101
25 APRILI, 2013 1 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 25 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII:- Randama za Makadirio ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

1

BUNGE LA TANZANIA

________________

MAJADILIANO YA BUNGE

________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 25 Aprili, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII:-

Randama za Makadirio ya Wizara ya Maliasili naUtalii kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

2

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni siku nyingineya Alhamisi Maswali kwa Waziri Mkuu tunao waliomba kamatisa bila kumjumuisha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Mkiulizamaswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi.Sasa namwita Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, aanzishemjadala huu.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kunipa nafasi ya kwanza ya kumwulizaMheshimiwa Waziri Mkuu swali.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, maji ni jambo ambalo ni lamsingi mkubwa mno kwa sababu linagusa Watanzania wotekwa maana ya Watanzania karibu milioni 45, na maji katikanchi yetu yanasimamiwa na Sera ya Maji ya mwaka 2002sambamba na Sheria ya Maji ya mwaka 2009; na kwa sababupameonekana kwamba kuna uzito mkubwa wa kutekelezaahadi pamoja na Sera ya Maji; na kwa sababu Wabungewalio wengi wame-complain kwa kiwango kikubwa mnokwamba hapajatolewa fungu la kutosha kuiwezesha Wizaraya Maji kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sera yamwaka 2002.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni kwa nini sasa pengineSerikali isione umuhimu wa kuondoa mjadala wa majiunaoendelea katika Bunge hili kwa sasa ikafikirie upya namnaya kutengeneza fungu maalum ambalo litawezesha majikweli kutumika kama resource ambayo itawasaidiaWatanzania mamilioni ambao wanateseka kwa ajili yakukosa maji? (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu maelezo.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, maji ni sualamuhimu kwa Watanzania lipo wazi na mimi ninakubali kabisa,na ndiyo maana kama Serikali tunafanya juhudi kulinganana uwezo wa kifedha uliopo kuona ni namna gani tunawezakuwa tunakabiliana na tatizo hili la maji. Kwa hiyo, hata ule

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

3

mradi ambao mliona tuliuibua kutokana na msaada wafedha kutoka Benki Dunia ilikuwa ni kwa nia njema ya kujaribukutatua tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, nataka tu nilihakikishie Bunge lakoTukufu kwamba kama Serikali jambo hili tunalijua na ndiyomaana tunajitahidi kufanya kila tunaloweza. Tatizo ni lakibajeti, tatizo zaidi ni uwezo wa kifedha. Tulipowasilisha hapaBajeti ya Kilimo, Chakula na Ushirika wote mlisema Bajetihaitoshi na mimi nina hakika katika Sekta zote zinazokujamtasema Bajeti hazitoshi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tatizo ni udogo wa kiasicha fedha ambacho inabidi tugawane katika kujaribu kukidhimahitaji ya Sekta zote ambazo ni muhimu. Sasa rai yako ninzuri, lakini sina hakika kama pengine huo ndiyo utakuwautaratibu muafaka kwa jambo hili.

Mheshimiwa Spika, mimi ninachoweza kumwomba nakuliomba Bunge, maadam kwa utaratibu wa Kanuni za sasaumetoa fursa nzuri ya siku kama sita kwa Serikali baada yakuwa tumepokea maoni ya Wabunge kutazama ni namnagani tunaweza tukaboresha baadhi ya maeneo kulinganana maoni na ushauri wa Wabunge.

Pengine hilo lingekuwa jambo muafaka zaidi na mimikama Kiongozi wa upande wa Serikali tumeishaanzakulitazama tunajaribu kuona namna gani tunaweza angalautukaokoteza okoteza fedha kutokana na fedha zinazotokanahasa na upande wa OC kwenye matumizi ya kawaidakupunguza katika baadhi ya maeneo ili tuweze kuongezakiasi fulani cha fedha katika eneo hilo la maji.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuunakushukuru kwa majibu yako ambayo ni ya msingi sana.

Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu utakubaliana na mimikwamba kupanga ni kuchagua. Ni kweli Sekta mbalimbalikatika nchi yetu zinahitaji msukumo wa kibajeti, lakini ni ukwelivilevile kwamba jambo la maji na suala la maji ni priority.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

4

Mimi nina imani kabisa hata katika kilimo kamahatutakuwa na utawala maalum wa Sekta ya Maji katikakukisaidia kilimo hatutaweza kuuondoa umaskini wawananchi wetu.

Pamoja na kwamba maji yanatumika zaidi kwamatumizi ya binadamu kama first priority, lakini vilevile majiyanastahili kutumika kama resource muhimu sana katikamasuala ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwawananchi wetu.

Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu umekirikwamba Serikali itaangalia uwezekano wa kuongeza Bajetiya Maji na Bunge lisaidie katika upande huo.

Vilevile tunatambua maji ni finite resources yaani nirasilimali inayokwisha na Sera ya Maji ya mwaka 2002haijabainisha kwa undani matumizi ama factor ya kuvunamaji ya mvua kama sehemu muhimu katika Water ResourceManagement.

Je, Serikali itakiri kwamba katika marejeo hayo yaBajeti ya Wizara ya Maji itaweka vilevile kipaumbele katikasuala la uvunaji wa maji ya mvua kama sehemu ya kukuzarasilimali maji?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu maelezo.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, katika jitihada hiziza Serikali suala la uvunaji wa maji ya mvua ni sehemu yautaratibu au mradi ambao Serikali tunakwenda nao. Mtaonakatika baadhi ya maeneo ambayo tumeibua uchimbaji wamabwawa kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua componentmoja ni matumizi ya binadamu, lakini nyingine ni mifugo, lakininyingine vilevile tumeitumia kwa ajili ya umwagiliaji.

Kwa hiyo, ni eneo moja tunalitambua ni muhimu sanana tunakwenda nalo kwa sababu tunajua ni eneo ambalolazima tulizingatie.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

5

Lakini tutakapokuwa tunatazama hili ambalo ni lasasa tutakachoona kwanza ni kiasi cha fedhatutakachoweza kukipata, halafu tuone ni maeneo yapiambayo pengine yapewe nafasi katika Bajeti hii kulinganana kiasi ambacho tutakuwa tumepata. Kwa sasa kiliokikubwa ni mahitaji ya maji kwa matumizi ya binadamu hasavijijini kwa sababu bado kunahitajika effort kubwa zaidi.(Makofi)

Kwa hiyo, kama ninaweza kupata fedha zakuwezesha kupata maji kwa Watanzania vijijini nitawekaumuhimu mkubwa sana katika eneo hilo kwa sasa kwakutumia vyanzo vyovyote vile tutakavyoweza kuvipata katikangazi ya vijiji. Kwa hiyo, tutaangalia tuone ni kiasi ganitutaweza tukiwa na fedha za kutosha wazo lako siyo bayahata kidogo.

SPIKA: Ahsante sana. Tumechukua dakika kumi. Sasanaomba mnaokuja msije na hotuba ndefu ili kusudi tuwezekupata idadi kubwa. Mheshimiwa Diana Mkumbo Chilolo.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa Watanzaniawamekubali kuondoka kwenye matumizi ya analogue nakujiunga na matumizi ya digital kwa kununua ving’amuzi nabei ya kununulia ving’amuzi ilikuwa ni shilingi 39,000 lakini sasahivi ving’amuzi hivi vimefikia shilingi 79,000 bei ambayo nikubwa sana, Watanzania walio wengi wanashindwakununua ving’amuzi hivyo.

Je, Serikali ipo tayari kufuatilia zoezi hili na kuonanamna ya kuzungumza na Mashirika haya kwa lengo lakuwasaidia Watanzania ili ipatikane bei ambayo kilaMtanzania atamudu kununua ving’amuzi hivi? (Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba tu nipokeeushauri wa Mheshimiwa Mbunge tutampa Waziri waMawasiliano, Sayansi na Teknolojia suala hilo alitazame, nanafikiri atakuwa na maelezo pengine mazuri zaidi wakatiwakiwasilisha Bajeti yake.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

6

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Waziri Mkuu,kwa kuwa baada ya kununua ving’amuzi hivi badoMtanzania anaendelea kununua channel kwa kila mwezi,anayehitaji channel chache anatoa shilingi 9,000 namwingine mwenye kuhitaji channel nyingi kidogo anatoashilingi 18,000 na mwenye kuhitaji channel nyingi zaidi anatoashilingi 36,000; kwa kuwa watanzania wote wanahitaji hizichannel zote.

Je, katika mazungumzo hayo Serikali itakuwa tayarikuangalia channel zitolewe zote kwa Watanzania na itolewebei ambayo kila Mtanzania atanunua channel hizo zote?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosemaeneo hili kidogo linahitaji maelezo ya wataalam zaidi si lakisera sana. Kwa hiyo, ndiyo maana naomba nilipokee tuhuo ushauri Wizara ya Kisekta inayohusika ili iweze kupatanafasi ya kutoa maelezo ambayo ni fasaha zaidi. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Mtutura AbdallahMtutura.

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, dhamira ya kutunga Sheria katikajamii yoyote duniani ni kuondoa kero ambazo jamiiinaizunguka. Katika nchi yetu na kupitia Bunge hili Tukufutulitunga Sheria ya Stakabadhi ya Mazao Ghalani, Sheria hiibadala ya kuondoa kero kwa wakulima hasa wa koroshoimeongeza kero. Hivi karibuni tumeona vuruga nyingizikitokea na watu wengine ambao hawana nia njema katikanchi yetu wamekuwa wakitumia kisingizio hiki cha Sheria yaStakabadhi Ghalani kuleta vurugu.

Je, Serikali haioni sasa hivi ni muda muafaka wakuiangalia sheria hii haraka iwezekanavyo na ikibidiwaisimamishe kwa misimu hii miwili mfululizo ili wakulima wakorosho waweze kunufaika na zao lao la korosho? (Makofi)

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

7

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwambatuliwasilisha mapendekezo ya kutunga Sheria ya StakabadhiGhalani na ilipitishwa na kama mtakumbuka lengo kubwakabisa la Sheria lile ilikuwa ni dhamira njema ya Serikali yakuona namna nzuri ya kumkinga au kumlinda mkulima huyuhasa kutokana na bei ambazo wakati mwingine wanunuziwalipokwenda vijijini wananunua bidhaa mbalimbali kwa beiya chini sana. Kwa hiyo, ilikuwa lengo kwamba tuwe nautaratibu ambao utawezesha wakulima kuwa na kauli ya beizao kwa maana ya kupanga bei na mtu akanunue kutokakatika vituo mahsusi ambavyo vimetengwa.

Sasa tunatambua kwamba inawezekana katikajambo hili kwa sababu linahitaji fedha na wakati mwingineinabidi kukopa benki inaweza kuwa imeleta tatizo katikautekelezaji wa Sheria yenyewe. Lakini bado nataka nisisitizekwamba nia ni nzuri. Mara ya kwanza nilipokwenda Mtwarakukumbana na jambo hili nilikuta korosho kilo moja walikuwawanainunua kutoka kwa wakulima kwa shilingi 50, iliniumasana sana. Ndiyo maana tukafikiria kwamba pengine namnabora ni hiyo. (Makofi)

Sasa kama yapo matatizo Serikali itayaangalia natutashirikiana kujaribu kuona namna gani tunawezatukaondoa kero hiyo na pengine kuiweka katika mazingiraambayo yanaweza kuwa ni muafaka zaidi. Lakini badotujaribu kumlinda mkulima kwa kiasi cha kutosha. (Makofi)

MHE. MTUTURA A. MTURURA: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri.Lakini moja ya kero ambazo zinaletwa na mfumo huo waStakabadhi Ghalani ni kuzaliwa kwa tozo mbalimbali ambazozinazalishwa na Vyama vingi vya Ushirika pamoja na Taasisimbalimbali za Kiserikali.

Je, katika mfumo huo mpya ambao sasa hiviinauangalia Serikali itakuwa tayari kutoa amri ya kuondoatozo hizi ambazo zina lengo la kumnyonya mkulima wakorosho? (Makofi)

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

8

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, analolisemaMheshimiwa Mtutura Abdalla Mtutura, ni kweli na ni jambola lazima tuliangalie. Kwa sababu ukichukua mfano wakorosho tu zipo tozo kumi kutoka Taasisi na vyombombalimbali na ukijumlisha kiwango cha fedha ambazozinatozwa kwa kilo moja ya korosho ni shilingi 220.

Kwa hiyo, mkulima anakosa kiasi kikubwa cha fedhaambazo zingeweza kumrudia yeye na nyingine kusema kwelihazina sababu. Nyingine ni mambo ya Bodi, Bodi wanailipakwa nini kwa sababu Bodi tunaigharamia Serikali, Vyama vyaMsingi, Vyama vya Ushirika, wapo transporters pale. Ni kweliwamejenga taratibu ambazo unaweza ukasema ni zakujinufaisha zaidi kuliko za kumsaidia mkulima. (Makofi)

Kwa hiyo, kimsingi tumelikubali na tumeishaanzakulifanyia kazi na ndiyo maana Waziri wa Kilimo aliahidi Bungelako Tukufu hapa kwamba tutafanya kila litakalowezekanakukaa na wadau na kuondoa baadhi ya maeneo ambayotunaona kwa kweli hayastahili. Siyo korosho tu, mifumo hiiutaikuta kwenye tumbaku, utaikuta kwenye pamba na ndiyomaana unakuta wakati mwingine inaleta zogo kubwa sanakwa sababu ya utaratibu ambao mifumo hiyo imeweka.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Tanzania ni moja kati yanchi kumi ambazo zinazalisha mkaa kwa wingi dunianiambapo asilimia 3 ya mkaa wote unaozalishwa dunianiunatoka Tanzania kiasi cha kwamba takriban ya tani milionimoja tunazalisha kwa mwaka ni sawa na tani 2650 kwa sikuambazo tunazalisha Tanzania.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, tani hizi ambazo tunazalishaTanzania zinasaidia katika uchumi wa Taifa takriban dollarmilioni 650.

SPIKA: Naomba swali liwe fupi.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

9

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Je, Serikali yako inamustakabali gani wa kisheria na kisera kuwatambua nakuwaendeleza wazalishaji hawa ambao ni wananchi wakawaida wa vijijini na wale ambao kwa kweli kipato chao niduni?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijaribukueleza suala hili ambalo Mheshimiwa Rajab ameliuzia.Mwanzoni nilipata tabu maana sikujua kama ni mkaa wamawe au ni mkaa unaotokana na kuni. Kumbe ni mkaaunaotokana na miti, misitu na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, analolisema ni kweli kwambaTanzania ni moja ya nchi ambazo tunatumia mkaaunaotokana na ukataji misitu kwa kiwango kikubwa sana.Tunaweza tukadhani ni neema lakini kwa kweli nichangamoto kwa upande wa Taifa letu. (Makofi)

Ni changamoto kwa sababu ukataji ule unachangiasana katika uharibifu wa misitu. Jambo ambalo lina atharikubwa sana kama Taifa, lakini kama ulimwengu vilevile. Sasawakati ninakubaliana na wewe kwamba hiyo ndiyo hali ilivyosasa si jambo ambalo ningependa kama Serikali tukatakatulihimize na kuliendeleza la hasha. Hatutakuwa tumefanyauamuzi wa busara.

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri la kukubaliana hapakama Serikali na kwa Watanzania tuone ni mambo ganimbadala ambayo mwananchi huyu anaweza akafanya nayakamwezesha kupata kipato chake.

Lakini wakati huo huo tujibu ni nini mbadala sasaambacho mwananchi atatumia kama nishati hasa Mijini.Ndiyo maana tunashukuru kwamba Serikali kwa jitihada zakesasa tuna fursa kubwa ya gesi. Kwa hiyo, imani yangu nikwamba tukijipanga vizuri, gesi hii itatusaidia sana katikamatumizi ya nyumbani na hivyo tutapunguza kwa kiasikikubwa matumizi ya ukataji wa misitu kwa ajili ya nishatiambayo mimi nadhani haitupeleki mahali pazuri sana.(Makofi)

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

10

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: MheshimiwaSpika, ahsante sana. Namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuukwa majibu yake mazuri.

Mheshimiwa Spika, wakati Serikali inajipanga natunasubiri manufaa ya hii gesi familia takribani milioni mojanchini zinategemea mauzo haya au uzalishaji huu wa mkaa.Je, Serikali ina tamko gani kwa sasa hivi?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukapike na hukonyumbani.

WAZIRI MKUU: Naona Mheshimiwa bado anatakatuseme tunatoa baraka kwa hayo, hapana. Mimi nafikiritusitoe baraka za namna yoyote ile tutaendelea kujaribukutumia sheria tulizonazo sasa na Kanuni tulizonazo sasakwamba ukataji wa misitu kwa ajili hiyo nao udhibitiwe,usimamiwe usiwe holela maana tukiliachia hilo likawa holelakama ninavyosema ni tishio kubwa sana kwa Taifa letumnaweza unatishia nchi yenu kuwa jangwa kama vilehamkuwa mnajua tatizo lenyewe.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni baadhi yaWabunge wamegeuka kuwa kama wasemaji wa Serikaliwanapokuwa kwenye Shughuli za Bunge hapa Bungeni nahivyo kuweza kulifanya Bunge letu kuweza kupotezamwelekeo katika suala zima la kuishauri na kuisimamia Serikaliipasavyo.

Je, Serikali yako iko tayari kuweza kutunga sheriaambayo itazuia Wabunge kutokuwa wasemaji kamaambavyo imejijengea kama ni utamaduni wetu?

SPIKA: Utamaduni gani? Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

11

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, namwomba arudiemaana swali lake naona sijamwelewa hata kidogo.

SPIKA: Halieleweki

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru Serikali iko tayari kuweza kutunga sheria yakuzuia baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ambaowamegeuka kuwa wasemaji, washauri au wasemaji waSerikali tunapokuwa kwenye vikao vyetu vya Bunge nahatimaye sasa Bunge letu linapoteza mwelekeo katika sualazima la kuishauri Serikali na kuisimamia Serikali ipasavyo?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu kama ni kweli.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, sina hakika kamakweli unahitaji sheria kwa jambo hili. Kwa sababu kamawewe unajifanya kuwa ni msemaji wa Serikali unatakanikutungie sheria ya kukuzuia usifanye hivyo, mimi nafikirihapana. Nadhani rai nzuri ingekuwa kutoa wito kwaWabunge wote kwamba katika kuishauri Serikali tuzingatieKanuni zetu za Bunge maana Kanuni zile zimewekwa kwaajili ya kutusaidia sisi. (Makofi)

Kwa hiyo, kwamba utahitaji sheria mahsusi kwa jambohili, mimi sidhani. Lakini ni kweli kabisa kwamba wakatimwingine na mimi napata taabu kidogo na hasayanapokuwa mambo yametokea hapa Bungeni au penginekwenye Kamati, lakini wakati mwingine hata halijafikia tamatilakini utamwona Bwana Machali yuko kwenye majukwaahuko analisemea na kadhalika. Sasa wakati mwingine nalosi zuri sana. Ndiyo maana nilikuwa nafikiri kwamba kubwa nikurudi kwenye Kanuni tukizifuata zimewekwa vizuri sanazitatusaidia sana.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu,wewe ndio Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni na kwanafasi yako una mamlaka na wajibu wa kuhakikisha Serikaliinatekeleza Maazimio ya Bunge.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

12

Mwezi Novemba, 2011 Bunge lilipitisha Maazimiobaada ya kufanya uchunguzi juu ya matumizi mabaya yafedha kwenye Wizara ya Nishati na Madini, kwa taarifaambayo iliitwa maarufu kama Sakata la Jairo.

Toka wakati ule mpaka hivi leo umepita mwakammoja na nusu Serikali haijawasilisha ndani ya Bunge hilitaarifa ya utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na taarifaile ya Kamati Teule na wala waliotakiwa kuchukuliwa hatuaza kisheria hawajachukuliwa hatua za kisheria mpaka hivi leo.Ni kwa nini Serikali yako imekuwa ikidharau kutekelezaMaazimio ya Bunge kwa wakati?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli hiyo nisehemu ya jukumu langu na jitihada zinafanyika kilatunapopata ushauri wa Wabunge tunayafanyia kazihatuyapuuzi hata siku moja. Kwa hiyo, hata hili pengineungeweza tu kusema kwamba Bwana Mheshimiwa WaziriMkuu lini utatuletea taarifa ya utekelezaji juu ya jambo hilina tutafanya tu hivyo kwa sababu si kwamba hakunakilichofanyika.

Tumeshachukua hatua kadhaa ambazo ndani yaSerikali pengine kilichokosekana sasa ni kurejesha mrejeshonini mpaka sasa tumejaribu kufanya na kipi badohatujakamilisha. Hilo nafikiri halina tatizo. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nilini utaleta Bungeni taarifa ya utekelezaji wa hayo Maazimioyote?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, wakati wowotekuanzia sasa. (Makofi/Kicheko)

MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa WaziriMkuu, Serikali ilikuwa na nia njema ya kudhibiti matumizi yakekwa kufanya manunuzi kwa kupitia zabuni.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

13

Lakini uhalisia uliopo katika maeneo mengi ni kwambabidhaa zinazonunuliwa kwa wazabuni zinakuwa za bei yajuu kuliko bei ya kawaida na hata kama ni majengoyanayojengwa kwa zabuni yanakuwa na bei ya juu kulikobei ya kawaida na wakati mwingine yanakuwa na bei yajuu wakati kiwango ni cha chini kuliko vya kawaida.

Je, Serikali inatoa kauli gani na itakuwa tayarikurekebisha kuleta Muswada ili kurekebisha kasoro ambazozimejitokeza?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, lengo la sheria ileilikuwa ni kuimarisha dhana ya uwazi katika usimamizi washughuli ya manunuzi, ilikuwa hasa ndio dhamira yake na ndiomaana katika sheria ile utaona uko mfumo umewekwa wakutangaza baadaye mnawasaili mnapata mtu ambayemnafikiri ana sifa stahiki huyo ndiye mnayempa kazi yakufanya.

Kama mtakavyokumbuka ndani ya sheria i leimewekwa bayana kwamba yule atakayekuwa ametoa beiya chini kutegemea na aina ya zabuni ilivyo basi huyo ndiyetutakayempa nafasi ya kwanza ama yule atakayetupa beiambayo ni ya juu zaidi kutegemea na aina ya zabuni huyondiye tutakayempa nafasi ya kwanza.

Kwa hiyo, dhamira yake ilikuwa ni nzuri sana. Tatizolililopo hapa sasa ni uaminifu wa wasimamizi na watendajiambao ndio wanaotumia ile sheria vibaya na hili jambo nichangamoto kubwa sana. Kwa hivyo kama anavyosemaMheshimiwa Mwigulu nadhani tukubali kwamba penginekuna haja ya kuitazama sheria ile tuone kama kwa namnatulivyokuwa tumeitunga hapa Bungeni kwamba iliweza kwelikuziba mianya yote ambayo inampa fursa mtu mwinginekuitumia vibaya.

Lakini si hiyo tu, liko tatizo vilevile la kucheleweshwasana na mlolongo mrefu sana kabla hamjafikia hatua ile yamwisho. Pengine nalo hili itabidi tuliangalie tuone namnagani tutashughulika na jambo hili. Upande wa Serikali

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

14

tulikwishaanza tayari timu ndogo ambayo inalifanyia kazinadhani tutakapokuwa tumekamilisha tutawasilisha baadhiya mawazo ambayo tunajaribu kuyapata ili Bunge naloliweze kutusaidia kutupa mchango zaidi. (Makofi)

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Waziri Mkuu tatizo la msongamano katika mijimikuu hasa Dar es Salaam imekuwa ni kero na ni gharamakubwa kwa maisha

SPIKA: Msongamano wa nini?

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Msongamano wamagari katika barabara ni tatizo kubwa na sasalimeongezeka linasababisha ajali nyingi sana kwa askari wausalama barabarani. Ili kuondoa hili ni lini Serikali itanunuahelikopta ili kuondoa kero ya misafara ya viongozi ambayoinakwamisha magari kila wakati?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, nina hakika kabisasiku tukinunua helikopta kwa ajili hiyo Bunge lote mtatugeukahapa. Wote mtageuka. (Makofi)

Naelewa analolisema Mheshimiwa Mangungu,sitakubaliana naye sana kwamba suluhu ni sisi akina Pindakununua mahelikopta ya mabilioni tuanze kuruka kwa sababusisi labda ndio tunasababisha misafara na kadhalika nakadhalika hapana.

Mimi bahati nzuri napata nafasi ya kutembea nchinyingi, viongozi wote wanatumia barabara hizi hizi na ni sualala utaratibu tu wa namna nzuri ya kuwezesha viongozi kupitana upande mwingine kuhakikisha kwamba askari wetu wakosalama.

Yako mambo mawili ambayo nayaona. Moja nimfumo tuliojiwekea wa namna ya kuwezesha viongozi kupitawakati ule ule kuwezesha magari mengine kupita. Ukiendahata Kenya kiongozi unaingia kwenye msafara lakini magarimengine yote yanaruhusiwa kuendelea na safari zake.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

15

Mnapishana kubwa tu ni wewe ambaye unaongozamsafara wa kiongozi ili msije mka-create msongamanoambao siyo wa lazima sana. Kwa sababu kinachotokeawakati mwingine mnapokuwa mmesimamisha magarilinapomalizika gari moja unapoachia magari menginekuanza kuingia wakati mwingine ndio kunatokea mtafarukuambao sio wa lazima sana.

