222
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Arobaini na Tatu – Tarehe 4 Juni, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Moja, leo ni Kikao cha Arobaini na Tatu. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU - KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 MHE. MASHAURI M. NDAKI (K.n.y. MHE. HAWA A. GHASIA - MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Arobaini na Tatu – Tarehe 4 Juni, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae.Tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Moja, leo ni Kikaocha Arobaini na Tatu. Katibu.

NDG. RUTH MAKUNGU - KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha2018/2019

MHE. MASHAURI M. NDAKI (K.n.y. MHE. HAWA A.GHASIA - MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI):

Taarifa ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji waMajukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka waFedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati juu yaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwakawa Fedha 2018/2019

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ndaki, Mbunge waMaswa Magharibi, kwa niaba ya Mwenyekiti. Katibu.

NDG. RUTH MAKUNGU - KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, swalilitaulizwa na Mheshimiwa Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe,Mbunge wa Kavuu.

Na. 360

Sharti la Kujiunga katika Vikundi ili Kupata Mikopo

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE aliuliza:-

Serikali imekuwa ikiwahimiza wananchi wajiungekwenye vikundi ili waweze kupata mikopo ya kuwasaidiakuendesha shughuli zao:-

Je, Serikali haoni kuwa sharti hilo linawakosesha fursabaadhi ya wananchi ambao pengine wanahitaji hudumahiyo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. PudencianaWilfred Kikwembe, Mbunge wa Kavuu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma zakifedha zinawafikia wananchi wake Serikali imetunga Seraya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2017 ambayoitawezesha kuchochea maendeleo stahiki na ubunifu wahuduma ndogo za kifedha ili kukidhi mahitaji halisi yawananchi wa kipato cha chini na hivyo kuongeza ukuaji wauchumi na kupunguza umaskini. Pia Serikali inalenga kutatuachangamoto inayowapata wananchi juu ya mtazamo wa

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

mifumo ya ukopeshaji kwa vikundi au mtu mmoja mmoja.Sera hii itapelekea kutungwa kwa sheria itakayowekautaratibu mzuri wa huduma ndogo ya fedha.

Mheshimiwa Spika, utoaji mikopo kwa kutumiavikundi ni mfumo ambao hutumika kutoa mikopo midogomidogo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali. Mfumo huuhutumika kutoa mikopo kwa watu ambao uwezo wao wakiuchumi ni mdogo, hasa kwa wakopaji ambao hawanadhamana. Pia mfumo huu husaidia kuweka dhamanambadala ya usalama wa mikopo inayotolewa kwakuwafanya wanakikundi kuwa na uwajibikaji wa pamoja juuya mkopo huo.

Mheshimiwa Spika, mfumo huu umekuwa ukitumiwana taasisi nyingi za kifedha ambazo zimekuwa zikitoa mikopokwa watu wenye kipato cha chini ikiwepo mifuko yauwezeshaji wananchi kiuchumi inayomilikiwa na Serikalikutokana na faida yake katika kuhakikisha kuwa usalamawa mikopo hasa kwa wakopaji wasio na dhamana. Mfumohuu pia husaidia kurahisisha ufuatiliaji wa kuwajengea uwezowanakikundi kupitia mafunzo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mfumo huu kutumikalakini ni pia mwananchi mmoja mmoja wamepatiwa fursaza uwezeshaji kupitia benki na mifuko mbalimbali yauwezeshaji kama vile Mfuko wa Kuendeleza Wajasiriamali,Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi na Mfuko wa Wajasiriamaliwadogo wadogo.

SPIKA: Mheshimiwa Kikwembe, swali la nyongeza.

MHE. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa Spika,ahsante. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri pamoja namajibu mazuri ya Serikali, kwa kweli leo nimefurahi kidogo.Naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri amenijibu vizuri.Naomba nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza:

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, sera hii inalengakutatua changamoto inayowapata wananchi kuhusu

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

mitazamo mbalimbali lakini umesema pia sera hii inalengakuwakopesha wanavikundi na mtu mmoja mmoja, swalilangu ni kwamba; ni kwa nini sasa Halmashauri nyingizimekuwa zikiwalazimisha wananchi wakope wakiwakwenye vikundi vya watu watano na kuendelea, jamboambalo kimsingi l inamnyima mkopaji mmoja mmojamwenye uwezo wa kukopa ambaye anaweza akajidhaminiili aweze kujiendeleza katika maisha yake?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, naishukuruSerikali yangu kwa sababu imeweza kuondoa riba katika hiimikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Halmashauri asilimiakumi, lakini, ni kwa nini sasa, bado tunasema kwamba, kwamfano kwenye Mifuko ya Akinamama na Vijana, wazee nawanaume hawapati mikopo hii, jambo ambalo tunawezatukawakopesha na wakaweza kuendeleza mifuko hiyo?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaatafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE):Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongezakipengele cha kwanza alichouliza Mheshimiwa PudencianaKikwembe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika swali lake anapendekezaingefaa tukaanza kum-address mtu mmoja mmoja badalaya vikundi ambalo kimsingi na yeye mwenyewe atakubalianana mimi na hata ukienda kule kwake, vikundi kwa maanaya ushirika ndiyo hasa njia ya kuweza kututoa sisi wanyonge.Naomba nimsihi Mheshimiwa Mbunge kuwa vyovyote, yuleambaye ana uwezo wa kuweza ku-access mabenki, windowhiyo ipo, lakini katika hii pesa ambayo inatolewa na Serikalini vizuri kwanza tukajikita katika vikundi maana tukisaidiavikundi tunasaidia watu walio wengi zaidi.

SPIKA: Kwa lile la pili, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisiya Waziri Mkuu, majibu tafadhali.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika utaratibuwa uwezeshaji wananchi kiuchumi, Serikali inachokifanya nikuona namna ya kuweza kuyagusa makundi yote kwa wakatimmoja. Ndiyo maana pamoja na kwamba tunayo Mifukoya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi lakini pia tunayomifuko maalum kwa ajili ya akinamama na vijana, lakinikundi la wazee na watu wengine ambao hawadondokeikatika sifa hizo, wenyewe pia kupitia Mifuko ya UwezeshajiWananchi Kiuchumi wanayo fursa ya kwenda kukopeshwamtu mmoja mmoja au kupitia vikundi pia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimwuondoe hofuMheshimiwa Mbunge ya kwamba bado hata kama kunamzee na mtu mwingine yeyote ambaye anahitaji kupatamikopo hii, hata kama hadondokei katika kundi la vijanana akinamama lakini fursa hiyo ipo kupitia Mifuko yaUwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambayo ipo 19 na imekuwaikifanya kazi hiyo kuwawezesha wananchi kiuchumi.

SPIKA: Mheshimiwa Kemilembe nilikuona, swali lanyongeza.

MHE. KEMILEMBE J. LWOTA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kumekuwa kuna hamasa ya uhamasishajimkubwa sana kwa wananchi wetu kujiunga na vikundi hiviili waweze kupata mikopo hii asilimia 10 kutoka kwenyeHalmashauri zetu, lakini kiuhalisia Halmashauri nyingi mikopohii haitoki. Nataka kujua, Serikali ina mpango gani wakuwezesha Halmashauri zetu ili mikopo hii iweze kutoka naakinamama, wazee na watoto waweze kupata mikopo hiikama inavyoonekana?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa, majibu tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Spika, swali hili limekuwa likijirudia mara kwa mara na majibuambayo tumekuwa tukitoa, tumekuwa tukielekeza kwambawakati tunakuja kuhitimisha bajeti kuna kipengele ambachokitaingizwa katika Finance Bill ambacho kitamlazimisha kilaMkurugenzi kuhakikisha kwamba pesa hizi zinatengwa nazisipotengwa sheria zitachukuliwa ili kutoa adhabu kwa walewote ambao hawatatimiza takwa hili la kisheria. Kwa sasahivi, imekuwa ni kama option lakini tutakuja na kipengeleambacho kitamlazimisha kila Mkurugenzi a-make surekwamba pesa hizi zinatengwa.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Ofsiya Waziri Mkuu, TAMISEMI, swali la Mheshimiwa John PeterKadutu, Mbunge wa Ulyankulu. Mheshimiwa Kadututafadhali.

Na. 361

Shule za Mkindo na Ulyankulu Kupewa Hadhi yaKuwa na Kidato cha Tano na Sita

MHE. JOHN P. KADUTU aliuliza:-

Kabla ya kuanzishwa Shule za Kata, kulikuwa nampango wa kujenga shule katika tarafa. Kwenye Jimbo laUlyankulu kulijengwa shule tatu ambazo ni Kashishi, Ulyankuluna Mkindo; Shule ya Kashishi hivi sasa ina kidato cha tano nasita:-

Je, ni lini Shule za Mkindo na Ulyankulu zitapewa hadhiya kuwa na kidato cha tano na sita ili kuwapunguziawanafunzi gharama za kufuata mbali masomo ya kidatocha tano na sita?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa JohnPeter Kadutu, Mbunge wa Ulyankulu, kama ifuatavyo:-

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, naomba kwaruhusa yako niondoe sentensi moja tu inayoanza na nenoTarafa mpaka pale mwisho na sita.

Mheshimiwa Spika, malengo ya Serikali kwa sasa nikuhakikisha kuwa, kila Tarafa angalau ina shule moja yenyekidato cha tano na sita. Mkakati uliopo kwenye maeneoambayo tayari kuna shule zinazotoa elimu ya kidato cha tanona sita ni kuziimarisha kwa kuziwekea miundombinu,kuzipatia vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuzipatiaWalimu wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, ili shule iweze kupandishwa hadhina hatimaye kusajiliwa kama Shule ya Kidato cha Tano naSita ni lazima itimize vigezo vifuatavyo:-

(i) Iwe na miundombinu inayojitosheleza kamamabweni, madarasa, bwalo, jiko na maktaba;

(ii) Iwe na huduma muhimu na za uhakika za majina umeme; na

(iii) Iwe na Walimu wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, kwa muktadha huo, Shule zaSekondari Ulyankulu na Mkindo bado zina changamoto yamiundombinu isiyojitosheleza kama mabweni, madarasa,bwalo, jiko na maktaba. Hivyo, naishauri Halmashauri yaWilaya ya Kaliua ifanye jitihada za makusudi kuwezesha shulehizo mbili kufikia vigezo vinavyohitajika ili ziweze kusajiliwa.Aidha, kwa kuwa bajeti ya Wizara ya Elimu pamoja na ileOfisi ya Rais, TAMISEMI kwa mwaka 2018/2019 zimeshapitishwana Bunge, itakuwa vigumu shule hizo kusajiliwa na kuanzakuchukua wanafunzi wa mwaka huo.

SPIKA: Mheshimiwa Kadutu, swali la nyongeza,tafadhali.

MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwa vile Naibu Waziri

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

ameona aondoe sentensi moja, mimi nasema paragraphyote majibu hayafanani na swali nililouliza. Mimi sitaki kuulizamaswali mengi, nimwombe tu Mheshimiwa Naibu Waziri auMawaziri wote watatu wa TAMISEMI wafike Ulyankulu kujioneahaya yaliyoandikwa, je ni kweli? Kwa sababu haya yoteyaliyoandikwa si kweli.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nimwombe NaibuWaziri au wenzake waweze kufika Ulyankulu na kujionea kilewanachopewa na wataalam na je, ndicho kilichoko site?

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Kakunda, leoumepiga Kisikongesikonge. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaSpika, naomba sana nimwombe Mheshimiwa John Kadutu,awepo Jimboni tarehe 10 Julai, ili tuweze kutembelea shulehizo kwa pamoja.

SPIKA: Mheshimiwa George Malima Lubeleje, swali lanyongeza, tafadhali.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali mojala nyongeza. Kwa kuwa, shule za sekondari za kidato chakwanza mpaka cha nne Serikali imezipandisha hadhibaadhi yake kuwa shule za kidato cha tano na cha sita,kwa mfano, Kibakwe, Berege, Mazae na Kongwa Mjini.Hata hivyo, watoto katika shule hizi wanasoma katikamazingira magumu sana kwanza madarasa, hostelipamoja na mabweni lakini hata chakula wanachopewahela ni kidogo sana. Mheshimiwa Naibu Waziri anasemajekuhusu suala la kuboresha shule za form five na six katikakata hizi?

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaSpika, kwanza napenda nichukue nafasi hii kumpongeza, yeyeni Mbunge mzoefu wa siku nyingi na kutokana na Ubungewake ndiyo maana ameweza kupata maendeleo makubwakatika Jimbo lake hadi shule hizo alizozitaja zimesajiliwa kuwakatika hadhi ya kidato cha tano na sita. Kuwa na shule tatuau nne kwenye Jimbo moja za kidato cha tano na sita siyokazi ndogo, ni kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika jibu hili, napenda kujibu kwaujumla kwamba shule zote za kidato cha tano na sita nahata za kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, zotezinapewa fedha sawasawa kwa nchi nzima. Kwa hiyo,haiwezekani kwa mfano tukasema kwamba, kwa sababushule hizi sasa Mheshimiwa Mbunge amesema zina matatizomakubwa, basi tuziongezee shule zile za Jimbo lake tu, nikitu ambacho hakiwezekani. Kwa hiyo, nakaribisha maonikama haya ili tuweze kuyajadili kwa pamoja kwa ajili ya shulezote nchini badala ya shule moja moja.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Alhaj Bulembo nilikuona, swali lanyongeza, tafadhali.

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaSpika, nakushukuru sana. Kwa kuwa swali la msingi laUlyankulu liko katika Majimbo mengi ya nchi hii, kutokuwana shule za form five na form six. Serikali inatoa commitmentgani na lini itaanza kufanya operation katika kila jimbokupata shule za form five na form six? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo, Naibu Waziri, MheshimiwaJoseph George Kakunda, tafadhali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): MheshimiwaSpika, maombi yaliyopo katika Wizara yetu ambayo sisi

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

tukiyapokea tunayapeleka Wizara ya Elimu kwa ajili ya usajilikwa sababu anayesajili ni Wizara ya Elimu ni mengi, lakinimengi yamekuja hivi karibuni, mwezi wa Nne mwishoni,mwezi wa Tano wakati tayari masuala ya bajeti yalikuwayameshakamilika. Kwa hiyo, naomba sana nimwahidiMheshimiwa Bulembo pamoja na Waheshimiwa Wabungewote na Bunge zima kwamba mwakani tutawekautaratibu maalum wa kuhakikisha kwamba inavyofikaDesemba, 2018, basi shule zote ambazo zina maombimaalum katika ofisi zetu za Serikali tutazisimamia ili ziwezekupata usajili.

SPIKA: Majibu ya nyongeza Mheshimiwa ProfesaNdalichako, Waziri wa Elimu, mmepeleka maombi mwishonisana. (Kicheko)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nimesimama kulihakikishiaBunge lako Tukufu Wizara yangu ambayo ndiyo ina jukumula kusajili shule haina tatizo lolote la kusajili wakati wowoteshule ambayo imekidhi vigezo. Kwa hiyo, nitoe wito kwaWaheshimiwa Wabunge na Wakurugenzi na Maafisa Elimukwa ujumla kama kuna shule ambayo inahitaji usajili, tunasajiliwakati wowote ilmradi shule imekidhi vigezo. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Tuendelee na swali la Wizarahiyo hiyo ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, linaulizwana Mheshimiwa Musa Rashid Ntimizi, Mbunge wa Igalula nakwa niaba yake Mheshimiwa Dkt. Kafumu nimekuona.

Na. 362

Matengenezo ya Barabara ya Buhekela-Miswaki-Loya-Iyumbu

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU (K.n.y. MHE. MUSSA R.NTIMIZI) aliuliza:-

Barabara ya Buhekela-Miswaki-Loya-Iyumbuinaunganisha Majimbo ya Igunga, Manonga, Igagula na

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Singida Magharibi, pia inaunganisha Mikoa miwili ya Taborana Singida, ina Mbuga kubwa ya Wembele ambapowananchi wanalima mpunga na kulisha Mikoa ya Tabora,Shinyanga na Singida lakini ni mbovu sana:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuitengenezabarabara hiyo kwa umuhimu wake huo wa kiuchumi nakimawasiliano?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibuswali la Mheshimiwa Musa Rashid Ntimizi, Mbunge wa Igalula,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, barabara ya Buhekela-Miswaki-Loya-Iyumbu inahudumiwa na Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA), katika Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauriya Wilaya ya Igunga yenye kipande chenye urefu wa kilometa102.79 ambayo ni barabara ya Igunga-Itumba-Simba naHalmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa maana ya Uyui yenyekipande chenye urefu wa kilometa 66.05 ambayo nibarabara ya Miswaki - Loya kilometa 28.68 na Loya-Nkongwakilometa 37.37.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018, TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imepangakufanya matengenezo ya muda maalum kilometa sita namatengenezo ya kawaida kilometa moja kwa gharama yaSh.225,000,000. Mpaka sasa barabara zenye urefu wa kilometasita zimeshachongwa na maandalizi ya kuziwekachangarawe yanaendelea. Vilevile TARURA Halmashauri yaIgunga imepewa shilingi milioni 297 kwa ajili ya kujenga boksikalvati tatu na kufanya matengenezo ya muda maalumkilometa 1.6.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa ujenzi wa boksi kalvatitatu umefikia asilimia 30. Katika mwaka wa fedha 2018/2019

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imetengewaSh.165,000,000 kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofikilometa 23 na ujenzi wa boksi kalvati moja.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)imeidhinishiwa Sh.400,000,000 kwa ajili ya matengenezo yabarabara ya kilometa 20 kwa kiwango cha changarawepamoja na kujenga kalvati moja. Serikali itaendelea kutoafedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara hii kwa kadriya upatikanaji wa fedha.

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kafumu, swali la nyongeza,tafadhali.

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika,nakushuru. Swali la kwanza, kwa kuwa barabara hii yaBuhekela-Miswaki-Loya mpaka Iyumbu na ile barabara yaIgunga-Itumba-Simbo ni barabara ambazo zinapita kwenyeMbuga ya Wembele mahali ambapo ni lazima ujenge tutakubwa ili barabara iwezekane siyo kuchonga, kwa hiyo, kunamadaraja mengi yanahitajika kujengwa.

Mheshimiwa Spika, Sh.225,000,000 za barabara yaIyumbu na zile Sh.297,000,000 za barabara ya Itumbahazitoshi kabisa kuzijenga barabara hizi. Waziri anatoacommitment gani kuhusu kuongeza bajeti ili kujenga hiibarabara kwa kiwango ambacho zitaweza kupitika wakatiwowote?

Swali la pili, kwa kuwa ile barabara ya Igunga-Itumba-Loya kipande cha Itumba - Loya hakina fedha, kwa sababuinaenda Simbo kwanza. Ni lini basi Serikali itatoa fedha kwaajili ya kile kipande cha Itumba-Loya?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, sijui hivyo vichochorovya Itumba-Loya huko unavifahamu Mheshimiwa NaibuWaziri, majibu tafadhali.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaSpika, ni kweli swali hili amekuwa akiuliza sana kuhusu kipandehicho cha Mbuga ya Wembele ambayo inahitaji specialconsideration na ni ukweli usiopingika kwamba inahitaji bajetikubwa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba kama Serikali tunalitambua hil i, lakinikinachogomba ni suala la bajeti, pale hali itakavyokuwaimeimarika hatutasahau kwa sababu eneo lile linahitaji pesanyingi. Naamini katika bajeti zijazo, kabla hatujafika 2020tutakuwa tumeshaikamilisha. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu nilikuona, swali lanyongeza.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo lanyongeza. Barabara ya Vigwaza - Kwala - Kimaramasaleinayounganisha Majimbo matatu ya Mkoa wa Pwani, Jimbola Bagamoyo, Kibaha Vijiji na Kisarawe, ni lini itaanzakujengwa kwa kiwango cha lami ikizingatiwa kule kunabandari kavu?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu tafadhali,Mheshimiwa Kwandikwa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaSpika, ahsante sana. Kwanza nishukuru kwa majibu mazuriya Mheshimiwa Naibu Waziri na nimshukuru MheshimiwaHawa Mchafu kwa swali lake.

Mheshimiwa Spika, niseme tu barabara hiiinahudumiwa na TANROADS na katika ule mpango mkakatiwetu tunao utaratibu wa kuitengeneza. Kwa sasatunajitahidi kuhakikisha barabara hii inapitika wakati wotena kwa umuhimu wa kipekee kwa sababu ya kuwa na hii

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

bandari kavu tutaipeleka kwenye kiwango cha lami. Kwahiyo, nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge avumilie kidogoutaratibu upo wa kuifanya hii barabara iwe nzuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa David Silinde nilikuona, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana, nami nina swali dogo la nyongeza. Tatizo lililopo katikaJimbo la Igalula lipo vilevile katika Jimbo la Momba hususankatika barabara ya kutoka Kakozi-Kapele - Ilonga ambakoni Jimbo la Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Kandege,Jimbo la Kalambo.

Mheshimiwa Spika, wakati tunasubiri ahadi yaTANROADS ya kutengeneza barabara hiyo na yeye sasa hivindiye Waziri, haoni sasa ni wakati muafaka kutengenezabarabara hiyo ambayo inaunganisha mikoa miwili ya Songwepamoja na Mkoa wa Rukwa, lakini vilevile Jimbo la Mombana Jimbo lake la Kalambo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mheshimiwa Kwandikwa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): MheshimiwaSpika, ahsante sana. Kwanza nataka nimwombeMheshimiwa Silinde tu avumilie kwa sababu sijatembeleaMkoa wa Songwe, lakini utaratibu wa Serikali kisera nikwamba umuhimu wa kwanza ni kuhakikisha tunaunganishamikoa. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi na katika bajeti yetutuna provision na nikienda kule tutazungumza kwa upanazaidi ili aone namna ambavyo tumejipanga kuijengabarabara hii Mheshimiwa.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

SPIKA: Tunaendelea na Wizara ya fedha na Mipango,swali linaulizwa na Mheshimiwa Juma Kombo HamadMbunge wa Wingwi.

Na. 363

Kero ya Ulipaji Kodi ya Mizigo Kutoka Zanzibar KwendaTanzania Bara

MHE. JUMA KOMBO HAMAD aliuliza:-

Mfumo wa ulipaji kodi za kusafirisha bidhaa kutokaZanzibar kwenda Tanzania Bara umekuwa ukilalamikiwa kwamuda mrefu kwamba unakwaza na kuvunja harakati zabiashara Zanzibar na hivyo kusababisha uchumi wa Zanzibarkushuka:-

Je, Serikali ipo tayari kuunda Kamati kwa ajili yakushughulikia mfumo wa ulipaji kodi za mizigo kutokaZanzibar kwenda Tanzania Bara?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedhana Mipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa JumaKombo Hamad, Mbunge wa Wingwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, chimbuko la malalamiko ya kodiwakati mizigo inaposafirishwa kutoka Zanzibar kuja TanzaniaBara linatokana na kuwepo kwa mifumo tofauti ya kuthaminibidhaa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara. Hali hiyoinasababishwa na viwango tofauti vya ushuru wa forodhavinavyopaswa kulipwa kwa bidhaa ya aina moja kutoka njeya nchi na kusafirishwa kwenda sehemu ya pili ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mfumo wa uthaminishaji bidhaazote zinazoingia Tanzania Bara unafanyika kwa kutumiamifumo ya TANCIS na Import Export Commodity Databaseikiratibiwa na kituo cha Huduma za Forodha kilichopo Dar

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

es Salaam. Hata hivyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarhaitumii mifumo hiyo na hivyo kusababisha kuwepo na tofautiya kodi kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, kutokana na utofauti wa mifumoinayotumika, bidhaa zote za nje zinazoingia Tanzania Bara,kupitia Zanzibar hufanyiwa uhakiki l icha ya kuwazimethaminiwa Zanzibar. Iwapo uthamini wa Tanzania Barautakuwa sawa na ule uliofanywa Zanzibar, hakuna kodiitakayotozwa Tanzania Bara. Ikiwa kodi iliyolipwa Zanzibarni kidogo, Mamlaka ya Mapato hukusanya tofauti ya kodiiliyozidi.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kukusanya tofautiya kodi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara kwa kutumiamifumo ya IECD na TANCIS haina lengo la kuua biasharaZanzibar, hatua hiyo inalenga kuleta usawa wa gharama zakufanya biashara na ushindani hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleakujadiliana ili kuona kuwa suala hili linapatiwa ufumbuzi wakudumu. Aidha, kwa kuwa Serikali zetu mbili hazijashindwakutatua changamoto hii, ni dhahiri kabisa kuwa hakunasababu ya kuunda Kamati ya kushughulikia mfumo wa ulipajikodi kwa mizigo inayotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Ibara ya 63(2), Bunge lako Tukufu ni Mhimiliunaojitegemea na hivyo Serikali haina mamlaka ya kuundaKamati ndogo ya Bunge kwa ajili ya jambo hili au jambololote lile.

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Wingwi, swali lanyongeza tafadhali.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika,ahsante. Zanzibar ni Kisiwa kidogo chenye wakazi wachachesana, wakazi wa Zanzibar ni kati ya 1,000,000 mpaka 1,500,000na kutokana na hali hiyo Zanzibar inategemea soko la bidhaakutoka nje. Maana yake Zanzibar inategemea soko la bidhaa

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

zinazotoka nje kusafirishwa nchi jirani au baadhi ya nchinyingine il i kutafuta soko na ndiyo maana Zanzibarimejiandalia mfumo wake mahsusi i l i kufanikishawafanyabiashara kutoka nchi nyingine ikiwemo TanzaniaBara wafike Zanzibar wachukue bidhaa zinazotoka nje kwaajili ya kwenda kufanya biashara sehemu nyingine.

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali haioni kwambakuilazimisha Zanzibar kufata mfumo wa TANCIS ndiyo maanaya kuua soko la bidhaa kutoka nje kwa pale Visiwa vyaZanzibar? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa Wazirikasema haiwezekani kuunda Tume, Bunge haliwezikuunda Tume. Naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, Je,Serikali kupitia Wizara ya Fedha ipo tayari kuunda KamatiNdogo wakiwemo Wabunge, Maafisa wa TRA na yeyemwenyewe kwenda Zanzibar kukutana na wadau,wafanyabiashara wa Zanzibar hususan Taasisi yaWafanyabishara Zanzibar ili kuangalia ukubwa wa tatizo hilina kulitafutia ufumbuzi?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu tafadhali yamaswali hayo.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi nikwamba hiki kinachotokea ni kuhakikisha kunakuwa naushindani katika soko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania. Ndiyo maana bidhaa zinazouzwa kutoka Zanzibarzilizotoka nje kuja Tanzania Bara lazima zifanyiwe uthamini ilikuhakikisha wafanyabiashara wanaotumia Bandari za Serikaliya Jamhuri ya Tanzania Bara wanapata ushindani ulio sawia.

Mheshimiwa Spika, amesema kwambawafanyabiashara kutoka nchi nyingine. Kumekuwa na tatizola wafanyabiashara kutoka nchi nyingine kwenda kununuabidhaa Zanzibar na kuja kuzi-dump katika soko la Jamhuri

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

ya Muungano wa Tanzania. Ndiyo maana kwa sababubidhaa zile hazijazalishwa Zanzibar lazima zinapoingiaTanzania Bara ziweze kulipa kodi husika ili ushindani huouweze kuwepo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, napendakumwambia Mheshimiwa Kombo kwamba nimesemakwenye jibu langu la msingi Serikali zetu mbili, Serikali yaZanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania zinalifanyia kazi tatizo hili na tuna uhakika kwambachangamoto hii itafika mwisho, kwa sababu majadilianoyamefika sehemu nzuri na tuna imani kubwa kwambachangamoto hii itafika mwisho sasa.

SPIKA: Mheshimiwa Khadija Nassir nilikuona, swali fupila nyongeza.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kuniona. Ni lini Serikali italeta marekebishoya Sheria Bungeni ili umeme unaonunuliwa Tanzania Barakwenda Zanzibar uweze kupatiwa msamaha wa kodi kamailivyo bidhaa nyingine zinazozalishwa Tanzania Bara kwendaZanzibar?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu WaziriFedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, wakati tunapitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati, Waziriwa Nishati alisema vizuri kabisa kuhusu jambo hili, kwambanalo ni katika mambo ambayo yapo katika mijadalakuhakikisha kwamba kodi inayotozwa kwa umemeunaouzwa Zanzibar inafanyiwa kazi. Nimwombe MheshimiwaKhadija Nassir pamoja na Wazanzibari wote na Watanzaniawote jambo hili litafanyiwa kazi kwa muda muafaka kabisa.

SPIKA: Mheshimiwa Lucia Michael Mlowe, uliza swalilako sasa.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

Na. 364

Watumishi wa Afya ambao Hawakuwepokwenye Mifuko ya Kijamii

MHE. LUCIA M. MLOWE aliuliza:-

Wapo Watumishi katika sekta ya afya, hususanMadaktari na Wauguzi ambao waliajiriwa katika miaka ya1980 kupitia Serikali Kuu, lakini wakati ule hapakuwa namakato ya mfuko wa kijamii na kuanzia mwaka 1999, Serikaliilianza kuwakata mishahara yao kwenye Mfuko wa PSPF:-

Je, Serikali inawafikiriaje Watumishi hao ambao fedhazao hazikukatwa na mifuko ya kijamii wakati huo hususanMfuko wa PSPF?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedhana Mipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa LuciaMichael Mlowe, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kabla ya Julai 1999, mfumo wamalipo ya mafao ya kustaafu kwa watumishi wa Serikali Kuuhaukuwa wa kuchangia. Kwa mantiki hiyo, watumishi wotewa umma waliokuwa kwenye ajira ya masharti ya kudumuwanastahili malipo ya uzeeni, wakiwemo watumishi wa sektaya afya hata kama hawakuchangia. Aidha, kwa mujibu waIbara ya tano (5) ya Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF,watumishi wote wa Serikali Kuu ambao waliajiriwa nakuthibitishwa katika ajira ya masharti ya kudumu na pensheni,wanakuwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPFkuanzia tarehe ya kuanzishwa kwa mfuko huo.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Mafaoya Hitimisho la Kazi Na.2 ya Mwaka 1999 kwa Watumishi waUmma, ambayo ilianzisha Mfuko wa Pensheni wa PSPF,wastaafu wote ambao ni wanachama wa Mfuko waPensheni wa PSPF na wanaoguswa na Sheria hii wanalipwa

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

mafao yao ya kustaafu na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwakipindi chote cha utumishi wao. Hii inamaanisha kwamba,mafao yao yanakokotolewa kuanzia tarehe ya kuajiriwa hadiwanapostaafu utumishi wao kwa mujibu wa Sheria na Kanuniza Utumishi wa Umma.

SPIKA: Mheshimiwa Mlowe nimekuona swali lanyongeza, tafadhali.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika, nakushurusana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza.Swali la kwanza; kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziriamesema kwenye jibu lake la msingi kwamba watumishiwanapaswa kulipwa mafao yao hata kama hawakuwawanakatwa, lakini hilo halifanyiki. Je, Serikali ina mkakati ganikuhakikisha kwamba hawa watumishi wanapata mafaoyao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa watumishiwastaafu wanapata pensheni yao ndogo sana, kunawatumishi wanapata Sh.50,000 kwa mwezi, kwa kweli kiasihicho ni kidogo sana. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikishainaongeza kiasi hicho cha pensheni? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa NaibuWaziri wa Fedha na Mipango.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, napenda kumwambia Mheshimiwa Mbunge na Bungelako Tukufu kwamba hili jambo analosema halifanyiki, siyosahihi. Kwa sababu watumishi wote ambao waliajiriwa nawalikuwa hawachangii kabla ya Mfuko wa Pensheni wa PSPFkuanzishwa walikuwa wakilipwa na Serikali Kuu kupitiaHazina. Kwa sasa kile kilichokuwa kinalipwa kupitia Hazinandicho kimeunganishwa na malipo yao ya PSPF nawanalipwa pensheni yao yote kama ambavyo wanastahilikulipwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, sina uhakika sanalabda nikae na Mheshimiwa Mbunge ni wastaafu gani

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

wanaolipwa pensheni ya Sh.50,000, kwa sababu Serikaliiliongeza pensheni ambayo ni kiwango cha chini kutokaSh.50,000 kwenda Sh.100,000 na Mifuko yote ya Hifadhi yaJamii inalipa Sh.100,000 kwa watumishi wote kama kiwangocha chini. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mlowe hujasema kweli leobwana, hakuna wa elfu 50.

MBUNGE FULANI: Wapo!

SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Mheshimiwa Joseph Mbilinyi swali la nyongeza tafadhali.(Kicheko)

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Ukiacha waaguzi lakini pia wafanyakazi wengi wa Idarazingine Serikalini wanacheleweshewa sana mafao. Mfano niAskari Magereza wanastaafu lakini wanakaa zaidi ya miakamiwili hawajaenda kwao. Wanaganda kwenye zile kota zaMagereza lane, mafao hamna, mtu kastaafu miaka miwilianadhalilika kwao Tanga, kwao Kilimanjaro, kwao wapi,hawezi kwenda kwa sababu hajapewa mafao yao walapensheni.

Mheshimiwa Spika, sasa hii Serikali inawaangalia kwajicho lipi hawa Askari Magereza kwa sababu, waowamezoea kuwa-support Polisi ambao wanatukamata,lakini wahalifu wako maeneo mbalimbali, wanakusanywayale maeneo mbalimbali, wanapelekwa eneo moja ambaloni Magereza. Wale jamaa wana kazi ngumu sana kuwatunzamle, lakini wanafanya utumishi wao, wanakuja wanastaafu,mtu anakaa Police Lane miaka miwili hajapewa pensionwala mafao yake, kwa nini wanawafanyia hivi AskariMagereza? (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Niliacha swali hilo refu liendelee maanalinatoka kwa mtu mwenye uzoefu, anazungumza vitu halisi,siyo maswali ya kutungatunga tu. Mheshimiwa Naibu Wazirikwa uzoefu huo wa Magereza, majibu tafadhali. (Kicheko)

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaSpika, ameuliza, kuhusu mkakati wa Serikali yetu, naombanimwambie Mheshimiwa Mbilinyi, mkakati wa kwanza waSerikali yetu ilikuwa ni kulipa madeni yote ya michango yamwajiri ambayo Serikali ilikuwa ikidaiwa na mifuko yaHifadhi ya Jamii. Napenda kumwambia MheshimiwaMbunge kwamba, mpaka leo ninapoongea madeni yoteyaliyokuwa yanadaiwa ya michango Serikali yetu yaAwamu ya Tano tayari imeshalipa zaidi ya shilingi bilioni 282ili kuhakikisha wastaafu wetu wanalipwa mafao yao kwamuda muafaka.

Mheshimiwa Spika, mkakati wa pili, ilikuwa ni kuonajinsi gani ya kuunganisha Mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii, ilipesa zilizopo ziweze kutumika inavyotakiwa na kuwanufaishawastaafu wetu pale wanapostaafu. NamwambiaMheshimiwa Mbunge kwamba, Julai Mosi, mifuko yoteimeshaunganishwa na sasa tuna mifuko miwili, tatizo hililitaondoka bila wasiwasi wowote.

SPIKA: Ahsante sana tuendelee. Waheshimiwa wenyehoja kwenye mambo haya, leo ni Wizara ya Fedha naMipango kwa hiyo, mtaweza kuchangia baadaye kidogo.Wizara ya Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Qambalo WillyQulwi, Mbunge wa Karatu. Mheshimiwa Qambalo,tafadhali.

Na. 365

Wanyamapori Kuharibu Mali na Kujeruhi Watu – Karatu

MHE. QAMBALO W. QULWI aliuliza:-

Matukio ya Wanyamapori kutoka nje ya Hifadhi yaNgorongoro kwenda katika vijiji vinavyopakana na hifadhihiyo Wilayani Karatu na kuharibu mazao ya wananchi nakujeruhi watu yamekuwa yakijirudia mara kwa mara:-

(a) Je, ni nini mkakati wa Serikali kuwadhibitiwanyama hao ili wabaki katika maeneo waliyotengewa;

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

(b) Fidia/Kifuta jasho kinachotolewa pindiwanyama wanapofanya uharibifu ni kidogo sanana imepitwa na wakati. Je, ni lini Serikali italetamarekebisho ya kifuta jasho, ili kuendana na mazingiraya sasa?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasilina Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Qambalo WillyQulwi, Mbunge wa Karatu, lenye sehemu (a) na (b) kwapamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, uharibifu wa mali na maisha yabinadamu kutokana na wanyamapori wakali na waharibifuunajitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa nipamoja na maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Ngorongoro.Katika Eneo la Ngorongoro uharibifu unajitokeza zaidi katikamaeneo ya mashamba na makazi ya wananchi wanaoishipembezoni mwa hifadhi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Hifadhi yaNgorongoro kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya yaKaratu inakabiliana na changamoto ya uharibifu wa malina maisha ya binadamu kwa kufanya doria za pamoja.Aidha, Mamlaka ya Ngorongoro ina vituo vitano katikamaeneo ya Kilimatembo, Elewana, Nitini, Bonde la Faru naMasamburai kwa ajili ya kudhibiti wanyamapori wakali nawaharibifu, vilevile magari mawili yamenunuliwa kwa ajiliya madhumuni hayohayo.

Mheshimiwa Spika, juhudi nyingine zinazofanyikani kuendelea kutoa elimu ya namna ya kujihami nakudhibiti wanyamapori, hususan tembo. Elimu hiyo,inahusisha matumizi ya pilipili, mafuta machafu na mizingaya nyuki kuzunguka mashamba kama njia ya kufukuzatembo.

Mheshimiwa Spika, fedha za kifuta jasho na kifutamachozi hazitolewi kama fidia bali hutolewa kwa ajili ya

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

kuwafariji wananchi walioathirika na wanyamapori wakalina waharibifu. Hivyo, fedha hizo kuwa ni kidogo nahazilingani na hali halisi ya uharibifu.

Mheshimiwa Spika, kulingana na wingi wa matukiopamoja na ufinyu wa bajeti Serikali imeamua kupitia Kanuniza Kifuta Machozi na Kifuta jasho ili kuondoa changamotozilizopo kiutendaji.

SPIKA: Mheshimiwa muuliza swali, Mbunge wa Karatu,swali la nyongeza.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogoya nyongeza. Pamoja na kuwa na doria za pamoja kati yahalmashauri na hifadhi hizo na pamoja na kuwa na hivyovituo vilivyotajwa bado kasi ya wanyama waharibifu nawakali kutoka ndani ya hifadhi na kwenda nje kwenye makaziya wananchi, imeendelea kuwa kubwa mno.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa ambayotunayo kwenye Halmashauri zetu ni Halmashauri hazina usafirikwa ajili ya kuwafukuza wanyama hao, Halmashauri hazinasilaha stahiki kwa ajili ya wanyama hao, lakini pia, bajetindogo ambazo Halmashauri tunazo, pia, uchache wawatumishi wa sekta hiyo ya wanyamapori.

Mheshimiwa Spika, hapa imesemwa kuna magarimawili yamenunuliwa kwa ajili hiyo. Magari hayo mawilinaamini yako Ngorongoro hayako Karatu huku ambakotatizo lilipo. Sasa Mheshimiwa Waziri anaweza akaongea nawatu wake wa Ngorongoro ili angalau gari moja liwekweHalmashauri, wale Maofisa wa Halmashauri pindi tatizolinapotokea waweze kwenda kushughulika?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, fedha hizi za kifutajasho au kifuta machozi, pamoja na kwamba, ni ndogo sanalakini pia, zinachelewa sana kuwafikia...

SPIKA: Mheshimiwa Willy, swali sasa.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Spika, swali;kwa nini fedha hizi zisilipwe kwenye hifadhi husika badala yamlolongo ambao sasa hivi zinalipwa kutoka Wizarani?

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mawili, Naibu Waziriwa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga, tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, ni kweli kabisa kumekuwa na changamoto hizi zakudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneomengi. Changamoto ziko katika upande wa usafiri,watumishi, pamoja na vifaa vile vinavyotakiwa kutumikakatika kupambana na hao wanyamapori.

Mheshimiwa Spika, sasa niombe kusema tu kwamba,kama nilivyosema kwenye swali la msingi, magari mawiliyameshanunuliwa na tayari kweli yako pale. jitihada ambazotutafanya ni kulingana na jinsi ambavyo amependekezaMheshimiwa Mbunge, kuhakikisha angalau gari mojalinakuwepo katika maeneo yale kusudi pale linapotokeatukio basi gari hilo liweze kusaidia katika juhudi hizo zakupambana na wanyama wakali.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, kuhusiana nafedha za kifuta jasho na kifuta machozi kwamba, ziwezinatolewa na hifadhi inayohusika, ni suala ambalo labdatutaliangalia wakati tunapitia upya hizi sheria ambazotutaona kama kweli, inafaa. Kwa hivi sasa ilivyo tuna mfukomaalum ambao unatumika kwa ajili ya kifuta jasho na kifutamachozi.

Mheshimiwa Spika, huu mfuko bado unakabiliwa nachangamoto ya kuwa na fedha za kutosha. Kwa hiyo, katikapendekezo analolileta nafikiri tutaliangalia, tutaona kamalinafaa, tunaweza tukalichukua. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Cecilia Paresso ni jirani wa hukohuko kwenye swali. Uliza swali la nyongeza.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.Changamoto ambazo zinakabili vij i j i hapa nchinivinavyopakana na hifadhi za wanyama zimekuwa nichangamoto za muda mrefu kwamba, wanyama wanaingiana kuharibu mazao na kuuwa watu, lakini ukiangalia nchimbalimbali zilizoendelea duniani wanaweka electrical fence,ili kudhibiti moja kwa moja tatizo hili. Je, Serikali kwa niniisianze kwa awamu kutekeleza na kuweka hizo electricalfence, ili angalau kukomesha kabisa tatizo hili? (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo fupi, Mheshimiwa NaibuWaziri.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Paresso,dada yangu ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu sanamatukio mbalimbali na amekuwa alifanya kazi nzuri sana,hongera sana.

Mheshimiwa Spika, sasa kuhusu electrical fencekuwekwa katika hifadhi zetu zote ni suala zuri, lakini uwezowa kifedha ndiyo changamoto. Ukiangalia ukubwa wahifadhi tulizonazo kwamba, zote tutaweka electrical fencekwa kweli, inaweza ikachukua muda mrefu sana. Sitaki kutoacommitment ya Serikali, lakini tutaendelea kulifanyia kazi ilituone kwamba, kama litawezekana, kama pale ambapobajeti itaruhusu basi tunaweza kulitekeleza.

SPIKA: Kwa sababu ya muda tunaendelea na swalila Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda.

Na. 366

Kuzuia Wanyama Waharibifu – Jimbo la Bunda

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-

Kila mwaka wanyama waharibifu wamekuwawanakula mazao ya wakulima katika Jimbo la Bunda na

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kulipa fidia yakifuta jasho na kifuta machozi kwa wakulima hao:-

Je, Serikali ina mikakati gani ya kuzuia wanyama haowakiwemo Tembo?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasilina Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa BoniphaceMwita Getere, Mbunge wa Bunda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua madharayanayosababishwa na wanyamapori waharibifu na wakali,hususan tembo, kwa wananchi waishio kandokando yamaeneo ya hifadhi, ikiwemo Wilaya ya Bunda. Katika Wilayaya Bunda Vijiji vinavyopata usumbufu wa mara kwa marakutokana na wanyamapori waharibifu na wakali ni Kunzugu,Bukore, Nyatwali, Balili, Tamau, Serengeti, Nyamatoke,Kihumbu, Hunyari, Mariwanda, Mugeta, Guta, Kinyambwigana Kinyangerere.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka mikakatimbalimbali ya kuwanusuru wananchi kutokana na madharaya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo yoteyanayopakana na maeneo ya hifadhi. Utekelezaji wamikakati hiyo unaendelea ambapo katika Wilaya ya Bundayafuatayo yamefanyika:-

(i) Umeanzishwa ushirikiano wa kudhibitiwanyamapori waharibifu kati ya watumishi kutoka KikosiDhidi ya Ujangili Bunda, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Pori laAkiba Ikorongo - Gurumeti, Halmashauri ya Wilaya ya Serengetina Mwekezaji Gurumeti Reserve;

(ii) Kutafuta vitendea kazi kwa ajili ya doria zawanyamapori waharibifu;

(iii) Vikundi 83 vimeanzishwa kwenye vij i j ivinavyopakana na maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuchukua

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

hatua za awali za kudhibiti wanyamapori hao pindikunapokuwa na matukio ya wanyamapori waharibifu,wakati wakisubiri msaada wa Askari Wanyamapori;

(iv) Wizara imetoa tochi 100 kwa Halmashauri yaWilaya ya Bunda. Mwanga mkali husaidia kufukuza tembousiku kwa vijiji vinavyounda vikundi hivyo vya kufukuzawanyamapori;

(v) Mafunzo kwa wananchi juu ya mbinu zakukabiliana na wanyamapori waharibifu yametolewa kwavijiji, sambamba na kuwashauri kuepuka kulima kwenyeshoroba za wanyamapori;

(vi) Kuweka madungu (minara) ambayo AskariWanyamapori wanaitumia kufuatilia mwenendo wa tembo;

(vii) Kutumia teknolojia ya mizinga ya nyukiambayo imewekwa pembezoni mwa mashamba; na

(viii) Mpango wa kutumia ndege zisizo na rubanikwa ajili ya kufukuza tembo unaendelea.

Mheshimiwa Spika, lengo la mikakati hii ni kuhakikishakwamba, matukio ya uvamizi wa tembo yanashughulikiwakwa haraka iwezekanavyo. Sambamba na mikakati hiyoWizara imekuwa ikitoa fedha za kifuta jasho au kifutamachozi pale ambapo mazao yameharibiwa au wananchiwamejeruhiwa au kuuawa na wanyamapori wakali,akiwemo tembo.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi Machihadi mwezi Oktoba, 2017, Wizara imelipa kifuta jasho nakifuta machozi cha jumla ya Sh.249,741,250 kwa wahanga1,284 na vijiji 14 katika Wilaya ya Bunda.

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa inayosababishamatukio ya wanyamapori wakali na waharibifu kuendeleakuwepo ni kuzibwa kwa shoroba na mapito yawanyamapori. Kutokana na hali hiyo Serikali ina mpango wa

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

kufufua shoroba za wanyamapori katika maeneo mbalimbalinchini kwa mujibu wa Kanuni za Shoroba, GN. 123 ya tarehe16 Machi, 2018. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Getere, swali la nyongeza,tafadhali.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika,ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naombakuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, niwapongezeWizara ya Maliasili na Utalii kwa kunipa gari la kusaidiakufukuza wanyama waharibifu kwenye maeneo yangu, lakinipia, najua wana mpango wa kupeleka fedha za kifuta jashokatika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa, sasani miaka 15 Vijiji vya Hunyali, Kihumbu, Maliwanda, Salakwa,Kyandege, Tingilima, wamekuwa ni wahanga wakuu wawanyama waharibifu wa mazao, sasa Serikali ina mpangogani sasa mbadala ikiwepo kupima vijiji hivyo ili kupata HatiMiliki za Kimila na kuendesha maisha ya wananchi wa makazihayo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa sasa kuonani kuamini na kuamini ni kuona, ni lini sasa Wizara au Waziriatatembelea maeneo haya, ili kujihakikishia hali halisi yauharibifu huo?

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Majibu ya swali hilo la Mheshimiwa Getere,tafadhali Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, kwanza nikweli kabisa kwamba, sasa hivi Wizara ina mpango mkubwamahususi wa kuhakikisha kwamba vijiji vyote ambavyovinazungukwa na Hifadhi za Taifa vinakuwa na mpango borawa matumizi ya ardhi. Hili tunalifanya kuanzia mwaka wafedha unaoanza Julai mwaka huu. Katika kutekeleza hilo

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

tunashirikiana na Wizara ya Ardhi, ambapo ndiyowamepewa hizi fedha kwa ajili kusaidia kupima vijiji vyotehivi ili wawe na mpango mzuri na kuhakikisha matumiziyanaeleweka vizuri kabisa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kuhusu kwendakutembelea na kujionea hali halisi, naomba nimwambie tuMheshimiwa Mbunge kwamba tuko tayari wakati wowotemara baada ya Mkutano huu wa Bunge kumalizikatutapanga ni lini tunaweza kufika kule ili tujionee hali halisiilivyo huko.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu yamuda tuendelee na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano. Mtaona muda wetu ni mdogo. Swali laMheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa MpakaniTunduma.

Na. 367

Ujenzi wa Barabara ya Mpemba hadi Ileje

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya Mpemba hadiIleje kwa kiwango cha lami ili kuunganisha na kuboreshampaka wa Malawi na Tanzania katika eneo la Isongole?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali la MheshimiwaFrank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mpemba – Isongoleambayo ni barabara kuu yenye urefu wa kilometa 50.3inaunganisha nchi yetu na nchi jirani ya Malawi inahudumiwana Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Songwe. Barabara hiyo inaanzia katika Barabara Kuu yaTANZAM, eneo la Mpemba, katika Mamlaka ya Mji waTunduma, Wilaya ya Momba. Barabara hii ni kiungo cha kufikakatika Mji wa Itumba ambao ni Makao Makuu ya Wilaya yaIleje na maeneo ya jirani ya nchi ya Malawi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali inatambuaumuhimu wa barabara hii kiuchumi na kijamii na kwa kuwa,ndiyo barabara inayounganisha wananchi wa sehemumbalimbali wa Wilaya ya Ileje na nchi jirani ya Malawi naZambia, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) inaendelea kujenga Barabara ya Mpemba –Isongole kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa utekelezaji wa mradiupo kwenye hatua za awali, zikiwemo ujenzi wa Kambi yaMhandisi mshauri ambayo imefikia 80%, kusafisha eneo laujenzi wa barabara kilometa 10, ujenzi wa makalvati mannena uwekaji wa tabaka la chini la barabara.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2017/2018Serikali imetenga shilingi bilioni 4.455 kwa ajili ya ujenzi wakiwango cha lami na katika mwaka wa fedha 2018/2019Serikali imetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuendelea naujenzi wa barabara hii, ili mradi huu uweze kukamilika kamaulivyopangwa.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri yanayotoa faraja kwa wananchiwa Tunduma pamoja na Ileje, ninayo maswali mawili yanyongeza. Swali la kwanza, wananchi wa Kata ya Bupigu,Kata ya Malangali, Kata ya Isoko na Kata ya Ikinga katikaWilaya ya Ileje wamekuwa na adha kubwa sana ya kuamkaSaa nane ya usiku na kusubiri usafiri kuja makao makuu yaMkoa wa Songwe. Ni lini Serikali itajenga barabara hii yakutoka Isongole mpaka Ikinga, ili kuondoa adha hii yaWananchi wa Ileje?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuna kipande chabarabara kilometa 1.6 kimejengwa katika Mji wa Tunduma

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

na kimejengwa kwa sababu, wananchi wa Mji wa Tundumawakati Mheshimiwa Rais akiwa Waziri wa Ujenzi, wakatianapita anakwenda Rukwa, walimsimamisha pale nawakamwomba barabara ile ijengwe haraka iwezekanavyona sasa Serikali imejenga kipande kile cha kilometa 1.6, lakinikipande kile kimejengwa chini ya kiwango. Je, ni lini Serikaliitakuja kuhakiki kipande kile cha barabara ili wananchi waTunduma waweze kufurahia mpango wa ujenzi wa barabarakwenye Mji wa Tunduma?

SPIKA: Majibu ya maswali hayo ya Mbunge waTunduma, Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa EliasKwandikwa tafadhali.

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Kama anavyouliza, anapenda kujua katika swali lakela kwanza, katika hizi Kata za Lupingu, Malangali na Ikinga,kuna sehemu ambayo ina uharibifu mkubwa, kwamba, kwakweli, maeneo mengi tumekuwa na uharibifu kutokana namvua zimekuwa nyingi, lakini kama tulivyopitishiwa bajetina Bunge lako, tumetenga fedha kwa ajili ya kufanyamatengenezo, ili kuhakikisha kwamba, maeneo hayayanapitika.

Mheshimiwa Spika, kabla hatujapata kipande chalami katika eneo hili nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbungena wananchi wa Tunduma kwa ujumla kwamba wakati hizimvua zinapungua tumejipanga kwa ajil i ya kufanyamarekebisho makubwa ili maeneo haya yapitike. Kwa hiyo,nimtoe tu wasiwasi kwamba tutafanya marekebisho iliwananchi waendelee kupata huduma ili waondokane nahii adha ambayo wanaipata.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kuhusu kilekipande cha kilomita 1.6 ambacho Mheshimiwa Mbungeanaona kwamba hakikujengwa katika standardinayotakiwa; niseme tu kwa sababu nitakuwa na ziara yamaeneo yale kwamba tutayaona kwa pamoja ili tuonekwamba hii kilomita 1.6 ina shida gani ili tuone kama kweli

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

ni kiwango hakikuwa kimefikiwa au labda saa nyingine ndiyoilikuwa kuna shida tofauti ya hapo kwa sababu kuna wakatimwingine barabara zinajengwa lakini mazingira ambayohayakutegemewa yanaweza yakatokea barabaraikaharibika.

Mheshimiwa Spika, tutaiona kwa pamoja naMheshimiwa Mbunge halafu tuone tutachukua hatua kamakutakuwa na shida yoyote kuhusu kipande hiki ambachoumekitaja.

SPIKA: Tunaendelea na swali l inalofuata laMheshimiwa Catherine Magige kwa niaba yake nimeokuonaMheshimiwa Amina Mollel.

Na. 368

Fidia kwa Wananchi wa Mkoa wa Arusha

MHE. AMINA S. MOLLEL (K.n.y. MHE. CATHERINE V.MAGIGE) aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi 55 wa Kataza Oldonyosambu na Mateves Wilayani Arumeru MkoaniArusha waliopisha ongezeko la barabara ya Arusha-Namanga toka mwaka 2013.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali la MheshimiwaCatherine Valentine Magige, Mbunge Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tathmini ya mali za wananchi 55wa Kata ya Oldonyosambu walioathiriwa na ujenzi wabarabara ya Arusha - Namanga ilifanyika mwaka 2013 nakiasi cha shilingi milioni 281.501 kilihitajajika kwa ajili yakuwalipa fidia. Uhakiki wa tathmini hiyo ulifanyika na

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

umekamilika, tayari Serikali imeshatoa Shilingi milioni 66.821katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kulipa sehemuya fidia hiyo.

