16
za mwambao wa Bahari ya Hindi na za kwenye Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Mbali na hilo TPA ilikabidhiwa majukumu zaidi ya kumiliki na kuendeleza Bandari zilizokuwa zinaendeshwa na Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Services Company Limited – MSCL) katika Maziwa Makuu. Majukumu mengine iliyokasimiwa ni pamoja na kuendeleza shughuli za Bandari, kutangaza huduma za Bandari, kushirikisha na kusimamia sekta binafsi katika uendelezaji, uboreshaji na uendelezaji wa Bandari za TANZANIA PORTS AUTHORITY www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047 TOLEO NO: 07 MEI 14 - MEI 27 2018 @tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq TPAHQ TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 01 05 WAFANYAKAZI WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA TPA YATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MUHIMBILI 03 NDANI amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake Aprili, 2005. TPA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004 ambapo awali ilikuwa ikiitwa Mamlaka ya Bandari Tanzania – THA ambayo ilianzishwa mwaka 1977 mara baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mwandishi Wetu Jumuiya hiyo ilikuwa inaendesha Bandari kupitia Shirika la Bandari la Afrika Mashariki lililoanzishwa mwaka 1967. Historia inaonesha kwamba THA ilikuwa na kazi ya kusimamia na kuendesha Bandari za mwambao wa bahari tu ambazo ni Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Mafia, Pangani, Lindi na Kilwa. TPA ambayo ilianza rasmi kufanya kazi tarehe 15 Aprili, 2015 ilikasimiwa kazi ya kuendeleza na kusimamia Bandari zote TPA YAADHIMISHA MIAKA 13 YA MAFANIKIO Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wafanyakazi wa TPA pamoja na baadhi ya Wadau wa TPA. M mwambao wa bahari na za kwenye Maziwa Makuu nchini. Katika kipindi cha miaka 13 sasa tangu ilipoanzishwa, TPA imeendelea kuhudumia wateja wake katika Bandari zake kwa kuwapatia huduma bora. Huduma hizo ni pamoja na za kuhudumia meli ambapo TPA imeendelea kuboresha miundombinu ya magati na kuwa na marubani wa 13 BANDARI TANGA YATOA MSAADA WA VITANDA 10 VYA KUJIFUNGULIA PANGANI! 07 WIKI YA KUADHIMISHA MIAKA 13 YA UTOAJI HUDUMA TPA YAHITIMISHWA KWA BONANZA..

TANZANIA PORTS AUTHORITY · Mradi huu upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na unakwenda sambasamba na mradi mwingine wa ujenzi wa Bandari mpya ya Mwambani Tanga. Aidha, TPA

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • za mwambao wa Bahari ya Hindi na za kwenye Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

    Mbali na hilo TPA ilikabidhiwa majukumu zaidi ya kumiliki na kuendeleza Bandari zilizokuwa zinaendeshwa na Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Services Company Limited – MSCL) katika Maziwa Makuu.

    Majukumu mengine iliyokasimiwa ni pamoja na kuendeleza shughuli za Bandari, kutangaza huduma za Bandari, kushirikisha na kusimamia sekta binafsi katika uendelezaji, uboreshaji na uendelezaji wa Bandari za

    TANZANIA PORTS AUTHORITY

    www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047

    TOLE

    O N

    O:

    07

    MEI

    14

    - M

    EI 2

    7 20

    18

    @tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq TPAHQ TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 01

    05

    WAFANYAKAZI WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA

    KUPIMA AFYA

    TPA YATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA

    MUHIMBILI

    03

    NDANI

    amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake Aprili, 2005. TPA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004 ambapo awali ilikuwa ikiitwa Mamlaka ya Bandari Tanzania – THA ambayo ilianzishwa mwaka 1977 mara baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

    Mwandishi Wetu

    Jumuiya hiyo ilikuwa inaendesha Bandari kupitia Shirika la Bandari la Afrika Mashariki lililoanzishwa mwaka 1967. Historia inaonesha kwamba THA ilikuwa na kazi ya kusimamia na kuendesha Bandari za mwambao wa bahari tu ambazo ni Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Mafia, Pangani, Lindi na Kilwa. TPA ambayo ilianza rasmi kufanya kazi tarehe 15 Aprili, 2015 ilikasimiwa kazi ya kuendeleza na kusimamia Bandari zote

    TPA YAADHIMISHA MIAKA 13 YA MAFANIKIO

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wafanyakazi wa TPA pamoja na baadhi ya Wadau wa TPA.

