6
1 WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Zamani nikiwa na umri mdogo nilifahamishwa kuwa ukiangalia sana Mwezi utaona Nabii Elia amekalia kiti na amevaa taji, kainama anasikitikia Dunia. Dunia iliyojaa Chuki, Dhiki,Dhambi na Damu ya Uasi wa kiroho. Nikawa naona ni kweli. Katika utu uzima wangu tarehe 7 Septemba, 2015 ghafla naangalia Mwezi naona picha ya John Magufuli, amekalia kiti, kashika Katiba ya Tanzania. Pembeni ya kiti kuna maneno yameandikwa “Ikulu Takatifu” yamezungukwa na maua ya rangi ya kijani na njano; picha ya nembo ya Taifa al-maarufu Adam na Eva na Bendera ya Taifa vimepamba kofia yake. Aidha, kuna imani kuwa, Mawingu hutoa maumbo au picha mbalimbali,mfano ukiliona umbo la samaki ni dalili ya neema kwako; umbo linaloonesha tendo la ndoa ukiliona ni Uchuro hapo kuna kifo au nuksi kubwa; lakini umbo la sura ya mtu ni kiashiria cha mateso na misukosuko ya kutafuta mafanikio bila kuyapata kwa mtu huyo. Naliangalia wingu naona picha ya Edward Lowasa, ina maneno ya Kiingereza No!, No! No! na mengine yakiwa “Ahsante Sana Watanzania, Mungu yu pamoja nami . Ghafla nazimia namuona Mwalimu Nyerere ameongozana na Wavuta kiko maarufu Sebastian Kinyondo na Kamanda Abdalah Natepe wanavuta kiko zao zinatoa harufu ya udi wanapiga kelele “Tunafukuza harufu ya chuki, damu, ufisadi, na kuilinda Ikulu”. Wananipa Waraka nimpe John Magufuli, Edward Lowasa, na Watanzania usemao; Watanzania wangu, hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa ndiyo wamiliki wa Ikulu kuliko Wagombea wenu? Na kuwa radhi yangu inakaa ndani yenu?. Kama mtu akiiharibu Ikulu kwa kumchagua Mgombea fisadi Mungu atamharibu mtu huyo, kwa maana Ikulu ni mahala patakatifu, na ni miliki ya Taifa lenu. Wagombea wote ni halali, bali si wote watakaoijenga hadhi ya Ikulu kwani John, na Edward wana karama tofauti lakini Tanzania ni ileile. Ikulu ilijengwa na Wajerumani mwaka 1891 na Gavana Chakosi Dikwe na kutumika kama ngome yake, hadhi na siri zake zingali zinakumbukwa huku Kuzimu. Damu za Askari walioiharibu Ikulu wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia inawalilia Wanangu mlio hai. Jasho la Gavana wa kwanza wa kijerumani ndugu Horrace Byatt aliyeboresha Ikulu Mwaka 1919 lingali linalowesha Sanda za Askari hao na kufuta damu zao kila siku. Byatt analia na ananiuliza “Mwalimu Watanzania wanajua kuwa baada ya mimi kuingia madarakani nililazimika kukaa katika makazi ya muda kwenye ofisi zao za wizara ya Afya ili Ikulu iwe Mahala patakatifu?”. Kama mnavyofahamu,

WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

1

WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM

(taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Zamani nikiwa na umri mdogo nilifahamishwa kuwa ukiangalia sana Mwezi utaona Nabii Elia amekalia kiti na amevaa taji, kainama anasikitikia Dunia. Dunia iliyojaa Chuki, Dhiki,Dhambi na Damu ya Uasi wa kiroho. Nikawa naona ni kweli. Katika utu uzima wangu tarehe 7 Septemba, 2015 ghafla naangalia Mwezi naona picha ya John Magufuli, amekalia kiti, kashika Katiba ya Tanzania. Pembeni ya kiti kuna maneno yameandikwa “Ikulu Takatifu” yamezungukwa na maua ya rangi ya kijani na njano; picha ya nembo ya Taifa al-maarufu Adam na Eva na Bendera ya Taifa vimepamba kofia yake. Aidha, kuna imani kuwa, Mawingu hutoa maumbo au picha mbalimbali,mfano ukiliona umbo la samaki ni dalili ya neema kwako; umbo linaloonesha tendo la ndoa ukiliona ni Uchuro hapo kuna kifo au nuksi kubwa; lakini umbo la sura ya mtu ni kiashiria cha mateso na misukosuko ya kutafuta mafanikio bila kuyapata kwa mtu huyo. Naliangalia wingu naona picha ya Edward Lowasa, ina maneno ya Kiingereza No!, No! No! na mengine yakiwa “Ahsante Sana Watanzania, Mungu yu pamoja nami”. Ghafla nazimia namuona Mwalimu Nyerere ameongozana na Wavuta kiko maarufu Sebastian Kinyondo na Kamanda Abdalah Natepe wanavuta kiko zao zinatoa harufu ya udi wanapiga kelele “Tunafukuza harufu ya chuki, damu, ufisadi, na kuilinda Ikulu”. Wananipa Waraka nimpe John Magufuli, Edward Lowasa, na Watanzania usemao;

