6
SIWA LA KISWAHILI ni kijarida ambacho kinachapishwa na Idara ya Kiswahili, Chuo Ki- kuu cha Nairobi. Hili ndilo toleo la pili. Karibuni ili mpate kufahamu habari za hivi punde kabisa kutoka katika Idara ya Kiswahili. Toleo hili pia linaangazia maswala mbali mbali yanayohusiana na shughuli za Idara, wahadhiri, wanafunzi na wafanyikazi wengine idarani. Wa- hadhiri kadhaa wamechapisha vitabu vipya, wengine wao wamehudhuria na kuwasilisha makala katika makongamano mbali mbali ya humu nchini na katika nchi za kimataifa. Vile vile toleo hili lina habari kuhusu shughuli za kufundisha Kiswahili ikiwa ni pamoja na mi- hadhara, safari na tafiti za nyanjani, uwasilishaji wa mapendekezo na matokeo ya utafiti unao- fanywa na wanafunzi wa kiwango cha uzamili, miongoni mwa mambo mengine. KARIBUNI! DIBAJI CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI DIbaji………………………….1 mkuu wa idara…………... TAhariri……………………. Machapisho………………. Makongamano………….. Ufundishaji………………. Mahafala…………………. Wahadhiri………………... Wanafunzi……………….. USHIRIKIANO……………. KIJARIDA CHA IDARA YA KISWAHILI JANUARI - MEI 2016 SALAMU ZA MKUU WA IDARA YALIYOMO Karibuni katika Idara ya Kiswahili. Nina furaha kubwa ku- waalika kusoma SIWA ambayo ndiyo mbiu yetu. Toleo hili linaonyesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na wa- hadhiri na wanafunzi wa Idara ya Kiswahili. Mathalani uta- julishwa kuhusu vitabu na machapisho ya hivi karibuni kabisa yaliyoandikwa na wasomi wetu wa Kiswahili, ushirikiano tulio nao na vyuo vingine ulimwenguni, makon- gamano yalioyoandaliwa ama kuhudhuriwa na wahadhiri wetu, pamoja na shughuli zao za utafiti. Vile vile, utasoma kuhusu shughuli za wanafunzi wetu wa Kiswahili. Singependa kukuondolea utamu wa mambo utakayofurahia utakaposoma taharasha hii tukufu. Karibuni! Prof. John Habwe Mkuu wa Idara

CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

SIWA LA KISWAHILI ni kijarida ambacho

kinachapishwa na Idara ya Kiswahili, Chuo Ki-

kuu cha Nairobi. Hili ndilo toleo la pili.

Karibuni ili mpate kufahamu habari za hivi

punde kabisa kutoka katika Idara ya Kiswahili.

Toleo hili pia linaangazia maswala mbali mbali

yanayohusiana na shughuli za Idara, wahadhiri,

wanafunzi na wafanyikazi wengine idarani. Wa-

hadhiri kadhaa wamechapisha vitabu vipya,

wengine wao wamehudhuria na kuwasilisha

makala katika makongamano mbali mbali ya

humu nchini na katika nchi za kimataifa.

Vile vile toleo hili lina habari kuhusu shughuli

za kufundisha Kiswahili ikiwa ni pamoja na mi-

hadhara, safari na tafiti za nyanjani, uwasilishaji

wa mapendekezo na matokeo ya utafiti unao-

fanywa na wanafunzi wa kiwango cha uzamili,

miongoni mwa mambo mengine.

KARIBUNI!

DIBAJI

CHUO KIKUU CHA NAIROBI

SIWA LA KISWAHILI

DIbaji………………………….1

mkuu wa idara…………...

TAhariri…………………….

Machapisho……………….

Makongamano…………..

Ufundishaji……………….

Mahafala………………….

Wahadhiri………………...

Wanafunzi………………..

USHIRIKIANO…………….