    Mmwambao wa bahari na za kwenye Maziwa Makuu nchini.

    Katika kipindi cha miaka 13 sasa tangu ilipoanzishwa, TPA imeendelea kuhudumia wateja wake katika Bandari zake kwa kuwapatia huduma bora. Huduma hizo ni pamoja na za kuhudumia meli ambapo TPA imeendelea kuboresha miundombinu ya magati na kuwa na marubani wa

    13

    BANDARI TANGA YATOA MSAADA WA VITANDA 10

    VYA KUJIFUNGULIAPANGANI!

    07

    WIKI YA KUADHIMISHA MIAKA 13 YA UTOAJI

    HUDUMA TPAYAHITIMISHWA KWA

    BONANZA..

  • 2 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Maadhimisho

    TPA yaadhimisha miaka 13 yenye mafanikio lukukikuongoza meli wenye ujuzi na uzoefu mkubwa.

    Pia kuwajengea uwezo wafanyakazi wengine wanaohusika na uhudumiaji wa meli wakati wa kuingia na kutoka Bandarini. Pia TPA imefanikiwa kupunguza muda wa kukaa meli Bandarini kwa kuongeza ufanisi kwa kushirikiana na wadau wa Bandari kama vile idara za Uhamiaji na Afya.

    Kwa upande wa kuhudumia mizigo ya wateja TPA imeboresha kwa kuwajengea uwezo wafanyakazi wake ili waweze kuhudumia wateja kwa kuwapatia huduma bora. TPA imeweza kuzinunulia Bandari zake vifaa bora na vya kisasa vya kuhudumia meli na mizigo ya wateja. TPA kwa kushirikiana na wadau wake imefanikiwa kutoa huduma kwa wateja wake kuchukua mizigo yao Bandarini kwa muda wa saa 24 kwa siku 7 za wiki. TPA imefanikiwa kuwawezesha wateja kulipia tozo za Bandari kwa kutumia mfumo wa E-payament.

    Ili kuweza kuhakikisha TPA inaendelea kutoa huduma bora katika Bandari zake, iliamua kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuboresha na kuendeleza Bandari zake kukabiliana na changamoto ya ongezeko la shehena na kuweza kuingiza meli kubwa katika Bandari zake.

    Kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam, TPA imeweza kukamilisha miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Boya la Mafuta (Single Point Mooring – SPM) kuhudumia meli kubwa za mafuta zenye uwezo wa kuchukua mafua hadi tani 150,000. Ujenzi wa Kituo Kimoja cha Huduma (One Stop Centre), Mradi wa kisasa wa ulinzi (Integrated Security System), ujenzi wa barabara za kuingia lango namba 4 na 8 na ujenzi wa karakana ya meli (Dock Yard).

    Mradi mkubwa unaotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam ni Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambao ni mradi wa uboreshaji na uongezaji wa kina katika gati namba 1 hadi 7, kuongeza kina cha mlango wa Bandari na mzunguko wa kugeuza meli pamoja na kujenga gati namba 13 na 14.

    Katika Bandari ya Mtwara, TPA imeongeza gati namba 2 kuipanua Bandari hiyo kuwa ya kisasa kwa lengo la kuiwezesha kuhudumia meli kubwa na shehena kubwa zaidi. Mradi huo una lengo la kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa mikoa ya Mtwara, Lindi and Ruvuma.

    Pia taifa kwa ujumla litanufaika kwa kuwapatia fursa wateja kuteremshia mizigo yao katika Bandari hiyo. Mradi huo uliwekwa jiwe la msingi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi, 2017.

    Pia katika Bandari ya Tanga Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Serikali ya Uganda kujenga bomba kubwa la mafuta la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda kupitia Bandari ya Tanga. Mradi huu upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na unakwenda sambasamba na mradi mwingine wa ujenzi wa Bandari mpya ya Mwambani Tanga.