Mheshimiwa Spika, malipo ya fidia yatafanyika kwapamoja kwa wananchi wote mara baada ya Wizara yangukupokea fedha zote zinazohitajika kwa ajili ya kulipa fidiahiyo.

Mheshimiwa Spika, napenda kumfahamishaMheshimiwa Mbunge kuwa wananchi wote wanne (4) kwaKata ya Mateves wameshalipwa fidia yenye jumla ya shilingibilioni 2.225, hivyo hakuna mwananchi wa Kata ya Matevesanayeidai Serikali fidia.

SPIKA: Mheshimiwa Amina Mollel, kama una swali lanyongeza.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, ninalo.Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja namajibu hayo ya Serikali lakini mpaka Mheshimiwa Mbungeanaandika swali hili ni kwamba katika Kata hiyo ya Matevesbado kuna wananchi ambao wanadai fidia ya malipo hayokwamba bado hawajatimiziwa. Je, Waziri yuko tayarikufuatilia na kuhakikisha kwamba wananchi hawa wotewanapata malipo yao kama ilivyokubalika awali? Hilo niswali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ningependa tu kupatacommitment ya Serikali amesema kwamba atakapopokeafedha hizo. Je, katika msimu huu wa mwaka 2017/2018 au nimpaka katika bajeti nyingine na pengine tu kwamba Waziriwenyewe yupo tayari kwenda sasa na Mheshimiwa Mbungeili kwenda kusikiliza hizo kero na malalamiko ya wananchina kuweza kuwakamilishia fidia yao.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo mafupi, MheshimiwaNaibu Waziri tafadhali.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, nimpongezesana Mheshimiwa Mollel na Mheshimiwa Mbunge CatherineMagige kwa ushirikiano wao namna ambavyo wanafuatiliaili kuhakikisha kwamba wananchi wao katika maeneo hayaya Arusha wanapata haki zao.

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya juhudi kubwasana kulipa fidia hizi. Ukiangalia kwa ujumla wakekwamba kulikuwa na jumla ya madai ya shilingi bilioni2.5, lakini mpaka sasa tunavyozungumza bilioni 2.291zimekwishalipwa ina maana kwamba asilimia 92 yamadai yote imeshalipwa. Hii inaonesha kwa jinsi ganiSerikali iko committed kuhakikisha kwamba hawawananchi wanaodai wanapata haki zao na kwaharaka.

Mheshimiwa Spika, nimtoe tu wasiwasi MheshimiwaMbunge kwamba hiki kiasi cha shilingi milioni kama 214kilichobaki ni kiasi ambacho ni kidogo, lakini ni muhimukilipwe mapema. Kwa hiyo, tunafuatia na niseme tukwamba ni wakati wowote na niko tayari kuhakikishakwamba fedha zikipatikana kutoka Hazina hawa wananchiwanalipwa mara moja. Kwa hiyo, wasiwe na wasiwasi,kama tulivyowalipa hawa wengine na wao watalipwa maramoja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu commitment ya Serikali ,nisema wakati niko committed kama nilivyoahidi hata wikiiliyopita wakati nikijibu swali lako Mheshimiwa Mbungekwamba nitafika maeneo haya ili sasa tuweze kuona piakwamba ni nini kinachotakiwa kufanyika ili mambo yaendesawia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Wizara ya mwishokwa siku ya leo ni Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Swalilinaulizwa na Mheshimiwa Balozi Adadi Mohamed Rajabu,Mbunge wa Muheza, tafadhali.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Na. 369

Tatizo la Maji Muheza

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB aliuliza:-

(a) Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi zake ikiwemoya Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni za kutoa maji MtoZigi kwenda Muheza na Vijiji vyake?

(b) Je, Serikali ina mpango gani zaidi ya huo wakuwaletea maji wananchi wa Muheza?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba na Waziri wa Maji naUmwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Balozi AdadiMohamed Rajab, Mbunge wa Muheza, lenye sehemu (a) na(b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaanza kutekelezaahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambapoimekamilisha usanifu wa kutoa maji kutoka Mto Zigi kwendaMji wa Muheza.

Mheshimiwa Spika, kazi zitakazotekelezwa katikamradi huo ni ujenzi wa kitekeo cha maji (Intake)katika Mto Zigi, ujenzi wa mtambo wa kutibu maji,ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa kilometa 23,uunganishaji wa vijiji vitakavyopitiwa na bomba kuuumbali wa kilometa 12 kila upande, pamoja na upanuzina ukarabati wa mtandao wa usambazaji maji katika Mjiwa Muheza.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imeendelea na utekelezaji wa oboreshaji wahuduma ya maji katika Mji wa Muheza, kwa mpango wamuda mfupi. Kazi zinazotekelezwa ni ulazaji wa mabomba

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

urefu wa kilomita 16.9 kutoka Pongwe Jijini Tanga hadi KitisaWilaya ya Muheza. Gharama za utekelezaji wa mradi huonishilingi milioni 413.5

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali imetenga kiasi cha fedha shilingi bilioni 3.17kwa ajili ya kuendelea na uboreshaji wa huduma ya majikatika Mji wa Muheza na vijiji mbalimbali katika Wilayahiyo.

SPIKA: Mheshimiwa Balozi Adadi, swali la nyongezatafadhali.

MHE. BALOZI ADADI. M.RAJABU: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswalimawili ya nyongeza: Kwanza napenda kuwapongeza sanaMawaziri wote yeye Naibu Waziri ameshafika Muhezapamoja na Waziri mwenyewe wiki iliyopita Ijumaa alikuwaMuheza na ameonesha ishara kwamba kweli Muhezainakaribia kupata maji. Isitoshe pia Mwewe katika kipindi chaClouds TV imesema kwamba Muheza itapata maji hivikaribuni.

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa Zigi kutoa majikutoka Mto Zigi mpaka Mjini Muheza ni kati ya miradi 17ambayo tunategemea kupata mkopo wa Serikali ya Indiaya dola milioni 500. Nataka kujua mradi huu utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, la pili, pale Muheza Halmashauriya Wilaya imenunua mtambo wa kuchimba visima, lakinimtambo huu tunashindwa kuutumia kikamilifu kwasababu ya ukosefu wa fedha. Kwenye bajeti hii ya wakatihuu tumepangiwa zaidi ya bilioni moja na tuna mpangowa kuchimba zaidi ya visima 50, Halmashauriimekwishapitisha.

Mheshimiwa Spika, nataka Waziri awahakikishiewananchi wa Muheza kwamba Urasimu utaondolewa,tunataka kuchukua kiasi cha fedha kutoka kwenye hiyo bilioniambayo tumepangiwa ili tuweze kutumia mtambo huu ili

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

tuweze kuchimba visima. Nataka Mheshimiwa Waziriawahakikishie wananchi kwamba urasimu huo utaondolewana utasaidia ku-facilitate mipango hii iweze kuendelea.

SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa NaibuWaziri wa Maji na Umwagiliaji tafadhali.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza napendanimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri, lakininiwahakikishie wananchi wa Muheza wana Mbungemfuatiliaji.

Mheshimiwa Spika, kwa kudhamiria kwa kutatuatatizo la maji kabisa katika Mji wa Muheza tumeona haja yakuwekeza mradi mkubwa wa maji kati ya miradi ile 17 nautekelezaji wa maji inategemea na upatikanaji wa fedha.Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mpaka sasa Serikaliimeshasaini mkataba na ile Serikali ya India mradi wa mkopowa milioni 500 katika kuhakikisha kwamba tunatatua tatizola maji.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie yeye pamoja nawananchi wa Muheza wakati wowote mradi ule utaanzamara moja. Sisi kama Wizara ya Maji tutasimamia nakufuatilia fedha zile mradi uanze mara moja na kwa wakatikatika kuhakikisha tunatatua tatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, kamaWizara ya Maji hatutakuwa kikwazo lakini tuwapongeze kwakununua mtambo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge leo saasaba tukutane na Katibu Mkuu wa Maji ili katika kuhakikishanamna gani tunaweza tukawasaidia wananchi wa Muhezawaondokane na tatizo hilo la maji katika kuhakikishatunawaunga mkono. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda hauko upandewetu naomba tuendelee na matangazo. Leo tuna wageniwengi kweli is a record. Nitaanza na wageni ambao wakokwenye jukwaa la Spika.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Wageni watatu ambao ni Watumishi kutoka Ofisi yaSpika wa Bunge la Ghana, our visitors from Ghana Head ofDeputy Speaker’s Secretariat – Mr. Mathew Tawiah, Head ofthe First Deputy Speaker’s - Secretariat - Ms. Janet Frimpong,Head of the Second Deputy Speaker’s Secretariat – Ms. AnitaPapafio, your most welcome. Inaonekana Bunge la Ghanalina Manaibu Spika wawili. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, pia tunao wageni 55 waMheshimiwa Waziri wa Fedha Philip Mpango ambao ni hawawafuatao:-

Naibu Katibu Mkuu - Ndugu Suzana Mkapa; NaibuKatibu Dkt. Hatibu Kazungu; Naibu Katibu Mkuu Ndugu AminaShaaban; Kamshina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) -Ndugu Charles Kichere; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali, Profesa Juma Assad; Kamshina wa Bajeti, NduguMary Maganga; Kamshina wa Sera (CPAD), Ndugu BenedictoMgonya; Mhasibu Mkuu wa Serikali, ndugu FrancisMwakapalila; Msajili wa Hazina, Ndugu Mafutah Bunini;Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, Ndugu Mohamed Mtonga;Kamshina Msaidizi wa Kitengo cha Utakasishaji wa FedhaHaramu, Ndugu Gilbert Nyombi; Katibu wa Tume ya Pamojaya Fedha (JFC), Ndugu Ernest Mchanga;

Wengine ni Kaimu Kamishna wa Idara ya usimamiziwa Sera ya Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, NduguJohn Mboya; Kamshina wa Idara ya Sera na Ununuzi waUmma, Dkt. Fredrick Mwakibinga; Mtendaji Mkuu, Ofisi yaTaifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa; Kamshina Msaidizi waBajeti, Ndugu Pius Mponzi; Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa(PPF), Ndugu William Erio; Mkurugenzi Mkuu wa Mfukowa Pensheni (GEPF), Ndugu David Msangi; MkurugenziMkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali(PSPF), Ndugu Adam Mayingu, wameambatana na Wakuuwa Taasisi, Mashirika, Idara na Vitengo vilivyo chini yaWizara hiyo.

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageni waMheshimiwa Raphael Chegeni wanaotoka Singapore, our

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

visitors from Singapore please! Madam Elaina Chong andMadam Farizan Demoran, your welcome. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao wageni wanne (4) waUmoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWTG) ambao niwanamitindo kutoka Jiji Dar es Salaam Ndugu KhadijaMwanamboka, Ndugu Fideline Iranga, Ndugu Frank Gongana Ndugu Richard Mlekoni. (Makofi)

Wapo pia wageni watatu (3) wa MheshimiwaRaphael Chegeni nimeshawataja.

Wageni 11 wa Mheshimiwa Juma Aweso, Naibu Waziriwa Maji na Umwagiliaji ambao ni Walimu tarajali kutokaMkoani Tanga, karibuni sana. (Makofi)

Wageni 10 wa Mheshimiwa Willy Qambalo ambao niwapiga kura wake kutoka Karatu. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Khadija Nassir Ali ambaye nimtoto wake kutoka Dodoma, Ndugu Abdulrahman FestoMselia. (Makofi)

Tunao wageni 45 wa Mheshimiwa Bonnah Kaluwaambao ni wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Tusiime iliyopoJijini Dar es Salaam, wanafunzi wa Tusiime wako wapi? Ooh!karibuni sana Tusiime. Hii ni moja ya shule bora kabisa katikanchi yetu. (Makofi)

Pia wapo wageni 14 wa Mheshimiwa Oran Njezaambao ni Viongozi wa CCM, Mji wa Mbalizi Mkoani Mbeyawakiongozwa na Ndugu Fred Mwampashi, karibuni sanawageni wetu toka Mbeya. (Makofi)

Wageni Watatu (3) wa Mheshimiwa Hassan Masalaambao ni wapiga kura wake kutoka Nachingwea, MkoaniLindi. (Makofi)

Wageni 51 wa Mheshimiwa Justin Monko ambao niwanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Dodoma wanaotokea

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wakiongozwa naNdugu Yohana Msita, Wanyampaa wako wapi? Inaelekeahawapo leo au wapo basement maana wageni ni wengi.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao wageni 22 waMheshimiwa Chief John Kadutu ambao ni wachezaji wa Timuya Ulyankulu Veterans kutoka Ulyankulu wakiongozwa naMheshimiwa Juma Hamduni, Diwani. Karibuni sanaWalyankulu. (Makofi)

Wapo pia wageni saba (7) wa Mheshimiwa VictorMwambalaswa ambao ni wapiganaji wake kutoka ChunyaMkoani Mbeya. Mheshimiwa Mwambalaswa ananiambiahawa ndiyo kiboko ya CHADEMA, Mbeya. (Kicheko)

Pia, wageni 94 wa Mheshimiwa Martin Msuha ambaoni Walimu na wanafunzi wa Shule ya Mount Everest kutokaDar es Salaam, Ooh! wanapendeza, karibuni sana Shule yaMount Everest, karibuni watoto wetu. (Makofi)

Wapo pia wageni watatu (3) wa MheshimiwaGoodluck Mlinga ambao ni jamaa zake kutoka MkoaniMorogoro. (Makofi)

Wageni Wawili wa Mheshimiwa Venance Mwamotoambao ni marafiki zake toka Jijini Dar es Salaam. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, wageni waliotembeleaBunge kwa ajili ya Mafunzo ni Wanachuo 40 kutoka Chuocha Taifa cha Usafirishaji (NIT) cha Jijini Dar es Salaam, karibunisana. Wanafunzi 30 na walimu watano (5) kutoka shule yaSekondari ya Denis ya Morogoro, karibuni sana watoto wetu.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Will iamNgeleja anatutaarifu kwamba timu yetu ya Mpira wa miguujana iliwafunga St. John’s bao moja na mchezaji aliyefungabao hilo ni Mheshimiwa Venance Mwamoto, mchezaji borawa jana alikuwa ni Mheshimiwa Hamidu Bobali. (Makofi)

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Kwa upande wa Bunge Queen’s lilipata magoli 75against St. John’s University ilipata magoli matatu tu. Nyotawa mchezo huo alikuwa Mheshimiwa Esther N. Matikoambaye peke yake Mheshimiwa Esther Matiko alifungamagoli 47 kati ya hayo 75. Hongera sana MheshimiwaMbunge. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, Jumapili timu yetu ya mpirawa miguu iliwafunga Kadutu Boys ambayo wapo hapo juumagoli matatu dhidi ya sifuri..

MHE. JOHN P. KADUTU: Aaah! (Kicheko)

SPIKA: Magoli matatu kwa mawili, wafungaji wetuwalikuwa Mheshimiwa Alex R. Gashaza na MheshimiwaAhmed Juma Ngwali na mchezaji bora katika mechi hiyoalikuwa Ahmed Juma Ngwali. Tunawasisitiza WaheshimiwaWabunge kuhudhuria michezo kila weekend kuwatia moyowachezaji wetu. (Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, naona niwatangaziekwamba Ofisi ya Bunge tumepokea barua kutoka Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ikitoa rai kwa Wabungeambao mlikopa matrekta kutoka SUMAJKT kulipa madeniyenu ya matrekta hayo na zana zake ambayo mliyakopaharaka sana.

Itakumbukwa kwamba tarehe 17 Mei, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli alitoa maelekezo kwa wadaiwa wote wa matrektana zana zake wa SUMAJKT warejeshe madeni yao ndani yakipindi cha siku thelathini. Kufuatia maelekezo hayoWabunge wote mnaodaiwa ni SUMAJKT mnatakiwa kureshamadeni hayo kabla ya tarehe 23 Juni, 2018. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Walipe!

SPIKA: Majina yenu ninayo hapa sijui niyasome?

MBUNGE FULANI: Soma!

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Waheshimiwa kuna wanaoafiki nisome na wasioafiki.Wasioafiki wameshinda. Kwa hiyo Waheshimiwa kwa kwelitulipe madeni haya. Nimeaangalia kwenye orodha ile yawanaodaiwa haya nikasema labda tuangalie kwenyemalipo yetu ya Bunge tuwakate kule, nikakuta kule nakohawana hata kitu, kwa hiyo sina pa kukata. (Kicheko)

Mheshimiwa Margaret Sitta, anaomba niwatangazieWaheshimiwa Wabunge kuwa, kutakuwa na mafunzopamoja na mazoezi ya maonesho ya mavazi (fashion show)kwa Waheshimiwa Wabunge mtakaoshiriki onesho lamavazi, siku ile ya hafla ya uchangishaji fedha za kuboreshamazingira ya mtoto wa kike shuleni kwa majimbo yote. Kwahiyo, tunawaomba sana wale ambao mtashiriki kwenyefashion show hiyo tuwataarifu kwamba MwanamindoMaarufu Khadija Mwanamboka yuko kwenye jukwaa letuhapo, ameshawasili kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo yamazoezi. Mazoezi hayo yatafanyika katika Ukumbi waMsekwa, C na D, saa saba mchana mara baada yakuahirishwa kwa shughuli za Bunge. (Kicheko)

Mheshimiwa Damas Ndumbaro, anawatangaziaWabunge wa Nyanda za Juu Kusini, Wabunge Vijana naWabunge wote kufika kwenye presentation ya Tamasha laMaji Maji Selebuka, leo tarehe 4 Juni, katika ukumbi wazahanati ya zamani saa 7.30 mchana.

Naona tumemaliza sasa inabidi tuendelee na mambomengine.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika,mwongozo.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Spika,Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Katibu nisomee majina:

NDG. LINAH KITOSI-KATIBU MEZANI: MheshimiwaMusukuma, Mheshimiwa Heche, Mheshimiwa Ryoba,

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Lucia Mlowe, Mheshimiwa Amina Mollel,Mheshimiwa Chegeni.

MWONGOZO WA SPIKA

SPIKA: Mheshimiwa Chegeni, kifupi jamani.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Spika,naomba tu kutumia kanuni ya 68(7), lakini naomba tu nielezekwamba, kuna baadhi ya mikoa ambayo ni mipya, lakinikwa bahati mbaya sana haina vitendea kazi vya zimamoto.Mkoa wa Simiyu ni mkoa mpya lakini, una gari la zimamotoambalo limeshakuwa chakavu halifanyi kazi.

SPIKA: Mheshimiwa Chegeni hilo jambo limetokea linikatika mambo yetu?

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwahalijatokea leo hii, lakini naomba tu nilieleze.

SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Chegeni, kinyumena kanuni uliyoisoma. Mheshimiwa Ryoba.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Nasimama kwa mujibu wa kanuni ya 68(7) na ileya 47, kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Spika, pale Serengeti katika Kijiji chaNyichoka, wameuawa simba tisa. Hali ya wanyama kutokanje ya hifadhi, ni mbaya sana. Tunakoelekea inaonekanaSerikali haiko serious na wanyama wanaotoka nje ya hifadhi.Sasa wanatoka nje ya hifadhi wanauawa, Serikali hainamkakati wowote mpaka sasa hivi wa kuzuia hawawanyama. Kwa hiyo, nataka mwongozo wako, Serikali inautaratibu gani wa kuhahikikisha kwamba inazuia hawawanyama wasitoke nje ya hifadhi?

Mheshimiwa Spika, hawa wanyama wanauawamwisho wataisha, maana wamekwenda wamekulang’ombe, bahati mbaya sana wafugaji wameweka sumu

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

kwenye mzoga, wameenda wamekula wamekufa; na sioSerengeti peke yake walikwenda pia na huku maeneo yaKaratu Karatu huku, ikawa hivyo hivyo na Serikali bado ikokimya.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ryoba, tumekupata.Maliasil i m-note down hilo li l i lotokea, ni taarifa nzuriMheshimiwa, Serikali wameipokea moja kwa moja. Ni jambola hatari, maana Serengeti ina simba wachache sana, kamaunaweza kuwaua tisa kwa mpigo ni hatari.

Mheshimiwa Mlowe.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Spika, nasimamakwa kanuni ya 68(7), naomba mwongozo wako kuhusujambo ambalo limetokea Bungeni mapema. Wakati NaibuWaziri wa Fedha akijibu swali langu nililouliza la 364, alisemakwamba si kweli kusema kwamba watumishi wastaafuwanapokea shilingi hamsini elfu. Nina ushahidi kabisa, kunahata wazazi wa baadhi ya Wabunge huku ndani wanapokeapesa hizo, hamsini elfu kwa mwezi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba mwongozowako kuhusu suala hili kwa sababu nimeambiwa ni mwongolakini hali kuwa najua ni ukweli, kuna watu wanapokeafedha hizo.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Mheshimiwa Mlowe, Naibu Waziri alipojibualisema yeye hana taarifa, lakini angependa kama unataarifa hizo basi uwapatie ili waweze kuzifanyia kazi. Kwahiyo ujumbe umefika, wewe wawasilishie ili muweze kuliwekavizuri kwa pamoja.

Mheshimiwa Amina Mollel.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nakushuru.Mwongozo wangu utatokana na swali namba 369, ambapokila wakati tulikuwa tukiulizia maswali...

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

SPIKA: Kanuni gani Mheshimiwa?

MHE. AMINA S. MOLLEL: Kanuni ya 68(7), kuhusu swalinamba 369, limetokea leo. Kutokana na swali hili tumekuwatukizungumzia masuala ya maji na shida kubwa ya majiiliyopo katika maeneo mengi. Hata hivyo, baadhi yawananchi katika Vijiji vya Oldonyosambu na Oldonyowasimaji wanayopata yana kiwango kikubwa cha madini yafluoride.

Mheshimiwa Spika, hili ni janga kwa sababu watotowanapata ulemavu wa kupinda miguu, pia akinamamawanapinda mgongo. Inaumiza sana, kwa sababu kizazikinachozaliwa pale kinapata ulemavu. Upo ulemavuunaokubalika lakini ulemavu huu unatokana na janga la majiyenye kiwango kikubwa cha madini ya fluoride haukubaliki.Tunazalisha kizazi ambacho watoto wale wanapata ulemavuambao kwa kweli kama Serikali tukipeleka maji tutaondoaulemavu huu.

Mheshimiwa Spika, naomba kauli ya Serikali ni jitihadagani za haraka, zinafanyika katika kuokoa kizazi kile ilikuondokana na hili janga la ulemavu ambao unawezakuepukika. Ahsante.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Amina Mollel, kwahoja yako muhimu sana. Wizara ya Maji ichukueni hiyo,namna gani ya ku-deal na fluoride ambazo zinasababishamatatizo makubwa kwa watoto.

Mheshimiwa Heche.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Nimesimama kwa kanuni ya 68(7), lakininikisoma pamoja na kanuni ya 47. Kama utaona inafaa nakwa udharura na unyeti wa jambo hili, ningeomba lijadiliwena Wabunge ili litolewe mwongozo. Juzi wakati Waziri waMadini anahitimisha hoja yake hapa, alipiga marufukukusafirisha carbon kutoka kwenye mkoa mmoja kwendamkoa mwingine.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Mheshimiwa Spika, wale wazalishaji wa dhahabuwanapokuwa wamezalisha dhahabu, wanapokuwawameichakata inakuwa in carbon form wanaipelekakwenye plant inayoitwa illusion, ile plant ndiyo inayotumikakukamata dhahabu na kuuza, sasa inakuwa dhahabu kamiliili iuzwe.

Mheshimiwa Spika, kwenye mikoa yetu ambayo mingitunazalisha dhahabu, kwa mfano Mkoa wa Mara, hatunahiyo plant ya illusion; Mkoa wa Mara hakuna kabisa hiyoplant na Mkoa wa Mara kuna wachimbaji wadogo wengisana, hasa kwenye Jimbo langu la Tarime, wengi wanafikahata mia nane mia tisa na wanategemea kuzalisha dhahabukwa ajili ya maisha yao, wamekopa kwenye Mabenki,wamekopa kwenye SACCOS na wengine wamekopa kwawatu binafsi. Kwa hiyo kitendo cha kupiga marufuku kuanziaJuni mosi ghafla tu, kwamba watu wasisafirishe carbon,inaenda kuharibu uchumi wa watu wengi sana na watuwengi majumba yao yatauzwa.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, kwenye hilo,uzalishaji wa carbon hii, uki-extract na ukakamata dhahabu,sehemu pekee ambayo kanda ya ziwa watu wanauzadhahabu ni Mwanza. Sasa, hata kama kungekuwa na illusionplant, ukisema watu wa-extract wasafirishe dhahabu ni hatarikweli kweli. Pia watumishi wa TMAA wa kukaa pale nakuangalia loyalty ya Serikali kwenye kila plantitakapozalishwa mimi naona ni kazi ambayo Serikali inajipaambayo ni ngumu.

Mheshimiwa Spika, ningeomba hil i jambo,lizungumzwe kama jambo la dharura, kwa sababu kunawananchi wengi sana, na nafikiri ni mikoa mingi sana,ambao wana carbon ndani na wanaenda kuzuiliwakusafirisha kuanzia jana na maisha yao wanadaiwa naMabenki na italeta usumbufu mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, naomba suala hili kama utakubalilijadiliwe na Wabunge hapa watoe mwongozo kwa Serikaliili watu hawa wasije wakaharibu uchumi wao.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

SPIKA: Hilo jambo tuachie tu, tulifanyie kazi, ili tuwezekujua nini ni nini, kwa sababu si wengi hapa ambaotunafahamu hii illusion ni kitu gani na kikoje. Wizaraisingeweza kukurupuka tu kusema hivyo lazima kuna sababuza msingi sana. Kwa hiyo, tupeane muda tutapata kwawakati muafaka maelezo kuhusu jambo hilo, sasa kamayatakuwa hayatoshi ndio tutakuwa na majadiliano kamaitabidi.

Mheshimiwa Musukuma, ndiye wa mwisho.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Nami nasimama kwa kanuni ya 68(7)ikisomwa na 47, nadhani nina imani busara yako mimi sinasababu ya kuomba suala hili lijadiliwe.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano,imefanya vizuri sana kuhamasisha wananchi nawafanyabiashara waweze kulipa kodi kwa kutumiamashine za EFD. Hata hivyo, tunavyozungumza ni zaidi yasiku 10 mashine za EFD nchi nzima, kupita kwenye shell,madukani na sehemu zingine hazifanyi kazi nawafanyabiashara wengi hawana mbadala hata ya risiti yamkono ambayo TRA hawaitambui, kwa hiyo watuwanafanya biashara bila ya kutoa risiti, leo karibu siku 10,Serikali imepoteza mapato.

Mheshimiwa Spika, sasa ni nini kauli ya Serikali, hasakwa supplier alie-supply EFD mashines ambayo sasa anazi-temper, tunakuwa tunakula hasara, hatukusanyi kodi nahatuna mbadala nyingine ya Serikali ni nini kauli yaSerikali?

Mheshimiwa Spika, nakushuru.

SPIKA: Kwa sababu leo ni Wizara ya Fedha naMipango, hilo Waziri analichukua moja kwa moja, yatakuwani moja ya maeneo ambayo atayatolea ufafanuzi wakutosha kabisa, kati ya leo na kesho pia. Kwa hiyo tuwemakini tu kufuatilia.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka,tumetangaziwa kwamba wale mabinti maarufu Maria naConsolata walifariki juzi, na huenda mazishi yao yakawa leoIringa. Kwa kweli kwa niaba ya Bunge hili ningependakutoa salamu za rambirambi kwa familia, walikuwa niwatoto ambao ni wa ajabu kidogo na watoto wenyeupendo mkubwa sana. Kifo chao kimetupa masikitikomakubwa sana, Mheshimiwa Waziri wa Elimu tufikishie polezetu huko.

La mwisho ambalo nataka kulisemea kidogo tu; kunajambo ambalo limesababisha sintofahamu kwa ummana lilitokea hapa, nalo ni jambo linaloendana na msibawa ndugu yetu na rafiki yetu Mwalimu Kasuku Bilago.Mtakumbuka hivi juzi hapa aliweza kupumzishwa kwenyenyumba yake ya milele, lakini katika process yakushughulikia suala la msiba ule, kulikuwa nasintofahamu za hapa na pale na maneno mengi yahovyo hovyo, mengine yakisemwa mbele yetu hapahapa Bungeni; maneno yasiyostahili kabisa kuzungumzwana viongozi ambao wana utulivu na nadhani tuzoee tumambo kama haya, lakini kwa kifupi sana kilichotokeani nini?

Wakati msiba ule unatokea siku ile ya Jumamosi, kuleMuhimbili walikuwepo maafisa wangu wa Bunge au maafisawetu, ikiwa ni pamoja na Katibu wa Bunge mwenyewe, palepale Muhimbili, pale pale I.C.U, na baadhi ya wanafamiliawalikuwa pale. Sina haja ya kwenda na hadithi hiyo kwaurefu wake.

Kwa hiyo tulipokaa siku ya Jumapili, amefarikiJumamosi sisi tukakaa kikao Jumapili, Kamati ya Uongozipamoja na Tume tukazingatia ushauri tuliokuwatumeupata toka kwenye familia na sisi wenyewe. Vikaohivyo vikaamua siku ya mazishi iwe Jumatano tarehe30. Nasema kwa kuzingatia ushauri tulioupata kwenyefamilia pamoja na sisi Kamati ya Uongozi na Tume kamailivyo ada kwa misiba mingine yote ambayo tuliyowahikupata.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Kwa hiyo mipango yote ikafanyika na tumewajibikakama Bunge katika kila hatua. Sitaki kwenda na kilajambo ambalo lilitokea katika kila hatua, ikibidi hukombele nitakuja kueleza, kwa sababu tulikuwa tunafahamukila kinachoendelea na tunajua kila kilichoendelea.Ilibidi sisi kama Bunge kama tulivyokuwa tumepangaratiba yetu iishie tarehe 30 ile ile na tulifanya hivyo, tulifikapale.

Tukumbuke msiba unakuwa ni wa familia, ndio wenyekauli ya mbele zaidi kuliko sisi au watu wengine. Hatakama tulikuwa tumekubaliana mwanzoni, iwe hivi iwetarehe 30 familia wana uwezo wa kubadili wakatiwowote maamuzi yao na wakafanya wanavyoona inafaa,lakini sisi kama taasisi tunapoishia pale tulipopangatunaishia pale.

Iko misiba mingine, kwa mfano nchi ya Nigeria nakwingine kule, ninyi mnafahamu, wanachukua hata miezimitatu kabla ya kumzika marehemu, wengine wanachukuamwezi. Sasa hatuwezi Bunge tukaenda mahali tukawekamatanga pale tukaa miezi mitatu tunasubiri mpaka sikuambayo familia itasema sasa ndipo izike, haiwezekani.Lazima tuwe na muda muafaka na muda ule unafahamikana kila mtu anakuwa anajua tunashiriki vipi na mwisho wetuni wapi.

Tulipata ushauri muhimu sana, kutoka kwa Mwenyekitiwa Wabunge wa Kigoma, Mheshimiwa Nsanzugwanko,tangu mapema na hata mahali pale, kwamba kwa kabilala Waha na kwa kweli Watanzania kwa ujumla huwahatugombei msiba, watu hawanyang’anyani marehemu.Kwa hiyo kwa busara iliyotokea pale baada ya kukaa nawenzetu tukakubaliana kwamba tuwakabidhi familia ilifamilia iweze kuendelea na hatua iliyobaki kwa sisi paletulipofika ikawa ndio mwisho wa zoezi letu na tukafanyahivyo kwa amani na salama kabisa.

Waheshimiwa Wabunge, isingetarajiwa hata kidogoSpika aende kwenye uwanja ulioandaliwa na vyama vya

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

kisiasa, nikae pale nianze kuingia kwenye siasa zakuanza kujadili hatma ya marehemu, kwamba Mbungegani atafuata, wa chama gani na kadhalika na miminiko pale, hata kumzika bado, hiyo biasharanisingeweza kufanya hivyo na sijawahi kufanya nahata Maspika walionitangulia hawajawahi kufanya.(Makofi)

Siku zote tunapowapeleka marehemu wetu huwatunawapeleka kwa familia, huwa tunaaga pale kwenyefamilia, tunakwenda makaburini kama jambo hilo likotayari, tunamalizia pale kwa wote. Kwa hiyo, utamadunimwingine wa kwenda kwenye viwanja na kadhalikahata kama awe ni Mbunge wa chama gani, Spikahawezi kwenda kwenye viwanja vya aina hiyo,haiwezekani.

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge, napenda tuniliweke sawasawa jambo hili na niwaombe rafiki zanguakina Selasini na wengine ambao tunashiriki vikao natunaamua kwa pamoja, halafu mkitoka huko mnahamiafacebook na mnaanza kusema maneno ya ajabu na ninyini watu wazima tunaheshimiana, kidogo haipendezi,kama mtataka tuwe tunajibishana hatua kwa hatua,kila hatua tunajibishana na kuwaumbua na ninilinakuwa ni jambo ambalo halitawaletea heshima kwenyemajimbo yenu.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo ni vizuritunapokuwa kwenye kikao na wewe mwenyeweumehudhuria na umeshiriki, unafahamu jambo lenyewemwanzo mwisho, halafu tena wewe ndiye unakuwa nambamoja kuzungumza mambo ambayo hayana mantiki naku-confuse watu ni jambo ambalo halina maana hatakidogo.

Tunawashuruku wale wote waliotupa ushirikianomahali popote katika jambo hili. (Makofi)

Katibu tuendelee.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

NDG. LINAH KITOSI-KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mpangotafadhali, karibu sana. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika,kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lakoTukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaBajeti, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako sasa lipokeena kujadili mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti yaWizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2017/2018 pamojana Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka ujao wafedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuruMwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kusimama mbele yaBunge lako Tukufu kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Fedha naMipango kwa mwaka 2018/2019. Aidha, napenda nitumiefursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakinipia Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa KassimM. Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa kuliongoza taifa letu kwa ujasiri na uzalendowa hali ya juu. Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema,hekima na busara ya kuliongoza Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kukushukuru wewebinafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwakuendesha vema majadiliano ya mapendekezo ya bajeti zaWizara mbalimbali kwa mwaka 2018/2019. Aidha, napendakumpongeza Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia, kwakuchaguliwa tena, pamoja na Mwenyekiti mpya,Mheshimiwa Jitu Soni. Aidha, nawapongeza na kuwashukuru

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti kwa maoni, ushauri namapendekezo waliyotoa ambayo yamesaidia sana katikakuboresha Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipangokwa Mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hii kuwapongezaMheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro, Mbunge wa Jimbo laSongea Mjini; Mheshimiwa Justin Monko, Mbunge wa SingidaKaskazini; Mheshimiwa Dkt. Stephen Kiruswa, Mbunge waJimbo la Longido; na Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel,Mbunge wa Jimbo la Siha, lakini pia Mheshimiwa MaulidMtulia, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa kuchaguliwakuwakilisha wananchi wa majimbo yao katika Bunge lakoTukufu.

Mheshimiwa Spika, aidha, natoa pole kwa Bunge lakoTukufu kwa kuwapoteza Mheshimiwa Leonidas Gamaaliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na MheshimiwaKasuku Samson Bilago aliyekuwa Mbunge wa Jimbo laBuyungu. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahalipema peponi. Amina.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoe shukrani zanguza dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji – Mbunge waKondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango kwaushirikiano anaonipatia katika kuhakikisha utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango unafanikiwa.Aidha, nawashukuru Bw. Doto James, Katibu Mkuu na MlipajiMkuu wa Serikali, Naibu Makatibu Wakuu Bi. Amina Shaaban,Dkt. Khatibu Kazungu na Bi. Susan Mkapa kwa kusimamiavizuri shughuli za kila siku za kiutendaji za Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, pia napenda kumpongeza kwadhati Profesa Florence Luoga, Gavana mpya wa Benki Kuuya Tanzania na kumshukuru yeye pamoja na Bw. CharlesKichere, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzaniana Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa yaTakwimu kwa kusimamia kwa weledi taasisi nyetiwalizokabidhiwa. Nawashukuru pia, Makamishna,Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara,

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Wakuu wa Vitengo na Wafanyakazi wote wa Wizara, kwakutimiza wajibu wao vema wa kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Spika, hotuba yangu imejikita katikamaeneo makuu mawili. Kwanza, ni Mapitio ya utekelezajiwa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2017/2018 na pili niMalengo na Maombi ya fedha kwa mwaka 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nianze na Mapitioya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka huu wafedha unaoenda ukingoni.

Mheshimiwa Spika, Wizara imetekeleza majukumuyake kupitia mafungu tisa ya kibajeti pamoja na taasisi namashirika 36 yaliyo chini yake na tumeonesha kwenye jedwalila kwanza ukurasa 136 wa kitabu cha hotuba. Mafungu hayoni: Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango; Fungu 21 – Hazina;Fungu 22 – Deni la Taifa; Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuuwa Serikali; Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha; Fungu 13 –Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; Fungu 7 – Ofisi yaMsajili wa Hazina; Fungu 66 – Tume ya Mipango; na Fungu 45– Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara ya Fedha naMipango pamoja na muhtasari wa mapato na matumizi yaWizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ni kamainavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa nne hadi ukurasa wa tisa.

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Majukumu kwaMwaka 2017/2018. Naomba kutoa taarifa mbele ya Bungelako Tukufu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara yaFedha na Mipango kwa mwaka 2017/2018 ambayoyameainishwa katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 10mpaka ukurasa wa 81.

Mheshimiwa Spika, kwanza ni Utekelezaji wa Sera zaUchumi Jumla. Katika kutekeleza jukumu hili Wizara ilijikitakatika kuhakikisha kuwa malengo ya ukuaji uchumi, mfumukowa bei na mapato na matumizi ya Serikali yanafikiwa. Katika

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

mwaka 2017 kasi ya ukuaji wa uchumi imeendelea kuwa yakuridhisha na kufikia wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwana ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2016.

Mheshimiwa Spika, ukuaji huo ulichangiwa na kasikubwa ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika sekta yamadini na uchimbaji wa mawe ambayo ilikua kwa asilimia17.5; sekta ya maji asilimia 16.7; sekta ya uchukuzi na uhifadhimizigo asilimia 16.6; na sekta ya habari na mawasilianoambayo ilikua kwa asilimia 14.7.

Mheshimiwa Spika, wastani wa mfumuko wa bei kwamwaka 2017 ulikuwa asilimia 5.3 na umeendelea kupunguahadi kufikia asilimia 3.8 mwezi Aprili, 2018. Kupungua kwamfumuko wa bei kulichangiwa zaidi na kuongezeka kwauzalishaji wa chakula, utulivu wa thamani ya shilingi yaTanzania dhidi ya sarafu za kigeni, kuimarika kwa uzalishajiwa umeme, utekelezaji thabiti wa sera za fedha, urari wamalipo, kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni pamojana usimamizi wa bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, mapato ya kodi kwa mwaka2017/2018 yanatarajiwa kufikia asilimia 13.0 ya Pato la Taifaikilinganishwa na asilimia 13.3 mwaka 2016/2017. Aidha, nakisiya bajeti inatarajia kufikia asilimia 2.1 mwaka 2017/2018ikilinganishwa na asilimia 1.5 mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni Uratibu wa Mipango yaMaendeleo ya Taifa; katika mwaka 2017/2018, Wizaraimeandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka2018/2019. Mpango huu ni wa tatu katika kutekeleza Mpangowa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Utekelezajiwa Mpango utasaidia kujenga msingi wa uchumi waviwanda ili kukuza uchumi na kuondoa umaskini. HivyoSerikali inaendelea kuandaa mazingira wezeshi ili kuhuishaushiriki wa sekta binafsi katika kugharamia utekelezaji wampango wa maendeleo.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara imekamilisha nakuchapisha Mkakati wa Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Maendeleo wa Miaka Mitano. Mkakati huo unatoamwongozo wa utekelezaji wa Mpango huo ambaoutaiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo2025. Mkakati unalenga maeneo yafuatayo:-

Viwanda vya nguo, ngozi, madawa, maeneomaalum ya kiuchumi, ukuaji wa miji na usimamizi wamaendeleo ya miji.

Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya ufuatiliaji wautekelezaji wa Miradi ya Kitaifa ya Maendeleo iliyobainishwakatika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano.Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Wizara za kisekta ilifanyaufuatiliaji wa miradi 29 katika Mikoa ya Morogoro, Shinyanga,Mwanza, Pwani, Iringa na Mbeya. Miradi iliyofuatiliwailijumuisha miradi ya sekta ya umma na binafsi na sekta zaviwanda, kilimo, uvuvi, maji, afya, elimu, mifugo, ujenzi namiundombinu.

Mheshimiwa Spika, malengo makuu ya ufuatiliajiyalikuwa kubainisha hatua halisi za utekelezaji wa miradihusika, changamoto na hatua stahiki za kuzitatua iliyazingatiwe katika maandalizi ya mpango wa mwaka wafedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, tatu, ni Uratibu wa Mikakati yaKupunguza Umaskini. Wizara imekamilisha taarifa ya mwanzoya Hali ya Umaskini na Malengo ya Maendeleo Endelevu yamwaka 2016/2017. Taarifa hii inabainisha mwelekeo wa haliya umaskini, changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo. Aidha,imeonesha viashiria vitakavyotumika na kubainisha wapitulipoanzia (baselines) ili kupima mafanikio katika utekelezajiwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Mwaka2030.

Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo inaonesha mafanikioyafuatayo:-

Wastani wa umri wa kuishi umeongezeka kutokamiaka 63.3 mwaka 2015 na kufikia miaka 64.4 mwaka 2017;

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka wastani wavifo 38 mwaka 2015 hadi kufikia vifo 34.5 kwa vizazi hai 1,000mwaka 2017. Pato la wastani la Mtanzania limeongezekakutoka Sh.1,918,931 mwaka 2015 na kufikia Sh.2,275,601mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 18.6. Kuongezekakwa umiliki wa samani katika kaya nao umeongezeka naupatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu, afya ya jamii,maji safi na salama, umeme na miundombinu ya barabaraumekuwa bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, tathmini ya hali ya umasikini nchiniiliyofanyika mwaka 2015/2016 kwa ushirikiano baina ya Ofisiya Taifa ya Takwimu na Benki ya Dunia ilionesha kuwaumaskini wa mahitaji ya msingi (basic need poverty)umeendelea kupungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/2012hadi asilimia 26.4 mwaka 2015/2016. Malengo ya Serikali nikupunguza umaskini hadi kufikia asilimia 12.7 mwaka wafedha 2025/2026.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ili kubainisha hali yaumaskini hususani wa kipato, Ofisi ya Taifa ya Takwimuikishirikiana na Benki ya Dunia hivi sasa inaendesha Utafiti waMapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (Household BudgetSurvey) kwa mwaka 2017/2018. Hatua iliyofikiwa ni ukusanyajiwa takwimu za mapato na matumizi ya kaya kwa miezi sitaya kwanza ya 2018 katika mikoa yote.

Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo tunatarajia kuwamatokeo rasmi ya hali halisi ya umaskini na hususan wa kipatokatika ngazi ya kitaifa, kimkoa na kiwilaya yatatolewa naOfisi ya Taifa ya Takwimu mwezi Machi, 2019. NiwaombeWaheshimiwa Wabunge wote kwamba katika kitabu changucha Hotuba ukurasa wa 13 sehemu hii ya Mikakati yaKupunguza Umaskini isomeke kama nilivyosoma sasa.

Mheshimiwa Spika, nne, Usimamizi wa Ukusanyaji waMapato ya Serikali, nikianza na Mapato ya Ndani. Katikamwaka 2017/2018 sera za mapato zililenga kukusanyamapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi trilioni 19.9ikijumuisha mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Aprili, 2018 jumla ya makusanyo ya ndani yakijumuishamapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa yalikuwa shilingitrilioni 14.8, sawa na asilimia 74 ya makadirio ya mwaka.

Mheshimiwa Spika, kati ya kiasi hicho, mapato ya kodiyalifikia shilingi trilioni 12.6, sawa na asilimia 74 ya lengo lamwaka la kukusanya shilingi trilioni 17.1. Mapato yasiyo yakodi yalifikia shilingi trilioni 1.78 sawa na asilimia 82 ya lengola mwaka la kukusanya shilingi trilioni 2.18; na mapato yaMamlaka za Serikali za Mitaa yalikuwa shilingi bilioni 437.6,sawa na asilimia 64 ya makadirio ya shilingi bilioni 687.3 kwamwaka.

Mheshimiwa Spika, vile vile, hadi kufikia Aprili 2018,Serikali ilikopa jumla ya shilingi trilioni 4.9 kutoka soko la ndanisawa na asilimia 80 ya shilingi trilioni 6.1 zilizotarajiwakukopwa kwa mwaka. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 4.12zilikopwa kwa ajili ya kulipia dhamana na hati fungani zaSerikali zilizoiva (rollover) na shilingi bilioni 832.3 zilikopwa ilikugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha,mikopo kutoka kwenye chanzo hiki, ilielekezwa kulipiasehemu ya madeni ya wakandarasi wa barabara, maji naumeme.

Mheshimiwa Spika, Misaada na Mikopo nafuu tokakwa Washirika wa Maendeleo. Hadi kufikia Aprili 2018 Serikaliimepokea kiasi cha shilingi trilioni 1.86 sawa na asilimia 47 yalengo la shilingi trilioni 3.9 na kati ya kiasi kilichopokelewa,shilingi bilioni 70.2 ni misaada na mikopo nafuu ya kibajeti,sawa na asilimia saba ya ahadi ya shilingi bilioni 941.26; shilingibilioni 180.52 ni mifuko ya pamoja ya kisekta sawa na asilimia33 ya ahadi ya shilingi bilioni 556.08 na shilingi bilioni 1,612.6kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 65 ya ahadiambayo ilikuwa ni shilingi trilioni 2.47.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na sekta,washirika wa maendeleo na wadau wengine ilifanikiwakuandaa na kukamilisha Mwongozo wa Ushirikiano waMaendeleo (Development Cooperation Framework) ambaouliidhinishwa na Serikali mwezi Agosti 2017. Mwongozo huu

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

umeanza kutekelezwa mwaka 2017/2018 na utadumu hadi2024/2025. Aidha, Wizara imeendelea kufuatilia na kutathminiutekelezaji wa programu na miradi ya maendeleoinayonufaika na fedha za nje ili kuhakikisha kwamba fedhahizo zinatumika kwa mujibu wa makubaliano kati ya Serikalina washirika wa maendeleo.

Mheshimiwa Spika, tano, ni Uandaaji na Usimamizi waUtekelezaji wa Bajeti ya Serikali. Katika uandaaji na usimamiziwa bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018, Wizara ilifanyauboreshaji wa mfumo wa uandaaji na usimamizi ya Bajeti yaSerikali (Central Budget Management System) ambaoumeanza kutumika rasmi katika uandaaji wa bajeti yamwaka 2018/2019. Pamoja na mambo mengine, mfumo huoutarahisisha utoaji na uchambuzi wa taarifa za mapato namatumizi na pia na utaondoa kabisa tatizo la uingizwajiwa takwimu za bajeti mara mbili kama ilivyokuwa kwenyemifumo iliyopita.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa nipamoja na:-

Kuendesha mafunzo ya mfumo wa CBMS kwamaofisa 246 kutoka kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemeana Sekretariati za Mikoa; Kuandaa, kuweka kwenye tovutiya Wizara, kuchapisha na kusambaza nakala 3,000 zaMwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti wa mwaka2018/2019; Ukamilishaji wa Vitabu vya Makadirio ya Matumiziya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Juzuu Na. I, II, III na IVambapo nakala 2,150 zilichapishwa na kuwasilishwa Bungenikwa ajili ya kujadiliwa na pia kusambazwa kwenye Wizara,Idara Zinazojitegemea na Sekretarieti za Mikoa na Wadauwengine; na Uandaaji wa Kijitabu cha Bajeti ya Serikali yamwaka 2017/2018 Toleo za Wananchi (Citizens Budget) kwalugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Mheshimiwa Spika, sita, ni Usimamizi na Udhibiti waMatumizi; katika mwaka 2017/2018, Wizara kupitia Idara yaMkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali imeendelea kufanyauhakiki wa madeni ya Serikali kama ifuatavyo:-

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Uhakiki wa madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF,PPF, PSPF, GEPF, LAPF na NHIF); Uhakiki wa madeni ya Mamlakaya Uchimbaji Visima (DDCA) uliofanyika katika Halmashaurimbalimbali za Mikoa ya Katavi, Morogoro, Arusha, Pwani naLindi ambapo kiasi cha shilingi Trilioni 1.1 kiliokolewa kutokanana uhakiki huo; na Uhakiki wa madeni ya Wizara, IdaraZinazojitegemea, Wakala za Serikali 61 na Sekretarieti za Mikoa26 umekamilika. Aidha, Wizara imefanya ukaguzi maalumkatika maeneo yafuatayo:-

Hospitali Teule ya Mvumi Dodoma; Mradi wa SELFMicrofinance Fund, kuchunguza ukwepaji wa kodi katikaBiashara ya vinywaji vikali; kukagua mfumo wa kukusanyamaduhuli na Wakala wa Usafiri wa Mwendo wa Haraka(DART) na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Mheshimiwa Spika, kutokana na kiasi kikubwaambacho kimeokolewa baada ya kufanya uhakiki, naombakusisitiza kuwa Wizara yangu itaendelea kuhakiki madeni yotekabla ya kuyalipa. Kama tungelipa madeni haya bilakujiridhisha tungekuwa tumepoteza fedha nyingi sana zawananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa chini ya Usimamizi na Udhibiti wa Fedha zaUmma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 19 hadi 24.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Malipo; katikamwaka wa fedha 2017/2018, Wizara imeendelea kuboreshausimamizi wa malipo kwa kuunganisha mfumo wa malipowa TISS katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mikoaya Lindi, Mtwara, Pwani, Kagera, Geita, Simiyu, Shinyanga,Mara, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Tabora na Kigoma.Aidha, mfumo wa TISS umeunganishwa katika Ofisi yaWaziri Mkuu (Fungu 25 na 37), Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa (Fungu 57), Jeshi la Polisi (Fungu 28), Jeshi laWananchi (Fungu 38), Jeshi la Kujenga Taifa (Fungu 39) nakuwapatia mafunzo Watumishi ili kuwawezesha kutumiamfumo huo.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Spika, vile vile, Wizara imesimika mfumowa malipo (EPICOR) kwenye Ubalozi wa Tanzania kuleNairobi-Kenya kwa lengo la kudhibiti matumizi nje ya bajeti.Kadhalika, Wizara imetoa mafunzo ya matumizi yaviwango vya kimataifa (IPSAS) kwenye uandaaji waHesabu kwa Wahasibu wa Wizara, Idara Zinazojitegemea naWakala, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali zaMitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma 650 na kuwezeshakuandaa Hesabu za Majumuisho kwa mwaka wa fedha2016/2017 kwa kutumia Viwango vya Kimataifa (IPSASAccrual Basis).

Mheshimiwa Spika, Deni la Serikali; Serikali imeendeleakusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo,Dhamana na Misaada, Sura 134. Mwezi Novemba 2017,Serikali ilifanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikalikwa kipindi kilichoishia Juni, 2017. Tathmini hiyo inaoneshakuwa deni ni himilivu kwa kipindi cha muda wa kati namrefu.

Mheshimiwa Spika, Uwiano wa Deni la Serikali kwaPato la Taifa ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo waasilimia 56; thamani ya sasa ya deni la nje pekee kwa patola Taifa ni asilimia 19.7 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia40; thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia81.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 150; na thamaniya sasa ya deni la nje kwa mapato ya ndani ni asilimia 117.1ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 250.

Mheshimiwa Spika, kazi ya viashiria hivyo vinne nikupima uwezo wa nchi kukopa. Viashiria vilivyobaki vinapimauwezo wa nchi kulipa deni. Kutokana na tathmini, ulipajiwa deni la nje kwa kutumia mapato ya ndani umefikiaasilimia 9.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20 na ulipajiwa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia13.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20. Kwa kuzingatiavigezo hivyo Tanzania bado ina uwezo wa kuendelea kukopaili kugharamia shughuli zake za maendeleo na pia ina uwezowa kulipa mikopo iliyoiva kwa kutumia mapato yake yandani na nje.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Spika, pamoja na uhimilivu huo wa deniSerikali imeendelea kuchukua tahadhari kwa kukopa kwenyevyanzo vyenye masharti ya gharama nafuu na kuhakikishakuwa mikopo hiyo inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleoitakayochochea ukuaji wa uchumi, ikiwemo ujenzi wamiundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege na ujenziwa mitambo ya kufua umeme.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali kwa kushirikiana nawadau mbalimbali kila robo mwaka inapitia viwango vyaDeni la Serikali ili kuhakikisha kuwa deni linaendelea kuwahimilivu. Vile vile, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali amekamilisha ukaguzi wa deni hilo na Serikaliinapitia taarifa hiyo kwa lengo la kuzingatia ushauriuliotolewa.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya malipo ya deni la Serikaliiko katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 26 hadi 28.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Mifumo ya Taarifaza Kifedha; katika mwaka 2017/2018, Wizara imeendelea nakazi ya kuboresha Mfumo wa kutolea taarifa za kulipiamishahara kwa watumishi wa umma kwa njia ya kielektroniki,ambapo mfumo wa kutolea taarifa za malipo ya mishaharaya watumishi wa umma na hati za mishahara (GovernmentSalary Slip Portal) umekamilika na kuanza kutumika mweziJulai, 2017. Watumishi wa umma wanaweza kupata hatiza mishahara kwa njia za kielektroniki mahali popotepalipo na mtandao. Aidha, maboresho hayayamepunguza gharama kubwa za usambazaji wa taarifaza mishahara.

