19
Mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo “Yesu akawaambia, ‘Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo” (Mathayo 16:6). Kila neno ambalo Yesu Kristo alisema limejawa na mafundisho kwa watu wake. Kumbuka kwamba tunasoma maneno ya Mchungaji wetu Mkuu. Kumbuka kwamba wakati tunasoma maneno ya Yesu Kristo tunasoma maneno ya Yule ambaye ni Kichwa cha kanisa lake akiwaongea na watu wake, tunasoma maneno ya Mfalme wa wafalme, maneno ya Bwana wa Ufalme wa Mungu. Ni Yeye ambaye anaongea na sisi watu wake. Pia, tunapaswa kukumbuka kwamba wakati Yesu aliongea, aliongea maneno ya Mungu Baba Mwenyewe. Yesu alisema, “Kwa maana si semi kwa ajili Yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema” (Yohana 12:49). Kwa hivyo kila wakati tunasoma maneno ya Yesu Kristo tunapaswa kusikia na uangalifu sana. Haya ni maneno ya Mwokozi wetu na haya ni maneno ambayo Mungu Baba amempa Kristo. Kwa hivyo, kila neno ambalo Yesu Kristo aliongea ni ya maana sana na ni muhimu sana. Mafundisho yake ni ya thamani sana; mifano yake na unabii wake ni ya thamani sana; mambo ambayo aliongea kuwafariji watu wake ni ya thamani; na maneno yake ya kutuonya pia ni ya thamani. Hatupaswi tu kumsikia wakati anasema, “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo.” Tunapaswa pia kumsikia wakati anasema, “Mwe mwanagalifu na jichungeni.” Katika sura hii ninataka kukufundisha kuhusu onyo moja ambayo Yesu Kristo aliwapatia wanafunzi wake ambayo ni onyo muhimu sana. Yesu alisema, “Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo” (Mathayo 16:6).” Ninataka kuwafundisha mstari huu kwa wale wote ambao wanataka kuokoka, ili wapate kujua bila mashaka njia ya kuokoka ni gani, na pia ninataka kuwafundisha wale ambao wameokoka ile waweze kuvumilia katika ukristo wao. Hili ni onyo muhimu sana na ni lazima sana kila mmoja wetu afahamu vizuri ni nini Yesu Kristo anatufundisha hapa. 1. Kwanza, ninataka kukufundisha ni nani ambao walionywa na Yesu katika kifungu hiki.

Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

  • Upload
    lamphuc

  • View
    343

  • Download
    5

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo

“Yesu akawaambia, ‘Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo” (Mathayo 16:6).

Kila neno ambalo Yesu Kristo alisema limejawa na mafundisho kwa watu wake. Kumbuka kwamba tu-nasoma maneno ya Mchungaji wetu Mkuu. Kumbuka kwamba wakati tunasoma maneno ya Yesu Kristo tunasoma maneno ya Yule ambaye ni Kichwa cha kanisa lake akiwaongea na watu wake, tunasoma ma-neno ya Mfalme wa wafalme, maneno ya Bwana wa Ufalme wa Mungu. Ni Yeye ambaye anaongea na sisi watu wake. Pia, tunapaswa kukumbuka kwamba wakati Yesu aliongea, aliongea maneno ya Mungu Baba Mwenyewe. Yesu alisema, “Kwa maana si semi kwa ajili Yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema” (Yohana 12:49). Kwa hivyo kila wakati tunasoma maneno ya Yesu Kristo tunapaswa kusikia na uangalifu sana. Haya ni maneno ya Mwokozi wetu na haya ni maneno ambayo Mungu Baba amempa Kristo.

Kwa hivyo, kila neno ambalo Yesu Kristo aliongea ni ya maana sana na ni muhimu sana. Mafundisho yake ni ya thamani sana; mifano yake na unabii wake ni ya thamani sana; mambo ambayo aliongea kuwa-fariji watu wake ni ya thamani; na maneno yake ya kutuonya pia ni ya thamani. Hatupaswi tu kumsikia wakati anasema, “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo.” Tunapaswa pia kumsikia wakati anasema, “Mwe mwanagalifu na jichungeni.”

Katika sura hii ninataka kukufundisha kuhusu onyo moja ambayo Yesu Kristo aliwapatia wanafunzi wake ambayo ni onyo muhimu sana. Yesu alisema, “Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo” (Mathayo 16:6).” Ninataka kuwafundisha mstari huu kwa wale wote ambao wanataka kuokoka, ili wapate kujua bila mashaka njia ya kuokoka ni gani, na pia ninataka kuwafundisha wale am-bao wameokoka ile waweze kuvumilia katika ukristo wao. Hili ni onyo muhimu sana na ni lazima sana kila mmoja wetu afahamu vizuri ni nini Yesu Kristo anatufundisha hapa.

1. Kwanza, ninataka kukufundisha ni nani ambao walionywa na Yesu katika kifungu hiki.

Tunasoma katika mstari huu kwamba Yesu alisema, “Jihadarini, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo” (Mathayo 16:6). Je, ni nani ambao aliwaonya hapa? Wakati tunasoma kifungu hiki tu-naona kwamba hakuwaonya wale ambao walikuwa watu wa dunia, wale ambao hawajaokoka na ambao walikuwa wenye dhambi wakuu. Kristo hapa anawaonya wanafunzi wake, yaani wale ambao walikuwa watu wake, wale ambao walimwamini na kumfuata na kumtumikia. Aliwayonya wale ambao walikuwa wahubiri wa kwanza wa Ufalme wake. Ni hawa ambao Yesu Kristo aliwaonya.

Hili ni jambo la kutushangaza. Tunaweza kuwaza kwamba hawa wanafunzi hawahitaji kuonywa hivyo. Tunajua kwamba wao waliacha vitu vyote vya dunia kumfuata Yesu Kristo. Tunajua kwamba wao waliteswa sana na kujaribiwa sana kwa ajili ya Yesu Kristo. Tunajua kwamba wao walimwamini Yesu Kristo na kufuata Kristo na kumpenda Kristo hata ile wakati watu wa Israeli wengi walimpuuza. Lakini hata baada ya haya yote, Yesu Kristo aliwaonya, “Jihadarini, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo”

Page 2: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Pia hili ni jambo la kutushangaza kwa sababu tunajua hawa wanafunzi wa Yesu walikuwa watu wa aina gani. Tunajua kwamba hawa wanafunzi walikuwa watu bila elimu na watu wa kiwango cha chini katika nchi ya Israeli. Wengi walikuwa wavuvi na mmoja wao alikuwa mtoza ushuru. Watu wa aina hii hawawezi kushirikiana na Mafarisayo na Masadukayo. Mafarisayo na Masadukayo wakati wa Yesu wa-likuwa kama wachungaji wa makanisa makubwa makubwa na maaskofu: watu ambao wanajitenga kwa watu wa kawaida. Tunajua kwamba mtu ambaye anafanya kibarua hawezi kuwa rafiki ya mchungaji wa kanisa kubwa ambaye ako na gari kubwa, hawa wawili hawawezi kushirikiana kila siku. Kwa hivyo, ni jambo la kushangaza kwamba Yesu Kristo aliwaonya wanafunzi wake kuhusu chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Lakini sisi sote tunapaswa kujifunza kwamba kuna jambo moja muhimu hapa sana. Biblia hapa inatu-fundisha kwamba watu wa Mungu wote wanahitaji kuonywa na wanahitaji kujilinda vizuri kila wakati. Hata yule ambaye ameokoka miaka mingi sana na amemtumikia Mungu miaka mingi sana na anajulikana kuwa mtu mtakatifu anahitaji kuonywa na kujilinda.

