekana kwamba kuna sehemu mbili
ambazo jua huchomoza na ambazo ziko mbali mbali sana, moja wakati wa majira ya baridi, na
nyingine wakati wa majira ya joto.
Hali kama hiyo vile vile ipo katika machweo; hivyo kuna mashariki mbili na magharibi mbili.
Ufuatao ni ufafanuzi wa kijografia na kifalaki:-
- Katika kizio cha kaskazini cha dunia (wakati wa majira ya joto), jua litakuwa juu ya Tropiki
ya Kansa, ambapo katika kizio cha kusini cha dunia (wakati wa majira ya baridi) husimama wima
juu ya Tropiki ya kaprikoni. Jua linaposimama wima wa Tropiki moja huwa sawa na pembe ya
Tropiki nyingine. Hivyo, jua huchomoza katika sehemu mbili zilizo mbali mbali wakati wa majira
ya joto na majira ya baridi, likidhihiri juu ya tropiki moja na kuiinamia ile nyingine. Qur‟an
inaeleza zaidi kuwa umbali uliopo kati ya hizi mashariki mbili ni mkubwa sana (10)
. Ndiyo, kama
kuna „mashariki mbili‟ lazima pawe na „magharibi mbili‟ zilizo mkabala nazo.
- Kanuni hiyo hiyo inazihusu pia „mashariki zote na magharibi zote‟, kwani kwa kipindi cha
mwaka mzima jua hudhihiri katika vituo vinavyofuatana baina ya Tropiki hizo mbili. Hivyo, kila
kituo tunaweza kukiita mashariki pamoja na magharibi inayoelekeana nayo. Kwa maana hii,
tunapata kuelewa kuwa kuna mashariki na magharibi nyingi.
Kuna mashariki na magharibi nyingi katika sayari nyingine (11)
. Basi utukufu ni wa Mola wa
mashariki zote na magharibi zote.
Katika kuhitimisha, je, hatuwezi kusema kuwa „hitilafu‟ zinazodaiwa zipo tu kwa yule
anayezielewa vibaya Aya hizo au anayefanya uovu wa kuzusha uongo huo kwa malengo yake
binafsi?
Rejea:
1. “Je hawaizingatii Qur‟an? Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa
Mwenyezi Mungu bila shaka wangekuta ndani yake khitilafu nyingi”
{4:82}
2. Tuhuma hizi zinatolewa na Goldziher pamoja na Losian Klimovitch ambao hawaitambui
Qur‟an kama kitabu cha Mungu bali kama kazi ya ubunifu wa Muhammad.
3. Qur‟an {36:51}
27
4. Qur‟an {8: 32-34}
5. Qur‟an {73: 9}
6. Qur‟an {55: 17}
7. Qur‟an {70:40}
8. Qur‟an - {7:153}
9. Qur‟an - {3:11}
10. “Hata atakapotufikia, atasema: Laiti ungelikuwa umbali wa mashariki na magharibi kati
yangu na wewe”
Qur‟an :{ 43:38}
11. “Mola wa mbingu na ardhi na yaliyomo kati yake, na ni Mola wa mashariki
zote na magharibi zote”.
Qur‟an {37:5}
28
KESI YA NNE
Uislam Kwa watu wote (1)
Hakimu: Uite Uislam
(Bawabu wa mahakama anauita Uislam)
(Uislam unaingia mahakamani, tabasamu linaonekana mdomoni mwake na kuwatupia jicho la
dhihaka wapinzani wake, unajiamini kikamilifu kuwa hauna hatia na pia Mtume wake naye hana
hatia.)
Hakimu: Mwendesha Mashtaka endelea!
Mwendesha Mashtaka: Fikra ya kuitangaza dini hii kwa watu wote ilikuja baada tu ya kifo cha
Muhammad; Muhammad mwenyewe hakufikiria hata kidogo kuhusu jambo hili, japokuwa fikra hii
inaungwa mkono na idadi kubwa ya Aya mbali mbali za Qur‟an pamoja na hadithi (maneno ya
Mtume). Kama itadaiwa kuwa Muhammad alikuwa na fikra hiyo, basi ilikuwa kwa mbali sana.
Mahali pa ujumbe wake hasa ilikuwa ni Arabia, na dini hii mpya ilikusudiwa kwa Arabia pekee.
Muhammad (S.A.W.) katika maisha yake yote alielekeza wito wake kwa Waarabu tu. Kamwe
hakupanga kuusambaza Uislam kila mahali, wala hakufanya mipango yoyote kwa ajili ya kuanzisha
jambo hili. Kama Uislamu uliendelea na kuenea dunia nzima (2)
ilitokana tu na sababu za nje ya
malengo ya dini hii. Muhammad (S.A.W) aliuweka wito wake ndani ya mipaka ya Arabia na
kamwe hakwenda nje ya mipaka hiyo kuyaita mataifa mengine kuingia katika dini yake (3)
.
Hatuwezi kueleza hasa kama Muhammad (S.A.W) mwenyewe alihisi kuwa alitakiwa kueneza
ujumbe huo kwa watu wote (4)
.
[Uislamu unatabasamu na, Kwa imani thabiti ya kuwa uko kwenye haki Na ukiwa na imani ya
ushindi, unasimama ili kujitetea]
Uislam: Mheshimiwa Hakimu! Je inaingia akilini kwamba Muhammad hakujua nchi yoyote
tofauti na Arabia na kwamba hakuwafikiria watu wengine? Kuna uthibitisho gani kuwa dini hii
ilikusudiwa kwa ajili ya Arabia pekee?
Kipindi watu wa kabila la Kiquraishi walipokuwa wakifanya biashara na nchi jirani wakati huo,
walipata taarifa na uzoefu wa mambo mengi ya nchi zinazowazunguuka. Muhammad mwenyewe
akiwa bado mdogo alisuhubiana na ami yake katika safari ya kibiashara kwenda Syria. Vile vile
alikwenda katika safari ya pili kwa niaba ya Khadija, aliyekuja kuwa mkewe hapo baadaye. Iweje
29
idaiwe kuwa Muhammad, ambaye akili yake, uaminifu na hekima yake vilikuwa mashuhuri,
kwamba hakujua chochote kuhusu nchi yoyote nje ya Arabia?
Mheshimiwa Hakimu! Kama tukilazimika kutumia mantiki ya hawa Mustashriqiina,
itawezekanaje mtu aliyefikia mafanikio yote haya na kuwa bwana pekee wa Arabia, aache
kuupanua utawala wake kwenda mbali zaidi, hususani kama alikuwa na shauku ya utawala na kuwa
na nguvu? Kama Mustashriqiina mwenye kiburi angeambiwa kuwa Alexander Mkuu (Alexander
the Great) alikuwa akipambana kuanzisha himaya ambayo ingemeza ulimwengu wote wa zamani na
kuipiga chapa ya utamaduni na lugha yake, hayo asingeyakataa. Kama angeambiwa kuwa
Napoleon alikuwa akifanya jitihada ili kuunda milki ambayo ingejumuisha ulimwengu wa kale na
wa sasa na hatimaye apate kukaa kwenye kiti chake cha utawala, hilo angeliamini. Kama
ingedaiwa kuwa Hitler alikuwa akijaribu kufanya yale yaliyofanywa na Genghis Khan kabla yake,
hilo nalo angeliamini. Lakini kama ingesemwa kuwa Muhammad bin Abdillah alikuwa akifikiria
kuwaita kwenye neno la Mungu watu wote waliokuwa wakiishi jirani na Arabia, ambao walikuwa
wakifanya biashara na Maquraishi, na ambao maisha yao yaliwategemea, wale wenye chuki na
inda, wenye kuongozwa na ushabiki wangedai kuwa Muhammad alikuwa mbali kufikiria jambo
hilo.
Kuhusu madai kwamba dini hii iliwahusu Waarabu pekee, ni madai ambayo hayakujengwa hata
kidogo kwenye msingi wa hoja na mantiki, kwa sababu hakuna ushahidi wowote au fununu hata
kidogo za kuyathibitisha. Muhammad (S.A.W) alipandikiza ndani ya Waumini wa Kiislam imani
ya kuwa dini yake inafaa kwa kila mahali na kila zama. Qur‟an inazunguka kila mazingira kwa
maelezo kamili:-
“Na tumekuteremshia kitabu kielezacho kila kitu, na ni muongozo
na rehma na khabari za furaha kwa wanaojisalimisha” (5)
Madai kwamba, kwa kuwa Qur‟an iko katika lugha ya Kiarabu basi itawahusu watu
wanaozungumza Kiarabu tu. Madai haya hayana msingi kwa sababu kila kitabu kilichoteremshwa
lazima kiwe katika lugha moja na kuwahutubia watu fulani kama hatua ya mwanzo. Zaidi ya hayo,
anayeisoma Qur‟an hatokuta mahali popote inaposema kuwa inawahusu watu fulani tu, na pale
inapoelezewa kuwa ni “Qur‟an ya Kiarabu”, inakusudiwa tu lugha iliyoteremshiwa hiyo Qur‟an.
Ushahidi wa wazi kuhusu ujumbe kuwa wa watu wote na kuhusu Uislam kuwa kwa walimwengu
wote, uthibitisho upo katika ukweli kwamba miongoni mwa wafuasi wa mwanzo wa Uislam ni
pamoja na „Bilal‟ kutoka Ethiopia, „Suhaib‟ kutoka Byzantium na „Salman‟ kutoka Fursi (Iran).
Ushahidi huu wa wazi hauachi shaka yoyote kwamba Uislam haukuhusu jamii ya Kiarabu pekee,
hata kabla ya Waarabu wenyewe hawajafikiria kufanya ufunguzi au vita nje ya Arabia.
Mheshimiwa Hakimu! Nina ushahidi wa ziada katika tabiri nyingi za Muhammad mwenyewe
zinazohusu ueneaji wa Uislamu baada yake. Tafadhali niruhusu nitoe baadhi yake:
30
1. Akiwa safarini kuelekea Madinah, wakati wa kuwakimbia jamaa zake wa Makka, na katika
nyakati ngumu sana za maisha yake, Muhammad (S.A.W) alimtabiria Suraqa bin Malik kuwa siku
moja yeye Suraqa atavaa majoho mawili na mkanda wa Khosro, mfalme wa Fursi (Iran). Miaka
mingi ilipita na hatimaye Fursi ikaangukia mikononi mwa Waislamu na hayo majoho mawili na
mkanda vilikuwa miongoni mwa ngawira za Waislamu. Vitu hivyo vilifaa kuvaliwa na mtu mrefu,
na hivyo vikakabidhiwa kwa Suraqa aliyekuwa mrefu kati ya watu wengine. Na hapo Suraqa
akaukumbuka utabiri uliotolewa na Muhammad (s.a.w.) alipomuahidi kuwa ndiye ambaye
angevivaa vitu hivyo.
2. Siku moja Muhammad (S.A.W), alisimulia ndoto yake kwamba baadhi ya wafuasi wake
walikuwa wakisafiri katika bahari kama vile wafalme walio juu ya vitanda vyao. Mwanamke
mmoja aliyeitwa Ummu Hiram alimuomba Mtume (S.A.W.) amuombee ili awe mmoja wao.
Akasema:- “Wewe ni mmoja wao”.
Miaka kadhaa baadaye, Um Hiram alikuwa miongoni mwa wale waliosafiri kwenda Cyprus,
ambapo alifariki dunia akiwa huko na kaburi lake bado lipo huko mpaka leo.
3. Mtume (S.A.W) aliwaamuru masahaba wake kuwatendea wema watu wa Misri pale
aliposema:- “Mwenyezi Mungu atawafungulieni Misri. Kuweni wema kwa watu wake”
Je, Misri na watu wake wako Arabia?
4. Kabla ya vita vya Khandaki na wakati handaki likichimbwa ili kuunusuru mji wa Madinah
dhidi ya wavamizi kutoka Makkah na washirika wao, Muhammad (S.A.W) aliwatabiria masahaba
wake kuwa makasri ya Syria na Fursi yangefunguliwa kwa ajili yao.
Je, maeneo haya yapo Arabia?
Tabiri hizo zisizokuwa na idadi zinakanusha uongo wa Mustashriqiina hao wenye viburi.
5. Mfano wangu wa mwisho: Katika maneno ya Muhammad (S.A.W) tunakuta maelezo
yasemayo yeye:- “Ametumwa kuwa rehma kwa walimwengu wote” (6)
Wakati fulani alimweleza gavana wa Yemeni ------ iliyokuwa ikitawaliwa na Fursi wakati huo-----
kwa maneno yafuatayo:- “Dini yangu na utawala wangu utapanuka na kufika mahali
utakapofika utawala wa Fursi”
Je, kulikuwapo na tangazo la wazi zaidi kuliko hili?
Kwa upande mmoja kuna Aya nyingi ndani ya Qur‟an zinazoelezea kuenea kwa Uislam na kuhusu
Uislam kuwa ni dini ya ulimwengu mzima. Hapa nitatoa chache kama mfano:-
“Huo sio ila ni ukumbusho na Qur‟an ibainishayo. Ili imuonye kila aliye
hai” (7)
“Mwenye baraka ni yule aliyeteremsha Qur‟an kwa mja wake ili awe muonyaji kwa walimwengu
wote” (8)
31
“Na hatukukutuma ila uwe Mtume kwa watu wote na uwe mtoaji wa khabari nzuri na
muongozaji, lakini watu wengi hawajui” (9)
“Waambie „Muhammad‟; Enyi watu hakika Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote” (10)
Hiyo ni tofauti kati ya ujumbe wake na ujumbe wa Mitume waliomtangulia. Ujumbe wa mitume
wengine unapoelezewa mahali popote unahusu watu wao tu, kwa mfano:-
“Hakika tulimpeleka Nuhu kwa watu wake, akawaambie: Enyi watu wangu, mwabuduni
Mwenyezi Mungu nyinyi hamna Mungu ila yeye” (11)
“Na kwa Thamudi tulimpeleka ndugu yao Saleh” (12)
“Na tulimpeleka Luti alipowaambia kaumu yake: Je, mnafanya uchafu ambao haja
kutangulieni yeyote kwa ufasihi huo katika walimwengu?” (13)
“Na kwa watu wa Madyana tulimpeleka ndugu yao Shuaib akawambia: Enyi kaumu yangu,
muabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu ila yeye” (14)
“Na kwa A‟di tulimpeleka ndugu yao Hud” (15)
Hivyo Nuhu, Saleh, Luti, Shuaib na Hud kila mmoja alitumwa kwa watu wake. Lakini Uislam
imeeleza wazi kuwa ni kwa ajili ya watu wote. Sasa inakuwaje Mustashriqiina pamoja na wao
kuifahamu vema lugha ya Kiarabu waseme kuwa maneno „watu wote‟ yana maanisha Waarabu
peke yao?
Ujumbe wa Muhammad ulienea kila mahali duniani na kuziweka pamoja jamii zote ulimwenguni.
Hakuna yeyote miongoni mwao aliyehisi kuwa ujumbe huu ulielekezwa kwa jamii moja tu au
kwamba unaifaa jamii moja bila nyingine. Wote waliridhika na kukubali kuwa ujumbe huo
uliwahusu wote na unayazunguka maisha na uhai wao wote.
Rejea:
1. “Huu siyo ila ni ukumbusho kwa walimwengu. Na ama mtajua khabari zake baadaye
kidogo” Qur‟an {38:87 – 88}
2. Muir – The Caliphate – Uk. 34 – 44
3. Caetani – Annal‟e de Islam –Jz.V – Uk. 323 – 324
4. Carl Brocklemann – The History of the Muslim Nations – Uk. 70 – 71
5. Qur‟an - {16:89}
6. “Nasi hatukukutuma, ila uwe rehema kwa walimwengu”
Qur‟an {21:107}
7. Qur‟an {36:69 - 70}
32
8. Qur‟an {25:1}
9. Qur‟an {34:28}
10. Qur‟an {7:158}
11. Qur‟an {7:59}
12. Qur‟an {7:73}
13. Qur‟an {7:80}
14. Qur‟an {7:85} 15. Qur‟an {9:50}
33
KESI YA TANO
Barua zilizobuniwa (1)
[Uislam umeitwa na kuingia chumba cha mahakama. Mwendesha mashtaka anasoma mashtaka
yafuatayo]
Mwendesha Mashtaka: Muhammad hakuwahi kutuma ujumbe kwa wafalme na maamiri wa nje
ya Arabia (2)
. Hili linakubaliana na maoni ya William Muir na Caetani, kwamba Uislam kamwe
haukuwafikiria watu wa nje ya Arabia.
Uislam: Mashtaka haya yana sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni uwepo
wa barua na ujumbe huo, sehemu ya pili ni tuhuma za William Muir na Caetani.
Nilijibu suala hilo la pili katika kesi iliyopita, hivyo sihitaji kulielezea zaidi. Jibu langu kwa suala
la kwanza ni kwamba hakuna ushahidi wowote unaothibithisha madai haya, bali mambo ni
kinyume chake, hasa pale tunapokuta kwamba baadhi ya barua hizi bado zipo mjini Istanbul. Barua
nyingine zinaweza kuwa zimepotea kwa sababu moja au nyingine, au zimechanika kama
ilivyotokea kwa barua iliyotumwa kwa mfalme Fursi wa wakati huo.
Je, sio jambo la kushangaza kuona kwamba Mustashriqiina wameshindwa kuzifuatilia barua hizi
katika historia ya wafalme na maamiri hawa, pale ilipozuka mizozo kuhusu hizi barua?
Ni muhimu kueleza kuwa historia ya taifa lolote haiwezi kuchukuliwa kutoka kwa wale walio
wageni nayo, hivyo historia ya Uislam haiwezi kuchukuliwa kutoka kwa Mustashriqiina ambao
masomo yao juu ya Uislam yanakosa busara na kutopendelea na wamejawa na chuki. Hili
linamhusu hasa Marguiliuth na wenzake, ambao kazi yao inatiwa alama na kupigwa chapa za
uwongo, vijembe na uadui. Kwa upande mwingine, wanahistoria wetu wa Kiarabu ambao ndio
chanzo cha taarifa tulizo nazo kuhusu urithi wetu, hawakuwa na shaka hata kidogo kwamba barua
hizi zilikuwepo kweli na zilitumwa kwa watawala hao.
Sasa tunatakiwa kumwamini nani, wanahistoria wetu wenyewe, au Mustashriqiina wa kigeni?
Mheshimiwa Hakimu! Sasa nitatoa rejea muhimu katika vitabu vya Kiarabu kuhusu historia ya
Kiislam, na kisha nitakuachia wewe utoe uamuzi wako.
1. Ibn Hisham – Jz 4 – Uk. 279 – 280 - {Ujumbe mbalimbali}
2. Yaqubi – Jz 2 – Uk. 83 – {Ujumbe mbalimbali}
3. Ibn Al-Athir, Al-Kamil Fi Tarekh – Jz 2 – Uk. 143 – {Ujumbe mbalimbali}
4. Al-Bidaayah Wanihaayah – Jz 4 – Uk. 362
5. Tabari – Jz 2 – Uk. 646 - {Ujumbe wa Muhammad kwenda kwa Wafalme mbali mbali}
34
Kwa mfano tuangalie kilichosimuliwa katika Tabari Juzuu ya 2 Ukurasa 649 ambapo tunakuta
ujumbe wa Muhammad kwenda kwa Heraclius, unaosema:-
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, mwenye kurehemu.
Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mungu, kwenda kwa Heraclius, Kaizari wa Rumi. Amani
iwe juu ya wale wanaofuata muongozo wa Mwenyezi Mungu. Fuata Uislam nawe utapata
amani. Fuata Uislam na Mwenyezi Mungu atakulipa mara mbili. Kama ukikataa basi dhambi
za Mafarisayo zitakuwa juu yako”
Hapa kuna barua nyingine ya Muhammad kwenda kwa Muqawqus:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, mwenye kurehemu.
Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mungu kwenda kwa Muqawqis, mtawala wa Misari. Amani
iwe nawe juu ya wale wanaofuata muongozo. Ninakuita kwenye Uislam, ufuate Uislam nawe
utapata amani na kulipwa mara mbili. „Sema‟: Enyi watu wa kitabu njooni kwenye neno lililo
sawa baina yetu na nyinyi. Kwamba tumuabudu Mwenyezi Mungu; na tusimshirikishe na
chochote”.
Na hii hapa ni barua kwenda kwa mfalme wa Ethiopia:-
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma na mwenye kurehemu.
Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mungu, kwenda kwa Najjashi mfalme aliyebarikiwa wa
Ethiopia. Amani iwe juu yako, ninamtukuza Mungu kwako. Ninashuhudia kwamba, masihi bin
Mariam ni roho wa Mungu na ni neno lake alilolitupa kwa Mariam mwema, mtakatifu na msafi.
Alimzaa Isa, ambaye Mungu alimuumba kutokana na roho wake na akampulizia uhai, kama
alivyomuumba Adam kwa uwezo wake na kumpulizia uhai. Ninakuita kwa Mungu wa pekee
asiyekuwa na mshirika, endelea kumtii na kunifuata mimi na kuamini ufunuo niliofunuliwa.
Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Nimemtuma binamu yangu Ja‟far pamoja na baadhi ya
Waislam, wakifika kwako basi wapokee vyema. Ninakulinganisha wewe na wanajeshi wako kwa
Mwenyezi Mungu, nimefikisha ujumbe wangu na nimekushauri uukubali. Amani iwe juu ya
wale wanaofuata muongozo”
Muhammad alituma ujumbe ufuatao kwa Kisra mfalme wa Wafursi:-
“Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwenda kwa Kisra mtawala wa Fursi.
Amani iwe juu ya wale wanaofuata muongozo na kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume
wake. Ninakuita kwenye ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ambae ndie Mkuu. Hakika mimi ni
Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, nimetumwa kutoa maonyo kwa wale walio hai na
adhabu itakuwa juu ya wale wanaoikataa haki. Fuata Uislam nawe utapata amani. Kama
ukikataa, basi dhambi ya mjusi itakuwa juu yako”
Mheshimwa Hakimu! Usahihi wa barua na ujumbe huu unaungwa mkono na ushahidi ufuatao:-
35
1. Mahojiano yaliyofanyika baina ya Heraclius, mfalme wa Rumi, na Abu Sufian, kiongozi wa
wapagani wa Makkah. Heraclius alikuwa Jerusalem pindi ujumbe na barua hiyo ulipofikishwa
kwake na Duhya Al-Kalbi, mjumbe wa Muhammad ambaye alikaribishwa vyema na mfalme huyo.
Baada ya muda mfupi mfalme aliwataka watu wake watafute na kuona kama wanaweza kumpata
Mwarabu yeyote kutoka Makkah, na kama wakimpata wamlete kwa ajili ya kuulizwa.
Wakati huo Abu Sufian na baadhi ya rafiki zake walikuwa mjini Jerusalem wakifanya biashara
pamoja na kununua bidhaa. Kama inavyojulikana vyema, Abu Sufian alikuwa mmoja wa maadui
wakubwa wa Uislam. Yeye pamoja na jamaa zake waliletwa mbele ya mfalme na mazungumzo
yalikuwa kama ifuatavyo:-
Heraclius: Unamfahamu mtu huyu, Muhammad, ambaye amenitumia ujumbe
akidai kuwa ni Mtume? Waweza kuniambia anatoka katika familia ya aina gani?
Abu Sufian: Anatokana na familia tukufu.
Heraclius: Kuna yeyote katika wahenga wake aliyewahi kuwa mfalme?
Abu Sufian: Hapana.
Heraclius: Je, kuna yeyote katika familia yake ambaye amewahi kuwa na
madai sawa na haya?
Abu Sufian: Hapana.
Heraclius: Watu ambao wameikubali dini yake ni masikini au matajiri?
Abu Sufian: Ni Masikini.
Heraclius: Je, wafuasi wake wanaongezeka au wanapungua?
Abu Sufian: Wanaongezeka.
Heraclius: Mlimtuhumu kwa uongo kabla ya kufanya madai hayo?
Abu Sufian: Hapana; kamwe hatujawahi kumuona akisema uongo.
Heraclius: Je, anakwenda kinyume na ahadi zake?
Abu Sufian: Hata kidogo, lakini lazima tuangalie kama ataendeleza makubaliano
mapya yaliyo baina yetu na yeye.
Heraclius: Je, mmewahi kupigana naye vita?
36
Abu Sufian: Ndiyo.
Heracliua: Matokeo yalikuwaje?
Abu Sufian: Wakati fulani sisi tulishinda na wakati mwingine yeye alishinda.
Heraclius: Anafundisha nini?
Abu Sufian: Anafundisha watu kumuabudu Mungu mmoja, na kutomfanyia
washirika, kuwa wasafi wa moyo, kusema ukweli tu, na kuchunga ahadi na
kutekeleza amana zao.
Kisha Heraclius akayatolea maoni maswali yake na kumfafanulia Abu Sufian sababu ya yeye
kumuuliza maswali hayo:
“Unasema kwamba anatokana na familia tukufu, siku zote mitume hutoka katika familia tukufu.
Unasema familia yake haijawahi kudai utume hapo kabla, kama ingekuwa imefanya hivyo,
ningesema kuwa anafanya hivyo sasa kwa sababu ya kutaka kurithi utume. Unakubali kuwa
hajakuwapo mfalme katika familia yake, kama ingekuwa hivyo, ningesema kuwa anatafuta taji la
ufalme. Unatambua kuwa hasemi uongo. Yule asiyewadanganya watu atawezaje kumzulia uongo
Mwenyezi Mungu? Unashuhudia kuwa maskini ndio wanaomfuata, siku zote watu maskini ndio
wanaowafuata mitume kabla ya watu wengine.
Unasema kuwa havunji ahadi zake, mitume hawadanganyi. Unasema kuwa anafundisha sala,
uchamungu na maadili mema, kama haya yote ni kweli, nina hakika ufalme wake utafika mahali
niliposimama. Nilikuwa na hakika kuwa kuna mtume anakuja, lakini sikufikiri kuwa angezaliwa
Arabia. Ninatamani ningekuwa pamoja na Muhammad ili niioshe miguu yake”.
Baada ya mahojiano hayo Abu Sufian aliondoka huku akiwaambia watu wake kuwa daraja ya
Muhammad imepanda juu.
Mwanahistoria mashuhuri, Tabari (3)
anaelezea zaidi kwamba kabla ya Heraclius kutoka Syria
kuelekea Constantinople, aliwakusanya watu wake na kusema:
“Enyi watu wa Rumi, nina masuala kadhaa ninayoyaleta mbele yenu na ningetaka ushauri
wenu. Mnajua huyu mtu ni Mtume aliyetumwa na Mungu, sifa zake zimetajwa katika vitabu
vyetu vitukufu. Tumfuate ili kuyaokoa maisha yetu hapa duniani na huko Akhera”
Wakasema:-
“Itawezekanaje sisi tujisalimishe kwa Waarabu, ufalme wetu ni mkubwa na tunawazidi kwa
wingi wa watu na mali?”
37
Akasema Mfalme:-
“Basi tumlipe kodi ili tuepuke mapambano naye”
Wakajibu:-
“Kamwe hatutojidhalilisha kwa kuwalipa Waarabu kodi wakati sisi ni wengi sana kwa idadi,
tuna nguvu kubwa zaidi yao na tuna hadhi na heshima kubwa”
Akawashauri:
“Basi tusuluhishe naye kwa kumpatia eneo la Syria wakati ambapo uendeshaji wa mambo ya
maeneo mengine ya ardhi zetu yabaki mikononi mwangu” .
Wakasema:
“Umpe ardhi ya Syria, moyo wa ufalme wetu? Tunaapa kwa Mungu, kamwe hatutalifanya hilo”
.
Akasema:
“Basi na iwe hivyo, kama mnaijali hivyo ardhi yenu basi kamwe hamtoshindwa”.
Kisha alimpanda Nyumbu wake, na wakati akiondoka Damascus aliiaga Syria.
Sasa ninaelekea kwenye kipande cha pili cha ushahidi wangu:
Wakati Margiliuth akikubali na akitambua kusilimu kwa Bazan, Gavana wa Kifursi nchini Yemen,
haelezi chanzo hasa cha kusilimu kwake.
Kisa hicho ni kama ifuatavyo:
Kisra, Mfalme wa Kifursi alimuagiza Bazan, gavana wake nchini Yemen, atume watu wawili
wenye nguvu waende kwa Muhammad na kumleta kwa mfalme huyo akiwa mateka.
Wakiwa njiani, watu hawa walikutana na Maquraish ambao walifurahi sana kusikia kuwa
Muhammad angechukuliwa mateka mpaka Fursi, na wakawaeleza kuwa wangeweza kumpata
Muhammad mjini Yathrib (Madinah).
Walipokutana na Muhammad na kumtaka aende nao kwa mfalme, Muhammad aliwataka waje
siku ya pili.
Pindi waliporejea, Muhammad aliwaambia kwamba Mola wake alikuwa amemuua bwana wao;
mtoto wa Kisra alikuwa amemuua baba yake usiku ule. Walimuuliza kama wangemueleza
38
Bazan kuhusu jambo hilo. Muhammad aliwaamuru kufanya hivyo, akiongeza kuwa wamweleze
wazi ya kwamba dini ya Muhammad ingefika mahali ulipoenea utawala wa Kisra.
Walipomsimulia Bazan tukio kamili, alisema kuwa yalikuwa ni maelezo ya mfalme, na kwamba
mtu huyo lazima atakuwa ni mtume kama alivyodai. Wangelazimika kusubiri ili kuthibitisha
maelezo hayo ya Muhammad: kama yatakuwa sahihi, basi atakuwa ni mjumbe wa Mungu, la
sivyo uamuzi utachukuliwa baadaye.
Ndani ya muda mfupi Bazar alipata barua kutoka kwa Shiraweih, akisema:
“Nimemua Kisra baada ya kukasirishwa na yale aliyoifanyia Fursi, akiwaua watu wasiokuwa na
hatia. Mara upokeapo barua yangu unaagizwa kusimamia utoaji wa kiapo cha utii kutoka kwa
raia wetu waliopo katika wilaya yako. Ama kuhusu mtu ambaye Kisra alikuandikia maagizo
yake (yaani Muhammad), usimdhuru mpaka utakapopata maelekezo zaidi”
Pindi Bazan alipomaliza kusoma barua hiyo alisema:-
“Bila shaka mtu huyu ni Mtume wa Mungu”, kisha akasilimu pamoja na Wafursi waliokuwa
naye huko Yemen
Margiliuth hakatai kisa hiki, lakini anasisitiza kuwa mawakala wa Muhammad waliripoti tukio hilo
la kifo cha Kisra kwake, jambo ambalo tutalitolea maoni hapo baadaye. Swali letu hapa ni,
anawezaje kukubali usahihi wa kihistoria wa tukio hili lakini akapinga sababu zake? Anaukataa
hata ujumbe wa Muhammad kwenda kwa Kisra. Wakati huo huo hatoi sababu ya Kisra kuwatuma
watu wawili wenye nguvu kwenda kumua Muhammad na wala hatoi sababu ya barua ya shrawih
kwenda kwa Bazan, au hata sababu ya Bazan na watu wake kuingia katika Uislam. Nitahitimisha
hoja yangu kwa kuelezea matukio mawili zaidi, vita vya muta na usia wa Muhammad kuhusu watu
wa Misri.
Baadhi ya Mustashriqiina, kama vile Brockelmann, wanakubali kuwa vita vya Muta, vilivyotokea
mwaka wa nane wa Hijra, ilikuwa katika ulipizaji kisasi dhidi ya Al-Harth bin Abi Shummar wa
Ghassan, kwa sababu ya kumuua mjumbe wa Mtume (s.a.w.), aitwaye Shuqa‟ bin Wahb Al-Asath.
Swali lililopo hapa ni, ilikuwaje kutokee vita kwa sabau ya mauaji ya mjumbe wa Mtume wakati
ambapo Margiluith na wengineo wanakanusha uwepo wa ujumbe huo?
Brockelmann anakubali pia kwamba Muhammad aliwaamuru masahaba wake kuwafanyia wema
Wamisri pale aliposema:-
“Mwenyezi Mungu atawafungulia Misri baada yangu. Ninawausia kuwatendea wema Wamisri.
Katika wao mnao ndugu na wenza”
Ukweli kwamba Maria, Mmisri alikuwa mke wa Muhammad, ni ushahidi wa kuaminika wa ujumbe
wa barua hizo. Kama isingekuwa ujumbe wa Muhammad kwa mfalme wa Misri Al-Muqawqis -----
ujumbe uliopelekwa na Habib bin Abi Baltaa----- Maria asingekuja Arabia kama zawadi ya mfalme
39
wa Misri kwa Muhammad na kisha kuwa mkewe. Al-Muqawqis mwenyewe asingetuma zawadi
hizo kwa Muhammad kama asingekuwa amejadiliana na mjumbe wa Muhammad.
Uwepo wa barua halisi ya Muhammad kwenda kwa Al-Muqawqis kwenye makumbusho ya Top
Kapi mjini Istanbul ni ushahidi usiopingika wa usahihi wa barua hizo ambazo hata Mustashriqiina
hawajaweza kuukanusha. Uwepo wa barua moja ni uthibitisho mzuri wa ukweli kwamba
Muhammad aliwatuma wajumbe wake kwenda kwa watawala wa enzi hizo wa nchi zinazoizunguka
Arabia.
Yote haya ni ushahidi wa kutosha kuwa Uislam ni dini ya walimwengu wote kama ilivyooneshwa
na Aya mbali mbali za Qur‟an ambayo nimekwishaitetea. Bila shaka Muhammad mwenyewe
asingewatuma wajumbe hao kwenda kwa wafalme na watawala wa enzi zake kama asingetakiwa na
Aya za Qur‟an kuwaita kwenye Uislam watu wote kila mahali kwa kutumia hekima na mahubiri
mazuri. Qur‟an inasema:-
“Uite watu wote kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema” (4)
Rejea: 1. “Mwenyezi Mungu ataifungua Misri kwa ajili yenu, baada ya kuondoka kwangu. Watendeeni wema
watu wake, katika nyinyi kuna ndugu na wenzi wao”.
{Maneno ya Mtume}
2. Madai haya yalitolewa na Mustashriqi aitwaye David Samwel Margiliuth
3. Tabari – Juzuu ya 2 – Uk. 651
4. Qur‟an - {16:125}
40
KESI YA SITA
Muhammad na ubashiri wake
Mwendesha Mashtaka: Majasusi wa Muhammad mara zote walimpatia habari mpya ndani ya
muda mfupi, na hivyo ninashaka kwamba sababu ya wajumbe wa Bazan kutomchukua Muhammad
kama mateka kwenda Yemen haikutokana na ubashiri wa Muhammad kwamba Kisra alikuwa
ameuawa. Kama kweli Muhammad aliweza kujua jambo hili la kuuawa kwa Kisra, lazima itakuwa
imetokana na misukosuko na ghasia zilizotokea katika ufalme wa Fursi punde tu baada ya mauaji
ya Kisra, zikiwawezesha majasusi wa Muhammad kumpatia habari hizo.
Hakimu: Ni upi utetezi wako, Islam?
Uislam: Lengo la Margiliuth na wenzake siku zote ni kuukadhibisha utume wa Muhammad ili
hatimaye waukadhibishe ufunuo na ujumbe wake wote. Ikiwa kile alichokuja nacho Muhammad
sio ufunuo, ujumbe na utume, je, ufunuo na utume ungetakiwa kuwaje na sifa za utume huo
zilitakiwa ziweje? Ni sifa zipi kati ya hizo ambazo hatukuzishuhudia kwa Muhammad? Margiliuth
na wale walio kama yeye waliitambua idadi ya mitume na manabii, kwa nini hawaukubali utume
wa Muhammad, wakati alikuwa na sifa zote walizokuwa nazo mitume waliomtangulia?
Hata hivyo, katika kuibua shaka hizi Margiliuth ameshindwa kutaja hata jina moja la „majasusi‟
waliomfanyia kazi Muhammad na kumpa habari na taarifa mpya, vile vile ameshindwa kueleza
kuwa ghasia alizodai kuwa taarifa zake zilimfikia Muhammad hazikutokea katika mji au wilaya ya
jirani, bali umbali wa zaidi ya maili elfu moja.
Margiliuth aliacha nukta muhimu kwamba Muhammad alitangaza kifo cha Kisra siku ile ile
aliyeuawa licha ya umbali uliopo baina ya Arabia na Fursi. Zaidi ya hayo taarifa za kifo cha Kisra
hazikufika Yemen ila baada ya ubashiri wa Mtume (S.A.W) na wajumbe wa Bazan walirejea
Yemen na kusubiri taarifa rasmi kutoka Fursi.
Hali ya Marqiliuth kupinga suala la wajumbe wa Bazan kukataa kutekeleza amri ya Kisra ya
kumuua Muhammad kwa sababu ya ubashiri wa Muhammad, upingaji wake huo unakanushwa kwa
sababu mbili:-
Eneo la:-
1. Kwa nini wajumbe hao walirudi Yemen bila kumpeleka Muhammad?
Margiliuth anakataa ubashiri wa Mtume kuwa ni sababu ya kurudi kwao. Lakini hakutoa sababu
mbadala.
41
Ni rahisi kutoamini baadhi ya matukio, lakini ni vigumu na haiwezekani kabisa kuwakinaisha
watu wengine juu ya kile tukisemacho kama hatutoi ushahidi na uthibitisho kamili. Tunauliza;
Margiliuth anatoa ufafanuzi gani kuhusu kusilim kwa Bazan?
2. Waarabu na majirani zao wakati huo wasingekuwa na wasiwasi wowote
wa kukubali ubashiri huo, ikizingatiwa kuwa walikuwa wakisubiri kudhihiri kwa nabii wa mwisho.
Hata Heraclius alimwandikia gavana wa Iliya akimuuliza kuhusu maudhui hii.
Hivyo, hoja yenye nguvu inayakanusha madai ya Margiliuth na kuyachukulia kuwa hayana msingi.
Tukiendelea mbele zaidi, tunaweza kumuuliza Margiliuth na wenzake maswali kadhaa:-
i) Anasemaje kuhusu maelezo ya Mtume juu ya matukio yaliyokuwa yakitokea kwenye uwanja wa
vita vya Mu‟ta iliyopo umbali wa mamia ya maili kutoka Madina, alipokaa msikitini adhuhuri moja
na kusimulia yaliyokuwa yakitokea wakati huo baina ya askari wake 3000 waliokuwa
wakipambana na askari 100,000 wa Kirumi?
Alikuwa akiwaelaza kuwa:-
“Bendera imebebwa na Zaid bin Haritha, ameendelea kupambana mpaka akauawa. Kisha
Jaafar ameishika na kupambana mpaka naye amefika mwisho wake”
Kisha baada ya kimya cha muda mfupi aliendelea kusema:-
“Abdullah bin Rawaha ameichukua bendera na kupambana mpaka kifo chake. Kisha
bendera ikachukuliwa na upanga wa Mungu- yaani Khalid bin Walid - naye sasa
anapambana vikali”
Majasusi waliwezaje kumpa Muhammad habari zilizokuwa zikitokea wakati huo huo?
Swali letu la pili: Margiliuth anatoa tafsiri gani kuhusu maelezo ya kina yaliyotolewa na
Muhammad kuhusu Msikiti wa Al-Aqsa alipokuwa akijibu swali la Abu Jahl na Maquraishi katika
kuthibitisha suala la safari yake ya kimiujiza aliyokuwa ameifanya ndani ya usiku mmoja tu
kwenda kwenye Msikiti huo na kisha kupaa juu kwenda mbinguni?
Katika tukio jingine aliwapa Maquraishi taarifa mpya kuhusu msafara wao wa biashara uliokuwa
njiani kutoka Syria kuja Makka. Alitangaza kuwa msafara huo ungewasili wakati wa
mapambazuko ukiongozwa na ngamia mkubwa, ambaye aliwaelezea sifa na muonekano wake.
Maquraishi walitoka kwenda kwenye viunga vya mji wa Makkah, sio kwa ajili ya kupokea msafara
huo, bali kuthibitisha uongo wa Muhammad, kwani hawakuamini kuwa angeweza kuwa hata na
taarifa za msafara wao katika wakati ambao yeye hakuondoka Makkah usiku ule. Wakiongozwa na
Abu Jahl, Maquraishi walikaa wakisubiri mapambazuko na hakika msafara ulijitokeza katika muda
na mahali husika. Maoni yao pekee yalikuwa ni kwamba ule ulikuwa uchawi wa Muhammad.
Swali letu la tatu: Margiliuth na wengine wangetoa ufafanuzi gani kuhusu tukio lifuatalo?
42
Muda mfupi baada ya vita vya Badr, ambavyo Muhammad aliwashinda maadui wake wa
Kiquraishi, Omair bin Wahb pamoja na Safwan bin Umayya walipanga kwenda kwa Muhammad
na kumuua huku wakijifanya kuwa wanaomba kuachiwa huru kwa mwanaye Omair aliyekuwa
mateka. Kama Omair akishindwa kutekeleza jambo hili basi Safwan atachukua jukumu la
kuwatunza watoto na mke wa Omair.
Omair alikwenda Madinah akiwa tayari ameunoa upanga wake na kuuwekea sumu. Alipoingia
Msikitini, mahali alipokuwa amekaa Muhammad, Omar bin Al-Khattab na masahaba wengine
walimkamata na kumfunga kamba kwa sababu walihofia kuwa alikuwa akikusudia kufanya shari.
Muhammad alimuamuru Omar amfungue, na akamtaka Omair asogee karibu naye. Alipoulizwa
kwa nini alikuwa amekuja Madinah, Omair alijibu kuwa alikuwa amekuja kutaka mwanaye
aachiwe huru. Kisha Muhammad alimtaka aseme ukweli hasa, lakini Omair alikataa kufanya hivyo.
Kisha Muhammad alimwambia kuhusu makubaliano ya siri aliyoyafanya pamoja na Safwan ili aje
kumuua.
Omair aliposikia siri yake ikifichuliwa alitamalakiwa na mshangao na kuapa kuwa yeye na Safwan
ndio pekee waliokuwa wakiyajua makubaliano yale ya siri na kwamba kweli Muhammad ni Mtume
wa Mungu na kwamba Mungu ndiye aliyemfunulia ukweli huo. Alisilimu papo hapo na kukiri
kuwa Muhammad alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hapo Muhammad alitoa amri ya
kuachiwa huru mtoto wa Omair na kuwaagiza masahaba wake kumfundisha Omair Uislam na
Qur‟an.
Mwisho, maelezo gani anayoweza kuyatoa Margiliuth kuhusu ubashiri mbalimbali wa Muhammad?
Kuna idadi nzuri ya ubashiri huo, ambao nitautaja.
“Mwenyezi Mungu ataifungua Misri kwa ajili yenu”, aliwaambia masahaba wake.
“Watendeeni wema watu wake”
Miaka kumi baada ya kifo cha Muhammad, ubashiri huu ulitimizwa.
Wakati wa vita vya makundi (Ahzab) pindi Maquraishi na washirika wao walipokuwa
wameuzunguka mji wa Madinah kwa lengo la kumng‟oa Muhammad na ujumbe wake, Muhammad
aliwambia masahaba wake kuwa Makasri ya Fursi na Damascus yangefunguliwa kwa ajili yao,
jambo ambalo lilikuja kuwa kweli katika harakati za mapambano ya ufunguzi ya Waarabu.
Akiwa njiani kwenda Madinah, akiwakimbia maadui wake wa Makkah, Muhammad alimbashiria
Suraqa ----- aliyekuwa akimfuatilia ili kumuua----- kwamba angevaa joho la Kisra, mfalme wa
Fursi. Hili lilitokea pindi Iraq ilipovamiwa kama nilivyoeleza katika kesi ya nyuma.
Muhammad alibashiri kuwa Um Hiram, mke wa Ubada, angesafiri baharini katika kumtumikia
Mwenyezi Mungu. Hili lilitokea wakati wa utawala wa Uthman.
43
Mfano wa mwisho; alibashiri kuwa mmoja wapo wa masahaba wake angezikwa chini ya kuta za
mji wa Constantinople. Na hili lilimtokea Abu Ayyoub Al-Ansari pale jeshi la Kiislam
lilipokwenda kuutwaa mji huo.
Swali letu sasa: Nani aliewza kumpa Muhammad taarifa hizi, majasusi wake au ni ufunuo na
miujiza kutoka mbinguni?
Sasa akili huru na ihukumu!
44
KESI YA SABA
Kuenea kwa Uislam
“Alinihusisha na tuhuma na fitna zake” – Methali ya Kiarabu.
Uislam unaingia mahakamani; hakimu anamuashiria mwendesha mashtaka kutoa tuhuma na
mashtaka yake, naye anasimama na kuutuhumu Uislam kwa haya yafuatayo:-
Mwendesha Mashtaka: Mwanafikra msomi, mwenye akili, anayetafuta ukweli,
anawezaje kuamini kwamba Uislam unatangaza uhuru wa kufikiri na kuamini pamoja na kudai
kuwa unafuata hoja, ushahidi na ushawishi kama inavyotajwa katika Qur‟an:- “Hakuna kulazimisha
katika dini, hakika uongofu umekwisha pambanuka katika upotovu” (1),
na: “sema: ukweli umetoka
kwa mola wenu, basi anayependa akubali, na anayependa akatae” (2)
na: “lakini wakikataa, basi
hakika juu yako ni kufikisha tu ujumbe uliowazi” (3)
inawezekanaje hivyo wakati bado dini hiyo
inatumia njia ya upanga kuwashurutisha watu kuukubali?
“Mwislam ni lazima atangaze kuwashambulia wasio kuwa Waislam popote awakutapo, kwa sababu
kupigana na wasiokuwa waislam ni wajibu wa kidini” (4)
“Ni hakika kwamba Uislam haukufaulu ila baada ya malengo yake kuwa katika uvamizi” (5)
Muir na Caetani walidai kuwa “ongezeko la idadi ya wafuasi wa Uislam ilitokana na uvamizi wa
kijeshi na kuwashurutisha watu kuyakubali mafundisho ya Uislam” (6)
“Upanga wa Uislam uliwatisha watu wa Afrika na Asia mmoja baada ya mwingine” (7)
“Historia ya Uislam ilikua ni mfululizo wa kutisha wa umwagaji damu, vita na mauaji” (8)
“Mnamo karne ya Saba A.D. aliibuka adui mpya upande wa mashariki: adui huyo ni Uislam
uliojengwa juu ya misingi ya matumizi ya nguvu na ukaanzisha ushabiki mkali wa kidini.
Muhammad aliuweka upanga mikononi mwa wafuasi wake. Alikuwa mzembe wa utaratibu
mtakatifu wa maadili; aliwaruhusu wafuasi wake kufanya ufisadi na kupora na akawaahidi wale
waliokufa katika mapambano kuwa wangepata furaha ya milele” (9)
.
“Muhammad aliwaamuru wafuasi wake kuwashurutisha watu wote ulimwenguni waukubali Uislam
kwa nguvu ya upanga inapolazimika” (10)
.
“Wale waarabu waliwalazimisha watu kuifuata dini yao kwa nguvu na kuwataka watu wakubali
kuutii Uislam au la wauawe. Wakati ambapo wafuasi wa Kristo walizivuta nyoyo za watu kwa
uadilifu na subira” (11)
.
45
Uislam ulisikiliza tuhuma hizi na ukasimama kwa ushupavu na uthabiti ili kukanusha shutuma za
hawa Mustashriqiina, na kwa bahati mbaya baadhi ya tuhuma hizi hufundishwa katika shule za
awali za misheni katika ardhi za Waarabu ili wanafunzi wanaomaliza masomo yao wawe na chuki
kubwa dhidi ya Uislam.
Uislam: Mheshimiwa Hakimu! Muhammad alianza kazi yake mjini Makkah kwa kuwafikishia
ujumbe na mahubiri yake rafiki zake wa karibu: hivyo Abu Bakr, Uthman, Ibn Al-Awwam, Saad,
bin Awf, n.k. waliingia katika dini mpya. Wakati wa kipindi cha mwezi wa Hijja aliufikisha
Uislam kwa watu wa makabila mbali mbali waliokuja Makkah na akawalingania kufuata dini ya
Allah. Kundi la koo za Aus na Khazraj zilitekeleza ombi lake na kuukubali wito wake. Muhammad
alibaki Makkah akivumilia mateso na kuathiriwa na dhulma na jinai za Maquraishi. Aliondoka
kwenda Madinah bila kumwaga tone lolote la damu. Akiwa ameasisi dola ya Kiislam mjini
Madinah, Mtume alipambana na maadui wafuatao:-
1. Maquraishi wakazi wa Makkah
2. Wayahudi mjini Madinah na Khaibar
3. Warumi wa Byzantium na Waarabu wa Ghassan.
Kwa nini Muhammad na Waislam waliingia katika vita dhidi ya wote hao?
1. MAQURAISH:-
Muhammad alimaliza miaka 13 mjini Makkah ----- mahali alipozaliwa ----- akiwashawishi watu
kuingia katika Uislam kwa hoja, hekima na mawaidha mema. Maquraishi walitumia kila aina ya
jinai na mateso dhidi ya Waislam ambao Allah aliwasaidia kuwa na msimamo na kuvumilia mateso
kwa uthabiti: “Basi subiri kama walivyosubiri wale Mitume wenye ustahimilivu mkubwa
(kama Nabii Nuhu na Ibrahimu na Musa na Isa); wala usiwahimizie (adhabu)” (12)
.
Allah alimfunulia kisa cha “watu wa mahandaki” walioteswa kwa kuchomwa moto kwa ajili ya
Allah. Alimweleza hayo katika Sura Al-Buruuji. Allah alimweleza Muhammad habari za mitume
mbali mbali akiwemo Yunus (Yona). Alimtaka Muhammad asiwe kama Yunus ambaye
hakuvumilia: - “Akaondoka akiwa ni mwenye ghadhabu”. Hivyo Muhammad alivumilia sana
mateso na akawataka masahaba wake kufanya hivyo. Muhammad alihama au alikimbilia Madinah.
Mali zake binafsi na zile za Waislam zilipokonywa kwa dhulma, hivyo Waislam walidhulumiwa na
kufanyiwa jinai.
Akiwa Madinah, Muhammad alitangaza vita vya kiuchumi dhidi ya Maquraishi kwa ajili ya
kulipiza kisasi ili kuwashurutisha Maquraishi watambue haki miliki za Waislam zilizo mjini
Makkah pamoja na kuwa na uhuru wa kutangaza mahubiri yake.
Waislam walipanga kuushambulia msafara wa biashara wa Abu Sufian lakini msafara huo
ulifanikiwa kutoroka. Hata hivyo Maquraishi walikuja katika makundi makubwa na jeshi imara,
hata watumwa wao nao walijumuishwa katika jeshi hilo. Kwa hali hiyo Allah akampa Mtume
46
wake ruhusa ya kupigana:- “Imeruhusiwa kupigana kwa wale wanaopigwa, kwa sababu
wamedhulumiwa na kwa hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia. Ambao
wametolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema: Mola wetu ni Allah” (13)
Vile vile anasema:- “Na wapigeni vita katika njia ya Mwenyezi Mungu ambao wanakupigeni vita,
wala msivuke mipaka hakika Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka. Na wauweni popote
muwakutapo, na muwatoe popote walipowatoa, na shirki ni mbaya zaidi kuliko kuua. Wala
msipigane nao katika eneo la Msikiti Mtukufu mpaka wawapigeni ndani yake. Na ikiwa
watakupigeni basi nanyi pia wapigeni, kwani hayo ndiyo malipo ya makafiri. Watakapo koma, basi
waacheni hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwenye kurehemu.Na wapigeni mpaka
yasiwepo mateso, na dini iwe ni ya Mwenyezi Mungu peke yake, watakapokoma, basi usiweko
uadui ila kwa madhalimu” (14)
Katika Aya nyingine Allah anasema:- “Na mna nini ninyi hampigani katika njia ya Mwenyezi
Mungu na wale wanaoonewa katika wanaume na wanawake na watoto ambao husema: Mola
wetu; tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu na utujaalie msaidizi kutoka kwako” (15)
Tunaona kuwa mapigano yaliruhusiwa katika kujilinda tu na kwa lengo la kulinda heshima na mali.
Kinachotufanya kuona fakhari na kuukumbuka kwa moyo mkunjufu uwezo wa hali ya juu wa
Muhammad ambaye maisha yake yote yamejaa utukufu, kujiheshimu na uadilifu ni kwamba katika
Badri hakudhamiria kupigana au kumwaga damu, alilenga shambulio la kiuchumi ili kurudisha yale
yaliyochukuliwa na kuporwa na Maquraishi.
Katika Uhud Muhammad alishauri kubaki Madinah na kuyafukuza majeshi ya Maquraishi kwa
hasara ndogo kadri iwezekanavyo. Katika vita vya handaki au makabila yaliyoungana, Muhammad
alichagua mfumo wa kujilinda na kuwasambaratisha wahujumu hao kwa kupandikiza mbegu ya
ugomvi miongoni mwao ili pasiwepo na hasara ya majeruhi katika pande zote mbili.
Alipotaka kuifungua Makkah, baada ya Maquraishi kwenda kinyume na mkataba wa amani wa
Hudaibiah, alifunga na kuzizuia njia zote zielekeazo Makkah ili kurudi mahali alipozaliwa ambapo
hapo awali alikuwa amefukuzwa, na ili kutoa somo kwa Maquraishi waliokiuka mkataba wa amani
na kuwaudhi Waislamu pale walipoingia katika Uislam kwa ushawishi na hoja nzuri, na ili
kuwathibitishia watu wa Makka kuwa yeye hakuwa mtabiri au mshauri, au mwendawazimu kama
walivyomshutumu. Waarabu walimchukulia Muhammad kuwa mwenye busara na hekima na habari
zake kuwa za kweli na mahubiri yake kuwa ya uadilifu.
Muhammad alipanga kuingia Makka bila kumwaga damu, hivyo baada ya kukaribia Makka Abu
Sufian alikuja kufanya majadiliano. Mtume alimtaka Al-Abbas kumchukua Abu Sufian kwenda
kulitazama jeshi la Allah lililokuwa kwenye njia nyembamba ya mlimani.
Lengo lake lilikuwa ni kuwathibitishia watu wa Makka kwamba jeshi lake lilikuwa kubwa mno na
lisingeweza kuzuilika. Kisha aliwatangazia kuwa walikuwa salama kama wangeingia katika
nyumba ya Abu Sufian, au nyumba ya Hakimu Ibn Hizan, au Msikitini au wangejifungia
47
majumbani mwao. Abu Sufian aliwafanya watu wa Makka watambue kuwa kweli jeshi la
Muhammad lilikuwa na nguvu na uwezo zaidi ya jeshi lao wenyewe.
Muhammad aliwaagiza wanajeshi wake wasimpige yeyote isipokuwa yule atakayewashambulia.
Shughuli muhimu ya Muhammad haikuwa kumwaga damu ya Waarabu ambayo aliipenda,
japokuwa ilikuwa ni ya makafiri, kwa sababu Allah aliitukuza hadhi ya Waarabu ambao ndio
wangebeba jukumu la kuulingania Uislam.
Kwa ajili ya ukweli wa kihistoria Uislam unakubali kwa Waislam pekee kuishi katika Peninsula ya
Arabia ili kulinda makao yake ya mwanzo, kuulinda Uislam ndani ya ardhi yake ya asili. Wakristo
wa Nejran ndio jamii ya mwisho iliyofukuzwa kutoka Arabia baada ya kupewa dhamana ya
usalama wa desturi na imani zao (16)
. Baadaye Omar ibn Al-Khattab aliwafanya waondoke katika
ardhi hiyo baada ya kukiuka mkataba wa amani waliowekeana na Mtume na baada ya kuwa chanzo
cha tishio na hatari dhidi ya Arabia (17)
.
Hivyo, tunahitimisha kuwa Muhammad alikuwa sahihi alipopambana na Maquraishi kwa sababu
alifanya hivyo katika kujilinda dhidi ya maadui waliomfanyia uhasama, ambao walifanya harakati
za kuyaangamiza mahubiri yake na kuitupa misingi yote ya kibinadamu, walimfukuza yeye pamoja
na masahaba wake, na wakawapokonya mali zao.
Ni kwa mapambano tu dhidi yao kwamba aliikomboa Peninsula ya Arabia dhidi ya shirki na
upagani kwa gharama ya hasara ndogo kadri ilivyowezekana na ndani ya muda mfupi tu.
Kisha Uislam ukamuuliza Hakimu: Mheshimiwa Hakimu! Je ilitokea kwa hao wenye msimamo
wa kishabiki wakahesabu idadi ya vifo katika kipindi cha miaka ishirini na tatu ya mahubiri ya
Muhammad katika harakati zote? Walikuwa ni Waarabu 440 tu (18)
.
Ni harakati gani iliyoshuhudiwa na ulimwengu ambayo ilipata ushindi kama huo katika kipindi cha
muda kama huo na kwa gharama ya vifo vya watu wachache?
Mwisho kabisa, wasome maelezo ya kukiri ya Margiliuth kwamba mapambano ya Muhammad
dhidi ya Maqurishi kilikuwa kitendo sahihi na halali (19)
.
2. MAPAMBANO YA MUHAMMAD DHIDI YA WAYAHUDI:
Wakati wa kujadili masuala ya Wayahudi, baadhi ya Mustashriqiina husema:- “Muhammad
alijaribu kuonesha kuwa walikuwa wahalifu na wenye hatia ya kuvunja mikataba na makubaliano
yao” (20)
.
“Akawashurutisha Wayahudi kuyaacha makazi yao kwa njia mbaya” (21).
"Muhammad alitumia miaka sita baada ya Hijra katika kupora, kuvamia na kufanya wizi.
Kunyang’anya ngawira za watu wa Makka kulihalamishwa kwa sababu alikuwa wamepoteza mali
48
zake na alikuwa amefukuzwa kutoka mahali alipozaliwa. Vivyo hivyo alikuwa sahihi, iwe kweli au
la; kufanya kisasi dhidi ya makabila ya Mayahudi wa Madina, lakini watu wa Khaibar iliyokuwa
mbali na mji wa Madina hawakufanya kosa kubwa ambalo lingechukuliwa kama tishio la kweli au
jinai iliyotendwa na wote. Hili linaonesha shauku kali ya Muhammad ya kuanzisha kampeni
mfululizo za kijeshi kama zile za Alexander na Napoleon. Uvamizi wa Waislam dhidi ya Khaibar
unaonesha ni kwa kiasi gani Uislam unavyotishia dunia" (22)
.
Na sasa tunaendelea mbele katika kukanusha na kupinga hoja za hawa Mustashriqiina na hasa
Margiliuth aliyejifanya kumwachia huru Muhammad dhidi ya hatia inayohusu vita vyake dhidi ya
Maquraishi na Mayahudi wa Madina na hakumtetea kuhusu Khaibar ili aonekane ni mwenye busara
na muungwana lakini alishindwa katika jaribio lake hilo kwa sababu zifuatazo:-
Muhammad alikuwa sahihi alipowafukuza Mayahudi wa Bani Qaynuq‟aa baada ya vita vya Badri
kwa sababu walikula njama na kuufanyia shari Uislam kwa majivuno makubwa mno. Wanahistoria
wanatueleza kuwa Wayahudi hao walikuwa wakisema:- “Muhammad, usidanganyike kwa sababu
ulipambana na watu wasiojua kupigana ukawashinda”
“Ndio lililokuwa kabila la kwanza la Kiyahudi kuvunja mikataba yao na kwenda kinyume na
makubaliano ya amani” anaandika hivyo Ibn Al-Atheer. Kisha anasimulia tukio ambalo
walimvunjia heshima mwanamke wa Kiislam aliyekuwa sokoni mwao.
Vile vile Muhammad alikuwa na haki halali alipowafukuza Mayahudi wa Bani Al-Nadeer baada ya
vita vya Uhudi kwa sababu wakishirikiana na Maquraishi walikula njama ya kumuua.
Muhammad alikuwa sahihi kabisa kuhusu hukumu yake juu ya Bani Quraidhah baada ya vita vya
handaki kwa sababu walivunja makubaliano waliyokuwa wamewekeana naye, wakawasaidia
Maquraishi na kuwachochea kumpiga katika mazingira na kipindi kigumu alichokuwemo.
Dr. Hassan Ibrahim Hassan katika kitabu chake “History of Islam” baada ya kuelezea njama na
uadui wao dhidi ya Mtume (s.a.w.), anasema:- “Hata hivyo Mtume alikuwa mpole kwa Wayahudi
pindi walipokiuka mikataba waliyokubaliana naye au alipowashinda. Adhabu yake kwao ilikuwa ni
kwa kiasi cha kuwafanya waache kuwatendea ubaya Waislam. Hata aliweza kuwaacha wachague
hukumu ambayo ingetoa uamuzi. Kwa kifupi, Muhammad aliamiliana nao kwa upole na huruma
sana kuliko alivyoamiliana na Maquraishi”.
Wayahudi ---– watu waliochaguliwa na Mungu kama wapendavyo kujiita ----- walikataa kuona
ukabila wao ukitishwa na uthabiti wa Waarabu pamoja na kukusanyika jirani na Mtume, hivyo
walilazimika kulinda daraja yao kwa kummaliza Mtume na harakati yake. Walikuwa wakivunja
makubaliano yao katika nyakati tete na kushirikiana na maadui wa Uislam kuwatendea shari
Waislam.
Walijaribu mara mbili kumuua Mtume: mara ya kwanza walifanya hivyo kwa kumwekea sumu
kwenye nyama ya Kondoo na mara nyingine kwa kudondosha jiwe kutoka kwenye paa la nyumba
49
aliyokuwa amekaa. Hivyo, mapambano ya Muhammad dhidi ya Wayahudi wa Madina yalikuwa
halali na ya haki.
Kuhusiana na Khaibar, swali ni kama ifuatavyo:-
Kwanza kabisa tunashangazwa na msimamo wa Margiliuth na wengine wanaoiangalia historia
katika mtazamo aliouchukua yeye. Wanahistoria wanatueleza kwa ukweli kwamba pindi Waarabu
wa Kiquraishi waliposhindwa kumuangamiza Muhammad, Wayahudi waliwaunganisha upya na
kupanga njama za kuishambulia Madina ili kuwashtukiza Waislam. Mtume aliitambua nia yao ya
kuivamia Madina na kuumaliza Uislam ndani ya ngome yake, hivyo akafanya haraka na kwenda
kuwapiga katika mji wa Khaibar, makao yao, na ngome kuu ya mipango ya njama zao hizo (23)
.
Msimamo wa Wayahudi wa Khaibar na chuki yao dhidi ya Uislam ni kitu kilichokuwa kikijulikana
vyema, jambo linalokanusha uzushi wa Mustashriqiina wenye chuki au wasio waadilifu kama vile
Margiliuth na mfano wake.
Rekodi za kihistroria zinaeleza kuwa Ali alimkamata jasusi mmoja aliyekiri kuwa alikuwa akienda
Khaibar kuwataarifu watu wake kuwa Wayahudi wa Fadak walikuwa tayari kutuma nguvu ya ziada
kama wangepewa matunda ya Khaibar kama badala. Pia jasusi huyo akasema kuwa Wayahudi
wote wangeisaidia Khaibar katika kuwapiga Waislam. Margiliuth na wanahistoria wa mfano wake
wanatilia shaka ukweli wa hitosria kuhusu suala hili kwa sababu ukweli huu unazipinga shutuma
zake dhidi ya Muhammad na Waislam.
