Transcript
  • Kitabu cha hadithi 5

    Tusome Early Literacy Programme

    Darasa la 2

    KiswahiliDarasa la 2Kitabu cha hadithi 5

    Vitabu vya hadithi vya Tusome vimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu ili kusaidia kuinua kiwango cha kusoma kwa wanafunzi wa darasa la 1 na la 2. Hadithi hizi zinawapa wanafunzi nafasi ya kufurahia hadithi na kuinua uelewa wa hadithi nje ya masomo ya kawaida darasani. Vitabu hivi vinaweza kutumiwa na yeyote anayejifunza Kiswahili. Tunashukuru kwa usaidizi wa SIL LEAD kwa mchango wao katika kuandika hadithi hizi. Ili kusaidia katika juhudi hii, hadithi hizi zimeandikwa kwa kuzingatia yafuatayo:-• Lugha rahisi kwa wanafunzi na sentensi zenye urefu unaofaa,• Picha za kuvutia ambazo hazielezi hadithi kikamilifu lakini zinamwezesha

    msomaji kusoma zaidi ili aelewe hadithi,• Hadithi za kufurahisha zenye maudhui na dhamira ambazo msomaji

    anayeanza kusoma ataweza kulinganisha na maisha yake ya kila siku,• Vichwa vya hadithi ambavyo vinamwezesha msomaji kutabiri.

    Hadithi katika msururu huu ni:Darasa la 1: ‣ Fisi Mjinga na Chura na Kiboko ‣ Mchezaji Banda na Kisa cha Simba na Mbuni ‣ Faida za Ng’ombe na Siku za Wiki ‣ Kwa nini Mzee Kobe ana magamba na Jitu la MtoniDarasa la 2: ‣ Shujaa Musa na Mnyama Nimpendaye ‣ Mama Mzee na Nguruwe na Juma na Sungura ‣ Fisi na Mbuzi na Kuku na Mwewe Wakosana ‣ Sababu ya Paka Kupenda Kukaa Jikoni na Kwa nini Twiga

    ana Shingo Ndefu ‣ Safari ya Mombasa na Masaibu ya Musa

    Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya) na Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza (DFID/Kenya) kupitia mradi wa Tusome Early Grade Reading Activity.

  • 1

    Safari ya MombasaMwandishi: Nashera Ara Kodawa

    Mchoraji: Bonface Andala

    “Amina!” Mamake Amina alimwita. “Umeshapanga vitu vyako? Fanya haraka usichelewe.”

    “Ndiyo mama, kila kitu kimepangwa,” Amina alimjibu.

    Amina na binamu yake walikuwa wamepanga kwenda Mombasa. Mipango yote ilikuwa imekamilika.

    Mara mlango ulibishwa. Amina alikimbia kuufungua. Alikuwa Sifa, mjomba wake Amina. Amina alimrukia na kumkumbatia, “Mjomba Sifa! Karibu sana!”

  • 2

    “Mko tayari? Twende, muda wetu umeisha,” mjomba alisema.

    Sifa akamsalimia mama yake Amina. Kisha wakaondoka kwenda katika stesheni ya garimoshi. Kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari barabarani. Sifa akasema, “Amina, leo mtaachwa na garimoshi.”

    “Tafadhali mjomba usiseme hivyo,” Amina alilalamika.

  • 3

    Walifika katika stesheni ya garimoshi ya Nairobi na kupanda garimoshi. Walikuwa Amina, Asha, Kadogo na Saidi.

    Baada ya muda mfupi, garimoshi liliondoka kwenye stesheni kwa mwendo wa kasi.

    “Lo! Karibu tuchelewe,” Amina alisema. Walimpa mjomba Sifa kwaheri kwa kumpungia mkono wakiwa na furaha tele.

  • 4

    Gari lilipofika Athi River watoto hao walifurahi kuona maeneo tofauti. Waliona kituo cha kuchinjia ng’ombe.

    “Tucheze mchezo wa kadi!” Alisema Saidi. Saidi alikuwa mkubwa wa watoto hawa wote. Walifurahishwa sana na mchezo wa kadi. Walitumia wakati huu pia kuzungumzia yale watakayofanya watakapokuwa Mombasa.

    Mara, mhudumu wa hoteli alipita na kuwaambia kuwa chakula cha jioni kilikuwa tayari.

