View
10
Download
0
Category
Preview:
Citation preview
MWONGOZO WA UZALISHAJI WA MBEGU ZA DARAJA LA KUAZIMIWA UBORA
(Quality Declared Seeds)
KITINI NAMBA 7:
November, 2019
2
YALIYOMO 1.0 UTANGULIZI .................................................................................................................................................... 3
1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora ............................................................................................... 3
2.0 UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA JAMII YA MIKUNDE, MAFUTA NA NAFAKA .......... 3
2.1. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu ............................................................................................ 4
2.2. Utenganisho wa shamba .......................................................................................................................... 4
3.0. UTAYARISHAJI WA SHAMBA ................................................................................................................ 5
4.0. CHANZO CHA MBEGU .............................................................................................................................. 5
5.0. UPANDAJI ....................................................................................................................................................... 6
5.1. Wakati wa kupanda ..................................................................................................................................... 6
5.2. Kiasi cha mbegu ...................................................................................................................................... 6
5.3. Nafasi ya kupanda .................................................................................................................................. 7
5.4. Matumizi ya mbolea .............................................................................................................................. 7
6.0. KUSAJILI SHAMBA LA MBEGU ............................................................................................................. 8
7.0. UDHIBITI WA WADUDU /WANYAMA WAHARIBIFU NA MAGONJWA ............................ 8
8.0. UKAGUZI WA SHAMBA LA MBEGU .................................................................................................. 12
9.0. UVUNAJI NA UHIFADHI WA MBEGU ............................................................................................... 12
9.1. Kupima ubora wa mbegu ......................................................................................................................... 12
9.2. Kufungasha na kuweka nembo yenye taarifa za mbegu ......................................................... 13
MBINU MUHIMU ZILIZOFUNDISHWA KATIKA SOMO HILI: .........................................................14
3
1.0 UTANGULIZI
1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora
Mbegu ni sehem ya mmea ambayo hutumika kuzalisha/kuotesha mmea mwingine, yaweza
kuwa ni zao la ua au sehem ya mmea iliyokomaa na kuwa tayari kuendelea kuoteshwa tena,
mfano vipando vya muhogo
Mbegu ni mojawapo ya pembejeo muhimu katika kilimo. Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora
(QDS) ni mojawapo wa vyanzo bora vya mbegu vya kutegemewa na wakulima. Mfumo wa
uzalishaji wa mbegu bora za kuazimiwa ubora ulianzishwa na shirika la kilimo na chakula
duniani (FAO) mwaka 1993 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2006.
Mbegu hizi ziliingizwa kwenye mfumo rasmi wa kuzalisha mbegu katika sheria ya mbegu ya
mwaka 2003, pamoja na kanuni, miongozo na taratibu zake za uzalishaji za mwaka 2007. Mbegu
hizi huzalishwa na mkulima mmoja mmoja au kikundi cha wakulima kilichosajiliwa na kupata
mafunzo kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa matumizi yao binafsi na/au kuuza kwa wakulima wa
maeneo ya jirani. Ni muhimu nasaba/asili ya mbegu hiyo ijulikane na hivyo mbegu ya msingi au
iliyothibitishwa kuwa ndizo pekee zinazotumika katika uzalishaji ili kuhakikisha ubora wa
mbegu.
Hapa nchini mbegu zilizopevushwa kiasili (OPV) ambazo zinapatikana katika orodha ya taifa ya
mimea ndizo zinazoweza kutumika katika uzalishaji wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora na
siyo mbegu za kizazi cha kwanza cha mbegu chotara (F1 Hybrids). Mfumo wa mbegu za daraja la
kuazimiwa ubora huwawezesha wakulima kupata mbegu bora kwa gharama nafuu na kwa
wakati. Mfumo huu wa QDS upo si kwa nia ya kuubadili mfumo rasmi wa uzalishaji mbegu
zilizothibitishwa ubora ila kujaza pengo lililoachwa na mfumo rasmi. Ni mfumo unaowahusu
wakulima wadogo wadogo walio kwenye vikundi kwa matumizi yao ndani ya wilaya husika.