Sasa tunaendelea kujaribu kuzungumza na wenzetuwa Polisi pamoja na vyombo vya usalama kuona namna nzurizaidi ya kuweza kuwapitisha viongozi hawa bila kulazimishapengine msongamano mkubwa ambao baadaye unaletatatizo katika kuwapisha watu wengine kuweza kupita salama.Kwa hiyo, ni changamoto lakini si kubwa tunaendeleakuitafutia ufumbuzi. (Makofi)

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibumazuri. Lakini gharama ya ununuzi wa helikopta ukiangaliatathmini iliyofanyika na wataalam wa usafirishaji kila siku siochini ya shilingi bilioni 4 zinapotea kwa wananchi na watumaijiwengine wa barabara.

Sasa ili kuondoa tatizo inaweza ikawa Bunge litaingiliakati lakini ningependa Serikali yako sasa ichukue wajibu najukumu la kufanya tathmini ipi ni gharama kubwa aidha kwakutumia vyombo hivyo vya usafiri lakini pia kwa kipindi champito itangazwe sasa ni misafara ipi ambayo inaruhusiwakuzuia magari maana yake sasa hivi misafara imekuwa mingi.Waziri Mkuu yuko Dodoma, Rais yuko nje ya nchi badounaona ving’ora vinaongezeka mitaani.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, MheshimiwaMangungu anatutakia mema lakini bado nafikiri wachatulitazame jambo hili kwa upana wake maana inawezekanatatizo pengine ni msongamano kwa sababu barabara zetuni nyembamba zinahitaji kuboreshwa zaidi.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

16

Ule mradi ambao tunaozungumza wa Mabasiyaendayo kwa kasi, siyo kwamba tunataka tu watu wengiwaweze kusafirishwa Dar es Salaam, lakini vilevile kuongezaupana wa barabara zetu ili kuruhusu magari mengi zaidikupita kwa namna ambayo ni salama zaidi. Kwa hiyo,tunachanganya mambo mengi katika kujaribu kutafutaufumbuzi wa jambo hili kwa pamoja.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge muda umekwisha.Tukushukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kujibu maswalina maswali kidogo yameenda kisekta zaidi kuliko yale yakisera. Kwa hiyo, tujaribu kuendelea kuuliza maswali vizuri.Tunaendelea, Katibu!

MASWALI YA KAWAIDA

Na. 105

Wizara ya Ardhi, Elimu na AfyaKupelekwa TAMISEMI

MHE. MOSSES J. MACHALI aliuliza:-

(a) Je, ni sababu gani inayofanya Serikali kuwekausimamizi wa baadhi ya mambo yanayohusu Ardhi, Elimu naAfya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) na hivyokuiongezea mzigo mkubwa?

(b) Je, ni lini Serikali itaondoa masuala ya Ardhi, Elimu naAfya kutoka TAMISEMI ili kupunguza urasimu katika utoajihuduma?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Moses Joseph Machali, Mbunge wa KasuluMjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

17

(a) Mheshimiwa Spika, chimbuko la upelekaji waMadaraka kwa Umma ni Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara ya 8(1), 145 na 146.

Aidha, Sheria Na. 7 ya mwaka 1982 (Mamlaka zaWilaya) na Sheria Na. 8 ya mwaka 1982 (Mamlaka za Miji)ambazo zinatambua uwepo wa Mamlaka za Serikali zaUmma kama vyombo huru vya kuwahudumia wananchi.Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma unazingatia misingi mikuuminne ambayo ni kupeleka madaraka ya kisiasa, rasilimalifedha, majukumu, na rasilimali watu kwenda kwenyeMamlaka za Serikali za Mitaa ambako ndiko utekelezaji waSera na Mipango ya Kitaifa unafanyika. Lengo kuu nikuimarisha na kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi.

Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kupeleka masuala yaArdhi, Elimu na Afya katika Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMIunatokana na Katiba, Sheria na Sera ya Upelekaji waMadaraka kwa umma ambayo inazipa Mamlaka za Serikaliza Mitaa madaraka na mamlaka ya kujiamulia mambo yaowenyewe kwa kujiletea maendeleo kwa kuzingatia matatizoyaliyopo. Serikali Kuu imebaki na jukumu la kutunga nakusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Miongozo mbalimbalina kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto zilizopo,utekelezaji wa Sera hii umekuwa na manufaa makubwayakiwemo kupungua kwa tofauti za kimaendeleo kati yaMkoa na Mkoa na Halmashauri moja na nyingine.

Hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI itaendeleakuratibu utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwaumma ambayo ni sera mtambuka inayohusisha sekta zotezikiwepo Ardhi, Elimu na Afya kwa kuziimarisha Sekretarieti zaMikoa ili ziweze kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaakatika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

18

(b) Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo niliyoyatajakatika sehemu (a) hapo juu, ni dhahiri kwamba uendeshajiwa masuala ya Ardhi, Elimu na Afya utaendelea kutekelezwana Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Serikali Kuu itaendelea kuzijengea uwezo Mamlakaza Serikali za Mitaa na kufuatilia kuona kwamba malengoya kuhamishia utekelezaji wa masuala yanayohusiana nautoaji huduma kwa wananchi yanafanikiwa. (Makofi)

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa fursa nimwuliza maswali madogomawili madogo ya nyongeza.

Kutokana na majibu mbalimbali ambayo yamekuwayanatolewa na Mawaziri wa Serikali yetu imedhihirisha wazikwamba sehemu kubwa huwa wanatupia mzigo TAMISEMIkatika suala zima la kuweza kufanya maamuzi na hivyokudhihirisha kwamba kauli ambayo imetolewa naMheshimiwa Naibu Waziri ya kwamba Serikali kuu imebakina jukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa Sera,Sheria na Miongozo hiki kitu hakipo.

Je, Wizara yako chini ya Mheshimiwa Waziri Mkuuhaioni kwamba ipo haja ya kuhakikisha kwamba sasainawapatia mamlaka Mawaziri wa Wizara nyingine kama zaArdhi, Elimu na nyinginezo ili kuhakikisha kwamba zinakuwana uwezo au mamlaka ya kutosha tofauti na ilivyo hivi sasa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, inaeleweka bayanakwamba sheria hizo umezitaja lakini sheria sio Msahafu kamailivyo Biblia na kadhalika. Wizara yako inaweza ikawa tayarikufanya mabadiliko ili kuhakikisha kwamba sasa Wizara zotezinaweza kuonyesha uwezo na hivyo kuwa na tija kwawananchi katika suala zima la kushughulikia mambombalimbali yanazihusu Wizara hizo ambazo ziko chini yaTAMISEMI?

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

19

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, hili ambalo Mheshimiwa Moses Machali analizungumziahapa sio mara yake ya kwanza analizungumza. Amewahikuja mpaka ofisini, nimekuja na hii sheria hapa nanilimwonyesha Katiba ya Nchi inasema nini. Kwa kweliakasema kwamba siyo Msahafu. Labda tuwe concretetueleze hapa kwamba nini kinachosemwa hapa.

Tulipoanzisha shule za sekondari katika Kata kwamaana hii anazungumza Mheshimiwa Machali ingemaanishamambo yafuatayo kwamba Mkuu wa Shule aliyekuwaMuleba au aliyekuwa Kasulu atoke kutoka Kasulu aende Dares Salaam kwenye Wizara ya Elimu kwenda kutafuta chakulacha watoto ndicho kinachosemwa hapa.

Mimi nataka tuelewane vizuri ili tuweze kufahamiana.I want to be concret. Hapa tunazungumza habari D by D(Decentralization by Devolution) na dunia nzima inasemapeleka madaraka, mamlaka, peleka resources zote kwawananchi kule waliko, leo unakuja unasema hivi kuanzia leotutarudisha tena yale madaraka kule tuliko.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu nataka niliambie Bunge lako Tukufu hapa katika Afrikanchi pekee ambayo inasifiwa kwa kuhakikisha kwambainapeleka madaraka na inapeleka rasilimali kwa wananchi,Tanzania ni ya kwanza. Wamekuja South Africa, Kenya,Rwanda na Burundi wamekuja kujifunza hapa. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge hapa hii kelele yotetunayopiga hapa ya kusema peleka mamlaka na madarakakule Siha, peleka kule Mtwara, Magu hiyo kelele kamatukisema leo tunarudi tena kulekule tulikotoka, maamuziyafanyikie huko!

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

20

Mheshimiwa Spika, tunachosema, Halmashaurifunction yake ya kwanza ni kupitisha bajeti, function yake yapili ni kupitisha Sheria ndogo, function yake ya tatu ni kutoahuduma muhimu kwa jamii. Hivi tulivyo sasa hivi na hayamatatizo yanayozungumzwa hapa, tukisema turudi tenanyuma, utaleta urasimu mkubwa hapa, tutawa-confusewananchi hapa.

Mheshimiwa Spika, it is my opinion kwa niaba ya Ofisiya Waziri Mkuu kwamba kama kuna matatizo nachangamoto zinazojitokeza hapa, tuzilete tuzizungumzehapa. Lakini tusikubali asilani kwamba tunarudi tena nyumakule tulikotoka, madaraka yanarudi kule. Wizara zibakie namambo ya quality control, mambo ya sera na mambomengine kama tulivyoeleza hapa.

Mheshimiwa Spika, namwalika Mheshimiwa MosesMachali na wale wengine wote wanaofikiri kwambatunaweza tukaendelea, tuzungumze zaidi kuhusu jambo hili.(Makofi)

SPIKA: Haya. Nitamwita mtu mmoja tu, MheshimiwaSoni.

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.Nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Wazirialiyoyatoa. Nilikuwa nauliza: Je, kama masuala yote hayoya ardhi, afya na elimu yako TAMISEMI, kwanini sasa hakunaushirikiano na maelewano katika Idara zote hizo wakatiwanapopanga na kutekeleza miradi mbalimbali? Inakuwakila moja inajitegemea. Lini watakuwa na coordination ilimambo yaende vizuri?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, naomba ujibu kwa kifupitu. Maana muda hautoshi!

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI):Mheshimiwa Spika, nimfahamishe tu Mheshimiwa Mbunge naWaheshimiwa Mawaziri wote walioko hapa wanafahamu, kilawakati tunapokuwa na jambo lolote linalohusu mambo ya

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

21

kisera tunakutana, kama linahusu mambo ya afyatunakutana na Waziri wa Afya tunakaa naye, anakuja natimu yake na sisi tunakuja na yetu ya TAMISEMI, tunazungumzawote kwa pamoja kuhusu mambo ambayo tunafikiri kwapamoja tunataka.

Mheshimiwa Spika, huyu Waziri aliyeko sasa hivianayezungumzia habari ya maji, tunakwenda Ofisini kwakena yeye anakuja Ofisi kwetu tunakuwa na vikao vya watuwa maji na sisi tunakuwa na vikao vya kwetu vya TAMISEMI.Wote tunashirikiana vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, kama kuna upungufu mtuambietu kuna upungufu, lakini to the best of my knowledge, wakatiwote tumekaa katika vikao, tumeshirikiana nao na ndiyomaana hata wakati wa kujibu maswali hapa wakatimwingine tunashirikiana. Kama ni barabara tunajibu wotekwa pamoja.

SPIKA: Tumetumia dakika kumi kwa swali moja. Kwahiyo, tunaendelea na Wizara ya Maji. Mheshimiwa YusuphNassir ndiye atauliza swali hilo.

Na. 106

Kero ya Maji Korogwe Mjini

MHE. YUSUPH A. NASSIR aliuliza:-

Kumekuwepo na kero ya muda mrefu ya majiKorogwe Mjini ambapo Serikali ilitoa taarifa ya miradi ya majiambayo mpaka sasa haitekelezeki:-

(a) Je, Serikali itaondoa lini kero hii ya maji kwawananchi wa Korogwe Mjini?

(b) Je, Serikali itatenga fedha kiasi gani kwa ajiliya kutatua kero hii; kwani visima vya Benki ya Duniavimeshindwa kukidhi matarajio ya haraka ya wananchi wa

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

22

Vitongoji vya Mahenge, Kwakombo, Mgambo, Kitifu naIwengera?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yusuph AbdallahNassir, Mbunge wa Korogwe Mjini, lenye sehemu (a) na (b)kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ili kuondoa tatizo la maji MjiniKorogwe, Serikali itaendelea kutenga fedha mwaka hadimwaka kwa ajili ya kazi za kubadili mabomba chakavu,kuongeza chanzo cha maji kwa kuchukua maji ya kutoshakutoka Mto Mashindei pamoja na kujenga chujio la kuchujana kutibu maji.

Aidha, Wizara ya Maji katika mwaka 2013/2014 (chiniya fungu 49), imeuweka Mji wa Korogwe katika orodha yaMiji ambayo ujenzi wa miradi ya maji inayoendeleautaharakishwa ili kuwapatia wakazi wake ufumbuzi wadharura wa matatizo ya maji. Wastani wa Shilingi milioni 200zimetengwa kwa ajili hiyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeendelea kutekelezamiradi ya vijiji 10 katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Miradihiyo inatekelezwa katika vijiji viwili vya Kwamndolwa naKwameta ambayo itakamilika mwezi Juni, 2013.

Aidha, zabuni za kuwapata Wakandarasi wa ujenzikatika vijiji vitatu vya Kwakombo, Kwasemagube na Kwamsisiambavyo ni vijiji vya nyongeza zimetangazwa. Vijiji sita vyaMgambo, Mgombezi, Kitifu, Mahenge, Msambiazi naLwengera Relini vitatekelezwa katika mwaka wa fedha 2013/2014. Kiasi cha Shilingi milioni 343.65 kimetengwa ili kutekelezamiradi ya maji katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

SPIKA: Ahsante. Swali la nyongeza Mheshimiwa Nassir!

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

23

MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwa kuwa suala la maji au tatizo la majiKorogwe Mjini lilikuwa pia ni sehemu ya ahadi ya MheshimiwaRais, lakini kadhalika makuzi ya Mji wa Korogwe ni miongonimwa Miji inayokua kwa kasi sana; na kwa kuwa pia siyo marakadhaa tumekuwa tukizungumza hapa Bungeni kuhusianana kadhia ya maji; na kwa kuwa katika michango ya maji natukiendelea kuchangia bajeti, vyanzo mbalimbali vyamapato vimeshauriwa na Waheshimiwa Wabunge; na kwakuwa kiasi cha pesa kilichotengwa kwa mujibu wa majibuya Mheshimiwa Waziri wa Maji kinaonekana ni kidogo, ni sawana kumpa pipi mtu mwenye njaa ya miaka mitatu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza kabisa tatizola maji Korogwe Mjini? (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji,majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikweli lipo tatizo kubwa la maji katika Mji wa Korogwe, naminilipata nafasi ya kutembelea pale. Lakini vilevile tutambuekwamba tunayo bajeti finyu ambayo imepelekea tupatefedha kidogo katika Mji huu wa Korogwe. Niseme tu kwamba,tunayo Miji mingi, Miji midogo na Miji Mikuu ya Wilaya ambayoinazidi zaidi ya 132.

Mheshimiwa Spika, kwa kuanzia, tumeupakipaumbele Mji wa Korogwe hata kwa kiwango kidogotuanze kutekeleza hii miradi. Lakini hapo tutakapopata fedhaza kutosha, Mji wa Korogwe utapewa kipaumbele ili tuwezekujenga miradi mikubwa kwa kutumia vyanzo vya majiambavyo nimeviainisha.

SPIKA: Tunaendelea, kwa sababu suala lenyewe lipokwenye mpango. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kuulizamaswali mengi. Mheshimiwa Esther Matiko swali linalofuata.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

24

Na. 107

Mradi wa Uchimbaji Bwawa Kata ya Nyahongo

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-

Wananchi wa Rorya wamekuwa na mahitajimakubwa ya bwawa na Serikali ilisharidhia kuchimba bwawakatika Kata ya Nyahongo na kwamba kati ya mwaka 2006 -2009 Serikali imekuwa ikiweka suala hili kwenye bajeti yakekabla ya kuliacha miaka ya hivi karibuni bila utekelezajiwowote:-

Je, ni sababu gani zilipelekea kuondolewa kwa sualahili kwenye bajeti wakati hakuna utekelezaji wowoteuliofanyika?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Esther Nicholaus Matiko, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Ujenziwa Mabwawa katika mwaka wa fedha wa 2007/2008 iliwekabwawa la Kanyisambo katika bajeti kwa ajili ya utekelezajiwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Bwawa hilolilipangwa kujengwa katika Kijiji cha Manyanyi kilichopo Kataya Nyahongo. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifuimekamilika mwaka 2010. Ujenzi wa bwawa la Kanyisambohaujaondolewa, bali haukufanyika kutokana na ufinyu wabajeti.

Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kujengamabwawa nchini, hususan katika Halmashauri ya Wilaya yaRorya kwa kipindi cha mwaka 2002/2003 hadi mwaka 2010/2011, Serikali imejenga na kukamilisha mabwawa saba yaChereche, Irienyi 1, Irenyi 2, Ochuna, Nyanjagi, Barack Parishna Nyambori. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

25

ujenzi wa mabwawa nchini kote likiwemo bwawa laKanyisambo kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, katika hatua za muda mfupi zakupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa Kata ya Nyahongo,Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa kushirikiana na Shirikala Maendeleo la Japan (JICA), imetekeleza miradi minne yavisima. Miradi hiyo imefungwa pampu za mkono katika Kijijicha Nyamkonge.

SPIKA: Ahsante. Swali la nyongeza Mheshimiwa EstherMatiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Licha ya kwamba Mkoa wa Maratumezungukwa na vyanzo vingi vya maji, lakini wananchi waMkoa ule hasa akinamama tumeendelea kuteseka kwakukosa maji.

Katika majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri anaainishakwamba upembuzi yakinifu ulikamilika mwaka 2010 naanakwenda mbali kwa kusema kwamba watatekelezakuchimba hilo bwawa la Kanyisambo wakishapata hela.Lakini mbaya zaidi anaainisha visima vinne ambavyovimechimbwa kwenye Kijiji cha Nyamkonge bila kuzingatiaumbali kijiografia kwa wakazi wa Kata ya Nyahongo.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni lini sasa Serikaliitaipa kipaumbele Kata hii ya Nyahongo na kuchimba hilobwawa la Kanyisambo ili kupunguza adha ya maji kwawananchi wa hii Kata?

La pili, wananchi wa Tarime wamekuwa wakiendeleakupata adha kubwa ya maji. Kwa mfano, Tarafa ya Inchuguyenye Kata ya Susuni, Mwema, Sirari na Nyamaraga, tangutumepata uhuru hatujawahi kuchimbiwa hata bwawa moja.Napenda kujua ni lini Serikali itawapa kipaumbele wananchiwa Tarime kama ilivyo kwingine Tanzania ili na sisi tuwezekupata hilo bwawa?

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

26

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naombaMheshimiwa Mbunge akubaliane na mimi kwamba Serikaliimefanya mambo makubwa sana katika Mkoa wa Mara hasakatika Mikoa ya Ziwa Victoria kwa kuweka miradi mikubwa.Sasa hivi tuna miradi mikubwa ambayo inajengwa paleMusoma kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Musoma maji.

Mheshimiwa Spika, tunao mradi mkubwautakaojengwa kutoka Misungwi kwenda Magu na Bariadikwa kutumia chanzo cha Ziwa Victoria; tunao mradi mkubwawa kupanua mtandao wa maji Ziwa Victoria kwenda katikamaeneo ya Vijijini milimani kama Ilemela; na tunao mradimkubwa wa kutoa majitaka katika Mji wa Bukoba. Kwa hiyo,Serikali imefanya mambo makubwa. Lakini tatizo hili ni kubwa,nimwahidi kwamba tutaendelea kuweka vipaumbelekulingana na fedha zinazopatikana.

Mheshimiwa Spika, lakini katika Vijiji kumi ambavyotumekuwa tukivitekeleza, mapendekezo yalianzia kwenyeHalmashauri. Kwa hiyo, pale itakapoonekana Kijiji hiki ndiyomuhimu zaidi, basi wao walete mapendekezo, Serikaliitakuwa tayari kutoa ushirikiano.

SPIKA: Ahsante. Tunakwenda Wizara ya Elimu naMaendeleo ya Ufundi. Mheshimiwa Kaika Telele atauliza swalihilo.

Na. 108

Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi (VETA) Nchini

MHE. KAIKA S. TELELE aliuliza:-

Serikali imekuwa ikiahidi mara nyingi hapa Bungenikuwa itajenga Vyuo vya Ufundi (VETA) katika Wilaya zotenchini:-

(a) Je, kwanini mradi huo umekuwa ukisuasuakwa muda mrefu?

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

27

(b) Je, Wilaya ya Ngorongoro ipo katika awamuya ngapi ya utekelezaji wa mradi huo?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Kaika Saning’o Telele, Mbunge wa Ngorongoro,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imeahidikujenga Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) katika WIlaya zotenchini kwa vile ni ahadi iliyotolewa kwenye Ilani ya Chamacha Mapinduzi ya mwaka 2005 na 2010. Katika kutekelezaazma hii, Serikali imedhamiria kujenga Vyuo vipya au kutumiaVyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa ujenzi wa Chuo chaWilaya ya Makete umeshakimilika na kinatarajia kuanzamasomo mwezi Mei, 2013. Aidha, Serikali imeanza maandaliziya awali ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya yaLudewa, Namtumbo, Chunya, Kilindi na Ukerewe na katikamwaka wa fedha 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, sambamba na jitihada hizo,Serikali itaviwezesha Vyuo 55 vya Maendeleo ya Wananchivilivyoko katika Wilaya mbalimbali nchini ili viweze kutoamafunzo ya ufundi stadi. Kwa mwaka 2012/2013 Vyuo 25 vyaMaendeleo ya Wananchi tayari vimejengewa uwezo navimeshaanza kutoa mafunzo ya ufundi stadi ambapo kilakimoja kimedahili wanafunzi 50.

(b) Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ngorongoro nikati ya Wilaya 50 ambazo bado hazijafanyiwa utafiti wakubaini stadi. Zoezi hil i l itafanyka mara fedhazitakapopatikana. Nachukua fursa hii kumshauri MheshimiwaMbunge na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kutumiaVyuo vya VETA vya Oljoro, Njiro na Chuo cha St. Joseph (VTC)kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro kupata mafunzo ya

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

28

Ufundi Stadi wakati jitihada za Serikali za kujenga Chuo chaVETA katika Wilaya ya Ngorongoro zikiendelea.

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Telele, swali la nyongeza.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, ahsantesana.

(a) Kwa kuwa azma hii ya Serikali ya awamu yanne ya kujenga Vyuo vya VETA katika kila Wilaya hapa nchini,ni azma njema sana. Lakini basi ni kwa kiasi gani nia hii njemaimezingatiwa katika bajeti ya mwaka huu?

(c) Mheshimiwa Spika, Makao Makuu ya Wilayaya Ngorongoro kutoka Arusha ni zaidi ya kilometa 400 na inamazingira magumu kwa maana ya kwamba barabarahakuna. Sasa Serikali kutuelekeza tutumie Vyuo vya VETA vyaOljoro na Njiro ni kazi ambayo ni ngumu sana. Sasa Serikaliinaweza kutuonea huruma na kutuingiza katika awamu yakwanza ya kufikiriwa kupewa Chuo Kimoja angalau katikaJimbo la Ngorongoro?

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimuna Mafunzo ya Ufundi, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa alitaka kujua tu bajeti yamwaka huu wa fedha 2013 kwamba tumetenga kiasi ganikwa ajili ya Vyuo vya Ufundi vya Wilaya? Kwenye swali langula msingi nimesema kwamba tunavyo Vyuo vinne ambavyotayari maandalizi yake yanaendelea kutafuta hati miliki kwaajili ya Halmashauri kukabidhi VETA ambayo ni Wilaya zaKilindi, Ukerewe, Namtumbo na Chunya na tulitenga Shilingibilioni nne.

Kuhusu swali la pili ni kwamba kule Ngorongoro nimbali sana na hivi Vyuo ambavyo nimevitaja vya Oljoro nakule Arusha, lakini nimesema kwamba stadi hizi za kazizilifanyika kwa kuona kila Wilaya ambako hakukuwa na Chuochochote hata kama ni cha binafsi au mashirika ya dini.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

29

Wilaya ya Ngorongoro kipo Chuo cha St. Joseph (VTC)ambacho ni Chuo binafsi, ndiyo maana Serikali haikuwezakufanya stadi kwenye maeneo hayo. Lakini tulikuwatunaangalia zile Wilaya ambazo hazina Vyuo kabisa.

SPIKA: Ahsante. Muda jamani tunakwenda nao. Sasanamwita Mheshimiwa Dkt. Pudenciana Kikwembe.

Na. 109

Chama cha Walimu Kuwakopesha Walimuili Kujikwamua Kimaisha

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE aliuliza:-

Walimu wamekuwa wakikatwa 2% ya mshaharakuchangia Chama cha Walimu Nchini, lakini wamekuwawakifanya kazi katika mazingira magumu:-

Je, Chama hicho hakioni umuhimu wa kuwakopeshaWalimu mikopo isiyo na riba kama ujenzi wa nyumba ilikuwakwamua katika mazingira magumu ya kimaisha?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe, Mbunge waViti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, makato ya asilimia mbili yamishahara ya Walimu kama ilivyo kwa Vyama vingine vyaWafanyakazi nchini ni kutetea maslahi ya Wanachama wao.

