40

Al hikma vol 27

Embed Size (px)

DESCRIPTION

 

Citation preview

Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila Ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali. (Suratul Haj: 27)

MKURUGENZI MKUUMorteza Sabouri

MHARIRI Maulidi Saidi Sengi

WAANDISHI NA WATARJUMIFatma Ali Othmani

Mohammed BandalyMSANIFU WA KURASA

Maulidi Saidi Sengi

KAULI YA MKURUGENZIMorteza Sabouri................................................................................2IBADA YA HIJA

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mahujaji -1434 .................3Ibada tukufu ya Hija................................................…………….………..6Hija na umuhimu wake…………………..................................…..……….8HISTORIASiku ya Ghadir, tukio adhimu katika historia ya Uislamu …......11Kulitokea nini siku ya Ghadiri?.................................................13HABARI ZA SIASARais Rouhan ahutubia Baraza kuu la UN…...........................14Sisitizo juu ya haki ya nyuklia, ajenda kuu.............................15John Kerry: Tunaweza kuelewana haraka na Iran…................16HISTORIA YA UISLAMUUmuhimu wa kutafiti na kuhifahi Historia.......................……………17AFYAUislamu na Afya yako……………..................................................…….18JAMII / MALEZIMalezi mema kwa Watoto…..................................................………20MASHAIRILabbaykallahumma.......................................................................23JAMIIKiigizo chema…...............................................................................24Kigezo chema kutoka katika Familia ya Mtukufu Mtume ......….25VIJANAWeledi juu ya Mustakbali wa Vijana….......................................26KAZIUmuhimu wa Kazi Katika Uislamu........................................….28HISTORIA / SIKU YA ASHURAMalengo ya vuguvugu la Ashuraa….....................................…..30Nafasi ya mwanamke katika tukio la ashura.......................…34

MCHAPISHAJI

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran

FEHERESI

MTAYARISHAJI

Kitengo cha Uhariri na Usanifu

ANUANI:Al-Hikma Jarida Maridhawa

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran

S.L.P. 7898Dar es Salaam

Tanzania

2

Sifa zote ni zake Allah (s.w.t) Mola wa viumbe wote. Sala na salamu zimfikie Mtume Mtukufu

Mwaminifu, Aali zake watoharifu pamoja na Sahaba zake Wema. Kwa mara nyingine tena umewadia msimu wa Hija ulojaa Baraka na Rehema kwa kila aliyejaaliwa kwenda katika miadi hii. Allah awajaze kheri na Nuru Inshaallah.

Waislamu wanawake kwa wanaume wameitikia wito wa Muumba wao kwa kusema “Labbayka Allahumma Labbayka; Wito wangu kwa Mahujaji wote ni kuitumia fursa hii adhimu ya uwepo wao katika Nyumba hii Tukufu kwa kujiimarisha kiroho na kujipamba kwa sifa na matendo mema bila ya kusahau mshikamano na kudumisha udugu wa Kiislamu baina yao.Hija ni kambi ya malezi na Mafunzo ya kupambana na Shetani na kila aina ya ubaguzi kwa kuonesha umoja na mshikamano kwa kuwa nyote ni umma mmoja mliokusanyika mahali pamoja kwa lengo moja. Mwenyezi Mungu

(s.w.t) amepafanya mahala hapo kuwa ni makutano ya Waislamu wote bila ya kujali tofauti zao. Hijja ni mahali ambapo Waislamu wanapata fursa ya kukaa, kutafuta na kutafakari kwa pamoja namna ya kutatua masuala yanayowahusu na kuwasibu Waislamu na jamii kwa ujumla, na hasa kungalia ni kitu gani kinausibu ulimwengu wa Kiislamu kuingia katika yale yanayowasibu Waislamu leo hii ulimwenguni na nini mustakbali wake.

Hijja ni sehemu pekee ambayo Waislamu wataimarika kiibada na kupata fursa ya kujikurubisha kwa Mola Muumba kwa kutekeleza amali zote zilizotukuka mbele ya Allah (s.w.t,) kama kutufu al-Kaba, kwenda Swafa na Marwa na hatimaye kuelekea katika kisimamo kimoja cha Arafa ambapo hapo kila mmoja atapata picha halisi ya siku ya ufufuo kwamba wanadamu wote watasimama katika uwanja mmoja siku ya kiyama.

Hijja ni ibada inayofufua nyoyo zilizokufa na kuzijaza nuru kwa kumpwekesha Allah (s.w.t) na ni ibada inayomfanya mwanadam kupambana na nafsi yake na kila aina ya uovu kwa kuongeza nguvu na imani ya kukabiliana na adui yake mkubwa ambaye ni Sheteni.

Ndugu Waislamu, mambo mawili ni muhimu na ni faradhi isiyopitwa na wakati na haijalishi mahali ulipo; kuijenga nafsi na kuujenga umoja wa Kiislamu. Kuijenga nafsi huanza pale tu mja anapofanya juhudi za kupambana na hisia za kishetani na kujiepusha na madhambi (madogo na makubwa). Na kujenga umma wa Kiislamu ni pale Waislamu watakapotekeleza majukumu ya kidini na kutumia vizuri akili ya

kumjua adui ni nani, nini njama zake na namna ya kukabiliana naye. Hivyo basi wakati Waislamu wakawa ni wageni katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, ni wakati muafaka kwao kukaa na kutafakari kwa pamoja kwa kuwa wote ni umma mmoja kwani hapo watapata nafasi ya kuinua na kutia nguvu neno la UISLAMU na pia wataweza kuangalia na kujadili matatizo yanayowakumba Waislamu ulimwenguni na hasa ndugu zetu wa Syria.

Hili ni jukumu la kila Hujjaj kunyanyua na kutoa sauti yenye sura ya umoja dhidi ya Mustakbirin (mabeberu) wa nchi za magharibi na vibaraka wao kusitisha mara moja mauaji yanayoendelea nchini Syria ili kunusuru umwagaji damu za watu wasiokuwa na hatia hasa wanawake na watoto.

Ndugu Waislamu! Yanayoendelea leo nchini Syria na katika ulimwengu wa Kiislamu ni fedheha na aibu kubwa kwa nchi za Kiislamu kunyamaza au kuunga mkono waasi wanaopinga utawala halali wa Bashir al Assad.

Ni wajibu wetu kutambua ya kuwa tuna dhima kubwa ya kuzuia unyama unaoendelea nchini Syria kwa kutumia mkusanyiko huu ambao haupatikani isipokuwa mara moja katika mwaka, na kuna haja ya kutathmini hali za Waislamu ulimwenguniNawatakia Hijja iliyokubalika na Sa’y iliyoshukuriwa.

Wassalaam Alaykum warahmatullahi wabarakaatuh

Morteza Sabouri.

Kauli ya Mkurugenzi Bwana Morteza Sabouri

UTANGULIZI

3

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mahujaji -1434

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu na sala na salamu zimshukie Bwana wa

Manabii na Mitume wa Mwenyezi Mungu na Aali zake watukufu na masahaba zake wema.Kuwadia kwa msimu wa Hija kunapaswa kutambuliwa kuwa ni sikukuu kubwa ya Umma wa Kiislamu. Fursa kubwa inayoletwa na siku hizi

zenye thamani katika miaka yote kwa Waislamu duniani ni kemia inayofanya muujiza ambayo iwapo itathaminiwa ipasavyo na kutumiwa vizuri inaweza kutibu magonjwa mengi ya ulimwengu wa Kiislamu. Hija ni chemchemi ya baraka tele za Mwenyezi Mungu. Ninyi Mahujaji mliopata saada, mumepata fursa ya kuosha nyoyo zenu katika amali na ibada

hii iliyojaa usafi na umaanawi na kutumia hazina hii ya rehma, izza na qudra kwa ajili ya kujiwekea akiba ya umri wenu wote. Msimu huu wa ibada ya Hija ni shule ya kujifunza na kujistawisha ambayo ina masomo ya kuwa wanyenyekevu na kujisalimisha kwa Mola Mlezi, kubeba majukumu waliyopewa Waislamu na Mwenyezi Mungu, kufanya jitihada,

ه فمن فرض فيهن الج فل رفث ول فسوق ول جدال في الج وما تفعلوا من خير يعلمه اللـوتزودوا فإن خير الزاد التقوى واتقون يا أولي اللباب البقرة ١٩٧

IBADA YA HIJA

3

4

IBADA YA HIJA

nishati na harakati katika kazi za dini na dunia, kurehemeana na kusameheana katika kuamiliana na ndugu, masomo ya ushujaa na kujiamini katika kukabiliana na matukio mazito na kuwa na matumaini na msaada wa Mola Karima katika kila mahala na katika kila kitu. Kwa ufupi tunasema kuwa, msimu wa ibada ya Hija ni uwanja wa kujenga shakhsia ya mwanadamu kwa mujibu wa vigezo vya Kiislamu.

Kwa msingi huo mnaweza kujipamba humo kwa vito hivyo vya kiroho na kufaidika na hazina hiyo tukufu na kuchukua matunda yake kwa ajili ya nafsi zenu na zawadi kwa nchi, mataifa yenu na Umma mzima wa Kiislamu.

Hii leo Umma wa Kiislamu unahitajia zaidi wanadamu wanaoambatanisha pamoja amali, imani, usafi wa roho, ikhlasi, muqawama mbele ya maadui wenye vinyongo pamoja na kuijenga nafsi kiroho na kimaanawi. Hii ndiyo njia pekee ya wokovu wa jamii kubwa ya Waislamu kwa kipindi kirefu kutoka kwenye matatizo iliyotumbukia ndani yake ama kwa mikono ya adui au kutokana na udhaifu wa azma, imani na busuri.

Hapana shaka kuwa kipindi cha sasa ni kipindi cha mwamko na kupata utambulisho wa Waislamu; uhakika huu unaweza kuonekana waziwazi kupitia changamoto zinazozikabili nchi za Waislamu. Ni katika mazingira haya ndipo azma na irada inayoegamia kwenye imani, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, kuona mbali na tadbiri vinapoweza kuyapatia ushindi na fahari mataifa ya Waislamu katika changamoto hizi na kuyafikisha kwenye mustakbali wenye izza na utukufu. Kambi nyingine ambayo haiwezi kustahamili mwamko na izza ya Waislamu, imejitosa katika medani kwa nguvu zake zote na inatumia nyenzo zake zote za kiusalama, kinafsi, kijeshi, kiuchumi na kipropaganda kwa

ajili ya kuwatibua na kuwakandamiza Waislamu na kuwashughulisha wao kwa wao. Hali ya nchi za magharibi mwa Asia kuanzia Pakistan hadi Syria, Iraq na Palestina, nchi za Ghuba ya Uajemi, na vilevile nchi za kaskazini mwa Afrika kuanzia Libya, Misri na Tunisia hadi Sudan na baadhi ya nchi nyingine, inaweka wazi mambo mengi.

Vita vya ndani, taasubiri kipofu za kidini na kimadhehebu, machafuko ya kisiasa, kuenea ugaidi uliojaa ukatili, kujitokeza makundi na mirengo yenye misimamo ya kufurutu mipaka ambayo yanatumia mbinu za kaumu zilizokuwa zikiishi maisha ya kishenzi katika historia kama kupasua vifua vya wanadamu na kutafuna nyoyo zao.

Watu wanaobeba silaha wanaoua watoto na wanawake, watu wanaochinja vichwa vya wanaume na kuwabaka wanawake na wakati mwingine kufanya jinai hizo za kukirihisha na kuchafua moyo kwa kutumia jina na bendera ya dini, yote hayo ni matokeo ya mpango wa kishetani na kibeberu wa mashirika ya kijasusi ya wageni na tawala vibaraka wao katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ambayo yanatayarisha mazingira ya ndani kwa ajili ya matukio hayo na kuyaonjesha shubiri mataifa mbalimbali.

Ni wazi kuwa katika hali kama hii hatuwezi kutarajia kuwa nchi za Waislamu zitajaza mapengo yao ya masuala ya kimaanawi na kiroho na kupata amani, hali bora ya maisha na maendeleo ya kisayansi na nguvu ya kimataifa ambavyo ndiyo baraka za mwamko na kupata utambulisho wa Kiislamu. Hali hii ya maafa inaweza kuutia ugumba mwamko wa Kiislamu na kuharibu utayarifu wa kiroho uliojitokeza katika dunia ya Kiislamu, na kwa mara nyingine kuyatumbukiza kwa muda mrefu mataifa ya Waislamu katika mkwamo, hali ya kutengwa na

mporomoko na hatimaye kusahaulisha kabisa masuala muhimu ya Waislamu kama kadhia ya kuikomboa Palestina na mataifa mengine ya Waislamu kutoka kwenye makucha ya Marekani na Wazayuni.

Tiba mujarabu na ya kimsingi inaweza kufupishwa katika sentensi mbili muhimu ambazo zote ni katika masomo muhimu ya ibada ya Hija:Kwanza: Umoja na udugu wa Waislamu chini ya bendera ya tauhidi.Pili: Kumjua adui na kukabiliana na njama na mbinu zake. Somo kubwa la ibada ya Hija ni kuimarisha udugu na mshikamano.

Hapa, katika ibada ya Hija, inazuiwa pia kufanya ubishani na malumbano. Vazi la aina moja, amali za aina moja, harakati za aina moja na mwenendo wa upole hapa katika Hija vina maana ya usawa na udugu wa watu wote wanaoamini tauhidi. Hili ni jibu la wazi la Uislamu kwa kila fikra, itikadi na wito unaowaondoa katika Uislamu baadhi ya Waislamu na watu wanaoamini al Kaaba na Tauhidi. Watu

4

5

wenye fikra za kuwakufurisha Waislamu ambao wamekuwa wanasesere wa siasa za Wazayuni mahaini na waungaji mkono wao wa Kimagharibi ambao wanafanya jinai za kutisha na kumwaga damu za Waislamu wasio na hatia, na wale wanaojidai kushikamana na dini na kuvaa mavazi ya wanazuoni wa dini wanaochochea moto wa hitilafu kati ya Shia na Suni na wengineo mfano wao, wanapaswa kuelewa kwamba ibada ya Hija inabatilisha madai yao.

Mimi, kama walivyo maulamaa wengi wa Kiislamu na wale wanaoumizwa na masuala ya Umma wa Kiislamu, ninatangaza tena kwamba, kila neno au amali inayochochea moto wa hitilafu kati ya Waislamu, kuvunjiwa heshima matukufu ya mojawapo ya makundi ya Waislamu au kukufurisha moja kati ya madhehebu za Kiislamu ni kuhudumia kambi ya ukafiri na shirki na kusaliti Uislamu; na amali hiyo ni haramu.

Kumtambua adui na mbinu anazotumia ndiyo nguzo ya pili. Kwanza kabisa hatupasi kughafilika na kumsahau adui mwenye kinyongo, na marasimu ya kumpiga mawe mara kadhaa shetani katika ibada ya Hija ni nembo ya kukumbuka suala hilo daima katika fikra na akili zetu. Pili ni kwamba hatupasi kufanya makosa katika kumtambua adui yetu asili ambaye hii leo ni kambi ya ubeberu wa kimataifa na kanali ya watenda jinai ya Kizayuni.

Tatu ni kuwa, tunalazimika kuainisha vyema mbinu za adui huyo mkaidi ambazo ni kuzusha hitilafu kati ya Waislamu, kueneza ufisadi wa kisiasa na kimaadili, kutoa vitisho na vivutio kwa shakhsia na watu mashuhuri, kuweka mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya mataifa mbalimbali na kuzusha shaka katika imani na itikadi za Kiislamu na vilevile kuwatambua vibaraka na vikaragosi wao wanaowafanyia kazi kwa kujua au bila ya kujua. Madola ya

kibeberu yakiongozwa na Marekani yanaficha sura zao halisi kwa kutumia msaada wa zana za kisasa za vyombo vya habari na kutumia hila na ujanja mbele ya fikra za mataifa mbalimbali kwa madai ya kutetea haki za binadamu na demokrasia. Madola haya yanadai kutetea haki za mataifa ilhali mataifa ya Waislamu kila siku yanaona kwa macho na kuhisi kwa nyoyo moto wa fitina zao.

Tunapotazama taifa linalodhulumiwa la Palestina ambalo kwa miongo kadhaa sasa linaendelea kujeruhiwa kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na waungaji mkono wake, au katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Iraq ambako ugaidi uliotengenezwa na siasa za ubeberu na vibaraka wao umeyafanya machungu kama shubiri maisha ya mataifa hayo, au nchini Syria ambayo inashambuliwa na chuki za mabeberu wa kimataifa na vikaragosi wao wa kieneo na imetumbukizwa katika vita vya umwagaji damu vya ndani. Kwa dhambi ya kuunga mkono harakati ya mapambano dhidi ya Wazayuni, au Bahrain au Myanmar ambako katika kila mojawapo ya nchi hizo Waislamu wanaosumbuliwa na mashaka mbalimbali wamesahaulika na maadui zao wanaungwa mkono, au mataifa mengine ambayo yanatishiwa mara kwa mara na Marekani na waitifaki wake kushambuliwa kijeshi au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi au kukabiliwa na uharibu wa kiusalama, yote hayo yanaweza kuonesha vyema sura halisi ya vinara hawa wa mfumo wa ubeberu kwa walimwengu wote.