    Aidha, TPA inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya Bandari zilizoko katika Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Bandari hizo zimejengewa na zinaendelea kujengewa uwezo kuhudumia meli, abiria na mizigo ya wateja.

    Pia ili kuhudumia mizigo ya wateja vizuri TPA inatekeleza mradi wa Bandari Kavu ya Kwala, Ruvu, ambapo imenunua maeneo ya Katosho Kigoma kwa ajili

    ya mizigo ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na eneo la Fela, Misungwi kwa ajili ya mizigo ya Uganda.

    Ili kusogeza huduma za Bandari karibu na wateja wake, TPA imefungua ofisi zake; Lubumbashi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lusaka nchini Zambia, Kigali nchini Rwanda na Bujumbura nchini Burundi. Pia, TPA ina mawakala Goma nchini DRC, Kampala nchini Uganda na iko mbioni pia kumpata wakala nchini Malawi.

    Kwa muda wa miaka 13, TPA imepata mafanikio mengi ya kujivunia katika Bandari zake ambayo yamechangia maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa Tanzania na nchi jirani zinazotumia Bandari za TPA.

    Aidha TPA kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake kwa kuwajengea uwezo wafanyakazi wake, kuboresha miundombinu pamoja na vifaa, kuendelea kutoa huduma bora kwa haraka na gharama nafuu kwa kutumia mifumo ya kisasa kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

    TPA kwa kumjali mteja ina kituo cha huduma kwa mteja ambacho kina simu ambazo mteja anaweza kupiga au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi bure kuuliza swali lolote au kupata

    ‘‘Kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam, TPA imeweza kukamilisha miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Boya la Mafuta (Single Point Mooring – SPM) kuhudumia meli kubwa za mafuta zenye uwezo wa kuchukua mafua hadi tani 150,000. Ujenzi wa Kituo Kimoja cha Huduma (One Stop Centre), Mradi wa kisasa wa ulinzi (Integrated Security System), ujenzi wa barabara za kuingia lango namba 4 na 8 na ujenzi wa karakana ya meli (Dock Yard).’’

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 3

    Msaada

    ‘‘Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando amesema kuwa TPA inawajibika kuiangalia jamii kwa kuisaidia mambo mbalimbali na kwamba Mamlaka imeamua kuwafariji watoto hao kwa kukabidhi msaada wa “wheelchairs” 20 na “thermometers” 40 kwa wodi ya watoto ya hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.’’

    BI. MTAWA AMEIOMBA JAMII KWA UJUMLA KUWASAIDIA WATOTO HAO KWA VITU MBALIMBALI MBALI NA VIFAA TIBA NA KWAMBA MSAADA ULIOUTOLEWA NA TPA UMEPOKELEWA NA UONGOZI PAMOJA NA WAZAZI WA WATOTO KWA MOYO MKUNJUFU NA UTAWASAIDIA KWA KIWANGO KIKUBWA.

    Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando amesema kuwa TPA inawajibika kuiangalia jamii kwa kuisaidia mambo mbalimbali na kwamba Mamlaka imeamua kuwafariji watoto hao kwa kukabidhi msaada wa “wheelchairs” 20 na “thermometers” 40 kwa wodi ya watoto ya hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.

    Tarehe 15 Aprili, 2018 TPA imetimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake tarehe 15 Aprili 2005. TPA ilianzishwa kupitia Sheria ya Bandari Na. 17 ya 2004” ikiwa na jukumu la kusimamia, kuendeleza na kuendesha Bandari

    amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA ambapo kilele chake ilikuwa ni Jumapili, Aprili 15, 2018.

    Focus Mauki

    TPA YATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MUHIMBILI

    Mzilizopo katika bahari na maziwa.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimmbili, Bi. Agnes Mtawa ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, amewashukuru sana TPA kwa kuwakumbuka watoto hao na kuiomba Mamlaka na watanzania wote kutowasahau na kuwatembelea wodini mara kwa mara ili kuwafariji watoto hao.

