136
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 26 Juni, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Moja, leo ni Kikao cha Hamsini na Nane. Katibu NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na litaulizwa na Mheshimiwa Aisharose Matembe Ndogholi. Na. 487 Kuboresha Huduma za Hospitali ya Mtakatifu Gaspar – Itigi MHE. AISHAROSE N. MATEMBE aliuliza:- Hospitali ya Mtakatifu Gaspar imekuwa Hospitali ya Rufaa tangu mwaka 2011 na inahudumia wananchi wa Mikoa ya Tabora, Singida na Mbeya. Wakati wa kampeni

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

  • Upload
    lekhanh

  • View
    214

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE_____________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 26 Juni, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutanowetu wa Kumi na Moja, leo ni Kikao cha Hamsini na Nane.Katibu

NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na litaulizwa naMheshimiwa Aisharose Matembe Ndogholi.

Na. 487

Kuboresha Huduma za Hospitali yaMtakatifu Gaspar – Itigi

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE aliuliza:-

Hospitali ya Mtakatifu Gaspar imekuwa Hospitali yaRufaa tangu mwaka 2011 na inahudumia wananchi waMikoa ya Tabora, Singida na Mbeya. Wakati wa kampeni

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

mwaka 2015, Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufulialiahidi kuipatia vifaa tiba, dawa na watumishi wakutosha ili kupunguza changamoto wanazokutana nazowagonjwa:-

Je, ni lini ahadi ya Mheshimiwa Rais itatekelezwa ilikusaidia hospitali hiyo kutoa huduma za afya kwa ufanisi nakuokoa maisha ya wananchi?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la MheshimiwaAisharose Ndogholi Matembe, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha ushirikiano katiya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika utoaji wahuduma za afya, Serikali inatoa ruzuku ya fedha kwa ajili yakulipia mishahara ya watumishi pamoja na ruzuku ya dawana vifaa tiba. Jumla ya watumishi 50 wa Hospitali ya MtakatifuGaspar wanalipwa mishahara na Serikali ambapo ni DaktariBingwa mmoja (Bingwa wa Upasuaji), Daktari mmoja,Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi 43na Mteknolojia wa Maabara mmoja.

Mheshimiwa Spika, mgao wa dawa na vifaa tibakutoka Bohari ya Dawa (MSD) unaendelea kutolewa naSerikali katika Hospitali ya Mtakatifu Gaspar ambapo katikamwaka wa fedha 2016/2017, Serikali ilitoa dawa zenyethamani ya shilingi milioni 105.67 na mwaka wa fedha wa2017/2018 dawa zenye thamani ya shilingi milioni 114.67zimetolewa katika hospitali hiyo. Aidha, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaandaamwongozo wa gharama za matibabu katika hospitaliambazo siyo za Serikali ili kuzifanya hospitali hizo kutoahuduma zenye gharama nafuu.

SPIKA: Mheshimiwa Aisharose, nilikuona.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswalimawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwahospitali hii inahudumia wagonjwa wengi kutoka Mkoa waMbeya, Singida na Tabora lakini ina Madaktari Bingwawachache; Madaktari Bingwa waliopo ni wanne tu. Je,Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha hospitali hii inakuwana Madaktari Bingwa wa kutosha ili kutoa huduma bora kwawakati wote?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa gharamaza hospitali hii ya Mission pamoja na gharama nyingine zahospitali za binafsi ni kubwa sana ambapo wananchi wakawaida hawawezi kumudu. Kwa mfano, mamaanapoenda kujifungua anatakiwa kulipa Sh.150,000 kwakawaida lakini anapojifungua kwa operesheni anatakiwakulipa Sh.450,000. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikishaWilaya ya Itigi inapata Hospitali ya Wilaya?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa JosephatKandege, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, kuhusiana na suala zima la kuwepo Madaktari Bingwawa kutosha, ni nia ya Serikali kuhakikisha kwambawanapatikana ili waweze kutoa huduma. Hivi karibuni Ofisiya Rais, TAMISEMI imeweza kutoa tangazo kwa ajili yaMadaktari. Naamini katika wale ambao watakuwawameomba na Madaktari Bingwa watapatikana kwa ajiliya kuwapeleka maeneo kama hayo.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Mbungeavute subira na swali hili limekuwa likiulizwa mara kwa marana Wabunge wa Mkoa wa Singida, mnamo tarehe 7 mwezi

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

huu swali hili liliulizwa na leo linaulizwa kwa mara ya pili.Kwa hiyo, inaonyesha jinsi ambavyo wanajali wananchi waokatika suala zima la afya.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na gharama zamatibabu ambazo zinatolewa na hospitali hii na hospitalizingine binafsi, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu lamsingi tunatarajia mwongozo kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa sababuSerikali inawekeza pesa zake, kuwe na bei ambazo wananchiwanaweza kumudu.

Mheshimiwa Spika, amechomekea na swali linginekuhusiana na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itigi, naombanimhakikishie ni azma ya Serikali baada ya kuwa tumemalizahizi hospitali 67, katika maeneo yote ambayo hakunaHospitali za Wilaya Serikali itaenda kujenga.

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Mama Margaret Sitta,swali la nyongeza la wananchi wa Urambo.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nakubali kwamba Serikaliinajitahidi sana kusaidia Hospitali ya Wilaya ya Urambo lakinibado tuna changamoto kubwa ambayo ni ukosefu watheater, ni mradi wa ADB ambao ulijenga theater pale ikafikialenta. Je, Serikali inawaliwaza vipi wapiga kura wangu waUrambo kuhusu kumalizika kwa theatre ambayo ipo katikahatua ya lenta?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kama unakumbukaujenzi wa hilo jengo la upasuaji Urambo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, nilipata nafasi ya kutembelea Urambo na naombanimpongeze kwa dhati kabisa Mheshimiwa Sitta amekuwa

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

ni mpiganaji kuhakikisha kwamba afya ya akinamama nawatoto kwa ujumla inaboreshwa. Wakafanya kazi nzuri sana,wameanzisha na wodi maalum kwa wale watu ambaowangependa wawe kwenye grade A, ni jambo lakupongezwa na wengine ni vizuri tukaiga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeona ile theater ambayoinajengwa ikafikia usawa wa lenta, naomba nimhakikishieMheshimiwa Sitta Serikali itahakikisha kwamba kazi nzuriambayo imefanyika haiachwi ikapotea, kwa kadri pesaitakavyopatikana tuna wajibu wa kuhakikisha kwambatunamalizia ile theater ambayo ilikuwa imekusudiwa kwaajili ya kutoa huduma kwa akinamama na watoto. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mwalimu Mulugo, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana na mimi kupata swali la nyongeza. Ni wikimbili zimepita alikuja Katibu wa Hospitali ya MwambaniBwana Kalindu na nikamwita Mheshimiwa Naibu Waziritukakaa, tukaongelea habari ya Hospitali ya Mwambani paleMkwajuni.

Mheshimiwa Spika, kama mnavyojua Songwe niWilaya mpya na hatuna Hospitali ya Wilaya lakini hii Hospitaliya Mwambani ndiyo inayotumika kama Hospitali ya Wilayaau Hospitali Teule, lakini watumishi mpaka sasa ni haba nahatupati dawa na hata mgao wa Serikali hauendi kamaambavyo inatakiwa ipewe Hospitali Teule. Ni nini Serikaliinatamka juu ya jambo hili na Mheshimiwa Waziri anajua?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa JosephatKandege.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, ni kweli Mheshimiwa Mulugo alikuja na tukakaapamoja na Daktari ambaye alikuwa ametoka Hospitali ya

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mwambani. Kimsingi Hospitali ya Mwambani kwa sababundiyo hospitali pekee iliyopo inatakiwa itumike kama DDH.Ni makosa tu ambayo yalifanyika na naomba nimhakikishieMheshimiwa Mbunge ndani ya muda mfupi tatizo litakuwalimeshatatuliwa na hospitali ile itatambuliwa kama DDH kwasababu ndiyo hospitali ambayo ni tegemeo kwa wananchiwa Mwambani na Chunya kwa ujumla wake. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini,uliza swali lako, tafadhali.

Na. 488

Mkopo na Posho kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH (K.n.y. MHE. HASSAN S.KAUNJE) aliuliza:-

(a) Je, ni lini Serikali itadhamini Wenyeviti waSerikali za Mitaa ili waweze kupata mikopo kama ilivyo kwaMadiwani na Wabunge?

(b) Je, ni lini Serikali itaanza kuwalipa posho/mishahara Wenyeviti wa Serikali za Mitaa?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais – TAMISEMI, napenda kujibu swali la MheshimiwaHassan Seleman Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini, lenye sehemu(a) na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, utaratibu wa Halmashaurina Bunge kudhamini mikopo kwa Waheshimiwa Madiwanina Waheshimiwa Wabunge umetokana na kuwepo kwautayari wa benki zinazokopesha mikopo hiyo, hususan NMBna CRDB ambazo baada ya kuonesha utayari, makubalianomaalum husainiwa ambayo ndiyo hutoa mwongozo wanamna mikopo itakavyotolewa pamoja na viwango vyake.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa aina hiyo hadi sasahaujawezekana kwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Mitaa naVitongoji kwa kuwa hadi sasa hakuna benki iliyoonesha utayariwa kutoa mikopo ya aina hiyo. Hata hivyo, ipo fursa kwakiongozi mmoja mmoja kuwasiliana na benki moja kwa mojakwa ajili ya makubaliano binafsi ya mkopo kulingana nakiwango cha amana alichonacho, thamani ya ardhi,nyumba anayomiliki au biashara.

(b) Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kazikubwa inayofanywa na Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Vitongojina Mitaa kupitia Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa,Serikali i l itoa mwongozo kuwa viongozi hao wawewanalipwa posho inayotokana na asilimia 20 ya mapato yandani ambayo hurejeshwa na Halmashauri kwenye Kijiji/Mtaahusika.

Mheshimiwa Spika, changamoto zil izopo zaukusanyaji hafifu wa mapato ya ndani zimekuwazikisababisha ugumu wa kutekeleza mwongozo huo katikabaadhi ya maeneo. Kwa sababu hiyo, Halmashauri zotezimeagizwa zifanye mapitio ya vyanzo vyote vya mapatona ziimarishe makusanyo ya ndani ili ziwe na uwezo wa kulipaposho hizo.

SPIKA: Mheshimiwa Hamida Abdallah, swali lanyongeza.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwanza nishukuru kwa majibu hayo ambayoyamejibiwa sasa hivi lakini naomba niulize maswali mawiliya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Madiwaniwanafanya kazi sawa na Wabunge. Kwa nini Serikali isiwalipemishahara kama ambavyo Wabunge wanapewamishahara? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kwa nini Wenyevitiwa Serikali za Mitaa, sasa hivi Serikali haijaona umuhimu wa

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

kuwalipa posho ambayo wanastahili kupata maanawanalipwa posho ndogo sana. Serikali ingeona umuhimukwa sababu wao wanasimamia kazi za miradi ya maendeleokatika mitaa. Kwa hiyo, ningeomba sasa Serikali ifanyemaamuzi ya kuwaongezea posho ili waweze kukidhi mahitajiyao. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mnapouliza maswalihaya msilinganishe sana na Wabunge kwa sababu naWabunge nao wana malalamiko posho haitoshi. (Kicheko/Makofi)

Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) : MheshimiwaSpika, katika swali lake la kwanza, ni kweli kwamba Madiwaniwamekuwa na mtazamo huo wa kuomba kwamba kuwena malipo hayo ya mshahara, Serikali iliyapokea na hatawakati Rais alivyohudhuria kikao cha ALAT mwaka janaalipokea maombi yao. Mimi nasema tu kwamba majibuyaliyotolewa pale ndiyo sahihi na hadi hapo Serikaliitakapotoa maelekezo mengine lakini kwa sasa hivitutaendelea na utaratibu ambao tunao.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili kuhusuWenyeviti wa Serikali za Vijiji, Vitongoji na Mitaa kwambaposho ni ndogo sana, msisitizo ambao tunautoa sisi kilaHalmashauri ifanye mapitio (review) ya vyanzo vyake vyandani pamoja na mbinu zao za makusanyo, wakusanyekiwango cha kutosha cha mapato ya ndani na wahakikishekwanza, hata hiyo ndogo maana maeneo mengine mengituna malalamiko kwamba hawalipi, hata hiyo ndogo basiinalipwa baada ya hapo sasa ndiyo tutaona tunaendajehuko mbele. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hasna Mwilima, nil ikuwanimekuona, swali tafadhali.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Posho ya Wenyeviti wa Serikali za Vijiji kwenye Halmashaurizingine hawalipwi kabisa. Sasa nataka niulize tu swali kwanini Wizara ya TAMISEMI isitoe Waraka Maalum kwenda chinikwa Wakurugenzi wote kuwaelekeza kwamba katika ownsource za Halmashauri wawe wanatoa kiasi fulani kwa ajiliya Wenyeviti wa Vijiji huku tukijua hao ndiyo wanaotusaidiakufanya kazi kubwa za maendeleo kwa niaba ya Serikali?(Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa, kule Halmashauri kuna hela basijamani? Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, majibutafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) : MheshimiwaSpika, kama nilivyojibu katika swali la msingi, huo Warakaambao Mheshimiwa Mbunge anaupendekeza ulitolewamwaka 2003, lakini kwa sababu umekuwa ni wa muda mrefupengine labda baadhi ya wenzetu wanaanza kuusahau, basitutachukua ushauri wake ili tutoe maelekezo tena.

Mheshimiwa Spika, msisitizo ni kwamba lazimaHalmashauri zote zifanye mapitio ya vyanzo vyao vyamapato, waongeze mbinu za ukusanyaji wa mapato yandani ili kusudi wawe na uwezo mzuri wa kuweza kulipa. Hiini kwa sababu hata taarifa za CAG zinaonesha kwamba ileasilimia 20 katika baadhi ya Halmashauri imekuwa hairudikule kwenye vijiji kwa sababu tu ya malalamiko kwambawamekusanya kidogo sana.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Waitara nilikuona, swali la mwishola nyongeza kwenye eneo hili.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Mimi ni Mwenyekiti wa Serikali ya MtaaMstaafu, Mtaa wa Kivule. (Makofi)

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kutokutoamaelekezo mahsusi ya Wenyeviti wa Mitaa kulipwa poshoinapelekea mzigo huu kupelekwa kwa wananchi ndiyomatokeo ya zile barua ambazo zinalipiwa, wananchiwanatwishwa mzigo huu. Kwa hiyo, ningeomba nijue, kwakuwa Serikali imechukua vyanzo mbalimbali vya mapatokutoka Halmashauri na Halmashauri haipeleki fedha hizokulipa Wenyeviti wa Mitaa na wanafanya kazi kubwa masaa24.

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini isiwekwe sheria mojakwa moja ili wadai kama haki? Kwa sababu sasa hivi ni poshokwa hiyo hawana uhalali wowote ule, Halmashauri inaamuailipe ama asilipe. Ni kwa nini Serikali isiwajali watu ambao niwengi sana katika nchi hii, wanafanya kazi kubwa sana yamiradi, ulinzi na usalama, usafi na ku- impose sheriambalimbali walipwe pesa ya kisheria badala ya hii ambayoni hiari?

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo la Mheshimiwa Waitarakutoka TAMISEMI, Mheshimiwa Joseph Kakunda, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) : MheshimiwaSpika, kama anavyosema ni kweli Wenyeviti wa Serikali zaVijiji, Vitongoji na Mitaa wanafanya kazi kubwa na nyingi nakweli mzigo ni mkubwa sana kwa upande wao. Sisi kamaWabunge na Serikali tunawategemea sana katika kazi zetuza kila siku. Ili kazi zetu na za Serikali ziende lazima walewafanye kazi.

Mheshimiwa Spika, sasa mapendekezo ambayoanayatoa na kuhusisha kwamba Serikali imechukua vyanzovingi vya mapato kwenye Halmashauri, mimi natakanimhakikishie kwanza kwamba vyanzo ambavyovimechukuliwa siyo vingi…

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) : MheshimiwaSpika, vyanzo vingi bado vipo katika Halmashauri na ndiyomaana tumewaambia kwamba wafanye mapitio.Wakishafanya mapitio Halmashauri ambayo itakuwa nachangamoto za ziada basi wataleta taarifa TAMISEMI natutaweza kuifanyia kazi.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na swalilinalofuata la Mheshimiwa Zuberi, Mbunge wa Liwale.

Na. 489

Mgogoro wa Mpaka wa Wilaya yaLiwale na Wilaya ya Kilwa

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:-

Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa mpakakati ya Wilaya ya Liwale na Wilaya ya Kilwa:-

Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro huo ili kuletaamani katika Wilaya hizo kabla amani haijatoweka?

SPIKA: Majibu ya swali hilo la wananchi wa Mirui,Mtawawa, Mkundi, Makonjiganga, tafadhali MheshimiwaNaibu Waziri. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ZuberiMohamed Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kilwa ilianzishwa kwaTangazo la Serikali Na. 91 la tarehe 16 Mei, 1947 na Wilaya yaLiwale ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na.185 la tarehe 5Desemba, 1980. Hadi hapo hakukuwa na mgogoro wowote.Tangazo la Serikali Na. 134 la mwaka 1983 lilianzisha

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Halmashauri za Wilaya ambapo Mirui iliorodheshwa kamakata na kijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale nahaikutajwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali inautambua mgogoro huounaohusu mkanganyiko ulioko kati ya Kitongoji cha Miruikatika Kijiji cha Nanjirinji A, Kata ya Nanjirinji, Wilayani Kilwakwa upande mmoja na Kijiji cha Mirui katika Kata ya MiruiWilayani Liwale kwa upande wa pili.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mgogoro huo nisehemu ya migogoro mingi inayoshughulikiwa na Serikali chiniya uratibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMakazi, nashauri Mbunge na wananchi wa maeneo husikawawe na subira wakati huu ambapo Serikali imetumawataalam kwenye eneo hilo la mgogoro wanaofanyamapitio ya kina ya matangazo ya kuanzisha wilaya zote mbilina tangazo la kuanzisha halmashauri zote mbili kwa lengola kuhakikisha mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi wakudumu ndani ya mwaka 2018/2019.

SPIKA: Swali la nyongeza, Mheshimiwa ZuberiKuchauka, Mbunge wa Liwale.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Pamoja na majibu yanayoridhisha ya MheshimiwaWaziri, mgogoro huu, kama mwenyewe anavyokiri ni wamuda mrefu na mimi nimeshakwenda kwa MheshimiwaWaziri wa Ardhi akaniambia kwamba mgogoro huu badouko kwenye ngazi ya mkoa, watakaposhindwa ngazi yamkoa watauleta Wizarani. Nimekwenda kwa Mkuu wa Mkoaameniambia kwamba yeye ameshauandikia Wizarani kwamaana ya kwamba wameshashindwa.

Mheshimiwa Spika, hata h ivyo, mimi mwenyewebinafsi nimemuandikia Mheshimiwa Waziri kumjulishamgogoro huu mpaka sasa hivi sijapata majibu yoyote. Sasakutokana na huu mkanganyiko wa kauli za Serikali, Mkuu waMkoa anasema hili na Waziri anasema lingine, nini kauli yaSerikali juu ya mgogoro huu yaani nani kati yao yuko sahihi?

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Spika, swali la pili, anasema mgogorohuu utashughulikiwa mwaka huu wa 2018/2019. Je,Mheshimiwa Waziri, yuko tayari kuandamana na mimi baadaya Mkutano huu twende akaangalie hali halisi? Kwa sababutayari watu walishaanza kuchomeana ufuta, juzi hapaufuta wa Kijiji cha Mirui umekatwa na wananachi wa kutokaKilwa.

SPIKA: Hivi upande wa Nanjirinji Mbunge wake niMheshimiwa Bwege au Mheshimiwa Ngombale?

MBUNGE FULANI: Ni Mheshimiwa Bwege.

SPIKA: Sasa Mheshimiwa Kuchauka mnashindwakukaa ninyi wawili mkalimaliza?

Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo. Naibu Waziriwa Ardhi amesimama, tafadhali Mheshimiwa Naibu Waziri,TAMISEMI. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi, MheshimiwaAngeline Mabula. Pole sana kwa msiba Mheshimiwa NaibuWaziri.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba yafamilia, napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wabungewote kwa namna ambavyo wameshiriki katika msiba huu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni wiki mbili tu kabla ya msibanilikuwa kule na nimefika mpaka kwenye jimbo lake. Taarifanilizozipokea kutoka mkoani, walisema migogoro yotewalikuwa wameorodhesha na wakasema kama mkoawameunda timu za kiwilaya wanashughulikia migogoro yao,itakapowashinda wataileta Wizarani na taarifa ya maandishiwamenipa.

Mheshimiwa Spika, nataka tu nimhakikishie kwambapamoja na kwamba timu ya Wizara iko kule katikakushughulikia ule mgogoro, lakini pia mkoa ulijiridhisha naukaniridhisha pia mimi nilipokuwa kule kwamba migogoro

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

yao wanaisimamia wenyewe kwa sababu haijawashinda nawakikamilisha Wizara itakwenda kuweka mipaka, hasakatika yale maeneo ambayo yana utata wa mipaka.

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, nimekuona,tafadhali.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Kama ilivyo Liwale,Wilaya ya Hanang kila upande imezungukwa na migogoroya mipaka kati yake na Mbulu, Singida na Kondoa. Natakakujua TAMISEMI itachukua hatua gani, kwa sababu imekuwamuda mrefu mno, hatimaye watu watauana kule ili hayamatatizo ya mpaka yanayotukabili yaweze kutatuliwa nawatu waishi kwa amani? Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi, majibutafadhali.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEOYA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Migogoro yamipaka iko mingi katika maeneo mengi lakini suluhisho lakwanza katika kutatua ile migogoro ni kwa pande zote mbiliza maeneo husika kukaa. Kwa hiyo, pale wanapokuwawamekaa wamekubaliana kwa pande zote mbili na hasapanapokuwa na utata, hapo ndipo Wizara inakuja kuingiakwa ajili ya kusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe tu, pamoja naswali la Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu na wengine ambaowana migogoro, pale inaposhindikana ndipo hapotunatakiwa kuingilia kati kwa sababu huwezi kuingilia katikabla pande zote mbili hazijakaa na kuridhia na kwakuangalia zile GN zilizounda maeneo hayo ziko katikautaratibu upi.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri.Twende Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, swali laMheshimiwa Jaku Hashim Ayoub, Mbunge wa Baraza laWawakilishi.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Nami nikushukuru na nikupongeze kwa dhatikabisa kwa jinsi unavyoendesha vikao hivi hasa ukiwa makinikutetea backbenchers.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naombaSerikali itoe majibu ya swali na.490 na naomba Mawaziriwasikasirike. (Kicheko)

Na. 490

Mawaziri Kutopatikana kwenye Simu

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:-

Mawaziri kama walivyo viongozi wengine wa Serikali,wapo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na kwambawananchi wamewachagua Wabunge na Mawaziri (Serikali)ili kuwasiliana, kushirikiana na kushauriana katika kutatua kerozao; lakini kwa bahati mbaya sana wapo baadhi ya Mawaziriambao kupatikana kwao hata kwenye simu ni jambo gumukupita kiasi:-

(a) Je, Serikali haioni kuwa ipo haja ya Mawaziriwenye tabia hiyo ya kujichimbia na kutopatikana kwenyesimu kuacha tabia hiyo kwa maslahi ya wananchi?

(b) Je, Serikali itakubaliana nami kuwa ipo hajaya kuweka utaratibu maalum wa kuifikia Serikali iwapowananchi kupitia Mbunge wao wana shida ya kumuonaWaziri anayehusika na akawa hapatikani hata kwa simu?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa KapteniMstaafu Mkuchika na unaombwa usikasirike. (Kicheko)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Jaku Hashim Ayoub, Mbunge anayewakilisha pia

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Baraza la Wawakilishi, lenye sehemu (a) na (b), kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa KanuniB.3(1) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka2009, simu ni moja ya njia za mawasiliano halali Serikalini.Waheshimiwa Mawaziri wanafanya kazi zao kwa lengo lakuwahudumia wananchi na wananchi nao wana nafasi yakutoa maoni na shida zao na hatimaye kupata mrejesho.Mpaka sasa Serikali haina ushahidi wa kuwepo Mawaziriambao kwa makusudi hujichimbia na kutopatikana kwasimu. (Makofi)

(b) Mheshimiwa Spika, zipo njia mbalimbaliambazo wananchi wanaweza kuzitumia kuwasilisha maonina kero zao ofisini kwa Waziri licha ya simu peke yake.Wananchi wanaweza kuandika barua, kupiga simu, baruapepe kwa viongozi na watendaji wa Wizara kamaMakatibu Wakuu au Makatibu wa Waheshimiwa Mawazirina taarifa za wananchi zitamfikia Mheshimiwa Waziri nakufanyiwa kazi.

SPIKA: Mheshimiwa Jaku, swali la nyongeza.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Wazirikutokuwa na afya kwa upande wangu, niwapongeze sanaNaibu Mawaziri; Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uchukuzi naMawasiliano, Mheshimiwa Engineer Atashasta Nditiye naNaibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, kwakupokea simu kwa wakati, niwapongeze sana kwa hili nawengine naomba wafuate mfano huu.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, hizoKanuni nani anazisimamia ili hao Mawaziri ambao wamohumu ndani, hawapokei simu zikiwemo za Wabunge, mbalina za wananchi, ili hatua zichukuliwe? Ikiwa namba za ma-RPC ziko hadharani na ziko katika mtandao, sababu ganizinazosababisha Mawaziri hao namba zao zisiwe hadharani?Hilo la kwanza.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Spika, la pili, Mheshimiwa Waziri kablaya kupata Uwaziri hapa, Mheshimiwa Spika ni shahidi, alikuwamkali kutetea wananchi wake na akawa ngangarikwelikweli. Ni lini Mawaziri namba zao zitatangazwahadharani ili wananchi na Wabunge watakapowapigia simuwapokee?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Utumishi na Utawala Bora, Mheshimiwa Kapteni MstaafuMkuchika, tafadhali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Spika,maswali yake kwa kweli ni moja lilelile limejirudia lakini pianafikiri kuna mchanganyiko kidogo katika swali lake.Analalamika kwamba Mawaziri hawapatikani kwa simulakini wakati huohuo analalamika kwamba namba zaohaziko hadharani. Sasa hao ambao huwapati kwa simu niwapi kama simu zao hunazo? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, sasa kwa kujibu swali lake, nanianazisimamia hizo Kanuni nil izozitaja? Kanunizinasimamiwa na Serikali, kila Wizara kuna viongozi wakena Wizara ya Utumishi inasimamia Kanuni zote za watumishiwa umma.

Mheshimiwa Spika, sasa ilimradi tumeshasema katikajibu la msingi kwamba hatuna ushahidi wa Waziri ambayekwa makusudi hataki kupatikana, ndiyo maanahatujamchukulia hatua maana hatuna taarifa hizo. KilaWaziri hapa ana mkubwa juu yake, akizileta kama mimi siyosize yangu nitazipeleka juu, lakini atuletee na siyo kwakowewe tu, Mtanzania yeyote yule ambaye anaonakwamba hakutendewa haki, hampati Waziri kwamakusudi, hilo kwa makusudi naliweka kwenye, Wazunguwanasema inverted commas, maana yake mimi sina ushahidinalo hilo.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana kila Wizara kunasanduku la maoni. Sanduku lile una jambo la kuishauri Wizara,

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

una jambo umetendewa vizuri na Wizara unaandikaunawapongeza, una jambo umefanyiwa vibaya na Wizaraunaandika unawasema.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Kapteni Mkuchikakwa majibu mazuri ya swali hilo kuhusu WaheshimiwaMawaziri. Mheshimiwa Mkuchika lakini WaheshimiwaWabunge wamekuwa wakiniandikia hapa, sina majibu,wananiuliza kuhusu Yanga, wanasema hivi Yanga bado ipoau? (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wizara yaMifugo na Uvuvi, swali la Mheshimiwa Joseph KashekuMusukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Naomba nikutaarifu tu kwamba Yangabado ipo. (Makofi/Kicheko)

Na. 491

Kuzuia Shughuli za Uvuvi Katika Ziwa Viktoria

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:-

(a) Je, ni utafiti gani umefanyika katika ZiwaVictoria mpaka kufikia hatua ya kuzuia uvuvi wa aina yoyotekwa kisingizio cha uvuvi haramu?

(b) Je, ni sheria gani inatumika kukamata nyavuna ndani ya dakika kumi zinachanwa bila ya kumpa mvuvinafasi ya kujitetea?

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa GeitaVijijini, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kamaifuatavyo:-

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Mheshimiwa Spika, Serikali haijazuia uvuvi wa ainazote kufanyika katika Ziwa Viktoria. Uvuvi unafanyika nchinikwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 naKanuni zake za mwaka 2009 pamoja na sheria nyingine zanchi yetu. Aidha, kwa sasa Serikali inapambana na uvuviharamu katika Ziwa Viktoria kama ilivyo katika maeneomengine kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimali zauvuvi hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, upo utaratibu wa kisheria wakukamata na kuharibu zana za uvuvi zinazotumika katikauvuvi haramu. Taratibu hizo zimeelezwa vizuri kwenye KanuniNa. 50(1), (2) na (5) ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009. Aidha,nyavu haramu huteketezwa kwa idhini ya Mahakama baadaya taratibu zote za kisheria kufuatwa.

SPIKA: Mheshimiwa Joseph Musukuma, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Dhana ya uvuvi haramu imeenea sana kwenyekauli za Mawaziri, lakini kule ziwani kuna aina za samakikama 30 na samaki pia wana makuzi tofauti, ni kamabinadamu. Ukichukua umri wa Musukuma ukachukua na umriwa Mwalongo, tuko sawa, lakini ukituangalia kwa maumbiletulivyo tuko tofauti na unapotupa nyavu ziwani inakuja nasamaki za aina tofauti wakiwepo wenye tabia kama yanguna Mwalongo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ukiwapima kwenye rulahawalingani lakini umri ni mmoja. Kwa kuwa sheria yenyewendiyo inajichanganya, ni lini Wizara itakuja na sheria ambayoitam-favour pia mvuvi anapokumbana na matatizo kamaya maumbile ya binadamu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mheshimiwa Waziriwakati operesheni hii inapoendelea, kumekuwa na tabia yakukamata nyavu saa nne na zinachomwa saa sita. Mfanomzuri ni kwenye Kisiwa cha Izumacheri kilichopo Jimbo laGeita Vijijini ambapo Maafisa Uvuvi walikamata nyavu

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

ambazo siyo haramu lakini wakanyimwa rushwa,wakachoma nyavu dakika 15 zilizofuata na nyavu hizi nihalali. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana na mimikwenda kusikiliza SACCOS hiyo na kutoa adhabu kwa walewaliohusika na suala hili? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Abdallah Ulega.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaSpika, kuhusu suala la lini Serikali itakuja na sheria mpyaitakayowasaidia wavuvi waweze kufanya shughuli zao kwauzuri zaidi, hasa ikizingatiwa hili analolisema la kwambasamaki wako wa aina tofauti na ile nyavu inapoingiainakwenda kuzoa hata wengine wasiohusika.

Mheshimiwa Spika, Serikali tupo katika hatua yamwisho ya maboresho ya Sheria yetu ya Uvuvi naitakapokuwa tayari itaingia humu Bungeni ambapoWaheshimiwa Wabunge watashiriki kikamilifu katikakuhakikisha kwamba sheria ile tunaiboresha kwa pamojakwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ameeleza juu yasuala linalohusu nyavu, ya kwamba nyavu hizizinapokamatwa ghafla tu zinachomwa moto na akanitakakama niko tayari niweze kufuatana naye kwa ajili ya kuwezakwenda kuwachukulia hatua wale watumishi wa Serikaliambao wanatenda kinyume.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie MheshimiwaMusukuma na Waheshimiwa Wabunge wote na hatawananchi wote wanaoshughulika katika shughuli hizi zauvuvi, Wizara yangu tuko tayari kabisa sisi kamaviongozi kwa specific cases kama hii anayoizungumziaMheshimiwa Musukuma, tutakwenda popote pale na endapotutabaini watumishi wetu wametenda kinyume sisi kamaMawaziri tuko tayari kuwachukulia hatua kwa ajili yamustakabali mpana zaidi wa wananchi na wavuvi wetu.(Makofi)

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

SPIKA: Hili swali tulibakize kulekule Kanda ya Ziwa,Mheshimiwa Constantine Kanyasu na Mheshimiwa JosephMkundi wa Ukerewe.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa nafasi. Naomba nimpongezeMheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Kwa mujibuwa Kanuni za Uvuvi, ukienda kifungu cha 45(3)(b), naombanisome, kinasema:-

“No person shall:

(b) fish, land or possess, process or trade in Nile tilapiaor fish locally known as “Sato” the total length of which isbelow 25 centimetres.”

