!. viromen-alSc:a MRADI WA UMEME WA GESI YA.. Environmental & Social
* Assessment & Management SONGO SONGO. 5: Plan Sum m ary - Sw ahili -- --- ------------ -- - ---- - ---- - ------- - - --- -------------- - - - - ------------------------------::Plan Summary - Swahili
*: - - ------ O TATHMINI ZAKIMAZINGIRA NA
KIJAMII NA MPANGOWA UDHIBITI
0 14 ~~~~Muhtasari wa Tafirti za Athari za Kimazingira na Mpangowa Kina wa Udhibiti
Oktoba 2001
E65 v.2October 2001
9.
9. .-.
0- ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~
*. .. , _ ;d.-- - v-~ = --l . . ,= D i (_ -t
* . .,.,. . ( * 0 .
. ,:;5! .i½. ' . ,' ' 'o P y
.. ~~ :. .... -i, ..:.E, ......... . .: .q :.;,-..
. .
S..
" ':y,, .D ,,,,s, 0 N;~~~('~~igu
0*
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
Pub
lic D
iscl
osur
e A
utho
rized
TA-HMINI Z KIMAZINGIR NA KIJAMII NA HMANGO WA UDuIBITI
Congas
Mradi wa Umeme wa Gesi ya Songo Songo
Tathmini za Kimazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti
Muhtasari waTafiti zaAthari za Kimazingira na Mpango wa Kina wa Udhibiti
Oktoba 2001
Kampuni ya Songas
Nyumba ya Maarifa
Mtaa wa Ohio
Dar es Salaam
Simu: +255-22-21 1-7313
Faksi: +255-22-21 1-3614
www.songas.com
TATHmINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
Mombasa- ,
Tanga,.Pernba
-~i1. -ZANZI BAR
I_____ 1'
__ I - ~~~~~Unguia
F____ Kh ha $Ka arLi -SMtambowaurjmc rvU DAR ES SALAAM
Mkuranga O'0
Mazomorao
_ ~~~~BunguO , ,-- ~NgulakulaVSW0
I. ! --4 -! - _ i,- ,0 ,AVYAMAFIA zMbvera _
Sormanga Visima vya GesinaMtarbowa a:
Kitwa Kivinieo Kusafisha Gsi <
Kitwa hlasokoLindi
Mitwara '
(Gesi iliyogunduliwa Mnazi Bay)
Ramani 1: Eneo la Mradi wa Gesi ya Songosongo
2
TATHMINI ZA KIMAZING,RA NA KIJAmII NA MPANGO WA UDHIBITI
SURAYA
UfupishoGesi asilia iligunduliwa mwaka 1974 katika kisiwa cha Songo Songo kilicho nje kidogo ya pwani ya
mashariki mwa Tanzania. Mradi wa gesi ya Songo Songo kuzalisha umeme umepangwa kuendeleza
na kuuza raslimali ya gesi asilia nchini Tanzania.
Wadhamini wa sekta binafsi wa mradi wa Songo Songo ni Shirika laAES na Kampuni ya Nishati
ya PanAfrica. Kampuni ya utekelezaji inaitwa Songas Limited (Songas), ambayo ni kampuni binafsi
kwa asilimia kubwa na imesajiliwa kwa mujibu wa sheria yaTanzania.Washiriki wa Mitaji wa CDC
pamoja na Shirika la Maendeleo ya Fedha laTanzania (TDFL) ni wawekezaji wa hisa pia.
Wakopeshaji wa mradi huu ni Benki ya Dunia na Benki yaWawekezaii ya Ulaya.
Maelezo kuhusu MradiMradi utatoa gesi asilia kutoka kwenye visima vya gesi huko Songo Songo na kuipeleka kwenye
mtambo wa kuzalisha umeme wa Ubungo unaoendeshwa na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO).Vilevile gesi itapelekwa kwenye kiwanda cha Saruji chaWazo, jijini Dar-es-Salaam.
Eneo lote la mradi limeonyeshwa kwenye ramani namba 1.
Sehemu kuu za mradi ni pamoja na:(i) visima vya gesi katika kisiwa cha Songo Songo (tazama picha ukurasa 3);
(ii) mfumo wa kukusanya gesi na kiwanda cha kuisafisha katika kisiwa cha Songo Songo;
(iii)kilomita 25 za bomba litakalolazwa chini ya maji kutoka kisiwa cha Songo Songo hadi
Somanga Funga na kilomita 207 za bomba litakalozikwa ardhini kutoka Somanga Funga hadi
Dar-es-Salaam;
(iv)kilomita 16 za bomba kuelekea kiwanda cha Saruji chaWazo;
(v) mitambo ya kuzalisha umeme (tabaini) iliyoko kwenye kituo cha umeme cha Ubungo yenye
uwezo wa kuzalisha megawati 112 za umeme na yenye uwezo wa kutumia gesi asilia;
(vi)udhibiti wa mfumo, kituo cha uendeshaji na miundombinu mingineyo pale Ubungo, na
(vii)utawala na mafunzo kwa mradi.
