Upload
prof-handley-mpoki-mafwenga
View
170
Download
10
Embed Size (px)
Citation preview
1
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN KUTOKA AHELA
Na Prof (Dkt) Handley Mpoki Mafwenga
Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Ilikuwa usiku wa tarehe 05 Julai Mwaka, 2010 majira ya saa tisa alfajiri nilipotokewa
kwenye ndoto na Waasisi wa Chama cha Mapinduzi Mwal Nyerere, Mzee Abeid Karume na
Mzee Thabiti Kombo, nilipokabidhiwa barua ifuatayo;
Dr Shein; ukumbuke kuwa una kazi kubwa sana ya kukabiliana na siasa za vijembe za
huko Zanzibar. Miaka mingi sasa toka umechukua uongozi kwa Dr Omar Ali Juma
umekuwa Mpole, Mkimya, Msikivu, na mwenye Hekima kubwa; Wewe ni binadamu wa
namna gani? Hata ulimi kujikwaa kidogo kisha ukasamehewa kama binadamu wengine
walivyo? Je wewe ni mithili ya Malaika?
Sisi tulifanya makosa kidogo kuondoa kofia ya Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais,
tukidhani tunaboresha Muungano. Lakini tumejikuta tafsiri ya Watanzania kuhusu
Zanzibar iko tofauti sana, Zanzibar inafananishwa na Mkoa. Tumefurahi sana kumsikia
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri akirekebisha mawasilisho ya maelezo kuwa
Zanzibar isijumuishwe na Mikoa ni vyema basi katika maelezo mseme “na huko Zanzibar”
baada ya kutaja Mikoa. Inaonyesha kuwa kugombea kwako uongozi na kuacha nafasi ya
Makamu wa Rais ni kielelezo kuwa Zanzibar ina uthamani wa tofauti ndani ya Utaifa wa
Tanzania.
Dr Shein, Zanzibar inaitwa kikatiba “Tanzania Zanzibar” hivyo bila Tanzania ukweli
Zanzibar haipo. Utaapishwa utakaposhinda chini ya Ibara ya 103(2) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano na Jaji Mkuu wa Zanzibar kulinda na kutetea Katiba ya Jamhuri
na kiapo kingine chochote chini ya Katiba ya Zanzibar katika kutekeleza majukumu yako.
Kuna kitu kinatusumbua sana. Imekuwaje leo mnaleta kauli za “Kero za Muungano”
tunaomba kuanzia sasa mseme “Changamoto za Muungano”hili ndilo neno tulilowaachia.
Muungano ni dhana ya upendo, mshikamano, na uvumilivu, ndani ya vitu hivyo vitatu
hakuna Kero; Mwambia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Kiongozi
Vuai Nahodha waepuke neno hilo”Please”.
2
Hata hizo ziitwazo kero za Muungano ni maombi yanayowasilishwa na upande Mmoja
yaani Zanzibar katika aidha kuubomoa au kuuimarisha Muungano; mengi hayajajitokeza
kurekebisha Nyongeza ya 1 ya Ibara ya 4 ya Katiba inayoelezea Mambo ya Muungano.
Uwaeleze mambo ya Muungano ni haya hapa; 1) Katiba ya Tanzania na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano 2) Mambo ya Nchi za Nje 3) Ulinzi na Usalama 4) Polisi 5)
Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya Hatari 6) Uraia 7) Uhamiaji 8) Mikopo na
Biashara za Nchi za Nje 9) Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano 10) Kodi ya
mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, Ushuru wa Forodha, na Ushuru wa
Bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha 11)
Bandari, mambo yanayohusika na Usafiri wa Anga, posta na simu 12) Mambo yote
yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki,
(pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na
usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni 13) Leseni ya viwanda na
takwimu 14) Elimu ya Juu 15) Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuta ain ya petrol na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia 16)
Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza
hilo 17) Usafiri na Usafirishaji wa Anga 18) Utafiti 19) Utafiti wa Hali ya Hewa 20)
Takwimu 21) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na 22) Uandikishaji wa
vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo
Ili mambo yaweze kutekelezeka pale Zanzibar inabidi Baraza la Wawakilishi liridhie
Sheria inayotakiwa kutekelezeka hadi Zanzibar lakini ni mambo machache yanayoridhiwa
kuna nini hapo? Aidha, kwa mfano kodi zote zilizo chini ya Jamhuri ya Muungano inafaa
ziletwe kwenye mahakama za kodi (TRAT na TRAB) lakini hakuna kesi hata moja
iliyoletwa kwenye mahakama hizo angalau basi Mahakama hizo zingekasimu usikilizaji wa
kesi pale Zanzibar.
