14
www.memorybooks.org.uk JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu This version of the original Memory Book was written in October 1999 with the help of many NACWOLA mothers who had made Memory Books for their children. Special thanks to Kayondo Farida, Kyabita Janet, Nabwire Jacqueline, Nakabazzi Rebecca, Nakku-Namagembe Irene, Nankabirwa Eleonor, Nazziwa Yudaya, Oundo Jane, and Were Beatrice. Carol Lindsay Smith, Rory O'Brine © 2006 Tafsiri: Shirika la Kuendeleza Makuzi, Malezi bora, Madili mema na Ustawi wa Familia - Adilisha Uhariri na Mpangilio: Michael Kimaryo Vielelezo: Jimmy Kisula Mwongozo wa Wosia: Chatles Mkude

JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

  • Upload
    others

  • View
    30

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

www.memorybooks.org.uk

JinsoYa KuandikaKitabu Cha

Kumbukumbu

This version of the original Memory Book was written in October 1999 with the help of manyNACWOLA mothers who had made Memory Books for their children. Special thanks toKayondo Farida, Kyabita Janet, Nabwire Jacqueline, Nakabazzi Rebecca, Nakku-NamagembeIrene, Nankabirwa Eleonor, Nazziwa Yudaya, Oundo Jane, and Were Beatrice.

Carol Lindsay Smith, Rory O'Brine © 2006

Tafsiri: Shirika la Kuendeleza Makuzi, Malezi bora, Madili mema na Ustawi wa Familia - AdilishaUhariri na Mpangilio: Michael Kimaryo

Vielelezo: Jimmy KisulaMwongozo wa Wosia: Chatles Mkude

Page 2: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

Makala hii ya Kitabu cha Kumbukumbu ni pamojamiongozo kwa wazazi, walezi na wasaidizi, vilevile nimapendekezo ya kurasa za vichwa vya habari au suraza kutosheleza habari muhimu ambazo watoto wanahitajikufahamu kutoka kwa wazazi wao.

Kwa busara inashauriwa kwamba, mtu yeyote ambayeangependa kujishughulisha na shughuli hii kamamkufunzi, mhudumu au mwandishi asome maandishihaya kwanza.

♦ Sehemu ya kwanza inatoa habari za kusaidiawakufunzi au viongozi wa jumuia kuelezeamawazo ya Kitabu cha Kumbukumbu kwa familiambalimbali.

♦ Sehemu ya pili inatoa mawazo kwa wazazi auwalezi wanaowatunza watoto kufikiria kabla

ya kuanza utengenezaji wa Kitabu chaKumbukumbu.

♦ Sehemu ya tatu inahusu mawazo ya j insi yakuanza uandishi wa Kitabu chaKumbukumbu.

♦ Sehemu ya nne inaelekeza kurasa au sura za vichw avya habari ili kutosheleza historia yafamilia na habari muhimu za kila mtoto.Sehemu hii inajumuisha mawazo kuhusuvipengele vilivyomo katika kila kichwa chahabari.

♦ Sehemu ya tano inahusu UKWELI MUHIMUambao watoto wanahitaji kuufahamu zaidi kwenyefamilia zao na historia binafsi.

1

Utangulizi KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 3: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

1.1 KITABU CHA KUMBUKUMBU NI NINI?Ikiwa wazazi watafariki au watatengana wakati watotowakingali wachanga kumbukumbu muhimu hutoweka, hiihuwafanya watoto kukua bila kujitambua wao ni nani.Siku hizi si rahisi watoto kujifunza habari za familia zaokutoka kwa wazazi wao kama hapo zamani. Hivyokuandika Kitabu cha Kumbukumbu ni muhimu sana.

Kitabu cha Kumbukumbu hutoa mwongozowa kuwasaidia wazazi, ndugu au marafikikuhifadhi habari mahususi kuhusiana nachanzo cha familia zao

Kitabu cha Kumbukumbu hakiwakingi watoto dhidi yaukiwa wa kifo cha wazazi wao ama walezi wao aumifarakano iliyopo kati ya wazazi wao. Lakini Kitabu hikikitawaelezea kuhusu asili yao, ukoo, mila, utamaduni,desturi na imani za kifamilia, pamoja na maisha ya utotonimwao. Watafahamu yaliyopita na kuwawezesha kuwawajasiri na imara wa kukabili yale yajayo.

1.2 WAZO HILI LILITOKA WAPI? Wazo la awali la kutengeneza vitabu vya Kumbukumbu lil-ianzishwa huko Uingereza mnamo mwaka 1993 na shirika laBarnardos lililowafadhili wazazi Waafrika walioishi jijiniLondon. Wazazi hawa waliathirika kwa VVU/UKIMWIhivyo walihofia kufariki wakati watoto wao wangali wadogo.Kwa sababu ya watoto kukulia nchi ya ugenini walihisi kuwawatoto hao watapoteza mahusiano na ndugu zao na nchi zaoza asili. Hivyo wazazi walihamasika kuandika mambo yakihistoria , habari muhimu za kifamilia na mazingira ya nduguzao mbalimbali wa ukoo. Wazazi hao walitaka kuendelezaimani na tamaduni zao vilevile kuonyesha matumaini yao juuya hatima za watoto wao.

Walidhamiria kuwaachia watoto wao urithi wamaneno ya busara na kumbukumbu muhimuna missing ya kuishi nayo.

Mnamo mwaka 1995na 1996 wazo la uandishi wa Kitabucha Kumbukumbu lililetwa Uganda na kuanza kufanyiwakazi na Bi. Beatrice Were (Mratibu wa Jumuia ya Kitaifa yawanawake Wanaoishi na VVU/UKIMWI- NACWOLA),kama njia muafaka ya kusaidia wazazi kuzungumzia waziwazi kuhusu UKIMWI kwa watoto wao. Uzoefu waoulionyesha kwamba wazo hilo liliweza kueleweka kwaurahisi kwa watu wa tamaduni mbalimbali na viwango mbal-imbali vya elimu. Kitabu cha Kumbukumbu cha sasa kimezingatia mchangowa mawazo na uwazi waliouonyesha akina mama hawawaasisi.

Tangu 1993 pamoja na kazi ya NACWOLA ya mwaka19995/6, mawazo ya Kitabu cha Kumbukumbu yamesambaaulimwenguni pote. Mashirika mengi makubwa ya Kimataifa

yanayojishughulisha na Watu Wanaoishi naVIRUSI/UKIMWI yamekuwa yakitumia mawazo ya kitabuhiki kwa kukinukuu, kutafsiri ama kuongezea maelezo zaidikwa yale ya awali ili yaweze kufaa.mazingira yao halisi. Kwasasa maelfu yawezekana mamilioni ya wazazi na waleziwamekwisha fanya maajabu kwa kutengeneza vitabu vyakumbukumbu, masanduku ya kumbukumbu, vikapu vyakumbukumbu hata mikoba ya kumbukumbu Hii ikiwa nikatika jitihada za kuweza kutunza kumbukumbu,habari,maelezo na vito vya thamani kwa ajili ya kuwahamasishawatoto kuwa na msingi imara juu ya utambulisho wao.

Ni muhimu kutosahaurika kwa kaziiliyoanzishwa na familia za Kiafrika walioishijiji la London na ile ya wenzi wao wa shirika laakina mama la NACWOLA- Uganda ambaondio walio kuwa wa kwanza kuzungumzia kwauwazi kuhusu kuathrika kwa afya zaokutokana na janga la UKIMWI.

1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI?Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi wao wameathirika naVVU/UKIMWI hii ilikuwa ni kuwarahisishia wazazi haokuwapatia watoto wao taarifa muhimu za kifamiliawatakazo hitaji wakati wanapokua. Pia wazo la Kitabu chaKumbukumbu limekuwa ni wazo la msaada kwa watotowaishio katika mazingira magumu hasa yatima nawaliotengana na wzazi wao kwa sababu zozote zile. (Ikiwawazazi au ndugu wakaribu wa ukoo hawapo kwa ajili yakuandika kitabu, taarifa zinaweza kukusanywa kutokakwa majirani, wanajamii, walimu ama kwa yeyote yuleanayeifahamu familia hiyo).