Ahadi za Songas za masuala ya mazingira na kijamiiSongas, kwa kupitia wafadhili wake pamoia na Serikali yaTanzania, inakusudia kwa dhati kuendeleza
mradi wa Songo Songo kwa utaratibu ambao utaweka mizania (wakati wote na kwa kuwajibika)
kati ya uhifadhi wa mazingira na sura ya kijamii ya Tanzania na uondoaji wa umaskini na faida za
kiuendeshaji za mradi. Kwa kutumia filosofia hii na mwelekeo huu, Songas itadumisha fursa bora
na za muda mrefu za kibiashara kwa ajili ya wadhamini wa mradi huu na maslahi yanayoambatana
nayo ya washikadau wa nchi, kanda, na mahali ambapo mradi unatekelezwa.
AES, kampuni inayoongoza kwa hisa, ina sera ya kuchangia hadi asilima 5 (5%) ya mapato halisi
kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Maamuzi yanayohusiana na kiwango na mahali ambapo msaada uta-
tolewa umeachiwa mameneja wa zaidi ya mitambo ya umeme 125 inayoendeshwa na kampuni ya
AES duniani kote. Kwa makubaliano na wanahisa wengine wa Songas, kampuni ya Songas itaanzisha
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KI.AMII NA MPANGOWA UDHIBITI
Kisima cha Gesi cha Nchi Kavu
i- - A - ;_____- - I__C
__
_ __ S _ |~~S
|~~~~~~ ~ _
-
Kisima cha Gesi cha Baharini
3
TATHiM NI ZA KImAZINGIRA NA KrJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
sera kama hiyo nchini Tanzania. Mwezi Juni mwaka 2000, sheria ya kodi ya Tanzania ilibadilishwa,
hivyo kuipa moyo zaidi Songas kuchangia maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.
Sera na Masharti ya Kiurekebishaji na ya KisheriaMradi wa Songo Songo umeandaliwa na utaendeshwa kwa kulingana na matakwa ya kanuni na she-
ria, ikiwa ni pamoja na zile za Serikali yaTanzania na Benki ya Dunia.
Mashauriano na Uarifu wa UmmaSehemu muhimu tatu za mradi wa Songo Songo, tayari zimekamilika. Mafanikio ya sehemu hizi
ndogo tatu za mradi yanaonyesha mawasiliano mazuri ya Songas na mashauriano yenye mafanikio
kati yake na watu waliothirika na mradi. Mradi wa Songo Songo unafahamika sana na umma wa
Tanzania na umeelezewa vizuri sana katika magazeti, redio na televisheni. Songas imepanga kuen-
delea kuwasiliana vizuri na washikadau wote na watu walioathirika na mradi ili kuwe na taarifa
sahihi zinazotolewa kwa washirika wote kuhusiana na mradi.
Zaidi ya kuwepo kwa majadiliano mengi na umma pamoja na tathmini, Songas imekubaliana na
masharti rasmi ya uarifu ya Benki ya Dunia kwa ajili ya tathmini za mazingira kwa kutoa taarifa zake
kwa Kitengo chaTaarifa cha Benki ya Dunia na hapa nchini. Kwa kuzingatia hilo, ripoti yaThathmini
za Mazingira na Kijamii na Mpango wa Udhibiti, ilisambazwa kwa washikadau wote ndani na nje
ya Tanzania.
1 - 1_ ; J
_N~L ,
4~~
_ F~~~~~71_
Mkutano wa wananchi walioathirika na Mradi
TATHMINI zA KIMAZNGIRA NA KilAmii NA MPANGO WA UDHIlM
Upembuaji waVibadala na Uteuzi wa NjiaSongas imechunguza vibadala vingi, ikiwa ni pamoja na njia mbadala za kuzalisha umeme, umbo
mbadala la mradi, na njia mbadala za bomba la majini na la nchi kavu ili kufikia mfumo unaokubali-
ka na usio na gharama kubwa.
Muhtasari waTafiti za Kimazingira na KijamiiKatika kuupa mwega mradi wa Songo Songo, Songas imegharamia utayarishaji wa ripoti maalum
zipatazo 28 zinazohusu mazingira na mada nyingine za kijamii tangu 1993. Kama ilivyodokezwa, kazi
hii ilifanywa i1i kutekeleza masharti ya tathmini ya Benki ya Dunia na Sekta mbalimbali zaTanzania
zinazohusiana na mazingira na wajibu wa kijamii. Kwa ufupi, ripoti hizo zinapendekeza kuwa mradi
hautakuwa na athari mbaya za kimazingira na kijamii kama Songas na makandarasi wake wakubwa
na wadogo watatekeleza hatua za kupunguza makali zilizopendekezwa, kusimamia na kufuatilia
hatua hizo.
