20
ubunifu zaidi ARUSHA TANZANIA JUNE 22-24 TANZANIA ADVENTIST INTERNET NETWORK 2015

2015 TAiN Presenters booklet

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Displays presenters topic, abstract and profile of Presenters of 2015 TAiN Meeting

Citation preview

Page 1: 2015 TAiN Presenters booklet

ubunifu zaidi

ARUSHAT A N Z A N I A

J U N E 2 2 - 2 4

TANZANIA ADVENTIST INTERNET NETWORK

2015

Page 2: 2015 TAiN Presenters booklet

KARIBU

TAiN 2015

Napenda kukukaribisha katika mkutano wa kwanza wa TAiN hapa Arusha Tanzania,TAiN ni kifupi cha maneno ya kiingereza yaitwayo Tanzania Adventist internet Network, maneno haya kwa tafsiri pana na yenye maana sahihi ni Mtandao wa Intaneti wa Waadventista Tanzania. Wazo la kuanzia TAiN lilianzishwa mwaka 2014 na Watanzania watano ambao ni Mch. Steven Bina, Mch. Musa Mika, Mch. Aston Mmamba, Mch. Christopher Ungani na Ndg. Gideon Msambwa, waliohudhuria mkutano mkubwa ya idara ya mawasiliano duniani ufahamikao kama GAiN jijini Baltmore nchini Marekani. Walifurahishwa na majadiliano ya mkutano ule wa GAiN na wakapendekeza kuanzisha mikutano ya namna ile katika nchi yetu ya Tanzania. Ndipo likazaliwa jina la TAiN.

Lengo kuu la mkutano huu wa TAiN ni kujadili ubunifu na njia za kisasa za teknolojia ya mtandao ili kutimiza utume wa kanisa la Waadventista wa Sabato.

Mikutano ya namna hii itaendelea kufanyika kila mwaka, Mwaka 2016 mkutano wa TAiN utafanyika Dodoma.

Ni matumaini yangu kwamba utaondoka katika mkutano huu wa TAiN ukiwa umejazwa mawazo mapya na roho mtakatifu atakuongoza kutumia njia za kisasa za teknolojia ya mtandao kumtumikia Mungu katika eneo lako la kazi.

Tuungane pamoja tuuambie ulimwengu Yesu anakuja tena

Gideon T. Msambwa

Mratibu wa TAiN 2015

tain.adventistafrica.orgfacebook.com/tainadventist

Page 3: 2015 TAiN Presenters booklet

WATOA MADA

UBUNIFU ZAIDI KATIKA KUPELEKA INJILI NA KULEA WASHIRIKI

Dr. Godwin Lekundayo

Pr. Steven Bina

Tunaishi katika ulimwengu uliojaa maarifa ya kila namna. Wakati watu wa dunia wanayatumia maarifa hayo kwa kufanikisha shughuli zao za Kidunia na wakati mwingine kufanikisha uovu, Kanisa lingeweza kuyatumia maarifa hayo hayo katika kufanikisha Upelekaji wa Injili na Malezi ya Washiriki. Ikiwa Kanisa lingejali kufanya hivyo, lingeweza kupeleka Injili kwa haraka zaidi na Kulea Washiriki katika namna ilio bora zaidi.

Ni Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu Kaskazini mwa Tanzania Ni mhitimu wa Uzamivu (PhD) katika fani ya ‘Missiology.’ Ni Mkuu (Chancellor) wa Chuo Kikuu cha Arusha. Pia ni Mchungaji wa Wachungaji mwenye upeo mkubwa wa kuelewa jinsi ambavyo Teknolojia inaweza kutumika kulisaidia Kanisa katika kazi ya Uinjilisti. Yeye hupenda kuhimiza mafunzo na ubunifu wa Kiteknolojia katika kazi ya Mungu kwenye Ofisi zote za Konferensi hii ya Kaskazini.

