52
Wananchi Wanasemaje? Insha na Michoro ya Washindi wa Shindano Lililoandaliwa na PCB na HakiElimu Rushwa katika Elimu

Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Wananchi Wanasemaje?

Insha na Michoro ya Washindi wa ShindanoLililoandaliwa na PCB na HakiElimu

Rushwa katika Elimu

Page 2: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Shukrani

Shukrani za dhati kwa wote waliotusaidia katika kutayarisha kijitabu hiki:

• Washiriki wote wa shindano la “Unafanya Nini Kupambana na Rushwa katika Elimu?”• Sabas Masawe, Consolata Mushi na Bashiru Ally kwa kutathmini na kupima insha na michoro yote

katika awamu ya kwanza• Dominick Mushi, Merchant Mtandika, Patrick Ngowi na Nsa Kaisi kwa kutathmini na kuchagua

washindi 17 na waliofanya vizuri 110• Wafanyakazi wa PCB-Makao Makuu: Lillian Mashaka, Mary Mosha, Stephen Mbelle na Jonathan

Semiti kwa mchango wao wa mawazo

WaandishiGodfrey Telli, Mary Nsemwa na Lilian R. Kallaghe

MhaririRakesh Rajani

Picha ya JaladaSteven Kipili

Mchapishaji© HakiElimu 2004

SLP 79401Dar es Salaam, TanzaniaSimu: (255 22) 2151852 au 3Faksi: (255 22) 2152449Barua pepe: [email protected]: www.hakielimu.org

Kwa kushirikiana na:Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB)SLP 4865Dar es Salaam, TanzaniaSimu: (255 22) 2150043-6Faksi: (255 22) 2150047Barua pepe: [email protected]: www.tanzania.go.tz/pcb

Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya kijitabu hiki kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwakufanya ni kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwa na kutuma nakala mbili kwa HakiElimu.

ISBN 9987- 8943-7-2

Page 3: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Yaliyomo

Dibaji (Joseph Sinde Warioba)

Utangulizi ……………………………………………………….………………………........... i

Maoni ya Washiriki………………………………………….…………………………............. ii

Insha na Michoro ya Washindi 17…………………………………………….………............ 1

Mchakato wa Kupata Washindi……………………………….………………………............. 40

Orodha ya Washindi……………………………………….…………………………............... 41

Page 4: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Dibaji

Page 5: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Utangulizi

Rushwa ni tatizo katika jamii yetu linalomgusa kila mtu. Wakati tulipopata uhuru, Mwalimu Nyererealitangaza maadui wakubwa watatu: Ujinga, Umaskini na Maradhi. Rais Mkapa baadaye naye aliongezaadui wa nne: Ukosefu wa Mitaji. Leo hapa wananchi wanatuambia kuna adui mwingine mkubwa zaidi:Rushwa.

Hayo ni maoni ya wananchi takribani 3,000 walioitikia shindano la “Rushwa katika Elimu.” Shindanohilo lilizinduliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) na HakiElimu mwezi Novemba,2003. Mada ya shindano ilikuwa ni “Unafanya Nini Kupambana na Rushwa katika Elimu?”

Shindano lililenga katika kujibu maswali mawili: “Ni aina gani za rushwa zinazojitokeza zaidi katikaelimu?” na “Ni njia gani za uhakika zinazoweza kutumika kupambana na rushwa katika elimu?”

Kijitabu hiki kimechapisha insha na picha zilizoandaliwa na washindi 17. Mapendekezo yao hayatakuwana maana kama tusipoyajadili na kuyafanyia kazi katika maeneo yetu.

Wananchi wanashauku kubwa ya kupambana na rushwa. HakiElimu na PCB tumechapisha kijitabu hikikuwapa wananchi taarifa na fursa ya kuchangia katika mapambano dhidi ya rushwa. Tutajitahidikukisambaza sehemu nyingi kwa wanajamii na viongozi wao. Kwa kufanya hivyo tunaamini shindanohili litakuwa limetoa mchango wenye maana katika jamii.

Shindano hili limetufundisha mambo mengi muhimu. Jambo la kwanza ni kwamba pamoja na fikratofauti za baadhi ya watu, ni kwamba rushwa imeota mizizi na kusambaa katika elimu nchi nzima.Imechukua sura nyingi, ambazo baadhi zimeelezewa katika insha na michoro katika kijitabu hiki.

Tunaweza kuchimbia vichwa vyetu mchangani, kama mbuni anayejaribu kukwepa ukweli. Amatunaweza kusikiliza kwa makini, kujifunza na kuchukua hatua.

Michango hii ya mawazo pia ni chanzo cha matumaini na matarajio mema. Wananchi hawajakatatamaa. Wanaamini kwamba bado kuna nafasi nzuri ya kufanya mambo mengi na kuitokomeza rushwa.Wametoa mawazo mengi ya jinsi ya kufanya hivyo. Sasa umefika wakati wa kutenda!

Viongozi wanatakiwa kuongoza na kuonyesha kuwa wao wenyewe ni wasafi na wanajali kupambana narushwa. Wana nia ya dhati na wako makini kufanya hivyo kwa vitendo.

Wananchi nao wana wajibu wa kuwa wasafi. Wakatae kuburuzwa na kuingizwa katika rushwa.Wawaitikie viongozi wao wanapowataka kupambana na rushwa. Wawe pia tayari kuwawajibishaviongozi wao. Ni kweli kwamba, kwa pamoja twaweza kuleta mabadiliko!