Ubinafsi, Chuki na Siasa zilizopitwa na wakati usiwe kimya yashughulikie pindi ukiwa
Rais; Kuna hili swala la “Muafaka”. kumbuka swala zima la “Utawala wa Sheria” na
maneno ya Engels kuwa” Power which is termed as State; arose from the society, but places
itself above it and alienates itself more and more from it. What does this power mainly
consist of? It consist of special bodies of armed men which have prisons etc. at their
command; public power which is attribute of every state does not coincide with the armed
population with its acting armed organization.‟ Engles alijaribu sana kuelezea nguvu ya
Umma “Public power” akisisitiza kuwa hiyo ndiyo muhimu zaidi kwani nguvu zozote za
kijeshi hazina mafanikio bila nguvu ya Umma ndani ya Utawala wa Sheria. Tunakuasa
Nguvu ya Umma ya Watanzania ni muhimu sana na haijengwi kutoka kwenye vyama ila
vyama hujengwa kutoka kwao; epuka neno muafaka linaloanzia kwenye vyama vya siasa
huo siyo msingi wa Utawala wa Sheria.
Maana ya kwanza ya Utawala wa Sheria ilitolewa kwenye Sheria ya Athens ya 1955; ya
pili kutoka kwenye „Delaration ya Delhi Mwaka 1959; na 1961 kwenye Sheria ya Lagos
ambayo ilijaribu kuleta maana ya Kiafrika; aidha, Tume ya Wanasheria ya Geneva Mwaka
3
1961; Utawala ni kuhakikisha Wanasheria wanawajibika katika kulinda na kukuza haki
za mtu za kiraia na kisiasa, kijamii, kuchumi, kielimu na kimila katika hali ya utu, uhuru
na kiitikadi bila kuingiliwa na Dola. Palipo na Muafaka ni dalili kuwa Utawala wa Sheria
una walakini na unaingiliwa zaidi na vyama vya siasa au Dola.
Kuna hili la mihimili mitatu ya dola; yaani Bunge, Mahakama, na Serikali. Imetokea
wabunge wanaiagiza Serikali badala ya kushauri ingawa Ibara ya 45 (2) Bunge laweza
kuweka utaratibu utakaofuatwa na Rais katika kutekeleza majukumu yake; Bunge
linaweza kupitisha Azimio la kumuonda Rais (Vote of No Confidence), madarakani endapo
itatolewa hoja ya Bunge kumshitaki Rais chini ya Sheria Na 20 ya Mwaka 1992 Ibara ya 8
na Sheria Na 12 ya Mwaka 1985 Ibara ya 4. Aidha, Bunge linaweza kupitisha hoja ya
kuunda Kamati ya Uchunguzi na ikiwa hivyo Rais atahesabika kuwa hayupo kazini ndani
ya siku saba na Bunge litampa Rais nafasi ya kujieleza na Kamati itatoa taarifa kwa Spika
ndani ya siku tisini n.k. Lakini ikumbukwe kwamba kwenye Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikisomwa pamoja na Sheria Na 15 ya Mwaka 1984
Ibara ya 12 Bunge lina wajibu kwa niaba ya Wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali
ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa Majukumu yake
kwa mujibu wa Katiba. Sasa hili la kuiagiza Serikali liko wapi ndani ya Katiba?
Hii imesababisha pia vyama vya siasa kukosa mwelekeo na nafasi ya utambuzi katika
Nchi, hasa kwa chama Tawala na ndiyo maana hivi karibuni kulitokea wabunge kutumia
Bunge kujibu hoja za maelekezo ya Halmashauri Kuu (NEC). Halmashauri Kuu ni
Chombo cha kuheshimika katika chama ndiyo maana Makamu wa Pili wa Rais Hayati
Rashid Kawawa October, 1968 alibainisha kuwa TANU na ASP ni vyama shika hatamu
lakini wabunge walipinga. Alisisitiza kuwa NEC ina uwezo wa kufukuza watu kwenye
chama; katika kikao cha NEC wabunge wawili Ndugu Oscar Kambona na Ndugu
Anangisye walifukuzwa kwa sababu ya kukiuka maadili, na misingi ya chama. Hii ni kwa
vile vifungu Na 27,30,32 na 33 vya Katiba ya Mpito vilibainisha kuwa Mwananchi yeyote
ili awe mbunge lazima awe mwanachama wa chama cha siasa; hivyo kufukuzwa kwao moja
kwa moja kunapoteza nafasi yao ya ubunge. Hii ipo pia katika Ibara ya 67(1) ukisoma
pamoja na Sheria Na 15 ya Mwaka 1984 Ibara ya 13. Katika hili tunaomba
muwakumbushe wabunge nafasi ya vyama vya siasa katika nchi. Hadhi ya chama isiwe
wakati wa mchakato wa kupata ubunge na urais bali wakati wote katika kulida heshima,
utu, na haki ya watanzania.
Kumbuka maneno ya Patrice Lumumba tarehe 30 Juni, 1960 alisema “We are going to re-
examine all former laws and make new ones which will be just and noble. We are going to
put an end to suppression of free thought and make it possible for all citizens fully to enjoy
the fundamental liberties set down in the declaration of the rights of man” Kama wabunge
wanataka kuagiza Serikali warundi kubadili Sheria zilizopo ku-enzi hata maneno ya
Lumumba. Tunajua wewe ni Muislamu lakini ebu Fungua Samwel 23(1)(b) neno linasema
“Atawalaye wanadamu kwa haki akitawala katika hicho cha Mungu, atakuwa kama nuru
ya asubuhi jua lichapo, asubuhi isiyo na mawingu” .
4
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika