12
Toleo namba 002 | 17 Machi 2019 Ninafuraha tena kujumuika na wasomaji na wapenzi wa soka katika toleo letu la pili la kila wiki la Jarida la TFF. Katika toleo la wiki hii,ningependa kuzungumzia michuano mbalim- bali inayozikabili timu zetu katika mashindano ya kimataifa. Kwa upande wa timu yetu ya taifa’ Taifa Stars’,ni wazi tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Uganda Cranes siku ya Jumapili,lakini tuna imani kubwa tutashinda mchezo huo. Ushirikiano mkubwa ambao Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF),lin- aupata kutoka kwa Serikali na Kamati ya ushindi-Taifa Stars-,tunaim- ani ya kushinda na kufuzu mchezo huo. Tumedhamiria kwa dhati kubwa kuhakikisha tunashinda mchezo huo,na kuweza kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa Afrika (Afcon). Ni muda sahihi kwa Watanzania wote kushikana na kuhakikisha tunaiombea timu yetu iweze kufanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Uganda. Halikadhalika,jicho letu pia lipo ka- tika maandalizi ya michuano ya vi- jana ambayo yanaendelea vizuri na tunaamini,yataweza kututoa kimaso- maso katika mashindano hayo. Hasa,ikizingatiwa sisi ndio tutakuwa wenyeji,kwahiyo tunakila sababu,ka- ma nchi kuandika historia ya kuweza kuandaa michuano hiyo pamoja na kuweza kuchukua kombe hilo. Pia,kwa upande wa timu yetu ya wanawake Twiga Stars wao na wanak- abiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Congo April 05,ambao tunakila sa- babu ya kuhakikisha tunashinda ka- tika ardhi yetu ya nyumbani. Shime Watanzania,kipindi hiki cha sasa ni muhimu tukashikamana kwa pamoja na kuhakikisha tunaziunga mkono timu zetu za taifa kwa hali na mali. Sisi kama Shirikisho tunaimani kub- wa timu zetu zitaweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Wallace Karia Rais wa TFF Neno la Rais Wallace Karia

- J # 1 :anew.tff.or.tz/wp-content/uploads/2019/03/TFF-Jarida-la...3. JKT Tanzania 4. Ndanda FC 5. Yanga SC KUNDI D 1. KMC FC 2. Mbeya City 3. Simba SC 4. Tanzania Prisons 5. Lipuli

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • J A R I D AL A W I K I

    Toleo namba 002 | 17 Machi 2019

    Ninafuraha tena kujumuika na wasomaji na wapenzi wa soka katika toleo letu la pili la kila wiki la Jarida la TFF.

    Katika toleo la wiki hii,ningependa kuzungumzia michuano mbalim-bali inayozikabili timu zetu katika mashindano ya kimataifa.

    Kwa upande wa timu yetu ya taifa’ Taifa Stars’,ni wazi tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Uganda Cranes siku ya Jumapili,lakini tuna imani kubwa tutashinda mchezo huo.

    Ushirikiano mkubwa ambao Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF),lin-aupata kutoka kwa Serikali na Kamati ya ushindi-Taifa Stars-,tunaim-ani ya kushinda na kufuzu mchezo huo.

    Tumedhamiria kwa dhati kubwa kuhakikisha tunashinda mchezo huo,na kuweza kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa Afrika (Afcon).

    Ni muda sahihi kwa Watanzania wote kushikana na kuhakikisha tunaiombea timu yetu iweze kufanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Uganda.

    Halikadhalika,jicho letu pia lipo ka-tika maandalizi ya michuano ya vi-jana ambayo yanaendelea vizuri na tunaamini,yataweza kututoa kimaso-maso katika mashindano hayo.

    Hasa,ikizingatiwa sisi ndio tutakuwa wenyeji,kwahiyo tunakila sababu,ka-ma nchi kuandika historia ya kuweza kuandaa michuano hiyo pamoja na kuweza kuchukua kombe hilo.

    Pia,kwa upande wa timu yetu ya wanawake Twiga Stars wao na wanak-abiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Congo April 05,ambao tunakila sa-babu ya kuhakikisha tunashinda ka-tika ardhi yetu ya nyumbani.

    Shime Watanzania,kipindi hiki cha sasa ni muhimu tukashikamana kwa pamoja na kuhakikisha tunaziunga mkono timu zetu za taifa kwa hali na mali.

    Sisi kama Shirikisho tunaimani kub-wa timu zetu zitaweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

    Wallace KariaRais wa TFF

    Neno la Rais Wallace Karia

  • Kocha Mkuu wa timu ya soka taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) akielezea: Oscar Mirambo.