Mheshimiwa Spika, ukisoma Kanuni hii, ni kamainafikiria source ya Sato ni moja tu, Nile Tilapia lakini sasaTanzania tuna-encourage watu kufanya aquaculture, maanayake sources za sato ziko nyingi, lakini tuna maziwa na mitona Kanuni hii imetumika kusababisha usumbufu mkubwasana kwa watumiaji wa sato nchi nzima. Ni lini Serikali au nikwa nini Serikali isisitishe sasa kukamata watu kwa kutumiaKanuni hii ambayo yenyewe tu inajichanganya na ina makosampaka itakapofanyiwa marekebisho? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mheshimiwa Luhaga Mpina, majibu tafadhali.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,nishukuru sana kwa swali hili la nyongeza la MheshimiwaKanyasu, lakini nimpongeze sana Naibu wangu kwa majibumazuri sana aliyoyatoa hapo awali.

Mheshimiwa Spika, kama alivyoisoma Kanuni yetu nakama Naibu Waziri alivyoeleza, mwezi huu wa Saba, Wizarayangu itakuwa imemaliza zoezi la kufanya mapitio ya Kanuniya Uvuvi pamoja na Sheria yenyewe ya Uvuvi Na. 22 yamwaka 2003. Vilevile kwa nyongeza ni kwamba opereshenihizi zinazoendelea na wananchi wetu ambao wanajishirikisha

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

na ufugaji wa samaki, kila wanapofikia kuvuna samaki waowanawasiliana na ofisi yangu ambayo inakuwa inazo taarifaza uhakika juu ya uvunaji wa samaki hao ili kusije kukatokeausumbufu wa aina yoyote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, katika kipindi ambachoKanuni inarekebishwa, utaratibu umewekwa na Wizarakwa maana ya kwamba mawasiliano yako proper yanamna ya uvunaji kwa sasa wakati tunatengenezaKanuni ambayo itakuwa ime-favour uvunaji wa samakikatika Ziwa Viktoria lakini wakati huohuo na walewafugaji wetu wa samaki ambao wanafuga samaki kwenyemaji.

SPIKA: Nilikuwa nimekutaja Mheshimiwa JosephMkundi, Mbunge wa Ukerewe na Mheshimiwa Dkt. Chegeniatakuwa wa mwisho kwenye eneo hili.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Kwa kuwa baada ya operesheni nyavuzinazotumika sasa ni mbovu sana, hazina kiwango na walahazistahili kutumika kwa uvuvi, zinawatia hasara sanawatumiaji. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kupatanyavu zinazostahili, zinazoweza kukabiliana na mazingira yaMaziwa Viktoria, Tanganyika na mengineyo ili wavuvi wetumbali na kupata hasara za kuchomewa nyavu wasiendeleekupata hasara za kununua nyavu kila siku chachezinapokuwa zinapita? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziriwa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Abdallah Ulega,tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaSpika, juu ya suala linalohusu ubora wa nyavu, ni kweli Wizarayangu imepokea malalamiko kutoka kwa wavuvi kutokapande zote za nchi yetu hasa wavuvi wa Ziwa Viktoria natumekwenda kujir idhisha. Tupo katika utaratibu wakuendelea kufanya tathmini ya hali hii. Nataka nimhakikisheMheshimiwa Mbunge kwamba tunashirikiana vyema na

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

wenzetu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa ajili yakuweza kupata viwango halisi vya ubora wa nyavu zetuzinazozalishwa nchini.

Mheshimiwa Spika, pale itakapobainika kwamba likotatizo juu ya ubora huu, la kwanza tutawataka amatunawataka wazalishaji wetu waongeze viwango vyao vyaubora, lakini ikibidi sisi kama Wizara tuko tayari kutafutampango mwingine wa kuweza kuwanusuru wananchi wetuili waweze kuendelea na shughuli hii ya uvuvi bila ya tatizololote.

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Chegeni, swali kutokaBusega.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza swali lanyongeza. Zoezi la uvuvi haramu limetekelezwa sivyo ndivyokatika maeneo mengi sana na wavuvi wengi sanawamepata hasara kubwa sana kutokana na zoezi hili. Zoezihil i l imefanywa na wafanyakazi ambao kwa kwelihawakuzingatia maadili na hata kanuni za kazi zao. Ilifikiamahali Mheshimiwa Waziri akasema kwamba yeye hanawapiga kura wavuvi hao wenye wapiga kura wavuvimtajijua wenyewe. Nataka kujua kauli ya Serikali, wavuviambao wameingizwa hasara kubwa sana watalipwa fidiakiasi gani na lini fidia hiyo italipwa?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri waMifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Mpina, tafadhali.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,suala la uvuvi haramu tumeeleza mara kwa mara hapaBungeni na jinsi ambavyo linaendeshwa. WaheshimiwaWabunge tumewaomba mara kwa mara kwamba kamakuna mtu ambaye ameonewa katika eneo lolote liletuletewe ili sisi tuweze kuchukua hatua. Leo ni miezi sitaWizara yangu inasisitiza suala la watu walioonewakuwasil isha malalamiko yao il i waliohusika wawezekuchukuliwa hatua.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo Wizara yanguhaiwezi kujua ni kitongoji, kijiji na kata gani, ni lini, Mkaguzinani na alifanya makosa yapi kwa sababu hatua zaukamataji zipo. Sasa ikiendelea kuzungumzwa hivi kilasiku kwamba watu wameonewa, halafu ushahidihupewi, Waziri huwezi kuwa kwenye nafasi ya kuchukuahatua.

Mheshimiwa Spika, hili Bunge ndiyo linalotunga sheria,kwa nini Waziri alaumiwe na kuandamwa kwa kuchukuahatua za watu ambao wamevunja sheria? Nataka nisemekwamba wananchi na watu wote wataendelea kuchukuliwahatua kwa mujibu wa sheria tulizonazo leo na kwa mujibuwa Katiba tuliyonayo sasa, watakaguliwa mahali popotena wakibainika watachukuliwa hatua. Watu wotewanaojihusisha na uvuvi haramu bila kujali vyeo vyao,wataendelea kuchukuliwa hatua mahali popote walipo kwamujibu wa sheria tulizonazo.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inasisitiza kamakuna mtu yeyote ambaye ana ushahidi dhidi ya manyanyasoau uonevu wa aina yoyote umefanywa na Afisa wangu sikuhiyo hiyo hatua zitachukuliwa.

SPIKA: Nami niongeze, Waheshimiwa Wabunge walemnaotoka Kanda ya Ziwa, kama kuna malalamikomleteeni Spika. Leteni hapa na sisi tutaipa Serikali iwezekuangalia kwa sababu si nia ya Serikali wala mtu yeyotekuona kwamba mtu yeyote anaonewa popote pale katikanchi hii.

Waheshimiwa Wabunge, kwenye zile Kanuniningeshauri sana pia, kwa sababu hili ni jukumu lenu pekeyenu Serikali lakini Kamati yetu inayohusika na mambo yauvuvi nao kidogo watazame ili waweze kutoa ushauri waujumla. (Makofi)

Tunaendelea na Wizara ya Kil imo na swali laMheshimiwa Njalu Daudi Silanga, Mbunge wa Itilima,Mheshimiwa Silanga, tafadhali.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Na. 492

Kuporomoka kwa Zao la Pamba Nchini

MHE. NJALU D. SILANGA aliuliza:-

Tanzania ni nchi yenye mazao ya biashara kamapamba, korosho, tumbaku na kahawa. Zao la pamba linazidikuporomoka kutoka wastani wa ekari moja kilo 400 hadi kilo120 kwa ekari moja ikilinganishwa na nchi kama China ekarimoja kilo 2,000, India kilo 1,500, Burkina Faso kilo 1,200 nawastani wa uzalishaji wa dunia ni kilo 1,200 kwa ekari moja:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kunusuru zao hilo?

SPIKA: Mheshimiwa Silanga, kule Kongwa kunangoma inaitwa Silanga acha kabisa, siku moja nitakupelekaukaione. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, majibu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Njalu Daudi Silanga,Mbunge wa Jimbo la Itilima, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Mkakati waKuendeleza Zao la Pamba unaoratibiwa na Bodi ya PambaTanzania kwa lengo la kuhakikisha kuwa tija na uzalishajiwa pamba nchini vinaongezeka. Kutokana na utekelezajiwa mkakati huo, uzalishaji wa pamba msimu 2017/2018unatarajiwa kufikia zaidi ya tani 600,000. Aidha, mafanikiohayo yanatokana na upatikanaji wa mbegu bora, viuatilifu,huduma za ugani, uchambuaji na uongezaji thamani wazao hilo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadauimeanzisha Mkakati wa Kuzalisha Pamba hadi Mavazi kwamaana ya (Cotton to Clothing Strategy 2016-2020) ambao

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

unatarajia kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka wastaniwa kilo 600 hadi 700 kwa ekari kwa sasa na kufikia kilo 1,800kwa ekari ifikapo mwaka 2020.

Mheshimiwa Spika, aidha, mkakati huo unalengakuongeza utengenezaji wa nyuzi kutoka wastani wa tani30,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 90,000 ifikapo mwaka2020 pamoja na kuongeza mauzo ya bidhaa za pamba njeya nchi kutoka wastani wa Dola za Marekani milioni 30 hadikufikia milioni 150 kwa mwaka 2020.

Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha ongezeko la tija naubora wa pamba, Serikali imechukua hatua ya kuimarishamfumo wa uzalishaji wa mbegu za pamba ambapo kuanziamsimu 2018/2019, maeneo yote yanayolima pambayatatumia mbegu aina ya UKM08 na kuachana kabisa nambegu aina ya UK91 ambayo haina ubora. Aidha, aina mpyaya mbegu za pamba UK171 na UK173 zilizoidhinishwa mweziJanuari, 2018 zinaendelea kuzalishwa kwa wingi na zitaanzakuwafikia wakulima kuanzia msimu wa kilimo cha pambawa 2021/2022.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Swali la nyongeza, Mheshimiwa Mbunge Itilima,tafadhali Mheshimiwa Silanga.

MHE. NJALU D. SILANGA: Mheshimiwa Spika, kwanzaahsante sana kwa kunialika kwenda kuona ngoma, nikotayari kwenda huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kwanzakumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa majibu yakemazuri aliyonijibu. Hivi sasa maeneo mengi yameonekanakuwa na ugonjwa wa mbegu hii UKM08. Je, Serikaliinatoa tamko gani kwa wakulima wa zao la pambakwa maeneo ambayo yanaathirika na ugonjwa huuFusarium hasa ikizingatia kwamba viuatilifu vinavyokujahavifikii viwango na kusababisha mashamba mengikuharibika?

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa NaibuWaziri ameelezea kwamba kuna mkakati mzuri kwa mwaka2016/2017 ekari moja imeweza kuzalisha kilo 300 lakini kwamwaka 2016/2017 wastani ambao tumeweza kukusanya kwanchi nzima kwa maana kwa mikoa 17 na wilaya 56 ni takribanikilo milioni 120. Kwa hiyo, atakubaliana nami kwamba zaola pamba linazidi kuporomoka. Ukigawanya kwa wastanikatika zao zima kwa nchi nzima ni Mkoa mmoja tu wa Simiyuwenye kuzalisha kilo 70,000 na mikoa 16 ndiyo unaigawanya.Kwa hiyo, kama Wizara iko shughuli ya kufanya kuhakikishazao hili linaongezeka kwa uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Majibu ya swali hilo la Mheshimiwa Silangapamoja na ushauri alioutoa.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awalikabisa, naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwasababu amekuwa akifuatilia sana juu ya zao zima la pambana hasa ukizingatia na yeye pia ni mfanyabiashara wa zaohili la pamba.

Mheshimiwa Spika, nikija kwenye maswali yake mawilimadogo ya nyongeza kwa ufupi kabisa na kwa pamoja nikwamba zao la pamba kama zao la pamba na mbegu, sisikwenye zao la pamba zile mbegu huwa inachukua mudamrefu sana na ukizingatia kwamba mbegu hizo tunazosemautafiti unafanyika muda mrefu muda wa karibu sana na kwaharaka ambao unaweza ukafanyika ni ile miaka mitano. Kwamaana hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge naWaheshimiwa Wabunge wote wajue kabisa kwamba sualazima la utafiti huwa linachukua muda mrefu na muda mfupiambao unaweza ukafanyika ni kipindi cha miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake lile la pili lanyongeza kwamba kwa nini kilimo hiki cha zao la pambakimeporomoka, ni kweli kwamba wakulima walikuwahawafuati zile kanuni bora za kilimo cha pamba. Nichukefursa hii kumpongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

Mkuu kwa sababu amekuwa ni champion, amekuwaakihamasisha na akiwaeleza hata Wakuu wa Mikoa juu yaufuatiliaji wa zao zima la pamba.

Mheshimiwa Spika, vilevile amemuagiza hataMheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kuboresha suala zima laugani. Pia kama Serikali tumejipanga kuhakikisha kwambakatika msimu wa 2018/2019, tutaboresha zao la pambakutoka hiyo tani 300,000 kwa ekari hadi tani 600,000 kwakuzingatia hayo maelezo ambayo nimesema ili wakulimawote nchini waweze kuhakikisha kwamba wanafuata kanunibora za kilimo cha pamba.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Tunaendelea na swali l inalofuata laMheshimiwa Albert Obama Ntabaliba, Mbunge wa Buhigwe.

Na. 493

Fidia kwa Wakulima wa Kahawa Buhigwe

MHE. ALBERT O. NTABALIBA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itawalipa wakulima 435 wa kahawawaliodhulumiwa katika Jimbo la Buhigwe?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Albert ObamaNtabalika, Mbunge wa Jimbo la Buhigwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika msimu wa 2011/2012,Kikundi cha Wakulima wa Kahawa cha Kalinzi Organickilipeleka jumla ya tani 15.8 za kahawa yenye thamani yaDola za Kimarekani 74,397.24 kwa Kampuni ya TanganyikaCoffee Curing Co.Ltd kwa ajili ya kukobolewa na baadayekuuzwa mnadani. Hata hivyo, baada ya kukoboa kampuniya TCCCo Limited ilitambulisha kimakosa kahawa ya Kikundi

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

cha Kalinzi Organic kuwa ni kahawa ya Kikundi cha KalinziCoffee Farmers kwa maana ya (KACOFA) na hivyo Bodi yaKahawa Tanzania kukilipa fedha za mauzo ya kahawakikundi cha KACOFA badala ya Kikundi cha Kalinzi Organic.

Mheshimiwa Spika, baada ya kugundulikamkanganyiko huo, taratibu za usuluhishi zilifanyika namaamuzi yalitolewa ambapo kikundi cha KACOFA kilikubalikurejesha fedha hizo kwa Kikundi cha Kalinzi Organic kupitiamauzo ya kahawa yao ya msimu ule wa 2012/2013. Hatahivyo, katika msimu wa 2012/2013 na 2013/2014 Kikundi chaKACOFA hakikupeleka kahawa ya kuuza kwenye soko lamnada hivyo fedha hizo hazikuweza kurejeshwa kwa Kikundicha Kalinzi Organic kama ilivyoamuliwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya mashauriano kati yauongozi wa kiwanda, Bodi ya Kahawa, Wizara ya Kilimo naviongozi wa Mikoa ya Kilimanjaro na Kigoma iliamuliwa kuwasuala hilo liwasilishwe kwenye vyombo vya usalama kwa ajiliya uchunguzi.

Mheshimiwa Spika, upelelezi wa suala hiloumekamilika na jalada la shauri hilo lipo kwa Mwanasheriawa Serikali ili atoe uamuzi na mapendekezo ya hatua zakuchukua kwa kikundi cha KACOFA. Aidha, naombanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba haki ya Kikundicha Kalinzi Organic itapatikana.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Obama Ntabaliba, nilikuona.

MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Naibu Waziri waKilimo kwa majibu mazuri na kihakika kama Wizarawanaonesha wanalitambua suala hili vizuri. Kwa hilo,nawapongeza sana kwa majibu haya.

Mheshimiwa Spika, kuanzia 2011 - 2018 ni miaka sabasasa, hawa wakulima 435 wanaodai zaidi ya milioni 150 au

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Dola 74,000 bado wanadai. Kwa kuwa Bodi ya Kahawailifanya makosa kumlipa mtu mwingine na Mheshimiwa Waziriamekiri kwenye majibu yako kwamba iko kwa Mwanasheria,wakulima hawa wanataabika na hii ni Serikali ya wakulima,ni lini fedha hizo zitapatikana na Mwanasheria atawezakuliharakisha suala hili?

Mheshimiwa Spika, la pili kwa kuwa hii inatokana namatatizo ya soko hili la kahawa, ni mkakati gani uliopo wabei na masoko ya kahawa kwa wakulima wetu? Wananchiwanataka kusikia. Nakushukuru.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, majibutafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanzanaomba nichukue fursa hii nimpongeze sana MheshimiwaMbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia sana sualazima la zao hili la kahawa katika jimbo lake. Kwenye maswaliyake madogo mawili ya nyongeza, mimi nimejibu kwenyemajibu yangu ya msingi kwamba hili suala liko Mahakamanina jambo linapokuwa Mahakamani, sisi kama Serikalitunaviachia vyombo vya sheria viweze kuchukua mkondowake na ukizingatia pia Mwanasheria Mkuu ndiyo in chargekatika suala zima hili.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili lanyongeza, ni kwamba, kama Serikali hata zao la kahawatumejipanga na tumesema tunafufua, tunaimarisha Vyamavya Ushirika kuhakikisha kwamba wakulima wetu waKitanzania hawaonewi na wanakuwa na strong bargainingpower kupitia Vyama vya Ushirika ili bei zao ziwe nzuri namazao yaweze kuwa bora. Nashukuru.

SPIKA: Nil ikuona Mheshimiwa Bulembo naMheshimiwa Peter Serukamba.

MHE. ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kutokana na swali la msingi, naomba kuulizaWizara ya Kilimo hapo. Kwa kuwa wakulima wa kahawa ni

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

sawasawa na wakulima wa pamba. Wakulima wa pambawamewaruhusu waliofanya biashara ya mkataba wawezekuendelea na shughuli hiyo, lakini wakulima wa kahawakatika nchi wa mkataba hawazidi watano mpaka sita. Kwanini Wizara inakuwa double standard, msimu umeanza sasahivi wiki ya pili watu hawa hawataki kuwapa kibali chakuweza kukusanya kahawa kwa sababu ni biashara yao.Naomba tujue hawa haki yao wanaipata wapi?

SPIKA: Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Dkt. Tizeba,majibu tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, utaratibutuliouweka sasa hivi lengo lake la kwanza ni kuhakikishakwamba wakulima wanapata malipo stahiki kwa jasho lao.Mfumo tuliokuwa nao sasa hivi kwa kiwango kikubwaulikuwa hautoi malipo stahiki kwa jasho la wakulima na mojaya njia zilizotumika kuwanyima haki wakulima ilikuwa nimfumo wa kununua kahawa kwa kulipa advance kutokakwa wafanyabiashara na hasa katika Mkoa ambakoMheshimiwa Bulembo anatoka maarufu kwa jina la Butura.Ili kukabiliana na Butura, lazima kuweka mfumo unaofafanamaeneo yote.

Mheshimiwa Spika, jana nilisema hapa ndani wakatinachangia hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwamba paleambapo mikataba hiyo iliingiwa officially kwamba kunamkataba na mamlaka za Serikali zinatambua mikataba hiyokama ilivyo kwenye pamba, pamba mtu haingii mkatabamtu na mtu mmoja, mikataba hiyo inaingiwa kupitiamamlaka za Serikali, kama wako wakulima wa kahawaambao wameingia mikataba kwa njia hiyo, nilielekezakwamba wapeleke habari hiyo haraka Bodi ya Kahawa iliwaweze kupata utaratibu wa kuuza kahawa kwa mtuwaliyeingia naye mkataba.

Mheshimiwa Spika, ile mikataba ya kuingia kienyejindiyo utaratibu uliokuwa unasababisha watu kupoteza hakiyao na jasho lao kwa kuuza kwa watu ambao wanawapamalipo kidogo kwa kahawa ya bei kubwa.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

SPIKA: Nilikutaja Mheshimiwa Peter Serukambaatafuatia Mheshimiwa Innocent Bilakwate.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.Kwanza KACOFA iko kwenye Kata yangu, Organic iko Kalinzeambako ni Kata yangu. Kwa masikitiko makubwa Wazirianasema kesi iko Mahakamani, si kweli hakuna kesiMahakamani.

Mheshimiwa Spika, kilichotokea, KACOFA walipelekaKahawa na hawa Organic-Kalinze walipeleka Kahawa. Kilekiwanda kil ipouza Kahawa ile kikawalipa KACOFA ,hakikuwalipa Kalinze Organic. Kalinze Organic walipoanzakufuatilia pesa zao wamefanya usuluhishi Wizarani na Bodiya Kahawa mwisho wake Kiwanda kikasema kitawalipa,naomba nitoe maelezo haya; kitawalipa Organic taratibu.

Mheshimiwa Spika, toka mwaka 2011 kiwanda kileambacho kilikubali kuanza kuwalipa watu wa KalinzeOrganic, kwamba tutawalipa taratibu mpaka leo hakijalipa.Waziri anakuja leo hapa anasema suala lipo kwa AttorneyGeneral wakati wameshakubaliana waanze kuwalipataratibu.

Mheshimiwa Spika, swali langu; naomba Wizaraisimamie watu wa Kalinze Organic waweze kulipwa fedhazao kwa sababu makosa haya yamefanywa na kiwanda kilecha Moshi.

SPIKA: Majibu ya swali hilo na ombi hili, MheshimiwaWaziri wa Kilimo, Mheshimiwa Dkt. Tizeba, tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jinsialivyojibu hili swali la msingi la Mheshimiwa Albert Obama.Jambo hili ni la siku nyingi na hatua za awali kamaanavyozisema Mheshimiwa Serukamba ni kweli zilichukuliwanamna hiyo. Kosa lililofanyika ni ku-identify nani anatakiwakulipwa baada ya yule kupeleka ile kahawa kule mnadani.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Bodi ya Kahawailivyopokea yale malipo ikapeleka kwa mtu ambaye alitajwana mtu aliyeleta kahawa kwamba ndiye beneficiary wa hiyokahawa; kwa hivyo wakamlipa na wale watu wakapokeapesa isiyo yao na wakaitumia.

Mheshimiwa Spika, baadaye ilipoonekana kwambawamepokea pesa isiyo yao na wametumia, kwanzawakatakiwa wasuluhishwe tu amicably, wakaitwa, wakakirikwamba watalipa msimu utakaofuata, kwambawatakapouza kahawa msimu unaofuata watalipa hilo deni.Wale waliokuwa wanadai Mheshimiwa Serukambawakakubaliana na hiyo position, kwamba watapewa pesayao msimu utakaofuata.

Mheshimiwa Spika, msimu uliofuata wale mabwanawa KACOFA hawakupeleka kahawa, kwa hivyo sasa kukawana default ya makubaliano hayo; na baada ya hapo ndipotaratibu zikaanza. Nikiri tu kwamba jambo hili liliendapolepole lakini sisi safari hii tulichokifanya tumelipelekakwenye vyombo vya uchunguzi kwanza tujiridhishe kwa niniwalitumia hela ambayo si yao at a time wakati ya kwaowalishalipwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, humu ndani kuna jinai katikati yahili jambo, kwamba mtu amekuta benki fedha ambayo sikwake lakini bila kuuliza benki hela hii imetoka wapi,ameitumia, Sheria za Fedha ziko wazi, umeona! Sasa katikahatua hiyo ndiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali atatushaurisasa hivi tuendelee na hatua gani.

Mheshimiwa Spika, kama atatushauri tuwapelekeMahakamani ili wale viongozi wa ule Ushirika wawezekuchukuliwa hatua wachukuliwe hatua, kwa sababu as wespeak hawa hela ya kuwalipa wale wenzao mara moja,kwamba tungewaambia leteni hizi pesa tuwalipe waleambao wanastahiki ya kupata hizo pesa.

SPIKA: Mheshimiwa Innocent swali la mwisho kwenyeeneo hili.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Sasa hivi nikipindi cha msimu wa kahawa. Vyama vya Ushirikavimeshindwa kuwahudumia wananchi kupata maturubai yakuvunia Kahawa na hii kahawa inaendelea kukaukiaMashambani, wananchi wamekosa msaada. Hata hivyo,hata wale ambao wamepata maturubai, maturubai hayahayana viwango yanachanika hovyo. Ni hatua zipi zadharura ambazo zitachukuliwa ili kunusuru zao hili namkulima aweze kulifaidi? Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziriwa Kilimo, kwa kifupi tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwelitumekuwa na matatizo sana katika suala zima la Vyamavyetu vya Msingi na Vyama Vikuu vya Ushirika na ndiyo maanakama Serikali tunasema kwamba, tuko katika mikakati yakuhakikisha tunafufua, tunaimarisha na kuboresha Vyama vyaUshirika.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo kutokana naswali lake hili la msingi katika Jimbo lake la Kyerwa, kwambampaka sasa hivi kunasuasua, naomba nichukue fursa hiikuagiza Chama Kikuu cha Ushirika cha Kyerwa kuanzia leowahakikishe kabisa kwamba, zoezi zima la mazao yakahawa katika Jimbo la Kyerwa wanafanya kazi yao kwaubunifu, wanafanya kazi yao kwa utii, wanafanyakazi yaokwa weledi, wanafanyakazi yao kwa uhakika.

Mheshimiwa Spika, lakini na mimi kama Naibu Wazirinikitoka hapa Bungeni ninaahidi kuwapigia Vyama Vikuu vyaUshirika vile AMCOS pale Kyerwa nikishirikiana na Mrajisiwangu kuhakikisha kwamba jambo hili halijirudii na linawezakufanikiwa kwa uhakika.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko nilikuona, swali lamwisho kabisa la nyongeza kwenye Wizara hii ya Kilimo.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru mimi nina swali dogo la nyongeza. Tarafa yaHerujuu huko Kasulu tunalima Kahawa nyingi na hasa Kataya Herujuu, Kata ya Muhunga na Kata ya Muganza lakini eneohilo halina Chama cha Ushirika na Chama cha Ushirika kikoBuhigwe kilometa 45. Ni kwa nini Mheshimiwa Waziri asitoeruhusa sasa wakulima hawa wakauza kwa watu binafsi?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, majibu tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, hatuwezikuwaruhusu kuuza kwa watu binafsi kwa sababu tutakuwatume-distort mfumo tunaojaribu kuujenga. Tunajaribu kujengamfumo hapa ambao tukiruhusu hicho anachokisematutakuwa tumeuvuruga tena wenyewe wakati tunajaribukutengeneza.

Mheshimiwa Spika, mimi binafsi Jimboni kwangutunalima kahawa, lakini wale wakulima wa kwangutumewaunganisha na vyama vingine ambavyo vina uwezowa kufika sokoni na sisi tunaendelea tu kumshauriMheshimiwa Nsanzugwanko kufanya namna hiyo. Jambomuhimu hapa ni kuangalia uwezekano wa wao wenyewekuwa na AMCOS yao; na AMCOS zinaruhusiwa kufikishaKahawa kwenye soko kule Moshi.

SPIKA: Ahsante sana, tunaendelea na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.

Na. 494

Mkanganyiko wa Watumishi wa ZimamotoKwenye Viwanja vya Ndege

MHE. LUCIA M. MLOWE (K.n.y. MARY D. MURO) aliuliza:-

Kumekuwepo na mkanganyiko wa watumishi wazimamoto kwenye viwanja vya ndege na viwanja hivyokutokuwa huru katika kuwatumia kutokana na kuwa sisehemu ya waajiri wao:-

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Je, nini kauli ya Serikali kuhakikisha viwanjavinajitegemea?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la MheshimiwaMary Deo Muro, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoajilinasimamiwa na Sheria Namba 14, Sura ya 427 ya Mwaka2007 iliyounganishwa Vikosi vya Zimamoto vilivyokuwa chiniya TAMISEMI na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuwa chiniya Kamandi moja ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamotona Uokoaji.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoajipamoja na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ni Taasisi zaSerikali ambazo hufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kutoahuduma ya kulinda mipaka ya nchi, hivyo hakunamkanganyiko wowote wa kiutendaji. Hata hivyo, naombakulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa upo ushirikianomzuri kati ya vyombo hivi vya ulinzi na usalama naMamlaka ya Viwanja vya Ndege katika kutekeleza majukumuyao.

SPIKA: Mheshimiwa Mlowe nimekuona.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswaliya nyongeza. Pamoja na majibu ya Waziri naomba niulizekama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwawatumishi wa Jeshi la Zimamoto wanafanya kazi katikamazingira magumu na mazingira hatarishi, lakini hawanavifaa vya kufanyia kazi. Je, Serikali ina mkakati ganikuhakikisha watumishi hawa anapata vitendea kazi nchinzima?

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa Mkoa waNjombe hadi sasa Jeshi la Zimamoto hawana Ofisi, je, Serikaliina mkakati gani kuhakikisha inajenga Ofisi pale Njombe?Ahsante.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri, Mhandisi Masauni kutoka kwa Mheshimiwa LuciaMlowe.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, ni kweli tuna changamoto ya vifaa ama vitende kazikwenye Jeshi la Zimamoto na tunafanya jitihada mbalimbalikukabiliana na changamoto hiyo. Moja katika jitihadaambazo tunafanya ni kutenga fedha kwenye bajeti yetu kilamwaka ili kuweza kununua vifaa zaidi ikiwemo magari navitendea kazi vingine mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, vile vile tunajaribu kuimarishamahusiano kati ya Jeshi la Zimamoto kupitia halmashauripamoja na majiji mengine. Wakati huo huo tumekuwatukibuni mikakati mbalimbali ikiwemo mikakati ya kuwezakuchukua program za mikopo ambazo sasa hivi tunamchakato ambao unaendelea. Nisingependeleakuzungumza sasa hivi kwa sababu haujafikia katika hatuaya mwisho, lakini ni moja katika jitihada ambazotunafanya kuhakikisha kwamba Jeshi la Zimamoto linapatavifaa.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la Njombe, nichangamoto ya Ofisi katika mikoa hii mipya. NimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba tunalifahamu hilo natunalichukulia kwa uzito na pale ambapo hali ya kifedhaitaruhusu tutakabiliana na changamoto ya Ofisi katikaMkoa wa Njombe na mikoa mingine hususani mikoamipya.

SPIKA: Mheshimiwa Julius Kalanga, nilishakuona.

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Spika, ahsante,nashukuru kwa kunipa nafasi. Tumekuwa na tatizo la kuungua

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

kwa majengo mbalimbali ya Serikali ikiwemo vyuo na shuleza sekondari hata katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.Je, nini mkakati wa kuhakikisha kwamba angalau kilahalmashauri inapata gari moja la Zimamoto?

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, swali lake linafanana sana na swali ambalo limeulizwakwenye swali la msingi ambalo nimeshalijibu. Kwa hivyo jibulake linakuwa vile vile, kwamba, mikakati ni ile ile ambayonimeizungumza kuhakikisha kwamba tuna dhamira hiyo hiyoya kuona kwamba magari yanafika katika maeneo takribaniyote. Ndiyo maana tumeanza jitihada sasa hivi za kutanuawigo wa kuweza kupeleka huduma ya Zimamoto katikaWilaya nyingi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kila mwaka tumefanya jitihadahizo kwa kufungua Ofisi, kupeleka Maaskari wetu kuanzakutoa huduma za kutoa elimu ili pale ambapo magariyatakapokuwa yamepatikana na vifaa vingine tuwezekuvifikisha huko viweze kusaidia jitihada hizi ambazotumeanza nazo kwa mafanikio makubwa.