Wewe ni sehemu ya jawabu. Unaweza kufanya mambo mengi kuleta mabadiliko. Soma kijitabu hiki.Kijadili na rafiki yako, jirani yako au mfanyakazi mwenzako. Fikiria rushwa iliyopo katika jamii yako nanini kinaweza kufanyika juu yake. Halafu tenda. Nenda kaongee na watu wanaohusika. Wasiliana naPCB katika wilaya yako au waandikie PCB makao makuu, SLP 4865 Dar es Salaam. Waandikie viongoziwako. Andika barua kwa wahariri magazetini. Shiriki katika mikutano ya serikali za mitaa, misikitini,makanisani na vilabu vya michezo.

Kumbuka rushwa itakwisha ikiwa watu – kama wewe – watasimama na kusema “sasa basi nitafanyakitu leo kuiondoa.”

iRushwa katika Elimu

Page 6: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

ii Rushwa katika Elimu

Maoni ya Washiriki

Aina za Rushwa

Washiriki wote walionyesha kukerwa na rushwa katika elimu. Walionyesha hamu kubwa ya kuona elimuikiendeshwa kwa uadilifu bila rushwa.

Waliainisha aina nyingi za rushwa zinazojitokeza katika elimu. Aina tano kuu ni:• Rushwa ya ngono• Rushwa ya fedha na zawadi• Wanafunzi kufanyishwa kazi kwa walimu wao• Kutumia madaraka vibaya• Undugu na upendeleo

“Shida ni msichana yatima mwenye umri wa miaka 14 tu. Amekaa chini ya mti, amejiinamia,analia. Machozi yanazidi kulowanisha shati lake la shule. Ameshikilia mfuko wake wamadaftari. Ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza na amefukuzwa shule kwa sababu ya kupataujauzito. Hana hakika ni mwalimu yupi kati ya walimu watatu aliofanya nao mapenzi iliwamsaidie kufaulu mtihani ndiye aliyemsababishia mimba hiyo… Shida ni mmoja kati yawanafunzi wengi wanaoathirika kwa kukatisha masomo kutokana na kushamiri kwa rushwa yamapenzi…” (Beatus A. Mwendwa, Mwanza)

1. Rushwa ya ngono imetajwa na takriban washiriki wote. Washiriki wanasema ngono inajitokeza zaidibaina ya walimu wa kiume na wanafunzi wa kike. Wapo washiriki wachache walioonyesha kwambarushwa ya ngono pia inatokea baina ya walimu wa kiume na wazazi wa kike. Hali hii inasikitisha kwasababu, mara kadhaa wazazi wa kike wanafanya hivyo ili kuwanusuru watoto wao wa kike.

Wapo washiriki walioonyesha kwamba rushwa ya ngono inafanyika baina ya walimu wa kike na viongoziwa elimu ngazi ya kata, wilaya au juu zaidi. Lengo likiwa ni kupata upendeleo wa kupandishwa cheo,kuzuia uhamisho, kuokoa ajira baada ya kufanya makosa, nk.

“Rushwa ya mapenzi hufanyika kati ya walimu na wanafunzi. Mapenzi hupewa mwalimu ilinaye atoe siri za mitihani hususan majibu ya mitihani. Pia upendeleo wa maksi nyingizisizofanyiwa kazi hupewa yule mpenzi wa mwalimu husika.” (Redempta B. Minga, Mbeya)

2. Aina ya pili ya rushwa ni rushwa ya fedha na zawadi. Aina hii ya rushwa imezoeleka hadi kuonekana kamani jambo lililokubalika katika jamii. Rushwa hii inahusisha kuuza na kununua nafasi za wanafunziwaliofaulu mitihani na kushindwa kuendelea na masoma ya juu. Rushwa ya aina hii imejitokeza piakatika kuvujisha mitihani, uandikishwaji wa wanafunzi shuleni na kujipatia vyeti vya kugushi.

“Sehemu za mijini wakati wa uandikishwaji shule walimu wakuu husema nafasi zimejaa ilimwombaji atoe kitu kidogo. Lakini sehemu za vijijini hususan katika jamii za wafugaji, watuhutoa mbuzi, ng’ombe, nk, kwa walimu ili watoto wao wasiandikishwe shule.” (Ngikundael E.Mghasse, Monduli)

Rushwa hii inajitokeza pia kwa kuhusisha vyakula, vinywaji na mavazi. Rushwa hizi zinajitokeza zaidiwakati wa kampeni za uchaguzi wa kamati za shule.

3. Aina ya tatu ya rushwa ni rushwa inayohusu wanafunzi kutumikishwa nyumbani au shambani kwawalimu. Aina hii ya rushwa imeenea sana maeneo ya vijijini japokuwa pia hujitokeza mijini. Kazi hizo nikama kukata kuni, kuteka maji, kulisha mifugo, kutengeneza bustani na kwa watoto wa kike kupikiawalimu chakula.

Page 7: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Kwa upande wa mijini rushwa hii hujitokeza zaidi kwa watoto kutumikishwa kwenye miradi midogomidogo ya walimu kama kuuza maandazi, karanga na pipi. Watoto wa kike wanatumikishwa kamawafanyakazi wa nyumbani kwa kazi kama kufua nguo, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, nk. Kazi zotehizi hufanyika wakati wa masomo.

4. Aina ya nne ni rushwa ya kutumia madaraka vibaya. Walimu na watendaji wa elimu kutowajibika ipasavyokatika majukumu yao na kujiingiza katika biashara ndogo ndogo. Mahudhurio ya mwalimu mkuushuleni yanaathirika kwa sababu ya kujihusisha na masuala yake binafsi nje ya shule. Hali hii huathiri piauwajibikaji wa walimu wengine.