Katika historia kuna ushahidi kwamba kila uvamizi ulikuwa na sababu na uhalali wake ambao ni
udharura wa kujilinda, ambapo ingempelekea Muhammad kutoa adhabu kali lakini alikuwa mpole
kuliko ilivyotegemewa. Vile vile alikuwa akishughulishwa na akifanya jitihada ya kutekeleza
makubaliano, kutoa fidia kwa wale waliouliwa na Waislam kwa bahati mbaya na kumsamehe
mkosefu yeyote aliyeingia katika Uislam. Lakini Margiliuth anajifanya kiziwi dhidi ya ripoti hizo
sahihi za kihistoria. Kwa nini?
Kama Margiliuth anamshutumu Muhammad na Waislam kwamba waliivamia Khaibar kwa sababu
tu ya kutaka mali na ngawira, hapendi kuipima historia kwani akifanya hivyo basi atapata ukweli
kuwa hawakuwa na upendeleo wa kupata mali na kamwe hawakupigana vita kwa ajili yake.
Waliondoka Makka wakiacha mali na majumba yao yote, walikabiliana na aina zote za mateso na
taabu, maumivu ya kutengwa wakiwa katika bonde la Abu Talib. Halikadhalika ugumu wa kukaa
uhamishoni nchini Ethiopia na kuwa mbali na mji wa asili pale walipokimbilia Madina. Wenyeji
wao (Ansar) waliwapa hifadhi na wakashirikiana nao katika mali walizokuwa nazo:- “Na wale
waliofanya maskani yao Madina na kushika imani kabla ya hao, wanawapenda waliohamia kwao,
wala hawapati dhiki nyoyoni mwao kwa hayo waliyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao
ingawa wenyewe wana hali ndogo” (24)
50
Yote haya yanakanusha uongo wa Margiliuth. Kila mtu mwenye akili timamu anaweza kutambua
kuwa Waislam ambao walikabiliana na hizi anuai za mateso kwa uvumilivu kamwe hawakuwa
wakitazamia au kutamani matunda ya kidunia bali walifanya hivyo kwa itikadi na imani yao thabiti
tu. Yeyote aliyejaribu kuleta taabu dhidi ya imani hii alipata adhabu stahili kwa watu waliotaka
kuiangamiza dini ya Allah: Kukamatwa kwa mji wa Khaibari ilikuwa ni adhabu stahili kwa wale
waliokuwa na tamaa ya kuifuta dini ya Mwenyezi Mungu.
3. VITA DHIDI YA WAGHASSANI NA WATAWALA WAO WABYZANTINE:
Vita vya Mu‟ta mwaka 8 A.H. na Tabuk mwaka 9 A.H.
Mu‟ta: Mnamo mwaka wa 8 baada ya Hijra (25)
Muhammad alituma mjumbe kwenda kwa Al-
Harith Ibn Abi Shummar, mfalme wa Ghassan akimwita kwenye Uislam. Al-Harith alimuua
mjumbe huyo aliyeitwa Shuja‟a Ibn Wahb Al-Assadi. Wajumbe hawatakiwi kutendwa na
kuamiliana nao kwa njia hii inayokiuka kanuni na desturi za kimataifa. Wajumbe hawauawi kwa
yale wayatendayo na lolote wasemalo. Al-Harith alijibu: - “Nitakwenda kupambana na mtu huyo
anayetaka kukwapua mamlaka yangu” (26)
Lakini Mtume hakukusudia kutwaa ufalme wake, bali
alitaka tu kumuongoa na kumtaka awe Mwislam. Hivyo, jeshi lenye askari elfu tatu likiongozwa na
Zaid Ibn Harithah lilitumwa kama tu kipimo cha adhabu dhidi ya wale waliomuuwa mjumbe wa
Mtume. Makabiliano baina ya Waislam kwa upande mmoja na majeshi ya Waghassani na
Wabyzantium kwa upande wa pili yalitokea katika eneo liitwalo Mu‟ta. Matukio hayo ya kijeshi
sio jambo la muhimu kwetu bali tunapenda kusisitiza kuwa Waislam hawakupanga kupigana na
Waghassani pamoja na mabwana wao Wabyzantium ila baada ya wao kuwa wamejiandaa kutuma
jeshi kuwapiga Waislam katika mji wa Madina, ndipo Waislamu nao walipotuma jeshi hilo. Hivyo,
operesheni hiyo ya kijeshi ya Mu‟ta ilikuwa ni kipimo cha kujilinda.
Tabuk: ni mji mdogo uliopo baina ya Wadi Al-Qura na Syria.
Muhammad alipata taarifa kuwa Wabyzantium wa Kirumi waliyakusanya majeshi yao mpakani
mwa Palestina, pamoja na baadhi ya makabila ya Waarabu Wakristo ili kuwapiga Waislam.
Muhammad akapanga kuwavamia ndani ya maeneo yao. Akaelekea Tabuk mahali ambapo yeye na
Waislam walikaa kwa siku kadhaa. Watu wa eneo hilo walifanya naye makubaliano ya amani
baada ya Wabyzantium kuondoka na kuelekea upande wa kaskazini. Kisha akafanya makubaliano
ya amani na magavana wa Dawmat Al-Jandel na Ailah kisha akarudi Madina bila kumwaga damu
yoyote.
Hivyo, safari ya Tabuk ilikuwa imejengwa kwenye msingi mzuri na sababu ya kisheria. Kwa ufupi,
Muhammad alilazimika kuingia katika medani ya vita kwa lengo tu la kujilinda japokuwa amani
ndio iliyokuwa jiwe la msingi la sera yake: Lengo lake lilikuwa kustawisha maisha ya watu na
kuwatia adabu madhalimu wenye majivuno kwa gharama ndogo ya umwagikaji damu. Ustahmilivu
ulianisha hatua zake na ndio lililokuwa lengo lake. Alitupatia mfano bora na kutupa somo la namna
ambavyo vita vitukufu dhidi ya washirikina vinavyopaswa kuwa.
51
Jihadi Maana yake, Misingi, Maadili, Malengo na Faida zake:
Msheshimiwa Hakimu! Uislam umepandikiza maadili ya kujiheshimu sana ndani ya nyoyo za
waumini na kuyafanya kuwa wito wao: - “Na utukufu hasa ni wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake
na Waumini” (27)
. Watu walioonewa na kudhulumiwa nao wanapaswa kuwa na utukufu huu, vita ni
nyenzo ya kueneza moyo huu. Uislam umezigawa sifa hizi za ziada zifuatazo na kuunga mkono
aidolojia ya kimafundisho hii:-
(1). Dhamira ya muumini wa kweli inaambatana na Allah, mwenye mamlaka yote. Hivyo,
hamuogopi na hajisalimishi kwa yeyote asiyekuwa yeye Allah.
(2). Waislam wanaagizwa kuwa juu na kuzishinda aina zote za majivuno yatokanayo na matabaka,
au mazazi, au asili, au mali, au ushawishi wa madaraka, au rangi, au jamii ….. Uislam umeyafanya
mambo na matendo mema kwa maslahi ya mtu binafsi na kwa ustawi wa jamii nzima hapa duniani
na akhera kuwa ndio kigezo cha mtu kupata shukrani na hadhi ya juu:- “Na wote wana vyeo sawa
na yale waliyoyatenda” (28)
(3). Kanuni au sheria ya usawa katika haki.
(4). Uadilifu kamili ni sehemu muhimu ya jamii na serikali. Hivyo, Uislam hautofautishi na kutoa
upendeleo kwa ndugu, jamaa au hasimu, n.k.
(5). Kizuizi kimewekwa juu ya uhalifu dhidi ya roho za binadamu au maisha yao, mali, hadhi na
heshima yao, n.k.
Nguvu haimaanishi ukuu au dhulma au mamlaka juu ya wengine. Hata hivyo nguvu hizo ni nyenzo
ya kutekeleza malengo adhimu ambayo ni mahusiano yenye amani ya kimataifa.
“Na kama wakielekea kwenye amani nawe pia ielekee na mtegemee Allah” (29)
.
Nguvu ni ngao inayokinga na kuilinda imani. Nguvu hiyo vile vile huwawezesha Waislam kutetea
mafundisho na kudhibiti uhalifu na dhulma
Vita vitakatifu ni nini na ni yapi malengo yake?
Allah hajawaagiza waumini wa dini ya Kiislam kufanya vita vitakatifu kwa ajili ya kuwalazimisha
watu kuingia katika Uislam kwa sababu nguvu haijengi imani: - “Hakuna kulazimisha katika dini,
uongofu umekwisha pambanuka katika upotovu” (30)
. Kwa hiyo Uislam hautumii nguvu au
kulazimisha, wala haumshurutishi mtu kufuata dini anayoikataa au anayoichukia. Ndani ya sheria
na katiba ya Uislam kuna uhuru kwa mtu kuchagua dini. Kama Uislam ungetumia upanga au
kuwalazimisha watu waufuate kwa nguvu ------ kama wanavyozusha baadhi ya watu ----- basi
kusingekuwepo na vifungu vya kodi ya kichwa kwa wasio Waislam waliochini ya utawala wa
Kiislam au raia wasiokuwa Waislam walioishi katika dola ya Kiislam. Hawa wa mwisho (yaani
watu walioishi katika dola ya Kiislamu) ni wale wakazi waliokataa kuingia katika Uislam.
Walikuwa raia huru waliofurahia uhuru wa kutekeleza ibada na huduma zao za kidini huku imani
na utukufu wao vikiheshimiwa na watawala wa Kiislam. Kuwafanyia jinai ni haramu kwani
52
Muhammad (S.A.W.) amesema: - “Mwenye kumdhuru au kumsumbua kwa makusudi raia asiye
Mwislam huyo ni adui yangu” (31)
.
Hoja na ushahidi ndivyo vitu pekee vilivyo rahisisha ueneaji wa Uislam.
“Waite watu kwenye njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa
namna iliyo bora” (32)
.
“Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume, na kama mkikengeuka, basi ni juu yake huo
(mzigo) aliotwika; (kazi aliyopewa kufikisha ujumbe). Na juu yenu (huo mzigo) mliotwikwa ----
(kutii). Na mkimtii mtaongoka; hapana juu ya Mtume ila kufikisha (ujumbe wake) wazi wazi” (33)
.
“Basi kumbusha hakika wewe ni mkumbushaji tu, wewe si mwenye kuwatawalia” (34)
.
“Sisi tunajua wanayoyasema, wala wewe si jabari juu yao, kwa hiyo mkumbushe kwa Qur’an
anayeogopa onyo langu” (35)
.
Misingi ya kutangaza vita vitakatifu ni hii ifuatayo:-
(1). Kuondosha vikwazo vya uhuru wa kiakili, kulinda „shakhsia ya binadam‟ dhidi ya kuanguka
kwenye upuuzi, kuipa fursa ya kuonesha tabia na sifa zake njema na mwisho kuisafisha dhidi ya
uchafu wa ushirikina, maono ya uwongo, kuabudu vitu na unyonyaji wa jasho la wanyonge ili
kuinua neno la Allah ulimwenguni.
(2). Kuzuia dhulma, ukandamizaji, mateso na uhalifu ili kwamba imani, nchi, ndugu, mali, watoto,
n.k…. visipate kufisidiwa.
“Imeruhusiwa kupigana kwa wale wanaopigwa kwa sababu wamedhulumiwa” 36)
.
(3). Kutoa uhuru wa kuamini na kuabudu.
(4). Kutengeneza na kuandaa njia ya uongofu kwa ajili ya dini ya Allah, kwa idhini yake kwa
sababu ni aina ya mabadiliko ya kijamii yaliyojengwa kwenye msingi wa ukweli, wema, haki,
usawa, undugu na kumuabudu Allah pekee.
(5). Kuwasaidia wanyonge na wale waliodhulumiwa.
“Na kama wakiomba msaada kwenu katika dini, basi ni juu yenu kuwasaidia isipokuwa juu ya watu
ambao yapo mapatano kati yenu na wao na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda” (37)
.
Kusema kwamba Waislam walitumia upanga kuwalazimisha watu kuingia katika Uislam ni uzushi
ulioenezwa na kushadidiwa na Kanisa huko Ulaya. Hapa tunaweza kumnukuu mwanahistoria
53
mkubwa Toinby kuhusu jambo hili; mwisho wa makala haya kuna nukuu mbalimbali kutoka kwa
mabigwa waadilifu katika historia ya Kiislam:
“Kwa haki ni rahisi kukanusha shutuma zinazosisitiza na kupiga chuku matumizi ya nguvu na
kulazimisha katika kuenea kwa Uislam, hizi shutuma ambazo zimekuwa zikienezwa ndani ya
ulimwengu wa Kikristo, kwa sababu katika nchi za Fursi na Wabyzantium wa Kirumi chaguo
mbadala lililotolewa halikuwa kati ya kuingia katika Uislam na upanga bali mtu alipewa hiari ya
kuchagua baina ya Uislam na kulipa kodi ya kichwa, ni mkakati unaostahili sifa ambao baadae
ulionesha mwangaza pale ulipofanyiwa kazi huko Uingereza wakati wa utawala wa Malkia
Elizabeth” (38)
.
Inakuaje kwamba mkakati wa Uislam au kodi uonekane kuwa wa kuaibisha na wenye ukatili pale
unapotumika mashariki, wakati ambapo huko magharibi na hasa Uingereza, mpango wa mtu
kuchaua Ukristo au kulipa kodi ulionekana kuwa kitu kinachostahili sifa na sera ya kishereia? Je
huu si upendeleo na chuki?
Hata hivyo, nchi zenye Waislam wengi ni zile zilizoshuhudia uvamizi mdogo sana wa Kiislam.
Kwa maneno mengine mamilioni ya Waislam wanoishi Afrika na Asia ya kusini kamwe
hawakukabiliana na majeshi ya Kiislam, bali walikutana tu na wahubiri wa Kiislam ambao
waliwaita kwenye Uislam.
Mwanzoni mwa kudhihiri kwa Uislam kamwe Waislam hawakupigana isipokuwa pindi
walipojitetea na pindi walipowazuia watu wasiwafanyie jinai wale waliotaka kuingia katika Uislam (39)
.
Je, Al-Harith hakumuua mjumbe wa Muhammad?
Je, Wabyzantium hawakuwashawishi na kuwasaidia Waghassani na kuamua kuwavamia Waislam
katika eneo lao?
Je, Kisra hakutuma watu wampeleke Muhammad mbele yake awe mfu au hai kwa sababu ya
kutakiwa kuingia katika Uislam?
Waislam wa mwanzo hawakuhama au kuutambulisha Uislam kwa watu bali waliwahamisha watu
kuwapeleka kwenye Uislam. Matokeo ya mapambano au ushindi wa Kiislam havikupelekea
kuibuka kwa vinyongo na chuki za kudumu mataifa yaliyoshindwa dhidi ya wale waliowavamia.
Uislam ulikaa katika nyoyo zao baada ya kuridhika na kuamini. Utawala wa kisiasa na wa kijeshi
wa Kiislam ulipofikia tamati imani ya Uislam ilibaki moja kwa moja na kukita mizizi katika nyoyo
zao.
Harakati za mapambano ya Kiislam hazina mfano katika historia ya binadam, ni za kipekee na
hazina kifani.
54
Maadili na Sheria za Jihadi:-
Msingi wa kimaadili ambao harakati za mapambano ya Kiislam zilikuwa zinasimama juu yake
unakubaliana na kila msingi salama wa kila imani iliyo kamili. Kanuni hizo ni mfano wa kudumu
wa sheria za vita.
Mheshimiwa Hakimu! Vita katika Uislam vina kanuni kadhaa maalum ambazo Khalifa Abu Bakr
alizielezea kwa ufupi wakati akiliaga jeshi lililokuwa chini ya uongozi wa Usamah Ibn Zaid.
Alisema:-
“Enyi watu zingatieni maelekezo kumi yafuatayo……
1. Msifanye khiyana wala kudanganya.
2. Msidhuru au kukata viungo vya miili ya watu.
3. Msiwauwe watoto.
4. Msiuwe wanawake au wazee.
5. Msikate wala kuchoma moto mitende.
6. Msikate miti ya matunda.
7. Msichinje Kondoo au Ng‟ombe au Ngamia isipokuwa kwa ajili ya chakula
8. Mtapita sehemu ambayo watu watakuwa wamejifungia ndani, msiwadhuru.
9. Mtawafikia watu watakaokupeni sahani za aina mbali mbali za vyakula, kama mkila kidogo
kidogo basi na iwe kwa jina la Allah.
10. Mtakutana na watu walionyoa katikati ya mataji yao (juu ya vichwa) na kuacha nywele zao za
pembeni kama mistari (bands) wapigeni kwa panga zenu.
Jiandaeni kwa jina la Allah (S.W.).
Maelekezo mengine ya kimaadili yanayoonekana katika vita za Kiislam ni haya yafuatatyo:-
Ni marufuku kukatakata miili, kuchoma moto maiti, kuwanyima maadui chakula, na
kuwatesa mateka.
Maadili mengine: ni lazima kutoa tangazo la vita kabla ya mapigano kuanza kuepuka hila na
ulaghai. Vita viwe baada ya kushindikana kwa njia zote za ushawishi wa kuwalingania na kuwaita
watu katika Uislam, na imekatazwa kujigamba kwa ushindi au kugeuza ukweli: “Wala msiwe kama
wale waliotoka katika majumba yao kwa fahari na kujionyesha kwa watu” (40)
. Kuasisiwa kwa maadili haya ya vita kulikofanywa na Abu Bakr ni jambo lisilo na mfano.
Sheria ya sasa ya kimataifa imeyaidhinisha haya maadili. Umoja wa Mataifa umezifanya kanuni
hizi kuwa wito kwa kibinaadam, lakini kwa bahati mbaya zimebakia kwenye makaratasi, wakati
ambapo zilitoa mafundisho thabiti kwa wapiganaji wa mwanzo wa Kiislam.
55
Mheshimiwa Hakimu! Vipengele vya sheria na kanuni hii ni kama ifuatavyo (41)
:-
1. Itolewe taarifa ya tahadhari kwenda kwa nchi inayotangaziwa vita katika tarehe husika (42)
.
2. Sheria ya kimataifa inatamka kwa dhati kuwa raia wasio na silaha au wasiokuwa wapiganaji
hawahesabiwi kama askari, hivyo wasijeruhiwe. Neno „wapiganaji‟ linamaana ya askari katika
majeshi ya ulinzi.
3. Sheria ya kimataifa inapiga marufuku kuwamalizia maisha askari waliojeruhiwa, kuwatesa
maadui au kuwaumiza.
4. Sheria ya kimataifa imeelezea kanuni na taratibu kadhaa za kuamiliana vyema na mateka na
kutowadhuru.
Vita vitakatifu huanzishwa kwa ajili ya Allah, hivyo popote pale vinapotajwa, maneno "katika njia
ya Allah" hujumuishwa. "Yule ambae anapigana ili kufanya neno la Allah liwe juu, basi anapigana
katika njia ya Allah".
Kwa ufupi, Uislam ulipambana dhidi ya wafalme waliojifanya nusu-miungu, kama wale wa Fursi,
lakini mapambano hayo hayakufanyika dhidi ya watu wengine au raia. Waislam walipigana ili
kuwafikia watu, kuondosha vikwazo na vizuizi njiani sio kuwalazimisha watu kuingia katika
Uislam, bali kuangaza njia ya imani kwa kuuacha utashi wao kuwa huru, kwani Uislam una hakika
kuwa imani ni matokeo ya utashi huru.
Je, kwa hali hiyo kuzivamia tawala dhalimu zilizowafanyia dhulma watu wake na kuzuia uhuru wao
na kuwashurutisha kodi za kidhulma na mafundisho ya imani, je uvamizi wa aina hiyo ni
ukandamizaji? Akili salama itaona kuwa ni muhimu kuwaokowa watu hawa, hivyo Uislam uliingia
katika nchi ambazo watu wake walikuwa wamefanywa kuwa watumwa. Uliingia kwa lengo la
kuwainua kuelekea kwenye kiwango cha ubinadamu wa kweli. Waliipenda dini mpya na miongoni
mwao wakatokea magavana, majenerali, na wasomi walioitetea dini ya wanaharakati hao. Watu
walikula kiapo cha utii kwa Uislam baada ya kushangazwa na kupendezwa na tabia za kimaadili za
waambanaji wa Kiislamu, ambao walitoa mfano mwema na hivyo watu hao wakaingia katika dini
mpya bila kutumiwa nguvu au kushurutishwa au kuuawa.
Yule ambaye hatoshelezwi na maoni yetu, basi hapa kuna mbinu nyingine ya ushawishi wa utetezi:-
Maquraishi walipiga hatua ya kwanza kuwafanyia dhulma Waislam. Wabyzantium wakachukua
uamuzi wa kutumia upanga dhidi ya Waislam. Wafursi walitaka kumkamata Muhammad akiwa hai
au amekufa, na ndio waliokuwa nyuma ya mapinduzi ya ndani katika jamii ya umma wa Waarabu
kwa kuwapatia wahaini silaha na pesa baada ya kifo cha Muhammad (43)
.
Nani aliyeanza kushambulia? Nani aliyefuatia kupigana katika kujitetea?
56
Sasa ni muda wa kuangalia iwapo dini nyingine zilienea kwa imani na mafundisho yake. Je
shutuma hizi dhidi ya Uislam usiokuwa na hatia, haziwezi kutumika kwa dini nyingine? Au
walitushutumu kuhusika nazo ili wajiweke huru dhidi ya makosa hayo, ikiwa ni mojawapo ya njia
za msingi za kujitetea? yaani kuwashutumu wengine kwa kasoro ambazo nao wanazo, kama vile
muongo anayewashutumu wengine kwa uongo ili aonekane yeye kuwa mkweli.
Sasa Mheshimiwa Hakimu, nitaleta mbele yako maelezo ya namna dini nyingine zilivyoenea.
1. Aminhotab, Firaun wa Kimisri, aliwalazimisha raia wake kumuabudu Atun, Mungu wa jua.
Aliyafunga mahekalu ya miungu wengine, akaharibu hadhi zao, akaziondosha picha na
majina yao. Yeyote aliyekataa kutekeleza amri hiyo aliadhibiwa na kuteswa (44)
. 2. Azuka aliingia katika dini ya Buddha, akaieneza dini hiyo nje ya himaya yake mpaka
Ceylon, Burma na kusini mashariki mwa Asia (45)
. 3. Qubadh, mfalme wa Fursi alijiunga na dini ya Masdak, akajaribu kuwashurutisha raia wake
na Waarabu wa Iraq kuingia katika dini hiyo. Alipokufa dini yake ikaanguka (46)
. 4. Kuhusu dini ya Zoroaster: ilienea baada ya ujio wa utawala wa Darius, ambaye aliieneza
kwa nguvu ya Kijeshi karne moja baada ya kifo cha Zoroaster na baada ya kuipeleka Athens,
mji mkuu wa Ugiriki.
5. Dini ya Confucius haikuenea nchini China ila baada ya Confucius kushika madaraka ya
Uwaziri Mkuu katika jimbo la Loo.
6. Mwisho kabisa, Ukristo usingeweza kuenea lau kama si Constantine aliyetaka kuiongoza
hdini hiyo, na hivyo akatumia fursa ya migogoro ya ndani ya Kanisa kufikia azma yake hiyo,
ambapo mwaka 313 A.D. alitoa kile kinachojulikana kama sheria ya Milan na kuutambua
Ukristo na kuupa misaada tele.
Charlemagne, aliyekuwa na hamasa ya hali ya juu, aliamini kuwa ilikuwa ni wajibu kwake
kuwabadilisha jirani zake kwenda kwenye Ukristo. Hakuamini kuwa majadiliano yalitakiwa
kuwepo katika kuwaongoza watu badala yake akachangua njia ya matumizi ya nguvu (47)
. Kwa
kipindi cha miaka ishirini na tatu alipigana kikatili dhidi ya Wasaksoni mpaka akawashinda na
kuwabadilisha dini. Ilimchukua kampeni nane mfululizo za kivita kuwashinda Waafarini ambao
mali zao nyingi ziliporwa na Charlemagne (48)
.
Chanzo kingine kinadai kuwa Charlemgane aliwalazimisha wapagani Wasaksoni kuingia katika
Ukristo baada ya kupoteza udhibiti wao kutokana na vita vingi na wakasalimu amri kwenye ufalme
wa Frankish (49)
. Mtakatifu Liudger na Willehad walisaidia katika mchakato wa kuwaingiza watu
kwenye Ukristo.
(A.) Dr. Gustav Lebon katika kitabu chake “Civilization of the Arabs” anasema:-
“Misri ililazimishwa kuamini katika Ukristo, hali iliyowapelekea wakazi wake kuingia kwenye
uharibifu mkubwa, ambapo baadaye Waarabu walikuja na kuwaokoa na kuwatoa katika hali hiyo.
Kabla ya Waarabu kuingia nchini Misri mateso na ufukara vilishamiri kutokana na nchi hiyo kuwa
57
uwanja wa migogoro mingi ya kidini. Migogoro hiyo iliwapelekea Wamisiri kuuana wenyewe kwa
wenyewe na kukabiliwa na mateso yaliyosababishwa na watawala wa Byzantium. Wananchi hao
wa Misri walikuwa wakingojea kuokolewa kutokana na dhulma za Makaisari wa Byzantium” (50)
.
(B.) Nchini Denmark mfalme Cnut aliueneza Ukristo katika majimbo ya himaya yake kwa
kutumia nguvu na vitisho. Kisha aliwashurutisha watu hao dhaifu kuingia katika dini ya Kikristo
baada ya kuwapiga kikatili Wabarbaria, akiongozwa na msukumo wake wa kuieneza dini hiyo (51)
.
(C.) Nchini Urusi kazi ya umisionari wa Kikristo ilienezwa na kundi la watu walioitwa “ndugu
wa upanga”, angalia tukta hiyo kwa makini, Mheshimiwa Hakimu! Kwa mujibu wa kitabu kingine
tunasoma kuwa: “kuhusu namna Ukristo ulivyopokelewa nchini Urusi suala hilo lilikuwa mikononi
mwa Vladimier Dukke wa Kiev (985 – 1015) mtoto wa Rurck. Alikuwa mfano kamili wa ushenzi
na asiyekuwa na mfano katika matamanio ya uasherati. Alirithi kiti cha miliki ya Duke baada ya
kumuua ndugu yake wa mwisho. Alikuwa na wanawake elfu tatu na mia tano (52)
. Pamoja na
maovu yake hayo Kanisa la Orthodox wa Byzantium lilimuona kuwa alikuwa mtu mtakatifu kwa
sababu yeye ndiye aliyeifanya Kiev na Warusi kuwa Wakristo. Aliwalazimisha watu wa milki ya
Duke ya Urusi wabatizwe katika mto Denieber (53)
.
(D.) Majemedari wa Ordo Fratrum Militiae Christ waliwalazimisha watu wa Levonia kujiunga
na Ukristo kwa nguvu (54)
.
Thomas Arnold anasema kuhusu eneo hili: - “Mateso na kushurutishwa kubadili dini kulichukuwa
mahali pa wito wa utulivu ili kuwafanya watu waliamini neno la Mungu” (55)
(E.) Nchini Norway Mfalme Olaf Trigfisan aliwachinja wale wote waliokataa kuwa Wakristo;
aliikata miguu na mikono ya watu wengine na kuwaweka wengine kizuizini.
Hivi ndivyo alivyousambaza Ukristo katika Viken yote, Norway ya Kusini.
(F.) Qadri Al-Qalaji anaandika katika kitabu chake Saladin Ayyoubi kinachojulikana pia kama
kisa cha mapambano baina ya Mashariki na Magharibi katika karne za 11 na 12:
“Basilius II aliyanyofoa macho ya mateka elfu kumi na tano wa Kibulgaria, isipokuwa watu mia
moja na hamsini ambao miongoni mwao alimuachia kila mmoja jicho moja ili awaongoze wengine
wakati wa safari ya kurudi nchini mwao.Huyu Basilius ndiye aliyeueneza Ukristo nchini Urusi”.
(G.) Dkt. Ashur akiwa amezungumzia mateso yaliyohusishwa sana na kazi ya kuueneza Ukristo
iliyofanywa na Charlemagne pamoja na mauaji ya kutisha aliyoyafanya dhidi ya maksoni na
Wanormandi, anafafanua mauaji yaliyofanywa na askari wa Tuton pamoja na askari wa taasisi ya
upanga wakati wakisonga mbele katika kueneza ukristo miongoni mwa Waprussia, Walithuania
na Waslav wengine katika kipindi cha karne ya 13 na 14. Kisha Dkt. Ashur anatoa vielelezo vya
kile walichokifanya wamisionari hao katika karne ya 17 nchini India wakati walipokuwa
wakiueneza Ukristo kwa namna ya ukatili (56)
.
58
(H.) Tahakiki na tafiti mbalimbali za kijiografia zilizofanywa na wazungu hazikufanywa kwa
sababu ya wao kuupenda ustaarabu, kwa mfano:-“Livingstone alitaka kuchunguza njia kwa ajili ya
safari za Wamisionari wala si kwa ajili ya kuupenda ustaarabu na maarifa” (57)
. Alipofikwa na
mauti akiwa Afrika wenzake waliuzika moyo wake chini ya mti aliofia, lakini mwili wake
ukazikwa huko Westminister Abbey, mjini London.
Wamisionari walioambatana na tafiti za kijiografia walitenda matendo machafu ambayo hayana
manufaa kwa binadamu.
Vasco da Gama aliyegundua njia ya kuelekea India alikuwa Mmisionari. Wachunguzi wa Kikristo
waliwafanyia nini wakazi asili wa Amerika, yaani Wahindi wekundu? Waliwaangamiza kabisa. Ni
maangamizi kama yale yaliukumba ustaarabu wa Antilles na Mayas kusini mwa Mexico, ustaarabu
wa Aztik katikati mwa Mexico na ule Anka huko
Peru (58)
.
Hapa kuna nukuu kutoka katika gazeti la kila siku la Beirut liitwalo “Al-Hayat” ikielezea ugunduzi
wa kisiwa cha Haiti kulikofanywa na Wahispania.
Mwanzo maofisa na wapambe wa kiongozi wa kampeni hiyo walishughulishwa na kuichunguza na
kuitwaa kwa nguvu Haiti (Hispaniola). Bado kulikuwa na eneo kubwa lililokuwa halijagunduliwa.
Diego Vlasquiza na Banfilo Dunarvis walichukua jukumu la kufanya kazi hiyo. Walifanya
unyama usiomithilika kama vile kuzikata ncha za vidole vya wakazi asilia wa eneo hilo na
kuyanyofoa macho yao, kuwamwagia mafuta yaliyochemshwa na risasi iliyoyeyuka kwenye
majeraha yao, au kuwachoma moto wakiwa hai kwa lengo la kutaka wawajulishe mahali dhahabu
ilipofichwa au kuwalazimisha kuingia katika dini yao (59)
.
Padri mmoja alijaribu kumshawishi Chifu Hanihey, aliyekuwa amefungiwa katika eneo la
kuchomea watu moto, kwamba ajiunge na Ukristo na akamwambia kuwa kama angebatizwa
angeingia peponi. Chifu huyo wa Kihindi alimuuliza: - “Je kuna Wahispania huko peponi?” Padri
huyo akajibu: - “Ndiyo, bila shaka wanamuabudu Mungu wa kweli”. Chifu wa Kihindi akajibu kwa
ukali: - “Basi kama ni hivyo sitaki kwenda mahali ninapoweza kukutana na watu waliolifanyia
ukatili taifa hili” (60)
.
Jarida la Cuba international Joulio 1972 chini ya kichwa cha habari „La Histoir‟ Uk. 6 lilikuwa na
picha ya mmisionari mmoja akiwa ameshika msalaba pamoja na picha ya chifu mmoja aliyefungwa
kwenye mlingoti na kufunikwa na majani makavu na magogo mengi yaliyomfika kiunoni akisubiri
kuchomwa moto. Mmisionari huyo alikuwa akiunyanyua msalaba mpaka kwenye uso wa chifu
huyo akimtaka kuingia katika dini yake kabla ya kukata roho.
(I.) Wapiganaji wa vita vya msalaba, ambao nembo yao ilikuwa msalaba, walishuhudia mauaji
yasiyokuwa na idadi. Wanamsalaba hao walitenda mauaji ya kinyama na ya kikatili mno kila
mahali walipopita.
59
Dk. A. S. Ashur katika kitabu chake adhimu kiitwacho “The Crusade Movement” anaandika
yafuatayo kwenye uk.294 sehemu 1:
“Pindi watu wa Caesarea walipokimbilia katika msikiti wa mjini wapiganaji wa vita vya msalaba
waliwafuatilia huko na kuwachinja wote wanaume, wanawake na watoto na msikiti ulikuwa kama
bwawa kubwa lililojaa damu ya Waislam”.
Mauaji ya Jesursalem, mwaka 1099, yalikuwa doa la aibu na fedheha kwa kampeni ya vita vya
msalaba kwa mujibu wa wanahistoria wa Kimagharibi (61)
.
Baldwin aliuchoma moto msikiti mkubwa wa Alfarma pamoja na misikiti mingine ya kawaida
katika mji huo.
Lebon anasema: - “Waislamu elfu kumi walichinjwa katika msikiti wa Omar pekee” (62)
.
Tunamnukuu Ibn Al-Adim: - “Katika kampeni hiyo askari wa vita vya msalaba walifanya mauaji
mengi: walifukua makaburi ya Waislam, wakayachukua majeneza na kuyapeleka kwenye hema zao
na kuyatumia kama viwekeo (Containers) vya vyakula vyao, wakaiba sanda, wakazifunga kwa
kamba maiti mpya zilizokuwa zimezikwa na kuziburuta mbele ya macho ya Waislam na kuwapigia
kelele watazamaji wakisema:- “Huyu ni Mtume wenu Muhammad, huyu ni jamaa yenu”.
Walitwaa nakala ya Qur‟an kutoka eneo moja takatifu la kitongoji cha Aleppo na kuita kwa sauti:-
“Enyi Waislam tazameni kitabu chenu kitakatifu”
Viongozi husika wa kampeni hizo na hususan Louis VII, mke wake Eleanor na Raymond de Poitie
walifanya kashfa na uovu wa aibu za kingono. Kwa ufupi, wanahistoria wa kimagharibi
walizielezea kampeni zote hizo kuwa ni ushenzi na ukatili. Hatupaswi kushangazwa na maelezo
haya kwani kampeni hizo za vita vya msalaba zilikuwa kurasa nyeusi katika historia ya Ulaya yote.
Je, mapadri hawakuweka chupa za mvinyo juu ya Mwamba mtakatifu? Je, hawakupiga kengele za
Kanisa katika Msikiti wa Aqsa baada ya kuondosha adhana ya Waislam kutoka katika minara ya
msikiti huo? Je imani na mahekalu yanaheshimiwa katika namna hiyo? Angalia maelekezo ya Abu
Bakr aliyoyatoa kwa wapiganaji wa Kiislam ambayo, pamoja na mambo mengine, yalijumuisha
“kuwaacha mapadri washughulike na kuendesha ibada zao katika makao yao kwa amani”.
Akiwa amezungumzia vitendo vya fedheha vilivyofanywa na mahakama za Kanisa nchini Hispania,
Dkt. Lubon katika ukurasa wa 270 na 271 wa kitabu chake kiitwacho Civilization of the Arabs,
anasema: “Padri Bleeda alifurahi sana alipowachinja wahamiaji laki moja katika msafara wa
wakimbizi wa kiislamu laki moja na elfu arobaini waliokuwa wakielekea Afrika”.
Kisha Bwana Lubon anataja hasara waliyoipata Waislam baada ya watu milioni tatu kuchinjwa,
kuchomwa moto na kufukuzwa. Kisha katika ukurasa wa 272 anasema:- “Hatuwezi kusaidia
60
kukubali kwamba katika wavamizi wakatili wa Kihispania hatukumkuta yeyote wa kumlaumu kwa
vitendo vya mauaji ya sawa na yale yaliyotendwa dhidi ya Waislam”.
(J.) Mwisho kabisa, kujadili historia ya Kanisa la Kikristo juu ya maelezo ya uhalifu huu itahitaji
majuzuu kadhaa ya vitabu, kwa hiyo inatosha tu kukinukuu kitabu cha “Missionaries and
Colonialism”, uk. 7, ambacho kinasema: “Kampeni na harakati hizi za Wamissionari zilikuwa na
madhara makubwa kwa nchi zetu kuliko hata ukoloni (ubeberu) wenyewe, kwa sababu ukoloni
ulipenya na kuingia katika nchi zetu kupitia nyuma ya pazia la kazi ya kimissionari, kusudio lenye
hatia ambalo mzigo wake unaapswa kubebwa na ubeberu wa kisasa kwa sababu ya taabu na jinai
zake zote za kihalifu”.
Mheshimiwa Hakimu! Ama kuhusu kuenea kwa Uislam, nitakupa ushahidi kutoka kwa
mwanahistoria mwadilifu wa kimagharibi ili kuthibitisha kuwa kamwe Uislam haujatumia au
kuzijua njia zilizotajwa hapo juu zilizopata kutumiwa na dini nyingine kama vile umwagaji damu,
ukatili, unyama, kuwalazimisha na kuwashurutisha watu kuzikubali dini hizo. Ushahidi huu wa haki
ulipatikana katika kitabu cha Sir Thomas Arnold kiitwacho “The Call to Islam” ambapo anajadili
juu ya ueneaji wa Uislam ulimwenguni. Sasa tusome aliyoyaandika:-
1. Maeneo ya Syria:-
Mabedui wa Kikristo waliitwa kwenye Uislam kwa njia ya uvumilivu. “Kwa nini watu waliingia
katika Uislam? Kwa sababu Omar aliweka katika kila mji watu wasomi ili kuwafundisha watu
Qur’an na kanuni za falsafa ya sheria”.
Nukuu nyingine kutoka katika kitabu hiki ni hii ifuatayo: - “Makabila ya Wakristo wa Kiaarbu
yaliyoingia katika Uislam yalifanya hivyo kwa moyo mmoja na utashi huru, na Wakristo wa
Kiarabu waishio katikati ya jamii za Kiislam leo hii wanathibitisha ustahimilivu huu”. Akili ya
kiovu ndiyo itakayopinga kile kilichotokea Syria, lakini matukio hayo ni mashada ya heshima juu
ya kichwa cha binadamu milele na milele na vilevile ni mwiba machoni mwa wabaguzi, wenye inda
na chuki kubwa dhidi ya Uislam.
Je umewahi kusikia kuhusu wakazi wa mji kama ule wa Homs, ambao walihuzunika na kulia baada
ya Waislam kuondoka baada ya kuwaokoa. Walikwenda kwa Abu Ubaidah, Amir Ibn Al-Jarrah ---
- pindi Waislam walipoamua kuondoka Homs na kuelekea upande wa kusini- wakalia huku
wakimwambia kamanda wa Kiislam: “Enyi Waislam, tunawapenda nyinyi zaidi kuliko
Wabyzantium japokuwa ni Wakristo kama sisi. Nyinyi ni waaminifu zaidi, wenye huruma sana,
wema, waadilfu na viongozi bora, lakini wao ---- Wabyazantium ---–walitutawala kimabavu sisi
pamoja na ardhi zetu (63)
. Kisha waliifunga milango ya mji wao dhidi ya majeshi ya Heraclius.
Je, watu hao walijiwasilisha au kujisalimisha kwa wakombozi wa Kiislam kwa nguvu ya upanga na
udhalilishaji, au walikinaishwa na kuridhika na hoja walizopewa?
Punde tu kabla ya kuanza kwa vita vya Yarmuk, Georigat mtoto wa Theodore alimuuliza Khalid: -
61
“Ni ipi hali (darja) ya wale wanaoikubali na kufuata dini yako sasa hivi?”
Khalid akajibu:-
“Hali yao ni sawa na hali yetu kuhusu kuwajibika kwetu kwa Allah, wale wa tabaka la juu ni sawa
na wale wa tabaka la chini, na wa kale ni sawa na wapya”.
Hii inaashiria kuwa lengo la vita hivi ni kuwafikia watu. Hivyo, watu wa Homs walipoona kuwa
makao yao yalikuwa yamechakaa, na mavazi yao yalikuwa yamechoka na wakalitazama jengo kuu
la Uislam na mavazi yake masafi, kwa thamani na kwa upendo adhim wakaipendelea dini hiyo
bora.
Mheshimiwa Hakimu! Ninakusihi kwa dhati ufikirie. Baada ya kuusoma waraka wa agano la
Omar kwa watu wa Syria, Je itakuwa sahihi kusema kuwa watu hao walilazimishwa kuukubali
Uislam? “Katika waraka huu, Omar mja wa Allah na kiongozi wa Waumini, anatoa ulinzi kwa watu
wa Ikya (Jerusalem): Maisha yao, mali, makanisa na misalaba yao, mgonjwa na mzima bila
ubaguzi kwa wafuasi wote wa imani yao, kamwe hakuna atakayebomoa au kuishi katika makanisa
yao, watalindwa dhidi ya hasara ya vitu hivi au mali yao yoyote, hawalazimishwi kuiacha dini yao
au kudhuriwa”.
Dalili nyingine inayothibitisha kuwa watu wa Syria waliukubali Uislam au maelezo ya kwamba
walamini na kusadikisha kwa utashi wao wenyewe ni vijitabu vilivyoandikwa na John the
Damascen. Aliishi katika zama za harakati hizi za ukombozi na vijitabu vyake vyote
vinazungumzia au kushughulikia midahalo mbali mbali baina ya Ukristo na Uislam. Hili
linakanusha uzushi kwamba Uislam ulienezwa kwa upanga au kulazimishana (64)
. Vijitabu hivi
viliandikwa katika mfumo wa majadiliano kama vile: - “Kama Mwarabu akikuuliza…” au “Kama
Mwarabu akikwambia ….. jibu …….”
Mwanafunzi wa Mt. John, Askofu Theodore Abu Qurrah, naye pia aliandika mijadala kadhaa
baina ya hizi dini mbili. Mijadala hii ilidumu mpaka wakati wa Ukhalifa wa Harun Al-Rashid
ambaye alihudhuria mijadala na mashindano haya ya hoja yaliyowashirikisha pia Timathaus na
Kadinali Tusuf wa Merv (Khurasan, Iran).
Je, kwa msingi huu Uislam uliingia Syria kwa msaada wa upanga na kwa nguvu, au baada ya
mjadala na mdahalo uliofanyika kwa ustahamilivu kamili uliopelekea watu kuusadiki, kuuamini na
kuutii uislam?
Ninakusihi, Mheshimiwa Hakimu, utoe uamuzi wako kwa busara.
Ama kuhusu kuenea kwa Uislam barani Afrika tutafakari kwa pamoja jinsi wakazi wa Misiri
walivyoishi kwa mujibu wa vyanzo vya nje (yaani vitabu vilivyoandikwa na wasiokuwa Waarabu),
ili kuzuia tuhuma na shaka zozote zinazoweza kuibuliwa kuhusu Wanahistoria wa Kiarabu. Hapa
kuna nukuu chache kutoka katika kitabu cha Thomas Arnold kiitwacho “Call to Islam”:- “Wakaazi
62
wa Misri waliteswa na kutupwa katika maji”. Katika uk. 123 wa sura ya 4 anaandika chini ya
kichwa cha habari “Harakati za ukombozi wa Waarabu nchini Misri na ukaribisho wa Wakhufti
kwa waliowaokoa dhidi ya utawala wa Byzantine”, anaandika yafuatayo: “Mafanikio ya haraka
ambayo wanajeshi wa Kiarabu waliyapata, kwanza kabisa, yalitokana na mapokezi yenye ukunjufu
kutoka kwa Wakristo waliouchukia utawala wa Wabyzantium pamoja na mateso yao na utawala
wao wa kidhalimu na kisha kutokana na Waarabu hao kutowatendea ubaya wanathiolojia”.
Je, Uislam uliwapa nini ili kubadili hali zao?
1. Uislam uliwafanya waondokane na kodi kubwa za ukandamizaji na kuwafanya walipe moja ya
kumi tu ya kodi hizo.
2. Uliwapa uhuru kamili wa kidini. Arnold anakubali kwamba ukombozi wa Kiislam uliwapa
Wakhufti (yaani Wamisri) uhuru wa kuamini ambao hawakuwa wameupata hapo kabla (65)
.
Vilevile, anakubali kuwa Amr Ibn Al-As aliwapa uhuru wa kufanya ibada na sherehe zao za kidini;
aliwaondoshea uingiliaji uliokuwa ukifanywa na Wabyzuntium kwenye mambo yao, kamwe
hakufanya aina yoyote ya utekaji au uporaji, wala hakunyang‟anya mali au milki zozote za
makanisa.
“Hakuna dalili ya ushahidi kwamba waliacha dini yao na kujiunga na Uislam kutokana na kuteswa
au “kushuritishwa’ kulikotokana na upande wa watawala wapya kukosa uvumilivu” (66)
“Wakhufti (Wamisri) wengi waliingia katika Uislam kabla ya ukombozi huo kufikia kikomo” (67)
Kwa sababu hiyo, Mheshimiwa Hakimu! Nani anayediriki kusema kuwa watu wa Kaskazini mwa
Afrika waliingia katika Uislam kwa njiya ya upanga?
2. Hispania:-
Helffererich katika ukurasa wa 82 anasema: - “Kamwe hatukuwahi kusikia kuhusu kuwashurutisha
watu kuingia katika Uislam au kuwatesa katika kipindi cha mwanzoni mwa harakati hizi za
Waislamu. Lililo hakika ni kwamba sera ya kuvumiliana kidini iliyotekelezwa na wanaharakati hao
kwa Wakristo ilikuwa na athari kubwa sana katika maandalizi ya kuikomboa nchi hii (Hispania)”.
Naye Dozy anataja uvumilivu wa Waarabu nchini Hispania na kusisitiza juu ya wema wa
wakombozi hao na kodi ndogo iliyotolewa na watu, ambayo ilikuwa ni sehemu ndogo kuliko zile
zilizotolewa kabla ya Waarabu hao (68)
.
John wa Gorz, shahidi aliyetembelea Hispania katikati mwa karne ya 10 anasema: - “Wakristo
walifurahia kuabudu katika maeneo yao mtakatifu na kuzifanyia mali zoa kile walichotaka kwa
uhuru katika kipindi cha ukombozi wa Uislam”.
63
Mwanahistoria mwingine anasema: - “Waislam hawakuwaingilia Wakristo wakati walipokuwa
wakitekeleza sherehe na taratibu zao za kidini” (69)
.
Baudissin katika ukurusa wa 11 – 13, 196 aliandika: - “Walishitakiwa katika mahakama zao
wenyewe kwa mujibu wa sheria za nchi yao”
“Utawala wa Waarabu nchini Hispania ulijiainishwa kwa busara; watu hawakulazimishwa kuingia
katika Uislam na walilipa kodi ya kichwa pekee. Wahispania katika zama za utawala wa Waarabu
waliishi katika maisha ya ustawi na raha” (70)
.
Ni jambo linalochosha sana kunukuu rejea nyingine. Hivyo, nitataja tu nukuu kutoka katika kitabu
cha „Call to Islam‟ Uk. 164: “Athari ya Uislam kwa Wahispania ilikuwa kubwa sana kwa ustaarabu
wake bora; vilevile Uislam ulivivuta na kuvikaribisha vipaji na ushairi, falsafa na sanaa yao
ambayo ilivichangamsha vipaji vyao na kuunganisha ubunifu wao”
Pindi Waarabu walipotoka Hispania mnamo tarehe 2 Januari 1492, “wakazi hao maskini bado
walikuwa wakifuata dini ya wahenga wao, japokuwa kwa zaidi ya karne moja walilazimishwa
kuonesha imani yao katika Ukristo” (71)
. Baadaye Waarabu hao walielekea Morocco katika safari
kwa ajili ya dini yao.
Je, Hispania iliingia katika Uislam kwa kulazimishwa na kwa upanga?
3. Ulaya ya Mashariki:-
Wakiwa wameiteka Constantinople mwaka 1453, Waothoman walipenya kuelekea Mashariki mwa
Ulaya. Je, Uislam uliingia katika nchi za Balkan, Yugoslavia na Albania kwa kutumia kitisho cha
upanga?
Tuangalie kile alichokifanya mtekaji wa Constantinople punde tu baada ya mji huo kuangukia
mikononi mwake. Alichokieleza Thomas Arnold kitatosha: - “Mojawapo ya kazi za mwanzo
ambazo Muhammad II, aliyeivamia Constantinople, alizotekeleza baada ya mji huo kuangukia
mikononi mwake na kuweka udhibiti wake, ilikuwa ni kulinda kiapo cha utii cha kuwatumikia
Wakristo kwa kujitangaza yeye mwenyewe kuwa mlinzi wa kanisa la Ugiriki. Alipiga marufuku
kabisa ukandamizaji dhidi ya Wakristo, na akampa askofu mkuu mpya sheria inayompa yeye na
walio chini yake haki ya kufurahia heshima waliokuwa nayo, mapato na misaada mbalimbali.
Gannadius, Askofu mkuu wa kwanza baada ya utekaji wa Waturuki alipokea fimbo ya uaskofu
kutoka mkononi mwa Sultan, fimbo ambayo ilikuwa ndio nembo ya ofisi yake, pamoja na mkoba wa
pesa uliojaa sarafu elfu moja za dhahabu” (72)
.
“Watekaji hawakuingilia masuala ya kanisa, lakini uongozi wa Kiraia wa ufalme wa Byzantium
ulikuwa umefanya hivyo” (73)
.
64
“Watu waliruhusiwa kutekeleza sherehe zao za kidini kwa mujibu wa taratibu zao za kitaifa” (74)
.
“Wanaharakati wa Kiislamu walipewa mapokezi ya bashasha kutoka kwa Wagiriki katika maeneo
mengi ya himaya ya Byzantium kwa sababu watekaji hao walichukuliwa kuwa wasaidizi na
wakombozi wao dhidi ya utawala wa kidhalimu na kionevu wa Wafrank na Wavenetia uliokuwa
umewaweka raia hao katika hali mbaya sana ya utumwa” (75)
.
Ni kweli harakati hizi za ukombozi zililenga kuwakomboa dhidi ya utumwa. Wanahistoria wengi
wamefafanua hali iliyokuwapo katika taifa la Byzantine kabla ya uvamizi na utekaji huo. Hapa
kuna nukuu moja: - “Taifa lolote lisiloheshimu sheria zake ni sawa na farasi jike bila hatamu.
Constatine na warithi wake waliruhusu watu maarufu wa ufalme huo kuongoza kama madikteta,
mahakama zao hazikuwa na uadilifu, nyoyo zao zilikosa huruma au ushupavu; Mahakimu
walijipatia mali nyingi kutokana na machozi na damu ya watu wasiokuwa na hatia” (76)
.
Hata hivyo, wanaharakati hao waliibadilisha hali na “kwa msaada wa uongozi wao makini na
madhubuti waliweza kueneza amani na nidhamu kwenye majimbo yote. Mambo ya kiraia na
kisheria yakapangiliwa kwa njia bora kabisa” (77)
.
“Waislamu wa Kituruki hawakumlazimisha yeyote kuiacha dini yake” (78)
. “Waturuki waliamini
kuwa kitu bora wanachoweza kumpa mtu ni kumuongoza kwenye Uislam” (79)
.
Arnold anasema: - “Kwa busara hii hawakuacha kutumia njia yoyote yyenye kuvutia na
kushawishi” (80)
.
Kwenye ukurasa wa 186 Arnold anasema: - “Wakazi hao waliyakubali mafundisho na maagizo ya
Uislam kwa ukarimu wa mapokezi, mafundisho ambayo yalikuwa yenye kueleweka na yaliyo
kwenye msingi wa umoja wa Mwenyezi Mungu” (81)
.
Tumesikia kuwa makundi makubwa ya watu, ambao hawakuwa wa hali ya kawaida, bali kutoka
katika matabaka ya watu wa hali ya juu na wasomi, waliingia katika Uislam (82)
.
Kwa nini watu hawa walibadili dini yao na kuuchagua Uislam? Wakati huo Uislam uligeuka
kuwa hifadhi ya kudumu kwa Wakristo waliokuwa waumini wa Kanisa la Mashariki (83)
. Hilo
lilikuwa jambo la kiasili na la kimaumbile kwa sababu ya migogoro ya ndani ya kanisa
iliyosababishwa na muamala mbaya wenye mkali usiokuwa na huruma walioupata kutokana na
misingi ya uasi wa Kanisa punde tu kabla ya ufunguzi wa Kiislam.
Ninakusihi, Mheshimiwa Hakimu mwenye busara! Tupatie uamuzi. Je Uislam ulipenya kwenda
Ulaya ya mashariki kwa nguvu?
65
Inafaa kueleza kuwa pindi vita vilipozuka kati ya Waturuki na Wahungari George Brankovich
alimuuliza John Hidai angefanya kitu gani kama angeshinda, alijibu kwamba angeanzisha imani ya
Roman Catholic; kisha akamuuliza Sultan kuwa angeifanyia nini dini yao kama angekuwa mshindi,
akajibu: “Nitajenga Kanisa pembezoni mwa kila msikiti na kumpa kila mtu uhuru wa kusali popote
atakapopachagua” (84)
.
4. Fursi (Iran) na ng‟ambo ya mto:-
Kuhusu kuenea kwa Uislam nchini Iran na maeneo mengine Thomas Arnold alifafanua historia ya
mambo yalivyo mwanzoni mwa sura ya 4 ya kitabu chake, lakini kabla ya hapo alielezea
ukandamizaji uliowapata watu wa himaya ya Sassani na dhulma iliyoonekana kwa vurugu na
matatizo. Waliwachukia na kukereheka na watawala wao hususan pindi dini ya Zoroaster
ilipotambulishwa na wakuu wa dini hiyo kushikilia mamlaka na hatamu za mambo mengi ya kiraia.
Hivyo, wanaharakati wa ukombozi wa Kiislam waliwakomboa watu hao dhidi ya utawala wa
Wassasani, ukombozi ambao Caetani anaukubali (85)
.
Mbali na hilo sio ajabu kama Mustashriqiina wengi wamekubali kwamba wakazi wa mijini hususan
wafanyakazi, wafanyabiashara na mafundi stadi waliukaribisha Uislam na wengi wao walijiunga
nao kwa shauku na mapenzi makubwa (86)
.
Dosobhai Framji katika kitabu cha History of Paris Juzuu 1 ukurasa 56 – 59 anasisitiza kuwa
“ukali na nguvu havikuhitajika kwa watu kuingia kwa wingi katika Uislam kwa sababu Waarabu
walikuwa wema kwa Waajemi (Wafursi au Wairan) hao ambao bado walikuwa wakifuata imani na
dini zao za awali”.
Hivyo, tunaweza kuhitimisha kwamba haiwezekani kuyakubali mawazo ya wanahistoria wenye
chuki ambao huzusha madai ya kwamba kutoweka kwa dini ya Zoroaster nchini Iran na kuupisha
njia Uislam ilitokea kwa nguvu au kwamba “ilisababishwa na wanaharakati wa ukombozi wa
Kiislam kutumia nguvu kuwalazimisha watu kuingia katika Uislam” (87)
.
Maeneo ya Ng‟ambo ya Mto:-
Uislam ulianza kuenea katika maeneo haya pindi Qutaibah Ibn Mustim Al-Bahili alipowasili huko.
Al Baladhuri katika ukurasa 421 anaandika: “Qutaibah (88)
alipowasili Samarkand aliona
masanamu mengi: Waabudu-Masanamu walikuwa wakiamini kuwa yeyote ambaye angeyakasirisha
na kuyaudhi masanamu hayo angekufa. Mwanaharakati huyo wa ukombozi wa Kiislam alipuuza
wasiwasi huo uliotokana na imani za kishirikina, hivyo akayachoma moto masanamu hayo kitendo
kilichopelekea idadi kubwa ya watu wakajiunga na Uislam”.
Katika zama za Ukhalifa wa Omar Ibn Abdul-Aziz, wahubiri wa Kiislamu walikuwepo katika eneo
hilo na watu wengi waliitikia mahubiri yao kwa mapenzi makubwa, na kundi kubwa la watu
66
walisilimu kwa msaada wa Abi Saida aliyekwenda na ujumbe huo kwenda Samarkand katika zama
za utawala wa Hisham wa pili.
Waseljuki wa Kituriki walibadili dini yao na kuingia katika Uislam bila vurugu wala mapigano
kwa sababu waliishi katika eneo jirani na Waislam la Turkestan, ambao walituma wahubir,i na kwa
sababu walijionea kwa macho yao usalama na nidhamu ambayo Waislam waliifurahia katika
kipindi cha karne ya 10 na 11 hususan pindi Seljuk na kabila lake walipoingia kaitka Uislam,
kutoka Turkestan mpaka Bukhara, na walikuwa waumini wenye shauku kubwa.
Je, Uajemi na maeneo yanayoizunguuka yaliingia katika Uislam kwa kitisho cha upanga au baada
ya kuupenda Uislam kwa kusadikisha mapenzi, amani na kupata usalama? Walikuwa wakweli,
waaminifu na wenye mapenzi ya dhati katika dini hii.
Ni jambo la kufurahisha kuwa watu wa maeneo haya waliupa Uislam huduma zenye thamani
kubwa mno, na ustaarabu wa Kiarabu na Kiislam ulirutubishwa na watu hawa. Walikuwa wafuasi
wa kweli walioinyanyua juu dini ya wanaharakati wa Kiislamu, lugha yao, hadithi za Mtume na
matawi mbali mbali ya elimu inayohusu ustaarabu huu mpya. Je, watu ambao wamelazimishwa
kwa nguvu kuingia katika Uislam wanaweza kuupa huduma na utumishi kama huo? Kama
wangekuwa wamelazimishwa wangetumia rasilimali zao zote za kiakili kuuangamiza na
kupambana na imani na dini ya wakombozi hao. Kwa kweli walikuwa wafuasi wa dhati waliojitoa
wakfu na mara zote walifanya juhudi kuvirutubisha viwanja vyote vya sayansi za Kiislam. Wengi
wao ambao walijipatia sifa na heshima, walibeba majina ya miji na wilaya mbalimbali kama vile Al
Tabari, mwanahistoria mkubwa na mfasiri wa Qur‟an tukufu, Ibn Khardadhabah, mwanajiografia
maarufu, Al-Shihristani, mtunzi wa kitabu „Imani na itikadi‟, Al Bukhari, mpokezi mkubwa wa
hadithi za Mtume (S.A.W) na idadi nyingine kubwa ya wasomi kama vile Avicenna (89)
, Abu Bakr
al Razzi, Abu Hanifa Al-Dainawari, Al Beiruni, Al Khawarizmi, Abu Al-Wafa Al-Buzanjani, n.k.
….
Je, watu hawa waliutumikia ustaarabu wa Kiislam kwa kushurutishwa au kwa imani na mapenzi ya
dhati, kwa ufuasi na kujitolea muhanga nafsi zao kwa ajili yake?
5. Wamongolia na Watartar:-
Makundi makubwa ya hawa wakatili yalikuja kutoka mashariki na majeshi ya Waislam
yakashindwa. Hakuna msiba au taabu kubwa iliyoufika ulimwengu wa Kiarabu inayoweza
kulinganishwa na uvamizi wa kishenzi wa Wamongolia waliouharibu na kuukanyaga ustaarabu, na
tamaduni walizoziondosha wakizishusha kwenye majangwa yaliyoangamizwa na maangamizi ya
kutisha. Katika Bukhara Wamongolia hawa waliifanya misikiti kuwa mazizi ya farasi wao,
wakazichana nakala za Qur‟an na kuzikanyaga kwa kwato za farasi wao. Walifanya vivyo hivyo
huko Samarkand, Balakh na miji mingine ya Asia ya kati ambayo hapo awali ilikuwa vito vya
ustaarabu wa Kiislam, makao ya wasomi na wanasayansi, na msiba kama huo uliikumba Baghdad (90)
.
67
Nywele za mwanahistoria mkubwa Ibn A-Athir zilisimama alipoanza kuelezea uvamizi huu wa
Wamongolia. Anasema: “Kwa miaka mingi, nilijizuia kuelezea matukio haya, nikichukia
kuuzungumzia ukatili wao wa kutisha, nikiogopa kuanza kusimulia: Nani ambaye hatotetemeka
kwa kuzungumzia matukio hayo ya maafa? Naapa kwa Allah laiti mimi nisingezaliwa na laiti mimi
ningekufa na ningekuwa nimesahaulika”
Wazo hili linatosha kuelezea msiba ulioukumba ustaarabu wa binadamu: Vitabu vya maktaba
kubwa sana ya Dar Al-Hikma (iliyoanzishwa na Harun Al-Rashid na iliyozaa matunda yake zama
za Al-Maamun) vilizamishwa katika maji ya mto Tigris na kujaa rangi nyeusi kwa siku kadhaa.
Ustaarabu na maarifa vilirudi nyuma kwa karne nyingi kutokana na hasara ya elimu na mafunzo
yaliyokuwa katika vitabu hivyo: maktaba hiyo ilikuwa ya kipekee isiyokuwa na kifani.
Mbele ya kizuizi hiki cha kijeshi kilichouathiri ulimwengu (kuanzia China mpaka Palestina),
Uislam ulithibitisha kwamba haukuwa kama imani au dini nyingine zote: mbali na utukufu wake
na kwa tabia yake ya kimiujiza kutoka kwa Mungu, Waislam waliwashinda na kuwaangusha
wavamizi hao.
Uislam ulielekea kunyanyuka na kukikwea kifusi cha utukufu wake wa awali na urithi wake wa
kifahari siki zote na katika njia nzuri. Ulizivamia nyoyo za watekaji hao wakatili kwa kutumia
wahubiri wake; kulikuwa na ushindani mkubwa baina ya dini mbalimbali kutaka kuwasogeza na
kuwavuta wapagani hao wakatili. Arnold anasema: “Mapambano yalikuwa makali kati ya dini ya
Budha, Ukristo na Uislam, kila dini ilikuwa katika mpambano mkali kuzivuta nyoyo na roho za
watekaji hao wagumu wenye taabu”
Wavamizi hao wasiostaarabika walirudi nyuma pindi wahubiri walipowafundisha Uislam, kanuni
za Kisuffi, hususan zuo la Naqshbandi (91)
.
Wavamizi hao walirudi kwenye nchi zao wakiuchukua Uislam pamoja nao kuwapelekea wananchi
wenzao. Walikuja mashariki ya kati wakibeba unyama, ukatili na maangamizi ya kikatili dhidi ya
binadamu, wakarudi nyumbani wakiwa wamebeba hisia za kibinadamu, huruma na upendo kwa
ulimwengu mzima. Uislam uliwasilimisha bila kutumia upanga au jeshi, majadiliano mema na ya
uchangamfu, busara na ushauri wa kirafiki ndivyo vitu pekee vilivyofanikisha lengo hili. „Kikosi‟
cha wahubiri wa Naqshbandi kilipenya katika nyoyo zao, hivyo tukawavuta wavamizi wetu na
tukazirejesha ardhi zetu.
Katika namna hii Uislam uliingia katika hali bora na ukaenea baada ya kuushinda upanga na sio
kwa kutumia upanga. Wahubiri wa Kiislam waliwafanya wapigapropaganda wa kimongoli kuwa
njia ya kuueneza Uislam, na kila mpanda farasi na mpiganaji katika jeshi la Barakah Khan akarudi
akiwa pamoja na busati (92)
lake la kusalia na kila aliposikia wito wa sala usemao “Njooni kwenye
Sala, njooni kwenye wokovu” alitekeleza ibada yake ya sala.