Athari za Kimazingira na Kijamii na Mpango wa UdhibitiSongas inakusudia kutumia "mwenendo bora" wa kimataifa katika udhibiti wa athari za kimazingi-
ra na kijamii za mradi wa gesi ya Songo Songo wa kuzalisha umeme. Songas itasanifu, kuunda na
kuendesha mradi na kutekeleza mfumo wa usimamizi wa mazingira, afya na usalama ambao
umeegemea kanuni za Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO), ISO 14001.
Muundo wa Utawala wa SongasSongas itakuwa na wajibu kamili kwa mambo yote yanayohusu mradi wa Songo Songo kwa kutu-
mia timu ya uongozi yenye uzoefu katika kuendesha majukumu yake.Wakati wa kipindi cha ujen-
zi, majukumu ya kuchukua hatua mbalimbali za kimazingira na kijamii kwa ajili ya udhibiti na usi-
mamizi yataachiwa makandarasi. Katika mazingira kama hayo, Songas itabaki na uwezo wa kusi-
mamia i1i kuhakikisha kuwa makandarasi wanatekeleza wajibu wao.
Wajibu wa MakandarasiSongas itahakikisha kuwa mikataba na makandarasi wakuu na wadogo wa ujenzi inazingatia vipen-
gele maalum vya mfumo wa usimamizi wa mazingira, afya na usalama ambavyo vitakuwa ndani ya
wigo na wajibu wa mkandarasi.
Maelezo kuhusu Masuala Muhimu:RidhaaUkuzaii wa mpango wa udhibiti wa kimazingira na kijamii kwa aiili ya mradi wa Songo Songo
umeridhia Sera za Utekelezaji na Maagizo ya Benki ya Dunia kama inavyoonyeshwa katika jedwalilinalofuata:
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA MA KIJAMII NA MPANGO WA UCDI-ITI
OP 4.01 :Tathmini ya Mazingira. Mradi unaridhia:Tathmini ya mazingira imetayarishwa kulingana namasharti ya mradi wa kategoria A.
OP/BP 4.04: Makazi Asilia Mradi unaridhia: Mradi umetumia mwelekeo wa kitahadhari katika usi-mamizi wa rasilimali za asili katika jitihada za kuhifadhi na kulinda makaziasilia, kuyaepuka makazi muhimu na kudumisha shughuli za kiekolojia. Kilainapokuwa budi hatua za kupunguza na kuondoa tatizo zimebainishwa ilikupunguza kasi ya upoteaji wa makazi pale ambapo hali haizuiliki.Mdhamini wa mradi atatoa pia uhakika wa fursa za maendeleo endelevuya muda mrefu katika nchi kwa kupitia mpango wake wa maendeleo yajamii, michango na ushiriki katika Bodi ya Mfuko wa Kanda ya Mashariki(The Eastern Arc Endowment Trust Fund) na Chama cha Hifadhi yaWanyamapori chaTanzania,
OP 4.09: Udhibiti wa wanyama Mradi Unaridhia: Mdhamini wa mradi hatatekeleza shughuli yoyote yaau wadudu waharibifu kudhibiti wanyama au wadudu waharibifu.
OPN 11.03: Mali ya Kijadi Mradi unaridhia: Usanifu kamambe wa njia utaepuka uharibifu mkub-wa kwenye mali za kitamaduni zinazofahamika na zisizoweza kurejeshwaupya. Zaidi ya hayc, mdhamini wa mradi atasanifu na kutekeleza programuya uandani ya kushughulikia'mali ya Kijadi itakayobahatika kuonekana'yaani 'Chance finds' wakati wa ujenzi wa mradi.
OD 4.20: Wenyeji Haihusiki: Hakuna mwenyeji, kama ilivyofafanuliwa na OP 4.20, ambayeataathinika na mradi.
OD 4.30: Kulazimika kuhamia Mradi unaridhia: Mdhamini wa mradi ametayarisha Programu ya tath-Makazi Mapya mini ya Kiuchumi-jamii ili kuhakikisha kuwa wale waathirika wa mradi
wanasaidiwa ipasavyo kwa ajili ya mali walizopoteza na kwamba mapatoyanarejeshwa au kuboreshwa kulingana na sera.Tafiti nyingine zinapen-dekezwa za kukagua uridhiaji wa sera na kuongezea kanzi ya data zakiuchumi-jamii kwa ajil. ya jambo hili.
