62
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI-MHE.AGGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 07 - 15 JANUARY 2013. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, S.L.P 128, Sumbawanga, RUKWA. Simu. Na. 025 - 2802137/2802138 Nukushi: 2802117/2802318 Baruapepe: [email protected] January, 2013 1

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI-MHE.AGGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 07 - 15 JANUARY 2013

Embed Size (px)

DESCRIPTION

MHE.MWANRI ZIARANI MKOANI RUKWA

Citation preview

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI-

MHE.AGGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE

MKOANI RUKWA

TAREHE 07 - 15 JANUARY 2013.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,S.L.P 128, Sumbawanga,RUKWA.Simu. Na. 025 - 2802137/2802138Nukushi: 2802117/2802318Baruapepe: [email protected] January, 2013

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWA NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI- MHE.

1

AGREY MWANRI (MB) KATIKA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA TAREHE 07 - 15 JANUARY, 2013.

1.0.UTANGULIZI.Mheshimiwa Naibu Waziri, Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha wewe na ujumbe wako hapa Mkoani Rukwa. Ni matumaini ya Uongozi wa Mkoa wa Rukwa na wananchi wake kuwa, ziara hii itakuwa ya manufaa makubwa kwa maendeleo ya Mkoa wetu na Ukanda wote wa Ziwa Tanganyika, kwani tunajua wazi kwamba tutapata ushauri, maelekezo na maagizo kwa ajili ya kuboresha utendaji wetu wa kazi.

Aidha, nichukue nafasi hii kutoa shukrani zetu kwa Serikali kwa kuwateua miongoni mwa viongozi wa Mkoa wa Rukwa kuanzisha Mkoa mpya wa Katavi, uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dr. Rajabu Rutengwe kuwa Mkuu wa kwanza wa Mkoa mpya wa Katavi na Eng. Emmanuel Kalobelo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa ni faraja kubwa kwetu.

Mheshimiwa Naibu Waziri, Taarifa hii ya Mkoa wa Rukwa inaeleza na kuainisha hali ya Ki-jiografia, Ki-utawala, Maendeleo katika Sekta za Ki-uchumi, Ki-jamii na ki-siasa. Aidha, taarifa hii pia itagusia fursa za maendeleo, mafanikio na changamoto zilizomo katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Ushirika, Uvuvi, Ardhi, Maendeleo ya Jamii, Biashara, Viwanda, Miundombinu, Mawasiliano, Masuala Mtambuka, Haki za Binadamu pamoja na Utawala Bora.

2.0 HALI YA KI-JIOGRAFIAMgawanyo wa Mkoa niliouelezea hapo juu unaonyesha kuwa, kwa sasa Mkoa wa Rukwa una eneo la kilometa za mraba 27,713 wakati kilometa za mraba 22,792 ni la ardhi na kilometa za mraba 4,921 ni eneo la maji. Mipaka ya sasa ya Mkoa wa Rukwa upande wa Kusini - Magharibi Mkoa unapakana na nchi ya Zambia, upande wa Kaskazini - Mashariki Mkoa wa Katavi, upande wa Kusini - Mashariki Mkoa wa Mbeya, na upande Magharibi nchi ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC). Mkoa wa Rukwa uko Kusini-Magharibi mwa Tanzania kwenye Latitudo 050 na 090 Kusini na Longitudo 30 - 330 Mashariki.

3.0 HALI YA ULINZI NA USALAMAMhe. Naibu Waziri, Kwa ujumla hali ya Ulinzi na Usalama katika Mkoa ni shwari na ya kuridhisha kwa kiasi kikubwa. Matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza

2

yameendelea kushughulikiwa na kudhibitiwa na Kamati za Ulinzi na Usalama za kila Wilaya kwa kushirikiana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Kwa upande wa Kisiasa viko vyama tisa (9) vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2010 wa Rais, Wabunge na Madiwani. Chama Cha Mapinduzi, ndicho chama chenye nguvu kisiasa katika Mkoa wa Rukwa. Kati ya Waheshimiwa Wabunge 7, wote wanatoka Chama Cha Mapinduzi na kati ya Wahe. Madiwani 86 wa kuchaguliwa, 78 wanatoka Chama Cha Mapinduzi, 6 kutoka CHADEMA, 1 kutoka CUF na 1 kutoka TLP.

4.0. KI-UTAWALA. Mhe. Naibu Waziri, Katika maeneo ya utawala, Mkoa wa Rukwa unazo Halmashauri za Wilaya tatu (3) ambazo ni Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri za Wilaya za Sumbawanga na Nkasi. Halmashauri ya nne ni ya wilaya mpya ya Kalambo ambayo bado haijaanza rasmi. Pia mkoa una jumla ya Wilaya tatu (3), Tarafa 14, Kata 64, Vijiji 313, mitaa 125 na Vitongoji 1,638 kwa mchanganuo ufuatao:-

WILAYA HALMASHAURIENEO KM. ZA MRABA TARAFA KATA VIJIJI

IDADI YA WATU

20032012

PROJECTION

SUMBAWANGA Sumbawanga MC 1,003 2 15 24 152,939 221,033Sumbawanga DC 8,203 4 15 101 214,979 296,327

KALAMBO Kalambo DC 4,211 5 17 101 167,260 220,423NKASI Nkasi DC 9,375 5 17 87 216,883 299,413

TOTAL 22,792 16 64 313 752,061 1,037,196

4.2 Maeneo Mapya ya UtawalaMkoa umepokea Wakuu wapya wa Wilaya zote tatu ambao ni Mhe. Mathew S. Sedoyeka - Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Moshi Musa Chang’a - Mkuu wa Wilaya ya Kalambo na Mhe. Iddi Hassan Kimanta - Mkuu wa Wilaya ya Nkasi. Mkoa Rukwa unajivunia kupokea Wilaya mpya ya Kalambo ambayo tayari imeshapatiwa baadhi ya viongozi na watumishi ngazi ya wilaya kama vile, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Polisi wa Wilaya, Afisa Usalama wa Wilaya, Afisa Tawala wa Wilaya. Mkoa ulishaainisha maeneo ya ofisi na makazi ya Viongozi wa ngazi ya wilaya pamoja na watumishi watakao kwenda kuanzisha eneo hilo jipya la utawala.

4.3 Changamoto 3

Kuna upungufu wa vitendea kazi; magari, samani za ofisi, nyumba na ofisi zitakapoanzia wilaya yetu mpya kwani ofisi na makazi yaliyopo kwa sasa ni ya kukodisha toka kwa watu binafsi. Utaratibu uliotumika kutoa fedha kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa mipya ungesaidia sana kama ungetumika kwa uanzishaji wa wilaya pia.

5.0 ELIMU5.1. ELIMU YA AWALIMhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa kwa mwaka wa 2012 una wanafunzi wa elimu ya awali 19,315 wakiwemo wavulana 9,894 na wasichana 9,421 wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 5 na 6.

5.2 ELIMU YA MSINGIMhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa umeweza kuandikisha wanafunzi 37,525 sawa na asilimia 109.11 kuanza darasa la kwanza 2012 wakiwemo wavulana 18,800 na wasichana 18,725 kutoka katika lengo la kuandikisha wanafunzi 34,392 hata hivyo zoezi la uandikishaji kwa wanafunzi wa mwaka 2013 lilianza mwezi Disemba na hivyo bado linaendelea.

5.2.1 MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2011 NA 2012Jumla ya watahiniwa 28,551; ambao ni wavulana 13,781 na wasichana 14,770 walifanya mtihani kati ya watahiniwa 30,070 waliosajiliwa ikiwa ni asilimia 94.69. Kati ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2011, vijana 14,612 walifaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2012 kati yao 8,221 ni wavulana na 6391 ni wasichana. Ufaulu huu ni sawa na asilimia 51.07 ya watoto waliofanya mtihani.

Mwaka 2012 jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba ni 18,683, waliofanya ni 17,518 na waliofaulu ni 10,219 kati yao wavulana ni 5,574 na wasichana ni 4,645 sawa na asilimia 58. Jumla ya wanafunzi waliochaguliwa ni 8,068 kati yao wavulana ni 4,430 na wasichana ni 3,638 sawa na asilimia 78. Asilimia 22 ni waliofutiwa matokeo, wasiojua kusoma na kuandika na wachache wamekosa nafasi.

5.3. ELIMU YA SEKONDARI.

4

Mhe. Naibu Waziri, Mkoa una jumla ya shule za Sekondari 80 zikiwemo 68 za Serikali na 12 zikiwa ni za watu binafsi na mashirika ya dini. Shule zenye kidato cha V-VI zipo 10 ambapo sita (6) za Serikali na nne (4) sio za Serikali. Mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 5,820 wakiwemo wavulana 3,694 na wasichana 2,126 walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne. Aidha, jumla ya wanafunzi 6,487 wa kidato cha pili wakiwemo wavulana 3,881 na wasichana 2,606 walifanya mtihani mwaka 2012. Matokeo ya mitihani ya Kidato cha pili na cha nne bado hayajatoka.

5.4. ELIMU YA UALIMU.Mhe. Naibu Waziri, Mkoa una chuo kimoja cha Ualimu cha Serikali kiitwacho Sumbawanga kinachotoa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti daraja la IIIA na mafunzo ya cheti cha Sayansi Kimu. Pia, Mkoa una vyuo viwili binafsi vya Ualimu vinavyotoa mafunzo ya ualimu daraja la IIIA vyote vikiwa vimepata usajili na hivyo Mkoa kuwa na vyuo vitatu vya mafunzo ya ualimu. Vyuo hivi vimesajiliwa kwa majina ya Rukwa Chuo cha Ualimu na St. Aggrey Chanji.

5.5. ELIMU YA UFUNDI Mhe. Naibu Waziri, Mkoa hauna Chuo cha VETA mbali na vituo vya ufundi stadi vinne (4) katika fani za Useremala, Uashi na Sayansi Kimu. Aidha, vipo vyuo vya ufundi viwili (2) katika fani za Ufundi Magari, Uchomeleaji na Kompyuta. Ni vema sasa Mkoa wa Rukwa ukawa na Chuo chake cha VETA kama ilivyo mikoa mingine nchini. Eneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo hiki limeainishwa.

5.6. UKAGUZI WA SHULEMhe. Naibu Waziri, Halmashauri za Wilaya zimekuwa zikisaidia ili Wakaguzi wa shule waweze kukagua shule za Msingi. Katika kipindi cha Julai 2011 - Juni 2012 shule za msingi 42 zilikaguliwa.

5.8. ELIMU YA JUUMhe. Naibu Waziri, Mkoa unacho Kituo cha Chuo Kikuu Huria chenye jumla ya wanachuo 150 katika kozi mbalimbali. Katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2012 jumla ya wanachuo 57 wamefuzu na kutunukiwa vyeti katika fani mbalimbali.

5.9 CHANGAMOTO

5

Mhe. Naibu Waziri, Zipo changamoto ambazo zinaikabili sekta ya Elimu mkoani Rukwa nazo ni:- Upungufu wa hosteli/daharia katika shule za sekondari Mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Ushiriki hafifu wa wananchi katika kuchangia utekelezaji wa MMEM na MMES

5.10 MATARAJIO YA BAADAYE:Matarajio ya Mkoa ni kuboresha taaluma kuanzia shule za awali, msingi, sekondari na vyuo ili kukidhi ushindani wa kielimu katika soko la kitaifa, Afrika mashariki na kimataifa.

6.0 SEKTA YA AFYA Sekta ya afya kwa mwaka 2011 iliendelea na jukumu lake la kutoa huduma kwa wagonjwa mbali mbali wanje na wa ndani (waliolazwa). Katika kutoa huduma jumla ya wagonjwa 149,580 walitibiwa kama wagonjwa wanje kati yao 67,145 walikuwa watoto chini ya miaka mitano. Kwa wagonjwa wanje magonjwa kumi sugu yalioongoza ni kama yanavyoonekana katika jedwali Na 1.

JEDWALI NA. 1:

IDADI YA WAGONJWA KWA MWAKA 2012 MKOA WA RUKWAMAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WA NJE.

WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO (‹5) UMRI WA ZAIDI YA MIAKA MITANO(5+)Aina ya Ugonjwa IDADI Aina ya ugonjwa IDADI

1 Diarrhoeal diseases 1,167 Malaria 3,4752 Malaria 2,684 Congestive Cardiac Failure 1273 ARI 255 Diarrhoeal diseases 5644 Pneumonia 1,055 Pneumonia 4915 Non infections

Gastrointestinal Disease129 Anaemia 422

6 Burns 110 Acute Respiratory Diseases 3247 Urinary Tract Infections 87 Fractures 2708 Other nutritional

Disorders65 Hypertension 245

9 Severe protein energy malnutrition

37 Urinary Tract Infections 181

10 Anaemia 265 Tuberculosis 162

Source of Data: DHMIS Reports 2011

6

Sekta pia ilitoa huduma kwa wagonja waliolazwa kwa magonjwa mbalimbali. Katika mwaka 2011 Jumla ya wagonjwa 27,716 walilazwa katika vituo vya kutolea huduma. Kati yao 14,117 walikuwa watoto chini ya miaka 5. Magonjwa kumi sugu yaliyoongoza kwa wagonjwa waliolazwa ni kama yaliyoonekana katika Jedwali Na 2.

JEDWALI NA 2: MAGONJWA 10 YALIYOONGOZA KWA WAGONJWA WALIOLAZWAWATOTO CHINI YA MIAKA MITANO (‹5) UMRI WA ZAIDI YA MIAKA MITANO (5+)

Aina ya Ugonjwa IDADI Aina ya ugonjwa IDADI1 Malaria 5,663 Malaria 4,7482 Intestinal worms 2,007 ARI 8223 Pneumonia 1,721 Diarrhoeal diseases 6854 Anaemia 689 Pneumonia 6605 ARI 847 Intestinal worms 6486 Urinary Tract Infections 349 Urinary Tract Infections 4227 Non Gastrointestinal Diseases 199 Genital Discharge syndrome 3358 Burn 173 Pelvic Inlammatory Diseases 328

9 Severe Protein Energy Malnutritions(PEM)

76 Minor surgical conditions 327

10 Other Nutritional Disorders 65 Skin infections 264

Kitengo cha kinga katika sekta ya afya kilitoa chanjo kwa ajili ya kukinga maradhii mbalimbali kwa kufuata miongozo na taratibu za kitaifa na kimataifa.Kwa mwaka 2011 chanjo ilitolewa kama inavvyoonekana katika Jedwali Na 3.

JEDWALI NA 3: CHANJO ILIYOTOLEWA 2011 KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANONo

District BCG DPT3Polio 3

Measles Vit A

Total Vaccinated

% Vaccinated

% Vaccinated

% Vaccinated

% Vaccinated

%

1 SBA MC

9243 1433 16 8469 92 8469 92 9262 100

9662 105

2 SBA DC

40927 21581 53 21660 53 20651 50 22090 54 22331 55

3 NKASI 13976 15450 11 13844 99 13551 97 14888 107

14888 107

TOTAL 64146 38464 60 43973 69 42671 67 46240 72 46881 73

6.1 UPATIKANAJI WA DAWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA7

Katika mwaka 2011 vituo vya kutolea huduma vilitoa huduma kwa wagonjwa kama kawaida pamoja na upungufu wa vifaa na dawa. Jedwali Na. 4 hapa chini linaelezaea idadi ya siku ambazo vituo havikuwa na dawa/vifaa kiwilaya. Idadi hii imekokotolewa kwa kujumlisha idadi ya siku za kukosa dawa kwa kila kituo.

JEDWALI NA.4.

AINA YA DAWA

WILAYA JUMLA WASTANI WA SIKU AMBAZO KITUO KILIKOSA DAWA

SBA MC

SBA DC NKASI DC

AMOXYCILLINE TABS 301 3,064 1,729 5,094 26

B.BEMULSION 335 9,306 3,264 12,905 65

BENZYLPENILLIN INJ. 7 3,053 1,155 4,215 13

COTRIMOXAZOLE SUSPENSION

695 0 0 695 4

COTRIMOXAZOLE TABLETS 362 0 0 362 2

DOXYCLINE TAB 220 0 0 220 1

ERGOMETRINE INJECTION 845 5,348 2,344 8,537 43

FOLIC ACID TABS 751 3,558 931 5,240 26

LIDOCAINE INJ 843 3,018 790 4,651 23

MEBENDAZOLE TABS 215 8,843 3,610 12,668 64

METRONIDAZOLE TABS 158 7,446 3,344 10,948 55

ORS 598 10,198 3,423 14,219 71

OXYTETRACYCLINE EYE

OINT.

1,565 7,113 2,001 10,679 54

PARACETAMOL TABS 307 5,164 3,416 8,887 45

P.P.F VAIL 1,298 13,187 3,440 17,925 90

WATER FOR INJECTION 550 12,329 4,516 17,395 87

EXAM. GLOVES 358 3,035 1,492 4,885 24

POVIDONE IODINE SOLN 663 11,968 5,148 17,779 89

SILK SUTURE 248 2,101 1,217 3,566 18

SURGICAL GLOVES 388 4,588 1,292 6,268 31

SYRINGE REUSABLE 2,050 3,939 2,791 8,780 44

6.2. CHANGAMOTO

Sekta ya Afya mkoani inakabiliwa na changamoto zifuatazo: Uhaba wa watumishi kutokana na watumishi wanaopangiwa kuja mkoa wa

Rukwa kutoripoti katika vituo vyao vya kazi. Upatikanaji wa madawa na vifaa kwa wakati kutoka bohari kuu ya madawa

(MSD).

8

Bado kuna maeneo magumu kufikika hasa mwambao wa Ziwa Tanganyika

7.0. SEKTA YA MAJI

Mhe. Naibu Waziri,Kiwango cha usambazaji maji safi na salama katika Mkoa wa Rukwa ni asilimia 43 tu. Jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa usambazaji unakidhi mahitaji ya watumiaji ifikapo 2025 kulingana na dira ya maendeleo. Upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ni kama unavyoonekana kwenye jedwali ambapo Manispaa ya Sumbawanga (Mjini) inaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa (54%) na mji wa Namanyere kuwa na kiwango kidogo (16 %) kama inavyoonekana kwenye jedwali.

JEDWALI NA.5: UPATIKANAJI WA MAJI MKOANI

Mahali Upatikanaji wa maji (%)Manispaa ya Sumbawanga (Vijijini) 41.8Manispaa ya Sumbawanga (Mjini) 54Sumbawanga vijijini 45Namanyere 16Nkasi vijijini 42

Mhe. Naibu Waziri, Vipo vyanzo vikuu viwili vya maji ambavyo vinatumika kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, vyanzo hivyo ni maji yaliyopo chini ya ardhi (Ground water) na yaliyopo juu ya ardhi (Surface water). Teknolojia zinazotumika kusambaza maji kutoka katika vyanzo vinavyofanya kazi ni, pampu za mkono za visima virefu zipatazo 384 na visima vifupi 194, pampu za umeme za visima virefu zipatazo 7, miradi ya kutiririsha maji kwa mserereko (Gravity) 38 mradi wa maji ya kusukuma kwa mashine (pumped scheme) 1. Pia kuna maji ya chemichemi zilizohifadhiwa (protected spring) 2. Jedwali Namba 6 hapa chini linaonesha mgawanyo wa vyanzo vya maji.

JEDWALI NA. 6: VYANZO VYA MAJI.

Halmashauri/ Aina ya mradi wa maji Hali ya mradi

9

Mamlaka Unafanya kazi

Haufanyi kazi

Nkasi DC Miradi ya mserereko 6 1Miradi ya kupampu 1 6Visima virefu vyenye pampu ya mkono 145 47Visima virefu vyenye pampu ya dizeli - 1Visima vifupi vyenye pampu ya mkono 82 57Chemchem zilizohifadhiwa 2 -

Sumbawanga DC Miradi ya mserereko 21 7Visima virefu vyenye pampu ya mkono 181 38Visima vifupi vyenye pampu ya mkono 111 76Chemchem zilizohifadhiwa 8 3

Sumbawanga MC Miradi ya mserereko 5 2Visima virefu vyenye pampu ya mkono 33 5Visima vifupi vyenye pampu ya mkono 1 2Chemchem zilizohifadhiwa 9 -

Mamlaka ya Maji Sumbawanga

Miradi ya mserereko 6 -Visima virefu vyenye pampu ya mkono 14 -Visima virefu vyenye pampu ya umeme 3 -Chemchem zilizohifadhiwa 2 -

Mamlaka ya Maji Namanyere

Visima virefu vyenye pampu ya mkono 11 -Visima virefu vyenye pampu ya umeme 4 -

7.1 MAJI VIJIJINIMhe. Naibu Waziri, Mipango ya Maendeleo ya Uboreshaji wa upatikanaji na usambazaji wa majisafi na salama ili kuhakikisha kiwango cha huduma ya maji kinapanda kwa kila Halmashauri inafanywa kupitia program ndogo ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kupitia mradi unaojulikana kama Quick win na Mradi wa Vijiji Kumi pia kupitia vyanzo vingine vya fedha.

7.1.1 Quick winMhe. Naibu Waziri, Kupitia Quick win ambayo ilitekelezwa mwaka 2007-2010 visima virefu vyenye pampu ya mkono 15 vilichimbwa na 6 vilikarabatiwa, visima vifupi vyenye pampu ya mkono 5 vilichimbwa pia miradi ya maji ya mserereko 3 ilikarabatiwa wakati miradi mipya 4 ilijengwa na uhifadhi wa chemichemi 2 ulifanyika. Miradi hii iligharimu kiasi cha Shilingi mia sita kumi na nane milioni mia moja arobaini na mbili elfu mia nne sitini na sita na senti tisini na tano (618,142,466.95).

7.1.2 Vyanzo vingine vya fedha

10

Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimekuwa zikitumia fedha za Wahisani na za ndani katika utekeleaji wa miradi ya Maji. kiasi cha shilingi mia saba arobaini na tatu milioni mianane sabini na nane elfu mia nane ishirini na tatu na senti tisini na tatu (743,878,823.93) zimetumika kujenga visima virefu 41 vyenye pampu ya mkono na kukarabati visima virefu 11. Miradi hii ilitekelezwa kati ya mwaka 2007 na mwaka 2012. Fedha hizo ni za Mfuko wa TASAF, Fedha za miradi ya maendeleo (LGCDG) na fedha za wahisani (Tanzania Rural Revival).

7.1.3 Mradi wa Vijiji 10Mhe. Naibu Waziri, Utekelezaji wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2010-2013 chini ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji unaojulikana kama mradi wa vijiji kumi unaendelea ambapo usanifu wa miradi umekamilika na uchimbaji wa visima vya majaribio umekamilika na jumla ya visima 11 vimechimbwa, kati ya hivyo visima tisa vina maji ya kutosha .

Vijiji 37 vimependekezwa kutekeleza miradi ya maji chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kama jedwali namba 7 hapa chini linavyoonyesha:

Jedwali Na.7: VIJIJI VITAKAVYOTEKELEZA PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI.

11

Halmashauri NaKijiji

Jimbo la uchaguzi Idadi ya Walengwa

Sumbawanga MC

1 Luwa

Sumbawanga

47732 Kanondo 38503 Mponda 20544 Malonje 30005 Mawenzusi 60006 Katumba Azimio 41407 Milanzi 43748 Nambogo 23729 Mlanda 6494

10 Matanga 239511 Kisumba 288412 Chelenganya 191413 Kasense 246714 Chipu 330615 Pito 264216 Tamasenga 475617 Malagano 4160

Sumbawanga DC

1 Kisumba-Kasote

Kalambo

60732 Matai 86013 Kamawe 11304 Mwimbi 52855 Mwazye 41726 Mpui

Kwela

59397 Ikozi 60668 Laela 121329 Kilyamatundu 4805

10 Nankaga 6037

Nkasi DC

1 Tambaruka

Nkasi Kaskazini

19332 Isale 30293 Matala 24394 Chala B 30055 Kabwe 101356 Kamwenda 90117 Kisula

Nkasi Kusini1757

8 Mpasa 68419 King’ombe 1632

10 Mkinga 11380

Mhe. Naibu Waziri, Utekelezaji wa miradi ya vijiji kumi utaanza kwa kutekeleza miradi 7 katika vijiji vya Nankanga, Matai, Kanondo, Kisumba, Chelenganya, Chala

12

na Kamwanda (Kirando) ambayo itaanza wakati wowote baada ya Halmashauri kupewa vibali (No-objection) vya Wataalam Washauri (Consultants) na ujenzi wa miundombinu. Tunaomba zoezi la utoaji wa vibali hivyo liharakishwe ili tuweze kuendelea na awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi kwani ni muda mrefu sasa wananchi wamesubiri kupata huduma bora ya Maji safi na salama. Kiasi cha Shilingi bilioni nne miatano sitini na moja milioni miambili ishirini elfu mia saba arobaini na mbili (4,561,220,742) kimetengwa kutumika kwa ajili ya Wataalam Washauri, Wachimbaji wa visima vya majaribio na Makandarasi wa ujenzi wa miundi mbinu ya maji katika miradi 7 itayotekelezwa kama inavyoonekana kwenye jedwali Namba 8 hapo chini. Jedwali Na.8: GHARAMA ZA MIRADI SABA (7).