Mheshimiwa Spika, shughuli hizo ni kudai nyongezaza mishahara, kupandishwa madaraja, kudai madenimbalimbali kama malimbikizo ya mishahara, uhamisho,matibabu na nauli za likizo pamoja na kutetea Walimu wenyekesi mbalimbali kwenye Mahakama pale wanapopatamatatizo wakiwa kazini.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

30

Mheshimiwa Spika, Chama cha Walimu Tanzaniakinaona upo umuhimu wa kuwapokea Walimu kutokana namichango inayotokana na makato ya asilimia mbili yamishahara yao. Kwa sasa Chama cha Walimu Tanzania kipokwenye hatua za mwisho kabisa za kufungua Benki ya Walimuambayo itaanza kufanya kazi mwezi Juni, 2013 na ikapoanza,kila mwalimu atakuwa na haki ya kukopa kwa ajili ya mahitajiyake kama vile kujenga nyumba, kusomesha watoto wakeau kujisomesha yeye mwenyewe na mahitaji mengine.

Mheshimiwa Spika, suala la msingi ni kwamba mikopoitakayotolewa na Benki ya Walimu haiwezi kukosa kuwa nariba kwa vile chombo kitakachowakopesha kinatakiwa kuwaendelevu. Nafuu itakayotokana mikopo kutoka katika Benkihii ya Walimu ni kwamba riba itakuwa ya kiwango kidogozaidi ikilinganishwa na Taasisi nyingine za fedha ambazo zipokibiashara zaidi.

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kikwembe, swali lanyongeza.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaSpika, ahsante kwa kunipa nafasi kuweza kuuliza maswalimawili ya nyongeza. Kwanza kabisa, napenda tu nisemeukweli kwamba nasikitika na majibu haya ambayo hayaelezeihali halisi Mwalimu. Siyo kweli kwamba hii asilimia mbiliinamsaidia Mwalimu kutatua matatizo yake. Kama ingekuwahivyo, Walimu wasingekuwa wanagoma, Walimuwasingekuwa hawaingii madarasani kufundisha.Wangefanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na watoto wetuwangefaulu vizuri.

Swali la kwanza, kwa sababu majibu yamekuwayakitolewa humu ndani kwamba Walimu walikaawakakubaliana hii asilimia mbili ikatwe na wakajaza fomu,jambo ambalo siyo kweli. Mimi pia ni Mwalimu nanimeshawahi kukatwa hizi asilimia bila makubaliano yoyote.Je, wapi walikaa wakakubaliana hiyo asilimia mbili? Kwaniniiwe asilimia mbili na isiwe chini ya asilimia mbili? (Makofi)

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

31

Swali la pili: Je, Walimu wameshirikishwa kutokana namakato yao haya ya 2% ili kuweza kuanzisha hiyo Benki?(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Kazi na Ajira!

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, hii 2%ni kwa Vyama vyote vya Wafanyakazi na ipo kisheria kamanilivyogusia jana. Lakini ni kwamba kabla mfanyakazihajakatwa hiyo pesa, Chama cha Walimu kinatakiwakuwasiliana na Mwalimu kupitia Mwajiri sehemu ya kazikuwaeleza na kuwaomba wajiunge na Chama hicho nakuwaomba wajaze fomu inayoitwa TOF 6.

Sasa kwa upande wa Walimu, Chama cha Walimukinakwenda Halmashauri, kinawasiliana na Mkurugenzi. Kwahiyo, assume kwamba Chama cha Walimu ndiyo Chamachenye Wafanyakazi wengi katika shule zote. Mkurugenzianakubaliana na Chama cha Walimu waendelee kukatwa2% lakini kwa wale ambao hawajaingia katika Chama,assumption ni kwamba kwa kuwa 50% ya Walimu wotewameshaingia katika Chama cha Walimu, wanakatwa helainatwa pesa ya Uwakala.

Mheshimiwa Spika, hii pesa ya Uwakala ni kwa ajili yakuwatetea wale Walimu ambao siyo Wanachama. Hatahivyo, maelekezo tuliyotoa ni kwamba Walimu wapyawanaojiunga na kazi wasikatwe hiyo pesa mpaka Chamacha Walimu kitoe elimu kiwaeleze na kiwapelekee hiyo fomuili wajaze, na pia wajaze fomu ya kukubali makato. Hiyotumeshawaelekeza Chama cha Walimu watuletee idadi yaWalimu waliojaza fomu ili tujue kuwa waliojaza fomu kweli ni50% kusudi wengine wote waweze kukatwa hiyo 2%.

SPIKA: Ahsante.

Waheshimiwa Wabunge, naomba muwe mnaangaliana saa halafu tutakuwa tunaelewana vizuri. Mkiwa mnatakatuseme mpaka mwisho, haiwezekani. Muda wa Maswaliumekwisha, sasa ni matangazo ya kazi.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

32

Kwanza kabisa, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaHuduma za Jamii - Mheshimiwa Margareth Sitta, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kuwa leo saa 7.00kutakuwa na kikao cha Kamati hiyo ambacho kitafanyikaUkumbi Namba 133, halafu Mwenyekiti wa Kamati ya Bungeya Hesabu za Serikali za Mitaa - Mheshimiwa RajabMohammed anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamatiyake kwamba leo saa 7.15 na kutakuwa na Kikao cha Kamatihiyo kwenye ukumbi wa Pius Msekwa C.

Halafu Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ardhi,Maliasili na Mazingira - Mheshimiwa Zakia Meghji, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba leo tarehe25 saa 7.15 watakuwa na kikao katika ukumbi namba 227.Halafu Katibu wa Wabunge wa CCM Bungeni anaombaniwataarifu Wabunge wa CCM kuwa leo saa 7.00 mchanakutakuwa na Kikao cha Wabunge wote wa CCM ukumbi waPius Msekwa.

MWONGOZO WA SPIKA

SPIKA: Mheshimiwa Nchemba!

MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Spika,nasimama kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) inayohusuMwongozo. Kwa ajili ya muda, naomba nisisome. Tangu janamjadala wa bajeti ya Serikali ya Maji unaoendelea hapaunatoa ishara kabisa kwamba bajeti iliyoletwa na Serikalibado haijaendana sawasawa na hali halisi ya maji Vijijini naMijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini Waziri Mkuu aliwahi kutamkakwamba katika ziara zake alizofanya alijionea hali halisi yamaji hapa nchini, na kwa kuwa leo katika maelezo yakeameona kuwa Serikali imeliona suala la maji na uzito wakena inatambua umuhimu wake, lakini ameelezea tatizo ninamna ya kuangalia mambo ya fedha na kuona wapiwanaweza kupata kuweza kuziweka fedha.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

33

Mheshimiwa Spika, tumekuja hapa kuwapa majibuWatanzania. Uliunda Kamati Ndogo ya Wabunge ambayoumeiita Kamati ya Bajeti, nami ni Mjumbe katika Kamati hiyona ninaamini katika mijadala ambayo imekuwa ikiendelea,Kamati ile inaweza kuishauri Serikali vizuri na ikaisaidia nchihii kuweza kupata fedha kwa ajili ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hata mjadalaukiendelea hapa itakuwa malalamiko tu siyo majibu, kwa niniusitoe mwongozo wa Serikali kukutana na Kamati ndogo yaBajeti, think tank yako uliyoiweka pale ili iweze kurekebishamahesabu na tukija hapa tuweze kuwapa Watanzaniamatumaini waweze kupata maji? Leo hii ukiwaulizaWanyiramba…

SPIKA: Mwongozo siyo hotuba jamani!

MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Spika, kwanini usitoe muda kwa Serikali kukutana na Kamati hiyo?

Mheshimiwa Spika, naomba Mwongozo wako.

SPIKA: Mheshimiwa Esther!

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, naminaomba Mwongozo wa Spika kwa Kanuni 68 (7).

Mheshimiwa Spika, wakati Naibu Waziri anajibumaswali yangu ya nyongeza mawili hususan swali nililoulizala Tarime ya Tarafa ya Inchugu kutokupata bwawa takribanimiaka 52 baada ya uhuru, hakujibu kabisa, matokeo yakeakaanza kuainisha miradi aliyoifanya ya Ilemela, Misungwi,Bukoba na kwingineko; nilikuwa naomba Mwongozo wako,likitokea jambo kama hili ambapo Mawaziri hawajibu maswaliyetu, badala yake wanakuwa wanapiga siasa, ni hatua ganiunachukua? Naomba Mwongozo wako.

SPIKA: Haya, ahsante. Mheshimiwa Mpina!

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

34

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, niliombaMwongozo jana kuhusiana na majibu yaliyotolewa naMheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha akijibu swali langu lanyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ufafanuzi huo alioutoaMheshimiwa...

SPIKA: Mheshimiwa Mpina!

MHE. LUHAGA J. MPINA: Ndiyo!

SPIKA: Tulisema Mwongozo wa Spika siyo hotuba.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Kwa kifupi sana.

SPIKA: Naomba tuelewane vizuri, kwanza ningeombaukae kwanza. Aspect ya Mwongozo siyo mahali pa kujadili,ni kitu ambacho wewe hufahamu kilichotokea kabla. Sasanamna ya kufanya; kwa mfano, hata jana mimi sikuwepohapa, alikuwepo Mheshimiwa Naibu Spika, lile lako kunamaelezo binafsi, ile ya kwako ili-fit vile.

Hata alivyozungumza Mheshimiwa Lugola jana, paleni maelezo binafsi ambayo yanakupa nafasi ya kujieleza vile.Lakini sasa Mwongozo unakuta ni hotuba, ni mabishano,Mwongozo hautaki namna hiyo. Someni kifungu chaMwongozo.

Kwa hiyo, nawaombeni sana, hilo suala lako limekaakama maelezo binafsi, na kifungu cha maelezo binafsi kipo.Tukitumia muda huu kusema Mwongozo kumbe tunahutubia,hatutakuwa tumelitendea haki Bunge. Nawaombeni sana,lile suala lako nimelisikia vizuri, haliwezi kuwa Mwongozo waSpika. Ile ni maelezo binafsi, na wengine nao wakajiandaewaje wajibu, lakini siyo kwamba tutaanza kubishana kamailivyotokea. Kwa hiyo, lile suala la Mheshimiwa Mwigulunitajibu baadaye, suala la Mheshimiwa Esther tutaangaliaMaswali na Majibu kwasababu yote yako kwenye Hansard.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

35

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwaMwaka 2013/2014 - Wizara ya Maji

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba niwaiteWafuatao kama wapo kwasababu kusudio la Wizara hiitunataka tufike asubuhi tu, kama wapo Mheshimiwa RitaMlaki, atafuatiwa na Mheshimiwa Herbert Mtangi, atafuatiwana Mheshimiwa Mariam Mfaki, kama wapo naomba waanzehalafu tutaendelea baadaye. Mheshimiwa Ritta Mlaki nilifikirinimemwona!

MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Spika, nakushukurusana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia hotuba hii yaWizara ya Maji. Kwanza, nichukue nafasi hii kumpongeza sanaWaziri na Wizara yake kwa hotuba nzuri pamoja namapendekezo mazuri kwa ajili ya maji kwa Mkoa wa Dar esSalaam.

Mheshimiwa Spika, Dar es Salaam ina watu takribanimilioni 4.5 ambao wanakaribia kufika milioni tano wakatiwowote. Jiji la Dar es Salaam limepata matatizo ya maji kwamuda mrefu na ninashukuru kwenye bajeti imejieleza kwakirefu mikakati ya nyuma na mikakati ijayo.

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2002, Serikali ilitengaama ilichukua mkopo wa Benki ya Dunia Shilingi bilioni 174kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji Mkoa wa Dar esSalaam ili upatikanaji uweze kuwa mzuri. Lakini ninasikitikakwamba pamoja na jitihada zote hizo, pamoja na kumwekaMkandarasi ambaye ilikuwa ni Kampuni ya Kichina, mpakasasa bado Jiji la Dar es Salaam maji hayatoshi.

Pamoja na hayo, kuna matatizo mbalimbaliyanayotokea katika Jiji letu kama milipuko ya magonjwaCholera na magonjwa mengine ya kuambukiza ambayo

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

36

kusema ukweli yanaletwa kwa ajili ya uchafu hasa majiambayo yanapatikana kwa shida sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika uchunguzi tumeonakwamba mabomba mengi katika Mkoa wa Dar es Salaamyamekatwa, watu wanaiba maji kwa kukata mambombana kuteka maji, lakini vilevile wanapomaliza kufanya namnahiyo, hayaungwi kwa hiyo, kunakuwa na upotevu mkubwasana wa maji kwa mpango huo.

Vilevile mambomba yaliyopo ni ya zamani ambayoyameziba na hayawezi kupisha maji kwa kiwango ambachokinahitajika kwa sasa. Lita tunazotaka kutumia auzinazohitajika kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni lita milioni 470kwa siku ambapo Waziri ameeleza kuwa mpaka sasa hivitunapata lita 300 na kitu.

Mheshimiwa Spika, kwa ajili ya tatizo hili kubwa,tulikuwa tunapendekeza, Serikali sasa badala ya kuweka hiziproject ndogo ndogo ambazo tunaona vyanzo vya majikutoka Ruvu Chini, Ruvu Juu, Mtoni na visima ambavyovinachimbwa hayatoshi, kwa nini Serikali isifikirie sasa kuwekadesalination plant kubwa pale Dar es Salaam ili tuwezekutumia maji ya bahari?

Mheshimiwa Spika, ilikuwa ni kigugumizi kwa mudamrefu kutumia maji ya Lake Victoria lakini tunashukuru Serikaliikaamua na maeneo mengi sasa katika Kanda ya Ziwayanapata maji na bado yataendelea kupata maji. Hebutufikirie sasa mpango huu wa maji kutoka baharini.

Mheshimiwa Spika, tukiwaza namna hiyo watu ni rahisikufikiria kuwa ni pesa nyingi na bajeti haitoshi au Serikali hainapesa. Lakini kuna mikopo. Nina hakika kuna nchi mbalimbalizitakuwa tayari au Benki ya Dunia hiyo hiyo kutukopesha kwaajili ya plant kubwa kama hiyo ya kusafisha maji ya baharituweze kuyatumia kwa matumizi ya binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kwa sasa hivi ninashauri Serikaliwafuatilie hayo mambomba kwa karibu mno. Kuna watu

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

37

wengi ambao wameajiriwa, kuna DAWASCO, kuna DAWASAambao wanapita katika majumba kufuatilia bili zao,wanaweza vilevile kuamua sasa wakishirikiana na Manispaahusika kuhakikisha kwamba tunaweza kuziba hiyo mianya.Maji yanayopotea ni asil imia kubwa sana ambayotunayaona na tuna uhakika nayo.

Mheshimiwa Spika, vilevile Serikali sasa iwaze sasakujenga reserve tanks. Nakumbuka katika mwaka wa 2004/2005 Serikali ilijenga reserve tank kubwa pale Kunduchi katikamwinuko katika kiwanda cha Wazo na hiyo ilitusaidia sanakupata maji katika maeneo ya Kata ya Kunduchi katika Jimbola Kawe.

Mheshimiwa Spika, kuna maeneo mbalimbaliambayo yako katika mwinuko kule Ubungo Chuo Kikuuambayo tunaweza pia kujenga matanki makubwa ya majiyakasaidia kuwa kama reserve ili tuweze kuyakinga yale majina kuyaweka tayari kwa kuweza kusaidia wananchi.

Mheshimiwa Spika, ningependa kuongelea pia tatizola majitaka katika Jiji la Dar es Salaam. Majitaka ni tatizokubwa sana na imekuwa kama ni kitu cha kawaida, unapitaeneo unakuta maji yametoka ya sewage yanamwagikabarabarani na watoto wadogo wanachezea katikamajumba ya watu.

Mheshimiwa Spika, sijui Serikali ina mpango gani katikahili. Ni kazi kubwa kwasababu miundombinu ya zamaniiliyowekwa ya majitaka imezeeka kwa sasa na niseme njiaambayo ilikuwa imejengwa kwa ajili ya zile sewage tanksambazo zilikuwa zimejengwa au njia ya kupeleka baharininyingi zimeziba: Je, Serikali ina mpango gani wa kushughulikiahili suala hasa katika Jiji ambalo lina watu takribani milionitano?

Mheshimiwa Spika, eneo la Mikocheni B, ukipita paleni harufu kali kuanzia kwa Nyerere mapa ufike njia Panda yaKawe, inasikitisha sana. Maji yatoka mengi, yatoka viwandani,yanatoka kwenye vyoo, yanakuja kama bahari na kule

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

38

baharini sijui kumezibwa! Ningeliomba hilo Serikali itazamekwa makini sana, kwa sababu ni hatari kwa maisha yabinadamu, ni hatari kwa watoto wetu, ni hatari kwa viwandana ni hatari pia kwa kila maendeleo yanayofanyika katikaeneo lile.

Mheshimiwa Spika, naomba vilevile watu hawa waDAWASA wawe wakali kidogo kwa watu ambaowanachukua maji machafu na kuyaweka katika mitaro yamaji masafi.

Kwa hiyo, drainage system pale kwa ujumla haijakaavizuri. Tunaliomba hilo liweze kufikiriwa. Tatizo la maji nchinzima ni kubwa, tatizo la maji katika Miji Mheshimiwa Waziriamesema angalau 86% katika Miji wanapata maji. Lakini kwaDar es Salaam nina hakika ni 55%.

Mheshimiwa Spika, nakumba sana Mheshimiwa Waziripamoja na Serikali yake watusaidie sana tatizo la maji katikaJiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naungamkono hoja nikiamini kabisa kuwa Mheshimiwa Waziriamesikia, Watendaji wake wamesikia, wawatusaidia katikampango wa dharura tuweze kupata maji kwa haraka katikaMkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nitamwita Mheshimiwa HerbertJames Mntangi, atafuatiwa na Mheshimiwa Mariam Mfaki.Mheshimiwa Mntangi hayupo, Mheshimiwa Mfaki hayupo…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mfaki yupo!

SPIKA: Yupo!

MBUNGE FULANI: Eh!

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

39

SPIKA: Aah, Mama Mfaki; haya, ahsante.Tunaendelea Mheshimiwa. Baada yake atafuatiaMheshimiwa Anna-Marystella, na Mheshimiwa John Mnyika.

MHE. MARIAM S. MFAKI: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi hii ya kuchangia.

SPIKA: Naona kama husikiki vizuri.

MHE. MARIAM S. MFAKI: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi hii ya kuchangia asubuhi ya leo.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuzungumza yaleambayo yanahusu Wizara hii, naomba uniruhusu niotoeshukrani.

Pamoja na kwamba umesema hapana, lakini miminaomba niseme machache.

Mheshimiwa Spika, kwanza nitoe shukrani za dhatikwako wewe binafsi, Naibu wako, Katibu wa Bunge, pamojana wote ambao kwa kweli kutokana na hali yangu yakuumwa mlinisaidia sana, mkaniwezesha nikatibiwaMuhimbili, nikaenda India na bahati nzuri nimerudi sasa haliyangu ni nzuri. Nawashukuruni sana. (Makofi)

Vilevile niwashukuru Madaktari wa Mkoa wa Dodomaakiwepo Mama Chaula pamoja na wenzake kwa msaadawalionipa na kunitibu katika Hospitali yetu ya Dodoma nawakaruhusu niende Muhimbili.

Vilevile niwashukuru Madaktari wa Hospitali ya Chenaikule India wakiongozwa na Dkt. Rajah ambao kwa kweliwalihangaika na mimi katika matibabu mpaka nikapatanafuu. Nawashukuru sana. (Makofi)

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

40

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumze machachekuhusu Wizara hii ya Maji, kwanza niishukuru Wizara ya Majikwa Mkoa wetu wa Dodoma ikiwemo Mji wa Dodomakwamba wamejitahidi sana kusambaza maji, tunawashukurusana.

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile niiombe Serikali, majiyamesambazwa lakini bado kuna tatizo la maji taka, maeneomengi bado maji taka hayajatengenezewa miundombinuyake. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iangalie sana juu ya sualahili, ni maeneo mengi ya Mji wa Dodoma hayana mtandaowa maji taka, kwa hiyo, hilo naomba lishughulikiwe.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, ningeomba nishukurusana kuhusu kuanza utafiti wa bwawa la Farkwa kule Kondoa.Naomba utafiti huo ufanyike haraka kwani lile bwawalikishakamilika litakuwa ni msaada sana kwa vijiji vilivyo jiranina kwa maeneo ambapo maji yatapita mpaka kufikaDodoma Mjini. Kwa hiyo, Serikali ijitahidi kufanya utafiti harakana bwawa lianze kuchimbwa na likamilike mapema ili liwezekusaidia wananchi.

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji kwa kweli ni la nchinzima, imeonekana kwa kuwa kila Mbunge amejaribukusemea suala hili, nisingependa niendelee kulisemea kwasababu tayari limekuwa ni tatizo.

Mheshimiwa Spika, naomba sana, kazi ambayoifanywe na Serikali ni kutafuta pesa. Fedha ikitafutwa naaminimiradi hii ya maji vijijini inaweza kabisa ikapunguza tatizo lamaji vijijini. Tunaomba hasa wangalie vijijini ambako wananchiwanapata shida sana hasa Mkoa wa Dodoma. Naamini ninyinyote mnajua shida ya Mkoa wa Dodoma, ni Mkoa ambaohauna mvua za kutosha. Kwa hiyo, tatizo la maji ni kubwana naamini pengine inawezekana ni kubwa hata kuliko mikoamingine.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutakapopata pesa,naomba sana Serikali ijitahidi kuondoa tatizo la Mkoa waDodoma, wakishachimbiwa mabwawa ya kuvunia maji, nina

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

41

25 APRILI, 2013

uhakika mabwawa hayo yatasaidia sana. Pia kuchimbavisima ambavyo vitasaidia kwa vijiji vingine.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali ijitahidikutafuta hizo hela na iweze kuendelea kutatua tatizo la majiVijijini, kuchimba visima, kutengeneza mabwawa ili yawezekusaidia.

Mheshimiwa Spika, sikuwa na mengi nilitaka kusemeahayo tu, kwa sababu mengi yameshasemwa sana naWabunge na kwa kweli limeonekana ni tatizo kubwa kulikokawaida.

Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono hoja.Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa John Mnyika atafuatiwana Mheshimiwa Dkt. Lucy Nkya.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spikanakushukuru. Nitaomba nizungumze mambo machacheyanayohusiana na hotuba hii iliyopo mbele yetu ya Waziriwa Maji.

Mheshimiwa Spika, naungana na Wabungewenzangu wote waliokataa kuunga mkono hoja hii kuwezakupitishwa hapa Bungeni kutokana na kutokukidhi haja yaidadi ya fedha zilizopo katika bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, pia nieleze tu masikitiko yangutarehe 4 Februari, 2013, niliwasilisha hoja binafsi hapa Bungenijuu ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji.Hoja ile iligusa maeneo makubwa mawili ambayo taarifa hiiiliyotolewa na Wizara sasa hivi ya utekelezaji kwenye hotubaya Waziri, bado sijaridhika kwamba imekidhi haja.

Mheshimiwa Spika, upande mmoja wa hoja ulihusumasuala yaliyohusiana na mpango wa maji Dar es Salaam,ambapo ndani ya kitabu hiki cha Waziri kuna mamboambayo Waziri ameyatolea maelezo ambayo sijaridhika

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

42

25 APRILI, 2013

nayo na ndiyo maana siungi mkono hoja na naungana nawote ambao hawaungi mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa hoja ulihusumasuala yanayohusiana na mradi wa maji vijijini ambaounatekelezwa Dar es Salaam lakini unatekelezwa vile vilekwenye Halmashauri zote za Wilaya nchi nzima. Tafsiri yakeni nini?