Watanzania wangu, hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa ndiyo wamiliki wa Ikulu kuliko Wagombea wenu? Na kuwa radhi yangu inakaa ndani yenu?. Kama mtu akiiharibu Ikulu kwa kumchagua Mgombea fisadi Mungu atamharibu mtu huyo, kwa maana Ikulu ni mahala patakatifu, na ni miliki ya Taifa lenu. Wagombea wote ni halali, bali si wote watakaoijenga hadhi ya Ikulu kwani John, na Edward wana karama tofauti lakini Tanzania ni ileile.

Ikulu ilijengwa na Wajerumani mwaka 1891 na Gavana Chakosi Dikwe na kutumika kama ngome yake, hadhi na siri zake zingali zinakumbukwa huku Kuzimu. Damu za Askari walioiharibu Ikulu wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia inawalilia Wanangu mlio hai. Jasho la Gavana wa kwanza wa kijerumani ndugu Horrace Byatt aliyeboresha Ikulu Mwaka 1919 lingali linalowesha Sanda za Askari hao na kufuta damu zao kila siku. Byatt analia na ananiuliza “Mwalimu Watanzania wanajua kuwa baada ya mimi kuingia madarakani nililazimika kukaa katika makazi ya muda kwenye ofisi zao za wizara ya Afya ili Ikulu iwe Mahala patakatifu?”. Kama mnavyofahamu,

Page 2: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

2

Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Ukoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo (state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana wa Kiswahili Sir Unapima Mkali aliyechukua utawala anawalilia Watanzania wasipoteze hadhi ya Ikulu. Ndugu J. H Sinclair - Mtaalam wa majengo wakati wa ukoloni aliyetia nakshi za jengo hilo anawaomba mboreshe Ikulu kwa dhana ya kuchagua Rais safi na alinde Uadilifu. Ikulu maana yake ni Itetemia lenye asili ya Kinyamwezi hasa enzi za mtemi Milambo, Makao Makuu ya ngome ya milambo yenye Uadilifu na hadhi paliitwa kwikulu, ndio neno ikulu likatoholewa.

Edward kichwa chake chenye mvi ni taji ya utukufu wa Mashabiki wa siasa wasio na weledi wa uchambuzi, lakini kikionekana katika njia ya haki kitalinda hadhi ya Ikulu na nje ya njia ya haki ni laana ya Watanzania karne na karne zijazo. Ushujaa wa uchapakazi na Uadilifu wa John ni Lulu ya Utulivu na Ushindi wa CCM unaozidi ustawi wa Ngome ya UKAWA yenye karama nyingi zinazojumuisha kuwapoteza Prof Haruna na Padre Mstahafu Wilbroad.

Kijana wangu Edward, unafahamu kuwa amdhihakiye Maskini humsuta Muumba wake, unapoongelea Umaskini katika safari ya Ikulu uwe makini, ukifika Ikulu uwe radhi kugawa nusu ya Mali zako kuwapa Maskini; na ujue kuwa changamoto ya Watanzania ni uwezo wa kugawanya rasilimali zao lukuki, Ugawanyaji wa Mapato yao na Uimarishaji wa Uchumi endelevu; dhana ya Umaskini ni Matokeo na siyo chanzo cha Changamoto; aidha, ujue kuwa ajitengaye na CCM hutafuta matakwa yake mwenyewe kwenda Ikulu; je una msingi imara wa muundo wa kichama kuenzi “Utatu wa Elimu” yaani “Elimu, Elimu,Elimu” unaoenzi Azimio langu la Musoma?. Mwanangu Edward nakutakia heri iliyo na nuru kuenzi Elimu maana kumbuka niliwaachia Imani kuwa “Elimu ni Ufunguo wa Maisha”.