    Bi. Mtawa ameiomba jamii kwa ujumla kuwasaidia watoto hao kwa vitu mbalimbali mbali na vifaa tiba na kwamba msaada ulitolewa na TPA umepokelewa na uongozi pamoja na wazazi wa watoto kwa moyo mkunjufu na utawasaidia kwa kiwango kikubwa.

    Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando akikabidhi msaada kwa wodi ya watoto Muhimbili kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

  • 4 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Ukaguzi/Mafunzo

    WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA TPA (BOARD OF SURVEY) WAKIKAGUA MALI CHAKAVU ZILIZOPO BANDARI YA DAR ES SALAAM.

    BAADHI YA VIONGOZI WA MENEJIMENTI YA TPA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAKUFUNZI WA PSPTB MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWAMAFUNZO YA UNUNUZI NA UGAVI YALIYOFANYIKA BANDARI YADAR ES SALAAM HIVI KARIBUNI.

    Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando akizindua zoezi la kupima afya kwa kupima afya yake katika wiki ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 5

    Afya/HQ/Dar

    Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando wakati alipomwakilisha Mkurugenzi Mkuu kwenye zoezi la kupima afya na uchangiaji damu lililofanyika katika eneo la idara ya zimamoto, Bandari ya Dar es Salaam.

    “Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wale wote ambao wamejitokeza leo kuchangia damu kwa wenye uhitaji pamoja na kupima afya zao, natoa wito kwa wafanyakazi wote kuwa na ari na moyo wa kusaidia wenye shida na damu na pia wapime afya zao mara kwa mara, hata mimi leo nitapima afya yangu na kuchangia damu ili kutoa hamasa,” amesema Bi. Mhando.

    Zoezi hilo kwa Wafanyakazi la kuchangia damu lilikuwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA mwaka 2005.

    Kwa upande wake akizungumza kuhusu zoezi hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam (DOWUTA), Bw. Mashaka Karume amesema zoezi hilo ni sehemu

    afanyakazi wameaswa kujenga utamaduni wa kupima afya kila wakati pamoja na kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika mahospitali mbalimbali nchini.

    Focus Mauki

    WAFANYAKAZI WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA

    W

    ya mambo ambayo walipanga kwa pamoja kama Chama na Menejimenti ili kuadhimisha miaka 13 ya TPA.

    “Damu ambayo tunachangia itatumika katika hospitali mbalimbali kwa wagonjwa wenye uhitaji, jambo hili tunajivunia kwamba tunasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu,” amesema Mashaka.

    Bw. Mashaka amefafanua zaidi kwamba, “Ni wajibu wa Wafanyakazi kuchangia damu kwa sababu Taifa linahitaji damu

    ya kutosha na wanaohitaji kutumia damu ni Watanzania wenzetu, kwa hiyo tunalolifanya sisi ni jambo jema kwa maslahi ya familia zetu na Taifa kwa ujumla.”

    Zoezi hilo la uchangiaji damu ambalo liliratibiwa vizuri kwa kushirikiana na Zahanati ya Mamlaka chini ya Mganga Mkuu Dkt. Mkunde Mlay lilikuwa la mafanikio makubwa huku wafanyakazi wengi wakitoa maoni kuwa liwe ni endelevu.

    Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando akizindua zoezi la kupima afya kwa kupima afya yake katika wiki ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA.

    Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali mbalimbali Jijini Dar es Salaam.

  • 6 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Afya/Tanga

    WAFANYAKAZI BANDARI YA TANGA WACHANGIA LITA 100 ZA DAMU

    Zoezi hilo la kuchangia damu lilianza Aprili 10 na likaendelea Aprili 11, 2018 likiwahusisha Wafanyakazi wa Bandari pamoja na baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga.

    Katika kipindi cha siku moja, takribani lita 35 za damu zilikusanywa huku lengo likiwa ni kukusanya lita 100 za damu.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hospitali ya rufaa ya Bombo peke yake inatumia takribani lita 3 hadi 5 kwa siku katika kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye kuhitaji damu kuokoa maisha yao.

    atika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 13 ya TPA, Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga na baadhi ya Wananchi wa Mkoa Tanga wameshirikiana kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.