    “Ni furaha iliyoje kula chakula katika hoteli ndani ya garimoshi.

  • 5

    “Ni muhimu garimoshi kuwa na mkahawa ndani. Hii ni kwa sababu linapitia kwenye sehemu ambazo watu hawawezi kupata chakula.

    Garimoshi pia husimama katika vituo maalumu pekee. Kwa hivyo haliwezi kusimama kama basi ili abiria wanunue chakula,” alisema Sifa.

    “Isitoshe, safari ya garimoshi huchukua muda mrefu sana njiani.”

  • 6

    “Hivyo, abiria wanahitaji chakula ili wasiwe na njaa,” aliendelea Sifa.

    “Ni kweli, ikiwa hapangekuwa na mkahawa ndani ya garimoshi, tungefika Mombasa tukiwa na njaa tele,” alisema Asha.

    Baada ya chakula, watoto walilala usingizi mzito. Walipoamka, gari lilikuwa limefika Mariakani. Walipiga meno mswaki, wakanawa uso na kuelekea hotelini kupata kiamshakinywa.

    “Tuanze kupanga mipango ya leo,” Amina alisema.

    “La! Kwanza tumpigie shangazi simu tumwambie tunaelekea Mazeras,” alisema Saidi.

  • 7

    Walimpigia shangazi yao simu akawaeleza kuwa wangempata kwenye stesheni Mombasa. Waliposhuka katika stesheni, shangazi yao aliwapokea na kuwapeleka nyumbani. Baada ya kuoga waliondoka kwenda kuzuru Fort Jesus.

    Huko Fort Jesus waliona ngome ya zamani sana. Ndani ya ngome hiyo waliona pia vitu vya zamani sana.

  • 8

    “Njoo Saidi! Njoo uone sanamu za Waswahili na vyombo walivyotumia zamani.”

    Waliona pia kisima cha zamani sana ambacho kilitumiwa na Wareno.

    Ilipofika saa saba na nusu, walienda kula chakula cha mchana na kuelekea sehemu iitwayo Bamburi Nature Trail kwa matembezi mwituni.

  • 9

    “Leo nataka nimpige picha yule kobe mwenye miaka zaidi ya mia moja,” Amina alisema. Kila mmoja wao alipigwa picha na huyo kobe.

    Waliporudi nyumbani shangazi yao aliwaandalia chakula mapema.

    “Nataka mle mapema ili muweze kulala mapema. Najua mmechoka sana,” shangazi yao aliwaambia.

  • 10

    Wakati wa chakula walizungumza juu ya yale waliyoona huko Fort Jesus na Bamburi Nature Trail.

    “Haya! Laleni mapema ili kesho muwe wachangamfu.” Shangazi yao aliwaambia. Usiku huo watoto wote walilala fo fo fo!

    Maswali1. Amina na binamu yake walipanga

    kwenda wapi?2. Ni nini kingefanya Amina waachwe na

    garimoshi?3. Watoto walifurahia kuona nini Athi

    River?4. Watoto walifanya nini baada ya kula

    chakula?5. Baada ya kuoga, watoto walienda

    wapi?

  • 11

    Masaibu ya MusaMwandishi: Nashera Ara Kodawa

    Mchoraji: Bonface Andala

    Musa alikuwa mvulana wa darasa la pili. Hakuwa amewahi kuendesha gari tangu alipozaliwa. Musa alikuwa akiangalia kila kitendo ambacho baba yake alikifanya alipokuwa akiendesha gari akimpeleka shuleni. Aliangalia jinsi baba yake alivyoingiza ufunguo mahali pake. Alitazama pia alivyoweka gia na kuzibadilisha. Asubuhi moja baba yake akimpeleka shuleni kama kawaida, Musa alifanya kitendo cha ajabu sana.

  • 12

    Baba yake Musa aliegesha gari kando ya barabara na kuingia dukani. Alitaka kumnunulia Musa daftari la mazoezi ya hesabu. Kwa haraka, Musa aliondoka kwenye kiti chake na kukikalia kiti cha dereva.

    Baba yake alikuwa amesahau ufunguo wa gari. Musa alizungusha ufunguo na gari likanguruma.