KIJARIDA CHA IDARA YA KISWAHILI JANUARI - MEI 2016

SALAMU ZA MKUU WA IDARA

YALIYOMO

Karibuni katika Idara ya Kiswahili. Nina furaha kubwa ku-waalika kusoma SIWA ambayo ndiyo mbiu yetu. Toleo hili linaonyesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na wa-hadhiri na wanafunzi wa Idara ya Kiswahili. Mathalani uta-julishwa kuhusu vitabu na machapisho ya hivi karibuni kabisa yaliyoandikwa na wasomi wetu wa Kiswahili, ushirikiano tulio nao na vyuo vingine ulimwenguni, makon-gamano yalioyoandaliwa ama kuhudhuriwa na wahadhiri wetu, pamoja na shughuli zao za utafiti. Vile vile, utasoma kuhusu shughuli za wanafunzi wetu wa Kiswahili. Singependa kukuondolea utamu wa mambo utakayofurahia utakaposoma taharasha hii tukufu. Karibuni!

Prof. John Habwe

Mkuu wa Idara

Page 2: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

TAHARIRI

MACHAPISHO

Wapenzi wa lugha teule ya Kiswahili ninawa-

karibisha katika toleo hili la SIWA. Hili ni

toleo la pili la kijarida hiki kinachochapishwa

na Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nai-

robi.

Ndani ya toleo hili, mtapata habari mbali mbali zinazohusu Idara ya Kiswahili. Habari hizi ni pamoja na shughuli za ufundishaji, utafiti na uchapishaji zinazofanywa na wa-taalamu wa lugha na fasihi ya Kiswahili waliomo katika Idara. Kumbuka kwamba

Idara hii ina wataalamu waliobobea katika nyanja mbali mbali za lugha na fasihi ya Kiswahili. Nina matumaini kwamba utafurahia kujisomea toleo hili la hivi karibuni kabisa la SIWA. Maoni yenu yanakaribishwa; yatume kwa [email protected]. Karibuni!

UKURASA 2 SIWA LA KISWAHILI

IDARA YA

KISWAHILI INA

WATAALAMU

WALIOBOBEA

KATIKA NYANJA

ANUWAI ZA

LUGHA NA

FASIHI YA

KISWAHILI

Dkt. Nyachae Michira Mhariri Mkuu

Tangu toleo la mwisho la SIWA, wataalamu kutoka Idara ya Kiswahili wameweza kuchap-isha kazi mbali mbali kama ifuatavyo. Prof. John H. Habwe akishirikana na wa-taalamu wengine ametoa kamusi ya kisasa ya lugha ya Kiswahili. Kamusi hii inajulikana kama KAMUSI ELEZI YA KISWAHILI (2016). Kamusi ni ya kisasa na imeandikwa kwa ufundi wa kipekee na ina maelezo mufti ya vidahizo. Miongoni mwa sifa kuu za KAMUSI ELEZI YA KISWAHILI ni kwamba ina: Vidahizo zaidi ya 45,000 Maneno yapatayo 1,000 mapya Matamshi ya kifonetiki ya vidahizo Ufafanuzi wa methali, semi na nahau Mifano mwafaka Michoro na picha maridhawa Upeo wa kimataifa

“KAMUSI ELEZI YA

KISWAHILI NI KA-

MUSI YA KISASA

ILIYOANDIKWA

KWA UFUNDI WA

KIPEKEE NA ILIYO

NA MAELEZO

MUFTI YA VIDA-

HIZO...ITAWAFAA

WATAALAMU,

WANAFUNZI NA

WATUMIZI WEN-

GINE WA LUGHA

YA KISWAHILI”

Page 3: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

MACHAPISHO

UKURASA 3 JANUARI - MEI 2016

Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

Kiswahili ambayo yametungwa na washairi mbali

mbali na kuhaririwa na Dkt. Iribe Mwangi na

wenzake. Diwani hii ilichapishwa na EAEP

mnamo mwaka wa 2015.

Pendo la Karaha ni riwaya iliyoandikwa na Prof.

