22
Conservaon Farming Unit www.conservaonagriculture.org Mwongozo wa Wakulima Kaka Kuchagua na Kutumia Viua Magugu – 2015

Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Conservation Farming Unit www.conservationagriculture.org

Mwongozo wa Wakulima Katika Kuchagua na Kutumia Viua Magugu – 2015

Page 2: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

2

ShukraniTafsiri ya Mwongozo huu wa Wakulima katika Kuchagua na Kutumia Viua Magugu imefanywa na kampuni ya CROPBASE (T) Ltd ya mjini Arusha kwa ufadhili wa CFU-Tanzania. CFU- Tanzania inatekeleza mradi wa miaka mitano wa Kilimo Hifadhi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Nchi ya Norway (Norad) kupitia Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) linalotekeleza programu ya Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) awamu ya pili.

Kwanza kabisa CFU-Tanzania inatoa shukrani zake za dhati kwa CFU-Zambia kwa kuruhusu kijitabu/kijarida hiki kutafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili ili kiweze kutumiwa na wakulima na maafisa ugani hapa nchini.

Pili CFU-Tanzania inawashukuru Norad na ACT kwa kufadhili kazi ya kutafsiri kijitabu/kijarida hiki.

Vile vile, CFU-Tanzania inaishukuru kampuni ya CROPBASE (T) Ltd kwa kutafsiri kijitabu/kijarida hiki.

Mwisho, sio rahisi kuwashukuru watu wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha zoezi hili la kutafsiri kijitabu hiki. CFU-Tanzania inawashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wamesaidia kufanikisha zoezi hili.

Kama una jambo lolote linalohusiana na Kijitabu/Kijarida hiki wasiliana nasi kwa anuani ifuatayo: CFU-Tanzania;

S. L. P. 78851; Dar Es Salaam; Barua pepe: [email protected]

Page 3: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

3

Maneno yaliyotumika sambamba/kwa kubadilishana

(i) Kunyunyiza Kupiga dawa(ii) Mnyunyuziaji Mpiga dawa(iii) Dawa Kiuatilifu (kiua magugu, n.k)(iv) Bomba la kunyunyuzia Bomba la kupiga dawa

Page 4: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

4

YALIYOMO UKURASA

Njia 16 za kufanikiwa 3 – 8Usalama 3 Viua Magugu visivyopendekezwa 5Bomba la kunyuniza na maelezo yake 7Jinsi ya kunyunyiza 9

Viuatilifu 9 - 17Glyphosate 9 - 10Atrazine 5, 11, 15 Atrazine and Cyanazine 11Topramesone and Dicamba, Mesotrione 12, 16Acetolchlor, Metolachlor 13Nicosulfuron 14, 15Halosulfuron 14Sulcotrione 152,4-D 15 MCPA 15Bromoxynil 15Fluazifop 16Quizalofop 16Haloxyfop 16Cethlodim 16

Conservation Farming Unit - CFUMwongozo wa Viua Magugu kwa Wakulima Wanaokutumia mabomba; Toleo la 2015

Zingatia: Kijitabu hiki kimetayarishwa kama mwongozo wa wakulima katika kuchagua na kutumia Viua Magugu. Japokuwa muda na umakini mkubwa umetumika wakati wa kuandaa mwongozo huu wa mafunzo, CFU aidha haitawajibika kwa madhara yoyote yatakayotokea kwenye mazao kwa matumizi yasiyosahihi ya kiua magugu chochote kilichotajwa kwenye kijitabu hiki au haitawajibika na ubora wa kiua magugu chochote kitakachotolewa na wauzaji wa Viua Magugu.

Viuatilifu (Inaendelea) Ukurasa

Prometryn and Fluometuron 16Chlorimuron 17Pendimethalin 17Metribuzin 17Bentazone 17

Mawasiliano 18

Page 5: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Hatua 1. Usalama kwanza

Mara zote soma maelekezo ya usalama kwenye kibandiko cha Kiuatilifu na fuata maelekezo husika;

Kamwe usinunue au kutumia viuatilifu ambavyo havina kibandiko halisi au hivijafungwa kwa sili. Usisafirishe Viua Magugu vikiwa vimechanganywa na vyakula au vinywaji;

Wakati wa kunyunyiza (kupiga dawa) hakikisha unavaa mavazi yafuatayo:- Suruali ndefu (ni vyema iwe ya kitambaa kisichopitisha kemikali), shati la mikono mirefu, buti, kofia, glovu na miwani ya kulinda macho;

Wakati wakupima Viua Magugu toka kwenye kifungashio chake mara zote vaa glovu na miwani;

Usile au kuvuta sigara wakati wa kupiga dawa;

Kama Bomba linavuja tafuta kunakovuja na hakikisha panazibwa mara moja;

Wakati wakusafisha nozo au chujio (filters) usipulize kwa mdomo;

Mara zote hifadhi chupa zenye Viua Magugu sehemu salama, mbali na nyumba yako na mbali na watoto;