SPIKA: Swali la mwisho kwa siku ya leo linaelekezwakwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na linaulizwana Mheshimiwa Flatei Gregory Massay.

Na. 495

Kukosekana kwa Mawasiliano ya Mtandaowa Simu-Mbulu Vijijini

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga minara yaSimu katika Kata za Yayeda, Ampa Arr, Tumati, Gidilim Gorati,Endaagichan na Haydere katika Jimbo la Mbulu Vijijini iliwananchi waweze kuwasiliana?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasil iano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko waMawasiliano kwa Wote (UCSAF) i l iyaainisha maeneombalimbali ya Jimbo la Mbulu vijijini yakiwemo maeneo yaYaeda, Tumati, Gidilim Gorati, Masieda, Endaagichan, naHyadere na kuyaingiza katika zabuni ya awamu ya tatuiliyotangazwa tarehe 5 Juni, 2018. Zabuni hii inategemewakufunguliwa tarehe 23 Julai, 2018. Endapo mzabuniatapatikana, mkataba kwa ajili ya kazi husika unatarajiwakusainiwa tarehe 29 Agosti, 2018 na ujenzi wa minaraunatarajiwa kuchukua miezi tisa tangu kusainiwa kwamkataba.

SPIKA: Mheshimiwa Massay, swali la nyongezatafadhali.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa katikamajibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri amesema mkatabaukisainiwa utachukua miezi sita mpaka mnara ujengwe. Ninaminara mitatu ambayo kimsingi imejengwa miaka miwilimpaka sasa haijamalizika, kwa mfano; mnara wa Airtelambao uko Maga, mnara wa Halotel ambao upo Gidilimna mnara wa Halotel mwingine ambao upo Tumatihaujakamilika. Je, Mheshimiwa Waziri atasaidiaje minara hiiikamilike kwa sababu Serikali imeweka fedha nyingi iliwananchi wa Mbulu vijijini wapate mawasiliano?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa vijiji ni vingiambavyo havina mawasiliano, Mheshimiwa Waziri yuko

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

tayari sasa kuja kuonja taste ya kukaa nje ya mawasiliano?Kwa mfano; Getereri, Mewadan, Migo, Harbaghe, Endadug,Eshkesh, Endamasaak, Gorad na Endamilai, yuko tayari sasakuja ili uone hali ya mawasiliano ilivyo vibaya Mbulu Vijijini iliakatupangia vijiji hivi kupata minara?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia AtashastaNditiye, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ATASHASTA J. NDITIYE) : MheshimiwaSpika, ni kweli kwamba kuna minara mitatu ambayoimefungwa muda mrefu na mpaka sasa haifanyi kaziipasavyo. Kuna mnara wa Maga ambao ulijengwa na Airtel,kuna matatizo yaliyotokea kati ya wakandarasi na jamiiinayozunguka eneo hilo iliyosababisha mpaka sasa hivimgogoro ambao unaendelea kutatuliwa kwa ngazi ya kata.

Mheshimiwa Spika, nahakikisha kwamba naendeleakuwafuatil ia hawa watu wa Airtel kwa sababu waowaliingia mkataba na UCSAF kwa aji l i ya kupelekamawasiliano. Masuala ya mgogoro kati ya Airtel na Katayanatakiwa yatatuliwe miongoni mwao lakini mawasilianoya wananchi wa maeneo ya Maga yapatikane.

Mheshimiwa Spika, vilevile eneo la Gidilim ambakoHalotel wamejenga mnara kuna kama miaka miwilihaujaanza kufanya kazi kutoka na Mkandarasi kutopatavifaa vya kutosha kupeleka maeneo hayo. NimhakikishieMheshimiwa Mbunge kwamba tunafuatilia yote hayopamoja na Yaeda, Ampa ambako Halotel vi le vilewamefunga ili kuhakikisha kwamba hiyo minara inaanzakufanyakazi kwa haraka sana.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ni kuhusukuambatana na yeye kuona maeneo hayo aliyoyataja.Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana MheshimiwaMassay, kwa kweli anafanya kazi kwa bidii sana. Mudamwingi sana huwa tunawasiliana kuhusu masuala ya

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

mawasil iano; na mimi kama mwenye dhamana yamawasiliano namhakikishia kwamba Serikali tunajuaumuhimu wa kuwa na mawasiliano kwa wote kwa sababumpaka sasa hivi tuna asil imia 94 ya Watanzaniawanawasiliana. Hatutaki wabaki hata kidogo inapofikamwisho wa mwaka huu, tunataka Watanzania wote wawewanawasiliana. Ahsante sana.

SPIKA: Waheshimiwa mtaona muda hauko upandewetu, nawaombeni tuendelee na mambo mengine yaliyokatika meza na kama mnavyojua leo mambo ni mengi sanana leo ni siku maalum.

Nitaanza na matangazo ya wageni, na tunao wageniwengi; Waheshimiwa Wabunge naomba tusikilizane kidogo:-

Mgeni wangu wa kwanza ni mtu ambaye ningependakumtambulisha kipekee kabisa Waheshimiwa Wabunge.Mtakumbukwa kwamba mwezi uliopita mwezi Mei, hebunaomba tusikilizane, tusikilizane wale wote mnaongeaongea. Please hasa huu upande wangu huu una shida huu,Chief Whip watu wako huku uwe unaangalia wanapiga sanakelele hawa.

Mwezi uliopita palikuwa na Harusi ambayo ilivuta hisiaza Watanzania wengi, nafikiri wengi mliona kwenye vyombovya habari ambapo bibi harusi alikuwa amembeba bwanaharusi ambaye ni mlemavu. Sasa maharusi hawa ni wageniwangu leo na ninao hapa Bungeni lakini pia ni wageni waMheshimiwa Zuberi Kuchauka, Mbunge wa Liwale, na ninaokatika jukwaa pale ni Ndugu yetu Jivunie Mbunda na mkewe.Naomba msimame hapo mlipo. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,ambebe tuone

SPIKA: …na Jivunie, mama hebu mbebe mzee hapo,asante sana, asante sana, sana. (Makofi/Kicheko/Vigelegele)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Baby! Baby!

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

SPIKA: Ahsante sana, ahsante sana mnaweza kukaasasa. Ni upendo ulioje, hebu tuwapigie makofi menginemaharusi hawa. (Makofi/Vigelegele)

Bwana Mbunda na mama kabla hamjaondokabaadaye kwenye saa saba nawaalika muonane naMheshimiwa Spika kidogo, tunong’one kidogo; ahsante sana;huo ndio upendo halisi kabisa kabisa.

Waheshimiwa tuendelee kusikil izana; wageniwengine tulionao katika majukwaa yetu ni wageni waMheshimiwa Januari Makamba Waziri wa Nchi, ofisi yaMakamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambao niwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaotokea Jimbola Bumbuli Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. UDOM walewageni wa Mheshimiwa Makamba, wale pale karibuni sana.(Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Japhet Hasunga, Naibu Waziriwa Maliasili na Utalii, ambaye ni mwimbaji wa nyimboza injili kutoka Dar es Salaam, Ndugu Catherine MadiLukindo, Catherine Lukindo, karibu sana Catherine.(Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa John Kadutu ambaye nimwandishi wa Jembe FM kutoka Jijini Mwanza ndugu JumaAyo, yule pale, karibuni. (Makofi)

Wageni wanne wa Mheshimiwa Allan Kiula ambaoni Madiwani wa CCM kutoka Mkalama Mkoani Singida,karibuni Waheshimiwa Madiwani. (Makofi)

Wageni 13 wa Mheshimiwa Philip Mulugo ambao niKamati ya Siasa ya CCM kutoka Wilaya ya Songwe, Kamatiya Siasa Songwe, wale pale, karibuni sana na mkihitajikufanya kikao cha Kamati ya siasa ya Songwe leo niambieniniwape ukumbi. (Makofi)

Wageni 40 wa Mheshimiwa Fatuma Hassan Toufiqambao ni viongozi wa UWT kutoka kata za Dodoma Mjini.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

UWT mmependeza kweli kweli, karibuni sana, karibuni sana,sana, sana. Jamani mnaona UWT hiyo, sasa hii BAWACHAmbona hatuonagi huku? (Makofi)

Wageni 46 wa Mheshimiwa Anna Lupembe ambaoni watumishi wa Mungu kutoka Kanisa la Sayuni GatewayMinistries kutoka Jijini Dodoma, karibuni sana wageni wetu,karibuni sana, sana, sana. (Makofi)

Hivi Umoja wa Wanawake wa CUF wanaitwaje?Wana umoja wa Wanawake wa CUF kweli? Sijawahi kusikia.(Kicheko)

Wageni 36 wa Mheshimiwa Bagwanji Meisuria naMheshimiwa Kanali Mstaafu Masoud Khamis ambao ni vijanawa Kanisa la Kilutheri, Dayosisi ya Morogoro wakiongozwana Mwenyekiti wao Inspekta Mwashibanda. Karibuni sana,sana, sana, karibuni sana wageni wa Bagwanji, Baniani pekeehumu ndani. (Makofi)

Wageni wawili wa Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabuambao ni wapiga kura wake kutoka Muheza, karibuni sanawale pale. (Makofi)

Wageni wa Mheshimiwa Khatib Saidi Haji ambao nindugu yake kutoka Zanzibar Mjini, ndugu Omari Ally Hassan,karibu. (Makofi)

Wageni wanne wa Mheshimiwa Joram Ismail Hongoliambao ni wadau wa habari kutoka Mkoani Njombe. Karibunipopote pale mlipo, wale pale. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Dkt. Rashid Chuachuaambaye ni mpiga kula wake kutoka Masasi, Ndugu AhmadSaid Masenga, karibu sana. (Makofi)

Wageni watatu wa Mheshimiwa Josephine Chagulaambao ni watoto wake kutoka Jijini Dar es Salaam, karibunisana. (Makofi)

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Kwa mara nyingi huku kulia kwangu kelele zimezidisana, Chief Whip watu wako bwana.

Mgeni wa Mheshimiwa Boniphance Mwita ambayeni Mwenyekiti wa CCM Hunyari kutoka Bunda, Ndugu MusaIramba karibu sana. (Makofi)

Wageni wanne wa Mheshimiwa Martin Msuha ambaoni viongozi wa CCM Kata ya Msigani karibu. (Makofi)

Wageni 24 wa Mheshimiwa Mary Chatanda ambaoni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, wanaotokeaKorogwe Tanga. Wako wapi wageni wa MheshimiwaChatanda? Karibuni sana popote pale mlipo. (Makofi)

Wageni wanne wa Mheshimiwa Justine Monkoambao ni marafiki zake wa maendeleo kutoka nchiniMarekani wakiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Ufundi kwaWatu Wenye Ulemavu, Ndugu Fatuma Hussein Malenga.Karibuni sana, karibuni sana, karibuni sana wageni wetukutoka Marekani. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Jumaa Aweso Naibu Waziriwa Maji na Umwagiliaji ndugu Shaban Sufiani MussaMwenyekiti wa Kijiji cha Boza kilichopo Wilayani PanganiMkoani Tanga, karibuni sana Mwenyekiti. (Makofi)

Wageni wawili wa Mheshimiwa Mariam Ditopileambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Umoja waVijana wa Mkoa wa Dodoma, karibuni sana, karibuni, walepale. (Makofi)

Wageni watano wa Mheshimiwa Venance Mwamotoambao ni Madaktari kutoka hospitali ya Aga Khan Jijini Dares Salaam. Karibuni Madaktari kutoka Aga Khan popote palemlipo. (Makofi)

Wageni sita wa Mheshimiwa Joshua Nassari ambaoni viongozi mbalimbali kutoka Jimbo la Arumeru, wale palekaribuni sana. (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Wageni watano wa Mheshimiwa Zuberi Kuchaukaambao ni familia yake na wapiga kura wake kutoka Liwale,karibuni sana, karibuni sana. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Alex Gashaza ambaye niMjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa wa Kagera nduguChristopher Kilaja, karibu sana Christopher. (Makofi)

Wanafunzi thelathini na sita kutoka Chuo cha Elimuya Biashara (CBE) kutoka Jijini Dodoma, majirani zetu wa CBEwale pale karibuni sana, sana, sana, karibuni CBE mjifunzekuhusu namna Bunge linavyofanya kazi. (Makofi)

Waheshimiwa tunaendelea, matangazo mengine,Kamati ya Bajeti saa saba mchana katika ukumbi wenu wakawaida mkutane ili muweze kukutana na MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango na Naibu wake ili muwezekuzungumzia mambo yanayohusu Muswada wa Sheria yaFedha ili muweze kukamilisha uandikaji wa maoni yenumapema. Saa saba Kamati ya Bajeti mkutane katikauwanja wenu wa kawaida na Mheshimiwa Waziri waFedha na Naibu wake watakuja huko pamoja na watalaamwao.

Tangazo kwa Waheshimiwa wote wa Imani yaKikristo, mnatangaziwa na Mheshimiwa Anna LupembeMwenyekiti wa ibada kwamba, leo kutakuwa na ibada naMtumishi wa Mungu Bishop Oscar Ongere kutoka SayuniGateway Ministries atahudumu katika ibada hiyo. Pia leokutakuwa na kwaya ya Mtakatifu Andrea kutoka Msalato.Kama mnakumbuka ile kwaya ya Mtakatifu Andrea ni mojaya kwaya top kabisa hapa katika Jiji la Dodoma.

Sasa Waheshimiwa Wabunge nina matangazokadhaa, ambayo naomba tusikilizane vizuri, mengine nimarefu kidogo. Kabla sijayatangaza haya, Mheshimiwa JumaNkamia jana alikuwa ameuliza swali ambalo baada yakulipima nikaona kwamba, basi niruhusu Serikali iweze kutoamaelezo yake kwa ufupi kuhusiana na suala ambaloMheshimiwa Nkamia aliliuliza, kwa sababu linahusiana na

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

mambo ambayo yanaweza yakatoa picha isiyo kuwa nzuriya nchi yetu. Kwa hiyo nikaona ni vizuri basi tuwape nafasiWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kama wana maelezokidogo kuhusiana na mwongozo alioomba MheshimiwaJuma Nkamia.

Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, MheshimiwaDkt. Mwigulu Nchemba, karibu tafadhali.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaSpika, nasimama kutoa maelezo mafupi kwa jambolililojitokeza kufuatia mwongozo wa Mheshimiwa JumaNkamia ambalo lilikuwa linahusu kuamuliwa kwa Mashehekuondoka waliokuwa wamepewa mwaliko kuendelea nashughuli hapa.

Mheshimiwa Spika, kwanza hakukuwepo na jambobaya la kusema kwamba kuna kushukiana ama vinginevyo,lilikuwa jambo tu la kiutaratibu ambapo kila nchi huwa inataratibu za masuala ya kiuhamiaji. Kwenye masuala yakiuhamiaji kuna nchi ambazo wageni wake wanapokujaTanzania hupata VISA wanapofika uwanja wa ndege na kunanchi ambazo huwa wanatakiwa wageni waombe VISAwangali bado wako katika nchi zao.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo ulitokea tumkanganyiko unaohusiana na utaratibu ambazo zinahusumasuala ya kiuhamiaji, lakini pia na masuala mengine yakimawasiliano ya ndani ya nchi ambayo yanahusiana nataasisi zinazosimamia mihimili ya kiimani katika dini husikapamoja na Idara yetu ya Uhamiaji.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kabla ya jambo hilikuwa limeletwa kupitia mwongozo, Serikali tulishapatamalalamiko hayo na kwa kuepusha migonganoinayoweza kujitokeza tayari Wizara nilishaelekeza kwamba,warekebishe kasoro zilizojitokeza kwa taasisi hiyo iliyokuwaimepata wageni kuwasiliana na taasisi nyingine husikana kuleta kumbukumbu zilizo sahihi katika Idara yetu yaUhamiaji.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Mheshimiwa Spika, kabla ya hapo tayari nilikuwanimeelekeza kuwa Mashehe hao waendelee na shughuli zaoambazo waliit iwa na huku viongozi wa taasisi hiyowakiendelea kuwasiliana na BAKWATA pamoja naUhamiaji kuweza kuweka kumbukumbu sawa hizo zakiutaratibu ili hao watu waweze kufanya shughuli zao bilakubughudhiwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naliarifu Bunge lakoTukufu pamoja na Waislam wote kwamba, jambo hilotulilimaliza na tulielekeza Mashehe hao waendelee na kazina tena hata wasibughudhiwe wafanye kazi kama ambavyowalikusudia.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba Serikali hii yaCCM inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli inaheshimu uhuru wa kuabudu wa wananchiwake na inaheshimu Katiba inayotoa uhuru huo wakuabudu kwa wananchi wote na jambo hilo tutaendeleakuliheshimu.

Mheshimiwa Spika, napenda tu nizikumbushie taasisizote zinazoalika wageni kuzingatia taratibu hizo za ualikajiwa wageni na taratibu na taratibu za kiuhamiaji ambazoziko kikatiba na kisheria kwa nchi ambazo wanahitajikupata Visa kabla hawajaja na vile ambazo wanahitajikupata Visa wanapofika uwanja wa ndege ili kuepushamigongano ambayo inaweza kujitokeza.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, labda tu kwaniaba ya Mheshimiwa Mkuchika, uliuliza Yanga wako wapi?Nikwambie tu hawako ligi za mchangani kwa sababu ni timupekee iliyosalia kwenye timu nane bora zinazochezamashindano ya kimataifa. Kwa jinsi Yanga wanavyojiandaamsimu ujao timu zingine zitapata tabu sana, tabu sanaikiwepo timu yako pendwa. (Makofi)

SPIKA: Wanapata taabu kujieleza wako wapi, huumwaka hatari kubwa. (Kicheko/Makofi)

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Waheshimiwa Wabunge, naomba nitoe uamuzikuhusiana na mwongozo ulioombwa Bungeni juu yaWimbo wa Taifa, Nembo ya Taifa na alama nyingine muhimuza Taifa.

Waheshimiwa Wabunge, mnamo tarehe 3 Aprili, 2018Mheshimiwa Sixtus Mapunda aliomba mwongozo kuhusudosari za maneno na melodia katika wimbo wa Taifa,unaopigwa na kuimbwa hapa Bungeni tunapoanza Bungena tunapofunga Bunge. Halikadhalika tarehe 6 Aprili, 2018Mheshimiwa Goodluck Mlinga aliomba mwongozo akiombaalama zinazotumika kwenye Nembo ya Taifa zirekebishwekwani haziakisi mazingira ya Tanzania.

Waheshimiwa Wabunge niliipa kazi Sekretarieti yanguya Bunge kufanya utafiti wa kina kuhusu hoja hizo na kubainikuwepo kwa dosari ndogondogo za baadhi ya maneno namuziki (lyrics na rhythms) katika uimbaji wa wimbo wa Taifaunaoimbwa hapa Bungeni wakati wa kufungua na kufungavikao kutokana na kukosekana kwa sheria mahususi yakuongoza uimbaji na kusimamia wimbo huo kama ilivyokwenye nchi nyingine. Mfano Kenya na Malaysia ambakozimewekwa maneno beti na (melody) nota za muziki kwenyesheria zao za Wimbo wa Taifa.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge alama muhimuza nchi yetu kufuatana na mwongozo wa MheshimiwaMlinga, alama muhimu za nchi yetu zinapaswa kulindwakikamilifu. Naishauri Serikali iunde timu, ni ushauri tu, iundetimu maalum ya wadau mfano Wizara ya Habari, Wizara yaElimu, Vyuo Vikuu, Sanaa, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,BASATA, Majeshi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka nakadhalika ili ikusanye taarifa kuhusu Wimbo wa Taifa naalama nyingine muhimu za Taifa kama vile ngao, benderana muhuri wa Taifa ili kubaini dosari za kimatumizi na kutoamapendekezo ya kurekebisha hali hiyo endapo kunaumuhimu wa kufanya hivyo.

Waheshimiwa Wabunge nawashukuru sana,Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Mheshimiwa Goodluck

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mlinga kwa hoja zao ambazo ni uthibitisho wa uzalendo waBunge hili katika kulinda na kudumisha historia, utamadunina utambulisho wa Taifa letu.

Vile vile naishukuru Sekretarieti ya Bunge kwa utafitina uchambuzi iliyoufanya. Naishukuru pia Wizara, Taasisi,Idara na ofisi zote za Serikali kwa utafiti wao na maoniwaliyotupatia hususan Profesa Boniventura Silivant RutinwaMakamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nawengine wote waliotuletea maoni na michango yao juu yasuala hili. (Makofi)

Kwa wale ambao hamkuwepo siku hiyo, MheshimiwaMlinga alikuwa na maoni kwamba, Nembo yetu ya Taifakama mnavyoiona pale juu, wale Bibi na Bwana kamawalikuwepo miaka ya 60 sasa leo watu wamebadilikakidogo. Alikuwa na maoni kwamba wangependeza zaidikuliko walivyo, maana huyu bwana amepiga shuka tu hukujuu kote hana hata fulana. Pia huyu mama naye, je, hawezikuboreshwa kidogo?

Kutokana na jambo hil i, kama nil ivyosemanitawasilisha Serikalini taarifa nzima hiyo ya utafiti nauchambuzi wa Wimbo wa Taifa na alama nyingine muhimuza Taifa ili zifanyiwe kazi kwa kadri itakavyoonekana inafaahasa Wizarani kwa Mheshimiwa Waziri Mwakyembe

Waheshimiwa Wabunge ili kuboresha upigaji nauimbaji wa wimbo wa Taifa hapa ndani ya Bunge kwamujibu wa kanuni ya 27(2) ya Kanuni za Bunge nimeona ipohaja ya kumuwezesha kila Mbunge kushiriki kikamilifu kwania ya kuamsha ari na uzalendo wa nchi yetu wakati wakuuimba wimbo huo.

Kwa muktadha huo Waheshimiwa Wabunge kwayale ambayo yanatakiwa kufanywa na Bunge letu,naagiza kwamba kuanzia sasa Wimbo wa Taifautakaopigwa na kuimbwa Bungeni utaongozwa na brassband itakayotoka miongoni mwa vyombo vyetu vya ulinzina usalama. (Makofi)

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Kwa hiyo ili kutofanya makosa makosa sasa tutaletabrass band wakati wa kufungua na kufunga Bunge, maanaule wimbo uliokuwa unaimbwa ulikuwa kidogo una kasorokadhaa.

Waheshimiwa Wabunge ratiba yetu ya leo ni nzitona ngumu, lakini niwaambie tu kwamba kuanzia mudamfupi baada ya matangazo haya tutaendelea naWaheshimiwa Mawaziri kujibu baadhi ya hoja na tutaanzana Mheshimiwa Angela Kairuki na wengine watafuata,Mheshimiwa Mpina na wengine watafuata dakika 10.

Waheshimiwa Wabunge, kuanzia saa 11.00 jioninitaomba kila mmoja wenu awepo hapa. Saa 11.00 juu yaalama kila mtu awe ndani kwa sababu ndipo tutaanza sualala kura ya uamuzi wa bajeti. Baada ya hapo tutakuwa naMuswada wa Appropriation kwa hatua zote na kura hii nimuhimu sana. (Makofi)

Sasa Waheshimiwa Wabunge kuna baadhi yaWabunge ambao huwa wanasumbuliwa na tofauti kati yautaratibu wa kupitisha bajeti wa kupitisha bajeti ya Serikaliambao leo tunashughulika nao na Muswada wa Sheria yaFedha (Finance Bill) ambao utashughulika kwa siku mbili katiya kesho na kesho kutwa.

Mjadala kuhusu Bajeti ya Serikali utahitimishwa naWaziri wa Fedha na baada ya hapo Bunge litapiga kura yawazi leo jioni kwa kuita jina la Mbunge mmoja mmoja ilikutoa uamuzi wa kupitisha au kutokupitisha bajeti hiyo. Hiini kanuni ya 107. Bunge likikataa kupitisha bajeti mara mojaRais atalivunja Bunge, ibara ya 90(2)(b) ya Katiba. (Makofi)

Narudia tena, endapo mlio wengi mtaikataa Bajetiya Serikali, Bunge hili litavunjwa mara moja na baadhi yawengine hapa mkirudishwa jimboni hamrudi humu. Kwa hiyoakili ya kuambiwa changanya na ya kwako.

Baada ya zoezi hilo la kupitisha bajeti kwishaMuswada wa Appropriation utasomwa kwa hatua zake zote

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

mfululizo, yaani Kusomwa Mara ya Kwanza, Mara ya Pili naMara ya Tatu; hapo mchakato wa kupitisha bajeti za SerikaliBungeni unakuwa umekamilika, Kanuni ya 108.

Sasa Muswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)unaainisha na kuzipa nguvu za kisheria taratibu zote zaukusanyaji wa kodi na maduhuli ya Serikali, usimamizi wafedha za umma na kwa ujumla utekelezaji wa taratibu zoteza kibajeti kama zilivyoainishwa kwenye Bajeti ya Serikali nakupitishwa na Bunge. Huwasilishwa na kujadiliwa kamaMiswada mingine yoyote ya Sheria.

Muswada huu ulishasomwa mwaka wa kwanzatarehe 18 juni 2018, tayari umechambuliwa na Kamati yaBajeti na wanaendelea kumalizia na utawasilishwa Bungenina Kusomwa Mara ya Pili kesho na taratibu zake zotezitafuata. Mjadala huwa ni wa siku mbili kama nilivyosema,Mheshimiwa Waziri atahitimisha siku ya pili, Kamati ya BungeZima itakaa na Wabunge watahojiwa kwa ujumla nakuamua.

Tofauti na Muswada wa Appropriation ni kwambakwenye Finance Bill, Kamati ya Wabunge wanaruhusiwakuwasilisha mapendekezo ya marekebisho Schedule ofAmendment kwa mujibu wa Kanuni ya 86(1). Kwa hiyoWaheshimiwa Wabunge na wapiga kura wanaotusikiliza kwaleo jioni wakati wa kupiga kura Mbunge hapigi kura kwajambo moja au mawili anapiga kura kwa Mfuko mzima waBajeti, begi zima. Kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaelewakwa sababu ni muhimu sana tukaelewana katika jambo hili.

Basi baada ya hayo ningeomba sasa tuendelee unlesskuna jambo la muhimu sana ambalo haliwezi kusubiri, ndiyoMheshimiwa ni moja tu ngoja kidogo, nawaomba kwa kifupisana tuanze na Mheshimiwa.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nasimama kwa msaada wa

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Kununi ya 68(7) kuhusu jambo ambalo limetokea hapaBungeni.

Mheshimiwa Spika, leo umepokea mgeni BwanaHarusi na Bi harusi wetu ambao wametutembelea hapaBungeni ni wana ndoa wa kihistoria. Kilichodhihirika nikwamba mwanamke akiamua kuitengeneza nyumba yakekwa kweli hashindwi, kwa gharama yoyote ile atawezakufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wanaume wenginewote nimpongeze sana Bi harusi wetu kwa kufanikisha kuingiakatika ndoa hii. Sasa umekuwa ni utaratibu wa Kitanzaniapale ambapo watu wanataka kufunga ndoa kuwakaribishawengine kwa ajili ya michango ili kufanikisha jambo hilo. Biharusi na Bwana harusi hawakutupatia nafasi ya kufanyahivyo wakati wanakwenda katika maandalizi yao ya ndoa.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa kuwa leo wameingiahapa Bungeni nilikuwa naomba mwongozo wako kwa ninikatika posho zetu za leo Wabunge tusikatwe angalauSh.20,000 ili iwe mchango katika kufanikisha ndoa hii ili nawao sasa waweze hata wakaanzie maisha kama pongeziyetu kwenye jambo hilo, naomba mwongozo wako. (Makofi)

SPIKA: Toa hoja tuone kama inaungwa mkono.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika, sasanaomba kutoa hoja.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, naafiki

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkononaomba kuwahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja ilitolewa na Kuafikiwa)

SPIKA: Kwa kauli moja, maharusi mtachangiwaSh.20,000 na kila Mbunge wa Bunge hili la Jamhuri ya

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Muungano hongereni sana na karibuni Bungeni. Hiyo ni zawadiya Bunge kwenu kwa kutambua jambo hili muhimu sana laupendo wa ajabu ambao hatujawahi kuuona, karibuni sana.Pia nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa takrimahii ambayo mmeifanya Mungu atawalipa, ahsanteni sana.(Makofi/Vigelegele)

Tunaendelea Mheshimiwa Lubeleje.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika,naomba mwongozo wako kwa kanuni ya 68(7) kuhusu swalinamba 488 linalohusiana na Wenyeviti wa Vijiji, Wenyevitiwa Vitongoji na Madiwani.

Mheshimiwa Spika, Wenyeviti ndio kiungo wakubwawa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na ndio wanaofanya kazikubwa ya kusimamia maendeleo katika vijiji vyetu. Sasanashauri, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu WaziriSerikali ingewafikiria kuwalipa posho hawa Wenyeviti kwasababu kazi wanayoifanya ni ngumu sana, pamoja naMadiwani.

Mheshimiwa Spika, Madiwani wanafanya kazi kubwaya kusimamia miradi ya maendeleo si kama Madiwani wazamani kama sisi hapana. Kwa hiyo nashauri Madiwaniwaongezwe posho na hao Wenyeviti wa Vitongoji naWenyeviti wa Vijiji uangaliwe uwezekano wa kuwalipa poshokwa kila mwezi.

Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Lubeleje,mwongozo wangu kama Serikali imesikia na kwa kweliitazingatia maoni hayo kadri watakavyoona inafaa.

Mheshimiwa Mbarouk kwa kifupi.

MHE. MUSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nasimama kwa kanuni ya 68(7), kuomba Mwongozo wangu,lakini kwanza nikumbushe kitu. Tarehe 14 nil iomba

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

mwongozo hapa baada ya Wizara ya Afya kupigamarufuku kununua na kuuza damu kwa wagonjwa,nikaambiwa mwongozo ule ungejibiwa Jumatatuitakayofuata ilikuwa ni siku ya Alhamisi, lakini mpaka leosijajibiwa.

Mheshimiwa Spika, lakini mwongozo wangu wa leo,Bunge letu hili ni Bunge la wananchi na inapotokea kunajambo linalowasumbua wananchi tukilijadili humu ndaniwakati mwingine tunaambiwa halijatokea mapema humundani. Sasa jana kama ulibahatika kuangalia vyombo vyetuvya habari, kuna zoezi la ukaguzi wa bima wa vyombo vyamoto. Sasa kuna mkanganyiko kati ya Agents wanaokatabima na hizi mashine za ukaguzi za sasa hivi; hata kamaulikata bima siku za nyuma…

SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk hilo ni katika ambalohalijatokea naomba umuone tu Mheshimiwa Waziri, halafumkishindwana utatuletea,

Mheshimiwa Mtolea. Mheshimiwa Mtoleahakusimama nafikiri ni wewe Mheshimiwa, samahani.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,naitwa Frank George Mwakajoka. Nami naomba mwongozowako. Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwenye maeneoyetu hasa mkoa wa Songwe na Mbeya kwa polisi kuzungukakwenye polisi na watu wa halmashauri na jiji kuzunguka katikanyumba za wageni usiku na kuanza kukagua vitabu vyawageni na baadaye kumekuwa na usumbufu mkubwasana…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwakajoka hilo limetokealini hapa?

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,tulikuwa tunajadili hapa na Mheshimiwa hapa kwa hiyotulikuwa tunajadili ndani ya Bunge humu, tulikuwa tunajadilina Mheshimiwa Mbilinyi, kwa hiyo inatokea humu ndani yaBunge. (Kicheko)

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

MWENYEKITI: Mheshimiwa Selasini, tafadhali.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kunipa nafasi. Mwongozo wangu nami ni kanuniya 68(7) kuhusu jambo lilitokea hapa Bungeni leo asubuhi.

Mheshimiwa Spika, ulipompa Mheshimiwa Chegeninafasi ya kuuliza swali la nyongeza kutokana na swali namba491 alisema kwamba Mheshimiwa Waziri wa Uvuvi amekuwana tabia ya kusema kwamba yeye hana wapiga kura wasamaki.