OP 4.36: Misitu Mradi unaridhia Mradi haujihusishi na biashara ya magogo au ununuziwa vifaa vya magogo. Kwa kuwa uoto fulani utafyekwa katika maeneoyaliyopangwa, mfadhili wa mradi atatekeleza hatua za kupunguza uharibi-fu ili kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara katika uoto pamoja na hatuanyingine yoyote ziiakazopendeke7wa na Idara ya Misitu yaTanzania.Mfadhili wa mradi atafanyakazi pia na wenyeji, na MashirikaYasiyo yaKiserikali (NGO's) kila inapobidi, ili kuendeleza hatua za uimarishaji naurejeshaji uoto juu ya ardhi.
OP/BP 4.37: Usalama wa Haihusiki: Mradi haujishughulishi na ujenzi wa mabwawa.Mabwawa
OP/BP/GP 7.50: Miradi iliyoko Haihusiki: Mradi utaendeshwa katika eneo la maji yaTanzania pekee.katika Njia za Maji za Kimataifa
OP/BP/GP 7.60: Miradi katika Haihusiki: Mradi hauko wala hautaingia hadi kwenye maeneo yenyeMaeneo yenye mgogoro mgogoro.
Sera ya Utoaji wa Habari Mradi unaridhia:Taarifa kuhusiana na mradi zimekuwa zikitolewa nazitaendelea kutolewa nchini Tanzania na katika Kitengo cha habari chaBenki ya Dunia.
Viwango vya Kazi Mradi unaridhia: Mdhamini wa mradi hatatumia ajira ya watoto au yanguvu.
6
TAT-MINI ZA KiMAZINGIRA NA KIJAMIl NA MPANGO A UDHIRcI
Masuala muhimu ya Kimazingira na KijamiiSura ya 7 ya ripoti ya mazingira ambayo huu ni muhtasari wake inajumuisha muhtasari na masuala
ya mazingira ya asili na pia tafiti za kijamii, matumizi ya ardhi na kiuchumi-jamii, ikiwa ni pamoja na
masuala ya afya, makazi na fidia. Sehemu hizi zinajumuisha haii za msingi za mazingira kufuatana na
aina na unyeti wa mazingira katika ukanda unaopita bomba.
Sura ya 8 inaeleza kwa kina athari zinazoweza kutokea za kijamii (ikiwa ni pamoja na za kiuchu-
mi-jamii) na athari za kimazingira pamoja na hatua zitakazochukuliwa na Songas ili kupunguza athari
hizo na kuongeza faida zinazotokana na mradi kwa wenyeji na taifa zima.
Masuala muhimu ya kimazingira na kijamii, yaliyo chanya na hasi, yaliyobainishwa wakati wa
uchanganuzi wa tathmini ya athari za mradi huu na namna Songas itakavyoyadhibiti yameorod-
heshwa hapa chini.
1. Bioanuwai - Spishi za kimamalia zinazohitajika kuhifadhiwa zinapatikana katika eneo la
mradi. Shughuli za mradi zitafanywa kwa namna ambayo haitaziathiri spishi hizi wakati wa
ujenzi na uendeshaji wa mradi.
2. Misitu - Haki ya njia inapitia katika maeneo yenye uoto wa asili. Songas itatumia njia zote
zinazowezekana kupunguza ukataji wa miti na itasaidia shughuli za usimamizi mzuri wa misitu
katika ukanda unaopita bomba.
3. Maji - Songas itawapatia wakazi wa kisiwa cha Songo Songo maji safi ya kunywa (pamoja na
umeme) kutoka kwenye kiwanda cha gesi.
4. Mmomonyoko wa Udongo - Mkandarasi atahakikisha kwamba maeneo yanay-
omomonyoka kirahisi yanaimarishwa baada ya kutibuliwa.
5. Taka - Songas itatekeleza mkakati wa kudhibiti taka ngumu kwa mradi wote ili kuhakikisha
kwamba taka zinaondoshwa kwa namna isiyohatarisha mazingira.
6. Hewa - Utoaji wa hewa kutoka kwenye mradi utazingatia miongozo ya Benki ya Dunia. Gesi
zitakazotolewa zitachangia kwenye utoaji wa gesi zenye kuongeza kiwango cha joto katika
angahewa duniani, lakini kwa kiasi kidogo zaidi kuliko kama mitambo ya kuzalisha umeme
(tabaini) zingeendelea kutumia fueli mafuta.
7. Bomba - (Majini na Nchi Kavu) - Ili kushughulikia uvujaji wa gesi utakaotokea kwa bahati
mbaya, Songas itaunda na kutekeleza mpango wa dharura wa kudhibiti hali itakayotokana na
uvujaji wa gesi.