2.0 UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA JAMII YA MIKUNDE, MAFUTA NA NAFAKA
Mbegu za jamii ya kunde, mafuta na nafaka zinatumiwa na wakulima wengi kwa ajili ya kuzalisha
chakula kwa matumizi ya binadamu na mifugo. Mbegu hizi hustawi kwenye udongo wa aina
tofauti kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali.
4
Jedwali 1: Aina ya udongo unaofaa
Aina ya mbegu Udongo unaofaa
Mbaazi Udongo wa aina mbalimbali kuanzia ule wenye mchanganyiko wa
kichanga na tifutifu na mfinyanzi na tifutifu. Lakini hufanya vizuri
zaidi kwenye udongo wa tifutifu
Alizeti Udongo wa aina mbalimbali lakini hukua vizuri zaidi kwenye
udongo wa tifutifu usiotuamisha maji
Mahindi Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji
Choroko Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji
Mpunga Udongo wa tifutifu nchi kavu na mabondeni
Kunde Udongo wa aina mbalimbali pia huweza kustawi vizuri kwenye
udongo wa kichanga
Maharage Udongo wa tifutifu usiotuamisha maji
Angalizo: Epuka kupanda mbegu za aina tofauti kwa misimu miwili inayofuatana
2.1. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu
Inashauriwa kuwa shamba la kuzalisha mbegu liwe msimu uliopita halikulimwa mbegu husika
ili kuepuka magonjwa yanayoweza kutokea.
2.2. Utenganisho wa shamba
Utenganisho wa mashamba ya mbegu unafanywa ili kuzuia vyanzo vyote vinavyoweza kuchafua
mbegu wakati wa kukua. Inahakikisha kwamba uchavushaji mtambuka (cross pollination) wa
chavua (pollen) kutoka kwenye aina nyingine za mimea au kutoka kwenye mimea ya daraja duni
na dhoofu hautokei. Pia inahakikisha kuwa hakuna uchanganyikaji wa mbegu wakati wa kuvuna
au uambukizi wa wadudu kutoka kwa mazao sawa au mazao mbadala.
Kuna aina kuu mbili za utenganisho wa shamba.
a. Utenganisho wa umbali
Shamba la mbegu linatakiwa kutengwa kutoka shamba lingine la aina hiyo hiyo ya mbegu kwa
umbali uliopendekezwa kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:
5
Jedwali 2: Utenganisho wa umbali wa shamba
Aina ya zao Utenganisho wa umbali kwa kila daraja la mbegu (mita)
Msingi Certified 1 Certified 2 QDS
Mahindi (OPV) 400 200 200 190
Maize (chotara) 400 200 200 190
Mtama 400 200 200 100
Uwele 300 300 300 100
Mpunga 5 5 5 3
Choroko 20 20 20 20
Karanga 3 3 3 3
Maharage 10 10 10 10
Kunde 5 5 5 5
Mbaazi 50 50 50 50
Alizeti 200 200 200 200
b. Utenganisho kwa kutumia nyakati
Uchafuzi unaweza kudhibitiwa kwa kupanda mimea/mbegu kwa nyakati tofauti. Hii inaweza
kuzuia utoaji wa maua na uchavushaji kwa wakati mmoja.
Zingatia
Epuka kulima mbegu zilizotajwa hapo juu kwenye mabonde yenye kutuamisha maji.
3.0. UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Tayarisha shamba mapema ili kutoa nafasi ya manyasi kuoza na hatimaye kuongeza mboji
kwenye udongo. Kama shamba linalotumika ni la zamani hakikisha limetifuliwa vizuri kwa
kutumia aidha wanyama kazi, jembe la mkono au trekta na mabonge ya udongo yapigwe ili
kupata udongo laini. Kama shamba linalotumika ni jipya, hakikisha kuwa visiki na mawe
yameondolewa ili kuwezesha matumizi ya trekta na wanyama kazi katika uandaaji wa shamba.
