142
i VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI Mhe. Dkt. Medard M. C. Kalemani (Mb.) Waziri wa Nishati Mhe. Subira K. Mgalu (Mb.) Naibu Waziri wa Nishati Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

  • Upload
    others

  • View
    19

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

i

VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI

Mhe. Dkt. Medard M. C. Kalemani (Mb.)

Waziri wa Nishati

Mhe. Subira K. Mgalu (Mb.)

Naibu Waziri wa Nishati

Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua

Katibu Mkuu

Wizara ya Nishati

Page 2: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

ii

Page 3: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

1

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI MHE.

DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA

KALEMANI (MB.), AKIWASILISHA

BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA

MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI

KWA MWAKA 2019/20

Page 4: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

2

Page 5: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

1

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia

Taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge

ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja

kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea

na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti

kwa Mwaka 2018/19 na kupitisha Makadirio

ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati

na Taasisi zake kwa Mwaka 2019/20.

2. Mheshimiwa Spika, napenda

nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,

mwingi wa rehema kwa kuendelea kuwajalia

afya njema Viongozi wetu Wakuu wa

Kitaifa, Waheshimiwa Mawaziri wenzangu,

Waheshimiwa Wabunge na Viongozi wengine

mbalimbali. Kipekee nimshukuru Mwenyezi

Mungu kwa kunijalia afya njema na

kuniwezesha kuendelea kusimamia Sekta

ya Nishati na leo kusimama mbele ya Bunge

lako Tukufu kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya

Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2019/20.

3. Mheshimiwa Spika, naomba

pia niungane na Mawaziri wenzangu,

Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwa

Page 6: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

2

ujumla kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John

Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yake

thabiti yanayonisaidia kuisimamia vema

Sekta ya Nishati. Ni dhahiri kuwa Rais wetu

amekuwa chachu katika kutekeleza mipango

mikubwa na yenye tija katika Sekta ya

Nishati hapa nchini. Mipango hiyo ni pamoja

na kuanza kutekeleza Mradi Mkubwa wa

kielelezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia

maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (MW

2,115). Napenda kuwaahidi Watanzania

kuwa Wizara yangu kwa kushirikiana na

Bunge lako Tukufu na wadau mbalimbali

tutasimamia vema Mradi huu ili ukamilike

kwa wakati.

4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa

hii kuwashukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan,

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa

Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo

mbalimbali wanayonipatia katika kusimamia

Sekta ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na

miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi

wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu

ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda

Page 7: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

3

kumpongeza pia Mhe. Dkt. Ali Mohamed

Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi

ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la

Mapinduzi kwa kuendelea kusimamia kwa

ufanisi utekelezaji wa shughuli za maendeleo

katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mheshimiwa Spika, nichukue

nafasi hii pia kuwapongeza Mawaziri

walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nampongeza Mhe. Prof. Palamagamba John

Aidan Kabudi (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri

wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika

Mashariki; Mhe. Angellah Jasmin Kairuki

(Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi

ya Waziri Mkuu (Uwekezaji); Mhe. Balozi Dkt.

Augustine Philip Mahiga (Mb.), aliyeteuliwa

kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Doto

Mashaka Biteko (Mb.), aliyeteuliwa kuwa

Waziri wa Madini; Mhe. Japhet Ngailonga

Hasunga (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa

Kilimo; na Mhe. Joseph George Kakunda

(Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda

na Biashara.

6. Mheshimiwa Spika, niwapongeze

pia Naibu Mawaziri Mhe. Dkt. Mary

Machuche Mwanjelwa (Mb.), aliyeteuliwa

Page 8: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

4

kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti

ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;

Mhe. Constantine John Kanyasu (Mb.),

aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili

na Utalii; Mhe. Innocent Lugha Bashungwa

(Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa

Kilimo; na Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara

(Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi

ya Rais - TAMISEMI. Nawatakia wateule wote

kila la kheri katika kutekeleza majukumu

yao ya Kitaifa.

7. Mheshimiwa Spika, napenda

nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika,

Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wote wa

Kamati Mbalimbali za Kudumu za Bunge

pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge

lako Tukufu kwa utendaji kazi wenu mahiri.

Kwa namna ya pekee natoa shukrani zangu

za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya

Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe.

Dunstan Luka Kitandula (Mb.), Makamu

Mwenyekiti Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri

(Mb.), na Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa

ushauri na maelekezo wanayotupatia. Nikiri

kuwa Kamati hii imefanya kazi kubwa ya

kuishauri Wizara katika masuala mbalimbali

na kuchambua kwa kina mapendekezo

Page 9: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

5

ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka

2019/20. Wizara itaendelea kushirikiana na

Kamati hii katika kusimamia kwa ufanisi

ustawi wa Sekta ya Nishati.

8. Mheshimiwa Spika, baada ya

utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha

Taarifa ya Mapato, Matumizi na Utekelezaji

wa Shughuli za Wizara ya Nishati kwa Mwaka

2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na

Matumizi kwa Mwaka 2019/20.

B. TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI

YA WIZARA KWA MWAKA 2018/19 NA

MWAKA 2019/20

Bajeti na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka

2018/19

9. Mheshimiwa Spika, Bajeti

iliyopitishwa kwa ajili ya Wizara ya Nishati

pamoja na Taasisi zake kwa Mwaka 2018/19

ni jumla ya Shilingi Trilioni 1.692 kwa

ajili ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya

Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Bajeti ya

Miradi ya Maendeleo ilikuwa Shilingi Trilioni

1.665 sawa na asilimia 98.4 ya bajeti yote

ya Wizara na Bajeti ya Matumizi ya Kawaida

ni Shilingi bilioni 27.15 sawa na asilimia

1.6 ya bajeti yote ya Wizara.

Page 10: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

6

10. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia

tarehe 15 Mei, 2019 Wizara ilikuwa imepokea

jumla ya Shilingi Trilioni 1.227. Fedha

hizi zinajumuisha Shilingi bilioni 688.65

ambazo ni malipo ya awali (advance payment)

kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Mradi wa

kuzalisha umeme wa Rufiji na Shilingi bilioni

169.71 ambazo ni fedha za nje zilizopelekwa

moja kwa moja (D-Funds) katika miradi ya

REA, TANESCO na Sustainable Energy for

All (SE4All). Kiasi hicho kilichopokelewa na

Wizara ni sawa na asilimia 87 ya fedha

zilizotarajiwa kupokelewa katika kipindi

husika ambazo ni Shilingi trilioni 1.410.

Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali

11. Mheshimiwa Spika, Wizara ya

Nishati katika mwaka 2018/19 ilipangiwa

kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 394.45.

Kati ya makusanyo hayo, jumla ya Shilingi

bilioni 394.44 zilitarajiwa kukusanywa

kupitia shughuli za mafuta na gesi asilia na

Shilingi milioni 10.0 kupitia shughuli za

utawala. Hadi kufikia tarehe 15 Mei 2019,

Wizara kupitia shughuli za TPDC za utafiti wa

mafuta na mauzo ya gesi asilia imekusanya

Shilingi bilioni 484.33. Makusanyo hayo ni

sawa na asilimia 123 ya lengo la makusanyo ya

Page 11: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

7

Shilingi bilioni 394.45 kwa mwaka 2018/19.

Sababu ya kuvuka lengo ni kuongezeka

kwa matumizi ya gesi asilia yanayotokana

na kuunganishwa kwa kituo cha kuzalisha

umeme cha Kinyerezi II na Kiwanda cha

Saruji cha Dangote. Matumizi ya gesi asilia

yameendelea kuongezeka na kufikia jumla ya

futi za ujazo bilioni 59.2 mwaka 2018 kutoka

futi za ujazo bilioni 32.2 mwaka 2015, sawa

na ongezeko la asilimia 84.

12. Mheshimiwa Spika, makisio

ya makusanyo ya maduhuli kwa mwaka

2019/20 ni Shilingi bilioni 602.05, sawa na

ongezeko la asilimia 52.6 ikilinganishwa na

Shilingi bilioni 394.45 lililokuwa lengo la

mwaka 2018/19. Ongezeko hilo la makisio

ya makusanyo limetokana na kuongezeka

kwa matumizi ya rasilimali ya gesi asilia.

C. UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA

2018/19

13. Mheshimiwa Spika, Maeneo ya

Kipaumbele ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka

2018/19 yalikuwa ni pamoja na: kuongeza

uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza miradi

mikubwa ikiwemo Mradi wa kuzalisha

umeme katika Mto Rufiji MW 2,115; miradi

Page 12: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

8

ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi

asilia ya Kinyerezi I - Extension MW 185 na

Kinyerezi II MW 240; kuimarisha mifumo

ya kusafirisha umeme nchini; kuendelea

na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi

Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini

(REA III); kuendelea na utekelezaji wa Mradi

wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha Mafuta

Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga

(Tanzania); kuimarisha shughuli za utafutaji

wa mafuta na gesi asilia; na kuendeleza

miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo

na umeme-jua).

14. Mheshimiwa Spika, Wizara pia

ilizingatia maeneo mengine ambayo ni pamoja

na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi

wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia

Sekta ya Nishati; kuboresha mazingira ya

ofisi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi

zake ili kutoa huduma bora zaidi; na

kuendelea kuelimisha umma na kuboresha

mawasiliano na wadau mbalimbali kuhusu

masuala ya nishati.

15. Mheshimiwa Spika, napenda

kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa kutokana

na utekelezaji wa maeneo hayo ya kipaumbele,

Wizara imepata mafanikio makubwa 22 ikiwa

Page 13: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

9

ni pamoja na nchi kutokuwa na mgawo wa

umeme katika kipindi chote cha utekelezaji

wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/19.

Aidha, pamoja na kutokuwa na mgawo wa

umeme, Taifa letu limeanza kuwa na ziada

ya umeme wa wastani wa MW 300 kwa siku

kwa mwaka 2018/19 tofauti na hapo awali

tulipokuwa na upungufu wa zaidi ya MW

100 kwa mwaka 2015. Mafanikio makubwa

21 ni kama ifuatavyo:

(i) Kuanza kwa utekelezaji wa mradi

mkubwa wa kuzalisha Umeme katika

Mto Rufiji wa MW 2,115 utakaokamilika

mwaka 2022. Ujenzi wa bwawa hili

kutaifanya Tanzania kuwa na umeme

wa uhakika, unaotabirika na gharama

nafuu. Aidha, Ujenzi wa bwawa la

mradi huu utaifanya Tanzania

kushika nafasi ya kwanza Afrika

Mashariki kwa kuwa na bwawa

kubwa, ya nne kwa Afrika na kuwa

kati ya nchi 70 Duniani zenye

mabwawa makubwa ya kuzalisha

umeme;

(ii) Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya

kusafirisha umeme msongo wa kV

220 kutoka Makambako, Madaba hadi

Page 14: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

10

Songea, pamoja na ujenzi wa vituo vya

kupoza umeme vya Madaba na Songea

na upanuzi wa kituo cha Makambako.

Kukamilika kwa njia hii ya kusafirisha

umeme kumefanya mikoa ya Njombe

na Ruvuma kuunganishwa katika

Gridi ya Taifa na hivyo kusitishwa

kwa matumizi ya mitambo ya mafuta

ambayo ilikuwa ikigharimu TANESCO

na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni

9.8 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika

kununua mafuta katika Vituo vya

Madaba, Ludewa, Songea, Mbinga na

Namtumbo;

(iii) Kuongezeka kwa kasi ya kusambaza

umeme vijijini ambapo hadi kufikia

tarehe 15 Mei, 2019 Serikali imepeleka

umeme katika vijiji 7,127 vya Tanzania

Bara ikilinganishwa na vijiji 2,018

vilivyokuwa vimeunganishwa umeme

Mwaka 2015. Hii ni sawa na ongezeko

la vijiji 5,109 katika kipindi cha miaka

mitatu iliyopita, ambalo ni ongezeko la

asilimia 253 ya vijiji vilivyokuwa na

umeme kufikia mwaka 2015. Aidha,

ifikapo mwezi Juni, 2020 vijiji zaidi ya

10,278 kati ya 12,268 vya Tanzania

Page 15: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

11

Bara vitaunganishwa umeme sawa na

asilimia 84 ya vijiji vyote. Hivi sasa

Wilaya na Halmashauri 15 za nchi

yetu zimefikishiwa umeme katika vijiji

vyake vyote na kazi inayoendelea ni

kuunganisha umeme katika vitongoji

vyake. Wilaya pamoja na Halmashauri

hizo ni Mafia, Iringa Vijijini (Isimani),

Pangani, Rufiji, Bahi, Siha, Moshi, Hai,

Mwanga, Rombo, Madaba, Buhigwe,

Makambako, Korogwe Mjini na

Mafinga. Pamoja na kukamilisha wilaya

na Halmashauri hizo, kwa sasa kazi

za kuunganisha umeme zinaendelea

katika wilaya nyingine nchini;

(iv) Serikali kupitia TANESCO kuanza

kuunganisha umeme kwa Shilingi

27,000 katika maeneo yote ya vijijini

kulingana na Mpango wa Kupeleka

Umeme Vijijini;

(v) Kuunganisha Gridi ya Taifa katika

maeneo mbalimbali yakiwemo Tunduru

na Liwale na hivyo kuokoa jumla

ya Shilingi bilioni 7.33 zilizokuwa

zikitumika kununua mafuta ya

kuendesha mitambo ya umeme katika

maeneo hayo;

Page 16: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

12

(vi) Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa

Kinyerezi II na kuongeza jumla ya MW

248.22 katika Gridi ya Taifa. Kituo

cha Kinyerezi II ni cha kwanza hapa

nchini kutumia teknolojia ya kisasa ya

combined cycle;

(vii) Kuendelea kutumia vifaa vya ndani

katika ujenzi wa miundombinu ya

kuunganisha umeme vikiwemo nguzo,

mashineumba (transfoma), nyaya na

mita za LUKU na hivyo kulipunguzia

gharama kubwa Shirika la Umeme

Nchini (TANESCO) na kuokoa wastani

wa Shilingi bilioni 162.57 kwa

mwaka. Mpango huu umetengeneza

ajira kwa watanzania wapatao 3,520 na

kuharakisha utekelezaji wa miradi ya

umeme. Kutokana na mafanikio hayo,

kwa sasa kuna zaidi ya viwanda vitatu

(3) vya kuzalisha transfoma badala ya

kimoja kilichokuwepo mwaka 2015,

viwanda tisa (9) vya nguzo badala ya

vitatu (3) vilivyokuwepo awali, viwanda

vitano (5) vya nyaya badala ya kimoja

cha East African Cables kilichokuwepo

na kujengwa viwanda vitatu (3) vya Mita

za LUKU tofauti na hapo awali ambapo

hapakuwa na kiwanda hata kimoja;

Page 17: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

13

(viii) Kuanza kutekeleza mradi wa kujenga

njia ya kusafirisha umeme kV 132

ili kuunganisha mikoa ya Kigoma na

Katavi katika Gridi ya Taifa kutoka

Tabora – Urambo - Kaliua, Nguruka

hadi Kidahwe (Kigoma) kilomita 391

na kutoka Tabora – Ipole, Inyonga hadi

Nsimbo (Katavi) kilomita 381;

(ix) Shirika la Umeme (TANESCO) kutohitaji

ruzuku ya Serikali katika shughuli zake

za uendeshaji kutokana na TANESCO

kujiendesha lenyewe na kuokoa wastani

wa Shilingi bilioni 143 zilizokuwa

zikitumika kama ruzuku kutoka

Serikalini kila mwaka;

(x) Kuimarika kwa mapato ya TANESCO

kwa kiwango cha ongezeko la asilimia

1.5 mwaka 2017/18 hadi asilimia 7.6

mwaka 2018/19. Hivyo ni matarajio

kuwa TANESCO itaweza kuanza kutoa

gawio Serikalini katika kipindi cha

Mwaka 2019/20;

(xi) Kuunganishiwa umeme kwa wateja

wapya 969,431 katika kipindi cha

kuanzia Julai, 2015 hadi tarehe 15

Mei, 2019 na kufikia jumla ya wateja

Page 18: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

14

2,442,648 ikilinganishwa na wateja

1,473,217 waliokuwepo kuanzia nchi

yetu ilipopata Uhuru hadi mwezi Juni,

2015 sawa na ongezeko la asilimia 66

kwa miaka mitatu;

(xii) Kuongeza mtandao wa kusambaza

gesi asilia viwandani na majumbani

kwa takriban kilomita 9.64 kwa

mwaka 2018/19 kutoka kilomita 6.31

kwa mwaka 2017/18. Mtandao huo

utawezesha kuunganisha wateja wa gesi

asilia majumbani zaidi ya 500 katika

Jiji la Dar es Salaam. Kwa upande

wa viwandani, viwanda vya: Dangote

(awamu ya pili); Knauf; Cocacola;

Lodhia; na kiwanda cha vifungashio

kinachomilikiwa na Goodwill Ceramics

Tanzania Limited vimeunganishwa.