Kijana wangu John moyo wako umechangamka na ni dawa nzuri ya kukimbilia Ikulu; hekima ipo machoni pako kwani una Ufahamu, isipokuwa uhamasike sana ndani ya Kampeni, hujafika bado Ikulu,usishibe kabla hujala, usioge hujavua nguo; ongeza kasi Ikulu inakukaribia. Tanzania yangu unataka iwe ya Uchumi wa viwanda utakaolinda utajiri wa Mafuta na Gesi ukifungamanishwa na Sekta zingine ili zisije zikafa kwa kukosa nguvu kazi itakayoweza kukimbilia kwenye Mafuta na Gesi, watakakolipwa ujira zaidi na kuacha Sekta zingine kama vile Kilimo. John ndoto zako za kuboresha Ujasilia-Mali ndani ya Uchumi wa viwanda ni wazi utapunguza Umaskini na Kuweka Maendeleo ya Uchumi endelevu; utapunguza gharama za Uzalishaji na kupanua uwezo wa Wananchi kulipa kodi. Lakini nakutakia heri katika jitihada za kufufua viwanda na Ikulu ipo ndani ya mboni zako. Wewe ni Mkemia hapana shaka Viwanda vya mbolea vitapata mtu, uhifadhi wa mazingira utaboreka na ukiwa Mwanahisabati Tanzania itafanya kazi ki-Mahesabu. Ukiwa Ikulu anzisha Mifuko miwili ya Hifadhi ya Mapato ya Mafuta na Gesi; mmoja wa kuimarisha Mapato dhidi ya Mnyumbo wa Uchumi (Stalization Fund), na mwingine wa Uhifadhi wa Mapato kwa Vizazi vijavyo (Saving Fund) ili uchumi wa viwanda uwe endelevu; hiyo iwe sambamba na Uadilifu wa Matumizi ya Mapato..

Nimetambua kuwa kuna vyama vinanipa tabu huku Kuzimu;ACT ni watu wasio na nguvu, lakini hujiwekea Hazina ya kisiasa wakati wa Heri ya Ikulu; NLD ni watu dhaifu lakini hujibanza ndani ya mabawa ya UKAWA huo ni ulaghai wa kisiasa; CHADEMA na CUF hawana Wafalme zao Wilboad na Haruna Ngunyuru waliozama chini ya kivuli

Page 3: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

3

kinachoficha demokrasia, lakini vyama hivyo vinakodi Wafalme huku wakienda pamoja vikosi vikosi ndani ya UKAWA; CCM hushika ubora wa Ilani yake wakimiliki Ikulu ya Kivukoni, wakifurahia Upendo kwa nyimbo na lugha zilizojaa Mithali. Vyama hivi huwachanganya Wananchi hawajui mwelekeo na Dira ya Uchaguzi Mkuu.

Kijana wangu John, nia yako ya kushughulikia maovu kwa moyo ni yako kama Mwanadamu, jawabu la ulimi wako wenye Upako hutoka kwetu huku Kuzimu na kwa Mungu. Mkabidhi Mungu Sera na Mawazo yako yatathibitika. Ulimi huo ni kama fedha yenye thamani ndani ya soko la ndani na la nje linalopambana na myumbo wa uchumi; fedha itakayofanikisha afya, elimu, maji, umeme na miundombinu laini na migumu, ili Ikulu ithibitike. Matunda yangu na akina Rashid Kawawa, Oscar Kambona, Job Lusinde, Amir Jamar, Nsilo Swai, Tewa Said Tewa, Chief Abdalah Fundikila, Dereck Bryceson, Paul Bomani, Sir Ernest Vasseey, Sir George Kahama, Chief Abdalah Fundikira, Chifu Lukumbuzya, Chief Adam Sapi Mkwawa, Mwami Theresia Ntare na wengine hupita thamani ya dhahabu na vito ndiyo maana Ikulu ililinda Haki. Ukifuata nyendo zangu ni mwanzo wa mwendelezo wa hekima na utakatifu utakaoongeza Ufahamu wako.