Pia Biblia hapa inatufundisha kwamba kila mmoja wa watu wa Mungu anahitaji kuwa mnyenyekevu sana na kukesha na kuoma ili asianguke dhambini. Hakuna mtu ambaye ni mtakatifu sana ili hawezi kuanguka dhambini. Sisi sote bado tuko na dhambi ndani yetu na sisi sote tunaweza kuanguka dhambini na kufanya mambo mabaya sana. Ni kweli kwamba ikiwa tumeokoka kwa ukweli hatuwezi kukaa tu katika njia ya dhambi na kufa huko. Ikiwa mtu ambaye ameokoka ataanguka dhambini, Mungu atamletea tena kwake, yeye hawezi kukaa tu katika dhambi. Lakini ukweli ni kwamba yeye anaweza kuanguka dhambini na kuwawezesha maadui wa Mungu kudharau kanisa Lake na neno Lake. Hakuna mkristo yeyote ambaye ni mwenye nguvu sana na hawezi kuanguka dhambini..

Ni kweli kwamba wale ambao wameokoka wameteuliwa na Mungu na kuhesabiwa haki kwa ajili ya imani yao ndani ya damu na haki ya Yesu Kristo na kutakaswa na Roho Mtakatifu, lakini hata baada ya haya yote wao bado ni wanadamu wadhaifu tu. Wao bado wako ndani ya miili yao ambayo ni midhaifu na wao bado wako katika ulimwengu huu ambao umejawa na dhambi. Dhambi kila wakati iko ndani yao na iko karibu sana nao na wao wanaweza kuanguka katika dhambi wakati wowote. Mioyo yao ime-fanywa mipya, lakini bado iko midhaifu; wao wamefahamu mambo mengi sana kumhusu Mungu na neno lake, lakini bado hawajafahamu yote. Watu wa Mungu wote wanahitaji kuishi kama wao wako katika nchi ya maadui wako na wanahitaji kuvaa silaha ya Mungu kila siku. Adui wetu shetani si mnyonge na yeye halali. Kumbuka kwamba watu wa Mungu wakuu kama Noa na Abrahamu na Loti na Musa na Daudi na Petro wote walianguka dhambini baada ya kuokoka. Tukumbuke mifano yao ili tuweze kuwa wanyenyekevu na kujichunga tusianguke.

Ni mafikira yangu kwamba wale ambao ni wachungaji na walimu wa neno la Mungu wanahitaji kusikia maonyo haya zaidi kuliko watu wote wengine. Usiwaze kwamba kwa sababu wewe ni mchungaji, basi wewe ni mtu mtakatifu na kwa hivyo huwezi kuanguka dhambini yoyote. Wakati tunasoma historia ya kanisa, tunaona kwamba ni wachungaji na walimu wa neno la Mungu ambao wameleta mafundisho ya uongo katika Ufalme wa Mungu. Wachungaji wengi wanawaza kwamba wao wanajua Biblia vizuri na kwa hivyo hawahitaji kuisoma na kujifunza Biblia kila siku, na kwa hivyo wanaanza kuacha njia ya uk-weli bila kujua. Pia, wachungaji wanaweza kuwa wakristo wa nje tu. Wao wanaweza kuvaa vizuri kila Jumapili na kusimama mbele za watu na kuhubiri, lakini moyoni wanaweza kuwa mbali sana na Mungu. Wakati tunasoma historia ya kanisa tunapata kwamba wachungaji wengi wameanguka katika dhambi kama kiburi na majivuno na upendo wa pesa na vitu vya dunia na kutaka kuheshimiwa na watu. Wachun-

Page 3: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

gaji wanahitaji kukumbuka kwamba wao pia ni wanadamu tu, na kwamba wao pia wako na dhambi moy-oni mwao na wao pia ni wadhaifu.

Mambo haya yanafaa kutufanya kuwa wanyenyekevu na kujitahidi sana kujilinda. Yanatufundisha kwamba hatuwezi kuamini mioyo yetu, na yanatufundisha kwamba tunahitaji kuomba sana tusianguke dhambini. Jambo muhimu sana ambalo tunahitaji kuomba na unyenyekevu. Watu wa Mungu wote wako katika hatari sana kuanguka katika dhambi ya kiburi na majivuno. Hizi ni dhambi ambazo ziko karibu nasi kila wakati, na kuna wengi ambao tayari wameanguka katika dhambi hizi bila kujua. Wao ni watu wa kiburi na majivuno na wanawaza kwamba wao ni watu wa Mungu na wako karibu sana na Mungu. Hawajafahamu kwamba wanatenda dhambi. Lazima tukumbuke sana maneno ya Yesu Kristo, “Ji-hadarini, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

2. Pili, ninataka kukufundisha ni hatari gani ambayo Yesu anaongea kuhusu hapa.

Yesu alisema. “Jihadarini, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo” Wakati tunasoma kifungu hiki, tunaona kwamba Yesu anaonya watu wake kuhusu mafundisho ya uongo. Wanafunzi wake walielewa kwamba Yesu anaongea kuhusu “mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo” (Mathayo 16:12).

Yesu hapa haongii kuhusu mateso ambayo watu wake watakumbana nao na haongeii kuhusu dhambi am-bayo wataona hapa ulimwenguni. Pia Yesu hapa hawaonya wanafunzi wake kuhusu upendo wa pesa na upendo wa anasa za dunia. Ni kweli kwamba wanafunzi wake walihitaji kuonywa kuhusu haya mambo yote, lakini Yesu katika mstari huu hakuongea kuyahusu. Katika kifungu hiki, kuna kitu kimoja tu amba-cho Yesu anaongea na hiki ni mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Wakati Yesu anaongea kuhusu mafundisho ya Mafaisayo na Masadukayo, je, ni nini yeye alimaanisha? Katika sehemu hii ya sura hii, ninataka kukueleza kuhusu mafundisho ya hawa wawili.

Mafundisho ya Mafarisayo yalijumlisha mambo matatu.