Aidha, matumizi ya gesi katika magari

yameongezeka kutoka magari 80 mwaka

2017/18 na kufikia magari zaidi ya 200

mwaka 2018/19 ikiwa ni ongezeko la

zaidi ya asilimia 150;

(xiii) Kukamilika kwa ukarabati wa vituo

vya kupoza umeme vya Kigamboni na

Kurasini na hivyo kuimarisha hali ya

Page 19: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

15

upatikanaji umeme katika Jiji la Dar es

Salaam ikiwemo maeneo ya Kigamboni;

(xiv) Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu

ya kupeleka umeme katika Mji wa

Serikali eneo la Mtumba, Jijini Dodoma

kwa kuunganisha umeme Wizara zote

katika muda mfupi;

(xv) Kuanzisha utaratibu mpya wa

mawasiliano baina ya wateja na TANESCO kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo kuanzisha makundi

ya whatsapp kwa kila wilaya

yanayopatikana masaa 24 kila siku

ili kuimarisha huduma kwa wateja na

hivyo kuongeza ufanisi na mapato ya

Shirika;

(xvi) Kuongezeka kwa ufanisi wa makusanyo

ya mapato ya Serikali ambapo hadi

kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Wizara

kupitia TPDC ilikuwa imekusanya

Shilingi bilioni 484.33 sawa na

asilimia 123 ya lengo la makusanyo

ya Shilingi bilioni 394.45 kwa mwaka

2018/19;

(xvii) Kuendelea kutekeleza kazi za awali

za Mradi wa Bomba la Kusafirisha

Page 20: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

16

Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda)

hadi Chongoleani (Tanga) zikiwemo

Geotechnical na majadiliano ya Host

Government Agreement – HGA. Kazi

hizo zitakamilika mwezi Juni, 2019 na

kazi nyingine za maandalizi ya ujenzi

zinaendelea;

(xviii) Kuongeza uzalishaji wa gesi asilia

kufikia Futi za Ujazo milioni 190 kwa

siku kwa mwaka 2018/19 kutoka Futi

za Ujazo milioni 175 kwa siku mwaka

2017/18. Ongezeko hilo ambalo ni

sawa na asilimia 8.6 limewezesha

upatikanaji wa gesi zaidi kwa matumizi

ya viwandani, majumbani na katika

kuzalisha umeme;

(xix) Kupungua kwa muda wa kushusha

mafuta katika Bandari zetu za Dar es

Salaam, Tanga na Mtwara kutoka kati

ya siku 30 na 60 hadi kati ya siku 3

na 8 kutokana na Serikali kuendelea

kuimarisha Mfumo wa Uagizaji wa

Mafuta kwa Pamoja na hivyo kupunguza

gharama zilizokuwa zinatokana na

gharama za meli kuchelewa kushusha

mafuta bandarini (Demurrage Charges);

Page 21: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

17

(xx) Kupatikana kwa mafuta ya kutosha na

ya uhakika katika kipindi chote cha

mwaka 2018/19 ambapo hadi sasa

kuna ziada ya lita milioni 125.22 za

dizeli, lita milioni 94.67 za petroli, lita

milioni 18.95 za mafuta ya taa na ndege

yanayotosheleza kwa zaidi ya siku 32;

(xxi) Kukamilika na kupitishwa kwa miundo

ya Wizara, PURA na TPDC ambayo

itawezesha Wizara na Taasisi zake

kuendelea kutekeleza majukumu kwa

ufanisi; na

(xxii) Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la

awamu ya kwanza la Wizara na kuhamia

Ofisi mpya katika Mji wa Serikali eneo

la Mtumba Jijini Dodoma.

D. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA

SHUGHULI ZA WIZARA KWA MWAKA

2018/19 NA MPANGO WA BAJETI

KWA MWAKA 2019/20

16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20, Wizara ya Nishati itaendelea

kutekeleza maeneo ya vipaumbele mbalimbali

yakiwemo: kuongeza uzalishaji wa umeme

nchini ili kufikia lengo la kuwa na MW 10,000

ifikapo mwaka 2025, kwa kutekeleza miradi

Page 22: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

18

mikubwa ikiwemo: mradi wa kuzalisha

umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji

(MW 2,115) na mradi wa kufua umeme kwa

kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I - Extension

(MW 185), Mradi wa kuzalisha umeme

wa Rusumo MW 80, Ruhudji MW 358 na

Rumakali MW 222; Kuimarisha mifumo ya

usafirishaji wa umeme nchini kwa kutekeleza

miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi

wa North - West Grid Extension kV 400 yenye

umbali wa kilomita 1,384 inayojumuisha

Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda –

Kigoma hadi Nyakanazi; Singida – Arusha

– Namanga kV 400, kilomita 414; Rufiji -

Chalinze – Dodoma kV 400, kilomita 512;

Rusumo – Nyakanazi kV 220, kilomita 98;

Geita – Nyakanazi kV 220, kilomita 133;

Tabora – Urambo – Kaliua – Nguruka hadi

Kidahwe Mkoani Kigoma kV 132, kilomita

391; na Tabora – Ipole – Inyonga hadi Nsimbo

(Katavi) kV 132, kilomita 381.

17. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine

ya kisekta yatakayozingatiwa na Wizara ni:

kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu

ya Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme

Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini

(REA), katika vijiji takriban 1,990 vilivyobaki

Page 23: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

19

kati ya vijiji 12,268; kuendelea na utekelezaji

wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha

Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi

Tanga, Tanzania (East African Crude Oil

Pipeline - EACOP); kuimarisha shughuli za

utafiti wa mafuta na gesi asilia; kuongeza

kasi ya usambazaji wa gesi asilia; kuendeleza

miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo

na jua); kuvutia uwekezaji katika sekta ya

nishati; na kuendelea kuimarisha utendaji

wa Taasisi za TANESCO, TGDC, REA, TPDC,

PURA na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa

Pamoja ili kuongeza ufanisi na ushindani

katika Sekta ya Nishati.

18. Mheshimiwa Spika, pamoja na

maeneo hayo ya kisekta, Wizara itazingatia

maeneo mengine ya kuboresha utendaji

ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea

uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake

katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuendelea

kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi

wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma

bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma

na kuboresha mawasiliano kati ya Wizara

na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya

nishati.

Page 24: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

20

SEKTA NDOGO YA UMEME

HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI

19. Mheshimiwa Spika, hali ya umeme

nchini imeendelea kuimarika katika kipindi

chote cha mwaka 2018/19. Aidha, mahitaji

ya umeme nchini yameendelea kuongezeka

mwaka hadi mwaka kutokana na kukua

na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi

zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha,

wa uhakika na wa gharama nafuu katika

uzalishaji. Katika mwaka 2018/19 uwezo

wa mitambo ya kuzalisha umeme (installed

capacity) nchini umeongezeka na kufikia MW

1,601.90 kutoka MW 1,517.47 zilizofikiwa

mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia

5.6. Kati ya jumla ya MW 1,601.90 zilizopo

nchini, MW 1,565.72 zimeunganishwa katika

mfumo wa Gridi ya Taifa na MW 36.18 zipo

nje ya mfumo wa Gridi ya Taifa.

20. Mheshimiwa Spika, matumizi ya

juu ya umeme yamefikia MW 1,116.58

ukilinganisha na MW 1,051.27 zilizofikiwa

mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la

asilimia 6.2. Aidha, umeme uliozalishwa

nchini uliongezeka kutoka GWh 7,114

mwaka 2017 na kufikia GWh 7,374 mwaka

Page 25: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

21

2018 sawa na ongezeko la asilimia 3.7. Hadi

kufikia mwaka 2015, nchi yetu ilikuwa na

uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 1,204

ikilinganishwa na uwezo wa sasa wa MW

1,601.90 sawa na ongezeko la asilimia 33.

Katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa

nchi ya uchumi wa viwanda, Serikali kupitia

Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme

wa MW 10,000 ifikapo mwaka 2025.

MIRADI YA KUZALISHA UMEME

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Mto Rufiji (Rufiji Hydro

Power Project) – MW 2,115

21. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme

wa MW 2,115 kwa kutumia maporomoko ya

maji ya Mto Rufiji. Mkataba wa ujenzi wa

mradi ulisainiwa tarehe 12 Desemba, 2018

kati ya TANESCO na Mkandarasi Kampuni

ya Arab Contractors na Elsewedy Electric

za nchini Misri. Tukio hili lilishuhudiwa na

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri

ya Misri. Mkandarasi huyo alikabidhiwa eneo

la mradi tarehe 14 Februari, 2019 na kuanza

utekelezaji wa kazi za awali. Katika kipindi

Page 26: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

22

cha mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa

ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa

miundombinu wezeshi ikijumuisha: njia ya

kusafirisha umeme wa MW 8 yenye msongo

wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi

eneo la mradi yenye urefu wa kilomita 170;

barabara za kiwango cha changarawe za

Ubena – Zomozi na Kibiti – Mloka hadi eneo

la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya

simu; na nyumba za kuishi Mkandarasi.

Vilevile, kulingana na mahitaji ya umeme

wakati wa ujenzi, TANESCO imeanza ujenzi

wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33

kutoka kituo cha kupoza umeme cha Gongo

la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la

mradi urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha

umeme wa MW 22.

22. Mheshimiwa Spika, katika kipindi

cha mwaka 2019/20 Serikali itaendelea na

utekelezaji wa mradi huu muhimu ambapo

kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kuanza

ujenzi wa bwawa (main dam and spillways);

kuanza ujenzi wa njia za kupitisha maji

(tunnels); na kukamilisha ujenzi wa njia ya pili

ya umeme msongo wa kV 33 kutoka Gongo

la Mboto. Fedha za ndani Shilingi trilioni

1.443 zimetengwa katika mwaka 2019/20

Page 27: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

23

kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Utekelezaji

wa mradi umeanza mwezi Desemba, 2018

na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni,

2022. Kwa ujumla Serikali imedhamiria

kwa dhati kutekeleza Mradi huu bila

kuyumbishwa, kucheleweshwa wala

kukwamishwa na mtu yeyote kutoka

ndani au nje ya nchi asiyeitakia mema

nchi yetu.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80

23. Mheshimiwa Spika, mradi huu

wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi

na Rwanda unahusu ujenzi wa kituo cha

kuzalisha umeme wa MW 80 kwa kutumia

maporomoko ya maji ya Mto Kagera kwa

mgawanyo sawa kwa kila nchi. Kwa upande

wa Tanzania, Mradi unagharimu Dola za

Marekani milioni 113 sawa na takriban

Shilingi bilioni 261.75 kwa ufadhili wa

Benki ya Dunia. Kazi zilizofanyika kwa

mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika

kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la

Mradi; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji

(coffer dam) na kukamilika kwa uchimbaji wa

eneo la kusimika mitambo (power house).

Page 28: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

24

24. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni

pamoja na kujenga miundombinu ya kukinga

na kuingiza maji katika handaki (Dam

and Intake); ujenzi wa kituo cha kuzalisha

umeme (powerhouse); ufungaji wa mitambo

katika kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa

kituo cha kupoza umeme (Switchyard); na

kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi

wanaozunguka eneo la mradi (Local Area

Development Plan – LADP na Livelihood

Restoration Program - LRP). Fedha za nje

Shilingi bilioni 3 zimetengwa na Serikali

katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya mradi

huu. Mradi huu umeanza mwaka 2017 na

unatarajiwa kukamilika mwezi Februari,

2020.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358

25. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kituo cha kufua umeme

wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya

maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe. Ujenzi

wa mradi huu utahusisha njia ya kusafirisha

umeme wa msongo wa kV 400 yenye urefu wa

kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha

kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa.

Page 29: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

25

Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika

ni pamoja na: Serikali kuanza majadiliano

ya ufadhili na Serikali ya China kwa ajili

ya kutekeleza mradi; na kumpata Mtaalam

Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi

Yakinifu. Ujenzi wa mradi unakadiriwa

kugharimu Dola za Marekani milioni 407.40

sawa na takriban Shilingi bilioni 943.70 na

ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo

wa kV 400 unakadiriwa kugharimu Dola za

Marekani milioni 53.2 sawa na takriban

Shilingi bilioni 123.23.

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na:

kukamilisha taratibu za ufadhili wa mradi;

kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of

feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri

wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata

Mkandarasi wa kujenga mradi. Jumla ya

Shilingi bilioni 12.50 zimetengwa katika

mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati

ya fedha hizo Shilingi bilioni 10.00 ni fedha

za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha

za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi

Mei, 2020 na kukamilika mwezi Aprili, 2023.

Page 30: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

26

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222

27. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha

umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya

Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya

kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye

urefu wa kilomita 150 kutoka katika mitambo

hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo

mkoani Mbeya. Gharama za mradi huu kwa

pamoja zinakadiriwa kuwa jumla ya Dola za

Marekani milioni 344.22 sawa na takriban

Shilingi bilioni 899.27. Katika kipindi

cha mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa

ni pamoja na: kumtafuta Mtaalam Mshauri

kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu wa

mradi uliofanyika mwaka 1998; na kuanza

usanifu wa miundombinu ya mradi.

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi; kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii (ESIA); na kulipa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 3.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya

Page 31: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

27

fedha hizo Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2023.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Kakono – MW 87

29. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha

umeme wa MW 87 kwa kutumia maji ya

Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme wa msongo wa kV 220 kutoka

Kakono hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita

38.8. Gharama za ujenzi wa mradi ni Dola

za Marekani milioni 380 zitakazotolewa na

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika

la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Shirika

la Maendeleo la Norway (NORAD). Kazi

zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja

na: kukamilisha utafiti wa kijiolojia na

haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa

mradi; kufanya maandalizi ya zabuni kwa ajili

ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi; kuhuisha

tathmini ya athari za mazingira na kijamii

(updating ESIA); na kukamilisha mpango wa

kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa

mradi (Resettlement Action Plan - RAP).

Page 32: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

28

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kutwaa

ardhi na kulipa fidia katika eneo la mradi;

na kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi

wa mradi na njia ya kusafirisha umeme ya

msongo wa kV 220. Jumla ya Shilingi bilioni

2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20

ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu

unatarajiwa kuanza mwezi Desemba, 2019

na kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 45

31. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme

wa MW 45 kwa kutumia maporomoko ya maji

ya Mto Malagarasi mkoani Kigoma na ujenzi

wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa

kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka

Malagarasi hadi Kidahwe mkoani Kigoma.

Gharama za utekelezaji wa Mradi ni Dola za

Marekani milioni 150.0 sawa na takriban

Shilingi bilioni 346.30. Katika kipindi cha

mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja

na kukamilisha: Upembuzi Yakinifu wa njia

ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV

Page 33: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

29

132; usanifu (design) wa miundombinu ya

mradi; upimaji na uthamini wa eneo la mradi

na njia ya kusafirisha umeme; na mpango

wa kuhamisha wananchi wanaopisha mradi.

32. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na:

kutwaa ardhi na kulipa fidia kwa wananchi

watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam

Mshauri na Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi

wa mradi na njia ya umeme msongo wa kV

132. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa

katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi

hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni

600 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni

2.40 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu

unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2020

na kukamilika mwezi Septemba, 2023.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Maji wa Kikonge – MW 300

33. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha

umeme wa MW 300 kwa kutumia

maporomoko ya maji ya Mto Ruhuhu mkoani

Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu

wa kilomita 53 kutoka Kikonge hadi kituo

Page 34: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

30

cha kupoza umeme cha Madaba. Gharama za

utekelezaji wa mradi zinakadiriwa kuwa Dola

za Marekani Milioni 750 sawa na takriban

Shilingi trilioni 1.737. Mradi huu pia

unahusisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya

umwagiliaji. Kazi zilizotekelezwa kwa mwaka

2018/19 ni kumpata Mtaalamu Mshauri

wa kufanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility

Study) na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira

na Kijamii (Strategic Environmental & Social

Assessment – SESA). Kazi hizi zinafadhiliwa

na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kukamilisha

Upembuzi Yakinifu pamoja na Tathmini ya

Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (SESA);

kukamilisha majadiliano ya ufadhili wa ujenzi

wa mradi na kumpata Mtaalam Mshauri wa

kusimamia mradi. Jumla ya Shilingi bilioni

2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20

ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu

unatarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2020

na kukamilika mwezi Oktoba, 2023.

Page 35: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

31

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia

Maji wa Murongo/Kikagati – MW 14

35. Mheshimiwa Spika, mradi huu wa nchi mbili za Tanzania na Uganda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 14 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kV 33 yenye urefu wa kilomita 0.7 kutoka Kikagati (Uganda) hadi Murongo (Tanzania). Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 58 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 134.35 na unatekelezwa na mwekezaji binafsi, Kampuni ya Kikagati Power Company Ltd (KPCL).

36. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi na miundombinu ya barabara za kuingia eneo la mradi; usanifu wa mitambo na vifaa ya umeme; na ujenzi wa miundombinu ya kukinga na kuingiza maji (Dam and Intake) na njia za kupitisha maji (waterways). Kazi zitakazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na: kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme; na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 33. Mradi huu ulianza mwezi Novemba, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2020.

Page 36: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

32

Matengenezo ya Mtambo wa Kuzalisha

Umeme wa Hale (Rehabilitation of Hale

Hydro Power Plant) – MW 21

37. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji

na ukarabati wa mitambo ya kufua umeme

kwa kutumia maji wa Hale mkoani Tanga.

Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa

SEK milioni 200 ambazo ni takriban Shilingi

bilioni 50.96 zitakazotolewa na Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

kushirikiana na Serikali ya Sweden kupitia

Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (Sida).

Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni

kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi

wa ukarabati wa mitambo.

38. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja

na kuanza uchimbaji wa handaki la kuingia

katika kituo cha kuzalisha umeme (access

tunnel). Jumla ya Shilingi bilioni 7.80

zimetengwa kutekeleza kazi hizo ambapo

kati ya fedha hizo Shilingi milioni 300 ni

fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.50 ni

fedha za nje. Kazi za ukarabati zinatarajiwa

kuanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika

ifikapo mwezi Desemba, 2021.

Page 37: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

33

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia

Gesi Asilia wa Kinyerezi II – MW 240

39. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa

mradi huu ulianza mwezi Machi, 2016 kwa

gharama ya Dola za Marekani milioni 344,

sawa na takriban Shilingi bilioni 794.12.

Mradi huu ulihusu ujenzi wa kituo cha

kuzalisha umeme wa MW 240 kwa kutumia

gesi asilia katika eneo la Kinyerezi Jijini

Dar es Salaam. Kituo hiki chenye jumla ya

mitambo nane (8), ambapo mitambo sita (6)

ni ya kutumia gesi asilia (gas turbines) na

mitambo miwili (2) ni ya kutumia mvuke

(steam turbines) kilikamilika na kukabidhiwa

rasmi kwa TANESCO mwezi Desemba, 2018.

Kukamilika kwa kituo hiki kumeongeza

jumla ya MW 248.22 katika Gridi ya Taifa.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I

Extension – MW 185

40. Mheshimiwa Spika, mradi huu

ambao upo katika hatua za mwisho za

utekelezaji unahusu upanuzi wa kituo cha

Kinyerezi I – MW 150 kwa kuongeza mitambo

itakayozalisha MW 185 na kufanya kituo

hicho kuzalisha jumla ya MW 335. Mradi

Page 38: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

34

huu unagharamiwa na Serikali ya Tanzania

kwa asilimia 100 kwa gharama ya Dola za

Marekani milioni 188 sawa na takriban

Shilingi bilioni 435.48. Katika mwaka

2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na:

kukamilika kwa utengenezwaji wa mitambo

yote minne (4) na kuanza kufungwa katika

eneo la mradi; kukamilika kwa upanuzi wa

kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV

220 na kuendelea na upanuzi (upgrade) wa

njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi

I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la

Mboto. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi

Juni, 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi

Agosti, 2019.