4.0. CHANZO CHA MBEGU
Mbegu zitakazotumika katika uzalishaji zisiwe chotara. Mkulima atumie mbegu ya daraja la
msingi, au kuthibitishwa ama QDS 1. Mbegu ya msingi na iliyothibitishwa hupatikana katika
mashamba ya wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seed Agency - ASA). Vilevile mbegu za
6
daraja la kuthibitishwa hupatikana katika makampuni ya mbegu, kupitia kwa wakala wao au
maduka ya pembejeo.
Mkulima anaruhusiwa kutumia mbegu ya QDS 1 iliyopatikana kutoka kwa mkulima wa mbegu
aliyesajiliwa na TOSCI, kama chanzo cha mbegu, lakini ajue ya kwamba, akishavuna hawezi
kuitumia kama mbegu tena.
Baadhi ya aina ya mbegu zinazopendekezwa na Wizara ya Kilimo ni kama zilizoonyeshwa
kwenye jedwali lifuatalo:
Jedwali 3: baadhi ya aina za mbegu zinazopendekezwa
Zao Baadhi ya mbegu zinazopendekezwa
Mahindi Kilima, staha, Katumani, Kito, Cholima 1, Lishe K1, Stuka- 2
Alizeti Rekodi
Karanga Mnanje, Red mwitunde, Nyota, Johari, Pendo 98, Sawia 98
Mbaazi Komboa, Mali, Tumia
Choroko Nuru, Imara
Kunde Tumaini, Fahari, Vuli -1, vuli - 2
Maharage Kabanima, Uyole 84, Uyole 90, Uyole 98, Seliani 90, Seliani
97, Jesca, Wanji
Angalizo
Kwa mkulima anayeanza kuzalisha mbegu, anashauriwa kutumia mbegu ya daraja la msingi.
5.0. UPANDAJI
5.1. Wakati wa kupanda
Mzalishaji anashauriwa kuzalisha mbegu wakati wa mvua za msimu. Kwa mfano, mbaazi za
muda mfupi hustawi zaidi ukanda wa chini na ni vyema zikapandwa mwishoni mwa mwezi wa
Februari kwani hukomaa katika muda wa siku 120.
5.2. Kiasi cha mbegu
Kiasi cha mbegu kwa ekari moja hutegemea aina ya mbegu kama inavyoonyeshwa kwenye
jedwali lifuatalo:
7
Jedwali 4: Kiasi cha mbegu kwa ekari
Aina ya mbegu Kiasi kwa ekari moja (kg)
Mbaazi Muda mrefu 2
Muda mfupi 3
Alizeti 6
Mahindi 8-10
Choroko 8-10
Kunde 6 - 10
Maharage 10
5.3. Nafasi ya kupanda
Panda mbegu kwa kuzingatia nafasi iliyopendekezwa kati ya mche na mche na kati ya mstari na
mstari kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:
Jedwali 5: Nafasi inayopendekezwa ya upandaji
Aina ya mbegu Utenganisho
kati ya mstari
na mstari (cm)
Utenganisho kati
ya mche na mche
(cm)
Kina (cm)
Mbaazi 20 50 5
Alizeti 90 25 4 - 6
75 30 4 - 6
Mahindi 75 30 4 – 5
75 60 4 - 5
Choroko 50 10 4 - 5
Karanga 50 10 2.5 - 5
50 15 2.5 - 5
Kunde 75 20 3 – 4
Maharage 50 15-20 2.5 - 3
5.4. Matumizi ya mbolea
Wakati wa kupanda mkulima anashauriwa kutumia mbolea mboji/vunde na/au samadi
kulingana na rutuba ya udongo iliyopo kwenye eneo husika. Mkulima azingatie ushauri wa
wataalam kuhusu matumizi ya mbolea zinazopendekezwa katika kilimo ikolojia.
