20
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 144, Agosti, 2019 ISSN 0856-874X CPJ yamtaka Rais kumfutia mashtaka Kabendera Polisi wahimizwa kuzingatia sheria Wanahabari wanaotuhumiwa waishukuru MCT Uk5 Uk 13 Uk 9 Wanahabari Watishwa Absalom Kibanda Simon Mkina Neville Meena Eddo Kumwembe

Baraza la Habari Tanzania Toleo la Agosti, 2019 ISSN ......ya unyanyasaji, vitisho na hata utekaji wa waandishi. Unavyosoma maoni haya , Polisi hawajatoa taarifa muhimu na za maana

  • Upload
    others

  • View
    4

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

    Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 144, Agosti, 2019ISSN 0856-874X

    CPJ yamtaka Rais kumfutia mashtaka Kabendera

    Polisi wahimizwa kuzingatia sheria

    Wanahabari wanaotuhumiwa waishukuru MCT

    Uk5 Uk 13Uk 9

    Wanahabari Watishwa

    Absalom Kibanda Simon Mkina Neville Meena

    Eddo Kumwembe

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

    MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

    MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI

    2003FREE MEDIA

    PIONEER

    2

    TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

    Vyombo vya habari viachwe vifanye uandishi wa kweliLicha ya hatua mbalimbali na miito ya kutaka kuwepo utulivu na umakini katika mahusiano ya kikazi kati ya wanahabari na vyombo vya usalama vya dola hasa Polisi, ukweli ni kwamba mambo ni kinyume kabisa na miito hiyo haizingatiwi. Imekuwa kawaida kwa vyombo vya usalama kuvitumia vyombo vya habari kwa ajili ya kujitangaza lakini kila wanapopata nafasi wao huwakamata na kuwanyanyasa wanahabari.

    Matukio ya kuwakamata na kuwanyanyasa waandishi wa habari ni mengi. Wakati mmoja polisi waliwafuata wanahabari hadi kwenye vyumba vya habari kuwahoji jinsi walivyoripoti mikutano ya kisiasa, hasa ya vyama vya upinzani..

    Polisi wamekuwa wakiwakamata waandishi na mara nyingi huwanyang’anya vifaa vyao vya kazi na hata kufuta picha wasizozipenda. Wanahabari hupigwa wakati wanakamatwa na huchukuliwa kama wahalifu ama watu hatari waliokuwa wakitafutwa muda mrefu.

    Rejista ya Ukiukaji wa Uhuru wa Habari ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imerikodi matukio kadhaa ya unyanyasaji, vitisho na hata utekaji wa waandishi. Unavyosoma maoni haya , Polisi hawajatoa taarifa muhimu na za maana kuhusu mwanahabari Azory Gwanda aliyetoweka Novemba 21, 2017.

    Sheria kandamizi zilizopitishwa – Sheria ya Makosa ya Mtandaoni, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari, Sheria ya Takwimu na mlolongo wa kanuni, zinafanya utendaji wa vyombo vya habari kuwa mgumu wakati zinavipa vyombo vya dola silaha ya kuendelea kuwakandamiza wanahabari na vyombo vya habari kwa jumla.

    Lakini kwa nini wenye mamlaka wanakuwa na tabia ya kuvibana vyombo vya habari? Hii ni nchi huru ambapo maoni ama ya kuunga mkono ama tofauti dhidi ya utawala lazima yaruhusiwe. Vyombo vya habari, siyo tu kama watoaji au wachagishaji, lazima vifanyekazi kwa uhuru bila kukwazwa.

    Hali inayojitokeza sasa nchini ni kwamba maoni ni haki ya upande mmoja tu na wengine ni wasikilizaji, wafuate na kutekeleza..

    Tunawakumbusha wenye mamlaka kuwa haisaidii kwamba vyombo vya habari viwe kwa ajili ya kusifia na propaganda. Viachwe viwe huru kufanya uandishi wa habari wa kweli wenye manufaa utakaosaidia kufichua maovu yanayostahili kuondolewa katika jamii. Ni vyombo vya habari makini , ukiacha vya kusifia tu vinavyopendwa na serikali, ambavyo vitatoa habari na kutoa mrejesho kwa wenye mamlaka na kutishia waovu. Hivyo, kwa vyombo vya dola, badala ya kuendelea kunyanyasa waandishi wa habari, wakuze mahusiano mazuri kwa lengo la kurahisisha kazi za pande zote mbili kwa manufaa ya taifa.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    3

    Habari

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Na Mwandishi wa Barazani

    Baraza la Habari Tanzania (MCT) kama mlezi wa waandishi wa habari na mtetezi wa uhuru wa vyombo vya habari limefuatilia taarifa kuhusu vitisho vilivyotolewa dhidi ya waandishi habari wanne waandamizi kuona ni kwa kiasi gani huo ujumbe umefanyiwa kazi na walengwa.

    Agosti 7, 2019, kulitokea taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikisema kuwa “Tumetonywa; wafuatao wakae maeneo yenye CCTV na waweke vitu vyao sawa. Walengwa wa ujumbe huo ni waandishi wa habari Simon Mkina, Neville Meena, Eddo Kumwembe na Absalom Kibanda.

    Wengine katika orodha hiyo ni Thabit Jacob, Aidan Eyakuze, Maria Sarungi, Fatuma Karume na Sammy Swami.

    Wanahabari watatu akiwemo Simon Mkina ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, , Abaslom Kibanda aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa Mtanzania , Rai na Bingwa na Neville Meena ambaye ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wameeleza

    walivyochukulia vitisho hivyo. Maelezo yao kuhusu hatua walizochukua ni kama yafuatavyo:-

    Simon MkinaMkina alisema ameongea na baadhi

    ya watu ili kupata ushauri wa kitu gani afanye hasa baada ya kupokea kitisho hicho. Alichokuja kugundua ni kuwa ujumbe huo umetoka kwa mtu anayedai ni mwanachama wa chama kimoja cha Upinzani (jina tunalo). Alifanya jitihada za kuwasiliana naye kupitia akaunti yake ya twitter lakini hakujibiwa.

    Aidha, alisema amewasiliana na wenzake wote waliopo kwenye orodha ya waandishi na wanaharakati waliotishiwa na wote wakaonyesha kulichukulia kwa uzito mkubwa.

    Mkina alimtaja mtu mmoja ambaye amekua akitumia vyombo vya habari anavyoviongoza au kuvimiliki “kuwachafua watu” (jina tunalo), kwamba aliandika jambo linalofanana na hilo kwenye gazeti lake na baada ya muda wahusika wakaanza kutafutwa. “Hili siyo la kulipuuza.”

    Mkina anaamini kuwa kitisho hicho kinatokana na kazi yake, anasema lengo kubwa ni kumtisha. Anasema kuna jamaa yake mmoja aliongea naye kuhusiana na “hiyo post”, yeye

    akamjibu kuwa baada ya dakika tano “hiyo post” itaondolewa na mwenye akaunti hiyo, na kweli baada ya muda mfupi “post hiyo” ikaondolewa.

    Pia anasema taarifa hizo zimesambazwa sana duniani na wana-Diaspora.

    Mkina ameripoti hili tukio polisi lakini pia anatarajia kuwasiliana tena na wenzake kujua wanaweza kufanya nini kama timu.

    Absalom KibandaAnatarajia kwenda kuripoti polisi

    kwa sababu tukio hilo limetokea yeye akiwa Kilimanjaro. Hivyo ataripoti polisi pamoja na kuwasiliana na mwanasheria wake kwa ajili ya ushauri zaidi.

    Alisema “kupuuzia kitu kama hiki unaweza kujikuta umesingiziwa kuwa uko kwenye magenge ya uhalifu.” Amesema akikamilisha hatua anazopanga kuchukua, atalitaarifu Baraza la Habari. Anasema hiki siyo kitisho cha kupuuza.

    Kibanda alishashambuliwa na watu wasiojulikana na akalazimika kupata tiba hapa nchini katika hospitali ya Muhimbili na baadaye Afrika Kusini.

    Neville MeenaAmevisikia vitisho hivyo na kwamba

    leo Agosti 9, 2019 anatarajia kwenda kuripoti hili tukio polisi. Anasema siyo jambo la kupuuza. Anasema familia yake imepata hofu sana hasa baada ya kuona “hiyo posti” kwenye mitandao ya kijamii. Anasema kwa sasa anaripoti polisi baada ya hapo kama kutakuwa na hatua nyingine atakazochukua ataliarifu Baraza.

    MCT yafuatilia vitisho dhidi ya waandishi

    Abasalom Kibanda pamoja na kufanyakazi za uhariri amekuwa pia akitoa mihadhara na kuwasilisha mada mbalimbali kuhusu uandishi wa habari kwa ama wanafunzi wa vyuo, wanahabari waandamizi na hata wanaochipukia.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    4

    Utaratibu

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    16

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Baraza la Habari Tanzania ni chombo huru kilichoundwa na wadau wa vyombo vya habari kusimamia weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

    Je! Una malalamiko juu ya habari au makala iliyotoka gazetini au kipindi chochote kilichorushwa hewani na radio au luninga?

    Kama una malalamiko, basi wasiliana na mhariri wa gazeti au chombo husika cha habari. Ikiwa hutaridhika na hatua za chombo hicho cha habari, basi peleka malalamiko yako Baraza la Habari Tanzania. Baraza litashughulikia shauri lako haraka kwa misingi ya maridhiano na uungwana.

    Jinsi ya kupeleka shauri katika Baraza• Kabla ya kuleta shauri katika Baraza dhidi ya chombo cha habari chochote au

    mwandishi wa habari yeyote, mlalamikaji ajiridhishe kuwa juhudi za kuleta maelewano na kupata upatanishi kati yake na walalamikiwa zimeshindikana.

    • Mlalamikaji anapaswa kuhakikisha kwamba wakati malalamiko yanaletwa kwenye Baraza habari zinazolalamikiwa hazikuchapishwa au kutangazwa zaidi ya wiki 12 zilizopita.

    • Malalamiko yoyote yaletwayo kwenye Baraza sharti yawe katika maandishi na yaonyeshe tarehe, jina la chombo cha habari kilichochapisha au kutangaza habari zinazolalamikiwa. Baraza linaweza kukiamuru chombo cha habari au gazeti kumuomba radhi mlalamikaji na, au kumpa nafasi ya kujibu, au kutoa amri yoyote itakayoona inafaa na ambayo ipo ndani ya mamlaka yake.

    • Iwapo mlalamikaji hataridhika na uamuzi wa Baraza anaweza kutafuta njia nyingine za kutatua shauri lake ikiwemo kulipeleka mahakamani. Hata hivyo, hatatumia uamuzi wa Baraza kama ushahidi Mahakamani. Hata hivyo, Mahakama inaweza kulialika Baraza wakati wowote kama “rafiki wa mahakama” (Amicus Curiae’) pale itakapohitaji ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya habari.

    Kwa mawasiliano na Baraza:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzania,Josam House, Kitalu B, Ghorofa ya Kwanza, Upande B, S.L.P 10160, Simu+255 22 2775728/ +255 22 2771947,Nukushi +255 22 2700370, Simu ya Kiganjani +255 732 998310Barua Pepe: [email protected]: mct.or.tz

    BARAZA LA HABARI TANZANIA

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) imemwan-dikia barua moja kwa moja Rais Joseph Pombe Magufuli kumtaka afute mashitaka yanayomk-abili mwandishi wa habari za uchun-guzi, Erick Kabendera na kutoa maelezo kuhusu hatma ya mwandishi Azory Gwanda aliyetoweka.