41. Mheshimiwa Spika, katika kipindi

cha mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa

ni kukamilisha ufungaji wa mitambo na

kuingiza jumla ya MW 185 katika Gridi ya

Taifa. Fedha za ndani Shilingi bilioni 60.00

zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili

ya kutekeleza kazi hizo.

Page 39: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

35

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa

Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara – MW 300

42. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha

MW 300 kwa kutumia gesi asilia katika Mkoa

wa Mtwara. Gharama za mradi zinakadiriwa

kuwa Dola za Marekani milioni 360 sawa

na takriban Shilingi bilioni 833.90. Mradi

huu utatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali

ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo

(JICA) kwa kushirikiana na Serikali. Kazi

zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni

pamoja na: kukamilika kwa Upembuzi

Yakinifu (Feasibility Study) wa kituo cha

kuzalisha umeme na miundombinu wezeshi

ya maji, barabara na gesi asilia.

43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na

kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa

wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi;

kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia

ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa

ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni

4.20 zimetengwa katika mwaka 2019/20

kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi bilioni 1.00 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 3.20 ni fedha za nje. Mradi

Page 40: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

36

huu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa

mwezi Machi, 2020 na kukamilika mwezi

Septemba, 2022.

Miradi ya Kufua Umeme Utokanao na Jua – MW 150, Upepo – MW 200 na

Makaa ya Mawe – MW 600

44. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2018, Serikali kupitia TANESCO ilitangaza miradi ya nishati jadidifu (Jua – MW 150 na Upepo – MW 200) na Makaa ya Mawe – MW 600 kwa wawekezaji binafsi. Lengo ni kupata miradi ya kuzalisha umeme wa jumla ya MW 950 kwa njia ya ushindani na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Hadi kufikia mwezi Februari, 2019 tathmini ya zabuni kwa kampuni zilizoshiriki ilikamilika. Taratibu zinazoendelea kwa sasa ni kampuni zilizopita hatua ya awali kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza

miradi husika baada ya kupatiwa Request for

Proposals (RFPs).

45. Mheshimiwa Spika, katika kipindi

cha mwaka 2019/20, TANESCO itakamilisha

taratibu za kuwapata wawekezaji binafsi

wenye bei nafuu na kuanza utekelezaji wa

miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi hii nafuu

utapunguzia Shirika gharama za uendeshaji

Page 41: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

37

na hivyo kuwepo matarajio ya kushuka kwa

bei ya umeme. Utekelezaji huo unatarajiwa

kuanza mwezi Novemba, 2019 na kukamilika

mwezi Oktoba, 2022.

MIRADI YA KUSAFIRISHA UMEME

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 wa Singida –

Arusha – Namanga

46. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa

kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga

kupitia Arusha. Mradi huu pia unahusisha

ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme

katika eneo la Kisongo mkoani Arusha,

upanuzi wa kituo cha kupoza umeme (bay

addition) cha Singida na usambazaji wa umeme

katika vijiji 22 vinavyopitiwa na mradi. Mradi

huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya

Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan

(JICA) na Serikali ya Tanzania. Gharama ya

mradi ni Dola za Marekani milioni 258.82

sawa na takriban Shilingi bilioni 599.53.

Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni

kulipa fidia na kuanza shughuli za ujenzi

wa mradi.

Page 42: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

38

47. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni:

kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla

ya Shilingi bilioni 4 fedha za nje zimetengwa

katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi

hizo. Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi

Machi, 2017 na unatarajiwa kukamilika

mwezi Machi, 2020.

48. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa

mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi

wa Backbone awamu ya pili (Backbone Phase

II) unaohusu kuongeza uwezo (upgrade)

wa vituo vya kupoza umeme kutoka kV

220 mpaka kV 400 katika mikoa ya Iringa

na Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya

Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na katika mikoa ya

Singida na Dodoma kwa ufadhili wa Benki

ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la

Maendeleo la Japan (JICA).

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 220 kutoka Makambako

hadi Songea na Kusambaza Umeme

Vijijini kwa Mikoa ya Njombe na Ruvuma

49. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi

wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa

Page 43: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

39

kV 220, yenye urefu wa kilomita 250 kutoka

Makambako hadi Songea kupitia Madaba

pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza

umeme vya Madaba na Songea na upanuzi

wa kituo cha Makambako ulianza mwezi

Mei, 2016 na kukamilika mwezi Septemba,

2018. Mradi huu ulizinduliwa rasmi na Rais

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.

Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe

06 Aprili, 2019. Hadi kufikia tarehe 15 Mei,

2019 jumla ya vijiji 112 kati ya 122 vilikuwa

vimeunganishwa umeme. Jumla ya wateja

wapatao 22,700 wanatarajiwa kuunganishwa

umeme kupitia mradi huu katika wilaya

za Makambako, Njombe na Ludewa katika

Mkoa wa Njombe; na Songea Vijijini, Songea

Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa

wa Ruvuma. Gharama ya mradi huu ilikuwa

ni Shilingi bilioni 216 chini ya ufadhili wa

Serikali za Tanzania na Sweden.

50. Mheshimiwa Spika, kazi

zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20

ni: kuendelea kuunganisha wateja ikiwemo

Vijiji vya Lutikila, Ifinga na Mbangamawe

mkoani Ruvuma vilivyoongezeka pamoja

na kukamilisha kazi ya kufunga Reactor na

Distribution Panels katika vituo vya kupoza

Page 44: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

40

umeme vya Makambako, Madaba na Songea.

Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa

katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi

hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 2 ni

fedha za ndani na Shilingi milioni 500 ni

fedha za nje.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita

51. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi ni kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 55 kutoka Bulyanhulu hadi Geita. Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kV 220, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu, usambazaji wa umeme katika vijiji 10 vilivyopo ndani ya eneo la mradi na kubadilisha mita za umeme za kawaida (conventional meters) 1,500 mkoani Geita. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 23 sawa na takriban Shilingi bilioni 53.28. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme; kupatikana kwa

Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini;

na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha

mradi.

Page 45: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

41

52. Mheshimiwa Spika, kazi

zitakazofanyika mwaka 2019/20 ni

kukamilisha: ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme

mkoani Geita; upanuzi wa kituo cha kupoza

umeme cha Bulyanhulu; ujenzi wa njia za

kusambaza umeme za msongo wa kV 33 na

kV 0.4 katika vijiji 10; na kuunganisha wateja

wapya 1,500. Jumla ya Shilingi bilioni

4.10 zimetengwa katika mwaka 2019/20

ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi bilioni 1.50 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 2.60 ni fedha za nje. Ujenzi

wa mradi huu ulianza mwezi Januari, 2019

na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2020.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa

Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi

53. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 220 yenye urefu

wa kilomita 133, kituo cha kupoza umeme

Nyakanazi na kusambaza umeme katika

vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi. Gharama za

utekelezaji wa mradi huu ni EURO milioni

45 sawa na takriban Shilingi bilioni 117.79.

Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni:

kukamilisha upatikanaji wa Mkandarasi;

Page 46: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

42

kukamilisha uhakiki wa mali za wananchi

watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia.

54. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni

kuanza: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

kutoka Geita hadi Nyakanazi; ujenzi wa

kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi;

upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha

Geita kitakachojengwa kupitia Mradi wa

Bulyanhulu – Geita; na usambazaji wa

umeme katika vijiji 32. Fedha za nje Shilingi

bilioni 1 zimetengwa katika mwaka 2019/20

kwa ajili ya kazi hizo. Ujenzi wa mradi huu

utaanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika

mwezi Julai, 2021.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 220 Rusumo – Nyakanazi

55. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita

98.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme

cha Rusumo hadi Nyakanazi. Gharama za

mradi ni Dola za Marekani milioni 35 sawa

na takriban Shilingi bilioni 81.07. Mradi

huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya

Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania. Katika

Page 47: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

43

mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja

na: kumpata Mkandarasi ambaye ni ubia

kati ya Kampuni ya Sterling & Wilson Pvt

ya India na Electromontaji S.A ya Romania;

kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha

mradi, ambapo takriban Shilingi bilioni

2.5 kutoka vyanzo vya ndani vya TANESCO

zitatumika kulipa fidia hiyo; na Mkandarasi

kuanza kazi za awali za ujenzi wa mradi. Kazi

zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni:

kujenga njia ya kusafirisha umeme. Fedha za

nje Shilingi bilioni 2.32 zimetengwa katika

mwaka 2019/20 kwa ajili ya shughuli za

mradi huu. Mradi huu unatarajiwa kuanza

Julai, 2019 na kukamilika mwezi Juni, 2020.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400, Iringa - Mbeya –

Tunduma - Sumbawanga – Mpanda -

Kigoma – Nyakanazi (North West Grid)

56. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 kutoka Iringa -

Mbeya – Tunduma - Sumbawanga – Mpanda

- Kigoma – Nyakanazi yenye urefu wa kilomita

1,384. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu

tatu kama ifuatavyo:

Page 48: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

44

Awamu ya Kwanza: Ujenzi wa Njia ya

Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400

kutoka Iringa – Mbeya – Tunduma hadi

Sumbawanga

57. Mheshimiwa Spika, awamu hii

inahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 400 kutoka Iringa kupitia

Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye

urefu wa kilomita 624. Mradi huu utahusisha

ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa,

Mbeya, Tunduma na Sumbawanga. Mradi

utagharimu jumla ya Dola za Marekani

milioni 465, sawa na takriban Shilingi

trilioni 1.08 na utafadhiliwa na Benki ya

Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa

(AFD) na Serikali ya Tanzania. Hadi sasa

Benki ya Dunia imetoa Dola za Marekani

milioni 365, sawa na takriban Shilingi

bilioni 845.49. Kazi zilizofanyika kwa mwaka

2018/19 ni pamoja na kukamilisha taarifa

ya awali ya Upembuzi Yakinifu kati ya Mbeya

na Sumbawanga; kuanza uthamini wa mali

kwa wananchi watakaopisha mradi pamoja

na kuanza taratibu za kumpata Mkandarasi

wa mradi.

Page 49: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

45

58. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni:

kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa

wananchi watakaopisha eneo la mradi;

kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia

ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi

wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 6.35

zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili

kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi bilioni 5 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 1.35 ni fedha za nje.

Shughuli za ujenzi zinatarajiwa kuanza

mwezi Desemba, 2019 na kukamilika

mwezi Novemba, 2022. Mradi huu ni kati ya

miradi ya kikanda itakayounganisha njia za

umeme kati ya nchi yetu na nchi jirani za

SADC kupitia Zambia. Serikali itaendelea

kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa

miradi ya namna hii ili pamoja na faida

nyingine, kuwezesha nchi yetu kuuza

umeme katika nchi nyingine.

Awamu ya Pili: Ujenzi wa Njia ya

Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400

kutoka Nyakanazi hadi Kigoma

59. Mheshimiwa Spika, awamu hii

itahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi

Page 50: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

46

Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi

wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani

Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza

umeme (bay addition) cha Nyakanazi na

usambazaji umeme katika vijiji 38. Gharama

za mradi ni Dola za Marekani milioni 187

sawa na takriban Shilingi bilioni 433.17

zitakazotolewa na Benki ya Maendeleo ya

Afrika (AfDB) pamoja na Shirika la Maendeleo

la Korea (EDCF). Kazi zilizofanyika kwa mwaka

2018/19 ni: kumpata Mtaalam Mshauri wa

kusimamia ujenzi wa mradi; uthamini wa

mali zitakazoathiriwa na ujenzi wa mradi;

na kupata eneo la kujenga kituo cha kupoza

umeme Kidahwe mkoani Kigoma.

60. Mheshimiwa Spika, kazi

zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20

ni: kuhakiki na kulipa fidia kwa wananchi

watakaopisha mradi na kumpata Mkandarasi

wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi

bilioni 4.50 zimetengwa katika mwaka

2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya

fedha hizo Shilingi bilioni 3.50 ni fedha za

ndani na Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za nje.

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza

mwezi Desemba, 2019 na kukamilika mwezi

Desemba, 2021.

Page 51: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

47

Awamu ya Tatu: Ujenzi wa Njia ya

Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400

kutoka Sumbawanga – Mpanda – Kigoma

61. Mheshimiwa Spika, awamu hii

inahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 400 kutoka Sumbawanga

hadi Kigoma kupitia Mpanda yenye urefu wa

kilomita 480. Mradi huu utagharimu Dola

za Marekani milioni 165 sawa na takriban

Shilingi bilioni 382.21. Benki ya Dunia

imeonesha nia ya kufadhili ujenzi wa njia ya

kusafirisha umeme na Shirika la Maendeleo

la Korea (EDCF) limeonesha nia ya kufadhili

kituo cha kupoza umeme cha Mpanda.

Kazi iliyofanyika kwa mwaka 2018/19 ni

kuendelea na majadiliano na Washirika wa

Maendeleo kuhusu upatikanaji wa fedha

kufadhili mradi huu.

62. Mheshimiwa Spika, kazi

zilizopangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20

ni: kufanya tathmini ya mali za wananchi

zitakazoathiriwa na mradi; kuendelea na

majadiliano na Washirika wa Maendeleo

kuhusu ufadhili wa mradi; na kuandaa

nyaraka za zabuni za kumpata Mtaalam

Mshauri wa kusimamia mradi. Jumla

ya Shilingi milioni 500 fedha za ndani

Page 52: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

48

zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza

mwezi Julai, 2021 na kukamilika mwezi

Juni, 2024.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze –

Dodoma

63. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa

kilomita 512 kutoka kituo cha kuzalisha

umeme Rufiji hadi Dodoma kupitia Chalinze

Mkoa wa Pwani. Mradi huu pia unahusisha

upanuzi wa vituo vya kupoza umeme (bay

addition) katika Mji wa Chalinze na Jiji la

Dodoma pamoja na kusambaza umeme

katika vijiji 37 vitakavyopitiwa na mradi.

Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola

za Marekani milioni 276.36 sawa na

takriban Shilingi bilioni 640.08. Katika

kipindi cha mwaka 2018/19 kazi iliyofanyika

ni kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya

kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi kutoka

Rufiji hadi Chalinze.

64. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha

Page 53: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

49

Upembuzi Yakinifu; kufanya uthamini wa

mali za wananchi watakaopisha mradi na

kulipa fidia; kumpata Mtaalam Mshauri wa

kusimamia mradi; na kumpata Mkandarasi

wa kujenga njia ya kusafirisha umeme.

Jumla ya Shilingi bilioni 11 zimetengwa

katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi

hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 8 ni

fedha za ndani na Shilingi bilioni 3 ni fedha

za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi

Machi, 2020 na kukamilika mwezi Desemba,

2021.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 kutoka Kinyerezi

hadi Chalinze

65. Mheshimiwa Spika, mradi huu

utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa

kilomita 115 kutoka Kinyerezi mkoani Dar es

Salaam hadi Chalinze mkoani Pwani pamoja

na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme

Kinyerezi. Gharama za mradi zinakadiriwa

kuwa Dola za Marekani milioni 120 ambazo

ni takriban Shilingi bilioni 282. Katika

kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika

ni pamoja na: kukamilisha taratibu za kulipa

fidia kwa wananchi watakaopisha mradi;

Page 54: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

50

na kuanza taratibu za kumpata Mtaalam

Mshauri kwa ajili ya kufanya Upembuzi

Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme.

66. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha

Upembuzi Yakinifu; kulipa fidia kwa

wananchi watakaopisha mradi; na kumpata

Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme na kituo cha kupoza umeme. Jumla

ya Shilingi bilioni 15 zimetengwa katika

mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati

ya fedha hizo Shilingi bilioni 12 ni fedha

za ndani ambazo zitatumika kulipa fidia na

Shilingi bilioni 3 ni fedha za nje. Mradi

huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2020

na kukamilika mwezi Desemba, 2021.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa

North – East Grid (Chalinze – Segera kV

400, Segera – Tanga kV 220,

Kibaha – Bagamoyo kV 220)

67. Mheshimiwa Spika, mradi huu

utahusisha ujenzi wa: njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 yenye urefu

wa kilomita 104 kutoka Chalinze kwenda

Segera; njia ya umeme msongo ya kV 220

yenye urefu wa kilomita 64 kutoka Segera

Page 55: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

51

kwenda Tanga na kilomita 40 kutoka Kibaha

kwenda Bagamoyo; na kujenga vituo vya

kupoza umeme (bay addition) vya Chalinze,

Segera, Bagamoyo na Tanga. Gharama za

mradi zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni

468. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi

zilizofanyika ni pamoja na: kumpata Mtaalam

Mshauri kwa ajili ya kufanya Upembuzi

Yakinifu wa mradi; na kuainisha mipaka

ya mkuza wa njia ya kusafirisha umeme na

kutathmini mali za wananchi watakaopisha

mradi katika eneo kati ya Segera na Tanga.

68. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa mwaka 2019/20 ni: kufanya

Upembuzi Yakinifu; na kuwapata Wakanda-

rasi wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme

na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya

Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka

2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha

hizo Shilingi bilioni 2 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za nje. Ujenzi

wa mradi huu unatarajiwa kuanzia mwezi

Julai, 2020 na kukamilika Juni, 2022.

Page 56: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

52

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 Mwanza – Masaka

69. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi

huu ni kuunganisha nchi ya Tanzania na

Uganda kwa kujenga njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 400 kutoka Mwanza,

Tanzania hadi Masaka, Uganda kupitia

mikoa ya Geita na Kagera. Gharama za mradi

huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani

milioni 75 sawa na takriban Shilingi bilioni

173.73. Kazi iliyofanyika katika mwaka

2018/19 ni majadiliano na Benki ya Dunia

ili kupata fedha za kudurusu taarifa ya awali

ya Upembuzi Yakinifu. Kazi zitakazofanyika

kwa mwaka 2019/20 ni kudurusu Upembuzi

Yakinifu wa mradi na kutafuta ufadhili wa

ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni

3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili

kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo

Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Mradi

huu unatarajiwa kuanza mwezi Machi,

2021 na kukamilika mwezi Septemba, 2023.

Utekelezaji wa mradi huo pamoja na

manufaa mengine, utaiwezesha nchi yetu

kuuza umeme kwa nchi jirani.

Page 57: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

53

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 kutoka Mtwara hadi

Somanga Fungu

70. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita

253 kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu na

ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika

Mkoa wa Mtwara pamoja na kusambaza

umeme katika vijiji 29 vinavyopitiwa na mradi.

