16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1069 JAMADUL THAN 1434, IJUMAA - MEI 3 - 9, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Hizi ni rasilmali Ametupa Allah. Tunazihitaji zote pamoja katika ibada ya Hijja. Allah Anatutaka tuzitumie mapema kabla hajatunyang’anya. Hakuna mwenye uhakika wa mwakani. Majuto mjukuu, hasa yale ya baada ya kufa. Unangoja nini? Usimwendekeze shetani (iblis). Karibu ujiandikishe na kulipa Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117. Kunuti maalum siku 21 kuanza leo Ni kuwaombea Kheri Masheikh Dr. Shein, Uamsho ni amri ya Mungu Hata ma-Rais wanahitaji ‘Fadhakkir’ Wasisahu siku FFU watakapowakimbia Nyingi ni uzushi, ufasiki, usanii Masheikh wetu wachunge ndimi Waulize maswali, sio kutoa kauli Habari za kiintelijesia! Mholanzi aliyesilimu asema Alipoingia Msikiti wa Mtume ‘Samahani Mtume’… RAIS Jakaya Kikwete SHEIKH Ponda Issa Ponda SHEIKH Azzan (kushoto), Sheikh Farid (katikati), Sheikh Mussa Juma wakiwa katika moja ya mihadhara ya Kiislamu Zanzibar kabla ya kuwekwa ndani. Habari Uk. 3 ARNOUD Van Doorn (kushoto), Mdachi aliyesilimu akionyeshwa namna kitambaa kinachofunika Ka'abah kinavyotengenezwa alipofanya Umrah hivi karibuni. Habari kamili ukurasa wa 4. (13) AFYA, UWEZO, NA NAFASI. Uk. 8

ANNUUR 1069

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Gazeti la kila wiki

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1069

ISSN 0856 - 3861 Na. 1069 JAMADUL THAN 1434, IJUMAA - MEI 3 - 9, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Hizi ni rasilmali Ametupa Allah. Tunazihitaji zote pamoja katika ibada ya Hijja. Allah Anatutaka tuzitumie mapema kabla hajatunyang’anya. Hakuna mwenye uhak ika wa mwakani. Majuto mjukuu, hasa yale ya baada ya kufa. Unangoja nini? Usimwendekeze shetani (iblis). Karibu ujiandikishe na kulipa Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

Kunuti maalum siku 21 kuanza leoNi kuwaombea Kheri MasheikhDr. Shein, Uamsho ni amri ya MunguHata ma-Rais wanahitaji ‘Fadhakkir’Wasisahu siku FFU watakapowakimbia

Nyingi ni uzushi, ufasiki, usaniiMasheikh wetu wachunge ndimi Waulize maswali, sio kutoa kauli

Habari za kiintelijesia!

Mholanzi aliyesilimu asema Alipoingia Msikiti wa Mtume

‘Samahani Mtume’…

RAIS Jakaya Kikwete SHEIKH Ponda Issa Ponda

SHEIKH Azzan (kushoto), Sheikh Farid (katikati), Sheikh Mussa Juma wakiwa katika moja ya mihadhara ya Kiislamu Zanzibar kabla ya kuwekwa ndani. Habari Uk. 3

ARNOUD Van Doorn (kushoto), Mdachi aliyesilimu akionyeshwa namna kitambaa kinachofunika Ka'abah kinavyotengenezwa alipofanya Umrah hivi karibuni. Habari kamili ukurasa wa 4.

(13) AFYA, UWEZO, NA NAFASI.

Uk. 8

Page 2: ANNUUR 1069

2 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Makala

JUZI siku ya Jumatano y a M e i M o s i m w a k a huu, zilifanyika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani, ambazo kwa hapa nchini zilifanyika kitaifa jijini Mbeya.

M g e n i r a s m i k a t i k a sherehe hizo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete alitumia fursa ya sherehe za Mei Mosi, kuzungumza na wananchi, hususan wafanyakazi na kuwajulisha namna serikali yao inavyojizatiti kutatua kero zao kazini.

Pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuzungumzia juu ya hatua inazochukua serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania, zaidi katika huduma za miundo mbinu na jitihada zinazofanyika katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa Watanzania.

Rais Kikwete alihitimisha hutuba yake kwa kuzungumzia tatizo la udini nchini, ambalo limeshika kasi siku za hivi karibuni.

Tatizo ambalo kwa kweli lina kila sura ya kufuta mila na desturi yetu ya umoja, mshakamano na upendo kwa Watanzania.

Akizungumzia tatizo hili kwa kina, Rais Kikwete alitoa tahadhari kwa wananchi, kuepuka kushabikia udini kwani n i ha tar i kubwa inayoweza kulisambaratisha Taifa.

Rais Kikwete alisema kuwa tayari serikali inafanya jitihada ya kutatua tatizo hilo, ambapo imepanga kukutana na viongozi wa dini mbili za Kiislamu na Kikristo, ili kujadili kwa pamoja kwa kina juu ya hatari iliyopo na namna ya kuikwepa ili kuleta nusura dhidi ya janga linaloweza kuliangamiza Taifa.

Aliyoyaeleza Rais Kikwete na hatua ambazo amekusudia kuzichukua dhidi ya tatizo zima la udini, ni mwanzo mzuri wa kulitatua tatizo.

Tunaamini hatua hiyo ni muafaka kwa kuwa itaruhusu pande zote tatu, yaani serikali, viongozi wa Kikristo na Kiislamu kubainisha vyanzo vya tatizo, athari za tatizo na namna ya kulimaliza.

Pande zote tatu zitakuwa na fursa kamili ya kuonana

HIVI karibuni Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr. Al i Mohammed She in amer ipot iwa akisema kuwa Zanzibar h a i h i t a j i U a m s h o kwani Wazanzibari walishaamka zamani.

Aliyasema hayo baada ya kufikishiwa malalamiko kwamba kuna maskani za CCM zimechomwa moto na watu wasiofahamika.

Maskani hizo ni pamoja na zile za Kisonge na Kachochora maarufu kwa vijembe na maneno ya kashfa kwa wapinzani wa muundo wa Muungano wa Serikali mbili na wakati mwingine matusi kwa Wapemba.

Kauli ya Rais Shein k u w a Wa z a n z i b a r i hawahitaji Uamsho baada ya kufikishiwa malalamiko hayo, imefasiriwa na wengi kuwa ni sawa na kuwahusisha Masheikh wa Uamsho na uhalifu huo.

Na kama ndio hivyo, sisi tunaona sio sahihi. Kwanza Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Miahadhara ya Kiislamu (JUMIKI) hawajasema kuwa wao ndio waliohusika na uhalifu huo. Lakini pili, suala na tuhuma kama hiyo halijafikishwa katika vyombo vya sheria na Mahakama ikahukumu kuwapata JUMIKI na hatia ya kufanya uhalifu huo.

Masheikh wa JUMIKI n i w a n a z u o n i w a Kiislamu, ni Maimamu na Makhatibu wa Misikiti. Wanaongoza Waislamu ka t ika swala ka t ika Misikiti yao. Kuwatukana Masheikh hawa ni sawa na kuwatukana waumini wao na Uislamu kwa ujumla.

Hii sisi tunaona sio sah ih i . Mwanadamu

Amesema kweli Mtume (s.a.w) wapo watakaodai damu na mali za watu

ameumbwa na utu wake na heshma yake vi tu ambavyo vimetajwa katika mafundiso ya Kiislamu kuwa ni vitu vitakatifu. Na kwamba katika makosa na madhambi makubwa, ni pamoja na kumwaga damu ya mtu au kumchafulia heshma yake. Hivi ni vitu vitakatifu kama alivyovitaja M t u m e M u h a m m a d (s.a.w). Na ndio maana pia hata katika sheria za kibinadamu, mtu hawezi kuitwa mwizi au mhalifu wa kosa fulani mpaka ahukumiwe. Kabla ya hapo anakuwa ni mtuhumiwa tu.

Leo tunapowahusisha Masheikh wa Uamsho na kuchomwa moto maskani ya Kisonge na Kachochora, je, tuna uhakika kuwa M a s h e i k h h a o n d i o waliochoma?

Kama hatuna, tutalipa vipi dhulma hii tunayowatendea M a s h e i k h h a w a y a kuwavunjia heshma yao kwa kuwasingizia uhalifu na mambo ya kihuni?

Tunadhani kuwa pamoja na mihemuko ya kisiasa, lakini wanasiasa na viongozi wetu wa Serikali inapasa wazingatie kuwa watu wengine nao ni binadamu kama wao. Wana haki zao zinazostahiki kuchungwa n a k u h e s h i m i w a . Muhalifu aitwe muhalifu kama imethibiti kuwa ni muhalifu.

A m e s e m a k w e l i M t u m e M u h a m m a d (s.a.w) kwamba, lau watu wangeaminiwa tu kwa madai yao, wapo ambao wangedai damu na mali za watu.

Kwa hiyo ni wajibu w a m w e n y e k u l e t a madai kuleta ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

Serikali ndiyo inayoleta udiniMwiba hutokea ulipoingialia

Na Shabani Rajabana kwa ana na kubainisha hoja za kila upande, tofauti na ilivyozoeleka ambapo hoja huishia kwenye vyombo vya habari.

H a t a h i v y o t u s e m e tu kwamba, tangu awali hakukuwa na tatizo lolote kati ya Waislamu na Wakristo nchini. Wote wamekuwa wakiishi pamoja mitaani kama ndugu, wakipanga nyumba moja, wakifanya kazi pamoja, wakitembeleana nk.

Tunavyoona as i l i na mzizi wa udini nchini, ni matokeo ya kuwepo mfumo mbaya wa serikali namna inavyowahudumia watu wa imani hizi mbili tofauti.

Kwa miaka mingi Waislamu wamekuwa wakilalamikia serikali juu ya utaratibu mbovu wa kihuduma unaotolewa kati ya jamii ya Waislamu na ile ya Kikristo.

Waislamu wanalalamika kuwa mfumo uliopo serikalini, una chembe chembe za ubaguzi, dhulma kwa misingi ya dini, hasa katika fursa za ajira, utumishi wa umma, uteuzi wa nafasi mbalimbali serikalini na kubwa zaidi na la awali ubaguzi katika elimu.

A i d h a W a i s l a m u wamekuwa wakilalamikia kuwa taasisi zao za kidini pia zimekuwa zikinyimwa fursa ya kiserikali katika kuwaendeleza Waislamu na jamii kwa ujumla, tofauti na wenzao wa Wakristo.

Wanaona kuwa kutokana na kukomaa kwa mfumo huo, imefikia mahali watu wa dini fulani wanaamini kuwa wao ndio wana haki miliki ya nafasi na fursa serikalini kuliko wale wa imani nyingine.

Na mara nyingi kisingizio kikubwa kinachotumika kutetea dhulma hii kwa Wa i s l a m u , n i k w a m b a hawajasoma.

Tumeona hata pale jamii ya Waislamu inapolalamika, huishia kupuuzwa, kukejeliwa na kudharauliwa.

Kukithir i malalamiko ya Wai s l amu dh id i ya serikali kuhusu kubaguliwa kwa misingi ya kiimani, imeonekana kuwa ndio chimbuko hasa la Wakristo nao kuamua kuja na hoja ya kudai kuchinja.

Vitendo vinavyofanywa na serikali kama vile mikataka ya kunufaisha watu wa dini moja kutoka serikalini kwa mfano MoU kati ya Makanisa na serikali mwaka 1992, lakini Waislamu wakitaka fedha za kuendesha Mahakama ya Kadhi wakakataliwa kwa

madai kuwa serikali haina dini, au ikadaiwa kuwa haiwezi kutoa fedha kufaidisha watu wa dini moja, ni dhahiri ndivyo vinavyoleta udini.

N a m a t a t i z o h a y a yanatokana na kujazana watu wa imani moja katika sekta mbalimbali za ajira na utumishi wa umma serikalini kuliko wa imani nyingine. Na hili limewafanya kukosa uadil i fu na kusukumwa na nafsi ya kiimani katika kutenda kazi zao.

Katika hali hii, ni vigumu kuamini kwamba hakuna Waislamu waadilifu, wasomi na wajuzi wanaostahi l i kuteuliwa au kuchaguliwa katika nyadhifa na ajira za serikali, na nafasi hizo kujazwa wakapewa Wakristo pekee.

Kwa mazingira haya ni rahisi mtu kutambuliwa na kuwezeshwa ‘mwenzao’ kuliko kutumikia watu kwa haki na uadilifu bila kutizama imani ya mtu. Bila shaka hali hii ndio inayolalamikiwa na Waislamu katika Baraza la Mitihani.

Kadha l ika Wai s l amu hawaamini kuwa sio udini kuhalalisha uwepo wa ubalozi wa Vatican nchini, lakini wakakataliwa mkataba kati ya serikali na OIC huku wapingaji wakubwa wakiwa ni viongozi wa Kikristo, na wasikilizwe na serikali kuliko viongozi wa Kiislamu.

Sisi tunadhani kwamba fursa hii ambayo amekuja nayo Rais Kikwete, basi iwe chanzo cha kuondolewa viini hivi vya udini nchini.

Tunaamini kabisa kwamba, iwapo Serikali itaachana na mazoea ya kutizama imani za watu, kwasababu tu ya wingi wa watu wa imani hiyo katika nyadhifa serikalini na katika idara zake au kwasababu ya ukali wa Maskofu, halafu uadilifu na haki vikashika mkondo wake, chanzo cha udini kitakuwa kimekwisha. Hakutakuwa na tatizo.