Mheshimiwa Spika, kama wakati ule Serikaliingetakiwa kutoa majibu kwa ukamilifu kwa maazimio yotenane ambayo yalipaswa kutolewa majibu wakati ule, kuanziamwezi Februari Serikali ingekuwa imeshaanza kuhangaikakutafuta pesa za nyongeza za kuongeza kwenye bajeti yamaji na kwa kweli tusingefikia katika hatua hii tuliyoifikia hivisana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni rai yangu kwa Wizara,Serikali na kwa Wabunge wenzangu safari hii michangotuliyoitoa na michango tutakayoendelea kuitoa isiwe yakinafiki ya kuonesha kukataa kuunga mkono hoja, lakinibaadaye mkishakaa vikao vya Chama chenu mnaamuakuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, kuna mambo mawili ya muhimusana hapa ambayo ni muhimu yakazingatiwa. Kwanza niukweli kwamba, kuna tatizo la uhaba wa pesa, lakini la piliambalo ni kubwa zaidi kuna tatizo la matumizi mabaya yapesa kwenye miradi ya maji na jambo hili ni muhimu Wizarakwenye majumuisho ikaja na majibu ni kwa nini kunakigugumizi cha kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali, kukagua pesa zilizotumika na ufanisi wa mradi wamaji ya mabomba ya Wachina ambayo hayatoi maji mpakahivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana tutaingiza pesa nyinginekwenye miradi, lakini kama hatushughulikii miradi ya zamaniambayo ni matatizo matupu, hizi nazo zitakwenda vibaya.Ni kwa nini kuna kigugumizi kila Mbunge anayesimamaanasema Wakandarasi kwenye miradi ya Vijiji Kumi wengine

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

43

25 APRILI, 2013

walichakachua ndiyo maana wametafuta maji nahayakupatikana. Ni kwa nini kuna kigugumizi kwa Serikalikumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanyaukaguzi maalum wa matumizi ya fedha za Mradi wa Vijiji Kumi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda sitakwendakiundani, lakini ukaguzi wa kawaida tu wa Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali kwa taarifa iliyoishia mwezi tarehe 30 Juni,2011 iliyowasilishwa Bungeni kuanzia ukurasa wa 99 wa ripotiya CAG mpaka ukurasa wa 117 wa ripoti ya CAG, umeainishanamna ambavyo Halmashauri 98 za Tanzania zilivyoshindwakutumia ipasavyo fedha za miradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hata tukienda kuongezapesa kama hatuwezi kushughulikia ufisadi na ukiukwaji wataratibu kwenye miradi ya maji, hatuwezi kufika kunakostahili.Kwa hiyo, hiki kielelezo nitaomba kifike mezani kwako ili Serikaliikubali kwenda kufanya ukaguzi kwenye miradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, hapa nina Ilani mbili za Uchaguziza CCM, nina Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005mpaka mwaka 2010 na nina Ilani ya Uchaguzi ya CCM yamwaka 2010-2015. Tukianza na Ilani ya Uchaguzi ya CCM yamwaka 2005, CCM iliwaahidi Watanzania mwaka 2005kwamba ifikiapo mwaka 2010 asilimia 65 ya wananchi vijijiniwatakuwa na maji safi na salama, ifikapo mwaka 2010 asilimia90 ya wananchi Mijini ikiwemo Dar es Salaam watakuwa namaji safi na salama. Mwaka 2010 umefika ilani hiyohaijatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, sasa kama ilani hii haijatekelezwani kwa vipi na katika hili kabla ya mtoa hoja hajaja kutoahoja, wachangiaji wengine wakishamaliza kuchangia,nitaomba unipe nafasi niweze kutoa hoja hapa ya kuahirishahuu mjadala kwani ahadi aliyoitoa leo Waziri Mkuu asubuhini ahadi ambayo ni maneno matupu.

Mheshimiwa Spika, tukishapita kwenye kupitia vifungukwa vifungu kwa mujibu wa Kanuni zetu, Bunge likikaa kamaKamati mchezo kimsingi utakuwa umemalizika. Tutaambiwa

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

44

25 APRILI, 2013

hizo pesa zinatoka kwenye OC, zikitoka kwenye OC, sisitumeshapitia vifungu kwa vifungu, ni wakati gani tutapitiatena kifungu kwa kifungu ili kuhakikisha kama kweli Wizaraya Maji tuliyoyasema yametekelezwa? Siamini kabisa hiiahadi ya Waziri Mkuu itatekelezwa kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu tulipopiga kelelekuhusu bajeti ya Nishati na Madini mjadala ukaahirishwa,Waziri Mkuu aliahidi kwamba tunakwenda kukata kwenyeOC tunatengeneza mpango wa dharura wa umeme. Ahadiilipokuja hapa Bungeni hawakukata kwenye OC, wakasemawanakwenda kukopa benki kwa ajili ya mpango wa dharurawa umeme ambao mpaka sasa haujatekelezwa kwa ufanisikwa sababu fedha hazikutolewa kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, sasa ni nini kinatufanya tuamini leokwamba pesa zitakwenda kukatwa kwenye OC kamahatutapitia kifungu kwa kifungu mpaka tujihakikishie kwambakweli pesa zipo.

Mheshimiwa Spika, nitaomba baadaye nitoe hiyohoja ili tuahirishe mjadala kama Kamati inakaa na Serikaliikakae, tusiuziwe mbuzi kwenye gunia, tuletewe hapa,tukiziona pesa kifungu kwa kifungu zikienda kwenye miradiya maji. Pia sikubaliani na Kamati kwamba tunahitaji bilioni181 tu peke yake. Ukisoma hotuba ya Waziri kwenye hiiprogram ya matokeo ya haraka Big Result Now, inasema pesazinazohitajika kwenye maji ni trilioni 1.85.

Mheshimiwa Spika, trilioni 1.85 kama tunakwenda kwakasi hii ya bilioni 181, tutahitaji miaka mingapi ili kutatua tatizola maji hapa nchini? Kwa maneno mengine, kinachohitajikahapa ni kama tulivyofanya mpango wa dharura wa umeme.Katika mpango wa dharura wa umeme tulisema tunatafutabilioni mia tano, hapa tukitumia bilioni mia tano; mwaka wakwanza bilioni mia tano, mwaka wa pili bilioni mia tano,mwaka wa tatu bilioni mia tano, tumemaliza tatizo la majinchi nzima siyo Dar es Salaam tu.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

45

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, hii inawezekana, bilioni mia tanoni nusu tu ya mapato ya Serikali kwa mwezi, tukiamuakujifunga mkanda kwa mwezi mmoja tu tunapata pesa yakwenda kuinusuru nchi na tatizo la maji.

Mheshimiwa Spika, kuna Mbunge alichangia janaakasema maji ni uchaguzi, lakini naona maji ni zaidi yauchaguzi kwa sababu maji ni maisha ya watu! Kama ninyimnashindwa mnatazama uchaguzi peke yake 2015 ondokenimadarakani watu wengine waingie watekeleze haya. Majini maisha ya watu na maji ni maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja na siungi mkonomaelezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu asubuhi kwa sababusina imani na ile kauli mpaka tupitie kifungu kwa kifungu,tuzikate hizo pesa kwenye OC tuzione, tuzielekeze kwenyemiradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuna nyongeza kidogo Dares Salaam na ni jambo zuri, kuna mkopo wa India umeongezapesa Ruvu Juu, kuna mkopo wa Marekani umeongeza pesaRuvu Chini kwa maana ya pesa za MCC.

Mheshimiwa Spika, lakini ni vizuri Waziri akakumbuka,mwezi Februari walipokaa kwenye kikao cha Baraza laMawaziri na Rais akaja akafanya mkutano na Waandishi waHabari akatangaza tatizo la maji Dar es Salaam litakuwahistoria mwaka 2013. Huu ni mwaka wa 2013, pesazilizotengwa wakati ule zilikuwa ni bilioni 654, kwa hiyo hizizilizotengwa hapa pamoja na kuwa zinaonekana ni nyingi nichini ya mpango wa Serikali, ni chini ya ahadi ya Serikali nakama hatutazingatia haya…

MBUNGE FULANI: Dakika kumi hazijafika kweli?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, walewananchi wa Dar es Salaam wako tayari kuendeleakuandamana kuja Wizarani kwako, kwa sababuwamekwishachoka. Waliahidiwa tatizo la maji itakuwahistoria mwaka 2010, halijawa historia. Wakaahidiwa mwaka

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

46

25 APRILI, 2013

2011, halijawa historia, mwaka 2012, halijawa historia namwaka 2013, halijawa historia!

Mheshimiwa Spika, katika hili hakuna masuala yaVyama, Itikadi, sijui na nini. Maji ni maisha, maji ni uhai namaji ni utajiri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nitamwita Mheshimiwa Dkt. LucyNkya sijui yupo? Kama hayupo atafuata Mheshimiwa MaryChatanda, kama hayupo atafuatia Mheshimiwa JeromeBwanausi, naye pia hayupo. Mheshimiwa JosephineChagula, wamekwenda wapi hawa? Mheshimiwa SylvesterKoka, hayupo; Mheshimiwa Fatma Mikidadi, naye hayupo;Mheshimiwa Josephat Kandege atafuatiwa na MheshimiwaChiligati na Mheshimiwa Rosemary Kamili na MheshimiwaJoshua Nassari wajiandae.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa kupata nafasi ya kuchangia hoja iliyombele yetu. Mengi yamesemwa na mengi yatasemwa, lakinitukubaliane kimsingi kwamba kinachotakiwa ni upatikanajiwa pesa.

Mheshimiwa Spika, bahati nzuri nipo kwenye Kamatiya Bajeti na kila Mbunge anayesimama hapa analia kilio chamaji, nadhani katika hili hata ndugu zetu wa upande waUpinzani wataunga mkono hoja ili pesa ipatikane twendekutatua kero ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa napitia ukurasa wa 52 nahil i ninalisema kwa makusudi wakati ndugu yanguMheshimiwa Machali anachangia alisema kwamb,a kunasehemu zinapendelewa na mradi ule unaongelea suala laMiji inayozunguka Lake Tanganyika. Katika Miji inayozungukaLake Tanganyika Kasulu siyo mmojawapo, lakini wamepatapesa za kutosha na nyingi tu.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

47

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni vizuri tunapokuwatunatoa kauli tuwe tunakumbuka na yale tunayoyasema.Tanzania hii ni ya kwetu sote, tusiigawane nchi kwa vipandevipande, naiomba Serikali ihakikishe kwamba tatizo la majini kwa Tanzania nzima, kwa hiyo tuiangalie Tanzania kamanchi yetu sisi sote, pale ambapo mradi unakuwa umekwendasehemu moja tusiwe watu wa kulaumu, ni zamu imefika kwamwenzako itakuja zamu yako itafika, tuwe na spirit hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nashangaa kuna baadhiya wachangiaji walikuwa wanasema eti MheshimiwaMaghembe mradi umekwenda Same na Mwanga kwasababu yeye ndiyo Waziri kipindi hiki. Hizi ni fikra potofu sana,kwa nchi hii si vizuri tukawa tunakwenda kwa mtazamo huo,ule mradi ulikuwepo kabla hata yeye hajakwenda kwenyesekta hiyo. Kwa hiyo, haiwezekani eti kwa sababu leowananchi wa Same na Mwanga wanapata maji na Korogwendiyo iwe nongwa, hii siyo sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Jimbo langu la Kalambo na Wilayampya ya Kalambo, ukitazama miradi ni michache sana.Naamini ndiyo maana safari hii tumesema kwamba mpakadakika ya mwisho tutaifumua bajeti na baada ya kusikilizamaoni ya Wabunge walio wengi basi kilio kitasikilizwa nakutekelezwa yale ambayo yanatakiwa. Naamini na Wilayaya Kalambo na Vijiji vyake, mwambao wa Ziwa Tanganyikakuanzia Kipwa kule tunakopakana na Zambia, nasitutasikilizwa.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana mwakahuu kuna wanafunzi wawili walikamatwa na mamba wakiwawanatafuta maji na wale ndiyo wako Ziwa Tanganyika, lakinimaji safari hii yanakwenda Kasulu sisemi sana, lakini ujumbeumefika.

Mheshimiwa Spika, kuanzia Kipwa, unakwendaKilewani, unakwenda Kasanga Port unakuja Muzi na vijiji vyotevile vya Ziwa Tanganyika, hali ya maji ni ya tabu kweli. Ndiyomaana kila mara inapofika kipindi cha masika magonjwa

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

48

25 APRILI, 2013

ya kuhara na kipindupindu ni kila mwaka. Naamini Wizarainasikia, ihakikishe kwamba, huu mradi wa kwenda kuletamaendeleo na kuleta maji unafanyika kwa nguvu kubwa.

Mheshimiwa Spika, siyo vijiji vya mwambao wa ZiwaTanganyika peke yake ambavyo vina shida ya maji ni Kijijikama Kalepula, Ulumi ambapo Waziri alifanya ziara na aliahidiyeye mwenyewe, naamini wakati anahitimisha atawaambiawananchi wa Kijiji cha Ulumi ni lini maji yatakwenda. Piaatawaambia wananchi wa Kafukula ni lini maji yatakwendana wananchi wa maeneo mengine. Ninachowaomba nduguzangu tushikamane katika hili, maji ni kwa Watanzania wote,hivyo hata Wizara zingine hawatapata tabu palewatakapoambiwa kwamba OC imepungua ili twendekutatua kero ya maji.

Mheshimiwa Spika, naamini hata ikifika kwa Vyamavya Upinzani wakiambiwa kwamba ruzuku inapungua ilitukatibu kero ya maji hawatasikitika na katika hilo hata waonaona wanapiga makofi. Tukubaliane kimsingi kwamba majini tatizo, hivyo ni lazima sisi zote tufunge mikanda tuhakikishekwamba tunawapelekea Watanzania maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwanzo ilikuwa nisiunge hoja,lakini kutounga mkono hoja maana yake ni nini? Maana yakeunasusa na sisi hatujafundishwa tabia ya kususa,unapambana unahakikisha kwamba, unatatua tatizo. Kwahiyo, naamini Serikali, itakuja na majibu mazuri sana kwendakutatua kero ya maji. Kwa sababu nataka kuhakikishakwamba, kwamba, we are promise solvers, twende tukatatuekero hiyo.

Mheshimiwa Spika, nitaunga mkono baada ya majibumazuri ya Serikali. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Rose Kamili atafuatiwa naMheshimiwa Joshua. Mheshimiwa Rose Kamili dakika tanona Mheshimiwa Joshua Nassari dakika tano.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

49

25 APRILI, 2013

MHE. ROSE K. SUKUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sanakwa kunipa fursa pia. Napenda kuchangia Hotuba ya Waziri,lakini naomba nianze na kusema siungi mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivyo, sio kwamba,hatupendi maji yaende Mwanga, wala Same, wala Korogwe,lakini utaratibu uliotumika sio sahihi kwa sababu, Watanzaniawote tunalia maji. Watu wanatembea kilomita 20,akinamama na wazee wote na vijana wanatafuta maji, lakinileo bilioni 56 ziende kwa awamu moja kwa mwaka mmojaMwanga, sisi hatukubaliani nalo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba hizo fedha tuzigawanye,ziweze kwenda Hanang, kwa ninyi msiotaka acheni, sisiHanang tuna shida ya maji. Tunahitaji bilioni 19 ambazo nifedha zilizotolewa na OPEC, USD milioni 12 zije kwetu kwasababu, katika bajeti yake Mheshimiwa Waziri alisema,estimate iliyofanyika ni bilioni 32 tu ndio zianze kazi, mradi wamwanzo wa mwaka huu; sasa wewe mwaka huu hela zoteunapeleka kwako, kwa nini tusione wivu? Hatukubaliani nalo.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba, sio kwambawao wana shida ya maji sana, Mwanga Mjini wana maji,vyanzo vya maji vipo, mnakwenda kuchimba kule Bwawa laNyumba ya Mungu ambalo linakauka kiangazi saa nyingine,kwa nini usiende kwenye Milima ya Kindoroko au Lambo?Maji yakateremka kwa gravity badala ya kutumia fedhanyingi? Hapa hamkutumia utaratibu mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumza kwamba,Mheshimiwa Waziri na timu yake ya Wizara, wana dharaukwa Wabunge. Hatujapitisha hii bajeti, Hotuba yake jana ndioalisoma. Gazeti la jana limetangaza tenda ya Mwanga, hivikweli Waheshimiwa Wabunge, hatujadharauliwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, gazeti la Mwananchi liko hapa,tangazo la Mwanga tayari kwa ajili ya tenda ya kujenga aukuanza mradi. Nani amempitishia hiyo hela na nani

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

50

25 APRILI, 2013

alimwambia atangaze kabla hatujapitisha? Hiyoanatudharau sisi, tunataka hizo hela tuzigawanye, tangazolake akalifute ili tuweze kufanya kazi inayotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la visima kumi; fedhazimekaa kwenye akaunti gani? Ameeleza kwenye Hotubayake yeye mwenyewe kwamba, fedha zimepatikana 2012zilikuwepo; 2013 ndio zinatolewa Machi, zilikuwa kwenyeakaunti ya nani na zilikuwa zinafanya nini? Akatukwamishiamiradi yetu ya maji ya visima vitano ambavyo, MheshimiwaWaziri mwenyewe katika Hotuba yake ya Bajeti ya 2012/2013,alitamka hapa na kwenye Hansard ipo, alisema kwamba,visima vitano-vitano kwenye kila Kijiji, mradi wa visima kumiutakamilika; haujakamilika mpaka leo, anatwambia nini sasasisi Wabunge? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka huu unasema visimavitano tena. Wilaya ya Hanang, iko hapa kwenye kitabuchako, umeonesha kwamba, ni visima viwili; inakuwaje visimaviwili na vingine vitatu viko wapi? Nataka kuvijua kwa sababu,tunapopitisha maana yake tayari kuna wengine watakosavile visima vitatu wasipate hayo maji.

Mheshimiwa Spika, wana Hanang wana shida sana,Watanzania wana shida sana, lakini kwenye mradi wa visima10 umekuwa ni fedha za kuliwa kuanzia ngazi ya Wizaranadhani au kama sijui ni Hazina, sijui, lakini kule Halmashaurinako ni sawa na ile Katuni inayoonesha kwamba, unamegahapa, unamega tena, yule bata akifika kwenye Halmashauriwanamalizia na ile meza yake kabisa, ndio kitu kilichofanyika.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niambiwe pia, zile fedhamilioni 700 mlizopeleka zimefanya nini...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Naona muda wako umekwisha. (Makofi)

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

51

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Nassari, dakika tano!

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwa sababu, ya muda, leo naomba niendemoja kwa moja kuzungumzia mambo ya wananchi wanguwa Arumeru Mashariki, waliyonituma hapa.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa Mbunge, bila kuhongashilingi, sikuwahi kumnunulia mtu kanga wala kumnunulia mtusukari. Wananchi wa Arumeru Mashariki, waliniamini kwamba,naweza kuja kuwasemea vizuri.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kangi Lugola, janaametoa nyoka wa shaba hapa. Nikim-complement yulenyoka wa shaba ambaye alikuwa amechorwa, leo nakuleteapicha zilizopigwa Jimboni kwangu Arumeru Mashariki,takribani wiki moja iliyopita kuonesha ni jinsi gani ambavyowananchi wanahangaika na adha ya maji.

Mheshimiwa Spika, nilishawahi kuzungumza hapa,nikasema maji sio kama umeme; unapokosa maji hataukipewa soda, huwezi kuishi. Ukikosa umeme unawezakuwasha kibatari, unaweza ukatumia petrol ukawashajenereta, mambo yanakwenda. Lakini ni aibu leo miaka 52ya uhuru wa nchi hii, bado tunajadili tatizo la maji kwenyeTaifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni aibu kubwa sana unakwendakwenye Jimbo kama Arumeru, ambalo lina Mlima Meruwenye maji mazuri ambayo hayajawahi kukatika hata sikumoja. Jimbo lenye Ziwa kama Ziwa Duluti ambalo lina majiya kutosha ambayo hayajawahi kukatika hata siku moja.Jimbo lenye Ziwa Momela ambalo lina maji; Jimbo lenyevyanzo vya maji kama vya Ngaresero Lodge, vya Tema kuleNkwaranga na maeneo mengine, lakini cha ajabu wananchihawana maji ya kunywa ilhali wako kilomita moja kutokaumbali wa chanzo cha maji.

Mheshimiwa Spika, ni aibu sana, katika picha hizininazokuonesha hapa leo na kwa sababu na wewe ni mama,

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

52

25 APRILI, 2013

naomba zifikishwe mezani kwako uzione. Kuna mama hapa,ambaye ni mama kama wewe, ambaye yuko na pundaametembea kilomita saba kwenda kufuata maji, anatokakatika Kijiji cha Samaria kwenda Kikatiti kutafuta maji kilometasaba. Hapa hapa kuna picha ya watoto tarehe 20 Aprili,juzi, siku ya shule saa 5.00 asubuhi wako wanatembeakutafuta maji, maana yake wanakosa shule.

Mheshimiwa Spika, kwa hali hii nitamshangaaMbunge yeyote, ambaye ataunga mkono bajeti hii.Wananchi wanatuona vizuri kwa sababu, wanatuonakwenye TV, Mbunge yeyote anayeunga mkono bajeti hii,wananchi Watanzania mnatusikiliza, hafai kurudi kwenyeBunge hili mwaka 2015. Tunajadili maji miaka 52 ya uhuru,halafu kuna Mbunge anasema Watanzania tuna maji 80%;80% ya wenye maji vijijini ni akina nani hao? Yuko nchi ganihuyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajadili maji hapa, halafuanakuja Waziri anatudanganya. Jana kwenye Hotuba yakehapa, wazi kabisa tena uwongo mkubwa, Wazirianalidanganya Bunge? Ameandika kitabu hiki hapaanasema kuna Kijiji kinaitwa Kasanumba, ambacho kwamwaka huu ambao unakwisha keshokutwa mwezi wa Sita,wameshatekeleza mradi wa maji wa Vijiji Kumi wakati hataKasanumba, hakijawahi kuwepo kwenye nchi hii; amekitoawapi? Amekitoa Mwanga? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kabisa tuambiwe vizurihapa. Pia tunaambiwa kwamba, kuna Vijiji vitano ambavyovimetekelezwa, Kasanumba ambacho hakipo, Kikuletwa,Mbuguni, Kwa Ubora, Namboreni, Mwaivaro; wakati leoukienda Arumeru ni Vijiji viwili peke yake ambavyo visimavimechimbwa, tena yakafukiwa na yakafungwa, hayajawahikutoka, hayajawahi kunywewa wala hayajawahi kufanyiwachochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunakwenda wapi? KamaWabunge, tunadanganywa hapa halafu tunashangilia,

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

53

25 APRILI, 2013

kidumu Chama cha Mapinduzi – kidumu Chama. Kidumunamna gani kwa hali hii? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kabisa niseme wazi,Mheshimiwa Mnyika amesema hapa kwamba, atatoa Hojaya kuomba kuahirisha Mjadala; naomba kila Mbunge aungemkono, Serikali, ikakae chini ijichimbie, ituletee majibu sahihiya maji hapa. Mbona akina Magufuli wanaweza kwenyebarabara, anashindwa vipi kwenye maji? Anashindwa vipi?Profesa na Dokta, wako wawili wasomi, wanashindwa vipi?Naomba tusaidiane katika hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini aibu nyingine watuwanakufa. Jimboni kwangu Arumeru kuna wananchiwamekufa, kuna yatima wameachwa kwa sababu, wazaziwanahangaika kutafuta maji mpaka usiku wa manane kwabaiskeli, wanagongwa na magari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Kata yangu ya King’ori,kuna mama ameacha watoto ndani kwenda kutafuta majiusiku, nyumba ikawaka moto, watoto wawili wakaungua,wakafa wote; naambiwa niunge mkono, nitaunga vipi mkonobajeti hii? Haifai. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kwa unyenyekevumkubwa na niwaombe Wabunge wenzangu wa Chama chaMapinduzi, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wao ndiowanaunga mkono hoja baada ya malalamiko marefukwamba, tukubaliane leo tuahirishe...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana, muda wako umekwisha.

Mheshimiwa Chiligati atafuatiwa na MheshimiwaMchungaji Mwanjale na Mheshimiwa Christine Ishengomaajiandae.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

54

25 APRILI, 2013

MHE. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi nichangie katika mjadala huu wamaji. Kwanza nikubaliane na wenzangu waliotanguliakusema kuhusu tatizo kubwa la maji na ni kweli kwamba,katika kero za wananchi hapa Tanzania, sasa hiviinayoongoza ni kero ya maji. Tatizo ni kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hapa tunataka kujadili jinsigani ya kukabiliana na hii kero yenyewe. Tusipoteze mudamwingi sana kushutumiana, kulaumiana, kunyosheana vidole,wananchi wanataka waone jinsi gani sisi nyumba hiitunaisaidia Serikali, kutatua tatizo hili, hilo ndio jambo kubwaambalo liko mbele yako. Wala siungi mkono hoja kwamba,baadaye tuahirishe kuzungumza, tuzungumze sasa hivimpaka tumalize, kwa nini tuahirishe jambo ambalolinawakabili wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hoja nyingi zimetolewa zenyelengo la kutufikisha kwenye kutatua tatizo lenyewe nawananchi ndio wanasubiri. Moja ambalo limetoka hapa nikwamba, bajeti ni finyu haitoshi na kwamba, sasa tutafutenamna ya kuiongeza.

Mheshimiwa Spika, namshukuru Waziri Mkuu, asubuhi.Wakati anajibu maswali, nadhani li l ikuwa ni swali laMheshimiwa Mbowe, ametoa ahadi kwamba, watakaakutazama, wanyofoe katika mafungu ya OC mbalimbali, ilibajeti ya maji iongezwe. Nadhani hili, kwa muda mfupituliunge mkono, wala tusitie mashaka. Kuna rafiki yangummoja kasema yeye ana mashaka kwamba, hii kauli yaWaziri Mkuu ina mashaka; kwa nini tuwe na mashaka na WaziriMkuu?

Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu hawezi akasimamahapa, akatoa kauli ambayo hataitekeleza. Kwa hiyo,naiomba Serikali, itekeleze ule ushauri wa asubuhi wa WaziriMkuu, watazame baadhi ya mafungu yale ya OC, tunyofoenyofoe ili tuongeze bajeti ya maji, tutatue tatizo la majiambalo wananchi wa Tanzania wanasubiri majawabu ndaniya nyumba hii. Wananchi hawasubiri malalamiko, wanasubiri

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

55

25 APRILI, 2013

majawabu, kwa hiyo, moja ya majawabu tupunguze katikamafungu mengine ya OC, tuongeze bajeti ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili ni la muda mfupi, lakini kwamuda mrefu tunaishauri Serikali, kwamba, tatizo hil itusiendelee kulitatua kwa utaratibu wa kawaida, kwa bajetiya kawaida, business as usual, hatuwezi. Lazima tutafute hatambinu zingine zaidi ya huo utaratibu wa kawaida. Wala huumradi wa World Bank, tusiutegemee sana kwa sababu, kwamiaka mingi haujaonesha matunda, twende zaidi nje ya box.

Mheshimiwa Spika, watu wameshauri hapa nanakubaliana nao kwamba, hebu sasa tuunde chombokingine, kama kwenye barabara tumeunda chombo(TANROAD) na kinafanya vizuri, barabara tunaziona.

Mheshimiwa Spika, pia kwenye umeme tumeundachombo (REA), kinafanya kazi nzuri na matunda tunayaona.Hebu nayo maji haya nayo tuyaundie chombo ambachokitapata bajeti ya Serikali, kitapata mikopo ya nje na ndani,ili tuongeze bajeti ya maji.

Mheshimiwa Spika, hii inawezekana kabisa, tuwe nakitu kama REA kwenye umeme na kitu kama TANROADkwenye barabara, hivyo kwenye maji nako tunahitaji chombokama hiki. Nadhani Serikali, hili mlichukue na mwakanitutakapokuja tusije katika hali kama hii, tuje katika halinyingine yenye kuleta matumaini makubwa zaidi kwawananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa niende Manyoni. Wilaya yaManyoni, kuna sehemu mbili, moja iko juu kwenye plateau,moja ni Bonde la Ufa. Sasa kwenye bonde la ufa ndio tunashida kubwa kabisa ya maji. Ni shida kubwa kwa sababu,tukichimba kule kwenye bonde la ufa, ama hupati maji auunapata maji ya chumvi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaishauri Serikali naMheshimiwa Waziri nimeshamweleza tatizo hili kwamba,

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

56

25 APRILI, 2013

tusiendelee kuchimba kule kwenye bonde la ufa kwa sababu,ama tunakosa maji ama tunapata maji ya chumvi; mkitakakutusaidia, tumewaambia.

Mheshimiwa Spika, pale kwenye Salanda escapment,ule mwinuko wa Salanda pale, wamechimba visima, maji nimengi. Naishauri Serikali kwa mara nyingine, hebu chukuenimaji kwenye mwinuko wa Salanda kule, kuna eneo linaitwaMbwasa, visima tayari vipo na vina maji mengi. Yale maji sasamyateremshe kwenye vijiji vyote vya bonde la ufa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Wazirinilishamkaribisha aje atazame eneo hilo, alishanikubalia nanadhani Bunge hil i kabla halijakwisha tutakwendanimwoneshe. Tukifanya hivyo Mheshimiwa Waziri, lile bondela ufa, Wilaya ya Manyoni, ambalo lina shida kubwa kabisaya maji hiyo shida itakwisha kwa sababu, maji yapo tenaunayateremsha kwa gravity kwa sababu, Salandaescapement, mwinuko ule uko juu na vijiji vyote viko chini yabonde huku. Ni kutandika mabomba na kuweka matenki,maji yanakwenda tu kwa kumiminika kwa sababu ni gravity.Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri, kabla Bungehalijakwisha twende nikamwoneshe hilo eneo;alishanikubalia, bajeti yake ikishakiwisha namkaribisha.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho kabla kengele haijalia,suala la uvunaji wa maji. Hili nalo Serikali tumeishauri, lakinitumelifanyia mzaha mzaha mwingi sana, sasa tuache. ngazimbili, ya kwanza, kila mtu anayejenga nyumba ya bati auya vigae kuwe kuna Kasheria kakumlazimisha achimbe liletenki la chini pale, maji yakitoka kwenye bati lake yaendechini, ni akiba yake. Hili linawezekana kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ngazi ya Serikali, mito hii ya muda,wakati wa msimu mito inapitisha maji mengi sana, lakinikuyakinga inabidi tupate mabwawa madogo madogo, naloni jambo ambalo hatujaliwekea mkakati. Naishauri Serikali,tuweke mkakati, kila Mto tuuzibe tu, tutapata maji ya kutoshakabisa. Hata sisi ambao tuko katika maeneo ya ukame huwa

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

57

25 APRILI, 2013

tuna mvua fupi, maji yanapita yanapotea. Sasa maji yaletunataka kwanza tuweke mkakati wa Wizara na Halmashaurizetu, tuweze kuziba ile mito, tupate mabwawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkonohoja.

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita MheshimiwaMwanjale atafuatiwa na Mheshimiwa Ishengoma naMheshimiwa Juma Nkamia ajiandae.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekuchangia katika hoja hii ya maji. Kwa kweli, tatizo la maji nikubwa.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika tathmini yaharaka haraka kwa kweli, maswali mengi yanayoulizwa hapayanahusu maji. Hiyo inaonesha kwamba kweli, tatizo la majini kubwa na hakuna Mbunge hapa ambaye atasema anausalama katika Jimbo lake kuhusu ya maji.

Mheshimiwa Spika, maji ni tatizo kubwa na nafikiritutashutumiana hapa, tutatukanana, tutasema haya na yale,lakini hayatasaidia kitu kwa sababu, hata tungemwambiaMaghembe, hela atapata wapi? Si ni lazima sisi tuamuehapa, tuzungumze hapa kitu cha maana hela zipatikanekuhakikisha kwamba, tunamsaidia Mheshimiwa Maghembena mwenzake, wapange mipango vizuri tena, lakini suala lamaji ni tatizo kubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli, tunahitaji kwamba,suala hili lingekuwa ni tatizo la ku-solve kwa haraka kwasababu, kuna miradi ya maji ya Vijiji Kumi imekwenda zaidiya miaka 10, hata kijiji kimoja kinashindwa kutekelezwa. Kwahiyo, nina maana kwamba, kwa hela ya Benki ya Dunia, kwakweli, hapa tumeshindwa.

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

58

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni vizuri Serikali, iangaliemfumo mpya wa kutafuta hela zingine, vyanzo vingine vyafedha, lakini kwa Benki ya Dunia, hapo nasema kwamba,kwa kweli, tumeshindwa. Kama kuna miradi imetekelezwakwa hela ya Benki ya Dunia ni michache sana.

Mheshimiwa Spika, miaka 10 vijiji 10 havijakwisha.Tutakwenda miaka zaidi ya 30 hapa kumaliza Vijiji Kumi namfano, mimi nina vijiji 148. Kwa hiyo, katika vijiji 148 ina maanampaka watu wote tutakuwa tumeshakufa humu ndani ndiowatapata maji wengine, kwa hiyo, kuna faida gani?(Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ni vizuri vyanzo vingine vya fedhaza maji vitafutwe na ingekuwa ni vizuri hela hilo zipatikanesasa, kwa mwaka huu 2013/2014. Tukienda 2014/2015,wananchi wataona hapa sisi tunakwenda kwa ajili yauchaguzi tu, wala haitakuwa na tija. Naomba itafutwe helaya kutekeleza Vijiji hivyo Kumi viishe wakati huu 2013 na 2014,angalau tuanze kwa hapo, maana vijiji ni vingi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwamba, kwakweli, suala hili la maji limetusikitisha sana kwamba,halitekelezwi. Miaka yote tumejaribu kuzungumza, kila tukikaahapa, ahadi ni zile zile, lakini maji hayaendi, tutafika wapindugu zangu?

Mheshimiwa Spika, mimi kwa pale Mbalizi, mji wanguule wa Mbalizi, ni mji ambao una watu wengi wanaelekeakwenye 60,000 au 70,000. Nimeahidi maji muda mrefukwamba, maji haya yataboreshwa, lakini mpaka sasa hiviinaelekea kwamba, katika bajeti, ukisoma vitabu hakuna kitukinaoneshwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba Serikali, ijitahidikuhakikisha kwamba, miradi hii ambayo iko kwenye mpango,

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

59

25 APRILI, 2013

kwenye programu, iishe kabla hatujafika huko mbele. Tuwena historia na sisi kwa sababu, kama hawatapata maji kwawakati huu, mwaka huu 2013/2014 kwa kweli, Mbeya itakuwani tabu; tunajiletea moto mbaya kabisa ambao utatuunguza.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali, iwe makini nanafikiri ni vizuri, kama walivyosema wengine, zitafutwe helaza haraka kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, miradi hii ambayokwa kweli ipo inatekelezwa kwa haraka zaidi. Nje ya hapotutakuwa tunapiga kelele tu ambayo haitakuwa na maana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, itakuwa si vizurikuzungumza jambo hilo hilo watu wote hilo hilo. Kwanzaingekuwa tangu asubuhi kuna hela mahali tungesemajamani, hata mjadala uishe, kama Serikali ingesema jamanikuna pesa zimepatikana mahali, tusingekuwa na manenoya kusema hapa. Lakini watu wanapiga kelele, watuwanataka kulia humu ndani, wanazungumza kwa emotionkwa sababu, shida ni kubwa katika Majimbo yao; barabaraangalau kidogo wanajitahidi, lakini suala la maji ni kubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wataalam wa maji ni kamahawapo, wako wachache sana, kwa hiyo, hata miradi ileikiambiwa kwamba itatekelezwa, inachukua muda mrefumno.

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

60

Mheshimiwa Spika, halafu pia pesa kutoka, ziendekwenye mradi huko nazo zinachukua muda mrefu mno. Kunanini huko, Serikalini jamani? Tupatieni hela haraka, kama kunamradi unatakiwa utekelezwe haraka, hela zitolewe kwaharaka lakini hela zinatolewa kwa shida kubwa sana. Kamahela hakuna si tuwaambie! Wananchi tumeshawaahiditumewaambia vijiji hivi vitapata maji, wanasubiri miakamitatu, minne, maji hayapatikani, tutaeleweka kwa watu?Unaweza kwenda kesho kifua mbele unasema jamanimnichague tena? Itakuwa ni mchezo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iliangalie sualahili kwa umakini tena wa hali ya juu kabisa kuhakikisha kwakweli maji yanapatikana kabla hatujafika mwaka 2014 zaidiya hapo hakuna. Aidha, nawaomba ndugu zanguWabunge, tuhakikishe kwamba Serikali kwa vyovyote vile,hata kama ungesema unanikata hela yangu, mimi ningesemasawa tu, cha msingi ni kwamba wananchi wangu wapatemaji. Mtu mmoja hapa alisema jana 15% ya hela za OC ziendekwenye maji, tunasita nini hapo kama hatuna hela! Tukisubirihela ya Benki ya Dunia hawa Wazungu wanatuchezea tu,wewe miaka kumi hela hazitoki, vijiji vimeshaainishwa tayarilakini hela haitoki na masharti yao ni makubwa mno. Kwahiyo, tukiangalia na kufikiria hela za Benki ya Dunia, tutakuwatumepotoka vibaya sana. Ni afadhali tufikirie hela zetuwenyewe, ombaomba mara nyingi anapata shida na mtuanayeomba mara nyingi kuna shida yake, kheri kutoa kulikokupokea. Tunapokea kila siku, tunapokea mara nyingine kwamatusi na kwa shida na kwa dharau kubwa sana halafumambo hayatekelezwi.

Mheshimiwa Spika, kule kwangu kulikuwa na mradiambao ulishakubaliwa kuwa utapewa hela yake lakiniumesumbua kwelikweli, mradi wa Iwahanje japokuwa sasahivi wanatengeneza lakini umechukua muda mrefu. Hiiinatokana na wataalam na hela ya benki wanasemamasharti fulani mmekiuka, sasa hii ya masharti tutafika nayowapi? Ndugu zangu wa Serikali, tunaomba hiyo hela ya majivijiji kumi ipatikane kwa mwaka huu, tukienda mpakamwaka kesho, mwaka 2014/2015 tumeshapotoka tayari.Watu watajua hawa ni waongo kwa sababu kwa miaka

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

61

kumi wametuvumilia na bado maji hawapati, mwishowatasema hawa watu waongo wameona uchaguzi ndiyowanaleta maji wakati huu, naomba hela zipatikane mwakahuu. Mimi naomba hela zipatikane sasa na tuzungumzie hiyoWabunge wenzangu, hela za vijiji kumi zipatikane sasa, siyomwaka kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo,nakushukuru. (Makofi)

SPIKA: Haya! Mheshimiwa Dkt. Christina Ishengoma,atafuatiwa na Mheshimiwa Nkamia.

MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: MheshimiwaSpika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, watu wote tunafahamu kuwatatizo la maji ni kubwa sana hapa nchini na hasa vijijini. Majini changamoto kweli. Maji safi na salama bado nichangamoto kweli kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, hali ya utoaji wa huduma ya majihapa nchini mpaka sasa hivi ni 58.6% kwa wastani katikamaeneo ya vijijini na wastani wa 86% katika maeneo ya mjini.Lengo letu tu nafahamu kuwa kuja kufikia mwaka 2015 ni95% kwa mjini na 65% vijijini. Nashauri hii Serikali yangu tuwezekujipanga tutatue kero hii ya Watanzania hasa huko vijijinina hasa kina mama ambao wanateseka kila siku kutafutamaji. Kwa kusimamia na kutekeleza malengo na mipangoyote, tunaweza tukafaulu kupatikana maji kwa hawaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni bajeti. Kamawalivyosema Wabunge wenzangu, kila mmoja anasemakuwa bajeti imepungua na kweli bajeti imepungua kilamwaka. Kwa hiyo, naungana na wenzangu tuweze kuonani wapi ambapo tunaweza kutafuta hela kusudi tuwezekuongezea bajeti na kutatua hili tatizo la maji hasa kwaWatanzania. Nashauri kuwa tuongee, tuangalie, ni wapi hasatunaweza tukapata hela tukaweza kutatua hili tatizo.(Makofi)

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

62

Mheshimiwa Spika, uharibifu wa mazingiraunachangia sana kutopata haya maji na nashauri wananchina mipango mizuri ya Serikali ya kupanda miti. Kila mmojaanajua kuwa miti inasaidia kwenye kuleta mvua kwa pamojatuweze kusaidia kulinda vyanzo vya maji na hasa kwakupanda miti rafiki ya maji pamoja na kupanda mipakakuzunguka vyanzo vya maji kusudi zisiweze kuharibiwa kwasababu vyanzo vya maji vinaharibiwa na binadamu hasakwa upande wa kulima na mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni upande wauvunaji maji. Uvunaji maji kwa makabila mengine ni tabia.Anapojenga nyumba ya bati, anaweka makinga maji. Kwahiyo, naomba wananchi tuwe na tabia ya kuweka makingamaji angalau tuweze kuvuna maji ya kutumia nyumbani piatuweze kuchimba mabwawa kwa matumizi ya mwakamzima hasa wakati wa mvua wakati ambapo majiyanakuwepo tuyatumie tusiache yaweze kuharibika bure.Kwa hiyo, tuwe na mipango kabambe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikija kwa Mkoa wa Morogoronapo bado hatujapata maji ya kutosha. Mara kwa maratumeona Manispaa hata vij i j ini watu wamekuwawanasumbuka sana kutafuta maji. Kwa hiyo, nashauri Serikaliyangu, narudia tena tuweze kutafuta hela za kuwasaidia.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Morogoro ni 64.5%vijijini ndio wanaopata maji na 62.3% mijini wanapata maji.Mtashangaa kwa nini mijini wanapata maji kidogo.Wanapata maji kidogo kwenye Manispaa kwa sababuMorogoro inapanuka, Manispaa inapanuka, kwa hiyo watuwamekuwa wengi wanahitaji maji, kwa hiyo, mipangokabambe iweze kuwekwa. Nashauri kuwa kwa kutatua hilitatizo, hii mipango mizuri ya vijiji kumi iweze kutimilika,ikitimilika tatizo la maji linaweza likapungua hasa kwawananchi wote kwenye Halmashauri zote kwa sababu vijijikumi vinapelekwa kwenye Halmashauri zote za nchi yetu yaTanzania na Watanzania wanaweza kupata maji salama namaji safi ya kutosha.

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

63

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, ujenzi wa Bwawala Kidunda ni mpango mzuri sana. Bwawa hili linapatikanaMkoani Morogoro Vijijini na maji haya yatakwenda kuongezamaji kwenye Mto Ruvu ambayo haya maji yatasaidia kwenyeMikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani. Ombi langu nikuwa hivi vijiji vinavyozunguka hili bwawa na vyenyeweviweze kupata hayo maji, wananchi waweze kufaidi hayomaji pamoja umeme ambao utatokana na bwawa hili. Vijijivyenyewe ni kama Selembala pamoja na Mzia, wananchiwana matatizo sana ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine nilikuwa naombatuweze kufikiria vijiji vya Mtego wa Simba, Lukole, Fulwe,Mikese pamoja na Mikumi, wana matatizo sana ya maji nawenyewe kwenye mipango hii ya maji waweze kupatiwamaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naongelea pia bwawa la Igurubapale Isimani Iringa, ilikuwa ni gumzo sana lakini safari hiinimeona kama tumetengewa hela. Naomba hizi hela zotezilizotengewa ziweze kufika huko kwa wananchi kusudiwaweze kufaidika kutumia hayo maji kwa kilimo pamojana matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana ila tatizo la maji bado ni kubwa, naombatuliangalie kwa macho yote mawili.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsantesana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa ni Mheshimiwa Juma Nkamia,Mheshimiwa Hussein Nassor Amar na baadaye.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi nimshukuruMwenyezi Mungu pia kwa kuniamsha salama ili niwezekuchangia bajeti hii ya Wizara ya Maji.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

64

Mheshimiwa Spika, nisipoongelea tatizo la maji katikaWilaya ya Chemba, nadhani hukumu yangu itakuwaimebakiza miaka miwili na nusu tu. Nianze tu na hili suala lamradi wa Ntomoko, Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokujaaliahidi na kwenye bajeti nimeona, naamini kwambautafanikiwa na wananchi wa Kinkima kule, Churuku, Hamaina maeneo mengine watakuwa wanasubiri kwa hamu sana.Kina Mzee Ikanda kule wamechoka kila siku kutembeakwenda kufunga yale mabomba ili maji yatoke, naamini sasasuala hili litafikia kikomo.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni suala la bwawa laFarkwa. Project hii imekuwa ikizungumzwa na katika bajetiya mwaka jana ilitengewa shilingi milioni 800 tulionawataalam fulani sijui ni wataalam au Wazungu walikuwawanakuja kule, inawezekana ndiyo wanafanya jambo hilo.Kwa hiyo, tunaamini kwamba kama jambo hili litafanyikakwa haraka tatizo la maji katika Wilaya Chemba litakuwalimepungua. Naiomba Wizara ifahamu kwamba hili bwawala Farkwa pia litumike kwa ajili ya kupeleka maji Chembana si kuleta Dodoma mjini peke yake.

Mheshimiwa Spika, kwenye miradi hii ya maji ya WorldBank, visima vya Benki ya Dunia, visima viko tayarivimechimbwa muda mrefu sana na vingine ambavyovilikuwepo kwenye project ya benki ya Dunia nilivichimbamimi kwa kutafuta wafadhili, kinachotakiwa sasa ni kwaWizara kupeleka hela tu kwa ajili ya kuweka pump watuwanywe maji. Jambo hili linachukua muda mrefu sana. Mserakuna kisima kipo tayari, Mwaikisabe kipo tayari, Chemba kipotayari tena cha ajabu Chemba ndio Makao Makuu ya Wilayahii ya Chemba hata kwenye bajeti ya mwaka huu hakipowala hakihitaji zaidi ya shilingi milioni 55. Jenjeluse kipo tayarina kina maji mengi zaidi ya 80,000 cubic per hour. Nadhanivitu hivi ni vizuri tuangalie, Kelemakuu shimo lipo maji yapotatizo ni hilo na Wizara waliomba tuwapelekeetumewapelekea, Chandama tuna matatizo, Mapango halikadhalika na Jangalo.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

65

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri anisaidie jambomoja dogo sana, Mlongia tumechimba kisima sisi kwa fedhatulizotafuta wenyewe, kinatoa karibu lita elfu nane na kitukwa siku kwa saa. Tukaambiwa tupeleke Wizarani ili wawezekukiingiza kwenye bajeti kwa ajili ya kufunga mitambo. Kilaukimuuliza Mhandisi anasema kwamba Wahandisi wa Wizarawamesema hawawezi kufanya lazima wao wenyewewaende Kondoa na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoaikawaambia tuko tayari kuwagharamia kutoka Dar esSalaam mpaka Kondoa, miezi minne sasa jambo hilihalijafanyika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo namwombaMheshimiwa Waziri jambo hili alitilie maanani, tatizo ni nini?Wahandisi wa Halmashauri hawaaminiki ama kuna nini hapampaka wataalam watoke Dar es Salaam waka-verifykwamba je kweli kisima hiki kipo? Basi naomba hawaWahandisi ambao pengine hawawaamini Wahandisi waKondoa waende basi wakatusaidie jambo hili.

Mheshimiwa Spika, kisima cha Mlongia kinaweza ku-save not less than twenty five thousand people kikasaidiaJangalo kikasaidia Itolwa lakini tatizo ni suala la kufanyamaamuzi tu. Najua kuna matatizo ya fedha, tofauti kwenyebarabara, hela nyingi inakuwa injected kwenye barabaralakini maji ni muhimu sana hata ukipita juu ya barabara yalami unahitaji kuoga pia. Kwa hiyo, naomba sana hilomtusaidie.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna baadhi ya maeneokatika visima hivi ambavyo tulishachimba kwa mfano Ombilipale, tumechimba kisima kinatoa karibu lita 7,000. Nikawekamashine mimi mwenyewe siyo chini ya shilingi milioni 25,efficiency yake ni kubwa zaidi kuliko hata zile mashinezinazowekwa na Halmashauri ama na Wizara. Kwa hiyo,ningeomba pengine wataalam wa maji wa Wizarawatakapokwenda kama watakwenda huko Kondoaangalau wapite pale Ombili wafanye feasibility study kidogo,ni namna gani tumeweza kufanikiwa kufunga mashine paleOmbili kwa gharama ndogo sana ya shilingi milioni 25 nakisima kinahudumia bila matatizo yoyote.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

66

Mheshimiwa Spika, siwezi kusema Waziri achotekidogo zile za kwenda Mwanga anipelekee pale Mlongialakini Waswahili wanasema paka si rangi, umuhimu nikukamata panya. Kwa hiyo, nakuomba jambo hili unisaidie.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, nasema naungamkono hoja. (Makofi)

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kuchangia hoja hiilakini kwanza napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu ambayeameniwezesha kunipa afya na kuweza kusimama hapa leo.

Mheshimiwa Spika, tatizo la maji, ni tatizo kubwa sanana Wabunge wote wamechangia. Yaliyowagusa katikaMajimbo yao hata mimi ni hivyo hivyo lakini kuna msemoWaswahili wanasema ukitaka kumlaza mtoto mwimbiewimbo mzuri. Pia mtoto huyo ukimwimbia wimbo huohuosiku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu inawezekana asilale.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kusema hivyo kwasababu Jimbo langu la Nyang’wale leo ni mwaka wanguwa tatu nazungumzia suala hili la maji, matatizo ni makubwasana katika Jimbo hilo. Ukiangalia matatizo hayoyamesababisha mpaka vifo kwa ajili ya kutafuta maji. Leotakribani mwezi wa pili kuna kifo ambacho kimetokea, kinamama wamegombana kisimani kwa ajili ya kugombea majina mmoja ikawa amefikia kupatwa na umauti.