    Licha ya kumwandikia Rais Magufuli, CPJ pia imeandika barua kwa Umoja wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu suala hilo na suala zima la uhuru wa habari na kujieleza kwa jumla katika nchi hizo.

    Katika barua ya Agosti 12, 2019, Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ, Joel Simon alikumbusha kuwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu kutetea vyombo vya habari, uliofanyika London mwezi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Prof. Palamagamba Kabudi alisisitiza

    kwamba serikali ya Tanzania inataka kuwezesha uanndishi wa habari za uchunguzi na kuhakikisha kuwa waandishi wanalindwa dhidi ya unyanyasaji na hatua zozote za aina hiyo.

    Kumruhusu Kabendera kuendelea na shughuli zake na kushughulikia suala la kutoweka kwa Gwanda ni hatua muhimu za kufanikisha ahadi hizi za serikali, CPJ imeeleza katika barua hiyo.

    Kabendera alichukuliwa kwa nguvu kutoka nyumbani kwake Julai 29, 2019 na kunyimwa kukutana na mwanasheria kwa saa 24. Polisi awali walidai walikuwa wanachunguza uraia wake.

    Hata hivyo siku chache baadae Polisi walibadili msimamo na kumfungulia mashtaka ya uchumi, ambayo hayamwezeshi kupata dhamana. Alihamishwa mara kwa mara katika vituo vya polisi wakati akihojiwa.

    Kwa jinsi alivyokamatwa na kuwekwa ndani kunaonyesha ni

    hatua za kumkomoa kutokana na uandishi wake ikiwamo suala la mgawanyiko ndani ya chama tawala, CPJ imeeleza katika barua yake.

    Kuhusu Gwanda , CPJ imesema

    mwandishi huyo pia alikuwa ni wa kujitegemea ambaye alitoweka katika Mkoa wa Pwani Novemba 21, 2017 akiwa amechukuliwa na watu wasiojulikana wanaoaminika kuwa ni askari wa usalama.

    Kabla ya hapo, Gwanda alikuwa ameandika habari za mauaji na utekaji wa watu mbalimbali wakiwemo maofisa wa chama tawala na polisi. Licha ya familia yake, vyombo vya habari na mashirika ya kijamii na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhimiza kufanyike uchunguzi, hakuna jitihada zilizochukuliwa kuhusu yaliyomsibu na hatma ya mwandishi huyo.

    Badala yake maofisa wamekuwa wakitoa kauli mchanganyiko mahali alipo mwanahabari huo huku wakiwa

    5

    Habari

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    CPJ yamtaka Rais Magufuli kumfutia mashtaka Kabendera

    Rais John Magufuli akiwa katika mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi za Ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

    Endelea Ukurasa wa 6

    l Pia yawasilisha barua kwa wakuu wa nchi za SADC

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    6

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    kimya kuhusu maendeleo ya uchunguzi wao.

    Barua ya CPJ imezungumzia matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kabudi, katika mahojiano ya Julai ambapo alisema Gwanda ni mmoja wa watu wengi waliotoweka na kufariki katika mkoa wa Pwani.

    Ingawa Kabudi baadaye alisema amenukuliwa vibaya na kwamba hajui kilichomfika Gwanda, matamshi yake yanakuza wasiwasi na kuhimiza haja ya kufanyika uchunguzi ya nini kilichomfika mwandishi huo..

    CPJ imemkumbusha Rais Magufuli kwamba malengo ya serikali yake, ikiwamo kukomesha rushwa, hayawezi kufanikiwa bila ya kuwa na vyombo vya habari vinavyofanyakazi kwa uhuru, salama na bila woga.

    Katika hatua nyingine CPJ imewasilisha suala la kukamatwa kwa mwandishi Kabendera na kutoweka kwa Gwanda kwa Marais wa nchi wanachama wa SADC.

    Katika barua kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dr. Stergomena Tax, CPJ imeeleza wasiwasi wa kipekee

    kuhusu Tanzania ambayo Rais wake Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa SADC, ambapo wanahabari wanafanyakazi katika mazingira magumu na hatarishi.

    Barua hiyo iliyotiwa saini na Robert Mahoney, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ Agosti 15, 2019 na kuwasilishwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC Agosti 17 Jijini Dar e s Salaam, imeeleza kuwa mwandishi Azory Gwanda ametoweka tangu 2017, na serikali kushindwa kutoa maelezo kuhusu suala lake kunatisha vyombo vya habari nchini humo.

    Mwezi uliopita CPJ ilieleza kuwa Kabendera alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya makosa ya uchumi kutokana na uandishi wake wa uchunguzi. Bado yuko ndani. CPJ pia ilieleza katika barua hiyo kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikifungiwa na kwamba kwa kutumia kanuni mpya Tanzania imeweka tozo za juu kwa uendeshaji wa mitandao na kudhibiti nini wananchi wake wanaweza kusema mitandaoni.

    Barua hiyo imemtaka Katibu

    Mtendaji wa SADC kutoa kipaumbele kwa uhuru wa habari na usalama wa waandshi katika eneo hilo. CPJ imekumbusha kuwa mkataba wa SADC unasisitiza nchi wanachama kuzingatia kanuni za haki za binadamu, demokrasia na utawala a sheria.

    Zaidi ya hapo , CPJ imesema Mkataba wa SADC wa Utamaduni, Habari na Michezo uansisitiza nchi wanachama zinahimizwa kuhakikisha vyombo vya habari vilivyo na uhuru wa uhariri ."

    H ata hivyo pamoja na makubaliano haya, CPJ imebaini ukiukaji mkubwa wa uhuru wa habari katika nchi mbalimbali za SADC ikiwa pamoja na kushambualia waandishi binafsi, kufungwa kwa vyombo vya habari, kufunga intaneti na sheria kandamizi. Vitisho hivi vingi vinaongezeka katika kipindi kuelekea uchaguzi ama wakati wakati wa uchaguzi. Zaidi ya nusu ya nchi wanachama wa SADC zinatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ama uchaguzi mkuu ifikapo mwisho wa mwaka 2020.

    Inatoka Ukurasa wa 5

    CPJ yamtaka Rais Magufuli kumfutia mashtaka Kabendera

    Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi za Ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ukiendelea.

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Kabla hata mwezi kupita, mwandishi mwingine wa habari za uchunguzi ame-kamatwa na polisi kwa kutekeleza kazi zake.

    Joseph Gandye, Mhariri wa Uzalishaji wa Runinga ya Mtandaoni ya Watetezi TV alikamatwa na Polisi Agosti 22, 2019 kufuatia kutangazwa kwa habari ya ukatili wa polisi kwa watuhumiwa.

    Kukamatwa kwa Gandye

    kunafuatia kukamatwa kwa mwandishi mwingine wa habari za uchunguzi Erick Kabendera, ambako kulipingwa vikali na taasisi mbalimbali za habari nchini na nje ya nchi.

    Kabendera amepachikwa mashitaka ya makosa ya uchumi ambayo hayana dhamana na yuko rumande. Alikamatwa Julai 29 nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam.

    Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelaani kukamatwa kwa mwandishi Gandye na inaona hatua hiyo ni mwendelezo wa Polisi wa kuzuia waandishi kutekeleza majukumu yao ya msingi ya kukusanya habari na kuwapasha habari Watanzania.

    MCT, katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza, Kajubi Mukajanga imeleeza kuwa imeridhishwa kuwa Gandye

    7

    Habari

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Mwandishi mwingine akamatwa

    Mhariri wa Uzalishaji wa Runinga ya Mtandaoni ya Watetezi, Joseph Gandye

    Endelea Ukurasa wa 8

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    8

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    alizingatia taratibu zote za uandishi ikiwemo kuwahoji wafanyakazi wa kiwanda alikopata taarifa husika.

    Mwandishi huyo pia aliwahoji polisi, madaktari katika hospitali ya Mafinga na wamiliki wa Kiwanda cha kampuni ya Hong Wei International na alitumia hati ya mashahidi wanaodaiwa kulazimishwa kulawitiana baada ya kuteswa.

    Katika hili MCT inashangazwa na kukamatwa mwandishi aliyezingatia taratibu zote za uandishi kabla ya kutangaza habari yake. Baraza limevitaka vyombo vya usalama kutowakamata wanahabari wanapofanyakazi zao na badala yake wawape ushirikiano.

    “Waandishi wanaofichua maovu ni rafiki wa wananchi na maofisa wa usalama, siyo maadui”, alisema Mukajanga katika taarifa hiyo.

    Katika matamshi yake ya awali, Mukajanga alisema ni bahati mbaya wale wanafanyakazi ya uandishi wa habari wa kweli wanaendelea kukamatwa na kunyanyaswa. “Wanataka uandishi upi? Kuna propaganda na kusifia katika uandishi…. ambao si uandishi makini na unaofaa”, alisema Mukajanga..

    Wakati huo huo Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wamelaani kukamatwa kwa mwandishi huyo wa kituo cha cha runinga na wametaka apewe haki zote za mtuhumiwa , asiteswe ama kunyanyaswa.

    THRDC imesisitiza haki ya mtuhumiwa kupata dhamana kwa kuwa kosa alilokamatiwa lina dhamana. Juni 17, 2019 waandishi wa Watetezi TV walipata taarifa ya vitendo vya udhalilishaji walivyofanyiwa watuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Mafinga, mkoani Iringa. Baada ya kupata ripoti hizo mwandishi Gandye alisafiri kwenda Iringa kuchunguza habari hizo na Agosti 9, 2019 runinga ya Watetezi TV iliripoti tukio la polisi kufanya unyama katika kituo hicho cha Mafinga katika Facebook, Twitter na You Tube.

    Katika tukio hilo , imedaiwa kuwa watuhumiwa sita (majina yao yanahifadhiwa) walikamatwa na polisi May 19, 2019 na wakawekwa ndani kwa siku 10 ambapo ilidaiwa

    walipigwa na kulazimishwa kulawitiana wenyewe mbele ya polisi wakati wakihojiwa. Baada ya runinga ya Watetezi kutangaza unyama huo wa Polisi Agosti 9, 2019, jeshi la polisi mkoani Iringa kupitia Kamanda wake wa Mkoa (RPC), ACP Juma Bwire, alikanusha ripoti hiyo kuwa ililenga kulidhalilisha jeshi na serikali kwa jumla.

    Kulingana na taarifa ya THRDC, Gandye ndiye mwandishi aliyeripoti kuhusu mwanafunzi aliyeadhibiwa na mwalimu mpaka pingili za uti wake wa mgongo kuvunjika mkoani Njombe.

    Pia aliripoti kuhusu ukiukaji wa haki Loliondo na kutokana na ripoti ya Watetezi TV, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola, aliweza

    kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua. Joseph Gandye pia ni mtayarishaji wa kipindi cha Haki za Binadamu kinachotangazwa Ijumaa kila wiki na studio za runinga ya Watetezi TV.

    Joseph Gandye aliachiwa kwa dhamana baadaye na mwandishi Haruna Hussein Mapunda wa runinga ya mtandaoni ya Gilly Bonny ambaye alikamatwa na polisi naye pia ameachiwa. Ofisa mmoja wa THRDC alisema kuwa Gadye aliachiwa kwa dhamana Agosti 24, 2019 baada ya kuripoti kwa Kamanda wa Uhalifu wa Mkoa wa Iringa na alitakiwa kuripoti

    tena Agosti 28, 2019. Kuhusu Mapunda ambaye

    alikamatwa akiwa na viongozi wa Act Wazalenda ofisa huyo wa THRDC alisema kuwa ameachiwa na hakuweza kutoa maelezo zaidi.