Mheshimiwa Spika, wakati anatoa majibu yakehakuzungumzia hili kwa kukanusha au vyovyote vile na miminaona hii ni tuhuma nzito angeweza akasema hapana labdawatu walini-quote vibaya na nini. Kwa sababu humu ndanikumezuka sasa tabia ya kutuhumiana, hata jana MheshimiwaMusukuma katika mchango wake alisema katika Mfuko waKuendeleza Zao la Korosho ana hakika kwamba kunaWabunge wezi na mimi niliomba mwongozo ili walau ifutweau wawaseme lakini alisisitiza.

Mheshimiwa Spika, sasa mambo kama hayayasiposemewa yakafutwa kwenye hansard, hansard inakujakusomwa na watoto wetu na wajukuu wetu, itaonekanakwamba Bungeni palipita Wabunge ambao walikaa si kwamaslahi ya nchi, walikaa kwa maslahi yao.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ningeomba mwongozowako ili Mheshimiwa Waziri aweze kulikanusha hili au awezekutoa maelezo na lile la jana kama linaweza likatolewaufafanuzi sababu Mheshimiwa Musukuma alisema anahakika ana majina ya Wabunge wezi wa Mfuko huo.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Sijui kama kuna haja ya Mheshimiwa Wazirikusimama na kujibu hilo maana alipata nafasi ya kujibuukiona amenyamaza ujue amepuuzia. Sidhani; kwa sababusisi wote tuko hapa ndani ingekuwa aliyetajwa ni mtu

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

ambaye hayuko miongoni mwetu, hata Musukumaalivyosema angesema watu ambao hawako miongonimwetu ingekuwa ni issue kwamba tunawalindaje. Sasaukitajwa Selasini halafu ukanyamaza maana yake ni kwambaumechagua, umeona ni bora hilo kuliacha lilivyo, unless kamaMheshimiwa Waziri unataka kujibu, Mheshimiwa Waziritafadhali Mheshimiwa Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo naUvuvi, tafadhali.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,maneno mengine ni ya kama ulivyosema, lakini niseme tukwa sababu limeongelewa hapa. Maneno mengine niuchonganishaji tu kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, mimi ni Waziri chini ya kiapo siwezikuwabagua wananchi wangu katika kuwasimami hata sikumoja na siwezi kutoa kauli kama hizo hata siku moja.Majukumu yangu ni kwa mujibu wa Katiba, kwa mujibuwa sheria zilizowekwa. Kwa hiyo, ninachotaka kusema tuni kwamba katika ulinzi huu wa rasilimali zetuwatuvumilie kwa baadhi ya watu ambao wakatimwingine hata wao wenyewe wanahusika na biashara hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile kumekuwa na mamboambayo yanazungumzwa, Wabunge wenginewanazungumza humu gari langu mimi lilikamatwa lakinihata hawaku-declare interest, halafu wanapata airtime yakumtukana Waziri wanavyoweza, hawana right hiyo. Mimikama Waziri, Bunge linanielekeza kwa mujibu wa sheria nataratibu zilizowekwa. Hakuna Mbunge ambaye ana uwezowa kumtukana Mbunge mwenzake kwa kadri awezavyo.Kwa hiyo mimi nilitaka tu niseme hayo.

SPIKA: Ahsante sana, hayo ndio majibu MheshimiwaSelasini. Tunaendelea na Mheshimiwa Musukuma.

MHE. MUSUKUMA J. KASHEKU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana; na mimi nasimama kwa Kanuni hiyo ya68(7). Wakati nimeuliza swali langu namba 491, Mheshimiwa

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Waziri amekiri kwamba Sheria ile ya Uvuvi, Namba 22imejichanganya na atakamilisha marekebisho yake mweziwa Saba lakini zoezi hili linaendelea na Wabunge wengi…

MWENYEKITI: Unazungumzia kanuni au sheriayenyewe?

MHE. MUSUKUMA J. KASHEKU: Mheshimiwa Spika,nazungumzia kanuni na Wabunge wengi wamekuwawakilalamika kuhusiana na watu wao kuonewa kwenyemajimbo na maeneo yao. Majibu mepesi sana ya Wazirianasema anasingiziwa na sasa hivi umemsikia anavyolezwakwamba watu wanazungumza hawaja-declare interestyaani majibu mepesi.

Mheshimiwa Spika, kauli yako umezungumza vizurisana kwamba naomba mniletee malalamiko. Sasa ni kazikubwa sana kwa Mbunge na muda tuliona kwanza kuanzakushughulika na mmoja mmoja pengine kuwabebakuwaleta Dodoma. Kwa nini kiti chako kisiunde Tume ikaendakuzunguka kutafuta hayo matatizo wakakuletea hicho kitabucha malalamiko, tukaondoa hii kauli na dharau ya Waziri yakusema tunamsema kwa kumsema sijui kwa kuvunja Katibasi sahihi. Ni kwamba kweli watu wetu wameonewa na wapona anawajua, hata kwa majina amepelekewa hajachukuaaction.

Mheshimiwa Spika, niombe sana kama kunauwezekano uunde tume ikafanye hii kazi ili hii fitna yakuzungumza ijiondoe. Nakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri unataka kusema chochote,karibu tafadhali.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,sijasema kwamba sheria i l iyotungwa na Bunge hil iimejichanganya sijasema hivyo. Nilichokisema ni kwamba nikawaida, sheria yetu hii tumeitunga mwaka 2003, leo ni miaka15 sasa na mambo mengi yamebadilika ya kiuchumi na

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

maendeleo kwa hiyo tunachofanya ni kuiboresha ili iendena wakati sawasawa.

Mheshimiwa Spika, la pili, hakuna mwananchi yeyoteambaye ananyanyaswa wala kuonewa katika hatua yaoperesheni zinazoendelea. Leo niseme kwamba Serikali ipokatika ngazi ya kitongoji, katika ngazi ya kijiji, katika ngaziya kata, katika ngazi ya wilaya, tunazo Kamati za Ulinzi naUsalama katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewananchi wanapopata matatizo hayo hayawezi kutokakatika level ya kijiji, level ya kitongoji, level ya kata, level yawilaya yakaja moja kwa moja kwa Waziri. Kwa hiyo ndiyomaana mimi nikawa nasema muda wote, kwamba kamakuna shida yoyote tutaishughulikia, iwe imewasilishwa naMbunge moja kwa moja kuja kwa Waziri au imewasilishwana Wenyeviti wetu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Mheshimiwa Spika, niseme na kusisitiza kwambahakuna mwananchi yoyote ambaye anaonewa na Serikalikwa mujibu wa nanii; sisi tunapambana na uvuvi haramu tuambao tumeapa lazima tuutokomeze. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Musukuma kwa sasahivi kuunda tume kwa maana ya Bunge sidhani, nadhani nimapema kidogo unless tupate ushauri mzito zaidi kutokakwenu huko mbele tunakoenda, lakini kwa sasa nadhanihebu tujaribu kwenda hivyo tunavyoenda tuone; na kamanilivyosema kama kuna shida yoyote kubwa tuambiane nasisi tutawaambia Wizara na Serikali kwa ujumla. Nina hakikasi nia ya Wizara wala ya Serikali kuona kwamba mtu yeyoteasiyekuwa na hatia anapata matatizo katika nchi yetu.

Sheria hii tuliitunga baadhi yetu tulikuwepo 2003,Mwenyekiti wa Kamati alikuwa Mama Makinda na sisi tulikuwawajumbe. Tuliichambua sana sheria ile, sasa kinawezakikatupita kitu fulani lakini katika madhumuni na sababuhaikuwa kwamba tuunde sheria itakayosababisha usumbufumkubwa kwa watu, hapana.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Pia mkumbuke Waheshimiwa Wabunge, wewemwenyewe kama Mbunge una uwezo wa kuleta marekebishowa sheria, Kamati yenu mnaweza kuleta mapendekezo yamarekebisho ya sheria kama kuna sheria ina matatizo, Serikaliina uwezo wa kufanya hivyo. Kwa hiyo badala ya kulalamikakila siku, basi hebu angalieni nafasi ambazo zipo katikakanuni na muweze kuzitumia vizuri.

Mheshimiwa Mulugo.

MHE. PHILIPO A. MLUGO: Mheshimiwa Spika,mwongozo wangu na mimi ulikuwa ni 68(7) ambao tayariMheshimiwa Mtolea ameutoa, ilikuwa ni juu ya wanandoawetu wa leo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja yaMheshimiwa Mtolea.

SPIKA: Ahsante sana. Wa mwisho ni MheshimiwaMkuchika.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika,nimesimama kwa kanuni ya 68(7).

Mheshimiwa Spika, kwanza nataka nikupongeze kwamaelekezo yako uliyoyatoa leo asubuhi kuhusu uimbaji wetuwa Wimbo wa Taifa. Naomba mwongozo wako kuhusujambo moja. Kila nchi ina mapokeo yake katika utamaduni.Kwa mfano, nchi nyingi ukienda hata Marekani na wapiwanapoimba Wimbo wa Taifa wanaweka mkono kifuani,ndiyo mapokeo ya nchi yao.

Mheshimiwa Spika, sisi Watanzania mapokeo yetutuna simama attention, awe mwanafunzi wa shule ya msingi,awe mgambo, awe askari, awe Spika tunasimama attention.Humu ndani tumeanza kuwachanganya watoto wa shule,ambao hawajui wafuate lipi? Wafuate mtindo wa Marekaniwa kuweka mkono kifuani, wasimame attention au wa-relaxau waendelee kuongea?

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako.

SPIKA: Huo ni mtihani mkubwa sana kwa MheshimiwaSpika, lakini kama ulivyoeleza Mheshimiwa Waziri kwa kwelimapokeo yetu sisi na wengi wenu mmepita JKT na mahalipengine ni kusimama attention. Sasa hii si sehemu yamapokeo yetu na wanapenda sana upande huu kufanyahivyo.

(Hapa Mheshimiwa Spika alionesha kwa vitendo jinsibaadhi ya Wabunge wanavyofanya wakati wa

uimbaji wa wimbo wa Taifa)

SPIKA: Kwa hiyo, turudi kwenye msingi jamani alikuwaanatukumbusha tu Mheshimiwa Waziri tuzingatie hilo. Katikamasuala Wimbo wa Taifa ni jambo rasmi inatakiwa tufuatemisingi ile inayoendana na jambo hilo tangu waasisi natunakoelekea.

Basi sasa muda ulipofikia sasa ni kuanza kwauchangiaji, Katibu.

NDG. RUTH MAKUNGU-KATIBU MEZANI

HOJA ZA SERIKALI.

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango waMaendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019; na

Mapendekezo ya Serikali Kuhusu Makadirio ya Mapato naMatumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Majadiliano yanaendelea, WaheshimiwaMawaziri kuna mwenye dakika kumi na wenye dakika tanokadri mlivyojipangia wenyewe. Nitaanza na MheshimiwaProfesa Ndalichako dakika kumi atafuatiwa na MheshimiwaMwakyembe dakika tano.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Profesa tafadhali.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwamchangiaji wa kwanza katika siku ya leo. Napenda kuanzakwa kutoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Fedha naMipango Dkt. Mpango, pamoja na Naibu Waziri,Mheshimiwa Kijaji pamoja na watendaji wote wa Wizara yaFedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt JamesDoto.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa nimpongeze kakayangu Dkt. Philip Mpango, kwa uwasilishaji wa umahiri kabisawa bajeti hii, alitumia saa moja na dakika arobaini na tanolakini hatukuchoka. Tunampongeza sana na naunga mkonohoja hii kwa sababu bajeti hii imeandaliwa kwa lengo lakutatua kero za Watanzania.

Mheshimiwa Spika, katika mchango wangunitapenda kuzungumzia masuala machache kwa sababuya muda na ningeanza na suala ambalo wachangiaji wengiwalikuwa wakilizungumzia kwamba Serikali haipeleki fedhakwamba tunakuwa tunapitisha hapa bajeti lakini mwishowa siku Serikali haipeleki fedha. Pia wengine walienda mbalina wakawa wanasema kwamba hii Serikali inaleta bajetihewa.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze kwa dhatiMheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Joseph Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni Raisishupavu, ni Rais ambaye anafanya vitu kwa vitendo, akiahidianatekeleza.

Mheshimiwa Spika, pongezi hizi nazitoa kwa sababukwenye sekta ya elimu fedha zimekuwa zikija kama ambavyozimepangwa. Wizara ya Elimu ilipangiwa jumla ya trilionimoja na bilioni mia tatu thelathini na sita na mpaka sasaSerikali imeshatoa trilioni moja na bilioni mia moja ishirini natisa.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Spika, Serikali pia imekuwa ikitekelezaahadi yake ya elimu bila malipo kila mwezi bila kukosa, fedhakwa ajili ya elimu bila malipo zimekuwa zikienda bilioni ishirinikwa wakati. Pia Serikali ilikuwa imetenga bilioni 427.54 kwaajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mpaka sasaninapozungumza tayari Serikali imekwisha pokea shilingibilioni 427.44 sawa na asilimia mia moja ya fedha zoteambazo zilitengwa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na upatikanaji huu wafedha katika sekta ya elimu Serikali imeweza kufanya mambomengi. Tumeweza kujenga madarasa kwa ajili ya kuongezaupatikanaji wa nafasi za elimu pamoja na kuboreshamazingira ya elimu ambapo jumla ya madarasa 1907yamejengwa lakini na matundu ya vyoo elfu nne mia tanona moja.

Mheshimiwa Spika, na nichukue nafsi hiikuwapongeza kwa dhati, umoja wa Wanawake Wabungekwa uchangishaji wa vyoo bora kwa mtoto wa kike ambaokwa kweli inaungana na juhudi za Serikali katika utoaji waelimu bora tunashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, pia tumeweza kujenga mabweni338, tumefanya ukarabati wa shule kongwe 45 na vilevileukarabati wa vyoo vya walimu 17. Vile vile kutokana naupatikanaji wa fedha hizi Serikali imeweza kuendeleakuimarisha tafiti katika nchi hii. Serikali ilitoa shilingi bilioni 3.2kwa ajili ya miradi nane ya tafiti na hii miradi imelenga katikakuimarisha viwanda pamoja na kilimo.

Mheshimiwa Spika, jana tulikuwa tunazungumziamasuala ya kilimo, tunajua kwamba kilimo ndio kinabebaWatanzania na kwa hiyo Serikali imetoa bilioni 3.2 ambazoni kwa ajili ya miradi minane ya utafiti. Kwa mfano na taasisiinayoshughulika na magonjwa ya binadam, (NIMR)imepata fedha kwa ajili ya kutengeneza maabara kwaajili ya dawa, pia Chuo Kikuu cha Afya na SayansiShirikishi (MUHAS) kimepata fedha pia kwa ajili ya masualaya dawa.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Spika, hatujasahau na hapa Mkoa waDodoma Makao Makuu tumetoa fedha kwa aji l i yakuimarisha utafiti wa zao la zabibu. Kwa hiyo tumetoa fedhakwenye hii Taasisi ya Utafiti wa Mifugo ya TALIRI kwa ajili yakuzalisha mifugo.

Mheshimiwa Spika, vile vile tumetoa fedha kwa ajliliya utafiti wa kuboresha mitambo ya kuzalisha mvinyo katikaTaasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Makutupora. Haya yotenayazungumza kwa uchache tu kuonesha kwamba Serikaliya Awamu ya Tano ni Serikali ambayo inatenda kwa vitendona hii yote imetokana na bajeti ambayo imetengwa.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kwenye Taasisi zaElimu ya Juu, Serikali hii imefanya mambo makubwa sanakwenye hizi Taasisi za Elimu ya Juu. Ukienda Chuo Kikuu chaDar es Salaam sasa hivi inajengwa maktaba ya kisasa na yakipekee katika Bara la Afrika, ambayo itakuwa na uwezowa kuweka wanafunzi 2,500 kwa wakati.

Mheshimiwa Spika,ile vile Tume ya Mionzi ya Taifainajenga Maabara kwa ajili ya kupima mionzi na maabarahiyo ikikamilika kwa kweli itakuwa ni maabara ya kipekeekatika Ukanda wa Afrika. Tayari vifaa kwa ajili ya maabarahizo vimekamilika. Nashukuru kwamba Serikali imeshatoafedha ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya hii Tume nazinaendelea kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, katika suala la kusema kwambaSerikali inatenga fedha haizitoi; kwa sababu ya muda siwezikumaliza taasisi, lakini niseme kwamba ukienda Mzumbe,ukienda Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, ukienda MbeyaChuo cha Utafiti, ukienda Arusha Technical utakuta mambomengi yanafanyika.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo lilikuwalinazungumziwa katika michango ni namna gani Serikaliinaimarisha elimu ya ufundi. Napenda kulihakikishia Bungelako Tukufu kama ambavyo imeainishwa katika Mpango waMaendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano na ambao umekuwa

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

ukitekelezwa mwaka hadi mwaka, Serikali ya Awamu ya Tanoimedhamiria kuhakikisha kwamba inaongeza ujuzi kwawananchi katika nyanja mbalimbali, maana kuna ujuzi wachini, kuna ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.

Mheshimiwa Spika, hivi tunavyoongea katika Chuocha Ufundi Arusha Karakana zote zinabadilishiwa vifaa iliziweze kutoa mafunzo ya kisasa. Kuna kontena kumi na sitaambazo zimefungwa, tayari vifaa vile vipo kwa ajili yakufungwa, kwa hiyo Serikali inaendelea kuimarisha.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la Walimu, kwa sababuelimu si majengo tu, ni pamoja na Walimu. Serikali imekuwaikiendelea kuimarisha utoaji wa mafunzo ya ualimu. Sasa hivitunafanya upanuzi wa vyuo vyetu vya ualimu; ukienda kuleKitangali utakuta Chuo cha Ualimu cha kisasa kimejengwa,nenda Mkuguso, nenda Ndala, nenda Shinyanga utaona kazinzuri ambayo inafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii ambayo MheshimiwaRais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais ambayeanaangalia wanyonge hajasahau wanafunzi wenye mahitajiwenye mahitaji maalum. Kwa hiyo katika mambo ambayotunafanya tumeendelea pia kuimarisha utoaji wa elimu kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maaalum.

Mheshimiwa Spika, hivi ninavyozungumza ujenzi washule maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maaluminaendelea katika Chuo cha Ualimu Patandi. Sambamba naujenzi huo lakini Serikali pia imepanga kununua vifaa kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum; na tayaritumeshatoa maelekezo kwamba katika shule zote katikamiundombinu yote ya kielimu inayojengwa lazima tuzingatiemahitaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niseme tu kwambaniwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu tuiungemkono bajeti ya Serikali kwa sababu ni bajeti ambayo italetamaendeleo, ni bajeti ambayo inakwenda kutatua kero zawananchi na ni bajeti ambayo inatusaidia hata sisi

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Waheshimiwa Wabunge kutekeleza ahadi ambazo tumezitoakwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nategemea kwambajioni kama ulivyoelekeza Wabunge wote watajitokezawapige Kura ya Ndiyo katika bajeti hii ili wanafunzi wa elimuya juu waendelee kupata mikopo ambapo tunategemeakutoa mikopo kwa wanafunzi 123,000.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naunga mkono hoja,lakini kwa heshima kubwa nawaomba WaheshimiwaWabunge wote tupige Kura ya ndio. Ahsante sana.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri wa Elimu,Profesa Ndalichako. Sasa ni zamu ya Mheshimiwa Dkt.Mwakyembe dakika tano na Mheshimiwa Waziri wa Maliasilina Utalii, dakika kumi.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii.Nianze kwa kuunga mkono hoja na vile vile kumpongezaWaziri wa Fedha na Naibu wake kwa kazi nzuri na yenyeviwango. Katika dakika tano pengine nigusie sualamoja tu, muda ukibaki nitaongelea suala la pili na penginela tatu.

Mheshimiwa Spika, jana lilijitokeza suala la ukabilahapa, ambalo haliwezi likabaki kwenye Hansard bila yaufafanuzi. Kwa bahati mbaya sana liliibuliwa na Mbungeambaye namheshimu sana na ambaye mimi mwenyewenajivunia kwa kumwita mdogo wangu Mheshimiwa JamesMbatia.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Wabunge wenzanguhapa, pamoja na maudhi yote ambayo tunaweza kuyapata,maana sisi wote ni binaadam, tuna upungufu mwingi sana;sisi viongozi tusikubali kwa njia yoyote ile kuwa abiria kwenyebasi la ukabila na basi la udini. Tukifanya hivyo, tutafutakabisa mafanikio makubwa ambayo Taifa hili limepata

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

kupita Taifa lolote lile katika Bara la Afrika hasa katika kujengaumoja wa kitaifa na sisi kujisikia ni Watanzania na si niwakabila.

Mheshimiwa Spika, ndugu yetu Mheshimiwa Selasinini Mheshimiwa mmoja Mbunge na ambaye vile vilenamheshimiwa sana; jana aliweza kutoa sababu kwa niniimekuwa hivyo, akagusia magazeti mawili, kwamba kunamagazeti mawili hapa, Tanzanite na Jamvi kwambandiyo sababu hasa nafikiri kwamba kuna ubaguzi waWachaga.

Mheshimiwa Spika, lakini haya magazeti yanawezakushtakiwa tu na Sheria ya Huduma ya Habari kifungu cha41, mtu akileta upuuzi upuuzi mpeleke Mahakamani. Sisikama Wizara ya Habari tutakuwa mashahidi wenututafungiaje, kesho tutafungia mtasema tunaminya uhuru wahabari.

Mheshimiwa Spika, Wizara hatuwezi kufungia kituambacho hakiko direct katika kuvunja usalama wa nchi hii.Kama umetukanwa wewe nenda Mahakamani, kifungu cha41 kinakuruhusu, lakini ukileta hapa kwa sababuumesema wewe ukaleta Wachaga wote wanabaguliwa nimaneno ambayo kwa kweli yanaturudisha nyuma sanaWatanzania.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme neno moja, hivileo Mchaga ni nani katika Taifa leo la Watanzania? Yupi hapaanaweza akashika jiwe akamtupia, akatupa jiwe kwenyekabila lingine asimguse mkwewe au mjomba wake kule?Hili Taifa limebadilika sana; mimi niko kwenye hali ngumuhapa, mimi natoka Mbeya huko lakini siwezi kutupa jiwe kwaMchaga, watoto wangu wenyewe ni Wachaga wana damuhiyo na ndiyo Tanzania nzima iko hivi.

Mheshimiwa Spika, mwaka 1961penginetukumbushane kwa vijana wadogo wadogo hapa;tulipopata Uhuru, ulikuwa ni uhuru wa makabila hayazaidi ya 120 ambayo hawakuwahi kukaa na

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

kukubaliana kwamba sisi ni Taifa. Kwa hiyo kazi kubwaaliyokuwa nayo Baba wa Taifa ni kuunda a Nation State;ataiundaje?

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana Baba wa Taifa ilibidiafanye kazi kubwa ambayo viongozi wengine wote Afrikawalidharau na ndiyo maana kwao bado ukabila ni mkubwa.Sisi hatuna ukabila hapa, yeyote yule anayepanda basila ukabila hana safari ndefu huyo, atapotea, ndiyo maanakitu cha kwanza Mwalimu ikabidi tusitishe mamlaka yaMachifu katika Serikali, ilikuwa nzuri tu, ili tuunde nationalstate.

Mheshimiwa Spika, pili lugha ya Kiswahili kuwa ndiyolugha yetu ya Taifa; lakini tatu education system yetu.Unakumbuka na viongozi wengine hapa, unamalizadarasa la saba wewe unatoka Kyela sekondariutakwenda Bukoba, wa Bukoba atakwenda Nachingwea,wa Nachingwea ataenda Tanga, wa Tanga ataendaKigoma.

Mheshimiwa Spika, tumejichanganya na tuna tafiti zakisosholojia hapa, watu wote waliopitia mfumo huo, asilimiazaidi ya 85 hawajaoa maeneo yao, wameoa maneomengine; na ndilo Taifa alilokuwa anataka kuliunda MwalimuNyerere.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana,nimeanza ndani ya Bunge hili tumeanza kupanda mabasi yaukabila, mabasi ya udini. Kuna sentensi za udini na za ukabila,tuache kabisa sisi ni viongozi, hawa watoto, bahati mbayanimepewa dakika tano, lakini ujumbe wangu ulikuwa nikwamba jana nilishtushwa, nikasema haya yasiongelewehapa, tusiongee kabisa, tumefika mbali, tumefanikiwa sanakama Watanzania.

Mheshimiwa Spika, nakuhakikishia hili ni Taifa jipya,hapawezi kabisa kuwa na mtu akisema watu fulanitunabaguliwa, haiwezekani utambagua nani? Maana woteni wale wale. Ahsante sana.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

SPIKA: Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri waHabari, Mheshimiwa Mwakyembe, kwa kweli ujumbe ulioutoani muhimu kweli kweli na mimi nipigie mstari kama kiongozikatika Bunge hili.

Waheshimiwa Wabunge, hili jambo la ukabila si lakuliendekeza, kulisema hapa. Tunaweza tukasema tukidhaniatunajenga lakini kumbe tunafanya makosa makubwa sana.Unaweza kujikuta wewe unayelalamika kuhusu jambo fulanindiyo ipo huko Serikalini na kila mahali kuliko hata jamiinyingine ambazo hazisemi.

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge, nawaombatujiepushe sana na kama kuna shida kama hizo hebu tujaribukunong’ona miongoni mwa viongozi ili tuone kama jambohilo lipo, basi tulirekebishe taratibu bila kulimwaga kwenyejamii bila utaratibu. Kwa kweli wa kujifunza na kurudi nyumakatika mambo haya ni sisi wote kama jamii yaWatanzania, katika makundi yetu yote; yawe makundi yakisiasa, yawe makundi ya kidini, yawe makundi ya kijamii,iwe ni timu za mipira, michezo na kadhalika tuendelee kuwaWatanzania wamoja namna hiyo.

Dalili za ukabila ni dalili mbaya sana na hatuwezikufika popote kama tunachochea ukabila. Kwa sababuMheshimiwa Selasini ndiye Chief Whip hapa nimwambie rafikiyangu katika watu ambao dada zao wameolewa kilamahali ni dada zako. Mna wajomba nchi nzima, wengi sana,dada zako ni liberal kweli kweli.

Kwa hiyo yaani nchi hii ni moja bwana huwezikumpata huyo Mchaga utampa wapi? Ikija siasa hizowajomba ni wengi mno kila mahali. Kwa hiyotumechanganyika upendo ule tuliouona ndio upendo waWatanzania yaani hivyo kabisa. Kwa hiyo sisi wanasiasatusiwe ni chanzo cha kuparaganyisha nchi yetu katikamambo ya kikabila.

Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, atafuatiwana Mheshimiwa Mkuchika, dakika tano

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi hii. Labda nianze kwanza kwakumkumbusha Mheshimiwa Selasini, wale anaowasema walendiyo shemeji zake wakubwa maana dada zake wana rangiambayo inavutia sana makabila ya wale anaowasema.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Selasini, hata Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla ni shemeji yako pia. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika,kwa hivyo hata nyumbani kwangu leo nimeondoka asubuhinimewaaga wajomba zake. Kwa hivyo, haya mambohayawezekani katika nchi yetu. Sisi ni wamoja na hataMheshimiwa Dkt. Mwakyembe ana wajomba zako wakutosha, Mheshimiwa Mwigulu, Mheshimiwa Makamba andthe list goes on and on! Huwezi kuzungumza ukabila Tanzania.Tuachane na haya mambo ya hovyo hovyo, hayatusaidii kitu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nianzekuchangia kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshiimwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli kwa jinsi ambavyo anaendelea kutoa dirana mwelekeo wa Taifa letu katika kuboresha maisha yaWatanzania na kuleta ustawi wa Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombanichangie hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Richard PhillipMbogo kuhusiana na uvunaji wa mazao ya maliasilikutoonekana kuchangia kikamilifu katika pato la Taifa letu.Alipenda kujua sababu hasa ni nini?

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Misitu inachangia patola Taifa kwa kiwnago cha asilimia 3.5 tu! Kinaonekana nikiwango kidogo sana na hata sisi tunaosimamia sekta hiitunaona kwamba kiwango hiki ni kidogo, lakini kiukwelikiwango hiki hakipaswi kuonekana kidogo ilakinachosababisha kikubwa ni formula ya mfumo wa fedhakwa namna ambavyo mchango wa Sekta ya Misitu

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

unakokotolewa, lakini mchango wa Sekta ya Misitu namazingira kwa ujumla ni mkubwa sana kwenye uchumi waTaifa letu kuliko ambavyo inasemwa kwamba ni asilimia 3.5tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ku-mention mambo machachetu, Sekta ya Misitu inachangia kwenye upatikanaji wa maji,umeme na kwenye kilimo. Ukitaka kuitazama kwa upanawake utaona kwamba kama Watanzania zaidi ya asilimia70 wanategemea kilimo kama shughuli yao ya msingi yakiuchumi na kama kilimo kinategemea maji ya mvua nakama mvua zinatokana na uwepo wa misitu iliyohifadhiwa,maana yake kwa kiasi kikubwa sana uchumi wa Tanzaniawa watu wetu walio wengi unategemea kwa kiasi kikubwamisitu ambayo inahifadhiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia, wanyama kuanziang’ombe au zaidi ya milioni 36 ambao Mheshimiwa Mpinakila siku hapa anajivunia nao wanategemea majiyanayotokana na uhifadhi wa vyanzo vya maji ambavyondiyo hiyo misitu inayohifadhiwa. Uzalishaji wa umeme, miradiya umeme ambayo kila siku Mheshimiwa Dkt. Kalemani hapaanajivunia na Waheshimiwa Wabunge kila siku mnaombaumeme kwa ajili ya wannachi wetu. Ule umeme unaozalishwakutokana na maji ukirudi kinyumenyume utakuja kugunduaunatokana pia na uhifadhi wa misitu ambao tunaufanyakatika Wizara yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, ukitaka kukokotoa vizuriukaangalia hizo factor zote utaona wazi kabisa kwambaSekta ya Misitu inachangia kwa kiasi kikubwa sana kwenyeuchumi wa nchi yetu kuanzia kwenye kuzalisha umeme,kilimo, mifugo, samaki, uhifadhi wa wanyamapori kwasababu kwenye hii misitu pia tunahifadhi wanyamapori.Sasa ni nani ambaye ana formula ya kiuchumi yakuangalia umuhimu wa misitu katika uhifadhi wake wabioanuai ambao unafanyika. Kwa kweli utaona ni kwakiasi kidogo sana formula inayotumika na wenzetu waWizara ya Fedha kukokotoa umuhimu wa misituinavyotumika.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Spika, pia misitu inatusaidia sanakuondoa madhara ambayo yangejitokeza kutokana nauwepo wa hewa ya ukaa. Kama tungekuwa hatuna misitumaana yake hewa ya ukaa ingeongezeka duniani namazingira yangeharibika maradufu na maradufu. Kwa hivyo,kwa kuhifadhi misitu tunaweza kupunguza ongezeko la hewaya ukaa angani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile kwenye misitu tunapataasali, uyoga, dawa na tunapata hewa ya oxygen ambayosisi sote tunaivuta. Sidhani kama formula za kiuchumizinaangalia hadi oxygen ambayo tunavuta kila siku ambayoinatokana na uwepo wa misitu ambayo inatusaidia ku-controlhewa ya ukaa hapa duniani.

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, kwa kweli mchangowa misitu katika uchumi na katika pato la Taifa hauwezi kuwani hiyo asil imia 3.5 tu ambayo inazungumzwa nawanatakwimu za kiuchumi. Sisi tunaamini ingepaswa kuwakubwa zaidi ya hiyo lakini kwa sababu ya formula inayotumikamchango wake unaonekana kuwa ni huo wa asilimia 3.5 yapato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili nilipenda kuzungumziailitolewa na Mheshimiwa Magdalena Sakaya ambayealisema kwamba utumiaji wa mazao ya misitu nchini kwakutengeneza samani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchiambapo tunapoteza chanzo cha mapato.

