5
WARAKA KWA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Nipashe Na Prof (Dr) Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Alfajiri ya saa tisa, naona mtu kasimama mlangoni ananieleza kuwa ametumwa na waasisi wa CCM Julius Nyerere, Abeid Karume, Thabiti Kombo, Rashid Kawawa na Bibi Titi Mohamed. Akanipa Waraka niupeleke kwa watanzania wenye maneno yafuatayo; Ndugu Watanzania, mnaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge; muelewe kuwa mnatekeleza wajibu wenu chini ya Sheria ya Umma Na 15 ya Mwaka 1984 na Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuchagua au kuchaguliwa katika shughuli za utawala wa Nchi. Tanzania ni nchi ya kwanza kwa SADC kuwa na mfumo wa vyama vingi ikifuatiwa na Botswana, Zambia. Ni nchi pekee iliyopigania Amani kusini mwa Afrika, na nchi ya kwanza kupata uhuru katika SADC Mwaka 1961. Ofisi zote za wapigania uhuru kama FRELIMO, ANC, Kamati ya Ukombozi ya OAU nk zilikuwa na makao yao makuu Dar-Es-salaam miaka ya sabini. Tumejijengea heshima Duniani na kuwa na sifa ya Umoja, Uvumilivu, Upendo na Mshikamano. Hii ilitufanya Mwaka 1969 tuanzishe vijiji vya Ujamaa kwa kuchukua mfano wa Ruvuma Development Association kilichoundwa Mwaka 1963 pale kijijini Litowa kuwa mfano (Model) na kumtumia mtaalamu wao makao makuu ya TANU na kuwa mshauri wetu wa Uchumi na Mipango Ikulu. Kwa

WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

WARAKA KWA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA

MRISHO KIKWETE

Nipashe

Na Prof (Dr) Handley Mpoki Mafwenga

Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

Alfajiri ya saa tisa, naona mtu kasimama mlangoni ananieleza kuwa ametumwa na

waasisi wa CCM Julius Nyerere, Abeid Karume, Thabiti Kombo, Rashid Kawawa

na Bibi Titi Mohamed. Akanipa Waraka niupeleke kwa watanzania wenye maneno

yafuatayo;

Ndugu Watanzania, mnaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge;

muelewe kuwa mnatekeleza wajibu wenu chini ya Sheria ya Umma Na 15 ya

Mwaka 1984 na Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuchagua au

kuchaguliwa katika shughuli za utawala wa Nchi.

Tanzania ni nchi ya kwanza kwa SADC kuwa na mfumo wa vyama vingi ikifuatiwa

na Botswana, Zambia. Ni nchi pekee iliyopigania Amani kusini mwa Afrika, na nchi

ya kwanza kupata uhuru katika SADC Mwaka 1961. Ofisi zote za wapigania

uhuru kama FRELIMO, ANC, Kamati ya Ukombozi ya OAU nk zilikuwa na makao

yao makuu Dar-Es-salaam miaka ya sabini.

Tumejijengea heshima Duniani na kuwa na sifa ya Umoja, Uvumilivu, Upendo na

Mshikamano. Hii ilitufanya Mwaka 1969 tuanzishe vijiji vya Ujamaa kwa

kuchukua mfano wa Ruvuma Development Association kilichoundwa Mwaka 1963

pale kijijini Litowa kuwa mfano (Model) na kumtumia mtaalamu wao makao

makuu ya TANU na kuwa mshauri wetu wa Uchumi na Mipango Ikulu. Kwa

Page 2: WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

sababu tulijua Uhuru bila Maendeleo ni kazi bure. Mfano huo ulitumika pia

kufundishia wanasiasa wetu chuo cha siasa kivukoni.

Tanzania ni nchi ya kwanza kuanzisha uhuru wa Bunge Mwaka 1961, Uhuru huo

ulikaa kwa muda mfupi kwa sababu hatukulenga kuwa na Serikali Imara

inatakayojali matatizo ya kijamii na kiuchumi na uwepo wa chama kushika

hatamu. Katiba ya Jamhuri ya Mwaka 1962 ilitatua matatizo ya kijamii na

kiuchumi wakati Katiba ya Chama kimoja ilitatua tatizo la chama kushika hatamu.