7
TATHmI-NI ZA KIMAZ NGIRA NA KjAmII NA MPANGO WA UDHIBITI
.
j ' -fI;'., I . , _
Kikundi cha wahasibu wakilipa fidia kwa walioathirika na mradi
8. Masuala ya Kiuchumi-jamii - Ujenzi na uendeshaji wa bomba utatoa ajira za kutosha
nchini Tanzania na katika eneo la mradi. Songas itamhitaji mkandarasi kutumia nguvukazi ya
wenyeji na kununua bidhaa na huduma za wenyeji wa eneo la mradi. Songas itaziunganisha
jumuiya zilizoathirika na mpango wa mikopo midogomidogo.Jumuia zitafaidika pia na ukuzaji
wa biashara ndogondogo.
9. Masuala yanayohusiana na Afya - Kwenye kisiwa cha Songo Songo, Songas itainua viwan-
go vya watumishi wa afya na kituo kinachotoa huduma ya afya ili kuhudumia vizuri zaidi
wananchi na watumishi wa mradi. Songas itaandaa mkakati wa kuthibiti ueneaji wa
VIRUSI/UKIMWI katika maeneo yote ya mradi.
Makazi MapyaShughuli za kuwapatia wananchi makazi mapya zilifanyika chini ya Mipango ya Utekelezaji ya Makazi
Mapya iliyopangwa kutekeleza masharti ya Benki ya Dunia na yale ya Serikali ya Tanzania, hii ni
pamoja naAgizo la Kiutendaji nambari 4.30 la Benki ya Dunia:Mpango wa Kulazimika kuhamia
Makazi Mapya. Songas imekwishafanya uchunguzi unaohitaiika, ikaandaa mipango inayotakiwa, na
katika baadhi ya maeneo ikaanza utekelezaji na ufuatiliaji wa programu zinazohitajika ili kuhakik-
isha kuridhia kwa sera za Benki ya Dunia za usalama wa kijamii, ikiwa ni pamoja na Mpango wa
Kulazimika KuwapatiaWananchi Makazi Mapya.
Programu za fidia za Songas ziliandaliwa mahsusi kuwarejeshea mapato watu walioathirika na
mradi. Mradi umelipa fidia kwa viwango vya soko, ambavyo ni vikubwa kuliko viwango vilivyowek-
wa na serikali yaTanzania.Viwango vya fidia ni vikubwa mara tatu zaidi ili kurejesha mapato ya watu
8
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIUAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
waliofidiwa na huku yakiwepo makusudio ya kuboresha, au kukaribia hali ya maisha yao kabla ya
kuathirika na mradi.
Kwa ujumla, jambo lililozingatiwa sana katika kupanga njia litakamopita bomba lilikuwa ni
kupunguza usumbufu na kuwapatia wananchi makazi mapya. Kutokea mahali bomba linapoibukakutoka majini na kuingia nchi kavu hadi viungani mwa Dar es Salaam (umbali na takribani kilomita
200), ni kaya 33 tu ndizo zilizohitajika kupatiwa makazi mapya. Zaidi ya hayo, ingawa bomba linapi-tia katika eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam, ni kaya 155 tu zilihitaji kuhamishwa kutoka kwenye
eneo la njia ya bomba katika maeneo ya mji.
Maeneo mawili yalichaguliwa kwa ajili ya makazi mapya ya familia katika eneo la Dar es Salaam
- Kinyerezi, kusini mwa Dar es Salaam, na Salasala, huko kaskazini (tazama ramani namba 2). Kaya
nyingine 155 zilizoathiriwa na mradi, ni kaya ambazo zilikuwa katika maeneo yaliyotengwa kwa
matumizi ya umma, zimefidiwa pia na kuhamishiwa humo humo ndani ya maeneo ya makazi mapya.
Makazi haya mawili yaliyopangwa vizuri ni rasilimali kubwa kwa jiji la Dar es Salaam.
Mpango wa Ufuatiliaji wa Mazingira na JamiiSongas inatekeleza Mpango wa Ufuatiliaji wa Mazingira naJamii ili kufuatilia athari za mradi. Mpango
huu unajumuisha maeneo yanayohusika na bomba la Songas, mitambo ya kuzalisha gesi na uende-
shaji wa mtambo wa kuzalisha umeme.
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
_A1TONGA A~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~At:,,, ; Nt -:~~~~~~~~~~~~A . _ .
-V
BAHARI HINDI
1, ~ ~ s S. lani
0~~~~~~~~~~~~
>111~ 'h 'Ii
/; I I' E, n e,
Xi-.z; D1ar-es Salaam- :
7 _ >_;F_ 1 ,-^ s~~~~~~Kituo .