Mheshimiwa Spika, tunakubaliana na yeye, lakinibado sana teknolojia ya wazalishaji wetu hapa ndaniimekuwa duni kwa kiasi kikubwa na mazao mengiyanayotokana na uvunaji wa misitu bado hayajatumikakikamilifu kwa matumizi mengine mbalimbali ikiwemo hiyoya kutengeneza samani za maofisini na majumbani, lakini piakutengeneza briquette kwa ajili ya mikaa na matumizimengine mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali imekuwa ikitoamaagizo mbalimbali mara kadhaa kuhusu taasisi mbalimbali

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

za Serikali kuanza kutumia samani za hapa ndani na mfanomzuri ni kwenye Bunge lako ambapo tunatumia samanizinazotokana na mazao ya misitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia mwaka huu kadriambavyo Ilani ya Uchaguzi inatuelekeza tutenge asilimia 10ya mazao ya misitu kwa ajili ya viwanda vya ndani, tunafanyahivyo. Huu ni mwaka wa pili sasa tumekuwa tukifanya hivyo,tunatenga uzalishaji kwenye misitu kwa asilimia 10 kwa ajiliya viwanda hususan katiak mashamba yetu ya Longuza namashamba ya Mtibwa.

Mheshimiwa Spika, hoja ya mwisho ambayo napendakuchangia inatokana na mchango alioutoa Mheshimiwa ZittoZuberi Kabwe hapa Bungeni kuhusiana na kwamba VATimepunguza kasi ya ukuaji wa Sekta ya Utalii hapa nchini.Introduction ya VAT inaweza ikasemwa kwamba imepunguzakasi ya ukuaji wa Sekta ya Utalii lakini sisi tunapenda kuonakwamba bado ni mapema mno kufanya tathmini ya ainayoyote ile kama introduction ya VAT imeathiri ukuaji wa sektaama la!

Mheshimiwa Spika, hatupingi wala hatukubali, lakinitunaona tu kwamba muda wa kufanya tathmini badohautoshi na sisi tunaona sababu za ku-introduce VAT kwenyeSekta ya Huduma za Utalii ilikuwa ni ya maana sana, kwambasekta hii kwa muda mrefu imekuwa ikionekana kama vile nisekta ipo na haizalishi sana kwa ajili ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, sasa, ili Watanzania wa kawaidawaweze kufaidika na Sekta ya Utalii ni lazima Sekta ya Utaliiitozwe kodi ili hizo kodi ziende kutumika kutekeleza miradi yakijamii ambayo itawagusa wananchi wengi, hilo ni jambo lakwanza. Pia, ni lazima wananchi wawezeshwe kushiriki katikaSekta ya Utalii ili nao wapate kipato kutokana na sektayenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kwa bahati mbaya sana,sekta hii kwa miaka mingi imekuwa ikiwa controlled nawawekezaji kutoka nje ambapo mawakala wapo nje ya nchi

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

na baadhi ya mawakala wapo ndani. Malipo kwa kiasikikubwa yamekuwa yakifanyika nje ya nchi na kwa hivyohapa Tanzania tunakuwa hatupati chochote. Piawafanyabiashara wa Tanzania walikuwa wachache kwamiaka mingi.

Mheshimiwa Spika, sasa tulichokifanya katika miakahii ni kutanua wigo wa kuwavutia wawekezaji wa ndani naowashiriki kwenye biashara ya utalii ili pia tuweze kupata kodi.Pia tunapo-introduce VAT maana yake walau tunapunguzaeconomic leakage ambayo ilikuwa inasababishwa kwamapato ya utalii kubaki nje na kutokuingia hapa ndani kwasababu tunachaji kwenye huduma ambazo ziko hapa ndani.Kwa kufanya hivyo, tunakuwa tuna uhakika sasa ulemchango mkubwa ambao unaonekana kwa sekta pana yautalii wa asilimia 17.6 kuwa na faida kwa wananchi wakawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja naahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla.Mheshimiwa Captain Mstaafu Mkuchika dakika tanoatafuatiwa na Mheshimiwa Januari Makamba, dakika kumi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika,nataka nianze kwa kuunga mkono hoja. Vile vile napendakumpongeza Waziri wa Fedha kwamba baada ya kutokaChuoni kufundisha akaja kwenye siasa. Hotuba aliyoitoamwaka huu ya utangulizi wa Serikali hii imefanya nini,ameshahitimu siasa. Alimaliza kila kitu katika yale mambokumi aliyoyasema yaliyofanywa na Serikali ya Awamu yaTano, basi hotuba ya Waziri wa Fedha hakuna hotuba yakoimenoga kama ya mwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, upandewangu Utumishi na Utawala Bora kulikuwa na hoja kama tatunitazieleza kwa kifupi. Kwanza ni suala la ajira, Wabungewengi wamesimama wametaka kufahamu suala la ajira

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

likoje. Nataka nieleze tu kwamba Serikali kwa makusudiilisimamisha ajira kwa muda katika kipindi cha kuhakikiwatumishi. Maana unaweza ukampa mtu promotion kumbemfanyakazi yule fake, unaweza kumpa mtu promotion kumbevyeti vyake sio halali. Ndio maana ikasimamishwa kwanza, ilizoezi la uhakiki likashakamilika zoezi lianze. Zoezi limekamilika,tumewabaini wafanyakazi hewa 19,708, tumewabaini vyetifake 14,409, tazama pesa kiasi gani tumeokoa. Malengo yauhakiki makubwa ni mawili:-

Mheshimiwa Spika, kwanza tuwapate watu wafanyekazi ambayo wanataaluma nayo. Mtu anaingia theatreanapasua watu awe ni mtu ambaye cheti chakekinamruhusu kupasua watu. Tumewabaini watu wanavaamajoho meupe wanaingia walikuwa wanafanya operationsasa hatuwezi kucheza na maisha ya watu. Ndio maanaSerikali ikasema kwanza, tuwe na uhakika kila mmojaanafanya kazi ambayo ana taaluma nayo.

Mheshimiwa Spika, lakini lingine nalo Utawala Bora nikusimamia rasilimali za umma zitumike vizuri. Unapowalipawafanyakazi hewa, unapowalipa watu ambao vyeti vyakesi sahihi, hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Kwahiyo, nataka niseme baada ya hil i zoezi kukamilikatumeshaanza ajira, mpaka Juni, tutakuwa tumeajiri watumishi22,150 mpaka tarehe 30 ya mwezi huu.

Mheshimiwa Spika, katika hao Walimu ni 7000 tayariprocess ya ajira inaendelea na Afya 8000. Kwa hiyo, natakaniwaombe Wabunge wenzangu wale ambao tunasimamiaujenzi wa zahanati tusiwe na mashaka, tumalize zahanatihakuna zahanati itakayokamilika ikaacha kufanya kazi etikwa sababu haina watumishi, tutawaajiri. Hilo ni la kwanza.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pil i, i l ikuwa upande wamishahara na hili limeongelewa na Mheshimiwa MasoudAbdallah Salim wa Mtambile, Mheshimiwa Susan Kiwangawa Mlimba na Ndugu yangu Mheshimiwa Mwita Waitara.Kifupi walisema kwamba, watumishi wa umma

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

hawajaongezewa mishahara kwa muda mrefu sasa na piahata nyongeza yao ya mwaka (increment) hawapewi. Halihii inasababisha wanapostaafu kupata mafao kidogo.Maelezo ya Serikali ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, si sahihi kwamba watumishi waumma hawajaongezewa mishahara kwa muda mrefu kwaninyongeza hiyo haikutolewa kuanzia mwaka 2016/2017. Kamanilivyoeleza kutokana na uamuzi wa Serikali kupitia Muundowake na kufanya zoezi la uhakiki watumishi. Aidha, hivi sasaSerikali inaboresha utoaji wa huduma ya elimu na afya nakutekeleza miradi maendeleo ambayo itakuwa chachu yaukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla katika siku zabaadaye.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uwezo wa kibajetiimekuwa vigumu kugharamia utoaji wa huduma ya elimu naafya, kutekeleza miradi hiyo mikubwa pamoja na kuongezamishahara kwa wakati mmoja. Uwezo wa bajetiutakapokuwa mzuri Serikali itatoa nyongeza na mishaharakwa watumishi wake.

Mheshimiwa Spika, tulipokuwa Iringa kwenye Sikukuuya Wafanyakazi, Mheshimiwa Rais alisema hali ya hewa,akiona kwamba hali ya hewa inaruhusu hatangojakupandisha siku ya sikukuu, hata ngoja kupandisha siku yamwaka mpya, muda wowote hali itakaporuhusu mishaharaitapanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika mwaka wafedha 2017/2018, Serikali ilitoa nyongeza ya mwaka AnnualSalary Increment kwa watumishi wa umma na itaendeleakutoa nyongeza hiyo katika mwaka wa fedha 2018/2019na miaka mingine kadri ya uwezo wa bajetiutakavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, suala la mwisho lilihusu upandishajivyeo. Hili lilitolewa na Mheshimiwa Sophia Mwakagenda naMheshimiwa Dkt. Prudenciana Kikwembe. Hoja ilikuwakwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilizuia stahiki mbalimbali

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

watumishi ikiwemo upandishwaji madaraja kupisha zoezi lauhakiki. Kwa kuwa zoezi l imekamilika watumishiwamepandishwa madaraja, kwa tarehe za sasa na sio kwatarehe walizostahil i kupanda madaraja. Hali hiyoinasababisha watumishi kustaafu na kupata mafao kidogo.Serikali iwalipe stahiki zao watumishi kwa vile zoezi la uhakikilimekamilika.

Mheshimiwa Spika, maelezo ya Serikali ni kweli Serikaliya Awamu ya Tano ilizuia stahiki mbalimbali za watumishiikiwemo upandishaji madaraja ili kupisha zoezi la uhakikiambalo lilifanyika kwa manufaa makubwa na kuokoa kiasikikubwa cha fedha za Serikali kwa kuondoka watumishi hewa.kama nilivyosema 19,708, watumishi wenye vyeti fake 14,405.Hata hivyo kwa watumishi…

SPIKA: Mheshimiwa Waziri malizia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika,paragraph moja tu naisoma.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa watumishi ambaowalikuwa na barua ya kupandishwa vyeo, mishahara yaoiendelee kubadilishwa katika mifumo shirikishi na taarifa zakumbukumbu za watumishi kila mwezi kwa kuzingatia tarehewalizostahili kadri ya tarehe yao ya kustaafu kazi kwa umriilivyokaribia.

Mheshimiwa Spika, iwapo kwa bahati mbaya yupomstaafu ambaye alikuwa na bahati ya kupandishwa cheolakini mshahara haujabadilika hadi alipostaafu; mstaafu wanamna hii anashauriwa aende kwa aliyekuwa mwajiriwake amjazie fomu maalum ya madai ya malimbikizo yamishahara inaitwa Mheshimiwa Spika, Salary Arrears ClaimsForm ili aweze kulipwa madai yake kwa njia za hundi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, kamanilivyosema naunga mkono hoja. (Makofi)

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mkuchika.Mheshimiwa Januari Makamba atafuatiwa na MheshimiwaAngella Kairuki, dakika kumi kila mmoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia bajeti hii nanianze kwa kukupongeza kwa jinsi unavyoongoza Bunge letuvizuri kwa busara na hekima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nimpongeze sana MheshimiwaDkt. Mpango, Waziri wa Fedha, Naibu Waziri wa Fedha,Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote. Nimefuatiliamijadala ya bajeti hata kabla ya hapo, mijadalambalimbali iliyohusu Wizara ya Fedha. Bahati mbaya sanakatika baadhi ya mambo niliyobaini ni mashambulizi binafsikwa Mheshimiwa Dkt. Mpango (personal attack), kwambakuna wakati tabia yake, kwamba ana kiburi, il ikuwainazungumzwa kuna wakati hata elimu yake inatiliwamashaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati mwingi kilichopo mezanihuwa ni hoja, lakini bahati mbaya, mimi bahati nzuri nimepatakumfahamu Mheshimiwa Dkt. Mpango miaka kumitumekuwa wote, alikuwa msaidizi wa Rais, Uchumi miminilikuwa Msaidizi wa Rais, Hotuba, nimefanya nae kazi kwakaribu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kujua humility auhumbleness ni Dkt. Mpango, hii habari ya kiburi, binafsi nawote ambao tuna-interact naye binafsi hiyo haipo. Kwahiyo nadhani wakati mwingine humu ndani ya Bungetupingane tu na ni haki na ni sahihi, kuwa na mawazo tofautiya alicholeta mezani lakini tunapomwendea binafsitunakuwa tunakosea. Wakati mwingine sio yeye tu hatahumu ndani baina ya Wabunge na Wabunge, umebainiMbunge anapotoa hoja kinachojibiwa sio alichosema balini yeye yukoje na anaishi wapi na anafanya shughuli gani nayote ambayo yamezungumzwa yanakuwa sio tena hoja.(Makofi)

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Bunge la namna hiyonadhani sio Bunge unalolitaka na sio Bunge linalostahili hadhina uzito wako kama wewe Spika. Kwa hiyo, nataka ni-vouch,nimtetee Dkt. Mpango kwamba namfahamu na piaukiondoa tu tabia yake ya kusikiliza na kuheshimu kila mtu,pia ni msomi mzuri bila shaka yoyote. Amefanya kazi Benkiya Dunia, ameaminiwa na Marais wawili, amepitia kwenyemikono ya Profesa Ndulu ambaye tunamsifu ni gwiji wauchumi hapa nchini, ameaminiwa nje ya nchi na ndani yanchi na pia ni mcha Mungu, kaka yake ni Askofu anatokahuko katika familia ya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Mheshimiwa Dkt. Ashatu woteambao tunapishana naye kwenye corridor hatuwezi kusemakwamba, ana kiburi, tunamjua kwamba mtu ana heshima.Vilevile watalaam wa Wizara ya Fedha wakiongozwa naBwana Dotto na wao pia ukimfuata bwana Dottoanakusikiliza na anafanya maamuzi akielewa jambo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nil iona wakatitunaongelea bajeti hawa viongozi wetu wakuu ambaotumewapa kazi kubwa sana ya kuandaa bajeti nakuiwasilisha na kujibu siyo kazi ndogo wanaifanya kwa niabayetu sisi Watanzania. Hivyo, tusiwapeleke kule ambapotutazidi kuwatia msongo wa mawazo kwamba kaziwanayofanya hatuithamini. Kwa hiyo, nawapongeza kwaweledi wao lakini pia kwa hulka zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kuna hoja mbili, tatuzimetolewa hapa…

SPIKA: Kabla hujaenda kwenye hoja MheshimiwaJanuary, wala usikae, nataka kumwambia Mheshimiwa Dkt.Mpango na Mheshimiwa Dkt. Ashatu, katika siasaalichokifanya January ndiyo kinachopaswa kufanywa. Yaanikatika siasa lazima upate watu wakusemee, lakini ukisemamwenyewe jamani mimi mtu mzuri, watu watasema unaona.Kwa hiyo, ni jambo zuri sana amelifanya, namshukuru sanakwa niaba yetu, endelea Mheshimiwa. (Makofi)

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, naombanikuthibitishie kwamba sikukaa chemba na Mheshimiwa Dkt.Mpango kabla ya kuzungumza hapa siku ya leo. Kwahiyo hizi ni hisia kabisa binafsi na zinawasilisha mawazomengi hapa katika Baraza la Mawaziri na Wabungewengi ambao tunafanya kazi na Mheshimiwa Dkt. Mpango.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mambo kadhaayamezungumzwa kuhusu muungano hasa kubwa ni hoja yaMheshimiwa Dkt. Ally Yussuf Suleiman ambaye ametajamambo matatu, ambayo napenda kuchukua nafasi hiikuyajibu harakaharaka.

Mheshimiwa Spika, la kwanza ni akaunti ya pamoja,amesema muda mrefu akaunti hii haijaanzishwa. Ni kweli naakaunti hii ya pamoja imewekwa ni hitaji la kikatiba kifungucha 133 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakinaelekeza kwamba kuwe na Mfuko wa Akaunti ya Pamojaya Fedha ambayo itakuwa sehemu ya Mfuko Mkuu waHazina ambapo kutawekwa fedha yote itakayochangwa naSerikali mbili kwa kiasi kitakachoaamuliwa na Tume ya Pamojaya Fedha. Hilo ndiyo neno la msingi, kwa kiasikitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Akaunti hii ya Pamojahaijakuwepo kwa sababu mapendekezo ya Tume ya Pamojaya Fedha kuhusu kiwango cha mgawanyo ndiyoyanafanyiwa kazi na Serikali sasa hivi. Hili ni jambokubwa linahitaji uamuzi wa Mabaraza yote mawili yaMawaziri ya pande zote mbili na linahitaji input kubwa yawataalam.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kinachoendelea sasahivi ni kusubiri maamuzi baada ya wataalam kuwawanamalizia kazi yao. Kwa hiyo, sisi kama Serikali azma yakutimiza matakwa ya kikatiba bado ipo palepale, lakini kwakuwa ni jambo kubwa lazima tuliendee kwa umakini nautaratibu ili liweze kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Spika, suala la pili lililozungumzwa kuhusuMuungano ni suala la mchakato wa sasa hivi unaoendeleawa usajili wa meli. Kama unavyofahamu Tanzania ina ainambili ya usajili wa meli; kuna usajili wa meli za ndani na usajiliwa meli za nje zinazopeperusha Bendera ya Tanzania.Kwamba mtu yuko nje ya Tanzania ana meli yake, lakinianataka atumie Bendera ya Tanzania. Usajili huounafanywa na Mamlaka Zanzibar ndiyo tulivyokubaliana,usajili wa meli za ndani unafanywa na SUMATRA. Sasakulitokea changamoto ya kutokuwepo na uangalifu naumakini katika usajili wa meli za nje zinazopeperusha Benderaya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kilichojitokeza nikwamba meli zinazopeperusha Bendera za Tanzania zilikutwanje ya nchi zinafanya makosa makubwa, kubeba silaha,magendo, madawa ya kulevya na kupaki kwenye Bandarizisizoruhusiwa. Kwa hiyo, Serikali ambacho tumeamuakufanya siyo kuinyang’anya Zanzibar mamlaka ya usajilihapana, kwamba hili jambo la usajili tushiriki wote. Kwambaasiwe mtu Dubai ana muhuri tu yeye anagonga tu nakukabidhi bendera, lazima vyombo vya Usalama vya nchivishiriki, kwa sababu tunapotoa bendera yetu, ni alama yanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tulikubaliana kwambawenzetu watafanya lakini wasifanye peke yao kuwe na inputya Vyombo vya Ulinzi na Usalama na due diligence wa melizote zinazoomba kutumia Bendera ya Tanzania. Kwa hiyo,hicho ndicho kinachofanyika na wala wenzetu Wazanzibariwasione tunawapora na kwa kweli ni muhimu haya mambokuyajua kabla ya kuyasema, kwa sababu yanaamsha hisiaambazo si sahihi.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni Kisiwa cha FunguMbaraka au Latham; kwamba Mheshimiwa Dkt. Ally YussufSuleiman alisema kwamba Tanzania Bara inataka kuporaKisiwa hiki kwa sababu kuna rasilimali. Labda niseme kwambanchi yetu ni moja hatujafikia mahali pa kugombea eneokatika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

SPIKA: Kinaitwaje Kisiwa hicho?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Naam.

SPIKA: Kisiwa hicho kinaitwaje?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, kinaitwaFungu Mbaraka au Latham kipo katikati hapa Bahari ya Hindi.Kwa hiyo, kuna dhana inajengeka kwamba kuna mgogorokati ya Bara na Zanzibar kuhusu umiliki wa Kisiwa hicho.

Mheshimiwa Spika, chanzo cha mgogoro nikwamba inawezekana eneo lile lina mafuta. Sasa hii dhanainaenea na inaamsha hisia. Sasa niseme tu kwamba hukonyuma wakati suala la mafuta ni la Muungano na TPDC ndiyoilikuwa inatoa leseni ni kweli pale mahali palitolewa blocksza kuchimba, kutafuta mafuta.

Mheshimiwa Spika, bahati mbaya wale waliyotafutamafuta hawakuyapata, kwa hiyo wakarudisha zile block, kwahiyo, mpaka leo lile eneo halina mtu anayetafuta mafuta.Kwa hiyo dhana kwamba tunagombea eneo katika Jamhuriya Muungano wa Tanzania siyo sahihi, Katiba zetu ziko wazikuhusu maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nanchi yetu hii ni moja, Zanzibar ikinufaika Tanzania imenufaika,Bara ikinufaika Tanzania imenufaika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwa wenzetuWanzazibari na Watanzania kwa ujumla kusijengeke dhanakwamba tunagombana kuhusu eneo lolote katika Jamhuriya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho, umezungumza kuhusulugha humu ndani za ukabila na ukanda na mengineyo. Hatahivyo, kuna moja ambalo ni muhimu kulizungumza lughazinazohusu Muungano wetu. Namna ambavyo tunauchangiana kuuelezea Muungano wetu ni kana kwamba badohatujakubaliana kuhusu umuhimu wake na kwamba

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

tumeamua kuungana. Kuna lugha kali sana ambazozinafadhaisha watu wa upande mmoja na kudhalilishaupande mmoja au mwingine.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ningependa utumierungu lako na kiti chako na joho lako na busara zako kukemeahizi lugha ambazo zina-condemn kwa ujumla watu waupande mmoja au mwingine kuhusu Muungano. Muunganowetu sisi tumeamua kuwa nchi moja, tumeamua kuwa jeurina kutengeneza mipaka yetu ya Tanzania. Kwa hiyo, naombaurithi huo tuulinde na Bunge lako lichukue uongozi katikakuulinda urithi huo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa January Makamba.Mheshimiwa Angellah Kairuki atafuatiwa na MheshimiwaLuhaga Mpina ambaye atakuwa wa mwisho kwenyemichango.

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kunipa nafasi nipende tu kusema kwamba naungamkono hoja hii ya Mheshimiwa Waziri kwa asilimia mia moja.Kipekee tu napenda kumpongeza sana yeye MheshimiwaNaibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Fedhakwa Hotuba nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la kwanza, kama msimamizi waSekta ya Madini nipende tu kutoa shukrani sana kwa Serikalikupitia kwake Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa kukubalikuweza kufuta tozo zilizokuwa zikitozwa katika chumvi, tozotakribani 10 kati ya 16 ambazo kimsingi zilikuwa zimesababishasana gharama za uzalishaji wa chumvi kuwa kubwa na piakumsababishia mchimbaji wetu mdogo wa chumvikutokuweza kupata faida.

Mheshimiwa Spika, ilikuwa kwa takribani gunia la kilo50 walikuwa wanapata faida ya Sh.150 tu ilikuwa ni faidandogo. Pia walikuwa wanashindwa kushindana kisoko na

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

matokeo yake ilikuwa chumvi ya kutoka nchi za jiraniilikuwa inaingia kwa wingi zaidi na hatimaye sisi ambaotuna chumvi nyingi humu kutoweza kufanya biashara aukuwa na ushindani. Kwa hiyo nipende tu kusema kwaniaba ya Sekta ya Madini na Wizara tunawashukuru sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna hoja yaMheshimiwa Musukuma kuhusiana na tozo au kiwangokikubwa cha kodi kinachotozwa katika madini yadhahabu au kwa wachimbaji wetu wadogo wa dhahabuna alikuwa ameeleza kwamba kuna tozo ya asilimia takribanikumi na nne (14%).

Mheshimiwa Spika, nipende tu kumwelezaMheshimiwa Musukuma kwamba kwa mujibu wa Sheria yetuya Madini Sura namba 123, wachimbaji wadogo wanatozwatakribani asilimia 12.3 ya kodi ambayo inajumuisha mrabahawa asilimia sita, inajumuisha kodi ya zuio ya asilimia tano, adaya ukaguzi wa uzalishaji wa madini asilimia moja, pamoja naushuru wa huduma au service levy kwa halmashauri kwaasilimia 0.3 ambayo jumla yake ni asilimia 12.3 na kwa upandewa wachimbaji wakubwa na wa kati wao wanatozwamkokotoo wa asilimia 37.3.

Mheshimiwa Spika, alipendekeza kodi kwawachimbaji wadogo ziondolewe; nipende tu kumwelezaMheshimiwa Mbunge kwamba tumekuwa tukiliona na kwakuwa Serikali yetu ni sikivu kama ambavyo tumefanya katikachumvi. Niendelee tu kuwaomba shirikisho la Vyama vyaWachimbaji Wadogo (FEMATA) tukae, tuweze kulizungumzasuala hili na kuliona ni kodi zipi au ni tozo zipi ambazo zinawezazikafikiriwa kuzingatiwa katika punguzo hilo au kuwezakuondolewa.

Mheshimiwa Spika, lengo letu kubwa kama Serikalinikuhakikisha kwamba tunakuwa na uchimbaji mdogo,uchimbaji mdogo ambao utakuwa na faida kwa wachimbajiwetu. Lakini pia sisi kama Serikali bado tunaendelea kuonani namna gani tunawasaidia kwa upande wa teknolojia,

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

masuala mazima ya mtaji, mafunzo, kupata masoko lakinizaidi kuwapa teknolojia mpya na waweze pia kujifunzateknolojia ya kisasa katika uchimbaji.

Mheshimiwa Spika, kwa kuanzia kupitia Serikali kupitiabajeti yetu ya Wizara ya Madini katika mwaka ujao wa fedhatutajenga vituo vya mifano vitano katika maeneo ya Chunya,Bukombe, Rwamgasa, Tanga pamoja na Kilwa. Pia tutajengavituo saba vya umahiri Mpanda, Handeni, Musoma, Songea,Bariadi, Bukoba na kwingineko.

Mheshimiwa Spika, lengo letu kubwa ni kuhakikishakwamba tunawafundisha kwa mfano ili waweze kuchimbakwa teknolojia ya kisasa kupitia vituo hivyo ambavyotumeviweka kwa gharama nafuu sana, lakini hatimaye lengoletu ni kuhakikisha kwamba tunawarasimisha ili wawezekuingia katika mfumo rasmi wa kibiashara pamoja na kikodi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mwisho nipende tu kuoa raikwa Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, kuhakikisha kwambawanazingatia viwango vya tozo za kodi vilivyoanishwa katikaSheria. Wako wengine unakuta wameenda katika maduaraya uchimbaji wa Madini, unakuta wanaambiwa wakivunamifuko 10, mifuko labda mitano inaenda kwenyeHalmashauri. Niombe sana tuzingatie viwango ambavyovimeainishwa kisheria ili kuhakikisha kwamba wachimbajiwetu hawa wadogo hatimaye wanaweza kukua.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo Sera yetu yaWizara ya Madini na Serikali kwa ujumla wachimbaji hawahadhi yao hii si ya kudumu wanatakiwa tu watumie hadhi yauchimbaji mdogo kama daraja hatimaye waweze kuwawachimbaji wa kati na hatimaye pia kuwa wachimbajiwakubwa kama ambavyo wengine kama wakina BusolwaMining pamoja na akina Mzee wangu Marwa wamewezakufanikiwa.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna hoja pia ya zuio lausafirishaji wa carbon, hoja hii nadhani leo nitakuwa

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

nasimama kwa mara ya tatu kuweza kuielezea. Kaka yanguMheshimiwa Musukuma ameweza kuieleza lakini nipende tukurudia maelezo ya Serikali kwamba zuio letu la usafirishajiwa carbon liko palepale kama nilivyotoa maelezo yangutarehe Mosi Juni, kama nilivyotoa maelezo yangu pia tarehe14 Juni.

Mheshimiwa Spika, nipende tu kwa kwelikuwapongeza sana wamiliki wa Illusion Plants takribaniwatano kwa Kahama tayari wameshaanza kujenga IllusionPlants hizo. Nipende pia kuwapongeza wawekezaji takribaniwatatu ambao wameshaanza kuonesha nia ya kuwekezaShinyanga, vile vile pia niwapongeze sana wawekezajiwengine watatu ambao wameonesha nia ya kuwekezakatika maeneo ya Tabora.

Mheshimiwa Spika, zaidi niwapongeze sana Kampuniya GEMAAfrica ambao tayari wameshakamilisha kujengamtambo wa Illusion Plants Wilaya ya Geita. Nipendekuwapongeza Kampuni ya Transco Gold pamoja naNyamigogo, Nang’ana Group pamoja na Busamu Companyambao nao wameshakamilisha ujenzi wa Illusion Plants katikaWilaya ya Kahama.

Mheshimiwa Spika, kipekee pia niwapongeze FramalInvestment ambao tayari nao wameshakamilisha ujenzi wamitambo yao katika Wilaya ya Musoma pamoja na DeepMine Service ambayo kwa sasa na wenyewe wanatafutaeneo la kujenga mitambo husika ya Illusion Plants katikaWilaya ya Kahama.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Geita na Tarimebado watu wengi wamekuwa wakionesha nia. Nipendetu kuwakaribisha sana wawekezaji na Watanzaniawengine kuona ni namna gani wanatumia fursa hiikuwekeza katika ujenzi wa Illusion Plants katika sehemuambazo bado wawekezaji hawajenda lakini piahuduma zao zinahitajika. Hata hivyo, nipende kusemakwamba agizo la Serikali bado linasimama palepale.(Makofi)

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kuhusiana naMheshimiwa Ole Millya alieleza kwa kina sana kwambamapendekezo ya Kamati Maalum ya Mheshimiwa Spikailiyochunguza mnyororo mzima wa biashara ya uchimbaji waTanzanite kwamba hayajatekelezwa. Nipende tukumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufuhata siku moja hatuwezi kudharau mapendekezo aumaazimio ya Kamati Maalum ya Spika ambayo tunaamini nimapendekezo ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, vilevile nipende tu kueleza tukwamba kama ambavyo tulieleza tarehe Mosi, Juni, 2018katika hotuba yangu ukurasa wa 46, tulieleza namnakabisa masuala mazima ya majadiliano kupitia ubia waKampuni ya Tanzanite One pamoja na STAMICOyanavyoendelea na tulieleza katika hotuba yangu ukurasawa 46 kwa wale ambao watakuwa nayo wanawezakufuatilia.

Mheshimiwa Spika, tumeotoa maelekezo kwaKampuni ya Tanzanite One pamoja na STAMICO kurudishaleseni ya uchimbaji ili iweze kuandaliwa utaratibu mpyaambao utaiwezesha Serikali na Taifa kwa ujumlakuweza kunufaika zaidi katika uchimbaji na biashara nzimaya Tanzanite kwa kuzingatia Sheria ya Madini, Sura namba123.

Mheshimiwa Spika, hayo mengine ya kusemayamegawia, sijui imekuwaje mara imehuishwa, nipende tukusema kwamba niwaombe Waheshimiwa Wabunge wajikitezaidi katika maelezo ya Mheshimiwa Kabudi aliyoyatoatarehe Mosi, Juni lakini pia wajikite katika kufanya referencekatika hotuba yangu niliyoitoa ya bajeti katika ukurasa ulewa 46. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nipende tu kusema kwambakatika makubaliano yale ambayo Kamati ya Majadiliano yaTaifa kupitia kwa Kiongozi Mheshimiwa Kabudi, makubalianoyaliyoingiwa tarehe 15 Aprili na Kampuni ya Tanzanite Onetayari wameshaanza kulipa mkupuo wa kwanza wa fidia

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

ambayo walikuwa wameelekezwa na obviously fidia hiiinaingia kwa Taifa na kuna taratibu zake kwa mujibu waWizara ya Fedha kwa malipo kama hayo yanalipwa kwataratibu gani.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru na napenda kusematu kwamba, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Angellah Kairuki,Waziri wa Madini, tunakushukuru sana. Sasa ni zamu yaMheshimiwa Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, tafadhalidakika 10.

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa nafasi uliyonipa ili niweze kuchangiakatika hotuba hii iliyo mbele yetu ya Bajeti Kuu ya Serikali yaMheshimiwa Dkt. Mpango pamoja na Naibu wake.