    Mwandishi mwingine akamatwa

    Mwandishi Haruna Mapunda wa wa runinga ya mtandaoni ya Gilly Bonny.

    Inatoka Ukurasa wa 7

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani,

    Taasisi tatu za habari – Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wametoa kauli ya pamoja kuhimiza vyombo vya usal-ama, hasa polisi kuzingatia taratibu za kisheria wanapokamata watuhumiwa.

    Tamko hilo lilitolewa na taasisi hizo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Agosti 11, 2019 Jijini Dar es Salaam.

    Tamko hilo limetolewa kufuatia kukamatwa mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera ambaye hatimaye polisi wamemfungulia mashitaka ya makosa ya kiuchumi yasiyo na dhamana.

    Wakuu wa taasisi hizo, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, Rais wa UTPC Deogtaius Nsokolo na Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile kwa pamoja wamesisitiza kuwa hawapingi watu kukamatwa bali sheria lazima zizingatiwe.

    Walieleza masikitiko jinsi mwandishi Kabendera alivyokamatwa huku familia, jamaa na hata wanasheria hawakujua alipo kwa kipindi kirefu na wakati huo huo akihamishwa katika vituo mbalimbali vya polisi. Katika tamko hilo taasisi hizo zilitoa

    ufafanuzi mpana na taratibu zinazostahili kuzingatiwa.

    Wamewataka maofisa wa Jeshi la Polisi wajiepushe na vitendo vinavyoweza kuashiria ukiukwaji wa haki za watuhumiwa kama uteswaji au udhalilishaji wa namna yoyote.

    Pia Polisi wametakiwa kuhakikisha wanawapeleka washtakiwa mahakamani ndani ya muda uliowekwa kisheria.

    Vile vile wametaka mashitaka yote yawe na dhamana.

    Tamko hilo ambalo ni la kwanza la aina yake kutolewa, hasa baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani limejikita zaidi katika stahiki na haki za kisheria za watuhumiwa kabla na baada ya kukamatwa.

    Tamko kamili ni kama lifuatavyo:-Erick Kabendera ni mwandishi wa habari

    za uchunguzi wa kujitegemea anayeandika kuhusu hahari za ndani ya nchi na za Kimataifa. Erick Kabendera alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi tarehe 29 Julai 2019 saa 12 jioni nyumbani kwake Mbweni, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, ambapo walivamia nyumba yake na kuondoka naye.

    Kwa mujibu wa maelezo ya mke wake na jirani zake, gari iliyotumika kumchukua haikuwa na namba za polisi na ilikuwa imesajiliwa kwa namba T746 DFS. Rekodi ya kamera za CCTV zinaonyesha watu waliojitambulisha kuwa ni askari polisi walimkamata na kuondoka naye nyumbani kwake. Mke wake alieleza kuwa kundi la

    watu sita waliojitambulisha kuwa ni askari polisi ambao hawakuvaa sare, walifika na gari na kuizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa tatu, kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni. Baadaye Bw. Erick Kabendera alikamatwa kwa maelezo kuwa wanampeleka kituo cha polisi cha Oysterbay.

    Kabla ya kukamatwa kwake, simu zake za mkononi zilikuwa hazipatikani na laini za simu zilikuwa hazifanyi kazi. Alipiga simu mtandao wa Vodacom kuulizia ambapo alijibiwa kuwa wamepokea maagizo kutoka katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzuia kadi zake za simu. Inasadikiwa kuwa ababu za kuzimwa kwa simu zake ni kwa kuwa alikuwa anawasiliana na majirani na viongozi wa Mtaa kuhusu uwepo wa gari lisiloeleweka getini kwake baada ya kuwachunguza kupitia CCTV.

    Utata wa Aliposhikiliwa Erick Kabendera kabla ya ndugu kumwona

    Mwanzoni maafisa wa polisi katika kituo cha Oysterbay na kituo Kikuu cha Kati walikataa kuwa wanamshikilia Erick Kabendera. Baada ya mivutano mingi na kuonesha ushahidi wa kuwa Kabendera amechukuliwa na Jeshi la Polisi, ndipo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alikiri kuwa Erick Kabendera alikamatwa na Jeshi la Polisi na ameshikiliwa kwa mahojiano kuhusu uraia wake.

    Jambo hili pia lilizua maswali mengi

    9

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Polisi wahimizwa kuzingatia sheria kwa watuhumiwa

    Endelea Ukurasa wa 10

    Habari

    Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mkujanga (wa pili kutoka kushoto) akizungumza wakati Baraza hilo na taasisi nyingine tatu zilipotoa tamko la pamoja kusisitiza vyombo vya usalama hasa polisi kuwatendea haki watuhumiwa. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Dedodatus Balile, kulia ni Rais wa Umoja wa Klabu za Waaandishi wa Mikoani (UTPC) Deogratius Nskolo na wa pili kutoka kulia ni Mratibu wa Kitaifa wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    10

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    yaliyosababisha Mtandao uanze mchakato wa kumtafuta Erick kupitia mahakama. Baada ya kushindwa kuwasiliana na Erick Kabendera, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kupitia mawakili wake, ulianza mchakato wa kumuombea dhamana katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mwandamizi Rwizile. Kabla ya kituo cha polisi alichoshikiliwa kujulikana, Mke wa Bwana Kabendera alizunguka vituo vingi vya polisi akijaribu kumtafuta mumewe lakini hakufanikiwa. Hata hivyo alifanikiwa kukutana na kamanda wa polisi, Lazaro Mambosasa, ambae alimwambia aende Kituo cha Polisi cha Kati mnamo tarehe 31 Julai, 2019 saa 2 asubuhi. Pia Mke wa mwandishi huyo aliripoti kuwa alipokea simu iliyomwamuru kusalimisha hati ya kusafiria ya mumewe na nakala za kitaaluma kwa Waziri wa Mambo ya ndani.

    Tabia ya kuwahamisha watu wanaotuhumiwa kutoka kituo kimoja cha polisi kwenda kingine imeongezeka sana sasa. Tatizo hili hufanyika bila taarifa kwa ndugu na hatimaye kuvunja haki za mtuhumiwa na kuzua taharuki kwa umma kuhusu usalama wa mtuhumiwa. Hii inanyima haki ya uwakilishi wa kisheria na kutembelewa na familia. Maafisa wa polisi walikiuka haki hizi kwa kuwa mke hakuweza kumuona mumewe, na mawakili wake hawakuweza kumpata kwa siku mbili mfululizo. Baada ya kufuatilia kwa kina na nguvu kubwa tulifanikiwa kujua kuwa Bwana Kabendera yupo katika kituo cha Polisi cha barabara ya Kilwa (Kilwa road), kituo ambacho hakikutajwa hapo awali na maafisa wa polisi. Zaidi ya saa 44 zilipita toka Bwana Kabendera akamatwe na kuwekwa kizuizini katika kituo cha polisi ambacho hakikufahamika mara moja, mpaka tarehe 31.07.2019 ilipodhihirishwa kuwa yupo katika kituo cha Polisi cha Barabara ya Kilwa.

    Matakwa ya Sheria kuhusu Haki za Watuhumiwa

    Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (The criminal procedure Act 1985 Cap 20 R.E 2002) imeelezea wazi taratibu za kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kumfungulia mtu mashtaka.

    Kwa namna alivyokamatwa, polisi hawakufuata taratibu mbalimbali za sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Utaratibu uliokiukwa ni kama ufuatavyo:

    1. Mshtakiwa hakujulishwa sababu za kukamatwa kwake

    Kifungu cha 23 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai hakikuzingatiwa. Alipokamatwa hakuambiwa chochote zaidi ya kuwa anapelekwa kituo cha polisi tena baada ya majirani kuzunguka gari na kuhoji ni wapi Kabendera anapopelekwa.

    Sababu za kukamatwa kwake zilikuja kuwekwa bayana baada ya siku kadhaa kupita katika mkutano na waandishi wa habari. Huu sio utaratibu sahihi wa kisheria. Mtuhumiwa alipaswa kujua sababu zilizopelekea akamatwe na kushikiliwa katika kituo cha polisi. Alipokamatwa tarehe 29 Julai 2019, polisi hawakutoa sababu za kukamatwa kwake na pia hawakutoa sababu za kuhoji utaifa wake kwa mara ya pili.

    Pamoja na tuhuma hizo na mahojiano Idara ya Uhamiaji haijatoa taarifa yoyote kuhusu uchunguzi uliofanywa. Badala yake walimkabidhi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi huku ikionekana hakuna tena tatizo la uraia. Changamoto kubwa ni kuwa hadi sasa Idara ya Uhamiaji haijamtangaza Erick kuwa sasa ni raia halali na pasi za kusafiria za Erick na Familia yake bado pia wanazishikilia.Ikumbwe suala la uraia ndilo lililokuwa kosa la kwanza alilotuhumiwa nalo Erick Kabendera baada ya kukamatwa.

    2. Kufikishwa mahakamani ndani ya wakati uliowekwa kisheria.

    Kifungu cha 32(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema kuwa:

    “Wakati mtu yeyote amewekwa mahabusu kwa kosa bila kibali, isipokuwa kwa kosa linaloadhibiwa kwa kifo, afisa msimamizi wa kituo cha polisi ambako ameletwa, katika jinsi yoyote, na kama inaonekana haiwezekani kumpeleka mbele ya mahakama inayofaa ndani ya saa ishirini na nne kuanzia alipowekwa mahabusu, anaweza kuichunguza kesi na, isipokuwa kama kosa linaonekana na afisa huyo kuwa ni kubwa, kumwachia mtu huyo baada ya kuweka dhamana kwa kiasi cha kutosha

    akiwa na wadhamini au bila ya wadhamini, na kumtaka kuhudhuria mbele ya mahakama katika muda na mahali palipotajwa kwenye dhamana; lakini kama atashikiliwa mahabusu atalazimika kupelekwa mbele ya mahakama haraka iwezekanavyo.”

    3. Haki ya kuwa na wakili na kuonana na ndugu au rafiki kipindi cha kuchukua maelezo ya mshitakiwa.

    Kifungu cha 54 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai mwaka 1985 kinaeleza kuhusu haki ya msingi ya mshitakiwa kuonana na wakili na ndugu wa karibu. Katika haki ya kuonana na mwanasheria wake au mtu wake wa karibu au familia, mwandishi huyu hapo mwanzoni amehojiwa bila kuwa na wakili wake au mtu wake wa karibu kinyume na utaratibu uliopo kisheria. Haki hii imeshindwa kutekelezeka kwa sababu hapo awali mawakili na familia yake walishindwa kuwepo wakati akitoa maelezo kwa sababu haikujulikana yupo katika kituo gani cha polisi.

    4. Kutokuwa na hatia mpaka itakapothibitishwa

    Ibara ya 13 (6)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kudhaniwa ametenda kosa hilo mpaka pale itakapothibitika ametenda kosa hilo .Ukiangalia jinsi alivyokamatwa, inaonekana wazi kuwa maafisa wa polisi waliohusika walienda mbele zaidi na kumdhania Bwana Kabendera kuwa na hatia kabla haijathibitishwa na mahakama.