60~~~~~~~~~~~~
~~~~~~~~~~~~~~
,.--,S'-~ ~ ~~>-~. I;; ,I - . ....
TA -- --- -- ---- , .
Maka, mapya Mkaz, Bambamin kgog Njla ya ges ya Songosongo
~~~~~~~~~~~~~~~~~~ -- Maneoy i'm a Yaal e. --u M starl ya kontuaRamMani k2: .Maeneo-kMto yMkzap
Ramani 2: Maeneo ya Makazi Mapya~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
TATHMINI ZA KiMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGO WA UDHIBIT
SURAYA
2
Shughuli za Programu yaMaendeleo ya Jamii hadi
Januari 2001
Fursa za kuboresha mapatoMapato ya watu walioathirika na mradi inawezekana hayakuwa hasi, hasa katika maeneo ya vijijini
ambako watu waliofidiwa na mradi bado wanaendelea kutumia mashamba ambayo tayari wame-
fidiwa. Hili lilifanyika i1i kujenga uhusiano mzuri kati ya mradi na jamii za wenyeji.
MajiKwenye kisiwa cha Songo Songo, mradi umejenga tangi la maii lenye mabomba kwa ajili ya kuwa-
patia wananchi maji yaliyowekewa dawa (maji safi na salama) kutoka mapangoni wakati wakisubiri
kupatiwa maii (yatakayofikishwa hadi kwenye mpaka wa mtambo wa gesi na mradi) kutoka kwenye
mtambo wa gesi. Kuwepo kwa mfumo wa kuwekea maji dawa kumeongeza sana ubora wa maji.
UsafiUtoaji wa maji kisiwani umeboresha afya na usalama, kwani ugumu wa kuchota maji toka kwenye
mapango yenye kina kirefu umepungua. Upatikanaji wa maji umesababisha kuwepo na mazingira
mazuri zaidi kwa wanakijiji.
Nyumba BoraKumekuwepo mabadiliko toka nyumba za kuezeka kwa makuti hadi nyumba za bati, hasa katika
maeneo yaliyofidiwa na mradi, kwa mfano: Rungungu, Bungu na Jaribu Mpakani.Wananchi wame-
boresha sana ubora wa nyumba zao na sasa wanapanga kuvuta umeme hadi vijijini mwao.
Mipango JijiMakazi mapya ya mradi huko Kinyerezi na Salasala yalikuwa maeneo yenye sifa za kijiji na ambayo
hayakupimwa. mradi umeyabadilisha na kuwa makazi yaliyopangwa yenye idhini kamili ya
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kama yanavyoonekana katika ramani namba 3 na 4.
ElimuMradi wa Songo Songo umesaidia katika ukarabati wa Shule ya Msingi ya Songo Songo, ambapo
mradi umechangia vifaa vya ujenzi kama vile mifuko ya saruji, mabati ya kuezekea na mbao za
kuandikia madarasani. Zaidi ya hayo, mradi uliwahamasisha watoto kwenda shule kwa kutoa ufad-
hili kidogo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ya sekondari na vyuo. Kalamu na madaftari
vimetolewa kama msaada kwa shule kadhaa katika maeneo litakamopita bomba na katika kisiwa
cha Songo Songo.
TATHM[NI ZA KIMAZINGIAm NA KIIAMl NA MPANGO WA UDHIRM
I., ~ ~ ~ *
_ _ _ _ _ _ , _ _ _ _ _ _ _ _ _
ak_ Mk2i Nj. Y g. Y. S---- -w,,):
*1.~~~~~~~~~~~~~1
q~~~~~~~~~~~ - -;{
- N N P-,
,. ~ ~ ~ ~ ~ ~ 6,, OAOg MAt'M
Msnoaionmkz -- MN we
Ramani 3: Eneo la Makazi Mapya Kinyerezi
12
Ramani 4: Eneo la Makazi Mapya Salasala
Machirnba ' MTONGANI
a i
' m~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ ya Mawe -~ '
Makazi m-pya 4 Makatl mapya Banabana n go _ __, Mlitatya bomba la gesl ya SongoM.sya Ma go
i.4
p~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
3 .4 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~-~~~~~~~~~~~~~I~~~~0
MaEEE, mapyE Makazi m~~~~~~~~~ya Barabara WI NilE ~~~~~~~E bombs Ia YEsI ya Songosongo~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~BambOo 09090 ~ ~~~~~~~~ 040001150 komua~ ~~~'P0 1
Mel Nia YE mig~~~~~~~~~~~~~~~~~~~a ~ ~ ~ ~ Mto ~ ~ ~ ~
TATHMINI ZA KIMAZINGtRA NA KIJAMil NA MPANGO WA UDHIBITI
UshauriWatumishi wa mradi waliwatembelea MaafisaWatendaji wa Kata na kuzungumza nao juu ya mata-
tizo kadhaa ya kijamii na kimazingira vijijini mwao. Maofisa wa mradi waliwapatia MaafisaWatendaii
Kata, viongozi na wazee wa kijiji changamoto mbalimbali. Matokeo yake ni kwamba watoto wengi
zaidi wameandikishwa shule na watu wengi zaidi wamehudhuria vituo vya afya.