  • 13

    Baada ya gari kunguruma, Musa alitoa breki ya mkono na kuweka gia ya kwanza. Gari lilianza kwenda. Mara Musa alishikwa na woga. “Gari laondoka! Nitalisimamisha vipi? Nilikuwa ninajaribu tu…” Musa aliwaza. Alimwona baba yake akitoka dukani akajua mambo yameharibika. Alijaribu kulisimamisha gari lakini hakufaulu. Gari liliendelea kuongeza kasi. Musa alijaribu kila aliloliwaza lakini yote hayakumsaidia. Moyo ulimdunda sana. Alihepa kwa karibu sana kugongana na pikipiki moja.

  • 14

    Musa alisikia honi za magari kila upande huku wengine wakimpita na kumtusi. Alitokwa na jasho mwili mzima. Gari lilifika kwa barabara kuu na hata kuongeza kasi zaidi.

  • 15

    Aliwaza sana jinsi ya kulisimamisha gari hilo lakini hakupata la kumsaidia. Kwa bahati ilikuwa asubuhi sana na kwa hivyo hapakuwa na magari mengi barabarani.

    Alifikia kivukio cha wanaotembea kwa miguu. Akakumbuka kupiga honi. Alipiga honi kwa mfululizo. Wanafunzi waliokuwa wakivuka walikimbilia kando ya barabara. Wakati huu gari lilianza kuyumbayumba. Alitoa mkono mmoja nje na kupiga honi. Madereva wengi walitoka barabarani na kumpa nafasi.

  • 16

    Mara baba yake alifika kando ya dirisha la gari akiwa juu ya pikipiki. Kumbe alikuwa amemfuata kwa pikipiki. “Musa! Umefanya nini? Utasababisha ajali! Simamisha gari!” Mara polisi wa pikipiki alifika na kushangaa kuona dereva aliyevalia sare ya shule.

  • 17

    Alishangazwa zaidi alipoona ni mwanafunzi mdogo wa shule.

    Kwa bahati nzuri, katika hali za kutafuta suluhisho, Musa aliisongesha gia na gari lilipunguza mwendo. Lilitembea taratibu hadi lilipogonga jiwe kando ya barabara na kusimama. Taa za gari zilivunjika. Musa alipata majeraha kwenye miguu.

  • 18

    Alishtuka sana hata hakujua alichofanya ili gari lisimame. Polisi na baba yake wakawa pia wameegesha pikipiki zao. Yule polisi alimkaribia Musa kwa hasira lakini baba yake akamtuliza. Akamwambia polisi kwamba yeye ndiye aliyekuwa mwenye gari. Polisi alikuwa amedhani kuwa Musa alikuwa ameiba gari hilo.

    Baba yake Musa alimwomba yule polisi msamaha. “Nakubali mimi ndiye mwenye makosa, nilisahau ufunguo ndani ya gari, tafadhali nisamehe,” babake Musa alimsihi polisi. Mwishowe polisi alikubali kumsamehe.

  • 19

    “Mwanangu Musa nitajua la kumfanyia tutakapofika nyumbani,” baba yake Musa alimweleza polisi.

    Wakati huu wote, Musa alikuwa akitetemeka sana huku jasho likimtoka mwili mzima. Musa alimuomba baba yake msamaha.

    Kabla ya kumsamehe, baba yake Musa alimuonya asirudie makosa hayo tena. Alimwambia ya kwamba alihatarisha maisha yake na ya watumiaji barabara wengine. Babake alimpeleka Musa hospitali. Alipewa dawa na kudungwa sindano.

  • 20

    Walipofi ka nyumbani, babake akamwambia kwamba hangemruhusu kumtembelea mjomba wake. Hii ilikuwa adhabu kwa Musa. Musa alikuwa akitarajia kumtembelea mjomba wake shule ikifungwa. Mjomba wake aliishi jijini. Tangu siku hiyo, Musa hakuwahi kurudia makosa kama yale.

    Maswali1. Musa alikuwa katika darasa gani?2. Babake Musa alitaka kumnunulia Musa

    nini?3. Kwa nini Musa alitokwa na jasho

    mwili mzima?4. Baba yake Musa alimfanya nini baada

    ya kosa?