Kwanza, Mafarisayo walikuwa watu wa dini ya nje tu. Dini yao haikuwa dini ya moyo, bali ilikuwa tu mambo ya nje kama ni nini mtu anavaa, ni namna gani ananawa mikono wake, ni namna gani anamwabudu Mungu kanisani.

Pili, Mafarisyo waliheshimu sana desturi ya mababu zao

Tatu, Mafarisayo waliwaza kwamba wao ni watu wazuri na wenye haki kwa sababu ya matendo yao.

Hawa Mafarisayo waliheshimu sana desturi ya mababu zao na kwa mawazo yao, hizi desturi zilikuwa sawa sawa na mafundisho ya Biblia. Hawa Mafarisyo walichunga sana mambao ya nje ya dini yao. Wao walikuwa na sheria yao kuhusu nguo ya kuvaa na ni namna gani wanaomba na ni namna gani wanamwabudu Mungu, na walikuwa waangalifu sana jinsi walifuata sheria hii. Wao walikuwa na kiburi sana kwamba walikuwa watu wa Abrahamu, na waliwaza kwamba kwa sababu walikuwa watu wa Abra-hamu, basi walikuwa watu wa Mungu na wataingia mbinguni bila shaka yoyote.

Hawa Mafarisayo walikuwa na sheria yao jinsi mtu anapaswa kunawa mikono yake na jinsi mtu anaweza kuwa safi mbele za Mungu. Wao walifanya bidii sana kuwaonyesha watu wote wa nchi yao kwamba wao

Page 4: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

ni watakatifu. Dini yao yote ilikuwa dini ya nje tu, ilikuwa mambo ya nguo na kunawa mikono, haikuwa mambo ya kiroho. Wao walitaka kuonekana kuwa wale ambao wanawaheshimu wale ambao wamekufa na kwa hivyo walijenga makaburi mazuri na kuchunga vizuri makaburi ya watu wao. Pia, wao walifanya bidii sana kuvuta watu wawe wafuasi wao, na kuwa watu ambao wanaheshimiwa na wengine. Wao walipenda sana kuitwa “Mwalimu, mwalimu.” Tunaweza kusoma kuhusu Mafarisayo katika Mathayo sura ya 15 na Marko sura ya 7.

Ni lazima tufahamu kwamba hawa Mafarisayo hawakukataa Agano la Kale hata kidogo, lakini wao walitengeneza sheria yao na kuweka sheria hii sawa sawa na Agano la Kale.

Kwa upande mwingine, Masadukayo hawakuheshimu Biblia kama neno la Mungu. Si wengi katika nchi ya Israeli ambao walifuata mafundisho ya Masadukayo, na hii ndiyo sabab hatusomi mengi kuwahusu. Kuna mambo mengi ambyo yamefundishwa katika Biblia ambayo hawa Masadukayo walikataa kuamini. Wao hawakuamini kwamba mwanadamu ako na roho, na kwamba watu wa dunia wote watafufuliwa siku ya mwisho, na kwamba kuna malaika. Tunaona mafundisho yao wakati walimwuliza Yesu swali kuhusu mwanamke mmoja ambaye alikuwa na mabwana saba, na kumwuliza, “Katika ufufuo yeye atakuwa mke wa nani?” (Mathayo 22:28). Hawa walisimama dhidi ya yale ambayo Biblia inatufundisha wazi, na wao walifundisha tu mawazo yao na si mafundisho ya Biblia.

Kumbuka kwamba hawa Masadukayo hawakuwa bila imani yoyote. Hawa hawakuwa wale ambao hawaamini kabisa Biblia. Wao walijaribu sana kwa uwezo wao kufuata sheria ya Musa, na wengine wao walikuwa kuhani ya hekalu katika Yerusalemu. Kuhani Kaifa ambaye alimhukuku Yesu Kristo kifo alikuwa Msadukayo. Lakini hawa hawakuamini kwamba yale ambayo Biblia inafundisha ni neno la Mungu. Wao waliwaza kwamba ikiwa kuna jambo fulani ambalo Biblia inafundisha ambayo hawa hawataki kuifuata, basi wao wanaweza tu kukataa kufuata jambo lile. Wao waliwaza kwamba mwanadamu ako na huru kuamua ni nini anaweza kupokea kutoka kwa neno la Mungu na ni nini anaweza kuacha tu kwa sababu yeye hapendi mambo fulani. Hii nidyo sababu Yesu Kristo alisema, “Ji-hadarini, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

Sasa, swali ambalo tunahitaji kuuliza ni hili: je, ni kwa nini Yesu Kristo aliwaonya watu wake kujilinda dhidi ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo? Yeye ni Mungu mwenyewe, na Yeye alijuwa kwamba baada ya miaka 40 ya kusema maneno haya jeshi la Warumi wataingia nchi ya Yerusalemu na kuharibu mji huu na watu wa Israeli wote watatoka nchi yao na kwamba Mafarisayo na Masadukayo wote wataisha. Lakini hata baada ya kujua haya yote, yeye alifundisha onyo hili. Je, ni kwa nini alifanya hivyo?

Jibu ni kwamba Yesu Kristo alitaka kuwaonya watu wake wa kila wakati kuhusu jambo hili. Yesu Kristo ni Mungu na anajua kila kitu. Yeye alijua kwamba watu wake wa kila wakati walihitaji kusikina onyo hili. Yeye ambaye ni Bwana wa kanisa lake na Kichwa cha kanisa lake alijua kwamba mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo yataendelea kuwa katika kanisa lake na kujaribu kuangusha watu wake, na kwamba wengi watapokea na kuamini mafundisho haya na kwa hivyo kuangamizwa. Haya yote Yesu Kristo alijua, na hii ndiyo sababu aliwaonya watu wake kuhusu mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. Yeye alijua kwamba watu kama Mafarisayo na Masadukayo wataendelea kuwa hapa ulimwenguni na kujaribu kuongoza kanisa lake katika njia isiyofaa. Yeye alijua kwamba kila wakati tutakuwa na watu ambao ni kama Mafarisayo na Masadukayo. Yeye alijua kwamba kila wakati tutakuwa na wale ambao watajaribu kuongeza kwa neno la Mungu mawazo yao, na pia alijua kwamba kila wakati

Page 5: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

tutakuwa na wale ambao wataondoa mambo mengi kutoka kwa neno kwa sababu hawapendi neno la Mungu na mafundisho yake kamwe. Hii ndiyo sababu Kristo aliwaonya watu wake, “Jihadharini, jilen-deni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”

Wakati tunasoma historia ya kanisa, tunaona kwamba kumekuwa na watu kama Mafarisayo na Masadukayo kila wakati. Kumekuwa na wale ambao wamejaribu kubadilisha neno la Mungu na kuondoa mafundisho ambayo wao hawapendi kamwe. Hata leo kuna wale ambao, kwa mfano, hawapendi ma-fundisho ya Biblia kuhusu wanawake ambao wanataka kuhubiri. Wao wanajua kwamba jambo hili haliruhusiwi katika Biblia na kwamba mafundisho ya Biblia kuhusu jambo hili ni wazi kabisa. Lakini wao hawataki kupokea au kufuata neno la Mungu, na kwa hivyo wanapuuza tu mafundisho ya Biblia na wanawaruhusu wanawake wahubiri. Pia kuna wale ambao ni kama Mafarisayo na wanaongoza neno la Mungu na mawazo yao. Wao wanajua ni nini neno linasema, lakini wao wanataka watu wafuate mawazo yao, na si ya Biblia, na kwa hivyo wanahubiri tu mawazo yao na mafundisho yao, na si mafundisho ya Biblia.