Vyombo vilivyoisha Viua Magugu visitumike kwa kazi nyingine. Safisha vyombo vilivyoisha kemikali kwa maji na vitoboe ili visifae kwa matumizi mengine. Teketeza vyombo husika kwa kuvitupa kwenye shimo la choo au kuvifukia. Ni njia sahihi zaidi kama vitachomwa moto kwenye maeneo mbali na makazi ya watu yaliyotengwa kwa kazi hiyo;

Baada ya kumaliza kazi ya kupiga dawa, oga kwa maji safi na sabuni, badilisha nguo, fua mavazi ya kujikinga (mavazi ya kunyunyizia) kwa kuyatenganisha na mavazi ya nyumbani ;

UKWELI MAHUSUSI: Hauhitaji kutumia Viua Magugu kutekeleza kilimo Hifadhi. Kama wewe ni mkulima wa jembe la mkono unaweza kuendelea kupalilia shamba lako kwa kutumia jembe la mkono. Kama kilimo chako ni cha jembe la kukokotwa na wanyama kazi (ng’ombe) unaweza kulima juu juu ila usipalilie kwa plau na usinyanyulie udongo. Hata hivyo kwa kuwa wakulima wengi tayari wanatumia Viua Magugu, mwongozo huu utakusaidia kuchagua Viua Magugu stahiki kwa ajili ya kudhibiti magugu yaliyopo shambani kwako.

Hatua 16 za kufanikiwa

5

Page 6: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

6

Hatua ya 2: Kamwe usinunue au kutumia Viua Magugu mpaka uwe umepata mafunzo yakutosha toka kwa mratibu wa wakulima wa CFU au Bwana shamba. Hudhuria mafunzo yanayoandaliwa na waratibu wa wakulima au wakulima wawezeshaji ili ujifunze jinsi ya kutumia mabomba yakunyunyuzia viuatilifu na kuyatunza, jinsi ya kuchagua Viua Magugu sahihi, jinsi ya kuchanganya Viua Magugu na unyunyizaji pamoja na usalama kwa ujumla. Hapa chini ni aina ya mabomba ambayo CFU inayapendekeza.

Hatua ya 3: Nunua bomba zuri la ujazo wa lita 16.

Hatua ya 4: Hakikisha una nozo mbili sahihi ili kunyunyiza Viua Magugu kwa usahihi- Hii ni muhimu sana. Pia fahamu jinsi ya kufunga nozo kwenye bomba lako kwa usahihi.

Nozo ya rangi ya Bluu Nozo ya rangi ya Chungwa (Orange)

JACTO XP - Lita 16 JACTO HD 400 – Lita 16 GUARANAY – Lita 16 MATABI – Lita 16

Hatua ya 5: Siku hizi kuna aina nyingi za Viua Magugu kwenye soko. Chunguza ni magugu gani sumbufu zaidi kwenye shamba lako ili ununue Viua Magugu stahiki. Fahamu ni Viua Magugu vipi inafaa kutumika kwenye mazao tofautiHatua ya 6: Jifunze majina ya viuatilifu vilivyoko ndani ya Viua Magugu. Viua Magugu vingi vina majina tofauti ya kibiashara lakini ndani yake vina viuatilifu vinavyofanana. Mfano – Kuna aina 100 za PANADO ila zote zina dawa aina moja ya PARACETAMOL inayotibu maumivu. Hata hivyo kiasi cha paracetamol ndani ya vidonge kinaweza kuwa tofauti aidha kingi au kidogo hivyo ni vyema kusoma kibandiko ujue ni vidonge vingapi unatakiwa kumeze. Hivyo hivyo kwa Viua Magugu- Soma kibandiko kwanza.Hatua ya 7: Hakikisha unajua jina la kiuatilifu unachoenda kununua kitadhibiti magugu shambani kwako kabla ya kwenda dukani. Kuna chupa nyingi sana ndani ya duka. Usitegemee ushauri wa muuza duka kwani anaweza kukuuzia kiua magugu ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye maelezo ili uelewe ni kiua magugu gani unaenda kununua. Hatua ya 9: Ukiwa dukani soma kibandiko ili uwe na uhakika kuwa kiuatilifu kilichopo ndani ya kiua magugu ni sahihi na ndicho unachotaka. Ili kufanikisha hili soma maelekezo humu ukurasa wa 9-17.

Page 7: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

VIUA MAGUGU AMBAVYO HAVIPENDEKEZWI NA CFU

Kwa kuwa jambo muhimu kwenye Kilimo Hifadhi ni Kilimo Mzunguko na kwa kuwa baadhi ya viuatilifu ni sumu na ni hatari kuvitumia, kuna idadi ya Viua Magugu ambavyo havipendekezwi na CFU na vinapaswa kuviepuka. Viua Magugu hivyo vimeorodheshwa hapa chini:

Viua Magugu vyote vyenye kiuatilifu paraquat havipendekezwi Kwani kiuatilifu hiki ni sumu sana na hatari kwa binadamu na wanyama.

