Wizara ya Mambo ya Waqfu ya Misri
Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu
ANGA ZA UTAMADUNI
MAKALA KATIKA DINI NA MAISHA
Profesa/ Muhammad Mukhtaar Juma
Waziri wa Mambo ya Waqfu
Raisi ya Baraza Kuu la Mambo ya kiislamu
Mjumbe Wa Baraza la Tafiti Za Kiislamu
AL-azhar
Kimefasiriwa Na
Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar
Kairo
1437 AH & 2016 CE
2
Yaliyomo
1 Mtume Muhammad ni nabii wa rehema
7
2 Kuelekea pamoja kwa jamii safi ya kisasa
13
3 Makosa yatokanayo na hutuba za dini
20
4 Utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na
wa kisiasa
25
5 Umuhimu wa juhudi za pamoja
32
6 Vyama vingi na utawala usiomil
38
7 Maana ya Usalama wa taifa
42
8 Miji mikuu, mipaka na ujenzi wa taifa
47
9 Sinai Ndani ya Kurani tukufu
50
10 Uhakiki kati ya marekebisho na ubomoaji
55
11 Vyombo vya habari vyenye malengo
62
12 Hofu ya kuzembea
65
3
13 Kisa cha masanamu na ubomoaji wa ustaarabu
71
14 Kati ya utendaji bora na utii 78 15 Mfano mzuri wa kugawanya mali ya zaka 85
16 Mfano mzuri wa kugawanya mali ya zaka 89
17 Baina ya Matumaini na Kazi 93 18 Uzuri, furaha na hisia njema 107
19 Rafiki tumtafutaye
112
20 Haki ya mwanamke katika kurithi na maisha
mazuri
117
21 Ujeuri na mwisho mbaya
125
22 Misri ni nchi kubwa kwa maadili yake na ustaarabu wake
130
23 Wizi wa mali za umma na kuzifuja 134
24 Mazungumzo ya ijumaa
Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa
139
25 Wito wa kuwa na matumaini
144
4
Utangulizi
Shukurani zote njema anastahiki mwenyzi Mungu, rehma na
amani zimshukie Mtume wa mwisho na mjumbe wake sayidna
Muhammad bin Abdillah, na jamaa zake na masahaba zake na
kila aliyemfuata mpaka siku ya mwisho.
Huu ni mkusanyiko wa makala za matukio mapya mbalimbali
: ya kidini, kitamaduni, kifikra, kijamii na kitaifa, nimependelea
kuyaandika chini ya anuani “Anga ya Utamaduni”. Nayo ni kwa
ajili ya kutilia mkazo juu ya makosa yaliyomo katika akili za
watu ya kutoelewa kutafautisha kati ya dini na tamaduni. Kuna
tafauti kubwa na kwa kuwa msomi anatakiwa awe na kiwango
kikubwa cha ufahamu wa vitu mbali mbali. Kwa kuwa hukumu
ya kitu ni sehemu ya ujuzi (ili uhukumu kitu inatakiwa uwe na
ujuzi nacho). Pamoja na kuchunga hali na sehemu ambazo pia
ni nguzo muhimu za ufikishaji, kitu kinachopelekea kwa msomi
awe na ufahamu wajamii iliyomzunguka na kwa matukio na
changamoto zinazojiri duniani.
Ulimwengu wa kiarabu na kiisilamu umefikwa na mbano
mkubwa wa taaluma au kiwango kidogo cha taaluma kwa watu
5
wengi, pengine ni kwa sababu ya kutowafikia kwa njia sahihi
kwa baadhi ya wakati. Na tatizo hili imebidi kuzungumziwa kwa
kuwa mtafutaji au msomi wa somo
maalumu huwa anazingatia ile fani yake pekee na kuacha kujua
ima kifikra au hata kimitaala fani nyengine kitu ambacho
huzalisha kizazi ambacho –pengine- huwa hakijaelimika au
kutoweza kufanya kazi kwa pamoja kwa roho ya timu au kuwa
na uhusiano wa karibu na jamii. Kwa sababu hajabobea kw
nyenzo za kitaaluma na ujuzi wa kisasa. Na huenda mwandishi
au msomi akatibu kimakosa baadhi ya kadhia au hata
akapelekea mkangamano sawa iwe kwa mihadhara ya
kusikikana au ya kuonekana.
Na nimejitahidi katika kuleta fikira mbalimbali katika makala
hizi ambazo ninaziandika katika kitabu hiki, hali ya kumuomba
Mwenyezi Mungu anikubalie, na niongeze kitu katika taaluma
za fikra ya kiisilamu, nikiwa niko sawa basi kwa fadhila za
Mwenyezi Mungu na kama si hivyo basi ni kwangu nami
nimejitahidi na kujaribu.
6
Mwenyezi Mungu yu nyuma ya kila lengo naye ni Mwafikishaji
na Msaidizi.
Prof. Muhammed Mukhtari Juma
Waziri wa Wakfu
Na Mjumbe wa Utafiti wa Al Azhar Sharif
7
Mtume Muhammad Ni Nabii Wa
Rehema
Mwenyezi Mungu Mtukufu amemleta Mtume Muhammad
(rehma na amani zimshukie) kuwa ni rehema kwa ulimwengu
mzima, akasema: {na wala hatujakutuma isipokuwa ni rehema
kwa ulimwengu mzima} na Mtume akajieleza mwenyewe kwa
kusema “enyi watu hakika mimi ni rehema yenye kuongoa.” Na
Qur’ani Tukufu inasisitiza kuhusu hilo na kusema { Hakika
amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe;
yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.
Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. }
Na kitabu chake alichoteremshiwa Mtume ni kitabu chenye
uongofu kwani Mweneyzi Mungu anasema {Na tunateremsha
katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini.
Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara}
Dini yake ni dini ya rehema,amani na usalama kwa viumbe
wote, dini yenye misingi thabiti ya kuwawezesha watu wote
waishi kwa amani. Inahifadhi kutomwaga damu, inahifadhi mali
8
zote kwa misingi ya kiutu bila ya kutafautisha watu kwa misingi
ya dini, rangi, jinsia na kabila, nafsi zote zimehifadhiwa,
heshima na mali pia zimehifadhiwa. Na amana zote hurejeshwa
kwa weneywe bila ya pingamizi. Na Mtume wetu (rehma na
amani zimshukie) wakati wa kuhamia kwake Madina alimuacha
Ali bin Abi Twalib nchini Makka ili azirudishe amana kwa
watu wake ingawa walimnyanyasa na kumkera.
Na siku walipokuwa mji wa Taifu watu wa mji ule
walipowaamuru watumwa na watoto wamrembee kwa mawe
mpaka akamwagika damu nyingi miguuni mwake, wakamjia
malaika wa majabali na kumwambia : “Ewe Muhammad hakika
Mweneyzi Mungu amesikia maneno ya watu wako kuhusu
wewe na mimi ni malaika wa majabali Mwenyezi Mungu
amenituka kwako ili uniamrishe kwa amri yako pindi ukitaka
niwagandamize katika majabali mawili. Mtume (rehma na
amani zimshukie) akasema: “lakini ninaema,ewe Mweneyzi
Mungu waongoe watu wangu kwani hawajui walitendalo, nami
ninataraji kuwa Mwenyezi Mungu atatoa katika migongo yao
atakaesema Lailaha illa llahu (hapana wa kuabudiwa kwa haki
isipokuwa Mweneyzi mungu).” Na alipoambiwa. “Waombee
9
washirikina” akasema: mimi sikutumwa kuwa ni mweneye
kulaani lakini nimetumwa kuwa ni rehema.
Uisilamu ni dini ya rehema na amani wa ulimwengu wote,
hakuna mauaji kwa sababu ya itikadi hata kidogo, na Mtume
(rehma na amani zimshukie) alipomuona mwanamke wa
kikafiri ameuliwa katika uwanja wa vita akasema: “ni nani
amemuua? Huyu haikupasa kuuliwa.” Hii inathibitisha kuwa
ukafiri si sababu ya kuuliwa, isipokuwa mauaji hutokea kwa
sababu ya kuondoa uadui kwani dini hailazimishi mtu na wala
haina maneno ya kejeli, Mweneyzi Mungu anasema
. Na lau ungeli kuwa mkali, kumwambia Mtume wake {
mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi
ika wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao kat
mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi
Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao
} na Qur’ani ilipowazungumzia makafiri kupitia mtegemea.
ulimi wa Mtume (rehma na amani zimshukie) na kwa ndimi za
masahaba wake akasema { Na hakika sisi au nyinyi bila ya
shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi.} na wala
hakusema “sisi tupo katika uongofu na nyinyi mupo katika
10
upotevu wa wazi, na misemo kama hii inajulikana kwa wasomi
wa ufasihi wa maneno kuwa ni “ kunyeyekea”. Na hii ndio
tamaduni yetu ambayo inamfanyia uadilifu mwengine hata
katika kuzungumza.
Uisilamu umeamrisha kusema maneno mazuri, mwenyezi
Mungu akasema Semeni na watu vizuri} na watu inakusudiwa
kwa ujumla pia semeni maneno mazuri {na sema kuwaambia
waja wangu waseme maneno ambayo ni mazuri} na watende
pia vitendo vyema. { Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu
kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana
uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu} huyu
ndiye Mtume wetu na hizi ndizo tabia zake akasema
“nimetumwa kukamilisha tabia njema”
Na iwapo dini yetu ni dini ya rehema na kitabu chetu ni kitabu
cha rehema na Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) ni wa
rehema sasa vipi kuhusu sisi? Tumefikwa na nini? Na ni kipi
kilichowafika wenye nyoyo dhaifu juu ya dini yetu hata
wakafikia kuwa wana nyoyo ngumu kiasi hiki? Na utatuzi wake
ni upi?
11
Hapana shaka kuwa vitendea kazi vingi vinahusika juu ya hili,
ikiwemo wasomi wasio na fani husika kuwa na mamlaka katika
kutoa hutuba za ulinganio na kushika nafasi hizo kwa muda
mkubwa. Na wengine kuamisi sivyo na kuzidisha itikadi kali
katika dini, yote haya ni ufahamu usio sahihi na ipo haja ya
kusahihisha pamoja na kusisitiza kuwa uisilamu ni dini ya
msamaha, rehema na wepesi. Na wasomi wamesema kuwa
“Fiqhi” ni utambuzi na uwepesishaji kwa dalili, na hakuna
aliyesema yeyote katika wenye kutegemewa elimu zao sawa
katika wale wa zamani au wa somi wa kisasa kuwa “fiqhi” ni
elimu yenye itikadi kali. Mweneyzi Mungu anasema {
Mweneyzi Mungu anakutakieni wepesi wala hakutakieni uzito}
na anasema {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika
Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi
Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii
(Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe
mashahidi kwa watu}. Pia anaendelea kusema {Na jueni kuwa
Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini
katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini
Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba
12
katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na
upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka, 8. Kwa fadhila za
Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kujua, Mwenye hikima. }. Na Mtume wetu (rehema na
amani zimshukie) hakuwa akichagua kati ya mambo mawili
isipokuwa akichagua lililo jepesi lao ilivyokuwa si katika maasi
au kuvunja undugu, na Mtume (rehema na amani zimshukie)
alikuwa ni mwenye kujiepusha sana katika maasi
13
Kuelekea Pamoja Kwa Jamii Safi Ya
Kisasa
Usafi ni maadili ya kisasa lakini hasa ni anuani ya ustaarabu, na
haiwezekani kwa wananchi wenye kuwa na ustarabu wa aina
mbili nazo zote ni kubwa mno ambazo historia ya mwanadamu
imezielewa wapuuzie jambo hili. Sisi ni wana wa ustarabu
tuliobobea na uliokita zaidi ya miaka elfu saba. Na ustaarabu
mwegnine ni wa kuwepo uisilamu, na zote mbili hizi
zimekusanyika pamoja na kutengeneza mwanaraia wa Misri.
Ustaarabu huu una wito wa kuwa watu wazuri na wenye haiba,
na kujiweka mbali na kila lenye makero na kuudhi na ambalo
halitakikana kwa mtu mwenye akili timamu. Mwenyezi Mungu
amewasifu watu wa msikiti wa Qubaa kwa pupa zao za kuwa
wasafi, Mwenyezi Mungu akasema: “ndani yake muna vijana
wanaopenda kujisafisha, na Mwenyezi Mungu huwapenda
wajisafishao ”
Na Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuchukua mapambo yetu
kila tuendapo misikitini akasema, {Enyi wanadamu, chukueni
mapambo yenu kila muendapo msikitini}. Na kutuamrisha
14
kujisafisha miili yetu na nguo zetu akasema {enyi mlioamni
mukisimama kwenya sala basi osheni nyuso zenu na mikono
yenu mpaka katika visugudi na pakeni vichwa vyenu na miguu
yenu mpaka kwenye visigino na muwapo na janaba basi ogeni}
. na pia Mweneyzi Mungu akasema kumwambia Mtume wake
(rehma na amani zimshukie {1 Ewe uliye jigubika! 2 Simama
uonye! 3 Na Mola wako Mlezi Mtukuze! 4 Na nguo zako,
zisafishe.}
Na Mtume (rehma na amani zimshukie) ameweka wazi kuwa
usafi ni nusu ya dini akasema: “Usafi ni nusu ya imani.” Si
hivyo tu bali uisilamu umefanyaa usafi wa mwili na nguo na
mahali ni sharti ya kukubaliwa ibada muhimu katika maisha ya
muisilamu na ni nguzo ya kimatendo iliyo ya juu kabisa katika
uisilamu baada ya kutoa shahada mbili, nayo ni sala. Mtume
(rehma na amani zimshukie anasema: “ Hakika Mweneyzi
Mungu Mtukufu haikubali sala bila ya tohara (usafi) na sadaka
kutoka mali haramu.
Na Mtume (rehma na amani zimshukie) kaenda mbali zaidi ya
hapoa katika hadithi ya usafi aliposema kuwa kuacha
kujisafisha baada ya kwenda haja ndogo ni sababu ya kupata
15
mtu adhabu ndani ya kaburi lake, na hii ni pale alipopita (rehma
na amani zimshukie) katika makaburi mawili akasema: “ hawa
wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama
mmoja wao alikuwa ni msengenyaji na mwengine alikuwa
hajisafishi kutokana na haja ndogo.”
Na dini yetu tukufu imekataza kutumia kila kinachoharibu maji
au sehemu au kuweka vizuizi kwa watu katika maisha yao au
lolote lenye kusababisha makero na kudharau. Imekataza pia
kukojoa ndani ya maji au kivulini au katika njia wapitazo watu
au maeneo ya watu wote. Mtume (rehma na amani zimshukie)
amesema: “waogopeni walaanifu wawili, wakasema: “Ni nani
hao ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” akasema: “ambao
wanajisaidia njiani na katika vivuli vya (kupumzikia) watu.”
Kama ambavyo uisilamu umekataza pia mtu kufanya haja
ndogo katika eneo analoogea sawa iwe ni mtoni, baharini au
hata katika bwawa la kuogelea au kufanya haja ndogo upande
unaotokea upepo, na jambo hili ukaliwekea adabu zake, zaidi
juu ya maudhui hii imeelezwa kwa kina katika vitabu vya fiqhi,
sehemu za tohara (usafi).
16
Na atakaehesabu idadi ya majosho ya lazima kwa mfano,
mwanamke anapomaliza hedhi, au damu ya ugonjwa, au ujusi
(baada ya kujifungua) au baada ya kukutana (mtu na mkewe),
aukutokwa na manii. Au hata majosho yasiyo ya lazima kwa
mfano; kuoga kwa ajili ya sala ya Ijumaa kwa wanaosema kuwa
ni sunna (baadhi ya wasomi), ingawa wengine wanasema kuwa
ni jambo la lazima, na kuoga kwa ajili ya sala za idi mbili, na
kuoga kwa anayeosha maiti, na kuingia Makka, na majosho
mengineyo yasiyo ya lazima (sunna), itafahamika kuwa ni
namna gani uisilamu umelipa uhuhimu jambo la usafi.
Na jambo jengine ni kuwa uisilamu umehimiza urembo na
kujipamba Mtume (rehma na amani zimshukie) aliposema “
hatoingia peponi mwenye chembe ya kiburi ndani ya moyo
wake, kijana mmoja akasema: “ kuna mtu hupenda nguo zake
na viatu vyake viwe vizuri.” Mtume (rehma na amani
zimshukie) akasema: “Mwenyezi Mungu ni mzuri na hupenda
uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.”
Uisilamu umefanya usafi wa kinywa (upigaji mswaki) kuwa ni
jambo la sunna, na ukasema pia ni wajibu kuosha katika mikato
ya nje na ya ndani ya mikono na miguu, na kueleza kuwa iwapo
17
itakuwa ni msimu wa baridi basi kutumia maji katika
kujitahirisha kunazidishiwa malipo mara mbili, Mtume (rehma
na amani zimshukie) akasema: “ Je niwafundishe
atakayokufutieni Mweneyzi Mungu makosa yenu na kukuinueni
daraja? Wakasema:” ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.
Akasema: “kueneza udhu wakati wa baridi, na kuenda sana
misikitini, na kungojea sala baada ya sala hayo ndiyo malipo
makubwa.”
Na uisilamu umetaka usafi wa njia (barabara) na kuondoa
uchafu na kuacha kabisa kuutupa (kiholela) kwani usafi ni
sehemu ya imani akasema: “imani ni sehemu sabini au ni
sehemu sitini, bora yao ni tamko la “Lailaha illa llahu (hapana
apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mweneyzi Mungu) na
ya chini yake ni kuondosha uchafu njiani.” na hadithi hii
inaweka wazi kuwa kuondosha uchafu njiani humpa mtu imani
na haya yanasisitizwa na kijana alipomuuliza Mtume (rehma na
amani zimshukie) kuhusu matendo yatakayomuingiza mtu
peponi akamwambia: “ondosha uchafu njiani”. Na katika
hadithi nyengine “kuondosha uchafu njiani ni sadaka.”
18
Na hayo yote yanatilia mkazo juu ya ustaarabu wetu kuhusu
usafi na uzuri, na kukataza aina zozote za uchafu na makero, na
katika mambo ambayo inabidi tuyaangalie kwa undani zaidi ni
usafi katika maisha yetu ili tusijikere na kuwakera wengine. Na
iwapo hatutasaidiana katika usafi wa mazingira yetu, jamii yetu
na mandhari yetu basi kwa uchache na tusiwe ni sababu ya
kuwakera watu sawa iwe kwa kutupa taka au masalio ya ujenzi
katika barabara (njiani) au kurembea matakataka katika njia
ipitayo maji-taka au kumwaga maji ya viwandani katika mto wa
Nile, na kutupa masalio na uchafu ndani yake na kuchafua uzuri
wake na kuharibu kingo zake.
Kila mmoja wetu ajitahidi katika usafi wa mwili wake, nguo
zake, sehemu yake, shule yake, sehemu afanyayo kazi na
asaidie pia katika usafi wa jamii, kwa kuondoa uchafu njiani, na
ajitahidi kadiri awezavyo katika kuifanya jamii ionekane nzuri
na safi na ya kisasa.
Na kwa jamii zilizoendelea zinaweza kuzibadilisha taka na
kuzifanya kuwa ni rasilimali yenye kurudisha faida kwa jamii
yake, je, sisi tuko tayari kwa hili? Na tunaweza? Bila shaka,
“ndio” tunaweza, lakini kwa sharti la kuacha maneno na
19
kufanya vitendo, na kuanza kila mmoja wetu.. na iwe kauli
mbiu yetu.. jamii safi ya kisasa."
20
Makosa Yatokanayo Na Hutuba Za Dini
Hapana shaka kuwa mabadiliko na urekebishaji wowote wa
utoaji wa hutuba za dini kwa kupitia historia ya viumbe
haiwezekani uwe ni kadhia ya jamii au makubaliano pasi na
kuainisha muda au wakati ambao huenda ukarefuka au ukawa
mfupi kwa mujibu wa wasomi wa wakati ule kupitia juhudi zao
na misimamo yao na pia uwezo wao wa kukinai kwa mawazo
mapya. Na kwa upande wa wasomi wa zamani na wenye
kunufaika kwa matukio ya hali iliyopo kwao inakuwa ni
vigumu kukubaliana kirahisi na kwa wepesi na wasomi wa
kisasa, na kwa mujibu wa mawazo ya wasomi wa kisasa na
mwenendo wao wa kimawazo uliofikia mbali (mara nyinyi)
jamii huwa tayar kuambatana nao kimawazo na kuacha njia ya
wasomi wenye mawazo mgando yasiyoleta tija. Isipokuwa njia
nyepesi ya kati na kati nayo imekuwa ni kitu chenye utata kati
ya makundi mawili haya.
Maudhui hii kwa upande huu itagawanyika katika mafungu
matatu makuu, nayo:- ufahamu uliosahihi (uliotakasika), hatari
21
ya kuacha maudhui husika na kumuelekea mtu binafsi, na uhuru
wa itikadi na wa maoni.
Fungu la kwanza: ufahamu uliosahihi (uliotakasika), wa zamani
na mtazamo wake kwa kuwa ni wa zamani kiasi ambacho
inakaribia kuonekana maneno yaliyozungumzwa na baadhi ya
wasomi wa zama hizo kwa mujibu wa nyakati zao na maeneo
yao yanaonekana kama ni maneno matukufu. Ama kwa nyakati
hizi itahitajika kuwepo kwa jitihada
mpya yenye kwenda sambamba na wakati tulionao na matukio
yake pamoja na matakwa yake, na tunakaribia kuona
wanaoyatukuza maneno ya baadhi ya wanahistoria na kile
walichokiandika katika vitabu vya ukoo (majina) na historia.
Na kwa upande mwengine tunaona wenye kuvuka mipaka kwa
njia ya kejeli kuhusu yale mambo yaliyothibiti (kidalili) au yapo
karibu sana na kuwa yamethibiti kwa kisingizo cha urekebishaji
kiasi ambacho baadhi yao huharibu kabisa kabisa. Na hili
huenda likawa kwa sababu ya uoni mdogo au kwa manufaa na
makusudia mabaya ingawa hatukanushi au kukubali kwani
nyoyo na nia zote zipo katika mikono ya Mwenyezi Mungu
(S.W) .
22
Msisitizo wetu tunaourejea rejea mara kwa mara ya kuwa sisi
tunahitajika turekebishe na kuifanyia akili kazi nasi tupo
kinyume na mawazo mgando na fikira za kizamani na kufunga
mlango wa jitihada na kudunisha upeo au kuufunga kabisa na
kuuziba. Na tupo kinyume na kuwaona kuwa wao ni makafiri
na kuwatuhumu kuwa wapo kinyume na taifa lao isipokuwa
kama mahakama itatoa hukumu ya jambo hilo. Na mimi
nakumbushia kuwa hakuna yeyote katika watu na itikadi zao
kuwa atakubali kuingiliwa katika kile anachokiamini na
kumfanyia uadui ndani yake hata kama itakuwa kwa kubatilisha
itikadi yake kwa njia za akili na dalili.
Fungu la pili: Na miongoni mwa makosa makubwa yatokanayo
na hutuba za dini ni kuacha kuacha maudhui na kumuelekea
mtu binafsi na kumdhalilisha mpaka inafikia kuonekana kuwa
ni matusi, au kurudishiana matusi ya nguoni kama si matusi ya
waziwazi. Sawa kati ya wanaogombana na wanaozungumza kati
ya maulamaa na wasomi. Iwapo msomi atakapozungumzia
maudhui Fulani na akawa nachunga heshima ya mazungumzo
na kutoa mawazo yake kisomi na kwa akili huyu itajulikana
kuwa anasema kwa mujibu wa upeo wa hoja, rai na akili ya
kimantiki. Lakini iwapo msomi au mtafutaji au mhakiki
23
atakapozungumzia maudhui na akawa anamzungumzia
mwengine kwa njia ya kumkweza sawa na iwe katika wasomi
wa zamani au wa kisasa na sawa awe kati wasomi wa dini au si
wa dini jambo hili katu halitakubaliwa. Na haiwezekani
kulikalia kimnya au kilisubiria, na hili linaweza kuwa ndio
chanzo cha kukujeliana na audui wa kifikra. Na kwa wafuasi wa
anayeshambuliwa wanaweza kutoka nje ya mipaka na wakaona
kuwa ni wajibu wao kisheria, kiakili na kiutu kuwakinga
wasomi wao, jambo ambalo huenda likapelekea kuzuka kwa
vita ya maneno na mijadala mipya au ya zamani yenye
kujirudiarudia au hata kusababisha matukio yenye kutenganisha
ndani ya historia ya taifa letu.
Fungu la tatu: ni lile lenye kuzungumzia ufahamu sahihi na
ufahamu usio sahihi kuhusu uhuru wa maoni, sisi
tunatenganisha uhuru wa itikadi na uhuru wa maoni, kama
tunavyotafautisha kati ya uhuru unaodhibitiwa na sheria au akili
au kanuni na machafuko ambayo hayana mipaka. Pamoja na
kuwa dini yetu haijambebesha mtu mzigo au kumlazimisha
kuikubali, mweneyzi Mungu anasema { Hapana kulazimisha
katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na
upotofu } na pia anasema : { Na Mola wako Mlezi angeli
24
penda angewafanya watu wote wakawa umma mmoja.
Lakini hawaachi kukhitalifiana} na anaendelea kusema {
Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi
Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua
zaidi waongokao}, pia anasema { Si juu yako ila kufikisha
Ujumbe tu.}Na anasema pia {3. Huenda labda ukajikera
nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. 4. Tunge penda
tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea
shingo zao.}
Uisilamu umeweka vidhibiti vya uhuru vilivyo imara na
vyenye kusisitiza msamaha wake mkubwa, lakini jambo hili na
ufahamu wa uhuru wa maoni halitakiwi liwe la kuvuka mipaka
au kuzidi kiwango juu ya yale yaliyothibiti kidalili au yale
yanayotukuzwa au hata kugusa heshima za watu kwa kisingizio
cha uhuru wa maoni . na kwa kuwa sisi tunahitajika zaidi
kufanya kazi na si kulombana na kujiweka pamoja kwa
lililokubaliwa pande zote, na kukubaliana juu ya kutofautiana
kwa maoni
yawengine, na wala tusielekee katika lugha ya matusi na
kurushiana madongo au kurudishiana matusi na mfano wake
hili ni kwa ajili ya kulinda uzuri wa jamii kwa ujumla. Kitu
25
ambacho (kulumbana) hakikubaliki katika akili na ni kigeni
katika jamii yetu na katika ustaarabu wa kiarabu na wa
kiisilamu.
Utendaji Wa Dini Kwa Muonekano Wa
Nje Na Wa Kisiasa
26
Hapana shaka kuwa utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na
kwa muonekano wa kisiasa hii ni changamoto kubwa sana
ambayo umma wa kiarabu na wa kiisilamu unakabiliwa nayo.
Na iwe sawa kwa hawa ambao wanazingatia umbo au
muonekano hata kama itakuwa ni kwa kuacha asili. Na kufanya
kuwa muonekano ndio kila kitu, na hata kama mwenye kujidai
muonekano huo hana utu wala tabia ambazo humfanya awe ni
kigezo na mfano wa kuigwa. Na hii inatokana na kuwa mwenye
kujionesha huwa tabia yake haiendani sambamba na mafunzo
ya kiisilamu na hii huzingatiwa kuwa moja ya uvunyaji na
ukiukwaji wa dini, kwani iwapo muonekano wa wenye
kujionesha ni tabia mbaya au uongo au kutengua ahadi au
khiyana au kula mali za watu kwa dhuluma, hapa jambo hili
kwa hakika huwa ni hatari sana.
Isitoshe mwenye tabia hizi huwa ni katika wanafiki, kwani
Mtume wetu (SWA) amesema : ”alama za mtu mnafiki ni tatu;
akizungumza husema uongo, akitoa ahadi haitimizi na
akiaminiwa hufanya khiyana. (imepokewa na Bukhari).
Vile vile kwa waichukuliao dini kuwa ni ibada na kufanya
jitihada ambazo zitapelekea kuifahamu dini vibaya na kufikiria
zaidi mambo yasiyohitajika na kubeba silaha na kujitenga na
27
watu wenzao, kama ilivyokuwa kwa madhehebu ya Khawarij
ambao walikuwa wakisali sana, kufunga na kusali usiku
isipokuwa wao hawajaisoma elimu ya sheria kama itakiwavyo
ambayo ingeweza kuwakinga na umwagaji wa damu na
kupelekea watu wawapinge kwa kutumia panga zao. Lau kama
wangetafuta elimu kwanza kama alivyosema imam shafii
“Mwenyezi Mungu amrehemu”, wangejikinga na mengi, kwani
uisilamu ni dini ya upole kabla ya chochote, na kila ambacho
kitakuweka mbali na upole basi hicho hukuweka mbali na
uisilamu, na kinachozingatiwa ni tabia njema si maneno
matupu. Kwani wamesema “Muungwana hujulikana kwa
matendo na si kwa maneno.”
Na hakika ibada zote haziwezi kuleta matunda yake isipouwa
tabia ya mwenyewe itakapokuwa njema, na yeyote ambae swala
yake haitamkataza juu ya uovu na machafu basi huwa hana
swala, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “hakika ya swala
inakataza maovu na machafu, na utajo wa Mwenyezi Mungu ni
mkubwa, naye Mwenyezi Mungu anajua yote muyatendayo”
(Ankabut, aya 45)
Na yeyote ambae funga yake haimzuii na maneno machafu basi
huwa hana funga, kwani Mtume SWA anasema “asiyeacha
28
maneno machafu na matendo machafu, basi hakika Mwenyezi
Mungu huwa hana haja ya mja huyo kuacha chakula chake na
kinywaji chake” (Imepokewa na Bukhari)
Mwenyezi Mungu huwa hakubali zaka wala sadaka isipokuwa
kwa mali halali, Mtume wetu (SWA) anasema “Hakika
Mwenyzi Mungu ni Mzuri na wala hakubali isipokuwa kizuri”
(Imepokewa na Muslim).
Mtume (SWA) anasema “ Swala haikubaliwi bila ya tohara na
wala sadaka haikubaliwi iwapo ina husuda (Imepokewa na
Muslim).
Na hata ibada ya Hijja ili ikubaliwe itategemea kipato cha halali
na tabia njema “Atakaehiji na akawa hajafanya uovu wala
machafu basi hurejea (na madhambi yake hufutwa) kama siku
aliyozaliwa na mama yake”. Na Mtume (SWA) ametaja “Mtu
ametoka safari ya mbali amejaa vumbi kisha ananyosha mikono
yake mbinguni anasema “Ewe Mola wangu ewe Mola wangu,
hali ya kuwa chakula chake ni haramu kinywaji chake haramu,
nguo zake ni haramu na amekula haramu iweje basi mtu huyu
kujibiwa” (Imepokewa na Muslim).
Na utendaji ulio mbaya zaidi ni utendaji wa dini kwa
muonekano wa nje kwa ajili ya kisiasa, hapa tunakusudia hili
29
kundi ambalo wameifanya dini kuwa ndio njia ya kupitia
kuelekea kwenye uongozi kwa kutumia upenzo wa dini na
kuwapendezesha watu hasa wale wasiojua kitu kuhusu dini yao.
Na kuwahadaa kuwa lengo la kushika madaraka ni kwa ajili ya
kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu pekee na kuinusuru na
kuifanya iwepo. Pamoja na kuwa sisi huwa hatuhukumu kupitia
nia na wala hatuingilii chochote kuhusu nia ya mtu kwani nia ni
kati ya mja na Mola wake, na kila mmoja wetu ana malengo
yake (nia yake), lakini ujuzi tulionao wa kuishi na kundi la
kigaidi la Ikhiwani na kwa wale wenye mwenendo kama wao au
kuwaunga mkono katika makundi mengine ya kiisilamu
tumejihakikishia mambo mawili, nayo:-
1. Tukio kwa upande wao si tukio la kidini hata kidogo
isipokuwa ni kupigania uongozi kwa makeke na mabavu,
hatukuwahi kuona mfano wake na kuwatendea wengine
kwa kujeli, kiburi na maguvu, kitu ambacho watu wengi
wakakipinga kwa kuwa ni mzigo katika dini, na ikawa
hakuna budi isipokuwa kuifuta sura hii mbaya ambayo
imeenea katika akili za wengi kati ya watu ambayo
imefungamana na tabia za watu wa kundi hili pamoja na
dini.
30
2. Jambo la pili jingine ni kuwa, wao wameiharibu dini yao
na kuipa sura mbaya pamoja na kuwa dini ina tamaduni
nzuri na ya upendo, na wakajithibitishia kuwa wao si
watu wa dini na wala hawawezi uongozi, kwa sababu, je
ni dini gani inayowakhini watu wake na taifa lake na
kutoa siri na kuuza hata nyaraka muhimu na kuwa
wapelelezi wa nchi yao kwa wasioitakia manufaa. Na je
kuna dini inayochochea vurugu, mauaji, ufisadi na
kuunda vituo vyenye lengo la kueneza maovu kwa
wafuasi wake pamoja na kufanya khiyana ambayo
haijawahi kutokea, ikiwemo khiyana ya taifa na
kutendeana na maadui wa nchi yake?
Imethibiti na ninazidi kuthibitisha kuwa kundi hili ambalo
limeifanya dini kuwa ndio chombo cha kuwahadaa watu na
kunufaisha malengo yao ya kuutaka uongozi si zaidi ya
kuungana na shetani, ili kutekeleza na kuhakikisha malengo
yao na tamaa zao za kutaka utawala na uongozi kwa kupitia
dini, au nchi au kwa umma.
31
Umuhimu wa Juhudi za Pamoja
Jamii yetu imeingiliwa na fatwa ngeni pamoja na rai zisizo
sahihi na baadhi ya wenye husuda na wasio na ujuzi na wenye
32
nafsi dhaifu ambao wanawaingilia maulamaa, kwa madhumuni
ya kupata umaarufu, vyeo na kutaka kuonekana tu, wakazitumia
rai zote zisizo sahihi na zilizo ngeni ili wapate kuonekanwa na
kwa ajili ya masilahi yao pamoja na makundi yao.
Na kwa kutokana na wingi wa kadhia pamoja na matukio
mapya yanayojiri na kugawanyika kwake na vuguvugu lake
pamoja na kutowafikiana kwa baadhi yake katika rai za
wanazuoni na wasomi waliotangulia ambao wao walitoa fatwa
kwa mujibu wa zama zao na wakati wao pamoja na sehemu zao.
Ukizidisha na ujinga wa wasio wasomi wa fani hiyo ambao
hawana ujuzi wa kuchambua na kufanya uhakiki, pia kuacha
kutendea baadhi ya hukumu bila ya vigezo, na hii ni kwa
sababu ya ujinga wa tukio pia ujinga wa kutofahamu sharti za
vipimo sahihi. Kwa sababu hizi ndio imepelekea kuwepo kwa
ulazima wa upatikanaji wa juhudi za pamoja.
Kwa ajili hiyo. Huu ukawa ndio wito wa Imamu Mkuu Prof.
Ahmed Twayyib, kiongozi wa Al Azhar Shariyf, katika hotuba
yake ya ufunguzi kwenye mkutano wa Kikao kikuu cha masuala
ya Waisilamu, uliofanyika katika mji wa Luxur, wenye anuani:
“Mtazamo wa viongozi na maulamaa katika kurekebisha hotuba
za dini, na kutengua fikira zisizo sahihi,” na kuwepo juhudi ya
33
pamoja ambayo itawaita wasomi wakubwa katika nchi tafauti
ulimwenguni, na kwa kila mwenye kuwa na hisia juu ya umma
na matatizo yake, ili wapinge kwa ushujaa wao wote masuala
yaliyopo kwa mfano; ugaidi, ufahamu wa hukumu juu ya pahala
pa kiisilamu, kujiunga na makundi ya kigaidi yenye kutumia
silaha, kuacha kuwa pamoja na wanajamii na kuwachukia,
kuhalalisha damu za raia wasio na hatia kwa kuwaua au kwa
kuwaripua, au kila chenye kuhusika na haki za kibinadamu na
uhuru, na kila lenye kuhusika katika masuala ya kijamii kwa
mfano, suala lenye kupewa kipaumbele ni masuala ya
mwanamke, kuanza kujua mwezi upi wa kiarabu ndio
unaotangulia kwa kupitia makadirio ya falaki, masuala ya Hijja
na hasa katika kuanza kuhirimia Jiddah kwa wale waendao
(kuhiji) kwa kupitia vyombo vya anga au kwa vyombo vya
bahari, pia kulenga mawe katika nyakati zote nyengine , na
masuala mengineyo ambayo yanashikana na haki za nchi, na
yanashikana na wakati na pia mahitajio ya watu.
Na ili umma uinuke inapasa kutoa fat-wa zenye kuwezekana
kutendeka na zenye kuharamisha kujibweteka na uvivu, na hii
ni kwa masharti isije ikatolewa fat-wa yenye kuhitaji
mazingatio ya kina kwa kuitolea fat-wa iliyokuja kwa ujumla na
34
kwa maelezo ya ujumla ambayo hayaendani na uhalisi uliopo na
ambazo pia hazitaweza kutoa jibu juu ya masuala au hata
kubadilisha kilichopo.
Na bila shaka juhudi za pamoja zitasaidia sehemu kubwa na
zitaweka wazi sana ili kufuta rai zisizo sahihi, na kwa ajili ya
kuondosha sababu za uasi, Kikao kikuu cha masuala ya
Waisilamu katika mkutano wake wa mwisho kimezungumzia
mambo muhimu, nayo ni:-
1. Kufunga, kuzuia, na kuacha kufuata bila ya mwelekeo, na
kuweka wazi ufahamu wa kuyafasiri maelezo kama
yalivyo katika asili yake na kujiepusha na uelewa wa
matukio ambayo matokeo ya fat-wa yake hayatafanana
na tukio, na kutofahamu misingi ya sheria kiujumla (pasi
na kujua asili yake), pia kuwapa nafasi wasio na elimu
katika kueneza ulinganio.
2. Baadhi ya watu kuitumia dini kama biashara, na kuitumia
kwa malengo ya kisiasa na kwa vikundi vya vyama, pia
kwa kujipatia faida katika vikundi na miasasa yao kwa
jina la dini na taifa, na kujifanya watendaji wa dini lakini
35
kwa mtazamo wa nje na wa kisiasa badala ya kuitendea
dini kwa ajili yake Mwenyezi Mungu pekee.
3. Kufanikiwa kwa baadhi ya watawala katika kuwatumia
vibaraka wao katika nchi nyingi za kiarabu na za
kiisilamu, sawa kama ni kwa ajili ya kubadilishana
masilahi, au kupewa ahadi za uongo kwa baadhi ya
makundi, au kwa njia ya kununuliwa na kuwa kama
watumishi.
Ikifanyika juhudi ya pamoja basi itapelekea kufikia lengo
kubwa hasa katika upande wa kuwepo pamoja kwa wasomi,
na sababu nyingi za mtengamano zitaondoka, na hii
itapelekea, bila shaka, umma kuwa kitu kimoja, na hasa hasa
katika kupambana na fikira zisizo sahihi, za uasi na zenye
kupotosha.
Vyama Vingi na Utawala Usiomili
Anuani hii inakusanya mambo mawili yanayokaribia kuwa
ni yenye kukinzana kwa kutowafikiana na kutokubalika, moja
wapo likiwa ni lazima lipatikane katika Nyanja za kidemokrasia
36
na jengine linaonekana kuwa ni hatari kubwa kwa kutengeneza
taifa kwani huenda likasababisha kuporomoka na kuanguka na
kudhoofisha. Kwa upande wa vyama vingi hili ni jambo la
kiadilifu kwa upande wa kidemokrasia, kwani ulimwengu wa
sasa ni sawa na mhimili mmoja (kijiji kimoja). Na mara nyingi
kukosekana kwa kujadili mambo kwa uadilifu hutokea hali ya
kidikteta na udhaifu na hasa pale inapokuwa hakuna upinzani
wa kweli wa kuweza kutimiza ahadi ya kweli juu ya kile
alichokiahidi na kukalifishwa.
Ama kwa kuwepo utawala unaomili katika nchi yoyote au
kuwepo kwa makundi yenye kujali masilahi yao pekee, hii
husababisha hatari kubwa sana ya ujenzi wa mshikamano wa
taifa. Na hasa iwapo utawala utajisitiri kwa vazi la kidini na
kujaribu kutumia madaraka yake na ushawishi wake kwa njia
hiyo.
Na kipimo pekee cha kujua kuwa utawala au jamii haina
au ina utawala unaomili ni kwa kuangalia kwa kina gani
wanatekelea sheria bila ya upendeleo au uficho na bila ya kusita
au kudhulumu. Na kutoruhusu kundi lolote au mtu yeyote
kushajiisha wafuasi wake waende kinyume na sheria au
kuiharibu sheria kwa nguvu.
37
Na kwamba wote wanahitajika kufuata mkondo wa sheria
katika kuelezea matakwa yao, na wafanye vile sheria nakanuni
ilivyoruhusu katika Nyanja zote, pia kuhakikisha kuwa
hairuhusiwi kutumia udanganyifu kwa kupitia sheria. Na kama
mfano wa kundi la kiisilamu la kisiasa linavyodai ya kuwa
“kwenye lengo hupatikana njia”, kwa kutumia njia hii jamii
ilishuhudia kutetereka na kuyumba na kama si usaidizi kutoka
kwa Mwenyezi Mungu taifa lingelikuwa lishatoweka. Na kwa
kutokana na umakini wa Mheshimiwa raisi Abul fatah Al sisi na
wasaidizi wake pamoja na jeshi lake shujaa na wengine wenye
kuipenda nchi yao, kitu ambacho kinachofanya kurudi kwa
kundi la kigaidi la Ikhwani katika kutengeneza dola lenye
kumili kuwa ni jambo lenye kupingwa na lazima lipingwe kwa
nguvu zote kwa ajili ya kuhifadhi heshima ya nchi.
Na iwapo tunaamni kuwa hakuna kulazimishana katika
dini, na nafasi ya wasomi ni kufikisha ujumbe kwa njia sahihi
na wao ni walinganiaji na si mahakimu au majaji basi jambo hili
linahitaji kuwekwa wazi katika mahusiyano yaliyopo kati ya
walinganiaji na watawala, kwa kuzingatia kuwa utawala wenye
kumili hujaribu kuutengeneza kwa wafuasi wake unaweza
ukawa umemili katika kisiasa au kifikira au kitamaduni na
38
inaweza kuwa pia kiuchumi au kijamii kwa kupitia baadhi ya
vitega uchumi vyake au kwa njia nyengine yoyote.
Kiufupi, kundi lolote ambalo litakuwa linahisi kwamba
lipo juu ya sheria na kuwa halishtakiwi jambo hili litapelekea
kuonekana kuwa utawala uliopo ni wa kumili nalo ni jambo la
hatari sana kwa serikali na kwa sheria zake. Kinachohitajika ni
kutimiza sheria kwa yeyote bila ya kumili hili ni jambo la
uadilifu kwa ajili ya kuokoa taifa na sheria zake. Na mtume weu
(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “hakika
wliokuwa kabla yenu waliangamia kwani walikuwa akiiba mtu
mwenye cheo walimuachilia huru na akiiba mnyonge walikuwa
wakimpa adhabu ya wizi, nami ninaapa kwa Yule ambae nafsi
yangu ipo mikononi mwake lau kama Fatuma bint Muhammad
angeliiba basi ningelimkata mkono wake.”
Na sayidna Ali (Mwenyezi Mungu amwie radhi) anasema
pale alipopewa uongozi: “enyi watu mimi nimepewa madaraka
juu yenu hali ya kuwa si mbora wenu, nikidhoofika basi nitieni
nguvu, nikifanya vyema basi nisaidieni, ukweli ni amana, uongo
ni khiyana, dhaifu kwenu basi kwangu ni mwenye nguvu mpaka
apewe haki yake kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na mwenye
nguvu kwenu kwangu ni dhaifuampaka apate haki yake kwa
39
uwezo wa Mwenyezi Mungu.. nitiini kadiri nitakavyokuwa
ninamtii Mwenyezi Mungu na mtume wake, na nikimuasi
Mweneyzi Mungu na mtume wake basi musinitii.”
Na mfano mwengine ni sayidna Umar bin Khatab
(Mwenyezi Mungu amwie radhi) anamuandikia Abi Musa Al
ash ariy (Mwenyezi Mungu amwie radhi) barua ya kihistoria
kuhusu uongozi, anasema: “ baada ya hayo, hukumu ni jambo la
lazima lenye hekima na ni mwenendo wenye kufuatwa, elewa
pindi ukifikwa na jambo kuwa usiseme isipokuwa ya
kweli,fanya usawa kwa watu kwenye uso wako na kikao chako
na uadilifu wako na wala dhaifu asikate tamaa katika uadilifu
wako, na wala mwenye cheo asiwe na tama katika uadilifu
wako.
Sayidna Omar bin Al Khatwab alimuandikia kingozi wa Kufa
Abi Mussa Al ashary kwamba awafanyie usawa watu katika
hukumu, akamwambia: “ fanya usawa kwa watu kwenye kikao
chako na katika uso wako.” Akikusudia hata katika mwenendo
na uwapo nao na hata
unapowaangalia. Usimpokee mmoja kwa kumchukia na
mwengine kwa bashasha, au mwengine ukamuita kwa jina lake
la kawaida na mwengine kwa jina la ukoo na la kupanga, ili
40
watu wasije wakawa na tamaa ya kusifiwa au madhaifu wasione
kuwa wanadhalilishwa bila ya haki yoyote.
Uadilifu ni kwa wote na kwa ajili ya kuhifadhi sheria
(kanuni) na kuinua taifa. Na kuhifadhi uongozi na hukumu. Ili
amani ya nafsi na utulivu wa jamii upatikane, kwani wasomi
wamesema: “ Hakina ya Mwenyezi Mungu huhifadhi nchi
yenye uadilifu hata kama ni ya makafiri na wala hainusuru nchi
yenye kudhulumu hata kama ni waumini.”
Na hatari kubwa inayokumbana na taifa lenye kumili ni ile
ya kuwepo makundi au vikundi vya madhehebu au ukabila
ambavyo hupata nguvu zake kwa kupitia nchi nyengine, kama
mfano tuonavyo kwa baadhi ya makundi ya kishia ambayo
hupata nguvu zake kutoka kwa Wafursi. Na kufanya uongozi
wa mwanzo na wa mwisho ni haki yao pekee na hujiimarisha
kwa kila hali.
Na la kushangaza kabisa ni kuona nchi ya Saudi Arabia
kutekeleza hukumu zake juu ya mwananchi wake na kisha
kujitokeza wanaowaunga mkono Wairani wakiingilia mambo
ya ndani ya nchi hiyo, na kufikia ujinga wa wafursi wa kisufi
hadi kuvunja mikataba ya kimataifa ya kuwahifadhi
wanadiplomasia, na hali ingekuwaje lau kama (Saudi
41
Arabia) angefanya hukumu ya kumnyonga raia wa Irani?
Na je, yupo yeyote anayeingilia kati kama hivi juu ya nchi ya
Iran na upotefu wake dhidi ya nchi za kiarabu kwa kuwanusuru
madhehebu ya sunni katika Ahwaz na sehemu nyengine? Au
haya ni maonyesho tu ya Irani kuonyesha nguvu zake kwa ajili
ya kutaka kudhihirisha nyama zake za kutaka kueneza fitina
katika eneo la mashariki ya kati kwa ajili ya adui mayahudi na
ubepari wa majigambo wa kifursi?
Maana ya Usalama wa Taifa
Hapana shaka kuwa taifa lolote ili liwe na utulivu ni lazima liwe
na utulivu na usalama wa taifa. Na kila mwananchi awe na
pupa katika kuhakikisha usalama wa taifa, bila ya kusita na
hasa pale taifa linapofanya maamuzi, na hasa maamuzi ambayo
42
yanahusika na utendaji wa ulimwengu wa nje au ambayo
yataathiri katika utendaji huu.
Iwapo usalama wa taifa lolote ni mstari mwekundu usiopaswa
kutengeukwa au kuupuuzia pasi na kuathiri kwa msitari huu
itapekelea kuwepo na ufahamu na elimu ya kuendelea ya
kuuelezea umuhimu wa usalama wa taifa. Ninaweza kusema: “
kufanya vipindi vya mara kwa mara kwa lengo hilo kwa kila
aliye na chezo au nafasi ya uongozi itakuwa ni jambo la lazima
sana na lenye msisitizo, kwa kuwa ujuzi wa fani, uendeshaji wa
idara na utendaji pekee hautofalia kwa ajili ya kuleta muono
ambao utapelekea kuelekea katika njia sahihi, na hii iwapo
hakuna muono mwengine mkubwa zaidi wenye athari ambao
utatekelezwa kwa asili ya usalama wa taifa.
Na wengi hawazingatii akilini katika yale maamuzi wayafanyayo
au wayasimamiayo yanayoshikamana na mahusiana ambayo
yanaweza kuleta athari katika usalama wa taifa. Inaweza kuwa
si kwa kukusudia isipokuwa kwa kutojua yanayohitajika katika
ulinzi wa usalama wa taifa, au yanayohitajika yakawa hayupo
kwa muhusika kwa kiwango kitakiwacho. Na kwa kipindi
ambacho taifa na eneo la Mashariki ya kati lilivyo, na
43
ulimwengu unahitaji mwananchi wa kawaida ukiachana na
mtoa maamuzi kwamba awe na ufahamu wa usalama wa taifa
lake. Sawa atoapo maamuzi au kuweka mahusiano au katika
makubaliano na itifaki.
Na iwapo umuhimu wa kujua ni jambo kubwa litakiwalo na ni
la hatari kwa kule kushikamana kwake na usalama wa taifa na
kutafautiana kati ya mtu na mwengine kwa kuzingatia vielelezo
tafauti kama; utamadunim hima ya kutaka masilahi ya taifa,
kujali shida za taifa, na kuweka masilahi ya taifa mbele zaidi ya
kila kitu, hivyo jambo hili litapelekea:
a. Kuelimisha zaidi kuhusu usalama wa taifa kwa kupitia
vipindi vya mara kwa mara kwa kila kiongozi.
b. Kuzindua umuhimu wa usalama wa taifa na ulazima
wa kuulinda hasa kwa wanasiasa na wasomi na
waandishi na wataalamu na vyombo vya habari, na
hasa kwa wale wenye kumiliki uoni mkubwa wa elimu
juu ya fani hii. Na kuweka katika mazingatio yao kuwa
hili nalo ni moja ya yaletayo utulivu wa taifa.
44
c. Ulazima wa kuwepo ushirikiano kwa vyombo husika
kabla ya kufanya makubaliano au itifaki pamoja na
vyombo vya nje, kwa kuzingatia isije ikatokea aina
yoyote ya uvujaji au athari zitakazoathiri masilahi ya
taifa hata kama itatokezea bila ya kukusudia.
Kwa kusisitiza ufahamu wa usalama wa taifa kwa nchi
yoyote itabidi pia kuzingatia hali ya kisiasa ya ndani na nje
na kimaeneo na kimataifa. Kutokana na kina chetu sisi
waarabu na kina chetu waafrika na ulimwengu wetu wa
kiisilamu pamoja na mahusiano yetu ya kimataifa yote hayo
inabidi yawekwe katika mazingatio wakati wa kuchukua
(kufanya) maamuzi muhimu na tendaji, pamoja na kusoma
upeo wa athari juu ya mahusiano hayo, na kujua faida zake
au hasara zake kwa pande zote, pamoja na kusoma yaliyo
muhimu na kumjuvya mwananchi uzito wa kila hatua
inayofanyika.
Hakuna shaka ya kuwa mahusiano ya kisiasa, kipolisi,
kiuchumi, kitamaduni, kifani na vyombo vya habari athari
zake zinaathiri wenyewe kwa wenyewe, kwa kuwa
haiwezekani kutenganisha kimoja na kuacha chengine,
45
ilivyokuwa kila taasisi inajitegemea kama vile ni ulimwengu
uliojikamilisha. Hivyo basi, inabidi kwa kila taasisi kuzingatia
utendaji wake na kuchunga utendaji wa taasisi nyengine. Na
bila shaka jambo hili linahitaji hisia za kizalendo za hali ya
juu na utambuzi mkubwa na kufanya kazi sote kwa pamoja
kwa roho ya timu na kufahamu usemi kuwa “ ufahamu wo
wote na utendaji wa baadhi”, kwa kuhakikisha kila
muhusika anahusika ipasavyo juu ya kazi alizoachiliwa na
tahasusi yake anaifanya kwa kiwango cha uelewa kwa roho
ya pamoja (timu) na wote alionao, na kutoa maamuzi kwa
mujibu wa jambo husika.
Na kwa kuhakikisha kuwa taifa haliwezi kuendelea kwa
kuwa tu tuna nia njema bila ya kuwa na mipangilio na
uamko, katika ulimwengu ambao asiyejikinga na mbwa
mwitu basi ataliwa naye.” Sayidna Umar bin Khatab (Mungu
amwie radhi) anasema: “ mimi si mjanja na mtu mjanja
hawezi kunihadaa.” Na Mughira bin Shuuba alikuwa
akisema: “ lau kama si uisilamu basi ningelifanya vitimbwi
visivyowezekana katika bara arabu.”
46
Na nia njema haina budi kuwepo ili matendo yakubalike,
Mwenyezi Mungu anasema: {Sema: Je, tukutajieni wenye
khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao juhudi
yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani
kwamba wanafanya kazi nzuri.} na kwa ajili hiyo kurani
imesisitiza sharti za amana na utendaji bora kwa kuwa
zinatoshelezana, kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu anasema
kupitia ulimi wa mtoto wa nabii Shuaib (rehma na amani juu
yake) { Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba
yetu!Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye
nguvu na muaminifu.} na pia anasema { Yusuf akasema:
Nifanye mshika khazina za nchi.Kwani hakika mimi ni mlinzi
mjuzi.
Miji Mikuu, Mipaka na Ujenzi wa Taifa
Uhusiano kati ya miji mikuu na mipaka yake ni uhusiano wa
kukamilishani na si wa kugombana na wala haitakikani iwe
hivyo, kwa kuwa hakuna taifa lolote ambalo linaweza
47
kujitosheleza kufanya kuwa mji mkuu ndio kitovu na kusahau
pande nyengine za taifa kwani bila ya mipaka taifa haliwezi
kusonga, isipokuwa tu mataifa mengi huifanya miji mikuu kuwa
ni kituo kikubwa walichokipa kipaumbele na mifano ya
kihistoria inaweka wazi ushahidi wa jambo hili. Isipokuwa kuna
tafauti kati ya mataifa yaliyoendelea na mataifa yasiyoendelea
katika kutoa umuhimu wa miji mikuu. Mataifa yaliyoendelea
haiwezekani kuzembea hata kidogo kuhusu hata kipande cha
ardhi, jengo au sehemu na kuiacha ikiharibika au kufanyia
uharibifu au hata fikira tu za kutaka kujitenga (kama ni
maeneo).
Mshairi mmoja alikwenda kwa Umar bin Abdul Aziz (Mungu
amwie radhi) akamsomea shairi akasema:
Iwapo unahifadhi unaowamiliki basi elewa
Wafanyakazi wa ardhi yako ni mbwa mwitu
Hawajaitikia wito wako uliowaita
Mpaka wapigwe viboko na kukatwa shingo
Na kwa kuwa ukuaji wa maeneo na sehemu za mipakani si
jukumu la serikali pekee au viongozi wa kisiasa, kwani hifadhi
na umuhimu pamoja na kazi za ukuzaji ni jukumu linalokusanya
taasisi zote za nchi, sawa na iwe taasisi rasmi au mashirika ya
kijamii, wafanyabiashara, watega uchumi, sekta za elimu, sekta
za afya, za ujenzi, za tamaduni, wizara ya wakfu, na wizara
nyengine na mashirika pia, pamoja na jumuiya za huduma za
kijamii.
Wote hawa inabidi watilie umuhimu mkubwa na hasa maeneo
ya mipaka. Na walipe kipaumbele na kuona kuwa ni suala
linalohusu usalama wa taifa kwa upande mmoja na la ukuzaji
kwa upande wa mwengine. Na inatakikana sote kwa pamoja
48
tuyageuze maeneo ya mipakani iwe ni maeneo ya kuvutia na si
ya kukimbiwa. Na inapotokezea taifa kutojali maeneo haya basi
huwa ni nafasi kwa makundi kufika katika maeneo haya na
kufanya kambi zao na kusababisha msongamano usio wa
kawaida kwa vituo vya huduma za kijamii na kupatikana uwepo
wa ujenzi wa kiholela, na hata kusababisha kukuwepo kwa
maisha ya kitabaka, maradhi na matatizo mengine ya kijamii
ambayo yatahitaji udhibiti usio wa kawaida ili kuyatatua.
Ama kwa upande wa taifa kujali na kutoa umuhimu wa maeneo
haya ya mipakani kwa upande wa vitega uchumi, ni kule
kuweka huduma za lazima kwa wananchi wake: makazi, afya,
elimu, utamaduni, na huduma nyenginezo ambazo zinahitajika
kuendeleza maisha katika ardhi yao. Pamoja na kuwepo kwa
nafasi za kazi na uzalishaji. Hayo yote yatapelekea kwa
wananchi kuipenda ardhi yao (taifa lao) na kuhifadhi chembe
ndogo ya mchanga ili isipotee pamoja na kuwafanya wawe
wazalendo.
Na panapokuwepo kwa vivutio na ushajiishaji wa kazi katika
maeneo haya na kuwepo kwa vitega uchumi madhubuti kama
nchi inayotilia mkazo ilivyo hivi sasa katika maeneo ya Sinai,
Matruh na Ismailia mpya, Halayib, Shalatin na Wadi Jadid, na
maeneo mengine kama yale ya jangwani. Maeneo haya karibuni
yatabadilika na kuwa ya kuvutia. Kitu ambacho kitapelekea
kuwepo kwa ugawaji sawa wa kijiografia, kimakazi na pia
utawezesha kuwepo kwa maisha mazuri kwa wananchi wa
maeneo hayo. Na kupunguza msongamano wa utoaji wa
huduma kwa wakazi wa maeneo hayo, au kupatikana huduma
kama zile zipatikanazo katika miji sawa huduma za kisiasa au
za kiuchumi. Na kuwepo kwa vivutiaji vitakavyowezesha
kuvutia watalii na kuushangaza ulimwengu na kuonyesha
ukubwa na upevu wa wanachi wa ukuaji wao.
49
Sinai Ndani ya Kurani Tukufu
Kurani tukufu imezungumzia kuhusu Sinai maneno ambayo
yanahitaji mazingatio, maelezo yanayotilia mkazo umuhimu wa
50
eneo kwa upande wa kidini na kihistoria. Maelezo ambayo
yanatufanya tufikirie sana umuhimu wa eneo hilo, na ukuaji
wake na uwekezaji wake na mali asilia zake pamoja na alama
zake kwa upande wa kitalii, kidini kitabia nchi na kimatibabu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuapia mlima Sinai ndani ya
kitabu chake kitukufu aliposema: {1 Naapa kwa mlima wa T'ur.
2 Na Kitabu kilicho andikwa. 3 Katika ngozi iliyo kunjuliwa. 4
Na kwa Nyumba iliyo jengwa. 5 Na kwa dari iliyo
nyanyuliwa,} (At tuur; 1-5). Na ametangulia kuapa kwa Tuur na
kuacha vyengine kutokana na umuhimu wake na nafasi yake
tukufu, si hivyo tu bali sura nzima imepewa jina na kuitwa
“sura at tuur”.
Na Mwenyezi Mungu anaapa kwa uwazi zaidi ndani ya kitabu
chake katika sura ya “At tiyn” aliposema {3 Na kwa mji huu
wenye amani! 2 Na kwa Mlima wa Sinai! 1 Naapa kwa tini na
zaituni!} (At tiyn;1-3). Na ametanguliza kuapia mlima Sinai
kabla ya kutaja mji wenye amani pamoja na kuwa ni mji wenye
utukufu mkubwa.
Kama ilivyoashiria Kurani Tukufu juu ya baadhi ya kheri na
neema zilizopo katika mlima Sinai, Mwenyezi Mungu anasema,
{ Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa
51
kitoweo kwa walao.} (Al muuminun; 20) na kuhusu mti huu
Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) anasema: “ kuleni
mafuta, na jipakeni nayo, kwani ni katika mti wenye Baraka.”
(Tirmidhy)
Na ndani mwake muna sehemu ya ardhi iliyobarikiwa na
imetajwa katika Kurani Tukufu Mwenyezi Mungu anasema kwa
kupitia mazungumzo yake na Mtume Mussa (rehma na amani
zimshukie) { Basi alipo ufikia aliitwa kutoka ng'ambo ya
bonde la kulia ni katika eneo lilio barikiwa kutoka kwenye
mti: Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola
Mlezi wa walimwengu wote.} (Al qasas; 30). Na kuna jangwa
tukufu la Tuwa ambalo Mwenyezi Mungu amelieleza ndani ya
kitabu chake alipokuwa akizungumza na Mussa (rehma na
amani zimshukie) aliposema {Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe
Musa! 12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu
vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.} (Taha; 11-
12).
Eneo hili la Sinai ambalo Mwenyezi Mungu amelitaja maalumu
linapasa kuwepo ndani ya nyoyo zetu, na kulilinda na kujitolea
muhanga kwa ajili yake kwa kila tunachokimiliki.
52
Hapana shaka ya kuwa jeshi letu kakamavu limevumilia kwa
ushujaa wa hali ya juu na limejitolea muhanga na halijaacha
kufanya hivyo kwa ajili ya kuhifadhi damu za wananchi wake
kwa ujumla. Pia kwa ajili ya kuihifadhi Sinai na kuisafisha
kabisa na makundi ya itikadi kali, kitu ambacho wanastahiki
pongezi na hongera kwa upande na kuwa safu moja yenye
nguvu na kutoa kila kinachobidi kwa ajili ya kuilinda kwa
upande wa pili, sawa iwapo hifadhi hii ni ya kimali au isiyo ya
kimali.
Na kwa jaribio letu la kuangazia upande wa kidini, na kitalii,
tabia nchi, kiustaarabu na kihistoria kuhusu kusini mwa mlima
Sinai tumeamua kama Wizara ya Wakfu ya Misri kufanya
mashindano ya kimataifa ya Kurani tukufu katika mji wa
Sharmi Alshaekh kwa kusaidiana na wizara ya Vijana na
Michezo na mkoa wa Kusini mwa Sinai pamoja na Taasisi ya
gazeti la Jamhuria ambayo itakuwa ni mmoja wa washirika
muhimu, na kundaa matembezi ya mandhari za kidini na
kiustaarabu, kihistoria na tabia nchi kwa kuwa Misri itapokewa
wageni kutoka mataifa mbalimbali ya ulimwenguni katika mji
wa At Tuur (Sinai) na Uyuun Mussa, na Saint Catherina na
53
alama mandhari mengine. Pamoja na kuwaelezea umuhimu wa
maeneo haya kwa upande wa dini na kihistoria.
Na kwa kuwa mashindano ya mkwa huu yatakuwa na mtindo
mpya utakaukuwa wa aina mbili: Aina ya kwanza; mashindano
ya kuhifadhi kurani tukufu ya vijana chini ya umri wa miaka
kumi na mbili na, aina ya pili; ni mashindano ya kuhifadhi
kurani kwa wenye ulemavu kwa uchache juzuu tatu. Na
mashindano haya yanafanyika kwa kusisitiza kuwa mji wa Sinai
ni mji wa amani na utabakia hivyo kwa Uwezo wa Mwenyezi
Mungu. Na kwa kuwa upo moyoni na akilini mwa kila Mmisri
mwenye kuipenda nchi yake. Na kuhusu majaribio ya kuvunja
tamaa ya baadhi ya maadui hayatotuzuia tusiweze kuiendeleza
Sinai nakuijenga na kuihifadhi kwa mapenzi yetu yote na
kushikamana na ardhi yake, pamoja na kuwa macho katika
kuondosha kabisha chimbuko la ugaidi.
Na hapa ninahimiza kwa maimamu ambao watapata nafasi ya
kuongoza eneo la Sinai wafanye kazi kwa ajili ya kuondoa
shinikizo la kigaidi, kama ninavyohimiza kwa wale wote ambao
watakuwa na kazi ya kueneza wito (ulinganio) sawa wawe ni
kutoka katika wizara ya Wakfu ndani ya mkoa wa Kusini mwa
Sinai au kutoka katika sehemu nyengine ambazo zipo chini ya
54
uangalizi wa Wizara ya Wakfu kuwa wafanye kazi zao kwa
mtindo wa kupishana.
Uhakiki Kati ya Marekebisho na
Ubomoaji
55
Mwanzo kabisa hatuna budi kutenganisha kati ya uhakiki ulio mzuri na ule mbaya, Na kinyume chake ambacho ni ubomoaji. Maana ya neno la kwanza nalo limechukuliwa katika mfano ule wa kusema “ dhahabu na fedha zimesafishwa” ikimaanisha kuwa zimetenganishwa kati ya dhahabu / fedha nzuri na ile siyo nzuri. Na maana ya neno la pili likiwa na maana ya ubomoaji (maporomoko) ni kama kusema “mtu Fulani amefariki chini ya maporomoko: ikiwa na maana yupo chini ya mabaki ya nyumba iliyoyabomoka. Na neno uhakiki katika lugha lina maana mbili: ya kwanza: aibu, tusi na lawama, mfano kama alivyosema Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) “ukiwatusi watu nao watakutusi na ukiwaacha nao watakuacha: ikiwa na maana iwapo utawatia aibu na lawamani nao pia watafanya hivyo, kwani iwapo kama una ulimi basi watu wana ndimi. Ama maana ya pili ni ile inayokusudiwa ya kupambanua kati ya jema na baya, inaweza kuwa ni kusifia na kupendezeshea na inaweza kuwa pia kukejeli na kutusi na inaweza kukusanyika ikakusanya yote mawili. Na uhakiki unaweza kuwa ni wa kibinafsi au wa kitabia, na unaweza kuwa ni wa kielimu na kimitaala na kimaudhui. Mfano
56
wa uhakiki wa kibinafsi ni; kwa mfano kusoma makala au kusikiliza hotuba au neno au hadithi au kuona ubao ulochorwa na fanani na ukashangazwa nao bila ya kutaka kujua undani wa fani au kujua sababu za uzuri wake, na unaweza usishangazwe kwa kutotaka kujua undani wa fani ile ambayo kwa mtazamo wako haina kiwango cha uzuri. Ama kwa upande wa uhakiki wa kielimu na kimitaala na maudhui ni ule uliopo na uliosimamia misingi ya kielimu na kimaudhui na kifani na uhakiki wa namna hii unahitaji nguzo tatu kuu:- Nguzo ya kwanza: Zana zenye kuhusika na utengenezaji au fani. Mhakiki wa kazi za ufasihi anahitajika kujua sana lugha kwa mfano nahau, sarufi, elimu ya mashairi, elimu ya ufasaha wa usemaji, na elimu ya uhakiki, na fasihi pamoja na kujua baadhi ya elimu nyengine za kibinaadamu, kijamii, kisaikolojia, fani za historia , ustaarabu wa jamii na ujenzi na masome mengine kwa ujumla. Mhakiki wa mahesabu au wa kisiasa au wa fani au uchoraji hana budi kuwa na kiwango kikubwa sana cha misingi ambayo anataamali nayo. Kinyume chake atakuwa anafanya uhakiki wa kijuujuu tu na atahitajika kuwepo wa
57
kumhakiki na wa kumkosoa pia, na pengine afikwe na kejeli kutoka kwa atakaemueleza vibaya na hata kumdharau. Nguzo ya pili: kwa mhakiki awe na utambuzi na ujuzi na umiliki, je huoni kuwa unaweza kusikia msomaji anasifia hutuba mbili nzuri zenye mvuto mkubwa au ukasoma vitabu viwili vya makala vya waandishi wakubwa ukawa una zana zote za ufahamu (inakusudiwa elimu kwa fani tafauti) au ukapata kuhakiki kazi za kielimu na kifani zilizo na ufanisi wa hali ya juu, isipokuwa unaweza ukapambanua kazi hizo kwa kitu chenye kufahamika lakini ikawa ni vigumu kuelezeka. Mfano kama alivyosema Al Amindiy: “ huoni kuwa unaweza kukutia farasi wawili wazuri wakawa na sifa zilizofanana kwa upande wa uhodari werevu na nguvu na uasili na ikawa kwa mwenye akili ni vigumu kuwapambanua, isipokuwa kwa wale wenye ujuzi wa farasi kwao ikawa wanaweza kuwatenganisha mmoja kutoka mwengine, vile vile mbao zilizochorwa kwa ustadi mkubwa na majengo yaliyojengwa kwa kiwango kwa wenye ujuzi ni rahisi kujua uzuri uko wapi na kasoro iko wapi kwa kuwa wanamiliki zana za utambuzi wa fani hiyo. Ama kuingilia tu fani ya uhakiki kwa wasio na ujuzi nayo na wala wasio miliki zana zake au hata kuisomea hili huwa ni
58
tatizo kubwa ambalo huchelewesha na lisiloleta maendeleo na lenye kuharibu na lisilojenga na humpa sifa mbaya mhakiki kabla ya alichokihakiki. Nguzo ya tatu: nayo ni muhimu sana nayo ni kutenda kwa moyo wote na kujiepusha na matamanio na kusifika kwa watu, kwani kuingia katika matatizo na matamanio na kuacha kutenda yanayotakikana ni janga kubwa ambalo inapasa kujiepusha nalo. Hii ni kwa kuwa baadhi ya nyoyo ni gonjwa hazielewi isipokuwa njia ya ubomoaji pekee na kama alivyosema Imamu Ali Bin Abdiaziz Al jarjani katika utangulizi wa kitabu chake, kinachoitwa Alwasatwatu baina almutanabiy wakhusumuhu. Ametaja kuwa upungufu upo wa makundi mawili: kundi hufanya kwa ajili ya kurekebisha mapungufu yao na kuficha aibu, na jambo hili ni jema kwa kuwa mhakiki amejishughulisha zaidi na nafsi yake na kujaribu kujiweka katika nafasi nzuri. Ama kundi la pili ni la wale wenye mapungufu ikawa wamejikali ima kutokana na kushindwa au kwa hiyari yao au kwa udhaifu au kwa uvivu na hakuna kitu kinachowalazimisha wawe na mapungufu au kuweza kuhifadhi aibu zao kutokana na mapungufu hayo, na wakawa
59
wanadhania kuwa na mwenendo huo kutawafanya waweze kunyanyuka na kupata vyeo vya juu. “ Na wengi wamefikwa na jaribio hili hata katika zama zilizotangulia ikawa wanachumia pato lao kwa kupitia sifa wanazosifiwa na maneno mazuri wanayopambiwa, na kujipatia pato kwa njia ya kusifiwa jambo hili lilikuwa ni maarufu tangu zama za kijahili kwani wapo waliojulikana kama chuo cha utunzi au cha uchumaji kupitia mashairi kwa mfano Zuheyri bin Abi Salma, Nabia Adhubiyan na wengineo, na wengine walijulikana kwa ufasaha hata mwanzoni mwa kuja kwa uisilamu kama Hutwaya ambae alikuwa akiwatishia watu kutokana na ufasaha wake wa kuweza kumsema mtu vibaya, mpaka kiongozi Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akamtishia sana pindi asipoacha kuhujumu tabia za watu, akasema: “ basi na wafariki watoto lakini nitanunua kutoka kwake (Hutwaya) heshima za watu kwa dirhamu elfu arobaini ili asije akamvunjia heshima yeyote. Na Hutwaya akaacha kuwakejeli watu kwa muda wa uongozi wa Umar kisha akarudia tena baada ya kufariki kwake. Haya yote hayawezi kutengeneza ustaarabu wa kweli au kuendelea kwa jamii yenye usawa ambayo inastahiki kusifiwa
60
na pongezi za kweli, lakini uhakiki wa aina hii hubomoa. Na uhakiki wa kweli wa kimaudhui uliojengeka kwa misingi ya kielimu na ujuzi wa utaalamu na uadilifu huu ndio utakaojenga. Kwa mfano kusema kwa aliyefanikiwa: “ umefanikiwa” na kwa aliyekosea, kumwambia kwa heshima kuwa “umekosea na umepunguza. kwani huenda akajirekebisha na kuitafuta njia ilizo sawa. Na huu ndio uhakiki wenye malengo ambao haubomoi bali hujenga na wenye uadilifu na kushajiisha na wakati huohuo unaweka wazi pamoja na kutahadharisha. Na iwapo uongozi ni majukumu na ni amana basi kuhakikisha uhakiki na uchambuzi ni amana na majukumu vilevile. Nasi sote tutaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kila mtu ataulizwa juu ya amana ambayo Mwenyezi Mungu amempa. Kama ambavyo tutaulizwa juu ya ujenzi wa taifa letu na kazi za uimarishaji wake na ukuaji wake kupitia njia za ujenzi na marekebisho na si kwa njia za uvunjaji na ubomoaji. Na si kwa njia ya kujinufaisha au kupenda kuonekana, kwa wengi wetu sasa wanaweza kutambua nini ngano na nini pumba. Na Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake kitukufu: “Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi.
61
Vyombo Vya Habari Vyenye Malengo
62
Hapana shaka kuwa nafasi ya vyombo vya habari duniani ni
muhimu sana na tendaji kubwa na wala haiwezekani
kuvizembea na kuvipuuzia, na vyombo vya habari vyenye
malengo ni vile vyenye kujenga na sio vile vyenye kubomoa.
Na hakuna yeyote apingaye kuwa vyombo vya habari vya
kisasa vinapita katika mikondo tafauti, baadhi yake
vinajishughulisha na masuala ya kitaifa, vyengine vya kisiasa
sawa imechama tawala au upinzani, viko pia visivyomili upande
wowote au vya kuajiriwa na baadhi ni vya biashara na vyengine
ni vya kijamii na kibinafsi.
Na kila chombo kinapimwa kutokana na kazi zake zifanyazo
kwa jamii na kujiweka kwake katika kufuata misingi ya kikazi
na maadili ya kiutangazaji, na kuacha kumili pamoja na kujadili
mambo kwa kina na kwa mitazamo ya viongozi na waandishi
wake na wasomi wake pamoja na wahabari wake pia kuzingatia
ubora wa wafanyakazi wake katika fani hiyo.
Na nilazima kwa kila taasisi ya utangazaji au isiyo ya utangazaji
iwe na chombo cha uchunguzi ambao utachunga namna za
ubora wa wafanyakazi wake katika kila sekta zake, kitu
kitakachopelekea kuzidisha ufanisi na uwezo wake wa kuweza
kushindana na vyombo vya habari sawa viwe vya kitaifa au vya
63
kimataifa. Na kikusudiwacho ni ufuatiliaji wa kweli wenye hisia
za kitaifa na dhamiri ya kikazi.
Na hapana shaka kuwa ulimwengu wa kimaarifa upo wazi zaidi
na una uwezo mkubwa wa kujipambanua, na kuweza kumjua
nani mwenye ujuzi wa kazi hii na nani asiye na ujuzi wa kazi hii
(ya utangazaji) kwa kuwa ni kazi yenye kuhitaji uwezo wa
kifikra na maarifa.
Na hakuna shaka kuwa taasisi za magazeti ya kitaifa yamesaidia
kwa kiwango kikuba katika kurekebisha mwenendo wa
utangazaji na ushirikiano wake wa kutoa huduma katika kujadili
masuala ya kitaifa. Na kuzifanya taasisi hizi kuwa na heshima
kubwa kwa wananchi kwa ujumla na kwa wasomi kwa
kuwahusisha wao pekee.
Na hapana shaka pia mikutano ya kiuchumi na ya kisomi
ambayo inafanywa na baadhi ya taasisi za magazeti makubwa
ni mojawapo ya shajiisho kubwa lenye kustahiki pongezi na
hongera. Vilevile kuzingatia masuala ya kisomi na uchambuzi
wa kina kwa kusaidia kuweka wazi sura na mitazamo. Na
pengine hata fikira zilizo nje ya sanduku kuziweka wazi mbele
ya watengenezao maamuzi.
64
Pamoja na kuweka wazi tafauti kati ya uhakiki ambao
unakusudia kubomoa na uhakiki wa maudhui ambao huleta
nyongeza kubwa sana katika Nyanja za kisomi nakitamaduni na
kiidara na kiuchumi nacho ni kitu ambacho kinahitajika
tukikaribishe sote na kukishajiisha na tufaidike nacho. Na kuona
kuwa ni nyongeza isiyo na upungufu ilivyokuwa inachunga
misingi ya kazi na masilahi ya taifa.
Na kumiliki hisia za kutosha za kupanga mambo, na katika
mambo ya kuzingatia pia ni kuendesha mafunzo ya vizazi
virithishane . Na wale wenye ujuzi wa kazi wawafunze vijana
na kuwajuvya uhumimu wa kuwasiliana na mazungumzo yenye
kuendelea kati ya wahusika na waandishi wa habari
(wanahabari), na kuwepo na uhusiano uliokamilika wenye kuwa
na masilahi ya kitaifa pamoja na kuhakikisha umaridadi. Na
kama alivyosema mmoja wa waandishi wa habari” “
nimejifunza kutoka kwa walimu wangu kuwa ni afadhali
kuzikosa habari mia moja kuliko kupoteza ukweli wangu katika
kueneza habari moja kwa njia isiyo sahihi.
Hofu ya Kuzembea
65
Taabira hii inamaanisha kuwa kuzembea ni jambo kubwa
mno kwani huhofisha mwili na roho pia, na si hivyo tu bali
inazidi mipaka ya kutia hofu ndani ya nafsi na kufikia hatua ya
umwagaji wa damu, kuteketeza mali za watu pengine hata na
heshima zao. Mambo haya yote yaweza kuwa kweli kwa bidii
katika kazi kwa ajili ya manufaa ya watu wote na nchi nzima.
Na lau kama tungeshikamana na hadithi ya mtume (rehma na
amani zimshukie juu yake) “nyote ni wachungaji na nyote
mutaulizwa juu ya mulivyovichunga..” (Bukhari) Mume ni
mchungaji wa nyumba yake na watu wake naye ataulizwa juu
ya aliowachunga. Mwalimu ni mchungaji kwa wanafunzi wake
na ataulizwa juu ya aliowachunga, mwalimu mkuu ni
mchungaji juu ya shule yake na ataulizwa juu ya
aliowachunaga, mkuu wa idara, mkurugenzi, mkuu wa sekta
wote hawa ni wachungaji na wataulizwa juu ya waliowachunga.
Katika sekta ya elimu, afya, usafi wa mazingira, kilimo, na
sekta nyenginezo lau kuwa tungeshikamana na hadithi hii basi
uzembe ungebadilika na kuwa mafanikio
66
Nasi tunaomba juhudi zizidishwe ndani ya taasisi za kitaifa na
kuweka sheria kali za kupambana na ugaidi, tunataka sheria hii
iwabane wote wenye kuzembea na pia kuwazuia wahalifu. Na
lau kuwa nafsi ya wanadamu tumeipa nafasi yake na kuelewa
heshima hii ina thamani gani basi tusingelimwaga damu na wala
kuidhulumu si kwa kuzembea wala kwa kuiogopesha. Na lau
kama tungeelewa kuwa mali ni mali ya Mwenyezi Mungu na
mali zote kwa ujumla sawa iwe ya mtu binafsi ya umma
inapaswa kuhifadhiwa na kuitunza na ni amana iliyo katika
mikono yetu mwenye kuilinda na kuijali na kunufaika nayo, na
kuwa sisi tuna majukumu juu ya mali hizo na ya kuwa
hautanyanyuka mguu wa mja siku ya kiyama mpaka aulizwe,
basi tungelizihifadhi sawa ziwe mali zetu au za wenzetu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu wenye kufanya
ubadhirifu kuwa wao ni ndugu wa mashetani akasema, {
Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni
mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi.} Israa,27. Sasa ni
vyema zaidi kujiepusha na kujiweka mbali na uzembe na
kuzembea kwani adhabu zake ni kali. Na Mtume (rehma na
amani zimshukie juu yake) amekataza kuwa nimemsikia huyu,
67
nimemsikia Yule na kufuja (kupoteza) mali, pasipo na haki kwa
kufanya isirafu na kwa kuzembea.
Sisi tunahitajika kuondoa utamaduni wa kutojali sawa kama
itakuwa ni kwa njia kueleweshana na kwa mafundisho ya kidini
na kuhisi jukumu la taifa. Kwa upande wa sheria itahitajika
kuweka adhabu kubwa itakayokuwa ni fundisho kwa kila
afanyaye ufisadi katika ardhi, kwani kuzembea ni ufisadi na {
Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi }Al baqara 205.
Na kuna matukio ambayo baadhi ya watu watayaona kuwa ni
mepesi lakini ukweli yanahitaji kuchukuliwa tahadhari, na
yanaweza kusababisha hatari kubwa au tukio kubwa. Kuacha
taa za barabarani wakati wa mchana zinawaka huku ni
kuzembea na kupoteza nguvu ambazo tunazihitajia sana, nayo
pia ni kupoteza mali za jamii ambazo jamii inahitajia.
Pia kufanya isirafu katika kutumia maji na kuacha kutengeneza
njia za maji taka na kuacha na inawezekana kutengeneza kwake
ni rahisi sana ama madhara yake ni makubwa kwa mfano nyaya
za umeme zilizo wazi, au mashimo ya maji taka yaliyo wazi au
kutozingatia yanayopaswa kuangaliwa kwa mfano kuacha
kuangalia matairi ya magari breki zake, vioo vya pembeni na
68
vya kuonea nyuma au kuacha vioo vya gari hali ya kuwa vina
ufa, na kuacha kuchukua tahari ipasavyo. Yote haya yanaweza
kusababisha hatari kubwa ambayo tungeweza kuepukana nayo
lau kama tungelijiepusha na sababu za kizembe na kutojali.
Na uzembe wa hali ya juu kwa mtu kuacha kile ambacho
Mweneyzi Mungu kampa akishughulikie, kwani jamii (taifa)
litamshitaki mbele ya Mwenyezi Mungu. Vyeo na uongozi wa
idara si burudisho la kitaifa na la kijamii – hakuna cha kufurahia
kwa wakati wowote – bali vyeo ni amana, na siku ya kiyama
itakuwa ni fedheha na majuto isipokuwa kwa yule aliyechukua
nafasi ya uongozi na kutekeleza amana hiyo kama itakiwavyo.
Athari za matatizo ya kuzembea zimezidi mara dufu na tishio la
mihadarati na vileo ambavyo vimeshafunika akili, na
kudhoofisha miili na kutuletea aina tofauti za kuzembea na
kutojali. Muhadarati ni mama wa madhambi kwani mtu pindi
akili yake ikatoweka na akawa anaenedelea na ugonjwa wake
huu hatoacha kutafuta mali kwa ajili ya kutaka kununua kwa
njia yoyote ile hata kama itakuwa ni kwa kufanya uadui kwa
jamaa zake wa karibu na hufikia hata kuua. Baadhi ya magazeti
na mitandao imeeleza kisa cha yule kijana muovu ambae
69
amejaribu kutaka kumvunjia heshima mama yake mzazi mzee
kwa sababu akili yake haipo.
Na hatari hii kubwa inahitajika msimamo madhubuti wa
jamii nzima kwa ajili ya kupambana na kutojali na kuzembea na
wale wote wasiotekeleza majukumu yao. Uuzaji wa madawa ya
kulevya ni kitendo kidogo chenye kupelekea ufisadi mkubwa na
ni chanzo kikubwa cha kuharibu akili za vijana wetu na
mustakbali wa taifa letu. Hii, inahitajika kwa taasisi za kidini,
kitamaduni, kielimu na vyombo vya habari kuchukua jukumu
lake ipasavyo bega kwa bega na vyombo vya serikali, vya
uchunguzi na vya kimahakama. Na kufahamu ya kuwa
apotezaye akili yake basi hatari huwa kwa nafsi, heshima na
mali na daktari pengine katika kutibu atahitajika kukata sehemu
katika mwili kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa roho yake. Na
mwanadamu anaweza kuwa mkali kwa baadhi ya wanawe kwa
ajili ya kuwahifadhi na kuwalinda na kuwalea malezi bora. Na
mshairi wa kiarabu anasema:
Haki ya taifa na haki ya jamii ni kuwa salama kwa namna zote,
na usalama tunaouzungumzia hauwezi kupatikana kwa upande
na kuachika katika upande mwengine, lakini kwa jamii nzima.
70
Na itapendeza zaidi lau kama kila mtu atakuwa na pupa ya
kuheshimu usalama wa jamii, kwani kuna maelfu kama si
mamilioni ambao wananufaika na usalama, na kama
utadumishwa basi kuna wengine pia wataudumisha na kama
utazembewa na kila mtu akawa hajali basi uzembe utaenea
katika jamii, na wa zamani walisema “mtendee mwengine vile
upendavyo kutendewa”. Wakasema “fanya utakavyo, kama
ulivyokopa utalipwa.” Na kwa asiyejua masilahi ya nafsi yake
jamii italazimika kumsaidia kulijua hili na kumrudisha katia
uongofu, kwani Mwenyezi Mungu humuondoshea kitu sultani
kila si chomuondoshea msomi wa kurani.
Kisa Cha Masanamu na Ubomoaji wa
Ustaarabu
71
Kwa kuanzia, hakuna muisilamu duniani mwenye kuabudu
sanamu. Au hata kuamini jambo hilo pia hata kulingani
kuabudiwa au kufikiria tu jambo hilo, si muisilamu tu mwenye
kuamini hivi lakini pia hata wale wa dini zilizoteremshwa.
Na iwapo uisilamu umekataza kutengeneza masanamu
mwanzoni mwa uisilamu basi hili lilikuwa kwa sababu mbili; Ya
kwanza. Watu walikuwa bado ni wapya katika uisilamu na
walikuwa wameacha kuabudu masanamu kwa muda mchache
(tangu kuingia kwao katika uisilamu) kwa kudhania kuwa
yanawaweka karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu. Kama
iliyoeleza kurani tukufu kwa ndimi zao pale Mwenyezi Mungu
aliposema { Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu
kumkaribia Mwenyezi Mungu }.
72
Sababu ya pili:Iwapo masanamu haya hutengenezwa
kwa ajili ya kuabudiwa au kutengenezwa kwake ni kwa ajili ya
kumfananisha na Mwenyezi Mungu. Na kati ya yenye
kuthibitisha hayo na kuwa tukiachilia mbali kuondosha
masanamu yaliyokuwa yakiabudiwa ndani ya Alkaaba kwa ajili
ya kuisafisha haikuthibiti kuwa kuna sahaba yeyote aliyevunja
sanamu au athari yoyote ile ya sanamu katika nchi yoyote
katika zile walizozifungua. Hii ni kwa kuwa walifahamu
malengo ya makusudio ya uisilamu ufahamu ulio sawa na wala
hawakusita kusimamia ufasiri wa aya kijuujuu.
Lakini waliangalia kwa undani zaidi juu ya makusudio na
malengo kwa dalili ya kuwa walijua madhumini ya aya, hata
sayidna umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) pale alipozuia
fungu la sadaka kwa wale wanaozoweshwa nyoyo zao katika
73
uisilamu pamoja na kuwa imethibiti ndani ya kurani, Mwenyezi
Mungu aliposema { Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na
masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao,
na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika
njia ya Mwenyezi Mungu,) na alipoulizwa Umar( Mwenyezi
Mungu amwie radhi) iweje unasimamisha fungu ambalo Mtume
(rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akilitoa?
Akasema: “ tulikuwa tukiwapa na uisilamu ni dhaifu na kwa
lengo la kuwazowesha lakini sasa Mwenyezi Mungu Mtukufu
ameupa nguvu uisilamu kwa fadhila zake kwa ajili hili fungu hili
halina kazi tena.
Na zaidi ya haya, alizuia kutimizwa hukumu ya wizi katika
mwaka wa njaa pale alipomwandkia mmoja wa wafanya kazi
wake, utafanya nini akikujia mwizi (mtu kaiba)? Akasema:
74
nitamkata mkono wake.” Akasema: “ mimi akinijia mwenye
njaa basi nitaukata mkono wako.
Isipokuwa umma wetu wa kiisilamu umefikwa na mitihani
mikubwa akili za watu wake zikasimama wakaanza kuhalalisha
na kuharamisha bila ya elimu, ufahamu na wala kujua,
wakajidhatiti kwa nafsi zao na za wanafunzi na wafuasi wao
kwa yale wasiyo kuwa na elimu nayo kwa kutoa fatwa,
wakapotea na kupoteza wengine, pia kufungua mlango mpana
wa kuwapa mwanya watawala na mabeberu kufuta athari za
ustaarabu wetu sawa ustaarabu wa kiarabu, kiisilamu,
kikiristu, kifirauni, kiashuri, kibabeli, kiyunani, kirumi na
ustaarabu mwengine. Hii ni kwa kufuta utajo wa waarabu na
pia ustaarabu wake na ustaarabu wa kiisilamu na pia wa
kikiristu. Kwa kuwa wao ni wajinga wa tabia na
75
wasio na dini na wala maadili. Kwao wao ni kufikia
malengo yao pasi na kutizama sababu na hata kama
kuangamiza wanadamu na majengo na kila kikavu na kibichi
pia hata kubomoa ustaarabu wa kibinaadamu.
Mbaya zaidi ni kuwa haya yanatendeka kwa jina la dini na
baadhi ya watu huidhania dini vibaya na kuona ni ya kiadui
kumbe dini ipo mbali sana na mambo haya. Na hata kama
watajidanganya wenyewe na kuwahadaa wahanga wao
(wafuasi wao) katika vijana wenye kujiunga nao kwamba wao
wapo sawa. Hao ni kama wale aliosema Mwenyezi Mungu
Mtukufu, {na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu. Kwa
hakika hao waliwafanya mashet'ani kuwa ndio marafiki walinzi
badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao
wameongoka} na anasema {Sema: Je, tukutajieni wenye
khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao
76
juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao
wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri} {. Na katika
watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya
kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi
Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye
mkubwa wa ukhasimu. 205. Na anapo tawala hufanya
juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea
na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.}
Na kiongozi mkuu wa Al Azhar Profesa Ahmad Al-Twayib
amesisitiza kama alivyosisitiza waziri wa wakfu na Dar Al-Iftaa
ya Misri, kuwa haifai kuharibu alama hizi za ustaarabu kwa
namna yoyote ile sawa iwe kwa kuzivunja, kuziharibu
mkuziuza, kuziiba au kuzibomoa na kuziharibu ni sawa na
kuharibu ustaarabu wa mwanadamu.
Na katika jambo lenye kuhitaji mazingatio na lenye kuleta hisia
na mshangao na kuleta masuala mengi ni msimamo wa nchi
za magharibi na mashirika ya kimataifa juu ya kimya chao
77
kikubwa juu ya makosa haya ambayo lau kama yangelitokea
sehemu yoyote hapa ulimwenguni ukiachilia mbali eneo la
mashariki ya kati (ukanda wa kiarabu) basi ulimwengu wote
ungelijua. Basi hii ndio tabia ya maadui zetu ambao
wanatushajiisha katika vita visivyo vya sheria, na lenye kuuma
zaidi ni zile Fatwa ambazo hutilia mkazo matendo ya aina hii,
hivyo basi tunahakikisha na kuthibitisha tena na tena kuwa
kuna haja
kubwa ya kuweka sheria ambazo zitazingatia utoaji wa
Fatwa kwa kutolewa na wale tu wenye ujuzi nazo na si
wengine.
78
Kati ya Utendaji Bora na Utii
Pindi nchi ikiwa na uetndaji bora pamoja na utiifu, utiifu
wa kazi, utendaji bora wa kazi na sehemu afanyayo kazi mtu
basi jambo hili huwa ndilo litakiwalo. Ama ikiwa ni utendaji kwa
ajili ya mtu Fulani au kundi Fulani au hata chama Fulani basi
jambo hili huwa ni la kujiweka rehani kwa kutumia utendaji
nalo huwa ni hatari sana, sawa kwa kipimo cha sheria au kwa
79
kipimo cha taifa. Utendaji bora na utiifu ni mambo mawili
yaliyoshikamana pamoja na wala hayatengani. Mtume wetu
(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “ yeyote
mwenye kumtumia mtu juu ya kundi naye akawa anatambua
kuwa (kufanya hivyo ni) kumtumikisha, basi atakuwa
amemfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake na
waisilamu wote.” Na uongozi uwe wa aina yoyote sawa uwe
mkubwa au mdogo huwa ni amana na huhitajika ufanisi na
utendaji bora. Mwenyezi Mungu anasema kwa ulimi wa mtoto
wa nabii Shuayb (rehma na amani juu yake) kuhusu Mtume
Mussa (rehma na amani juu yake): { Akasema mmoja katika
wale wanawake: Ewe baba yetu!Muajiri huyu. Hakika mbora
wa kumuajiri ni mwenyenguvu na muaminifu.} uaminifu pekee
hautoshi pia na elimu pekee haitoshi ,Abu dhari alipomtaka
Mtume (rehma na amani zimshukie) ampe uongozi, mtume
80
(rehma na amani zimshukie) akamwambia: “ ewe Aba dhari
wewe ni dhaifu uongozi ni amana na siku ya kiaya ni fdheha
na majuto isipokuwa kwa atakaeuchukua kwa haki na
kutekeleza yapasayo.” Na Mtume akawapa uongozi wa
kuongoza jeshi Khalid bin Al-Walid na Amru binAl- A`s na
wengineo pamoja na kuwa walisilimu muda mchache sana
kutokana na utendaji wao na ujuzi wa fani za kivita na
mazingira ya mapigano na malumbano.
Ama utendaji wa ubinafsi huturudisha katika miaka ya
kiza iliyokuwa makabila na watu maalumu ndio wakiongoza
kupitia utiifu wa watu maalumu na kuacha kutii wengine. Pia
huturudisha katika kipindi ambacho ufisadi ulienea katika idara
zote na hadi hivi sasa bado tunaendelea kupata athari zake,
kwani ilikuwa hutangulizana wenyewe kwa wenyewe na baadhi
81
ya wanafiki na wenye kusifiana wenyewe kwa wenyewe na
wale wenye kuamini njia ya ulaji rushwa kuwa ndio njia pekee.
Dhuluma na uvunjaji moyo zikawa ndio vilivyopo na kusitiriana
pamoja na kujiweka mbali na utendaji wa unaostahiki na ikawa
wanafichiana aibu zao, pamoja na kuhakikisha kuwa kile
walichokitoa katika mali (kipindi cha kampeni) wanahakikisha
kuwa kinarudi tena mifukoni mwao kwa njia yoyote. Hivyo, vita
kuu ya raisi ni kupambana na ufisadi na mafisadi wote na
kung`oa ufisadi kabisa kutoka katika mashina yake.
Hapana shaka kuwa utiifu kwa wale wapandao mabega
ya watu watii kwa njia zisizo za kisheria wala za kikanuni hawa
huwa hawaelewi zaidi ya kuwanufaisha wakubwa wao pekee
hata kama ni kwa kuitumia dini yao na dhamira zao watafanya
hivyo kwa masilahi ya pande zao na kuacha masilahi ya taifa.
82
Na hapana shaka kuwa hawa wenye kujitakia manufaa ya
nafsi zao hawawezi katu kulinufaisha taifa na wala taasisi kwa
amana ya aina yoyote. Kwa kuwa hawastahiki na wala hawana
shime ya kutekeleza uamnifu, isipokuwa kwa nafsi zao zilizo
na chuki kwa kuwatendea wale walio na utii. Na wala
haiwezekani kuwakosoa au kuwaingilia kwa lolote katika
matendo yao au hata kuwasahihisha ukosefu wa matendo yao.
Na katika kosa kubwa sana lililofanywa na chama cha
kisiasa cha kiisilamu ni kule kuwahadaa watu kwa mtazamo wa
nje na kuitumikisha dini kwa juujuu na kufanya kuwa
kujilazimisha kuitendea dini katika baadhi ya mambo ni
sehemu ya uongozi bali pia ni shuruti muhimu na mambo ya
lazima kufanyika. Watu wengi walotii kundi la kisiasa la kidini
wakawa ndio wengi waliopata vyeo, unaweza muona yule
83
ambae jana hakuwa akijua kitu chochote katika dini leo hii
keshapata nafasi kubwa na hatari sana ya uongozi. Cheo
ambacho hana iuhusiano unacho wala ujuzi nacho. Na mfano
mkubwa ni yale yaliyotokea katika Wizara ya Wakfu ya Misri
pale kilipotawala chama cha Kigaidi. Waliwaweka watu wasio
na ujuzi wowote kwenye wizara hiyo wala katika idara zake ili
tu ionekane kuwa kundi hilo ndilo lenye kuongoza. Na si
katika wizara ya wakfu pekee bali pia khiyana ilienea katika
vyombo vya dola kwa mfano bei kupanda na uroho wa kutaka
madaraka.
Na utengwaji pengine historia ya nchi haijawahi
kushuhudia namna hiyo isipokuwa baada ya kutawala kundi hili
uongozi wa taifa, kitu ambacho kikapelekea kuanguka kwao
kukawa ni kukubwa historia ya karibuni haijawahi kuona tukio
84
kama hilo na kuweka wazi ukweli wao mbele ya ulimwengu
wote. Kitu ambacho kinatupa uhakika kuwa mwisho wa kundi
hili kuwa limeitumia dini kama biashara na kuiweka katika
mnada ulio rahisi, na lilikuwa likiwadanganya watu kwa muda
mwingi mpaka Mwenyezi Mungu akafichua mambo yao, kila
mtu akaelewa ubaya wa nia zao, na pole za wale
wanaowatetea hazikusaidia kitu.
Na juu yetu kukunufaisha kwa kukuweka mbali na utiifu
usio wa kweli na wa uongo na usiokubalika kisheria na taifa.
Na kuwapa wenye kustahiki kulisimamia jambo hili kwani
wakati tulionao unahitaji nguvu madhubuti za mwenye ujuzi na
mpenda nchi.
Mfano Mzuri wa Kugawanya Mali ya
85
Zaka
Hapana shaka kuwa iwapo zaka itagaiwa kama itakiwavyo
kisheria basi itaziba pengo kubwa la mahitajio ya mafakiri na
wenye shida sana na masilahi ya taifa zima. Pindi nafsi za
matajiri na wenye uwezo wakifanya ukarimu na kutenda
wajibu wao wa kuwalisha wenye njaa, kuwavesha wasio na
nguo, kuwatibu wagonjwa, kuwasaidia wenye kuhitaji na kutoa
mchango wa kuboresha na kudumisha kwa taifa basi ni lazima
nchi ibadilike. Na hapatakuwa na raia ambaye atakuwa
anahitajia na kuomba, imamu Ali (mwenyezi Mungu amwie
radhi) anasema: “Hakika ya Mwenyezi Mungu Mtukufu
amegawa chakula cha masikini katika mali za matajiri, na katu
masikini hatokuwa na njaa isipokuwa tajiri atakuwa ameshiba,
na akipatikana masikini mwenye njaa, tambua kuwa pana tajiri
dhalimu na hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake,
na hakutekeleza wajibu wake kwa upande wa jamii yake.”
Na iwapo (tajiri) ataekeza vitega uchumi kwa njia sahihi kwa
ajili ya masilahi ya taifa lake jambo hili litapelekea kuinuka
kwa taifa letu zuri kama itakiwavyo. Bali pia huenda manufaa
86
yakaenea katika nchi nyengine nyingi za kimasikiniambazo nasi
tunahitajika kuzisaidia kwa mfano wa nchi za mto wa Nile
ambazo inatubidi kuwa na mawasiliano nazo na kusaidiana
kielimu, kitamaduni, kimanufaa na kiutu kwa kiwango cha
kiserikali na cha kiraia na kwa taasisi zake za kitaifa ambazo
tunaweza kufanya vitega uchumi vikubwa na imara katika nchi
hizi na nyenginezo katika nchi za Afrika zilizo na umasikini,
kama ni mojawapo ya mbinu na himaya ya usalama wa raia
wetu. Na kwa jambo hili kuna mifano mingi inyoshukuriwa
kwa upande wa taasisi za kiraia.
87
Zaka ni Haki ya Lazima Katika Mali
Nasisitiza juu ya ukweli, na wa kwanza ni: hakika ya zaka ni
hali ya lazima katika mali na ni nguzo kuu kati ya nguzo za
kiisilamu mfano wa sala na funga bila ya kutafautiana, na
Sayidna Abdallah Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi)
amesema: “Vitu vitatu ndani ya kurani tukufu vimeteremshwa
kwa kuambatanishwa sambamba na vitu vitatu (vyengine)
kimoja wapo hakikubaliwi bila ya chengine, navyo neno lake
Mwenyezi Mungu “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtiini
Mtume wake.” Na neno lake, “Na Simamisheni sala na toeni
zaka” mwenye kuacha kutoa zaka pamoja na kuwa anajua
kama ni lazima basis ala yake haitomnufaisha kitu mbele ya
Mwenyezi Mungu. Na neno lake, “na unishukuru mimi na
wazazi wako wawili na kwangu ni marejeo.”
Asiyewashukuru wazazi wake wawili kwa wema wao na
matendo mazuri yao basi pia hatomshukuru Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wanaoweka hazina za mali
na kujizuia na utoaji wa zaka {Na wanao kusanya dhahabu na
fedha, wala hawazitumii katika Njia yaMwenyezi Mungu,
88
wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu. 35. Siku zitapo
tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, nakwazo
vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao namigongo
yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu,
basi onjeni mliyo kuwamkilimbika. }
Jambo la pili: hakika uisilamu umetoa wito wa kutoa sadaka
kwa wingi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Mfano wa
wanao tumia mali zao katika Njia yaMwenyezi Mungu ni
kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba.
Katika kila shuke zimo punjemia. Na Mwenyezi Mungu
humzidishia amtakaye, naMwenyezi Mungu ni Mwenye
wasaa na Mwenye kujua.} ( Surat Albaqarah.Aya,261). Na
Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake anasema) “ mali
haipungui kwa kutoa sadaka.” Na anasema: “sadaka bora ni
ile uitaoyo hali ya kuwa ni mzima kabisa, unataraji utajiri
na kuogopa umasikini, usiicheleweshe hadi pale roho
inafikia kooni kasha ndio unasema, Fulani apewe hiki na
Fulani hiki na ilikuwa kwa Fulani (hiki) na ilikuwa kwa
Fulani (hiki).” Na pia anaendelea kusema: “hakuna siku
isipokuwa malaika wawili huita na mmoja wao husema
“ewe Mola mpe kila atoe (mpe) ziada, ewe Mola mpe kila
89
ajizuiaye uharibifu.” Na anasema Mwenyezi Mungu
Mtukufu:{ Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya
Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya
ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili
mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio
wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu,
nao hawatakuwa kama nyinyi}. ( Surat Mhammad,Aya 38) .
Huondosha na kutibu mwanya:
Hapana shaka kuwa mwanya utakuwa ima katika vyombo
(taasisi) vyenye kutoa zaka au vyenye kupokea zaka au
vyombo vyenye kuunganisha na sawa iwe ni mtu, jumuiya au
taasisi.
Mwanya unaopatikana kupitia vyombo vitoavyo zaka itakuwa
ima kwa kutotoa hiyo zaka kabisa, au kwa kuipunja au itakuwa
inatolewa lakini si kwa umakini kwa wahusika wake.
Hivyo basi, ni wajibu kuzingatia katika hutuba za dini juu ya
ulazima wa kutoa zaka na umuhimu wake na madhambi
makubwa ayapatayo mwenye kuzuia kutoa zaka mbele ya
Mwenyezi Mungu, pamoja na kusisitiza ya kuwa tajiri
hatoepukana na dhima yake kwa kuitoa mali yake kiholela. Na
baadhi ya wasomi wa elimu ya sheria wameona ya kuwa iwapo
90
tajiri amempa mali yake kwa anayedhania kuwa ni masikini
kasha akaja kuelewa kuwa si masikini basi itamlazimu kutoa
tena zaka. Ni wajibu wake ahakikishe kuwa anatoa kwa mujibu
wa sheria na kwa amana na kwa uchunguzi na kwa vyombo vya
kisheria ambavyo hupewa zaka ili dhima yake iondoke mbele
ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ili zaka yake ilete matunda
mazuri ambayo yanapatikana kwa utoaji wa zaka.
Na mwanya upatikanao kwa upande wa mpokeaji, unakuja
kutokana na udhaifu wa ugawaji kwa baadhi ya wenye nia
mbaya za kutaka kujilimbikizia mali kwa njia yoyote hata kama
ni kwa kulaghai. Ni wajibu wetu kuwakumbusha muongozo
sahihi wa kiisilamu na utu wa kibinaadamu ambao unakataza
kwa mwenye uwezo kulaghaia na kujidhalilisha. Mtume
(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “haifai kuomba
isipokuwa kwa Yule mwenye ufakiri uliopindukia mipaka,
au mwenye madeni makubwa, au mwenye damu ya
maumivu ”. Na anasema; “Mwombaji ni kama pambo
ambalo mtu hujipambia usoni mwake, akitaka huliacha
usoni mwake na akitaka huliondoa.” Na ima Ali (radhi za
Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) anasema;
91
Ni afadhali kubeba kima cha jabali * kuliko kufadhiliwa na
watu
Watu hunambia kazi ni aibu * nami huwambia “aibu ni kuomba
watu”
Na Mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema
“ katika mambo ambayo watu waliyapata kutokokana na
maneno ya utume ya mwanzoni ni kuwa, usipokuwa na
haya basa fanya utakacho.”
Lazima tuhakikishe ya kuwa uisilamu umekataza kuomba pasi
na sababu ya msingi, na mtu mwenye heshima hawezi
kuishusha nafsi yake kwa kuomba, na mkono wa juu (utaoa) wa
juu ni bora kuliko wa chini (usiotoa). Pamoja na kuhakikisha
umuhimu wa kufanya kazi na thamani yake na msisitizo wa
uisilamu juu ya kazi. Na kuweka wazi ya kuwa anayekwenda
mbio kwa ajili ya wajane na masikini ni sawa na apiganiaye
jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mbora wa watu ni
Yule alaye kwa mkono wake na si kwa kuomba kwa wengine.
Ama kwa upande wa mwanya wa tatu: ni ukusanyaji na
ugawaji, pamoja na imani yetu kwa baadhi ya taasisi za kijamii
kuwa zinapunguza mzigo mkubwa kwa mafakiri na wasi na
uwezo sawa kwa upande wa kuwapa mahitajio kwa kupitia
92
vitega uchumi na hasa kwa upande wa matibabu, isipokuwa
nionavyo kuwa taasisi hizi zinahitaji yafuatayo:-
A. View chini ya uangalizi wa vyombo vya kiserikali, na
vyombo hivi viwe vinafutilia na kuchunguza ipasavyo, na
kuwe na uwazi wa kutangaza uwezo wake, mahitajio
yake na mafao yake pamoja na kuwaongoza katika
utendaji wa kiidara kadiri wawezavyo.
B. Kuwe na ramani ya wazi juu ya taasisi hizi, na upeo
wake wa kijiografia na utendaji wake, ili ijulikane
mipaka yake na kikomo chake na isije ikatokezea
kupatikana uzembe kwa baadhi ya sehemu pengine
zingelikuwa zinahitaji msada mkubwa zaidi.
C. Kuwe na idara ambayo itashughulikia taasisi hizi kwa
mfano Wizara ya Ushirikiano wa jamii. Kuwe na
kiunganishi chenye kuwaunganisha watoaji na wapokeaji
na taasisi za kijamii kwa mwelekeo wake wa kijiografia
au mwelekeo wa kihuduma, ili pia wahusika wajulikane
na iepukane kutowafikia walengwa halisi wanaohitajia
zaka.
D. Malengo na madhumuni yawe wazi yajulikane kwa wote,
au kila chombo au jumuiya ijulikane ina dhumuni gani
93
iwapo ni kuwalisha wasio na uwezo au kuwatibu
wagonjwa, kulipia madeni ya watu, nahyo haya ni
miongoni mwa malengo wanayoyaendea mbio Wizara ya
Wakfu ya Misri.
Baina ya Matumaini na Kazi
Maisha yamejaa matumaini. Hakuna kukata tamaa
maishani. Na wala maisha hayawi pamoja na kukata tama. Na
mwenye akili hupata jibu kwa kila jambo gumu au kwa uchache
huwa anajaribu kufanya hiyo. Na mjinga huwa anaona katika
kila suluhisho lina msongo (fundo) uliokamatana. Basi huwenda
jambo lililo sahihi kisheria haiyumkini kupingana na usahihi wa
akili kwani sheria zote zinaelekea kuwa ni kwa masilahi ya
watu. Basi wanachuoni wanachukulia kuwa kukata tamaa na
kukatisha tamaa ni kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu
94
Mtukufu na ni miongoni mwa madhambi makubwa. Basi
kutoka kwa Ibn Abaas R.A. anasema kwamba mtu mmoja
alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni yapi Madhambi
makubwa? Mtume S.A.W. akasema: Kumshirikisha Mwenyezi
Mungu na kukatia tamaa kwa Nguvu ya Mwenyezi Mungu, na
kukata tamaa kwa rehema za Mwenyezi Mungu, aliyelindwa na
Mwenyezi Mungu kwa mambo hayo na kuepushwa nayo
nimemuhakikishia kuingia peponi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwa ulimi wa
Bwana wetu Ibrahim (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu
yake) katika mazungumzo yake pamoja na Malaika
waliombashiria Ishaq (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu
yake): {Akasema: "Oh!" Mnanipa khabari hii, na hali yakuwa
uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanipa khabari njema
hivyo?" (54) Wakasema: "Tumekupa khabari njema iliyo haki;
basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa." (55) Akasema:
"Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola wake isipokuwa
wale waliopotea?" [AL HIJR 54-55-56]
Na huyu ni Yaaqub (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu
yake) anawaambia watoto wake: {"Enyi wanangu! Nendeni
mkamtafuta Yusuf na nduguye na wala msikate tamaa na
95
rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na rehema ya
Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri"} [YUSUF 87].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema; {Sema, "Enyi
waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! msikate tamaa na
rehema ya Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu
husamehe dhambi zote; hakika yeye ni mwingi wa kusamehe
(na) mwingi wa kuehemu."} [AZ ZUMAR 53].
Basi mwenye dhambi asikate tamaa kwa usamehevu,
kwani Mwenyezi Mungu alifungua wazi mlango wa toba, na
katika Hadithi ya Qudisi kwamba Mtume S.A.W: asema "Ewe
mwanadamu! Wewe ukiniomba na ukinitarajia Mimi
nikakusamehe madhambi yako na sisiti, ewe mwanadamu
ukinijia kwa kiasi cha ardhi makosa lakini hunishirikii na kitu
cho chote basi tutakupa msamaha kiasi chake" [Imetolewa na Al
Tarmiziy].
Na mgonjwa hakati tamaa kwa kutopona hata kama
ugonjwa wake ni mkali kabisa, basi lazima atafute njia ya
kujitibu, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika
uponyaji, na sisi tuna mfano wa Ayyubu (amani ya Mwenyezi
Mungu iwe juu yake), Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
{Na (mtaje) Ayyubu alipomwita Mola wake (akasema) "Mimi
96
yamenipata maradhi, nawe ndiwe unayehurumia kuliko wote.
(83). Basi tukamkubalia (wito wake) na tukamwondolea
ugonjwa aliyokuwa nao, na tukampa rehma yeye na watu wake
na mfano wao pamoja nao. Ni rehemu inayotoka kwetu, na
ukumbusho (mzuri) kwa wafanyao ibada.} [AL ANBIYAA 83-
84].
Na kama ulikuwa tasa huzai, basi usikate tamaa kwa
rehema ya Mwenyezi Mungu mwingi wa utoaji. Basi
mwangalie huyu ni mke wa Ibrahimu (amani ya Mwenyezi
Mungu iwe juu yake) alipobashiriwa mtoto na Malaika ingawa
umri wake ulikuwa mkubwa, anasema: {(mkewe Ibrahimu)
akasema: "Ee Mimi we! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na
huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo la
ajabu." (72). Wakasema (wale Malaika): "Je, Unastaajabu amri
ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka
zake juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye
(Mwenyezi Mungu) ndiye anayestahiki kusifiwa na
kutukuzwa"} [HUD 72-73].
Na Zakaria (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake)
alipomwomba Mola wake basi akasema: {Akasema: "Mola
wangu! Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa
97
kimejaa mvi, wala sikuwa mwenye bahati mbaya, (mwenye
kuhasirika, Mola wangu, kwa kukuomba wewe." (4). "Na
hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu (kuharibu
dini). Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi (anijie) kutoka
kwako."} [MARYAM 4-5]. Jibu lilimjia kutoka kwa Mola
wake kwa haraka... {(Akaambiwa) "Ewe Zakaria! Tunakupe
habari njema ya (kuwa utazaa) mtoto, jina lake ni Yahya:
Hatujafanya kabla yake aliye na jina namna hilo.} [MARYAM
7].
Na Zakaria (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake)
alipoulizia: {Akasema (Zakaria) "Mola wangu!) Nitapataye
mtoto, na hali uzee umenifikia, na mke wangu ni tasa?"
Akasema: (Mwenyezi Mungu) "Ndiyo vivyo hivyo; Mwenyezi
Mungu hufanya apendavyo."} [AALI IMRAN 40]. Basi jibu
lilimjia: {Akasema: "Ni kama hivyo. Akasema Mola wako.
"Haya ni sahili kwangu. Na kwa yakini Nilikuumba zamani
nawe hukuwa cho chote.} [MARYAM 9].
Na kama ulikuwa masikini, basi jua! kuwa fakiri wa leo
labda atakuwa tajiri wa kesho, tajiri wa leo pengine atakuwa
fakiri wa kesho, na siku huzunguka, na kwamba Mwenyezi
Mungu Mtukufu atakapo jambo kwa mja hulipitisha: {Hakika
98
amri yake anapotaka cho chote (kile kitokee) ni kukiambia
"kuwa" basi mara huwa.} [YASIN 82]. Na Mwenyezi Mungu
Mtukufu anasema: {Rehema Anayoifungua Mwenyezi Mungu
kwa watu, hakuna wa kuizuia na Anayoizuia hakuna wa
kuipeleka mbele (isipokuwa Atake) Naye ni Mwenye nguvu,
Mwenye hikima.} [FATIR 2].
Na hata nyakati za hasiri zinapokuwa na ugumu katika
maisha yako basi ushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu. Basi huyo ni Maryam (amani ya Mwenyezi Mungu
iwe juu yake), dunia ilipoingia giza machoni mwake na
hakupata kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa
kwake akasema: {Akasema: "Laiti ningekufa kabla ya haya, na
ningekuwa ni mwenye kusahaulika kabisa.} [MARYAM 23].
Basi msaada na rehema zilikuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu katika kauli yake: {Mara ikamfikia sauti kutoka chini
yake (inamwambia): "Usihuzunika! Hakika Mola wako
Ameweka kijito cha maji chini yako." (24) "Na litikisie kwako
shina la mtende huo, litakuangushia tende nzuri, zilizo mbivu."
(25) "Kisha ule na unywe na litue jicho (lako) (furahi, pumua
moyo wako). Na kama ukimwona mtu yoyote (anataka
kukuuliza habari ya mtoto huyu), sema: "Hakika mimi
99
nimeweka nadhiri ya kufunga kwa ajili ya (Mwenyezi Mungu)
Mwingi wa rehema, kwa hivyo leo sitasema na mtu."}
[MARYAM 24-25-26].
Na wale waislamu katika vita vya Ahzabu; mushrikina
waliwazingira kila upande, lakini ushindi uliwajia ambapo bila
kutegemea kama vile Quraani tukufu ilivyoyazungumzia haya
katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini
kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu;
yalipokufikieni majeshi, Tukayapelekea upepo na majeshi
msiyoyaona (ya Malaika), na Mwenyezi Mungu Anayaona
(yote) mnayoyafanya." (9) Walipokujieni (kukushambulieni)
kutoka juu yenu na kutoka chini yenu, na mlipoyakodoa macho
yenu na nyoyo zikapanda kooni nanyi mkaanza kumdhania
Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. (10). Hapo waislamu
walitiwa mtihani (kweli kweli) na wakatetemeshwa kwa
matetemesho makali.} [AL AHZAB 9-10-11].
Na huyu ni Bwana wetu Ibarahim (amani ya Mwenyezi
Mungu iwe juu yake) watu wake walipomtupia motoni kuokoka
kwake kulitoka kwa Mwenyezi Mungu: {Tukasema; "Ewe
moto! kuwa baridi na salama juu ya Ibrahim. (69) Na walimtaka
100
ubaya, lakini tukawafanya wao ndio wenye kupata hasara.} [AL
ANBIYAA 69-70].
Na huyu ni Yunus (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu
yake) alipomezwa na nyangumi basi alielekea kwa Mwenyezi
Mungu Mtukufu, na aliendelea kumtegemea Mwenyezi Mungu,
na ikawa rehema na uokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu, anasema: {Na (mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alioondoka
hali amechukia, na akadhani ya kwamba hatutamsaidia. Basi
(alipozongwa) aliita gizani (akasema): "Hakuna aabudiwaye
isipokuwa wewe, Mtakatifu, hakika mimi nilikuwa miongoni
mwa wenye kudhulumu (nafsi zao)" (87) Basi tukampokea na
tukamwokoa katika huzuni ile. Na hivyo ndivyo tuwaokoavyo
walioamini.} [AL ANBIYAA 87-88].
Na miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu
nasi kuwa anatuamrisha juu ya kutafuta njia, ama matokeo ya
kinachofanyiwa kai tuyarudishe kwake Mwenyezi Mungu
Mtukufu, basi kama tukifanya mema kwa kufuata njia
inayotakiwa na tukifanya mema katika kumtegemea Mwenyezi
Mungu Mtukufu atatufungulia milango ya rehema zake katika
dunia na Akhera. Imepokelewa na Omar Bin Al Khattab R.A.
kuwa yeye alimsikia Mtume S.A.W akisema: "Kama nyinyi
101
mtamtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea
atawaruzuku kama afanyavyo kwa ndege ambao huondoka
matumbo yao yakiwa matupu na hurejea yakiwa yamejaa."
[Imetolewa na Imamu Ahmad].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na anaye
mwogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu)
humtengenezea njia ya kuokoka (katika kila balaa). Na humpa
riziki kwa namna asiyoitazamia.} [AT TALAQ 2, 3]. Na
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {"Na anayemtegemea
Mwenyezi Mungu Yeye humtosha, kwa yakini Mwenyezi
Mungu anatimiza kusudio lake (lo lote alitakalo; hakuna wa
kumpinga). Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila
kitu kipimo chake.} [AT TALAQA 3].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na
anayemwogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu)
humafanyia mambo yake kuwa mepesi.} [AT TALAQA 4]. Na
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Je, Mwenyezi Mungu
hamfikii (hamtoshelezi) mja wake? Na wanakuogopesha kwa
aliye duni (masanamu; kuwa watakudhuru kama hutawaabudu,
wanaweza wapi kudhuru, ukiachana na kunufaisha!. Na
102
aliyehukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hana wa
kumuongoa.} [AZ ZUMAR 36].
Lakini matumaini bila ya kazi ni matumaini matupu, na
ni amani ya uongo yenye makosa. Na Bwana wetu Omar Bin Al
Khattab R.A anasema: "Asijibwetekee yeyote miongoni mwenu
na akaacha kutafuta riziki, na kisha anasema ewe Mola wangu,
niruzuku! na hakika ni kwamba mbingu hainyeeshi dhahabu na
wala fedha na wala haitoshi kufanya kazi tu, bali kazi ni lazima
iwe kamilifu na kwa ujasiri zaidi na ifanywe vizuri. Na kutoka
kwa Aisha R.A. amesema kwamba Mtume S.A.W. anasema:
"Hakika Mwenyezi Mungu anampenda yule ambaye afanyapo
kazi huifanya kwa ukamilifu." [Musnad Abi Yaaliy], na
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika wale walioamini
na kufanya vitendo vizuri (tautawalipa mema ya hayo). Hakika
sisi hatupotezi ujira wa wale wanaofanya vitendo vizuri.} [AL
KAHF 30].
Na Uislamu haukutoa wito wa kufanya kazi tu, bali kazi
lazima ifanyike vizuri na kwa kuikamilisha. Na kutoka kwa
Aisha R.A kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Kwamba
Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda yule ambaye afanyapo
103
kazi huifanya kwa ukamilifu." [Ilipokelewa na Al Baihaqiy
katika Al Shaab].
Na hivyo ni pamoja na udharura wa kumwogopa
Mwnyezi Mungu Mtukufu, kwa siri na wazi wazi, kwani ni
vigumu mno bali pengine ilikuwa jambo lililoepushwa au labda
ni muhali kwamba tutajaalia mlinzi kwa kila mwanadamu ili
amlinde, au mwangalizi ili amwangalie, na hata lau tuliyafanya
hayo, basi mlinzi pengine anahitaji mlinzi mwingine ili
amlinde, na mwangalizi anahitaji mwangalizi ili amwangalize,
lakini ni jambo jepesi kujenga malezi ya dhamira njema kwa
kila mwanadamu, dhamira iliyo hai inapumua haki na inatoa
msukumo wa kuelekea katika heri. Kwani dhamira hiyo
inalindwa na asiyepatwa na usingizi wala wala kulala.
Na kwa kukazia umuhimu wa kazi, Uislamu umetutolea
wito kuwa tufanye kazi hadi mwisho wa maisha yetu. Hata
kama hatutayapata matunda ya kazi hiyo. Na jambo hili
halikuwa isipokuwa kwa ajili ya kubainisha thamani ya kazi na
umuhimu wa uzalishaji kwa watu na mataifa. Na kutoka kwa
Anas Bin Malik R.A. anasema: Mtume S.A.W.
amesema;"Kama kikija Kiyama na katika mkono wa mmoja
104
wenu kuna mche basi akiweza kuupandikiza kabla ya kuja
Kiyama basi aupande." [Katika Al Adab Al Mufrad].
Kama ambavyo Quraani imetoa wito wa kufanya kazi, na
ikaifanya kazi hiyo kuwa katika kiwango cha ibada. Na
Mwenyezi Mungu Mtukufu ametutolea wito kwa ajili ya sala ya
siku ya Ijumaa -ibada hiyo tukufu- kwa amri, kisha
ametuelekeza kufanya kazi baada ya swala kwa amri iliyo sawa
na nyingine, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
{Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala ya siku ya
Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni
biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua hivi, basi
fanyeni!" (9) Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika ardhi
mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni
Mwenyezi Mungu kwa wingi (ili msipate kufanya mabaya), ili
mpate kufaulu.} [AL JUMUA 9-10]
Na Bwana wetu Iraak Bin Malik R.A alikuwa pindi
anapomaliza kuswali sala ya siku ya Ijumaa huondoka na
akasimama katila mlango wa msikiti kisha akasema: Mola
wangu! Mimi niliuitikia wito wako na nikaswali faradhi yako,
na nikaondoka kama ulivyoniumuru, basi niruzuku fadhila zako,
na wewe ndio mbora wa kuruzuku. [Tafsiri ya Ibn Katheer]. Na
105
kwa kuwa Uislamu unatoa wito wa kufanya kazi na uzalishaji
basi pia unapinga -na kwa nguvu- ukosefu wa ajira, uzembe na
kuombaomba, kwani hayo ni miongoni mwa sababu ya
kuchelewa kwa taifa na uharibifu wa watu, na Mtume S.A.W.
alikuwa akijikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na
kushindwa na uzembe. Na kutoka kwa Anas Bin Malik R.A.
akasema: Mtume S.A.W. alikuwa akisema: "Mola wangu!
Najikinga kwako kutokana na kushindwa na uzembe, woga,
uzee na ubahili, na najikinga kwako kutokana na adhabu ya
kaburini, na fitina za uhai na umauti." [Muslim akaitoa].
Kwa hivyo Mtume S.A.W alikuwa akiwavutia watu
katika kufanya kazi, na alikuwa akikataza ukosefu wa ajira na
uzembe. Na kutoka kwa Abi Huraira R.A. anasema: Mtume
S.A.W. anasema: "Kwani kuwa mtu mmoja miongoni mwenu
anakata kuni, na kuubeba mzigo wa kuni juu ya mgongo wake
ni bora zaidi kuliko kuwa anaombaomba, anaweza kupewa au
asipewe." [Al Bukhariy aliitoa]. Na kutoka kwa Ibn Omar R.A.
kwa wote wawili, alisema: Mtume S.A.W. aliulizwa juu ya
chumo zuri zaidi kuliko yote, basi akasema: "Kazi ya
mwanamume kwa mikono yake, na kila uuzaji bora."
106
[Imetolewa na Imamu Ahmad katika Musnadi yake na Al
Ttabaraniy katika Al Muajam Al Kabeer].
Na kutoka kwa Al Meqdaam R.A. kutoka kwa Mtume
S.A.W. anasema: "Hakuna Mtu yeyote aliyekula chakula kizuri
zaidi isipokuwa anapokula chakula kutokana kazi ya mkono
wake, na kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Dawud (amani ya
Mwenyezi Mungu iwe juu yake) alikuwa akila kutokana na kazi
ya mkono wake." [Al Bukhariy aliitoa]. Na kutoka kwa Abi
Huraira R.A alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Hakika kuna
madhambi miongoni mwa madhambi yasiyofutwa na sala wala
kufunga (saumu), wala Hija na wala Umra." Wakasema basi ni
yepi yanayoyafuta ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?
Akasema: " Shime ya kutafuta maisha." [Al Ttabaraniy aliitoa].
Na kutoka kwa Abi Huraira R.A., kutoka kwa Mtume
S.A.W anasema: "Mwenye kumkimbilia mjane na masikini ni
kama mpiganaji wa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu -na
nilidhani kuwa alisema: na kama vile mwenye kusali sala bila
ya kupumzika, na kama vile mfungaji hafuturu." [Inaafikiana
juu yake].
Na hayakuwa hayo yote ila kwa sababu ya kutilia mkazo
umuhimu wa kazi na uzalishaji. Na kwamba nchi yoyote haina
107
kauli na wala utashi isipokuwa kwa watu wake wote kufanya
kazi ili kuiendeleza na kuistawisha. Na ili iweza kuzalisha
chakula chake, vinywaji chake, mavazi yake, dawa zake, silaha
zake na misingi yote ya maisha yake. Na haya yote
hayawezekani isipokuwa kwa elimu, kazi na mikakati mizuri.
Nayo ndio tutakayoyazungumzia kwa kirefu katika hotuba yetu
ijayo kama Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda.
Uzuri, Furaha na Hisia Njema
Uisilamu ni dini ya ustaarabu na upendo, dini ya furaha na
maelezo yake na njia zake zote zinathibitisha hili na hata kurani
tukufu na hadithi za mtume (rehma na amani zimshukie juu
yake) pia zinathibitisha hili. Mwenyezi Mungu anasema katika
kurani { Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa
vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.
6. Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na
mnapo- wapeleka malishoni asubuhi.}
108
Na anasema pia { Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko,
na akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni kutoka
mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za
mimema.} na kuendelea kusema { na tukaiotesha mimea mizuri
ya kila namna.} {, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni,
na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi
hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja
na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.} na
kusema pia {17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo
umbwa?18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?19. Na milima jinsi
ilivyo thibitishwa?20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} na
anasema pia { Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi
wa Rehema.}ama kuhusu mbingu zilizo juu anasema { na
tumezipamba kwa wenye kuangalia.} { Na kwa hakika
tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa,}
Kurani tukufu imetuamrisha kujipamba kwa mapambo mazuri
na tuchukue mapambo yetu kila tuendapo misikitini (tusalipo).
Mwenyezi Mungu anasema { Enyi wanaadamu! Chukueni
pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na
kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye
hapendi wanao fanya israfu 32. Sema: Ni nani aliye harimisha
109
pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo
vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai
wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna
hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.} Na Mtume (rehma
na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ haingii peponi mtu
mwenye chembe ndogo ya kiburi (dharau). Mtu mmoja
akasema: “kuna mtu hupendelea nguo yake iwe nzuri na viatu
vizuri.” Mtume akasema: “ Mwenyezi Mungu ni mzuri hupenda
uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.” (muslim). Na
sayidna Mughira bin Shuuba (Mungu awie radhi) alipomueleza
kuwa yeye amemchumbia mwanamke, mtume (rehma na amani
zimshukie juu yake) akamwambia: “mwangalie kwani
itapelekea kudumu kati yenu.” (Tirmidhiy).
Mtume (rehma na amani zimshukie alikuwa kipenda uzuri, na
alilingania pia uso wa bashasha akasema: “jambo jema lolote
usilidharau hata kama utakutana na mwenzio basi iwe kwa uso
wa bashasha.” (Muslim). Na kusema kuwa kuingiza furaha kwa
watu ni kitu kimuwekacho mtu karibu na Mwenyezi Mungu
akasema: “ mwenye kuingiza furaha katika nyoyo ya muisilamu
basi ni haki ya Mwenyezi Mungu kumridhisha siku ya kiyama.”
Na akasema “ amali zipendwazo sana na Mwenyezi Mungu ni
110
furaha uiingizayo kwa muisilamu.” Na akawataka masahaba
zake kuvaa nguo nzuri wakati wanapokutana na katika sherehe
na minasaba
Pamoja na kuwa uzuri wa kweli haupo katika mandhari ya
muonekano na uzuri wa vitu lakini unavuka mipaka zaidi nao ni
uzuri tabia na mwuonekano. Mustafa Saadiq Rafii (Mungu
amrehemu) anasema: “ mwanamke mbora ni yule mwenye sura
nzuri kama tabia zake na akili yake ikawa uzuri wake wa tatu.
Mwanamke huyu akiwa na mwanamke mwenye kuendana nae
basi atamfurahisha na kumfurahisha na kumfurahisha. Mshairi
anasema
Mtu iwapo hajalaumiwa kwa heshima yake
Basi nguo yoyote aivaayo huwa nzuri
Tunaelewa kuwa kidogo huwa ni kingi
Nikasema kuwa ukarimu huona kidogo
Sikudhurika kwa kidogo na jirani yetu
aliye mwema ni mwenye nguvu
na jirani mwenye wengi ni dhalili
Inatulazimu sote kujipamba kwa tabia za kiisilamu katika
muonekano wetu, mazingira yetu, mashule yetu, vhuo vyetu,
111
bustanini mwetu, matembezini mwetu na katika sehemu zote.
Na wala tusifanye yenye kuondosha furaha na ucheshi.
Na katika alama kubwa sana za ucheshi na ziletazo furaha ni
neno zuri lililo jema, sayidna Umar bin Khatab (Mungu amwie
radhi) alipita kwa watu waliokuwa wakiota moto akachukia
kuwasalimia kwa kusema “amani iwe juu yenu enyi watu wa
motoni” isipokuwa akasema” amani iwe kwenu enyi watu wa
kivulini”. Na kama ulivyotulingania uisilamu kuwa tuchague
majina yenye maana nzuri na kujiepusha na majina mabaya
yasiyoendana na hisia za kiutu, kwani kurani imetuamrisha
kufanya kila lililo zuri na jema na kusema kila lililo jema.
Mwenyezi Mungu anasema { nasemeni na watu kwa wema,}
Albaqara 83. Na akasema { Waambie waja wangu waseme
maneno mazuri,} Israa 53. Basi kauli mbiu yetu ni “hisia njema
na uzuri”. Hisia nzuri ni kigezo cha kujua uzuri na kuueneza
kwa waliotuzunguka katika wanajamii.
112
Rafiki Tumtafutaye
Rafiki tumtafutaye ni yule aliyesema Mustafa Sadik Al rafiy
(Mungu amrehemu): ni yule anapokuwa hayupo husemi kuwa
Fulani hayupo bali unasema kuwa sehemu katika wewe haipo,
sehemu katika wewe, si rafiki akupakae mafuta kwa mgongo wa
chupa na kukuhadaa kama anavyohadaa fisi au kudonoa kama
anavyodonoa kalunguyeye (aina ya mnyama mfano wa panya)
na marafiki hawa huwapatikani isipokuwa pale tatizo
linapokuwa limeshamalizika nao ni kama inzi hawaonekani
isipokuwa pale penye asali.
113
Rafiki wa kweli tumtafutaye ni kama alivyosema Imam Shafi
(Mungu amrehemu) :
Rafiki wa kweli ni Yule anaekuwa nawe
Na kuidhuru nafsi yake kwa ajili yako
Ambaye wako unapokuwa mgumu hukusaidia
Na hujikimu nasfi yake ili akuunge.
Na siyo kama alivyosema kadhi Abu-Surur:
Mbona uko hivyo nami nilikuona kuwa ni rafiki,
wakati ukanitenganisha na kwa haki zote,
Nilikuwa ninakuhesabu kuwepo katika tabu zangu ,
hata kama wakati utanitafuna kwa dhiki,
Ulipata habari kama wakati ulinikaba,
ukabakia wewe kunipigia makofi,
Na ulipofahamu yakini kuwa mimi,
nimepata nafasi kubwa,
Ukanijia na kunipongeza kwa furaha,
unashangaza sana mambo yako ya kuvunja undugu,
Hakika upendo sehemu yake ni moyoni,
114
lakini ukweli wake huonekana pale penye matatizo
Mmoja wao aliulizwa: “ ni nani rafiki yako? Akasema:
“simjui” akaulizwa: “kwa nini” akasema: “kwa kuwa dunia
imenigeukia na itakapogeuka upande mwengine nitamfahamu
nani rafiki yangu kwani watu wengi huzunguka na dunia kila
iendapo, ukiwa nao basi wapo nawe na ukiwa mbali nao huwa
kinyume nawe. Na ndio maana wakasema: rafiki wa kweli
hujulikana wakati wa shida. Na mshairi akasema:
Mweneyzi Mungu ayalipe matatizo heri zote,
kwani kupitia hayo nimeelewa rafiki yangu na adui yangu
Na mwengine akasema:
Nimewaona watu wameenda,
kwa wenye dhahabu.
Na kwa wasio na dhahabu,
wakawa wananyenyekea kwa wenye fedha.
Nimeeona watu wameenda,
kwa wenye fedha kuelekea.
115
Na kwa asiye na fedha ,
wakawa wananyenyekea kwa wenye fedha.
Nimeona watu wamemili,
kwa wenye mali .
Na kwa wasio na mali ,
wakawa wananyenyekea kwa wenye mali .
Na mwengine akasema:
Tajiri husalimiwa kwa salamu ,
na bakhili hunyimwa salamu .
Kwani mauti kwao si mamoja tu ,
pindi wakifa na wakiwa makaburini?
Neno rafiki ni mnyumbuliko wa neno Sidqi (Ukweli) nalo
lina ujumbe wa anayekuamini katika hali ya siri na dhahiri na
katika hali ya raha na tabu katika uchangamfu na
unyongonyevu, anayekupendelea kile akipendacho nafsi yake
na kukichukia kwako kile akichukiacho katika nafsi yake.
116
Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) anasema: “
hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee mwenzake kile
anachokipenda katika nafsi yake.” (Bukhari). Na anasema
(rehma na amani zimshukie): “ mambo matatu mwenye kuwa
nayo basi atapata utamu wa imani; awe Mwenyezi Mungu
na Mtume wake anawapenda kuliko wengine wasiokuwa
hao. Na ampende mtu asimpendee kwa chochote isipokuwa
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na achukie kurudi katika
ukafiri kama anavyochukia kutumbukizwa motoni.”
(Bukhari) na pia anasema (rehma na amani zimshukie):” watu
saba Mwenyezi Mungu atawafunika kwa kivuli chake siku
isiyokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake; kiongozi
muadilifu, Kijana aliyeishi katika kumuabudu Mwenyezi
Mungu. Na mtu moyo wake umefungamana na misikiti. Na
watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
wanakutana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuagana kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kijana aliyeitwa na
mwanamke mwenye cheo na uzuri (kwa ajili ya kufanya
maovu) akasema (kijana) “Mimi ninamuogopa Mwenyezi
Mungu.” Na kijana anaetoa sadaka akaificha mpaka mkono
wake wa kushoto ukawa haujui kinachotolewa katika
117
mkono wa kulia. Na kijana anaemtaja Mwenyezi Mungu
hali ya kuwa yu pekee mpaka akatokwa na machozi.”
(Bukharin a Muslim).
Na imepokuwa kuwa kuna mzee mmoja alimtembelea
mwenzake katika kijiji chengine Mwenyezi Mungu akamwekea
katika njia yake malaika, alipomfikia akamwambia:
“unakwenda wapi?” akasema “kwa ndugu yangu aliye katika
kijiji hiki.” Akasema: je unaneema yoyote unayoitaka kutoka
kwake? Akasema: “ hapana, isipokuwa mimi nimempenda kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu. Akasema: “hakika mimi ni
mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwako na hakika ya
Mwenyezi Mungu anakupenda kama unavyompenda ndugu
yako kwa ajili yake (Mwenyezi Mungu).” (Muslim). Nakatika
hadithi Kudsiy, “mapenzi yangu yamewajibika kwa
wapendanao kwa ajili yangu, na wakaao pamoja kwa ajili
yangu, na wenye kutembeleana kwa ajili yangu.” (Ahmad).
Na mtume wetu (rehma na amani zimshukie): “wapendanao
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wana mimbari za nuru siku
ya kiyama wanapendwa na mashahidi.” (kitabu cha
Mustadrik). Hivyo, ni uzuri ulioje kuwepo kwa mahusiano na
urafiki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, uhusiano
118
utakayokuwa na upendo na utu na athari iliyojengekwa kwa
maadili na tabia njema, mbali na aina yoyote ua ubinafsi na
masilahi na kujinufaisha kimasilahi.
Haki ya Mwanamke Katika Kurithi na
Maisha Mazuri
Kadhia ya urithi ni moja kati ya kadhia kubwa sana amabazo
mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) ameisisitiza
katika hotuba yake ya kuagana aliposema: “hakika Mwenyezi
mungu amempa kila mweye haki amempa haki yake, tambueni
kuwa hakuna wasia kwa anaerithi.” (Ibn Majah). Naye
Mwenyezi Mungu ameweka wazi mafungu ya wanaorithi na
suala hili hakumuachia yeyote katika viumbe vyake, akasema
{11. Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu:Fungu
la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.Na ikiwa
wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za
119
alichokiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja,
basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja
wao apate sudusi ya alichokiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa
hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi
wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao
ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya
kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu,
nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa
manufaa. Hiyo ni Sharia iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila
ya shaka Mwenyezi Munguni Mjuzi na Mwenye hikima.}.
Na haikuishia hapo kutaja mafungu tu, lakini pia kurani tukufu
imetaja na adhabu kali mno kwa kila atakaefanya dhuluma
katika haki hizi, akasema Mwenyezi Mungu mtukufu, {13.
Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi
Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo
mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu
kukubwa.
14. Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na
akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni
adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.}. Na
ikawakemea watu majahili kwa kule kula kwao mali za baadhi
120
ya warithi bila ya haki, akasema {Sivyo hivyo! Bali nyinyi
hamuwakirimu mayatima, 18. Wala hamhimizani kulisha
masikini; 19. Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, 20. Na
mnapenda mali pendo la kupita kiasi. 21. Sivyo hivyo! Itakapo
vunjwa ardhi vipande vipande, 22. Na akaja Mola wako Mlezi
na Malaika safu safu, 23. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo,
siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa
nini? 24. Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!
26. Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. 25. Basi siku
hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.}. Na mtume
wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “mwenye
kukata mirathi ambayo mwenyezi Mungu na Mtume wake
wamefaradhisha, basi Mwenyezi Mungu atamkatia urithi wake
peponi.”
Na inasimuliwa kuwa kuna mtu alimnyima mtoto wake wa kike
mirathi, akangoja hadi muda wa kufariki (kwa mzazi wake) na
kukutana na Mola wake, alipoingizwa sehemu ya kuoshwa
(naye mtoto wa kike) akaingia, akawa anamwangalia na
kusema: “ewe Mola wangu hakika unaelewa kuwa ameninyima
baadhi ya neema za dunia name nakuomba umnyime neema za
akhera.”
121
Kasha kitendo cha kuwanyima wanawake urithi huenda ikawa
kinasababishwa na tabia ovu au tamaduni na mila zilizopitwa na
wakati ambazo hazina asili yoyote katika sheria, na kama
kwamba Yule anayemnyima mwengine na kumpa mwengine
anadhani ya kuwa amefanya jambo la masilahi kwa
anayestahiki na kwa siye stahiki kwa Mola wa viumbe vyote,
muumbaji wa kila kitu na Mbora wa mahakimu, na kama
kwamba (anayegawa mirathi kwa dhuluma) anasema ndani ya
moyo wake: “mgao wa Mwenyezi Mungu haunipendezi” au
“mimi nitagawa vizuri zaidi kuliko hata Mwenyezi Mungu” –
Mungu atuepushe mbali- kwani angelikuwa ni muumini wa
kweli na kuamini kuwa mgao wa mwenyezi Mungu ni bora na
wa haki basi mtu huyu asingelifadhilisha mwengine na
kumuacha mwengine.
Ama kuhusu mwanamke kwa ujumla sawa awe ni dada,mke,
mtoto wa kike au yeyote, ieleweke kuwa dini yetu imekataza
kuwadhulumu na kupunja haki zao, bali ikasema kuwa uadilifu
kwao na kwa watoto wa kiume ni njia nzuri ya kupata radhi za
Mwenyezi Mungu na kupata pepo yake, mtume (rehma na
amani zimshukie juu yake) anasema: “Yeyote atakaekuwa na
mwanamke na akawa hajamzika akiwa haina wla
122
hakumdhulumu ْ na wala mzazi wake hakumpendelea zaidi ya
mwengine (kamfanyia usawa) basi Mwenyezi Mungu
atamuingiza peponi.” Na katika hadithi hii kuna maana kubwa
na ufasaha wa hali ya juu kabisa kwani mtume amesema
“yeyote” ambayo inamaanisha mjumuiko na pia akasema
“mwanamke” na wala hakusema “mtoto wa kike” kwa sababu
mwanamke inakusanya jinsia ya kike sawa awe mtoto,
dada,mtoto wa kike n.k.
Na mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameusia
kuwakirimu na kuwatendea wema wanawake katika nyanya
zote, kwani katika hadithi kudisiy ambayo imepokewa na
mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) kutoka kwa Mola
mtukufu anasema: “Niridhisheni kupitia madhaifu wawili,
mwanamke na yatima.” Na mtume (rehma na amani zimshukie
juu yake anasema: “mwenye kuwa na watoto wa kike watatu,
akawa na subira kwao, akawalisha, na kuwavisha kwa kipato
chake, basi hao watakuwa kwake ni kinga ya moto siku ya
kiama.” Na katika mapokezi mengine, mwenye kuwa na watoto
wakike wawili au ndugu wa kike wawili. Na katika mapokezi
mengine pia inasisitiza hata kama atakuwa na mtoto wa kike
mmoja tu akamfundisha na kumpa malezi mema atakuwa
123
kwake ni kinga ya moto siku ya kiama. Na alipokuwa mzee
mmoja amekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie
juu yake) akaja mtoto wake wa kiume,akamchukua na kumbusu
na kumuweka mapajani mwake, kasha baadae akaja mtoto wake
wa kike akamchukua na kumuweka ubavuni mwake, mtume
(rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ unaonaje lau
kama ungeliwafanyia uadilifu”. Hapa anakusudia kama
ulivyomuweka mtoto wa kiume mapajani ilibidi pia ufanye
hivyo hivyo kwa mtoto wa kike kwa kumuweka kwenye paja
jengine.
Ingawa kwa wakati tulionao tunaona aina tafauti za
utenganishaji usiohitajika, ndani ya nyumba moja ya familia
kwa baadhi ya watu, mtoto wa kiume huwa ni bora kuliko wa
kike, na katika sekta ya elimu hushughulikiwa zaidi wavulana
kuliko wasichana, kwenye mirathi –ambayo tunatoa tolea lake-
ima atakuwa hapewi kabisa au atapewa lakini kwa kuridhisha tu
(na si kama haki yake), nalo ni jambo lisilokubalika hata kidogo
hiyo ni aina ya kumkandamiza na kutumia mabavu au
unyanyasaji. Ita utakavyo isipokuwa kinachohitajika ni mirathi
ya haki kwa ajili ya kumfuata sheria ya uadilifu wa Mwenyezi
124
Mungu na kwa ugawaji kama ambavyo sheria, haki, uadilifu
inavyotaka.
Ujeuri na Mwisho Mbaya
Ujeuri na mwisho mbaya ni mambo mawili yaondayo
sambamba wala hayatengani. Mwenyezi Mungu Mtukufu
anasema :{ Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe.
Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni
kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.}
(Yunus; 23). Na anasema pia {Ama kina A'di walijivuna
katika nchi bila ya haki , na wakasema: Nani aliye kuwa na
125
nguvu kushinda sisi ? Kwani wao hawakuona kwamba
Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu
kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!.
16 Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika sikuza
ukorofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwa hizi katika uhai wa
duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina
ukali(khezyy) zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.}
(Fussilat; 15-16). Na anaendelea kusema { Walipo
jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni
manyani wa kudharauliwa } (Al aaraf; 166). Na wasomi
wameeleza kuwa Mwenyezi Mungu huunusuru umma ulio
na uadilifu hata kama ni wa kikafiri na wala haunusuru
umma ulio na dhuluma hata kama ni waumini.
Ujeuri unaweza kuwa ni kwa mtu au kwa kundi nalo ni lile
liitwalo “kundi la kijeuri” na inaweza pia kuwa ujeuri kwa
taifa. Ama kuhusu mtu au kikundi au makundi
yatakayofanya ujeuri na kuvuka mipaka ya haki basi
mwenyezi Mungu hatowaacha anatashika na kuwapa
malipo wanayostahiki, kwani anasema: { Na ndio kama
hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata
126
miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni
mchungu na mkali.} (Hud;102).
Na anasema Mwenyezi Mungu kuhusu Qaruni, {Hakika
Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia
dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo zake
zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo
mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi
Mungu hawapendi wanao jigamba. 77. Na utafute, kwa
aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala
usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama
Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala
usitafute kufanya ufisadi katika ardhi.Hakika Mwenyezi
Mungu hawapendi mafisadi. 78. Akasema: Kwa hakika
nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo. Je!
Hakujua kwamba Mwenyezi Mungu kesha waangamiza,
katika vizazi vya walio kabla yake, watu walio kuwa wenye
nguvu zaidi kuliko yeye,na wenye makundi makubwa zaidi
kuliko yake. Na wakosefu hawataulizwa khabari ya dhambi
zao. 79. Basi akawatokea watu wake katika pambo
lake.Wakasema wale walio kuwa wanataka maisha ya
duniani:Laiti tungeli kuwa tunayo kama aliyo pewa Qaruni!
127
Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa. 80. Na wakasema
wale walio pewa ilimu: Ole wenu!Malipo ya Mwenyezi
Mungu ni bora kwa mwenye kuamini naakatenda mema.
Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye subira. 81. Basi
tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala
halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi
Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojitetea.}(Al
qasas; 76-81)
Na kuhusu kisa cha nabii Saleh pamoja na watu wake,
Mwenyezi Mungu anasema {Na wakamuuwa yule ngamia,
na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe
Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa
Mitume. 78. Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na
kulipokucha wakawa majumbani mwao kifudifudi
wamekwishakufa.} (Alaaraf; 77-79).
Ama kuhusu kisa cha nabii Shuib (rehema na amani
zimshukie) pamoja na watu wake Mwenyezi Mungu
anasema {95. Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia
walivyoangamia watu wa Madyana, kama walivyo angamia
watu waThamud!Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa
128
Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa rehema
yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na
wakapamba ukiwa majumbani mwao wamekufa
kifudifudi!} (Hud; 94-95)
Na Mtume wetu (Rehma na amani zimshukie) “Mwenyezi
Mungu humpa muda dhalimu mpaka anapoamua
kumchukua basi hapo hatowezatoroka.” Dhuluma ni kiza
siku ya kiyama, na vitimbwi havirudi isipokuwa kwa
wenyewe.
Hivyo basi, ninasisitiza zaidi kuwa mwisho wa taifa lenye
dhuluma ni kutoweka, na amesema kweli mashairi Hafidh
Ibrahim aliposema katika ushairi wake mzuri:
Misri inajieleza wenyewe.
Nchi ngapi zimenifanyia ujeuri
Kisha zikatoweka, kwani huo ndio mwisho
wake
Na hakuna aliyenilenga kisha akawa salama
Mwenyezi Mungu amelihifadhi jeshi lake tokea zamani.
Nchi itendayo dhuluma na mataifa yaliyojijenga kidhuluma
zinajiwekea sababu za kuporomoka na kuanguka kwa
haraka sana.
129
Na makundi ambayo yanayofanya utumiaji wa mabavu,
dhuluma, ujeuri na kuvuka mipaka katika kutenda maovu
kwa mfano wa yale makundi yanayotelekeza mauaji ya
kujitolea muhanga na kungamiza, na kurikodi namna
wanavyowachinja watu na kuunguza mwili wake. Pamoja
na kudhalilisha watu, na kuuza wanawake kama ni mateka
wa kivita, kubomoa tamaduni na majengo na kuangamiza
kila kilicho na roho na kisicho na roho, hao wanajibebesha
sababu za kuanguka kwao na kuangamia, kwani Mwenyezi
Mungu hapendi uharibifu wala wenye kufanya uharibifu.
Na kwa ajili hiyo mimi ninatoa bishara ya kuwa kuangamia
kwa kundi la wapiganaji wa dola la kiisilamu na makundi
mengine ya Alqaida na maadui wa nyumba tukufu ya
Qudsi, boko haramu na makundi mengineyo ya kikatili -
kuangamia – kwao kupo karibuni, {NaMwenyezi Mungu
ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu
wengi hawajui.} (Yusuf; 21)
130
Misri ni Nchi Kubwa Kwa Maadili Yake
na Ustaarabu Wake Hakuna shaka kuwa Misri ni nchi kuwa kwa uongozi
wake, wasomi wake, wanaume wake, wanawake wake,
wavulana wake, wasichana wake, historia yake, ustaaarabu
wake, nafasi yake ya uongozi katika eneo la mashariki ya kati
kimawazo, kielimu, kitamaduni kijeshi na kiutu. Na pengine
kitu kinachofanya kuonekana kuwa ni nchi kubwa ni masafa
yake makubwa na uwezo wake wa mkubwa na msamaha ulip
131
nao na kuachana na mambo madogo madogo na yasiyo na
uhumimu kwani hutaamali kiakili. Wapo wasemao:
Mjinga hunikabili kwa kila njia * nami nachukia kumjibu
Ujinga wake ukizidi nami hekima zangu huzidi * kam ujiti
wa udi unapo kila unapounguzwa ndio huzidi kutoa harufu
nzuri
Lakini kuna tafauti kubwa kati ya upole na nguvu, na kati
ya udhaifu na unyenyekevu . Misri ina upole na wala si dhaifu,
ni kaka mkubwa kwa anaetaka mafanikio na iko tayari kusaidia
kwa kila anachomiliki bila ya kutenganisha familia na kuvunja
udugu na haiku tayari kumuacha mkono wakati wa shida hata
kwa Yule aliyemfanyia ubaya katika ndugu zake.
Na iwapo hii ndio hali ya kaka mkubwa juu ya ndugu zake,
basi Misri itabakia kuwa ni kiongozi na haitoachana kutaamali
na matukio ya taifa lake na wakati huohuo haitojiingiza katika
matatizo ambayo yatafanya makundi hasimu kuwemo katika
machafuko zaidi yenye mwisho mbaya.
Misri kwa kipindi chote cha historia yake kubwa na
iliyojaa utu na maadili, watu wake hawakuelewa khiyana na
uvunjaji ahadi, na wala kumfanyia mwengine uadui bila ya
haki, isipokuwa ilisimama wima kwa ndugu zake na marafiki
132
zake na kipindi chote cha historia ilijulikana kwa ujirani
mwema, na usamehevu wa watu wake na ujirani mwema na
upole wa roho zao, haikuwa ukifahamu matumizi ya nguvu na
wala itikadi kali. Ama yanayojiri katika matumizi ya nguvu
haya ni matukio ya kupita na ni mageni ambayo jamii ya kimisri
katu hawajayashuhudia na ni kama mawingu tu ambayo
mwisho wake yatatoweka.
Misri imechukua ustaarabu wa nchi nyingi, na ikafaidika
kwa ustaarabu huo sana, na kupitia msamaha wa Al zhar na
usawa wake unaojulikana kwa mujibu wa historia ambayo
imelea kwa kipindi cha maelfu ya miaka imekuwa ni moja ya
dhamana ya usamehevu na usawa huu, si Misri pekee na wala si
katika ulimwengu wa kiarabu pekee na wala si katika
ulimwengu wa kiisilamu pekee lakini ni kwa ulimwengu wote
kwa ujumla.
Na kwa hili nimeandika beti zifuatazo:
Misri tukufu iliyohifadhika
Kitabu kitukufu kimetaja amani yake
Na ikidhoofisha siku moja itapona haraka haraka
Na uisilamu utarudi hali ya kuenea
133
Na umma wa kiarabu utakuwa na nguvu zake
Atakaekuja kwa amani atapokewa
Na atakaekuja kwa vita basi sisi ndio wenyewe
Hatufanyi uadui na wala haturidhii khiyana
Nguzo yeu ni ujanadume
Moja ya mawili ndio tutakacho
Ushindi mkubwa au kuonekana mashahidi
Iulizeni historia kuhusu mashujaa wake
Na lieleweni jeshi la mtume
Jeshi bora ni jeshi la Misri, liheshimuni
Ardhi bora ni haki yake na ni cheo chake
Na Azhari yake ni ni yetu pia na ambayo
Imehifadhi elimu kwa karne
Ikawa inafundisha kila sehemu duniani
Usamehevu ni dini yetu na anuani yake
Msalieni aliyechaguliwa Ahmad
Kwani yeye ni mbora wa viumbe na ni kiongozi wao
134
Wizi wa Mali za Umma na Kuzifuja
Hapana shaka kuwa uisilamu umeweka uharamu wa mali
kama ulivyoweka uharamu wa kumwaga damu, pale Mtume
(rehma na amani zimshukie) aliposema katika hijja ya kuaga
akiwahutubia watu wote: “enyi watu hakika ya damu zenu na
mali zenu ni haramu kwenu kama ilivyokuwa ni haramu
siku yenu hii (siku ya Arafa) na katika mji wenu huu
(Makka mji wa Mwenyezi Mungu), ewe Mola wangu
shuhudia, tambueni, na aliyekuwepo amfikishie
135
asiyekuwepo. Na anasema: “mwili wowote uliojengeka kwa
haramu basi moto ni bora kwake.” Na pia anasema Mtume
(rehma na amani zimshukie): “ Hakika ya watu wenye
kulumbukiza mali za Mwenyezi Mungu bila ya haki
watakuwa na moto siku ya kiyama.” Na Mwenyezi Mungu
anasema. {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa
dhulma,isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.
Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kuwarehemuni.30. Na mwenye kutenda hayo kwa uadui na
udhaalimu,basi huyo tutamwingiza Motoni. Na hilo ni jepesi
kwa Mwenyezi Mungu.} (Anisaa, 29-30).
Na hapana shaka ya kuwa kuiba mali za umma na kuzitumia
vibaya ni katika makosa makubwa kuliko kutumia mali za mtu
binafsi. Kwa kuwa mali za umma zina haki nyingi ni mali ya
jamii kwa pande zote. Na atashtakiwa mbele ya Mwenyezi
Mungu siku ya kiyama kila mwenye kuzinyooshea mkono wake,
Mwenyezi Mungu anasema: { Na haiwezekani kwa Nabii
yeyote kufanya khiyana.Na atakaye fanya khiyana, atayaleta
Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu
atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala
hawatadhulumiwa.} (Al Imraan, 161).
136
Na wakati Abdallah bin Umar bin Al-Khatwab (Mwenyezi
Mungu awawie radhi) alipoingia kwa Ali bin Amir Al-
hadharamiy kumuangalia alipokuwa katika kitanda cha umauti
akasema Al-hadharamiy: “Tuombee Mwenyezi Mungu ewe
mtoto wa Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) akasema Ibn
Umar: “ hakika ya Mwenyezi Mungu haipokei swala bila ya
udhu (tohara) na wala sadaka kwa kujionesha mnawe ulikuwa
kiongozi nchini Basra na huenda ukawa umechanganya mali za
umma na mali zako kitu kitakachopelekea kubadilisha hali ya
maombi ya dua zako na kukubaliwa kwako hii iwapo kama
dhamira yako ilikuwa iko safi, na imeepukika na vijikasoro na
iko mbali na shaka au kutiliwa wasiwasi, na kwa namna hiyo
imesemwa,: wacha Mungu wameitwa wacha Mungu kwa sababu
wao huogopa vile ambavyo watu wengine hawaviogopi. Na
baadhi ya masahaba na wanaowafuata na wafuasi wao katika
wachaji Mungu walikuwa wakiacha baadhi ya vitu vya halali
kwa kuogopea isije ikawa ndani yake muda wasiwasi wa
kuwepo kitu cha haramu. Na Mtume wetu (rehma na amani
zimshukie) anasema: “ halali ipo wazi na haramu ipo wazi, na
katikati yake pana vitu vinavyoshabihiana, watu wengi
hawavielewi, na ajiepushae na vitu vyenye utata (shubuhati)
137
basi atakuwa ameilinda dini yake na heshima yake, na
atakaeingia katika vitu vyenye utata atakuwa ameingia katika
haramu, kwa mfano mchungaji anayechunga kandokando ya
mipaka, inaogopewa asije akaivuka, tambueni kila mmiliki ana
mipaka, eleweni mipaka ya Mwenyezi Mungu ni yale
aliyoyaharamisha. Na katika mwili kuna pande, pindi
likitengemea basi nao mwili wote hutengemea, na likiharibika
nao mwili mzima huharibika, tambueni pande hilo ni moyo.”
(Bukharin a Muslim)
Na pengine wengine wanaweza kudhani kuwa wizi wa mali za
umma unakusudiwa ni ule wa kuiba au ubadhirifu lakini ni zaidi
ya hapo, kwani kuacha kulipa kodi zenye kustahiki katika
wizara husika na taasisi husika nayo pia hujulikana kama ni wizi
wa mali za umma bali ni wizi uliokamilika vitendo kabisa.
Na tumetoa toleo la Wizara ya wakfu kubainisha kuwa wizi wa
huduma hauhitilafiani na wizi wa mali na kuzitumia vibaya.
Kwani uhalisi wa huduma ni mkusanyiko wa mali, aibaye
umeme, maji, au kuacha kulipa nauli ya garimoshi au metro na
vyengine, huwa sana na aibaye mali.
Na kama afanyae ujanja wa kutumia pesa bandia ili apate ruzuku
zake huyu nae ni mla haramu, kwani anachukua mali
138
asiyostahiki. Na iwapo sheria imeweka kiwango maalumu na
pato maalumu kwa mwezi kwa bidhaa za mgao unaotolewa na
serikali basi kila atowaye bidhaa hizi kwa kwenda kinyume na
shuruti itakuwa nae yumo makosani. Kwa kuwa atakuwa ametoa
kwa wasiostahiki na kuwaacha wenye kustahiki au kwa wale
wenye kuhitaji zaidi. Vilevile kwa upande wa makazi wenye
kufanya hila za kutaka kujinufaisha wao na kuhalifu shuruti
zilizowekwa.
Hawa na kila anayewasaidia watakuwa ni washirika katika
makosa au wakawa wanazembea katika kutaka kurekebisha
kasoro au wakawa wana nia ya kupata kitu chochote kutoka
katika mali za umma kupitia uzembe wanaoufanya.
Siku zote na tukumbuke maneno ya Mtume wetu (rehma na
amani zimshukie): “nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa
juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa
juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake
naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika
nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga,
mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye
ataulizwa juu ya alichokichunga.” (Bukhari). Na Mwenyezi
139
Mungu atauliza kila mchungaji kwa kile alichokichunga iwapo
amekihifadhi au amekipoteza.
Mazungumzo ya Ijumaa
Wizi wa Kielimu na Athari Zake Kwa
Taifa
Kila tendo lina jawabu lake lililo sawa, na pia lina jawabu la
kinyume, kushajiisha kufanyika kwa utafiti, uchunguzi na
ugunduzi wa kielimu na kuendelea nao kwa ajili ya mustakabali
wa kweli inahitajika kuwepo nguvu na kuchukua hatua
madhubuti za kuweza kupambana na wizi wa kielimu na mfano
wake. Na hasa katika Nyanja za mafunzo ya taaluma na utafiti
140
wa kielimu, kuwepo na adhabu kali kwa kila aibae matokeo ya
utafiti wa mwengine na izingatiwe kuwa ni moja kati ya makosa
yenye kuondosha heshima ambayo hayahitajiki kwa mtu
ambaye atapewa wadhifa wa uongozi kwani uongozi unahitaji
uaminifu na usafi na kuwa na tabia njema na heshima.
Na kujifunza kuwa muaminifu katika Nyanja za kielimu
inapaswa ianze mapema katika shule za msingi mpaka mwisho
wake na kuendelea katika Nyanja zote za kielimu.
Tukingalia uhalisi wetu tutafahamu kuwa baadhi ya sekta
ambazo hutoa elimu za ukamilisho kama zile zifunzazo malezi
na mafunzo ya mwisho kwa mfano, ukiongeza vyuo vitoavyo
vyeti vya sanaa huenda vikawa vinatoa mitihani isiyo kwenda
sambamba na hali halisi ya uwezo unaohitajika, jambo hili
inabidi lipelekee kuwepo kwa nidhamu ya ufatiliaji na
uchunguzi.
Tukikiri kuwa baadhi ya wahitimu wa diploma (uzamili) ya
sanaa hawawezi kusoma na kuandika kama ipasavyo na miaka
ambayo wamesoma tutaelewa kuwa ipo haja ya kubadili
mwenendo wa kitaaluma kwa namn ya utoaji wa mitihani na
upasishaji. Na kuhakikisha kuwa khifadhi nidhamu za kisayansi
na kielimu na utafiti na hasa nay ale yanayoshikamana na
141
mitihani na namna ya kuitathmini kwani nayo pia ni amana. Na
kukengeuka ni khiyana na kumpa kwa asiyestahiki na
asiyekuwa na uwezo wa kumiliki, kitu ambacho kunatoa
wanafunzi wasio na uwezo hali ya kubeba vyeti visivyokwenda
sambamba na ukweli wa elimu zao, na wala hawawezi kuingia
katika soko la la wafanyakazi. Na kupelekea vyuo vilivyotoa
vyeti hivi kukosa thamani yake na nafasi yake na ubora wake
ndani ya nchi na nje pia. Si hivyo tu, bali hata mwanafunzi
mwenyewe kukosa hisia za kujua thamani ya cheti ambacho
amekipata na thamani ya nafsi yake, na kukosa uwezo wa kuishi
kwa mujibu wa hali halisi.
Na iapo udanganyifu umekatazwa katika hali zote, kwani
mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema:
“adanganyae si katika sisi”. Udanganyifu katika fani ya elimu
na fikira ni haramu zaidi na huondoa heshima na utukufu wa
mtu.
Na japokuwa kuna aina mbaya sana za udanganyifu ambazo
wengi hawawezi kuzijua (kwa mfano) ile ya kuiba kazi za tafiti,
kwa kumtaka mmoja wa wanafunzi au rafiki yake kumuandika
jina lake katika kazi ya utafiti ambayo hakushiriki hata kidogo
na wala hakutumia juhudi yoyote, kitu ambacho ninaomba
142
ipatikane juhudi ya kumuhoji mtafiti kwa utafiti alioufanya kwa
njia ya mazugumzo ili tuhakikishe uwezo wake wa ufahamu.
Kwa ajili hiyo inapasa kwa pande zote husika zenye
mfungamano na fikira na elimu kuweka mipangilio ambayo
itafanyika bila ya kuiba elimu, au kumzuia asiye na uwezo
kupatia asichostahiki. Na ni lazima kutekelezwa sheria kwa
umakini na ukali kwa kila anayevunja sheria na nidhamu za
kielimu na kimalezi katika vyuo, na kuwepo na ufuatiliaji
unaoendelea kwa walimu na wengine. Ufuatiliaji uwe wa kweli
na sio wa kuzuga ili anayejitahidi aone matunda ya juhudi zake.
Na kwa siyejitahidi nae apate kujikaza kaztika juhudi na kuinua
kiwango chake au apewe kazi kwa mujibu wa uwezo wake, na
liwe hili waziwazi na si kwa ajili ya upendeleo wa aina yoyote.
Iwapo tunaamini thamani ya elimu kuwa ni njia pekee
itakayotuwezesha kuvuka na kuelekea katika usalama, basi njia
hii inapasa iwe ya ukweli na tuipe juhudi ya kweli inayostahiki
na kutaabika nayo, na kujikaza na kushikamana mabega hadi
tufikie katika manufaa yanayotarajiwa. Na tupate kigezo kizuri
kutokana nayo, na kuanzisha katika kila kituo cha elimu utafiti
au kuwepo na idara yenye kushughulikia suala la wizi wa
kielimu, ili tuelekee katika ulimwengu wa kielimu na taaluma,
143
na taifa letu na watu wake wapate kusimama katika ulimwengu
ambao nguzo kuu za maendeleo ni elimu na teknolojia na kujua
anga za nje na ili vita yetu kubwa iwe ni ya kifikra na elimu na
teknolojia vita ambayo mshindi wake ni Yule mwenye kumiliki
vyanzo madhubuti na endelevu.
Kwa kutilia mkazo kuwa uisilamu umeipa elimu thamani
Mwenyezi Mungu anasema {Je huwa sawa wanaojua na
wasiojua, hakika wenye kukumbuka ni wale wenye akili}. Na
mtume wetu (rehma na amani ziwe juu yake anasema: “wasomi
(maulamaa) ni warithi wa mitume, na hakika ya mitume
hawakurithiwa dinari wala dirhamu (mali) lakini wamerithiwa
elimu na atakaeichukua basi kachukua fungu kubwa.” Na
akasema (rehma na amani zimshukie): “mwenye kupita elimu
yenye kushikamana na elimu basi Mwenyezi Mungu
atamuwepesishia njia ya kwenda peponi.” Na neno “elimu”
limekuja bila ya kuhusishwa elimu Fulani bali elimu yoyote ile.
Ikiwa na maana kuwa makusudio ni ile faida ipatikanayo
kupitia elimu, na msomi wa kweli, na mwanafunzi mwenye
juhudi na sio kwa mwenye kubeba cheti cha uongo au
kilichopatikana kwa njia ya udanganyifu na kilichokosa ukweli
na heshima.
144
Wito Wa Kuwa na Matumaini
Uzuri ulioje wa kuwa na tama, na ubaya na hatari ilioje ya
kukata tama, kukata tamaa kuangamiza nafsi, na kuondosha
matarajio na huzalisha unyongevu na kutia simanzi. Kwa ajili
hiyo uisilamu umekataza kukata tamaa na kukatisha tamaa na
kujichangabya na kuchangaya na baadhi ya wasomi wakasema
hilo ni miongoni mwa madhambi makubwa.
Mwenyezi Mungu mtukufu anasema kwa ulimi wa Mtume
Yakubu (rehma na amana zimshukie juu yake: { Enyi wanangu!
Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye,wala msikate tamaa na
145
faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakikahawakati tamaa na faraji ya
Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri } na anasema
kupitia ulimi wa mtume Ibrahim (rehma na amani zimshukie
juu yake) { Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika!
Basikwa njia gani mnanibashiria? 55. Wakasema:
Tunakubashiria kwa haki; basi usiwemiongoni mwa wanao kata
tamaa. 56. Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema
yaMola wake Mlezi ila wale walio potea?
Na kutoka kwa Ibn Abass (radhi za Mwenyezi mungu
ziwashukie) amesema: Kijana mmoja alisema: “ ewe mjumbe
wa Mwenyezi Mungu, ni yepi madhambi makubwa? Akasema:
“ kumshirikisha mwenyezi Mungu na kutokuwa na matumaini
na upole wa Mweneyzi Mungu na kukata tamaa katika rehema
za Mwenyezi Mungu
Na tunamwambia mgonjwa hata kama ni maradhi ya
kudumu au ya vipindi kuwa usikate tamaa ya kutopona, na
kumbuka Mwenyezi Mungu alivyomponya mtume Ayubu
(rehma na amani ziwe juu yake) na akashikamana kwa
kumuomba mola wake na akamfanya kuwa ni kigezo pale
aliposema Mtukufu: { Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake
Mlezi, akasema:Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye
146
unaye rehemukuliko wote wanao rehemu. 84 Basi tukamwitikia,
na tukamwondolea madhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu
wake na mfano wao pamojanao kuwa ni rehema inayo toka
kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.}
Na iwapo ni tasa basi usisahau neema ya Mwenyezi Mungu
kwa mtume Zakariyya (rehma na amani zimshukie juu yake)
pamoja na umri wake mkubwa na utasa ambao hakutarajia
kupata mtoto, nah ii ni pale alipoita zakaria (rehma na amani
zimshukie juu yake) Mola wake “{Akasema: Mola wangu
Mlezi! Mafupa yanguyamedhoofika, na kichwa
kinameremeta kwa mvi; wala,Mola wangu Mlezi, sikuwa
mwenye bahati mbaya kwakukuomba Wewe 5. Na hakika
mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu.Na mke wangu
ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako. 6. Atakaye nirithi
mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub.Ewe Mola wangu Mlezi!
Na umjaalie awe mwenyekuridhisha.} na anasema Mwenyezi
Mungu mtukufu {89 Na Zakariya alipo mwita Mola wake
Mlezi: Molawangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe
ndiye Mborawa wanao rithi. .90 Basi tukamwitikia, na
tukampa Yahya natukamponyeshea mkewe. Hakika wao
147
walikuwa wepesi wakutenda mema, na wakituomba kwa
shauku na khofu. Naowalikuwa wakitunyenyekea.}
Na kikawaida kuwa mwanamke anapokuwa ni gumba ambae
hazai huwa anafanyiwa dawa kwanza ili azae. Lakini aya za
kurani hazikusema hivi isipokuwa mwenyezi Mungu anasema:
{ Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya natukamponyeshea
mkewe.} wamebashiriwa mtoto kwa kutibiwa mke, na kama
kwamba Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kumpa mtoto bila ya
sababu, sawa mke akitibiwa au hapana {hakika jambo lake
atakapo huwa anasema kuwa likawa}. Nayo ni kama
ilivyoelezwa katika kisa cha Nabii Ibrahimu (rehma na amani
zimshukie juu yake) wakati malaika walipombashiria mtoto
pamoja na kuwa alikuwa na umri mkubwa, Mweneyzi Mungu
anasema { Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka.
Basitukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-
haqYaaqub 72. Akasema: Je, hivyo mimi nizae, na hali
yangu nikikongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika
haya nimambo ya ajabu! 73. Wakasema: Je, unastaajabia
amri ya Mwenyezi Mungu?Rehema ya Mwenyezi Mungu na
baraka zake ziko juu yenu,enyi watu wa nyumba hii!
Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa kutukuzwa.}
148
Na mtu awapo katika tabu au maafa aelewa kuwa hazina
za Mwenyezi Mungu ni nyingi na wala hazishi, na masiku
huzunguka kati ya mazuri na mabaya, tajiri wa leo huenda
akawa masikini kesho, na masikini wa leo huenda akawa tajiri
kesho.
149
Huoni Kuwa Fakiri Hutaraji Utajiri
Na Tajiri Huogopea Ufakiri
Mwenyezi Mungu anasema {Na anaye mcha Mwenyezi Mungu
humtengezea njia ya kutokea. .3 Na humruzuku kwa jiha asiyo
tazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye
humtosha.} na anasema pia { Na anaye mcha MwenyeziMungu,
Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.} na
anaendelea kusema {Rehema ambayo Mwenyezi Mungu
anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana
wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu,
Mwenye hikima.}
Na kwa kuupokea mwaka mpya hapana budi tujiweke
kuwa na tamaa ya muda ujao ulio bora na wenye kuchomoza,
kwani ufunguzi wa Mwenyezi mungu upo karibu. Tusikate
tamaa wala kufadhaika na wala tusiwe wa kutarajia mabaya.
Kwani dui wetu huwa anataka tukate tamaa na kuvunjika moyo,
na kwa kuwa dini yetu haijatufundisha kukata tamaa na wala
haijui kuvunja moyo sisi ni umma wenye tamaa kubwa.
150
Mbingu yenye huzuni imesema kwa ubaya
Nikasema: tabasamu wacha ubaya uwepo juu
Ikasema: Nyusiku zimeniumiza
Nikasema: wewe tabasamu tu hata kama zimekuumiza
Kwani mwengine wakikuona upo sawa
Basi huzuni huweka kando na wao huwa sawa.