Rushwa hii pia inaelezewa kuwa ni ya maneno na matendo ambayo hutumiwa kumlainisha mtu hadikutoa huduma. Mfano, kusifia matendo ‘mazuri’ yanayofanywa na wakubwa ili kuficha makosa yao yakiutendaji.

5. Aina ya tano ya rushwa ni rushwa ya undugu. Inahusisha ndugu mmoja mwenye madaraka kuwasaidiandugu wengine wasio na uwezo wa kazi bali ni kwa sababu tu wana undugu naye. Katika manunuzi yavifaa vya shule tenda hupelekwa kwa ndugu. Pia katika kuchagua watu kuhudhuria mafunzo, mikutanoau warsha ndugu huchaguliwa kwa lengo la kujipatia posho.

Aina hii ya rushwa inajitokeza pia panapotokea uhaba wa nafasi za kuandikisha wanafunzi darasa lakwanza. Mzazi anatumia uhusiano wa kindugu alionao na kiongozi wa elimu au mwalimu mkuu ilimwanae aweze kuandikishwa.

Njia za Kupambana na Rushwa

Washiriki waliorodhesha njia nyingi za kupambana na rushwa. Tunaweza kuzigawa njia hizo katika makundimakuu mawili:Hatua za muda mrefu

• Kupeleka rasilimali ya kutosha ya fedha na nguvukazi katika Idara ya Elimu• Kuanzisha kampeni dhidi ya rushwa katika ngazi za jamii. Kampeni hizi zihusishe makundi yote na

ziwe hai na za kudumu• Kutoa elimu ya uraia kwa wananchi

Hatua za muda mfupi• Kutoa adhabu kali na bila huruma kwa maofisa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa• Kuwahusisha zaidi wanajamii katika maamuzi na uongozi wa shule• Kutoa maslahi mazuri na kwa wakati kwa walimu• Kuajiri watumishi waaminifu na waadilifu

“Walimu wapewe motisha na wasogezewe huduma na kupewa mishahara yao kwa wakatiuliopangwa. Watatumia muda wao mwingi kufundisha na kulea wanafunzi” (ZainabuRamadhani, Kibiti – Rufiji, Pwani)

Kwa ujumla shindano hili limetoa changamoto na kuhamasisha washiriki wengi kutoa mapendekezo kwajamii katika ngazi zote kuanzisha mashindano yatakayoshindanisha uadilifu wa taasisi mbalimbali zaSerikali.

Washiriki wengi waliona kuwa njia bora za kupambana na rushwa katika elimu ni zile zinazojumuishamakundi yote. Yaani wananchi, Serikali katika ngazi zote, PCB na vyombo vingine vyote vya dola.Walipendekeza makundi yote hususan katika ngazi ya jamii kujumuika pamoja na kufanya kampeni kubwaza kila mara za kupambana na rushwa. Kampeni hii itawajumuisha wanajamii wote kushiriki katikakutekeleza mipango ya kuchambua mianya ya rushwa na kuweza kupambana nayo.

iiiRushwa katika Elimu

Page 8: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

iv Rushwa katika Elimu

“Viongozi pamoja na watumishi mbalimbali wa umma wamewekwa kwa ajili ya kuwahudumiawananchi na sio kuwachuna kwa njia za udanganyifu. Hivyo wanapaswa kuwa karibu nawananchi ili maamuzi pamoja na vitendo vyao wavifanye bila kificho ili wananchi wayaonewaziwazi matendo yao na kutambua kinachoendelea.” (Padri Michael Kumalija, Shinyanga)

Wako ambao wametoa mapendekezo ya kulifanyia kazi tatizo la rushwa kwa kutumia vyombo vya serikalihususan Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) nchini. Wanatoa mapendekezo kwamba wawepo makacherowatakaofanya kazi kwa vipindi vifupi vifupi katika idara za elimu. Wafanye kazi kwa siri bila kutambulika.Hawa watabainisha mianya ya rushwa na watawatambua wala rushwa kwa urahisi.

“Yaweza pia kuwepo njia ya makachero ndani ya idara tuhumiwa ili kufichua uozo wakiutendaji na kutoa taarifa sahihi juu ya suala zima la rushwa. Makachero hao ni lazima wawena kipindi maalumu ambacho ni kifupi cha kukaa katika eneo moja ili kudhibiti uhusianounaoweza kuharibu kazi.” (Norbet Mpunga, Tandahimba, Mtwara)

Wako wengine waliotoa maoni kwamba mishahara na marupurupu ya walimu iangaliwe upya. Hii itafanyapato la walimu kuongezeka na kuwawezesha kumudu maisha. Hali hii itawaondolea tamaa ya kujipatia patola ziada.

“Njia ya kwanza ambayo ndio msingi wa njia nyingine ni kurekebisha mishahara ya walimu.Kama tunavyojua walimu wamekuwa wakipata mishahara midogo sana ambayo haitoshikutimiza mahitaji yao na ya familia zao. Walimu wanafanya kazi kubwa katika kuwafundishawanafunzi. Kuwapa mishahara midogo kunawavunja moyo na kupelekea elimu nchinikushuka. Hali hii pia inawasababishia kupata tamaa na kuamua kuomba rushwa ili kukidhimahitaji yao.” (Leah Anku Sanga, Dar es Salaam)

Serikali kwa kushirikiana na wananchi wajenge shule nyingi za msingi, sekondari na vyuo ili kutoshelezaongezeko la watoto wanaojiunga na shule na vyuo hivyo.