Tunaamini kwamba iwapo serikali itaamua kutenda haki kwa kuzingatia uwiano wa watu wa imani hizi mbili, uadilifu na haki vikachukua mkondo wake bila kujali imani ya mtu isipokuwa ujuzi, uadilifu, weledi na uwezo wa mtu kutenda, suala la udini nchini litayeyuka mithili ya barafu juani.

Page 3: ANNUUR 1069

3 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Habari

Kunuti maalum siku 21 kuanza leoJANA ilikuwa siku ya funga na leo inaanza Kunuti maalum katika swala ya Ijumaa.

Kunut i h i i ka t ika Misikiti yote itaendelea kwa siku 21 mfulululizo i l i kuwaombea dua Masheikh na Waislamu kwa ujumla.

U a m u z i h u o umefanywa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar kwa ushi r ik iano na Maulamaa mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mara baada ya kikao cha Maimamu Aprili 27 mjini Zanzibar, ili kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu, Waislamu walitakiwa kufunga jana funga ya Suna ya kila Alhamisi na kushiriki Kunuti leo Ijumaa itakayoendelea katika kila swala kwa siku 21.

Taarifa hiyo imesema kuwa pamoja na kuiombea amani nchi, huu ni wakati muafaka “kuwaombea Masheikh wetu... kwa kutanguliza kufunga siku ya Alkhamisi tarehe 2/5/ sawa na mwezi 21 Mfunguo 9 na baadae kufuatiwa na Kunuti kuanzia swala ya Ijumaa inayofuatia kwa muda wa siku 21 katika kila swala.”

Dua hii inakuja wakati baadhi ya viongozi na Masheikh wa JUMAZA na JUMIKI wapo bado ndani kwa zaidi ya miezi sita sasa ambapo wamenyimwa haki yao ya dhamana katika tuhuma zinazowakabili.

A i d h a i m e k u j a siku chache baada ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kur ipot iwa akisema kuwa Zanzibar haihitaji Uamsho.

“ U a m s h o wanamuamsha nan i al iyelala Zanzibar”, ndivyo gazet i moja lilivyoandika likisema k u w a R a i s S h e i n haiwahitaji Uamsho kwa sababu hakuna aliyelala.

Na Mwandishi Wetu “Uamsho unamuamsha nani, ni nani aliyelala wakat i Wazanzibar i waliamka kitambo na ilipofika mwaka 1964 w a z e e w a k a f a n y a Mapinduzi ya umma yaliyoongozwa na Mzee Abeid Karume.”

Dk. Shein alitoa tamko hi lo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika tawi la CCM Kinuni na kuwahutubia wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa CCM Zanzibar, mapema wiki hii.

Hata hivyo baadhi y a M a s h e i k h n a wananchi waliochambua kauli hiyo walisema kuwa, wanachofanya Masheikh wa Uamsho ni ‘Fadhakkir’ na hii ni amri ya Mwenyezi Mungu haihitaji kibali cha Rais wala kamanda wa Jeshi.

Kwa upande mwingine wakasema kuwa kuamsha watu na kuwakumbusha juu ya wajibu wao kwa Allah, ni kama ilivyo Adhana katika Swala.

Japo watu wana saa, lakini kila ikifika wakati w a S w a l a , A d h a n a itasikika.

Zaidi wakasema kuwa Uamsho na Fadhakkir inawafaa pia ma-Rais na viongozi wa Serikali kwa ujumla kwani kutokana na madaraka yao na dhamana waliyobeba, ni rahisi kujisahau wakajiona kuwa ni miungu watu au wakahini amana zao na kusahau kuwa wao ni wachunga.

“Hawa wanahi ta j i k u a m s h w a n a kukumbushwa kila wakati kuwa wao ni wachunga na kila mchunga ataulizwa Siku ya Kiyama, siku ambayo FFU na Vikosi vinavyowalinda hivi l eo hav i takuwepo.” Amesema mwananchi mmoja akitoa maoni yake.

“Alikuwepo Mzee Abeid Aman Karume yupo wapi leo katangulia m b e l e y a h a k i , walikuwepo akina Dr.

SHEIKH Azzan.

Omari Ali Juma, katika Barzakh wametulia, na hapo ni ama bustani katika mabustani ya Peponi au shimo katika mashimo ya motoni.”

Aliongeza na kusema k u w a i n a t a k i k a n a k u w a a m s h a n a kuwakumbusha mara kwa mara viongozi wa Serikali waji tambue kuwa wao ni viumbe wa Allah ipo siku pumzi waliyo nayo itakatika na kwamba madaraka waliyo nayo ni amana tu, ni wachunga na ipo siku watasimamishwa mbele ya Hakimu na Mfalme wa wafalme kujieleza walivyowaongoza watu na kuchunga haki zao.

Kwa upande mwingine, baadhi ya Waislamu w ames ik i t i s hw a na kitendo cha Rais Shein

kuwahusisha Masheikh na vitendo vya kihalifu.

Wamesema, kitendo cha kuwataja Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) na kuwahusisha na uchomaji moto wa matawi ya CCM uliodaiwa kufanyika Kinuni, ni kuwadhalilisha Masheikh na Waislamu kwa ujumla.

Wa m e s e m a h i v y o kwa sababu kauli ya Mheshimiwa Rais Shein ameisema baada ya kulalamikiwa na wan-CCM kuwa tawi la chama hicho katika eneo la Kununi lilichomwa moto na watu wasiojulikana z i k i w a m o p i a n a maskani kuu za Kisonge na Kachochora mjini Zanzibar.

M a t a w i h a y o y a l i c h o m w a m o t o zilipoibuka vurugu mara baada ya Sheikh Farid kutoweka na yaliyojiri baadae.

Hata hivyo, Masheikh wa JUMIKI walishatoa kauli za kukaunusha na kulani kitendo cha kuhusishwa na uhalifu huo.

“ M a s h e i k h w a JUMIKI tunawajua, ni watu na heshma zao, ni wachamungu, hawawezi kufanya mambo ya k i h u n i k a m a h a y o hii ni kuwatukana na kuwatukana Waislamu w a n a o w a t e g e m e a kama viongozi wao na Maimamu wao,” amesema mkazi mmoja wa Mji Mkongwe akitoa maoni yake.

Page 4: ANNUUR 1069

4 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Makala/Tangazo

ARNOUD Van Doorn, Mdachi aliyesilimu hivi kar ibun i amefanya Umrah na kujistukia ak i sema ‘ samahani M t u m e ’ a l i p o s w a l i katika Msikiti wa Mtume Madina.

Van Door pamoja na mambo mengine katika ibada yake ya Umrah, alichukua muda kumtaka m s a m a h a M w e n y e z i Mungu ku tokana na kushiriki kwake katika k u f a n i k i s h a f i l a m u iliyozua ghasia kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu kwa vile ilikuwa i k i m t u k a n a M t u m e Muhammad (s.a.w).

Lakini kwa upande mwingine, Fitna hiyo ndiyo iliyomfanya mwanasiasa huyo mashuhuri huko Uholanzi, kusilimu.

Kwa maelezo yake mwenyewe, Van Doorn , anasema kuwa hasira za Waislamu zilizoibuka baada ya kutoka filamu hiyo na taarifa nyingi za kupakazia Uislamu matope na chuki dhidi ya Uislamu, zilimfanya aone sababu ya kusoma Qur’an na vitabu vya Hadithi ili kujua kwa uhakika Imani na mafundisho ya dini hiyo.

Anasema, aliyosoma katika utafiti wake huo ndiyo yaliyompelekea kutamka Shahada na kuwa Muislamu.

K w a s a s a a n a j u t a kuwa alishiriki katika k u f a n i k i s h a f i l a m u i l iyomtukana Mtume Muhamad na kwamba muda wote anaomba toba kwa Mwenyezi Mungu.

Fitna ni filamu fupi ya kiasi cha dakika 17 iliyotolewa katika internet mwaka 2008 ambapo Uislamu unaonyeshwa kama dini ya watu wa shari, wauaji na magaidi na kwamba uovu huo w a n a f u n d i s h w a n a Qur’an.

I l i tengenezwa kwa kuchukua baadhi ya aya na kuzipotosha maana yake na kisha kuziunganisha na taarifa na matukio mbalimbali katika vyombo vya habari.

Fi lamu hiyo i l izua maandamano na harakati mbalimbali za Waislamu kupinga kashfa hiyo.

Maandamano kama hayo yalifanyika pia hapa Dar es Salaam.

‘Samahani Mtume’…Mholanzi aliyesilimu asema Alipoingia Msikiti wa Mtume

Van Doorn anasema kuwa kile kilio, zile sauti na lile zogo la Waislamu duniani kote, ndio lililomfanya asilimu maana il ibidi achukue muda kuwasoma Waislamu na kuusoma Uislamu.

Akiendelea na shughuli zake za k is iasa japo amejitoa katika chama chake cha The Party for Freedom, ambacho ni maarufu kwa kutukana na kusambaza chuki dhidi ya Waislamu, anaendelea kuwa mbunge na Diwani katika Baraza la Madiwani la jiji la The Hague.

Ameandika barua rasmi kwa Meya wa jiji hilo kuwa, kila ikifika wakati wa swala lazima apatiwe ruhusa ya kwenda kuswali.

Anasema anashukuru amejifunza kuwa maisha yana lengo na kwamba kila uzoefu na kila hatua na mabadiliko anayopitia m t u k a t i k a m a i s h a , bas i yanaweza kuwa msaada muhimu ila hili lililompelekea kuusoma na kuujua Uislamu limekuwa

muhimu sana katika maisha yake na ni uchaguzi sahihi aliofanya.

“Nimefanya makosa mengi sana katika maisha

kama inavyokuwa kwa binadamu yoyote, na n i m e j i f u n z a m e n g i ku tokana na makosa hayo.”

Amesema na kuongeza kuwa ha tua yake ya kusilimu anaichukulia kuwa amejitambua na kuipata njia ya sawasawa.

Ewe Muislamu usikose kuhudhuria Dua Maalum ya kujikurubisha na kumlilia Allah (s.w.) dhidi ya dhulma kwa Waislamu nchini.

Mahali: Masjid Mtoro Kariakoo, Dar es Salaam.Siku: Jumatano Mei 8/2013Muda: Saa 8 mchana

Masheikh mbalimbali watakuwepo.

NB: Hukumu ya Sheikh Ponda Issa Ponda ni tarehe 9/05/2013 (Alhamisi) - Waislamu tuhudhurie kwa wingi

Wabillah Tawfiiq

JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU (T)

Dua - Masjid Mtoro

ARNOUD Van Doorn (kushoto), Mdachi aliyesilimu alipofanya Umrah hivi karibuni.

Page 5: ANNUUR 1069

5 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Habari za Kimataifa

RIYADHSERIKALI ya Saudi Arabia imelaz imika kuacha mpango wake wa kubomoa mahala a l i p o z a l i w a M t u m e M u h a m m a d ( S AW ) , ili kupanua ujenzi wa Masjidul Haraam baada ya hatua hiyo kukabiliwa na upinzani mkubwa wa wananchi na Maulamaa wa nchi hiyo.

Msaidizi wa Mkuu wa Baraza la Mji wa Makka anayehusika na masuala ya ustawi, A’ref Qadhi, amesema kuwa maktaba ya Makka haitabomolewa k w a n i i k o m a h a l a alipozaliwa Mtume SAW.

Hatua hii inakuja katika hali ambayo Sheikh Abdul Aziz Aal Sheikh, Mufti wa Saudi Arabia katoa fat’wa ya kuruhusu kubomolewa athari za Kiislamu kwa ajili ya kupanuliwa Masjidul

Saudia kutoharibu alipozaliwa Mtume SAWHaram.

Naye Sheikh Abdul Wahhab Abu Suleiman, ambaye ni miongoni mwa Maulamaa wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini humo, amesema k u w a k u b o m o l e w a maktaba hiyo ni sawa na kuondoa athari kubwa zaidi za kihistoria katika dini ya Kiislamu na kwamba, suala hilo litaziumiza nyoyo za Waislamu ulimwenguni kote.

Pamoja na kushindwa zoezi hilo la kubomoa mahali alipozaliwa Mtume SAW, lakini inaelezwa kuwa athari nyingine nyingi za kale za Kiislamu, zilizoko pambezoni mwa Masjidul Haram zimeshaharibiwa na kubomolewa kwa amri ya utawala kifalme wa Aal Saud.

MTAWALA wa zamani wa Kijeshi wa Pakistan, Gen. Pervez Musharraf, amewekwa katika kizuizi cha nyumbani ambapo baadae a ta f ik i shwa kizimbani.

B a a d a e M a h a k a m a ya kupambana na ugaidi itamfikisha kizimbani kwa kuhusishwa na mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhuto 2007.

K u k a m a t w a k w a Musharraf ina maana amekosa kushiriki uchaguzi unaoendelea kufanyika nchini humo.

Mwendesha Mashitaka M k u u w a F e d e r a l Investigation Agency, Chaudhry Zulfiqar Ali, alisema kuwa hadi kufikia Jumanne wiki hii tangu akamatwe, Musharraf alikuwa bado hajafikishwa kizimbani kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni za kiusalama.

I n g a w a M u s h a r a f alishikiliwa mahabusu kwa siku 14, bado ataendelea kuwa kizuizini katika makazi ya shambani kwake Chak Shahzad, nje kidogo ya jiji la Islamabad, ambako pameonekana kama ni ‘nusu jela’.

