172
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Tatu – Tarehe 7 Septemba, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kwa mwaka wa fedha ulioisha tarehe 30 Juni, 2016 (The Annual Report and Audited Accounts of National Environment Management Council (NEMC) for the year ended 30 th June, 2016) NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi (Convention on the Establishment of a Joint Songwe River Basin Commission Between the

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA NANE

Kikao cha Tatu – Tarehe 7 Septemba, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA):

Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Barazala Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kwa mwaka wa fedhaulioisha tarehe 30 Juni, 2016 (The Annual Report and AuditedAccounts of National Environment Management Council(NEMC) for the year ended 30th June, 2016)

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwajiwa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yaJamhuri ya Malawi (Convention on the Establishment of aJoint Songwe River Basin Commission Between the

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Government of the United Republic of Tanzania and theGovernment of the Republic of Malawi).

MHE. SALUM MWINYI REHANI (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):

Maoni ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji juu yaAzimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji waKamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe Kati ya Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuriya Malawi (Convention on the Establishment of a JointSongwe River Basin Commission Between the Government ofthe United Republic of Tanzania and the Government of theRepublic of Malawi).

MHE. HAMIDU H. BOBALI - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA MAJI NAUMWAGILIAJI:

Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu yaWizara ya Maji na Umwagiliaji kuhusu Azimio la Bunge laKuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamojaya Bonde la Mto Songwe Kati ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi(Convention on the Establishment of a Joint Songwe RiverBasin Commission Between the Government of the UnitedRepublic of Tanzania and the Government of the Republic ofMalawi).

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YANCHI):

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani naUsalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East AfricanCommunity Protocol on Peace and Security).

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

MHE. ROSE C. TWEVE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NAUSALAMA):

Maoni ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamajuu ya Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African CommunityProtocol on Peace and Security).

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM - NAIBU MSEMAJIMKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARAYA MAMBO YA NDANI YA NCHI:

Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu yaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu Azimio la Bungela Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki (The East African Community Protocol on Peaceand Security)

NAIBU SPIKA: Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza namaswali na tunaanza na Ofisi ya Rais (TAMISEMI), MheshimiwaBupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum sasaaulize swali lake.

Na. 30

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga na Nkasi

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:-

Halmashauri za Wilaya ya Nkasi na Sumbawanga Mjinihazina Hospitali ya Wilaya; wanawake na watoto wanapatashida ya matibabu wakati wa kujifungua na huduma zawatoto.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali katika Wilaya hizo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mheshimiwa Selemani Jafo, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Rukwa umeanzataratibu za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa katika eneola Milanzi. Hospitali ya Mkoa inayotumika sasa itabaki kuwaHospitali ya Manispaa ya Sumbawanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa wananchi waManispaa ya Sumbawanga wanapata huduma za afyakatika Hospitali Teule ya Dkt. Atman inayomilikiwa na Kanisaambayo imeingia mkataba na Serikali wa utoaji huduma zaafya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya yaNkasi imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 100kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Taratibu zakulipa fidia wananchi waliopisha ujenzi huo zinakamilishwa.Kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika HospitaliTeule iliyopo pamoja na vituo vya afya na zahanati. Serikaliitajitahidi kutafuta fedha na kushirikiana na wananchi waNkasi ili kufanikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bupe NelsonMwakang’ata, swali la nyongeza.

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakinimaswali mawili ya nyongeza ni kama ifuatavyo:-

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwaSera ya Afya inasema itajenga zahanati kila kijiji na piaitajenga vituo vya afya kila kata na pia itajenga Hospitali zaWilaya kila wilaya. Je, ni lini sera hii itatekelezwa kikamilifu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa afyani kipaumbele cha mwanadamu hasa kwa mama na mtoto,je, Serikali haioni umuhimu wa kuupa kipaumbele Mkoa waRukwa kwa kuwa hauna Hospitali ya Wilaya hata moja?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli serayetu inatueleza hivyo na ndiyo maana ukiangalia mchakatowa Serikali kwa kushirikiana na ninyi Waheshimiwa Wabunge,wananchi na wadau mbalimbali mnaona ni jinsi ganitunajitahidi kwa kadri iwezekanavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli naomba nitoepongezi zangu za dhati, katika maeneo mbalimbali nilikopitanimekuta Wabunge wengi sana na wengine wakitumia Mfukowa Jimbo na kuungana nguvu na wananchi katika sualazima la ujenzi wa zahanati na vituo vya afya. Nilishawahikuzungumza hapa siku za nyuma kwamba katika bajeti yamwaka 2017/2018 tumetenga shilingi bilioni 251 lakini katikahizo shilingi bilioni 68 ni kwa ajili ya ku-top up shughuli hizo zaujenzi wa zahanati huko tunakokwenda kumalizia hayamaboma.

Kwa hiyo, mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwambatunafanya kila liwezekanalo sera hii iweze kutekelezwa.Najua kila jambo lina time frame, katika miaka hii mitanomtaona mabadiliko makubwa sana katika sekta ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mahsusi katika Mkoawa Rukwa, ni kweli kuna changamoto kubwa sana ndiyomaana Serikali tukaona katika Halmashauri zake kutokana

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

na changamoto lazima tuboreshe kwanza vituo vya afyavilivyopo. Leo hii kwa kaka yangu Mheshimiwa Ally Keissy kuleNkasi amepigia kelele sana Kituo chake cha Kirando,tumefanya utaratibu tunaenda kujenga theatre na majengomengine. Ukienda pale Sumbawanga DC halikadhalika kunasuala la ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mirepa lakini hilotutafanya kwa kadri iwezekanavyo na ndiyo maana katikaHalmashauri ya Wilaya ya Kalambo hivi sasa tumepelekakaribia shilingi milioni 340 kwa ajili ya zoezi la ujenzi waHospitali ya Wilaya.

Kwa hiyo, ni jukumu la Serikali kuhakikisha Mkoa waRukwa nao uweze kujengewa miundombinu ili wananchi wakule waweze kupata huduma nzuri za afya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Badwel, swali la nyongeza.

MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili nami niulize swalimoja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wilaya ya Bahinayo ni miongoni mwa Wilaya hizo kadhaa ambazo hazinaHospitali ya Wilaya na kumekuwa na matatizo mengi sana,lakini pale Bahi tuna kituo cha afya ambacho hakijafikia levelya upasuaji.

Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kuwaambiawananchi wa Bahi kwamba labda upo mpango wowotemzuri wa kusaidia kile Kituo cha Afya Bahi ili angalau hatuaya upasuaji hasa akina mama na huduma zingine muhimuziwepo? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli nimefikamara mbili kwenye Halmashauri ya Bahi na juzi juzi tulikuwana Mheshimiwa Mbunge jimboni kwake takribani mwezi

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

mmoja na nusu na bahati mbaya Bahi hawana Hospitali yaWilaya wala vituo vya vya afya na kile kimoja kiko katikahali mbaya. Kutokana na maombi ya Mbunge tayaritumeshapeleka shilingi milioni 500 ndani ya wiki hii. Tunaendakukiimarisha Kituo cha Afya cha Bahi, tunakijengeamiundombinu ya upasuaji na maabara. Nia yetu ni kwambaBahi pale huduma zote za msingi ziweze kupatikana kwaukaribu zaidi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, ombi lakolimekubaliwa na Serikali na tunalifanyia kazi. Lengo letu nikwamba wananchi wa Bahi wapate huduma nzuri kamawananchi wengine.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Aida Khenani, swali lanyongeza.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwa kuwa ni zaidi ya miaka 53 toka nchiimepata uhuru sehemu yenye hadhi ya mkoa kama Mkoawa Rukwa hatuna Hospitali ya Wilaya hata moja. Serikalihaioni umuhimu sasa wa kuondoa aibu hiyo angalau hatawilaya mbili zipate hospitali ya wilaya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu,Wabunge wote wa Rukwa wakisimama hapa ajendakubwa ni afya kwa sababu ni kweli siyo jambo la uongo.Ndiyo maana hata nilivyokuwa nikimjibu Mheshimiwa Bupeswali lake lile la msingi la kwanza nilizungumza kwa ujumlawake. Ndiyo maana tumesema mipango ya Serikali katikaHalmashauri ya Kalambo sasa hivi kati ya shilingi bilioni 1.4tuliyoitenga tumepeleka karibu shilingi milioni 340 lakini hilitutalisimamia vizuri katika mwaka huu wa fedha angalauKalambo ujenzi uende kukamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika ukiangaliapale Sumbawanga DC hali ni mbaya vilevile, lakini hivi sasakatika Kituo cha Afya cha Mwimbe tumepeleka fedha

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

karibuni shilingi milioni 500 lakini kule Nkasi tumeshaanzakushughulikia matatizo yake. Jukumu hili lote ni la Serikali.Naomba muwe na imani kwamba Serikali hii ya Awamu yaTano, commitment yake ile mikoa ambayo ina changamotokubwa sana tutafanya kila liwezekanalo kuhakikishawananchi wa mikoa hiyo wanapatiwa huduma.

Kwa hiyo, Mheshimiwa dada yangu naomba nikusihikwamba Serikali hii iko nanyi Wabunge wa Rukwa walamsiwe na hofu, tutajitahidi kufanya kila liwezekanalokuhakikisha huduma ya afya inapatikana vizuri zaidi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Halima Bulembo, swali lanyongeza.

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. RCC ya Mkoa wa Kagera ilishatoa kibali kuhusuujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe, lakini suala hilolinakwamishwa na Wizara ya TAMISEMI kwa sababu haitakikutoa usajili ili hospitali hiyo itengewe bajeti na ujenzi uanzemara moja. Je, ni lini Wizara ya TAMISEMI itaamua kutoa usajilihuo ili ujenzi uanze mara moja ili kuokoa akina mama nawatoto?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibuswali la dada yangu Mheshimiwa Halima Bulembo na kwanzanimpe hongera sana kwa kazi kubwa aliyofanya katika sektahii ya afya, hongera sana. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, bahati nzurinimefika Karagwe, bahati nzuri pia anafahamu hata paleKaragwe kulikuwa hakuna DMO. S isi TAMISEMI ndiyotukamchukua kijana mmoja anaitwa Sobo tukampelekapale, ni daktari mzuri sana wa upasuaji. Hata Karagwe paletulikuwa hatuna centre ya Serikali ya kufanya upasuaji sasahivi upasuaji pale Karagwe katika kituo cha afya umeanza.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Si hivyo tu, lilivyotokea tetemeko la ardhi, Serikali imefanyajuhudi kubwa sana kuboresha kile kituo cha afya na hivi sasatunapeleka takribani shilingi milioni 500 kufanya wananchiwa Karagwe wanapata huduma nzuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwahakikishiekwamba katika ofisi yetu hakuna kibali kitakachokwamaisipokuwa wakati mwingine ni changamoto ya bajeti.Tunachukua mawazo yote ya Wabunge wa Karagwe,tutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo kutekeleza vipaumbelevyenu mlivyoweka katika mpango wa bajeti maana siyosuala la kibali, kibali sisi hamna tatizo isipokuwa ni pamojana kuona ni jinsi gani tutenge bajeti kuhakikisha tunajengahospitali ya wilaya.

Kwa hiyo, ni jukumu la Serikali, tutafanya kilaliwezekanalo wananchi wa Karagwe kama tunavyofanyasasa tutaendelea kufanya hivyo ili mradi huduma ya afyaipatikane vizuri katika Wilaya ya Karagwe na Halmashauriyake kwa ujumla. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Swali la mwisho, Mheshimiwa Kakoso.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukurusana kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Tanganyika nimiongoni mwa wilaya mpya ambazo hazina huduma yahospitali ya wilaya. Kwa nyakati tofauti, Serikali imekuwaikiahidi Kituo cha Afya kijiji cha Majalila ambako ni MakaoMakuu ya Wilaya. Nilikuwa nataka kujua kauli ya Serikali, je,Kituo kile cha Majalila, ni lini kitaanza kupewa fedha nahatimaye kuanzisha ujenzi wa kituo cha afya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Wilayaya Tanganyika imegawanyika kutoka Mpanda na mimi

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Mbunge nafahamu tulifika pale kwake ni kweli kuna tatizokubwa sana. Kwa mfano wananchi wanaotoka Mwesewakija Mpanda Mjini ni tatizo na tulifika pale Majalilaambapo Makao Makuu ya Wilaya ile inataka ijengwe,nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasatumetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya Halmashauri yakoya Wilaya. Juzi nilikuwa naongea na Mkurugenzi wako waMpanda DC kuangalia jinsi gani tutafanya.

Kwa hiyo, kuna shilingi milioni 500 tunawaletea na hiisisi tunasema kama ni kingiambago tu, ni fedha ya kwanzatutatoa fedha nyingine kwa ajili ya kununua vifaa ambayojumla yake itakuwa karibuni shilingi milioni 720. Kwa hiyo,naomba niwahakikishie wananchi wa Tanganyika hili nijukumu la Serikali kuwafikia watu wote hata ndugu yanguwa Kakonko tulifanya jambo hili kwa sababu siku ile tuliyofikashida ilikuwa kubwa. Hii ni kazi ya Serikali na itafanya kazikila mahali kwa manufaa ya wananchi wake wa Tanzania.

NAIBU SPIKA: Tunaendelea, Mheshimiwa James FrancisMbatia, Mbunge wa Vunjo, swali lake litaulizwa kwa niabana Mheshimiwa Selasini.

Na. 31

Ujenzi wa Barabara Inayoanzia Uchira - Kolaria

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. JAMES F.MBATIA) aliuliza:-

LEKIDIA imeweza kushirikiana na wananchi wa Kataya Kirua Vunjo Mashariki na kufanikiwa kukarabati barabaraza kata hiyo zenye urefu wa kilometa 17 kwa gharama yashilingi milioni nane, lengo kuu ni ujenzi wa barabarainayoanzia Uchira hadi Kolaria yenye urefu wa takribanikilometa 12 kwa kiwango cha lami; na LEKIDIA wamefanikiwakufanya harambee na kupata shilingi milioni 130 ambaposhilingi milioni 60 zimetumika kununua mapipa 300 ya lamina kubakiwa na shilingi milioni 70.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Je, Serikali itashirikianaje na LEKIDIA kutekeleza mradihuo kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi wa Kataya Kirua Vunjo Mashariki?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa James Francis Mbatia, Mbunge wa Vunjo, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Uchira -Kisomachi - Kolaria yenye urefu wa kilometa 12 ilijengwa kwakiwango cha changarawe kwa gharama ya shilingi milioni300 kutoka katika Mfuko wa Barabara katika mwaka wafedha 2013/2014. Barabara hiyo imeendelea kufanyiwamatengenezo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017zilitumika shilingi milioni 74.2 ili kuifanya ipitike wakati wote.Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imepangakutumia shilingi milioni 31 kwa ajili ya matengenezo yakawaida kilometa nane na matengenezo ya sehemu korofikilometa mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapongeza juhudi kubwainayofanywa na LEKIDIA. Serikali kupitia Wakala wa BarabaraMijini na Vijijini (TARURA) itafanya tathmini ya barabara zotenchini pamoja na barabara ya Uchira hadi Kolaria ili kuonanamna bora ya kuziboresha barabara hizo kwa kiwangokinachohitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakushirikiana na wananchi na wadau wengine wa barabaraili kuhakikisha barabara hiyo inafanyiwa matengenezokurahisisha usafiri na usafirishaji.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Selasini, swali la nyongeza.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika,swali la kwanza, LEKIDIA imekuwa ikishirikiana na wananchikatika kuibua vipaumbele vya maendeleo katika Kata yaKirua Vunjo Mashariki kwa muda mrefu na kipaumbele chasasa ni hii barabara ya Uchira - Kisomachi - Kolaria ambaowamejitahidi kuchanga fedha na sasa wana lami pipa 300.Kipaumbele chao ni kwamba hii barabara ijengwe kwakiwango cha lami.

Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kusaidiaili lami hii isije ikaharibika kujenga walau hatua kwa hatuakilometa tano na baadaye kilometa nyingine tano ilihatimaye hii barabara iweze kukamilika kwa kiwango lamibadala ya kutumia fedha nyingi kwa ukarabati mara kwamara?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, wananchiwamekuwa wakishiriki sana katika kuchangia maendeleo,wamekuwa wakichangia ujenzi wa zahanati, vituo vya afya,shule na kadhalika. Katika Jimbo langu la Rombo karibu kilakijiji kuna miradi ya maendeleo inayoendelea kwa michangoya wananchi lakini kwa upande wa Serikali fedha zimekuwahaziendi kwa wakati jambo ambalo sasa linawavunja moyowananchi.

Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu upelekaji wa fedhaza maendeleo jinsi ambavyo zimekubaliwa kwenye bajeti ilikuwatia moyo wananchi hao waendelee kuchangia shughuliza maendeleo ambazo tayari zimeshaanza?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli LEKIDIAwamechanga wamenunua mapipa takribani 340 kwa rekodiniliyokuwa nayo. Ndiyo maana katika jibu langu la msinginimesema kwa sababu sasa hivi tumeunda Wakala mpyawa TARURA na bahati nzuri tumepata Meneja maalum wamradi katika Halmashauri ya Rombo na katika Halmashauri

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

zote Tanzania. Meneja hawa jukumu lao sasa ni kufanya needsassessment katika kila Halmashauri. Tuagize Meneja wetuapitie barabara hiyo then ataleta tathmini halafu tutajua ninicha kufanya katika barabara hiyo. Kwa hiyo, ni jukumu kubwala Serikali kuhakikisha barabara hizi zote zinafanyiwamatengenezo. Kwa hiyo ni commitment yetu Serikali kwaTanzania nzima, hili jambo tutaenda kulifanya nikitambuajuhudi kubwa ya wananchi wanayoendelea kuifanya, lazimatuwaunge mkono. Kwa hiyo, kazi itafanyika baada yatathmini ya Mameneja wetu walioko site kuangalia kipikilichopo na kipi kifanyike katika utaratibu gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala zima la upelekajiwa fedha, nimesema hapa kwa mfano fedha za barabaratumetenga karibuni shilingi bilioni 263 lakini hizi kuna fedhaza barabara zenye vikwazo lakini zingine za road fund namaeneo mbalimbali. Ni jukumu la Serikali kuhakikishatunapata fedha hizi na bahati nzuri jana tulikuwa na Waziriwa Fedha katika kikao chetu cha mambo ya lishe amesemacommitment ya Serikali katika mwaka huu wa fedha nikuhakikisha fedha zote za maendeleo zinafika katika maeneohusika. Kwa hiyo, ondoa hofu, jukumu letu sasa hivi naombatuungane mkono wote kwa pamoja tukusanye mapato,tulipe kodi na mwisho wa siku kwamba fedha hizozitapelekwa katika vijiji vyetu kwa ajili ya kuhakikisha kwambawananchi wanapata huduma nzuri katika maeneombalimbali.

NAIBU SPIKA: Tunaendelea na Ofisi ya Rais, Utumishina Utawala Bora, Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbungewa Mafinga Mjini, swali lake litaulizwa kwa niaba naMheshimiwa Mgimwa.

Na. 32

Kupandisha na Kuongeza Morali yaKazi kwa Watumishi wa Umma

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA (K.n.y. MHE. COSATOD. CHUMI) aliuliza:-

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Serikali ina utaratibu wa kuwalipa watumishi waumma gharama za nauli ya likizo mara moja katika miakamiwili wakati wanaenda likizo.

Je, Serikali ipo tayari kuanzisha utaratibu wa kuwalipagharama za nauli za likizo watumishi wa umma kila mwakakatika kuongeza, kupandisha morali ya kazi na piakupunguza makali ya maisha?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, likizo ya mwaka ni haki yakila mtumishi wa umma na haki hii imebainishwa katikakifungu cha 31 cha Sheria ya Kazi na Mahusiano KaziniNamba6 ya mwaka 2004 na Kanuni ya 97 ya Kanuni zaUtumishi wa Umma za mwaka 2003.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa kulipagharama za nauli kwa watumishi wa umma kwa ajili ya likizoumeainishwa katika Kanuni H. 5 (1) (a), (b) na (c) ya Kanuniza Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009. Kwamujibu wa kanuni hiyo, mtumishi wa umma anatakiwakulipiwa gharama ya nauli kwa ajili yake, mwenza wake nawategemezi wasiozidi wanne kutoka kituo chake cha kazihadi nyumbani kwake mara moja katika kipindi cha miakamiwili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni kuwapamotisha watumishi wa umma ili kuwaongezea morali ya kazi.Hata hivyo, motisha inayotolewa inapaswa kuzingatia haliya uchumi wetu. Hali ya uchumi wetu kwa sasa inaruhusu

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

utaratibu huu wa kulipa gharama za nauli ya likizo kwawatumishi wa umma mara moja katika kipindi cha miakamiwili. Aidha, Serikali itaendelea kuboresha motisha kwawatumishi wa umma kadri uchumi unavyoimarika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa, swalila nyongeza.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimwa NaibuSpika, pamoja na maelezo ya Serikali, naomba kuulizamaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, natakatupate tamko la Serikali lini wataanza kulipa malimbikizohayo ya likizo za wafanyakazi ambao kwa muda mrefuwamekuwa wakisubiri haki zao hizo za msingi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni mwaka wapili sasa hakuna increment yoyote kwa walimu walakupandishwa madaraja. Nataka kauli ya Serikali ni liniwataanza kupandisha madaraja na kuongeza incrementhasa za walimu ambao morali zao zimeanza kushuka katikamaeneo yao ya kazi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza nipende tu kusema kwamba Serikali imekuwaikijitahidi kulipa malimbikizo mbalimbali ya mishaharapamoja na madai mengine yasiyokuwa na mishahara kwawatumishi wa umma na itaendelea kufanya hivyo kila mara.Nipende tu kusema kwamba katika mwaka huu wa fedhakupitia bajeti za OC mbalimbali za waajiri wetu wametengaulipaji wa madeni, lakini vilevile kupitia Serikali kwa ujumlawake tumetenga fedha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajiliya kulipa madeni ya watumishi pamoja na madeni yawazabuni wengine mbalimbali waliotoa huduma katika

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Serikali. Kwa hiyo, wakati wowote tu kuanzia sasa pindi tumadeni hayo yatakapokuwa yameshahakikiwa basiwatumishi wataweza kuona madeni hayo yakilipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusianana increment na kupanda madaraja, nilipokuwa nikijibu swalihapa Jumatatu au Jumanne nilieleza kuhusiana na suala hili.Tayari taratibu zimeanza na hivi sasa tunakamilisha tutaratibu za mwisho ili kuweza kuanza kulipa nyongeza hiyoya mwaka ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande waupandishwaji wa madaraja, nil ishasema fedhazimeshatengwa na niwahahakishie tu watumishi wote waumma wenye stahili za kupanda madaraja hakuna ambayeataachwa. Niendelee tu kuomba waajiri wahakikishe kilaambaye anastahili kupanda daraja basi ameingizwa katikaorodha, lakini bila kuacha kuzingatia seniority list ili watumishiwenye stahili waweze kupatiwa madaraja hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kurudia kusematena tumeshatenga fedha kwa ajili ya watumishi 193,166ambao watapanda madaraja mwaka huu. Niendeleekuwatoa hofu watumishi wa umma hakuna ambayeatakakosa daraja lake analostahili katika mwaka huu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa hapa mbele sijalijua jinalako hebu jitambulishe, taja jina lako unapouliza swali lanyongeza.

MHE. NURU A. BAFADHILI: Mheshimiwa Naibu Spika,mimi naitwa Nuru Awadh Bafadhili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniruhusukuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa kuna baadhi ya walimu mfano katikaHalmashauri ya Jiji la Arusha katika Shule ya Msingi Olkerian,Kata ya Olkerian mpaka leo wanasumbuliwa kulipwa fedhazao za likizo na wakati huo huo tayari walishatumia fedha

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

zao. Wanapouliza wanaambiwa andikeni barua ili muwezekulipwa pesa zenu. Je, Waziru anatuambiaje kuhusu sualahilo? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora,majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa NaibuSpika, awali ya yote, nimpongeze kwa kurudi tena Bungeni,alikuwa ni Mbunge kipindi cha mwaka 2005-2010, hongerasana na karibu tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua yako madenimbalimbali ya watumishi wanaodai fedha zao za likizo.Nipende tu kusisitiza kwa waajiri ki la mwaka pindiwanapoandaa mapendekezo ya bajeti za mwakawahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya nauli za likizokatika bajeti ya matumizi ya kawaida au bajeti za OC. Vilevilenipende kusema kwamba kwa yeyote ambaye hakulipwafedha hizo hilo ni deni na kama Serikali tunalitambua natunalichukua na tutaendelea kufuatilia kuhakikisha kwambawatumishi hawa wanapatiwa malipo yao. Niombe tuanisaidie huko baadaye taarifa kamili ili tuweze kushirikianakatika ufuatiliaji, lakini ni haki ya msingi ya mtumishi na nilazima walipwe.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bashungwa, swali lanyongeza.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuipongezaSerikali kwa mpango wa kupandisha watumishi madarajawale wanaostahili lakini kuna changamoto ya walewatumishi ambao wanapandishwa madaraja mishaharahuwa inachelewa ku-reflect l i le daraja ambalo

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

amepandishwa. Je, ni nini maelezo ya Serikali kuhusu sualahili?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala Bora,majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YAUTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza kabisa niseme kwamba ni kweli wako baadhiya Maafisa Utumishi ambao wamekuwa hawatekelezi wajibuwao kama inavyopaswa na wamekuwa wakicheleweshakurekebisha mishahara katika mfumo wetu wa ulipaji wamalipo ya mshahara wa LAWSON. Nipende kutoa tamkohapa na maelekezo kwa mara nyingine tena, tulishachukuahatua katika Halmashauri ya Bagamoyo, Kilombero, Temekena nyingine nyingi, hatutamvumilia Afisa Utumishi yeyote aumhusika yeyote katika mamlaka ya ajira ambayeatachelewesha kurekebisha malipo ya mshahara baada yamtumishi kupandishwa daraja.

Nipende kusema sasa hivi tumeenda mbali itafikawakati tutaanza kuwafungia hata Wakurugenzi waHalmashauri mishahara yao ili na wenyewe waweze kuonauchungu wa kuchelewesha upandishwaji wa madaraja wawatumishi hao.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,tunaendelea na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mheshimiwa Neema William Mgaya,Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

Na. 33

Kuiboresha MSD

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaboresha MSD ili dawa zifike kwawakati?

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naombakujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbungewa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanyamabadiliko makubwa katika utendaji wa MSD. Kutokanana malalamiko mengi juu ya utendaji wa MSD siku za nyuma,katika mwaka wa fedha 2015/2016 Serikali iliajiri Kampuni yaUshauri wa Kitaalam ya Deloitte ili kupitia mfumo wa utendajikazi wa MSD kwa minajil i ya kuuboresha. Deloittewalitengeneza ripoti ya utendaji wa MSD na kuletamapendekezo ya maboresho ambayo iliwasilishwa Wizaranimnamo mwezi Januari, 2016. Taarifa hiyo ilikuwa namapendekezo 21 ya utekelezaji ili kuiboresha MSD nakuhakikisha dawa zinafika vituo vya afya kwa wakatikulingana na mahitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mapendekezo hayoyalikuwa pamoja na kuimarisha mifumo ya uwajibikaji yaMSD, kuongeza mtaji wa usambazaji dawa, kulipwa kwadeni la MSD, kuboresha mifumo ya kusimamia rasilimali watu,kuupitia mnyororo wa ugavi wa dawa nchi nzima nakuondoa kero ya uhaba wa dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kupokea ripotihiyo, Wizara iliunda timu maalum ya kusimamia utekelezajiwa mapendekezo ya Deloitte kuhusu uboreshaji wa MSDikiongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali. Napendakukujulisha kuwa hadi kufikia tarehe 31/7/2017 MSD ilikuwaimetekeleza mapendekezo 19 kati ya 21 ya Deloitte.Mapendekezo mawili yaliyosalia ya kuongeza upatikanaji wadawa na kufuta deni la MSD yanaendeea kufanyiwa kazi nayanatarajiwa kukamilika kabla ya Juni, 2019.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na maboreshohayo ndani ya MSD, kwa sasa hali ya upatikanaji wa dawamuhimu imeendelea kuimarika hadi kufikia wastani waasilimia 80. Aidha, ununuaji wa dawa kutoka moja kwa mojakwa wazalishaji kumepunguza gharama za ununuzi wa dawakwa wastani wa asilimia 40 na hivyo kuwawezesha wananchiwengi kupata dawa nyingi zaidi kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kukujulishakuwa ili kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati, Wizara kupitiamsaada wa Mfuko wa Dunia (Global Fund to Fights Aids,Malaria and Tuberculosis) inatarajia kuipatia MSD magari yausambazaji 181 kwa ajili ya usambazaji wa dawa, vifaa navifaa tiba ili ufanyike kila baada ya miezi miwili badala yamiezi mitatu ya sasa. Utaratibu huu utaongeza upatikanajiwa dawa kuanzia mwezi Januari, 2018.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Neema William Mgaya,swali la nyongeza.

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, napendakumuuliza kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, denila MSD lilikuwa ni kiasi gani na kiasi gani kimeshalipwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, nataka kujuaMSD tayari wameshapewa pesa, ni maboresho ganiwaliofanya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata dawakwa wakati? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzanianze kwa kumpongeza kwa jitihada anazofanyakuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu afya zawananchi wa Mkoa wa Njombe na ndiyo maana amenialika

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

kwenye mkoa wake mara mbili i l i kwenda kutatuachangamoto zinazowakabili.

Mheshimiwa Naibu Spika, deni la MSD mpaka kufikiamwezi Juni, 2016 lilikuwa linafikia shilingi bilioni 143.4 na uhakikiulikuwa bado unaendelea. Sehemu kubwa ya deni ilikuwaimehakikiwa na mpaka sasa bado uhakiki wa deni hilounaendelea kufanywa na wenzetu wa Hazina. Tayari piahatua mbalimbali za kuanza kulipa deni la MSD zilikwishaanzakuchukuliwa kwa wenzetu wa Wizara ya Fedha kutuleteapesa kwa ajili ya kulipa deni hilo kila baada ya muda wamiezi mitatu. Mpaka sasa tayari deni la MSDl imeshapunguzwa kwa takribani shilingi bilioni 12 nalinaendelea kuhakikiwa lakini pia kulipwa taratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tuna changamotomoja kwamba kuanzia 2016 - 2017 Juni, kipindi hiki chamwaka mmoja hapo, deni pia limeongezeka tena kwashilingi bilioni 11 na ni kwa sababu ya miradi misongeambapo kwa kiasi kikubwa inafadhiliwa na taasisimbalimbali za kimataifa ikiwemo Global Fund to FightsMalaria, HIV/AIDS and Tuberculosis. Kwa msingi huo,wanatupa dawa na vifaa tiba lakini tunatakiwa sisi tuingiegharama za ku-clear. Sasa pesa hizi zimekuwa zikichelewakuja kutoka kwa wenzetu wa Hazina. Kwa hiyo, denilimeendelea tena kuongezeka mpaka kufikia tena shilingibilioni 144 kufikia Julai, 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye majibu yaswali ya msingi niliyoyatoa hapa nilieleza maboreshombalimbali ambayo tumeendelea kuyatekeleza kufuatanana ushauri wa kitaalam tuliopewa na taasisi ya kutoa ushauriya kimataifa ya Deloitte and Touche na mpaka sasatunaendelea kufanyia kazi mapendekezo yao 21 ambayoyalitolewa. Kutilia msisitizo tu ni kwamba changamotokubwa ambazo zilijionesha katika ripoti ile, pamoja nakuwepo changamoto ya deni, magari machache yakusambaza dawa na mtaji wa MSD kwisha kutokana namadeni kuwa makubwa lakini pia kulikuwa kuna

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

changamoto nyingine ya kukosekana kwa maoteo(quantification) kutoka kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni mambo ambayotumekuwa tukiyaboresha kwa ukaribu sana katika kipindi hikina sasa upatikanaji wa dawa kwa kweli imekuwa ni sualala kihistoria. Mimi nazunguka sana kwenye vituo vya afya,Hospitali za Wilaya nakuta upatikanaji wa dawa upo kwazaidi ya asilimia 90 na mpaka sasa wastani umefika asilimia80. Hakuna mtu atasimama leo hii na kulalamika kwambakuna upungufu wa dawa kwenye eneo lake. Ukionaimejitokeza hivyo basi ujue DMO ama Mkurugenzi hawafanyikazi yao ipasavyo na wala siyo suala la MSD ama SerikaliKuu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Khadija Nassir, swali lanyongeza.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na malalamikomengi kwenye Halmashauri zetu juu ya uhaba au ukosefuwa dawa lakini taarifa za Naibu Waziri hapaanasema kwamba dawa zipo. Sasa nilikuwa naomba tuMheshimiwa Naibu Waziri atupe maelezo juu ya hili kwa kinazaidi. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, utakapokuja kujibuhapa naomba uchukue muda mfupi kwa sababu umeshatoamaelezo marefu ya mwanzo, kwa hiyo, yeye anahitaji tumsisitizo. Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimeonanisimame kwa sababu Naibu Waziri ametoa majibu mazurisana lakini bado mdogo wangu Mheshimiwa Khadija Nassiranauliza swali kuhusu upatikanaji wa dawa. Kwa hiyo,nataka kidogo nitoe uelewa, tunapima vipi upatikanaji wadawa.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapima upatikanaji wadawa, dawa ziko zaidi ya elfu mbili, elfu tatu, elfu nne, lakinikatika ngazi ya MSD tumechagua dawa 135 muhimu zaidikwa mujibu wa Mwongozo wa WHO kwamba hizo ndiyodawa muhimu zaidi ambazo zinatakiwa kuwepo mudawote katika ngazi ya MSD katika nchi. Kwa hiyo, kamaalivyosema Naibu Waziri, MSD kati ya hizo aina 135 za dawa,tuna zaidi ya asil imia 82. Kwa hiyo, Mkurugenzi waHalmashauri au DMO anapoomba aina 100 za dawa atapataangalau aina 82 za dawa mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya pili ya kupimaupatikanaji wa dawa, katika zile dawa 135 tumechaguaaina 30 za dawa ambazo tunaita life serving medicines, zamalaria, maambukizi ya bakteria, HIV, dawa za akina mamawajawazito na kila kitu. Kwa hiyo, ndiyo maana Naibu Wazirisasa hivi na mimi ambavyo tunaenda kwenye vituotunamuuliza Mganga Mkuu wa Wilaya katika zile tracermedicine 30 leo mgonjwa akiumwa ziko aina ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo taarifa ya TAMISEMI,anachosema Naibu Waziri ni sahihi. Mikoa hii imeoneshakwamba sasa hivi hali ya upatikanaji wa dawa katika mikoana katika vituo ni zaidi ya asilimia 80 mpaka 90. Kwa hiyo,huo ndiyo ufafanuzi na ndiyo ukweli…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini natakakutoa changamoto moja, dawa hazipatikani bure,wananchi wanatakiwa kuchangia kupata dawa. Kwa hiyo,lazima pia tuwahimize watu wakate bima za afya.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, tuko vizuri nanataka kurudia, hata NGOs kama SIKIKA ambazo zilikuwazinatuandikia taarifa mbaya kuhusu hali ya upatikanaji wa

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

dawa wametoa taarifa na kuthibitisha dawa ni zaidi yaasilimia 80. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pia Jarida laKimataifa la Famasia limethibitisha hali ya upatikanaji wadawa muhimu Tanzania ni zaidi ya asilimia 80. Kwa hiyo,tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuwekeza kwenyeupatikanaji wa dawa nchini Tanzania. Ahsante sana. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche, kama unatakakuzungumza na Waziri, zunguka huku nyuma uendeukazungumze naye pale.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wizara yaUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mheshimiwa Jumaa HamiduAweso, Mbunge wa Pangani, sasa aulize swali lake.

Na. 34

Barabara Kichocheo Kikubwa cha Maendeleo

MHE. JUMAA H. AWESO aliuliza:-

Ujenzi wa barabara ni kichocheo kikubwa chamaendeleo ya kiuchumi na hata ajira na mawasiliano.

Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani –Saadani hadi Bagamoyo utaanza?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, Mbunge wa Pangani,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi kwa kiwango chalami wa Barabara ya Tanga – Pangani – Saadani - Bagamoyoyenye urefu wa kilometa 246 unajumuisha madarajamakubwa ya Pangani na Wami Chini, barabara za mchepuokatika Jiji la Tanga na Mji wa Pangani pamoja na barabarazinazoingia kwenye hoteli za kitalii za ufukwe wa Bahari yaHindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni sehemu yaMradi wa Kikanda wa Barabara ya Malindi – Mombasa –Lungalunga – Tanga – Pangani - Saadani haadi Bagamoyona unaratibiwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya upembuzi yakinifuna usanifu wa kina ilikamilika mwezi Juni, 2015 chini ya ufadhiliwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank).Aidha, kutokana na gharama za mradi huu kuwa kubwa,taratibu za kupata fedha kutoka African Development Bankna washirika wa maendeleo wengine zimechukua mudamrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018 Serikali imetenga shilingi milioni 4,435 kwa ajili yakuanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwabarabara ya Tanga – Pangani – Saadani - Bagamoyo wakatitaratibu za kupata fedha zaidi kutoka African DevelopmentBank na washirika wa maendeleo zinaendelea.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso,swali la nyongeza.

MHE. JUMAA H. AWESO: Mheshimiwa Naibu Spika,nikushukuru. Napozungumzia ujenzi wa barabara ya Tanga– Pangani – Saadani, nazungumzia uchumi na maisha yawananchi wangu wa Jimbo la Pangani.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwabarabara hii ni ahadi ya muda mrefu na ujenzi wakeumekuwa wa kusuasua yaani ahadi hii tangu mimi sijazaliwampaka sasa hivi nimekuwa Mbunge. Kwa kuwa Serikaliimesahatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii yaTanga – Pangani – Saadani, nini kinachokwamisha kuanzakwa ujenzi wa barabara hii na wananchi wangu kulipwafidia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pamoja na nianjema ya Serikali kuhakikisha kwamba inajenga barabaraya Tanga – Pangani – Saadani, yapo maeneo korofi ambayoyanasababisha matatizo na usumbufu kwa wananchiwangu, mfano ni eneo la kutoka Mkwaja kwenda Mkaramo,Tundaua kwenda Kirare.