Inaweza kuonekana kwamba mimi ni mtu mkali kwa sababu ninaongea wazi kabisa juu ya mambo haya. Kuna wengi ambao wanafunga macho yao na kusema, “Ndiyo ninajua huyu mzee anafundisha nini, lakini mimi sioni hatari yoyote kwa kanisa.” Na kwa sababu hawa hawaoni hatari, wanawaza tu kwamba yote ni sawa na kanisa la Mungu hapa ulimwenguni linaendelea vizuri. Lakini kwa ukweli maadui wa kanisa la Mungu wanafundisha mambo mengi maongo hapa ulimwenguni na wao wanafurahi wakati wanaone kwamba watu hawajui ni nini wanafundisha. Wanafurahi wakati watu wanasema, “Hatuoni hatari yoyote hapa.”

Mimi ninahisi mambo haya sana moyoni mwangu. Ninajua kwamba mtu akiongea kuhusu mafundisho mabaya na hatari ambayo kanisa liko ndani, watu hawapendi mafundisho yake na wanataka kuyapuuza. Wengi wanawaza kwamba yule mhubiri ambaye anahubiri kuhusu mambo haya hana upendo moyoni mwake, bali ni mtu kali na mtu ambaye anawachukia wengine. Kuna wale ambao wanasema, “Je, ni kwa nini huyu anahubiri dhidi ya wanawake wahubiri na wachungaji wengine?”

Pia, kuna wengi ambao hawafahamu mambo haya vizuri. Kuna wengi ambao wako tayari kusikia ma-fundisho ya yeyote ambaye anajiita mchungaji na mwalimu wa neno la Mungu ni mtu wa kweli. Kwao, yeyote ambaye anasimama mbele ya watu na kuhubiri ni mtu wa Mungu na mwalimu wa ukweli. Wao hawaelewi kwamba kuna wale ambao ni walimu wa ukweli na wale ambao ni walimu wa uongo. Hawafahamu kwamba mtu anaweza kujiita mchungaji na mwalimu ya Biblia na awe yeye hafundishi mambo ya ukweli bali mafundisho maongo.

Lakini ninataka kuwaambia watu wote kwamba wakisoma Agano Jipya, wataona kwamba kuna maonyo mengi kuhusu wale ambao wanaonekana kuwa watu wa Mungu na walimu wa ukweli, ambao kwa ukweli ni walimu wa uongo. Agano Jipya linasema hii:

“Jihadharini na mabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali” (Mathayo 7:15).

“Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Wakolosai 2:8).

Page 6: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

“Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine nyingine, nay a kigeni; maan ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, wao waliokwenda navyo hawakupata faida” (Waebrania 13:9).

“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1 Yohana 4:1).

Pia wakati tunasoma nyaraka ambazo tunapata katika Agano Jipya, tunaona kwamba mara mengi, waan-dishi wa nyaraka hizi wanawaonya watu wa Mungu kujichunga sana kwa sababu kuna wengi ambao wanaonekana kuwa watu wazuri na watu wa Mungu na wahubiri wa ukweli ambao kwa ukweli ni wahu-biri wa uongo.

3. Tatu, ninataka kuangazia ni namna gani Yesu Kristo aliongea kuhusu haya mafundisho ya Ma-farisayo na Masadukayo.

Kila wakati Yesu Kristo alifundisha neno la Mungu, alitumia maneno ambayo yanafaa vizuri kabisa ku-fundisha ukweli. Hapa, angeweza kusema, “Kuwa waaminifu na jichungeni dhidi ya mafundisho ya Ma-farisayo na Masadukayo.” Lakini Yesu hakusema hivyo. Yeye alitumia neno moja ambalo linaweza ku-tushangaza. Kristo alisema, “Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”

Sisi sote tunajua chachu ni nini. Mwanamke ambaye anapika mkate anaweka chachu kidogo ndani ya unga. Wakati wa kupika, chachu ni kidogo sana kulingana na unga yote. Vilevile, mafundisho maongo yanaanza kwa njia kidogo kidogo tu. Chachu inafanya kazi yake ndani ya unga kwa njia pole pole, na vilevile mafundisho maongo yanafanya kazi yake kwa njia polepole miongoni mwa watu wa Mungu, hadi wengi wamedanganywa na hawajui ukweli ni nini na uongo ni nini. Haya ni mafundisho Yesu Kristo anatufundisha kuhusu mafundisho mabaya miongoni mwa watu wake. Wakati tunachunguza vizuri ma-fundisho yake, tunaona kwamba yanaweza kutufundisha mambo mengi muhimu sana.

Wale ambao ni walimu wa uongo hawasimami miongoni mwa watu wa Mungu na kusema, “Mimi ni mwalimu wa uongo!” Mwalimu wa uongo huja kwa watu wa Mungu kwa njia ya urevu na ujanja na kwa siri. Wao wanakuja kwa ile njia ili watu wa Mungu hawana shaka kwamba wao ni walimu wa uongo. Wao ni mbwa mwitu ambao wamevaa nguo ya kondoo, kama tu shetani anaonekana kuwa malaika ya nuru. Ni wao ambao ni watu wa hatari sana kwa watu wa Mungu.

Mwalimu wa uongo atakuja kwa njia pole pole na ataonekana kuwa mtu mema sana na mtu wa Mungu na mtu mtakatifu. Yeye atakuambia kwamba yeye anakubali kila kitu ambacho kinapatikana katika Biblia, lakini anasema kwamba unahitaji kuongeza mambo fulani madogo madogo kwa imani yako ili imani yako ikuwe kamili. “Mimi pia ninaamini Biblia ni neno la Mungu. Lakini wewe unahitaji kujua kwamba kuna wale leo ambao wanasikia neno la Mungu kutoka mbinguni na wanahubiri neno hili. Wao wamepata mafundisho kutoka kwa Mungu kwa watu wa leo na sisi sote tunapaswa kusikia ni nini Mungu anasema leo. Ukiwasikia walimu hawa na kufuata mafundisho yao, basi ukristo wako utakuwa kamili na kukuletea furaha nyingi.”