Shakhsia wa kisiasa, kiutamaduni na kidini katika maeneo yote ya ulimwengu wa Kiislamu wanalazimika kufichua uhakika huu. Huu ni wajibu wetu sote wa kidini na kiakhlaki. Nchi za kaskazini mwa Afrika ambazo kwa masikitiko makubwa zimekumbwa na hitilafu kubwa za ndani, zinalazimika

kuliko nchi nyingine, kutilia maanani wajibu huu adhimu, yaani kumtambua adui, mbinu na njama zake. Kuendelea hitilafu kati ya mirengo mbalimbali ya kitaifa na kughafilika na hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hizo ni hatari kubwa ambayo hasara zake kwa Umma wa Kiislamu haziwezi kufidika haraka.

Hatuna shaka kwamba mataifa yaliyosimama kidete katika eneo hilo linaloonesha kielelezo cha Mwamko wa Kiislamu, kwa idhini yake Mwenyezi Mungu, hayataruhusu mshale wa saa urejee nyuma na kurejesha kipindi cha watawala waovu, vibaraka na madikteta; hata hivyo ni wazi kuwa kughafilika na nafasi ya madola ya kibeberu katika kuzusha fitina na kuingilia mambo yao ya ndani vitatatiza kazi zao na kuchelewesha kwa miaka mingi kipindi cha izza, usalama na hali bora ya kimaisha.

Tuna imani kubwa na uwezo wa mataifa na nguvu iliyowekwa na Mwenyezi Mungu Mwenye hikima katika azma, imani na busuri ya watu na tumeiona na kuijaribu nguvu hiyo kwa macho yetu katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hima yetu ni kuyalingania mataifa ya Waislamu tajiriba hii ya ndugu zao katika nchi hii yenye fahari na isiyochoka.

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu arekebishe hali za Waislamu na kuwaepusha na vitimbi vya adui. Vilevile namuomba Mwenyezi Mungu atakabali Hija na kuwapa uzima wa mwili na roho na tunu kubwa ya kimaanawi ninyi nyote Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Sayyid Ali Khamenei.

IBADA YA HIJA

5

6

Hija ni ibada inayokusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa

Mola wake Karima. Ni shule ya kutoa malezi na maarifa kwa waja kwa msingi wa tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Safari ya Hija huanza kwa kuwekwa nia safi na ikhlasi na kukamilika kwa ibada na amali makhsusi.

Kwa mara nyingine tena imewadia safari ya uja na mapenzi kuelekea katika ardhi tukufu ya Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada tukufu ya Hija. Ni safari fupi lakini iliyojaa

nembo na siri kubwa. Ni safari ya siku chache lakini yenye matunda na manufaa makubwa mno. Ni safari ambayo wenye uwezo wa kifedha na kiafya ndio wanaoweza kuitekeleza baada ya kupata tawfiki ya Mwenyezi Mungu. Ni safari ya kuelekea katika kitovu cha Wahyi; ardhi ambazo ni mahala pa maarifa, mlima wa mahaba na mahala pa uja na unyenyekevu. Mbali na kutekeleza ibada ya kimaanawi na kisiasa ya ibada ya Hija, akiwa Makka hujaji hupata fursa ya kujionea athari muhimu za Uislamu. Katika safari hii ya kimaanawi Hujaji hupata nafasi

ya kunufaika kihistoria na kimaanawi na athari za Uislamu katika mji wa Makka na Madina. Kwa hakika al-Kaaba ni nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyobarikiwa na yenye uongofu. Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 96 ya Surat al-Imran kwamba, "Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ajili ya ibada ni ile iliyoko Makka, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote."

Wanahistoria wana kauli moja kuhusiana na kujengwa nyumba ya al-Kaaba katika zama za Nabii Adam AS. Imekuja katika kitabu cha Taarikh al-Yaaqubi kwamba, baada ya Nabii Adam kumaliza kujenga al-Kaaba alifanya tawafu. Katika kipindi chote cha historia, Kaaba ikawa ni mahala pa kufanya ibada manabii wengi wa Mwenyezi Mungu. Nabii Ibrahim aliamrishwa na Mwenyezi Mungu aikarabati al-Kaaba. Mwenyezi

Ibada Tukufu ya Hija

Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili, Radio Tehran

Bwana Mtume SAW anasema: Mwenyezi Mungu anajifakharisha na watu wanaofanya tawafu, na laiti ingelikuwa imeamuliwa kwamba, malaika wapeane mikono na mtu, basi wangepeana mikono na wenye kufanya tawafu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu.

IBADA YA HIJAIBADA YA HIJA

7

Mungu anasema katika aya za 26 na 27 za Surat al-Haj kwamba, "Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kut'ufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanaosujudu. Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali."

Hivyo basi Kaaba ni nembo ya wanatawhidi na wampwekeshao Mwenyezi Mungu na jambo hilo lilikuwa hivyo katika kipindi chote cha historia. Nafasi muhimu iliyobainishwa na Qur'ani kuhusiana na al-Kaaba ni ile hidaya na kuongoza kwake watu. Mwanzoni mwa Uislamu al-Kaaba hakikuwa kibla cha Waislamu. Kwa muda wa miaka kumi na tatu aliyokuwa mjini Makka na muda kidogo mjini Madina, Mtume SAW na wafuasi wake walikuwa wakisali ibada zao

wakielekea Baytul Muqaddas. Hii ni katika halia ambayo, wananchi wa Makka walikuwa wameigeuza Kaaba na kuwa nyumba ya waabudu masanamu. Nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaaba ina nafasi muhimu katika ibada za Kiislamu na vile vile uhai wa kijamii wa Waislamu. Waislamu kwa siku huelekea mara tano upande wa al-Kaaba wakati wa kusali.

Hii kwamba, kwa siku mamilioni ya watu usiku na mchana na kwa wakati maalumu tena kwa pamoja husali na kuelekea upande wa al-Kaaba, kwa hakika hili ni jambo ambalo huzifanya nyoyo za Waislamu kuwa pamoja na kuzikurubisha zaidi.

Mwenyezi Mungu amewataka Waislamu popote watakapokuwa kuelekea upande wa Makka wakati wa ibada zao, kwa sababu nyumba ya al-Kaaba daima inapaswa kuwa mhimili na kitovu cha kukusanyika wanatawhidi wote. Fadhila muhimu ya Al-Kaaba ni kuwa, nyumba hii, ni nyumba ya tawhidi na haina msukukumo mwingine usiokuwa wa Kimwenyezi Mungu katika kupatikana kwake na katika kuendelea kwake kuweko.

Mahujaji wakiwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu hufanya tawafu katika mahala ambapo malaika wanatufu na mahala ambapo Mitume wa Mwenyezi Mungu na mawalii wake walikuwa kando ya eneo hilo na kumhimidi Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume SAW anasema: Mwenyezi Mungu anajifakharisha na watu wanaofanya tawafu, na laiti ingelikuwa imeamuliwa kwamba, malaika wapeane mikono na mtu, basi wangepeana mikono na wenye kufanya tawafu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Kaaba ni

mahala pa amani na usalama kwa wanaadamu wote. Mwenyezi Mungu anasema katika Suratul Baqara aya ya 125 kwamba, "Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani."

Hivyo basi kila mtu atakayekuwa kando ya Kaaba, anakuwa yuko katika amani kimwili na kiroho na huwa na utulivu. Usalama na amani ya Nyumba hii ya Mwenyezi Mungu unatokana na dua aliyoiomba Nabii Ibrahimn AS kama inavyosema aya ya 126 ya Suratul Baqarah, "Na alipo sema Ibrahim:

Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho." Mwenyezi Mungu aliijibu dua ya Ibrahim AS.

Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana kwa karne nyingi, al-Kaaba imesalimika na shari ya waitakiao mabaya. Kisa cha Abraha na jeshi lake la askari waliokuwa wamepanda tembo ni jambo linaloweka wazi uhakika huu.

Abraha Aliyeandaa jeshi kubwa lililokuwa limesheheni tembo wengi ili kwenda kuivunja al-Kaaba na yeye mwenyewe alikuwa amempanda tembo mkubwa sana kuliko wote alikumbwa na hatima mbaya. Waarabu wa Makka waliliogopa sana jeshi lile. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu alilishushia jeshi la Abraha, jeshi la ndege lililodondosha mawe. Mtu yeyote aliyepatwa na jiwe alisagikasagika yeye na tembo wake na kuwa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa kama tunavyosoma katika Qur'ani.

IBADA YA HIJAIBADA YA HIJA

7

8

Msimu wa Hija ni machipuo ya Kiroho na kung'ara kwa Tauhidi katika upeo wa

dunia; na ibada ya Hija, ni chemchemi safi inayoweza kuwatakasa Mahujaji na uchafu wa madhambi na mghafala, na kurejesha ndani ya nyoyo na nafsi zao atia ya Mwenyezi Mungu ya nuru ya fitra na maumbile.

Kulivua vazi la majivuno na la kujipambanua na wengine katika makutano ya Hija, na kuvaa vazi la pamoja na la rangi moja la Ihramu, ni alama na nembo ya kuwa na hali moja umma wa Kiislamu, na ni hukumu ya dhihirisho la umoja na kuwa kitu kimoja Waislamu wa sehemu zote duniani. Upande mmoja wa Sha'ar ya Hija ni

ر وبش أسلموا فله واحد إله فإلهكم بتني ال

"Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimishieni Kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu." Na upande wake wa pili ni

والسجد الرام الذي جعلناه للناس سواء

العاكف فيه والباد

"Na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni." Na ndivyo hivyo, kwamba al Kaaba, mbali ya kuwa ni kiwakilishi cha kalima ya tauhidi, ni dhihirisho pia la Tauhidi ya kalima (neno la kumpwekesha Allah), udugu na usawa wa Kiislamu.

Waislamu waliokusanyika hapo kutoka pembe nne za dunia wakiwa na shauku kubwa ya kutufu al Kaaba na kuzuru Haram ya Mtume Muhammad SAW wanapaswa kuithamini na kuitumia ipasavyo fursa hii kwa ajili ya kuimarisha mfungamano wa kidugu baina yao, ambao ni dawa ya masononeko makubwa uliyo nayo umma wa Kiislamu. Leo hii tunajionea waziwazi jinsi mkono wa wasioutakia mema ulimwengu

wa Kiislamu unavyofanya kazi zaidi ya ulivyokuwa huko nyuma, ya kuwafarakanisha Waislamu. Na hii ni katika hali ambayo leo hii umma wa Kiislamu unahitajia mshikamano na kuwa kitu kimoja, zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma.

Leo makucha yaliyoroa damu ya maadui, yanaonekana hadharani yakiendelea kuleta maafa katika sehemu mbali mbali za ardhi za Kiislamu; Palestina iko kwenye mateso na madhila yanayoongezeka kila uchao, ya ukandamizaji wa kikhabithi wa Wazayuni; msikiti wa al Aqsa unakabiliwa na hatari kubwa; baada ya mauaji yale ya kimbari yasiyo na mfano, wananchi madhulumu wa Gaza wangali wanaendelea kuishi katika hali ngumu kabisa; Afghanistan iliyoko chini ya ukandamizaji wa kijeshi wa wavamizi, kila siku inapatwa na maafa na masaibu mengine mapya; wananchi wa Iraq wamekuwa hawana

IBADA YA HIJAIBADA YA HIJAIBADA YA HIJA

Imeandikwa na M. Baraza wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

HIJA NA UMUHIMU

WAKE

9

raha kutokana na machafuko na kukosekana amani nchini humo; na mauaji baina ya ndugu na ndugu nchini Yemen yameutia jeraha jengine jipya moyo wa umma wa Kiislamu.

Waislamu wa dunia nzima wakae na kutafakari, fitna na vita hivi, na milipuko na mauaji haya ya kigaidi na ya kiholela, ambayo yamekuwa yakijiri katika miaka ya hivi karibuni katika nchi za Iraq, Afghanistan na Pakistan yanatokea vipi na yanapangwa na kuratibiwa wapi?

Kwa nini hadi kabla ya uingiaji wa

kijeuri na wa kujifanya wamiliki, wa majeshi ya Magharibi katika eneo hili wakiongozwa na Marekani, wananchi wa mataifa haya hawakushuhudia misiba na masaibu yote haya?

Kwa upande mmoja wavamizi wanazipa harakati za mapambano za wananchi wa Palestina, Lebanon na maeneo mengine jina la magaidi, na kwa upande mwingine wanaratibu na kuongoza ugaidi wa kinyama wa kimapote na kikaumu kati ya mataifa ya eneo hili. Katika kipindi kirefu, na kwa zaidi ya miaka mia moja, nchi za eneo la Mashariki ya Kati na la Kaskazini mwa Afrika zilikuwa katika madhila, uvamizi na unyonyaji wa madola ya Magharibi,

ya Uingereza, Ufaransa na mengineyo, na baadaye Marekani; maliasili zao ziliporwa, moyo na hisia za kujihisi kuwa ni binadamu huru zilizimwa, na wananchi wao wakafanywa mateka wa uchu na tamaa za madola machokozi ya kigeni.

Na mara baada ya madhalimu wa kimataifa kung'amua kwamba haiwezekani tena kuendeleza hali hiyo kutokana na mwamko wa Kiislamu na harakati za mapambano za mataifa, na baada ya kuona kuwa suala la kuwa tayari kufa shahidi na katika njia ya Mwenyezi Mungu

limeingia tena katika damu ya Jihadi ya Kiislamu likiwa ni fikra madhubuti isiyo na mithili, (madhalimu hao wa kimataifa) waliamua kutumia mbinu za hila na ujanja, na hivyo ukoloni mamboleo ukachukua nafasi ya

mbinu za huko nyuma. Lakini leo hii zimwi lenye nyuso kadhaa la ukoloni, limeamua kutumia nguvu na uwezo wake wote ili kuupigisha magoti Uislamu kwa kutumia vikosi vya kijeshi, mkono wa chuma na uvamizi wa waziwazi, mlolongo wa kazi za kishetani za propaganda, maelfu ya mifumo ya uenezaji uwongo na uvumi; kuandaa makundi ya kufanya ugaidi na mauaji ya kikatili, kusambaza vitu vya kushamirisha ufuska na maovu ya kiakhlaqi; kueneza mihadarati na kuharibu azma, nyoyo na akhlaqi za vijana, kuanzisha mashambulio na hujuma za kisiasa za kila upande

dhidi ya ngome za mapambano, kuamsha na kuchochea ghururi za kikaumu na taasubi za kimapote, pamoja na kuanzisha uadui baina ya ndugu wa Kiislamu.

HIJA NA UMUHIMU

WAKE

IBADA YA HIJA

Nasaha zangu ninazozitilia mkazo kwa mahujaji wote waliopata saada, hususan maulamaa na makhatibu wa nchi za Kiislamu ambao wamehudhuria katika makutano haya matukufu, na makhatibu wa Ijumaa wa Haramain tukufu, ni kwamba wawe na uelewa sahihi wa hali halisi, na kulitambua leo hii jukumu walilo nalo linalohitaji kutekelezwa kwa haraka. Kwa uwezo wao wote wawabainishie wasikilizaji wao njama za maadui wa Uislamu, na kuwalingania watu wito wa upendo na umoja.

10

Ikiwa upendo, dhana njema na masikilizano yatatawala baina ya mataifa ya Kiislamu, madhehebu za Kiislamu na kaumu za Waislamu, badala ya dhana mbaya na kutizamana kwa jicho la uadui ambayo ndiyo matakwa ya maadui,

Waislamu wataweza kuzima sehemu kubwa ya njama na mipango ya wale wasiowatakia mema, na kutibua mipango yao miovu ya kutaka kuendelea kuuweka umma wa Kiislamu chini ya udhibiti wao.Hija ni mojawapo ya fursa bora kabisa kwa ajili ya kufikia lengo hili tukufu.

Waislamu waelewe kwamba kwa kushirikiana na kushikamana na misingi yao mikuu ya pamoja ambayo imeelezwa na Qur'an na Sunna wataweza kuwa na nguvu na uwezo wa kukabiliana na shetani hili lenye nyuso kadhaa na kulishinda kwa imani na irada zao.

Iran ya Kiislamu ni mfano dhahiri wa istikama iliyofanikiwa kutokana na kushikamana kwake na mafunzo ya Imam Khomeini (MA). Wameshindwa katika Iran ya Kiislamu. Kwa miaka thelathini sasa maadui hao wanafanya njama mbali mbali dhidi ya Iran ya Kiislamu. Kuanzia kujaribu kufanya mapinduzi hadi vita vya miaka minane vya kujihami

kutakatifu. Kuanzia vikwazo na kutaifisha mali hadi vita vya kisaikolojia na kipropaganda vinavyofanywa na vyombo vyao vya habari vilivyojipanga safu moja.

Kuanzia njama zao za kuizuia Iran isipate maendeleo ya kisayansi na teknolojia za kisasa kama vile teknolojia ya nyuklia hadi kufanya uchochezi na kuingilia waziwazi katika masuala ya uchaguzi uliofana kabisa wa hivi karibuni nchini Iran.

Lakini njama na vitimbi vyote hivyo vya maadui vimeshindwa na hivyo kuwalazimisha maadui hao wachanganyikiwe na wachukue maamuzi ya hasira na pupa. Kwa mara nyingine ile aya ya Qur'ani tukufu inayosema:

يطان كان ضعيفا إن كيد الشHakika vitimbi vya shetani ni dhaifu… imethibiti kivitendo na kwa uwazi kabisa mbele ya macho ya Wairani.