Gramoxone Uniquat Afriquat Paraquat 20% Mupaxarone Leader 24 Herbikill Paraforce Harpoon Parabat

Viua Magugu vyote vyenye kiuatilifu atrazine pekee au atrazine na terbulthylazine kwa ajili ya kudhibiti magugu kwenye mahindi havipendekezwi kwasababu kama utaotesha mimea jamii ya mikunde au mazao mengine kwenye shamba hilo hilo msimu unaofuata yanaweza kudhurika. Viua magugu vifuatavyo vina atrazine pekee au atrazine na terbuthylazine.

Atracell Agrazine Atraforce Farmizine 600C

Atrazine 500SC

Afrizine Atraprime Bullet Cheetah Scorpion

Emerald Ballistic Gold

Rhino

Viua Magugu vyote vyenye viuatilifu formesafan na imazethapyr kwa ajili ya kudhibiti magugu kwenye Maharage ya Soya na Karanga havipendekezwi kwasababu kama utaotesha Mahindi kwenye shamba hilo hilo msimu unaofuata yanaweza kudhurika.

Flex Caddy Formesafan Quizafom Imax Image Zephyr Imaze Legume Weed Killer

Hatua ya 10: Jifunze Viua Magugu vya kuepuka na ambavyo vistahili kutumika

Kuna baadhi ya Viua Magugu ambavyo vinamatumizi mahsusi na vinavyostahili kutumiwa kwa tahadhari kama unataka kuzungusha mazao yako msimu unaofuata. Maelezo ya Viua Magugu hivyo yako ukurasa wa 12.

7

Page 8: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

8

USHAURI MAHUSUSI.Kama kibandiko cha kiua magugu hakina maelezo yakutosha kuhusu kiuatilifu kilichopo ndani yake na kiasi cha kemikali yake kwenye vipimo vya gramu au asilimia usinunue kiua magugu hicho . Tumia muongozo huu kutafuta mbadala wake au pata ushauri toka kwa mtaalamu wa CFU.

Hatua ya 12: Hakikisha una vifaa vya vipimia stahiki vya kupima kiasi sahihi cha kiua magugu cha kuchanganya na maji katika Bomba lako la lita 16. Kuna aina nyingi tofauti za vifaa hivi na vya ukubwa tofauti kuanzia milimita 50 hadi lita moja na zaidi. Badhi ya Viua Magugu huambatanishwa na vipimio vidogo. Kipimio cha ukubwa wowote ulicho nacho hakikisha kimeandikwa kwa nje kuonyesha vipimo vyake kama picha pembeni inavyoonyesha. Kamwe usikadirie kiasi cha kiua magugu chakuweka kwenye bomba lako ni vyema kuwa na uhakika. Ili kujua kiasi sahihi cha kiua magugu cha kutumia fuata maelekezo yaliyoko ukurasa x hadi y. Kamwe usitumie kipimio cha Viua Magugu kwa kazi nyingine. Safisha vipimio vyako kwa maji safi baada ya kumaliza kunyunyiza na hifadhi mbali na watoto.

50ml--

75ml--

100ml--

125ml--

150ml--

175ml--

200ml--

225ml--

250ml--

Hatua ya 13: Hakikisha nozo imefungwa sehemu stahiki katika uelekeo sahihi kuelekea kwenye lance ya bomba.

Hatua ya 14: Ili kuchanganya Viua Magugu kwa usahihi, jaza maji safi nusu tenki kupitia kwenye chujio la mfuniko wa Bomba lako, ongeza kiasi stahiki cha kiua magugu halafu jaza maji safi hadi kwenye alama inayoonyesha lita 16 nje ya bomba. Funika bomba lako halafu tikisa bomba lako vyema kuchanganya kiuatilifu na maji .

Uelekeo wa nozo

Hatua ya 11: Mara zote tumia maji safi kuchanganyia Viua Magugu. Kama maji yana matope au ni machafu kiua magugu hakitafanya kazi vizuri, chujio (filters) za bomba lako zitaziba na bomba linaweza kuharibika.

Page 9: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Hatua ya 15: Jifunze utunzaji sahihi wa Bomba lako

4. Mkono wa pampu (Pump

handle )

1. Valvu ya kufungulia

dawa (Trigger valve)

2. Valvu ya kudhibiti presha

5. Lance

3. Pampu

9. Tenki

8. Mfuniko

7. Mpira wa kupitisha dawa

6. Nozo na kishikio chake

9

Kichujio cha kwanza hupatikana chini ya mfuniko wa tenki (8*)

Kichujio cha pili mara nyingi hupatikana ndani ya valvu ya kuruhusu dawa (1*)

Kichujio cha tatu hupatikana kwenye kishikio cha nozo nyuma ya nozo (6*) Aina hii ya kichujio hujulikana kama “top hat”.

Bomba bora lina aina 3 za vichujio (Filters) vinavyozuia nozo kuziba. Mara zote hakikisha chujio zote na nozo ni safi.

Jifunze sehemu zote za Bomba lako ambazo hufanya lifanye kazi na ujue kazi zake.

