16
BANDARI TANGA MABINGWA “INTER-PORTS GAMES 2018” kujipanga kuchukua ubingwa na siyo vinginevyo. Michezo hiyo maarufu ya Bandari ya 12, kwa mwaka huu imefanyika katika mkoa wa Morogoro katika viwanja vya Jamhuri na bwalo la JKT la Umwema kuanzia Oktoba 15 mpaka Oktoba 19, 2018. TANZANIA PORTS AUTHORITY www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047 TOLEO NO: 11 OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 @tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @TPAHQ TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 01 04 BANDARI “INTER-PORTS GAMES 2019” KUFANYIKA ZANZIBAR… MICHEZO YA BANDARI IWE CHACHU YA KUONGEZA UFANISI 03 NDANI andari Tanga imetia fora kwa kunyakua vikombe na medali nyingi zaidi ya Bandari nyingine na kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa michezo maarufu ya 12 ya “Bandari Inter-Ports Games” kwa mwaka 2018. Na Focus Mauki-Morogoro Watu wengi walitarajia kama ilivyo ada katika michezo ya mwaka huu Bandari ya Dar es Salaam ingeibuka na ushindi wa jumla lakini kwa mwaka huu hali ilikuwa tofauti ambapo tangu michezo ilipoanza Bandari Tanga walionesha B Kwa ujumla wachezaji wa Bandari Tanga walionesha kuwa na timu zilizoandaliwa vyema na zenye ushindani kwa timu pinzani jambo ambalo wachezaji wa timu nyingine hawakulitarajia. Wachezaji wa timu zote za Bandari Tanga za pete, kikapu, kuvuta kamba, riadha, soka, bao, kwa ujumla walionesha 07 TPA RUDISHENI SIFA YENU KWENYE MICHEZO 06 MSIONEANE HAYA, KOSOANENI NA KUPONGEZANA PALE INAPOBIDI..... Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Lutengano Mwambona (kushoto) akikabidhi kikombe cha ushindi wa jumla wa jumla wa michezo ya Bandari kwa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bi. Moni Jarufu.

BANDARI TANGA MABINGWA NDANI “INTER-PORTS GAMES 2018” · Katika michezo ya mwaka huu 2018 timu za soka na kuvuta kamba kutoka Bandari Zanzibar na TICTS ziliomba kushiriki michezo

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • Toleo Maalum Michezo

    BANDARI TANGA MABINGWA“INTER-PORTS GAMES 2018”

    kujipanga kuchukua ubingwa na siyo vinginevyo.Michezo hiyo maarufu ya Bandari ya 12, kwa mwaka huu imefanyika katika mkoa wa Morogoro katika viwanja vya Jamhuri na bwalo la JKT la Umwema kuanzia Oktoba 15 mpaka Oktoba 19, 2018.

    TANZANIA PORTS AUTHORITY

    www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047 TOLE

    O N

    O:

    11

    OK

    TOB

    A 2

    8 -

    NO

    VEM

    BA

    11

    2018

    @tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @TPAHQ TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 01

    04

    BANDARI “INTER-PORTS GAMES 2019” KUFANYIKA

    ZANZIBAR…

    MICHEZO YA BANDARI IWE CHACHU YA KUONGEZA UFANISI

    03

    NDANI

    andari Tanga imetia fora kwa kunyakua vikombe na medali nyingi zaidi ya Bandari nyingine na kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa michezo maarufu ya 12 ya “Bandari Inter-Ports Games” kwa mwaka 2018.

    Na Focus Mauki-Morogoro

    Watu wengi walitarajia kama ilivyo ada katika michezo ya mwaka huu Bandari ya Dar es Salaam ingeibuka na ushindi wa jumla lakini kwa mwaka huu hali ilikuwa tofauti ambapo tangu michezo ilipoanza Bandari Tanga walionesha

    BKwa ujumla wachezaji wa Bandari Tanga walionesha kuwa na timu zilizoandaliwa vyema na zenye ushindani kwa timu pinzani jambo ambalo wachezaji wa timu nyingine hawakulitarajia.

    Wachezaji wa timu zote za Bandari Tanga za pete, kikapu, kuvuta kamba, riadha, soka, bao, kwa ujumla walionesha

    07

    TPA RUDISHENISIFA

    YENU KWENYE MICHEZO

    06

    MSIONEANE HAYA, KOSOANENI

    NA KUPONGEZANA PALE INAPOBIDI.....

    Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Lutengano Mwambona (kushoto) akikabidhi kikombe cha ushindi wa jumla wa jumla wa michezo ya Bandari kwa Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bi. Moni Jarufu.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    2 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    BANDARI TANGA MABINGWA “INTER-PORTS GAMES 2018”kuwa wamejiandaa vilivyo kutokuwa wasindikizaji katika michezo hiyo ambayo ilifunguliwa rasmi siku ya Jumatatu, Oktoba 15 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe.

    Akizungumza wakati wa kufungua michezo hiyo, Dkt. Kebwe alimshukuru,Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko kwa kutoa kibali na kuruhusu michezo hiyo kufanyika katika Mkoa wa Morogoro.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 3

    Bi. Nyimbo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa michezo ya Bandari iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, Oktoba 15.

    “Michezo ni nyezo muhimu ambayo inampa mfanyakazi motisha ya kuongeza tija inayokusudiwa lakini pia inajenga afya ya akili na mwili hivyo ni muhimu sana tukaitumia michezo hii katika kuongeza tija na ufanisi katika sekta nzima ya uchumi wa nchi huku bandari ikiwa ni moja ya eneo nyeti ambalo limewekwa katika vipaumbele vya Serikali Kuu kwa lengo la kuwa chachu ya kuelekea kwenye uchumi wa kati na uchumi wa viwanda” amefafanua Bi. Nyimbo.

    Kwa upande mwingine, Bi. Nyimbo ameahidi kwamba Bodi ya Wakurugenzi ya TPA kwa kushirikiana na Menejimenti imedhamiria kuiendeleza michezo ya ‘inter-ports’ kwani ni sehemu ya kuimarisha afya za Wafanyakazi na kuongeza ufanisi wa kazi.

    jumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimaliwatu ya TPA, Jayne Nyimbo amewataka wafanyakazi kuitumia michezo ya Bandari kama nyenzo muhimu ya kuongeza motisha ya kuongeza ufanisi katika kazi.

    Na Focus Mauki

    MBi. Nyimbo pia alitumia fursa hiyo kumshukuru, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka pamoja na Bodi nzima ya

    Wakurugenzi kwa kuridhia Wafanyakazi kushiriki katika michezo.

    Michezo ya Bandari ya mwaka huu imewahusisha zaidi ya wanamichezo 400 kutoka katika bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Bandari za Maziwa na Makao Makuu ambao katika muda wa siku tano wachezaji walishiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, bao, riadha na mpira wa kikapu.

    Wakati huohuo, Bi Nyimbo ametumia fursa hiyo kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kwa mchango unaotolewa na Mkoa wake katika kuhakikisha mizigo yote ambayo inasafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam inapita katika Mkoa huo salama ikielekea katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kama vile Zambia, DRC,Rwanda na Burundi.

    Amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Mkoa wa Morogoro katika usafirishaji kwenye ushoroba wa kati (central corridor) ndio maana Mamlaka iliona kuna umuhimu wa kuifanya michezo hiyo katika mkoa wa Morogoro.

    Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Rasilimaliwatu, Bi. Jayne Nyimbo akizungumza na Wanamichezo wakati wa ufunguzi wa michezo ya Bandari iliyofanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambae alikuwa mgeni rasmi katika tukio la ufunguzi wa michezo hiyo.

    Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipiga penati kuashiria ufunguzi wa michezo ya Bandari.

    MICHEZO YA BANDARI IWE CHACHU YA KUONGEZA UFANISI

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    4 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    Na Focus Mauki

    “Napenda kuwafahamisha kwamba Kamati Kuu ya Michezo imependekeza michezo ya mwakani 2019 ifanyike mjini Zanzibar, tutajipanga na kuona namna ya kufanikisha jambo hili,” amefafanua Msabimana.

    Msabimana amesema moja kati ya lengo la kupendekeza michezo ya mwaka 2019 kufanyika Zanzibar ni kuendeleza undugu na urafiki baina ya TPA na Bandari Zanzibar lakini kubwa zaidi ni kubadilishana uzoefu katika

    kutoa huduma za Bandari.

    Katika michezo ya mwaka huu 2018 timu za soka na kuvuta kamba kutoka Bandari Zanzibar na TICTS ziliomba kushiriki michezo ya Bandari ambayo ilifanyika mjini Morogoro kwa muda wa siku tano (5).

    Kwa upande mwingine, Msabimana amewapongeza wanamichezo na wafanyakazi wote TPA, Bandari Zanzibar na TICTS ambao walijumuika

    kwa pamoja kwa amani na utulivu mkubwa mjini Morogoro katika kipindi cha juma moja.

    Mbali na wanamichezo pia ameipongeza Kamati Kuu ya ya Michezo kwa umahiri walioonesha wa kuandaa mashindano ya mwaka 2018 na kutimiza malengo ya kujenga afya, mshikamano na uhusiano mwema.

    Amewaambia wanamichezo kuwa ni vyema wakakumbuka kuwa katika

    wenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bandari, Said Mussa Msabimana ametangaza kwamba michezo ya 13 ya Bandari itafanyika mjini Zanzibar endapo mipango itaenda kama ilivyopendekezwa.M

    BANDARI “INTER-PORTS GAMES 2019” KUFANYIKA ZANZIBARV

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 5

    michezo hii, Mamlaka inatumia gharama kubwa kwa lengo la kuboresha rasilimali watu iliyopo hivyo ni vyema michezo hiyo ikatumika vizuri katika kuongeza tija na uzalishaji kiwandani.

    Ameongeza kuwa kwa upande wa Menejimenti haina tatizo la kuboresha na kuongeza idadi ya michezo na wanamichezo isipokuwa ni kwa kigezo cha kuona wafanyakazi wameongeza tija na faida ndani ya Mamlaka na siyo vinginevyo.

    Michezo ya Bandari imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kuongeza tija ndani ya Mamlaka na Menejimenti imeahidi kuitumia sera ya michezo ili kuhakikisha sera hiyo inatoa dira ya

    kutumia michezo kama mojawapo ya kipimo cha tija.

    Kwa mwaka huu 2018 takribani michezo nane (8) imechezwa ikiwa ni pamoja na Mpira wa miguu, Mpira wa kikapu, Mpira wa pete, Kuvuta kamba, kurusha tufe, mkuki, bao na Riadha (Mita 100 na 400).

    Katika michezo ya mwaka huu zaidi ya wachezaji 400 wameshiriki michezo hii kutoka vituo vya Makao Makuu, Bandari za DSM, Tanga, Mtwara, Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na Kyela), Bandari Zanzibar na TICTS.

    Michezo ya Bandari kwa mwaka huu imefanikiwa kufikia malengo yake ambayo ni pamoja na kujenga afya na

    ukakamavu kwa wafanyakazi, kujenga na kudumisha urafiki, mshikamano, ushirikiano (team spirit) na kuimarisha nidhamu baina ya wafanyakazi.

    Wakizungumza na gazeti hili wanamichezo wengi wamethibitisha kuwa katika michezo ya mwaka huu timu zilicheza kwa nidhamu na uadilifu, zilishindana bila kugombana na washangiliaji walishangilia timu zao kwa juhudi bila kuzozana na wapinzani wao.

    Timu zote zimeahidi kuwa katika michezo ijayo ya 13 ya 2019 zitaongeza juhudi katika mazoezi ya kujiandaa na kutafuta vipaji vichanga ili kuwa vichocheo katika uzalishaji na hatimaye kuboresha tija ndani ya Mamlaka.

    BANDARI “INTER-PORTS GAMES 2019” KUFANYIKA ZANZIBARV

    2018takribani michezo nane (8) ime-chezwa ikiwa ni pamoja na Mpira wa miguu, Mpira wa kikapu, Mpira wa pete, Kuvuta kamba, kurusha tufe, mkuki, bao na Riadha (Mita 100 na 400).

    Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya TPA, Bw. Said Mussa Msabimana (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza Bandari ya Tanga. Aliyebeba kikombe ni Mwenyekiti wa DOWUTA Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mashaka Karume na kulia ni Mwenyekiti wa DOWUTA Bandari ya Tanga, Bw. Sankole.

    Mashabiki wa Bandari ya Mtwara wakiishangilia timu yao ya mpira wa kikapu, Bandari hiyo iliibuka na zawadi ya kikombe cha ushangiliaji bora.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    6 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    Na Focus Mauki

    Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wanamichezo kwenye hafla fupi ya kufunga michezo ya 12 ya Bandari iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri na Bwalo la JKT la Umwema mjini Morogoro hivi karibuni.

    Akizungumza na wanamichezo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Msaidizi wa Afisa Tawala wa Wilaya, Bw. Lutengano Mwambona amewapongeza wanamichezo na washindi na kuwakumbusha kuwa uboreshaji wa utendaji kazi na mustakabali wa TPA ni jambo lisiloepukika.“Daima mkumbuke wajibu wenu na dhamana kubwa mliyopewa na Taifa lenu kusimamia Mamlaka hii kubwa kabisa hapa nchini ya jukumu la kujiendesha kwa ufanisi na tija,”

    amesema Lutengano.

    Amewakumbusha Wafanyakazi kurudi katika vituo vya kazi wakiwa na hamasa, na kuwavutia wengine ili matokeo ya kazi ya msingi yawe ya ushindi.

    Amewataka wafanyakazi kutumia nadharia ya michezo ya kupata ushindi itumike kutaka kupata ushindi katika majukumu ya kazi za kila siku.

    “Baada ya michezo hii sasa ninawaomba nyote mseme uteja wa kushika mkia katika kutekeleza majukumu yenu ya kazi sasa basi lazima msonge mbele kwa kuongeza ufanisi, uadilifu na bidii katika utendaji kazi wenu,” amefafanua zaidi Lutengano.

    Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Wilaya pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wafanyakazi kwa ukakamavu na umahiri waliouonesha katika mashindano hayo ambayo yamewajenga kiafya na kuwaongezea ari na nguvu mpya ya kuwajibika katika vituo vyao vya kazi.

    Amewataka kujiuliza swali la msingi mara baada ya michezo hili kuwa wataongeza asilimia ngapi katika kiwango cha tija na kuvuka malengo yaliyowekwa na Bodi na Menejimenti kupitia kauli mbiu ya Serikali ya ‘Hapa Kazi Tu’.