Mheshimiwa Spika, pia Wizara imesimika mfumo wamakusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, (Governmentelectronic Payment Gateway - GePG) ambapo hadi sasataasisi 86 zimeunganishwa na kati ya hizo taasisi 51 zimeanzakukusanya maduhuli kwa njia ya kielektroniki.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Mali za Serikali; ilikuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa mali za Serikali,

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Wizara imeendelea kufanya uthamini wa mali katika Wizara,Idara na Wakala za Serikali. Hadi Aprili 2018, uthamini waardhi na majengo ya Serikali katika mafungu 48 ulifanyika ilikuwa na taarifa sahihi za mali za Serikali za mafungu hayo.Aidha, Wizara imefanya uhakiki maalum wa mali za watubinafsi zilizo chini ya uangalizi wa Serikali katika vituo 145 vyaPolisi Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuipunguziaSerikali mzigo wa kulipa fidia zinazotokana na upungufu wauangalizi na usimamizi wa mali hizo.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika katikausimamizi wa mali za Serikali ni kama inavyooneshwa katikakitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 31 mpaka32.

Mheshimiwa Spika, Ununuzi wa Umma; katika mwaka2017/2018, Wizara imetoa mafunzo kwa Maafisa Ununuzi naUgavi 75 juu ya matumizi ya mfumo wa uagizaji wamahitaji ya hati ya ununuzi (Local Purchase Order-LPO’s)kupitia Mfumo wa Malipo ya Serikali (Epicor); na kukamilishazoezi la tathmini ya Ufanisi wa Mfumo wa Ununuzi wa Ummana kuandaa mikakati ya utekelezaji wa matokeo yazoezi hilo.

Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwachini ya ununuzi wa umma, rufani za zabuni za umma,huduma ya ununuzi Serikalini na kupitia Bodi ya Watalaamwa Ununuzi na Ugavi ni kama inavyooneshwa katika kitabucha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 32 mpaka 35.

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi wa Hesabu za Serikali; Ofisiya Taifa ya Ukaguzi katika kutekeleza majukumu yake kwamujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania imefanya ukaguzi wa mapato na matumizi yaSerikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017. Ofisiilifanya ukaguzi wa hesabu za Wizara na Idara za SerikaliZinazojitegemea 55, Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, Wakalaza Serikali 37, Mifuko Maalum 15, Taasisi nyingine za Serikali 60na Balozi za Tanzania nje ya nchi 40. Aidha, ukaguzi ulifanyikakwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 na Mashirika yaUmma 105.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine za ukaguzi wahesabu za Serikali zilizofanyika ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 35mpaka 37.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Mashirika na Taasisiza Umma; katika mwaka 2017/2018, Ofisi ya Msajili wa Hazinaimefanya tathmini na uchambuzi wa mikataba ya utendajiKazi 31 iliyoingiwa baina ya Msajili wa Hazina na Wenyevitiwa Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma katika mwaka wa2016/2017.

Mheshimiwa Spika, lengo la zoezi hilo ni kupimautekelezaji wa mikataba hiyo kwa mujibu wa viashiria vyamafanikio, ambapo mambo ya msingi yanayozingatiwakatika tathmini ni pamoja na utawala bora, usimamizi wafedha, usimamizi wa rasilimali watu na huduma kwa mteja.Katika zoezi la mikataba ya utendaji, kigezo ni taasisi husikakuwa na bodi hai na kuwa na bajeti iliyoidhinishwa. Matokeoya tathmini yanaonesha wastani wa taasisi kufanya vizuri kwaasilimia 70.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msaji l i wa Hazinaimeendelea kufanya uchambuzi wa taasisi na mashirikaya umma ambayo majukumu yao kwa namna mojaau nyingine yanafanana kwa lengo la kuunganishataasisi hizo ili kuongeza tija na kupunguza gharama zauendeshaji.

Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwakatika kusimamia mashirika na taasisi za umma ni kamainavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 37 mpaka39.

Mheshimiwa Spika, Mafao ya Wastaafu na Mirathi;katika mwaka 2017/2018, Serikali ilitenga kiasi cha shilingitrilioni 1.0 kwa ajili ya kulipia michango ya mwajiri kwenyemifuko ya hifadhi ya jamii. Hadi kufikia Aprili, 2018 kiasi chashilingi bilioni 716.19 sawa na asilimia 71 kilitumika kulipamichango ya mwajiri kwa watumishi wa umma.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Spika, aidha, nitumie fursa hii kuiagizaMifuko ya Hifadhi ya Jamii iandikishe wanachama wake,kuwapa vitambulisho vya uanachama na kutunza vizurina kwa usahihi taarifa za uchangiaji kwa kipindi chotecha utumishi wa wanachama ili kuwaondoleausumbufu siku za kustaafu kwao kama ilivyoelekezwa naMiongozo ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhiya Jamii.

Mheshimiwa Spika, vile vile, nawakumbushawatumishi wa umma wawe na tabia ya kukagua taarifa zamadaraja ya mishahara, makato ya lazima na yale yasiyo yalazima kutoka kwenye mishahara yao na kutoa taarifa kwawakati kwa mamlaka husika ili kama kuna makato hayakosawasawa mamlaka husika zichukue hatua za kurekebishamapema na kuisaidia Serikali kuepuka tozo zinazowezakutozwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na taasisi nyingine zafedha.

Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwakatika kusimamia mafao ya wastaafu na mirathi ni kamailivyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 39 mpaka 41.

Mheshimiwa Spika, Udhibiti wa Utakatishaji FedhaHaramu na Ufadhili wa Ugaidi; katika mwaka 2017/2018,Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidikimeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti waFedha Haramu na kufanya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kupokea na kuchambuataarifa 254 za miamala shuku inayohusu fedha haramu naufadhili wa ugaidi na kuwasilisha taarifa za kiintelijensia 32kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwaajili ya uchunguzi. Aidha, katika kujenga uwezo wa watumishi,maafisa wa kitengo walipata mafunzo ya namna bora yauchambuzi na upembuzi wa taarifa za miamala shuku katikaKituo cha Kudhibiti Fedha Haramu (Financial IntelligenceCentre) cha Afrika ya Kusini na Maafisa wanne (4)walihudhuria mafunzo ya Financial Action Task Force

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Standards yaliyofanyika nchini Korea Kusini ambayo ni muhimukatika nyanja ya udhibiti wa fedha haramu na ufadhili waugaidi.

Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwakatika kusimamia utekelezaji wa Udhibiti wa Fedha Haramuna Ufadhili wa Ugaidi ni kama ilivyooneshwa katika kitabucha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 41 mpaka 43.

Mheshimiwa Spika, Ubia kati ya Sekta ya Umma naSekta Binafsi (PPP). Katika mwaka 2017/2018, Wizaraimeendelea kuratibu na kuchambua miradi ya ubia kati yasekta ya umma na sekta binafsi na kuishauri Serikali juu yautekelezaji wa miradi hiyo. Aidha, kulingana na Sheriaya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura103, uchambuzi wa miradi ya ubia hupitia hatua tatuzifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, mamlaka za utekelezajikuwasilisha andiko la awali la mradi kwa ajili ya uchambuzi;pili, mamlaka kuandaa taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu;na tatu mamlaka ya utelekezaji wa miradi ikishirikiana naMshauri Mwelekezi huandaa na kuwasilisha taarifa yaupembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, Wizara hufanya uchambuzi wataarifa hizo kwa kuangalia, pamoja na mambo menginemaeneo makuu matatu. Kwanza, ni uhamishaji wa mianyahasi ya mradi kwenda kwa sekta binafsi; pili ni uwezo waSerikali kugharimia mradi; na tatu ni manufaa ya mradi kwaSerikali na wananchi kwa ujumla. Endapo mradi unakidhivigezo utaidhinishwa na Kamati ya Wataalam wa PPP kwaajili ya kuendelea na hatua ya kumpata mbia.

Mheshimiwa Spika, Wizara imefikia hatua mbalimbaliza uchambuzi wa miradi itakayotekelezwa kwa utaratibuwa PPP. Upembuzi yakinifu wa mradi wa uzalishaji wamadawa muhimu na vifaa tiba wa Bohari Kuu ya Madawa(MSD) umekamilishwa na kuwasilishwa kwenye kitengo chaubia kwa ajili ya hatua za uidhinishaji.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimiwa Spika, mradi wa kujenga na kuendeshavyuo 10 vya VETA kwa utaratibu wa PPP katika Mikoa ya Dares Salaam, Arusha, Manyara, Tabora na Shinyanga. Wizaraimefanya uchambuzi wa Taarifa ya Upembuzi Yakinifu nakuwasilisha kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojiamapendekezo yanayotakiwa kuzingatiwa ili mradi uwe natija kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Barabara ya Tozo kutokaDar es Salaam hadi Chalinze. Taarifa ya upembuzi yakinifuwa mradi imefanyiwa uchambuzi ambapo Wizara imetoaidhini yenye masharti (Conditional Approval) ya kutekelezakabla ya kuendelea na hatua ya kumpata mbia.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Uendeshaji wa Hudumaya Usafiri jijini Dar es Salaam awamu ya kwanza. Zabuni kwaajili ya ununuzi wa mtoa huduma wa kudumu, mkusanyajiwa mapato na mwendesha Mfuko zil itangazwa nawazabuni wamepatikana; na Wizara imekamilishauchambuzi wa andiko la awali la mradi wa Mradi waMwambani Port lililowasilishwa na Mamlaka ya BandariTanzania; hatua inayoendelea ni maandalizi ya upembuziyakinifu.

Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwakatika kusimamia utekelezaji wa PPP zimeoneshwa kwenyekitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 44 mpaka 46.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi na Uratibu wa Taasisina Mashirika ya Umma Chini ya Wizara. Kama nilivyoelezahapo awali, Wizara yangu inaratibu na kusimamia mashirikana taasisi za umma 36. Utekelezaji wa majukumu ya taasisina mashirika haya kwa mwaka 2017/2018 ni kamailivyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu ukurasa wa47 mpaka 78.

Mheshimiwa Spika, aidha, utekelezaji wa miradi yamaendeleo chini ya Wizara kwa mwaka 2017/2018yameoneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 79 mpaka 81.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Spika, Changamoto na HatuaZilizochukuliwa; pamoja na mafanikio yaliyopatikana katikautekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango,changamoto zilizojitokeza ni pamoja na ukwepaji wa kodi,kuchelewa kupatikana kwa misaada na mikopo ya mashartinafuu pamoja na mikopo ya kibiashara kwa ajil i yakugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, uelewamdogo wa wananchi juu ya dhana ya utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi ambayo ni pana na inabadilikakwa kasi. Pia baadhi ya wawekezaji kutelekeza maliwalizouziwa na Serikali wakati wa zoezi la Ubinafsishaji, nauelewa mdogo wa dhana ya ubia kati ya Sekta ya Ummana Sekta Binafsi. Hatua zilizochukuliwa ni zifuatazo:-

Kwanza, ni kutekeleza mkakati wa ulipaji kodi kwahiari na kuendelea kuboresha makusanyo ya mapato yasiyoya kodi kwa kujenga mifumo ya kielektroniki ya ukusanyajiwa mapato; Kuendelea kuelimisha wadau mbalimbalikupitia makongamano, mikutano na warsha kuhusu dhanaya utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi;kuendeleza mazungumzo na Washirika wa Maendeleokuhusu njia mpya za kutoa na kupokea misaada na mikopo;Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imeongeza nguvukatika kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa wawekezaji wote ilikuhakikisha wanaendesha viwanda na mali walizouziwa kwakuzingatia masharti ya mikataba ya mauzo; na Kuendeleakutoa mafunzo kuhusu ubia kati ya sekta ya umma na sektabinafsi kwa watumishi wa umma na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nieleze malengo yampango na bajeti kwa mwaka 2018/2019. Mpango na Bajetiya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka ujao wa fedhaumeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya2025, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030,Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Sheria yaBajeti Na.11 ya Mwaka 2015, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(2015 – 2020), Hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati wa Uzinduziwa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,pamoja na masuala mtambuka kama vile jinsia, watu wenyeulemavu, mazingira, UKIMWI, makundi mengine yaliyo katika

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

mazingira hatarishi na masuala ya lishe kwa jamii pamojana maelekezo na ahadi zilizotolewa kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Utekelezaji waMajukumu ya Wizara. Kwanza kwa upande wa kusimamiautekelezaji wa sera za uchumi jumla. Katika kipindi chamwaka wa 2018/19 shabaha zitakuwa ni zifuatavyo:-

(i) Pato la Taifa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka2018 kutoka ukuaji halisi wa asilimia 7.1 mwaka 2017;

(ii) Mfumuko wa bei kuendelea kubaki katikawigo wa tarakimu moja;

(iii) Mapato ya ndani kufikia asilimia 15.8 ya Pato laTaifa mwaka 2018/2019 kutoka matarajio ya asilimia 15.3mwaka 2017/2018 na asilimia 15.6 mwaka 2016/2017;

(iv) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.6 ya Patola Taifa mwaka 2018/2019 kutoka matarajio ya asilimia 13mwaka 2017/2018 na asilimia 13.3 mwaka 2016/2017; na

(v) Nakisi ya bajeti kufikia asilimia 3.2 ya Pato laTaifa mwaka 2018/2019 kutoka asilimia 2.1 mwaka 2017/2018na asilimia 1.5 mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Uratibu wa Mipango ya Maendeleoya Taifa; kutokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Tume yaMipango na Wizara ya Fedha, imebidi kuupitia muundo waWizara ili uweze kuyaingiza mabadiliko haya ili kutoathiriutekelezaji wa majukumu pamoja na maslahi ya watumishikwa ujumla. Muundo wa Wizara uko katika hatua za mwishoza kuidhinishwa na mamlaka husika, ambapoimependekezwa iundwe Divisheni ya Mipango ya Maendeleoya Taifa itakayoongozwa na Kamishna na kuwa na kifunguchake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo katika mwaka 2018/2019,shughuli za kipaumbele zitakazotekelezwa katika uratibu waMipango ya Maendeleo ya Taifa ni pamoja na:

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa waMwaka 2019/2020; Kufuatilia utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019; Kufanya tathminiya muda wa kati katika utekelezaji wa Mpango waMaendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano; Kukamilisha uundwajiwa mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa miradi ya kitaifaya maendeleo; na Kufuatilia matumizi ya Mwongozo waUsimamizi wa Uwekezaji wa Umma (Public InvestmentManagement Operational Manual).

Mheshimiwa Spika, Uratibu wa Mikakati ya KupunguzaUmaskini; katika mwaka ujao wa fedha Wizara itaendeleakusimamia na kuratibu utekelezaji wa juhudi za kupunguzaumaskini ikiwemo:-

Kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji waJitihada za Kuondoa Umaskini nchini (Poverty MonitoringSystem); Kufuatilia utekelezaji wa malengo yaliyoainishwakatika mipango ya kitaifa na kisekta na Malengo yaMaendeleo Endelevu (SDGs) ya mwaka 2030 na programuzinazolenga kuondoa umaskini katika maeneo ya vijijini namijini; Kufanya uchambuzi wa kina juu ya utafiti wa mapatona matumizi ya kaya ya mwaka 2017/2018; Kutoa mafunzokwa Maafisa Mipango na Maendeleo ya Jamii wa Mamlakaya Serikali za Mitaa kuhusu jitihada za kupambana naumaskini na kutunza mazingira ili kuweza kujumuisha katikamipango na bajeti zao.

Mheshimiwa Spika, mipango mingine katika uratibuwa Mkakati wa Kupunguza Umaskini iko kwenye hotubayangu kuanzia ukurasa wa 87 hadi 89.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Ukusanyaji waMapato ya Serikali. Katika kuboresha ukusanyaji wa mapatoya ndani kwa mwaka ujao wa fedha, Wizara imepangakutekeleza yafuatayo:-

Kusimamia sera za fedha na za kibajeti zinazolengakuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara; Kuhamasishaulipaji kodi kwa hiari kwa kuimarisha mkakati shirikishi wa

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

mawasiliano na walipa kodi na kuboresha utaratibu wautozaji kodi; Kujenga uwezo wa watumishi ili kukabiliana natatizo la uhamishaji faida (Transfer Pricing) unaofanywa nakampuni zenye mitandao ya kimataifa kwa lengo la kukwepaau kupunguza kodi; Kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji waulipaji kodi kupitia mfumo wa vitalu vya walipakodi;Kusimamia zoezi la uunganishaji wa Wizara, Idara,Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma kwenye Mfumowa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ilikuboresha ukusanyaji na kudhibiti upotevu wa mapatoya Serikali; na kuongeza kasi ya uthaminishaji wamajengo ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi yamajengo.

Mheshimiwa Spika, mikakati mingine iko katikahotuba yangu ukurasa wa 89 hadi 90.

Mheshimiwa Spika, Mikopo na Misaada; katikamwaka 2018/2019, Wizara itaendelea na uratibu waupatikanaji wa fedha za misaada na mikopo nafuu kutokakwa washirika wa maendeleo kwa ajili ya kugharamiaprogramu na miradi ya maendeleo mbalimbali nchini.Washirika wa maendeleo wameahidi kuchangia Bajeti yaSerikali kiasi cha shilingi bilioni 2,676.64. Kati ya fedhahizo, shilingi bilioni 545.76 ni kwa ajili ya misaada na mikoponafuu ya kibajeti (General Budget Support), shilingi bilioni125.86 kwa ajili ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta nashilingi bilioni 2,005.02 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zil izopangwakutekelezwa ni pamoja na kukamilisha mpango kazi wakutekeleza Mwongozo Mpya wa Ushirikiano (DevelopmentCooperation Framework); na Kukagua miradi inayofadhiliwana washirika wa maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Uandaaji na Usimamizi waUtekelezaji wa Bajeti ya Serikali. Katika mwaka ujao wa fedhaWizara imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemokuendelea kuboresha mfumo mpya wa uandaaji na

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

usimamizi wa bajeti ya Serikali ili kurahisisha utoaji wa mgaowa fedha za matumizi kila mwezi na kuendesha mafunzo yamfumo huo.

Mheshimiwa Spika, kufanya marekebisho, kuchapishana kusambaza nakala 2,200 vitabu vya Makadirio yaMatumizi ya Serikali ya mwaka 2018/2019 kamayalivyopitishwa na Bunge, kuchapisha na kusambazaMwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka2019/2020, Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali za kilaRobo Mwaka, vitabu vya Makadirio ya Matumizi ya Serikaliya mwaka 2019/2020 na kuviwasil isha Bungeni nakuvisambaza kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarietiza Mikoa kwa wadau wengine.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zil izopangwakufanyika ziko katika hotuba yangu ukurasa wa 92 hadiukurasa wa 93.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi na Udhibiti wa Matumiziya Serikali; katika mwaka 2018/2019, Wizara itaendeleakudhibiti matumizi ya fedha za umma kwa kufanya ufuatiliajiwa uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya ukaguzi wandani i l iyotolewa na Wizara na kutoa mafunzo kwaWakaguzi wa Ndani katika maeneo ya ukaguzi wa miradi,ukaguzi wa kiufundi, usimamizi wa vihatarishi, mfumo wausimamizi wa kazi za ukaguzi na mfumo wa kusimamiautekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, mipango mingine ambayo Wizarainatarajia kutekeleza katika usimamizi wa udhibiti wafedha za umma iko katika hotuba yangu ukurasa wa 94mpaka 95.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Malipo; katikamwaka ujao wa fedha, wizara imepanga kusimamia mfumowa udhibiti wa matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamojana uanzishwaji wa Akaunti Jumuifu (Treasury Single Account)kwa lengo la kuboresha mfumo wa matumizi ya umma ili

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

kuiongezea Serikali uwezo wa kugharamia shughuli zakekwa wakati. Aidha, Wizara itaendelea na usimikaji nausimamizi wa mifumo ya malipo ya kieletroniki ili kuondoaucheleweshaji wa malipo kwa wadau mbalimbali wakiwemowastaafu, watoa huduma kwa Serikali pamoja na watumishiwa umma. Vile vile Wizara itaendelea na uunganishaji wamfumo wa malipo kwenye Balozi saba ili kudhibiti matumizinje ya bajeti.

Mheshimiwa Spika, Deni la Serikali; katika mwaka ujaowa fedha, Serikali itahakikisha kuwa deni la Serikalilinaendelea kuwa himilivu na kutokuwa mzigo kwa uchumiwetu na kuendelea kuwa fursa na kichocheo cha maendeleokwa nchi yetu. Aidha, Serikali itaendelea kukopa kwauangalifu kwa kuzingatia masharti nafuu. Mikopo hiyoitatumika kwenye miradi ya maendeleo ya kuchochea ukuajiwa uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mchango wa Mwajiri KwenyeMifuko ya Hifadhi ya Jamii; Wizara itaendelea kuwasilisha kwawakati michango ya kisheria ya mwajiri ya kila mwezi kwaajili ya watumishi wa umma kwenye mfuko mpya wa hifadhiya jamii utakaochukua nafasi ya mifuko ya hifadhi ya jamiiiliyounganishwa ya PSPF, GEPF, LAPF na PPF pamoja na mifukoambayo haitaunganishwa ya NSSF, ZSSF, WCF na Bima ya Afya.

Mheshimiwa Spika, natumia fursa hii kuwasisitizaMaafisa Utumishi wote wanaohusika na kuingiza taarifa zawatumishi wa umma kwenye mfumo wa kompyuta wakutunza taarifa za watumishi wa umma, waingize taarifa zawatumishi kwa ukamilifu na kwa usahihi ili uwasilishaji wamichango ya mwanachama na mwajiri kwenye Mifuko yaHifadhi ya Jamii iwe kamili na sahihi kwa kipindi chote chautumishi na hatimaye kurahisisha malipo ya mafao, penshenina mirathi wakati wa hitimisho la utumishi wa umma ilikuwaondolea usumbufu watumishi wa umma walioitumikianchi yao kwa weledi na uaminifu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Mifumo ya Taarifaza Kifedha; katika mwaka 2018/2019, Wizara imepanga

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

kusimamia na kuboresha uendeshaji na utumiaji wamfumo wa taarifa za mishahara ya watumishi wa umma(Government Salaries Payment Platform) kwa kuunganishamfumo huo na taasisi za kibenki na mfumo wa penshenikwa ajili ya urahisishaji wa huduma za mikopo napensheni.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara itaendeleakuunganisha taasisi 260 katika mfumo wa kukusanya mapatoyasiyo ya kodi (Government Electronic Payment GatewaySystem) ili kuweza kufanikisha ukusanyaji wa maduhuli yaSerikali. Vile vile Wizara itaunganisha mifumo 10 yakielektroniki ya taarifa za fedha kwa lengo la kuiwezeshamifumo iweze kubadilishana taarifa.

Mheshimiwa Spika, Usimamizi wa Mali za Serikali;katika mwaka 2018/2019, Wizara imepanga kufanya kaguziza mali za Serikali katika Balozi kumi, kufanya kaguzi maalumna kutoa elimu ya utumiaji na utunzaji bora wa mali katikataasisi mbalimbali za Serikali ili kuepusha hasara zinazowezakuzuilika.

Mheshimiwa Spika, Ununuzi wa Umma; katika mwakawa fedha wa 2018/2019, Wizara imepanga kufanyayafuatayo:-

Kukamilisha uandaaji na kuzindua Sera ya Ununuzi waUmma pamoja kuanza utekelezaji wa sera hiyo; Kukusanyamaoni ya wadau kuhusu changamoto zinazowakabili katikautekelezaji wa Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma kwalengo la kuzifanyia marekebisho pale itakapohitajika;Kuwajengea uwezo Maafisa Ununuzi na Ugavi Serikalini juuya matumizi ya mwongozo wa utekelezaji wa shughuli zaununuzi na ugavi; Kuendesha mafunzo kwa Maafisa Ununuzina Ugavi kuhusu matumizi ya mfumo wa malipo waEPICOR katika ununuzi; Kuandaa mpango kazi wausimamizi wa ununuzi wa umma katika Serikali Kuu naMamlaka ya Serikali za Mitaa; na Kutekeleza mapendekezoya taarifa ya tathmini ya ufanisi wa mfumo wa ununuziwa umma.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zil izopangwakufanyika katika eneo hili ziko kwenye hotuba yangu ukurasawa 98 mpaka 101.

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi wa Hesabu za Serikali;katika mwaka ujao wa fedha Ofisi ya Taifa ya Ukaguziimelenga kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumizi yaSerikali kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazikwenye matumizi ya rasilimali za umma. Ili kufikia malengohayo, ofisi imepanga kutekeleza vipaumbele vinane kamaifuatavyo:-

Kufanya ukaguzi wa mafungu ya bajeti za Wizara,Idara zinazojitegemea, wakala na Taasisi za Serikali,Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Mashirikaya Umma na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa nawahisani.

Kufanya ukaguzi wa sekta ya gesi, mafuta na madini,kufanya maboresho ya mfumo wa ukaguzi kwa kutumiaTEHAMA na kukagua ukusanyaji wa mapato ya kodi nayasiyo ya kodi. Aidha, ofisi imelenga kufanya ukaguzi wakiufanisi na kaguzi maalum katika maeneoyatakayoainishwa.

Pia kuwajengea wakaguzi uwezo wa kufanya ukaguzikatika maeneo mapya ya ukaguzi kwenye sekta ya gesi asiliana mafuta, sekta ya madini, sekta mtandao na katika uhalifuwa kifedha kwa kutumia mtandao (Financial crimesauditing). Vile vile, ofisi itaendelea na ujenzi wa majengo yaOfisi za Ukaguzi katika Mikoa ya Rukwa na Mara.

Mheshimiwa Spika, kazi nyingine ambazo zitafanyikakwa upande wa usimamizi wa mashirika na taasisi za ummalakini pia upande wa mafao ya wastaafu na mirathi, upandewa udhibiti wa utakatishaji wa fedha haramu, Tume yaPamoja ya Fedha lakini pia upande wa PPP zote zimeelezwakwenye kitabu cha hotuba yangu; na naomba yote yaliyopokwenye kitabu cha hotuba yapokelewe kwenye Taarifa Rasmiza Bunge (Hansard).

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Mheshimiwa Spika, Makadirio ya Mapato na Maombiya Fedha kwa mwaka 2018/2019; mwaka ujao wa fedhawizara inakadiria kukusanya maduhuli shilingi bilioni 597.8kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauzoya nyaraka za zabuni, kodi za pango na mauzo ya leseni zaudalali.

Mheshimiwa Spika, Maombi ya Fedha; Wizara yaFedha na Mipango imepanga kutumia kiasi cha jumla yashilingi bilioni 12,058.71 kwa Mafungu yote Nane. Kati ya fedhahizo, shilingi bilioni 10,763.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaidana shilingi bilioni 1,295.21 ni kwa ajili ya matumizi yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaidayanajumuisha shilingi bilioni 65.76 kwa ajili ya mishahara;shilingi bilioni 693.26 kwa ajili ya matumizi mengineyo;na shilingi bilioni 10,004.48 ni malipo ya deni la Serikalina michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Aidha,katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi bilioni1,266.03 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 29.18 ni fedhaza nje.

Mheshimiwa Spika, Maombi ya Fedha; Fungu 50 –Wizara ya Fedha na Mipango. Kwenye Fungu hili Wizarainaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Matumizi ya kawaida – Sh.57,022,927,000 ambapomishahara ni shilingi bilioni 7.58 na matumizi mengineyoshilingi bilioni 49.44. Miradi ya maendeleo Sh.28,790,817,000.Kati ya hizo shilingi bilioni 19.64 ni fedha za ndani na fedha zanje shilingi bilioni 9.15.

Mheshimiwa Spika, Fungu 21 – Hazina. Wizarainaomba kuidhinishiwa fedha kwa ajili ya Fungu hili kamaifuatavyo:-

Matumizi ya kawaida Sh. 531,890,056,000. Kati ya fedhahizo shilingi bilioni 21.47 ni mishahara, matumizi mengineyoshilingi bilioni 510.42.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Spika, upande wa miradi yamaendeleo Shilingi bilioni 1,247.61, ambapo fedha zandani ni bilioni 1,236.19 na fedha za nje ni shilingi bilioni11.42.

Mheshimiwa Spika, Fungu 22 – Deni la Taifa. KwenyeFungu hili kwa mwaka ujao wa fedha, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaidaSh.10,013,706,140,000 ambapo mishahara ni shilingi bilioni9.23 na matumizi mengineyo Shilingi bilioni 10,004.48.

Mheshimiwa Spika, Fungu 23 – Mhasibu Mkuu waSerikali. Katika Fungu hili, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasicha fedha kama ifuatavyo:-

Matumizi ya kawaida Sh.46,725,409,000. Kati ya fedhahizo mishahara shilingi bilioni 7.91, matumizi mengineyoshilingi bilioni 38.82. Kwa upande wa miradi yamaendeleo Sh.3,200,000,000 kati ya fedha hizo shilingi2,000,000,000 ni fedha za ndani na fedha za nje ni shilingibilioni 1.2.

Mheshimiwa Spika, Fungu namba 7 – Ofisi ya Msajiliwa Hazina. Kwa ajili ya fungu hili, matumizi ya kawaidatunaomba Sh.54,592,065,000; kati ya fedha hizi mishahara nibilioni 2.36 na matumizi mengineyo ni shilingi bilioni 52.23.Miradi ya Maendeleo, Sh.1,650,000,000 ambapo fedha zandani ni shilingi bilioni moja na fedha za nje ni shilingi bilioni0.65

Mheshimiwa Spika, Fungu namba 10 – Tume yaPamoja ya Fedha; katika Fungu hili tunaomba Bunge lakoTukufu lituidhinishie matumizi ya kawaida Sh.2,155,075,000ambapo kati ya hizo mishahara ni bilioni 0.57 na matumizimengineyo ni shilingi bilioni 1.58.

Mheshimiwa Spika, Fungu namba 13 – Kitengo chaKudhibiti Fedha Haramu. Katika fungu hili kwa mwaka ujao

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

wa fedha tunaomba matumizi ya kawaida Bunge lakolituidhinishie Sh.2,015,586,000 na miradi ya maendeleo –Sh.248,363,000.

Mheshimiwa Spika, Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.Kwa fungu hili kwa mwaka ujao wa fedha tunaombakuidhinishiwa matumizi ya kawaida Sh.55,394,216,000ambapo mishahara ni bilioni 16.65 na matumizi mengineyoshilingi bilioni 38.75. Upande wa miradi ya maendeleotunaomba Sh.13,712,092,000 ambapo kati ya fedha hizoshilingi bilioni 7.20 ni fedha za ndani na bilioni 6.51 ni fedhaza nje.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hiikuzishukuru nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifaambayo kwa namna moja ama nyingine yamesaidia katikautekelezaji wa bajeti ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kuwashukurusana wafanyakazi na wananchi wote ambao wameendeleakulipa kodi kwa hiari na pia kushiriki katika ujenzi wa Taifaletu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa napendakuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizarawww.mof.go.tz.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Hoja imetolewana imeungwa mkono, tunakushukuru sana MheshimiwaWaziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpangokwa hotuba yako hiyo nzuri.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

HOTUBA YA MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB.), WAZIRI WAFEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGOKWA MWAKA 2018/19 – KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 TANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifailiyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa Hojakwamba, Bunge lako sasa lipokee na kujadili mapitio yautekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha naMipango kwa mwaka wa fedha 2017/18 pamoja naMakadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka ujao wafedha 2018/19.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuruMwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kusimama mbele yaBunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Fedha naMipango kwa mwaka wa fedha 2018/19. Aidha, napendanitumie fursa hii kuwapongeza Mhe. Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb.),Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuliongoza Taifa letu kwa ujasiri na uzalendo wa hali ya juu.Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema, hekima nabusara katika kuliongoza Taifa letu.

3. Mheshimiwa Spika, napenda pia kukushukuruwewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwakuendesha vema majadiliano ya mapendekezo ya bajeti zaWizara mbalimbali kwa mwaka 2018/19. Aidha, napendakumpongeza Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia, (Mb.) kwakuchaguliwa tena pamoja na Makamu Mwenyekiti mpyaMhe. Jitu Vrajlal Soni (Mb.). Aidha, nawapongeza nakuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti kwamaoni, ushauri na mapendekezo waliyotoa ambayoyamesaidia sana katika kuboresha Mpango na Bajeti yaWizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2018/19.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

4. Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hiikuwapongeza Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro - Mbunge waJimbo la Songea Mjini, Mhe. Justin Monko – Mbunge waSingida Kaskazini, Mhe. Dkt. Stephen Kiruswa - Mbunge waJimbo la Longido, Mhe. Dkt. Godwin Mollel - Mbunge waJimbo la Siha na Mhe. Maulid Mtulia - Mbunge wa Jimbo laKinondoni kwa kuchaguliwa kuwakilisha Wananchi wamajimbo yao katika Bunge lako Tukufu. Aidha, natoa polekwa Bunge lako Tukufu kwa kuwapoteza Mhe. LeonidasGama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Mhe.Kasuku Samson Bilago aliyekuwa Mbunge wa Jimbo laBuyungu. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahalipema peponi, Amina.

5. Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoeshukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. AshatuKachwamba Kijaji - Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri waFedha na Mipango, kwa ushirikiano anaonipatia katikakuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedhana Mipango unafanikiwa. Aidha, nawashukuru Bw. DotoJames - Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, NaibuMakatibu Wakuu Bibi Amina Kh. Shaaban, Dkt. Khatibu M.Kazungu na Bi. Susan Mkapa kwa kusimamia vizuri shughuliza kila siku za kiutendaji za Wizara yangu. Pia napendakumpongeza kwa dhati Prof. Florens Luoga - Gavana mpyawa Benki Kuu ya Tanzania na kumshukuru yeye pamoja naBw. Charles Kichere - Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya MapatoTanzania na Dkt. Albina Chuwa – Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Taifa ya Takwimu, kwa kusimamia kwa weledi taasisi nyetiwalizokabidhiwa. Nawashukuru pia, Makamishna,Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara,Wakuu wa Vitengo na wafanyakazi wote wa Wizara, kwakutimiza wajibu wao vema wa kuwatumikia Watanzania.

6. Mheshimiwa Spika, hotuba yangu imejikitakatika maeneo makuu mawili yafuatayo: Kwanza, ni Mapitioya utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2017/18 napili, Malengo na Maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha2018/19.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

2.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NABAJETI KWA MWAKA 2017/18

7. Mheshimiwa Spika, Wizara imetekelezamajukumu yake kupitia mafungu tisa ya kibajeti pamoja naTaasisi na Mashirika 36 yaliyo chini yake (Jedwali Na. 1 ukurasa136). Mafungu hayo ni Fungu 50-Wizara ya Fedha na Mipango,Fungu 21-Hazina, Fungu 22-Deni la Taifa, Fungu 23-Idara yaMhasibu Mkuu wa Serikali, Fungu 10-Tume ya Pamoja yaFedha, Fungu 13-Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu,Fungu 7- Ofisi ya Msajili wa Hazina, Fungu 66-Tume ya Mipangona Fungu 45-Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

8. Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara yaFedha na Mipango pamoja na muhtasari wa mapato namatumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18 ni kamainavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 4 hadi ukurasa wa 9.

2.1 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA MWAKA2017/18

9. Mheshimiwa Spika, naomba sasa kutoataarifa mbele ya Bunge lako Tukufu kuhusu utekelezaji wamajukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2017/18 ambayo yameainishwa katika hotuba yangu kuanziaukurasa wa 10 hadi ukurasa wa 81.

2.1.1 Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla

10. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumuhili, Wizara imejikita katika kuhakikisha kuwa malengo yaukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, na mapato na matumiziya Serikali yanafanikiwa. Katika mwaka 2017, kasi ya ukuajiwa uchumi imeendelea kuwa ya kuridhisha na kufikia wastaniwa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa wastani waasilimia 7.0 mwaka 2016. Ukuaji huo ulichangiwa na kasikubwa ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika sekta yamadini na uchimbaji mawe (asilimia 17.5), sekta ya maji

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

(asilimia 16.7), sekta ya uchukuzi na uhifadhi mizigo (asilimia16.6) na sekta ya habari na mawasiliano ambayo ilikua kwaasilimia 14.7.

11. Mheshimiwa Spika, wastani wa mfumuko wabei kwa mwaka 2017 ulikuwa asilimia 5.3 na umeendeleakupungua hadi kufikia asilimia 3.8 mwezi Aprili, 2018.Kupungua kwa mfumuko wa bei kulichangiwa zaidi nakuongezeka kwa uzalishaji wa chakula, utulivu wa thamaniya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kigeni, kuimarikakwa uzalishaji wa umeme, utekelezaji thabiti wa sera zafedha, urari wa malipo, kuongezeka kwa akiba ya fedha zakigeni pamoja na usimamizi wa bajeti ya Serikali. Mapato yakodi kwa mwaka 2017/18 yanatarajia kufikia asilimia 13.0 yaPato la Taifa ikilinganishwa na asilimia 13.3 mwaka 2016/17.Aidha, nakisi ya bajeti inatarajia kufikia asilimia 2.1 mwaka2017/18 ikilinganishwa na asilimia 1.5 mwaka 2016/17.

2.1.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa

12. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wamwaka 2018/19. Mpango huu ni wa tatu katika kutekelezaMpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano(2016/17-2020/21). Utekelezaji wa Mpango utasaidia Taifakujenga msingi wa uchumi wa viwanda ili kukuza uchumina kuondoa umaskini. Hivyo, Serikali inaendelea kuandaamazingira wezeshi ili kuhuisha ushiriki wa sekta binafsi katikakugharamia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo. Aidha,Wizara imekamilisha na kuchapisha Mkakati wa Utekelezajiwa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17-2020/21. Mkakati huo unatoa mwongozo wa utekelezajiwa Mpango huo ambao utaiwezesha Tanzania kuwa nchiya kipato cha kati ifikapo 2025. Mkakati unalenga maeneoyafuatayo: viwanda vya nguo, ngozi, madawa, maeneomaalum ya kiuchumi, ukuaji wa miji na usimamizi wamaendeleo ya miji.

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

13. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya ufuatiliajiwa utekelezaji wa Miradi ya Kitaifa ya Maendeleoiliyobainishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo waMiaka Mitano. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Wizara zakisekta ilifanya ufuatiliaji wa miradi 29 katika mikoa yaMorogoro, Shinyanga, Mwanza, Pwani, Iringa na Mbeya.Miradi iliyofuatiliwa ilijumuisha miradi ya sekta ya Umma naBinafsi, na sekta za Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Maji, Afya, Elimu,Mifugo, Ujenzi na Miundombinu. Malengo makuu ya ufuatiliajiyalikuwa kubainisha hatua halisi za utekelezaji wa miradihusika, changamoto na hatua stahiki za kuzitatua iliyazingatiwe katika maandalizi ya Mpango wa mwaka 2018/19.

2.1.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini

14. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilishaTaarifa ya mwanzo ya Hali ya Umaskini na Malengo yaMaendeleo Endelevu ya mwaka 2016/17. Taarifa hiiinabainisha mwelekeo wa hali ya umaskini, changamoto najinsi ya kukabiliana nazo. Aidha, imeonesha viashiriavitakavyotumika na kubainisha wapi tulipoanzia (baselines)ili kupima mafanikio katika utekelezaji wa Malengo yaMaendeleo Endelevu ya Dunia 2030.

15. Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo inaoneshamafanikio yafuatayo: wastani wa umri wa kuishiumeongezeka kutoka miaka 63.3 mwaka 2015 na kufikiamiaka 64.4 mwaka 2017; vifo vya watoto wachangavimepungua kutoka wastani wa vifo 38 mwaka 2015 hadikufikia vifo 34.5 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2017; Pato lawastani la Mtanzania limeongezeka kutoka shilingi 1,918,931mwaka 2015 na kufikia shilingi 2,275,601 mwaka 2017 sawana ongezeko la asilimia 18.6; kuongezeka kwa umiliki wasamani katika kaya nao umeongezeka na upatikanaji wahuduma za jamii ikiwemo elimu, afya ya jamii, maji safi nasalama, umeme na miundombinu ya barabara umekuwabora zaidi.

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

16. Mheshimiwa Spika, tathmini ya hali yaumaskini nchini iliyofanyika mwaka 2015/16 kwa ushirikianobaina ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Benki ya Dunia ilioneshakuwa umaskini wa mahitaji ya msingi umeendelea kupunguakutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka2015/16. Malengo ya Serikali ni kupunguza umaskini hadi kufikiaasilimia 12.7 mwaka 2025/26. Hata hivyo, ili kubainisha haliya umaskini hususan wa kipato, Ofisi ya Taifa ya Takwimuikishirikiana na Benki ya Dunia hivi sasa inaendesha Utafiti waMapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (Household Budget Survey-HBS) kwa mwaka 2017/18. Hatua iliyofikiwa ni ukusanyajiwa takwimu za mapato na matumizi ya kaya kwa miezisita ya kwanza ya 2018 katika mikoa yote. Kwa msingi huotunatarajia kuwa matokeo rasmi ya hali halisi ya umaskinina hususan wa kipato katika ngazi ya kitaifa, kimkoa nakiwilaya yatatolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mweziMachi, 2019.

2.1.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato yaSerikali

(a) Mapato ya Ndani

17. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,sera za mapato zililenga kukusanya mapato ya kodi na yasiyoya kodi ya shilingi bilioni 19,977.0 ikijumuisha mapato yaMamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi Aprili, 2018 jumla yamakusanyo ya ndani yakijumuisha mapato ya Mamlaka zaSerikali za Mitaa yalikuwa shilingi bilioni 14,838.5, sawa naasilimia 74 ya makadirio ya mwaka. Kati ya kiasi hicho,mapato ya kodi yalifikia shilingi bilioni 12,611.0 sawa naasilimia 74 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni17,106.4; mapato yasiyo ya kodi yalifikia shilingi bilioni 1,789.9sawa na asilimia 82 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingibilioni 2,183.4; na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaayalikuwa shilingi bilioni 437.6, sawa na asilimia 64 ya makadirioya shilingi bilioni 687.3 kwa mwaka.

Vile vile, hadi kufikia Aprili 2018, Serikali ilikopa jumlaya shilingi bilioni 4,958.0 kutoka soko la ndani sawa na asilimia

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

80 ya shilingi bilioni 6,168.9 zilizotarajiwa kukopwa kwamwaka. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 4,125.7 zilikopwakwa ajili ya kulipia dhamana na hati fungani za Serikalizilizoiva (rollover), na shilingi bilioni 832.3 zilikopwa ilikugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha,mikopo kutoka kwenye chanzo hiki, ilielekezwa kulipiasehemu ya madeni ya wakandarasi wa barabara na maji naumeme.

(b) Misaada na Mikopo nafuu toka kwaWashirika wa Maendeleo

18. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2018Serikali imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1,865.76 sawa naasilimia 47 ya lengo la shilingi bilioni 3,971.10. Kati ya kiasikilichopokelewa, shilingi bilioni 70.2 ni Misaada na Mikoponafuu ya Kibajeti (GBS) sawa na asilimia 7 ya ahadi ya shilingibilioni 941.26, shilingi bilioni 180.52 ni za mifuko ya pamoja yakisekta sawa na asilimia 33 ya ahadi ya shilingi bilioni 556.08na shilingi bilioni 1,612.61 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleosawa na asilimia 65 ya ahadi ya shilingi bilioni 2,473.77.

19. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naSekta, Washirika wa Maendeleo, na Wadau wengineilifanikiwa kuandaa na kukamilisha Mwongozo wa Ushirikianowa Maendeleo (Development Cooperation Framework -DCF) ambao uliidhinishwa na Serikali mwezi Agosti 2017.Mwongozo huu umeanza kutekelezwa mwaka 2017/18 nautadumu hadi 2024/25. Aidha, Wizara imeendelea kufuatiliana kutathmini utekelezaji wa programu na miradi yamaendeleo inayonufaika na fedha za nje ili kuhakikishakwamba fedha hizo zinatumika kwa mujibu wamakubaliano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo.

2.1.5 Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji waBajeti ya Serikali

20. Mheshimiwa Spika, katika uandaaji nausimamizi wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18, Wizarailifanya Uboreshaji wa Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi ya

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Bajeti ya Serikali (Central Budget Management System – CBMS)ambao umeanza kutumika rasmi katika uandaaji wa bajetiya mwaka 2018/2019. Pamoja na mambo mengine, mfumohuo utarahisisha utoaji na uchambuzi wa taarifa za mapatona matumizi na pia na utaondoa kabisa tatizo la uingizwajiwa takwimu za bajeti mara mbili kama ilivyokuwa kwenyemifumo iliyopita.

Kazi nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na: kuendeshamafunzo ya mfumo wa CBMS kwa maofisa 246 kutokakwenye Wizara, Idara Zinazojitegemea na Sekretariati zaMikoa; kuandaa, kuweka kwenye tovuti ya wizara,kuchapisha na kusambaza nakala 3,000 za Mwongozo waMaandalizi ya Mpango na Bajeti wa mwaka 2018/19;ukamilishaji wa Vitabu vya Makadirio ya Matumizi ya Serikalikwa mwaka 2018/19 Juzuu Na. I, II, III na IV ambapo nakala2,150 zilichapishwa na kuwasilishwa Bungeni kwa ajili yakujadiliwa na pia kusambazwa kwenye Wizara, IdaraZinazojitegemea na Sekretarieti za Mikoa na Wadau wengine;na uandaaji wa Kijitabu cha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18 Toleo za Wananchi (Citizens Budget) kwa lugha ya Kiswahilina Kiingereza.

2.1.6 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikaliimeendelea kufanya uhakiki wa madeni ya Serikali kamaifuatavyo: Uhakiki wa madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii(NSSF, PPF, PSPF, GEPF, LAPF na NHIF), uhakiki wa madeni yaMamlaka ya Uchimbaji Visima (DDCA) uliofanyika katikaHalmashauri mbalimbali za mikoa ya Katavi, Morogoro,Arusha, Pwani na Lindi ambapo kiasi cha shilingi bilioni1,166.85 kiliokolewa kutokana na uhakiki huo; na uhakiki wamadeni ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali61 na Sekretarieti za Mikoa 26 umekamilika. Aidha, Wizaraimefanya ukaguzi maalum katika maeneo yafuatayo;Hospitali Teule ya Mvumi Dodoma; Mradi wa SELFMicrofinance Fund, kuchunguza ukwepaji wa kodi katikaBiashara ya vinywaji vikali; Kukagua mfumo wa kukusanya

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

maduhuli (ITS/AFCS system) wa Wakala wa Usafiri wa Mwendowa Haraka (DART) na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

22. Mheshimiwa Spika, majukumu mengineyaliyotekelezwa chini ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha zaUmma ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 19 hadi ukurasa wa 24.

2.1.7 Usimamizi wa Malipo

23. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2017/18, Wizara imeendelea kuboresha usimamizi wa malipokwa kuunganisha mfumo wa malipo wa TISS katika Mamlakaza Serikali za Mitaa kwa mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani,Kagera, Geita, Simiyu, Shinyanga, Mara, Kilimanjaro, Manyara,Singida, Tabora na Kigoma. Aidha, mfumo wa TISSumeunganishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Fungu 25 na 37),Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (Fungu 57), Jeshi laPolisi (Fungu 28), Jeshi la Wananchi (Fungu 38), Jeshi la KujengaTaifa (Fungu 39) na kuwapatia mafunzo Watumishi ilikuwawezesha kutumia mfumo huo. Vile vile, Wizaraimesimika mfumo wa malipo (EPICOR) kwenye ubalozi waTanzania kule Nairobi-Kenya kwa lengo la kudhibiti matumizinje ya bajeti. Kadhalika, Wizara imetoa mafunzo ya matumiziya viwango vya kimataifa (IPSAS) kwenye uandaaji waHesabu kwa Wahasibu wa Wizara, Idara Zinazojitegemea naWakala, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa,Taasisi na Mashirika ya Umma 650 na kuwezesha kuandaaHesabu za Majumuisho kwa mwaka wa fedha 2016/17 kwakutumia Viwango vya Kimataifa (IPSAS Accrual Basis).

2.1.8 Deni la Serikali

24. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleakusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo,Dhamana na Misaada SURA 134. Mwezi Novemba 2017,Serikali ilifanya tathmini ya uhimilivu wa Deni la Serikali kwakipindi kilichoishia Juni 2017. Tathmini hiyo inaonesha kuwadeni ni himilivu kwa kipindi cha muda wa kati na muda mrefu.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Uwiano wa Deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 34.4ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56; thamani ya sasa yaya Deni la nje pekee kwa pato la Taifa ni asilimia 19.7ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 40; thamani ya sasa yadeni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 81.8 ikilinganishwana ukomo wa asilimia 150; na thamani ya sasa ya deni la njekwa mapato ya ndani ni asilimia 117.1 ikilinganishwa naukomo wa asilimia 250.

25. Mheshimiwa Spika, kazi ya viashiria hivyo vinneni kupima uwezo wa nchi kukopa. Viashiria vilivyobakivinapima uwezo wa nchi kulipa deni. Kutokana na tathmini,ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mapato ya ndani umefikiaasilimia 9.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20 na ulipajiwa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia13.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 20. Kwa kuzingatiavigezo hivyo, Tanzania bado ina uwezo wa kuendelea ilikugharamia shughuli zake za maendeleo na pia ina uwezowa kulipa mikopo inayoiva kwa kutumia mapato yake yandani na nje.

26. Mheshimiwa Spika, Pamoja na uhimilivu huoSerikali imeendelea kuchukua tahadhari kwa kukopa kwenyevyanzo vyenye masharti na gharama nafuu na kuhakikishakuwa mikopo hiyo inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleoitakayo chochea ukuaji wa uchumi, ikiwemo ujenzi wamiundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege na ujenziwa mitambo ya kufua Umeme. Aidha, Serikali kwakushirikiana na wadau mbalimbali kila robo mwaka inapitiaviwango vya Deni la Serikali ili kuhakikisha kuwa denilinaendelea kuwa himilivu. Vile vile, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali amekamilisha ukaguzi wa deni hilo naSerikali inapitia taarifa hiyo kwa lengo la kuzingatia ushauriuliotolewa.

27. Mheshimiwa Spika, taarifa ya malipo ya Denila Serikali iko katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 26hadi ukurasa wa 28.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

2.1.9 Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa za Kifedha

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara imeendelea na kazi ya kuboresha Mfumo wa kutoleataarifa za kulipia mishahara kwa watumishi wa Umma kwanjia ya Kielektroniki (Government Salaries Payment Platformand Government Online Salary Slip Portal) ambapo mfumowa kutolea taarifa za malipo ya Mishahara ya watumishi waUmma na hati za mishahara (Government Salary Slip Portal)ulikamilika na kuanza kutumika mwezi Julai, 2017. Watumishiwa umma wanaweza kupata hati za mishahara kwa njia yakielektroniki mahala popote palipo na mtandao. Aidha,maboresho haya yamepunguza gharama kubwa zausambazaji wa taarifa za mishahara. Pia Wizara imesimikamfumo wa makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi,(Government electronic Payment Gateway - GePG) ambapohadi sasa taasisi 86 zimeunganishwa na kati ya hizo taasisi 51zimeanza kukusanya maduhuli kwa njia ya kielektroniki.

2.1.10 Usimamizi wa Mali za Serikali

29. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kunakuwana usimamizi bora wa Mali za Serikali, Wizara imeendeleakufanya uthamini wa mali katika Wizara, Idara na Wakalaza Serikali. Hadi Aprili 2018, uthamini wa ardhi na majengoya Serikali katika Mafungu 48 ulifanyika ili kuwa na taarifasahihi za mali za Serikali za Mafungu hayo. Aidha, Wizaraimefanya uhakiki maalum wa Mali za Watu binafsi zilizo chiniya uangalizi wa Serikali kwa vituo 145 vya Polisi Tanzania Barana Zanzibar kwa lengo la kuipunguzia Serikali mzigo wakulipa fidia zinazotokana na upungufu wa uangalizi nausimamizi wa Mali hizo.

30. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyikakatika usimamizi wa Mali za Serikali ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 31-32.

2.1.11 Ununuzi wa Umma31. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,

Wizara imetoa mafunzo kwa maafisa ununuzi na ugavi 75

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

juu ya matumizi ya mfumo wa uagizaji wa mahitaji wa Hatiya Ununuzi (Local Purchase Order-LPO) kupitia Mfumo waMalipo ya Serikali (Epicor); na kukamilisha zoezi la tathminiya Ufanisi wa Mfumo wa Ununuzi wa Umma na kuandaamikakati ya utekelezaji wa matokeo ya zoezi hilo.

32. Mheshimiwa Spika, shughuli nyinginezilizotekelezwa chini ya Ununuzi wa Umma, Rufaa za Zabuniza Umma, Huduma ya Ununuzi Serikalini, na kupitia Bodi yawatalaam wa Ununuzi na Ugavi ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 32 hadiukurasa wa 35.

2.1.12 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali

33. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzikatika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara ya143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanyaukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali kwa kipindi chamwaka wa fedha 2016/17. Ofisi ilifanya ukaguzi wa hesabuza Wizara na Idara za Serikali zinazojitegemea 55, mikoa yote26 ya Tanzania Bara; Wakala za Serikali 37, Mifuko maalum15, Taasisi nyingine za Serikali 60, Balozi za Tanzania nje yanchi 40. Aidha, ukaguzi ulifanyika kwenye Mamlaka za Serikaliza Mitaa 185 na Mashirika ya Umma 105.

34. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine za Ukaguziwa Hesabu za Serikali zilizofanyika ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 35 hadiukurasa wa 37.

2.1.13 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

35. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Ofisiya Msajili wa Hazina imefanya tathmini na uchambuzi waMikataba ya Utendaji Kazi 31 iliyoingiwa baina ya Msajili waHazina na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi na Mashirika ya Ummakatika mwaka 2016/17. Lengo la zoezi hilo ni kupimautekelezaji wa mikataba hiyo kwa mujibu wa viashiria vyamafanikio ambapo mambo ya msingi yanayozingatiwa

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

katika tathmini ni pamoja na: utawala bora; usimamizi wafedha; usimamizi wa rasilimali watu; na huduma kwa mteja.Katika zoezi la Mikataba ya Utendaji, kigezo ni taasisi husikakuwa na bodi hai na kuwa na bajeti iliyoidhinishwa. Matokeoya tathmini yanaonesha wastani wa taasisi kufanya vizuri kwaasilimia 70.

36. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazinaimeendelea kufanya uchambuzi wa taasisi na mashirika yaumma ambayo majukumu yao kwa namna moja au nyingineyanafanana kwa lengo la kuunganisha taasisi hizo ilikuongezea tija na kupunguza gharama za uendeshaji.