Wakati unasikia maneno kama haya, kumbuka sana mafunisho ya Yesu Kristo, ‘Jihadharini, jilendeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” Je, ni kwa nini ninasema maneno haya? Ni kwa sababu ma-fundisho maongo huwa yanaanza kwa njia ndogo ndogo na kuongezeka hadi yanapatikana kila mahali.

Page 7: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

1. Kuna wale ambao wanasema, “Kumbuka kwamba kanisa ni muhimu sana,” na baada ya muda unaona kwamba watu hawafuati Kristo, bali wanafuata kanisa.

2. Kuna wale ambao wanasema, “Kumbuka kwamba wachungaji ni watu muhimu kanisani,” na baada ya muda utaona kwamba watu wanafuata mchungaji na si Kristo. Kwao, mchungaji ndiyo mtu muhimu sana na kwa mawazo yao, wao wanahitaji kutii kila kitu ambacho yeye anafundisha.

3. Kuna wale ambao wanasema, “Kumbuka kwamba ubatizo na meza ya Bwana ni mambo muhimu sana,” na baada ya muda utaona kwamba wao wanafundisha watu kwamba mtu akitaka kuokoka, anahi-taji kubatizwa kwa sababu ubatizo unaosha dhambi za watu. Na pia mtu akitaka kuokoka anahitaji kuhudhuria meza ya Bwana kwa sababu ni hapa wokovu hupatikana. Haya yote ni mafundisho maongo, lakini ni wengi ambao wanafundisha mambo haya, na ni wengi ambao wanayaamini.

Kuna wale ambao wanasema, “Maaskofu ni watu muhimu sana kanisani,” na baada ya muda utaona kwamba maaskofu sasa ni viongozi wa kanisa na si Yesu Kristo. Watu wanawaheshimu sana maaskofu na kusahau kwamba Bwana wao ni Yesu Kristo na si askofu fulani.

Haya yote ni mafundisho ya Mafarisayo ambao walidai kuamini kwamba Biblia ni neno la Mungu lakini kwa ukweli waliongeza mafundisho yao, na baada ya muda, mafundisho yao yalikuwa muhimu sana ku-liko mafundisho ya Biblia.

Zaidi ya mafundisho ya Mafarisayo, tunapata mafundisho ya Masadukayo. Wao walikataa kuamini kwamba Biblia ni neno la Mungu na walifuata mawazo yao badala ya Biblia.

Wale ambao wanafuata na kufundisha mafundisho ya Masadukayo pia wanaanza mafundisho yao kwa njia pole pole, na baada ya muda kidogo wanaongoza watu wengi kufuata mafundisho yao. Kwa mfano, mtu anasema, “Ni kweli kwamba Biblia ni neno la Mungu, lakini kuna mafundisho ingine ambayo Mungu anataka tufuate na haya hayapatikani katika Biblia. Paulo anasema wanawake hawawezi kuhu-biri, lakini haya ni mafundisho ya Paulo. Siku hizi wanawake pia wanaitwa na Mungu kuhubiri neno.”

Pia, watu kama hawa wanafundisha, “Si vizuri kusema wanawake hawawezi kufundisha au kusema mtu fulani ni mwalimu wa uongo. Sisi hatujui mambo yote. Pengine huyu ni mwalimu wa ukweli ambaye ametoka kwa Mungu, na pengine mafundisho yake na ya kweli. Si mambo mazuri kusema huyu ni mwongo!”

Mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo ni ya aina hii. Haya ni mafundisho ya uongo ambao yanaanza kwa njia pole pole na baada ya muda yanawashika watu na yanawaongoza katika njia ya uongo. Tuna-paswa kujilinda sana na kujichunga sana dhidi ya mafundisho kama haya. Kama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana, lakini kwa kweli mafundisho haya yatawaongoza watu wa Mungu dhambini mbaya sana.

Tujichunge sana dhidi ya yale mafundisho ambayo yanaanza kwa njia pole pole na yanaanza kuwa madogo sana. Mafundisho yote maongo yalianza hivyo. Watu wachache tu walifundisha mafundisho haya mabaya, lakini baada ya miaka mingi, watu wengi wanayaamini. Mtu akitaka kupanda mti mkubwa sana, anahitaji tu mbegu mdogo na baada ya miaka mingi, atakuwa na mti mkubwa. Mtu ambaye anataka kujenga nyumba kubwa sana ya gorofa mingi anahitaji tu kuanza na mawe madogo madogo. Safina am-

Page 8: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

bayo Noa alijenga ilikuwa na miti midogo midogo! Mwanamke ambaye anataka kupika mkati mkubwa anahitaji tu chachu kidogo, na baada ya muda, chachu hii itasambaa kila mahali katika mkati ule. Vilevile mafundisho maongo, hata kama ni madogo sana yanaweza kuharibu kanisa lote. Wakristo wa Galatia waliheshimu siku fulani na miezi fulani. Hii haionekani kuwa dhambi kubwa. Lakini Paulo ali-waandikia, “Ninaogopa kwa ajili yenu” (Wagalatia 4:10-11).

Wakati unasoma mambo haya, usiseme, “Ni kweli watu wa Mungu wanaweza kuanguka katika ma-fundisho mabaya na wanahitaji kujichunga, lakini mimi si kama wao. Mimi ni mtu wa Mungu na ninajua Biblia vizuri. Mimi siwezi kuanguka katika mafundisho maongo.” Kuna wengi ambao waliwaza hivi lakini sasa wameshikwa na mafundisho mabaya na hata hawajui jambo hili. Kumbuka kwamba yule ambaye anaanguka katika dhambi anaanguka kwa hatua moja baada ya moja na hatua hii si kubwa, ni ndogo ndogo. Kumbuka kwamba Kristo mwenyewe ametuamuru kwamba unataka kujichunga dhidi ya mafundisho mabaya.

4. Jinsi ya kujilinda leo kutokana na mafundisho ya uongo kama yale ya mafarisayo and masadukayo.

Sisi sote leo tunahitaji uwepo wa Roho Mtakatifu katika mioyo yetu ili aweze kutuongoza, kutufundisha na dkutuwezesha kuenenda katika imani ya kweli. Tunafaa kuomba kwamb Roho Matakatifu atatulinda ili tusidanganywe na walimu wa uongo. Ikiwa tutaweza kulindwa kutokana na mafundisho ya uongo, ni lazima tuzungatia ukweli fulani katika maisha yetu. Ninasema hivi kwa sababu kuna wakati katika Kanisa la kristo ambapo tunapaswa kuwa na msimamo bora wa Biblia. Ikiwa tutakuwa na msimo wa kweli wa Biblia, ni waiz kwamba tutakuwa na nafais bora sana kuyapinga mafundisho ya uongo na walimu wa uongo.