    Moni Jarufu

    K

    ‘‘Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hospitali ya rufaa ya Bombo peke yake inatumia takribani lita 3 hadi 5 kwa siku katika kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye kuhitaji damu kuokoa maisha yao.’’

    Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali mbalimbali Jijini Tanga.

    Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali mbalimbali Jijini Tanga.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 7

    Michezo/Mtwara

    Maadhimisho hayo yaliitimishwa kwa kupambwa na Bonanza kabambe lililohusisha mazoezi ya viungo (aerobic) kwa wafanyakazi wote, Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, mchezo wa bao na Mpira wa Pete kwa timu za Menejimenti na Wafanyakazi.

    Akifungua bonanza hilo Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali aliwasisitiza wafanyakazi kuwa na tabia ya kushiriki kwenye mazoezi mbalimbali ya mwili kwa ajili ya kujenga Afya njema pia kuepuka magonjwa mbalimbali ili kuleta ufanisi mzuri katika Utendaji kazi.

    Bonanza hilo lilimalizika kwa timu za wafanyakazi kuibuka washindi kwenye michezo yote na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo kuku na fedha taslimu.

    Wafanyakazi waliishukuru Mamlaka kwa kuwapa nafasi ya kujumuika pamoja katika kusherekea maadhimisho ya miaka 13 ya utoaji huduma kwa TPA na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza Tija.

    amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeadhimisha Kumbukumbu ya Miaka 13 Ya utendaji kazi kuanzia tarehe 09 hadi 15 Aprili, 2018 Kupitia Bandari zake zote za Tanzania ikiwemo Bandari ya Mtwara. Katika kuadhimisha wiki hiyo Mamlaka iliandaa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ‘Press Conference’, Kutembelea na kutoa misaada kwa Jamii, Wanajamii Kutembelea Bandari kujifunza vitu tofauti na kumalizika na Bonanza lililohusisha michezo mbalimbali.

    Fassie Obadia

    WIKI YA KUADHIMISHA MIKA 13 YA UTOAJI HUDUMA TPA YAHITIMISHWA KWA BONANZA KABAMBE BANDARI YA MTWARA

    M

    Wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakijumuika pamoja katika kufanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 13 ya TPA.

    Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali, akimkabidhi zawadi kocha wa timu ya mpira wa pete Bi. Mariam Said.

  • 8 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Michezo/HQ/Dar

    Michezo hiyo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kutimiza Miaka 13 ya TPA tangu kuanzishwa kwake Aprili 2005, ilijaa burudani hasa katika michezo ya kufukuza kuku na kukimbia na magunia.

    Shindano la mpira wa miguu lilikuwa kati ya timu ya iliyokuwa THA na TPA. Mpaka kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa sare ya 1-1.

    Kwa upande wa Mpira wa Pete matokeo yalikuwa vijana TPA vikapu 4-10 THA. Mchezo wa kukimbiza kuku (wanaume) ambao ulikuwa na burudani ya aina yake ushindi ulienda kwa Ibrahimu Mbatto huku mchezo wa kukimbia na gunia (wanawake), Bi. Modesta Kaunda akiibuka kidedea na Bw. Jonas Bwoma akiibuka kidedea kwa upande wa wanaume.

    Mwaka huu TPA inaadhimisha miaka 13 tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo awali ilikuwa ikitambulika kama THA.

    atika kusherekea Maadhimisho ya Wiki ya TPA, Wafanyakazi wa Makao Makuu na Bandari ya Dar es Salaam, wameshiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo Kandanda, mpira wa pete, kukimbiza kuku na Gunia michezo iliyochezwa katika viwanja vya klabu ya Bandari Kurasini.

    Innocent Mhando

    WAFANYAKAZI WASHIRIKI MICHEZO KUADHIMISHA MIAKA 13

    K

    Wanamichezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati waliposhiriki michezo ya kuadhimisha miaka 13 ya TPA.

    Wanamichezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati waliposhiriki michezo ya kuadhimisha miaka 13 ya TPA.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 9

    Msaada/Mwanza

    Msaada huo umetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mkuu wa Bandari hiyo, Bw. Daniel Sira ambaye aliongozana na Wafanyakazi mbalimbali wa Bandari hiyo. Msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa kusherehekea miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake mnamo Aprili 15, 2005.

    ongozi wa Bandari ya Mwanza umetoa msaada wa mchele, sabuni, mafuta ya kupikia na unga wa sembe kwa kituo cha kutunza wazee cha Bukumbi jijini Mwanza.

    Mwandishi Wetu

    BANDARI MWANZA YASAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA BUKUMBI!

    U

    Baadhi ya Wafanyakazi wa Bandari ya Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kituo cha Bukumbi mara baada ya kuwakabidhi misaada mbalimbali.

    ‘‘Uongozi wa Bandari ya Mwanza umetoa msaada wa mchele, sabuni, mafuta ya kupika na unga wa sembe kwa kituo cha kutunza wazee cha Bukumbi jijini Mwanza.’’

    Aliyekuwa Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Bw. Daniel Sira akikabidhi msaada kwa wazee wa kituo cha Bukumbi.

  • 10 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Ziara/Mtwara

    Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake kwenye Bandari ya Mtwara ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuadhimisha miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake Aprili 15, 2005.

    Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za Bandari ambapo amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa Ujumla.

    kuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa ameipongeza TPA kwa jitihada inazozifanya za kuimarisha ulinzi katika Bandari zake hususani Bandari ya Mtwara.

    Fassie Obadia

    MKUU WA MKOA MTWARA AIPONGEZA TPA KWA KUTIMIZA MIAKA 13!

    M

    Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za Bandari ambapo amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa Ujumla.

    Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa (kushoto) akiwa na Mwenyeji wake Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali (katikati).

    Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa (kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali (kushoto) wakiwa ndani ya boti ya ulinzi.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 11

    Msaada/Mtwara

    Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Dickson Sahini aliishukuru Mamlaka kwa msaada walioutoa kwa kuwa Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa ukosefu wa mashuka ambapo walikuwa na upungufu wa mashuka 992 ya kulalia wagonjwa jambo ambalo limekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.

    Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za kiBandari ambapo amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa Ujumla.

    Mashuka hayo yenye thamani ya Tshs. 1,335,000/= yalikabidhiwa na Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali. Akikabidhi mashuka hayo Bw. Mlali alisema kwamba TPA inaadhimisha miaka 13 ya Utoaji huduma toka ilipoanzishwa mwaka 2005.

    Hivyo Mamlaka imeona ni vyema kuishukuru Jamii kwa kuipa ushirikiano toka ilipoanzishwa kwa kutoa kile kidogo ambacho imepata kwa kipindi chote hicho ikiwa ni shukrani kwa jamii

    atika wiki ya kuadhimisha miaka 13 ya utoaji huduma kwa TPA toka ianzishwe Bandari ya Mtwara imetoa msaada wa mashuka mia moja (100) katika hospitali ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula.

    Fassie Obadia

    HOSPITALI YA LIGULA YANUFAIKA NA MASHUKA 100 KUTOKA BANDARI YA MTWARA

    kwa kuunga mkono kazi mbalimbali za Mamlaka. Vilevile Mamlaka inaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuboresha utoaji huduma katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na ustawi wa Jamii.

    Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Dickson Sahini aliishukuru Mamlaka kwa msaada walioutoa kwakuwa Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa ukosefu wa mashuka ambapo walikuwa na upungufu wa mashuka 992 ya kulalia wagonjwa jambo ambalo limekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.

    Vile vile alitoa rai kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano wa Mamlaka kwa kusaidia Hospitali hiyo kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa ‘Sunction Machine’, ‘Wheel Chairs’, ‘Autoclaves’ nk.

    K

    Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali akikabidhi msaada wa shuka kwa Kaimu Daktari Mfawidhi hospitali ya Mkoa wa Ligula Dkt. Dickson Sahini

  • 12 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Wadau/Masoko

    Mkutano huo ambao umewakutanisha wateja na wadau wa TPA ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja namna wanavyoweza kushiriki kwa pamoja katika kuboresha huduma za Bandari.

    Mkutano huo umefanyika kwa siku moja katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

    aibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye ameiagiza TPA kuongeza shehena ya mzigo katika Bandari zake hususani Bandari za maziwa. Ametoa agizo hilo wakati alipofungua rasmi mkutano wa wadau wa TPA ambao ulifanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

    Focus Mauki

    NAIBU WAZIRI AZINDUA KONGAMANO LA WADAU

    N

    Mkutano huo ambao umewakutanisha wateja na wadau wa TPA ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja namna wanavyoweza kushiriki kwa pamoja katika kuboresha huduma za Bandari.

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye akizungumza na wadau wa TPA kwenye mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

    Wadau mbalimbali wa TPA wakifuatilia mada zilizowasilishwa kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 13 ya TPA.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 13

    Msaada/Tanga

    Mkuu huyo wa Bandari amekabidhi msaada huo kwa naibu waziri wa maji na umwagiliaji na mbunge wa pangani, mhe. Jumaa aweso na mkuu wa wilaya ya pangani, mhe. Zainab abdallah.

    Msaada huo uliotolewa na TPA ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake aprili 15, 2005.

    ‘‘Msaada huo uliotolewa na TPA ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake aprili 15, 2005.’’

    Mkuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Percival Salama akikabidhi msaada wa vitanda vya kujifungulia kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Zainab Abdallah. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Pangani, Mhe. Jumaa Aweso.

    Baadhi ya vitanda vilivyotolewa msaada na TPA kwa Wilaya ya Pangani.

    BANDARI TANGA YATOA MSAADA WA VITANDA 10 VYA KUJIFUNGULIA PANGANI!

    kuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Percival Salama amekabidhi msaada wa vitanda 10 vya kujifungulia kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Pangani.

    Moni Jarufu

    M

  • 14 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Wanafunzi/Mtwara

    Wakiwa Bandarini hapo wanafunzi hao pia walipata fursa ya kujifunza kuhusiana na utendaji kazi wa Bandari ikiwa ni pamoja na namna Bandari ilivyojizatiti kikamilifu kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo ya moto. Mbali na elimu ya nadharia Wanafunzi hao pia wamepata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna ya uzimaji wa moto wa aina mbalimbali kwa kutumia chombo maalumu cha kuzimia moto ‘Fire Extingusher’.

    anafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari wa Mkoa wa Mtwara wamepata fursa ya kupata elimu kuhusiana na shughuli za Bandari hususani elimu ya zimamoto ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 13 ya TPA.

    Fassie Obadia

    MAADHISHO YA MIAKA 13WANAFUNZI MTWARA WANUFAIKA NA ELIMU YA BANDARI!

    W

    ‘‘Mbali na elimu ya nadharia Wanafunzi hao pia wamepata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna ya uzimaji wa moto wa aina mbalimbali kwa kutumia chombo maalumu cha kuzimia moto ‘Fire Extingusher’.’’

    Wataalamu wa zimamoto na usalama wa Bandari ya Mtwara wakitoa elimu kuhusiana na vifaa vinavyotumika wakati wa kuzima moto.

    Mtaalamu wa zimamoto na usalama wa Bandari ya Mtwara akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusiana na vifaa vinavyotumika wakati wa kuzima moto.

  • TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 15

    Tamasha/Dar

    “Michezo hii ilianzishwa mahsusi ili kujenga, kuimarisha Muungano na undugu bila kusahau kuboresha afya za Wafanyakazi wa pande zote za Bara na Visiwani,” amefafanua Eng. Kakoko na kuongeza kuwa michezo hii itaendelea kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.

    Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko wakati akifunga michezo ya Tamasha la Pasaka ambayo kwa mwaka huu imefanyika katika vwanja vya Klabu ya Bandari Kurasini jijini Dar es Salaam.

    “Michezo hii ilianzishwa mahsusi ili kujenga, kuimarisha Muungano na undugu bila kusahau kuboresha afya za Wafanyakazi wa pande zote za Bara na Visiwani,” amefafanua Eng. Kakoko na kuongeza kuwa michezo hii itaendelea kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.

