16
1 TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba Toleo Namba 23 23 14 - 20 Oktoba, 2013 Tumieni elimu mliyoipata kusaidia Jamii – Msangi Uk. 14 Dk. Mwakyembe: TPA mmenifurahisha Uk.3 Soma utekelezaji wa maagizo ya Waziri Uk.5 Inaendelea Uk. 2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Gati la Bandari ya Maa, kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Uzinduzi wa Gati la Maa ambao ulifanyika Oktoba 3 mwaka huu pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (watatu kushoto) na Mbunge wa Maa, Mh. Abdulkarim Shah (wa pili kushoto) pamoja na Maasa wengine wa Wizara na Serikali. Kulia ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete. Na Janeth Ruzangi R ais Jakaya Kikwete amelifungua rasmi gati la Mafia na kuiagiza Mamlaka kutengeneza utaratibu maalum wa magari ya kuwabeba abiria kutoka melini na kwenda melini hasa wagonjwa, wazee na watoto ambao umbali wa kilomita 1.3 wa gati hilo ni mrefu kwa kundi la watu hao. Gati la Mafia lafunguliwa rasmi

Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

1

TANZANIA PORTS AUTHORITY

www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba Toleo Namba 2323 14 - 20 Oktoba, 2013

Tumieni elimu mliyoipata kusaidia Jamii – Msangi

Uk. 14Dk. Mwakyembe: TPA mmenifurahisha

Uk.3 Soma utekelezaji wa maagizo ya Waziri

Uk.5

Inaendelea Uk. 2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Gati la Bandari ya Mafi a, kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Uzinduzi wa Gati la Mafi a ambao ulifanyika Oktoba 3 mwaka huu pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (watatu kushoto) na Mbunge wa Mafi a, Mh. Abdulkarim Shah (wa pili kushoto) pamoja na Maafi sa wengine wa Wizara na Serikali. Kulia ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

Na Janeth Ruzangi

Rais Jakaya Kikwete amelifungua rasmi gati la Mafi a na kuiagiza Mamlaka kutengeneza utaratibu maalum wa magari ya kuwabeba abiria kutoka melini na kwenda melini hasa wagonjwa, wazee na watoto ambao umbali

wa kilomita 1.3 wa gati hilo ni mrefu kwa kundi la watu hao.

Gati la Mafialafunguliwa rasmi

Page 2: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

2

“Nimetembea mpaka kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais.

Rais aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifungua rasmi gati hilo baada ya ujenzi wake kukamilika ambapo pia alishuhudia meli ya kwanza ya abiria ikifunga na abiria wake kushuka katika gati hilo.

Katika kutekeleza utaratibu huo Rais alitaka mpango huo ufanyike kwa umakini ili kuepusha ajali na kusisitiza kwamba suala la usalama ni muhimu na linaingia kwenye kundi la maeneo muhimu, ‘vital installations’ na kuitaka Mamlaka kuijenga bandari ya Mafi a ili ifanane na bandari kwa kuweka sakafu badala ya mchanga uliopo, maeneo ya kukatia tiketi, jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya watu wasiohusika kuingia ndani ya bandari na hivyo kupunguza vitendo vya uhalifu na hujuma.

Akiongea na wananchi wa Mafi a waliofi ka kushuhudia ufunguzi huo, Rais alisema ahadi ya Serikali ya kumaliza kero mbili za Wilaya ya Mafi a za ujenzi wa gati na uwanja ndege zimekamilka na kuipongeza Wizara ya Uchukuzi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa kazi nzuri na kuwataka wananchi wa Mafi a kuitunza gati hiyo. “Itunzeni gati hii ili iwatunze, itunzeni

idumu,” alisisitiza.

wa Mafi a kulitunza gati hilo lisihujumiwe na wachache wenye uchu wa vyuma chakavu na kuwataadharisha kwamba “kwa kunyofoa nati moja, uwezo wa daraja hilo unakuwa umeathirika,” alisisitiza.

Gati hilo lenye urefu wa kilomita 1.3 lina nguzo 124 za chuma ambazo ndani yake ni zege, lina uwezo kufunga meli za ukubwa wa tani laki sita na kubeba malori ya mzigo ya uzito wa tani 10 ambayo hutembea kilomita 15 kwa saa limejengwa kwa ubia na kampuni za US Bridge na Farm Equip na Midroc Foundation na kusimamiwa na Msimamizi Mshauri Ambicon Engineering.