Kwa hivyo nataka tutazama baadhi ya mambo ambyo tunapaswa kuamini na tusiyache kamwe, bali yawe msimo wetu katika kila jambi. Mambo ni kulingana na mafundisho ya Biblia.

a).Kwanza, tunapaswa kuamini kwamba, mwanadamu ameanguka katika dhambi, na kwamba dhambi imedhuru kila sehemu ya maisha yake yote.

Kwanguka kwa mwanadamu katika dhambi ni jambo la muhimu sana kwa sababu kutokana na dhambi, mapenzi, hekima, hisia na dhamira, yote imeharibiwa. Mwanadamu hajafanya mambo mabaya hapa na pale tu, au kwamba dhambi zake ni kodogo tu machoni pa Mungu. Mwanadamu ni mwenye hatia na anastahili hukumu ya dhambi.

Kuna wengi ambao wanawaza kwamba shida ya mwanadamu ni kodogo tu na kwamba yeye anauwezo fulani wa kujitoa kwa hali hii. Lakini ukweli ni kwamba, ikiwa hatutafamu vyema uovu wa dhambi, basi ni wazi kwamba hatutapata tibu ya kweli ya ugonjwa wa dhambi.

b) Pili, tunapaswa kuamini kwamba Biblia ni neno la Mungu.

Tunafaa kuendelea kuamini na kushikilia ukweli kwamba Bibli imepeanwa kwa nguvu za Roho Matakatifu, na kwamba Biblia yote ni neno la Mungu, yaani Kutoka kitabu cha Mwanzo hadi kitubu cha Ufunuo. Biblia si kama vitabu vingine, hiki ni kitabu ambacho ndani mwake Mungu anazungumza na mwanadmu.

Page 9: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Ni ukweli kwamba katika Biblia kuna mambo mengi sana ambayo hatuelewi. Ikiwa hatutaamini kabla ya kuelewa kila kitu, basi ni wazi kwamba tutaamini mambo machache sana katika Biblia. Hatufai kuogopa matusi au maneno mabaya ya wale wote amabo hawaiamini Biblia. Tangu siku za mitume, Neno la Mungu limekuwa likitukanwa, lakini limeendelea kuwa neno la kweli. Kile Mungu amesema, kamwe kimetimia na kile ambacho hakijatimia kitatimia. Biblia inasema kwamba, “Mungu si mtu aseme uongo, wala si mwanadamu ajute, iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena hatalifiliza?” (Hesabu 23:19). Hatufai kuogopa lolote, kwa sababu kila wakati Biblia itadhirika kwa kitabu cha Mungu ambacho kime-jawa na ukweli ambo hakuna mwanadamu anaweza kubadilisha. Sauti ya Mungu na kazi ya mikono ya Mungu, yote kitu kimoja. Hakuna siku ambapo sauti ta Mungu itasema jambo ambalo ni kinyume na kazi ya mikono yake. Hakuna mtu ambaye atavumbua jambo au kitu ambachi kiko kinyume na Neno la Mungu.

Pia tunapaswa kuendela kuamini na kushikilia kwamba neno la Mungu ndio msingi wa imani na maisha ya ukristo. Chochote ambcho hakimo katika neno la Mungu, hakiwezi kutumika na kumsaidia mwanadamu kupata wokovu. Mafundisho yote yote ambayo hayamo katika neno la Mungu, hatufai kuwayafuata, kuyatii au kuyazingatia kwa njia njia yote ile. Haijalishi ni nani ambayo anafundisha ma-fundisho hayo, iwe askofu au mchungaji yeyote. Haijalishi elimu ya ule ambaye anafundisha, ikiwa ha-fundishi neno la Mungu, hatufai kwamwe kumsikiliza.

Tunapaswa pia kuitumia Biblia kwa njia ambayo inadhirisha kwamba kweli tunaimini. Tunafaa kuitumia kwa njia ya heshima na kusoma maneno yake kwa unagalifu sana kwa sababu ni maneno ya Baba we tu wa mbinguni. Tukumbuka kwamba, kwa sababu Biblia ni neno la Mungu amblo limevuviwa na Roho Mtakatifu, ni lazima tutapata mambo mengi ambayo hatuyafahamu. Hivi ndivyo ilivyo. Kwa hivyo kila wakati tunafaa kusoma Biblia kwa moyo wa unyenyekevu tukiomba Mungu atusaidie na ataufundishe Neno Lake. Biblia si kitabu cha mwanadamu, lakini kimeandikiwa mwanadmu. Kwa hivyo tukisoem kwa njia ya kutaka kufunzwa na wala si kufundisha; si kama mtu ambaye anafahamu kila kitu ndani yake, bali kama mwanafunzi mnyenyekevu ambaye anataka kufundishwa ili ajue ukweli na aweze kumtukuza Baba yake.

c) Tatu, tunapaswa kuamini katika kifo cha Yesu Kristo na dkazi yake akiwa kuhani Mkuu.

Kifo cha yesu Kristo msalabani Kalivari hakikuwa kifo cha kawaida. Hakikuwa kifo cha yule ambaye alikufa kwa ajili ya imani yake. Hakikuwa kifo cha kutuonyesha tu mfano wa kujitolea katika mambo ya Mungu. Kifo cha Kristo yesu kilikuwa sadak ambayo ilitolewa kwa Mungu kwa njia ya mwili na damu ya Kristo Yesu kama njia kumtosheleza Mungu kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Kilikuwa sadaka na kilikusudia kumtosheleza Mungu; kilikuwa kifo ambacho kilizungumziwa katika sadaka za sheria ya Musa; kilikuwa kifo cha kubadilisha maisha ya wanadamu. Bila kumwagwa kwa damu, hakuna ondoleo la dhambi. B ila kifo cha Kristo Yesu kamwe hakuna msamaha wa dhambi za wanadamu.

Pia tunapaswa kukumbuka kwamba huyu mwokozi ambaye alisulibishwa msalabani, ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba akiendela kuwaombea wote ambao wanakuja kwa Mungu kupitia kwake. Pia kwamba anaendelea kuwaombe a wote ambao wamemwamini na kwamba Yeye bado ndiye Kuhani Mkuu na hajamweka mwanadamu yeyote kutekeleza majukumu ya afisi hii ya kuwa kuhana Mkuu. Kwa hivyo hatumhitaji mwingine yeyote Krist Yesu anatosha. Hatumhitaji maria mama wa Yesu au malaika au kasisi au mtakatifu yeyote, au mchungaji yeyote kuwa mwakilishi kati yetu na Mungu, isipokuwa mwakilishi mmoja ambaye ni kristo Yesu.