  • Kitabu cha hadithi 5

    Tusome Early Literacy Programme

    Darasa la 2

    KiswahiliDarasa la 2Kitabu cha hadithi 5

    Vitabu vya hadithi vya Tusome vimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu ili kusaidia kuinua kiwango cha kusoma kwa wanafunzi wa darasa la 1 na la 2. Hadithi hizi zinawapa wanafunzi nafasi ya kufurahia hadithi na kuinua uelewa wa hadithi nje ya masomo ya kawaida darasani. Vitabu hivi vinaweza kutumiwa na yeyote anayejifunza Kiswahili. Tunashukuru kwa usaidizi wa SIL LEAD kwa mchango wao katika kuandika hadithi hizi. Ili kusaidia katika juhudi hii, hadithi hizi zimeandikwa kwa kuzingatia yafuatayo:-• Lugha rahisi kwa wanafunzi na sentensi zenye urefu unaofaa,• Picha za kuvutia ambazo hazielezi hadithi kikamilifu lakini zinamwezesha

    msomaji kusoma zaidi ili aelewe hadithi,• Hadithi za kufurahisha zenye maudhui na dhamira ambazo msomaji

    anayeanza kusoma ataweza kulinganisha na maisha yake ya kila siku,• Vichwa vya hadithi ambavyo vinamwezesha msomaji kutabiri.

    Hadithi katika msururu huu ni:Darasa la 1: ‣ Fisi Mjinga na Chura na Kiboko ‣ Mchezaji Banda na Kisa cha Simba na Mbuni ‣ Faida za Ng’ombe na Siku za Wiki ‣ Kwa nini Mzee Kobe ana magamba na Jitu la MtoniDarasa la 2: ‣ Shujaa Musa na Mnyama Nimpendaye ‣ Mama Mzee na Nguruwe na Juma na Sungura ‣ Fisi na Mbuzi na Kuku na Mwewe Wakosana ‣ Sababu ya Paka Kupenda Kukaa Jikoni na Kwa nini Twiga

    ana Shingo Ndefu ‣ Safari ya Mombasa na Masaibu ya Musa

    Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya) na Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza (DFID/Kenya) kupitia mradi wa Tusome Early Grade Reading Activity.

    /ColorImageDict > /JPEG2000ColorACSImageDict > /JPEG2000ColorImageDict > /AntiAliasGrayImages false /CropGrayImages true /GrayImageMinResolution 300 /GrayImageMinResolutionPolicy /OK /DownsampleGrayImages true /GrayImageDownsampleType /Bicubic /GrayImageResolution 300 /GrayImageDepth -1 /GrayImageMinDownsampleDepth 2 /GrayImageDownsampleThreshold 1.50000 /EncodeGrayImages true /GrayImageFilter /DCTEncode /AutoFilterGrayImages true /GrayImageAutoFilterStrategy /JPEG /GrayACSImageDict > /GrayImageDict > /JPEG2000GrayACSImageDict > /JPEG2000GrayImageDict > /AntiAliasMonoImages false /CropMonoImages true /MonoImageMinResolution 1200 /MonoImageMinResolutionPolicy /OK /DownsampleMonoImages true /MonoImageDownsampleType /Bicubic /MonoImageResolution 1200 /MonoImageDepth -1 /MonoImageDownsampleThreshold 1.50000 /EncodeMonoImages true /MonoImageFilter /CCITTFaxEncode /MonoImageDict > /AllowPSXObjects false /CheckCompliance [ /None ] /PDFX1aCheck false /PDFX3Check false /PDFXCompliantPDFOnly false /PDFXNoTrimBoxError true /PDFXTrimBoxToMediaBoxOffset [ 0.00000 0.00000 0.00000 0.00000 ] /PDFXSetBleedBoxToMediaBox true /PDFXBleedBoxToTrimBoxOffset [ 0.00000 0.00000 0.00000 0.00000 ] /PDFXOutputIntentProfile () /PDFXOutputConditionIdentifier () /PDFXOutputCondition () /PDFXRegistryName () /PDFXTrapped /False

    /CreateJDFFile false /Description > /Namespace [ (Adobe) (Common) (1.0) ] /OtherNamespaces [ > /FormElements false /GenerateStructure false /IncludeBookmarks false /IncludeHyperlinks false /IncludeInteractive false /IncludeLayers false /IncludeProfiles false /MultimediaHandling /UseObjectSettings /Namespace [ (Adobe) (CreativeSuite) (2.0) ] /PDFXOutputIntentProfileSelector /DocumentCMYK /PreserveEditing true /UntaggedCMYKHandling /LeaveUntagged /UntaggedRGBHandling /UseDocumentProfile /UseDocumentBleed false >> ]>> setdistillerparams> setpagedevice


Recommended