Mradi wa ujenzi wa gati la Mafi a umegharimu takriban kiasi cha Tshs. 20 bilioni ulianza mwaka 2009 na ulitegemewa kukamilika mwaka 2010.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Mafi a, Wabunge, Viongozi wa Vyama mbalimbali vya Siasa na Wananchi wa Wilaya ya Mafi a na vitongoji vyake.

Akimkaribisha Rais, Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Wizara yake imetimiza kazi ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 kwa kumaliza ujenzi wa gati hilo katika kipindi cha Miaka Mitano ya Ilani hiyo gati ambalo ni la aina yake lililojengwa kwa kutumia fedha za hapa nchini.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabaan Mwinjaka alisema Wizara ya uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari itahakikisha changamoto zilizopo bandarini hapo zinatatuliwa ipasavyo na kusema ili kulinda usalama wa watoto wanapopita katika gati hilo inakusudiwa kuwekwa wavu ili kuongeza usalama, kuweka lami ili hali ya mchanga uliopo uwe ni historia, kujenga gati eneo la Nyamisati na kuhakikisha boya linawekwa kwa ajili ya vyombo vidogo kutia nanga.

Akizungumza katika sherehe hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Madeni Kipande aliwasihi wananchi

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ma-nahodha wa meli ya ‘Pride Of Pangani’ mara baada ya kushusha abiria kwa mara ya kwanza katika gati jipya la Bandari ya Mafi a hivi karibuni.

Inatoka Uk. 1

Uzinduzi

Page 3: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

3

Na Focus Mauki

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wa Mamlaka ambapo amesema tangu alipofi ka kwa mara ya kwanza na kukutana na uongozi na wafanyakazi

kumekuwa na mabadiliko makubwa ya utendaji na ufanisi.

“Nimekuja na furaha kubwa kwenu kwa sababu TPA toka nimekuja mabadiliko makubwa yameonekana, mmenikuna mnachapa kazi kwelikweli, nawapongeza sana,” amesema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe: TPA mmenifurahisha kwa uchapaji kazi wenu

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na Wafanyakazi wakati wa mku-tano. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shabaan Mwinjaka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Madeni Kipande (kulia).

Waziri ametoa kauli hiyo Septemba 14 mwaka huu wakati alipokutana na uongozi na Wafanyakazi katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam. Dk. Mwakyembe pia ametumia fursa hiyo kumtambulisha

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shabaan Mwinjaka ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Inaendelea Uk. 4

Pongezi

Page 4: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

44

Pamoja na kumtambulisha Dk. Mwinjaka, Waziri alisema Wizara imepata Naibu Katibu Mkuu mpya ambaye ni Bibi Monica Mwamunyange.

Wakati huohuo Waziri ameiagiza Menejimenti kuanza kutekeleza muundo wa utumishi ‘scheme of service’ kabla ya mwisho wa mwaka huu, “nafurahi kwamba uandaaji umekamilika lakini sasa utekelezwe haraka iwezekanavyo na isipite mwaka huu pitishieni kwenye Bodi haraka na muanze kuufanyia kazi,” amefafanua Dk. Mwakyembe.

Kwa upande wa ‘fl oating dock’ Waziri ameitaka Menejimenti kuweka katika bajeti yake ununuzi wa ‘fl oating dock’ kwa ajili ya Bandari ya Dar es Salaam. “wekeni kwenye bajeti mnunue fl oating dock kwa ajili ya Bandari ya Dar es Salaam,” amefafanua Waziri Mwakyembe.

Waziri pia imeitaka Menejimenti kutumia wahitimu wa Chuo cha Mabaharia (DMI) kwa ajili ya kutatua tatizo la uhaba wa wafanyakazi uliopo

amesema, “tunao wafanyakazi wachapa kazi na waadilifu na udokozi umepungua kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba nchi ya Zimbabwe sasa inaitumia Bandari ya Dar es Salaam na kusema ni salama sana.”

katika kitengo cha ‘marine’. Katika mkutano huo Waziri aliwaomba wafanyakazi kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu mpya kwa lengo la kupeleka nchi yetu mbele.

Waziri pia amewasifu DOWUTA kwa kutoa ushirikiano na Menejimenti wakati wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wafanyakazi. Kuhusu udokozi waziri

Pongezi

Inatoka Uk. 3

Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti wakifuatilia majadiliano ya mkutano.