    Kimsingi mashindano ya vijana ya kimataifa ya UEFA ASSIST, am-bayo tumemaliza hivi karibuni nchini Uturuki, yametusaidia kwa kia-si kikubwa kutazama kikosi chetu mahala ambapo panahitajika kufa-nyiwa marekebisho.

    Mashindano hayo licha ya kutupa sisi benchi la ufundi kubaini mapungufu mbalimbali ya vijana wetu,lakini pia yamesaidia kuwaweka vijana katika wigo mpana kwa kuwawezesha kucheza Ulaya na timu mbalimbali.

    Pia,yametusaidia kuwaona wapinzani wetu ambao nao wamefuzu katika fainali za michuano ya Mataifa ya vijana chini ya miaka 17,itakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

    Ingawa kulikuwa na changamoto ya hali ya hewa,hususan mchezo wa kwanza,ambao tulipoteza,lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda vijana walianza kuzoea hali ya hewa.

    Kikubwa mashindano hayo,yametusaidia sana benchi la ufundi,kuelekea maandalizi yetu ya AFCON,ha-likadhalika pia kwa wachezaji nao,michuano hiyo imewajenga na kuwaongezea kujiamini zaidi.

    Kwahiyo,tunaimani kubwa,maandalizi ambayo tumeyafanya huko Uturuki na ambayo tunatarajia kuyafanya huko nchini Dubai,yatawasaidia vijana wangu kuwaweka vizuri kabla ya michuano ya Afcon kuanza.

    Ningependa kuwatoa hofu Watanzania,kuwa vijana wetu wapo tayari kwa mashindano na sisi benchi la ufundi tunajitahidi kuwapa kila mbinu ili ziweze kuwajenga zaidi.

    Ni kwa vipi Mashindano ya UEFA ASSIST yameisaidia Serengeti Boys?

    1 CONFEDERATION AFRICAINE DE FOOTBALL

    3 Abdel Khalek Tharwat Street, El Hay El Motamayez, P.O. Box 23 6th October City, Egypt - Tel.: +202 38247272/ Fax : +202 38247274 – [email protected]

    Calendrier du tournoi final de la Coupe d’Afrique des Nations U17, TOTAL, Tanzanie 2019 Fixtures of the Final Tournament of the TOTAL U17 Africa Cup of Nations, Tanzania 2019

    No

    Match

    Gp

    Date

    K.O.

    Lieu/Venue:

    Matchs de Groupes /Group matches

    A 14/04/2019 16:00hrs National Stadium 1. TANZANIA V NIGERIA

    2. ANGOLA V UGANDA A 14/04/2019 19:00hrs National Stadium

    3. GUINEA V CAMEROON B 15/04/2019 16:00hrs Chamazi Stadium

    4. MOROCCO V SENEGAL B 15/04/2019 19:00hrs Chamazi Stadium

    5. NIGERIA V ANGOLA A 17/04/2019 16:00hrs National Stadium

    6. UGANDA V TANZANIA A 17/04/2019 19:00hrs National Stadium

    7. CAMEROON V MOROCCO B 18/04/2019 16:00hrs Chamazi stadium

    8. SENEGAL V GUINEA B 18/04/2019 19:00hrs Chamazi stadium

    9. TANZANIA V ANGOLA A 20/04/2019 16:00hrs National stadium

    10. NIGERIA V UGANDA A 20/04/2019 16:00hrs Chamazi stadium

    11. GUINEA V MOROCCO B 21/04/2019 16:00hrs Chamazi stadium

    12. CAMEROON V SENEGAL B 21/04/2019 16:00hrs National Stadium

    Demi-Finales/ Semi-Finals

    13. 1st Group A V 2nd Group B 24/04/2019 16:00hrs National Stadium

    14. 1st Group B V 2nd Group A 24/04/2019 19:30hrs National Stadium

    Match de Classement /3rd Place match

    15. Los.-Perd.: 13 v Loser-Perdant: 14 27/04/2019 16:00hrs National Stadium

    Finale/Final match

    16. Win./Vainq.:13 v Win./Vainq.: 14 28/04/2019 16:00hrs National stadium

    Viwanja viwili vitakavyotumika katika michezo ya AFCON U17 2019 Tanzania

    Taifa

    Azam Complex

    RATIBA

  • UEFA Assist; Serengeti Boys

  • Taifa Stars

    Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’kinachojiwinda na mchezo wake kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Uganda,kinatarajia kuingia kambini Machi 17.

    Makamanda hao ambao wanakibarua kigumu cha kuhakikisha kinapata tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika,kinatarajia kuweka kambi yake Bahari Beach Ledger Plaza.