Mahakama imepanga siku ya kusikilizwa kesi

Musharraf kizimbanikuwa ni Mei 14, zikiwa ni siku tatu baada ya k u f a n y i k a u c h a g u z i uliopangwa kufanyika Mei 11 mwaka huu, uchaguzi ambao ndio uliomrejeshwa nyumbani mwezi uliopita kutoka uhamishoni miaka minne.

Mamlaka za Pakistani tayari zilimwondolea sifa za kushiriki uchaguzi huo, jambo ambalo limemwathiri katika nia yake ya kurejea katika siasa nchini humo.

Benazir Bhutto, aliuliwa kwa bomu kutoka kwa mtu aliyejitoa muhanga wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mkuu huko Rawalpindi Desemba 2007.

Katika kusilikizwa kesi yake April 26, Musharraf aliwekwa mahabusu ya FID kwa siku nne, kwa ajili ya kuhojiwa juu ya mauaji ya Bhuto.

K a b l a y a k u r e j e a Pakistan, kikundi cha Tehreek-e-Taliban Pakistan kiliwahi kutangaza kuwa kilishaandaa kikosi maalum cha kummaliza kiongozi huyo wa zamani iwapo angekanyaga ardhi ya nchi hiyo.

Timu ya uchunguzi ya FIA imedai kukamilisha uchunguizi wake dhidi

ya Musharraf na kudai kukusanya kilichotajwa k u w a u s h a h i d i w a kutosha unaomhusisha moja kwa moja kiongozi h u o w a z a m a n i n a tuhuma za kufadhili jinai inayomkabili.

“Mara kadhaa Musharraf amejaribu kukana kuhusika na kuelekeza makosa kwa wengine, lakini kuna ushahidi wa uhakika unaothibitisha kuwa ana hatia.” alisema Chaudhry Zulfiqar Ali.

Aw a l i M u s h a r r a f alikamatwa na maofisa wa FIA Aprili 25 baada ya mahakama ya kupambana n a u g a i d i k u w a t a k a wapelelezi kumuingiza kat ika uchunguzi wa mauaji.

A l i s h i t a k i w a k w a kushindwa kutoa ulinzi m a k i n i k w a B h u t t o baada ya kurejea kutoka uhamishoni.

Wanasheria walipitisha shauri mahakama kuu la kumfungulia mashitaka kwa uchochezi wa kutangaza hali ya hatari mwaka 2007 na pia anakabiliwa na shitaka la kuuliwa kiongozi wa Baloch, Bw. Akbar Bugti mwaka 2006 katika operesheni ya kijeshi.

WAZIRI Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa miradi ya nyuklia ya Iran bado haijavuka mstari mwekundu.

A k i z u n g u m z a n a wanachama wa chama cha Likud, Netanyahu amedai kuwa Iran bado inaendeleza miradi yake ya nyuklia japokuwa bado haijavuka mstari m w e k u n d u , l a k i n i inaukaribia mstari huo.

Netanyahu alirejea

Hofu ya Netanyahu Adai Iran bado haijavuka mstari mwekundu

maneno yake dhidi ya Iran ambapo alisisitiza kuwa, Israel haiko tayari kutoa mwanya kwa Iran kuvuka mstari huo mwekundu.

Hata hivyo Meir Dagan, Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD, amekosoa vikali matamshi hayo ya Netanyahu na kusema kuwa, vitisho vya mara kwa mara vinavyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel vya kutaka kuishambulia kijeshi Iran, vimesababisha kuchafuka haiba ya utawala wa Israel ulimwenguni.

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

WAUMINI wa dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni wakiwa katika Ibada ya Hijja, Makkah Saudi Arabia.

Page 6: ANNUUR 1069

6 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013MAKALA

AWALI ya yote, ni ukweli usiopingika kuwa ibara ya 1 na ya 2 ya katiba ya jamhuri y a m u u n g a n o w a Tanzania, zinafafanua kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Aidha, inaonesha kuwa eneo la Tanzania ni Tanzania B a r a , T a n z a n i a Visiwani na eneo la bahari linalopakana na Tanzania.

Ukweli ni kwamba kuna mambo yasiyo ya muungano ambayo pande hizi mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) huyashughulikia wakati yale ya bara h u s h u g h u l i k i w a n a Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO ni Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano , Mambo ya Nchi za Nje, Ulinzi na Usalama, Pol is i , Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, u shuru wa fo rodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa

n c h i n i Ta n z a n i a unaosimamiwa na Idara ya Forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni. Leseni ya viwanda na takwimu, Elimu ya juu, Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya

Kero hizi katika Muungano mpaka lini?Na Abu Hudhaifah motokaa na mafuata ya

aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia, Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo, Usafiri na usafirishaji wa anga, Utafiti, Utafiti wa hali ya hewa, Takwimu, Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kuwa Tanzania ni nchi moja. Kuthibitisha hili rejea Ibara ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977(iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008).

Kwa kuwa Tanzania ni nchi moja ya Muungano wa mambo hayo pekee tajwa hapo juu bila shaka yapo ambayo si ya muungano ambayo yanaifanya Tanzania Bara na Zanzibar kuwa nchi mbili zilizoungana huku kila moja ikishughulikia mambo yake kivyake pasipo nyingine kutaka kujua yanafanyikaje, kwa wakati gani na nani mwenye dhamana ya kushughulikia.

Ifahamike kuwa hata haya yaliyounganishwa na kuifanya Tanzania moja, bado kuna matatizo lukuki kiasi kwamba yaliundiwa tume kadhaa na hata kuwa chini ya Waziri na Wizara au Ofisi ya Waziri.

Tatizo ni nini wakati i m e e l e w e k a k u w a tuliyoungana ni moja, mbili na tatu.. kama orodha inavyoonekana hapo juu? Inawezekana m a k u b a l i a n o yanakinzana na uhamisho w a m a k u b a l i a n o yaliyo katika orodha iliyokubaliwa na utendaji halisia au kila upande kufanya mambo fulani fulani kivyake vyake

kama yale yasiyo ya muungano.

Kwa kuzingatia ibara ya kwanza ya katiba na orodha ya hapo juu ni wazi kuwa bado kuna tatizo katika kuyatendea kazi yale ya muungano. Kwa mfano, usafirishaji wa bidhaa kutoka na k w e n d a Z a n z i b a r , Mtanzania anatakiwa kulipia ushuru kwa TRA na ushuru wa bandari Zanzibar kwa mzigo huo huo kwa mfano TV inapofika upande wa pili ijapokuwa katiba ina tuambia n i nchi moja na orodha ya mambo ya muungano inaonesha kuwa TRA pekee ni chombo chenye dhamana ya kukusanya kodi Tanzania bara na Zanzibar.

Kama suala la ushuru/kodi ni suala la muugano, kwanini uonevu huu uendelee kujitokeza? Iweje friji moja itozwe ushuru mara mbili na chombo kimoja? Kama h i l o l i n a w e z e k a n a inashndikana nini kwa friji inayosafirishwa toka Dar es Salaam kwenda Kigoma isilipiwe kila inapovuka mpaka wa mkoa mmoja kwenda mwingine na TRA? Au hili linawezekana kwa Dar es Salaam na

Zanzibar tu na je, ni halali?

N j i a z a k u o n d o a kero za muugano ni kuondoa taratibu kama hizi ambazo zinatufanya tushindwe kuuelewa e l e w a m u u n g a n o huu ni wa aina gani. Kwa serikali ambayo ina dhamira ya dhati ya kuongeza ajira kwa wananchi wake kujiajiri na kuwaajiri wenzao, huwa inajaribu kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa wakulima na kwa wafanya biashara wadogo wadogo na wakubwa.

H a k u n a m u u j i z a wa kutatua matatizo ya Watanzania bi la kuhakikisha kuna uwepo wa utawala unozingatia usawa kwa watu wake, usawa wa ugawanaji wa pato la taifa, ujenzi ulio sawa wa miondo mbinu, uwajibishaji wa watendaji wabovu na ufatiliaji wa utendaji wa waliopewa dhamana ili kuhakikisha kuwa wanawajibika.

Ifahamike kuwa sauti za wanyonge wa kundi dogo zapaswa kusikilizwa na wale walalamikiwa na si kuwapuuza kwa namna yeyote. Kiongozi bora ni yule anayesikiliza na si mpuuzaji wa malalamiko

ya kundi fulani bila kutafakari wanasema nini, kwa nani, kwa nini wanasema hivyo na akajiuliza ni nini suluhisho la tatizo lao?

Suala la usafirishaji wa mizigo kutoka Zanzibar kwenda Dar au kutoka Dar kwenda Zanzibar lahitaji utatuzi na kuwaondolea mzigo Watanzania wa hali ya chini kwani hata gharama za uchukuzi katika boti zinatisha, kwa mfano TV ndogo ya nchi 14 unatakiwa kulipia sh. 5000 hadi 10000/= ukijumlisha na ushuru wa bandari zote mbili (Dar na Zanzibar) pamoja na ushuru wa TRA unaotozwa pande zote mbili ni hatari.

Bila shaka wenye b u s a r a w a t a j a r i b u kutafakari mambo haya bi la kukurupuka na kuyatafutia ufumbuzi hasa baada ya kupima ukweli. Na kiongozi wa kweli ataonekana daima kwa kuyashughulikia matatizo ya kundi dogo linalolalamika. Nami n i m e c h u k u a k a l a m kuliwakilisha kuonesha li l ipo tatizo ingawa pengine hawajaliona au wameliona lakini hawajapata fursa ya kuzungumzia.

WAZANZIBARI wakiwa katika moja ya mikutano yao ya hadhara kisiwani humo.

Page 7: ANNUUR 1069

7 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Makala

TUMEAMBIWA kuwa ‘mafuta yametolewa katika orodha ya mambo ya muungano’. Tumeambiwa hivyo katika mfululizo wa vikao vingi. Cha mwisho kilikaa Zanzibar Beach Resort, mara tu baada ya sherehe za mapinduzi January 12-2013, chini ya uenyekiti wa Makamo wa Rais, Dr. Bilali na huku Balozi Seif Ali Iddi.

Vilifuata vikao vya chama – CCM, pia viliridhia hilo. BLW, na Bunge limeambiwa hivyo mara elfu kidogo. Hii imekuwa nyimbo ya wanasiasa wa pande zote mbil i – Tanganyika na Zanzibar.

Karibuni hivi, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda al i l iar i fu Bunge kuwa ‘mafuta yametolewa katika orodha ya mambo ya Muungano’. Msimamo wa Jaji Warioba na Tume yake ya Katiba ni kuwa ‘suala hilo litajadiliwa kama sehemu ya kutengeneza katika mpya’. Halina haraka?

Hivi karibuni Mheshimiwa Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamo wa PILI wa Rais aliliarifu BLW kuwa ‘bado majadiliano yanaendelea kuhusu suala hilo’ ama yawe ya Zanzibar au Muungano au…..vipi si jui . Yaani, suala hilo bado halijatolewa

Tunapanga orodha ya wachezaji Arsenali huku Zanzibar inakwenda

Siasa hizi ni Mafuta ya Zanzibar au Muungano?

Na Mwandishi Maalum‘Tanganyika’ au Muungano. Umakini ungalikuwapo, Wawakilishi wangaliweza kumbana Waziri Mohammed A b o u d a t u p e u k w e l i wa mambo! Jamani nchi inateketea, inatutoka hiyo.

Ms imamo wangu au imani yangu: ‘Tanganyika’ hawakubali wala hawathubutu kuyatoa mafuta ka t ika ulingo wa muungano, na kama watayatoa, basi ni ‘kimaandishi tu’; wao ndio signatories wa mikataba yote ‘….na ushirikiano wa kimataifa….’

Tanganyika hawakubali aslan Abadan kuitoa Zanzibar au kuiwacha Zanzibar. Mfanye mnavyoweza, wala msijilinganishe na ex-USSR au Yugoslavia au wapi na wapi sijui. Sisi tusubiri, siku moja, tuimbishwe Aleluyah, na tutakwenda kuimba na huku tumevaa misalaba. Na Hatutokataa.

Tutabaki kucheza keram, na kupanga list wa wachezaji wa Asernal, Manchester United, Liverpool, na Real Madrid. Tutabaki kuhadithi mipira kila asubuhi tu, na nchi inazidi kututoka. Kigezo cha kuwa mstaarabu – ni kujua mpira na kuangalia mpira wa Man United, na kumhadithi Sir Alex Ferguson/na upumbavu kama huo. Mtoto wa miaka saba, juzi ninamsikia anapanga list ya majina ya wachezaji wataocheza usiku wake, na ilikuwa hivyo hivyo.

maamuzi, ndio maana yake. Sasa hapa tukamate lipi?

Hapa ndio panaponiuma mimi kuwa tunachukuliwa Wazanzibari ‘just for granted’, na ‘just for ride.’ Na nyie

wenzangu wengi mnakubali. Hii ndio hali inayotukabili Z a n z i b a r . T u m e k o s a muelekeo, tumekosa mawazo mbadala.

Tumegeuzwa kama mpira wa kona. Hatuoni uimara wala umakini wa wabunge na wawakailishi wetu katika masuala kama haya, hasa yanapogusa masilahi ya

SHUKRANI zote anastihiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote na Rehema na Amani zimfikie yule aliye tumwa kuwa ni Rehema kwa viumbe vyote ambae ni mtume wetu Muhamad.

Ama baada ya utangulizi huu umefikia Uislamu msamaha wake ukomo wa ukubwa ambao haujapata kufikia hapo kale wale hautofikiwa baadae katika sheria. Maisha ya Amani yemeletwa na Uislamu kwa watu wote. Basi mazungumzo yetu ya leo ni juu ya vyanzo vya fikra na nadharia juu ya msamaha huu.