Wafanyakazi wakifuatilia mazungumzo katika mkutano.

Baadhi ya Viongozi wa DOWUTA wakijitambulisha kwa mgeni rasmi.

Michezo

Page 5: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

5

Wafanyakazi

Na Mwandishi Wetu

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Madeni Kipande, amesema Uongozi umetekeleza maagizo yote 17 yaliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake aliyoifanya Bandarini

Desemba 21 mwaka jana.

Akijibu hoja hizo zilizotolewa na Wafanyakazi, Mhandisi Kipande amesema, mojawapo ya hoja ilikuwa ni Wafanyakazi kubaki vibarua kwa miaka mingi huku ajira za kudumu zikipewa watu wa nje.

Akijibu hoja hii Mhandisi Kipande amesema tayari Uongozi umelifanyia kazi agizo hili ambapo Menejimenti iliunda kamati kulifanyia kazi jambo hili na kazi na utekelezaji wa uchambuzi wa nafasi umekamilika na kilichobakia sasa ni kufanya mchujo wa awali.

Akitoa ufafanuzi wa mchujo huo, Mhandisi Kipande amesema utafanyika kwa kuangalia waliongia bila kufuata taratibu pamoja na kupata majina ya wanaostahili kupata ajira. Kuhusu hoja ya pili ya marekebisho ya mishahara ya Wafanyakazi kuchelewa licha ya mtaalamu mwelekezi kumalizia kazi yake ya kuandaa ‘scheme of service’, Mhandisi Kipande amesema jambo hili limekamilika na litawekwa wazi.

Baadhi ya hoja ambazo zilijibiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu na kupatiwa ufafanuzi na Kaimu

Mkurugenzi wa Utumishi na Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na Dock Yard.

Agizo lingine kutoka kwa Waziri lilihusisha ‘dock yard’ kutelekezwa na kuachwa bila vitendea kazi na Wafanyakazi wake kutopanda vyeo na kupewa fursa za kujiendeleza kitaaluma. Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema taratibu zinaendelea za kufanyia kazi maagizo ya Waziri, na kwamba jambo la kupanda vyeo tayari limejibiwa kupitia ‘scheme of service.’

Ajira za upendeleoKuhusu TPA kuajiri watu wasio na utaalamu wa mambo ya Bandari na ajira za upendeleo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema jambo hili limefanyiwa kazi na tayari Mamlaka imeingia mikataba na wadau ili kuboresha mafunzo kwa upande wa ‘Marine Serice Staff’ na kwamba katika siku za karibuni wapo Wafanyakazi waliopelekwa Misri, na taratibu zinafanywa kwenda nchi za Afrika Kusini na Singapore.

Wafanyakazi wa mikatabaKatika Menejimenti kuboresha ‘gratuity’ asilimia 25 kwa Wafanyakazi wa mikataba,

Mhandisi Kipande amesema Uongozi umeanza taratibu za kutekeleza agizo la Waziri kwa awamu.

Wadau kufanya kazi saa 24Katika agizo namba saba la Waziri kwa Taasisi zote zilizopo ndani ya Bandari kufanya kazi kwa saa 24, Waziri ameeagiza apewe orodha ya Taasisi ambazo bado zinasita kufanya kazi saa 24 ili achukue hatua mwafaka.

Scanner na MamlakaKuhusu huduma ya ‘scanner’ ambayo Waziri aliiagiza Mamlaka iifunge katika Bandari ya Dar es Salaam, Mhandisi Kipande amesema Uongozi umetenga kiasi cha fedha katika mwaka huu wa fedha ambapo Mamlaka imepanga kununua ‘scanner’ mbili.

MarineKuhusu hoja ya Wafanyakazi wa idara ya ‘marine’ kuhusishwa katika mambo ya Uongozi wa mamlaka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema tayari ‘Harbour Master’ anashiriki katika vikao vyote vya Menejimenti. Kwenye mafunzo ya ‘marine engineering’ Uongozi umeingia makubualiano ya kushirikiana

Mhandisi Kipande: tumefanyia kazi maagizo yote ya Waziri

Inaendelea Uk. 6

Page 6: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

6

Wafanyakazi/DOWUTA

na Bandari kubwa duniani ambapo Wafanyakazi wanne wa Mamlaka watahudhuria mafunzo na jambo hili litakuwa endelevu.