Mheshimiwa Spika, kwanza niungane kwa dhatikabisa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwakazi kubwa anayoifanya katika Taifa hili katika kupiganiamaendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nifunguke tu kwambaBunge lako hili kabla ya mimi sijawa Waziri hapa nimepitiamaeneo mengi sana na Bunge hili limenipeleka kwenyeTaasisi mbalimbali kwenye Mabunge ya Afrika, nimeendakwenye Mikutano mingi ya kikanda na ya Kimataifa sijawahikuona Kiongozi ambaye committed kama Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli. Nampongeza sana kwa kazi kubwaanayoifanya katika nchi yetu hii ya Tanzania katika kupiganiamaendeleo ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nikupongeze wewe sana, mojaya sifa ya Kiongozi ni kutengeneza viongozi. Toka ulivyokuwaMwenyekiti wa Bunge hili, baadaye ukawa Naibu Spika,baadaye ukawa Spika umetengeneza viongozi wengi sanakwenye Bunge hili. Kwa hiyo, uwezo wako siyo wa kutiliwamashaka yoyote na mtu yeyote anayejua historia na mimi

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

pia tu nikuombe kwamba kwa baadhi ya wale Wabungewageni ambao hawaijui historia wasiwe wanakurupukakushambulia watu wasiowajua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo na nirudiepia kumpongeza sana Waziri wa Fedha na MipangoMheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Naibu wake Ashatu Kijajikwa kazi kubwa sana ambayo wanayoifanya katika kulindauchumi wa nchi yetu. Katika kipindi hiki kifupi chaUtawala huu wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufulina Serikali hii ya Awamu Tano mambo mengi yamefanyikasana, mageuzi makubwa yamefanyika ya kiuchumiambapo Mheshimiwa Dkt. Mpango tunampongeza sanakwa kazi hiyo kubwa kwa kuendesha hilo gudurumu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtakumbuka na Wabungewatakumbuka hapa na wengine wameni-refer kwenyemichango yao niliwahi kulia mbele ya Bunge hili nakukataa Bajeti ya Serikali, kipindi ambacho kilikuwakigumu sana kwangu pia kwa chama changu, lakiniyalikuwa ni baadhi ya mambo ambayo leo hiiyamefanyiwa marekebisho makubwa na mageuzi makubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, yapo mambo makubwa nsihukuru,nimpongeze hapa Mheshimiwa Stanslaus Mabula ambayealipata nafasi hapa ya kuchangia kuna mambo makubwakatika Taifa hili ambayo tulikuwa tukiingia hasara kubwa natulirekodiwa kati ya nchi ambayo ina-facilitate zoezi la IllicitFinancial Flow kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo,mapambano yaliyowekwa, mechanism zilizowekwa, kupigavita suala la Illicit Financial Flow katika nchi yetu, huwezikuamini leo akina nanii ambao wanafanya tathmini yaIllicit Financial Flow, tunawakaribisha Tanzania waje watu-access.

Mheshimiwa Spika, watakuja kuona jinsi udhibitimkubwa uliyofanyika na sasa zoezi hili linafanyika kwakiwango cha chini sana hapa nchini kwetu. Pia mambo ya

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

transfer pricing vilevile, mambo ya dollarization vilevile nasuala gumu hili lilishindikana siku zingine suala la credit ratingna lenyewe katika kipindi hiki limeweza kufanyika. Kwa hiyo,viongozi wetu ambao wanaongoza jukumu hili, Waziri waFedha na msaidizi wake, pamoja na Katibu Mkuu wake nawengine wote wanaohusika katika usimamizi wa uchumiwetu tunawapa heko na tunawapongeza sana kwa bidii hizoza kazi.

Mheshimiwa Spika, basi baada ya kusema hayo,niweze kuzungumza kidogo kuhusu baadhi ya mamboambayo yamezungumzwa ambayo yanatekelezwa katikaWizara yangu:-

Mheshimiwa Spika, moja ni jambo la chanjo nauogeshaji wa mifugo kwamba, tunayo shida kubwa. Ni kwelikabisa nakubali kwamba, suala la chanjo na uogeshaji wamifugo ambapo mifugo mingi inakufa kila mwaka kwa kukosachanjo na mifugo mingi inakufa kila mwaka kutokana na kupena kwa kutokana na kutokuogeshwa. Sasa tunafanyakila aina kuhakikisha kwamba, jambo hili tunalifanya vizurizaidi.

Mheshimiwa Spika, Chuo chetu cha Utafiti chaUzalishaji wa Chanjo cha Kibaha kinaendelea vizuri kuzalishachanjo hapa nchini. Vilevile tumepata bahati ya kupatamwekezaji mpya kutoka India ambaye naye anakuja kujengakiwanda hapa kwa ajili ya kuzalisha chanjo kwa wingi.Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuwahakikishia wananchi wetuna kuwa-guarantee kupatikana kwa chanjo kwa muda nakwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kama hiyo haitoshi pia,kwamba, Wizara yangu inatengeneza sasa mpango ambaoutawezesha chanjo kupatikana kiurahisi, lakini vilevileuogeshaji wa mifugo kuwezekana kwa urahisi na vilevile kwabei ambazo wafugaji wetu watazimudu. Kwa hiyo, jukumuhilo linafanyika na mpango huo tutahakikisha kwamba,wafugaji wote, halmashauri zote zinashirikishwa katikakuutekeleza.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Spika, kuna suala lingine la pili liliwahikuzungumzwa hapa Bungeni kuwa ni suala la uzalishaji wamaziwa hapa nchini na hasa ikilinganishwa nchi yetu na nchiya Kenya kwamba, sisi tunazalisha mpaka sasa hivi lita zamaziwa bilioni 2.4 wakati Kenya wanazalisha bilioni 5.2.

Mheshimiwa Spika, katika ulinganifu huo ni kwelikabisa, lakini nataka kuwa-assure Waheshimiwa Wabungekwamba, kutangulia si kufika, tumejipanga vizuri katikakuhakikisha kwamba, tunakuja na uzalishaji mkubwa wamaziwa hapa nchini. Sisi hatuwezi kushindana na Kenya,hatuwezi kushindana na nchi yeyote ile ya Afrika kwa sababu,sisi kama ninavyosema, ni nchi ya pili tu kuwa na mifugo mingihapa Afrika ikiwa nchi ya kwanza inayoongoza mpaka sasahivi ni Ethiopia.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, sisi tuna malisho mazurikuliko mtu yeyote, tuna maji bora kuliko mtu yeyote pamojana kwamba, ng’ombe wa maziwa sasa hivi ni 789,000 tu, lakinimpango tulioanzisha sasa hivi wa kuhimilisha mifugo yetuambao tunaita this is a massive artificial insemination ambapotutahimilisha kila mwaka kutafuta mitamba milioni moja kwamwaka, kwa miaka mitatu tutakuwa na mitamba milioni tatuna tutaweza ku-compete na yeyote na tutaweza kuzalishamaziwa mengi kuliko mtu yeyote. Tuna mifugo, tuna maeneomazuri na swali hili limenifurahisha na liliulizwa na MheshimiwaJesca. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini niseme kwamba, Kituo chetucha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) tumekifanyia ukarabatimkubwa sana ambao utawezeasha kuzalisha mbegu nyingiza kutosha. Tumenunua madume bora 11, kuna mtu mmojaaliwahi kuchangia hapa Bungeni akasema kwamba,madume hayo 11 hayawezi kutosheleza na kwamba, nikidogo mno na kwamba, Serikali haiko serious.

Mheshimiwa Spika, niwaambieni kwamba, hayamadume 11 yanaweza kuhimilisha ng’ombe zote wa AfrikaMashariki. Mbegu zinazozalishwa na madume 11 zinawezakuhimilisha mahitaji yote ya uhimilishaji katika nchi za Afrika

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Mashariki. Kwa hiyo, tumejipanga vizuri na tutakuwa namaziwa mengi ya kutosha katika nchi yetu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Asante sana Mheshimiwa Waziri wa Mifugo naUvuvi, duuh! Haya madume 11 haya, naona madume yaKisukuma haya, yanaweza kushughulikia ng’ombe wote nchihii hatari kubwa, lakini ndio taarifa za kisayansi hizo. (Makofi/Kicheko)

Sasa tunakuja kwa Mtoa Hoja na Msaidizi wake. Kamamnavyojua tumeongea kwa siku saba mfululizo, mambo nimengi. Kwa kweli, sio rahisi kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedhakuyagusa yote, tunawashukuru Waheshimiwa Mawaziriambao wametangulia kupunguza baadhi ya mamboambayo yalikuwa yanagusa Sectoral Ministries, basi sasamoja kwa moja nimwite Mheshimiwa Naibu Waziri Fedhana Mipango, Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji, ili aanzekwa dakika 20 halafu tutamwita mtoa hoja ahitimishe hojayake.

Mheshimiwa Naibu Waziri karibu tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii. Kablasijaanza kuchangia hoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedhanaomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingiwa rehema aliyetujalia sote fursa hii ya kuwepo katika jengolako hili Tukufu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, pia baada ya kumshukuruMwenyezi Mungu, kama il ivyo kawaida, napendaniwashukuru wazazi wangu wawili, Mzee Kijaji na Mke wakeMama Aziza Abdallah, nawashukuru sana kwa malezi yaokwangu yaliyonifikisha hapa nilipo siku hii ya leo.

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru MheshimiwaRais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kazi kubwa

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

anayoifanya katika Taifa hili kwa kutekeleza Ilani ya Chamacha Mapinduzi ambayo alizunguka Taifa hili kuinadi ilani hiyo.Nampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, hakika yukomakini anatekeleza kile ambacho aliwaahidi Watanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza pia, MheshimiwaMama yetu Mama Samia Suluhu Hassan, mama wa mfanokwa Taifa la Tanzania. Amekuwa ni mama yetu wa mfano,sisi wanawake tunajivuna kuwa na mama kama yeye,aendelee kupambana sisi wanawake wenzake tuko nayesambamba kuhakikisha tunayatenda kwa ajili ya watoto wakitanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshukuru na nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa miongozo yake kwetu sisi tulio chini yake.Kwa kweli, ni kiongozi imara, ni kiongozi makini, busara zakezinatuwezesha kufika hapa tulipo siku hii ya leo.

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru wewe pia,kaka yangu, Mheshimiwa Spika Job Yustino Ndugai, kwauongozi wako imara kwa Bunge letu Tukufu na WaheshimiwaWenyeviti na watendaji wote wa Bunge letu Tukufu. Naombaniseme kwamba, najivunia na najisikia faraja kuwa ni Mbungekutoka moja ya Majimbo ya Dodoma ambako wewe ni mleziwetu, najivunia sana Mheshimiwa Spika, ahsante sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nimshukuruMheshimiwa Waziri wangu wa Fedha. Kwa mara ya kwanzaniliposimama ndani ya Bunge hili, miaka miwili iliyopita, tukiwatunawasilisha bajeti ya Serikali kama hivi, nilimwambiaMheshimiwa Waziri wa Fedha kwamba, najivunia kufanya kazichini yake. Miongozo yake, ushauri wake kwangu kwa kweli,ameweza kunifanya nisimame na kuwa ni mmoja waManaibu Waziri imara kabisa.

Mheshimiwa Spika, ulisema huwezi kujisifu mwenyewe,lakini naomba nijisifu mwenyewe na sijafika hapa ni kwa

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

sababu, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ananipa nafasiya kutenda haya ninayoyatenda. Nakushukuru sanaMheshimiwa Waziri na nakuombea kwa MwenyeziMungu azidi kukuimarisha, busara yako inatungoza sisi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia, niwapongeze sanawatendaji wote ndani ya Wizara ya Fedha na Mipangowakiongozwa na Katibu Mkuu Mheshimiwa Dotto James.Nil iwaeleza tulipoanza mchakato huu mwezi Machinikawaambia, kama ni siku basi ilikuwa alfajiri ule mwezi waMachi na leo hii tarehe 26 mwezi Juni basi ni saa 12.00 jioni.Naomba niwaambie siku yetu tumeikamilisha kwa ufanisimkubwa, Watendaji wote wa Wizara ya Fedha najisikia farajasana kufanya nanyi kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kusema na kamailivyo kawaida yangu naomba ni-site Aya mbili ndani yaKitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu, Quran na hii naombaiende kwa Mheshimiwa Rais wetu. Mheshimiwa Raisnamwambia maneno haya ya Mwenyezi Mungu kutoka SuratAl-qalam, Aya ya 7 - 8; Mwenyezi Mungu anasema katikaAya ya 7 kwamba:

“Falaatutwiil-mukadhdhibina, waddu lautudihinufayudihinuun” Mwenyezi Mungu anasema hivi, wala usiwatiiwale wanaokadhibisha yale unayoyatenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namwambia Mheshimiwa Rais,asiwatii hata kidogo wale wanaokadhibisha jitihada zakeanazozifanya kwa ajili ya wananchi wanyonge waTanzania. Dunia inaona, jamii inaona, Watanzaniawanaona, Watanzania wanasema. Pia nimwambieMheshimiwa Rais wangu kwamba, hii yote Aya ya pilinil iyosema, Mwenyezi Mungu anasema, haowanaokadhibisha wanatamani ulegeze japo kwa sekundemoja, ili waweze kutulia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namwambiaMheshimiwa Rais aendelee kupambana. Sisi tunaona,

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Watanzania wanaona na Mwenyezi Mungu akipenda 2019haya ninayoyasema yatadhihirika ndani ya Taifa laTanzania. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais endelea kuchapa kazi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sasa niseme machachekatika hoja ambazo zimewekwa mezani naWaheshimiwa Wabunge wamesema. Hoja ya kwanza nayoimekuwa ni kuhusu Serikali ya Awamu ya Tano kuelekeakuziua halmashauri zetu. Jambo hili limesemwa kwauchungu na msisitizo mkubwa na WaheshimiwaWabunge ndani ya Bunge lako Tukufu. Naomba nisemeyafuatayo:-

Mhesimiwa Spika, limesemwa jambo hili kwa kisingiziocha kwamba, Serikali ya Awamu ya Tano imechukuamakusanyo ya property tax, lakini pia makusanyo yaushuru wa mabango. Tulipitisha sheria ndani ya Bunge lakoTukufu na ndipo tulipoanza kutekeleza hil i ambalolinalalamikiwa leo.

Mheshimiwa Spika, na sheria tuliyoipitisha, Sheria yaFedha ya Mwaka 2017 ilituruhusu kukusanya mapato hayakwenye halmashauri zetu zote ndani ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania. Serikali siku zote ni sikivu na hasaSerikali hii ya Chama cha Mapinduzi, ni Serikali sikivu; ilisikilizamaoni yaliyotolewa katika ripoti ya Kamati yako Maalum,maarufu kama Chenge One. Chenge One katika taarifa ilewalisisitiza kwamba, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapatoya Tanzania ikusanye kodi ya majengo, ikusanye na kodiya mabango na Serikali iko sikivu tukaanza kuyatendahaya.

Mheshimiwa Spika, kwa nini tumefanya hivyo?Tumefanya hivyo, ili kama ilivyoshauriwa ndani yaChenge One ni kuimarisha makusanyo ya mapato hayo,ili tuweze kuyapeleka kwa Watanzania kwa Taifa zima.Nimshukuru sana na niwashukuru Waheshimiwa Mawaziriwaliosema kabla yangu, wale waliokema ile kuligawa Taifaletu.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Spika, nilisema mwaka jana wakatinachangia Bajeti ya Wizara ya Fedha kwamba, tuko kwenyehatari kubwa ya kuligawa Taifa hili vipandevipande, ule umimituuache ndugu zangu. Tunachokifanya Serikali ya Awamuya Tano ni kuyakusanya mapato haya na kuhakikishatunayarejesha kwenye halmashauri zetu kulingana na bajetiza halmashauri husika na ndicho ambacho tumekuwatukikifanya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, niwaombe sana WaheshimiwaWabunge waelewe hiyo dhamira njema ya Serikali yetu,tumekuwa tukifanya hivyo, hakuna halmashauri ambayoimekosa bajeti ya maendeleo, wala bajeti ya matumizi yakawaida katika utendaji wetu ndani ya miaka mitatu iliyopita.Katika kudhihirisha haya Serikali yetu imekuja na mpango wakuziwezesha halmashauri zetu kuweza kuja na mipangoimara, mipango mikakati kwa ajili ya kuongeza mapato yahalmashauri.

Mheshimiwa Spika, hili napenda kulisema, tuelewanejambo moja, Wakurugenzi wa Halmashauri ni watendajiwakuu wa halmashauri zetu. Hawa wanaitwa ni CEO wahalmashauri zetu zote na misingi ya mafanikio ya mtendajiyoyote wa taasisi haijawahi kubadilika kati ya sekta binafsina sekta ya umma. Ndio maana sasa Serikali imekuja nampango huu kwamba, tunataka kupima ubunifu wawatendaji wetu, ili tuweze kuwawezesha kuwapa pesa, iliwaweze kutekeleza mipango ya maendeleo, lakini yenye tijakwa wananchi wanaowaongoza. Kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge sisi ni madiwani katika halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kaka yangu Jafotulifanya kikao tarehe 14 Mei, pale Wizarani tukisaini mikatabaya shilingi bilioni 131.5 kwa ajili ya halmashauri zile zilizooneshaubunifu wa kubuni miradi ya maendeleo itakayoleta tija kwawananchi wao, itakayoleta tija kwa halmashauri zaokujiongezea kipato.

Mheshimiwa Spika, naomba niwasifu sana Wakuu waMikoa wafuatao: Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mkuu

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu waMkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mkuu waMkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Mkoawa Lindi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Mkuu wa Mkoa waKigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawasifu Wakuu hawa wa Mikoakwa sababu, wana-vision, wana ndoto ndani ya mikoayao. Wamekaa na watendaji wao baada ya sisi kutoamwongozo wa kuja na mikakati hii kwa ajili yakuongeza mapato ya halmashauri, Wakurugenzi waowakaja na maandiko mazuri ambayo yamepata fedha hizi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, juzi Jumamosi nilikuwa MkoaniSimiyu. Wengi wakanishangaa, unakwenda kuhitimisha bajetikesho kutwa, umefikaje Simiyu leo? Nikawaambia niko Simiyukwa sababu, ni utekelezaji wa bajeti tunayoipitisha.Nilikwenda Simiyu kuangalia viwanda vilivyoanzishwa ndaniya Mkoa wa Simiyu na Halmashauri za Wilaya ndani yaMkoa wa Simiyu. Nikawa namuuliza Mkurugenzi waHalmashauri ya Maswa, nikamwambia baada ya kuanzishakiwanda hiki cha chaki kwa mwaka mmoja unakusanyamapato kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, akaniambia ndio wameanza,wanakusanya zaidi ya milioni 600 kwa mwaka kwa kiwandahicho kimoja. Nikamwambia una sababu sasa wewe naBaraza lako la Madiwani la kwenda kusimama kusubirimapato ya kusubiri mtu anayetoka kujisaidia chooni kwamba,unakusanya mapato? Akaniambia hana sababu kwasababu, ana miradi ambayo inamuongezea mapato nahana sababu ya kulalamika hajapata mapato kutoka SerikaliKuu.

Mheshimiwa Spika, hili napenda lieleweke na liendekwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri zote 185 kwamba,Serikali iko tayari. Mkoa wa Simiyu peke yake mikatabatuliyosaini juzi wamepata shilingi bilioni 8.2 kwa ajili yaviwanda vidogo vidogo na ndio maana nimekuwa

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

nikisema tatizo la Serikali ya Awamu ya Tano sio pesa, tatizounataka pesa ukafanye nini. Hilo ni jambo la msingi sana,lazima tukae pamoja tuelewane kama viongozi, ili tujue ninini tunakwenda kufanya na Watanzania tunaendakuwapa nini.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hili niwaombe sanaWaheshimiwa Wabunge hili la kulalamikia mapato hayayaliyokusanywa yamekusanywa yanakwendawapi?Yamekusanywa halafu yanarejeshwa kwenyehalmashauri kulingana na bajeti.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ukiacha hiyo yakurejeshewa hiyo tumekuja na mkakati wa kuongeza mapatoya halmashauri. Kwa nini tusikae na Wakurugenzi wetutukaelekezana, wakaandaa maandiko, tukatekeleza, Serikalihaijazuia kuanzisha viwanda vidogovidogo.

Mheshimiwa Spika, naomba sisi tuwe wa kwanzakutenda maono ya Mheshimiwa Rais, tuwe sisi ni wa kwanzakutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, iliyosema 2025Tanzania itakuwa ni Tanzania ya viwanda. Mwaka 2025Tanzania itakuwa ni Tanzania ya watu wenye kipato cha kati.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hayawezekani haya kamatusipokuwa wabunifu sisi viongozi na tukawaelekezawananchi wetu, tukaainisha fursa zilizomo ndani ya maeneoyetu katika kutenda ili kuja kuiona Tanzania ya viwanda naTanzania ya uchumi wa pato la kati. Haya yanawezekana,mikoa niliyoitaja wameonesha dhamira hii kwa kuanzakutenda, wengine tuige ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili ambayo ningependakuitolea ufafanuzi, naomba niziseme hizi mbili tu, najua mudasio rafiki, ilikuwa ni Serikali ya Awamu ya Tano kuvunjaKatiba na Sheria kwa kukusanya pesa za Mifuko Maalumna kuziingiza kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali bila kuzipelekakwenye matumizi yaliyokusudiwa.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mheshimiwa Spika, naomba nirudie hili, hakunaSerikali inayoheshimu Katiba, Serikali inayoheshimu sheriazilizotungwa na Bunge lako kama Serikali ya Awamu ya Tano.Nasema haya kwa sababu tunaielewa Katiba, Ibara ya135 (1) na (2), Ibara ya 136(2), Ibara ya 143(2)(a) na (b)tunaifahamu kama Wizara ya Fedha na tunaifahamuSheria ya Bajeti iliyotungwa na Bunge lako Tukufu. Hatukotayari kuvunja Katiba yetu wala kukiuka sheriazilizotungwa.

Mheshimiwa Spika, nasema haya kwa sababukwanza mapato ya Serikali yako ya aina mbili, hayoyanayokusanywa kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali ambayoyametajwa katika Katiba 135(1) na (2), ambayo hayoyakikusanywa kutoka kwenye Revenue Collection Accountya TRA moja kwa moja huenda katika Mfuko Mkuu wa Hazinayakisubiri kupangiwa matumizi ili yapelekwe yanakotakiwa.Aina ya pili ni haya yaliyotajwa 135(2) na 136(2) ambayo nimapato yenye Mifuko Maalum, matumizi yake ni maalum.

Mheshimiwa Spika, naomba kuliambia Bunge lakoTukufu, tunailinda Katiba, tunatekeleza Sheria. Hakunamapato yoyote kutoka kwenye vyanzo maalum yanayoingiakatika Mfuko Mkuu wa Hazina. Mapato hayayakishakusanywa kutoka kwenye Petroleum Levy DepositCollection Account yanakwenda moja kwa moja kwenyemifuko husika. Naomba kusema yafuatayo kwa datazifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, Mfuko wetu wa Nishati Vijijini,mpaka kufikia tarehe 30 Mei, tulishakusanya shilingi bilioni309.209. Nini tumepeleka kwenye Mfuko wa REA? Tumepelekazaidi ya shilingi milioni 333.528 zaidi ya asilimia 108 yatulichokikusanya kwenye kipindi hiki cha miezi 11. Kwa ninizimezidi hizi asilimia nane? Zimezidi kwa sababu huwa kunalag period. Zinazokusanywa Juni, huwa zinakwenda kwenyeREA Account mwezi Julai.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndiyo maana mnaonahii 8% inayozidi. Ndiyo maana napenda kuliambia Bunge lako

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Tukufu kwamba tuko tayari, tuliapa kuilinda Katiba nakuisimamia Sheria. Hatuko tayari kuvunja Katiba wala Sheria.

Mheshimiwa Spika, huo ulikuwa ni Mfuko wa REA.Tukienda kwenye Mfuko wa Barabara, mpaka tarehe 30Mei, 2018 tumekushanya zaidi ya shilingi milioni 740,655.Nini tumepeleka kwenye Mfuko wa Road Fund?Tulichokipeleka ni shilingi milioni 783,141 zaidi ya asilimia100 imezidi 6%. Kwa hiyo, hakuna sehemu ambakofedha hizi za Mifuko Maalum zinakwenda kwenye MfukoMkuu wa Hazina, hapana. Tutalinda sheria na piatutaisimamia.

Mheshimiwa Spika, tukienda kwenye Mfuko waMaendeleo ya Reli, mpaka tarehe 30 Mei, 2018 tumekusanyashilingi milioni 203,974 na tumepeleka shilingi milioni 221,971zaidi ya asilimia 109.

(Hapa kengelei lilia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, najua ni kengele ya pili, yako mengi ya kusema, lakininataka kusema haya yanayoonesha image ya Wizara yaFedha kwamba tunavunja Katiba na Serikali yetu, nasemahapana, hatuvunji Katiba. Tuko tayari kufanya kazikwa ubunifu wa hali ya juu, kuhakikisha Taifa hililinasimama kiuchumi, tunafikisha maendeleo kule kwawananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kile nilichomwambia MheshimiwaRais wangu nil ipoanza kusema hapa, naombanimwambie Mheshimiwa Waziri wangu wa Fedha kwambaFalatutwii-l-mukadhdhibina, waddu Lautudihinu, fayudihinuun.Wala usigeuke nyuma, utageuka jiwe MheshimiwaWaziri. Chapa kazi, tuko tayari kukusaidia kufanya kazi yako.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkonohoja. (Makofi)

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

SPIKA: Ahsante sana Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt.Ashatu Kijaji kwa maneno yako mazuri na muhimu ya kutiamoyo. Tunakushukuru sana kwa jinsi unavyomsaidiaMheshimiwa Waziri wa Fedha. Sasa ni wakati wa mtoa hoja,Mheshimiwa Dkt. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha naMipango. Karibu sana sasa uhitimishe hoja yako. Karibu sana,una dakika 40. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwaRehema zake na kuniwezesha kusimama tena mbele yaBunge lako Tukufu kuhitimisha mjadala wa Hotuba ya BajetiKuu ya Mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, siku ya Alhamisi tarehe 14 Juni, 2018niliwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Hali yaUchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleowa Mwaka 2018/2019 na pia Mapendekezo ya Serikalikuhusu Makadirio Mapato na Matumizi kwa mwaka wafedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba hizo nilielezamambo mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali kwa kipindicha mwaka 2017/2018. Matokeo ya utekelezaji, changamotozilizojitokeza, mambo ya msingi ambayo Serikali inakusudiakutekeleza katika mwaka 2018/2019 na mapendekezo yabajeti.

Mheshimiwa Spika, baada ya mawasilisho hayo,Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi kwa siku saba;tarehe 18 – 22 na tarehe 25 na leo tarehe 26 Juni, 2018 yakujadili Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mujibu wa Kanuni ya106(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.Hivyo napenda kutumia fursa hii kukushukuru kwa dhati kabisawewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwakuendesha mjadala huu vizuri ambao unatarajiwakuhitimishwa leo jioni kwa kura.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea zaidi, napendakutambua michango mizuri iliyotolewa na Kamati ya Kudumu

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake MheshimiwaHawa Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Pia MakamuMwenyekiti, Jitu Soni, Mbunge wa Babati Vijijini.

Mheshimiwa Spika, nakiri kuwa Kamati hii ilihojimambo mengi na pia kutoa ushauri kuhusu hatua mbadalaau maboresho. Mimi na wenzangu katika Wizara ya Fedhana Mipango, tunaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwaKamati maana tunaamini kwamba Wajumbe wote waKamati ya Bajeti wataendelea kuongozwa na maslahi yaWatanzania walio wengi, hasa wanyonge katika kuishauriSerikali. Ahsanteni sana Kamati ya Bajeti.

Mheshimiwa Spika, aidha, nawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwakuzungumza na kwa maandishi. Jumla ya Wabunge 208wamechangia hoja nil iyowasil isha. Kati ya hao, 180wamechangia kwa kuzungumza na 28 kwa maandishi.Naomba niseme kwa niaba ya Serikali, ahsanteni sanaWaheshimiwa Wabunge kwa michango yenu mliyoitoakwenye bajeti hii kwa niaba ya wananchimnaowawakilisha.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru pia wananchi wotewaliotoa maoni na ushauri juu ya Hotuba ya Bajeti ya Serikalikupitia majukwaa mbalimbali na vyombo vya habari.Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inathamini sanamichango hiyo, nami na wataalam wa Wizara ya Fedha naMipango na taasisi zilizo chini yake tumeyapokea natumejipanga kuyafanyika kazi mambo yote waliyotushaurikwa maslahi ya Tanzania. Baadhi tutayazingatia katika bajetihii na mengine katika bajeti zijazo.

Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kabisa,tumeyapokea pia mawazo ya Wabunge kutoka Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni. Hata hivyo, napenda nisisitize kuwatumepokea yale tu yanayoendana na Dira ya Maendeleo yaTanzania 2025 (The Tanzania Development Version 2025),Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliopitishwana Bunge lako Tukufu na Ilani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

Mkuu wa Mwaka 2015 ambayo imebeba ahadi za ChamaTawala kilichochaguliwa na wananchi na kukipa ridhaa yakuongoza nchi.

Mheshimiwa Spika, nyaraka nil izozitaja ndiyochimbuko la ajenda za Serikali ya Awamu ya Tanoinayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wetu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.Kamwe hatutasita kumsifia Rais wetu kwa kazi nzuriiliyotukuka anayowafanyia Watanzania wote. Hatuko tayarikuyumbishwa na agenda za kuandikwa. Sisi tunaandikawenyewe na tunatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Tanzania wanayomacho na hawalazimiki kuambiwa tazama. Wale wa BukobaMjini wanaona Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyojengwa upyabaada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi. Wananchi waMwanza wanafurahia daraja la waenda kwa miguu laFurahisha na kivuko kipya katika Ziwa Victoria. Wakazi waJiji la Arusha wanaona barabara mpya kutoka Arusha mpakaTengeru ilivyopendezesha Jiji lao. Wananchi wenzangu waKigoma wanaona barabara ya Kidahwe hadi Kasulu imeanzakuwekwa lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Dar es Salaamwanaona barabara za juu katika makutano ya TAZARAikielekea kukamilika na bandari ikipanuliwa na kuongezewakina. Wanaifakara sasa wanavuka mto Kilombero kupitiaDaraja la Magufuli kwa usalama. Wananchi wa Mtwarawanaona uwekezaji mkubwa wa upanuzi wa Bandari yaMtwara.

Mheshimiwa Spika, vilevile, wananchi wa Masasisasa wataondokana na adha ya ukosefu wa maji,kufuatia ukarabati wa miundombinu ya kusambaza majina ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji Chiwambo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakazi wa Jij i la Dodomawameikaribisha Serikali na sasa tuko hapa. Wananchi wa

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Tanga wanashuhudia kuanza kazi ya ujenzi wa bomba lamafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga.Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka nchi nzima.Watoto wetu kote nchini wanafaidi elimu bila ada nakadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa yote hayo na mengine mengi,kwa nini tusiisifie Serikali ya CCM na Jemedari wetu Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nirejee kwa muhtasarimapendekezo yaliyoungwa Mkondo na wachangiaji wengi.Kwanza, kufuta kodi ongezeko la dhamani kwa taulo za kike;pili, kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya makampunikutoka asilimia 30 hadi asilimia 20 kwa wawekezaji wapyawa viwanda vya madawa ya binadamu na viwandavinavyotengeneza bidhaa za ngozi; na kulinda wawekezajiwa ndani kwa kuongeza ushuru kwenye bidhaa zinazotokanje ya nchi ambazo zinaweza kuzalishwa na viwanda vyandani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nne, ni kusamehe VAT kwenyevifungasho vya madawa ya binadamu vinavyotengenezwamahususi kwa ajili ya viwanda vinavyozalisha dawa hapanchini; na tano, kusamehe VAT kwenye virutubishovinavyotumika kutengeneza vyakula vya mifugo kwa lengola kupunguza gharama kwa wafugaji na kuhamasisha ufugajibora.

Mheshimiwa Spika, sita, ni kuanzisha utaratibumaalum wa kusamehe kodi ambao unalenga kusamehemalimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu kwa kiwango chaasilimia 100 na pia kuweka msisitizo katika utekelezaji wamiradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli kwakiwango cha standard gauge, mradi wa kufua umeme Rufiji,mradi wa makaa ya mawe na chuma, Liganga naMchuchuma.