8
6.0. KUSAJILI SHAMBA LA MBEGU
Mzalishaji wa mbegu analazimika kusajili shamba lake kwenye Taasisi ya Udhibiti wa ubora wa
mbegu (TOSCI) muda usiozidi siku 30 baada ya kupanda. Uasjili hufanyika katika vituo vya
Morogoro, Mwanza, Njombe, Arusha na sasa Mtwara. Usajili unatoa nafasi kwa Taasisi kupanga
utaratibu wa ukaguzi.
Kung’oa mimea isiyofaa
Hakikisha kuwa shamba lako linabaki safi wakati wote. Ondoa mimea yote ambayo ina
magonjwa, mimea iliyoharibiwa na wadudu. Kwenye alizeti ondoa mimea yenye vichwa vingi.
Zingatia: Shughuli ya kuondoa mimea isiyofaa ifanyike kwa kushirikiana na afisa ugani aliye
karibu.
7.0. UDHIBITI WA WADUDU /WANYAMA WAHARIBIFU NA MAGONJWA
Baadhi ya wadudu waharibifu wanaoshambulia mbegu zikiwa shambani na namna ya
kuwadhibiti ni kama ilivyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo.
Jedwali 6: Baadhi ya wadudu wanaoshambulia mimea na udhibiti wake
Zao Mdudu anayeshambulia Udhibiti
Mbaazi Pod borer, spotted pod borer, podfly,
plumemoth, blue butterfly, pod bug na
blister beetles
Tifua ardhi kwa kina kipindi cha
kiangazi ili kuwaibua wadudu
funza wa wadudu waliojificha
ardhini. Tumia kilimo
mchanganyiko cha
mtama/mahindi. Weka mitego ya
limbwata (pheromone traps) na
pulizia dawa za asili. Kuwaua
blister beetle kwa kutumia mitego
na/au kuwakamata na
kuwaharibu.
Alizeti Sunflower Beetles (Mbawa kau wa
alizeti)
Funza wakatao miche, panzi, minyoo
ya ardhini (cutworms) na funza wa
vitumba (sunflower borers)
Hakikisha shamba linakuwa safi
wakati wote kabla na baada ya
kupanda. Pulizia dawa za asili kwa
mchanganyiko maalum kama
ilivyoelekezwa na wataalam wa
9
kilimo ikolojia kama vile
mwarobaini, pilipili za kuwasha,
majivu, maziwa mabichi, majani
ya mpapai n.k.
Mahindi Maize stalk boarer Ili kudhibiti bungua, tumia mfumo
wa kilimo wa fanya juu fanya chini
(push-pull) kwa kupanda mstari
mmoja wa majani jamii ya
mikunde ya Desmodium
(silverleaf au greenleaf) kila baada
ya mistari mitatu ya mahindi. Pia
panda mistari isiyopungua mitatu
ya Napier grass katika ukingo wa
shamba. Desmodium inatoa
harufu ya kuwafukuza wadudu na
Napier inatoa ute mzito ambao
hunasa larvae na kufa.
Unga wa mwarobaini
Choroko 1) Wadudu wanaoshambulia mabua
(stem feeders)
(2) Wadudu wanaoshambulia majani
(foliage feeders: leaf folder,
caterpillars)
(3) Wadudu wanoshambulia mbegu
(pod feeders)
Matumizi ya mbegu bora
zinazotoa ukidhani dhidi ya
mashambulizi ya wadudu.
Kurekebisha tarehe za kupanda,
matumizi ya aina ya sugu na
kupanda mazao mchanganyiko
(choroko na mahindi) au mazao ya
mtego yanaweza kufuatiwa
kulingana na upatikanaji na
ufanisi katika eneo fulani.