68
Ushindi mwingine uliofuata ni: kupenya kwa Uislam mpaka Urusi, pasipo kutumia operesheni za
kijeshi bali kwa wema na uadilifu ambao wanahistoria wananuita “Uwezo au nguvu ya Kiroho
ambayo Waislam walisifika nayo” (93)
. Nguvu hii ya imani iliyochanganyika na mifupa na damu, ni
nguvu imara iliyojificha katika Uislam, ni nguvu ya uzima, na uzima ni kwa wakakamavu. Arnold
anasema wazi wazi kuwa: - “Uislam ulianza kuyatelekeza mabaki ya utukufu wake uliopita na
kuirejesha daraja na nafasi yake upya kama dini yenye nguvu na ukuu” (94)
. Dini hii, licha ya maafa
yaliyoletwa na Wamongolia, ilienea katika mawimbi makubwa miongoni mwa Watartar wa Asia ya
Kati na huko Urusi.
Kinachoonesha nguvu isiyo na mwisho ya mahubiri ya Uislam, ambayo imejengwa kwenye mizizi
ya kutafiti na kutafakari, ni kwamba kushamiri kwa Uislam kuliimarishwa na Waislam wa Crimea
baada ya sheria ya uhuru wa kuamini iliyotolewa mwaka 1905 (95)
.
Aidha, makabila ya Qargheez yaliingia katika Uislam kwa muongozo wa wahubiri ambao katika
kazi ya kuwafikishia watu ujumbe wa Uislam walitegemea njia ya kuwaita watu kwenye njia ya
Allah kwa hekima na ushauri wa kirafiki. Mji wao wa Qazan ulikuwa kituo kikuu cha harakati hizi;
maelfu ya machapisho ya vitabu yalitolewa kila mwaka.
Uislam uliingia Siberia (bila upanga au vita). Kwa namna gani? “Mwaka 1745 kwa mara ya kwanza
Uislam ulienea miongoni mwa makabila ya Tartar yaliyoitwa Baraba Tartars (96)
.
Mheshimiwa Hakimu! Kuhusu Uislam kuenea kwa njia ya hekima na mazungumzo ya kirafiki au
uchangamfu, kwa ushawishi na kutafakari bila ya kulazimishana, mjadala wake kamwe hautafikia
tamati. Wale wanaoamini kuwa Uislam ulienezwa kwa nguvu, hawastaajabu jinsi Uislam
ulivyofika kusini mwa India, Ceylon, Lakdaif na visiwa vya Maladaif (97)
vilivyopo katika bahari
ya Hindi; kwenda Tibet maeneo ya pwani za China Philippines, visiwa vya Indonesia hadi
Peninsula ya Malaya? Uislam ulieneaje Afrika ya kati, Senegal, Nigeria, Somaliland, Tanzania,
Madagascar na Zanzibar? Uislam ulifikaje kwenye nchi hizo za mbali? Kwa upanga? Je, majeshi
yenye silaha yalikwenda huko?
Uislam ulikwenda huko pamoja na wafanyabiashara ambao imani zao ziling‟ara nyoyoni mwao;
katika biashara zao (za kuuza na kununua) waliutangaza Uislam na kuhubiri kwa njia ya hotuba
maridhawa. Njia ya kuufanyia kazi ukweli, upendo, haki na uaminifu ni mazoezi tosha ya
kuwahubiria watu kuingia katika Uislam.
Ili kujua kwa ndani jinsi Uislam ulivyoenea India (98)
kwa njia ya mahubiri bila kutumia silaha,
soma Sura ya 9 ya kitabu cha “Call to Islam” uk. 285. Kuhusu China, soma Sura ya 10 (99)
; kuhusu
Afrika, soma Sura XI inayofafanua namna taratibu, nidhamu na mafundisho ya Kisuffi
yalivyoushamilisha Uislam kwenye pwani ya mashariki mwa Afrika, nchini Uganda, katika maeneo
ya mashariki mwa Afrika (100)
na Somaliland mpaka Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope).
Kufahamu namna Uislam ulivyoenea huko Archipelago ya Malaya bila kutumia nguvu, soma Sura
69
ya XII Uk. 401 ambapo utafahamu jinsi Uislam ulivyofika Sumatra, Java, Visiwa vya Malox,
Borneo, Silibis, Ufilipino na Solo. Je, hivi sasa huko Amerika Uislam unaenea kwa kuwalazimisha
na kuwashurutisha watu?
Ushahidi wa haki na uadilifu:
“Historia haijapata kushuhudia wanaharakati wenye huruma mno kuliko Waarabu” Gustav Lebon.
Thomas Carlyle alikuwa mmoja wa waandishi wachache wa kimagharibi waliokuwa na nia njema
na uelewa kamili wa vita vitakatifu katika Uislam. Anafahamika kama mbashiri wa waandishi
anayehitimisha hoja zake kwa kueleza kuwa wale wanaohusisha kushamiri kwa Uislam na upanga
ni wafinyu wa mawazo duni na wapumbavu. Hakubaliani hata kidogo na mawazo hayo finyu na
huzichukulia shutuma hizi kuwa ni uongo wa kihistoria kwa sababu ni rahisi sana kuukana na
kuubatilsha kwa hoja. Anasema kuwa madai haya ni sawa na kusema kwamba mtu aliushika
upanga wake na kuwashambulia maadui wake ili kuwatisha na kuwashurutisha waamini kile
wasichokikubali na hivyo wakaitika kwa kukubali na kuamini kisha wanashirikiana naye
kuuchukua upanga ili kuwatisha wengine (101)
.
Laura Veccia Valgalieri ana ufafanuzi unaovuita kuhusu Uislam kuendelea kuenea Asia na Afrika
kwa sasa, naye anasema: “Hakuna awezaye kudai leo hii kwamba kuna upanga wa mvamizi
ulioandaa njia kwa ajili ya Uislam, bali kinyume chake ni kwamba, katika nchi ambazo hapo awali
kuliwepo na mataifa ya Kiislam na sasa kuna serikali mpya pamoja na dini nyingine kushika
hatamu, taasisi za kimisionari zenye mamlaka na nguvu ni nyingi sana zikifanya juhudi kubwa
kuwabadilisha watu kwenda kwenye dini nyingine, lakini hakuna chochote kilichotokea kwani
wameshindwa kuuondosha Uislam au kuukwepa.
Nguvu iliyoje ya kimiujiza yenye kujificha katika dini hii! Nguvu gani halisi ya ushawishi
inayoungana nayo! Ni katika kina gani cha moyo wa binadamu ambapo wito wake hutoa jawabu la
ngurumo? (102)
.
“Ushindi mbalimbali walioupata Waarabu ulitokana na sababu mbalimbali na iliyo kubwa zaidi ni
tabia tukufu walizojazwa na zinazotokana na Uislam” (103)
.
“Tunapojadili harakati za ukombozi za Waarabu na sababu zake, msomaji ataona kwamba
matumizi ya nguvu na upanga havikuwa nguzo katika kushamiri kwa Qur’an na kwamba Waarabu
waliwapa wale waliowashinda katika medani ya vita uhuru wa kuendelea na dini zao” (104)
.
“Qur’an haikuenezwa kwa upanga; wahubiri ndio walioieneza na watu wakaiamini” (105)
.
70
Robertson katika kitabu chake “History of Charlecan” anasema: - “Waislam ndio watu pekee
waliojumuisha vita na ustamilivu kwa wafuasi wa dini nyingine ambao waliwashinda na
wakawaacha huru watekeleze ibada zao za kidini”
Michaud anasema katika kitabu chake “History of the Crusades”:- “Uislam ambao unafanya vita
vitakatifu kuwa wajibu wa kidini una uvumilivu kwa waumini wa dini nyingine: uliwasamehe kodi
maaskofu, mapadri pamoja na watumishi wao”.
Count Henry de Catray, katika kitabu chake “Islam – Ideas and thoughts”, baada ya kuelezea
harakati za ukombozi wa Kiislamu na kuenea kwa dini hii miongoni mwa mataifa mbali mbali,
anasema: “Hawakuwaua wale walioupinga Uislam” .
Vile vile anasema: “Hakuna yeyote aliyelazimishwa kwa upanga au ulimi kuingia katika Uislam;
dini hiyo ilipenya katika nyoyo zao kwa shauku na moyo mmoja, kutokana na mvuto na ushawishi
mkubwa uliomo ndani ya Qur’an”.
Thomas Carlyle anasema kwenye ukurasa wa 76 wa kitabu chake “Heroes” wakati akikanusha
madai kwamba Uislam ulienea kwa nguvu:
“Wanasema kwamba lau isingekuwa nguvu ya upanga dini hii isingelienea; lakini kitu gani
kilichoutengeneza huo upanga? Ilikuwa ni nguvu ya hiyo dini. Ni kweli pindi taifa lolote jipya
linapoibuka hufanya hivyo katika ubongo wa mtu mmoja, mtu binafsi dhidi ya ulimwengu mzima.
Akichukua upanga na kusimama dhidi ya ulimwengu wote, takriban hupata hasara au hupotea kwa
ujumla. Ninaamini kwamba ukweli hujieneza wenyewe kwa njia yoyote iliyo muhimu. Je, huoni
kwamba wakati fulani Ukristo haukuacha kutumia upanga? Inatosha kukumbuka kile alichokifanya
Charlemagne dhidi ya makabila ya Wasaxon. Sijali kama ukweli ulienea kwa upanga au kwa ulimi
au kwa njia nyingine yoyote. Basi ukweli na uenee kwa kufanya hotuba au kwa kutumia majarida
ya habari au kwa moto. Waache wafanye juhudi na bidii kwa kutumia mikono, miguu na ncha zao
za vidole: hawatashindwa isipokuwa wale wanaostahili kushindwa”.
Rejea:
1. Qur‟an {2:256}
2. Qur‟an - {18:29}
3. Qur‟an - {16:82}
4. 4. Carl Brockelann “History of Islamic Peoples” uk. 78
5. Muir 2 Juz. 4 – uk. 107 – 8 na The Religions of the World uk. 28 kilichoandikwa na Fredrick
Demison Morris; na Caetani Juz. 1 – uk. 663.
6. The Religions of the World Uk. 28
71
7. Islam and Mission Uk. 43
8. Lutfi Levonian 9.
9. Search for the True Religion – Uk. 220 la 28 maoni ya M. Colly.
10. Mihadhara ya Isaac (Isaac's Lectures).
11. History ya France – Kilichondikwa na Guillaman na Lusiter.
12. Qur‟an - {46:35}
13. Qur‟an - {22:39 -40}
14. Qur‟an - {2:190 – 193}
15. Qur‟an - {4:75}
16. Defense of Islam – uk. 34 cha Lauravichia Viglairy.
17. The Arab State – uk. 23 cha Julius Fulhauzen.
18. Idadi hii inajumuisha vifo vyote baina ya Waislam na wasiokuwa waislam kwa kipindi cha
miaka 23, ambayo sio kitu ikilinganishwa na mbinu za zamani na za kisasa katika ujenzi wa
mataifa mbali mbali kutoka kwenye sifuri.
19. Muhammad at the Rise of Islam – uk. 462 – 3
20. Julius Vulhauzen – History of the Arab State – uk. 22
21. Julius Vulhauzen – History of the Arab State –uk. 15
22. The History of Islam – Juz. 1 – uk. 133 – 134.
23. “Muungano wa makabila ya Kiyahudi ulijumuisha wale walitoka Taima, Fadak, na Wadi el
Qura”
24. Qur‟an - {59:9}
25. Linganisha – Barua zilizobuniwa ambayo hukanusha shutuma kwamba Uislam ulienea kwa
upanga.
26. Historia ya Al-Kamil
27. Qur‟an - {63:8}
28. Qur‟an - {6:132}
29. Qur‟an - (8: 6)
30. Qur‟an - {2:256}
31. Hadithi hii imepokelewa na Al-Khatib kutoka kwa Ibn Masud
32. Qur‟an - {16:125}
33. Qur‟an - {24:54}
34. Qur‟an - {89:21}
35. Qur‟an - {50:45}
36. Qur‟an - {22:39}
37. Qur‟an - {8:72}
38. What is said – uk. 27
39. Katika kitabu chake –“Fanaticism and Toleration” – uk. 90 Profesa Muhammad Al Ghazali
anaandika:- “Lau kama Uislam ungetumia nguvu za kijeshi dhidi ya serikali zilizotoa uhuru
wa kidini na haki za mtu mmoja mmoja basi ungekuwa umetenda uhalifu unaotisha sana”.
40. Qur‟an - {8:47}
41. “The Internatinal Code in Islam” cha Dr. Najib Al-Armanazi.
42. Rejea {8:58} „Na kama ukiogopa Khiyana kwa watu, basi watupie ahadi yao kwa usawa,
hakika Allah hawapendi wafanyao Khiyana‟
72
- {9:2} “Basi tembeeni katika nchi miezi mine, na jueni kwamba nyinyi hamuwezi
kumshinda Allah, na kwamba Allah ndiye mwenye kuwahizi makafiri”
- Rejea tafsiri ya Qur‟an ya Ibn Al-Atheer Juz. 2 – uk. 331.
43. The Civilized and Political History of the Arabs in Ancient and Middle Ages”
Juz. 2 – uk. 48.
44. “Old History of Middle East” cha Abdul Aziz Othman.
45. “History of Civilization” cha George Haddad
46. “History of Muslim Nations” sehemu 1 cha Al-Khudari
47. Ma‟rifah Encyclopedia Na. 8 – uk. 122
48. Hisory of Medieval Euope cha Fischer – Juz. 1 – Uk. 61
49. “Enhardi Fuldensis Annales” na “Monumenta Germanise Hisorica”.
50. “Civilization of the Arabs” – uk. 336 – Sura 4 The Araba in Egypt
51. “The Call to Islam” Tanbihi – uk. 30
52. Camb. Med. Hist. IV – uk. 208 anasema katika kuongezea kuwa katika wake watano wa
halali alikuwa na vimada mia moja pekee.
53. “History of Europe in Middle Ages” cha Fischer,
54. “The Call to Islam” – uk. 31 cha Thomas Arnold.
55. Kitabu hicho hicho – uk. 223 – Wabushgardian nchini Hungari walikuwa Waislam mpaka
mwaka 1340 Charles Robert alipowashurutisha raia wake wote wasio Wakristo ima
wajiunge na Ukristo au waondoke nchini humu.
56. The Crusade Movement sehemu 1 – uk. 30 cha Dk. Ashur.
57. Missionaries and Colonialism – uk. 51 cha Dk. Khalidi na Dk. Faroukh
58. History of Modern Times – uk. 69
59. Tofauti kubwa na maelekezo ya Abubakr yaliyoelezwa hapo nyuma.
60. Al Hayat Na. 2494 la 23 Juni 1954 likinukuu kutoka kitabu cha “Missionaries and
Colonialism”.
61. Greusset‟s Histoir des Croisades 1 – uk. 161 Runciman op. cit. 1 – uk. 287
62. The civilization of the Arabs –uk. 326
63. Azdi – uk. 97 – Al-Baladhuri uk. 137 – The Call – uk. 73
64. Rejea kitabu cha mtunzi kiitwacho A-Yarmuk – uk. 45.
65. Arnold – Uk. 123 – Sawyers – Uk. 106 – Renaudot – Uk. 161
66. Call to Islam – Uk. 124 – Kutoka kwa Bell and Weltgeschichte Juz. 5 – Uk. 153
67. Rejea zilizotangulia
68. Dozy 2 Tom, ii – Uk. 39
69. Eulogui, Men, Sanct, Lib 130
70. The Marifah Encyclopedia sehem 43 – Uk. 684 “Athari ya Kiarabu”
71. The Call to Islam – Uk. 168 akinukuu kutoka kwa bea The Moriscos – Uk. 259
72. Phrantees – Uk. 305 – 6
73. Call to Islam – Uk. 171
74. Finaly Jz. 3 – Uk. 522
75. A Contemporary Tourist; The Travels of Martin Baumgarten – Uk. 373
76. Call to Islam – Uk. 173
73
77. Kitabu hicho hicho – Uk. 174
78. turchieae Spurciiae Suggillacio – Jz. 17
79. Scheffler 51, 53
80. Arnold – Uk. 184
81. Kitabu hicho hicho – Uk. 186
82. Kitabu cha mtunzi aliyeishi 1458. kitabu kilichotangulia – Uk. 186
83. Kitabu kilichotangulia – Uk. 186
84. Call to Islam – Uk. 237 kutoka kwa Enrique Dupuy de Lome: Los Eschavos Y. Turqufa –
uk. 17 - 18
85. Caetani Ju. 2 – Uk. 910 – 911
86. De Govineau – Uk. 306 – 316
87. Call to Islam – Uk. 293
88. Jeneali wa kijeshi ambaye Al-Hajjaj alimfanya kuwa kiongozi wa Khurasan na akamruhusu
kuikomboa sehemu ya ng‟ambo ya mto, hivyo akaitwaa Balkh, Beykand, Bukhara n.k. …..
89. Alizaliwa Afashnah, kijiji kilicho jirani na Bukhara (980 – 1037)
90. Call to Islam – Uk. 249
91. Arnold alielezea kuhusu madhehebu hii ya kisufi iliyokuwa na nguvu na ushawishi mkubwa
huko Asia katika karne ya 14 A.D.
92. Call to Islam – Uk. 259, 226 - 270
93. Kitabu kilichotajwa – Uk. 276
94. Kitabu kilichotajwa – Uk. 269
95. Islam and Mission – Uk. 257
96. Radloff Juz. 1 – Uk. 241
97. Watu wa Maladaif waliingia katika Uislam kwa msaada wa wafanyabiashara wa Kiarabu na
Kiajemi waliokuwa wakiishi huko. Call to Islam – Uk. 302
98. Wafanyabishara wa Kiislam waliueneza Usilam huko Pirmahaibir lenye maana ya Kiongozi
mkubwa wa kitawa aliueneza Uislam katika eneo la Dakn.
99. Wafanyabiashara waliosafiri kwa kupitia njia ya bahari ya zamani walifanya kazi hiyo.
100. Sheikh Yusuf Shamsuddin aliyetokea Tabriz Iran aliutangaza Uislam nchini Mali.
101. Arab Civilization Jack S. Rasier – Uk. 27
102. The Civilization of Arabs – Uk. 145 cha Gustav Lebon, kimetafsiriwa na M. Adil
Zuaiter.
103. Kitabu kilichotajwa hapo juu – Uk. 128
104. uk. 35 – Tafsiri ya A. Fathi Zaghful
105. Kitabu kilichotajwa hapo juu – Uk. 39 – 40
74
KESI YA NANE
Wasiokuwa Waislam na Kodi ya Ushuru (Jizyah)
Uislam unaingia katika ukumbi wa mahakama na kesi ya nane inaanza.
Mwendesha Mashtaka: Uislam uliamiliana na watu, Wakristo na Wayahudi, waliokuwa chini ya
himaya yake, kwa namna ya ushenzi na ufedhuli na ukawanyima uhuru wao sanjari na
kuwabebesha mzigo wa ushuru ulioitwa “Jizya” (kodi).
Raia wasio Waarabu, chini ya utawala wa kikabaila wa wanamgambo wa Kiarabu, walikuwa ni
mojawapo ya nguzo za kiuchumi kwa serikali ambayo iliwatoza kodi kubwa zaidi ya “Zakaat”,
kodi ya maskini iliyokuwa ikitolewa na Waislam. Serikali hiyo ya Kiarabu iliingilia mambo yao ya
ndani, bila sababu kuliko ilivyoingilia mambo ya makabila mbalimbali yaliyounda taifa hilo la
Kiislam.
Jambo kubwa ambalo serikali hii ilijihusisha nalo sana ni mapato ya hazina.
“Watu waliokuwa chini ya maagano walikuwa kama ng‟ombe ambaye mapembe yake yalikamatwa
na mtawala ili kumtuliza huku mtoa kodi akimkamua” (1)
.
Madai yangu haya yanaweza kubainishwa na Aya moja iliyomo ndani ya Qur‟an isemayo:-
“Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyzio Mungu wala siku ya mwisho wala hawaharamishi
alivyoviharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala hawashiki dini ya haki, miongoni
mwa wale waliopewa kitabu mpaka watoe kodi kwa mkono hali wametii” (2)
.
Uislam unasimama, ukiudhika sana na tuhuma hizi za ushabiki wa kidini, hali ukishangazwa na
namna Uislam unavyofundishwa na kuelezewa huko ulaya. Pamoja na tuhuma zote hizi Uislam
unadhamiria kuweka ukuta mrefu baina ya tuhuma hizi na ukweli.
Uislam: Kwa kuanza tunaweza kusema kwamba katika nchi zote za Kiislam, Wakristo na
Wayahudi wamekuwa wakiishi pamoja na Waislam kwa amani muda wote. Wakati huo huo
Waislam wamekuwa wakiishi katika nchi zisizokuwa za Kiislam. Je kila upande uliamiliwa na
kutendewa vipi katika nchi yake? Fanya ziara katika ulimwengu wa Kiislam, ukitafuta lalamiko
kutoka kwa Mkristo au Myahudi yeyote kuhusu Waislam.
Bali kinyume chake ndicho kinachoonekana katika nchi zisikuwa za Kiislam ambazo Waislam
waliishi. Tunasoma maelezo yafuatayo kama yalaivyonukuliwa kutoka katika kitabu cha Bwana
Gustav Lebon „The History of the Arab‟ uk. 194:
75
“Ukatili ndio iliyokuwa alama ya wapiganaji wa vita vya msalaba nchini Palestina. Wapiganaji
wetu wa kweli wa vita vya msalaba, hawakuishia kwenye unyanyasaji, uonevu na mateso.
Waliitisha mkutano wa halaiki mjini Jerusalem na wakachukua uamuzi wa kuwateketeza watu wote
wa Jerusalem waptao elfu sitini, Waislam na Wayahudi. Waliwaangamiza ndani ya siku nane bila
kubagua mwanamke, mtoto na hata mzee.
Wapiganaji hao wa msalaba walikuwa waovu, wafidhuli na wakana Mungu, wenye dhambi. Kama
mwandishi ataelezea uovu wao wa kikatili hatoendelea kuwa tena kuwa mwanahistoria, bali
atageuka na kuwa mtenda dhambi”.
Hispania ya leo inatuelezea kuwa hakuna hata Mwislam mmoja anayeishi huko. Waislam
waliokuwa wakiishi huko waliteketezwa. Walishurutishwa kuuacha Uislam na kuingia katika
Ukristo. Mnamo Februari, 1502, sheria iliwekwa ili kuwafukuza Waislam wenye asili ya Morocco
(walioitwa maadui wa Mungu) waondoke katika mji wa Seville na vitongoji vyake kama
wasingekubali kubatizwa. Walitakiwa kuondoka Hispania mwezi Machi. Hawakuruhusiwa kubeba
dhababu au shaba yoyote. Hawakuruhusiwa kupita njia yoyote ambayo ingewapeleka kwenye nchi
yoyote ya Kiislam, hivyo hatma yao wote ikawa ni kifo kisichokuwa na shaka ndani yake.
Taasisi ya mahakama ya Kanisa Katoliki kukomesha uasi, miaka ya 1232 – 1820 iliwashinikiza
Waislam kuwa Wakristo. Mamlaka za Kanisa zilitegemea mbinu za matumizi ya nguvu kupita
kiasi. Ahadi zilizotolewa kwa Waislam ili kuwalinda na kampeni hii ya msalaba, hazikutekelezwa.
Sera ya Kihispania ilivishwa vazi la dini na uchamungu.
Kisha mnamo mwaka 1501, Wafalme wawili wa Kikatoliki, Ferdinand na Isabella, walitangaza
kuwa walikuwa wamechaguliwa na Mungu kuitakasa Granada kutokana na wapagani kwa
kuwapiga marufuku Waislam kuishi huko. Yeyote ambaye angevunja agizo hili angekabiliwa na
adhabu ya kifo huku mali na utajiri wao vikichukuliwa kwa nguvu.
Baada ya huu utangulizi sasa tuyadurusu maisha ya wasiokuwa Waislam katika taifa la Kiislam.
1. Qur‟an Tukufu:
Qur‟an takatifu, pamoja na hadithi za Mtume (S.A.W) na matendo ya makhalifa wenye busara
vimeelekeza njia sahihi kwa Waislam kuamiliana na watu wasiokuwa Waislam na jamii ya Kiislam
ilifuata njia hiyo kwa vitendo.
Qur‟an inasema: “Allah hakukukatazeni kuwafanyia ihsani na uadilifu wale ambao hawakupigana
nanyi kwa ajili ya dini wala hawakukufukuzeni katika nchi yenu. Hakika Allah anawapenda wenye
kufanya uadilifu” (3)
. Vilevile inasema: “Na chakula cha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu, na
chakula chenu ni halali kwao” (4)
.
76
Ikitokea kwamba mtoto amesilimu na wazazi wake wakaendelea kuwa wasiokuwa Waislam,
Uislam unamtaka mtoto huyu kuendeleza uhusiano mwema na wazazi wake licha ya kutofautiana
katika dini: “Na kama wakikushurutisha kunishirikisha na yule ambaye huna khabari naye, basi
usiwatii na kaa nao kwa wema hapa duniani” (5)
.
Waislam wanapojadiliana na “watu wa Kitabu” (Wakristo na Wayahudi) wamewekewa kanuni
kadhaa zinazotakiwa kuzingatiwa: “Wala msibishane na watu wa kitabu ila kwa yale yaliyo bora,
isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tunaamini yaliyoteremshwa kwetu na
yaliyoteremshwa kwenu na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja nasi ni wenye kunyenyekea
kwake” (6)
.
2. Hadithi za Muhammad (S.A.W.) na matendo yake:-
Muhammad, amani ya Mungu iwe juu yake, alikuwa akihudhuria dhifa za wasiokuwa Waislam na
kushiriki katika mazishi yao na kuwatembelea wagonjwa wao. Pindi ujumbe wa Kikristo kutoka
Najran Yemen, ulipomtembelea aliwatandikia joho lake ili wakae juu yake. Alikuwa akiazima pesa
kutoka kwa watu wa kitabu na kuwekeana nao rehani. Alipofariki dunia vazi lae la kivita lilikuwa
limewekwa rehani kwa Myahudi mmoja mjini Madina.
Yote hayo yalikuwa ni somo kwa Waislam kujifunza na kufuata. Miongoni mwa wafuasi wake
kuna waliokuwa tayari kumuazima pesa au hata kuyatoa muhanga maisha yao kwa ajili yake.
Siku zote alikuwa akisema: “Amuumizaye mtu asiye Mwislam basi huyo si katika mimi”. “Amuuaye
mtu tuliye na agano naye hatonusa harufu ya pepo”. “Atakayemtendea ubaya tuliye na agano naye
na kumbebesha mzigo mzito atasiamam mbele yangu siku ya hukumu ili ajieleze”. “Allah
atamuadhibu yule anayewaadhibu na kuwatesa watu hapa duniani”. Hakusema “Waislam” bali
“watu”( wa madhehebu zote).
Zaid bin Saghna, mmojawapo wa Wayahudi anahadithia kuwa siku moja alimpa Muhammad
mkopo ili aweze kuwahudumia baadhi ya wale ambao mioyo yao ilihitaji usuluhishi. Kabla ya
deni kulipwa alikwenda kwa Muhammad kutaka pesa yake. Anaendelea kusema: “Nilipokuja kwa
Muhammad nilishikilia joho lake na kumtazama kwa uso wenye chuki nikisema: “Ee Muhammad
hutanilipa pesa yangu? Unatoka katika familia ambayo siku zote hufanya usiri na kuwafukuza watu
na kutolipa kwa wakati”. Kisha Omar alinitazama na macho yake yakizungukazuka kwa hasira
nakusema: “Ee adui wa Mungu, unawezaje kusema na kumfanyia Muhammad hicho ninachokiona?
Ninaapa kwa jina la Mungu ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, lau isingekuwa kumchukiza
Muhammad ningekikata kichwa chako kwa upanga wangu”.
Muhammad akanitazama kwa upole na akasema: “Ee Omar, tunahitaji kitu bora zaidi kuliko
upanga. Unatakiwa kunishauri kulipa vizuri, nawe kumtaka aulize katika namna nzuri. Mchukue
mtu huyu na umpe zaidi ya pesa yake kwa sababu umemtisha”.
77
Zaid anaendelea kusema: Omar akanichukua na kunilipa mkopo wangu na zaidi ya hapo akanipa
kilo ishirini za tende. Nilipomuuliza Omar kwani alikuwa amefanya hivyo, akasema:
“Muhammad ameniamuru kukulipa zaidi kwa sababu nilikuogofya na kukutisha”.
3. Waislam na matendo yao:-
Katika sheria ya Kiislam, Mwislam anatakiwa kuwa mkarimu kwa ndugu yake Mwislam kwa
kipindi cha muda wote. Kama akikiuka sheria hii, mtawala ana mamlaka ya kumlazimisha
kutekeleza sheria hiyo madam anaweza kufanya ukarimu huu.
Omar aliagiza kutowaadhiri wasio Waislam kwa desturi hizi za Kiislam, hata wakati wa vita.
Alimuamuru Saad bin Abi Waqas, kamanda wa jeshi lake nchini Iraq katika mpaka wa Faris,
akisema: “Askari wako wakae mbali na vijiji vyao (wasio Waislam) na wale tu waaminifu
waruhusiwe kuingia humo na wasiwadhuru wakazi hao. Majaribu yako ni kutekeleza wajibu wako
na majaribu yao ni kulivumilia hilo”.
Hivyo, tunaona kuwa hawakutakiwa tu kuamiliana nao kwa wema, bali kiubinadamu. Kauli mbiu
ya Omar haikuwa “Taabu kwa waliotekwa kutoka kwa watekaji” bali ilikuwa ni “Onesha huruma,
ulinzi, wema na ustahimilivu kwa walio shindwa katika mapambano”.
Mara zote Omar aliwakumbusha viongozi na magavana wake kwamba walitakiwa kutowanyanyasa
watu wa kitabu na wawapunguzie matatizo yao na wasiwabebeshe mzigo mzito wa mambo.
Alipoombwa kutoa ushauri na usia kabla ya kifo chake, Omar aliwaambia:-
“Ninakuusieni kukiangalia vyema kitabu cha Mwenyezi Mungu. Mkikifuata hamtapotea;
Ninakuusieni kuwaangalia kwa wema Muhajirin (watu wa Makka waliokuwa wa kwanza kuslimu)
kwa sababu watu wanaongezeka na wao wanapungua. Ninakuusieni kuwaangalia Ansar
(Waliounusuru Uislam) kwa sababu Uislam ulikimbilia kwao wakati ukikimbia kutoka Makka.
Ninakuusieni kuwaangalia watu walio kwenye maagano na Waislamu (Wakristo na Wayahudi
wasio Waislam) kwa sababu Muhammad alituusia kuhusu wao na wao ndio wasaidizi wa watu
wenu.”
Katika mikataba yake ni huu ufuatao: “Haya ndiyo ambayo Khalifa Omar mja wa Mugu ameagiza
kwa watu wa Eliya kwa ajili ya misalaba yao. Makanisa yao hayatatwaliwa na Waislam wa
kubomolewa. Ustawi wao hautaguswa na hawatalazimishwa kufuata dini nyingine yoyote, hakuna
madhara yatakayotendwa dhidi yao na hakuna Myahudi yeyote atakayeshirikiana nao katika nchi
yao ya asili”.
Kimatendo, Omar ambaye harakati nyingi za ukombozi zilifanyika enzi zake, alikuwa mwenye
subira sana na aliamiliana na kila mtu vizuri.
78
Alipokuwa ndani ya Kanisa la Ufufuo, mjini Jerusalem, muda wa yeye kusali ukafika alitoka na
kwenda nje ya viwanja vya Kanisa na kutekeleza sala yake.
Alipoulizwa na mkuu wa Kanisa kwa nini hakusalia ndani ya Kanisa, alisema kuwa alikhofia
kwamba siku moja Waislam wangesema kuwa wana haki ya kujenga Msikiti mahali hapo kwa
sababu ni mahali ambapo Omar alitekeleza sala yake.
Siku moja Omar alimuona mzee wa Kiyahudi akiwaomba watu sadaka. Alipoulizwa mtu huyo
akasema: “kuwa hali hiyo ilitokana na shida kubwa itokanayo na uzee wangu”. Omar aliposikia
hayo alimchukua kwa mkono wake kumpeleka nyumbani kwake na kumpa mali nyingi. Kisha
alimuagiza mtunza hazina kuendelea kumpatia mzee huyo stahili yake kutoka katika mfuko
uliowekwa maalum kwa ajili ya watu maskini na wale wenye shida, na akaongeza kuwa haikuwa
haki kumtoza kodi wakati wa ujana wake na kisha kumkana wakati wa uzee wake. Mtu huyo
alikuwa miongozi mwa maskini katika watu wa kitabu, hivyo alistahili kupata fungu lake kutoka
katika zaka na sadaka za Waislam.
Siku nyingine Omar alipita eneo lililokuwa na Wakristo wenye ukoma, nchini Syria na akaagiza
kuwa wanatakiwa kuendelea kupewa zaka kutoka katika sadaka za Waislam.
Siku moja Wakristo wa kabila la Taghlib walimpinga gavana wao wa Kiislam Walid bin Waqus
kwa hofu ya kwamba anaweza kufanya kisasi yeye mwenyewe, Omar alimtaka kamanda huyo
ajiuzulu na kisha akamuweka mahali pake mtu mwenye huruma na uvumilivu zaidi ili kuwaangalia
vyema Wakristo hawa na kuamiliana nao kwa upendo.
4. Maoni ya Wakristo kuhusu muamala wao na wanaharakati wa Kiislam:-
Mwanamfalme wa Nistoria, Yashou Baf III, alituma barua kwenda kwa
Samaan, Askofu mkuu wa Fursi akisema:-
“Waarabu ambao Mungu amewajaalia kuitawala hii dunia, wanaamini kile unachokifuata na
kuishi ndani mwake. Licha ya kwamba hawaipigi vita dini ya Kikristo, wanaijali na kuilinda na
wanawaheshimu maaskofu na watakatifu wetu, Wanatoa misaada kwa makanisa yetu”.
Isho Babeh kiongozi wa Kikristo anasema:-
“Waarabu ambao wamewezeshwa na Mungu kuutawala ulimwengu, wanaamiliana nasi katika
namna uijuayo. Wao si maadui wa Ukristo wanaitukuza dini yetu wanawaheshimu makasisi wetu
na wanayasaidia makanisa na dayosisi zetu”.
Kwanini wasiokuwa Waislam walipe kodi?
Kodi hiyo kwa lengo gani?
Ni kiasi gani?
Inawakilisha nini miongoni mwa Waislam?
79
Watu wa Kitabu wanaweza kunufaika na huduma za umma, kama vile mahakama, polisi, madaraja
na ujenzi wa barabara, miradi ya umwagiliaji, n.k. mambo ambayo yanahitaji gharama ambazo kwa
kiasi kikubwa zilitekelezwa na Waislam na kwa kiasi kidogo zikatekelezwa na watu wa Kitabu kwa
kodi au Jizyah (Poll-tax) wanayotoa kwa serikali ya Kiislam.
Vilevile kwa kutoa kodi hii wale wenye uzima wa mwili hawahitajiki kufanya kazi yoyote ya
kijeshi kulinda nchi. Jukumu hili linabebwa na Waislam pekee. Hivyo, kodi hii inawafanya wasio
Waislam wasamehewe kushiriki katika kazi yoyote ya kijeshi.
Kama wakilazimika kujilinda, inapotokea kuwa serikali ya Kiislam haiwezi kufanya kazi hiyo, basi
hawatoi kodi yoyote.
Mwanzo Waislam waliingia Homs nchini Syria na kupokea kodi kutoka kwa wakazi hao ambao
hawakujiunga na Uislam. Kisha wakalazimika kusalimu amri pindi jeshi kubwa la Byzantine
lilipokuwa likija kutokea kaskazini. Walifahamu vyema kuwa wasingeweza kuwalinda watu hao
wa Homs, hivyo waliwarudishia kodi yao. Baada ya kuona hivyo watu hao wa Homs wakawaambia
Waislam: “Utawala na uadilifu wenu ni vitu vyenye thamani kubwa kwetu kuliko unyanyasaji na
uonevu wa Wakristo wa Byzantium, waliokuwa wakitutawala. Tutaulinda mji wetu pamoja nanyi”.
Kwa sababu hii muhimu watu hao walisamehewa kutoa kodi yoyote.
Kiwango chake:-
Mtu mwenye mali nyingi alikuwa akitoa dirham 48 kwa mwaka au takriban sarafu mbili za paundi.
Mtu wa kawaida alikuwa akitoa dirham 24 na mfanyakazi dirham 12. Hivyo, ni kiwango kidogo
cha pesa kilichokuwa kikitolewa kwa mwaka na kilitofautiana kulingana na hali ya kifedha ya
mwananchi wa Kikristo au Myahudi. Wale ambao hawakuwa na kipato walisamehewa kutoa kodi
hiyo.
Ilieleweka kwamba kodi hiyo haikuwa aina ya adhabu kwa wale waliokataa kuukubali Uislam, bali
ilikuwa tu fidia kwa ajili ya ulinzi walioutoa Waislam kwa ajili yao. Watu wa Hira walipolipa kodi
walitoa masharti mawili ambayo ni:-
“Kutulinda na shari kutoka upande wenu (Waislam) na shari kutoka nje” (7)
, ambapo Waislam
walijibu wakisema: “Kama tukiwalinda basi tunahaki ya kuchukua Jizya, la sivyo hapana” (8)
.
Haki za kijamii za watu wa Kitabu (9)
:-
1. Usalama wa nafsi:-
Damu ya raia wasio Waislam ina thamani sawa na ya Waislam.
80
(a) Imesimuliwa na Omar bin Hassan kuwa Mwislam mmoja alimuua mwananchi asiye Mwislam.
Taarifa hizi zilipomfikia Muhammad alisema “Mimi ndiye ninayewajibika kulinda haki yake” kisha
akaagiza kuwa Mwislam yule muuaji auawe.
(b). Wakati wa utawala wa Omar, mtu mmoja wa kabila la Bakr bin Wael alimuua raia asiye
Mwislam kutoka Hira. Omar akaagiza kuwa muuaji apelekwe na kukabidhiwa kwa kabila la
marehemu ambao nao waliamua kumuua.
(c) Wakati wa utawala wa Ali, Khalifa wa nne, Mwislam mmoja alikamatwa kwa mauaji ya raia
asiye Mwislam na adhabu ya kifo ilihitajika kutekelezwa. Ndugu wa marehemu alikubali kuchukua
fidia na akamsamehe. Ali aliposikia hivyo alitaka kujua kama ndugu huyo alikuwa ametishwa na
familia ya muuaji na kushurutishwa kukubali fidia badala ya kutekeleza adhabu ya kifo. Lakini
akamwambia Ali kuwa hapakuwepo vitisho vyovyote.
Na hapo Ali akasema: “Damu ya yule aliyepewa dhamana ya ulinzi wetu ina thamani sawa na
damu yetu na fidia yake ni sawa na fidia yetu.”
2. Sheria ya Uhalifu:-
Raia Waislam na wasio Waislam wote wana haki sawa mbele ya sheria. Huadhibiwa kwa kosa
moja sawia, wizi, kuzusha uwongo na uzinzi. Lakini asiye Mwislam haadhibiwi kwa kunywa
pombe.
3. Sheria ya Kiraia:-
Ali Khalifa wa nne anasema: “Mali zetu na mali zao (wasio Waislam) zina haki sawa mbele ya
sheria. Wao (wasio Waislam) wanaruhusiwa kutengeneza pombe, kuziuza na kuzinywa.
Wanaruhusiwa kufuga na kula Nguruwe. Kama Mwislam yeyote akiharibu pombe au Nguruwe
yeyote anayemilikiwa na asiye Mwislam analazimika kumlipa fidia. Hii ni kwa sababu wao
wameamua kufuata dini yao nasi tuna yetu hakuna kuwakera.
4. Utunzaji wa Heshima:-
Raia asiyekuwa Mwislam hatakiwi kudhuriwa kwa mkono au ulimi, hapaswi kupigwa, kutukanwa
au kukashifiwa.
5. Kudumisha Makubaliano:-
Makubaliano kati ya serikali ya Kiislam na raia wasio kuwa Waislam yanawashurutisha na
kuwafunga Waislam dhidi ya kuyavunja. Lakini raia wasio kuwa Waislam wana hiari ya kuyafuata
au kuyavunja kwa utashi wao. Licha ya kosa au jinai yoyote kubwa inayotendwa na raia asiyekuwa
Mwislam, bila kujali ukubwa wake, kosa hilo halivunji makubaliano hayo hata kama akimuua
81
Mwislam au kutolipa kodi. Bali hapa ataadhibiwa kama mvunjaji wa sheria na hatazamwi kama
mtu anayetakiwa kutengwa na taifa.
Lakini vitu viwili pekee ndivyo vinavyoweza kuvunja agano hilo: Moja, kuondoka katika taifa la
Kiislam na kuungana na jingine katika kulipiga la Kiislam. Pili, kuinua upanga hadharani dhidi ya
taifa akikusudia kueneza uasi au mapinduzi.
6. Sheria za Kibinafsi:-
Raia wasiokuwa Waislam wana haki kamili ya kurejea kwenye sheria zao wenyewe. Wakati
mmoja Khalifa wa Ki-bani Umayyah Omar bin Abdul Azizi, alimuandikia Imam Hassan Al Basri
akitaka fatwa yake ya “kwa nini Makhalifa wenye busara waliwaacha raia wasiokuwa Waislam
kutumia sheria zao wenyewe za ndoa, Pombe na Nguruwe?”
Hassan Al Basri akajibu akisema: “Walitoa kodi ili waachwe wafuate imani zao wenyewe.
Unatakiwa kufuata mfano wa wale waliokutangulia na hupaswi kuanzisha mambo yanayokwenda
kinyume na mafundisho ya Uislam”. Akaongeza akisema: “Wewe ni mfuasi sio mwanzilishi”.
Lakini ikiwa pande mbili, zisisokuwa za Kiislam, zitaiomba mahakama kutumia sheria ya Kiislam
kusuluhisha tofauti zao basi mahakama lazima ifanye hivyo na kutumia sheria ya Kiislam.
Lakini mmoja wao akiwa Mwislam na kesi yake inahusu sheria binafsi basi ni lazima kutumia
sheria ya Kiislam.
7. Taratibu na Ibada za Kidini:-
Raia wasiokuwa Waislam wana uhuru kamili wa kutekeleza taratibu za dini yao katika majumba
yao ya ibada. Serikali ya Kiislam haina haki ya kuingilia ibada hizo, vilevile wana haki ya
kukarabati mahekalu yao.
8. Uvumilivu katika kuchukua kodi:-
Magavana wa Kiislam wanaamriwa kutowalazimisha raia wasio Waislam katika kuchukua kodi.
Wanatakiwa kuichukua kwa upole na heshima. Hawatakiwi kushinikiza au kuuza mali zao ili
kupata kodi hiyo. Khalifa wa nne Ali alimwandikia mmoja wa magavana wake akisema: “Katika
kuchukua kodi usiuze Punda, Ng’ombe au Nguo yoyote ya mtu, si katika kipindi cha joto na wakati
wowote”.
Maulamaa wa Kiislam walitoa hukumu kwa wale waliokataa kulipa kodi ya kila mwaka kwa
kuwaweka gerezani, lakini bila kuwapa kazi ngumu, na kwa kuwahudumia ipasavyo mpaka walipe.
Yule aliye maskini sana sio tu kwamba husamahewa kulipa kodi hii bali pia hupewa fungu lake
kutoka katika hazina.
82
Mtu akifa na deni la serikali kwa kutolipa kodi yake serikali haina haki ya kutaka kodi hiyo kutoka
kwa warithi wala kutoka katika urithi wake.
Raia wasiokuwa Waislam wana uhuru wa kuelezea fikra zao, wana shule zao na wanaweza kufanya
kazi za serikali isipokuwa kazi chache zilizo katika ngazi za juu. Waislam na wasiokuwa Waislam
huamuliwa kwa sifa zao (10)
. Wana uhuru wa kujipatia pesa katika viwanda, biashara, kilimo au
katika utaalam wao.
Hivyo, tunaona kuwa watu wasio Waislam waliishi chini ya mwavuli wa Uislam, wakifurahia
uhuru kamili, haki isiyokuwa na upendeleo na uhuru wa kuabudu, yote hayo yakitokana na mfumo
wa Kiislam ambao msingi wake ni kumuogopa Mwenyezi Mungu katika shughuli zote na katika
kutekeleza misingi thabiti ya Uislam.
Ushahidi wa Haki:-
Mheshimiwa Hakimu! Naomba niwasilishe baadhi ya ushahidi wa haki. Dryder anasema:
Waislam chini ya utawala wao walichukua kiasi kidogo tu kutoka kwa watu ikilinganishwa na kiasi
ambacho serikali zao za kitaifa zilihitaji kutoka kwao.
Montisques anasema: Kodi kubwa walizolipa watu kwa wafalme wao ziliwarahisishia Waislam
kuzitwaa nchi zao kwa sababu walikuta kwamba hawa Waislam walikuwa na huruma na upole sana
kuliko watawala wao wenyewe.
Laura Veccia Volglieri ana maoni yafuatayo kuhusu mikataba iliyosainiwa na Waislam:
“Mikataba hii iliwapa watu hao uhuru wa kuendelea na dini na desturi zao za zamani ikizingatiwa
kuwa wale wasiojiunga na Uislam wanatakiwa kuilipa Serikali ya Kiislam kodi ya kichwa ambayo
ilikuwa ni kiasi kidogo zaidi ya kodi ambazo Waislam wenyewe walitakiwa kuzilipa Serikali zao.
Kwa kodi hiyo wasiokuwa Waislam walipewa ulinzi kamili uliokuwa ukifurahiwa na jamii ya
Kiislam. Hivyo, sio tu kwamba Uislam ulilingania subira na kuvumiliana bali uliyafanya mambo
hayo kuwa kitu kisichotengana na falsafa yake ya kisheria”.
Vaglieri anaendelea kusema: “Lipa kodi ndogo ya kichwa ufurahie ulinzi kamili au ingia katika
Uislam ufurahie haki zote tunazofurahia”.
Gustav Lebon anasema: “Ni kodi ndogo zaidi kuliko zile walizokuwa wakiwalipa watawala wao wa
zamani” (11)
.
83
Rejea:
1. Madai haya yamenukuliwa kutoka katika kitabu cha “The History of the Arab State” – uk. 27
cha Julius Felhausen.
2. Quer‟an {9:29}
3. Qur‟an - {60:8}
4. Qur‟an - {5:5}
5. Qur‟an - {31:15}
6. Qur‟an {29:46)
7. Tabari – uk. 2055
8. Tabari – uk. 2050
9. „The rights of the non-Muslim subjects‟ cha Maududi – uk. 13
10. Maududi „The Rights of the Non-Muslim – the Islamic State‟ – Uk. 34
11. The Civilization of the Arabs.
84
KESI YA TISA
Uislam na Ukoloni
Mwendesha Mashtaka: Pindi uislam ulipoingia Palestina, uliambatana na malengo ya
kisiasa na kijeshi. Hilo lilitendeka kwa mikono ya Khalifa Omar mkoloni wa Kiarabu.
Muhammad aliweka upanga mikononi mwa wale waliomfuata na akavunja sheria tukufu
sana za maadili. Kisha aliwaruhusu kutenda kila aina ya uharibifu na uporaji pamoja na
kuwaahidi kuwa wale waliokufa katika medani ya vita wangeyaridhisha matamanio yao yote
huko akhera. Muda mfupi tu wakaikamata Asia ndogo, Afrika na Hispania. Waislam wa
Kiarabu walikuwa kama upande wa kaskazini kutokana na mazao yake mazuri walikuwa
kama wavamizi ambao binadamu amewashuhudia katika maisha yake kutoka zama moja
kwenda zama nyingine.
Hakimu: Islam ni upi utetezi wako?
Uislam: Mheshimiwa Hakimu, madai kwamba Uislam ni harakati ya ukoloni sawa na
harakati nyingine za aina hiyo, yanachukuliwa na madai kwamba Waarabu wa Kiislam
walifanikiwa katika harakati za vita vya ukombozi kutokana na moyo na tabia yao ya
kuhamahama iliong‟arisha nguvu zao katika jangwa. Ngamia alikuwa mhimili mkuu wa
utekaji huo kwani alisafirisha vifaa, majeshi na mawasiliano baina ya Hijza, kitovu cha taifa
lao linaloendelea, na safu za mapambano.
Tunasema kwamba moyo na tabia ya kuhamahama haikuwa na mchango wowote katika hili.
Waislam walishinda licha ya idadi yao kuwa ndogo na washirikina wa Kiarabu
wakashindwa licha ya idadi yao kuwa kubwa?
Hoja ya pili ni kwamba katika vita vya Yarmuk, ambayo ni maajabu na muujiza wa kudumu
wa Uislam, Warumi wa Ki-Byzantium wapatao askari laki moja na elfu arobaini na wakiwa
na msaada wa askari laki moja kutoka katika kabila la Ghassasin waliokuja kuwasaidia
wakati ambapo jeshi la Kiislam lilikuwa na askari elfu arobaini tu. Kwa nini Waislam
walishinda?
Ngamia hakuwa na ulazima kama angekuwa muhimu hata kidogo kwenda kwenye taifa la
Farsi au Rumi kwa sababu medani ya vita ilikuwa katika ardhi yao na hawakuhitaji Ngamia
kutoa nyenzo za mawasilano na kubeba chakula.
Pili, Ngamia angebeba nini kutoka Hijaz huko Arabia? Je, angesafirisha tende? Mtu
anayesikia kuhusu misaada atadhani kuwa ni maelfu ya misafara ambayo kila mmoja
85
unakuwa na Ngamia mia moja wanaosafiri baina ya Hijaz na Syria na baina ya Hijaz na Iraq
wakiwa wamebeba chakula, nguo, silaha na misaada mingine. Je, jambo hilo ni sahihi?
Je, Ngamia ndiye aliyekuwa sababu na chanzo cha ushindi uliopatikana Armenia, Iran,
Afrika ya kaskazini na Indonesia?
Ngamia huyo alikuwa wapi katika vita vya mpakani mwa India na China?
Saunders anayedai kuwa Uislam ni vuguvugu la kikoloni ameghafilika na vitu viwili: -
(1) Ukiulinganisha utekaji mbalimbali ulioshuhudiwa na historia za harakati
za ukombozi wa Kiislam tutaona tofauti haraka sana.
(2) Ukoloni na athari zake vinahitaji kuchambuliwa ili kujua ikiwa Uislam nao
uliacha athari kama hizo.
1. Historia ya harakati mbalimbali za Uvamizi wa Nchi:-
Historia ilishuhudia watekaji wanao hamahama walio muhimu zaidi
Wakiwa:-
(a) Hixus „wafalme wachunga Kondoo‟ walioivamia Misri na kuitwaa
kwa nguvu, lakini baadaye waliondoka wakiwa wameshindwa na wakibeba
pamoja nao ustaarabu wa bonde la mto Nile, dini yake, njia na mbinu za
maisha.
(b) Alexander the Great aliyefanya uvamizi wake na kujaribu kuanzisha
ustaarabu wa ulimwengu kwa kufuata mfano wa Ugiriki. Ustaarabu mpya
ulioibuka chini ya jina la “Kigiriki” ambao walikuwa ni mchanganyiko wa
Kigiriki na ustaarabu wa nchi zilizokaliwa.
(c) Wahunes, Wajerumani na Wafindal, makabila haya yalikuja Ulaya
yakitokea Asia ya kati na pwani za Bahari ya Khazar. Waliweza kuubadili
wajihi wa kisiasa wa Ulaya, uvamizi wa makabila haya ulipewa jina la vita vya
kishenzi kwa sababu uliambatana na ukatili, umwagaji damu, uharibifu na
uchomaji moto wa miji.
Makabila haya ya kuhamahama yaliweza kuweka vitengo vya kisiasa na falme
zenye nguvu kuanzia Hispania mpaka Ujerumani lakini punde tu upanga wao
ukawa na kutu na ufalme wa Kirumi ukawameza wachunga Kondoo hawa wa
86
kuhamahama na kuwayeyusha na huo ukawa mwisho wa mfunuo wao wa
kufikiri.
(d) Makabila ya Mongoli yaliubadilisha wajihi wa Asia kutoka China
mpaka Palestina. Ufalme wa Gengiz Khan ukawa mkubwa sana na
Hulagu akaweza kuikamata Baghdad mji uliokuwa umestaarabika zaidi wakati
huo.
Lakini je, Wamongoli waliweza kuweka ustaarabu ambao ungeweza kuumeza
ustaarabu wote wa nchi walizoziteka? Sisi wote tunafahamu kwamba
hawakuweza kufanya hivyo, waliyeyushwa katika ustaarabu wa nchi
walizoziteka na wakaungana na dini zao. Hivyo, utekaji wao ulibadilisha
mifumo yao ya kufikiri na wakaingia katika Uislam.
Mwisho kabisa, kwanini ustaarabu wa Byzantium kwa upande mmoja na ustaarabu wa
Kifursi kwa upande mwingine, hazikuweza kuumeza Uislam wa Waarabu wanaohamahama?
Jawabu liko wazi kabisa wale waliotokea katika Peninsula hii waliupelekea ulimwengu
ustaarabu madhubuti. Walibeba ujumbe wa Mungu wakiongozwa na malezi na utakasifu wa
Muhammad kwao. Hivyo waliweza kushamiri sio kutawanyinywa, wakang‟ara sio kufutwa.
Walikuja na upendo, undugu, usawa na ukombozi kwa watu waliowapokea kwa moyo
mkunjufu.
Staarabu zenye umri mkubwa hazikuwameza kwa sababu sio tu kwamba hazikufanikiwa
katika uwanja wa vita bali pia katika uwanja wa udugu wa kibinadamu, sayansi, fikra na
falsafa, kufuta tofauti zote za kimatabaka pamoja na utimbakuwiri na kiburi cha watawala.
Harakati za ukombozi wa Kiislam hazikupelekea kuwepo kwa tabaka la wavamizi na
wavamiwa, mtu bora na mtu duni. Bali zilipelekea kuwepo kwa uhuru na amani miongoni
mwa wanaharakati hao na watu husika zilipelekea kuwepo kwa umoja wa imani na fikra.
Miongoni mwa sababu za ushindi na kuendelea kwa Uislam ni maasi ya hali ya juu
waliyosifika nayo wanajeshi wa Kiislam ambapo kwa ujinga Mustashriqiina waliita kuwa
„nguvu ya siri‟. Walikataa kukubali kuwa ni nguvu ya imani iliyokuwa katika nyoyo za
wanajeshi waaminifu, walioonesha kiwango kikubwa cha ujasiri ambao ungewapatia
umashuhuri duniani kote, kama wangeyaweka wazi majina yao au wangejionesha. Lakini
walifanya waliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwani walitaka mali kutoka kwake
tu. Kuna matukio kadhaa yanayoweza kuthibitisha hoja yetu.
87
Katika medani fulani ya mapambano Waislam walipata mashambulizi na hujuma nyingi
kutoka kwa adui maalum. Suala hili lilimfanya kiongozi wa Waislam hao atangaze zawadi
ya dinari elfu moja kwa atakayemuua adui huyo. Walipoamka asubuhi walikikuta kichwa
cha adui hemani mwa kiongozi wao, hawakumtambua mtu aliyemuua adui yao mara nyingi
walimtaka askari huyo shujaa aliyetekeleza mauaji hayo ajitokeze lakini hakuna
aliyejitokeza.
Kisha kiongozi huyo aliomba na kusihi sana kwa jina la Mungu kwamba askari huyo
ajioneshe, mtu mmoja asiyejulikana alijitokeza huku akiwa amevaa kinyago „Mask‟ usoni
mwake. Alipewa zawadi lakini aliikataa akisema kuwa alifanya alivyofanya kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu tu. Alikataa hata kutaja jina lake kwa sababu alichelea kwamba
wangelitangaza kila mahali na hivyo kumpotezea thawabu zake na kumfanya ajifakharishe,
kwa hiyo akawasihi wamuache.
Wakati mmoja, Khalifa Omar alitaka ushauri juu ya mtu atakayeteuliwa kama gavana wa
jimbo moja muhimu. Aliikataa idadi ya majina ya watu, hata Abd-al-Rahman ibn Auf,
akisema: kuwa Abdul-Rahman alikuwa mtu laini na hapo wakamuuliza kuwa alitaka mtu
wa aina gani.
Omar akasema: “Nataka mtu atakyeonekana kuwa mtu wa kawaida anapokuwa kiongozi
katika kundi la watu wake, na aonekane kama kiongozi wao anapokuwa si kiongozi wao.”
Kisha walimpendekeza Al-Rabi Al-Harithi, akakubali pendekezo hilo.
Uchaguzi makini wa magavana ni miongoni mwa sababu zilizowafanya watu wawapende
wale walioziteka nchi zao. Gavana sio tu kwamba alikuwa baba wa Waislam, bali pia
alikuwa mtumishi wao.
Vijana wengi ambao nchi zao zilitekwa walisimama imara kuutumikia Uislam na elimu
zake. Waliweza hata kua viongozi na mashujaa waliobeba bendera ya watekaji na kwenda
nao Sanjari kuueneza Uislam kwa moyo wa dhati na kujitolea.
Dounty anasema: kwamba mazungumzo ya Waislam siku zote yalihusu Uislam na imani
popote pale walipokwenda. Iliwapa furaha na faraja wote kwa sababu mazungumzo hayo
yalielezea dini sahihi ambayo msingi na malengo yake ni „Hakuna Mungu isipokuwa
Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake‟
Marocci, aliyeishi karne ya kumi na saba, anasema: Bila kujali siri za maumbile
zinavyoweza kuwa rahisi ni vigumu sana kuzielewa ikilinganishwa na uwazi na urahisi wa
Qur‟an, unaoifanya iwe rahisi kuisoma na kuielewa.
88
Uislam katika chimbuko lake ni dini ya umma kwa maana kamili ya neno hilo ikiwa na
mfumo rahisi sana. Hapa ndipo ilipo siri ya mafanikio na ufanisi wa juhudi za walimu
„wahubiri‟ wa Kiislam. Dini ya Kiislam siku zote imekuwa na nguvu ya kufaulu kuingia
katika ufahamu na uelewa wa watu.
Askofu Lefray anaamini kuwa siri ya nguvu ya ajabu ya Uislam ipo katika imani thabiti ya
kuwepo kwa Mungu, ambayo ndio ukweli halisi wa ulimwengu huu. Imani hiyo iliwapa
Waislam wengi uwezo usioshindikana wa kupambana iliwashawishi kukidharau na kukibeza
kifo, kitu ambacho hakikuwepo hata kidogo katika tawala zote zilizotangulia. Uti wa
mgongo wa sifa yao ilikuwa ni msimamo, nguvu ya utashi na subira yao, ambayo haikupata
kujua kitu kinachoitwa “malalamiko”. Iliwafanya wawe wema na wazuri.
Hamasa ya hali ya juu ya wanaharakati hao dini yao iliyojumuisha fikra na misingi
iliyoafikiana kikamilifu na hoja na sifa yao iliyojionyesha katika sekta zao zote za kijeshi na
kiuongozi, vilimfanya Mwislam kuwa mtu wa kipekee katika udhanifu “Idealism”
akiuwakilisha umma wote na hata kuwa kitovu cha ulimwengu.
Zaidi ya hayo jeshi la Kiislam lilijiainisha kwa sifa ambayo ilikuwa nadra, na hata
kutopatikana katika jeshi au taifa lolote, yaani Mwislam wa kawaida au mwanajeshi
asingeweza kusalimu amri au kushindwa kama kiongozi wake angekufa katika uwanja wa
mapambano, kwani kiongozi mpya angechaguliwa haraka sana kama ilivyotokea katika vita
vya Muta, Buwaib na Nahawand. Katika historia tunasoma kwamba Wahune, Wajerumani
na Wamongoli walikuwa kama kundi la Kondoo likimfuata mchungaji wake, lingetawanyika
pindi mchungaji huyo angefariki kama ilivyotokea baada ya kuuliwa kwa Atilla au Genghiz
Khan. Wakati fulani ililichukua kundi hili miaka mingi kujikusanya tena chini ya uongozi
wa mchungaji mpya.
Mwislam alikuwa sehemu ya msafara ambao uelekeo na malengo yake vilikuwa tayari
vimepangwa ambapo kifo cha kiongozi husika kisingeathiri au kuzuia safari ya msafara huo,
kwani kiongozi mpya angejitokeza kuja kuuongoza kwenye njia iliyopangwa pamoja na
kukamilisha kile kilichokuwa kimeanzishwa na mtangulizi wake.
Na sasa, ingawa utawala wa kisiasa wa wanaharakati hawa ulipita muda mwingi uliopita,
ustaarabu wa Kiislam ---- licha ya harakati za kimisionari za Kikristo kuupiga vita ---- bado
upo katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Uislam.
Nyoyo na nyuso za mamia ya mamilioni ya watu wa maeneo haya bado zinaelekea Makkah
katika sala mara tano kwa siku na huelekea Hijja au kutembelea maeneo haya matakatifu ya
Uislam, na anapotajwa Mtume wa Uislam, Muhammad watu hawa humtakia rehma na
89
kumpelekea salamu zao kwa heshima kubwa na upendo. Sasa nguvu ya kisiasa au ya kijeshi
ya Uislam ipo wapi?
Uislam umeendelea kuwapo huko kwa sababu Waislam hawakuwa sawa na wavamizi
wengine. Hawakuupeleka Uislam kwenye mataifa hayo, bali waliyapeleka mataifa hayo
kwenye Uislam. Uislam ni dini ya kipekee ililazimika kupigana vita tatu kwa pamoja; vita
dhidi ya Byzantine huko Syria, makabiliano na Fursi huko Iraq na makabiliano na Afrika
huko Misri, ambapo katika vita hizi tatu Uislam ulishinda kwa sababu ulijaaliwa nguvu hii
isiyoonekana.
Mheshimiwa Hakimu, Sasa niruhusu nizungumzie ukoloni na kuonesha tofauti iliyopo
baina yake na harakati ya Kiislam.
Ukoloni una maana ya mtu kumtawala mtu mwingine, au jamii fulani kuitawala jamii
nyingine au taifa moja kulitawala taifa jingine, kwa lengo la unyonyaji. Baada ya uvumbuzi
wa kijiografia wa zama za sasa ulimwengu ulipata kujua pupa ya ushindani wa kikoloni
mbali mbali za ukoloni.
(1) Ukoloni wa Makazi:-
Hapa taifa fulani huwaangamiza wakazi asilia wa eneo fulani au kuwatoa
katika nchi yao na kuwabadilisha na raia wake wenyewe kama ilivyotokea katika
kadhia ya Amerika na Australia, ambapo Wahindi wekundu hapo zamani na wakazi
wa asili hapo baadaye waliangamizwa na huko Palestina ambapo Wapalestina
walitawanywa kila mahali.
(2) Ukoloni wa Kijeshi:-
Hapa tunakuwa na utawala wa jeshi la kigeni ambalo hudhibiti moja kwa
moja mambo ya nchi fulani na kuinyonya bila huruma, kama ilivyokuwa kwa ukoloni
wa Kiingereza nchini India.
(3) Hadhi ya Nchi iliyochini ya himaya ya Nchi nyingine:-
Hapa mambo ya nje, usalama, ulinzi na uchumi wa nchi fulani hudhibitiwa
na mamlaka ya kigeni, huku mambo ya ndani yakiachiwa wananchi wa nchi hiyo.
(4) Kukabidhi madaraka ya nchi kwa nchi nyingine (Mandate):-
Mfumo huu ulitengenezwa na Shirikisho la Mataifa „League of Nations‟
90
kufuatia vita vya kwanza vya dunia, „ibara 22 ya azimio lake‟. Ni aina iliyoboreshwa
ya ukoloni inayolenga, lakini mara nyingi ilibadilika na kuwa unyonyaji mkubwa
dhidi ya nchi husika.