Steve Bina ni Mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato aliyewekewa mikono. Hivi sasa anafanya kazi katika Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati kama Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Uinjilisti kwa njia ya Satalaiti. Kabla ya majukumu yake ya sasa, amewahi kulitumikia kanisa kama mwalimu, mchungaji wa mtaa, mhariri wa nyumba ya uchapishaji, na mkurugenzi wa idara. Zaidi ya hayo amewahi kuwa Katibu wa Konferensi, Mwenyekiti wa Konferensi, Katibu wa Union na Mwenyekiti wa Union.Kiu yake kubwa ni kuona mafanikio makubwa zaidi ya upelekaji wa injili kupitia matumizi bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano .

MAKUSUDI NA SHUGHULI ZA IDARA YA MAWASILIANO

Kuna njia nyingi sana za mawasiliano zinazoweza kutumiwa na kanisa leo. Njia zenye ufanisi zaidi za kutimiza utume wa Kanisa ni vyombo vya habari na huduma za kiunjilisti zinapokuwa zimeunganishwa na wachungaji pamoja na washiriki.Kwa kuwa kazi ya idara ya mawasiliano ni kujenga madaraja ya matumaini, idara ya Mawasiliano ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, pamoja na Kituo cha Habari cha ECD imedhamiria kutumia njia hizi zote kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa wokovu kwa ulimwengu.

Page 4: 2015 TAiN Presenters booklet

Mr. Edward Onyango

Mrs. Jullie Ochieng

Ni mtaaluma katika teknolojia na mawasiliano. Amefunga ndoa na Jullie Ochieng, ambaye pia ni mkufunzi katika mkutano huu. Edward anafanya kazi kama Msaidizi wa Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, ECD. Pamoja na mapenzi yake makuu ya matumizi ya teknolojia ya habari katika utimizwaji wa utume wa Kanisa, yeye pia ni mpenzi wa simulizi za kiroho. Amehitimu stashahada ya Electrical and Electronics Engineering; pamoja na Shahada ya Kwanza ya Broadcast Journalism. Hivi sasa anafanya shahada ya Pili ya MBA in Information Systems Management.

KUZIKUBALI NJIA MPYA ZA KUTENGENEZA MAUDHUI

Wito wa Waadventista ni maalum sana kwa ajili ya kusimulia kisa cha Tumaini Kuu, Imani na Wema. Ingawa maudhui ya ujumbe wetu hayawezi kubadilika, hadhira yetu na mazingira yanabadilika siku baada ya siku. Ili kuufikia ulimwengu huu mpya ubadilikao kwa kasi, hatuna budi kubadilisha namna tunavyoandaa maudhui na ujumbe tunaotoa kupitia vyombo vyetu vya habari.

MAENDELEO YA TEKNOLOJIA! MITANDAO YA KIJAMII! MAVUMBUZI.

Ulimwengu unakimbia kwa mwendokasi mkubwa sana kupitia njiia mbalimbali. Tunaishi katika zama za jukwaa la tatu kinachounganisha kwa pamoja njia nyingi zaidi za mawasiliano. Kama Waadventista tunapaswa kuchagua zana sahihi za teknolojia zinazoweza kuleta tija katika ukuzaji wa ufalme wa Mungu.

Jullie amebobea katika taaluma za mbalimbali za habari na mawasiliano. Hivi sasa anafanya kazi kama mwangalizi wa wavuti ya Sekretarieti ya Divisheni na miradi maalum katika ofIsi za Divisheni

Page 5: 2015 TAiN Presenters booklet

Mr. Haggai Abuto

Pr. Musa MikaNi raia wa Tanzania mwenye uzoefu wa miaka 22 katika tasnia ya habari na mawasiliano. Amebobea hasa katika usanifu wa picha, uhariri, upangaji mikakati, ufasiri wa lugha, teolojia, utengenezaji wa programu za komputa, na sheria za habari na mawasiliano mtandaoni. Hata hivyo ana uzoefu wa uandaaji wa vipindi vya redio na televisheni.Amelitumikia Kanisa kama Mfasiri, Mhariri Mkuu, Mchungaji wa Mtaa na Mkurugenzi wa Idara.Ni mhitimu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania katika Shahada ya Uzamili ya Sheria za TEHAMA na Mawasiliano ya Simu. Utafiti alioufanya ulijikita katika Uhalifu Mtandaoni na athari zake kwa mfumo wa sheria za Tanzania.