Idara na vyombo vyote vinavyojihusisha na mapambano dhidi ya rushwa kuanzia ngazi za jamii viimarishwena kupewa uwezo na nyenzo za kupambana na rushwa, mfano mafunzo kazini, usafiri, mawasiliano (simu,kompyuta), nk. Vyombo hivyo ni pamoja na mahakama, polisi, PCB na mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Kuwepo na masanduku mengi ya maoni katika taasisi za elimu ambayo yatakuwa chini yaTaasisi ya Kuzuia Rushwa” (Jodos S. Gwemela, Tabora)

Elimu zaidi kwa kutumia vyombo vya habari na madhehebu ya dini pia imeonekana na wengi kama njiamuafaka ya kupambana na rushwa katika elimu kwa mfano, watu waelimishwe kupitia redio, magazeti namahubiri ya kanisani/misikitini. Washiriki wengi wamehusisha vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili.

Mwisho washiriki wamependekeza adhabu kali zitolewe kwa wale watakaobainika kujihusisha na vitendovya rushwa. Hii inasemekana itakuwa pia ni fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

“Wanaopatikana na makosa ya rushwa wawajibishwe na/au wafukuzwe kazi kabisa badala yakuwahamishia sehemu zingine za kazi ambako wataendeleza uovu huo.” (Ngikundael E.Mghasse, Monduli, Arusha)

Page 9: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Insha na Michoro ya Washiriki

1Rushwa katika Elimu

Page 10: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

2 Rushwa katika Elimu

1. Leonida J. Kasoga (Mwanamke, Miaka 13, SLP 141, Tabora)

Leonida anaelezea kwa ufasaha aina za rushwa zinazojitokeza katika elimu. Anataja aina hizo kuwa ni rushwa ya fedha, rushwa ya ngonona rushwa ya kutumia madaraka vibaya. Anasema mbinu muafaka za kupambana nayo ni kwa njia ya elimu, kuweka mambo wazi nakuwaadhibu kwa ukali wale wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Page 11: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

3Rushwa katika Elimu

1. Leonida J. Kasoga (Mwanamke, Miaka 13, SLP 141, Tabora)

Page 12: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

4 Rushwa katika Elimu

2. Theresia Gervas (Mwanamke, Miaka 15, SLP 1184, Mwanza)

Theresia anasema rushwa zinazojitokeza zaidi ni rushwa za ngono, uuzaji wa nafasi za wanafunzi walioacha shule na kuvujisha majibu yamitihani. Anasema njia za kupambana na rushwa ni kuienzi kazi ya ualimu kwani ualimu ni wito. Walimu waongezewe motisha ili naowaongeze bidii na kuwaondoa wananchi katika hali ya ujinga na wawe na sauti ya kupambana na rushwa.

Page 13: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

5Rushwa katika Elimu

2. Theresia Gervas (Mwanamke, Miaka 15, SLP 1184, Mwanza)

Page 14: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

6 Rushwa katika Elimu

3. Leah A. Sanga (Mwanamke, Miaka 15, SLP 9533, Dar es Salaam)

Leah anazitaja na kuzielezea aina za rushwa ya fedha na rushwa ya mapenzi kama ni rushwa zinazojitokeza zaidi katika elimu. Anasemanjia muafaka ya kupambana na rushwa ni kuhakikisha kwamba sheria kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuripotiwa polisi nakusimamishwa kazi zichukuliwe dhidi ya wakosaji.

Page 15: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

7Rushwa katika Elimu

3. Leah A. Sanga (Mwanamke, Miaka 15, SLP 9533, Dar es Salaam)

Page 16: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

8 Rushwa katika Elimu

4. Twaha Hamis Ubwa (Mwanaume, Miaka 17, SLP 807, Singida)

Twaha anatoa maelezo yanayokolezwa na michoro yenye kutoa picha halisi ya aina za rushwa zinazojitokeza katika elimu. Anamaliziakwa kusema kwamba ni jukumu la kila mzalendo kupambana na tatizo hili.

Page 17: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

9Rushwa katika Elimu

4. Twaha Hamis Ubwa (Mwanaume, Miaka 17, SLP 807, Singida)

Page 18: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

10 Rushwa katika Elimu

4. Twaha Hamis Ubwa (Mwanaume, Miaka 17, SLP 807, Singida)

Page 19: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

11Rushwa katika Elimu

5. Mercy Charles Masasi (Mwanamke, Miaka 19, SLP 9131, Dar es Salaam)

Mercy anasema wazazi wenye uwezo kiuchumi wananunua nafasi za masomo kwa watoto wao waliofeli mitihani. Wenye uwezo darasaniwanakosa nafasi ya kuendelea na masomo kwa sababu tu ya umasikini wa wazazi wao. Anaongelea pia juu ya wachache wanavyozitumiakwa manufaa binafsi fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuendeleza elimu. Ni fedha kidogo tu zinazofika hadi katika ngazi ya shule.

Page 20: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

12 Rushwa katika Elimu

5. Mercy Charles Masasi (Mwanamke, Miaka 19, SLP 9131, Dar es Salaam)

Page 21: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

13Rushwa katika Elimu

6. Hamis Mtingwa (Mwanaume, Miaka 19, SLP 77693, Dar es Salaam)

Hamisi anatoa ufafanuzi mzuri kwa kutumia michoro. Michoro yake inaonyesha juu ya rushwa ya pesa na mapenzi inavyojitokeza shuleni.Anaonyesha kuwa njia muafaka ni kuelimisha jamii na kuwaadhibu kwa kufuata sheria wale wanaobainika kujihusisha na vitendo vyarushwa.