Sisi waislamu tunaamini tupo katika haki na wengine wapo katika batili. Sisi tupo katika uongofu na wengine wapo katika Upotevu sisi ni waumini na wengine ni makafiri katika

Na Sheikh Abou Bakar Soliman

Mashina ya msamaha katika Uislamumtazamo wetu na vipi tuishi nao makafiri kwa mshamaha huu ambao Uislamu umeuleta. Msamaha huu una shina na msingi wa kifikra muhimu.

Mwanzo wa shina hilo ni imani yetu kuwa kutofautiana na watu ni kwa uwezo wa mwenyezi Mungu na yeye ndiye anayetaka haya yote yatokee na hakuna wa kuzuia anayoyataka Mungu na uwezo wa Mwenyezi Mungu umeambatana na hekima zake kwani yeye halifanyi jambo isipokuwa lina hekima. Anaijua atakaejua na ataekosa kuijua na hivyo sio kwa tama za Muislamu hii ni kinyume cha matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amesema mwanyezi Mungu Mtukufu. (Lau angetaka Mola wako wangeamini watu wote duniani hivi wewe unawachukia watu hadi wawe waumini”

Na shina la pili ni kwamba kafiri na muumini hisabu zao sio hapa duniani na hazitolewi ni kiumbe bali hesabu zao juu ya ukafiri au Imani inakua ni huko akhera na inatoka kwa mwenyezi Mungu Mtukufu anasema Allah “Na wakikujia wambie Mwenyezi mungu anaya jua n inayoyafanya . Mwenyezi Mungu atahukumu kazi yenu siku ya kiama kwa

yale mnayotofautiana hadi 68 – 69” hukumu siku ya kiama inatoka kwa Mwenyezi Mungu na sio kutoka kwako wewe. Na pia anasema Mola Mtukufu “Mwenyezi Mungu ni Mola wetu na Mola wenu sisi tunamatendo yetu na kati yenu mwenyezi Munga atatukusanya kati yetu na kwake tutarejea.

Na hii hupelekea kupumzisha moyo wa Muislamuu.

Mtu huyu ni kafiri Mwenyezi Mungu ndiye atamlipa juu ya ukafiri wake huyu mtu anastahiki jahanamu Mwenyezi Mungu ndiye anaejua ikiwa alikufuru kwa ujinga au kwa ukaidi basi huu ndio mfano wa pili katika shina la msamaha katika Uislamu.

Shina la tatu Imani ya Muislamu juu ya utukufu na Binadamu ni u tukufu wa kibinabamu. Anasema Mwenyezi Mungu “kwa hakika tumemtukuza binadamu Israi (70) utukufu sio wa Muislamu peke yake bali ni kwa watu wote. Utukuf huu ni wa binadamu wote kila aliye binadamu hauangalii:-

Rangi yake – Mweupe au mweusi

Utaifa wake – Mwarabu au Mwafrika

Bara lake – Mmashariki au Mmagharibi

Tabaka lake - Masikini au Tajiri

Utamaduni wake – Msomi au mjinga

Binadamu kama binadamu ni Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu.

Na katika mifano ya kazi juu ya hayo ni kwa yale aliyopokea Imamu bukhari katika sahihi yake toka kwa jabiri Bin Abdillah (R.A) kwamba Mtume (SAW) walipita na jeneza Mtume akasimama wima wakasema ewe Mtume hilo ni jeneza la Myahudi!! Akasema Jee hiyo sio nafsi? Ndio………………hiyo ni nafsi ya Binadamu na kila nafsi ya binadamu ina utukufu wake na thamani yake.

Shina la nne:- Kwamba Uislamu unaamrisha uadilifu (usawa) kwa watu wote na usawa sio kwa Waislamu peke yao. Akasema Allah “Na mnapo hukumiwa kati ya watu hukumianeni kwa usawa (Uadilifu Nisai 58) Basi uadilifu wa mwenyezi Mungu ni kwa viumbe wake wote kwani zimeteremshwa aya tisa katika Surat nisai 105-113 kwa kumtetea myahudi ambaye alituhumiwa wizi na ilikuwa walio iba ni ni Waislamu

au katika walio tuhumiwa juu ya unafiki. Walijaribu kumbandikizia hizi tuhuma huyu myahudi na alikusudia mtume kutaka kuwatetea wezi hawa na ikateremka Qur-ani ili kumtakasa huyu Myahudi na kumtetea.

Na kuwaonyesha hawa ambao wal i ja r ibu kumpa tuhuma asiyehusika basi usawa haugawanyiki na wala haupimiki kwa mizani bali ni kwa uadilifu na usawa na mwenyezi Mungu anasema:-

“Enyi mlioamini kuweni na msimamo kwa ajil i ya mwenyezi Mungu mashahidi wa Usawa (uadilifu) na wala zisikudanganyeni uadui wa watu hadi mkaacha uadilifu (USAWA) fanyeni uadilifu huko ndio karibu na ucha Mungu na mcheni Mwenyezi Mungu” Su-rat – Maidah.

Uadui maana yake sawa ikiwa uadui huo na dharau hizo ni kwenu nyinyi kwao au bughudha yao kwenu isikuchukulieni vitu hivyo mkaacha kufanya uadilifu (usawa) na katika hadithi (……………Dua ya aliyedhulumiwa hata kama ni kafiri haina pazia kati yake na mwenyezi Mungu”

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atufundishe yaliyo na manufaa na atunufaishe kwa yale tunayojifunza.

Page 8: ANNUUR 1069

8 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Makala

KATIKA jumla ya habari zilizopewa uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki iliyopita, ni pamoja na yale madai ya Serikali ya Marekani kuwa Rais Bashar El Assad anatumia silaha za kemikali katika kupambana na wapinzani wake. Akitangaza taarifa hiyo, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Charles Timothy "Chuck" Hagel amenukuliwa na Kituo cha Utangazaji cha CNN akisema kuwa Marekani ina ushahidi kuwa silaha za kemikali zimetumika Syria.

Taarifa hiyo inakuja siku mbili baada ya jasusi wa Israeli naye kudai kuwa Damascus ilikuwa inatumia silaha zilizopigwa marufuku chini ya sheria ya kimataifa dhidi ya watu wake yenyewe katika vita vya wao kwa wao nchini humo. Akizungumzia suala hilo, Rais Barack Obama alisema serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake yenyewe nchini humo ingebadil i muundo wa kinachotokea. Kwamba kwa sasa Marekani i t a a n g a l i a u w e z e k a n o wa kuingilia kijeshi (eti) kuwanusuru wananchi wa Syria wasiangamizwe.

Taar i fa ya gaze t i l a Washington Post ikasema kuwa Mashirika ya ujasusi ya Marekani yanazo taarifa za kijasusi kuwa Assad alitumia silaha za kemikali likamnukuu Hagel akisema kuwa hitimisho la tathmini iliyofanywa na mashirika ya kijasusi lilifikiwa katika ‘viwango tofauti vya usahihi,’ ikimaanisha kuwa hitimisho hilo halina ushahidi usio na kipingamizi.

Barua ya Ikulu kupitia gazeti la Washington Post i l idhihirisha zaidi j insi ushahidi huo ulivyokuwa ni wa kulazimisha tu: “Jumuia yetu ya kijasusi inatathmini kwa viwango tofauti vya usahihi kuwa utawala wa Syria umetumia silaha za kemikal i kwa kiwango kidogo nchini Syria, hasa kemikali ya sarin. Tathmini hi i kwa upande mmoja imeegemea katika sampuli zenye miundo inayoeleweka. Viwango vyetu vya ushahidi vinahitaji kutumia msingi huu wa tathmini za kijasusi wakati tunaendelea kutafuta ushahidi halisi ambao umethibitishwa. Kwa mfano, mlolongo wa

Habari za kiintelijesia!Nyingi ni uzushi, ufasiki, usaniiMasheikh wetu wachunge ndimi Waulize maswali, sio kutoa kauli

Na Omar Msangi

nani alikuwa ameshika nini (kuhusiana na kemikali sarin) hauko wazi, hivyo hatuwezi kuthibitisha jinsi kemikali hivyo ilivyotumika na katika mazingira gani. Tunaamini kuwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria ungetokana bila shaka na utawala wa Assad.”

C h a k u s h a n g a z a n i kuwa Marekani inajaribu kurudia hadithi za silaha za maangamizi nchini Syria, kama ilivyofanya kwa ulaghai uliochukiza kote duniani kule Iraq na kuwa sababu ya kuangamiza mamilioni ya roho za watu wakiwemo askari wapatao 5000 wa Marekani na maelfu wengine kutiwa vilema.

Kisingizio cha Marekani kuvamia Iraq kilikuwa kuwa Saddam Hussein ana silaha za kemikali na ana kiwanda cha kutengeneza silaha hizo. Na ulimwengu wakati ule uliambiwa kuwa ‘zilikuwa taarifa za kiintelijensia na kijasusi za kuaminika.” Lakini miaka 10 tu baadae Rafid Ahmed Alwan al-Janabi raia wa Iraq aliyetumiwa kusuka uwongo ule, sasa ametoka hadharani na kusema wazi kuwa ulikuwa uwongo na yeye ndiye aliyetumika kuandaa taarifa na vielelezo vya uwongo ambavyo alivitumia aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani wakati ule Collin Powell

kuhutubia Umoja wa Mataifa Februari 5, 2003 akitamba kuwa wana uhakika kuwa Iraq ina silaha za maangamizi na kwamba wao watakwenda vitani hata kama Baraza hilo halitaidhinisha. Alijenga hoja kuwa kwa ushahidi walio nao wanakwenda kuwanusuru wananchi wa Iraq.

“Defec tor admi t s to WMD lies that triggered Iraq war”, ndivyo vichwa vingi vya habari vilivyobeba habari hiyo katika magazeti mbalimbali ambapo Rafid Ahmed Alwan al-Janabi, jina la kazi za kijasusi akijulikana kama Curveball (codenamed Curveball).

“They gave me this chance. I had the chance to fabricate something to topple the regime.”

Anasema al-Janabi akieleza alivyotumika kutunga uwongo na kuusambaza. Na kufafanua kuwa yeye kwa vile alikuwa Muiraq na muhandisi wa kemikali (chemical engineer), ilikuwa rahisi uzushi wake kukubalika kuliko angekuwa mtu wa nje.

Janabi kabla ya hapo alikuwa akitumiwa na Idara ya Usalama ya Ujerumani Bundesnachrichtendienst (BND). Taarifa zake alikuwa akiziwasilisha BND na hawa BND ndio wakizifikisha kwa CIA.

Kama i l ivyor ipot iwa katika gazeti la The Guardian

(Uingereza) , baada ya kukamilisha uzushi huo alipewa hadhi ya ukimbizi na kupewa nyumba ya kukaa Karlsruhe, Kusini-Maghari ya Ujerumani. Pamoja na nyumba, BND walimpa gari aina ya Benz (Mercedes Benz) na posho ya Paundi 2,500 (Euro 3000) kwa mwezi.

A k i f a f a n u a walivyotengeneza ushahidi wa uwongo anasema kwa miezi sita akitumia taaluma yake ya Uhandisi wa kemikali (chemical engineering), alikaa na makachero wa Ujerumani na kutengeneza mchoro na picha za kiwanda cha silaha za kemikali kinachoweza k u h a m i s h w a k u t o k a sehemu moja hadi nyingine (mobile weapons trucks). Akamtaja kachero mmoja wa Ujerumani akijitambulisha kwa jina la Paul kwamba alikuwa ndiye mtaalamu wa Silaha za Maangamizi (expert on weapons of mass destruction) aliyeongoza jopo la kutunga uwongo huo. Na kwamba baada ya michoro kukamilika, ikadaiwa kuwa yeye, Curveball, ndiye aliiba au kupiga picha kutoka Iraq akitajwa kuwa alikuwa mhandisi aliyeshiriki katika kuunda kiwanda hicho hadi kilivyoanza kuzalisha silaha za kemikali. Michoro na hadithi hii ya urongo, ndiyo aliyoitumia Waziri wa Mambo ya Nje, Collin Powell, katika

kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pale aliposema:

“We have f i rs t -hand descriptions of biological weapons factories on wheels. The source was an eyewitness — an Iraqi chemical engineer who supervised one of these facilities. He was present during biological agent production runs. He was also at the site when an accident occurred in 1998. Twelve technicians died.”

A k i m a a n i s h a k u w a Marekani ina ushahidi kutoka kwa Injinia Muiraq aliyehusika kujenga kiwanda hadi kinaanza kuzalisha silaha. Lakini Injinia mwenyewe, ndio huyo anayesema leo kuwa alitumiwa kubuni urongo huo!

Baada ya hotuba hiyo ya Powell katika Umoja wa Mataifa ambapo ilikuwa wazi sasa kuwa Marekani inaivamia Iraq, Rafid Ahmed Alwan al-Janabi alimpigia simu kachero wa BND ambaye ndiye alikuwa akiripoti kwake akimweleza alivyomwona Powell akitumia urongo wake kuhalalisha uvamizi na vita Iraq.

Anasema baada ya kuongea naye akamwambia kwamba kuanzia siku hiyo, hali si shwari kwake kwa hiyo ni lazima afichwe. Inavyoonekana ni kuwa baada ya kuona nini kinafuata, kwamba Iraq inavamiwa, watu wasio na hatia watauliwa, ubinadamu ulimjia, ikaanza kumshika huruma, kuwaonea huruma wananchi wenzake.

Kuanzia siku hiyo Janabi alifichwa kama mtu aliye kifungoni na hakutakiwa kuonana na mtu yeyote wala kuona TV au kusoma magazeti. Kwa hiyo vita inaanza ndugu zake wa Iraq wanauliwa, hana habari anapata habari za juu juu tu za kuokoteza. Inawezekana waliomtuma kazi hiyo walihofia kuwa akiona watu wasio na hatia wanavyouliwa, ubinadamu ungemshika akatoa siri. Na angesema kabla malengo ya kuisambaratisha Iraq haijakamilika, ingekuwa kizaa zaa. Hivi sasa, miaka 10 baadae ndio anasema. Lakini isaidie nini?

Hivi sasa Rafid Ahmed Alwan al-Janabi ana hali ngumu sana. Alionekana wa maana mwaka 2003 akapewa nyumba, pesa za kumtosha matumizi na kupewa gari la kifahari-Mercedes Benz.

Inaendelea Uk. 13

Rafid Ahmed Alwan al-Janabi,

Page 9: ANNUUR 1069

9 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013TANGAZO

Page 10: ANNUUR 1069

10 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Makala

TUNAISHI katika kipindi ambacho, kwa lugha ya kiungwana, tungesema kina changamoto nyingi sana. Tunahitaji kuzama kwenye kina kirefu zaidi kuweza kufahamu nini kinatokea, hapa nyumbani na duniani kote, kuhusu Waislamu wakweli, waadilifu, ambao wamej i toa kwa dhat i kupigania haki zao, ikiwa ni pamoja na kuendesha harakati za kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu.

Inaonekana kuna kipengele kinachoingilia jitihada za Waislamu kupigania haki zao zinazoporwa, ikiwa ni pamoja na kueneza mafunzo sahihi ya dini yao. Kipengele hiki ni kipengele cha woga. Wa i s l a m u w a n a o g o p a kupigania haki zao! Woga wa namna hii siyo tabia ya Kiislamu. Haupo kwenye Saikolojia ya Muislamu halisi na unapotosha jamii nzima ya Waislamu. Lazima tuupige vita woga kwa nguvu zote!

Wote tunakubali kwamba, njia ya kutatua changamoto zetu, hata zikiwa ngumu kiasi gani, ni kufuata nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hauwezi kukuta katika maisha ya Mtume w a M w e n y e z i M u n g u kwamba alionyesha woga wa kutekeleza jukumu, ingawa alipata mitihani mizito kweli kule Makka na Madina.

Moja ya mitihani mizito aliyokumbana nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ni wakati ule alipokuwa vitani na majesh i ya maadui yalipoonekana kuwazidi nguvu Waislamu. Wakati Waislamu walipohisi wako hatarini katika nyakati zile za kujitoa muhanga, maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuwa faraja kubwa katika nyoyo zao na yaliwaangazia njia yao.

Hayo ndiyo maelezo ya wale Waislamu, ambao wamejitoa kwa dhati, wao na maisha yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakati wanapokuwa katika mitihani mizito kutoka kwa madhalimu. Mwenyezi Mungu anasema kulikuwa na kundi la Waislamu wa kweli, chini ya uongozi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambao waliambiwa kwamba kuna kundi la majeshi ya kukodiwa ya Maquraysh, yaliyojikusanya kwa lengo la kuwashambulia:

“Wale ambao waliwaambia ( W a i s l a m u ) : “ W a t u wamekukusanyikieni. Kwa hivyo waogopeni”. Lakini (maneno hayo) yakawazidishia imani (Waislamu), wakasema:

Woga katika kupigania hakiNa Said Rajab

“ M w e n y e z i M u n g u anatutosha. Naye ni mlinzi bora kabisa” Qur(3:173).

Nguvu zote, ziwe za kijeshi, kisiasa, vyombo vya habari, mahakama, propaganda na nyinginezo, zimeelekezwa dhidi ya Waislamu. Nini unadhani lilikuwa jibu la Waislamu? Je? walihisi wafanye mazungumzo ya kujinusuru kutoka kwenye mtihani ule mgumu? Je? walihisi warejee tena kwenye makabrasha na kuanza kuandika upya sera, dira na mikakati ya harakati zao? Hapana hata kidogo!

Mi t ihan i kama h iyo inapowatokea Waislamu kutoka kwa madhalimu, huchangia tu kuimarisha imani zao, ikiwa ni pamoja na kuwaongezea juhudi katika harakati zao kama tulivyoona kwenye Aya, na kamwe siyo sababu ya kusalimu amri au kuleta visingizio vya kukwepa wajibu. Misukosuko ni lazima kwa Waislamu wakweli! Hiki ni kipimo kwa wale wanaosema wamemuamini Mwenyezi Mungu:

“Je, Watu wanadhani wataachwa (wasitiwe katika misukosuko) kwa kuwa wanasema “Tumeamini?” Basi ndiyo wasijaribiwe ( w a s i p a t e m i t i h a n i ) ? Qur(29:2).

Hiyo siyo njia ya jinsi imani inavyofanya kazi! Hivyo sivyo alivyotufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mara ngapi tunasoma kwenye Qur’an (na wengi wetu ni wasomaji wazuri) kwamba hakuna hofu itakayowapata vipenzi vya Mwenyezi Mungu

wala kuhuzunika: “Sikilizeni! Vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika” Qur(10:62).

Tukiliangalia hili katika istilahi za kitabibu, vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawaugui maradhi ya ‘neurosis’ wala ‘depression’. Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama tunavyoifahamu historia yake, na ndiye kiigizo chetu, alikabiliana na majeshi na nguvu kubwa ya wakati ule. Makafiri walimkejeli, walimtisha, walimsumbua, walimwagia utumbo wa mnyama aliyechinjwa na mateso mengine mengi.

Je, Kuna dalili yoyote kwenye vitabu vya Sira, mahal i popote ambapo ukisoma, unaweza kuhisi hapa Mtume wa Mwenyezi Mungu ameonyesha woga au hofu kwa makafir i? Hakuna! Alitengwa na jamii yake - jamii ile ile ambayo ilimkubali kwamba yeye ni “As-saadiq al-ameen” (mkweli, mwaminifu). Kwa miaka mitatu, Waislamu walilazimika kula ngozi kwa kuwa hawakuwa na chakula; kulikuwa na dalili yoyote ya woga kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu au wale waliokuwa naye? Miye sijaiona!

Kinyume chake, Mitume wote wa Mwenyezi Mungu na watu waliokuwa karibu nao hawakuogopa kupoteza maisha yao. Wakati Mtume alipoona mateso ya Ammar na Al Yaasir, Mwenyezi Mungu awawie r adh i , alisema vumilieni - hakika

mmeahidiwa Pepo. Mtume hakusema “Subiri kidogo, mambo yanakwenda kombo sasa, itabidi tutafute njia ya kuzungumza nao lugha laini kwa maslahi ya taifa!” Katika maisha yote matukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hutopata rejea au tukio linaloonyesha kwamba alishadidia mawazo ya kijinga namna hii.

Kama binadamu, bila shaka Mitume walikuwa na hofu, lakini hofu yao ilikuwa ni kwa jamii na watu waliowazunguka. Mara ngapi inaelezwa ndani ya Qur’an kuhusu maneno ya Mitume katika kipindi chote cha historia:

“Ya kwamba msimuabudu yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu; hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya siku (kubwa hiyo) inayoumiza” Qur(11:26)

Hiyo Aya inatufundisha kwamba Mitume hawakuwa na hofu ya kutaka kunusuru n a f s i z a o a u z a w a l e walioshikamana nao; bali hofu yao kubwa ilikuwa ni kwa wale waliopotea njia ya Mwenyezi Mungu. Sasa linganisha hofu hii yenye akili na ile ya woga, ambayo huonyeshwa na baadhi ya Waislamu, ambao wapo katika nafasi za kusema ukweli, lakini wanaogopa kusema ukweli.

Wana uwezo wa kushiriki mapambano ya kudai haki zao, lakini wanaogopa changamoto zinazoendana na shughuli hiyo.

Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwenye hadith

ambayo mara nyingi hatupendi kuinukuu, amesema Jihad kubwa zaidi ni kumwambia ukweli mtawala muovu. Wako wapi Waislamu wenye sifa hizi leo? Lengo hasa si kuwanyooshea watu vidole, bali kutafuta mzizi wa tatizo na kuweza kubadilisha hali hii isiyopendeza.

Ni rahisi sana kunukuu Aya hii ambayo inapendwa s a n a : “ N y i n y i n d i y o umma bora kuliko umma zote zi l izodhihir ishiwa wa tu (u l imwengun i ) - mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu na mnamwamini Mwenyezi Mungu” Qur(3:110).

Najua ni rahisi zaidi kusema kuliko kutenda, lakini Waislamu wa aina ya Sheikh Ponda Issa Ponda wao hutenda zaidi kuliko kusema. Haki ya Waislamu imeporwa s e h e m u , b a s i S h e i k h Ponda atakuwa wa kwanza kuifuatilia na kuipigania kwa namna zote. Msimamo wake usioyumba katika kupigania haki za Waislamu wa nchi hii, umemfanya awe mwiba kwa watawala, kipenzi kwa Waislamu, na tatizo kwa wanafiki.

Kama She ikh Ponda angekuwa mwoga katika kupigania haki za Waislamu, kama tulivyo sisi wengine, ‘wapiga porojo’ basi a s i n g e p a t a m a t a t i z o anayoyapata sasa. Ukweli wake, Msimamo wake usioyumba na hofu yake kwa Mwenyezi Mungu, mara zote vimemfanya aonekane kero kwa madhalimu. Ponda amekuwa ajenda i s i y o k w i s h a k w e n y e v i k a o v y a o ! K w a Waislamu wa Tanzania wanaodhulumiwa, Ponda ni hazina kubwa, lakini kwa madhalimu na wanafiki ni balaa kubwa!!

Ndugu zangu katika i m a n i , t u n a j u k u m u kubwa kwa jamii yetu inayotuzunguka. Jukumu hili litatushinda kutekeleza, i w a p o b a a d h i y e t u tutajiona ni wanyonge na wengine kudandia mfumo unaokandamiza Waislamu.Kazi ya kupigania haki zetu, katika mfumo wa utawala unaokandamiza Waislamu ni yetu wenyewe. K a m a h a t u t a k u w a w e n y e k u j i a m i n i n a w e n y e k u m t e g e m e a Mwenyezi Mungu kwa dhati kabisa, basi hatuna sifa ya kufanya kazi hii. Tutakuwa vikaragosi tu vya madhalimu.

Page 11: ANNUUR 1069

11 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Makala/Tangazo

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu.Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika ofisi zifuatazo:-1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987.3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 4538384. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 4445. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 7861016. Dukani kwa Abdala Hafidh Mazrui wete pemba 0777 482 6657. Dukani kwa Mohamed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 4569118. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 6796929. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736Wahi kulipia. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444.Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987.Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC

Tanbih:Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu.Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu.Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo.Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo.Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi.

Nyote mnakaribishwa

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

April 02, 2013 ‘Mtandao wa kupashana habari’

ZAIDI ya miaka 11 tangu mkasa wa kuvunjiliwa mbali kwa Kituo cha Biashara cha Kimataifa, serikali ya jiji la New York mwishowe inauliza: Nini katika dunia hii kingeweza kutokea kwa waliokufa 1,116 ambao hawajapatikana?

Katika historia ya kuanguka majumba kote duniani , miili ya waliokufa wote imepatikana ikiwa katika hali ya kawaida. Hii ni kwa sababu jengo linaloanguka linavunja miili ya watu. Hayaiteketezi kuwa vipandepande vidogo, au kuisababisha kupotea kiajabu.

H a t a h i v y o m n a m o Septemba 11, 2001, kuanguka kwa majengo kwenye sifa zaidi katika historia kwa nj ia moja au nyingine kulisababisha miili ya zaidi ya waliokufa 1,000 kupotea kana kwamba ni kwa miujiza. Hakuna hata kipande cha ngozi, kichembe cha ukucha, au cha mfupa kimeonekana kutoka kwa miili yote hiyo au kupatikana wakati wowote ule, licha ya umakini mkubwa wa juhudi za ‘kupeta na kutia kwenye ndoo’’ za waokozi na watafutaji miili.

N i n i k i l i t o k e a k w a karibu miili 3,000 ambayo iliteketezwa katika upoteaji kwa sekunde kumi wa minara hiyo miwili ya ghorofa 110? Jibu: Ni kile kilichotokea kwa samani za ofisi, kabati za chuma kuwekea mafaili, simu, makompyuta, na vitu vingine vilivyokuwa katika minara hiyo. Hakuna mabaki yaliyopatikana ya takriban chochote kile. Vifaa hivyo, kama miili ya watu, kwa njia fulani vilibadilishwa na kubakia kama vijipande vya taka na vumbi la chini ya micron 100 za upana (au 1/1000 ya sentimeta moja), vumbi tu ambalo lilisambaa katika bahari ya Atlantiki. Kama mmoja wa wapepetaji n a w a p a k u a j i k w e n y e ndoo, kipande kikubwa zaidi cha samani ya ofisi kilichopatikana kilikuwa ni kipande kidogo tu cha ubao wa herufi za kuandikia wa kompyuta.

