3
1 WARAKA WA UPENDO DHIDI YA JOHN MAGUFULI [CCM] NA EDWARD LOWASA [UKAWA] KUTOKA KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE Rai ya Mtanzania Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Ninavuta shuka langu ghafla Napata usingizi mzito, ndoto yanijia naona Kwanya za dini zote zinaimba nyimbo za kuomboleza; kulia yupo Kapteni John Komba analia sana, kushoto yupo Brigedia Hashimu Mbitah kanuna sana; nyuma yangu naitwa na Mwalimu Nyerere ameongozana na Peter Kisumo, Abdalah Natepe, Thabiti Kombo, Bibi Titi Mohammed na Mama Rhoda Kahatano; Mwalimu ananipa waraka niwape Watanzania kwa ajili ya wagombea wawili John Magufuri na Edward Lowasa usemao; Nijaposema kwa lugha za kuzimu na za Winston Churchil, Mao Tse-tung, Augustine Neto, Gamal Abdel Nasser Hussein na Kwame Nkrumah, kama Watanzania hamna Upendo mmekuwa sawa na Bunduki SMG itakayomwaga damu yenu, na upatu uvumao kumpata Rais Mbabaishaji. Tena nijapokuwa na Unabii kama Rais wa Kwanza wa Tanzania na kujua siri zote za Taifa langu na Maarifa yote niliyoyafanya na kuwaachia Watanzania, nijapokuwa na Imani timilifu dhidi ya Wagombea wenu John Magufuri na Edward Lowasa kiasi cha kuweza kuhamisha Akili za Watanzania kuwa na Moyo wa Maendeleo, tofauti na nilivyowaacha tarehe 14 Oktoba, 1999 kama hamtakuwa na Upendo basi si Kitu nyie na mtakuwa kama Bweha wanyemeleao mizoga iliyotanda ndani ya Uwanja wa Siasa Barani Afrika. Tanzania itakuwa kama Ethiopia, Sudan au Rwanda Amani itapotea. Watoto wachanga watanyonya matiti ya Maiti za mama zao, watainua maiti za mama zao wakilia bila mafanikio, wapendeni watoto kama Mtume Muhammad (saw) anavyosema “Mtu anayembusu mtoto wake, Mwenyezi Mungu humwandikia amali njema, na mtu anayemfurahisha mtoto wake Mwenyezi Mungu atamfurahisha Siku ya Kiyama". (Usulul Kafi: 6-49); aidha, ndugu zangu, akina mama watabakwa, vikongwe watakufa njaa, na mafuvu yatatapakaa nchi nzima. Tena nilitoa Mali na akili zangu kuwalisha Maskini wa Tanzania kwa kile nilichokiita Kuondoa Ujinga, Umaskini na Maradhi , tena nilijitoa kuutafuta Uhuru niliteseka na Azimio la Arusha [Ujamaa na Kujitegemea], Azimio la Iringa [Siasa ni Kilimo], Azimio la Musoma [Elimu kwa Wote] mithiri ya kuungua moto, kama Watanzania hamna Upendo haifai kitu. Msipende kuilaumu CCM kwani sikupumzika na Matatizo toka tulipopata Uhuru. Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano toka 1961 tulikabiriwa na Jeshi la Tanganyika Rifles kuasi Mnamo tarehe 20 Januari, 1964 Jeshi langu likiongozwa na Jenerali Morisho Sarakikya, hali ya kisiasa ikawa tete, Uchumi ukayumba; Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia 1969 baada ya Azimio la Arusha tulikumbwa na Ukame, mazao yetu kama Karafuu, Katani, Pamba, Kahawa, Pareto na Almasi yalikosa soko na kushuka bei katika soko la Dunia; ukuaji wa pato la taifa ulikuwa hauzidi asilimia 4.8%, aidha, lilishuka tena hadi asilimia 3%; mnamo 1972 tulikuwa na Matatizo ya Kisiasa Afrika Mashariki na Jumuiya ikavunjika na wakati huohuo tarehe 7 Aprili, 1972 nilimpoteza kaka yangu kipenzi Sheh Abeid Karume; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano hadi 1977 tukapata shida ya njaa iliyotokana na Ukame wa 1974, nililazimishwa na Wahisani

WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE

1

WARAKA WA UPENDO DHIDI YA JOHN MAGUFULI [CCM] NA EDWARD LOWASA

[UKAWA] KUTOKA KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE

Rai ya Mtanzania

Na

Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Ninavuta shuka langu ghafla Napata usingizi mzito, ndoto yanijia naona Kwanya za dini zote

zinaimba nyimbo za kuomboleza; kulia yupo Kapteni John Komba analia sana, kushoto yupo

Brigedia Hashimu Mbitah kanuna sana; nyuma yangu naitwa na Mwalimu Nyerere ameongozana na