Katika sehemu nyingine yoyote pia, ambako istikama iliyotokana na azma na imani imewawezesha wananchi kusimama na kukabiliana na Waistikbari wenye majigambo, ushindi umewaendea waumini, na kipigo na fedheha imekuwa ndiyo hatima ya uhakika iliyowafika madhalimu. Ushindi wa dhahiri wa vita vya siku 33 nchini Lebanon na jihadi ya kujivunia na ya ushindi ya

Gaza katika miaka mitatu ya hivi karibuni, ni shahidi hai wa kuthibitisha uhakika huo. Nasaha zangu ninazozitilia mkazo kwa mahujaji wote waliopata saada , hususan maulamaa na makhatibu wa nchi za Kiislamu ambao wamehudhuria katika makutano haya matukufu, na makhatibu wa Ijumaa wa Haramain tukufu, ni kwamba wawe na uelewa sahihi wa hali halisi, na kulitambua leo hii jukumu walilo nalo linalohitaji kutekelezwa kwa haraka. Kwa uwezo wao wote wawabainishie wasikilizaji wao njama za maadui wa Uislamu, na kuwalingania watu wito wa upendo na umoja.

Wajihadhari sana na kila kinachosababisha Waislamu kudhaniana dhana mbaya; na kwa kadiri ya motisha waliyo nayo, na kwa kiasi wawezavyo kupaza sauti zao, wafanye hivyo dhidi ya Waistikbari, maadui wa umma wa Kiislamu na viranja wa fitna zote, yaani Uzayuni na Marekani na wadhihirishe kwa maneno na matendo yao kujibari na kujiweka mbali kwao na washirikina.

Kwa unyenyekevu, ninamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atupe mimi na nyinyi nyote uongofu, taufiki, msaada na rehma Zake.

Wassalaamu Alaykum

IBADA YA HIJA

10

11

HISTORIA / GHADIR KHOM

Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuhu Matukio makubwa na yenye kuleta ghera katika

historia ya dini au itikadi ni ishara ya uhalisi na ukweli wa dini hiyo na hivyo huongeza idadi ya wafuasi wake.

Tukio la Ghadir ni kumbukumbu kubwa na tukio la kihistoria lenye adhama ambalo liliainisha kigezo cha uongozi na hatima ya Ummah wa Kiislamu. Sisi hapa katika Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran tunachukua fursa hii kutoa salamu za kheria na fanaka kwa Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa siku kuu hii muhimu ambayo huahdimishwa tarehe 18 Dhul Hijja.

Sheikh Mufid, msomi mkubwa wa Kiislamu katika kitabu chake chenye anwani ya 'Kitab al-Irshad ameandika hivi: ‘Baada ya kujiri makabiliano ya Rasulullah SAW na Wakristo wa Najran katika tukio la Mubahala, Mtume alitekeleza hija ya mwisho. Kidogo kabla ya tukio hili, Mtume SAW alimtuma Ali bin Abu Talib hukoYemen ili apokee fedha ambazo Wakristo wa Najran walikuwa wameahidi kutoa. Imam Ali AS alielekea alikokuwa ametumwa na

Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume SAW hakumuamini yeyote isipokuwa Ali katika kutekeleza jukumuhilo na miongoni mwa watu hapakuwa yeyote aliyestahiki kupewa jukumu hili. Katika kipindi hicho, Mtume SAW alitoa tangazo la Hija na akiwa ameandamana na idadi kubwa ya watu, tarehe 25 Dhul Qaada aliondoka Madina.

Sambamba nahilo, Mtume SAW alimtumia Ali barua akiwaYemenna kumtaka aondokeYemenna aelekee Makka. Lakini hakuandika lolote kuhusu Hija yake na namna ya kuitekeleza. Ali AS akiwa na jeshi alilokuwa ameandamana

nalo hadiYemenalifunga safari na kuelekea Makka. Ali ambaye alikuwa na hamu na raghba kubwa ya kumuona Mtume kipenzi chake, alipokaribia Makka, alikabidhi jukumu la kusimamia jeshi kwa mtu mwingine na kisha yeye akaharakisha kumfikia Mtume kiasi kwamba alifanikiwa kukutana na Mtume SAW kabla hajaingia Makka.

Mtume alielezea kufurahishwa kwake kumuona Ali na hapo akamuuliza: "Ewe Ali ni kwa nia gani umefunga Ihramu?"

Ali alijibu kwa kusema: "Kwa vile sikujua ulitia nia gani, wakati wa kuvaa Ihramu nilisema: Ewe Allah, mimi naweka nia ya Ihramu sawa na ile aliyoweka Mtume Wako." Hapo Rasulullah SAW akasema: "Allahu Akbar, Ali kipenzi, hakika wewe ni mshirika wangu katika kutekeleza Hija, amali zake na kuchinja."

Hija hii ya mwisho ya Mtume ilikuwa mwanzo wa kuteuliwa Ali AS kuchukua nafasi ya Rasulullah SAW."

Katika Qur'ani Tukufu limeashiriwa suala la Uimamu na kupata uungaji mkono wa Mwenyezi Mungu. Aya ya 124 ya Surat Baqara inasema hivi kumshusu NabiiIbrahimAS:

Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema: "Wilaya ni ibara yenye maana kuhusu utawala katika Uislamu na ni kigezo cha mfumo wa kijamii na kisiasa katika Uislamu. Ubora na umaanawi wa duniani katika Uislamu uko katika Wilayah ya Allah SW

11

12

nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu.

Katika aya nyingine, wakati Nabii Mussa AS alipomuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kaka yake, Harun awe waziri na muungaji mkono wake, Mwenyezi Mungu alisema hivi kama tunavyosoma katika Surat Taha aya ya 36:

Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa!

Nabii Dawood AS vile vile ni kati ya mitume walioteuliwa kuwaongoza wanaadamu. Allah SWT anasema hivi katika aya ya 26 ya Surat Sa'ad:

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye njia ya Mwenyezi Mungu.

Tab'an katika Uislamu wilaya na uongozi haumaanishi tu kusimamia masuala ya maisha ya kila siku ya watu.

Uongozi katika Uislamu unamaanisha pia kuwaongoza kimaanawi watu. Katika kusimamia maisha ya wanaadamu Uislamu unazingatia pia suala la ukamilifu na kufikia uhakika.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema: "Wilaya ni ibara yenye maana kuhusu utawala katika Uislamu na ni kigezo cha mfumo wa kijamii na kisiasa katika Uislamu. Ubora na umaanawi wa duniani katika Uislamu uko katika Wilayah ya Allah SWT…Ni kwa sababu hii ndio katika mfumo wa Kiislamu Walii hajatenganika na watu…. Ghadir ni idi ya Wilaya, siasa na kuhusishwa wananachi katika utawala."

Katika tukio la Ghadir. Mtume Mtukufu wa Uislamu, ili kuhakikisha kuwa baada ya kuaga dunia kwake bahari tulivu ya jamii ya Kiislamu haikumbwi na dhoruba na vita vya kupigania madaraka na ili wenye kujitakia makuu wasitumie vibaya malumbano yanayoweza kuibuka na kwa upande wa pili kufuatia amri ya Mwenyezi Mungu, aliainisha atakayechukua nafasi yake kuongoza Ummah. Rasulullah

SAW katika mjumuiko wa umma na usio na kifani baada ya Hija katika eneo la Ghadir Khum, alimuarifisha Imam Ali AS kama mrithi na wasii wake. Katika kuonyesha nafasi ya juu ya chaguohilo, Mtume SAW alibainisha bayana kustahiki Ali nafasi hiyo kwa kusema:

“Enyi Watu! Jueni kuwa hakuna elimu yoyote iliyobakia isipokuwa Mwenyezi amenifunza nami pia nimemfunza Ali ambaye ni kiongozi wa watenda mema. Enyi Waislamu! Msiondoke kutoka katika njia ya Ali, msimuache na msipinge uongozi wake; kwani yeye atawaongoza wote katika haki na atatenda kwa mujibu wa haki, ataangamiza batili na atajiepusha nayo na katika njia ya Allah haogopi chochote.

Enyi Watu! Ali alikuwa mtu wa kwanza kumuamini Allah na Mtume wake, alijitoa muhanga kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na daima alikuwa na Mtume na hakuna aliyejisalimisha zaidi kumliko yeye mbele ya maamurisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Enyi Watu! Ali ni ndugu na mrithi wangu, mwenye kueneza elimu yangu, kiongozi wa umma wangu, mwenye ujuzi kuhusu tafsiri ya Qur’an, mwenye kuongoza watu kuelekea katika kitabu cha Allah SWT na mtekelezaji wa maamurisho ya Qur’an. Ali anatenda amali kwa ajili ya ridhaa yake Allah SWT, anapigana na maadui wa Mwenyezi Mungu na ni rafiki ya waja wa Mwenyezi Mungu na kuwazuia kumuasi Mola Muumba.” (Hotuba ya Ghadir).

Kabla ya tukiohilo, Rasulullah SAW pia alikuwa ametaja sifa za kipekee za Ali AS katika sehemu mbali mbali. Riwaya

ambayo imenukuliwa kutoka kwa Ibn Abbas, Hudhaifa na Aisha inabainisha kuwa miongoni mwa watu walioishi katika zama zake, Ali AS alikuwa kiumbe bora zaidi wa Allah SWT baada ya Mtume SAW. Hakuna ambaye angeweza kufikia takwa, ushujaa na uhodari wake. Jabbir bin Abdullah Ansari anasema: ‘Nilikuwa na Mtume SAW wakati Ali AS alipokuja. Mtume SAW alisema: ‘Naapa kwa mtu ambaye moyo wangu uko katika nguvu zake.

Huyu Ali na wafuasi wake katika siku ya kiyama watakuwa watenda mema.’ Katika hali hiyo ilishuka aya ya saba ya Surat Al Bayyinah inayosema:

‘Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio wabora wa viumbe.’

Tokea hapo kila wakati Masahaba zake Rasulullah SAW walipomuona Ali AS walikuwa wakisema Kheirul Bariya yaani mbora wa viumbe.

Kwa maelezo hayo, kwa kumuarifisha Ali AS, Ghadir ilipata thamani na nguvu na kuwa Idi kubwa ya Waislamu. Hii ni kwa sababu katika siku hii Allah alikamilisha dini yake na kutumiza neema zake kwa Ummah wa Kiislamu. Kwa hivyo kushukuru neema hii kubwa ni wajibu kwa Waislamu wote na ni kwa sababu hii ndio maana Waumini wanapokutana Siku ya Ghadir hukumbuka na kutamka dhikri ifuatayo:

بولیة کین التمس من جعلنا الذی ل المد

أمیر الؤمنین

Yaani Hamdu ni zake Allah ambaye ametujaalia kuwa miongoni mwa wale ambao wameshikamana na Wilaya ya Kiongozi wa Waumini Ali AS.

HISTORIA / GHADIR KHOM

13

Ghadir Khum ni sehemu iliyoko maili kadhaa kutoka Makka katika njia

inayoelekea Madina. Wakati Mtume (s.a.w) alipopita sehemu hiyo tarehe 18 Dhul’Hijja (10 March 632) wakati anarudi kutoka Hijja yake ya mwago (Kuaga), aya, “Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa...”

Iliteremshwa, kwa hiyo alisimama ili kutangaza kwa mahujaji ambao alifuatana nao kutoka Makka na ambao walikuwa watawanyike njia panda hapo kila mtu kuelekea sehemu yake. Kwa amri ya Mtume (s.a.w) mimbari maalum ilitengenezwa kwa kutumia matandiko ya ngamia kwa ajili yake.

Baada ya Sala ya mchana Mtume (s.a.w) alipanda mimbari na akatoa Khutuba yake ya mwisho mbele ya mkusanyiko mkubwa kabla ya kifo chake miezi mitatu baadae.

Sehemu ya kuvutia ya Khutuba yake, ni pale alipomchukuwa ‘Ali (a.s) kwa mkono wake, Mtume s.a.w. aliwauliza wafuasi wake iwapo yeye ana mamlaka zaidi (awla) kwa waumini kuliko wao wenyewe.

Kundi kubwa lile la watu likaitikia kwa sauti kubwa “Hivyo ndivyo ilivyo , Ewe Mtume wa Allah”. Kisha akatangaza: “Yule ambaye kwamba mimi ni (mawla) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali vile vile ni (mawla) mwenye mkumtawalia mambo yake. Ewe Allah, kuwa rafiki

kwa yule ambaye ni rafiki kwake, na uwe adui kwa yule ambaye ni adui kwake.” Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kumaliza khutuba yake, aya ifuatayo iliteremshwa:....Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni (juu yenu) neema yangu, na nimekupendeleeni (kwenu)Uislamu uwe ndiyo Dini.

Baada ya Khutuba yake Mtume (s.a.w) alimtaka kila mtu kula kiapo cha utii kwa Ali (a.s) na kumpongeza. Miongoni mwa waliofanya hivyo ni Umar bin al-Khattab, ambaye alisema: “Hongera Ali Ibn Abi Talib! Leo umekuwa bwana wa waumini wote wanaume na wanawake.”

Mwarabu mmoja aliposikia tukio la Ghadir Khum, alikuja kwa Mtume (s.a.w) na akasema: “Ulituamrisha tushuhudie kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah na kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah, tumekutii.

Umetuamrisha kusali sala tano kwa siku, tukakutii.Umetuamrisha kufunga (saumu) mwezi wa Ramadhani, tumekutii. Kisha umetuamrisha kwenda kuhiji Makka tukakutii. Lakini kukutosheka na yote haya yote ukamnyanyua binamu yako kwa mkono wako na ukamuweka juu yetu kama mtwala kwa kusema ‘Ali ni mawla wa yule ambaye mimi ni mawla kwake: je, amri hii yatoka kwa Allah au yatoka kwako wewe?”

Mtume (s.a.w) akasema: “Kwa jina la Allah ambaye ndiye Mola Pekee! Haya yanatoka kwa Allah, Mwenye nguvu na Mtukufu”. Aliposikia jibu hili aligeuka na kuelekea aliko ngamia wake jike huku akisema: “Ewe Allah! Kama asemayo Muhammad ni sawa, basi vurumisha jiwe juu yetu kutoka angani na tupatie sisi adhabu kali na mateso.” Kabla hajamfikia ngamia wake Allah alimvurumishia jiwe ambalo lilipiga juu ya kichwa chake na kupenyeza ndani ya mwili wake na kumuacha akiwa amekufa.

Ni katika tukio hili kwamba Allah (swt) aliteremsha aya ifuatayo:” “Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea. Kwa makafiri ambayo hapana awezaye kuizuia. Kutoka kwa Allah, Mola wa mbingu za daraja.” (Qur’an 70:1-3)

لم على من اتبع الهدى والس

Imetafsiriwa na: Dr M S KanjuKwa Hisani ya Alitrah Foundation. Tovuti: www.ibn-tv.org

HISTORIA / GHADIR KHOM

13

14

HABARI ZA SIASA

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amehutubia mkutano wa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Marekani na kutoa wito wa kuweko umoja ili kupatikana amani ya kudumu duniani. Rais Hassan Rouhani amesema kuwa suala linalopasa kuzingatiwa ni kuweko umoja utakaopelekea kupatikana amani ya kudumu duniani kote na si kufikiria suala la kuendesha vita katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Katika mkutano huo wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwa makini mazingira na hali ya mambo ya sasa kieneo na kimataifa, na kuwasilisha mapendekezo ya Iran kwa ajili ya kutatua mgogoro unaoikabili jamii ya kimataifa. Katika hotuba yake hiyo ya jana usiku, Rais Rouhani ameashiria pia vikwazo vya Magharibi dhidi ya Iran na kueleza kuwa vikwazo hivyo vinakiuka haki za msingi za binadamu

kama haki ya kuwa na amani, haki ya maendeleo, haki ya kupata huduma za afya, elimu na muhimu kuliko zote, ni ile ya uhai wa mwanadamu.Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Rais Hassan Rouhani amesema Iran si tishio kwa ulimwengu na kwamba Tehran iko tayari kufanya mazungumzo kuhusu miradi yake ya nyuklia katika mazingira ya uwazi kamili.

Amesema, kama alivyoeleza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, njia nyepesi zaidi ya kutatua kadhia ya nyuklia ya Iran ni kukubali haki ya kisheria, ya kimsingi na ya wazi ya Tehran katika uwanja huo.

Rais Rouhani amesema taifa la Iran liko tayari kushirikiana na jamii ya kimataifa na pande nyingine husika kwa msingi wa kuheshimiana pande mbili. Rais wa Iran amemtaka Rais Barack Obama wa Marekani kutounga mkono maslahi ya makundi

ya mashinikizo iwapo anataka kutatua hitilafu mbalimbali. Dakta Hassan Rohani ameuambia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba hakuna shaka kuwa Iran si tishio kwa ulimwengu, bali nchi hii ni sababu ya kupatikana amani na usalama katika eneo lililotumbukia kwenye hali ya mchafukoge. Ameongeza kuwa silaha za kemikali na nyingine za maangamizi ya umati hazina nafasi katika mfumo wa ulinzi na usalama wa Iran na zinakinzana na misingi ya kidini na kiakhlaqi ya taifa hili.