Page 22: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

14 Rushwa katika Elimu

6. Hamis Mtingwa (Mwanaume, Miaka 19, SLP 77693, Dar es Salaam)

Page 23: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

15Rushwa katika Elimu

6. Hamis Mtingwa (Mwanaume, Miaka 19, SLP 77693, Dar es Salaam)

Page 24: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

16 Rushwa katika Elimu

6. Hamis Mtingwa (Mwanaume, Miaka 19, SLP 77693, Dar es Salaam)

Page 25: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

17Rushwa katika Elimu

7. Martin Peter Mkumbo (Mwanaume, Miaka 19, SLP 7878, Dar es Salaam)

Martin anafafanua kwa undani maana ya rushwa na kuzitaja rushwa zinazojitokeza zaidi katika elimu kuwa ni rushwa ya ngono na rushwaya fedha. Ameambatanisha mchoro kutoa picha halisi ya maelezo yake. Anasema njia za kupambana na kuitokomeza kabisa rushwa nikukishughulikia chanzo chake. Hivyo anasema chanzo ni hali duni ya walimu. Kuboresha hali za walimu, kutoa mafunzo tangu shule zamsingi na kuwaadhibu wahusika; ndiyo njia muafaka za kupambana nayo.

Page 26: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

18 Rushwa katika Elimu

7. Martin Peter Mkumbo (Mwanaume, Miaka 19, SLP 7878, Dar es Salaam)

Page 27: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

19Rushwa katika Elimu

7. Martin Peter Mkumbo (Mwanaume, Miaka 19, SLP 7878, Dar es Salaam)

Page 28: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

20 Rushwa katika Elimu

8. Beatus Mwendwa (Mwanaume, Miaka 23, SLP 1411, Mwanza)

Beatus anasimulia hadithi yenye kugusa hisia juu ya wasichana na watu masikini wanavyoathirika na rushwa katika elimu. Anasemarushwa ziko katika mfumo wa zawadi ili kupata nafasi finyu wakati wa kuandikisha watoto shule. Naye pia anaiongelea rushwa yamapenzi kama ni rushwa inayojitokeza zaidi katika elimu. Anasema njia muafaka ya kupambana nayo ni kutoa elimu. Elimu yakawaida tu haitoshelezi bila kuwapa watoto elimu ya maadili ya kuikataa na kuichukia rushwa.

Page 29: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

21Rushwa katika Elimu

8. Beatus Mwendwa (Mwanaume, Miaka 23, SLP 1411, Mwanza)

Page 30: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

22 Rushwa katika Elimu

9. Steven Kipili (Mwanaume, Miaka 25, SLP 63096, Dar es Salaam)

Kwa njia ya michoro yenye mvuto, Steven anaelezea kwa ufasaha jinsi rushwa ya zawadi na hata mifugo inavyotumika katikauandikishwaji wa wanafunzi shuleni. Anaonyesha pia kwamba masomo ya ziada hutolewa kwa wanafunzi wenye uwezo tu. Njia muafakaya kupambana na rushwa hii anasema ni kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii, mishahara ya walimu kutolewa kwa wakati bila kuchelewana elimu ya kupambana na rushwa itolewe kwa wanafunzi.

Page 31: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

23Rushwa katika Elimu

9. Steven Kipili (Mwanaume, Miaka 25, SLP 63096, Dar es Salaam)

Page 32: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

24 Rushwa katika Elimu

10. Jodos S. Gwemela (Mwanaume, Miaka 31, SLP 2069, Tabora)

Jodos pamoja na aina nyingine za rushwa, anaitaja rushwa ya fedha na ngono kama rushwa inayojitokeza zaidi katika elimu. Anasema njiamuafaka ya kupambana nayo pamoja na mbinu nyingine ni Serikali kufanya ukachero kwa kutengeneza vyeti vya bandia na kuwanasawatakaovinunua na kuvitumia katika kutafuta ajira au masomo ya juu.

Page 33: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

25Rushwa katika Elimu

10. Jodos S. Gwemela (Mwanaume, Miaka 31, SLP 2069, Tabora)

Page 34: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

26 Rushwa katika Elimu

11. Rajabu A. Ngimba (Mwanaume, Miaka 32, SLP 23, Ngerengere, Morogoro)

Rajabu ametaja na kueleza kwa ufasaha rushwa ya fedha na ngono kama aina kuu za rushwa. Anaeleza jinsi jamii inavyoweza kupambana na rushwa. Anatoa mwito kwa mishahara ya walimu kuongezwa na kutoka kwa wakati bila kuchelewa.Pia anashauri adhabu kali zitolewe kwa watakaobainika kujihusisha na rushwa, na adhabu hizo ziwekwe wazi ili kila mmoja azifahamu.

Page 35: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

27Rushwa katika Elimu

11. Rajabu A. Ngimba (Mwanaume, Miaka 32, SLP 23, Ngerengere, Morogoro)

Page 36: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

28 Rushwa katika Elimu

12. Ngikundael G. Mghasse (Mwanaume, Miaka 32, SLP 46, Monduli, Arusha)

Ngikundael ametoa ufafanuzi mzuri kuhusu maana ya rushwa na kutaja sababu za rushwa katika elimu. Moja ni rushwa itokanayo naukarabati na ujenzi wa madarasa na majengo mengine shuleni chini ya mpango wa MMEM. Njia moja ya kupambana na rushwa nimaamuzi mbalimbali ya Serikali kuwekwa wazi ili wananchi washiriki vizuri katika mapambano.

Page 37: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

29Rushwa katika Elimu

12. Ngikundael G. Mghasse (Mwanaume, Miaka 32, SLP 46, Monduli, Arusha)

Page 38: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

30 Rushwa katika Elimu

13. Redempta B. Minga (Mwanamke, Miaka 38, SLP 3114, Mbeya)

Redempta anataja na kuelezea vizuri aina za rushwa zinazojitokeza katika elimu. Anafafanua rushwa ya walimu na watendaji wa elimukutowajibika ipasavyo katika majukumu yao na kujiingiza katika biashara ndogondogo. Anapendekeza njia moja muafaka ya kupambanana rushwa ni vyombo vya habari kutoa elimu kwa jamii kwamba rushwa ni adui wa haki.