Page 10: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Hatua ya 16: Jifunze kunyunyuzia Viua Magugu kwa Usahihi

Mita 50

Sentimita 50

Kupata matokeo mazuri wakati wa unanyunyiza kwa kutumia nozo za rangi ya chungwa (Orange) au Bluu unatakiwa uzinyanyue kimo cha sentimita 50 juu ya magugu husika. Pia kasi ya kutembea iwe sahihi. Ukitembea haraka kiasi cha kiua magugu kitakachotumika kinaweza kuwa kidogo sana, na ukitembea taratibu sana utatumia kiua magugu kingi zaidi. Fanya mazoezi hadi ufanye kwa usahihi.. Funga kipande cha kamba kwenye nozo na funga kitu kizito chini umbali wa sentimita 50 (angalia picha hapo juu). Chimbia mambo/pegi mbili ardhini kwenye umbali wa mita 50. Jaza maji safi kwenye bomba halafu nyunyiza ukiwa umenyanyua nozo yako kwenye kimo sahihi kadiri unavyotembea. Tafuta mtu wa kukusaidia kuangalia muda unaotumia kutembea toka mambo moja kwenda nyingine kwa kutumia saa au simu. Kwa kawaida unatakiwa utumie sekunde 45 hadi 50 kutembea umbali huo wa mita 50.

Wakati wa kupiga dawa tembea katikati ya mistari ya mazao ukiwa umenyanyua nozo kimo cha sentimita 50 juu ya magugu au juu ya ardhi kama unanyunyiza kiua magugu kinachotumika kabla mimea au magugu kuota.

Kumbuka ushauri huu ni kwa mazao yaliyooteshwa umbali wa sentimita 90 mstari hadi mstari. Chochea mkono wa pampu taratibu na kwa kuendelea ili kuwa na presha inayofanana.

MAZOEZI NI MUHIMU ILI KUWA NA UJUZI MAHILI WA UNYUNYIZIAJI VIUA MAGUGU.

Tumia saa au simu kujua muda uliotumika kutembea kati ya mambo mbili zenye umbali wa mita 50.

UKITUMIA VIUA MAGUGU VISIVYO SAHIHI, KWA MAZAO YASIYO SAHIHI, KWA MUDA USIO MUAFAKA NA KWA KUTUMIA BOMBA LISILOTUNZWA VIZURI NA KUPATA MATOKEO YA KUKATISHA TAMAA UJILAUMU MWENYEWE.KAMA UTADONDOKA KWENYE BAISKELI KUTOKANA NA KUTOJIFUNZA KUENDESHA BAISKELI KWA USAHIHI, JE NI KOSA LA BAISKELI?

Page 11: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

MUONGOZO WA VIUATLIFU VYA KUDHIBITI MAGUGU

Jina Aina Lita kwa Hekta.

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo Ushauri

ROUNDUP Kimiminika 3 650 MLS (CC) NOZO YA RANGI YA CHUNGWA YA FLAT FAN

(ORANGE FLAT FAN)

Round-Up hutengenezwa na MONSANTO, kampuni ya kwanza kugundua glyphosate.Bidha za Round up zenye rangi ya kijani zina kiasi kidogo cha glyphosate kwa lita kuliko za rangi ya njano hivyo dawa nyingi inatumika.

HOCKPHOSATE Kimiminika 3 650 MLS (CC)GLYPHADER Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYPHON 360 Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GUARD Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYPHOSNOW Kimiminika 3 650MLS (CC)Bidhaa zenye rangi ya njano zina kiasi kikubwa cha glyphosate kwa lita hivyo kiasi kidogo kinatumika.

Hata hivyo kabla ya kununua piga mahesabu kama lita 2 ya kiua magugu hiki zitagharimu pesa nyingi zaidi au kidogo ukilinganisha na lita 3 za kiua magugu chenye rangi ya kijani

PIRANAH Kimiminika 3 650 MLS (CC)

TWIGASATE Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYPHOSATE Kimiminika 3 650 MLS (CC)

WOUND OUT Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYFORCE Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYPHOCURE Kimiminika 3 650 MLS (CC)

GLYPHOSATE. Kiuatilifu hiki kinatumika kuua magugu yanayoota shambani kabla mazao hayajaoteshwa. Pia kinaweza kutumika mara tu baada ya kuotesha ila kabla mbegu hazijaanza kuota. Kamwe usinyunyize juu ya mazao yaliyoota kwani Glyphosate inaua mimea mingi ya kijani. Kiatilifu hiki kinaua magugu mengi jamii ya nyasi ikiwa ni pamoja na kapinga na magugu mengine lakini haidhibiti ndago vizuri .Matokeo bora yanapatikana kama magugu ni machanga na ya kijani na si marefu zaidi ya kimo cha futi moja, pia kama kuna upepo kidogo au hakuna kabisa na hakuna mvua masaa 4 baada ya unyunyizaji kufanyika. Kuwa makini na upepo kwani ukipeleka dawa kwenye mazao yaliyoko jirani yatakufa. Kama magugu yamekuwa marefu itakulazimu kutumia dawa nyingi zaidi ya kiasi kinachoonyeshwa hapa chini na itagharimu pesa nyingi . Gyphosate inaweza kutumika kabla yakuotesha zao lolote.