JINA LA HALMASHAURI

KIASI CHA FEDHA KAZI

Sumbawanga MC 463,124,141 Uchimbaji wa visima 2 vya majaribio

73,000,000 Usimamizi wa miradi (phase1)

696,350,672 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji

Sumbawanga DC 213,421,631 Usimamizi wa miradi (phase1)

273,237,000 Uchimbaji wa visima 4 vya majaribio

98,366,238 Usimamizi wa miradi (phase2)

1,423,092,000 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji

Nkasi DC 225,855,500 Usimamizi wa miradi (phase1)

110,514,000 Uchimbaji wa visima 12 vya majaribio

24,591,560 Usimamizi wa miradi (phase2)

959,668,000 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji

7.2. MAJI MJINIMhe. Naibu Waziri, Serikali imeanza kushughulikia tatizo la maji katika Mji wa Sumbawanga kwa kutekeleza Miradi miwili yenye kuleta mafanikio ya haraka. Miradi hiyo ni Uchimbaji wa visima virefu 13 katika bonde la mto Lwiche na ukarabati wa mabomba ya zamani ikiwa ni pamoja na ufungaji wa bomba mpya za kutoa Maji kwenye visima hadi Mjini. Hadi sasa visima 13 vimechimbwa ambapo visima nane vina maji na vinaweza kutoa jumla ya lita 4,000,000 kwa siku. Ukarabati wa mabomba maeneo ya mjini umekamilika km. 46. Usanifu wa bomba za kutoa maji kwenye visima hadi Mjini umekamilika pia ujenzi wa tanki la maji ya visima eneo la Mto Lwiche umefikia asilimia 80%. Kazi zilizosalia ni kufunga pampu

13

za umeme katika visima na kulaza bomba za kutoa maji katika visima hadi mjini.

Mhe. Naibu Waziri, Gharama za mradi wa visima ni Sh. 393,640,200.00 na gharama za mradi wa kulaza mabomba mapya na kukarabati bomba za zamani ni Sh. 4,944,594,450.00. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Mradi huu utakapoanza kufanya kazi uzalishaji maji wakati wa kiangazi unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 30% ya sasa na kufikia asilimia 80% ya mahitaji ya maji ya mji ambayo ni lita 9,000,000 kwa siku. Wakati wa msimu wa Mvua, huduma ya maji kutoka katika visima na vyanzo vya sasa vya mito, itatosheleza mahitaji ya maji ya sasa. Mradi ulitarajiwa kukamilika Mwezi Octoba, 2012, lakini kumekuwa na changamoto za kiutendaji.

7.2.2: MAJI MJI WA NAMANYERE.Mhe. Naibu Waziri, Huduma ya Maji katika Mji wa Namanyere si ya uhakika kwani maji ya visima vya kupampu yanapatikana kulingana na upatikanaji wa umeme ambao si wa uhakika, Pia maji kutoka bwawa la Mfili si ya uhakika kutokana na gharama za uendeshaji wa mradi kuwa juu kulingana na bei ya dizeli. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi iliandaa mpango kabambe wa Maji katika Mji wa Namanyere, mpango huu uliwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

7.2.3 MRADI WA SEVEN (7) TOWN URBAN UPPER PROGRAM.Mhe. Naibu Waziri, Mradi wa Seven (7) Town Urban Upgrading Programme unalenga kukidhi mahitaji ya maji ya muda wa kati na muda mrefu kwa miji saba ya Lindi, Mtwara Musoma, Sumbawanga, Kigoma, Babati na Bukoba. Kazi ya Usanifu na uandaaji vitabu vya zabuni za ujenzi wa miundo mbinu ya maji safi na usafi wa mazingira katika mji wetu umekamilika. Taratibu za kuwapata Wakandarasi wa ujenzi zinaendelea na ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Januari 2013 kupitia ufadhili wa umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani.

7.3. CHANGAMOTOMhe. Naibu Waziri, Sekta ya maji inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kudumisha Huduma ya Maji katika Mkoa wetu. Changamoto hizi ni: Uharibifu wa mazingira hasa kuchoma moto misitu kunakosababisha kukauka

kwa vyanzo vya maji, Wizi wa miundombinu ya maji,bomba na mifuniko ya chemba za maji, Ucheleweshwaji wa kupatiwa msamaha wa kodi ya mapato (VAT) kwa miradi, Utekelezaji wa miradi inayoendelea umekuwa hauendi kama ilivyopangwa

14

kutokana na fedha kutopatikana kwa wakati pia ucheleweshwaji wa vibali vya Wataalam Washauri.

8.0. MAENDELEO YA JAMII.Mhe. Naibu Waziri, Sekta ya Maendeleo ya Jamii inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996,

8.1. HALI HALISI YA MKOA KIJINSIA:Mhe.NaibuWaziri, Katika Mkoa wa Rukwa hali ya ujinsia bado hairidhishi, kwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vinaendelea miongoni mwa wanandoa wakiwemo wanawake na wanaume na ukatili dhidi ya watoto. Jumla ya wanawake 7,463 wamepatiwa mafunzo ya Sheria kuhusu masuala ya Sheria ya Mikataba, Sheria za Kazi, Sheria za Ndoa, Sheria za Mirathi, Sheria za Ardhi na Sheria ya Mtoto. Lengo mafunzo lilikuwa kuwajengea uwezo wanawake kuzitambua haki zao za msingi katika maisha yao ya kila siku.

8.2. WEZESHAJI WA KIUCHUMI.Mhe. Naibu Waziri, Mkoa unawezesha jamii kiuchumi katika juhudi za kuondokana na umaskini wa kipato kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF). Mafunzo ya ujasiriamali yametolewa kwa vikundi 806 na jumla ya vikundi vya Akinamama vipatavyo 117 ambavyo vimepatiwa mikopo yenye thamani ya Shilingi. 91,000,400 kati ya hizo fedha zilizorudishwa ni Shilingi 45,469,800. Deni lilobaki ni Shilingi millioni 45,930,200 ufuatiliaji bado unaendelea.

8.5. HUDUMA KWA MAKUNDI YENYE UHITAJI.Mhe.NaibuWaziri, Mkoa umetoa misaada yenye thamani ya Shilingi. 28,689,100 kupitia NMSF Grant kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji kama Watoto Yatima, wajane, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 899. Mkoa umewatambua walemavu wa ngozi (Albino) wanawake 448 nawanaume 349, jumla797. Vilevile, Mkoa una vituo sita (6) vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi: Manispaa ya Sumbawanga vituo vinne (4), Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga kituo kimoja (1) na Nkasi kituo kimoja (1):

8.6. MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI:Mhe.NaibuWaziri, Mkoa unafanya ufuatiliaji na utaratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI. Jumla ya watu 83,000 wamejitokeza kupima VVU/ UKIMWI kwa mwaka

15

2012 ikiwa wanaume ni 41,519 na wanawake ni 42,481. Waliokutwa wameambukizwa jumla ni 27,196 ikiwa wanaume ni 10,525, wanawake ni 16,671 na watoto wenye maambukizi ni 1,754 kwa mwaka 2012. Mkoa umeendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa njia ya hamasa kwa kutumia gari la sinema (cinema van) na pia kutoa misaada ya kibinadamu kwa makundi yenye uhitaji katika kata 27,WAVIU 313 wamepatiwa misaada,watoto yatima 2,747 wamelipiwa ada shule za sekondari na msingi.

8.7 UFUATILIAJI WA ASASI ZA KIRAIA.Mhe.NaibuWaziri, Mkoa umefanya ufuatiliaji na kuzijengea uwezo jumla ya Asasi za Kiraia 115 zilizo hai. Pia Mkoa unawezesha usajili wa Asasi mbalimbali zinazoomba usajili . wadau hao wanatambuliwa na Mkoa wanatoa huduma za kijamii kama utoaji wa huduma za kibinadamu kwa WAVIU, watoto yatima, wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi,pia hutoa hamasa dhidi ya mapambano dhidi ya UKIMWI, hamasa ya kilimo cha kisasa, hamasa ya afya ya uzazi, na kuwajengea uwezo wavuvi kwa kuwapatia elimu ya UKIMWI, uvuvi na utunzaji wa rasilimali maji na mazingira yanayowazunguka kwa ujumla.

9.0. KILIMO:Mhe.NaibuWaziri, Hali ya maendeleo ya kilimo kwa msimu wa 2011/2012 ni ya kuridhisha. Kulikuwa na athari za mwenendo wa unyeshaji mvua ambapo mwanzoni (Desemba – Januari 2012) zilinyesha kwa wingi kiasi cha kuathiri kalenda za upandaji na ukuaji wa mimea. Baadaye mwezi Machi kulitokea ukame wa karibu majuma matatu hali iliyoathiri uwekaji mbolea ya kukuzia mashambani na ubebaji wa mazao hasa mahindi.

Mkoa wa Rukwa ulilenga kulima jumla ya hekta 395,141 za mazao ya chakula kwa matarajio ya kupata tani 1,409,869.5. katika utekelezaji zimelimwa jumla ya hekta 380,671 sawa na 96% na kutupatia mavuno ya tani 1,000,349.2 sawa na 71% ya malengo.

Katika msimu wa kilimo wa 2012/2013 Mkoa umelenga kulima jumla ya hekta 401,837.0 za mazao ya chakula na hekta 93,103.0 za mazao ya biashara ambazo tunatarajia kupata tani 1,357,836.0 za mazao ya chakula na tani 184,731.4 za mazao ya biashara.

9.1 Hali ya chakula

16

Mhe.NaibuWaziri, Mahitaji ya chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Rukwa wapatao 1,037,196 (projection 2012) ni sawa na tani 280,043, hivyo tulikuwa na ziada ya tani 820,306, kati ya hizo ziada ya mahindi ni tani 239,766.

Kulingana na hali mbaya ya chakula nchini hususan mikoa ya kanda ya kati, kanda ya ziwa na Kaskazini, na kwa kuwa Mkoa wetu umekuwa kimbilio la wengi kwa mahitaji ya chakula, kiasi kikubwa cha ziada hiyo kimenunuliwa na kusafirishwa nje ya Mkoa.

9.1. Matumizi ya PembejeoMhe.NaibuWaziri, Mkoa wa Rukwa tulipatiwa jumla ya vocha za pembejeo zenye ruzuku 316, 779 zinazotosheleza jumla ya ekari 105,593 kwa idadi hiyo hiyo ya kaya za wakulima. Vocha hizo zina thamani ya Shilingi bilioni 7.6. Mgawanyo na matumizi yake kwa Halmashauri ni kama ilivyo katika jedwali Namba 9 hapa chini.

Jedwali Na.9: MGAWANYO WA VOCHA ZA PEMBEJEO KI-HALMASHAURI.