Ukoloni umeendelea katika mtindo mpya uitwao ubeberu ambao ni mfumo au muundo mpya
wa ukoloni wenye malengo ya kutawala uchumi na maliasili za nchi nyingine na wakati huo
huo ukiiruhusu nchi hiyo kuwa na jeshi lake, uwakilishi wa kimataifa pamoja na kujiunga na
umoja wa mataifa. Mbali na picha ya kijeshi na kiuchumi ya ukoloni mambo mengine
mabaya yalitokea kama vile:-
Ununuzi na usafirishaji wa Waafrika weusi waliotoroshwa mamilioni kwa mamilioni
na kupelekwa Marekani na Ulaya ili watumike katika kazi ngumu za mikono kama
vile uchimbaji wa madini.
Maangamizo makubwa ya watu wa Amerika na Australia na ufukuzwaji wa
Wapalestina uliofanywa na Wayahudi.
Ubaguzi wa rangi huko Amerika, Rhodesia „Zimbabwe‟ na Afrika ya kusini au
ubaguzi wa kidini katika nchi inayokaliwa kimabavu ya Palestina.
Migogoro ya kuendelea miongoni mwa nchi za Kikoloni, ambazo hupigana ili kupata
mali nyingi zaidi kutoka nchi zinazotawaliwa kama ilivyotokea kati ya Hispania na
Ureno kati ya Ireland na Uingereza na Ureno na Uingereza na Uholanzi.
Uporaji wa mali za watu hususan mali ghafi pamoja na uanzilishwaji wa uzalishaji
mpya huko Ulaya na Marekani uliofanywa kwa gharama za watu hawa.
Kuendelea kwa ukoloni kuwa wa changamoto zaidi na wa kibepari, unaolenga kuwa
na ukiritimba wa kiuchumi, uwekezaji rasimali na shinikizo za kiuchumi.
Kuzifukarisha nchi zenye mashamba na kuzifanya kuwa mashamba yao pamoja na
kuzibana kwa mikopo ya muda mrefu yenye mashariti ya mashirikiano mbali mbali
pamoja na mambo ya kijeshi.
Madhara yatokanayo na Ukoloni:-
Matokeo ya Ukoloni:-
- Kugawa na kupokonya ardhi.
91
- Madhara ya kiuchumi kwa nchi zilizotawaliwa.
- Kuzifanya nchi zilizotawaliwa ziendele kuwa tegemezi juu ya nyenzo za msingi za
uzalishaji na kilimo.
- Uingiliaji wa mahusiano ya kiuchumi na kuweka vizuizi vya kiuchumi kama vile
ukiritimba na uporaji.
- Uharibifu wa viwango vya maisha katika nchi zilizotawaliwa huku viwango hivyo
vikiimarika katika nchi za Wakoloni kwa gharama ya nchi zilizokaliwa kikoloni.
- Uduni wa huduma za afya na huduma mbali mbali za msingi.
- Kushamili kwa ujinga na kiwango cha chini cha elimu.
- Upungufu wa wataalam wachumi na wasomi mbali mbali, jambo lililozuia
maendeleo ya kiuchumi.
- Kushamiri kwa utumwa huko Ulaya na Marekani.
- Nchi za kibaguzi bado zipo, ambapo weupe wachache huwatawala weusi walio
wengi, kama ilivyo katika Rhodesia na Afrika ya kusini.
Mheshimiwa Hakimu: Sasa je, tunawezaje kuiita harakati ya Kiislam kuwa Ukoloni baada
ya kuwa tumedurusu maana ya ukoloni na madhara yake? Hakika Uislam haukuwa ukoloni
katika maana hii kwa sababu zifuatazo:
(1) Uislam uliwakomboa watumwa.
(2) Uislam haukubali maangamizo dhidi ya watu wote tunayakumbuka
maagizo ya Abu Bakr Khalifa wa kwanza wa Uislam kwa askari wa Kiislam.
(3) Uislam ulipinga ubaguzi wowote wa rangi au ukaliaji wa kimabavu.
Msimamo huu wa Uislam umeelezwa kwa uwazi na Mtume. Hakuna
tofauti kati ya Mwarabu na asiye Mwarabu au kati ya mtu mweupe na mweusi
isipokuwa kwa ucha Mungu „unyoofu wa imani‟. Uislam ulimnyanyua mtumwa
mweusi, Bilal juu kwenye Kaaba akawaita watu kwenye Sala akisema “Allahu
Akbar” Uislam ulimfanya Salman Muajemi kuwa mwanafamilia ya Muhammad.
92
(4) Ama kuhusu unyonyaji wa mali za watu tunakurejesha kwenye kesi
tuliyozungumza kuhusu watu wasio Waislam walioishi katika nchi ya Kiislam na jinsi
walivyoondolewa mzigo wa kodi kubwa zilizotozwa na watawala wao huko Uajemi
na Byzantium. Kile walichokuwa wakikitoa kwenye hazina ya Serikali ya Kiislam
kilikuwa si chochote ikilinganishwa na kile walichokuwa wakikitoa kwenye Serikali
zao za awali na ikilinganishwa na huduma walizopewa na Serikali ya Kiislam kama
fidia ya kodi yao hiyo. Kodi iliyotolewa na Waislam ilikuwa kubwa zaidi ya ile
iliyotolewa na wasio Waislam.
(5) Ustawi mkubwa wa nchi husika uliongezeka sambamba na usalama na
amani iliyoshamili kila mahali kama ilivyotokea katika bonde la mto Nile na Iraq,
ambapo gavana mpya wa Kiislam alipendwa na kuheshimika sana kuliko watawala
wao wa awali. Walishuhudia kwake mema yote ya Uislam kwa vitendo sio kwa
maneno matupu.
Mwamko mkubwa katika sayansi na tiba ulishamili, hospitali zikafunguliwa, vitabu
vikatafsiriwa, maarifa ya zamani yakapitiwa upya na Waislam wa kiarabu, wakazi wa
Kiislam, na wananchi wa nchi zilizotekwa. Wasomi wengi ambao umashuhuri wao ulienea
kila mahali walitokana na nchi hizi zilizotekwa, kama vile Avicenna, Al Razi, Al Bukhari,
Beiruni na Khawarizmi ambao walitoka Uajemi na mashariki ya mbali.
Wakati mmoja Gustav Lebon aliulizwa juu ya kile ambacho kingeitokea Ulaya iwapo
Waarabu wangeshinda vita ya Poitie huko Ufaransa. Alijibu akisema: Ulaya ya kishenzi
ingebadilika kama Hispania ilivyobadilika chini ya ustaarabu wa Kiislam uliostawi huko
chini ya bendera ya Mtume Mwarabu, Muhammad. Hakuna tofauti na migogoro ya kidini au
uasi ambao ungetokea au umwagaji damu ulioshamili Ulaya nzima ambapo ungetokea kwa
karne nyingi yaani yote hayo yangekoma iwapo Uislam ungeshinda huko.
Pamoja na imani ya kuamini Mungu mmoja, je Uislam ulishamilisha maarifa au ujinga, nuru
au giza? Sisi wote tunafahamu vyema kwamba ukoloni ni ujinga na Uislam ni elimu na
maarifa. Sasa vitu viliwezaje kukutana? Ukoloni ni uharibifu na Uislam ni ujenzi, sasa
viliwezaje kuwa sawa? Wimbo uliokuwa ukiimbwa na jeshi la Ki-Italia lililovamia Libya
mwaka 1911 ni huu ufuatao:-
“Mama, kamilisha sala yako na usilie, cheka na utafakari. Hujui kwamba Italia inaniita?
Nina kwenda Tripoli nikiwa na raha na furaha kumwaga damu yangu katika kulipiga taifa
lenye laana na kupambana na dini ya Kiislam. Nitapambana kwa nguvu zangu zote
kuingamiza Qur’an. Kama sitorudi usimlilie mwanao kama ndugu yangu akikuuliza kwa
nini huna huzuni mwambie nilikufa nikiupiga Uislam”
93
Kutokana na maelezo hayo tunapata kuona yafuatayo:
1. Kuliomba Taifa lililolaaniwa:-
Mwislamu hawapigi watu hovyo hata wakuu wa wilaya au nchi zilizotekwa kwa
sababu yupo kwa ajili ya uongofu. Katika wimbo uliotangulia tunasikia mauaji, lakini
katika Uislam tunakuta uhai wa watu ambao nchi zao zimetekwa.
2. Kuiangamiza Qur‟an na Uislam:-
Tunasoma katika Qur‟an:
“Sema: Enyi watu wa Kitabu njooni katika neno
lililo sawa baina yetu na baina yenu, tusimwabudu ili Mwenyezi Mungu tu, wala
tusimshirikishe na chochote” (3)
Hivyo, Uislam ni tangazo la wito, lakini ukoloni ni uvunjanji na maangamizi, kwa
hiyo kamwe havitokuwa sawa.
Hapa kuna ushahidi usiokuwa wa kibaguzi uliotolewa na Lirden Hodis, Mmsionari
katika bara la Afrika alioutaja katika kitabu chake „Islam in East Africa‟. Baada ya
kudurusu tofauti kubwa iliyopo baina ya athari ya walioiacha Waarabu huko Afrika ya
kaskazini na ile ya watu wa Ulaya, alieleza kwamba Wareno walikaa miaka mia mbili
barani Afrika na hawakuacha athari yoyote yenye maana. Kitu pekee walichokiacha
nyuma yao ni kumbukumbu ya uharibifu katika shule na maeneo matakatifu ya
Waislam. Kila mahala walipokwenda walifanya uporaji na maangamizi, lakini
Waarabu waliokwenda maeneo ya Pwani, walipeleka huko uandishi, ujenzi (usanifu
wa majengo) na nyenzo za ustaarabu wakiacha mahali hapo alama mbalimbali katika
vipengele vingi vya maisha.
Kushamiri huku kwa uharibifu kulikofanywa na mabeberu wa kikoloni,
hayakutokana barani Afrika pekee, bali pia katika maeneo mengine.
Wachunga Ng‟ombe (Cow Boys) waliwafanyia nini Wahindi Wekundu, wenyeji wa
Marekani?
Ufaransa ilifanya nini huko Algeria?
Jibu ni “Vifo vya Waalgereia milioni moja” na kabla ya hapo sera ya ardhi
iliyochomwa.
94
Uingereza ilifanya nini huko Australia au Afrika ya Kusini?
Jibu ni maangamizo na ujenzi wa makazi ya kikoloni na ubaguzi wa rangi.
Hispania na Ureno zilifanya nini huko Amerika ya Kusini?
Jibu ni kufifia kwa usataarabu wa Innca, Moya na Aztik na maangamizo makubwa
dhidi ya wakazi wake asilia na misafara isiyokoma ya dhahabu na fedha kwenda
Hispania na Ureno.
Uholanzi ilifanya ninn katika Indonesia?
Jibu ni kuwanyonya watu, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha. Pindi askari wa
Kikoloni alipotaka kumpanda farasi wake, alikuwa akikanyaga kwa kiatu chake cha
kijeshi juu ya mgongo wa raia wa Indonesia.
Marekani iliyostaarabika ilifanya nini huko Vietnam?
Jibu ni; mamilioni ya mabomu yaliyodondoshwa juu ya vichwa vya watu wasiokuwa
na hatia.
Juu ya yote hayo, ujinga, uduni na ukiritimba wa kiuchumi vilienea na kushamili kila
walipokwenda wakorofi hawa.
LAKINI KUHUSU UISLAM:-
1. Mara zote tulizoea kuwasikia Waislam wakiwaambia watu wa nchi
walizoziteka: “Sisi sote pamoja tuna haki sawa na majukumu sawa”
2. Kama watu wa Homs wangekuwa wameona Ukoloni wowote ndani ya
Uislam wasingelia, pindi Waislam walipotaka kuondoka katika mji wao. Walilia kwa
sababu waliwaona kuwa ni waaminifu kwa maneno na vitendo; waaminifu kimwili na
kiroho.
3. Je, Uislam haukumweka katika daraja sawa mtoto wa jemedari aliyeiteka
Misri na kijana wa Kimisri pindi Omar Ibn Al-Khattab alipomwambia huyo Mmisri:
“Mpige mtoto wa bwana (bosi/lodi)”
95
Tukio hili linaonesha namna Khalifa wa Kiislam alivyowatendea Mwislam na Mmisri
kwa usawa kama wananchi wenye haki ya kupewa ulinzi na kupewa uhuru dhidi ya
dhulma.
4. Je, wanaharakati wa ukombozi wa Kiislam hawakuwaambia wananchi wa
nchi zilizotekwa: “Ingieni katika Uislam nasi tutaondoka” yaani njooni katika nuru
na uongofu ambao Mwenyezi Mungu ametuamuru kuueneza nasi tutaondoka kwa
sababu hatuna mamlaka yoyote juu yenu. Je, huo ni ukoloni? Je, Omar ni Mkoloni?
Je, hakutangaza haki za binadamu mamia ya miaka iliyopita pale aliposema: Kwa nini
unawafanya kuwa watumwa watu ambao mama zao wamewazaa wawe huru?
Mwangwi wa maelezo kama hayo ulijaa duniani kote baada ya kufanywa kuwa alama
ya mapiduzi ya Kifaransa ya mwaka 1789. Wakati ambao Omar alitoa maelezo hayo
na kuyatumia ilikuwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Je, huu si ushahidi wa wazi
kwamba walikuwa na imani kubwa katika uhuru? Zaidi ya hapo, hapa kuna tukio
linaloonesha uadilifu mkubwa waliokuwa nao Waislam.
Mji wa Samarkand ulio katika eneo la Asia ya kati uliwekwa chini ya ulinzi wa
Waislam kwa kiasi kadhaa cha pesa kilichotolewa na watu wa mji huo kulingana na
makubaliano ya kawaida yaliyokuwepo baina ya pande hizo mbili.
Inasimuliwa kuwa Qutaiba, kiongozi wa jeshi la Kiislam, alikitweza kiasi kile cha
pesa akavunja masharti ya mkataba na kuuteka mji huo na kuuweka chini ya utawala
wa ukhalifa wa ukoo wa Umayya mnamo mwaka 715 A.D.
Miaka mingi baadaye, pindi Omar Ibn Abdul Aziz alipokuwa Khalifa, ambaye
umashuhuri wa uadilifu wake ulienea kila mahali, ujumbe kutoka Samarkand ulikuja
kwake na kulalamika kwamba mji wao ulichukuliwa kwa nguvu kinyume na kanuni
zote za Kiislam.
Aliuagiza ujumbe huo kwenda kwa gavana wa Kiislam huko Samarkand, Salman Ibn
Abi Sarh, wakiwa na mielekezo ya kutaka kuhakikisha kisa hiki.
Hakimu aliteuliwa na mashahidi kutoka pande zote mbili wakaitwa. Kutokana na
maelezo ya askari waliokuwa katika jeshi la Qutaiba wakati wa tukio hilo, hakimu
alikuta kwamba Qutaiba hakuwa amewapa watu wa Samarkand chaguo lolote zaidi ya
vita na aliitwaa nchi yao kimabavu.
96
Baada ya kusikia hayo hakimu alitoa amri za wazi kwamba jeshi la Kiislam linatakiwa
kuondoka Samarkand haraka sana pamoja na Waislam wote walioingia nchini humo
baada ya uvamizi ule.
Hakuna mtu aliyetarajia hakumu hii, au kwamba hakimu angeweza kuwa na nguvu ya
kuliamuru jeshi kuondoka katika mji fulani baada ya kuuteka.
Khalifa alipotaarifiwa juu ya hukumu ile na kuombwa ushauri wake, Khalifa
alimuagiza gavana kutekeleza kabisa hukumu hiyo bila kuchelewa hata kidogo.
Gavana akaliagiza jeshi lijiandae kuondoka na Waislam waondoke mjini hapo.
Maandalizi yakiwa yamefanyika, kambi zikahamwa, mali zikauzwa na Waislam
wakiagana kitu ambacho hakutarajiwa hata kidogo kilitokea. Ujumbe kutoka kwa
watu Samarkand ulikwenda kwa gavana ukamuomba kubatilisha amri ya kuhama,
kwani hawakuwa wakitarajia kwamba hakimu angethubutu kuliamuru jeshi liondoke
katika nchi iliyotekwa kawa upanga. Kamwe hawakundelea kiasi kikubwa namna ile
kwa kufikia hatua ya kutoa hukumu dhidi ya raia wenzake.
Waliendelea kusema kwamba haikuwahi kuwatokea kwamba Khalifa mwenyewe
akaunga mkono uamuzi wa hakimu na kuliamuru jeshi lake kuondoka licha ya
kuathiriwa na mashambulizi mengi.
Kwa hiyo waliachana na matakwa yao yote na wakalitaka jeshi la Kiislam na Waislam
waendelee kubaki Samarkand kwani wasingetendewa vibaya na watu hao na hakuna
madhara yoyote ambayo yangetendwa dhidi yao.
Kwa kutambua kwamba walikuwa na nia ya dhati ya kutaka jeshi la Kiislam libaki,
amri ilitolewa kwa jeshi hilo kuanza tena majukumu yake na Waislam wakatakiwa
kurudi kwenye shughuli zao ambapo pande zote mbili zilijawa na furaha kubwa. Sio
ajabu kuona kwamba suala hili likawa mhimili mkubwa kwa watu wa Samarkand
kuingia katika Uislam.
Waislam hawa wapya waliweza hata kuwa wasomi wakubwa wa Uislam,
waliutangaza Uislam na kuufanya mji wao kuwa miongoni mwa vitovu vikubwa vya
Uislam ambapo watu wengi kutoka kila mahali na kila namna waliutembelea kwa
lengo la kupata elimu na maarifa. Tukio hili la kipekee huwafanya Waislam wote
waone fakhari juu ya uadilifu unaondelea kuwepo katika Uislam kwa miaka mingi.
97
Sasa inawezekanaje kwa mtu mwenye akili adai kwamba Uislam ulikuwa na ukoloni
katika vita vyake? Kama Uislam ungekuwa ukoloni, watu wa Samarkand
wasingekwenda kwa Khalifa Omar Ibn Abdul Aziz, kutaka maamuzi ya kisheria, jeshi
lisingeondoka na watu wa Samarkand wasingeliomba jeshi hilo kuendelea kubaki.
Katika kuhitimisha tunanukuu maoni ya mwanafikra na mwanahistoria wa Kihispania
Sansit Olbernot, kuhusu utekaji uliofanywa na Waislam huko Hispania:
Utwaaji wa Hispania uliofanywa na Waarabu ulileta mema tupu. Je ukoloni wa
Ulaya au wa Kiamerika ulileta mema kwenye nchi walizozitwaa kwa nguvu?
Aliendele kusema:
“Wananchi wa nchi zilizotwaliwa walimtukuza Mwenyezi Mungu kwa sababu ya
kuwa Waislam, nao wakajiunga dini ya watu waliitwaa nchi yao. Je watu wa
makoloni ya Waitalia, Wareno au Waingereza walimtukuza Mungu kwa kutawaliwa
na Wafaransa au Waitalia? Hapana kabisa kwa nini?”
Rejea:
1. Saunders kutoka gazeti la History Today
2. Marier Koli: The Search for True Religion (kilichotolewa na Union of Christian
Teaching Institution, Paris, 1978.
3. Qur‟an (3:64)
98
KESI YA KUMI
Uislam na Utumwa
Mwendesha Mashtaka anasema: Utumwa ndio uliokuwa mhimili wa maisha ya kiuchumi
ya watu wa zamani na Muhammad hakuutendea mfumo wa utumwa lolote jema kuliko ulivyofanya
Ukristo wa mwanzzo”. “Hakukomesha utumwa kikamilifu”. “Hivyo utumwa ni mashaka
yaliyoletwa na Uislam”.
Baada ya mwendesha mashtaka kukamilisha hoja yake, hakimu mwenye busara aliutaka Uislam
kujitetea. Uislam ukasema:
“Mheshimiwa Hakimu! Utumwa katika Uislam umekuwa silaha kubwa ya kampeni kali
zinazofanywa dhidi ya Uislam. Watu walio nyuma ya kampeni hizi ni wakanaji wa dini, makundi
ya mahubiri na baadhi ya Mustashriqiina ambao kazi yao ni kuchafua jina la Uislam na kuusingizia.
Lengo la watu hawa ni kueneza mawazo yao miongoni mwa vijana wa Kiislam, hususan wale
wasioielewa dini yao, ili kupandikiza mbegu ya shaka dhidi ya Uislam ndani ya akili zao, hasa hasa
kuhusu suala la utumwa. Hakika Uislam ndio dini ya kwanza kutunga sheria kwa maslahi ya
watumwa. Hata ustaarabu wa Kimagharibi haukuweza kufanya chochote kilicho sawa na kile
kilichofanywa na Uislam kwa ajili ya haki na uhuru wa watumwa.
Wale wanaoushambulia Uislam wanaitambua vyema historia ya biashara ya utumwa. Wanajua kwa
yakini kuwa biashara hiyo ilifanywa na makampuni ya Ulaya na yale ya Kimarekani yaliyokuwa
yakiwatumia madalali mbalimbali wasiokuwa Waarabu na wasiokuwa Waislam. Ukweli huu
haujulikani kwa vizazi vya Waarabu wa sasa ambao wamesoma katika shule za kimisionari.
Hakika, Qur‟an Tukufu haina Aya hata moja inayohamasisha utumwa. Halikadhalika hadithi za
mtukufu Mtume Muhammad (S.A.W.).
Na sasa, Mheshimwa Hakimu, nitatazama namna mataifa mbalimbali yalivyoshughulika na
utumwa:-
1. Misri: Mapiramidi, mahekalu na minara mirefu iliyo mashuhuri ilijengwa na watumwa.
2. China: Utumwa ulikuwa jambo la kawaida kwa sababu ya umasikini. Mtu aliweza kujiuza au
kuwauza wanae ili kupata pesa.
3. India: Walikuwa na mfumo wa kimatabaka. Watumwa ambao ndio waliokuwa wengi hawakuwa
na haki ya kumiliki kitu chochote.
4. Uajemi: Waliamini kuwa watawala walikuwa na damu ya Mungu katika mishipa yao ya vena.
Hivyo walichukuliwa kuwa juu ya binadamu wengine na watu wote walikuwa watumwa wao.
99
5. Ugiriki: Utumwa ulikuwa wa dhahiri na kitu kilichozoeleka sana. Maharamia wa Kigiriki
waliwateka watu kutoka mataifa mengine na kuwauza katika masoko ya Athens na miji mingine.
Kulikuwepo na masoko maalumu ya watumwa na kaya za Kigiriki zilikuwa zimejaa watumwa
wanaume kwa wanawake.
Wanafalsafa wa wa Kigiriki waliwagawa watu katika sehemu mbili: Mtu aliye huru kwa asili na
yule aliye mtumwa kiasili. Waliamini kwamba watumwa waliumbwa kwa ajili ya kuwatumikia
mabwana zao tu. Mtumwa alipaswa kufanya kazi za kimwili, wakati ambapo Mgiriki ambaye
alikuwa huru kwa asili alifanya kazia za kiakili pamoja na kazi muhimu ya utawala.
Plato, katika Jamhuri yake ya Mfano, aliamini katika kuwanyima watumwa haki yoyote ya uraia na
kwamba walitakiwa tu kuwatii mabwana zao. Mwanafunzi wa Plato, Aristotle alikubaliana na
mwalimu wake na kuamini kuwa neno “raia” ni kisawe cha neno “huru”. Aliamini pia kwamba kazi
ya watumwa ilikuwa kuipatia pesa familia husika na kuitumikia.
6. Warumi: Wafanyabiashara ya utumwa katika zama za Warumi walipata faida kubwa, hususan
wakati wa vita mbalimbali zilizotokea. Baada ya ushindi mkubwa uliochukuliwa kuwa heshima na
utukufu kwa Warumi, huku ushindi huo ukiwa aibu machoni mwa binadamu, mfanyabiashara
mmoja angeweza kununua watumwa elfu moja kwa wakti mmoja. Kulikuwepo na masoko maalum
kwa ajili ya watumwa katika mji wa Roma. Mara nyingi watumwa walikuwa wanaume na
wanawake, wazee na watoto ambao waliachwa uchi wa mnyama wakiwekwa tayari kwa wanunuzi
kuwaona na kuigusa miili yao kabla ya kuamua kuwanunua au la.
Sheria ya Kirumi haikumchukulia mtumwa kama mtu mwenye haki zozote za kibinadamu, bali
kikorokoro kama bidhaa nyingine inayoweza kuuzwa na kununuliwa.
Warumi pia walikuwa wakimfanya kuwa mtumwa mtu aliyeshindwa kulipa deni la aliyemkopa.
7. Wayahudi: Agano la Kale liliruhusu utumwa kwa kuwauza au kuwanunua mateka wa vita.
Myahudi angeweza kumnunua Myahudi mwenzake aliye maskini na iwapo angetaka kujiuza kwa
mtu tajiri. Wakati mwingine Myahudi angekuwa mtumwa wa tajiri aliyempa mkopo mpaka pale
atakapoweza kulipa deni.
Katika Agano la Kale tunasoma: “Kama ukimnunua mtumwa Myahudi atakutumikia kwa
kipindi cha miaka sita na katika mwaka wa saba atakuwa huru”.
Torati ilimruhusu Myahudi kumuuza binti yake awe mtumwa kwa Myahudi mwingine ambaye
alikuwa amemnunua binti huyo.
Na ama kuhusu vita, Torati inasema:
“Utakapokaribia mji katika vita, waite watu wake kwenye amani. Kama wakikubali na mji
ukawa wazi kwa ajili yako basi watu wote ni wako kwa ajili ya kuwafanya watumwa. Kama
wakikupiga, basi usiingiie na kama Bwana akikupa mji huo, wauwe wanaume wote kwa
upanga wako, lakini wanawake, watoto, wanyama na ngawira zote zitakuwa kwa ajili yake
100
kuzifurahia. Hivyo, ndivyo utakavyofanya kwa miji yote iliyo mbali nawe, miji isiyokuwa
katika mataifa yaliyokaribu na hapa. Lakini miji ya watu hawa uliopewa na Bwana wako
wauwe watu wake wote bila kuchagua”.
8. Ukristo: Dr. George Brest anasema kwamba Ukristo haukupinga utumwa. Iwe kisiasa au
kiuchumi, Ukristo haukuwahamasisha waumini wake kupinga desturi za vizazi vyao kuhusu
utumwa. Ukristo haukulijadili hata kidogo tatizo hilo na haukusema chochote kilicho kinyume na
haki za wamiliki wa watumwa na kimsingi haukutaka watumwa waachwe huru.
Paulo aliwataka watumwa wawatii mabwana zao kama wanavyomtii Yesu Kristo. Katika waraka
wake kwa watu wa Efeso, Paulo alisema:
“Enyi watumwa! Watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka,
kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo, walaa si kwa utumwa wa macho tu
kama wajipendekezao kwa wanadamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda
yampendezayo Mungu kwa moyo, kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si
mwanadamu mkijua kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa hilo hilo na Bwana,
kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru” (1)
.
Petro alitoa pendekezo kama hilo na kuwaagiza mapadri na makasisi kulifuata kwa sababu utumwa
ni ukombozi wa makosa ya binadamu, yaliyotendwa na watu kwa ajili ya kumghadhibisha Mungu
Mkuu. Mtakatifu Thomas Aquinas aliongezea mtazamo wa kifalsafa kwenye mawazo ya viongozi
wa kidini lakini hakuupinga utumwa, bali aliusifu, kwa sababu yeye, kama ilivyo kwa mwalimu
wake Aristotle, aliamini kuwa utumwa ni kadhia ya kiasili ambapo baadhi ya watu kiasili huzaliwa
wawe watumwa. Pia aliamini kuwa utumwa haukuwa ukienda kinyume na dini na kwamba
wanadamu wanapaswa kuridhika na bahati na maajaliwa yao ya hali ya chini.
Katika Larouse kubwa ya karne ya 19 mtu anaweza kuona maneno yafuatayo:
“Mtu hastaajabu kuwepo kwa utumwa na kuwa ni jambo la kawaida miongoni mwa
Wakristo mpaka leo. Wawakilishi wa kidini walikubali na kuamini kwamba utumwa ni
halali.
Kwa ufupi, Ukristo unaukubali utumwa moja kwa moja mpaka zama zetu za leo na ni vigumu sana
kuthibitisha kwamba Ukristo ulifanya juhudi ya kufuta utumwa.
9. Ulaya: Ulaya haina historia yoyote bali kama ile ya Wajerumani. Bwana Shafiq Basha katika
kitabu chake “Slavery in Islam” anazungumzia mawazo ya Wajerumani kuhusu utumwa kwa
kusema: “Wakati mwingine kamari iliwapalekea wale wachezaji sugu, kucheza michezo ya bahati
nasibu na kamari, kwa kuwatoa wake au watoto wao na hata kwa kuutoa uhuru wao. Kwa
Wajerumani hilo lilikuwa chanzo cha utumwa”.
101
Katika miaka ya kati mfumo wa kikabaila ulienea sana na wanavijiji walimilikiwa na malodi wao.
Wanavijiji hao wangeuzwa pamoja na ardhi pale ardhi hiyo inapouzwa. Hakuna yeyote kati ya
wanavijiji aliyekuwa na haki ya kwenda kwenye ardhi nyingine kwa sababu alikuwa mali ya
mwenye ardhi, kama ilivyo kwa mali nyingine.
Ilikuwa karne ya 19 tu ambapo utumwa ulikomeshwa. Kwa hakika utumwa ulikomeshwa Ulaya
pekee na kubakia Asia na Afrika. Utumwa ulienea kwa jina la ukoloni huko Asia wakati ambapo
katika Afrika ulikuwa ni utumwa wa kweli kweli na masoko ya watumwa yaliyofunguliwa na
wazungu yalistawi sana na kuleta faida kubwa kwa waendeshaji wake.
Katika karne za 16, 17, 18, na 19, waendeshaji wa biashara ya utumwa, wakishirikiana na baadhi ya
machifu wa makabila ya Afrika walikuwa wakizishambulia nyumba za Waafrika na kuwateka
watoto wao ili wakauzwe katika masoko ya watumwa.
Katika Ensaiklopidia ya Britanica Juz. 2 Uk. 779 chini ya neno “Slavery” kuna maelezo
yafuatayo: “Ukamataji wa watumwa kutoka katika vijiji vyao vilivyozungukwa na misitu
minene ilitokea namna hii: moto uliwashwa katika mbuga za miti mikavu zilizozunguka
vibanda vyao na wakazi husika walipokimbilia msituni Waingereza waliwakamata kwa vifaa
vilivyoandaliwa kwa kazi hiyo. Katika kazi hii ya kuwawinda binadamu baadhi ya watu
walikufa wakati wakipelekwa pwani kwenye meli za Waingereza na zile za makampuni
mengine. Theluthi moja ya mateka waliobaki walikufa kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya
hewa, na wakati wa kuwasafirisha kwa meli 4.5% na 19% walikufa wakati wa safari. Wale
waliokufa katika makoloni hawakuwa na idadi.
Mwaka 1520 karibu watumwa laki nane waliingia katika koloni la Jamaika na watumwa laki
tatu na elfu arobaini pekee ndio waliobaki kuwa hai mwisho wa mwaka huo.
Malkia Elizabeth I alikuwa mshirika katika biashara ya utumwa. Mshirika wake alikuwa John
Hawkins, mfanyabiashara mkubwa wa watumwa katika historia. Malkia alimpa cheo cha hadhi ya
mtu mwenye heshima ya kutumikia taifa lake na kuitwa „Sir‟ kabla ya jina lake. Alimpa cheo hicho
baada ya Malkia huyo kushangazwa na ujasiri wake na akaifanya nembo yake kuwa na alama ya
mtumwa aliyefungwa katika minyororo na pingu. Ni jambo la kejeli kusoma kuwa meli
iliyoandaliwa na Malkia kwa ajili ya Hawkins ilipewa jina la “Jesus” yaani Yesu, na idadi ya meli
zilizotengenezwa kwa ajili ya biashara ya watumwa ilifikia 192 ambapo kila meli iliweza kubeba
watumwa 47,146. Uingereza iliwataka viongozi wa Kanisa kutafuta maandiko yatakayohalalisha
hii biashara na hatimaye maandiko kutoka katika Agano la Kale yaliyotajwa hapo juu kuhusu
Wayahudi na utumwa yalipatikana na kuweza kutumika.
Waarabu na Utumwa:
Utumwa ulikuwa umeshamiri sana kabla ya Uislam. Chanzo cha hali hiyo ni vita vilivyokuwa
vikindelea baina ya makabila ya Kiarabu. Wale walioshinda walikuwa wakiwachukua
walioshindwa kuwa watumwa na wakati mwingine, kabila lote lilichukuliwa na kabila jingine kuwa
102
watumwa. Wakati mwingine, mtu au kundi la watu waliokuwa wakisafiri bila ulinzi walitekwa na
kuchukuliwa kama watumwa.
Katika kadhia zote zilizotajwa hapo juu utumwa ulujumuisha mwili na akili, yaani mtumwa
alimfuata bwana wake katika mfumo wake wa kufikiri pamoja na imani yake ya kidini. Mtumwa
alikatazwa kuwa na fikra inayokwenda kinyume na fikra ya bwana wake. Bwana huyo alikuwa na
kila haki ya kutumia adhabu yoyote dhidi ya mtumwa wake, kwa sababu alikuwa akimmiliki moja
kwa moja.
Uislam na Utumwa:
Msimamo wa Uislam kuhusu utumwa kwa muda wa karne kumi na nne zilizopita tunaweza
kuufupisha kwa maneno machache. Uislam ulipiga marufuku utumwa kwa ujumla wake na
ukaruhusu tu mfumo uliozoeleka katika zama zetu hizi. Uislam ulifanya juhudi kufuta utumwa
katika namna ambayo kwamba binadamu hajaweza kufanya kitu kizuri kama hicho mpaka sasa.
Uislam haukukomesha utumwa kwa maneno tu bali kwa vitendo, msimamo imara na michakato
iliyopangiliwa vizuri. Sababu za hatua hizi za kidogo kidogo ni kama ifuatavyo:-
1. Kuamiliana na adui katika njia ile ile wakati wa vita baada ya kila upande kuwachukua mateka na
kuwahesabu kama watumwa. Sasa tunawauliza wale wanaojifanya kuwa waungaji mkono wa
uhuru katika zama za sasa. Kungetokea nini leo hii kama mabadilishano ya mateka wa vita
yasingekubalika miongoni mwa mataifa mbalimbali?
2. Uislam una falsafa yake binafsi katika kushughulikia mambo yasiyokuwa ya msingi. Falsafa hii
inaelekea kushughulikia mambo mbalimbali kwa subira na kwa amani mpaka Uislam unapofikia
malengo yake, bila kusababisha shida yoyote miongoni mwa wafuasi wake. Vitu kama vile pombe,
utumwa na ndoa za mitala yalisawazishwa kidogo kidogo, lakini kuhusu mambo muhimu kama vile
Tawhiid na ushirikina, Uislam uliyashughulikia moja kwa moja na kwa dhahiri na ulikuwa katika
hali ya uwazi sana.
Sasa, Uislam ulilishughulikia vipi swala la utumwa katika namna isiyo ya moja kwa moja? Uislam
ulitumia njia mbili muhimu: Kuziba njia za utumwa na kufungua njia ya kuwakomboa watumwa,
yaani uliziba vyanzo vya utumwa na kuhimiza njia mbalimbali za kuwaacha huru watumwa.
1. Kupunguza vyanzo mbalimbali vya Utumwa:
Kabla ya Uislam kulikuwepo na njia mbalimbali za utumwa kama vile kuuza au kucheza kamari,
utekaji, ulipaji deni, vita, uharamia na mfumo wa matabaka.
Uislam ulikomesha njia zote hizo na moja pekee ndiyo iliyobaki. Uislam pia ulifanya juhudi ya
kuziba chanzo hiki, mpaka pale utumwa ulipopungua sana. Chanzo hicho ni Jihad (kupigana vita
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu).
103
Jihad ilikusudiwa kukabiliana na aina yoyote ya uonevu kutoka kwa maadui wa Uislam na
ilikuwa ni sharti kwamba mateka husika asiwe tayari ni Mwislam, hata kama angekuwa kwa
upande wa adui.
Hivyo, hakukuwepo na utumwa, lakini katika vita halali ----- yaani vita kwa ajili ya kujilinda. Aina
ya utumwa iliyoruhusiwa na Uislam uliruhusiwa pia na mataifa yaliyostaarabika, ambayo
yalikubaliana kukomesha utumwa mnamo karne ya 18.
Mataifa haya yaliruhusu uchukuaji wa mateka wa vita, kuwashikilia au kuwakomboa kwa kulipa
fidia au faini. Hicho ni kitu kilichofanywa na Uislam karne 14 zilizopita.
Wanafalsafa wa sheria za Kiislam, wanasema kwamba ikiwa mvulana atakamatwa kisha akaja
Mkristo akadai kuwa ni mwanaye na Mwislam akaja na kudai kuwa ni mtumwa wake basi hakimu
atamkabidhi mtoto huyo kwa Mkristo ili asije kuwa mtumwa hata kama kufanya hivyo
kutampelekea mtoto huyo kubadilishwa dini.
Uislam pia uliweka baadhi ya masharti katika kuwabadilisha mateka wa vita kuwa watumwa. Moja
wapo ikiwa ni kwamba mkuu wa nchi atatakiwa kutangaza kuwa mateka hao watahesabiwa kama
watumwa na kabla ya hatua hiyo mambo kadhaa yanatakiwa kufanyika.
(a) Mabadilishano ya mateka wa vita baina ya Waislam na maadui zao kama yale mabadilishano
yaliyofanyika katika kingo za mto Lams. Baada ya mabadilishano hayo fidia zilitolewa iwapo
mateka yeyote aliendelea kushikiliwa upande wa pili.
(b) Kuwaacha huru mateka wa vita bila masharti au ulipaji wowote wa pesa, kwa kufuata mfano
wa Mtume Muhammad (S.A.W) aliyesma:
“Mtembelee mgojwa, mpe chakula mwenye njaa na waache huru mateka wa vita”
2. Kufungua njia ya Kuwaoa Watumwa:
Uislam uliutazama utumwa kama suala la muda mfupi na ukajaribu kuukomesha, hivyo ukafungua
milango yote ya kuwaacha huru watumwa kwa:-
(a) Kuwaacha huru watumwa (manumission) jambo lililohamasishwa na Mwenyezi Mungu ndani
ya Qur‟an Tukufu: “Lakini mwanadamu hakupita njia nzito. Na nini kitakujulisha njia nzito
ni nini? Ni kumwacha huru mtumwa” (2)
.
Mtume (S.A.W.) amesema: - “Ukimuacha huru mtumwam, Mwenyezi Mungu atauacha huru
mwili wako dhidi ya moto wa Jahannam”
104
(c) Kumwacha huru mtumwa ilikuwa njia ya kutimiza kiapo kilichowekwa na Mwislam
iwapo hakuweza kukitekeleza. Au ilitumika kama ulipaji fidia kwa makosa
aliyoyatenda. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur‟an Tukufu:
“Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni
kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini
kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au
kumkomboa mtumwa” (3)
.
Na: “Mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye
Muumini” (4)
.
Hatua ya kuwaacha huru watumwa ni suala ambalo baadaye lilihalalishwa na Uislam huku ukipiga
marufuku utumwa ambao ulichukuliwa kuwa halali kabla ya Uislam. Uislam ulizitangulia sheria za
kimataifa katika kuyalazimisha mataifa mbalimbali kuwaacha huru wafungwa wa kivita na
kuwaacha huru watumwa, na ukahimiza suala hilo kwa njia binafsi pindi watumwa
wanapomilikiwa na mabwana zao.
Hatuwezi kusema kuwa kazi hii ilikuwa kubwa au la, lakini angalau tunaweza kusema kwamba
ilikuwa njia pekee ya kuwaacha huru watumwa na kwamba hakuna taifa jingine lolote lililoweza
kufanya lolote jema kuliko hatua hiyo ya Uislam.
(c) Makubaliano ya kuachwa huru ni yale yaliyofanywa baina ya watumwa na wale wanaowamiliki
ambapo wangeachwa huru iwapo wangelipa kiasi fulani cha pesa au kwa kuwafanyia kazi wamiliki
wao kwa kipindi fulani cha muda.
Baadhi ya wanafalsafa ya sheria za Kiislam wanaamini kuwa juhudi hii ni wajibu kutekelezwa
iwapo mtumwa akimuomba mmiliki wake kufanya hivyo, kwa sababu katika Qur‟an tunasoma:
“Na wanaotaka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi
waandikieni kama mkiona wema kwao” (5)
.
Baada ya makubaliano hayo ana haki ya kufanya biashara au kufanyakazi na ana haki ya kumiliki
mali na kufanya kazi kwa maslahi yake binafsi. Hivyo hamfanyii kazi bwana wake bali atafanya
kazi ili apate pesa ya kumlipa mmiliki wake kidogo kidogo.
Uislam pia ulitenga sehemu ya Zaka ilipwe katika kuwasaidia watumwa wapate uhuru wao kutoka
kwa wamiliki wao. Katika Qur‟an tunasoma: “Hakika sadaka ni kwa mafakiri na masikini, na
wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao, na katika kuwapa uhuru watumwa” (6)
.
(d) Kuwa huru kwa utashi, ikiwa na maana ya mtumwa kuwa huru pindi bwana wake anapofariki.
Hili lilifanywa ili kwamba bwana angemtumikisha mtumwa wake katika kipindi anachokuwa hai,
ambapo mtumwa huyo angekuwa huru baada ya kifo cha bwana wake. Hii pia ingekuwa sehemu
105
ya jambo jema ambalo lingechukuliwa kama sadaka na kumsaidia mtu katika ulimwengu
mwingine (Akhera).
(e) Kama mtumwa mwanamke akibeba ujauzito kutoka kwa bwana wake na kujifungua mtoto basi
mwanamke huyo hapaswi kuuzwa au kupewa mtu mwingine na atahesabiwa kuwa yupo huru pale
bwana wake atakapokufa. Na hapo mtoto wake angekuwa huru. Hii ilikuwa kinyume na sheria za
Waarabu zilizokuwapo kabla ya Uislam. Mfumo wao wa kabla ulitaka kwamba mtumwa
mwanamke angeendelea kuwa mtumwa kama awali, hata kama angejifungua mtoto, pia mtoto wake
huyo naye angekuwa mtumwa, japo baba yake angekuwa huru.
Antara wa kabila la al-Abs alikuwa mtumwa kutokana na baba yake. Alikataa kulitetea kabila lake
japo alikuwa mtu shujaa zaidi katika kabila hilo. Baba yake akamwambia: “Ewe Antara, pambana”,
Antara akajibu: “Lakini mtumwa hajui kupambana, bali anajua kukamua maziwa na kumlisha
Ngamia”. Kisha baba yake akasema: “Pambana na hapo utakuwa huru”. Hivyo asingepata uhuru
wake kama isingekuwa watu wake kumhitaji wakati wa shida.
Mtume (S.A.W.) alipopambana dhidi ya watu wa kabila la Bani Al-Mustalik alifikiria kumuoa
mwanamke kutoka katika kabila hilo lililoshindwa ili kuwafariji. Wafuasi wake wakaona kuwa ni
jambo lisilofaa kuchukua mateka kutoka katika watu ambao wamekuwa na mahusikano ya ndoa ya
Mtume (S.A.W.).
(f) Iwapo mtu angemwacha huru mtumwa wake kwa sehemu moja, mtumwa huyo angekuwa huru
moja kwa moja. Hilo hutokea pale watu wawili au watu wengi wanashirikiana katika kummiliki
mtumwa na mmoja wapo wa wamiliki akaliacha huru fungu lake, mmiliki huyo atawalipa wamiliki
wengine thamani ya hisa yao. Kama mmiliki huyo asipoweza kuwalipa washirika wake, basi
mtumwa huyo atatakiwa kufanya kazi ili kuwalipa washirika hao.
(g) Kama baba na mtoto ni watumwa chini ya mmiliki mmoja na kumwacha huru mmoja wao,
kisha yule mtoto au baba aliye huru akahusiana na mwenzake katika utumwa, basi mtumwa yule
atakuwa huru moja kwa moja.
Hapa swali linaweza kuibuka; kwanini mtumwa hawi huru pindi tu anapoingia katika Uislam?
Katika kujibu tunaweza kusema kuwa Waislam hawakutaka kuhadaiwa na wanafiki ambao
wangejifanya kuwa Waislam na pale wanapokombolewa wakarudi kwa watu wao na kurudi
kupambana dhidi ya Waislam.
Kama mfungwa wa kivita alikuwa mkweli katika imani yake asingedhurika sana kwa yeye kusubiri
kwa muda fulani ili aachiwe huru katika moja ya njia mbali mbali zilizotajwa hapo juu. Tunaona
kwamba Uislam ulikomesha utumwa kwa matendo. Mwanamke angekuwa huru punde tu
anapojifungua kutoka kwa mmiliki wake, na hili hufanya iwe rahisi sana kwa wanawake kuwa
huru. Ama wanaume kuwa huru, kuna njia nyingi kwao kupata uhuru wao kama ilivyoelezwa hapo
juu.
106
Uislam na Muamala kwa Watumwa:-
Uislam ulijitahidi sana kuondoa tofauti zote baina ya watumwa na wamiliki wao. Kitu cha muhimu
sana ni kwamba mtumwa humfanyia kazi bwana wake kwa kiwiliwili chake, huku akiwa na uhuru
kamili kiakili na kiroho. Ana uhuru wa kufikiri na kuamini katika dini na hakuna yeyote awezaye
kumshurutisha katika uwanda huu. Waarabu katika siku za mwanzo za Uislam walilichulia jambo
hili kama mapinduzi makali sana ambapo waliwatesa na wakati mwingine kuwaua watumwa wao
pale walipojichagulia imani na dini yao na wakaita kwa sauti ya juu machoni pa wamiliki wao:
“Tumeingia katika Uislam na hamna Mamlaka yoyote juu ya fikra zetu. Mnatawala tu miili
yetu katika namna isiyopingana na imani yetu ya kidini au kimaadili”.
Ibnul Qayyim, mwanachuoni maarufu wa Kiislam anasema: “Mwenye mtumwa hana haki juu
ya utu au akili ya mtumwa wake, haki yake pekee ni ya kimwili”.
Vile vile, Uislam uliwafanya watumwa na wale walio huru kuwa sawa katika vipengele vingi vya
maisha. Mtume Muhammad (S.A.W.) katika moja ya hadithi zake anasema:- “Mwenye kumuua
mtumwa wake naye atastahiki kuuawa na mwenye kumtesa kwa njaa mtumwa wake naye
atastahiki kuteswa kwa njaa”
Uislam uliuchukulia uchamungu kuwa kiwango bora kwa binadamu, wale waliohuru au watumwa.
Kwa sababu hii Mtume (S.A.W.) alimuozesha binamu yake Zainab kwa kijana aliyekuwa mtumwa
hapo awali, Zaid. Alimfanya Zaid kuwa kiongozi wa jeshi la Waislam lililokwenda kupambana na
Warumi katika eneo liitwalo Mu‟ta. Katika jeshi hilo kulikuwa na malodi wengi wenye
kuheshimika. Baadaye Mtume (S.A.W) alimfanya Usama, mtoto wa Zaid kuwa kiongozi wa jeshi
kubwa la Kiislam kwenda tena kupambana na Warumi. Chini ya uongozi wake pia walikuwapo
watu wenye shakhsia kubwa za Kiislam.
Katika masahaba waliokuwa karibu zaidi na Mtume (S.A.W.) walikuwemo watumwa walioachwa
huru, kama vile Bilal wa Ethiopia, Salman Muajemi na Suhaib Mrumi.
Uislam uliwaagiza wenye watumwa wasiwachoshe kwa kazi ngumu sana. Vile vile Uislam
uliwataka wenye watumwa waamiliane nao kwa namna iliyo bora kwa kuwapa chakula kile kile
wanachokula wao na kuwapa nguo sawa na zile wanazovaa wao wenyewe. Hiki chaweza kuwa
kiwango cha juu sana katika usawa. Al-Maru bin Suwail amesema: “Nilikutana na Abu Dhar,
sahaba maarufu wa Mtume, katika eneo la Ribdha na tukaona kwamba yeye na mtumwa wake
walikuwa wamevaa mavazi sawa. Tukasema: Kwa nini huchukui kipande cha nguo ya mtumwa
wako na kukiongeza kwenye nguo yako ili uwe na suti na kumpa mtumwa wako kitambaa kingine?
Abu Dhar akasema kwamba alimsikia Mtume akisema: - “Watumwa ni ndugu zenu. Mwenyezi
Mungu aliwaweka katika mikono yenu hivyo mnatakiwa kuwapa chakula sawa na kile
mnachokula na kuwapa mavazi sawa na yale mnayovaa na msiwatumie katika kazi ngumu,
lakini mkilazimika kuwapa kazi basi mnapaswa kuwasaidia”
107
Uislam uliwapa heshima watumwa kwa namna ambayo iliwafanya wafurahi na kuhisi ubinadamu
wao na ukuu wa roho yao pale ulipowafanya watumwa kuwa viongozi katika sala pindi
walipokuwa na elimu nzuri ya Qur‟an na mafundisho ya dini kupita wenzao walio huru.
Inasemekana kuwa Bibi Aisha (R.A.), mke wa Mtume alikuwa na mtumishi aliyekuwa
akimuongoza katika Sala.
Tunasoma ndani ya Qur‟an: Muabuduni Mwenyezi Mungu na msimshirikishe na chochote na
watendeeni wema wazazi wawili na ndugu na mayatima na masikini na jirani walio ndugu zenu,
na jirani wa mbali na rafiki aliye jirani yenu na msafiri na wale wanaomilikiwa na mikono yenu
(watumwa)(7)
.
Mtume (S.A.W.) anasema:- “Mnamjua aliye mbaya miongoni mwenu? Yule anayekula peke
yake, asiyemsaidia yeyote na ampigaye mtumwa wake”
Siku moja Mtume (S.A.W) alimuona mtu akiwa juu ya farasi huku mtumwa wake akimfuata kwa
kutembea kwa miguu. Mara moja Mtume akaipaza sauti yake kumwambia yule aliyempanda
farasi: “Ewe Abdullah mchukue pamoja nawe, yeye ni ndugu yako na roho yake ni kama yako”
Kutokana na mafundisho hayo tunaona matukio mengi ambayo watumwa walitendewa wema na
heshima kubwa. Abu Aziz, ndugu wa sahaba maarufu wa Mtume, aitwaye Mus‟ab bin Umeir,
wakati mmoja alisema kwamba baada ya vita ya Badr alichukuliwa kama mateka kupelekwa
Madinah na kwa sababu Mtume alikuwa ameagiza kwamba mateka wa vita watendewe wema,
wanajeshi wa Kiislam walikuwa wakimpa chakula bora walichokuwa wakikitumia wao wenyewe.
Wakati mmoja Mtume (S.A.W) alimpa Abu Haitham mtumwa na kumtaka aamiliane naye vizuri.
Alipomweleza mkewe kuhusu ushauri wa Mtume, mkewe akasema: “Hatuwezi kutenda jambo
jema zaidi ya kumwacha huru huyu mtumwa”.
Baada ya vita ya Badr Mtume (S.A.W.) alimwacha huru kila mtumwa aliyewafundisha Waislam
kumi kusoma na kuandika. Ibn Hisham ambaye aliandika historia ya maisha ya Mtume, anasema
kwamba mfungwa mmoja aliyeitwa Thumana Al Hanafi aliamiliwa vyema sana na Waislam
ambapo Mtume (S.A.W) aliiamuru familia yake (Mtume) kumpa maziwa (Thumana) kila siku
asubuhi na jioni sanjari na kuumpelekea chakula kizuri walichokuwa wakikitumia wao wenyewe.
Siku tano kabla ya kifo chake, Mtume (S.A.W) alisema: “Muogopeni Mwenyezi Mungu katika
kuamiliana na watumwa wenu‟
Ali, Khalifa wa nne baada ya Muhammad aliwahi kusema: Ninaona haya kuwa na mtumwa
anayesema “Mola wangu ni Allah”. Na wakati mmoja aliwapa watumishi wake pesa ili
wamnunulie nguo yeye na mtumishi wake. Pindi mtumishi huyo alipoleta hizo nguo, alimpa
mtumishi wake nguo yenye thamani kubwa na iliyo bora na kumwambia: “Unastahili kupata hii
iliyo bora kuliko mimi, wewe ni kijana na unatakiwa uonekane maridadi na mwenye kupendeza
hali ya kuwa mimi ni mzee”
108
Mfano mmoja ulio bora katika usawa uliotokea pindi Omar Ibnul Khattab alipokwenda Jerusalem
pamoja na mtumishi wake aliyekuwa juu ya Ngamia. Walifanya zamu ya kumpanda Ngamia
ambapo walipofika langoni mwa mji ilikuwa ni zamu ya mtumishi kupanda juu ya Ngamia. Na
hapo Omar akawa anatembea kwa miguu huku mtumishi wake akiwa juu ya Ngamia. Abu Ubaida,
mmoja wapo wa viongozi wa jeshi la Kiislam akamlaumu Khalifa kwa kitendo hicho akisema:
“Ninaona unatenda kitu kisichokufaa. Watu wote wanakutazama”. Khalifa akasema kwa uthabiti:
“Tulikuwa watu duni na dhalili lakini Mwenyezi Mungu akatufanya kuwa imara na wenye
kuheshimika kwa sababu ya Uislam. Kama tukitaka fakhari nje ya Uislam tutashindwa”.
Wakati mmoja Omar alimwacha huru mtumwa mwanamke kwa sababu bwana wake alikuwa
amempiga, kwani Mtume alisema: “Ampigaye au kuumiza uso wa mtumwa wake, lazima
amuache huru mtumwa wake kama fidia na kafara ya kosa hilo”
Siku moja mtumwa alimleta Kondoo aliyevunjika mguu mpaka mbele ya bwana wake Zainul
Abidiin, mjukuu wa Mtume, ambaye alimuuliza mtumwa huyo kwa nini alikuwa ameuvunja mguu
wa Kondoo? Mtumwa akasema kuwa alikuwa amefanya vile ili kumkasirisha bwana wake. Zain al
Abidiin akasema: “Nami nitamkasirisha shetani aliyekufundisha hivyo. Nenda; uko huru
katika njia ya Mwenyezi Mungu”.
Mtu mmoja alimtembelea Salman Mwajemi na kumkuta akikanda ngano. Mtu huyo alishangazwa
na akamuuliza: “Kitu gani hiki ewe Abu Abdillah?” Salman akasema: “ Nimemtuma mtumishi
wangu kupeleka ujumbe mahali fulani nami ninachukia kumuongezea kazi nyingine”.
Mtawala mmoja wa Tunisia (1845) aliona kwamba watu wengi waliokuwa na watumwa walikuwa
hawaamiliani vyema na watumwa wao, hivyo aliweka sheria ya kuwaacha huru watumwa wote na
viongozi wa mamufti wa kidini walikubaliana naye.
Siku moja Yahia Bin Said alisema: “Khalifa Omar bin Abdul Aziz alinituma kwenda Afrika
kukusanya Zaka, nikafanya hivyo lakini nilipotaka kuzigawa pesa hizo kwa watu waliokuwa
na haja nazo sikuona mtu yeyote mwenye shida, kwani kipindi cha Omar bin Abdul Azizi
kilikuwa ni kipindi cha ustawi mkubwa sana kiasi cha kila mtu kuwa tajiri na hakuna
maskini waliokuwa wamebaki. Hivyo, niliitumia pesa hiyo kununua idadi kubwa ya
watumwa na kuwaacha huru”.
Suluhisho hili la kivitendo kwa ajili ya tatizo la utumwa na muamala mwema lilikuwa suluhisho la
kimataifa ambalo Uislam ndio ulioonesha njia. Uislam uliwasaidia watumwa kwa kipindi kifupi
mpaka waraka wa kimataifa ulipoweza kufikiwa na kukubaliwa.
Hatimaye tunaweza kusema kwamba Uislam ulikuta mfumo wa utumwa ukiwa tayari upo na
ukaweka mpango na mikakati ya kuukomesha na ukafanya vita halali kuwa chanzo pekee cha
utumwa. Kisha baadaye Uislam ukatangaza kwamba mateka wa vita wanapaswa kuwa huru au
kukombolewa kwa fidia.
109
Kitu kilichofanywa na Uislam karne kumi na nne zilizopita ni kikubwa sana kuliko kile
kinachofanywa sasa na nchi zilizostaarabika katika kuwatendea haki wafungwa wao wa kivita au
watumwa wao na hatuwezi kufikiri jinsi walivyoweza kufanya kitu kizuri zaidi.
Katika kipindi cha chini ya miaka hamsini, wafanyabiashara ya utumwa kutoka magharibi
waliwachukua watumwa na kuwapeleka kaskazini na kusini mwa Amerika. Idadi ya watumwa hao
ilifikia watu milioni ishirini waliobaki baada ya mauaji na manyanyaso. Idadi hii ni mara tano ya
zaidi ya watumwa waliokuwapo katika ulimwengu wa zamani, zaidi ya miaka elfu moja iliyopita.
Na tofauti iliyopo baina ya watumwa wa ulimwengu wa zamani na ulimwengu wa sasa ni kubwa
sana kiasi kwamba Wanegro katika eneo la Amerika bado ni jamii yenye nasaba iliyotengwa,
isiyoheshimika na haina haki za kikazi na kiraia.
Mtu hawezi kulikuta jambo hili katika nchi yoyote ya mashariki. Mtu mweusi anayekuja katika
nchi yoyote huko, huhesabiwa kuwa raia ndani ya takriban kizazi kimoja. Ana haki na majukumu
sawa na hahitaji ulinzi wa sheria au kanuni. Hata hivyo, historia ya Ulaya ilikuwa na baadhi ya
waandishi waadilifu waliohuru na wenye ujasiri walioelezea hali ya utumwa katika Uislam.
Van Denburg anasema: “Sheria nyingi zimewekwa na Uislam, zikionesha hisia adhimu
aliyokuwa nayo Mtume Muhammad na wafuasi wake juu ya watumwa. Katika sheria hizo
tunakuta kwamba faida za mfumo wa Uislam ni tofauti na mifumo yote iliyotumika na mataifa
mbalimbali mpaka katika miaka ya hivi karibuni, mataifa yanayodai kuwa na ustaarabu na
maendeleo makubwa”.
Abbas M. Al-Aqqad anasema kwamba kadhia ya utumwa ni nyenzo nzuri ya kufanya mahubiri
miongoni mwa vijana wa Kiislam na mataifa ya Kiafrika yanayopata uhuru wake na kutafuta imani
na ustaarabu bora wenye kuwavutia na kuwakinaisha. Ni nyenzo ya kuutangaza Uislam na wala sio
propaganda dhidi ya Uislam. Lakini tunapoona hali iliyo kinyume, na kuwaona mawakala wa
ubeberu na wamisionari wakilitumia suala la utumwa kama silaha dhidi ya Uislam, huku Waislam
wakisikia na kuona bila kutoa jawabu lolote, basi Waislam wanatakiwa kujilaumu wenyewe.
Sauti ya Uislam iliendelea kuunguruma kwa muda wa karne nyingi mpaka iliposikika.
Ukomeshaji wa utumwa ni moja wapo ya zawadi zilizoletwa na Uislam kwa binadamu.
110
Rejea:
1. Waefeso 6:5 – 8.:
Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa
hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; wala si kwa
utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu; bali kama watumwa wa Kristo,
mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema kama kumtumikia Bwana, wala
si mwanadamu; mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana,
kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.
2. Qur‟an - 90:11 – 13.
3. Qur‟an - 5:89.
4. Qur‟an - 4:92}
5. Qur‟an - 24:33
6. Qur‟an - 9:60
7. Qur‟an - 4:36
111
KESI YA KUMI NA MOJA
Ngawira ndio Lengo
Mwendesha Mashtaka: Mazingira mabaya ya uchumi wa Waarabu na kupenda kwao
ngawira ni kichocheo kikuu cha vita vyao mbalimbali na kama anavyosema Thomas Arnold katika
kitabu chake „The Call to Islam‟ Uk. 40 “Waarabu ni watu wenye nguvu walioongozwa na njaa na
shida wakayatelekeza maeneo yao yenye ukame wakaenda kuzishambulia nchi za jirani zilizokuwa
na utajiri na ustawi.
“Tuna shaka kama hamasa ya kidini pekee ilitosha kuwafanya Waarabu wapambane na nchi kubwa
za jirani. Inaonekana kwamba waliendeleza uvamizi wao kwa sababu ya shida kubwa ya kiuchumi
waliyokuwa nayo”.
Katika kitabu chake kiitwacho “Arabs in Spain” Mt. Paul anasema kwamba: “Utajiri mkubwa wa
Makaisari na wafalme wa Uajemi, ardhi zenye rutuba na miji yenye ustawi ya falme za jirani,
zilikuwa nguzo muhimu kwa Waislam kueneza dini yao”.
Philip Hitti katika kitabu chake “History of the Arab” Juz. 1 Uk. 195 – 199 anasema: “Ingawa
baadhi ya Waarabu walishiriki katika uvamizi kwa sababu ya kupenda pepo na maisha ya Akhera,
kwa kweli wengi wao walikwenda kupigana vita kwa matarajio ya kupata maisha ya raha katika
ustaarabu wa nchi zenye rutuba za upande wa kaskazini mwa Arabia”.
Baada tu ya mwendesha mashtaka kukamilisha hoja zake, hakimu aliutaka Uislam kusimama na
kujitetea.
Uislam: Shutuma hii inafanana na ile iliyoelekezwa kwa Mtume Muhammad katika hatua zake
za awali za kuutangaza Uislamu. Wakati huo, watu walidhani kwamba alihitaji pesa au mali, hivyo
walitangaza na kuahidi kumpa kiasi kikubwa cha pesa lakini yeye alisema: “Ninaapa kwa
Mwenyezi Mungu lau mngeliweka jua katika mkono wangu wa kuume na mwezi katika mkono
wangu wa kushoto nisingeacha mahubiri haya mpaka yafanikiwe au nife”
Muhammad (S.A.W.), baada ya kuwa mtawala wa Arabia yote angeweza kujenga majumba ya
kifakhari, angeoa wasichana warembo zaidi wa kiarabu na wasichana wa Kiajemi na wa Kirumi
wenye mvuto sana, angejipatia yeye na familia yake chakula na mavazi yenye thamani kubwa,
lakini je alifanya hivyo baada ya mafanikio yake? Je, alifanya hivyo katika maisha yake ya awali?
Hapana! Kwa kweli alifanya kinyume chake na wakati mwingine alikaribia kuwakosa wake zake
kwa sababu ya maisha ya kimasikini waliyoishi katika nyumba yake.
Muhammad alikuwa masikini badala ya kuwa tajiri, na vivyo hivyo Makhalifa Abu Bakr na Omar
ambao walizishinda falme kuu mbili za wakati wao, falme za Rumi na ile ya Uajemi. Othman naye
112
alikuwa maskini. Hata hivyo bado kuna tuhuma kwamba Waislam walipigana tu ili kupata mali na
ngawira.