Akitolea ufafanuzi kuhusu mafunzo haya, Kaimu Mkurugenzi wa Utumishi, Bw. Peter Gawile amesema watakaoudhuria mafunzo tayari wamekwisha andaliwa.

Zawadi kwa wafanyakazi wa muda mrefuKuhusu hoja ya zawadi ya mabati na saruji kwa Wafanyakazi wa muda mrefu kwamba haitolewi kwa wakati na hukatwa kodi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema tuzo zimeboreshwa kwa kuongeza kiwango cha zawadi ili kufi dia makato ya kodi.

“Endapo mfanyakazi atapaswa kupewa mifuko 60 ya saruji kama zawadi yake, Mamlaka itamuongezea mifuko 20 ya ziada ili kufi dia gharama za kodi, ambapo baada ya kodi atapata mifuko 60 kamili badala ya pungufu kama ilivyokuwa awali,” amefafanua Mhandisi Kipande.

Mazingira HatarishiKuhusu agizo la Waziri kwa Mamlaka kuboresha vifaa vya kinga katika mazingira hatarishi, Kaimu

Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe amesema tayari Uongozi umechukua hatua madhubuti kwa kuwa na jitihada endelevu za kuwa na mahali salama sehemu ya kazi ambapo mpango huu utahusisha utoaji wa elimu kwa kushirikiana na Idara ya Zimamoto na Usalama.

Bonasi ya MwakaKuhusu hoja ya kulipa Wafanyakazi bonasi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema Menejimenti na DOWUTA imelifanyia kazi jambo hili ambapo lilifi kishwa Wizarani pamoja na hazina ili kupata kibali ambacho tayari kimeshatolewa. “Ndugu Wafanyakazi kibali hiki tumekipata mwezi wa saba mwaka jana, kwa maana hiyo bonasi inatakiwa kulipwa kwa mwaka wa fedha 2012/13, kwa sasa tunafanya ukaguzi wa hesabu za Mamlaka tulipe kuendana na mahesabu,” amefafanua Kipande.

Posho ya mazingira magumuKuhusu posho ya mazingira magumu, Mhandisi Kipande amesema kwa kuwa sio kila mfanyakazi yupo katika mazingira magumu ameagiza kila idara kufanya utafi ti wa nani anastahili kulipwa posho hii ya mazingira magumu ambayo tayari imekwishakubaliwa kwenye vikao vya baraza na DOWUTA na italipwa mapema iwezekanavyo.

Inatoka Uk. 5

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) amesifu juhudi

na jitihada zilizoonyeshwa na wafanyakazi katika kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na kusema kuanzia sasa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka itakuwa na mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (DOWUTA).Waziri amesema, “mmefanya kazi nzuri sana tumekaa na Katibu Mkuu tukasema tuweke nafasi kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya TPA sasa awepo mwakilishi wa chama cha wafanyakazi.”

Waziri amefafanua zaidi kwamba, uamuzi wa nani mwakilishi wa wafanyakazi awepo

itakuwa ni uamuzi wa wafanyakazi wenyewe.

Uamuzi wa Waziri umepokewa kwa furaha na wafanyakazi ambao wameonesha kufurahishwa na jambo hilo kwani sasa watakuwa na uwakilishi katika ngazi ya juu ya Mamlaka.

Waziri amesema wafanyakazi wakionyesha uchapaji kazi mzuri Menejimenti ikazanie motisha kwa wafanyakazi.

Dk. Mwakyembe amesema Bandari ndio kichocheo cha uchumi na kuongeza kuwa anawasifu wafanyakazi kutokana na wizi kupungua ndani ya bandari na kwa upande wa TICTS ambapo pia udokozi umepungua kwa kiwango kikubwa.

Waziri ametumia fursa hii kuwapongeza walinzi wa Mamlaka ya Bandari na kumuomba Katibu Mkuu kuwatafutia motisha mara baada ya kuzuia jaribio la wizi katika kitengo cha SPM.

DOWUTA yapata kiti Bodi ya Wakurugenzi

Page 7: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

7

Ulinzi

Inaendelea Uk. 9

Na Cartace Ngajiro

Askari saba (7) wa Mamlaka wametunukiwa vyeti mara baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi mitatu katika ngazi ya ukoplo yaliyofanyika katika Chuo Cha Maafisa wa Polisi Tanzania kilichopo Kidatu mkoani

Morogoro.Jumla ya askari 15 kutoka TPA, Manispaa ya Temeke, Manispaa ya Moshi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (DUCE) na Chuo Cha Usimamizi wa Biashara (CBE) walipata fursa ya kuudhuria mafunzo hayo yaliyoanza juni 18 na kukamilika septemba 20 mwaka huu.

Askari saba wa Mamlaka wamefanikiwa kuhitimu mafunzo hayo ambapo Mgeni Rasmi Mkuu wa Chuo hicho Kamishna Msaidizi wa

Polisi, Andrew Mwang’onda, aliwapongeza wahitimu kwa kuonesha nidhamu, uvumilivu, na juhudi wakati wote wa mafunzo hayo.

Mwang’onda aliwataka wahitimu hao kuwa chachu katika kupambana na uhalifu na kutoa huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vyema askari walio chini yao kwa kuwa mfano bora na kuleta tija katika maeneo ya kazi.

Askari Saba wa TPA wahitimu mafunzo

ngazi ya Ukoplo

Mkuu wa Chuo cha Maafi sa wa Polisi, Kidatu Kamishna Msaidizi wa polisi Andrew Mwang’onda (wanne kutoka kulia) akiwa na maofi sa wa jeshi hilo katika picha ya pamoja na askari kutoka Taasisi mbalimbali waliohitimu mafunzo ya ngazi ya Ukoplo (Polisi Wasaidizi) katika Chuo Cha Maafi sa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro hivi karibuni. Wa nne kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fortunatus Musilimu ambaye pia ni Msimamizi wa Majukumu ya Kipolisi Kanda ya TPA.

Page 8: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

8

Matukio mbalimb

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akizungumza na Kaimu Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Bw. Edwin Kasyupa (kushoto) wakati ali-potembelea Banda la TPA katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ba-hari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North hivi karibuni.

Wachezaji na wanachama wa BAVE, wakiwa katika picha ya pamoja katika kiwanja cha Mwanakalenga Bagamo

Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Bpamoja.

Page 9: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

9

mbali katika picha

Mfanyakazi kutoka Idara ya Utumishi, Bw. Frank Simbeya ameiaga rasmi kambi ya makapera kwa kufunga ndoa takatifu na mke wake, Bi. Judith Mkude katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa hafl a ya nguvu iliyofanyika katika ukumbi wa Twalipo. Wengine katika picha ni Wafanyakazi kutoka Idara ya Utumishi.

Picha ya pamoja ya wahitimu wa mafunzo ya huduma ya kwanza bandarini Tanga. Wa Tano kutoka kulia ni Muwakilishi wa Mkuu wa Bandari ya Tanga Bwana Bushiri Ramadhani Msangi na kushoto kwake ni Kaimu Af-isa Zimamoto na Usalama Bwana Ramadhani Mapinda. Wa kwanza kulia mstari wa mbele ni Afi sa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Bibi Cecilia Korassa

gamoyo hivi karibuni.

ya BAVE wakiwa katika picha ya

Page 10: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

1010

Ulinzi

Nae Msimamizi wa Majukumu ya Kipolisi kanda ya TPA, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fotunatus Musilimu ametoa pongezi kwa wahitimu na Taasisi zilizowawezesha wafanyakazi kuhudhuria mafunzo na kuwaasa kuwa imara na shupavu katika kukabiliana na uhalifu.

“Nawapongeza kwa dhati wahitimu wote pamoja na Taasisi zenu kwa kuwawezesha kuhudhuria mafunzo haya, mjione ni lulu katika sehemu zenu za kazi na muwe imara na kutekeleza kwa vitendo mafunzo mliyoyapata katika kukabiliana na uhalifu,” amefafanua Musilimu.

Musilimu ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizotajwa na wahitimu hao katika risala yao. Pamoja na changamoto wahitimu hao pia wamewapongeza wakufunzi wao kwa kutumia mbinu shirikishi wakati wa mafunzo, jambo ambalo liliwapa ari ya kujifunza na kuboresha viwango vyao vya uelewa.

Mwanafunzi bora katika mafunzo hayo ametajwa kuwa ni Koplo Peter Bujiku kutoka TPA. Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa likitoa mafunzo katika vyuo vyao kwa askari wanaotoka kwenye taasisi mbalimbali kwa lengo la kujiimarisha kiulinzi katika maeneo yao ya kazi.