HALMASHAURI MAPOKEZI MATUMIZI BAKI

Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga 140,157 139,296 861

Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga 55,401 53,924 1,477

Halmashauri ya Wilaya Nkasi 121,221 121,116 105

JUMLA 316,779 314,336 2,443

ChangamotoMkoa ulikabiliana na changamoto zifuatazo katika kutekeleza Mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa kutumia vocha:- Bei za mbolea ya kupandia kuwa juu tofauti na ilivyotegemewa na kufanya

baadhi ya wakulima walengwa kushindwa kuchangia tofauti ya bei. Uwezo mdogo wa wakulima kuchangia gharama za ‘package’ nzima zinazofikia

Sh. 124,000 hadi 133,000/=, hivyo kuchagua aina moja ya pembejeo mfano, mbegu tu au mbolea ya kukuzia tu. Hali hii imefanya malengo ya uzalishaji (tija) yasifikiwe.

Baadhi ya mawakala kutokuwa na elimu ya uhifadhi na utunzaji wa pembejeo za kilimo.

Mwitikio mdogo wa wakulima katika kutumia mbolea ya Minjigu kutokana na sababu mbalimbali.

17

Kukosa mawakala wakutosha wenye mitaji ya kusambaza pembejeo vijijini kabla ya malipo

Uadilifu mdogo kwa baadhi ya mawakala na watendaji kusimamia zoezi zima la ruzuku.

Kutoeleweka vizuri mfumo wa kutumia hati za kukiri kupokea pembejeo kwa mkulima badala ya vocha kabla ya kuleta vocha.

Kuchelewa kwa malipo kwa mawakala kulishusha morali wa kuhudumia wakulima.

9.2. Ununuzi wa mahindiMhe.NaibuWaziri, Wakala wa hifadhi ya chakula cha Taifa kituo cha Sumbawanga walikadiria kununua kiasi cha tani 60,000 za mahindi katika msimu wa 2011/2012 kwa kutumia vituo 13 vya Mazwi, Bohari, Matai, Mwimbi, Katazi, Legezamwendo, Laela, na Mtawisa katika wilaya ya Sumbawanga na Namanyere, Mtenga, Kasu, Swaila na Ntalamila katika wilaya ya Nkasi. Ununuzi ulianza mwezi Agosti 2012, hadi kufikia mwezi Desemba 2012, tani zipatazo 7,346.42 zilinunuliwa sawa na asilimia 12.24. Hali hii ilitokana na mahindi mengi kuuzwa mapema na kwa bei ya juu kwa wafanya biashara kutoka mikoa iliyokuwa na upungufu wa chakula.

9.3. KILIMO CHA UMWAGILIAJI.Mhe. Naibu Waziri, Mpango kabambe wa Umwagiliaji Taifa wa mwaka 2002, ulibaini kuwa Mkoa wa Rukwa una jumla ya Hekta 527,721 zenye uwezo wa kumwagiliwa. Kati ya eneo hilo kekta 14,310 zina uwezo wa juu, hekta 42,294 zina uwezo wa kati na hekta 471,117 uwezo wake ni wa chini. Kwa sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 14,382.08 sawa na 25.41% ya eneo lenye uwezo wa juu na kati wa kumwagiliwa.

Mkoa una jumla ya Miradi ya Umwagiliaji 10 ambayo inaendelezwa kwa njia ya kisasa na Miradi ya Umwagiliaji 16 ambayo haijaendelezwa inamwagilia kwa kutumia njia za asili (Traditional Irrigation).

Kwa mwaka 2011/2012 Mkoa ulipangiwa jumla ya Sh.1,322,000,000/=kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF). Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Sh.1,072, 000,000/= na Wilaya ya Nkasi Sh.250, 000,000/= .

18

Aidha kwa mwaka 2012/2013 Mkoa umepangiwa jumla ya Sh.1,031,250,000/= kutoka Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF). Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:- Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Sh.515,625,000/= na Wilaya ya Nkasi Sh.515,625,000/=.

9.4.1. CHANGAMOTO ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI:Mhe.NaibuWaziri, Katika utekelezaji wa shughuli za Umwagiliaji mkoa unakabiliwa na changamoto zifuatazo. Upungufu wa wataalamu na vitendea kazi, katika ngazi ya Halmashauri za

Wilaya. Kutokuwepo na wakandarasi wa ndani (Private Sector) wa kutosha mkoani

wenye uwezo wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji. Kutokuwepo na wawekezaji(Investors involved in Irrigation Agriculture) toka

sekta binafsi (Private Sector) kwenye Kilimo cha umwagiliaji. Elimu ndogo kwa wakulima juu ya kuzingatia matumizi bora ya maji utunzaji

bora wa mimea na matumizi bora ya zana za kilimo katika skimu za umwagiliaji. Elimu ndogo kwa wakulima kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira. Hii

inasababisha athari za mazingira, mfano kukata miti na kulima kwenye vyanzo vya mito au kando kando ya mito.

Elimu ndogo Kwa Wakulima juu ya umuhimu wa uibuaji wa miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya vijiji.

Mkoa umejipanga kutatua changamoto kama ifuatavyo:- Halmashauri za Wilaya zimeelekezwa kuajiri wataalam wa umwagiliaji angalau

mhandisi mmoja wa umwagiliaji, mpimaji mmoja na fundi mchundo wa umwagiliaji watatu.

Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakandarasi wa ndani (Private Sector) waliopo mkoani wenye uwezo wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji wafanye kazi hizo.

Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa ili sekta binafsi (Private Sector) wawekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji (Investing in Irrigation Agriculture).

Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya kuzingatia matumizi bora ya maji, utunzaji bora wa mimea na matumizi bora ya zana za kilimo katika skimu za umwagiliaji.

Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira.

19

Halmashauri zimeelekezwa kuweka sheria ndogo ndogo kuzuia ukataji wa miti na kulima kwenye vyanzo vya mito au kando kando ya mito.

Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa uibuaji wa miradi ya umwagiliaji katika ngazi ya vijiji .

Mkoa umetoa maagizo kwa kila Halmashauri kuwa na Mpango wa matumizi bora ya ardhi.

9.4.3 MATUMIZI YA ZANA ZA KILIMO:Mhe.NaibuWaziri, Matumizi ya wanyamakazi (maksai) kwa mwaka 2011/2012 ni asilimia 80% ya nguvu kazi iliyotumia wanyamakazi katika kulima hekta 405,016 za mazao ambalo ni sawa na 324,012.8 hekta ya eneo lililolimwa kwa wanyamakazi kwenye msimu wa kilimo. Mkoa wa Rukwa una jumla ya trekta kubwa 60 na matrekta madogo 199 Mwaka 2011/2012 hekta 40,501.6 zimelimwa kwa kutumia trekta kubwa na hekta 32,401.0 kwa kutumia matrekta madogo na hekta 8,100.32 kwa wanaolima kwa mikono. 9.4.4 Miradi ya Sekta ya Kilimo.Mhe.NaibuWaziri, Katika mwaka 2011/2012 Mkoa umepangiwa jumla ya Sh. 2.659 bilioni za miradi ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo. Pamoja na kupangiwa fedha hizo mwisho wa mwaka wa fedha wa 2011/2012 Mkoa ulivuka na kiasi cha Sh. 2.665 bilioni. (Sumbawanga Sh.1.77 bilioni na Nkasi Sh. 0.885 bilioni). Miradi iliyolengwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa masoko, ujenzi wa maghara, ujenzi wa skimu za umwagiliaji, ukarabati wa nyumba za maafisa ugani, ujenzi wa vituo vya rasilimali za kilimo, ujenzi wa majosho, marambo ya Kilyamatundu na Mtenga, ujenzi wa machinjio, ujenzi wa machinjio,ujenzi wa minada ya mifugo na Majosho.

Pamoja na Serikali kuendelea kuzipatia Halmashauri fedha kwa ajili ya Miradi ya ASDP kumekuwepo na changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa miradi hiyo zifuatazo:- Kasi ndogo ya wakandarasi katika kutekeleza miradi ya DADPS iliyopo

Wilayani. Uchangiaji mdogo wa wananchi katika Miradi ya maendeleo ya kilimo (DADPS) Baadhi ya Miradi kutekelezwa chini ya viwango. Uhaba wa wahandisi wa Umwagiliaji katika wilaya za Mkoa wetu. Uhaba wa wakandarasi wenye uzoefu katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji Umakini mdogo wa watendaji wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya

maendeleo ya kilimo.

20

Halmashauri kutumia fedha za miradi kwa shughuli zisizoendana na utekelezaji wa miradi.

Ushirikiano hafifu kati ya idara na idara katika Halmashauri. Ucheleweshwaji wa fedha za Miradi ya Sekta ya Kilimo toka Serikali kuu.

10.0 MIFUGO10.1 Rasilimali za Ufugaji.

Mhe.NaibuWaziri, Kulingana na Sensa ya Kilimo ya 2003, asilimia 34 ya wananchi wa vijijini katika Mkoa wa Rukwa hujishughulisha na ufugaji. Hivyo ufugaji ni shughuli ya pili kwa umuhimu kiuchumi baada ya kilimo cha mazao. Mifugo ni rasilimali (asset) muhimu inayomilikiwa na wananchi wa vijijini baada ya ardhi. Mbali na kutumika kama benki hai mifugo hii pia hutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa njia ya nguvukazi na samadi. Zaidi ya asilimia 70 ya wakulima wa Mkoa wa Rukwa hutumia nguvukazi ya wanyama katika shughuli mbalimbali. Maeneo yanayotumika katika malisho Mkoani ni hekta 1,136,218 na malisho yasiyotumika kutokana na mbung’o ni hekta 18,952.

Mkoa mpya wa Rukwa unakadiriwa sasa kuwa na ng’ombe 438,953, mbuzi 152,899, kondoo 22,686, nguruwe 49,989, kuku 470,595 na punda 6,171. Utekelezaji katika eneo la ufugaji ulihusisha yafuatayo:-

10.2 Shughuli zilizofanyika katika kipindi kilichopita ni kama ifuatavyo (i) Kuratibu usambazaji na matumizi ya dawa ya kuogesha mifugo yenye

ruzuku. Mwezi Juni, 2012 mkoa ulipokea jumla ya lita 5,600.5 za dawa ya kuogesha mifugo yenye ruzuku ya Serikali kwa 40%. Jumla ya lita 2,400.5 za dawa zilipelekwa mkoa wa Katavi. Kutokana na matumizi hafifu ya dawa hii katika baadhi ya maeneo, wasambazaji waliopangiwa na serikali kuleta dawa hii mikoa ya Rukwa na Katavi bado wanayo dawa ya mwaka uliopita lita 14,437.6 ambayo inaendelea kusambazwa. Kati ya majosho 62 yaliyopo, yanayofanya kazi ni 35 (56%).

(ii) Kufuatilia matukio na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko. Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (CBPP) umeendelea kuenea katika maeneo mengi ya Mkoa. Wilaya ya Nkasi imeendesha chanjo dhidi ya ugonjwa huu kwa ufanisi mkubwa ambapo jumla ya ng’ombe 111,381 (82%) walichanjwa

21

mwezi Juni/Julai baada ya wafugaji kuchangia gharama ya Sh. 200/= kwa ngombe. Aidha kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na kondoo katika baadhi ya mikoa, chanjo dhidi ya ugonjwa huu inaendelea kutolewa katika wilaya za Sumbawanga na Nkasi ambapo hadi sasa wanyama 6,000 wamechanjwa katika wilaya ya Sumbawanga.

(iii) Mashindano ya wafugaji kitaifaMfugaji kutoka Wilaya ya Nkasi aliwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika mashindano ya wafugaji kitaifa mjini Dodoma na kuibuka mshidi wa kwanza katika kundi la wafugaji wadogo wa ng’ombe wa nyama. Ushindi huu unaendelea kutangaza fursa zilizopo katika Mkoa wa Rukwa.

10.3 MIKAKATI YA SEKTAMhe.NaibuWaziri, Mkoa wa Rukwa unazo fursa nyingi za ufugaji ikiwa ni pamoja na ardhi ya kutosha, mvua za kuaminika, rasilimali ya mifugo ya kutosha na soko zuri la ndani na nchi jirani ambazo hazina rasilimali ya kutosha ya mifugo. Mkoa unayo machinjio ya kisasa yenye uwezo wa kuchinja kwa wakati mmoja Ng’ombe 200 na Mbuzi zaidi ya Hamsini.