K w a b a h a t i m b a y a , uwezekano wa kupa ta mabaki ya zaidi ya waliokufa wachache ni mdogo. Kwa hali yoyote, taka ya minara miwili -ambayo ilikuwa ni chini ya asilimia 5- ya uzito wa minara hiyo (nini kilitokea kwa uzito uliobaki) - ilishapepetwa kwa uangalifu na kujazwa kwenye ndoo zaidi ya muongo mmoja uliopita. Uamuzi wa jiji wa kupeta katika mabaki ya ujenzi uliofanyika hivi karibuni (kutafuta mabaki)

9/11: Kukosekana uhalali wa serikali ya MarekaniJiji la New York lauliza: Nini kilitokea kwa waliokufa 1,116 wa 9/11 waliopotea?Na Dk. Kevin Barret

inafanana kiasi fulani na uamuzi wa (aliyekuwa Rais wa Marekani) George W. Bush kupiga magoti kuangalia chini ya meza yake (ya ofisi) kama ‘silaha za maangamizi’ za Irak (ambazo hazikuonekana) zimefichwa hapo. Hivi hii ni aina ya mzaha wa Siku ya Wajinga ya Aprili Mosi?

Kukosekana kwa miili iliyovujnika lakini ipo jumla, samani za ofisi au vifaa, na takriban asilimia 50 ya uzito wa majengo minara kunaonyesha kuwa minara miwili haikuanguka, ililipuka. (Angalia filamu ya Youtube ‘ M n a r a w a K a s k a z i n i Ukilipuka’). Hii ingetoa mwanga kwanini vijipande vya mifupa ya binadamu viligunduliwa vimesambaa katika dari ya jengo la Benki ya Ujerumani karibu na minara ilipokuwa, mwaka 2006. Hakuna kuanguka kwa kawaida, kama ilivyoelezwa na taarifa rasmi ya serikali ya Marekani, kungeweza kupasua miili ya watu kuwa vijipande na kuvisambaza kote katika jengo lililo karibu na hapo.

Hivi minara miwili, na maelfu ya watu waliokuwa h u m o , i l i t e k e t e z w a kwa mil ipuko? Ndicho wanachoamini wengi kati ya wanafamilia ya waliokufa katika tukio la 9/11. Robert McIlvaine, ambaye mwanae Bobby a l iuawa ka t ika minara miwili mnamo 9/11, amesema kuwa takriban n u s u y a w a n a f a m i l i a wanasadiki kama yeye kuwa minara hiyo ilivunjwa kwa kulipuliwa kwa kutumia mbinu ya kijeshi ya ‘kukosea walengwa wa mashambulio.’ William Rodriguez, shujaa anayefahamika sana wa 9/11 ambaye amezungumza na mamia ya maelfu ya watu kote duniani (kuhusu tukio hilo), ni mmoja kati ya waliopona 9/11 anasema kuwa ushahidi wa ‘ubomoaji uliopangiliwa’ ni siri iliyo wazi.

Mwanasayansi Carl Sagan aliwahi kuonyesha kuwa “kutokuwepo ushahidi siyo ushahidi wa kutokuwepo” ( k w a k i n a c h o t a f u t w a ) kuhusiana na 9/11, Baadhi ya maeneo mengine ya ‘ushahidi unaokosekana’ ni:

(1) Kukosekana kwa video zaidi ya 80 za serikali ya Marekani kuhusu shambulio la Pentagon (makao makuu ya Jeshi la Marekani), baadhi (ya video) zikiwa vimekamatwa na kuzuiliwa na wapelelezi wa FBI (shirika la upelelezi la Marekani) punde tu baada ya shambulio. Ni vielelezo vichache tu vimetolewa tangu wakati huo. na vielelezo hivyo vinaonyesha mlipuko katika Pentagon bila kuwepo

ndege kubwa.(2) Kukosekana kwa kilo

100,000 za dege la Boeing 757 ya abiria ambayo ilisemekana kuingia jengo la Pentagon. Hakuna vielelezo vyovyote vya kilo hizo laki moja za mabaki ya ndege hiyo, au mabaki ya mizigo iliyokuwa ka t ika ndege au wa tu waliokuwamo kuondolewa katika mojawapo ya maeneo m a t a t u y a l i y o v u n j w a , yaliyotengana kwa umbali mkubwa katika jengo la Pentagon.

(3)Kukosekana kwa kilo 100,000 za dege la abiria la Boeing 757 ambayo ilisemekana kujichimbia katika ardhi laini chini ya pango dogo la wazi la upana wa mita 15 eneo la Shanksville j imboni Pennsy lvan ia . Hakuna ushahidi wa tani 100,000 za dege lililoanguka, pamoja na mabaki ya abiria na mizigo kuondolewa chini ya ardhi katika eneo linalodaiwa dege hilo lilianguka hapo.

(4)Kukosekana kwa rasimu ya abiria waliokuwamo katika ndege hizo, video za kamera za usalama (uwanja wa ndege), vigunzi vya tiketi zilizouzwa, ushuhuda wa wafanyakazi wa ndege, au ushahidi mwingine wowote kuwa vijana wale 19 wa Kiarabu waliosemekana (kusababisha ndege hizo kugonga minara , n .k . ) walikuwa katika ndege hizo.

( 5 ) K u k o s e k a n a k w a minaso ya sauti ya maofisa wa Mamlaka ya Usafiri

wa Anga (ya Marekani) wakieleza kiofisi kuhusu walichokihisi kikitokea mnamo 9/11. Minaso hii i l inyang’anywa (kutoka kwa maofisa wengine) na msimamizi wa FAA (mamlaka hiyo) na kuchanwachanwa kuwa vijipande, ,ambavyo vilitawanywa katika vikapo vya takaratasi tofauti hivyo visiweze kukusanywa na kuundwa upya.

( 6 ) K u k o s e k a n a kwa v i sanduku vyeus i visivyoharibika vya ndege zilizogonga minara miwili. S e r i k a l i y a M a r e k a n i inadai kuwa visanduku hivyo hakupatikana, lakini walioshuhudia kilichotokea wanasema wal ikuwepo vilipopatikana na kuchukuliwa na maofisa wa FBI.

( 7 ) K u k o s e k a n a k w a ushahidi wa serikali uliotajwa sana: Minaso ya sauti na mikanda ya video ya masaa meng i ya u t e swa j i na kuandikwa taarifa za uwongo za kukiri kwa taahira Abu Zubaydah aliyesemekana ndiye kinara wa mashambulio ya 9/11 na ‘kinara mwenzake’ Khalid Sheikh Muhammad. (Sh i r ika l a Ujasus i l a Marekani) CIA linakiri kuwa liliteketeza kinyume cha sheria minaso hiyo ya sauti, wakati taarifa za kudakiza kuhusu k i l i chokuwepo zikitajwa katika Ripoti ya Tume ya 9/11 kama ushahidi pekee wa kuwepo wateka nyara 19 (katika tukio hilo).

(8)Kutokuwepo maelezo yoyote yale yenye hisia ya ukweli kuhusu taarifa ya awali ya BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza) kuhusu kuanguka kwa jengo namba saba (mmoja wa minara), kukiri kwa Larry Silverstein kuwa alillivunja jengo la WTC-7 na (bila shaka) operesheni ya kuvunjwa kwa milipuko wa jengo hilo.

Kat ika k i la moja ya maeneo haya, kama katika suala la miili 1,116 ambayo haikuonekana - kukosekana kwa ushahidi ni ushahidi tosha (wa kilichotokea).

Serikali ya Marekani sasa inakabiliwa na kukosa hadhi kabisa ya kutawala.

(Hii ni tafsiri ya makala, “9/11: Illegitimacy of US Government -New York City asks: What happened to the 1,116 missing 9/11 victims?” iliyoandikwa na Dr. Kevin Barrett. Dk. Kevin Barret, m w e n y e s h a h a d a y a uzamivu katika masuala ya Uarabu na Uislamu, ni mmoja ya wakinzani wanaofahamika za id i Marekani kuhusu ‘Vita dhidi ya Ugaidi.’ Dk. Barret ameonekana mara nyingi katika vituo vya televisheni vya Fox, CNN, PBS na vituo vingine vya utangazaji, na kuwezesha kuandikwa makala na tahariri katika magazeti yenye sifa kama New York Times, Christian Science Monitor, Chicago Tribune na mengineyo.)

Page 12: ANNUUR 1069

12 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013

MAKALA

K WA N Z A n a p e n d a kunena kabisa kwamba mimi ni mtoto wa Mkulima niliyezaliwa kule kijijini Mea-Mtwaro, Wilyani Tunduru ambaye nimekuwa na uwezo wa kuandika barua kama hii kutokana na zao la korosho ambalo kwalo Wazazi wangu walilitumia kuninunulia k a l a m u a m b a y o l e o naitumia kuandika makala hii. Hivyo naliheshimu sana zao la Korosho na kuchukia pale zao hili linapobezwa na kutwezwa na baadhi y a w a t u w a l i o s h i k a mamlaka ya kusimamia zao hili na hivyo kupelekea kukemea vitendo vya hovyo vinavyoashiria kulizika zao hili huku nikijua kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwazika ndugu zangu wa Tunduru na kusini kwa ujumla kwani zao hili ni uti wa mgongo wa uchumi wa Wanakusini.

Aidha, kabla sijanyanyua mguu mbele, ni bora nieleze japo kwa ufupi kuhusu Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaoashir ia kul ipeleka zao la korosho Shimoni ili kwayo wale walotandwa na utandu machoni mwao waweze kutanduka. Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ni utaratibu ulioanzishwa mwaka 2005 chini ya Sheria ya ‘Ware House Receipts Ac t ‘ ya Mwaka 2005 ambapo kupitia mfumo huo, Wakulima wa mazao ya biashara huikopesha Serikali kupitia vyama vya Ushirika huku Serikali ikitanguliza nusu ya bei ya zao husika na nusu nyingine hubakia ghalani mpaka pale Serikali itakapouza mazao hayo kwa wanunuzi kutoka Ng’ambo.

Mfumo huu ulianzishwa chini ya sheria ya mwaka 2005 ya ‘Ware House Receipt Act’ ya mwaka 2005 ambapo pamoja na malengo mengine, kubwa lilikuwa kuwasaidia Wakulima baadaya wanunuzi binafsi kununua mazao hayo kwa bei ya ‘kuwalalia Wa k u l i m a ’ . L i c h a y a Serikali kuwa na nia nzuri ya kuwasaidia wakulima, bado mfumo huo haufai kwani baada ya mfumo huo kuwa ni nyenzo ya kulisukuma gurudumu la maendeleo umekuwa kinyume chake.

M f u m o h u u n d i o unaowafanya wakulima

Mfumo wa Stakabadhi GhalaniNi maafa kwa mkulima, umefeli

Na Bakari Madaya kupokea fedha katika awamu mbili. Upokeaji wa fedha katika awamu mbili haufai kwani wakulima wadogo wadogo wanaouza korosho zao robo hadi tani moja huambulia kuwapeleka watoto wao shuleni kwa fedha za awamu ya kwanza huku wakisubiri fedha za awamu ya pili kwa kununua mbolea na mambo mengine ambapo kwasababu za kii t i lafu za uongozi fedha hizo za awamu ya pili huja machi hadi Aprili wakati Wakulima wakijiandaa kuvuna mazao yao ya Mahindi na Mpunga yaliyokosa mbolea kwa sababu ya ucheleweshaji wa fedha hizo na hivyo kupelekea mavuno madogo yanayosabab i sha n j aa ambayo kwayo huistua Serikali na kuanza kupanga safari kwenda Ng’ambo kuomba chakula.

M f u m o h u u n d i o unaopelekea Wakulima wadogowadogo kuchelewa kujenga nyumba za bati kwani Wakulima wadogowadogo huuza korosho zao na kupata fedha za awamu ya kwanza na hivyo kujikongoja kununua bati huku wakisubiri zile zilizopo ghalani ili wamalizie kununua nondo, misumari, boriti na simenti tayari kwa ujenzi. Kwa bahati mbaya Wakulima hawa hupata maradhi na hivyo kulazimika kukopa fedha kwa Wajasiliamali i l i w a k a n u n u e d a w a walizozichangia wenyewe huko hosptalini na hatimaye kusababisha fedha za awamu ya pili kuwa ni kwa ajili ya kulipa madeni na hatimaye ujenzi kuzorota.

M f u m o h u u n d i o uliosababisha mahudhurio f i n y u y a Wa n a f u n z i waliofaulu kwenda kidato cha kwanza Wilayani Tunduru kwani mpaka sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya Wanafunzi ambao hawajaripoti Shuleni kutokana na wazazi wao kukosa soko la kuuza Korosho zao kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, vyama vya Ushirika Wilayani Tunduru vilivyokuwa na dhamana ya kununua korosho hizo vilikuwa vinadaiwa na Benki ya NMB na hivyo kupelekea korosho hizo kuuzwa ‘Kangomba’ kwa bei ya ‘kutupa’ na hivyo hasara kubwa kwa Wana-Tunduru.

Utaratibu wa Stakabadhi Ghalani ndio unaosababisha

Uhasama kati ya Wakulima na Serikal i yao kwani wakulima wanauona mfumo huu ni nyonyaji na kandamizi kwani unaonekana kunukia Ufisadi na kuwapelekea wananchi kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa serikali na vyama Ushirika kama ilivyotokea huko Liwale jioni ya Aprili, 23 mwaka huu.

Kule Liwale Mkoani Lindi, Wakulima wa zao la korosho wamekataa kupokea shilingi 200/= kati ya shilingi 600/= zilizokabaki ghalani ambazo hata hivyo zimechelewa kufika. Ni mfumo huu ndio ulosababisha Wana-Liwale kukataa fedha hizo na hatimaye kusababisha vurugu.