Mheshimiwa Spika, pia mradi wa kusindika gesi asiliakuwa kimiminika kule Lindi. Pia kuna shamba la miwa na

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

shamba la sukari Mkulazi na uendelezaji wa maeneo maalumya uwekezaji. Hatua zote hizi zililenga kuhamasisha ujenzi waviwanda hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia niseme kwa kifupihoja na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza tulishauriwa kuongezatozo ya Sh.50/= kwa lita ya dizeli na petrol lakini pia zilitolewahoja kuhusu pendekezo la Serikali la kuanzisha mfumo wastamp za kodi za kielektroniki kwamba itekelezwe kwauangalifu. Pia tulishauriwa kwamba Serikali itoe mara mojabakaa ya fedha za ushuru wa korosho zinazosafirishwa njeya nchi kwa Bodi ya Korosho; nne, kwamba kwenyekuanzishwa kwa akaunti jumuishi ya Hazina tuelezwakwamba hatua hii ni kinyume cha Katiba ya nchi na vilitajwavifungu; tano, kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwakuzingatia umuhimu wa sekta hii.

Mheshimiwa Spika, pia kulikuwa na hoja kuhusuuhalisia wa bajeti ya Serikali, umuhimu wa kuboreshamazingira ya uwekezaji na kufanya biashara nchini. Vile vileilitolewa hoja kwamba kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi siyohalisia.

Mheshimiwa Spika, ilielezwa kwamba ni muhimukuboresha mifumo ya ulipaji kodi na kuheshimu sheriazinazosimamia masuala ya ukusanyaji wa kodi, lakini piailielezwa kwamba mwenendo wa Sekta ya Fedha hauridhishi;lakini pia kwamba vyanzo vikuu vya mapato ya Halmashaurivinachukuliwa na Serikali Kuu bila kuvirejesha. Lingine nikwamba Serikali sasa ichukue hatua za madhubuti zaidikulipa madai mbalimbali na kwamba deni pia la Taifa linakuakwa kasi mno na hivyo lidhibitiwe.

Mheshimiwa Spika, mawazo mengine ni pendekezola kufuta sheria iliyoanzisha Tume ya Mipango kwamba siyojambo jema kwa maendeleo ya nchi. Pia kulikuwa namasuala mbalimbali yanayohusu mahusiano ya kiuchumi na

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

kibiashara kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikalina Muungano wa Tanzania; na vile vile tulishauria kwambaSerikali iangalie tena baadhi ya hatua mpya za mapato kwamwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kama ulivyosema mwenyewe, niwazi kabisa kuwa hoja na michango mbalimbali iliyotolewakwa siku saba na Waheshimiwa Wabunge haiwezikufafanuliwa kwa muda wa hizi dakika 40. Hivyo kama ilivyoada, napenda kuliahidi Bunge lako Tukufu kuwa Wizara yanguitatoa ufafanuzi wa kina wa hoja zote na kuziwasilisha kwamaandishi kupitia kwa Katibu wa Bunge kwa ajili ya rejea yaWaheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hiikuwashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawazirina Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kufafanuavizuri baadhi ya hoja zinazohusu sekta wanazozisimamia.

Mheshimiwa Spika, wakati wote wa mjadala humuBungeni kuhusu mapendekezo ya Serikali ya Makadirio naMapato ya Matumizi kwa mwaka ujao wa fedha, Serikalii l is iki l iza kwa makini maoni na ushauri kutoka kwaWaheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Serikali sikivu ya CCM ilipokea na kufanyiakazi ushauri wa kizalendo kutoka kwa WaheshimiwaWabunge na wadau mbalimbali na sasa napendakuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu mapendekezo yakufanya marekebisho ya baadhi ya kodi na tozo kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni Sheria ya Michezo yaKubahatisha Sura ya 41. Napendekeza kuwianisha viwangona msingi wa ukokotoaji wa kodi ya Michezo ya Kubahatishahasa inayoshabihiana. Kwanza, kubashiri matokeo (SportBetting for land based and on line). Pili, ni sehemu ya mashine40 (forty machine sites); ya tatu ni Bahati Nasibu ya SMS Lotteryna Casino za mtandao (internet casino).

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mheshimiwa Spika, kiwango cha kodikinachopendekezwa katika michezo hii inayoshabihiana niasilimia 25 ya mauzo halisi (Gross Gaming Revenue - GGRA)badala ya viwango na wigo uliopo sasa. Pili, kwa michezoya Bahati Nasibu ya Taifa (National Lottery) napendekezakutoza kodi kwa kiwango cha asilimia 20 kwa mauzo halisi(GGR) badala ya asilimia 10 ya mauzo ghafi (Gross Sales)inatozwa sasa.

Tatu, ni kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadiya ushindi (Gaming Tax on Wining) kutoka asilimia 18 hadiasilimia 20 kwenye Bahati Nasibu ya SMS Lottery. Michezo yakubashiri matokeo Sports Betting, Slot Machine Operations,Bahati Nasibu ya Taifa, sehemu ya mashine 40 na casino yamtandaoni (internet/online casino). Nne, kupunguza kiwangocha kodi, kwenye zawadi ya ushindi yaani Tax on Winningskwa michezo ya Casino ya ardhini (Land Based Casino) kutokaasilimi 18 hadi asilimia 12 au chini.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo hayo yamarekebisho ya Sheria ya Kodi ya Michezo ya Kubahatisha,yanatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi chashilingi bilioni 29.7.

Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanyamarekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,Sura 148 ili kwanza kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko lathamani kwenye mashudu yanayotumika kutengenezachakula cha mifugo kama ifuatavyo:-

(a) Mashudu ya Soya HS Code 2304.00.00;

(b) Mashudu ya Pamba HS Code 2306.10.00; na

(c) Mashudu ya Alizeti HS Code 2306.30.00.

Mheshimiwa Spika, lengo la marekebisho haya ni kwakuwawezesha wafugaji kupata chakula cha mifugo kwa beinafuu zaidi na hivyo kuhamasisha ufugaji bora na kuongezamchango wa Sekta ya Ufugaji katika pato la Taifa.

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

Mheshimiwa Spika, lakini pili, ni vifaa vya kukusanyiakodi taxi instruments ambazo ni stamp za kodi za kielektronikiHS Code 4907.00.90 na pili, ni mashine za kielektroniki zakutolea risiti (Electronic Fiscal Devices) HS Code 8470.50.00.

Mheshimiwa Spika, lengo la mapendekezo haya nikutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, kwenyestamp za kodi za kieletroniki na mashine za kielektroniki zakutolea risiti ili kuwapatia unafuu wazalishaji wa bidhaazinazobandikwa stamp za kodi za kielektroniki pamoja nakutoa hamasa juu ya matumizi ya mashine za kielektronikiza kutolea risiti. Hatua hizi pia zinatarajiwa pia kuimarishausimamizi na udhibiti wa mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo haya ya Sheria zaKodi za Ongezeko la Thamani yatapunguza mapato yaSerikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.6.

Mheshimiwa Spika, marekebisho ya Sheria ya Michezoya Kubahatisha pamoja na Sheria ya Kodi ya Ongezeko laThamani kwa ujumla wake yataongeza mapato ya Serikalikwa shilingi bilioni 639.0 hadi shilingi bilioni 646 sawa naongezeko la shilingi bilioni saba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewengi walichangia hoja kuhusu marekebisho katika Sheriaya Tozo ya Huduma ya Bandari, Sura 264 kwa kurekebishakifungu cha (3) kinachohusu kuongeza tozo za huduma zabandari kutoka Sh.500/= hadi Sh1,000/= kwa wasafiri ambaoni wakazi nchini na kutoka Dola za Marekani tano (5) hadi 10kwa wasafiri ambao ni wageni nchini na kuomba kuwamsamaha uendelee kutolewa. Serikali imewasikia namsamaha huo utaendelea kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabungewalizungumzia pia marekebisho katika Sheria ya VAT aya ya22, sehemu ya kwanza ya jedwali, kwa kufuta msahama wakodi ya ongezeko la thamani kwa ndege ndogo zakukodisha na kuiomba Serikali iendelee kutoa msamaha huo.Nichukue fursa hii kulieleza Bunge lako Tukufu kwamba Serikali

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

ya CCM imefanyia kazi hili na sasa msamaha huo utaendeleakutolewa kama kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 75 wa hotubayangu nilipendekeza kufuta leseni ya kukidhi matakwa yaSheria ya Afya na Usalama. Napenda kufanya marekebishoeneo hilo lisomeke, “kufuta ada ya leseni ya kukidhi matakwaya Sheria ya Afya na Usalama.”

Mheshimiwa Spika, nirudie tena kusema, Chama chaMapinduzi kimeielekeza Serikali yake kuwa sikivu namaboresho nil iyoyaeleza yanathibitisha hilo. Aidha,tutaendelea kufanyia kazi mapendekezo yote na ushauriuliotolewa na Waheshimiwa Wabunge na wananchi wenginekwa maslahi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niende kwenye baadhi yahoja na ushauri uliotolewa na Wabunge wengi. Kwanzakulikuwa na hoja kwamba Serikali iongeze tozo ya Sh.50 kwalita ya mafuta ya petrol na desel kwa ajili ya Mfuko wa Maji ilikuwe na chanzo kinachotabirika (ring fence).

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uwepo wachangamoto ya upatikanaji wa maji katika sehemumbalimbali nchini, mij ini na vij i j ini. Katika kutatuachangamoto hii Serikali imekuwa ikitenga fedha kwenyebajeti kwa ajili ya miradi ya maji. Aidha, baadhi ya miradiiligharamiwa moja kwa moja na wadau wa maendeleo wanje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi hizi za Serikalina wadau wa maendeleo, bado maeneo mengi mijini navijijini yanakabiliwa na uhaba wa maji. Kutokana na hali hii,Waheshimiwa Wabunge walipendekeza kuongeza tozo yaSh.50/= kwa kila lita moja ya mafuta ya petrol na dieselkwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, Serikali imechambua kwa kinapendekezo hili. Pendekezo hili ni zuri lakini wakati huu siomuafaka kwa sababu zifuatazo:-

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Mheshimiwa Spika, kwanza, tumetazama mwenendowa matarajio bei ya mafuta kwenye Soko la Dunia natunaona wazi kabisa kwamba kwa takwimu tulizonazomwenendo wa bei ya mafuta ulimwenguni inakwenda juu,kwa hiyo, huu siyo wakati muafaka. Tutatoa takwimu kupitiakwenye Ofisi ya Katibu wa Bunge, kuonesha uchambuziambao tumefanya.

Mheshimiwa Spika, kutokana na Ripoti ya Hali yaUchumi wa Dunia (World Economic Outlook ya IMF)iliyotolewa mwezi Aprili, bei ya mafuta ghafi inatarajiwakuongezeka hadi kufikia kati ya wastani wa Dola 60 hadi 70kwa pipa, ikilinganishwa na matarajio ya awali ya Dola zaMarekani 50 mpaka 60 kwa pipa kwa mwaka 2018.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019, bei ya mafutaghafi inatarajiwa kufikia wastani wa Dola 65.5 kwa pipa naongezeko hilo linachangiwa na makubaliano ya kupunguzauzalishaji wa mafuta kwa wanachama wa OPEC na baadhiya wazalishaji wasio wanachama wa OPEC na hali hiiinaweza kusababisha ongezeko la kasi ya mfumuko wa bei,nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kodi na tozo zilizopo kwenyemafuta kwa sasa ni nyingi sana; na bidhaa za mafuta yapetrol na diesel zina kodi nyingi. Pendekezo lililotolewa naWaheshimiwa Wabunge kama lingekubaliwa, ingekuwa nimzigo mkubwa sana. Kwanza kuna tozo na kodi kwa ajili yamamlaka mbalimbali za umma, hizo ziko 11; ziko kodi zaSerikali Kuu tatu, ziko kodi na tozo za mauzo ya jumla yamafuta, ziko mbili; kuna tozo na kodi kwa mauzo ya rejarejaya mafuta, ziko tatu.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kodi na tozo hizi,ni wazi kabisa kwamba bidhaa za mafuta ya petrol na dieselzimebebeshwa mzigo mkubwa sana katika kuchangiamaendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, baada ya kufanyatathmini, tumeona kwamba tozo hii ingeongeza bei ya

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

mafuta nchini na kusababisha kupanda kwa pump pricesya mafuta ya diesel na petrol. Tunayo mifano ambayotumechambua kwa Dar es Salaam, kiasi gani ambachobei ya mafuta ingeongezeka. Vile vile ingeleta atharikwenye utulivu wa uchumi kwa ujumla (macroeconomicstability) na kusababisha bei za bidhaa na hudumaambazo zinazalishwa hapa nchini kuongezeka (second roundeffect).

Mheshimiwa Spika, wakati wa Hotuba ya Wizara yaMaji na Umwagiliaji, zilielezwa njia mbadala za Serikali katikakugharamia Miradi ya Maji Nchini. Kwa hiyo, nisingependakuzirejea, itoshe tu kusema kwamba tumetenga shilingi bilioni673.2 kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha kugharamia miradiya maji mijini ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, ahadi ya Serikali ni kwamba tunadhamira ya dhati ya kupeleka fedha kwenye utekelezaji wamiradi ya maji kama ilivyopitishwa na Bunge lako Tukufu kwaajili ya mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile tumepokea fedha katikamwaka uliokwisha. Tumeshasaini mkataba na Benki ya Eximya India, Mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili yautekekelezaji wa miradi ya maji katika Miji 21, Tanzania Barana Zanzibar. Pia tumeshakamilisha majadiliano na Benki yaDunia ambapo Dola za Marekani milioni 350 zinatarajiwakupatikana na kati ya kiasi hicho Dola za Marekani 60 sawana asilimia 17 kitatolewa mwezi Julai, 2018.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja juu ya pendekezola Serikali la kuanzisha mfumo wa stamp za kodi zakielektroniki. Serikali ilishauriwa itengeneze yenyewe mfumowa ETS ili kiasi cha fedha ambacho kitalipwa kampuni yaCIPA iwe ni sehemu ya mapato ya Serikali, badala yamapato yatokanayo na stamp ya kuchukuliwa na KampuniBinafsi.

Mheshimiwa Spika, tumelichambua sana hili, nisemetu kwamba teknolojia ya kutengeneza mfumo huu ni mpya

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

hapa nchini na hivyo hapakuwa na kampuni au taasisi yaSerikali iliyokuwa na uwezo wa kutengeneza mfumo huo.Kutokana na hilo, ililazimu Serikali itangaze Zabuni yaKimataifa kwa uwazi na ndipo tulipompata Mzabuni mwenyeuwezo na uzoefu wa kutengeneza mfumo huu kati yaMakampuni tisa yaliyojitokeza na hapakuwepo Kampuni yandani iliyojitokeza.

Mheshimiwa Spika, pia uwekezaji wa mradi huu nizaidi ya mwaka mmoja na hivyo gharama za mradizimezingatia muda huo ili kufidia gharama ya uwekezaji.Mapato yatokanayo na stamp za kodi kwa mudawa mwaka mmoja hayawezi kulingana na gharama zauwekezaji wa mradi huo katika mwaka wa kwanza.

Mheshimiwa Spika, vilevile mfumo huoutakapokamilika kujengwa, utaanza kuunganishwakwenye viwanda vya uzalishaji kwa awamu kulinganana uhatarishi wa upotevu wa mapato katika bidhaahusika.

Mheshimiwa Spika, napenda niseme tu kwambamfumo huu una faida nyingi sana ambazo zinazidi hizogharama ambazo ilikuwa ni wasiwasi wa WaheshimiwaWabunge.

Mheshimiwa Spika, niseme kuhusu ushuru wa koroshozinazosafirishwa nje ya nchi na matumizi yake. MheshimiwaMwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Kil imowalifafanua jambo hili kwa ufasaha jana na nisingependakurudia. Ni vyema niseme na Watanzania wasikie na ikaekwenye Kumbukumbu Rasmi za Bunge lako Tukufu. MimiPhillip Mpango siwezi kamwe kuwahujumu wananchi,wakulima wa korosho wa Mikoa ya Mtwara na Lindi au mkoamwingine wo wote ule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwahikikishie Watanzania kuwaMtwara na Lindi nitakwenda, iwe katika kutelekezamajukumu yangu ya kikazi au kuwatembelea ndugu namarafiki. Hakuna anayeweza kunizuia, ni haki yangu na uhuru

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

wangu kama Mtanzania ambayo haiwezi kupokonywakwa vitisho. Hata ikibidi kufa katika kutumikia Taifa na iwe.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika nafasi mbalimbalinilizotumikia Serikali ya CCM na Taifa hili kwa ujumla,nimetumia uwezo wangu wote kuwatumikia Watanzaniawa mikoa yote, nimefundisha wanafunzi wakiwa nipamoja na wanaotoka Mikoa ya Kusini, nilipokuwaMhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Dar es Salaam bilaupendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, kati ya mambo niliyofanyanikiwa Mshauri wa Rais, Uchumi katika Serikali ya Awamu yaNne na nilipokuwa Mkuu wa Tume ya Mipango, nilikuwamstari wa mbele kuishawishi Serikali kuifanya Mtwara iwekitovu cha ukuaji wa uchumi hapa nchini (Mtwara GrowthPole) na kuingiza miradi mikubwa ya maendeleo, kwa mfanoupanuzi wa Bandari ya Mtwara, LNG Plant Lindi, Barabara zauchumi na kadhalika katika Mpango wa Maendeleo wa Taifawa Miaka Mitano.

Mheshiomiwa Spika, mimi na wenzangu tuliishauriSerikali kutenga nafasi za upendeleo kwa vijana kutoka Mikoaya Kusini kusoma masomo ya sayansi ili baadaye wawezekufanya kazi katika viwanda vinavyohusiana na Sekta ya GesiAsilia; niliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania inayotaka pamoja na mambomengine kuhakikisha maendeleo ya Uchumi wa Taifayanakuzwa na kupangwa kwa uangalifu na kwa pamojaambayo iko kwenye Ibara ya 9 (d). Iweje leo niwahujumuwananchi wa Mtwara na Lindi?

Mheshimiwa Spika, kama yupo mtu ana chuki binafsina Phil l ip Mpango, pasipo chembe ya ukweli, miminamwombea msamaha kwa Mungu. Nasema tena,sitayumba katika kusimamia matumizi bora ya fedhaza umma kwa mujibu wa sheria. Nawakumbushawabadhirifu wa fedha za umma, wajue wanakula sumu.(Makofi)

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Mheshimiwa Spika, najua muda siyo rafiki, nilitarajianingesema sana leo, lakini naomba niseme jambo mojakabla sijaenda kwenye kuhitimisha. Kulikuwa na hoja kuhusumapendekezo ya Serikali ya kufuta sheria iliyoanzisha Tumeya Mipango.

Mheshimiwa Spika, nil ieleza katika hotubaniliyowasilisha tarehe 14 Juni, kwamba mapendekezo hayoni mabadiliko ya kimuundo na siyo kufuta kazi muhimu zakupanga mipango ya maendeleo ya Taifa letu kwa kipindicha muda wa kati na muda mrefu. Ukifuatilia historia yamuundo ya Taasisi ya Tume ya Mipango, iko wazi kuwaimekuwa inahama, kwa nyakati tofauti toka tulipopataUhuru, Taasisi hiyo kuna kipindi ilikuwa peke yake kama Wizarakamili au Tume na wakati mwingine ikawa sehemu ya Wizaraya Fedha.

Mheshimiwa Spika, tena jambo hili siyo kwa Tanzaniapekee, hata katika nchi jirani za Uganda na Rwanda hivisasa, fedha na mipango vinaunda Wizara moja (Ministry ofFinance and Economical Planning). Lengo kuu ni kuwianishaMipango ya Maendeleo ya Taifa na ugawaji wa rasilimalifedha, jambo ambalo ni gumu pale ambapo Taasisi hizizinapokuwa zimetenganishwa.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza, kazi yakuandaa na kusimamia mipango ya maendeleo yaTaifa ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango,itaongozwa na Kamishna atakayekuwa na fungu lakekuwezesha utekelezaji wa kazi za idara hiyo. Kazi hizozimeendelea kufanyika vizuri baada ya kuhamishawataalam wa iliyokuwa Tume ya Mipango ndani ya Wizaraya Fedha.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha. Kamanilivyoeleza katika hotuba yangu, hatua zilizopendekezwakwenye Bajeti hii zinalenga kujenga msingi madhubuti wauchumi wa viwanda na kupanua fursa za ajira na biashara.Dhamira yetu sote ni kufikia kiwango cha uchumi wa kipatocha kati itakapofika mwaka 2025. Ili kushiriki katika mafanikio

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

hayo, ni lazima kila mmoja wetu ashiriki katika shughuli halaliza kuzalisha na afanye hivyo kwa juhudi na maarifa ili kuletatija.

Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa Bajeti hii kunahitajinidhamu ya hali ya juu katika usimamizi wa mapato namatumizi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alituusia,nitasema kwa Kiingereza; mwanzo wa kunukuu: “our watchword must be frugality, this must run through the wholeexpenditure.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, hii inatoka kitabu cha Freedomand Socialism. Ili kufikia azma hii, juhudi za pamoja katiya Serikali na wadau wote zinahitajika ikiwa ni pamojana kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika uchumikwa kuwekeza zaidi katika maeneo ya kipaumbele.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, najua Watanzania tuna kiu kubwaya kuendelea, tena haraka, lakini tukumbuke kuwa kilasafari inaanza na hatua moja ikifuatiwa na nyingine.Vile vile njia ya maendeleo ina vikwazo vingi na haiwezekanikutatua changamoto zote za nchi hii kwa mara moja.

Mheshimiwa Spika, hata nchi zilizoendelea kamaMarekani na Uingereza na kadhalika bado wanazochangamoto, bado nao wanajenga barabara, reli, hospitalina kadhalika. Hivyo ni muhimu Watanzania tuendeleekufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kudumisha amani naumoja wa Taifa letu. Changamoto zitaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nawashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge wote, mjadala wetu wa siku sabaumeyatendea haki mapendekezo ya Bajeti niliyowasilishatarehe 14 Juni, 2017. Kukosoa kwa haki i l i kujenga(constructive criticism) na kujikosoa ni sehemu muhimu sanakatika harakati za maendeleo ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa jambo kubwa la Kitaifa kamahili la Bajeti ya Serikali, ningestaajabu sana kama kila Mbunge

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

angesimama na kusifia tu mapendekezo niliyowasilisha.Ndiyo maana mwanzo kabisa mwa Hotuba ya Bajeti Kuunil ibainisha kwa makusudi changamoto kubwazinazotukabili kama Taifa na kwa ukweli, ili tujielekeze kwapamoja katika kuzitatua.

Mheshimiwa Spika, imani yangu ni kuwa lazima tuwewa kweli sisi wenyewe na kwa Taifa letu, lakini ni muhimupia tuishi katika dunia, tusiishi katika dunia ya kufikirika. KwaKiingereza, we have to be honest ourselves, honest to ourcountry and be as pragmatic as possible. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatukuandaa bajeti hiikujifurahisha. Tumekuwa wakweli katika kutathmini utekelezajiwa Bajeti 2017/2018, tuliyoifanya. Katika mapendekezotuliyoleta hapa Bungeni juu ya hatua ambazo tunaamini kwadhati zitatupeleka mbele kama Taifa. Ukweli ni kwamba nirahisi sana kusema, rahisi sana kwa rafiki zangu wa upandewa pili kukosoa, lakini nao wanajua kuwa ni vigumu kutenda,ndiyo maana hata walichokisema ni Bajeti Mbadalawaliandikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalize kwa kumshukurutena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake. Namshukuru sanaNaibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.Ashatu Kijaji, wewe mama ni mahiri kweli kweli, umekuwa nimsaada mkubwa sana. Namshukuru sana Katibu Mkuu naWataalam wote wa Wizara ya Fedha kwa kuendelea kufanyakazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, nawaomba sanaWaheshimiwa Wabunge wote kuunga mkono Bajeti hii yaSerikali kwa mwaka 2018/2019 ikiwa ni hatua nyingine thabitiya Kujenga Uchumi wa Viwanda Nchini Tanzania nakuboresha maisha ya wananchi wetu. Natanguliza ahsantekwa kura yenu ya ‘Ndiyooo!’

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naafiki.

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono. Ahsantesana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango. Ahsantesana Mheshimiwa, tunakushukuru sana kwa kuhitimisha hojayako.

Waheshimiwa Wabunge, kama alivyosemaMheshimiwa Waziri, haikuwa rahisi kwake kugusa kila hojaambayo ilizungumzwa huku ndani kwa dakika ambazotulikuwa tumempa. Ametuahidi kwamba watapitia hotubazetu na watatengeneza majibu ambayo yatapita hapaMezani na tutapeana majibu hayo katika utaratibu wetu wakawaida kwa wakati muafaka kupitia pigeon holes zetu.

Tunakushukuru tena Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpangona Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji kwa majibuyenu kwetu ambayo kwa kweli yanatia moyo kwa kiwangokikubwa. (Makofi)

Moja ya mambo ambayo ameyasema hapa ni kufutakodi kwenye mashudu. Najua au nahisi kuwa ziko baadhi yaHalmashauri nazo zina vikodi kodi huko, sasa ni vizuri nazohuko mbele zikajiangalia ili ziendane na sprit hii ya Serikali. Nimpango ambao unaenda kuboresha sana habari ya ufugajiwa mifugo na kukuza masuala ya ufugaji bora katika nchiyetu. (Makofi)

Nina matangazo mawili madogo. La kwanza kamanilivyosema kabla, Wajumbe wa Kamati ya Bajeti mtaendakatika ukumbi wenu wa kawaida ili muweze kupitia lilependekezo la Muswada wa Sheria ya Fedha. MheshimiwaWaziri na Naibu na Wataalamu wao wataelekea huko maratukitoka hapa.

La pili, ni kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Hudumaza Jamii, Mheshimiwa Peter Serukamba, anawaombaWajumbe wote wa Kamati hiyo mkutane kwenye ukumbiambao kwa kawaida huwa mnakutana, mara tu baada yamambo haya ili muweze kukutana na ndugu zetu wa TCRA,

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

kuna mambo ya kuelimishana na ni muhimu sana kufanyahivyo leo. (Makofi)

Narudia tena Kamati ya Huduma, ambayoMwenyekiti wake ni Mheshimiwa Peter Serukamba,anawaomba Wajumbe wote mkutane katika ukumbi wenuwa kawaida, mkutane na TCRA.

Mwisho, Waheshimiwa Wabunge, tukutane tena saa11.00 kwa kazi kubwa maalum na sisi tutakuwatumeshaandaa mambo yetu hapa. Naomba tuwahi, kwasababu mara tu mkifika, zoezi lile muhimu litaanza ili tuwezekufanya maamuzi kuhusiana na shughuli nzima hii tuliyoianzamwezi Aprili yote, Mei yote na Juni karibu yote. Kwa maanahiyo,tutakuwa tumetekeleza wajibu wetu kamaWaheshimiwaWabunge, tukifanya hivyo.

Baada ya hapo basi, niseme tu kwamba naahirishashughuli za Bunge hadi saa 11.00 juu ya alama. Ahsante sana.

(Saa 11.00 Mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Aah, leo full House! Waheshimiwa Wabunge,tukae. (Kicheko)

Ngoja tutoe nafasi ya Waheshimiwa Wabungewanaoingia waweze kuingia, halafu tuelezane mamboyanayohusu taratibu.

Sasa namwomba Sergeant-at-Arms, igongwe kengeleili kuwahimiza Waheshimiwa Wabunge ambao wakosehemu nyingine za jengo hili au walioko njiani wawezekujiunga nasi ili tuweze kuanza zoezi lililo mbele yetu. Kwahiyo, naomba kengele igongwe kufuatana na kanuniinavyotaka.

(Hapa kengele iligongwa ili kuruhusu WaheshimiwaWabunge kuingia ndani ya ukumbi)

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Kwa kweli mahudhurio ya leo ni mazuri. Naona hataMheshimiwa Silinde naye amerudi, maana yake alikuwahaonekani. Sasa kesho tuna Muswada wa Fedha, usijeukasema tena maoni yako hayajaingizwa kwenye OrderPaper na lawama nyingi. Kama wameshakuandikia, basituletee mapema ili… (Kicheko/Makofi)

Bunge hili ni zuri kweli, ndiyo maana mtu akitokaBungeni ana-miss. Lina mambo yake na vionjo vyake.(Kicheko)

Basi Waheshimiwa Wabunge, natumaini tunawezatukaanza sasa. Nawaomba sana katika zoezi linalokuja,basi wale wanaotembea tembea, au wale wanaokaamaeneo sio yao, hebu tupunguze hilo ili zoezi letu liwezekwenda vizuri. Naona wenzetu wengine bado wanazidikuingia, karibuni sana. Naona bado kuna haja yakuvuta muda kidogo. Nadhani tunaweza tukaendeleasasa.

Waheshimiwa Wabunge, nina maelezo mafupi kwenuna naomba tusikilizane kidogo ili twende pamoja. Kwakuwa tumehitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa2018/2019 na Mtoa hoja akaja kuhitimisha hoja yakehapa, tunatakiwa sasa katika hatua hii kufanyamaamuzi kwa kuyapitisha au kutokuyapitisha makadiriohayo.

Kanuni ya 107(2) inaeleza kuhusu utaratibu wakuidhinisha Makadirio ya Matumizi ya Serikali na inasomekakama ifuatavyo:

“Uamuzi wa Bunge wa kupitisha au kutokupitishaBajeti ya Serikali utafanywa kwa kupiga kura ya wazi, kwakutaja jina la Mbunge mmoja mmoja.”

Ibara ya 94(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Kanuni ya 77(1) ya Kanuni za Bunge, pamoja namambo mengine zinaelekeza kwamba Akidi ya Kikao cha

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Bunge wakati wa kufanya maamuzi ni nusu ya Wabungewote.

Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa idadi yaWabunge wote ni 393, ukiondoa mwenzetu mmoja kamamnavyokumbuka, kwa hiyo, sasa hivi idadi ya Wabunge woteni 392. Hivyo, kabla ya kuanza zoezi la kupiga kura,tunatakiwa kuwa na Wabunge wasiopungua 196 humundani.

Katibu wa Bunge atatumia utaratibu unaofaakutuhakikishia kama tunazidi idadi ya 196. Katibu atafanyahivyo kwa utaratibu wa kuhesabu au atakavyoona inafaa,lakini mwisho atatujulisha.

Kanuni ya 79(1) inafafanua kuwa, mambo yoteyanayohitaji kuamuliwa na Bunge, yataamuliwa kwa kufuatamaoni ya Wabunge walio wengi, waliohudhuria na kupigakura Bungeni. Hivyo katika zoezi letu la leo tutafuata utaratibuufuatao:-

Kwanza, kengele itapigwa kama nilivyoelekeza iliWaheshimiwa Wabunge walio nje ya ukumbi waingie ndani.Pili, Katibu atawahesabu Wabunge wote ili kuona kamaakidi inatimia, kwa maana ya kwamba tunafikia na kuzidi196.

Tatu, zoezi la kupiga kura litaanza ambapo Katibuatasoma majina ya Wabunge mmoja baada ya mwinginena kila anayeitwa, atatoa uamuzi wake kwa kusema ‘Ndiyo’au ‘Hapana.’

Waheshimiwa Wabunge, baada ya hapo, tutapatiwamatokeo ya kura kuhusiana na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa2018/2019.

Waheshimiwa Wabunge, sasa namkaribisha Katibuwa Bunge ili atupatie idadi yetu tuweze kuendelea na zoezihili baada ya hapo. Katibu.

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

NDG. STEVEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:Mheshimiwa Spika, idadi kamili ya Wabunge waliopo ndaniya Ukumbi wa Bunge kwa sasa ni 303 na inawezekanaikaongezeka kwa kuwa baadhi ya Wabunge badowanaendelea kuingia.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa idadi hiyo inatoshakuendelea na zoezi la kupiga kura, naomba uridhie tuendeleena hatua inayofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa orodhailiyoandaliwa kwa madhumuni ya kupiga kura hii yaBajeti, tutaanza kuita majina ya viongozi waliomohumu ndani, Mawaziri, Wenyeviti wa Kamati zaKudumu za Bunge na kufuatiwa na Wabunge wenginewote.