    5. Kubadilishwa mashtaka zaidi ya mara tatu ndani ya siku 5

    Jambo ling ine lililoonyesha uonevu kwa Erick na ukiukwaji wa Sheria ni dhamira ya kulazimisha kumkuta Erick na tuhuma hata ambazo hazikuwa msingi wa kukamatwa kwake. Tukio la kukamatwa, kuhojiwa , limehusisha tuhuma kuu tatu (Uraia, Taarifa za Uongo na Uchochezi) kabla ya kufikishwa mahakamani kwa tuhuma nyingine tatu (Utakatishaji fedha, Kutokulipa Kodi na kushiriki mtandao wa uhalifu).

    a) Kuhojiwa kuhusu UraiaBaada ya kukamatwa kwa mara ya

    kwanza Bwana Erick alihojiwa na maofisa wa uhamiaji kuhusu uraia wake. Ni vyema ikumbukwe hii ni mara ya pili mwandishi huyu kukamatwa na kuhojiwa kuhusu uraia wake, mnamo mwaka 2013, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, Emmanuel Nchimbi, alitoa tamko la kuondoa utata juu ya madai ya kuwa Bw. Kabendera sio Mtanzania, alieleza kuwa ni Mtanzania na hata wazazi wake ni Watanzania. Vilevile kauli iliyotolewa na Afisa wa Uhamiaji kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ilisema kwamba uraia wa mwandishi huyu pamoja na wazazi wake haukuwa na utata wowote.

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaoro Mambo sasa akizungumza kufuatia kukamatwa kwa mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera.

    Polisi wahimizwa kuzingatia sheriaInatoka Ukurasa wa 9

    Endelea Ukurasa wa 12

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Vyombo vya habari vinashuhudia matumizi ya sheria kuvikandamiza pamoja na mashirika ya kiraia, Ripoti ya mwaka 2018 ya Baraza la Habari Tanzania inaeleza.

    Sheria mbaya zimekuwepo kama sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na sheria zingine, lakini vyombo vya habari havijawahi kubanwa kama inavyotokea sasa.

    Ripoti hiyo inazungumzia baadhi ya sheria zenye vipengele kandamizi ambazo zilitumika kwa

    ukamilifu mwaka 2018 na kuathiri vyombo vya habari na mashirika ya kiraia ikiwa ni pamoja na sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari (MSA) ya mwaka 2016, Sheria ya Takwimu ya 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2018, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015 na Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018 ya Sheria ya Eletroniki na Posta.

    Kutokana na kubanwa vyombo vya habari sasa vimekuwa ni vya kusifia tu na kujidhibiti vyenyewe na aina ya habari zinazotangazwa ama kuchapishwa na kwamba uandishi wa uchunguzi unapotea.

    Hali inazidi kuwa mbaya zaidi

    na Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni na sheria ya Takwimu kwa kufanya iwe hatari kufanya uandishi wa habari huru hata katika masuala ya maendeleo.

    Pia kupitishwa kwa kanuni za sheria ya MSA pia kumeathiri uchumi wa vyombo vya habari, kwa kuwa vingi vinategemea matangazo yanayotolewa na serikali.

    Kanuni hizo zimeweka utaratibu mmoja wa kutoa matangazo na yamempa madaraka Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoa matangazo kwa vyombo vya habari.

    Wahariri wanalalamika

    11

    Habari

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Kibano cha kupindukia kwa vyombo vya habari

    Endelea Ukurasa wa 14

    Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za uhalifu wa kiuchumi.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Waziri huyo aliagiza kuwa maafisa wawili wa Uhamiaji waliomkamata na kumhoji juu ya uraia wake waadhibiwe kwa kumdhalilisha yeye pamoja na familia yake.

    Mnamo mwaka 2013, Mkurugenzi wa Malalamiko katika Idara ya Uhamiaji, Bwana Augustine Shio, alisema kwamba zoezi lote la kufuatilia na kuamua utaifa wa Kabendera pamoja na wa wazazi wake halikuwa sahihi na halikushughulikiwa kitaaluma. Alifafanua kwamba uraia na utaifa wa Erick Kabendera na ule wa familia yake haukuwa na shaka yoyote.

    Kufuatia kauli hizo za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Afisa wa Uhamiaji, kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu sababu za kumkamata kwa mara ya pili ikiwa walishathibitisha kuwa ni Mtanzania. Na kama si Mtanzania ni raia wa wapi?.

    b) Kuhusu tuhuma za UchocheziBaada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa na

    maofisa wa Uhamiaji, Bwana Erick alishikiliwa na kuhojiwa kuhusu tuhuma za uchochezi mitandaoni. Tuhuma hizi zilihusishwa na makala yake aliyoitoa kwenye jarida la “The Economist” lililochapishwa tarehe 31 Julai 2019. Hata hivyo tuhuma hizo za uchochezi na utoaji wa taarifa za uongo zilibadilishwa tena pale alipofikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa makosa mengine matatu.

    c) Tuhuma za kushindwa kulipa kodi, kupanga njama ya kutenda uhalifu na utakatishaji fedha

    Wakati mahojiano yakiendelea, makazi ya Bwana Erick Kabendera yalikaguliwa mara kadhaa. Mara ya mwisho katika kukagua nyumba yake, askari polisi waliamuru awapatie hati ya nyumba, kadi za benki na magari.

    Erick Kabendera aliwasilisha nyaraka alizokuwa nazo kwa muda huo na alitoa ushirikiano wa kukamilisha uwasilishwaji wa baadhi ya nyaraka ambazo hazikuwepo ndani kwa wakati ule, alitoa maelekezo ya wapi vinaweza kupatikana .

    Baada ya vuta nikuvute ndani ya siku 6 mfululizo za jitihada za kumuombea dhamana bila mafanikio, hatimaye siku ya 7 mnamo tarehe 5 Agosti 2019, polisi walimpeleka Erick Kabendera Mahakamani. Mawakili walikuwa wamejiandaa kwa kusikilizwa kwa ombi la kupatiwa dhamana kwa kuwa mpaka muda huo hakua amefunguliwa shitaka lolote.

    Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Erick Kabendera alipofikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu alisomewa mashtaka matatu ikiwemo kushindwa kulipa kodi, kupanga njama ya kutenda uhalifu na utakatishaji fedha. Makosa anayotuhumiwa nayo Erick Kabendera hayana dhamana kwa mujibu wa sheria na hivyo mwandishi huyo anabakia kuwa mahabusu hadi uchunguzi wa kesi yake utakapokamilika na kesi yake kusikilizwa katika Mahakama Kuu yenye

    mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.Sheria hizi za Uhujumu Uchumi na

    Utakatishaji fedha ni moja ya sheria kandamizi zinazoonekana kwa sasa kukiuka sana haki za watuhumiwa za kupata dhamana, lakini pia haki ya kusikilizwa mahakamani kwa wakati. Ni kinyume na haki za binadamu kumkamata mtu ambaye uchunguzi wa awali haukujitosheleza kumtia hatiani. Makosa haya hufanya watu wakae mahabusu kwa miaka mingi bila mashauri yao kusikilizwa. Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma alishauri watu wasikamatwe hadi pale uchunguzi utakapokuwa umefikia kiwango cha kuridhisha. Erick alibadilishiwa makosa dakika za mwisho. Swali linabaki walipata muda gani kufanya uchunguzi wa kutosha kumshitaki Erick kwa makosa haya makubwa ambayo hayakuwa makosa ya awali wakati wa ukamataji.

    Katika kipindi hiki ambapo Jumuiya za Kimataifa zinafuatilia kwa ukaribu masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini, suala la kukamatwa na kushtakiwa kwa Erick Kabendera limeleta taswira mbaya ya nchi yetu. Balozi mbalimbali zimeshatoa matamko kuonyesha masikitiko yao kuhusu hali ya haki za binadamu na namna ambavyo watuhumiwa kama Erick wamekuwa wakivunjiwa haki zao kabla ya kupelekwa mahakamani.

    WITO WETUa. Kutokana na ukweli kwamba awali

    Bwana Erick alihojiwa kuhusu uraia wake na maofisa wa Uhamiaji kabla ya kubadilishiwa tuhuma, tunawasihi maofisa wa uhamiaji watoe tamko kwamba Erick ni Raia wa Tanzania au vinginevyo kwa mujibu wa uchunguzi wao;

    b. Tunashauri pia suala la uraia lisitumike kama silaha ya kuwanyamazisha Watanzania wanaopenda kuhoji mambo ya msingi ya kitaifa;

    c. Tunawaomba maofisa wa uhamiaji wamrudishie Bwana Erick, Mke na Watoto hati zao za kusafiria ikiwa hawakuthibitisha kuwa Bwana Erick si raia wa Tanzania;

    d. Tunalisihi Jeshi la Polisi kufuata utaratibu katika kukamata watu, ikiwemo kuwataarifu sababu za kukamatwa, ndugu wafahamu kituo cha polisi alichopelekwa na kushikiliwa ili kuepuka sintofahamu na kudhaniwa kuwa mtu ametekwa kumbe amekamatwa na vyombo vya usalama;

    e. Maofisa wa jeshi la Polisi watoe haki zote za mshatakiwa kama kuonana na mwanasheria pamoja na familia yake pindi wanapokuwa wanawashikilia watuhumiwa;

    f. Maofisa wa Jeshi la Polisi wajiepushe na vitendo vinavyoweza kuashiria ukiukwaji wa haki za watuhumiwa kama uteswaji au udhalilishaji wa namna yoyote;

    g. Polisi wahakikishe wanawapeleka washtakiwa mahakamani ndani ya muda

    uliowekwa kisheria;h. Wito kwa wanasheria wote nchini

    kutafakari na kuchukua hatua ya kupinga sheria ya utakatishwaji fedha na uhujumu uchumi haswa katika suala la dhamana;

    i. Katika kipindi hiki ambacho serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, inapitia upya Mfumo wa Haki na Jinai nchini, wanasheria na Watetezi wa Haki za Binadamu kote nchini wanapaswa kupinga nguvu na mamlaka makubwa aliyopewa mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) katika kuendesha kesi hizi na haswa katika upatikanaji wa vielelezo na ushahidi mbalimbali katika mashtaka ya aina hii;

    j. Makosa yote yawe na dhamana. Sheria zote zinazominya haki ya watuhumiwa kupata dhamana zifanyiwe marekebisho ili kuwapa watuhumiwa haki yao ya kuwa huru wakati vyombo vya usalama vinapoendelea na uchunguzi au Mahakama inapoendelea na kesi.

    k. Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lipitishe sheria itakayoruhusu makosa yote yawe na dhamana.

    l. Mahakama ipewe mamlaka ya kutoa maamuzi kuhusu dhamana. Sheria zisizuie dhamana bali mahakama iamue kuhusu dhamana ya mtu kulingana na mazingira na uzito wa shauri.

    m. Masharti ya dhamana katika mahakama zetu na Jeshi la polisi yalegezwe ili kuweka masharti nafuu yatakayowawezesha watuhumiwa kupata haki yao ya dhamana.

    n. Jeshi la Polisi na vyombo vyote vinavyohusika na utoaji haki visikamate watuhumiwa kabla ya kumaliza upelelezi. Tunaungana na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma ya kuhakisha watu hawakamatwi hadi pale uchunguzi wa kutosha uwe umefanyika. Hii itapunguza muda mwingi wa watuhumiwa kukaa mahabusu.

    o. Sheria itamke wazi kwamba ikifika kipindi fulani cha muda na upelelezi haujakamilika basi kesi ifutwe.

    p. Tunapendekeza kuwepo utaratibu wa polisi kupeleka shauri la kusikiliza ushahidi (evidential Hearing). Hii itasaidia upatikanaji wa haki na kwa wakati. Katika mchakato huu polisi wanatakiwa kuleta shauri hilo wakiwa na vielelezo vyote na ushahidi wote mbele ya mahakama. Mahakama isikilize na mtuhumiwa ajibu ndipo mahakama ikiridhishwa kuwa mtuhumiwa ana kesi na anaweza kutiwa hatiani itoe amri ya kukamatwa mtuhumiwa. Shauri hili litasaidia kupunguza muda ambao polisi wanatumia kufanya upelelezi huku mtuhumiwa akinyimwa haki zake za msingi ikiwa kudhaniwa hana hatia mpaka atakapokutwa na hatia, vilevile ushahidi ukiwa umekamilika kesi itaendelea kwa

    12

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Habari

    Inatoka Ukurasa wa 10 Polisi wahimizwa

  • Waliomeremeta

    Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

    Na Mwandishi wa Barazani

    Waandishi wa habari Christopher Gamaina, Zephania Mandia na Manga Msalaba ambao walifunguliwa kesi namba 11/2018 ya

    unyang’anyi wa kutumia nguvu katika Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani

    Mwanza wamelishukuru Baraza la Habati Tanzania (MCT) kwa kuwapatia mawakili wa kuwatetea katika kesi yao.