Je, Serikali ina mkakati gani wa muda mfupi na waharaka il i kuhakikisha kwamba maeneo hayayanarekebishwa ili wananchi wangu wasipate tabu kwamuda huu?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoelezakatika swali la msingi, barabara hii imetengewa fedha shilingimilioni 4,435. Nimhakikishie tu hiyo ndiyo dalili njema, huondiyo ushahidi kwamba sasa Serikali imedhamiria kuijengabarabara hii kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara hii nipamoja na kuwalipa fidia wale wote wanaostahili fidianamna barabara hii itakavyopita.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge nawananchi wa Pangani na wengine ambao wanaguswa nabarabara hii, dhamira ya Serikali ya kuijenga barabara hii ikopalepale na tumeshaanza na tunatarajia muda si mrefuwashirika wa maendeleo pamoja na African Development

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Bank kwa namna mazungumzo yanavyoendelea tutakujakuongezewa fedha ili tukamilishe kazi hiyo kwa umakiniunaotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kipande chaMkaramo hadi Mkwaja, nimhakikishie tu MheshimiwaMbunge kwamba Meneja wetu wa TANROADS Mkoa waTanga ataliangalia hili alete taarifa yake, gharama yakurekebisha hiki kipande kidogo ili mawasiliano yawepokatika muda wote wa mwaka.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hussein, swali la nyongeza.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Rais wa Awamuya Nne alifanya ziara yake katika Wilaya ya Nyang’hwale nakuahidi ujenzi wa barabara kutoka Kahama –Nyang’holongo – Bikwimba – Karumwa – Nyijundu – Busolwa– Ngoma - Busisi (Sengerema) kwa kiwango cha lami. Pia2010 Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano na yeye alifanyaziara katika Wilaya hiyo ya Nyang’hwale na kuahidi ahadihiyo hiyo ya ujenzi wa barabara hiyo hiyo. Je, kauli ya Serikalini lini upembuzi yakinifu utaanza kwa ujenzi wa barabarahiyo ya lami kutoka Kahama - Karumwa - Busisi? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia sanakuhusu ujenzi wa barabara hii na kwa sababu hiyoanafahamu mimi niliamua kupita barabara hii wakati nikitokaMwanza na Geita na kweli nimeona umuhimu wa barabarahii walau sasa wataalam watakachokuwa wanaelezanitakuwa nafahamu wanachosema ni nini. Nikuhakikishie,mara fedha zitakapopatikana kwa shughuli hii kazi hiiitafanyika.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bwanausi, swali lanyongeza.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa barabara yaMtwara – Tandahimba – Newala – Masasi imeshaanzakujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Mtwara. Je,Mheshimiwa Waziri anawathibitishia nini wananchi ambaowalipaswa kulipwa fidia zao wanalipwa fidia haraka ilikupisha ujenzi huo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimuombeMheshimiwa Mbunge, tulishajadiliana kuhusu suala hili natulikubaliana kwamba tuangalie namna zile fedhazilizotengwa ni kiasi gani kitumike kwa ajili ya fidia na kiasigani kiendelee kukamilisha ujenzi wa barabara ile. Nimuombetu tuwasil iane il i hatimaye tukubaliane yeye na sisi.Ninachomhakikishia wote wanaostahili kulipwa fidia katikabarabara ile watalipwa fidia, hakuna ambaye hatalipwafidia. Hilo ndilo ninalokuhakikishia na nilikwambia hivyokabla, nakushukuru sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rhoda Kunchela, swali lanyongeza.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Nilitaka nipate ufafanuzi kutoka kwa MheshimiwaWaziri, kuna ujenzi wa barabara ambao unaendelea yakutoka Sumbawanga – Stalike – Kigoma. Barabara ile kunamaeneo ambayo tayari ujenzi umeshapita na wananchiwanaoishi pembezoni mwa barabara ya kwenda Kigomawameshahamishwa na baadhi ya wananchi tayariwalishalipwa fidia lakini kuna wengine wamerukwa. Sasa

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Serikali inatumia utaratibu gani kuendelea kuwabaguakuwalipa baadhi ya wananchi fidia na wengine kuwaruka?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ujenzi wabarabara hii ya kutoka Sumbawanga - Stalike - Kigomaunaendelea na unafahamu kwamba kwa sasa tunajengavile vipande viwili ambavyo wakandarasi wako kwenyeeneo na lingine lile la kutoka Mpanda - Tanganyikaunafahamu kwamba tuna fedha lakini napo tunatarajiamkandarasi hivi karibuni atakuwepo site na tunaendeleakutafuta fedha kukamilisha kabisa hadi Kigoma. Nikuombetu kwa kawaida ulipaji wa fidia ni kutegemea na makadirioyaliyofanywa na valuers waliopita katika maeneo hayo. Maranyingi inatokea maeneo mengine kuna watu amawanarukwa na wakati mwingine wanarukwa kwa sababuwakati ule valuation inafanyika pengine yule mtu hakuwepo.Kwa hiyo, nikuombe tu suala hili tutaendelea kulishughulikiana tushirikiane kuhakikisha kwamba wale waliosahaulika nakama kweli wana haki wapate haki yao. Sisi muda wotetunasema mwenye haki ya kulipwa fidia ni lazima alipwefidia na kwa vyovyote kama kuna watu ambao hawanahaki ya kulipwa fidia hatutawalipa fidia.

NAIBU SPIKA: Tunaendelea na Mheshimiwa OmarAbdallah Kigoda, Mbunge wa Handeni Mjini sasa aulize swalilake.

Na. 35

Ujenzi wa Barabara ya Handeni - Kiberashi- Kiteto - Nchemba

MHE. OMARI A. KIGODA aliuliza:-

Serikali iliahidi kutoa kipaumbele kwa barabarazinazounganisha mikoa.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

Je, ni lini barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto –Nchemba na Singida itaanza kujwengwa ili kuunganishamikoa minne ambayo ni ya kiuchumi hususan kilimo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali laMheshimiwa Omari Abdallah Kigoda, Mbunge wa HandeniMjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya upembuzi yakinifuna usanifu wa kina kwa Barabara ya Handeni – Kiberashi –Kijungu – Chemba – Kwamtoro hadi Singida yenye urefu wakilometa 461 umekamilika. Aidha, katika mwaka wa fedhawa 2017/2018, Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 500kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimuwa barabara hii kiuchumi na kijamii, Serikali inaendeleakuhakikisha kuwa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabarahii unatekelezwa ili kuunganisha mikoa inakopita na maeneomengine hasa ukizingatia hivi sasa tuna mradi wa kujengabomba la mafuta linalotoka Uganda kwa maana ya Hoimahadi Tanzania kwa maana ya Tanga.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Omari Abdallah Kigoda,swali la nyongeza.

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amesema kila kitukaribia kimeshakamilika, wananchi wa Handeni, Kiberashi,Kijungu, Kiteto na Nchemba wao wanataka kujua ni lini huumradi utaanza? Ahsante sana. (Makofi)

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, niombe tukuwahakikishia wananchi wa maeneo hayo yote aliyoyatajakuanzia Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kiteto – Nchemba -Kwamtoro hadi Singida ambako barabara hii itapita, Serikaliimedhamiria kwa dhati kuijenga barabara hii kwa kiwangocha lami. Mwaka huu wa fedha ndiyo tunaanza kufanyamaandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lamina tumetenga shilingi milioni 500 kama nilivyosema kwenyejibu langu la msingi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stanslaus Mabula, swali lanyongeza.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niishukuru Serikalikwa ujenzi wa barabara ya lami inayotoka Nela kuelekeaKiwanja cha Ndege. Niulize swali dogo, kwa kiwango hichohicho ni lini Serikali sasa itaanza mpango wa kuboreshabarabara kwa kiwango cha njia nne kutoka mjini katikatikwa maana ya barabara ya Kenyatta kwenda Shinyangakupitia Kata za Mkuyuni, Igogo, Mkolani, Nyegezi pamoja naBuhongwa ili na yenyewe iweze kufanana na yale mazingirayaliyopo? Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naombakumhakikishia Mheshimiwa Stanslaus Mabula na wananchiwa Mkoa wa Mwanza, ni kweli Jiji lile sasa lina hadhi kubwana kwa kweli barabara zake nazo lazima tuhakikishezinakuwa katika hadhi inayostahili Jiji lile. Nimepokea

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

maombi yake, mimi nimechukulia hayo kama ni maombi,nitakwenda niyawasilishe kwa wataalam waanze kuangaliauwezekano wa kufikiria hilo ombi ambalo MheshimiwaStanslaus Mabula amelieleza.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mussa Mbarouk, swali lanyongeza.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwanza niseme nashukuru kwa Serikali kutengatakribani shilingi bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa barabaraya Pangani. Je, ni lini kazi rasmi ya ujenzi wa barabara hiyoitaanza?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naombakumpongeza sana huyu Mheshimiwa Mbarouk kwa sababuanashirikiana vizuri na Wabunge wenzake wa Tanga katikakuhakikisha maendeleo katika maeneo yao yanafanikiwabila kujali itikadi. Nikupongeze sana kwa sababu hatimayeni wananchi wanaotuleta humu ndani na hatimaye niwananchi watakaotuondoa tusipoangalia interest zawananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikuhakikishie kamaambavyo nilijibu kwenye swali la msingi la Mheshimiwa Awesoni kwamba mwaka huu wa fedha tumetenga shilingi milioni500 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuijenga barabara hiikwa kiwango cha lami. Ujenzi wa barabara una hatua, hiindio hatua ya kwanza tunaianza mwaka huu wa fedha.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hussein Bashe, swali lanyongeza.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Wazirikwamba mwaka 2010 wananchi wa Jimbo la Nzega

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

waliahidiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kilometa 10 zalami ndani ya Mji wa Nzega. Mwaka 2014, Waziri wa Ujenziambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasaaliwaahidi tena mbele ya Rais Kikwete ahadi hiyo hiyo.Mwaka 2015 Rais wa sasa, Rais John Pombe Magufulialiwaahidi wananchi wa Jimbo la Nzega ujenzi wa Darajala Nhobola na kilometa kumi za lami ndani ya Mji wa Nzega.Waziri wa TAMISEMI ndani ya Bunge hili mwaka 2016 akijibuswali langu la msingi alisema Serikali inashughulikia ujenzi waDaraja la Nhobola katika bajeti ya 2016/2017 na Naibu WaziriNgonyani katika Bunge lililopita aliahidi daraja hili litajengwana Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka Naibu Waziri anijibuni lini ahadi ya daraja hili itatimizwa katika Halmashauri yaMji wa Nzega? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naombakumhakikishia Mheshimiwa Hussein Bashe na wananchi waNzega kwamba ahadi zilizotolewa na viongozi mbalimbaliama ndani ya Bunge kwa kujibu maswali, wakati wa ziaraama wakati wa kampeni kuhusu ujenzi wa hayo maeneomawili aliyoyasema, ujenzi wa kilometa kumi pamoja nadaraja la Nhobola maana yake hii siyo mara kwanza kuliulizahili suala, nikuahikikishie kama ambavyo tumekuhakikishiasiku za nyuma kwamba ahadi hii itatekelezwa katika Serikalihii ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilimhakikishia MheshimiwaMbunge hilo, na ni kweli tulisema kwamba tungewekakwenye bajeti ya 2016/2017 na unafahamu kwamba bajetini mchakato, kikubwa nachokwambia ni kwamba Serikaliitatekeleza ahadi hii ya viongozi mbalimbali pamoja na sisiambao tumekuwa tukijibu maswali hapa kwa niaba yaSerikali.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Fedha na Mipango, Mheshimiwa MasoudAbdallah Salim, Mbunge wa Mtambile, sasa aulize swali lake.

Na. 36

Kuboresha Mafao ya Wastaafu Nchini

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM aliuliza:-

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwawastaafu ambao wakati wa utumishi wao walilitumikia Taifahili kwa uaminifu na uadilifu mkubwa lakini kumekuwa nahali ya kucheleweshewa mafao yao ya uzeeni yasiyolinganana kupanda kwa gharama za maisha, hali inayosababishakuwa na maisha magumu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha mafao yauzeeni ili kuondoa malalamiko hayo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango, napenda kujibu swali la MheshimiwaMasoud Abdallah Salim, Mbunge wa Mtambile, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mafao ya kustaafuhukokotolewa kwa kutumia muda wa utumishi ambaomtumishi alikuwa katika utumishi na mshahara ambaomtumishi alikuwa analipwa kabla ya tarehe ya kustaafu.Ukokotoaji huo ndiyo unaotoa kiwango cha kiinua mgongoanachostahili kulipwa kwa mkupuo na kiwango chapensheni atakachoendelea kulipwa kila mwezi. Kwautaratibu huo, viwango vya pensheni hutofautiana kati yamstaafu mmoja na mwingine kutegemea muda wake wautumishi na mshahara kabla ya tarehe kustaafu. Iwapo katika

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

ukokotoaji, itajitokeza pensheni ya mstaafu kuwa chini yakima cha chini cha kiwango cha pensheni anacholipwa,mstaafu atalipwa kima cha chini cha pensheni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambuaumuhimu wa kuboresha viwango vya pensheni ili kukidhimahitaji muhimu ya kila siku ya wastaafu. Kwa kutambuahivyo, Serikali iliboresha viwango vya pensheni mwezi Julai2015 ambapo kima cha chini kiliongezwa kutoka shilingi50,114 hadi shil ingi 100,125 kwa mwezi. Hata hivyo,maboresho ya viwango vya pensheni kwa wastaafuyasiyoendana na maboresho ya miundombinu ya kiuchumina huduma za kijamii hayawezi kuondoa malalamiko yawastaafu wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunatambua kwambamapato ya Serikali ni madogo ikilinganishwa na mahitajimuhimu ya kitaifa. Kwa kutambua kuwa ni miaka miwili tutangu tuongeze kima cha chini cha pensheni, Serikali kwasasa imejielekeza zaidi katika kuboresha miundombinu yausafiri na usafirishaji, nishati ya umeme, maji, huduma za afyana elimu. Maeneo haya yana uhitaji mkubwa sana warasilimali fedha. Aidha, matokeo mtawanyiko ya maboreshoya maeneo haya yanaleta unafuu mkubwa wa maisha yawastaafu wetu na wananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kulitaarifu Bungelako Tukufu kwamba Serikali inafanya juhudi za makusudi zakuboresha mifumo ya kukusanya mapato sambamba nakuboresha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kujengauwezo wa kuboresha maisha ya wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyongeza ya pensheni kwawastaafu, mishahara na maslahi mazuri kwa watumishi waumma itawezekana tu kama tutafanikisha mikakati na azmaya Serikali ya kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wetu. Hivyobasi, tuendelee kuiunga mkono Serikali yetu katika juhudi zakeza kujenga uchumi imara, uchumi wa viwanda ambao ndiyomsingi mkuu wa kuimarisha mapato ya Serikali.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim,swali la nyongeza.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kupata nafasi ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, imekuwani mazoea ripoti kadhaa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) katika miaka mbalimbali zimekuwazikionyesha kwamba mafao ya wastaafu yanakuwayakipunjwa kwa makusudi na Serikali imekuwa ikielezakwamba ni wakati wa kukokotoa ndiyo matatizo hayoyanatokea.

Je, ni kwa nini basi mmekuwa mkiwapunja nakuwanyanyasa kwa makusudi na hali zao za maishazimekuwa ni mbaya na tatizo hili limekuwa la muda mrefu,CAG analalamika lakini Serikali imekuwa haifuatilii kwamakini, tabia hii mbaya ya Serikali ya kuwapunja/kuwadhulumu wastaafu mtaacha lini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, majibu yaMheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba shilingi 50,000 ambayoilikuwa miaka iliyopita mkapandisha mpaka shilingi 100,000ambayo ni wastani wa shilingi 3,300 kwa siku. Katika majibuyako ukasema kwamba sasa mnajielekeza kwenyemiundombinu ya usafiri, usafirishaji, nishati na umeme, hiviwatu hawa ambao mliwatuma wakiwa wazima wakafanyakazi hii kwa uadilifu na uaminifu mkubwa mnawapatia shilingi3,300, mtuambie waziwazi mkakati wa Serikali wa ziada wakuboresha maisha ya wastaafu kwa kuongeza pensheni hiiutafanyika lini siyo kubakia na majibu haya tu kwambamnajielekeza kwenye usafirishaji na usafiri hawa mnawatumawakiwa na nguvu sasa mmewaacha mnawatelekeza, tabiahiyo mbaya Serikali mtaacha lini? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Sasa Mheshimiwa Masoud mbona kamaumetoa majibu mwenyewe kwa hilo swali? MheshimiwaNaibu Waziri wa Fedha na Mipango, majibu.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaNaibu Spika, kwa swali lake la kwanza, kusema kwambaSerikali ina tabia mbaya ya kuendelea kuwapunja wastaafuwetu, hii siyo sahihi hata kidogo. Nasema siyo sahihi hatakidogo kwa sababu nimemueleza mafao ya wastaafuhukokotolewa kwa kanuni ambayo imekubalika ndani yaSerikali na wastaafu, kwa hiyo, hakuna sehemu yoyoteambako mstaafu anapunjwa na Serikali yetu, hilo halipo hatakidogo. Kwa hiyo, kanuni iko wazi na inatumika na kilamstaafu anapojiunga na mfuko wowote huiona kanuni hiikabla ya kujiunga na mifuko hii.

Kwa hiyo, napenda wananchi wetu waelewe, Serikaliyetu ina nia njema na dhamira ya dhati ya kuhakikishawastaafu wanalipwa katika msingi ambao ni mzuri kabisana ndicho ambacho Serikali tumekuwa tukifanya. Ndiomaana 2015 tumeongeza kiwango hiki kutoka shilingi 50,000mpaka shilingi 100,000 kima cha chini. Wapo wanaolipwavizuri zaidi kwa sababu nimesema formula hii inategemeana muda wake wa utumishi pamoja na mshahara wake wamwisho aliostaafu nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pilikwamba Serikali ina mkakati gani, nimemueleza vizuri kabisakwamba Serikali yetu na sote sisi ni mashahidi tunapambanakuhakikisha tunaongeza mapato ya Taifa letu, tunawezakukusanya kodi yetu na sote tunaona.

Pia nimesema wazi, ukiongeza pensheni kwa ajili yawastaafu tu wakati hakuna dawa, maji na huduma nyinginemuhimu za jamii haitoleta maana yoyote kwa Taifa letu.Tunawathamini wastaafu wetu, tunaendelea kufanya naokazi vizuri na tutaendelea kuwalipa jinsi ambavyo mapatoya Taifa letu yanavyoimarika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko, swali lanyongeza.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Ni kweli kabisa kwamba wastaafu

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

wanateseka sana na wengi wao wanapoteza maisha. Nikatika Bunge hili hili, Mheshimiwa Naibu Waziri aliliahidi Bungekwamba wastaafu wote wanaodai malimbikizo baada yamarekebisho ya kima cha chini kutoka shilingi 50,000 kwendashilingi 100,000 watalipwa fedha zao kwa maana arrears zotelakini ni takribani miaka miwili sasa wastaafu hawahawajalipwa fedha zao sana sana ni wale ambao walikuwakwenye PSPF na PPF.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningetaka kujua ni kwa niniSerikali haijaweza kuwalipa hawa wastaafu haya malimbikizokama ambavyo Naibu Waziri uliahidi Bunge hili na jemnavyoenda kuwalipa…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko ni maswaliya nyongeza kwa hiyo unauliza moja tu. Mheshimiwa NaibuWaziri wa Fedha na Mipango, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nianze kwa kukanusha kwamba nimiaka miwili wastaafu hawa hawajalipwa ile nyongeza, siyosahihi hata kidogo. Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamiiwameanza kulipa kima cha chini kilichoongezwa na Serikalikuanzia mwezi Januari, 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hili aliloli-quote yeyekwamba niliahidi hapa, nakumbuka wakati najibu swali hilinililieleza Bunge lako Tukufu kwamba kulingana na Sheria yaSSRA, regulator anaye-regulate Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii,ni Bodi za Wadhamini za mifuko husika baada ya actuarialvaluation ndizo zinazoamua sasa kulipa kiwango hiki nandipo baada ya kufanya actuarial valuation Bodi zotezimeidhinisha na tumeanza kulipa kwa kipindi chote kuanziaJanuari mpaka leo tunapoongea wote wanalipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua yapo malalamikowanasema kwamba wengine hawaoni hizo transaction lakininaomba niwaambie kwamba hasa kwa wastaafu wetuwanaolipwa na PSPF siku za nyuma pensheni zao za kilamwezi zilikuwa zikianza kulipwa kabla ya hii addition kwa

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

hiyo kulikuwa kunaonekana kuna two transaction ndani yamwezi mmoja kwa utofauti wa wiki moja au wiki mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali yetu inalipanyongeza hii kwa sababu nyongeza hii hasa kwa PSPF hulipwakutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina, tunalipa kwa wakatina wanalipwa siku moja pensheni yao pamoja na ilenyongeza yao. Kwa hiyo, hakuna sehemu yoyote ambapohawalipwi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu, swali lanyongeza.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Kwa kuwa Waraka wa SSRA Namba 1 wamwaka 2006 unasema kwamba mstaafuatakayecheleweshewa mafao yake, Mfuko husika wa Hifadhiya Jamii utatakiwa kumfidia, waraka huo unaonekanakutokuwa na nguvu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni nini sasa mkakatikabambe wa Serikali kuhakikisha tabia ya ucheleweshaji wamafao ya wastaafu inakoma? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziriwa Fedha kwa majibu yake mazuri na nampongeza sana.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa waajiri wengilakini na mifuko kwa maana nyingine wamekuwawakichelewesha ulipaji wa mafao ya wastaafu wetu kwanamna moja ama nyingine. Kupitia SSRA tumeweka sasamkakati maalum na kupitia maboresho pia ya Sheria za Kaziambayo yalifanyika ndani ya Bunge lako hili Tukufu, tumewapanguvu pia Maafisa Kazi wetu ambao sasa wamepata ya

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

kukagua, wanapokwenda kukagua masuala ya kazi,wanakwenda pia kukagua compliance ya mifuko na waajirikatika kushughulikia pensheni za wastaafu na michango yawaajiri kwenye mifuko ya pensheni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombanimhakikishie Mbunge kwamba Serikali inalisimamia hilikupitia SSRA lakini pia kupitia ofisi zetu za kazi tutaendeleakuhakikisha kwamba waajiri na mifuko ya pensheni inafanyacompliance katika sharia zote tulizonazo na wastaafu wetuwapate mafao yao kwa wakati na waajiri wapelekemichango yao kwa wakati.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Taofiq, swali la nyongeza.

MHE. FATMA H. TAOFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Naona swali nililotaka kuliuliza ameshaliulizaMheshimiwa Mchafu, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea na Wizaraya Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Joyce Bitta Sokombi,Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake.

Na. 37

Tatizo la Tembo katika Mkoa wa Mara

MHE. JOYCE B. SOKOMBI aliuliza:-

Katika Mkoa wa Mara kuna usumbufu mkubwaunaosababishwa na tembo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti tembo hao?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii,majibu.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Joyce Bitta Sokombi, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na madharayanayosababishwa na wanyamapori, hususan tembo, Serikaliimechukua hatua mbalimbali ili kunusuru maisha na mali zawananchi waishio kando ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Kwanza, Serikali imeunda timu ya udhibiti wa wanyamaporihatari na waharibifu ambayo inajumuisha watumishi 14kutoka kikosi dhidi ya ujangili kilichopo Bunda, Hifadhi ya Taifaya Serengeti, Pori la Akiba Ikorongo – Gurumeti, Halmashauriya Wilaya na Gurumeti Reserves. Lengo ni kuhakikishakwamba tukio lolote la uvamizi wa tembo linashughulikiwamara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuweka minara(observations towers) ambayo askari wanyamaporiwanatumia kufuatil ia mwenendo wa tembo il i palewanapotoka nje ya hifadhi, hatua za kuwadhibiti zichukuliwena tatu, kuweka mizinga ya nyuki pembezoni mwamashamba ili tembo wanapoingia katika mashambawafukuzwe na nyuki.

Nne, kutumia ndege zisizokuwa na rubani (unmannedaerial vehicles) kwa ajili ya kufukuza tembo. Mafunzo yakutumia ndege hizo yametolewa kwa watumishi kwakushirikiana na Shirika la World Animal Protection.Kwa ajilihiyo, Pori la Ikorongo limepewa ndege moja, Halmashauriya Serengeti imepewa moja na Kikosi Dhidi ya Ujangili Bundakimepewa ndege moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tano, kuendelea kutoaelimu ya uhifadhi kwa jamii ili wananchi waepuke kulimakatika shoroba za wanyamapori. Sita, kuendelea kufanyautafiti na kushauri wananchi kulima mazao ambayo hayavutiikuliwa na wanyamapori na saba, kuhamasisha Halmashauriya Wilaya kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na jitihada hizi,matukio ya uvamizi wa tembo yamepungua kutoka 128mwaka 2015/2016 hadi 105 katika mwaka 2016/2017. Aidha,katika mwaka 2015/2016, tembo waliweza kufanya uharibifuhadi umbali wa kilometa 30 kutoka kwenye hifadhi, lakinikwa mwaka 2016/2017 umbali huo umepungua hadi kilometa12 tu.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika sana. Majangaya tembo katika Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla nimakubwa sana, lakini majibu ya Waziri yamekuwa ni mepesisana. Nitanukuu, naambiwa kwamba kuanzia mwaka 2015mpaka 2016 ni matukio 128 na mwaka 2016 mpaka 2017wamepunguza hadi 105, kwa maana hiyo matukiowaliyoweza kuyapunguza ni 23 tu. Hatuoni kwambaitachukua muda mrefu sana mpaka kuhakikisha kwambatatizo la tembo hapa Tanzania kwa ujumla litakuwa badoni tatizo kubwa sana kwa wananchi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine, hawa tembozamani wananchi walikuwa wanajichukulia wenyewe hatuamikononi na tembo hawa walikuwa hawasumbui wananchi.Lakini kwa sababu Serikali imeona kwamba tembo ni wathamani kuliko binadamu, na ukiua tembo ni shidaunafungwa miaka mingi, na tembo akiua binadamu nihalali. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri aje na majibu mazurikwa wananchi wa Mkoa wa Mara, je, warudi kule kulewajichukulie hatua mkononi? Kwa sababu ile nyama yatembo inaliwa na wanasema kwamba aidha…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sokombi si umeshaulizamaswali mawili tayari? Umeshauliza mawili, labda kamaunafuta mojawapo ya hayo mawili ambacho sikushauri, kwahiyo tumpe nafasi Mheshimiwa Waziri ajibu hayo maswalimawili.

Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, majibu.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza, ni kweli kwamba uvamizi wa tembo katikamaeneo ya wananchi ni changamoto kubwa katika maeneoya Bunda, Tarime na Serengeti. Hata hivyo Serikali inachukuakila aina ya hatua kuhakikisha kwamba inapambana nakuzuia hali hii, na orodha ya hatua ambazo zimechukuliwanimezitaja. Pamoja na hayo, tunaendelea na utafiti wakuweza kutambua njia nyingine bora zaidi za kukabilianana jambo hili. Na Mheshimiwa Mbunge atakuwa ni shahidikwamba wafanyakazi wetu pamoja na wafanyakazi waHalmashauri wanafanya juhudi kubwa sana ya kusaidiawananchi katika jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, si kweli kabisa kwambatembo ni bora kuliko wananchi. Lakini ni jambo lisilopingikakwamba wanyamapori ni rasilimali kubwa yetu sisi sote kamawananchi wa Tanzania na tunawashukuru sana wananchiwa Mara kwa juhudi kubwa ambazo wanafanya kusaidianchi nzima katika kuwahifadhi wanyama hawa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mmesimamawengi, hili tatizo la tembo liko maeneo mengi sana. Sasainanipa wakati mgumu sana kumchagua nani na naninimuache, maana mmesimama wengi sana.

Mheshimiwa Willy Qambalo, swali la nyongeza.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, uko utaratibu kama si sheriaau kanuni katika nchi hii, kwamba mifugo ya wananchi auwananchi wenyewe wakiingia kwenye hifadhi kuna tozoinawakuta. Je, Mheshimiwa Waziri haoni ili kuondokana nahili tatizo la wanyama kutoka nje umefika wakati sasawanyama wakitoka nje kwenye maeneo ya wananchi, tozohiyo hiyo ambayo wananchi wanatozwa wakiingia kwenyehifadhi nayo itozwe? Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa NaibuSpika, wanyamapori si binadamu na wanyamapori hawanaakili za kibinadamu, ni wanyama wa porini. Kwa hiyo,tujitahidi sana kuwalinda kwa kuwaeleza askariwanyamapori pale wanapotokea na mimi nasema kwa kwelini furaha kubwa kwamba kwa mara ya kwanza sasa tembowameongezeka kutokana na hali mbaya ya ujangiliiliyokuwepo hapa nchini na sasa wanaonekana, wanakujampaka kwenye maeneo ya watu. Rai yangu kwa kwelitushirikiane il i tuwataarifu askari wanyamapori palewanyama hao wanapotokea na sisi tunachukua hatuaharaka iwezekanavyo kila tukio la namna hii linapotokea.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Raphael Chegeni swali lanyongeza.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri katoamajibu mazuri sana, lakini mimi nina concern moja kubwakwamba hawa tembo madhara yao ni makubwa sanakatika Wilaya ya Busega ambayo inapakana na Wilaya zaBunda na Serengeti. Maelezo ya Mheshimiwa Waziri katikamajibu yake amesema kwamba hawa tembo wanazidikudhibitiwa, lakini mwishoni amesema kwamba tembowameongezeka zaidi, sasa sijaelewa kwamba sasa kwa vilewameongezeka zaidi madhara yatakuwa makubwa kwawananchi. Serikali sasa kupitia Wizara yake ina mkakati ganikuwaokoa wananchi ambao wanasumbuliwa na tembokwa kusababishiwa hasara kubwa zaidi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utaliimajibu.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa NaibuSpika, huko nyuma nchi yetu ilikuwa na tembo wengi sana,wanafika 110,000, hivi sasa hatua tuliyofikia hapa wanyamahawa walipunguzwa sana na ujangili wakafika chini ya10,000. Sasa hivi ndiyo idadi hiyo inaanza kukua na tunaanza

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

kuwaona. Katika eneo lile la Serengeti na eneo la Maswatunafanya utafiti kuangalia kama tunaweza kujenga uzio wakuwatenganisha watu, mashamba yao na hifadhi. Tunafanyamazungumzo na wawekezaji wakubwa hapa nchini kwetuna mazungumzo yanaelekea vizuri. Sikupenda nifike mahalininasema jambo hili, lakini Serikali inalichukulia jambo hili kwauzito mkubwa sana na ndiyo maana tunafanya utafiti wauwezekano wa kujenga uzio wa kilometa 140 tuone kwambaitaleta afueni kiasi gani katika kuwadhibiti wanyama hawa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumalizie swaliletu la mwisho kwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge waKalambo sasa aulize swali lake.

Na. 38

Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji – Kata ya Ulumi

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-

Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika Kijiji cha Ulumikilichopo Kata ya Ulumi ambao ulianza kujengwa mwaka2010 haujakamilika mpaka sasa.

(a) Je, ni sababu zipi zimefanya mradi huokutokamilika mpaka sasa na ni lini utakamilika?

(b) Je, Serikali ilitenga kiasi gani cha fedha katika bajetiya mwaka 2017/2018 ili kukamilisha mradi huu?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji na Umwagiliaji, naomba kujibu swali la MheshimiwaJosephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Jimbo la Kalambolenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa ujenzi waMradi wa Umwagiliaji Ulumi ulianza kujengwa mwaka 2012

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

kwa kujenga banio lenye gharama ya shilingi milioni213,279,000 kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Msaada waChakula baina ya Serikali ya Tanzania na Japan bila kuhusishaujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji mashambaniambapo jumla ya shilingi bilioni 1.3 zinahitajika kukamilishakazi zote. Aidha, Wizara yangu hivi sasa inafanya mapitio yaMpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2002kwa lengo la kuihuisha ili uendane na hali ya sasa. Kazi hiiinatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka 2018 nakupitia mpango huu Mradi wa Ulumi ni miongoni mwa miradiiliyopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji wa kilimo chaumwagiliaji kwa manufaa ya wananchi wa Ulumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimuwa mradi huu kwa wananchi wa Kalambo, Wizara yangukatika mwaka wa fedha 2018/2019 itaingiza mradi huu katikabajeti kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ili mradi huu uwezekuanza utekelezaji.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali. Kwakutambua na kukiri umuhimu wa mradi huu, naombanipatiwe majibu; lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, naombacommitment ya Serikali kwamba hiyo 2018/2019 hakika pesaitatengwa kwenye bajeti.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na swali la MheshimiwaMbunge kwamba lini utakamilika, mradi huu kujua ni liniutakamilika ni baada ya kukamilisha usanifu na kuingiamikataba ndipo tarehe itapangwa, kulingana na scope yakazi itakayojitokeza ndiyo tutajua ni lini mradi utakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pil i nicommitment. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwambaSerikali yetu iko commited kuhakikisha kwamba inanyanyuakilimo cha umwagiliaji ili tuweze kuondokana na njaa. NaMkoa wa Rukwa ni miongoni mwa mikoa mitano ambayo

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

inazalisha chakula kwa wingi, kwa hiyo kwa mikoa hii Serikaliiko commited kuhakikisha kwamba tunaendeleza kilimo chaumwagiliaji; tutahakikisha kwamba bajeti hii tunaitenga.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dunstan Kitandula swali lanyongeza.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa fursa niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya Skimu ya Umwagiliajiya Ulumi inafanana sana na Skimu ya Umwagiliaji yaMwakijembe. Mwaka 2010 Serikali ilitumia shilingi bilioni 1.2kujenga Skimu ya Umwagiliaji ya Mwakijembe, lakini bahatimbaya sana skimu ile mifereji haikujengewa wala hakunabwawa lililojengwa kuvuna maji. Matokeo yake, leo hiitunapozungumza its hardly 10 percent ya mradi ndiyoimetumika. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha skimu ile inafanyakazi?

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa, ndiyo maanaSerikali kwa kupitia msaada wa Serikali ya Japani sasa hivimhandisi mshauri anapita nchi nzima ili kubaini matatizo yamiradi ya umwagiliaji ambayo imefanya efficiency ya miradiya umwagiliaji isiwe nzuri. Ni kweli kabisa kwamba miradimingi imejengwa lakini imekuwa na matatizo kwambainalimwa mara moja tu, kipindi cha masika, baada ya hapokilimo hakuna, kunakuwa hakuna maana. Ndiyo maanampango huu unaoendelea wa mwaka 2002 kupitia miradiyote ya umwagiliaji kubaini shida ni nini ndipo tutagunduakwamba kumbe skimu zilijengwa lakini hazina maji kwa hiyotuna mpango wa kujenga mabwawa. Lakini tusubiri ripotiya wahandisi washauri, watakapokuwa wameikamilishandipo tutaendelea sasa kurekebisha mapungufu yote ilimiradi hii iweze kufanya kwa uwezo mkubwa uleunaotarajiwa.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mtulia swali la nyongeza.

MHE. MAULID SAID A. MTULIA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokanana taarifazilizotolewa na TMA wameeleza kwamba baadhi ya mikoayetu katika Tanzania itapata chini ya wastani wa kiwangocha mvua, kwa maana ya Pwani, Tanga, Zanzibar naMorogoro Kaskazini. Je, Serikali ina mpango gani kukabilianana tatizo litakalotokana na upungufu huo wa mvua?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Serikali yetu kwa kushirikianana wataalam mbalimbali duniani tunaanza kuandaa miradiambayo itakuwa na efficiency kubwa kwa maana ya kutumiamaji kidogo kwenye uzalishaji wa mimea. Teknolojia hiyotunazidi kuichukua na kuiendeleza il i maji kidogoyanayopatikana yaweze kutumika vizuri na uzalishaji uwemkubwa. Kwa hiyo, tumejiandaa, taarifa ya TMA tunayo nasisi tunaendelea kuifanyia kazi ili kuhakikisha kwambaproduction ya mazao hasa ya chakula itaendelea kuwakama ambavyo matarajio yapo.

NAIBU SPIKA: Swali la mwisho Mheshimiwa VenanceMwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo la majikwenye Wilaya ya Kilolo ni kubwa na kwa kuwa Wilaya yaKilolo ina utajiri mkubwa wa mito na vyanzo vya maji; nakwa kuwa tayari kuna utekelezaji mkubwa wa mradi wa majiambao uliahidiwa na Mheshimiwa Rais ambao Wizara hiiinafanya; je, kwa maeneo yale mengine ambayo tumekuwatukipigia kelele kwa mfano Ruaha Mbunyuni, Wambingetona sehemu nyingine, Waziri anasemaje? Ni pamoja na kujakutembelea miradi hiyo ambacho ndicho kilio cha mudamrefu cha wananchi; Serikali inasemaje?

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa Jimbo lake nimiongoni mwa Majimbo ambayo yaliahidiwa kupatamsaada kutoka Austria. Mpango huo unaendelea lakini kwakuona kwamba unachelewa, sasa tumeanza utekelezaji kwakutumia fedha za ndani. Mfano, Ilula sasa hivi tumepatachanzo cha maji kizuri kutoka Mkombozi na mradi umeanzaambao unatekelezwa na Mamlaka yetu ya Maji ya Iringa(IRUWASA) na pale ni kilometa 14, kilometa mbilizinatekelezwa na tutakuongezea shilingi bilioni tanokuhakikisha kwamba sasa maji yanafika mpaka Mji wa Ilula;na mipango mingine yote uliyoomba Mheshimiwa Mbungetunaifanyia kazi ikiwemo Ruaha Mbuyuni, lakini pamoja nakuchukua maji Mto Mtitu kupeleka kwenye Makao Makuu yaWilaya pale Kilolo, tunaendelea kuifanyia kazi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumefikamwisho wa kipindi cha maswali na majibu, tutaendelea naratiba yetu. Sasa nilete matangazo tuliyonayo asubuhi ya leo.