    Amebainisha kuwa Watanzania wanaitegemea TPA ambayo inakabiliwa na mahitaji makubwa ya kuboresha utendaji kazi wake lakini bila kusahau maendeleo ya rasilimali watu wake ambayo ndio uti wa mgongo wa uendeshaji wa Bandari.

    kuu wa Wilaya ya Morogoro amewataka Wafanyakazi wa TPA kutoona haya kukosoa makosa ya kiutendaji, kupendana, kurekebishana pale mfanyakazi anapokosea na kupongezana pale inapobidi.M

    MSIONEANE HAYA, KOSOANENINA KUPONGEZANA PALE INAPOBIDI-DC MOROGORO

    Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Lutengano Mwambona akizungumza na wanamichezo wakati wa kufunga michezo ya Bandari. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Bi. Ediltruda Maseko na wengine ni wageni waalikwa na wanakamati wa michezo ya Bandari.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 7

    Na Focus Mauki

    Dkt. Kebwe ametoa rai hiyo wakati alipozungumza na wanamichezo kwenye hafla ya uzinduzi wa michezo ya 12 ya Bandari inayofanyika mara moja kila mwaka.

    “Wengi bado tunakumbuka jinsi ambavyo miaka iliyopita Bandari ilivuma kwa kuwa na timu nzuri na wachezaji wenye vipaji katika michezo ya mpira wa pete na mpira wa soka hata masumbwi, ambapo timu hizi zilikuwa zikicheza na kutambulika katika madaraja ya juu katika mashindano ya kitaifa, michezo hii iwe ni changamoto ya kungalia namna ya kurudisha heshima yenu katika michezo,” amebainisha Dkt. Kebwe.

    Ameongeza kuwa anawashukuru sana Wanabandari kwa kutambua ukweli kwamba michezo pekee inawaunganisha wafanyakazi kwa karibu na kuwa familia moja na kutujenga kiafya.

    Akifafanua zaidi, Dkt. Kebwe amesema, “natambua kwamba katika juma hili kutakuwa na ushindani mkali kwa timu zote za soka, riadha, kuvuta kamba, bao, mpira wa pete na mpira wa kikapu, lakini pia nafahamu kwamba michezo hii italeta mwamko kwa wakazi wa mji wa Morogoro ambao nao watashuhudia Wanabandari kutoka Tanga, Mtwara, Mwanza, Kigoma, Kyela, Dar es Salaam, Makao Makuu, TICTS na Zanzibar wakipimana nguvu na kuonesha vipaji vyao katika michezo.”

    Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa jitihada zake kubwa za kuboresha michezo ya Bandari tangu ilipoanza tena mwaka 2007 baada ya kuwa ilisimama kwa muda.

    Michezo hiyo iloporejeshwa mwaka 2007 kulikuwa na michezo mitatu tu ambapo tangu iliporejeshwa idadi ya michezo imeongezeka na kufikia mitano huku wafanyakazi 400 wengi zaidi wakipata fursa ya kushiriki.Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kuangalia mashindano hayo ambayo yalikuwa chachu ya pekee kwa wakazi wa Morogoro hususani wafanyabiashara wenye Mahoteli ambao kwao pia ilikuwa ni fursa ya kufanya biashara.

    Dkt. Kebwe ambaye kitaaluma ni daktari wa binadamu amesema ili Wafanyakazi wawe na tija na afya njema katika kutekeleza kazi zao ni muhimu kwa kila Taasisi husika kuhamasisha na kuendeleza michezo.

    Aliwaasa wanamichezo kushindana kwa nidhamu na kutokukamiana mpaka kuvunjana au kuumizana na kukumbuka kwamba michezo ni undugu si uadui, na kuwa wasikivu kwa viongozi na walimu ili kudumisha ushirikiano miongoni mwa wanamichezo na kuwa kioo mbele ya wapenda michezo kote nchini.

    “Mara baada ya kukamilika kwa michezo hii isiwe ni mwisho wa kushiriki michezo na kujenga afya zenu, endeleeni kushiriki michezo na kujijengea utamaduni wa kushiriki michezo kwa ajili ya afya zenu ili muweze kufanya kazi kwa tija, kwani bila afya njema huwezi kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi,” amesisitiza Dkt. Kebwe.

    Mkuu wa Mkoa amewataka wanamichezo kujituma katika kazi ili kuongeza tija, kufanya kazi kwa umakini, uadilifu na kwa ufanisi mkubwa na kumalizia kwa kusema kuwa, “sina hofu na wanamichezo, wanamichezo siku zote ni wachapakazi wazuri kwa kuwa na afya njema na akili zilizochangamka.”

    kuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewataka wafanyakazi wa TPA

    kurudisha sifa waliyokuwa nayo katika michezo ndani ya Taifa la Tanzania katika miaka ya zamani.