Kutengeneza mandhari ya
shamba (farmscaping) ambayo ni
mbinu ya kiikolojia ya usimamizi
wa wadudu; ikiwa ni pamoja na
matumizi ya safu za miti
10
zinazofanya ua (hedgerows),
mimea ya wadudu, mazao
yanayofukina ardhi, na mabwawa
ya maji ili kuvutia na kusaidia
viumbe wenye manufaa kama vile
wadudu, popo na ndege wa
mawindo.
Karanga Vidukari (mafuta) Dhibiti kwa kupanda mapema na
kwa nafasi iliyopendekezwa.
Tumia dawa za asili za utupa,
pilipili, mwarobaini n.k.
Inzi wa karanga Panda mapema na pia pilizia dawa
za asili za utupa, pilipili,
mwarobaini n.k.
Mchwa Bomoa vichuguu ambavyo ni
mazalia ya mchwa.
Kunde Aphids/vidudu mafuta Panda aina za mbegu zinazotoa
ukinzani dhidi ya wadudu hao.
Shamba liwe safi lisiwe nan a
magugu na vichuguu vya mchwa.
Pia fanya kilimo mzunguko,
badilisha tarehe za upandaji,
mitego ya wadudu.
Maharage Foliage beetles, flower thrips, pollen
beetles, pod borers, pod bugs, and sap
suckers kama vile aphids
Wadudu hawa wanaweza
kudhibitiwa kwa kutumia mbinu
shirikishi (IPM) ambazo
zinahusisha: kupanda kwa wakati,
kilimo cha mazao mchanganyiko,
kilimo mzunguko.
Baadhi ya magonjwa yanayoshambulia mbegu ni kama yalivyoonyeshwa kwenye jedwali
lifuatalo.
11
Jedwali 7: Baadhi ya magonjwa yanayoshambulia mimea na udhibiti wake
Zao Magonjwa Udhibiti
Mbaazi Mnyauko Ng’oa na kutupa nje ya shamba
Alizeti Madoa ya majani, kuoza
mizizi, kuvu ya majani
na ukoma
Tumia mbegu zilizothibitishwa ambazo
zinastahamili magonjwa
Mahindi Virusi vya milia (maize
streak vírus), Fugwe (
smut disease)
Ng’oa na kufukia mimea ilyoathirika. Tumia
viuatilifu vya asili kudhibiti wadudu.
Choroko Kuoza mizizi na majani,
kutu
Choma mimea iliyoathirika na ugonjwa.
Pulizia mafuta ya muarobaini.
Karanga Ugonjwa wa kuoza
(aflatoxin), , ukoma,
maganda matupu.
Zuia mikwaruzo wakati wa kuvuna, karanga
zikaushwe vizuri na kuhifadhiwa kwenye
magunia na siyo viroba katik sehemu isiyo
na unyevu.
Kuoza majani na kutu Kupanda mapema, kuondoa maotea, kilimo
cha mzunguko na kutumia mbegu
zinazostahimili magonjwa
Ukoma Panda mapema na kwa nafasi, palilia
mapema, ondoa maotea na panda mbegu
bora
Maganda matupu Ongeza virutubisho vya chokaa na tumia
mbegu za muda mfupi
Kunde Kuoza kunde (Cowpea
rot and damping),
Kukauka majani
(Southern blight) ,
unyaufu wa mmea
kuanzia majani ya chini
(cowpea mosaic vírus),
Mnyauko fusari/Ukoma
(cowpea fusarium wilt)
Kuondoa mimea iliyoathiriwa na virusi,
kudhibiti magugu na kupanda mbegu
zilizothibitishwa zinazotoa ukinzani dhidi ya
magonjwa.
12
Maharage Chule (anthracnose),
baka jani (halo blight),
mnyauko bakteria
(bactérial wilt), unyaufu
wa mmea kuanzia
majani ya chini (bean
common mosaic virus)
Tumia mbegu zilizothibitishwa ambazo
hazina vimelea vya magonjwa
Ili kuepuka magonjwa haya mkulima anashauriwa kutumia mbegu zilizothibitishwa ambazo
zinastahimili magonjwa.