1.4 KUTAFUTA UELEWA WA WATOTO WANAJUA JAMBO GANI.Hata hivyo kutengeneza Kitabu cha Kumbukumbukunahitaji kufahamu au kutafuta kila mtoto anaufahamugani binafsi juu ya chimbuko la familia yake. Kwa njiamoja au nyingine ni muhimu kwa watoto ambao tayari niyatima au wametengana na wazazi wao kutoka kwenyefamilia kutafuta wanakumbuka nini kuhusu chimbuko lafamilia zao. Kazi hii inahitajika kufanyika mapema bilakuchelewa kwa sababu ya kukabili msongo mawazo wawatoto juu ya mifarakano ya wazazi, kufiwa wazazi nauhamaji wao unaweza kuwaacha watoto wamechanganyikiwakuhusu ukweli wa mambo mbalimbali.

1.5 NANI ANAWEZA KUTENGENEZA KITABU CHA KUMBUKUMBU? NI WAKATI GANI ULIO SAHIHI?

Mtu yeyote anaweza kutengeneza Kitabu chaKumbukumbu, watu wengi walioshiriki katika mradi huuushauri kuwa ni suala ambalo watu wote tunapaswakulifanya.

2

1. Habari Kwa Wakufunzi Na Viongozi Wa Vikundi KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 4: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

♦ Hakuna haja ya kusubiri kuugua au kuwepomifarakano katika familia kabla ya kuanzakuandika.

♦ Wazazi wanaweza kutengeneza kitabu chao binafsikwa kila mtoto au kitabu kikubwa cha familia yotena kitunzwa sehemu maalamu inayoeleweka.

♦ Watoto wakubwa wasichana kwa wavulanawanaweza kusaidia kutengeneza kitabu kwa ajiliya wadogo zao katika familia.

♦ Ndugu au walezi wanaweza kutengeneza kitabucha Kumbukumbu kwa yatima au watotowaliotengwa walio chini ya uangalizi wao.

♦ Utengenezaji wa kitabu cha Kumbukumbuunaweza kuwa mradi kwa ajili ya ukoo au jumuiya.

♦ Taarifa ndani ya kitabu cha Kumbukumbuzinaweza kuongezewa kadri miaka inavyokwenda.

♦ Watoto wakielewa kuhusu kitabu chaKumbukumbu wanaweza pia kushiriki kwa kuulizamaswali, kutafuta picha na kuongezea habari zaokadri wanavyokua na kunapotokea mabadiliko.

1.6 KUJIWEKA WAZI (DISCLOSURE). Wazazi wengi waishio na VVU/UKIMWI hubeba mzigomzito wa siri; wanahofia ni lini, kwa namna gani na wapiwaweze kuwa wazi kwa watoto wao. Uzoefu wa akinamama wa NACWOLA ni kwamba, wakati walipoanzakutengeneza Kitabu cha Kumbukumbu kiliwasaidia kuanzakuzungumza katika njia ya kawaida kuhusu janga laUKIMWI na matatizo mengine katika familia. Baadayewalipata ujasiri wa kuanza kutengeneza mipango yaoya baadaye na ikawa rahisi kuwaandaa watoto waokukabiliana na kupoteza wazazi pia mabadiliko yatakayoweza kujitokeza siku za usoni. Mwishowe waligunduakuwa upya huu wa uwazi na uaminifu uliwaondolea mzigokatika mioyo yao. Walipata nguvu na matumaini yakukabiliana na magumu mbalimbali katika siku zao za usoni.

1.7 WAZAZI WANAWEZA KUPATA MSAADA WAPI WA KUANDIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU?

Mnamo mwaka 1996 na 1997 NACWOLA ikisaidiwa nashirika la Save the Children Uganda (UK) walianzisha mradiwa mafunzo ya uandishi wa Kitabu cha Kumbukumbu kwawazazi waishio na VVU/UKIMWI. Mafunzo hayo ni ya siku5 yalihusu namna ya uandaaji wa Kitabu cha Kumbukumbupia yalijumuisha masuala mengine ya malezi kwa wazazi/waleziyakiwemo:

♦ Habari kwa wazazi juu ya maendeleo ya makuzi yamtoto;

♦ Mawazo juu ya namna na lini kuanzakuzungumuza wazi kuhusu maradhi na matatizomengine katika familia;

♦ Uhamasishaji wazazi kuhusu kupanga mipango yabaadaye, ushauri, vitendo vya kuandaa wosia namirathi, mipango ya kuandaa walezi sawia naulinzi wa mali;

♦ Mapendekezo ya njia za kurithisha maarifa nastadi zitakazowasaidia watoto kukabili siku zausoni kwa uimara na kujiamini.

Upatikanaji wa taarifa hizi na mafunzo mengineyoyamejumuishwa katika tovuti ya Kitabu cha Kumbukumbu.Vipengele muhimu vya mpango wa mafunzo juu ya Kitabu chaKumbukumbu pia vimeingizwa katika tovuti. Wakati huo huomashirika au wazazi binafsi wanaotaka nakala ya Kitabu chaKumbukumbu Kwa Afrika wanaweza kuwasiliana moja kwamoja na shirika la "Teaching Aids at Low Cost" – TALC P.OBox 49, St. Albans, Herts AL1 5TX UK. Simu + 44 (0) 1727853869. Barua pepe - [email protected] au kwenye tovutiwww.talcuk.org.

Waweza pia kuwasiliana na Shirika la Malezi bora na MaadiliMema la ADILISHA nchini Tanzania, linatoa mafunzo juuya uandishi wa Kitabu cha Kumbukumbu. SLP 11098 Mwanza –Tanzania:- Simu +255 028 2540864Barua pepe [email protected] Tovuti:- www.Adilisha.com

1.8 JE, WAZAZI WANAWEZA KUFANYA KAZI HII PEKE YAO?Hakuna wasiwasi ni vizuri sana wazazi kufanya kazi

hii pekee yao, lakini ni vema zaidi wazazi hawa kupatamsaada wakati wa kutengeneza Kitabu chaKumbukumbu. Kwa sababu ya kuweza kuhimili misisimukopia majonzi yanayoweza kujitokeza wakati wa uandishivilevile wakati wa kujiweka wazi kwa kwa watoto.Lakini, hat kama hakuna kikundi cha kijamii wazaziwengi wameonyesha kuwa wanaweza kufanya vizurikwa kufuata mwongozo huu. Inapobidi wazazi uhitajimsaada kutoka kwa rafiki mwaminifu ama mtu yeyoteambaye humuzungumzia kumbukumbu zenyemichomo pia kumsaidia muzazi kutafakari majibu yamaswali ya kitundu ya watoto. Baada ya kazi zaokukamilika watahitaji watu wa kuwasaidia kusheherekeamafanikio yao makubwa waliyo yapata.

1.9 JE , WAZAZI WANAWEZA KUTEKELEZA KAZI HII WAKIWA TAYARI WAGONJWA AU WAMETENGANA NA WATOTO WAO?

Uzoefu unaonyesha kuwa hata wazazi wanapokuwawagonjwa sana au wana msongo wa mawazokutokana na kutengana wanaweza kusaidiwa kutoahabari kwa watoto wao. Njia mojawapo ni rafiki aumsaidizi, msimamizi/mlezi kupitia vichwa vya habariza Kitabu cha Kumbukumbu kwa kuuliza maswala nakuandika majibu. Rafiki wa karibu na ndugu wa ukoowanaweza kukumbuka historia na hadithi kuhusuukuaji wa watoto. Kila habari ina thamani kwa watoto.Wazazi wenyewe wataliwazika kwa sababu watakuwawamefanya kila wawezalo kuwapatia watoto taarifa zaukweli kuhusu utambulisho wao.