    MTPA RUDISHENI HESHIMA YENU KWENYE MICHEZO

    Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wanamichezo katika kilele cha ufunguzi wa michezo ya Bandari hivi karibuni.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    8 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    MATUKIO MBALIMBALI YA MICHEZO YA BANDARI

    8 | TPA GAZETI JULAI 02 - JULAI 14 2018

    Wajumbe wa Baraza kuu la Wafanyakazi wakifuatilia mkutano wa 24 uliofanyika chini ya Mwenyekiti Mhandisi Deus Dedit Kakoko hivi karibuni.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 9

    Mjumbe akichangia Mada katika Mkutano wa Baraza kuu la Wafanyakazi chini ya Mwenyekiti Mhandisi Deus Dedit Kakoko hivi karibuni.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    10 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    MATUKIO MBALIMBALI YA KUKABIDHI ZAWADI KWA WACHEZAJI

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 11

    Na Fassie Obadia

    Michezo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kuzikutanisha bandari zote ilijumuisha michezo ya Mpira wa Miguu, Mpira wa pete, Mpira wa Kikapu, Kuvuta Kamba, Mchezo wa bao na Riadha.

    Jambo lililokuwa kivutio katika michuano hiyo ni jinsi wachezaji wa bandari ya Mtwara walivyoweza kukonga mioyo ya watazamaji kwa aina ya ushangiliaji waliouonesha katika mji wa Morogoro ya kutumia manyanga, tarumbeta na vikoi huku wakicheza ngoma maarufu ya Mkoani Mtwara iitwayo Sindimba.

    Kutokana na ubunifu wa staili ya kushangilia Kamati ya Michezo iliridhishwa kuamua kuwapa Wachezaji hao zawadi ya kombe la ushangiliaji ambalo hutolewa katika michuano hiyo kwa Bandari ambayo inashangilia na kuonyesha hamasa katika michuano hiyo.

    Mbali na Kombe hilo la ushangiliaji

    Bandari ya Mtwara ilifanikiwa kuchukua kombe la ushindi wa pili katika mchezo wa Kikapu na Kuvuta Kamba Wanawake. Vile vile mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa Riadha waliweza kujinyakulia Medali mbalimbali za mchezo huo na kuweza kuiletea sifa bandari yao.

    Pia katika Mpira wa Kikapu mchezaji chipukizi kutoka Mtwara Kelvin Ikungura

    aliteuliwa na Kamati kuwa Mchezaji bora wa mpira wa kikapu kwa mwaka huu na kupewa zawadi ya kikombe.

    Shamra shamra hizo ambazo zilidumu takribani kwa wiki nzima zilihitimishwa mnamo tarehe 19 Oktoba, 2018 na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro .

    Michezo hii imeandaliwa na Mamlaka kwa madhumuni ya kusaidia Wafanyakazi wa Mamlaka kufahamiana, kubadilishana mawazo katika utendaji kazi, kuimarisha mahusiano na Afya za wafanyakazi kwa Ujumla.

    andari ya Mtwara wamekuwa washindi wa kombe la ushangiliaji katika michuano ya Interport Games, 2018 iliyotimua vumbi mkoani Morogoro hivi karibuni. B

    MTWARA WAIBUKA MABINGWA WA USHANGILIAJI INTER-PORT GAMES 2018

    Mwakalishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Lutengano Mwambona akikabidhi zawadi ya kikombe cha ushangiliaji bora kwa Bandari ya Mtwara.

    Timu ya kuvuta kamba wanawake ya Bandari ya Mtwara.

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    12 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    Timu zilizoshiriki katika michezo ya mwaka huu ni pamoja na Makao Makuu, Bandari ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Maziwa pamoja na wageni Bandari Zanzibar na TICTS.

    Katika michezo ya mwaka huu zaidi ya wanamichezo 400 wameshiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na soka, pete, kikapu, bao, riadha (mita 100, 200, 400, mbio za kupokezana vijiti,

    ichezo ya Bandari Inter-Ports Games 2018 imefanyika mjini Morogoro katika uwanja wa Jamhuri na Bwalo la JKT la Umwema kuanzia Oktoba 15-19, 2018 imehitimishwa huku Bandari ya Tanga ikiibuka kuwa mabingwa wa jumla kwa kunyakua vikombe na medali nyingi zaidi mbele ya Bandari washindani.

    Na Focus Mauki

    Mkurusha mkuki na tufe) na kuvuta kamba (wanawake na wanaume).

    MATOKEO YA MCHEZO WA BAOKwenye mchezo wa bao uliochezwa katika bwalo la JKT la Umwema Lake Ports waliibuka washindi kwa kupata alama 20 mbele ya Bandari Tanga waliopata alama 19. Timu nyingine kwenye mchezo huu na alama walizopata ni pamoja na Mtwara (14),

    “TANGA PORT” NYUMBANI KUMENOGA…• YAWA KINARA WA MICHEZO MINGI• BAHATI HERMAN KINARA WA MICHEZO

    Dar Port (10) na Makao Makuu (9).

    Katika mchezo huu mwanamichezo Herman Shimbe wa “Lake Ports” aliibuka kuwa Mchezaji bora wa mchezo wa bao.