Tangazo la kwanza ni la wageni. Tunao wageniwalioko Jukwaa la Spika na hawa ni wageni watano waMheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi na hawa ni viongozi wa Idara na Taasisi zaWizara hiyo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Meja JeneraliMstaafu Projest Rwegasira, karibuni sana

Tunao pia wageni wa Mheshimiwa Ester MichaelMmasi ambao wanatoka katika Taasisi binafsiinayojishughulisha na masuala ya TEHAMA vyuo vikuu na hawani ndugu Dossi Said Dossi na ndugu John Sarita. Karibuni sana

Tunao pia wageni waliotembela Bunge kwa ajili yamafunzo na kundi la kwanza ni wanafunzi 45 na walimuwatano kutoka shule ya sekondari Kihesa iliyoko Mkoa waIringa wakiongozwa na Mwalimu Pius Mwachuvaka, karibunisana.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Tunao pia vijana 60 kutoka Kanisa la RedeemAssemblies of God Tanzania la Mkoani Dodoma, karibuni sanawageni wetu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tangazo lingine ni kuhusukukaimu nafasi ya Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni.Mheshimiwa Spika ametaarifiwa kwamba Mheshimiwa WaziriMkuu amesafiri kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya shughuliza kikazi kuanzia jana na kwa hivyo kuanzia leo atakayekuwaanakaimu nafasi hiyo ni Mheshimiwa Profesa JumanneMaghembe. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya matangazo hayo,tunaendelea na ratiba tuliyonayo.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Naibu Spika,Mwongozo.

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Kiwanga naombaukae Chief Whip wako amesimama, naomba ukaeMheshimiwa Susan Kiwanga. Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana na naomba kuomba mwongozo chini yaKanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako Tukufuna Kanuni ninayoiombea mwongozo ni kanuni ya 120(1), (2)na (3) na Kanuni ya 122 (1), (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu zaBunge lako Tukufu

Mheshimiwa Naibu Spika, jana Kamati mbili Teule zaBunge lako Tukufu zimewasilisha taarifa ya Kamati hizo kwaWaziri Mkuu na tunaambiwa hizo taarifa sasa zinawasilishwakwa Mheshimiwa Rais kwa hatua zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Kamati Teule za Bungehizo mbili zimeundwa kwa mujibu wa Kanuni ya 120(1), (2)na (3) ya Kanuni za Kudumu na Wajumbe wake waliteuliwana Mheshimiwa Spika kwa mujibu ya 120(4) ya Kanuni za

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Kudumu; na kwa mujibu wa Kanuni ya 122 fasiri ya (1), (2) na(3) ya Kanuni za Kudumu, taarifa ya Kamati Teule za Bungezilipaswa kuwasilishwa ndani ya ukumbi wa Bunge lako Tukufuna kujadiliwa na Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa hiyoKanuni ya 122(3) ya Kanuni za kudumu za Bunge hili

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mwongozoninaoumba ni ufuatao:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, tunaomba useme,uliambie Bunge hili Tukufu ni kwa utaratibu gani wa Kikanuni,taarifa mbili za Kamati Teule za Bunge zimewasilishwa kwaWaziri Mkuu badala ya kuwasilishwa kwa Bunge kamainayotakiwa na Kanuni za Kudumu za Bunge hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, tunaomba utuongoze,ni lini sasa kama itawezekana ni lini sasa taarifa hizo mbilizitawasilishwa kwenye ukumbi huu wa Bunge ili zijadiliwe kwamujibu wa Kanuni za Bunge hili. Nakushukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge nimeombwamuongozo na Mheshimiwa Tundu Lissu kwa kutumia kanuniya 68(7). Katika maelezo yake anaomba mwongozo kuonakama Kanuni ya 120 (1), (2) na (3) na Kanuni ya 122(1), (2) na(3) na ametaja pia Kanuni ya 120(4)

Waheshimiwa Wabunge, katika maelezo yakeameeleza kuhusu tukio lililotokea jana ambapo ameombamwongozo juu ya mambo mawili kwa yale yaliyotokea janaambayo sina haja ya kuyaeleza lakini anaomba mwongozo;kwanza kwamba ni utaratibu gani wa kikanuni uliosababishaama ulioruhusu taarifa za Kamati kupelekwa kwaMheshimiwa Spika nje ya Bunge hapo na kisha MheshimiwaSpika kumkabidhi taarifa hizo Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Na jambo la pili aliloliomba ili Bunge hili liwezekuongozwa, ameuliza ni lini taarifa hizo mbili zitaletwa sasaBungeni ili Bunge liweze kujadili kwa mujibu wa Kanunitulizonazo.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Waheshimiwa Wabunge, nitaeleza mambo mawili;jambo la kwanza; Kanuni ya 68(7), mwongozo unaombwakwa jambo lililotokea Bungeni, sasa ili tuende vizuri nitaisomahiyo fasili:-

“Hali kadhalika Mbunge anaweza kusimama wakatiwowote ambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema nakuomba Mwongozo wa Spika kuhusu jambo ambalolimetokea Bungeni mapema ili Spika atoe ufafanuzi kamajambo hilo linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanunina taratibu za Bunge na majibu ya Spika yatatolewa papohapo au baadaye kadri atakavyoona inafaa.”

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, jamboaliloliombea muongozo Mheshimiwa Tundu Lissu kwa mujibuwa Kanuni ya 68(7) halijatokea Bungeni mapema. Nimesemanitazungumza mambo mawili, jambo la pili, kwa ajili yakuweka kumbukumbu sawa sawa; Waheshimiwa Wabunge,kanuni ya 120(1) inasema hivi:-

“Kamati teule inaweza kuundwa na Bunge kwamadhumuni maalum, kwa hoja mahususi itakayotolewa nakuafikiwa.”

Waheshimiwa Wabunge, masharti mengine ya kuhusuKamati Teule yako kwenye Kanuni ya 121(1) inasema:-

“Kila Kamati teue itakuwa na Wajumbe wasiozidiwatano.”

Nimechangua machache ili kupunguza muda wakuzungumza ili tuwezekuendelea na ratiba iliyo mbele yetu.

Ukisoma Kanuni ya 120 utagundua kwamba, Bungehili hakuna mahali ambapo hoja ilitolea humu ndaniikaafikiwa kwamba sasa zinaundwa Tume ama inaundwaKamati Teule ya Bunge. Kwa sababu hiyo ndiyo maanaMheshimiwa Spika yeye amechangua utaratibu alioona borawa Kamati alizoziunda yeye na si zilizoundwa na Bunge.(Makofi)

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Waheshimiwa Wabunge tusikilizane kidogo ili twendepamoja, maana hata waliouliza maswali naona na wenyewewanazungumza.

Kwa hiyo, ikiwa zile Kamati alizoziunda MheshimiwaSpika, tunataka kusema zilikuwa ni Kamati Teule za Bungehakuna ushahidi uliopo kwenye Hansard kuonyesha kwambaBunge hili liliziunda hizo Kamati. Kamati ziliundwa naMheshimiwa Spika na akaja kutangaza majina ya waleambao watakuwepo kwenye hizo Kamati, hilo ni moja.(Makofi)

La pili, Waheshimiwa Wabunge ninyi mliwaona waleWaheshimiwa waliokuwa kwenye hizi Kamati mbili.Mheshimiwa Spika asingeweza kuzidisha Wajumbe waKamati Teule kwa kiasi kile ambacho tumewaona, kwa hivyoKanuni ya 121 ingekuwa imevunjwa kitu ambachohakijafanywa. Kwa hiyo, pamoja na kwamba jambolimetokea jana halitakiwi kutolewa mwongozo ndani yaBunge hili, nimetoa hayo maelezo kwa sababu kumekuwana upotoshaji hapa na pale. (Makofi)

Sasa kuhusu haya mambo ambayo MheshimiwaTundu Lissu ameyaomba, naomba tu WaheshimiwaWabunge tujue kwamba hata katika mazingira yale ambayoKamati inazo taarifa ambazo inataka kuishauri Serikali,ukisoma Kanuni ya 117 tuko pamoja naamini; Kanuni ya117(17) itakupa maelekezo kwamba Mheshimiwa Spikaanaweza kuiambia Seriakli juu ya yale mapendekezo yaKamati mahususi kwahiyo tuelewane hilo na likae vizurinamna hiyo. Kamati zimeundwa na Mheshimiwa Spika, Bungehili halijawahi kuhojiwa wala hoja haijawahi kuletwailiyoafikiwa ili Kamati hizo mbili ziundwe, ni Mheshimiwa Spikaaliziunda. (Makofi)

Baada ya Mwongozo huo Waheshimiwa Wabungesasa tunaendelea na ratiba iliyo mbele yetu.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba Mwongozo wako.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

NAIBU SPIKA: Naomba ukae Mheshimiwa Mwakajoka.Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA-KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji waKamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikaliya Jamhuri ya Malawi (The Convention on the

Establishment of the Joint Songwe River Basin Commissionbetween the government of united republic of Tanzania and

the Government of Republic of Malawi)

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania, naomba kuwasilishamapendekezo ya Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba waKuanisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe katiya Tanzania na Malawi (Convention on the Establishment ofthe Joint Songwe River Basin Commission between Tanzaniaand Malawi).

Mheshimiwa Naibu Spika, utangulizi; Mto Songwe nirasilimali ya maji shirikishi na unafanya mpaka kati ya Tanzaniana Malawi katika ukanda wa chini umbali wa kilometa 200kutoka mto unapoingia katika Ziwa Nyasa. Bonde la mtohuo lina kilometa za mraba 4,243 na wakazi wapatao341,104. Eneo hilo linajumuisha maeneo ya Wilaya ya Kyela,Ileje, Mbozi, Mbeya Vijijini na Momba nchini Tanzania na Wilayaza Kitipa na Karonga nchini Malawi.

Eneo la uwanda wa chini wa bonde hilo limekuwalikikabiliwa na mafuriko ya mara kwa mara. Mafurikoyamekuwa yakisababisha mkondo wa mto kuhamahamana kusababisha mpaka wa nchi ya Tanzania na Malawikuhamia kila mafuriko yanapotokea. Kutokana na hali hiyo,wakazi wa eneo hilo hujikuta wapo katika eneo la nchinyingine kila mkondo wa mto unapohama.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mheshimiwa Naibu Spika, kubadilika kwa mpakamara kwa mara kunaweza kusababisha mgogoro wampaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye eneo husika nakuathiri muskabali wa usalama katika nchi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana nachangamoto za mafuriko na kuhama hama kwa mkondowa mto kuanzia mwaka 1976, Serikali za Tanzania na Malawizimekuwa zikifanya mazungumzo katika ngazi mbalimbalikutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Mwaka 1991 Serikalihizo zilisaini makubaliano ya ushirikiano kwenye masualambalimabli (General Corporation Agreement) ya kutatuamatatizo yanayozikabili nchi zote mbili. Katika kutekelezamakabliano hayo, mwaka 2001 hado 2003 nchi hizozilitekeleza mradi wa kudhibiti mkondo wa Mto Songwe (TheStabilization of the Course of the Songwe River Project) ambaoulihusu upembuzi yakinifu, lengo likiwa ni kubaini njia boraya kiufundi ya kuimarisha kingo za Mto Songwe na kupatasuluhisho la mpaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo ya upembuzi huoyalibaini kuwa mafuriko yanayosababisha kuhama hamakwa mkondo wa mto Songwe yanaweza kudhibitiwa kwakujenga Mabwawa makubwa matatu ya Songwe Chini,Songwe Kati na Songwe Juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua hiyo pia ingewezeshakutumia rasil imali ya maji kwenye Mabwawa hayo,kuendeleza fursa nyingine zilizopo kwa faida za kijamii nakiuchumi kama vile uzalishaji wa umeme, umwagiliaji, uvuvi,utalii na kadhalika. Kwa hiyo lengo kuu la uimarishaji wakingo za mto lilirejewa na kujumuisha uboreshaji wa hali yakijamii na kiuchumi ya wakazi wa bonde hilo kwa kutumiarasilimali zake. Hivyo kupitia upembuzi huo iliamuliwakuanzishwa kwa programu ya kuendeleza bonde la MtoSongwe (Songwe River Basin Development Program).

Mheshimiwa Naibu Spika, program hiyoimegawanywa katika awamu tatu na kutekelezwa kupitiahati ya makubaliano baina ya nchi hizo mbili. Awamu ya

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

kwanza ilihusu upembuzi yakinifu 2001-2003, awamu ya piliilihusu usanifu wa kina na maandalizi ya miradia ya uwekezaji2012 - 2013.

Awamu ya tatu inahusu utekelezaji wa miradi 2016-2026 ambapo utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Bwawa laSongwe Chini litakalojumuisha miundombinu ya uzalishajiumeme na umwaguiliaji, shughuli za uvuvi na utalii pamojana miradi ya kuboresha huduma za kijamii kama vile maji,shule, hospitali na barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha pandezote mbili zinanufaika na rasilimali za Bonde la Mto Songwe,nchi za Tanzania na Malawi zimeamua kuanzisha Kamisheniya pamoja ya kuendeleza Bonde la Mto Songwe (JointSongwe River Basin Commission) itakayosimamia nakuendeleza rasilimali za bonde hilo pamoja na kutekelezamiradi iliyoibuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, uanzishwaji wa vyombombalimbali vya ushirikiano katika kusimamia na kuendelezarasilimali za maji shirikishi unatekelezwa kupitia mkataba naitifaki zinazoridhiwa na nchi washirika kama ilivyoelekezwakupitia Itifaki ya Maji ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo yaKusini mwa Afrika (SADC) Revised Protocol on shared watercauses 2000 kifungu cha 53 ambayo ni shared water causeinstitutions.

Mheshimiwa Naibu Spika, itifaki hiyo inaelekeza nchizinazopakana kwenye bonde moja lenye maji shirikishikuanzisha taasisi za ushirikiano kama vile Kamisheni za Maji,Mamlaka za Maji na Bodi za Maji kwa lengo la kuendelezakutumia na kuhifadhi rasilimali za maji katika bonde husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania liliridhia itifaki hiyo ya SADC mweziAgosti, 2003. Vilevile Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002kipengele cha 2.12 na Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali zaMaji Na. 11 ya mwaka 2009 kifungu 9(d) zinaelekeza na kuipamamlaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikiana

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

na nchi nyingine katika umiliki, utunzaji na matumizi yarasilimali ya maji shirikishi kwa manufaa ya nchi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, maadhumuni ya azimio hilini kuwasilisha Bungeni mapendekezo ya kuridhia mkatabawa kuanzishwa kwa Kamisheni ya Pamoja kati ya Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri yaMalawi kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza rasilimali zamaji katika Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, vipengele muhimu vyamkataba; mkataba una jumla ya vipengele 20. Baadhi yavifungu ni pamoja na vifuatavyo. Kifungu cha tatu;madhumuni na msingi ya kamisheni.

Mheshimiwa Naibu Spika, madhumuni; kwanzaitauwa kutoa ushauri kwa pande zote mbili kuhusu usimamizi,uhifadhi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali zamaji kwenye bonde.

Pili, kuainisha maeneo ya ushirikiano katika usimamizina uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji (intergratedwater resources management and development) nakuyajumuisha kwenye Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa naWilaya inayohusu bonde.

Tatu; kuratibu na kutekeleza mipango ya maendeleoiliyo chini ya Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe,usimamizi wa miundombinu ikijumuisha mabwawa,mitambo ya kuzalisha umeme, mifumo ya umwagiliaji namiundombinu ya kutoa huduma za kijamii kwa nchi zotembili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Misingi ya Kamisheni.Kwanza ni ushirikiano unaozingatia uhuru, usawa na heshimakwa nchi husika na mipaka yake.

Pili, maendeleo endelevu, usawa na matumizi sahihiya rasilimali za maji za pamoja kwenye bonde hususan MtoSongwe na vijito vingine vinavyoingiza maji kwenye mto huo.

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Tatu, kuchukua tahadhari na kuzuia madharayanayoweza kujitokeza na usawa wa uwiano katika masualayote yanayohusu ushirikiano katika bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha tano; Mamlakana Majukumu ya Kamisheni; kwanza itakuwa kusaidiakukusanya na kuchakata taarifa muhimu zinazohitajikakuhusu bonde kwa ajili ya kutoa ushauri kwa pande zote nakutekeleza jukumu lolote litakalotekelezwa na nchi zote mbiliau kufanya maamuzi yanayohusu suala husika endapoitakuwa imeridhiwa, kutoa ushauri na mapendekezo kwapande zote kuhusu suala lenye maslahi ya pamoja, tatu,kuunda Kamati mbalimbali na vikosi kazi vitakavyopewamajukumu ya kusimamia rasilimali za maji na rasilimalinyingine za bonde kulingana na mahitaji ya kamisheni.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne; kuajiri wataalamwashauri, wakandarasi na watoa huduma kulingana namahitaji na tano, kuandaa kanuni na taratibu za kamishenikulingana na madhumuni na misingi ya mkataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 12 ni masualaya fedha; Kamisheni itagharamia ushiriki wa wajumbe kutokapande zote kwenye mikutano inayohusu shughuli zakamisheni kwa fedha zinazotokana na michango ya nchiwashirika au mapato kutoka kwa vyanzo vya kamisheni.Aidha, kamisheni itagharamia ushiriki wa wajumbe wenginewatakaoalikwa katika vikao vya kamisheni kwa ajili ya kutoaushauri wa kitaalam kama itakavyokubalika na pande zotembili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia gharama nyingine namadeni yatokanayo na utekelezaji wa majukumu yakamisheni yatalipwa kwa usawa na pande zote isipokuwakama itakubalika kulipa kupitia michango ya nchi washirikana mapato ya kamisheni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 13 ni usuluhishiwa migogoro. Kwanza mgogoro wowote utakaojitokezakati ya pande hizo mbili kuhusiana na tafsiri au utekelezaji

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

wa mkataba utatatuliwa kwa njia ya maelewano ya amani.Pili, endapo nchi zitashindwa kutatua mgogoro ndani ya siku90, upande wowote utaomba msaada wa usuluhishi kutokakwa taasisi au mtu yeyote atakayekubalika na pande zotembili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, endapo usuluhishiutashindikana pande zote zitawasilisha suala husika kwamaandishi kwenye Baraza la Usuluhishi la SADC au kwamaamuzi (Adhoc Arbitrator) kwa makubaliano maalum yapamoja. Maamuzi ya mwamuzi huyo yatakuwa ya mwishona pande zote zitawajibika kutekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo ya kuridhiamkataba; kuridhiwa kwa mkataba huo kutawezeshakuanzishwa kwa kamisheni ya pamoja ya Bonde la MtoSongwe itakayosimamia na kuendeleza rasilimali za majikatika bonde hilo ikiwa ni pamoja na yafuatayo:-

i. Kutekeleza mradi wa ujenzi wa mabwawa kwa ajiliya kudhibiti mafuriko ambayo huharibu kingo za mto nakusababisha mkondo wa mto kuhama na kuathiri mpakawa nchi hizo mbili.

ii. Kuanza ujenzi wa mradi wa bwawa Songwe chinilitakalotumika kuzalisha umeme megawati 180.2, kutoahuduma za maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani,viwandani, kil imo cha umwagiliaji, uvuvi, hifadhi yamazingira na utalii na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi nakuboresha hali ya maisha ya wakazi wa eneo la bonde.

iii. Kuwa na chombo madhubuti kitakachoweza,pamoja na kazi nyingine, kutafuta rasilimali fedha kwa niabaya nchi husika kwa ajili ya kutekeleza miradi itakayokusudiwakatika bonde.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuridhiwa kwamkataba huu kutakuwa na faida mbalimbali kwenye sektanyingine kama ifuatavyo:-

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Naibu Spika, kisiasa; ulinzi na usalama,wananchi wa eneo husika watakuwa na makazi ya kudumukatika nchi zao na kuepuka kuhamahama nchi nyingine bilahiari yao. Vile vile ulinzi na usalama mpakani utaimarika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiuchumi; fursa za kiuchumizitapatikana kutokana na upatikanaji wa umemeutakaowezesha uanzishwaji wa viwanda vya kusindikamazao ya kilimo na uvuvi. Vilevile ujenzi wa mabwawa nahifadhi ya mazingira utaongezeka, vivutio kwa utalii nakuboresha kilimo na hivyo kuongeza mapato kwa wakaziwa Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiteknolojia; upatikanaji waumeme utachochea matumizi ya teknolojia mbalimbali zauzalishaji viwandani na kilimo cha umwagiliaji pamoja nakuimarika kwa huduma za mawasiliano kama vile simu nacomputer.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne ni kimazingira; ujenziwa mabwawa utazuia mafuriko ambayo huharibu mazingiravile vile miradi ya kuhifadhi mazingira kwenye bonde itasaidiakurudisha uoto wa asili, kuzuia mmomonyoko wa udongona kuhifadhi rasilimali za maji kwa matumizi endelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tano ni huduma za kijamii;uboreshaji wa huduma za jamii hususan maji, afya na umemeutawapunguzia wanawake muda wanaotumia kutafutahuduma hizo na kutumia muda huo katika shughuli nyingineza uzalishaji na hivyo kuongeza kipato cha familia. Vilevileuboreshaji wa huduma hizo utaongeza mahudhurio yawanafunzi mashuleni. Kiutamaduni, wakazi wa bondewataishi bila wasiwasi wa kuathiriwa na mafuriko na hivyokuendelea kuenzi tamaduni, mila na desturi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa kuridhia;kifungu cha 15 cha mkataba kinaelekeza kwamba mkatabahuo utakuwa na nguvu za kisheria baada ya nchi zotewanachama kuridhia kwa mujibu wa taratibu za Katiba zanchi zao hivyo Tanzania inahitaji kuridhia mkataba huo kama

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977inavyoelekeza katika Ibara ya 63(3)(e).

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu gharama za kuridhia;katika utekelezaji wa awamu ya tatu ya programu ni yamiaka kumi inayotarajiwa kugharimu jumla ya dola zaMarekani milioni mia nane ishirini na tisa ambazo zitatumikakutekeleza miradi iliyosanifiwa katika awamu ya pili. Fedhahizo zinatarajiwa kupatikana kupitia vyanzo vifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, michango kutoka nchiwanachama, mikopo ya masharti nafuu na misaada kutokakwa washirika wa maendeleo na taasisi za fedha na zakimataifa na uwekezaji wa hisa kutoka Sekta Binafsi.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Wizara yaMaji na Umwagiliaji imetenga kiasi cha shilingi milioni miasaba na nane kwa ajili ya kulipa madeni, kuratibu maandaliziya miradi ya kijamii na mazingira na kuendesha Sekretarietiya Pamoja ya Mpito ya Kamisheni ya Bonde la mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kongamano lawawekezaji la kujadili upatikanaji wa fedha za kutekelezamiradi ilifanyika mwezi Mei, 2017 nchini Malawi, wengi wawawekezaji hao walionesha nia ya kushiriki kwenyeutekelezaji wa miradi inayotarajiwa kutekelezwa katikaawamu ya tatu na wanasubiri mtaalam maalum (transactionadvisor) aajiriwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuundwa kwakamisheni gharama za kuchangia kwa kila nchi husikazitabainishwa. Gharama hizo zitahusu kwanza, mchango wakila mwaka utakaotolewa na kila nchi kwa ajili ya uendeshajiwa kamisheni, pili, mahitaji ya fedha kwa ajili ya miradiitakayotekelezwa na tatu gharama nyingine kamazitakavyoridhiwa na pande zote mbili.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Naibu Spika, Ushirikishwaji wa Wadau.Katika kuandaa azimio hili la Bunge Wizara imeshirikishawadau wafuatao:-

Kamati za Kudumu za Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Nishatina Madini; Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Sheriana Mambo ya Katiba; Fedha na Mipango; Kilimo, Mifugo naUvuvi; Maliasili na Utalii; Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi;Elimu, Sayansi na Teknolojia; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto; Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Mambo ya Ndani yaNchi na Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, taasisi zinazoshirikishwa nipamoja na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira; Tumeya Taifa ya Umwagiliaji; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; ChuoKikuu cha Kilimo cha Sokoine na Taasisi Zisizokuwa za Serikaliambazo n Tanzania Country Water Partnership na TAWASANET.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mikoa ya Mbeya naSongwe pamoja na Halmashauri za Kyela, Mbeya Vijijini, Ileje,Mbozi na Momba zimeshirikishwa kwa kutoa maoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ratiba ya utekelezaji;kifungu cha 15 cha mkataba kinaelekeza kwamba mkatabautakuwa na nguvu ya kisheria siku 30 baada ya nchi zotembili kuridhia na kupeana taarifa kwa maandishi kuhusuhatua hiyo, hivyo utekelezaji wa mkataba utaanza baadaya pande zote mbili kuridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, baada ya maelezohayo ya utangulizi naomba sasa niwasilishe Azimio la Bungela Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Kamisheni ya Maji yaPamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawikama ifuatavyo:-

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Azimio la Bunge Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji waKamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuriya Malawi

KWA KUWA Tanzania ni mwanachama wa Jumuiyaya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC);

NA KWA KUWA Tanzania ni moja ya nchi zilizoridhiamkataba wa SADC na Itifaki ya Maji za Nchi za SADCinayoelekeza uanzishwaji wa vyombo vya ushirikiano katikakusimamia na kuendeleza rasilimali za maji;

NA KWA KUWA, Tanzania na Malawi zilishiriki katikamajadiliano ya pamoja yaliyofanyika mwaka 1976 kuhusunamna ya kutatua changamoto zinazosababishwa na mtoSongwe kwa madhumuni ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu;

NA KWA KUWA tarehe 20 Februari, 2004 Tanzania naMalawi zili-sign hati ya makubaliano (MoU) ambayo pamojana mambo mengine ilitoa mamlaka kwa pande zote mbilikuanzisha kamisheni mbalimbali za pamoja ikijumuishaKamisheni ya Pamoja na Bonde la Mto Songwe;

NA KWA KUWA Tanzania ilishiriki kikamilifu katikamajadiliano yaliyowezesha kusainiwa kwa Mkataba waKimataifa wa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bondela Mto Songwe na hatimaye kusaini mkataba huo katika Mjiwa Lilongwe, nchini Malawi tarehe 18 Mei, 2017;

NA KWA KUWA Bonde la Mto Songwe ndilo linalofanyampaka kati ya nchi ya Tanzania na Malawi na ambapo Wilayaza Kyela, Ileje, Mbozi, Mbeya Vijijini na momba nchini Tanzaniazimo katika bonde hilo;

NA KWA KUWA Mto Songwe umekuwa ukifurika marakwa mara na kusababisha uharibifu wa miundombinu, malina mashamba na hivyo kuleta madhara, hasara nausumbufu mkubwa kwa wakazi wa bonde hilo;

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

NA KWA KUWA mafuriko ya Mto Songwe yamekuwayakisababisha kuhamahama kwa mkondo wa mto na hivyokusababisha kuhamahama kwa mpaka baina ya nchi yaTanzania na Malawi na kusababisha wasiwasi wa kiusalamajuu ya uwezekano wa kutokea mgogoro wa mipaka bainaya nchi hizi mbili;

NA KWA KUWA Tanzania na Malawi zinatekeleza mradiwa kudhibiti mkondo wa Mto Songwe ambaounapendekeza kujengwa kwa mabwawa makubwa matatuambayo ni Songwe Chini, Songwe Kati na Songwe Juu kwamadhumuni ya kudhibiti mafuriko;

NA KWA KUWA Ibara ya 2.12 ya Sera ya Taifa ya Majina kIfungu cha 98 cha Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali zaMaji Sura 331 kwa pamoja zinaipa mamlaka Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kushirikiana na nchi nyingine katikaumiliki, utunzaji na utumiaji wa pamoja wa rasilimali za majikwa manufaa ya nchi;

NA KWA KUWA mkataba huu unalenga kuimarishausimamizi, uhifadhi, uendelezaji, matumizi endelevu yarasilimali ya maji ya Mto Songwe;

NA KWA KUWA Ibara ya 15 ya mkataba huu inaelezakuwa mkataba huu pamoja na masharti mengine utaanzakutumika kwa kuzingatia matakwa ya kisheria ya kila nchiambapo kwa nchi yetu ili mkataba wa Kimataifa uwezekutumika, pamoja na mambo mengine ni budi uridhiwe naBunge;

NA KWA KUWA Tanzania kuweka saini ya kuridhiamkataba huu pamoja na kutekeleza itanufaika kisiasa,kiuchumi na kijamii ikijumuisha kutekeleza mradi wa ujenziwa mabwawa kwa ajili ya kudhibiti mafuriko ambayoyanakuwa yakiharibu kingo za mto na kusababisha mtokuhama hama na kuathiri mipaka ya nchi hizi mbili;

(b) Bwawa la Songwe Chini ambalo litajengwabaada ya kusainiwa mkataba huu litatumika kuzalisha

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

umeme wa megawati 180.2, kutoa huduma za maji kwaajili ya matumizi ya majumbani, viwandani, kilimo chaumwagiliaji, uvuvi, hifadhi ya mazingira na utalii na hivyokuongeza fursa za kiuchumi na kuboresha hali ya maisha yawakazi wa eneo la Bonde la Mto Songwe;

Na (c) ni kuhifadhi mazingira kurudisha uoto wa asili,kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuhifadhi rasilimali zamaji kwa matumizi endelevu.

HIVYO BASI kwa kuzingatia manufaa yatokanayo namkataba huu kwa Tanzania na umuhimu wa kuridhiamkataba huu, Bunge hili katika Mkutano wa Nane kwamujibu wa Ibara ya 63(3)(a) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977 linaazimia kuridhiaMkataba wa Kimataifa wa Kuanzisha Kamisheni ya Pamojaya Bonde la Mto Songwe (Joint Songwe River BasinCommision).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono, tutaendeleana utaratibu mwingine. Sasa nimuite Mwenyekiti wa Kamatiya Kilimo, Mifugo na Maji.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA - MAKAMUMWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaMwenyekiti, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Azimio la Bungekuridhia Mkataba wa kuanzisha Kamisheni ya Pamoja yaBonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawi.

Mheshimiwa Naibu Spika, utangulizi; kwa mujibu waKanuni ya 53(6) (b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo laJanuari, 2016 kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji naomba kuwasilisha maonina ushauri wa Kamati kuhusu Azimio la Bunge kuridhiaMkataba wa Kuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde laMto Songwe kati ya Tanzania na Malawi (Convention on theEstablishment of a Joint Songwe River Basin Commissionbetween Tanzania and Malawi).

Mheshimiwa Naibu Spika, Nyongeza ya Nane kifungucha 7(1)(b) ya Kanuni za kudumu za Bunge toleo la Januari,2016 inazipa Kamati za Kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumuya Bunge, Kilimo, Mifugo jukumu la kushughulikia Miswadaya Sheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwakuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia.Jukumu hili pia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3)(e)ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Nyongezaya Nane kifungu cha 6(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji inasimamia Wizara mbili ambazozinashughulikia sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia Kanunitajwa hapo juu, tarehe 31 Agosti, 2017 uliiletea Kamati yaKilimo, Mifugo na Maji kazi ya kuchambua mapendekezo yaAzimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Kamisheniya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania naMalawi kama yalivyowasilishwa na Serikali ili Kamati iwezekutoa maoni na ushauri kwa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Azimio la Bunge la KuridhiaMkataba wa Kuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde laMto Songwe Kati ya Tanzania na Malawi liliwasilishwa mbeleya Kamati siku ya Jumatatu tarehe 4 Septemba, 2017 na Waziriwa Maji na Umwagiliaji, Mheshimiwa Engineer GersonLwenge (Mbunge).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya82(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

inazitaka Kamati za Bunge zinapokuwa zinashughulikiaMiswada ya Sheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwakuridhiwa na Bunge ialike wadau ili kwa kutumia utaalamuwao waisaidie Kamati kuchambua na kuboresha maudhuiyanayopendekezwa. Kufuatia ufinyu wa muda uliotolewakushughulikia azimio husika, Kamati haikuweza kupatawadau wowote na hivyo kushindwa kutekeleza Kanuni hiyoya Bunge. Hata hivyo, Kamati iliweza kutekeleza jukumuiliyopewa kwa niaba ya Bunge ilipitia na kuchambua azimiotajwa na kukamilisha taarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, chimbuko, madhumuni nafaida ya Mkataba wa Kuanzisha Kamisheni ya Pamoja yaBonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, historia fupi ya kuanza kwaMkataba wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe;mchakato wa kuanzisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde laMto Songwe ulianza mwaka 1976 ambapo mwaka 2004Tanzania na Malawi zilisaini Hati ya Makubaliano ambayopamoja na mambo mengine hati hiyo ya makubalianoinazipa mamlaka nchi ya Tanzania na Malawi kuanzishaKamisheni mbalimbali za pamoja, ikijumuisha Kamisheni yapamoja ya Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia hati hiyo yamakubaliano, Tanzania ilishiriki kikamilifu katika majadilianoyaliyowezesha kusainiwa kwa Mkataba wa Kimataifa waUanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja na Bonde la MtoSongwe na hatimae kusaini Mkataba huo katika Mji waLilongwe nchini Malawi tarehe 18 Mei, 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, madhumuni ya Mkatabawa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe; dhumunila msingi la kuanzishwa kwa Mkataba wa Kamisheni yaPamoja ya Bonde la Mto Songwe ni kuimarisha usimamizi,uhifadhi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali yamaji ya Mto Songwe. Kuanzishwa kwa mkataba huu nimuhimu kufuatia faida zitakazopatikana kwa nchiwanachama, kwani unalenga kuwezesha:-

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

(i) Kutekeleza mradi wa ujenzi wa mabwawa kwaajili ya kudhibiti mafuriko ambayo huaribu kingo za mto nakusababisha mkondo wa mto kuhama na kuathiri mpakawa nchi hizi mbili.

(ii) Kuanza ujenzi wa mradi wa Bwawa la SongweChini litakalotumika kuzalisha wa umeme megawati 180.2,kutoa huduma ya maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani,viwandani, kil imo cha umwagiliaji, uvuvi, hifadhi yamazingira na utalii na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi nakuboresha hali ya maisha ya wakazi wa eneo la Bonde.

(iii) Kuwa na chombo madhubuti kitakachoweza,pamoja na kazi zingine kutafuta rasilimali fedha kwa niabaya nchi wanachama kwa aji l i ya kutekeleza miradiiliyokusudiwa katika Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na faida hizo zakiujumla, kuridhiwa kwa Mkataba huu kutakuwa na faidambalimbali kwenye sekta nyingine kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kisiasa, ulinzi na usalama;eneo la uwanda wa chini wa Bonde la Mto Songwelimekuwa likikabiliwa na mafuriko ya mara kwa maraambayo yamekuwa yakisababisha mkondo wa mtokuhamahama na kusababisha mpaka wa nchi za Tanzaniana Malawi kuhama kila mafuriko yanapotokea. Hivyokuridhiwa kwa Mkataba huu pamoja na mambo menginekutasaidia kupata suluhisho la mpaka na kuwawezeshaWananchi wa eneo la mpakani kati ya Tanzania na Malawikupata makazi ya kudumu katika nchi zao na kuepukakuhamia nchi nyingine bila hiari yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiuchumi; kuridhiwa kwamkataba huu kutawezesha ujenzi wa bwawa la SongweChini, ambalo mara baada ya kukamilika kwake litatumikakuzailisha umeme megawati 180.2 ambapo fursa za kiuchumizitapatikana kutokana na umeme utakaowezeshauanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo nauvuvi. Aidha, ujenzi wa mabwawa na hifadhi ya mazingira

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

utaongeza vivutio vya utalii na kuboresha kilimo na hivyokuongeza kipato kwa wakazi wa eneo la Bonde na Taifakwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma za kijamii; ujenziwa mabwawa na uzalishaji wa umeme utaboresha piahuduma za jamii kama vile upatika wa maji ya uhakikaambayo ni safi na salama, upatikanaji wa umeme wauhakika na afya za jamii. Kuboreka kwa huduma hizikutawasaidia wanawake kupunguza muda mrefuwanaotumia kutafuta huduma hizo na kuwawezeshakutumia muda huo kufanya shughuli zingine za uzalishaji nahivyo kuongeza kipato cha famila.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa mkataba wakuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe.Mkataba wa kuanzisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde laMto Songwe una jumla ya vifungu 20.

Kamati ilipitia vifungu vyote, hata hivyo taarifa yaKamati ninayoiwasilisha inataja kwa kifupi vifungu muhimuvilivyoko kwenye mkataba huu. Vifungu hivyo ni pamoja na:-

(i) Kifungu cha 3 kinahusu madhumuni na misingi yaKamisheni.

(ii) Kifungu cha 5 kinafafanua kuhusu mamlaka namajukumu ya Kamisheni.

(iii) Kifungu cha 11 kinataja majukumu, wajibu na hakiza msingi za kila nchi katika kutekeleza mkataba.

(iv) Kifungu cha 12 kinaelezea upatikanaji wa rasilimalifedha za kuendesha Kamisheni.

(v) Kifungu cha 13 kinafafanua jinsi ya kushughulikiautatuzi wa migogoro endapo itatokea.

(vi) Kifungu cha 16 kinahusu utaratibu wa nchikujiondoa katika Mkataba.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

(vii) Kifungu cha 17 kinahusu utaratibuutakaozingatiwa na nchi katika kufanya marekebisho katikavifungu vya mkataba.

(viii) Kifungu cha 19 kinahusu sharti la kuzingatia usirikatika utekelezaji wa Mkataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Kamati kufanyauchambuzi kwenye vifungu hivyo muhimu, Kamati ilitakakujiridhisha kwenye maeneo ya msingi na hivyo kuhitajiufafanuzi kwenye maeneo hayo ambayo ni pamoja na:-

(i) Hatua iliyofikiwa kati ya Tanzaia na Malawi katikakushuhulikia mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa il ikujiridhisha kuwa mgogoro uliokuwepo hauwezi kuathiriutekelezaji wa mkataba. Mantiki ya hoja hii nikutokana naukweli kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe, na ukwelikwamba Ziwa Nyasa lina umuhimu mkubwa kwenye uchumiwa Tanzania.

(ii) Ufafanuzi kuhusu namna nchi itakavyonufaika naZiwaNyasa na Mto Songwe, na ni kwa kiasi gani utekelezajiwa Mkataba huu hautaathiri manufaa yaliyokuwayakipatikana awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bungelako kuwa Kamati imeridhishwa na maelezo yaliyoko kwenyeMkataba huu pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Serikalikuhusu hoja zilizoibuliwa na Wajumbe.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni na ushauri waKamati; baada ya kufanya uchambuzi wa Mkataba wakuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe,Kamati inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

(i) Kwa kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe, nakwa kuwa mkataba huu unahusisha nchi za Tanzania naMalawi ambazo zimekuwa na mgogoro wa mara kwa marakuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa, Kamati inaishauri Serikalikuchukuwa tahadhari na kuhakikisha utekelezaji wa

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

mkataba huu hautaathiri faida ambazo nchi imekuwaikipata kutoka Ziwa Nyasa na Mto Songwe.