Mungu amewachukua Mashujaa wangu wote, wachache waliobaki watumieni; Mimi nilipata mateso ya Watanzania na fimbo yangu hadi mkaniita “Musa” na kwavile niliwatoa kwenye bwawa la mateso ya Kikoloni; Mungu aliniongoza katika giza wala si katika nuru nilipokuwa Ikulu; nilichakaa nyama yangu na ngozi yangu; hadi nikafariki mapema kuliko Nelson Mandela kwa kuwapenda Watanzania kubeba mzigo wa Ikulu. Wanangu Watanzania; mmegeuza njia zangu zenye neema, mnararua rarua Sanda yangu; mmenifanya mkiwa huku Butiama kwa ushabiki wa kisiasa, uliokosa tija ya fikra na uchambuzi wa kina. Kumbukeni msiba wangu mlipolia mimi niliililia Ikulu, na Ikulu ilinililia “Baba yangu, Baba yangu wa Taifa Mbona Unaniacha?” nami nikatamka “Unyerere Umekwisha” nikakata roho.

Macho yangu yanatoa machozi hayakomi, ningali naililia Ikulu yangu; babu na bibi zenu waliowarithisha Ikulu wanalia, watoto zenu waliowakopesha Ikulu ambao ni samani ya Tanzania wataomboleza kama mtachagua Rais kwa ushabiki wa kisiasa. Wanangu John na Edward, urithi wenu umegeuka kuwa mali ya Wageni na utajiri kuwa mali ya Mafisadi. Watanzania wangu wamekuwa yatima walionyang’anywa urithi wao. Ondoeni pepo la unyonyaji wa rasilimali zetu ili mlinde ushindani wa Wawekezaji wa nje na wa ndani katika Mnyororo wa Thamani wa Uwekezaji; kumbukeni, Kiatu cha Mwanangu Jakaya Kikwete kiliisha sori kulinda hadhi ya Ikulu, aliwatafutia Neema ndani na nje ya nchi; Watanzania walio wengi hamkumsaidia, kazi yenu ikawa kulalama badala ya kufanya kazi, mkitaka akae Msoga aende Ikulu kila siku mithiri ya Mfanyakazi wa kawaida; mkatenganisha Ikulu na Urais kwa kupigwa upofu wa fikra mkilinganisha gharama za Ikulu na za kununua bamia. Lakini mmesahau Yesu Kristo, Mtume Mohammad (S.A.W), Nabii Musa na wengine hawakutulia kuwaletea Waja wa Mola Neema na Ukombozi; yu heri Rais Jakaya Kikwete aliyeenzi Mila na Desturi ya ki-Afrika kuwa Muwindaji (Mfwimi) kwa kuwapa Neema na Ukombozi wa ki-Uchumi.

Watanzania wangu, Albino mmewafanya wanyama¸ Binti Kabula Nkalango, Said Abdalah, Nainana Daud,, Rukia Halfan na Fatma Halfan damu zao na viungo vyao vingali vinavuja damu; Wauaji waliohukumiwa kunyogwa; Joseph Lugala,, Masumbuko Madata, Emmanuel Masangwa, Charles Masangwa, Nchenyewe Kisiwa, Sayi Gamaya, Mboje Mawe, Sayi Matizi, na Kazimir Mashauri roho zao zinatuchefua huku Kuzimu;

Page 4: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

4

Chozi la Peter Kayanza Pinda halijakauka katika Sanda zetu. Vijana wangu John na Edward mnapokwenda Ikulu zibeni Chemchem ya damu za Albino anzeni alipomalizia Mhe Jakaya.

Mama zenu wamekuwa kama wajane mbali ya Mwanangu Jakaya Kikwete kuwajali kwa hali na mali kwa mfano ameteua Wanawake wengi kuwa Majaji, hii ni kuenzi kazi yetu ya tarehe 1 Septemba, 1970 ambapo Tanzania ilikuwa Nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuteua Hakimu Mkaazi Mwanamke; tulikuwa na uchache wa Mahakimu Wakazi wakiwa 44 tu kati yao watatu wa-Nigeria, watano wa-Malawi na 36 wa-Tanzania. Jaji Mkuu wa kwanza alikuwa Jaji Said aliyeteuliwa 1971 na Jaji Mkuu wa kwanza wa Mhakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki alikuwa Raia wa Tanzania; Ahsante Jakaya Kikwete umetusetiri huku kuzimu akina mama wanakuombea maisha marefu kwani wanaamini majaji wanawake watalinda Utawala wa Sheria mithiri ya binti wa Faraoh aliyelinda Utawala wa Sheria dhidi ya Nabii Musa ndani ya nyumba ya Faraoh baada ya kuokotwa baharini.