37. Mheshimiwa Spika, shughuli zinginezilizotekelezwa katika kusimamia Mashirika na Taasisi zaUmma ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 37 hadi ukurasa wa 39.

2.1.14 Mafao ya Wastaafu na Mirathi

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 1,008.61 kwa ajili yakulipia michango ya mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi yaJamii. Hadi kufikia Aprili, 2018 kiasi cha shilingi bilioni 716.19sawa na asilimia 71 kilitumika kulipa michango ya mwajirikwa watumishi wa umma. Aidha, nitumie fursa hii kuiagizaMifuko ya Hifadhi ya Jamii iandikishe wanachama wake,kuwapa vitambulisho vya uanachama na kutunza vizuri nakwa usahihi taarifa za uchangiaji kwa kipindi chote chautumishi wa wanachama ili kuwaondolea usumbufu siku zakustaafu kwao kama ilivyoelekezwa na Miongozo ya Mamlakaya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Vile vile, ninawakumbusha watumishi wa Ummawawe na tabia ya kukagua taarifa za madaraja yamishahara, makato ya lazima na yale yasiyo ya lazima kutokakwenye mishahara yao na kutoa taarifa kwa wakati kwamamlaka husika ili kama kuna makato hayako sawasawamamlaka husika zichukue hatua za kurekebisha mapema na

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

kuisaidia Serikali kuepuka tozo zinazoweza kutozwa na Mifukoya Hifadhi ya Jamii na Taasisi nyingine za fedha.

39. Mheshimiwa Spika, shughuli zinginezilizotekelezwa katika kusimamia Mafao ya Wastaafu naMirathi ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha hotubayangu kuanzia ukurasa wa 39 hadi ukurasa wa 41.

2.1.15 Udhibiti wa Utakasishaji Fedha Haramu naUfadhili wa Ugaidi

40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidikimeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti waFedha Haramu kwa kufanya yafuatayo: Kupokea nakuchambua taarifa 254 za miamala shuku inayohusu fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi na kuwasilisha taarifa zakiintelijensia 32 kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezajiwa sheria kwa ajili ya uchunguzi. Aidha, katika kujenga uwezowa watumishi, Maafisa wa Kitengo walipata mafunzo yanamna bora ya uchambuzi na upembuzi wa taarifa zamiamala shuku katika Kituo cha Kudhibiti Fedha Haramu(Financial Intelligence Centre – FIC) cha Afrika ya Kusini naMaafisa wanne (4) walihudhuria mafunzo ya Financial ActionTask Force (FATF) standards yaliyofanyika nchini Korea Kusiniambayo ni muhimu katika nyanja ya udhibiti wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi.

41. Mheshimiwa Spika, shughuli zinginezilizotekelezwa katika kusimamia utekelezaji wa Udhibiti waFedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 41 hadiukurasa wa 43.

2.1.16 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi(PPP)

42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18,Wizara imeendelea kuratibu na kuchambua miradi ya ubiakati ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuishauri Serikali

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

juu ya utekelezaji wa miradi hiyo. Aidha, kulingana na Sheriaya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Sura 103;uchambuzi wa miradi ya Ubia hupitia hatua tatu zifuatazo;(i) Mamlaka za utekelezaji kuwasilisha andiko la awali la mradikwa ajili ya uchambuzi (ii) Mamlaka kuandaa taarifa ya awaliya upembuzi yakinifu (iii) Mamlaka ya utelekezaji wa miradiikishirikiana na Mshauri Elekezi kuandaa na kuwasilisha Taarifaya Upembuzi Yakinifu.

Wizara hufanya uchambuzi wa taarifa hizo kwakuangalia, pamoja na mambo mengine maeneo makuumatatu: (a) Uhamishaji wa mianya hasi ya mradi kwendakwa sekta binafsi; (b) Uwezo wa Serikali kugharimia mradi;na (c) Manufaa ya mradi kwa Serikali na wananchi kwaujumla. Endapo mradi unakidhi vigezo utaidhinishwa naKamati ya Wataalam wa PPP kwa ajili ya kuendelea na hatuaya kumpata mbia.

43. Mheshimiwa Spika, Wizara imefikia hatuambalimbali za uchambuzi wa miradi itakayotekelezwa kwautaratibu wa PPP. Upembuzi Yakinifu wa Mradi wa Uzalishajiwa Madawa muhimu na Vifaa Tiba wa Bohari Kuu yaMadawa (MSD) umekamilishwa na kuwasilishwa kwenyeKitengo cha Ubia kwa ajili ya hatua za uidhinishaji; Mradi waKujenga na Kuendesha Vyuo 10 vya VETA kwa Utaratibu waPPP katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Taborana Shinyanga.

Wizara imefanya uchambuzi wa Taarifa ya UpembuziYakinifu na kuwasilisha kwa Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia mapendekezo yanayotakiwa kuzingatiwa ili mradiuwe na tija kwa Taifa; Mradi wa Barabara ya Tozo kutokaDar Es Salaam hadi Chalinze, taarifa ya upembuzi yakinifuwa mradi imefanyiwa uchambuzi ambapo Wizara imetoaidhini yenye masharti (Conditional Approval) ya kutekelezakabla ya kuendelea na hatua ya kumpata mbia; Mradi waUendeshaji wa Huduma ya Usafiri jijini Dar es Salaam Awamuya kwanza, zabuni kwa ajili ya ununuzi wa mtoa hudumawa kudumu, mkusanyaji mapato na mwendesha mfukozilitangazwa na wazabuni wamepatikana; na Wizara

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

imekamilisha uchambuzi wa andiko la awali la mradi waMradi wa Mwambani Port lililowasilishwa na Mamlaka yaBandari Tanzania, hatua inayoendelea ni maandalizi yaUpembuzi Yakinifu.

44. Mheshimiwa Spika, shughuli zinginezilizotekelezwa katika kusimamia utekelezaji wa PPP ni kamainavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 44 hadi ukurasa wa 46.

2.2 USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NAMASHIRIKA YA UMMA CHINI YA WIZARA

45. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapoawali, Wizara yangu inaratibu na kusimamia mashirika nataasisi za umma 36 zilizo chini yake. Utekelezaji wa majukumuya taasisi na mashirika haya kwa mwaka 2017/18 ni kamainavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangu kuanziaukurasa wa 47 hadi ukurasa wa 78. Aidha, utekelezaji wamiradi ya maendeleo chini ya Wizara kwa mwaka 2017/18 nikama unavyooneshwa katika kitabu cha hotuba yangukuanzia ukurasa wa 79 - 81.

2.3 CHANGAMOTO NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA

2.3.1 CHANGAMOTO46. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio

yaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedhana Mipango, changamoto zilizojitokeza ni pamoja na:

i. Ukwepaji wa kodi;ii. Kuchelewa kupatikana kwa misaada na

mikopo ya masharti nafuu pamoja na mikopo ya kibiasharakwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

iii. Uelewa mdogo wa wananchi juu ya dhanaya utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidiambayo ni pana na inabadilika kwa kasi;

iv. Baadhi ya wawekezaji kutelekeza maliwalizouziwa na Serikali wakati wa zoezi la Ubinafsishaji; na

v. Uelewa mdogo wa dhana ya ubia kati yaSekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

2.3.2 HATUA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

47. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto za utekelezaji wa bajeti, Wizara inaendeleakuchukua hatua mbalimbali zikiwemo:

i. Kutekeleza mkakati wa ulipaji kodi kwa hiarina kuendelea kuboresha makusanyo ya mapato yasiyo yakodi kwa kujenga mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wamapato;

ii. Kuendelea kuelimisha wadau mbalimbalikupitia makongamano, mikutano na warsha kuhusu dhanaya utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi;

iii. Kuendeleza mazungumzo na Washirika waMaendeleo kuhusu njia mpya za kutoa na kupokea misaadana mikopo (New Financing Instruments);

iv. Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazinaimeongeza nguvu katika kufanya ufuatiliaji wa karibu kwawawekezaji wote ili kuhakikisha wanaendesha viwanda namali walizouziwa kwa kuzingatia Masharti ya Mikataba yaMauzo; na

v. Kuendelea kutoa mafunzo kuhusu ubia katiya sekta ya umma na sekta binafsi kwa watumishi wa ummana sekta binafsi.

3.0 MALENGO YA MPANGO NA BAJETI KWAMWAKA 2018/19

48. Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara yaFedha na Mipango kwa mwaka 2018/19 umeandaliwa kwakuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo yaMaendeleo Endelevu 2030, Mpango wa Pili wa Maendeleowa Miaka Mitano (2016 /17- 2020/21), Sheria ya Bajeti Na.11ya Mwaka 2015, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi – CCM (2015– 2020), Hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati wa Uzinduzi waBunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

na masuala mtambuka kama vile Jinsia, watu wenyeulemavu, Mazingira, UKIMWI, makundi mengine yaliyo katikamazingira hatarishi na masuala ya lishe kwa jamii pamojana maelekezo na ahadi zilizotolewa Kitaifa.

3.1 MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAWIZARA

3.1.1 Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya UchumiJumla

49. Mheshimiwa Spika, shabaha za uchumi jumlakatika kipindi cha mwaka 2018/19 ni kama ifuatavyo:-

(vi) Pato la Taifa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka2018 kutoka ukuaji halisi wa asilimia 7.1 mwaka 2017;

(vii) Mfumuko wa bei kuendelea kubaki katikawigo wa tarakimu moja;

(viii) Mapato ya ndani kufikia asilimia 15.8 ya Patola Taifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 15.3mwaka 2017/18 na asilimia 15.6 mwaka 2016/17;

(ix) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.6 ya Pato laTaifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 13.0 mwaka2017/18 na asilimia 13.3 mwaka 2016/17; na

(x) Nakisi ya bajeti kufikia asilimia 3.2 ya Pato laTaifa mwaka 2018/19 kutoka matarajio ya asilimia 2.1 mwaka2017/18 na asilimia 1.5 mwaka 2016/17.

3.1.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa

50. Mheshimiwa Spika, kutokana nakuunganishwa kwa iliyokuwa Tume ya Mipango na Wizaraya Fedha, imebidi kuupitia muundo wa Wizara ili uwezekuyaingiza mabadiliko haya ili kutoathiri utekelezaji wamajukumu pamoja na maslahi ya watumishi kwa ujumla.

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Muundo wa Wizara uko katika hatua za mwisho zakuidhinishwa na Mamlaka husika, ambapo imependekezwaiundwe Divisheni ya Mipango ya Maendeleo ya Taifaitakayoongozwa na Kamishna na kuwa na kifungu chake.

51. Mheshimiwa Spika, hivyo katika mwaka 2018/19, shughuli za kipaumbele zitakazotekelezwa katika uratibuwa mipango ya maendeleo ya Taifa ni pamoja na: KuandaaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20;Kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifawa mwaka 2018/19; Kufanya tathmini ya muda wa katikatika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa waMiaka Mitano; Kukamilisha uundwaji wa Mfumo waKielektroniki wa usimamizi wa miradi ya kitaifa ya Maendeleo;na Kufuatilia matumizi ya Mwongozo wa Usimamizi waUwekezaji wa Umma (Public Investment Management -Operational Manual - PIM – OM).

3.1.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umaskini

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara itaendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wajuhudi za kupunguza umaskini ikiwemo kusimamia utekelezajiwa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Jitihada za Kuondoa Umaskininchini (Poverty Monitoring System - PMS); kufuatilia utekelezajiwa malengo yaliyoainishwa katika Mipango ya kitaifa nakisekta na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 2030 naprogramu zinazolenga kuondoa umaskini katika maeneo yavijijini na mijini; kufanya uchambuzi wa kina juu ya Utafiti waMapato na Matumizi ya Kaya (HBS-2017/18); kutoa mafunzokwa Maafisa Mipango na Maendeleo ya Jamii wa Mamlakaya Serikali za Mitaa kuhusu jitihada za kupambana naumaskini na kutunza mazingira ili kuweza kujumuisha katikamipango na bajeti zao.

53. Mheshimiwa Spika, Mipango mingine katikauratibu wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini iko katikahotuba yangu kuanzia ukurasa wa 87 hadi ukurasa wa 89.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

3.1.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato yaSerikali

(a) Mapato ya Ndani

54. Mheshimiwa Spika, katika kuboreshaukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2018/19, Wizaraimepanga kutekeleza yafuatayo: kusimamia sera za fedhana za kibajeti zinazolenga kuboresha mazingira ya uwekezajina biashara; kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwakuimarisha Mkakati Shirikishi wa Mawasiliano na Walipa kodina kuboresha utaratibu wa utozaji kodi; kujenga uwezo wawatumishi ili kukabiliana na tatizo la uhamishaji faida (TransferPricing) unaofanywa na kampuni zenye mitandao yakimataifa kwa lengo la kukwepa au kupunguza kodi;kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa ulipaji kodi kupitiaMfumo wa Vitalu vya Walipakodi; kusimamia zoezi lauunganishaji wa Wizara, Idara, Wakala, taasisi na mashirikaya umma kwenye Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki waukusanyaji wa mapato (GePG) ili kuboresha ukusanyaji nakudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali; na kuongeza kasiya uthaminishaji wa majengo il i kuongeza mapatoyatokanayo na kodi ya majengo.

55. Mheshimiwa Spika, mikakati mingineiliyopangwa iko katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa89 hadi ukurasa wa 90.

(b) Misaada na Mikopo

56. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19Wizara itaendelea na uratibu wa upatikanaji wa fedha zamisaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika waMaendeleo kwa ajili ya kugharamia programu na miradi yamaendeleo mbalimbali nchini. Washirika wa Maendeleowameahidi kuchangia Bajeti ya Serikali kiasi cha shilingi bilioni2,676.64. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 545.76 ni kwa ajiliya Misaada na Mikopo nafuu ya Kibajeti (GBS), shilingi bilioni125.86 kwa ajili ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta na shilingibilioni 2,005.02 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

57. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizopangwakutekelezwa ni pamoja na: kukamilisha Mpango Kazi wakutekeleza Mwongozo mpya wa ushirikiano (DevelopmentCooperation Framework- DCF); na kukagua miradiinayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo.

3.1.5 Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji waBajeti ya Serikali

58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19Wizara imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo:kuendelea kuboresha Mfumo mpya wa Uandaaji naUsimamizi wa Bajeti ya Serikali (CBMS) ili kurahisisha utoaji wamgao wa fedha za matumizi kila mwezi na kuendeshamafunzo ya mfumo huo; kufanya marekebisho, kuchapishana kusambaza nakala 2,200 Vitabu vya Makadirio yaMatumizi ya Serikali ya mwaka 2018/19 kama yalivyopitishwana Bunge, kuchapisha na kusambaza: Mwongozo waMaandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2019/20, Taarifaza Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali za kila Robo Mwaka, Vitabuvya Makadirio ya Matumizi ya Serikali ya mwaka 2019/20 nakuviwasilisha Bungeni na kuvisambaza kwa Wizara, IdaraZinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa kwa Wadau wengine.

59. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizopangwakufanyika ziko katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 92hadi ukurasa wa 93.

3.1.6 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Serikali

60. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2018/19,Wizara itaendelea kudhibiti matumizi ya fedha za umma kwakufanya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa miongozo mbalimbaliya ukaguzi wa ndani iliyotolewa na Wizara na kutoa mafunzokwa wakaguzi wa ndani katika maeneo ya ukaguzi wamiradi, ukaguzi wa kiufundi, usimamizi wa vihatarishi, mfumowa usimamizi wa kazi za ukaguzi na mfumo wa kusimamiautekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

61. Mheshimiwa Spika, mipango mingine ambayoWizara inatarajia kutekeleza katika usimamizi wa udhibiti wafedha za umma iko katika hotuba yangu ukurasa wa 94 hadiukurasa wa 95.

3.1.7 Usimamizi wa Malipo

62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara imepanga kusimamia mfumo wa udhibiti wamatumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na uanzishwajiwa Akaunti Jumuifu (Treasury Single Account) kwa lengo lakuboresha mfumo wa matumizi ya Umma ili kuiongezeaSerikali uwezo wa kugharamia shughuli zake kwa wakati.Aidha, Wizara itaendelea na usimikaji na usimamizi wamifumo ya malipo ya kieletroniki (EFT na TISS) ili kuondoaucheleweshaji wa malipo kwa wadau mbalimbali wakiwemowastaafu, watoa huduma kwa Serikali pamoja na watumishiwa Umma. Vile vile, Wizara itaendelea na uunganishaji wamfumo wa Malipo (Epicor) kwenye Balozi saba (7) ili kudhibitimatumizi nje ya bajeti.

3.1.8 Deni la Serikali

63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Serikali itahakikisha kuwa Deni la Serikali linaendelea kuwahimilivu na kutokuwa mzigo kwa uchumi wetu na kuendeleakuwa fursa na kichocheo cha maendeleo kwa nchi yetu.Aidha, Serikali itaendelea kukopa kwa uangalifu kwakuzingatia masharti nafuu. Mikopo hiyo itatumika kwenyemiradi ya maendeleo yenye kuchochea ukuaji wa uchumi.

3.1.9 Mchango wa Mwajiri (Serikali) kwenye Mifukoya Hifadhi ya Jamii

64. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendeleakuwasilisha kwa wakati michango ya kisheria ya mwajiri yakila mwezi kwa ajili ya watumishi wa umma kwenye MfukoMpya wa Hifadhi ya Jamii utakaochukua nafasi ya Mifuko yaHifadhi ya Jamii iliyounganishwa ya PSPF, GEPF, LAPF na PPFpamoja na mifuko ambayo haitaunganishwa ya NSSF, ZSSF,WCF na Bima ya Afya (NHIF).

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

65. Mheshimiwa Spika, ninatumia fursa hiikuwasisitiza maafisa utumishi wote wanaohusika na kuingizataarifa za watumishi wa umma kwenye mfumo wa kompyutawa kutunza taarifa za watumishi wa umma waingize taarifaza watumishi kwa ukamilifu na usahihi ili uwasilishaji wamichango ya mwanachama na mwajiri kwenye Mifuko yaHifadhi ya Jamii iwe kamili na sahihi kwa kipindi chote chautumishi na hatimaye kurahisisha malipo ya mafao, penshenina mirathi wakati wa hitimisho la utumishi wa umma ilikuwaondolea usumbufu watumishi wa umma walioitumikianchi yao kwa weledi na uaminifu.

3.1.10 Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa za Kifedha

66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara imepanga kusimamia na kuboresha uendeshaji nautumiaji wa mfumo wa taarifa za mishahara ya watumishiwa umma (Government Salaries Payment Platform - GSPP)kwa kuunganisha mfumo huo na taasisi za kibenki na mfumowa pensheni kwa ajili ya urahisishaji wa huduma za mikopona pensheni. Aidha, Wizara itaendelea kuunganisha taasisi260 katika mfumo wa kukusanya mapato yasiyo ya kodi(Government Electronic Payment Gateway System - GePG),ili kuweza kufanikisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali. Vilevile, Wizara itaunganisha mifumo 10 ya kielektroniki ya taarifaza kifedha kwa lengo la kuiwezesha mifumo iwezekubadilishana taarifa.

3.1.11 Usimamizi wa Mali za Serikali

67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara imepanga kufanya kaguzi za mali za Serikali katikabalozi kumi (10), kufanya kaguzi maalum na kutoa elimu yautumiaji na utunzaji bora wa mali katika taasisi mbalimbaliza Serikali ili kuepusha hasara zinazoweza kuzuilika.

3.1.12 Ununuzi wa Umma

68. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kukamilisha uandaaji

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

na kuzindua Sera ya Ununuzi wa Umma pamoja kuanzautekelezaji wa sera hiyo; kukusanya maoni ya wadau kuhusuchangamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa sheria nakanuni za ununuzi wa umma kwa lengo ya kuzifanyiamarekebisho pale itakapohitajika; kuwajengea uwezomaafisa ununuzi na ugavi serikalini juu ya matumizi yamwongozo wa utekelezaji wa shughuli za ununuzi na ugavi;kuendesha mafunzo kwa maafisa ununuzi na ugavi kuhusumatumizi ya mfumo wa malipo wa EPICOR katika ununuzi;kuandaa mpango kazi wa usimamizi wa ununuzi wa ummakatika Serikali Kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa; nakutekeleza mapendekezo ya taarifa ya tathmini ya ufanisiwa mfumo wa ununuzi wa umma.

69. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizopangwakufanyika ziko katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 98hadi ukurasa wa 101.

3.1.13 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali

70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imelenga kuimarisha ukaguzi wamapato na matumizi ya Serikali kwa lengo la kuimarishauwajibikaji na uwazi kwenye matumizi ya rasilimali za umma.Ili kufikia malengo hayo, Ofisi imepanga kutekelezavipaumbele nane (8) kama ifuatavyo: kufanya ukaguzi wamafungu ya bajeti za Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakalana Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikaliza Mitaa, Mashirika ya Umma na Miradi ya maendeleoinayofadhiliwa na wahisani; kufanya ukaguzi wa sekta yagesi, mafuta na madini; kufanya maboresho ya mfumo waukaguzi kwa kutumia TEHAMA; na kukagua ukusanyaji wamapato ya kodi na yasiyo ya kodi. Aidha, Ofisi imelengakufanya ukaguzi wa kiufanisi na kaguzi maalum katikamaeneo yatakayoainishwa; kuwajengea wakaguzi uwezowa kufanya ukaguzi katika maeneo mapya ya ukaguzikwenye sekta ya gesi asilia na mafuta, sekta ya madini, Serikalimtandao na katika uhalifu wa kifedha kwa kutumiamtandao (Financial crimes auditing). Vile vile, ofisi itaendelea

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

na ujenzi wa majengo ya Ofisi za Ukaguzi katika Mikoa yaRukwa na Mara.

3.1.14 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

71. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Ofisi ya Msajili wa Hazina imepanga kutekeleza yafuatayo:kufanya mapitio na kufuatilia kampuni ambazo Serikali inaHisa chache na hazijawasilisha gawio serikalini; kufanyauchambuzi wa uwekezaji unaofanywa na Mashirika ya Ummakatika Kampuni Tanzu na kampuni nyinginezo; kushirikianana Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kufanyaurejeshaji wa viwanda vinavyosuasua na kuwapatiawawekezaji mahiri; kusimamia kwa karibu ukusanyaji wamadeni ya ubinafsishaji wa il iyokuwa Benki ya NBC;kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Mifuko ya Jamii, Taasisi za Fedha pamoja na wadaumbalimbali katika suala zima la uwekezaji na ufufuaji waviwanda, kampuni na mashamba yaliyobinafsishwa.

72. Mheshimiwa Spika, Mipango mingine katikakusimamia Mashirika ya Umma iko katika hotuba yanguukurasa wa 102 hadi ukurasa wa 103.

3.1.15 Mafao ya Wastaafu na Mirathi

73. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendeleakuboresha, kutunza na kusimamia huduma za Pensheni kwawastaafu wanaolipiwa Hazina ikiwa ni pamoja na kuendeleakulipa kwa wakati mafao na pensheni kwa wastaafu waSerikali, mirathi na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishiwa Serikali walio kwenye mikataba. Aidha, wizara itaendeleakuboresha masijala ya pensheni kwa kuendelea kuhifadhikumbukumbu za wastaafu kielektroniki, ili kurahisisha malipokufanyika kwa wakati.

74. Mheshimiwa Spika, naomba nisisitize kwamaafisa utumishi wote wanaohusika kuandaa mapemanyaraka za watumishi wanaotarajia kustaafu na kuziwasilisha

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Hazina zikiwa zimekamilika ili malipo ya mafao, pensheni namirathi ya wastaafu wa kawaida yafanyike kwa wakati nakuwaondolea adha ya usumbufu watumishi pindiwanapokuwa wamestaafu. Aidha, nahimiza ofisi zote zaumma zitunze taarifa za watumishi wa umma kielektronikikwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao.

3.1.16 Udhibiti wa Utakasishaji Fedha Haramu naUfadhili wa Ugaidi

75. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Kitengo cha Udhibiti wa Utakasishaji Fedha Haramu naUfadhili wa Ugaidi itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheriaya Udhibiti wa Fedha Haramu ya Mwaka 2012 na Sheria yaUdhibiti Fedha Haramu na Mali Athirika ya Zanzibar ya Mwaka2009 kwa kutekeleza yafuatayo: kufanya marekebisho yaSheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu (The Anti-MoneyLaundering Act, 2006) na kanuni zake za mwaka 2012 ilikuendana na mahitaji; kuendelea na utekelezaji wa mikakatiya kitaifa na kimataifa ya udhibiti wa utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi; kuendelea kupokea nakuchambua taarifa za miamala shuku zinazohusu utakasishajiwa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi na taarifa zausafirishaji wa fedha kutoka na kuingia nchini kupitiamipakani; na kuendelea kuwasilisha taarifa za intelijensiakwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria.

3.1.17 Tume ya Pamoja ya Fedha

76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Tume ya Pamoja na Fedha imepanga kufanya uchambuziwa Mapato na Matumizi yanayohusu utekelezaji wa Mamboya Muungano.

3.1.18 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara imepanga kufanya marekebisho ya Sheria na Kanuniza Ubia ili kuimarisha usimamizi wa mifumo ya usimamiajiwa miradi ya ubia na kupunguza mlolongo wa uidhinishaji

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

wa miradi hiyo; kusimamia uibuaji na utekelezaji wa miradiya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP);kuandaa miongozo ya kitaalam ya kuainisha na kufanyauchambuzi wa miradi ya PPP; na kutoa mafunzo kuhusuutekelezaji wa miradi ya ubia kwenye Wizara, Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma nataasisi binafsi.

78. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana namamlaka husika inategemea kukamilisha maandiko ya ujenziwa reli ya Mchuchuma/ Liganga – Mtwara na reli ya Tanga –Arusha – Musoma kwa kiwango cha standard gauge; ujenziwa miundombinu ya reli katika jiji la Dar Es Salaam kwa ajiliya treni ya abiria na mradi wa kusambaza gesi asilia nchini.Aidha, Wizara itaendelea na hatua ya kutangaza mradi waujenzi wa viwanda vya uzalishaji wa madawa muhimu navifaa tiba chini ya MSD ili kuwapata wawekezaji.

3.1.19 Programu ya Maboresho ya Usimamizi waFedha za Umma

79. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19,Wizara kupitia Programu ya Maboresho ya Usimamizi waFedha za Umma itaendelea kuziwezesha Wizara, IdaraZinazojitegema, Wakala, Taasisi za Serikali, Sekretarieti zaMikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutekelezamaboresho ya usimamizi wa fedha za umma katika maeneombalimbali, hususan: marekebisho ya sheria za kodi ili sheriahizi ziendane na Sheria ya Uwekezaji; kuhuisha mikataba yamadini ambayo inapata misamaha ya kodi na mfumo wakufanya maoteo ya viashiria vya uchumi jumla.

80. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine yamaboresho ni pamoja na: kuandaa na kukamilisha Sera yaKitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini; kuhuisha mikataba yamakubaliano na Washirika wa Maendeleo ili iendane naSheria za Kodi za Tanzania; kufanya tathmini ya matokeo yakiutendaji ya mfumo wa vihatarishi katika Wizara, Taasisi,Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuimarisha mfumowa udhibiti wa ndani; kuanzisha Ofisi mpya za Mhakiki Mali

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

wa Serikali katika mikoa ya Simiyu, Katavi na Songwe; kufanyamarekebisho ya sheria ya Udalali ya mwaka 1928; nakuimarisha ununuzi wa Umma.

3.1.20 Mradi wa Kimkakati wa kuongeza mapatokwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa (Strategic RevenueGeneration in LGAs Project)

81. Mheshimiwa Spika, kupitia Mradi huu, Wizaraitatoa fedha katika Serikali za Mitaa zitakazokidhi vigezo vyamiradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya Serikali za Mitaa.Aidha, Wizara imepanga kutoa mafunzo kwa wawezeshajiwa kitaifa juu ya Usimamiaji na Uandaaji wa Miradi yaKimkakati ya kuongeza mapato kwenye Mamlaka ya Serikaliza Mitaa.

3.2 USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NAMASHIRIKA YA UMMA CHINI YA WIZARA

82. Mheshimiwa Spika, mipango na malengo yabajeti kwa mwaka 2018/19 kwa upande wa mashirika nataasisi za umma zilizochini ya wizara ni kama inavyooneshwakatika kitabu cha hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 109 hadiukurasa wa 127.

4.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MAOMBI YAFEDHA KWA MWAKA 2018/19

4.1 MAKADIRIO YA MAPATO

83. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19Wizara inakadiria kukusanya maduhuli kiasi cha shilingi bilioni597.81 kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja namauzo ya nyaraka za zabuni, kodi za pango, mauzo ya leseniza udalali, gawio, marejesho ya mikopo na michango kutokakatika Taasisi na Mashirika ya Umma.

4.2 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2018/19

84. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha naMipango imepanga kutumia kiasi cha jumla ya shilingi

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

12,058,714,013,500 (Bilioni 12,058.71) kwa mafungu yote nane.Kati ya fedha hizo, shilingi 10,763,501,474,000 (Bilioni 10,763.50)ni kwa aji l i ya matumizi ya kawaida na shilingi1,295,212,539,500 (Bilioni 1,295.21) ni kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi65,764,075,000 (Bilioni 65.76) kwa ajili ya mishahara, shilingi693,257,399,000 (Bilioni 693.26) kwa ajili ya matumiziMengineyo (OC) na shilingi 10,004,480,000,000 (Bilioni 10,004.48)ni malipo ya deni la Serikali na michango ya Mifuko ya Hifadhiya Jamii. Aidha, katika fedha za matumizi ya maendeleo,shilingi 1,266,033,128,500 (Bilioni 1,266.03) ni fedha za ndanina shilingi 29,179,411,000 (Bilioni 29.18) ni fedha za nje.

MAOMBI YA FEDHA

4.2.1 FUNGU 50 – WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

85. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 57,022,927,000(bilioni 57.02). Kati ya hizo:

(i) Mishahara - Shilingi 7,577,332,000 (bilioni 7.58)

(ii) Matumizi mengineyo – Shilingi 49,445,595,000(bilioni 49.44)

(b) Miradi ya Maendeleo - Shilingi 28,790,817,000(bilioni 28.79). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani - Shilingi 19,642,535,000(bilioni 19.64).

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 9,148,282,000 (bilioni9.15).

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

4.2.2 FUNGU 21 - HAZINA

86. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya Kawaida – Shilingi 531,890,056,000(bilioni 531.89). Kati ya fedha hizo:

(i) Mishahara ya fungu hili - Shilingi 21,467,017,000(bilioni 21.47).

(ii) Matumizi Mengineyo – Shilingi510,423,039,000.00 (bilioni 510.42) ambazo ni kwa ajili yamatumizi ya idara, taasisi zilizo chini ya Fungu hili, pamojana matumizi maalum.

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi1,247,611,267,500 (bilioni 1,247.61). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani - Shilingi 1,236,190,593,500(bilioni 1,236.19)

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 11,420,674,000 (bilioni11.42)

4.2.3 FUNGU 22- DENI LA TAIFA

87. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi10,013,706,140,000 (bilioni 10,013.71). Kati ya fedha hizo:-

(i) Mishahara - Shilingi 9,226,140,000 (bilioni 9.23)

(ii) Matumizi Mengineyo (Malipo ya Madeni naMichango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii) – Shilingi10,004,480,000,000 (bilioni 10,004.48)

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

4.2.4 FUNGU 23 – MHASIBU MKUU WA SERIKALI

88. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya Kawaida - Shilingi 46,725,409,000(bilioni 46.72). Kati ya fedha hizo:

(i) Mishahara – Shilingi 7,908,675,000 (bilioni 7.91)

(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi Shilingi38,816,734,000 (bilioni 38.82)

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 3,200,000,000.00(bilioni 3.20). Kati ya fedha hizo:

(i) Fedha za Ndani - Shilingi 2,000,000,000.00 (bilioni2.00).

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 1,200,000,000.00(bilioni 1.20).

4.2.5 FUNGU 7 – OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

89. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi54,592,065,000.00 (bilioni 54.59). Kati ya fedhahizo:-

(i) Mishahara - Shilingi 2,362,279,000.00 (bilioni2.36)

(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi Shilingi52,229,786,000.00 (bilioni 52.23).

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 1,650,000,000.00(bilioni1.65). Kati ya fedha hizo:

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

(i) Fedha za Ndani – Shilingi1,000,000,000.00 (bilioni 1).

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 650,000,000.00(bilioni 0.65).

4.2.6 FUNGU 10 – TUME YA PAMOJA YA FEDHA

90. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya Kawaida - Shilingi 2,155,075,000(bilioni 2.15). Kati ya fedha hizo:-

(i) Mishahara - Shilingi 574,933,000 (bilioni 0.57)

(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi 1,580,142,000(bilioni 1.58).

4.2.7 FUNGU 13 – KITENGO CHA KUDHIBITI FEDHAHARAMU

91. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:

(a) Matumizi ya kawaida - Shilingi 2,015,586,000(bilioni 2.01).

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 248,363,000(bilioni 0.25) ambazo ni fedha za nje.

4.2.8 FUNGU 45 – OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI

92. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwamwaka 2018/19, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi chafedha kama ifuatavyo:

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

(a) Matumizi ya kawaida – Shilingi 55,394,216,000 (bilioni 55.39). Kati ya fedha hizo:

(i) Mishahara - Shilingi 16,647,699,000 (bilioni16.65).

(ii) Matumizi Mengineyo - Shilingi 38,746,517,000(bilioni 8.75).

(b) Miradi ya Maendeleo – Shilingi 13,712,092,000 (bilioni 13.71). Kati ya fedha hizo:

(i) Fedha za Ndani – Shilingi 7,200,000,000 (bilioni7.20).

(ii) Fedha za Nje - Shilingi 6,512,092,000(bilioni 6.51).

5.0 SHUKRANI

93. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hiikuzishukuru nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifaambayo kwa namna moja ama nyingine yamesaidia katikautekelezaji wa bajeti ya Wizara. Aidha, napendakuwashukuru sana Wafanyakazi na wananchi wote ambaowameendelea kulipa kodi kwa hiari na pia kushiriki katikaujenzi wa Taifa letu.

94. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa napendakuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara(www.mof.go.tz).

95. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasa nitamwitamsemaji wa Kamati ya Bajeti aje asome ripoti yake kwa nususaa na akimaliza tu kusoma Mwenyekiti wa Bajeti ambayehotuba yake itasomwa na Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Jitu Soni, mchangiaji wa kwanza atakuwa MheshimiwaDaniel Nsanzugwanko na atafuatiwa na MheshimiwaMchungaji Peter Msigwa na Mheshimiwa Juma KomboHamad ajiandae.

Mheshimiwa Jitu, karibu sana.

MHE. JITU V. SONI – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Ifuatayo ni Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusuUtekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwaMwaka wa Fedha 2017/2018, pamoja na Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2018/2019.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(7)na (9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajetikuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipangokwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, pamoja na Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2018/2019; ambayo inajumuisha Fungu 07 – Ofisi ya Msajili waHazina; Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha; Fungu 13 –Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu; Fungu 21 – Hazina;Fungu 22 – Deni la Taifa; Fungu 23 – Mhasibu Mkuu wa Serikali;na Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 9(1)(c) cha Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 kinaipa mamlakaKamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kupitia na kuridhiaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko wa Ofisi ya Taifaya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Fungu45). Kamati ilitekeleza jukumu hili na kufanya mashaurianona Serikali na mwisho kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Mfuko wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu haya,Kamati ilifanya vikao na Wizara ya Fedha na Mipango katiya mwezi Machi na Aprili, 2018, Dodoma na kupokea Taarifaya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango na

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Mafungu yaliyo chini yake kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018,pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, Mapitio ya Ujumla KuhusuUtekelezaji wa Bajeti na Majukumu ya Wizara ya Fedha naMipango kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Katika Mwakawa Fedha 2017/2018, Wizara ya Fedha na Mipango kwaMafungu yote manane yaliidhinishiwa kutumia jumla yaSh.11,676,591,286,252.00. Kati ya fedha hizo shilingi 10.26zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Mafungu yotena shilingi trilioni 1.41 zilikuwa kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Aidha, mchanganuo wa fedha za matumizi yakawaida ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, shilingi bilioni 72.53 ilikuwa ni kwaajili ya mishahara na shilingi bilioni 727.5 ilikuwa kwa ajili yamatumizi mengineyo na shilingi trilioni 9.4 ni kwa ajili ya kulipiaDeni la Serikali na huduma nyingine. Kwa upande wa fedhaza maendeleo zilizoidhinishwa na Bunge, shilingi trilioni 1.37ni fedha za ndani na shilingi bilioni 42.3 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Februari Wizaraya Fedha na Mipango pamoja na mafungu yake ilikuwaimepokea jumla ya shilingi trilioni 7.21, sawa na asilimia 62.2ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge. Kati ya fedha hizo shilingitrilioni 7.1 sawa na asilimia 72 ya lengo zilikuwa ni kwa ajili yamatumizi ya kawaida na shilingi bilioni 69.5 zilikuwa ni kwaajili ya miradi ya maendeleo sawa na asilimia tano tu yabajeti.

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Bajeti kwa Mafunguya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha wa2017/2018. Hotuba iliyotolewa na Waziri wa Fedha naMipango imetoa taswira halisi ya utekelezaji wa bajeti yaMafungu yake nane kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.Kamati imefanya uchambuzi katika mafungu manane yaliyochini ya Wizara hii na kuona kuwa baadhi ya Mafungu yaWizara yamepata fedha za kutosha na hivyo kutekelezamajukumu yake kikamilifu.

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

Mheshimiwa Spika, vile vile, kuna Mafungu ambayohayakupatiwa fedha za kutosha hivyo kuathiri utendaji wakewa kazi. Hata hivyo, hali sio nzuri kwa upande wa utolewajiwa fedha za maendeleo kwenye Mafungu yote manane(rejea jedwali namba moja).

Mheshimiwa Spika, ukirejea jedwali namba moja,utaona kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2018; kati ya Mafungunane yaliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ni Mafungumawili tu yalikuwa yamepokea fedha zaidi ya asilimia 60 yabajeti iliyoidhinishwa na Bunge (matumizi ya kawaida namiradi ya maendeleo).

Mheshimiwa Spika, Mafungu yaliyopokea zaidi yaasilimia 60 ni; Fungu 22 – Deni la Taifa na Fungu 10 – Tume yaPamoja ya Fedha. Aidha, Fungu 50 – Wizara ya Fedha naMipango; Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu zaSerikali; na Fungu 23 – Mhasibu Mkuu wa Serikali yamepokeafedha chini ya asilimia 60 kwa kipindi husika. Kwa upandewa Fungu 7 – Msajili wa Hazina amepokea asilimia 17.25 naFungu 21 – Hazina imepokea asilimia 21.2.

Mheshimiwa Spika, hali ya utolewaji wa fedha kwaMafungu haya siyo ya kuridhisha hata kidogo ukilinganishana utekelezaji wa majukumu ya msingi wa Mafungu haya.Katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hakuna hataFungu moja ambalo limepokea bajeti ya maendeleo kwazaidi ya asilimia 50.

Mheshimiwa Spika, tathmini inaonesha kuwamwenendo wa ugawaji wa fedha kwa baadhi ya Mafunguya Wizara ya Fedha na Mipango si wa kuridhisha. Hii ni dhahirikuwa utekelezaji wa shughuli nyingi za Wizara hii umeathirikakwa kiasi kikubwa ukizingatia kuwa mgawanyo na wajibuwa Serikali (Government Instrument) kwa Wizara ya Fedhana Mipango ni kutafuta na kusimamia ukusanyaji wa mapatopamoja na kuandaa na kusimamia utelekelezaji wa bajetiya Serikali kwa Mafungu mbalimbali. Kamati inaona kuwamwenendo huu wa utolewaji wa fedha kwa Mafungu yakehautoi tija kwa Mafungu husika kutekeleza majukumu yao.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Spika, Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zilizo chini yakekwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Wizara ya Fedha naMipango katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, imekadiriwakutumia jumla ya shilingi trilioni 12.1 kwa Mafungu yote nane.Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.8 ni kwa ajili ya matumiziya kawaida na shilingi trilioni 1.29 ni kwa ajili ya matumizi yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaidayanajumuisha kiasi cha shilingi bilioni 313.6 kwa ajili yamishahara na shilingi bilioni 495.3 ni kwa ajili ya MatumiziMengineyo (OC) na shilingi trilioni 10.04 ni kwa ajili ya ulipajiwa Deni la Taifa na huduma nyingine. Aidha, kwa upandewa fedha za matumizi ya maendeleo, Wizara imepangakutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.29 ambayo inaoneshwakatika jedwali namba mbili.

Mheshimiwa Spika, Maombi ya Fedha kwa Wizara yaFedha na Mipango na Mafungu yaliyo chini Wizara kwaMwaka 2018/2019. Makadirio ya mapato na matumizihaya yanahusisha pia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali (Fungu 45). Kamati ya Bajetiinaipongeza Wizara ya Fedha kwa kuongeza shilingibilioni 6.23 kwenye Fungu 45 ili Ofisi ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali iweze kutimiza majukumuyake vizuri.

Mheshimiwa Spika, Maoni na Mapendekezo ya Kamatiya Bunge ya Bajeti. Baada ya Kamati kupitia utekelezaji waBajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisi zakekwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, pamoja na maombi yafedha ya Mafungu husika kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019;Kamati inapenda kutoa maoni na mapendekezo yake kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mwenendo wa Utolewaji waFedha kwa Mafungu yaliyo chini ya Wizara ya Fedha na Wizaranyingine kama yalivyoidhinishwa na Bunge. Tathmini yaujumla ya mwenendo wa utoaji wa fedha za utekelezaji wa

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa mafungu yaliyo chini yaWizara ya Fedha unaonesha kuwa siyo wa kuridhisha kwabaadhi ya Mafungu.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mwezi Machi 2018, katiya Mafungu nane yaliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango,mafungu mawili tu yalikuwa yamepokea fedha zaidi yaasilimia 60 ya Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa upandewa matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Mafunguyaliyopokea zaidi ya asilimia 60 ni; Fungu 22 – Deni la Taifa naFungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha. Kamati inaonakuwa mwenendo huu wa utolewaji wa fedha kwaMafungu yake hautoi tija kwa mafungu husika kutekelezamajukumu yao.

Mheshimiwa Spika, Wizara imejitahidi kutoa fedha zamatumizi ya kawaida kwa Mafungu mbalimbali ya SerikaliKuu na mikoa kwa wastani wa asilimia 100. Hata hivyo,pamoja na mwenendo huu mzuri wa utolewaji wa fedhakwenye mafungu husika, bado utekelezaji wa majukumu yamafungu haya unaathiriwa na bajeti isiyojitoshelezakutokana na ukomo wa bajeti uliowekwa na Serikali hapoawali wakati mafungu hayo yakiomba fedha kwa ajili yakutekeleza majukumu yao. Aidha, kwa upande wa utoajiwa fedha za maendeleo kwa kipindi cha mwezi Julai 2017hadi Machi 2018, hali si ya kuridhisha.

Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha kuwa kati yamafungu 47 ya Wizara mbalimbali yanayostahili kupata fedhaza maendeleo ni mafungu 16 tu yamepata fedha zaidi yaasilimia 50. Hali hii pia tunaiona kwa upande wa fedha zamiradi ya maendeleo kwa baadhi ya mafungu ya Mamlakaza Serikali za Mitaa ukilinganisha na bajeti waliyoidhinishiwana Bunge. Kamati inashauri Wizara ya Fedha na Mipangoiangalie namna bora ya kutekeleza majukumu yake nakutatua changamoto za utekelezaji wa bajeti.

Mheshimiwa Spika, Fungu 66 – Tume ya Mipango;itakumbukwa kuwa Tume ya Mipango (Fungu 66) ilianzishwakwa Mujibu wa Sheria ya Tume ya Mipango ya Mwaka 1989

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

(iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002) ikiwa chini ya Ofisi ya Raiskwa lengo la kuwa Msimamizi Mkuu wa Mipango ya Serikaliikiwemo kubuni miradi ya maendeleo ya kimkakati pamojana kufuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradihiyo. Tume hii imeweza kutekeleza majukumu yake kwaufanisi ikiwa huru chini ya Ofisi ya Rais.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kuwa, kwa kuwamfumo wa Serikali umebadilika ni vyema Serikali ikarudishaTume ya Mipango pamoja na Fungu 66 chini ya Wizara yaFedha na Mipango kwa lengo la kusimamia na kuendelezashughuli zilizokuwa zinafanywa na Tume ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, hatua hii itasaidia kulinda uhuruwa upangaji wa mipango na usimamizi wa mapato namatumizi ya Serikali ili kuondokana na hali iliyopo sasaambapo Serikali imekuwa ikiegemea zaidi kwenye mapatona matumizi kuliko mipango ya nchi na hivyo kutokuwa nauwajibikaji mzuri katika masuala ya kibajeti (checks andbalances).

Mheshimiwa Spika, Uhakiki na Ulipaji wa Madeni yaWatumishi na Wakandarasi na Wazabuni. Katika Mwaka waFedha 2015/2016, Serikali ilichukua hatua madhubuti yakuhakiki na kulipa madeni mbalimbali, hatua ambayoinapongezwa sana na Kamati ya Bajeti. Hadi Mwaka waFedha 2017/2018, Serikali imehakiki na kulipa jumla ya shilingibilioni 939.5 kwa mchanganuo ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, wakandarasi wamelipwa jumlaya shilingi bilioni 618.9; wazabuni shilingi bilioni 81.2; watumishibilioni 133.4; watoa huduma mbalimbali shilingi bilioni 77.2na madeni mengineyo shilingi bilioni 27.5. Pamoja na ulipajihuo wa madeni ya watumishi bado kuna malalamiko yabaadhi ya watumishi kama Walimu, kwamba fedhawalizolipwa ni pungufu ya madai halisi wanayoidai Serikali.Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhakikisha inakamilishaulipaji wa madeni yote yaliyohakikiwa ili kupunguzagharama kwa Serikali hasa kwa madeni yenye ongezeko lariba.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Miradi kwa Njia yaUbia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Bunge lakoTukufu lilipitisha Sheria ya Ubia baina ya Sekta Binafsi na Sektaya Umma mwaka 2009 mara baada ya kukamilika kwa Seraya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Katikautekelezaji wa Bajeti ya Fungu 21, imeainishwa miradimbalimbali iliyo katika hatua ya kufanyiwa upembuzi yakinifuili itekelezwe kwa njia ya PPP. Miradi hiyo ni Dar Rapid TransportPhase I, Mradi wa Uzalishaji wa Madawa na Vifaa Tiba Muhimu,Ujenzi wa Reli ya Mchuchuma/ Liganga – Mtwara, Mradi waBandari na Kituo cha Biashara cha Kurasini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizi muhimu,Kamati imebaini kuwa maombi mengi ya miradi inasuasuakutekelezwa kwa njia ya PPP kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, moja; Serikali kuchelewa kuwalipawakandarasi wanaofanya upembuzi yakinifu kwa miradi hiyo(feasibility study) mfano Reli ya Mchuchuma/ Liganga hadiMtwara; Dar es Salaam – Tanga – Moshi; na Moshi – Arusha –Musoma. Pili, kuchelewa kufanya maamuzi kwa miradiinayoweza kutekelezwa kwa njia ya ubia mfano Mradi waKituo cha Biashara cha Kurasini ambacho mwekezaji hivi sasaameamua kuwekeza nchi ya jirani.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Wizara ya Fedhana Mipango kuhakikisha Kitengo cha PPP kilichopo Wizaranikinatekeleza jukumu lake kwa ufanisi la kuratibu nakusimamia maandiko na maombi ya utekelezaji wa miradiya maendeleo kwa njia ya ubia baina ya sekta ya umma nasekta binafsi kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali(Contracting Authorities).

Mheshimiwa Spika, aidha, Kamati inaishauri Serikalikutenga fedha za kutosha kwa ajili ya PPP Facilitation Fund.Mfuko huu una jukumu la kutenga fedha kwa ajili yakuandaa maandiko kwa aji l i ya kubainisha miradimbalimbali inayoweza kutekelezwa kwa njia ya ubia nakuhifadhi fedha kwa ajili ya ushiriki wa Serikali kwenyemiradi ya ubia.

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Village Empowermentmaarufu kama Milioni 50 kwa kila Kijiji yaaani (Fungu 21).Katika mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ya Fedha naMipango ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 60, kwa ajili yakufanya utafiti wa majaribio yaani (pilot study) kwa baadhiya mitaa, vijiji, kata na shehia kwa ajili ya kutekeleza Mradiwa village empowerment maarufu kama milioni 50, kwa kilakijiji.

Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulilenga “Kutenga Kiasicha Shilingi bilioni 50, kwa ajili ya Kila Kijiji kwa ajili ya kukopeshaVikundi vya Ujasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopayaani (SACCOS) katika vijiji husika”. Hata hivyo, fedha hizozilizotengwa katika miaka yote na hakuna fedha yoyoteiliyotolewa licha ya Serikali kuahidi kuweka utaratibu maalumwa utekelezaji wa miradi hiyo kupitia TAMISEMI. Kamatiingependa Bunge lako Tukufu lipewe taarifa ya utekelezajiwa mradi huo ikiwemo hiyo ya ‘pilot study’ iliyofanyika.

Mheshimiwa Spika, Mchezo wa Kubahatisha, katikamwaka wa fedha 2017/2018, Bunge lako Tukufu kupitiaKamati ya Bajeti ilishauri Serikali kufanyia mabadiliko katikaSheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura 41. Lengo lamabadiliko ilikuwa ni kuipa Mamlaka ya Mapato (TRA) uwezowa kukusanya mapato yatokanayo na michezo hii na piakufanya marekebisho ya viwango vya tozo. Mafanikiomakubwa yaliyopatikana ni kutokana na ushauri huo waKamati.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali kwa kupitiaMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuweza kukusanyashilingi bilioni 39.1ni sawa na ongezeko la asilimia 12 hadikufikia mwezi Machi, 2018. Pamoja na kuwa michezo hiiimekuwa kwa kasi sana na kuipatia Serikali mapato, Kamatiinashauri Serikali kupandisha ada, tozo na kodi mbalimbalikatika michezo hii kwa sababu kimsingi michezo hii sio yakiuzalishaji na imekuwa na madhara makubwa kwa jamii.

Mheshimiwa Spika, katika Nchi za Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo inaongoza kwa kiwango cha chini cha

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

mapato ghafi katika michezo hii kuliko nchi nyingine. MfanoKenya wanatoza asilimia 35, Rwanda wanatoza asilimia 13na Uganda wanatoza asilimia 20 ya mapato ghafi. Aidha,Kamati inaitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kusimamiakikamilifu Sheria hii kuhakikisha kwamba wanaoshiriki katikamichezo hii ni wale wanaofikisha umri wa miaka 18 kamasheria inavyotaka.

Mheshimiwa Spika, Ukusanyaji wa Kodi wa Majengo;mwaka 2015/2016, Serikali ilichukua jukumu la ukusanyaji wakodi ya majengo na mabango kutoka katika Serikali za Mitaana kuipeleka Serikali kuu kwa lengo la kuongeza ufanisi katikaukusanyaji na baadaye kuzirejesha mapato hayo katikahalmashauri husika. Mwaka huo huo Serikali ilishushamakadirio ya makusanyo ya kodi kutoka shilingi bilioni 58.08zilizokuwa zimekadiliwa na Serikali za Mitaa na kuwa Shilingibilioni 47.6.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika mwaka wa fedha2017/2018, Serikali ilifanya mabadiliko kupitia Sheria yaFedha na kuondoa takwa la kurejesha fedha zamakusanyo ya mabango na majengo kwa Serikali zaMitaa na badala yake kurejesha kulingana na mahitaji yamatumizi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, Serikali imeweza kukusanya kodi ya majengo kwa ufanisiwa asilimia 61.08 ambapo kiasi ya fedha Shilingi 20.22 zilikuwazimekusanywa. Baada ya Kamati kufanya tathmini yamwenendo huu, nina masuala yafuatayo kiushauri kwaSerikali:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kurudisha chanzo hikicha mapato katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa sababubado Mamlaka ya Mapato hawajawa na uwezo wa kutoshakukusanya chanzo hiki; na Pili, ni utaratibu wa kutumiaDhamana ya Serikali za Mitaa yaani (Municipal Bonds) katikakupata fedha za Maendeleo kwa Serikali za Mitaautashindikana kwa sababu halmashauri hazitakuwa nauwezo wa kulipa riba pindi amana hizo zinapoiva; na

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Tatu, Kamati inaishauri Serikali kutumia Wanafunzi waChuo cha Ardhi kufanya shughuli ya kufanya tathimini yamajengo wakati wa mafunzo ya vitendo ili kuongeza tija yaukusanyaji wa mapato husika.

Mheshimiwa Spika, ukusanyaji na utoaji wa fedha kwaajili ya Mifuko mbalimbali yenye vyanzo Mahususi. Bunge lakoTukufu lilipitisha sheria mbalimbali zilizokuwa na lengo lakubainisha vyanzo vya mapato mahsusi kwa ajili ya Mifukombalimbali. Mfano asilimia 1.5 yaani kwa bill of lading wakatiwa kuingiza bidhaa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Reli,na tozo ya Sh.100 ya mafuta kati ya tozo hiyo Sh.50 ni kwa ajiliya Mfuko wa Umeme Vijijini (REA) na Sh.50 kwa ajili ya Mfukowa Maendeleo wa Maji.

Mheshimiwa Spika, aidha, kifungu cha 17(a) chaSheria ya Uendelezaji wa Tasnia ya Korosho inatoamgawanyo wa makusanyo ya ushuru wa usafirishaji wakorosho ghafi nje ugawanywe kwa asilimia 35 ziende Serikalikuu na asilimia 65 ziende kuendeleza zao la korosho nchini.Kamati imebaini kwamba pamoja na Sheria mbalimbalikuainisha matumizi ya fedha hizo kwenye maeneo yakimkakati utoaji wa fedha hizo umekuwa ukichelewa na maranyingi hazitolewi.