Viua Magugu vyenye kiuatilifu kiitwacho Glyphosate

11

Page 12: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Jina Aina Lita/paketi kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

NOZO Ushauri/ Maelekezo

CYCAT KIMIMINIKA 2 450 MLS (cc) NOZO YA RANGI YA CHUNGWA YA FLAT FAN (ORANGE FLAT

FAN)

Kama ilivyo kwa Viua Magugu vingine vyote kiasi kinachotakiwa kufanya kazi vyema kinatategemea urefu na aina ya magugu, ujuzi wa mnyunyizaji na mazingira wakati wa kupiga dawa.

Mara nyingi ni jambo zuri kuchagua sehemu ya kunyunyiza kiasi kidogo na na sehemu nyingine ya kunyunyiza kiasi kikubwa na kuangalia matokeo kwa ajili ya rejea siku zijazo.

AGRICELL KIMIMINIKA 2 450 MLS (cc)

AFRICALE KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

GARUD KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

GLYCEL KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

KALACH 700 KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

TOUCHDOWN KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

GLYPHOMAX KIMIMINIKA 2 450 MLS(cc)

WEED ALL UNGA 12 PAKETI 1 NOZO YA RANGI YA CHUNGWA YA FLAT FAN (ORANGE FLAT

FAN)

Mara zote angalia kibandiko cha paketi kionyeshe – ‘Paketi 1 kwenye lita 16 za maji’ kama maelekezo haya hayapo usinunue. Tumia paketi 2 /kwa bomba kama magugu aina ya kapinga lipo shambani

MUSCLE UP UNGA 12 PAKETI 1

ERASE UNGA 12 PAKETI 1

Viua Magugu vingine vyenye kiuatilifu Glyphosate

12

Kila mwaka viuatilifu vyenye glyphosate huingia sokoni. Kama huna uhakika wa kiasi gani cha kutumia soma kibandiko. Kama kibandiko kinaonyesha 360 TINDIKALI ( ACID) kiasi cha kutumia ni lita 3 kwa hekta na kama kinaonyesha 480 TINDIKALI (ACID ) kiasi cha kutumia ni lita 1 kwa hekta. Kama kibandiko kinaonyesha CHUMVI ( SALT ) pekee muulize Afisa ugani wako kabla ya kununua.

Page 13: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Viua Magugu vyenye viuatilifu Atrazine na Cyanazine kwa kudhibiti magugu kwenye MAHINDI

Jina Aina Lita kwa Hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16 na kwa aina ya udongo

Nozo Angalia kibandiko kujua uwezo wa Kiuatilifu

ILI KUPATA MATOKEO BORA UDONGO UWE NA UNYEVU AU UWE UMELOA NA EPUKA KUNYUNYIZA WAKATI WA UKAME

Udongo wa kichanga

UDONGO TIFUITIFU

UDONGO MFINYAN

ZI

Kila mwaka kuna aina nyingi za Viua Magugu vyenye kiuatilifu kile kile zinaingia sokoni, ila vinakuwa na majina tofauti ya kibiashara. Pia kiasi cha kiuatilifu ndani ya kiua magugu kinaweza kubadilika.

HIVYO KWA AINA HII YA VIUA MAGUGU SOMA KIBANDIKO KABLA YA KUNUNUA.KIBANDIKO LAZIMA KIONYESHE AIDHA ASILIMIA 25% ATRAZINE, ASILIMIA 25% CYANAZINE KWA LITA AUGRAM 250g ATRAZINE ,GRAM 250g CYANAZINEKWA LITA

Kama kibandiko hakionyeshi chochote usinunue.

BLAZINE KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS (CC) 280 MLS(CC 320 MLS NOZO ZA BLUU AINA YA

FLAT FAN (BLUE FLAT

FAN)

ATRAPACK PLUS KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 280 MLS(CC 320 MLS

MAIZE WEEDKILLER

KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 280 MLS(CC 320 MLS

FARMAZINE KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

EXCEL KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS(CC 320 MLS

SCORPION KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

SUCCESS KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

CYATRA KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS (CC 28O MLS (CC 320 MLS

INFERNO KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

KRIMIX KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

AFRISTICK KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

ETHANO KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS (CC 28O MLS (CC 320 MLS

MAIZE WEEDER KIMIMINIKA 2.75 to 4.0 220 MLS(CC 28O MLS (CC 320 MLS

ATRAZINE + CYANAZINE: Kiua magugu hiki kinaweza kutumika kwenye shamba la mahindi baada ya kuotesha ila kabla ya kuota au mara tu baada ya kuota. Kwa matokeo bora, magugu yasizidi urefu wa inchi 1 - 2. Viua Magugu hivi ni maarufu miongoni mwa wakulima na mara nyingi vinatumika kuua magugu yanayoota baada ya Glyphosate kutumika. kinadhibiti magugu mbalimbali jamii ya nyasi na pia magugu yenye majani mapana (BLW) ila sio mulungwe, ndao na magugu ya zamani yenye mizizi mirefu na yale ambayo huishi wakati wa kiangazi kila mwaka.

13

Page 14: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Kiua magugu chaguzi (selective herbicide) chenye kiuatilifu Topramezone na Dicamba kwa kudhibiti magugu kwenye MAHINDI

STELLA STAR: Kiua magugu hiki ni maarufu miongoni mwa wakulima na kinatumika kudhibiti magugu kwenye mahindi baada ya mazao kuota. Hudhibiti magugu jamii ya nyasi (grass weeds) na magugu yenye majani mapana (BLW). Magugu yanadhibitiwa vyema zaidi yakiwa na majani 3 – 4 ila pia yanaweza kudhibitiwa yakiwa na kimo zaidi ya hicho kama yatakuwa yanashindana na mazao kwenye kuchukua mbolea, mwanga na maji. Magugu yaliyonyunyizwa STELLA STAR huchukua siku 7 - 10 kuonyesha matokeo hivyo kuwa mvumilivu. Usinyunyize juu ya mazao baada ya mahindi kufikia kimo cha sentimita 80. Magugu yasiwe yamesinyaa kwa ukame wakati wa kupiga dawa.

Jina Aina Lita kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo Ushauri/Maelekezo

Haihitajiki udongo uwe na unyevu, STELLA STAR haihitaji mvua baada ya kutumika ndipo iweze kudhibiti mulungwe au ndao. Hiki ni kiua magugu muhimu na kinaweza kutumika katika mazingira tofauti tofauti.

STELLA STAR KIMIMINIKA 1 80 MLS (CC) BLUE FLAT FAN

Kiua magugu chenye kiuatilifu Mesotrione kwa ajili ya kudhibiti magugu kwenye MAHINDI

MESOTRIONE: Mesotrione pia hutumika baada ya mahindi na magugu kuota.. Magugu lazima yawe yameota vyema na sio kwa taabu kutokana na ukame. Inaweza kudhibiti magugu nyasi (grass weeds) na magugui yenye majani mapana (BLW). Soma kibandiko kujua ni magugu gani yanathibitiwa na kiua magugu hiki

Jina Aina Lita kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo Ushauri/Maelekezo`Si lazima udongo kuwa na unyevu wala mesotrione haihitaji mvua baada ya kunyunyiza ili kufanya kazi vizuri. Haiwezi kudhibiti mulungwe au ndao.

MESOTRIONE SC KIMIMINIKA 0.35 30 MLS BLUE FLAT FAN

BALLISTIC SC 480G KIMIMINIKA 0.35 30 MLS

MESOTRIONE 480G KIMIMINIKA 0.35 30 MLS

14

Page 15: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Kiua magugu chenye kiuatilifu Acetochlor au Metalochlor kwa ajili ya kudhibiti magugu kwenye MAHINDI

Jina Aina Lita kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16 kwa aina za udongo

Nozo Angalia kibandiko kujua uwezo wa Kiuatilifu

ILI KUPATA MATOKEO BORA LAZIMA UDONGO UWE NA UNYEVU AU EPUKA KIPINDI CHA KIANGAZI

Udongo Kichang

a

Udongo TIFU TIFU

Udongo Mfinyanzi

Viua Magugu hivi vina aidha gramu 900g, 750g au 500g za viuatilifu kwa lita hivyo viwango tofauti vya kutumia vinapendekezwa. Acetochlor itadhibiti aina mbalimbali za magugu jamii ya nyasi ya msimu na baadhi ya magugu yenye majani mapana (BLW) kwenye mahindi na karanga.

Changanya na atrazine/cyanazine ili kupata matokeo mazuri kwenye zao la mahindi pekee.

ACETOCHLOR 900g KIMIMINIKA 0.75 – 1.8 90 MLS 12O MLS 180 MLS BLUE FLAT FAN

JAGUAR 900g KIMIMINIKA 0.75 – 1.8 90 MLS 120 MLS 180 MLS

HURRICANE 750g KIMIMINIKA 0.9 – 2.0 100 MLS 150 MLS 220 MLS

SAPPHIRE 750g KIMIMINIKA 0.9 – 2.0 100 MLS 150 MLS 220 MLS

ACETOCHLOR 500g KIMIMINIKA 1.4 – 3.25 160 MLS 220 MLS 320 MLS

METALOCHLOR

ILI KUPATA MATOKEO BORA LAZIMA UDONGO UWE NA UNYEVU AU EPUKA KIPINDI CHA KIANGAZI

Udongo Kichang

a

Udongo TIFU TIFU

Udongo Mfinyanzi

TOLLA 960g KIMIMINIKA

0.9 – 2.0 85 MLS 100 MLS 140 MLS BLUE FLAT FAN

Metolachlor inadhibiti magugu jamii ya nyasi ya msimu na baadhi ya magugu yenye majani mapana (BLWs) kwenye mahindi na pia kwenye Pamba, Maharage ya Soya, Karanga na Alizeti.

METALOCHLOR 960g KIMIMINIKA

0.9 - 2.0 85 MLS 100 MLS 140 MLS

DUAL GOLD 960g KIMIMINIKA

0.9 – 2.0 85 MLS 100MLS 140 MLS

BUCCANEER 960g KIMIMINIKA

0.9 – 2.0 85 MLS 100MLS 140 MLS

DUAL MAGNUM KIMIMINIKA

0.6 – 1.3 55 MLS 70 MLS 115 MLS

S-METOLACHLOR KIMIMINIKA

0.6 – 1.3 55 MLS 70 MLS 115 MLS

ACETOCHLOR: Kiua magugu hiki kinaweza kutumika baada ya mahindi kuoteshwa ila kabla ya kuota au punde yanapoanza kuota. Hutumika kama atrazine/cyanazine zinavyotumika. Acetochlor inadhibiti ndao za Njano na yaweza kuchanganywa na cyanazine/atrazine ili kufanya kazi vizuri zaidi. Nyunyiza wakati udongo una unyevu, lazima mvua inyeshe ndani ya siku 14 ili kupata matokeo mazuri.

15

Page 16: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Viua Magugu vyenye kiuatilifu nicosulfuron kwa ajili ya kudhibiti magugu ya Mulungwe kwenye Mahindi

Jina Aina Gramu kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo TAHADHARI

MULUNGWE WEED KILLER UNGA 60 G 4.8 G BLUE FLAT FAN Usioteshe Karanga kwenye eneo hili kwa misimu miwili.

POSI POST UNGA 60 G 4.8 G

FORTRESS UNGA 60G 4.8 G

Viua Magugu hivi vina kiuatilifu kiitwacho nicosulfuron. Kwa kuwa kiasi kinachohitajika kuweka kwenye bomba la lita 16 ni kidogo sana, wazalishaji husambaza nicosulfuron kwenye vipimo vinavyotosha kwa Bomba moja, kama sivyo usinunue kiua magugu hiki. Tumia Viua Magugu hivi mara moja baada ya magugu na mahindi kuota.

Jina Aina Gramu kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo TAHADHARI

HURRICANE UNGA 50 G 4 G BLUE FLAT FAN Usioteshe Maharage ya Soya au Karanga katika eneo moja kwa misimu miwili. Mvua ikinyesha ndani ya masaa 6 baada ya kunyunyiza itapunguza kasi ya kudhibiti magugu husika.

BRIGADIER UNGA 50 G 4 G

NUTGRASS KILLER UNGA 50 G 4 G

Viua Magugu vyenye kiuatilifu kiitwacho halosulfuron kwa ajili ya kudhibiti magugu ya Njano ya Ndao (Yellow Ndao) kwenye Mahindi

Viua Magugu hivi vina kiuatilifu kiitwacho halosulfuron . Kwa kuwa kiasi kinachohitajika kuweka kwenye bomba la lita 16 ni kidogo sana, wazalishaji husambaza nicosulfuron kwenye vipimo/ujazo vinavyotosha kwa Bomba moja, kama sivyo usinunue kiua magugu hiki. Tumia baada ya Mahindi na Ndao kuota.

16

Page 17: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Aina nyingine za Viua magugu kwa ajili ya kudhibiti magugu jamii ya nyasi (Grass weeds) na magugu yenye

majani mapana (BLW) kwenye Mahindi

Jina Aina Lita kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16 kwa aina mbalimbali za udongo

Aina ya Nozo 

Udongo kichanga

Udongo tifutifu Udongo mfinyanzi

ARMADILLO KIMIMINIKA O.8 – 2.0 1.2  1.5 2.0  BLUE FLAT FANSUCCEED KIMIMINIKA ?  ? ? ?  BLUE FLAT FANLUMAX KIMIMINIKA 4 - 5 320 - 400 BLUE FLAT FAN

ARMADILLO ina viuatilifu sulcotrione na atrazine. SUCCEED na LUMAX vina viuatilifu atrazine mesotrione na nicosulfuron. Viua magugu vyote hivi vinaweza kutumika baada ya magugu na mazao kuota . Vyote vinyunyizwe kwenye ardhi yenye unyevu na vinahitaji mvua ndani ya siku 10 – 14 ili vifanye kazi ipasavyo.

Jina Aina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Aina ya Nozo

2,4-D KIMIMINIKA 2.0 160 MLS BLUE FLAT FAN

MCPA KIMIMINIKA 2.5 200 MLS BLUE FLAT FAN

BROMOXYNIL KIMIMINIKA 1.5 – 2.0 120 – 160 MLS BLUE FLAT FAN

2,4-D, MCPA na bromoxinil ni viua magugu ambavyo vinaua magugu yenye majani mapana (BLWs) pekee kwenye Mahindi na Mtama. Vyote vinatumika baada ya mimea na magugu kuota.