Gharama za mradi ni Dola za Marekani

milioni 230 sawa na takriban Shilingi bilioni

532.77. Fedha hizi zitatolewa na Serikali

ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo

(JICA), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)

na Serikali ya Tanzania. Katika kipindi cha

mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja

na kukamilisha Upembuzi Yakinifu.

71. Mheshimiwa Spika, kazi

zilizopangwa kwa mwaka 2019/20 ni:

kufanya tathmini ya athari za mazingira

na kijamii; kufanya uthamini na kulipa

fidia kwa wananchi watakaopisha mradi;

kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya

usimamizi wa utekelezaji wa mradi; na

kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi.

Jumla ya Shilingi bilioni 10 zimetengwa

Page 58: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

54

katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi

hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 3 ni

fedha za ndani na Shilingi bilioni 7 ni fedha

za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza

mwezi Machi, 2020 na kukamilika mwezi

Aprili, 2022.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 400 kutoka Somanga

Fungu hadi Kinyerezi

72. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi

huu ni kujenga njia ya kusafirisha umeme wa

msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu

mkoani Lindi hadi Kinyerezi Mkoani Dar es

Salaam yenye urefu wa kilomita 198. Gharama

za Mradi ni Dola za Marekani milioni 150

sawa na takriban Shilingi bilioni 347.46.

Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19

ni kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu

na kuendelea kulipa fidia kwa wananchi

wanaopisha mradi. Hadi kufikia mwezi Mei,

2019 wananchi 3,085 kati ya 3,901 sawa na

asilimia 79 walikuwa wameshalipwa fidia ya

Shilingi bilioni 56 kati ya Shilingi bilioni

69.14.

73. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha

Page 59: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

55

malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha

mradi; kumpata Mtaalam Mshauri; na

kumpata Mkandarasi. Jumla ya Shilingi

bilioni 8.65 zimetengwa katika mwaka

2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya

fedha hizo Shilingi bilioni 5.80 ni fedha za

ndani na Shilingi bilioni 2.85 ni fedha za

nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza

mwezi Desemba, 2020 na kukamilika mwezi

Februari, 2022.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi

Kidahwe Mkoani Kigoma na kutoka

Tabora hadi Nsimbo Mkoani Katavi

74. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme msongo wa kV 132 yenye urefu wa

kilomita 391 kutoka Tabora hadi Kidahwe

mkoani Kigoma kupitia Urambo, Kaliua na

Nguruka na vituo vyake vya kupoza umeme

pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu

wa kilomita 381 kutoka Tabora hadi Nsimbo

mkoani Katavi kupitia Ipole na Inyonga.

Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa

Dola za Marekani milioni 92 sawa na

takriban Shilingi bilioni 213.11. Mradi huu

Page 60: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

56

unatekelezwa na TANESCO kwa kutumia

wataalam wa Shirika na utafanikisha azma

ya Serikali ya kuiunganisha mikoa ya

Katavi na Kigoma katika Gridi ya Taifa. Kazi

zilizofanyika mwaka 2018/19 ni pamoja na:

kukamilisha Upembuzi Yakinifu wa awali

(Pre-feasibility Study); kuainisha mipaka ya

mkuza wa njia ya usafirishaji umeme; na

upatikanaji wa eneo la kujenga vituo cha

kupoza umeme.

75. Mheshimiwa Spika, kazi

zilizopangwa kwa mwaka 2019/20 ni:

kufanya tathmini ya athari za mazingira na

jamii; kufanya uthamini wa mali za wananchi

watakaopisha mradi; kulipa fidia; na kuanza

ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni

1.50 fedha za ndani zimetengwa katika

mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo.

Aidha, TANESCO imetenga Shilingi bilioni

4.80 kutoka katika mapato yake kwa ajili

ya utekelezaji wa mradi huo ambao ulianza

mwezi Januari, 2019 na unatarajiwa

kukamilika mwezi Agosti, 2020.

Page 61: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

57

Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme

Msongo wa kV 220 na Kituo cha Kupoza

Umeme katika Mkoa wa Simiyu

76. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme

msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita

160 kutoka kituo cha kupoza umeme cha

Ibadakuli Mkoani Shinyanga hadi kituo cha

kupoza umeme cha Imalilo Mkoani Simiyu.

Gharama ya mradi inakadiriwa kuwa Shilingi

bilioni 75. Kazi zilizopangwa kwa mwaka

2019/20 ni: kufanya Upembuzi Yakinifu;

kufanya tathmini ya athari za mazingira na

kijamii; kuainisha mipaka ya mkuza wa njia

ya usafirishaji umeme; na kufanya uthamini

wa mali za wananchi watakaopisha mradi.

Jumla ya Shilingi milioni 100 fedha za

ndani zimetengwa katika mwaka 2019/20

ili kutekeleza kazi hizo. Aidha, TANESCO

imetenga Shilingi milioni 300 kutoka katika

mapato yake kwa ajili ya kutekeleza mradi

huo. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza

mwezi Julai, 2020 na kukamilika mwezi

Desemba, 2021.

Page 62: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

58

MIRADI YA KUBORESHA NJIA ZA

USAMBAZAJI UMEME

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa

Usambazaji Umeme katika Jiji

la Dodoma

77. Mheshimiwa Spika, mradi huu

utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha

umeme ya msongo wa kV 220 kutoka Zuzu

kwenda Msalato na kutoka Zuzu kwenda

Kikombo pamoja na ujenzi wa vituo viwili (2)

vya kupoza umeme katika maeneo ya Msalato

na Kikombo mkoani Dodoma. Gharama ya

mradi ni Dola za Marekani milioni 167.7

sawa na takriban Shilingi bilioni 388.46.

Kazi zilizofanyika mwaka 2018/19 ni pamoja

na kukamilisha Upembuzi Yakinifu wa njia

ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220;

njia ya kusambaza umeme msongo wa kV

33; vituo vya kupoza umeme vya Haneti na

Narco; na kuendelea na taratibu za kupata

ufadhili wa mradi kutoka Serikali ya Japan

kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa

(JICA).

78. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kwa mwaka 2019/20 ni kukamilisha

taratibu za ufadhili wa mradi na kuanza

Page 63: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

59

utekelezaji. Katika mwaka 2019/20 jumla

ya Shilingi bilioni 5.4 zimetengwa kwa

ajili ya kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha

hizo Shilingi milioni 400 ni fedha za ndani

na Shilingi bilioni 5 ni fedha za nje. Mradi

huu unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2020

na kukamilika mwaka 2022.

79. Mheshimiwa Spika, pamoja na

juhudi hizo za ujenzi wa njia za usafirishaji

umeme katika Jiji la Dodoma, Serikali pia

imedhamiria kuufanya Mji Mpya wa Serikali

kuwa Mji wa kisasa na wa Kimataifa. Katika

hatua hiyo, Serikali kupitia TANESCO

inadhamiria kusambaza umeme katika Mji

huo kwa kutumia nyaya za chini ya ardhi

(underground cables). Gharama za Mradi huo

zinakadiriwa kuwa jumla ya Shilingi bilioni

16.9.

Mradi wa Usambazaji Umeme kwa

Maeneo ya Mijini

(Urban Electrification Program)

80. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi

huu ni kuwezesha TANESCO kuongeza kasi

ya kuunganisha wateja maeneo ya mijini

kwa kupanua miundombinu ya kusambaza

umeme ili kuhamasisha ujenzi wa viwanda.

Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni

Page 64: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

60

kuendelea na ujenzi wa njia za usambazaji

umeme katika maeneo mbalimbali ambapo

jumla ya kilomita 592 za msongo wa kV

33, kilomita 1,550 za msongo wa kV 0.4

zimejengwa na kufunga mashineumba 683

na kuunganisha jumla ya wateja 112,308.

Utekelezaji wa kazi hizo umegharimu jumla

ya Shilingi bilioni 82.2 kupitia mapato ya

ndani ya TANESCO. Serikali imeendelea

kujadiliana na washirika wa maendeleo

wakiwemo Benki ya Dunia na Benki ya

Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya utekelezaji

endelevu wa mradi.

81. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kutekelezwa kwa mwaka 2019/20

ni: kuendelea kutanua wigo wa usambazaji

wa umeme mijini na maeneo ya pembezoni

mwa miji yanayohitaji umeme katika mikoa

yote ya Tanzania Bara. Jumla ya Shilingi

bilioni 4.0 zimetengwa katika mwaka

2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya

fedha hizo, Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za

ndani na Shilingi bilioni 3.0 ni fedha za

nje. Aidha, TANESCO kupitia mapato yake

ya ndani, imetenga Shilingi bilioni 188.70

kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu katika

maeneo ya mijini mikoa yote.

Page 65: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

61

MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme

Vijijini Awamu ya Tatu (REA – III)

82. Mheshimiwa Spika, Mradi wa

Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya

Tatu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (Rural

Energy Agency - REA) unaendelea. Mradi

huu unalenga kufikisha umeme katika vijiji

ambavyo hadi kufikia mwezi Desemba, 2015

vilikuwa havijafikiwa na miundombinu ya

umeme. Katika kipindi cha kuanzia mwezi

Januari, 2016 hadi kufikia mwezi Mei, 2019

jumla ya vijiji vipya vilivyoongezeka kwa

kuunganishwa umeme kupitia mradi huu

ni 5,109 zaidi ya vijiji 2,018 vilivyokuwa

na umeme hadi mwezi Desemba, 2015

na hivyo kufikisha jumla ya vijiji 7,127

vilivyounganishiwa umeme. Mzunguko wa

Kwanza wa mradi huu utakapokamilika

mwezi Juni, 2020 jumla ya vijiji 10,278

vitakuwa vimeunganishiwa umeme kati ya

vijiji 12,268 sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote

Tanzania Bara. Vijiji 1,990 vitakavyobaki

sawa na asilimia 16 ya vijiji vyote vitaanza

kupelekewa umeme kuanzia Julai 2020 na

kukamilika ifikapo Juni, 2021 na kuifanya

Tanzania kufikisha miundombinu ya umeme

Page 66: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

62

vijijini katika vijiji vyote Tanzania Bara.

Aidha, hadi sasa jumla ya Taasisi za Elimu

3,165; Maeneo ya Biashara 3,451; Pampu za

Maji 210; Taasisi za Afya 1,211 na Nyumba

za Ibada 984 zimefikishiwa umeme.

83. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa

Miradi iliyopo chini ya Mpango wa REA III ni

kama ifuatavyo:

(i) Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini

Awamu ya Tatu (Grid Extension) –

Mzunguko wa Kwanza

84. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unatekelezwa katika vijiji 3,559 vya mikoa

yote ya Tanzania Bara na kuhusisha ujenzi

wa njia za kusambaza umeme na ufungaji

wa mashineumba. Hadi kufikia tarehe

15 Mei 2019, kazi zilizofanyika ni pamoja

na: kuendelea kujenga miundombinu ya

kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali

yamradinahivyokuunganishawatejawaawali

zaidi ya 56,920. Kazi zilizopangwa kufanyika

katika mwaka 2019/20 ni: kuendelea

kujenga miundombinu ya usafirishaji na

usambazaji wa umeme; na kuunganisha

wateja. Utekelezaji wa usambazaji wa

umeme vijijini umeongezeka kwa kasi

Page 67: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

63

ambapo hadi kufikia tarehe 31 Desemba,

2016 upatikanaji wa umeme vijijini

ulifikia asilimia 49.5 ikilinganishwa na

upatikanaji wa umeme vijijini wa asilimia

21 mwaka 2015. Hata hivyo, kwa sasa

upatikanaji wa umeme umeongezeka

zaidi ya kipindi hicho kufikia vijiji 7,127

mwezi Mei, 2019. Ongezeko hili linaifanya

Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa nchi

za Afrika Mashariki katika kusambaza

umeme vijijini. Inatarajiwa kuwa ifikapo

mwezi Juni, 2020 vijiji 10,278 ambavyo ni

sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote nchini

vitakuwa vimefikishiwa umeme.

(ii) Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini

Awamu ya Tatu (Grid Extension) – Mzunguko wa Pili

85. Mheshimiwa Spika, Mradi wa

Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu

Mzunguko wa Pili utahusisha kusambaza

umeme katika vijiji vilivyobakia 1,190 sawa

na asilimia 16 ya vijiji vyote 12,268 vya

Tanzania Bara. Mradi huu utahusisha ujenzi

wa kilomita 35,581 za njia za umeme msongo

wa kV 33; ujenzi wa kilomita 21,777 za umeme

msongo wa kV 0.4; kufunga mashineumba

7,386; na kuunganisha wateja wa awali zaidi

Page 68: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

64

ya 582,937. Kazi zitakazofanyika katika

mwaka 2019/20 ni kutangaza zabuni za

kuwapata wakandarasi na kuanza kazi.

(iii) Mradi wa Usambazaji Umeme katika

Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji

(Peri-Urban Rural Electrification

Program)

86. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusisha kusambaza umeme katika jumla

ya maeneo 250 yakiwemo ya kibiashara, mitaa

na vitongoji/vijiji. Jumla ya wateja wa awali

zaidi ya 37,843 wataunganishwa umeme

katika wilaya za Mikoa ya Pwani na Dar es

Salaam ikiwemo Kigamboni ili kujazilizia

vitongoji vilivyoachwa na kuboresha

huduma za umeme katika maeneo hayo.

Katika mwaka 2018/19, kazi zilizofanyika

ni pamoja na kuwapata wakandarasi kwa

ajili ya kazi ya ujenzi wa miundombinu ya

kusambaza umeme ambapo zitafanyika kwa

muda wa miezi 9 kuanzia mwezi Mei 2019.

Kazi zitakazofanyika kwa mwaka 2019/20 ni

pamoja na Wakandarasi kuanza kazi za ujenzi

wa miundombinu ya kusambaza umeme na

kuunganisha wateja.

Page 69: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

65

(iv) Mradi wa Usambazaji Umeme katika

maeneo ambayo yamefikiwa na

Miundombinu ya Umeme Mzunguko

wa Pili (Densification Round Two)

87. Mheshimiwa Spika, baada ya

Mradi wa Ujazilizi Mzunguko wa Kwanza

katika mikoa nane (8) ambayo ni Arusha,

Iringa, Mara, Mbeya, Njombe, Pwani, Tanga

na Songwe kukamilika, Serikali inaendelea

na utekelezaji wa mradi huo katika awamu

ya pili. Mradi wa ujazilizi mzunguko wa pili

unahusisha kuongeza wigo wa kuunganisha

umeme katika vitongoji vilivyobaki

(alimaarufu kurukwa) na kufanya wananchi

wengi kufikiwa na umeme. Kazi zilizopangwa

kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni

kukamilisha taratibu za zabuni na kuwapata

wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi

huo.

88. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia

tarehe 15 Mei, 2019, Wakala wa Nishati

Vijijini ulikuwa umepokea jumla ya Shilingi

bilioni 393.31 kati ya Shilingi bilioni 412.08

zilizopangwa kutumika kwa mwaka 2018/19

sawa na asilimia 95.4 ya bajeti. Aidha, katika

mwaka 2019/20 fedha zilizotengwa kwa ajili

ya kutekeleza miradi ya kusambaza umeme

Page 70: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

66

vijijini ni Shilingi bilioni 423.10, kati ya hizo

Shilingi bilioni 363.10 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 60 ni fedha za nje.

SEKTA NDOGO YA NISHATI JADIDIFU

89. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

EWURA imekamilisha mapitio ya utaratibu

wa uendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme

(Review of Small Power Projects Framework) ili

kuvutia wawekezaji na kutatua changamoto

zilizojitokeza kwa wadau wakati wa

utekelezaji. Katika kukamilisha mapitio hayo,

EWURA imerekebisha Kanuni za Uendelezaji

wa Miradi Midogo ya Umeme za Mwaka 2018

(The Electricity (Development of Small Power

Projects) Rules, 2018) yaliyohusisha kikokotoo

cha bei ya umeme kwa miradi hiyo inayouza

umeme kwa TANESCO na ile ya gridi ndogo

(mini/micro grids) zinazouza moja kwa moja

kwa wateja. Kanuni hizo za Mwaka 2019

(The Electricity (Development of Small Power

Projects) Rules, 2019) zimetangazwa kupitia

Gazeti la Serikali GN No. 380 ya tarehe 10

Mei, 2019. Kanuni hizi zitasaidia kudhibiti

bei za umeme kutoka kwa wazalishaji

wadogo ambapo kwa sasa wanajipangia bei

wenyewe na bei hurekebishwa kunapokuwa

na malalamiko kutoka kwa wateja asilimia

15 au zaidi.

Page 71: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

67

90. Mheshimiwa Spika, ili kuleta

usawa katika bei ya umeme kwa maeneo

ambayo yanapata huduma za umeme

kupitia mfumo wa Solar Mini Grid hususan

maeneo ya Visiwani na ambayo hayajafikiwa

na Gridi ya Taifa, maeneo hayo yataendelea

kuunganishiwa umeme kwa gharama sawa

na zinazotozwa na REA na TANESCO.

Nishati inayotokana na Nguvu ya Jua,

Upepo na Maporomoko Madogo ya Maji

91. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19 Serikali iliendelea kuhamasisha

matumizi ya nishati itokanayo na nguvu

ya jua katika nyumba (Solar Home System)

na taasisi za huduma za jamii. Kupitia

mfumo huu, matumizi ya nishati ya jua

yaliongezeka kwa jumla ya MW 10 na hivyo

kufanya matumizi ya nishati hiyo hadi sasa

kufikia MW 26. Vilevile, Serikali iliendelea

na jitihada za kuhamasisha na kuvutia

uwekezaji wa sekta binafsi katika nishati jua

kwa kutumia mfumo wa gridi ndogo. Aidha,

kwa mwaka 2019/20 mchango wa miradi

midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia

maporomoko madogo ya maji na upepo

unatarajiwa kuongezeka kwa jumla ya MW

7.7 kutokana na kukamilika kwa miradi ya

Page 72: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

68

Lugarawa MW 1.7 Wilayani Ludewa; Maguta

MW 1.2 Wilayani Kilolo; Luponde MW 1.0

Wilayani Njombe; Suma MW 1.4 Wilayani

Rungwe; na Mradi wa Upepo wa Mwenga MW

2.4 Wilayani Mufindi.

Matumizi Bora ya Nishati

(Energy Efficiency)

92. Mheshimiwa Spika, katika kipindi

cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni

pamoja na: Serikali kuridhia utekelezaji wa

Mpango Kazi wa Kitaifa wa Matumizi Bora

ya Nishati (Energy Efficiency Action Plan);

na kukamilika kwa rasimu ya Mkakati

wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Nishati

(Energy Efficiency Strategy). Aidha, Taasisi

ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Shirika

la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Utafiti

na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Chuo

cha Ufundi Arusha (ATC) zilibainishwa kama

taasisi zitakazoshiriki katika utekelezaji wa

Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati

na kuanza kujengewa uwezo wa jinsi ya

kutekeleza Mpango kazi huu.

93. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

pangwa kutekelezwa katika Mpango Kazi

wa Matumizi Bora ya Nishati kwa mwaka

Page 73: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

69

2019/20 ni pamoja na: kuboresha Mpango

Kazi huo kwa kuoanisha na Mkakati wa

Kitaifa wa Matumizi Bora ya Nishati; kuandaa

muundo thabiti wa kitaasisi utakaokuwa na

jukumu la kusimamia utekelezaji wa Mpango

Kazi huu; na kutoa elimu ya matumizi bora ya

nishati kwa wananchi na Taasisi za Serikali.

Programu ya Nishati Endelevu kwa Wote

(Sustainable Energy for All – SE4ALL)

94. Mheshimiwa Spika, katika

programu ya upatikanaji wa nishati endelevu

kwa wote inayolenga kuongeza mchango wa

nishati jadidifu na kukuza matumizi bora ya

nishati hapa nchini, kwa mwaka 2018/19

Serikali ilikamilisha maandalizi ya miongozo

ya utekelezaji wa programu hii ikiwemo:

mkakati wa upatikanaji wa rasilimali kwa ajili

ya kufikia malengo ya programu; Mkakati wa

Mawasiliano; Mpango wa ushirikishwaji wa

mamlaka zote na wananchi (Regionalization);

na kuzijengea uwezo Wizara na Taasisi

mbalimbali katika kusimamia utekelezaji wa

miradi ya nishati. Aidha, kupitia programu

hii, Mpango wa Kijinsia wa Utekelezaji wa

Jitihada za Upatikanaji wa Nishati kwa

Wote (Gender Action Plan for Implementation

of Sustainable Energy for All Initiatives)

Page 74: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

70

uliandaliwa na mfumo wa ukusanyaji na

utunzaji wa takwimu za nishati jadidifu hapa

nchini ulianza kuandaliwa.

95. Mheshimiwa Spika, katika kipindi

cha mwaka 2019/20 kazi zilizopangwa

ni pamoja na: kuanza kwa utekelezaji

wa Tanzania Energy Gender Action Plan;

kukamilisha uandaaji wa mfumo wa

ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za

nishati jadidifu; na kuendelea kuwajengea

uwezo watumishi wa Serikali na Sekta Binafsi

katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya

nishati jadidifu nchini. Jumla ya Shilingi

bilioni 3 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi

milioni 500 fedha za ndani na Shilingi

bilioni 2.50 fedha za nje zimetengwa katika

mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo.

Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi

(Geothermal)

96. Mheshimiwa Spika, katika kutimiza

azma ya nchi kuwa na usalama wa nishati

(energy security) kwa kuzalisha umeme

kwa kutumia vyanzo mbalimbali ambavyo

ni nafuu, endelevu na rafiki kwa mazingira

ikiwemo jotoardhi, Serikali kupitia Wizara ya

Nishati imelenga kuzalisha umeme MW 200

Page 75: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

71

utokanao na Jotoardhi ifikapo mwaka 2025.

Pamoja na uzalishaji wa umeme, rasilimali

ya jotoardhi ina manufaa mengine mengi

kupitia mchango wake katika maendeleo ya

sekta nyingine za uchumi kama vile kukausha

mazao, ufugaji wa samaki, mabwawa ya maji

moto kwa ajili ya kuogelea, uchakataji wa

bidhaa za viwandani na hivyo kuboresha pato

na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

97. Mheshimiwa Spika, Serikali

inatekeleza miradi mitano (5) ya kipaumbele

katika maeneo ya Ngozi na Kiejo-Mbaka

mkoani Mbeya, Songwe mkoani Songwe,

Luhoi mkoani Pwani na Natron mkoani

Arusha. Utekelezaji wa miradi hii upo katika

hatua ya uhakiki wa rasilimali ya Jotoardhi

kwa kuchoronga visima vya utafiti isipokuwa

mradi wa Natron ambao upo katika hatua

ya utafiti wa kina. Kwa kawaida, utekelezaji

wa miradi ya jotoardhi hupitia hatua

mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na (i)

utafiti (exploration), (ii) uhakiki (test drilling),

(iii) uendelezaji (development), (iv) uvunaji

(exploitation) na (v) utumiaji (utilization).

98. Mheshimiwa Spika, hatua hizo

hutekelezwa kwa mpangilio maalumu bila

kuruka hatua yoyote na unachukua muda

Page 76: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

72

wa kati ya miaka 6 hadi 8 ili kukamilisha

hatua hizi. Pamoja na kwamba hatua za awali

za uendelezaji wa jotoardhi huchukua muda

mrefu na ni wa gharama kubwa, umeme

utokanao na jotoardhi ni wa uhakika na bei

nafuu kwa kuwa uzalishaji wake hautegemei

mafuta wala hali ya hewa. Miradi mitatu (3)

ambayo itatekelezwa katika mwaka 2019/20

ni Ngozi, Songwe na Kiejo-Mbaka.

(i) Mradi wa Ngozi (Mbeya)

99. Mheshimiwa Spika, Mradi huu

unahusu uzalishaji wa umeme unaotokana

na Jotoardhi katika eneo la Ngozi, mkoani

Mbeya kwa kuanza na uzalishaji wa MW 30.

Kwa sasa mradi upo katika hatua ya uhakiki

wa rasilimali ya Jotoardhi kwa kuchoronga

visima vitatu (3) vya utafiti (exploratory wells).

Shughuli za maandalizi ya uchorongaji wa

visima hivyo vya utafiti zilizofanyika katika

mwaka 2018/19 ni pamoja na: kuajiri

Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuandaa

mpango na kusimamia uchorongaji; taratibu

za ununuzi wa mtambo wa uchorongaji wa

visima vya utafiti; na maandalizi ya upimaji

na uthamini wa ardhi hitajika kwa ajili ya

uchorongaji. Katika mwaka 2019/20 Serikali

itaendelea na taratibu za ununuzi wa mtambo

Page 77: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

73

wa kuchoronga visima vya utafiti. Aidha,

Serikali imetenga fedha Shilingi bilioni 8

kwa ajili ya kuchoronga visima vitatu (3) vya

utafiti katika eneo la Ngozi. Kati ya fedha hizi

Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na

Shilingi bilioni 7.50 ni fedha za nje. Ujenzi

wa mtambo wa kuzalisha umeme unatarajiwa

kuanza mwaka 2021 na kukamilika mwaka

2023.

(ii) Mradi wa Songwe (Mkoani Songwe)

na Mradi wa Kiejo-Mbaka (Mbeya)

100. Mheshimiwa Spika, Miradi hii

inahusu uzalishaji wa umeme na matumizi

mengineyo (direct uses) katika maeneo

ya Songwe, mkoani Songwe na Kiejo-

Mbaka, mkoani Mbeya ambapo imefikia

hatua za uchorongaji wa visima vya utafiti.

Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi

zilizokamilika katika mradi wa Songwe ni

Upembuzi Yakinifu wa Awali (Pre-feasibility

Study) wa matumizi mengineyo ya Jotoardhi

ambayo ni pamoja na kukaushia mazao ya

kilimo na mifugo, mabwawa ya kuogelea na

shughuli za utalii.

101. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

fanyika hadi sasa katika mradi wa

Page 78: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

74

KiejoMbaka ni pamoja na kuwasilisha

maombi ya ufadhili wa mradi kwa Mfuko wa

Maendeleo ya Jotoardhi Afrika (GRMF) kwa

ajili ya uchorongaji wa visima vya utafiti. Kazi

zilizopangwa kufanyika katika kipindi cha

mwaka 2019/20 ni: kufanya maandalizi ya

uchorongaji wa visima vya utafiti; na kuanza

ujenzi wa miradi ya matumizi mengineyo

ya jotoardhi katika maeneo hayo. Shilingi

bilioni 1.31 fedha za ndani ya Kampuni

(TGDC) zimetengwa katika mwaka 2019/20

kugharamia utekelezaji wa kazi hizo.

Utekelezaji wa miradi ya matumizi mengineyo

unaendelea na unatarajiwa kukamilika

mwaka 2021.

102. Mheshimiwa Spika, sambamba

na utekelezaji wa miradi ya jotoardhi,

Serikali inaendelea na juhudi za kuandaa

mazingira wezeshi ya uendelezaji na

utumiaji wa jotoardhi. Kwa sasa leseni za

utafiti za jotoardhi zinasimamiwa na Sheria

ya Madini ya Mwaka 2010. Hata hivyo,

Serikali inaendelea kutathmini changamoto

za utekelezaji wa miradi ya jotoardhi kwa

kutumia sheria husika na kuchukua hatua

stahiki. Aidha, Serikali imeendelea kutoa

fedha za uendelezaji wa miradi ya jotoardhi

Page 79: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

75

kupitia bajeti ya kila mwaka na kujenga

uwezo wa wataalam wa ndani. Katika kipindi

cha mwaka 2015 hadi mwezi Mei, 2019

zaidi ya wataalamu 15 walipata mafunzo

mbalimbali ya muda mrefu katika nyanja za

utafiti na uhakiki wa jotoardhi ikilinganishwa

na wataalamu 7 waliokuwepo wakati TGDC

inaanzishwa.

SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA

GESI ASILIA

Shughuli za Utafutaji, Uzalishaji na

Usambazaji wa Mafuta na

Gesi Asilia Nchini

103. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia

mwezi Mei, 2019 jumla ya Futi za Ujazo

Trilioni 57.54 za gesi asilia zimegunduliwa

hapa nchini. Katika kipindi cha mwaka

2018/19, shughuli za utafutaji, uendelezaji

na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia

zimeendelea kutekelezwa na Shirika la

Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa

kushirikiana na Kampuni za Kimataifa

za Mafuta (IOCs). Uchukuaji wa data za

mitetemo (seismic data acquisition) za 2D

zenye kilomita 442 za mstari katika Kitalu

cha Ruvu umekamilika. Uchakataji na tafsiri

Page 80: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

76

ya data hizo ili kubaini ukubwa wa mashapo

na eneo zuri la kuchoronga visima vya

utafutaji na uendelezaji bado unaendelea.

Aidha, maandalizi ya awali ikiwemo ujenzi

wa barabara na kupatikana kwa vibali kwa

ajili ya kuchoronga visima vya Hammerkop-1

na Kito-1 katika Kitalu cha Rukwa Kusini na

Kilosa-Kilombero sawia yamekamilika.

104. Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa

gesi asilia nchini katika vitalu vya Mnazi

Bay na Songo Songo umeongezeka hadi

kufikia Futi za Ujazo Milioni 190 kwa siku

kwa mwaka 2018/19, ikilinganishwa na

wastani wa Futi za Ujazo Milioni 175 kwa

siku kwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko

la asilimia 8.6. Ongezeko hili la uzalishaji

wa gesi asilia limetokana na ongezeko

la mahitaji katika matumizi viwandani,

majumbani na kuzalisha umeme. Gesi asilia

inachangia zaidi ya asilimia 60 ya umeme

unaozalishwa nchini. Mahitaji ya gesi asilia

katika kuzalisha umeme yameendelea

kuongezeka ambapo yalifikia Futi za Ujazo

bilioni 50.53 kwa mwaka 2018 kutoka Futi

za Ujazo bilioni 42.79 mwaka 2017, sawa na

ongezeko la asilimia 18.

Page 81: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

77

UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI

UNAOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA

MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)

105. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa

miradi ya kimkakati ya utafutaji wa mafuta

na gesi asilia kupitia TPDC unaendelea kwa

kutoa kipaumbele katika Vitalu vya Eyasi –

Wembere,4/1B,MnaziBayKaskazininaSongo

Songo Magharibi. Aidha, Serikali inaendelea

kukamilisha maandalizi ya Mkataba Kifani

wa Ushirikiano katika Utekelezaji (Model

Joint Operating Agreement) utakaosainiwa

baina ya TPDC na Wabia katika kuendeleza

vitalu vya kimkakati.

(i) Kitalu cha Eyasi – Wembere

106. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

TPDC imeendelea kutekeleza mradi wa

utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu

cha Eyasi – Wembere kilichopo katika Bonde la

Ufa la Afrika Mashariki. Kwa mwaka 2018/19,

kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kumpata

Mshauri Mwekelezi wa kufanya Tathmini ya

Athari za Mazingira kwa ajili ya ukusanyaji

wa data za mitetemo za 2D; kuandaa mkataba

wa awali (MoU) kati ya Serikali za Tanzania

Page 82: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

78

na Uganda kwa ajili ya utafiti wa awali;

kukamilisha Hadidu za Rejea kwa lengo la

kumpata Mbia wa Kimkakati; kukusanya

taarifa za awali (reconnaissance survey); na

kukamilisha maandalizi ya uchorongaji wa

visima vifupi vya utafiti wa tabaka za miamba

(Stratigraphic Boreholes) ambapo Mkandarasi

wa kutekeleza kazi hiyo amepatikana.

107. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka

2019/20, kazi zitakazotekelezwa ni pamoja

na: kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira

kwa ajili ya ukusanyaji wa data za mitetemo

za 2D; kuainisha na kufanya tathmini ya

eneo litakaloathiriwa na mradi; kuchoronga

visima vifupi vitatu (3) vya utafiti wa tabaka

za miamba; kufanya utafiti wa kimaabara

wa sampuli zitakazokusanywa kutoka katika

visima vya stratigraphic; na kukusanya,

kuchakata na kutafsiri data za mitetemo za

2D zenye urefu wa kilomita 150. Jumla ya

Shilingi bilioni 1.00 zimetengwa kwa ajili ya

utekelezaji wa kazi hizo.

(ii) Uchorongaji wa Kisima katika

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

108. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

TPDC imeendelea na mpango wa kuchoronga

Page 83: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

79

kisima cha utafutaji mafuta na gesi asilia

katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini

kufuatia matokeo chanya ya tafsiri ya data

za awali za mitetemo (3D) zenye kilomita za

mraba 132. Tafsiri ya data hizo imeonesha

uwezekano wa kuwepo kwa gesi asilia katika

Kitalu hiki. Kwa mwaka 2018/19, Serikali

imetekeleza kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja

na: kukamilisha uchakataji na tafsiri ya data

za mitetemo kiasi cha kilomita za mraba 132;

kuandaa Mpango wa Uchorongaji wa Kisima

(Drilling Programme); na kukamilisha taratibu

za kumpata Mbia wa Kimkakati.

109. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazo-

tekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na:

kumpata Mtaalamu Mshauri wa uchorongaji

(drilling management consultant); kupitia na

kutafsiri taarifa za kijiolojia; na kuchoronga

kisima cha utafutaji mwezi Mei, 2020. Fedha

za ndani Shilingi milioni 800 zimetengwa

kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

Page 84: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

80

(iii) Uchukuaji wa data za mitetemo

katika Vitalu Na. 4/1B na Mnazi

Bay Kaskazini

110. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ukusanyaji na uchakataji wa data

za mitetemo katika Kitalu Na. 4/1B na Mnazi

Bay Kaskazini ili kubaini uwepo wa mashapo

yenye viashiria vya mafuta au gesi asilia.

Kwa mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni

pamoja na: kuboresha Mpango wa Usimamizi

wa Mazingira (Environmental Management

Plan); na kukamilika kwa Hadidu za Rejea

za kumpata mbia wa kimkakati. Kwa

mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa ni

pamoja na: kumpata Mshauri Mwelekezi

wa kukusanya, kuchakata na kutathmini

taarifa za mitetemo ya 3D zenye ukubwa wa

kilomita za mraba 693.1 kwa kitalu cha 4/1B

na Mnazi Bay Kaskazini kwa maeneo ambayo

hayajafanyiwa utafiti; na kumpata Mshauri

Mwelekezi kwa ajili ya kutathmini athari za

mazingira. Jumla ya Shilingi milioni 850

zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.

(iv) Kitalu cha Songo Songo Magharibi

111. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia

Page 85: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

81

katika kitalu cha Songo Songo Magharibi

chenye mashapo yenye viashiria vya uwepo

wa gesi asilia. Kwa kipindi cha mwaka

2018/19, TPDC imekamilisha kazi za

awali za kukusanya data za mitetemo za

3D (seismic scouting) za kilomita za mraba

183.4. Aidha, Hadidu za Rejea za kumpata

mbia wa kimkakati zimekamilika. Vilevile,

katika kipindi hicho, TPDC imeendelea na

taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa

kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira.

Katika mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa

kutekelezwa ni pamoja na: kufanya tafiti za

kijiolojia na kijiofizikia; kumpata mbia wa

kimkakati wa kutekeleza mradi; na kufanya

maandalizi ya awali ya uchorongaji wa kisima

cha utafiti. Jumla ya Shilingi milioni 55

zimetengwa na TPDC kutekeleza shughuli

hizo.

MIRADI YA KUSAFIRISHA NA

KUSAMBAZA GESI ASILIA NCHINI

112. Mheshimiwa Spika, Serikali

imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya

kusafirisha na kusambaza gesi asilia kwa

lengo la kuhakikisha gesi hiyo inatumika

kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya

viwandani, majumbani, katika magari na

Page 86: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

82

kuzalisha umeme. Miradi hiyo ni kama

ifuatayo:

(i) Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia

Viwandani

113. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19, TPDC imekamilisha ujenzi wa

miundombinu ya kusambaza gesi asilia

katika Kiwanda cha Dangote (awamu ya pili),

Lodhia, Cocacola, kiwanda cha vifungashio

kinachomilikiwa na Goodwill Ceramic

Tanzania Limited na kazi ya kuunganisha

kiwanda cha Knauf imefikia asilimia 80.

Aidha, TPDC imekamilisha majadiliano ya

mauziano ya gesi asilia na Kiwanda cha

Shreeji Silcates. Katika kuendelea kutafuta

wateja zaidi wa viwandani, TPDC imeanza

majadiliano ya mauziano ya gesi asilia na

kiwanda cha MM-1 Intergrated Steel Mills

Ltd kilichopo Mikocheni – Dar es Salaam,

pamoja na LN Future Building Materials Co.

Ltd na Kings Alluminium vilivyopo Mkuranga

- Pwani.

114. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka

2019/20, kazi za mradi zitahusu ujenzi wa

miundombinu ya kuunganisha viwanda

vya Shreeji Silicates Tanzania Limited,

Page 87: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

83

LN Future na Kings Aluminium. Vilevile,

TPDC inatarajia kujenga trunk-line kutoka

Mwenge hadi Tegeta na kuunganisha wateja

mbalimbali wakiwemo Estim Construction,

Chem & Cortex, Polypet, Interchik, Giraffe

Hotel, Jangwani Sea Breeze, Ramada Resort

Hotel, Landmark Hotel, Seascape Hotel

na White Sands Hotel. Katika kutekeleza

mpango huo, Shirika litafanya majadiliano

na kusaini mikataba ya mauziano ya gesi

asilia na wateja hao pamoja na kumtafuta

Mkandarasi (EPC contractor). Fedha za ndani

za Shirika Shilingi bilioni 11.22 zimetengwa

kwa ajili ya kutekeleza mradi huu.

(ii) Miradi ya Kusambaza Gesi Asilia

Majumbani na Ujenzi wa Vituo vya

Kujazia Gesi Asilia katika Magari

115. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

TPDC inaendelea kusambaza gesi asilia

kwa wateja wa majumbani walio karibu na

miundombinu iliyopo katika Mkoa wa Dar

es Salaam. Mradi wa kuunganisha wateja

wa majumbani ulianza kutekelezwa mwaka

2016 na ni endelevu kupitia GASCO, kampuni

tanzu ya TPDC. Katika mwaka 2018/19, kazi

zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha

ujenzi wa mtambo wa kupunguza msukumo

Page 88: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

84

wa gesi (Pressure Reduction Station) eneo la

Ubungo Kibo; kukamilisha kazi za awali za

ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi

asilia kutoka Ubungo Maziwa kupitia Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam, Savei, Mlalakuwa,

Changanyikeni, Makongo Juu kuelekea

Tegeta. Miundombinu hiyo itawezesha

kuunganisha wateja wa gesi asilia majumbani

zaidi ya 500 katika Jiji la Dar es Salaam. Ili

kuhamasisha Watanzania wengi kutumia gesi

hii na hivyo kupunguza gharama za maisha

na kukabiliana na uharibifu wa mazingira,

gharama ya bei ya gesi majumbani ina

punguzo la asilimia 40 ukilinganisha na bei

ya gesi ya mitungi (LPG).

116. Mheshimiwa Spika, maandalizi ya kusambaza gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara yanaendelea ambapo kwa upande wa Mkoa wa Mtwara, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha taratibu za manunuzi ya mabomba, mita za gesi na vifaa vya kupunguza mgandamizo wa gesi (pressure reduction stations); kukamilisha michoro ya usanifu wa ujenzi wa miundombinu; na kupatikana kwa vibali vya ujenzi wa mradi. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kutandaza mabomba makubwa (trunk-lines) katika njia mbili, ya kwanza ikielekea Shule ya Sekondari

Page 89: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

85

Ufundi Mtwara kwa ajili ya kusambaza gesi katika taasisi mbalimbali na makazi ya watu zaidi ya nyumba 125 za awali pembezoni mwa bomba la gesi.

117. Mheshimiwa Spika, miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika njia ya pili itaelekea Gereza la Lilungu ikiwa na matoleo kwa wateja walio pembezoni mwa miundombinu hiyo. Maandalizi ya usambazaji wa gesi majumbani kwa Mkoa wa Lindi yameanza ambapo kazi ya kutoboa bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa eneo la Lindi itakamilika mwezi Januari, 2020. Ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi na kazi ya kuunganisha wateja itaanza mwezi Juni, 2020 na itakuwa endelevu.

118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20, Serikali kupitia TPDC imepanga

kuunganisha wateja wa awali zaidi ya

nyumba 1,000 katika Jiji la Dar es Salaam

na nyumba zaidi ya 300 mkoani Mtwara.

Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja

na: kumpata Mshauri Mwelekezi kwa ajili

ya kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira

Jijini Dar es Salaam kupitia maeneo ya

Bagamoyo Road, Kilwa Road na Mandela

Page 90: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

86

Road (Changombe, Kurasini, Keko); kumpata

Mshauri Mwelekezi wa kufanya Tathmini ya

Athari za Mazingira mkoani Mtwara kwa kata

za Railway, Shangani, Chikongola, Tandika,

Likombe, Magomeni, Chuno na Majengo; na

kuwapata wakandarasi (EPC contractors) wa

kuunganisha gesi asilia majumbani Jijini

Dar es Salaam na mkoani Mtwara.

119. Mheshimiwa Spika, TPDC pia

itajenga kituo mama cha kupunguza

mgandamizo wa gesi asilia (Compressed

Natural Gas – CNG Mother Station) chenye

kituo cha kujazia gesi katika magari eneo la

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, vituo

vidogo vya kupunguza mgandamizo wa gesi

asilia (CNG Daughter Stations) vitajengwa

maeneo ya Hospitali ya Muhimbili, Soko la

Samaki Feri na Ubungo. Kituo cha Ubungo

kitatumika kujaza gesi katika Mabasi ya

Mwendokasi zaidi ya 300 pamoja na magari

mengine zikiwemo daladala. Serikali imetenga

Shilingi bilioni 1.10 fedha za ndani kwa ajili

ya kutekeleza mradi huo.

120. Mheshimiwa Spika, katika

kuendelea na juhudi za kuwezesha mikoa

mingine nchini kunufaika na rasilimali ya

gesi asilia, Serikali itaendelea kufanya tafiti za

Page 91: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

87

namna bora ya kuunganishia mikoa hiyo na

miundombinu ya kusafirisha na kusambaza

rasilimali hiyo. Kwa kuanzia, usambazaji

wa gesi asilia unatarajiwa kufanyika katika

mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro, Dodoma,

Kilimanjaro, Mwanza na Arusha. Mpango

huu unatarajiwa kutekelezwa kati ya sasa

na mwaka 2025. Kutokana na kuongezeka

kwa mahitaji ya gesi asilia majumbani,

TPDC itaongeza kasi ya kusambaza gesi

asilia katika maeneo mbalimbali nchini.

(iii) Mradi wa Usambazaji wa Gesi Asilia

kwa kuhusisha Sekta Binafsi katika

Mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es

Salaam

121. Mheshimiwa Spika, Serikali

kupitia TPDC imeanza kutekeleza mradi wa

kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Lindi,

Mtwara na Dar es Salaam. Mradi huu ni

sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe

wa Matumizi ya Gesi Asilia nchini (Natural

Gas Utilization Master Plan - NGUMP).

Mradi unahusu ujenzi wa miundombinu

ya kusambaza gesi asilia kwa kushirikisha

wawekezaji binafsi kwa baadhi ya maeneo

katika mikoa husika.

Page 92: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

88

122. Mheshimiwa Spika, Wawekezaji wa

sekta binafsi watapatikana kwa njia ya zabuni

za ushindani wa kimataifa ili kuweka usawa

na kupata wawekezaji wenye uzoefu na uwezo

wa kiteknolojia na fedha za kugharamia mradi

kwa masharti nafuu kwa Serikali. Kupatikana

kwa wawekezaji kutaharakisha ujenzi wa

miundombinu ya kusambaza gesi asilia na

hivyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa

muda mfupi. Katika mwaka 2018/19, kazi

zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha

Upembuzi Yakinifu wa Awali (Pre-Feasibility

Study) wa mradi; na kuendelea na taratibu

za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya

Upembuzi Yakinifu wa mradi anayetarajiwa

kupatikana mwezi Juni, 2019.

123. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni

kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi na

kuwapata wawekezaji binafsi kwa ajili ya

utekelezaji wa mradi. Baada ya kupatikana

kwa wawekezaji, ujenzi unatarajiwa kuanza

mwezi Juni, 2020 na awamu ya kwanza

ya ujenzi inategemewa kukamilika mwezi

Desemba, 2021.

Page 93: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

89

(iv) Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha

Mbolea Mkoani Lindi

124. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa kiwanda cha mbolea

chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni

1.3 za urea kwa mwaka. Kiwanda hiki

kinatarajiwa kujengwa eneo la Kilwa Masoko

– Lindi na Kampuni ya Tanzania Mbolea and

Petrochemicals Company Limited (TAMPCO)

ambayo ni ubia wa TPDC, Ferrostaal

Industrial Project GmbH ya Ujerumani, Fauji

Fertilizer Company Limited ya Pakistan na

Haldor Topsoe ya Denmark. Ujenzi wa mradi

huu utafanikisha upatikanaji wa uhakika

wa mbolea aina ya urea na hivyo kuchochea

ukuaji wa Sekta ya Kilimo nchini. Manufaa

mengine ni pamoja na: mapato yatokanayo

na gawio na kodi mbalimbali; kutoa ajira za

moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 400;

kuongeza fursa za utoaji huduma na ugavi wa

bidhaa kwa kampuni za Tanzania; kujenga

uwezo wa Watanzania katika uendeshaji wa

viwanda vya mbolea; na kuongeza matumizi

ya gesi asilia kwa wastani wa futi za ujazo

milioni 70 hadi 100 kwa siku.

125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19 kazi zilizotekelezwa ni: kuendelea

Page 94: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

90

na majadiliano ya namna bora ya utekelezaji

wa mradi kati ya wawekezaji na Serikali;

kuandaliwa kwa moduli ya kiuchumi ya

mradi; na kukamilika kwa tathmini ya madai

mapya ya fidia kwa wananchi watakaopisha

mradi. Kazi zitazotekelezwa kwa mwaka

2019/20 ni kukamilisha majadiliano kati ya

Serikali na wawekezaji ambako kutawezesha

kuanza kwa ujenzi wa mradi. Ujenzi wa

mradi unatarajiwa kuanza mwaka 2021 na

kukamilika mwaka 2024. Gharama ya mradi

ni Dola za Marekani bilioni 1.9 sawa na

takriban Shilingi trilioni 4.401.

(v) Mradi wa Kusafirisha Gesi Asilia

kutoka Tanzania kwenda Uganda

126. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha

gesi asilia kutoka Tanzania hadi Uganda

kwa kutumia mkuza wa bomba la mafuta

ghafi la kutoka Uganda hadi Tanga. Mradi

unalenga pia kusambaza gesi asilia maeneo

yatakayopitiwa na bomba hilo. Katika mwaka

2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja

na: kusainiwa kwa Makubaliano ya Awali

(Memorandum of Understanding – MoU) kati ya

Serikali ya Tanzania na Uganda mwezi Agosti,

2018; kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya

Page 95: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

91

Wataalamu (Joint Technical Committee - JTC)

kutoka nchi zote mbili; kuandaa Mpango

Kazi wa Mradi (Project Workplan); na kuanza

taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi

atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi.

Katika mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa

kutekelezwa ni pamoja na kumpata Mshauri

Mwelekezi kwa ajili ya kufanya Upembuzi

Yakinifu wa mradi. Serikali imetenga Shilingi

milioni 800 kwa ajili ya kutekeleza kazi za

awali za mradi huu kwa mwaka 2019/20.

(vi) Mradi wa Ujenzi wa Bomba la

Kusafirisha Gesi Asilia kutoka

Tegeta hadi Bagamoyo

127. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unalenga ujenzi wa bomba la kusafirisha

gesi asilia kutoka Tegeta hadi Bagamoyo ili

kusambaza gesi asilia katika eneo la viwanda

la Zinga, Bagamoyo pamoja na wateja wengine

waliopo katika maeneo yanayopitiwa na mradi

yakiwemo Bagamoyo Export Processing Zone

– EPZ, majumbani na taasisi mbalimbali.

Bomba la kusafirisha gesi asilia kwenda

maeneo hayo linakadiriwa kuwa na urefu wa

kilomita 30 na uwezo wa kusafirisha futi za

ujazo milioni 250 kwa siku. Gharama za mradi

huu ni Dola za Marekani milioni 22.74

Page 96: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

92

sawa na takriban Shilingi bilioni 52.67.

Kukamilika kwa mradi huu kutachochea

ukuaji wa viwanda katika eneo la Bagamoyo

kwa kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa

nishati ya bei nafuu na kuongeza matumizi ya

gesi asilia kwa wateja mbalimbali wanaopitiwa

na miundombinu hiyo.

128. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

tekelezwa hadi sasa ni pamoja na kukamilisha

utafiti wa masoko (market survey) kwa eneo

litakalopitiwa na mradi, usanifu wa mradi

(project design) na Upembuzi Yakinifu wa

mradi (feasibility study). Katika mwaka

2019/20, shughuli zilizopangwa kutekelezwa

zinajumuisha kufanya Tathmini ya Athari

za Mazingira na Kijamii zitakazotokana na

utekelezaji wa mradi na kumpata Mkandarasi

(EPC + Financing) wa kutekeleza mradi.

Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi

Juni, 2020 na kukamilika mwezi Juni, 2021.

Serikali imetenga Shilingi milioni 300 fedha

za ndani kwa ajili ya kutekeleza kazi za awali

za mradi huu.

Page 97: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

93

MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA

GESI ASILIA (Liquefied Natural Gas - LNG)

129. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

TPDC imeendelea na maandalizi ya ujenzi

wa mitambo ya kuchakata na kusindika gesi

asilia iliyopo kina kirefu cha bahari katika

Vitalu Na. 1, 2 na 4. Mitambo hiyo kwa ujumla

itakuwa na uwezo wa kusindika tani milioni

10 za gesi asilia kwa mwaka (10 MTPA).

Pamoja na gesi itakayosindikwa kusafirishwa

nje, kipaumbele ni kupatikana kwa gesi ya

kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani ya

nchi. Ili kuhakikisha mradi unatekelezwa

kwa maslahi mapana ya Taifa, Serikali

iliekeleza Timu ya Majadiliano ya Serikali

(Government Negotiation Team - GNT) kukutana

na mwekezaji mmoja mmoja na si kwa pamoja

kama ilivyokuwa awali. Katika kutekeleza hilo,

GNT ilianza majadiliano na wawekezaji hao

mwezi Aprili, 2019 na yanatarajiwa kukamilika

ndani ya miezi saba (7).

130. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

tekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni:

kukamilisha Tathmini ya Athari za Mazingira

na Kijamii (ESIA); kukamilisha Mpango wa

uhamishaji wananchi watakaopisha Mradi

(Resettlement Action Plan); kuanza kwa

Page 98: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

94

majadiliano ya kimkataba (Host Government

Agreement – HGA) baina ya Serikali na

wawekezaji na kuandaliwa kwa moduli ya

kiuchumi (economic model) ya Mradi.

131. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unatarajiwa kuleta manufaa makubwa

nchini yakiwemo: kuongezeka kwa mapato

ya Serikali yatakayotokana na mauzo ya

gesi asilia; kuongezeka kwa fursa za ajira

kwa Watanzania; kupatikana kwa gesi

kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini;

fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania

kutoa huduma na bidhaa katika mradi; na

kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika

mikoa ya Lindi na Mtwara. Katika mwaka

2019/20, kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na

kukamilisha majadiliano ya mradi na kulipa

fidia kwa wananchi watakaopisha mradi.

Jumla ya fedha za ndani Shilingi bilioni 6.7

zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Gharama za mradi ni Dola za Marekani

bilioni 30 sawa na takriban Shilingi trilioni

69.49. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza

mwaka 2022 na kukamilika mwaka 2028.

Page 99: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

95

MIRADI YA KUHIFADHI NA

KUSAFIRISHA MAFUTA

(i) Mradi wa Hifadhi ya Kimkakati ya

Mafuta ya Akiba na Dharura Nchini

132. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya

Petroli, 2015. Mradi huu pia unahusu ujenzi

wa miundombinu ya kuhifadhi mafuta ya

akiba ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta

ya kutosha nchini wakati wote. Kwa kuanzia,

TPDC imeainisha maeneo katika Mikoa ya

Dar es Salaam, Morogoro na Tanga ambapo

miundombinu hiyo itajengwa. Kwa upande

wa Dar es Salaam, tathmini ya awali ya

ardhi imekamilika na maandalizi ya kufanya

tathmini kwa mikoa ya Tanga na Morogoro

inaendelea.

133. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo-

tekelezwakwamwaka2018/19ni:kuandaliwa

kwa Andiko la Biashara (Business Plan)

pamoja na moduli ya kiuchumi; kuandaliwa

kwa Hadidu za Rejea za kumpata mbia wa

kimkakati; na kukamilika kwa kazi ya ukaguzi

na usanifu wa Tenki Na. 8 litakalotumika

kuhifadhia mafuta. Kazi zitakazotekelezwa

kwa mwaka 2019/20 ni kukarabati Tenki Na.

8 na kuendelea na taratibu za kutwaa ardhi

Page 100: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

96

katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na

Tanga. Shilingi milioni 400 fedha za ndani

zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi

hizo. Jumla ya Dola za Marekani milioni

250 sawa na takriban Shilingi bilioni

579.10 zinahitajika kwa kuanza uagizaji wa

mafuta ya hifadhi.

(ii) Mradi wa Bomba la Kusafirisha

Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki

(EACOP) kutoka Kabaale (Uganda)

hadi Bandari ya Tanga (Tanzania)

134. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha

mafuta ghafi (crude oil) kutoka Kabaale nchini

Uganda hadi mkoani Tanga nchini Tanzania.

Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa

Dola za Marekani bilioni 3.5 ambazo ni

takriban Shilingi trilioni 8.1. Katika mwaka

2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na:

kuendelea na majadiliano ya mkataba kati

ya kampuni ya mradi na Nchi Hodhi (Host

Government Agereement – HGA); kuendelea

na maandalizi ya majadiliano ya Mkataba wa

Ubia (Shareholding Agreement – SHA) ambayo

yanategemewa kukamilika mwezi Juni 2019;

na kukamilika kwa tathmini ya fidia kwa

maeneo ya kipaumbele (camps and coating

yard) na eneo lote la mkuza.