    Kwa upande mwingine Eng. Kakoko ameridhia timu za Shirika la Bandari ya Zanzibar (ZPC) na Shirika la Meli Zanzibar (SHIPCO) kushiriki katika michezo ya “Bandari Interports” ambayo kwa mwaka huu 2018 imepangwa kufanyika Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma.

    amasha la Pasaka ambalo huwakutanisha Wafanyakazi wa Bandari za Tanzania Bara na Visiwani litaendelea kufanyika kila mwaka kwa lengo la kuenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.

    Innocent Mhando

    TAMASHA LA PASAKA LA BANDARI KUTUMIKA KUENZI WAASISI WA MUUNGANO!

    TKwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam (DOWUTA), Bw. Mashaka Karume amepongeza ushirikiano na upendo uliopo baina ya Wafanyakazi wa pande zote mbili hususani katika kufanikisha michezo ya Bonanza la Pasaka.

    Nae Bw. Hassan Ahmed akiongea kwa niaba ya uongozi wa Klabu ya Bandari na Wanamichezo kutoka TPA ameishukuru Menejimenti ya TPA kwa kutoa idhini na hatimaye kufanikisha Tamasha hilo na kuahidi kwamba Wafanyakazi watafanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuuenzi Muungano kwa vitendo.

    Katika mchezo wa soka timu ya Makao Makuu waliibuka kidedea kwa 3-1 dhidi ya Shirika la Meli Zanzibar na kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam walishindwa kufurukuta mbele

    ya Shirika la Bandari Zanzibar kwa kuchapwa bao 2-0.

    Katika mchezo wa kuvuta kamba Makao Makuu Wanaume na Wanawake waliwavuta Shirika la Meli Zanzibar kwa seti zote mbili huku katika mchezo wa Kamba Bandari ya Dar es Salaam waliwagalagaza wavuta kamba wa Shirika la Bandari Zanzibar kwa seti zote mbili.

    Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bandari ya Dar ea Salaam walipata alama 32 -20 dhidi ya timu ya Shirika la Bandari Zanzibar na kwa upande wa Makao Makuu mpira wa pete walishindwa kufurukuta mbele ya Wanzibari kwa kufungwa kwa alama 11 -19 na Shirika la Meli Zanzibar.

    Wafanyakazi wa TPA, Shirika la Bandari ya Zanzibar (ZPC) na Shirika la Meli Zanzibar (SHIPCO) wakiserebuka kwenye tamasha la Pasaka ambalo linafanyika mara moja kwa mwaka kwa lengo la kujenga mahusino mema ya kazi.

  • 16 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018

    Geti GetiMasoko

    Akiongea na Waandishi wa Habari wa nchini Uganda, Kakoko amesema kufunguka kwa kipande hicho kutafungua fursa nyingi za kibiashara na kurahisisha usafirishaji wa shehena kati ya Tanzania na Uganda.

    Pichani Mkurugenzi Mkuu huyo anaonekana akiwa anakagua ukarabati wa reli hiyo ambapo pia walikutana na Uongozi wa URC kwenye Kikao Kazi.

    kurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amekutana na Uongozi wa Shirika la Reli Uganda (URC) na Wafanyabiashara wa Uganda ili kupanga mkakati madhubuti wa matumizi ya kipande cha reli cha Kilomita 9 kati ya Port Bell na Kampala ambacho kinafanyiwa ukarabati mkubwa ili kuanza kutumika kwa ajili ya kupitishia shehena ya Uganda kutokea Bandari ya Mwanza.

    Mwandishi Wetu

    TPA YAKUTANA NA URC NAWAFANYABIASHARA WA UGANDA

    M

    Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (wa tano kushoto) akiwa katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Uganda (URC), Eng. Charles Kateeba (katikati). Wengine katika picha ni Menejimenti ya TPA na URC.

    ‘‘Akiongea na Waandishi wa Habari wa nchini Uganda, Kakoko amesema kufunguka kwa kipande hicho kutafungua fursa nyingi za kibiashara na kurahisisha usafirishaji wa shehena kati ya Tanzania na Uganda.’’