Rais Rouhan a h u t u b i a Baraza kuu la UN

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amehutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Marekani na kutoa wito wa kuweko umoja ili kupatikana amani ya kudumu duniani.

New York - Marekani:Kwa Hisani ya Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

15

HABARI ZA SIASA

Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye yuko New

York kwa ajili ya kushiriki kwenye vikao vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena amesisitiza juu ya haki ya wazi ya Iran ya kurutubisha urani.

Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Marekani ya ABC, Zarif ameeleza kuwa Iran iko tayari kufanya mazungumzo na kusisitiza kuwa Tehran haina haja ya kurutubisha urani kwa malengo ya kijeshi. Hata hivyo amesema kuwa haki ya Iran ya kurutubisha urani si suala la kujadiliwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa hakuna shaka yoyote kuwa

Iran haitaelekea upande huo wa kijeshi. Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo duru mpya ya mazungumzo kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA imeanza huko Vienna Austria ikiwa zimepita siku kadhaa tu kufuatia hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa sambamba na kufanyika mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na wa kundi la 5+1 huko New York.

Katika upande mwingine, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ameleekea Washington Marekani ambapo jana alikuwa na mazungumzo na Rais Barack

Obama wa nchi hiyo. Netanyahu ameweka wazi lengo la safari yake huko Marekani kwa kueleza kuwa kwa mara nyingine tena anataka kuithibitishia dunia kwamba tishio la nyuklia la Iran halijapungua. Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia hakukaa kimya na kuyaacha hivi hivi bila ya kuyapatia jibu matamshi hayo yasiyo na msingi ya upotoshaji fikra za waliowengi ya Netanyahu.

Bali Muhammad Javad Zarif ameyajibu matamshi hayo kwa kusema kuwa Israel ambayo ndio pekee inayomiliki silaha za nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati na tishio kwa amani na usalama wa dunia imehusika katika kuwaua kigaidi wasomi wa Kiirani bila kulalamikiwa na yoyote.

Sisitizo juu ya haki ya nyuklia, ajenda kuu ya mazungumzo ya

Iran na Magharibi ...Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia hakukaa kimya na kuyaacha hivi hivi bila ya kuyapatia jibu matamshi hayo yasiyo na msingi ya upotoshaji fikra za waliowengi ya Netanyahu...

15

16

Netanyahu na viongozi wengine wa utawala wa Kizayuni tangu mwaka 1991 wamekuwa wakidai kuwa umebaki muda wa miezi sita tu kabla Iran kuunda bomu la nyuklia. Zarif ameeleza kuwa Iran haitamiliki silaha za anyuklia si katika miezi sita, wala miaka sita au miaka sitini mingine. Hii ni kwa sababu Iran haina lengo la kumiliki silaha hizo hatari bali Tehran inaamini kuwa silaha za nyuklia ni kwa madhara ya usalama

wa nchi hii.Ni zaidi ya miaka kumi sasa ambapo utawala haramu wa Israel unafanya kila unaloweza ili kuishawishi Marekani iishambulie kijeshi Iran ambapo imekuwa ikitumia kila uwongo kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani ili kufanikisha lengo lake hilo. Licha ya kuweko ripoti bandia zilizowasilishwa na Israel kuhusu Iran, lakini inaonekana kuwa siasa za nje za Marekani hivi sasa ni

zile zilizojielekeza katika kujaribu kukurubisha misimamo ya nchi hiyo na ya ile ya Iran na kutambua kinagaubaga suala hili kwamba Iran ni nchi kubwa katika eneo na isiyopenda vita. Hata hivyo viongozi wa Marekani wanaelewa vyema kuwa ripoti zilizotolewa na upande wa Israel kuhusu Iran ni za uwongo na lengo lake ni kuzusha uchochezi dhidi ya taifa hili.

HABARI ZA SIASA

Serikali ya Marekani ni serikali ya kibeberu ambayo inajipa haki ya

kuingilia masuala ya ndani ya mataifa yote ya dunia.

Kadhia ya nyuklia inatumiwa kama kisingizio tu na nchi hiyo (Marekani) ili

kuendeleza uadui wake dhidi ya Iran.

Miamala ya kibeberu ya Marekani imeyafanya mataifa mengine duniani

kutoiamini hata kidogo nchi hiyo, kama ambavyo pia uzoefu umethibitisha kuwa

taifa na serikali yoyote inayoiamini Marekani mwisho wake hupata pigo hata

kama ni miongoni mwa mataifa rafiki wa Marekani.

Tangu zamani tulisema, hivi sasa tunasema na katika siku za usoni pia

tutasema kwamba, utawala wa Kizayuni ni utawala usio wa kisheria, bali ni

mwana wa haramu.

Kauli ya Kiongozi Muadhamu Ayatullahil Udh'ma Seyyid Ali Khamenei (D.I)

16

1717

Kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sasa nimekuwa nikifanya utifiti na kupiga picha

juu ya misikiti ya kale nchini Tanzania (ikiwemo Unguja na Pemba), kwa lengo la kujua historia ya Uislamu Tanzania. Katik utafiti huu nimejifunza mengi, lakini hali ya misikiti hiyo ya kale sio nzuri na inatia aibu Waislamu.

Japokuwa kuna maeneo ambayo yametengwa, na Serikali ya Muungano na ya Zanzibar, kuwa ni maeneo ya kihistoria na utalii, Kama vile Mikindani, Kilwa, Tongoni, na Pemba, lakini ukweli ni kwamba misikiti haitunzwi na hakuna dalili kuwa ukarabati utafanyika hii karibuni, na hata Mwakani.

Msikiti wa kala wa Mkambuu unaweza kuchukuliwa na bahari wakati wowote kama ambavyo visima vya maji vilivyoliwa tayari. Msikiti wa Mvita pale Mikindani (Pemba mnazi) umebaki jina tu, maana nje ndani umeharibika, na majani yanaunyemelea. Msikiti wa Ijumaa wa Pemba Mnazi, kwa kweli unatia aibu. Na msikiti yote hii ina umri wa zaidi ya miaka mia moja. Kituko kikubwa zaidi ni kule Bagamoyo. Nilikuwa napasaka mahali ambapo Bushiri-bin-Salim al-Harith (Mpinzani wa utawala wa Wajerumani), alipojenga Msikiti. Ilinitumia siku mbili

kujua mahala hapo. Na wazee wa Kiislamu wa miaka 65 na zaidi wa eneo hilo la Nzole walikuwa hawajui ulipo. Nilipofika eneo hilo nikakuta makaburi ya mama Muislam, Kaunde bin Mwalimu, anaonekana ni Mnyamwezi, liko chini ya mti wa mwembe halina historia wa tarehe. Ingawa niliambiwa hapo alikuwa akiishi Muarabu aliyekuwa tajiri sana miaka ya 1950. Nikakuta Msikiti uliobaki Nguzo nne tu.

Na nilipofika kwenye msikiti wa Bushiri, nikakuta hakuna kitu zaidi ya dalili ya ujenzi kuwa hapo paliwahi kuwa makazi. Japo kumetokewa Waislamu nisiowajua wamejenga msingi wa tofari tano kuzungukia msikiti ulivyojengwa. Na ndio mwisho. Na aliyefanikisha nikauona ni kaka wa Kisukuma, mhamiaji, ambaye hakuwa Muislamu.

Baadaye nikgundua kuwa kuna kijiji kinaitwa Utondwe, kusini ya Mji wa Saadani, ambacho kilikuwepo kabla ya miaka ya 1400. Kuwa kijiji hicho kilikuwa maarufu kwa Uislamu, biashara ya chumvi nawatu wake hodari kwa kupiga mishale vitani. Haya aliyaandika Bwana Al-Masood. Msafiri na mwandishi maarufu enzi hizo, na kushadidiwa na Ibn Batuta katika maandishi yake ya Periplus. Nilisafiri kwa pikipiki kwa kilo meta 50

kwenda na 50 kurudi. Nikaufikia msikiti huo wa Utondwe. Lakini nilisononeka, kwani msikiti ulikuwa katikati yam situ mkubwa. Hauna mtunzajji na kaburi la Imam na Binti yake yako vichakana. Kuna dalili kuwa kuna watu huenda kule kwa Hija na dua, lakini hakuna matunzo yoyote. Makuburi mengine yamefukiwa na mchanga, mengine yameliwa na mto Utondwe, na hakuna linguine.

Nina ushahidi wa picha kuwa maandishi ya kiarabu yaliyokuwa katika makaburi yalichukuliwa na watafiti wa kizungu, na hatuwezi kuyapata. Je Waislamu mnafikiriaje juu ya hili? Tumezembea kwa kudhani kuwa tunaweza kuaachia wasio sisi kutuandikia historia, na kututunzia pahala petu pa Ibada. Historia inaimarisha imani, na kuwasaidia waumini kujua wapi wametoka na wapi walipo, na nini kifanyike kuikuza imani yao. Wengi wa Waislamu wanajua wapi dini hii tukufu ilianzia, Maka, Madina na kwengineko.

Lakini hawajui dini hii ilikujaje Tanzania, na ilisambaaje kufika huko iliko sasa hivi. Na nani aliwajibika. Ni wajibu wa Waislamu wenyewe kufikiria mbinu bora ya kutunza amali hii muhimu.Wabilahi Tawfiq! [email protected]

Nina ushahidi wa picha kuwa maandishi ya kiarabu yaliyokuwa katika makaburi yalichukuliwa na watafiti wa kizungu, na hatuwezi kuyapata. Je Waislamu mnafikiriaje juu ya hili?

Umuhimu wa Kutafiti naKuhifadhi Historia ya Uislamu

Na: Mohamed Mustapha Kayoka

HISTORIA YA UISLAMU

Kauli ya Kiongozi Muadhamu Ayatullahil Udh'ma Seyyid Ali Khamenei (D.I)

18

Uislamu na Afya yako

Uislamu ni mfumo kamili aliyouweka Allah (swt) ili uwe ni muongozo kwa wanaadamu

katika kila nyanja ya maisha yao iwe kiroho au kimwili.Allah (swt) alimuumba mwanadamu na kumjalia kuwa na kiwiliwili na roho. Uhai na maisha mazuri yanategemea afya njema ya mwili na roho. Ni dhahiri kabisa kwamba mwanadamu anahitaji afya njema ili aweze kufanya kazi na ibada yoyote ile. Kwa hiyo katika maisha ya mwanadamu suala la afya ni la msingi, kiasi kwamba neema hii ikitoweka, basi neema zote zimetoweka. Hakuna mtu binafsi, jamii au taifa, linalopiga hatua ya maendeleo iwe kielimu, kiuchumi au kisiasa ikiwa linakabiliwa na tatizo la afya.

Kwa sababu hii tunakuta kwamba Qur’ani na pia Sunnah ya Mtume Muhammad (s) imezungumzia masuala ya afya na tiba kwa umuhimu wa pekee.Katika utangulizi huu tutanukuu baadhi ya aya na hadithi zinazozungumzia msingi huu muhimu wa mafanikio ya mwanadamu.

1-Uhai ni Amana ya Allah, lazima iheshimiwe na ihifadhiwe. Msingi wa Tawhiid unatufundisha ya kwamba muumbaji pekee ni Allah (swt). Yeye ndiye aliyeumba, na Yeye ndiye Mmiliki pekee wa uhai. Kwa sababu hiyo, Uhai ni amana na kila mtu ataulizwa namna gani alivyo chunga amana hiyo. Ni

haramu kabisa kwa mtu kujidhuru au kudhuru wengine. Ndani ya Qur’an, hizi ni baadhi ya aya zinazokataza kudhuru au kujidhuru kwa namna yoyote ile:Suratul Maida,5:32Kuuwa nafsi kwa kudhamiria ni sawa na kuua watu wote, na kuhuisha nafsi ni sawa na kuhuisha watu woteSuratul Nisaa, 4:93Kitendo cha kuua ni kibaya sana na hatari kwa uhai wa waliwengu kwa ujumla. Kwa sababu hiyo yeyote anayeua muumini kwa kudhamiria basi jaza yake ni ghadhabu na laana ya Allah na kukaa milele motoni.

Suratun Nisaa, 4: 29-30Kama ilivyo haramu kuua, pia mtu hana haki ya kujiua na kukata uhai aliyopewa na Allah (swt). Surah Baqarah, 2:195 Katika ayah hii, Allah (swt) ameharamisha mtu kujidhuru kwa njia yoyote ile. Sheria nyingi za Kiislamu zinazohalalisha au kuharamisha zinasimama kwenye msingi huu muhimu. Hata katika masuala ya ibada. Hii ni baadhi ya mifano: ni haramu -mtu kufunga, kuhiji, kuoga (kwa mwenye janaba) ikiwa kufanya hivyo kutasababisha ugonjwa au kuhatarisha maisha yake.-kupuuzia kutumia dawa au kwenda hospitali na baadae kudhurika na ugonjwa. Suratul An’am, 6:151/ Suratul Israa, 17:31/ Suratul Takwir, 81:8Katitka aya hizi Allah amekataza:- Mtu kumuua mtoto wake kwa sababu ya ufakiri, au kuogopa ufakiri-kuwaua watoto wachanga wa kike, kitendo cha kikatili kikifanywa zama za ujahilia, bara Arabu.

Ama katika Sunnah ya Mtukufu Mtume (s), ikiwa ndiyo tafsiri ya Qur’an, haikuacha kutilia mkazo mafunzo ya kuheshimu uhai na viumbe vya Allah (swt). Hizi ni baadhi ya hadithi:1-Miongoni mwa hadithi mashuhuri ni ile inasema: “kila mtu siku ya kiama ataulizwa kuhusu namna alivyotumia

Na: Sheikh Mulaba Saleh Lulat

Uislamu ni mfumo kamili aliyouweka Allah (swt) ili uwe ni muongozo kwa wanaadamu katika kila nyanja ya maisha yao iwe kiroho au kimwili.Allah (swt) alimuumba mwanadamu na kumjalia kuwa na kiwiliwili na roho. Uhai na maisha mazuri yanategemea afya njema ya mwili na roho.

AFYA

19

maisha yake, alivyotumia elimu yake, namna alivyochuma mali yake, na namna alivyotumia afya yake”.

2-hata katika hali ya vita, Mtume (s) alihimiza mafunzo haya ya msingi kwa kusema: “ msiue watoto, wanawake na vikongwe. Msiwaguse watawa katika nyumba zao za ibada, msikate miti, wala kuua wanyama (ila kwa chakula). Msiwaue majeruhi na waliojisalimisha...”3-katika ‘hijjatul wadaa’’ (hijja ya kuaga), Mtume akiwa Arafat alikumbusha na kuhusia msingi huu muhimu ambao ni nguzo ya ubinadamu, kwa kusema: “enyi watu, kama vile mnavyoutazama mwezi huu kuwa ni mtakatifu, na siku hii kuwa ni takatifu, na mji huu kuwa ni mtakatifu, basi hivyo hivyo tizameni uhai na mali na heshima ya kila Muislamu kuwa ni amana takatifu...”

2-Uhai ni Amana ya Allah: Lazima itunzwe na ihuishwe Uhai unahitaji kutunzwa na kuhuishwa kwa kuchunga misingi bora ya afya. Afya njema ni Neema ambayo mwanadamu anatakiwa kuishukuru kwa kuitumia vyema. Ili kuwa na afya njema tunahitaji:- Kujiepusha na kila kinachoharibu na kudhuru afya1. Mazingira

Mwanadamu anaishi katika mazingira ambayo ndiyo yanampa mahitaji yake yote ya maisha. Mwanadamu kama khalifa wa Allah ndani ya ardhi anajukumu la kuheshimu na kutunza mazingira anayoishi ndani yake. Leo suala la uharibifu na uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya maendeleo ya kisanyansi na kiteknolojia linathibitisha kwamba mwanadamu anaweza kujiangamiza ikiwa hataweza kuheshimu na kuchunga mazingira yake. 2. Chakula na lishe boraKila mwanadamu anahitaji chakula bora ili aishi. Zaidi ya chakula, anahitaji kuchunga adabu za kula. Bila shaka lishe duni ni tatizo, lakini tatizo la kula kwa ulafi na israfu ni kubwa zaidi. Hizi ni baadhi ya aya kuhusu umuhimu wa chakula na adabu za kula:1. Suratul Baqarah, 2:173Katika vyakula vilivyopo, mwanadamu anahitaji kula vilivyo vizuri tu. 2. Suratul Baqarah, 2:168Vyakula vya kuliwa ni vile tu vilivyo halali na vizuri3. Suratu Taha, 20:81Katika kula na kunywa, lazima kujiepusha na kufanya israfu.4. Suratul Rahman, 55:7-9Kusimamisha mizani na kujiepusha na israf ni kanuni ya msingi katika maisha ya mwanadamu.

