7
Huduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama vile usafiri,hospitali, maji au posta kwa mujibu wa TUKI(2004:118) Katika shule za msingi ziko huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanafunzi ili kusaidia kwa namna moja au nyingine katika kuinua kiwango cha elimu baadhi ya huduma hizo ni huduma ya chakula,huduma ya afya ,huduma ya maji safi na salama huduma ya ushauri nasaha pamoja na huduma ya mawasiliano na usafiri. Huduma zote hizi ni muhimu katika kumfanya mwanafunzi aweze kukua kiakili,kimaono na kimwili na kiroho na kufanya shule kuwa sehemu salama kwa wanafunzi na kwa mwalimu pia. Miongoni mwa huduma hizo tunaangalia changamoto za utoajia wa huduma za afya pamoja na mbinu za kukabiliana na changamoto hizo. Afya maana yake ni kitendo cha mtu kuwa mzima kimwili,kiakili na kijamii na situ kutokuwa na magonjwa au ulemavu wa aina yeyote. Huduma ya afya ni hali ya ukamilifu kimwili,kiakili , kijamii na kisaikolojia Mbinu ni namna ya kufanya jambo.TUKI(2004) Changamoto nijambo linalomkabili mtu kulifanya. Kwa mujibu wa Mdee, J,Shafi ,k na Njogu (2013:56)

Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

  • Upload
    lamque

  • View
    278

  • Download
    14

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

Huduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema

huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama vile

usafiri,hospitali, maji au posta kwa mujibu wa TUKI(2004:118)

Katika shule za msingi ziko huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanafunzi ili kusaidia

kwa namna moja au nyingine katika kuinua kiwango cha elimu baadhi ya huduma hizo ni

huduma ya chakula,huduma ya afya ,huduma ya maji safi na salama huduma ya ushauri nasaha

pamoja na huduma ya mawasiliano na usafiri. Huduma zote hizi ni muhimu katika kumfanya

mwanafunzi aweze kukua kiakili,kimaono na kimwili na kiroho na kufanya shule kuwa sehemu

salama kwa wanafunzi na kwa mwalimu pia.

Miongoni mwa huduma hizo tunaangalia changamoto za utoajia wa huduma za afya pamoja na

mbinu za kukabiliana na changamoto hizo.

Afya maana yake ni kitendo cha mtu kuwa mzima kimwili,kiakili na kijamii na situ kutokuwa na

magonjwa au ulemavu wa aina yeyote.

Huduma ya afya ni hali ya ukamilifu kimwili,kiakili , kijamii na kisaikolojia

Mbinu ni namna ya kufanya jambo.TUKI(2004)

Changamoto nijambo linalomkabili mtu kulifanya. Kwa mujibu wa Mdee, J,Shafi ,k na Njogu

(2013:56)

Utoaji wa huduma ya sfya katika shule za msingi unakabiliwa na changamoto nyingi ambazo

zimekuwa ni kikwazo katika utekelezaji wa huduma hiyo .

Changamoto hizo nikama zifuatazo pamoja na mbinu zinazoweza kutumia kutatua changamoto

hizo.

Ukosefu wa rasilimali fedha ,hali ya ukosefu wa fedha ni changamoto kubwa kwa

sababu hupelekea kukosa kwa mahitaji muhimu yanayohitajika katika utoajia wa huduma ya

afya kwa mfano zipo changamoto kama ukosefu wa madawa muhimu kama vile panado,yuso,

Iyodini,asali na madawa mengine muhimu kama albendazole ni muhimu sana zikawepo

shuleni. Pia kunachangamoto za vifaa kama vile pamba, makasi,sabuni, na vifaa vingine kwa

ajili ya kufanyia usafi ili vitu hivi viweze kupatikana vinahitaji fedha.