Miongoni mwa kozi zilizotolewa katika mafunzo hayo ni pamoja na polisi na uongozi, haki za binadamu na mahusiano ya kijamii, uongozi na usimamizi, sheria na makosa ya jinai, sheria ya mwendo wa makosa ya jinai, sheria ya ushahidi, afya ya jamii na ulinzi wa mazingira.

Kozi nyingine ni stadi za mawasiliano, matumizi ya silaha na usalama, mafunzo ya jumla pamoja na gwaride maalumu.

Koplo Joseph A. Nyoni

Koplo Peter Bujiku

Koplo Shabani I. Hegga

Koplo Kelvin Millanzi

Koplo Peter Madiya

Koplo Zahoro M. Kiumbi

Koplo Omary Makame

Inatoka Uk. 7

Page 11: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

11

Ulinzi

Koplo, Peter Bujiku wa TPA wa pili mstari wa nyuma akiwa na wahitimu wezanke kutoka Taasisi mbalimbali kwenye Gwaride katika sherehe ya kufunga mafunzo ya polisi wasaidizi ngazi ya koplo yaliyofanyika chuo cha maafi sa wa polisi Kidatu Morogoro hivi karibuni.

Mkuu wa Chuo cha Maafi sa wa Polisi, Kidatu Kamishna Msaidizi wa polisi Andrew Mwang’onda (wanne kutoka kulia) akiwa na maofi sa wa jeshi hilo katika picha ya pamoja na askari kutoka Taasisi mbalimbali waliohitimu mafunzo ya ngazi ya Ukoplo (Polisi Wasaidizi) katika Chuo Cha Maafi sa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro hivi karibuni.

Page 12: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

12

Mkutano mkuu waBandari Veterani wafanyika Yapongezwa kwa kuwa na wanachama wengi Muasisi Keny Mwaisabula astaafu Mkutano mwingine kufanyika Mombasa

Mwenyekiti wa Bandari Veterani akimkabidhi kapteni wa timu ya Bagamoyo, Veterani, Widy Steven kitita cha pesa kama mchango kwa timu hiyo.

Na Innocent Mhando

Bandari Veterani (BAVE) imefanya mkutano wake mkuu wa mwaka katika ukumbi wa “Double M” mjini Bagamoyo hivi karibuni na kupongezwa kwa kuongeza wigo wake wa wanachama. Mgeni Rasmi katika mkutano huo Meneja Rasimali watu Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Jones Macha amepongeza juhudi za umoja huo wa maveterani kwa kuhusisha wafanyakazi kutoka vituo vingine ikiwemo Makao Makuu na Bandari ya Tanga.

Akizungumzia jambo hilo Mwenyekiti wa BAVE, Mangasa Sosela amesema kwa sasa chama kimejitanua ambapo mbali na kuwa na wanachama

kutoka Bandari ya Dar es Salaam pia wapo wanachama kutoka katika Bandari nyingine.

Akizungumizia maendeleo ya chama yaliyofi kwa mpaka sasa Sosela amesema chama kimetanua mipaka yake na kifi kia hatua ya kusaidiana miongoni mwa wanachama katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo misiba, harusi na matukio mengine mbalimbali.

Sosela ametoa wito kwa vijana ambao ni wafanyakazi wa Bandari kujiunga na kikundi hicho kwani kina manufaa mengi mojawapo ikiwa ni kushiriki katika mabonanza ya michezo, kujenga afya na kuimarisha utendaji kazi.

“Vijana ambao ni wafanyakazi wa mamlaka nawahusia washiriki katika mabonanza mbalimbali ikiwemo ya maveterani hii itawajenga kiafya hata baadae wakifi kia umri kama

Michezo

Page 13: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

13

JIC

Shabiki namba moja wa timu ya Bandari Veterani, Fred Temu “Papaa Temu” akitoa mawaidha kwa maveterani mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

kuwa mlezi wa kikundi baada ya aliyekuwa Mlezi wao Fredrick Mdemu kustaafu kazi ombi ambalo Macha ameahidi kulifi kisha.

Wakati huohuo Bandari Veterani imepitisha ombi la kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Bw. Keny Mwaisabula ambapo wananachama kwa pamoja walipitisha ombi hilo kwa kupiga kura. Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka unatarajiwa kufanyika mwakani mjini Mombasa Kenya.

Katika kikao hicho wana BAVE walikusanya jumla ya shilingi laki moja na elfu nne na kuikabidhi kwa kapteni wa timu ya Bagamoyo Veterani, Bachu Pishok ikiwa ni ubani kwa

kufi wa na mmoja wa mchezaji wake.

Bandari Veterani “BAVE” ambayo ilianza rasmi kazi zake mwaka 2006 imeasisiwa na Keny Mwaisabula, Marehemu Celina Lukindo, Juma Taliata, Hassani Hemedi, Method Andrew na Anthony Kifaro ikiwa na lengo la kuimarisha na kutunza afya za wananchama wake.

BAVE ilianza ikiwa na wanamichezo waanzilishi 15 kutoka Bandari ya Dar es Salaam pekee ambapo mpaka sasa imefanikiwa kufi kisha wanachama 91 na juhudi za kupanua shughuli zake zinaendelea.

wetu itakuwa rahisi kuwapa jukumu la kusimamia kikundi na kuboresha afya zao kwa ujumla,” ameongeza Sosela.

Kwa upande wao wanachama wa BAVE wameushukuru uongozi wa Mamlaka kwa kuwawezesha kushiriki katika mkutano huo na kuomba ushirikiano huo udumishwe. Wanachama hao wametaja changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na ugumu katika kukusanya michango ya wanachama kutokana na kusitishwa kwa utaratibu wa ukusanyaji wa ada kupitia mishara ya kila mwezi yaani “Payroll”.

Pamoja na hayo wanachama wamemuomba Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam

Michezo

Page 14: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

14

Tumieni elimu mliyoipata kusaidia

Jamii MsangiNa Cecilia Korassa

Mwakilishi wa Mkuu wa Bandari ya Tanga Bw. Bashiri Msangi amewaasa wahitimu wa mafunzo ya Huduma ya Kwanza ‘First Aiders’ kutumia elimu waliyoipata kikamilifu.

Msangi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la “Bandari House” mjini Tanga hivi karibuni.

“Nyie mnaomaliza mafunzo haya leo, mnatakiwa muwe mstari wa mbele popote pale ambapo kutakuwa na tukio linalohitaji kuokoa jamii. Iwe nyumbani, barabarani, sehemu ya kazi au mahali popote kwenye tukio ambalo huduma ya kwanza inahitajika, muwe wa kwanza kusaidia. Mmepata mbinu nyingi hivyo mkazitumie ipasavyo,” amesisitiza Msangi.

“Tuipende huduma hii ili tuweze kuifanya kwa moyo mmoja kwa kujituma wenyewe bila kushurutishwa na endapo litatokea tatizo inabidi kuwajibika kwa upendo, ili kuokoa maisha ya watu wengine,” amefafanua zaidi Msangi.

Kwa upande wake mhitimu wa mafunzo hayo Bw. William Elias wa Idara ya Zimamoto na Usalama, ameushukuru Uongozi wa Bandari Tanga kwa kuwapatia mafunzo hayo, ambayo amesema yamekuwa ni muhimu na kuuomba uongozi kuwapatia mafunzo kama hayo wafanyakazi wengine.

“Hivi sasa magonjwa ni mengi, ajali ni nyingi, hivyo sote tukiyajua haya tutakuwa

Bwana William Elias wa Idara ya Zimamoto na Usalama Tan-ga, akifafanua jambo wakati

wa ufungaji wa mafunzo ya Zimamoto na Usalama katika Bandari ya Tanga.

tumeisaidia jamii, lakini pia tumekumbana na changamoto ya kuwa na muda mfupi wa mafunzo na tunaomba Uongozi

Elimu

Page 15: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

15

uongeze muda wa masomo,” amefafanua Elias.

Amebainisha changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa vifaa vinavyotumika kufanyia mazoezi kwa vitendo na kupatiwa vitambulisho vitakavyowarahisishia kutoa huduma ya kwanza wakiwa eneo la tukio.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Zimamoto na Usalama Bandari ya Tanga, Bw. Ramadhani Mapinda amesema mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Zimamoto na Usalama kwa kushirikiana na taasisi ya ST. John Ambulance, Tawi la Tanga.