Peter Kisumo, Abdalah Natepe, Thabiti Kombo, Bibi Titi Mohammed na Mama Rhoda Kahatano;

Mwalimu ananipa waraka niwape Watanzania kwa ajili ya wagombea wawili John Magufuri na

Edward Lowasa usemao;

Nijaposema kwa lugha za kuzimu na za Winston Churchil, Mao Tse-tung, Augustine Neto, Gamal

Abdel Nasser Hussein na Kwame Nkrumah, kama Watanzania hamna Upendo mmekuwa sawa na

Bunduki SMG itakayomwaga damu yenu, na upatu uvumao kumpata Rais Mbabaishaji. Tena

nijapokuwa na Unabii kama Rais wa Kwanza wa Tanzania na kujua siri zote za Taifa langu na

Maarifa yote niliyoyafanya na kuwaachia Watanzania, nijapokuwa na Imani timilifu dhidi ya

Wagombea wenu John Magufuri na Edward Lowasa kiasi cha kuweza kuhamisha Akili za

Watanzania kuwa na Moyo wa Maendeleo, tofauti na nilivyowaacha tarehe 14 Oktoba, 1999 kama

hamtakuwa na Upendo basi si Kitu nyie na mtakuwa kama Bweha wanyemeleao mizoga iliyotanda

ndani ya Uwanja wa Siasa Barani Afrika. Tanzania itakuwa kama Ethiopia, Sudan au Rwanda Amani

itapotea. Watoto wachanga watanyonya matiti ya Maiti za mama zao, watainua maiti za mama zao

wakilia bila mafanikio, wapendeni watoto kama Mtume Muhammad (saw) anavyosema “Mtu

anayembusu mtoto wake, Mwenyezi Mungu humwandikia amali njema, na mtu anayemfurahisha

mtoto wake Mwenyezi Mungu atamfurahisha Siku ya Kiyama". (Usulul Kafi: 6-49); aidha, ndugu

zangu, akina mama watabakwa, vikongwe watakufa njaa, na mafuvu yatatapakaa nchi nzima.

Tena nilitoa Mali na akili zangu kuwalisha Maskini wa Tanzania kwa kile nilichokiita Kuondoa

Ujinga, Umaskini na Maradhi , tena nilijitoa kuutafuta Uhuru niliteseka na Azimio la Arusha [Ujamaa

na Kujitegemea], Azimio la Iringa [Siasa ni Kilimo], Azimio la Musoma [Elimu kwa Wote] mithiri ya

kuungua moto, kama Watanzania hamna Upendo haifai kitu.

Msipende kuilaumu CCM kwani sikupumzika na Matatizo toka tulipopata Uhuru. Mpango wa

Maendeleo wa Miaka Mitano toka 1961 tulikabiriwa na Jeshi la Tanganyika Rifles kuasi

Mnamo tarehe 20 Januari, 1964 Jeshi langu likiongozwa na Jenerali Morisho Sarakikya, hali ya kisiasa ikawa tete, Uchumi ukayumba; Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka

Mitano kuanzia 1969 baada ya Azimio la Arusha tulikumbwa na Ukame, mazao yetu kama Karafuu,

Katani, Pamba, Kahawa, Pareto na Almasi yalikosa soko na kushuka bei katika soko la Dunia; ukuaji

wa pato la taifa ulikuwa hauzidi asilimia 4.8%, aidha, lilishuka tena hadi asilimia 3%; mnamo 1972

tulikuwa na Matatizo ya Kisiasa Afrika Mashariki na Jumuiya ikavunjika na wakati huohuo tarehe 7

Aprili, 1972 nilimpoteza kaka yangu kipenzi Sheh Abeid Karume; Mpango wa Maendeleo wa Miaka

Mitano hadi 1977 tukapata shida ya njaa iliyotokana na Ukame wa 1974, nililazimishwa na Wahisani

Page 2: WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE

2

nimrudishe nchini John Samuel Malecela aliyetambuliwa kuwa mmoja ya watu wenye Busara

Duniani na akifananishwa na Mwanadiplomasia na Mwanasayansi wa Marekani Henry Kisinger

asimamie Kilimo na Mawasiliano.

Mpango huu wa Pili wa Maendelo ya Miaka mitano ulizingatia zaidi kujenga siasa ya Ujamaa na

Kujitegemea, Maendeleo vijijini, na kujenga sekta ya Umma kwa kufikia lengo la asilimia kati ya 85

hadi 95. Sekta ya Urazinishaji na Uimarishaji wa Mashirika ya Umma ulizingatia ujenzi wa uwezo wa

usimamizi na kupunguza gharama. Hatua za Kukuza mafunzo ndizo zilitufanya tuanzishe Chuo cha

Uongozi Mzumbe (IDM), sekta ya Utalii na Madini kuwa chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa

(NDC) na kuhamisha masuala ya Utalii kuwa chini ya Shirika la Utalii la Taifa (TCC) na kilimo kuwa

chini ya Shirika la Kilimo na Chakula (NAFCO). Tuliingia Mkataba wa Kimataifa wa kulinda soko la

sukari ingawa Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EEC), Marekani, Cuba na Urusi hawakuwa sehemu ya

Mkataba. Ukweli hatukuwa hata na uwezo wa kulipa mafao ya wastahafu.

Tulilazimika kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ili kutoa Mafunzo ya Uongozi na Uhasibu kwa

wazawa mnamo Oktoba, 1966 na hususan kuwajenga imani ya Ujamaa ambapo kozi 67 zilizohusisha

watu 1500 ziliendeshwa. Mwaka 1964 watoto walioingia shule za Msingi walikuwa chini ya asilimia

50% na shule za Sekondari zilishindwa kupeleka vitivo vya sayansi ambapo Mnamo Mwaka 1968

kati ya wanafunzi 296 waliohitajika ni wanafunzi 254 tu waliofanikiwa. Aidha, tulifanya mabadiliko

ya ukomo wa elimu ya Msingi kutoka Darasa la Nane na kuwa hadi darasa la saba, tukafuta mitihani

ya darasa la nne na wanafunzi wa darasa la Tatu na la Nne waliokuwa wakisoma nusu siku ikabidi

wasome siku nzima. Hapa tukalazimika kuandaa Mpango wa Elimu kwa Wote (UPE) Mwaka, 1969.

Tulianzisha Chuo cha Ufundi Mwaka 1968 (DAR-TECH) kikianza na wanafunzi 66 waliofanya

mitihani ya Cambridge hapa alikuwepo Mhe Prof Mark Mwandosya. Chuo Kikuu kikapanuliwa hadi

kuwa na Kitivo cha Udaktari kwa kuwa na Wanafunzi 20, Kitivo cha kilimo kilianzishwa Morogoro

na wanafunzi 20 pia. Vyeti vilitolewa na Baraza la Mitihani la Afrika ya Mashariki. Aidha, huduma

ya Maktaba ya Taifa ilianzishwa pia. Benki ya Taifa ya Biashara ilianzisha huduma za Mobile kule

Dodoma maeneo ya Kongwa, Kondoa na Mpwapwa na Tawi la Sumbawanga likiwa Tawi la 30

lilianzishwa April, 1968 ingawa liliathiriwa na Sarafu za Zambia katika biashara hususan za Mpakani.

Sikupumua Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuishia 1981 tukakumbwa na Vita vya Idd

Amin Rais wa Uganda aliyevamia eneo la Misenyi Kagera tarehe 30 Oktoba, 1978 Jeshi langu

likiongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo na kuathiri sana zao la sukari, kahawa na miundombinu

Mkoani Kagera; mnamo miaka ya 80 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90 Mgogoro na Vita vikazuka

nchini Urusi na Dola likafa chini ya Michael Gorberchev kwenye mabadiliko ya siasa na Uchumi

yaani Perestoroika na Glasnost hizi zikatumaliza katika ushindani wa soko la Dunia na ujenzi wa soko

la Mtaji nchini; ikabidi 1985 nimwachie Alhaji Ali Hassan Mwinyi Mpango wa Maendeleo wa Miaka

Mitano na 1987 nilingátuka nafasi ya Uenyekiti wa CCM. Watanzania tokea hapo Mageuzi ya

Uchumi yalipoanza muda huo hadi miaka ya 1989 na 1995 nchi yenu ina changamoto nyingi

zinazohusisha myumbo wa soko la Dunia na Kukosekana kwa Amani miongoni mwa nchi rafiki zetu

ulioathiri kwa kasi Maendeleo yetu. Hata hivyo, jitihada za CCM chini ya Ali Hassan Mwinyi,

Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete zimeinyenyua Tanzania kwa kasi.

Upendo huvumilia katika dhiki na karaha, hufadhili katika ufinyu wa mawazo ya kisiasa; Upendo

hauhusudu, Upendo hautakabari, haujivuni ndani ya medani ya kupambana na Umaskini, haukosi

kuwa na Adabu mbele ya Watawala wa Dola, hautafuti mambo yake bila kuwajali Watanzania,

hauoni Uchungu pale panapokuwa na Mapungufu ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii; hauhesabu

mabaya yoyote yafanywayo na wenye Mamlaka wala Watawaliwa, haufurahii udhalimu unaofanywa

kwa njia ya kutafuta haki au kutoa haki, bali hufurahi pamoja katika Jamii ya Watanzania wenye Dini

na Kabila Tofauti, huvumilia yote, huamini yote, hautumaini yote, hustahimili yote, Upendo

haupungui neno wakati wowote, kwa maana Mimi na wenzangu huku Kuzimu tunafahamu kwa

sehemu na tunafanya Unabii kwa sehemu bila nyie kujua.