Page 2: Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

Hivyo ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa raslimali fedha ,ni budi kuanzisha miradi

midogomidogo itakayosaidia kuondokana na changamoto kwa mfano shule inaweza kuanzisha

kilimo cha mazao ya mbogamboga ,migomba ,mahindi,maharage na matunda ya muda mfupi

kama vile mananasi na matikiti maji. Pia ufugaji mdogo kama vile kuku wa mayai,kuku wa

nyama, ufugaji wa shungura na ng’ombe wa maziwa. Kupitia miradi hii utajipatia fedha za

kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa raslimali fedha.

Ukosefu wa waatalamu,hii ni miongoni mwa changamoto ya utoaji wa huduma ya afya

katika shule za msingi kwani shule nyingi hazina wahudumu wa afya. Walimu wanaotoa

huduma ya afya shuleni hawana taaluma yoyote inayohusiana na maswala ya afya badala yake

hutoa huduma hii kwa udhoefu wa kawaida bila kufuata utaratibu unaotakiwa kwa sababu

matukio hukea shuleni ajali mbalimbali au hata kuugua gafla wakiwa shuleni hivyo walimu

hutoa huduma hii kwa kutumia maarifa kidogo waliyonayo.

Mbinu ya kukabiliana na changamoto hii ni kwamba ,serikali inapaswa kuweka mpango wa

muda mfupi na wamuda mrefu kwa ajili ya uendeshaji wa semina wa namna yakutoa huduma ya

chakula shuleni, Mfano walimu wa afya shuleni wapewe kipao mbele yaani yapelekwe

semina ,na warudipo vituoni mwao wawezeshe walimu wenzao maarifa hayo ili kuweza kutoa

huduma stahiki kwa mwanafunzi.

Ukosefu wa maji safi na salama,shule nyingi za msingi nchini hazina vyanzo vya maji

safia na salama jambo ambalo hupelekea wanafunzi kutumia maji yasiyo safi na salama kwa ajili

yakula na matumizi mengie ambayo huwapelekea kuugua magonjwa ya tumbo mfano shule

nyingi za Moshi vijijini hutummia majia ya mfereji au miti iliyo karibu na shule na watoto

hutumia maji hayo kwa kunywa pia hakuna utaratibu wa kuweka madawa yakuuwa vijidudu

vilevile hakuna vyombo vya kuhifadhia maji ambavyo ni salama kwa ajilili ya kunywa .

Hivyo ili kuondokana na changamoto hii shule inapashwa kuwa na utaratibu wa kuwa na

majisafi na salama kwa kushirikisha uongozi wa kijiji kupitia uongozi wa kijiji utaweka utaratibu

wa upatikanaji wa maji safi mfano baadi ya shule viko vyanzo vya maji kama vile chemchem

hivyo kijiji kinaweza kusaidia kuweka bomba kutoka kwenye chanzo hiko pia kupitia ruzuku ya

shule uongozi wa shule unaweza kununua vifaa vyakuhifadhia maji mfano majaba au kuwa na

matangi ya maji pia kupitia mashirika yasiyo yakiserikali ya mradi wa maji yanaweza kusaidia

Page 3: Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

kutatua changamoto hii ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi na afya zao kwani maji ni

muhimu kwa mujibu wa Alan Peakock(2003:23) Anasema,sehemu kubwa ya damu imeundwa

kwa maji hivyo maji safi na salama ni muhimu kwa afya.

Ukosefu wa chakula bora au lishe,ili kuwa na afya bora nimuhimu pia kuwepo na

chakula bora hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya shule za msingi Tanzania kwa

sababu mwanafunzi akikosa lishe bora hata masomo yanakuwa ni tatizi kw sababu lishe bora ni

muhimu kwa afya ya akili ili kuwezesha kuwa na kumbukumbu na uelewa wa haraka,pia

ukosefu wa chakula bora na lishe ni changamoto katika huduma ya afya kwasababu kutokula

chakula bora kunasababisha maradhi mfano kwashakoo,marasmasi na udumavu wa afya akili na

mwili pia .