3

1. Habari Kwa Wakufunzi Na Viongozi Wa Vikundi KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 5: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

2.1 KWA NI NINI KUANDIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU? Watoto wote wanahitaji kujua kuhusu chimbuko la famil-ia zao na habari binafsi zinazowahusu, Kitabu chaKumbukumbu husaidia kuandika ukweli juu yako piamatarajio ya mbeleni juu ya wanao. Hiki ni kitu halisiambacho utawapatia watoto wako. Wakati wowote katikamaisha ya usoni mwa watoto, kila mara watakuwa naukweli utokanao na maneno yako mwenyewe. Hivyo kilamara watajua WAO NI NANI. Wataweza kufahamumaelezo ya maisha yao ya utotoni hata kama watakumb-wa na migogoro katika familia

2.2 JE, MAMBO GANI YA KUWEKA? Kurasa muhimu katika Kitabu cha Kumbukumbu nihabari kuhusu taarifa za wazazi wote wawili na maisha yamakuzi ya kila mtoto. Unaweza kuandika kuhusu imani namaisha unayoishi pia matarajio yako kwa wanao hapo

baadaye. Unaweza pia kueleza mila na matukio yaliyomuhimu katika familia na kwenye ukoo. Unaweza kukum-buka nyakati za furaha na mizaha ya kifamilia. Unawezakuongezea methali, misamiati, vitendawili na misemomuhimu itumikayo katika familia na kwenye ukoo wenukwa jumla. Aidha elezea njia zitumikazo kuadilisha wato-to, kuwafundisha majukumu yao mbali mbali ya kifamiliahasa maarifa ya upishi, kilimo na ufugaji. Toa taarifa zandugu zako wa ukoo na marafiki, tengeneza mti wa famil-ia pia chora ramani kuonyesha mahali ulipo zaliwa piaulipohamia, sehemu za makaburi ya wanafamilia.Maelekezo na ushauri jinsi ya kukamilisha mada zote ukokatika sura ya 5.

2.3 KUKABILI MADA NGUMU.Kumbukumbu hizi hazilengi kukumbusha vifo au majangabali kuwasaidia watoto kujitambua wao ni nani na kuwap-atia taarifa sahihi zitakazowasidia wafanikiwe maishani

mwao. Habari za masikitiko kuhusu maradhi na misibaitashughulikiwa kwa urahisi kama taarifa zimetolewa kwamlinganisho wa kumbukumbu, habari za vitendo maishanimwako na mipango ya hapo baadaye kwa wanao.

Kila Kitabu cha Kumbukumbu kitakuwa na taarifatofauti kwa kila mtoto na kadri utakavyo endelea kuandi-ka utakuwa unapata uzoefu na mawazo mapya na sahihijuu ya kutengeneza Kitabu chako cha Kumbukumbu.

2.4 NITAJISIKIAJE? Wakati unapokuwa unaandika Kitabu cha Kumbukumbu,baadhi ya maelezo yatakuwa yanakukumbusha vipindi vyawakati mzuri na mbaya. Unatakiwa kutafuta maneno yakuelezea hali yako ya sasa, matumaini yako na hofu zakojuu ya maisha ya mbeleni ya wanao. Kumbuka maishayako ya nyuma na kuandika ukweli wake wakati mwinginekutakutia huzuni, na ikawa kazi ngumu kwako, hasa

endapo maisha yako yote hayakukuendea kamaulivyokuwa umekusudia. Lakini wazazi wengi wamewahikusema kwamba kukumbuka, kuzungumza na hatimayekuandika kitabu cha kumbukumbu kumeweza kuwapatiaamani akilini mwao. Mwishowe wameweza kuwa hurukabisa kuendelea na maisha yaliyobaki.

2.5 JE, NI NANI ANAYEWEZA KUNISAIDIA KUCHAMBUA VIZURI HABARI ZANGU?

Wakati utakapoanza kuandika kitabu hiki, mawazo mengiyatajaa kichwani mwako, hata kukuchanganya. Itakuwavigumu kwako kuelewa uanzie wapi na wazo lipi. Katikahali hii unashauriwa kumweleza rafiki yako wa karibu juuya mawazo hayo, ili aweze kukusaidia kukumbushamatukio yaliyopita na kuyapanga katika lughaitakayoweza kueleweka kwa watoto watakapokuwawakiyasoma.

4

2. Habari Kwa Wazazi Na Walezi Wengine Wanaotunza Watoto KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 6: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

2.6 JE, LINI NINAWEZA KUANZA KUANDIKA KITABU CHAKUMBUKUMBU?

Kazi hii haiwezi kumalizika kwa siku moja, hivyo usipendekusubiri hadi ukapatwa na tatizo. Anza kuandika mapemaiwezekanavyo, ukikumbuka kuwa utakapokamilishakuandika utakuwa umejipunguzia mzigo mzitoulioubeba.

2.7 JE, NINAWEZA KUANDIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU IKIWA SIJUI KUANDIKA?

Watu wengi inawawia vigumu sana kuandika kitabu chakumbukumbu, na hasa wanapokuwa na maradhiwaliyonayo pamoja nahisia zenye maumivu. Wazo mojani kuwa wanashauriwa kumwona rafiki au mtoto waoaweze kukusaidia kuandika. Mtu huyu atakuuliza maswalikulingana na kurasa au sura zilizomo kwenye mwongozohuu. Ni muhimu umjibu kwa sauti kubwa ili aandike yaleunayoyasema mwenyewe.

2.8 JE, NI SAHIHI WATOTO KUSHIRIKI KATIKA KUANDAA KITABU CHA KUMBUKUMBU?

Wazazi wengi wamesema inasaidia endapo utawafahamishawatoto wako unachokifanya na kuwashirikisha katika uan-daaji wa kitabu hicho. Wanaweza kukusaidia kutafutapicha za foto, kuchora picha ndani ya kitabu, piakuandika habari mbalimbali za familia. Hii inawapa piafursa ya wao kukuuliza maswali yatakayowaondolea hofuwalizo nazo na kuhusu mambo yatakavyokuwa siku zausoni. Maisha ya familia yanakuwa na unafuu palemnapoweza kuongea kwa uwazi miongoni mwenu.Watoto wanapoelewa matatizo ya familia, mara nyingihuwawezesha kuchukua majukumu zaidi. Hata watotowadogo kabisa wanaweza kuchangia kwa kukumbushianyakati za furaha, watu waliowafurahisha na kuchorapicha zitakazoingizwa kwenye kitabu.

Wakati mwingine watoto watapendelea kutengenezakitabu chao wenyewe. Hali hii itawasidia sana kwani watotowanaweza kuongeza habari zao zitakazowasaidia kubadilishamaisha yao. Ni jambo jema wakalinganisha maisha ya wakatiuliopita na yale ya ule ujao.

2.9 JE, NI LINI WATOTO WATAKIONA KITABU CHAO CHA KUMBUKUMBU?

Kama watoto waliwasaidia wazazi wao kuandika kitabu,hakuna siri tena.Lakini baadhi ya wazazi wanaamuakukitunza Kitabu cha Kumbukumbu mpaka baada ya vifovyao au mpaka watato watakapo kuwa wakubwa. Kamaunaogopa kwamba unaweza kufa au kutengana na watotowako kabla hawajakiona Kitabu cha Kumbukumbu,

unahitaji kumkabidhi mtu ambaye unamwamini atakitunzahadi muda utakapofika.Huyu anatakiwa kuwa mtumakini, anayekufahamu vizuri na ambaye ataweza kujibumaswali yatakayoulizwa na watoto baada ya kusomahistoria ya familia. (Maelekezo megine yako sura ya 5)

2.10 JE, NIFANYE NINI NA TAARIFA NGUMU?Unaweza ukadhani kuwa mambo mengine yanaumizasana au ni ya binafsi sana kuweza kuyaandika kwenyeKitabu cha Kumbukumbu ambacho kitasomwa nawatoto wako. Au kinaweza kuwa na taarifa za siriambazo hutaki zijulikane kwa watu wengine ambaowatasoma kitabu hicho. Mathalani, taarifa kuhusukilichosababisha kifo cha mzazi au kuvunjika kwandoa.Unachoweza kufanya ni kuandika kumbukumbuza matukio ya huzuni kwa kifupi sana kwenye kitabu.Halafu andika barua tofauti yenye taarifa za kina zaidina umkabidhi mtu unayemwamini aitunze hadi watotowakue vya kutosha kuweza kusoma wenyewe.(Hakikisha unadokeza kwenye Kitabu chaKumbukumbu ukionesha nani mwenye barua hiyo).Hata hivyo, watoto wako ikiwa ni wakubwa vya kutoshani vizuri zaidi ukawaeleza wewe mwenyewe. Kitumuhimu ni kutafuta njia ya kuwaeleza watoto ukwelikatika maneno yako wakati huo huo ukijaribukutokutoa maamuzi au kuwalaumu wengine maamuzi.