10.4 CHANGAMOTO ZA SEKTA

Mhe.NaibuWaziri, Mkoa unakabiliana na changamoto mbalimbali katika kuendeleza sekta ya ufugaji. Baadhi ya changamoto zinazoathiri ufugaji katika Mkoa wa Rukwa ni pamoja na zifuatazo:Baadhi ya changamoto muhimu zinazoathiri ufugaji katika Mkoa wa Rukwa ni pamoja na zifuatazo: Ukosefu wa mipango ya matumizi bora ya ardhi; pale ilipo mipango hii

haizingatiwi. Uhamiaji holela wa mifugo kutoka mikoa jirani. Mbali na kusababisha migogoro

ya ardhi hali hii huchangia sana kuenea kwa magonjwa ya mifugo. Msongamano wa mifugo katika baadhi ya maeneo, hasa yale yenye vyanzo vya

maji vya uhakika. Huduma duni za ugani kutokana na uhaba wa wataalam na wachache waliopo

kutotumika ipasavyo. Sekta binafsi dhaifu na ukosefu wa asasi za wafugaji. Uhaba wa miundombinu ya huduma za mifugo

22

12.0 UVUVI.Mhe.NaibuWaziri, Kutokana na sensa ya mwaka 1999 uzalishaji wa samaki toka Ziwa Rukwa unakadiriwa kuwa ni tani 7,000 na Ziwa Tanganyika linakadiriwa kuzalisha samaki kiasi cha tani 165,000 hadi tani 200,000 kwa mwaka wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 80 hadi milioni 100.

Kuna aina mbali mbali ya samaki wanaopatikana katika maziwa na mito iliyopo katika Mkoa wetu. Ziwa Tanganyika linatupatia samaki aina ya dagaa, migebuka, sangara, kuhe, kambale na samaki wa mapambo. Ziwa Rukwa linatupatia kambale, gege na mamba. Dagaa na migebuka wanaopatikana ziwa Tanganyina na gege toka ziwa Rukwa mara nyingi hukaushwa na kupelekwa kuuzwa kweye masoko makubwa ndani na nje ya nchi mfano Zambia, Kongo na Burundi.

12.1. CHANGAMOTO. Ukosefu wa nishati ya umeme kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika . Ukosefu wa zana bora za uvuvi kwa wavuvi.

13.0. USHIRIKA.Mhe.NaibuWaziri, Hadi kufikia mwezi 31 Disemba, 2012 Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika 93 zikiwemo SACCOS 80 zenye jumla ya Wanachama 10,938 na Hisa za jumla ya Sh.286,600,000/= akiba za Sh.1,581,083,000/= na amana zenye thamani ya Sh.27,999,000/= hivyo kufanya jumla ya mtaji wenye thamani ya Sh.1,872,682,000/=. Jumla ya Sh.5,732,891,000/= zimetolewa kama mkopo kwa wanachama na kiasi cha Sh.4,085,820,000/= kimerejeshwa sawa na asilimia 71.3 ya kiasi cha fedha zilizokopeshwa. 13.1: CHANGAMOTO.Mhe.NaibuWaziri, Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kuendeleza sekta ya Ushirika Mkoani Rukwa unakabiliwa na changamoto zifuatazo:- Upungufu wa Maafisa ushirika katika Halmashauri. Upungufu wa vitendea kazi kwa maafisa ushirika ikiwemo vyombo vya usafiri. Baadhi ya Halmashauri kuchelewesha makato (deductions) ya SACCOS za

wafanyakazi. Baadhi ya wanachama wa Vyama vya Akiba na Mikopo kuchelewesha ama

kutorejesha kabisa mikopo.

23

14.0 SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARAMhe. Naibu Waziri, Katika sekta hii kuna viwanda vidogo na vya kati vinavyoendeshwa, Viwanda hivyo vinajihusisha na shughuli za usindikaji wa nafaka, samaki, nyama utengenezaji wa sabuni. Hadi sasa Mkoa una Viwanda saba ambavyo ni:- SAAFI Co.LTD, Tropical grain Co.LTD, Fantashiru Milling, Ikuwo Enterprises, Energy Milling.Co.Ltd, Migebuka Premium (Premji).

14.1. BIASHARAMhe.NaibuWaziri, Mkoa unaendelea kuhakikisha kuwa unawakwamua wananchi wake kiuchumi. Katika jitihada hizo maafisa biashara wamekuwa wakitoa elimu na ushauri kwa wajasiriamali juu ya kuendesha biashara zao kwa mafanikio na uboreshaji wa vifungashio kwa wasindikaji ili kuwavutia wateja. Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) imekuwa mstari wa mbele katika kuiendeleza sekta ya biashara.

14.2. BEI ZA VYAKULA NA BIDHAA MBALIMBALI Mhe. Naibu Waziri, Tokea tupate agizo la kuangalia mwenendo wa bei hapa Mkoani, hali ya upatikanaji wa bidhaa mbalimbali imekuwa ya kuridhisha na bei ya baadhi ya bidhaa imekuwa ya kupanda na kushuka kama ifuatavyo; Vyakula: Bei ya rejareja kwa kilo moja ya Sukari ni kati ya Sh. 2,000 hadi 2300. Mafuta ya kula lita 10 ni Sh. 30,000 sawa na Sh. 3,000 kwa lita Unga wa Sembe kilo moja inauzwa kwa Sh. 700/-1,000 Mchele unauzwa Sh. 1,400 hadi Sh. 1,700 kwa kilo. Bidhaa nyingine bei zake ni kama ifuatavyo:- Petrol lita moja Sh. 2,262 /=, Diesel lita moja Sh. 2,300/=, Mafuta ya taa, lita moja Sh. 2,221/=, Gesi kilo 15 ni Sh. 57,000/= na Saruji mfuko wa kilo 50 unauzwa kwa shilingi 21,000/=.

14.3. CHANGAMOTO ZILIZOPO: Ubovu wa miundombinu Ukosefu wa nishati kwa baadhi ya maeneo Ukosefu wa masoko ya baadhi ya mazao

15.0 MALIASILI NA MAZINGIRAMhe. Naibu Waziri, Mkoa wa Rukwa una fursa nyingi za maliasili (utalii, misitu na ardhi) ambazo bado hazijatumiwa kikamilifu kama Maporomoko ya mto Kalambo yenye mita 235, wanyama waliopo katika mapori tengefu ya Lwafi, mbega

24

wekundu waliopo katika msitu wa hifadhi wa Mbizi. Uwepo wa makaa ya mawe, uwepo wa ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa pamoja na mito midogo midogo mingi. Katika kutekeleza sera ya Taifa na sheria ya Mazingira, Mkoa umeendelea kuhamasisha wananchi katika kuhifadhi Mazingira kwa njia mbalimbali zikiwemo za upandaji miti na utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira.

15.1. HIFADHI YA MAZINGIRA (i) UPANDAJI MITI;

Jumla ya miti 2,468,052 ilioteshwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Rukwa mwaka 2011/2012.

(ii) MATUMIZI BORA ARDHIJumla ya vijiji 13 vimeshatekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi (Land Use Plan) kati ya vijiji 259 vilivyopimwa.

(iii) ELIMU YA MAZINGIRA; Elimu hii inatolewa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya ziwa Tanganyika, mradi uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Divisheni ya Mazingira, Taasisi ya kuhifadhi wanyama iliyopo Mbeya (WCS - Wildlife Conservation Society), REYO - Rukwa Environment Youth Organization, KAESO, ADAP - Association for Development for Areas Protected, REDESO, GMU n.k,

15.2. MRADI WA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKAMhe.NaibuWaziri, Katika Mkoa wa Rukwa, Programu hii inatekeleza miradi miwilikama ifuatayo:- Mradi wa usimamizi wa Bonde (Catchments Management) Mradi wa uendelezaji wa Uvuvi na Hifadhi ya Mazingira ya ziwa Tanganyika.

Mambo ambayo yanapelekea kuandaa mkakati wa kuhifadhi ziwa Tanganyika yanatokana na mambo yafuatayo;-- Uchafuzi wa ziwa (environmental pollusion)- Kuongezeka kwa tabaka la udongo (sedmentation)- Uharibifu wa makazi ya viumbe ( destruction of breeding site)- Uvuvi usio endelevu ( unsustainable fisheries)

15.3. MISITU NA NYUKI

25

Mhe.NaibuWaziri, Katika kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya Misitu na nyuki kazi zifuatazo zimetekelezwa kwa mwaka 2011/2012 Mkoa umekusanya Shs.201,559,099/= kutokana na ushuru utokanao na mazao

ya misitu na ukataji wa leseni za biashara ya mzao ya misitu. Jumla ya mita za ujazo 3000 zimetolewa kwa ajili ya ukusanyaji wa kuni Tani 420 za asali zimepatikana kutokana na urinaji wa asali Kamati 15 za wafuga nyuki zimeanzishwa katika vijiji 15 na vikundi 77

vimenufaika na elimu ya ufugaji nyuki. Jumla ya mizinga 684 ya kisasa imewekwa katika maeneo mbalimbali ya

Halmashauri zetu za Mkoa wa Rukwa. Jumla ya miti 2,468,052 imeoteshwa maeneo mbalimbali katika Mkoa wa

Rukwa kwa mwaka 2011/2012.

15.4. WANYAMAPORIMhe.NaibuWaziri, Katika kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya wanyamapori kazi zifuatazo zimetekelezwa kwa mwaka 2011/2012. Jumla ya watu 2800 waliondolewa kwenye Mapori ya Akiba, ambapo walikuwa

wakiendesha shughuli za kibinadamu (kilimo, ufugaji na uvuvi), ambapo wawaliokuwa wanaendesha shughuli za uvuvi wamepewa muda wa kuondoka (mwisho mwezi wa kumi) wafugaji walioachia mifugo 17 walitozwa faini na mmoja alifungwa na wawili wanatafutwa. Aidha zoezi hilo la kuwaondoa wavamizi litaendelea katika msitu wa hifadhi wa Kalambo na misitu mingine ya hifadhi.

Jumla ya doria 2 kubwa na doria 4 ndogo zimefanyika katika maeneo misitu ya asili na Mapori ya Akiba.

15.5. CHANGAMOTO: Uelewa mdogo wa wananchi dhidi ya hifadhi ya mazingira. Ukataji wa miti holela kwa ajili ya nishati ya kuni, mkaa, ujenzi na upanuzi wa

mashamba. Uchungaji holela wa mifugo na wa kuhamahama, na Uchomaji moto ovyo.

15.6. MIKAKATI: Kuwashirikisha wananchi katika uibuaji wa miradi ya maendeleo inayohusisha

masuala ya mazingira, mfano mradi wa utengenezaji wa sabuni. Kuendelea kuzijengea uwezo kamati za mazingira za vijiji ( VNRC)

26

16.0. MIUNDOMBINU16.0. SEKTA YA BARABARA

16.1. MATENGENEZO YA BARABARA KUUMhe. Naibu Waziri, Hadi kufikia tarehe 31, Novemba 2012, kazi za matengenezo ya barabara kuu na za Mkoa zilizopangwa kufanyika katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 zilikuwa zimekamilika ambapo km 447, madaraja 25 yalijengwa ama kutengenezwa kwa gharama ya Shilingi. 1,452,759,000. Matengenezo ya barabara kwa bajeti ya 2012/13 yanaendelea kufanyika na yapo katika hatua tofauti za utekelezaji.

16.1.1 UKARABATI NA UJENZI WA BARABARA KUU NA ZA MKOA.Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 ukarabati/ujenzi kwa kutumia fedha za ndani (bajeti ya maendeleo) tulitarajia kutengeneza km 101, barabara hizi zimekamilika kwa kutumia Sh. millioni 3,014,797.

16.2 MIRADI YA MAENDELEO YA BARABARA16.2.1 UKARABATI NA MATENGENEZO KUPITIA MPANGO WA PMMR (Performance–Based Management and Maintenance of Roads).

Mhe. Naibu Waziri, Mradi wa PMMR kwa sasa unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 ambayo mikataba iliyopo ni ya Miaka Mitano. Katika kipindi cha 2010/2011 hadi 2011/2012 kiasi cha km 111.59 za barabara zimekarabatiwa ambapo zimeigharimu Serikali Sh.5,763,432,621.72.