Nyuso za vikongwe hazipewi heshima huitwa Wachawi utafikiri nyie hamtazeeka, mlidiriki kuchoma nyumba zao zaidi ya 20 wakati mnajua Katiba niliowaachia inazuia Mauwaji,Ukandamizaji na Utesaji ambacho ni kinyume hata cha Sheria ya Makosa ya Jinai na Sheria ya Uchawi ya Mwaka 1928; damu za waliouwawa kwa imani za Uchawi Agripina Thomas, Anamaria Theda, Monica Spron wote wa Kagera, Amana Shawishi wa Mwanza, Lyatoga Venance wa Makongoro Nansio, Cheupe Mwananzyuni wa Rukwa na Frank Mwasha wa Nzega zinaililia Ikulu na Upendo kwa Watanzania;

Mabinti zenu wanabakwa na kukatizwa masomo, mabikra ni wa kuhesabu. Watoto wa kiume hulawitiwa kinyume na Kifungu Na 156(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai. Roho zetu zinamuombolezea mtoto wa miaka 13 wa Sumbawanga aliyetelekezwa na mama yake muuza bia bar mjini Mbeya, mtoto aliyefiwa na baba yake akiwa na miaka saba aliyelawitiwa kwa siku tatu na baba wa miaka 51 aliyekuwa akifanya kazi Kampuni ya Majembe Auction Mart Sumbawanga kwavile mtoto aliishi katika mazingira magumu; Aidha, Wakulima na Wafugaji mnauwana mashamba na mifugo imekuwa bora kuliko roho zenu.

Enzi zangu moja ya Madhumuni ya Mwongozo wa TANU wa 1971 ilikuwa kulinda maslahi ya Wananchi. Hata China baada ya nguvu ya dola kuwa mikononi mwa Wananchi Rais Mao Tse Tung alisema; “Hamtaki kuangusha nguvu ya Dola? Ndiyo, tunataka, lakini siyo kwa sasa , hatuwezi kufanya sasa; kwa nini? Kwasababu Ubeberu bado upo, kwasababu migogoro ya ndani bado ipo, tofauti ndani ya jamii bado ipo. Kazi yetu kwa sasa ni kuboresha vyombo vya Dola; Jeshi la Ulinzi, Polisi, na Mahakama ili kuunganisha ulinzi wa Taifa na kuwalinda watu na maslahi yao” Watanzania wangu msikimbilie kuondoa Dola linaloongozwa na CCM,kwani changamoto zilizopo zinahitaji pia kuboresha ulinzi na usalama. Wanajeshi waboreshewe maisha yao, ili Ugaidi umalizwe. Wanajeshi wakazane kuwalinda wasije wakatamani Ikulu kama yaliyonikuta Mwaka 1964 ambapo nilimkimbia Mpenzi wangu Mariah hadi leo hamjui wengine husema niliivaa baibui kutorokea Kigamboni, wengine hudai nilijificha Kanisa la St Peter Oysterbay kila mtu anasema anachojua, msilogwe ndugu zangu Ikulu pagumu.

Waulizeni Sir George Kahama, Job Lusinde Mawaziri wangu Ofisi ya Rais wawaeleze, aidha,Uchovu alioupata Waziri mwenzao wa Ofisi ya Rais Bwana A.K Hanga

Page 5: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

5

unashuhudia Uasi huo huku Kuzimu. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu sasa cheo mnakiita Katibu Mkuu Dkt Amon James Nsekela (1963-1964) anaomba msiguse machungu ya majonzi dhidi ya Uhaini aliyonayo huku Kuzimu. Aliyempokea na kudumu kwa muda mrefu Bwana H.K Talawa (1964-1980) na kuteseka pia na vita ya Uganda anatoa chozi la kuiombea Tanzania Amani. Makatibu Wakuu Viongozi wa wakati huo Danstun Afred Omari (1962-1964) na Joseph Augustino Namata (1964-1967) wametandika mikeka huku Kuzimu wakiombolezea Hatma ya Tanzania.