Watanzania wangu, ufuateni Upendo na kutaka sana Karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate

kuhutubu, Maana Mgombea Urais anenaye kwa lugha ya Kisiasa na Itikadi zilizojengwa nami ndani

ya TANU na CCM, hasemi kwa Watanzania bali husema na Mungu, maana hakuna asikiaye lakini

Page 3: WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL JULIUS NYERERE

3

anena mambo ya siri katika roho yake; Bali yeye ahutubuye asema na Watanzania maneno kwa lugha

ya Kisiasa na hujijenga nafsi yake; na ahutubuye huijenga Tanzania yangu niliyowaachia.

Basi nawasihi mnifuateni mimi Julius Nyerere, nawakumbusha njia zangu zilizo katika Katiba ya

Serikali na Katiba ya CCM kama vile nilivyowafundisha kila mahali nchini Tanzania. Kila Chama

kisiangalie mambo yake chenyewe bali kiangalie mambo ya Watanzania. Pendo na lisiwe na Unafiki

lichukulieni lililo Ovu kwa kila mgombea mkiambatana na lililo jema, kwa pendo la udugu,

mpendane ninyi kwa ninyi kwa heshima mkiwatanguliza Watanzania kwa bidii, si walegevu, mkiwa

na juhudi katika roho zenu mkiitumikia Tanzania, kwa Tumaini mkifurahi katika dhiki. Msitukanane

kwenye kampeni; Qur’ani Tukufu inawahimiza kusema maneno mema na mazuri. Sehemu moja ya

aya ya 83 ya Suratul Baqara inasema: Na semeni na watu kwa uzuri..”Miongoni mwa mambo

yanayosisitizwa sana katika mafundisho ya Uislamu kuhusu adabu za kusema na kuzungumza ni

kutafakari kabla ya kusema. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, yumkini maneno ambayo

hayakupimwa yakazusha matatizo makubwa yasiyoweza kutatuka kirahisi. Kwa msingi huo

mwanadamu anashauriwa kutafakari kabla ya kufungua kinywa kuzungumza na kufikiria athari

zinazoweza kusababishwa na maneno yake. Amirul Muumin Ali bin Abi Twalib (as) anasema:

“Muumini hutafakari kabla ya kuzungumza. Kama maneno yake ni mazuri huyasema na kama

hayafai huyaacha na kuyafunika.”

Basi imetupasa sisi tulio na nguvu huku kuzimu kuuchukua udhaifu wenu msio na nguvu ndani ya

Taifa la Tanzania, wala hatupaswi kujipendeza wenyewe kwani huku tumepumzika tungependa nanyi

mpumzike kama sisi. Zaidi iweni na juhudi nyingi katika kupendana kwa sababu upendano husitiri

wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi pasipo kunungúnika. Maana twaenenda kwa imani si

kwa kuona, na kumbukeni “Binadamu Wote ni ndugu Zangu na Afrika ni Moja” na hii ndiyo Imani

ya CCM niliyowaachia kwa sababu mtu akiwa ni msiakiaji anajiangalia uso wake katika kioo. Basi

toeni Boriti kwenye Jicho la Dira ya Chama chenu ndipo Mtazame Kibanzi katika Jicho la Dira ya

Chama kingine. Nawakumbusha maneno yangu “the people and the Government of United Republic

are aiming to build a just society of free and equal citizens who live in healthy conditions, who control

their own destiny and who cooperate together and with other people in a spirit of human brotherhood

for mutual benefit”

Basi tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi huku kuzimu, tuliona vema tuwatembelee Tanzania, ili

kuwafanya ninyi muwe Imara na kuwafariji kwa habari ya Imani Yetu huku kuzimu. Nasi

tumefahamu pendo alilo nalo Mungu kwenu nyie na kuliamini. Mungu ni pendo, naye akaaye katika

pendo hukaa ndani ya Tanzania yenye Upendo, na Tanzania yenye Upendo hukaa ndani yake katika

hili pendo lililokamilishwa kwenu, ili muwe na ujasiri katika siku ya tarehe 25 Octoba, 2015

mtakapochagua Rais Mtakatifu na Jasiri. Hii ndiyo raha yetu huku kuzimu na tafadhali mpeni raha

yeye aliyechoka na Matatizo ya Watanzania na huku ndiko kuburudika. BWANA atawaletea taifa juu

yenu kutoka mbali, kutoka ncha ya Dunia kama warukavyo Tausi niliowaacha Ikulu, taifa

msiloufahamu ulimi wake unapotamka jina tamu la Tanzania, taifa lenye uso mkali, ambalo

haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana kwani ni taifa la rika zote.

“MUNGU IBARIKI TANZANIA IBARIKI AFRIKA”