3. Hali ya kinafsi Kuwa na matumaini, utulivu, furaha na kutosheka ni hali inayojenga afya ya mwanadamu. Ama kuishi na wasiwasi, hasira, chuki, kukata tamaa, ni hali inayoharibu afya na kusababisha magonjwa hatari. Aya nyingi zimehimiza kumuamini Allah na kumtegemea:Suratul Maa’rij, 70:19-35 Aya hizi zinaonyesha hali mbili za mwanadamu na matokeo yake. Mwanadamu ni mwenye pupa, akifikwa na shari anakuwa na wasiwasi, woga,

hana subira, na akipata kheri ni mchoyo na mwenye kuzuia wengine (hali ambayo inazaa wasiwasi na matatizo zaidi).Ama yule mwenye imani, ibada, akamuogopa Allah na kuamini atalipwa siku ya Qiyama, anaishi kwa utulivu, amani na mapenzi kwa wanadamu wenzake.-Kujenga mwili kwa mazoeziLeo ni dhahiri kwamba mazoezi ni njia muhimu ya kujenga afya na kujiepusha na maradhi mengi hatari. Zipo aya kadha zinaonyesha fadhila ya kuwa na nguvu, na kwamba wenye kufanya jihadi ni bora kuliko wenye kukaa. Jihadi ya aina yeyote inahitaji nguvu za mwili na uwezo. Mwili kuwa na nguvu unahitaji mazoezi.

Mtukufu Mtume (s) alitilia mkazo suala la mazoezi na kujenga mwili. Katika moja ya hadithi anasema: “wafundisheni watoto wenu kuogelea, kulenga mishale na kupanda farasi”.

-kutafuta tiba pindi maradhi yanajitokezaAllah (swt) aliyeumba kila kitu, alikipa kila kiumbe umbile na mfumo maalum. Patholojia (hali ya ugonjwa) inasababishwa na fiziolojia (utendaji wa mfumo) kuwa na matatizo (kuingiliwa, kuvurugwa, kasoro...). Mfumo huo unapoingiliwa au kuwa na kasoro, lazima hali ya ugonjwa inajitokeza.Mtukufu Mtume (s) alifundisha kwamba ‘kila ugonjwa una sababu na tiba. Hakuna ugonjwa isipokuwa Allah ameweka tiba yake.’ Aya nyingi zimezungumzia ubora wa baadhi ya vyakula na kutaja baadhi ya tiba kama vile Qur’an, funga, dua, asali... InshaAllah, katika makala zijazo tutazungumzia kwa mapana nyanja mbalimbali za afya katika Uisalmu.

AFYA

20

JAMII / MALEZI

Malezi mema kwa watoto...Kwa hali yoyote ile, ipo haja ya kutaja hapa kwamba, mazingatio ya Uislamu kwa watoto yameanza zamani na yanarejea nyuma zaidi ya miaka elfu moja na mia nne. Uislamu kwa mfululizo unaadhimisha na kuonesha huruma yake kwa mtoto, si baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla ya kuzaliwa, na umeelezewa kwa makini haki zake...

Wakati wa utoto katika Uislamu umepewa picha ya ulimwengu mzuri wa

furaha, uzuri, ndoto, mapenzi na ruya njema. Na aya za Qur'ani zinaonyesha mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa watoto, na ndipo akaapa Mwenyezi Mungu:"Naapa kwa mji huu, (wa Makkah). Na wewe utahalalishwa katika mji huu. Na (kwa) mzazi na alichokizaa." (90:1-3).Watoto wameelezwa katika Qur'ani kuwa ni bishara njema. Amesema Mwenyezi Mungu: "Ewe Zakaria tunakupa habari njema ya (kupata) mtoto jina lake ni Yahya…." (19:7).

Pia watoto ni kiburudisho cha macho yetu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Ewe Mola wetu, tupe katika wake zetu na watoto wetu watakaoyaburudisha macho yetu…."(25:74).Na watoto ni pambo la maisha katika ulimwengu huu: "Mali na watoto ni pambo la maisha ya duniani…." (18:16).Mtume (s.a.w.) anatudhihirishia ya kuwa ulimwengu wa utoto ni kama pepo,

pale aliposema: "Watoto ni vipepeo vya Peponi." Kuwatunza watoto ni jambo la lazima, na kuwapenda humleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.) amesema: "Lau kama si watoto wanyonyeshwao, na wazee wanaorukuu (kwa kuswali) na wanyama walishwao mashambani, basi mngelipatwa na adhabu kali."Inaonyesha wazi kwamba huruma na uangalifu wa Mwenyezi Mungu kwa watoto ndiyo uliofanya Mwenyezi Mungu kuzuia adhabu juu ya watu wake.

Kumjali mtoto hata kabla ya kuzaliwa:Kutilia maanani kwa Uislamu kuhusu malezi ya mtoto hakuanzi baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla hajaanza kupata umbo (tumboni) kwani Uislamu unamuamuru mtu kuoa mke mcha Mungu na mtulivu. Mtume (s.a.w.) amesema: "Jitahidi umpate mwenye kushikamana na dini, basi furaha zote ni zako."Uzuri, na utajiri si sifa pekee za kutosha kuchagua mke, sambamba

Na: Zahra Ally.

JAMII / MALEZI

20

21

na sifa hizo, pia mke ni lazima awe na sifa zingine, kwa mfano kumpata aliye na dini, na awe ametoka kwenye nyumba yenye mema. Kwa sababu watoto wake atakaowazaa mke huyo watarithi tabia, adabu na mwenendo wake. Mwenyezi Mungu amekataza kuoa mwanamke mzuri tu asiye na tabia nzuri na nidhamu. Mtume (s.a.w.) amekataza: "Jihadharini na wanawake wazuri wenye sifa mbaya."

Mtume (s.a.w.) ameweka mwongozo kwa mwanamke ambaye yu tayari kuolewa: atafute mume mcha Mungu, mwenye tabia za kidini, atakayeangalia jamii yake kwa ukamilifu, kutekeleza haki za mke, na kusimamia malezi ya watoto. Mtume (s.a.w.) amesema:

"Atakapowajia mtu mtakayeridhishwa na dini yake, na tabia yake, basi muozeni, ama msipofanya hivyo, mtaleta fitina na ufisadi mkubwa duniani."Hii inaweza kuonekana kwamba Uislamu umezitangulia (kwa uvumbuzi) kanuni za kisayansi na elimu ya 'tabia zinazorithishwa' (Heredity) kwa kuonyesha umuhimu ulioko katika sehemu ya urithi wa tabia, na namna gani uteuzi mzuri wa watu wawili wanaooana utakavyopelekea kupata watoto ambao ni tuzo la Mwenyezi Mungu na furaha ya maisha.Kwa kuwa mtoto atachukua mwenendo wa wajomba na shangazi zake, asili ya undani ya baba yake na mama yake, na akajifunza kupitia kwa urathi ambao

umepitia kutokana kwa muungano wa baba yake na mama yake, na ndipo Uislamu ukazitengeneza asili hizi kwa njia hiyo ili kumhifadhi mtoto awe ni kiumbe mwenye heshima na nidhamu, na hivyo kuepukana na upungufu wowote. Mara tu mtu anapoanza kufikiria kuoa na kutunza familia, Uislamu unamuongoza kupitia katika njia hizo.

Pendo la wazazi:Mtoto ni matokeo ya kimaumbile ya uhusiano imara wa wazazi, ubaba na umama ni matamko mawili ambayo Mwenyezi Mungu ameyazatiti kwa ihsani na mapenzi Yake, akayatajirisha na kuyapitia kwa maana ya kuungana watu wawili na kuendelea kuwa pamoja. Uhusiano wa karibu zaidi baina

ya wazazi na watoto wao, ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule wa kibinaadamu. Uhusiano huo umehifadhiwa na Mwenyezi Mungu, naye amehakikisha kuwa unaendelea na kustawi; kwa sababu kufanya hivyo ni kuendelea kwa jamii ya binaadamu na uhai. Upendo wa wazazi kwa watoto wao hauna nafasi yoyote ya kutia shaka, kwani ni alama ya Mwenyezi Mungu na ni neema Yake kubwa kwa walimwengu.

Mwenyezi Mungu amesema: "Na katika alama zake, ni huku kuwaumbia wake zenu, kutoka miongoni mwenu ili mpate utulivu kwao, na akajaalia mapenzi na huruma baina yenu." (30:21).

Mtume (s.a.w.) mara kwa mara alikataza kuwapendelea watoto wa kiume zaidi ya wa kike pasi na sababu yoyote, kwa maana hiyo, ndiyo akaipa daraja la juu heshima ya watoto wa kike na akaipa nguvu thamani na staha yao.Amesema Mtume (s.a.w.): "Bora ya watoto wenu ni mabinti."Mtume (s.a.w.) alipopewa habari ya kuzaliwa bintiye Fatima (a.s.), nyuso za maswahaba zilionekana kuparama, Mtume (s.a.w.) akawaambia: "Mna jambo gani linalowahuzunisha? (kumzaa Fatima) ni kama kupata ua la mrehani niunusao, na riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu."

JAMII / MALEZIJAMII / MALEZI

21

22

Baadhi ya wafasiri wameeleza 'penzi' na 'huruma' hapa, kwa maana ya mtoto ambaye ameupa nguvu uhusiano baina ya wazazi na ameupa amani na usalama. Familia ndicho kitu cha kwanza ambacho Uislamu unakichukulia kuwa ni cha kwanza katika jamii ya watu. Familia huunda nyoyoni mwao penzi lisilo na kikomo kwa watoto wao, penzi hili ni nuru waliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Mtume (s.a.w.) aliwaambia maswahaba zake na huku akiwaonyesha mwanamke akasema: "Je Mnaweza kufikiria kwamba siku moja mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanawe motoni?" Wao wakasema: "La", akasema: "Basi Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma zaidi kwa waja wake kuliko mama huyu alivyo na huruma kwa mtoto wake."

Basi haya ni maumbile, na ni aina ya pendo la kiasili ambalo hapana yeyote awezaye kulizuia au kushindana nalo, na kwa sababu hii ndipo Mwenyezi Mungu akawausia wazazi kuwaangalia watoto wao. Mwenyezi Mungu amefanya kuwapenda watoto na kuwahurumia ni sehemu ya maumbile ya kiasili ya kibinaadamu yasioepukika. Pia ameziingiza hisia hizi thabiti ndani ya nyoyo za wazazi.

Ni kwa ajili hii basi ndipo maelezo haya yote pamoja na wasia yameelekezwa moja kwa moja kwa watoto, kwa ajili ya kuwatendea wema na kuwapa heshima wazazi wao. Maelekezo haya amepewa mtoto ili kuzivutia hisia zake.Ni maelekezo ya hali ya juu ambayo yanategemeza uhusiano wa karibu na hisia ya kibinaadamu ambazo ndio sababu kubwa ya kuwepo kwetu duniani.Watoto wa kike:Kadri Uislamu unavyochukulia watoto kuwa ni kiburudisho cha macho yetu,

ni lazima hii idhihiri kwa vitendo na kwa njia zake. Usawa baina ya watoto hauna budi kutekelezwa hata katika kuwabusu. Uislamu unataka usawa ufanywe kulingana na maagizo yake matukufu. Siku moja Mtume (s.a.w.) alimwona baba ambaye alikuwa na watoto wawili, akambusu mmoja na kumwacha mwingine, kisha Mtume mtukufu akamuuliza: "Je huwezi kuwafanyia usawa?"

Tukiangalia mvuto wa kumpendelea mtoto mmoja zaidi ya mwingine au jinsia moja (wa kike au wa kiume) zaidi ya nyingine, hii ni kinyume kabisa na maadili ya Kiislamu, mila na fikra za usawa ambazo Uislamu umejengewa.

Uislamu hautofautishi baina ya mwanamume na mwanamke, wala hautofautishi baina ya mvulana na msichana. Wote sawa, hapana yeyote ampitaye mwenzake ila kutokana na baadhi ya sifa alizonazo kitabia alizojipatia yeye mwenyewe, Mwenyezi Mungu amesema: "Mola akawakubalia (maombi yao), ya kwamba mimi sipotezi amali ya mwenye kutenda, awe ni mwanamume au mwanamke, baadhi yenu kwa baadhi nyingine…."(3:195).Kwenda kinyume na misingi hii kunafuatia kwenda kinyume na fikra za usawa, maarifa, na haki. Kwa ajili hii, Uislamu unawaamuru

Waislamu kuwafanyia usawa watoto wao ili kwamba kusiwe na yeyote yule atakayekuwa na kinyongo au kusononeka. Kwa njia kama hiyo, Uislamu unazuia kuzagaa kwa chuki badala ya mapenzi, na kusema maudhi badala ya amani. Mambo haya iwapo yataendelea, hatimaye yataleta matatizo ya kinafsi, majonzi, na utengano, na haya yote huvunja hisia za moyo.

Mtume (s.a.w.) mara kwa mara alikataza kuwapendelea watoto wa kiume zaidi ya wa kike pasi na sababu yoyote, kwa maana hiyo, ndiyo akaipa daraja la juu heshima ya watoto wa kike na akaipa nguvu thamani na staha yao.

Amesema Mtume (s.a.w.): "Bora ya watoto wenu ni mabinti." Mtume (s.a.w.) alipopewa habari ya kuzaliwa bintiye Fatima (a.s.), nyuso za maswahaba zilionekana kuparama, Mtume (s.a.w.) akawaambia: "Mna jambo gani linalowahuzunisha? (kumzaa Fatima) ni kama kupata ua la mrehani niunusao, na riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu."

Hapa Mtume (s.a.w.) kwa ubaba wake mtukufu alijaribu kubadilisha mawazo ya watu ya kuwapendelea watoto wa..

itaendelea Toleo lijalo Inshaallah...

Kwa kuwa upendo wa wazazi kwa watoto ni sehemu ya maumbile yao (wazazi) ya kiasili, ndipo ikawa hapana haja ya kuagizwa juu ya jambo hilo, kwa hivyo Uislamu umetilia mkazo zaidi umuhimu wa 'matunzo' ya watoto na ukaonya vikali wazazi wasizembee katika jambo hilo, ili familia na jamii ziweze kuishi kwa raha na furaha.

JAMII / MALEZI

23

MASHAIRI

Al-Akh. Alhaaj Osan Omari Ngulangwa. (LILENGANE)' (DIWANI YA ALHAAJ OSAN). Nyaminywili, Rufiji. 1 Dhul Hijjah 1434 / 7 Oktoba 2013.

Naanza kwa kutamka, Jina lako ya Aleema. Ni msimu umefika, Uliojaa neema.

Niwezeshe kuandika, Maneno yenye hekima. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Naandika kwa hisia, Thawabu nikitaraji. Dua ninawaombea, Ndugu zangu mahujaji.

Ibada 'yende sawia, Haji is'ende na maji. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Labbaykallahumma, Wito wameuitika. Wamekuja hima hima, Arafah 'mekusanyika.

Wasamehe ya Raheema, Na wamwagie baraka. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Yaa Rabb Jalla Jalali, Muweza uso mipaka. Toba zao zikubali, Yaa Tawwabu Mtukuka.

Iwe haji maqbuli, Iwatakase hakika. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Kalamu naweka chini, Tamati nimefikia. Twakuomba yaa Dayyani, Kwako tukinyenyekea.

Tuliobaki nyumbani, Tuende kuhiji pia. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Madhambi waghufirie, Utusamehe na sisi. Na kamwe tusirudie, Maovu na kukuasi. Waja wema sote tuwe, Tuwafikishe Quddusi. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Nyumbani wakirejea, Warudi wamesafika. Moyo safi na tabia, Wazidi dini kushika. Wadumu katika njia, Sahihi ilonyooka. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Na sisi tujaalie, Twakuomba waja zako. Wepesi utufanyie, Tuizuru nyumba yako. Ameen tukubalie, Hakuna kigumu kwako. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

Rabb wewe nd'o pekee, kwake yote yumkini. Dua zetu zisikie, Yaa Wahabu yaa Muini. Hata mwenzangu na mie, Ahiji huko usoni. Labbaykallahumma, Usie na mshirika

LABBAYKALLAHUMMA..

24

Kiigizo chema

Wakati Waislamu wakishughulika na ujenzi wa Msikiti wa Mtume Muhammad

s.a.w mjini Madina , walikuwa wakibeba mawe na vifaa vingine mbali mbali vya ujenzi ili kukamilisha jengo la msikiti. Mtume s.a.w naye kwa upande wake hakubakia nyuma katika kazi hiyo tukufu, bali alikuja akawa anabeba mawe.

Kwa bahati alikutana na sahaba aliyekuwa akiitwa Usaid bin Khudhair ambaye alimwambia Mtume s.a.w kuwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu nipe miye jiwe hilo nilibebe.” Bwana Mtume s.a.w alijibu akamwambia: “Hapana wewe nenda kachukuwe jiwe jengine.” Ushiriki huu wa Mtume katika kazi ya kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa msikiti, ni dalili tosha inayotuonesha kuwa ujenzi wa msikiti ni jambo lenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, malipo ambayo Mtume s.a.w alikuwa akitaraji kuyapata kutokana na kazi hiyo.

Kadhalika kitendo hicho cha Mtume s.a.w ilikuwa ni njia ya kuwahamasisha wengine kuifanya kazi ile ya thawabu na ndiyo maana alimtaka Usaid bin Khudhair kubeba jiwe jengine, badala ya kumpokea lile alilokuwa amelibeba yeye.Mwenyeezi Mungu anasema: “Bila shaka mnacho kiigizo chema kwa Mjumbe wa

Mwenyeezi Mungu, kwa yule mwenye kumtarajia Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho na akamkumbuka Mwenyeezi Mungu kwa wingi.” Qur 33:21.

Kuwalea MayatimaMwenyeezi Mungu Mtukufu anasema: “Wanakuuliza (ewe Mtume) kuhusu mayatima. Waambiye: Kuwatendea mema ni bora. Na mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu…” Qur 2:120.