    Meneja wa timu za Taifa,Danny Msangi,amesema maandalizi yote kuhusina na kambi hiyo yanaendelea vizuri na wachezaji wanaocheza nje ya nchi wanatarajia kujiunga katika kikosi hicho kuanzia Machi 18.

    Taifa Stars yaingia kambini kujiwinda na Uganda

    Tujitokeze kwa wingi siku ya Tarehe 24.03.2019 Saa 12:00 Jioni kuishangilia Timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) itakapokuwa ikicheza na Uganda kufuzu AFCON 2019

  • KATIKA kuwajengea uwezo Makatibu wakuu wa Klabu za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara,Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), liliendesha semina ya siku moja,iliyofanyika Machi 12,Dar es Salaam.

    Semina hiyo iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi,Steven Mnguto,lengo kuu lilikuwa ni ku-wanoa na kuwakumbusha watendaji hao wakuu wa klabu jinsi ya uendeshaji wa taasisi zao (klabu).

    Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya ligi,Mnguto,alisema ya kuwa semina hizo ni muhimu sana kwa watendaji wa klabu nchini,kwakuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto katika soka letu pamoja na kuwajengea uwezo zaidi Makatibu.

    Makatibu wa Klabu Ligi Kuu wapigwa msasa

    Kwa mara ya kwanza Tanzania imeingia kwenye his-toria,baada ya mwamuzi wa kike nchini Jonesya Rukyaa,kuteuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), kuchezesha michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya AFCON.

    Mbali na Rukyaa kupata nafasi hiyo ya kuchezesha mi-chuano hiyo mikubwa ya vijana,mwamuzi mwingine Mohamed Mkono naye ameteuliwa kupuliza kipyenga.

    Michuano hiyo ambayo,itafanyika nchini mwezi ujao kuanzia Aprili 14 hadi Aprili 28,itazishirikisha timu nane ambazo ni mwenyeji Tanzania,Senegal,Moroc-co,Guinea,Nigeria,Angola,Cameroon na Guinea.

    Rukyaa aandika historia AFCON U17

  • Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 20,Juma Mgun-da,ametaja kikosi cha wachezaji 26,ambacho kinatarajia kuingia kambini Machi 20,mwaka huu.

    Mgunda amekitaja kikosi hicho,ambacho kitaingia kambini kwa ajili ya kujiwinda na michuano mbalimbali ya kimataifa ya kirafiki inayotaraji kufanyika hivi karibuni.

    Wachezaji walioitwa katika kikosi hicho ni Ramadhan Kabwili (Yanga),Ali Salim (Simba),Zubeiry Masoud (Makongo Sekondari),Israel Mwende (Alliance),Nixon Kibabage (Mtibwa Sugar),Hans Msonga (Alliance),Ali Msengi (KMC),Muhsin Makame (Coastal Union),Habib Kyombo (Singida United),Mohamed Musa Kijiko (Coastal Union) na Rashid Juma (Simba).

    Wengine ni Dickson Job (Mtibwa Sugar),Mohamed Rashid (Singida United),Akram Muniri (Coastal Union),Jafari Mtoo (Arusha Academy),Abubakari Juma (Mtibwa Sugar),Najib Mohamed (Changanyikeni),-Said Musa (African Lyon),Nashon Naftari (JKT Tanzania),Kelvin Sospeter (KMC),Henrick Nkosi (Ndan-da),Hamis Kiza (Coastal Union), Asaad Juma (Singida United), Issa Abushehe (Coastal Union), Maurice Paul Sweya (Electrical FC - Ureno) na Super Jamhuri Kihwelo (AD Sanjoanese - Ureno)

    Kikosi cha U20 chatajwa

    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeandaa programu maalum ya mazoezi ya viungo (Soka Aerobic),ambayo itakuwa ikifanyika kila siku ya Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa Karume.

    Mratibu wa Programu hiyo,Jonathan Kasano,alisema kwamba wameamua kuanzisha programu hiyo maalum kwa ajili ya wa-namichezo wote ili kujenga miili yao na kujiweka vizuri kiafya.

    Alisema:Wanamichezo wote ambao wa-nataka kushiriki katik programu hiyo wanakaribishwa na ni bure,kwahiyo tun-awakaribisha tujumuike kwa pamoja.”

    Kasano amesema kwamba,program hiyo ambayo itakuwa ikifanyika kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa mbili,itafuatiwa na michezo mbalimbali ya Beach Soccer inayoendelea katika uwanja wa Karume.