Mheshimiwa Spika, kwanza nasema siungi mkonohoja. Kwa nini ninasema hivyo, wananchi wa Jimbo laNyang’wale kutokana na matatizo ya maji waliyonayo kwamuda mrefu watanishangaa sana kwa nini naunga mkonohoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli Serikali naiombaiongeze bajeti yake, bajeti hii haitoshi. Nikiangalia kwenyekitabu hiki tumepangiwa kama shilingi milioni 316, mimi ninakata 12 vijiji 54 na mahitaji ni makubwa sana kuliko hizo

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

67

shilingi milioni 316. Mwaka jana niliuliza swali hili la maji,nikaambiwa nimetengewa shilingi milioni 30 kwa ajili yaupembuzi yakinifu lakini pesa hizo hazijaingia na walahazijulikani ziko wapi lakini maji haya yako ndani ya Jimbolangu, Ziwa la Victoria liko Jimboni kwangu, ni nusu kilomitatu lakini kijiji cha mwanzo kutoka Ziwani pale kinaitwaNyamtukuza hakina maji na Jimbo langu kutoka ZiwaVictoria kwenda kijiji cha mwisho kwenye Jimbo langu nikilomita 40 lakini Jimbo hilo halina maji. Niliishauri Serikalikwamba itenge pesa kwa ajili ya kufufua mtambo wa majiuliopo Ziwa Victoria pale ambao umesimama tangu mwaka1975 na ulikuwa unasambaza maji zaidi ya vijiji 15 lakinihakuna jibu lolote mpaka leo hii, kwa hiyo, sina haja ya kuungamkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, matatizo yaliyosababishwa namaji, kuna matatizo mengi, maradhi mengi, minyoo, typhoidna malazi mengine ambayo yanasababishwa na unywaji wamaji machafu na yasiyo salama. Pia maji yamesababishamimba zisizo rasmi kwa mabinti zetu, yamesababisha ndoanyingi kuvunjika, yamesababisha hata wanafunzi wetukutofanya vizuri katika mitihani yao kwa sababu ya mudamwingi kupoteza kwenda kutafuta maji. Kwa kweli Jimbola Nyang’wale lina matatizo makubwa sana ya maji na majiyametuzunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa ushauri kwaSerikali yangu kwamba iwahamasishe sasa wananchiwaweze kuchimba ama kujenga visima katika maeneo yaona pia katika shule za msingi na sekondari ili kuwezakupunguza tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Jimbo langu kunamaporomoko mengi ya maji, kuna mabwawa ambayoyameshapasuka zaidi ya miaka 15 na mabwawa hayoyalikuwa yanaweza kusaidia zaidi ya vijiji 15. Kuna bwawala maji lililoko Nyang’hwale ambalo limebomoka zaidi yamiaka 15 na kuna bwawa ambalo limebomoka kwenye kataya Shabaka, sehemu ya Shabaka panaitwa Nyamgogwa,bwawa lile na lenyewe lilikuwa linasaidia sana zaidi ya vijijikumi. Kwa hiyo, naiomba Serikali, bajeti hii iongezwe ili na

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

68

Nyang’hwale iweze kupata maji na kupunguza tatizo la majikwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo, mimisiungi mkono hoja mpaka Serikali ituongezee pesa katikabajeti hii ndiyo nitakapoweza kuunga mkono hoja kwasababu wananchi wa Jimbo la Nyang’hwale hivi sasawananisikiliza, tatizo ni kubwa sana. Viongozi mbalimbaliwamefika katika Jimbo hilo, kina mama wanawaimbiavizuri, wanawakuta wamependeza ni kwa ajili ya ugeni huolakini baada ya hapo ukienda ghafla kwenda kuwatembeleautakuta hali zao si nzuri kutokana na ukosefu wa maji.Viongozi wahurumieni hao kina mama ambao sasa hiviwanaota vipara kwa ajili ya kufuata maji kwa umbali mrefu.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kina mama hao, wanawaimbienikwa furaha, hawahitaji zile pesa ambazo huwa mnawatunzashilingi 2000/3000, wanahitaji muwahudumie hususani upandewa maji. Serikali ninaiomba ituangalie kwa jicho la huruma.Hata Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye kampeni mwaka2010, alituahidi kupata maji kutoka Ziwa Victoria. Mtandaohuo siyo kwamba haupo, upo! Mpaka leo matenki ni mazima,baadhi ya mabomba yapo, tunashangaa kwa nini mtambohuo haufufuliwi na ni asilimia labda sabini na tano tuulioharibika lakini asilimia ishirini na tano mitambo yote nimizuri.

Mheheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais alipotuahiditulikuwa na matumaini mazuri. Mimi nasema kipaumbele chakwanza kwa Jimbo la Nyang’hwale maji, kipaumbele chapili maji, kipaumbele cha tatu maji, hatuhitaji umeme,hatuhitaji barabara, tunahitaji kwanza maji. Maji, halafuvifuate vitu vingine kama barabara pamoja na umeme,vyote ni muhimu lakini maji ni uhai. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo siungimkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

69

SPIKA: Namwita Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya,halafu Mheshimiwa Abdulsalaam Ameir, yupo? Atafuatiwana Mheshimiwa John P. Lwanji.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuungana naMheshimiwa Moshi Chang’a, DC wa Wilaya ya Kalamboambaye amefiwa na mke wake. Naomba Mwenyezi Munguawape faraja na mazishi yatakuwa kesho saa tisa, kwa hiyo,naungana nao na Mungu awepe faraja.

Mheshimiwa Spika, kimsingi Waheshimiwa Wabungewengi wamechangia kwa huzuni kubwa juu ya tatizo la majinchini Tanzania. Hali kadhalika nami siwezi kuwa kinyumejuu ya suala hilo kwa sababu ni ukweli ambao uko wazi nawananchi wengi wanahitaji maji.

Mheshimiwa Spika, kuna mambo ambayo sisiWabunge au viongozi tunaweza tukayaona kama ndiyopriority hasa kutegemea na taswira au dira ya nchitunakotaka twende lakini ukienda kwa wananchi hawa wakawaida, wao wana vipaumbele vyao na ni vile ambavyovinawagusa katika maisha ya kila siku. Ukienda kuongea nawananchi, ukawauliza nini kipaumbele chao, wanaumewatakuambia elimu, watakuambia barabara; wanawakewatakuambia maji, watakuambia suala la afya. Hayo ndiyomambo yaliyopo huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli, maji ni kikwazokikubwa cha maendeleo ya kiuchumi. Kwa sababu kamahakuna maji salama, ina maana ndipo inakuwa chimbukola magonjwa na ndipo tunapofikiria kuwa na dawa nyingikatika vijiji, dawa nyingi kwa ajili ya watu ambayo nayo yanaathari katika miili yao. Kwa hiyo, kama tutaweza kuwa namaji safi na salama, tunaweza kupunguza bajeti katikamaeneo mengine hasa ya afya.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

70

Mheshimiwa Spika, maeneo ya vijijini hata katikaZahanati, unakuta hakuna maji safi na salama na ndikowanakojifungulia akina mama, ndiko wanakopatamagonjwa na ndiko tunapojaribu kupunguza vifo vya akinamama na watoto. Maji yana mchango mkubwa katikakupunguza vifo vya akina mama na watoto hasa waliokochini ya miaka mitano, wasiojitambua na wanaowezakunywa maji ambayo hayajachemshwa.

Mheshimiwa Spika, suala langu hili naomba nilielekezekatika sura hii. Wote tumezungumza juu ya tatizo hili, lakinitunalizungumza sasa. Najaribu kuona kwa upande wetu sisiwenyewe, kama Wabunge, hivi leo sisi Wabunge tukiulizwakatika mijadala yetu yote tunayoijadili humu ndani,kipaumbele chetu namba moja ni kipi, namba mbili ni kipi,namba tatu ni kipi? Mtakubaliana na mimi kwamba maranyingi kadri ya bajeti inavyokuja hapa, kila bajetiinachangiwa kwa kipaumbele kilekile. Tukifungua sasa hiviHansard, siku ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, tukifungua siku yaUtumishi, tukifungua siku ya Kilimo, utakuta kila aliyechangiaalitoa priority kwa eneo lile. Kwa hiyo, tunakuwa hatunamawazo ya pamoja kwamba sisi tuko katika msimamo upikama nchi.

Mheshimiwa Spika, mimi nasema kwamba, kwanzapamoja na kwamba Mheshimiwa Spika unasema pongezisiyo za muhimu, mwanamke mwenzetu lazima tukupongezekwa kutoa huu mtindo mpya wa kusema kwamba Bungetuanze kujadili bajeti muda huu kabla ya muda ule ambaounatakiwa mwezi wa saba ili kuwezesha mabadiliko yamsingi. Suala hilo, watu wanaweza wakaliona ni mabadilikomadogo. Haya ni mabadiliko makubwa sana, yana impactkubwa sana na yana mchango mkubwa sana katika bajetiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hali hiyo basi, mimi najaribupia kujiuliza. Kwa mfano, sasa hivi tunasema tukate kwenyeOC sioni taabu lakini kila wakati napenda kujiridhisha. HiyoOC tunayoikata ilikaa hapo kwa ajili gani? Nini maana yaOC, ipo hapo kwa ajili gani? Kwa sababu hata katika hii

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

71

miradi ya maendeleo, utakuta kama gari litahitajika kutumiamafuta kwenda kutembelea huo mradi au shughuli yoyoteinayoendana na mafuta, package yake inajitokeza kwenyeOC. Kwa hiyo, unaweza ukaweka pesa ya maendeleo yakufanya ile shughuli ukajikuta hauna fedha ya kufuatilia ulemradi, nalo hilo ni tatizo. Pia, nasema kwamba tusiangalieOC kama kitu hasi, lakini tuende ndani zaidi. OC hiiiliyowekwa hapa ni kwa ajili ya nini? Ile ambayo ipo kwa ajiliya mambo ya viburudisho, mambo ambayo siyo ya lazima,posho labda pengine kama za sisi Wabunge hapa ndani,basi hizo tunaweza tukasema labda pengine tupunguze sisihayo lakini tuwezeshe ile miradi kuweza kwenda mbele.

Mheshimiwa Spika, katika hii miradi ya maendeleohuwa ina utaratibu wake wa mchakato. Kwa mfano, mradihuu uzungumziwa zaidi, mradi wa Same - Mwanga. Mradihuu haujanza leo na mpaka wale wanaotoa pesa wamekujakuukagua wakaridhika, wakasema basi tutoe pesa kwa ajiliya mradi fulani ambao gharama yake ni kiasi fulani. Leotukisema tunakata zile pesa tunapeleka sehemu nyingine,siyo hiari ya wahisani. Wahisani wetu wanapotoa pesawanatoa kadri wanapovyojisikia na matakwa yao. Ndiyomaana unakuta kwamba, hata kama una shida kwenye eneojingine, lakini kama wao kwa wakati huo siyo priority yao,unakuta hatuwezi kuhamisha. Kwa mfano, wao sasa hiviwao priority yao ni kusaidia vyama vya siasa, labda priorityyao ni kusaidia demeokrasia, kwa hiyo, unakuta hata kamawewe unalia maji, kama hiyo siyo priority yao sasa hivi,hawawezi kupeleka pesa huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa nashauri mradi huotusiupige, siyo kwa sababu Mheshimiwa Waziri wa Majianatoka huko, basi wananchi wake wapate shida, eti kwasababu sisi tunasema amepeleka kwao, hapana. Lazimawananchi wale watendewe haki sawa na wananchi wamaeneo mengine. Mradi huu mimi kwa kumbukumbu zangunaamini ulipita wakati wa Waziri wa Fedha, tenaMheshimiwa Mkulo hapa amenipa ushahidi na wengine sikuza wa nyuma hata wakati huyu Waziri hajawa kwenye eneohili. Tusimfanyie hivyo, wananchi sasa watasema tusimchague

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

72

mtu ambaye atachaguliwa kuwa Waziri kwa sababututakuwa tunanyimwa miradi, nadhani siyo sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nami kwa kusisitiza hilo, ukiangaliatatizo la maji katika Bonde la Ziwa Nyasa, maeneo yaNgumbo, Nkili, Lundo, kwa kweli ni kubwa mno. Kuna visimavimechimbwa kule miaka nenda rudi mpaka leohavijaunganishwa. Hali kadhalika nikirudi upande wa Rukwa,bonde la Ziwa Rukwa, lile limekuwa mapped kama maeneochronic kwa magonjwa sugu ya kuhara. Kila mwaka Mkoawa Rukwa lazima upate aibu ya kipindupindu katika bondela Ziwa Rukwa, simply kwa sababu maji yanatoka kule juumilimani yanaenda kule chini, hakuna visima, hakunamabomba sawa na ambavyo Mheshimiwa Mbunge waSingida, Mheshimiwa Chiligati alipokuwa anaeleza. Maeneohaya yanakaribiana sana tabia zake na za kule Singida.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa mazingira kamahayo, mimi nachokiomba sisi kama Wabunge tukae pamojalakini pia tushauriane na Serikali yetu, kuweza kuona hatasasa hivi kama tunaongeza hiyo hela inaenda wapi? Maanasiyo tu kwamba tunapata OC shilingi milioni 600 tupelekekwenye maji, lakini kwa mradi upi? Lazima ijulikane zinaendakwenye mradi fulani na Fulani otherwise unatawanya helana miradi haikamiliki.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni juu yamakandarasi wa maji. Makandarasi wa maji hawatutendeihaki, wanalipwa hela hawatokei site kwa wakati….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika,ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa namwita Mheshimiwa JohnLwanji atafuatiwa na Mheshimiwa Ahmed Ali Salum naMheshimiwa Lusinde ajiandae.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

73

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi na mimi nichangie juu ya hoja hii ya Wizaraya Maji.

Mheshimiwa Spika, muda huu tunafikia mwisho wamvua kwa msimu huu. Ni kipindi cha kipupwe sasa kinaanzalakini siyo muda mrefu watu wetu wataanza kuhangaikakutafuta maji. Kwa muda wa miezi saba inayokuja, kwa kwelini kipindi cha kuhuzunisha na ni chakusikitisha.

Mheshimiwa Spika, nchi hii imepata misaada sanakatika eneo hili. Wafadhili wengi wamemwaga pesa kwaajili ya kutanzua tatizo la maji lakini tatizo hili linakuwa sugu.Kama alivyosema Mheshimiwa Chiligati, Wilaya ya Manyoniina maeneo mawili, eneo la juu na la chini. Sasa miminakotoka ni kwenye plateau, lakini kila wanapochimba maji,maji hayapatikani, ni maeneno machache na paleyanapopatikana labda wataalamu huwa wamekwendakushirikisha wenyeji wa maeneo hayo, wanaweza wakajuamaeneo hayo maji yanaweza yakapatikana wapi, lakinimara nyingi magari yamekuwa yakija, yanaweka mitamboyao hapo, wanasimika mitambo na kuchimba maji lakinihakuna maji. Magari yamekuwa yakirudi na watu kuwaachawakifadhaika. Wakati magari yanapofika watu wanakuwana matumaini makubwa lakini magari yanapoondokayanaacha huzuni.

Mheshimiwa Spika, mimi ninashangaa sana jinsitunavyopoteza pesa kwenye eneo hili. Katika mchakato huo,kuna watu wawili hapa, yule anayekwenda kutafiti maji,kujua eneo lile lina maji au hapana, ni mtumishi wa Serikali.Wanakwenda wanapima, wanasema eneo hili lina maji,wanaweka alama pale, halafu ndiyo mchakato wa tendaunaanza kumpata Mkandarasi wa kuja kuchimba lakini kwabahati mbaya mara nyingi inatokea, anapokuja kuchimbahuyo mchimbaji naye ni mtu mwingine; ndiyo kapewa tendahiyo, sijui ni mtu binafsi anachimba pale na anatoka palemaji hakuna. Pesa iliyoteketea pale kwa kisima kimoja siyochini ya shilingi milioni 30 na kuendelea, sasa hasara hii

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

74

imekuwa ikitokea kila siku, nani hasa anayeibeba,inamwangukia mwananchi.

Mheshimiwa Spika, mimi ningeomba tuwe seriouskwenye eneo hili. Naomba huyo mtu basi atakayekujakupima, basi apewe na dhamana ya kuchimba huyohuyokwamba akipima pale akasema hapa kuna maji, basihuyohuyo yeye mwenyewe apewe kazi hiyo ya kuchimba kwamakubaliano kwamba kama maji yatapatikana utalipwa,kama hayakupatikana hasara ni juu yako wewe. Mimi nafikiriwangekuwa na uangalifu zaidi katika kutafiti na kupimamaji, akisema hapa kuna maji, basi maji yawepo lakiniutaratibu wa sasa hivi unaliingizia Taifa hasara na wananchiwanapata shida sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaomba Wizara hii iniambie basijuu ya ahadi ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa mwaka janaalipokuja Mji Mdogo wa Itigi. Mhandisi wa Maji wa Wilayaalisimamishwa pale nusu saa, awaeleze wananchi juu yamkakati unaofanyika ili kuupatia Mji Mdogo wa Itigi maji yakutosha na mji huo unaandaliwa na baadaye utakapokuwaWilaya ikute miundombinu ya maji ikiwa safi lakininimeangalia kwenye kitabu cha bajeti sioni. Napenda kupatajibu, inaangukia wapi ahadi hii ya Rais ili watu wawezekuelewa kwamba kuna tofauti kati ya ahadi ya Rais namipango ya kawaida. Mkuu wa nchi amekuja pale naakaahidi, baada ya Mhandisi kueleza, akasema nataka hiim-fast truck, akasema anataka kuona mji huu unapatiwamaji ya kutosha lakini sijaona mpango huu na miminasimama hapa Itigi siyo mbali, napigiwa simu, wenyejiwanakuja hapa mara kwa mara na leo ninao wageni hapa,wameniuliza je mpango wa Itigi kuhusu maji ahadi ya Raisaliyoitoa je, iko katika bajeti safari hii? Kwa hiyo, ninaombamajibu wakati wa kuhitimisha ili tuweze kutendeana haki.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, watu waRungwa walikuwa na bwawa miaka nenda rudi lakini kwabahati mbaya sana, lile bwawa lilipopasuka, Serikali ilikujana ahadi nzuri na ikatenga fedha wakati ule wa Bunge laTisa, mwanzo tu tulipoingia hapa, ilitenga shilingi milioni 250,kujaribu kujenga kuta za bwawa hilo. Nasikitika mpaka leo

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

25 APRILI, 2013

75

na mimi sioni coordination yoyote kati ya Wizara ya Maji naWizara hizi nyingine zinazochangia kwenye miradi ya maji.Hii miradi ya DADPS sijui hii miradi inayochangiwa na Wizaraya Maliasili na Utalii na wao ile coordination yao iko halfhazard, sijaona seriousness yoyote. Sasa wanachi hawaeliwi,wanachotaka ni maji. Hawahitaji kitu kingine. Naombamaelezo kuhusu hilo bwawa ili na mimi niweze kuona kamanaunga mkono hoja au siungi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Wizara hii ifanye utafitijuu ya maeneo ya Jimbo langu. Kata ya Idodyandole, Kataya Gondi, Kata ya Sanjaranda, Kata ya Ipande, Kata ya Itigi,Kata ya Kitaraka mpaka kule juu unapoelekea Kata yaMgando, Mitundu mpaka Mwamaghembe ni eno la juu, majihayakai. Mvua zinanyesha vizuri lakini maji hayakai lakinikuchimba maji kama nilivyosema mwanzo linakuwa tatizo.Maji yanakuwa ni kirefu na mara nyingi maji hayapatikani.Ningeomba Serikali ifanye utafiti na ije na mkakati wakuchimba mabwawa katika maeneo hayo. Ukiweka bwawamoja pale Idodyandole, ukaweka bwawa moja paleKashanga, ukaweka bwawa lingine pale Mbungani, Kataile utakuwa umeshamaliza. Kwa kweli, haya mambomengine ya watu kutafuta maji waachwe, wafanye waowenyewe, lakini maji ya uhakika kwa ajili ya wakulima nawafugaji wa maeneo hayo, yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.Naomba sana tuwe serious katika eneo hili. Mimi sishangaikwa nini sasa hivi watu tunagombana hapa. Toka mwaka1961 tatizo hili la maji mpaka hivi sasa bado limekuwa sugu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa mimi kamawenzangu wanavyosema katika kuliangalia tatizo hili, miminaona eneo hili litafutiwe fedha za kutosha, bila hivyonadhani kutakuwa na tatizo katika bajeti hii. Mimi nawezanikasema kabisa kwamba niko njia panda, sijui niungemkono au nisiunge, ninatafakari, mpaka haponitakapopatiwa majibu ya kutosha, mimi ninasimama kamanilivyo na ninaomba nikae labda nitamke tu kwa muda huusasa hivi siungi mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

76

25 APRILI, 2013

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza, naungana nawenzangu, nasema siungi mkono hoja hii, kutokana naumuhimu wa suala zima la maji katika Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea, World FoodProgram tulikuwa tumepata shilingi milioni 104 kwa ajili yamatenki ya kuvunia maji kwenye shule zetu za msingi. Kwamasikitiko makubwa, nimepata barua tarehe 23 Aprili,wakiniambia kwamba, wametuondolea tena zile fedha kwasababu hatukusaini MoU.

Mheshimiwa Spika, sasa namwomba MheshimiwaWaziri wa Maji anisaidie hili, siyo kweli kwa sababu MoU hiihapa, siku waliyotuletea na siku waliyosaini wao tarehe 28Machi, siku hiyohiyo Mkurugenzi alisaini na aliirudisha. Sasakama wamei-misplace wao, ni suala lingine. Maamuziwaliyofanya hayakunifurahisha na mimi mwenyewe nikitokahapa nadhani nitamtafuta ili nimwonyeshe vitu hivi.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ziwa Victoria,KASHUWASA, wanafanya kazi nzuri sana katika Mkoa waShinyanga na maeneo yote unapopita Mradi huu. Tatizolililojitokeza ni kwamba, kuna tatizo baina ya KASHUWASA naSHUWASA; KASHUWASA wanaidai SHUWASA shilingi milioni 900na kuna shilingi milioni 200, almost 1.1 trillion, mpaka hivi sasaSHUWASA wanashindwa kuilipa. Sasa udhaifu huu uliojitoezaumeifanya KASHUWASA kutokufanya kazi vizuri katikakuwaletea maji Wananchi wa Shinyanga na Kahama.

Mheshimiwa Spika, mimi naomba sana, udhaifu huuunawaletea matatizo makubwa Wananchi wa maeneo yale,hasa Jimbo la Solwa, pamoja na Wananchi wa ShinyangaMjini. Serikali ifikirie kuvunja vyombo vyote hivi na kutengenezachombo kimoja tu, ambacho kitakuwa responsible katikamasuala yote ya kukusanya maji, kukusanya fedha au kodiwanayolipa wanaotumia maji haya ili sasa fedha zile zisipitiekwenye mikondo mingine.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

77

25 APRILI, 2013

Kuwe na Bodi moja na kazi hii ifanyike SHUWASA ndiyowanaochukua fedha na mpaka sasa hawajawalipaKASHUWASA. KASHUWASA wanashindwa hata kuendelezahuu Mradi, inakuwa tatizo kubwa kweli na hii inapelekea hataWananchi wa Jimbo la Solwa, ambao wamepitiwa na Mradihuu kusubiri kwa muda mrefu, kuona kwamba sasa Mradihatuupati na huduma imekuwa mbaya kweli kweli.

Mheshimiwa Spika, namwomba sana MheshimiwaWaziri wa Maji, alitazame hili, tatizo liko SHUWASA. Kuna Mradiambao sasa hivi Serikali inaufanyia upembuzi yakinifu kutokaKahama kupitia Tinde kwenda Nzega. Ninaomba sanakutokana na hii hali iliyojitokeza ya awamu ya kwanza naawamu ya pili kwenye Mradi huu wa Kahama kuja Tinde naNzega, kusiwepo na awamu ya pili. Wanapofanya upembuziyakinifu wafanye pamoja na vile vijiji vilivyopo ndani yakiliometa 12, navyo vipate maji kwenye awamu moja hiyohiyo na Mradi huo huo, siyo tena tutapitisha bomba, baadayetena Mradi wa pili, imetuchukua zaidi ya miaka minne sasahivi tangu Mradi huo utoke Helele kuja Solwa, kuja Shinyangana kwenda Kahama, miaka minne hii tunasubiria maji yaawamu ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maji ya Ziwa Victoria, uwezo wakeni lita milioni 120, sasa hivi maji yanayotumika ni lita 17 milionitu, utaona ni percent ndogo sana ya capacity ya majiambayo mashine ile inaweza ikahudumia katika Mikoa yotehiyo inayopitiwa na maji ya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Spika, naiomba sana Serikali na leoWaheshimiwa Wabunge kwenye Party Caucus ni suala hilihili la maji. Ziongezwe fedha ili Wananchi wa maeneo yotekatika Tanzania hii waweze kunufaika na maji na hasa Mradihuu wa Ziwa Victoria. (Makofi)

Hakuna msalie Mtume, mimi nasema no, tunatakafedha za kutosha, tumechoka na ukizingatia hili limo hatakwenye ahadi za Rais. Mpaka hivi sasa fedha tulizopata nishilingi 4.8 bilioni, ukitazama gharama zote hizi ni kama vijijikumi tu vya mradi mzima wa Ziwa Victoria; hivi ni kweli?

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

78

25 APRILI, 2013

Tupunguze fedha kwenye matumizi ya kawaida, ambayotumechukua mkopo wa shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya matumiziya kawaida, hebu tukamue kule kama tunakula vitumbuavinne tule kitumbua kimoja tu, safari nne tunywe safari mojatu, lakini hii tuokoe hali ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mimi sina majibu kwa Wananchiwangu zaidi ya kusema wasubirie tuone Bajeti hii itasemajekatika Miradi yao.

Mheshimiwa Spika, maji ya World Bank, nilipouliza swalilangu la nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri wa Maji, hakulijiu,sasa atakapo-wind up nataka nijue; kuna documents zetu,kuna Mkataba wetu katika Halmashauri yetu ya ShinyangaVijijini.

Katika Mradi wa Didia na wa Mshepo, ambao mpakasasa inasubiriwa kusaini kwa maana ya kumpata mshaurimwelekezi. Sasa huyu mshauri mwelekezi ni nani na hili sualala ushauri uelekezi mbona linachukua muda mrefu naunachukua fedha nyingi? Hivi Wizara wanakosa nini kuletamajibu ya haraka haraka na kama suala liko World Bank, basitunaomba majibu au myafanyie kazi. Huu Mradi uanze kazi,kwa sababu Kata ya Didia, Kata ya Mshepo, Kata ya Itwangina Kata ya Tinde, sasa hivi ni Kata ambazo Wananchiwanakuwa wengi, maji yamekuwa ya shida. Nikiendakufanya ziara yangu kule katika Jimbo la Solwa, katika watukumi wanouliza maswali, watu wanane wanauliza maswaliya maji. Hatuna majibu nayo zaidi ya kutenga fedha zakutosha kwa ajili ya kwenda kutatua tatizo hili la maji.