Bila ya shaka Uislamu ni utaratibu uliyo kamilika katika kila nyanja za maisha, kwani haukuwacha jambo lolote kubwa au dogo isiipokuwa umelishughulikia. Muundo wa jamii uliyomo ndani ya Uislamu, ni muundo unaojenga maingiliano kati ya makundi mbali mbali ya wana jamii.

Muundo huo wa jamii ndani ya Uislamu umepangika na hauna aina yoyote ile ya tofauti hasi. Kwa hali hiyo basi, kuwepo kwa mayatima ndani ya jamii kwa kawaida linaweza likawa ni jambo lenye kuleta mgawanyiko na hasa inapozingatiwa kwamba kundi la mayatima ni kundi lililo kosa walezi au halina mtu wa kuwaliwaza na kuwaonesha upendo na huruma.

Sheria tukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja ili kuweka utaratibu na

mwongozo wa jinsi ya kuwalea na kuwatazama vyema mayatima hawa, bali imeandaa malipo mengi kwa yeyote mwenye kusimamia kazi ya kuwalea mayatima, awe mwana mume au mwana mke.

Imamu Ali (a.s) Mlezi wa Mayatima .Katika mji wa Kufah pekee, Imam Ali bin Abii Talib alikuwa akiwalea mayatima zaidi ya mia mbili, na alikuwa akiwalisha kwa mkono wake mwenyewe na kuwaliwaza.

Inasimuliwa kwamba; katika kipindi ambacho yule mal-uun Ibn Muljim alipompiga Imam Ali a.s kwa upanga wenye sumu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, tabibu aliyekuwa akimtibu Imam a.s aliagiza yaletwe maziwa amnyweshe ili kumpunguzia athari ya sumu mwilini mwake.

Habari hizi zilienea mjini Kufah na mara ghafla mlangoni kwa Imam walifurika mayatima kwa wingi na kila mmoja akiwa amebeba maziwa na anataka kumpa Imam Ali a.s.

Usia wa Imam Ali a.s kuhusu Mayatima.Hapo kabla tumeona ya kwamba Imam Ali a.s alikuwa mlezi wa mayatima. Historia inatuonesha pia kwamba jambo hilo alilisisitiza mno mpaka mwishoni mwa

JAMII

Na: Musabah Shaaban Mapinda

JAMII

24

25

Kiigizo chemauhai wake hapa duiani akasema: “Allah Allah! Nakuhimzeni kuhusu mayatima, msiwaache na njaa na wala wasipotee mbele ya macho yenu (hali ya kuwa mnaona). Kwa hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu akisema: Yeyote mwenye kumlea yatima mpaka akaweza kujitegemea mwenyewe, basi Mwenyeezi Mungu amemuwajibishia pepo mtu huyo, kama alivyo wajibisha (adhabu ya) moto kwa mtu anaye kula mali ya yatima.”

Malipo ya wenye kuwalea Mayatima.Kuna hadithi nyingi za Mtume s.a.w na Maimamu zinazowabashiria kheri nyingi watu wanaofanya kazi ya kuwalea mayatima, na zinaeleza kuwa jambo hilo ni miongoni mwa mambo mema ambayo inawapasa watu

wote wake kwa waume kuisimamia kazi hiyo. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Maryamu Al ansari amesema: “Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu s.a.w amesema: Kwa hakika yatima anapolia Arshi tukufu (ya Mwenyeezi Mungu) hutikisika na Mola Mtukufu husema: Ni nani huyo anayemliza mja wangu niliye mnyang’anya wazazi wake wawili katika umri wake mdogo? Basi naapa kwa Utukufu Wangu hatamnyamazisha yeyote isipokuwa nitamuwajibishia pepo.”

Kuna hadithi nyingine iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Ja’far a.s amesema kuwa: “Mambo manne akiwa nayo mtu, basi Mwenyeezi Mungu atamjengea mtu huyo nyumba peponi: Mwenye kumlea yatima, na mwenye kumhurumia

mnyonge, na mwenye kuwahurumia wazazi wake wawili…..” Na ndani ya hadithi nyngine mashuhuri Mtume s.a.w.w anasema: “Yeyote mwenye kumlea yatima na akamlisha, basi mtu huyo atakuwa pamoja nami peponi mfano wa viwili hivi….” Mtume akaashiria kwa vidole vyake viwili cha kati na kile cha shahada.

Shime enyi ndugu wa kike na wa kiume kuhusu jambo hili lenye malipo makubwa mbele ya Mwenyeezi Mungu. Itumiyeni vizuri fursa hii tukufu ya uhai mliyo nayo, kwani ni yenye kupita kwa haraka mno, kama ambavyo umri nao unapungua kadiri siku zinavyo kwenda. Basi je! Ni kitu gani tulicho kiandaa kwa ajili ya siku hiyo ya kutisha inayo tungojea?

Imam (a.s) alikuwa ni mfano wa juu kabisa katika ubora, elimu, utoaji, sharafu, furaha na ukarimu, ibada,

unyenyekevu na tabia zingine nyingi njema, na alikuwa ni mfano wa kuigwa na kigezo chema kwa wengine, na alikuwa ni mwenye urefu wa wastani na mzuri wa umbile, mwenye uso mzuri na kiwiliwili cha wastani, mwenye heshima na hadhi kubwa kwenye nyoyo na mwenye nafasi ya juu na tukufu katika nafsi za watu, na Imam (a.s) alikuwa akimfanana sana babu yake Mtume (s.a.w) katika tabia zake na mwendo wake mwema na uzuri wa kuishi vema

na watu. Na miongoni mwa visa vya ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na Ismail kisemacho: Nilimkalia na kumsubiri Imam (a.s) katikati ya njia, alipo fika na kupita mahala nilipo kuwa nikamueleza ufukara wangu. Imam akasema (a.s): Unaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo kwani umefukia Dinari miambili chini ya Ardhi na kusema kwangu maneno haya si kwa sababu ya kuto taka kukupa, ewe ghulam (Mhudumu) mpatie ulicho nacho, akasema: Yule mhudumu akanipatia Dinari mia moja. Na kuna mtu mwingine alimwendea Imam-alipo

sikia ukunjufu wake na ukarimu wake-na alikuwa akihitaji Dirhamu mia tano, Imam (a.s) akampatia Dirham mia tano na kumuongezea Dirhamu zingine mia tatu. Na kwa hakika watu wote walitoa ushahidi na kuthibitisha ubora wake na ukarimu wake, hata wakiristo walimshuhudia (a.s) ya kuwa yeye anafanana na masihi (Yesu) katika ubora, elimu, ukarimu na miujiza yake, na Imam (a.s) alikuwa ni mwenye kufanya sana ibada, akisali sala za usiku (tahajjud) daiama na alikuwa ni mwenye mandhari ya wema, na mwenye heba kubwa.

JAMII

Kigezo chema kutoka katika Familia ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) Imam Hassan bin Ali Al-askariy (a.s)

25

26

VIJANA

una hotuba kutoka kwa Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema:“Mtu ambaye anatambua kwa ukamilifu kile kipindi ambamo yeye anaishi, kamwe hatazidiwa na kiwewe (cha mambo yaliyomzunguka yeye).”

Hii ina maana kwamba, yule mtu anayejua, ambaye anatambua na kuelewa ule wakati au kipindi ambamo anaishi, yeye hawezi kusumbuliwa na mkanganyiko au wasiwasi kuhusu mambo yanayotokea katika mazingira yake yanayomzunguka.

Katika Hadith hii Imam (a.s.) ametwambia kwamba, “Kama mtu anatambua mazingira yake basi hatasumbuliwa kamwe na kuchanganyikiwa na kiwewe juu ya yale mambo ambayo yanamzunguka yeye, kiasi kwamba kwa wakati anaangalia na kusahau hata mikono na miguu yake mwenyewe, na akawa hana uwezo wa

Weledi juu ya Mustakbali wa Vijana

Na: Hemedi Lubumba

kuzitumia nguvu na nishati yake mwenyewe wala hana uwezo wa kukusanya mawazo yake kuweza kutatua tatizo.” Hii kwa hakika ni Hadith mashuhuri sana.

Viko vifungu vya maneno vingi vyenye umuhimu kama hiki katika Hadith hii ingawa sikuvihifadhi vyote, hata hivyo mstari mwingine unasema kwamba: “Mtu ambaye hatumii akili yake hatakuwa mwenye kufanikiwa, na yule mtu ambaye kwamba hana elimu hataweza kuitumia akili yake.”

Maana ya akili ni nguvu au uwezo wa kuhitimisha na kuangalia jambo kwa mantiki na kuanzisha uhusiano kati ya hoja mbili – ikiwa na maana ya kutoa masharti juu ya jambo na kufikia uamuzi. Akili huchukua chanzo cha msukumo kutoka kwenye elimu na hivyo, akili

ni taa ambayo mafuta

Kizazi kipya mbinu mpya

K

VIJANA

27

Weledi juu ya Mustakbali wa Vijana

yake yanayoiendesha ni elimu. Hadith hii kisha inaendelea kusema: Hii ina maana kwamba, yeyote anayeelewa (jambo fulani), basi matokeo yake ni kwamba atakuwa na tabia njema na ya kuheshimiwa kwani matokeo ya hazina au bidhaa isiyo na thamani ya bei ni kupitia ile kazi inayoitanguliza mbele. Kwa hili ina maana kwamba tusiwe wenye kuiogopa elimu na ni lazima tusiifikirie elimu kuwa kama ni kitu ambacho ni cha hatari.

Hata hivyo kwa hali halisi, sisi ni maana tofauti kabisa na udhihirisho wa Hadith hii, kwani wengi wetu hatutambui zile zama ambamo tunaishi. Tumejikalia chini tu, bila ya kutambua mazingira yetu, huku tukisinzia. Wakati mmoja tunakabiliwa kwamba, kwa mfano, ardhi hii ni lazima igawanywe na kwamba ardhi hii ni lazima isafishwe na kulimwa (ili kuifanyia matumizi).

Bila kujua, inakuwa kana kwamba jambo hili (kuhusiana na usafishaji na ulimaji wa hiyo ardhi) linaanzisha machukizo juu yetu kwa vile hatuzitambui kabisa zile zama ambamo sisi tunaishi. Hatuna kule kuona mbali au makisio ya nini kinaweza kuja kutokea hapo baadae na hatukupanga lolote ili kuamua kwamba wajibu wetu utakuwa ni nini au ni kitu gani ambacho tunachotakiwa tuwe tunafanya.

Sisi, katika hali halisi, hatujui ni nini kinachoendelea katika ulimwengu huu na ni nini kinachofanyika nyuma ya mapazia. Tumekabiliana ghafla na suala la haki za kijamii za wanawake. Hapa, hatuna muda wa kutosha kufikiri juu ya hili na kuchambua vipengele vyake vyote ili kubaini umuhimu wake. Hivi wale wanaozitetea hizi haki za kijamii za wanawake wamedhamiria ukweli? Hivi kweli wanataka kuvutia mashabiki wengi?

Au kuna faida nyingine yoyote wanayonuia kuipata kutokana na kuibua masuala kama haya? Pamoja na haya, yatakuja kutokeza mambo mengine yenye mashaka na mageni yasiyojulikana kwetu sisi. Miaka sitini hadi mia iliyopita miongoni mwa nchi nyingine za ulimwengu, hili suala la kuwaongoza na kuwaelekeza vijana lilikuwa limekwisha kufikiriwa, wamekuwa wakishughulika sana katika kulitafakari na kulijadili jambo hili kuliko sisi tulivyo sasa.

Ni nini ambacho ni lazima kifanyike?Kile ambacho ni muhimu sana kuliko kuandaa mpango kwa ajili ya uongozi wa kizazi hiki ni kwamba, ni lazima tuziimarishe imani katika vichwa vyetu wenyewe kwamba uongozi na mwongozo wa kizazi hiki ni tofauti katika utaratibu na mbinu zake,

mwote katika vipindi mbalimbali vya nyakati, na unatofautiana kulingana vile vikundi vya watu ambao tunafanya kazi nao. Hivyo, ni lazima tuondoe kabisa yale mawazo kutoka vichwani mwetu, kwamba kizazi hiki kipya lazima kiongozwe kwa kufuata zile taratibu zilizotumiwa na vizazi vilivyotangulia.

Kwanza kabisa, ni lazima tukielewe vizuri kabisa hiki kizazi kipya, na Kufahamu ni aina gani za sifa bainishi na tofauti ambazo wanazo. Kuhusiana na kizazi hiki, kuna namna mbili za fikira ambazo ni za kawaida, na kwa kawaida kuna njia mbili ambazo zinaweza zikashughulikiwa kwazo.

Kutokana na maoni ya baadhi ya watu, vijana hawa ni kundi la watu ambalo lisilojali na fidhuli, ambao wamedanganywa na kupendezwa mno na tamaa zao duni. Wao ni wenye kuabudu nafsi zao na wana maelfu (mengine) ya mapungufu. Hawa watu (wanaofikiria hivi juu ya kizazi hiki kipya) wakati wote wanawafinyia nyuso na kila mara wanazungumza vibaya juu ya kizazi hiki.

Hata hivyo, vijana hawa wanajiona wenyewe kama wako kinyume kabisa na hali (picha) hii. Vijana hawajioni wenyewe kama ni wenye mapungufu

VIJANAVIJANA

28

Kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kumkabidhi Mola Mlezi kazi zetu, hakuna maana

ya kwamba, mwanaadamu akae na kubweteka na kuacha kunufaika na suhula za kimaumbile zilizoko kwa ajili ya kufikia malengo yake. Kutawakali

kwa Mwenyezi Mungu hakuna maana ya kutozishughulisha suhula zilizoko ambazo kimsingi ziko kwa ajili yetu.Mja muumini, hutawakali kwa Mwenyezi Mungu na hufadhilisha kumtegemea Mwenyezi Mungu Muumba badala ya kuwategemea asiyekuwa Yeye.

Mwenyezi Mungu anazungumzia suala la kutawakali kwake katika Surat ya Aal Imran aya ya 159 kwa kusema: «Na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.» Katika aya hii Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume Wake kwamba, baada ya kukata shauri kwa maana kwamba, baada ya kutathmini hali ya mambo na jambo lenyewe na kuandaa suhula za lazima, basi ifanye kazi hii hali ya kuwa unatawakali na kumtegemea Mola Muumba.

Ayatullah Murtadha Mutahhari msomi mtajika katika ulimwengu wa Kiislamu anasema: «Mafuhumu ya kutawakali ni mafuhumu na fasili hai. Yaani kila mahala ambapo Qur'ani Tukufu inataka

yoyote. Wao wanajidhania kuwa ni sanamu (picha) la akili, sanamu la busara, sanamu la sifa za hali ya juu kabisa. Kizazi cha zamani kinafikiri kwamba kundi hili limeangukia kwenye utovu wa maadili na kwamba limetumbukia kwenye dhambi, ambapo hicho kizazi kipya kinadhani kwamba kizazi cha zamani wana akili nyepesi (mapunguani) na wajinga wasiojua kitu.

Kizazi cha zamani kinawaambia kizazi kipya kwamba wamejishusha wenyewe kwenye kuabudu nafsi zao wenyewe na wamekuwa watovu wa maadili, ambapo hicho kizazi kipya kinawaambia kizazi cha zamani kwamba wao hawakijui kile ambacho wanakisema na kwamba hawawaelewi! Kuzungumzia

kwa kawaida jinsi mambo yalivyo, inawezekana kwamba kizazi kimoja kinaweza kukiona kizazi kilichotangulia kana kwamba ni watu wenye haki lakini pia inawezekana kwamba wakawaona kama waliopotoka.

Vijana wa Kisasa:Kizazi chetu kichanga cha leo kina sifa zote nzuri na kasoro kadhaa ndani yao. Kizazi hiki kina mlolongo wa uelewaji na hisia ambazo vizazi vilivyotangulia havikuwa nazo na kwa hiyo, sisi lazima wakati wote tuwape faida ya mashaka yao. Wakati huo huo, wao wanayo mawazo potovu na sifa bainifu za kimaadili za kinyume ambazo ni lazima ziondolewe kwenye tabia zao. Haiwezekani kuziondoa sifa bainifu hizi kutoka kwao

bila ya kuzingatia na kuziheshimu zile sifa nzuri ambazo vijana hawa wanazo – kwa maana ya kwamba, kule kuelewa kwao na hisia zao, na sifa bainifu zao bora na tabia hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwao kuhusiana na haya.

Hakuna mwisho kabisa katika maisha. Katika vizazi vilivyotangulia, mawazo na akili za watu hazikuwa wazi kama za kizazi cha sasa. Hisia hizi na sifa nzuri hazikuwepo kwa watu wa siku za nyuma, na kwa hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwa vijana kwa ajili ya sifa zao bora – na ni Uislamu wenyewe, ambao umeonyesha heshima kwenye sifa bainifu hizi.

Umuhimu wa Kazi Katika Uislamu

VIJANA / KAZI

29

kumfanya mwanadamu afanye kazi na kumuondolea woga na hofu, humwambia kwamba, tawakali kwa Mwenyezi Mungu na umtegemee Yeye. Songa mbele na ufanye hima.»