(ii) Kwa kuwa nchi ya Tanzania na Malawi zimekuwana mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kwa muda mrefu,na kwa kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe; pamojana kwamba mkataba huu unahusu Mto Songwe, Kamatiinaishauri Serikali kupitia fursa ya mkataba huu kufanyautambuzi wa mipaka ya Ziwa Nyasa hatua ambayo inawezakumaliza kabisa tatizo la mgogoro wa mpaka wa ZiwaNyasa.

(iii) Kwa kuwa Mkataba huu unahusisha nchi mbili nivyema baada ya kuridhiwa na Bunge, Serikali iharakisheutungwaji wa Sheria na Kanuni zake ili wananchi wa Tanzaniawaanze kunufaika na faida zilizoainishwa kwenye mkatabahuu.

(iv) Baada ya nchi wanachama kuridhia utekelezajiwa Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe, elimu yakutosha itolewe hususan kwa wananchi waishio maeneoyampaka wa Tanzania na Malawi kuhusu utunzaji wamazingira kwenye eneo la Mto Songwe pamoja na kutumiavizuri faida zitakaopatikana kutokana na mkataba huupamoja na kutoa elimiu kuhusu mipaka ya nchi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho; mwisho, napendakukushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuwasilishamaoni ya Kamati. Aidha, sina budi kukupongeza wewe binafsipamoja na Mheshimiwa Spika na Wenyeviti wa Bunge kwakuliongoza Bunge kwa weledi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nitumie nafasi hiipia kumshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji, MheshimiwaEngineer Gerson H. Lwenge (Mbunge), pamoja na NaibuWaziri wa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Engineer Isack A.Kamwelwe (Mbunge), Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo nawatendaji wa Wizara kwa ushirikiano walioutoa wakatiKamati ilipokuwa inachambua na kujadili mkataba huu.

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee nawashukuruWajumbe wa Kamati kwa kazi nzuri ya kuupitia,kuuchambua na hatimaye kutoa maoni na ushauri waMkataba husika, naomba majina ya Wajumbe yaingizwekwenye Kumbukumbu Rasmi za Bunge kama yalivyoandikwakwenye taarifa hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile napendakuwashukuru kwa dhati watumishi wote wa Ofisi ya Bunge,chini ya Uongozi wa Dkt. Thomas D. Kashillah, Katibu waBunge, kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake.Aidha, nawashukuru Makatibu wa Kamati Ndugu RachelNyega, Ndugu Martha Chassama na Ndugu Virgil Mtuiwakisaidiwa na Msaidizi wa Kamati Ndugu Mwimbe Johnkwa kuratibu vyema kazi za Kamati na kuhakikisha Taarifahii inakamilika kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja. Ahsanteni kwa kunisikiliza. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMOMIFUGO NA MAJI KUHUSU AZIMIO LA BUNGE KURIDHIAMKATABA WA KUANZISHA KAMISHENI YA PAMOJA YA

BONDE LA MTO SONGWE KATI YA TANZANIA NA MALAWI(CONVENTION ON THE ESTABLISHMENT OF A JOINT SONGWE

RIVER BASIN COMMISSION BETWEEN TANZANIA ANDMALAWI) – KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

_______________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, kwaniaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha Maoni na Ushauri waKamati kuhusu Azimio la Bunge kuridhia Mkataba wakuanzisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto SongweKati ya Tanzania na Malawi (Convention on The Establishment

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

of a Joint Songwe River Basin Commission Between Tanzaniaand Malawi)

Mheshimiwa Spika, Nyongeza ya Nane Kifungu cha 7(1) (b)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, inazipaKamati za kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumu ya BungeKilimo, Mifugo na Maji, jukumu la kushughulikia Miswada yaSheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwana Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia. Jukumu hilipia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3) (e) ya Katibaya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Nyongeza ya NaneKifungu cha 6 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari 2016, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugona Maji inasimamia Wizara mbili ambazo zinashughulikiasekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Kanuni tajwa hapo juu,tarehe 31 Agosti, 2017 uliiletea Kamati ya Kilimo, Mifugo naMaji kazi ya kuchambua mapendekezo ya Azimio la Bungekuridhia Mkataba wa kuanzisha Kamisheni ya pamoja yaBonde la Mto Songwe kati ya Tanzania na Malawi(Convention on The Establishment of a Joint Songwe RiverBasin Commission Between Tanzania and Malawi), kamayalivyowasilishwa na Serikali ili Kamati iweze kutoa maonina ushauri kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Azimio la Bunge kuridhia Mkataba wakuanzisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto SongweKati ya Tanzania na Malawi (Convention on The Establishmentof a Joint Songwe River Basin Commission Between Tanzaniaand Malawi), liliwasilishwa mbele ya Kamati siku ya Jumatatutarehe 4 Septemba, 2017 na Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhe. Eng. Gerson H. Lwenge, Mb.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 82(2) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 inazitaka Kamatiza Bunge zinapokuwa zinashughulikia Miswada ya Sheria,Maazimio na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwa na

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Bunge ialike wadau ili kwa kutumia utaalamu wao waisaidieKamati kuchambua na kuboresha maudhuiyanayopendekezwa. Kufuatia ufinyu wa muda uliotolewakushughulikia Azimio husika, Kamati haikuweza kupatawadau wowote na hivyo kushindwa kutekeleza kanuni hiyoya Bunge. Hata hivyo, Kamati iliweza kutekeleza jukumuiliyopewa kwa niaba ya Bunge ilipitia na kuchambua Azimiotajwa na kukamilisha taarifa hii kwa wakati.

2.0 CHIMBUKO, MADHUMUNI NA FAIDA YA MKATABA WAKUANZISHA KAMISHENI YA PAMOJA YA BONDE LAMTO SONGWE

2.1 Historia fupi ya kuanza kwa Mkataba waKamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe

Mheshimiwa Spika, mchakato wa kuanzisha Kamisheni yapamoja ya Bonde la Mto Songwe ulianza Mwaka 1976,ambapo Mwaka 2004 Tanzania na Malawi zilisaini Hati yaMakubaliano ambayo pamoja na mambo mengine Hati hiyoya Makubaliano inazipa mamlaka nchi ya Tanzania naMalawi kuanzisha Kamisheni mbalimbali za pamoja,ikijumuisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Spika, kufuatia Hati hiyo ya Makubaliano,Tanzania ilishiriki kikamilifu katika majadiliano yaliyowezeshakusainiwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa uanzishwaji waKamisheni ya pamoja na Bonde la Mto Songwe na hatimaekusaini Mkataba huo katika Mji wa Lilongwe nchini Malawitarehe 18 Mei, 2017.

2.2 Madhumuni ya Mkataba wa Kamisheni ya Pamojaya Bonde la Mto Songwe

Mheshimiwa Spika, dhumuni la msingi la kuanzishwa kwaMkataba wa Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songweni kuimarisha usimamizi, uhifadhi, uendelezaji na matumiziendelevu ya rasilimali ya maji ya Mto Songwe.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Spika, kuanzishwa kwa Mkataba huu ni muhimukufuatia faida zitakazopatikana kwa nchi wananchama,kwani unalenga kuwezesha -:

i) Kutekeleza mradi wa ujenzi wa mabwawa kwa ajili yakudhibiti mafuriko ambayo huaribu kingo za mto nakusababisha mkondo wa mto kuhama na kuathiri mpakawa nchi hizi mbili;

ii) Kuanza ujenzi wa mradi wa Bwawa la Songwe Chinilitakalotumika kuzalisha umeme (Megawati 180.2), k u t o ahuduma ya maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani,viwandani, kilimo cha umwagiliaji, uvuvi, hifadhi yamazingira na utalii na hivyo kuongeza fursa za kiuchumi nakuboresha hali ya maisha ya wakazi wa eneo la Bonde; na

iii) Kuwa na chombo madhubuti kitakachoweza, pamojana kazi zingine, kutafuta rasilimali fedha kwa niaba ya nchiwanachama kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyokusudiwakatika Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Spika, pamoja na faida hizo za kiujumla,kuridhiwa kwa Mkataba huu kutakuwa na faida mbalimbalikwenye sekta nyingine kama ifuatavyo:-

KISIASA, ULINZI NA USALAMA

Mheshimiwa Spika, eneo la uwanda wa chini wa Bonde laMto Songwe limekuwa likikabiliwa na mafuriko ya mara kwamara ambayo yamekuwa yakisababisha mkondo wa mtokuhamahama na kusababisha mpaka wa nchi za Tanzaniana Malawi kuhama kila mafuriko yanapotokea. Hivyokuridhiwa kwa Mkataba huu pamoja na mambo menginekutasaidia kupata suluhisho la mpaka na kuwawezeshaWananchi wa eneo la mpakani kati ya Tanzania na Malawikupata makazi ya kudumu katika nchi zao na kuepukakuhamia nchi nyingine bila hiari yao.

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

KIUCHUMI

Mheshimiwa Spika, kuridhiwa kwa Mkataba huukutawezesha ujenzi wa bwawa la Songwe Chini, ambalomara baada ya kukamilika kwake litatumika kuzailishaumeme Megawati 180.2 ambapo fursa za kiuchumizitapatikana kutokana na umeme utakaowezeshauanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo nauvuvi. Aidha, ujenzi wa mabwawa na hifadhi ya mazingirautaongeza vivutio vya utalii na kuboresha kilimo na hivyokuongeza kipato kwa wakazi wa eneo la Bonde na Taifakwa ujumla.

HUDUMA ZA KIJAMII

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa mabwawa na uzalishaji waumeme utaboresha pia huduma za jamii kama vile upatikawa maji ya uhakika ambayo ni safi na salama, upatikanajiwa umeme wa uhakika na afya za jamii. Kuboreka kwahuduma hizi kutawasaidia wanawake kupunguza mudamrefu wanaotumia kutafuta huduma hizo na kuwawezeshakutumia muda huo kufanya shughuli zingine za uzalishaji nahivyo kuongeza kipato cha famila.

3.0 UCHAMBUZI WA MKATABA WA KUANZISHAKAMISHENI YA PAMOJA YA BONDE LA MTO SONGWE

Mheshimiwa Spika, Mkataba wa kuanzisha Kamisheni yapamoja ya Bonde la Mto Songwe una jumla ya vifungu 20.Kamati ilipitia vifungu vyote, hata hivyo taarifa ya Kamatininayoiwasilisha inataja kwa kifupi vifungu muhimu vilivyokokwenye Mkataba huu. Vifungu hivyo ni pamoja na:-

i) Kifungu cha 3; kinahusu Madhumuni na Misingi ya Kamisheni;

ii) Kifungu cha 5; kinafafanua kuhusu Mamlaka na Majukumuya Kamisheni;

iii) Kifungu cha 11; kinataja majukumu, wajibu na haki zaMsingi za kila nchi katika kutekeleza Mkataba;

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

iv) Kifungu cha 12; kinaelezea upatikanaji wa rasilimali fedhaza kuendesha Kamisheni;

v) Kifungu cha 13; kinafafanua jinsi ya kushughulikia utatuziwa migogoro endapo itatokea;

vi) Kifungu cha 16; kinahusu utaratibu wa nchi kujiondoakatika Mkataba;

vii) Kifungu cha 17; kinahusu utaratibu utakaozingatiwa nanchi katika kufanya marekebisho katika vifungu vya mkataba;na

viii) Kifungu cha 19; kinahusu sharti la kuzingatia usiri katikautekelezaji wa Mkataba

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kufanya uchambuzikwenye vifungu hivyo muhimu, Kamati ilitaka kujiridhishakwenye maeneo ya msingi na hivyo kuhitaji ufafanuzi kwenyemaeneo hayo ambayo ni pamoja na:-

i) Hatua iliyofikiwa kati ya Tanzaia na Malawi katikakushuhulikia mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa il ikujiridhisha kuwa mgogoro uliokuwepo hauwezi kuathiriutekelezaji wa Mkataba. Mantiki ya hoja hii ni kutokana naukweli kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe, na ukwelikwamba Ziwa Nyasa lina umuhimu mkubwa kwenye uchumiwa Tanzania.

ii) Ufafanuzi kuhusu namna nchi itakavyonufaika na ZiwaNyasa na Mto Songwe, na ni kwa kiasi gani utekelezaji waMkataba huu hautaathiri manufaa yaliyokuwa yakipatikanaawali.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako kuwaKamati imeridhishwa na maelezo yaliyoko kwenye Mkatabahuu pamoja na ufafanuzi uliotolewa na Serikali kuhusu hojazilizoibuliwa na Wajumbe.

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

4.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya uchambuzi waMkataba wa kuanzisha Kamisheni ya pamoja ya Bonde laMto Songwe, Kamati inatoa maoni na ushauri ufuatao:-

(i) Kwa kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe,na kwakuwa mkataba huu unahusisha nchi za Tanzania na Malawiambazo zimekuwa na mgogoro wa mara kwa mara kuhusumpaka wa Ziwa Nyasa, Kamati inaishauri Serikali kuchukuwataadhari na kuhakikisha utekelezaji wa mkataba huuhautaathiri faida ambazo nchi imekuwa ikipata kutoka ZiwaNyasa na Mto Songwe.

(ii) Kwa kuwa nchi ya Tanzania na Malawi zimekuwa namgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kwa muda mrefu, nakwa kuwa uhai wa Ziwa Nyasa ni Mto Songwe, pamoja nakwamba mkataba huu unahusu Mto Songwe, Kamatiinaishauri Serikali kupitia fursa ya Mkataba huu kufanyautambuzi wa Mipaka ya Ziwa Nyasa hatua ambayo inawezakumaliza kabisa tatizo la mgogoro wa mpaka wa ZiwaNyasa.

(iii) Kwa kuwa Mkataba huu unahusisha nchi mbili ni vyemabaada ya kuridhiwa na Bunge, Serikali iharakishe utungwajiwa Sheria na Kanuni zake ili wananchi wa Tanzania waanzekunufaika na faida zilizoainishwa kwenye mkataba huu.

(iv) Baada ya nchi wanachama kuridhia utekelezaji waKamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe, elimu yakutosha itolewe hususan kwa wananchi waishio maeneoya mpaka wa Tanzania na Malawi kuhusu utunzaji wamazingira kwenye eneo la Mto Songwe pamoja na kutumiavizuri faida zitakaopatikana kutokana na mkataba huupamoja na kutoa elimu kuhusu mipaka ya nchi hizo.

5.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kukushukuru wewebinafsi, kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha maoni ya Kamati.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

Aidha, sina budi kukupongeza wewe binafsi MheshimiwaSpika, Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwakuliongoza Bunge kwa weledi.

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii piakumshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mheshimiwa Eng.Gerson H. Lwenge, Mb pamoja na Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji Mhe. Eng. Isack A. Kamwele, Mb, Katibu MkuuDkt. Kitila Mkumbo na Watendaji wa Wizara kwa ushirikianoalioutoa wakati Kamati ilipokuwa inachambua na kujadiliMkataba huu.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru Wajumbe waKamati kwa kazi nzuri ya kuupitia, kuuchambua na hatimayekutoa maoni na ushauri wa Mkataba husika, naomba majinaya Wajumbe yaingizwe kwenye Kumbukumbu Rasmi zaBunge kama yalivyoorodheshwa hapa chini.

1. Mhe. Dkt. Michael M. Nagu, Mb Mwenyekiti2. Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma,Mb M/Mwenyekiti3. Mhe. Dkt. Immaculate Sware Semesi, Mb Mjumbe4. Mhe. Mahmoud H. Mgimwa, Mb “5. Mhe. Salum Mwinyi Rehani, Mb “6. Mhe. Khadija Hassan Aboud, Mb “7. Mhe. Marwa Ryoba Chacha, Mb “8. Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki, Mb“9. Mhe. Mattar Ali Salum, Mb “10. Mhe. John John Mnyika, Mb “11. Mhe. Hamidu Hassan Bobali, Mb “12. Mhe. James Kinyasi Millya, Mb “13. Mhe. Njalu Daudi Silanga, Mb “14. Mhe. Pascal Yohana Haonga, Mb “15. Mhe. Salim Mbaraku Bawazir Mb “16. Mhe. Deo Kasenyenda Sanga, Mb “17. Mhe. Abdallah Hamis Ulega, Mb “18. Mhe. Haji Ameir Haji, Mb “19. Mhe. Daniel N. Nsanzugwanko, Mb “20. Mhe. Philipo Augustino Mulugo, Mb “21. Mhe. Upendo Furaha Peneza, Mb “22. Mhe. Emmanuel Papian John, Mb “

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

23. Mhe. Kunti Yusuph Majala, Mb “24. Mhe. Oliver Daniel Semuguruka “

Mheshimiwa Spika, vilevile napenda kuwashukuru kwa dhatiWatumishi wote wa Ofisi ya Bunge, chini ya Uongozi wa Dkt.Thomas D. Kashillah - Katibu wa Bunge, kuiwezesha Kamatikutekeleza majukumu yake. Aidha, nawashukuru Makatibuwa Kamati Ndg. Rachel Nyega, Ndg. Martha Chassama naNdg. Virgil Mtui wakisaidiwa na Msaidizi wa Kamati Ndg.Mwimbe John kwa kuratibu vyema kazi za Kamati nakuhakikisha Taarifa hii inakamilika kwa wakati .

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono Hoja.

Dkt. Christine Ishengoma, MbM/MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI7 SEPTEMBA, 2017

NAIBU SPIKA: Sasa tutamsikia msemaji wa KambiRasmi ya Upinzani, kwenye Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

MHE. HAMIDU H. BOBALI – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA MAJI NAUMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwakunipa fursa hii ili niweze kuwasilisha kwa ufupi sana maoniya Kambi Rasmi ya Upinzani, Kuhusu Azimio Kuridhia Mkatabawa Uanzishwaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la MtoSonngwe kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi (The Conventionon the Establishment of a Joint Songwe River Basin CommissionBetween the Government of The United Republic of TanzaniaAnd The Government of The Republic of Malawi)yanayotolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 86(6) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kubwanaomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu na

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

afya nzuri inayoniwezesha kusimama mbele ya ukumbi huuna kuweza kutoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzanikuhusiana na azimio hili. Aidha, nitoe shukrani kwa wananchina wanachama wote wa Chama cha Wananchi (CUF) kwaimani yao kwangu na kwa chama chetu katika kuhakikishakuwa tunapambana kwa nguvu zote ili kushinda nguvu zaaina yoyote kutoka nje ya chama chetu zinazokusudiakukidhuru na kukihujumu chama chetu kil ichobebamatumaini ya Watanzania wapenda mabadiliko nademokrasia ndani ya ushirikiano madhubuti ujulikanao kamaUKAWA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitakuwa si mwingi wafadhila kama sita mshukuru Naibu wangu, Mheshimiwa PeterAmbrose Lijualikali kwa msaada wake katika maandalizi yamaoni haya. Sambamba na hili niwashukuru waheshimiwawajumbe wenzangu wote wa Kamati ya Kilimo, Mifugo, Majina Uvuvi kwa ushirikiano mkubwa tulionao ndani ya Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kutoa utangulizihuo, naomba kuelezea baadhi ya mambo ambayo kwamtazamo wetu tumeona yanahitaji kupatiwa maelezo yakina na Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Azimio la Bungelinavyosema kwamba Bonde la Mto Songwe ndilo linalofanyampaka kati ya Tanzania na nchi ya Malawi na Wilaya za Kyela,Ileje, Mbozi Mbeya Vijijini na Momba zimo ndani ya Bondehilo. Kutokana na ukweli kwamba mto huo umekuwaukihama hama na hivyo kusababisha mpaka baina ya nchihizi nao kuhama hama jambo ambalo linaweza kusababishamtafaruku na jirani zetu hao.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya MheshimiwaWaziri aliyoileta kwenye kamati inaonesha kuwa Tanzaniana Malawi zinatekeleza Mradi wa Kudhibiti Mkondo wa MtoSongwe (Stabilization of the Course of Songwe River Project)kwa kujenga Bwawa la Songwe Chini ambalo litajengwabaada ya kusainiwa Mkataba huu na bwawa hilo litatumikakuzalisha umeme wa Megawati 180.2, kutoa huduma ya maji

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

kwa ajili ya matumizi ya majumbani, viwandani, kilimo chaumwagiliaji, uvuvi, hifadhi ya mazingira na utalii na hivyokuongeza fursa za kiuchumi na kuboresha hali za maisha yawakazi wa eneo la Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo hayo niliyosomayameelezwa kwenye Ibara ya 8 ya mkataba kuwa ni baadhiya kazi za Kamati ambayo inaundwa chini ya Ibara ya Nneya Mkataba. Kazi hizo za Kamati kama ilivyoundwa chini yaibara tajwa zitatekelezwa na kusi mamiwa na sekretarietiinayoanzishwa na Ibara ya nne. Ibara ya Tisa inaainishamajukumu ya Sekretariat, pamoja na majukumu mengineIbara ya 9(6)(g) kinasema kwamba:-

“Manage on daily basis the construction, operationand maintenance of all infrastructure under Songwe River BasinDevelopment Programme, including flood warning,hydropower, irrigation systems and operation of the dam;social infrastructure and regularly obtain, update andexchange information and data as necessary, including thedevelopment and use of decision support system.”

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu hicho kinaoneshakuwa kazi hizo zote zinatakiwa zifanywe na sekretarieti, lakinitukumbuke kwamba ustawi wa wananchi katika wilayahusika utakuwepo kama wananchi mmoja mmoja au kwavikundi vyao au kampuni zao (local content) watanufaikakwa kuwa wamiliki katika miradi itakayoanzishwa naKamisheni hiyo. Sambamba na hilo ni kwamba, ushiriki huowa wananchi utawezekana kwa sheria yetu ya PPP kati yaKamisheni na wananchi (sekta binafsi).

Mheshimiwa Naibu Spika, japokuwa Ibara ya 18inaongelea mawanda ya mkataba ni kwamba washirika wamkataba wanaweza kuingia mkataba baina au ya kimataifakwa aji l i ya utekelezaji wa miradi au programuzitakazotakiwa kutekelezwa na Kamisheni. Kambi Rasmi yaUpinzani inasema bado Ibara hiyo haijatoa uhakika waushiriki wa wanufaikaji katika kumiliki na kutekeleza miradihusika.

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli ulio wazi kwamba,miradi mingi ambayo ilianzishwa na Serikali kwa ufadhili kwaajili ya wananchi imekufa kutokana na kutokuwepo kwadhana ya umiliki kutoka upande wa wanufaikaji, wananchi.Tukumbuke kwamba, watangulizi wa Serikali hii ya Awamuya Tano waliliona hilo na ndio sababu ya ubinafsishajijapokuwa kutokufanya vizuri kwa ubinafsishaji haikuwa nidhana hiyo, bali utekelezaji wake. Kushindwa kwakekulitokana na ulegelege na kutowajibika ipasavyo kwawahusika waliokuwa wasimamizi wa zoezi hilo la ubinafsishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinashauri kwamba, kwa kuwa, moja ya lengo la uundwajiwa Kamisheni hii ni utumiaji endelevu (sustainable) warasilimali ya maji kwa wananchi wa Wilaya tajwa hapo awali,hivyo basi ni lazima ushiriki wa wananchi uonekane wazikwenye mkataba huu il i sheria zetu za utekelezajizitakapotungwa domestication, vipengele vya uhusishwajiwa wananchi kwenye maeneo tajwa uakisiwe kwenye sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, kinyume cha hapo, KambiRasmi ya Upinzani inaona kwamba, Kamisheni hii namalengo yake hayatakuwa na manufaa kwa maendeleoya wananchi hasa wa maeneo husika, bali itakuwa kamamamlaka ya uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji ambalobadala ya kuwa mkombozi au mleta kicheko kwa wananchiwa maeneo husika imekuwa ndio mleta kilio kwa wananchina hivyo, Taifa kuendelea kubaki kuwa mtazamaji tu warasilimali hiyo adhimu, bila kunufaika nayo. Serikali kuachakulifanyia kazi stahiki Bonde la Mto Rufiji ni muendelezo wakutotumia vizuri rasilimali zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli kabisa kuwa hiiKamisheni sio kama itajikita kwenye maji tu, bali ni kweli ardhiambayo wakulima wengi wanaendesha shughuli za maishayao ya kila siku. Kwa maana hiyo, basi ni muhimu MheshimiwaWaziri akaweka wazi kuhusiana na mfumo mzima wa vibalivya matumizi ya ardhi hiyo ambayo imo ndani ya himaya yaKamisheni. Kwa maana nyingine ni kwamba, maisha yawananchi wa Wilaya husika yataathirika kwa kiwango

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

kikubwa sana. Jambo hilo pia, lifanywe kwa kuzingatia sualazima la usalama wa Taifa letu. Kamisheni ni vema pia,ikahusisha Idara zetu zinazohusika na ulinzi na usalama waTaifa kwani isije ikatumika kama ndio ufunguaji wa mipakayetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayamafupi, Kambi Rasmi ya Upinzani haioni sababu yakutokuridhia Azimio la Kuridhia Mkataba wa Kuanzishwa kwaKamisheni hii ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU AZIMIO LAKURIDHIA MKATABA WA UANZISHWAJI WA KAMISHENI YA

PAMOJA YA BONDE LA MTO SONGWE KATI YA SERIKALI YAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA

JAMHURI YA MALAWI (CONVENTION ON THE ESTABLISHMENTOF A JOINT SONGWE RIVER BASIN COMMISSION BETWEENTHE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAAND THE GOVERNMENT OF THE REPUBLIC OF MALAWI) –

KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

“Yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Bunge,Toleo la Januari, 2016”

Mheshimiwa Spika,Kwa heshima kubwa naomba nimshukuru Mwenyezi Mungukwa kunipa nguvu na afya nzuri inayoniwezesha kusimamambele ya ukumbi huu na kuweza kutoa maoni ya KambiRasmi ya Upinzani kuhusiana na azimio hili. Aidha, nitoeshukrani kwa wananchi na wanachama wote wa chamacha wananchi-CUF kwa imani yao kwangu na kwa chamachetu katika kuhakikisha kuwa tunapambana kwa nguvuzote ili kushinda nguvu za aina yoyote kutoka nje ya chamachetu zinazokusudia kukidhuru na kukihujumu chama chetu

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

kilichobeba matumaini ya watanzania wapenda mabadilikona demokrasia ndani ya ushirikiano madhubuti ujulikanaokama UKAWA.

Mheshimiwa Spika,Nitakuwa si mwingi wa fadhila kama sita mshukuru Naibuwangu, Mheshimiwa Peter Lijualikali kwa msaada wakekatika maandalizi ya maoni haya, sambamba na hiliniwashukuru waheshimiwa wajumbe wenzangu wote waKamati ya Kilimo, Mifugo, Maji na Uvuvi kwa ushirikianomkubwa tulionao ndani ya kamati.

Mheshimiwa Spika,Baada ya kutoa utangulizi huo, naomba kueleza baadhi yamambo ambayo kwa mtazamo wetu tumeona yanahitajikupatiwa maelezo ya kina na Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika,Kama azimio la Bunge linavyosema kwamba Bonde la MtoSongwe ndilo linalofanya mpaka kati ya Tanzania na Nchiya Malawi na wilaya za Kyela, Ileje, Mbozi Mbeya Vijijini naMomba zimo ndani ya Bonde hilo. Kutokana na ukwelikwamba mto huo umekuwa ukihama hama na hivyokusababisha mpaka baina ya nchi hizi nao kuhama hama,jambo ambalo linaweza kusababisha mtafaruku na jirani zetuhao.

Mheshimiwa Spika,Taarifa ya Mheshimiwa Waziri aliyoileta kwenye kamatiinaonesha kuwa Tanzania na Malawi zinatekeleza Mradi wakudhibiti Mkondo wa Mto Songwe (Stabilization of the Courseof Songwe River Project) kwa kujenga Bwawa la SongweChini ambalo litajengwa baada ya kusainiwa Mkataba huuna bwawa hilo litatumika kuzalisha umeme wa Megawati180.2, kutoa huduma ya maji kwa ajili ya matumizi yamajumbani, viwandani, kilimo cha umwagiliaji, uvuvi, hifadhiya mazingira na utalii na hivyo kuongeza fursa za kiuchumina kuboresha hali za maisha ya wakazi wa eneo la Bonde lamto Songwe.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Mheshimiwa Spika,Maelezo hayo niliyosoma yameelezwa kwenye Ibara ya 8 yamkataba kuwa ni baadhi ya kazi za Kamati ambayoinaundwa chini ya Ibara ya 4 ya Mkataba.

Mheshimiwa Spika,Kazi hizo za Kamati kama ilivyoundwa chini ya ibara tajwayanatekelezwa na kusimamiwa na Secretariat inayoanzishwana Ibara ya 4, Ibara ya 9 inaainisha majukumu ya Sekretariat,pamoja na majukumu mengine Ibara ya 9, kifungu cha 6(g)kinasema kwamba:

“ Manage on daily basis the construction, operation andmaintenance of all infrastructure under Songwe River BasinDevelopment Programme, including flood warning,hydropower, irrigation systems and operation of the dam;social infrastructure and regularly obtain, update andexchange information and data as necessary, including thedevelopment and use of decision support system;”

Mheshimiwa Spika,Kifungu hicho kinaonesha kuwa kazi hizo zote zinatakiwazifanywe na Secretariat, lakini tukumbuke kwamba ustawiwa wananchi katika wilaya husika utakuwepo kamawananchi mmoja mmoja au kwa vikundi vyao au Kampunizao (Local Content) wapanufaika kwa kuwa wamiliki katikamiradi itakayoanzishwa na Kamisheni hiyo. Sambamba nahilo ni kwamba ushiriki huo wa wananchi utawezekana kwasheria yetu ya PPP kati ya Kamisheni na wananchi (Sektabinafsi).

Mheshimiwa Spika,Japokuwa Ibara ya 18 inaongelea mawanda ya Mkataba nikwamba washirika wa mkataba wanaweza kuingiamkataba baina au ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji wamiradi au programe zitakazotakiwa kutekelezwa naKamisheni. Kambi Rasmi ya Upinzani inasema bado Ibara hiyohaijatoa uhakika wa ushiriki wa wanufaikaji katika kumilikina kutekeleza miradi husika.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Spika,Ni ukweli uliowazi kwamba miradi mingi ambayo ilianzishwana Serikali kwa ufadhili kwa ajili ya wananchi imekufakutokana na kutokuwepo kwa dhana ya umiliki kutokaupande wa wanufaikaji(wananchi), na tukumbuke kwambawatangulizi wa Serikali hii ya tano waliliona hilo na ndiosababu ya ubinafsishaji japokuwa kutokufanya vizuri kwaubinafsishaji hakukuwa ni dhana hiyo bali utekelezaji wake.Kushindwa kwake kulitokana na ulegelege na kutowajibikaipasavyo kwa wahusika waliokuwa wasimamizi wa zoezi hilola ubinafsishaji

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kwamba kwa kuwa mojaya lengo la uundwaji wa Kamisheni hii ni utumiajiendelevu(sustainable) wa raslimali ya maji kwa wananchiwa wilaya tajwa hapo awali, hivyo basi ni lazima ushiriki wawananchi uonekane wazi kwenye Mkataba huu ili sheria zetuza utekelezaji zitakapotungwa(domestication), vipengelevya uhusishwaji wa wananchi kwenye maeneo tajwauakisiwe kwenye sheria.

Mheshimiwa Spika,Kinyume cha hapo Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwambaKamisheni hii na malengo yake hayatakuwa na manufaa kwamaendeleo ya wananchi hasa wa maeneo husika, baliitakuwa kama mamlaka ya uendelezaji wa Bonde la MtoRufiji ambayo badala ya kuwa mkombozi au mleta kichekokwa wananchi wa maeneo husika imekuwa ndio mleta kiliokwa wananchi na hivyo Taifa kuendelea kubaki kuwawatazamaji tu wa raslimali hiyo adhimu bila kunufaika nayo.Serikali kuacha kulifanyia kazi stahiki Bonde la Mto Rufiji nimuendelezo wa kutotumia vizuri rasilimali zetu.

Mheshimiwa Spika,Ni ukweli kabisa kuwa hii kamisheni sio kama inajikita kwenyemaji tu, bali ni kweli ardhi ambayo wakulima wengiwanaendesha shughuli za maisha yao ya kila siku. Kwamaana hiyo basi ni muhimu Mheshimiwa Waziri akaweka wazikuhusiana na mfumo mzima wa vibali vya matumizi ya ardhi

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

hiyo ambayo imo ndani ya himaya ya kamisheni. Kwa maananyingine ni kwamba maisha ya wananchi wa wilaya husikayataathirika kwa kiwango kikubwa sana. Jambo hilo pialifanywe kwa kuzingatia pia suala zima la usalama wa taifaletu. Kamisheni ni vyema pia idara zetu zinazohusika na ulinzina usalama wa Taifa kwani isije ikatumika kama ndioufunguaji wa mipaka yetu.

Mheshimiwa Spika,Baada ya kusema hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani hainasababu ya kutokuridhia azimio la kuridhia Mkataba waKuanzishwa kwa Kamisheni hii ya pamoja ya Bonde la MtoSongwe.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

………………………Hamidu H.Bobali (Mb)

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani-Wizara yaMaji na Umwagiliaji.

7/9/2017

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea.Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

AZIMIO LA BUNGE

Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African

Community Protocol on Peace and Security)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza naomba maelezo yote niliyoyaleta kwaajili ya Azimio hili yaingie kwenye Hansard.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupatafursa hii ili jiweze kuwasilisha mapendekezo ya kuridhia Itifakiya Amani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (TheEast African Community Protocol on Peace and Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na mkataba wakuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Mwaka 1999pamoja na marekebisho yake, hatua nne za mtangamanoambazo ni kuwepo kwa umoja wa forodha, ikifuatiwa nasoko la pamoja, kisha umoja wa fedha na hatimaye shirikishola kisiasa, vilipangiliwa. Aidha, Ibara ya 124 ya mkataba huoinaelezea kuwa nchi wanachama zimekubaliana kuwaamani na usalama ndio nguzo kuu ya maendeleo yakiuchumi na kijamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Ibara ya 151 yamkataba huo inatoa mamlaka kwa nchi wanachamakuandaa na kuridhia itifaki katika maeneo mbalimbali yaushirikiano. Ili kuweza kutekelezwa kwa itifaki iliyoidhinishwani lazima nchi zote wanachama kuridhia, kulingana nataratibu za ndani ya nchi husika na kisha kuwasilisha hati zakuridhia kwa itifaki hizo kwa Katibu Mkuu wa Jumuya ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Itifaki ya Amani na Usalamaya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The East African Protocol onPeace and Security) iliidhinishwa kwa Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutanouliofanyika Novemba mwaka 2012 na kisha kusainiwa naMawaziri wa nchi tano wanachama wa Jumuiya ja AfrikaMashariki, tarehe 15 mwezi wa Februari, 2013. Mpaka sasanchi tatu ambazo ni Kenya, Rwanda na Uganda zimeridhiaitifaki hiyo kulingana na matakwa ya mkataba, Ibara ya 152niliyoitaja.

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

Mheshimiwa Naibu Spika, vipengele muhimu vyaushirikiano vimeainishwa kwenye Ibara ya Pili Na. (2), (3) nipamoja na kuzuia na kutatua migogoro ya ndani ya nchi nanje ya nchi wanachama ambapo nchi wanachamazimekubaliana kutatua migogoro itakayojitokeza namiongoni mwao ni pamoja na kushughulikia matatizoyanayojitokeza na kuleta mauaji ya kimbari, kupambana naugaidi, kupambana na uharamia, kushiriki katika operesheniza kulinda amani, kukabiliana na kupunguza madharayanayotokana na majanga ambapo nchi wanachamazimekubaliana kuanzisha mifumo ya kupashana taarifa zamajanga il i kupunguza au kukabiliana nayo kablahayajajitokeza ili kutoleta madhara.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kusimamiamasuala ya wakimbizi kwa nchi wanachama, kuhuisha sera,sheria na mikakati na programu zinazosimamia masuala yawakimbizi kulingana na makubaliano ya Mkataba wa Umojawa Mataifa wa Wakimbizi wa Mwaka 1951 na Mkataba waUmoja wa Nchi za Afrika wa Mwaka 1969 unaohusu matatizoya wakimbizi Barani Afrika. Aidha, kuoanisha taratibu juu yakutafuta na kuhifadhi wahusika wanaoshughulikia upashanajiwa habari katika masuala ya mitandao.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengine muhimuya itifaki hii ni kudhibiti uzagaaji wa silaha haramundogondogo na nyepesi, kukabiliana na uhalifu wa Kimataifana uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kuzuia nakupambana na wizi wa mifugo na utoaji wa hudumaMagerezani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuridhia itifaki hiikutarahisisha uainishaji wa sera, sheria, programu za ndaniya Jumuiya zenye uwiano katika masuala ya amani nausalama. Kuwepo kwa mazingira mazuri ya amani nausalama hivyo, kuwezesha wananchi kufanya shughuli zaoza kiuchumi na za kijamii bila kuwa na hofu. Kingine nikujenga mazingira ya ujirani mwema kwa jamii za wafugajiwa ndani ya nchi pamoja na jamii zao ambazo wanafanya

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

shughuli zinazowiana ikiwemo pia na kuimarisha ushirikianokatika kupambana na kuondoa wizi wa mifugounaojitokeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuimarisha nakuimarika kwa uzoefu na pia, nchi zitaweza kuwa na mpangowa kubadilishana wafungwa; nchi zitaweza kutunga sheriana kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha amani nausalama wa nchi wanachama na makosa yanayovukamipaka yatadhibitiwa kwa pamoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya haya maelezoya utangulizi, naomba sasa kuwasilisha Azimio lenyewe kwaBunge ili liweze kuridhiwa, kama ifuatavyo:-

KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimiongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki, kwa mujibu wa Ibara ya 3(1) cha Mkatabaulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulisainiwa naWakuu wa nchi wanachama uliofanyika Mjini Arusha tarehe30 Novemba,1999;

NA KWA KUWA, Ibara ya 151 ya Mkataba huo waUanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatoa mamlakakwa Nchi Wanachama kuandaa na kuridhia itifaki katikamaeneo mbalimbali ya ushirikiano ili kuleta maendeleo yakiuchumi na kijamii katika Jumuiya;

NA KWA KUWA, mkataba huo unaelekeza kwambakila itifaki itakayoandaliwa itaidhinishwa na Mkutano waWakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikina itakuwa wazi kwa ajili ya kusainiwa na hatimaye kuridhiwana nchi wanachama kwa mujibu wa taratibu zao;

NA KWA KUWA, Itifaki ya Amani na Usalama waJumuiya ya Afrika Mashariki iliidhinishwa na Mkutano Mkuuwa 14 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2012 Mjini Nairobi,Kenya na kusainiwa na Mawaziri kutoka katika nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 15

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Februari, 2013 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniani mojawapo ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki iliyosaini Itifaki hii;

NA KWA KUWA, lengo la Itifaki hii ni kuimarisha amanina usalama na utulivu katika Jumuiya ya Afrika Masharikipamoja na kukuza ujirani mwema kwa nchi wanachama.

NA KWA KUWA, kwa kujiunga kwa Itifahi hii yaJumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania itaimarisha ushirikianowake na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikikatika kutatua migogoro mbalimbali katika Jumuiya ya AfrikaMashariki hivyo, kuimarisha ujirani mwema, kuwepo kwaamani na usalama kutokana na kubadilishana taarifa zauhalifu na uhalifu unaovuka mipaka, kupata taarifa zakuibuka kwa makosa mapya, kuimarisha mapambano dhidiya ugaidi, dawa za kulevya, biashara haramu za binadamu,kuenea kwa silaha haramu ndogondogo na nyepesi, wizi wamitandaoni na vilevile kusaidia katika kubadilishana ujuzi nauzoefu katika kubadilishana wahalifu.

HIVYO BASI, kwa kuzingatia manufaa yatakayotokanana itifaki hii kwa Tanzania na pia, umuhimu wa kuridhia itifakihii, Bunge hili katika Mkutano wake wa Nane kwa mujibuwa Ibara ya 63(3)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia Itifaki hii iitwayoItifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(The East African Community Protocol on Peace and Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

MAELEZO YA UTANGULIZI YA KURIDHIA ITIFAKI YA AMANINA USALAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAST

AFRICAN COMMUNITY PROTOCOL ON PEACE AND SECURITY)KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa hiiniweze kuwasilisha mapendekezo ya ya kuridhia Itifaki yaAmani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani EastAfrican Community Protocol on Peace and Security.

Mheshimiwa Spika, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Kulinganana Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki wamwaka 1999 pamoja na marekebisho yake umeainisha hatuanne za Mtangamano ambazo ni kuwepo kwa Umoja waForodha ikifuatiwa na Soko la Pamoja kisha Umoja wa Fedhana hatimaye Shirikisho la Kisiasa. Aidha, Ibara ya 124 yaMkataba huo inaeleza kuwa nchi wanachamazimekubaliana kuwa Amani na Usalama ndiyo nguzo kuu yamaendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Jumuiya. Kwamsingi huo, nchi wanachama zimekubaliana kujenga nakuimarisha mazingira mazuri ya amani na usalama kwakushirikiana katika nyanja hiyo kwa lengo la kuzuia uhalifuna kutatua migogoro itakayojitokeza kwa njia ya amani,kuimarisha ujirani mwema, kuandaa mfumo wa pamoja wamenejimenti ya wakimbizi na kuimarisha mfumo wakupambana na wahalifu wa kimataifa.

Mheshimiwa Spika, vile vile, Ibara ya 151 ya Mkataba inatoamamlaka kwa nchi wanachama kuandaa na kuridhia Itifakikatika maeneo mbalimbali ya ushirikiano. Ili kutekelezwa kwaitifaki iliyoidhinishwa ni lazima nchi zote wanachama kuiridhiakulingana na taratibu za ndani za nchi husika na kishakuwasilisha Hati ya kuridhia Itifaki hiyo kwa Katibu Mkuu waJumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiyaya Afrika Mashariki yaani iliidhinishwa na Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutanouliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kisha kusainiwa na

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

mawaziri wa nchi tano wanachama wa Jumuiya kwa wakatihuo tarehe 15 Februari, 2013. Mpaka sasa nchi tatu ambazoni Kenya, Rwanda na Uganda zimeridhia Itifaki hiyo kulinganana matakwa ya Ibara ya 152 ya Mkataba.

Mheshimiwa Spika, Vipengele muhimu vya ushirikianoyameainishwa kwenye Ibara ya 2(3) ni pamoja na Kuzuia nakutatua migogoro ndani na nje ya nchi wanachamaambapo nchi Wanachama zimekubaliana kutatua migogoroitakayojitokeza miongoni mwao au na nchi nyingine kwanjia ya amani. Vile vile, Jumuiya imekubaliana kushirikianana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (United NationsSecurity Council) na Baraza la Amani na Usalama la Umojala Afrika (Peace and Security Council of the African Union)katika kutatua migogoro ya nchi mwanachama au nchinyingine kwa njia ya Amani.

Mheshimiwa Spika, itifaki hii imekusudia kuzuia mauaji yakimbari, Kupambana na ugaidi, Kupambana na uharamia,Kushiriki katika operesheni za kulinda amani, Kukabiliana nakupunguza madhara yatokanayo na majanga ambapo nchiwanachama zimekubaliana kuanzisha mifumo ya kupashanataarifa za majanga ili kupunguza au kukabiliana nayo kablahayajajitokeza na kuleta madhara, Kusimamia masuala yaWakimbizi kwa nchi wanachama kuhuisha Sera, Sheria,Mikakati na Programu za usimamizi wa masuala ya wakimbizikulingana na makubaliano ya Mkataba wa Umoja waMataifa wa Wakimbizi wa mwaka (1951) na Mkataba waUmoja wa nchi za Afrika wa mwaka (1969) unaohusu matatizoya wakimbizi barani Afrika. Aidha, kuoanisha taratibu juu yawatafuta hifadhi kwa kuwa na mitandao ya kupashanataarifa.

Mheshimiwa Spika, maeneo mengine muhimu ya itifaki hii niKudhibiti uzagaaji wa silaha haramu ndogondogo na nyepesi,kukabiliana na uhalifu wa kimataifa na uhalifu unaovukawa mipaka,Kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo naUtoaji wa huduma za Magereza.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Mheshimiwa Spika, kuridhia itifaki hii kutarahisisha uainishajiwa Sera, Sheria na Programu za ndani ya Jumuiya zenyeuwiano katika masuala ya amani na Usalama, Kuwepo kwamazingira mazuri ya amani na usalama hivyo kuwawezeshawananchi kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii bila hofu,Kujenga mazingira ya ujirani mwema kwa jamii za wafugajindani ya Jumuiya, Kuimarisha ushirikiano katika kupambanana kuondoa wizi wa mifugo, kuimarika kwa uzoefu na pianchi zitaweza kuwa na mpango wa kubadilishanawafungwa, nchi zitatunga sheria na kuweka mikakati yapamoja ya kuimarisha Amani na Usalama wa nchiwanachama na Makosa yanayovuka mipaka yatadhibitiwakwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya, sasa naombakuwasilsha Azimio la Bunge la kuridhia kama ifuatavyo:-

AZIMIO LA BUNGE NA. ............................. LA MWAKA 2017

AZIMIO LA KURIDHIA ITIFAKI YA AMANI NA USALAMA YAJUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN

COMMUNITY PROTOCOL ON PEACE AND SECURITY)______________

KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongonimwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (TheEast African Community - EAC) kwa mujibu wa Ibara ya 3(1)ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaoulisainiwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa EACuliofanyika mjini Arusha, tarehe 30 Novemba, 1999;

NA KWA KUWA, Ibara ya 151 ya Mkataba huo wa Uanzishwajiwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 1999 (The Treatyfor the Establishment of the East African Community) inatoamamlaka kwa nchi wanachama kuandaa na kuridhia Itifakikatika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ili kuleta maendeleoya kiuchumi na kijamii katika Jumuiya;

NA KWA KUWA, Mkataba huo unaelekeza kwamba kila Itifakiitakayoandaliwa itaidhinishwa na Mkutano wa Wakuu wa

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na itakuwawazi kwa ajili ya kusainiwa na hatimaye kuridhiwa na NchiWanachama kwa mujibu wa taratibu zao;

NA KWA KUWA, Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya yaAfrika Mashariki (East African Community Protocol on Peaceand Security) iliidhinishwa na Mkutano Wakuu 14 wa Wakuuwa Nchi Wanachama wa EAC uliofanyika tarehe 30Novemba, 2012 mjini Nairobi Kenya na kusainiwa na Mawazirikutoka nchi wanachama wa Jumuiya tarehe 15 Februari,2013 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimojawapo ya Nchi Wanachama wa EAC iliyosaini Itifaki hii;

NA KWA KUWA, Lengo la Itifaki hii ni kuimarisha amani,usalama na utulivu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki pamojana kukuza ujirani mwema kwa nchi wanachama;

NA KWA KUWA, Kwa kujiunga na Itifaki hii Jamhuri yaMuungano waTanzania itaimarisha ushirikiano wake na nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutatuamigogoro mbalimbali katika Jumuiya na hivyo kuimarishaujirani mwema, kuwepo na amani na usalama kutokanakubadilishana taarifa za uhalifu na uhalifu unaovuka mipaka,kupata taarifa za kuibuka kwa makosa mapya, kuimarishamapambano dhidi ya ugaidi, dawa za kulevya, biasharaharamu ya binadamu, kuenea kwa silaha haramu ndogondogo na nyepesi, wizi wa mtandaoni na vilevile kusaidiakatika kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kukabiliana nauhalifu;

HIVYO BASI, Kwa kuzingatia manufaa yatokanayo na Itifakihii kwa Tanzania na pia umuhimu wa kuridhia Itifaki hii, Bungehili katika Mkutano wa nane na kwa mujibu wa Ibara ya63(3) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yamwaka, 1977 linaazimia kuridhia Itifaki hii iitwayo ITIFAKI YAAMANI NA USALAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI(EAST AFRICAN COMMUNITY PROTOCOL ON PEACE ANDSECURITY)

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

NAIBU SPIKA: Tutaendelea na utaratibu wetu. Sasatutamsikia Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzina Usalama.

MHE. STEPHEN J. MASELE (K.n.y. MHE. BAL. ADADI M.RAJABU - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZINA USALAMA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba yaKamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoamaoni na ushauri wa Kamati kuhusu Azimio la Bunge laKuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya AfrikaMashariki (The East African Community Protocol on Peaceand Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya53(6),(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016, kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naombakuwasilisha maoni na ushauri wa Kamati kuhusu Itifaki yaAmani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EastAfrican Community Protocol on Peace and Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, Nyongeza ya Nane yaKifungu cha 7(1)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari, 2016 inazipa Kamati za kisekta ikiwemo Kamati hiijukumu la kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikatabainayopendekezwa, kuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizarainazozisimamia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sambamba na hilo, jukumuhili pia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3)(e) ya Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha,kwa mujibu wa kifungu cha 6(3) cha Nyongeza ya Nane yaKanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumuya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inasimamia Wizara tatuambazo ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, masuala yaliyomo katikaitifaki hii yanazigusa moja kwa moja Wizara hizi.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mheshimiwa Naibu Spika, mnamo 5 Septemba, 2017,Kamati yangu ilikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba na kupokeamaelezo ya Serikali kuhusu chimbuko, vipengele vya muhimuna faida ya kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiyaya Afrika Mashariki. Baada ya maelezo hayo, Kamati ilipatafursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hoja hiyo ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo ya msingiyaliyozingatiwa na Kamati. Kwa kuzingatia wajibu wa Kamatikuliwezesha Bunge kutekeleza madaraka yake ipasavyo,Kamati ilizingatia masuala mbalimbali katika kujiridhisha nahoja iliyotolewa na Serikali. Kamati ilifanya mapitio yamkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Mwaka1999 ambapo Ibara ya 124 ya mkataba huo inaeleza kuwanchi wanachama zimekubaliana kuwa amani na usalamawa Kanda ya Afrika Mashariki ndiyo nguzo ya maendeleo yakiuchumi na kijamii katika Jumuiya hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Aidha, Kamati ilijiridhishakuwa Ibara ya 151 ya mkataba huo, inatoa mamlaka kwanchi wanachama kuandaa, kuridhia itifaki, katika maeneombalimbali ya ushirikiano likiwemo suala la amani nausalama. Itifaki iliyoridhiwa kwa mujibu wa Ibara ya 124 naIbara ya 151 ya mkataba huo inakuwa ni sehemu ya mkatabana hivyo kuweka misingi ya kisheria na kuilazimisha nchimwanachama kuitekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Kamati ilijiridhishakuhusu muda kipindi ambacho itifaki hii ilisainiwa na nchiwanachama. Katika kufanya hivyo, Kamati ilibaini kuwaitifaki hii ilisainiwa na Mawaziri wa Nchi zote Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi Julai mwaka 2013.mpaka sasa ni nchi tatu tu; Kenya, Rwanda na Ugandazimeridhia itifaki hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 152 ya mkatabamama na kuzifanya Tanzania na Burundi kuwa nchi pekeeambazo bado hazijaridhia itifaki hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, chimbuko, malengo namadhumi ya Itifaki hii. Kama ilivyoelezwa katika sehemu ya

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

kwanza ya taarifa hii, Ibara ya 124 ya mkataba wa kuanzishaJumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 1999 inaeleza kuwanchi wanachama zilikubaliana kuwa amani na usalama nimaeneo muhimu katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamiindani ya Jumuiya. Kwa kuzingatia jambo hilo nchiwanachama zinawajibika kusaini na kuridhia itifaki husika ilikufanikisha utekelezaji wenye tija wa mkataba wa Jumuiyaya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Itifaki hii nikuimarisha amani, usalama na utulivu katika Jumuiya yaAfrika Mashariki, pamoja na kukuza ujirani mwema kwa nchiwanachama. Itifaki hii inataja maeneo muhimu ya ushirikianoambayo yote yanalenga kuimarisha amani, ulinzi na usalamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Maeneo haya ni pamoja:-

(i) Kuzuia na kutatua migogoro ndani na nje ya nchiwanachama;

(ii) Kuzuia mauaji ya kimbari ikiwa ni pamoja na kuzuiavitendo vya kuharibu kwa jumla au sehemu ya Utaifa,uasili, ubaguzi wa rangi ama dini;

(iii) Kupambana na ugaidi;

(iv) Kushiriki katika operesheni za kulinda amani;

(v) Kukabiliana na kupunguza madhara yatokanayo namajanga;

(vi) Kusimamia masuala ya wakimbizi;

(vii) Kudhibiti kuzagaa kwa silaha haramu ndogondogona nyepesi;

(viii) Kukabiliana na uhalifu wa kimataifa na uhalifuunaovuka mipaka;

(ix) Kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo; na

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

(x) Kushirikiana katika utoaji wa huduma za magerezaikiwemo kubadilishana wafungwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kufanikisha utekelezaji wamaeneo hayo muhimu, nchi wanachama zimekubalianakuanzisha mifumo, sera na operesheni na mikakati ya pamojakupambana na uhalifu wa aina zote. Aidha, nchiwanachama zimekubaliana kuhuisha sera, sheria, mikakatina programu za usimamizi wa masuala ya wakimbizikulingana na makubaliano ya Mkataba wa Umoja waMataifa wa Wakimbizi wa mwaka 1951 na Mkataba waUmoja wa Nchi za Afrika wa mwaka 1969 unaohusu matatizoya wakimbizi Barani Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la kushirikianakatika utoaji wa huduma za magereza, nchi wanachamazimekubaliana kushirikiana katika ubadilishanaji wawafungwa, mahabusu na urekebishwaji wa tabia za wahalifupamoja na kushirikiana katika kuboresha mifumo ya utawalakatika Magereza na huduma za marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, faida na changamoto zakuridhia Itifaki hii. Zipo faida nyingi ambazo zinapatikanaTanzania kuridhia itifaki hii. Faida hizo ni pamoja na Jamhuriya Muungano wa Tanzania itaimarisha ushirikiano wake nanchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katikakutatua migogoro mbalimbali na hivyo kuimarisha ujiranimwema, kuwepo kwa amani na usalama katika nchikutokana na kubadilishana taarifa za uhalifu na uhalifuunaovuka mipaka, kupata taarifa za kuibuka kwa makosamapya, kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi, dawa zakulevya, biashara harama za usafirishaji wa binadamu,kuenea kwa silaha haramu na wizi wa mitandaoni. Mwishokubadilishana ujuzi na uzoefu katika kukabiliana na uhalifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika upande waJumuiya ya Afrika kuridhiwa kwa Itifaki hii kunarajiwa kuwana matokeo yafuatayo:

(i) Itifaki itarahisisha uainishaji wa sera, sheria za program

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

za ndani ya Jumuiya zenye uwiano katika masualaya amani na usalama.

(ii) Kuwepo kwa mazingira mazuri ya amani na usalama,kuwawezesha wananchi wa nchi wanachamakufanya shughuli za kiuchumi bila hofu.

(iii) Kujenga mazingira ya ujirani mwema kwa jamii zawafugaji ndani ya Jumuiya.

(iv) Kuimarisha ushirikiano katika kupambana nakuondoa uhalifu wa aina zote.

(v) Kuimarika kwa uzoefu wa kukabiliana na makosa yajinai na pia nchi wanachama zitaweza kuwa namipango madhubuti ya kubadilishana wafungwa.

Itifaki hii itahusisha operations zote ambazo zitakuwana viashiria vya uvunjifu wa amani na haki za binadamu.

Changamoto kuridhia Itifaki hii. Zipo changamotokadhaa zinazoweza kujitokeza kwa Tanzania kuridhia Itifakihii, changamoto hii ni pamoja na gharama za kuendeshaoperations mbalimbali za pamoja kama vile operations zaukamataji wa bidhaa bandia mipakani na kuwa na mafunzoya pamoja kwa nyakati tofauti.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na changamotohizo Kamati yangu imejiridisha kuwa faida zinazopatikanakwa Bunge kuridhia Azimio hili ni nyingi na zenye manufaa situ kwa Tanzania pekee bali wa Jumuiya ya Afrika Masharikikwa ujumla wake, hususan katika kufanikisha maendeleo yakiuchumi na kijamiii ya nchi wanachama.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni na ushauri waKamati. Baada ya kujadili kwa kina hoja ya Serikali kuhusuAzimio la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya yaAfrika Mashariki. Kamati ina maoni na ushauri ufuatao:-

Kwanza, ucheleweshwaji wa kuridhia Itifaki. Kamatiilipokuwa ikifanya uchambuzi wake ilibaini kuwa Itifaki hii

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

ilisainiwa na nchi wanachama, husika tarehe 12 Julai, 2013.Itifaki hii imechukua miaka minne kuletwa Bungeni kwa ajiliya kuridhiwa licha ya kuonekana kuwa ina manufaamakubwa kwa nchi. Kamati inaishauri Serikali kuwasilishaItifaki zote zilizosainiwa ambazo zinahitaji kuridhiwa na Bungekwa kuzingatia matakwa ya sheria.

Pili, masuala ya wizi wa kimtandao kuingizwa katikaItifaki. Ibara ya 12 ya Itifaki hii inaainisha maeneo ambayonchi wanachama zimekubaliana kuandaa mifumo, sera namikakati ya pamoja, kuzuia na kukabiliana na ainambalimbali za uhalifu wa Kimataifa na uhalifu unaovukamipaka ikiwemo wizi wa magari, biashara haramu yausafirishajij wa binadamu, mapambano dhidi ya ugaidi nadawa za kulewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, Kamati ilibainikuwa hakukuwa na kipengele mahususi kinachoongeleamasuala ya kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia wizi wamitandaoni (cybercrime) ambao ukuaji wake ni wa kasiduniani kote. Hivyo, Kamati inaishauri Serikali kuona umuhimuwa Itifaki hii kujumuisha kipengele hicho kwa siku za usoni,hatimaye kuwa na mkakati wa pamoja wa Jumuiya katikakudhibiti tatizo hili.

Tatu, utungaji wa sheria na mikakati ya pamoja.Katika utekelezaji za Itifaki hii nchi wanachama zitatungasheria na kuweka mikakati ya pamoja, kuimarisha amani nautulivu ndani ya Jumuiya. Pamoja na jambo hili jema Kamatiinaishauri Serikali kuhakikisha kuwa sheria zitakazotungwapamoja na mikakati itakayowekwa ziwe zenye manufaa natija kwa Taifa letu.

Nne, ubadilishaji wa wafungwa katika Jumuiya. Sualala ubadilishaji wa wafungwa katika Jumuiya ya AfrikaMashariki limekuwa lina ugumu kwa muda mrefu. Kamatiinaishauri Serikali kuwa mara Itifaki hii itakaporidhiwa nakuwa tayari kwa utekelezaji wake mikakati ya namna yakushirikiana katika kubadilishana wafungwa iandaliwe kwaumakini mkubwa il i iweze kuwezesha wafungwa

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

wanaotumikia vifungo katika nchi ambazo wao siyo raiakurejeshwa na kutumikia vifungo katika nchi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho, baada yakuwasilisha maoni na ushauri wa Kamati sasa naombakuchukua fursa hii kuwashukuru Wajumbe wa Kamati yaMambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwa michango yao mizuriwakati wa kuchambua hoja ya Serikali. Michango yaoimewezesha kukamilika kwa taarifa hii kwa wakati. Naombakuwatambua Wajumbe hao kwa majina kama ifuatavyo;wakiongozwa na Mheshimiwa Balozi Mohamed Adadi RajabMbunge, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Masoud Ali KhamisMbunge, Makamu Mwenyekiti; Mheshimiwa Capt. GeorgeHuruma Mkuchika, Mbunge...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stephen Masele majinahuwa hayasomwi Kikanuni. Kwa hiyo, wewe omba tu yaingiakwenye Hansard.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa uendeshaji mzuriwa Bunge letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa niaba ya Wajumbewa Kamati kumshukuru Mheshimiwa Mwigulu LameckNchemba, Mbunge na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchikwa uwasilishaji na ufafanuzi wa kina alioutoa wakati waKamati ikichambua Itifaki hii. Aidha, nawashukuru watalaamwa Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao michango yaoimewezesha Kamati kuchambua kujiridhisha kuhusu faida zakuridhia Itifaki hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, napendakumshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah kwakuratibu vema shughuli za Kamati na Bunge. Aidha,nawashukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge,Ndugu Athumani Hussein, Mkurugenzi Msaidizi Bi. AngelinaSanga, Makatibu wa Kamati hii Ndugu Ramadhani Abdallah,

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Ndugu Grace Bidya wakisaidiwa na Ndugu Rehema Kimbekwa kuratibu vema shughuli za Kamati kuhakiki taarifa hiiinakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono Azimio hilina naomba Bunge letu Tukufu liridhie Itifaki hii kamailivyowasilishwa na mtoa hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MAONI NA USHAURI WA KAMATI KUHUSU AZIMIO LA BUNGELA KURIDHIA ITIFAKI YA AMANI NA USALAMA YA JUMUIYA

YA AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN COMMUNITYPROTOCOL ON PEACE AND SECURITY) – KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI——————

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b) yaKanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016, kwa niabaya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo yaNje, Ulinzi na Usalama, naomba kuwasilisha Maoni na Ushauriwa Kamati kuhusu Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiyaya Afrika Mashariki (East African Community Protocol onPeace and Security).

Mheshimiwa Spika, Nyongeza ya Nane ya Kifungu cha 7(1)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016,inazipa Kamati za kisekta, ikiwemo Kamati hii, jukumu lakushughulikia Miswada ya Sheria na Mikatabainayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizarainazozisimamia. Sambamba na hilo, Jukumu hili pia ni jukumula kikatiba chini ya Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya Jamuhuriya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (3) cha Nyongeza yaNane ya Kanuni za Bunge, Toleo la Januari 2016, Kamati yaKudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inasimamiaWizara tatu ambazo ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Wizara ya Ulinzi na JKT, na Wizara ya Mambo ya Nje na

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Masuala yaliyomo katika Itifakihii yanazigusa moja kwa moja Wizara hizi.

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 05 Septemba, 2017 Kamatiyangu ilikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba, Mb, na kupokeo maelezo yaSerikali kuhusu chimbuko, vipengele vya muhimu na faidaza kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya AfrikaMashariki. Baada ya maelezo hayo, Kamati ilipata fursa yakutafakari na kujadili kwa kina Hoja hiyo ya Serikali.

1.1 Mambo ya Msingi yaliyozingatiwa na Kamati

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia wajibu wa Kamati katikakuliwezesha Bunge kutekeleza madaraka yake ipasavyo,Kamati ilizingatia masuala mbalimbali katika kujiridhisha naHoja iliyotolewa na Serikali. Kamati ilifanya Mapitio yaMkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Mwaka1999 ambapo Ibara ya 124 ya Mkataba huo inaeleza kuwanchi wanachama zimekubaliana kuwa Amani na Usalamawa Kanda ya Afrika Mashariki ndio nguzo kuu ya maendeleoya kiuchumi na kijamii katika Jumuiya hiyo.

Aidha, Kamati ilijiridhisha kuwa Ibara ya 151 ya Mkataba huoinatoa Mamlaka kwa nchi wanachama kuandaa na kuridhiaItifaki katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano likiwemosuala la Amani na Usalama. Itifaki inayoridhiwa kwa mujibuwa Ibara ya 124 na 151 ya Mkataba huo, inakuwa sehemuya Mkataba na hivyo kuweka misingi ya Kisheria nakuilazimisha nchi mwanachama kuitekeleza.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Kamati ilijiridhisha kuhusu muda/kipindi ambacho Itifaki hii ilisainiwa na nchi wanachama.Katika kufanya hivyo, Kamati ilibaini kuwa, Itifaki hii ilisainiwana Mawaziri wa nchi zote wananchama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki Mwezi Julai, 2013. Mpaka sasa, nchi tatu za Kenya,Rwanda na Uganda zimesharidhia Itifaki hiyo kwa mujibu waIbara ya 152 ya Mkataba mama, na kuzifanya Tanzania naBurundi kuwa nchi pekee ambazo bado hazijaridhia Itifakihii.

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

1.2 Chimbuko, Malengo na Madhumuni ya Itifaki

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa katika sehemu ya 1.1ya taarifa hii, Ibara ya 124 ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiyaya Afrika Mashariki wa mwaka 1999, inaeleza kuwa nchiwanachama zilikubaliana kuwa Amani na Usalama ni eneomuhimu katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii ndaniya Jumuiya. Kwa kuzingatia jambo hilo, nchi wanachamazinawajibika kusaini na kuridhia itifaki husika ili kufanikishautekelezaji wenye tija wa Mkataba wa Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Spika, Lengo la itifaki hii ni kuimarisha amani,usalama na utulivu katika jumuiya ya Afrika Mashariki pamojana kukuza ujirani mwema kwa nchi wanachama.

Mheshimiwa Spika, Itifaki hii inataja maeneo muhimu yaUshirikiano ambayo yote yanalenga kuimarisha amani, ulinzina usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Maeneo haya nipamoja na:-

i) Kuzuia na kutatua migogoro ndani na nje ya nchiwanachama.ii) Kuzuia mauaji ya Kimbari ikiwa ni pamoja na kuzuiavitendo vya kuharibu kwa jumla au sehemu ya utaifa, uasili,ubaguzi wa rangi au dini.iii) Kupambana na ugaidi.iv) Kushiriki katika operesheni za kulinda amani.v) Kukabiliana na kupunguza madhara yatokanayo namajanga.vi) Kusimamia masuala ya wakimbizi.vii) Kudhibiti kuzagaa kwa silaha haramu ndogo ndogona nyepesi.viii) Kukabiliana na uhalifu wa kimataifa na uhalifuunaovuka mipaka.ix) Kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo.x) Kushirikiana katika utoaji wa huduma za magerezaikiwemo kubadilishana wafungwa.

Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wa maeneo

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

hayo muhimu, nchi wanachama zimekubaliana kuanzishamifumo, sera, operesheni na mikakati ya pamoja katikakupambana na uhalifu wa aina zote. Aidha, nchiwanachama zimekubaliana kuhuisha Sera, Sheria, Mikakatina Programu za usimamizi wa masuala ya wakimbizikulingana na makubaliano ya Mkataba wa Umoja waMataifa wa Wakambizi wa Mwaka 1951 na Mkataba waUmoja wa Nchi za Afrika wa Mwaka 1969 unaohusu matatizoya wakimbizi Barani Afrika.

Mheshimiwa Spika, katika suala la kushirikiana katika utoajiwa huduma za Magereza, nchi wanachama zimekubalianakushirikiana katika ubadilishanaji wa wafungwa, mahabusuna urekebishwaji wa tabia za wahalifu pamoja nakushirikiana katika kuboresha mifumo ya utawala katikamagereza na huduma za marekebisho.

2.0 FAIDA NA CHANGAMOTO ZA KURIDHIA ITIFAKI HII

2.1 Faida za Kuridhia Itifaki

Mheshimiwa Spika, zipo faida nyingi ambazo zitapatikanakwa Tanzania kuridhia Itifaki hii. Faida hizo ni pamoja na:-i) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaimarishaushirikiano wake na nchi wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki katika kutatua migogoro mbalimbali na hivyokuimarisha ujirani mwema.

ii) Kuwepo kwa amani na usalama katika nchikutokana na kubadilishana taarifa za uhalifu na uhalifuunaovuka mipaka.

iii) Kupata taarifa za kuibuka kwa makosa mapya.

iv) Kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi, dawa zakulevya, biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu,kuenea kwa silaha haramu na wizi wa mitandaoni.

v) Kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kukabiliana nauhalifu.

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

Mheshimiwa Spika, aidha, kwa upande wa Jumuiya ya AfrikaMashariki, kuridhia kwa Itifaki hii kunatarajiwa kuwa namatokeo yafuatayo:-

i) Itifaki itarahisisha uainishaji wa Sera, Sheria naProgramu za ndani ya Jumuiya zenye uwiano katika masualaya amani na usalama.

ii) Kuwepo kwa mazingira mazuri ya amani na usalamakuwawezesha wananchi wa nchi wanachama kufanyashughuli za kiuchumi na kijamii bila hofu.

iii) Kujenga mazingira ya ujirani mwema kwa jamii zawafugaji ndani ya Jumuiya.

iv) Kuimarisha ushirikiano katika kupambana nakuondoa uhalifu wa aina zote.

v) Kuimarika kwa uzoefu wa kukabiliana na makosa yajinai na pia nchi wanachama zitaweza kuwa na mipangomadhubuti ya kubadilishana wafungwa.vi) Itifaki hii itahusisha operesheni zote ambazo zitakuwana viashiria vya uvunjifu wa amani na haki za binadamu.

2.2 Changamoto za Kuridhia Itifaki

Mheshimiwa Spika, zipo changamoto kadhaa zinazowezakujitokeza kwa Tanzania kuridhia Itifaki hii. Changamoto hizini pamoja na gharama za kuwa na operesheni mbalimbaliza pamoja kama vile operesheni za ukamataji wa bidhaabandia mipakani; na kuwa na mafunzo ya pamoja kwanyakati tofauti.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Changamoto hizo, Kamatiyangu imejiridhisha kuwa faida zitakazopatikana kwa Bungekulidhia Azimio hili ni nyingi na zenye manufaa si tu kwaTanzania pekee bali kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwaujumla wake hususan katika kufanikisha maendeleo yakiuchumi na kijamii ya nchi wananchama.

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

3.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kujadili kwa kina Hoja yaSerikali kuhusu Azimio la kuridhia Itifaki ya Amani na Usalamaya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kamati ina maoni na ushauriufuatao:-

i) Uchelewashwaji wa kuridhia Itifaki

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokuwa ikifanya uchambuziwake, ilibaini kuwa Itifaki hii ilisainiwa na nchi wananchamahusika tarehe 12 Julai, 2013. Itifaki hii imechukua miaka minnekuletwa Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa licha ya kuonekanakuwa ina manufaa makubwa kwa nchi yetu. Kamatiinaishauri Serikali kuwasilisha Itifaki zote zilizosainiwa ambazozinahitaji kuridhiwa na Bunge kwa kuzingatia matakwa yaSheria.

ii) Masuala ya Wizi wa Kimtandao kuingizwa katikaItifaki

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 12 ya Itifaki hii inaainisha maeneoambayo nchi wananchama zimekubaliana kuandaamifumo, sera na mikakati ya pamoja ya kuzuia nakukabiliana na aina mbalimbali za uhalifu wa Kimataifa nauhalifu unaovuka mipaka ikiwemo wizi wa magari, biasharaharamu ya usafirishaji wa binadamu, mapambano dhidi yaugaidi, dawa za kulevya nk.

Hata hivyo, Kamati ilibaini kuwa, hakukuwa na kipengelemahususi kilichoongelea masuala ya kuweka mikakatimadhubuti ya kuzuia wizi wa mtandaoni (cybercrime)ambao ukuaji wake ni wa kasi duniani kote.

Hivyo, Kamati inaishauri Serikali kuona umuhimu wa Itifaki hiikujumuisha kipengele hicho kwa siku za usoni na hatimayekuwa na mikakati ya pamoja ya Jumuiya katika kudhibititatizo hili.

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

iii) Utungaji wa Sheria na Mikakati ya Pamoja

Mheshimiwa Spika, Katika utekelezaji wa Itifaki hii, nchiwanachama zitatunga sheria na kuweka mikakati ya pamojaya kuimarisha amani na utulivu ndani ya Jumuiya. Pamojana jambo hili jema, Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kuwaSheria zitakazotungwa pamoja na mikakati itakayowekwaziwe ni zenye manufaa na tija kwa Taifa letu.

iv) Ubadilishanaji wa wafungwa katika Jumuiya

Mheshimiwa Spika, suala la ubadilishanaji wafungwa katikaJumuiya ya Afrika Mashariki limekuwa lina ugumu kwa mudamrefu. Kamati inaishauri Serikali kuwa, mara Itifaki hiiitakaporidhiwa na kuwa tayari kwa utekelezaji wake,Mikakati ya namna ya kushirikiana katika ubadilishanaji wawafungwa iandaliwe kwa umakini mkubwa. Hii itawezeshawafungwa wanaotumikia vifungo katika nchi ambazo waosi raia kurejeshwa na kutumikia vifungo katika nchi zao.

4.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwasilisha maoni na ushauriwa Kamati, sasa naomba kuchukua fursa hii kuwashukuruWajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamakwa michango mizuri wakati wa kuchambua Hoja ya Serikali.Michango yao imewezesha kukamilika kwa taarifa hii kwawakati. Naomba kuwatambua Wajumbe hao kwa majinakama ifuatavyo:-

1. Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mb, Mwenyekiti2. Mhe. Kanal (Mst) Masoud Ali Khamis, Mb, M/Mwenyekiti3. Mhe. Capt. George Huruma Mkuchika, Mb Mjumbe4. Mhe. Salma Rashid Kikwete, Mb “5. Mhe. Mussa Hassan Mussa, Mb “6. Mhe. Prosper J. Mbena, Mb “7. Mhe. Mhe. Victor Kilasile Mwambalasa, Mb “8. Mhe. Mch. Peter Simon Msigwa, Mb “9. Mhe. Cecilia Daniel Paresso, Mb “10. Mhe. Alphaxad Kangi Lugola, Mb “

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

11. Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Mb “12. Mhe. Cosato David Chumi, Mb “13. Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb “14. Mhe. Bonnah Kaluwa, Mb “15. Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mb “16. Mhe. Kiswaga Boniventura Destery, Mb “17. Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mb “18. Mhe. Joel Mwaka Makanyaga, Mb “19. Mhe. Haji Khatib Kai, Mb “20. Mhe. Lucy Simon Magereli, Mb “21. Mhe. Masoud Abdalla Salim, Mb “22. Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda, Mb “23. Mhe. Lazaro S. Nyalandu, Mb “24. Mhe. Stephene J. Masele, Mb “25. Mhe. Machano Othman Said, Mb “26. Mhe. Hasna Sudi Katunda Mwilima, Mb “27. Mhe. Khamisi Yahya Machano, Mb “28. Mhe. Yahya Omari Masare, Mb “

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuruwewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwauendeshaji mzuri wa Bunge letu.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wajumbe wa Kamati,namshukuru Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba, Mb,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa uwasilishaji naufafanuzi wa kina alioutoa wakati Kamati ikichambua Itifakihii. Aidha, nawashukuru wataalamu wa Wizara ya Mamboya Ndani ya Nchi na wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki ambao michango yaoimeiwezesha Kamati kuchambua na kujiridhisha kuhusu faidaza kuridhia Itifaki hii.

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuru Katibu waBunge Dkt. Thomas Kashililah kwa kuratibu vema shughuli zaKamati na Bunge. Aidha, nawashukuru Mkurugenzi wa Idaraya Kamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein, MkurugenziMsaidizi Bi. Angelina Sanga na Makatibu wa Kamati hii Ndg.Ramadhan Abdallah na Bi. Grace Bidya wakisaidiwa na Bi.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Rehema Kimbe kwa kuratibu vema shughuli za Kamati nakuhakikisha taarifa hii inakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono Azimio hili na naombaBunge lako Tukufu liridhie Itifaki hii kama ilivyowasilishwa namtoa hoja.

Balozi Adadi Mohamed Rajab, MbMWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA7 Septemba, 2017

NAIBU SPIKA: Sasa tutamsikia Msemaji wa KambiRasmi ya Upinzani kuhusu Azimio hili.

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAUPINZANI KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI):Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Msemaji Mkuu waKambi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi, naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki yaAmani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EastAfrican Protocol on Peace and Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, amani na usalama nimahitaji ya msingi kwa ustawi wa Taifa lolote duniani. Ili watuwaweze kutulia na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi,kisiasa na kijamii, wanahitajika kuhakikishiwa usalamaambao msingi wake ni amani na utulivu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba nchiyetu ipo katika historia ya dunia kutokana na kudumisha tunuzake za amani na utulivu, historia hiyo haiondoi ukwelikwamba amani na utulivu katika Mataifa mbalimbali duniavimeporomoka kwa kiwango kikubwa sana na hivyokuhatarisha usalama wa watu katika Mataifa hayo. Siyojambo la kubishaniwa kwamba kuongezeka kwa vitendovya kigaidi na kiharamia duniani, kuongezeka kwa uhasamakati ya Mataifa, uhasama ambao umesababisha au

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

matikisiko ya kivita na kuongezeka kwa aina mbalimbali zauhalifu kumefanya hali ya usalama duniani kuwa katika halitete.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na hali hiyoMataifa mbalimbali duniani yameanza kubuni mbinumbalimbali za mashirikiano katika nyanja za ulinzi wa amanina pia namna ya kujilinda na kujihami dhidi ya uvamizi auuhalifu unaoweza kujitokeza katika nchi moja au ukandaambao uko katika ushirikiano ili kuhakikisha usalama wawananchi wa nchi washirika unalindwa ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Tanzaniaimetajwa kuwa ni kisiwa cha amani cha Afrika na kwa kuwatangu enzi za utawala wa Mwalimu Julius KambarageNyerere, nchi yetu ilijipambanua kwa kusimamia misingi yahaki, demokrasia na utawala wa sheria, misingi ambayo ndioza amani na utulivu tunaojivunia leo; na kwa kuwa Tanzaniailijitoa mhanga kupigia vita vya kupinga ubaguzi wa ainayoyote, unyonyaji, unyanyasa na dhuluma dhidi ya binadamumwingine chini ya kauli mbiu ya wakati huo, binadamu woteni ndugu zangu na Afrika ni moja kwa lengo la kuhakikishakwamba amani na usalama kwa Waafrika wote vinalindwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa kuwa nchi yetuiliandika historia wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanzakwa kudiriki kuzitenga hata baadhi ya Serikali za nchi zaKiafrika zil izokuwa haziheshimu utawala wa kisheria,demokrasia na haki za binadamu; hivyo basi, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni haipingi wazo au nia ya kuanzisha itifakihii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu ushirikiano katikamasuala ya amani na usalama kwa kuwa ushirikiano huoutasaidia kuhuisha misingi ya kidemokrasia, utawala wa sheriana haki za binadamu ambayo kwa pamoja huzaa amani,amani ambayo hatimaye huzaa usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababuamani na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki vikokatika hatari ya kuporomoka kutokana na kuongezeka kwavitendo vya baadhi ya Viongozi kutokuheshimu misingi ya

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.Tumeshuhudia baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya yaAfrika Mashariki wakibadili na wengine wanaendeleakushawishi kubadili Katiba zao za nchi ili waendelee kutawalakwa awamu nyingine kinyume kabisa na Katiba hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha viongozi wenginewamediriki kudhoofisha Upinzani katika nchi zao, Upinzaniambao uko Kikatiba kwa kuwazuia kufanya mikutano yakisiasa, kuwakamata, kuwashtaki kwa kesi za uchochezi nakuwafunga gerezani baadhi ya viongozi wa Upinzani iliwatawale bila kupingwa au kukosolewa na wenginewamediriki kukandamiza uhuru wa habari kwa kuweka Sheriangumu za Vyombo vya Habari ili visiweze kukosoa maovuyanayofanywa na baadhi ya Viongozi wa Serikali wa nchizao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo niliyoyataja pamojana mengine ya namna hii huzua chuki kati ya Serikali namakundi mbalimbali ya jamii yanayoona kwambayanaonewa na matokeo yake ni kuzuka kwa vikundi vyawaasi na hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe nakatika hatua hiyo amani na usalama vinakuwa vimetowekakabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili mambo haya yasiendeleekutokea katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, KambiRasmi ya Upinzani Bunge ina mtazamo kwamba itifaki hiiimekuja wakati muafaka na kwamba Bunge liliridhie Itifakihii. Sababu za kuunga mkono Itifaki hii ni kutokana naumuhimu wa masuala yanayopendekezwa katika Itafiki hiikwa mstakabali mwema wa nchi washirika.

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala hayo ni pamojana ushirikiano katika usuluhisho wa migogoro baina ya nchiwanachama wa Afrika Mashariki au Mataifa mengine,kudhibiti na kukomesha mauaji ya kimbari, kukomeshaugaidi, kukomesha na kutokomeza uharamia, operesheni zakulinda amani, kukabiliana na majanga, uhifadhi wawakimbizi, udhibiti wa uingizaji haramu wa silaha, udhibiti

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

wa uhalifu wa Kimataifa kama vile wizi wa magari, usafirishajiwa magendo uhamiaji haramu, biashara haramu yabinadamu na kadhalika, pia kudhibiti uswagaji wa mifugokuvuka mipaka na kuingia nchi nyingine na pia kubadilishanamahabusu na wafungwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani inatoatahadhari wakati wa utekelezaji wa Itifaki hii kamaifuatavyo:-

Kwamba pamoja na masuala hayo ambayotunapendekeza Bunge hili liliridhie, lakini tunatoa wito kwaBunge na Serikali pia kuchukua tahadhari katika masualakadhaa kabla ya kuridhia na wakati wa utekelezaji wa itifakihii inayopendekezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inashauri Bunge hili na Serikalikutoitetea au kuilinda Serikali yoyote ya nchi zinazoridhia Itifakihii ambayo itakataliwa na wananchi wake kwa kisingiziocha ushirika kupitia Itifaki hii. Azimio hili lisiwe kinga kwa Serikaliambazo zitakuwa zimekataliwa na wananchi wake, kwamaneno mengine hatutarajii kuona Serikali ya nchi mojaikisaidia Serikali ya nchi zingine ndani ya Jumuiya kubakimadarakani kimabavu au kuingia madarakani kwa njia zaudanganyifu kwa kisingizio kwamba zipo katika ushirikiano.

Mheshimiwa Naibu Spika, vitendo vyote visivyo vyakidemokrasia vinavyotendwa na Serikali yoyote katikaJumuiya ya Afrika Mashariki lazima vikemewe na vilaaniwena Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki ili kusudio la kuwa naitifaki hii ya Amani ya Kudumu ya Usalama liweze kufikiwa.Hii ni kwa sababu kukitokea vitendo vya baadhi ya Serikalikusaidia au kubebana katika uovu machafu ya kisiasayatatokea, amani itapotea na hatutakuwa na usalama tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, Kambi Rasmiya Upinzani inashauri nchi zitakazoridhia itifaki hii kutokushirikikatika ukandamizaji wa raia wa nchi zao na kusababishaukosefu wa amani na usalama katika nchi zao, halafu

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

zikategemea kupata ushirikiano wa ulinzi wa amani kutokanana itifaki hii. Kwa kuwa, itifaki hii inahusu masuala ya amanina usalama basi nchi wanachama ziwe mfano wa kuigwakwa kudumisha amani na usalama ndani mwao kwanzabadala ya kuwa chanzo cha machafuko zenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ili itifaki hiiifikie malengo yaliyokusudiwa na iwe na manufaa ya kudumukatika nchi zitakazoiridhia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinashauri na kupendekeza kwamba nchi washiriki wa Itifakihii ziweke kipaumbele zaidi katika mazungumzo yakidiplomasia katika maeneo yenye migogoro kuliko kutumianguvu nyingi za kijeshi kulinda amani.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inazishauri nchi zitakazoridhia itifaki hiikupitia mara kwa mara taarifa za makubaliano ya azimiohili na utekelezaji wake ili kuhakikisha hakuna mabadilikohasi ya Azimio kulingana na wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tano, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inashauri kuwa, Serikali yetu ihakikishekuwa inaendeleza na kuziimarisha sababu zinazofanya nchiwashirika kukubali kuwa na Azimio hilo ikiwa ni sababu zakisiasa, kiuchumi na kiusalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho. Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inapenda kuweka bayana kwambambalimbali na tofauti ndani za kisiasa na baada ya kutoamaangalizo au tahadhari za kuchukua wakati wa kuridhiana kutekeleza Itifaki hii sasa tunakwenda pamoja kama Taifakatika kusaidia utekelezaji bora wa Azimio hili. Ikumbukwekwamba amani na utulivu tulionao ni zawadi kutoka kwaMwenyezi Mungu na kwa hiyo, hatuna budi kuilinda si kwamitutu ya bunduki bali kwa kutenda haki kwani amani nitunda la haki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumalizia kwakusema kwamba, kama kweli tunaipenda amani tuliyonayona kama kweli tunakuwa mfano wa kuigwa na Mataifa

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

mengine kwa kudumisha amani na utulivu, basi Viongoziwetu waliopewa dhamana ya kuongoza Taifa hili hawanabudi kuongoza wa kuzingatia misingi ya demokrasia, utawalawa sheria na kuheshimu haki za binadamu, kutokuoneanahaya kwa Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nawengineo wanaovunja misingi hiyo kwa uchu wa madaraka.Aidha, vitendo vyote vya kibaguzi na vya unyanyapaa waitikadi tofauti za kisiasa, havina budi kukomeshwa kwa nguvuzote kwani hiyo ndio huzaa chuki na machafuko na hatimayeamani na usalama kutoweka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inazihakikishia nchi wanachamaushirikiano katika utekelezaji wa Itifaki hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni, naomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, KUHUSUAZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA ITIFAKI YA AMANI NA

USALAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (THE EASTAFRICAN COMMUNITY PROTOCOL ON PEACE ANDSECURTIY) KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndaniya nchi, naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki yaAmani na Usalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EastAfrican Protocol on Peace and Security).

Mheshimiwa Spika, amani na usalama ni mahitaji ya msingikabisa kwa ustawi wa taifa lolote duniani. Ili watu wawezekutulia na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, kisiasana kijamii wanahitaji kuhakikishiwa usalama ambao msingiwake ni amani na utulivu.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba nchi yetu ipo katikahistoria ya dunia kutokana na kudumisha tunu zake za amanina utulivu; historia hiyo haiondoi ukweli kwamba amani nautulivu katika mataifa mbalimbali duniani vimeporomokakwa kiwango kikubwa sana, na hivyo kuhatarisha usalamawa watu katika mataifa hayo. Si jambo la kubishaniwakwamba; kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi na kiharamiaduniani; kuongezeka uhasama kati ya mataifa, - uhasamaambao umesababisha vita au matishio ya kivita nakuongezeka kwa aina mbalimbali za uhalifu kumefanya haliya usalama duniani kuwa katika hali tete.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hiyo; mataifambalimbali duniani yameanza kubuni mbinu mbalimbaliza mashirikiano katika nyanja za ulinzi wa amani na pianamna ya kujilinda na kujihami dhidi ya uvamizi au uhalifuunaoweza kujitokeza katika nchi moja au ukanda ambaouko katika ushirikano, ili kuhakikisha usalama wa wananchiwa nchi washirika unalindwa ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania imetajwa kuwa nikisiwa cha amani cha Afrika, na kwa kuwa tangu enzi zautawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, nchi yetuilijipambanua kwa kusimamia misingi ya haki, demokrasiana utawala wa sheria – misingi ambayo ndiyo nguzo zaamani na utulivu tunaojivunia leo; na kwa kuwa Tanzaniailijitoa mhanga kupigana vita vya kupinga ubaguzi wa ainayoyote; unyonyaji, unyanyasaji na dhulma dhidi ya binadamumwingine chini ya Kauli mbiu ya wakati huo “Binadamu woteni ndugu zangu na Afrika ni Moja’ kwa lengo la kuhakikishakwamba amani na usalama kwa waafrika wote vinalindwa;na kwa kuwa nchi yetu iliandika historia wakati wa Serikaliya awamu ya kwanza kwa kudiriki kuzitenga hata baadhiya Serikali za nchi za kiafrika zilizokuwa haziheshimu utawalawa sheria, demokrasia na haki za binadamu; Hivyo, basi,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haipingi wazo au nia yakuanzisha itifaki hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusuushirikiano katika masuala ya amani na usalama; kwa kuwaushiriakiano huo utasaidia kuhuisha misingi ya demokrasia,

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

utawala wa sheria na haki za binadamu ambayo kwapamoja huzaa amani; - amani mbayo hatimaye huzaausalama.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu, amani nausalama katika ukanda wa Afrika Mashariki viko katika hatariya kuporomoka kutokana na kuongezeka kwa vitendo vyabaadhi ya viongozi kutoheshimu misingi ya demokrasia,utawala wa sheria na haki za binadamu. Tumeshuhudiabaadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikiwakibadili na wengine wanaendelea kushawishi kubadilikatiba za nchi zao ili waendelee kutawala kwa awamunyingine kinyume na katiba hizo. Aidha, viongozi wenginewamediriki kudhoofisha upinzani katika chi zao; - upinzaniambao uko kikatiba, kwa kuwazuia wapinzani kufanyamikutano ya kisiasa; kuwakamatama, kuwashtaki kwa kesiza uchochezi na kuwafunga gerezani baadhi ya viongoziwa upinzan,i ili watawale bila kupingwa au kukosolewa; nawengine wamediriki kukandamiza uhuru wa habari kwakuweka sheria ngumu za vyombo vya habari ili visiwezekukosoa maovu yanayofanywa na baadhi ya viongozi waSerikali wa nchi hizo.

Mheshimiwa Spika, hayo niliyoyataja pamoja na mengineya namna hiyo, huzua chuki kati ya Serikali na makundimbalimbali ya jamii yanayoona kwamba yanaonewa namatokeo yake ni kuzuka kwa vikundi vya waasi na hatimayevita wa wenyewe kwa wenyewe; - na katika hatua hiyo,amani na usalama vinakuwa vimetoweka kabisa.

Mheshimiwa Spika, ili mambo hayo yasiendelee kutokeakatika ukanda wetu wa Afrika Mashariki; Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni ina mtazamo kwamba Itifki hii imekujawakati mufaka na kwamba Bunge liridhie itifaki hii. Sababuza kuunga mkono itifaki hii ni kutokana na umuhimu wamasuala yanayopendekezwa katika ifaki hii kwa mustakabalimwema wa nchi washirika. Masuala hayo ni pamoja naushirikiano katika:-

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

i. Usuluhishi wa migogoro baina ya nchi wanachamawa Afrika Mashariki na au mataifa mengine.ii. Kudhibiti na kukomesha mauaji ya kimbari(Genocide)iii. Kukomesha ugaidiiv. Kukomesha na kutokomeza uharamiav. Operesheni za kulinda amanivi. Kukabiliana na majangavii. Uhifadhi wa Wakimbiziviii. Udhibiti wa uingizaji haramu wa Silahaix. Udhibiti wa uhalifu wa kimataifa kama vile wizi wamagari, usafirishaji wa magendo, uhamiaji haramu, biasharaharamu ya binadamu nk.x. Kudhibiti uswagaji wa mifugo kuvuka mipaka nakuingia nchi nyinginexi. Kubadilishana mahabusu na wafungwa nk

2. TAHADHARI WAKATI WA UTEKELEZAJI WA ITIFAKI

Mheshimiwa Spika, pamoja na masuala hayo ambayotunapendekeza Bunge hili liridhie, lakini tunatoa wito kwaBunge na Serikali pia kuchukua tahadhari katika masualakadhaa kabla ya kuridhia na wakati wa utekelezaji wa itifakihii inayopendekezwa.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza: Kambi Rasmi yaUpinzani inalishauri Bunge hili na Serikali kutoitetea au kuilindaSerikali yoyote ya nchi zilizoridhia itifaki hii ambayo itakataliwana wananchi wake kwa kisingizio cha ushirikiano kupitia itifakihii. Azimio hili lisiwe kinga kwa Serikali ambazo zitakuwazimekataliwa na wananchi wake. Kwa maneno mengine,hatutarajii kuona Serikali ya nchi moja ikiisaidia Serikali yanchi nyingine ndani ya Jumuiya, kubaki madarakanikimabavu au kuingia madarakani kwa njia za udanganyifukwa kisingizio kwamba zipo katika ushirikiano. Vitendo vyotevisivyo vya kidemokrasia vinavyotendwa na Serikali yeyotekatika Jumuiya ya Afrika Mashariki lazima vikemewe navilaaniwe na Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki ili kusudio lakuwa na amani ya kudumu na usalama liweze kufikiwa. Hiini kwa sababu kukitokea vitendo vya baadhi ya Serikali

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

kusaidiana au kubebana katika uovu – machafuko ya kisiasayatatokea, amani itapotea na hakutakuwa na usalamatena.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Kambi Rasmi ya Upinzaniinazishauri nchi zitakazoridhia itifaki hii kutoshiriki katikaukandamizaji wa wa Raia wa nchi zao na kusababishaukosefu wa amani na uslama katika nchi zao halafuzikategemea kupata ushirikiano wa wa ulinzi wa amanikutokana na itifaki hii. Kwa kuwa Itifaki hii inahusu masualaya amani na usalama; basi nchi wanachama ziwe mfanowa kuigwa wa kudumisha amani na usalama ndani mwaokwanza badala ya kuwa chanzo cha machafuko zenyewe.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu; ili itifaki hii ifikie malengoyaliyokusudiwa na iwe na manufaa ya kudumu katika nchizitakazoiridhia, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashaurina kupendekeza kwamba nchi washirika wa itifaki hii ziwekekipaumbele zaidi katika mazungumzo ya kidiplomasia katikamaeneo yenye migogoro kuliko kutumia nguvu za kijeshikulinda amani.

Mheshimiwa Spika, jambo la nne, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inazishauri nchi zitakazoridhia itifaki hii kupitia marakwa mara taarifa za makubaliano ya Azimio hili na utekelezajiwake ili kuhakikisha hakuna mabadiliko hasi ya Azimiokulingana na wakati.

Mheshimiwa Spika, jambo la tano, Kambi Rasmi ya Upinzaniinashauri kuwa Serikali yetu ihakikishe kuwa inaziendeleza nakuziimarisha sababu zilizofanya nchi washirika kukubali kuwana azimio hili, ikiwa ni sababu za kisiasa, kiuchumi nakiusalama.

3. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kuweka bayana kwamba; mbali na tofauti zetuza ndani za kisiasa; na baada ya kutoa maangalizo autahadhari za kuchukua wakati wa kuridhia na kutekeleza

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

itifaki hii; sasa tunakwenda pamoja kama taifa katikakusaidia utekelezaji bora wa azimio hili. Ikumbukwe kwambaamani na utulivu tulio nao, ni zawadi kutoka kwa MwenyeziMungu na kwa hiyo hatuna budi kuilinda si kwa mitutu yabunduki bali kwa kutenda haki kwani amani ni tunda la haki.

Mheshimiwa Spika, naomba kumalizia kwa kusema kwambakama kweli tunaipenda amani tuliyonayo, na kama kwelitunataka kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine kwakudumisha amani na utulivu basi viongozi waliopewadhamana ya kuongoza taifa hili hawana budi kuongoza kwakuzingatia misingi ya demokrasia, utawala wa sheria nakuheshimu haki za binadamu, na kutowaonea haya viongoziwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nyinginezo,wanaovunja misingi hiyo kwa uchu wa madaraka. Aidha,vitendo vyote vya kibaguzi na vya unyanyapaa wa itikaditofauti za kisiasa havina budi kukomeshwa kwa nguvu zotekwani hivyo ndiyo huzaa chuki na machafuko na hatimayeamani na usalama kutoweka. Mwisho kabisa Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inazihakikishia nchi wanachamaushirikiano katika utekelezaji wa itifaki hii.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, naomba kuwasilisha.

Cecilia Daniel Paresso (Mb)Kny. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI

BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI7 Septemba, 2017

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumemalizamawasilisho sasa tutaanza na wachangiaji. Kwa orodhailiyonifikia hapa mezani Vyama vyote vinavyowakilishwaBungeni vimeleta majina. Kwa hiyo, ninao Wabunge waCCM, CHADEMA na CUF. Tutaanza na Mheshimiwa Tundu Lissuambaye atachangia kwa dakika 15. Atafuatiwa naMheshimiwa Masoud Abdallah Salim, Mheshimiwa JanetMbene ajiandae ikiwa muda wetu utakuwa umetosha.

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Naomba nisemekwamba nitachangia hoja ya Kuridhia Mkataba wa KuanzishaTume ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe, kati ya Tanzaniana Malawi. Kwa sababu ya muda naomba nijielekeze kwenyesuala moja tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkataba kati ya Tanzaniana Malawi juu ya Bonde la Mto Songwe ni Mkataba waKimataifa, it is an International Treaty, tuanzie hapo. Nimkataba wa Kimataifa kati ya nchi mbili. Pili, kwa vile nimkataba wa Kimataifa, mkataba wa Kimataifa huu kamakuna sheria nyingine yoyote ya Tanzania inayokwendakinyume na matakwa ya mkataba huu wa Kimataifa,mkataba wa Kimataifa unasimama sheria ya nchiinatanguka, basic International Law 101. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, kitu ambacho nimuhimu sana na ambacho tunahitaji majibu ya Serikalikuhusiana na mkataba huu wa Kimataifa ni ule unaohusuutaratibu wa utatuaji wa migogoro chini ya mkataba huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Ibara ya13(3) ya mkataba huu, The Songwe River Basin Convention,endapo kutakuwa na mgogoro kati ya Tanzania na Malawiambao ndiyo wahusika wa mkataba huu, endapo kutakuwana mgogoro kuhusiana na masuala mbalimbaliyanayohusiana na mkataba huu wa Kimataifa, Ibara ya 13(3)inasema mgogoro huo utapelekwa kwenye Mahakama yaSADC; the parties shall refer the matter to the SADC Tribunalor shall appoint an adhoc arbitrator through mutualagreement which shall be in writing. The arbitrator’s decisionshall be final and binding on the parties.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikipelekwa kwenyeMahakama ya SADC au ikapelekwa kwa msuluhishi waKimataifa, uamuzi wa Mahakama ya SADC au uamuzi wahuyu msuluhishi wa Kimataifa utakuwa ni wa mwisho nautatufunga sisi pamoja na Malawi, sasa shida iko hapo.

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkataba wa Bondela Mto Songwe unahusu rasilimali ya maji, unahusu acquaticresources, unahusu water resources, unahusu lakes, unahusurivers. Haya yote niliyoyataja yanajulikana katika sheria, ilesheria ilipitishwa kwa shamrashamra sana humu ndani, ilesheria ya kutangaza mamlaka ya kudumu ya utajiri wa nchi;The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Actiliyopitishwa hapa mwezi Julai. Sheria ile imesema, hizonilizozisema, rasilimali za maji, vile vitu vilivyoko kwenye maji,samaki and so on and so fourth, lakes, rivers, everything, kifungucha 11 cha sheria ile kimesema kwamba ni marufuku kwarasilimali hizi zilizotajwa kuamuliwa nje ya Mahakama zaTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na WaheshimiwaWajumbe wajiridhishe wakaangalie kifungu cha tatu chasheria ile, waangalie na kifungu cha 11(1), (2) na (3) cha sheriaile ili wajiridhishe juu ya hiki ninachokisema.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo letu la miaka yotena tatizo letu hasa la Bunge hili ni ushabiki usiokuwa namaana yoyote. Tumeruhusu Bunge linapitisha sheria zamambo makubwa bila kuzitafakari, matokeo yake ndiyohaya. Sasa tuna mkataba wa Kimataifa unaosema rasilimalizetu za maji, maziwa, mito, kuhusiana na Bonde la MtoSongwe zitaamuliwa kama kutakuwa na mgogoro katikaMahakama ya SADC. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wale walioenda ku-negotiate huu mkataba na umesainiwa tarehe 18 ya Mei,hakukuwa na watu wa Attorney General’s Office, hakukuwana watu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?Hakukuwa na watu wa Wizara ya Katiba na Sheria na tunamaprofesa pale! Niliposema proffesorial rubbish, this is what Imeant, hawakuwepo? Hawa ambao walileta baadaye hiiSheria ya Natural Wealth and Resources (PermanentSovereignty) hawakujua kwamba kuna mkataba umekuwanegotiated, ume… (Makofi)

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Tundu Lissu, kunaMheshimiwa Mbunge amesimama. Mheshimiwa JanetMbene.

T A A R I F A

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,naamini Mheshimiwa Tundu Lissu anaweza akatoa maoniyake bila kutumia maneno ya karaha. Hana haja yakutukana, hana haja ya kusema maneno ya hovyo, yeyeaeleze kilichoharibika kinachoweza kutengenezwa na niniambacho kimekosewa ili kifanyiwe kazi. Sidhani kama kunahaja ya kutumia maneno ya kuwaambia wenzake rubbishwala chochote.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Naibu Spika, Iwill not…

NAIBU SPIKA: Kaa kidogo Mheshimiwa Tundu Lissu.

Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu tunaendeleana huu mjadala na ili tuweze kwenda wote sawasawa,tukumbushane zile Kanuni zinazohusu majadiliano, lakini hatazile zinazohitaji kupata fursa ya kuzungumza ikiwa Mbungemwingine anazungumza. Kwa hiyo, twende vizuri kwasababu huu mjadala tunaendelea nao. (Makofi)

Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Maneno ya Mheshimiwa Mbene wala hayahitajiheshima ya kujibiwa, naomba niendelee.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hivi, nimeuliza swali lamsingi hapa, huu mkataba umesainiwa tarehe 18, Mei 2017.Je, Mheshimiwa Waziri wa Maji Gerson Lwenge alienda pekeyake? Yeye Engineer mambo ya sheria anaweza asiyafahamu,alikuwa peke yake? Hakupata ushauri wa Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali? Hakupata ushauri wa Waziri

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

wa Sheria? Wale walioleta Sheria hii ya PermanentSovereignty over Natural Wealth hawakujua matakwa yamkataba huu?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge,matokeo yake nimezungumza na nitaendelea kuzungumzatena, matokeo yake ni aibu hizi! Mmetunga sheria miezi miwiliiliyopita, leo mnaleta mkataba mnatunga sheria nyingine yakuitengua na mtaitengua. Waheshimiwa Wabunge,nawaomba sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo hili la mgongano katiya sheria inayosema maliasili na utajiri wa nchi yetuushughulikiwe na Mahakama zetu uko vilevile kwenyeMkataba ambao unakuja kesho wa Bomba la Mafuta,kaangalieni. Mkataba wa Bomba la Mafuta unasematukigombana Uganda na Tanzania kwa sababu ya bombala mafuta mgogoro ule unaenda kuamuliwa London nahawa ambao wanajifanya ndio watetezi wa rasilimali za nchihii, hatuoni! (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nawaombeni, mimi ninamaneno makali sana, lakini nani aniambie kama hayaambayo tumeyapitisha yako sahihi. Aniambie hayaninayoyasema ni ya uwongo, kwamba hatujaletamkanganyiko wa kisheria hapa, kama tumeleta mkanganyikowa kisheria tunatunga mkataba wa Kimataifa, tunapinduakile tulichokipitisha hapa kwa majidai mengi. Tunakitenguamiezi miwili baadaye, sisi ni watu wa aina gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge,hasa Waheshimiwa Wabunge mlio wengi, narudia tena witowangu, haraka haraka haina baraka, maangamizi ya Taifahili na maanguko ya Bunge hili ni hicho kinacholetwa kilaleo kwa hati ya dharura. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa MasoudAbdallah Salim atafuatiwa na Mheshimiwa Janet Mbene.

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru. Tunagawana muda na MheshimiwaHamidu Bobali, nusu kwa nusu, sijui dakika ngapi, sijaelewani 10 au 15.

NAIBU SPIKA: Kama mnagawana maana yake weweni saba na nusu na yeye saba na nusu. Ama wewe saba mpeyeye nane, ama wewe nane yeye saba. Kwa hiyo, kubalianenikwanza useme hapo ili Katibu aweke vizuri.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nitaongea dakika nane na Mheshimiwa Bobaliataongea dakika saba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naminitajielekeza kwenye Azimio moja tu ambalo ni Azimio laKuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya AfrikaMashariki (East African Community Protocol on Peace andSecurity). Katika muktadha wa shughuli nzima za ulinzi nausalama na jinsi ambavyo articles zilivyokuja, naomba nianzena Article 12 ambayo inasema combating trans-national andcross border crimes. Katika mambo ambayo yameelezwa,sitaki nisome sentensi zote lakini nataka niende kwenye ile(e) illegal migration (uhamiaji haramu).

Mheshimiwa Naibu Spika, katika dhana nzima hii yauhamiaji haramu, imeonekana kwamba wakati tukiwezakupitia Azimio hili kuridhia Azimio hili, naunga mkono Azimiohili lakini tuangalie ni kwa jinsi gani kwa muda mrefu, pamojana vipengele vilivyomo katika Azimio hili, vya kuwezakuchukua taratibu, sheria na kanuni, lakini tuangalie ni kwanini baadhi ya wahamiaji haramu wanaotoka Eritrea,Ethiopia, Somalia wanafika kwetu Tanzania ilhali wanapitakatika nchi ya Kenya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo hapa yakujifunza, tunataka kwenda katika utaratibu ambaotunataka kwenda vizuri na wenzetu kuona kwamba kunahatua ambazo zitachukuliwa, kuna mikakati ambayo

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

itafanywa, lakini wasiwasi ambao unakuja hapa sasa nimahusiano, maelewano ya ziada katika shughuli nzima yakutoka wahamiaji haramu kutoka Eritrea, Ethiopia, Somaliawanaopita Kenya kuja kwetu. Naomba hilo liwe angalizokubwa katika mkataba wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nenda katika Article 13;preventing and combating cattle rustling, ule wizi wa mifugo.Katika shughuli nzima hii ya wizi wa mifugo kumekuwa naoperesheni nyingi sisi wenyewe kwanza hapa. Tulikuwa naOperesheni Tokomeza ambayo ukiangalia Ukanda ule waKigoma kulikuwa na mambo mengi, lakini katika maeneomengine ambayo viongozi hasa wa mipakani walio katikamaeneo yale ya wafugaji, wamekuwa wakipata matatizosana na malalamiko sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kutekeleza itifakihii na kuiridhia inaonekana viongozi walioko mipakani,Watendaji wa Vijiji, Viongozi wa Chama, sisemi ni chamagani lakini inaonekana wale walio wengi zaidi kwa sababundio waliopata ushindi katika maeneo haya wengiwanapata, chama hicho, sitaki kutaja kwa sababu nikitajaitakuwa ni ukakasi, wataanza mambo ya hapa na pale lakinihili ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Viongozi hawa wanapokearushwa, viongozi hawa ndio wanaoingiza mifugo, tumesemamara nyingi lakini bado Serikali imekuwa ikisema kwambaitachukua hatua hii, utaratibu unakwenda, tuna mipangokabambe, mikakati hapa na pale, lakini hakuna kitu. Hilo nitatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakwenda kuridhiamkataba huu, mimi sina pingamizi nimesema naungamkono kabisa, lakini tuangalie jambo lingine, tunakwendakuridhia itifaki hii, lakini tuna tatizo kubwa la urejeshaji waalama za mipaka (beacons). Hili suala ni la ulinzi na usalama,amani na utulivu. Mheshimiwa Shamsi anajua, MheshimiwaHussein Mwinyi anajua na wengine wanajua. Tuna tatizokubwa la urejeshaji wa mipaka katika maeneo mbalimbali,

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

ripoti kadhaa zimesema kwamba baina ya Tanzania paleTarime na Migori Kenya beacons zimeondolewa kwa mudamrefu, Serikali inasema tuna mkakati, suala hili ni mtambuka,itachukuliwa hatua hapa na pale, hakuna kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumetaja maeneo, kunaVijiji vya Panyakoo, Ronche, Ikoma, leo kila wakati unasikiakwamba beacons zimeng’olewa, zimeondolewa, lakiniutaratibu maalum haupo. Sasa tunakwenda kwenye Itifakihii lakini kuna mambo sisi wenyewe kwanza kwa kuwamambo haya ni mtambuka, Wizara ya Ulinzi, Wizara yaMambo ya Ndani, TAMISEMI, Mambo ya Nje, zote tukae kwapamoja katika nchi hizo husika wakati tunakwenda kuridhiaitifaki hii kuweka utaratibu wetu, hili jambo likae vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, maana inaonekana kamatunasukumwa tu, kwanza tumechelewa. Tangu tarehe 12,Machi iliposainiwa tumekaa miaka minne, tumebakia sisi naBurundi tu, sisi Watanzania ni watu wa mwisho tu, kunamambo kidogo ya kujifunza hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mambo hayaambayo tunakwenda nayo, basi napenda kusema kwambaMsemaji wa Kambi ya Upinzani alisema kwamba ni vemanchi zetu za Kiafrika ziendelee kujifunza katika kudumishaamani na utulivu katika mambo ya demokrasia pale ambapommoja kashindwa akubali matokeo. Unafuta uchaguzi, kwanini ufute uchaguzi? Kwa mantiki ipi, kwa dhana ipi? Kwamanufaa ya nani? Umeshindwa kaa pembeni kwa sababuhakuna mwenye hatimiliki ya kuongoza, nchi ni yetu sote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo amesema Msemajiwa Kambi ya Upinzani, namshukuru sana Msemaji,Mheshimiwa Cecilia Paresso, amesema jambo kubwa kweli,jambo zuri, jambo jema, amewaambia kwamba katikakudumisha amani na utulivu katika demokrasia hizi za mfumowa Vyama vingi pale ambapo mmoja atashindwa basi akaepembeni, ni jambo jema sana, na hili tupate kujifunza katikamaeneo mbalimbali.(Makofi)

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo machache,bila kupigiwa kengele ile ya mwisho, nashukuru sana nanaunga mkono Azimio hili la Amani na Usalama, lakini amaniiwe ya kweli, isiwe ile amani ya kuigiza igiza. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masoud, baada yakonilimtaja Mheshimiwa Janet Mbene, lakini WaheshimiwaWabunge tunapojadili humu ndani lazima tujue pamoja nakwamba huwa tuna masihara ya hapa na pale, lakini tusiletemtafaruku kwenye mambo ambayo nchi husika ndiyoinayopaswa kujua nini cha kufanya. Hili lililotajwa la mfano,Katiba yao ndivyo inavyosema. Kwa hiyo, tuwaachewamalize mambo yao salama, wao wenyewe waliamuahivyo na ndivyo inavyofanywa huko kwao, tuwaachie. Lakininje tukitoka hapo tunaweza kujadili ila humu ndani hayotuyaache yasije yakatuma ujumbe ambao uko tofauti kidogohuko nje.

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea. MheshimiwaMasoud anajaribu kusema amemkumbuka sana Jecha.

Mheshimiwa Janet Mbene, kama muda utakuwabado upo atafuatiwa na Mheshimiwa Richard Mbogo.Hakuna aliyerukwa, kila mtu atachangia, kwa sababu hataCHADEMA kuna ambao wamegawana dakika saba na nusuna sijawaita, kwa hiyo msitie shaka muda wako ukopalepale.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Nami napenda kuchangia hoja hii iliyopombele yetu. Kwanza naipongeza Serikali kwa kuleta hili Azimiohapa Bungeni kwa sababu hili suala la mradi wa Bonde laMto Songwe ni la muda mrefu lakini sasa naona linafikiatamati na inasaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napendakupongeza Serikali kuwa sasa hivi pia imeongeza wigo wazile Wilaya ambazo zitaguswa na mradi huu au programuhii kutoka zile mbili za mwanzo iliyokuwa Ileje na Kyela, sasa

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

mpaka Momba, Mbozi na Mbeya Vijijini, kwa hiyo hii vilevileitaleta manufaa zaidi kwa wananchi wa sehemu hizo zaSongwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda vilevilekuzungumzia kuwa kwa kweli hii programu imekuja wakatimzuri, kwa sababu kwa muda mrefu sana Mto Songweumekuwa ukisumbua sana pale ambapo kunakuwa namafuriko ambayo yanaletea kingo zake kuleta madharamengi sana ya kimazingira pia kuharibu miundombinu yaeneo husika na kwa kudhibiti sasa hivi itatusaidia sanakuhakikisha kuwa Mto Songwe unadhibitiwa lakini vilevileunatumika vizuri zaidi kiuchumi kulinda mazingira, vilevilekuboresha maisha ya wananchi wa maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na maendeleohayo inaonekana kuwa programu hii pia itasababisha ujenziwa miundombinu mbalimbali ya barabara, vituo vya afya,elimu na masuala ya utalii. Napenda kutoa rai kwa Serikalikuwa wakati wanapofikiria kufanya miradi hii basi wazingatiemiradi au mipango ya miradi iliyoko pale kwenye eneo hiloili tusiwe tuna miradi ambayo inakwenda sambamba wakatikuna haja ya kumalizia ile iliyopo ili tusilete ile duplication aukuzidisha ukiritimba kwenye shughuli za maendeleo za eneohusika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda sana kutoarai kwa Serikali juu ya kuhusisha wadau muhimu. Kwa sababuhata hapo nyuma ambapo mradi ulikuwa umefikiriwakufanywa, kuna wananchi mpaka leo walikuwawameambiwa kuwa maeneo yao wasiyatumie kwa sababumradi utapita, kama mnavyojua ni miaka mingi tangu wazoliwekwe na wamekuwa kwenye hali ya sintofahamuwakisubiri nini kinaendelea. Kwa hiyo, safari hiitutakapomaliza kuridhia na itakapoanza kufanya hiiprogramu basi wananchi wafahamishwe, Halmashauri husikazihusishwe moja kwa moja ili sasa wananchi watambue ninini kitakuja kuendelea katika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuzungumzia

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

masuala ya kujifunza kutoka kwenye matokeo ya miradimingine ya haya mabonde, tumesikia hapa kuwa kulikuwakuna mabonde kama tisa nchini ambayo yamekuwa namiradi lakini yamekuwa na ufanisi ambao wakati mwinginesio mzuri sana. Sasa hii ingekuwa ni fursa nzuri kwa mradihuu na wenyewe kuangalia jinsi gani watajifunza tusiingietena katika matatizo yale ambayo yaliingiwa katika miradiya huko nyuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, Ruaha tunajuajinsi ambavyo shughuli za kibinadamu zimeathiri sana mtoule na mpaka sasa hivi unaathirika hata kina chake na kwahiyo inaleta shida. Sasa na huu mradi nao ukaangaliwe katikamtazamo huo na zile Wizara zote ambazo zinahusika katikamradi huu basi ziwe na ushirikiano wa karibu ili kila mmojaasimame katika nafasi yake kuhakikisha kuwa mradi huuunakuwa wa manufaa kuliko kuwa wa hasara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala amelizungumziaMheshimiwa Lissu pale ningependa kusema pamoja na kuwaamelizungumza kwa njia ambayo haikufurahisha basilikaangaliwe, ingawa mimi kwa uelewa wangu mdogoingawa siyo Mwanasheria, huu ni mradi ambao unahusisharasilimali zinazogusa nchi mbili. Kwa hiyo, naamini kutakuwana makubaliano mazuri ya jinsi gani ya kusuluhisha usimamiziwake na sikuona kama kulikuwa kuna sababu ya kutoamaneno makali ambayo kwa kweli hayajengi.

Mwisho kabisa nataka kupongeza sana na kuombaWaheshimiwa Wabunge turidhie Azimio hili kwa sababulinakwenda kujenga na kuboresha miundombinu na rasilimalihii nzuri itatumika vizuri zaidi kuliko jinsi ilivyo sasa hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Janet Mbene.Mheshimiwa Richard Mbogo nilikuwa nimekutaja, kamamuda utakuwa umebaki atafuatiwa na MheshimiwaSelemani Kakoso.

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa hii nafasi. Kwanza nitoe tu hoja kwambaWabunge na Bunge zima tuunge mkono hizi hoja mbiliambazo zimewasilishwa ya kuhusu Bonde na hili la Amanina Usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na hili Azimio laBonde la Songwe, napendekeza kwamba kwa ujumla wetutuangalie umuhimu wa haya mabonde. Sehemu kubwa,watu bado hawajatambua kwamba umuhimu wa bondeuko kwa kiasi gani katika nchi, tunaangalia kuyalindamabonde kwa kwanza kuangalia vyanzo vyetu vya hayamabonde ne mito yote. Tumekuwa na sehemeu kubwa snaya uharibifu wa mazingira ambapo imepelekea mtu wa chinihafaidiki tofauti na mtu wa juu, kwa lugha nyepesi ya kigeniwanaita upstream na downstream users. Sasa kwa kuwekahuu mkataba kati ya nchi mbili tunaona kwamba kutakuwana usawa katika utumiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala zima la Bonde hili pialinakwenda kutujengea ushirikiano mzuri kati ya nchi hizi mbili,kati ya Malawi na Tanzania, kwa hapo nyuma kuna manenoyalishapita ya mtaani ambayo yalikuwa siyo mazuri lakinitunatumaini sasa kwa Mkataba huu ambao umesainiwa namatumizi haya ya bonde na faida zake zote ambazozimeelezwa na Waziri mwenye dhamana, tunatumainikwamba tutafaidika kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, faida ya kwanza ambayonimeiona kwanza ni ushirikiano ambapo tutakuwa kwapamoja na ukiangalia katika mipaka yetu watu wanafananatamaduni na lugha, kwa hiyo ushirikiano utaendeleakuimarika.

Lingine ambalo naona litakuwepo ni suala zima lakiusalama. Nchi mbili mnapokuwa mmeshirikiana katikashughuli za kiuchumi kama hili ambalo tumesaini maana yaketutakuwa na uelewa wa pamoja, tutakuwa na usalama katiya nchi na nchi, kwa hiyo, tunapongeza sana Serikali kwakufanya hii jitihada.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambachoningesema ni kwamba tuhusishe pia Wizara yenye dhamanaupande wa Mazingira, iendelee kupitia Sheria zake zaMazingira kuendelea kulinda vyanzo vyote ambavyovinakwenda kwenye hili bonde, tumeona kwamba nchi sasahivi imezungukwa sana na shughuli za kiuchumi ambazohazizingatii sana Sheria ya Mazingira, ile mita 60 kutokakwenye kingo za mito, mita 500 kutoka kwenye vyanzo vyamaji na Serikali imekuwa inahimiza sana. Kwa hiyo, naombasana Wizara inayohusika na mazingira waendelee kulindahaya mabonde yote katika nchi yetu ili vizazi na vizaziambavyo vinafuatia viweze kufaidika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hii nita-commentkidogo kwenye Commission, tuombe Wizara inayohusikaiangalie Commission ambayo imeundwa, waangaliematatizo ambayo yamewahikutokea, kwa mfano TAZARAambapo kwenye upande wa reli kati ya Tanzania na Zambia,waangalie changamoto zilizopo upande wa TAZARA naupande wa huku sasa hii Commission ambayo imeundwazisiweze kujirudia na utendaji wake uwe wenye tija na ufanisi.Kwa hiyo, tunaomba sana na hata staffing yenyewe izingatiekama mkataba vile ulivyo na namna bora ambayo wataonani ya kuboresha na itapendeza zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeelezwa faida nyingi namimi napendezwa sana kuona kwamba litajengwa bwawana tutaweza ku-control mafuriko ambayo huwa yanatokeana tutaweza kupata umeme, shughuli za kiuchumi zitawezakufanyika. Naunga mkono na naomba Wabunge wotetuunge mkono Azimio hili ambalo ni muhimu sana kwamustakabali wa maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuzungumziaAzimio hili la bonde la Mto Songwe, naomba nigusie pia nakuhusiana na kuridhia Itifaki, Amani na Usalama ya Jumuiyaya Afrika Mashariki. Kiujumla Tanzania ni nchi ambayoilijengwa kwa misingi mizuri na hasa Rais wetu wa kwanza,Hayati Julius Kambarage Nyerere alitengeneza amani kubwasana katika nchi yetu ya Tanzania na vitu vingi aliweza

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

kuviondoa. Kwa mfano; aliondoa utawala wa Kichifuikapelekea nchi inakuwa inatawalika vizuri, ukabila vyotehivyo vimekuwa vimesaidia sana Tanzania tumekuwa naamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nchi yetu Tanzaniailipokea sana Wakimbizi kutoka nchi za jirani ambazo niCongo, Burundi, Rwanda yote yalitokea kwa sababuwenzetu hawakuwa na amani. Sasa kwa misingi yamaazimio haya ambayo yanaletwa na tayari tuko kwenyeUmoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maana yake tutajikitakwenye haya maazimio ambayo yatakuwa yamesainiwakwa ajili ya amani na usalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu wanapokuwahawana amani matatizo yale yanaleta migogoro katika nchiyetu ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakimbizi, imetokeamatukio wamekamatwa na silaha katika Kambi zaWakimbizi na wengine matukio ya kiujambazi, sasa kwaminajili hiyo kwa kulinda amani itatusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengi ya nchi zajirani kuna Tume zimewahi kuundwa, kuna mojawapo RaisMstaafu Benjamin Mkapa amekuwa Mwenyekiti, HayatiNelson Mandela amewahi kuwa Mwenyekiti, marehemuHayati Mwalimu Nyerere amewahi kuwa Mwenyekiti katikakusuluhisha nchi za jirani kwa kutokuwa na amani. Nchi nyingiduniani zinasumbuliwa na masuala ya ugaidi, kwa hiyotunavyokuwa na umoja kama Jumuiya ya Afrika Mashariki,tutaweka msimamo wa kulinda amani na wananchi wakewote watakuwa kwenye hali ya utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba kuunga mkono hoja zote hizi mbili na nawashawishiWabunge wote tuziunge mkono. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa SelemaniMoshi Kakoso kama na yeye atakuwa amechangia mudamfupi basi tutamaliza na Mheshimiwa Pascal Haonga

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nishukuru sana kunipa nafasi hii kuchangia maazimio ambayoyamewasilishwa kwenye Bunge hili. Kwanza ninapongezekwa uwasilishaji ambao wawasilishaji wote wameyaelezeakwa ufasaha zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la amani suala lamsingi sana katika nchi yetu. Ili nchi iweze kufanya kazi vizurini sharti tuwe na amani ya kutosha, kwa hiyo MheshimiwaWaziri alipokuwa anawasilisha ni vema sasa kama Bungetuli-support Azimio hili kwa ajili ya kulinda amani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sisi tunaoishi mipakanibado kuna shida kubwa sana ya Watanzania ambaowengine wanaishi bila kuwa na uhakika mzuri wa maishayao, tunaiomba sana Serikali iimarishe suala zima la ulinzi nausalama hasa maeneo ya mipakani. Mimi natoka Mkoa waKatavi ambao tumepakana na Ziwa Tanganyika pia nchi yaCongo tumepakana nayo. Wapo Watanzania ambaowanaishi mazingira ambayo siyo sahihi. Naomba sana Serikaliiweze kuangalia mazingira hasa nchi zile zinazopakana naMaziwa kama ilivyo Mkoa wa Katavi, Rukwa na Kigomamaeneo haya tunahitaji sana kuweka ulinzi shirikishi katikanchi zote tunazopakana nazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania ni watuwakarimu, tumeweza kuwapokea wananchi wa Mataifambalimbali kama Congo, Burundi lakini mazingira tunayoishikule ni mazingira ambayo Serikali inahitaji kuweka ulinzishirikishi ili kupunguza haya matatizo ambayo yanawezayakajitokeza. Naipongeza Serikali kwa Azimio lililoletwa,naamini litakuwa suluhisho kwa nchi zote za Afrika Masharikina zile ambazo ziko nje ya Afrika Mashariki kama DRC-Congotuweze kuazimia yale ambayo yamewekwa ili yawe na tijakwa Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni juu ya Bondela Mto Songwe. Bonde la Mto Songwe, Azimio lililoletwa nimuafaka lakini lina mazingira ambayo yanafanana namaeneo mengine. Nizungumzie maeneo ya Mkoa wa Katavi.

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

Tunayo mabonde ambayo yametoka, tuna mito ambayoimetoka maeneo ya kwetu na imeenda mpaka nchi ya DRC-Congo, tuna Mto Lwegere ambao umevuka ZiwaTanganyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna madhara ya sualazima la mazingira. Upande wa Congo, Ziwa Tanganyikalinapeleka maji ambayo yanaleta athari kwa nchi yetu, sasani vema tunapoweka mikataba hii tuangalie na maeneomengine ambayo kimsingi yanaweza yakachangia sualazima la maendeleo na suala zima la mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, nje ya hapo tuna Mto Nileambao unatoka Ziwa Victoria. Ni vema sasa tuangaliemazingira ambayo yatakuwa ni mazuri kwa nchi yetu,kuwatengenezea mazingira mazuri hasa Watanzania. Mfano,Mto Nile ni mto ambao unatoka kwenye maeneo yetu lakiniWamiliki wakubwa wa Mto Nile ni wenzetu watu wa Misri, nivizuri tukaangalia maeneo haya, tukayapitia upya ili yawena manufaa kwa Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mazingira ni sualaambalo linahitaji sasa liwekewe kipaumbele na Wizarahusika ili tuweze kulinda Mabonde na mito ambayo kimsingiinahama. Bonde la Mto Songwe linahama na ndiyo maanalimeletwa hapa kwa sababu mipaka huwa inahama kutokasehemu moja hadi sehemu nyingine, lakini bado kwenyemaeneo yetu ya ndani, leo hii tunapozungumzia mabondehaya ambayo chanzo ni uharibifu wa mazingira, tuna MtoKatuma ambao unapeleka maji kwenye hifadhi ya Katavina unapeleka maji mpaka kwenye Ziwa Rukwa, leo hii ZiwaRukwa linapoteza thamani yake na upo uwezekano wakutoweka kabisa, ni kwa sababu hakuna ulinzi mzuri wamazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana Wazirimwenye dhamana aendelee na jitihada ambazozitatengeneza mazingira mazuri ili kujenga mikakati yakulinda suala zima la mazingira, lakini cha kufurahisha kwenyeAzimio hili ni juu ya mpango wa uwezeshwaji wa kiuchumi

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

kwenye maeneo yote. Tuwaombe sasa Wataalam wawezekushughulikia uhalisia wa kutengeneza mazingira ambayoyatalinda hadhi ya Watanzania waweze kuwezeshwakiuchumi ili waweze kuendana na uhalisia wa mabonde hayaambayo wamezungukwa nayo kwenye maeneo yamipakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado tuwaombe sanawataalam wetu watengeneze mazingira ya kisheriayatakayolinda nchi yetu ili Watanzania na wale ambaowanazunguka katika maeneo hayo wawe na faida na hayaMaazimio tunayoyakubali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana nanaunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Nilikuwa nimemtajaMheshimiwa Pascal Haonga ambaye ana dakika saba nanusu na nadhani hizo zinakamilika pale. Mheshimiwa Haonga.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, hayupo.

NAIBU SPIKA: Hayupo eehh?

MBUNGE FULANI: Ndiyo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ryoba Chacha dakikaSaba na nusu.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Nami niweze kuchangia Itifaki hii naombanianze na hii Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kuipitia vizuri nanimeilewa ni nzuri. Sisi kama nchi tunapaswa kuiridhia lakinikuna mambo machache ningetaka niseme, kwamba kunanchi zimejiunga na zingine hazijajiunga na kwa kuwa Itifakihii lengo lake ni kutatua migogoro ndani na nje ya nchiwanachama, kuzuia mauaji ya kimbari, kupambana na

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

ugaidi, kupambana na uharamia na kadhalika ni jambo zurisana. Hata hivyo, nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Masharikizinaongozwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi zao na Katibahizi zimetoa haki kadha wa kadha, lakini unakuta katika nchihizi, viongozi ambao wako madarakani wanaamuakukanyaga Katiba ya nchi hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba imetoa fursa yademokrasia, Katiba imetoa fursa ya uhuru wa mawazo,Katiba imetoa fursa ya uhuru wa kujieleza, Vyama vya Siasana kadhalika, anatokea mtu anakwenda kinyume na Katiba,huyu mtu siyo gaidi? Kwa hiyo, gaidi siyo wale wa kuvamiapeke yake ni pamoja na viongozi wanaokwenda kinyumena Katiba ya nchi, wanaokwenda kinyume na sheria ya nchi.Kwa hiyo, nimefurahi kuona hii Itifaki kwamba pamoja nawale wanaozuia vyama vya siasa visifanye mikutano kwamujibu wa sheria itawashughulikia, nimefurahi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni vizuri mfahamukwamba, amani siku zote ni tunda la haki. Kama viongoziwa nchi hizi ambao wako madarakani hawataki kutendahaki, hakutakuwepo na amani, ni vizuri tufahamu Muasisiwa amani ni Mungu mwenyewe. Kama viongozi wa nchihizi ambao wako madarakani wanawaona wananchiwenzao hawana haki ambayo haki imetolewa kwa mujibuwa Katiba, Mungu atawahukumu siku moja na namshukuruMungu ameanza kuwahukumu wengine leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi kamaMheshimiwa Ryoba ninaikubali hii Itifaki iko sawa sawa, Bungeliridhie ili wale viongozi wanaokwenda kinyume na Katibaya nchi, kuzuia vyama vya siasa visifanye mikutano kwamujibu wa sheria waweze kushughulikiwa na umoja huu waJumuiya ya Afrika Mashariki. (Makofi)

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lucy taarifa.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Naibu Spika,tunachochangia hapa kilichopo mbele yetu ni kitu kingine,lakini Mheshimiwa Mbunge anazungumza jambo linginekabisa ambalo haliko mbele yetu. Naomba ajikite kwenyemada kwa sababu hicho anachokiongea hapa siyo mahalipake na wala hayo anayoyaongea siyo ya kweli. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ryoba Chacha unapokeataarifa hiyo?

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,huyu mtu hata hajasoma Kanuni, kwanza hajui Kanuni, lakinila pili hii Itifaki inaongelea amani na ukisoma ndani yakekuna kuzuia ugaidi, mauaji ya kimbari, nini source ya mauajiya Kimbari? Ni Viongozi walio madarakani kutokutenda haki.Fuatilia kule Rwanda na Burundi nini kilitokea? Viongoziwaliokuwa madarakani hawakutenda haki. Msipotenda hakikunaweza kukatokea mauaji ya kimbari, kwa hiyo ni vizurihaki itendeke ili watu wote wawe na amani. Msipofanyahivyo haina maana, ndiyo maana nikasema hii ni nzuri sana,kwa sababu itawazuia wale viongozi ambao hawatendi hakikwa wenzao. (Makofi)

Jambo lingine nilitaka niongelee hii Commission yapamoja ya Bonde la Mto Songwe. Pamoja na Mbunge waSingida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu ametoa tahadharihapa kwa sheria iliyopitishwa. Pia niungane naye kwambani vizuri jambo hili liangaliwe vizuri ingawa maudhui ya Itifakihii ni mazuri sana kwa sababu jambo hili kimsingi lilitakiwalifanyike muda mrefu sana kwa ajili ya kutoa manufaa kwawananchi wa maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo pia mabonde mengisana, kuna Bonde la Mto Rufiji, kuna Bonde la Mto Mara naMabonde mengine ambayo kama mabwawayangetengenezwa, kilimo cha umwagiliaji kikafanyika,wananchi wa maeneo husika wangepata faida kubwa sana.Kwa hiyo, pamoja na weakness za kisheria ambazozimeonekana, ambazo naamini kupitia Bunge hili mtazipitiamkaangalia nini kinaweza kufanyika ili Commission hii iweze

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

kutekelezwa, lakini kimsingi maudhui yake ni mazuri lakiniangalizo kubwa ni mgogoro wa mpaka.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wa kipindicha Bunge cha Asubuhi. Kabla sijasitisha shughuli za Bunge,niwakumbushe tena kuhusu michango hasa ileinayozungumzia nchi nyingine. Mheshimiwa Ryoba mambouliyokuwa unayasema sijajua wewe umesoma historia kiasigani kuhusu nchi hizo, lakini ni mambo mazito kwenye nchihizo balaa! Sasa sisi hapa tunazungumza kana kwamba nimchango wa kuufanyia mfano kirahisi namna hiyo, hayamambo hata kwao yametungiwa sheria namna yakuyazungumza. Kwa hiyo, tusiyachukulie kirahisi sanatukaonekana Bunge la nchi hii kuna namna labda inayajadilimambo yale kinyume na Katiba zao lakini na taarifa zileambazo wao wanazo kule kwao.

Waheshimiwa Wabunge, ningewaomba sana tujikitekwenye yale ya kwetu sisi, kama tunatumia mfano wa njetutumie kwenye yale wanayofanya vizuri kwa sababu kilamtu atataka kusikia anavyofanya vizuri, lakini kwenye yaleambayo hayajakaa vizuri huko kwao tuwachie wao kamawanavyotuachia ya kwetu. (Makofi)

Baada ya kusema hayo, niwataje WaheshimiwaWabunge watakaopata fursa ya kuchangia mchana;Mheshimiwa Rashid Shangazi, Mheshimiwa Hawa Ghasia,Mheshimiwa Oran Njeza, Mheshimiwa Ester Michael Mmasi,Mheshimiwa Pascal Haonga na Mheshimiwa Hamidu Bobali.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayonasitisha shughuli za Bunge mpaka saa kumi na moja jionileo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 Jioni)

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naombatukae. Kabla hatujaendelea, baadhi yenu mnaweza kuwammepata taarifa kuhusu Mheshimiwa Tundu Lissukushambuliwa kwa risasi mchana huu. Mpaka sasa kamaBunge, Mheshimiwa Spika yuko hospitali na vyombo vyausalama pia vinafanya kazi yake. Kwa hiyo, naomba kwawakati huu tumwombee mwenzetu, Madaktariwanapoendelea kufanya kazi yao naye apate ahueni.

Nadhani Mheshimiwa Spika atakapomaliza hukotutapata taarifa, aidha mchana huu ama kesho asubuhi.Tuendelee kuwa watulivu kwa hili lililompata mwenzetu, kamanilivyosema tuendelee kumwombea ili afya yake irejee. Yukohospitali, Madaktari wanaendelea kumshughulikia, vyombovya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake nasi WaheshimiwaWabunge tuendelee kumwombea mwenzetu.

Baada ya kusema hayo, tutaendelea na kilichopombele yetu. Kama kuna jambo litakaloifikia meza, basimtataarifiwa.

Waheshimiwa Wabunge, nilikuwa nimetaja majinakadhaa ya watu watakaochangia mchana huu. Kwa hiyo,nitaanza kuita kwa kadri ninavyoona watu walioko humundani kwa sasa. Mheshimiwa Rashid Shangazi, atafuatiwana Mheshimiwa Oran Njeza halafu Mheshimiwa EstherMichael Mmasi ajiandae.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. Nami nachukua nafasi hii niungane naWaheshimiwa Wabunge pamoja na Mheshimiwa Spika,kutoa pole kwa mwenzetu kwa jambo ambalo limempatana tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie ili afya yakeiweze kurejea katika hali ya kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nami nitoemchango mbele ya Bunge lako Tukufu juu ya Azimio la Bungekuridhia Mkataba wa Kuanzishwa Kamisheni ya pamoja ya

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Bonde la Mto Songwe sambamba na kuridhia Azimio la Itifakiya Amani na Usalama kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya hivi karibuni sualala maji limekuwa ni suala ambalo linaelezwa kuwezakusababisha Vita Kuu ya Tatu ya Dunia. Maji yamekuwa nitatizo, lakini chanzo kikubwa cha ukosefu wa maji ni uharibifuwa mazingira. Pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ambayokimsingi yanashahibiana moja kwa moja na mabadiliko yatabia za binadamu hasa pale ambapo tunaharibu mazingira,basi maazimio kama haya yakija kwenye Bunge letu Tukufu,hakuna namna zaidi ya kuridhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe rai tu kwamba pamojana nia nzuri ya Serikali kuridhia hili, lakini sasa iwe ni mwanzowa changamoto pia kuhifadhi mabonde mbalimbali yaliyokokatika Taifa letu. Kwa mfano, tumeona hivi karibuni kulikuwana wadau wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu lakini pia kuleMkoani Rukwa na Katavi kuna bonde pia, nimeonaMheshimiwa Waziri anayehusika na mazingira walikuwawanafuatilia pia uhifadhi wa lile bonde; na kuna mabondemengine kama Malagarasi, bonde la Mto Pangani nayo piabado hayako katika hatua nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitoe rai kwambatunapokwenda kuridhia mikataba hii ya Kamisheni ya Pamojaya Bonde la Mto Songwe kwa maana kwa nchi ya Tanzaniana Malawi, basi pia tuone umuhimu wa kuangalia kwamapana haya mabonde mengine ambayo yanazungukakatika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe rai, kama ambavyokwenye Kamati wameshauri kwamba nchi yetu haikuwa namahusiano mazuri sana na Malawi hasa katika eneo hili laziwa, lakini nadhani kwamba itifaki hii iende pia kuamsha arimpya katika kutengeneza mahusiano, siyo tu ya kidiplomasialakini ya kiuchumi, ya kijamii na ya kimazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kwamba mkatabahuu ukiridhiwa utoe tija ambayo inategemewa kwa

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

wananchi wa pande zote mbili. Pia ni kipaumbele kwambakwa kuwa hata Mkoa huu wa Songwe ni mkoa mpya,tunaamini kwamba fursa mbalimbali zitakazopatikana kupitiauanzishwaji wa hii Kamisheni utasaidia hata kusukumamaendeleo mengineyo hasa katika Sekta za Kilimo nauzalishaji wa umeme; tumeona hapa takriban megawatt 180zinaweza zikazalishwa kupitia bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto nyingineambayo naiona ni suala zima tu la eneo kwa wananchi juuya utunzaji wa jumla wa mazingira hasa tunavyoona kwambamto huu unatiririsha maji kuelekea katika Ziwa Nyasa na maranyingi shughuli za kilimo wakati mwingine zinachangiakusababisha uharibifu na kusababisha vina vya maziwakupanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitoe rai kwambapia wananchi waelimishwe ili wale ambao wanalimapembezoni mwa mabonde haya, wawe waangalifu kiasikwamba tuweze kulinda siyo bonde peke yake, lakini piahata mtiririko wa maji kuelekea katika Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili nizungumziekuhusu kuridhia kwa Itifaki hii ya Amani na Usalama waJumuiya ya Afrika Mashariki. Napenda kupongeza kwa hatuahii. Pia natoa rai kwamba naunga mkono moja kwa mojaAzimio hili, kwa sababu tumeona kwamba sasa hivi nchi hiziza Afrika Mashariki tuna tatizo la ugaidi. Tumeona mara nyingikule upande wa Kenya hasa eneo la Garissa na Mombasamara kwa mara wamekuwa wakishambuliwa na magaidihasa hawa wanaotokana na wenzetu wale wa kutokaSomalia, Al-Shabaab.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni, mwaka mmojauliopita, hata katika Mkoa wa Tanga katika maeneo yaMapango ya Amboni kulipatikana vikundi ambavyo vilikuwana dalili zote kwamba ni vikundi vya kigaidi na hata haliinayotokea pale katika eneo la Kibiti, Mkuranga ni viashiriaambavyo siyo vizuri sana kwa ustawi wa amani na usalamakatika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niseme wazikwamba protocol hii itatusaidia ili tuwe na ulinzi wa pamojakama ambavyo tunafanya na hata juzi hapa, tuliona kuleTanga kulikuwa na zoezi la pamoja kwa nchi za SADC. Kwahiyo, tutafarijika sana kwamba zoezi hili sasa nje ya SADClifanyike pia kwa nchi hizi za Afrika Mashariki hasa kwakuzingatia kwamba sisi mipaka yetu hii karibu nchi zote tanoukiondoa Sudan Kusini ambayo ni mwanachama mpya, lakininyingine zote tunapakana nazo kila mahali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia hii itasaidia kama hapaambapo wamezungumza pia kwamba wakati mwinginekuna minada ya mifugo inafanyika katika hizi nchi, hata mimikatika Jimbo langu la Mlalo pia ni mwathirika wa hii minada.Ni kwamba katika Bonde la Mkomazi ambako kuna wafugajiambao wanapatikana katika Wilaya za Same, LushotoMkinga na Korogwe, mara nyingi kule hatuna minada katikahaya maeneo kwa upande wa Tanzania. Kwa hiyo, hawawafugaji huwa wanapeleka kuuza mifugo katika upande waKenya. Kwa hiyo, kwa kupitia itifaki hii, naamini kwamba sualahili litaimarisha mahusiano haya na tunaweza hata tukawana masoko mazuri yenye amani na usalama na kusaidiabiashara hizi ziweze kufanyika vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, nitoerai kwamba ipo mipaka katika Jumuiya ya Afrika Masharikiambayo siyo mipaka rasmi, lakini kwa Serikali hizi kwakushindwa kuirasimisha, inachochea sasa hata vitendo vyauhalifu kufanyika na biashara za magendo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pamoja nakwenda kusaini Azimio hili la Amani na Usalama wa Jumuiyaya Afrika Mashariki, lakini pia Serikali sasa ione pia chachuna ione pia mwanya wa kwenda kurasimisha ile mipaka, hataisiwe katika ngazi za Kimataifa lakini angalau katika ngazizi le zi le za ujirani mwema kwamba tuwe tunawezakubadilishana mazao ambayo yanapatikana katika nchi hizitunazopakana. Tofauti na hivyo, bado unabaki mwanya kwawananchi wa kawaida kuitumia kuvusha kwa njia zamagendo.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitoe rai kwambatunapokuwa na maazimio mazuri kama haya ni vizuri piatukayatumia haya haya kuongeza tija nyinginezo zakiuzalishaji, isibaki tu kwa ulinzi na usalama, lakini pia zauzalishaji na kuinua uchumi wa wananchi katika maeneohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana nanaunga mkono Maazimio yote mawili. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Oran Njeza,atafuatiwa na Mheshimiwa Esther Michael Mmasi.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana. Nami kwanza niungane na WaheshimiwaWabunge wenzangu kumwombea mwenzetu uponyaji waharaka kwa haya yaliyompata.

Mheshimiwa Naibu Spika, Azimio hili la leo ni muhimusana kwa nchi yetu, hata kwa nchi zinazotuzunguka. Labdaningeanzia pale kwenye Azimio, nafikiri kunahitaji masahihishokidogo ya jina la Wilaya. Kuna Wilaya pale imetajwa, MbeyaVijijini. Hatuna Wilaya ya Mbeya Vijijini, ila tuna Wilaya yaMbeya. Kwa hiyo, labda kwa ajili ya kumbukumbu sahihi zaBunge, ingebadilishwa na kusahihishwa kuwa Wilaya yaMbeya.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo,niende zaidi kwenye maoni. Niungane kwanza na maoni yaKamati, walivyosisitiza kuwa katika mkataba huu labda ndiyowakati muafaka wa Serikali kuangalia ni namna gani huumkataba vile vile unaweza kutusaidia katika kutatua tatizola mgogoro wa mpaka ulioko katika Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri hiki kinaweza kuwani chanzo kizuri sana na Ziwa Nyasa linatokana na Mtosongwe na Mto Songwe kwa kiasi kikubwa unatoka kwetu,kwa hiyo, nafikiri hiyo inaweza kuwa ni chanzo kizuri ni namnagani tukaondoa hili tatizo la mgogoro wa Ziwa Nyasa.

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili katika maoni yaKamati, vile vile waligusia elimu kwa wananchi. Nafikiri hili nijambo muhimu sana kuangalia ni namna gani wananchiwakashirikishwa kikamilifu na kuwapa elimu ya namna yakuhifadhi haya mabonde yetu na hivi vyanzo vya mito.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia tunapozungumziabonde la Mto Songwe, kuna Mto Songwe ambao unakwendaZiwa Nyasa na kwa kweli kilichonifurahisha hapa ni namnagani yatajengwa yale mabwawa matatu na faida za yalemabwawa matatu ambayo yatazalisha umeme takribanMegawatt 182.2. Pamoja na hilo, hayo maji yatatumika kwaajili ya umwagiliaji na vile vile kwa ajili ya matumizi yamajumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia yale maeneo yakwetu hasa katika Wilaya yangu, pamoja na kuwa na mitomingi ambayo ndiyo vyanzo vya mito hii inayokwendaSongwe na ile Songwe inayokwenda Rukwa, vile vile ndiyochanzo cha Mto Ruaha, lakini yale maji kwa kiasi kukubwawananchi hawayafaidi. Kwa hiyo, kwa mtazamo huu uliopokwenye mkataba huu nina imani ya kwamba Serikaliitaangalia ni namna gani wananchi nao wafaidike na hayamaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoliangalia bonde laMto Songwe ambao unaelekeza maji yake kwenye ZiwaNyasa, napendekeza kuwa Serikali vile vile iangalie bondela Rukwa ambalo nalo lina Mto Songwe ambao unapelekamaji Ziwa Rukwa. Hili ni bonde muhimu sana na kwa kiasikikubwa Ziwa Rukwa karibu linaanza kupotea kwa ajili yaudongo na mmomonyoko ambao unasongwa na mtoSongwe kupelekwa Ziwa Rukwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa katika huu mtazamoambao tunauona hapa leo, nafikiri itakuwa ni jambo jemasana, tuanze sasa hivi kuangalia kuchukua hatua za haraka,ili haya yanayofanyika kwenye Bonde la Mto Songweunaopeleka maji Ziwa Nyasa, vile vile iende na kwenye MtoSongwe unaopeleka maji Ziwa Rukwa. Tufanye hivyo hivyo,

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

kwa vyanzo vingine vya mito vilivyoko kwenye milima yaUporoto na Kitulo ambao maji yake ndiyo chanzo cha MtoKiwira ambao unapeleka maji vile vile Ziwa Nyasa na vile vilendiyo chanzo cha Mto Ruaha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hivi vyanzo vyoteni muhimu sana. Kwa hiyo, elimu itakuwa muhimu sana kwawananchi, lakini tufanye mikakati ya makusudi, ni namna ganituwasaidie hawa wananchi ili waone manufaa vile vile, naowahusike katika kuhifadhi hivi vyanzo vya hii mito.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ester MichaelMmasi, atafuatiwa na Mheshimiwa Rehani.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaheshima ya pekee kusimama kwenye Bunge lako Tukufu namikuweza kuchangia kwa kifupi sana kuhusiana na documentshizi tatu ambazo tumeletewa, tuweze kuzipitia kwa minajiliya kuweza kulinda na kuhifadhi maliasili ya Tanzania, kuwezakulinda amani na usalama wa nchi yetu na kuinua uchumiwa Tanzania kupitia mradi wa Hoima - Tanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajielekeza tu kwenyeAzimio hili moja la mkataba kuanzisha Kamisheni ya Pamojaya Bonde la Mto Songwe, kwa sababu kimsingi sikuwezakupitia documents zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza kabisa na kurasaya saba Article No. 7, uundwaji wa hii Council, tukisoma paleSection (1) tunasema kwamba Board Memberswatakaoiunda hii Council, tume-mention kwambahatutakuwa na zaidi ya watu sita.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika watu sita, tuka-mention relevant Ministries ambazo tunafikiri zitatengenezahii Board Composition kwenye kusimamia hii Council. Pia tuka-

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

mention Wizara ya Maji, Ardhi, Energy, Irrigation, Agricultureand Local Government. Katika hawa watu sita, ukiangaliahizi Wizara hapa, tunapata watu watano, lakini hii nafasimoja tumeacha kwenye discretion power ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri pengine ni vizuriWizara ikajaribu kuangalia au ku-consider technical personellambaye ana specified background ya finance auaccounting management.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababuukiangalia kwenye majukumu haya ya hii Bodi, utaona palekwenye page eight Section (c), tunasema kwamba pamojana majukumu mengine hii Council itakuwa na majukumu ya:“to establish guidelines for financial and technical assistanceand development of projects and programs.” Pia ukienda(d) tunasema kwamba, pamoja na majukumu mengine, hiiCouncil itakuwa na majukumu ya ku-approve the budget ofthe Commission by the joint Steering Committee and suchblah blah blahs.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, concern yangu,nafikiri ni vyema kwa kuwa tume- consider Deputy Ministersndio ambao watatengeneza hii Council, kwenye nafasi zawatu sita tume consider Deputy Minister’s watano. Ni concernyangu kwamba pengine either tu-consider na Deputy Ministerfrom the Ministry of Finance ama tuwe specified tusemekabisa tutahitaji kuwa na technical personnel mwenyespecified background in financing or accounting. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo, nikija page nine,kwenye the Committee; uundwaji wa hiyo committee,ukisoma pale Section One inasema kwamba hiyo Committeeitaundwa na Wajumbe watano, lakini hatujaona backgroundof the relevant Ministries ambao wataunda hii Committeekama ambavyo ilikuwa kwenye Council.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni ushauri wangupia tuseme hawa members wana background gani; au

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

watatoka kwenye Bodi gani; au ni Ministries gani? Tusiachetu hivyo ina-hang. Kismsingi naona kama vile tunahitajikuongeza kitu hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukija pale theChairmanship of the Committee, tumesema kwamba huyuChairman atakuwa anaishi kwenye nafasi yake kwa mudawa mwaka mmoja na itakuwa ina-rotate, lakini pia nikawanahoji ni vyema basi tungeona the life span au projectduration kwa maana kwamba mimi ningeweza kusemambona one year haitoshi? Sasa napata shida kwa sababuhata sijui life span ya hii project, yaani the Shared WatercourseProjects. Kwa hiyo, ni vyema basi tukaona kabisa hii projectni ya muda gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kimsingi naonahivyo, kwa sababu naweza nikasema kwamba mwakammoja hautoshi au nikashindwa kupata relevance yamwaka mmoja kwa sababu kimsingi sijui hata life span ya hiiproject. Kwa hiyo, concern yangu kwenye section hiyo ilikuwani hiyo niliyoi-mention.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nikienda section 12kwenye Sekretariet, tunasema pamoja na Bodiitakayoteuliwa; appointing authority of cource imekuwamentioned, lakini pia tukasema itakuwa headed na ExecutiveSecretary pia itakuwa assisted na Deputy Executive Secretarylakini who are the body? Hatujaona bado hii bodi ni akinanani? Wako wangapi? Wanatoka wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukiangalia functions, itmeans zinatakiwa ziwe performed na a certain number ofpeople, lakini siyo tu Executive Secretary au Deputy Secretary.Kwa hiyo, kimsingi naona tuna haja kabisa ya kusema idadiya Board Members, ikibidi pia na background zao, lakini siyotu kusema kwamba itakuwa headed na nani kwa sababutayari tuna duties and responsibilities to be performed by acertain number of people.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kwenda kwaharaka haraka page number 15, kuhusu dispute resolution.Ukiangalia kwenye hii dispute resolution, the way imekuwadrawn, hutaona who is the specified body to deal with thedisputes or misunderstandings. Nadhani ingekuwa ni muhimukabisa na itakuwa na tija kama tutaweka the governingboard ya kuweza ku-overseas disputes au misunderstandings.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka mpaka ZiwaMalawi, ile misunderstanding ambayo tuliyokuwa nayo,nafikiri ni fundisho tosha. Kwa hiyo, kimsingi napenda kablaya ku-question kwa nini SADC Tribunal iwe ndiyo AppellateBoard lakini pia ni muhimu tukaona kwamba kunakuwa nagoverning board ya ku-overseas any dispute that may ariseduring the execution of this project.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukisoma hii documentinakwambia host country ni Tanzania na Makao Makuuyatakuwa Mbeya kule Songwe. Sasa kama host country niTanzania, kwa nini Appellate Board inabaki kuwa SADCTribunal? Kimsingi niki-refer hata kuna Mjumbe mmojaameongea humu ndani, lakini siangalii kwake, naangaliakama nilivyoelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipitisha hapa juzi Miswadaya kuweza ku-govern our natural resources, ile PermanentSovereignty Act ambayo tulijikita na tukasema kabisakwamba any dispute or misunderstands zitakuwa dealt withinthe country. Kimsingi ukiangalia hii document na ukiangaliavitu ambavyo tumepitisha Miswada na Sheria ambazotumepitisha nadhani hapa kunaleta ukakasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba naungamkono hoja asilimia mia, mawasilisho yaliyoletwa na Wizarahusika katika muktadha mzima wa kuijenga Tanzania yenyeuchumi wa kati, lakini pia ni subject to minor correctionswhere necessary. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Rehaniatakuwa mchangiaji wetu wa mwisho kwa upande wa

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

Wabunge, utafuata upande wa Serikali. Mheshimiwa Rehaniatafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Olensha halafu atafuatiaMheshimiwa Dkt. Mwakyembe.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana na mimi kupata fursa hii adhimu. Kwanzaniunge mkono hoja hii ya kuanzisha Commission hii ya Bondela Mto Songwe ambayo kimsingi, the highly potential areakwa nchi yetu, kwa uchumi wa nchi hii, lakini vilevile kwamustakabali wa wananchi wale wa Wilaya zile tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwamba mimikwa bahati nzuri nimeusoma huu mkataba vizuri nanimeuelewa madhumuni yake. Ikiwa dhumuni kubwa nikuhifadhi, kuendeleza na kuondoa athari za maji ambayoyanasababisha mto ule uweze kuhama kutoka sehemu mojakwenda nyingine na tishio la athari ya wananchi ambaowanakaa pembezoni mwa mto ule.