Haki bunifu zinalinda mbunifu dhidi ya usambazaji, ubadili, na matumizi ya kibiashara visivyoidhinishwa, pamoja na wizi wa maandishi/mawazo.Ingawa ni vitu vya kugusika, ni raslimali zilizobuniwa na kutengenezwa na watu/kampuni, zaweza kununuliwa, kuuzwa, kuwa na hati ya kuzimiliki na kutumika kama dhamana kama raslimali nyingine yoyote.

HAKI BUNIFU MTANDAONI

Binadamu kwa asili, ni viumbe wanaohusiana. Kama vile ulivyo ulimwengu wa teknolojia ya mawasiliano, kanuni za jamii ya binadamu ni mfuatano wa sheria zilizofungamana na maelekezo ya jinsi mwanadamu apaswavyo kuishi anapokuwa amechangamana na wanadamu wengine.. Mifumo yote ina njia zilizobainishwa za matumizi sahihi kwa mifumo hiyo japo njia zisizofaa zinaweza kutumika wakati njia sahihi zinaeleweka. Ungana nasi tunapojadili usalama wa mtandao, yale upaswayo kuyafanya, na yale usiyopaswa kuyafanya.

Ni Meneja wa IT wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, Mtaalamu wa Sayansi ya Komputa na Mjumbe wa bodi ya Teknohama ya ADRA Ulimwenguni. amethibitishwa kuwa mtaalamu wa maadili ya udokozi wa Kiimtandao (Certified Ethical Hacker)

USALAMA WA MTANDAO

Page 6: 2015 TAiN Presenters booklet

TAARIFA YA KONFERENSI YA NYANZA KUSINI

TAARIFA YA KONFERENSI YA MASHARIKI NA KATI MWA TANZANIA

Pr. Christopher Ungani

Pr. Aston Mmamba

Ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Uchapishaji na Utume wa Waadventista katika Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania. Kabla ya majukumu haya, amewahi pia kulitumikia kanisa kama Mwinjilisti Mlei na baadaye, Mchungaji wa Mtaa. Anafurahia sana Uadventisishaji kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano. Mch. Christopher Ungani ni Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Teolojia (BATh) ya Chuo Kikuu cha Eastern Africa Baraton na Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Umma (MAMC) itolewayo na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania, inajumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro, Baadhi ya maeneo ya mikoa wa Pwani na Dar es salaam, pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja. Makao makuu ya Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania yapo mjini Morogoro.

Konferensi ya Nyanza Kusini, inajumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita na Simiyu. Makao makuu ya Konferensi ya Nyanza Kusini yapo jijini Mwanza.

Kwa sasa ni mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano ya Umma. Kanda ya nyanza Kusini (SNC)ni mhitimu wa BTh Bugema University na MTh Christian Life School of Theology.Amekuwa mchungaji,Mwalimu, Chaplin na mkurugenzi wa Idara katika Conference kwa miongo miwili sasa.Ni mpenzi na mdau wa Tekinolojia habari na mawasiliano. Kwa ajili ya Uinjilisti na malezi ya waumini amewahikuandaa vipindi katika Redio ya Waadventista Ulimwenguni (AWR), Na alifanikiwa kupitishia mahubiri yote ya Sattelite kutokea Kampala yaliyokuwa yanaongozwa na Dr. Ruguri katika Barmedas TV na vile vile ameandaa vipindi katika Star TV, Ana mke aitwaye Neema, na wamepata neema ya watoto wawili Safiness na Alfred.