    MATOKEO YA MCHEZO WA PETE “NETBALL”Bandari ya Tanga imeibuka na ushindi katika mchezo wa pete kwa kupata

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 13

    SACCOs YAPATA WAJUME WAPYA MKUTANO MKUU

    alama sita (6) mbele ya washindani wao huku nafasi ya pili ikinyakuliwa na timu iliyoonesha ushindani kutoka Makao Makuu ambao walipata alama nne (4).

    Bandari nyingine na alama walizopata katika mabano ni pamoja na Dar es Salaam (2) na Bandari Mtwara (0).

    Mchezaji bora wa mpira wa pete kwa mwaka huu ni nyota Bahati Herman wa Bandari ya Tanga.

    MATOKEO YA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU “FOOTBALL”Kwa upande wa mpira wa miguu, timu ya Lake Ports aliibuka na ushindi wa kwanza kwa kumaliza ligi ikiwa na alama 9.

    Timu nyingine za soka na alama walizopata katika mabano ni pamoja na

    mshindi wa pili Tanga Port (7), watatu Dar Port (5), nafasi ya nne Makao Makuu (4) na wa mwisho Mtwara Port (2).

    MATOKEO YA MCHEZO WA KIKAPU “BASKETBALL”Katika mchezo kikapu Bandari ya Tanga iliibuka na ushindi wa kwanza, Mtwara mshindi wa pili na Lake Ports aliambulia nafasi ya tatu.

    Katika mchezo huu, Kelvin Kingula kutoka Bandari ya Mtwara aliibuka kuwa mchezaji bora au kama inavyofahamika kama “MVP” (Most Valuable Player) huku mkongwe Dkt. Omary Khupe wa Bandari Mtwara akiibuka kuwa “Best Defensive Player”.

    Katika mchezo huu wa kikapu Tanga Port iliinyuka Dar Port kwa vikapu 73-23, Mtwara waliishughulikia Makao Makuu kwa 43-38, Tanga waliitandika Lake Ports 80-48, Mtwara wakaibomoa Dar Port kwa 43-37, Tanga wakaishikisha adabu Makao Makuu kwa 72-45 na Tanga wakaimenya korosho ya Mtwara kwa 76-48.

    Matokeo mengine ni Lake Ports waliibamiza Dar Port kwa 58-43, Makao Makuu wakaivuruga Dar Port kwa vikapu 71-40 na Mtwara wakaifundisha kazi Lake Ports kwa kuitandika vikapu 67-52.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KUVUTA KAMBA-WANAUMEKwa upande wa matokeo ya kuvuta kamba wanaume, Bandari Tanga waliibuka washindi kwa kupata alama 9, Bandari Dar mshindi wa pili alama 7, Makao Makuu wa tatu alama 4, Mtwara wa nne alama 2 na Lake Ports ilishika mkia kwa kutopata alama yoyote.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KUVUTA KAMBA-WANAWAKEKwa upande wa matokeo ya kuvuta kamba wanawake, Bandari Dar waliibuka washindi kwa kupata alama 10, wa pili Bandari Mtwara alama 8, wa tatu Makao Makuu alama 5 na Lake

    Ports ilishika nafasi ya nne kwa kupata alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 100-WANAUMEKwa upande wa mchezo wa riadha mita 100 wanaume, Shagi Lugua wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 12:72 na kupata alama 7. Wengine ni mshindi wa pili Eliasi Mtili Bandari ya Tanga aliyeshika nafasi ya pili kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 13:06 na kupata alama 5.

    Ramadhani Madebe wa Bandari ya Dar es Salaam aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya sekunde 13:16 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne Ernest James, Lake Ports sekunde 13:44 alama 3, nafasi ya tano Clever Macha, Mtwara sekunde 14:03 alama 2 na wa mwisho ni Herry Mandoa, Mtwara Ports sekunde 14:12 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 100-WANAWAKEKwa upande wa mchezo wa riadha mita 100 wanawake, Bahati Herman wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 16:60 na kupata alama 7. Wengine ni mshindi wa pili Naomi Mwaipopo Lake Ports aliyeshika nafasi ya pili kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 17:09 na kupata alama 5.

    Monica Mlay wa Bandari ya Mtwara aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya sekunde 18:46 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne Suzan Kanyika, Tanga Ports sekunde 19:41 alama 3, nafasi ya tano Anna Chale, Dar Port sekunde 19:59 alama 2 na wa mwisho ni Hellen Sempambo, Mtwara Ports sekunde 20:28 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 200-WANAUMEKwa upande wa riadha mita 200

    Inaendelea kurasa 14>>

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    14 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    wanaume, Shagi Lugua wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 24:25 na kupata alama 7. Wengine ni mshindi wa pili Damian Mkumbukwa Bandari ya Dar aliyeshika nafasi ya pili kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 25:28 na kupata alama 5.