Mheshimiwa Naibu Spika, fursa hasa za kuangalia kitugani ambacho kitaweza kutusaidia kama nchi, eneo lile laMto Songwe kwa Tanzania ni belt ya uzalishaji wa mazaombalimbali. Kinachotakiwa baada ya kuridhiwa Kamishenihii; Kamisheni itengeneze mpango mkakati ambao utawezakuridhiwa na pande zote mbili kwa sababu yale yoteyaliyoainishwa katika Kamisheni hii, kila mmoja yanamgusahasa kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango mkubwa pale wakuanzisha mabwawa matatu yale ya Songwe Juu, SongweKati na Songwe Chini, kwa kweli kwa Tanzania ni fursa kubwakwanza kwa upatikanaji wa maji hasa ya mvua. Ile dhanaya rainfall harvesting pale ndipo itakapotimia. Tutakapowezakuyavuna yale maji, tutaweza kuu-shape ule mto uwezekwenda kwa mujibu wa mwelekeo tunaoutaka sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mto ule unafunguauwanja mpana wa kuanzisha maeneo ya umwagiliaji majikwa eneo lile la Kyela. Tutaweza kuzalisha mpunga kwakutumia yale mabwawa kama wanavyozalisha Moshi Chini

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

na Moshi Juu. Tufanye uwekezaji wa maana ili nchi ionekanekwamba kuanzisha ile Kamisheni imeleta manufaa na isiweKamisheni tu kama nyingine ambazo baada ya miakamitano, kumi tukija kutathmini, hakuna kilichofanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba Mawaziriwatakaosimamia, pawe na uwekezaji ambao utaleta fursakwa kila sekta. Tukizungumza Sekta ya Kilimo, zaidi ya hekta15,000 pale tunaweza kuzifanya zote kuwa za umwagiliaji majina zikaweza kutuzalishia zaidi ya tani laki tatu za mchele.Hilo linawezekana, suala ni kujipanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika eneo lile kunamazao ya biashara, kuna ndizi ambalo ni zao kubwa katikamaeneo yale ya Tukuyu na Kyela. Fursa ya uzalishaji kwakutumia irrigation ipo, kutumia mabwawa yatakayoanzishwakule. Tuhamasishe wananchi wajipange kwenye uzalishaji watija kuliko uzalishaji wa kutegemea mvua ambao haunauhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo yale, badounaweza kuzalisha mahindi kwa mpango maalum na nchiikaweza kunufaika na kuondokana na tishio la njaalinalotokana na ukosefu wa maji wa kila siku. Isitoshe, kazikubwa inayotaka kufanywa pale ni kuhifadhi mazingira yavyanzo vya mto ule toka vinavyotokea huko kwenye zilechemchemi za kutilia maji katika eneo lile, kwa sababu majikatika eneo lile ni mwaka mzima. Hiyo siyo kwambayanavunwa yale ya mvua, lakini maji yanatoka kwenyechemchemi ambazo ziko katika maeneo mbalimbali nandiyo maana tunapata fursa na nguvu ya kuanzisha yalemabwawa ya kuzalisha umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pale panategemewakuzalishwa umeme zaidi ya megawati 180, kitu ambachotunafikiria tu kwamba mgawanyo uwe nusu kwa nusu.Nasema, bwana, kila mwamba ngoma huvutia kwakevilevile. Asilimia kubwa ya ule mto na eneo kubwa ni letu siye,lakini na zile infrastructure ambazo zinahitajika kujengwakatika eneo lile ziko kwetu. Nafikiri hao watakaoenda kukaa;

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Mawaziri na watu wengine, waangalie uwiano wakugawana na siyo tu kwa kujenga mahusiano ya kusemakwamba tunaridhiana nusu kwa nusu, hapo tupaangalie kwaundani zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nitachangiakatika hii Kamisheni ni uanzishwaji wa viwanda. Tuhamasishemaeneo yale ambayo yanazalisha kokoa katika maeneombalimbali ya Kyela, basi kuwepo na kiwanda ambachokitaweza kuzalisha Chocolate na vitu vingine kuanzishiawananchi wetu ajira na fursa nyingine mbalimbali za kiuchumizitakazokuwepo kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo vilevile inafunguacorridor ile kuweza kuwa na mpango wa kujengwa reli kutokahuko Mchuchuma mpaka Lindi lakini ikaunganisha mpakakwenye reli ya TAZARA. Itazidi kufungua fursa kubwa zakiuchumi na kulifanya eneo lile kuwa moja katika eneo,wanaita economic zone. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili kwa nchi yetulimekuwa likitumika isivyo na faida; yaani l ikitumikakikawaida. Hii sauti ya kuanzisha Kamisheni ilianza miakamingi, lakini tushukuru Mungu sasa hivi Serikali imefika mahalipa uamuzi wa kuianzisha na kuanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba wataalammbalimbali wa Wizara zote zinazohusika na Kamisheni hiikukaa na kuanzisha miradi ambayo itaweza kuwasaidiawananchi kushiriki nao hasa kwenye uhifadhi wa mazingiraya eneo lile, kwa sababu kila eneo mto unapopita mazingirayanakuwa ni mazuri, lakini kutokana na kazi na shughuli zakibinadamu, mazingira yale yanaharibiwa kwa njia moja aunyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, wito wangu niombe hasaWizara ya Kilimo kupitia mifugo, eneo hili lilindwe na lisiingizwemifugo. Tutalimaliza! Tutauua ule mto na matokeo yake majiyale yatashindwa kutiririka kama yanavyotiririka hivi sasa.Haya ni mambo ya msingi. Tunaweza kuanzisha mambo

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

mazuri, lakini kuna lingine tukalisahau ambalo linaathirimazingira ya pale. Kwa hiyo, nawaomba sana wahusika waMikoa, Wilaya na maeneo mengine kuweza kuepukauingizwaji wa ngombe wengi katika maeneo yale paleambayo yanatumika kwa kilimo sasa hivi kikubwa. KuleZanzibar wanasema mchele wote unaoletwa kutoka Mbeyandio wenye soko kubwa. Kwa hiyo, nawaomba wazalishajina viongozi walioko katika maeneo yale tuweze kutilia mkazosana uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nimelionakwamba ni fursa kubwa, zile meli za bandari za Itui, Itumbi nasehemu nyingine, pale sitaweza kufanya kazi vizuri zaidi, kwasababu ufungukaji wa ile Kamisheni itaanzisha fursa kubwaya wafanyabiashara, lakini na wenzetu wa Malawi watapatafursa kubwa ya kuleta mizigo yao katika maeneo yale nahasa kwa kutumia ile meli mpya iliyoundwa hivi sasa iliyokuwainaanza kazi kuwa na manufaa zaidi kuliko vile ambavyotulivyokuwa tumetegemea. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rehani, kengele ya pili hiyo.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa William TateOlenasha, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe,halafu Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliajiajiandae.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru nami kupata fursa yakuchangia mjadala unaoendelea. Napenda kuungana naWaheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole sana kwaMheshimiwa Tundu Lissu kwa yaliyompata na kuungana naovilevile kumwomba Mwenyezi Mungu amjalie apate afyanjema na arudi katika shughuli zake za kawaida.

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajikita katika hoja mojailiyotolewa kuhusiana na Azimio la Kuridhia Mkataba KuanzaKamisheni ya Pamoja Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Azimio hili ni muhimu sanakwa nchi yetu na katika hali ya kawaida, limechelewa sana.Kumekuwepo na majadiliano ya kuanzisha Kamisheni yakusimamia bonde hili kati ya Tanzania na Malawi tokeamwaka 1976. Kwa kweli imechelewa sana kwa sababurasilimali ambayo inatumika na nchi zaidi ya moja katika haliya kawaida ingetakiwa iwe na utaratibu wa pamoja wakusimamia; na katika hali ya kimazingira ambayo bonde lilelipo kwa sasa, kwa kweli Kamisheni hii ni muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja ilitolewa kwambakifungu cha convention hii inayozungumzia kuhusu usuluhishiwa migogoro inapingana na sheria ambayo tulipitisha yaNatural Wealth and Resource Permanent Sovereignty Act ya2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Tundu Lissualitoa hoja kwamba kwa sababu itifaki ambayotunaizungumzia inaanzisha utaratibu ambao kama kutakuwana mgogoro kati ya Malawi na Tanzania kuhusu usimamiziwa Bonge la Mto Songwe, basi itapelekwa kwenye Tribunalla SADC. Yeye aliona inaingiliana na inavunja sheria ambayotumepitisha hivi karibuni ya kusimamia rasilimali zetu, sheriaambayo nimeitaja ya Natural Wealth and ResourcePermanent Sovereignty Act of 2017, hasa katika Kifungu cha11(1) mpaka (3).

Mheshimiwa Naibu Spika, mikataba hii au sheria hizini tofauti. Wakati Mkataba wa Kuanzisha Kamisheni yaPamoja ya Usimamizi wa Bonde la Mto Songwe inashughulikana uhusiano wa nchi na nchi, yaani katika maana ya bilateralagreement, sheria yetu ile ambayo nimeitaja ya PermanentSovereignty, yenyewe inahusika na uhusiano wa nchi yetuna wawekezaji au makampuni ambayo yanawekeza katikarasilimali zilizoko katika nchi yetu.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Kwa hiyo, katika hali ya kawaida ni mikataba tofauti;mwingine ni mkataba wa Kimataifa ambao unaongozaushirikiano kati ya nchi mbili lakini nyingine ni sheria ya ndaniinayohusiana tu na mikataba ya kutumia rasilimali zilizopondani ya nchi yetu. Kwa hiyo, niwahakikishie tu WaheshimiwaWabunge kwamba, ni vitu tofauti na wala hakuna hatariyoyote katika sisi kuridhia itifaki hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ni lazima tufahamukwamba katika hali ya kawaida kama rasilimali ambayoinalindwa na sheria inatumika na zaidi ya nchi moja,haiwezekani sheria ya nchi moja ikawa ndiyo inayotawalarasilimali ile. Kwa hiyo, kwa sababu rasilimali ya Bonde laMto Songwe ni shared resource, ni rasilimali ya nchi zaidi yamoja, katika hali ya kawaida ni lazima isimamiwe kwapamoja na kwa sheria ambayo ni ya pamoja. Itifaki hiyoambayo ndiyo tunasema sasa tunataka ianze kufanya kazi,imetengenezwa kwa utaratibu wa itifaki za Jumuiya ya Kusinimwa Afrika SADC ambayo sisi ni wanachama na Malawivilevile ni mwanachama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa pamoja tulishakubalihuko nyuma tulipojiunga kwamba masuala yote ambayoyanahusiana na maji au rasilimali ambazo zinamilikiwa kwapamoja, kama kuna migogoro, migogoro ile itaamuliwa kwakutumia Tribunal au Mahakama ya SADC. Kwa hiyo,niwahakikishie tu Waheshimiwa Wabunge kwamba hakunasheria yoyote iliyovunjwa, tuko sahihi kabisa. Sisi tukiridhiaAzimio hili wala hatutakuwa tumevunja sheria yetu ambayosisi wenyewe tumeipitisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile hoja ile iliekeakutaka kujenga hoja kwamba sisi hatuheshimu sheria zaKimataifa tunapotunga sheria kama ile ya kwetu The NaturalWealth and Resources Permanent Sovereignty Act, 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunaheshimu sheria zaKimataifa na ndiyo maana hata leo hii tupo hapatunazungumzia kuhusu Bilateral Convention, ni sheria ambayokwa mwonekano wake, kwa hali yake ya kawaida ni Sheria

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

ya Kimataifa, bado tunaendelea kuheshimu, lakini kuheshimukule haitunyimi sisi kuendelea kulinda rasilimali zetu ikiwa nipamoja na kuweka utaratibu wa kusuluhisha migogoroambapo tunafikiri italinda zaidi rasilimali zetu, itatupa nafasikubwa zaidi ya kuweza kusimamia rasilimali zetu bilakuingiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo machache,napenda kuunga mkono hoja ya Azimio lililopo mbele yetu.Nashukuru sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Naibu Waziri wa Maji naUmwagiliaji, atafuatiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika…

NAIBU SPIKA: Samahani, kumbe nil ishamtaja.Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursanami nichangie kwa kifupi tu kuhusu moja ya mazimio yaliyokombele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mshitukomkubwa nilioupata kwa taarifa uliyotupa hapa kuhusuMbunge mwenzetu, naungana nawe kabisa kumwombeamwenzetu apate ahueni haraka na vilevile namwombaMwenyezi Mungu atupe ustahimilivu mkubwa katika kipindihiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nalazimika kusimama kamanilivyosema, kuchangia kuhusu Azimio la Kuanzisha Kamisheniya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Tanzania naMalawi. Kuanzishwa kwa Kamisheni hii ambako kuna miradichini yake kadhaa ya maendeleo kwa wananchi, ni sawakabisa na kutumia jiwe moja na kuua ndege watatu kwapamoja.

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa Azimio hililitawanufaisha watu zaidi ya laki tatu; ni idadi kubwa sanahii ambayo iko katika hilo bonde hasa kupitia miradi yaohiyo ya umwagiliaji, miradi hiyo ya maji safi na vilevile miradiya umeme, kama ambavyo wenzangu wameelezanisingependa kurudia.

Pili, tutakuwa tumetatua tatizo sugu la muda mrefula Mto Songwe kupindapinda kubadilisha njia yake kila wakatina kusababisha watu waliokuwa Tanzania kuwa wa Malawimara nyingine na Wamalawi kuwa Watanzania. TRA najuawatashangilia sana kusikia hili, maana wanaowadai kodi,mara nyingine wanashindwa kwenda kuwadai maana tayariwako Malawi kutokana na maamuzi ya huo mto.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingine wenginehapa tunategemea kura kwa Watanzania wetu. Kuna kipindinimewahi kukuta ngome yangu kubwa yote imehamiaMalawi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa haya ndiyo mamboambayo watu wote kwa kweli katika Bonde hili watashangiliasana kwamba Azimio hili linaenda kutatua tatizo lililokuwasugu kati ya Tanzania na Malawi kuhusu mpaka huo ambapotuliwahi kufikia hata mahali hata eti kufikiria kujenga nguzokatikati ya huo mto. Kutokana na haya mabwawa matatu,hakutakuwa na mafuriko ya kutushangaza tena eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Azimio hili linatupafursa maalum, fursa muhimu ya maelewano zaidi kati yaTanzania na Malawi. Sasa hivi tumeanza ushirikiano, nami ninauhakika huu utakuwa ndiyo msingi wa maelewano zaidi nazaidi kati ya nchi zetu hizi mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikuhakikishie tu kitu kimojakwamba nilikuwa namwangalia rafiki yangu ananiangaliahapa, kwamba mimi eneo langu pale Kyela halijawahikuhamia Malawi. Sasa tusije tukaanza kueleweka vibaya

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

hapa, halijawahi. Muda wote mimi niko mbali kidogo nahuo mto, lakini naongelea tu kwa meneo yote ambayoyanahusika Wilaya ya Kyela.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii kuipongezasana Serikali kwa Azimio hili, kwa uamuzi huu kupitia Wizarayetu ya Maji na Umwagiliaji, kwa sababu watakaofaidikasana katika mradi huu; ni pamoja na Wilaya yangu, Jimbolangu la Uchaguzi la Kyela, hasa Kata zetu za Ngana,Katumbasongwe, Ikimba, Njisi, Ikolo, Ngonga, Bujonde, wotehapa katikati tutafaidika sana na Azimio hili tunalolipitishaleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nisipoteze muda wakomwingi, naomba tu kusema, naunga mkono Azimio hili.Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Engineer Isack Kamwelwe,Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, atafuatiwa naMheshimiwa Engineer Lwenge, Waziri wa Maji. MheshimiwaDkt. Susan Kolimba ajiandae.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, nianze kwa kuungana na wenzangu kwamasikitiko makubwa sana kwa tukio ambalo limetokeamchana wa leo. Mimi nakaa Area ‘D’, nimesikia bunduki,lakini baadaye nakuja kupata taarifa kwamba ni Mbungemwenzangu ambaye amejeruhiwa. Kwa kweli inasikitishasana, kwa siku ya leo inaleta uwoga kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kutoa shukranikwa Kamati ya Bunge ambayo inashughulikia miundombinuya maji kwa michango yao mizuri ambayo wametushaurikuanzia tulipoanzia michango hii kwenye Kamati. Pianashukuru sana Maoni ya Kambi ya Upinzani ambaowameunga mkono moja kwa moja kwenye jambo hili.Nashukuru kusema kwamba kwenye masuala kama haya,kwa sababu tunajenga nchi kwa pamoja, sisi wote niWatanzania, kwa hiyo, inabidi tuungane tuache suala latofauti za itikadi.

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyoongea, tayarituna Interim Secretariat na imeshafanya kazi kubwa sana. HiiInterim Secretariat Ofisi yake iko Kyela, naminimeshatembelea pale. Ndani ya Watumishi; tuna Watumishiwa kutoka Malawi na Watumishi wa kutoka upande waTanzania. Makubaliano yaliyopo ni kwamba hatatutakapokuwa tumekamilisha hii Kamisheni, ikisharidhiwa nikwamba Ofisi zitakuwa Kyela.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tangu Sekretarietii l ipoanza, Serikali ya Malawi na Serikali ya Tanzaniawanachangia hela kuendesha ile Sekretarieti ya mpito; naimefanya kazi kubwa sana. Imeshakamilisha feasibility study,imeshakamilisha detailed design na imefanya seminambalimbali na mikutano mbalimbali na Wafadhili nakutangaza kuhusu huu Mradi wa Bonde la Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari kuna indicationkubwa kwamba Wafadhili wanasubiri tupitishe hili ili sasamazungumzo ya mwisho yaweze kufanyika, tufanikiwekutekeleza ule mradi. Kwa hiyo, suala kama hili WaheshimiwaWabunge kwa kuliunga mkono, sisi kwa kweli kamaWatanzania na kama Wabunge na Wizara ya Maji tunafarijikazaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia juzi kulikuwa naMkutano wa SADC, nami Mheshimiwa Waziri alinitumaniende kule. Katika miradi miwili ambayo imepita;imepitishwa na SADC, ni pamoja na huu Mradi wa Songwe.Umepitishwa kwa sababu una components tatu ndani yakekama alivyokuwa amezungumza Mheshimiwa Mwakyembe.Tutazalisha umeme pale, tutatengeneza skimu za umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna hekta za mwanzo6,200; na kati ya hekta hizo, hekta 3,150 ziko upande waTanzania na hekta 3,050 ziko upande wa Malawi. Kwa hiyo,wananchi wa maeneo ya Tanzania na huku watafaidika naumeme na bado watafaidika na kilimo cha umwagiliaji,kilimo chenye uhakika.

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Mheshimiwa Naibu Spika, pia maji yatachakatwamajisafi na salama. Kwa hiyo, sehemu ya maji yatakwendaupande wa Tanzania na sehemu ya maji watatumia watuwa Malawi. Kwa hiyo, sioni katika mpangilio kama huoambao tuna-share umeme, tuna-share huduma ya maji safina salama na tuna-share kilimo cha umwagiliaji, jamaniundugu utazidi hapo. Unatarajia kuwe na ugomvi kwelihapo? Hata matatizo mengine yaliyopo kwenye lile ZiwaNyasa, tuna imani kabisa kwamba utatuzi wake sasautakuwa rahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungekatika michango yao wamezungumzia suala la ushirikishajiwa jamii. Tangu mwanzo hii Interim Secretariat ilivyoanza,imeshirikisha wananchi kutoka ngazi za Vitongoji, imekujakwenye Vijiji, mpaka Kata, mpaka Wilaya. Wameshirikishwana minutes zipo na taarifa hizi tumezitoa kwenye Kamati. Kwahiyo, kila mwananchi yuko aware na suala hili na wanalisubirikwa hamu kabisa kwamba Kamisheni hii ipitishwe na Bungeletu ili ianze kufanya kazi, wao wanasubiri kupata maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, hebu tujaribukuiangalia mipaka kwa wale ambao wanaishi kwenyemipaka. Kama maendeleo yakiwa upande mmoja kwinginekukawa hakuna maendeleo, maisha yanakuwaje katika hiloeneo? Kwa maana ya hii Kamisheni kwamba maendeleoyatakayopatikana yatakuwa shared upande wa Tanzania naupande wa Malawi. Kwa hiyo, tutazidi kuimarisha unduguwetu na ushirikiano utakuwa mkubwa. Migogoro minginemidogo midogo wakati mwingine unaitatua automaticallykwa kuweka huo ushirikiano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge, tunawashukuru sana na tunawaomba kwa kupitiakwenye michango ambayo wengi mlipata nafasi yakuchangia, wengi mnaridhia na hili. Kwa hiyo, mwisho kabisatunawaomba mridhie ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo, namaliziakwa kushukuru tena, ahsanteni sana. (Makofi)

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri waMaji na Umwagiliaji, Mheshimiwa Engineer Lwenge.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, naomba nami nitoe masikitiko yangu kwaMbunge mwenzetu kushambuliwa na majambazi. Kwa kweli,tunampa pole sana na tunamwombea kwa MwenyeziMungu aweze kumsaidia apone haraka aje afanye kazi zakeza Kibunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nawashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge wote kwa ujumla wenu kwa namnamlivyochangia, hakuna hata mmoja aliyepinga kwambatusiianzishe hii Kamisheni ya kuendeleza Bonde la Mto Songwe.Nashukuru kwa sababu siyo kawaida, mara nyingi kunawengine wanapinga tu hata mazuri, lakini kwa leo angalaukwa namna moja au nyingine wote wameunga mkonokwamba hii Kamisheni ni muhimu ianzishwe kwa ajili yamaendeleo ya wananchi wetu walioko kwenye Wilaya tano.Katika Wilaya hizi tano vijiji 48 vitanufaika na miradi hii ambayoimeibuliwa kwa manufaa ya nchi zote mbili upande waTanzania na upande wa Malawi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza kwa maoniambayo yametolewa na Kamati ya Bunge, yote haya katikamkataba huu ambao tumesaini kati ya Malawi na Tanzania,vifungu hivi vyote viko very flexible kwamba hakuna kifunguambacho hakina namna ya kurekebisha. Madaraka yote yakurekebisha vifungu hivi tumeipa lile Baraza la Mawaziri.Baraza la Mawaziri la pande zote mbili watakuwa na uwezowa kuongeza jambo lolote jema.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwamba mambomengi mazuri haya ambayo mmeyaleta WaheshimiwaWabunge, tutaangalia namna ya kuyapeleka katikakuboresha mkataba wetu ili uweze kuleta manufaa zaidi ilituweze kuendeleza bonde hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa sababuhawa wananchi wa vijiji 48 ambao ni zaidi ya 315,000, kwanza

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

watapata umeme wa uhakika. Kwa awamu ya kwanzaambayo tunajenga Bwawa la Songwe Chini ambalo litawezakutoa megawati 180 Tanzania tutaanza na mgawo waMegawati 90 ambazo tutaziingiza kwenye gridi ya Taifa. Kwasababu azma yetu ni kupeleka umeme vijijini kwa sehemukubwa, hivi vijiji 48 nina hakika kwa mpango huu watapataumeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna hizi hekta 6,000 zakilimo cha umwagiliaji. Wakati madhara ya mto huuulivyokuwa unafurika mara kwa mara, hata hiki kilimo chaumwagiliaji kilikuwa kinakuwa tatizo kwa sababu mashambaya wananchi maeneo ya Kyela na Ileje, yalikuwa yanajaamaji kiasi ambacho iliathiri sana kilimo cha umwagiliaji katikamaeneo yale. Tukija kuboresha sasa tukajengeamiundombinu ambayo imeboreshwa, nina hakika sasakutakuwa na kilimo endelevu na tunainua uchumi kwa ajiliya wananchi wanaoishi maeneo haya. Kwa hiyo, ni kamawengine walivyosema, kwamba mkataba huu umechelewa,ungekuja mapema zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, tujue kabisa kwambatumeanza kuzungumza uanzishwaji wa kitu cha namna hiitoka mwaka 1976, lakini tumekuwa tunapanda ngazi kidogokidogo. Tulipofika mwaka 2001 ndiyo tukaanzisha ileKamisheni ya Mpito au Interim Secretariat ambayo nayoimefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kujenga hii Ofisi yaMakao Makuu hapo Kyela. Kwa hiyo, ofisi tayari ipoimeshajengwa; na tutaanzia pale katika kusimamia sasamiradi hii iliyoibuliwa itakayoleta manufaa kwa wananchiwetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Lissu alikuwana mashaka, alifikiri kwamba katika kusaini mkataba huualienda Lwenge peke yake. Naomba nimtoe wasiwasikwamba hakwenda Mheshimiwa Lwenge peke yake,il ikwenda kama Serikali ikiwa na wataalam wotewaliobobea katika sheria, akiwepo Mwanasheria Mkuu waSerikali. Kwa hiyo, masuala ya sheria yote yamezingatiwa.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Olenashaamefafanua vizuri namna ya kutekeleza miradi inayokuwainashirikisha zaidi ya nchi moja, lakini katika kutatuamigogoro, hili suala la kwenda kwenye SADC au UN, hiki nikitu cha mwisho kabisa. Tumeweka hatua ya kwanza na kwamaelewano tuliyokuwanayo katika miaka yote hii hatufikihuko, kwa sababu kazi tunayoifanya ni ya manufaa kwa nchizote mbili. Ndiyo maana nasema kwamba sasa tunaimarishauhusiano wetu kwa nguvu zaidi kwa ku-develop miradiinayotunufaisha Malawi na Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hata hili suala lamgogoro wa mpaka au mgogoro wa Ziwa Nyasa nina hakikatumeanza vizuri kwa sababu hiki kitakuwa ni kichocheokimojawapo ambacho kimetuunganisha zaidi Malawi naTanzania katika kufikia muafaka wa jambo hili ambalolinazungumzwa la matumizi au rasilimali za Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkataba wetu una namnaya kutoka kama nchi moja ikionekana inakiukamakubaliano, tumesema kwenye Kifungu cha 18 kwambanchi moja inaweza ikavunja mkataba inapoona mwenziehatekelezi yale tuliyokubaliana kwa kutoa notice ya miezisita kwa maandishi, kwa hiyo, kuna namna ya kutoka, lakinisitaki tukifike huko kwa sababu hatuwezi kutoka na kwasababu pia, hii miradi ambayo imeibuliwa ya kujenga umemena miradi mingine, tayari wafadhili wameshaonesha nia,kama nilivyowasilisha pale mwanzo. Wameshaonesha niaya kutusaidia ili tuweze kuendeleza Bonde hili la Mto Songwekwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka nisemetu kwamba maoni yote ambayo Waheshimiwa Wabungemmetoa, tutaendelea kuyaboresha. Kwenye Council, katikazile Wizara sita, kuna Wizara ya Fedha pia ipo. Kuna mmojaalikuwa anataka kuhakikishiwa kama kuna wataalam wafedha watakuwepo. Wizara ya Fedha ni mojawapo katikaWizara ambazo zinaingia kwenye Council, kuna Wizara yaArdhi, Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa,Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na Wizara ya maji. Ila kwenye

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Mkataba wetu tumeweka nafasi ya ku-opt advisor yeyoteau Wizara yoyote ambayo tunafikiri kwa muda uletunapokuwa tunajadili tunaweza tukamwingiza kwenyeCouncil ili kusudi aweze kusaidia, kutegemea ni jambo ganitunalolishughulikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mkataba ukovizuri, uko flexible. Kwa hiyo, nawaomba sana WaheshimiwaWabunge kwa namna mlivyochangia, niwashukuru tena kwamaana kwamba sasa tunakwenda kuanzisha hii Kamisheniambayo itatusaidia kwa maendeleo ya wananchi wetu wapande zote mbili. Pia, tutaondoa huu wasiwasi wa wananchiwetu ambapo mto kila mara ukifurika walikuwa marawanakuwa Malawi, mara wanakuwa Tanzania; ili kusudiwaweze kufanya maendeleo endelevu, sasa watakuwa nauhakika wako Tanzania na wameshaendelezwa,wameshapata mahitaji mengi ya kuwainua kiuchumi. Kwahiyo, nina imani kabisa baada ya utekelezaji wa mradi huu,tutakuwa na jambo la kujivunia kwa kuendeleza rasilimali zamaji za Bonde la Mto Songwe kwa faida ya nchi zote mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema manenohayo, nirudie tena kukushukuru wewe kwa namnaulivyoendesha mjadala huu. Nawashukuru WaheshimiwaWabunge wote wa pande zote mbili kwa namnawalivyochangia; na nawashukuru Waheshimiwa Mawaziriwengine ambao pia wameweza kuchangia na kuungamkono hoja hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo,kwa heshima kubwa naomba kutoa hoja ili Kamisheni hii sasaiweze kuanzishwa, ya Ushirikiano Kati ya Malawi na Tanzaniakwa ajili ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji waKamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi liliridhiwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono na kwa hiyo,Bunge limeridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Kamisheni yaPamoja ya Bonde la Mto Songwe kati ya Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi.

Sasa namwita Naibu Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. SusanKolimba. Tutamalizia na Mheshimiwa Mwigulu Mchemba.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwaruhusa yako na kwa heshima kubwa niweze kuchangia hojahii iliyopo mbele yetu, hoja ya kuridhia Itifaki ya Amani naUsalama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kuchangiahoja hii, nitachangia hoja ambazo zimetolewa na baadhi yaWabunge kuhusu hoja iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kwanza ilitolewana Mheshimiwa Kanali Mstaafu Masoud Ally Khamis ambayealikuwa anaitaka Serikali iweke mkazo katika kusimamiaalama za mipaka kwani tayari kumekuwa na tuhuma zakuondoa alama hizo katika mipaka ya Sirari na maeneomengineyo. Naomba nitoe maelezo juu ya utekelezaji waSerikali juu ya hoja ambayo imetolewa na MheshimiwaMbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la urekebishwaji wamipaka ya nchi linafanyika kupitia mazungumzo baina yanchi na nchi. Tayari Serikali imekwishaanza majadiliano nanchi ambazo zinapakana nazo na hivi karibuni nafikirimmesikia, Tanzania ilifanya majadiliano na Serikali ya Ugandakuhusu mpaka katika Mkoa wa Kagera ambayo

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

yameshakamilika na hatua inayofuata sasa ni kujenga nakuimarisha alama za mpaka ule. Aidha, Serikali inajiandaakupitia upya mpaka wa nchi hizi mbili hasa kwenye upandeule wa ziwani kati ya Tanzania na Uganda.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kwa upande wa mpakawetu wa nchi ya kwetu pamoja na Kenya, mazungumzoyalishakamilika na tayari Serikali imeshatoa mchango wakekatika kugharamia, kujenga na kuziimarisha alama zamipakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, kwa upande wa nchiza Malawi, majadiliano bado yanaendelea. Kama mlivyosikiamara ya mwisho, Tanzania pamoja na Malawi waliitwa nalile jopo la Marais Wastaafu kule Kusini ili kujadili suala lampaka wa Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeleakuhakikisha kuwa tofauti zozote zinazojitokeza kati ya nchina nchi na hasa zinazohusu masuala ya mipaka, zitakuwazinaendelea kusuluhishwa kwa njia ya mazungumzo na kwaamani kwa faida ya pande zote mbili kwa sababu hawa nimajirani zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja ya pili ambayoilitolewa na Mheshimiwa Kanali Mstaafu Masoud Ally Khamis.Hoja hii ilikuwa inahusu Ibara ile ya 12 (e) ya Itifaki inayozitakanchi wanachama kushirikiana katika kukabiliana nawahamiaji haramu. Niseme tu kwamba nchi yetu imekuwaikipokea wahamiaji haramu kutoka nchi za Eritrea na Ethiopiawanaokwenda Afrika Kusini, ambapo tatizo ambalo kwaTanzania tumeshalisikia mara nyingi na limekuwa nichangamoto; Serikali ihakikishe kuwa nchi ya Kenyahaiwaruhusu watu hao kupitia kuja kwetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri kwa kusaini Itifakihii, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikiwatatumia mikakati ambayo iko ndani ya Itifaki nakuhakikisha kwamba hivi vyanzo na njia kuu na Vituo vya

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Wahamiaji haramu ambavyo vipo kwa sasa hivi,vitaondolewa kwa kupitia Itifaki hii ambayo sasa hivitunairidhia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, WaheshimiwaWabunge nawaomba sana tuweze kuiunga mkono Itifakihii ipite ili mikakati iliyowekwa na Serikali na kwa kupitia Itifakihii, changamoto hii ambayo inapatikana kwenye nchi yetuna nchi za jirani itakuwa imekwisha kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkonohoja hii. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa MwiguluNchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuhitimishahoja, lakini kwa ruhusa yako, kabla sijahitimisha hoja, naombaniseme mambo mawili. La kwanza, kama ambavyommesikia Mbunge mwenzetu ameshambuliwa kwashambulio baya na watu wasiojulikana, lakini taarifa rasmimtapewa. Tutatoa kwa utaratibu kadiri tutakavyoongozwana Bunge hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa tu za awali nikwamba Madaktari wamejitahidi kwa kiwango cha hali yajuu kuweza kutoa huduma ya kwanza. Nimechelewa kujahapa, nilikuwa pale na Mheshimiwa Spika, briefing ya mwishotuliyopewa ni kwamba wamefanya vizuri wamewezakudhibiti damu zilizokuwa zinatoka. Kwa hiyo, wamesemahatua ya awali ya huduma ya kwanza waliyotoa imeendavizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la awali tu kwaupande wa Wizara ya Mambo ya Ndani, japo tutatoa tamkorasmi, lakini tunasema jambo hili lililotokea ni jambo ambalohalikubaliki; nasi kama Wizara ya Mambo ya Ndani na kamaSerikali, hatutaruhusu na hatutaacha jambo hili lipite hivi hivi.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeelekeza Polisi Mkoa waDodoma waweke vizuizi njia zote zinazotoka Dodoma nazinazoingia Dodoma na wasambae kuweza kuwasaka haowote ambao wamehusika na tukio hili, tukio ambalolinapaka matope sura na heshima ya nchi yetu na tukioambalo linapaka matope Serikali yetu ambayo inashughulikiamasuala ya usalama wa raia.

Mheshimiwa Naibu Spika, iwe kwa sababu za kisiasa,iwe kwa sababu ya hujuma, iwe kwa sababu za ugomvi naiwe kwa sababu za za kijambazi, yote hayo tutasakakuhakikisha kwamba wale wote ambao wamehusika najambo hilo wanafikishwa katika mkono wa sheria ili kuwezakukomesha vitendo hivyo viovu ambavyo havijazoelekakatika nchi yetu. Watanzania wote tumwombee mwenzetuili Mungu ampe afya njema na afya yake iimarike awezekuendelea na kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, taarifarasmi itatolewa kwa utaratibu ambao Kiti chenyewe kitatoakwa masuala yote ya kiusalama pamoja na kiafya baadaya kuwa wenzetu wamefikia hatua ambayo wanawezawakatoa taarifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema hayo,nawapongeza Waheshimiwa Wabunge ambaowamechangia, nimeona wameunga mkono Azimio hili. Naminiendelee kusisitiza kwamba Azimio hili ni zuri, lina faida nyingi.Mambo mengi yalikuwa yakifanyika bila kuwa na misingi hiiambayo itakuwa imewekwa na Azimio na baadaye ambayoitapelekea uwepo wa sheria, kanuni na taratibu za kuwezakuyashughulikia mambo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nilisemawakati wa kutoa hoja; na kama ambavyo wachangiajiwameelezea nikitoa na pongezi kwa Mheshimiwa NaibuWaziri wa Mambo ya Nje aliyetoka kusema hivi punde,yatatusaidia katika kushughulikia masuala yaliyo ya kimipakalakini na yaliyo ya kiujirani mwema hasa yanayohusiana na

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

masuala ya kiusalama wa watu wetu pamoja na mali zaowa nchi hizi mbili na wageni wanaokuja katika nchi zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, itatusaidia hata kwenyemaisha ya kila siku, masuala haya ambayo tumeyasemeayanayohusu mambo ya migogoro, shughuli za kiuchumizinazoingiliana katika mipaka yetu. Kwa mfano, watu wetuwanaokaa jirani na mipaka ambao wana shughulizinazoendana na zinazoingiliana, wao kwa asil i zaohawatambui mipaka. Tunaamini uwepo wa Azimio nataratibu za kubadilishana taarifa na kubadilishana uzoefuwa kushughulikia uhalifu, itawasaidia watu wetu wawezekufanya shughuli hizo kwa njia ambayo ni salama naendelevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata kutimiza matakwa yamikataba ambayo nchi yetu imeingia, nchi yetu ni nchikiongozi katika uanzilishi wa jumuiya hii na katika uendeshajiwa jumuiya hii. Kwa hiyo, yale ambayo yanakubaliwa kamanchi wanachama ni wajibu wetu pia kama nchi kuwezakutekeleza na kuridhia na hasa baada ya kuwatumeshajiridhisha na manufaa ambayo nchi yetu itapatakupitia jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, huku tukipokeahoja zote zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge, naombasasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liridhie Azimiolake la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama ya Jumuiya yaAfrika Mashariki (The East African Community Protocol onPeace and Security).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamulia na Kuafikiwa)

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA … SEP 2017.pdf · NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA NANE Kikao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

(Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Amani na Usalamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki liliridhiwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono. Kwa hiyo,Azimio la kuridhia Itifaki ya Amani na Usalama wa Jumuiyaya Afrika Mashariki limeshakubaliwa na Bunge.

Waheshimiwa Wabunge, nawashukuru sana kwa kazinzuri mliyoifanya na nawapongeza Mheshimiwa Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Maji na Umwagiliajikwa hoja zao ambazo walizileta mbele ya Bunge ambazoBunge limeridhia. Nachukua fursa hii kuwapongeza kwasababu ni mara chache ambapo hoja zinaletwa nazinaungwa mkono na pande zote za Wabungewaliowakilishwa humu Bungeni. Kwa hiyo, nawapongezasana.

Waheshimiwa Wabunge, pamoja na pongezi hizo,nalazimika kuwakumbusha masharti ya Kanuni ya 154 nasitaisoma kwa sababu ni ndefu kidogo, lakini kanuni hiitumejiwekea kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kutoasalamu za pongezi na pole. Kwa sababu kesho Bungelitaendelea, niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge kufuatamasharti ya Kanuni ya 154. Spika kesho kama nilivyosemakwamba atazungumza kuhusu mambo haya, lakini Bungelitakapoendelea basi tuzingatie masharti hayo.

Kwa upande wa Bunge, Mheshimiwa Spika akitoapole ama pongezi, anakuwa amesema kwa niaba yaWabunge wote; na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni,akisema pole ama pongezi, anakuwa ametoa kwa niabaya Serikali.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nawashukuru sana kwa kazi nzuri mliyoifanya leo. Kwa mujibuwa Kanuni ya 28(4) naahirisha shughuli za Bunge mpaka sikuya kesho Ijumaa, tarehe 8 saa tatu asubuhi.

(Saa 12.15 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Ijumaa,Tarehe 8 Septemba, 2017, Saa Tatu Asubuhi)