Page 7: 2015 TAiN Presenters booklet

TAARIFA YA KONFERENSI YA NYANDA ZA JUU KUSINI MWA TANZANIA

TAARIFA YA KONFERENSI YA MARA

Pr. Haruni Kikiwa

Pr. Yoseph Otieno

Hivi sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na katika Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini, SHC. Kabla ya majukumu haya, amewahi pia kulitumikia kanisa kama Mchungaji wa Mtaa na Meneja wa Radio (AWR). Amehitimu Shahada ya Kwanza ya Teolojia (BATh) ya Chuo Kikuu cha Eastern Africa Baraton na Shahada ya Kwanza ya Mawasiliano ya Umma (MAMC) itolewayo na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.Anafurahia sana matumizi ya Facebook kama njia ya kupeleka injili na upashanaji habari.

Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania, inajumuisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Iringa,Rukwa na Njombe. Makao makuu ya Konferensi ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania yapo Jijini Mbeya.

Konferensi ya Mara, inajumuisha mkoa wote wa Mara Makao makuu ya Konferensi yapo Mjini Musoma.

Hivi sasa ni mkurugenzi wa mawasiliano katika konference ya Mara, pia amewahi kutumika kama kiongozi katika ngazi ya mtaa,konferensi na Union.Amehitimu shahada ya kwanza ya Theolojia BATh katika huko Andrews University (USA),MA in Pastoral Ministry Solusi University ( Zimbabwe) pamoja na Doctor of Ministry Andrews University (USA).

Page 8: 2015 TAiN Presenters booklet

TAARIFA YA KONFERENSI YA KASKAZINI MASHARIKI MWA TANZANIA

TAARIFA YA KONFERENSI YA KUSINI MASHARIKI MWA TANZANIA

Pr. William Sinyaw

Pr. Abraham YouzeNi Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Uchapishaji, Elimu na Utume wa Waadventista katika Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania. Kabla ya majukumu haya, amewahi pia kulitumikia kanisa kama Mwalimu na baadaye, Mkurugenzi wa idara ya Mawasiliano na Elimu SHC. Anafanya kazi kama Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Elimu na Utume wa Waadventista katika Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania, SEC.Amehitimu Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili ya katika maswala ya Elimu zitolewazo na Chuo Kikuu cha Eastern Africa Baraton.

Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania, inajumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Mtwara na Lindi. Makao makuu ya Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania yapo Jijini Dar es salaam.

Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania, inajumuisha mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara. Makao makuu ya Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania yapo Mjini Same.

Hivi sasa ni Mkurungenzi wa Mawasiliano katika Conference ya Kaskazini mashariki mwa Tanzania,Ametumika katika ngazi mbalimbali za Uongozi katika serikali na kanisa, Amehitimu Shahada ya Kwanza ya Theolojia, BATH Baraton University.

Page 9: 2015 TAiN Presenters booklet

KULEA NA KUTUNZA WASHIRIKI

Pr. Davis Fue

ACMS ni mfumo wa usimamizi wa makanisa ya Waadventista wa Sabato duniani, Mfumo huu unatunza

Mara nyingi Kanisa la Waadventista wa Sabato hujishughulisha sana nakutunza kumbukumbu za fedha kuliko kutunza kumbukumbu za washiriki, ikumbukwe kwamba kinachokwenda mbinguni ni washiriki sio fedha.

Ni Katibu Mkuu wa Unioni Konferensi ya kaskazini mwa Tanzania, Na mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Arusha. Pia ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD).

kumbukumbu za makanisa, washiriki, viongozi na wachungaji kuanzia ngazi ya kanisa mahalia hadi makao makuu ya kanisa duniani. Mfumo huu ndio mfumo rasmi wa kutunza kumbukumbu kwa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwengu mzima. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambayo inatumia mfumo huu kutunza kumbukumbu zake.

Mr. Gideon Msambwa Ni mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Unioni Konferensi ya kaskazini mwa Tanzania, mratibu wa ACMS (Adventist Church Management System) nchini Tanzania na mtengenezaji wa Programu tumishi za Nyimbo za Kristo na Ibada.