Vipi kuhusu watu wale masikini: Bilal Mhabeshi, Ammar, Sumayya na Khubaib? Je, walivumilia
mateso kwa sababu walitabiri mustakbali wa kwamba utajiri wa wafalme wa Rumi na Uajemi
ungeletwa kwao au walivumilia mateso hayo kwa sababu ya imani iliyojaa mioyoni mwao? Imani
iliyomfanya Rustam kiongozi wa jeshi la Kiajemi, ashindwe pindi alipotangaza kuwapa Waislam
zawadi dhahabu, chakula na nguo kabla ya vita vya Qadisya. Rustam alimwambia Zuhra bin Al-
Huwayya, mmoja wa wajumbe wa Kiislam: “Kama wewe na watu wako mkirudi bila kupigana
tutakupeni mali nyingi”. Lakini Zuhra akajibu: “Hatukuja kwako kwa ajili ya Ngawira na mali za
huu ulimwengu, lengo letu ni Akhera”. Mjumbe mwingine, Al-Mughirah Ibn Shu‟ba alikutana na
Rustam kabla ya vita. Rustam akasema: “Ninajua kwamba mmekuja kupigana nasi kwa sababu ya
umasikini na shida kubwa mliyo nayo. Tutawapa chakula ili kujaza matumbo yenu na mali nyingi
zitakazowafurahisha na kuwaridhisha”. Mjumbe huyo wa Kiislam akamcheka Rustam, mawazo
yake na pesa zake na kumpazia sauti akisema: “Unapaswa kuchagua mojawapo ya mambo haya:
Uislam, Jizya (kodi inayolipwa ili kuilinda dini ya mtu chini ya utawala wa Kiislam) au
mapambano”.
Kama Waislam wangetaka kupata mali bila ya kuieneza dini yao wangekuwa wamekubali pesa bila
ya kumwaga damu na wangekuwa wemeyaokoa maisha yao na kupata mali nyingi bila kazi yoyote,
jitihada ngumu, mayatima au wajane.
Mtawala wa China alikuwa na fikra kama za Rustam. Mnamo mwaka 666 A.D. Qutaiba A-Bahili
alimtuma Hubaira Al-Kilabi kwenda kukutana na mfalme wa China aliyekuwa ameomba jambo
hilo. Mfalme huyo akamwambia Hubaira: “Rudi kwa kiongozi wako umwambie asalimu amri
kwa sababu ninajua jinsi gani alivyo na tamaa na jinsi wafuasi wake walivyokuwa wachache.
Asipofanya hivyo, nitalituma jeshi litakalowasambaratisha nyinyi wote”. Hubaira akajibu:
“Watakuwaje wachache wafuasi wa kiongozi ambaye farasi wake wanaanzia katika ardhi
yako na kuishia katika ardhi ya Mizaituni? Anawezaje kuwa mwenye tamaa mtu
aliyeutweza ulimwengu huu na raha zake licha ya kuwa na uwezo wa kupata vyote
avitakavyo, na akapendelea mapambano, shida na akaivamia ardhi yako? Unatutisha
kutuua, lakini tunajua kwamba kila binadamu ana majaliwa ya kufa, na kuuwawa katika vita
ni mwisho mwema tunaoufikiria na kuukusudia. Hatuchukii au kuogopa kifo”.
Jawabu hili la Hubaira linabainisha wazi kuwa lengo la kwanza na la awali la harakati za Kiislam ni
kueneza dini. Tunaitaka akili yenye busara ihukumu na kuwafanya wenye chuki watambue kuwa
mali ni matokeo tu ya asili yaliyotokana na harakati za mapambano na kamwe mali hizo hazikuwa
lengo la harakati hizo.
Dr. Shalabi anataja baadhi ya nukta zinazotetea lengo la harakati za mapambano na huu hapa ni
muhtasari wake:-
113
1. Waislam walipambana dhidi ya ushirikina katika Peninsula ya Arabia kwa zaidi ya miaka
ishirini, kipindi ambacho baadhi ya Waislam wazuri waliuawa hususan katika mapambano dhidi ya
wakanaji wa dini, wale waliojifanya kuwa Mitume pamoja na wale waliokataa kulipa zaka. Vita
hivyo vilitokea katika ardhi kavu za majangwa yenye ukame mbali na kile kinachoitwa ardhi ya
rutuba katika upande wa kaskazini. Sasa basi; nini chanzo cha shida zote hizo?
Mbali ya hilo, siku zote Waislam walijaribu kushinda bila kupigana vita na bila ya ngawira, kama
ilivyokuwa katika kadhia ya ufunguzi wa Makkah.
Mara nyingi Waislam walipata ngawira na kuzirejesha kwa wenye nazo pindi wamiliki hao
walipoingia katika Uislamu, kama ilivyokuwa katika kadhia ya vita vya Hunain na Taif.
2. Kwa kipindi cha miaka elfu moja Waarabu waliishi katika jangwa lao masikini wakijua kwamba
kulikuwa ardhi yenye rutuba na utajiri katika upande wa kaskazini. Kwa nini hawakwenda huko
kaskazini hapo kabla?
Sio sahihi kusema kwamba Waarabu waliwahofia Warumi na Waajemi na kwamba ni pale tu
mataifa haya yalipodhoofika ndipo Waarabu waliwavamia, kwa sababu Waarabu waliendelea
kuwaogopa Warumi na Waajemi hadi pale walipowashinda katika vita vya Qadisya na Yarmouk.
Katika enzi za Omar Ibn Al-Khattab, Waislam walikuwa na wasiwasi kuhusu matokeo ya
kupambana na Waajemi katika namna ile ile waliyohofia kukabiliana na Warumi huko Syria.
Abdul Rahman Ibn Auf, mmojawapo wa masahaba mashuhuru wa Mtume aliwahi kusema: “Ni
Warumi na Banul Asfar (Waajemi) ndio wenye nguvu ya chuma na uwezo mkubwa katika vita”.
Lakini imani kubwa ambayo Mtume aliipandikiza katika nyoyo za wafuasi wake iliwafanya wawe
imara zaidi ya chuma na ikawapa ujasiri mkubwa ukiongezewa na hisia ya ukuu wa Mwenyezi
Mungu waliyokuwa nayo katika nyoyo zao, viliwafanya wawashinde Warumi na Waajemi.
3. Wajumbe wa Muqawqis (mtawala wa Misri) waliporudi kutoka kwenye kambi ya jeshi la
Kiislam, lililokuwa chini ya uongozi wa Amr Ibn Al-As baada ya kuizingira ngome ya Babeli,
walimwambia kiongozi wao kuhusu hali ya Waislam wakisema: “Tumeona watu ambao kifo
kina thamani zaidi kwao kuliko uhai, na staha ni bora kuliko maringo. Hakuna kati yao
mwenye hima na uhai. Hukaa juu ya mchanga na kiongozi wao ni kama yeyote miongoni
mwao. Huwezi kumtofautisha mtu wa cheo cha chini na yule wa kawaida wala humtofautishi
bwana na mtumwa”.
Ni meelezo gani baada ya haya yanayoweza kutolewa juu ya mwanajeshi Mwarabu wa Kiislam?
4. Vita vya Waislam dhidi ya Waberber wa Afrika ya kaskazini vilitokea jangwani ambapo
Waislam wengi waliuawa. Kuna yeyote aliyesema chochote kuhusu “ardhi ya rutuba”?
114
Tunaweza kuongezea kwa kuuliza: “Nani ambaye angeweza kukibeba kichwa chake mkononi
mwake kwenda kupigana na jeshi lenye nguvu sana la maangamizi ili kufurahia maisha ya utajiri
katika mabustani ya ardhi hiyo yenye rutuba”?
Je, huo sio uongo na uzushi wenye lengo la kupotosha ukweli?
Yawezekana vipi kwa mpenda maisha ya dunia akakitafuta kifo?
Historia ya Kiislam imejaa visa vya ushujaa ambao hakuna yeyote ambaye angeweza kuufanya
isipokuwa muumini imara ambaye imani yake imekita mizizi moyoni mwake na kujaa katika akili
na maisha yake.
Matendo hayo ya kishujaa yasingeweza kuja isipokuwa kutoka kwa mtu aliyekuwa kama malaika
na akafahamu kwa nini alikuwa akiyatoa muhanga maisha yake na ni kitu gani alichokuwa
akikitaka badala ya maisha hayo. Ni nadra sana kukuta ushujaa kama huo katika taifa lolote la
ulimwengu huu.
Katika vita ya Qadisiya askari mmoja wa Kiajemi aliita kwa sauti: “Nani atakayethubutu
kupambana nami?” Mwarabu mmoja aliyeitwa Elbaa bina Jahsh Al-Ujaili alijitokeza na kupambana
na askari yule wa Kiajemi. Alimpiga mtu yule kifuani mwake. Mwajemi akapiga kwa upanga
wake kwenye tumbo la Mwarabu. Muajemi akafa mara moja lakini Elbaa akaanguka chini ardhini
na hakuweza kusimama. Alijaribu kuurudisha utumbo wake lakini hakuweza. Kisha Mwislam
mwingine alipita jirani na Elbaa ambapo alimuomba mtu huyo amsaidie kuurejesha utumbo wake.
Mtu huyo alipomsaidia, Elbaa aliishikilia ngozi ya tumbo lake na kutambaa kuelekea mahali
walipokuwa Waajemi lakini alikufa akiwa kwenye umbali wa dhiraa 30 kutoka kwenye ardhi ya
Waajemi.
Katika vita ya Yarmouk watu wengi walipaza sauti zao wakisema: “Nani wa kujitokeza kupambana
mpaka kifo? Sio kupambana kwa lengo la ngawira za vita?
Waraqa Ibn Muhalhal Al-Tanoukhy ----- mshika bendera wa Abu obeida katika vita ya Yarmouk ---
-- alisema kwamba kijana mmoja kutoka katika kabila la Azd alikuwa miongoni mwa watu wa
mwanzo kuanza mapambano.
Kijana huyo alimwambia kiongozi wake Abu Obeida: “ Ewe Amiri ninataka kukata kiu ya moyo
wangu kwa kupambana na adui yangu na adui wa Uislam. Ninataka kuitoa roho yangu
katika njia ya Mwenyezi Mungu ili niweze kupata heshima ya kufa shahidi. Ninakuomba
uniruhusu, ewe Amiri. Isitoshe kama wataka nipeleke ujumbe wako kwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu nitafanya hivyo kwa ajili yako!”
Huyu ni mmoja katika vijana wa Kiislam. Itakuwaje kuhusu wanaume pamoja na watu wazima?
Hakika walitaka kuueneza Uislam au kufa kwa ajili yake.
115
Huko Nahawand, katika mapambano makubwa zaidi dhidi ya Waajemi, Al-Nuiman Ibn Muqarren
Al-Mazani alitamka maneno yafuatayo kabla ya kwanza kwa mapambano: “Ewe Mwenyezi
Mungu ipe nguvu dini yako, wape ushindi waja wako na nijaalie mimi kuwa mtu wa kwanza kufa
shahidi siku hii ya leo!! Ee Mwenyezi Mungu ninakuomba moyo wangu ufurahike kwa ushindi
mkubwa utakaoipa nguvu dini yako ya Uislam. “Ndugu zangu semeni Amen”.
Kwenye mpaka wa kaskazini ----- katika Asia ndogo ----- kiongozi wa Kiislam Habib Ibn Maslama
alimwambia mkewe Um Yazid Al-Kilabiya kwamba usiku ule angemuua Murayan, kiongozi wa
Kirumi. Habib alipokwenda kwenye hema la kiongozi yule wa kirumi alikuta tayari Murayan
ameuliwa na askari wa Kiarabu. Aliandamana na askari yule mpaka kwenye kambi ya Waislam.
Iligundulika kuwa askari aliyetenda kitendo kile cha kishujaa alikuwa ni yule mke wa kiongozi wa
Kiislam.
Je, umma unaotaka mali ungeweza kuonesha ushujaa na kujitolea muhanga katika kiwango hicho?
Sahaba mmoja wa Mtume (S.A.W.) aitwaye Amru Bnul Jamouh alikuwa mlemavu. Alikwenda
kushiriki katika vita vya uhudi japo angeweza kusameheka kama angeamua kutokwenda. Lakini
alisema: “Ninapenda niingie peponi nikiwa na mguu wangu wenye ulemavu”. Kitu gani
kilichomsukuma mtu huyu kwenda kupambana kama sio kwa sababu ya kupenda kifo na akhera?
Kwa kweli tunaweza kusema kwamba historia ya Ulaya ilikuwa na baadhi ya wasomi ambao
hawakuwa na chuki dhidi ya Waislam na ambao walifahamu sababu ya kweli ya mapambano yao.
Stanley Lane Poal katika kitabu chake “Arabs in Spain” anasema: “Shauku ya Waarabu
kufanya harakati za mapambano ilichochewa na hamu kubwa ya kueneza mafundisho ya dini
yao. Walipambana dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walipambana
kwa sababu walitarajia kupata thawabu za kufa shahidi huko mbinguni”.
Hapa kuna baadhi ya Nukta za Kuzingatiwa
1. Vita mbalimbali baina ya Waajemi na Warumi vilidumu kwa kipindi cha karne nne kwa sababu
za kimaada lakini hakuna yeyote kati yao aliyeweza kupata ushindi wa wazi dhidi ya mwingine.
Hilo lilitokana na ukosefu wa imani. Mabedui wenye silaha ya imani walipozishambulia tawala
hizo mbili waliweza kupata ushindi na hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yao.
2. Mtume wa Mwenyezi Mungu alituma barua mbalimbali kwenda kwa wafalme, maamiri na
watawala wote wa zama zake akiwataka wauamini Uislam, na waendelee kubaki na tawala na falme
zao. Katika mwelekeo huu, uroho wa mali uko wapi?
3. Waislam walikuwa wakiwataka maadui zao kuchagua moja ya mambo matatu: Uislam, Jizya na
vita. Wale waliochagua Uislam walikuwa katika amani na wakawa kama ndugu zao, wakiwa na
“haki na majukumu sawa” kama Mwislam mwingine yeyote.
Jizya ni kiasi kidogo cha pesa kilichokuwa kikitolewa kwa sababu ya muhusika kuwa chini ya
ulinzi wa Waislam na ili kufaidika na mfumo wa ustawi wa taifa hilo. Kwa hakika Jizya kilikuwa ni
116
kiwango kidogo zaidi ya kile kilicholipwa na Waislam kwenye hazina yao wenyewe. Na
mwishowe vita lilikuwa kimbilio la mwanzo katika juhudi zao za kuwafikia watu na kuwafikishia
mahubiri.
4. Kiongozi mkubwa wa kijeshi katika historia ya Waislam, Khalid Ibn Al-Waleed, alikufa na
kuacha nyuma yake mtumishi, farasi mmoja na upanga. Ngawira ziko wapi?
5. Askari wa Kiislam walioshiriki katika vita mbalimbali idadi yao haikuzidi laki moja ---- kama
tukizidisha idadi hiyo mara mbili. Na Sawad (sehemu ya kaskazini mwa Iraq), Palestina, Syria au
Delta ya Misri zingetosheleza mahitaji yao ya kimaada kama hilo lingekuwa ndio lengo lao tu.
Wangeweza kuwa matajiri na wenye furaha. Lakini walisonga mbele na kufika China kwa upande
wa mashariki na Hispania na Ufaransa kwa upande wa magharibi. Iko wapi tamaa na pupa ya
dunia?
6. Kwenye matukio mengi tunaona kwamba baadhi ya Waislam walioshikwa mateka katika vita
walifanya kazi ya kuihubiri dini yao hata pale walipouawa na maadui zao. Thomas Arnold katika
kitabu chake “A History of the Call to Islam” alieleza kuwa Wabelgiji walitaka kumuua kiongozi
mmoja wa Kiislam. Kiongozi huyu alizitumia saa zake za mwisho katika kumfikishia Uislam
mhubiri wa Kikristo aliyekuwa amepelekwa kwa kiongozi huyo wa Kiislam kwa lengo la kumfariji.
Arnold pia anaandika kwamba Uislam ulienea mashariki mwa Ulaya kupitia kwa mfungwa wa
Kiislam aliyekuwa amekamatwa wakati wa vita vya Waislam na Wabyzantine. Arnold anasema
kwamba Sheikh Ahmad Al-Mujaddid alikuwa gerezani pindi alipowasilimisha mamia ya wapagani
waliokuwa pamoja naye gerezani. Arnold pia anasema kwamba Waingereza walimfunga mmoja
wa Mawlawiya (mfuasi wa kundi la Sufi) kwa kumtenga katika kisiwa cha Armadan. Mwislam
huyo aliwasilimisha watu wengi kabla ya mauti kumfika akiwa kizuizini.
Enyi Mustashriqiina! Kwanini mmesahau kichocheo hiki cha ndani katika kuhubiri Uislam na
mkachukulia ardhi yenye rutuba huko kaskazini kuwa ndio sababu ya harakati hizi za mapambano?
Acheni kuwa na chuki na vinyongo. Acheni ulaghai, kwani jua linawaka nanyi hamuwezi kuukataa
mwanga wake.
117
KESI YA KUMI NA MBILI
Uislam na Sayansi
Mwendesha Mashtaka: Uislam unapingana na sayansi na falsafa kwa hiyo siyo dini ya maisha
na haistahiki kuwepo.
Hakimu: Tafadhali tuambie ukweli kuhusu suala hili?
Uislam: Itakuwa ni kama kurudia hoja kwa sababu tayari tumekwisha jadili mada kuhusu Uislam
na kwamba ni dini ya sayansi, elimu, maarifa na hoja. Ni rahisi sana kulithibisha hilo kwa sababu
vitabu vingi sana vimeandikwa kuhusu mada hii. Lakini kwa sasa tutajibu kwa kukanusha tuhuma
hizo za Renan hali kadhalika tuhuma zilizodai kwamba Waislam waliichoma moto Maktaba ya
Alexandria baada ya kuivamia Misri kama Gibbon, Butler, Sidio na wengine walivyodai.
Ustaarabu wa Kiislam ulioipatia dunia maendeleo makubwa katika medani zote za maisha, ulifanya
hivyo kwa sababu Qur‟an Tukufu inawataka Waislam wafanye hivyo. Qur‟an inasema:-
“Sema (ewe Muhammad) je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika
hutanabahi wale wenye akili tu” (1)
.
Hivyo basi, tunaona kwamba Mwenyezi Mungu anaitukuza elimu na watu wenye elimu na
kuwachukulia kuwa wenye heshima juu ya watu wengine.
Mwenyezi Mungu ameufanya ushuhuda wa wasomi kuwa sawa na ushuhuda wake na ule wa
Malaika pale anaposema ndani ya Qur‟an Tukufu:-
“Mwenyezi Mungu Na Malaika Na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakuna aabudiwaye ila
yeye tu, ni mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna aabudiwaye isipokuwa yeye tu Mwenyezi
Mungu, mwenye hekima” (2)
.
Hivyo, Mwenyezi Mungu anawatukuza wasomi kwa kuufanya ushuhuda wake kuwa sawa na ule
wa Malaika na ule wa wasomi.
Mwenyezi Mungu vilevile anamuagiza Muhammad (S.A.W.) kuomba dua kwa kusema “Mola
wangu nizidishie elimu” (3)
.
Uislam umeifanya mantiki hii kuwa msingi wa kuhukumu na kuamua kila kitu. Katika Qur‟an
Tukufu tunakuta Aya nyingi sana zenye maneno kama “Ulul albab” au “Ulunnuha” yenye maana ya
watu wenye utambuzi au akili. Katika maeneo mengine tutakuta maneno mbali mbali
yanayozungumza na watu wenye ujuzi.
118
Uislam unawataka watu wasome aina mbali mbali za elimu zinazofuta ujinga katika maisha au
katika dini.
Qur‟an inamtaka binadamu asome na kudurusu sayansi na elimu mbalimbali za mazingira: “Je!
Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni? na kwayo tumeyatoa
matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye
rangi mbali mbali, na myeusi sana. Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao
zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni
wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe” (4)
.
Watu wenye ujuzi hapa ni wale wenye kujua ushuhuda na siri za uumbaji ambazo Mwenyezi
Mungu ameziweka vitu mbalimbali. Hakuna mtu awezaye kujua jinsi mvua inavyonyesha kutoka
mawinguni bila kusoma fizikia na kemia, na wala hakuna awezaye kujua namna mimea
inavyokuwa bila kusoma kitu chochote kuhusu botania wala hatuwezi kujua chochote kuhusu
milima pamoja na aina na mitindo yake mbalimbali bila ya sayansi ya Jiolojia. Mwenyezi Mungu
anasema ndani ya Qur‟an Tukufu: “Hakika wanaomuogopa kweli kweli ni wasomi” (5)
. Anasema
kuwa wanaomuogopa kwa dhati kabisa ni wale wanaodurusu shuhuda mbalimbali za ulimwengu.
Kama wasomi wangemuamini Mungu, elimu yao ya siri za uumbaji ingewafanya wamuogope
Mungu, Muumba aliye Mkuu aliyekiwekea kila kitu utaratibu na kanuni maalum.
Vile vile, katika Qur‟an tunakuta wito wa kusoma baiolojia: “Basi mtu ajitazame ameumbwa kwa
kitu gani; ameumbwa kwa maji yanayotoka kwa nguvu. Yatokayo katikati ya mifupa ya mgongo
na kifua” (6)
. Awamu na hatua mbalimbali za uumbaji wa kiinitete ni sehemu ya elimu na sayansi
ya baolojia na tiba.
Vile vile, Uislam unatutaka kusoma historia ya sayansi ya jamii:“Je, hawatembei katika nchi na
kuona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa wenye nguvu zaidi
kuliko hawa na wakiilima ardhi na kuistawisha zaidi kulik hawa walivyoistawisha na Mitume
wao waliwafikia kwa miujiza ya wazi wazi lakini waliikataa (wakajisababishia maangamizi), basi
hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu
(7).
Mungu pia anasema: “Na ni umma ngapi tuliziangamiza kabla yao zenye nguvu kuliko wao?
Kisha wakapita katika nchi. Je, kulikuwa na makimbilio kwa ajili yao?” (8)
.
Vile vile, katika Qur‟an kuna wito wa kusoma habari za nyota. Baadhi ya majina ya sura za Qur‟an
ni kama vile Radi, Mwanga "Nuru", Moshi, Nyota, Mwezi, Njia za upaaji kuelekea mbinguni,
mkunjo wa jua, mpasuko wa mbigu, nyota za zodiaki, nyota ipitayo usiku, alfajiri, jua, usiku,
dhuha, tetemeko la ardhi. Sura zote zilizotajwa hapo juu zinatoa wito wa kufanya utafiti wa
kisayansi kuhusu mbingu na ardhi.
119
Tunasoma ndani ya Qur‟an: “Sema tazameni ni nini yanayotokea katika mbingu na ardhi na
dalili zote hizi na maonyo hayawafai watu wasioamini” (9)
.
Na “Hakika katika kuumba mbingu na ardhi na kutofautiana kwa usiku na mchana ni dalili
kwa wenye akili” (10)
.
Hadithi nyingi za Mtume (S.A.W.) zinawataka Waislam kuchukua hatua ya matibabu pindi
wanapopatwa na maradhi. Hadithi zote zinazohusu utunzaji wa afya na kufuata kanuni za kula na
kunywa zimekusanywa chini ya kichwa cha habari cha "Tiba ya Mtume".
Kama tungetaka kueleza kila kitu kuhusu wito wa Kiislam unaowataka watu kusoma aina
mbalimbali za elimu ingetuchukua muda mrefu sana. Inatosha kujua kwamba Uislam unaichukulia
jamii nzima kuwa yenye hatia iwapo hawatokuwa na idadi ya kutosha ya wasomi katika kila fani ya
ubobezi. Wanafalsafa wa sheria za Kiislam wamekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kama
umma ulikuwa ukihitajia wasomi mia moja katika fani moja lakini wao wakawa na wasomi tisini
tu, basi umma wote utahesabiwa kuwa wenye hatia mpaka watakapoweza kupata idadi inayotakiwa.
Wanasayansi na wasomi wengi wa kimagharibi wametambua na kuyakubali maendeleo makubwa
yaliyofanywa na Uislam katika fani za tiba, kemia, bailojia, hisabati, sayansi ya jamii, jiografia,
historia na nyota. Kitabu cha Zigrid Honke kinachozungumzia athari za ustaarabu wa Waarabu
kwa bara la Ulaya ni ushahidi tosha wa shukrani anazozitoa kwa Waarabu kwa sayansi na elimu
waliyoitoa kwa binadamu.
Gustav Lebon naye anasema kwamba “Uislam ni dini iliyokuwa karibu zaidi kwenye ugunduzi
wa sayansi kuliko dini nyingine yoyote ile" (11)
.
Dreilber, profesa katika chuo kikuu cha New York aliyetunga kitabu kiitwacho "The conflict
between religion and science" anasema kwamba Baghdad ilikuwa ni kitovu kikuu cha sayansi na
maarifa ulimwenguni wakati wa Khalifa wa ukoo wa Abbas Al-Maamoun mwaka 813, ambaye
alikusanya vitabu vingi, akawatukuza wenye elimu na kuwakirimu. Dreiber akaongeza kuwa
Waarabu waliendeleza sana elimu za zamani pamoja na kugundua elimu mpya ambazo hazikuwa
zikijulikana kabla.
Vyuo Vikuu vya nchi za Kiislam vilikuwa wazi kwa wanafunzi wa Ulaya waliosafiri kwenda
kwenye vyuo hivyo kwa ajili ya kutafuta elimu na maarifa. Hata wafalme na watoto wa wafalme
wa Ulaya walikwenda katika nchi za Kiislam kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali za nchi
hizo.
Sedillot katika kitabu chake "History of the Arabs" anasema "katika miaka ya kati Waarabu
walikuwa watu wa kipekee katika sayansi, falsafa na sanaa. Welieneza elimu popote pale
walipokwenda, utaalamu wao ukaenea mpaka Ulaya na hiyo ikawa sababu ya kuibuka na kustawi
kwake". Sedillot anaendelea kusema: "Pindi Waislam walipozungumzia juu ya ardhi kuwa
katika muundo wa tufe kulikuwa na mgogoro mkubwa katika ulimwengu wa Kikristo.
Kanisa likatangaza kwamba Chrisotper Columbus alikuwa kinyume na dini baada ya
120
kuizunguka bahari ya Atlantic akitumaini kuvumbua na kugundua nchi mpya! Mkutano wa
Salamouk ulikubaliana na hukumu hiyo na hakuna kilichoweza kumuokoa isipokuwa
mashambulizi ya baadhi ya wafalme wa Ulaya. Watu wa Kanisa walitafuta muongozo wa
maelezo ya Mapadre, maandiko ya Manabii, Biblia, Torati na Agano la kale wakamtia
Columbus hatiani".
"Inachekesha sana kujua kuwa Kanisa lilighadhibika na kukasirika pale mwanamama
mmoja aitwaye Mary Montag, mnamo mwaka 1721, alipotambulisha mbinu ya kuchoma
sindano kwenye ngozi kama njia ya matibabu. Kwa hakika njia hii ilikumwa
imeshagunduliwa na Waislam" (12)
.
Gustav Lebon katika kitabu chake "Arab civilizations" anasema: "Katika historia hatuoni
umma uliokuwa na athari hiyo kubwa kuliko Waislam wa Kiarabu. Mataifa yote yaliyokuwa
na mahusiano na mawasiliano nao walichagua kufuata ustaarabu wa Waarabu hata kwa
muda mfupi". Anaongeza kwa kusema: "Athari ya Waarabu huko mashariki haikuwa ya
wazi katika dini, lugha na sanaa pekee bali pia katika utamaduni wa kisayansi".
Profesa Libri anasema: "Kama Waarabu wasingekuwepo katika jukwaa la historia, uibukaji
na uchomozaji na maendeleo ya Ulaya vingechelewa kwa karne nyingi".
Maktaba wa Alexandria:
Yote yaliyosemwa hapo juu yamethibitisha kwamba Uislam unatetea sayansi na maarifa, ni dini ya
akili na fikra. Lakini Mustashriqiina mwingine anaweza kusema: "kama Uislamu uko hivyo, kwa
nini basi Amr Ibn Al-As, kwa amri ya Omar Ibn Al-Khattab aliichoma moto maktaba ya Alexandria
iliyokuwa imejaa vitabu? Kitendo hiki kimemnyima binadamu hazina kubwa ya elimu. Maktaba
hiyo ilichomwa moto na Waarabu waliofikiri kwamba fasihi na maandiko katika maktaba hiyo
yalipingana na mtazamo na desturi za Kiislam. Dini ya sayansi inaelezeaje uchomaji wa maktaba
ya Alexandria?
Kwa kweli, waandishi kadhaa wa kimagharibi walishughulikia mada hii ya maktaba ya Alexandria
kama vile Gibbon, Butle, Sedillot na wengineo lakini hawakufikia hukumu na tija ya mwisho.
Waandishi wengi walitilia shaka kisa kizima.
Gustav Lebon katika kitabu chake cha "The Arab Civilization" anasisitiza kwamba kisa hicho ni
uwongo mtupu na kusema kwamba: Uchomaji uliosemwa wa maktaba wa Alexandria ni tendo la
kishenzi, ambalo halikubaliani na maadili ya Mwarabu au Mwislam. Mtu angeweza kuhoji:
"Wasomi wakubwa waliwezaje kukiamini kisa hicho kwa muda mrefu? Kisa hiki kilichopingwa
katika zama zetu hakihitaji kujadiliwa tena. Hakuna kitu rahisi sana kuliko kuthibitisha kwamba
Wakristo wenyewe walichoma vitabu vingi vya washirikina kabla ya harakati za ukombozi wa
Kiislam".
121
Jack S. Wrestler katika kitabu chake aliuchukulia moto wa Alexandria kuwa uwongo. Wanahistoria
waliokuwepo wakati wa harakazi za ukombozi wa Kiislam kama vile Otikha hawakuwa na
chochote katika vitabu vyao kuhusu hizi shutuma. Vitabu vya wanahistoria wa Kiarabu wa zamani
kama vile Al-Yaqubi, Balathery, Ibn Abdil Hakam, Tabari, Al-Kindi, Al-Maqrizi, Abu Mahasin,
Al-Suyouti na wengineo, navyo pia havikutaja kisa chochote cha aina hiyo.
Mtu wa kwanza kudai kwamba Amr Ibn Al-As alichoma moto maktaba hiyo alikuwa ni Abdul Latif
Al-Baghdadi 1231, kisha akaja Ibnul Qafti 1248 na Abul Faraj Gregorius almalti, anayejulikana
kama Ibunul Ibri (au mtoto wa Myahudi) bila kutoa uthibitisho wowote. Wanahistoria wa leo
waliowanukuu watu hao walitaka kuthibitisha yafuatayo, kwamba:
1. Waislam walikuwa na hamu kubwa ya kuharibu kitabu chochote isipokuwa
Qur‟an na Hadithi.
2. Kisa cha moto hakikusimuliwa na Abul Faraj pekee bali pia kilielezewa na
wanahistoria wawili wa Kiislam: Al Baghdadi na Ibnul Qafti.
3. Wanaharakati hao wa Kiislam walichoma moto vitabu vya Waajemi pia, kama
ilivyoelezewa katika kitabu cha Haji Khalifa kiitwacho "Kashful Zunoon".
4. Uchomaji moto vitabu ni kitu cha kawaida kilichokuwa kikitendwa na kila aliyetaka
kuwaadhibu wale waliompinga kama alivyofanya Hulagu wa Tartar pale alipovitupa vitabu
vya Waislam katika mto Tigris.
Tunasema kwamba wazo la kwanza halikubaliki kwa sababu ilikuwa ni tabia ya Waislam
kuhamasisha na kuhimiza elimu. Abul Faraj mwenyewe alisema kwamba Amr Ibn Al-As
alimsikiliza Yuhanna "Yohana" Mgrammaria.
Ama kuhusu madai ya Haji Khalifa tunaweza kusema kwamba hachukuliwi kama rejea nzuri katika
masuala ya kihistoria kwa sababu alikufa mwaka 1657 A.D. Na kama Waislam wangekuwa
wamevichoma moto hivyo vitabu, wanahistoria wengine walioishi kabla ya Haji Khalifa
wangekuwa wamelitaja tukio hilo katika vitabu vyao.
Haipaswi kumlinganisha Hulagu na Omar Ibn Al-Khattab kwa sababu huyo wa kwanza alitaka
kuharibu na kubomoa staarabu mbali mbali za zama zile, wakati ambapo huyo wa pili alikusudia
kueneza utamaduni na maarifa.
Baadhi ya wanahistoria wa zama zetu walieleza mengi kuhusu simulizi ya Abul Faraj kuhusu
maktaba hiyo. Wanahistoria hawa wanaamini kwamba Amr na Omar hawana hatia na hawahusiki
hata kidogo na tuhuma ya uchomaji moto. Haya hapa aliyosema Abul Faraj: "Pindi Waarabu
walipoingia Misri palikuwapo mtu mmoja mashuhuri aitwaye Yahia “Yohana‟ Mgrammaria. Mtu
huyu alikuwa kasisi katika mji wa Alexandria. Aliamini katika Ukristo wa Yakobo na kuitukuza
imani hiyo (ya Sauri). Baadaye alilikataa wazo la utatu. Maaskofu walikutana naye na kumtaka
122
arudi katika imani yao lakini alikataa, hivyo wakaishusha hadhi na nafasi yake. Aliendelea kuishi
mpaka wakati Waarabu walipoifungua Alexandria, akakutana na Amr ambaye alijulikana sana kwa
kuhimiza na kuhamasisha elimu na sayansi.
Amr alimheshimu na kusikiliza hotuba zake za kifalsafa akafurahishwa sana na jambo hili kwa kiasi
kwamba alisuhubiana naye sana na kumfanya kuwa mtu wake wa karibu sana. Siku moja Yahia
alimwambia Amr: "umetaifisha kila kitu katika mji wa Alexandria, unachokihitaji au kukiona kina
manufaa kwako unakichukua bila pingamizi lakini usichokitaka ningependa kukichukua". Amri
akasema: "Unataka kitu gani?" Yahia akasema: "Vitabu vya falsafa vilivyopo katika makabati ya
kifalme". Amr akasema: "Siwezi kufanya hivyo bila kumsikiliza kiongozi wa Waumini Omar Ibn
Al-Khattab". Hivyo alimwandikia Ibn Al-Khatabu (Omar) akitaka ushauri wake. Omar akajibu
akisema: "Ama kuhusu vitabu ulivyovitaja ninasema kwamba vile vinavyokubaliana na kitabu cha
Mwenyezi Mungu (Qur‟an) vinatakiwa kudhibitiwa kwa sababu Qur‟an inatosha. Kama vina
mambo yanayopingana na Qur‟an, basi vinatakiwa kutupiliwa mbali. Hivyo Amr alivigawa vitabu
hivyo kwenye hamami ili vichomwe moto. Vitabu hivyo viliteketezwa kwa muda wa miezi sita!
Sikia hayo na ushangae!"
1. Kwanza tunaweza kusema kwamba simulizi hii inaonekana kuwa ni ngano na uwongo. Ibn Al-
Ibri alisema kwamba hivyo vitabu vingetosha kuchomwa katika hamami elfu nne zilizo kuwepo
katika mji wa Alexandria kwa muda wa miezi sita na hili linaonekana kutoingia akilini kwa sababu
vitabu vinavyodaiwa kuchomwa moto vilikuwa ni laki saba. Kama vilikuwa vimechomwa katika
hamami 4000 basi kila hamami ingekuwa imechukua vitabu 175, idadi hii ingeteketea kwa muda
wa siku chache tu sio kwa muda wa miezi sita.
Vile vile, tunashaka kwamba palikuwa na vitabu laki 7 au vijarida kwa sababu tukichukulia
kwamba kila mtunzi aliandika vitabu ishirini basi idadi ya watunzi itakuwa ni elfu thelathini na tano
na hilo linaonekana kuwa la kufikirika yaani sio kweli kwa wakati huo wa enzi za ulimwengu wa
zamani bila kuhesabu watunzi waliokuwa Ugiriki na Roma.
Mbali na hayo, kama Ibn Al-As angetaka kuiteketeza maktaba hiyo angeweza kuichoma moto mara
moja na asingeikabidhi kwa wamiliki wa hamami zinazodaiwa kuwepo. Yuhanna au watu wengine
wangevichukua vitabu hivyo kutoka kwa wamiliki wa hamami kwa gharama yoyote ile na vitabu
vingi vingeonekana hapo baadaye, kitu ambacho kamwe hakikutokea.
2. Butler ameeleza pia kwamba Yuhanna aliyesemwa alifariki dunia miaka thelathini au arobaini
kabla ya Waislam kuingia Misri.
3. Kama kisa hicho kingekuwa cha kweli wanahistoria wa mwanzo wangekizungumzia hata kwa
mukhtasari.
4. Maktaba inayosemwa ilichomwa moto mara mbili: Mara ya kwanza mwaka 48 B.C.
ilipochomwa moto na askari wa Kaisari Julius, na mara ya pili ni mwaka 391 A.D. zama za Kaisari
123
Theodosis „338 – 395‟. Hivyo basi, kisa hiki cha uchomaji moto maktaba kilielezewa kwa matukio
haya mawili kama mfano.
5. Orazius aliizuru Alexandria katika sehemu ya kwanza ya karne ya tano na kusema kwamba
katika ziara yake kwenye maktaba hiyo alikuta rafu tupu bila ya vitabu. Kwa hiyo vitabu
vilivyokuwa katika maktaba tokea enzi za Ptolemy havikuwepo tena mwishoni mwa karne ya nne
A.D. yaani zama za Theodosis, wakati wa tukio la pili la uchomaji moto.
Maktaba hiyo pia haikutajwa katika fasihi ya karne ya sita au ya saba. Inafahamika kwamba Misri
kabla ya ujio wa Waislam tangu zama za Diocletian ilikuwa katika hali ya uchakavu na udhaifu
mkubwa katika kilimo, uzalishaji, sayansi, elimu na fasihi. Na sio sahihi kwamba watu wa zama
hizo wangejali kuitunza tena maktaba kama ilivyokuwa hapo awali.
6. Mafundisho ya Kiislam yanahimiza na kutetea heshima ya dini zote na vitabu vyake na bila
shaka Waislam wanaweza kufaidika na vitabu hivyo. Hivyo, kisa hicho kinaonekana kupingana na
matendo ya Kiislam ambayo yasingeruhusu kitendo chochote kibaya dhidi ya kitu chochote
kinachobeba jina la Mungu.
7. Chukulia kwamba maktaba ilikuwepo mpaka wakati wa ujio wa Waislam, hakuna kilicho
wazuia Warumi kuibeba maktaba hiyo na kuipeleka Constantinople wakati wa makubaliano ya
usitishaji vita walioufanya na Waislam. Mbali na hilo, Amr aliwaruhusu kuchukua chochote
walichoweza kuchukua. Walikuwa na muda wa kutosha kubeba na kuhamisha maktaba nyingi, sio
moja tu. Na hivyo kisa hicho ni uwongo mtupu.
8. Kifungu kisemacho "Sikia hayo na ushangae!" kilichoandikwa na Abul Faraj mwishoni mwa
kisa chake kinaweza kueleweka katika namna mbali mbali:
1. Kwamba kisa hicho sio cha kweli na haiwezekani.
2. Kwamba aliamini kisa hicho na alikuwa na chuki dhidi ya Omar na Amr.
Vyote vile, ndani ya mshangao huo na wito wa kusikia kuna kitu kisichokuwa kweli na
kisichokuwa sahihi, ambacho kinafanya kisa hicho kiwe uwongo mtupu.
Rejea: 1. Qur‟an - {39:9}
2. Qur‟an - {3:18}
3. Qur‟an - {20:114}
4. Qur‟an - {35:27 – 28}
5. Qur‟an - {30:25}
6. Qur‟an - {86:5 – 7}
7. Qur‟an - {30:9}
8. Qur‟an - {Surah 26}
9. Qur‟an - {10:101}
124
10. Qur‟an - {3:190}
11. Gustav Lebon – The Arab Civilization – Uk. 126
125
KESI YA KUMI NA TATU
Uislam na Mwanamke
Mwendesha Mashtaka: Uislam uliwanyima wanawake haki zao kwa kuwapa nusu ya fungu la
wanaume katika mirathi, kuwaruhusu wanaume kuoa hadi wanawake wanne kwa wakati mmoja, kuifanya
talaka kuwa haki ya wanaume tu, kuwafanya wanaume kuwa na mamlaka juu ya wanawake na hivyo
Uislam uliwanyima wanawake haki nyingi walizopewa wanaume.
Hakimu: Islam, jitetee!
Uislam: Mada hii ya haki za wanawake katika Uislam haikutakiwa kujadiliwa hapa kwa sababu suala
hilo kwa sasa liko wazi kabisa kama lilivyo suala la dunia kuwa tufe, ambapo wanajiografia hawaendelei
tena kuwafanya watu waliamini kama walivyofanya katika kizazi kimoja kilichopita.
Uislam uliwapa wanawake haki nyingi sana ambazo wanawake wa huko magharibi wamekuja kuzipata
baada ya kupita karne nyingi. Wamepewa haki hizo katika karne ya sasa tu na katika baadhi ya masuala ya
wanawake wa magharibi mpaka leo bado wanapigania kupata haki hizo. Hapa hatutajadili madai ya Cara
De Foe kuhusu wanawake na haki zao za kusoma na kufaidika na mali zao, kufanya biashara, kutumia
mirathi zao, au katika kuchagua mume. Waandishi wengi sana wameandika kuhusu mada hizi na hapa
tutakanusha tuhuma zilizotolewa na De Foe kwa utaratibu ufuatao:
Wanawake kabla ya Uislam.
Mtazamo wa Uislam kuhusu wanawake.
Ndoa ya wake wengi.
Talaka.
Udhibiti katika ndoa.
Adhabu katika ndoa.
Tatizo la wanawake kuchanganyika na wanaume.
Wanawake hapo Zamani:
Ustaarabu wa Kirumi ulimchukulia mwanamke kama mtumwa anayemilikiwa na mwanaume, alikuwa na
haki wakati akiwa mdogo au wakati mwingine hakuwa na haki kabisa.
Dini za kale za India ziliamini kwamba "balaa, kifo, jahannam, sumu, nyoka na moto vyote ni bora kuliko
mwanamke" na kwamba mwanamke anatakiwa kufa mara tu mume anapokufa, kwani mume ndiye bwana
na mmiliki wake. Kama akiuona mwili wa mumewe kwenye moto alitakiwa kujitupa ndani ya moto huo au
la laana ya milele ingekuwa ndio majaaliwa yake.
Katika sheria za Manu Dahr Ma Sastra tunasoma yafuatayo kuhusu wanawake:
“Mwanamke yeyote, awe binti, mwanamke mdogo au mwenye umri mkubwa haishi kwa hiari yake.
Msichana au mtoto wa kike anaishi kwa utashi au hiyari na mapenzi ya baba yake, mwanamke aliyeolewa
anaishi kwa utashi wa mumewe na mwanamke wa umri mkubwa anaishi kwa hiari ya watoto wake wa
126
kiume kama atakuwa mjane. Kamwe mwanamke hawezi kujitegemea. Hawezi kuolewa baada ya kifo cha
mumewe, anatakiwa kuacha raha zote za maisha na hatakiwi kuolewa tena. Katika uhai wake mali zake
zote zinamilikiwa moja kwa moja na mumewe".
Wagiriki walimchukulia mwanamke kama aina ya mali na bidhaa iliyoweza kuuzwa na kununuliwa,
walikuwa wakimhesabu kama kazi ya shetani.
Katika Agano la Kale tunasoma maneno yafuatayo: "Nikageuka na moyo wangu ulikazwa katika kujua
na kupeleleza na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko ili nifahamu ya kuwa uovu ni
upumbavu na upumbavu ni wazimu. Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani
mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo" (1)
.
Kuhusu Kanisa Katoliki mwandishi wa Kidenmark Wieth Knudesen aliandika kuhusu wanawake katika
zama za kati akisema: "Wakati huo Kanisa Katoliki lilimchukulia mwanamke kama kiumbe wa daraja
la pili".
Huko Arabia hali ya mwanamke ilikuwa mbaya sana. Mwanaume angekasirika sana baada ya kuambiwa
kwamba alikuwa amepata mtoto wa kike (katika familia yake). Angeepuka kukutana na watu kwa sababu
ilichukuliwa kuwa kitu cha aibu kuwa na mtoto wa kike. Baadhi ya makabila ya Kiarabu yalikuwa
yakiwazika watoto wa kike mara baada tu ya kuzaliwa. Kama mtoto huyo angepata bahati ya kuishi basi
angekuwa na maisha mabaya ya taabu. Hakuwa na haki ya kurithi na wakati mwingine alilazimishwa
kufanya kazi ya umalaya na baada ya kifo cha mumewe angerithiwa kama vitu vingine vilivyoachwa na
mwanaume husika.
Katika mji wa Roma kulikuwa na mkutano mkubwa kujadili masuala ya mwanamke, ambapo iliamuliwa
kuwa mwanamke ni kiumbe asiyekuwa na roho, na hivyo asingerithi katika maisha yake yote na kwamba
ni kitu kichafu na hakupaswa kula nyama wala kucheka. Walimwamuru mwanamke kukaa kimya na
walifikia hatua ya kuwekwa kufuli ya chuma mdomoni mwake. Wanawake kutoka familia tajiri au maskini
waliendelea kubaki nyumbani au kutembea mitaani wakiwa na kufuli kwenye midomo yao.
Qassem Amin anaelezea kwa ufupi hali ya mwanamke akisema: "Mkuu wa familia katika jamii za
Kirumi, Kigiriki, Kijerumani Kihindi, Kichina na Kiarabu ndiye aliyekuwa mmiliki wa mkewe.
Angeweza kumnunua au kumuuza kama kitu chochote kile. Mkataba wa ndoa ulimruhusu
mwanaume kuamiliana na mkewe katika namna yoyote aitakayo. Haki zote za mama zingehamia
kwa mume na angeweza kumuuza mkewe kwa mtu yeyote".
Hiyo ndiyo hali ya hapo zamani. Lakini katika zama za sasa, mnamo mwaka 1586 ulifanyika mkutano
nchini Ufaransa kujadili suala la mwanamke iwapo alikuwa binadamu au la. Baada ya majadiliano
iliamuliwa kwamba mwanamke ni binadamu aliyeumbwa kumtumikia mwanaume.
Mnamo Februari 1938 sheria maalum ilianzishwa kwa lengo la kukomesha sheria zote za awali ambazo
hazikumruhusu mwanamke kutumia na kushughulikia mali zake. Kwa mara ya kwanza katika historia ya
mwanamke wa Kifaransa mwanamke aliweza kuwa na akaunti ya benki iliyokuwa na jina lake.
Katika kitabu chake kuhusu haki za binadamu katika Uislam, Dr. Ali Abdul Wahed ameandika kwamba
kifungu namba 217 katika sheria ya Ufaransa kiliainisha kwamba mwanamke aliyeolewa, hata kama
127
kulikuwa na sharti la kutenganisha mali za mke na za mume, mwanamke huyo hakuwa na haki ya kutoa,
kuhamisha au kuweka rehani mali yake bila ridhaa ya mumewe. Dr. Abdul Wahed anaongeza kusema
kwamba sheria hiyo hiyo, hata baada ya kufanyika marekebisho hadi sasa bado ina kasoro nyingi.
Nchini Uingereza, mpaka mwaka 1850, wanawake hawakuhesabiwa kama raia. Mpaka mwaka 1882
wanawake hawakuwa na haki binafsi na hawakuwa na uwezo wa kumiliki mali yoyote. Mwanamke
angemfuata baba au mume wake.
Chuo Kikuu cha Oxford hakikuwachukulia wavulana na wasichana kuwa na haki sawa kwenye vyama na
taasisi za wanafunzi mpaka baada ya sheria ya Julai 26/1964.
Msimamo wa Uislam kwa Mwanamke:
Uislam ulitangaza kwamba mwanaume na mwanamke wako sawa katika kila kitu isipokuwa katika masuala
ambayo yanahitaji kutofautishwa. Tunasoma ndani ya Qur‟an kwamba:- Na "Waumini wanaume na
Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi" (2)
.
“Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni
mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi" (3)
.
“Wanaume wana fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliowakaribia, na wanawake wana
fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliowakaribia” (4)
.
Aya zilizotajwa hapo juu zinawashughulikia na kuamiliana na wanaume na wanawake kwa usawa. Hata
hivyo, kuna baadhi ya maeneo ambayo yalidhaniwa na maudui wa Uislam kuwa ni kasoro zilizoweza kuwa
na athari dhidi ya Uislam. Na hivyo wakapiga kelele kwa huzuni dhidi ya Uislam kwa kudhani kuwa
Uislam ulimnyima mwanamke haki zake. Miongoni mwa mambo waliyodhani kuwa ya dharura sana ni
pamoja na ndoa ya wake wengi, talaka, kumdhibiti na kumuadhibu mke husika.
Kabla ya kujadili mada hizi tunapaswa kutambua kwanza kwamba Uislam ni dini ya silika, maumbile na
uhalisia. Kwa kweli mwanaume hufanya vyema zaidi ya mwanamke katika baadhi ya nyanja zinazohitaji
nguvu, ustahimilivu, kazi ngumu na juhudi nzito sana. Misuli ya mwanaume ni imara zaidi ya ile ya
mwanamke. Mwanamke huathiriwa na ukosefu wa damu katika kipindi cha hedhi ambayo huathiri mwili
wake. Huathiriwa pamoja na ujauzito na uzazi ambapo bila shaka huudhoofisha mwili wake. Al Aqqad
anasema: "Siku zote wanaume wamekuwa wakifanya vizuri kuliko wanawake hata katika nyanja
ambazo kwa kawaida ni za wanawake, kama vile upishi, mavazi na vipodozi".
Ndoa za wake wengi:
Qur‟an Tukufu inasema:
“Oweni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu watatu au wanne wanne, na mkiogopa kuwa
hamuwezi kuwafanyia uadilifu basi oweni mmoja tu” (5)
.
Na “hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, japokuwa mtajitahidi” (6)
.
128
Kwa kweli, mke mmoja ni jambo maarufu katika Uislam ambapo takriban asilimia 98 ya Waislamu wana
mke mmoja mmoja. Lakini mazingira fulani fulani humlazimisha mwanaume, awe Mwislam au la, kuoa
mke mwingine.
Baadhi ya mazingira hayo yasiyokuwa ya kawaida ni pamoja na maradhi sugu na ya kudumu ya mke
husika, utasa au mwanaume kushindwa kuvumilia wakati wa hedhi au baada ya uzazi. Hata hivyo matibabu
yanapaswa kufanyika kulingana na kadhia husika.
Abu Zuhra, mmoja wa wasomi wakubwa wa Kiislam anasema kwamba kuowa wanawake wengi wa halali
ni bora sana kuliko kuwa vimada wasio wa halali kama hali ilivyo katika ulimwengu wa Kimagharibi.
Ndoa ya wake wengi inaweza kuchukuliwa kuwa ufumbuzi wa suluhisho kwa zile jamii zenye ziada ya
wanawake wengi hasa baada ya vita. Hakuna shaka kwamba ni bora kwa wanawake kumkubali mwanaume
aliyeoa kuliko kukubali kuwa na uhusiano kama kimada, ambaye hawezi kudai haki yake yoyote wa ajili
yake au watoto wake kutoka kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano naye. Pia mwanamke anaweza
kuheshimika zaidi kuliko kuachwa kuwa mwanamke aliyepita muda wa kuolewa na kuwa mseja katika haya
maisha ambayo mara zote yanahatarishwa na umasikini na ufukara.
Katika baadhi ya jamii, ndoa ya wake wengi ni njia bora ya kuongeza kizazi cha baadaye hasa katika
mazingira ambayo kuna shida na haja ya nguvu kazi kwa ajili ya utendaji kazi, kama ilivyo katika nchi za
mashamba, au kwa ajili ya mapambano ya vita.
Waislam wana jukumu la kufanya juhudi kwa ajili ya dini yao. Katika hali hii ndoa ya wake wengi inaweza
kuwa ufumbuzi wa kufidia idadi ya watu waliokufa katika vita na mapambano. Ndoa pia huwafidia wake
wengi waliopoteza waume wao katika vita. Ni njia ya kuzuia ongezeko kubwa la wanawake ambao la sivyo
wangeachwa bila ya kuolewa.
Ndoa ya wake wengi, kwa upande mwingine sio kitu kipya kilichozushwa na Uislam. Ni kitu kilichokuwa
kikijulikana katika staarabu zote, katika Agano la Kale na kutambuliwa na Agano Jipya isipokuwa kwa
Askofu asiyeweza kuendesha maisha yake ya kidini akiwa na wake wengi. Katika hali hiyo anatakiwa
kuwa na mke mmoja. Sheria zilizotengenezwa na binadamu ndizo zilizopiga marufuku ndoa ya wake wengi
katika ulimwengu wa Kimagharibi. Bwana M. F. Hashimy, msomi wa Kikristo aliyeingia katika Uislam
alisema katika kitabu chake "Al Adiyaan fi Kaffat Al Mizan" uk. 105 – 106 kwamba Ukristo ulikuwa
ukitambua ndoa ya wake wengi mpaka karne ya 17 na viongozi wa Kanisa huko Ulaya waliiruhusu na
kuwatambua watoto halali wa Kifalme kutoka kwa wake mbalimbali wa familia za kifalme. Hilo ni
ungamo la mfuasi wa Kanisa na msomi wa sheria za Kimagharaibi.
Staarabu za zamani hazikuweka kikomo cha ndoa za wake wengi, lakini Uislam uliweka kikomo cha ndoa
za wake wengi pamoja na kuziwekea kanuni na masharti. Uislam pia ulibadilisha mfumo wa utumwa,
ukawaruhusu Waislam kuwaoa baadhi ya watumwa wa kike baada ya vita au baada ya ongezeko kubwa la
idadi ya wanawake. Katika hali hii wanaume walipata kuwatunza hawa watumwa, wakiwalinda na
wakawapa majina yao watoto waliotokana na hawa watumwa. Katika hali hii hawa watumwa wasingekuwa
kitu kinachochezewa na kila mtu. Wasingeiuza miili yao kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi na
kifiziolojia. Ungekuwa mzigo mkubwa kwa jamii kama kungekuwa na watoto wengi wasiokuwa wa halali.
129
Ni muhimu kutanabahisha hapa kwamba katika Jamhuri ya Muungano wa nchi za Kiarabu "United Arab
Republic" mwaka 1963 kulikuwa na maswala kwa ajili ya sheria ya kudhibiti ndoa za wake wengi na
talaka, na ukaruhusu maswala hayo kupelekwa mbele ya hakimu maalumu na kwa sababu zenye kuridhiwa.
Mswada huo ulikataliwa na kamati iliyoujadili. Kamati hiyo iligundua kuwa kiwango cha ndoa za mitala ni
asilimia 2 tu na ikagundua pia kwamba nusu ya matukio haya yalikuwa halali na yenye kuridhiwa.
Walikuta pia kwamba matukio na kesi za talaka nazo vile vile zilikuwa halali na kiwango cha talaka
kilikuwa kikiendelea kupungua muda hadi muda. Wakaamua kwamba hakukuwa na sababu ya kuweka
sheria hiyo.
Mwisho, nilisoma katika gazeti liitwalo "Saut Al Islam" toleo la 90 (Sauti ya Uislam) kwamba hatimaye
Ujerumani ilikuwa imeruhusu ndoa za wake wengi. Kwa hiyo tunaona kwamba kitu kile kile
kilichohesabiwa kama aibu na tusi dhidi ya Uislam kilifanywa na nchi ya Kikristo ya huko Ulaya. Kwa
nini? Ninafikiri ni hitajio la dharura lisilozuilika.
Talaka:
Uislam unaichukia talaka na kujaribu kuizuia. Unatetea ndoa ya kudumu na ya daima. Tunasoma katika
aya zifuatazo za Qur‟an Tukufu:-
“Na katika dalili zake ni kuwa amekuumbieni wenzi wenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye
amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika hayo mna mazingatio kwa watu
wanaofikiri” (7).
“Wao (wake zenu) ni nguo kwenu na nyinyi ni nguo kwao” (8)
.
Uislam haukuipenda talaka na ulifanya na kuweka michakato muhimu ya kutatua matatizo ya kijamii bila ya
kukimbia kwenye talaka pindi ilipowezekana. Qur‟an Tukufu inasema:-
“Na kaeni nao (wake zenu) kwa wema, na ikiwa mmewachukia basi huenda mkachukia kitu na
Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake” 9)
.
“Na wanawake mnaoogopa uasi wao, basi waonyeni kwanza na waacheni peke yao katika vitanda, na
mwishowe wapigeni kidogo na kwa ulaini. Watakapo watii, basi msiwatafutie njia ya kuwaudhi hakika
Mwenyezi Mungu ni mtukufu mkuu”(10)
.
“Mtakapochelea kuwepo mfarakano baina yao, basi pelekeni mwamuzi katika watu wa mume na
mwamuzi katika watu wa mke. Kama wote wawili wakitaka mapatano, Mwenyezi Mungu atawawezesha,
Mwenyezi Mungu ni mjuzi, mwenye khabari za mambo yote” (11)
.
“Na Kama mke akiogopa Kwa mume wake kutomjali au kumpa nyongo, basi si vibaya kwao kusikilizana
Kwa suluhu baina Yao, na suluhu ni bora” (12)
.
130
Na hapa kuna baadhi ya Hadithi za bwana Mtume (S.A.W.):
- “Mwenyezi Mungu amelaani kila mwanaume anayeoa sana na kuacha sana”
- “Owa lakini usiache kwani talaka huifanya Arshi ya Mwenyezi Mungu itikisike”
- “Miongoni mwa vitu vinavyochukiwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni talaka, japokuwa ni halali
au imeruhusiwa”
Huo ndio msimamo wa Uislam kuhusu talaka. Lakini katika maisha tunaona kwamba upendo unaweza
kufuatiwa na chuki, na mapatano yakafuatiwa na mfarakano, Uislam ni dini ya uhalisia na unaikubali talaka
kama suluhisho la mwisho.
“Talaka ni mara mbili: Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri” (13)
.
Talaka ni dawa yenye ladha chungu, lakini tatizo la mfarakano ni mbaya zaidi na ni hatari. Kama
inavyotokea wakati mwingine madaktari wakakata kiungo fulani cha mwili wa mtu ili kuviokoa viungo
vingine.
Talaka ni bora sana kuliko hali ilivyo huko Magharibi pale uhusiano baina ya mume na mke unapoharibika
na kuwa mbaya sana. Kwa kuwa hawawezi kutalikiana huwa hawana njia ya usuluhisho, hivyo kila mmoja
wa wanandoa husika humtafuta rafiki. Mke husuhubiana na rafiki wa kiume na mume naye husuhubiana na
rafiki wa kike. Hiyo ni kwa sababu hakuna yeyote kati yao anayeweza kuoana na mtu mwingine kabla ya
talaka, ambayo ni vigumu kuipata. Hivyo basi, suluhisho la mahusiano yao huwa ni kufanya maasi na
uchafu.
Baadhi ya nchi za Ulaya hatimaye zilitambua kuwa talaka ni kipimo kinachoingia akilini, na hivyo
wakarahisisha njia ya kuipata. Nchi ya mwisho ilikuwa ni Italia iliyoruhusu talaka mnamo mwaka 1971,
zaidi ya matukio milioni moja yalitokea mara tu baada ya sheria ya talaka kupitishwa nchini humo. Hapa
tunatakiwa kufikiria maisha yenye maumivu ya familia milioni moja yaliyokuwepo kabla ya talaka
kuruhusiwa. Familia zote hizo zilikuwa zikiishi katika hali duni, na mgawanyiko. Hali hiyo ya kutokuwepo
na talaka ilipelekea kuwa na mfumo wa kijamii usio halali, mfumo wa kuwa na vimada ambao sasa
unaziathiri jamii za Ulaya. Tunatakiwa kufikiria kile ambacho kingetokea iwapo pande mbili husika
zingetumia haki ya kutalikiana baada ya kujaribu kila njia ya usuluhishi. Wangeyafurahia maisha yao na
kuunda familia yenye furaha, ambayo ni ukuta imara wa jamii husika.
Kwa nini Uislam uliiweka talaka mkononi mwa wanaume badala ya wanawake?
Kwa sababu mwanaume anawajibika kwa familia, mahitaji yake ya maisha na ustawi wa watoto. Pingu za
ndoa ndio msingi na mhimili wa yote haya na ingekuwa kitu cha hatari sana kuiweka dhamana hii mikononi
mwa mtu asiyekuwa na wajibu husika. Nasi tunajua vema kwamba ni hali ya maumbile kwa wanawake
kuonyesha hisia sana, kuwa wepesi kwa mambo yasiyokuwa ya muhimu sana. Kama haki ya kuacha
ingewekwa mkononi mwa mwanamke, basi angekuwa na mwenendo wa kufanya maamuzi kwa pupa na
hivyo kuhatarisha uhai wa familia.
131
Uislam ulimfanya mwanaume atoe mahari yote kwa kuangalia hali ya talaka. Hasara hii ya kifedha pamoja
na gharama nyingine za ndoa mpya zitamfanya mwanaume husika afikirie mara mbili kabla ya kuchukua
uamuzi wa kutoa talaka. Kwa upande mwingine Uislam uliwapa wanawake haki ya kuachana na waume
zao kama wangehitaji kufanya hivyo. Hivyo mwanamke huyo, kwa makubaliano na mumewe, anaweza
kuandaa taratibu za talaka lakini katika hali hii atalazimika kutoa kiasi fulani cha pesa kama fidia ya hasara
ya mume: “Na kama (mahakimu) mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi
Mungu basi hakuna lawama juu yao kupokea atakachojikombolea mwanamke” (14)
.
Hata hivyo, Qur‟an Tukufu ilimuonya mwanaume dhidi ya kubishania bei na mke wake au kumtendea
ubaya kwa lengo la kumtisha na kumchukulia pesa yake: “Wala msiwazuie kuolewa ili mpate
kuwanyang‟anya baadhi ya vile mlivyowapa … na ikiwa mnawachukia huenda mkachukia kitu na
Mwenyezi Mungu akatia kheri nyingi ndani yake” (15)
.
Hapa kuna kisa kifupi chenye mazingatio:-
Wakati mmoja Mwislam mmoja mwenye busara alitaka kumwacha mkewe kwa sababu alifikiri kwamba
wasingeweza kupatana. Aliona kwamba litakuwa jambo jema kwa kila moja wao kutafuta mwenza
mwingine anayefaa. Watu wakamuuliza mume: “Ni vitu gani usivyovipenda kwa mkeo?” Akajibu:
“Mwanamume mwenye busara hawezi kumsaliti mkewe na haweki wazi na kufichua siri zake”. Baada ya
talaka walimuuliza mwanaume huyo: “sasa umekwishamuacha je, waweza kutueleza kwa nini ulifanya
hivyo?” Akasema: “kwa nini nimzungumzie sasa hivi ambapo yeye si mke wangu tena?”
Udhibiti katika Ndoa:
Uzoefu na uhalisia wa binadamu vimethibitisha kwamba udhibiti na usimamizi ni kitu muhimu kwa kila
aina ya makutano au muungano, mdogo na hata mkubwa. Mfarakano unaweza kuibuka ndani ya familia
hivyo, ni lazima awepo mtu katika nyumba husika ili kusawazisha mambo na kuchukua maamuzi pamoja na
kuwajibika kwa ajili ya mambo hayo. Na hiyo ikawa sababu ya kuwepo usimamizi. Ni jambo la asili pia
kwamba mwanaume kwa sababu ya kuwajibika kwa ajili ya familia ni msimamizi juu ya familia husika:
“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhili baadhi yao kuliko
wengine na kwa sababu ya mali yao waliyoyatoa” (16)
.
Usimamizi huu unatakiwa kuwa na huruma ukihusisha ushirikiano na uadilifu “Nao wanawake wanayo haki
kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye nguvu na Mwenye hikima” (17)
.