    Elias Mtili wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya sekunde 25:30 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne Heri Mandoa, Mtwara Ports sekunde 25:44 alama 3, nafasi ya tano Ramadhan Madebe, Dar Port sekunde 25:97 alama 2 na wa mwisho ni Halfan Yakub, Mtwara Ports sekunde 29:03 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 200-WANAWAKEUpande wa riadha mita 200 wanawake, Bahati Herman wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 32:31 na kupata alama 7. Wengine ni mshindi wa pili Anna Esau Dar Ports aliyeshika nafasi ya pili kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa

    sekunde 35:25 na kupata alama 5.

    Hawa Senkoro wa Bandari ya Dar aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya sekunde 35:78 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne Monica Mlay, Mtwara Ports sekunde 37:88 alama 3, nafasi ya tano Beatrice Siliwa, Tanga Port sekunde 39:10 alama 2 na wa mwisho ni Ashura Msisi, Makao Makuu sekunde 42:04 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 400-WANAUMEMichezo ya riadha kwa mwaka huu pia ilishuhudia mbio ndefu kabisa za mita 400 ambapo, Damian Mkumbukwa wa Bandari ya Dar aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa sekunde 00:59:34 na kupata alama 7. Mshindi wa pili aliibuka Ramadhan Madebe Bandari ya Dar katika muda wa dakika 1:00:40 na kupata alama 5.

    Moses Komba wa Lake Ports aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya dakika 1:01:13 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne

    Msafiri Mabalwe, Tanga Ports sekunde dakika 1:01:13 alama 3, nafasi ya tano Halfan Yakub, Mtwara Port sekunde 1:03:28 alama 2 na wa mwisho ni Elias Mtili, Tanga Ports sekunde 1:05:56 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA MITA 400-WANAWAKEKwa upande wa riadha mita 400 wanawake, Bahati Herman wa Bandari ya Tanga aliibuka mshindi wa kwanza kuwa kumaliza mbio hizo katika muda wa dakika 1:25:75 na kupata alama 7. Wengine ni mshindi wa pili Anna Esau Dar Port aliyeshika nafasi ya pili kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa dakika 1:26:16 na kupata alama 5.Naomi Mwaipopo wa Lake Ports aliibuka mshindi wa tatu kwa kumaliza mbio hizo ndani ya dakika 1:29:94 na kupata alama 4. Wengine ni nafasi ya nne Hawa Senkoro, Dar Port dakika 1:34:37 alama 3, nafasi ya tano Anna Challe, Mtwara Port dakika 1:46:68 alama 2 na wa mwisho ni Hawa Salum, Makao Makuu dakika 1:53:43 alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KURUSHA TUFE-WANAUMEMchezo mwingine uliochezwa ni wa kurusha tufe ambapo kwenye kundi la warusha tufe wanaume, Adam Mshindo wa Dar Port aliibuka mshindi kwa kurusha mita 9.9 na kunyakua alama 7 huku Bakari Hema wa Tanga akiibuka mshindi wa pili kwa kurusha umbali wa mita 9.5 na kupata alama 5.

    Warusha tufe wengine wanaume ni pamoja na Mohamed Fazal wa Bandari Tanga, aliyeshika nafasi ya tatu kwa kurusha mita 9.2 na kupata alama 4, nafasi ya nne Siraj Slim wa Dar Port aliyerusha mita 8.5 na kupata alama 3, Idrissa Mustafa wa Lake Ports nafasi ya tano aliyerusha mita 8.3 na kupata alama 2 na wa mwisho ni Samson Kamsa wa Mtwara aliyerusha mita 7.8 na kuambulia alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KURUSHA TUFE-WANAWAKEKwa upande wa kurusha tufe

    Inaendelea kutoka 13>>

  • Toleo Maalum Michezo Toleo Maalum Michezo

    TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018 | 15

    wanawake, mchezaji mkongwe Amina Kubo wa Tanga Port aliibuka mshindi wa kwanza kwa kurusha mita 8.4 na kunyakua alama 7 huku Monica Mlay wa Mtwara akiibuka mshindi wa pili kwa kurusha umbali wa mita 8.2 na kupata alama 5.Warusha tufe wengine wanawake ni pamoja na Jacobeth Pallangyo wa Tanga, aliyeshika nafasi ya tatu kwa kurusha mita 7.2 na kupata alama 4, nafasi ya nne Modester Mujumali wa Dar Port aliyerusha mita 6.7 na kupata alama 3, Patricia Kasendeki wa Dar Port nafasi ya tano aliyerusha mita 6.6 na kupata alama 2 na wa mwisho ni Leticia Njunju wa Mtwara aliyerusha mita 6.4 na kuambulia alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KURUSHA MKUKI-WANAUMEMchezo mwingine uliochezwa ni wa kurusha mkuki ambapo kwenye kundi la warusha mkuki wanaume, Focus Baba wa Lake Port aliibuka mshindi kwa kurusha mita 36.3 na kunyakua alama 7 huku Samson Kanisa wa Mtwara akiibuka mshindi wa pili kwa kurusha umbali wa mita 29.7 na kupata alama 5.

    Warusha mkuki wengine wanaume ni pamoja na Siraj Yusuf wa Bandari ya Dar, aliyeshika nafasi ya tatu kwa kurusha mita 29.6 na kupata alama 4, nafasi ya nne Maron Gumbo wa Mtwara Port aliyerusha mita 29.1 na kupata alama 3, Fred Katembo wa Dar Port nafasi ya tano aliyerusha mita 28 na kupata alama 2 na wa mwisho ni Abdul Zahuya wa Tanga aliyerusha mita 27.1 na kuambulia alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA KURUSHA MKUKI-WANAWAKEKurusha mkuki wanawake, Amina Kubo wa Tanga Port aliibuka mshindi kwa kurusha mita 21.6 na kunyakua alama 7 huku Hawa Senkoro wa Dar Port akiibuka mshindi wa pili kwa kurusha umbali wa mita 17.3 na kupata alama 5.

    Warusha mkuki wengine wanawake

    ni pamoja na Gladness Mwandiga wa Bandari ya Tanga, aliyeshika nafasi ya tatu kwa kurusha mita 14.8 na kupata alama 4, nafasi ya nne Hawa Nassoro wa Mtwara Port aliyerusha mita 14.6 na kupata alama 3, Modester Mujumali wa Dar Port nafasi ya tano aliyerusha mita 13.3 na kupata alama 2 na wa mwisho ni Lucy Magele wa HQ aliyerusha mita 12.8 na kuambulia alama 1.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA KUPOKEZANA VIJITI-WANAUMEKwa upande wa mbio za riadha wanaume kupokezana vijiti, timu ya Bandari Tanga iliibuka na ushindi wa kwanza kwa kumaliza ndani ya dakika 00:53:25 na kunyakua alama 12 huku timu ya Bandari ya Dar ikimaliza ndani ya dakika 00:56:60 na kupata alama 10.

    Mshindi wa tatu ni Bandari ya Mtwara waliomaliza ndani ya dakika 1:00:03 na kupata alama 08 na wa mwisho ni Makao Makuu waliomaliza ndani ya dakika 1:00:75 na kuambulia alama 6.

    MATOKEO YA MCHEZO WA RIADHA KUPOKEZANA VIJITI-WANAWAKEKwa upande wa mbio za riadha wanawake kupokezana vijiti, timu ya Bandari Tanga iliibuka na ushindi wa kwanza kwa kumaliza ndani ya dakika 1:12:18 na kunyakua alama 12 huku timu ya Bandari ya Dar ikimaliza ndani ya dakika 1:15:88 na kupata alama 10.

    Mshindi wa tatu ni Bandari ya Mtwara waliomaliza ndani ya dakika 1:20:10 na kupata alama 08 na wa mwisho ni Makao Makuu waliomaliza ndani ya dakika 1:32:71 na kuambulia alama 6.

    Kwa matokeo hayo mshindi wa jumla wa michezo ya riadha wanaume ni Bandari ya Tanga ambao wamejinyakulia alama 50, mshindi wa pili Dar Port waliopata alama 49, Mtwara 26, Lake Ports 16 na Makao Makuu walioambulia alama 6.

    Kwa upande wa mshindi wa jumla wa michezo ya riadha wanawake ni Bandari ya Tanga ambao wamejinyakulia alama

    60, mshindi wa pili Dar Port waliopata alama 41, Mtwara 27, Lake Ports na Makao Makuu waliofungana kwa alama 09.

    WACHEZAJI BORA WA MICHEZO MBALIMBALI

    RIADHAMchezaji bora riadha wanawake ni Bahati Herman na wanaume ni Shagi Ligua wote kutoka Bandari ya Tanga.

    KAMBAWachezaji bora katika mchezo wa kuvuta kamba wanaume ni Wilfred Tondoko wa Bandari Tanga na kama wanawake ni Halima Abeid wa Bandari ya Mtwara.

    PETEMchezaji bora wa mchezo wa pete ni Bahati Herman wa Bandari Tanga.

    SOKAMchezaji bora wa mpira wa miguu ni Hassan Ahmed wa Bandari Dar es Salaam.

    SOKAMchezaji bora wa kikapu ni Kelvin Kingula wa Bandari ya Mtwara.

    BAOMchezaji bora wa mchezo wa bao ni Herman Shimbe wa Bandari Maziwa.

    WACHEZAJI WAKONGWE WALIOPATA ZAWADIWachezaji wakongwe katika mchezo wa inter-ports 2018 ni pamoja na Dkt. Hawa Senkoro na Hassan Ahmed wote wa Bandari ya Dar es Salaam na Zubeir Shekhe wa Bandari Tanga.

    KIKOMBE CHA NIDHAMUMakao Makuu waliibuka na kikombe cha nidhamu.

    MSHANGILIAJI BORA WA MICHEZOBandari ya Mtwara iliibuka na kikombe cha mshangiliaji bora wa michezo ya 12 ya 2018.

  • Toleo Maalum Michezo

    16 | TPA GAZETI OKTOBA 28 - NOVEMBA 11 2018

    MATUKIO MBALIMBALI YA MICHEZO YA BANDARI