John H. Habwe. Riwaya hii ina hadithi ya

kusisimua kuhusu changamoto ambazo vijana

wanapitia wanapokimbilia katika nchi za kigeni

wakitoroka umaskini kwao.

Kaza Macho ni diwani ya mashairi yaliyotungwa na

Prof. Wadi Wamitila. Diwani hii inasheheni

mashairi yenye ubunifu mkubwa pamoja na yana-

tathmini maswala mbali mbali yanayomkumba

mwanadamu. Diwani hii ilichapishwa na Vide

Muwa Publishers.

Ukuzaji wa Kiswahili: Dhima na Majukumu ya Asasi

Mbali Mbali ni kitabu kinacholeta pamoja makala

na tahakiki za wasomi mbali mbali kuhusu

maendeleo na ukuaji wa Kiswahili. Wasomi hao

wametathmini majukumu ya asasi kama vile elimu,

vyombo vya habari na mawasiliano, bunge, wizara

na vyuo vikuu katika maendeleo ya Kiswahili.

Kitabu hiki kimehaririwa na Dkt. Nyachae Mi-

chira na wenzake na kuchapishwa na Focus Books.

Page 4: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

Idara ya Kiswahili ina muafaka wa kubadil-

ishana wanafunzi na vyuo vikuu vingine vya

kimataifa. Kwa mfano, tuna mwanafunzi wa

Kiswahili anaysomea shahada yake katika

Chuo Kikuu cha Humboldt kule Ujeru-

mani. Mwanafunzi huyo anaitwa Shadrack

Kirimi (kulia).

Mpango huu wa ubadilishanaji wanafunzi

umewafaidi wanafunzi kutoka Idara ya

Kiswahili. Vile vile, Idara huwa inawapokea

wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya kigeni.

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Wanafunzi katika Nchi za Kigeni

Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nai-

robi ina muafaka na Chuo Kikuu cha

Masomo ya Kigeni cha Hankuk, Korea ya

Kusini ambapo msomi wa Kiswahili

anakwenda kufundisha Kiswahili katika

chuo hicho kwa muda wa miaka miwili.

Kwa hivi sasa, Dkt. Tom Olali anaelekea

kukamilisha kipindi chake cha miaka mi-

wili katika chuo kikuu hicho cha Hankuk.

Chuo hicho cha Hankuk, kupitia kwa

Idara ya Kiswahili, kimemteua Dkt. Nya-

chae Michira kuchukua nafasi hiyo kwa

miaka miwili kuanzia mwezi wa Agosti,

2016. Dkt. Michira anafundisha fasihi ya

Kiswahili na vile vile ni mtalaamu wa

maswala ya mitalaa.

Idara ya Kiswahili inampongeza Dkt. Mi-

chira kwa uteuzi huo na inamtakia kila la

kheri atakaposafiri kwenda Korea Kusini.

UKURASA 4 SIWA LA KISWAHILI

Idara ya

Kiswahili ina

muafaka na

chuo kikuu

cha masomo

ya kigeni cha

hankuk, kule

korea ya

kusini ambako

dkt. Michira

atakwenda

kuchukua

nafasi ya dkt.

Olali

Dkt. Tom Olali

Dkt. Nyachae Michira

IDARA INA

MPANGO WA KU-

BADILISHANA

WANAFUNZI NA

VYUO VIKUU VYA

KIGENI KWA

MANUFAA YA

WANAFUNZI

WETU

Page 5: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

Wataalamu wa Kiswahili Prof. RayyaTimammy na Dr. Iribe Mwangi

walihudhuria Kongamano la 29 la Swahili kule Bayreuth, Ujerumani kutoka

tarehe 6 hadi 8 Mei, 2016. Wasomi hao waliwasilisha makala yanayohusu

mada mahususi katika nyanja zao.

Prof. Timammy ni mtaalamu wa fasihi huku Dkt. Iribe ni mwanaisimu.

Wote wawili wamechapisha kazi nyingi kuhusu maswala mbali mbali ya

Kiswahili.

Prof. Timammy aliwasilisha makala juu ya “Tamathali za usemi na taswira

katika Utenzi wa Ukimwi ni Zimwi”.

Dkt. Iribe naye akazungumza kuhusu maswala ya fonolojia ya Kiswahili katika makala aliyoiita “Analytical Problems in Standard Kiswahili Pho-nology”.

Katika kongamano hilo, kulikuwepo waandishi watajika wa Kiswahili kama vile Prof. Abdilatif Abdalla mtunzi wa diwani maarufu ya Sauti ya Dhiki.

KONGAMANO LA 29 KISWAHILI LA BAYREUTH

Page 5 VOLUME 1, ISSUE 1

KONGAMANO LA

BAYREUTH

LILIWALETA

PAMOJA

WATAALAMU NA

WAANDISHI

WATAJIKA WA

LUGHA YA

KISWAHILI KAMA

VILE PROF.

ABDILATIF

ABDALLA, PROF.

RAYYA TIMAMMY,

DKT. IRIBE

MWANGI, NA

WENGINE WENGI

Dkt. Iribe (kulia) na Prof. Abdilatiff Abdalla, Mohamed Kellef na Gikambi wakiwa Bayreuth

Prof. Timammy (ameketi kulia) akiwa na washiriki wengine katika kongamano la Bayreuth

Page 6: CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya

Shairi la Shabaan Robert Akisifu Kiswahili

Idara ya Kiswahili,

Chuo kikuu cha Nairobi,

s.l.p. 30197 00100 Nairobi, kenya

kijarida hiki cha

siwa

kinachapishwa

na idara ya

kiswahili, chuo

kikuu cha

nairobi.

haki zote

zinamilikiwa na

idara.

Education Building

Ghorofa ya 3

Mwenyekiti: Ed. 311

Mhariri Mkuu: Ed. 316

TITI LA MAMA

Titi la mama li tamu, hata likiwa la mbwa,

Kiswahili naazimu, sifayo inayofumbwa,

Kwa wasio kufahamu, niimbe ilivyo kubwa,

Toka kwa chemchemu, furika palipozibwa,

Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.

Lugha kitu kitukufu, hapana nichukiayo,

Kila lugha ashirafu, kwangu kwa masaidiyo,

Lugha zenu nazisifu, yangu nachieni nayo,

Hapana lugha dhaifu, sitatii wabezayo,

Lugha yangu taisifu, mpaka kukoma moyo,

Ama mwili kuwa mfu, maisha tembe sinayo.

Wasiliana nasi kwa barua-pepe: [email protected]

Tutembelee kwenye tovuti: www.kiswahili.uonbi.ac.ke

KUHUSU IDARA YA KISWAHILI

Idara ya Kiswahili ilianzishwa mnamo mwaka wa 2013. Kabla ya

hapo, taaluma ya Kiswahili ilijumuishwa na kufundishwa chini ya

Idara ya Isimu na Lugha. Kwa kuwa hadhi ya lugha ya Kiswahili ili-

badilika kwa mujibu wa katiba mpya, Chuo Kikuu cha Nairobi kil-

ionelea bora kuasisi idara huru ya kushughulikia maswala ya Kiswa-

hili.

Idara ya Kiswahili ina malengo ya kutoa mchango wake katika ku-

fanikisha Kiswahili kitekeleze ipasavyo majukumu yake kama lugha

rasmi na lugha ya taifa. Idara inanuia kufanya hivyo kupitia kufun-

disha, kufanya utafiti, kuchapisha vitabu na majarida.

Hivi sasa, Idara ya Kiswahili ina wahadhiri wapatao 20 pamoja na

wanafunzi wanaosomea shahada za awali, za uzamili na za uzamifu

katika nyanja tofauti tofauti za lugha na fasihi ya Kiswahili.

CHUO KIKUU

CHA NAIROBI