ADVENTIST CHURCH MANAGEMENT SYSTEM (ACMS)

Page 10: 2015 TAiN Presenters booklet

Pr. Lusekelo Mwakalindile

Mr. Mazara Matucha

Mada hii itajikita katika mambo ya muhimu katika mawasiliano yenye ufanisi. Kanuni za Msingi katika kuzungumza kupitia kwa redio, na sifa za habari (newstory) inayoweza kukubaliwa na Mhariri katika redio, na jinsi ambavyo redio na internet vinavyofanyakazi pamoja.

REDIO, INTERNET NA MAWASILIANO

Alijiunga na kazi ya Uchungaji mwaka 1992. Amefanya kazi kama Mchungaji wa mtaa kwa miaka miwili na nusu, Mwinjilisti wa vitabu kwa miaka miwili, Mkurugenzi wa idara ya uchapishaji wa Field kwa mwaka mmoja, Studio Manager na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Waadventista Ulimwenguni kwa miaka mitano na nusu, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Arusha, kinachomilikiwa na Kanisa la SDA kwa miaka mitatu, amekuwa akitumika Morning Star Radio (MSR) kwa miaka mitatu na nusu. Sasa yeye ndiye Mkurugenzi na Mhariri Mkuu wa MSR.

MSTV CHOMBO MAHUSUSI CHA UPENYAJI KATIKA ULIMWENGU UNAOWAYAWAYA

Tunaishi katika ulimwengu wa zama zilisemwa na manabii kuwa nyakati za mwisho. Wakati kukiwa na kiu na njaa kubwa ya neon, kuna uhaba mkubwa wa chakula cha kiroho hivyo kuwafanya wengi kufa kwa kihoro. Ujumbe wa zama hizi ni wa kasi ya kupaa. MSTV ni chombo muafaka kupenya kuta sizopitika, kuwafikia, kuwafundisha, kuwalea, kuwatunza na kuwaandaa kwa marejeo ya Yesu Kristo yaliyodhahiri kuliko hapo mwanzo.

Ni mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha Morning Star TV ambako kabla ya kuijunga alikuwa akitumika Katika Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania katika nafasi ya Meneja wa Mifumo ya Kompyuta. Kabla ya kujiunga na utumishi kanisani amewahi kufanya kazi na Africa Media Group limited kuanzia mwaka 2007 ambako alitumika kama Mhariri msanifu, Mtayarishaji wa Kipindi cha Click IT, na kisha meneja wa mifumo ya Kompyuta.

Page 11: 2015 TAiN Presenters booklet

UFUNUO PUBLISHING HOUSE

Pr. Tumaini Mahwago

Mch. Tumaini Mahwago ni Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Teolojia (BATh) ya Chuo Kikuu cha Eastern Africa Baraton na Shahada ya Uzamili ya Masomo ya Teolojia (MATh) itolewayo na Chuo Kikuu cha Lampeter (Kampasi ya Newbold).

Hivi sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Vijana na Chaplensia katika Konferensi ya Magharibi mwa Tanzania, WTC. Kabla ya majukumu haya, amewahi kuwa chaplain na mchungaji wa mtaa.

Mr. Ghuheni Mbwana

TAARIFA YA KONFERENSI YA MAGHARIBI MWA TANZANIA

Ni mtumishi katika kazi ya Bwana tangu 1978, Mungu amembariki na kumwezesha kupata Elimu ya juu katika utaalamu wa Graphic Design na Photography shahada ya kwanza.Kwa sasa anamalizia shahada yake ya Pili katika maeneo ya International Development na chuo chetu kikuu cha Andrews. Ndugu Mbwana ni mmoja wa watenda kazi ambaye ameiona na kutumia computer katika mabadiliko yake toka enzi za dos mpaka windows ya leo. Picha inabeba habari nyingi na ni hitaji lisilokwepeka leo.

Kiwanda cha Uchapishaji cha Ufunuo kilichopo Mjini Morogoro ndicho kiwanda pekee Nchini Tanzaniakinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato, Kiwanda hiki kimejipanga vizuri sana kutumia Teknolojia kuboresha na kuzalisha kazi zenye viwango vya hali ya juu.

Page 12: 2015 TAiN Presenters booklet

UNIVERSITY OF ARUSHA

MATOKEO YA MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI KWA MKRISTO NA KANISA LA LEO.

Pr. William Izungo

Mr. Joshua Ndege

Kwa sasa ni Afisa mahusiano ya Umma na masoko katika chuo kikuu cha Arusha ,Ni mdau wa TEKNOHAMA,ametumika katika kanisa la Waadventista wa Sabato katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na idara ya chaplensia pamoja na Canada Youth Challenge.

Chuo kikuu cha Arusha ni chuo pekee kinachomilikiwa na kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, Kinachotoa elimu kwafalsafa ya elimu kamilifu yaani Kiakili, kimwili, kimaadali na Kiroho.

Page 13: 2015 TAiN Presenters booklet

KULIUNGANISHA KANISA KWENYE MTANDAO

Mr. Kavishe Kavuta

r

Pr. Steven Letta

MATUMIZI YA MTANDAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI KWA KUBORESHA SHUGHULI ZA KANISA MAHALIA.

Mavumbuzi Katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, yanaliongezea Kanisa mahalia fursa nyingi zaidi za kurahisisha shughuli zake za kila siku. Hata makanisa yaliyo katika maeneo yasiyo na umeme, upo mlango kwa ajili yao.

Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Teolojia (BATh) ya Chuo Kiku cha Eastern Africa Baraton. Pia amefuzu na kupewa cheti cha Fani za Matumizi ya Komyupta toka Aptech International kilichomfanya kubobea katika matumizi ya kompyuta na mambo ya mtandao.Amelitumikia Kanisa kama Mchungaji wa Mtaa, Katibu Mkuu wa Konferensi, na hivi sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Shule ya Sabato Huduma, Huduma za Familia na Katibu wa Chama cha Wachungaji katika Union ya Kusini mwa Tanzania (STU)

Mhadhiri Chuo Cha Uhasibu Arusha kitengo cha Teknolojia ya habari na sayansi ya Kompyuta. Pia ni mtumishi wa MUNGU mzee wa kanisa la waadventista wa sabato Arusha Central.Elimu: Amesoma stashahada ya juu ya Teknolojia ya Habari (Advanced Diploma in Information Technology) – Chuo cha Uhasibu Arusha, Tanzania Na Shahada ya pili ya Sayansi Mawasiliano na Mitandao (Master of Science in Data Communication and Networking) - Chuo Kikuu cha Kingston, UK.

Kutumia teknolojia mpya na mbinu kuu za kiteknolojia vyenyewe haviwezi kufanya kanisa kukua. Lakini kutotumia teknolojia za kisasa katika kupeleka injili itasababisha kanisa lisiwe na uzoefu mkubwa wa kukua na kudumu katika kuleta mabadiliko ya ukuaji wa kiroho. Hivyo basi kanisa linatakiwa lisibaki nyumba katika kutumia mbinu za za kisasa za kiteknolojia zilizopo ili kuleta ufanisi zaidi katika ukuaji wa kiroho na kanisa kwa ujumla. Maeneo muhimu ya kuangalia ni kama kutumia wavuti, kuwa na database iliyounganisha na wavuti, kutumia program za simu za mkononi, na kompyuta katika mawasiliano

Page 14: 2015 TAiN Presenters booklet

TUZO YA JUMANNE S. MADUHU

MUSSA D. MIKA

2015Mwaka 2007 akishirikiana na wanafunzi wenzake watatu wakati anasoma Diplomaya IT katika Chuo Learn IT Institute of Business & Technology cha j i j ini Dar es salaa walianzisha Kipindi cha Maisha na Teknohama ambacho husikika Morning Star Radio kila jumapili saa 3:00asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi,kipindi hiki ambacho hutoa habari na maarifa mbalimbali yahusuyo teknolojia ya habari

na mawasiliano kimekuwa ni miongoni mwa vipindi vya Morning Star Radio vinavyopendwa na wasikilizaji wa rika mbalimbali na viwango vya elimu tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi bila kujali tofauti za imani na dini zao. Kipindi hiki pia kimewezesha kutambulika kwa wadau wa teknolojia ya habari na mawasiliano na wabunifu wa mifumo mbalimbali ya teknolojia ya habari na mawasiliano kanisani na nje ya kanisa hapa nchini toka taasisi za kanisa, wajasiriamali, watu binafsi taasisi za serikali hasa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia BUNI Innovation Hub, pia kushirikiana na Mtaalamu wa masuala ya usalama mtandaoni toka Wizara ya Mambo ya Ndani.Jumanne Maduhu kwa kushirikiana na wafanyakazi wenzake wa Morning Star Radio amefanikisha kuwezesha matangazo ya Morning Star Radio kusikika mtandaoni kupitia www.morningstaradio.or.tz na kwenye program tumishi ya Ustream, pia kuwepo kwa mfumo unaowawezesha wasikilizaji walioko Marekani kusikiliza matangazo kwa kupiga simu nambari 1518 800 1102.

Akiwa mtendaji mkuu wa Tanzania Adventist Media Centre (TAMC), 2011 – 2014.Walipanua Redio ya Morning Star Radio kutoa mkoa mmoja(Dar es salaam) hadi mikoa kumi (Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Tanga, Iringa, Musoma, Tabora, and Morogoro) ndani ya miaka miwili.Walifanya maandalizi ya kuanzishwa Morning Star TV kwa kuhuisha mpango mkakati, Kuutetea TCRA kwa mafanikio, kupata kibali cha kupewa lesseni ya Utangazaji, kuhamasisha fedha na kununua

vifaa, kuandaa studio na vipindi mpaka hatua za mwisho mwisho za maandalizi ya uzinduzi. Walianzisha kongamano za kila mwaka za matumizi ya TEHAMA katika utume kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.Walianza kuendesha semina kuwezesha makanisa ya Waadventista Tanzania kutengeneza Tovuti kwa mfumo wa netAdventist. Walianzisha utaratibu wa Kanisa kukutana na vyombo vya habari vya umma kila mwaka kwa nia ya kulitangaza Kanisa na kulinda taswira njema ya Kanisa.

Page 15: 2015 TAiN Presenters booklet

MORNING STAR TV

WAWEZA SIKILIZA MSR KATIKA SATELLITE KUPITIA MASAFA YA

ENDELEA KUSIKILIZA MORNING STAR RADIOMOROGORO 98.9 FM, MHzTANGA 104.1 FM, MHzMWANZA 102.1 FM, MHzMUSOMA 98.9 FM, MHzKIGOMA 103.3 FM, MHz

MBEYA 106.9 FM, MHzIRINGA 104.9 FM, MHzDSM 105.3 FM, MHzTABORA 102.9 FM, MHzARUSHA 102.5 FM, MHz

FREQUENCY 0.4 075 au 0407

SYMBOL RATE0.4 340 au 04340

Horizontal www.morningstaradio.or.tz

KOLWEZI 95.5 FMKISANGANI 107 FMGOMA 98.9 FMRWESI 103.5 FMBUKAVU 98.5 FMLUBUMBASHI 96.0 FM

(DRC)DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO

MORNINGRUNINGA IBADISHAYO MAISHA YAKO

JIPATIE KING’AMUZI CHENYE MORNING STARPIGA +255 769 070 714

SIKILIZA ADVENTISTWORLD RADIOKATIKA SHORT WAVES (SW)

PATA MASOMO YA BIBLIAKUTOKA SAUTI YA UNABII(VOP - Voice of Prophecy)

Page 16: 2015 TAiN Presenters booklet

ADDRESSLocation: University of Arusha is located 24 km from Arusha town to Usa-River trading center – Moshi road. From Usa-River the institution can be reached by taking Momela National Park road, a distance of 6 km from the main road. University has also a town center located in Mega Complex

(for Graduate Programs) and on Jacaranda Street, opposite Uhuru Primary School (Undergraduate Programs). The University also runs an Extension in Musoma.