Ili kutatua changamoto hii uongozi wa shule ushirikishe wadau katika kuchangia utoaji wa

chakula bora na lishe pia kuomb a msaada katika mashirika yasiyo yakiserikali mfano

PCI,WFP,FAO na UNICEF haya yatasaidia kutatua changamoto hiyo ili kuwezesha kutoa

chakula bora na lishe hasa kwa wanafunzi wanaosoma shule za kulala Alan Peakock(2003:26)

Anasisitiza kwa kusema kila baada ya kipindi Fulani lazima uhakikishe kuwa unakula vyakula

vitoavyo nishati vyakula vyakujenga mwili na vyakula vyakukinga mwili hivyo hatuna budi

kuhakikisha tunaondokana na changamoto hii.

Miundo mbinu mibovu isiyoridhisha isiyotosheleza mfano vyoo na mabafu , Baadhi ya

shule nyingi nchini huduma ya choo hairidhishi jambo linalopelekea kuwa changamoto kwa

utoaji wa huduma ya afya shuleni.Pia vyoo vilivyopo siyo rafiki kwa kwa wanafunzi mfano

choo cha shimo kwani ni hatari kwa watoto,pia hata vyoo vya maji vilivyopo havikizi viwango

kutokana na ubovu na uchakavu pia maji kwa ajili ya matumizi ni changamoto pamoja na vifaa

muhimu kwa ajili ya kusafishia hakuna .Mture Educational Publisher(2006:19,20) anasema choo

cha maji kinapaswa kusafishwa mara kwa mara na pia vifaa muhimu vitumike kama brashi

maalumu pamoja na kutumia kiuwa vijidudu kusafisha choo. Pia mazingira ya nje yasafishwe

ili kufanya kuwa safi na kuzuia wadudu kama nzi,mbu na wanyama hatari kama nyoka.

Mbinu yakuondokana na changamoto hii ni kutoa elimu na kuhamasisha umuhimu wa kuboresha

na kujenga vyoo vya kisasa na mabovu ili kuwasaidia vijana wa kike hasa wanapopatwa na

dharura zao. Jamii inapaswa kupewa elimu na kuhamasishwa ujenzi wa vyoo na mabafu kwa

Page 4: Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

ajili ya usalama na afya ya watoto wao kwani ukosefu wa huduma ya choo huweza kusababisha

magonjwa . Mture Education Publisher limited 2006:17 amefafanua magonjwa hayo ni kama

kuhara ,kipindipindu hivyo huduma hii ni muhimu kwa wanafunzi mashuleni.

Pamoja na kuwepo changamoto serikali imeendeleza kutoa kipaombele katia huduma za

afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao . serikali inatambua

umuhimu wa afya wa wananchi wake kwani afya ni raslimali muhimu kwa maebdeleo ya taifa

letu la Tanzania, maendeleo yataletwa na wananchi wenye afya bovu kwasababu ndiyo wenye

uwezo wa kuzalisha mali katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ,pia serikali

imeendelea kushikamana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwakuzingatia sera na

miongozo iliopo.

Page 5: Web viewHuduma ni shughuli ifanywayo kwa manufaa ya mtu mwingine, pia tunaweza kusema huduma ni mambo mbalimbali ambayo mtu anayahitaji katika maisha yake kama

Rejea

Alan Peakock(2003)Sayansi ya msingi Tanzania,kitabu cha mwanafunzi darasa la 5,Macmillan

Aidan,Dar es salaam Tanzania ukurasa 26,23.

Mture Educational Publisher Ltd(2006) Sayansi kwa vitendo kitabu cha mwanafunzi darasa la

tatu, Mture Educational Publisher Ltd, Dar es salaam Tanzania ukurasa 17,19 na 20.

Mdee J.S,Shafi k,Njogu A(2013) Kamusi ya Kiswahili karne ya 21,toleo la pili, Longhorn

Publisher Ltd,Dar es salaam.

TUKI(2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu,Taasisi ua uchunguzi wa Kiswahili (TUKI),Dar es

salaam.