Kwa maana nyingine, mfumo huu ndio uliopelekea nyumba 20 kuteketezwa kwa moto huko Liwale. Nyumba mbili za Mbunge wa Liwale zimeteketezwa, nyumba za viongozi wa CCM, Serikali na vyama vya Ushirika hazikuachwa nyuma kuteketezwa. Vurugu hizo zilizotokana na mfumo huu, ndizo zilizopelekea kuuawa kwa Ng’ombe 10 wa Meneja wa chama cha Ushirika Mkoani Lindi, Bw. Hamza Mkungura, ndizo zilizochoma nyumba ya Katibu enezi CCM Wilaya ya Liwale Bw. Abdallah Chande, zimechoma nyumba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bw. Mohamed Chande. Vurugu zimechoma nyumba ya Diwani wa kata ya Liwale Mjini.

Mfumo huu haukuacha nyuma kusababisha kuteketea kwa nyumba ya Meneja Mikopo wa Benki ya NMB Bw. Khalfani Mpaliluka na nyumba ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Bw. Mohamedi Ndemane.

Aidha, mfumo huu ndio utakaoiingiza Serikali hasara ya kujenga Miundombinu iliyoharibiwa na Wana-Liwale. Barabara ya Liwale-Nachingwea ni miongoni m w a m i u n d o m b i n u hiyo ambapo Wakulima wamechimba mashimo katika barabara hiyo, takribani kilometa 15 zimechimbwa na kuweka vitu vyenye ncha kali kuzuia Polisi kutoka sehemu nyingine wasiingie Wilayani humo.

Utaratibu huu uliopelekea Inaendelea Uk. 13

Someni ‘PARTNERSHIP’, kitabu cha muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, mintarafu muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, enyi wana muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, jembe na nyundo Chamwino,Someni ‘PARTNERSHIP’, ngangari jino kwa jino,Someni ‘PARTNERSHIP’, na wana-maandamano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, si hekaya wala ngano,Someni ‘PARTNERSHIP’, zi hoja si malumbano,Someni ‘PARTNERSHIP’, ni kitabu cha mfano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, risala ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, uketo wa muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, nje-ndani muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano,

Someni ‘PARTNERSHIP’, usuli wa muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, sababu za muugano,Someni ‘PARTNERSHIP’, natija ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, mazonge ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, mafyongo ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, upogo wa muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, fichuo la mafichano,Someni ‘PARTNERSHIP’, ndani Jumbe kwa mifano,Someni ‘PARTNERSHIP’, abaini migongano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, taswira ya muungano, Someni ‘PARTNERSHIP’, nyaraka za muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, takwimu za muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano .

Someni ‘PARTNERSHIP’, ni pevusho la muono,Someni ‘PARTNERSHIP’, si tambo la kimaono,Someni ‘PARTNERSHIP’, yakini ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, dhamira si utengano,Someni ‘PARTNERSHIP’, bali ni utangamano,Someni ‘PARTNERSHIP’, dira ya mshikamano,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, watoto wa muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, Mwanakombo na Machano,Someni ‘PARTNERSHIP’, wenyewe neno kwa neno,Someni ‘PARTNERSHIP’, muujue muungano.

Someni ‘PARTNERSHIP’, suluhu ya muungano,Someni ‘PARTNERSHIP’, kwa utuvu tena mno,Someni ‘PARTNERSHIP’, usia wangu kwa wino,Tusome ‘PARTNESHIP’, tuumanye muungano.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

SOMENI ‘THE PARTNER-SHIP’

Page 13: ANNUUR 1069

13 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013

MAKALA/TANGAZO

Vitabu vya Al-haj Aboud Jumbe Mwinyi The Partnership” (Kiswahili)

- “Muungano wa Tanganyika na Zanzibar miaka 30 ya dhoruba.”

Kwa bei ya jumla na rejareja vinapatikana Masomo Bookshop,

Zanzibar.

Kwa mawasiliano piga:-0777 46 47 48024 223 1048.

Mfumo wa stakabadhi ghalaniInatoka Uk. 12

machafuko na hasara kubwa Wi layan i L iwa le nd io unaoendelea kutumika kule Tunduru ambako mpaka sasa wakulima hawajalipwa shilingi 50 zao (Kwa kilo) za 2011- 2012, ndio unaotumika Masasi ambako mpaka sasa vyama vya Ushirika havijauza korosho za mwaka jana, ndio unaotumika maeneo mengine ambayo hulima Korosho na mazao mengine ya biashara. MUNGU epusha vurugu katika maeneo hayo.

Hivyo, nimeamua kuandika Makala hii ili kutumia Ibara ya 18 (1) inayoruhusu raia wake kuwa na uhuru wa kutoa mawazo na Fikra zao kuhusu Nchi yao.

Mosi, Serikali kupitia Bodi ya Korosho inayoongozwa na Mwenyekiti Anna Abdallah ha ina budi kuuangal ia tena mfumo huu na ikibidi kuuondoa kabisa kwani baada ya kuwa neema umekuwa Janga kwa Wakulima

Pili, Serikali isione aibu kuurejesha Mfumo uliokuwa uki tumika mwanzo wa kuwaruhusu wanunuz i binafsi kununua korosho hizo wenyewe vituoni isipokuwa tu Se r ika l i i hak ik i she inatangaza bei ya korosho baada ya majadiliano ya kina na Wanunuzi, kitu ambacho hakikuwa kinafanyika hapo awali.

Tatu, Serikali isihofie kwamba, kuurejesha mfumo

huo ni sawa na kuwazika Wakulima kwani Mfumo huu wa sasa ndio zikifu zaidi kuliko ule wa awali. Aidha hakuna hata mnunuzi atakayeng’ang’aninia bei ile ya shilingi 350-700 ya miaka ya nyuma hasa ukilinganisha gharama za maisha ya sasa. Pia ikizingatiwa kwamba wanunuzi hao hao huzinunua korosho hizo kwa shilingi 2000-2500 pale Bandarini Mtwara. Wenye Mamlaka mtusikilize.

( N i n a i t w a B a k a r i Madaya (Mwanatunduru). Ninapatikana simu namba: 0789 357 823 au barua Pepe: [email protected])

Habari za kiintelijesia!Inatoka Uk. 8Lililotakiwa limepatikana. Leo si BND, CIA wala White House wenye haja naye tena. Iraq nako hatakiwi. Hata hii serikali kibaraka, inamwona yeye ndiye kibaraka zaidi. Haitaki kumwona akirudi Iraq.

“I will be honest with you. I now have a lot of problems because the BND have taken away my flat, taken my mobile phone: I’m in a bad position.”

Anasema Rafid Ahmed Alwan al-Janabi akiongea na mwandish i wa The Gurdian Alhamisi iliyopita akimaanisha kuwa hivi sasa anaishi maisha ya tabu kwa sababu kanyang’anywa nyumba, hapewi posha na hata simu yake, pia amenyang’anywa.

Lakini zaidi anasema kuwa anajihisi hayupo salama, maisha yake yapo hatarini na hawezi kutoroka na kukimbia Ujerumani kwa sababu anachungwa na makachero muda wote. Hiyo ndiyo hatma ya usaliti.

Hata hivyo pamoja na somo hilo, lakini muhimu katika makala hii ni kuonyesha hiki kinachodaiwa kuwa ni taarifa za kiintelijesia’ zinavyoangamiza watu na nchi.

Tumesema kuwa baada ya uwongo huo ulioiangamiza Iraq na kuuwa mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kama sio mamilioni, hivi sasa Marekani inakuja na kisingizio hicho hicho kutaka kuivamia Syria. Inadai kuwa habari za kijasusi zinaonyesha kuwa Bashar El Assad anatumia silaha za kemikali kuwapiga wapinzani wake/raia na kwa hiyo lazima watimize jukumu la kuingia Syria kumng’oa madarakani Assad.

Hivi karibuni Kamishna mmoja wa Polisi alisema kuwa vyombo vya usalama vinazo taarifa za kiintelijesia kuwa nchini kuna makundi ya kigaidi ya Al Qaidah na Al Shabab.

“Taarifa za kiintelijensia zinatutahadharisha kuhusu uwapo wa magenge ya kigaidi Al Qaeda na Al Shabab nchini mwetu pamoja na kuibuka makundi ya kigaidi ya ndani,” alisema Kamishna Mwandamizi wa Polisi, SACP, Hussein Nassor Laisseri.

S A C P L a i s s e r i a l i s e m a h a y o k a t i k a semina iliyowashirikisha

Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Spika wake Mheshimiwa Kificho.

Misamiati hii Al Qaida, magaidi, wenyewe ndio hawa wanaowatumia akina Alwan al-Janabi kutengeneza uzushi ili wapate kuvamia nchi za watu. Upo ushahidi mwingi kuwa hawa akina al-Janabi wanatumika pia kufanya mashambulizi bila kujali kuwa watauliwa watu wasio na hatia. Haya hufanyika na kutafuta mtu wa kumpakazia i l i ipatikane sababu ya kufanya uhalifu kama ule wa Iraq.

K w a b a h a t i m b a y a katika nchi zetu hizi, hawa tumewaamini kuwa ndio wataalamu wetu, hata ukitokea uhalifu kidogo tu, tunaona fahari kukimbilia kuwaita watusaidie. Na misamiati yao tumeimeza haitutoki mdomoni. Tunaimba kama kasuku huku tukijidanganya kuwa ni ‘tungo’ zetu.

U p o u s e m i k u w a u k i m k a b i d h i m c h a w i mwanao ili amlee, basi ujue atabeba mikoba wakiruka usiku kwenda kuwanga. Kwa maana kuwa naye atafundishwa uchawi. Sasa huku kuwafanya hawa jamaa ndio walimu na wataalamu wetu, tunaposikia kauli hizi za polisi wetu kwamba taarifa zao za kiitelijesia zinaonyesha kuwepo ugaidi; lazima tuwe na wasiwasi kuwa yawezekana wameanza kurithishwa ungo wa kuwabeba akina al-Janabi kwenda kuwanga usiku.

Baada ya shambulio la Boston (Boston Marathon Bombing), mwandishi mmoja akiwa Chechnya aliwahoji baadhi ya watu wanajisikiaje kusikia kuwa Mchechen m w e n z a o , M u i s l a m u mwenzao kafanya shambulio lile lililouwa watu watatu wasio na hatia. Mtu mmoja, kama alivyoonyeshwa katika televishen alifoka akisema kuwa vijana hao wa Kichechen wamewatia aibu, wamewatia doa Wachechen wote na kuutukanisha Uislamu na Waislamu.

Nimalizie kwa kusema kuwa hili ndio kosa kubwa wanalolifanya baadhi ya Masheikh wetu hapa nchini. I t ada iwa kuwa kan i sa limechomwa moto halafu inadaiwa kuwa waliohusika ni Waislamu (siasa kali au Uamsho). Kisha wanasiasa au vyombo vya habar i v i n a m w e n d e a S h e i k h

wanamuuliza, nini maoni yako kuhusiana na kitendo hiki cha baadhi ya Waislamu kuchoma makanisa.

K w a k u f u a t w a kuulizwa Sheikh anaona kuwa kathaminiwa sana, anajimwaga. Anashutumu na kutoa aya na Hadithi kuwa kitendo hicho ni cha kulaaniwa na waliofanya hivyo hawajui Uislamu. Wanautukana Uis lamu. Kesho yake vyombo vya habari/na maadui wa Uislamu wanasherehekea kwa jinsi ulivyowabamiza Waislamu wenzako. Unakazia tuhuma, uchafuzi na uzushi kuwa

‘Waislamu ni magaidi’ au wakorofi, watu wa shari na wavuruga amani!

Mtu akikujia na swali kama hilo, kwanza lazima ujue kuwa kuna uwezekano wa kuwepo mchezo wa kuigiza ili ipatikane sababu ya kuwatukana Waislamu na kuwatafutia sababu. Lakini pili ni kuwa kanuni ya Qur’an ipo wazi, kwamba huwezi ukalisema jambo ambalo hujajua hakika yake. Kutoa maoni ni kuwa ushalijua jambo vizuri. Unajua kwa uhakika kilichotokea na nani kahusika.

Marehemu Profesa Sethy

Chachage aliwahi kuulizwa na msomi mwenzake mmoja kuwa anaonaje udini wa Mheshimiwa Rais Kikwete kuteuwa mabalozi wengi Waislamu. Aliulizwa kufuatia uteuzi uliokuwa umefanywa wa Mbalozi sita (6) ikatokeza kuwa wengi wao walikuwa Waislamu.

Akijibu swali hilo Prof. Chachage alisema kuwa ili aweze kutoa maoni ni lazima ipatikane kwanza orodha ya Mbalozi wote iangaliwe Waislamu wangapi na Wakristo wangapi.

Majibu ya namna hii ndiyo tunayotegemea kuyasikia kutoka kwa Masheikh wetu. Wahoji maswali ya msingi sio kukimbilia kutoa maoni ya jambo wasilolijua hakika

Page 14: ANNUUR 1069

14 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013Habari/Tangazo

Askofu apotosha kero za MuunganoInatoka Uk. 16uzushi mtupu na wanazushiwa hayo kutokana na Uislamu wa Wasomali hao na si vinginevyo, huku akiwataka Waislamu kuwa makini na tuhuma hizo kwani alidai, taarifa kama hizo huwa hazitoki bali kunakitu kimelengwa mbele dhidi ya Waislamu nchini.

“ G a z e t i l i m e a n d i k a ‘Wafadhili wa Al-Shabab hawa hapa’ utadhani wamefanya uchunguzi wa kina na wana lengo la kuonyesha ni nani hao wafadhili wa kikundi hicho, lakini ukisoma humo ndani

vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi zao.