Mheshimiwa Spika, tunaomba kila Mbunge anayeitwaasiwe na maneno mengine zaidi ya kujibu ‘Ndiyo’ au‘Hapana’ kwa sababu hizo ndizo tu zinazotakiwakurekodiwa.

Mheshimiwa Spika, sasa tutaanza kuita majina kamaifuatavyo:-

SPIKA: Mpaka hapo kabla ya Katibu hajaanza, kunaneno? Hakuna.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tunaanza shughuli.Katibu sasa anza.

NDG. NENELWA WANKANGA - KATIBU MEZANI:

Mhe. Dkt. Tulia Ackson - NdiyoMhe. Kassim Majaliwa Majaliwa - NdiyoMhe. Freeman Aikaeli Mbowe - HakuwepoMhe. Mussa Azzan Zungu - NdiyoMhe. Andrew John Chenge - NdiyoMhe. Najma Murtaza Giga - Ndiyo

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Mhe. Dkt. Adelardus Lubango Kilangi - NdiyoMhe. Capt. Mst. George Huruma Mkuchika - NdiyoMhe. Selemani Saidi Jafo - NdiyoMhe. January Yusuf Makamba - NdiyoMhe. Jenista Joakim Mhagama - NdiyoMhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba - NdiyoMhe. William Vangimembe Lukuvi - NdiyoMhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa - NdiyoMhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi - NdiyoMhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe - NdiyoMhe. Angellah Jasmine Kairuki - NdiyoMhe. Dkt. Charles John Tizeba - NdiyoMhe. Dkt. Philip Isdor Mpango - NdiyoMhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga - HakuwepoMhe. Charles John Mwijage - NdiyoMhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako - NdiyoMhe. Ummy Ally Mwalimu - NdiyoMhe. Prof. Paramagamba John Kabudi - HakuwepoMhe. Luhaga Joelson Mpina - NdiyoMhe. Dkt. Medard Matogoro Kalemani - NdiyoMhe. Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla - NdiyoMhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe - NdiyoMhe. Joseph Sinkamba Kandege - NdiyoMhe. Joseph George Kakunda - NdiyoMhe. Kangi Alphaxard Lugola - NdiyoMhe. Antony Peter Mavunde - NdiyoMhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa - NdiyoMhe. William Tate Ole Nasha - NdiyoMhe. Abdallah Hamis Ulega - NdiyoMhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji - NdiyoMhe. Dkt. Susan Alphonce Kolimba - NdiyoMhe. Angeline Sylvester Mabula - NdiyoMhe. Elias John Kwandikwa - NdiyoMhe. Eng. Stella Martin Manyanya - NdiyoMhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile - NdiyoMhe. Eng. Hamad Yussuf Masauni - NdiyoMhe. Eng. Atashasta Justus Nditiye - NdiyoMhe. Subira Khamis Mgalu - NdiyoMhe. Japhet Ngailonga Hasunga - NdiyoMhe. Jumaa Hamidu Aweso - Ndiyo

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Mhe. Juliana Daniel Shonza - NdiyoMhe. Stella Ikupa Alex - NdiyoMhe. Stanslaus Haroon Nyongo - NdiyoMhe. Doto Mashaka Biteko - NdiyoMhe. Mohamed Omary Mchengerwa - NdiyoMhe. Jasson Samson Rweikiza - NdiyoMhe. Peter Joseph Serukamba - NdiyoMhe. Vedasto Edgar Ngombale - HapanaMhe. Dkt. Raphael Masunga Chegeni - NdiyoMhe. Moshi Selemani Kakoso - NdiyoMhe. Dunstan Luka Kitandula - NdiyoMhe. Emanuel Adamson Mwakasaka - NdiyoMhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka - HakuwepoMhe. Suleiman Ahmed Saddiq - NdiyoMhe. Oscar Rwegasira Mukasa - NdiyoMhe. Nape Moses Nnauye - NdiyoMhe. Abdallah Dadi Chikota - NdiyoMhe. Dkt. Christine Gabriel Ishengoma - NdiyoMhe. Kemilembe Julius Lwota - NdiyoMhe. Mwanne Ismail Mchemba - NdiyoMhe. Mariam Ditopile Mzuzuri - NdiyoMhe. William Mganga Ngeleja - NdiyoMhe. Juma Selemani Nkamia - NdiyoMhe. Salum Mwinyi Rehani - NdiyoMhe. Zaynabu Matitu Vulu - NdiyoMhe. Khalfan Hilaly Aeshi - NdiyoMhe. Innocent Lugha Bashungwa - NdiyoMhe. Dkt. Jasmine Tisekwa Bunga - NdiyoMhe. Hawa Mchafu Chakoma - NdiyoMhe. Raphael Japhary Michael - HapanaMhe. Ruth Hiyob Mollel - HapanaMhe. Ally Saleh Ally - HapanaMhe. Ester Amos Bulaya - HakuwepoMhe. Halima James Mdee - HakuwepoMhe. James Francis Mbatia - HapanaMhe. John John Mnyika - HakuwepoMhe. Mch. Peter Simon Msigwa - HakuwepoMhe. Juma Hamad Omar - HakuwepoMhe. Godbless Jonathan Lema - HakuwepoMhe. Wilfred Muganyizi Lwakatare - Hapana

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mhe. Esther Nicholas Matiko - HakuwepoMhe. Antony Calist Komu - HapanaMhe. Susan Anselm Jerome Lyimo - HapanaMhe. Joseph Osmund Mbilinyi - HapanaMhe. Hamidu Hassan Bobali - HapanaMhe. Tundu Antiphas Mughwai Lissu - HakuwepoMhe. Joseph Michael Mkundi - HapanaMhe. Pauline Philipo Gekul - HapanaMhe. Yussuf Kaiza Makame - HapanaMhe. David Ernest Silinde - HapanaMhe. Qambalo Willy Qulwi - HapanaMhe. John Wegesa Heche - HakuwepoMhe. Dkt. Immaculate Sware Semesi - HapanaMhe. Mwita Mwikabe Waitara - HapanaMhe. Masoud Abdallah Salim - HapanaMhe. Cecilia Daniel Paresso - HapanaMhe. Cecil David Mwambe - HapanaMhe. Dkt. Suleiman Ally Yussuf - HapanaMhe. Zubeda Hassan Sakuru - HakuwepoMhe. Devotha Mathew Minja - HapanaMhe. Peter Ambrose Paciens Lijualikali - HapanaMhe. Abdallah Ally Mtolea - HapanaMhe. Rashid Ali Abdallah - HapanaMhe. Maida Hamad Abdallah - NdiyoMhe. Hamida Mohamed Abdallah - NdiyoMhe. Munde Tambwe Abdallah - HakuwepoMhe. Bahati Ali Abeid -NdiyoMhe. Abdul-Aziz Mohamed Abood - HakuwepoMhe. Khadija Hassan Aboud -NdiyoMhe. Lameck Okambo Airo - HakuwepoMhe. Ajali Rashid Akbar - HakuwepoMhe. Abdallah Haji Ally - HapanaMhe. Jamal Kassim Ali - HakuwepoMhe. Khadija Nassir Ali -NdiyoMhe. Khamis Mtumwa Ali -NdiyoMhe. Mbarouk Salim Ali - HapanaMhe. Hussein Nassor Amar -NdiyoMhe. Wanu Hafidh Ameir -NdiyoMhe. Zainab Mndolwa Amir -Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

MBUNGE FULANI: Uzalendo, uzalendo.

(Hapa Waheshimiwa Wabunge waliongea bila utaratibu)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, order, order!

NDG. NENELWA WANKANGA- KATIBU MEZANI:

Mhe. Ussi Salum Pondeza -NdiyoMhe. Saul Henry Amon -NdiyoMhe. Jaku Hashim Ayoub -NdiyoMhe. Omary Ahmad Badwel -NdiyoMhe. Nuru Awadh Bafadhil -Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Mhe. Faida Mohamed Bakar -NdiyoMhe. Zainab Mussa Bakar -HakuwepoMhe. Hussein Mohamed Bashe -NdiyoMhe. Mbaraka Salim Bawazir -NdiyoMhe. Innocent Sebba Bilakwate -NdiyoMhe. Lolesia Jeremia Bukwimba -HakuwepoMhe. Abdallah Majura Bulembo -NdiyoMhe. Halima Abdallah Bulembo -NdiyoMhe. Selemani Said Bungara -HapanaMhe. Felister Aloyce Bura -NdiyoMhe. Jerome Dismas Bwanausi -NdiyoMhe. Marwa Ryoba Chacha -HapanaMhe. Josephine Tabitha Chagula -NdiyoMhe. Lathifah Hassan Chande -HapanaMhe. Mary Pius Chatanda -NdiyoMhe. Sikudhani Yassini Chikambo -NdiyoMhe. Dkt. Rashid Mohamed Chuachua - NdiyoMhe. Cosato David Chumi - NdiyoMhe. Mbaraka Kitwana Dau - NdiyoMhe. Dkt. David Mathayo David - NdiyoMhe. Makame Mashaka Foum - NdiyoMhe. Tauhida Cassian Galoss Nyimbo -NdiyoMhe. Alex Raphael Gashaza - NdiyoMhe. Josephine Johnson Genzabuke - Ndiyo

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mhe. Boniphace Mwita Getere - NdiyoMhe. Anna Joram Gidarya - HapanaMhe. Seif Khamis Said Gulamali -NdiyoMhe. Haji Ameir Haji -HakuwepoMhe. Mwantumu Dau Haji -NdiyoMhe. Othman Omar Haji - HapanaMhe. Khatibu Said Haji - HapanaMhe. Azza Hillal Hamad - NdiyoMhe. Juma Kombo Hamad - HapanaMhe. Pascal Yohana Haonga -HapanaMhe. Joseph Leonard Haule - HapanaMhe. Juma Othman Hija - NdiyoMhe. Mansoor Shanif Hiran - NdiyoMhe. Augustine Vuma Holle - NdiyoMhe. Joram Ismael Hongoli - NdiyoMhe. Yusuph Salim Hussein - HapanaMhe. Khalifa Mohamed Issa - HapanaMhe. Zacharia Paulo Issaay - NdiyoMhe. Asha Mshimba Jecha - NdiyoMhe. Emmanuel Papian John - HakuwepoMhe. Asha Abdallah Juma - NdiyoMhe. Juma Ali Juma - NdiyoMhe. Mwantakaje Haji Juma - NdiyoMhe. Hamoud Abuu Jumaa - HakuwepoMhe. Jafar Sanya Jussa - NdiyoMhe. Ritta Esnepher Kabati - NdiyoMhe. Risala Saidi Kabongo - HapanaMhe. Mgeni Jadi Kadika - HapanaMhe. John Peter Kadutu - NdiyoMhe. Dkt. Dalaly Peter Kafumu - NdiyoMhe. Alfredina Apolinary Kahigi - Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Mhe. Haji Khatib Kai - HapanaMhe. Bonnah Moses Kaluwa - NdiyoMhe. Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala -NdiyoMhe. Vicky Paschal Kamata - NdiyoMhe. Maria Ndila Kangoye - NdiyoMhe. Costantine John Kanyasu - NdiyoMhe. Sebastian Simon Kapufi - Ndiyo

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mhe. Rukia Ahmad Kassim - Ndiyo (Makofi/Vigelegele)

Mhe. Katani Ahmad Katani - HapanaMhe. Zainab Athuman Katimba - NdiyoMhe. Hassan Selemani Kaunje - HakuwepoMhe. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa - NdiyoMhe. Kanali Mst. Masoud Ali Khamis - NdiyoMhe. Yussuf Haji Khamis - HapanaMhe. Sadifa Juma Khamis - NdiyoMhe. Ali Salim Khamis - HapanaMhe. Fakharia Shomari Khamis - NdiyoMhe. Mohamed Juma Khatib - HapanaMhe. Munira Mustapha Khatibu - NdiyoMhe. Aida Joseph Khenani - HapanaMhe. Omari Abdallah Kigoda - NdiyoMhe. Mendrad Lutengano Kigola - NdiyoMhe. Omari Mohamed Kigua - NdiyoMhe. Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe- NdiyoMhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete - NdiyoMhe. Salma Rashid Kikwete - HakuwepoMhe. Ali Hassan Omar King - NdiyoMhe. Elibariki Emmanuel Kingu - NdiyoMhe. Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa - NdiyoMhe. Mariam Nassoro Kisangi - NdiyoMhe. Jumanne Kibera Kishimba - NdiyoMhe. Jesca David Kishoa - HapanaMhe. Boniventura Destery Kiswaga - NdiyoMhe. Charles Muhangwa Kitwanga - NdiyoMhe. Allan Joseph Kiula - NdiyoMhe. Suzan Limbweni Kiwanga - HapanaMhe. Grace Sindato Kiwelu - HapanaMhe. Silvestry Francis Koka - NdiyoMhe. Leah Jeremiah Komanya - NdiyoMhe. Yosepher Ferdinand Komba - HapanaMhe. Kiteto Zawadi Koshuma - NdiyoMhe. Saed Ahmed Kubenea - HapanaMhe. Zuberi Mohamed Kuchauka - HapanaMhe. Rhoda Edward Kunchela - HapanaMhe. Julius Karanga Laizer - Hapana

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mhe. George Malima Lubeleje – NdiyoMhe. Riziki Said Lulida – HakuwepoMhe. Anna Richard Lupembe – NdiyoMhe. Livingstone Joseph Lusinde – NdiyoMhe. Eng. Gerson Hosea Lwenge - NdiyoMhe. Hamad Salim Maalim – HapanaMhe. Amina Iddi Mabrouk – NdiyoMhe. Stanslaus Shing’oma Mabula – NdiyoMhe. Khamis Yahaya Machano – HakuwepoMhe. Lucy Simon Magereli – HapanaMhe. Prof. Jumanne Abdallah Maghembe - NdiyoMhe. Catherine Valentine Magige – NdiyoMhe. Sonia Jumaa Magogo - HakuwepoMhe. Esther Alexander Mahawe – NdiyoMhe. Almas Athuman Maige – NdiyoMhe. Ezekiel Magolyo Maige - NdiyoMhe. Kunti Yusuph Majala – HapanaMhe. Salome Wycliffe Makamba – HapanaMhe. Makame Kassim Makame – NdiyoMhe. Eng. Ramo Matala Makani - NdiyoMhe. Joel Mwaka Makanyaga – NdiyoMhe. Amina Nassoro Makilagi – NdiyoMhe. Hussein Ibrahim Makungu – NdiyoMhe. Tunza Issa Malapo – HapanaMhe. Anne Kilango Malecela – HakuwepoMhe. Angelina Adam Malembeka – NdiyoMhe. Ignas Aloyce Malocha – NdiyoMhe. Issa Ali Mangungu - NdiyoMhe. Vedastus Mathayo Manyinyi - NdiyoMhe. Sixtus Raphael Mapunda – NdiyoMhe. Agness Mathew Marwa – NdiyoMhe. Gimbi Dotto Masaba - HapanaMhe. Hassan Elias Masala – NdiyoMhe. Stephen Julius Masele – HayupoMhe. Augustino Manyanda Masele – NdiyoMhe. Susanne Peter Maselle – HapanaMhe. Yahaya Omary Massare – NdiyoMhe. Janeth Maurice Masaburi - NdiyoMhe. Flatei Gregory Massay – NdiyoMhe. Aisharose Ndogholi Matembe - Ndiyo

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Mhe. Silafu Jumbe Maufi - NdiyoMhe. Lucy Thomas Mayenga - NdiyoMhe. Kiza Hussein Mayeye – Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Mhe. Mussa Bakari Mbarouk – HapanaMhe. Prosper Joseph Mbena – HakuwepoMhe. Janet Zebedayo Mbene – NdiyoMhe. Richard Philip Mbogo – NdiyoMhe. Taska Restituta Mbogo – NdiyoMhe. Gibson Blasius Meiseyeki – HapanaMhe. Bhagwanji Maganlal Meisuria – NdiyoMhe. Neema William Mgaya – NdiyoMhe. Mahmoud Hassan Mgimwa – NdiyoMhe. Godfrey William Mgimwa – NdiyoMhe. Suzana Chogisasi Mgonukulima – HapanaMhe. Omary Tebweta Mgumba – NdiyoMhe. Joseph Kizito Mhagama – NdiyoMhe. Mboni Mohamed Mhita – NdiyoMhe. Esther Lukago Midimu – NdiyoMhe. Rehema Juma Migilla – Ndiyo(Makofi/

Vigelegele)

Mhe. James Kinyasi Millya – HapanaMhe. Desderius John Mipata – NdiyoMhe. Nimrod Elirehema Mkono – HakuwepoMhe. Martha Moses Mlata – NdiyoMhe. Goodluck Asaph Mlinga – NdiyoMhe. Lucia Michael Mlowe – HapanaMhe. Ester Michael Mmasi – HakuwepoMhe. Ally Keissy Mohamed – NdiyoMhe. Twahir Awesu Mohammed – HapanaMhe. Ibrahim Hassanali Mohammedali – NdiyoMhe. Amina Saleh Mollel – NdiyoMhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel – NdiyoMhe. Justin Joseph Monko – NdiyoMhe. Daimu Iddi Mpakate – NdiyoMhe. Dkt. Hadji Hussein Mponda – NdiyoMhe. Maryam Salum Msabaha – HapanaMhe. Jacqueline Ngonyani Msongozi – Ndiyo

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mhe. Martin Mtonda Msuha – NdiyoMhe. Shamsia Aziz Mtamba - Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Mhe. Daniel Edward Mtuka – NdiyoMhe. Maulid Said Mtulia – NdiyoMhe. Muhammed Amour Muhammed – HakuwepoMhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo – NdiyoMhe. Joyce John Mukya – HapanaMhe. Phillipo Augustino Mulugo – NdiyoMhe. Mary Deo Muro – HapanaMhe. Benardetha Kasabago Mushashu – NdiyoMhe. Mussa Hassan Mussa – NdiyoMhe. Joseph Kasheku Musukuma – NdiyoMhe. Hawa Subira Mwaifunga – HapanaMhe. Frank George Mwakajoka – HapanaMhe. Sophia Hebron Mwakagenda – HapanaMhe. Bupe Nelson Mwakang’ata – NdiyoMhe. Fredy Atupele Mwakibete – NdiyoMhe. Edward Franz Mwalongo – NdiyoMhe. Victor Kilasile Mwambalaswa – NdiyoMhe. Venance Methusalah Mwamoto – NdiyoMhe. Zainabu Nuhu Mwamwindi – NdiyoMhe. Hasna Sudi Katunda Mwilima – NdiyoMhe. Abbas Ali Mwinyi – NdiyoMhe. Maftaha Abdallah Nachuma –Ndiyo (Makofi/

Vigelegele)

Mhe. Dkt. Mary Michael Nagu – NdiyoMhe. Shamsi Vuai Nahodha – NdiyoMhe. Joshua Samwel Nassari – HapanaMhe. Suleiman Masoud Nchambi – NdiyoMhe. Mashimba Mashauri Ndaki – NdiyoMhe. Richard Mganga Ndassa – NdiyoMhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro – NdiyoMhe. Deogratias Francis Ngalawa – NdiyoMhe. Eng. Edwin Amandus Ngonyani – NdiyoMhe. Stephen Hillary Ngonyani – HakuwepoMhe. Ahmed Juma Ngwali – HapanaMhe. Oran Manase Njeza – Ndiyo

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mhe. William Dua Nkurua – NdiyoMhe. Daniel Nicodemus Nsanzugwanko – NdiyoMhe. Albert Obama Ntabaliba – NdiyoMhe. Musa Rashid Ntimizi – NdiyoMhe. Nassor Suleiman Omar – HapanaMhe. Lucy Fidelis Owenya – HapanaMhe. Upendo Furaha Peneza – HakuwepoMhe. Haroon Mulla Pirmohamed – NdiyoMhe. Balozi Adadi Mohamed Rajab – NdiyoMhe. Shally Josepha Raymond – NdiyoMhe. Catherine Nyakao Ruge – HakuwepoMhe. Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare – NdiyoMhe. Conchesta Leonce Rwamlaza – HapanaMhe. Machano Othman Said – NdiyoMhe. Magdalena Hamis Sakaya – Ndiyo

(Makofi/Vigelegele)

Mhe. Mattar Ali Salum – NdiyoMhe. Ahmed Ally Salum – NdiyoMhe. Salum Khamis Salum – NdiyoMhe. Saada Mkuya Salum – NdiyoMhe. Deo Kasenyenda Sanga – NdiyoMhe. Edwin Mgante Sannda – NdiyoMhe. Njalu Daudi Silanga – NdiyoMhe. Joseph Roman Selasini – HapanaMhe. Oliver Daniel Semuguruka – NdiyoMhe. Ahmed Mabkhut Shabiby – NdiyoMhe. Rashid Abdallah Shangazi – NdiyoMhe. Shaabani Omari Shekilindi – NdiyoMhe. Prof. Norman Adamson Sigalla King – NdiyoMhe. Mussa Ramadhan Sima – NdiyoMhe. George Boniface Simbachawene – NdiyoMhe. Margaret Simwanza Sitta – NdiyoMhe. Joyce Bitta Sokombi – HapanaMhe. Jitu Vrajlal Soni – NdiyoMhe. Rose Kamili Sukum – HakuwepoMhe. Khalifa Salum Suleiman – NdiyoMhe. Sabreena Hamza Sungura – HapanaMhe. Grace Victor Tendega – HakuwepoMhe. Anatropia Lwehikila Theonest – Hapana

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Mhe. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka – NdiyoMhe. Fatma Hassan Toufiq – NdiyoMhe. Salim Hassan Turky – NdiyoMhe. Rose Cyprian Tweve – NdiyoMhe. Martha Jachi Umbulla – NdiyoMhe. Ally Seif Ungando – NdiyoMhe. Khamis Ali Vuai – NdiyoMhe. Anastazia James Wambura – NdiyoMhe. Selemani Jumanne Zedi – HakuwepoMhe. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto – Hakuwepo

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:Mheshimiwa Spika, tumemaliza zoezi la kupiga kura.

SPIKA: Ahsante Katibu. Sasa uendelee na kufanyatallying, mkishapata hesabu kamili mtatujulisha.

Kwenye kura ya wazi huwa hatuna wakala kwasababu ni ya wazi, kila mtu anaona, ingekuwa kura ya siritungeweka wakala. Mtaona kwamba Spika hajapiga kurani kwa sababu zikifungana basi inakuwa zamu yangu kupigakura ya Ndiyo. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya zoezi la kupigakura kukamilika, Katibu na Wasaidizi wake waliendakuhesabu kura na sasa wameshakamilisha zoezi hilo, naombasasa nimwite Katibu ili aweze kutoa matokeo ya kazi yetu.Katibu.

MATOKEO YA UPIGAJI KURA WA BAJETI YA SERIKALI

NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:Mheshimiwa Spika, idadi ya Wabunge waliopo na ambaowalipiga kura walikuwa 348; Wabunge ambao hawakuwepoBungeni ni Wabunge 43. Kura za Hapana zilikuwa 82, hakunakura ambayo haikuamua na kura za Ndiyo ni 266. (Makofi/Vigelegele)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa matokeo hayosasa natangaza kwamba Bunge limekubali na kuyapitisha

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato naMatumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa jinsi hiyo, nitoe pongezinyingi sana kwa Serikali kwa ujumla wake, tukianzia na RaisMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli; Makamu waRais, Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu; Waziri Mkuu,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa; WaheshimiwaMawaziri wote, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu naWataalam wao wote waliohusika na hii bajeti circle yotetangu ilikoanzia huko mpaka tumefika leo hapa ni safarindefu sana. (Makofi)

Nawapongeza Mawaziri wote ambao walilazimikakufika hapa na kuomba bajeti za Wizara zao moja baadaya nyingine, kazi kubwa sana mlifanya, mmeenda kwenyeKamati zetu, mmejieleza na kujieleza tena na tena namlipokuja hapa moto uliwaka.

Kipekee tumpongeze sana Mheshimiwa Waziri waFedha na Naibu wake ambao wao sasa wakabeba ule mzigowote katika ukubwa wake kwa maana ya bajeti nzima nakuiwasilisha hapa na tukawa na mjadala mkali sana.Naamini mjadala huu ulikuwa ni wa afya tu, naamini kabisaSerikali wenzetu tutakapokuwa tunaondoka tukifunga Ijumaamtaondoka mkiwa mmesheheni ushauri mwingi sana kutokakwa Wabunge. Ushauri huo ndio maoni ya wananchimtaenda kuangalia maana ushauri ni ushauri, mtatazamamtaona nini cha kufanya. (Makofi)

Pia Waheshimiwa inabidi tuwakumbushe, muwemnawakumbuka waliowapa bajeti hii mpaka ikapita, Eeeh!Siyo unapewa bajeti na hawa, unatumikia hawa, sasainakuwa kidogo…! Siku nyingine wanaotoa bajeti watakujakununa sasa sijui itakuwaje.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila utaratibu)

SPIKA: Ninyi semeni hivyo tu bahati nzuri hawa ni watuwa Mungu sana, lakini wangeamua mwaka fulani kura zote

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

zingekuwa za ndiyo hizi, maana hawezi mtu akakukataliabajeti halafu Bunge linalokuja anakuuliza swali una mpangogani wa daraja langu? Bajeti wewe si ulikataa? (Makofi/Kicheko)

Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Mpangohivyo hii Mawaziri msikate tamaa, unajua hivi vitu, alikuwaananikumbusha rafiki yangu mmoja enzi hizo tuko kuleMlimani Chuo Kikuu, palikuwa pana wanafunzi wanalipwakiasi hiki lakini wakawa wanataka kiasi kile kiongezeke marambili, sasa wakaitana Nkurumah Hall wamejaa kama hivi,akaitwa Vice Chancellor, ndiyo wanatoa maoni yao kwamara ya kwanza, wanamwambia Vice Chancellor tunatakaiongezeke kuanzia hapa mpaka hapa, we want our money,wanamwambia we want our money today, here and now.

Kwa hiyo, unaweza ukaona ukiwa unashughulika nauongozi, magumu siyo ya kwako peke yako mpaka hukokwingine kote, mambo ya hela huwa ni magumu sana. Sasawatu wanakwambia, we want our money today, here andnow yaani unafanya fanyaje mpaka zishuke, unakuwa ni Yesu,ni Mana ya kwamba zinateremka tu kwamba mikate hii sasaimeshakuwa kadhaa? Ni ngumu sana. (Makofi)

Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Phillip Mpangokwa hiyo, nasi tunataka yaani kikapu kile cha samaki kitutosheWatanzania kwa wakati mmoja lakini kwa kawaida rasilimalihazitoshi. Katika kutokutosha kwa rasilimali ndiyo kelele zotehizi na lawama eeh! Hata utaasikia ana kiburi huyu, ana ninini kwa sababu ya hizo rasilimali hazitoshi, zingekuwazinatosha ni kicheko tu, kila mtu anaondoka na mafunguyake hapa na mafurushi, basi inakuwa hivyo, otherwise kwakweli tunawashukuru kwa uvumilivu mkubwa ambaommekuwa nao.

Vile vile Waheshimiwa Wabunge nanyi niwashukurusana na kuwapongeza kwa jinsi ambavyommewachachafya Mawaziri, kabisa kabisa!Mnawachachafya kweli hasa upande huu, maana upandehuu mmekataa hata kutoa maoni tangu tuanze hawaleti

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

maoni, hata maoni ya kesho hawana! sababuhawajaandikiwa, looh! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa David Silinde alitoa mpya siku hiyo, basitunatumaini Bunge lijalo watawaandikieni halafu tutapatamaoni mbadala.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya pongezi hizonyingi sana ambazo tunazitoa kwa Serikali, tunawatakia kilala kheri katika utekelezaji wa bajeti hii, tunaamini kwambabajeti hii itatusogeza sana kutoka pale tulipo, kwenda hatuakadhaa mbele kiasi ambacho mwakani wakati huututakapokutana Inshaallah, basi tutakuwa tunazungumzamambo mengine na tutakuwa tunapongezana zaidi.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya maneno hayo,sasa Katibu kinachofuata.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE:

MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

Muswada wa Sheria kwa ajili ya kuidhinisha jumla yaShilingi Trilioni Thelathini na Mbili, Bilioni Mia Nne Sabini na Tano,Milioni Mia Tisa Arobaini na Tisa, Laki Nne Themanini na MbiliElfu na Mia Nne Kumi na Nane (32,475,949,482,418) kwaMatumizi ya Serikali kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazinakwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2019; Kutumia fedhazilizoidhinishwa kwa mwaka huo, kuruhusu kuhamisha baadhiya fedha pamoja na mambo yanayohusiana na malengohayo. (A bill for an Act to Apply some of Thirty Two Trillion, FourHundred Seventy Five Billion, Nine Hundred Forty Nine Million,Four Hundred Eighty Two Thousand Four Hundred EighteenShillings (32,475,949,482,418) out of the Consolidated Fund tothe service of the year ending on the 30th June, 2019, toappropriate the supply granted for that year, to authorizesthe reallocation of certain appropriations and to provide formatters connected with those purpose).

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

(Kusomwa Mara ya Kwanza)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama ambavyoKatibu ametuongoza tuko kwenye Muswada wa Sheria waKuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2018 (TheAppropriation Bill, 2018). Utaratibu wa Muswada huo nikwamba utapitishwa mfululizo kwa hatua zake zote bilamjadala, kwamba hautapelekwa kwenye Kamati yoyote yaBunge ya Kudumu wala Kamati ya Bunge Zima, mashartikusuhu Muswada huu kusomwa kwa mara ya kwanzahayatatumika, hautatangazwa kwenye Gazeti kablahaujawasilishwa Bungeni. Tunaendelea, Katibu.

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

Muswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikaliwa Mwaka 2018 (The Appropriation Bill, 2018)

(Kusomwa Mara ya Pili)

SPIKA: Katibu tena.

NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

Muswada wa Sheria kwa ajili ya kuidhinisha jumla yaShilingi Trilioni Thelathini na Mbili, Bilioni Mia Nne Sabini na Tano,Milioni Mia Tisa Arobaini na Tisa, Laki Nne Themanini na MbiliElfu na Mia Nne Kumi na Nane (32,475,949,482,418) kwaMatumizi ya Serikali kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazinakwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2019; Kutumia fedhazilizoidhinishwa kwa mwaka huo, kuruhusu kuhamisha baadhiya fedha pamoja na mambo yanayohusiana na malengohayo. (A bill for an Act to Apply some of Thirty Two Trillion, FourHundred Seventy Five Billion, Nine Hundred Forty Nine Million,Four Hundred Eighty Two Thousand Four Hundred EighteenShillings (32,475,949,482,418) out of the Consolidated Fund tothe service of the year ending on the 30th June, 2019, toappropriate the supply granted for that year, to authorizes

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1536904010-26 JUNI, 2018.pdf · Daktari Wasaidizi (AMO) wawili, Tabibu wawili, Wauguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

the reallocation of certain appropriations and to provide formatters connected with those purpose).

(Kusomwa Mara ya Tatu)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa hatua hiyo nakwa utaratibu wa Muswada huu, huwa hatuwahoji. Kwa hiyo,niwatangazie tu moja kwa moja kwamba Muswada huu kwamaana ya hapa Bungeni tumeshaupitisha. Kwa kuupitishakwetu maana yake sasa tutaupeleka kwa Mheshimiwa Raisili tuweze kupata baraka za sahihi yake na ukishasainiwa basitunaitakia Serikali utekelezaji mwema wa sheria hiyo maraitakapokuwa imeshawekwa sahihi na Mheshimiwa Rais.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, mmefanya kazi kubwa kwasiku ya leo ni kazi ambayo itaingia katika historia ya Bunge laKumi na Moja kama moja ya majukumu makubwa ambayotumeyatekeleza, niwapongeze sana, kwenye meza yangu yashughuli hapa, shughuli zote za leo zimekamilika,niwakumbushe tu kwamba kesho tutakuwa tunashughulikana ile Finance Bill.

Waheshimiwa Wabunge, kwa vile shughuli zanguzimekamilika hapa, naomba sasa niahirishe shughuli za Bungehadi kesho saa tatu kamili asubuhi.

(Saa 12.30 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumatano, Tarehe 27 Juni, 2018, Saa Tatu Asubuhi)