Mheshimiwa Spika, tunamsaidia Mheshimiwa Waziriwa Maji hapa na nyumba hii yote kwa pamoja bila kujalivyama vyetu, tusimame kuona angalau shilingi bilioni 300nyingine zinaongezeka kwa ajili ya Miradi hii ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono ule Mfuko waFedha ambazo Wizara ya Maji imeuunda kwa ajili ya kutafutafedha kwa ajili ya kutatua tatizo hili la maji. Ushauri wangukatika ule Mfuko, tusiende tu kwenye masuala haya ya kutoa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

79

25 APRILI, 2013

shilingi moja kwenye maji au sijui mnafanyaje, kunamakampuni ambayo katika utafiti uliofanywa, makampuniya madini, makampuni ya simu, hivi tukitengeneza tu percentfulani kwenye makampuni hayo kwamba wanapolipa kodikatika fedha au katika mazungumzo ya simu, shilingi mojaau shilingi mbili tu kwa sekunde, basi Mfuko huu utapata fedhanyingi sana na hata katika mjadala mzima huu wa maji kwakweli utafika mahali tutakuwa hatuna matatizo makubwasana ya kupata fedha za maji.

Sasa hivi katika Jimbo la Solwa tatizo bado ni kubwa,tunahitaji visima, kuna upungufu wa visima zaidi ya 100 nahapa ninaposema, sina namna yoyote zaidi ya Serikalikutusaidia. Mfuko huu mimi nawaomba sana WaheshimiwaWabunge tuuharakishe ili ukafanye kazi vizuri na mtoe fedhaza kutosha.

MHE. AHMED A. SALUM: Wizara ya Maji mwaka janana mwaka huu, tulipitisha fedha kwa ajili ya kupata Mradiwa Maji, 2010/2011 au 2011/12, ukitazama mwenendo mzimahapa, hakuna fedha zozote walizopata zilizoidhinishwa naBunge. Mwaka 2000…

(Hapa kengele il i l ia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante.(Makofi)

SPIKA: Haya, ahsante sana. Kitu gani, aah, sawa, simaoni yake jamani vipi! Mheshimiwa Lusinde, MheshimiwaNatse na Mheshimiwa Anna MaryStela Mallac atafuatia.

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika,kwanza, namshukuru Mungu kupata fursa hii ya kuzungumzandani ya Bunge lako tukiwa na mjadala unaohusu maji.

Mheshimiwa Spika, nianze na msemo unaosema;kwenye miti mingi hakuna wajenzi. (Makofi)

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

80

25 APRILI, 2013

Watafiti wengi ambao wamewahi kutafiti masuala yamaji, wanaitaja Tanzania kuwa ni nchi mojawapo yenye majimengi sana. (Makofi)

Tuna maji mengi sana kwenye ardhi yetu, lakinitunashindwa kuyatoa hayo maji tuweze kuyatumia, ndiyomaana nimetumia msemo kwenye miti mingi hakuna wajenzi.

Tutazungumza sana hapa, tutajaribu kumhoji Profesana Dokta; ni kweli kwamba, wana elimu kubwa, lakini elimuyao haiwezi kusaidia kama hawana fedha. Kwa hiyo, hapatufanye kila linalowezekana, kuwasaidia wapate fedha iliwaweze kusimamia hiyo kazi, lakini tukianza kuhoji tu, mbonawewe Profesa, mbona wewe Dokta, tunao Madaktari wengina Maprofesa wengi wameshashindwa Urais zaidi ya maratatu, lakini bado tunawaheshimu. Kwa hiyo, kuwa Dokta auProfesa haisaidii kama huna nguvu za kiuchumi za kuwezakusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia suala la maji,Wataalam wa Afya wanasema, tukimaliza au tukiweza kufikaasilimia 80 kuwapatia Wananchi maji safi, tutakuwatumepunguza Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kiwango kikubwasana; kwa sababu maradhi yote yanayosababishwa naungonjwa wa matumbo yataondoka, kama tu Wananchiwatakuwa na maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapozungumza suala la maji,hapa tusiingize siasa, tuzungumze kwa ukweli hoja nzito iliyokombele yetu. Katika Jimbo la Mtela, tuna vijiji zaidi ya 40,Wananchi wanakunywa maji pamoja na ng’ombe. UkipitaFufu, Manzase, Mlodaa, ukipita maeneo yote hayo ambayoni barabara kuu mnapita Waheshimiwa Mawaziri, mtakutanana hali mbaya sana ya maji na kila tukija kwenye Bajeti hapatunakuta orodha tu na sasa hivi Mheshimiwa Waziri ulikuwaumetupatia, tusingeangalia kwa makini, kila Mbunge kunaorodha ya vijiji vyake, yaani hapa kila Mbunge angesomaangekuta orodha imeorodheshwa angejua mwaka huugoma limo, kumbe hakuna maji, ukija kwenye Bajeti unakutafedha hazipo. (Kicheko/Makofi)

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

81

25 APRILI, 2013

Kwa hiyo, tukusaidie, mimi niombe kusema kwamba,tukitoka hapa, Kamati ya Bajeti ikutane, wala sitaki kuelekezasijui ni OC sijui ni wapi, ninyi mnajua namna ya kwendakufanya, muwaongezee fedha hawa Waheshimiwa Mawaziriili waje watugawie hapa tuweze kupata visima vya maji.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, ingekuwa vyemaBunge lako likawa na utaratibu wa kupata mrejesho uliosahihi; kwa mfano, kabla ya Bajeti ya Maji kusomwa, kwanza,tungeelezwa ni Miradi gani imetekelezwa; hiyo ya Benki yaDunia, vijiji vingapi vimepata maji, wapi wanakunywa maji, ilituelewe kwamba kumbe kazi iliyobaki ni kutoka hapakwenda mbele zaidi. Tukiwa tunafanyia kazi ujumla ujumlahivi, hatuwezi kujua wapi kuna maji, wapi watu hawajapatamaji, tutakuwa tunasikia tu World Bank, World Bank.

Katika huo Mradi wa Vijiji Kumi, ingekuwa vyemaWaheshimiwa Wabunge wote tupate orodha ya vijijiambavyo tayari wanakunywa maji, tungejua kwamba ahaa,kumbe katika vijiji vyote hivi, limepunguzwa kiasi kadhaa.Tukizungumza kwa ujumla wake, tutakuwa tunapoteza mudabure. Maji yenyewe ya Benki ya Dunia gharama yake nikubwa mno, unakuta mradi wa kijiji kimoja shilingi milioni 488wakati unaweza kuzigawa zile ukapata maji katika vijiji vinne.

Maji yanachimbwa kwa gharama kubwa,yanasambazwa kwa gharama kubwa, bila sababu yoyoteya msingi. Kwa hiyo, niishauri Serikali, hakuna sababu, kamawametupa zile fedha, namna gani ya kuzitumia watuachiesisi na Halmashauri, tuangalie kwamba ukikaa mahali kwenyekijiji chako, gharama ya shilingi milioni 100 unaweza kupatamaji ukatumia shilingi milioni 100 badala ya shilingi milioni 488.(Makofi)

Tunapoteza muda bure, tunayo maji kila sehemuyamechimbwa yamefunikwa, watu hawayatumii, ukijakuiangalia Bajeti, kila kijiji milioni 400, wakati wenyewetukichimba maji hata kwenye visima vyetu binafsi,tunayapata kwa fedha kidogo sana. (Makofi)

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

82

25 APRILI, 2013

Utaratibu huu tunawezekana kabisa na sitegemeikwamba hata matumizi yetu ya ndani ya namna yakupangua Bajeti yetu ili itoshe vijiji vingi, nalo Banki ya Duniawanatusimamia, itakuwa ajabu sana. Wao wametupa fedhasisi tuchukue fedha hiyo tuigawanye.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninalotakakulizungumza hapa ni mtiririko wa fedha kutoka Hazina.Wizara ya Maji haina kipaumbele chochote, ukiendakutazama pale kila siku unawaona akina Mheshimiwa ProfesaMaghembe wako Wizara ya Maji wanaomba fedha. Hiviwenzetu wa Wizara ya Fedha hamwoni umuhimu wa majiwa sababu ninyi mnakunywa maji? (Makofi)

Mimi nataka kutumia fursa hii kuwasihi Watanzania,kuanzia leo, ziara iwe ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, iwe yaMbunge au ya Spika, msimuwekee maji ya chupa, wekenimaji mnayokunywa ninyi. Maana hii tabia ya Watanzaniawakishaona mkubwa umekuja pale wananunua Kilimanjaro,wewe mkubwa unajisahau unafikiri wale wana maji kumbehawana. Piga jagi, weka pale kipeo chako, mwekee paleMzee Pinda, akiona mabaya basi ataenda kuhakikishaanaleta maji pale ya kunywa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili nawaomba Watanzaniawalizingatie sana wala viongozi wa ngazi ya chini wasiogopekwamba watafukuzwa kazi, hawawezi kufukuzwa, sisiWabunge tutawatetea. Leteni maji hayo hayo machafumnayokunywa kwenye meza za Mawaziri ili na wao wanywe,wakishindwa waende wakahakikishe wanaleta maji safi kwaajili ya nchi nzima. (Makofi)

Hatuwezi kukubali utaratibu huu, kila mtu ukifanyaziara wanakuwekea maji ya Kilimanjaro wakati wenzakowanakunywa maji machafu, kuna watu wanaoga sikuwakisikia ziara ya Waziri tu; haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala lingine la aibu sana,kama leo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere angefufuka,angeshangaa sana, mabwawa mengi ambayo

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

83

25 APRILI, 2013

waliyachimba leo yamefukiwa, hata kufukua tu tunashindwa!(Makofi)

Ukitembea katika Vijiji vya Mlowa Bwawani, Idifu,Mvumi Mission, Mkulabi, utakutana na mabwawa mengiyaliyochimbwa enzi zile za Mwalimu. Unajiuliza hivi Mwalimualiwezaje wakati ule na uchumi ulikuwa mgumu na sisitunashindwaje! (Makofi)

Tumekuwa tunapata habari hapa, tumepigana wee,tumetumia muda mrefu kwenda Wizara ya Maji kuombaBwawa la Sasajila likamilishwe pale, lakini hakuna lolote, kunaubabaishaji mtupu kwa watendaji wetu. Hebu tuangalie,tunaweza tukafikiri adui mkubwa wa CCM ni CHADEMA,kumbe adui mkubwa ni Watendaji waliomo ndani ya Serikali.(Makofi)

Tutapoteza muda bure, twende tukapambane nabaadhi ya Watendaji wasiokuwa waaminifu ili Wananchiwetu wapate maji.

Mheshimiwa Spika, niombe sana maji katika vijijiambavyo tangu Uhuru havijawahi kupata maji. Kijiji kamacha Igandu, Nghaelezi, Chinoje, Chanhumba, hawajawahikupata maji tangu Uhuru. Unashangaa hatujawahikuwaweka hata katika orodha; kwa mfano, nimeona kwenyeorodha ya kitabu hiki cha Mheshimiwa Waziri wa Maji,ametaja kuna Kijiji kinaitwa Chinoje kwamba kuna Mradi waMaji wa World Bank.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie MheshimiwaWaziri, pale wamechimba zaidi ya mita 120 hawakupata maji.Kwa hiyo, hiki hakipo kwenye mpango wowote, kwa sababumaji pale chini hayapo, labda twende mbali zaidi. Kwa hiyo,ni vyema tukawapa taarifa sahihi ili wakati mnatusaidiamtusaidie. Nenda katika Kijiji cha Mvumi Mission, kina watu21,000, lakini pale tangu Uhuru hakuna kisima cha majikilichochimbwa na Serikali. Maji yaliyoko pale ni kidogo yaKanisa. Sasa Kanisa lina miradi mingi pale; wana Shule yaoya DCT, wana High School, wana shule ya wenzetu wenye

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

84

25 APRILI, 2013

ulemavu wa macho, wana vyuo vitatu pale. Kwa hiyo,unakuja maji yao hayawatoshi wao wenyewe, sembusekuwapa Wananchi; tuna matatizo makubwa sana ya maji.

Tunawaomba sana, Mheshimiwa Spika na wewevilevile tunajua nguvu yako ya Kiti ni kubwa, unawezakuwaambia hawa leo wakutane waongeze fedha ili na Jimbolako nalo nalisemea lipate maji. Kwa sababu shida ya majiipo kuanzia kwenye back bencher hadi kwa Waziri Mkuu.

Tunapozungumzia vipaumbele, zipo Wizara wakatimwingine tunaweza tukasema mwaka huu tulipe mishaharatu Wizara hii, fedha zote za maendeleo tupeleke kwenye maji.Tuangalie vipaumbele vya Wizara, tukitaka kufanya kazi yamaji mwakani, tabu yake ni kwamba, hawa wenzetuwatafikiri tunafanya kwa ajili ya uchaguzi, kwa hiyo, tufanyesasa.

Tufanye sasa watu wetu wapate maji. Watuwakishapata maji na nikwambie Mheshimiwa Spika, tukipatamaji tutaokoa nguvu kazi kubwa sana ya Taifa, kwa sababuakina mama wengi badala ya kufanya kazi ya kuhangaikakutafuta maji, watafanya kazi ya kuzalisha. Wataungana nawenzao kwenda kuzalisha mali badala ya kuhangaikakutafuta maji. Hapa Dodoma hatuna mto unaotiririka maji.(Makofi)

SPIKA: Ahsante sana, tena na magonjwayatapungua.

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Siungi mkono hoja.(Makofi)

SPIKA: Haya, nashukuru. Sasa nimwite MchungajiNatse na Mheshimiwa Anna Mary Stella Mallac, dakika tanotano.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Nitumie dakika chachenilizonazo kujikita katika Jimbo langu la Karatu. Kama wengi

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

85

25 APRILI, 2013

walivyosema, Bajeti hii ya Wizara ya Maji haitoshi na Serikalihaina nia ya dhati kuhakikisha Wananchi wake wanapatamaji, kwa sababu ukiangalia vitabu vya maendeleo, sehemukubwa ni fedha za nje na siyo za ndani na katika Halmashaurinyingi, hakuna Bajeti kwa ajili ya maji. Maji wanasubiliwafadhili walete fedha.

Nije kwenye Miradi ya World Bank; ni kweli ni Miradiambayo ipo hoi na haitatusaidia. Fedha nyingi, shilingi milioni400 plus, haiwezi kuleta maji kwa kijiji kimoja, kwa sababuasilimia kubwa ya fedha zile zinaliwa na wakandarasi. Hii tabianafikiri tuiache kama Serikali, wakandarasi hao waogopenikama ukoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tarehe 18 Machi, 2013,Mheshimiwa Waziri Profesa Maghembe, alifika Karatu kwaajili ya kero ya maji na akatoa kauli nzito kwamba, Karatutumesikia kilio chenu na ni kwa mara ya kwanza nafikiri Serikaliimekumbuka kupeleka maji Karatu. Akasema watawekapampu kwenye kisima ambacho kipo tayari, watachimbavisima viwili, watajenga vioski kumi na kujenga matenki.Ndani ya siku kumi kazi hii itakuwa tayari. NaombaMheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha anipe majibumaana hata sasa hakuna kinachoendelea pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kutunza vyanzovya maji. Hili ni muhimu sana, pasipo kuonea aibu mtu yeyoteawaye, vyanzo vya maji vitunzwe kwa gharama zote.Ninakumbuka tunayo mabonde mengi ambayo kimsingiyanahitaji kuangaliwa, siyo kukaa ofisini, hawa watu wamabonde hasa Bonde la Kati, waende kwenye mabondewaangalie skimu zinakuwaje.

Katika Bonde la Eyasi, matatizo yaliyoko paleninaweza kudiriki kusema kwamba, yanasababishwa na watuwa Bonde la Kati, wanatoa maagizo toka ofisini, hawafikikwenye site. Ninakuomba Mheshimiwa Waziri, ufike kwenyeBonde la Eyasi kwenye chanzo cha Kandend uangalie,maana maji ni uhai wa Wananchi wote wa eneo lile. (Makofi)

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

86

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, naomba kuweka kumbukumbusawasawa, katika Hotuba ya Waziri Mkuu, MheshimiwaMwigulu Nchemba, alilipotosha Bunge lako na Wananchi waTanzania; Jimbo la Karatu linaongozwa na CHADEMA nakatika Mabaraza ya Katiba, Jimbo lile limepewa members75, CHADEMA ina members 45, CCM na wengine waliobaki,ilishangaza kudanganya Bunge na Wananchi kwamba hatakule Karatu CCM ilishinda; shame to him!

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, naomba uondoe hayomaneno yako ya mwisho.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Ahsante, naondoa.

Kwa kuwa tumekubali Vyama Vingi, twende pamojakwa nchi hii maana ni nchi yetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni suala la uvunajiwa maji. Naiomba Serikali iwekeze katika kuvuna maji hasakatika Taasisi zetu kama shule za sekondari na msingi, hospitalina zahanati. Tuvune maji kwa ajili ya mahitaji ya binadamuna hili linawezekana, kujenga matanki, kuweka gutters katikashule zote na taasisi zetu zote, kwa namna hii tutasaidia sanashida kubwa ya maji inayowakabili Wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kweli bajeti hii inahitajikuongezwa kama wengi walivyoomba, naiomba Serikali iruditena ikae, kabla ya kupitisha watuletee kitu.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Anna MaryStellaMallac dakika tano.

MHE. ANNA MARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, ahsante sana. Nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu, kwa kunipa afya siku hii ya leo.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa narudia manenowaliyoongea wenzangu kwamba maji ni kitu muhimu sana

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

87

25 APRILI, 2013

kuliko hata KILIMO KWANZA, kwa sababu KILIMO KWANZAhakiwezi kutekelezwa kama hakuna maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea shida ya maji siyokwamba tunahitaji maneno matamu kuyasikia masikioni namipango isiyokamilika. Ninaomba Waziri wa Maji, aelekezemacho yake ya huruma katika Mkoa wa Katavi na Mkoa waRukwa. Wanakatavi watanishangaa sana ikiwa nitaungamkono bajeti hii ya maji pamoja na Wanarukwa. Kwa kwelitunajiona kama ni watu ambao tumetengwa sana, naombaMheshimiwa Waziri wa Wizara hii ya Maji, awahurumie sanaWananchi wa Rukwa na Katavi, ambao wapo pembezonimwa nchi, ambao tupo nyuma kwa kila kitu kuanziabarabara, maji na elimu. Vitu vyote hivyo tumesahaulika sana.Kwa hiyo, naomba hili suala la maji alipe kipaumbele hasavijijini. Siwezi kuongelea sana mjini, naongelea vijijini ambapondipo kuna wazalishaji wakubwa, asilimia 80 ya Wananchiwako kule wanahangaika sana kutafuta maji. Jamaniwanawake wa vijijini wanahangaika sana, Mheshimiwa Waziriwa Maji hebu waonee huruma wanawake wale.

Leo hii Tanzania miaka 52 tangu tumepata Uhuru,bado ni wa kuchota maji kwa kichwa tena kuchota kwa katakwenye madimbwi, maji ambayo yamebadilika rangi na yakijani yanateleza kama mlenda; jamani! Wananchiwanakunywa maji Mheshimiwa Waziri kama togwa!

Mimi nimekuwa natembelea sana vijijini, naona aibuninapowazungukia Wananchi wananiandalia chakula halafuwananiwekea maji mazito kama togwa. Kwa kuwawanaokunywa ni Wananchi wenzangu na mimi nalazimikakunywa huku naomba Mungu nisaidie nisipange foleninyumbani ya kuingia sehemu muhimu. Jamani, wahurumienisana Wananchi wa vijijini.

Kuna vijiji nilivyovitaja mwaka jana na mwaka huusitavirudia, kwa sababu nitakuwa napoteza muda dakika nichache. Naona Serikali imevipanga kwenye kitabu chakokwamba vipo kwenye mpango wa vijiji kumi. Nitashukurukama mpango huo utatekelezeka, kwa sababu Serikali

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

88

25 APRILI, 2013

imekuwa na maneno mengi kama ni mama mpaka watototutakuchoka.

Naomba Wananchi wa vijijini waangaliwe hasa kwamaji, siwezi kuvitaja vijiji itakuwa ni kurudia. Kijiji cha Majimoto,Kata ya Majimoto, naomba uwakumbuke sana MheshimiwaWaziri, watu wale wana adhabu, wanakunywa maji ya motoyanayofuka moshi. Hebu niwaulize Wabunge wenzangukwamba; leo hii tuambizane kuanzia kesho wote tunapokulachakula tuanze kunywa maji ya moto kama chai yanakidhikumaliza kiu? Ndiyo wenzetu Majimoto wanakunywa majihayo ambayo yanafuka moshi, ni maji ya kunywa hayo naukikuta mwananchi anayekunywa maji ya baridi amenunua,debe la lita 20 amenunua kwa shilingi 2,000 au 1,500 na majihayo wanunuzi wanayatoa kilomita nane kijiji kinachoitwaMamba.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo…

(Hapa kengele Ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Dakika tano zimeisha mama. Ahsante. Sasanitamwita msemaji anayefuata, Mheshimiwa Dkt. Kebwe,atafuatiwa na Mheshimiwa Selemani Jafo, atafuatiwa naMheshimiwa Aliko Kibona.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,nashukuru sana kwa nafasi hii na mimi nichangie katika Wizarahii nyeti ya Maji. Nianze na ninaomba nieleweke kwamba,siungi mkono hoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja kwa sababuzifuatazo:-

Nashukuru Mheshimiwa Waziri anafahamu historia yaBwawa la Manchira. Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete,anafahamu Bwawa la Manchira. Mheshimiwa ProfesaMwandosya anafahamu sana historia ya Bwawa la Manchira.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

89

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, kilichofanyika katika Bwawa laManchira pale Serengeti, Mji wa Mugumu, unapata majikutoka katika Bwawa hili. Tunaishukuru Serikali kwanigharama kubwa sana imetumika, lakini Mradi umeishia njiani,haiwezekani maji yapatikane ambayo hayatoshelezi, lakinimfumo wake ule wa mtandao haujakamilika.

Mheshimiwa Spika, kibaya zaidi, Wanaserengeti kiliokikubwa ni kule kufananishwa sasa na sisi tuishi kamawanyama walio mbugani pale. Haiwezekani tupewe majiambayo hajatibiwa. Hii ni kinyume kabisa hata naubinadamu, yale maji kama hayatibiwi; hivi ilikuwaje RaisJakaya Kikwete alipelekwa pale kufungua Mradi ule? Ninahakika labda alidanganywa, sidhani kama angefahamu yalemaji angekwenda kukata utepe, hayatibiwi halafu aruhusuWatanzania, Wanaserengeti na Wanamugumu, wayanyweyale maji. Tunaiomba Serikali sikivu ya Chama cha Mapinduzi,kunapokuwa na ziara hizi za viongozi mbalimbali, vilevile nisehemu ya kujionea uhalisia, kwa nini hawa viongoziwanaotembelea Miradi mikubwa kama hii ya Kitaifawanadanganywa? (Makofi)

Hivi ni Mawaziri wangapi ambao walishatembeleaBwawa la Manchira? Imekuwa kama ni Mradi wa Maonesho,kila Kiongozi wa Kitaifa anayetembelea Serengeti ni lazimaapelekwe Bwawa la Manchira, kufanya nini kama Mradi huuhaukamiliki? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachoomba ni Serikali iongezefedha na ndiyo sababu mimi siungi mkono. Iongezwe fedha,hili ambalo linazungumzwa la shilingi bilioni 30 kupelekwaMwanga ni sehemu ya mradi wa utekelezaji kama ambavyoBwawa la Manchira linatakiwa lipewe fedha. Fedha hizizikiongezeka, naomba Bwawa la Manchira, mtambo wakusafishia, ile Water Treatment System uwekwe, fedhaambayo ilikuwa imekadiriwa, shilingi bilioni 17.5, pamoja namtandao wa kwenda kwenye vijiji vya sehemu ya Manchira,Kwamichanga, Miseke, Bwitengi na sehemu zote za mtandaozikiwemo Kibeo na Kisangura, ni vizuri utazamwe. Fedhaambazo zilikuwa zimekadiriwa hizo shilingi bilioni 17.5 basi

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

90

25 APRILI, 2013

zingekuwa zinatolewa hata kwa awamu. Kwa hiyo, fedha hiiikiongezeka kama zile shilingi bilioni 30 pale Mwangazitaendelea kuwa hivyo, mimi sitaendelea kuunga mkono.Ni vizuri keki inapokuwa ndogo basi kila mtu apate kidogo,lakini suala hili ni la ubinadamu, Wananchi wa Serengetiwanapewa maji ambayo hayatibiwi.