Page 10: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Pia tunapaswa kukumbuka kwamba amani katika dhamira zetu hainunuliwi na kutubu dhambi kwa kasisi. Amani hii katika dhamira inapatikana kwa kuenda kwa Bwana Yesu Kristo ambaye ndiye Kuhani Mkuu. Ni Kwake Kristo ambako tunakiri dhambi na wal si kwa mwanadamu yeyote. Ni Yeye Kristo Yesu pekee ambaye anasamehe dhambi. Tukienda Kwake pekee, Yeys atatuambia, “Dhambi zenu zimesamehewa, enendeni kwa amani.

Pia tunapaswa kukumbuka kwamba baada ya kuokolewa na Mungu, lazima tuendelea kuishi maisha yetu, kwa imani ndani ya kristo Yesu. Maisha ya ukristo si tu kuwa mtu wa dini au kuenda kanisani kial wakati au kula meza ya Bwana kila siku, hata kama haya mambo ni mazuri, bali ni kila wakati kumtazama Kristo kwa imani na kuendela kuish maish matakatifu ambayo yanamletea Mungu utukufu. Ni kula mwili na kunywa damu ya Kristo kwa imani kila siku. Ni kuendelea kutakasika katika mfano wa kristo yesus mwenyewe. Mtumishi mmoja wa Mungu ambaye alitwa John Owen, alisema kwamba kuna kitu kimoja amabcho ikiwa shetani angeweza kuchukua kutoka kwa Kristo, hicho ni kazi ya Kristo ya kuwa Kuhani Mkuu wa watu wake. Shetani anajua kwamba kazi hii ya Kristo kama Kuhani mkuu ndio msingi wa imani na faraja ya kanisa la Kristo. Ikiwa tunataka kuemndelea katika ukweli wa imani ya kikristo, ni laz-ima tufahamu vyema kazi hii ya Kristo Yesu ya Ukuhani.

(d) Nne, tunapaswa kuamini mafundisho kuhusu kazi ya Mungu Roho Mtakatifu.

Tunapaswa kujua kwamba kazi ya Roho Mtakatifu, ni kazi ambayo haifichiki tu katika moyo wa mwanadamu. Si ukweli kwamba wakati manyunyu yapo kwamba hayaonekani kamwe na kwamba wakati yananyesha huwa hayaonekani. Pia tujue kwamba, penye kuna uhai ndani ya mwanadamu huwa unaonekana kwa sababu yeye huwa anapumua. Hivi ndivyo ilivyo na kazi ya Roho matakatifu katika maisha ya mwanadmu. Pale ambpo Roho Mtakatifu yupo, kuna kiumbe kipya na mtu mpya. Pale ambapo apo, kuna kufahamu kupya, imani mpya, utakatifu upya; matunda mapya katika jamii, katika dunia na katika kanisa. Pahali ambapo hakuna mambo haya mapya, ni wazi kwamba hapo hakuna kazi ya Roho Mtakatifu. Tunaish katika nyakati ambapo sisi sote tunapaswa kuwa waangalifu juu ya kazi ya Roho mtakatifu. Mwandishi mmoja ambaye aliitwa Mademe Guyon alisema kwamba, kuna wakati wengi watauliua kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati huo ni sasa. Katika mafundisho memngi ya kikristo utapata kwamba mafundisho kuhus kazi ya Roho Mtakatifu ndio mafundisho ambayo yamefundishwa kwa njia mbaya sana.

Ninataka kusiitiza umuhimu wa mambo haya manne kwa wasomaji wangi wote.

(a) Mtazamo bora juu ya uovu wa mwanadamu.

(b) Mtazamo bora ya neno la Mungu

(c) Mtazamo bora juu ya kifo na kazi ya Kuhani mkuu ya kristo Yesu

(d) Mtazamo bora juu ya kazi ya Roho Mtakatifu

Ninaamini kwamba mafundisho mabaya kuhusu kanisa, huduma, njia za neema, upendo wa Mungu, kifo cha Kristo Yesus na hukumu wa milele; haya ndio mambo manne ambayo tunafaa kuyaamini na kushik-ilia ikiwa tutajiepusha na chachu ya Mafarisay nad Masdukayo, yanni walimu wa uongo.

Page 11: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Ninataka kumalizia mafundisho haya kwa kuonyesha jinsi tunapaswa kuishi maisha yetu kulingana ma-fundisho haya. Nia yangu ni kuhakisha kwamba wale wote ambao watasoma masomo haya, watafaidika kiroho sana. Pia ninataka kujaribu kuyajibu maswali yote ambayo yamo katika mioyo yao.

Swali ni je, tunapaswa kufanya nini and ni ushauri gani ambao tutanaweza kutoa katika siku hizi?

a)Kwanza, ninataka kumwuliza kila msomaji wangu kama ameokoka?

Hili ndilo swali muhimu sana katika maswali yote mtu anaweza kukuuliza. Haiwezi kumfaidi mtu yeyote kuwa mshirika wa kanisa ambalo linahubiri vizuri, ikiwa mtu huyu hajaokoka. Haitamsaidia mtu yeyote kuwa anafahamu Biblia ikiwa Kristo hayumo katika moyo wake. Je, hii ndio hali yako? Je, wewe un-aweza kukiri kwa ujasiri kwamba kweli moyo wako uko sawa mbele za Mungu? Je, moy wako umebadil-ishwa na Roho mtakatifu? Je, Kristo anaishi ndani mwako kwa imani? Ninakusihi, kwa usipumzike hadi kweli unajibu sahihi juu ya maswali haya. Mtu ambaye anakufa bila kuokoka, hata kama yeye alikuwa anafahamu maandiko vyema, yeye ataingia jahanum, kama tu Mafarisayo na Masadukayo.

b)Pili, ninataka kukuhimiza msomaji wangu ambaye unataka kujua ukweli wa Biblia kwamba un-afaa kusoma Biblia kwa uangalifu sana.

Biblia imepeanwa iwe nuru ya miguu yetu na iangaze njia yetu (Psalms 119:105). Mtu ambaye anasoma Biblia kwa njia ya unyenyekevu, heshima, kwa maombi na kila wakati ambaye atakosa kujua njia ya mbinguni. Tunafaa kuchunguza kila mafundisho kulingana na mafundisho ya biblia.

Je, unataka kujua ukweli? Je, wewe umechanganyika na mambo mengi ambayo unayasikia katika dini mingi? Je, wewe unataka kujua kile ambacho anapaswa kufanya ili uweze kuokoka? Jawabu ni, soma bib-lia yako na uache kuyasikia maneno matupu ya wanadamu. Soma Biblia yako kwa na uombe kwamba Roho Mtakatifu akufundishe neno lake. Soma Biblia na nia ya kutaka kutii kile ambacho Mungu anasema katika neno Lake. Soma Biblia yako na uangalifu sana na kwa uvumilivu mwingi, na utaona nuru. Mungu atakulinda kutokana na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo (walimu wa uongo) na atakuleta katika uz-ima wa milele. Tafadhali kuchukuwa uchari wangu na utafaidika sana.

c)Tatu, ninataka kushauri msomaji wangu ambaye anatumaini la kweli kwamba anapaswa kuen-delea kushikilia ukweli wa neno la Mungu.