8.0. UKAGUZI WA SHAMBA LA MBEGU
Ili kuhakikisha kuwa taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu
zimefuatwa shamba la mbegu ni lazima likaguliwe. Ukaguzi unafanywa na wataalam kutoka
taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI) na mkulima. Mkaguzi ataangalia kama utenganisho
wa umbali umezingatiwa. Pia ataangalia kama kuna mimea mingine ambao haitakiwi kuwepo
shambani, magonjwa na hali ya ujumla ya mazao. Kwa uchache ukaguzi utafanyika mara mbili
kabla ya mimea kutoa maua na kabla ya kuvuna.
9.0. UVUNAJI NA UHIFADHI WA MBEGU
Vuna kwa kuangalia dalili za kukomaa kwa mbegu.
Safisha mbegu kwa kuondoa uchafu, vumbi, mbegu zilizopasuka na mbegu zisizokomaa.
Mbegu ihifadhiwe sehemu iliyo safi, kavu na yenye mzunguko mzuri wa hewa.
Hakikisha kuwa vyombo vya kuhifadhia kama vile gunia zinapewa kitambulisho.
9.1. Kupima ubora wa mbegu
Kabla ya mbegu kuhurusiwa kuuzwa ni lazima ipimwe ubora wake kwa mfano; uotaji, usafi,
unyevu n.k. Upimaji unafanyika kwenye maabara ya mbegu katika Taasisi ya kudhibiti ubora wa
mbegu (TOSCI). Afisa wa TOSCI au wakala Wake huchukua sampuli ya mbegu na kuzipeleka
maabara ya mbegu ya TOSCI kwa ajili ya kuthibitisha ubora Wake.
Ubora wa mbegu
Mbegu ikithibitika kama ina ubora unaotakiwa inaweza kuuzwa.
13
9.2. Kufungasha na kuweka nembo yenye taarifa za mbegu
Weka mbegu katika mifuko ya ujazo wa kilo 2, 5 na 10 kulingana na mahitaji ya mteja. Ikiwa
mbegu itabaki kwa kipindi kitakachozidi miezi sita ni lazima mbegu ichukuliwe sampuli nyingine
na kupelekwa TOSCI ili ikafanyiwe tena uchunguzi.
14
MBINU MUHIMU ZILIZOFUNDISHWA KATIKA SOMO HILI:
1.1 Mbegu za daraja la kuazimiwa ubora
2. Uzalishaji Wa Mbegu Bora Za Jamii Ya Mikunde, Mafuta Na Nafaka
3. Sifa za ziada katika uzalishaji mbegu
4. Utenganisho wa shamba
5. Utayarishaji wa shamba
6. Chanzo cha mbegu
7. Upandaji
7.1 Kiasi cha mbegu
7.2 Aina ya mbegu
7.3 Kiasi kwa ekari moja (kg)
7.4 Nafasi ya kupanda
8. Kusajili shamba la mbegu
9. Udhibiti wa wadudu /wanyama waharibifu na magonjwa
10. Ukaguzi wa shamba la mbegu
11. Uvunaji na uhifadhi wa mbegu
12. Kupima ubora wa mbegu
13. Kufungasha na kuweka kitambulisho
SHUK RANI
Kitini hiki cha “ Mwongozo wa uzalishaji wa mbegu za daraja la kuazimiwa ubora” kimeandaliwa
na shirika la Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO) kwa ushirikiano na SWISSAID Tanzania.
Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa O�si ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara,
Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Naliendele, Sustainable Agriculture Tanzania
(SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity
(TABIO), Tanzania O�cial Seed Certi�cation Institute (TOSCI-Mtwara), Shirika la Uhifadhi
Misitu Asilia Tanzania (TFCG), wawakilishi wa wakulima na SWISSAID Tanzania katika
warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia,
msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Liechtenstein Development
Service (LED) na Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa
kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji, kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.
“Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”
"This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"
Recommended