    Waandishi hao wanaodai kubambikiwa kesi hiyo na Polisi walitetewa na mawakili Linus Amri

    na Constantine Mutalemwa na hivi sasa wako nje kwa dhamana kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa kesi hiyo isikilizwe upya.

    Aprili 18, 2019 mahakama ya Magu chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Edmund Kente iliwahukumu kwenda jela miaka 30 wakiwa wanatetewa na wakili Amri pekee, lakini wamesema walifurahishwa na hatua ya wakili Mutalemwa kushirikiana na Amri kuwakatia rufaa ya kupinga hukumu hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Ziwa.

    Jitihada za mawakili hao, kwa gharama za MCT, zilijenga

    hoja za kisheria zilizoishawishi

    Mahakama Kuu hiyo, chini ya Jaji Mohammed Siyani, kutoa uamuzi wa kuwafutia kifungo hicho Julai 24, 2019 na kuelekeza kesi hiyo irejeshwe katika Mahakama ya Wilaya ya Magu kwa ajili ya kusikilizwa upya na hakimu mwingine.

    Agosti 5, 2019 waandishi hao walitolewa gerezani na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu na kusomewa upya kesi hiyo mbele ya Hakimu

    Lugakingira kabla ya kudhaminiwa (kila mmoja na wadhamini wawili), na kurejea uraiani kuungana na familia zao.

    Walipangiwa kurudi mahakamani hapo Agosti 19, 2019 ili upande wa Jamhuri usome/uwasilishe hoja za awali za shitaka dhidi yao.

    Akiandika barua hiyo ya shukrani kwa niaba ya wenzake Gamaina amesema, “tunaishukuru na kuipongeza MCT kutokana na hatua hiyo ambayo hakika imetupatia matumaini kwamba siku moja tutaachiwa huru kabisa kwani hata Mungu anajua tulibambikiwa kesi hiyo ili kutuzima sisi kama waandishi wa habari tusitangaze maovu ya Nestory Kubu na mke wake,

    Tizila wanaotulalamikia”.“Tunaishukuru tena na tena MCT,

    tukiamini itaendelea kutushika mkono katika kila juhudi za kukabiliana na kesi hiyo hadi tuachiwe huru na Mungu atakuwa pamoja nasi daima”, aliandika Gamaina.

    13

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Habari

    Wanahabari wanaotuhumiwa mahakamani waishukuru MCT

    Wanahabari Christopher Gamaina(kushoto) na Zephania Mundia (kulia) wakiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi ya Mwanza (MPC), Edwin Soko baada ya kuachiwa kwa dhamana.

  • Waliomeremeta

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    14

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    kwamba vyombo ambavyo havizingatii msimamo wa serikali katika habari zao, vinanyimwa matangazo.

    Sheria mbaya pia zinatumika kukwaza haki ya wananchi kupata taarifa pamoja na haki ya kujieleza kwa kiasi kwamba mashirika ama taasisi zinazohusika na masuala ya uwajibikaji, haki za binadamu na kupata taarifa hayakuwa na uhakika nini kitatokea siku inayofuata, taarifa hiyo ya mwaka ya MCT imeeleza.

    Kulingana na Ripoti hiyo inayoelezea shughuli zilizofanywa na Baraza kwa mwaka, wadau wamekubali ukweli kwamba hali haiwezi kubadilika hivi karibuni na wameamua kuwa njia iliyobakia kutafuta haki ni mahakamani.

    “Baadhi ya mashirika ya kiraia yameungana katika kutafuta tafsiri ya sheria na kanuni zinazobana watu “, Ripoti hiyo imeeleza. Mwishoni mwa mwaka 2018, kesi tano zilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania na mbili katika Mahakama ya Afrika Mashariki.

    Maamuzi ya Serikali kuyafungia magazeti yalilalamikiwa kortini na yalipigwa chini.

    Katika mkutano wa hali ya juu wa wamiliki wa vyombo vya habari na wahariri ulioandaliwa na Baraza mwaka jana, ilielezwa kwamba vitendo vya ukiukwaji wa uhuru wa habari vimeongezeka ambapo vitisho, mashambulizi, kupigwa, kutozwa faini , kunyimwa kupewa taarifa, kutoweka, kufungiwa vyombo vya habari kumeongeza hofu kwa wamiliki wa vyombo vya habari.

    Baraza na wadau mbalimbali, kulingana na Ripoti hiyo wamekuwa wakishirikiana kusaidia wanahabari na vyombo vya habari ambavyo haki zao zimekiukwa.

    Ilipofika mwishoni mwa mwaka,

    vyombo vitano vya habari na wanahabari wanne wamekuwa wanasaidiwa kupata haki.

    MCT ilipata mafanikio katika kesi nne ilizokuwa ikiunga mkono ambazo ni za magazeti ya MwanaHALISI, Mawio na Mseto yaliyofungiwa na serikali na wanahabari Christopher Gamaina na mwenzake George Ramadhani walioachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mwanza kutokana na tuhuma ya kubambikiwa.

    Licha ya hali kuwa ngumu, Baraza na washirika wake wanadhamiria kuendeleza majadiliano na serikali kupitia wizara mbalimbali na maofisa na kupitia Bunge pia.

    Baraza, Ripoti hiyo inaeleza, limekuwa na mahusiano mazuri na Wizara ya Katiba na Masuala ya Sheria na wamekubaliana kufanyakazi pamoja kuhusiana na kujenga uwezo wa maofisa wa habari wa serikali kuhusiana na sheria ya Haki ya Kupata taarifa.

    Baraza pia limekuwa na mashauriano na maofisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Habari , akiwemo Katibu Mkuu.

    Ni imani ya Baraza kwamba mazungumzo yatawezesha serikali kutambua kuona na kuelewa kilio cha wadau, Ripoti hiyo imeeleza.

    Ujumbe uliojumuisha wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Baraza na Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ulifanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Masuala ya Sheria Prof. Palamagamba Kabudi Agosti 15, 2018.

    CoRI – inayoongozwa na MCT inajumuisha taasisi mbalimbali zikiwemo – Sikika, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA- Tan), Twaweza, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Chama cha Wamiliki wa Vyombo

    vya Habari Tanzania (MOAT), Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Policy Forum, TCIB na Article 19.

    Katika mkutano na Waziri , MCT iliwasilisha masuala kadhaa ikimuomba aboreshe Kanuni za Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa.

    Masuala hayo yanajumuisha :• Kama mtu ananyima

    taarifa kuweko na Bodi ya kushughulikia malalamiko;

    • Kanuni za ATI lazima zieleze wazi gharama za taarifa ni kwa ajili ya kutoa nakala au kutengeneza CD/DVD;

    • Sheria ya ATI haisemi nini kitatokea kwa wataka taarifa kama hawataridhika;

    • Sheria hiyo pia iruhusu watu wasio raia kupewa taarifa ili mradi hazitotumiwa vibaya.

    Pande hizo mbili zilikubaliana kufanyakazi pamoja kuhakikisha kuwa semina za uhamasishaji zinafanyika nchi nzima kuwafanya maofisa wa habari wa serikali kufahamu sheria ya ATI.

    Wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mei 3, 2018 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Dk. Harrison Mwakyembe aliuambia ujumbe wa MCT kuwa serikali inakaribisha mazungumzo katika masuala ambayo vyombo vya habari inayaona si mazuri kwao.

    Waziri pia alisema kwamba ingawa kuchukua hatua kama kufungua mashtaka ni haki ya kila mmoja, lakini mazungumzo kati ya serikali na wadau ni mazuri zaidi.

    Kwa upande wa Zanzibar , Baraza na washirika walikutana na maofisa wa serikali waandamizi na mazungumzo yao yalijikita zaidi katika suala la kuifuta sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu Namba 5 ya mwaka 1988.

    Msimamo wa Baraza ni kuendelea kufanyakazi na Wizara ya Habari Visiwani kuchangia kufanikisha kupatikana kwa sheria hiyo mpya.

    Inatoka Ukurasa wa 11

    Kibano cha kupindukia kwa vyombo vya habari

  • 15

    Maoni

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Na Saidi Nguba.

    Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetoa chapisho jingine kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini. Chapisho hili la sasa ni taarifa kuhusu “Hali ya Vyombo vya Habari Tanzania 2017 – 2018”. Ni kama ada, kila mwaka Baraza hutoa taarifa hiyo kuibua mambo muhimu yaliyotokea kuhusu vyombo vya habari, kuwataka wahusika waingilie kati pindi itakapo-hitajika kufanya hivyo na muda utakapowadia na kutoa mapendekezo ya nini cha kufanya. Ripoti hiyo imeandaliwa na washauri watatu - Dkt. Joyce Bazira, ambaye ni mkufunzi na mtafiti katika tas-nia ya habari; mwandishi wa habari mkongwe, Henry Muhanika na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Dkt. Ali Uki. Ripoti hiyo imetoa mapendekezo manne kwa vyombo vya habari, mashirika ya kijamii na wanaharakati wa haki za binadamu kuwa, kwanza, lazima kuendelea na kampeni ya kuzifanyia mabadiliko sheria zinazo-onekana kuwa ni kandamizi zinazohusu vyombo vya habari; pili, kupinga sheria na kanuni zinazo-bana mawasiliano ya kimtandao; tatu, kuandaa mwongozo wa maadili ya mawasiliano ya kimtan-dao na mwisho kudai mafunzo yatakayowaweze-sha wanahabari na vyombo vyao kuwa huru.