Wakati wa Programu ya Kufidia Haki ya Kupita Njia, watumishi wa mradi walishauriana mara
kwa mara na wanavijiji katika jamii zilizoathirika juu ya masuala yanayohusu maisha yao na masu-
ala mengine yanayohusiana na mradi kama vile elimu na afya. Hili lilifanyika katika mikutano kadhaa
wakati wa kuzitembelea ofisi mbalimbali vijijini.
MiundombinuWakazi wa kisiwa cha Songo Songo hurusiwa kutumia viti vilivyo wazi kwenye ndege za kukodish-
wa kutoka kisiwani hadi mikoa ya Dar es Salaam na Lindi. Zaidi ya hayo, wanatumia gati la saruji
(ambalo linahitaji kukarabatiwa) kufunga vyombo vyao wakati wa kupakia na kupakua mizigo na
abiria, kwani gati lao la zamani la mbao halitumiki tena.
Mabadiliko ya Hali ya MaishaKumekuwepo na mabadiliko ya hali ya maisha katika maeneo kadhaa kama vile Kinyerezi na kati-
ka kisiwa cha Songo Songo kwani watu sasa wanaishi katika nyumba nzuri zaidi baada ya kulipwa
fidia na baada ya programu ya uhamasishaii iliyofanyika kisiwani. Programu ya uhamasishaji ilifanyi-
ka ili kuwaandaa wakazi wa kisiwa kwenda sambamba na mabadiliko yanayohusiana na mradi kati-
ka vipengele vingi kwa mfano: kutayarisha nyumba zao kwa ajili ya kuingiza umeme.
14
TA:HMINI ZA KIMAZINGIPA NA KIrAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
SURAYA
3
Mpango wa Shughuli zaBaadaye za Programu ya
Maendeleo ya Jamii
ElimuKwenye kisiwa cha SongoSongo, Songas hutoa ada kwa wanafunzi watatu wa kwanza wanaochag-
uliwa kuendelea na elimu ya sekondari baada ya kufaulu mtihani wa taifa wa darasa la saba.
Programu hii ilianzishwa mwaka 2000 na itaendelea wakati wa utekelezaji wa mradi. Hadi sasa
wanafunzi watatu (3) wanafaidika na programu hii.
Programu nyingine za kielimu na misaada zitatolewa kwa kisiwa cha Songo Songo na jamii zilizomo
katika maeneo linakamopita bomba la gesi. Hii itakuwa huduma moja miongoni mwa huduma nyin-
gi zitakazotolewa kwa jamii zilizoko kwenye maeneo linakamopita bomba la gesi, kulingana na
wajibu wa kimazingira na kijamii ambao Songas imeahidi kutekeleza.
Maji na UmemeSongas itawapatia wakazi wa kisiwa cha Songo Songo maji na umeme bure hadi kwenye mpaka
wa mtambo wa gesi. Usambazaji wa maji na umeme katika maeneo muhimu ya jamii utafanywa na
Programu ya Usambazaji UmemeVijijini.
MiundombinuSongas itapanua na kuboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na barabara na upatikanaji wa maji
na umeme kwa jamii za makazi mapya ya Kinyerezi na Salasala jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kurejesha mapatoSongas itaziunganisha jumuiya zilizoathirika kwenye mipango ya mikopo midogomidogo. Jumuiya
zitafaidika pia na uendelezaji wa biashara ndogondogo. Mipango hii itaendelezwa kupitia mashauri-
ano kati ya wanavijiji na watumishi wa mradi.
UshauriSongas ina mpango wa kuendelea kuwa na mashauriano na wanavijiji katika jamii zilizoathirika juu
ya masuala ya Programu ya Maendeleo yajamii hasa yanayohusu mipango ya mikopo midogo mido-
go, uendelezaji wa biashara ndogo ndogo na masuala mengine yanayohusiana na mradi.
Mpango wa Usambazaji UmemeVijijiniMpango wa kusambaza umeme unaotokana na miale ya jua (umeme wa sola) unachunguzwa kwa
ajili ya familia zilizo karibu na njia ya bomba. Uchunguzi huu umeonyesha pia kwamba watu waishia
15
TATH-MINI ZA KIMPZINGIrIA NA KIJAMI, NA MPANCO WA UDHIBITI
4:S
L~~~~',
#_'_ s
p~~~~~~~~~~~ -- t.^
2 B . j. :1 m .2' .- . -
i r ______ &iX
Ene Ia Mrd Kiiw cha Songosong-
;' pes' 11ri,,;9S,.,^,,q,...16
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KIJAM I NA MPANGC WA UDHIBITI
~~- r ~~ S S v : e M5 Lr- ,r --- i:''
W.~~~~~~~~~N
_i~~~ ~ J- -- _
4:- _ ---#> ' -- 3i '. 4 S
,-11 _ A . . . .Ai_
Mitambo wa Umeme - Ubungo
17
TATHMIN ZA KIMAZINGIRA NA KIJAMII NA MPANGOWA UDHIBrTI
karibu na njia ya bomba wanatoa kipaumbele cha juu kwa maji na elimu. Hivyo kuna uwezekano
kwamba baadhi ya fedha zilizotengwa kupitia mradi huu zitatumika kwa aiili ya shughuli nyingine
za jamii zilizopewa kipaumbele, licha ya umeme. Songas itashiriki na kusaidia dhana yoyote itakay-
oonekana inafaa kwa aiili ya utoaii wa gesi na/au umeme na huduma nyinginezo.
Ahadi ya Songas ya Kutimiza Majukumu ya KijamiiSongas itachangia kwenye miradi ya maendeleo ya kijamii na ya kitaifa, ikitilia mkazo maalum kati-
ka miradi iliyomo kwenye maeneo ya mradi,yaani kisiwa cha Songo Songo,eneo linamopita bomba
na Ubungo. Mahitaji ya haraka sana kwenye kisiwa cha Songo Songo na katika maeneo linamopita
bomba yanahusu afya na elimu.Aidha Songas itachangia kulinda na kuboresha mazingira na pia
kuwa kichocheo cha kuleta mawasiliano miongoni mwa serikali za mitaa, serikali kuu na mashirika
yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Wakati ambapo miradi yote ya maendeleo ya namna hii huzua mambo na masuala mbalimbali,
mradi wa Songo Songo utafuata:-
* Sheria, Sera naViwango vya Tanzania;
* Sera za Usalama za Benki ya Dunia;
* Miongozo ya Benki ya Dunia ya Kupunguza Uchafu wa mazingira, na
* Miongozo ya Afya na Usalama ya Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kwa ujumla, masuala yamkini hasi ya kimazingira na kijamii yanayoweza kuibuliwa na mradi wa gesiya Songo Songo yanaweza kudhibitiwa ili kwamba athari zake zipungue. Songas inaamini kuwa
athari zozote hasi zitafidiwa kwa kiwango kikubwa na mazuri mengi yatakayotokana moja kwa
moja na mradi katika maeneo ya mradi na faida kubwa kwa nchi kutokana na kuendeleza rasilimali
hii muhimu.
18
TATHMINI ZA KIMAZINGIRA NA KJAMII NA MPANGO WA UDHIBITI
USAMBAZAJIWA RIPOTIYA UHAKIKIWA MAZINGIRA
Uhakiki wa athari za mazingira, kijamii- uchumi na namna ya kuzirekebisha umekwishafanyika kama
ilivyoelezwa hapo awali. Uhakiki wa kwanza ulikamilika mwaka 1994 na tangu hapo ripoti 28
za utafiti wa mazingira na kijamii - uchumi zimekwishatengenezwa. Ripoti zote hizo zimeungan-
ishwa pamoja na kupata ripoti moia kuu ambayo niTathmini za Kimazingira na Kijamii na Mpango
wa Udhibiti.
Ripoti hiyo ambayo huu ni muhtasari wake imesambazwa kwa washikadau wote. Baadhi ya sehe-
mu ambazo inaweza kupatikana ni kwa wakuu wa mikoa ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam; wakuu
wa wilaya za Kilwa, Rufiji, Mkuranga,Temeke, llala na Kinondoni.Vile vile inapatikana katika sehemu
zifuatazo:-
Katibu Mkuu Mkurugenzi Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini TANESCO
Barabara ya Sokoine na Mkwepu Mtaa wa Samora
Dar es Salaam Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu Mratibu wa Mazingira,Afya na Usalama
Baraza la Usimamizi wa Mazingira Songas
Barabara ya Sokoine Nyumba ya Maarifa
Dar es Salaam Mtaa wa Ohio
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Ofisi ya Benki ya Dunia
Barabara ya Ali H. Mwinyi Kitalu namba 50
Dar es Salaam Mtaa wa Mirambo
Dar es Salaam
19