Mapinda amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapatiwa huduma kwa haraka na umakini pale inapotokea ajali kabla ya kumfikisha majeruhi kwa daktari kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa wiki moja na yamehusisha wafanyakazi 20 kutoka Idara mbalimbali za Bandari ya Tanga ambapo hadi sasa Wanafunzi 52 tayari wamenufaika na mafunzo hayo tangu yaanzishwe mwaka 2010.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara mbalimbali katika Bandari ya Tanga ambao walihudhuria mafunzo ya huduma ya kwanza.

Pichani ni Muwakilishi wa Mkuu wa Bandari Tanga Bwana Bushiri Ramadhani Msangi akifunga mafunzo ya huduma ya Kwanza katika ukumbi wa mafunzo Bandari House Tanga. Kushoto ni Afi sa Ma-wasiliano Mwandamizi Bibi Cecilia Korassa

Elimu

Page 16: Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es ... · kwenye gati, ni mbali, kwa Kijana atakwenda mchakamchaka, kwa mtu mzima ni umbali mrefu, kwa mgonjwa ni maili elfu moja”, alichagiza Rais

1616

ADO ADO

Ndugu zangu wastaafu, Ujumbe pokeeni Ujumbe mintarafu, Utieni akiliniNawaombea raufu, Msiutupe kapuni Mwaondoka na vinono, Muendako adoado

Tahadhari chukueni, Ndugu zangu nawaambia Halahala mitaani, Msije kuangamia Mafao yenu chungeni, Majambazi yazengeaMwaondoka na vinono, Muendako adoado

Majambazi wapo wengi, Hila nyingi hutumia Wako watakwita dingi, Meno wakukenulia Sifa iso na msingi, Mafao kukuchomoa Mwaondoka na vinono, Muendako adoado

Vimini mtavaliwa, Minyama kutingishiwa Macho mtarembuliwa, Sauti talegezewaNa tai mtafungiwa, Ni mitego metegewaMwaondoka na vinono, Muendako adoado

Elimu mumeshapewa, Kuyalinda mafaoJizuie Kupagawa, Usemee wako moyoBure wachanganyikiwa, Lilaani hilo payoMwaondoka na vinono, Muendako adoado

Kuepuka Migogoro, Shirikishe familiaKamilisheni viporo, Nyuma vilivyobakiaZijadilini kasoro, Malengo kujiwekeaMwaondoka na vinono, Muendako adoado

Mwite mkeo karibu, Mueleze yalojiriMume kwa mke Tabibu, Watoto msiwasiriHuo ndo Utaratibu, Wafamilia JASIRIMwaondoka na vinono, Muendako adoado

MDIKANG’ANDU ARS (GHOSHI – JA - MBAZI)TANGA PORT CONTROL TOWERSimu: +255 784/0715390684

WASOMI OYEE

Bandari imeshamiri, Watu wake kujisomea,Waenda ka utitiri, Vyuoni huelekea,Ni moyo wa kijasiri, Unataka kuamua,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Kwa sasa ina hazina, Ya wasomi wenye vyeti,Wamefanya la maana, Katika shirika nyeti,Vyeti vimeongozana, Wamejipandisha chati,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Nitawataja wachache, Kwa majina gazetini,Mwenye nyingi hachehache, Abiduna Athumani,Malombe asijifiche, Ni msomi kajihini,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Ndeshi na Mchalaganya, Chuoni wajisomea,DMI nilihenya, Kitabu nilibukua,Kitentya aisanya, Shahadaye ya sheria,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa

Gwamala Kitangalala, Yumo Fikiri Msiba,Manga Gasaya Kaula, Mtunze Sudi Yeba,Kimario hajalala, Elimu kwake ni tiba,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Ombi langu kwa wasomi, Mlotunukiwa vyeti,Utumieni usomi, Bandari ipande chati,Muachane na umimi, Kutambiana kwa vyeti,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Jicho letu liko kwenu, Nini mtatufanyia,Kiburi si haki yenu, Ni kisare cha jalia,Epukeni usununu, Mungu atawajalia,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

Ambao hawajasoma, Hima wajibiidishe,Elimu haina koma, Tupunguze mishemishe,Binadamu ukisoma, Hazikutishi kashehe,Hongera wafanyakazi, Shahada kutunikiwa.

MDIKANG’ANDU ARS (GHOSHI – JA - MBAZI)TANGA PORT CONTROL TOWERSimu: +255 784/0715390684

Malenga