Postal Address: P.O. Box 7 Usa River, Arusha, Tanzania.Telephone Numbers: (+255) 27 254 000 0 (+255) 27 254 000 3

E-mail:[email protected]; [email protected]: www.uoa.ac.tz

School of Education

Faculty of Business

and Human Resource

Entrepreneurship

with Education

Faculty of Theology

UNIVERSITY OF ARUSHA

LIST OF DEGREE PROGRAMS

Page 17: 2015 TAiN Presenters booklet

FOMU ZINAPATIKANAARUSHA – Shuleni Mariado/ Matto Stationery Arusha CCM Mkoa Dar es Salaam – Office za mawakili ya TM Law Chambers, Jengo la DDCKariakoo - Msimbazi Centre Room No. 19 (kwa mama Haleluya) - Magomeni SDA Church

Mwanza - Mr. Ntane 0784 491 774, Kuboja – 0765 4338 33 na kwenyemakanisa ya Wasabato (SDA)Mbeya – Dr. Mhaye 0754 297939, 0756 297339 na kwenye makanisa yaWasabato (SDA)Lushoto - Mwalimu Kilonzo 0782 549 597

USAFIRIShule italipia usafiri wa mtoto wako kuja shuleni na kurudi nyumbani chini ya usimamizi wa walimu wetu kutoka miji ifuatayo- Dar es Salaam- Mwanza- Shinyanga- Kahama- Mbeya- Lushoto - Tanga

MARIADO SCHOOLS ARUSHA

- Ni shule ya msingi hadi kidato cha sita, iko usa – river mkoani Arusha- Ni shule ya bweni, pia ya kutwa kwa wenye sababu maalum, ni mchanganyiko wavulana kwa wasichana- Shule inamilikiwa na kampuni ya mshiriki wa kanisa la S.D.A mjini kati – Arusha- Shule inaendeshwa kwa maadili na miiko ya kanisa la Waadventista wa Sabato

INAWEZEKANA- Una wasiwasi na tabia ya mtoto wako?- Unafikiri maisha ya mtoto wako ya baadaye yatakuwaje?- Unatafuta mwalimu mzuri, mcha Mungu kwa ajili ya mtoto wako?

TULETEE hapa MARIADO, hutajuta, kwa neema ya Mungu tumekusudia kufanya kitu kipya kwa mtoto wako na jamii:

ELIMU BORA, MALEZI MAZURI NA MAADILI MEMA KWA JAMII NA KWA MUNGU WA MBINGUNI

JENGA MAISHA YA MTOTO WAKO NA MARIADOAdvanced Level Combinations- PCM, PCB, CBG, PGM- HGL, HKL, HGE- ECA NA EGM

Huna sababu ya kumsindikiza mtoto wako unapoteza gharama na muda wako, walimu wetu wanafanya hizo kazi kwa niaba yako, unatukabithi mtoto wako mikononi mwetu nasi tunamrudisha mikononi mwako hapo ulipo kwa gharama zetu.

Tel: +255 767 796 262 /+255 715 796 262 Hotline 24 Hours: +255 784 796 262

Page 18: 2015 TAiN Presenters booklet
Page 19: 2015 TAiN Presenters booklet

DOWNLOAD IBADA APPDOWNLOAD NYIMBO ZA KRISTO APP

MADE IN TANZANIA

Page 20: 2015 TAiN Presenters booklet

TANZANIA ADVENTIST INTERNET NETWORK

2016 DODOMA