16.3. UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI (SUMBAWANGA -LAELA- TUNDUMA (228.40 KM)

16.3.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA - LAELA (95.31 KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Aarsleff-BAM International Joint Venture V.O.F kutoka Denmark na Uholanzi kwa gharama ya USD 97 Milioni chini ya mhandisi

27

mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe Novemba, 2012 yalikuwa yamefikia 49.9% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri.

16.3.2. SEHEMU YA LAELA - IKANA (64.2 KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China New Era International Engineering Corporation kutoka China kwa gharama ya Sh. bilioni 76.1 chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa.

Maendeleo ya jumla ya mradi Desemba, 2012 yalikuwa yamefikia 65.51% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri.

16.3.3. SEHEMU YA IKANA - TUNDUMA (63.7 KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Consolidated Contractors Group S.A (offshore) (CCC) kutoka Ugiriki chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufaransa kwa gharama ya Sh. billion 82.5. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi Desemba 2012, yamefikia 44% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri.

16.3.4 SUMBAWANGA-NAMANYERE-MPANDA/KIZI-KIBAONI (274 KM)16.3.5 SEHEMU YA SUMBAWANGA-KANAZI (75 KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikana na Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia Desemba, 2012 yalikuwa 25.1% ya kazi zote zilizopangwa. Kuchelewa kwa malipo ya Mkandarasi kumeathiri kasi ya utekelezaji wa mradi, ambapo mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012.

16.3.6 SEHEMU YA KANAZI-KIZI-KIBAONI (76.6 KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group Corporation kutoka China, chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania, kwa gharama ya Sh.82.84 bilioni.

28

Maendeleo ya jumla ya mradi Desemba, 2012 yalikuwa 30.12% ya kazi zote zilizopangwa. Mkandarasi anaendelea vizuri ingawa kuchelewa kwa malipo ya Mkandarasi kumeathiri kasi ya utekelezaji wa mradi ambapo mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba,2012.

16.3.7 SUMBAWANGA-MATAI-KASANGA PORT (112KM)Eneo hili linajegwa na Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company Ltd chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd kutoka Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh.133.3 billion.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia Desemba, 2012 yalikuwa 30.29% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and Build Contract). Usanifu wa kina wa kilometa 70 za kwanza umekamilika na Mkandarasi ameruhusiwa kuanza kazi katika kilometa 60 za kwanza. Usanifu wa kilometa 42 zilizobaki unaendelea.

16.3.8 MIRADI YA UPEMBUZI YAKINIFU NA USANIFU WA KINAMiradi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Mkoa ni:-i). Barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda: Sehemu ya Kizi-Sitalike -

Mpanda (123 km)

ii). Barabara ya Matai-Kasesya (47 km)

16.4 CHANGAMOTO Mhe.Naibu Waziri, Tunakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo:(i) Uhaba wa mitambo ya matengenezo na ujenzi wa barabara pamoja na

Magari kwa Wakandarasi na hata Wakala (TANROAD)(ii) Ugumu wa makandarasi kupata dhamana (bonds/guarantees) kutoka katika

vyombo vya fedha na hivyo kuchelewa kuanza kazi.

17.0. KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA NA ENEO JIPYA LA KISUMBA17.1. HISTORIA FUPI YA KIWANJAMhe.NaibuWaziri, Kiwanja hiki kipo katika daraja la “3C” ambapo miundombinu yake huruhusu kutua na kuruka kwa ndege za uzito usiozidi tani 20. Barabara ya kutua na kuruka kwa ndege (runway) katika kiwanja hiki ni changarawe na ina urefu wa km. 1.6 tu. Kiwanja kina hudumia ndege za ndani ya nchi (charter flights)

29

za kukodi, ndege za abiria, ndege za serikali na nyakati nyingine nchi za jirani kama vile Zambia kwa ajili ya huduma za jamii za kuangamiza wadudu waharibifu.

17.2.UENDESHAJI KIWANJAMiundombinu: Katika majukumu yetu ya uendeshaji kiwanja tunawajibika kuhakikisha kuwa wakati wote miundombinu ya kiwanja hususani barabara ya kutua na kuruka ndege ziko katika hali salama kwa ndege kutua na kuruka.

17.3. HUDUMA ZA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.Kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kiko katika daraja la sifuri (0) la viwango vya zimamoto (fire service category zero). Hii kutokana na kutokuwepo kabisa kwa gari la kutoa huduma ya zimamoto na uokoaji.

17.4. MAPATO NA MATUMIZI YA KIWANJAKiwanja hiki ni moja ya viwanja vingi vinavyoendeshwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ambavyo havina mapato ya kutosha kujiendesha chenyewe. Hivyo matumizi ya kiwanja ni makubwa mara 36 ya mapato, kuanzia mwaka 2005 hadi 2011 kiwanja kimepata jumla ya Sh.8,437,900.00 na kutumia jumla ya Sh. 398,800,282.00 kwa kujiendesha, kama inavyoonyesha hapo chini katika jedwali namba 10.

Jedwali Na.10: MAPATO YA KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGASN Mwaka Mapato (Tsh.) Matumizi (Tsh.)

1 2010/2011 5,640,022 109,042,1432 2009/2010 4,785,000 8,749,69743 2008/2009 1,163,500 86,465,7864 2007/2008 1,918,200 86,966,6585 2006/2007 285,600 75,601,6856 2005/2006 285,600 62,269,179

Jumla 8,437,900 398,800,282

17.5. CHANGAMOTO ZINAZOKABILI KIWANJAMhe.NaibuWaziri, Kiwanja cha ndege cha sumbawanga kinakabiliwa na changamoto zifuatazo:- Kiwanja chetu hakina jengo la Watu Mashuhuri (VIP). Hivyo hupelekea

tunapopata ugeni wa kitaifa inatulazimu kuchanganyika na abiria wa kawaida.

30

Kiwanja hakina mitambo ya ukaguzi wa kiusalama kama mashine za kukagulia mizigo ya abiria (X-ray machine), mashine za kubaini vifaa vya chuma(walk through metal detectors). Hali hii huwalazimu maafisa wa usalama wa kiwanja kufungua mizigo ya abiria kwa ajili ya ukaguzi(Physical search) na kasha kutumia Hand held metal detectors kwa ajili ya ukaguzi wa abiria kabla ya kupanda ndege. Hali ya kukosekana kwa mitambo hiyo hupelekea ugumu wa kazi na kusababisha usumbufu na kero kwa abiria wanadai kuwa hali hiyo inawadhalilisha.

Ukosefu wa gari la zimamoto; kituo hiki hakina kabisa gari la zimamoto. Migogoro ya ukatishaji watu kiwanjani. Kutokana na ukosefu wa uzio wa usalama kuna tatizo la ukatishaji watu

kiwanjani la mara kwa mara.

17.6. MIPANGO YA MAENDELEOKiwanja cha sumbawanga ni mojawapo ya viwanja saba vilivyofanyiwa usanifu wa kina (feasibility study and Detailed Engineering Design) kwa ufadhili wa benki ya Dunia katika mwaka 2007/08. Baada ya usanifu wa kina serikali imekuwa ikitafuta fedha kutoka kwa vyanzo mbalimbali ili kuweza kukarabati miundombinu ya kiwanja. Na kwa sasa serikali imeshafanikiwa kupata mkopo wa Euro million 50 kutoka European Investment Bank (EIB) kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vitano ikiwemo Sumbawanga.

Serikali ya Mkoa wa Rukwa imeshatenga eneo jipya la kujenga kiwanja kikubwa cha ndege katika eneo la Kisumba umbali wa km 20 toka Sumbawanga mjini.

Serikali ya Mkoa kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ilipendekeza ianze kujenga kiwanja katika eneo la Kisumba badala ya kuendeleza kiwanja cha sumbawanga mjini kwa kutumia mkopo wa fedha kutoka EIB uliokusudiwa kukiendeleza kiwanja cha Sumbawanga mjini.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imetenga Shilingi milioni 20 katika mwaka wa fedha 2012/13 kwa ajiri ya kufanya tathmini ya eneo la kisumba kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja kipya.

18.0. BANDARI YA KASANGAMhe.NaibuWaziri, Bandari ya Kasanga huendesha shughuli zake kwa kusimamiwa na Kampuni ya Agro Truck Investment Ltd. Kampuni hii inakarabati ghati kwa

31

kuongeza eneo la kuegesha meli pamoja na ujenzi wa ghala ili kukidhi mahitaji ya abiria na mizigo. Fedha za ukarabati zilipatikana kwa msaada wa Serikali ya Norway kupitia ushirikiano wa Rukwa Association of Non Governmental Organization (RANGO). Ujenzi wa Bandari ya Kasanga unatarajiwa kugharimu kiasi cha Dola Laki Mbili za Kimarekani ($ 200,000).

18.1. MAFANIKIO:Mhe.Naibu Waziri, Bandari inatazamiwa kupanuliwa kwa kujenga Maghala na majengo mengine ili kukidhi mahitaji ya bandari. Kwa hivi sasa tayari Maghala 2 yamejengwa na yanatumika kikamilifu. Maghala hayo yanauwezo wa kuhifadhi takriban tani 3,000 kila moja na yamegharimu Shilingi bilioni 1.1 fedha toka Mamlaka ya Bandari ya Tanzania.

18.2. CHANGAMOTO:Mhe.Naibu Waziri, Bandari ya Kasanga inakabiliwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wake. Changamoto hizo ni pamoja na:- Ukosefu wa fensi kuzunguka eneo la bandari Ukosefu wa nyenzo za kufanyia kazi ikiwepo focal lifts, winchi na safari chache

za meli zinazofanywa kwa mwezi, na Ukosefu wa huduma ya umeme wa uhakika.

19.0. SEKTA YA ARDHI.Mhe. Naibu Waziri, Mkoa hutegemea ardhi yake kwa ajili shughuli za Kilimo na kiuchumi katika kuleta maendeleo endelevu na kupunguza umaskini, mchango wa Sekta ya Ardhi katika maendeleo ya Mkoa ni pamoja na uhakika wa kupata chakula na kipato. Mkoa wa Rukwa una jumla ya vijiji 288, vijiji 201 kutoka Wilaya ya Sumbawanga na Vijiji 87 kutoka Wilaya ya Nkasi. Kati ya vijiji 237 (82.3%) tayari vimepimwa mipaka yake indaendelea katika Halmshauri zote husika. Aidha Mkoa wa Rukwa una mpango wakuhakikisha matumizi bora ya ardhi katika miji, vitongoji na vijiji vyake inaendelea kutayarishwa kulingana na upatikanaji wa fedha kwenye bajeti. Hadi kufikia Oktoba 2012 vijiji 19 vilikuwa tayari vimeandaliwa matumizi bora ya ardhi ambapo ni asilimia (6.6%) ya vijiji vya Mkoa wa Rukwa. Taratibu zinaendelea ili kuhakikisha kwamba vijiji vyote vinaandaliwa matumizi bora ya ardhi. Mkoa una mpango pia unaolenga kuhakikisha miji yetu inakuwa safi na salama kwa wakazi wa mijini. Mipango inayoelekezwa ni pamoja na:- Kuhakikisha ardhi yote iliyoko mijini inapangwa na kupimwa. Kuboresha Miundombinu, huduma za jamii na makazi endelevu.

32

Kuibua fursa na ajira na kuweka mikakati ya kuondoa umaskini uliokithiri mijini. Kuhakikisha wadau wote wa maendeleo mijini wakiwepo NGOs, CBOs,

Cooperatives wanahusishwa kwenye mipango ya kuendeleza miji yetu Kuhakikisha wakati wote wa kuendeleza miji yetu mazingira yanalindwa. Kuhakikisha kwamba wakati wote wa kushughulia masuala yote ya ardhi sheria,

kanuni na miogozo inafuatwa na kuzingatiwa ili kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.

Mafanikio:- Katika kipindi kilichoishia Octoba, 2012 Mkoa umeweza kufanya kazi mbalimbali kama inavyoonyesha katika jedwali namba 11 hapa chini.