Ninasema hivi kwa sababu ni lazima tuhakishe kwamba hatubagui ukweli wa Biblia. Ni lazima tuhakikishe kwamba ukweli wote wa Biblia tunauamini. Hatufai, kufanya yale ambaya ni kwanza kuwa ya pili au ya pili kuwa ya kwanza. Kwa kusema hivi ninamaanisha kwamba, hatufai kusema kwamba kanisa iko juu ya Kristo. Wachungaji hawafai kupewa vyeo au heshima ambyo Kristo mwenyewe hajawapa. Njia ambazo Mungu ameweka za neema hazifai kuonekana kwamba hizo ndizo njia za waokovu. Ni lazima tuwe waangalifu juu ya jambo hili kwa sababu kuna makosa mengi ambayo yamefanywa katika jambo hili. Hii ndio sababu tunafaa kusoma neno la Mungu kwa uangalifu. Tunafaa kulisoma bila kuondoa lolote wala kuzingatia sehemu moja au kitabu kimoja cha Biblia. Hii pia inamaanisha kwamba tunafaa tuwe kuzingatia ukweli wa biblia katika mawazo yetu kila wakati.

(4) Nne, ninataka kuwaelezea wakristo wote kwamba wasije wakadanganjwa na walimu wa uongo.

Page 12: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

Msomaji wangu ninakuonya kwamba usije ukadanganywa kwamba kila mtu ambaye anajii mwalimu wa dini anapaswa kusikilizwa. Tusiwaze kwamba kwa sababu mtu fulani ana ukweli nusu, basi tunapaswa hata yeye kumsikiliza. Mtu kama huyu ni hatari sana kwa sababu ataumiza nafis yako. Yeye ni mtu am-baye anakupataia sumu mbaya, lakini anafanya hivyo pole pole. Sumu mbaya sana inapeanwa pole pole ikiwa imechanganywa na chakula kizuri. Kuwa mwangalifu usije ukadanganywa na kujitahidi kwa wal-imu wengi wa uongo. Kumbuka kwamba kujitahidi kwingi si ishara ya kwamba mtu huyu anafanya kazi ya Kristo na kwa hivyo tunapaswa kumsikiliza.

Petro alimaanisha kile alisema wakati alimwambi Kristo kwamba hafai kufa msalabani. Lakini hata hivyo, Kristo alimjibu, kaa nyuma yangu Shetani. Sauli ambaye abaadaye aliitwa Paulo, alikuwa na bidii sana wakati alikuwa ana litatiza kanisa la Kristo. Alifanya haya yote kwa bidii lakini biddi yake hakuwa inatokana na ukweli wa neno la Mungu. Kuna walfame ambao wamewaua na kuwatatiza wakristo. Wali-fanya hivyo kwa biddi sana wakiwa walikuwa wanamtumikia Mungu, ilhali walikuwa wanawaua watu wa Mungu. Ni ukweli kwamba shetani mwenye huwa anajigeuza kama malaika wa nuru (2 Wakorintho 11:14). Miongoni mwa makosa mengi ambayo wengi wamefanya, makosa makubwa sana ni kuwaza kwamba ikiwa mtu anajitolea kwa bidii katika kazi ya Mungu, basi mtu huyu ni lazima awe anaenda mbinguni. Tuwe waangalife tusije tukadanyika. Tuwe waangalifu tusije tukaongozwa vibaya na wale am-bao wanaonekana kuwa watu wenye biddi sana katika mambo ya Mungu. Kuwa na bidii katika mambo ya Mungu ni jambo zui sana, lakini ikiwa bidii hiyo msingi wake si Kristo na neno lake, basi bidii hiyo ni ya uongo na hafai kabisa. Mambo mengi ambayo huwa inaheshimika miongoni mwa wanadmu mara mingi huwa ni chukizo machoni pa Mungu.

(5) Tano, ninataka kumshauri kila mtumishi wa Mungu kwamba unapaswa kila wakati kuchun-guza moyo wako kwa makini kuhusu hali yako mbele za Mungu.

Hili jambo la manufaa kila wakati katika siku hizi ambazo tumoishi. Katika siku hizi ambao tunaishi, tu-napaswa kuchunguza mioyo yetu kwa uangalifu sana. Tunafaa kuwa watu ambao tunawaza juu ya neno la Mungu kila wakati na kujichunguza hali ya mioyo yetu. Ikiwa tutalindwa ili tusianguka katika dhambi, ni lazima tuwe watu ambao tunamaliza muda miwngi katika ushirika na Mungu. Tunafa kuwa watu wa ku-soma neno la Mungu na kuomba kila wakati na pia kuwa na ushirika na watu wake kila wakati.

(6) Sita, ninataka kuwahimiza wakristo wote kwamba wanapaswa kuendelea katika imani ambayo wengi ambao wameokoka waliendela ndani.

Wakristo wote wanapaswa kujipeana kwa kanisa amblo linawajenga kiroho, ambalo linahubiri injili ya kweli, kanisa ambalo linajitoa kuwaeleza wenye dhambi kuhus dhambi zao na kuwaonyesha njia ya wokovu. Kila wakati neno la Mungu linapaohubiriwa kwa uaminifu, na wale ambao wanalihubiri waishi maisha ambayo inaambatana na neno hilo, hizo ndizo nguvu za Mungu. Paulo aliandika na kusema, injili ni nguvu za Mungu ambzo zinaleta wokovu (Warumi 1:16). Ni ukweli kwamba wengi watalitukana lakini hivi ndivyo mambo yamekuwa hata wakati wa mitume. Neno hilo linaweza kuhubiriwa kwa udhaifu na wale ambao wanalihubiri, lakini matunda yake au matokeo yake, ni ya kuleta sifa. Matunda yake hayawezi kuletwa na jambo lingine lolote isipokuwa neno la Mungu pekee.

Mahali ambapo neno la Mungu linahubiriwa kwa ukweli bila kulichanganya na uongo, hapo ndipo kunap-atikana nafsi ambazo zinaokolewa. Mungu ametuokoa na kutuita tuhubiri neno lake na kwa hivyo hatufai kuwa na aibu yoyote kushuhudia kwamba Kristo Yesu ndiye mwokozi na kwamba ndani mwake ndimo

Page 13: Web viewKama lile tunda ambalo Adamu na Hawa walikula, mafundisho haya yanaonekana kuwa vizuri sana na yale ambayo yanaweza kuwasaidia watu wa Mungu sana,

kuna ukweli. Tuko na ukweli na kwa hivyo hatufai kuogopa lolote kusema ukweli huu. Siku ya hukumu, ukweli utadhihirika kwamba ni nani ambaye ni wa ukweli.