Mafuhumu na fasili ya kweli ya kutawakali ni kwamba, mwanadamu anapaswa kumfanya Mwenyezi Mungu Muumba kuwa tegemeo na kiegemeo chake cha pekee na kuwa na imani nae kamili na wakati huo huo atake msaada na kutumia suhula na nyenzo zote za kidunia ambazo ni nyenzo za kimaada kwa ajili ya kuboresha maisha yake. Na mtu mwenye kutawakali anapaswa kufahamu kwamba, nyenzo zote za kimaada ziko kwa ajili ya mwanadamu kwa mujibu wa mipango na irada ya Mwenyezi Mungu.

Katika mazingira kama haya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu hakuwezi kuwa sababu na hoja ya kuacha kufanya kazi na hivyo kuukumbatia uvivu.Katika Qur'ani Tukufu tunasoma kisa cha Dhul Qarnein na kuona jinsi gani alivyotumiwa nyenzo zote za kimaada alizopatiwa na Mwenyezi Mungu katika kupambana na dhulma na uonevu. Hata alipofanikiwa kujenga kizuizi cha chuma baina ya watu na maadui alisimama na kusema:''Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu Mlezi. Na itapofika ahadi ya Mola wangu Mlezi atauvunja vunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni kweli tu».

Wakati mwingine mtu huandaa mipango kwa ajili ya kazi fulani na kuchunguza vizuri engo na pande za kazi hiyo na kidhahiri hupata natija kwamba, hakuna kizuizi cha kumfanya ashindwe kuifanya vizuri kazi hiyo na kufikia malengo aliyoyakusudia iwe ni kazi ya biashara au kazi ya ujenzi na kadhalika. Hata hivyo hutokea tukio dogo tu ambalo huja kuvuruga mahesabu yake yote na hivyo kuifanya kazi yake

kutokuwa na natija. Hii inatokana na kuwa, elimu ya mwanadamu ina mipaka na mwanadamu hana habari na matukio au mishkili tarajiwa. Zaidi ya hayo, wakati mwingine mwanaadamu anapoamua kufanya kazi fulani au anapokata shauri kuiacha huwa hana habari ya maslahi yaliyoko katika kazi hiyo.Kwa mtazamo wa dini, mwanaadamu hukabiliwa na hakika yenye matumaini nayo ni kwamba, Mwenyezi Mungu ndiye mtawala mutlaki wa ulimwengu na hekima na elimu isiyo na kikomo iko kwake. Mola Muumba ana uwezo wa kufanya kazi zote na vile vile ana ufahamu juu ya maslahi ya kweli ya waja wake. Hatua ya mja ya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu mwenye sifa hizi humfanya ujudi wake ufungamane na nguvu isiyo na kikomo. Mja anayetawakali kwa Mwenyezi Mungu hushuhudia na kuona nguvu za Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu katika kazi na mambo yake na hunufaika na nguvu maalumu.

Marhumu Allama Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai mfasiri mkubwa wa Qur'ani Tukufu anaandika hivi kuhusiana na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu:«Wakati mwingine mwanadamu akiwa nia ya kufikia lengo lake fulani, huingia katika medani na kuona kuwa anayo

mahitaji yote ya lazima, lakini baadhi ya sababu za kiroho kama kuwa na irada inayotetereka, woga, pupa na tajiriba ndogo huingia baina yake na kazi husika.

Kama mtu atatawakali kwa Mwenyezi Mungu katika mazingira kama haya, irada yake huwa na nguvu, azma yake huwa thabiti na vizingiti vya kiroho huondoka. Kwani mwanadamu akiwa na hali ya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu huungana na chemchemi ya mambo yote yaani Mwenyezi Mungu na kwa muktadha huo, wasi wasi na vishawishi hutoweka.» Kutawakali kunamfanya mtu awe na ujasiri wa kufanya jambo na kwa hatua hiyo hufanikiwa kuondoa vikwazo na viziuzi vyote viwe vya kifikra au kimuamala.

Mtu mwenye kutawakali kwa Mwenyezi Mungu sambamba na kutumia nyenzo na suhula zilizoko katika maisha kwa ajili ya kazi na kufanya hima ili kufikia lengo lake, huwa na imani kwamba, Mwenyezi Mungu atamsaidia kufikia lengo lake kupitia suhula au kupitia njia nyingine ambayo mwanadamu hawezi kuifikiri wala kuitasawari.

Kwa msingi huo tunapaswa kusema kuwa, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu hakuna maana ya mtu kujishughulisha tu na ibada, dua na kunong'ona na Allah na hivyo kuacha kufanya kazi.

KAZI

Imepokelewa kwamba, «siku moja Bwana Mtume SAW alishuhudia kikundi fulani cha watu ambacho hakikuwa kikijihusisha na kazi. Mtume akawauliza: Mnaendesha vipi maisha yenu? Watu wale wakamjibu kwa kusema, sisi ni watu wanaotawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Baada ya Bwana Mtume S.A.W.W kusikia kauli yao hiyo akawaambia: «Nyinyi sio mnaotawakali kwa Mwenyezi Mungu bali nyinyi ni mzigo katika jamii.»

29

30

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

Malengo ya vuguvugu la Ashuraa.

Mapema sana baada ya kifo cha Mtume wa mwisho, Mtukufu Muhammad s.a.w, muasisi

wa usawa na uhuru, Uislamu ulikuwa kwenye hatari ya kutoweka kwa sababu ya matendo mabaya na mkengeuko wa Bani Umayyah. Uadilifu ukiwa umewekwa chini ya nyayo za madhalimu. Ni katika hatua hii kwamba Hussein (a.s) alianzisha mapinduzi makubwa ya Ashura.

Utawala duni wa Bani Umayyah ulikuwa ukijaribu kutoa picha ya uislamu kama mfumo wa kidhalimu na muasisi wake kuwa mtu mwingine zaidi ya ulivyokuwa. Fikiria kuwa Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko katika vikao vya pombe na kamari? na tena kwa aina ya kipekee , mrithi huyo wa Mtume wa Allah anaongoza sala ya jamaa msikitini? Hii ilikuwa ndiyo hatari kubwa iliyoutikisa uislamu na hili ndilo lililomfanya Bwana wa mashahidi asimame kupinga hali hiyo.

Suala hilo halikuhusika tu na utwaaji wa ukhalifa, kusimama kwa Imamu Husseini (a.s) ilikuwa ni maasi dhidi ya uhuru wa madhalimu, utawala dhalimu wa kifalme, ambao ulikusudia kuuchafua uslamu kwa madoa yaliyotajwa hapo juu. Bwana wa mashahidi (a.s) aliona kuwa aidolojia ya Kiislamu ilikuwa imeharibiwa. Kusimama

kwa Imamu Husseini ( a.s) au mapambano ya kiongozi wa waumini, Imam Ali ( a.s) dhidi ya Muawiyah na kampeni za Mitume dhidi ya madhalimu na wapagani wakubwa sio suala la kutwaa ardhi, kwani dunia yote sio chochote kwao. Hawakuwa na nia ya kutwaa ardhi.

Imamu Hussein (a.s) hakusimama kumpinga Yazidi kwa nia tu ya kuutwaa ufalme wa Yazid, inaelezwa kuwa Imamu (a.s) alilitambua hilo, lakini hata hivyo alisimama akitambua kuwa alitakiwa kupambana dhidi ya utawala dhalimu, na wa kikatili hata kama atalazimika kuyatoa maisha yake na maisha ya familia pamoja na ndugu zake.

Hivyo alisimama, akahatarisha maisha yake akaua idadi kadhaa ya waovu kwa ushupavu na hatimaye akafa kishahidi. Kadri ashura (siku ya 10 ya Muharramu, siku ambayo Imamu Husseini (a.s) aliuwawa) ilivyozidi kusogea ndivyo Imamu Husseini (a.s) alivyozidi kuwa na yakini juu ya shahada yake.

Uso wake ulizidi kung’ara, vijana wake walikuwa wakishindana ili kuipata shahada. Adhuhuri ya siku ya Ashura wakati mapambano yakiendelea na wote wakiwa hatarini, mmoja katika wafuasi wake alitoa

Dhamira ya Imam Hussein (a.s) kuanzia mwanzo wa maasi ilikuwa ni kuanzisha uadilifu. Alieleza kuwa mema yalikuwa hayafanyiwi kazi lakini maovu yakifanyiwa kazi. Lengo ni kuimarisha mema na kung’oa uovu.Upotovu wote unasababishw ana kufanya vitu vilivyokatazwa. Chochote kiovu lazima kindolewe. Na sisi, ambao ni wafuasi wa Bwana wa mashahidi lazima tuangalie namna alivyoishi.Dhamira ya vuguvugu lake ililenga kubomoa kila baya na ovu ikiwemo utawala wa kikatili.

31

taarifa kuwa ilikuwa ni wakati wa sala ya adhuhuri. Imam Husseini (a.s) alisema: “umenikumbusha juu ya sala. Allah akuhesabu kama mtekelezaji wa sala! Kisha akasimama na kusali, hakusema, “tuendelee na mapambano”, hapana, kwa sababu mapigano hayo yalikusudia kuilinda sala.Kama isingekuwa Ashura na muhanga wa kizazi cha Mtume s.a.w, basi dhalimu wa zama hizo angeharibu lengo la mahubiri na juhudi za Mtume s.a.w. Kama isingekuwa Ashura, tusingeijua Quran na Uislamu kwa ujumla.

Imam Husseini (a.s) aliuokoa Uislamu.Kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume s.a.w. “Husseini anatokana na mimi nami ninatokana na Husseini…”

Hii ina maana kuwa Imam Husseini (a.s) ni sehemu ya Mtume s.a.w. na harakati za Mtume s.a.w. zimehuishwa na Imam Husseini (a.s) . Hili linatokana na baraka zilizoambatana na shahada ya Imam Husseini, kwani ilivuruga njama za

kiovu za Muawiya na mwanaye, Yazidi, zenye malengo ya kupambana na Bani Hashim na hata kuufutilia mbali Uislamu na kuanzisha taifa la kiarabu mahali pa Uislamu. Kama alivyosema muaissi wa mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (r.a); “Maasi ya Ashura ni mfano adhimu kwa watu huru. Mtukufu Imam Husseini (a.s), Bwana wa Mashahidi, kwa kitendo chake alitufundisha sisi wote namna ya kusimama dhidi ya ukatili, dhidi ya serikali ya Kidhalimu. Tangu

mwanzo alitambua kuwa njia aliyopita ilikuwa ni njia ambayo wafuasi wake wote na familia yake wangetolewa muhanga. Lakini pia aliutambua mwisho na matokeo yake. Zaidi ya hapo alitufundisha kuwa katika historia yote hii ndiyo itakuwa njia ya kufuatwa; na kwamba uchache wa watu isiwe sababu ya hofu. Sio idadi bali ni sifa ya watu

ndiyo inayofaa, vilevile sifa ya jihadi ya watu dhidi ya adui ndiyo inayohitajika. Idadi inaweza kuwa kubwa lakini ikawa na kasoro au kutofaa. Vile vile idadi ya watu inaweza kuwa ndogo bado ikawa madhubuti na yenye mafanikio kutokana na sifa yao ya juu. Imamu huyo wa Uislamu alitufundisha kusimama pindi dhalimu anapowatawala waislamu kwa ukatili hata kama nguvu zetu ni ndogo. Na iwapo heshima ya Uislamu iko hatarini, tunatakiwa kuyatoa maisha

yetu katika kuutetea”. Likitiwa nguvu na tukio la Ashura, taifa adhimu la Iran lilianzisha maasi ya kihistoria ya tarehe 15, khordad (Juni 5, 1963). Kama Ashura isingetokea na nguvu Lake Lisiwepo, basi maasi hayo yasiyokuwa na mfano katika hali yoyote yasingefanyika katika Uislamu. Wakati tukiwa tumepoteza vijana na wataalamu wengi, tulipata

kitu ambacho thamani yake ni zaidi ya fikra hizi. Hilo ndilo lengo ambalo Bwana wa Mashahidi (a.s) alilitolea muhanga wa mke wake, watoto na hata yeye mwenyewe. Ndilo lengo ambalo Mtume s.a.w. alitumia maisha yake yote kwa ajili ya UIslamu. Hali kadhalika Maimam wetu watakatifu (a.s) walikabiliana na taabu na pingamizi za kila aina. Maombolezo na kuhuzunika huhifadhi na kudumisha harakati hiyo. Imesimuliwa kuwa anayelia (kwa

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi. Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame, kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.

Aidha Sheikh Salum alisema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupinga Dhulma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Kifo cha Imam Hussein (AS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

32

ajili ya kifo cha Imam Husseini) au kuwafanya wengine walie au hata kuwa na muonekano wa kulia, ataingizwa peponi. Mtu huyo ambaye huonekana kuwa na huzuni, ambaye uso wake unaonekana kuwa na majonzi, kwa hakika anasaidia kuhifadhi vuguvugu na harakati ya Imam Husseini (a.s).

Sio machozi bali kuwa na malengo ya kisiasa na kisaikolojia. Kama suala lingekuwa ni machozi tu, kwa nini kujinasibisha kwalo? Bwana wa mashahidi anahitaji machoci kwa ajili gani?

Kama wasomi wetu wangejua mwelekeo wa kisiasa na kijamii wa mikusanyiko hii ya huzuni na maombolezo, nyimbo hizi za huzuni na masikitiko wasingetuuliza kwa nini tunayakumbuka na kuyaheshimu. Katika hotuba nyingine Imam Khomeini (r.a) anasema , “ Baadhi ya watu wanawauliza vijana wetu, mtalia mpaka lini? Mtaomboleza mpaka lini?” Acha tufanye maandamano katika kupinga! Hayo ni kwa sababu watu hao hawajui maana na malengo ya maombolezo ya Ashura na ni jinsi gani yamekuwa yakitunzwa. Hili

hawalitambui, na hivyo hawawezi kujua”. Hawaoni kwamba maombolezo haya (Kwa heshima ya maimamu) huwastawisha watu na kuwajenga wanajeshi. Maombolezo ya Ashura ni silaha dhidi ya dhulma, dhidii ya fikra za kiburi, kwa sababu yanasimulia historia ya ukandamizwaji wa wanyonge na na hivyo yanatakiwa kuendelea moja kwa moja.

Malengo ya vuguvugu la ashura.Mitume wote wametumwa kufanya mbabadiliko katika jamii. Wote walitambua kuwa mtu anatakiwa kujitoa kwa ajili ya jamii. Mtu bila kujali ukuu, hata kama ni mtu wa cheo cha juu au mtu mwenye thamani kuliko wote, anatakiwa kujitoa na kusimama kwa ajili ya mema ya jamii.

Bwana wa Mashahidi alisimma kwa sababu ya msingi huu akayatoa maisha yake, wafuasi na wasaidizi wake. Jamii lazima ifanyiwe mabadiliko, “kwa kiasi kwamba watu wanalazimika kushughulika na usawa” Uadiifu unatakiwa kutendeka na kutambulika miongoni mwa watu na katika jamii. Kifo cha Imam Hussein (a.s) kililenga kuanzisha amani ya Mwe nyeziMungu

na kuilinda nyumba ya MwenyeziMungu. Maisha ya Bwana wa Mashahidi na yale ya Sahibu Zaman (a.s), yaani Imam wa kumi na mbili ambaye yuko katika ghaiba na yale ya mitumne wote, kuanzia Nabii Adam mpaka leo hii yote yalikusudia kitu kimoja tu, nacho ni kuanzisha utawala wa uadilifu katika kupinga ukatili.

Dhamira ya Imam Hussein (a.s) kuanzia mwanzo wa maasi ilikuwa ni kuanzisha uadilifu. Alieleza kuwa mema yalikuwa hayafanyiwi kazi lakini maovu yakifanyiwa kazi. Lengo ni kuimarisha mema na kung’oa uovu.Upotovu wote unasababishw ana kufanya vitu vilivyokatazwa. Chochote kiovu lazima kindolewe. Na sisi, ambao ni wafuasi wa Bwana wa mashahidi lazima tuangalie namna alivyoishi.Dhamira ya vuguvugu lake ililenga kubomoa kila baya na ovu ikiwemo utawala wa kikatili.

Bwana wa Mashahidi (a.s) aliumiam aisha yake yoet katika kuondosha uovu, kukumoesha utawala wa kikatili na kuzuia mambo machafu na ufisado ambao serikali iliuanzisha duniani. Hivi ndivyo alivyotumia maisha yake na ya yale ya wanaye. Alijua matokeo ambayo yangetokea kwa hatua yake hiyo.

Yeyote aliyesuhubiana na Imam (a.s) tangu alipoondoka Madina, akaingia Makkah na kuondoka Makkah tena mpaka mwisho, aliweza kuona na kusikia yote yaliyosemwa na Imam na kutambua kuwa Imam Hussein (a.s) alijua vyema kile am bachpo alikuwa kikifanya. Sio kwamba alikuwa anakwenda kuangalia nini kingetokea (Kusimama na kupambana ukiwa na askari wachache dhidi ya jeshi lenye mafunzo), nali, alikuwa amesimama ili kuichukua serikali (kutoka kwa wanyang’anyi). Hili lilikuwa ni lengo muhimu. Baadhi ya watu hufikiri kimakosa kwamba Imam (a.s) alikuw ahana serikali katika fikra yake alikuja

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

BALOZI wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mehdi Aghajafari (katikati) akiongoza ''Masiyr'' ya Imam Hussein, kulia kwake ni Morteza Sabouri, na kushoto kwake ni Sheikh Alhad Mussa

33

kuirudisha serikali ya Kiislamu, kwa sababu serikali ya Kiislamu ilitakiwa kuwa mikononi mwake yeye na wafuasi wake.