Hii ndiyo chanzo hasa cha kufuata mfumo (Model) ya kikatiba ya Westminster

kutofautisha Bunge na Mahakama hadi leo.

Mwaka 1958 hadi 1961 tulikuwa tukitembelea shule ya msingi ya Msonga na

kumkuta kijana akiongoza wanafunzi wenzake huyu si mwingine ni Jakaya

Kikwete. Mara nyingi alitusogelea akitaka busara zetu mara tukasikia amefauru

na kwenda Lugoba Middle School Mwaka 1962.

Tulipotembelea Kibaha Mnamo Mwaka 1966 tukamkuta akatueleza kuwa

angependa sana kuwa kama Winston Chuchil Waziri Mkuu wa Uingereza kwa vile

anapenda sana maneno yake(Maxims). Tukamwambia, kwa nia hiyo hakika

utakuwa hivyo.

Mwaka 1970 hadi Mwaka 1971 alisoma Tanga shule ya Sekondari. Alipenda somo

la “Political Economy” kwani alipenda pia kusoma maandishi ya akina Lennin, Carl

Max na wengine. Nilipokuwa nakwenda Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam (Mwal

Nyerere) kutunuku wanafunzi Mwaka 1972 hadi 1977 nilikuwa nikimkuta pale

akiuliza sana maswali hasa ya Uchumi na Maendeleo aliyokuwa akisomea akiwa

na wenzake akina Edward Lowasa ambaye alisoma pia Shahada ya Uzamili ya

Sayansi katika Maendeleo huko Bath Uingereza.

Kikwete alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha TANU Mwaka 1975 hadi 1977.

Nilimshangaa sana kuona ameacha hata kuajiriwa kwenye Mashirika kama

Mchumi wasomi wakiwa wachache wakati huo, hakupenda sana fedha, wala

kukimbia kondoo wa Bwana bali kuwatumikia.

Mwaka 1977 baada ya Kuunda Katiba Mpya na kuunganisha TANU na ASP nikiwa

Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, nilitembelea Zanzibar ambapo Ali Hassan

Page 3: WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

Mwinyi alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, niliona ni vyema aende huko

Zanzibar kuwa Makamu Katibu wa CCM. Nilifanya hivyo mara baada ya kuona

amehitimu mafunzo ya kijeshi pale Monduli kuanzia Mwaka 1976 hadi 1977.

Alipanda daraja kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Tabora Mwaka 1981 hadi

1983. Na ikizingatiwa alipigana vita ya Kagera ilikuwa vyema afundishe wanajeshi

wenzie pale Monduli Mwaka 1983 hadi 1986.

Mwaka 1986 alihamia Nachingwea na Masasi kuwa Katibu wa CCM. Mwenzangu

Ali Hassan Mwinyi aliona ni vyema Kikwete alitumikie Taifa zaidi kwa kuwa

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mwaka 1988 hadi 1990, Waziri kamili Mwaka

1990 hadi 1994, Waziri wa Fedha Mwaka 1994 hadi 1995, Waziri wa Mambo ya

Nchi za Nje Mwaka 1995 hadi 2005 na Wananchi mkaona vyema kumchagua

Mwaka 2005 kwa kura zilizoonyeshwa kwenye Jedwali Na1.

Jedwali 1: Matokeo ya Uchaguzi Mwaka 2005

Mgombea Chama Kura Asilimia

Jakaya Kikwete CCM 9,102,952 80.24

Ibrahim Lipumba CUF 1,327,125 11.7

Freeman Mbowe CHADEMA 668,736 5.89

Augustine Mrema TLP 84,901 0.75

Sengondo Mvungi NCCR-Mageuzi 55,819 0.49

Christopher

Mtikila

DP 31,083 0.27

Emmanuel

Makaidi

NLD 21,574 0.19

Anna Senkero PPT-Maendeleo 18,783 0.17

Leonard Shayo Demo-Makini 17,070 0.15

Paul Kyara SAU 16,414 0.14

Wanasaikolojia, Drs. Steven Rubenzer, Thomas Fasschingbauer na Deniz Ones,

walifanya usahili kuhusu historia ya Maraisi mia moja. Wataalamu hao wakaweka

tabia ya kisaikolojia kwa miaka mitano kabla Marais hawajawa madarakani. Hata

hivyo, hawakuangalia tabia ya marais wakiwa ndani ya ofisi kwa sababu “pressure”

za kazi zao wakiwa nje hutofautiana.

