They go to school, but do they learn?

Preview:

DESCRIPTION

The comic book debates the quality of learning in primary schools in Tanzania. Despite notable achievements in enrollment, constructions of classrooms and teacher training, children learn too little. Uwezo assessed learning in East Africa and found that children in the final year of primary school do not have basic numeracy and literacy skills. This booklet encourages citizens to distinguish between the success in enrollment and school infrastructure on one hand and the learning on the other. The characters in the comic book make suggestions on how everyone can make a contribution to improve learning.

Citation preview

Kijitabu hiki kimetayarishwa na watendaji wa Twaweza Tanzania.

Waandishi: Abella Bateyunga na Evarist KamwagaMchoraji: Marco TibasimaMhariri: Rakesh Rajani

©Hivos/Twaweza 2011

SLP 38342, Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 266 4301Faksi: +255 22 266 4308Barua pepe: info@twaweza.orgTovuti: www.twaweza.org

Unaruhusiwa kunakili sehemu yeyote ya kijitabu hiki kwa sababu zisizo za kibiashara tu. Unachotakiwa kufanya ni kunakili chanzo cha sehemu uliyonakilia na kutuma nakala mbili kwa Twaweza.

Utangulizi

Ndugu msomaji:

Wengi wetu tunaamini ‘elimu ni ufunguo wa maisha’. Serikali yetu vilevile

inatambua hivyo na ndio maana imeweka juhudi kubwa ka�ka elimu.

Madarasa mengi yamejengwa, uandikishwaji wa watoto umepanda, na walimu

lukuki wameajiriwa. Zaidi ya haya Tanzania iko mstari wa mbele ka�ka

kuyafikia malengo ya maendeleo ya milenia (MDGs), ka�ka hili tumepata tuzo

za kimataifa kwa kuvuka malengo ka�ka uandikishaji watoto mashuleni

(asilimia 95).

Mafanikio haya ni makubwa na Serikali inastahili kupewa pongezi.

Lakini, hebu tujiulize, ji�hada hizi zimezaa matunda gani? Tutumie kipimo kipi

kujua kama watoto wetu wameelimika?

Lengo la elimu ni kuleta mabadiliko ya maisha. Mwalimu Julius Nyerere ka�ka

Elimu ya Kujitegemea alituhimiza kwamba “Elimu inayotolewa ni lazima ijenge

mambo matatu kwa kila mwananchi; akili ya kuuliza, uwezo wa kujifunza na

uwezo wa kujiamini”. Ka�ka haya yote mkazo upo ka�ka ‘ubora’ na si

vinginevyo, yaani kumjengea mtoto maarifa ka�ka kusoma, kufanya

mahesabu, uwezo wa kudadisi, kufikiri, kusikiliza, kuuliza maswali,

kupambanua na kuwasiliana kwa kujiamini.

Ndiyo maana matokeo ya utafi� uliofanywa hivi karibuni na Uwezo yana�sha.

Utafi� umeibua matokeo tofau� na wengi wanavyotazamia elimu ya nchi yetu.

Imegundulika kuwa watoto wengi wapo madarasani lakini hawajifunzi. Kwa

mfano, watoto 9 ka� ya 10 wa darasa la tatu hawawezi kusoma Kiingereza cha

darasa la pili, 8 ka� ya 10 hawawezi kufanya Hisaba�, na 7 ka� ya 10

wanashindwa kusoma Kiswahili ipasavyo.

i

Tafakari kwa hali kama hii, miaka kumi ijayo tutakuwa na taifa la namna gani?

Kizazi hiki kipya cha waka� huo kitafanya nini? Hali hii inafanana na nyumba

iliyopambwa lakini yenye msingi mbovu, matokeo yake ni nyufa

zitakazopelekea anguko lake.

Lakini tusikate tamaa. Kuna mengi ya kufanya. Kila mmoja ana uwezo wa

kuleta mabadiliko. Unaposoma kijitabu hiki usikae kimya, shirikisha wenzio,

jadili na chukua hatua ka�ka eneo lako. Ongea na watoto na vijana, wasaidie

na kuwafariji. Wasiliana na viongozi kujadili jinsi ya kuboresha elimu. Andika

barua kwa mamlaka au kwenye vyombo vya habari kuwasilisha maoni yako.

Pamoja Twaweza! Ni sisi!

Rakesh RajaniMkuu, Twaweza

ii

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

18

19

20

21

22

23

24

25

26

27

Recommended