2.11 JE, NIFANYE NINI KAMA SINA MAJIBU YOTE? Kama baadhi ya taarifa zinakosekana, ni vizuri kuachanafasi wazi kama lilivyo au kusema sina uhakika wa ukweliwa habari. Vinginevyo kama watoto wakigundua baadayekuwa baadhi ya vipengele vilivyoandikwa vimekosewa,watashindwa kujua kipi cha kuamini. Inawezekana kwawakati huo usiwepo pale kutoa ufafanuzi.

5

2. Habari Kwa Wazazi Na Walezi Wengine Wanaotunza Watoto KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 7: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

3.1 KURASA ZIPI ZA KUTUMIA? Mwongozo huu unahusisha mawazo ya kurasa au surazitakazoweza kujumuisha matukio yote katika maisha yafamilia. Hata hivyo unaweza ukaondoa baadhi ya sehemuna kuweka za kwako mwenyewe kulingana na jinsihistoria ya familia yako ilivyo.

Watoto wako pia wanaweza wakaongezea kurasa zakwao nyingine. Kama inawezekana durufu kurasa zenyevichwa zilizotolewa katika sehemu ya 6 na kuzikata kwakufuata misitari.

3.2 NIANZIE WAPI. Hakuna utaratibu maalumu wa mahali pa kuanzia wakatiwa kuandika Kitabu cha Kumbukumbu,unaweza ukaanziana sehemu nyepesi, unaweza kuchagua sehemu ambayounajisikia amani kuandika habari zake mfano ukurasakuhusu kijiji au mji uliokulia. Utakavyokuwa unaendeleautajisikia jasiri na kuendelea kuandika kuhusiana nahabari nyeti au zenye hisia kali zaidi. Kidogo kidogoKitabu cha kumbukumbu kitaanza kupata mwelekeomzuri.

3.3 MAMBO MENGINE YA KUONGEZA KWENYE KITABU CHA KUMBUKUMBU.

Unaweza kuweka picha zako, maelezo ya namna yakutengeneza vitu mbalimbali, beti za nyimbo au mashairi,picha za watoto walizochora shuleni, kadi maalumu auhata barua muhimu. Unaweza kuweka vitu hivi karibu namaandishi yako mwenyewe ili kuwasaidia watotokukumbuka maisha yao ya kawaida ya kila siku. Endapohuna picha nyingi za watoto wako unaweza kutumia pichaza watoto wa umri mbali mbali kutoka kwenye magazetina kuziwekea maelezo yanayoonyesha uhusiano wake nawatoto wako. Kwa mfano “picha hii inanikumbusha weweulivyokuwa mdogo”.

3.4 3.4 KUTUMIA KINASA SAUTI AU KAMERA YA VIDEO. Kama unaweza hata kuazima kinasa sauti utakuwa umewapa

watoto wako zawadi kubwa! Sauti ya baba au mamaakisimulia hadithi, akiimba nyimbo au sehemu yamajadiliano kati ya wazazi na watoto- ni hazina kubwasana ya baadaye. Ukiweza pia kuazima kamera ya videomuombe rafiki yako achukue picha za shughuli aumatukio ya kawaida katika familia kwa dakika chache.

3.5 THE MEMORY BASKET. Unapoanza kutengeneza Kitabu cha Kumbukumbuunaweza kuanza kufikiria vitu vidogo vidogo ndani yafamilia ambavyo vinathamani. Hazina hii inaweza kuwakitambaa cha baba kilichopambwa, shuka lililopambwa,shanga za mama, nguo za watoto, kitabu ulichokipenda,kikombe au sahani ambazo watoto walitumia kila siku.Hata mawe, mbegu na majani makavu ya bustaninivinaweza kurejesha kumbukumbu. Vifaa hivi vidogovinaweza kutunzwa kwa usalama katika sanduku la chumaau kikapu cha asili" ukielelezea watoto wako watatakakuongeza yanayopendeza katika mkusanyiko huo. Kilakitu kidogo kitasaidia kuelezea historia ya familia.

3.6 HIFADHI YA NYARAKA ZA KISHERIA ZA KIAFYA NA VITO VYA THAMANI.

Si vema kutunza kumbukumbu zako ndani ya Kitabu chaKumbukumbu au katika kikapu cha kumbukumbu vituvyako vya thamani ndani ya kikapu cha Kumbukumbu.Vitu kama cheti cha kuzaliwa, hati ya ndoa, vyeti vyahospitali, hati za mikataba, kitabu cha benki na wosiavinatakiwa kutunzwa sehemu nzuri na salama. (Kwamfano benki, kwa mwanasheria, kiongozi wa jumuia,kanisani, msikitini, ndugu wa karibu au rafikimwaminifu). Ndani ya kitabu chako cha kumbukumbuweka taarifa kuwa hati hizo na vitu vyako vya thamanivimetunzwa na nani au wapi.

3.7 JE, NANI ZAIDI ATASAIDIA KUANDIKA KITABU CHA KUMBUKUMBU ?

Kama inawezeka, wazazi wote wawili yaani baba na mamakila mmoja aandike habari zake mwenyewe na baadayeziunganishwe pamoja kwenye kitabu kimoja. Hata hivyo,endapo mmoja au wote wameishafariki dunia, au kamawatoto wao wametengana, bado habari za familiazinaweza kukusanywa kutoka kwa babu au bibi, kaka,dada, ndugu wengine, marafiki wa karibu, walimu,viongozi wa jamii n.k hawa wanaweza kuulizwa nawakatoa habari kuhusu wazazi hao. Baada ya habari hizokupatikana watoto wenyewe wanaweza kusaidia kuandikakadri wanavyoweza kukumbuka. Kama kitabu chakumbukumbu kimeaandikwa kwa njia hii mtu mmoja wakutumainiwa anaweza kukusanya taarifa kutoka katikavyanzo mbalimbali mfano. Hata kama baadhi ya taarifasahihi zinzkosekana watoto watakuwa na kitu chkuwasaidia wao cha kukumbuka katika uwasilia wao.

6

3. Mawazo Halisi Ya Kutengeneza Kitabu Chako Cha Kumbumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 8: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

3.8 JE, KITABU NI KWA KILA MTOTO? Kila mtoto anahitaji kumbukumbu zake binafsi. Lakini

inachukua muda mwingi na pesanyingi kutengeneza kitabu cha

kila mmoja. Wazazi ambaowamekwisha tengeneza

kitabu cha watoto waowanashauri ifuatavyo:

♦ Kwanza andika kurasa za mwanzoni zenyemambo ya jumla kuhusu historia ya familia,ukoo, uzoefu katika ukuaji wao, ramani na mtiririko wa vizazi katika ukoo. Haya yanawezakunakiliwa kwa ajili ya kila mtoto.

♦ Kisha andika kurasa zenye habari za kila mtoto:kuzaliwa kwake, mambo anayoyapenda naasiyoyapenda, na uzoefu wake kwa ujumlakatika makuzi.

♦ Baada ya hapo tayarisha muhtasari kuhusuhabari za kaka na dada, na endapo watoto wanababa tofauti, ni muhimu sana kuainisha wazikuhusu wazazi wao na uhusiano wao kwa kilammoja.hii itawasaidia watoto kuelewa muundomzima wa familia hata kama huwa mara kwamara hawaishi pamoja.

♦ Toa nakala ya muhtasari huu kwa kila mtoto.♦ Wakati kunapojitokeza uhaba wa picha ili

kuokoa gharama inapendekezwa kuweka pichazote kwenye karatasi moja, toa nakala.

♦ Halafu gawa nakala hizo kwa watoto wote.