    Kwa mara nyingine tena ni vilio tu kutokana na sheria na kanuni kandamaizi kwa vyombo vya habari, kutozingatiwa kwa haki za binadamu, mahitaji ya mafunzo na uhuru kwa wanahabari. Ripoti nyingine iliyozinduliwa mapema mwaka huu na ambayo nayo iliangalia mwenendo wa vyombo vya habari, iliyoandaliwa kwa niaba ya Baraza la Habari ilibainisha kuwa habari nyingi zinazotolewa na vyombo vya habari, labda ni kwa sababu ya woga, ni za matukio rasmi yaliyokwishapangwa na yanayojulikana na siyo habari zinazoibuliwa na wanahabari wenyewe. Ripoti hiyo kuhusu “Ubora wa Maudhui ya Vyombo vya Habari Tanzania kwa mwaka 2018” ilitayarishwa baada ya utafiti na Bw. Christoph Spurk wa Kampuni ya Ushauri kwa Vyombo vya Habari ya Spurk Ltd. ya Berne Uswisi na Bw. Abdallah Katunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ripoti hiyo ilibainisha kudorora kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini katika miaka mitatu iliyopita ikikariri viwango vya uhuru wa habari vinavyotambulika kimataifa vinavyochapishwa na taasisi huru iitwayo Reporters Without Borders. Tanzania imeanguka kwa nafasi 22 mwaka jana na kuwa nchi ya 93, kati ya nchi 180 kutoka nafasi ya juu kidogo ya 71,

    mwaka 2016.Kwa hiyo maswali muhimu ya kujiuliza ni je,

    kwa nini wanahabari wanakuwa waoga? Kwa nini zinatungwa sheria zinazoonekana kuwa kandamizi na kuvibana vyombo vya habari? Nini kinachokusudiwa kupatikana? Kabla ya kuyajibu maswali hayo inafaa kuichambua zaidi ripoti hii mpya kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini.

    Mambo muhimu yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ni katika maeneo ya sheria na udhibiti; hali ilivyo kuhusu magazeti, vyombo vya elektroniki kama redio na televisheni na mitandao ya kijamii kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani. Ripoti hiyo imeelezea maoni ya wadau wa vyombo vya habari kuwa sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari iliyopitishwa hivi karibuni yenye vipengele vya kutoa leseni kwa wanahabari na madaraka makubwa aliyopewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya kusimamisha uchapishaji wa magazeti au kuyafungia kabisa inatishia uhuru wa wanahabari binafsi, vyombo vya habari vyenyewe na tasnia yote ya habari kwa jumla.

    Ripoti pia imeeleza kuwa kipindi ambacho utafiti umefanywa kimeshuhudia mwelekeo mpya wa “kuingiza siasa katika ajenda ya maendeleo” kwamba wanahabari au wadau wengine wanapopaza sauti kuhusu utendaji mbovu wa watendaji wa serikali basi wanaonekana kuwa ni “maadui” na “wanapinga maendeleo ya taifa”. Kuhusu vyombo vya kielektroni ripoti imesema, vyombo hivyo vimekabiliwa na matukio ya vitisho na kutoa mfano wa uvamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiambatana na askari polisi waliokuwa na silaha kuingia kwa nguvu ndani ya kituo cha televisheni cha Clouds, ikisemekana kuwa alitaka kulazimisha kituo hicho kionyeshe video fulani. “Hali ya vyombo vya habari nchini Tanzania katika mwaka 2017/18, hasa upande wa Bara,” ripoti imesema “kamwe haitii matumaini”.

    Imemaliza kwa kusema vyombo vya habari “kama ni magazeti, utangazaji au mitandao vimeathirika sana ikiwa ni pamoja na kufanyakazi katika mazingira magumu ya kisiasa yakitawaliwa na sheria kandamizi. Adhabu kama vile kusimamisha kuchapwa au kufungiwa magazeti, kufungwa kwa vituo vya utangazaji ambako kumeonekana dhahiri kuwa ni ukiukwaji wa haki, pamoja na matumizi ya nguvu, vitisho, kufunguliwa mashitaka na kuwabugudhi na kuwasumbua wanahabari ni miongoni mwa madhila yaliyoshuhudiwa katika miaka miwili iliyopita.” Hata hivyo ripoti hiyo ya hali ya vyombo

    vya habari nchini Tanzania imeelezea pia mwelekeo mzuri kama vile utaratibu ulioanzishwa na serikali wa kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ya kutumbukiza mambo machafu katika mitandao hiyo. Kwa upande wa Visiwani Zanzibar, ripoti hiyo pia imeelezea mwelekeo mzuri ulioleta kuchipuka kwa wingi televisheni za mtandaoni na kusema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika jitihada za kuupasha umma habari na taarifa mbalimbali.

    Imeelezwa nyakati mbalimbali kuwa uhuru wa habari maana yake siyo kuongezeka kwa idadi ya machapisho au vyombo vya habari, bali ni namna gani wanahabari wanafanya kazi zao kwa kuzingatia kanuni kuwa mawasiliano na kutoa maoni ni haki inayotakiwa ipatikane kwa uhuru. Uhuru huo hautakiwi kuingiliwaingiliwa. Na cha kustaajabisha ni kwamba wakati Rais Magufuli mwenyewe amekuwa mara kwa mara akivipongeza vyombo vya habari kwa kufanyakazi kwa ufanisi na kutoa mchango mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo kwa kuwapasha watu habari kwa usahihi bila ya upendeleo na kusaidia kuibua matendo maovu, baadhi ya wasaidizi wake wengi na baadhi ya watendaji serikaini hawaonekani kama wanakwenda pamoja na Rais na kutekeleza ajenda yake. Waziri wa Habari, Utangazaji, Sanaa na Michezo, Dkt. Harisson Mwakyembe, naye amewahi kukaririwa akisema yuko tayari kukaa na wadau wa vyombo vya habari kuangalia nini kinaweza kufanyika kuleta mabadiliko au marekebisho ya taratibu au kanuni zinazoonekana hazieleweki vizuri, zinaleta karaha au ni za uonevu. Ila bado hatua madhubuti hazijaonekana kuelekea huko. Kinachoonekana sasa ni kwamba wakati sheria ni hizo hizo zinazotumika huku baadhi ya vyombo vya habari vikiadhibiwa, vingine vinavyojinasibu kuwa ni wanaharakati, vinavyotoa taarifa zenye nia mbaya na kuleta chuki, vinaachwa tu. Haijapata kutokea. Hapakuwepo na hali ya namna hii hata wakati nchi ikiwa changa mara baada ya uhuru wala katika kipindi kabla ya ulegezaji wa masharti ya siasa na uchumi katika miaka ya mwanzo ya 1990. Haieleweki kwa nini mambo haya yanatokea sasa hivi. Watafiti wanasema wakati katiba ya Tanzania inataka kuwepo kwa uhuru wa kutoa mawazo, haihakikishi moja kwa moja kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari. Sheria kadhaa zilizopo zinavibana vyombo vya habari kwa misingi ya kuzingatia “usalama wa taifa” na “maslahi ya umma”. Lakini haki ya wananchi au vyombo vya habari kutoa, kupata, kujadili na kutoa mawazo na maoni bila ya hofu ya kushitakiwa ni kitu ambacho kila mtu angekipenda – raia wa kawaida na hata wale walio madarakani. Hata Rais Magufuli mwenyewe huwa anapenda sana kutoa maoni yake na kufanya hata utani, dhihaka na masihara kwenye mikutano ya hadhara na asingependa abanwe kufanya hivyo. Huwa anafurahia sana kuwa huru kuyasema anayoyataka kuyasema, mara kwa mara.

    Mwandishi ni Mwanahabari na Mhariri mkongwe. Anapatikana kupitia Barua-pepe: [email protected] Simu: 0754-388418.

    Ni vilio tu vya kudai Uhuru na kupinga Sheria kandamizi

    TAARIFA YA HALI YA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA MWAKA 2017 – 2018:

  • 16

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Kitabu

    Kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa waandishi wa habari na wahariri kukisoma ili kuelewa takwimu na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi katika habari

  • 17

    Uchambuzi

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    Na Gervas Moshiro

    Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe alisema kuwa jukumu lake kubwa mwaka huu ni kuanzisha vyombo vya usimamizi vilivyoainishwa kwenye sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari, 2016. Sehemu ya III ya sheria hiyo inaanzisha Bodi ya Ithibati kushu-ghulikia majukumu mawili: Ithibati ya Waandishi wa Habari na Mfuko wa Mafunzo ya Vyombo vya Habari. Sehemu ya IV ya sheria hiyo in-aanzisha Baraza Huru la Vyombo vya Habari. Waziri Mwakyembe kwa hiyo ana vyombo vitatu vya kuanzisha : Bodi ya Ithibati, Mfuko wa Mafunzo na Baraza Huru la Habari.

    Toka kupitishwa kwake, sheria hiyo imekuwa inapingwa na wanahabari, sio kwa kuwa haitakiwi ila ni kwamba mamlaka anazotaka kuanzisha Waziri Mwakyembe zitaongeza maumivu zaidi kwa wanahabari. Tayari kuna Idara ya Habari inayovibana vyombo hivyo kwa leseni na ithibati ya watendaji, mamlaka ya Mawasiliano nayo inafanya hayo hayo kwa vyombo vya utangazaji na vya mtandaoni. Makali hayo yanazidishwa na vifungu vingine vya sheria mbalimbali zinazohusiana na utendaji wa vyombo vya habari nchini. Yafuatayo ni maoni yangu kuhusu mjadala wa uanzishwaji mamlaka hizo. Sheria nzuri huongozwa na nia ya sera ya sekta au kama inavyofahamika, dira. Baada ya sheria, kanuni, miongozo na jitihada za utawala , ni nini kitakachotokea jamii husika? Katika sura ya utangulizi ya Sera ya Habari na Utangazaji iliyochapishwa na Idara ya Habari mwaka 2003, imeelezwa kuwa dira ya sera hiyo ni «kuwepo kwa vyombo vingi vya habari, vinavyomilikiwa na umma na sekta binafsi, na vilivyo imara na anuwai, na vinavyozingatia maadili ya taaluma na ya jamii, ili viweze kuchangia katika kufanikisha

    malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

    Malengo na madhumuni ya sera yanaelezwa kuwa ni “kuweka mazingira yanayowezesha ukuaji wa sekta ya habari na utangazaji nchini, kuhamasisha vyombo vya habari kutoa huduma kwa kuzingatia maadili ya taaluma na ya jamii, kuhamasisha wanahabari kuanzisha na kuendeleza chombo cha kusimamia maadili ya taaluma ya habari na utangazaji na kuweka utaratibu wa kujenga uwezo endelevu katika sekta”.

    Sera hiyo haijawahi kupitiwa upya licha ya mabadiliko makubwa na ya haraka ya teknolojia ya mawasiliano ya habari. Uzuri wa habari ni kwamba licha ya teknolojia ya vifaa na mitambo kubadilika, kiini cha habari hakidhuriki. Pengine hii ndiyo imefanya watu wasijali sana kutopitiwa upya kwa sera hiyo, ili mradi wananchi wanapata habari kwa njia zozote zile.

    Je, anachoenda kuanzisha Dk. Mwakyembe, kipo kwenye sera? Ibara ya pili ya dira ya sera inasema :

    “Aidha dira ya sera inahimiza kuwepo kwa taasisi za mafunzo, utafiti na ushauri wa kitaalam kwa lengo la kuboresha tasnia ya habari na zinazochangia kukuza sekta ya filamu na video kwa minajili ya kuibua na kukuza vipaji na kulinda historia na utamaduni wa Tanzania”.

    Sera hiyo ilionekana kuwa ya kimaendeleo sana kwa wadau na kama mapendekezo yake yakitekelezwa ipasavyo, basi haki zilizotajwa kwenye katiba ya nchi Kifungu cha 18 zitakuwa zimetekelezwa, hivyo kuwa na uhuru wa habari.

    Kwa sisi wengine tuliokuwa tunahanikiza uundwaji wa sera hiyo, tulichokuwa tunajali zaidi ni kwa nyanja ya habari na utangazaji kuhudumia wananchi kulingana na matakwa yao inavyotaka katiba ya nchi na matamko mengine, hasa lile la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.

    Ilichukuwa Serikali miaka 15

    kuja na sheria zilizopendekezwa - mwaka 2015 – Sheria ya Kupata Habari 2015 na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari 2016. Miaka miwili baadaye, ndio sasa wananchi wanasikia kuanzishwa kwa taasisi zitakazosimamia utoaji wa huduma za sekta hiyo.

    Sitaona ajabu kama baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vikawa vimepitwa na wakati kwa sababu mazingira kiteknolojia, kiuchumi na kimtazamo yamebadilika kiasi kwamba inahitajika mapendekezo mengine kuendana na hali ya sasa. Mimi nadhani tunahitaji mkabala mwingine ili wananchi wanufaike na taasisi zinazokusudiwa kuanzishwa.

    Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ni kati ya taasisi ambazo wanahabari wanasema kuwa sio ya lazima kwa kuwa kazi zake zimekuwa kwa miaka mingi zikifanywa na Idara ya Habari. Kwa hakika Kitengo kidogo tu kingetosha na sio bodi kubwa yenye urasimu na mbwembwe zote za mishahara na marupurupu makubwa kama tunavyoona kwenye bodi za sekta nyingine.Tayari sheria inataja kuwa atakuweko Mkurugenzi mkuu, kwa maana kuwa chini yake watakuweko wakurugenzi wengine lukuki.

    Kwa wakati fulani wa utawala wa Baba wa Taifa, mashirika na bodi nyingi zilitawala utoaji huduma kwa wananchi. Zilikuja kuwa mzigo mkubwa miaka ya tisini na ikabidi zivunjwe. Sasa naona zinarudi tena kwa majina ya mamlaka, bodi na mengine. Huu ni mkumbo usiohitajika sekta ya habari. Sio kila kilichoandikwa kwenye sheria lazima kitekelezwe kilivyo, hasa kama imegunduliwa kuwa hakina manufaa yaliyokusudiwa. Isitotoshe sheria yoyote yaweza kubadilishwa kifungu chochote au hata kufutwa wakati wowote kama kuna haja ya kufanya hivyo. Serikali yaweza kuwa na sababu zake za kuanzisha bodi hiyo lakini binafsi nadhani ni mzigo kiuchumi hasa wakati huu tunapohitaji kujenga miundombinu ya kukwamua nchi.

    Yawezekana Waziri Mwakyembe hana namna kwani ameikuta sheria imekwisha tungwa na yahitaji utekelezaji. Hata hivyo bado anao uwezo wa kuomba ushauri wa weledi na wajuzi wa taaluma wa namna ya maslahi zaidi ya kuanzisha vyombo vilivyotajwa. Ana haki pia kisheria kupendekeza mabadiliko ya sheria hiyo ili iendane

    Mamlaka za udhibiti zitazika uhuru wa habari

    Endelea Ukurasa wa 18

  • Uchambuzi

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    18

    na maslahi mapana ya pande zote, hasa ya wananchi.

    Mkurugenzi wa Habari hutoa leseni kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa ama na serikali, watu binafsi au jamii. Wanahabari (waandishi wa habari) ni watu wenye kujitegemea wanaotumikia vyombo hivyo kutokana na ujuzi kikazi. Maoni yangu ni kwamba serikali haitakiwi iwe na uhusiano wa moja kwa moja na mwanahabari, bali ipitie kwa chombo cha ajira au cha umoja wao kitaaluma kwani ndio wanaowajibika kiutendaji.

    Uanaharakati wa kudai sheria mpya ulianza miaka ya 80 ilipoonekana kuwa sheria ya magazeti ya 1976 haiendani na wakati na ni kandamizi kitaaluma. Ushajiishaji uliongezeka miaka ya 90 na matokeo ya awali yakawa kupata Baraza la Habari linalojitegemea, kufutwa kwa sheria ya uhodhi ya shirika la habari – SHIHATA na kuruhusiwa vyombo binafsi vya utangazaji. Wakati huo huo ongezeko la mahitaji ya watendaji likafanya vyuo vya elimu vilivyokuweko na vingine vipya kuanzisha mafunzo ya habari, na hii leo karibu kila chuo kikubwa nchini kinatoa mafunzo ya uandishi wa habari. Maoni yangu ni kwamba serikali isijihusishe na ufundishaji wa waandishi wa habari, bali iviachie vyuo vilivyopo kufanya kazi hiyo kwa utaratibu utakaowafaa wanahabari wenyewe.

    Tayari kuna watu wengi waliofuzu taaluma za habari wasiokuwa na kazi. Ni juu ya vyuo hivyo kuthibitisha kuwa vinatoa wataalam wenye ujuzi sawa sawa kwani ushindani ni mkubwa katika vyuo hivyo. Serikali isijihusishe kama ilivyotajwa kwenye Kifungu 13 cha sheria hiyo, bali tuachie nguvu za soko kurekebisha mwenendo huo.

    Tatizo, kwa sasa, sio mafunzo ya waandishi wa habari. Ilikuwa hivyo miaka iliyopita. Wako wanahabari wengi wenye mafunzo ya ngazi za juu kabisa na wako barabarani hawana kazi. Tayari, kwa kupitia uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), mtaala wa mafunzo ya kiustadi umeanza kutumika kwenye vyuo vya uandishi wa habari. Juhudi za MCT zinajumuisha pia mafunzo ngazi za shahada.

    Hata hivyo, kama ilivyo kwa

    taaluma zote, elimu haina mwisho. Mabadiliko ya teknolojia, uvumbuzi, mikakati mipya, mabadiliko ya vionjo, maudhui mahususi na mengine – vyote vinahitaji kufundishwa upya ili kwenda na mahitaji ya wakati. Hapa ndipo inapohitajika mshikamano kati ya vyuo vya mafunzo na bodi za kitaaluma zinazosimamia maendelo ya taaluma.

    Tangu MCT ianzishwe miaka ya 1990 hadi leo na pia hadi hivi karibuni Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), jukumu lao kubwa limekuwa kutoa nafasi za mafunzo kwa wanahabari walio kazini kwa lengo la kuongeza maarifa na ujuzi kulingana na mahitaji ya chombo. Ni wanahabari wachache nchini watasema kuwa hawajafaidika na mafunzo hayo. TMF ilienda mbali zaidi kwa kuwezesha vyombo vya habari kuweza kujiendesha ili shughuli zao ziwe endelevu.

    Udhaifu mkubwa wa taasisi hizo mbili umekuwa ni ukosefu wa fedha kufanya shughuli zake ziwe endelevu. Je, itakuwa tofauti kwa chombo kinachokusudiwa kuanzishwa?

    Bodi ya Ithibati pia itaanzisha Mfuko wa Mafunzo wa Habari. Mfuko huu utatoa fedha kwa mafunzo kwa wanataaluma ya habari, kukuza programu za kuendeleza maudhui ya ndani ya nchi na kukuza na kuchangia utafiti na maendeleo katika nyanja za mawasiliano ya umma.

    Maeneo yatakayofadhiliwa na Mfuko nadhani ni muhimu sana, hasa msaada kwa watafiti, uga ambao unakosekana kwenye taaluma ya habari.

    Misaada, ruzuku na zawadi na wakati mwingine michango ya vyombo vya habari ndizo zilizokuwa njia kuu za mapato kwa MCT na TMF. Vyanzo hivi vinakauka mfadhili anapoamua kusitisha msaada kutokana na sababu mbalimbali. Njia hii ni ya shaka kubwa.

    Mfuko mpya utakaoanzishwa na sheria utakuwa na vyanzo hivyo pamoja na fedha kutoka mfuko wa serikali kupitia bungeni. Kwa kuwa hatuna mfano wa ni kiasi gani Hazina itatoa kwa mfuko huu, ninachoweza kutabiri kutokana na mwelekeo wa malipo kwa taasisi, ambapo hata mamlaka za serikali za

    mitaa zinalia ukosefu wa fedha, licha ya kugawiwa na Bunge, na pia mzigo mkubwa wa deni la taifa linalozidi kukua, ni kwamba vyombo vya habari vitakuwa wa mwisho kuonewa huruma na Serikali. Yawezekana nimekosea, kwani mara nyingine inategemea ushawishi wa kiongozi aliyeko juu ya sekta hiyo, ambaye ni Dk. Harrison Mwakyembe.

    Mwaka 1989 na 1990 tulikuwa na waziri wa Habari, Balozi Ahmed Hassan Diria (marehemu). Aliweza kushawishi serikali kuiweka sekta ya habari kwenye kundi la sekta muhimu za kipaumbele nchini. Habari ikawekwa chini ya Ofisi ya Rais. Kwa bahati mbaya mpangilio huo ulidumu kwa muda mfupi, lakini kwa waliokuweko wanakumbuka tofauti kubwa iliyojionesha kwenye sekta wakati ule ya heshima, hadhi na uchangamfu katika kushughulikia mipango ya habari. Ninafahamu kuwa suala la kupata rasilimali wakati mwingi hutegemea ushawishi wa kiongozi wa mahali.

    Taasisi nyingine itakayoanzishwa na sheria ni Baraza Huru la Habari. Maelezo yaliyo kwenye sheria yanaendana na muundo na kazi za baraza lililopo la wanahabari la MCT. Kuna tofauti ndogo hapa na pale lakini kazi zake zitakuwa sawa na zinazotekelezwa na MCT.

    Uanachama wa baraza jipya utakuwa ni wa kila mwanahabari aliye na ithibati. Hii ni njia mojawapo ya kupanua wigo wa vyanzo vya mapato kwa kuwa wako wengi na bila kujali vyombo wanavyohudumu.

    Kutokana na maelezo ya sheria, baraza linaonekana kuwa huru, jambo ambalo ni zuri. Itaendelea kuwa vizuri ikiwa tutahakikisa kuwa haliingiliwi na nguvu za kisiasa na kichumi. Baraza kwa hiyo lazima liwe na utawala wenye watu wanaoelewa vizuri maana ya dhima na nafasi yao katika jamii.

    Kinachosikitisha ni utengano unaoendelezwa kisheria kati ya wanahabari wa vyombo vya utangazaji na magazeti, kuwa baraza hilo litashughulikia malalamiko yahusuyo magazeti tu. Kwa nini wakati taaluma ya habari ni moja tu? Katika hili nadhani sheria inafanya jambo baya : ubaguzi, hata kama wale wengine

    Mamlaka za udhibiti zitazika uhuru wa habariInatoka Ukurasa wa 17

    Endelea Ukurasa wa 19

  • wanashughulikiwa na sheria tofauti. Maagizo ya sera ni kwamba iwepo sheria moja tu kwa wanahabari wote, kitu ambacho hakijatekelezwa.

    Ukamilishaji wa mamlaka hizo tatu za udhibiti utafanya tasnia kuminywa kiasi cha kuona kwamba kheri hali ya zamani ingerejea. Kwa nini matarajio hasi. Vyombo vya habari, pamoja na vya serikali au umma itabidi vijiendeshe kibiashara. Vitahitaji ada za usajili, leseni kila mwaka, ada za makazi, ada za kuhama, ada za kubadili chochote kwenye muundo wa chombo, kodi, ripoti za utendaji kila mwaka na mengine mengi ambayo hayaendani na usimamizi mwema wa taasisi kimataifa.

    Huo ndio utaratibu wetu, na hakuna anaoubishia ili mradi utozaji kodi uwe wa haki. Kulazimisha kodi na tozo nyingi kwenye utoaji wa huduma ni kushawishi wenye huduma kutafuta fedha kwa njia zisizo kawaida, la sivyo ikikosekana huduma hiyo itasitishwa. Kuendelea na huduma za habari itabidi mtumiaji alipe zaidi.