    TFF yaanzisha program ya mazoezi ya viungo Habari za Beach Soccer

    Savannah BoysSix Home CityMburahati Fc

    Vingunguti Kwanza FcTanzania Prisons Fc

    Ilala Fc

    Kijitonyama Sands HeroesFriends of MkwajuniTabata Souls Sc

    Kisa FcBuza FcFriends Rangers

    Matokeo 16/03/20193 - 64 89 - 3

    4 - 73 - 45 - 6

    Matokeo 17/03/2019

  • Ligi Kuu ya Soka ya Vijana chini ya miaka 20,inata-rajia kuanza kutimua vumbi,katika viwanja mbalim-bali nchini kuanzia Aprili 7 mwaka huu.

    Michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini,itasimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kuviwezesha klabu katika ush-iriki wa michuano hiyo.

    Timu za vijana ambazo zitashiriki michuano hiyo zitakuwa ni zile ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tan-zania Bara na zitakuwa katika makundi manne am-bapo kila kundi kutakuwa na timu tano.

    Mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu yaan-zishwe mwaka huu ndio yanafanyika katika mtindo wa nyumbani na ugenini

    Ligi ya Vijana U20 kuanza Aprili

    KUNDI A1. Kagera Sugar2. Mbao FC3. Biashara United4. Stand United5. Mwadui FC

    KUNDI B1. Alliance FC2. Singida United3. Mtibwa Sugar4. Ruvu Shooting5. Coastal Union

    KUNDI C1. African Lyon2. Azam FC3. JKT Tanzania4. Ndanda FC5. Yanga SC

    KUNDI D1. KMC FC2. Mbeya City3. Simba SC4. Tanzania Prisons5. Lipuli FC

    MakundiLigi ya Vijana

    U20

    Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), inatarajia kuanza kushika kasi katika viwanja mbalimbali nchini kuanzia Machi 27 hadi Aprili 11,2019.

    Michuano hiyo itachezwa katika Mikoa ya Tanzania Bara,ipo katika hatua ya makundi na itachezwa katika vituo vinne ambavyo ni Simiyu (Uwanja wa Halmashauri Bariadi),Katavi (Uwanja wa Azimio Mpanda na Dodoma (Uwanja wa Mgambo-Mpwapwa).

    Katika Ligi hiyo,timu mbili za juu za kila kundi zitafuzu na kucheza hatua ya Nane bora katika kituo kitak-achotangazwa na TFF

    Wakati hatua ya nane bora itakuwa na makundi mawili yenye timu nne ambapo timu mbili za juu zitafuzu hatua ya Nusu fainali na baadaye Fainali.

    Patashika ya RCL kuanza Machi 27

    Kalenda ya Mashindano ya U15 na U17 Kuanzia April - JuniApril 01-30,2019Yatafanyika mashindano ya U15 na U17 katika ngazi ya Wilaya (Mashule,academy etc)kisha itachaguliwa timu ya kombaini ya Wilaya.

    Mei 01-25,2019Yatafanyika mashindano ya U15 na U17 katika ngazi ya Mkoa kisha itachaguliwa timu ya kombaini ya Mkoa

    Mei 15-28,2019Mikoa itadhibitisha ushiriki na usajili wake katika Ngazi ya taifa

    Juni wiki ya kwanza:Yataanza mashindano ya U15 NA U17 katika ngazi ya taifa

  • Ligi Kuu Wanawake

    Ligi Kuu Tanzania Bara

    1. Salum Iyee 142 . Meddie Kagere 123 . Haritier Makambo 114 . Said Dilunga 105 . Eliud Ambokile 106 . Ayoub Lyanga 97 . Vitalis Mayanga 88 . Amissi Tambwe 89 . Blais Bigirimana 710 . Emmanuel Mvuyekure 7

    Wanaoongoza kwa Ufungaji mpaka sasa.

    Matokeo ya Michezo iliyochezwa16.03.2019

  • Ligi Kuu Tanzania Bara

  • RATIBA YA MATUKIO YAJAYO

    Taifa Stars vs Uganda

    Twiga Stars vs DR Congo

    Total AFCON U17

    24.03.2019

    05.04.2019

    14 - 28.04.2019

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)Karume Memorial StadiumUhuru/Shaurimoyo Road P.O.Box 1574Telefax: +255 22 286 1815 Ilala - Dar es SalaamEmail: [email protected]: www.tff.or.tz

    27.03.2019 KMC FC vs African Lyon27.03.2019 Lipuli FC vs Singida United29.03.2019 Kagera Sugar vs Azam FC30.03.2019 Alliance FC vs Yanga SC

    Ratiba ya Kombe la Shirikisho Hatua ya Robo Fainali

    @tanfootball tfftanzania TFF TV