Page 4: WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

Wanasaikolojia hao walibainisha sifa za Marais kumi wa Marekani, ikaonekana

kuwa Marais hao siyo wawazi na hupindisha mambo ili mambo yao yaende vizuri.

Lakini imeonekana kuwa Marais wa Karne hii ni "extraverts," na wanajumuika

sana na jamii.

Rais anatakiwa awiwe na Mafanikio, shabaha ya kuongoza, uwezo, ufanisi pamoja

na uwezo wa kitaalamu, wenye kudhibiti hasira.,w enye imani ya kiroho na

waadilifu.

Watu kama Richard Nixon, Teddy Roosevelt Nyerere, Mkapa, Abeid Karume,

Kenyata, Salmi Amour wababe; John Adams, Nixon, Nasser, Jumbe ni “Introverts”;

Rutherfor Hays, Gerald Ford, George Washington, Nyerere, Augustine Neto,

Kaunda, Kikwete, Mwinyi, Nkrumah wana roho nzuri; Warren Harding, Nyerere,

Kikwete, Neto, Lumumba, wanyoofu; Reagan, Warren Harding, Clinton, Chisano

waigizaji; Bush, Ford, Truman, Mkapa, Kikwete, Nyerere, Chisano wana Msimamo;

Lincoln, Jefferson, Madison, Carter, Mwinyi, Nyerere, Nkrumah, Kikwete

wanafilosofia; FDR Kennedy, Clinton, Theodore Roosevelt, Nyerere, Kikwete na

Reagan ni "Extraverts".

Rais Kikwete kafanya yafuatayo; Kushusha kodi ya ongezeko la thamani kutoka

asilimia 20 hadi 18, kodi ya mapato asilimia 30 hadi 25, kuimarisha Sera ya

Medium Term Pay Policy kwa kiwango cha asilimia 60, kuimarisha ushiriki wa

Elimu ya Msingi na Sekondari kupitia Kata, kuboresha miundombinu, Kuimarisha

Umoja wa Kitaifa katika Muungano, na kuimarisha Pato la Taifa kama

ilivyooneshwa kwenye Picha Na 1,

Aidha, Kuimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwa ni pamoja na kuanzisha

soko la Pamoja, Kudhibiti Soko la Madini hasa ya Tanzanite na Kuanzisha Ukaguzi

hivyo kusababisha baadhi ya Makampuni ya Madini kuanza kulipa kodi, Kudhibiti

Ushukaji wa Pato la Taifa wakati wa Mdororo wa Uchumi kwa wastani wa asilimia

7.0, kupunguza kasi ya mfumuko wa bei, kuongeza uwezo wa Mikopo kwa sekta

binafsi kutoka wastani wa asilimia 10 Mwaka 2005 hadi wastani wa asilimia 55

Mwaka 2009, Kuongeza wigo wa uwekezaji (FDI) kutoka Dola za Marekani

494.1milioni Mwaka 2005 hadi 695.5milioni Mwaka 2008, Kuongeza nafasi za

Page 5: WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE

Uongozi kwa Wanawake (Mawaziri 7), (Wabunge 98), (Viti Maalum 75), Wakuu wa

Mikoa 3, Ma-RAS 9, Makatibu Wakuu 8, Manaibu Katibu Wakuu 2, Makamishna 4,

Wakurugenzi kutoka 133, Wakuu wa Wilaya 25, Ma-DAS 34, Majaji Mahakama ya

Rufaa 18 na Mahakama Kuu 15,

Mengine ni Kuongeza udhibiti wa umiliki wa viwanja, Mifugo na zao la samaki,

Kuimarisha Kilimo cha Umwagiliaji pamoja na usambazaji wa Maji, na Kuboresha

huduma ya Afya katika udhibiti Maradhi. Orodha ni ndefu sana.

Picha Na 1: Mapato ya Ndani kwa asilimia ya Pato la Taifa

Chanzo: Wizara ya Fedha na Uchumi

Tunawaomba mchague Rais mzoefu, atakayelipeleka Taifa mahala penye neema.

Tunawatakia safari njema.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA