Transcript

2

YALIYOMO

Gazeti hili la Habari Ilala, ni gazeti la kila Mwezi

linalotolewa na Manispaa ya Ilala, Ambapo ndani

yake utaweza kusoma Habari mbalimbali na matukio

yaliyojiri Ndani ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha

mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa

Miradi ya kimaendeleo

TAHARIRI

UTANGULIZI

SEHEMU YA MAONESHO NDANI YA JENGO

HABARI KATIKA PICHA

MEYA AKABIDHI VIFAA VYA

CHIMBUKO LA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE

SEHEMU YA MAONESHO NJE YA JENGO

MASABURI AIBUKA KIDEDEA NAIBU MEYA

MANISPAA YA ILALA

3

UTANGULIZI

1

CHIMBUKO LA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE

Nane Nane ni sikukuu ya wakulima nchini Tanzania ambayo huwapa fursa wakulima, taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kote nchini kuonesha bidhaa zao na mafanikio yao katika mwaka husika.

Mwanzo, sikukuu hii ya Nane Nane iliitwa ‘Saba Saba’ ambapo ilikuwa ikiadhimishwa kila

tarehe 7 ya mwezi Julai. Baadaye ilihamishiwa Agosti, 8 ya kila mwaka baada ya Saba Saba

kufahamika zaidi kwa maonyesho ya wafanyabiashara.

Sikukuu ya maonyesho ya wakulima iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 ili

kuongezea nguvu sera ya Serikali ya wakati huo ya ‘ Siasa ni Kilimo ‘, ambapo wakulima

katika wilaya, mkoa na kitaifa walionesha mazao yao halisi ya kilimo, pembejeo za kisasa za

killimo pamoja na kufundishwa namna ya kutumia pembejeo hizo kwa ustawi wa kilimo na

taifa.

Jijini Dar es Salaam sikukuu hii ilitengewa eneo maalum katika barabara ya Kilwa ambapo

hutumika mpaka leo kwa maonyesho mbalimbali. Kadri miaka ilivyozidi kwenda mbele sera

ya ‘Siasa ni Kilimo’ ilibadilika na kuwa ‘ Siasa ya Kilimo’ na wengine wakiitafsiri kama

‘Kilimo cha Siasa’ kwasababu sikukuu hiyo ilionekana kujaa siasa zaidi huku watu

wakilenga kuitumia kibiashara zaidi kuliko malengo ya awali.

Ndipo katikati ya miaka ya 1990 serikali iliamua kuihamisha sikukuu hiyo Agosti nane kila

mwaka na kuiacha sikukuu ya Saba Saba kuwa ya wafanyabiashara.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kila mwaka hushiriki katika maonesho ya Wakulima

nane nane katika kanda ya Mashariki ambayo hufanyikia mkoani Morogoro katika Viwanja

vya Mwl. J. K. Nyerere kuanzia tarehe 1 – 8 Agosti kila mwaka ambapo hushiriki Halmas-

hauri zote kutoka mikoa ya Dar es Saaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

Katika mwaka 2019 Maonesho ya kilimo - Nanenane ambayo ni maonesho ya 26 yalibeba

Kaulimbiu “KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”

4

2

Maonesho haya yaliyofunguliwa rasmi tarehe 01/08/2019 na Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu na kufungwa rasmi tarehe 08/08/2019 na Mhe. Samia Suluh Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo banda la Maonesho la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala lilitembelewa na Makamu wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania .

Maonesho ya Nanenane katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala huratibiwa na kuandaliwa

na Idara mbili ambazo ni Idara ya Kilimo na Ushirika pamoja na Idara ya Mifugo na Uvuvi.

Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Bibi Esther Masomhe akitoa Maelekezo ya

Teknolojia ya Umwagiliaji kwa njia ya Matone kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu

wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu wakati

alipotembelea banda la Nanenane la Manispaa ya Ilala Mwaka 2019

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Bidhaa

mbalimbali katika banda la Nanenane la Ilala

5

3

Katika banda la maonesho ya Wakulima nane nane la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilikuwa na sehemu kuu mbili

katika maonesho hayo ambayo ni Sehemu ya maonesho ndani ya jengo na Sehemu ya maonesho nje ya jengo.

Sehemu ya maonesho ndani ya jengo

Sehemu hii ilikuwa na mazao/vipando vilivyoainisha maumbo mbalimbali ya kilimo cha mjini, bidhaa za usindikaji

wa mazao mbalimbali, teknolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone, mazao ya nyuki, zana za uvuvi, huduma za

mifugo, wauzaji wa madawa ya mifugo na kilimo, bidhaa za ngozi, vifaa bora vya ufugaji kuku, wajasiriamali wa

sabuni na wanachama wa SACCOS. Aidha Makala ya shughli za kilimo, mifugo na uvuvi ilioneshwa kwa njia ya TV

na pia majalida, vipeperushi mbalimbali vya kilimo, mifugo na uvuvi yalikuwepo.

Picha za maonesho ndani ya banda

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia

Mjema akiuliza jambo kwa Msindikaji

Bibi Christina Magesa wa Kata ya kiwalani

Baadhi ya wakuu wa Idara wakipata

maelekezo ya mazao ya baharini toka

kwa Bw. Said Mussa ambaye ni Mvuvi wa

kata ya Kivukoni

Mdau wa Usindikaji akiwa anatoa

maelekezo ya Bidhaa kwa baadhi ya

Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya

Ilala

Pichani katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.

Sophia Mjema na kulia kwake ni Mstahiki meya

Mhe.Omary Kumbilamoto wakipata maelekezo

ya ufugaji wa jamii ya Ndege Mapambo

6

4

Sehemu ya maonesho nje ya jengo

Sehemu hii ilikuwa na Utoaji wa huduma ya kwanza, Ramani ya vipando, Teknolojia ya kilimo bila udon-

go (HYDROPONIC SYSTEM), Kitalu nyumba cha kuhamishika (Movable green house), ufugaji bora wa

kuku na njiwa njiwa wa mapambo, utotoleshaji wa vifaranga vya samaki, utengenezaji wa chakula cha

samaki, ufugaji bora wa samaki katika mabwawa, ukaushaji wa samaki kwa njia ya moshi, usindikaji wa

mazao mbalimbali, mapishi ya unga wa mhogo, usindikaji wa maziwa, jokofu la asili, huduma ya vyakula

na vinywaji, kilimo cha mjini, maumbo mbalimbali kwa ajili ya kilimo cha mjini, vifaa vya umwagiliaji na

teknolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone, umwagiliaji kwa kutumia chupa, matumizi ya matandazo

kudhibiti upotevu wa unyevu katika udongo, uzalishaji wa malisho ya mifugo, kilimo cha uwiano, jaruba

la mpunga, kilimo cha uyoga, ufugaji bora wa kuku kuchi, ufugaji bora wa kuku chotara, ufugaji bora wa

kuku wa mayai, ufugaji bora wa kuku wa nyama , ufugaji bora wa kuku wa asili, ufugaji bora wa bata

maji, ufugaji bora wa mbuzi na ng’ombe wa maziwa, ufugaji bora wa kanga na sungura, usindikaji wa

ngozi, matumizi bora ya ardhi na udhibiti wa mmomonyoko wa udongo, vipando vya mazao mbalimbali

yakiwemo ya jamii ya mboga, matunda, nafaka, mizizi, viungo na mikunde.

Mstahiki Meya Mhe. Omary

Kumbilamoto akiwa katika banda la

usindikaji wa maziwa la kampuni ya

PROFETE kata ya Segerea

Kaimu Mkurugenzi Bi. Elizabeth

Thomasi akiwa katika mahojiano na

Television ya Taifa TBC

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi

Bw. Majaliwa Andrea akitoa maelezo ya

ufugaji wa samaki

Muoneshaji Bw. Mseti Gitido akiwa

katika banda la ufugaji wa kuku,

kutokea kata ya Mzinga

7

5

HABARI KATIKA PICHA

Maumbo mbalimbali ya Kilimo cha

ghorofani Kilimo cha Mabiringanya

Kilimo cha Magorofani Miche ya Matunda Iliyobebeshwa

Kilimo cha Nyanya

Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi

akionesha baadhi ya Majani ambayo ni

chakula lishe kwa mifugo

8

7

Bw. Edward Mboya akielezea teknolojia ya umwagiliaji kwa

njia ya matone {Drip Irrigation } akiwa na mkulima toka

kata ya Chanika Bw. Ambonisye Ambwene akielezea Teknolojia ya kilimo

bila udongo toka katika banda la Green fish kutokea kata

ya Kitunda kilichowezeshwa na Manispaa ya Ilala

Picha ya pamoja ya waoneshaji ambao ni wadau mbalimbali wa sekta ya Kilimo, Mifugo na uvuvi wakiwa

mbele ya Jengo la Nanenane la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mfugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Bw.

Ismail Kibona akitoa maelezo kwa

Wananchi

Afisa Kilimo Bibi. Sije Lebi akielezea

teknolojia ya kilimo cha Magorofani

kwa Wananchi

9

6

Halmashauri Iling’ara na kuchukua ushindi katika ushiriki wa maonesho ya kilimo – Nanenane kwa mwa-

ka 2019,ambapo iliweza kupata ushindi katika maeneo yafuatayo:-

Mshindi wa KWANZA kwa Manispaa za Kanda ya Mashariki na kukabidhiwa zawadi ya kombe

na cheti.

Mshindi wa TATU wa jumla kanda ya mashariki na kukabidhiwa zawadi ya kombe na cheti .

Kukabidhiwa cheti cha Ushiriki .

Mshindi mkulima bora ngazi ya Mkoa ndugu Ambonisye Ambwene mkulima wa mboga aina ya

Letuce kwa kutumia teknolojia ya kilimo bila udongo – HYDROPONIC kutoka Kata ya

Kitunda alikabidhiwa hundi ya Tshs 1,000,000 na cheti.

Mshindi mkulima bora ngazi ya Halmashauri ndugu Ambonisye Ambwene mkulima wa mboga

aina ya Letuce kwa kutumia teknolojia ya kilimo bila udongo – HYDROPONIC kutoka Ka-

ta ya kitunda alikabidhiwa hundi ya Tshs 500,000 na cheti.

Mshindi mfugaji bora ngazi ya Halmashauri ndugu Karim Kolla mfugaji wa kuku wazazi wa

mayai kutoka Kata ya Buyuni alikabidhiwa hundi ya Tshs 500,000 na cheti.

Mstahiki Meya Mhe.Omary Kumbilamoto akiwa amebeba vikombe vya ushindi kwa Manispaa

ya Ilala ikiwa ni ushindi wa Kwanza kwa Manispaa na Ushindi wa Tatu kwa washiriki wote wa

Maonesho 26 ya Wakulima kanda ya Mashariki.

10

8

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Omary Kumbilamoto amekabidhi vifaa vya choo (masinki 10) pamoja na bati 20 katika shule ya sekondari kinyamwezi iliyoko kata ya pugu Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.

Makabidhiano hayo niutekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati kamati ya fedha ilopofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo. Katika shule ya Sekondari Pugu Kinyamwezi Kamati ilibaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu na ubovu shuleni hapo

Akisoma risala kwa Mgeni Mh. Omary Kumbilamoto, Mkuu wa Shule hiyo Bi.Sifa Mwaruka amesema wanakabiliana na changamoto ukilinganisha na mafanikio wanayopata, changamoto hizo ni uchache wa matundu ya vyoo vya wanafunzi na walimu kwani walimu wanatumia vyoo vinne ambavyo wanaume wanatumia viwili na wanawake viwili, na idadi ya walimu nikubwa ukilinganisha na idadi ya vyoo, uchache wa viti vya wanafunzi na walimu pamoja na meza za kusomea.

kufuatia tukio hilo Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala amezipokea changamoto hizo na kuahidi kuzifanyia kazi. Aidha Mstahiki Meya ametoa wito kwa wanafunzi kuzingatia maudhui yaliyopo katika wimbo wa shule ili kuepuka vishawishi ili wafikie malengo yao na kusisitiza usafi.

Meya wa Manispaa ya Ilala Akabidhi Vifaa vya Choo Shule ya Sekondari Pugu Kinyamwezi

11

8

Mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Mh. Deoglas Masaburi ameibuka mshindi wa unaibu Meya

manispaa ya Ilala kupitia uchaguzi uliofanyika Leo tarehe 19 Agosti 2019 katika ukumbi wa Arnatouglou

Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo ulihusisha wagombea kutoka vyama viwili vya Siasa ambao ni Mh.DeoglasMasaburi kuto-

kana chama cha mapinduzi CCM na Mh. Hellen Liyatula wa chama cha demokrasia na maendeleo

CHADEMA. Jumla ya wapiga kura walikua 54 ambao ni madiwani na wabunge wa Manispaa ya Ilala.

Akitangaza Matokeo hayo Afisa tawala wilaya ya Ilala Jabiri Makama amesema " Mgombea kupitia Cha-

ma cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Mh Hellen amepata kura 21 sawa na asilimia 39% nae

Mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi( CCM )Mh. Deoglas Masaburi amepata kura 33 sawa na asilim-

ia 61%”.

Baada ya uchaguzi huo Naibu Meya aliyechaguliwa alitoa neno la shukrani kwa wajumbe wote kwa kum-

chagua kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo na kuwaahidi Madiwani na wananchi wa Manispaa Ya Ilala

kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo ya Manispaa hiyo .

"Nawashukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi( CCM )wilaya ya Ilala, Madiwani naamini kura ni

imani nashukuru kwa kuniamini naahidi sitowaangusha". Amesema Mh. Masaburi.

Uchaguzi huo ulifanyika kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekua Naibu Meya wa

Manispaa ya Ilala Mh.Omari Kumbilamoto ambaye kwa sasa ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala.

MASABURI AIBUKA KIDEDEA NAIBU MEYA

MANISPAA YA ILALA

12


Recommended