Mheshimiwa Spika, mfano, Mfuko wa REA kwa mwakawa fedha 2017/2018, Serikali iliweza kukusanya jumla ya shilingibilioni 263.7 ambapo kiasi kilichokuwa kimetolewa REA nibilioni 261.3. Mfuko wa Uendelezaji wa zao la Korosho ulikuwaumepokea shilingi bilioni 10 tu kati ya shilingi bilioni 91,zilizokuwa zimekusanywa katika msimu wa mwaka 2016/2017.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kuzingatiasheria mbalimbali za fedha, hususan zilizoanzisha Mifukombalimbali pamoja na Sheria ya Bajeti ili mapato husikayaende yakatumike kwenye shughuli zilizokusudiwa, kwakuzingatia kuwa Mifuko hiyo ipo kisheria na Bungelilishaidhinisha matumizi ya fedha husika kwenye Mifukohusika.

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Mheshimiwa Spika, aidha, ukifuatilia Taarifa yaMkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali wa mwaka wa fedha2016/2017, utaona kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)ilikusanya kiasi cha Shilingi trilioni 1.67 kama tozo ya ushuruuliokusanywa kwa niaba ya Taasisi zingine. Makusanyo hayoyanahusu tozo za barabara, tozo ya petroli, ada yamaendeleo ya maji, tozo ya maendeleo ya reli na tozo yabandari. Hata hivyo, ilibainika kuwa, kati ya makusanyo yotehayo, kiasi cha shilingi bilioni 410, hazikuweza kuwasilishwakwenye Taasisi husika kinyume na matakwa ya sheria. Kamatiinaishauri Serikali kwamba pindi fedha zinapokusanywa naMamlaka ya Mapato na kupelekwa katika Akaunti yaMapato iliyoko Benki Kuu, fedha hizo zikitoka ziende moja kwamoja kwenye Mifuko husika na badala ya kusubiria tena kibalikutoka Wizara ya Fedha na Mipango kama inavyofanya sasa.

Mheshimiwa Spika, utendaji kazi katika kikosi cha kodi(Task Force). Kamati ya Bajeti ilikuwa na vikao mbalimbali naSekta Binafsi ambapo kupitia vikao hivyo masuala mbalimbaliyanayohusu changamoto ya kikodi zinazowakabili zilijadiliwa.Pamoja na mambo mengine Sekta Binafsi imekuwaikilalamikia utendaji kazi wa Kikosi Kazi cha Kodi hasa kwaupande wa idadi ya wajumbe wa Sekta Binafsiwanaoruhusiwa katika kikosi hicho; Pili, ufinyu wa mudawanaopewa kujadili masuala ya kodi; na Tatu, mapendekezomengi kutofanyiwa kazi na Serikali bila ya kutoa sababumaalum au mrejesho kwa wadau.

Mheshimwa Spika, ieleweke kwamba uwepo waSekta Binafsi ulikuwa ndio msingi madhubuti wa Serikalikukusanya mapato ili iweze kuhudumia wananchi. Kwakuzingatia hilo, Kamati inaishauri Serikali kuangalia upyamuundo wa Kikosi Kazi hicho ili kuondoa upungufu uliojitokezapamoja na kuangalia upya sera ya utozaji kodi katikamawanda mapana ya kiuchumi na ya kijamii na sio katikaukusanyaji wa mapato tu.

Mheshimiwa Spika, uendelezaji wa Sektazinazochangia kwa kiasi kikubwa Mapato ya Serikali. Katikamuda tofauti tofauti Kamati imekuwa ikishauri Serikali

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

kuhakikisha kwamba inaendeleza Sekta zinazochangia kwakiasi kikubwa mapato ya Serikali lakini hali imekuwa siyo hivyo.Mfano Sekta ya mawasiliano kwa mujibu wa Taarifa ya TCRAinaonesha watu zaidi ya milioni 2.5 wameondoka katikamfumo wa usafirishaji wa fedha kwa njia ya kielectroniki.

Mheshimiwa Spika, aidha, mapato yatokanayo naushuru wa usafirishaji wa fedha na bidhaa zinazotozwa ushuruwa bidhaa kama pombe kali (spirits) zimeshuka kwa asilimia30. Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuhakikisha kwambasera zake za kikodi kwa sekta zinazokua ziwe zina lengo lakulea na kuendeleza sekta hizo na sio kukusanya kodi kiasiambacho kinaathiri hata ukuaji wa sekta husika.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Utawala wa Kodi(Institute of Tax Administration) kimechaguliwa na Jumuiyaya Afrika Mashariki kuwa kituo cha Umahili cha Masuala yaMasomo ya Kodi na Forodha (Centre of Excellency). Kamatiinaipongeza Serikali kwa kuratibu na kuisimamia vyemashughuli za Chuo cha Utawala wa Kodi kupitia Mamlaka yaMapato (TRA). Hata hivyo, kwa sasa eneo la chuo hicho nifinyu na miundombinu yake haijawa ya kisasa ili kukiwezeshakukidhi ubora wa kimataifa katika masuala ya kodi na ushuruwa forodha. Kamati inaishauri Serikali kuongeza Bajeti kwachuo hiki ili kiweze kutanua na kujenga Campus mpya katikaeneo la Chuo la Misugusugu pamoja na kununua vifaa vyakuboresha miundombinu ya chuo ili kukidhi vigezo vyakimataifa.

Mheshimiwa Spika, hitimisho, napenda kuwashukuruWajumbe wote wa Kamati, kwa kuchambua na kutoa maonina mapendekezo mbalimbali yaliyowezesha kuboreshataarifa hii hatimaye kuletwa mbele ya Bunge lako Tukufu.Aidha, naomba nitumie nafasi hii kuwatambua Wajumbe waKamati ambao wameorodheshwa hapo chini kwa kaziwanayofanya.

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru MheshimiwaDkt, Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango naMheshimiwa; Mheshimiwa Dkt, Ashatu K. Kijaji, Naibu Waziri

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

wa Fedha na Mipango; Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuupamoja na wataalam wote wa Wizara ya Fedha na Mipangokwa kuwa tayari kutoa ufafanuzi na kupokea maoni naushauri kutoka kwa Wajumbe wa Kamati wakati wote wamijadala ya makadirio haya. Aidha, Kamati inatoa shukranikwa Taasisi na Idara zote zilizo chini ya Wizara ya Fedha naMipango na wadau wa Sekta Binafsi kwa ushirikianowalioutoa kwa Kamati katika kipindi chote cha utekelezajiwa majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee tunaombakukushukuru wewe binafsi, pia kumshukuru Mheshimiwa Dkt.Tulia Akson, Naibu Spika; Ndugu Stephen Kagaigai, Katibuwa Bunge; pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bungekwa kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Aidha, kwa namna ya pekee tunapenda kuwashukuruSekretarieti ya Kamati ya Bajeti ikiongozwa na KaimuMkurugenzi, Ndugu Lina Kitosi; Kaimu Mkurugenzi Msaidizi,Ndugu Michael Kadebe; na Makatibu wa Kamati hii NduguGodfrey Godwin, Emmanuel Rhobi, Lilian Masabala naMaombi Kakozi kwa kuratibu shughuli za Kamati pamoja nakutoa ushauri wa kitaalam na hatimaye kukamilika kwataarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya naombaBunge lako Tukufu sasa lijadili na kuidhinisha Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipangopamoja na Mafungu nane (8), yaliyo chini ya Wizara kwaMwaka wa Fedha 2018/2019, kama yalivyowasilishwa naMheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango, naombakuwasilisha na taarifa yote hii basi iingie katika Hansard.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa MakamuMwenyekiti wa Kamati ya bajeti Mheshimiwa Jitu Soni,tunakushukuru sana kwa kusoma vizuri sana maoni ya Kamatiyenu.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUHUSU UTEKELEZAJIWA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKAWA FEDHA 2017/18 PAMOJA NA MAKADIRIO YA MAPATO NAMATUMIZI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19.KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1.0 UTANGULIZI.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (7) na (9) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuhusuutekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwamwaka wa fedha 2017/18 pamoja na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19ambayo inajumuisha Fungu 07 - Ofisi ya Msajili wa Hazina,Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya Fedha, Fungu 13 - Kitengocha Kudhibiti Fedha Haramu, Fungu 21- Hazina, Fungu 22 -Deni la Taifa, Fungu 23 - Mhasibu Mkuu wa Serikali na Fungu50 - Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) (c) chaSheria ya Bajeti ya mwaka 2015 kinaipa mamlaka Kamati yaKudumu ya Bunge ya Bajeti kupitia na kuridhia Makadirio yaMapato na Matumizi ya Mfuko wa Ofisi ya Taifa ya Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Fungu 45). Kamatiilitekeleza jukumu hili na kufanya mashauriano na Serikali namwisho kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfukowa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu haya,Kamati ilifanya vikao na Wizara ya Fedha na Mipango katiya mwezi Machi na Aprili, 2018 Dodoma na kupokea Taarifaya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango naMafungu yaliyo chini yake kwa Mwaka wa Fedha 2017/18pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2018/19.

2.0 MAPITIO YA UJUMLA KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETINA MAJUKUMU YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWAMWAKA WA FEDHA 2017/18

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

2.1. Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa Fedha 2017/18, Wizaraya Fedha na Mipango kwa mafungu yote manane (8)yaliidhinishiwa kutumia jumla ya Shilingi 11,676,591,286,252.00.Kati ya fedha hizo Shilingi 10.261,308,284,511.00 zilikuwa kwaajili ya matumizi ya kawaida ya mafungu yote na Shilingi1,417,433,000,000 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.Aidha, mchanganuo wa fedha za matumizi ya kawaida nikama ifuatavyo Shilingi 72,533,604,000.00 ilikuwa ni kwa ajiliya mishahara, Shilingi 727,341,680,511.00 kwa ajili ya matumizimengineyo na Shilingi 9,461,433,000,000 kwa ajili ya kulipiaDeni la Serikali na Huduma nyingine. Kwa upande wa fedhaza Maendeleo zil izoidhinishwa na Bunge, Shilingi1,374,975,800,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi42,307,201,741.00 ni fedha za nje

Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia mwezi Februari Wizara yaFedha na Mipango pamoja na mafungu yake ilikuwaimepokea jumla ya Shilingi 7,212,352,493,767.63 sawa naasilimia 62.2 ya Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge. Kati ya fedhahizo Shilingi 7,106,866,350,742.37 sawa na asilimia 72 ya lengozilikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi69,587,632,847 zilikuwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleosawa na asilimia 5 tu ya Bajeti.

2.2. Utekelezaji wa Bajeti kwa mafungu ya Wizara yaFedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Mheshimiwa Spika, hotuba iliyotolewa na Waziri wa Fedhana Mipango imetoa taswira halisi ya utekelezaji wa bajeti yamafungu yake manane kwa mwaka wa fedha 2017/18.Kamati imefanya uchambuzi katika mafungu manane yaliyochini ya Wizara hii na kuona kuwa baadhi ya mafungu yaWizara yamepata fedha za kutosha na hivyo kutekelezamajukumu yake kikamilifu. Vilevile, kuna mafungu ambayohayakupatiwa fedha za kutosha hivyo kuathiri utendaji kaziwake. Hata hivyo, hali sio nzuri kwa upande wa utolewaji wafedha za maendeleo kwenye mafungu yote Nane (rejeajedwali namba moja)

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Spika, ukirejea Jedwali namba 1, utaona kuwahadi kufikia mwezi Machi 2018; kati ya Mafungu manane (8)yaliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ni mafungumawili tu yalikuwa yamepokea fedha zaidi ya asilimia 60 yaBajeti iliyoidhinishwa na Bunge (Matumizi ya Kawaida naMiradi ya Maendeleo). Mafungu yaliyopokea zaidi ya asilimia60 ni; Fungu 22 - Deni la Taifa na Fungu 10 Tume ya Pamojaya Fedha. Aidha, Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango,Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali naFungu 23 - Mhasibu Mkuu wa Serikali yamepokea fedha chiniya asilimia 60 kwa kipindi husika. Kwa upande wa Fungu 7 -Msajili wa Hazina (17.25) na Fungu 21 – Hazina (21.26) hali yautolewaji wa fedha kwa mafungu haya sio ya kuridhisha hatakidogo ukilinganisha na utekelezaji wa majukumu ya msingiwa mafungu haya. Katika utekelezaji wa miradi yaMaendeleo hakuna hata fungu moja ambalo limepokeaBajeti ya Maendeleo kwa zaidi ya asilimia 50.

Mheshimiwa Spika, tathmini inaonesha kuwa mwenendo waugawaji wa fedha kwa baadhi ya mafungu ya Wizara yaFedha na Mipango sio wa kuridhisha. Hii ni dhahiri kuwautekelezaji wa shughuli nyingi za Wizara hii umeathirika kwakiasi kikubwa ukizingatia kuwa mgawanyo na wajibu waSerikali (Government Instrument) kwa Wizara ya Fedha naMipango ni kutafuta na kusimamia ukusanyaji wa mapatopamoja na kuandaa na kusimamia utelekelezaji wa bajetiya Serikali kwa mafungu mbalimbali. Kamati inaona kuwamwenendo huu wa utolewaji wa fedha kwa mafungu yakehautoi tija kwa mafungu husika kutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, Mathalani, Ofisi ya Msajili wa Hazina inajukumu la Kusimamia Mashirika ya Umma na imepokeaasilimia 17.25 tu ya Bajeti iliyoidhinishiwa na Bunge. Ni vizuriBunge lijiulize kwa Bajeti hii, je Ofisi hii itawezaje kutimizamajukumu yake ya msingi? Kamati ya Bajeti inajiuliza kuwa,kama Wizara ya Fedha na Mipango imeshindwa kuwezeshakuwa baadhi ya mafungu yake kupata fedha za kutosha kwaajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya msingi, itawezajekuhakikisha mafungu ya Wizara nyingine kupata fedha zakutosha kutekeleza majukumu yao ya msingi? Kamati ya

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

Bajeti inaona kuwa bado kuna changamoto kubwa kwaWizara hii kuweza kusimamia vizuri sera, sheria, kanuni nataratibu za fedha (Monetary Policy) na Sera ya Mapato naMatumizi (Fiscal Policy)

JEDWALI NAMBA 1. Utekelezaji wa Bajeti Kwa Mafungu yaWizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2017/18

FUNG

U JINA LA FU

NGU 

BAJETI ILIYOIDHINISHWA 

2017/18 

 

FEDHA ILIYOTOLEWA HADI 

MACHI , 2018 

ASILM

IA 

MATUM

IZI YA

 KAW

AIDA

 NA

 MAEND

ELEO HADI 

MACHI, 2018 

ASILIMIA  

KIASI CHO

TE 

KILICHO

TOLE

WA 

 Aina ya Matum

izi 

Matum

izi ya 

kawaida

Maendeleo

Matum

izi ya 

Kawaida 

Maendeleo

Matum

izi ya 

Kawaida 

Maendele

o (%)

50 

Wizara ya Fedha na 

Mipango 

55,039,643,000

11,570,500,000 41,171,372,242.5

6 3,799,510,000 

74.80

32.84

 53.63

 

21 

Hazina 

570,429,248,00

0 1,395,636,701,

741 

339,050,386,897.

84 

63,125,192,84

6.70 

59.44

4.52 

21.26

 

22 

Deni la Taifa 

9,519,322,300,0

00 

‐ 6,821,053,221,47

2.90 

‐71.69

‐ 67.88

 

13 

Kitengo 

cha 

Udhibiti 

Fedha H

aram

u 1,515,586,000 

‐ 869,078,757.39 

‐ 57 

‐ 57.00

 

10 

Tume ya P

amoja ya 

Fedha 

1,386,817,511 

‐ 800,399,408 

‐57.71

65.00

 

07 

Msajili wa H

azina 

104,917,488,00

0 2,000,000,000 

17,695,190,675 

750,000,000 

16.87

37.5 

17.25

 

23 

Idara 

ya 

Mhasibu 

Mkuu w

a Serikali 

45,960,838,000

3,600,000,000 

36,323,843,086 

1,171,000,000 

79.03

32.53

 57.43

 

45 

Ofisi 

ya 

Taifa ya 

Ukaguzi w

a Hesabu ya 

Serikali 

49,832,948,000 

11,800,948,000

31,923,227,835 

778,195,000 

64.06

6.59 

57.39

 

 

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

FUNG

U JIN

A LA FU

NGU 

BAJETI ILIYOIDH

INISHW

A 2017/18 

 

FEDH

A ILIYO

TOLEWA HA

DI 

MACHI , 2

018 

ASILM

IA  

MATUM

IZI YA KA

WAIDA

 NA

 MAEND

ELEO

 HAD

I MACHI, 2018 

ASILIMIA  

KIASI CHO

TE 

KILIC

HOTO

LEWA 

 Aina ya

 Matum

izi 

Matum

izi ya 

kawaida

Maendeleo

Matum

izi ya

 Kawaida 

Maendeleo

Matum

izi ya 

Kawaida 

Maendele

o (%)

50 

Wiza

ra ya Fedha 

na 

Mipango 

55,039,643,000 

11,570,500,000 41,171,372,242.5

6 3,799,510,000 

74.80 

32.84 

53.63 

21 

Hazin

a 570,429,248,00

0 1,395,636,701,

741 

339,050,386,897.

84 

63,125,192,84

6.70 

59.44

4.52 

21.26 

22 

Deni la Taifa 

9,519,322,300,0

00 

‐ 6,821,053,221,47

2.90 

‐ 71.69

‐ 67.88 

13 

Kitengo 

cha 

Udhibiti 

Fedha Haramu 

1,515,586,000 

‐ 869,078,757.39 

‐ 57 

‐ 57.00 

10 

Tume 

ya Pamoja 

ya 

Fedha 

1,386,817,511 

‐ 800,399,408 

‐ 57.71 

 65.00 

07 

Msajili w

a Hazin

a 104,917,488,00

0 2,000,000,000 

17,695,190,675 

750,000,000 

16.87

37.5 

17.25 

23 

Idara 

ya 

Mhasib

u Mkuu wa Serikali 

45,960,838,000 

3,600,000,000 

36,323,843,086 

1,171,000,000

79.03

32.53 

57.43 

45 

Ofisi 

ya 

Taifa 

ya 

Ukaguzi w

a Hesabu ya 

Serikali 

49,832,948,000 

11,800,948,000

31,923,227,835 

778,195,000 

64.06

6.59 

57.39 

   

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

2.2.1. Fungu 50 -Wizara ya Fedha na Mipango

Mheshimiwa Spika, Fungu hili lina jukumu kubwa la kuratibuna kusimamia shughuli za utawala (Wizara pamoja na taasisizake), ununuzi wa umma, mali za Serikali, ukaguzi wa ndaniserikalini pamoja na kuratibu na kusimamia huduma zakisheria. Kwa mantiki hii, fungu hili ndio kitovu cha Wizara yafedha na Mipango. Hadi kufikia mwezi Machi 2018 fungu hilipamoja na umuhimu wake lilikuwa limepokea jumla yaShilingi 44,970,882,242.56 sawa na asilimia 67 ya Bajetiiliyoidhinishwa, kati ya fedha hizo Shilingi 41,171,372,242.56 nimatumizi ya kawaida na shilingi 3,799,510,000 ni fedha zamaendeleo. . Kamati inaona kuwa kutolewa kwa fedhakidogo au kuchelewa kutolewa fedha kwa wakati kwa funguhili kunaathiri utekelezaji wa majukumu ya msingi kwa Wizaraya Fedha na Mipango na hivyo kuathiri shughuli za kiutawalandani ya Wizara pamoja na upelekaji wa fedha kwa mafunguya Wizara nyingine. Kamati inaishauri kuwa, Wizara itekelezevema mipango yake ili kufikia malengo iliyojiwekea ikiwa nipamoja na kuhakikisha mafungu mengine ya Wizarayanapata fedha za bajeti zao kama zilivyoidhinishwa naBunge.

2.2.2. Fungu 21- Hazina

Mheshimiwa Spika, jukumu kubwa la hazina ni kuandaa nakusimamia sera ya fedha (monetary policy), sera ya mapatona matumizi (fiscal policy), kuandaa na kusimamia utekelezajiwa Bajeti ya Serikali pamoja na kusimamia na kudhibiti Denila Taifa. Katika mwaka wa Fedha 2017/18 halikuwezakupokea fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, kwanitakwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwezi Februari 2018kati ya kiasi cha Shilingi 1,395,636,701,741 kilichoidhinishwana Bunge, fungu hili lilikuwa limepokea kiasi cha Shilingi63,125,192,846.70 tu (sawa na asilimia 4.51). Baadhi ya miradihaijatekelezwa kutokokana na kukosekana kwa fedha zamaendeleo. Jedwali Namba 2 linaonyesha mchanganuohapo chini:-

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Jedwali Na 2: Utolewaji wa fedha za Maendeleo kwa Miradiya Fungu 21

Chanzo Wizara ya Fedha na Mipango fungu 21

Mheshimiwa Spika, Kati ya miradi saba iliyoainishwa hapojuu ni mradi mmoja tu wa PFMRP ndiyo umepokea fedhawakati miradi iliyobaki sita (6) haijapokea fedha hata kidogo.Kamati ya Bajeti inashauri ihakikishe inapeleka fedha kwenyemiradi husika kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, Hazina ndio inaratibu na kusimamiamifumo mbalimbali ya kibajeti. Hata hivyo, imekuwa na tabiaya kuanzisha na kusitisha mifumo mingi ya ukusanyaji,usimamizi, na ufuatiliaji wa masuala ya Bajeti ambayoimekuwa ikiigharimu Serikali fedha nyingi katika kuiandaa,kuifundisha na kuitumia. Kamati imebaini kuwa kuna mifumombalimbali ya ukusanyaji, usimamizi na ufuatiliaji wa masualaya bajeti na programu mbalimbali ambayo haijahuishwapamoja na hivyo kuongeza gharama na kero kwa wadau.Mfano, hapo awali tulikuwa na Mfumo wa Strategic BudgetAllocation System (SBASS) na sasa tumehamia kwenyeCentral Budgeting Management System (CBMS); Kulikuwa naMfumo wa Ukusanyaji wa Kodi ya Majengo na Mabango waSerikali za Mitaa uitwao Local Government RevenueCollection System (LGRCIS) Baada ya ukusanyaji wa mapatokuhamia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), naowakaanzisha mfumo mpya wa Property Rate Management

 

Na Mradi  Bajeti  Fedha zilizotolewa 

    Ndani  Nje  Ndani  Nje 1.  Village  empowerment 

Fund  60,000,000,000  ‐  0  ‐ 

2.  Regional  Support  on Budget Process  

100,000,000  135,354,000  0  0 

3.  Public  Management Reform  Programme (PFMRP)  

1,2000,000,000  1,000,000,000  0  328,080,000 

4.  Global  Fund Management Project  

0  2,293,002,878  0  0 

5.  Program Support to NAO     1,195,020,526  0  0 6.  PPP facilitation Fund   5,000,000,000  0  0  0 7  Poverty  Monitoring 

Master Plan (PMMP)  200,000,000  0  0  0 

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

System (PRMS). Hivi sasa, Serikali inaandaa Mfumo mwinginewa ufuatiliaji wa umasikini Poverty Monitoring System (PMS).Kamati inashauri Serikali kuangalia uwezakano wa kuhuishamifumo iliyopo ili kupunguza gharama na kukidhi mahitaji yawadau kwa muda mrefu badala ya kubadilisha mara kwamara.

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa, katika mwaka wafedha 2017/18 Bunge li l i idhinisha kiasi cha shilingi60,000,000,000 kwa ajili ya kufanya majaribio ya programuya uwezeshaji wananchi vijijini kupitia TAMISEMI. Hata hivyo,hadi mwezi Machi 2018 fedha hizo zilikuwa hazijatolewa naSerikali. Aidha, Serikali iliahidi kuweka utaratibu maalumutakaotumika katika kuchagua vijiji hivyo ili kutekelezaprogramu hiyo. Kamati haijajulishwa kuhusu utoaji wa fedhahizo kupelekwa kwenye maeneo husika. Hivyo inashauriSerikali kutekeleza program hii ikiwa pamoja na kutoa fedhahizo na kukamilisha utaratibu huo haraka utakaozingatiausawa kwa Mikoa yote, hali ya umasikini, aina ya shughuli naushirikishwaji wa vyombo vya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ilikupata taswira itayakowezesha program hii kutekelezwa kwaufanisi.

2.2.3. Fungu 22 – Deni la Taifa

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua na kuthamini umuhimuwa kuwepo kwa kitengo cha Usimamizi wa Deni la Taifa ndaniya Wizara ya Fedha na Mipango kikiwa na jukumu lakuhakikisha kinatunza na kusimamia taarifa muhimu zamadeni (Public Debt Database) pamoja na kusimamiakikamilifu ulipaji wa madeni ya ndani na nje (Domestic andExternal Debts). Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mweziFebruari 2018, Serikali ilikuwa imelipa jumla ya madeni ShilingiTrilioni 5.54 kati ya fedha hizo Shilingi Trilioni 4.094 ni madeniya ndani na Shilingi Trilioni 1.446 ni madeni ya nje. Kulinganana Tathmini ya Uhimilivu wa Deni (Debt Sustainability Analysis)unaonyesha Deni letu ni himilivu kwa asilimia 34.4ukil inganisha na ukomo wa asil imia 56. Hata hivyoukilinganisha makusanyo ya Ndani yanayotokana na kodi namalipo ya Deni la Taifa utaona kuwa, mpaka mwezi Desemba

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

2017 makusanyo ya Ndani yalikuwa Shilingi Trilioni 7.678 naMalipo ya Deni Mpaka Februari ya Shilingi Trilioni 5.54 utaonakwamba kiasi kikubwa cha makusanyo ya fedha za ndanikinakwenda kulipa Deni la Taifa.

Mheshimiwa Spika, Napenda Bunge lako tukufu lifahamukuwa deni la Serikali limeongezeka kwa asilimia 16.2 katikakipindi cha miezi 12 yaani kuanzia mwezi Machi 2017 hadimwezi Machi 2018. Licha ya kuwepo kwa mikakati mbalimbaliya kudhibiti ongezeko la deni la Serikali, bado mikakati hiyohaijaweza kuwa na matokeo chanya. Miongoni mwamikakati hiyo ni Mkakati wa Ushirikiano wa Maendeleo.Kamati inaishauri Serikali kutekeleza Mkakati wa Ushirikianowa Maendeleo (Development Cooperation Framework-DCF)wenye lengo la kupanua wigo wa upatikanjai wa mikopona misaada yenye masharti nafuu na kuongeza mitaji yauwekezaji wa moja kwa moja. Aidha, Serikali ifanyemazungumzo na wahisani mbalimbali wakiwemo wale wa‘Non Paris Club’ ili kuona namna ya kuweza kupunguziwa aukusamehewa Deni hilo na hivyo kutoa nafuu kwa mapatoya ndani kuweza kugharamia Bajeti ya Serikali.

2.2.4. Fungu 13 – Kitengo cha kudhibiti Fedha Haramu

Mheshimiwa Spika, kitengo cha udhibiti wa fedha haramu(Financial Intelligence Unit) kimeanzishwa kwa mujibu waKifungu cha 4 cha Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu yaMwaka 2006 (The Anti-Money Laundering Act). Kifungu chaSita cha Sheria hiyo kinaelezea majukumu na kazi za Kitengohicho ikiwa pamoja na kufuatilia ufadhili wa kigaidi. Pamojana majukumu haya makubwa, kitengo hiki badokinatengewa bajeti ndogo na hivyo kushindwa kutekelezamajukumu yake ipasavyo. Mathalani, Katika mwaka wafedha 2017/18 kitengo kilitengewa shilingi 63,000,000 tu kwaajili ya uchambuzi wa Taarifa mbali mbali za miamala shuku(suspicious transations) inayohusu fedha haramu na ufadhiliwa kigaidi.

Mheshimiwa Spika, kitengo hiki ni muhimu pia katika kudhibitiupotevu wa fedha kupitia njia haramu, kwani utafiti wa taarifa

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

ya Illicit Financial Flow 2011 maarufu kama Ripoti ya Mbekiinaonyesha kwamba Nchi za Afrika kwa mwaka zinapotezakiasi cha takribani Dola za Marekani Billioni 50 kupitia njiaharamu. Kamati inashauri fungu hili liongezewe bajeti yake ililitekeleze majukumu yake vizuri.

2.2.5. Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya FedhaMheshimiwa spika, Tume ya pamoja ya Fedha imeanzishwakwa mujibu Ibara 134 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. Majukumu ya Tume hiyo yameainishwa katikaIbara ya 134(2) ambayo ni pamoja na kutunza akaunti yapamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuchambuamapato na matumizi yanayohusu utekelezaji wa masuala yaMuungano pamoja na kutekeleza majukumu mengineitakayopangiwa na Rais. Hadi kufikia mwezi Februari 2018,Tume ilikuwa imepokea kiasi cha shilingi milioni 800.399 katiya shilingi bilioni 1.386 iliyoidhinishiwa (Sawa na asilimia 58 yafedha yote). Kutokana na majukumu yake ya Msingi Kamatiinashauri Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inatoafedha iliyopangwa kwa tume hii ili iweze kukamilishamajukumu yake ya kimsingi kama yalivyoainishwa kwenyeKatiba.

2.2.6. Fungu 7 - Ofisi ya Msajili wa HazinaMheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mujibu waSheria ya Msajili wa Hazina Sura ya 370; Ofisi hii ina jukumu lakusimamia na kulinda mitaji na uwekezaji wa Serikali katikamashirika na taasisi za umma. Pamoja na majukumu mengineOfisi ya Msajili wa Hazina inasimamia ukusanyaji wa mapatoyasiyo ya kodi kwenye mashirika ya umma kwa niaba yaSerikali. Takwimu zinaonesha hadi kufikia Mwezi Februari, Ofisihii imekusanya mapato yatokanayo na asilimia 15 ya mapatoghafi kiasi cha Shilingi bilioni 498.2 kati ya Shilingi bilioni 524.6zilizopangwa kukusanywa katika mwaka wa Fedha 2017/18(sawa na asilimia 94.9 ya lengo). Pamoja na Ufanisi huumkubwa bado Wizara ya Fedha na Mipango imetoa kiasikidogo tu cha fedha (asil imia 17.25 ya fedha yoteiliyoidhinishwa na Bunge) kwa ofisi hii ili iweze kutekelezamajukumu yake.

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Mheshimiwa Spika, aidha, katika mwaka wa fedha 2017/18,Fungu hili lilitengewa kiasi cha Shilingi bilioni 95.0 kwa ajili yakusaidia Mashirika ya Umma yenye matatizo ya Kimtaji. Hatahivyo, hadi kufikia mwezi februari mwaka huu, Serikali imetoakiasi cha Shilingi Bilioni 12.998 zilikuwa zimepokelewa. Hii nichangamoto kubwa kwa Serikali katika kuyawezeshamashirika yake ili yaweze kufanya kazi kwa ufanisi. Kamatiinaikumbusha Serikali kuwa ‘Ukitaka kukusanya mapato zaidilazima uwekeze zaidi sio kutegemea mapato bila yakuwekeza’. Aidha, Kamati inashauri Serikali kuangalia upyautaratibu wa kukusanya asilimia 15 ya Pato ghafi bilakuangalia gharama za uzalishaji kwa kuwa kwa kufanya hivyokuna baadhi ya mashirika yameanza kujiendesha kwa hasarana hivyo kuwa mzigo kwa Serikali hasa kwa yale ambayoyanategemea ruzuku kutoka kwa Serikali.

2.2.7. Fungu 23- Mhasibu Mkuu wa SerikaliMheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Idara hii kwa kuwezakusimamia na kuboresha mfumo wa malipo SerikaliniIntegrated Financial Management system (IFMS). Aidha,Kamati inasisitiza Idara hii kuhakikisha inaendelea kusimamiamatumizi ya fedha za Serikali na kutoa miongozo ya mifumoya kifedha kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti na Sheria yaUsimamizi wa Fedha za Umma. Hadi kufikia mwezi Machi 2018,Fungu hili limepokea kiasi cha asilimia 57.43 ya fedha yoteiliyoidhinishwa na Bunge. Kama ilivyojitokeza kwenyemafungu mengine, maoteo ya mahitaji ya fedha kwamafungu mbalimbali hayakuzingatia mahitaji halisi namajukumu ya kazi ya mafungu husika, hivyo ukomouliowekwa umeathiri shughuli za utekelezaji wa mafunguhusika.

Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya UkaguziMheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2017/18 Mfuko waOfisi ya Taifa ya Ukaguzi uliidhinishiwa jumla ya kiasi chaShilingi Bilioni 73.63 kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 44.51zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida (OC), ShilingiBilioni 17.31 kwa ajili ya mishahara na Shilingi Bilioni 11,80 kwaajili ya miradi ya maendeleo ambapo fedha za ndani zilikuwashilingi Bilioni 8.00 na shilingi 3,800,948,000 ni fedha za nje.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Ofisi ilikadiriwa kukusanya kiasi cha shilingi 12,000,000,000pamoja na fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali zikiwa kamaruzuku ya Serikali kiasi cha shilingi 32,519,192,267.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Februari, 2018 Ofisiilikuwa imepokea jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 37.36 kutokaHazina. Kati ya kiasi hicho, shilingi 27,505,331,083.85 ni kwaajili ya OC sawa na asilimia 73.6 ya bajeti iliyotengwa (ruzukuya Serikali), shilingi 9,084,318,726 kwa ajili ya mishahara sawana asilimia 52.5 ya makadirio na shilingi 778,195,000 tuambazo ni fedha za nje kwa ajili ya miradi ya maendeleoikiwa ni asilimia 20 ya makadirio ya fedha za nje na asilimia6.6 ya bajeti nzima ya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwahadi kufikia mwezi Februari 2018, Wizara ya Fedha naMipango ilikuwa haijaweza kutoa kiasi chochote cha fedhaza ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleokwa fungu hili. Kufuatia changamoto hiyo, Ofisi hii imeshindwakutekeleza miradi yake ya maendeleo iliyopangwa katikamwaka 2017/18; mathalani kushindwa kukamilisha ujenzi wamajengo mapya ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa. Hapo awaliSerikali ilikubali kutoa kiasi shilingi 8,000,000,000 kila mwakaambazo ni fedha za ndani kwa ajili ya ujenzi wa majengomawili. Hata hivyo, fedha hizo zilikuwa hazijatolewa mpakamwezi Machi 2018.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa ukusanyaji wa maduhuli,hadi kufikia mwezi Februari 2018, Ofisi hii imeweza kukusanyamaduhuli yenye jumla ya shilingi 9,555,780,296 ikiwa ni sawaasilimia 80 ya makadirio ya mwaka. Kamati inaipongeza Ofisiya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwaukusanyaji huo wa maduhuli na ikiwezekana kuongeza juhudiili kuvuka lengo lililowekwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada za Ofisi hii katikakukusanya maduhuli na kusimamia ukaguzi wa Wizara nataasisi za umma, bado mwenendo wa upatikanaji wa fedhaza matumizi mengineyo na Maendeleo kutoka Mfuko Mkuuwa Serikali sio wa kuridhisha na haukidhi utekelezaji wa

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

majukumu ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabuza Serikali. Suala hili linasababisha Ofisi kushindwa kutekelezamajukumu yake ipasavyo kulingana na viwango vyakimataifa vya kiukaguzi.

3.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARAYA FEDHA NA MIPANGO PAMOJA NA TAASISI ZILIZO CHINIYAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19.

3.1 Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wafedha 2018/19.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na Mipango katikaMwaka wa Fedha 2018/19 imekadiriwa kutumia jumla yaShilingi 12,106,390,621,500 kwa mafungu yote manane (8).Kati ya fedha hizo, Shilingi 10,813,501,149,000 ni kwa ajili yaMatumizi ya Kawaida na Shilingi 1,295,212,539,500 ni kwa ajiliya Matumizi ya Maendeleo. Matumizi ya Kawaidayanajumuisha kiasi cha Shilingi 313,677,166,000 kwa ajili yamishahara, Shiligi 495,343,983,000 kwa ajili ya MatumiziMengineyo (OC) na Shilingi 10,004,480,000,000 ni kwa ajili yaulipaji wa Deni la Taifa na Huduma nyingine. Aidha kwaupande wa fedha za Matumizi ya Maendeleo, Wizaraimepanga kutumia kiasi cha Shilingi 1,295,212,539,500.

Jedwali Namba 2. Maombi ya Fedha Kwa Wizara ya Fedhana Mipango na Mafungu yaliyo Chini Wizara kwa Mwaka2018/19.

Fungu  Matumizi Mengineyo (OC) 

Mishahara  Miradi ya Maendeleo 

Jumla 

50  22,632,514,000  34,390,413,000  28,790,817,000  85,813,744,000 21  295,550,354,000  242,567,027,000  1,247,611,267,500  1,785,728,648,500 22  10,004,480,000,000  9,226,140,000  ‐  10,004,480,000,000 13  2,015,586,000  0  248,363,000  2,263,949,000 10  1,580,142,000  574,933,000  ‐  2,155,075,000 07  102,229,786,000  2,362,279,000  1,650,000,000  106,917,488,000 23  38,816,734,000  7,908,675,000  3,200,000,000  49,925,409,000 45  32,518,867,000  16,647,699,000  13,712,092,000  69,106,308,000 

Jumla  10,499,823,983,000  313,677,166,000  1,295,212,539,500  12,106,390,621,500 

 

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Mheshimiwa Spika, makadirio ya mapato na matumizi hayayanahusisha pia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali (Fungu 45) ambapo kwa mujibu wa kifungu cha9(1) kipengele (a) cha Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015,Kamati ya Bunge ilikutana na Waziri wa Fedha na Mipangopamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikaliili kujadiliana na kufanya mashauriano kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi ya Ofisi hii kwa mwaka wa fedha 2018/19. Ofisi kwa mwaka wa fedha 2018/19 imelenga kuimarishaukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali kuimarishauwajibikaji na uwazi kwenye matumizi ya rasilimali za umma.

Mheshimiwa Spika, kwa muhtasari, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi(NAOT) kwa mwaka wa fedha 2018/19 imeidhinishiwa fedhazake kama walivyoomba kwenye mapendekezo ya bajetiyao yenye jumla ya shilingi 69,106,308,000. Kati ya fedha hizo,shilingi 16,647,6999,000 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi,shilingi 32,512,867,000 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali,shilingi 6,227,649,907 ni fedha kutoka ukaguzi wa Wakala/Taasisi na Mashirika ya Umma na shilingi 13,712,092,000.

Mheshimiwa Spika, Hatua hii ilifikiwa baada ya mashaurianona Wizara ya Fedha na hivyo kuongeza kiasi cha shilingi6,232,325,000 kwenye Mfuko husika na kufikia kiasi hicho chafedha. Kamati ya Bajeti inaipongeza Wizara ya Fedha naMipango kwa hatua hii muhimu. Aidha, Kamati badoinasisitiza umuhimu wa kuhakikisha Mfuko huu, unapatiwarasilimali fedha za kutosha zinazoendana na mahitaji halisiya Mfuko ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kikatiba.

4.0 MAONI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI YA BUNGE YABAJETI

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kupitia utekelezaji waBajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisizake kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 pamoja na maombi yaFedha ya mafungu husika kwa Mwaka wa Fedha 2018/19;Kamati inapenda kutoa maoni na mapendekezo yake kamaifuatavyo:-

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

4.1 Mwenendo wa Utolewaji wa Fedha kwa Mafunguyaliyochini ya Wizara ya Fedha na Wizara nyinginekama yalivyoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, tathmini ya ujumla ya mwenendo wautowaji wa fedha za utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/18kwa mafungu yaliyo chini ya Wizara ya Fedha unaoneshakuwa sio wa kuridhisha kwa baadhi ya mafungu. Hadi kufikiaMwezi Machi 2018, kati ya Mafungu manane (8) yaliyo chiniya Wizara ya Fedha na Mipango, mafungu mawili tu yalikuwayamepokea fedha zaidi ya asilimia 60 ya Bajeti iliyoidhinishwana Bunge kwa upande wa Matumizi ya Kawaida na Miradiya Maendeleo. Mafungu yaliyopokea zaidi ya asilimia 60 ni;Fungu 22 - Deni la Taifa na Fungu 10 Tume ya Pamoja yaFedha. Kamati inaona kuwa mwenendo huu wa utolewajiwa fedha kwa mafungu yake hautoi tija kwa mafungu husikakutekeleza majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, Wizara imejitahidi kutoa fedha zamatumizi ya kawaida kwa mafungu mbalimbali ya SerikaliKuu na Mikoa kwa wastani wa asilimia 100. Hata hivyo,pamoja na mwenendo huu mzuri wa utolewaji wa fedhakwenye mafungu husika, bado utekelezaji wa majukumu yamafungu haya unaathiriwa na bajeti isiyojitosheleza kutokanana ukomo wa bajeti uliowekwa na Serikali hapo awali wakatimafungu hayo yakiomba fedha kwa ajili ya kutekelezamajukumu yao. Aidha, kwa upande wa utoaji wa fedha zamaendeleo kwa kipindi cha Mwezi Julai 2017 hadi Machi2018, hali sio ya kuridhisha. Takwimu zinaonesha kuwa kati yamafungu 47 ya Wizara mbalimbali yanayostahili kupata fedhaza maendeleo ni mafungu 16 tu yamepata fedha zaidi yaasilimia 50. Hali hii pia tunaiona kwa upande wa fedha zaMiradi ya Maendeleo kwa baadhi ya mafungu ya Mamlakaza Serikali za Mitaa ukilinganisha na Bajeti waliyoidhinishiwana Bunge.

Mheshimiwa Spika, Kamati inataka Wizara ya Fedha naMipango iangalie namna bora ya kutekeleza majukumu yakena kutatua changamoto za utekelezaji wa Bajeti.

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

4.2 Fungu 66 – Tume ya Mipango

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa Tume ya Mipango(Fungu 66) ilianzishwa kwa Mujibu wa Sheria ya Tume yaMipango ya Mwaka 1989 (iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002);ikiwa chini ya Ofisi ya Rais kwa lengo la kuwa Msimamizi Mkuuwa Mipango ya Serikali ikiwemo kubuni miradi ya maendeleoya kimkakati pamoja na kufuatilia na kufanya tathmini yautekelezaji wa miradi hiyo. Tume hii imeweza kutekelezamajukumu yake kwa ufanisi ikiwa huru chini ya Ofisi ya Rais.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mabadiliko ya muundo waSerikali katika awamu ya tano kwa sasa Tume ya Mipangoimeunganishwa na Wizara ya Fedha na Fungu 66 limefutwana kujumuishwa chini ya Fungu 50 – Wizara ya Fedha naMipango. Kamati inaona kufutwa kwa fungu hili ni kinyumena Sheria hasa ukizingatia kwamba, Tume hii ilikuwa ni ‘thinktank’ ya Serikali na ilikuwa pamoja na majukumu mengine nikuhakikisha kwamba Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025inafikiwa. Kamati inaitaka Wizara ya Fedha na Mipangokurudisha Fungu hili na ikiwezekana kuanzisha Chombomaalumu chini ya Ofisi ya Rais kitakachoshughulikia Mipangoya Taifa. Nchi nyingi Duniani zimefanikiwa kuwa na nguvukubwa ya uchumi kwa kuwa na Tume za Mipango zenyenguvu kubwa ya ushawishi wa mipango na utekelezajipamoja na kupewa kipaumbele kwenye maamuzi yakiuchumi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kuwa, kwa kuwa mfumowa Serikali umebadilika ni vema Serikali ikarudisha Tume yaMipango pamoja na Fungu 66 chini ya Wizara ya Fedha naMipango, kwa lengo la kusimamia na kuendeleza shughulizilizokuwa zinafanywa na Tume ya Mipango. Hatua hii,itasaidia kulinda uhuru wa upangaji wa mipango na usimamiziwa mapato na matumizi ya Serikali ili kuondokana na haliiliyopo sasa amabpo Serikali imekuwa ikiegemea zaidikwenye mapato na matumizi kuliko mipango ya nchi na hivyokutokuwa na uwajibikaji mzuri katika masuala ya kibajeti(checks and balance)

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

4.3 Uhakiki na Ulipaji wa Madeni ya Watumishi naWakandarasi na Wazabuni.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2015/16 Serikaliilichukua hatua madhubuti ya kuhakiki na kulipa madenimbalimbali, hatua ambayo inapongezwa sana na Kamatiya Bajeti. Hadi mwaka wa fedha 2017/18 Serikali imehakikina kulipa jumla ya Shilingi Bilioni 939.5 kwa mchanganuoufuayao; Wakandarasi (Shilingi Milioni Bilioni 618.9), Wazabuni(Shilingi Bilioni 81.82), Watumishi (Bilioni 133.84), WatoaHuduma (Shilingi Bilioni 77.259) na Madeni mengineyo(Shilingi Bilioni 27.595). Pamoja na ulipaji huo wa madeni yaWatumishi bado kuna malalamiko ya baadhi ya Watumishikama Walimu kwamba fedha walizolipwa ni pungufu yamadai halisi wanayoidai Serikali. Kamati inaendelea kuishauriSerikali ni kuhakikisha inakamilisha ulipaji wa madeni yoteyaliyohakikiwa ili kupunguza gharama kwa Serikali hasa kwamadeni yenye ongezeko la riba.

4.4 Ulipaji wa Kodi (Paying Taxes)Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya UNCTAD yaMwaka 2017 inayohusu Mazingira ya Uwekezaji na UfanyajiBiashara, Tanzania inashika nafasi ya 137 kati ya nchi 186 naina mizania ya asilimia 54.04. Moja ya vigezo vianvyotufanyatusifanye vizuri ni suala la ulipaji wa Kodi ambalo tumeshikanafasi ya 154. Kamati imefanya utafiti na kuona kuwa ili tuwena vigezo bora vya kufanya vizuri katika ulipaji wa kodi,mambo yafuatayo hayana budi kufanyika:- Kwanza;kuharakisha kutoa maamuzi ya Kodi kwa Mashauri ambayoyako kwenye Baraza la Rufaa la Kodi, mfano katika mashauri320 yaliyosajiliwa katika Baraza la Rufaa (TRAT-Tax RevenueAppeals Board) ni kesi 99 tu zimetolewa maamuzi sawa naasilimia 31 ya kesi zote; Pili; kuihuisha sekta isiyo rasmi katikamfumo wa kodi ili iweze kulipa kodi stahili na Tatu; kupunguzautitiri wa kodi, tozo na ada usiokuwa na tija kwa wakulimana wafanyabiashara.

Mheshimiwa Spika, pamoja na haya, ni muhimu Serikaliikazingatia kanuni mbalimbali za kikodi kama vile “BestJudgement Rule” ambayo inamtaka mtu anayefanya

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

marekebisho ya makadirio ya Kodi (Adjutment of taxAssesment) aangalie mambo makuu yafuatayo:-. Kwanza,aina ya biashara zinazoshabihiana; Pili, taarifa alizowasilishaanayefanyiwa marekebisho na:- Tatu, ni mazingira ya sokokatika ufanyaji wa biashara.

Mheshimiwa Spika, maofisa wengi wa Kodi wanaofanyatathmini kwa wafanyabiashara (tax assessment) wamekuwahawafuati kanuni hizi na hivyo tathmini wanazofanyazimekuwa za viwango vya juu kuliko uwezo au faida yabiashara husika hali inayosababisha wafanyabiashara wengikufunga biashara, kukwepa kulipa kodi, kurudi kwenye sektaisiyo rasmi au kuhamia nchi jirani na hivyo kupelekeaukusanyaji hafifu wa mapato ya Serikali.

4.5 Utekelezaji wa Miradi kwa Njia ya Ubia baina ya Sektaya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

Mheshimiwa Spika, Bunge lako tukufu lilipitisha Sheria ya UbiaBaina ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma mwaka 2009 marabaada ya kukamilika kwa Sera ya Ubia baina ya Sekta yaUmma na Sekta Binafsi (PPP). Katika utekelezaji wa Bajeti yaFungu 21, imeanishwa miradi mbalimbali iliyo katika hatuaya kufanyiwa upembuzi yakinifu ili itekelezwe kwa njia ya PPP;Miradi hiyo:- Dar Rapid Transport Phase I, Mradi wa uzalishajiwa Madawa na Vifaa Tiba Muhimu, Ujenzi wa Reli yaMchuchuma/ Liganga –Mtwara, Mradi wa Bandari na Kituocha Biashara cha Kurasini. Pamoja na hatua hizi muhimu,Kamati imebaini kuwa maombi mengi ya miradi inasuasuakutekelezwa kwa njia ya PPP kwa sababu zifuatazo:-

Moja; Serikali kuchelewa kuwalipa wakandarasi wanaofanyaUpembuzi yakinifu wa miradi hiyo (feasibility study) mfano Reliya Mchuchuma/ Liganga hadi Mtwara, Dar es Salaam-Tanga-Moshi na Moshi-Arusha-Musoma;

Pili, kuchelewa kufanya maamuzi kwa miradi inayowezakutekelezwa kwa njia ya ubia mfano mradi wa Kituo chaBiashara cha Kurasini ambacho muwekezaji hivi sasaameamua kuwekeza nchi ya jirani. Kamati inaishauri Wizaraya Fedha na Mipango kuhakikisha Kitengo cha PPP kilichopo

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Wizarani kinatekeleza jukumu lake kwa ufanisi la kuratibu nakusimamia maandiko na maombi ya utekelezaji wa miradiya maendeleo kwa njia ya ubia baina ya Sekta ya Umma naSekta Binafsi kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali(Contracting Authorities).

Mheshimiwa Spika, Aidha, Kamati inaishauri Serikali kutengafedha za kutosha kwa ajili ya ‘PPP Facilitation Fund’’. Mfukohuu una jukumu la kutenga fedha kwa ajili ya kuandaamaandiko kwa ajil i ya kubainisha miradi mbalimbaliinayoweza kutekelezwa kwa njia ya ubia na kuhifadhi fedhakwa ajili ya ushiriki wa Serikali kwenye miradi ya ubia.

4.6 Mradi wa Village Empowerment maarufu kama Milioni50 kwa kila Kijiji. (Fungu 21)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17, Wizaraya Fedha na Mipango il itenga kiasi cha Shilingi60,000,000,000 na katika mwaka wa fedha 2017/18 Wizaraimetenga tena Shilingi Bilioni 60,000,000,000 kwa ajili yakufanya utafiti wa majaribio (pilot study) kwa baadhi yamitaa, vijiji, kata na shehia kwa ajili ya kutekeleza Mradi waVillage Empowerment maarufu kama Shilingi 50,000,000 kwakila Kijiji. Mradi huu ulilenga “Kutenga Kiasi cha Shilingi50,000,000 kwa Kila Kijiji kwa ajili ya kukopesha Vikundi vyaUjasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS)katika vijiji husika”. Hata hivyo, fedha hizo zilizotengwa katikamiaka yote hakuna fedha yoyote iliyotolewa licha ya Serikalikuahidi kuweka utaratibu maalumu wa utekelezaji wa mradihuo kupitia TAMISEMI. Kamati ingependa Bunge lako tukufulipewe taarifa ya utekelezaji wa mradi huu ikiwemo ‘pilotstudy’ iliyofanyika.

4.7 Michezo ya KubahatishaMheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2017/18 Bungelako Tukufu kupitia Kamati ya Bajeti ilishauri Serikali kufanyamabadiliko katika Sheria ya Michezo ya Kubahatisha Sura 41Lengo la mabadiliko ilikuwa ni kuipa Mamlaka ya Mapato(TRA) uwezo wa kukusanya mapato yatokanayo na Michezohii na pia kufanya marekebisho ya viwango vya tozo.

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mafanikio makubwa yaliyopatikana ni kutokana na ushaurihuo wa Kamati. Aidha, Serikali kupitia Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) kwa kuweza kukusanya Shilingi Bilioni 39.11sawa na ongezeko la asilimia 12 hadi kufikia Mwezi Machi2018. Pamoja ya kuwa michezo hii imekuwa kwa kasi sanana kuipatia mapato Serikali, Kamati imeishauri Serikalikupandisha ada, tozo na kodi mbalimbali katika michezo hiikwasababu kimsingi michezo hii sio ya kiuzalishaji na imekuwana madhara makubwa kwa jamii. Katika Nchi za AfrikaMashariki, Tanzania ndio inayotoza kiwango cha chini kwenyemapato ghafi ya michezo hii kuliko nchi nyingine. MfanoKenya wanatoza asilimia 35, Rwanda wanatoza 13 naUganda wanatoza asilimia 20 ya mapato ghafi. Aidha,Kamati inaitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kusimamiakikamilifu Sheria ili kuhakikisha kwamba wanaoshiriki katikaMichezo hii ni wale waliofikisha umri wa miaka 18 kama sheriainavyotaka.

4.8 Ukusanyaji wa Kodi ya Majengo

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2015/16 Serikali ilichukua jukumula ukusanyaji wa Kodi ya Majengo na mabango kutoka katikaSerikali za Mitaa na kuipelekea Serikali kuu kwa lengo lakuongeza ufanisi katika ukusanyaji na baadae kuyarejeshamapato hayo katika halmashauri husika. Mwaka huo huoSerikali ilishusha makadirio ya makusanyo ya kodi hiyo kutokashilingi 58,008,196,553 zilizokuwa zimekadiliwa na Serikali zaMitaa na kuwa Shilingi 47,672,784,729 Aidha, katika mwakawa fedha 2017/18 Serikali ilifanya mabadiliko kupitia Sheriaya fedha na kuondoa takwa la kurejesha fedha zamakusanyo ya mabango na majengo kwa Serikali za Mitaana badala yake kurejesha kulingana na mahitaji ya matumizi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/18 Serikaliimeweza kukusanya kodi ya majengo kwa ufanisi wa asilimia61.08 ambapo kiasii cha Shilingi 20,229,39 0,000 kilikuwakimekusanywa. Baada ya Kamati kufanya tathmini yamwenendo huu ina masuala yafuatayo ya kuishauri Serikali;Kwanza kurudisha chanzo hiki katika mamlaka ya Serikali zamitaa kwa sababu bado Mamlaka ya Mapato haijawa na

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

uwezo wa kutosha kukusanya Chanzo hichi na Pili ni utaratibuwa kutumia Dhamana za Serikali za Mitaa (Municipal Bonds)katika kupata fedha za Maendeleo kwa Serikali za Mitaautashindikana kwasababu Halmashauri hazitakuwa na uwezowa kulipa riba pindi amana hizo zinapoiva na Tatu Kamatiinaishauri Serikali kutumia Wanafunzi wa Chuo cha Ardhikufanya shughuli ya kufanya tathmini ya majengo wakati wamafunzo ya vitendo ili kuongeza tija ya ukusanyaji wa mapatohusika.

4.9 Ukusanyaji na utoaji wa fedha kwa ajili ya mifukombalimbali yenye vyanzo Mahususi.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilipitisha sheriambalimbali zilizokuwa na lengo la kubainisha vyanzo vyamapato mahsusi kwa ajili ya mifuko mbalimbali. Mfanoasilimia 1.5 ya Bill of lading wakati wa uingizaji wa bidhaakwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Reli, na tozo ya Shilingi100 ya mafuta kati ya tozo hiyo shilingi 50 ni kwa ajili ya Mfukowa Umeme Vijijini (REA) na Shilingi 50 kwa ajili ya Mfuko waMaendeleo ya Maji. Aidha, kifungu cha 17A cha Sheria yaUendelezaji wa Tasnia ya Korosho inatoa mgawanyo wamakusanyo ya ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi njeugawanywe kwa asilimia 35 ziende Serikali kuu na asilimia 65ziende kuendeleza zao la korosho nchini. Kamati imebainikwamba pamoja na Sheria mbalimbali kuainisha matumiziya fedha hizo kwenye maeneo ya kimkakati utolewaji wafedha hizo umekuwa ukichelewa na mara nyingine hazitolewikabisa. Mfano, Mfuko wa REA katika mwaka wa fedha 2017/18 Serikali ilikuwa imekusanya jumla ya Shilingi 263,700,000,000ambapo Kiasi ki l ichokuwa kimetolewa ni Shilingi261,3000,0000. Mfuko wa Uendelezaji wa zao la Koroshoulikuwa umepokea Shilingi 10,000,000,000 kati ya Shilingi91,150,303,392.92 zilizokuwa zimekusanywa katika msimu wamwaka 2016/17. Kamati inaishauri Serikali kuzingatia sheriaza mbalimbali fedha, hususan zilizoanzisha mifuko mbalimbalipamoja na Sheria ya Bajeti ili mapato husika yaendeyakatumike kwenye shughuli zilizokusudiwa, kwa kuzingatiakuwa Mifuko hiyo ipo kisheria na Bunge lilisha idhinishamatumizi ya fedha husika kwenye mifuko husika.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Spika, aidha, ukifuatilia Taarifa ya Mkaguzi naMdhibiti Mkuu wa Serikali ya mwaka wa fedha 2016/17,utaona kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanyakiasi cha Shilingi 1,671,096,919,536.3 kama tozo na ushuruuliokusanywa kwa niaba ya Taasisi nyingine. Makusanyo hayoyanahusu tozo za barabara, tozo ya petroli, ada yamaendeleo ya maji, tozo ya maendeleo ya reli na tozo yabandari Hata hivyo, ilibainika kuwa, kati ya makusanyo yotehayo, kiasi cha Shilingi 410,448,166,098.44 hakikuwezakuwasilishwa kwenye taasisi husika kinyume na matakwa yasheria. Kamati inaishauri Serikali kwamba pindi fedhazinapokusanywa na Mamlaka ya Mapato na kupelekwakatika Akaunti ya Mapato iliyopo Benki Kuu, fedha hizo zikitokaziende moja kwa moja kwenye mifuko husika na badala yakusubiria tena kibali kutoka Wizara ya Fedha na Mipangokama inavyofanya sasa.

4.10 Utaratibu wa Serikali kufikisha mapendekezo namaoni ya Tanzania kwenye Jumuiya ya AfrikaMashariki Kuhusu Sheria ya Forodha ya AfrikaMashariki.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka mingi, Bunge lako limekuwalikipitisha mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Forodhaya Afrika Mashariki bila kuwa na nafasi ya kushirikishwa nakutoa mapendekezo yake kupitia Kamati zake za Kibunge.Ieleweke kwamba, pamoja na mapendekezo hayo kuletewaBungeni kupitia sheria ya Fedha (Finance Bill), bado Bungelinakuwa halina mamlaka ya kubadili au kupendekezamabadiliko hayo katika sheria hiyo kwa kuwa tayari Serikaliza Nchi wanachama zinakuwa zimeisharidhia na kuamuakwa niaba ya nchi zao. Kamati ya Bajeti kwa nyakati tofautiimekuwa ikiomba fursa kwa Waziri wa Fedha na Mipangokuwasilisha mapendekezo hayo mbele ya Kamati ili yajadiliwekwa niaba ya Bunge kwa kuwa yanahusika katika kuongezaau kupunguza Mapato ya Serikali, hata hivyo Kamatihaijawahi kupewa fursa hii. Hatua hii inatokana na ukwelikwamba si kanuni za Bunge wala Sheria ya Bajeti inayoipaMamlaka Kamati ya Bajeti kupitia mapendekezo hayo kablaya kupelekwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Spika, ieleweke kwamba utaratibu namchakato wa maoni na mapendekezo ya mabadiliko yaSheria ya Ushuru wa Forodha ni jukumu la nchi husika na siola Afrika mashariki na hakuna Sheria inayomzuia Waziri waFedha na Mipango kushirikisha Bunge kabla ya kuyafikishakatika ngazi ya Jumuiya hiyo. Kamati ya Bajeti imefanya utafitina kuona kuwa, utaratibu huu uliopo sasa una mapungufumakubwa matatu:- kwanza; Bunge, kutokuwa na Mamlakaya kufanya mabadiliko kwenye vifungu vya Sheria ya Ushuruwa Forodha; Pili; Sekta binafsi nchini kuathiriwa na mabadilikoyanayofanyika katika Sheria hiyo ; Tatu, kutozingatiwa vizurikwa usalama wa kiuchumi (economic intelligence).

Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hii, Kamati ya Bajeti inaliombaBunge lako tukufu liridhie na kutoa maelekezo kwa Wizaraya Fedha na Mipango kuwasilisha maoni na mapendekezoya mabadiliko ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiyaya Afrika Mashariki ili yajadiliwe na Kamati ya Bajeti kwa niabaya Bunge kabla ya kuwasilishwa kwenye Jumuiya nahatimaye Kamati iweze kuwasilisha Taarifa yake kwamanufaa ya Bunge na wananchi wote kwa ujumla.

4.11 Utendaji Kazi wa Kikosi Kazi cha Kodi (Tax Task Force).

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilikuwa na vikaombalimbali na Sekta Binafsi ambapo kupitia vikao hivyomasuala mbalimbali yanayohusu changamoto za kikodizinazowakabili zilijadiliwa. Pamoja na mambo mengine SektaBinafsi imekuwa ikilalamikia utendaji kazi wa Kikosi Kazi chaKodi hasa kwa upande wa idadi ya wajumbe wa Sekta Binafsiwanaoruhusiwa katika kikosi kazi hicho; Pili, ufinyu wa mudawanaopewa kujadili masuala ya kodi na Tatu, mapendekezomengi kutofanyiwa kazi na Serikali bila ya kutoa sababumaalum au mrejesho kwa wadau.

Mheshimwa Spika, ieleweke kwamba uwepo wa Sekta Binafsiinayokuwa ndio msingi madhubuti wa Serikali kukusanyamapato ili iweze kuhudumia wananchi. Kwa kuzingatia hilo,Kamati inaishauri Serikali kuangalia upya muundo wa Kikosi

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Kazi hicho ili kuondoa mapungufu yanayojitokeza pamojana kuangalia upya sera za utozaji kodi katika mawandamapana ya kiuchumi na kijamii na sio katika ukusanyaji wamapato tu.

4.12 Uendelezaji wa Sekta zinazochangia kwa kiasikikubwa Mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, katika muda tofauti tofauti Kamatiimekuwa ikishauri Serikali kuhakikisha kwamba inalea nakuendeleza Sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa mapatoya serikali lakini hali imekuwa si hivyo. Mfano Sekta yamawasiliano kwa mujibu wa Taarifa ya TCRA inaonyesha watuzaidi ya milioni 2.5 wameondoka katika mfumo wa usafirishajiwa fedha kwa njia ya kielectroniki. Aidha, mapatoyatokanayo na ushuru wa usafirishaji wa fedha na bidhaazinazotozwa ushuru wa bidhaa kama pombe kali spiritszimeshuka kwa asilimia 30. Kamati inaendelea kuishauri Serikalikuhakikisha kwamba sera zake za kikodi kwa Sektazinazokuwa ziwe zina lengo la kulea na kuelendeleza sektahizo na sio kukusanya kodi kiasi ambacho kinaathiri hataukuaji wa Sekta husika.

4.13 Chuo cha Utawala wa Kodi (Institute of TaxAdministration)

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Utawala wa Kodi (Institute ofTax Administration) kimechaguliwa na Jumuiya ya AfrikaMashariki kuwa kituo cha Umahili cha Masuala ya Masomoya Kodi na Forodha (Centre of exellency). Kamatiinaipongeza Serikali kwa kuratibu na kusimamia vemashughuli za Chuo cha Utawala wa Kodi kupitia Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA). Hata hivyo, kwa sasa eneo la chuoni finyu na miundombinu yake haijawa ya kisasa zaidi ilikukiwezesha kukidhi ubora wa kimataifa katika masuala yakodi na ushuru wa forodha. Kamati inaishauri Serikali kuongezaBajeti ya chuo hiki ili kukiwezesha kujitanua na kujengakampasi mpya katika eneo la chuo la Misugusugu pamojana kununua vifaa na kuboresha miundombinu ya chuo ilikikidhi vigezo vya kimataifa

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

5.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendakumshukuru Mheshimiwa Jitu Vrajlal Soni, Mbunge wa BabatiVijijini na Makamu Mwenyekiti, kwa ushirikiano anaonipatia.Pia, napenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati, kwakuchambua na kutoa maoni na mapendekezo mbalimbaliyaliyowezesha kuboresha taarifa hii hatimaye kuletwa mbeleya Bunge lako Tukufu. Aidha, naomba nitumie nafasi hiikuwatambua Wajumbe wa Kamati kwa majina yao kamaifuatavyo:-1. Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia, Mb – Mwenyekiti2. Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb - Makamu Mwenyekiti3. Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mb4. Mhe. Ali Hassan Omar, Mb5. Mhe. Abdallah Majura Bulembo, Mb6. Mhe. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Mb7. Mhe. Albert Obama Ntabaliba, Mb8. Mhe. Dalaly Peter Kafumu, Mb9. Mhe. David Ernest Silinde, Mb10. Mhe. Freeman Aikael Mbowe, Mb11. Mhe. Hasna Sudi Katunda Mwilima, Mb12. Mhe. Dkt. Immaculate Sware Semesi, Mb13. Mhe. Ibrahim Hassanali Mohammedali Raza, Mb14. Mhe. Makame Kassim Makame, Mb15. Mhe. Maria Ndilla Kangoye, Mb16. Mhe. Martha Jachi Umbulla, Mb17. Mhe. Mendrad Lutengano Kigola, Mb18. Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki, Mb19. Mhe. Mbaraka Kitwana Dau, Mb20. Mhe. Oran Manase Njeza, Mb21. Mhe. Riziki Said Lulida, Mb22. Mhe. Stephen Julius Masele, Mb23. Mhe. Andrew John Chenge, Mb24. Mhe. Hussein M. Bashe, Mb25. Mhe. Shally Josepha Raymond, Mb26. Mhe. Suleiman A. Sadiq, Mb

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mhe. Dkt PhilipMpango (Mb) Waziri wa Fedha na Mipango na Mhe. Dkt

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Ashatu K. Kijaji Mb, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, KatibuMkuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na wataalamuwote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwa tayari kutoaufafanuzi na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa Wajumbewa Kamati wakati wote wa mjadala wa makadirio haya.Aidha, Kamati inatoa shukrani kwa Taasisi na Idara zote zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wadauwa Sekta Binafsi kwa ushirikiano walioutoa kwa Kamati katikakipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naombanikushukuru wewe binafsi Mhe. Spika, Dkt. Tulia Akson, Mb -Naibu Spika na Ndugu Stephen Kagaigai - Katibu wa Bungepamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge kwakuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Aidha, kwa namna ya pekee napenda kuishukuru Sekretarietiya Kamati ya Bajeti ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi NduguLina Kitosi, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ndg. Michael Kadebena Makatibu wa Kamati hii Ndg. Godfrey Godwin, EmmanuelRhobi, Lilian Masabala na Maombi Kakozi kwa kuratibushughuli za Kamati pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamuna hatimaye kukamilika kwa taarifa hii kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naliomba Bungelako tukufu sasa lijadili na kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja namafungu manane (8) yaliyo chini yake kwa Mwaka wa Fedha2018/2019 kama yalivyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri waFedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja hii.

Jitu Vrajlal Soni (Mb)MAKAMU MWENYEKITI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI04 Juni, 2018

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

SPIKA: Sasa tunaingia katika uwanja wa uchangiajiwa hoja iliyo mbele yetu iliyowekwa mezani naMheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. PhilipMpango. Kama nilivyokuwa nimeahidi mwanzotutaanza na Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko,atafuatiwa na Mchungaji Peter Msigwa, MheshimiwaNsanzugwanko.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika,naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotubahii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Hata hivyo, naomba kwaruhusa yako kabla sijasema ninayotaka kusema, nitoeshukrani za dhati kabisa kwako wewe mwenyewe, Katibu waBunge na timu yenu ya wafanyakazi wa Bunge kwa jinsimlivyokuja kutufariji huko Kakonko. Wewe mwenyeweumesafiri kilometa 816 hadi Kakonko, tunakushukuru sana.Umeonesha mapenzi makubwa sana na kwa kweli familiainashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee pianaomba niwashukuru Wabunge wote, lakini hasa waleWabunge 27 waliokuja Kakonko pale, tunawashukuru sanakwa kuja Kakonko, kwa kuja kutuhani.

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako nimeagizwa piana familia ya marehemu kwako wewe mwenyewe, menginenitakwambia tukiwa faragha, lakini mama yake mzazi, kakazake na mke wake wanashukuru sana, sana kwa kaziiliyofanywa na Bunge, kwa jitihada iliyofanywa na Bunge hadikufikisha mwili wa marehemu Mheshimiwa Bilago nyumbanikwao. Tunasema ahsante sana na Mungu awape nguvu naafya tele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombasasa niende kwa Wizara, kwanza, naunga mkono hoja hii,hoja muhimu sana. Pia niwape hongera ya kazi MheshimiwaWaziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango na Naibu wake MheshimiwaDkt. Kijaji; Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu na timu yoteya Wizara bila kumsahau Mkurugenzi Mtendaji wa TRAwanafanya kazi nzuri, hongereni sana, mazingira haya ni

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

mapya, wachape mwendo, tuko vizuri na wao wako vizuri.Sisi Wabunge wengi tunawapa hongera ya kazi, tunawatakiakazi njema katika mazingira haya mapya, hakuna kukatatamaa, ni kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina machache, nina mambomatatu hivi, nitakuwa na hili la Wazabuni, nitazungumzia TRAKasulu, nitazungumzia miradi ya PPP na mwisho kama mudautaniruhusu nitazungumzia soko la bidhaa, commodityexchange market katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na hili la malipoya Wazabuni, nashauri sincerely hili jambo nimesoma kwenyekitabu cha Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 24 mpaka 26amezungumzia malipo ya wazabuni. Hata hivyo, lipo tatizokubwa kati ya madai ya Wazabuni, muda wanaotoa hudumazao, uhakiki wa madeni haya na hadi hawa watu kulipwajamani.

Mheshimiwa Spika, hivi inawezekanaje Mzabunianalisha shule zetu za sekondari na zingine za msingi hizi zashule maalum, anawezaje kukaa anadai Serikali miezi 11?Huu uhakiki maana yake nini? Nafikiri wenzetu wa Wizaraya Fedha hii waichukue k ama changamoto, hawasuppliers wetu waki-supply, nitoe mfano tu mdogo, kwasababu kuna wapiga kura wangu walitoka Kasulu,Buhigwe na Kibondo kuja hapa na nikakutana nao; wanadaiTAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, Katibu Mkuu wa TAMISEMIamewaandikia Hazina madai mbalimbali ambayoyameshahakikiwa. Madai hasa hasa ya Wazabuni wa elimuna wiki jana hiyo barua mwenyewe nimebahatika kuionakwa sababu i l ikuwa ni pressure kubwa sana.Inawezekanaje Mzabuni adai Serikali miezi 11. Naombasana kupitia Wizara hii na wenzake Serikalini, warekebisheutaratibu, kweli wafanye uhakiki, tujiridhishe kwambamadeni haya ni halali, lakini Wazabuni wenye madenihalali walipwe kwa wakati jamani. Inachukua muda mrefusana, sana.

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Spika, kwa mfano katika Jimbo langu laKasulu peke yake Wazabuni wanayodai elimu, wanadai elimuzaidi ya shilingi milioni 500 na wamesubiri zaidi ya miezi kumina kwa bahati nzuri kile kitabu cha madai mwenyewenimekiona. Naomba sana wenzetu wa elimu mjaribu ku-fasttrack, wafanye uhakiki kweli, tujiridhishe na madeni, lakinihatimaye madeni haya yalipwe.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika madeni yaMawakala wa mbolea. Hilo limekuwa sasa ni kizungumkuti.Mawakala hawa tangu niko Kamati ya Kilimo miaka miwliiliyopita tuliletewa orodha na orodha ilikuwa inahakikiwa basituombe Mheshimiwa Waziri wale ambao wameridhikakwamba wana madai halali ya pembejeo walipwe basifedha zao.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani…

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge walemnaoongeaongea hapo hasa kule kushoto yaani watu wakosokoni kabisa, kule mwisho kule, nawasikia kule mwisho yaaniwana mikutano ya hadhara kabisa. Tunawaombeni sanatumsikilize mchangiaji. Endelea Mheshimiwa.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika,naomba ulinde muda wangu wa dakika moja, mbili huotafadhali.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nazungumzia juu ya hawawazabuni ambao wame-supply mbolea. Nakumbuka tangukwenye Kamati ya Kilimo limejadiliwa jambo hili na Waziri waalituletea orodha ya wanaodai, lakini kukawa kwambalinafanyiwa uhakiki. Ni jambo jema, lazima tujue nani hasatunamlipa, lakini wale waliohakikiwa tafadhali sana, waleambao wamejiridhisha kwamba hawa ni wadai halaliwalipwe fedha zao, muda umekuwa mwingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii sintofahamu ya Mabenkikuwatisha, kuuza mali zao, nadhani haijengi heshima yaSerikali, nina uhakika wala hata haijengi heshima ya Chama

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

cha Mapinduzi. Naomba sana, wazabuni halali walio-supplyhuduma ya pembejeo na kadhalika walipwe baada yakuwa wamefanya uhakiki na kuwe na timeframe kwambawazabuni hao wanalipwa kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni jambo kidogo ambaloliko local, sisi Mkoa wa Kigoma, Wilaya ya Kibondo naKakonko, Wilaya ya Kasulu na Buhigwe hatuna ofisi za TRA.Naomba kupitia kwa Mheshimiwa Waziri sina uhakika kamaanaijua Buhigwe, Kasulu na Kibondo iliko sina uhakika.Haiwezekani TRA waendelee kukaa kwenye vijumba vyakupanga panga…

SPIKA: Mheshimiwa Nsanzugwanko huna uhakikakama Mheshimiwa Waziri anapajua Buhigwe?

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Spika,eehhh! Maana yake angekuwa anapajua pengineangekuwa ameshajenga Ofisi ya TRA, ndivyo ninavyofikirihivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana watujengee Ofisiza TRA angalau wenzetu wa Wilaya ya Kakonko na Kibondowanaweza kuwa na TRA moja pale Kibondo wakai-share nasisi Kasulu na Buhigwe tukawa pia na Ofisi ya TRA.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri anajua sisiHalmashauri ya Mji wa Kasulu tumeshatoa Kiwanja bure kwaajili ya kujenga Ofisi za TRA. Sasa kile kiwanja kinakuwa chaka,kinakuwa pori, ningeshauri sana kupitia yeye na MkurugenziMtendaji wa TRA nadhani ananisikia hapa watujengee Ofisiya kisasa ya TRA. Mji wa Kasulu na Mji wa Kibondo ni mijiinayokua kwa haraka sana, inahitaji huduma za kibiashara.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, ambalo napendanilisemee ni hii miradi ya PPP; nimesoma kwenye kitabu chabajeti, umezungumzia PPP karibu kurasa tatu, lakini katikamaelezo ya Waziri haoneshi exactly ni mradi gani wa PPPambao Serikali ume-finalize sasa unatekelezwa hakuna hatammoja, ni maelezo tu.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Spika, Sheria ya PPP tangu tumeitungandani ya Bunge hili ni zaidi ya miaka 10 sasa. Sasa ningependapengine Waziri atakapokuja atueleze ni miradi ipi hasawamei-finalize ya PPP ambayo inakwenda kutekelezwa napengine ikibidi pia waitofautishe kati ya miradi ya hudumana miradi ya uzalishaji. Nawiwa sana hii PPP tungejielekezakwenye miradi ya kilimo na ufugaji maeneo ambayotuna uhakika yatazalisha fedha ili tuweze kupata fedhazingine.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ambalo ningependanilisemee, ni hii commodity exchange market. Waziriameileza sana ukurasa wa 63 mpaka ukurasa wa 65, hili nijambo geni. Kwanza ningeomba kupitia kwako pengineWabunge wote tungepitishwa kwenye somo hili, hii stockexchange ni kitu gani? Kuna maelezo mengi sana pale nabaadhi ya Makampuni ambayo yamekuwa registered kwaajili ya kuhudumia hii commodity exchange.

Mheshimiwa Spika, ni vyema Wabunge wenyewetungepata semina kubwa tukaelewa maana ya jambo hili.Ni jambo kubwa sana na nchi zingine zinatumia jambo hilikwa ufanisi mkubwa sana, lakini hapa bado ni kitu kipya, sisiwenyewe Wabunge hatukielewi vizuri, ningeshauri kupitiakwako tuwe na semina ya Bunge zima kuhusu hiki kitukinachoitwa commodity exchange market. Ni kitumuhimu sana, lakini sina uhakika kama kinafahamika vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, kwa sababuWizara hii ya fedha ndiyo wanagawa rasilimali fedha,naomba niendelee kuwakumbusha na hili nitalisema sanahata kwenye bajeti kuu, miradi ile ambayo tumeshaanzanayo itekelezwe, ikamilike.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyakanazi ileuliyopita kutoka Airport mpaka Kakonko ndiyo inaitwabarabara ya Nyakanazi, umeiona, hipitiki. Sasa kwa sababunakumbuka tangu mwaka jana ni moja ya miradi yavielelezo…

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Nsanzugwankonakushukuru sana.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Miradi ya vielelezonaomba itekelezwe.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkonohoja hii. (Kicheko)

SPIKA: Nakushukuru sana. Mheshimiwa Peter Msigwaatafuatiwa na Mheshimiwa Kombo.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,nikushukuru kwa kunipa nafasi. Niungane na MheshimiwaNsanzugwanko kuhusiana na barabara ya Nyakanazi tokeanimekuwa Mbunge hapa nasikia Kigoma-Nyakanazi tokanimekuwa Mbunge kipindi cha kwanza, kwa kweli watu waKigoma mnaonewa inabidi tuwasaidie, mpigiwe debe, mpoporini sana, mmetengwa. Nadhani Wizara watasaidia kidogo,ilikuwa mara ya kwanza kufika Kigoma kwa kweli mko nje yaTanzania.

Mheshimiwa Spika, nikirudi kwenye Wizara hii; naaminiWizara hii ya Fedha na Mipango ni Wizara ya Fedha naMipango, lakini kwa mtazamo wangu naona wamejikita zaidikwenye fedha kuliko kwenye mipango na kwa kuwa wao niWizara ya Fedha na Mipango walipaswa wawe ni Dira kubwaya Taifa ili kuliongoza namna gani ya kupata hizo fedha halafukisha wakusanye, lakini Wizara hii katika utendaji waowamekuwa kama vile ambavyo wanataka wamkamueng’ombe ambaye hawamuandalii mazingira mazuri ya kutoamaziwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ndiyo inayosimamia Diraya Taifa, Wizara hii ndiyo inasimamia Mpango waMiaka Mitano wa Taifa, lakini kwa bahati mbaya tokaSerikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani kunamipango mingi ambayo inatekelezwa na Wizara hii niile ambayo haipo kwenye Mpango wa Miaka Mitano waTaifa.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Mheshimiwa Spika, sasa mimi siyo Mchumi, I amTheologian by professional, inanichanganya kidogo kwambasasa hiyo mipango ni ipi wanayoisimamia kwa sababutunakuwa na priorities, tunaweka mikakati, lakini mwisho wasiku tunapokuja kwenye utekelezaji wanaleta vitu vinginekabisa ambavyo havikuwepo kwenye mpango wa nchi,wanaanza kufanya vitu ambavyo havipo.

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri, hakuna mtuanayekataa move ya kuhamia Dodoma, lakini haikuwepokwenye Mpango wa Miaka Mitano, it was more of a politicalthan economical, imetulete shida, tunahangaika, hatukuwana Ofisi, imechanganya mambo mengi sana katikakuendesha nchi yetu. Kwa hiyo Mheshimiwa Mpango…

SPIKA: Sasa hapo Mheshimiwa Msigwa unamgusaSpika.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,najua hapo umeguswa. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nirudie tena, hatukatai kuhamiaDodoma lakini hatukuwa na mpango huo, hela tumeitoawapi? Natoa mifano kama hiyo.

Mheshimiwa Spika, mpango mwingine ambaonaweza kusema, mipango hii ambayo inafanywa ambayohaikuwepo kwenye mpango wa nchi, inaleta tabu katika nchiyetu. Nitoe mfano mmoja wa haraka haraka, kwa wastaniTRA wanasema kwa sasa hivi wanakusanya wastani wa trilioni1.3 mapato kwa mwezi. Hata hivyo, mapato haya ukiangaliawao wamekuwa kama Wakala tu, hela nyingiwanazokusanya siyo za kwao.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, wanachukuawharfage, wanachukua hela zote za halmashauri, propertytax kwa mfano za majengo wamechukua, wamechukua zileVAT refundable, wamechukua mpaka zile levy za korosho,wamechukua hela nyingi ambazo siyo za kwao halafuwanapita mitaani, barabarani kwa wananchi kisiasa

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

wanasema sasa hivi tumedhibiti mapato yanakuwa mengi.Wakati huo huo hizo hela walizotunyang’anya kwenyehalmashauri zetu mnazi-ground halmashauri, hazifanyi kazivizuri, yaani hadi hela za REA nazo wanasema za kwao.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, wamezi-ground halmashauri, sasaleo hiyo mipango una-match vipi mipango na jinsi ambavyowanakusanya hizo pesa. Matokeo yake katika halmashauriwameshindwa kupeleka wataalam wazuri, wameamua tenaku-centralize ambapo ni mipango iliyoshindikana tokatumepata uhuru, tulijaribu tukakwama.

Mheshimiwa Spika, kwenye Majukwaa wanasimamakwamba wanakusanya pesa nyingi, lakini zile pesa ambazowametunyang’anya kwenye halmashauri hazirudi kwasababu hakuna mipango mizuri. Nilitegemea MheshimiwaWaziri katika mipango yake angeishauri Serikali hii kwambakupeleka watendaji katika halmashauri ambao hawanaweledi, ambao wameenda kisiasa kunaharibu utendaji wakazi kwa sababu nchi hii mtu akiwa Mwanasiasa anaaminikakwamba anajua kila kitu.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka siku moja Katibualiyeondoka Dkt. Kashilillah alisema hapa Wabunge tukianzahapa kuzungumzia masuala ya nuclear tutataka tuchangiehata kama hatuyajui. Pia tunaamini kwamba mtu akiwamwanasiasa anajua kila kitu na nategemea Wizara yaMheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango ingekuwandiyo dira ya kuishauri Serikali hii. Tumekuwa na mipangomingi ambayo iko nje ya bajeti.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia wakati wa Dkt. Kikwete,Dkt. Kikwete ameondoka hapa tunakusanya 900.0 billion900.0 ambazo hakukusanya hizi hela za wengine. Inaoneshayeye system zake zilikuwa zinafanya kazi vizuri lakini waowame-intefere maeneo mengine yote, wanataja pesakubwa hii lakini bado utekelezaji haupo. Sasa wanatangazahizo pesa zote zipo zinakusanywa, kwa nini kwenye pesa zamaendeleo pesa hazirudi kwenye maeneo yetu tunapotoka

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

kama hizi pesa zote wanazikusanya? Mfano mzuri, kwenyekitabu cha Kamati wamezungumza mpaka Disemba, 2017Serikali ilikuwa imekusanya 7.6 trillion na mpaka Februari, 2018walilipa deni la nje trilioni 5.5 maana yake tulibakiwa na trilionimbili.

Mheshimiwa Spika, sasa tunaendeshaji hii nchi kwautaratibu huo kama hela zote tunazokusanya tunalipamadeni na bado kwenye kitabu cha hotuba chaMheshimiwa Waziri ukisoma ukurasa wa 96 amezungumza nahawa wamesema, anasema kwamba deni bado linahimilikalakini mzigo mkubwa bado anabeba mwananchi waTanzania. Wakitoka nje kisiasa wanasema kila kitu kipo safi,tunapongezana hapa, mtumbwi unazidi kuzama, kiuhalisiatuna-suffocate, hakuna oxygen katika nchi hii badotunazama. Kila mtu anaamua anavyotaka, tutapigianamakofi hapa lakini hela hamna. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye kila Wizara kamani Wizara zipo zimepata pesa zaidi ya asilimia 50 na kitu nichache sana, zote ziko chini ya kiwango. Kama tunakusanyamapato hayo Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwa niniWizara zote zinapata pesa chini ya kiwango? Haya nimasuala ambayo anatakiwa atujibu na ningeomba katikasuala hili anijibu hela halisi ambayo anakusanya kodi ya TRAbila kuchanganya na hizi nilizomtajia, wharfage zile zaHalmashauri, sijui VAT refundable za watu wengine ambazowanashika ni shilingi ngapi? Tujilinganishe na Serikali iliyopitana ya sasa kama tunakwenda pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine kamanilivyozungumza, mipango mingi anayotekeleza sasa hiviMheshimiwa Waziri haikuwepo kwenye Mpango wa MiakaMitano. Hatukuwa kwenye mpango wa miaka mitanokwamba we will move from Dar es Salaam to Dodoma,kwenye mpango wa miaka mitano hatukuwa na standardgauge, where are we getting the money?

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, hizi hela ukiangaliakiutaratibu wamekopa mikopo ya commercial ambayo ni

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

very expensive. Tunakopa mkopo kwa sababu commercialunakopa mkopo, unaanza kulipa mkopo huo mapema kablaya ule mradi wa longterm haujaanza kuzalisha sasa ku-service huu mkopo tuta-service kupata hela, itatoka wapi?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri atupe majibuhapa. Ukiangalia Ethipoia au Kenya wao walipataconcession loan ambayo ukikopa wale watu watamaliza ulemradi, halafu wakishamaliza ule mradi, unapoanza kufanyakazi ndipo unaanza kulipa. Ni kitu gani kimesababishawasiende kwenye mikopo hiyo, wameenda kwenye mikopohii ya commercial loan? Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mpangoningeomba anijibu. Kwa hiyo, kuna mipango mingi ambayotunafanya lakini haikuwepo kwenye utaratibu.

Mheshimiwa Spika, tumeenda kwenye mambo yaStiegler’s gorge hapa, tatizo la Tanzania siyo kwamba tunatatizo la umeme, tatizo ni kuuhamisha umeme ulipo kwendakwa walaji. Hizo megawatts zote tunazozitaka tunatakatuzifanyie nini? Ambapo tutachukua hela ya sasa, kwenyelongterm loan ambazo zinakuwa ni mzigo kwa Watanzaniawakija hapa wanasema mkopo bado unabebeka. Haya nimambo siyo suala tuje tushangiliane hapa. Bado nam-challenge Mheshimiwa Mpango yeye ndiye dira ya nchi yetu.Hii mamlaka inatoka wapi ya kwamba wanaleta mipangoambayo haipo kwenye mipango ya miaka mitano? Hayandiyo yanayotuchanganya, yanatuchanganya kama Taifahatuelewi tushike lipi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yote yaliyofanyika, sasa hivinimezungumza hapo mwanzo kwamba, tumefika mahalituna-centralize kila kitu ambapo hayo mambo yalishindikanahapo mwanzoni, sasa hivi halmashauri zote tumezi-groundtunarudi kule kule ambako tulishindwa. Ilitumika pesa nyingisana kuunda Serikali za Mitaa, kuzi-empower Serikali za Mitaatulitumia pesa nyingi sana hizi D by D leo tena tumerudikule kule kitu kinafanyika Dar es Salaam, kila kituwanataka kifanyike sijui Dodoma ambako tumezi-groundHalmashauri.

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Spika, hii mipango inekuwa ina-empowerwatu wa kule chini inge-empower watu wa chini waonekama wana-own, wame-complicate. Naamini na elimuyangu ndogo hii niliyonayo, elimu hai-complicate mambo,elimu ina-simplify mambo, lakini ukiangalia mipango yotetunapiga mapambio mengi kwenye vyombo vya habari.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana wakati nasoma report haponimesikia kwenye report wenzangu walifanya siwa-challengelakini nilishangaa wanashangaa mtu analipwa milioni 96(Dola 40,000) tunashangaa mtu analipwa eti Dola 40,000,this is poverty mentality. Yule mtu kwanza ameingiamkataba na wale watu, zile hela siyo za kwetu, akilipwamilioni 96 kwanza atalipa kodi milioni 30 si zitakuja hapanchini, tuna hasara gani sisi? Kodi milioni 30 zitakuwahapa nchini, tutawaaminisha Watanzania kwamba mtuakilipwa milioni 40 kama ni laana, that is povertymentality.

Mheshimiwa Spika, watu wangelipwa hela zaidi yahizo ilimradi hawavunji sheria, sasa kwa mfano, waki-importexpert ambaye huwezi kumpata tena ni wa gharamautamlipa Sh.200,000 tunazolipana lipana hapa? Wachezajiwa mpira wanalipwa hela nyingi kwa sababu yaprofessionalism walizonazo, sasa tusifike mahali tunakuwasadist, tunawachukia watu wanapolipwa hela nyingi badalaya ku-encourage watu walio chini walipwe zaidi, sisitunasema analipwa zaidi, kwa hiyo ashuke chini, are weserious?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwaujumla, I am Theologian anyway I am not an economistlakini nataka kusema Mheshimiwa Mpango atuongoze,atusaidie…

SPIKA: Yaani hakuna hata taarifa hata katika uongohuo jamani?

WABUNGE FULANI: Aaaaah! (Kicheko/Makofi)

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

SPIKA: Tayari? ya pili? Oohhh! basi Bwana kumbendiyo maana hawakukupa taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,umeshindwa kuvumilia kidogo?

SPIKA: Tayari imeshakwisha. Mheshimiwa Juma KomboHamad, tafadhali.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika,nashukuru kuwa miongoni mwa wachangiaji wa Wizara hiikubwa, Wizara ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Spika, kabisa niungane na waliopitakuzungumza japo kwa ufupi au hata kuitaja barabara ileinayokwenda Kigoma kutoka Nyakanazi kwamba nibarabara muhimu na ni barabara ambayo nilipata fursa namimi kwenda kwenye msiba ule wa kumsitiri Mwalimu wetu,Mbunge mwenzetu Mwalimu Bilago, nikaona mazingirayalivyo, nikaona barabara ilivyo kwa kweli inahuzunisha nainatia huruma sana.

Mheshimiwa Spika, naamini kwamba ni miongonimwa barabara zile ambazo siku za mvua magari yanazamakwenye mito ikisubiri siku mbili au tatu wananchi wapatekupita kwa ajili ya kufika Kigoma na maeneo mengine yakule. Kwa hiyo, ni vyema Wizara ya Fedha barabara ilewaingalie kwa jicho la huruma sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ukiangalia kitabu chaKamati ukurasa wa 26 kumezungumzwa hizi milioni 50 kila kijiji,lakini ikiwa Serikali ya Awamu ya Tano hii inakwenda ukingonitena tunakwenda kwenye mwaka wa tatu sasa, Waziri waFedha anakuja hapa kutuaminisha kwamba sasakumetengwa jumla ya bilioni 60 ambazo zinakwenda kufanyautafiti yaani pilot studies kwa ajili ya kuona kwamba vipitutafanikisha mpango huu wa milioni 50 kila kijiji.

Mheshimiwa Spika, hii maana yake ni kwamba, kwamiaka mitatu sasa bado tunakwenda kwenye pilot studies,

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

kwenye kufanya research kuona vipi tutafanikisha utoaji wafedha hizi, lakini tukumbuke kwamba milioni 50 kila kijiji niahadi ya Rais na imo ndani ya Ilani ya Chama chaMapinduzi. Hii inamaanisha kwamba wananchiWatanzania tuliwadanganya. Tuliwadanganya kwasababu kama hadi leo miaka mitatu fedha hii haijatokaina maana hakuna dalili na bado tunakwenda kufanyastudy, bado hakuna dalili ya Watanzania kupata fedhahii na ni wazi kwamba huu ulikuwa ni usanii wa kisiasa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la tatu ni kuhusu mfumo wakodi ambao mara nyingi tumekuwa tukiuliza na umekuwa niwenye utata kwa kiasi kikubwa sana. Naomba nitoe maelezokwamba mifumo ya kodi kwenye bandari hizi za AfrikaMashariki inatofautiana sana kutokana na interest za nchina tozo ambazo zimo katika kila nchi ambayo inahusika naBandari hizo husika. Kwa mfano, container ambalolina futi 20, ina uzito sawa, thamani sawa, bandari yaDar es Salaam wanatoza dola 240 wakati bandari yaMombasa wanatoza dola 70 tu, hii ni tofauti kubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kontena ambayo urefu wa futi 40,bandari ya Dar es Salaam wanatoza dola 420, wakati bandariya Mombasa wanatoza dola 105, hii ni tofauti. Gari ambayoina thamani ya dola 10,000 bandari ya Dar es Salaamwanatoza 1.6% wakati Bandari ya Mombasa inatoa 0.8% hiini tofauti kubwa. Kuonesha kwamba utofauti huu haupo tubaina ya Bandari ya Zanzibar ambayo kila sikuinakandamizwa, inaonewa kwa sababu tu ya mfumo huowa kodi lakini suala hili haligusi bandari nyingine za Mombasana bandari nyingine ambayo ziko ndani ya Afrika Masharikina Kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kusema nini,nitakachokizungumza hapa, tumekuwa tukiuliza mara nyingikwamba, vipi mifumo hii ya kodi ambayo inaenda kuuauchumi wa Zanzibar, inaenda kuua bandari ya Zanzibar, liniitapatiwa ufumbuzi na lini Wanzanzibari wataachwa

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

waendeleze masuala yao ya biashara bila kulazimishwakwamba eti wafuate mfumo wa TANCIS,kwa sababu tofautihii zipo kila mahali.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukilalamikia suala hilisana, nataka nioneshe sisi kama Wabunge kutoka Zanzibarkwa sababu sisi Wabunge kutoka Zanzibar Jimbo letu ni kamaZanzibar. Kwa sababu kama Mbunge siwezi kuzungumziasuala la maji Jimboni kwangu, siwezi kuzungumzia suala lakilimo jimboni kwangu, kwa hiyo, jimbo langu ni Zanzibar sasa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumezungumzia masuala hapa,hata leo tumezungumzia masuala ya kodi ya umeme. Sisitumeuziwa umeme na TANESCO lakini tumeuziwa kwa beiambayo si sahihi. Tumekuwa tukilalamikia, Serikali kupitiaWizara ya Fedha inatuambia tunazungumza. Tumekuwatukizungumzia tozo za bandari haziko katika mazingira sahihikwa bandari ya Zanzibar. Kodi zile zinaua bandari ya Zanzibar,tumeambiwa suala hili tunazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumezungumza masuala yavyombo ya moto, tumelalamika sana, leo ni vitu vya ajabusana, leo mtu kutoka Burundi, mtu kutoka Kongo, mtu kutokaZambia anaingia Tanzania na gari lake, anatumia miezi miwilikwa kujaza tu fomu pale mpakani, halafu anaweza kuongezatena miezi miwili lakini mtu kutoka Zanzibar huu ni uonevu,udugu uko wapi? Mtu kutoka Zanzibar hana uwezo wa kuletagari Tanzania Bara akaweza kutumia. Huo udugu wa damuuko wapi?

Mheshimiwa Spika, kila siku tunasema udugu wadamu, tunadumisha, tunadumisha ndio ni sahihi, hakunaanayekataa umoja lakini umoja uwe na nia njema.Tukizungumza haya tunaambiwa tunazungumza,tutazungumza mpaka lini? Miaka 54 ya Muungano, kero hizizimeanza muda mrefu zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kila siku akija Waziri wa Fedhatutazungumza, akija Waziri mwingine yoyote, tunazungumza,

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

tunazungumza mpaka lini? Juzi hapa tumelalamikia masualaya Akaunti ya Pamoja ya Fedha. Leo tumeona kwenye kitabukwa ajili ya Tume ya Pamoja ya Fedha inafanya kazi gani?Mheshimiwa Mpango kwenye hotuba yake amesema kabisakwamba, tayari tume ile imekamilisha kufanya utafiti. Sasahii fedha iliyotengwa hapa ya nini? Maana amesemamshahara ni zero points.

Mheshimiwa Spika, sasa kama kuna mshahara zeropoints sasa ile bilioni ngapi uliyoitenga imo kwenye kitabu niya kazi gani kama watu wamekamilisha utafiti na hii akauntiitaanzishwa lini ili tuone sasa kuna equality kwenye masualaya mgawanyo wa fedha za muungano. Kuna equality katikamakusanyo ya fedha za muungano, tujue nani anahusika.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, yote haya tunaambiwatunazumgumza. Huu unaoendelea unaitwa ulaghai wakisiasa ambao hakika kila siku unaendelea kudumaza na kuuamaendeleo ya upande mmoja wa Muungano. Kwa sababuhizi zote ambazo nimezizungumza hapa hizi ndizo channelza maendeleo katika Taifa, katika nchi. Zanzibar ni nchiya visiwa inajitegemea kimaendeleo ina Serikali yake.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuendelee kuangalia, MheshimiwaMpango aje atujibu sasa haya masuala ya kodi bandari natozo. Leo Zanzibar pale unasafirisha hata vitenge 10, kanga10 au tano, TV moja ya kuja kuangalia mwenyewe ukija paleunapigwa difference. Leo wafanyabiashara wote soko lote,tulilokuwa pengine lingekuwa soko linaloenda kuchukuabidhaa Zanzibar kuleta maeneo ya Tazania Bara mikoatofauti leo wamehamia Uganda.

Mheshimiwa Spika, tukitoka hapo nje tu hapowajasiliamali wapo wanasema hili shati linatoka Uganda hili,shati hili linatoka Kongo, kitenge hiki kinatoka wapi, wale wotewalikuwa wanakuja Zanzibar wanachukua bidhaa na kuletaTanzania Bara kuuza, leo soko lile wafanyabiashara waZanzibar limekufa. (Makofi)

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Mheshimiwa Spika, mwisho niseme mwisho leotunaambiwa hapa bidhaa zinazotoka na inasikitisha sanamaji, kama kuna maji Zanzibar yanayozalishwa na kiwandakilichopo Zanzibar hayaruhusiwi kuuzwa Tanzania bara.Inaashiria nini? Tulipiga marufuku sukari wakasema Zanzibarhaitoshi. Hivi vifaa vyote, bidhaa zote zinazouzwa TanzaniaBara, zinazozalishwa Tanzania Bara ndio zikavushwa Zanzibar?

Mheshimiwa Spika, sio kweli huu ni usanii wa kisiasaambao kimsingi haukubaliki, lakini tukisema tunazungumzahivi tunazungumza na nani? Tunazungumza na mtu ambayehana mamlaka, mtu ambaye hana uwezo wa kusema, mtuambaye wanaenda kuzungumza naye asubuhi j ioniwanamwona mpuuzi wanasema achana naye yule. Sisitunaendelea na mambo yetu, hili haliwezekani.

SPIKA: Mheshimiwa Juma, lugha unazozitumia kidogo.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika,samahani sitorudia tena

SPIKA: Hawa wanaozungumza ni watu wazima na akilizao sasa, waheshimu tu kwa mazungumzo yao. Endelea tuMheshimiwa.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Spika,ahsante nitajirekebisha.

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumze hayo kwamasikitiko makubwa nikijua kwamba Wizara ya Fedha naMipango itakuja na majibu ya haya sasa kuona kwamba vipitunaenda kutatua hizi changamoto ambazotumezizungumza hapa, kwa nia njema kabisa na kwa nianjema kwa nchi hizi. Hizi story za kwamba tunazungumza,tunazungumza at least zifikie mwisho sasa tuone kwambamaendeleo haya yanakuwa kwa Tanzania nzima na sioupande mmoja wa Muungano.

Mheshimiwa Spika, Zanzibar haina pa kwenda,Zanzibar hatulimi mahindi, Zanzibar hatulimi nyanya, Zanzibar

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

hatulimi, yote tunatumia kutoka Tanzania Bara nayanaingia vizuri tu, lakini leo kinachozalishwa Zanzibarunaambiwa lazima tukifikie kiwango hiki, lazima tutoe hiki.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Kombo JumaHamad. Ulipokuwa unachangia nilikuwa najitahidi sanaMheshimiwa Ally Keissy asisimame nikawa nahakikishakabisa hatapata nafasi maana yake, ulikuwa unalitibuatayari.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, kunamaboksi mawili ya mitandio kutoka Uturuki yaliingia huku juzi.

SPIKA: Hapana Mheshimiwa Keissy, maanaMheshimiwa Juma ulikuwa unachokoza nyuki. MheshimiwaLeah Komanya tafadhali.

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipatia nafasi na mimi niweze kutoa mchango wangu.Awali ya yote napenda kupongeza Wizara ya Fedha kwakazi wanazofanya ikiwemo za upelekaji fedha katika Serikaliza Mitaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini katika kitabu cha hotubaukurasa wa 32 Wizara imetoa mafunzo kwa Maafisa Uganina Ununuzi 75 kwa ajili ya mafunzo ya kutumia mfumo wamalipo wa Serikali EPICOR. Hata hivyo, mafunzo hayahayatakuwa na tija kama Serikali haitarekebisha upungufuuliomo katika mfumo wa EPICOR, kwa sababu mfumo huuunatumia cash basis. Kwa hiyo LPO sasa hivi zinaandaliwakwa kutumia cash tu, asilimia kubwa ya LPO zinatumiwa njeya mfumo, kwa hiyo dhana zima ya internal control au udhibitiwa ndani haipo.

Mheshimiwa Spika, upungufu mwingine pia upoikiwemo asset management bado hazijawekwa humo,

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

naishauri sasa Wizara ione namna inavyoweza kutekelezakuweza kuingiza package ambazo zinazopungua katikamfumo mzima wa EPICOR.

Mheshimiwa Spika, nishauri pia Wizara ijitahidi kuwekamfumo ambao utaweza ku-link mifumo mbalimbalikama PLANREP ili sasa taarifa mbalimbali ziwezekutoka katika mfumo wa EPICOR badala ya taarifanyingine kutengenezwa nje ya mfumo ama taarifabaadhi za ufungaji wa hesabu zikafanyikia nje yamfumo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba pia niipongeze Wizarakwa namna inavyopeleka fedha za elimu bila malipo,inapeleka vizuri, nimeangalia katika kitabu cha CAG hojailiyopo ni ndogo tu shilingi bilioni moja haikupelekwa naupungufu huu ulitokana na Wizara yenyewe kule ya Elimuambako kulikuwa kuna utofauti wa takwimu. Kwa hiyo,naipongeza kabisa kwa namna inavyopeleka fedha za elimubila malipo. Niipongeze pia Wizara kwa kupeleka fedha zaujenzi wa vituo vya afya au kuboresha vituo vya afya. Vituovyetu sasa hivi vilivyoboreshwa vina hadhi nzuri kiasi kwambawananchi sasa hivi wana mvuto wa kwenda hospitali zaSerikali.

Mheshimiwa Spika, nipongeze pia kwa namnainavyopeleka halmashauri ruzuku za matumizi ya kawaida.Kumekuwa hakuna na matatizo ya upelekaji wa ruzuku zakawaida, lakini tukumbuke kwamba ruzuku hizi zilipunguzwakutoka asilimia 100 mpaka 40. Ukiangalia pale pale mahitajiya halmashauri yako pale pale, stahiki za watumishi ziko palepale, mtumishi anatakiwa aende likizo, mtumishi anatakiwaagharamiwe masomo.

Mheshimiwa Spika, kwa kupunguza hiyo asilimiakutoka 100 mpaka 40 kumekuwa na changamoto kubwasana inayozikumba halmashauri katika upungufu wa fedha.Pamoja na hayo halmashauri zilitegemea sasa wangetumiafedha za mapato ili kuweza ku-accommodate shughuli zaidara zinazopata ruzuku.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine ilizozikumbahalmashauri ni mapato mengine kuchukuliwa na Serikali Kuuna mapato mengine kupunguzwa. Kwa mfano, Mkoa waSimiyu ushuru wa pamba ulipunguzwa kutoka asilimia tanohadi tatu kwa ajili ya standardize bei ya pamba. Halmashauriza Mkoa wa Simiyu zaidi ya asilimia 60, bajeti yake inatumiaushuru wa pamba.

Mheshimiwa Spika, changamoto zimeendeleakuzikumba halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa shughulizake. Ukiangalia kazi ziko pale pale, Waheshimiwa Madiwaniwako pale kwa mujibu wa Sheria, wanahitaji kulipwa,wanahitaji kufanya ziara, lakini saa hizi Madiwani haowamekuwa wakikopwa fedha kwa muda mrefu zaidi hataya miezi sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hao hao Madiwani tunategemeawakasimamie miradi ya maendeleo. Ukiangalia sasa hiviSerikali imejikita kutumia force account hilo ni jambo jema.Hapo hapo ukiangalia force account hiyo Wahandisi wengiwemeenda TARURA. Kwa hiyo, Madiwani ambao ni Wenyevitiwa WDC wanapaswa kusimamia ile miradi. Changamotoukiangalia wenyewe kwanza hawana fedha wamekopwa,halafu wanaenda kusimamia force account ambayo kwakiasi kikubwa ina-involve cash, pale Serikali ifanye tathmini.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwamba Wizaraya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha wafanyereview kwa sheria ambazo tumezipitisha. Kwa mfano wakupunguza rukuzu ya matumizi ya kawaida kutoka asilimia100 hadi asilimia 40, kuondoa vyanzo vya mapato, wafanyereview waangalie ni athari gani zilizopo katika halmashauri.Ikiwezekana sasa halmashauri hizi ziweze kupewa fidia, kamailivyofanyika 2013 baada ya kupunguza vyanzo vilivyokuwakero kwa wananchi, halmashauri zilipatiwa fidia mpaka leohiyo fidia inaletwa. (Makofi)

Mheshimia Spika, naomba pia niongelee kuhusuupelekaji wa fedha za miradi ya maendeleo, nikijikita katika

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

ruzuku ya uendelezaji wa mitaji za Serikali za Mitaa LGCDGau inavyojulikana kwa CDG. Ni miaka mitatu sasa hivi fedhahiyo imekuwa haipelekwi, fedha hiyo ni ya Wafadhili lakinisio asilimia 100. Kuna sehemu ambayo ni fedha ya mapatoya ndani ambayo inajulikana, kama Local kuna foreign naLocal. Hata hivyo, ukiangalia hata zile fedha za local hakunafedha iliyopelekwa katika miradi ya CDG. Kama wafadhilihawaleti je, Serikali ambayo inakusanya kwa nini haipeleki?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali sasa ione namnainavyoweza kuinusuru miradi hii iliyotekelezwa kwa fedha yaCDG kwa sababu kila mwaka tunaopanga wananchi lazimawaibue miradi na kuianzisha kwa ule mfumo wa C-matching.Kwa hiyo, miaka mitatu tumekuwa tukilimbikiza magofu,magofu, magofu kiasi kwamba tunawapelekea wananchiwanakuwa hawana imani sasa na Serikali waanza kupotezaimani kwa Serikali. Wananchi sasa hivi wametokea kuiaminisana Serikali ya Awamu Tano, sasa tusiwakatishe tamaa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara ya TAMISEMI ilifanya kikaoiliwaita Waheshimiwa Wenyeviti na Wakurugenzi kwamba,waainishe miradi inayoweza kutekelezwa ambayo inawezakumalizwa na fedha ya CDG ili sasa iletwe, lakini mpakaninavyoongea sasa hivi fedha haijaletwa. Tukumbukehalmashauri zingine ziliitisha Mabaraza Maalum, wakatumiafedha ili kuweza kupitisha miradi ambayo sasa inawezaikatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, namwomba sana MheshimiwaWaziri tuone namna tunavyoweza kui-rescue hii miradi,mingine ina miaka 10, mingine ina miaka mitano na kamaMfadhili haleti fedha kwa nini tunaendelea kubajeti? Nashaurikama mfadhili hajaonesha nia ya kuleta basi kwenye hichokifungu tuweke token figure ili mfadhili atakapoleta tufanyesupplementary budget, kuliko kuendeleza kulimbikizamagofu, watoto wetu hawana madarasa, zahanati zetuhazijakamilika. (Makofi)

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Leah umegusa nyoyo zaWaheshimiwa Wabunge. Kwa kweli fedha hizi za CDGmuhimu kweli kweli, sana sana, vinginevyo Wabunge sijuikeshokutwa tutakwenda kusema nini.

Basi tutaendelea na uchangiaji wakati wa jioni,orodha yote ambayo ninayo hapa nitaanza na MheshimiwaMasoud Abdalah Juma, atafuata Mheshimiwa Silinde naMheshimiwa Mlinga utafuata na wengine. Wote ambao mpokwenye orodha mtapata nafasi jioni ya leo.

Mheshimiwa Mchungaji alikuwa anasema kuhamiaDodoma umekuwa ni mpango wa dharura akawaamenigusa kweli. Mimi ninavyojua kutoka mwaka 1973 kwaIlani zote za Chama cha Mapinduzi ambacho kimechaguliwaall along hakuna Ilani ambayo haikutaja habari ya kuhamiaDodoma hata moja. Waliokuwa hawaweki ni wale ambaowalikuwa hawataki kuhamia Dodoma, kwa hiyo, walikuwahawakipi kitu hicho preference. Hakuna mpango ambao niwa muda mrefu constantly ukitaja all the time kama wakuhamia Dodoma na hautekelezwi. (Makofi)

Kwa hiyo, hiki ni kitu kimekuwepo throughout. Ndiomaana mpaka leo bado ile sheria ya kusema kwamba,Dodoma ni Makao Makuu haijaja. Ndio hiyo tunasema safarihii Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, katikaSheria zitakazosomwa mara ya kwanza safari hii Bunge hilihiyo lazima iwepo. Isipokuwa hiyo, safari hii hakuna sheriahata moja itasomwa kwa mara ya kwanza. Tulishasema,tukasema, sasa safari hii ni utekelezaji. Mwambie kabisa AG,kabisa, kama hiyo kitu haiko safari hii hakuna sheriaitakayosomwa mara ya kwanza safari hii, kwa hiyo Bunge lamwezi Oktoba, halitakuwepo.

Waheshimiwa Wabunge tunaahirisha shughuli zaBunge mpaka saa 10.00 jioni. (Makofi)

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 10.00 Jioni)

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae.

Waheshimiwa Wabunge, majadiliano yanaendeleatulikuwa tumeshamtangaza toka asubuhi MheshimiwaMasoud Abdallah Salim, Mheshimiwa Masoud AbdallahSalimu tuanzishie session ya jioni.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi MunguSubhanahu wataala aliyetujalia uzima na afya njema katikamwezi huu Mtukufu wa Ramadhani katika kumi hili la Maghfiraikiwa ndio siku ya 19 na nikimwona rafiki yangu MheshimiwaAlly Keissy ametulia kweli kweli leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Watanzania tulitegemeamakubwa kutoka Wizara ya Fedha. Tulitegemea fedhaambazo Waheshimiwa Wabunge tunazipitisha sisi katikamaeneo mbalimbali fedha hizi za maendeleo zitakuwazikitolewa, lakini imekuwa ni kizungumkuti; haifahamiki, halini mbaya, tatizo limekuwa ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, fedha za maendeleo katikaWizara mbalimbali hazitolewi kwa wakati hata zikitolewa basiinakuwa ni pungufu sana na inaonekana hadi sasa ni chiniya asilimia 40 ya fedha za maendeleo katika maeneombalimbali ya Wizara ambazo tumezipitisha. Hili ni jangakubwa, ni tatizo kubwa, tatizo ambalo wananchi mategemeoyao waliyokuwa na huyo yameondoka. Mheshimiwa Waziriwa Fedha atuambie tatizo hasa ni nini kwake Wizara yafedha? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia kwenye volume IITreasury mambo ambayo waliyojipangia katika maeneombalimbali, ukienda kwenye book four, nimwambie Waziriwa Fedha, kama kuna tatizo la vyanzo vya fedha, hana fedharipoti ya Spika ambayo imewekwa juzi Jumamosi pale Mezanikuna fedha ambazo zilipatikana kwenye uvuvi wa bahari kuu,hivyo ni vyanzo, kuna mambo tayari yapo kwenye ripoti ya

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Tume ya Spika aliyoiunda, vyanzo vya kutoka bahari kuu kunamatrilioni ya fedha, hebu aingie atafute fedha tatizo nini,mbona haeleweki, hasomeki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kuhusu wastaafu,hali ya wastaafu ni mbaya sana, wastaafu wetu kwa kipindikilichopita walikuwa kwenye kima cha chini kutoka Sh.50,000hadi Sh.100,000 baadhi yao walio wengi, lakini ahadi yetukwa wastaafu kwa hivi sasa inaonekana kama Serikali hainadhamira ya dhati kuboresha hawa wastaafu wetu ambaowastaafu walikuwa ni watumishi wetu, walifanya kazi kwauadilifu kwa muda wa kipindi kirefu lakini hali zao za maishani mbaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye hotuba hii ukiangaliaWaziri hana jambo ambalo la kushika zaidi akasema kwambalabda wastaafu hawa wataweza kupata maslahi yaliyomazuri ukurasa 104 kaeleza mengi, lakini kasema tu kunamoja, mbili, tatu.

Mheshimiwa Spika, nimwombe sana MheshimiwaWaziri, wastaafu wetu katika kada mbalimbali hali zao nimbaya sana. Nitoe mfano mmoja, wakati wastaafu kwenyeJeshi la Wananchi kuanzia cheo cha private hadi BrigadierGeneral Jeshini mafao yao yanakuwa ni madogo sana mbaliya hao wengine, hawa walifanya kazi, walikwenda kwenyevita, vita va Kagera, walikwenda Msumbiji na kwingineko, leowanayafungua mageti kwa watu binafsi inaumiza kweli kwelihasa kuanzia cheo cha private, Brigadier General hata hawawalinzi wetu hatuwathamini hawa walinzi wetu walipiganavita na Kagera, waliokwenda kuokoa Msumbiji hata hilo?Mwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hili nimwombe sanaMheshimiwa Waziri, mwenzake Waziri aliyepita MheshimiwaSaada Mkuya aliweza kufanikisha kupandisha hizipension za wastaafu kwa kila mwezi, hebu naye ajiandae,aandae mazingira mazuri apandishe hizi pension zawastaafu za kila mwezi kwa sababu hali imekuwa nimbaya sana.

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aangalievilevile katika suala la wastaafu pale wanapostaafu, kwanzamafao yao wanacheleweshewa sana, lakini yeye amesemakwamba wataandaaa mazingira, mazingira hayapo kwasababu gani kumekuwa na kudhulumiwa, kumekuwa nakunyonywa kwa wastaafu kwa muda mrefu hata ripoti zaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mbalimbalizimekuwa zikisema kwamba mafao ya wastaafuwanapunjwa.

Mheshimiwa Spika, watu wamefanya kazi kwauadilifu, wamechoka hata mafao yao, ripoti za CAG zipokibao, nyingi sana ripoti mbalimbali kwamba mafao yawastaafu wanapunjwa tangu mwaka 2013, angalieniripoti za CAG, jinsi wastaafu wanavyonyonywa nakupunjwa. Kumbe wazee wetu maskini kwa sababu yaSerikali wanawadhulumu na kuwapunja tatizo nini?Mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme pale ambapomstaafu anafariki. Anapofariki mstaafu wanafamiliawanafungua mirathi, lakini niseme tu kwamba inakuwa namilolongo mikubwa sana kuzipata zile haki. Familiainapofungua ile mirathi wakifika pale mahakamani ndani yamuda mfupi sana Hazina wanaambiwa kwamba hicho kitufaili lake halionekani. Baada ya mwezi mmoja kufa faili lakehalionekani na hayo yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mzee Bobali, baba yake mdogoMheshimiwa Bobali hapa, muda mrefu tangu amestaafu huuni mwaka wa kumi na hajapata mafao yake, ni tatizo kweliwanaofariki na wao mafaili yao wanaambiwa hayapo.Kwa kweli wastaafu wametupwa, wanaonewa hili nijambo kubwa sana na jambo ambalo kwambahalikubaliki.

Mheshimiwa Spika, nadhani kwamba hakuna kitukinachoumiza kwamba watu hao walitumika katika hali nzurisana wakati wakiwa na nguvu lakini wameachwaMheshimiwa Waziri atuambie tatizo ni nini alilonalo na ahadi

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

ya Serikali kwa wastaafu, kuna kipi kikubwa zaidi ambachowanawapelekea mpaka leo wanakuwa maskini sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, niache hilo, pale Hazina kunabwana anaitwa nadhani Kasekwa, yule huyu ni mtu mmojaambaye namwamini sana, kwa hiyo yale mafao ambayoyakitengenezwa na bila shaka hapa atakuwa yupo. Huyuaungane na wale na wenzake, ashauriane na wenzake ilihayo mambo yaende vizuri, ni mtu mmoja mzuri sana nadhanianakuwa ni Katibu Mtendaji si ndio ana cheo fulani pale,nina imani kubwa kwamba hili jambo wataweze kulifanyavile ambavyo inavyohitajika.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalolinawaumiza sana ni suala zima la shilingi milioni 50 kwa kilakijiji. Volume four ukurasa wa 24, Poverty EradicationDepartment, subvote 81,000, item 6508 hapa wameweka.Wanaweka nini humu na hawatekelezi, huku nikudanganyana bure. Najua ikifika wakati wanakuja kifunguhicho kimeafikiwa na ni cha mwisho kifungu hichokimeafikiwa ohh, waoo, hamna kitu, hawatoi fedhawanadanganya, wananchi wanasubiri kwa muda mrefu nahawajatoa hizi fedha, wanaandika kwenye vitabu, lakinihakuna kitu, tatizo nini, bora muwaambie tu kwamba, ni kwelihizi fedha hazipatikani sababu ni moja, mbili, tatu.

Mheshimiwa Spika, ni ahadi kweli ya Mheshimiwa Rais,akishasema jambo, jambo hilo ni lazima litekelezwe,Mheshimiwa Waziri tatizo lake nini, kama hana vyanzo hatajuzi Kamati ya Gesi imesema kuna mabilioni mengine hayochukua fanyieni kazi, mbali ukiachia leo uvuvi wa bahari Kuu,nawashangaa.

Mheshimiwa Spika, nawauliza Serikali kuna nini hukomwaka huu, hayo ndiyo maisha, mbaya mzunguko wa fedhahakuna, kila tunaposema tuna vyanzo fulani wachukuevyanzo fulani wavifanyie kazi hawataki, sasa wanatakaushauri kutoka wapi na sisi ndio Wabunge wao, tenaWabunge, Wabunge kweli, shauri yenu. (Makofi)

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Spika, randama hii hapa, wameelezakatika hii randama, ukurasa wa 119 mpaka 120, wamewekahii maelezo yao waliweka hapa, naombeni sana sisi niWabunge waelewa sana, wasitufanye hivi, Wabunge woteni waelewa sana humu, waandae mazingira basi hizi fedhamilioni 50 kwa kila kijiji wametenga bilioni 60, hizi kila mwakawanatenga, lakini fedha hizi wananchi wanalalamikaWabunge wanasema labda jambo hili limewashindaWaheshimiwa Wabunge, tunawaambia lakini Serikali siowasikivu, Serikali haitaki kusikia.

Mheshimiwa Spika, naomba kwa hili tena leoRamadhani kumi la maghfira hili, anajua Mheshimiwa Ashatunazungumza hivi taratibu sana, kama ingekuwa miezi mingineningesema maneno mengine, wajitahidi sana waandaemazingira hizi fedha zitolewe, hali ni ngumu sana .

Mheshimiwa Spika, nimalizie jambo moja dogo, kwanikuna tatizo gani katika hali ya maisha wanayoionaWatanzania na mzunguko wa pesa na maelezo yaMheshimiwa Waziri kuwa deni bado himilivu, tuendeleekukopa, sawa na utaalam wake mimi siko huko, lakini kwanini kwenye hotuba yake ya mwaka jana alituambia hapakwamba nia yake ni kuandaa mazingira, wale wanaokulamlo mmoja kutoka asilimia 9.7 sasa waende mpaka asilimia5.5, hotuba yake ya mwaka jana hiyo, ni maelezo yake, lakinimbona wanaokula mlo mmoja wameongezeka, umaskiniumeongezeka.

Mheshimiwa Spika, sasa alichokisema mwaka janahajakisimamia Mheshimiwa Waziri, sisemi kama yeye nimwongo lakini hakusema kweli, simwambii kwamba mwongohapana, siwezi na Ramadhani hii, lakini hakusema kweli kwasababu haya ni maandishi yake kwamba tutahakikisha katikabajeti zinazofuata wanaokula mlo mmoja wataondoka katikaasilimia 9.7 mpaka asilimia tano, leo maskini wameongezeka,hiyo asilimia aliyosema haipo, wanaokula mlo mmojawengi, wengine hakuna mlo, maisha magumu, halimbaya kupita kiasi, tukisema kuna vyanzo chukueni…(Makofi)

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

SPIKA: Mheshimiwa Masoud wewe takwimu yakounaitoa wapi, ya Waziri hiyo ya kwako wewe kwambaumaskini umeongezeka.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Spika,kwa wananchi, nenda Kongwa, nenda Mpwapwa, nendaDar es Salaam , nenda Mbeya, nenda Iringa kusanya watuupate hiyo, tunaangalia takwimu yake ambayo ametupaawamu iliyopita, sisemi kwamba ni muongo lakini jambolimemshinda fedha ziko wapi, tatizo nini? Hamueleweki!Nawashangaa mwaka huu! Kama kweli Serikali sikivu andaenimazingira basi msikie.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya fedha ni tegemeokubwa sana kupita kiasi, Watanzania wote wako na sikiokuangalia Wizara ya Fedha itafanya nini kuboresha maishaya Watanzania. Leo maisha ya Watanzania yamekuwani ombaomba walio wengi, kila siku umaskiniunaongezeka, uchumi unakua umaskini unaongezeka nchigani duniani hakuna uwiano baada ya uchumikuongezeka…

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Masoud.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Umaskiniumeongezeka na uchumi unaongezeka…

SPIKA: Mheshimiwa Masoud tayari muda haukoupande.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mwaka huu, hayatutawaona! (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge muwe mna-relykwenye statistics, yuko mama wa National Bureau of Statisticshapo anatusikiliza, ukisema hiki kimeongezeka unasemakufuatana na tafiti iliyofanywa na taasisi fulani, hii nimeitoakwenye reference fulani. Hata hivyo tunakushukuruMheshimiwa Masoud.

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

Sasa namwita Mheshimiwa David Silinde atafuatiwana Mheshimiwa Goodluck Mlinga na Mheshimiwa SalumRehani ajiandae.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Wizara ya Fedha naMipango. Kwa lugha nyepesi kabisa adui namba moja wamaendeleo ya Taifa hili ni Wizara ya Fedha na Mipango. Aduinamba moja na nina sababu, sababu namba moja Wizaraya Fedha inashindwa kutoa fedha ambazo zipo kisherianamba moja.

Mheshimiwa Spika, hili nalisema, nenda kwenye ripotiya Mkaguzi, angalia fedha ambazo Wizara kwa kupitia TRAwamekusanya na ambazo wamepeleka na zile ambazohawajapeleka, hawapeleki fedha. Leo ukienda kuangaliawatu wa korosho wanalalamika, wamekuja watu wa Bodiya Korosho kwetu wamelalamika juu ya Wizara ya Fedhawamekusanya bilioni 91, wamepelekewa bilioni 10, fedha yaohalali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, railway development levy, hakunahata senti iliyopelekwa kule, angalia kila kifungu Wizaraya Fedha wana sababu moja tu wanasema siku hizi uhakiki,yaani Serikali hiyo moja kigezo chao ni uhakiki na ndio kichakacha kujifichia kutokupeleka fedha.

Mheshimiwa Spika, Mawaziri hapa wanakuja wanaliafedha hakuna na fedha zao ambazo zipo kisheria, waojukumu lao ni kuchukua, kukusanya na kurudisha kule,hawafanyi wanalitakia mema Taifa hili, the answer is no,hawatakii mema Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, fedha za miradi ya maendeleoangalia kilimo chini ya asilimia 10, miradi ya maendeleo;viwanda ambavyo ndio tunahubiri, Wizara ya Viwanda naBiashara asilimia tisa, leo uchumi wa Taifa ambao tunaliakwamba tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

unapeleka asilimia tisa na Wizara hawawezi kuleta majibuhawa na tunawaona. Pia wana sababu za ajabu, maagizokutoka juu, maagizo gani, yaani huko juu ni wapi mbinguniyaani ambako sisi kama Taifa hatuwezi kufika.

Mheshimiwa Spika, hivyo tuulizane swali dogo,unapoagizwa kutoka juu, hivyo mtu anayekuagiza kuvunjasheria you need to know one thing. Leo mpo ninyi, keshoutawala utakuja awamu nyingine, itakuja Awamu ya Sitaatakayekuwa responsible ni ninyi Mawaziri kwa sababu sisihatutamgusa Mheshimiwa Rais ana kinga Mheshimiwa Raisyoyote yule awe ni Mheshimiwa Dkt. Magufuli, afanyechochote kibaya ana kinga, ninyi hamna kingatutawachukulia hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa haya ndio ambayoyanapelekea haya madudu kuendelea kufanyika natumekuwa tukishuhudia kila wakati, sasa kuna maamuziambayo Wizara inayafanya ambayo sisi kama Taifa ndiyotunaingia hasara, kwa mfano unajua unapojenga reli yastandard gauge ni jambo jema na sisi kama wananchihatupingiki tunakubaliana na hilo jambo, lakini unapoamuakukopa mkopo wa kibiashara kwenda kuhudumia reliambayo malipo yake ni baada ya miaka 20 ni kuliingizia Taifahasara, yaani unatumia current asset to finance the long termliability, ni nini ninachokisema? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mikopo ya mabenki wanakupamuda wa grace period ya miezi sita, mradi wako hujakamilikaunaanza kulipa fedha, lakini ukitumia concessional loan niwatu wanakwenda kwenye mradi, wanatekeleza mradi,mradi unakwisha, baada ya mradi kuisha unapewa mudafulani miaka mitatu, baada ya hapo ndio unaenda kuwalipa.Sasa leo hii miradi ni mema Kwa Taifa lakini tutaanza kulipakabla miradi haijakamilika.

Mheshimiwa Spika, baada ya miaka 20 ndio mradi ilepay back period yake kuanza kutoa faida ndio unaanza

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

kuiona, unajua matokeo yake ni nini? Hakuna maendeleoyatakayoendelea kufanyika, ndio maana leo tukija humundani kilimo wanalia, afya wanalia, elimu wanalia, majiwanalia, hakuna mradi unaofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa haya wanaosimamia niWizara ya Fedha, sijawahi kuona Wizara ambayo inashindwakuelewa kama Wizara ya Fedha na hii inabidi uwe mkali sana,bila kuisimamia Wizara ya Fedha kupeleka fedha hizi zotetunazosema hapa ni ngonjera, kwa sababu kilakilichoandikwa mwisho wa siku lazima kitafsiriwe na fedhaiende pale. wanatamka mapato yameongezeka, sisitunashangilia huko mtaani, haya tuonyesheni hela basi,hazionekani.

Mheshimiwa Spika, lLeo unakwenda angalia tu mfanomdogo tu deni la Taifa ndani ya miezi 12 wamekopa trilionisaba, hilo deni limeingia kwenye deni la Serikali, trilioni saba,haya waambieni hili deni la trilioni saba hela zake basituonyesheni na zile mlizokusanya ndani tuonyesheni vileviletuone hii miradi na utekelezaji wake mnafanyajewanakwambia tu hili ni himilivu kwa asilimia 34.4 ukomo wetuni 56%, hawazungumzii tax to GDP yaani makusanyo ya kodiagainst pato la Taifa, tuko kwenye 14.5%, ndio ambayo tukosasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa duniani kote siku hizi watuwalishaacha kutumia mfumo wa debt to GDP siku hizi watuwanatumia mfumo wa kodi kwa pato ghafi la Taifa. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Silinde hivi kweli unamfundisha Dkt.Mpango, uchumi?

MHE. DAVID E. SILINDE: Namfundisha vizuri!

SPIKA: Endelea bwana. (Kicheko)

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana umenielewa.Tunakumbushana, ni Mwalimu lakini ni mwananadharia. Miminayaishi haya maisha practically. Hii ndiyo changamotoinayo-face nchi. Maprofesa wengi wamefeli kwenye uongoziduaniani kote walipokabidhiwa. Kwa sababu hivi vitu, unajuakuzungumza na kutekeleza ni vitu viwili tofauti. Sasa hilotumezungumza, tunaona hali halisi. Sasa kuna mambo mengiambayo hawa wanasimamia, leo wanasimamia rufaa zakodi, angalia kule, kuna rufaa kibao; lakini wanasema ilitumsikilize mtu tupokee ombi lake lazima ulipe moja ya tatuya kodi. Ndiyo kazi ya Wizara ya Fedha, yaani ni kukandamiza.

Mheshimiwa Spika, angalia mikakati yao Wizara yaFedha. Mikakati yote ni kodi, kodi, ongezeko la kodi. Hakunamahali popote wanayoweza kukuonesha namnawatakavyozalisha ama namna ya watakavyotengezamkakati wa wale watu wetu kwenda kulipa kodi. Hawa ndiowanaosimamia, sisi tunawahoji kila siku. Kuna majibu menginetunayavumilia, lakini kiukweli wanataka kuvuna mahaliambapo hajawapanda, ndiyo kitu kibaya sana ambachohawa watu wanacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatizo lingine ambalo wanalo, nikutokutaka kuelewa. Kama walichokipanga waowameshakipanga, maelezo yote tutakayotoa ndani yaBunge hakuna jambo lolote watakalolisikia. Hilo ndilo tatizo.Wizara ya Fedha ina kiburi cha hali ya juu, sijawahi kuonakatika nchi hii!

Mheshimiwa Spika, imezungumzwa hapa awali,wamejikita kwenye fedha, kwenye mipango ni kama hamna.Hiyo ndiyo imekuwa changamoto katika nchi hii kwa miakamingi. Yaani inapofika suala la mipango, waulize hawaMipango, ndiyo hii mipango inakuja mambo mapya. CAGameshatoa mapendekezo mengine, wao wenyewewanayakimbia. Haya yote ni kwa sababu wanashindwakutusikiliza, wanashindwa kuelewa.

Mheshimiwa Spika, ubaya sana kwenye hizi nchi,inafika mahali watu wanawaachia haya nendeni basi

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

tuwaone, mtafikia wapi? Mtashindwa! Sasa ninachofahamu,Mheshimiwa Rais anahitaji kushauriwa vizuri. Yeye nibinadamu, hata kama kuna wakati ana-push jamboukimwelewesha usiku atalala peke yake, atasema lakini lilejambo Mheshimiwa Waziri Mpango alinimbia kweli. Sasa ileakikwambia tu “nimesema kuanzia leo, toa hela hizi pelekahuku.” Unasema sawa mzee. Hakuna Taifa la namna hiyo!Lazima umwambie hapana Mheshimwa Rais. Nitatekelezahilo jambo lako, lakini lazima tufuate utaratibu. Ni mambo yakawaida. Hata Mbinguni kule kwa Mungu ili uende Mbingunilazima ufuate utaratibu, hakuna dunia inaendeshwa bilautaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya ndiyo yaliyotufikisha leohapa. Ni kwa sababu mambo mengi na fedha nyingi,zinakwenda bila utaratibu. Mwisho wa siku wanasema malibila daftari huishia bila habari. Kwamba unaweza ukakusanyamali nyingi, lakini kama unashindwa kurekodi, kuwa namipango, yaani hutafanya kitu chochote. Miaka mitano;imebaki miwili, itakwisha, mtakuja na the same story. Mtaishiakupiga kelele tu kwamba tumetekeleza; tuoneshenimlichokitekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, shilingi milioni 50 kila kijiji, ipokwenye rekodi hapa; leo mwaka wa wangapi? Wa tatu huu,ndiyo bajeti ya tatu; tumebakiwa na bajeti mbili tu.Wanatenga, lakini hawajapeleka hata shilingi mia. Ipokwenye taarifa yao. Walitenga shilingi bilioni 59, wakasematunakwenda kwenye pilot study; hawajapeleka hata shilingimia. Mwaka 2017 wakatenga shilingi bilioni 60, hawajapelekahata shilingi mia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tukija tukiwahojitunaonekana tunakosea, lakini ni kweli hizi takwimuwameziandika wenyewe; wanaotudanganya ni waowenyewe; lakini yote hii ni kwa sababu wanaamini sisihatuelewi. Sisi tunajua, tunaweza kuwa katika ujinga wetutunaelewa kidogo, lakini kwenye hiki cha ujinga kinatoka kwawananchi. Wewe unafika Jimboni mtu anakuuliza,Mheshimiwa Mbunge shilingi milioni 50 hazijaja hapa kwa

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

sababu wewe Mbunge ni mzembe, lakini unajua kabisa nikwa sababu Mheshimiwa Waziri wa Fedha kasema helaitakuja. Namwuliza hela iko wapi? Anakwambia helaitakapopatikana. Si mmetuelezaa hela zipo nyingi huku! Sasahilo ndiyo tatizo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Silinde.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Mlinga naMheshimiwa Rehani.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwanza nataka nimpe taarifa kaka yanguMheshimiwa Silinde amesema kwamba Serikali inatumiakichaka cha uhakiki kama kujificha. Kwa faida ya Bunge,mimi professional yangu ni Mtawala. Elimu ya juu nilisomaUtawala na ya juu zaidi nikasoma Sheria za Upatanishi naUsuluhishi. Kwa hiyo, migogoro hapa ni kaburi lake.

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia uhakiki waWatumishi Serikalini, hata wale wanaoenda kuhakikiwawanajiandaa jinsi ya kukwepa ule uhakiki. Kwa hiyo,mnaweza ukazungumza uhakiki kwamba Serikali haimaliziuhakiki, mkumbuke hata wale wanaoenda kuhakikiwa nawale waliowaingiza wale watumishi hewa, kwa sababuwanajua wakigundulika na wenyewe watakuwa matatani,kwa hiyo wanajiandaa jinsi gani ya kukwepa huo uhakiki. Kwahiyo, wasiituhukumu Serikali tu wakasema uhakiki hauishi. Sisiwatawala tunaelewa uhakiki maana yake ni nini nachangamoto zake ni zipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo langu la pili ambalonilikuwa natamani sana kulizungumza leo kwa kupata nafasihii, nchi yetu mwanzo ilikuwa nchi ya wakulima, wafanyakazi

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

na wafanyabiashara. Kuna kundi lingine limeongezekakubwa sana. Sasa hivi nchi yetu ni ya wakulima, wafanyakazi,wafanyabiashara na wacheza kamari. Bahati nzuriimezungumzwa, sasa hivi wanafunzi wote wa Vyuo Vikuuwakipata mikopo wanajazana kwenye vituo vya kuchezakamari.

Mheshimiwa Spika, pia wazee wetu wakipata pensionwanaenda kucheza kamari; wake zetu, zamani sisi enzi zetuwakati tunaoa, unaambiwa ili uwe na maisha mazuri, ukipatakahela kako mpelekee mkeo akatunze. Ukimpelekea mke,ukija kuchunguza simu zake, unakuta meseji za Biko na TatuMzuka. Madereva wa Bodaboda wote, yaani vijana wotetunavyozungumza sasa hivi, wote wanacheza kamari. Hili nijanga la Taifa. Gaming Board watafute namna gani yakuliratibu.

Mheshimiwa Spika, madhara ya kamari ni makubwakuliko biashara nyingine. Rafiki yangu Mheshimwia Musukumahapa alikuja na zao lake mbadala kwa ajili ya kutuleteauchumi tukalikataa, tukasema lina madhara, lakinininavyokwambia kamari madhara yake ni makubwa kulikobangi au kuliko hata viroba. Kwa hiyo, tutafute utaratibuwa kuendesha kamari, lakini siyo kama sasa hivi inavyoenda.

Mheshimiwa Spika, labda tu kwa watu ambaohawajui madhara ya kamari; kwanza, imevunja nguvu kaziza nchi yetu. Zamani ilikuwa ukienda vijijini unawakuta vijanawanacheza pool table. Sasa hivi pool table haipo, vijanawote kwenye betting maana kamari zenyewe ziko nyingi,zimeongezeka, mara kuna Tatu Mzuka, Biko, sijui Mkeka Bet,sijui nini bet, yaani ziko nyingi kweli kweli na zinaongezekakwa kasi, umeona.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nguvu kazi ya vijanaimepotea. Vijana wote wanaamini watakuwa matajiri, kwasababu matangazo yale ambayo tumeyaruhusu kiholela sasahivi inawafanya vijana wengi wawe na tama. Mtu anasemanitapata kesho, nitapata kesho. Kwa hiyo, akipata kihelakidogo, kwenye kamari.

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Spika, madhara mengine ni addictive.Mtu yeyote anayecheza kamari hawezi kuacha. Naowalivyokuwa wataalam, anakupa Sh.5,000/= leo umeshinda.Ukishinda Sh.5,000/= hiyo huwezi kuacha, hata ucheze shilingimilioni 20 hutaacha. Kwa hiyo, inasababisha hiyo addictive,wenyewe wanaita uteja.

Mheshimiwa Spika, lingine madeni. Watu sasa hiviwanaenda kukopa kwenye Vicoba ili wacheze kamari. Kwahiyo, inasababisha Taifa la watu kuwa na madeni. Ndiyomaana hata ukienda kwenye Vicoba mikopo hailipiki, watuwanakopa kwa ajili ya kwenda kuchezea kamari. Hivyo,malengo ya Taifa letu yanapotea kwa sababu wengiwanaweka malengo kwa kutegemea kamari.

SPIKA: Mheshimiwa Mlinga ukiona kuna Mbungeyeyote anacheza kamari, tupate jina tumpeleke maadili.(Kicheko/Makofi)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Sawasawa. (Kicheko)

SPIKA: Endelea Mheshimiwa.

MHE. GOODLUCK A MLINGA: Kwa hiyo, ndiyo hivyo.Ninachoomba Gaming Board watafute utaratibu wakuendesha haya mazoezi ya kamari, lakini siyo kwa mfumohuu. Watafute mfumo mwingine. Wametoa matangazo; kunatangazo wamelitoa zuri, lakini hilo tangazo linapita kwa watukiasi gani? Maana yake wanasema, usitumie fedha yenyemalengo mengine kuchezea kamari. Hebu niwaulize, leo hiiTanzania nani ambaye ana pesa ambayo haina malengoimekaa tu? Kila pesa tunayoipata ina shughuli , ada za shule,nini na vitu vingine, lakini watu wanaishia kwenye kamari.

Mheshimiwa Spika, kuna mwanafunzi mmojaalijinyonga juzi juzi hapa kwa sababu alitumia pesa ya adakwenye kamari na akaliwa. Kwa hiyo, naomba MheshimiwaWaziri wakati ana wind-up atuambie ni namna gani GamingBoard watatafuta utaratibu wa kuendesha kamari bilakusababisha matatizo ambayo yanatokea sasa hivi? (Makofi)

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Mheshimiwa Spika, suala la pili, wakati Serikali yetuya Awamu ya Tano inaingia madarakani, tulikubaliana Serikalinzima tubane matumizi yasiyo na tija ili hiyo pesa tuipelekesehemu nyingine ya maendeleo. Kweli tulifuta safari za njekama Bunge, sasa hivi hatuendi nje. Taasisi za Serikali zilitoafedha zao kutoka kwenye mabenki ya biashara wakapelekaBenki Kuu. Pia pakatolewa maelekezo kuwa tutumie hudumazinazozalishwa na taasisi za Serikali. Hata matibabu ya njeyalizuiliwa. Mpaka mtu aende kutibiwa nje inatakiwautaratibu mrefu na ionekane kuna haja ya muhimu kabisahuyu mtu kwenda kutibiwa nje.

Mheshimiwa Spika, hivi ninavyoongea, Benki Kuu yaTanzania ndiyo taasisi inayotumia fedha nyingi katikamatibabu bila msingi wowote. BoT Mfanyakazi akiwa namafua anaenda kutibiwa Uingereza au India. Wanatumiafedha nyingi na wamesahau kuwa hizi fedha ni za walipakodi.

Mheshimiwa Spika, Taasisi zetu za Serikali zimewekewautaratibu maalum kwa aji l i ya kupatiwa matibabu.Tunaitumia NHIF, hata Bunge tulikuwa tunatumia PrivateCompany sasa hivi tumeingia NHIF, BoT wanatumia PrivateInsurance gharama ya matibabu ambayo wangeitumia NHIFshilingi bilioni moja wanatumia shilingi bilioni 12 kwamwaka. Angalia ufisadi wa hali ya juu uliopo. Shilingi bilionimoja kwa shilingi bilioni 12 kwa sababu watu wana maslahibinafsi.

Mheshimiwa Spika, wewe ni shahidi, wanasema waohawawezi kwenda NHIF kwa sababu haina matibabu nje yanchi. Sasa naomba niulize, wao wanasema taasisi yao ni nyeti,Usalama wa Taifa wako NHIF, Bunge tuko NHIF, PCCB wakoNHIF. Mke wa Rais aliugua, alilazwa Muhimbili, lakini BoThawakubali. Wanasema wao taasisi yao ni nyeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge tulikubalihadi matezi dume tulipimwa kwenye Dispensary ya Bungehapa hatukuona tatizo, lakini wao mtu akiugua kidogowanataka kwenda nje.

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mheshimiwa Spika, naomba ulisimamie hili. Kunaufisadi mkubwa katika mchakato huu wa BoT kwendakupata matibabu kwa kutumia Private Insurance.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, siungimkono hoja ya Mheshimiwa Waziri mpaka atakapokuja namajibu ya haya niliyoyatoa. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, endapo Mheshimiwa Mlingaunachokisema ni kweli, kwamba wametoka kwenye onebillion sasa watumia shilingi bilioni 12 hawa BoT, nakuagizaMwenyekiti wa PIC kuiita Bodi ya BoT ndani ya wiki moja naManagement yake, wajieleze kwa nini wanafanya matumiziya aina hiyo kwenu? Maana yake, ni kwamba baada ya hiyowiki moja mtaripoti kwangu kwamba ni kitu ganikinachondelea. Hatuwezi kufanya mambo ya namna hiyo.

Mheshimiwa Salum Rehani, hayupo eeh? MheshimiwaMendrad Kigola.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika, naminashukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia.Kwanza nianze kutoa pongezi kwa Wizara ya Fedha. Wizaraya Fedha imeweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri sana. Bahatinzuri taarifa tuliyoisoma ipo wazi. Pale walipo-perform vizuriwanasema na pale wanapojua hawaja-perform wanasema.Huo ndiyo tunasema uwazi. Ndiyo maana kila mmojaanasema labda kwenye kilimo amepeleka asilimia kadhaa,ipo wazi; kuliko asingesema vitu ambavyo ame-perfom. Kwahiyo, nimempongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwauwazi huo.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Wizara ya Fedhandiyo moyo wa Serikali, ndio moyo wa maendeleo ya nchihii na ndiyo inayo-control mapato yote ya nchi hii. Ili Serikali i-perform vizuri, lazima Wizara ya Fedha ikae vizuri. Tunajuakwamba ili Serikali ifanye vizuri lazima makusanyo ya kodiyakae vizuri. Kuna Mbunge mmoja alisema kwamba Wizarahii inataja kodi tu, lazima itaje kodi tu kwa sababu isipotajakodi haiwezi kupata fedha ya kuendesha shughuli za Kiserikali.

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Kwa hiyo, nasema waendelee kutaja kodi tu ili na wananchiwaelewe kwamba lazima wananchi walipe kodi ili Serikaliifanye vizuri kwenye miradi ambayo tunahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kuangalia, wameelezavizuri kwamba wanataka kupunguza umaskini. Natakanijikite vizuri sana kwenye kupunguza umaskini. Wanatakawafanye ufuatiliaji kwenye vijiji ili waangalie umaskiniumepungua percent ngapi? Tuna changamoto nyingi sanavijijini.

Mheshimiwa Spika, nataka niiombe Wizara ya Fedha,lazima isimamie vizuri kuhakikisha kwamba mahitaji yawananchi kule vijijini kweli yanapungua. Nataka nitoe mfanomdogo tu, tukisema kupunguza umaskini kwa wananchi,lazima tuhakikishe miradi ile inayolenga wananchi inafanyikakiusanifu na kwa bei inayojulikana. Wengine wanasema,Serikali isifanye uhakiki, wanasema kila siku ni kuhakiki.Nasema kuhakiki kuongezeke kwa sasabu unaweza ukaonaSerikali imelipa fedha nyingi sana lakini mradi wenyewehauonekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haiwezekani Serikali ikawa inatoafedha nyingi, halafu mradi ule hauonekani. Kwa mfano,wanachimba kisima cha maji vijijini, wananchi hawajapatamaji, lakini fedha zinaonekana zimetumika pale. Hiihaitakubalika hata siku moja. Zamani miaka mitano iliyopita,unaweza ukaona wananchi wanahitaji maji pale kijijini,wanasema kwamba Mkandarasi ametumwa na Serikali,labda Wizara akachimbe kisima cha maji. Maji hajapata,unaenda kuangalia gharama kubwa pale zimetumika nawananchi hawajapata maji. Hii kweli itakubalika? Hii haiwezikukubalika. Lazima tuone impact. Kama fedha zimetumikakwa ajili ya kuchimba kisima, basi wananchi wapate majipale. Hilo lazima Serikali ihakikishe inafuatilia vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna changamoto kubwa sana.Kwa mfano miradi ya maji. Naiomba Serikali, miradi ya majimpaka sasa hivi kama tunapunguza umaskini, basitupunguze kwenye mradi ya maji, tuhakikishe wananchi wetu

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

wote wamepata maji. Kuna Wakandarasi wengine badowanadai fedha hazijalipwa. Kwa mfano, hata kwenye Jimbolangu, kuna kata moja ya Sawala, Mkandarasi sasa hivi kunamiezi sita alishasaini mikataba lakini mpaka leo hajapatafedha na mradi ule umesimama na wananchi wanatakaimpact ya maji. Kama tunapunguza umaskini, basituwapelekee maji.

Mheshimiwa Spika, kuna sehemu nyingine wananchiwanatembea kwa mguu kilomita nne au kilomita tatuwanatafuta maji. Sasa tusipokijita vizuri, hata hii perceptionya kusema tunapunguza umaskini, tutakuwa hatujapunguzaumaskini. Wananchi wanataka wapate maji. NamwombaMheshimiwa Waziri wa Fedha, wananchi wanataka kupatamaji. Miradi ile ya maji ambayo tumetenga kwenye bajeti,basi wapeleke tuhakikishe inafanyika kwa ufanisi kamailivyopangwa ili wananchi waweze kupata maji.

Mheshimiwa Spika, suala lingine, kwenye makusanyo.Serikali i j itahidi kufanya makusanyo. Lazima kwanzaitengeneze urafiki na wafanyabiashara, TRA watoe elimu yakutosha ili kuhakikisha kwamba kila mtu anayelipa kodi asionekama adhabu, aone ni wajibu wake kulipa kodi. Ili ajuekwamba ni wajibu wake kulipa kodi, lazima utaratibu waulipaji kodi uwe mzuri. Kuna point moja nimeipenda sanakwamba Wizara ya Fedha kushirikiana na TRA wanatakautaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba kila mtu anayelipakodi asikwepe. Hiyo nimeipenda, huo ni mfumo mzuri wakuhakikisha kwamba kila mtu analipa kodi, hiyo ni njiamojawapo. Hata hivyo, lazima tuhakikishe kwamba walewalipa kodi, tunajenga urafiki nao, tunawapa elimu, ili kilammoja nayelipa kodi asione kama adhabu.

Mheshimiwa Spika, kuna masuala ya fedha zilezinazopelekwa kwenye Halmashauri za maendeleo. NaishauriSerikali kwa sababu wanapeleka quarterly, sijajua system yakupeleka, lakini fedha ziende kwa muda unaotakiwa, ontime. Unaweza ukaona Mkandarasi ameingia mkatabalabda wa mwaka mmoja. Usipopeleka fedha on time kamamkataba unavyosema, matokeo yake ukichelewesha fedha,

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

inatokea Mkandarasi baadaye anaanza kuidai Serikali,baadaye ule mradi bei inaongezeka, Serikali inaanza kulipariba.

Mheshimiwa Spika, mradi wa shilingi bilioni mojabaadaye inakuja kusomeka hata shilingi bilioni tano. Kwahiyo, naiomba Serikali ipeleke fedha kwenye miradi mikubwa,kwenye Halmashauri kwa muda uliopangwa. Hii itasaidiasana kuhakikisha miradi ile inakwisha on time.

Mheshimiwa Spika, suala lingine nataka niipongezeSerikali kwenye point moja. Serikali kufikiri miradi mikubwa yakimaendeleo ndani ya nchi yetu ndicho kinachotakiwa.Hatuwezi kuwa tunafikiri miradi midogo midogo tu halafutunasema nchi itafikia uchumi wa kati, haiwezekani hatasiku moja. Lazima ifikiri miradi mikubwa ambayo inajengauchumi ndani ya nchi yetu. Kwa mfano, ule mradi wa umemewa Rufiji ni mradi ambao utatutoa katika hali ya umaskini.Kwa sababu ule umeme tunaweza kuuza hata nje.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, Malawi watanunua,Zambia watanunua na nchi nyingine za East Africawanaweza wakanunua umeme kutoka pale. Ndiyo nchi yetuitapata fedha za kigeni, ndiyo tutafikia uchumi wa kati.Ukisema kwamba unataka kufikia uchumi wa kati, wewe unaplan kulimalima mboga, bustani na kadhalika, uchumi wakati utaufikia wapi? Lazima tuwe na miradi ya kimkakatiambayo inaleta uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, point nyingine ambayo nimeiona,Serikali kufikiria kujenga reli, hiyo ni point kubwa ana katikanchi zinazoendelea. Hata ukienda Ulaya utakuta kuna relizimejengwa standard. Kwa mfano, sasa hivi kuna standardgauge, ni kitu cha msingi sana. Kwa hiyo, nataka niwaambie,kama tuna-plan uchumi, lazima tufikiri vitu vya kiuchumiambavyo vinaleta hela kubwa ili uchumi wa kati ufikiwe.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna watu wengine wanakatishatamaa, wanasema Serikali sijui haifanyi kazi. Sasa hivi

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

tunaingia kwenye vitu vikubwa ambavyo ni pigo kubwa kwauchumi ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Tukitaka kupata fedhanyingi, lazima tufikiri vitu ambavyo vinaweza vikatuingizia.Hata wawekezaji wanapokuja, wanauliza vitu vya msingi.Kwa mfano, atauliza barabara, miundombinu ya umeme,maji, hospitali; wafanyakazi wakiugua wanatibiwa wapi?Hivyo ndivyo vitu wanavyouliza wawekezaji. Wewe hunabarabara, umeme, maji wala hospitali halafu unasemaunatafuta mwekezaji, utampata wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali inapobuni vitu vyamsingi lazima tui-support na sisi Waheshimiwa Wabunge. Bilakui-support Serikali kwa vitu vya msingi hatutaendelea hatasiku moja. Kwa hiyo, nataka nimwambie Mheshimiwa Waziriwa Fedha, akaze buti, afikiri vitu vya msingi ili nchi yetu iwezekusonga mbele. Hatuwezi kuwa tunarudi nyuma kila siku,Waheshimiwa Wabunge tunauliza maswali madogo madogoambayo Serikali inaweza kutatua kwa muda mfupi sana. Kwahiyo, tunafuta maswali sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, hatupendi sisi Wabunge tukifikahapa tunauliza masuala ya maji, tunauliza kuhusu barabarandogo ndogo, zahanati ndogo ndogo; Serikali inakuwaimeshatatua. Sasa ili kutatua lazima tujifunge mkanda. Bilakujifunga mkanda, kujibana vizuri hatuwezi kuendelea hatasiku moja. Lazima Serikali ibane vizuri lakini ilete maendeleo,tuone impact. Siyo Serikali ibane halafu tuwe na njaa,hapana. Ubane vizuri, tunakula lakini tuhakikishe kila mmojaanafanya kazi kwa nafasi yake vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala lingine la utendaji kazi.Unaweza ukaona document moja inapelekwa kwenye ofisi,inazunguka miezi mitatu. Namwomba Mheshimiwa Waziriwa Fedha, document isizunguke. Mtu anatoka Halmashaurikule anafuatilia document hapa, inachukua siku mbili au tatu.Hii haiwezekani, unaweza ukaona gharama za ufuatiliaji wadocument, inataka kukaribia mradi unaofuatiliwa. Hiiinakuwa ni system mbaya sana. Kwa nini tusitafute system,mtu yuko Halmashauri kule, ana-lodge document yakemtaalam huko anasoma kwenye computer, analipa

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

malipo, simple. Anaona hiki kipande nimeelezwa vizuri, anadocument… (Hapa microphone ilikata)

Muda umeisha?

MBUNGE FULANI: Aah, endelea.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Niendelee, ahsante sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu yuko Halmashauri kule ana-search tu document kwenye computer, mtaalam hukuanasoma. Akishasoma ana-reply within the minute, yule kuleatakuwa ameshaiona. Akishaiona, basi inajibiwa. Sasa mtuanaanza kufuatilia wiki moja, mbili, anafuatilia document. Hiiinarudisha nyuma maendeleo. Kwa hiyo, nataka nihamasishewafanyakazi, hasa wale wa Idara ya Fedha, kwenye hiliwasimame vizuri, wasilimbikize kazi ambazo hazina msingi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni wastaafu. KunaMheshimiwa Mbunge aliuliza asubuhi kwamba wastaafu waobado wanadai, wanalipwa kiasi kidogo sana. Wale wastaafuni wa kuwaheshimu, wamefanya kazi nyingi sana mpaka sasahivi nchi imefika hapa. Wewe mtu amestaafu, alifanya kazinzuri, kwa nini usimlipe haki yake vizuri? Lazima tuhakikishewale wazee ambao na wenyewe wanatuombea na sisitufanye kazi vizuri, tuwalipe stahili zao kama inavyotakiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, haiwezekani mstaafu unamlipaSh.50,000/=. Kama sheria inasema alipwe Sh.100,000/=, mlipeSh.100,000/= yake. Kama inasema Sh.200,000/= mlipeSh.200,000/= yake, sasa mzee amestaafu anafuatilia mafaokuna watu wengine hawajapata mafao mpaka leoinachukua miezi mitatu na zaidi na mtu anastaafu yukokwenye system. Kwa nini anastaafu leo, kesho humlipi helayake? Mtu yuko kijijini, kwa mfano yuko Mufindi, afuatilieDodoma au Dar es Salaam wakati system inasoma. Kwa niniasilipwe on time? (Makofi)

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Spika, naiunga mkono Serikali, naungamkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mendrad Kigola.Baada ya muda atafuata Mheshimiwa Deo Sanga. Kablaya Mheshimiwa Deo Sanga, nimekuona Mwenyekiti wa PACsasa umeshaingia. Mwenyekiti wa PAC, ametoka tena! Basiwajumbe wa PAC mpo hapa, mpo si ndiyo?

MBUNGE FULANI: Yes!

SPIKA: Nimesema Kamati yenu ifanye kazi kabla yaJumatatu, kuanzia keshokutwa Jumatano mna-ample time,Alhamisi, Ijumaa mwite Bodi ya BoT na Senior Managementyake, kabla ya kukaa na BoT na Senior Management Teamya BoT muwe mmekaa na Mheshimiwa Mlinga kuhusu hilijambo aliloeleza na muwe mmekaa na National HealthInsurance Fund, mmenielewa? Mnakaa na MheshimiwaMlinga, mnakaa na NHIF halafu sasa ndiyo mnawaita hawaBoT.

Baada ya kufanya kazi yote hiyo, haraka sanamtaniletea majibu ya kazi yenu ili niweze kumwandikiaMheshimiwa Rais, il i kama wao hawawezi ku-reverseimmediately baada ya mkataba wao kwisha, tuhakikishebasi mkubwa wa nchi anaingilia kati. (Makofi)

Mheshimiwa Deo Sanga.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia. Kwanza nianzekwa kumshukuru Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, KatibuMkuu pamoja na Watendaji wote wa Wizara ya Fedha kwakazi nzuri waliyoifanya kwa kuwapa fidia wananchi wanguwa Jimbo la Makambako. Nawashukuru sana, kwa dhatikabisa kwa sakafu ya moyo wangu, nawashukuru sana,wamefanya kazi nzuri. Kwa sababu fedha hizi wamezidaikwa muda mrefu, lakini kupitia ahadi ya MheshimiwaRais imetekelezwa. Narudia tena kuwashukuru sana.(Makofi)

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Spika, ninaposhukuru, kuna ombi tenakuhusu fidia nyingine. Pale Makambako kupitia Wizara yaUjenzi, wana eneo ambalo waliomba, tuwaombe wananchikwa ajili ya kujenga One Stop Centre katika Kijiji cha Idofili,kilometa tano tu kuingia Mjini Makambako ukitokea barabaraya Iringa. Katika eneo hilo, vile vile kunatakiwa kulipwa fidiaili waanze kujenga One Stop Centre. Namwomba sanaMheshimiwa Waziri katika hitimisho lake, basi aseme neno iliroho za wananchi wangu wa Jimbo la Makambako wawezekupona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, tuna Liganga naMchuchuma. Imezungumzwa kwa muda mrefu sana kuhusuuchumi wa Liganga na Mchuchuma. Namwomba sanaMheshimiwa Waziri wa Wizara ya Fedha, atuambie ni ninikinachokwamisha Liganga na Mchuchuma isitekelezwe auisianze? Kwa hiyo kwenye hitimisho pia nitaomba nipatemajibu, tatizo ni kitu gani ambacho kinafanya isianze?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine tumejenga zahanatinyingi sana katika nchi yetu ambayo magofu haya ni mengiikiwepo Jimbo la Makambako. Makambako tuna zahanatiya vijiji zaidi ya 13 ambazo wananchi, WaheshimiwaMadiwani, Serikali, Mfuko wa Jimbo pamoja na mimi Mbungewao tumejenga zahanati hizi. Ombi langu kwa Wizara yaFedha, tuone sasa ni namna gani kwa nchi nzima na kupitiahata Halmashauri yangu ya Makambako tuzimalize zahanatihizi ili zianze kufanya kazi kusogeza huduma kwa wananchiwetu na hasa akinamama na watoto. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Wacha!

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, jambo linginenapenda sana Mheshimiwa Waziri atakapokuwaanahitimisha, nipate majibu hasa ya miradi ya maji 17 nchiniikiwepo na Makambako kwa fedha za kutoka Serikali ya Indiakwa mkopo nafuu. Maana mpaka sasa hatuelewi kazi hiiinaanza lini. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Waziri piakatika miradi hii 17, mmojawapo upo Njombe, Makambako,

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

Wanging’ombe na mahali pengine Zanzibar kule kuna mradimmoja nadhani. Basi ni vizuri Mheshimiwa Waziri atuambieni lini miradi hii itaanza ili wananchi waweze kupata hudumahii ya maji kama ilivyokusudiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, katika Wizarambalimbali ambazo tumekuwa tukichangia hapa ndani,Waheshimiwa Wabunge wengi wamesema, nami naombaniseme Mheshimiwa Waziri. Namwomba Waziri wa Fedha,fedha hizi za miradi mbalimbali basi ziende kwa wakati ilishughuli zilizopangwa kule kwenye Halmashauri yetu ziwezekwenda vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa Waziri, kupangani kuchagua. Kuna watu walizungumzia habari ya kununuandege, habari ya reli, habari ya huo umeme kwamba huoumeme wa kutoka Bonde la Rufiji hauna manufaa na relihaina manufaa. Niseme kwamba Bunge lililopita la mwaka2010 - 2015, Waheshimiwa Wabunge walisema hapa, ni nchiya ajabu hii kutokuwa na ndege zake yenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Serikali imetii kupitiaMheshimiwa Rais wetu, maana alikuwepo Bungeni hapawakati ule akiwa Waziri, leo ametii, amenunua ndege katikanchi yetu, tunasema kwa nini amenunua ndege, hazinamanufaa. Tukiwa hapa Bunge la mwaka 2010/2015tulizungumzia hapa, ni nchi gani haina reli? Reli hii ya kati nireli ambayo imepitwa na wakati, tunataka standard gauge.Mheshimiwa Rais ametii, amekubali, sasa ametafuta fedhatunajenga reli ya standard gauge. Kupanga ni kuchaguandugu zangu, ni lazima tusiwe vigeugeu, tuiunge mkonoSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulizungumzia hapa kwambawawekezaji wanashindwa kuja ni kwa sababu umemehautoshi. Leo ufumbuzi umeme kutoka Bonde la Rufiji,tunasema ule mradi haufai. Sasa tunajikatisha tamaawenyewe kwa wawekezaji wanaokuja kwamba kumbeumeme kule haupo. Tuunge mkono jitihada za Serikali yaAwamu ya Tano juu ya mipango mizuri ambayo ipo. Kwa

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

hiyo, Mheshimiwa Waziri Mpango na Wizara yake naWatendaji wake, achape kazi asonge mbele. Mipango nimizuri sana. Kwa hiyo, sisi tuko nyuma yako, tunamuungamkono kupitia bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, wenzangu wamesema hapa,Mheshimiwa Waziri amekuwa muwazi, ameeleza kila jambo;hili liko hapa, hili bado hivi, hili liko hivi. Tunamuunga mkono,achape kazi, asonge mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Deo Sanga.Mheshimiwa Sebastian Kapufi, atafuatiwa na MheshimiwaWilfred Lwakatare.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwa ajili ya muda, nianze kwa kuunga mkonohoja. Naomba nianze na kipengele cha kwanza kinachogusiarasilimali fedha. Najua kwa kupitia Taarifa ya Kamati, ukurasawa tatu na wa nne kwa ujumla wake naomba kipengelehiki muhimu tukione kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa tatu ule,kipengele hiki kinagusa hilo suala la rasilimali fedha, anasema:“Baadhi ya mafungu ya Wizara yamepata fedha za kutoshana hivyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Vile vile kunamafungu ambayo hayakupewa fedha za kutosha, hivyokuathiri utendaji kazi wake.” Hilo ni eneo la fedha.

Mheshimiwa Spika, kama haitoshi, tunaambiwa,kama Wizara ya Fedha na Mipango imeshindwa kuwezeshakwa baadhi ya vifungu vyake kupata fedha za kutosha kwaajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya msingi, itawezajekuhakikisha mafungu ya Wizara nyingine kupata fedha zakutosha?

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa rasilimali fedha,najua Wizara hii ni muhimu. Kama yenyewe tu inapata shida

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

eneo la fedha, vipi kuhusu Wizara nyingine? Naomba hiloliangaliwe sana. Nalisema hilo kwa maana ya suala hilohilo la rasilimali fedha, kuna huu mradi wa LGDG ambapokwa nia njema kabisa, Serikali ilikuwa imekusudia kwa wakatimmoja kutoa fedha ili kumaliza miradi viporo, lilikuwa nijambo jema sana. Kwa mfano, kule kwangu kwa kupitiaruzuku y a Serikali, kwa kupitia TAMISEMI of course, lakiniWizara ya Fedha iki-facilitate hilo jambo, kuna zaidi yaSh.923,475,000. Fedha hizi zilikuwa zimelenga maeneo yaelimu na afya.

Mheshimiwa Spika, leo mashaka yangu ni kwambatunakwenda karibu robo ya mwisho na bahati mbaya fedhahizi ambazo Serikali ilikuwa imekusudia kupeleka huko katikawilaya na maeneo mbalimbali, kwa bajeti hii inayokuja,hakuna sehemu fedha hii inasomeka. Kwa hiyo, nilichokuwanaomba kwa namna yoyote ile, tuhakikishe fedha hizizimekwenda huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hilo, kuhususuala la rasilimali fedha, napongeza kwamba kwa kupitiaTaarifa ya Kamati kuna maeneo mbalimbali yanazungumziasuala la Wizara kuendelea kufanya mazungumzo ili amakupunguziwa au kusamehewa madeni. Najua hilo likifanyika,litaendelea kutoa nafasi ya fedha za ndani zinazopakanakugharamia bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, nikitoka hapo, najua nanakubaliana na wale wote na Wizara tunaomba MheshimiwaWaziri alielewe vizuri, nakubaliana na maelezo yaliyotokakwenye Kamati kwamba ukitaka kukusanya mapato zaidi,ni lazima uwekeze zaidi, siyo kutegemea mapato bilakuwekeza. Kwa hiyo, naendelea kuomba namna yoyote ileambayo itatusaidia kwenda kuongeza mapato.

Mheshimiwa Spika, katika hili niendelee kushauri,najua ndugu zetu wa TRA lengo ni kuhakikisha nchi inapatafedha kwa kupitia kodi. Bado nashauri namna rafiki,najua suala la kudai kodi siyo jambo jepesi, linatakakusukumana, lakini kwa kupitia namna rafiki, bado

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

inaweza ikamfanya mtoaji wa kodi akaona umuhimu wakutoa kodi ikienda sambamba na elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikitoka hapo, eneo la mafao yawastaafu na mirathi, naona hili katika Taarifa ya Wizara,ukienda ule ukurasa wa 39 na 40, najua kimetengwa kiasicha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulipia michango ya mwajirikwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hadi kufikia Aprili, 2018kiasi cha shilingi bilioni 716.1 sawa na asilimia 71 kilikuwakimetengwa.

Mheshimiwa Spika, nasema suala hilo ni jemaMheshimiwa kwa maana ya kujali mafao ya wastaafu namirathi. Niendelee kusisitiza Mheshimiwa Waziri, wafanyakazihawa, wastaafu hawa ni uti wa mgongo wa Taifa hili, niwatu ambao waliitumikia nchi hii kwa uzalendo mkubwa.Inapofika sehemu mtu kastaafu, ni wajibu wa Serikalikuendelea kumwangalia mtu huyu. Nashauri sana hiloliendelee kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikitoka hapo Mheshimiwa, kunasuala la uhakiki wa madeni ya watumishi na Wakandarasi naWazabuni pia. Eneo hili la madeni najua mara ya mwishoSerikali ilitoa kiasi cha fedha kwenye kuonesha jitihada zakuanza kupunguza madeni ya wafanyakazi. Nafahamu kwaujumla wake, katika eneo hili kule Mkoani kwangu Katavi,eneo tu la madeni ya watumishi kuna takribaniSh.501,918,296/= ambapo humo ndani pia tuna madeniyanayowagusa Wazabuni, kuna Watumishi wasiokuwaWalimu na kuna Walimu.

Mheshimiwa Spika, ninachoomba, ili kuondelea kutoatija kwa watu wetu, eneo hili la madeni ya Watumishi naWazabuni kama ambavyo imesomeka katika maeneombalimbali, nilikuwa naomba liendelee kufanyiwa kazi.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikitoka hapo, najua kuna sualalinazungumziwa kuhusu kupuangua kwa mfumuko wa bei.Kati ya vipengele vilivyoongelewa kuhusu suala la kupungua

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

kwa mfumuko wa bei, limeongelewa suala la kuongezekakwa uzalishaji wa chakula kama baadhi ya vitu vilivyosaidiakupunguza mfumuko wa bei. Narudi kwenye point ile ile yamsingi, tunapofarijika na kuongezeka kwa uzalishaji wachakula, mtu wa kawaida ambaye hana elimu ya uchumi,anatamani kuona kumbe kama hili linachangia kwenyekufanya mfumuko wa bei usiwepo lakini yeye aliyeshirikikuzalisha chakula kwa namna gani anapata moja kwa mojamafao ya yeye kukizalisha chakula. Nikilisema hilo, tafsiri yangutuendelee kuangalia namna ambapo huyu mzalishaji wachakula na yeye anapata manufaa ya moja kwa moja.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikitoka hapo, najua lugha zotehizi zinazoongelewa hapo, tunaambiwa kwamba kutokamwaka 2017 kwa maana ya mfumuko wa bei ilikuwa 5.3,napongeza hilo, lakini kwa maana ya 2018 umeshuka mpaka3.8. Huu mfumuko wa bei na kushuka kwake ni jambo jema,lakini naendelea kuishauri Serikali yangu, namna pekee yamtu wa kawaida kuliona hilo, usomeke kwenye mifuko yake.Ikisomeka kwenye mifuko, tunakuwa tunaimba wimbommoja, wananchi na Serikali yao.

Mheshimiwa Spika, najua kwa maana ya malengoya mpango wa bajeti kwa mwaka 2018/2019, umeandaliwakwa kuangalia dira ya 2025, lakini kuna malengo endelevuya 2030. Ukija katika ukurasa wa 85 kwa maana ya Hotubaya Mheshimiwa Waziri kwa maana hii ya malengo ya mpangowa bajeti, inasema hivi:

“Baadhi ya vitu ambavyo wamezingatia ni pamojana masuala mtambuka kama vile jinsia, watu wenyeulemavu, mazingira, UKIMWI, makundi mengine yaliyo katikamazingira hatarishi na masuala ya lishe kwa jamii pamojana maelekezo na ahadi zilizotolewa Kitaifa.”

Mheshimiwa Spika, niendelee kushauri. Kama kumbebajeti hii malengo na mipango yake inazingatia suala hilo;masuala ya walemavu, masuala yanayogusa UKIMWI,nilikuwa naomba suala hili liendelee kusomeka. Walengwa

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

kwa maana ya walemavu wafike sehemu wakutane na kileambacho mipango inaelekeza kwamba watu hawawameguswa moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama haitoshi, eneo la UKIMWInaomba niendelee kushauri, mara nyingi na watu wenginewamekuwa wakiliongelea hili. Wakati tukitenga fedha kwaajili ya kusaidia masuala ya watu wenye maambukizo navinginevyo, nashauri eneo la watu wazima kutumia sehemukubwa ya fedha na walengwa wakawekwa pembeni, jambohili naliona halina tija. Kwa hiyo, naomba niendelee kusisitiza,wakati tunazungumzia suala hilo tujaribu kuendeleakuangalia kwamba walengwa, fedha sehemu kubwa iendeikawaguse walengwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo, naminiendelee kupongeza kama nilivyosema mwanzo. Naungamkono hoja. Nakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Nakushukuru sana MheshimiwaSebastian Kapufi. Nilitarajia kwenye Wizara kama hii wenzetuwa Kamati ya Bajeti wangekuwa ndio wachangiaji wengi.Kwa sababu ndiyo mmekaa na Wizara hii mwaka mzima kwaniaba yetu; na tulipanga wachumi wengi, wahasibu wengi,na ni ambao tuliamini kufuatana na maandishi yenu kwenyeCV zenu kwamba mna degree hizo, sasa matokeo yakesiwaoni. Majina yote niliyonayo ni ya akina Mzee Sanga nawengine. (Kicheko/Makofi)

Itabidi tuiangalie upya hii Kamati, nanyi ndio mnakaamasaa mengi kuliko Kamati nyingine yoyote. Hichomlichokuwa mnakiangalia mwaka mzima kiko wapisasa? Mnatuangusha sana. Nyie ndio mnatakiwamchambue sasa mtuambie, what is happening? Kwa hiyo,mlikuwa mnakaa tu huko mnakunywa chai halafuhamna kitu!

Haya Mheshimiwa Lwakaratare halafu MheshimiwaRiziki ambao wala sio Wajumbe wa hizo Kamati, tuendelee.(Makofi)

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa Spika,ahsante. Awali ya yote nitoe pole kwa familia ya MarehemuMheshimiwa Bilago kwa kuondokewa na mpendwa wao. Piapole kwa Waheshimiwa Wabunge wote hususan Chama chaCHADEMA. Pia namwomba Mwenyezi Mungu awezekumsimamia na kuweka mkono wake kwenye operation yaMheshimiwa Lissu ambayo inasemekana ni ya mwisho ili iwezekufanyika vyema na aweze kupona na kuweza kuungananasi pia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja zangu ni mbili ambazonimetumwa na wananchi wa Bukoba Town, ambazo kimsingizinawagusa Watanzania wote kwa ujumla wao. La kwanzani suala la property tax. Siku chache zilizopita, namshukuruMheshimiwa Naibu Waziri ambaye ni shemeji yangu, alitoaufafanuzi mzuri sana kuhusiana na nyumba ambazozinapaswa kulipa property tax na categories ambazozimepangwa.

Mheshimiwa Spika, kuna nyumba ambazo kimsingi,kiutaratibu zilipangiwa kulipa Sh.10,000/= ambazo ni nyumbazilizopo kwenye squatters ambazo ni unsurveyed na nyumbaza ghorofa ambazo zipo katika maeneo hayo. Nyumba hiziza squatters ni Sh.10,000/= na nyumba za ghorofa ambazozipo kwenye sehemu ambazo haziko surveyed na walahazijafanyiwa evaluation ni Sh.50,000/=. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ninayoileta hapa, wananchiwa Bukoba wanaamini wanatapeliwa na TRA, kwa sababuhivi sasa TRA inatoza karibu almost nyumba zaidi ya asilimia70 za ndani ya Mji wakidai kwamba zimefanyiwa evaluation;wakati utaratibu uliotumika kuzungumzia hicho kiwangoambacho kinasemekana kilifanyiwa evaluation ni kwambataratibu za Sheria ya Uthamini hazikufuatwa.

Mheshimiwa Spika, kilichotokea ni kwamba ni watuwameunda kikundi wakawaendea wataalam ndani yaHalmashauri husika. Wanakwenda kwenye nyumbambalimbali, wao wana-dictate terms wana-dictate zile rateskwamba hii nyumba thamani yake shilingi milioni 50, hii ni

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

shilingi milioni 100 bila kufuata Sheria ya Uthamini. Kwa hiyo,hivi sasa ni disaster na naamini iko katika maeneo mbalimbaliya miji mbalimbali hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wamebambikiwa ratesambazo siyo sawasawa na thamani ya nyumba; na nyumbazenyewe ziko vichochoroni. Mbaya zaidi tunajua Sheria yaUthamini lazima iwe shirikishi, aidha na Uongozi ulioko katikaeneo hilo la mitaa, eneo ambalo watu wenyewe, wahusikawenye nyumba hizo, wanapaswa washirikishwe, wanapaswawataarifiwe. Sasa watu wamekuwa wanakutana na bili zaTRA wakishangaa zinatoka wapi, kwa sababu wakati wazoezi la evaluation hawakushirikishwa wala hawajui lilifanyikalini? Kwa hiyo, huu mimi naweza nikausema ni utapeli wahali ya juu na kwa kweli wananchi wa Bukoba Townwamenituma kwamba wanataka maelezo yenye misingiiliyosimamiwa na Sheria ya Tathmini.

Mheshimiwa Spika, vinginevyo, kwa kuwa kule kunawatafiti wengi, hivi sasa zoezi tunalolifanya, tunakusanya dataza nyumba ambazo evaluation imefanyika kinyemela nabaada ya kukusanya hizo data tutatafuta ushauri wa hatuagani ya kuchukua na hata ikibidi kuipeleka TRA Mahakamani,kusimamisha zoezi hili mara moja kwa sababu halikufuatautaratibu wa kufanya tathmini.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa nyumba zinazotozwahela, unakuta mtu ni mzee kabisa amestaafu, anaambiwaile nyumba ambayo masikini ameijenga katika mazingiramagumu kwa hela ya pensheni mtu anaambiwa atoeSh.150,000/= kwa mwaka, atazitoa wapi? Kuna nyumba watuwengine wamerithi kutoka kwa wazazi wao ambaowameshafariki, unakuta amebaki mjane, wote haowanatozwa hela kwa rates ambazo kwa kweli niunaffordable, hawana uwezo wa kuzilipa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sambamba na majibu aliyoyatoaMheshimiwa Waziri, namshukuru alitoa majibu ambayoyamesimama vizuri, lakini kwa mazingira ya Bukoba Town nikwamba lile zoezi la evaluation ambalo wanadai ndiyo

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

linasimamia rates ambazo zinatozwa na TRA, zoezihalikufanyika katika taratibu za kisheria. NamwombaMheshimiwa Waziri anapo-wind-up azungumzie Bukoba,tutakwenda hivyo au twende na route ya kutafuta haki mbeleya vyombo vingine.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo kimsingi nalolinalalia huko huko, ni kwamba Mheshimiwa Waziri amekuwakatika takwimu zake na katika vyombo vya Habari na taarifazinazotolewa na TRA kwamba wanakusanya vizuri, hongerakwa hilo. Kwa mtu anayekusanya vizuri, vilevile kuwepo navielelezo na taswira na mazingira ya kuonesha anakusanyavizuri lakini pia analipa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimekuwa katika bajeti ya Wizarakwa kuwa nimo ndani ya Kamati, kwa nini fedha hazitoki?Mbona Wakandarasi wengi wanadai? MbonaWakandarasi wanasaini mikataba nje ya wakati?Naomba kabisa Mheshimiwa Mpango, asione haya, pesainakwenda wapi? Nieleze linalozungumzwa, mimi sinaminong’ono, wanasema yeye anabana mno, mpakapenalty. Pesa hazitoki. Zina mlango mmoja wa kuingia,lakini wa kutoka ni mwembamba kama uletunaoambiwa wa kwenda Mbinguni. Kwa nini pesahaitoki? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilifikiria labda hapa tukiwapamoja na Kambi ya Upinzani na wenzetu wa CCM, kamaanatuonea haya, hebu wakiwa kwenye caucus hukowazungumze, wanong’one, kwa nini pesa haitoki? Kwa hiyo,maendeleo ambayo tutaendelea kuyazungumza kimsingiyanakuwa ni maendeleo ya vitu, siyo ya watu. Watuwamechacha ile mbaya, maisha hayatamaniki.

Mheshimiwa Spika, kuna watu wanakula mlo mmojapamoja na kwamba wengine hawakufunga Ramadhani,lakini inabidi wafunge kwa sababu hela haiko katikamzunguko. Watu wa Bukoba wanauliza hela iko wapi? Helanyingi inayokusanywa, inakwenda wapi? Naomba atupemajibu hapa. Kama ataona hapa kuna soo, wakikutana

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

huko, najua caucus watakutana, hebu awaeleze Wabungewenzetu wa CCM hela inakwenda wapi? Mbona matatizo!(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili sambamba na hilo kuhusumadeni, nawazungumzia wapiga kura…

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Lwakatare. Pokea taarifa.

TAARIFA

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, natakanimpe taarifa mzungumzaji kwamba siyo Watanzania wengikwamba wanakula mlo mmoja. Watanzania wote tunakulamlo mmoja, ila tunakula mara tatu. Kwa sababu asubuhi uji,mchana ugali, jioni ugali. Kwa hiyo, mlo ni ule ule mmoja,lakini tunakula mara tatu. (Kicheko/Makofi)

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa Spika,nimepokea na kukupongeza kwa hilo.

Mheshimiwa Spika, nazungumzia specifically madeniya Wakandarasi wa Mji wa Bukoba na Mkoa wa Kageraambao wamenituma. Tunazungumzia kwa mfano,Wakandarasi wa Mradi wa REA ambao tunaambiwa mpakaleo wanadai. Kimsingi, bahati nzuri wale Wakandarasiwakubwa wana watu wa kuwazungumzia. Natakakuzungumzia kwenye local content, niite local content basiya miradi hii, kwamba kuna ma-supplier wadogo wadogoambao wanakuwa wanawa-supply hawa Wakandarasiwanaowadai. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina ma-supplier zaidi ya 20 hapaambao wamem-supply contractor aliyekuwa anasimamia nakuendesha mradi wa REA katika Mkoa wa Kagera. Hawawatu wanadai zaidi ya Sh.1,300,000,000/= hawajalipwa.Wengine majuzi Benki zimetangaza kuwafilisi na kunadishanyumba zao. Kuna mama mmoja alikuwa ana-supply vyakulakwa wafanyakazi wa Kampuni hii, yule mama ameukimbiamkoa kwa sababu ya madeni. (Makofi)

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

Mheshimiwa Spika, nataka watueleze haya madeniyanalipwa lini? Kwa sababu yasipolipwa yana-affect hatawengine ambao wapo chini wanao-supply vitu mbalimbalikwa hawa Wakandarasi. Kuna bwana mmoja ambayempaka katika kituo chake cha mafuta ameshindwa kununuamafuta mengine kwa sababu alikuwa supplier wa huyuMkandarasi, anadai mamilioni ya hela.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Wazirianapo-wind-up atueleze kwa sababu haya madeni hayawa-affect hawa Wakandarasi wakubwa tu, yanawa-affect hatama-supplier wadogo ambao kimsingi ndio wapo wengi kulechini. Ndiyo maana circulation ya hela inakuwa haipo nawatu wanaishia kwenye umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la tatu ambalo naombaMheshimiwa alifafanue, ni hiki kitu ambacho kinaitwa uhakiki.Nashangaa na nitaomba kwa kweli nipewe tuition kidogo...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Wilfred Lwakatare.Mheshimiwa Riziki Lulida, atafatiwa na Mheshimiwa ShallyRaymond.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote,nakushukuru nami kunipatia hii nafasi ya kuchangia hojailiyokuwa mezani. Kwanza nakupongeza kwa kazi kubwauliyoifanya kwa kuunda Tume ya Bunge kuangalia udhaifuuliojitokeza katika makinikia pamoja na uvuvi. Hii imeletafaraja kubwa katika Bunge letu, kuwa sasa hivi Bungelinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, mwanzo lilikuwa Bunge ambalounaona kabisa lipo lipo lakini naona sasa hivi umeliamshadude ndani ya Bunge na Bunge liko vizuri. Nakuomba tena,tunataka Bunge Live ili hayo unayoyaunda watu wayasikiekule mtaani. Wananchi, wapiga kura wanataka kusikia niniunazungumza, Wabunge wako wanafanya nini? Hii kazi

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

itasaidia kuweza kuleta uelewa kwa wale watu, watakuwawanajua kinachoendelea ndani ya Bunge. Hoja za Wabungewao zinazungumzia nini? Tukikaa humu ndani wananchihawaoni hayo unayoyafanya. Kwa hiyo, ningeshukuru sanana hilo nalo ungeliamsha ingeleta tija zaidi. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Sawa kabisa. (Makofi)

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, naona kunahoja nzito ya wafanyabiashara, wakulima dhidi ya kuwa namahusiano mabaya na mabenki. Benki zimeamuakuwakandamiza wafanyabiashara hasa wakulima. Tumeonakatika miaka miwili wakulima wako katika hali ngumu sana,wamelima mazao, lakini baada ya kulima mazao Serikaliimewasimamishia maendeleo yao kwa kutokununua mazaoyao. Matokeo yake benki hazikai chini kuangalia ninitatizo la hawa wakulima? Matokeo yake sasa hivi kilabenki inataka kuuza mali za wakulima, mali zawafanyabiashara. Nafikiri Mheshimiwa Waziri akae chini nawatu wa benki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Benki Kuu imepunguza riba kubwasana kwa benki nyingine, nafikiri ni kama 9%, lakini benki hizobadala na wao kupunguza riba, wameongeza riba imekuwakubwa sana. Imekuwa kubwa kiasi kwamba hakunamfanyabisahara wa kawaida ambaye anaweza kukidhi haja.Ukiweka pesa wanaweka percent, ukitoa pesa wanawekapercent na ndani yake kuna udhaifu mkubwa. Nafikiri hatana maeneo haya ya benki yaangaliwe kuna nini? Kama BenkiKuu imepunguza riba, kwa nini bado wao wanaongezeamzigo mkubwa kwa wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali hii inakatisha tamaa kwawakulima. Nataka nikupe mfano, nachukua mfano wawakulima wako wa Kibaigwa. Pale palikuwa nawafanyabiashara wakubwa wa mazao, miaka mitatuwamekutana na crisis za mvua na pametokea mafurikomakubwa, wao bado wanaendelea na interest, lakinihawaangalii kuwa je, wenzao ambao wamekutana namafuriko ambayo siyo wao, ni mipango ya Mwenyezi Mungu,

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

wangekaa chini wakapunguza riba ile ili na wao wawezekufanya biashara. Matokeo yake wanawakandamiza nakutaka kuuza mali zao bila kuangalia nini tatizo.

Mheshimiwa Spika, Kenya, Waziri wa Fedha na watuwa benki wamesimama na wanafanya biashara. Nami ninaimani kuwa Mheshimiwa Waziri ananisikia, atasimama nabenki na kuangalia wafanyabiashara wakubwa wanaathirikavipi na mikopo ya benki ili kuweza kuisaidia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia TRA. Ukiona mahalingoma inachezwa sana, basi haikawii kuharibika. TRA waliletaEFD machine. Kuna siku nilifika katika petrol station karibumara mbili, nikifika wananiambia mashine haifanyi kazi.Nikauliza kwa nini haifanyi kazi? Hela zinaendeleakuchukuliwa, lakini zile hela ambazo zinatakiwa ziingie katikaSerikali haziingii. Nataka nijue idara ya ICT ya TRA inafanyakazi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama mpaka Mbunge amekujakuliona hili suala humu ndani, baada ya siku ya pili tumeonamashine zinafanya kazi, hii ni hujuma. Hujuma kamahamuisimamii itakuwa ni hujuma kubwa sana. Kwa vile ICTDepartment ndiyo inaweza kuingiza data ndani ya programya Serikali na kuingizia pato Serikali, lakini kama ICTDepartment ikicheza na ma-hackers kwa kufunga hizi EFDMachines hizi pesa zote badala ya kuingia katika Mfuko waSerikali zitaingia katika mifuko ya watu wengine ambao sisihatuwajui. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nijiulize swali, MheshimiwaWaziri atakapokuja kumaliza ku-wind up aniambieDepartment yake ya ICT iko makini? Huwa ni network, maanakatika ICT inabidi ianzie TRA, iende mpaka katika mabenki,iende mpaka TCRA kuona je, humo ndani yake kuna nini iliangalau huu uovu, utasema Serikali haipokei mapato,kumbe mapato yanaingia kwa watu binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia suala la miradimbalimbali ambayo imesimama kwa muda mrefu. Nataka

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

nitoe mfano wa LNG (Liquefied Natural Gas) ambao uko Lindi.Tulitegemea mradi ule ungekuwa tayari umeshaanza kazi,lakini pamesuasua kwa muda mrefu, hatuambiwi mpaka leoule mradi umesimama wapi? Huu ni mwaka wa tanowananchi wamechukuliwa maeneo yao hawajalipwa, lakinikinachoendelea hakijulikani.

Mheshimiwa Spika, hii inawapa mwanya wawekezajikuchukua ile miradi kuipeleka Mozambique. Sasa hivi kilamradi ambao tunaukataa Tanzania, wenzetu Mozambiquewanauchukua, matokeo yake badala ya kwenda mbeleitakuwa sisi tumesimama na miradi yetu tukiwa na urasimuambao mimi sijajua, lakini naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja kujibu aniambie.

Mheshimiwa Spika, kuna kitengo ambacho ni Taasisiya CAG ya Ukaguzi. Kwa kweli hapa pana mtihani mzito sana.Kuna maeneo ambayo Serikali imeyaachia yasikaguliwe.Kwa nini? Kama Jeshi linakaguliwa na Bunge linakaguliwa,maeneo hayo ndiyo mianya mikubwa ya kupoteza helaambazo sisi hatuzijui.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano. Wafanyakazi wotewa Serikali mishahara yao inapitia NMB. Madaktari mishaharayao inapitia NMB na taasisi zote za Serikali zinapitia NMB, lakinihapakaguliwi. Sasa hivi nataka kufikia mwisho mpakabinadamu yule au biashara yao imekufa unakwenda kufukuamakaburi. Tuache biashara ya kufukua makaburi. Kama nisheria, walete Bungeni, Bunge lipitie sheria, wakaguliwe NMB,NBC na taasisi zote ambazo inabidi zikaguliwe. Kamahawakagui ndiyo mianya inapita ya pesa kwenda nje. Kamahawaiangalii mianya hii, leo kama taaisisi kubwa, mikopoyote ya Serikali iwe ya wanafunzi, inapitia NMB, halafuwanasema hawaikagui, wanalionaje hili neno? Ni hatarikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni lazima CAG awe nameno. Sheria ya CAG iletwe irekebishwe, apate fedha zakutosha ili awe na uwezo wa kukagua. Ama la, CAGanakagua chini ya 40%, ina maana maeneo mengi

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

anashindwa kukagua. Kama anashindwa kukagua, ni vipiwataweza kujua athari ambazo zinapatikana katika maeneombalimbali? Leo hii unamwona CAG anashindwa kukaguamaeneo mengine. Hakuna haja ya kufichaficha, tuseme aah,hapa TAKUKURU tusikague.

Mheshimiwa Spika, kwa nini TAKUKURU isikaguliwe?Pesa zinazokwenda pale ni za Watanzania. Matumizi ya paleni ya Watanzania. Kama watu hawa hawakaguliwi, ndiyomianya hiyo, maana watu wanatumia pesa bila kukaguliwa.Maana Jeshi wanakagua, ndiyo ambapo nilitegemea nisehemu nyeti sana, lakini anasema maeneo menginehatukagui. Hiki ni kigugumizi ambacho hakina maana,naomba Mheshimiwa Waziri atakapoingia katiak ku-wind-up anipe majibu kwa nini maeneo mengine yameachwayasikaguliwe, tunaachia watu tu wanatumia wanavyotakawao, wanakuwa na viburi vya kutosha? Hivyo naiombaSerikali iifanyie kazi.

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia suala la barabara.Leo hii Mikoa ya Lindi na Mtwara ndiyo kwenye uchumi.Tunaona uchumi wa Mkoa wa Lindi kwa ajili ya koroshoimekuwa ni green gold kulinganisha hata na madini mengine,lakini hatuna barabara. Tumekuwa maskini watu wa Mkoawa Lindi, hapapitiki leo kwenda Liwale, Liwale ina Selous,lakini hakuna barabara, Liwale ina korosho, hakunamaendeleo ya barabara, Nachingwea hakuna barabara,Kilwa hakuna barabara. Sasa wanapelekaje uchumi bilakupeleka na barabara? Uchumi utakwenda sambamba namiundombinu. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziriatuambie, bajeti i l iyopelekwa katika maeneo yaleyanayozalisha, Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvumainakwendaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Riziki Lulida.Nilishamtaja Mheshimiwa Shally Raymond, atafuatiwa naMheshimiwa Rose Tweve.

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa nafasi hii. Kipekee kabisa namshukuruMungu kwa kutupa sisi sote zawadi ya uhai, tupo hapatunazungumza mambo ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakupongeza tena na niunganena mwenzangu aliyetangulia kwa wewe jana kupokea ripotizile mbili na kuzikabidhi Serikalini, Ripoti ya Natural Gas na ileRipoti ya Uvuvi. Tumeona kazi yako na nia yako njema katikakudhibiti mianya yote ambayo inatupotezea mapato katikanchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hiinimpongeze sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha naniipongeze hotuba yake ambayo kwa kweli imeandikwa vizurina tumeielewa na ndiyo maana unaona mijadala yote ikomoto.

Mheshimiwa Spika, kabla sijasimama nilipokuwanajiandaa ilinilazimu kwenda kule Library nikachukua Hansardya mwaka 2017 ambayo pia wenzetu walikuwawamechangia. Niseme wazi kwamba nimei-miss michangoyao na sijui kwa nini mpaka leo hatupati michango yaupande wa pili? Kwa nini nimevutiwa kwenda kuchukuamichango yao? Nilitaka kuona mambo waliyoyazungumziamwaka 2017 leo yameendaje? Mengi waliyokuwawamelalamikiwa yametekelezeka na lazima niseme wazikwamba Mheshimiwa Waziri Mpango mambo yako yakovizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ni moyo wauchumi na ndiyo maana wote wanaozungumza wanaipigamawe, lakini tunasahau kwamba kuna mambo mazuriyamefanyika hapa katikati. Mwaka 2017 kipindi kama hikikila mtu alikuwa analalamika bei juu, walio kwenye MweziMtukufu wa Ramadhani vyakula viko juu, sukari hakuna,mahindi hakuna, mchele ghali; lakini leo kila mtu amekaaraha mustarehe. Kila kitu kinapatikana, Mwenyezi Munguamesikia kilio chetu, uji upo, mchele upo na sukari ipo.Mambo hayo yote wanadamu tumezoea kila siku kulalamika;

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

hata mambo mazuri hamwoni sasa? Hata mvua zilizokujahamzioni? Hata watu wanafuturu vizuri, wakiwepo naWaheshimiwa Wabunge wanafuturishwa kila leo, hawaoni?Bado wanalalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu akiwa na hulka yakulalamika, hakuna namna unavyoweza kumbadilisha, lakininamshukuru Mungu mfungo huu umekuwa mzuri. Nisemekwamba na hiyo iweze kumpa pia, ahueni huyu MheshimiwaWaziri wa Fedha.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombaniende katika ule ukurasa wa 87 wa Hotuba ya MheshimiwaWaziri unaozungumzia uratibu wa mikakati ya kupunguzaumasikini. Nilipokwenda Library nilichukua pia kitabu chaWizara hiyo cha mwaka 2017, kama hiki na nikaenda ukurasahuo huo katika uratibu wa mikakati ya kupunguza umaskini.Kilichozungumzwa mwaka 2017, mwaka jana ilikuwa ukurasawa 76 mwaka huu ni 87, hayapishani sana. Ni mambo mazurindiyo, lakini yote ni kwenye makaratasi.

Mheshimiwa Spika, mwananchi wa kawaidaukimwambia unapunguziwa umaskini kwa kuzidi kuboreshaau kuandika maandiko ya SDGs, maandiko ya PovertyMonitoring System, tunazidi kuboresha mifumo, tunazidikuboresha, haimuingii akilini. Nami pia niliyetumwa hapa nawanawake wa Kilimanjaro wanaonisubiri waone tumepigahatua kwenye kupunguza umaskini, naomba kutamkakwamba sielewi. Ni kwa nini sasa sielewi?

Mheshimiwa Spika, nilitaraji sasa baada ya wasomikuangalia hizo SDGs waje na pendekezo au waje na maagizokwa Serikali; jamani, tumeamua kupunguza umaskini,tunaomba au tunaagiza sasa tupeleke projects ambazowananchi watazisimamia na wanawake walio hapa wengini Viti Maalum, wanajua ambavyo wanaombwa kulekwenye maeneo yao semina ya kujifunza ujasiriamali,semina za kuboresha maeneo, za mazingira, semina zaufugaji, l akini wanafuga nini? Hakuna mifugoiliyoboreshwa. (Makofi)

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri wangu waFedha akatuzungumzie kunakopatikana mitamba bora,wanawake wakopeshwe. Miaka ya nyuma Mwalimu Nyererepeke yake katika awamu zote aliweza kutoa projectsambazo zinafanya kazi watu wakarejesha. Ilikuwa inaitwakopa ng’ombe lipa ndama; na mpaka leo ndiyo iliyowatoawatu. Watu waliweza kuboresha maisha yao, wanapatamaziwa, wanapata samadi, wanapata nyama nzuri nangozi.

Mheshimiwa Spika, ni Mwalimu tu katika awamu zotetano, yeye alitoa projects na zikalipa mpaka leo. Ndiyoakaweza kuchanganya wale ng’ombe wa kiasilia nang’ombe wa kisasa. Maeneo mengi yaliyoboresha kipatoni yale ambayo yaliweza kufaidi mradi huo.Namwomba Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mpango aangalie niprojects zipi zitaweza kwenda kuboresha kipato chaakinamama?

Mheshimiwa Spika, tumeona wanawake wanaingiakwenye VICOBA, Serikali inasema kwamba inakwendakusimamia VICOBA, mnasimamiaje VICOBA ambavyo hamjuivimeanzishwaje? VICOBA hivyo ni vya kudunduliza,amechangia mmoja akasema na ile hela ya VICOBA sasainakwenda kwenye kucheza kamari. Tunafanyaje?Tunatokaje hapo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba wanawake hawawapewe elimu ya VICOBA kila mara. Hapa wenyewe sisi,wengi wa Wabunge wako ni wasomi, lakini kila leoumejitahidi kutuletea semina za mambo mbalimbali ili tuwezekuendana na wakati. Sasa wanawake waletunawapelekeaje semina hizo? Haitoshi kabisa kuzungumziavitu vyao walivyoanza halafu tukasema tunasimamiaSACCOS. Unasikia Serikali inaingia kwenye SACCOS. SACCOSni uanzishaji wa hiari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwamba Serikaliimeweza kwenda kuangalia wasiuze zile mali za SACCOS,lakini uanzishwaji wa SACCOS ni wa hiari. Wenyewe wanakaa

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

wanakubaliana. Maeneo ambayo SACCOS zimeshamiri nikule ambako hazijaingiliwa. Leo Serikali ukienda ukaingilia,umeharibu.

Mheshimiwa Spika, nakuomba, dakika chachezilizopita umesimama umetoa amri. Najua, amri yako au yourwish ni kutekelezwa na ikitekelezwa kwenye hili jumba lakoTukufu wewe ndio umesema. Naomba siku moja ikupendeze,zile hela zinazotolewa au zilizowahi kutolewa na Marais sikuza nyuma zikaenda kwa wanawake, zikaenda kukopeshwa,halafu zikaishia ziliko, mimi najua ziko kwenye benki kwenyesuspense accounts. Tuma Tume yako fedha hizo zikakaguliwe,iwe ni NMB, iwe ni NBC, iwe ni CRDB, zile hela zirudi kwenyemzunguko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zile hela ni revolving funds, zirudi.Hazina inajua ni kiasi gani kilitoka. Mara ya mwisho tulipatamabilioni ya JK, mpaka leo yako wapi? Waliojifurahishawameyafungia, zime-lock mahali. Utashangaa hata viongoziwakubwa au wake wa viongozi walienda na waowakakopeshwa. Hivi walikuwa wanastahili hizo hela?Nakuomba, siku itakapokupendeza zile hela zirudi kwenyemzunguko, wanawake wakopeshwe, vijana wakopeshwehela hiyo ikombolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye ripoti tumeelezwa waziubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, hili ni jambojema. Naomba ubia huu usimamiwe na Serikali sasa iwemakini kuangalia ni jinsi gani ubia huu unaendeshwa. Tunabahati moja nzuri sana ya kupata Wakaguzi wa Serikaliambao ni makini, ambapo tulikuwa huko nyuma na Uttoh,sasa hivi tuna Profesa Assad. Ukiona ripoti zake, ziko wazi,hakuna anapoficha. Pamoja na madaraka yake hayomakubwa, nafasi yake amepewa; tukitaka sasa kujua valuefor money kwenye projects inashindikana maana naonawataalam hawa hawapo.

Mheshimiwa Spika, mara nyingi ameagizwa, lakiniamepewa majukumu na amefungwa mikono, hana namnaya kuajiri watu ambao wana uelewa kwenye eneo hilo. Sasa

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

inamwia ngumu. Tunamhoji tunasema, aah, umemalizaukaguzi sasa tunataka tuwe tena na ukaguzi ule mahususi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Shally Raymondkwa mchango mzuri sana. (Makofi)

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Naunga hoja mkono. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana kwa mchango mzuri sanaulionao. Tulikuwa tunatamani kuendelea kukusikiliza.Mheshimiwa Rose Tweve tafadhali.

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, nakushukurusana kwa kunipa nafasi nami niweze kutoa mchango wangusiku ya leo. Awali ya yote naomba nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri na Watendajiwote wa Wizara kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya. Nimatumaini yangu Watanzania wanatambua mchangomkubwa ambao wanautoa kwenye Wizara yao na kwa Taifahili.

Mheshimiwa Spika, nina jambo moja tu ambalonitapenda kuliongelea siku ya leo ambayo ni issue ya hawandugu zetu wa TIRA (Tanzania Insurance Regulatory Authority).Mwaka 2009 Bunge lako lilipitisha Sheria Ndogo, Sheria yaBima Na. 10 na lengo lilikuwa ni kutatua changamoto kwawananchi, hasa pale wanapopata ajali, kama mtuamepoteza maisha, basi ndugu zao waweze kupata fidiana kama kuna upotevu wa mali, basi waweze kupata stahikizao.

Mheshimiwa Spika, kama Mheshimiwa Waziri alivyokirikwenye hotuba yake ukurasa wa 60 kumekuwa na upungufumkubwa kwenye chombo hiki ambacho kilipewa mamlakaya kusimamia na kuratibu taratibu zote zinazohusu bimanchini. Kwenye ukurasa wa 60 Mheshimiwa Waziri anasema,

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Wizara imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchihasa ya ucheleweshaji wa fidia pale wanapopatwa namajanga. Hiki kimekuwa ni kilio kwa nchi nzima hasawananchi wangu wa Mkoa wa Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, chombo hiki kimekuwa naupungufu mkubwa, kwanza hakijulikani na hao wachachewanaokijua chombo hiki, notion iliyopo inakuwa ina-benefitsana makampuni ya Insurance badala ya wananchi wakawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, chombo hiki kiliundwa kuhakikishakinaratibu shughuli zote za bima, lakini suala hili niliulizailikuwa tarehe 3 Aprili, nikataka kujua takwimu ni ajali ngapizimetokea na watu wangapi walikuwa wamelipwa stahikizao? Mheshimiwa Waziri alitoa maelekezo hapa kuanzia 2016- 2018 ni majeruhi na vifo ilikuwa ni zaidi ya 14,000. Mpakatarehe hiyo 3 Aprili, Mheshimiwa Waziri alipokuwa anatoleahapa ufafanuzi ni watu 1,500 tu ndio ambao walikuwawamelipwa stahiki hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Waziri, hiki chombo kifanyiwe mapitio,kumekuwa na upungufu mkubwa sana. Kuna hata hili sualaambalo wameweka la Msuluhishi wa Bima. Chombo hikihakitambuliki na ofisi yao ipo moja tu Dar es Salaam. Sasakwa hali halisi Mheshimiwa Waziri mtu atoke sijui Makete,Njombe, Iringa aende kwa huyu Msuluhishi wa Bima inakuwani kazi kubwa. Kwanza umbali na pili ni gharama.

Mheshimiwa Spika, juu ya hilo, kuna upungufu, huyuMsuluhishi wa Bima anataka kuonana na mdai mwenyewe,hawaruhusu Mwanasheria au Mwakilishi yeyote kukutana nachombo hiki. Namwomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha,kwa sababu hawa TIRA wako chini ya Wizara yake, hebutuangalie tena kwa namna ya utendaji wao kazi. Moja,watoke maofisini waweze kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Spika, elimu ya Bima bado ipo nyumakwa wananchi wetu, wengi wanajua tu ni Bima pale ajali

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

inapotokea. Kuna wananchi wengi mkoani kwetu Iringa palewanajishughulisha na shughuli nyingi za kilimo, mashambayanaungua pale lakini hawajui bidhaa ambazo zinapatikanakwenye hizi huduma za bima ili pale wanapopata majangawaweze kupata stahiki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwambakwanza tupitie sheria, kama kuna upungufu wowote ziletwehapa zipitiwe ili tuweze kufanya mabadiliko tuwasaidieWatanzania. Pia TIRA wapewe pesa za kutosha. Najua sasahivi wameanzisha Website yao, nawapongeza kwa hilo, atleast inafanya kazi, watu wanaweza ku-check wamelipwapremium zao wanaweza kufanya follow-up kujua kamazimelipwa na hayo makampuni. Kwa hiyo, wapewe pesa zakutosha, watoke maofisini wasiishie Dar es Salaam, wawezekufika sehemu mbalimbali hata zile za vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hizi dakika chache zilizobaki,naomba pia niwasemee Walimu. Kumekuwa namanunung’uniko makubwa juu ya kulipa malimbikizo yao.Tunajua wana mchango mkubwa sana kutuandaa na nakutulinda. Wengine tumefika hapa Bungeni ni mchango waWalimu.

Mheshimiwa Spika, najua Mheshimiwa Naibu Wazirialitoa ufafanuzi mzuri asubuhi, tunaomba kuendelea ku-keepupdate kuhakikisha tunalipa hizi stahiki zao kwa wakati,wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanajenga Taifa hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nashukuru kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Rose Tweve.Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, Rose Tweve ni Mbunge waMkoa wa Iringa. Yuko vizuri, eeh! Sawasawa kabisa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Saul Amon uwe mchangiaji wa mwisholeo.

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

MHE. SAUL H. AMON: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi adimu ndani ya Bunge hili kuchangia.Kwanza kabla ya yote, naunga mkono hoja nisije nikasahau.Pili, naomba ku-declare interest kwenye uchangiaji wangukwa sababu nitachangia kuhusu biashara nami nimfanyabiashara, kwa hiyo na-declare interest mapemakabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza, nataka kutoa pongezikwa Serikali yangu ya Tanzania hasa kwa Mheshimiwa Raiskwa ununuzi wa ndege. Pamoja na kwamba kuna watuwanaopinga, lakini nawashangaa kweli kweli kwamba nchiinaweza kuwa bila ndege! Hata nchi ndogo zina ndege, sisitusiwe na ndege; kwa kweli nampongeza sana na hiliwanipelekee hiyo taarifa kwamba nampongeza kutokandani ya moyo wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pil i, kuna wenzanguwamechangia kuhusu property tax. Nataka nimkumbushetu Mheshimwa Waziri wa Fedha kwamba wakumbuke hilialilochangia mchangiaji mwingine simtaji j ina, lakiniMheshimiwa Rais ali l izungumza, akawaambia nyiewakusanya kodi mnafanya kodi zisikusanywe kwa sababumnaweka kodi zisizobebeka. Hili amezungumza mchangiajimwenzangu amesema kwa sisi viongozi; kiongoziakizungumza yanakuwa ni maamuzi sahihi na kama linamatatizo au ukakasi, namwomba Mheshimiwa Waziri waFedha, basi lije hapa lizungumzwe ili hizo kodi za propertytax ziweze kupunguzwa.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka aliongeaMheshimiwa Rais, sio mtu mwingine; akaongea bei mpakaakaongea akaweka mfano, nyumba ya ghorofa changisheniSh.100,000/= sijui Sh.50,000/= lakini wanawaambia watu kodiambazo haziwezi kubebeka. Ndiyo kweli aliyokuwaanazungumza mchangiaji mwingine aliyepita, wanaletamakadirio ya ajabu. Anakwambia ulipie kodi shilingi milioni30 wakati hilo jengo wewe hupati hata shilingi milioni 30 kwamwaka. Wanawatwisha watu mizigo ambayo haiwezikubebeka. (Makofi)

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, aliyeongea niMheshimiwa Rais na watu wote walisikia. Tunachotakiwa nikumuunga mkono Mheshimiwa Rais na naamini kwamba kodihii ikiwa ni ya kiasi ya watu kutaka kwenda kulipa wenyeweitalipika, lakini kwa haya mamilioni yanayotajwa kwa kwelisidhani kama watu wengi, kama alivyozungumzamchangiaji mwingine, mzee kastaafu, unamwambiaakalipie Sh.200,000/=, ndivyo walivyoenda kukagua na kutoatathmini ya hiyo nyumba yake. Kwa kweli ni ghali sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, kuna haya matatizo navikwazo katika biashara tunazozifanya na ndiyo maana nime-declare interest. Kuna hizi taasisi za umma zinaingiliana mnona zinaenda zote kwa pamoja; lakini nitazungumzamojawapo ambayo ni hii ya uingizaji wa mizigo. Unakuta,TFDA, kwa mfano, tunaweza kuiondoa TRA. Sasa hivi katikawatu wanaofanya kazi nzuri kupita maelezo, ni TRA lakinivikwazo vinavyowekwa na hizo Idara nyingine za Serikali ndizozinazofanya uchangiaji wa uchumi kukua upungue. Kwa nini?(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitazungumza katika eneo langula vipodozi. Nchi nyingi kwenye vipodozi wanaoshughulikiani watu wanaoshughulika na afya. Hapa kwetu naaminikwamba TFDA ndiyo wanaoshughulika na mambo ya dawa,vyakula pamoja na vipodozi. Unakuta TFDA wamekupacertificate, hawana matatizo. Wamekupa, wanakwambiakabla hujaingiza mzigo wako, lete tuukague, tuupime,tunakupa certificate.

Mheshimiwa Spika, unapewa certificate na TFDA,unayo. Unaenda kuleta mizigo, TBS wanakwambia huu mzigohaufai. Hapo wanakinzana mno na ndiyo maanawamesababisha watu wengi wapite porini. Siyo watu wotewana nguvu za kuweza kupita moja kwa moja. Naombahilo liangaliwe na hapa siwezi kulizungumza sana kwa sababunilikuwa nimekuja na hayo mawili. Pongezi kwa MheshimiwaRais kuhusiana na property tax na hiyo ya mambo yakupingana kwa Idara za Serikali. Kwa kweli zinapingana sana

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

kiasi kwamba wale wadogo wadogo ambao wamekujakabisa na kwamba wamelipia wana karatasi za DFTA, lakinihuyu anakataa. Kwa hiyo, unakuta wanakinzana.

Mheshimiwa Spika, TRA wako very efficient,unakwenda unafika siku tatu. Maana tulikuwa tunachukuawiki tatu au nne, lakini sasa hivi TRA siku mbili au tatuwamemaliza kazi yao. Unaanza kupiga kwata huku TFDA,wamemaliza; unaanza na TBS . TBS umemaliza naowanakwambia kuna vipimo. Jamani, Kampuni iliyotengenezahiyo mizigo ni ya Kimataifa, nitatoa tu mfano labda Procterand Gamble, watengenezaji wakubwa ambao wako katikakila nchi na vipimo vinajulikana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu anakwambia lazima tupimetu hii chupa kama kweli ni mills 50, naye umlipe. Tupime hiichupa ni mills 100 naye umlipe. Ni kweli kabisa na siyokwamba nazungumza kwa kuambiwa, ni vitu ambavyonavisikiliza. Kwa hiyo, wangekaa pamoja ili wahakikishekwamba tunafanya shughuli za uzalishaji na kukusanya kodiiwe rahisi. Itakuwaje rahisi? Ni kwa kuchukua hizi mamlakakwamba wewe ndio utashughulika na hili, wewe ndioutashughulika na hili, kuliko kila mmoja huyu kikwanzo, huyuhapana.

Mheshimiwa Spika, nitampa Mheshimiwa Wazirimifano mingi lakini hapa muda sina, kwa hiyo, mudanitautafuta mwenyewe nimpelekee mifano nimwambiekwamba na hawa wanamkwamisha kukusanya mapato nandiyo sababu ya watu kupita porini, siyo kwamba watuhawapiti porini na vitu havingii.

Mheshimiwa Spika, nchi hii ni kubwa, mipaka yake nimikubwa. Wewe mwenyewe ukiangalia kutoka Mombasauje ufike Mtwara, utoke Mtwara umalize yote Malawi; utokeMalawi uende Zambia; yaani mpaka ni mkubwa sana.Nakumbuka tukirudi huko nyuma, kulikuwa na uongoziuliwahi kulegeza, walikuwa wanakusanya mapatomakubwa sana. Vikwazo havileti mapato, wala kodi kubwahaileti mapato. (Makofi)

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

Mheshimiwa Spika, la tatu, naomba kumalizia, nalohili Mheshimiwa Waziri wa Fedha nakushukuru kwa sababukwanza namfahamu ni rafiki yangu kwa muda mrefu,mkaliangalie. Vipodozi siyo kweli kwamba ni anasa, vipodozisiyo sigara wala siyo pombe. Kama siyo sigara wala pombena kila aliyepo hapa ndani hakuna ambaye hakupakaakipodozi. Wanapoweka tax kubwa namna ile mpaka naexcise duty utafikiri unauza sigara au pombe kali,hawamtendei haki huyu mlaji wa mwisho. Mimi nitaleta, lakiniatakayeumia ni huyu aliyemo humu. Sasa wanaponiwekeahiyo kodi kubwa…

SPIKA: Wabunge wanawake mbona hii hoja nilifikirimtaiunga mkono! (Makofi/Vigelegele)

MHE. SAUL H. AMON: Mheshimiwa Spika, siamini hatakwamba Mheshimiwa Dkt. Mpango anataka watu wanukevikwapa humu ndani, haiwezekani. Kwa hiyo, vipodozi,nataka nimwambie kabisa siyo kitu cha anasa. Nenda nchiyoyote; nenda Amerika, nenda Ulaya vipodozi vinaingizwakwa sababu wanajua faida yake, hakuna asiyepakaa. Kwahiyo, waangalie hilo na waliangalie vizuri sana. Hayo mambomatatu; Idara zinazokinzana wakae pamoja...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Saul.

MHE. SAUL H. AMON: Mheshimiwa Spika, nashukurusana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Saul. Nilikuwanajaribu ku-imagine siku moja vingekosekana vipodozi kabisa,halafu na Waheshimiwa Wabunge wote ikabidi waje hapabila kipodozi hata kimoja, huenda wengine tusingewezakuwatambua. Spika anasema nani huyu? Nani?

Mheshimiwa Mbaraka Dau kwa dakika zilizobaki,unaweza ukazitumia? Mheshimiwa Mbaraka Dau.

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

MBUNGE FULANI: Ametoka.

SPIKA: Ametoka. Basi nina dakika kama tano. Basihakuna aliye tayari, mtamalizia kesho. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, sasa nawashukuru sanakwa michango yenu. Kesho tutaendelea na uchangiaji wahoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipangoaliyoiweka mezani na jioni kama saa hizi tutakuwatunaifanyia uamuzi kuhusiana na hoja hiyo. Nashukurutunakaribia kumalizia Wizara, hii ndiyo huwa inafunga geti.

Sasa toka tulivyoanza shughuli hizi za Bunge hili laBajeti pamekuwa na zoezi la kushika shilingi ya mshaharawa Waziri. Sikutaka kusema mapema, lakini leo nisemekidogo, siyo wote tunafahamu, maana ya kushika shilingi yaWaziri.

Katika Jumuiya ya Madola ambako ndiko utaratibuhuu ulikoanzia, unaitwa kushika shilingi ya Mheshimiwa Wazirikwa jambo la Kisera na kadhalika. Hivi jaribu tu ku-imaginekwamba kweli shilingi Waheshimiwa Wabunge mmekubalikwamba ushikwe. Kwa hiyo, Waziri akipata mshahara wakeminus shilingi moja, ina impact gani kwa Mheshimiwa Waziri?Haina maana yoyote, si ndiyo! Kwa nini kwenye Mabungehaya kuna hicho kitu kinaitwa kushika shilingi? Ndichoninachotaka kukielezea kwa dakika chache hapa.

Ni kwamba katika uzoefu huo wa haya Mabungeyaliyo mengi, kama Mbunge akishika shilingi ya MheshimiwaWaziri, halafu Wabunge mlio wengi mkaunga mkono kabisakwamba Waziri huyo, shilingi hiyo ikatwe, itoke kwenyemshahara wake; hoja hiyo itapita minus shilingi moja, lakinimaana yake na tafsri yake ni kwamba Waziri huyo anatakiwamuda mfupi baadaye ajiuzulu. Sijui kama wengi mnajua,ndiyo hivyo. Hiyo maana yake, Wabunge hawana imani naWaziri huyo. Ndiyo tafsiri yake ilivyo. (Makofi)

Kwa hiyo, wengi tunashikaga tu, tunafanya kamautani hivi na nini, lakini kwa sababu mimi huwa najua shilingi

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1541694878-04 JUNI,2018.pdf · NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

itarudishwa, kwa hiyo, huwa sina wasiwasi. Ni vizuri mjuekuanzia leo kuwa ni indicator; na ndiyo maana inatakiwausimame kwa jambo la msingi kwa kweli siyo tu nashikashilingi, nashika shilingi. Siyo kitu cha kucheza kucheza nachohivi. Kwa sababu kama kweli wenzako wakikuunga mkono,maana yake kwa kweli umemweka pabaya sanaMheshimiwa Waziri anayehusika na Wizara hiyo.

Waheshimiwa Wabunge kwa kusema hivyo sinamaana sasa ndiyo muanze mchezo huo, kwambamkishakuwa na kisasi, basi inatumika hii. Hapana, hatuitumiikulipa kisasi wala nini, ni kitu serious. (Makofi)

Mheshimiwa Mkuchika, Simba wameshinda huko leo.Rafiki zetu wa Yanga jana wamerudi, basi tunawakaribishanyumbani, hakuna shida. (Kicheko/Makofi)

Waheashimiwa Wabunge, kuna pochi hapa Mbungealiisahau. Jinsi ilivyo nadhani inaweza ikawa ni ya Mbungemwanamke, lakini ina pesa nyingi kweli humu ndani. Kabisakabisa. Kwa hiyo, mwenye pochi yake na pesa hizi atakujakuchukua mezani kwa Makatibu hapa baadaye. Hirizihamna, ni pesa tu. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, nawashukuruni sana kwaushirikiano mliotupatia kwa siku ya leo. Niseme tu kwambasasa tumefikia mwisho wa shughuli zetu kwa siku ya leo. Kwahiyo, naahirisha shughuli za Bunge hadi kesho saa 3.00 asubuhi.

(Saa 12.00 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumanne,Tarehe 5 Juni, 2018, Saa Tatu Asubuhi)