Jedwali Na.11: UPIMAJI WA VIWANJA.H/Mashauri Viwanja

vilivyopangwaViwanja

vilivyopimwaViwanja

Vilivyoandaliwa

Mashamba yaliyopimwa

Vijiji Vilivyopimwa

mipaka

Vijiji Vilivyoandaliwa matumizi bora

ya ardhi

Viwanja vilivyopimwa

kwa uwekezaji

S’ wanga DC 397 436 4 19 155 15 -

S’wanga MC 5500 1500 1237 32 - - 13

Nkasi 2327 587 30 3 82 4 10

Jumla 8224 2523 1271 54 237 19 23

19.1. CHANGAMOTO:Mkoa unakabiliwa na changamoto zifuatazo:-(i) Mipango ya matumizi bora ya ardhi; Halmashauri hazijafanya kazi ya

kutosha ya kubainisha matumizi bora ya ardhi kutokana na kinachoelezwa kuwa ni ufinyu wa bajeti. Kazi hii ikifanyika kikamilifu itasaidia kuepusha migogoro ya Wakulima na Wafugaji katika Mkoa wetu pamoja na maliasili zilizopo.

20.0 MKONGO WA TAIFAMhe. Naibu Waziri, Shughuli za kutandaza Mkongo wa Taifa zimekamilika katika Mkoa wetu na hadi sasa hakuna tukio lolote la hujuma dhidi ya Mkongo lililolipotiwa kutokea Mkoani kwetu. Hata hivyo Mkongo huu haukupitia katika Mji wa Namanyere ambapo ndio makao makuu ya Wilaya ya Nkasi.

21.0 SEKTA YA NISHATI21.1. MITAMBO YA KUFUA UMEME

33

Mhe. Naibu Waziri, Mji wa Sumbawanga unategemea umeme kutoka nchi jirani ya Zambia. Katika mwaka wa 2010, Serikali ilinunua na kufunga Generator nne zenye uwezo wa kuzalisha megawati tano (5). Kazi ya kusimika Mitambo ya kufua Umeme ilianza mwanzoni mwa mwezi April,

2011 na kumalizika mwanzoni mwa mwezi Juni, 2011. Mitambo ilianza kufua Umeme kuanzia tarehe 02.08.2011 japokuwa kwa

vipindi tofauti tofauti umeme huu umekuwa haupatikani kwa sababu ya kukosekana kwa mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo.

21.2. MRADI WA UMEME NAMANYEREMhe.NaibuWaziri, Awali mradi huu ulitarajiwa kukamilika mnamo mwezi wa Disemba 2011. Kazi ya kuweka nguzo na kutandaza nyaya kutoka mjini Sumbawanga hadi Namanyere wilayani Nkasi imekamilika. Ni matumaini ya mkoa kuwa umeme utawaka katika mji mdogo wa Namanyere vikiwemo vijiji 12. Mkoa unahitaji msukumo kutoka ngazi ya juu katika kuhakikisha kuwa umeme unapatikana Katika makao makuu ya wilaya zake zote na hasa wiliya mpya ya kalambo Mjini Matai na Namanyere.

22.0. MFUKO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATUMISHI MKOA WA RUKWA (RCSFF)Mhe.NaibuWaziri, Mfuko wa kuboresha mazingira ya Watumishi Mkoa wa Rukwa (Zamani ukijulikana kama ‘Mfuko wa Mwalimu Nyerere’) tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2007 umewezesha upatikanaji wa jumla ya walimu wa sekondari 380 pamoja na watumishi wa idara ya afya 36 ( katika kada za Madaktari na Wauguzi).

22.1. HALI YA KIFEDHA YA MFUKO Mhe.NaibuWaziri, Hadi kufikia Desemba 2012, mfuko una jumla ya shilingi milioni moja. Kwenye akaunti zake mbili zilizo katika benki za CRDB na NMB. Aidha, Mfuko umewekeza fedha sehemu mbili tofauti kama ifuatavyo:- UTT zimewekezwa Sh.200,000,000/= ambazo zimeishatoa faida ya

Sh.57,000,000/=. Benki ya CRDB zimewekezwa Sh.35,000,000/= ambazo zimetoa faida ya

Sh.4,500,000/= .

22.2. CHANGAMOTO NYINGINE ZINAZOUKABILI MFUKO.(i) Halmashauri hazichangii Mfuko wa kuboresha Mazingira kwa Watumishi

34

(ii) Wananchi wengi bado hawajafahamu umuhimu wa kuchangia mfuko huu kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za mfuko.

(iii) Usimamizi usioridhisha wa mfuko wenyewe.

23.0. KONGAMANO LA UWEKEZAJI.Mhe. Naibu Waziri, Mkoa Umeweza kuandaa kwa mafanikio makubwa Kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika lililofanyika Wilayani Mpanda kuanzia tarehe 15-18/10/2011 na kufunguliwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 17/10/2011. Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuzinadi fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika Ukanda huu. Jumla ya washiriki zaidi ya 300 walishiriki kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo mabalozi 34 kutoka nchi mbalimbali.

Aidha tathimini ya kongamano hilo ilifanyika tarehe 25/11/2012 ambapo Mkoa ulikuwa umepokea maombi toka kwa wawekezaji kumi na moja (11) walioonesha nia ya kuwekeza katika shughuli za Uvuvi, Hotel za kitalii, usafili wa Anga. Kati ya wawekezaji hao, tayari wapo waliokwisha kamilisha taratibu za uwekezaji na wanaendelea na kazi, mfano yapo makampuni mawili ya Auric Air Na Mission Aviation Fellowship (MAF) wanaotoa huduma ya usafiri wa Anga mara tano kwa wiki, ujenzi wa Hotel mbili za kisasa za New Holland na Kalambo Falls lodge. Aidha kwa upande wa uwekezaji katika kilimo wapo wakulima nane(8) ambao wameingia mkataba na kampuni ya bia ya TBL kwa ajili ya uzalishali wa shairi ambapo jumla ya Ekari 2,050 zitalimwa.

24.0. MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARAMhe. Naibu Waziri, Mkoa umefanikiwa kutoa kitabu maalumu kinachoelezea wapi tulipokuwa wapi tulipo na wapi tuendako, kitabu hicho kinaitwa ‘‘Taarifa ya Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa Desemba 1961 - Desemba, 2011”

Mkoa umeweza kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya maonesho Viwanja vya Sabasaba vya Mwalimu J.K. Nyerere vilivyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 - 12 Desemba, 2011. Katika ngazi ya Mkoa maadhimisho yalifanyika Mjini Namanyere, kwa kuambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya Umma zikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wajasiriamali na Wadau wengine wa Maendeleo.

35

25.0 UTAWALA BORA.25.1. TAARIFA YA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA. 25.1.1 MAPATO YA HALMASHAURI Mhe. Naibu Waziri, Katika mwaka wa fedha wa 2012/2013, hadi kufikia Novemba 2012, Halmashauri zetu zililkuwa zimekusanya jumla ya Sh.941,795,132.5 ikiwa ni makusanyo yake ya ndani sawa na asilimia 20.5 ya lengo la mwaka. Mchanganuo wa Mapato kwa kila Halmashauri ni kama inavyoonekena katika Jedwali namba 12 hapa chini.Jedwali Na.12: MAPATO YA HALMASHAURI MKOANI RUKWA.

HALMASHAURI MAKISIO MAKUSANYO ASILIMIA

MANISPAA YA SUMBAWANGA 1,651,147,210 433,166,507 26

HALMASHAURI YA SUMBAWANGA 1,902,858,000 350,779,748.50 18

HALMASHAURI YA NKASI 1,027,078,000 157,828,877 15

JUMLA 4,581,083,210 941,775,132.5 20.5

25.1.2 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.Mhe.Naibu Waziri, Katika mwaka wa fedha 2011/2012 Halmashauri zilitengewa jumla ya Sh.27,969,707,000/= ambapo hadi Juni 2012 fedha zilizopokelewa ni Sh.24,049,435,915.86/= sawa na asilimia 86 tu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Aidha kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Halmashauri zilitengewa jumla ya Sh.14,276,905,000/= ambapo hadi Novemba 2012, fedha zilizopokele- wa ni Sh.6,637,374,275/= sawa na asilimia 46 ya lengo la mwaka. Mchanganuo wa utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo itapatikana katika Halmashauri husika wakati wa ziara.

25.1.3 Changamoto katika utekelezaji wa miradiMhe.Naibu Waziri, Miradi ya maendeleo imekuwa ikitekelezwa kulingana na fedha zinavyopokelewa. Aidha, Halmashauri zinakabiliwa na changamoto zifuatazo; Kuchelewa kupata fedha kutoka Serikali Kuu. Ukosefu wa vipaumbele madhubuti katika bajeti zao. Uwepo wa miradi viporo mingi. Kukopwa kwa fedha za miradi ya maendeleo kwenda matumizi mengineyo. Usimamizi usio wa viwango wa miradi. Fedha kutoletwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa. Wakandarasi wengi kutokuwa waminifu katika kutekeleza miradi kwa viwango.

36

25.1.3. VIKAO VYA KISHERIA.Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimeendelea kuendesha vikao vyao vya Kisheria kama kawaida japo kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 baadhi ya Halmashauri hazikufanya vikao vya kisheria kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.

25.1.4. HALI YA WATUMISHI.Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zote tatu za Mkoa wa Rukwa zinao Wakurugenzi. Aidha, kutokana na muundo mpya wa Vitengo na Idara za halmashauri ulivyo kwa sasa, nafasi nyingi za Wakuu wa Idara na Vitengo bado zinakaimiwa na ni jukumu la halmashauri husika kupendekeza na/ama kujaza nafasi zilizowazi kwa kutumia watumishi wenye sifa waliopo katika halmashauri ama kuomba kwa wizara husika. Kwa mfano jedwali Namba 13 hapo chini linaainisha mahitaji ya wakuu wa idara na vitengo:Jedwali Na 13: MAHITAJI YA WAKUU WA IDARA KATIKA HALMASHAURI

No. Jina La Halmashauri

Nafasi Zilizojazwa Nafasi Zinazokaimiwa Hatua zilizochuku liwa.

1. Manispaa ya Sumbawanga

Idara nane (8) za zamani na kitengo kimoja cha ukaguzi wa ndani

Nafasi 5 (tano) vitengo vipya. Nafasi 2 (mbili) za idara mpya na nafasi 3 (tatu) idara za zamani

Mchakato wa kuteua watumishi kukaimu nafasi mpya unaendelea.

2. Halmashauri ya Sumbawanga

Nafasi saba (7) idara za zamani zimejazwa.

Nafasi 4 (nne) vitengo vopya na idara mpya 2 (mbili)Nafasi 4 (nne) idara za zamani.

Wameteuwa watumishi wenye sifa kukaimu nafasi mpya unaendelea.

3. Halmashauri ya Nkasi

Idara tisa (9) na kitengo kimoja cha ukaguzi wa ndani.

Vitengo vitano (5) vipya

Idara mpya mbili (2) na idara nne (4) za zamani

Mchakato wa kuteua watumishi wenye sifa kukaimu nafasi mpya unaendelea

Aidha kwa upande wa watumishi, halmashauri zinakabiliwa na uhaba wa watumishi ambapo uhaba mkubwa unaonekena katika katika Sekta ya Afya na Elimu kama Jedwali Namba 14 linavyoonyesha hapa chini.

Jedwali Na 14: MAHITAJI YA WATUMISHI.

No. Jina La Halmashauri Watumishi waliopo

Mahitaji ya watumishi

Upungufu wa watumishi

1. Manispaa ya Sumbawanga 1,876 2,550 713

2. Halmashauri ya Sumbawanga 3,663 6,114 2,45137

3. Halmashauri ya Nkasi 491 701 210

26.0 HOJA ZA UKAGUZI.Mhe. Naibu Waziri, Halmashauri zimeendelea kujibu hoja za ukaguzi za ndani na nje za mwaka 2009/2010 hadi 2010/2011 hii inalenga pia kuboresha hali ya usimamizi wa matumizi ya fedha. Kwa mwaka wa fedha 2010/2011 Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga zilipata hati safi na Hati ya mashaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Kutokana na ripoti hiyo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa umekwisha chukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha hoja hazijitokezi, mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Dodoma, pia Katibu Tawala Mkoa pamoja na wataalam wake kuzitembelea Halmashauri zote tatu (3) na kufanya nao vikao kwa ajili ya kuhakikisha hoja zinajibiwa kwa wakati na kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupitia Mkaguzi Mkazi aliyepo Rukwa.

26.1. AINA YA HATI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU (2008/09 - 2010/2011Jedwali Na 15: HATI ZA UKAGUZI KATIKA HALMASHAURI.

Na HALMASHAURI 2008/2009 2009/1010 2010/2011

1. Manispaa Sumbawanga Hati ya mashaka

Hati ya mashaka Hati safi

2. Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Hati safi Hati ya mashaka Hati safi

3. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Hati safi Hati ya mashaka Hati ya mashaka.

26.2 MUHTASARI WA HOJA KATIKA HALMASHAURI KWA MIAKA 2008/09 - 2010/2011.

Jedwali Na 16: MUHTASARI WA HOJA.

S/N HOJA S’WANGA MC

S’WANGA DC

NKASI DC

1. “CAG Audit Queries” 2010/2011 6 7 3

2. Current year Management Queries 27 21 24

38

3. “Management previous ordinary queries” 26 15 1

4. Management previous project queries 5 3 8

5. Maelekezo ya LAAC 10 23 11

JUMLA 74 69 47

Katika hoja zilizohojiwa kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zilisababishwa na mambo yafuatayo (mapungufu): Kutopatikana fedha kwa wakati (fedha za miradi ya maendeleo). Kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Kutokuwa na tathmini halisi ya fedha inayotakiwa katika gharama za miradi. Suala la kazi na thamani halisi (value for money) kwa shughuli nyingi

zilizofanyika. Udhaifu katika utekelezaji/usimamizi.

Katibu Tawala Mkoa ameweka mikakati ya kuhakikisha hoja hizo hazijitokezi tena na hasa kwa kudhibiti visababishi ambavyo vimeainishwa hapo juu kwa kufanya yafuatayo: Kukamilisha miradi yote viporo (Mkoa na Halmashauri zake zote). Kuomba Serikali ilete fedha kwa wakati (kabla ya kuisha mwaka wa fedha) Kila Halmashauri kutokuanza miradi mipya. Kutoa Elimu kwa wanasiasa wanaozuia wananchi kushiriki katika

utekelezaji/kuchangia miradi ya maendeleo. Kuimarisha miundombinu ya barabara ili kufikisha vifaa katika maeneo ya

miradi. Kuwa na wataalam wa kutosha na wenye weledi katika fani za IT, ukaguzi na

manunuzi.

Kuandaa na kufuatilia miongozo ya fedha inayotolewa na Wizara mama,Wizara ya fedha na uchumi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

Aidha Halmashauri wamejibu hoja zote za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa hoja hizi hazijitokezi tena. Majibu ya hoja hizo yamekabidhiwa kwa Mkaguzi Mkazi wa Rukwa kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji.

27.0. MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

39

Mhe.Naibu Waziri, Elimu imetolewa kupitia vipindi vya redio mara tatu, machapisho (1325), Semina kumi na mbili (12), mikutano ya hadhara thelathini (30) na vilabu vya wapinga rushwa Mashuleni sitini na mbili (62). Aidha, TAKUKURU pia imeendelea kuchunguza makosa ya rushwa hasa katika pembejeo za kilimo ambapo kati ya Julai 2011 hadi Januari 2012 kesi za pembejeo zipatazo (12) zimefunguliwa mahakamani ambapo washitakiwa wapatao thelathini (30) wakiwemo mawakala na watendaji wa Serikali wamefikishwa mahakamani.

28.0. HALI YA MAGEREZA MKOANIMkoa wa Rukwa una magereza matatu ambayo ni Gereza Mollo, Mahabusu Sumbawanga, na Kitete.

(i) Magereza ya Kilimo na Mifugo:Kilimo kina fanyika katika magereza ya Mollo, na Kitete yenye ukubwa wa ekari 37790.5, kati ya hizo ekari 16,365 zinafaa kwa kilimo, ekari 21,425.5 zinafaa kwa malisho. Eneo linalolimwa na magereza yetu yana ukubwa wa hekta 371.2 na jumla ya mifugo inayofugwa ni 350 ikihusisha Ng’ombe, Mbuzi na Nguruwe.

(ii) Magereza ya MahabusuMkoa una gereza moja la Mahabusu la Sumbawanga lenye uwezo wa kuhifadhi wahalifu 108. Kwa sasa linahifadhi wahalifu/wafungwa mpaka 368.

28.0. CHANGAMOTO: Ukosefu wa jengo la Ofisi ya Gereza la Mkoa kwani inayotumika sasa ni nyumba

ya mtumishi na mabanda yaliyoongezwa kwa muda. Ukosefu wa gereza la mahabusu wilaya ya Nkasi.

29.0. USALAMA WA RAIA:Kumekuwepo na ongezeko la makosa na uhalifu kama vile mauaji kwa imani za ushirikina, unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuchoma nyumba moto na uvunjaji kuongezeka.

29.1. MAFANIKIO:Juhudi za Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu tumefanikiwa kupunguza mauaji ya vikongwe wanaotuhumiwa kwa imani za kishirikina, jakapokuwa katika

40

takwimu zetu zinaonesha kuwa mauaji yamezidi, sio kwa vikongwe ni kwa rika mbali mbali hasa umri wa kati ya miaka 40 hadi 50.

29.2. CHANGAMOTO:

a) TATIZO LA ARDHI: wananchi wengi vijijini wanauana kugombea mashamba.b) MIFUGO: Ongezeko la mifugo vijijini imekuwa ni chanzo cha migogoro kati ya

wakulima na wafugaji.c) MATUKIO YA KUCHOMA NA KUBOMOLEANA NYUMBA:

Baada ya mavuno wananchi huchomeana na kuboleana nyumba kwa kisingizio cha imani za kishirikina.

30.0. MASUALA YA UHAMIAJI:Mkoa ulibaini kuwa na wahamiaji haramu elfu kumi na nne mia nne thelathini na tatu (14,433) kutoka Congo DRC, Burundi, Zambia na Rwanda.

30.1. MAFANIKIO:Wahamiaji haramu 255 wamekamatwa kwa mwaka 2011, wengine walipelekwa Mahakamani wengine walifungwa na wengine 172 walipewa hati ya kufukuzwa nchini (PI. NOTICE).

30.2. CHANGAMOTO:Vituo vya mipakani ukiondoa kituo cha Kasesya havina majengo ya Ofisi. Suala la usafiri ni tatizo kwa vituo vyote.

31.0. ULINZI WA MGAMBO:Mkoa huendesha mafunzo ya Mgambo kila mwaka, lengo la mwaka uliopita lilikuwa ni kutoa mafunzo ya Mgambo kwa wanamgambo 600, mafunzo yalianza Julai, 2011. Mafunzo yalitolewa katika vituo vinne (4) ambapo washiriki 596 walianza mafunzo na waliohitimu ni 420 na kufanya Mkoa wetu kuwa na jumla ya wanamgambo 15,155.

32.0. SENSA YA WATU NA MAKAZI, PAMOJA NA KATIBA.Mhe. Naibu Waziri,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya watu na makazi nchi nzima ifikapo tarehe 26/8/2012, ambapo maandalizi ya zoezi hili yapo katika hatua mbali mbali, ikiwemo: Kutenga maeneo madogo madogo (EA) ya

41

kuhesabia watu, mafunzo ngazi ya Taifa (TOT) mafunzo ya ngazi ya Mkoa, mafunzo ngazi ya Tarafa, nyaraka mbali mbali za Sensa pamoja na fedha kwa ajili ya kuendesha zoezi la Sensa. Viongozi wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya na viongozi wa dini wameendelea kuhamasisha shughuli za Sensa na Katiba katika ngazi zote.

32.1. Maeneo ya Kuhesabia.Jumla ya maeneo madogo madogo 2986 kwa mkoa mzima wa Rukwa yametengwa kwa mchanganuo ufuatao: Nkasi 855, Manispaa ya Sumbawanga 210, Halmashauri ya Sumbawanga 800 na Kalambo 621.

Kama sehemu ya maandalizi ya Sensa mkoa uliendesha mafunzo ngazi ya mkoa kuanzia tarehe 17/07/2012 hadi tarehe 28/07/2012, ambapo waliofunzwa ngazi hii ya mkoa wamekwenda kuwafunza wasimamizi na makarani ngazi ya tarafa, mafunzo haya yalihusisha makundi yafuatayo:1. Maafisa Elimu Kata zote 64 za mkoa wa Rukwa2. Maafisa maendeleo ya jamii, Halmashauri zote3. Maafisa Afya toka kila Halmashauri4. Maafisa ardhi toka kila Halmashauri5. Maafisa Kilimo toka kila Halmashauri6. Maafisa Elimu toka kila Halmashauri7. Maafisa toka Wizara ya Mambo ya ndani8. Maafisa toka Ofsi ya Mkuu wa Mkoa9. Wawakilishi wa walemavu.

Baada ya kukamilika mafunzo ngazi ya Mkoa yalifuatia mafunzo mengine ngazi ya Tarafa kuanzia tarehe 09/8/2012 hadi 19/8/2012, ambapo katika ngazi hii makarani na wasimamizi wa Sensa waliweza kufunzwa namna ya kwenda kukusanya taarifa hizi za sensa kwenye maeneo yaliyopangiwa. Makarani/wasimamizi walipatikana kupitia taratibu zote zilizoelekezwa na Serikali, ambapo walimu na watu wengine wasio walimu waliweza kupata nafasi za kuwa makarani wa Sensa.

32.2. VIFAA NA NYARAKA ZINGINE ZA SENSAVifaa na nyaraka zingine za Sensa toka Kituo cha Vifaa kilichopoo Kibaha - Pwani zililetwa mikoani kwetu japo baadhi ya vifaa vililetwa kwa kuchelewa katika hatua ya mafunzo.

42

32.3. FEDHA:Fedha kwa ajili ya mafunzo ngazi zote mbili (2) Mkoa na Wilaya/Tarafa pamoja na mafunzo ya madiwani zililetwa kupitia Hazina ndogo Rukwa na kuzigawa kwenye Halmashauri husika kwa kuzingatia mgawanyo wa bajeti.

32.4. CHANGAMOTO:Pamoja na kuwa Sensa ilifanyika vizuri, lakini kulikuwa na changamoto nyingi zifuatazo; Kuchelewa kupata fedha za kujikimu na mambo mengine siku za mwanzo za

mafunzo katika hatua zote mbili za (Mkoa na Tarafa). Baadhi ya vifaa vya mafunzo kuchelewa kuletwa mkoani ikiwemo Ramani na

bags za kutunzia vifaa na nyaraka zingine. Upungufu wa vyumba vya kulala (ngazi ya Tarafa) na hivyo wengine kulazimika

kulala madarasani. Kutopata maeneo ya kuaminika (usalama wa chakula) kwenye baadhi ya

maeneo/vituo vya mafunzo ngazi ya Tarafa. Upungufu wa madawati kwenye baadhi ya vituo vya kufundishia (ngazi ya

Tarafa). Halmashauri zetu kutokuwa na fedha za kutosha kukabiliana na maagizo toka

HQ Dar es Salaam ya kugharamia/kuwapa fedha za kuendesha zoezi la Sensa jambo ambalo halikuwa jukumu letu.

Uhaba wa magari Mkoani/Wilayani. Baadhi ya vifaa kutoletwa kabisa (Calculators, Sale za kuvaa n.k.)

32.5Namna zilivyotatuliwa baadhi ya changamoto: Washiriki waliamua kununua magodoro/mikeka ya kulalia na hivyo kulazimika

kulala madarasani. Madawati yalibebwa kwa gharama nafuu kutoka maeneo ya karibu kwenda

vituo vya mafunzo.

33.0. HITIMISHOMhe. Naibu Waziri, Napenda kuchukua fursa hii kwa mara nyingine tena kukukaribisha Mkoani kwetu wewe na ujumbe wako nawatakia afya njema na kila la kheri katika kipindi chote cha ziara yako Mkoani Rukwa.

Tupo tayari kutekeleza yote utakayotuagiza na kutuelekeza katika kipindi chote utakachokuwa pamoja nasi.

43

“KARIBU SANA”

44