    Ninakaa Mbagala, eneo la Dar es Salaam ambalo si la watu wakwasi sana. Nilikuwa ninanunua gazeti kila siku siku za nyuma lakini sasa ni mara chache kwa wiki. Muuza magazeti analalamika kuwa hana wateja kwani wanalalamikia bei ya shilingi 1,000 kuwa ni kubwa mno.

    Watu wengi wamekimbilia mitandao ya kijamii kwa habari na mawasiliano mengine, lakini wasiwasi wangu ni kwamba huko tuendako mitandao itakuwa ghali sana kuitumia kama chombo cha habari. Sababu kubwa ni kwamba magazeti na vyombo vya utangazaji vitakapobanwa sana vitakimbilia kutumia mitandao na hii itahalalisha mamlaka kutoza mitandao hiyo kiasi cha kutosheleza uendeshaji wa vyombo hivyo – Bodi ya Ithibati, Mfuko wa Mafunzo na Baraza Huru.

    Demokrasia itadumu nchini na itafika wakati serikali itaona kuwa kuna manufaa katika kushauriana na tasnia ya habari na kuachia baadhi ya majukumu yanayowekwa kisheria yatekelezwe na tasnia yenyewe bila kuwa mzigo kwa serikali. Serikali ikipunguza tozo zake kwa vyombo hivyo, maana yake ni kwamba huduma za habari kwa mwananchi zitakuwa rahisi zaidi.

    Nadhani serikali inaelewa kwa nini wanahabari wanapinga baadhi ya vipengele vya sheria. Tasnia haioni mantiki ya kugharimia mamlaka ya udhibiti inayosaliti dhima ya msingi ya habari kama mtetezi wa wananchi. Hutarajii wanahabari kuihoji serikali ambayo ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kuhusu leseni, uandikishaji, msaada wa mafunzo na usuluhishi. Neno ‘suluhu’ halipo kabisa katika matini ya sheria hii, labda limechukuliwa kuwa ni neno dhaifu sana kwa ukali wa sheria, na badala yake yanatumika maneno kama “kushughulikia” na “kuamua” badala ya ‘kusuluhisha’ na ‘kupatanisha’. Hakuna upole wa kujuana hapa, ni ama u mkosaji au huna hatia. Vyombo hivi vimekaa kimahakama zaidi.

    Hofu ya wanahabari inaongezeka pale wanapofahamu kuwa maudhui ya kazi zao yanachunguzwa kutafuta ukiukaji wa maadili yaliyopitishwa na serikali. Kwa kuwa hata maadili yanakuwa ni sehemu ya sheria, basi ukiukaji wake unakuwa ni uvunjifu wa sheria na kuchukuliwa kuwa ni uhalifu wa kijinai.

    Hofu hizi hazistawishi utamaduni wa kitaaluma na hasa uhuru wa habari. Bila vyombo huru vya habari hakuna demokrasia. Katika kifungu cha 7(1) cha sheria ya huduma ya habari kimetaja wajibu wa chombo cha habari bila kutaja pia haki ya vyombo vya habari ya kukusanya na kupata habari kutoka vyanzo mbalimbali, uhuru wa kuchakata na kuhariri habari kulingana na maadili ya taaluma na uhuru wa kuchapisha na kutangaza habari.

    Kimsingi huu ndiyo haki inayong’ang’aniwa vipewe vyombo vya habari ambayo sasa imenyimywa na kusiginywa na baadhi ya vyombo vya serikali. Haki hizi hazitajwi mahali popote katika sheria, hivyo kuifanya iwe na maslahi ya upande mmoja na kuacha watoa huduma ambao ndio wanaotegemewa na wananchi kwa huduma ya habari.

    Vyombo vya habari vinahitaji kukaa na serikali na kuainisha nini maana ya haki ya habari kama inavyotaja katiba ya nchi. Kwa hakika kuna mengi ya kujadiliana baada ya mamlaka za udhibiti kuundwa kama nia ya sheria na dira ya sera yatahitaji kutimia.

    Nina hakika Waziri Mwakyembe ana mashinikizo makubwa ya

    kutaka vyombo vya habari vidhibitiwe, lakini nina hakika watu hao hao wanamtegemea kwa ushauri na uongozi kwani wao si wataalam wa habari. Mwakyembe anahitaji kuwashauri washinde mioyo ya hofu na chuki kwa wanahabari wanapoandika au kutangaza jambo ambalo hawalipendi kama serikali.

    Ama hakika kuna mengi ya kujifunza kutokana na Waraka aliotoa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa anatangaza kutaifisha gazeti la The Standard mwaka 1970 jijini Dar es Salaam. Ninukuu baadhi ya aya za waraka huo uliotolewa kwa kiingereza. Tafsiri hii ni yangu na sio rasmi.

    “The Standard litakuwa linaunga mkono sera za Serikali ya Tanzania, lakini litakuwa huru kujiunga kwenye mijadala ya kukubali au kukataa jambo lolote litakalokuwa limependekezwa kwa wananchi, ama na Serikali, TANU au chombo kingine.

    Litakuwa huru kuanzisha mjadala wowote wenye kuleta maendeleo ya kijamaa na jamii ya kidemokrasia nchini. Litakuwa likiongozwa na kanuni ya kuwa mijadala huru ni kitu muhimu kwa ujamaa wa kweli, na litajitahidi kushawishi viwango vya hali ya juu vya madadiliano ya kijamaa.

    “Standard mpya litakuwa huru kukosoa kitendo chochote cha viongozi binafsi wa TANU au Serikali na kutangaza mapungufu yoyote katika jamii yaliyosababishwa na mtu yeyote. Litakuwa huru kukosoa utekelezaji wa sera zilizokubaliwa, ama kwa jitihada zake au kufuatia lawama au mapendekezo kutoka kwa wasomaji wake”.

    Hivyo ndivyo alivyokuwa Mwalimu Nyerere na falsafa yake kuhusu vyombo vya habari. Kama vyombo vyetu vya habari vingeachiwa kutekeleza japo nusu ya falsafa ya Waraka huo kuendana na mazingira ya sasa, tungekuwa na uhakika kuwa tunafuata nyayo za baba wa Taifa.

    Kwa sasa tusikitike tu kuwa vyombo vya usimamizi vinavyokusudiwa kuanzishwa bila kuzingatia mapendekezo ya wadau ndio utaokuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la uhuru wa habari nchini.

    Mamlaka za udhibiti zitazika uhuru wa habariInatoka Ukurasa wa 18

    Uchambuzi

    Toleo la 144, Agosti, 2019

    19

  • Na Mwandishi wa Barazani

    Kesi dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mwanasheria Mkuu ya kuli-funga gazeti la Raia Mwema kwa siku ti-sini imeruhusiwa kusikilizwa.

    Jaji Kiongozi Dk. Eliezer M. Feleshi ametupilia mbali pingamizi nne zilizowasilishwa na walalamikiwa kuzuia kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba 23, 2017.

    Kufungiwa kwa gazeti hilo kuliamriwa kuanze siku ya tarehe 29, Septemba 2017.

    Walalamikaji walipinga amri hiyo kulifungia gazeti hilo kwamba ilikuwa kinyume cha sheria na kwamba Waziri hana mamlaka hayo.

    Pingamizi nne zilizowasilishwa na walalamikiwa ni kama ifuavyo:-:

    Ombi limepitwa vibaya na wakatiKiapo cha maombi hayo kina

    mapungufu kupitilizaTaarifa ya maombi hayo imejumuisha

    uongo na inabidi idhihirishwe.Ombi hilo halifai na halitoshelezi

    matakwa ya mapitio ya kisheria.Katika uamuzi wake alioutoa Julai 26, 2019

    mbele ya Dk. Rugemeleza Nshala,

    wakili wa Raia Mwema na Bi. Janeth Makondoo, Wakili Mwandamizi wa Serikali kwa niaba ya walalamikiwa, Jaji Feleshi alisema pingamizi zote nne hazina mashiko kisheria na hivyo

    zinatupwa.

    Pingamizi hizo zilitolewa na walalamikiwa Mei 16 na 24, 2019.

    Mawakili wa pande zote waliwasilisha hoja zao kwa maandishi.

    Hoja za walalamikiwa zilijengwa na Wakili wa Serikali Erigh Stephen Mugisha na za walalamikjai zilijengwa na Wakili Rugemeleza Nshala.

    Baada ya kuzingatia hoja zote kuhusu pingamizi la kwanza kuhusu suala la muda, mahakama imelitupa kwa maelezo kuwa badala yake lingejenga hoja za kisheria.

    Kuhusu pingamizi la pili, Mwanasheria wa serikali alidai kuwa kiapo cha walalamikaji kilikuwa na taarifa za uongo au zisizo kweli, dai ambalo lilipingwa na wakili wa walalamikaji ambaye alisema kuwa kiapo hicho kina ukweli tu ingawa alikiri kuwepo mkanganyiko kiasi.

    Mahakama ilisema kuwa madai ya uongo ni masuala yanayohitaji kuthibitishwa na mpaka fursa hiyo ikitolewa, hakuna haki itatendeka.

    Kwa kuzingatia ukweli huo, pingamizi la pili nalo linakataliwa.

    Kwa pingamizi la tatu, Wakili wa serikali alidai kuwa ombi halikuwa na vithibitisho na hivyo kutoaminika kisheria, wakili wa walalamikaji alisema wakili wa serikali hakuonyesha wazi aya zisizokuwa na uthibitisho na kuiomba Mahakama kulikataa pingamizi hilo.

    Katika uamuzi wake Mahakama ilieleza kuwa sehemu zote zilithibitishwa akitoa mfano:”Uthibitisho – Mimi, Boas Moses, naapa kwamba yote yaliyomo kwenye aya za 1,2,3,6,7,8,9,11 na 12 kwa ufahamu wangu ukiacha aya 4 na 5 ambazo nimeambiwa na Bw. Godfrey Dilunga na yaliyomo kwenye kiapo ni maelezo ya kweli. ”

    Mahakama imesema haioni pointi yoyote jinsi uthibitisho huo unaweza kuwa dhaifu kama Wakili wa Serikali alivyosema na hivyo inaona hakuna msingi wa kuwepo pingamizi.Mahakama pia imeona pingamizi la nne halina mashiko kisheria pia. Pingamizi hilo lilidai kuwa ombi la mlalamikaji ni dhaifu kwa kukosa vigezo vinavyotakiwa kuhitaji mapitio ya kisheria.

    Hata hivyo Mahakama ilikataa ombi la walalamikaji la kuondolewa kwa amri ya kufungiwa kwa siku 90 mpaka shauri hilo limalizike kwa kuwa siku hizo zilishapita Desemba 2017 na kwamba mlalamikaji hakuwa ametoa ombi kuhusu amri hiyo na hata hivyo amri hiyo haitakuwa na maana.

    Pingamizi la awali la walalamikiwa ambalo lilidai kuwa shauri hilo lilipitwa na wakati lilikataliwa na Jaji Zainabu G. Muruke ambaye aliamuru shauri hili kusikilizwa Februari 6, 2019.

    Hata hivyo amehamishiwa kituo kingine na shauri hilo likakabidhiwa kwa Jaji Kiongozi , Feleshi.Wakili Rugemeleza Nshala

    Jaji Kiongozi Eliezer Feleshi

    20

    Habari

    Jarida la Baraza la Habari Tanzania

    Raia Mwema waruhusiwa kupinga kufungiwa