Maalim Bassaleh, alisema hata wakati wa kupigania Uhuru raia wa nchi nyingi za Kiafrika husani kutoka kusini mwa jangwa la Sahara, walikuwa wakikimbilia Tanzania.

Maalim Bassaleh, alisema ukichunguza kwa umakini, utagundua kuwa hapo tatizo sio Usomali, bali ni udini kwa

sababu nchi hii imekuwa na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, lakini hazisikiki lawama kutoka kwa raia wa nchi hizo.

“Hii ni kwa sababu takriban wakimbizi kutoka nchi zote hizo ni Wakristo au wapagani. Lakini Wakimbizi kutoka Somalia wote ni Waislamu, na kama ndio wanahusika na haya yanayotokea sasa nchini mbona hawajawekwa hadharani hata mmoja.” Alisema Maalim Bassaleh.

utashangaa.” Alisema Maalim Bassaleh.

Akionyesha kustaajabu na taarifa hiyo Maalim Bassaleh, alisema Gazeti hilo limedai kwamba, uwepo wa kundi hilo unathibitishwa na matokeo ya utekaji na mauaji yanayojiri nchini kwa kuwa yanafanana na matendo yafanywayo na kikundi cha Al-Shabab.

“Ukweli ni kuwa, hapa

nchini wapo wakimbizi wa Kisomali, ambao wameingia nchini kukimbia mapigano yanayoendelea nchini mwao, hilo si jambo geni kwa Tanzania.” Alisema Maalima Bassaleh.

Alisema, nchi hii imekuwa na historia kubwa ya kupokea wakimbiz i kutoka ka t ika nchi jirani za Afrika kama vile Wanyarwanda, Warundi, Wakongo ambao hukimbia vita

STUDENTS ADMISSION 2013/2014

UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION – ZANZIBAR INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA – KHARTOUM

The University College of Education invites qualified applicants to apply for first degree courses in the following specializations:Bachelor of Science with Education1. Physics & Mathematics 2. Chemistry & Biology 3. Physics & Chemistry 4. Computer Science & Mathematic 5.Chemistry & Mathematics 6. Biology & Geography Bachelor of Science1. Computer ScienceBachelor of Arts with Education 1. English & Kiswahili 2. English & Geography 3. English & History 4. English & Islamic 5. Arabic & Kiswahili 6. Arabic & English 7.Arabic & Geography 8.Arabic & History 9. Arabic & Islamic 10. Kiswahili & Geography 11. Kiswahili & History 12. Kiswahili & Islamic 13. Islamic & Geography 14. Islamic & History 15. History & Geography ADMISSION REQUIREMENTSApplicants should:1. Have at least, a minimum of two principal passes in Tanzania Advanced Certificate of Secondary Education (ACSE) in the appropriate subjects or equivalent qualifications.2. Be proficient in English( All students where their medium of instruction was not English, must produce language proficiency certificate.)3. Provide a medical certificate from UCEZ Dispensary.4. Be a full time studentFEES

Tuition

1,800,000/= (1200 US $) per annum

Physics & MathematicsChemistry & BiologyPhysics & Chemistry Chemistry & MathematicsBiology & Geography

1,500,000/= (1000 US $)

Computer Science & MathematicComputer ScienceEnglish & GeographyKiswahili & GeographyArabic & GeographyArabic & HistoryKiswahili & HistoryIslamic & HistoryEnglish & HistoryIslamic & GeographyHistory & Geography

1,300,000/= (870 US $) per annum

Arabic & Kiswahili Arabic & EnglishArabic & Islamic English & IslamicEnglish & KiswahiliKiswahili & Islamic

Accommodation 180,000/= (120 US $) per annum

Graduation 30,000/= (20 US $)Students Union 10,000/= ( 7 US $)C o m p u t e r services

40,000/= (27 US $) per annum

Registration 40,000/= (20 US $) Medical Care 30,000/= (20 US $)Application Form 25,000/= (17 US $)Meals 1,800,000/= ( 1200 US $) OptionalStationeries 200,000/= ( 134 US $) Optional

The College reserves the rights to change these fees at any time.

Application forms are obtained fromAcademic Office, University College of Education Zanzibar at Chukwani P.O. Box 1933 Zanzibar, Mobile: 0773774838 OR 0772912181, Email: [email protected]

Application forms are also available from the following offices;- -Africa Muslims Agency, Mabaoni–Chake Chake Pemba: Tel: 024-2452337- Africa Muslims Agency, Tabata - Dar es Salaam: Tel: 022-2807843- Africa Muslims Agency, Kaloleni -Moshi- Africa Muslims Agency, Pongwe- Tanga.

Application fee should be paid through the following account numbers:- (i) The peoples Bank of Zanzibar (Islamic Banking division) Account No. 51120100002450- Mwanakwerekwe, Zanzibar(ii) Barclays Bank Account No. 003 – 4000387

All completed forms together with payment receipts should be returned to the Academic Office, University College of Education Zanzibar.N.B: All Applicants intending to pursue Bachelor of Arts with Education in Arabic or Islamic Studies with another combination will be required to attend three months comprehensive course in Arabic Language which will start on 2nd July, 2013 and ought to pay 400,000/=.

The deadline for receiving applications is Friday 30th 2013 and for applicants who are waiting for form six results should return the forms two weeks after the results. For further information contact:

Registrar,University College of EducationP.O BOX 1933, ZanzibarMOBILE: 0778698127E.mail:[email protected] the main campus at Chukwani, West District, Unguja, two kilometers from the new House of Representatives Building.

Page 15: ANNUUR 1069

15 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013TANGAZO

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

• KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – SAME – KILIMANJARO • NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – MWANZA • UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L – DAR ES SALAAM

1. Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu.2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, ‘Combinations’ za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA.3. Muombaji awe na ‘Crediti’ 3 au zaidi na angalau ‘D’ ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana ‘F’ au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano.4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /20135. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

• Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha – 0654 723 418 - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075• Tanga - Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 - Ofisi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770• Musoma - Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193• Kagera - Bukoba: Alhuda Café Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA. - 0688 479 667 • Shinyanga - Msiikiti wa Majengo-0718866869 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 • Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 - Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin – 0655144474 • Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086• Singida - Ofisis ya Islamic Ed. Panel – karibu Nuru snack Hotel – 0714285465 • Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575• Kigoma - Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860 - Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663• Mtwara - Amana Islamic S.S 0786 729 973• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU – 0715 681701/0716791113 - Mkuzo Islamic High School. 0716 791113• Mbeya - Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole – 0713 200209 - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209• Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122• Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331• Unguja - Madrasatul – Fallah: 0777125074- • Mafia - Ofisi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu – 0653705627

6. Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

Wabillah Tawfiiq

MKURUGENZI

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO – 2013/2014

Page 16: ANNUUR 1069

16 AN-NUURJAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 JAMADUL THAN 1434, IJUMAA MEI 3 - 9, 2013

IMEELEZWA kwamba, si sahihi kudai kwamba kero za Muungano zimeanza katika awamu ya utawala huu, kwa madai ya kuchochewa na kikundi cha watu wachache Visiwani humo.

H a y o y a m e b a i n i s h w a na Maalim Ally Bassaleh, akiwahutubia Waislamu mara

Askofu apotosha kero za MuunganoNa Bakari Mwakangwale baada ya swala ya Ijumaa,

wiki iliyopita katika Msikiti wa Idrisa, Kariakoo Jijini Dar es salaam.

Maalim Bassaleh, alikuwa akikanusha madai ya Askofu Seveline Niwamugiza, wa jimbo la Kanisa Katoliki, Lurenge, Ngara, aliyedai kwamba kuna kikundi cha watu wachache chenye lengo la kuvunja Muungano wa Tanzania.

Askofu huyo amenukuliwa

akidai kuwa watu hao ndio wanao sababisha fujo na kero za Muungano pamoja na vurugu Visiwani Zanzibar, zilizosababisha watu kuuwana, na kuibua neno la ‘kero za Muungano’.

Maalim Bassaleh, alisema Askofu huyo aliyenukuliwa na Gazeti la Tumaini Letu, la April 26, 2013, kufuatia mtazamo wake huo, akaitaka Serikali kudhibiti wavurga amani kwa

kuwa hawana nia njema na Taifa hili.

“Serikali imetakiwa kudhibiti na kutosikiliza matwakwa ya kikundi kidogo cha watu chenye lengo la kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kuwa watu hao hawana nia njema na Taifa hilo”. Alinukuu Maalim Bassaleh, maneno ya Askofu Niwamugiza, kutoka katika gazeti hilo.

Maalim Bassaleh, alisema yeye ni Mzanzibar, kwamba anapozungumzia suala hilo anajua nini anachoongelea na kudai kimsingi hakuna Mzanzibar, anayetaka kuvunja Muungano, bali wanachotaka ni kero za Muungano zipatiwe ufumbuzi.

Alisema, na si kweli kama anavyosema Askofu huyo wa Kikatoliki, kwamba eti madai ya kero za Muungano zimeanza katika awamu hii ya nne na kikundi hicho kidogo kama anavyodai.

Akikosoa madai hayo, Maalim Bassaleh, alisema kero za Muungano zilianza tokea awamu ya kwanza ya kipindi cha Mwl. Julius Nyerere, pale Wazanzibari walipodai Muungano una kero na kutaka kero hizo zitatuliwe.

Lakini, alisema majibu juu ya suala la kero za Muungano kutoka kwa Mwl. Nyerere, wakati huo wa utawala wake yalikuwa ni mengi katika sura tiofauti tofauti, lakini alidai moja wapo ni pale alipodai kuwa ‘Muungano huo ni sawa na ndoa ya Kikatoliki’, (isiyo na talaka).

Hata hivyo, Maalima Bassale aliendelea kuanisha ukongwe wa kero za Muungano akasema, katika awamu ya pili ya utawala, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, aliandika kitabu kiitwacho ‘The Partner Ship’ na kuweka wazi kero za Muungano.

“Hivyo utaona kwamba hizi kero za Muungano zipo muda mrefu si kama anavyodai huyu Askofu wa Katoliki, yeye anadai kero hizi zimeanza juzi tu kwa maana katika awamu hii ya nne, kumbe kero za Muungano zimeanza tokea awamu ya Mwl. Nyerere.” Alisema Maalim Bassaleh.

Alisema, ikiwa Mwl. Nyerere, kwa mtazamo wake aliona Muungano huu ni sawa na ndoa ya Kikatoliki, je, akahoji akitokea mwingine akasema kwamba Muungano huo ni sawa na ndoa ya Kiislamu, kuna ubaya?

“Tena hiyo ndoa ya Kikatoliki pamoja na kusema hakuna kuachana, lakini wanakubali kutengana ikiwa kero za ndoa zikizidi, lakini kwa Waislamu kuna talaka nayo ni kutengana na mkitaka mnarejeana, baada ya suluhu.” Alisema Maalim Bassaleh.

Akifafanua alisema, hiyo maana yake ni kama ndoa ya Kiislamu, ikiwa pana mgogoro uwe ni wa kindoa, kitaasisi, iwe ni wa kijumuiya, au ni wa Muungano, kinachotakiwa ni pande mbili hizo zikae pamoja zizungumze.

Alisema, hata Serikali kupitia Waziri katika Ofisi ya Rais, inakubali kwamba zipo kero na kwamba kero tisa tayari zimeshatatuliwa na zingine zipo mbioni kutatuliwa.

Maalim Bassaleh, alisema jambo hilo ndilo Wanzibar w a n a l o l i h i t a j i n a w a l a h a w a g o m b a n i i k u v u n j a Muungano, bali wanataka haki itendeke baina ya pande hizo mbili.

Maalim Bassaleh, alisema Zanzibar, ilikuwa na kiti chake Umoja wa Mataifa kabla ya Muungano kama ilivyokuwa Tanganyika, na viti hivyo vyote viliwekwa kando na kutengewa kiti kimoja cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maana wote wanahaki sawa, bila kuangalia ukubwa au wingi wa raia wao.

“Wakati huo haikuangaliwa kwamba Zanzibar, ilikuwa ndogo kiasi gani na watu wangapi, hapana. Ikumbukwe Zanzibra ilikuwa na kiti chake na mamlaka kamili. Hivyo inahaki ya kutoa Rais kama ilivyo Tanganyika, ilikuepuka kuongeza kero juu ya kero zil izopo.” Aliasa Maalim Bassaleh.

Akizungumzia taarifa zilizochapishwa katika gazeti la Dira, juu ya kuwepo kwa wafadhi l i wa Al-Shabab nchini, kutokana na madai kuwa kumekuwa na wakimbizi wengi wa Kisomali nchini, Maalim Bassaleh, alisema kama hukuisoma taarifa hiyo utadhani kwamba gazeti hilo limefanya uchunguzi makini.

Akinukuu sehemu ya taarifa ya gazeti hilo, Maalim Bassaleh, alisema anashangaa habari hiyo ianada kuwa eti miongoni mwa mipaka wanayo tumia kuingia nchini Wasomali hao kwa wingi kuwa ni Mbeya, Iringa na Kigoma.

Alisema, tuhuma hizo ni Inaendelea Uk. 14

Masjid Allah Karim Kazimzumbwi Kisarawe Inawaalika waislamu wote katika Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kazimzumbwi Kisarawe, Tarehe 25/05/2013,

siku ya Jumamosi Saa 2:30 Baada ya Swalatul Ishaa , Inshaalah.

Wafadhili wa maulidi Hii ni.1. Sheikh Juma Sadiki Muyenga2. Mohamed Rafi ki Nurmohamed Satya3. Ndugu wa Familia ya Madenge

MAULID!!! MAULID!!!