Dhana ya vyama vingi ilenge kujenga umoja; demokrasia ilenge kuwaunganisha kama ndugu, na Taifa moja. Enzini sera za Kwame Nkrumah wa Ghana na Castro wa Cuba 1969. “Mabadiliko ya utawala yalichukuliwa kuwa siyo kuleta demokrasia, ila kuwaunganisha Waafrika; mfumo wa utawala wa ukoloni ulizingatia kuengua demokrasia mpya na ya zamani; na kuweka lengo la mbali la Serikali huru ya Waafrika, kwa ufupi ulikuwa utawala wa ukoloni wa Waafrika” Hivyo ni vyema kufikiria kuutoa ukoloni wa kiafrika ndani ya vyama vyenu kuliko kufikiria kuiuwa CCM chama changu kitakatifu. Ukoloni upo pia kwa CUFists na CHADEmists, kwani nguvu ya vyama vya upinzani huzuka wakati wa Uchaguzi tu na kujaza ndugu wa kabila moja,dini moja au Ukanda; hii ni hatari kwa Mustakhbari wa Ikulu endelevu na Taifa kwa ujumla. Hofu ni kuwa mkichagua UKAWA itachukua muda mrefu kujenga mnyororo wa thamani baina ya chama kimoja na kingine ndani ya UKAWA, badala ya kuimarisha uchumi na Taifa endelevu katika nchi yangu; kwani Ikulu itawanogea watu hao. Na hii itahusisha kodi za Wananchi. Hili ni Angalizo tu sipendi kuhukumu.

CCM yangu; yu heri Edward aliyekengeusha msimamo wake na kukaa kwenye Bwawa lenye kelele mithiri ya Bwawa lililojaa vyura wajawazito; kuliko Oscar Kambona, Anangisye, na Wabunge watano tuliowasimamisha Mwaka 1968 kwa kukiuka Imani za TANU na Sera zake. Mchukulieni Edward kama Kasanga Tumbo kiongozi wa Chama cha People’s Democratic (PDP) Mbunge aliyewekwa kizuizini kuanzi Januari 1964 hadi Julai 1966 aliyekuwa mkorofi dhidi ya Sheria ya kuwekwa kizuizini ya tarehe 26 Septemba, 1962; Edward alipinga utaratibu wa ngazi ya mchujo kwa kukengeusha nafsi yake kisiasa, kuitafuta demokrasia yake Kikatiba, akafuatwa na wengine na sasa ni mithiri ya Mpiga filimbi wa Hamelini; amejiweka kizuizini ndani ya uwanja wa siasa. Msishangae ni elimu ya Utamaduni aliyopata Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na ile ya Maendeleo yaki-Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha Barth Marekani, yafaa sasa alinganishwe na Mwanahisabati na Mkemia Mkufunzi John ili kumpata Mkalia Ikulu mahala patakatifu.

Siyo ajabu kutofautiana, hata sisi tulipoanzisha Operasheni Vijana tarehe 3 Oktoba 1968 kuzuia nguo fupi zilizoigwa kwa Wazungu, na muziki wa Marekani, alitokea Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyewahamasisha Wamasai kuacha nguo za Mataifa ya Magharibi walinde mila, desturi na asili yao wavae nguo zilizowaacha utupu kuliko hata za Magharibi. Mnamo Agosti, Afisa wa Ubalozi wa China alishindwa kulazimisha uzuiaji wa picha za Marekani, viatu vya uvuvi, kwavile vilikinzana na Utawala wa China.

Watanzania wangu, maana kwa ajili yenu mmepewa Guru wa kazi, na uweza wa dola la Ikulu utakuwa begani mwake, naye ataitwa uzao wa ajabu, Rais mwenye nguvu. Ole wao wapiga kura Wanafiki, maana kilio cha majuto kitakuwa kingi kuliko mafuriko ya Upendo ya kushangaa Kampeni. Siwakatazi Watanzania wangu, jikusanyeni bila haya kabla hamjaanza kupiga kura, mtafuteni Rais enyi nyote mlio wanyenyekevu wa

Page 6: WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZANIA

6

Tanzania, itafuteni haki ya Ikulu, kwani miongoni mwa wote waliompenda Edward hakuna hata mmoja amfarijiye, rafiki zake wote wa kisiasa wamemtenda hila sasa wamekuwa adui zake anakaa kati ya makafiri wa kisiasa, haoni raha iwayo yote na wote waliomfuata wamempata katika dhiki yake. Watu wake wote wana tafuta chakula, yumkini kuwatuhumu kuwa ni Wanafiki.

MUNGU IBARIKI TANZANIA IBARIKI AFRIKA