Kuna usemi unasema kwamba, kinga ni bora kulikotiba. Kwa takwimu ambazo zipo kidunia, ukieleza vizuri katikasuala la mazingira na suala la maji, asilimia 80 ya magonjwaya kuambukiza yanatoweka na ndiyo sababu hata wenzetukwa nchi ambazo zimepiga hatua kidogo walifanya hivyo,hawalii mambo ya matumbo, kuharisha na nini havipo kwasababu ya suala la maji. Ukiangalia mwanafalsafa mmoja,Wiliam Fisher, ambaye alijaribu kutengenisha haya magonjwakutokana na matatizo ya maji ikiwemo water related, waterwaste, water based na kadhalika. Kwa njia hii ndiyo ambayoilisaidia kuondokana na maradhi haya ya kuharisha nakuhara.

Kwa hiyo, naomba sehemu ya pili, mradi mkubwa wamaji ambao unaendelea pale Musoma, pampu yakeikikamilika inaweza kusukuma kwa gravity mpaka kilomita 50,ambayo inakuwa imebakia kilomita kumi kuingia Serengeti.Kwa hiyo, ni vizuri tutumie fursa hii kusudi mtandao ule wamaji kutoka Ziwa Victoria usambae mpaka Serengeti, ni kiasicha kuweka pampu ya kusogeza nguvu kwenda Wilaya yaSerengeti, ndiyo njia pekee ya kusambaza maji ya ZiwaVictoria. Kwa nini tuyaachie maji haya ambayo asilimia 70ya maji yanayongia Ziwa Victoria yanatokea Tanzania? Kwahiyo, ni vizuri fursa hii nzuri ambayo tunayo tusiiachie, majiyale yanaenda katika nchi za wenzetu wanajengamabwawa na kufanya kazi nzuri za kimaendeleo, ikiwemoMisri na Sudan, maji yale yanatokea kwetu na tunayazalishasisi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba suala hili lifanyekazi ya kimkakati, wataalamu ambao wako Wizara ya Majitumieni fursa hiii ili utaalamu wenu ufanye kazi ambayoitawasaidia Watanzania. (Makofi)

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

91

25 APRILI, 2013

Jambo lingine ninaloshauri ni kwamba, miradi ya Benkiya Dunia, tunaiita hivyo lakini ni sehemu ya support ya Benkiya Dunia, haijafanyiwa evaluation, nina hakika, ingekuwaimeshafanyiwa tathmini, sidhani kama tungeendelea nautaratibu huu. Haiwezekani Mradi unakuwepo miaka kumishughuli haziendi halafu bado tunakwenda; nini maana yamonitoring and evaluation? Ufuatiliaji na tathmini unakusaidiakuchukua uamuzi kwamba, are you on truck; yaaniunakwenda kulingana na mpango wenyewe ulivyo; kamahauko on truck unabadilisha utaratibu.

Kwa hiyo, ushauri wangu ni kwamba, ni vizurituachane na mambo ya visima ambavyo vinatumiagharama kubwa katika Mradi huu. Tukijielekeza katikamabwawa inakuwa ni multipurpose; kivipi? Utapata maji kwaajili ya mifugo, kwa ajili ya Ndama wakiwemo, unatengenezatrough halafu unaweka na DP kusudi maji yale yatumike kwaajili ya mifugo na binadamu katika uwanja mpana. Kwa hiyo,ni vizuri hili liangaliwe upya.

Mheshimiwa Spika, naomba tuwekewe mita katikaMji wa Mugumu. Siyo vizuri mtandao wa maji ambao upokwa watu wachache wenye mabomba katika maeneo yaohalafu unakuta Wananchi wengine wanakwenda kuchotamaji pale wanalipishwa kwa sababu hakuna mita. Kwa hiyo,ni vyema Wizara ikae vizuri ifanye ufuatiliaji wa karibu naisimamie ili kama ni Serikali kutoa seed money, iwepo kwaajili ya kununua mita, hii itasaidia kuongeza wigo waukusanyaji wa fedha kuliko watu wachache wanahodhi majihalafu wao ndiyo wanakuwa wafanyabiashara wakubwa wamaji kuliko matumizi ya jamii. Hii itasaidia kupiga hatua katikausambazaji wa maji.

Mheshimiwa Spika, lakini pia ninachokiona kikubwacha msingi, Miradi hii ambayo tunaanzisha halafu tunaishiakatikati, haitusaidii sana. Katika Bunge mwaka juzi niliulizakwamba Bwawa lile la Nyamitita hivi limeishia wapi? Jibunililopata ni kwamba, zimepangwa fedha shilingi milioni 700.Je, fedha hizo mpaka leo zipo wapi? Mradi umesimamahakuna kinachoendelea. Katika kujibu hoja, Mheshimiwa

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

92

25 APRILI, 2013

Waziri anapokuja kuhitimisha, aje na majibu ya kuelewekaya kuwasaidia Wanaserengeti. Hii ndiyo njia pekee ambayotutaachana na Miradi hii ambayo tunaanzisha halafu inaishiakatikati, at the end of the day, inakuwa very expensive, kwasababu kulingana na muda unavyokwenda na thamani yafedha nayo inabadilika, ni dhahiri itakuwa gharama kubwa.

Mheshimiwa Spika, kikubwa cha msingininachopenda kushauri Kamati ya Bajeti hii ambayoimeanzishwa, tuone kazi yake, performance yake ikoje, iliwenzetu warudi wakawatafutie fedha. Nimepitia katikavitabu vyote, Wizara mbalimbali maeneo yapo mengi yakubana matumizi, haiwezekani vitafunwa na chai inachukuabillions of money! Fedha hizi nyingine zipunguzwe na fedhanyingine za matumizi ya kawaida. Ukienda katika ile 250300unakuta kifungu kile ni perdiem domestic, kinachukua fedhanyingi kwelikweli; ni vizuri maeneo mbalimbali yaangaliwe.Wataalamu ambao wapo katika Kamati ya Bajeti wapitieupya. Hii itasaidia.

Kikubwa na cha kushangaza ninachokiona,tumepigia kelele kwenye suala la maji na nina hakika kamautakubali tufanye majaribio, basi maji yasipatikane katikamaeneo haya ya Bunge ikiwemo Bunge hapa tulipo, japokwa siku moja, kelele tutakazopata na maandamano yaWabunge …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Haya ahsante, kwani unatakaje mgawanamatatizo? Tunaganga huko yaliko.

Sasa nimwite Mheshimiwa Selemani Jafo naMheshimiwa Aliko Kibona ajiandae.

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, ahsante.Awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu, mchana waleo na mimi kupata nafasi.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

93

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, lakini sisi kwetu kule kuna kitukinaitwa timbwili, ukiona kila Mbunge hapa anajadili sualala maji kwa uchungu basi ujue suala hili ni kubwa sana. Jambohili kwa nini maji? Nikinukuu vitabu vya dini kwa Lugha yaKiarabu, Mwenyezi Mungu anasema: “Wahuwa radhi haraka-mina-l-imai-bashara, farajaharahum nasaba waswilawakana-rabuka kadira”. Kwamba, hakika Mwenyezi Mungundiyo amemwumba mwanadamu kwa maji, akamjaliaujungu wa damu na udugu wa kuoana. Kwa hiyo, ndiyomaana unaona kila mtu anaguswa na suala zima la maji,ndiyo maana naomba Wabunge wote kwanza tuache jazbatuseme kwamba jambo hili ni kubwa kweli kwa mustakabaliwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mimi kama unakumbuka sikuzote nikisimama Bunge hili nalilia sana shida ya maji katikaJimbo langu la Kisarawe na sijasimama hata siku moja kuachakuzungumzia shida ya maji. Wananchi wangu wana shidakubwa kwelikweli ya maji na hili nitaendelea kulisema ndaniya miaka yangu yote mitano, shida ya maji Wilaya yaKisarawe na ndiyo maana vipaumbele vyangu vitano katikaJimbo langu la Kisarawe ni shida ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini Mwenyezi Mungu anasemausipomshukuru binadamu mwenzako hata Mwenyezi Munguutashindwa kumshukuru. Naishukuru sana Serikali, imenisikiakwa shida ya maji Wilaya ya Kisarawe. Juzi tumepata shilingimilioni 700 kwa ajili ya kuweka miundombinu katika visimavitano vilivyokamilika hivi sasa. Katika Kisima cha Kihara,Kikwete, Mradi wa Mafizi, Kisima cha Boga na Msanga; kwakweli Wizara nawashukuru sana kwa sababu watu waKisarawe wana shida kubwa ya maji.

Mheshimiwa Waziri, nakushukuru sana. Katika ukurasawa 15 na mpaka nikapiga simu kwa Engineer wangu waWilaya, nashukuru sana kupata ufadhili kutoka China kwavisima 20. Nimepata taarifa pale Wilaya yetu ya Kisarawe,ndugu zangu Wanabunge hili, Kisarawe tunataabika kwelishida ya maji. Serikali imefanya hili kwangu mimi na mimikama binadamu lazima niridhike niseme kwamba, haiwezi

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

94

25 APRILI, 2013

kumaliza shida yote ya maji lakini angalau kidogo tumeanzakupiga safari hii. Nina imani kwamba, taratibu Wanakisarawemwisho wa siku tutapata nafuu katika shida ya maji.

Nakumbuka juzijuzi ofisi yako ilipata taarifa kwamba,wakati Mheshimiwa Mwandosya akiwa Waziri, tulipata Mradiwa Maji wa shilingi milioni 540, Mji wa Kisarawe ulipata shidakubwa sana ya maji. Mradi ule umeanza kufanya kazi vizuri,lakini mota yetu ikawa imeungua pale, bahati mbaya majikidogo yana changamoto kubwa kwa sababu ya kuwepokwa madini mengi sana ya iron. Nadhani Ofisi ya DAWASAwameshapata taarifa hii, naomba ndugu zetu wa DAWASAwashirikiane na wataalamu wetu pale Wilayani, kuhakikishakile kiwango cha madini ya chuma kinarekebishwa ili watuwangu wa Kisarawe waweze kupata maji mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii tunazungumza shida yamaji, lakini tujue kwamba, ndani ya miaka kumi iliyopita,Tanzania imeongezeka zaidi ya watu milioni kumi. Watumilioni kumi maana yake ni sawasawa na lita milioni 250zinatakiwa kwa siku. Ina maana kwamba, mahitaji yetu yamaji kwa Tanzania sasa ni makubwa. Hapa tuna kilachangamoto kubwa ya kutafakari kwa kina jinsi ganitutafanya ili tupambane na shida yetu ya maji katika nchiyetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri na Ofisi yako, Serikali, naishukurusana kwa kuweka shilingi milioni 35 kwa Mradi wa Kimbiji naMipera ambayo Mradi huu kwa mujibu wa taratibu utasaidiaJiji la Dar es Salaam, lakini utasaidia kwa kaka yangu paleMheshimiwa Adam Malima, Mkuranga pale, lakini nakutusaidia sisi watu wa Mji wa Kisarawe. Naomba aendeleekuweka nguvu sana Mradi wa Kimbiji uweze kukamilika.Wananchi wangu wa Mji wa Kisarawe pamoja na kwambawanaweza kupata maji salama, lakini angalau na waowaweze kujisikia sehemu yenye amani ya kuweza kuishi.

Mheshimiwa Spika, haya ndiyo maana nimesemamimi nikiwa Mbunge na sehemu yangu imeguswa, lazimanishukuru. Mwaka jana tulikuwa tunapitisha bajeti ya

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

95

25 APRILI, 2013

barabara hapa miundombinu, kwangu Kisarawesikutengewa hata barabara moja ya lami, ukiangalia mikoaya Kaskazini wamejengewa lami mpaka vyooni huko na watutulipitisha ile bajeti. Bajeti hii ya mwaka huu mimi naiungamkono na ndugu zangu wanasema sijui Mwanga,tuzungumze mambo ya Kitaifa, tukiwa tunawanyoosheawenzetu vidole wenzetu wa Mwanga na Same wale nao nibinadamu, watajisikia vibaya. Serikali yetu imetumiamamilioni ya shilingi kutoa maji Ziwa Victoria yanakwendampaka Tabora; mbona watu hawakusema? (Makofi)

Jamani Mradi wa Kitaifa lazima ugharimu pesa nyingisana, lazima kama Wabunge tuwe na jambo moja la Kitaifa,tutakuja kubaguana kwa sababu Mikoa ya Kaskazini sisiwengine lami na mambo mengine, tutakuja kubaguanahumu. Hata ukiangalia katika kitabu cha barabara, ujenziwa barabara mwaka huu, tutaanza kushikana mashati hapa.Kuna mikoa mingine wamewekewa mabilioni ya fedha.

MBUNGE FULANI: Kweli!

MHE. SELEMANI S. JAFO: Tutashikana mashatiWabunge hapa, tujadili kwa pamoja kama pesa haitoshitutafanyaje kuongeza pesa ili kusaidia Sekta ya Maji,tusinyoosheane vidole. Kila mtu anazungumzia Jiji la Dar esSalaam, ndiyo, lakini tuangalie hata investment ya kiasi ganipesa imewekwa Dar es Salaam kulinganisha na sehemunyingine tunakotoka.

Kwa hiyo, tuzungumze kwa pamoja kwamba kwelipesa ya maji haitoshi, kama Wabunge tukae tutafute njia ilipesa iongezeke na Mheshimiwa Maghembe hapendikudhalilishwa mtu mzima na Dokta wangu pale, hawapendikudhalilishwa. Wao siyo kwamba wana pesa mifukoni,hapana. Kazi ya Wabunge maana yake kuishauri Serikali nakuielekeza na kuisimamia. Sisi Wabunge tuishauri Serikalikwamba pesa ile ni ndogo.

Jana Mheshimiwa Serukamba alishauri kwamba,tukate OC hata ya asilimia 15, mimi nimesema hata asilimia

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

96

25 APRILI, 2013

kumi tutapata zaidi ya bilioni 300 au 400, tutaongeza katikaSekta ya Maji na itasaidia maji vijijini. Ndiyo maana nasemakama Wabunge, tukubaliane kwamba bajeti ya maji haitoshi.Bahati nzuri sana, nawashukuru sana Mheshimiwa ProfesaMsolla, Kamati yako imefanya kazi kubwa sana kusemakwamba, bajeti hii haitoshi. Nimesikitika sana, Mbungeanasimama hapa anailamu Kamati; Kamati imejaa akinaProfesa Msolla halafu mnaidhalilisha hapa! Kazi kubwawanayofanya akina Mama Makilagi, akina Subira Mgalu naWataalamu wamekaa wamejadili na kuishauri Serikalikwamba tuongeze shilingi bilioni 185, unasema Kamatihijafanya lolote! Kamati ndiyo imetuonesha njia kwambabajeti haitoshi. (Makofi)

Kwa hiyo, kama Wabunge, nakushauri MheshimiwaSpika kwamba, ikiwezekana tukitoka hapa Serikali iendeikakae itupe majibu jinsi gani pesa zitaongezwa. Hakunasababu ya kutafuta ujiko au sijui kutoa hoja, hakuna haja yakutoa hoja hapa, hoja tunachotaka ni kwamba, Serikaliikaongeze pesa tu. Hakuna kutafuta ujiko wa burebure hapa,Wabunge wote tumesema kwamba tunataka pesaiongezeke ili Wananchi wetu wapate maji na ndiyo maanatunaiagiza Serikali kwamba ikakae ikafanye mawazo ya kinakatika kutusaidia kutatua shida ya maji, wote tuna shida yamaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukitatua tatizo la maji tutakuwatumewagusa Watanzania wote. Sote tuna shida ya maji nasuala la maji ni jambo la msingi na ni jambo la kulisimamia.

Nawashukuru sana ndugu zangu wa DAWASA,nimepata taarifa kwamba wiki ijayo wataanza kuchimba majikatika maeneo ya Chole. Nawashauri watu wangu wa Choleambao sasa hivi mnanisikiliza kwamba, Wataalamu waDAWASA wakifika huko shirikianeni nao mhakikishe majiyanakwenda kuchimbwa sehemu ambayo tulikusudiakuchimba maji tuweze kupata maji.

Vilevile nawaomba Wataalamu wangu waHalmashauri pale Kisarawe, wahakikishe hivi visima vya

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

97

25 APRILI, 2013

Wachina vinavyokuja kule kwa kushirikiana na Serikali, viwezekusimamia kuwapelekea watu wa maeneo ya Mzenga,Malumbo na Manelomango, wapate maji katika maeneoyote ya Wilaya ya Kisarawe. Shida kubwa ni kwamba,Wananchi wetu hawawezi kupata maji.

Mheshimiwa Spika, samahani, maana nilitaka nisemeKisarawe oyee, nimejisahau nilidhani nipo katika majukwaaya kisiasa. Ni kwamba, lazima kama Wabunge tuhakikishekwamba, tunashikamana kwa pamoja. Naiomba Wizara,tuweze kuangalia na vilevile uharibifu wa tabia nchiumekuwa mkubwa kwelikweli. Sasa hivi takwimuzinatuonesha kwamba, kuna maeneo mengine mvuaimeshuka kutoka milimita 1500 kwa mwaka mpaka milimita780.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante na ninaomba nimwite MheshimiwaAliko Kibona.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kupata nafasi ili na mimi niweze kuchangiahoja iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, kuna msemo unasema,anayeshukuru maana yake anaomba tena. Niseme tukwamba, namshukuru Mheshimiwa Dkt. Mahenge, alifika Ilejekwa ajili ya kufungua Mradi wa Maji katika Kijiji cha Mbebe.Ninashukuru sana. Ninaposhukuru maana yake ajiandaeninataka kuomba tena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwamba,Mradi mkubwa wa Maji unaendelea katika Kijiji cha Ruswisina unaelekea katika hatua za mwisho. Kwa muda mrefu kilanikisimama katika Bunge lako Tukufu, nimekuwa nikitoa kiliokwa ajili ya Mji wa Isongole. Alikuwepo mama mmoja, alikuwana mtoto mgonjwa, akasikia Yesu Mnazareti anahubiri mahalina kuponya wagonjwa. Yule mama akakimbia akamwachamtoto wake nyumbani, alipofika akaenda moja kwa moja

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

98

25 APRILI, 2013

kwa Bwana Yesu akamwambia mtoto wangu ni mgonjwayu hawezi. Yesu akasema yuko wapi? Akasema yukonyumbani. Yesu akasema nifanyaje? Yule mama kwa imaniakasema sema neno tu na mgonjwa wangu atapona. Yesuakasema sijapata kuona imani kubwa namna hii.

Nimekuja kwako Mheshimiwa Waziri, nimeachamgonjwa yuko Isongole anahitaji shilingi milioni 500, usiniulizeyuko wapi, nasema sema neno tu na mgonjwa wanguatapona. (Makofi)

Mji wa Isongole ni mkubwa, unakua kwa kasi, panaBoda na Uhamiaji, wageni wanatoka nchi mbalimbaliwanachukua vibali vyao pale ili kuendelea na safari zaokwenda nchi za Kusini mwa Afrika. Mji ule hauna maji kwamuda mrefu toka tumepata Wilaya ya Ileje hatuna maji. Majiyaliyopo yaliwekwa miaka ya 1978 na wakati wa masikayakitoka kidogo yanakuja na tope la kutisha, watotowanakunywa maji yale hawawezi kuhudhuria masomo kwasababu ya homa za matumbo. Mheshimiwa Waziri, naombasema neno tu, katika hiki ambacho wenzangu wamesemakwamba, Serikali iende ikajipapase iangalie mahali penginetuweze kupata hela ya nyongeza. Naomba uelekeze katikakuongezaongeza kila mahali usinipite na mimi, uwekenyongeza katika Mji wa Isongole. (Makofi)

Ninakushukuru kwa aji l i ya visima vifuatavyo:Mheshimiwa Waziri ameniambia katika mwaka wa fedhaujao Serikali italeta maji katika Vijiji vya Ibaba, Shikunga,Ipande, Mtula, Chibila, Malangali, Kalengo, Bulanga, Kafule,Kapelekesi, Kikota na Sange. Ninashukuru maana yakeninaomba, nikitoka hapa ninakwenda kifua mbele,nakwenda kuwaambia Wananchi wa maeneo hayo majiyanakuja. Wakiniuliza nani amekwambia maji yatakuja?Nitawaambia Mheshimiwa Profesa Maghembe kupitia kauliyake kwa niaba ya Serikali amesema maji yanakuja katikavijiji hivyo. Ninaomba maji yafike katika vijiji hivyo ili furahayangu na shukrani yangu kwako isije ikageuka tena kuwalawama kwa watu wale wa vijiji nilivyovisema.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

99

25 APRILI, 2013

Mheshimiwa Spika, maji kama walivyosemawenzangu, mimi Wananchi wa Ileje wamenikataza kusemakama alivyosema fulani, lakini niseme kwamba,ninavyofahamu maji ni kila kitu. Mama anapokwendakuchota maji kilomita tano, akifika kule anakuta foleniwenzake wamewahi, anaweka debe lake au ndoo yake,anaanza kusubiri saa kumi na moja alfajiri, zamu yake yakuchota maji inakuwa saa tatu asubuhi, akirudi nyumbanimuda wa kwenda shambani umekwisha. Uchumi hauwezikwenda kwa njia hiyo, maji ni kila kitu, maji hospitalini hakunaoperesheni bila maji, hakuna kunywa dawa bila maji.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, uchumi wa nchi hauwezi kwendabila maji. Nasisitiza sana; Wananchi wa Isongolewanashindwa kufanya kazi hasa akina mama na ninashukurukwamba Mheshimiwa Waziri ninamwona, roho zinawasilianakwamba ananisikiliza. Naomba shilingi milioni 500 kwa ajili yaIsongole.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu lengo langu lilikuwakulia kwa ajili ya Isongole, niwape nafasi wachangiajiwengine. Nashukuru kwa kunipa nafasi hii na kwa yaleniliyotendewa katika Wilaya ya Ileje, kwa mara ya kwanza,Vijiji vya Ilanga, Miradi inaendelea, nimeambiwa pesa imefikaIkumbilo na Chitete. Naishukuru sana Serikali ya Chama chaMapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naombasasa nitofautiane na wenzangu kwa kuunga mkono hoja.Ninaunga mkono hoja hii nikitegemea hautanipita na mimikatika nyongeza ambayo Serikali itajipapasa.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mwanzoni tu baadaya maswali, kulikuwa kuna mtu aliomba mwongozo,Mheshimiwa Nchemba, kama ingewezekana kuendelea namazungumzo katika hali iliyokuwepo. Toka jana mpaka leo,

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

100

25 APRILI, 2013

ukweli ni kwamba, sisi tunaoangalia hakuna anayeungamkono suala hili zima.

Pia mkumbuke kwamba, utaratibu tuliojianzishia sisiwenyewe, upo utaratibu wa mashauriano, tunashaurianakatika bracket hiyohiyo, Bajeti ya Serikali kama ilivyowekwakatika framework, lakini tunaweza kupitia Kamati ya Bajetikuangalia. Pamoja na shutuma zote anazopewa Spika kwaKamati ya Bajeti, jamani mpaka tumefikia mfumo huu,haikuwa rahisi, kulikuwa na ubishi, woga, hofu na kila kitu,bahati nzuri mimi nilishajaribu, maji niliyaribu.

Kipindi kilichopita, bajeti ya mwaka jana, nilikuwanimetumia fedha za Legislative Support Program ya Bunge.Waliotupa pesa zile walikuwa wanasema tuwe tunakwendaMajimboni, nikasema kwenda Majimboni, Majimbo yapo 239huwezi kutumia dola milioni 3,500,000 zikatumika kwa Majimbokwa miaka mitano ambayo ni kudanganya toto. Tukasematufanye kitu kimoja, tuunde Kamati ndogo tuangalie hivi kweliSerikali imeshindwa kukusanya mapato katika maeneo fulani?Bahati nzuri Kamati ile ilifanya kazi bila kujitangaza kisiasa.Imesaidia sana kuona kwamba, tunaweza kufungua mahalipengine pa kukusanya kodi na Mwenyekiti wake alikuwaaliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi wakatiule, Mheshimiwa Chenge.

Sasa mtu kama mimi, watu wana hofu ya mabadilikona kila kitu, nimetumia kifungu changu cha tano kumteuaMwenyekiti wa Budget Committee, sijavunja sheria walasijavunja demokrasia ila nilitaka nijihakikishie kwamba kazininayofanya kweli inazaa matunda. Kwa hiyo, kwa maanahiyo, sasa naiona kabisa call ya Wabunge wote na ninadhanina Wananchi wote wanaotusikiliza, suala la maji hatuwezikufanya utani. (Makofi)

Kwa hiyo, naitaka Kamati ya Bajeti na Serikali kwamaana ya Hazina na Wizara ya Maji na Kamati ya Sekta,naahirisha Bunge sasa hivi wakafanye kazi na kazi hiitutaimaliza Siku ya Jumatatu. Kwa hiyo, Siku ya Jumatatu

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/... · maswali yenu kwa kifupi tunaweza kufikia idadi kubwa zaidi. Sasa namwita Kiongozi

101

25 APRILI, 2013

tuweze kupata maelezo kamili kama zimeongezeka basizimeongezeka vipi na addendum inakuwaje. (Makofi)

Kwa hiyo, naahirisha Kikao cha Bunge mpaka Siku yaJumatatu, saa tatu asubuhi. (Makofi)

(Saa 6.33 mchana Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumatatu, Tarehe 29 Aprili, 2013 Saa Tatu Asubuhi)