Page 39: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

31Rushwa katika Elimu

13. Redempta B. Minga (Mwanamke, Miaka 38, SLP 3114, Mbeya)

Page 40: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

32 Rushwa katika Elimu

14. Norbert N. Mpunga (Mwanaume, Miaka 39, SLP 44, Tandahimba, Mtwara)

Norbert anaelezea rushwa ya maneno na matendo ambayo hutumiwa kumlainisha mtu hadi kutoa huduma. Anatoa mfano wa kusifiamatendo mazuri yanayofanywa na wakubwa ili kuficha makosa ya kiutendaji kwa watendaji wa ngazi za kati na za chini. Anasemamashindano ya kufichua uozo katika elimu yatasaidia kupunguza rushwa. Pia kitengo kitakachoonekana kuwa safi wazawadiwe nawatakaoshindwa wafuatiliwe.

Page 41: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

33Rushwa katika Elimu

14. Norbert N. Mpunga (Mwanaume, Miaka 39, SLP 44, Tandahimba, Mtwara)

Page 42: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

34 Rushwa katika Elimu

15. Ephraim E. Baruti (Mwanaume, Miaka 44, SLP 169, Igunga, Tabora)

Ephraim anaelezea kwa undani kuhusu rushwa kwa wafugaji inayohusu wazazi kukwepa kuwaandikisha watoto shule kwa kuwahongawalimu mifugo. Pia wasichana huachishwa shule ili kuolewa kwa nia ya kupata mahari ya mifugo. Njia za kupambana na rushwaanasema ni pamoja na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kujenga shule za msingi, sekondari na vyuo kwa wingi ili kuongeza nafasikwa wanafunzi wapya.

Page 43: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

35Rushwa katika Elimu

15. Ephraim E. Baruti (Mwanaume, Miaka 44, SLP 169, Igunga, Tabora)

Page 44: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

36 Rushwa katika Elimu

16. Padri Michael Kumalija (Mwanaume, Miaka 50, SLP 2109, Shinyanga)

Pd. Michael amegusa maeneo mengi ya rushwa. Baadhi ya maeneo hayo ni kama uandikishwaji, fedha, tuisheni, ngono, kukaririmadarasa, n.k. Anaainisha njia muafaka za kupambana na rushwa kuwa ni pamoja na demokrasia, utawala bora, haki na usawa, ushirikiwa wananchi, uwajibikaji na uwazi.

Page 45: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

37Rushwa katika Elimu

16. Padri Michael Kumalija (Mwanaume, Miaka 50, SLP 2109, Shinyanga)

Page 46: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

38 Rushwa katika Elimu

17. Gerald W. Ndyamukama (Mwanaume, Miaka 55, SLP 102, Muleba, Kagera)

Gerald ameongelea rushwa za kuvujisha mitihani na upatikanaji wa vyeti vya kugushi. Anasema njia muafaka ya kuizuia ni kuingia vitani,kupigana kikamilifu na kuwakamata mateka na majeruhi wote ambao ni maadui wala rushwa.

Page 47: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

39Rushwa katika Elimu

17. Gerald W. Ndyamukama (Mwanaume, Miaka 55, SLP 102, Muleba, Kagera)

Page 48: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

40 Rushwa katika Elimu

Mchakato wa Kupata Washindi

Walioshiriki

Wakazi wote wa Tanzania bila kujali umri walikaribishwa kushiriki katika shindano hili. Jumla yawashiriki waliotuma insha na michoro yao walikuwa ni 2,898; kati yao wanaume ni 2,160 na wanawakeni 483. Wengine 255 walishiriki kama vikundi au hawakutaja jinsia zao. Washiriki walikuwa na umritofauti - wakiwemo watoto na wazee - na kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Tathmini

Shindano liliwataka washiriki kujibu maswali mawili. Swali la kwanza lilikuwa ni kutaja aina za rushwazinazojitokeza zaidi katika elimu. Swali la pili ni kupendekeza njia muafaka za kupambana na tatizo larushwa katika jamii.

Mapendekezo ni lazima yaambatane na sababu. Zaidi ya hayo insha na michoro ilitakiwa iwe ni yakiubunifu, iliyoandikwa vizuri na/au mchoro uliochorwa kwa unadhifu na kwa kuvutia na inayolengamoja kwa moja kwenye wazo muhimu.

Kila swali lilikuwa na alama 50%. Na kila insha au mchoro ulifanyiwa tathmini katika mfumo wa jedwalilifuatalo:

Taarifa kwa kila mshiriki Kigezo Alama

• Namba ya ushiriki Ubunifu/Upya/Utambuzi 20

• Jina la Mshiriki Sababu za kina/zenye uchambuzi 10

• Anapotokea (Wilaya, Mkoa) Iliyoandikwa vizuri/fupi/iliyo wazi 10

• Umri Bonasi kwa insha/mchoro bora 10

• Jinsia Jumla 50

Watu watatu kutoka katika nyanja tofauti waliteuliwa kufanya tathmini iliyoainishwa hapo juu. Walitokakatika sekta ya elimu na Asasi Zisizo za Serikali (AZISE). Mara baada ya kufanya tathmini, waliteuawashiriki 150 waliofanya vizuri.

Tathmini ya awamu ya pili ilifanyika ili kuwapata washindi na waliofanya vizuri. Washiriki walikuwa nikutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wizara ya Elimu na Utamaduni na AZISE inayohusika namasuala ya elimu– Action Aid. Wengine ni wawakilishi wawili kutoka PCB na mmoja kutoka HakiElimu.

Baada ya kufanya tathmini jopo lilifanikiwa kupata washindi 12 na waliofanya vizuri 100. Mchakato wauteuzi ulikuwa mgumu kwani insha nyingi ziliandikwa vizuri sana. Pia mtawanyiko wa washindi na walewaliofanya vizuri haukuwa katika uwiano mzuri kijiografia na kijinsia. Kwa sababu hizo washindi watanowaliongezwa hadi kufikia 17 na wale waliofanya vizuri waliongezwa 10 kufikia 110.

Page 49: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

41Rushwa katika Elimu

Orodha ya Washindi

Kila mshindi kati ya 17 bora alipata Tshs. 100,000/= kwa ajili yake na nyingine 100,000/= kwa ajili yashule aliyoichagua. Na kila mmoja katika washiriki wengine 110 waliofanya vizuri kila mmoja alipatafulana na kofia ya PCB. Washindi wote na wale waliofanya vizuri kila mmoja alitumiwa nakala moja yakijitabu cha “Shule Nzuri ni Ipi?”chenye maoni ya washiriki 17 wa shindano letu lililotangulia.

Hapa tunaorodhesha washindi wote 17 na shule walizochagua.

Jina Umri Jinsia Anapotoka Shule iliyochaguliwa

Leonida J. Kasoga 13 Ke Tabora Chemchem Shule ya Msingi SLP 141, Tabora

Theresia Gervas 15 Ke Mwanza Nyamanoro D Shule ya MsingiSLP 1184, Mwanza

Leah A. Sanga 15 Ke Dar es Salaam Mlimani Shule ya MsingiSLP 35091, Dar es Salaam

Twaha Hamisi Ubwa 17 M Singida Utemini Shule ya MsingiSLP 1066, Singida

Mercy Charles Masasi 19 Ke Dar es Salaam Kimara Baruti Shule ya MsingiSLP 55084, Dar es Salaam

Hamis Mtingwa 19 M Dar es Salaam Majimatitu Shule ya MsingiSLP 46343, Dar es Salaam

Martin P. Mkumbo 19 M Dar es Salaam Segerea Shule ya Msingi SLP 20950, Dar es Salaam

Beatus Mwendwa 23 M Mwanza Sumve Shule ya MingiSLP 41 Mwanza

Steven D. Kipili 25 M Dar es Salaam Ubungo NH Shule ya MsingiSLP 16600, Dar es Salaam

Jodos S. Gwemela 31 M Tabora Nyakimue Shule ya MsingiSLP 100, Manyovu, Kigoma

Rajab A. Ngimba 32 M Ngerengere, Morogoro Njianne Shule ya MsingiSLP 37 Ngerengere, Morogoro

Ngikundaeli E. 32 M Monduli, Arusha Olarash Shule ya MsingiMghasse SLP 8, Monduli

Redempta B. Minga 38 Ke Mbeya Mkombozi Shule ya MsingiSLP 6135, Mbeya

Norbert N. Mpunga 39 M Tandahimba, Mtwara Matogoro Shule ya MsingiSLP Tandahimba

Ephraim E. Baruti 44 M Igunga, Tabora Igunga Shule ya SekondariSLP 169, Igunga

Padri Michael Kumalija 50 M Shinyanga Mwasele Shule ya MsingiSLP 28, Shinyanga

Gerald W. 55 M Muleba, Kagera Kishoju Shule ya Msingi Ndyamukama SLP 102, Muleba, Kagera

Page 50: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

42 Rushwa katika Elimu

Zainabu Ramadhani Ke Kibiti-Rufiji Pwani

Josephine William Ke Iringa

Raphael Msabila Me Morogoro

Philemon Mfuruki Me Karagwe, Kagera

Jackson Luka Nkya Me Milambo, Tabora

Apolinary Andrew Me MorogoroSeiya

Wilbert Mgeni Me Dar es Salaam

Mwinondi Filbert Me SUA, Morogoro

Godfrey Alphonce Me Morogoro

Simon Malya Me Moshi, Kilimanjaro

Elisha K. Mwalugembe Me Biharamulo, Kagera

John M.S. Mwamlima Me Kidatu, Morogoro

John M. Msaki Me Moshi, Kilimanjaro

Eddie G. Jacque Me Dar es Salaam

Mohamed Ally Me Dar es Salaam

Francis Rwahama Me Dar es Salaam

Novatus Rweyemamu Me Dar es Salaam

George S. Davis Me Shinyanga

Mmari Enock Me Dar es Salaam

Mamboleo Jumanne Me 14 Kibaha, Pwani

Emmanuel Robert Me 15 Dar es Salaam

Paulina Fidelis Ke 16 Mbeya

Grace James Ke 17 Dar es Salaam

Abrahan Mema Me 17 Mbeya

Elifuraha E.Kazaula Me 17 Bukoba, Kagera

Chrispin Mkerebe Me 17 Dar es Salaam

Caroline Mtui Ke 18 Marangu, Moshi

Devotha L. Sanga Ke 18 Iringa

Ibrahim M. Thomas Me 18 Dar es Salaam

Stanley Francis Me 18 Tunduru, Ruvuma

George James Me 18 Sengerema, Mwanza

Aziz Chuma Me 18 Dar es Salaam

Benedict K. Simon Me 18 Mwanza

Ally Msunda Me 19 Manyoni, Singida

Caroli E. Klimenze Me 19 Singida

Dotto F. Miraji Me 19 Mbinga, Ruvuma

Shafii Ramadhani Me 19 Dar es SalaamOthman

Filbert V. Kotira Me 19 Dar es Salaam

Mnasaeli M. Urio Me 19 Usa-River, Arusha

Tito John Bondo Me 19 Mbeya

Eyya Ngollo Ke 20 Dar es Salaam

Glory E. Mponzi Ke 20 Dar es Salaam

Lilian Katyega Ke 20 Zanzibar

Husna Mwakiuno Ke 20 Dodoma

Happiness Chaula Ke 20 Iringa

Mussa Gunda Me 20 Dar es Salaam

Maryam Simba Ke 21 Dar es Salaam

Bakari Mbonde Me 21 Dar es Salaam

Hamad R. Msami Me 21 Dar es Salaam

Yassin Chikoyo Me 21 Dar es Salaam

Emmanuel Joseph Me 22 Dar es SalaamMgana

James B.S. Kyando Me 22 Dar es Salaam

Dianus Mutalemwa Me 22 Dar es SalaamSerapion

Alloys C. Mallelo Me 22 Kiabakari, Musoma

Simon Mbatiani Me 22 Kisarawe, Pwani

Jennifer Daniel Ke 23 Dar es Salaam

Christopher Shimwelah Me 23 Tanga

Yona Melita Me 23 Mto wa Mbu, Arusha

Hashim Salehe Me 23 Dar es Salaam

Patrick Khama Ayiemba Me 23 Dar es Salaam

Deodatus L. Mkambi Me 23 Mbozi, Mbeya

Celestin W. Kapelela Me 23 Mbozi, Mbeya

Malulu Bulima Me 24 Tabora

Gilbert M. Gosbert Me 24 Maswa, Shinyanga

Shule zilipewa uhuru wa kuamua jinsi watakavyotumia zawadi zao. Hata hivyo tulitegemea shulezitumie zawadi kwa kufuata misingi na dhamira ya shindano lenyewe. Shule zilitumiwa fomu zenyemwongozo wa jinsi ya kushirikisha makundi mbalimbali kuamua jinsi ya kutumia zawadi ya shindano.Zilitakiwa pia kuweka habari kuhusu zawadi hii wazi kwa jamii inayowazunguka. Na mwisho,waibandike taarifa hii kwenye mbao za matangazo.

Washindi 110 waliofuatia:

Jina Jinsi Umri Anapotoka Jina Jinsi Umri Anapotoka

Page 51: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

Elibariki John Me 25 Morogoro

John Philip Me 25 SUA, Morogoro

Paul Emmanuel Me 25 Mwanza

Nyamagalula N. Me 25 TaboraMachumu

Peter Andrew Me 25 Dar es Salaam

Alesco Seth Mpangile Me 25 Kijiji cha Nsonyanga, Mbeya

Geoffrey Marwa Me 25 Dar es Salaam

Yethiro Chongolo Me 25 Makambako, Iringa

Furaha Henjewele Me 26 Morogoro

C. M. Gichogo Me 26 Mwanza

Emmanuel R. Me 26 Moshi, KilimanjaroNyambuka

Lilanga Iddi Zuma Me 26 Dar es Salaam

Florian B. Tinuga Me 26 Moshi, Kilimanjaro

Deogratias Rwegoshora Me 26 Dar es Salaam

Emmanuel Kisyeri Me 26 Dar es Salaam

Hatibu O. Jongo Me 27 Ntoma Bukoba, Kagera

Maximillian S. Mondu Me 27 Dar es Salaam

Emmanuel Hungu Me 28 Butimba, Mwanza

Malimi Joram Me 29 Mwanza

Charles H. Kasigwa Me 30 Dar es Salaam

Lucas Ogutu Ojanje Me 30 Dar es Salaam

Elisaria S. Pallangyo Me 30 Dar es Salaam

Kitandu Paulo Ugula Me 30 Mwadui, Shinyanga

Jumanne Yusuf Mlacha Me 31 Dar es Salaam

Philip L. Sanga Me 31 Dar es Salaam

Niyonsaba D. Isaack Me 32 Bukene-Nzega, Tabora

John S.Chigongo Me 32 Singida

Musyangi S. Ramadhani Me 33 Dar es Salaam

Said Mbiliza Me 33 Nzega, Tabora

Leonard Joseph Me 34 SingidaMasawe

Markalio Godson Peter Me 35 Tanga

Filbert Millinga Me 37 Dar es Salaam

Narsis Fulgence Me 37 Bukoba, Kagera

Ephrain J.R. Kibona Me 37 Uyole, Mbeya

Razack A. Kijombe Me 39 K/Masoko, Lindi

Wenceslaus Patrick Me 40 Bukoba, Kagera

Timothy Kitundu Me 40 Dar es Salaam

Fernand Mnyasa Me 40 Muleba, KageraFulgence

Sophia G. Range Ke 41 Bagamoyo, Pwani

Hussein R. Mabodya Me 41 Kyaka, Bukoba

Mligi Martin Mligi Me 42 Singida

Mollen Masaka Ke 45 Itigi-Manyoni, Singida

Ndambile Kalasa Me 52 Itigi-Manyoni, Singida

Mary Maufi Ke 62 Mpanda

F. Byelembo Kishenyi Me 65 Karagwe, Kagera

Henry H. Mpungwe Me 67 Manyoni Singida

43Rushwa katika Elimu

Jina Jinsi Umri Anapotoka Jina Jinsi Umri Anapotoka

Page 52: Rushwa katika Elimu - HakiElimu : Homehakielimu.org/files/publications/document3rushwa_katika...ii Rushwa katika Elimu Maoni ya Washiriki Aina za Rushwa Washiriki wote walionyesha

44 Rushwa katika Elimu