3.9 KITABU CHA FAMILIA NZIMA?Kama haitawezekana kuandika kitabu kwa kila mtoto,unaweza kutengeneza kitabu kimoja kwa watoto woteambacho watakitumia kwa pamoja. Amua naniatakitunza Kitabu hicho cha Kumbukumbu na mpekila mtoto barua inayoelezea nani aliyekitunza kitabuhicho au kimetunzwa wapi.

3.10 KUHIFADHI KITABU CHA KUMBUKUMBU SALAMA.Kitabu hiki kitasomwa kila wakati, kwa kipindi chamiaka mingi ya mbeleni, hivyo kurasa zilizoandikwa napicha zilizomo vinahitaji kutunzwa na kuhifadhiwavizuri na kwa uangalifu. Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo:

♦ Tumia kalamu yenye wino mzuri ili maandishiyasififie au kufutika;

♦ Kila utakapo andika jitahidi kuacha sehemu ndogo

wazi katika kitabuchako chakumbukumbu.Nafasi au kurasa zazaidi utazitumiakuandika habarinyingine utakazokumbuka aukuongezea picha;

♦ Ukimaliza kitabuhakikishahakinyeshewi aukuliwa na wadudukwa kwa kuwekakaratasi hizo ndani ya vifuko vya plastiki;

♦ Hakikisha watoto ndugu wa familia au waleziwanajua sehemu uliyotunza Kitabu chaKumbukumbu!

3.11 KUANZA UANDISHI.

♦ JE NINAANDIKA KITABU HIKI KWA AJILI YANANI? Kitabu hiki kitakuwa kimoja kwa familianzima au ni kwa kila mtoto binafsi?

♦ NANI ATAANDIKA KITABU HIKI? Utaandikapeke yako? Au utataka kusaidiwa na familia yakoau rafiki zako?

♦ JE, WATOTO WAKO NI WAKUBWA KUWEZAKUSHIRIKISHWA? Ikiwa utawashirikishaitakuwa ni fursa nzuri ya kuwaelezea masualamuhimu kadri utakavyokuwa unaendelea.

♦ KAMA WATOTO WAKO BADO WADOGO…utatumia lugha gani rahisi ili waweze kuelewa? Auutawaandikia ili waje wakasome miaka michacheijayo?

♦ JE, UNAANDIKA KITABU KWA AJILI YAWATOTO AMBAO TAYARI NI YATIMA? Naniatakayekusaidia kupata habari muhimu za familiahiyo na za kila mtoto binafsi?

♦ KAMA WEWE SIYO MZAZI? Lakini unaandikakitabu kwa ajili ya watoto ambao tayari ni yatimaau wametengana na wazazi wao. Nani atakayesaidia kutafuta taarifa muhimu na ukweli kuhusuwatoto.

♦ JE HABARI NI SAHIHI? Kama kitabu kinaandikwana mtu zaidi ya mmoja (mf. Wazazi wote au mamana ndugu mwingine) ni muhimu kukubaliana juu ya majina, tarehe na matukio.

7

3. Mawazo Halisi Ya Kutengeneza Kitabu Chako Cha Kumbumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 9: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

Sehemu hii inatoa mawazo yanayosaidia kutengeneza ayambalimbali au sura za kitabu chako cha kumbukumbuunaweza kuacha mada au kuongeza ukurasa kamautakavyoona inafaa. Kama unatengeneza kitabu cha kilamtoto unaweza kuokoa muda kwa kuandika nakala moja yaukurasa zinazoelezea (habari za jumla kuhusu familiaimeelezwa chini katika aya ya 4. 2- 4.6) halafu durufu nakalaya uliyoandika au nakiri kwa mkono kwa kila mtoto.

4.1 KURASA ZA SHUKURANI (UKURASA WA MBELE)Kwenye ukurasa huu unaweza kuandika (au kutumiakichwa cha habari kilichochapwa) kuelezea yafuatayo:

♦ Kitabu hiki ni kwa ajili ya♦ Kitabu hiki kimeandikwa na………(mama, baba,

malezi n.k.)♦ Tarehe na mahali kilipoandikiwa Kitabu cha

Kumbukumbu.

4.2 HISTORIA YA FAMILIA YETU.Hii itawasadia watoto wako kuelewa yaliyomo katika Kitabucha Kumbukumbu ikiwa utaanza na maelezo juu ya familiakwa muhtasari wa matukio muhimu. Wape tarehe na elezasababu za mabadiliko makubwa katika njia zako za maisha.Mathalani familia kuhamia mjini kutoka vijijini au nchinyingine. Elezea jinsi na wapi familia inaishi kwa wakati huu.

4.3 TAARIFA SAHIHI ZA NDUGU WA FAMILIA YETU. Tegeneza orodha ya ndugu wote wa karibu katika familia.Andika majina yao kamili, tarehe zao za kuzaliwa, naanwani zao. Hii huwasaidia watoto kuwakumbuka watumuhimu katika familia. Hata kama wamekwisha fariki auhawaishi karibu . Katika orodha hiyo andika wafuatao.

♦ Baba wadogo/mama wadogo/wajomba/shangazi/binamu /wapwa,

♦ Kaka na dada zako (kama kaka na dada wanababa tofauti ni muhimu kuweka wazi ili watotowaelewe uhusiano wao na ukubwa wa familia yao.)

♦ Ndugu wengine wa karibu unaowalea nyumbanikwako na nasaba zao;

♦ Kama kuna watoto wa ndugu wa familia waliofariki,andika majina yao, tarehe za vifo vyao na sehemuwalipozikwa ili wasisahaulike;

♦ Marafiki zako wa karibu sana;♦ Wasimamizi wa dini/ndoa nk.ili wasisahulike.

4.4 NYUMBANI KWETU. Elezea nyumbani kwenu na mazingira na weka picha aumichoro hii itawasaidia watoto wako kuelewa yaliyomokatika kitabu cha kumbukumbu, kama utaanza kuelezeakuhusu familia na maelezo mafupi kuhusu matukio muhimu.Andika tarehe na elezea sababu ya mabadiriko makubwayaliyojitokeza katika maisha yako – kwa mfano, mara yakwanza fami l ia i l ipohamia mjini kutoka kijijini aukwenye nchi nyingine. Elezea jinsi familia ilivyoishi nasehemu unayoishi kwa sasa.

4.5 IMANI YETU- (VITU TUAMINIVYO). Kama watoto wako bado wadogo, ni muhimu kuwaelezeakuhusu imani yako, taja kama ni dhehebu au kanisa na toajina la kiongozi wa thehebu ama kanisa hilo. Kamawatoto wako wamebatizwa au ameshiriki katika ibadanyingine yoyote ya dini, ni muhimu kujumuisha maelezoya kina ya kumbukumbu hizi na weka katika sehemu yasalama pamoja na nyaraka nyingine muhimu.

4.6 UTAMADUNI WA FAMILIA NA MATUKIO MUHIMU. Kama kuna uwezekano wa watoto kutengana na wazazi aundugu zao wa karibu (kwa sababu ya ugonjwa au matatizomuhimu) ni muhimu sana wakue wakijua mila, desturi nautamaduni wa ukoo wao. Sehemu hii ina kupatia fursa yakuandika juu ya mila, miiko na desturi ambazo ni muhimukatika ukoo wako wa baba na mama. Unaweza kuongeza habari juu ya:

♦ Sherehe na taratibu wakati mtoto anapozaliwakatika familia;

♦ Jinsi jina la mtoto linavyochaguliwa;♦ Taratibu za kijadi juu ya makuzi ya wasichana na

wavulana;♦ Taratibu za kijadi juu ya utunzaji wa wazee na

kuwaheshimu wakubwa katka jamii; ♦ Mila na desturi za mazishi na namna ya

kuwakumbuka marehemu katika familia.