Hali ya mwanamke kuhisi kuwa na udhaifu, shida, wasiwasi na kukosa furaha anapokuwa akiishi na
mwanaume asiyetekeleza usimamizi huu na anayekosa sifa na tabia linganifu ni miongoni mwa uthibitisho
wa hulka ya kiasili ya hitajio la usimamizi wa mwanaume.
Ni aina ya uongozi wa masuala ya familia, ni ulinzi na usimamizi. Aidha, uwepo wa kiongozi katika taasisi
yoyote haubatilishi na hauondoi haki za watu wengine katika taasisi hiyo. Na Uislam umebainisha na
kuweka wazi haki na majukumu ya usimamizi huo. Majukumu ya kifedha katika maisha ya mwanaume
ndivyo vinavyotawala katika kuamiliana na mke na watoto. Ni wema, matunzo, ulinzi na uwajibikaji kwa
maana yake pana.
132
Usimamizi wa mwanaume humaanisha kwamba anawajibika kusimamia utaratibu na nidhamu katika
familia yake ambayo ni taasisi yake ndogo. Ina maana ya kufanya marekebisho sahihi ya mambo yake yote,
kugawa majukumu na uwajibikaji mbalimbali ndani ya familia na kuondosha mandhari na hali inayokwenda
kinyume na upendo, huruma na utengamano.
Hata hivyo, Uislam umempa mwanamke haki ya kuchagua mume. Kwa namna hiyo huweza kumchagua
msimamizi wake na kuweza kutambua kama mwanaume huyo anaweza kumudu vyema usimamizi huo au
la.
“Kama tukilichukulia suala la usimamizi kama jambo la kiutawala, nani kati ya pande mbili hizi
anayetakiwa kuwa msimamizi? Je ni mwanamke au mwanaume? Je haki za watoto zitakuwa jukumu la
mwanamke huyo au mwanaume?”
Adhabu katika Ndoa:
Uislam umependekeza baadhi ya mbinu za kutatua matatizo ya mfarakano unaoweza kuibuka baina ya
mwanaume na mwanamke kabla ya kukimbilia kwenye hatua ya juu zaidi na ya wazi, yaani: talaka. Kuna
hatua nne zinazobainishwa katika aya zifuatazo za Qur‟an tukufu: “Na wanawake mnaogopa uasi wao, basi
waonyeni kwanza, na kisha waacheni peke yao katika vitanda, na mwisho wapigeni kidogo kwa ulaini.
Watakapowatii basi msiwatafutie njia ya kuwaudhi, hakika Mwenyezi Mungu ni mtukufu, mkuu.
Mtakapochelea kuwapo mfarakano baina yao, basi pelekeni mwamuzi katika watu wa mume na mwamuzi
katika watu wa mke. Kama wote wawili wakitaka mapatano, Mwenyezi Mungu atawezesha, Mwenyezi
Mungu ni mjuzi, mwenye khabari za mambo yote” (18)
.
Onyo ni tiba nzuri na rahisi inayojaribu kuondosha mfarakano kwa wema na upendo. Kama njia hii haikufaa
basi kukiacha kitanda itakuwa hatua ngumu zaidi. Njia zote mbili ni rahisi na ni ngumu. Kama hili nalo
halikufaa basi kupiga (kama itafaa) itakuwa ndiyo tiba kabla ya kukimbilia kwenda kwa wapatanishi, jambo
litakalofichua siri za pande husika na kufanya maisha yao kuwa hadithi na simulizi isiyobanduka katika
ndimi za watu.
Maadui wa Uislam, wahubiri au Mustahriqiina (orientalist), walilitumia ovyo wazo la kupiga katika mfumo
wa adhabu katika Uislam. Walilia na kutoa machozi sio kwa sababu kwamba sheria hiyo ni kali bali kwa
sababu wao ni wagojwa. Hebu tuzitafakari hadithi zifutazo za Mtume (S.A.W.):
“Mwenye kuwatukuza wanawake naye ni mwenye kutukuzwa na mwenye kuwafedhehesha
basi huyo ni mtu duni”
“Wabora miongoni mwenu ni wale walio wema na wabora kwa familia zao nami ni mwema
na mbora kwa familia yangu”
“Kamwe watu bora miongoni mwenu hawawapigi wake zao”
“Waumini bora ni wale wenye tabia bora, na wabora miongoni mwenu ni wale walio bora
kwa wake zao (kwa kuwatendea wema).”
“Wosia wangu kwenu ni muamiliane vema na wanawake”
133
“Je haoni haya mwanaume ampigaye mkewe kama kwamba anampiga ngamia wake?”
Kupiga kunatumika tu katika mazingira fulani fulani yaliyo maalum. Haitumiki kwa mwanamke
anayependelea suluhi (upatanishi) au anayependelea talaka. Hakuna shaka kwamba ina athari kwa baadhi ya
wanawake. Al Akkad anasema katika kitabu chake Mukaranat Al-Adian: “Ni upumbavu mkubwa kusema
kwamba wanawake hujipambanua kutokana na mwanamke anayekubali kupigwa na kwamba hakuna
kinachomfanya kuwa mwema zaidi ya kupigwa. Tunasema ni upumbavu kwa sababu ni jambo lenye
madhara, na lisilofaa kwa yeyote”
Tunamtaka Brocklemann na Mustashriqiina wengine waelekeze juhudi zao zote kwenye kutatua tatizo la
wanawake wa Kimagharibi wanaokabiliwa na matatizo makubwa yanayohatarisha familia zao na
mustakbali wa kizazi kipya.
Kile kinachoitwa “Mama mrembo” huko Magharibi na maelefu ya watoto wasiokuwa na baba ni mambo
yanayohitaji suluhisho ambalo litatoa aina ya uangalizi kwa mama na watoto. Takwimu mbalimbali
zinaonesha kuwa mtoto mmoja katika kila watoto tisa waliozaliwa London mwaka 1960 hawakuwa na baba.
Uwiano huu ni mkubwa sana. Uwiano huu ulifikia watoto 57368 mwaka huo. Sasa suluhisho liko wapi?
Je, suluhisho hilo halipo katika Uislam?
Mirathi:
Qur‟an Tukufu inasema: “Mwenyezi Mungu anawausia kwa watoto wenu; mwanaume apewe na fungu la
wanawake wawili” (19)
.
Kwa nini?
Jibu ni rahisi sana na halihitaji maelezo mengi sana. Mwanamke hawajibiki kifedha, iwe kabla ya ndoa au
baada yake. Kabla ya kuolewa, baba anawajibika kumhudumia kwa kumpatia kila kitu, na baada ya
kuolewa mume ndiye anayewajibika kumpa kila kitu. Baadhi ya waandishi wanaamini kuwa mwanamke ni
mwenye bahati zaidi ya mwanaume katika muktadha huu. Kama mwanamke huyo atapata tano na
kuziweka akiba, hiyo itakuwa bora kuliko kumi atakazopata mwanaume halafu akatumia zote.
Je, karne mbalimbali zimempa nini mwanamke zaidi ya vile alivyovipata kwa haki na uadilifu wa Uislam?
Tuanze kutafakari nukta zifuatazo:-
Mnamo mwaka 1960 ilifanyika kura ya maoni nchini Ujerumani kuhusu mwanamke bora katika fikra na
mtazamo wa wanaume. Maoni hayo yalionesha kuwa mwanaume wa Kijerumani hana wazo hata kidogo
kuhusu mwanamke mfanyakazi na hapendelei kumuoa. Mwanamke bora kwake ni “mke wa nyumbani”
anayesimamia nyumba na kuwatunza watoto bila msaada wa mama yake. Ni mke anayepika chakula kizuri
na kufanya kila juhudi katika kumfariji mume.
Ofisi ya takwimu nchini Marekani mwaka 1975 ilieleza kwamba kulikuwa na ziada ya wanawake 3,600,000
kwa sababu ya ugonjwa uliokuwa umeua wanaume wengi zaidi kuliko wanawake.
Ofisi hiyo ilieleza pia kwamba kulikuwa na ongezeko la idadi ya wajane milioni 2 kila baada ya miaka
kumi. Hiyo ina maana kwamba mnamo mwaka 1975 kulikuwapo na zaidi ya wajane wakike wapatao
milioni kumi na moja. Dr. Marione Langer, mtaalam bingwa wa Saikolojia katika mashauri ya ndoa,
134
anasema wazi wazi kuwa: “Kuna masuluhisho mawili yanayowezekana ili kumaliza ongezeko la ziada
katika idadi ya wanawake: ndoa ya wake wengi au kutatufa njia ya kuwafanya wanaume waishi muda
mrefu, jambo ambalo halikutokea”
Gazeti la kila siku la Al-Akhbar lilitoa habari ifuatayo: “Imeelezwa kwamba wanafunzi wa kike
waliochaguliwa kuwa malkia wa urembo walishindwa katika mitihani yao kwa zaidi ya mara moja na
baadhi yao waliweza hata kuacha masomo yao katika chuo kikuu”.
Shirika la habari la Reuter lilieleza kuwa watoto 25,000 wasiokuwa wa halali walionekana katika jimbo la
Luisiana nchini Marekani. Kamati iliyokuwa ikihusika kwa ajili ya watoto hao iliwataka wananchi wa
Marekani wawasaidie watoto hawa kupata chakula na mavazi. Bila shaka suala hili ni matokeo ya
ustaarabu wa Kimagharibi na matunda ya mchanganyiko wa jinsia hizi mbili.
Mnamo mwaka 1960 nchi sabini na nne zilikutana mjini London kujadili masuala ya uhalifu (Crime
Conference). Katika kongamano hilo iliamuliwa kwamba sababu za ongezeko la uhalifu miongoni mwa
vijana ni mambo mawili: wanawake kwenda nje ya nyumba zao kwa ajili ya kufanya kazi na muda wa
uhuru unatokana na jambo hilo.
Uchunguzi wa maoni ulifanywa na shirika la habari la Marekani (American Press) kuhusu maoni ya
wanawake juu ya ndoa za wake wengi. Mmoja wa wanawake hao alisema: “Itakuwaje kama ungetaka
kununua pai na rafiki yako naye akahitajia keki nyingine, lakini ikawepo hiyo hiyo moja, je, wote wawili
msingeweza kushirikiana katika hiyo pai moja?” Binti mwingine akasema: “Ndoa ya wake wengi katika
nuru ya mchana na katika ulinzi wa Mungu ni bora zaidi kuliko kuwa na vimada katika giza la usiku na
katika ulinzi wa shetani?”
Mwaka 1961 ripoti ya kila mwaka ya wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilionesha kuwa mabinti elfu
kumi walio chini ya umri wa miaka ishirini walitiwa nguvuni kwa uhalifu wa kupindukia, uzururaji na
uhamasishaji wa vitendo vya uvunjifu wa maadili.
Na mkurugenzi wa Makao Makuu ya Idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai wa Uingereza alitangaza kuwa
makundi ya vijana wa kike na wanawake yalikuwa yakitishia usalama wa Uingereza.
Wahubiri wa Kanisa, wakisaidiwa na ukoloni wa Ulaya na Marekani, waliruhusu kuoa mpaka wanawake
wawili kwa bara la Afrika tu. Tafakari! (Saut Al-Islam Vol. 112).
Inakuwaje hawa wahubiri wanaruhusu ndoa za wake wengi kwa upande mmoja na kwa upande mwingine
wanautuhumu na kuukebehi Uislam kwa ndoa za wake wengi? Je ni tamaa zao zilizowafanya kuwa
watumwa?
Wanawake wa Kifaransa walikataa kujiunga na kamati ya umoja wa mataifa ya haki za wanawake kwa
sababu walipinga usawa wa moja kwa moja usiozingatia mazingira, masharti au mipaka mbali mbali kwa
sababu jambo hilo lingewagharimu wanawake kwa kuwapa majukumu mengi (20)
.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na chama cha kutetea usawa wa wanawake ulionesha kwamba nusu ya
wanawake ulimwenguni hawakuwa wakipendezwa na suala la ulinganifu na waliamini kuwa usawa ulikuwa
umeongeza mizigo mizito zaidi kwenye maisha yao (21)
.
135
Mnamo Mei 29/1961 gazeti la kila siku la Al Ahram lilichapisha makala kuhusu Profesa wa kike kutoka
chuo kikuu aliyewashauri wanafunzi wake kuoa/kuolewa kwanza. Mbele ya mamia ya wanafunzi wake,
alisimama katika sherehe ili kutoa hotuba juu ya tukio la kustaafu kwake. Alisema: “Mimi hapa, nikiwa
katika mwaka wangu wa sitini, nipo kwenye mojawapo ya nafasi za juu sana. Nimefanikiwa katika kila
mwaka wa maisha yangu, nimekamilisha na kutimiza mambo mengi. Kila dakika katika maisha yangu
ilikuwa yenye faida. Nimepata umashuhuri, pesa nyingi, na nilikuwa na bahati ya kusafiri ulimwenguni
kote. Lakini je nina furaha baada ya hayo yote? Nimesahau kitu kilicho muhimu zaidi kuliko hayo yote:
ndoa na watoto. Nimesahau kutulia ndani ya nyumba yangu mwenyewe. Niliyafikiria haya baada tu ya
kuamua kuiacha nafasi yangu. Katika kipindi hicho ndipo nilipotambua kuwa sikuwa nimefanya chochote
katika maisha yangu. Kazi yote ngumu niliyofanya imepotea, kwani nitajiuzulu kazi na mwaka mmoja au
miwili itapita na kisha kila mtu atanisahau kwa sababu ya kushughulishwa na maisha yao. Kama
ningekuwa nimeolewa na kuwa na familia yangu ningekuwa nimeacha kitu bora na chenye athari kubwa
katika haya maisha. Kazi pekee ya mwanamke ni kuolewa na kupata watoto. Kazi yoyote kinyume na hii
haina manufaa kwa maisha yake binafsi. Nami ninamshauri kila mwanafunzi wa kike anayenisikiliza
aiweke kazi hii katika fikra yake na baada ya hapo aweze kufikiria juu ya kazi na umashuhuri”.
Kwa kweli mwanamke akiacha kuolewa atakosa kitu ambacho hakiwezi kufidiwa na umashuhuri,
uheshimiwa, wadhifa wala pesa. Atakosa mapumnziko yenye furaha ya moja kwa moja. Uzoefu huu wa
miaka sitini uko mbele ya kila mtu ili apate kutafakari!
Nukta nyingine iliyoshughulikiwa na Uislam ni mchanganyiko wa jinsia mbili.
Mwanamke anaruhusiwa kufanya kazi lakini kwa mipaka kadhaa na bila ya kuchanganyika na wanaume.
Katika mapambano ya awali ya Uislam mwanamke alishiriki katika mapambano lakini katika mazingira
masafi na ya staha pande zote mbili zilikuwa safi:Wanajeshi wa Kiislam na wanawake waliowahudumia na
kuwasaidia wanajeshi.
Tukienda mbali zaidi suala la mchanganyiko linaweza kupelekea moja ya vitu viwili: kuchochea na
kuongeza matamanio ya kijinsia baina ya jinsia mbili, au kinyume chake yaani kuyadhoofisha na kuyazuia
matamanio hayo.
Mchanganyiko husababisha mvuto kwa wanaume na wanawake kutokana na silika za kimaumbile. Lakini
kama hakuna mipaka au utaratibu maalum wa mchanganyiko huu mambo yatakuwa mabaya na maradhi
mbali mbali yataenea miongoni mwa watu kutokana na uzinzi. Katika hali hiyo jamii itatumbukia katika
uchafu na uharibifu mkubwa. Chuki na vinyongo vitaibuka miongoni mwa wazazi ambao mabinti zao
wamedhuriwa, waume waliotendewa ubaya na wake zao, watoto waliotendewa ubaya na mama zao, na
wanaume na wanawake wanaoshindana na kupigana vikumbo kwa ajili ya mpenzi mmoja.
Kwa upande mwingine inasemekana kwamba mchanganyiko uliozidi kiwango baina ya wanaume na
wanawake katika mikutano mingi husababisha upungufu wa shauku na mvuto baina ya jinsia hizi mbili
jambo linalosababisha udhaifu wa matamanio ya kijinsia au kubadili matamanio hayo kwenda kwenye
uelekeo mwingine kama wanasemavyo baadhi ya wanasaikolojia. Wanaamini kwamba wanaume na
wanawake hupata aina fulani ya raha kwa kufurahia mikusanyiko yenye mchanganyiko pale tu
wanapoongea au kuitazama jinsia nyingine. Wakiwa pamoja wanaweza kuhisi aina fulani ya urafiki na
ujamaa, si zaidi ya hapo. Kukizoea kitu hukifanya kiwe na taathira ndogo. Kuishi katika eneo lenye harufu
mbaya kwa muda mrefu huweza kuwa kitu cha kawaida na chenye kuvumilika, na kunusa harufu nzuri ya
136
manukato kwa muda mrefu huifanya isiwe chochote baada ya muda mfupi tu, na hali ni hiyo hiyo kwa
upande wa wanaume na wanawake.
Watetezi wa matamanio ya kijinsia wanadai kuwa kubadili mkondo/uelekeo inaweza kuwa sahihi katika
baadhi ya maeneo ingawa baadhi ya matamanio imara ni vigumu sana kuyadhibiti na kuyazuia. Lakini
tuseme nini kuhusu juhudi za hawa watu? Je, huu si ubaridi/udhaifu wa kijinsia?
Kama mwanaume amemuona mwanamke halafu akawa hajahisi msukumo huo wa maumbile ya kijinsia.
Kama mwanaume ameiona mikono, miguu, kifua na mgongo wa mwanamke, halafu kisifuate kitu chochote
zaidi ya kuongea na kuonana. Kama mikono na miguu ya huyo mwanamke iko wazi lakini hakuna mvuto
wa kijinsia uliotokea, je huo sio ubaridi na udhaifu wa kijinsia? Katika hali kama hiyo huo ni ubaridi wa
kijinsia kwa pande zote mbili. Je, huo sio ungonjwa ambao watu huomba ushauri wa madaktari ili
kuondokana nao? Sasa inakuwaje tunaelekea kwenye hali hiyo kwa kisingizio cha kutuliza aibu ya kijinsia
au kubadilisha mkondo wa kijinsia?
Itakuwaje kama kanuni ya mvuto baina ya hasi na chanya iliyo katika viumbe vyote ikibadili mkondo wake
au kudhoofika? Je, kila kitu katika ulimwengu si kitafisidika?
“Kama haki ingelifuata matamanio yao, zingeliharibika mbingu na ardhi” (22)
.
Mhemko na nguvu ya mvuto wa kijinisa hupelekea kupata vizazi bora vyenye tabia na sifa nzuri. Na
kinyume chake mvuto hafifu na dhaifu ni chanzo cha kuwa na kizazi dhaifu chenye sifa na tabia mbaya.
Msomi mashuhuri, Imam Al Ghazali, aliitambua hatari ya msukumo dhaifu wa kijinsia na kuandika katika
kitabu chake “Ihyaa Uluum A-Diin” kwamba: “Miongoni mwa sababu za ndoa nzuri na yenye furaha ni
kuchangua mwanamke asiyekuwa ndugu wa karibu wa mume kwani jambo hilo hudhoofisha mhemko na
mvuto wa kijinsia”.
Maoni haya yanakubaliana na Hadithi ya Mtume (S.A.W.) isemayo: “Usimuoe ndugu wa karibu kwani hilo
huleta mtoto dhaifu”
Kuenea kwa ubaridi wa kijinsia kumesababisha tatizo jingine: usenge au ushoga. Mwanaume aliyezoea
kuona uzuri wa mwanamke lakini akawa hashtuki kijinsia huhitajia mwelekeo na misimamo mingine
isiyokuwa ya kawaida kwake ili aweze kushtuka. Ubaridi huu humfanya akose hisia ya uanaume wake
jambo ambalo hupelekea kwenye maumivu makali katikati ya kina cha moyo/nafsi yake. Hujihisi
kuandamwa na fedheha na uduni. Suala hili humfanya ajaribu kufurahia mahusiano ya kijinsia kwa
kukutana na kuungana na vimada na machangudoa ikiwa ni pamoja na kufuata njia na misimamo ya ajabu.
Hilo linaweza pia kumfanya awe muhanga wa madawa ya kulevya ili kufidia furaha alizozikosa. Vile vile
anaweza kukimbilia kwenye harakati za kihalifu na safari za hatari ili kuthibitisha uanaume wake katika
njia nyingine. Usenge unaweza kuwaathiri wanaume na halikadhalika wanawake.
Gazeti la Kimisri la “Al-Musawar” Vol. 1689 uk. 4 liliripoti kuwa Profesa Sarokin ----- Mkurugenzi wa
utafiti katika chuo kikuu cha Harvad ----- katika kitabu chake kiitwacho (Sexual Revolution) “Mapinduzi
ya kijinsia” alieleza kwamba Marekani inaelekea kwa kasi kubwa kwenye janga kubwa kutokana na
mfumo wa ngono huria. Akaongeza kusema kuwa Marekani inafuata njia ile ile iliyopelekea kuanguka kwa
tawala za kigiriki na kirumi huko zamani. Aleongeza kwamba: “tumezungukwa kila mahali na wimbi kubwa
la ngono inayovamia kila kona ya jengo letu la kiutamaduni na kila sekta ya maisha yetu ya kijamii”.
137
Mapinduzi haya yanabadilisha maisha ya kila mwanaume na mwanamke katika Marekani kuliko mapinduzi
yoyote katika zama hizi.
Gazeti la kila siku la Al-Akhbar liliripoti pia kwamba mwanasaikolojia wa Kimarekani, John Keshler wa
Chikango, alisema: “Mwanamke wa Kimarekani ni baridi” na “asilimia tisini ya wanawake wa
Kimarekani wameathirika na ubaridi wa kijinsia, na asilimia arobaini ya wanaume wameathirika na
utasa. Matangazo yanayowaonesha wasichana wakiwa uchi ndio chanzo cha upungufu mkubwa wa
kijinsia kwa Wamerekani”
Gazeti la Al-Tahrir katika toleo la 234 liliripoti kwamba kamati ya Bunge la Marekani, inayoshughulika na
uchunguzi wa uhalifu wa vijana, ilifikia hatima kwa kusema kwamba maadili ya Wamarekani yanazidi
kuharibika. Kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya na pombe kali vinatumiwa na vijana na baa nyingi
zinafunguliwa, idadi kubwa ya vitabu, visa na filamu za ngono vinaenezwa kwa wingi, na klabu za uchi
zinafunguliwa sana, hasa kwenye maeneo ya pwani na fukwe za upande wa mashariki.
Kamati moja ya Bunge la Uingereza ilijadili tatizo la usenge na mwisho ikafikia maamuzi ya kuuruhusu
kisheria kwa wale wenye zaidi ya umri wa miaka ishirini na moja, kama ilivyoripotiwa na gazeti la kila siku
la Kimisri la Al-Akhbar.
Kwa kweli, suala la mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake huko Uingereza limepelekea
kupatikana kwa “jinsia ya tatu” ambayo inatofautiana na wanaume kimaumbile na kisifa na inatofautiana
pia na wanawake katika kazi na mpangilio wa shughuli zao.
Mwanaume anayefanya kazi ngumu nje ya maskani yake, pindi arejeapo nyumbani anahitaji kula chakula
kizuri, kukuta nyumba ikiwa safi, na mwanamke nadhifu mwenye mapenzi ambaye atapata furaha awapo
pamoja naye. Mwanamke huyo anaweza kumfanya asahau shida na athari mbaya za matatizo
yanayomkwaza katika maisha.
Kazi ya mwanamke katika maeneo ya umma inaweza kuwa kikwazo cha kumtunza mume na watoto kwa
sababu atarudi nyumbani akiwa ni mwenye kuchoka na asiye na furaha. Katika hali kama hiyo basi nani
atakayemburudisha mwenzake. Mwanaume au mwanamke? Nani atakayestahimili kuwapa watoto upendo
na huruma? Je, Mume, mke na hata mtoto kila mmoja wao si atakuwa jino la gurudumu la mashine
isiyofanya kazi kabisa katika maisha yasiyokuwa na utulivu na uthabiti?!
Itakuwaje kama ikielezwa kuwa tutakuwa na nusu ya jamii isiyokuwa na kazi? Tutajibu: kazi zitatakiwa
kujazwa kwanza na wanaume wasiokuwa na kazi kabla ya kumruhusu mwanamke yeyote kuwa na kazi.
Mwanaume mwenye kazi atajisimamia na kujisaidia yeye pamoja na mkewe katika nusu nyingine ya jamii
pia.
Mara zote mkakati wa Kizayuni umekuwa ni kuyaharibu maisha ya familia ulimwenguni kote. Kanuni na
misingi ya mkakati huo imeelezwa kwa undani katika kitabu kiitwacho “The Protocals of the Zionist
Sagers”. Inafahamika vyema kuwa Freud ndiye mtetezi mkuu wa dhana mpya za kisaikolojia zilizojengwa
kwenye msingi wa kile kinachoitwa akili ya nafsi iliyofichika. Nadharia hizi zinaichukulia silika ya kijinsia
kuwa ndio mhimili wa shakhsia ya binadamu. Freud alikuwa Myahudi mwenye ushabiki wa kidini, alikuwa
akichagua wasaidizi wake waliokuwa Wayahudi tu. Uvunjifu wa familia hutokea pindi wanawake
wanapowekwa katika mazingira yasiyofaa, lakini wenye heshima na ukarimu. Jambo hili linaweza
138
kusababisha uchovu na ukosefu wa furaha kwa wanaume ambao, kama watafanya kazi, watabeba uzito wao
na wa familia zao pia.
Rejea: 1. Mhubiri - {7:25 – 26}
2. Qur‟an - {9:71}
3. Qur‟an - {3:195}
4. Qur‟an - {4:7}
5. Qur‟an - {4:3}
6. Qur‟an - {4:129}
7. Qur‟an - {30:21}
8. Qur‟an - {2:187}
9. Qur‟an - {4:19}
10. Qur‟an - {4:34}
11. Qur‟an - {4:35}
12. Qur‟an - 4:128}
13. Qur‟an - {2:229}
14. Qur‟an - {2:229}
15. Qur‟an - {4:19}
16. Qur‟an - {4:34}
17. Qur‟an - {2:228}
18. Qur‟an - {4:34 – 35}
19. Qur‟an - {4:11}
20. Al-Ahram Daily - Na. 27126, 2.10.1380 H
21. Al-Ahram Daily - Na. 27131
22. Qur‟an 23: 71
139
KESI YA KUMI NA NNE
Wake wa Muhammad
Mwendesha Mashtaka ananukuu kutoka kwa Mustashiriqiina mbalimbali kama vile Muir, Durminghan,
W. Irving na Lamance ambao waliamini kuwa Muhammad, baada ya kifo cha mkewe wa kwanza Khadija,
alikuwa na ashiki kubwa isiyo ya kawaida ya kuwa na mahusiano ya kijinsia na hiyo ndiyo sababu
iliyomfanya aowe wake wengi.
Uislam unasimama ili kukanusha uwongo huu.
Uislam: Watu wemekuwa na mitazamo mbalimbali na tofauti kuhusu suala hili. Baadhi yao,
wakiongozwa na imani, waliamini kuwa Mtume alikuwa ni zaidi ya binadamu wengine, ingawa Qur‟an
Tukufu ilithibisha kuwa Muhammad alikuwa binadamu kama binadamu wengine, na watu wengine
wakiongozwa na chuki na ushabiki wa kidini katika kielelezo hiki cha maisha ya Mtume wamepata kitu cha
kulipizia kisasi na kuonyesha kinyongo chao. Mustasriqiina (orientalist) wamesema mengi kuhusu ndoa ya
wake wengi na ndani yake hawakuona kitu zaidi ya kwamba inatokana na kuzidiwa na ashiki. Mtazamo
huu ni matokeo ya chuki za kijinga na tama za kiupofu, zilizo kinyume na njia ya utafiti wa kisayansi
ambayo ingeliwafanya walidurusu suala hili kwa mujibu wa viwango tofauti na vile vya zama zetu. Leo hii
watu wa Magharibi hawawezi kudai kwamba ndoa ya mke mmoja inafuatwa kikamilifu miongoni mwa
watu wao.
Hata hivyo, baadhi ya watu hao wa Magharibi wanamshambulia Muhammad kwa kuwa na wake wengi
karne kumi na nne zilizopita ambapo ndoa ya wake wengi ni desturi iliyokuwa mashuhuri isipokuwa katika
baadhi ya hali maalum. Mfumo huu haukuwa mfumo wa khiyari bali ni mfumo uliolazimishwa na
mazingira ya zama na mahali katika eneo la jangwani na katika hali ya maisha ya kibedui, katika zama
zilizokuwa zimetawaliwa na mfumo wa kikabila ambapo watoto walichukuliwa kuwa vitu vya thamani
zaidi katika maisha. Wanaume katika zama hizo walikuwa wakijivunia kuwa na watoto wengi na
wanawake walikuwa wakijivunia kuwa na uzazi.
Ndoa ya wake wengi inaweza kuonekana katika zama zetu hizi kuwa kama kielelezo cha kuwatia utumwani
wanawake wa Kiarabu, na kuwa tu nyenzo ya kumfurahisha mwanaume. Lakini kwa kweli ndoa hiyo
ilikuwa mzigo mzito kwa wanaume na wakati huo huo ndoa ya wake wengi iliwaokoa wanawake wa
Kiarabu dhidi ya hali mbaya zaidi ambayo ni “utumwa mamboleo”, mfumo unaomtambua mke mmoja tu na
kuwaacha wanawake wengine wawe katika maisha ya mwanaume bila kupata haki zozote na kuwaacha
katika hali ya kutelekezwa na kufedheheka. Mwanamke huyo asiye na bahati huadhibiwa na kuteseka kwa
hayo pamoja na jamii duni ya binadamu isiyokuwa na furaha. Gharama yake ni idadi kadhaa ya watoto
wanaotelekezwa na kutupwa na wazazi wao, jambo ambalo halikuwapo hata kidogo katika jamii ya Kiarabu
ambayo iliamini kwamba kuwa na watoto wengi hata kwa njia ya kuasili au kuwateka ni matokeo ya ustadi
wa mwanaume na kujivunia kuwa na idadi kubwa ya watoto.
Ama kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) na wake zake mbalimbali kuna ukweli ambao watu wengi
hawaujui. Ukweli huu ni kwamba wanaume hawalingani, na mwanamke anaweza kuchagua kwa ridhaa
kubwa kuwa mke mwenza katika maisha ya mwanaume kuliko kuwa mke pekee katika maisha ya
mwanaume. Mwanamke anaweza kupendelea kuwa mke wa Mtume, kuliko kuolewa na vijana wa Arabia,
anaweza kufanya hivyo ili kufurahia heshima kubwa ya kuwa mke wa Mtume, ambapo kumbukumbu yake
140
itaandikwa katika historia kama mke wa mwanaume bora wa Arabia, mke wa mpatanishi, mkombozi wa
Waarabu, ili jina lake lipate kuhusishwa na jina la Mtume milele na milele.
Na sasa tuyatazame mazingira yaliyoambatana na ndoa za Mtume.
1. Khadija bint Khuwailed:
Maisara, mtumishi wa Khadija, alirejea kutoka Syria katika safari ya biashara akiwa na Muhammad,
ambaye alikuwa kijana. Maisara alimweleza Khadija kila kitu kuhusu biashara hiyo na jinsi Muhammad
alivyokuwa na mafanikio na busara ya hali ya juu. Baada ya Maisara kuondoka, Khadija alitafakari juu ya
sifa na tabia bora za Muhammad ambaye alilelewa kama yatima na maskini. Khadija alikuwa mwanamke
mwenye uzoefu mzuri katika maisha, aliwahi kuolewa mara mbili na wanaume kutoka katika familia za
Kilodi katika Arabia. Alikuwa amewaajiri wanaume kadhaa ili kusimamia biashara zake. Lakini hakuwa
ameona yeyote mithili ya Muhammad. Hakika Muhammad alikuwa mtu wa kipekee. Je, Khadija
atamwambia ombi lake la kutaka kuolewa naye pamoja na kwamba alikuwa amewakataa viongozi na
machifu kadhaa wa Kiquraish?
Khadija aliongea na mtumishi/mpambe wake aliyeitwa Nafisa. Mara moja mtumishi huyu akaenda kwa
Muhammad na kumuuliza kwanini alikuwa hajaoa ambapo alijibu: “Sina mali ya kuniwezesha kuoa”.
Nafisa akasema: “kama ukitakiwa na mwanamke mzuri, mwenye mali, mwenye heshima na sifa njema,
utakubali?” Baada tu ya kusikia hivyo, Muhammad akasema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, huyo ni
Khadija”. Na hapo tu Nafisa akampa mwaliko maalum. Nyumbani kwa Khadija alikuwapo Abu Talib na
Hamza, na kwa niaba ya Khadija alikuwapo ami yake, Amru Ibnu Asad. Hapo Muhammad alimuoa
Khadija na ndoa yao ilidumu kwa muda wa miaka ishirini na tano na kupata watoto wa kiume na wa kike.
Al-Qassim na Abdullah watoto wa kiume, Ruqayya, Zainab, Um Kulthoom na Fatma watoto wa kike.
Kwa kweli Khadija alikuwa msaada mkubwa kwa kijana Muhammad katika mambo yake mbali mbali.
Msimamo wake katika kipindi cha mwanzo wa utume unajulikana vema. Alikwenda kwa binamu yake,
Waraqah ibn Nawfal na kumtaka ushauri kuhusu yaliyokuwa yakimtokea mumewe ambapo alimhakikishia
kuwa Muhammad alikuwa ni Mtume.
Mwisho Khadija alifariki dunia akimuacha Muhammad akilindwa na Malaika Jibril na akiwa amezungukwa
na waumini waliokuwa tayari kumlinda na kumtetea kwa miili na roho zao, wakichulia kuuwawa kwa ajili
ya dini ya Muhammad, kuwa ni njia ya kuelekea kwenye heshima na utukufu.
Siku zote Khadija aliendelea kubaki katika fikra na akili ya Muhammad pamoja na kwamba alioa wanawake
wengi baada yake. Pamoja na kuowa wake wengi lakini kamwe daraja yake katika moyo wa Muhammad
haikupata kuchukuliwa na yeyote. Hilo lilimfanya Aisha bint wa Abu Bakr amuonee wivu Khadija. Siku
moja Aisha alimwambia Mtume: “Kama vile hakuwepo katika ulimwengu huu mwanamke mwingine zaidi
ya Khadija!”
Mtume akajibu: “Alikuwa muhimu sana kwangu, na nilipata watoto kutoka kwake tu”. Kila
alipokuwa akichinja Kondoo, Mtume alikuwa akisema: “Wapelekeeni marafiki wa Khadija sehemu ya
nyama”. Siku moja Aisha akamuuliza kwa nini alikuwa akifanya hivyo, akajibu: “Ninawapenda wale
aliokuwa akiwapenda”. Aisha alikuwa akisema: “Sikuwahi kumuonea wivu mtu yeyote kama
141
nilivyofanya kwa Khadija, kwani mara zote nilikuwa nikimsikia Mtume akimsifia. Naye alinioa miaka
mitatu baada ya kifo chake”.
Margiliuth anasema kwamba pesa za Khadija zilimvuta Muhammad na kumfanya aisahau tofauti ya umri
iliyokuwepo kati yao. Lakini Placher katika kitabu chake kiitwacho “La Probleme de Mohamed”
anadhani kwamba kilichomvuta Muhammad kwa Khadija ni heshima na huruma kubwa aliyokuwa nayo
Khadija. Jambo la ajabu zaidi kuliko hili ni Muir aliyeandika katika kitabu chake “Life of Muhammad and
the History of Islam” kwamba Muhammad alihofia nafasi ya kiuchumi na ya kijamii ya Khadija na
akachelea kuwa Khadija angemtaka amtaliki. Kwa kweli waandishi hawa wote hawaelezi ukweli. Ukweli
hasa ni kwamba Khadija ndiye aliyemfikiria Muhammad na kumuomba amuowe. Muhammad angewezaje
kumfikiria Khadija ambaye tayari alikuwa amewakataa wanaume wazuri wa Kiquraish? Yule anayedai
kwamba Muhammad alitaka kumuoa kwa sababu ya pesa hali ya kuwa ana umri wa miaka ishirini na tano
na Khadija akiwa ni mama mwenye umri wa miaka arobaini, mtu huyo haijui vizuri historia na pia hayajui
maisha ya Mtume. Kwa hiyo tunakuta kuwa maoni hayo hayana ukweli wa kielimu wala uzoefu mzuri.
Uaminifu wa Muhammad kwa Khadija hata baada ya kifo chake ni uthibitisho mkubwa wa upendo wake
kwake na kwamba walikuwa na furaha na kufurahia maelewano katika ndoa yao. Je, inaingia akilini
kusema kuwa Muhammad katika kipindi cha maisha yake na Khadija alikuwa akihofia kuwa mke wake
huyo angemtaka amuache, hali ya kuwa tunaona kwamba baada ya kifo chake alimkasirikia Aisha pale
alipokuwa akimuonea wivu? Aliwezaje kuhofia talaka hali ya kuwa mwaka ambao Khadija alifariki dunia
aliuita kuwa “mwaka wa huzuni” ambao ni mwaka wa tatu kabla ya Hijra?
Uthibitisho mwingine wa maelewano yao ndani ya ndoa ni kwamba baada ya kifo cha Khadija Mtume
hakuwa amefikiria kuoa mke mwingine bali Khawla bint Hakeem aliufikiria upweke aliokuwa nao
Muhammad katika maisha na hivyo akamshauri kumuoa Sawda bint Zuma‟.
Kuhusu Khadija, Mtume anasema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sikupewa mwanamke bora kuliko
yeye, aliniamini pindi watu walipokadhibisha wito wangu. Alinisadikisha pindi watu waliponichukulia
kuwa muongo. Alinipa mali yake pindi watu walipotaka kuninyima, na Mwenyezi Mungu alinipa watoto
kutokana naye na hakunipa kutoka kwa wanawake wengine”.
Hivyo basi, Mustashriqiina wamejenga dhana zao kwenye ushahidi, hadithi au historia gani? Bila shaka
mawazo yao ni uwongo, uovu, chuki na hukumu isiyokuwa na mashiko na hivyo hayana maana.
2. Sawda bint Zuma‟:
Siku moja Khawla bint Hakeem alikuja kwa Mtume na kumshauri kuwa alitakiwa kuoa. Mtume akasema:
“Nani baada ya Khadija!?” Mara moja Khawla akasema: “Aisha binti wa rafiki yako mpendwa”. Mtume
akatafakari je, amkatae binti wa Abu Bakr? Lakini nafasi ya Abu Bakr katika moyo wake na urafiki wao wa
muda mrefu vilimfanya atafakari upya. Kisha akasema: “Lakini bado yu mdogo”. Khawla akasema:
“Waweza kushauriana na baba yake leo na kusubiri mpaka atakapokuwa mkubwa”. Lakini wakati huo nani
angeiangalia nyumba ya Mtume na kuwatunza wanaye? Khawla akashauri: “waweza kumuoa Sawda bint
Zuma” na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mtume aliombwa kumuowa (Sawda) ili kumfidia na kumfariji
kutokana na kifo cha mumewe, Assakran ibn Am, aliyekuwa ameshiriki katika hijra ya Ethiopia kisha
akarudi baada ya kudhani kuwa Maquraish wamemuamini Muhammad. Lakini alipofika Makka aliikuta
142
hali ikiwa tofauti na kuuawa siku tatu baada ya kuwasili kwake akimwacha mkewe akiwa mjane, sanjari na
kuwa mgeni katika mji wa Madina. Mtume aliifikiria hali ya mwanamke huyo baada ya kifo cha mumewe
na akaunyoosha mkono wake wa rehma kwa lengo la kumsaidia katika umri wake mkubwa na kumuondolea
machungu na shida za maisha.
Sawda alikubali kuwahudumia mabinti wa Mtume ili kupata heshima ya kuwa katika nyumba ya
Muhammad. Pindi Aisha alipokuja kama mke, Sawda alimpa daraja ya kwanza katika nyumba na
kumtunza. Siku zote Mtume alikuwa mwema kwa Sawda naye aliendelea kuishi katika nyumba ya Mtume
mpaka mwisho wa uhai wake. Aliridhia kuutoa usiku wake kwa wake wengine wa Mtume na badala yake
akajishughulisha na ibada na kutumaini kuwa Mwenyezi Mungu atamfufua siku ya kiyama akiwa kama
mke wa Mtume. Alikuwa akisema: “Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sina shauku sana na ndoa lakini
ningependa nifufuliwe siku ya kiyama nikiwa miongoni mwa wake wa Mtume”.
Hivyo, ndoa ya Mtume kwa Sawda ilikuwa ni aina ya rehma na maliwazo kwa mjane mwenye umri
mkubwa. Je, tunaweza kusema kuwa hayo yalifanyika kwa sababu ya matamanio yaliyozidi kiwango kama
inavyodaiwa na Mustashriqiina?
3. Aisha Bint Abu Bakr:
Khawla bint Hakeem alimshauri Mtume kumuoa Aisha naye akayapokea mawazo hayo kwa sababu jambo
hilo lingeimarisha mahusiano mema yaliyokuwepo baina ya Mtume na sahaba wake mpendwa Abu Bakr.
Aisha aliwahi kuchumbiwa na Jubair Ibn Al-Mutim bin Adi, hivyo alikuwa amelelewa na kukuzwa kama
binti. Lakini mama wa Jubair hakuwa Mwislam na alihofia kuwa ndoa hii ingepelekea mwanaye kubadili
dini na kuwa Muislam. Hivyo, uchumba ulivunjwa. Baba yake Aisha ni Abu Bakr na mama yake ni Um-
Ruman.
Mtume alimuoa Aisha na watu wa Makka hawakushangazwa na taarifa hizi. Walilipokea kama jambo la
kawaida. Hakuna yeyote katika maadui wa Mtume aliyeona katika ndoa hiyo chochote cha kuweza
kukitumia kama silaha ya kumshambulia Mtume, japokuwa waliwahi kumshambulia Mtume kwa vitu vingi
sana hata kama vingekuwa vya uzushi.
Watu wa zama hizo hawakuona ajabu yoyote katika ndoa ya binti mdogo mwenye umri kama wa Aisha na
mwanaume mwenye umri wa miaka hamsini na tatu. Kitu gani kingekuwa cha ajabu kuhusu ndoa hiyo
katika mazingira ambayo mabinti wengi walikuwa wakiolewa na wanaume wenye umri sawa na baba zao?
Mzee Abdul Muttalib kiongozi wa Makka alimuoa Hala binam yake Amina siku ile ile ambayo kijana wake
Abdullah alimuoa “Amina mama wa Mtume”.
Hala na Amina walikuwa na umri ulio sawa. Baadaye Omar ibn Al-Khatab alimuoa binti wa Ali ibn Abi
Talib, wakati ambapo Omar alikuwa na umri ulio sawa na ule wa babu wa binti huyo. Siku moja pia Omar
alimshauri Abu Bakr ampe binti yake Hafsa kuwa mkewe, ingawa tofauti ya umri baina yao ilikuwa sawa
na ile ya Mtume kwa Aisha.
Hata hivyo, idadi kadhaa ya Mustahsriqiina wamekuja sasa baada ya miaka elfu moja na mia nne na kutojali
tofauti mbalimbali za umri na nchi. Wanazungumzia kile wanachokiita “ndoa ya ajabu baina mtu mwenye
umri wa miaka hamsini na binti aliye bikra”. Kwa kutumia jicho la chuki, wanajaribu kulinganisha kati ya
143
ndoa iliyofanyika katika mji wa Makka kabla ya Hijra na kile kinachotokea leo katika Magharibi
iliyoendelea, ambapo mabinti hawaolewi kabla ya kufikisha umri wa miaka ishirini na tano. Japokuwa umri
huu bado unachukuliwa kama uliopitiliza kwa watu wa Arabia na nchi zilizo jirani na Misri na sehemu
nyingi za Mashariki. Hili liligunduliwa na Mustashriq mwadilifu Baudly aliyetembelea Arabia kisha
akasema: “Ingawa Aisha alikuwa mdogo bado alikuwa haraka sana kama ilivyo kwa msichana yeyote wa
Arabia. Makuzi haya ya mapema husababisha uzee wa mapema katika umri wa miaka ishirini. Lakini ndoa
hii iliwashughulisha baadhi ya wanahistoria wa Muhammad na waliitazama kwa mtazamo wa zama za sasa
wakisahau kwamba ndoa kama hiyo bado inaendelea kuwa kitu kilichozoeleka huko Asia na mashariki mwa
Ulaya. Ndoa hiyo ilikuwa ni mazoea pia katika nchi za Hispania na Ureno miaka kadhaa iliyopita. Sio ada
ya ajabu hata kidogo katika maeneo ya mbali yenye milima huko Marekani.
Tunatakiwa kufahamu kuwa wasichana waishio katika maeneo yenye joto hukomaa katika umri wa mapema
sana wa miaka 8, wakati ambapo wasichana wanaoishi katika maeneo yenye baridi ya upande wa kaskazini
kama vile, Sweden, Norway, Canada na Siberia hukomaa katika umri wa miaka ishirini na moja”.
Miongoni mwa ushahidi wa kwamba Aisha alikuwa mkubwa na mwenye utambuzi ni kwamba mara tu
alipoingia katika nyumba ya Muhammad kila mtu alihisi uwepo wake. Aisha alikuwa akijua vema kuwa
atakuwa nani, aliweka misingi ya shakhsia yake tangu siku ya kwanza kuingia katika nyumba ya Mtume
iliyokuwa ubavuni mwa msikiti.
Ushahidi mwingine ni kwamba alikuwa akitoa maoni yake katika mambo mbalimbali ya mapambo na
urembo. Alikuwa akisema: “Kama una mume na ukawa na uwezo wa kutoyaonyesha macho yako na
kuyahifadhi katika namna hiyo basi fanya hivyo”.
Alikuwa akichukia kwa mwanamke kukutana na mume wake akiwa amevaa nguo inayoashiria huzuni na
msiba. Alisema: “Mwanamke anayemuamini Mwenyezi Mungu haruhusiwi kuwa katika majonzi zaidi ya
siku tatu, isipokuwa kwa ajili ya mumewe”.
4. Hafsa bint Omar:
Mtu anaweza kuuliza kwa nini Mtume alioa mke mwingine baada ya Aisha hali ya kuwa alikuwa
amemwambia kuwa upendo wake ndani ya moyo wake ulikuwa thabiti?
Aisha alikuwa akimuuliza ni kwa kiwango gani alikuwa akimpenda naye alikuwa akijibu kuwa hakuwa
amebadilika, alikuwa akimpenda sana tu sasa basi kwa nini alioa mwanamke mwingine jambo ambalo
lingekuwa na maana ya kumdhuru Aisha?
Baadhi ya Mustashriqiina kama vile Muir, Durminghan W. lrving, Lamance, Fidensio na wengineo ambao
hawakuwa wakiujua ukweli wa Uislam na malengo yake, walidhani kuwa ndoa za Mtume baada ya Khadija
zilikuwa na dosari na hawakujua kuwa ndoa hizo zilifanyika kwa malengo ya kidini na kisiasa.
Mtume aliwaoa wake zake wote baada ya kifo cha Khadija alipokuwa na zaidi ya miaka hamsini. Zaidi ya
hapo alikuwa akimpenda sana Aisha ambapo hakumuoa yeyote baada yake kwa lengo la uzuri. Hivyo,
inakuwa rahisi kutambua kuwa ndoa zake zilikuwa tu kwa malengo ya kidini na ya kisiasa. Baadhi ya
matokeo ya ndoa hizo ni kuzitumia kama nyenzo ya kuleta utiifu wa makabila yaliyohusisha ndoa hizo.
Vile vile inabainisha sababu za yeye kuoa wanawake wengi kutoka kabila la Quraish ambalo ndilo
144
lililokuwa kabila kuu katika Arabia. Ndoa zake ziliwafanya Waarabu wengi waupende Uislam na kuufuata,
wakati mwingine Mtume alikuwa akioa wanawake kama aina ya rehma na faraja kwa watu
waliodhalilishwa katika vita mbali mbali.
Sasa kwa nini Mtume alimuoa Hafsa? Kwa sababu mumewe, Khunais Ibn Qais Ibn Adi Assahmi, alikuwa
amefariki na Omar alitaka kumuozesha kwa Abu Bakr au Othman lakini wote walikataa. Omar alikasirika
na akaenda nyumbani kwa Mtume na kumueleza yale yaliyokuwa yametokea. Mtume alitabasam na
kusema: “Hafsa ataolewa na mtu bora kuliko Othman (yaani mwenyewe Mtume) na Othman atamuoa mtu
bora kuliko Hafsa (yaani binti wa Mtume)”.
Watu wote wa Madina walimshukuru Mtume kwa kuunyoosha mkono wake ili kumpa heshima Omar Ibn
Al-Khattab na kumfariji bintiye, Hafsa. Japokuwa Abu Bakr na Othman walikuwa wamekataa kumuoa,
lakini Omar aliona fakhari kwa kitendo hicho cha Mtume. Hivyo basi, Mtume alimfurahisha Omar kwa
ndoa hiyo na hakuacha katika moyo wake chochote kilicho dhidi ya Abu Bakr na Othman.
5. Zainab Bint Khuzaima:
Aliachwa akiwa mjane baada ya mumewe kuuawa katika vita vya Uhud. Mtume alimuoa kwa lengo la
kutoa heshima kwa mume wake aliyekufa kishahidi na kwa lengo la kumfariji. Aliishi pamoja na Mtume
kwa miezi mitatu hadi minane kisha akafariki dunia.
Baudly katika kitabu chake kiitwacho “The Messenger” anasema yafuatayo kuhusu hii ndoa: “Muhammad
alimuoa kwa sababu ya kumhurumia tu. Aisha na Hafsa hawakuijali hii ndoa na Zainab alifariki dunia miezi
minane baadaye”. Vile vile anasema kwamba Zainab alikuwa mwema na mkarimu. Wanahistoria wa
Kiarabu wanamuelezea kama mtu aliyekuwa mwema sana kwa maskini. Alikuwa akiwahurumia na
kuwasaidia. Dr. Haikal anasema kuwa “Hakuwa mrembo lakini alijulikana kwa wema na ukarimu wake
kiasi kwamba alifahamika kwa jina la “Um Al Masakeen” yaani “mama wa maskini”. Ni hakika kwamba
alifariki dunia katika umri wa miaka thelathini kwa mujibu wa Al-Waqidi. Ibn Hajar katika kitabu chake
“Al-Isaba” anasema kwamba umri huu ulihesabiwa na baadhi ya watu kama umri wa kati na uliojuu ya
ujana. Watu hao wanasahau kuwa uzingatiaji huo unatosha kuyapinga madai yao kuhusu “utoto” wa Aisha.
6. Um Salama (Hind bint Abi Umayya Ibn Al-Mughira):
Mtume alimuoa baada ya kifo cha mumewe Abu Salama Abdullah ibn Abdul Asad Ibn Al-Mughira,
aliyekuwa binamu wa Mtume kwa upande wa baba. Um Salama alikuwa amehamia Ethiopia na pindi
aliporejea Makka alitaka kuondoka kwa mara nyingine kuelekea Madina. Lakini watu wake walimzuia na
idadi kadhaa ya watu kutoka Bani Asad, kabila la mumewe, walikuja kwa lengo la kumchukua mwanaye
“Salama”. Pande hizo mbili ziliingia katika ugomvi na kusababisha mkono wa mtoto huyo uteguke.
Mwishowe watu wa upande wa mumewe walimchukua Salama, kisha mumewe aliondoka kuelekea Madina
na kumuacha Makka. Alikaa Makka kwa muda wa mwaka mmoja akimlilia mtoto wake pamoja na
mumewe na hatimaye ndugu zake walimhurumia na kumruhusu kwenda kuungana na mumewe. Alisafiri
peke yake katika jangwa akielekea Madina, muda mfupi baadaye mumewe alifariki dunia akimuacha na
watoto kadhaa, miezi kadhaa baada ya kumalizika kwa kipindi cha msiba na majonzi Abu Bakr alimueleza
nia yake ya kutaka kumuoa lakini kwa upole kabisa alikataa, kisha akaja Omar kwa lengo hilo hilo lakini
kwa mara nyingine akakataa, mwishowe alikuja Mtume na kumchumbia naye akasema kuwa yeye ni mtu
mwenye wivu, mtu mzima na mwenye watoto kadhaa. Mtume akasema: “Ama kuhusu utu uzima, mimi
145
nina umri mkubwa zaidi yako, kuhusu kuwa mwenye wivu Mwenyezi Mungu atakuondolea hilo na ama
kuhusu watoto Mwenyezi Mungu na Mtume wake watawatunza”. Mtume aliamiliana naye kwa heshima
kubwa sana na kuwapenda sana watoto wake kiasi kwamba alimchagua mwanaye Salamah kuwa mume wa
binti wa ami yake Hamza, “Bwana wa Mashahidi”.
7. Zainab bint Jahsh:
Muhammad alimuoa Zainab bint Jahsh kwa lengo la kuasisi taratibu za kisheria. Waarabu walikuwa na
desturi ya kuwaasili watoto na kuwaharamishia wazazi wa kupanga kuwaoa watalaka wa watoto hawa.
Walikuwa wakidhani kuwa mke huyo ni sawa na binti wa mhusika. Mtume alimuoa Zainab kwa lengo la
kuvunja imani hii. Awali Mtume alikuwa akihofia kile ambacho wanafiki na Wayahudi wangekisema,
lakini Mwenyezi Mungu aliona hali hiyo na akamteremshia Muhammad Aya za Qur‟an zisemazo: “Basi
Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao
wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za talaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni
yenye kutekelezwa” {33:37}
Kwa upande mwingine ndoa hii ilitekelezwa ili kuhifadhi heshima na utu wa Zainab baada ya kuwa
ameolewa na mtumwa aliyeachwa huru. Alikuwa ni binti wa shangazi wa Mtume (S.A.W.), Umaima bint
Abdul Muttalib. Pindi Mtume alipomshauri kwa mara ya kwanza ili aolewe na Zaid, hakulipenda wazo hilo
na kuliona kuwa ni tusi kubwa akisema: “Nisingependa kuolewa naye kwa sababu mimi ni msichana bora
kwa watu wangu wa ukoo wa Abdi-Shams”.
Kaka yake Abdullah naye pia hakupenda kumuona dada yake wa kabila bora la Kiquraish akiolewa na mtu
aliyekuwa mtumwa. Lakini Mtume alisisitiza kwanza juu ya ndoa hiyo na kisha Aya ya Qur‟an ikateremka
kwa Mtume: “Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika
jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi
Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi”. {33:36}
Hivyo, Mtume (S.A.W.) alikomesha ubaguzi wa matabaka katika jamii ya Kiarabu na neno la Mungu
likatimia. Hata hivyo, Zainab alimchukia Zaid na kuonesha fakhari na maringo yake mbele ya Zaid. Suala
hili lilimfanya Zaid aende kwa Mtume na kumwambia kuwa asingeweza kuivumilia hali hiyo. Mtume
alijaribu kumtuliza na kumshauri aivumilie hali hiyo kwa kusema: “Shikamana na mkeo na umche
Mwenyezi Mungu”. {33:37}.
Lakini mwishowe Mtume aliamriwa kuisitisha ndoa hiyo na kulitatua tatizo hilo kwa yeye mwenyewe
kumuoa Zainab ili kuirudisha hadhi ya msichana huyo wa kabila tukufu baada ya kutekeleza shughuli
muhimu ambayo ni kuwatukuza wale waliowahi kuwa watumwa na kutoa funzo la namna wanavyopaswa
kutendewa.
Mustashriqiina na wahubiri wa Kikristo waliifanya ndoa hiyo kuwa kisa na hadithi ya mapenzi. Kwa kweli
Mtume (S.A.W.) alitaka kumuoa Zainab kwa lengo la kumfariji kwa sababu alikuwa amelazimishwa
kuikubali ndoa ya mwanzo kwa lengo tu la kupata radhi ya Mungu na Mtume wake. Alitaka kumuoa kwa
lengo tu la kutoa mfano wa demokrasia ambayo ni kielelezo muhimu cha Uislam. Ibn Al-Athir anasema
wazi kabisa kuwa Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtume wake ---- katika ufunuo aliomfunulia -----
kwamba amuoe Zainab mtalaka wa Zaid ili kuwafundisha watu kuwa kuasili watoto hakukubaliwi ndani ya
Uislam.
146
Mtume alihofia upingamizi wa wapinzani wake kwa sababu suala hilo halikuwa la kawaida kwao, na hivyo
akaificha amri hiyo moyoni mwake. Hivyo, akateremshiwa kauli nzito ndani ya Qur‟an isemayo: “Na
ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha na wewe pia umemneemesha:
Shikamana na mkeo na umche Mwenyezi Mungu, na ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi
Mungu kuyatoa na ukawachelea watu hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea
…..” {S. 33:37}.
Aya hizi zinaonesha kuwa Mtume alimtaka Zaid kushikamana na mkewe na kumcha Mwenyezi Mungu.
Lakini mgogoro baina ya hao wanandoa ulizidi kukua na talaka ikawa kitu kisichoepukika, na hapo Mtume
akaamriwa kumuoa Zainab kwa lengo la kuasisi sheria. Lakini Mtume akaificha amri hiyo kwa kuwaogopa
maadui zake wenye wivu ambao wangelichukulia jambo hilo kama silaha ya kumshambulia.
Kwa namna hiyo, desturi ya kuasili watoto ilikomeshwa kwa maneno na kwa vitendo. Na Mwenyezi Mungu
akiwazungumzia watoto walioasiliwa anasema: “Waiteni kwa (ubini wa) baba zao, maana huo ndio
uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu” {S. 33:5}. Na “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume
wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii” {33:40}.
Hiyo ndiyo demokrasia iliyojengwa na Mtume kupitia ndoa hii. Kama Mtume angetaka kumuoa kwa sababu
ya matamanio angefanya hivyo zamani alipokuwa binti kigori kabla ya kuolewa na kijana aliyewahi kuwa
mtumwa wake. Alimfahamu tangu alipokuwa mtoto mdogo na kumshuhudia akikuwa na kuwa binti
mkubwa. Yeye mwenyewe Mtume ndiye aliyemposa kwa niaba ya kijana wake, Zaid.
Mustashriqiina walidai kuwa Mtume alikwenda nyumbani kwa Zaid akamuona Zainab na kushangazwa na
urembo wake na hivyo akampenda sana moyoni mwake.
Yote haya ni uwongo ambao hatumtarajii muumini wa kawaida katika zama zetu kumtazama mke wa jirani
au rafiki yake kwa kumtamani au bila kumtamani. Tunawezaje kuamini kwamba kitu kama hicho kinaweza
kumtokea yule aliyepandikiza imani katika nyoyo za binadamu na kuwafundisha uchaji na kumuogopa
Mungu?
8. Juwairiya Binti Al-Hareth:
Ndoa ya Mtume na Juwairiya ilifanyika kwa malengo ya kisiasa na kidini. Mtume alikusudia kutumia
uhusiano huu kupata uungwaji mkono kutoka kwa makabila mbalimbali. Hatua yake ya kuoa katika kabila
la Kiquraish, kabila kubwa na lenye nguvu kuliko makabila yote ya Arabia, ilizifanya nyoyo za watu wa
makabila mengine zilainike na kuukubali Uislam. Zaidi ya hilo jambo hili linaonesha huruma na wema wa
Mtume hususani kwa wale waliokuwa na nafasi kubwa kisha wakatiishwa katika nyakati za vita.
Mtume alimuoa Juwairiya ili kuwa karibu na kabila lake ili kwamba waweze kuingia katika Uislam.
Hakuangalia urembo na uzuri kwa sababu tayari alikuwa amekwisha fundisha wafuasi wake kwamba
wanapotaka kuoa kwanza wazingatie dini na uchaji Mungu, sio kutazama uzuri na urembo.
Baba wa Juwairiya alikuwa amelikusanya jeshi kubwa kupambana dhidi ya Waislam katika vita vya bani
Al-Mustaleq. Lakini jeshi hilo lilishindwa na Juwairiya akachukuliwa mateka. Alikuwa katika fungu la
ngawira ya Mwislam mmoja aitwaye Thabit Ibn Qais. Akataka kujikomboa kwa kutoa fidia kubwa. Alihisi
fedheha kuwa mfungwa na hivyo akaenda kwa Mtume kuomba msaada na kuhurumiwa. Moyo wa Mtume
147
wenye heri ulimuonea huruma na kusema: “Waweza kuolewa nami iwapo nitalipa fidia yako? Juwairiya
alifurahi sana na kusema: “Ndiyo, bila shaka”. Hivyo, Mtume akamuoa na kumpa baba yake mahari ya
dirham mia nne. Baba yake alikuwa ameleta pesa nyingi ili kumkomboa kwa fidia binti yake lakini
alipokutana na Mtume na kujulishwa juu ya yaliyotokea kwa binti yake alitangaza Uislam wake na kuingia
katika dini hii. Ndoa hii ya kisiasa ilipelelea kutokea yafuatayo:
1. Askari wote wa Kiislam waliwatoa wafungwa wao na kuwaacha huru kwa kusema kuwa: “ Hawa ni
ndugu wa Mtume wa Mungu”. Hakuna mwanamke aliyekuwa na thamani kwa watu wake kuliko Juwairiya.
Pindi alipoolewa na Mtume mamia ya watu kutoka familia za kabila la Bani Al-Mustaliq waliachwa huru
kwa ajili yake.
2. Kwa ndoa hiyo Mtume alimpa hadhi na heshima na kumuokoa dhidi ya utumwa.
3. Aliingia katika Uislam na Uislam wake ulithibitika kuwa mzuri.
4. Baba yake naye pia aliingia katika Uislam, halikadhalika watu wengi katika kabila lake walifanya hivyo.
Ieleweke kuwa hapo kabla ya kuolewa na Mtume, Juwairiya aliwahi kuolewa mara moja na Musafi Ibn
Safwan.
9. Safiya Bint Huyay:
Baada ya vita vya Khadaq, Mtume alielekea Khaibar kwa ajili ya kuwaadhibu Bani Al-Nadeer, Wayahudi
waliowasaliti Waislam na kwenda kinyume na makubaliano walioyafanya na Mtume (S.A.W) kwa kufanya
hujuma katika vita hivyo. Khaibar ilitiishwa na kuangukia mikononi mwa Waislam ambapo mmoja wapo
wa mateka alikuwa Safiya Bint Huyay bin Akhtab. Inasemekana kuwa nasaba yake inakwenda mpaka kwa
Harun, ndugu wa Musa (A.S). Mama yake ni Barra bint Samawal. Hapo kabla, Safiya aliwahi kuolewa
mara mbili: mara ya kwanza aliolewa na Salam Ibn Mishkam na baadaye akaolewa na Kinana Ibn Al-Rabi
Ibn Abil-Haqiq. Inasemekana kuwa alipochukuliwa mateka, Mtume alimuuliza: “Utapenda kuolewa nami?
Akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nilikuwa nikitamani kuolewa na wewe kabla sijawa
Mwislam na sasa ninauamini Uislam, nitaikataaje hii ndoa hali ya kuwa Mungu ameifanya iwezekane?”
Hivyo, Mtume (S.A.W.) alimuacha huru, kisha akamuoa. Alikuwa muumini mzuri na hadithi nyingi
zilizungumzia juu ya uthabiti wa Uislam wake. Mtume alipokuwa akiugua katika kipindi cha mwisho cha
uhai wake, Safiya alisema: “Ninaapa kwa Mungu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, natamani ningekufa
mimi badala yako”.