Bwana wa Mashhaidi (a.s) aliona kuwa dini ilikuwa ikiharibiwa. Kuibuka kwa Imam Hussein (a.s) na kiongozi wa waumini, Imam ali ( a.s) dhidh ya Muawiyah, kusimama kwa Mitume dhidi ya Madhalimu na wapagani sio suala la kuteka nchi fulani , kwa sababu ulimwengu mzima si chochote kwao; hawakuwa na dhamira ya kutwaa ardhi.

Kile kilichompeleka Imam Husein (a.s) huko Kufa na Karbala ili kupambana dhidi ya uovu na dhulma, ilikuwa ni imani. Imani yake ndiyo iliyomfanya atoe kila kitu kwa ajili yake; aliuawa kwa sababu ya imani yake ya Uislamu na itikadi yake na kwa kuuawa kwake aliushinda utawala wa kidhalimu.

Imam Hussein (a.s) alisimama kumpinga Yazidi na labda alikuwa na uhakika kuwa asingeuondosho ufalme wa Yazid; imesimuliwa kuwa Imam ( a.s) alilijua hili na bado alisimama akijua kuwa alilazimika kupambana na utawala dhalimu na katili hata kama angelazimika kuyatoa maisha yake kwa ajili ya imani yake. Hivyo, alisimama akayatoa maisha ya watu, akaua wengi na yeye mwenyewe akachinjwa.

Imam alishughulishwa na Mustakbali wa Uislamu na waislamu. alitoa changamoto, kupambana na akauawa ili utetezi wake mtukufu na muhanga wam aisha ya watu wake katika uwanja wa vita viweze kutanganzwa na mpango wa siasa ya kijamii uweze kuanzishwa katika jamii yetu . Bwana wa mashahidi a.s aliona kuwa ni wajibu wake kupinga utawala huu na kuuawa ili hali iweze kuchochewa na kwa muhanga wake na muhanga wa wale waliokuwa pamoja naye, utawala wa kikandamizaji uweze kufichuliwa na kuaibishwa hadharani.

Alitambua kuwa utawala wa kimabavu ulikuwa umeshikilia mwelekeo w ataifa lake na akatambua kuwa wajibu wake wa kidini ni kupinga nakuutweza kwa gharama yoyote ingawa ilikuwa wazi kwa kanuni zinazojlikana kuw aile idadi ndogo (Imam hussein (a.s) na watu wake) isingeweza kupambana na idadi kubwa, lakini ilikuwani wajibu wa kidini. Lakini (kwa Bwana wa Mashahidi) ilikuw ani wajibu kusimama, kuitoa damu yake mwenyewe ili ummah upate kufanyiwa mageuzi na bendera ya

Yazid ipate kushushwa na kwa kweli jambo hili ndilo lililotokea – alitoa damu yake na damu ya wanawe, alitoa kila alichonacho kwa ajili ya Uislam.Imam Hussein ( a.s) alisimama wakati hakuw ana jeshi kubwa. Kama naye pea angekuwa mzembe, angekaa na kusema ,” sio wajibu wangu kisheria kusimama”. Hilo lingeufarahisha utwala wa Bani Umayyah.

Wangemfanya akae na asiseme lolote ili wapinzani waendelee kufanya mambo yao mabaya.Lakini Imam Husseini ( a.s) alimtuma Muslim Aqil kwenda kuwaita watu wale kiapo cha kuungana naye ili kuunda serikali ya Kiislam na kuiondosha serikali fasidi ( ya Yazid). Imam ( a.s) angebaki tu Madina na ngemkubali wakala wa Yazid na kula kiapo ch autii, jambo hilo lingewafurahisha ( Yazid) na

wangeubusu mkono wa Imam ( a.s).Imam Husein (a.s) ayatoa maisha yake kama zawadi kwa uislamu. Bwana wa mashahidi alisimama kuuimarisha Uislamu, kupinga dhulma na kupambana dhidi ya utawala wa wakati huo ambao ulikuwa umepata upeo wa tawala za zama za sasa. Katika kufanya hivyo aliwatoa muhanga watoto wake wadogo, wafuasi wake na hatimaye maisha na damu yake mwenyewe hakuwa na vitu vya kidunia ili apate kuvitoa. Bwana wa Mashahid (a.s) , naye pia aliuwawa hakufanya

hivyo ili kulipwa. Malipo ni suala ambalo halikuwa na nafasi kwake. Alikwenda katika hali ya kuinusuru itikadi, kuuendeleza a kuuhuisha Uislamu.

Imam Hussein (a.s) aliuwawa, lakini hilo lilikuwa katika kutii amri ya Mwenyezi Mungu; ilikuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ilikuwa ni heshima na hadhi yake na hivyo, hakushinwa, alitii amri ya Mwenyezi Mungu.

Wassalam alal Hussein wa As -Habul Husseini. وسيعلم الذين ظلموا أي منقلب ينقلبون

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

34

Katika Uislamu kuna mambo muhimu kama vile swala, Hijab, Imani, na kutofautisha

baina ya halali na haramu, kulingana na sheria za kiislamu, kuwapenda ahlul bait ( tawalla) na kujiepusha na maadui wa ahlul bayt (tabarra). Haya yote yamekuwa yakifanywa na kila mtu, wanawake na wanaume. Kati ya mambo mengi yaliyojitokeza siku ya ashura ni pale mwenyezimungu Mtukufu alipowapa taufiki na fadhila za pekee wanawake, kwa kutekeleza jukumu hili tukufu kwa makini kabisa.

MwenyeziMungu ameonesha uhusiano ulio bora kabisa baina ya mwanamke na amemfundisha mwanamke huyo namna ya kuilinda dini yake tukufu ya uislam, kwa kutekeleza wajibu wake katika nafasi yake akiwa kama mke, mama, dada na binti katika mtazamo wa kidini na kuondoa vurugu, kwa, kujitoa muhanga na kuupa ulimwengu mtazamo mpya wa kidini. Hebu jiulize maswali haya muhimu; ni lipi hasa ambalo Imam Hussein a.s alilotaka kulibadilisha? Na utaratibu upi aliuhitaji kufanikisha mabadiliko haya? Je alikuwa amejizatiti katika mapambano

haya kwa silaha gani? Je ni vipi aliweka utaratibu wa kuwatuma wajumbe kwenda sehemu mbalimbali ili tukio la Ashura lisiweze kusahaulika? Je vigezo vyake katika kuwachagua watu ambao wangeshiriki kikamilifu katika tukio hili la huzuni la Karbala vilikuwa ni nini?

Ukiangalia kwa makini utaona ya kwamba, uwanja wa Karbala ulikuwa ni mahali finyu licha ya ufinyu wake lakini paliweza kupanua akili ya mwanadamu kufikia upana ulio sawa na dunia hii au hata upana wa ulimwengu mzima.

Imam Hussein a.s alikuwa na mtazamo mpana juu ya matatizo yote halisi na yale yanayotarajiwa ambayo yanamwaza mwanadamu asipate kuendelea na alitaka kuuondoa mzizi wa matatizo haya ili hatari yake isiishie siku ya Ashura tu, bali mapamabano haya yawe kwa watu wote wa kwa nyakati zote. Ni nini ilikuwa mipango ya Imam Husein a.s siku ya Ashura? Imam Hussein a.s alichukua tahadhari zote dhidi ya fursa ya adui ambaye alitaka kuiua dini na kuitoa iwe nje kabisa ya utaratibu wa kimaisha. Bila shaka Wanawake nao

walikuwa ni miongoni mwa masuala haya muhimu ya kuhujumiwa na adui. Imam Hussein a.s alikuwa na mtazamo tofauti kwa wanawake, mtazamo ambao ulitoa fursa ya kuwapa moyo wanawake, kuienzi nafasi yao na uhodari wao ambao dini ya kweli ya uislamu ilijitahidi kuitoa na kuepukana na mitazamo isiyofaa na kuweka kando suala la ubaguzi dhidi ya wanawake,

Mtazamo na sera mbaya za adui, walidhani ya kwamba wanawake ni viumbe wasiojiweza kufanya chochote, kwamba wao ni kama midoli ya kuchezea na wasio na dhima yoyote, na si mwanadamu aliye huru.lakini kwa upande wa Imama Hussein a.s ilikuwa ni tofauti kabisa na sera hiyo, kwani hapo ndipo dhima mpya ya wanawake ilitangazwa siku ya ashura ili kuwafahamisha watu wote kwamba wanawake ni hazina wenye fadhila kubwa.

Matokeo ya juhudi zote za Ahl bait a.s yalikuwa sasa yanatoa matunda ikiwa ni katika kizazi cha pili tangu kuja Uislamu na wanawake waliona kwamba hapo ndipo mahali pao panapowafaa kijamii

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA TUKIO LA ASHURA

Na: Fatma Ali Othmani

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

35

HISTORIA / SIKU YA ASHURA

ambapo wanaweza wakaonesha ubora wao. Wana historia wanasema kwamba katika kila mapambano kuna hali mbili; “Kufa ukiwa ni mshindi (shahid)” na kushindwa na hatimaye kutekwa nyara (Mateka)”, yote haya yalikuwa ni mambo mawili aliyojitokeza katika mapambano ya Ashura. Wanawake walikuwa na nafasi yao kubwa katika mambo hayo mawili.

Mapambano ya siku ya Ashura yalikuwa ni ya Imam Hussein a.s akiwa na watu wachache na hatimaye alikufa akiwa ni Shahid, na pia wanawake na watoto ambao walionesha dhima ya mwanaume yeyote na mwanamke yeyote kama mwanadamu waliweza kutekwa na kuchukuliwa kama Mateka wa vita. Mtume Mtukufu s.a.w.w alijitahidi kuwafahamisha wanawake na kwa kutekeleza hili yeye mwenyewe kwa vitendo na aliwaongoza masahaba wanawake kwa kuongeza ufahamu wao na utamaduni wao.

Natija ya hayo ni vitendo na mwenendo wa Bibi Fatma Zahra a.s Binti wa Mtume s.a.w.w katika kumsaidia Imam Ali a.s na kuendelezwa na binti yao Bibi Zainab s.a vinaonesha ni jinsi gani juhudu hizi zimekuwa ni chachu na chanzo cha nuru katika jamii ambayo masahaba wengi wanawake walipata mwongozo na kuonesha ushujaa wao.

Matokeo ya juhudi za kuwaelimisha wanawake zilifanywa kwa kipindi cha miaka 61 yalitoa matunda katika uwanja mdogo wa karbala, kwa kutekeleza wajibu wao na dhima yao baada ya kushuhudia tukio la Ashura na nafasi ya Bibi Zainab s.a ambaye alipata ujumbe juu ya kuitekeleza dhamira hii toka kwa kaka yake Imam Hussein a.s na alianza kuifanyia kazi ilipofika jioni ya siku ya Ashura. Alianza utaratibu wake wa kuwahubiria watu kwa nguvu kiasi ambacho kilimfanya adui aweze kujibu.watu wakawa na hamu ya kutaka kujua

majibu yake na hii ilipunguza njama za siri ambazo serikali ilikuwa inafanya kwa kificho. Wazo la kuwa na utaratibu wa ‘kujibu maswali’ peke yake ambalo Zainab s.a alilitumia, lilikuwa ni aina ya mapambano kuilazimisha serikali kujibu maswali kutokana na vitendo vyake. Ustaarabu huu ulifanywa katika hali ambayo watu waliwaona watawala kuwa ni wenye makosa na waliwatuhumu kwa dhulma waliyoitenda kwa watu wa nyumba ya Bwana Mtume s.a.w.w.

Bibi Zainabu s.a alifanikisha jambo hili kwa kutekeleza majukumu makuu matatu:i. Kumtambulisha kwa watu kiongozi wa kiroho kwa kuwapa watu maelezo ya kutosheleza.ii. Tathmini ya Yazid na vitendo vya maofisa wake kabla na baada ya Ashura.iii. Kuwasihi na kuwafahamisha watu wakabiliane na sera za adui.

Katika sura hii Wanawake walishiriki katika matukio yote katika siku kabla na baada ya huzuni ya Karbala, kama vile kujenga msingi wa mapambano, kutoa msaada ulohitajika na kuwapa moyo wanaume wao kumuunga mkono Imama Hussein a.s na kuungana na uongozi mtukufu wa Kizazi cha Mtume s.a.w.w na pia kuungana na masahaba wa Imam na kuwa pamoja na Bibi Zainab s.a. kabla ya Ashura ambapo wanaume wengi waliogopa kuwasaidia Ahlul bait s.a , wanawake shupavu walijiweka hatarini wenyewe ili kumlinda ImamHussein a.s.

Kulikuwa na wanawake ishirini ambao walokuwepo katika ardhi ya Karbala, kumi kati yao wanatokana na Ahl bait a.s na waliosalia walikuwa ni wanawake wa masahaba wa Imam Hussein a.s, ambao kila mmoja alitekeleza wajibu na dhimma alokuwa nayo kuanzia Asubuhi hadi mchana siku ya terehe Kumi ya mwezi Muharram. Naam!

Ilikuwa ni mapenzi ya MwenyeziMungu kwamba jambo jipya kihistoria na kubwa kiroho la mwanadamu litokee na kile kilicho pandwa na Mtume wa MwenyeziMungu s.w.t kivunwe na Fatimatu Zahra na Ali Murtaza a.s, kwani, wanawake waliokuwepo Karbala siku ile walichaguliwa kwa umakini wa hali juu ili kudhihirisha moyo wa kujitoa muhanga kwa Imam wao.

Kwa sababu hii kiwango cha kujitoa muhanga baina ya masahaba wanawake kilikuwa hakijawahi kutokea hapo kabla baada ya kutawafu Mtume s.a.w.w katika ulimwengu huu.

Inasemekena kwamba usiku mmoja kabla ya siku ya Ashura, Imam Hussein a.s baada ya kuwapa wafuasi wake ruhusa waondoke, alisema; “Yeyote aliye na mke ampeleke mahali salama usiku huu. Kesho wanaume watauwawa na wanawake wetu watachukuliwa kuwa mateka”. Imam a.s hakutaka ukatili ule ule utakaofanyiwa Ahl bait a.s wafanyiwe wanawake masahaba.

Inasemekena kwamba baada ya Ibn Mazhar kuingia kwenye hema lake, mkewe akamuuliza;” Je ni kitu gani ambacho mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu a.s amesema juu ya wanawake? Ibn Mazhar akamueleza yale ambayo Imam alisema, mkewe akaanza kulia na akasema.” Ewe mwana wa Mazhar hii si sawa! unataka wewe mwenyewe uenda peponi!... ibn Mazhar akaenda kwa Imam a.s na kumweleza ; “Ewe mwana wa Mtume wa MwenyeziMungu, mke wangu Asadia hataki mimi nimpeleke mahali salama” Imam a.s alikuwa bado hajatoa jibu wakati ambapo yule mwanamke alilia na kusema| “Ewe mwana wa Zahra s.a , Je sisi hatustahili kuwahudumia binti zako na dada zako?’... Itaendelea Toleo lijalo Inshaallah, Wassalaam alaykum.

وسيعلم الذين ظلموا أي منقلب ينقلبون

36

FOMU YA MAONI

Maoni / Barua

Ili kuliboresha Jarida hili tafadhali jaza fomu hii ili utoe maoni yako kuhusu muundo mzima wa Jarida hili, kukosoa, kushauri au mapendekezo yoyote uliyonayo, bila shaka tutayafanyia kazi Maoni yako. Tutumie kupitia anuani zilizoko nyuma ya Jarida hili

Jina kamili........................................................................................................................Unapoishi (Mkoa / Wilaya / Kijiji)…………………………………………………….…...............…Sanduku la Posta……………………………………………………………………….............................Barua Pepe (E-mail)………………………………………………………………………….................….Namba ya Simu…………………………………………………………………………............................Weka alama katika moja ya masanduku utakayochaguaA: Muonekano wa Jarida / Picha Mpangilio:Nzuri Nzuri kiasi Nzuri sana Mbaya Mbaya kiasi Mbaya sana B: Sifa za Jarida / Makala zote:Nzuri Nzuri kiasi Nzuri sana Mbaya Mbaya kiasi Mbaya sana

C: Baadhi ya Makala: Nzuri Nzuri kiasi Nzuri sana Mbaya Mbaya kiasi Mbaya sana

Tumia nafasi hii kueleza chochote ulichonacho kuhusu Jarida hili..........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................Mwisho tunatoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye Makala nzuri (za Dini, Jamii, Utamaduni

Historia za Kiislamu nk.) atutumie kwa anuani zetu. Pia tunakaribisha Barua za wasomaji ikiwa na anuani na picha ndogo (Passport Size) (kwa mwenye

kutaka makala au barua itoke na picha yake)

Tutakuwa na utaratibu wa kukutumia Nakala (moja) ya Jarida hili kwa njia ya Posta, pia unaweza kusoma Jarida hili kupitia mtandao (Web Site) kwa anuani hizi:- http://issuu.com/al-hikma/docs/al-hikma_26Asante kwa ushirikiano wako na kuchagua Jarida hili.Maulidi Saidi Sengi.

MAONI

اجمللة الفصلية تصدر من مركز الثقافة للجمهورية اإلسالمية اإليرانية - دار السالم - تانزانيا