4.7 TAARIFA ZA KILA MTOTO.Aya ya 4.8 – 4.17 zinataka kumwandikia kila mtoto kitabucha kumbukumbu peke yake.

4.8 KUZALIWA KWAKO. Taarifa hii inarejea katika kuzaliwa kwa mtoto. Watotowote wanapenda kujua sehemu, muda na tarehe walipozaliwana walikuwaje ndani ya saa moja baada ya kuzaliwakwao.Andika kila jambo unalokumbuka. Nani alikuwepo?Je, mtoto mwenyewe alilia vizuri wakati alipozaliwa katikadunia hii. Uzito wake ulikuwaje, labda ulikuwa na jinalake kabla ya kutoka hospitali. Kuna picha zake zilizochukuliwa baada ya kuzaliwa. Kama hauna picha za utotounaweza kuangalia pia za mtoto mwingine aliyezaliwakutoka kwenye magazeti. Hii ni kumpa mtot wako taswiraya jinsi alivyokuwa akifanana wakati wa kuzaliwa kwake.

8

4. Kurasa Za Kitabu Cha Kumbukumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 10: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

4.9 NAMNA ULIVYOPATA JINA LAKO. Watoto wanapenda kujua jinsi majina yao yalivyochaguliwa,na kama waliitwa baada ya ndugu au rafiki kuwasili, ni nanialiwaita majina hayo. Pia wanapenda kujua kama jinahilo ni la ukoo wake. Je kuliwa na ubatizo au shereheya kupewa jina? Je, ni nani mzazi wa ubatizo aumdhamini?4.10 WAKATI ULIPOKUWA MTOTO.Simulia kidogo maisha ya utotoni ya mwanao.Je mtotoalikuwa akitembeatembea na mama yake. Je kaka, dadawakubwa au bibi walimlea wakati mama akiwa kazini.Kama alikuwa mkali, analia au mpole wa kulala sana nakama alifanana alifanana na yeyote katika familia. Je, aliishina wazazi wake au alipelekwa kwa ndugu wengine kamababu au bibi? Alipatwa na magonjwa katika umri wautotoni, kama nindiyo yapi yaliyokuwa yakimsumbua? Nichakula gani mtoto alichokuwa akipendelea? Husishapicha zake za utotoni.

4.11 MARA YAKO YA KWANZA.Unakumbuka ni lini mtoto wako alipochukua hatua yakwanza, alipozungumza maneno ya kwanza na yalikuwamaneno gani? Nini ulikuwa uzoefu wako wa kwanzauliougundua alipotengana na mama yake, alipoendashuleni mara ya kwanza, alipoenda hospitali aualipotembelea nyanya /babu yake? Kila mara ulifanyajewewe kumtia moyo mtoto wako.

4.12 SIKU ZAKO UKIWA SHULENI NA MAKUZI YAKO.Eleza maisha ya mwanao alipokuwa akisoma. Taja majinaya shule alizokuwa akisoma, masomo aliyoyapenda,walimu aliokuwa akiwaogopa au kuwapenda na matukiomengine kama ushiriki wake katika michezo. Ni zipizilikuwa sare za shule, masomo gani yalikuwa mazuri aumagumu sana, taja matukio pekee.

4.13 UPENDELEO WAKO NA SHUGULI ZAKO. Simulia mambo au shughuli mtoto wako alizopendeleakufanya. Elezea kuhusu marafiki zake tabia ya kufugawanyama, kusaidia wazazi, chakula alichokipenda,uhusiano wake na wadogo zake na maisha yake kwaujumla.

4.14 KUMBUKUMBU ZANGU KWAKO. Ni kitu gani cha pekee kuliko vyote unacho kikumbukamaneno ya mwanao wakati anajifunza kusema huyo?Kinaweza kuwa cha kufurahisha au kuhuzunisha. Lakinikuandika vitu vidogovidogo kuhusu tabia na mwenendowa mwanao ni jambo kubwa sana kwake.

4.15 MATEGEMEO NA MATARAJIO YANGU KWAKO. Hapa ni mahali pa kuandika unayoyatarajia kwa mtotowako kwa siku za baadaye. Unaweza pia kutoa ushari

au nasaha juu ya namna anavyopaswa kuishi, mathalaniumuhimu wa kuzingatia elimu, umuhimu wa kujiwekeamalengo, kujiepusha na marafiki wabaya, kuepukavishawishi akiwa kijana na uwajibikaji atakapokuwamzazi. Ni vizuri ukatoa uzoefu wako mwenyewe katikakumwelekeza.

4.16 WATU MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO. Andika maelezo mafupi kuhusu watu muhimu au wapekee kwa huyu mtoto. Pamoja na ndugu au waleziunaweza pia ukataja wengine kama vile majirani, viongoziwa dini, walimu, wataalamu wa afya n.k. hawa ni watu

wanaomfahamu mtoto kwa undani na wanaowezakumsaidia au kumshauri katika maisha yake ya kila siku.

4.17 TAARIFA KUHUSU AFYA YAKO. Toa maelezo mafupi kuhusu afya ya mtoto. Andikakuhusu maradhi au maumivu yaliyowahi kumpata sikuza nyuma. Pia taja hali au tatizo lolote la kiafyaaliloweza kurithi kutoka kwa ndugu zake. Orodheshamajina ya zahanati/hospitali pamoja na watendaji waafya ambao wamekuwa wakimhudumia mtoto ili awezekuomba maelezo zaidi au ushauri utakapohitajika.Karatasi za kumbukumbu za afya, kama vile chanjokamwe isiwekwe kwenye kitabu cha kumbukumbu balizihifadhiwe mahali pa salama.

4.18 TAARIFA KUHUSU WAZAZI.Watoto wote wanahitaji kuwa na taarifa sahihi na zawazi kuhusu wazazi wao wote. Endapo mmojawapo wawazazi amefariki au hayupo ili aweze kuandika kurasahizi itakuwa ni lazima kupata taarifa kutoka kwa nduguau jamii, hata kama taarifa si za kutosha, chochotekitakachopatikana bado ni muhimu kwa huyu mtotokatika kumpa hisia za kutambulika.

9

4. Kurasa Za Kitabu Cha Kumbukumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 11: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

4.19 TAARIFA KUHUSU MAMA.Ikiwa watoto wote wamezaliwa na mama mmoja, taarifaza aya ya 4.20- 4.28 ziandikwe mara moja tu na kutolewanakala kwa ajili ya kila mtoto.Iwapo watoto wamezaliwana mama tofauti au wamelelewa na familia nyingine,taarifa itabidi iandikwe ikielezea hali halisi ya kila mtoto.

4.20 TAARIFA ZA MAMA. Anza na mambo yafuatayo:

♦ Jina lako kamili, kabila lako na ukoo, ♦ Tarehe na mahali pakuzaliwa , ♦ Kama umeolewa, tarehe na mahali ulipofungia

ndoa, ♦ Mahali unapoishi sasa.

Halafu simulia kidogo ilivyokua: ulikuwaje ulipokutana nahuyo mmeo/ baba wa mtoto huyo? Ulijisikiaje kwa maraya kwanza? Baadaye nini kilifuata? Ulikuwa ukiishi wapiwakati ulipo wazaa watoto wako?

4.21 MAKUZI YA MAMA. Watoto wako watahitaji kujua historia ya nyuma ya familiayao. Kama mmekulia maeneo au jamii tofauti, ni muhimukuwaeleza utamaduni wenu, maisha yenu yote kwaujumla kama uliishi mjini au kijijini. Nyumbani kwenukulifananaje? Mlipanda nini katika eneo linazungukanyumba? Familia yenu walikuwa wakifuga mifugo gani?Nani walikuwa wakiishi kwenye mji huo – kaka nadada,babu, bibi? Kazi zako zikuwa ni zipi pale nyumbani– kulea watoto, kuchota maji. Au kumsaidia bibi yakokutayarisha chakula cha familia? Ulikwenda shule?Ulipenda masomo gani na yapi uliyachukia? Ulikuwaunacheza michezo yoyote au kushiriki katika kikundichochote cha burudani? Usisite au kuona aibu kutajamambo yako ya shuleni na usichana wako.

4.22 KIPINDI CHA KUKUA NA UTU UZIMA WA MAMA. Je, ulienda shuleni na uliendelea na masomo au mafunzoyoyote baada ya shule ya msingi /sekondari?Umeajiriwa- unaenda kazini – au muda wako mwingiunautumia kulea watoto na kutunza nyumba? Ukiangalianyuma, matarajio yako uliyafikia? Changamoto gani uli-zokabiliana nazo na mbinu gani ulizotumia kupambananazo?