Page 101: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

97

135. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unatarajiwa kuleta manufaa makubwa nchini yakiwemo: kuongeza mapato ya Serikali

kutokana na gawio la uwekezaji katika mradi

kupitia TPDC na kodi mbalimbali; kuongeza

ajira kwa Watanzania; fursa kwa Watanzania

kutoa huduma na bidhaa katika mradi;

kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika

mikoa itakayopitiwa na Bomba; na ukuaji wa

Bandari ya Tanga. Kwa mwaka 2019/20 kazi

zilizopangwa kutekelezwa ni kukamilisha

majadiliano ya Mkataba wa Ubia (SHA) kati

ya nchi washirika na kampuni zilizowekeza

katika mradi pamoja na kulipa fidia wakazi

watakaohamishwa kupisha eneo la mkuza

litakapopita bomba hili. Serikali imetenga

Shilingi bilioni 7 kwa ajili ya utekelezaji wa

Mradi. Ujenzi wa mradi unategemewa kuanza

mwezi Septemba, 2019 na kukamilika mwaka

2021.

(iii) Mradi wa Ujenzi wa Bomba la

Kusafirisha Mafuta Safi (White

Petroleum Products) kutoka Dar

es Salaam (Tanzania) hadi Ndola

(Zambia)

136. Mheshimiwa Spika, mradi huu

unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha

Page 102: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

mafuta safi (white petroleum products)

98

kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola

(Zambia). Mradi utakuwa na matoleo (take–

off points) katika maeneo ya Morogoro, Iringa,

Njombe, Mbeya na Songwe. Utekelezaji wa

mradi huu utaongeza uhakika wa upatikanaji

mafuta katika mikoa inayopitiwa na bomba

hilo sambamba na kuongeza mapato na

ajira. Aidha, utekelezaji wa mradi utaepusha

uharibifu wa miundombinu ya barabara na

kupunguza msongamano wa magari jijini Dar

es Salaam. Mradi huu vilevile utapunguza

changamoto ya usambazaji mafuta kwa nchi

zinazotumia bandari zetu kuingizia mafuta

yao na pia utafungua fursa za kibiashara

katika ukanda wa nyanda za juu kusini.

Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano

baina ya Tanzania na Zambia.

137. Mheshimiwa Spika, hadi sasa, kazi

zilizotekelezwa ni pamoja na: kuandaa Andiko

la Mradi; na kuandaa Hadidu za Rejea za

kumpata Mshauri Mwelekezi atakayefanya

Upembuzi Yakinifu wa mradi na Tathmini

ya Athari za Mazingira na Kijamii (ESIA).

Kazi iliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka

2019/20 ni kufanya Upembuzi Yakinifu

(feasibility study) utakaoainisha gharama za

Page 103: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

99

mradi na namna bora ya kutekeleza mradi.

Serikali imetenga Shilingi milioni 800 kwa

ajili ya kazi hiyo. Gharama za mradi huu

zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni

1.5 sawa na takriban Shilingi trilioni 3.474.

UDHIBITI WA SHUGHULI ZA MKONDO WA

JUU WA MAFUTA NA GESI ASILIA

138. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19, Serikali kupitia PURA imeendelea

na udhibiti wa shughuli za utafutaji,

uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na

gesi asilia nchini katika vitalu 11 kupitia

mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato

(Production Sharing Agreements – PSAs).

Mikataba iliyopo ilisainiwa katika miaka ya

2001 hadi 2012 kabla ya Sheria ya Petroli ya

Mwaka 2015. Aidha, Sheria za Natural Wealth

and Resources (Permanent Sovereignty)

pamoja na Natural Wealth and Resources

(Re-negotiations of unconscionable terms) za

mwaka 2017 zinahitaji mikataba mbalimbali

kupitiwa upya ili iendane na mahitaji ya sasa

yanayolenga rasilimali ya gesi kunufaisha

ipasavyo Serikali na wananchi. Kutokana na

matakwa hayo, kazi ya kudurusu mikataba

hii inaendelea kutekelezwa chini ya Ofisi ya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Page 104: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

139. Mheshimiwa Spika, katika

100

kutekeleza jukumu la kudhibiti shughuli

za mkondo wa juu wa petroli kwa mwaka

2018/19, Serikali kupitia PURA imeendelea:

kusimamia uchukuaji wa data za mitetemo za

2D zenye kilomita 442 za mstari katika Kitalu

cha Ruvu; na kusimamia maandalizi ya awali

ya uchorongaji wa Visima vya Hammerkop-1

na Kito-1 katika vitalu vya Rukwa Kusini na

Kilosa-Kilombero sawia. Vilevile, Mamlaka

imeendelea kufanya kaguzi katika maeneo

ya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia.

140. Mheshimiwa Spika, PURA

imeendelea na shughuli za uhakiki wa

gharama za uwekezaji, ambapo hadi kufikia

mwezi Aprili, 2019 gharama na mapato kwa

mikataba yote 11 kwa miaka ya 2016 na

2017 vimehakikiwa. Lengo ni kuhakikisha

kuwa nchi inaendelea kupata stahiki yake

kulingana na mikataba iliyopo. Vilevile,

Mamlaka hiyo imehakiki na kupitisha

Mpango Kazi na Bajeti ya mwaka 2019 kwa

kampuni zote zinazotekeleza shughuli za

utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia.

141. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka

2019/20, Serikali kupitia PURA itadhibiti

shughuli za uchorongaji wa kisima cha Kito-

Page 105: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

101

1 katika Kitalu cha Kilosa-Kilombero, Kisima

cha Hammerkop-1 katika Kitalu cha Rukwa

Kusini na visima viwili katika Kitalu cha

Ruvu. PURA itasimamia uchukuaji data za

mitetemo za 2D zenye jumla ya kilomita za

mstari 150 katika Kitalu cha Eyasi-Wembere

na data za 3D zenye jumla ya kilomita za

mraba 693.1 katika kitalu cha 4/1B na

Mnazi Bay Kaskazini. Serikali imetenga

Shilingi billioni 1.69 kwa ajili ya kuwezesha

Mamlaka hiyo kutekeleza shughuli zake kwa

mwaka 2019/20.

HALI YA UPATIKANAJI WA

MAFUTA NCHINI

142. Mheshimiwa Spika, hali ya

upatikanaji wa mafuta nchini imeendelea

kuimarika. Serikali kupitia Wakala wa

Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk

Procurement Agency - PBPA) inaendelea

kuagiza na kupokea mafuta ya kutosha

wakati wote. Kampuni za mafuta zimeendelea

kuagiza mafuta kupitia Mfumo wa Uagizaji

wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement

System - BPS) kupitia PBPA. Kati ya mwezi

Januari hadi Desemba, 2018 jumla ya lita

bilioni 5.70 za mafuta ziliagizwa kupitia

Bandari za Dar es Salaam, Tanga na

Page 106: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

102

Mtwara sawa na ongezeko la asilimia 6.3

ikilinganishwa na lita za mafuta bilioni 5.36

zilizoagizwa mwaka 2017. Kati ya kiasi hiki,

lita bilioni 3.27 sawa na asilimia 57.4 ya

mafuta yote yaliyoingizwa yalikuwa ni kwa

ajili ya matumizi ya ndani, sawa na ongezeko

la asilimia 2.5 ikilinganishwa na lita bilioni

3.19 zilizoingizwa mwaka 2017.

143. Mheshimiwa Spika, kwa upande

mwingine, lita bilioni 2.43, sawa na asilimia

42.6 ya mafuta yote yaliyoingizwa yalikuwa

ni kwa ajili ya nchi jirani (on transit) sawa

na ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa

na mafuta ya transit yaliyoingizwa mwaka

2017. Kiasi cha mafuta ya dizeli yaliongezeka

kwa asilimia 1.3 tu wakati mafuta ya taa na

mafuta mazito yalipungua kwa asilimia 11

na asilimia 54.4 sawia ikilinganishwa na

mwaka 2017. Hii inatokana na kupungua

kwa matumizi ya mafuta ya dizeli na mafuta

mazito katika uzalishaji wa umeme. Pia,

matumizi ya mafuta ya taa yanaendelea

kupungua kutokana ongezeko la usambazaji

wa umeme nchini hasa vijijini.

144. Mheshimiwa Spika, kuanzia mwezi

Julai, 2018 Bandari ya Mtwara ilianza

kupokea mafuta kwa ajili ya matumizi ya ndani

Page 107: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

103

sambamba na Bandari za Dar es Salaam na

Tanga. Kuanza kutumika tena kwa bandari

hii kupokea mafuta kumeleta unafuu wa

bei na upatikanaji wa mafuta kwa wananchi

wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Unafuu huu wa bei umetokana na kupungua

au kuondolewa kabisa kwa gharama za

usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda

mikoa hiyo. Mathalan, kwa Mkoa wa Mtwara

takriban Shilingi 72 kwa lita zilizokuwa

zinatumika kusafirisha mafuta kutoka Dar es

Salaam hadi Mtwara zimeondolewa. Pamoja

na unafuu wa bei, kuanza kutumika kwa

bandari hii kumepunguza muda uliokuwa

ukitumika kusafirisha mafuta kutoka Dar

es Salaam hadi mikoa hiyo ya kusini na

kupunguza uharibifu wa barabara.

145. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa

Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja umewezesha

upatikanaji wa mafuta ya kutosha

yanayotabirika na gharama nafuu. Manufaa

mengine ni pamoja na: upatikanaji wa

mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi

na yenye viwango vya ubora unaotakiwa;

kupungua kwa gharama za uagizaji wa

mafuta ikiwemo Demurrage Charges ambazo

zimeshuka kutoka kati ya siku 30 na 60 hadi

Page 108: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

104

kati ya siku 3 na 8; kupatikana kwa takwimu

sahihi za mafuta nchini na hivyo kuimarisha

ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali

za Serikali; kuvutia uwekezaji katika

miundombinu ya kupokelea na kuhifadhi

mafuta katika Bandari za Tanzania na sehemu

mbalimbali za kimkakati (Strategic Areas)

nchini; na kuendelea kuvutia nchi za jirani

(Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia na

Malawi) kupokea mafuta yao kupitia Bandari

za Tanzania na hivyo kuongeza mapato ya

nchi.

146. Mheshimiwa Spika, pamoja na

manufaa hayo Serikali inaendelea kuvutia

wawekezaji zaidi kutumia mfumo huu ambapo

Serikali ya Tanzania imeanza majadiliano

na Rwanda ili kuanza kutumia Bandari ya

Kemondo iliyopo Bukoba kupokea mafuta

kwa ajili ya matumizi ya nchi hiyo. Mafuta

hayo yatasafirishwa kwa njia ya reli kutoka

Dar es Salaam au Tanga. Aidha, Serikali ya

Tanzania imedhamiria kukamilisha ujenzi

wa miundombinu ya Bandari ya Mbamba

Bay pamoja na barabara ili kuleta wepesi

kwa nchi ya Malawi kupitisha mafuta yake

nchini kupitia Bandari ya Mtwara.

Page 109: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

105

147. Mheshimiwa Spika, Serikali

inaendelea na tafiti za namna bora ya

kutekeleza uagizaji wa pamoja wa gesi ya

mitungi kwa ajili ya kupikia majumbani

(Liquefied Petroleum Gas LPG) nchini kwa

Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (BPS). Kiwango

cha uagizaji wa gesi ya LPG kimeongezeka

kufikia tani 142,940 kwa mwaka 2018

ikilinganishwa na tani 107,263 kwa mwaka

2017, sawa na ongezeko la asilimia 33.

Ongezeko hili linatokana na: kuongezeka kwa

uelewa wa watumiaji kuhusu faida za kutumia

gesi; na kuongezeka kwa miundombinu ya

kujazia, kuhifadhia, na kusambaza LPG.

148. Mheshimiwa Spika, Serikali

inatambua kuwa katika maeneo mengi ya

vijijini mafuta yanatunzwa na kuuzwa kwa

namna hatarishi. Hali hiyo imetokana na

kusuasua kwa uwekezaji wa ujenzi wa vituo

vya mafuta katika maeneo hayo. Katika

kutafuta ufumbuzi wa suala hilo, mwezi

Septemba, 2018 EWURA iliingia mkataba na

Kitengo cha Ushirikiano na Viwanda (Bureau

of Industrial Cooperation - BICO) cha Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam ili kubuni namna

bora na salama ya kusambaza mafuta vijijini

kwa kutumia vituo vinavyohamishika (mobile

Page 110: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

106

fuel dispensing facilities). Tayari BICO

wameshaanza kutengeneza mfumo huo

kwa ajili ya majaribio ambao unatarajiwa

kukamilika mwezi Juni, 2019. Ili kuwezesha

Mfumo huo kufanya kazi, EWURA

imeshaandaa Kanuni zitakazotumika

kusimamia mfumo husika na zitapelekwa

kwa wadau ili kupata maoni kabla ya kuanza

kutumika. Lengo la Serikali ni kuhakikisha

usalama na upatikanaji wa mafuta katika

maeneo ya vijijini.

MRADI WA KUJENGA UWEZO KATIKA

SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI

ASILIA

149. Mheshimiwa Spika, Mradi wa

Usimamizi wa Rasilimali za Mafuta na Gesi

Asilia Nchini (Institutional Support Project for

Domestic Resource Mobilization and Natural

Resource Governance) una lengo la kujenga

uwezo kwa watendaji wa tasnia ya uziduaji

(extractive industry). Lengo kuu likiwa ni

kuwezesha Serikali kusimamia mapato

hususan katika sekta ndogo ya mafuta na

gesi asilia. Mradi huu unatekelezwa kwa

makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa

Maendeleo ya Afrika (African Development

Page 111: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

107

Fund) ulio chini ya Benki ya Maendeleo ya

Afrika.

150. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19 kazi zilizotekelezwa ni: kukamilisha

mikataba itakayowezesha ujenzi wa skana

ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na

ununuzi wa vifaa vya kuhifadhia data za

Petroli za PURA. Aidha, kupitia mradi huu

TPDC imefanikiwa kuchakata na kutafsiri

data za mitetemo za 3D na kuandaa Mpango

wa Uchorongaji kisima cha utafiti katika

Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini. Vilevile,

mradi umewezesha mafunzo ya muda mrefu

kwa watumishi 8 kutoka TPDC na mafunzo

ya muda mfupi kwa watumishi 50 wa Wizara,

PURA, EWURA, TRA na Timu ya Majadiliano

ya Mradi wa LNG katika masuala ya usimamizi

na uendeshaji ya miradi ya mafuta na gesi

asilia.

151. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka

2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni

pamoja na: ununuzi wa mifumo ya ukusanyaji

mapato, skana, mfumo wa kielektroniki wa

uondoshaji shehena bandarini na katika

mipaka, kukamilisha ununuzi na ufungaji

wa vifaa vya kuhifadhia data za petroli.

Page 112: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

108

Jumla ya Shilingi bilioni 6.34 zimetengwa

kwa ajili ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka

2019/20 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi

bilioni 2.60 ni fedha za ndani na Shilingi

bilioni 3.74 ni fedha za nje.

E. UIMARISHAJI WA MAWASILIANO

KATI YA WIZARA NA JAMII

152. Mheshimiwa Spika, katika hatua

ya kuimarisha mawasiliano kati ya Wizara

na Jamii kuhusu masuala yanayotekelezwa

na Serikali chini ya Sekta ya Nishati, Wizara

imeendelea kuandaa na kutoa taarifa kwa

wadau wa ndani na nje ya nchi. Taarifa

hizo zinajumuisha: kuratibu mahojiano kati

ya Waziri wa Nishati na Jarida la Forbes

Afrika litakalochapisha mafanikio ya Sekta

ya Nishati; kuratibu mikutano ya wadau wa

umeme kuhusu Mradi wa Rufiji iliyofanyika

katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya,

Njombe na Pwani kwa lengo la kujenga

uelewa kwa wananchi na kuwahamasisha

juu ya utunzaji wa vyanzo vinavyotiririsha

maji katika Mto Rufiji; kuratibu uandaaji

na urushaji wa makala (documentary)

iliyoeleza mafanikio ya Sekta ya Nishati ya

miaka mitatu (2015-2018) ambayo ilirushwa

na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1)

Page 113: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

109

tarehe 13 Septemba, 2018; na kusambaza

habari za Wizara na Taasisi zake katika

Magazeti na Mitandao ya Kijamii ikiwemo

ya facebook, Twitter, Instagram na You Tube

pamoja na kushughulikia kero za wananchi

zinazotumwa katika mitandao hiyo. Aidha,

Wizara imezindua jarida (Nishati News

Bulletin) linalotoa taarifa mbalimbali kuhusu

Sekta ya Nishati.

153. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2019/20, Wizara kwa kushirikiana na

wadau mbalimbali itaendelea kuimarisha

mawasiliano na Jamii ili kuendelea kukuza

uelewa wa masuala yanayotekelezwa na

Serikali chini ya Sekta ya Nishati. Pamoja

na mambo mengine, Wizara itaendelea kutoa

taarifa mbalimbali katika maeneo muhimu

na miradi mikubwa inayotekelezwa na Wizara

katika kipindi husika.

F. AJIRA NA MAENDELEO YA

RASILIMALIWATU

154. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza

majukumu ya Wizara kwa ufanisi baada

ya kugawanywa kwa iliyokuwa Wizara

ya Nishati na Madini, Wizara ya Nishati

iliandaa na kutekeleza Muundo wake ambao

Page 114: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

110

uliidhinishwa mwezi Juni, 2018. Kutokana

na kuidhinishwa kwa Muundo huo, Wizara

imeandaa Mahitaji ya Kazi (Job Listing);

Maelezo ya Kazi (Job Descripitions) na

mapendekezo ya kujaza nafasi mbalimbali za

Uongozi kulingana na Muundo huo. Nyaraka

hizo ziliwasilishwa katika Mamlaka husika

kwa hatua zaidi. Wizara pia ilisimamia

maandalizi ya Miundo ya Taasisi zilizo chini

yake (TPDC na PURA) baada ya Miundo yake

kuidhinishwa. Taratibu za kujaza nafasi

kulingana na Miundo hiyo zinaendelea

kutekelezwa. Vilevile, Miundo ya TANESCO

na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja

(PBPA) bado inaendelea kukamilishwa

ili kuziwezesha Taasisi hizo kutekeleza

majukumu yake kwa ufanisi.

155. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza

tija na motisha kwa Watumishi, katika

mwaka 2018/19 Wizara iliwapandisha

vyeo Watumishi 41 na kubadilisha kada

(re-categorization) Watumishi watatu (3).

Katika mwaka 2019/20, Wizara inatarajia

kubadilisha kada za Watumishi wanne (4),

kujaza nafasi 13 za uongozi na kuwapandisha

vyeo Watumishi 48. Aidha, Wizara na Taasisi

zake zinatarajia kuajiri jumla ya Watumishi

Page 115: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

111

217 ambapo kati ya idadi hiyo, Wizara itaajiri

Watumishi 53; TPDC Watumishi 116; REA

Watumishi 9 na PURA Watumishi 39.

156. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua

umuhimu wa masuala ya mafuta na gesi asilia

nchini, Wizara imeendelea kushirikiana na

Washirika wa Maendeleo ili kutoa ufadhili wa

masomo kwa Watanzania katika Shahada ya

Kwanza, Uzamili na Uzamivu ili kuhakikisha

kuwa nchi inakuwa na Wataalamu wake wa

kutosha katika sekta hiyo. Katika mwaka

2018/19 Watanzania 18 walipata fursa

ya ufadhili wa masomo kutoka Serikali ya

Jamhuri ya Watu wa China katika tasnia

ya mafuta na gesi asilia. Aidha, Watanzania

wengine 22 wanatarajiwa kwenda masomoni

kupitia ufadhili wa Serikali ya China kwa

mwaka 2019/20. Wizara imewasilisha

Ubalozi wa China mapendekezo ya waombaji

wenye sifa kwa ajili ya kukamilisha hatua

muhimu za uchambuzi.

157. Mheshimiwa Spika, vilevile, katika

kuwajengea uwezo Watumishi wa Wizara na

Taasisi nyingine za Serikali, katika mwaka

2018/19 Wizara imewezesha na kutoa

ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu kwa

Watumishi 10 na mafunzo ya muda mfupi

Page 116: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

112

kwa Watumishi 47. Kwa mwaka 2019/20,

Watumishi 10 wanatarajiwa kupata fursa ya

mafunzo ya muda mrefu na Watumishi 75

mafunzo ya muda mfupi.

158. Mheshimiwa Spika, Wizara

imeendelea kutoa huduma ya lishe na mlo

kamili pamoja na fedha kwa ajili ya usafiri

wakati wa kuhudhuria matibabu kwa

watumishi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

ili waendelee kulitumikia Taifa. Wizara pia

iliendesha mafunzo ya namna ya kujikinga

na Virusi vya UKIMWI na Magonjwa Sugu

Yasiyoambukizwa (MSY), Ushauri Nasaha

na Lishe Bora. Sambamba na jitihada hizo,

Wizara pia inaendelea kuwahamasisha

Watumishi kufanya mazoezi ya mwili na

kupima afya hususan katika Magonjwa

Sugu Yasiyoambukiza kama vile magonjwa

ya shinikizo la damu, kisukari na saratani.

159. Mheshimiwa Spika, katika mwaka

2018/19, Wizara imekamilisha awamu ya

kwanza ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao

Makuu ya Wizara katika Mji Mpya wa Serikali

eneo la Mtumba Jijini Dodoma. Utekelezaji

wa mradi huo ulianza mwezi Desemba 2018

na kukamilika mwezi Aprili 2019. Aidha,

jengo hilo la Wizara limeanza kutumiwa rasmi

Page 117: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

113

tarehe 15 Aprili, 2019 na Viongozi Wakuu

wa Wizara, Wakuu wa Idara na baadhi ya

Wakuu wa Vitengo na Sehemu. Katika mwaka

2019/20 Wizara inatarajia kuanza ujenzi wa

jengo la pili la ofisi litakalokidhi mahitaji ya

watumishi wote ambapo Shilingi bilioni 2.4

zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza ujenzi

huo.

G. USHIRIKIANO WA KIKANDA NA

KIMATAIFA

160. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia

Wizara ya Nishati inapenda kuwashukuru

Washirika wa Maendeleo na nchi wahisani

ambao wameendelea kutoa michango yao

katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli

mbalimbali za Wizara. Kwa niaba ya Serikali,

napenda kutambua mchango wa: Benki ya

Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia

(WB), Benki ya Ushirikiano wa Kimataifa

ya Japan (JBIC), United Bank for Africa

(UBA); Economic Development Cooperation

Fund (EDCF - Korea), Mfuko wa Uendelezaji

Jotoardhi (Geothermal Risk Mitigation

Facility - GRMF) pamoja na Taasisi na

Mashirika ya: JICA (Japan), KfW (Germany),

AFD (Ufaransa), Sida (Sweden), Umoja wa

Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Umoja

Page 118: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

114

wa Mataifa (UNDP), Shirika la Maendeleo la

Canada (CIDA) na USAID (Marekani).

161. Mheshimiwa Spika, pia natoa

shukrani kwa Serikali za Burundi, Canada,

China, Finland, Iceland, Japan, Sweden,

Ufaransa, Ujerumani, Norway, Korea ya

Kusini, Misri, Rwanda, Uganda na Zambia

kwa ushirikiano wao katika kuendeleza

Sekta ya Nishati. Vilevile, nishukuru

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

(SADC) kwa ushirikiano katika masuala ya

kikanda yanayohusu Sekta hii. Kwa kipindi

cha mwaka 2019/20 Wizara itaendelea

kushirikiana kwa karibu na Washirika

hawa wa maendeleo na wadau wengine

watakaojitokeza ili kuhakikisha kuwa

Sekta ya Nishati inaendelea kuwa

chachu ya sekta nyingine katika kuleta

maendeleo nchini.

H. SHUKRANI

162. Mheshimiwa Spika, naomba

kutumia fursa hii kumshukuru Naibu Waziri

wa Nishati, Mhe. Subira Khamis Mgalu, (Mb.)

kwa kunisaidia kwa kiasi kikubwa na kwa

dhati kabisa katika kutekeleza majukumu

Page 119: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

115

yangu. Aidha, napenda kumshukuru Katibu

Mkuu Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua kwa

uchapakazi mahiri na ushirikiano anaonipa

katika kutekeleza shughuli za kila siku za

Wizara. Vilevile, nawashukuru Makamishna,

Wakuu wa Idara na Vitengo, Wenyeviti na

Wajumbe wa Bodi, Wakuu wa Taasisi zilizo

chini ya Wizara na Watumishi wote kwa

ujumla kwa ushirikiano wao na juhudi

zao wanazofanya kwa ajili ya kufanikisha

kufikiwa kwa malengo ya Wizara.

163. Mheshimiwa Spika, kwa kipekee

napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru

wananchi wa Jimbo la Chato kwa ushirikiano

wanaonipa katika kutekekeleza shughuli

mbalimbali za maendeleo ya jimbo. Nawaahidi

kuwa sitawaangusha na nitaendelea

kushirikiana nanyi katika kubuni mikakati

mbalimbali ya kuendeleza shughuli za jimbo.

Naishukuru sana familia yangu ikiongozwa

na mke wangu Mama Kalemani pamoja na

watoto wangu kwa kuendelea kuniombea

na kuniunga mkono katika kutekeleza

majukumu ya kitaifa.

Page 120: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

116

I. HITIMISHO

164. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya

Mwaka 2019/20 inalenga kutekeleza

dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa

inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika,

unaotabirika na wenye gharama nafuu.

Vilevile, bajeti imelenga kuimarisha shughuli

za utafutaji na biashara ya mafuta na gesi

asilia pamoja na kuwezesha wananchi

kunufaika na rasilimali hizo. Lengo ni

kuiwezesha Serikali kufikia azma ya kujenga

uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa

kati ifikapo mwaka 2025.

165. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka

2019/20, Wizara ya Nishati inakadiria

kutumia jumla ya Shilingi trilioni 2.142

ikilinganishwa na Shilingi trilioni 1.692

iliyotengwa kwa Mwaka 2018/19, sawa na

ongezeko la asilimia 26.6. Ongezeko hili

limetokana na kuanza kutekelezwa kwa

mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha MW

2,115.

166. Mheshimiwa Spika, fedha nyingi za

ndani za miradi ya maendeleo zilizotengwa

kwa mwaka 2019/20 zimeelekezwa katika

miradi mitatu (3) ya kimkakati ambazo ni

Page 121: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

117

Shilingi trilioni 1.86, sawa na asilimia

95.1 ya Bajeti yote ya Ndani. Miradi hiyo ni:

Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji,

MW 2,115 (Shilingi trilioni 1.44); Mradi

Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini

Awamu ya Tatu (Shilingi bilioni 363.11); na

Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I

Extension MW 185 (Shilingi bilioni 60).

167. Mheshimiwa Spika, naomba

kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu

sasa liidhinishe bajeti ya jumla ya Shilingi

2,142,793,309,000 kwa ajili ya matumizi

ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

(i) Shilingi 2,116,454,000,000 sawa

na asilimia 98.8 kwa ajili ya Miradi ya

Maendeleo. Kati ya fedha hizo za maendeleo,

Shilingi 1,956,372,000,000 ni fedha za

ndani na Shilingi 160,082,000,000 ni fedha

za nje; na

(ii) Shilingi 26,339,309,000 sawa na

asilimia 1.2 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Kati ya fedha hizo Shilingi 15,025,821,000

kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na

Shilingi 11,313,488,000 kwa ajili ya

mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na

Page 122: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

118

Taasisi zilizo chini yake.

168. Mheshimiwa Spika, naomba tena

nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa

Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.

Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya

Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz.

Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali

ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya

ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu

Sekta ya Nishati.

169. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa

hoja.

Page 123: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

119

1A: Mfumo wa Gridi ya Taifa

Na.

Jina la Kituo

Uwezo (MW)

1 Kidatu 204.00

2 Kihansi 180.00

3 Mtera 80.00

4 New Pangani Falls 68.00

5 Hale 21.00

6 Nyumba ya Mungu 8.00

7 Uwemba 0.84

8 Mwenga 4.00

9 Yovi 0.95

10 Matembwe 0.59

11 Darakuta 0.32

12 Andoya 1.00

13 Tulila 5.00

Jumla Ndogo - Maji

573.70

1 Songas 189.00

2 Ubungo Gas PP I 102.00

3 Tegeta Gas PP 45.00

VIELELEZO KUHUSU SEKTA YA

NISHATI

1.0 UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Kielelezo Na. 1: Uwezo wa Mitambo ya

Kufua Umeme Nchini hadi Mwezi Mei,

2019

Page 124: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

120

4 Ubungo Gas PP II 129.00

5 Kinyerezi I 150.00

6 Kinyerezi II 248.22

7 Mtwara Gas PP 22.00

8 Somanga Gas PP 7.50

Jumla Ndogo - Gesi 892.72

1 Zuzu 7.40

2 Nyakato 63.00

3 Biharamuro 4.14

4 Ngara 2.50

5 Songea 7.67

6 Namtumbo 0.34

7 Ludewa 1.27

8 Mbinga 2.00

9 Madaba 0.48

Jumla Ndogo - Mafuta 88.80

1 TANWAT 1.50

2 TPC 9.00

Jumla Ndogo - Biomass 10.50

Jumla - Gridi 1,565.72

Chanzo: TANESCO

Page 125: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

121

1B: Mfumo Nje ya Gridi ya Taifa

Na.

Jina la Kituo

Uwezo (MW)

1 Bukoba 2.56

2 Kasulu 2.50

3 Kibondo 2.50

4 Kigoma 8.25

5 Liwale 0.85

6 Loliondo 5.00

7 Mafia 1.89

8 Mpanda 4.16

9 Sumbawanga 5.00

10 Tunduru 3.00

11 Inyonga 0.48

Jumla – Nje ya Gridi 36.18

Jumla Kuu 1,601.90

Chanzo: TANESCO

Page 126: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

122

Kielelezo Na. 2: Njia za Kusafirisha

Umeme na Vituo vya Kupoza Umeme

Na.

Njia za Usafirishaji Umeme

(Transmission Lines)

Urefu (km)

hadi Mei,

2019

1 Njia kuu za msongo wa 400kV 670

2 Njia kuu za msongo wa 220kV 2,940.7

3 Njia kuu za msongo wa 132kV 1,697.47

4 Njia kuu za msongo wa 66kV 543

Jumla 5,851.17

Na. Vituo Vya Kupoza Umeme

(Substations)

Idadi

1 Vituo vya msongo wa 220kV 20

2 Vituo vya msongo wa 132kV 27

3 Vituo vya msongo wa 66kV 7

4 Vituo vya msongo wa

33/11kV

67

Jumla 121

Na. Urefu wa Mkongo wa

Mawasiliano wa TANESCO

Urefu

1 Mkongo wa Mawasiliano (Op-

tic Fibre Cable) – km

3,200

Chanzo: TANESCO

Page 127: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

123

Kielelezo Na. 3: Taasisi Zilizopatiwa Umeme Kupitia REA hadi

kufikia tarehe 15 Mei, 2019

Na Mradi Taasisi

za Elimu

Biasha-

ra

Pump

za Maji

Taasisi

za Afya

Nyumba

za Ibada

1 Miradi ya Awali 1,099 1,648 64 412 813

2 Turnkey Phase II 1,931 1,743 126 752 53

3 Turnkey Phase III 38 27 10 22 15

4 BTIP_VEI 25 15 3 7 7

5 Densification Round I 21 10 4 1 3

6 Makambako-Songea 45 8 3 11 66

7 Solar za Makonteina 6 0 0 6 27

Jumla 3,165 3,451 210 1,211 984 Chanzo: REA

Page 128: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

Kielelezo Na. 4: Maeneo yenye Viashiria

vya Jotoardhi Nchini

Chanzo: TGDC

124

Page 129: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

125

2.0 MAFUTA NA GESI ASILIA

Kielelezo Na. 5: Matumizi ya Gesi Asilia katika Kipindi cha

Mwaka 2016 – 2018 (BCF)

Chanzo: TPDC

Page 130: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

126

Kielelezo Na. 6: Mwenendo wa Uagizaji Mafuta kwa Matumizi

ya Ndani kwa Mwaka 2018

Chanzo: PBPA

Page 131: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

127

Kielelezo Na. 7: Ujenzi wa Miundombinu ya Kusambaza Gesi

Asilia Majumbani (Mikocheni – Dar es Salaam)

Chanzo: TPDC

Page 132: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

128

Kielelezo Na. 8: Mtambo wa Kupunguza Msukumo wa Gesi

Asilia (Pressure Reduction and Metering Station – PRSM)

uliosimikwa Ubungo Kibo katika Valvu Na. 15

Chanzo: TPDC

Page 133: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

129

Kielelezo Na. 9: Mpango wa Kusambaza Gesi Asilia Mtwara

(kwa kuanzia eneo la Bandari)

Chanzo: TPDC

Page 134: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

Kielelezo Na. 10: Mpango wa Kusambaza

Gesi Asilia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

(UDSM)

Chanzo: TPDC

130

Page 135: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

131

Kielelezo Na. 11: Gesi ya Kupikia (LPG) iliyoagizwa Nchini kwa

Mwaka 2010 – 2018

Chanzo: EWURA

Page 136: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

132

Kielelezo Na. 12: Wastani wa Mauzo ya Mafuta Kimkoa katika

Vituo mbalimbali Nchini

Mikoa Wastani wa Matumizi

ya Mafuta kwa

Mwaka (Lita)

Idadi ya

Vituo vya

Mafuta

Wastani wa

Mauzo kwa

Kituo kwa

Mwaka

(Lita)

Arusha 96,950,638 98 989,292

Coast 74,434,223 94 791,853

Dar es Salaam 493,472,968 200 2,467,365

Dodoma 54,953,984 66 832,636

Geita 18,332,546 55 333,319

Iringa 43,023,787 34 1,265,405

Kagera 32,530,523 70 464,722

Katavi 4,839,897 9 537,766

Kigoma 13,708,412 44 311,555

Kilimanjaro 52,070,384 92 565,982

Page 137: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

133

Mikoa Wastani wa Matumizi

ya Mafuta kwa

Mwaka (Lita)

Idadi ya

Vituo vya

Mafuta

Wastani wa

Mauzo kwa

Kituo kwa

Mwaka

(Lita)

Lindi 14,020,811 32 438,150

Manyara 15,105,887 48 314,706

Mara 14,038,293 55 255,242

Mbeya 80,767,764 62 1,302,706

Morogoro 61,203,623 73 838,406

Mtwara 51,121,346 36 1,420,037

Mwanza 137,426,041 88 1,561,660

Njombe 29,818,207 32 931,819

Rukwa 13,741,841 17 808,344

Ruvuma 30,352,084 39 778,259

Shinyanga 35,280,506 53 665,670

Simiyu 3,654,477 26 140,557

Page 138: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

134

Mikoa Wastani wa Matumizi

ya Mafuta kwa

Mwaka (Lita)

Idadi ya

Vituo vya

Mafuta

Wastani wa

Mauzo kwa

Kituo kwa

Mwaka

(Lita)

Singida 16,445,910 20 822,296

Songwe 9,187,073 28 328,110

Tabora 18,125,550 30 604,185

Tanga 59,305,549 59 1,005,179

Jumla 1,473,912,325 1,460 20,775,220

Chanzo: EWURA

Page 139: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

135

Kielelezo Na. 13: Mwenendo wa Bei za Mafuta Safi katika

Soko la Dunia kwa Mwaka 2017 na 2018

Chanzo: EWURA

Page 140: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

136

Kielelezo Na. 14: Idadi ya Vituo vya

Mafuta Nchini hadi Mwezi Aprili, 2019

MKOA

JUMLA YA

VITUO VYA

MAFUTA HADI

TAREHE 31

DESEMBA 2018

JUMLA YA

VITUO VYA

MAFUTA HADI

TAREHE 30

APRILI 2019

Arusha 98 98

Coast 94 104

Dar es Salaam 200 220

Dodoma 66 64

Geita 55 60

Iringa 34 35

Kagera 70 65

Katavi 9 11

Kigoma 44 39

Kilimanjaro 92 92

Lindi 32 25

Manyara 48 50

Mara 55 56

Mbeya 62 64

Morogoro 73 71

Mtwara 36 36

Mwanza 88 89

Njombe 32 32

Rukwa 17 18

Ruvuma 39 37

Shinyanga 53 59

Page 141: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

137

MKOA

JUMLA YA

VITUO VYA

MAFUTA HADI

TAREHE 31

DESEMBA 2018

JUMLA YA

VITUO VYA

MAFUTA HADI

TAREHE 30

APRILI 2019

Simiyu 26 28

Singida 20 22

Songwe 28 29

Tabora 30 31

Tanga 59 65

JUMLA YA

IDADI YA

VITUO VYA

MAFUTA

1460

1500

Chanzo: EWURA

Page 142: VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI · Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa

138

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori (wa kwanza kushoto), wakiwasha jiko linalotumia gesi asilia tayari kwa matumizi ya nyumbani katika eneo la Mikocheni Mtaa wa TPDC jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Palangu wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,

Pololiti Mgema.