10. Um Habiba „Ramla bint Abu Sufian‟:
Aliingia katika Uislam yeye pamoja na mumewe, Ubaidullah Ibn Jahsh Al-Asdi. Kisha walihamia Ethiopia.
Siku moja aliota ndoto ya kutisha ambayo ilikuja kuthibitika pale mumewe alipoingia katika Ukristo
wakiwa huko Ethiopia . Alijaribu hata kumbadilisha dini Ramla, lakini Ramla alikataa na kustahimili shida
nzito kwa ajili ya kuilinda imani yake. Alikaribia kufariki dunia kwa sababu ya huzuni na masikitiko.
Alitafakari: “Kwa nini Ubaidullah alihama? Ukandamizwaji, kuhama, manyanyaso yote yalikuwa ya nini?
Sasa hivi, anaucha Uislam kwa kile ambacho Ramla amekihangaikia na kukisumbukia na hata kumfanya
148
baba yake, Abu Sufian akumbwe na huzuni na msongo. Ramla afanye nini? Arudi Makka ambapo baba
yake amewasha moto wa vita dhidi ya Uislam au aendelee kukaa Ethiopia akiwa na majonzi, msongo na
mume aliyebadili dini?
Katika hali hii mmoja wa watumishi wa mfalme Najashi alikuja kumwambia Ramla kwamba Mtume
angependa kumuoa kwa sababu alichukuliwa kama mtu aliyeachika. Mtume alimtuma mtu kwa lengo la
kumchumbia. Alipopata habari, Um Habiba alichukua mikufu miwili ya fedha na kumpa mtumishi huyo
kama zawadi. Kisha akamuomba Khalid Ibn Said Ibn Al-As awe mwakilishi wake katika hii ndoa. Mfalme
Najashi alimpa Um Habiba dinari mia nne kama mahari. Alipokuja kutoka Ethiopia, Mtume alimkirimu
akamkaribisha na kumfariji kwa ndoa yake iliyovunjika. Akawa mmoja wa mama wa waumini. Na hata
baba yake, Abu Sufian, ambaye ni kiongozi wa Maquraish alipopata habari za ndoa hii alisema kuhusu
Muhammad: “Ni mwanaume ambaye hawezi kukimbiwa”. Wakati huo Um Habiba alikuwa mwaminifu na
mtiifu kwa mwanaume aliyemuokoa kutoka katika mateso, wasiwasi na huzuni.
Pindi mkataba wa amani wa Hudaibiya ulipovunjwa na Maquraish, Abu Sufian alikwenda kukutana na
Mtume na kumuomba kufanya upya mkataba huo. Alikwenda nyumbani kwa binti yake aliyeshangaa
kumuona kwa sababu hakuwa amemuona baba yake tangu alipohamia Ethiopia. Abu Sufian alitaka kukaa
juu ya mkeka lakini (Um Habiba) alifanya haraka kuutoa na kuukunja. Abu Sufian akasema kwa namna ya
upole: “Binti yangu, je umeukunja kwa sababu haunifai, au kwa sababu sistahiki kuutumia?” Akasema:
“Ni mkeka wa Mtume wa Mungu, na wewe ni kafiri, hivyo sikutaka ukae juu yake”
Abu Sufian alifedheheka sana akasema kwa namna ya kusikitika: “Ewe Binti yangu, baada yangu
umeathiriwa na uovu”. Kisha akaondoka akiwa na hasira.
Hivyo, Mtume alimuoa Um Habiba kwa lengo la kumuondolea huzuni, kumfariji na kuumaliza ugeni na
upweke aliokuwa nao katika nchi ya kigeni. Alimuoa huyu Binti wa Abu Sufian, kiongozi wa Makka, kwa
madhumuni ya kisiasa. Alifanya hivyo akitumaini kwamba Abu Sufian atasalimu amri na kukomesha
mapambano ya Maquraishi dhidi ya Waislamu.
11. Maria:
Al-Muqauqis, mtawa wa Misri alimtuma Maria kama zawadi kwa Mtume. Alimtumia zawadi kadhaa
kupitia kwa mjumbe wa Mtume, Hatib Ibn Abi Baltaa. Miongoni mwa zawadi hizo ni vipande elfu moja
vya dhahabu na nguo laini zipatazo ishirini zilizotengenezwa kutokana na vitambaa vya Kimisri. Zawadi
nyingine alikuwa ni Maria na dada yake.
Walipofika Madinah, wanawake hao walikuwa ni wenye huzuni kutokana na kuhisi ugeni. Mtume alimuoa
Maria ambapo dada yake aliolewa na mshairi wa Mtume aliyeitwa Hassan Ibn Thabit. Ndoa hii ilipelekea
kuwepo kwa mahusiano mema na Wamisri. Mtume (S.A.W.) alisema: “Amilianeni vizuri na Wamisri
kwani wana uhusiano wa damu pamoja nasi na tunajukumu la kudumisha usalama”.
Wakati wa mazungumzo ya amani pamoja na Mua‟wiya, Al-Hassan Ibn Ali alimtaka muawiya awasamehe
watu wa Hafna wasilipe kodi za kila mwaka, Kharaj. Hafna ni mahali alipozaliwa Maria na ni makazi ya
wajomba wa Ibrahimu, mtoto wa kiume wa Mtume (S.A.W.) aliyezaliwa na Maria. Baada ya ufunguzi wa
149
Misri, Ubada Ibn Al-Samit alikitafuta kijiji hicho cha Hafna na kwenye makazi ya Maria akapajengea
Msikiti.
12. Maymouna Bint Al-Harith:
Waislam katika mji wa Madinah walisubiri kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya mkataba wa amani wa
Hudaibiya ili wapate kwenda Makkah kwa ajili ya ibada ya Umra. “Hakika Mwenyezi Mungu
amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu,
Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na
khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni” {48:27}. Kwa hakika
waumini waliingia katika mji wa Makka wakiita kwa sauti: “Labaika Allahumma Labbaika”
wakimaanisha: “Tumeitika wito wako Ee Mwenyezi Mungu”. Mji wa Makka ulitikiswa na kundi hilo
lililokuwa likiita kwa sauti moja, wapagani walitishika na kuogopa sana na kuhisi kana kwamba milima ya
Makka ilikuwa ikipasuka na kuvunjwavunjwa na sauti hizo zilizoendelea kuita “Hakuna Mungu ila Allah
tu, ametimiza ahadi yake, amempa ushindi mja wake Muhammad na jeshi lake, na Yeye pekee
ameyashinda majeshi ya muungano wa washirikina”. Ni wakati huo ambapo watu wote walitambua kuwa
siku ya ushindi mkubwa kwa Waislam ilikuwa imewadia.
Mandhari hayo yalikuwa na athari ya mvuto kwa watu wa Makka. Miongoni mwa wanawake wazuri wa
Makka, Barrah Bint Al-Harith Al-Hilaliya, mjane mwenye umri wa miaka ishirini na sita, alihisi kumpenda
sana Muhammad na kumwambia dada yake, “Ummul Fadl”, mke wa Al Abbas Ami yake Mtume, kwamba
alikuwa tayari kujitoa nafsi yake kwa ajili ya kuolewa na Muhammad. Hivyo, Mtume (S.A.W.) akamuoa na
kumpa jina la “Maymouna” lenye maana ya mtu aliyebarikiwa. Alimpa jina hilo kwa sababu lilikuwa ni
tukio lenye baraka kuingia Makka kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba ya kuuacha katika tukio la
Hijrah.
Katika kuhitimisha mjadala huu, tunaweza kusema kuwa Mtume (S.A.W.) alioa wanawake kumi na moja,
baada ya Khadija, ambao sita miongoni mwao ni wa kabila la Quraish na watano walitokana na makabila
mengine ya Kiarabu. Alifanya hivyo kwa lengo la kuanzisha mahusiano mema na makabila yao.
Aliziunganisha nyoyo za watu kupitia ndoa hizo na akawataka wafuasi wake kuiga mfano wake. Al-Tabari
anahadithia kwamba Mtume (S.A.W.) alimtuma Abdul Rahman Bin Awf kwenda Dawmat Al Jandal, eneo
lililopo kaskazini mwa Arabia, na akamwambia: “Kama wakikufuata katika Uislam, basi muoe binti wa
Mfalme wao”. Hii inaonesha kuwa ilikuwa ni sera iliyofuatwa na Muhammad na wafuasi wake kwa lengo la
kuimarisha mahusiano pamoja na makabila mbalimbali ili kwamba wasivunje au kwenda kinyume na
makubaliano yao na ahadi zao kwa Waislam. Kutokana na sera hii watawala na watawaliwa wakawa ndugu
wenye uhusiano wa damu.
Mustashriqiina wamekifanya kipengele kimoja wapo cha Uislam chenye kung‟aa sana kionekane kuwa
chenye giza, lakini giza hilo litaendelea kubaki katika akili zao na akili za wafuasi wao. Waliona uaminifu
wa Mtume katika maadili yake, maisha yake na mahubiri yake yote kuwa ni kitu cha uwongo. Waliisawiri
rehema na huruma ya Mtume kama uonevu mkubwa. Waliusawiri mfumo wake wa utawa na upole kuwa ni
tamaa ya kuhukumu na kutawala.
150
Kwa kufanya hivyo hawakuifuata haki, wala hawakuwa waaminifu na waadilifu kihistoria. Hawakuwa
sahihi katika tabia yao mbaya dhidi ya Mtume aliyetumwa na Mungu. Uko wapi uaminifu wao na uadilifu
wao katika kufanya utafiti?
Walimtuhumu Mtume kuwa alizidiwa na tamaa ya kijinsia, walidhani kuwa kwa kuzungumzia ndoa zake
mbali mbali kwamba wengeweza kuthibithisha hoja yao. Lakini kama tukiuliza akili ya kawaida tutakuta
kwamba mawazo yao si sahihi.
Walidai kuwa Mtume aliwakataza wafuasi wake kuowa zaidi ya wake wanne kwa wakati mmoja huku yeye
akioa wake wanane. Tukiirejea historia ya usimikaji wa sheria tunapata kujua kwamba aya zinazoweka
kikomo cha idadi ya wanawake ziliteremshwa mwishoni mwa mwaka wa nane wa Hijrah, kipindi ambacho
Mtume alikuwa amekwisha kuoa wake zake wote.
Kabla ya kuteremshwa aya hizo hapakuwepo na kikomo cha kuoa mpaka wake wanne tu. Hivyo,
hakuna hoja yenye mashiko ya kumtuhumu Mtume (S.A.W.) kwamba alijipa ruhusa ya kufanya kitu fulani
na kuwakataza wafuasi wake kukifanya.
Aidha, Mtume (S.A.W.) hakuwa mtu pekee katika zama zake (miaka 1400 iliyopita) kuoa wake wengi.
Lilikuwa ni jambo mashuhuri na la kawaida miongoni mwa watu wa enzi hizo. Omar Ibn Al-Khattab katika
kipindi chake cha kabla ya Uislam alikuwa ameoa wanawake saba kwa uchache. Nao ni:-
1. Zainab bint Maz‟oun bin Habib, bin Wahab, bin Huzafa.
2. Mulaika bint Jarwal Al-Khuzai.
3. Quraiba bint Abi Umayya Al-Makhzoumi.
Wanawake wengine aliowaoa baada ya kusilimu ni hawa wafuatao:
4. Um Hakeem bint Al-Harith bin Hisham Al-Makhzoumi.
5. Jameela bint Thabit bin Abil Aklah Al-Awsi Al-Ansari.
6. Um Kulthoum bint Ali bin Abi Talib
7. Fakaiha Al Yamania.
Alitaka kuoa wanawake wengine lakini walikataa kwa sababu alikuwa mkali sana mwenye kutisha.
Khalifa wa tatu, Othman bin Affan aliwaoa:
1. Ruqayya bint wa Mtume (s.a.w).
2. Um Kulthoum, dada wa Ruqayya
3. Fatima bint Ghazwan bin Jabir
4. Um Amr bint Jundub bin Amr
5. Fatima bint Al-Waleed bin Al-Mughira Al-Makhzoumi
6. Um Al Baneen bint Uyayna
7. Naila bint Al-Farafisa
8. Ramla bint Shuhaiha.
Naye Khalifa wa 4, Ali alioa wanawake wafuatao:
151
1. Fatima bint wa Mtume (S.A.W) ambaye alikuwa mke wake wa pekee hadi alipofikwa na umauti.
2. Um Al-Baneen bint Hizam
3. Laila bint Massoud bin Khalid
4. Asmaa bint Umaith
5. Al-Sahbaa bint Rabi‟a
6. Umama bint Abil As bin Al-Rabie‟a
7. Um Said bint Urwa bin Massoud
8. Mukhabbia bint Emriel Qais bin Adi.
Kwa hiyo tukisoma historia za maisha ya wanaume wa wakati huo tutaona kwamba ndoa ya wake wengi
kilikuwa ni kitu mashuhuri na cha kawaida. Kwanini Mustashriqiina walimuona Mtume pekee kuwa mtu wa
ajabu? Kwanini hawakuitazama zama yote kwa ujumla? Kwanini hawakuyadurusu mazingira
yaliyokuwepo?
Kama wangekuwa waadilifu wangejifunza kwamba upeo wa hisia ya furaha ya Mtume ulikuwa katika Sala,
sio katika kuoa.
Mtume (S.A.W.) wakati wote alikuwa na saa moja ambayo aliitumia kuwa karibu na Mungu, ukaribu
ambao hakuna malaika wala Mtume mwingine yeyote aliyeupata. Katika saa hiyo ndipo ilipopatikana
furaha yake, sio katika wanawake. Lakini chuki ndiyo iliyoyatia upofu macho ya Mustashriqiina.
Katika Suala hili, Thomas Carlyle anasema: “Muhammad hakuwa mtu wa matamanio licha ya yote yale
ambayo yamekuwa yakisemwa dhidi yake bila ya uthibitisho. Tutakuwa tunakosea sana kama tukidhani
kuwa alikuwa mtu wa matamanio ya kijinsia ambaye alifikiria tu kuhusu matamanio yake. Hapana;
alikuwa mbali kabisa na tuhuma hizo” (1)
.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Hakimu, tunaona kuwa tuhuma hizi zinathibitika kuwa ni za uwongo kama ilivyo
kwa tuhuma nyingine.
Rejea:
1. Carlyle katika mihadhara yake ijulikanayo kama: “Heroes and Hero Worship” {1838 – 1841}
152
KESI YA KUMI NA TANO
Chembechembe za Upagani
Mwendesha Mashtaka: Tunakubali kwamba Hija ni mkusanyiko wa Kiislam wenye faida
nyingi, lakini huoni kwamba bado ina taratibu za kipagani kama vile Kaaba, kubusu na kulitukuza
jiwe jeusi ambalo linaonekana kuwa kama mawe mengine matukufu yaliyokuwa mashuhuri kwa
wapagani?
Hakimu: Kwa kweli tunataka kujua kwa nini Waislam wanalibusu Jiwe Jeusi, kwa nini Kaaba
ilifanywa kuwa Qibla na uelekeo kwa ajili ya sala, na kwa nini mahujaji wa Kiislam hutupa na
kurusha mawe wakati wa Hija. Tunataka kujua mambo mbalimbali kuhusu sala na kwa nini
iliagizwa kutekelezwa? Je, ni kawaida za kidini tu? Ina faida gani katika zama za sayansi na
maendeleo?
Uislam: Hivyo basi, ninatarajiwa kufafanua nukta tatu, ambazo ni:
1. Kaaba na Jiwe Jeusi.
2. Kutupa mawe wakati wa Hijja.
3. Sala, asili yake na uhalali wake
Ama kuhusu Kaaba tunajua kuwa Nabii Ibrahim (A.S.) alimuomba Mungu akisema: “Mola wangu
zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao (kizazi changu) {S. 14:37}. Mwenyezi Mungu aliyakubali
maombi ya Ibrahim na kuufanya msikiti alioujenga kuwa mahali panapopendwa na kutembelewa na
mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Vile vile, Mungu alitaka kuwapa heshima Waarabu,
hivyo akaufanya mji wao kuwa kituo ambacho watu wote wanatakiwa kukielekea wakati wa sala
zao.
Hatudhani kuwa mtu mwenye akili anaweza kufikiri kwamba aliitukuza nyumba ya Ibrahim na
Ismail kwa sababu ya mawe na kuta zake. Tunajua kuwa utukufu uliokusudiwa hapa ni utukufu wa
kiroho sio wa kimwili/Kimaada. Siku zote mtu hamtembelei rafiki yake mpendwa kwa ajili ya
mawe ya nyumba yake bali hufanya hivyo kwa ajili ya rafiki yake mwenyewe. Hivyo basi, Kaaba
ni alama ya utukufu ambao Mungu alimpa Nabii Ibrahim (A.S.) na Muhammad (S.A.W.).
Allah anamwambia Muhammad ndani ya Qur‟an:
“Hakika tumeona uso wako ukielekea mbinguni kwa ajili ya kutaka muongozo, basi bila shaka
tutakugeuza kwenye Qibla ukipendacho. Basi elekea uso wako upande wa Msikiti mtukufu, na
popote mtakapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo” {2:144}. Hivyo basi, Kaaba ni alama ya
kuziunganisha akili na nyoyo za wanadamu. Ushahidi ni kwamba Qur‟an Tukufu imetueleza kuwa
153
Qibla ni uelekeo wa Mwenyezi Mungu tu: “Mahala popote muelekeapo ndipo kwenye uelekeo
wa Mwenyezi Mungu” {2:115}.
Kwa hiyo, utukufu wa eneo hilo haupo kwa ajili ya Kaaba kama Kaaba bali kwa sababu ni amri ya
Mungu. Kutii amri yake ndio jambo la muhimu katika suala hili. Kama amri ya Mungu
isingekuwepo katika suala hili tusingeona utukufu wowote katika eneo husika. Kinadharia tunaona
kwamba Waislamu kuelekea katika uelekeo mmoja ni alama ya umoja wa imani na malengo
yao.
Hivyo kutokana na maelezo hayo tunapata kujua kwamba:
1. Kuelekea upande wa Kaaba kunafanywa na mwili pekee ilhali roho na moyo vinaelekezwa kwa
Mwenyezi Mungu.
2. Hakuna Mwislam yeyote atakayefikiri kwamba anaielekea Kaaba kwa sababu ya mawe yake.
Mwislam hutambua kwamba wakati wa sala, akili, roho na moyo wake humuelekea Mwenyezi
Mungu: “Mahala popote muelekeapo ndipo kwenye uelekeo wa Mwenyezi Mungu”. {2:115}
3. Kulizunguka jengo la Kaaba katika Hijja, ingawa hufanywa na mwili, lakini ulimi wa hujaji na
moyo wake hurudiarudia maombi haya: “Labbaika Allahumma Labbaika, La sharika Laka
Labbaika” (Nimekuitika mola wangu nipo hapa kwa ajili ya kukuabudu, huna mshirika). Maombi haya huambiwa Mwenyezi Mungu, sio Kaaba.
Hatujawahi kumsikia yeyote akisema: “Ewe Kaaba nipo hapa kwa ajili ya kukuabudu”. Jambo hili
linafafanuliwa vizuri na maneno ya hujaji mmoja wa Kiislam pale anaposema: “Mwili wangu
umeizunguka nyumba hii, lakini moyo wangu umemzunguka Bwana wa nyumba hii”.
Ama kuhusu Jiwe Jeusi tunapaswa kuzungumzia Hijja kwa ujumla wake ili kuweza kufafanua suala
la kulibusu Jiwe au kulinyooshea kidole. Inatosha kunukuu hapa aya ya Qur‟an inayozungumzia
malengo na faida za Hijja. Mwenyezi Mungu anamwambia Ibrahim akisema: “Na watangazie
watu Hjija; watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila ngamia aliyekonda
(kwa machovu ya njiani) wakija kutoka katika kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa
yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu ---- katika siku maalumu ---- juu ya yale
aliyowaruzuku, nao ni wanyama wenye miguu minne. Basi kuleni katika wanyama hao na
mlisheni mwenye shida aliye fakiri” {22:27 – 28}.
Hivyo basi, katika Hijja kuna faida na manufaa ya kimwili, kimaadili, kiroho, kijamii na kiuchumi.
Mkutano huu mkuu unaofanyika katika viwanja vya Arafat (jirani na Makka) ni ishara ya umoja wa
Waislam wote. Mambo na matatizo yote ya ulimwengu wa Kiislam hupata kujadiliwa katika
mkutano huo. Kila taifa la Kiislam lina biashara na bidhaa zake na kwa kupitia kongamano hili
mikataba na makubaliano mengi hupata kufanywa katika nyanja za kiuchumi, elimu, afya ….. n.k.
154
Katika Hijja mtu huweza kushuhudia usawa wa kweli wa kimatendo baina ya watu wa daraja la juu
na wale wa kawaida. Wote huvaa aina moja ya nguo, na wote huishi maisha ya aina moja. Hakuna
ukuu katika ufahari wa mali, utukufu, cheo au madhihirisho mengine yoyote ya kimaada/kimwili.
Mkutano huu wa Kiislam ni wa kipekee. Wakati ambapo katika dini nyingine Hijja hufanywa
kwenye makaburi, katika Uislam hufanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Katika zama za leo tunaona kwamba watu walijaribu kuuiga Uislam katika kongamano lake
linalohusisha watu mbalimbali, wakaunda Umoja wa Mataifa baada ya kuanzisha shirikisho la
mataifa (League of Nations). Lakini makongamano haya yalipotoshwa na yakakosa sifa kwa sababu
yalijengwa kwenye misingi ya fikra za kimaada huku wakiusahau upande wa kiroho ambao,
unapokosekana binadamu huwa sawa na jiwe.
Ama kuhusu kulibusu Jiwe Jeusi, tunapaswa kutambua kwamba Waarabu walikuwa wakiabudu vitu
mbalimbali, lakini Jiwe hilo halikuwahi kuchukuliwa kama Mungu. Lilichukuliwa tu kama kitu
kitukufu kwa sababu ni miongoni mwa kumbukumbu za jengo na ujenzi wa Nabii Ibrahim (A.S.).
Hivyo basi, Uislam haukuwahi kuikubali aina yoyote ya upagani wa zama za kabla ya Uislam.
Isitoshe kuligusa au kulibusu Jiwe Jeusi wakati wa Hija ni kitendo cha mfano tu na wala sio kwa
kusudio la kulitukuza Jiwe hilo kama Jiwe. Pindi Maquraish walipoijenga upya Kaaba, koo
mbalimbali zilizozaana juu ya yule ambaye angestahiki kuliweka Jiwe Jeusi mahali pake. Tukio
hilo lilitokea miaka mitano kabla ya Muhammad kuwa Mtume. Alilitatua tatizo hilo kwa kutandika
kitambaa chake, akaliweka Jiwe katikati mwa kitambaa hicho na kuzitaka koo zote za Kiquraish
kukinyanyua kitambaa hicho. Kisha yeye mwenyewe alilichukua Jiwe na kuliweka mahali pake.
Siku moja Khalifa wa pili, Omar Ibn Al-Khattab alisimama mbele ya Jiwe Jeusi akaliambia
akisema: “Ninajua kwamba wewe ni jiwe ambalo haliwezi kunufaisha wala kudhuru,
nisingekubusu kama nisingemuona Mtume akikubusu”. Kwa hiyo kulibusu hili Jiwe sio wajibu
na Hijja inaweza kukamilika bila kufanya tendo hilo.
Kutupa mawe kwenye sanamu la shetani wakati wa Hijja ni ishara ya hali itakavyokuwa baada ya
kumalizika kwa ibada ya Hijja. Pindi shetani atakapomtaka hujaji amuasi Mwenyezi Mungu yeye
atakumbuka kitendo hicho cha kumpiga mawe na atatambua kuwa siku zote yuko vitani dhidi ya
shetani na mara zote atamfanya kuwa adui yake. Baada ya Hijja jambo hili litapelekea
kushikamana na tabia na matendo yatakayokuwa kinga madhubuti dhidi ya ushawishi wa shetani.
Hijja ya kweli inayokubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ile inayombadilisha hujaji kuwa mtu mpya,
inayomfanya mtu kuwa binadamu wa kweli, mwenye tabia njema na mahusiano mazuri na
Mwenyezi Mungu.
Hujaji atarudi nyumbani huku akiendelea kufuata mfano wa Nabii Ibrahim (A.S.) katika utii wake
wa kweli kwa Mwenyezi Mungu hata kama angetakiwa kumtoa kafara mwanaye wa pekee. Hijja ni
hamami ya kiroho na haitakuwa Hijja ya kweli kama haitakuwa na athari kubwa kwa Hujaji. Hijja
ni fikra, roho, elimu na manufaa mbalimbali. Hivi ni vitu muhimu katika ibada ya Hijja.
155
Katika zama za leo tunashuhudia vipengele mbalimbali vya upopoaji au ulengaji. Mtazame
mwanajeshi akifanya mazoezi kwa kutumia mwanasesere, anauchoma kwa kisu na kuulenga kwa
bunduki,. kwa nini? Je, wote huo ni wendawazimu? Hapana! Ni mazoezi anayoyafanya katika
kujiandaa kwa ajili ya siku ya kweli atakapokabiliana na adui. Tunajua kwamba majeshi ya kisasa
yanafanya maajabu makubwa kwa kutumia mwanasesere na vifaa vya bandia. Je, wanapoteza
muda na pesa zao? Hapana. Wanafanya mazoezi kwa kutumia vitu vya mfano katika kujiandaa kwa
ajili ya mapambano ya kweli yanayotarajiwa kutokea, kama inavyokuwa katika tukio la kumpiga
mawe shetani wakati wa ibada ya Hijja. Tukio hilo ni ishara ya tangazo la vita dhidi ya shetani, vita
ambayo huendelea mpaka mwisho wa maisha ya hujaji pamoja na kuendelea kumtii Mwenyezi
Mungu pekee.
Sala:
Sala ina makusudio na malengo mbalimbali kama vile umoja wa lengo ambalo hutokana na ukweli
kwamba Waislam wote huelekea kwenye Qibla kimoja, humuabudu Mungu mmoja, husema
maneno ya aina moja na kufanya harakati za aina moja. Philip Hitti katika “History of the Arabs”
anasema kwamba, lau kama mtu angepewa uwezo alionao ndege wa angani, kisha akautazama
ulimwengu wa Kiislam wakati wa Sala, na akaweza kuzitazama pande zote kwa uhuru bila kujali
mistari ya latitude na longitude, mtu huyo angeshuhudia mistari mikubwa ya waumini
wakijikusanya kukizunguka kituo kimoja, Kaaba, wakiwa katika mviringo mkubwa.
Sala hupelekea kuwapo na usawa pale watu wote, tajiri au maskini, walalahoi na waheshimiwa,
wanaposimama bega kwa bega wakijisalimisha mbele ya Mungu mmoja katika Sala zao. Wakati
wa Sala watu hupata kujuana kwa ukaribu. Pale mmoja wao anapokosekana msikitini wenzake
humuulizia na watamtembelea kama atakuwa mgonjwa na watamsaidia kama atakuwa na shida.
Sala ina utajiri wa kiroho ambao wale tu walioshikamana nayo ndio wanaouona na kuushuhudia.
Sala ni taa ya moyo. Mtu anaweza kujishughulisha na masuala ya kidunia na kumsahau Mungu
pamoja Akhera na kifo, lakini pindi anaposikia wito unaomtaka kwenda kwenye Sala (adhana)
hufanya haraka kwenda kusali, na kwa hivyo miale ya imani huendelea kuwa taa na nuru katika
moyo wake.
Binadamu wa leo anaihitajia sana Sala kwani ni mahali anapoweza kupata faraja na kuufurahia utu
wake katika vipengele vyote vya kimwili na kiroho. Mwislam mzuri husali mara tano kwa siku.
Kila mara huwasiliana na Mwenyezi Mungu na kutamani muda wa mawasilano hayo uwe mrefu.
Lakini wale wasiotekeleza Sala ya kweli inayomuongoza mtu kwenye tabia njema, maadili mema
na mahusiano mazuri na watu, watu hao ni kama kipofu anayesimama mbele ya kazi nzuri ya
kisanaa lakini akawa hawezi kufurahia uzuri wa kazi hiyo hata kama atasimama hapo kwa muda
mrefu kiasi gani.
Sala inayosaliwa katika zama hizi sio Sala ya kweli na hakika. Watu wengi huitekeleza kwa namna
ya mazoezi tu na harakati za kimwili bila kuwepo na mawasiliano ya kiroho baina ya muhusika na
Mwenyezi Mungu.
156
Sala inayotakiwa na Uislam ni ile ambayo muhusika huwa na mawasiliano ya kiroho na Mwenyezi
Mungu, akasimama mbele ya utukufu na ukuu wake. Ni shule kuu ambayo Profesa wake ni
Mwenyezi Mungu ambapo mtu huwa ni kama mwanafunzi anayepokea maarifa kutoka kwake.
Sala ya kweli humnyanyua mtu mpaka kwenye daraja ya malaika, na kuua ubinafsi uliopo katika
moyo wake. Sala isiyomkataza mtu kufanya maovu na mabaya sio sala ya kweli, bali sala
inayomfanya mtu awe katika mawasiliano na Mwenyezi Mungu humtengeneza binadamu kamili
katika jamii, binadamu mwaminifu, mwenye huruma, mwenye kuaminiwa na mwenye imani
kamili. Mtu kama huyo atawezaje kusema uongo, kuwa msaliti, kutapeli au kumdhuru mtu.
Hawezi kufanya hivyo hali ya kuwa muda mfupi tu uliopita alikuwa amesimama mbele ya
Mwenyezi Mungu wakati wa Sala yake. Anawezaje kufanya kitu kibaya hali ya kuwa anajua
kwamba muda mfupi ujao ataachana na maisha haya na kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu?
Mwislam wa kweli kila sekunde huhisi kwamba yuko mbele ya Mwenyezi Mungu; roho na moyo
wake huhisi kitu hicho!
Montesque aliwahi kusema: “Mwanadamu huhisi kuvutiwa zaidi na dini yenye matukio
mengi kuliko dini yenye ada ndogo za kidini. Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mtu
hushikamana kwa nguvu zote na vitu ambavyo huendelea kuitawala akili yake”. Dini ya
Kiislam siku zote ipo katika akili ya Mwislam na Sala za kila siku huimarisha hisia hii.
Said Ibnul Hassan, Myahudi kutoka Alexandria aliyesilimu mwaka 1238, siku moja alisema
kwamba tukio la kuwaona Waislam wakisali Sala ya Ijumaa katika jamaa ndio iliyokuwa chanzo
cha kusilimu kwake. “Niliwaona Waislamu wakiwa wamesimama kwa ajili ya sala wakiwa katika
mistari kama malaika. Pindi msoma hotuba alipotokeza akiwa amevaa joho lake jeusi nilijawa na
hali ya kumheshimu na pindi alipomalizia hotuba yake kwa kusema: “Mwenyezi Mungu anaamuru
kufanya uadilifu, kutenda wema, na kuwapa ndugu wa karibu haki zao, na anakataza kutenda
maovu na machafu na dhulma na maasi: anakuwaidhini ili mpate kukumbuka”, nikahisi kitu fulani
kikinisukuma kusimama na kujiunga katika safu za waumini wa Kiislam ambazo zilionekana kuwa
kama safu za malaika! Katika kurukuu na kusujudu kwao mtu huweza kuhisi kuwa yupo mbele ya
Mwenyezi Mungu. Nilijiambia: “Mungu aliongea na wana wa Israeli mara mbili, lakini anaongea
na Waislam kila wanapotekeleza Sala zao. Nikatambua kuwa nilikuwa nimeandikiwa kuwa
Mwislam”.
Naye Renan anasema: “Kila nilipokwenda msikitini nilihisi mhemko na hisia kubwa; huzuni na
simanzi ya kwamba nilichelewa kuingia katika Uislam”.
Kutokana na hali hiyo tunaweza kutambua ni jinsi gani Sala ya moja kwa moja iliyosaliwa na
mfanyabiashara wa Kiislam mbele ya Waafrika au Waindonesia na Wafilipino ilivyowafanya
waingie katika Uislam. Sala hiyo na athari zake ziliufanya Uislam uenee kila mahali.
Mheshimwa Hakimu! Mwisho kabisa, je, katika suala la Hijja, Kaaba, Jiwe Jeusi, kupopoa mawe
na Sala, umekuta chembechembe zozote za kipagani? Je, huoni kuwa vitu hivi hupelekea mtu kuwa
na furaha na ubinadamu?
157
KESI YA KUMI NA SITA
Kikao cha Mwisho
Swali la Kwanza:
Hakimu: Islam, katika kesi zilizotangulia ulikanusha idadi kadhaa ya tuhuma. Leo tunataka
tuhitimishe huu mjadala, lakini kuna idadi kadhaa ya maswali tunayotaka uyajibu kwa ufupi.
Una maoni gani kuhusu madai ya Sydney Ficsher katika kitabu chake kiitwacho “The Middle
East in the Islamic Era” ambapo ameeleza kuwa Uislam ni aina ya Uyahudi lililopotoshwa, madai
ambayo yanaungwa mkono na Naphtali Wieder katika kitabu chake kiitwacho “The influence of
Islam on Jewish Worship”. Madai kama hayo yalitolewa pia na J. Isaac katika kitabu chake
“Lectures on the Near East”, ambapo anasema: “Ilitokea kwamba Muhammad alijifunza mambo
fulani fulani kuhusu dini za Kikiristo na Kiyahudi wakati wa safari zake”.
Unasemaje kuhusu madai yafuatayo ya Goldziher: “Mahubiri ya Muhammad hayakuwa chochote
zaidi ya mchanganyiko wa fikra na mawazo ambayo alipata kujifunza kutokana na mawasiliano ya
moja kwa moja aliyokuwa nayo, kutokana na misingi ya Kiyahudi na Kikristo iliyomuathiri sana,
na kumsukuma kupandikiza hisia kubwa ya kidini ndani ya wafuasi wake”.
Islam: Hili ni kosa lililokaririwa kwa mfululizo na Mustashriqiina pamoja na
Wamagharibi walioamini kwamba Wayahudi ndio asili na chimbuko la imani zote za kidini
zilizowekwa ndani ya Taurati halafu wakateremshiwa wao tu na Mitume wao, na kwamba hapo
kabla hakuna aliyewahi kupewa imani hizo zaidi yao.
Lakini haihitaji kufanya juhudi na jitihada yoyote kutambua uwongo wa madai haya. Usomaji wa
kawaida wa Taurati ya sasa unaonesha kuwa Wayahudi walipokea fikra zao nyingi kuhusu
ulimwengu pamoja na mafundisho yao ya kijudisheria kutoka kwa mitume wa zamani au kutoka
kwa watu walioishi au kuchanganyika nao.
Taurati iliyopo sasa inaanza na kitabu cha mwanzo ambacho ni jiwe la msingi la imani zao za
kidini. Haihusishwi na Mtume yeyote wa wana wa Israeli, hivyo sio lazima kusema kuwa
kiliendeleza ubashiri wa Wayahudi na walijifunza kutoka kwa wale waliokuja kabla yao, bila
kuangalia kama kiliteremshwa kwa Mitume wa zamani au ilikuwa ni desturi na mila iliyorithiwa
kutoka kwa wahenga.
Katika kuisoma Taurati, kwa nini Mustashriqiina wanasisitiza juu ya uasili wa Uyahudi na
kuuchukulia Uislam kuwa si chochote zaidi ya kuwa tawi la mti wa Uyahudi hali kuwa
imethibitika kuwa Uyahudi wenyewe ni tawi la mti au miti ya zamani? Katika misingi ya imani
kama vile Uungu, Utume, Kiama, Thawabu na Adhabu, n.k. tunaona kuwa kuna taofuti kubwa kati
ya Uislam na Uyahudi au dini nyingine yoyote.
158
Kwa mujibu wa Wayahudi, Mungu wao, Yehova, ni Mungu wa kabila moja, ambaye neema zake
zinalihusu kabila hilo tu, lakini Mungu wa Uislam ni wa viumbe wote na hakuna anayependelewa
naye isipokuwa kwa uchamungu tu.
Utume kama unatazamwa na Wayahudi ni kufanya miujiza, kufichua siri na kufuta vitu
vilivyopotea, lakini katika Uislam ni ujumbe wa mafundisho na muongozo unaozungumza na akili
na ufahamu wa binadamu na kuwafikia watu kwa ushawishi unaotokana na hoja, uthibitisho na
dalili sio kwa njia ya upigaji chuku, mambo yasiyo ya kawaida au miujiza.
Kiama kwa Wayahudi huwabebesha watoto madhambi ya wazazi wao. Adhabu huwakumba dhuria
wa mbali kutokana na makosa yaliyofanywa na wahenga wao. Katika Uislam kila mtu atawajibika
kwa makosa na dhambi zake mwenye.
Hekalu katika tamaduni za Kiyahudi hupokea sadaka za waja wa Mungu ambazo zisingeweza
kupokelewa isipokuwa na makasisi wa hekalu. Lakini ndani ya Uislam hatuna kitu kama hicho
kabisa.
Kama tukienda kwenye suala la kulinganisha mizizi na matawi tunaweza kusema kuwa Uislam ni
mti tofauti unaotoa matunda mazuri ya dini zilizotangulia baada ya kuyachuja na kuyathibitisha.
Matunda ya mti wa Uislam yasingeweza kuzaliwa na mti ambao mizizi yake ni ya Kiyahudi kwa
sababu hata Uyahudi wenyewe ni tawi la miti ya zamani.
Imethibiti kwamba Wayahudi walijifunza mambo mengi kutoka katika lugha, fasihi na hekima za
Waislam hasa hasa katika zama za sasa. Kwa upande mwingine Waislam hawakupata chochote
kutoka kwa Wayahudi isipokuwa yale matukio ya Kiyahudi ambayo baadhi ya Waislam wasiokuwa
na maarifa walikuwa wakiyaeneza na ambayo hivi karibuni yameondolewa katika akili zao na
wanachuoni na wasomi wa Kiislam.
Lugha ya Kiyahudi haikuwa na kanuni za kimfumo na kiusanifu kabla ya karne ya kumi. Iliendelea
kuwa katika hali hiyo mpaka pale S‟aadia Jaoun alipojifunza utamaduni wa Kiarabu nchini Misri
katika karne hiyo na hapo ndipo kanuni za lugha ya Kiyahudi zilipowekwa. Kisha Adonim bin
Tameem, Mbabelon akaandika kitabu katika lugha ya Kiyahudi kwa kulinganisha na lugha ya
Kiarabu na kunukuu mifano mbalimblai kutoka katika Kiarabu kwa lengo la kuifafanua lugha ya
Kiyahudi.
Aidha Wayahudi hawakuwa na utaalam wa arudhi (Metrics) katika mashairi yao, walijifunza sanaa
hiyo kutoka kwa Waarabu wa Andolesia na Misri. Mwanafalsafa wa Kiyahudi Musa bin Maimun
alikuwa mwanafunzi wa wanafalsafa kadhaa wa Kiislam nchini Morocco. Kwa hiyo basi, tunaona
kwamba Uyahudi ulinufaika na elimu za Kiislam na Kiarabu hali ya kuwa Uislam haukuchukua
chochote kutoka kwa Wayahudi.
Katika kitabu chake kiitwacho “The Biography of Muhammad” bwana Boadly anakanusha
uzushi wa Margiliuth, Askofu Canon Sil na Durmingham waliodai kwamba sura zinazozungumzia
159
Ukristo ndani ya Qur‟an ni sura ambazo Muhammad alijifunza kutoka kwa Suhaib, mtu aliyebadili
dini zamani na kuwa Mwislam, halikadhalika kutoka kwa Jabir bin Abdullah kwa mujibu wa
madai ya Margiliuth. Boadly alijenga hoja yake juu ya ukweli kwamba hakukuwepo na tafsiri
zozote za Biblia kabla ya kudhihiri kwa Muhammad na tafsiri za Kiarabu za Agano la Kale
na Agano Jipya zilikuja baada ya karne nyingi kupita. Hivyo, itawezakanaje kudai kwamba
Muhammad alijifunza au kunukuu tamaduni zozote za Kibiblia?
Kudai kwamba Uislam ni toleo la dini nyingine kwa sababu una Sala, Funga na ada za kidini
nyingine, zile zinazopatikana katika Uyahudi na Ukristo, ni madai yasiyokuwa na maana kwa
sababu dini zote zinahubiri unyoofu wa moyo kwa kutumia matendo haya ya kiibada. Ufanano sio
kiamuzi cha kwamba dini moja imechukua kitu fulani kutoka dini nyingine.
Madai hayo hayana msingi kabisa na yanapingana na mantiki na akili salama. Aidha, matendo ya
kiibada ndani ya Uislam yanatofautiana sana na yale yaliyopo katika Uyahudi kama ilivyo kwa
upande wa misingi ya Kiimani.
Swali la Pili:
Mwendesha Mshtaka: Uislam ni zao la zama za kati (Middle Ages) ambazo
zilikuwa zama za giza na hazikuleta lolote jema. Ni zama zilizokuwa kinyume na sayansi,
wanasayansi na maarifa.
Islam: Ninakubaliana nawe kwamba zama za kati zilikuwa ni zama za giza, kuwachoma moto na
hataa kuwaua wanasayansi na kutangaza vita dhidi ya maarifa. Hili ni jambo lisilopingika,
lakini linaihusu tu Ulaya ambayo wakati ikiwa imelala katika giza, Waislam walikuwa
katika zama za Dhahabu (Golden Age), zama za nuru, sayansi, maarifa, utafiti, ugunduzi na
ufahamu wa hakika ya mambo katika nyanja zote.
Kwa kweli ninawasikitikia wale vijana wanaokariri kariri, kama kasuku, madai ya baadhi ya
Mustashriqiina (Orientalists) wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri kwa kutaja matatizo ya zama
za kati (Middle Ages), wakati huo huo wakisahau kwamba yaliyoikumba Ulaya hayakuzihusu zama
zetu za Dhahabu.
Katika zama hizo hatukushuhudia mgogoro wowote baina ya sayansi na dini, mgogoro kama ule
ulioikumba Ulaya. Uislam unamtaka Mwislam kutafuta elimu na maarifa katika nyanja zote.
Wakati miji ya Baghdad na Cordova ikiwa vituo vya sayansi na elimu vyenye vyuo vikuu, maktaba
na wanasayansi waliojaa tele, Ulaya ilikuwa imezama katika giza la ujinga. Wasomi, wanafikra na
wanasayansi walihukumiwa kwa madai kwamba utafiti wao ulikuwa kinyume na mafundisho
ya Kanisa na wengi wao waliuawa kwa sababu hiyo.
160
Wakati ensaiklopidia ya Larous chini ya neno “dini” ikirudiarudia kile ambacho katika karne ya
kumi na tisa viongozi wa kanisa huko Ulaya walikuwa wakisema: “Tekeleza ukiwa umefumba
macho yako”, Qur‟an kwa upande wake inasema: “Leteni ushahidi wenu ikiwa mnasema kweli” (1)
na “Je mnayo elimu? Basi mtutolee hiyo, nyinyi hamfuati ila dhana tu, wala hamsemi ila
uongo tu” (2)
.
Kwa msingi huo tunaona tofauti kubwa sana kati ya madai yao na ukweli ulio dhahiri kabisa.
Katika kitabu chake “The Conflict Between Science and Religion” Bwana Draper, Profesa
katika chuo kikuu cha New York anaonesha ukweli huu kwa uwazi kabisa pale anaposema: “Vyuo
vikuu vya Waislam vilikuwa wazi kwa wanafunzi wa Ulaya waliotoka katika nchi zao na kuja
kutafuta elimu na maarifa katika Vyuo hivyo. Wafalme na maamiri kutoka Ulaya walikuja
katika nchi za Kiislam kwa ajili ya kupata matibabu. Nchi za Kiislam ndizo zilizokuwa chanzo
cha mwanga na nuru kwa Ulaya katika nyanja za kifikra, kisayansi na kiutamaduni”.
Bwana Gerbert kutoka Ufaransa alisoma katika shule za Siville na Cordova ambapo alijifunza
utamaduni wa Kiislam na wa Kiarabu na baadaye akawa Papa huko mjini Roma akijulikana kama
Silvester II, na kuyatambulisha maarifa ya Waarabu wa mashariki na magharibi kwa watu wa Ulaya (3)
.
Wanafunzi wanaotafuta elimu wasingemiminika katika nchi zetu kutoka kila mahali kama nchi zetu
hizo zingekuwa zimezama katika giza. Profesa Libry anasema: “Kama Waarabu wasingetokea
katika jukwaa la historia, basi kipindi cha mwamko wa elimu na maarifa ya Ulaya kingechelewa
kwa karne nyingi”.
Jua la Arabia liliangazia magharibi katika zama za kati. Mwamko wa sasa wa Ulaya ulianza baada
ya kutokea kwa vita vya msalaba na watu wa Ulaya walikabiliana na kukumbana na medani za
kielemu na maarifa ya Kiaarabu na ya Kiislam. Kwa kipindi cha karne sita chanzo pekee cha
maarifa kwa Vyuo Vikuu vya Ulaya ilikuwa tafsiri kutoka katika Kiarabu. Tunaweza kusema
kwamba athari za Waarabu katika baadhi ya masuala ya kisayansi, kama vile madawa, zimeendelea
kuwapo hadi wakati wa sasa. Mpaka mwishoni mwa karne iliyopita, vitabu vya Avicenna vilikuwa
vikifundishwa katika Chuo Kikuu cha Montpelier.
Pindi Louis XIV alipokuwa akitaka kitabu cha tiba na madawa kwa ajili ya kupata maelezo kamili
ya tatizo lake alikuwa akilazimika kutoa kiasi kikubwa cha pesa, kama dhamana ya usalama wa
nakala pekee ya kitabu cha kiarabu iliyokuwapo Ufaransa wakati huo.
Wazungu wanasema kuwa uharibifu na uteketezaji wa mji wa Baghdad na maktaba yake ya Umma
(Darul Hikma) uliofanywa na Hulagu wa Mongolia, ulichelewesha maendeleo ya ustaarabu wa
dunia kwa kipindi cha karne sita. Mheshimiwa Hakimu! Naomba kuuliza: “Ni kipi kilichokuwa
zao la enzi za giza, je, ni dini ya Uislam au ni jaribio la kuuangamiza urithi wa Uislam lililomletea
binadamu giza na kuchelewesha maendeleo yake kwa karne sita?”
161
Kitu gani zaidi tunachoweza kukiongeza kwenye maelezo ya Bwana Gustav Lebon pale
alipotamani kuwa laiti kama Waarabu wangeitwa Ufaransa na mji wa Paris, kama ilivyokuwa kwa
mji wa Cordova nchini Hispania, ukawa kituo cha utamaduni na elimu, ambapo mtu wa kawaida
aliweza kuandika, kusoma na hata kuandika mashairi, wakati ambapo watawala wa Ulaya
hawakuwa wakijua hata kuandika majina yao na badala yake wakatumia stempu na muhuri.
Akiwadhihaki wale waliowalingalisha Waarabu na zama za kati na Wazungu wa wakati huo,
Bwana Gustav Lebon anasema: “Hali ilikuwa tofauti na vile tunavyojua leo hii. Waarabu
walikuwa ni watu waliostaarabika na Wazungu walikuwa washenzi wasiostaarabika (Sabages).
Hakuna uthibitisho uliokuwa bora zaidi kuliko pale tunapoiita historia ya Ulaya ya wakati huo
kuwa Zama za Giza”.
Katika kuhitimsha, ili kuipa mada hii haki na uzito wake stahili, kuna idadi kadhaa ya vitabu
ambavyo ni muhimu kuvirejea kwa lengo la kupata habari zaidi. Vitabu hivyo ni kama vile “The
History of Andolesia Duringi the Muslim Rule”, cha Dr. Ahmad Badr, “The History of Europe
During the Middle Ages” cha Bwana Ficsher. Vitabu hivi viwili vinazungumzia juu ya kipindi
kimoja cha muda na kuangazia juu ya zama zetu za kati, na zama za kati kwa upande wa Ulaya.
Kitabu kingine ni “The Sun of the Arabs Rises on the West” cha Zigrid Honike. Katika sura ya
mwisho ya kitabu chake kiitwacho “The Crusade Movement” cha Dr. Said Abdul Fattah Ashour,
anangazia juu ya athari ya vita vya msalaba kwenye mwamko wa ustawi wa Ulaya kwa kusema:
“Biashara ya Waarabu na kwa kufuata mfano wa maisha yao, viliibadilisha tabia ya utovu wa
nidhamu waliyokuwa nayo wanawake wa Ulaya katika kipindi cha zama za kati, na kumfanya
muungwana ajifunze zaidi hisia za wema, uadilifu na huruma.
Mheshimiwa Hakimu! Maelezo yetu yanaungwa mkono na ushahidi na uthibitisho kamili, lakini
mashtaka hayo yaliyotolewa dhidi ya Uislam ni ya uzushi na hayana ushahidi wala uthibitisho ulio
wazi. Ni madai yaliyosimama kwenye misingi ya chuki na uovu.
Swali la Tatu:
Mwendesha Mashtaka: Tunasoma ndani ya Qur‟an kuwa “Tumewainua
baadhi yao daraja kubwa juu ya wengine ili baadhi yao wawafanye wengine kuwa
watumishi” (4)
. Hapa tunaona kuwa Uislam unatambua tofauti za kimatabaka katika namna
ambayo mtu mmoja anafaywa kuwa mtumishi wa mtu mwingine.
Uislam: Kabla sijaangazia juu ya msimamo wa Uislam kuhusu mfumo wa kimatabaka, ninatakiwa
kulitolea dokezo jinsi lilivyokuwa likifanywa huko Ulaya. Katika zama za kati pengo baina ya
matabaka lilikuwa kubwa sana miongoni mwa jamii ya watu wa Ulaya. Kulikuwepo na tabaka la
mamwinyi, tabaka la viongozi wa dini na lile la makabwela. Kisha tabaka la mabwanyenye
likaibuka na kujenga utajiri wake kwa gharama ya walalahoi. Mamwinyi (Malodi) na viongozi wa
dini walikuwa wakipendelewa sana kwa kuwa katika mavazi maalum, kipato cha hali ya juu na
kutolipa kodi. Walikuwa na mamlaka juu ya watu wengine pamoja na haki ya kupata asilimia
162
fulani ya kodi yote. Matabaka haya mawili yalikuwa yenye kurithiwa. Baadaye mapinduzi ya
Ufaransa, kwa dhahiri yaliondoa mfumo wa matabaka na kinadharia yakatangaza misingi ya uhuru,
undugu na usawa.
Katika zama za sasa, tabaka la kibepari limeibuka katika Ulaya na magharibi. Tabaka hili ndilo
linalomiliki mtaji, nguvu na kuhodhi madaraka. Katika nchi ya Uingereza, Bunge la Malodi bado
linafurahia upendeleo wake lililourithi. Sheria ya Kikabaila ilikuwa ikiwanyima watoto wa mtu haki
ya kurithi huku ikimrithisha mtoto mkubwa wa kiume peke yake, ili kwamba mali ile isigawanyike
huku na kule, na hiyvo kuendelea kutunza na kuhifadhi uwepo wake. Mchakato huu bado
unatekelezwa siku hizi kwa gharama ya warithi wengine wote.
Kimsingi, mfumo wa kikabaila unakubali kwamba tabaka linalomiliki pesa ndilo linalokuwa na
madaraka ya kiserikali, kwa sababu ndilo linaloendesha vyombo vya utungaji sheria kwa maslahi
yake moja kwa moja, au kwa namna isiyo ya moja kwa moja kwa malengo ya kujilinda na
kuwadhibiti watu wa kawaida kwa njia ya kuwanyima haki zao na hali kadhalika kwa kuwawekea
mzigo mkubwa wa kodi na ushuru.
Hili linatukumbusha mfumo wa kikabaila uliokuwa ukitekelezwa katika nchi za India, Ugiriki,
Roma na Iran ambapo matabaka ya watu wa hali ya chini yalinyimwa haki na heshima yao pamoja
na kubebeshwa mzigo wa majukumu. Matabaka ya juu yalirithi heshima na mali, lakini watu
wengine walirithi fedheha, umasikini na utumwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Katika Uislam hakujawahi kuwepo na mfumo wa kitabaka. Ubwana na Ulodi havirithiwi. Tukio la
kijana wa Kimisri na mtoto wa gavana wa Misri, Amr Ibn Al-As, ambalo limekwishasimuliwa
katika hiki kitabu, ni uthibitisho mzuri kwamba watu wote wako sawa mbele ya Uislam. Khalifa
wa pili Omar alisema: “Kwa nini unawatia utumwani watu ambao mama zao wamewazaa kama
watu huru?” Kwa hiyo watu wote wako huru na hakuna tofauti yoyote baina yao isipokuwa kwa
uchaji na unyoofu wao.
Katika Uislam utajiri na mali za urithi hugawanywa miongoni mwa warithi wote bila ubaguzi
wowote wala ucheleweshaji. Baada ya mmiliki wake kufariki dunia, mali hiyo haiachwi
ikalundikana na kujikusanya bali hugawanywa. Tajiri wa leo anaweza kuwa maskini wa kesho na
maskini wa leo anaweza kuwa tajiri wa kesho. Qur‟an Tukufu inasema: “Ili isiwe inayorudia
baina ya matajiri wenu tu” (5)
. Kwa hiyo hakuna mipaka ya vizuizi bandia vinavyoruhusiwa
kuwepo baina ya tajiri na masikini.
Sayansi ya sheria ya Kiislam (Fiqhi) sio ukiritimba wa tabaka moja, bali ni sheria ya Mungu
iliyowekwa kwa ajili ya furaha ya watu wote bila ubaguzi, chuki, dhulma au unyonyaji wa nguvu za
watu wengine.
Mfumo wa ukabaila unasimama wapi katika Uislam na kitu gani kilichoundeleza? Na sasa aya ya
Qur‟an iliyonukuliwa na mwendesha mashtaka ikisema: “Tumewainua baadhi yao daraja
163
kubwa juu ya wengine, ili baadhi yao wawafanye wengine kuwa watumishi” (6)
, Aya hii ina
maana kwamba duniani kote watu wako tofauti katika daraja na kipato. Wote tunajua vema
kwamba mtu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii tangu akiwa katika umri wa mapema ili aweze kuwa
na kipato kizuri.
Wale wanaokimbilia kwenye uvivu na uzembe bila shaka watakuwa chini ya watu wengine katika
daraja na mali. Mtu wa kawaida kuwa mwajiriwa na mwingine kuwa mhandisi, sio suala la bahati
nasibu au sadfa. Aya zifuatazo za Qur‟an zinathibitisha hoja yetu:
“Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu na walipewa elimu daraja za
juu” (7)
. “Na wote wana vyeo sawa na yale waliyoyatenda, na Mola wako si mwenye
kughafilika na yale wanayoyatenda” (8)
.
Na wote wana madaraja kwa yale waliyoyatenda na ili Mwenyezi Mungu awalipe malipo ya
vitendo vyao, nao hawatadhulumiwa” (9)
.
Neno “mtumishi” lililonukuliwa hapo juu halihusishi uduni na udhalili, wala tabaka moja kujiweka
juu ya wengine kwa majivuno na ushaufu. Kila mtu ni mtumishi wa mwenzake kwa namna moja
au nyingine na hivyo gurudumu la maisha ndivyo linavyozunguuka. Wasionacho hufanya kazi kwa
wenye nacho, kibarua kumfanyia kazi mhandisi na mmiliki wa kiwanda. Mhandisi kumfanyia kazi
kibarua na mmiliki wa kiwanda pia, ambaye naye humfanyia kazi mhandisi na kibarua pia.
Maisha ya juu ya mgongo wa ardhi yanawezekana tu kutokana na tofauti zetu za vipawa, uwezo,
utendaji na nyenzo za maisha. Hivyo, chini ya mfumo wowote tunawezaje kuifanya mishahara ya
askari kuwa sawa na ile ya ofisa au mishahara ya mhandisi kuwa sawa na ile ya kibarua? Kwa
hivyo, hiyo ndio kanuni ya maisha. Kila mtu humfanyia kazi mwenzake lakini bila kuwepo
mitazamo ya udhalilishaji na uduni bali kwa namna ya kuthaminiana. Kwa ufupi hii ndiyo maana
ya utumishi inayokusudiwa na Uislam.
Swali la nne:
Hakimu: Ni upi msimamo wa Uislam kuhusu mfumo wa Kikabaila?
Uislam: Ukabaila ni mfumo ambao mzalishaji wa moja kwa moja anakuwa
na wajibu fulani kwa bwana wake au mmiliki wa eneo husika. Mahitajio haya ya kiuchumi yapo
katika namna mbalimbali kama vile kumtumikia au kulipa pesa taslimu au bidhaa yenye thamani ya
mali.
Katika mfumo wa Kikabaila/Kimwinyi kuna matabaka mawili: Tabaka moja ni lile la wamiliki wa
ardhi, na tabaka la pili linajumuisha wakulima, wapangaji wa mashamba na ardhi na watumwa wa
mashambani ambao walitumikishwa kufanya kazi za mashambani. Bwana mkubwa wa Kikabaila
ndiye anayetawala na kuyadhibiti maisha yao ya kijamii na kisiasa.
164
Wakulima hufanya kazi kwa kulazimishwa au kutumikishwa bila kuwajali na kwenda kinyume na
maslahi yao. Zaidi ya hayo ulazima wa kulipa kiasi fulani cha kodi kama ishara ya utiifu na
kujisalimisha mbele ya bwana mkubwa.
Msheshimiwa Hakimu! Kwa lengo la kufupisha mjadala huu tunaweza kuitaja misingi ya ukabaila
ili tuilinganishe na kile kilichotokea katika jamii ya Kiislam.
1. Utumishi wa kudumu kwa mfalme wa Kikabaila.
2. Mizigo ya lazima waliyopewa wakulima kutoka kwa mwenye ardhi, ambayo ni:
(a) Kazi za lazima zisizokuwa na malipo yoyote kwenye shamba la mkabaila siku moja kwa wiki.
(b) Kazi za lazima zisizokuwa na malipo wakati wa sikukuu na siku za matamasha.
(c) Kumpa mfalme zawadi mbalimbali katika siku za sherehe na sikukuu.
(d) Kulazimishwa kupeleka nafaka zao kwenye kiwanda cha mkabaila.
3. Lodi (Mfalme) ndiye anayeamua apendavyo na kuteua eneo la ardhi ambalo hupewa mtwana,
kazi zinazotakiwa pamoja na kodi.
4. Kutokana na kutokuwepo kwa sheria ya umma/kiraia, mfalme huyo hutoa hukumu na maamuzi
kutokana na atakavyo na aonavyo yeye.
5. Wakulima walilazimishwa kupata uhuru wao kwa kulipa pesa pindi mfumo wa Kikabaila
ulipokuwa ukielekea kuanguka.
Hii ndiyo hali ya mambo katika mfumo wa Kikabaila. Kwa upande mwingine katika Uislam kila
kitu kipo tofauti kabisa:
1. Ukandamizaji wa kuendelea ni kitu ambacho hakipo kabisa katika Uislam, nje ya hali ya utumwa
ambao tayari tumekwisha uelezea kwa mapana na kubainisha jinsi ya kujikomboa dhidi yake.
Mipaka huwekwa na Mwenyezi Mungu pekee.
Katika mtazamo wa kiuchumi, Uislam haujengi mfumo wake wa uchumi kwenye msingi ya mtu
mmoja kumtisha mtu mwingine, isipokuwa katika hali ya utumwa tuliouelezea na ambao kilikuwa
ni kitu kisichoepukika wakati wa enzi za zamani. Kiroho na kiuchumi, Uislam umepiga marufuku
Ukabaila na kuwaokoa binadamu kabla hawajatumbukia katika shimo la utumwa na kutumikishwa.
2. Ama kuhusu mizigo ambayo wenye ardhi waliwabebesha wakulima, Historia ya Kiislam
haikuwahi kukabiliwa na kadhia hiyo. Katika Uislam uhusiano pekee kati ya mkulima na mmiliki
wa shamba/ardhi ni ule wa kukodishiana au ukulima wa kushirikiana kwa maana kwamba mkulima
165
kulingana na uwezo wake, hukodi ardhi kutoka kwa mwenye ardhi husika ambapo ana uhuru wote
wa kulilima shamba kwa gharama zake mwenyewe na hivyo kuvuna mazao yote yeye mwenyewe.
Au anaweza kushirikiana na mwenye ardhi katika mchakato wa kilimo, ambapo mmiliki huyo
hugharamia mambo yote na mkulima akashughulikia kazi za mikono, na mwisho wa mavuno wote
wawili wakagawa faida baina yao.
Katika hali zote mbili hakuna wajibu wa kulazimishana au kufanya kazi isiyokuwa na malipo au
kazi yoyote ya bure ambayo mkulima analazimika kumfanyia mwenye shamba. Bali kuna
majukumu sawa kwa pande zote mbili juu ya misingi ya uhuru, haki na uwajibikaji. Mkulima ana
uhuru wa kutofanya kazi kama haoni mapatano yenye faida. Mmiliki wa shamba hana mamlaka ya
kumlazimisha au kumshurutisha kufanya kazi iwapo mkulima atakubaliana kuhusu kilimo cha
kushirikana, bali majukumu yake yatakuwa sawa na yale ya mwenye shamba na yatatekelezwa na
wote, na fungu lake ni sawa na lile la mwenye shamba.
Ama kuhusu misaada na zawadi, mmiliki wa ardhi ndiye anayetakiwa kumpa mkulima, kwa sababu
maskini siye anayetakiwa kumpa zawadi tajiri kama „misaada‟ ya Ulaya inavyotaka.
Ama kuhusu vinu vya kusaga, imekuwa ni jambo la ada katika maeneo ya Uislam kwamba vinu
hivyo humilikiwa na watu maskini ambao maisha yao yanapata kuwa mazuri kwa kuvimiliki.
Mashine za kusaga hazikuwa zikimilikiwa na wamiliki wa mashamba ambao waliwalazimisha
wakulima kuleta nafaka zao kwenye vinu hivyo walivyovimiliki.
Katika Uislam hakuna kazi isiyolipiwa au ya bure: Kuna mahusiano yaliyojengwa kwenye misingi
ya kuheshimiana na usawa kamili katika utu wa binadamu. Wajibu wa malodi huko Ulaya wa
kuwalinda wakulima, ulilipwa kwa kazi hii ya bure na udhalilishaji wa kidhalimu, lakini matajiri
katika Uislam wamezoea kutoa huduma hizo kwa ajili ya watu maskini kwa hiari na kwa uhuru,
kwa sababu wanategemea kupata fidia ya kazi yao kutoka kwa Allah, kutokana na kutekeleza
wajibu wao wa kuwatumikia waja wake. Hiki ni kielelezo cha wazi kinachoutofautisha utawala
ambao misingi yake imejengwa kwenye mafundisho ya kidini na ule usiokuwa na dini na kanuni za
kiimani.
Uislam ulianzisha vita dhidi ya ukabaila kwa nguvu zote. Mwenyezi Mungu anasema: “Na
hakika tumewatukuza wanadamu”. Mtume Muhammad (S.A.W.) anasema: “Wanadamu
wote ni sawa kama safu za chanuo”. Omar alitangaza haki za binadamu pale aliposema:
“Wawezaje kuwatia Utumwani watu waliozaliwa huru?”
3. Kuhusu eneo la ardhi lililohodhiwa na lodi na hali kadhalika kazi walizobebeshwa wakulima,
mambo haya hayapo ndani ya Uislam ambao haukujenga misingi yake juu ya ubwana wa lodi na
utumwa wa mkulima. Ardhi anayokodi mkulima inategemea utashi wake huru na msimamo wake
wa kifedha; lakini katika mfumo wa kilimo cha pamoja eneo la ardhi husika linategemea nguvu na
uwezo wa kimwili wa mkulima na huduma inayohusika ni ile inayohitajika kwa ardhi/shamba
ambalo linamilikiwa kwa pamoja baina ya mkulima na mmiliki wa ardhi mpaka mazao
166
yanapovunwa. Eneo lililobaki la ardhi halihesabiwi na mkulima halazimiki kufanya kazi ndani
yake.
4. Mambo ya maamuzi na mamlaka ya kisheria yamekabidhiwa kwa Serikali Kuu yenye sheria ya
kawaida. Serikali ndiyo inayosimamia uendeshaji wa sheria na haki kwa kuwateua mahakimu na
gavana anayesimamia sheria ya Uislam. Hakuna yeyote mwenye mamlaka juu yao isipokuwa
wanapofanya makosa au uhalifu. Hivyo, mmiliki wa ardhi hana mamlaka yoyote ya kufunga na
kuzua sheria dhidi ya wakulima. Matakwa na kanuni za Allah kwa watu wote ndizo sheria pekee
zinazotakiwa kutumika juu ya wote kwa usawa, sio tu kati ya mkulima na mmliki wa ardhi, ambao
wote wawili ni watu huru, bali pia kati ya mtumwa na mmiliki wake, jambo lililokuwa la kipekee
ambalo Uislam ulilenga kulikomesha tangu mwanzo wa kudhihiri kwake na kwa bahati nzuri
lilikomesheka.
Hakuna shaka kuwa kuna matukio machache sana, ambapo ilitokea kwamba mahakimu walikosea
au kutoa maamuzi ya kimakosa yanayokwenda kinyume na sheria, kwa lengo la kuwaridhisha
wamiliki wa ardhi au watu wenye nguvu za kimamlaka: Kesi na matuko haya sio kanuni.
Tunapaswa kuyazingatia matukio makubwa yenye kukumbukwa, ambapo hakimu alikuwa akitoa
maamuzi yanayowapa haki watu masikini na wanyonge. Maamuzi haya, sio tu kwamba yalikuwa
kinyume na lodi au gavana au mmoja wapo wa mawaziri, bali pia kinyume na Khalifa mwenyewe
ambaye alifurahishwa na maamuzi hayo na wala hakumfanyia kisasi hakimu au kumfukuza kazi
kutokana na ukuu wa sheria uliopunguza nguvu za kila aina ya mamlaka.
5. Katika Uislam hapakuwepo na wakulima waliokimbia, kama ilivyotokea Ulaya, kwa sababu
wakulima walikuwa na uhuru sio tu wa kuhama kutoka shamba moja kwenda jingine bali pia
walikuwa na uhuru wa kuhama nchi moja kwenda nchi nyingine ya ulimwengu wa Kiislam.
Hakuna kitu kilichowazuia kuhama isipokuwa tamaa yao huru ya kuendelea kukaa katika eneno
fulani la ardhi/nchi.
Ama kuhusu wakulima kununua uhuru wao, bila shaka hakuna kitu kama hicho kilichotokea katika
ulimwengu wa Kiislam, kwa sababu walikuwa huru moja kwa moja na hivyo hawakuhitaji kutafuta
uhuru.
Aidha, ulimwengu wa Kiislam ulikuwa na kiwango kikubwa sana cha mali ndogo za mashamba,
ambayo wamiliki wake binafsi walikuwa ni wenye kujitosheleza pamoja na fursa zisizokuwa na
idadi zilizokuwepo kwa ajili ya watu kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ya biashara na uzalishaji
wa wakati huo. Jambo hili lilifuatia uwepo wa ukabaila wa kidhalimu uliopata kushamiri Ulaya
katika kipindi cha zama za kati, na ambao uliendeleza ujinga wa kijahilia na giza la kiroho hadi pale
eneo hilo la Ulaya lilipopata mawasiliano na ulimwengu wa Kiislam katika kipindi cha vita vya
msalaba au kupitia uwepo wa Hispania, ndipo Ulaya ikapona na kuweza kuamka kutoka katika giza
la usingizi na kuelekea kwenye mwamko na ustawi wa kielimu.
Hakimu: Lakini leo hii ukabaila umepata kuenea katika nchi za Kiislam.
167
Uislam: Hilo ni kweli, lilitokea katika kipindi cha mwisho cha utawala wa Ottoman baada ya
chemchem ya mafundisho ya haki na imani kukauka, na baada ya watawala waliokuwa Waislam
kwa majina tu kushika madaraka. Mazingira yaliharibika zaidi baada ya ubeberu kutoka Ulaya
uliposhika hatamu wakati walipofanya uvamizi, na hivyo uwajibikaji wa pamoja na ukarimu
vikatoweka au kuharibiwa, jambo lililotoa nafasi kwa matumizi ya matajiri wenye ubinafsi na
utumwa wa utiifu mbaya wa watu maskini. Hili halikusababishwa na Uislam na pia Uislam
hautakiwi kulaumiwa kwa jambo hili, unatakiwa kulaumiwa tu iwapo sheria yake inatekelezwa
kikamilifu na hali hiyo ikaendelea kuwepo.
Swali la Tano:
Hakimu: Vipi kuhusu ubepari, na je mnauruhusu?
Uislamu: Ubeberu haukuzaliwa na kukulia katika ulimwengu wa Kiislam. Uliingia baada ya
eneo hilo kudhoofishwa na uvamizi wa kimagharibi na kupelekea kuzama katika lindi la umaskini,
ujinga, maradhi na uduni wa ukosefu wa maendeleo. Hivyo, Uislam umekuwa ukieleweka
kimakosa kwa madai kwamba unapendelea ubeberu katika sheria na kanuni zake, kwa sababu ya
kuruhusu umiliki binafsi.
Inatosha kujibu kwa kutaja usemi wa kweli, ambao unajulikana vema kwa kila mwanafunzi wa
masuala ya uchimi, yaani, ubepari haudhihiri na kustawi bila ya riba na ukiritimba, ambavyo
Uislam ulivipiga marufuku karne kumi na nne kabla ya ubeberu haujazaliwa, lakini hatuna haja ya
kujibu kwa namna ya haraka. Ubepari ulidhihiri baada ya uvumbuzi wa mashine zilizopelekea
utajiri kujikusanya mikononi mwa mabepari huku vibarua wakizikosa au kuwa na uhaba wa
kuzipata. Kisha bepari aliwafanya vibarua wake wazalishe kiwango kikubwa cha bidhaa bila
kuwalipa mishahara ya kutosha ambayo ingewafanya waishi maisha mazuri. Hivyo, bepari huyo
alipata faida kubwa na kuishi maisha yenye kila aina ya anasa zenye kuchukiza.
Aidha, mishahara midogo ya vibarua huwazuia kutumia bidhaa zote za viwandani, kwa sababu
iwapo watapokea kiwango kinachotosheleza kutumia bidhaa zote au nyingi katika vikorokoro
vinavyozalishwa, faida za bepari huyo zitapungua, jambo ambalo halikubaliwi na ubepari kwa
sababu malengo yake ni faida na wala si ulaji.
Hivyo, bidhaa hujazana na kusongamana mwaka hadi mwaka na mataifa ya kibepari hutaka masoko
mapya na safi ili kuuza bidhaa zao, jambo linalopelekea kwenye ubeberu au ukoloni, na matokeo
yake hutokea na kuibuka migogoro na uhasama, upinzani au ushindani kwa lengo la kutafuta na
kudhibiti masoko na malighafi na hivyo kuishia katika mapambano na vita.
Kwa upande mwingine, kazi ya kudumu ya Uislam ni kuimarisha ustawi na kueneza maendeleo na
uadilifu katika uso wa ardhi, hivyo haumkwazi mtu binafsi kuwa na ustawi na maendeleo na wakati
huo huo Uislam hauyapuuzi masuala yanayowahusu watu binafsi. Huweka sheria na kanuni kwa
lengo la kudhibiti mahusiano yao na jamii na hivyo kukomesha unyonyaji wa kijinga, ambao ima
168
utatokana na dhamira ya kishetani ya bepari au itaibuka kutokana na asili ya ubepari wenyewe
kama ubepari.
Aidha, baadhi ya wanasheria wa madhehebu ya Maliki wanaona kwamba wafayakazi lazima
wagawane faida na mwenye mali. Wanaeleza kuwa tajiri atalazimika kutoa gharama zote na nguvu
kazi ya wafanyakazi itatosha kuwafanya wawe washirika katika faida. Hivyo, takriban mgao wao
wa faida unakuwa sawa sawa kwa kila upande. Hili linaonesha juhudi maridhawa ya Uislam katika
kutenda haki na usawa.
Ubepari umejengwa kwenye misingi ya mikopo, jambo lililopelekea kuibuka kwa mifumo ya
Kibenki, ambayo inathibiti na kutamalaki michakato mikubwa ya kibepari na kutoa mikopo ya
uwekezaji kwa kubadilishana na faida na riba. Benki hizi zimejengwa kwenye msingi wa riba,
ambao umepigwa marufu katika Uislam kwa namna ya moja kwa moja.
Makampuni madogo yalivunjwa au kuunganishwa na kuanzisha mashirika makubwa kwa lengo la
kufanya ukiritimba na kuhodhi, kitendo ambacho hakikubaliki ndani ya Uislam. Katika hadithi
moja Mtume Muhammad (S.A.W) anasema: “Mwenye kuhodhi na kufanya ukiritimba
ametenda dhambi”.
Kwa hiyo, ubepari (ungekuwa chini ya uangalizi wa Uislam) usingestawi na kwenda kwenye
mielekeo yake mibaya na ya kutisha na wakati huo huo ukisababisha dhulma, ukoloni, ubeberu na
vita. Ungestawi kwa namna gani? Je ungesimamishiwa kwenye bidhaa hafifu zilizokuwapo katika
kipindi cha mwanzoni mwa mwamko wa sayansi, au ungeendelezwa kuelekea kwenye mikondo
mingine iliyojaa mema na isiyokuwa na uovu wa kutisha?
Uislam unapinga vizuizi dhidi ya maendeleo ya viwanda: Uislam unapendelea uvumbuzi na
maendeleo. Ama kwa mwelekeo mwingine wa mageuzi na mabadiliko ya mahusiano katika
uzalishaji, tofauti na yale yaliyotokea Ulaya katika karne ya 19 na ya 20, zoezi hili lingeweza
kutekelezwa kwa kuunda kanuni na taratibu za kiuchumi kufuatana na sheria ya Kiislam kama
tulivyoona katika suala la kugawa faida nusu kwa nusu kwenye kadhia ya ujira na ajira. Kwa
kufanya hivyo Uislam ungekuwa umefuta maovu mawili kwa wakati mmoja: riba na ukiritimba,
uliopigwa marufuku na Uislam, na uonevu wa kidhalimu ambao unawakumba wafanyakazi ambao
ni waathirika wa ubepari unaonyonya nguvu za vibarua hao na kuwaacha wakiwa maskini na
dhalili, vitu ambavyo Uislam unapambana navyo.
Uislam, ambao uliweza kutatua tatizo la utumwa na kuzuia ukabaila mbele ya wanadamu wote,
vivyo hivyo ukiongozwa na msukumo wake wa dhati, uliziangusha nguzo za ubepari, riba,
ukiritimba, faida zilizozidi na ambazo sio za halali. Vile vile, uliwalinda wafanyakazi na kuwafanya
washiriki katika kupata faida.
Uislam haujaacha kutatua tatizo la kikundi cha watu kujilundikia mali na kuwaacha watu wengi
wakiishi katika taabu na umasikini, kwani jambo hilo linapingana na sheria yake iliyowazi
inayotaka utajiri na mali vigawanywe baina ya watu wote.
169
Katika aya ya 7 ya Surah Hashir Allah anasema: “Mali isiwe inayorudia baina ya matajiri wenu
tu”.
Zaidi ya hili ni kwamba, mfumo wenyewe wa sheria ya Kiislam unapiga marufuku chanzo cha
kujikusanyia mali ambapo sheria za mirathi huzigawanya mali na mirathi kwa kila kizazi. Mfumo
wa zaka, dhamana ya pamoja, marufuku ya kulimbikiza mali na ulaji wa riba, sifa njema ambayo
imekuwa stahili ya jamii ya Kiislam yote haya ni madhihirisho na kielelezo cha wazi cha usalama
wa pamoja wa jamii nzima.
Uislam haukujaa sheria na kanuni za uchumi pekee, bali pia unaweka nguvu kwenye uenezaji wa
maadili ya kiroho. Maadili haya ya kiroho hayatenganishwi hata kidogo na mfumo wa uchumi wa
Kiislam, kwani Uislam unahimiza juu ya uchanganyaji wa utakaso wa roho na taasisi ya uchumi
katika jamii.
Maagizo ya kiroho ya Uislam yanakataza na kupiga vita anasa yenye kuchukiza. Anasa ambazo,
kama ilivyokuwa kwa starehe za kimwili, zilistawi baada ya mali kulundikana mikononi mwa
kikundi cha watu wachache.
Vile vile, Uislam unapiga marufuku dhuluma na uonevu wowote dhidi ya wafanyakazi, uonevu
ambao unapelekea ukiritimba na mali kulundikana kwa mtu mmoja.
Uislam unawataka watu watoe mali zao kwa ajili ya Allah, kwani hatujui kwamba watu huendelea
kudidimia katika umasikini baada ya matajiri kujipendelea wao wenyewe tu? Sifa ya maadili ya
kiroho ni kiunganishi baina ya mwanadam na Mwenyezi Mungu kinachomshurutisha kujizuia dhidi
ya anasa na tamaa za kidunia kwa ajili ya kumridhisha Allah, na kwa lengo la kupata maisha
mbadala siku ya Kiyama. Je, mtu mwenye mafungamano imara na Allah anaweza kukimbilia
kwenye kujilundikia mali na utajiri?
Kazi ya maadili na maagizo ya kiroho ni kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa sheria ya kiuchumi
inaoufuta ubepari ili kwamba watu waweze kuzitii sheria zao kwa moyo na kwa hiari, sio kwa woga
na hofu.
Ubepari, ambao baadaye ulienea katika ulimwengu wa Kiislam, haukuzaliwa katika ulimwengu
huo, bali uliletwa kutoka nje na kusambazwa. Hivyo, Uislam haupaswi kulaumiwa kwa ujio wa
ubepari katika ulimwengu wa Kiislam, kwa sababu hilo linatokana na watu kutotii sheria za Kiislam
katika maisha yao pamoja na biashara/uchumi wao.
Swali la Sita:
Hakimu: Mwisho kabisa, je hukubaliani nami kwamba Uislam umesababisha ukosefu wa
maendeleo kwa Waislam kwa sababu umewashurutisha kuachana na maisha na kuzifanya akili zao
zisishughulike, jambo lililosababisha uzembe na kutoshughulikia maisha yao? Kama wangeachana
170
na dini ya Kiislam, wangepata maendeleo kwa sababu dini hiyo ndiyo chanzo cha wao kuwa na
hisia ya kutojali na ndio kikwazo cha wao kutopata maendeleo.
Uislam: Ewe Hakimu mwenye busara! Ninashangazwa kushtakiwa kwa tuhuma hizo, yaani
kwamba mimi ni kikwazo, chanzo cha uzembe na kuzifanya akili zisifanye kazi, na yote kwa yote
kuwashurutisha watu kuachana na kushughulikia maisha. Mimi ndiye niliyekuwa chagizo
lililowasukuma na kuwachochea Waarabu wa zamani kueneza ujumbe wa maisha mashariki na
magharibi. Nina uhakika kwamba sababu ya Waislam kudumaa inatokana na wao kuacha ujumbe
huo na kukimbilia kwenye kitu kingine.
Ndani ya Uislam kuna nguvu za uvumbuzi na juhudi, nguvu za utendaji na kuchapa kazi, lakini
Waislam walizitelekeza na kuzitupa na kukimbilia au kupendelea usingizi, ambao nimeukana na
kuupiga vita. Mahasimu na maadui zao wametumia mwanya wa ulegevu wa Waislam kuwaacha
walale katika usahaulifu mkubwa ili waweze kuitumia vema fursa ya kutokuwa na
mshindani/mpinzani.
Uislam unaikataa hali ya kujiamini kusikokuwa na umakini au uzembe baridi ambao umewanyima
Waislam aina zote za maisha imara. Qur‟an inaanza kutufundisha ushupavu na azma kabla ya
tawakali (kutegemea). Aya ya 159 ya Surah Al-Imran inasema: “Shauriana nao katika
mambo; na ukishakata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu
huwapenda wanaomtegemea”. Hivyo, kukata shauri, uthabiti na nguvu ya utashi ndio zana
dhahiri za utayari na kisha huja tawakali (tumaini) ambayo hukaa moyoni. Ama kuhusu utawa na
kujinyima mambo ya halali, Qur‟an Tukufu inawahimiza Waislam kufurahia mambo mazuri ya
kidunia na kupendelea maisha mazuri ya Akhera. Lakini wameupuuza huu ulimwengu na kuamini
kuwa ni ufahari wa kujivuna na ni mchezo kutojali uamuzi wa Allah katika kujishusha thamani kwa
mambo ya kidunia ili kwamba wasijitaabishe katika kuyahangaikia na kuyazembea maisha ya
baadaye.
Uislam unakataa hali ya mtu kujishughulisha katika ibada pekee, kuudhulumu na kuutaabisha
mwili. Tunao mfano bora kwa Mtume Muhammad (S.A.W): alikuwa akimuabudu sana Allah,
lakini hakuwa mzembe, aliendeleza mahubiri yake kwa nguvu zote na kusonga mbele katika
harakati za mapambano na maisha. Alikuwa akisema kuwa mtu anayeingia katika Uislam halafu
akapiga marufuku kuvaa nguo nzuri na kula chakula kizuri, basi mtu huyo haijui Aya ya 168 ya
Surah Al-Baqarah isemayo: “Enyi watu kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri” na aya
ya 87 ya Surah Maidah: “Enyi mlioamini msiharamishe vizuri alivyokuhalalishieni Mwenyezi
Mungu” na Aya ya 172 ya Surah Al-Baqarah: “Enyi mlio amini kuleni vizuri
tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Menyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu”.
Na aya ya 201 ya Surah ya Al-Baqarah: “Mola wetu mlezi tupe duniani mema na Akhera
mema, na utulinde na adhabu ya moto” na aya ya 77 ya Surah Al-Qasas: “Na utafute kwa
aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi ya Akhera wala usisahau fungu lako la dunia”
Hali ya kugeuka jiwe ni maradhi thabiti yanayotokana na uzembe wa Waislam. Uislam uliingia
kwa nguvu na kuizunguka dunia nzima, lakini sasa tunaona kuwa hauwezi kusimama au kuhimili
171
na kustahimili sana kwa kiasi kwamba Waislam ni kama wameuacha na dini sasa imegeuka kuwa
huduma za sala na utawa na wanapotakiwa au kuhimizwa kufanya harakati na kufanya kazi hujibu
kwa kusema: “Tuna kazi gani na hii dunia?”.
Japokuwa Uislam unahimiza sana sala na matendo ya kuabudu, lakini haushurutishi kufanya haya
tu, bali unawahimiza Waislam kufanya kazi na kuweka juhudi na bidii katika mambo mbali mbali.
Wale wanaopuuza kufanya kazi na wakawa wanajihusisha na ibada za kawaida kwa hoja ya kutaka
utawa na uchamungu, wanauweka Uislam katika hali ya uzembe na kuganda. Hatua yao ya kujitoa
katika maisha sio aina sahihi ya utawa na uchamungu wa kweli kama ule wa Abu Bakar, Omar na
masahaba wengine wa Mtume Muhammad (S.A.W.) waliopata kuutawala ulimwengu, lakini
wakawa hawajajiingiza ndani yake. Hawakuupa thamani umuhimu wake na wala haukuzifanya
nyoyo zao zighafilike hata kidogo. Walikuwa wachamungu wenye kuchapakazi na wenye uhai
katika matendo yao, hawakuwa wenye kulala na kuwa kama mawe; lakini hawa watawa wa leo
wameacha kuitii na kuiweka vitendoni Aya ya 105 ya Surah Tawbah isemayo: “Na sema:
Tendeni vitendo na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini wataviona vitendo vyenu
na mtarudhishwa kwa mwenye kujua siri na dhaahiri naye atakuambieni mliyokuwa
mkiyatenda”, na aya ya 11 ya Surah Mujaadalah: “Mwenyezi Mungu atawainua walioamini
miongoni mwenu na walio pewa elimu daraja za juu na Mwenyezi Mungu anazo khabari za
mnayoyatenda”.
Kuna aya nyingi sana zinazowataka Waislam watembee duniani na wajionee…
Hali hii ya uzembe na kulala imedumu kwa muda mrefu sana kutokana na kuwepo kwa aina tatu za
viongozi wa dini:
1. Tabaka la wale wanaoona kuwa dini ni maisha au uwanda unaohusika na roho na moyo tu, na
hivyo wakayapuuza mambo na shughuli nyingine za kimaisha na kufuata Usuffi ambao kwa hakika
sio Uislam wote bali ni sehemu tu ya moyo na roho, ambapo kuna vipengele vingine pia vya
maisha.
2. Tabaka lenye uhafidhina mkubwa na wenye fikra finyu. Hushikilia maana ya juu juu ya
maandiko ya kidini bila kuyasoma na kuyadurusu kwa undani na kwa kina. Hawajui kupendekeza
na kuweka mipango ya kidini katika zama hizi tulizo nazo: wanaketi kama mahakimu wakali
wanaotoa hukumu na maamuzi ya kukurupuka, wakisema kuwa mtu fulani ni muumini wa kweli,
na yule ni mkarimu na mwingine hana maadili au yule ni mshirikina au ni muasi wa dini au mhaini.
Aina hii ya utoaji hukumu ni hatari sana na hupelekea vijana wengi kuichukia dini na kuudhika
nayo.
Tabaka hili la viongozi wa kidini japokuwa ni waaminifu kwa dini yao, wanatakiwa kuwa na busara
na akili ya kuzaliwa nayo katika kuitangaza na kuieneza imani ya Kiislam. Mwanadini anatakiwa
kuwa mtu wa kiroho na kimwili na sio kuwa “hakimu.”
172
3. Tabaka la tatu linajumuisha wale ambao sio wazuri katika kujenga. Wanakosoa sana kwa namna
ya kuharibu na kubomoa yale yote yaliyojengwa na waboreshaji na wakombozi mbalimbali, iwe
kwa makusudi au kwa kutojua na kutokuwa na nia njema.
Ama kuhusu watu wa kawaida, tunaona kwamba wanapotea na hawawezi kuzielewa kanuni za
sheria za kidini au kuzitekeleza kama wasomi. Ni watu wachache tu ndio wanaofahamu kiasi
kidogo cha sheria ya dini, hivyo hatuwatarajii kuishi au kuzitekeleza ipasavyo.
Mojawapo ya sababu za msingi zilizopelekea kuwepo kwa hali hii ya kukakamaa katika ulimwengu
wa Kiislam ni shule za kimisionari za Kikristo zilizotia sumu katika itikadi zetu na kusingizia na
kuharibu sifa ya dini yetu. Waliwapotosha vijana wetu na kuwatisha kwa kudai kuwa Uislam
umepitwa na wakati na haufai kwa zama hizi. Hivyo, vijana wetu wanapohitimu masomo yao
hugeuka kuwa wanapropaganda wabaya dhidi ya Uislam na kuwa na chuki na uhasama dhidi ya
imani na dini yao wenyewe.
Siku moja kijana mmoja aliniuliza: “Tutawezaje kuondokana na hali ya kutuama na uduni ambao
umeuvamia umma wetu kwa muda mrefu?
Nilimuuliza kama alikuwa na fikra gani?
Akajibu kwa huzuni kubwa: “Ni muhimu kwamba kizazi hiki kitoweke na baada yake kizazi kipya
kizaliwe”
Nikamuuliza: “Hali yako ya kukata tamaa na kutotegemea mazuri ni ya nini? Je Umma wetu hauna
vipengele vya mambo ya msingi vinavyotutaka tufanye kazi, tufanye utafiti wa kisayansi, umoja na
maarifa?”
Nikasema: “Je, Umma wetu haukushika nafasi za juu katika uwanda wa elimu katika zama za
Khalifa Al-Rasheed na Al-Maamun?”
Nilimuuliza iwapo hakutaka kuwa na nafasi kubwa ya maendeleo kama wao. Akajibu: “Ndiyo
tunapenda kufanya tafiti mbalimbali, maendeleo, kuungana, na kuwa wavumbuzi”.
Nikauliza: “Waarabu walikuwa na nafasi gani ya maendeleo ya ustaarabu kabla ya kuja kwa
Uislam? Je, walifanya tafiti au maendeleo yoyote katika elimu au ustaarabu?” Akajibu kwa
kukataa.
Nikamuuliza: “Nguvu gani iliyowafanya watafiti, wawe wanafikra, watafsiri vitabu vya elimu na
taaluma mbalimbali na kuanzisha vituo vya mafunzo/elimu na maktaba nyingi?” Akasita kidogo
kisha akajibu: “Uislam”.
Nikamwambia: “Kama tukiurejea na kuugeukia Uislam ipasavyo tutapata umoja, ustaarabu na
maendeleo ya kiakili na kisayansi, halikadhalika tutapata upendo na mapatano yanayofaa”
173
Kama tunataka umoja, basi Uislam ndio dini ya umoja na umma mmoja. Aya ya 92 ya Surah Al-
Anbiyaa inasema: “Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu,
Kwa hiyo niabuduni Mimi” na Aya ya 52 ya Surah Al-Muuminun inasomeka: “Na kwa yakini
huu umma wenu ni umma mmoja na Mimi ni Mola wenu basi nicheni Mimi”.
Kama tunataka kuwa na maendeleo katika elimu ni lazima tuzifikirie na kuzitilia maanani zile aya
kumi zinazojumuisha na kuhusisha amri ya wazi inayowataka watu kusoma na kupata maarifa,
taamuli na tafakari za kiakili na kuwahimiza kuutafakari sana ulimwengu na vilivyomo ndani yake,
kutafakari uumbaji wa binadam na maisha yake kama tulivyokwisha eleza hapo awali kuhusu
msimamo wa Uislam juu ya kufanya kazi na ambapo tulihitimisha kwa kanuni ya utamaduni wa
Kiislam kwa kauli na fundisho lake lifuatalo: “Fanya majaribio kwa vitendo au jitahidi sana
fanya bidii kwa ujuzi na busara na chungua, utakuwa msomi”
Mlango na njia hii ya kisayansi ni tofauti kabisa na ada na utamaduni wa watu wa Ulaya
uliokuwapo baada ya karne ya kumi A.D. Kanuni iliyokuwa imeenea kwao ni: “Soma vitabu na
urudierudie (kama kasuku) kile kinachotajwa na maprofesa, nawe utakuwa msomi”
Hakuna shaka kwamba hali ya Waislam kuyatii na kuyafuata maamrisho ya Qur‟an ndio iliyokuwa
nguvu na kichocheo kilichowapa nafasi ya mbele katika ustawi wa elimu. Waliandika na kubuni
maeneo mbalimbali ya maarifa, wakayapangilia katika mpangilio sahihi na kuyasanifu vema. Kisha
walifanya nyongeza kwenye maeneo ya awali wakaleta vitu vipya na kuvumbua vyombo vipya.
Kila mtu bado anakumbuka vema kwamba Albert aliandika kuhusu Avicenna na Thomas Aquinas
kuhusu falsafa ya Averroes; wote Albert na Thomas walikuwa chini ya viwango vya wasomi wa
Kiislam kama alivyotathmini mwanafalsafa wa Kifaransa Bwana Renan.
Hakuna awezae kukanusha kuwa utaalam wa dawa na utabibu, elimu ya nyota, fizikia na sosholojia,
vilivyopo huko Ulaya, vilitokana na vyanzo vya kweli vya Kiislam ambavyo msingi wake
unatokana na uelewa wa kweli wa Uislam.
Hivyo, tunathibitisha kuwa Uislam haujawahi kuwa dini ya kusali tu au dini ya utawa au maisha ya
kujinyima pekee au kuwa njia ya ulegevu, utepetevu na unyongevu, bali ni dini ya mapinduzi ya
kudumu, dini ya kuzaliwa upya na maendeleo katika fani zote za elimu.
Mheshimiwa Hakimi! Yumkini ukashangaa kuwa dini hii itawezaje kubadilisha hali iliyopo sasa
katika jamii ya Kiislam na wapi kilipo kiunganishi baina ya Uislam na Waislam. Jibu ni sawa na
kile tulichokielezea katika mijadala yetu ya awali, yaani tunahitaji sana kundi la wasomi wanaojua
maana ya Uislam na mafundisho yake. Kila mmoja wao lazima awe na ujuzi wa falsafa na utawa
wa moyo, yaani awe na mchanganyiko wa ustadi/akili nyingi na moyo uliotakaswa.
Tunabaki kuwa na haja ya mwanachuo ambaye, kwa kutumia akili na busara zake, anaweza
kuingiza hekima katika mawazo, fikara na matendo ya watu. Mwanachuoni, ambaye kwa kutumia
usafi wake wa moyo, anaweza kuzitakasa na kuzisafisha nyoyo na roho za watu.
174
Tunawatarajia wasomi wa aina hiyo kwani wanaujua msingi wa Uislam, mazingira ya kweli ya
zama hizi na wanaelewa hekima ya Uislam inayoweza kutumika katika mambo mapya ya zama
hizi. Nina imani kuwa ulimwengu wa Kiislam hauwezi kuwakosa watu hao, lakini Mustashriiqiina
wametushawishi kutowatambua wasomi kama hao na hivyo kutoshirikiana nao na kutilia shaka kile
wanachosema au kukifanya.
Pindi tutakapoondokana na hisia za uduni zilizopandikizwa kwetu na hao Mustashriqiina na
tutakipata “kiunganishi kilichopotea” baina ya Uislam na Waislam na hapo nuru ya Mungu
itaangaza na kumulika katika njia ya furaha ya watu wote. Aya ya 4 na 5 za Surah Ruum
zinasema: “Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla na baadaye, na siku hiyo waumini
watafurahia kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, Mwenye kurehemu”.
Punde tu Uislam ulipokuwa ukinukuu aya hizo Mwendesha Mashtaka akaingilia kati na
kumwambia hakimu, huku akimuashiria mshtakiwa kwa kutumia kijiti kilichokuwa mkononi
mwake na kusema: “Mheshimiwa Hakimu! Katika ncha ya kijiti hiki kuna mhalifu ambaye
ameutikisa ulimwengu na kuupa matatizo; ni bahati nzuri kwamba binadam amemtia hatiani.”
Hakimu aliinamisha kichwa chake akijaribu kuyakumbuka maamuzi na hukumu zake alizozitoa
katika vikao kumi na sita vya mahakama yake katika hii kesi. Kisha alimtazama Mwendesha
Mashtaka na kumwambia: “Ndiyo, kweli katika ncha ya kijiti hicho kuna mhalifu anayetakiwa
kutiwa hatiani, lakini ncha hiyo ni hiyo iliyopo katika mkono wako”.
Rejea: 1. Qur‟an - {11:3}
2. Qur‟an - {6:148}
3. “The General History of the Arabs” cha L. A. Sidio.
4. Qur‟an - {43:32}
5. Qur‟an - {59:7}
6. Qur‟an - {43:32}
7. Qur‟an - {58:11}
8. Qur‟an - {6:132}
9. Qur‟an - {46:19}
175
RUSHDI NA AYA ZA KISHETANI
Baina ya Ngano ya Kihistoria yaliyozushwa na Ukweli wa Kisayansi
uliothibitishwa
Imekwishafahamika vema kwamba harakati za umisionari zinajirudiarudia mwanzoni mwa kila
kizazi: kazi-mkakati wa zamani na hata sasa imesimamia kwenye kuupiga vita Uislam kwa kuunda
madai ya uongo na tuhuma dhidi ya Uislam, Mtume Muhamma (S.A.W.) pamoja na mamlaka za
Kiislam. Zaidi ya hapo ni kwamba kampeni hii inalenga kuwapotosha Wakristo kuhusu Uislam
ili kuwazuia wasiuelewe ukweli wake na kusilimu. Wamisionari hao wanafanya bidii kubwa kwa
lengo la kuwabadilisha Waislam wapate kuingia katika Ukristo kwa kuwatumia Mustashriqiina
(orientalists).
Mkuu wa umoja wa Waislam wa Uingereza bwana Lord Headley(1)
anasema: “Hakika inasikitisha
kuwaona wamisionari na viongozi wengi wa Kikristo wakiielezea dini yetu nzuri kwa wengine
katika namna mbaya. Mara nyingi katika majadialiano niliambiwa kuwa tunamuabudu
Muhammad, kwamba tunaoa wanawake wanne au kwamba tunaamini kuwa wanawake hawana
roho na kwamba hawaruhusiwi kuingia Misikitini. Ninafikiri maelezo haya yalitamkwa kwa nia
njema, lakini kwa uwazi kabisa, yanaashiria propaganda za upotoshaji na kueneza madai ya uongo.
Ni jambo la unyonge na uduni mkubwa kujaribu, kwa makusudi kabisa, kutangaza imani za dini ya
mtu kwa kuzusha uongo dhidi ya dini ya watu wengine” (2)
.
Mwanzoni mwa karne ya sasa, Kanisa la Anglikana lilifanya propaganda kwa ajili ya kitabu
kilichoandikwa na Bi. Lora Supridge kiitwacho “The Woman, her dreams and Message”.
Katika dibaji ya kitabu hiki Askofu wa mji wa London anakisifia kuwa ni kitabu kizuri na kuusia
kisomwe na Wakristo wote pamoja na viongozi wa Kanisa. Lora katika kitabu chake anasema:
“Tazama hili tishio zito na onyo la kutia hofu! Hilali ya Mtume inazunguuka juu ya wanadam
million 222 (3)
. Hilali hiyo inajitahidi kwa nguvu kuyatawala mataifa dhidi ya msalaba wa Kristo.
Hilali hii, inayofanana na upanga wenye kombo, inawakilisha moyo wa kimataifa uliowalazimisha
watu kujiunga na dini yake kwa kitisho cha upanga, dini inayokuza mambo na tamaa za kimwili” (4)
.
Bila shaka kitabu hiki kimejaa uongo, uzushi na chuki dhidi ya Uislam na Mtume wake. Ni
masikitiko kusema kuwa sio kwamba, ujinga tu ndio ulioyafunika macho ya watu wa Ulaya na
kuwazuia wasiione “nuru” ya Muhammad (S.A.W), bali pia nyoyo zao zimetiwa kifuniko kizito
kwa sababu ya matendo, uongo unaozushwa, ukweli unapotoshwa na hakika inayofichwa.
Kila alipojitokeza mwandishi mwadilifu huko Ulaya, ambaye hakuogopa lawama yoyote katika
kutetea haki, waandishi wa kulipwa wakitumiwa na tawala za kikoloni walifanya haraka sana na
kumlaumu au kumtia ila. Mfano wa hilo ni mwanahistoria wa Kiingereza Gibbon (5)
, ambaye
176
alihukumiwa kama mpagani kwa sababu ya kitendo chake cha kumsifu Muhammad (S.A.W.) na
kuelezea, kwa haki kabisa, juu ya mazingira halisi waliyokuwa nayo Wakristo na Ukristo katika
zama za Muhammad (S.A.W.), katika namna ambayo haikuwaridhisha wakoloni hao.
Baadaye Carlyle alipoliinua pazia la ujumbe wa kweli wa Muhammad (S.A.W.) na kuufanya
Uislam uwe wazi machoni mwa watu wa magharibi, makelele ya hasira yalipigwa kwa ukali dhidi
yake. Naye mkuu wa Chuo Kikuu cha Edinburgh (6)
alilazimika kukutwa na hali kama hiyo licha ya
nguvu kubwa aliyokuwa nayo na hivyo kuinyanyua sauti ya masifio yake hapo baadaye, hata hivyo
jambo hilo lilipelekea macho yenye upofu na masikio yasiyosikia kufunguka.
Baada ya kitabu cha Carlyle kiitwacho “The Heroes” vilikuja vitabu vya Higgins wa Devonbert na
Bosworch Smith wa Uingereza, Girhil na Grimens wa ujerumani na kisha Kaetani wa Italia. Vitabu
hivi viliwafanya wasomi wa kimagharibi waamini kuwa hoja zenye kukaririwa kaririwa na
waandishi wa Kikristo zilikuwa zimeshindwa na kuanguka. Kwa ufupi, mtazamo wa watu wa
magharibi kuhusu Muhammad (S.A.W.) umebadilika, sasa hachukuliwi kuwa ni mdanganyi bali
sasa anachukuliwa kama mwanamageuzi mkubwa. Hatuhumiwi tena kuwa alikuwa akisumbuliwa
na maradhi ya kushindwa kujizuia kama vile kifafa, bali sasa machoni mwao ametwaa sifa ya
utulivu na azma imara. Na sasa hahesabiwi kuwa mfalme jeuri anayesukumwa na raghba za nafsi
yake, bali anaonekana kuwa kiongozi mwenye maono ambaye huwajaza raia wake upendo na
huruma tele. Hachukuliwi tena kuwa mtaka maslahi binafsi, bali sasa anaonekana kuwa Mtume
mwenye maadili na sifa imara ambazo hakuwahi kuzitupa au kuzipoteza. Wamagharibi sasa
wamezitambua kikamilifu sifa hizi (7)
.
Hata hivyo, utambuzi huu haujaleta usumbufu kwa mahasimu wa Uislam kwani yote yanayohusu
huo utumbuzi yamewekwa ndani ya vitabu na ni wasomi wachache sana wanausoma, lakini pindi
Wakristo wanaoheshimika wanapousadiki Uislam na kuamua kusilim ndipo watu wa magharibi
hujishughulisha sana kuusoma Uislam na kuona faida zake, jambo ambalo lilipelekea kuibuka kwa
chuki na uhasama wa waandishi waovu na ghasia zao. Pindi kitabu cha Salman Rushdi (Satanic
Verses) kilipochapishwa kwa gharama kubwa kutoka magharibi na katika mazingira ya ukosefu wa
chaguo lenye ustaarabu mbadala ili kukaa mahali pa maadili yake yaliyokuwa yakiporomoka na
pindi wanamageuzi kadhaa walipotamani kuingia katika Uislam baada ya kugundua kuwa ndio
mkombozi wa pekee wa mwanadam, suluhisho la tatizo lao lililowakabili likawa ni kuupotosha
utukufu wa chaguo hilo mbadala lenye kuhitajika sana na la thamani kubwa, yaani Uislam.
Vyombo vya habari vya magharibi, vilitumia muda mwingi kupita kiasi, vikitoa wasifu na sifa za
kitabu hicho bila hata ya kuchunguza kwa makini au kuyachambua yale yaliyomo katika kitabu
hicho au hata kuvipitia vichwa vyake vya habari.
Gazeti la “Sunday Times” la mjini London liliandika kwamba kitabu hicho ni kazi bora
iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa na yenye mvuto zaidi kuliko kitabu chochote kilichowahi
kuchapishwa (8)
.
177
Magharibi bado inatangaza uovu duniani kote bila kukoma. Tatizo hili la kijinga ni kubwa zaidi ya
Salman Rushdi na kitabu chake na vile vile ni kubwa zaidi ya kile kinachoitwa “uhuru wa
kujieleleza au kutoa maoni”, ambao Uislam haupingani nao hata kidogo. Uislam unaunga mkono
na kulitetea hili la uhuru wa kujieleza kwa moyo mmoja. Uislam unakubali uhuru wa mtu kusema
kile anachokiamini “Hakuna kulazimishana katika dini”. Kwa kweli, Salman Rushdi hakueleza
au kutoa mtazamo uliosahihi juu yetu. Kitu pekee alichofanya ni kumshambulia Muhammad
(S.A.W.) kwa namna ya matusi na ufidhuli. Maelezo yake marefu kuhusu Uislam na Qur‟an ni ya
dharau. Hatupingani au kuzuia uhuru wa kufikiri au kujieleza, lakini tunapingana na shari dhidi ya
alama zetu takatifu. Ingekuwa kazi rahisi kukanusha hoja za kitabu hicho kama zingekuwapo au
kama kitabu hicho kingekuwa na hoja yoyote. Kuna tofauti kubwa kati ya fikra zinazotolewa katika
namna ya uthibitisho wa kisayansi na kati ya maelezo machafu na kashfa zinazotamkwa kiuzushi.
Kamwe hatupingani na magharibi kuhusu uhuru wa kufikiri, bali hitilafu ipo katika utetezi wa kweli
wa uhuru wa mawazo, kwani magharibi haiamini moja kwa moja katika hilo kwa sababu za
kiusalama: Bi. Thacher binafsi aliingilia kati kuzuia uchapishaji wa kitabu kiitwacho “Spy Catch”
kilichoandikwa na Peter Right, kwa maelezo au kwa kisingizio cha mambo ya lazima kiusalama!
Ulimwengu unaomuunga mkono Salman Rushdi na kitabu chake unawakilisha chuki na inda za
kimagharibi dhidi ya Uislam. Wameubadilisha uhuru wa kufikiri na kuwa uhuru wa shutuma na
matusi. Kuna tofauti kubwa baina ya uhuru wa kujieleza na kuamini kwa upande mmoja, na haki
ya kusingizia na kukashifu. Lini matusi na kutumia maneno ya kifedhuli, kwa lengo la
kuyashambulia mambo matukufu ya Kiislam, ikawa ni alama ya mazungumzo na uhuru wa
kufikiri?
Nukuu zifuatazo kutoka katika kitabu hicho cha “Satanic Verses” zinaonesha kuwa Salman Rushdi
alikuwa mbali mno na ukweli wa kisayansi uliothibitishwa. Aidha nukuu hizo ni uthibitisho wa
dhahiri wa nia yake mbaya na kielelezo cha uovu wake, halikadhalika ni maandiko ya ajabu
yaliyokusudiwa kutumikia malengo yaliyopangwa mapema na kwa kipindi cha muda maalum.
Anampa Muhammad (S.A.W.) jina la “Mahound” (9)
lenye maana ya Mtume bandia, roho muovu
na shetani. Neno “Hound” lina maana ya “Mbwa mwindaji”. Kwenye ukurasa wa 95 Rushdi anadai
kwamba Nabii Ibrahim (A.S.) alikuwa mwanaharamu. Anaeleza kuwa sahaba mmoja wa Mtume
(S.A.W.) aitwaye Khalid ni jitu la dubwana. Anadai kuwa Salman Al-Farissy alikuwa na mkia
mkubwa na kwamba alikuwa mlevi. Bilal anadaiwa kuwa alikuwa mtu wa tatu katika watu duni
sana (uk. 101).
Katika ukurasa wa 363, Rushdi anayaelezea maadili ya Uislam na kuyaita kuwa yaliyolaaniwa,
maadili hayo ambayo humuelekeza mtu hata namna ya kuihifadhi na kuisitiri tupu yake, ni mkono
upi anaotakiwa kuutumia katika kustanji, na hata namna ya kulala na mkewe, hayo yote ameyataja
kuwa yaliyolaaniwa. Kisha kwa namna ya dharau anasema: “Mungu ndiye anaweka mipango na
Muhammad mfanyabiashara aliyelaaniwa ameifunga mikono yetu kwa sheria na amri nyingi mno”.
Kwenye ukurasa wa 364 anasema: “Muhammad hataki mtu yeyote amjibu. Anapelekea Salman Al-
Farissy aseme pindi anapolewa: “Muhammad sio malaika na wanawake wamemfanya awe na
nywele za kijivu”
178
Katika ukurasa wa 366, Rushdi anasema: “Katika vita vya Handaki (10)
Waislam wengi walikufa
ambapo mtu mmoja aliweza kuoa hata wajane wanne, jambo ambalo lilimchukiza Salman Al-
Farissy na kuamua kumtelekeza Mtume na kuiasi dini. Alijipeleka mbele ya Mungu Baal, ambaye
alimuuliza juu ya kilichomtokea baada ya kuwa mmoja wa marafiki wa karibu wa Muhammad.
Salman akajibu kuwa, kadiri nilivyomkaribia mwanamazingaombwe huyo (yaani Muhammad),
ndivyo nilivyozidi kuujua ulaghai na ujanja wake.
Kwenye ukurasa wa 364, Rushdi anadai kwamba Uislam unaruhusu na kuhalalisha ulawiti, madai
ambayo ni ya uongo. Ni njama zinazochekesha na nyepesi kusoma katika ukurasa huo huo wa 364,
kwamba Malaika Jibril alimwambia Muhammad: “Haiwezekani kutembea juu ya mwezi bila shaka
ya aina yoyote”
Kitabu hicho kinaitwa “Satanic Verses” (yaani, Aya za Kishetani), kwa sababu katika ukurasa wa
113 Rushdi anadai kwamba Muhammad anatoa sauti kubwa ya ukali kwa “kuapa kwa nyota”,
maandiko yanayoanza kusema: “Naapa kwa nyota inapoanguka”. Ingawa anatia maneno ya ziada
wakati wa kuzitafsiri aya hizo, Rushdi anadai kuwa Mtume alimuona Mungu kwa macho yake:
“Niliona dalili za Mola wangu”. Anataja tukio la Gharaaniiq, ambayo ameitafsiri kama „korongo‟.
Salman Rushdi sio wa kwanza kuzusha au kubuni tukio hili au jina hili. Ensaiklopidia ya kizamani
ya Cambridge ililitaja. Carl Brocklemann alilizungumza katika kitabu chake kiitwacho “History of
Muslim Nations” (11)
. Vile vile lilitokea katika kitabu kiitwacho “Historical Studies in English” (12)
chini ya kichwa cha habari “The Beginning of Opposition”. Mwandishi wa kitabu hicho
anaeleza wazi moja kwa moja kwamba ni kweli, kwa sababu Al-Tabary amekiingiza katika kitabu
chake cha Historia. Simulizi hii ya “Gharaaniiq” inakanushwa na kukadhibishwa kutokana na
uthibitisho wa Qur‟an, Sunnah, Lugha na historia.
Katika Surah Al-Haaqqah 44–46, Mungu anasema: “Na kama angelizua juu yetu baadhi ya
maneno lazima tungelimshika kwa mkono wa kulia, kisha tungelimkata mshipa mkubwa wa
moyo” (13)
.
Katika Surah An-Najmi 3–4, Mungu anasema: “Wala hasemi kwa tamaa ya nafsi yake, haya
kuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa” (14)
.
Mwandishi wa kitabu kiitwacho Al-Ibriz ameitupilia mbali simulizi yote (15)
kwa sababu hata Iyad
na Ibn Araby waliikataa kwa sababu mapokezi yake ni dhaifu na kuna mkanganyiko katika dhana
nzima ya kisa hiki. Anasema: “Kama tukio hili lingekuwa kweli Waislam wengi wangeiacha dini
yao, jambo ambalo halikutokea. Anaielezea kwa kina aya hiyo inayonukuliwa na waenezaji wa
simulizi hii”. Surah Al-Hajj 52 inasema: “Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala nabii
kabla yako ambaye shetani hakutia fitna katika matakwa yake, lakini Allah huondoa
anayoyatia shetani na huumakinisha ufunuo wake” (16)
. Aya hii inaonesha kwamba Mitume
wote akiwemo Mtume wetu (S.A.W.) hua na shauku ya kutaka watu wake wamuamini Mungu na
179
kuingia katika dini yake. Mwenyezi Mungu anasema katika Surah Al-Kahf 6: “Basi huenda
ukajiangamiza nafsi yako kwa kusikitikia hali yao ikiwa hawayaamini mazungumzo haya” (17)
. Hivyo watu hao hawakujali na walikuwa tofauti tofauti, “wapo kati yao walio amini, na
wengine kati yao walio kufuru” (18)
. Shetani alinong‟ona na kuwatia fitna wale wasiokuwa na
imani, fitna iliyowapelekea na kuwafanya wasiwe waumini. Waumini wa kweli hawawezi
kupatikana bila ya majaribu na fitna ambayo haionekani kwa macho. Allah huondoa anayoyatia
shetani katika nyoyo za wafuasi wa mitume na kuumakinisha ufunuo wake ambao huthibitisha
umoja wake na dini yake, lakini fitna hizo huendelea kuishi ndani ya nyoyo za wanafiki na waongo (19)
.
Yumkini kwamba Maquraishi walizusha kisa hiki cha Gharaniiq na washirikina wakakieneza kwa
sababu mpango wao ni kama tuambiwavyo na Mwenyezi Mungu katika Aya ya 73 ya Surah Al-
Israa: “Walitaka kukushawishi uache tuliyokufunulia ili upate kutuzulia mengineyo, na hapo
bila shaka wangelikufanya rafiki” (20)
.
Maquraishi waliunda kisa hiki ili kwamba wakimbizi wa Kiislam waweze kurudi Makkah kutoka
Ethiopia. Walikuwa wemekimbilia huko baada ya mateso makali waliyotendewa na Maquraishi
ambao walituma ujumbe kwenda kwa Najashi, mfalme wa Ethiopia wakimtaka awafukuze
wakimbizi hao na kuwarudisha Makkah.
Ama kuhusu Sunnah (historia ya maisha ya Muhammad), hakuwahi kuabudu sanamu katika zama
za kabla ya Uislam. Imeripotiwa kuwa alisema: “Allah ameyafanya masanamu na ushairi kuwa
vitu vichukizavyo kwangu”. Ali naye pia hakuwahi kuyasujudia masanamu.
Mtu huyu ambaye Mwenyezi Mungu alimtunza na kumlea katika malezi bora hawezi kulisujudia na
kulithamini sanamu, kwa sababu Mungu alikwishamlinda dhidi ya matendo yasiyofaa ambayo
angeyakusudia kuyatenda kabla ya Uislam.
Ibn Khuzaimah anasema kuwa hadithi hiyo ya Gharaaniiq ilizushwa na wapagani. Al-Baihaqi
anasema kuwa sio ya hakika na haina utaratibu wa upokezi wa hadithi, wasimuliaji wake sio wenye
kuaminika. Bukhari hakuitaja kabisa hadithi hii ya Gharaaniiq.
Ibn Katheer, ambaye tafsiri yake ya Qur‟an ni mashuhuri sana, anasema kwamba hadithi hii ina
mapungufu ya nyororo ya wapokezi wake (ambao walikuja baada ya kizazi cha pili, baada ya kifo
cha Mtume), ikiwa na maana kwamba ni dhaifu sana na haina usahihi (21)
.
Imam Ibn Hazm anasema kuwa hadithi inayodaiwa kuwa ni ya Mtume yenye maneno yafuatayo:
“Hao ni waungu watukufu na kwamba maombezi yao bila shaka yanatarajiwa” ni hadithi ya uongo
kabisa kwa sababu haina nyororo (Sanad) sahihi ya mapokezi yake na hivyo haistahiki hata
kujihusisha au kujishughulisha nayo, kwani kila mtu ana uwezo wa kuzusha uwongo (22)
.
180
Tukija kwenye matumizi ya lugha ya Kiarabu, Imam Muhammad Abdu anaibatilisha hadithi au
simulizi hii kwa sababu kamwe Waarabu hawakuwapa waungu wao jina hili, halikuwahi kutokea
katika mashairi yao, insha zao au maongezi yao. Neno “Gharaaniiq” halikuwa likitumika isipokuwa
katika maana yake ya kawaida ambayo ni ndege-maji wenye rangi nyeusi na nyeupe, yaani
korongo. Wakati mwingine lilitumika kistiari kumaanisha kijana mzuri mweupe.
Mwanzoni mwa mahubiri yake ya kiutume, Muhammad hakuwa akisali katika Kaaba isipokuwa
anapokuwa pekee yake. Licha ya uadui wao Maquraishi kamwe hawakumpa fursa ya kuwasomea
Aya za Qur‟an na kuzisikiliza. Inajulikana vema kuwa Waislam wa mwanzo walikuwa wakijificha
maeneo ya mbali ili wapate kusali wakihofia kwamba makafiri wangewadhuru. Siku moja kundi la
wafidhuli wa Kiquraishi waliwaona Waislam hao wakisali wakataka kuwanyanyasa, na hivyo
ikapelekea kutokea mapigano baina yao.
Katika mtazamo wa kihistoria, kama asemavyo marehemu Dr. Omar Farrouk, Wamisionari (23)
na
baadhi ya Mustashriqiina na waliitumia fursa hii na kushikilia simulizi hii. Walidai kuwa
Muhammad aliwasifu na kuwatukuza Waungu wa washirikina baada ya kuwa dhidi yake kwani
alitamani kupata fursa ya kuwa na maingiliano nao, walilichukulia tendo hili kuwa ni safari ya
kuachana na mashambulizi na kuwabeza miungu wao. Dr. Farroukh anaendelea kusema:
“Ninaamini kwamba majibu bora ya kuukanusha huu uzushi ni yale yaliyotolewa na msomi
mashuhuri kutoka India, Maulana Muhammed Ali (24)
aliposema: “Al-Taabari na Al-Waqidi
waliitaja hii simulizi, hata hivyo simulizi yao hiyo haina mashiko kwa sababu vitendo vyote vya
Mtume wetu (S.A.W.) vinapingana na mwelekeo huu, zaidi ya hilo ni kwamba Al-Wagidi ni
maarufu sana kwa kunukuu masimulizi, visa na hadithi za uongo za Kiyahudi. Katika kitabu cha
“Deaths of Eminent Persons” imeandikwa kuwa Al-Waqidi huripoti hadithi zisizokuwa na
usahihi (25)
. Ashafii anasema: “Kazi zote za Al-Waqidi zimejaa uongo”.
Katika kitabu chake “History of Apostles and Kings” (25)
, Al-Tabari amekijumuisha kisa cha
tukio la Ghraaniiq; lakini wale waliokipa kisa hiki umuhimu mkubwa wanasahau kwamba mfumo
wa Al-Tabari wa ukusanyaji wa hadithi ni ule wa wasimuliaji wa visa, yaani anaelezea matukio tu
na wingi wake alioupata bila ya kutoa maoni yake juu ya matukio hayo au kuyachambua maandiko
yake kimantiki, na hivyo watafiti wengi wanamkosoa yeye pamoja na mfumo wake. Wanasema:
“Mfumo wa kutoa maelezo ya matukio na kuyasimulia tu bila kuyafanyia uchunguzi na
utafiti wa ndani hakuwafai wanahistoria wenye utambuzi na ustadi (26)
. Al-Tabari anaweza
kusamehewa kama ilivyo kwa wapokezi wengine wote wa hadithi ambao huinukuu hadithi husika
huku wakiwataja wapokezi wake pamoja na matini zake na kumpa msomaji fursa ya kuamua kwa
ajili ya usomaji makini na maarifa yenye uchanganuzi. Al-Tabari anasema katika utangulizi wa
kitabu chake: “Ningependa wasomaji wangu wajue kwamba katika matukio yote ninayoyaelezea na
habari ninazozinasibisha na wasimulizi wake, ninafanya hivyo bila kutumia juhudi kubwa ya hoja
za kiakili kutoa mukhtasari au kuhitimisha, isipokuwa kwa kiasi kidogo kinachowezekana, kwani ni
kwa njia tu ya utawanyaji wa habari za wasimulizi na wapokezi, kwamba maarifa ya taarifa na
matukio ya zamani huweza kupatikana na wala sio kwa uamuzi na ushawishi wa kiakili. Kama mtu
ataona katika kitabu hiki vipande kadhaa vya taarifa kuhusu matukio ya zamani ambayo anataka
181
kuyakataa au kuyabeza kutokana na kuwa linachukiza basi sio kosa letu kwani tumeelezea taarifa
hizo tulizozipata kama zilivyotufikia” (27)
.
Kwa upande mwingine, tukirudi kwenye masimulizi ya Ibn Is-Haq au hadithi sahihi za Bukhari
ambazo hazikuacha kipengele chochote cha maisha ya Muhammad (S.A.W.) hatuikuti hii hadithi
iliyotengenezwa.
Ibn Is-Haq aliishi miaka 40 kabla ya Al-Waqidi aliyefariki mwaka 823 A.D. na zaidi ya karne moja
na nusu kabla ya Al-Tabari.
Al-Bukhari aliishi zama za Al-Waqidi na hakuitaja hata kidogo hadithi hii.
Mwisho, mbinu ya kuchukiza ya Mustashriqiina na Wamisionari ni ile ya kurudiarudia na kukariri
matukio au visa visivyokuwa na mashiko, huku wakiupuuza ukweli unaobainisha uongo wa visa
hivyo. Hivyo, huyataja madai yao mara kwa mara, wakidhani kuwa maelfu ya wasomaji wenye
fikra finyu au wasikilizaji wepesi wa kuamini, wataelekea kuyakubali na kuyasadiki. Wanafanya
hivyo ili kufikia malengo na madhumuni yao maalum.
Lord Headley anasema: “Hapa kuna hila, ambapo hufululiza bila ya kuchoka katika kufanya hivyo
kwa lengo la kuzisuta dini nyingine. Mmojawao huitaja juu juu fikra fulani, mwingine huja na
kutetea uwezekano wa fkra husika, wa tatu huja na kuunyanyua uwezekano huo kwenye
daraja ya kuwa fikra au nadharia iliyopendekezwa, mtu wa nne huinyanyua juu zaidi na
kusema kuwa fikra hiyo ni kweli au ni jambo sahihi. Hivyo, fikra hiyo huzunguka na kupitia
katika hatua nne kati ya tano mpaka inapofikia hatua ya kukubalika na kuanza kutumika dhidi ya
dini au staarabu nyingine ambazo wanataka kuzikosoa, kuzisuta au kuzitia ila” (28)
Inafahamika vema kwamba visa au masimulizi ya kihistoria yanakusanya mambo kadhaa ya maisha
ya mwanadamu, yanajumuisha muelekeo wake na maono yake katika jukwaa la kihistoria. Hili
linahusisha mambo hayo kwenye msingi wa mambo mawili:
- Kushikamana na historia ya kuuelewa undani wake na uhalisia wa taarifa zake.
- Kuielewa tabia ya binadam na kuifahamu vizuri au kuupima umuhimu wake katika maisha (29)
.
Salman Rushdi alichagua mada au kisa cha uzushi wa kihistoria ili kuyapa mawazo yake ya
kuchekesha fumbo la bure na la daima kwa kadiri awezavyo, ingawa utiaji chumvi kwenye hadithi
ya kihistoria hauna nafasi kwenye sifa bora za msingi au matukio makubwa na ya muhimu. Hivyo,
mwandishi wa uzushi wa hadithi yoyote ya kihistoria anatakiwa kuitwa kujieleza na kubebeshwa
jukumu/mzigo wa maandiko ambayo silka yake inayaendeleza hususan pale shujaa wa hadithi
husika anapofanywa kwamba aseme kitu ambacho sio cha kweli au hakina usahihi wowote wa
kihistoria. Kwa maana hiyo Rushdi anatakiwa kuwajibishwa kwa yale yote aliyoyaeleza katika
hadithi yake yakiovu, na anatakiwa kutoa uthibitisho. Tunalaani uzushi huo pamoja na mtunzi wake
na kuusihi ulimwengu wa magharibi kwa heshima na busara, elimu, mambo matakatifu ya kidini na
182
maadili mema, waachane na Rushdi na hadithi yake ya uzushi kwa nia njema kabisa. Tunazitaka
taasisi za kielimu na vituo vya utafiti watoe hukumu yao kuhusu kile kilichoandikwa na Rushdi kwa
nia ya kuutendea haki ukweli tu.
Tunapenda kumkumbusha Rushdi na wale wanaomuunga mkono juu ya haya yafuatayo:
Kuna tofauti kubwa sana baina ya uhuru wa maoni na utafiti kwa upande mmoja, na uhuru
wa kutengeneza uongo na kuzua mambo kwa upande mwingine.
Kuna tofauti kubwa kati ya ukweli wa kihistoria uliothibitishwa, na masimulizi
yaliyozushwa yasiyo na usahihi na ya kufikirika. Kuna tofauti kamili baina ya utafiti wa
kitaalam unaoungwa mkono na kuthibitishwa na ushahidi, na baina ya simulizi ya
kuchekesha iliyojaa uongo na uzushi wa kutengenezwa.
Mwenyezi Mungu anasema katika Surah Al-Tawbah Aya 109–110: “Je mwenye kuweka msingi
wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka
msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linaloburugunyika, na likaburugunyika naye
katika moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu. Na jengo lao
hilo walilolijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo
zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima” (30)
.
Himidi njema ni za Allah, mwanzo na mwisho.
183
Rejea:
1. Lord Headley alifariki mwaka 1935 mjini London akiwa na umri wa miaka 81. Alihitimu
masomo yake katika ChuoKikuu cha Cambridge. Alikuwa ni mtu mwenye kuheshimu mawazo ya
watu wengine, mwenye busara, akili, ujuzi, mwadilifu na aliyejaliwa azma imara na uthabiti.
Hakuacha kutoa juhudi yoyote na mali katika njia ya kuueneza Uislam. Hata katika umri wake wa
miaka 70 aliweza kusafiri mpaka Misri, India na Afrika kusini kwa ajili ya kazi hiyo.
2. The Ideal Prophet – cha Khouja Kamal Al Deen uk. 18.
3. Tarakimu hizi zinahusu idadi ya Waislam mwanzoni mwa karne ya 20 kwa sasa idadi yao ni
takriban billion moja.
4. The Ideal Prophet uk. 21
5. Edward Gibbon 1737 – 1794 ni mwanahistoria wa Kiingereza aliyeandika kitabu kiitwacho “The
Decline and Fall of the Roman Empire” ambacho kilipendwa sana.
6. Thomas Carlyle alizaliwa kusini mwa Scotland mwaka 1795. Aliishi miaka 86. Aliandika vitabu
maridhawa katika nyanja za historia na falsafa. Kitabu chake mashuhuri zaidi ni “The Heroes”.
7. The Ideal Prophet – uk. 25
8. Toleo la Kiarabu la Kihan Na. 1601 la 4.3.89
9. Angalia maana ya neno „Mahound‟ katika kamusi ya Cassells.
10. Vita vya Handaki vilitokea mwezi wa Februari 727 wakati wa mapigano Waislam 6 walikufa
shahidi, Saad Ibn Uadh, Anas Ibn Aus Ibn Ateek, Abdullah Ibn Sahl, Al Tufail Ibn Al Niman,
Thaalabah Ibn Atmah na Kaab Ibn Zaid.
11. Kilichapishwa na kampuni ya Learning for Millions House 1965 Uk. 34 na 35
12. Chuo Kikuu cha Damascus idara ya Historia uk. 1 – 22.
13. Surah Al-Haqqah 44, 45, 46.
14. Surah An Najmi 3 – 4
15. Ahmad Ibn Al-Mubarak toleo la Al-Babi Al-Halabi 1961, 240 – 244.
16. Al-Hajj - 52
17. Al-Kahf - 6
18. Al-Baqarah - 253
19. Al-Ibriz „Pure Gold‟ uk. 243
20. Surah Al-Israa - 73
184
21. Ibn Katheer J.3, 229 – 230
22. Islam between Equity and Repudiation uk. 69 – 72
23. Carlyl Brockelmann – History of Islam Nations 1965 uk. 25.
24. Ibn Khillikan – Deaths of Eminent Persons J.4 Uk. 34.
25. History of Apostles and Kings J.2 uk. 338 – 340
26. History of Apostles and Kings J.1 uk. 25
27. Introduction to Previous Reference Book uk. 7 na 8
28. The Ideal Prophet uk. 28
29. Art of Novle cha Dr. Muhammad Yusuf Najm.
- System of Historical Research cha Dr. Hassan Othman
- Modern Literature cha Omar Dusuqy.
30. Al-Tawbah 109 –110