Eleza kama wewe mama ulichukua mafunzo/koziyoyote baada ya siku za shule yako.Maeneo ambayoumewahi kuajiriwa, mafanikio ambayo uliyowahi kuyapatapia changamoto ulizokutanazo. Je malengo yakouliyokusudia umeyafikia na umeyatekeleza? Na ndotoyako umeifikia?

4.23 SHUGHULI NA MAMBO MUHIMU ANAYOPENDELEA MAMA.

Hii ni sehemu ya kuelezea mambo na shughuli una-zopenda kufanya ukiwa nyumbani hasa wakati ukiwa

huru. Je unao muda wa kupumzika? Je unasaidiajamii/familia/shule? Unashiriki katika shughuli zadini? Ni jambo gani unalolifanya ambalo linawavutiawatu hadi wakakusifia? Kama vile kupika chakula chaasili, kusitawisha maua ambayo ni ya pekee, ufinyanziau ufumaji, kuimba au kuchezaq katika kikundi Jemwanachama katika kikundi cha kijamii.

4.24 MAMBO AMBAYO MAMA ANAYAPENDELEA NA ASIYO YAPENDELEA.

Unaweza kutaka kuandika jinsi gani unavyo sherehekeasikukuu za kidini kama vile: Krismas, Pasaka, Maulidiama mfungo wa Ramadhani vilevile wakati ambao familiahukutana pamoja. Nyimbo ama mashairi uliyojifunzashuleni; aina za vyakula ambavyo bibi yako alikufundishajinsi ya kupika. Aina gani ya vitu vinavyokufanya ukasirikeau ujisikie huna furaha: watu - wakiwemo wanasiasawasiojali ahadi? Watoto wasiotii? Wanyama waharibifuwalioharibu bustani yako? Majirani wenye majungu amawanaoingilia mambo ya familia yako?

4.25 KUMBUKUMBU MAALUMU ZA MAMA.Fikiria kuhusu baadhi ya siku za furaha maishani mwako.Kumbuka jambo maalum au tukio muhimu katika familialililoleta furaha au majonzi. Kumbuka kwamba vitu vidogovidogo vinaweza kuwa na uzito sawa na tukio kubwa katikafamilia. Mfano, suala la mtoto kushangaa anapoona yai likitoakifaranga, linaweza kuwa na umuhimu kama wa sherehe yakumaliza shule.Wazazi wengine wanaweza kuamuakuelezea nyakati ngumu walizowahi kukutana nazo na jinsiwalivyoweza kupambana na changamoto hizo.

4.26 IMANI YA MAMA NA MTAZAMO WAKE KATIKA MAISHA.

Inawasaidia watoto kukuelewa na kuheshimu maadili yakokama utawafahamisha mambo yaliyokuongoza maishani. Hilisi swala tu la imani ya dini bali pia msukumo kutoka kwawazee wa ukoo, walimu, babu na bibi na watu wengine wotewaliokusaidia kupambana katika maisha yako.

10

4. Kurasa Za Kitabu Cha Kumbukumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 12: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

4.27 AFYA YA MAMA. Hii ni sehemu ya kuandika hali ya afya yako ili watotowaweze kuelewa ukweli na hali halisi juu ya afya yako kwamaneno yako mwenyewe. Andika habari kuhusu hali yoyoteya kiafya inayoweza kurithishwa. Ikiwezekana elezea kwakina kwenye karatasi tofauti majina ya madaktari nahospitali ambazo umekuwa ukitibiwa ili watoto wakowaweze kwenda kupata habari zaidi kama zitahitajikabaadaye.

4.28 MAISHA YA MAMA KWA SASA.Ni muhimu kuelezea hali ya maisha yako kwa sasa nakama familia imewahi kukumbwa na balaa la kifo amawewe kutengana na mwenzako. Kama sasa uko peke yakounaweza kuelezea jinsi unavyoweza kujikimu na maishaya kila siku. Endapo umepata mwenza mpya, pengineunaweza ukawafahamisha wanao jinsi maisha yakoyalivyobadilika na nafasi yao katika familia kwa sasa.

4.29 TAARIFA KUHUSU BABA.Kama kuna uwezekano kurasa (zinazoelezea masuala yaaya 4.30-4.38) ziandikwe na baba mzazi wa mtotomwenyewe.Ikiwa baba huyo hapatikani ili aandikemwenyewe, au ameisha aga dunia, ni muhimu kwa mama aumwanafamilia kutoa taarifa sahihi kadri anavyozifahamu.Ikiwa watoto wote wamezaliwa na baba mmoja, taarifaziandikwe mara moja tu na kutolewa nakala kwa ajili yakila mtoto.Iwapo watoto wamezaliwa na baba tofauti,taarifa itabidi iandikwe ikielezea hali halisi ya kila mtoto.

4.30 TAARIFA ZA BABA. Anza kwa mambo yafuatayo:

♦ Jina lako kamili , ♦ Tarehe na mahali pa kuzaliwa ,♦ Kama umeoa, tarehe na mahali ulipofungia ndoa ,♦ Unapoishi sasa.

Halafu endelea kuandika hadithi (maelezo) yako.Unaweza kuweka namna ulivyo kutana na mama watotowako. Upi ulikuwa mtazamo wake? Ulifanikiwajekumpata? Uliishi wapi watoto walipozaliwa?

4.31 MAISHA YA UTOTO WA BABA. Watoto wako watapenda kujua maisha ya familia. Kamaumeishi katika eneo tofauti na hapo ulipo sasa elezea mazin-gira yake kiutamaduni na kijamii. Uliishi kijijini au mjini?Nyumbani kwenu kulifananaje? Mlikuwa mnapanda ninikwenye eneo linalozunguka nyumba yenu? Familia yenuilikuwa ikifuga wanyama? Ulikuwa ukiishi na nani – kaka nadada, babu na bibi? Ulijifunza nini kutoka katika familia?Ulikuwa ukifanya kazi gani nyumbani – kuwatunza wadogozako, kuchota maji, kulima, kupika, kuchunga, uvuvi n.k.Ulienda shule? Ni masomo gani ulikuwa ukipendelea nayapi hukuyapenda? Ulipenda kushirikisha katika mambogani – kuimba, kucheza au burudani gani nyingine? Watotowako watapenda kujua mafanikio yako shuleni – kufaulumitihani au kuwa bingwa katika michezo.

4.32 MAISHA YA MAKUZI NA UTU UZIMA WA BABA. Elezea kama ulisoma shule masomo gani uliyoyapendelea nayapi uliyachukia na toa sababu zake. Pia elezea masualamuhimu uliyoyapenda : kama ulikuwa mwanakwaya?Mcheza ngoma? Ulikuwa katika chama cha maskauti?,Mwanamichezo? Watoto wako watataka kuelewa juu yamafaniko yako kama ulikiwa ukifauli katika mitihani auulikuwa mkibiaji sana. Eleza mafunzo uliyopata baada yakumaliza shule. Wafahamishe watoto kuhusu ujuzi wako nakazi uliyokuwa ukifanya – ulikuwa ukijishughulisha na kazi zanyumbani au ulikuwa ukienda kufanya kazi nje ya nyumbani?Ukifikiria kipindi cha nyuma, matarajio yako yalikuwa yapi –na je, yamefikiwa?

4.33 SHUGHULI NA MAMBO MUHIMU BABA ANAYOPENDELEA.

Hapa ni mahali huru pa kusema jinsi ulivyotumia mudawako wa mapumziko. Ulijifunza maarifa gani kutoka kwawazazi wako na ni ujuzi gani unaoweza kuurithisha kwawatoto wako? Je, mtazamo wa watu kwako ukuje –wanakuona kama mwanaume anayewajibika katika famil-ia yake? Unashiriki kikamilifu katika shughuli za kijamiiau za dini. Kuna vitu unavyopendelea au michezo yoyoteunayoshiriki?

4.34 MAMBO ANAYOYAPENDELEA NA ASIYOPENDELEA BABA.

Unaweza kuelezeajinsi ulivyokuwau k i s h e r e h e k e asikukuu za kidiniau sherehe nyingine zakifamilia. Unawezapia ukaandikakumbukumbu zavitu vingine vyazamani kama vilechakula alichokuwaak ip ika b ib i ,ulivyokuwa ukiangalia

mpira, ukiimba au kucheza. Lakini pia usisahau kuandikajuu ya vitu ulivyokuwa vikikuuthi au kukuchanganya!Wanaweza kuwa watu kama wanasiasa wasiotekeleza ahadizao, watoto wasiokuwa watii, au majirani wambea na wenyemajungu. Au labda wanyama waliokuwa wakiharibu mazao?

4.35 KUMBUKUMBU MAALUM ZA BABA. Fikiria matukio yaliyokusisimua maishani mwako hususanimambo mazuri ambayo umekuwa ukifurahia na watotowako. Kumbuka kwamba vitu vidogovidogo vinawezakuwa na uzito sawa na tukio kubwa katika familia.mfano,kitendo cha mtoto wako kushangaa anapoona mbegualiyopanda imechipua kinaweza kuwa na uzito kamasherehe fulani ya ndoa! Yote haya ni kukifanya kitabu chak u m b u k u m b u k i v u t i e n a k i s i w e m a r a z o t ek i n a m s o n o n e sha mtoto.

11

4. Kurasa Za Kitabu Cha Kumbukumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 13: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

4.36 IMANI NA MTAZAMO WA BABA KATIKA MAISHA. Inawasaidia watoto kukuelewa na kuheshimu maadiliyako kama utawafahamisha mambo yaliyokuongozamaishani. Hili si kuhusu imani ya dini pekee bali ushauriuliokuwa ukipata kutoka kwa wazee wa ukoo, walimu,babu na bibi na watu wengine wote waliokusaidiamaishani kwa namna moja au nyingine.. hii pia ni nafasiyako kuwaeleza watoto kuhusu msimamo wako juu yamaswala ya siasa, mila na desturi.

4.37 AFYA YA BABA. Hapa ni mahali pa kuandika afya yako ili watoto watapate

fursa ya kufahamu hali halisi ya afya yako kwa uwazi nakwa maneno yako mwenyewe. Wafahamishe watoto kwaufasaha (ikiwezekana tumia karatasi tofauti ) majina yamadaktari na wahudumu wengine wa afya waliokuwawakihudumia, pamoja na hospitali au zahanati kuuliziataarifa zaidi kama zitahitajika hapo baadaye.

4.38 MAISHA YA BABA KWA SASA.Ni muhimu kuelezea mazingira yako kwa sasa. Hiiitawasaidia watoto kuelewa kwa nini mambo yako hivikwa sasa na kwa jinsi gani yanaweza kuathiri mahusianoyako na wao.

12

4. Kurasa Za Kitabu Cha Kumbukumbu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

Page 14: JinsoYa Kuandika Kitabu Cha Kumbukumbu · 2013-02-04 · 1.3 KITABU HIKI NI KWA AJILI YA NANI? Kitabu cha kumbukumbu kwa mara ya kwanza kiliandik-wa kwa ajili ya watoto ambao wazazi

(Sehemu ya mwisho inatoa nafasi ya taarifa ambazo hapoawali hazikuwekwa katika kitabu cha kumbukumbu. Piainatoa nafasi ya kuweka majina na taarifa mbalimbalimuhimu kutoka katika sehemu zilizotangulia. Taarifa hizoni pamoja na ramani za maeneo na michoro inayoonyeshamtiririko wa vizazi katika ukoo ili kuwasaidia watotokuelewa muundo mzima wa familia na kufahamu nduguwalikotokea au walipokwenda endapo hawaonekani)

5.1 MAJINA NA ANWANI ZA WATU MUHIMU KATIKA FAMILIA.Hii ni muhimu sana kama watoto wametengana auwametawanyika. Orodhesha majina kamili na anwani zawatu muhimu kwa watoto na maeneo wanapoishi watuwafuatao:

♦ kaka na dada pamoja na ndugu wengine wa karibu♦ wakuu wa ukoo:ndugu wa karibu♦ wanajamii, walimu na viongozi wa dini ♦ mashirika au vikundi vya msaada ♦ marafiki na majirani wakutumainiwa ♦ Wanaukoo wakongwe

5.2 TAARIFA KUHUSU MATUKIO MENGINE MUHIMU NA WATU.

Hizi ni pamoja na:♦ Maelezo kuhusu kifo cha ndugu wa karibu au

marafiki na mahali walipozikwa♦ Taarifa kuhusu ndoa au talaka♦ Maelezo ya kina ya ndugu au marafiki ambao

wako mbali au wanaishi nje ya nchi♦ Taarifa nyingine yoyote muhimu ambayo

haikuandikwa awali katika Kitabu chaKumbukumbu.

5.3 RAMANI YA TAIFA NA KIMATAIFA.Unaweza kutumia ramani kuonesha jinsi ndugu mbalimbaliwanavyohama kutoka sehemu moja hadi nyingine, mahaliwalipozaliwa, mahali walipokwenda,makazi yao ya sasa auwalipozikwa endapo wamefariki.

5.4 MCHORO WA MTI WAFAMILIA (family tree).Kama watoto ni lazima waendemahali fulanai au kuishi na watuwengine mara nyingi huwawanachanganyikiwa juu yauhusiano wa familia. Mchorohuu unatakiwa kuonyesha nakuelezea msingi wa familia yenu.Mti huu unatakiwa kuanzia kwababu na bibi wa kwanza hadikwako wewe baba/mama piakwa watoto. Hii itasaidiawatotokufahamu kwa usahihi ninaniwazazi waona ni nanibabu/bibi zao, na kufahamu uhusiano wao wa kweli, kaka,dada, mjomba, shangazi na binamu.

5.5 MTI WA MWEMBE.Huu unatoa nafasi kwa wazazi kujaza majina ya watu wakaribu na muhimu kwa mtoto, wanaweza kuwa ndugu,marafiki au wanajumuia. Baadhi ya wazazi wanabandikapicha za watu hawa kwenye matunda katika familianyingine watoto wanachagua watu wanaowahitaji na hatakuchora picha zao katika matunda.

5.6 WAPI PA KUPATA NYARAKA NA KUMBUKUMBU.Kitabu cha kumbukumbu si mahali sahihi panapofaakutunza nakala halisi za nyaraka au vitu vyovyote vyathamani, unahitaji kutafuta mahali salama au watuwanaoaminika kutunza nyaraka za familia na vitu vinginemuhimu hadi watoto watakapokuwa wamejitegemea.Mahali salama ni pamoja na jamaa mashuhuri, benki,mwanasheria kiongozi wa jumuiya au kanisa, mwanakamati wa kikundi fadhili au rafiki mwaminika.

Ni muhimu kutengeneza orodha ya yaraka na vitu nakupata risiti. Ndipo watoto watajua kilichotunzwa na wapikitapatikana.Nyaraka muhimu zinaweza kujumuisha:

♦ Vyeti vya kuzaliwa na ubatizo ♦ Vyeti vya ndoa (na kama inafaa vyeti vya talaka.)♦ Vyeti vya hospitali pamoja na chanjo.♦ Wosia na nyaraka zao kumilki mali♦ Maandishi ya maelekezo au makubaliano ya kawaida

kuhusu ulezi au mtunzo ya watoto mbeleni.♦ Pasi za kusafiria na nyaraka zingine kuhusu utaifa

na kisheria.

Sasa umekamirisha kitabu cha kumbukumbu.Lakini maelezo yanaendelea.…..na inawezekana wewe auwatoto wako wataalam kuweka rekodi kulingana nawakati wa kuongezea habari mpya na mawazo kadrimiaka inayopita..

13

5. Taarifa Nyingine Muhimu KUMBUKUMBU

www.memorybooks.org.uk

“Maandishi yako ni hazina kubwa kwa kizazi chako” - Adilisha 2005“Usemi wako kwa leo waweza kutothaminiwa bali kwa usoni utakuwa ni lulu” Adilisha 2007