17

Aina nyingine za viua magugu kwa ajili ya kudhibiti magugu yenye majani mapana ( BLW) kwenye mahindi pekee

Page 18: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Viua magugu vyenye viuatilifu Fluazifop, Quizalofop, Haloxyfop au Clethodim kwa ajili ya kudhibiti magugu jamii ya nyasi kwenye Pamba, Maharage ya Soya, Karanga, Alizeti na Maharage Matamu (Sugar Beans).

Viua magugu vifuatavyo vinatumika kudhibiti magugu jamii ya nyasi kwenye mazao haya pekee:- Pamba, Maharage ya Soya, Karanga, Maharage Matamu na Alizeti. Vyote vinatumika baada ya mazao na magugu kuota. Aina yoyote ya magugu yenye majani mapana (BLWs) hayawezi kufa kwa Viua Magugu hivi. Magugu aina ya Kapinga yanaweza kuota tena baada ya kunyunyizwa Super Grass Killer na Select 120 EC. Viua magugu hivi viwili vina kiuatilifu kiitwacho clethodim.

Jina Aina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Aina ya Nozo Ushauri/Maelekezo

GRASS KILLER KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls BLUE FLAT FAN Tumia kiasi kidogo sana cha dawa ili kudhibiti magugu machanga jamii ya nyasi.

Tumia kiasi kingi cha dawa ili kudhibiti magugu jamii ya nyasi yaliyokomaa ya Kapinga na magugu mengine yakudumu (perennial grass weeds).

PANTERA KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

NOVA KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

BLACK PANTHER KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

PANTHER KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

QUIZATE KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

QUIZALOFOP KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 Mls

QUIZAFOM KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 MlsHI CASE KIMIMINIKA 1.0 – 3.5 80 – 280 MlsFUSILADE FORT 150SC KIMIMINIKA 0.75 – 1.5 60 – 120 MlsORCA 25E KIMIMINIKA 0.75 – 1.5 60 – 120 MlsMIYIDIMA KIMIMINIKA 0.375 – 1.5 30 – 120 MlsSUPER GRASS KILLER KIMIMINIKA 0.125 – 1.5 10 – 120 MlsSELECT 120EC KIMIMINIKA 0.125 – 1.5 10 – 120 Mls

18

Viua magugu chaguzi vyenye viuatilifu Prometryn na Fluometuron kwa jili ya kudhibiti magugu jamii ya nyasi na magugu yenye majani mapana (BLW) kwenye Pamba

Jina Aina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Nozo Ushauri/Maelekezo

COTTON WEEDKILLER KIMIMINIKA 3 L 240 MLS BLUE FLAT FAN Nyunyiza wakati wa kuotesha au baada tu ya kuotesha.

SAPPHIRE KIMIMINIKA 3 L 240 MLSHERBICOTTON KIMIMINIKA 3 L 240 MLS

Page 19: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Viua Magugu chaguzi (Selective herbicides) vyenye kiuatilifu Chlorimuron kwa ajili ya kudhibiti Magugu yenye majani mapana (BLWs) kwenye Maharage ya Soya na Karanga

19

Viua magugu chaguzi vyenye kiuatilifu Pendimethalin kudhibiti magugu nyasi na BLW kwenye Pamba, Maharage ya Soya, Maharage Matamu (Sugar Beans) , Karanga na Mahindi

Jina Aina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16 kwa aina mbalimbali za udongo

Aina ya Nozo Ushauri/Maelekezo

Sandy Soils Medium Soils Clay Soils Tumia kiwango cha chini kudhibiti magugu ya msimu pekee.

PENDIMETHALINKIMIMINIKA

1.3 L – 3.0 L 100 – 160 MLS 160 – 240 MLS 240 - 320 MLS BLUE FLAT FAN

Kiua magugu chaguzi chenye kiuatilifu Metribuzin Kwa ajili ya kudhibiti magugu jamii ya nyasi na BLW’s kwenye Soya Beans na Mahindi

Jina Aina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16 kwa aina mbalimbali za udongo

Nozo Ushauri/Maelekezo

Udongo wa kichanga

Udongo Tifutifu

Udongo mfinyanzi

Hudhibiti aina nyingi za magugu yenye majani mapana (BLWs) na baadhi ya magugu nyasi pekee.

METRIBUZIN SCKIMIMINIK

A0.6 L –M 0.7 L 50 MLS 60 MLS - BLUE FLAT FAN

Viua magugu chaguzi vyenye kiuatilifu Bentazone kwa ajili ya kudhibiti BLW’s na Ndao kwenye Maharage soya, Karanga na Mahindi

JinaAina Lita kwa hekta Kiasi cha chini kwa

bomba la lita 16Aina ya Nozo Ushauri/Maelekezo

BENTAZON WSKIMIMINIKA 3.0 L – 5.0 L 240 MLS – 400 MLS BLUE FLAT FAN Tumia kiwango cha juu cha dawa kudhibiti

Ndao.

BASAGRANKIMIMINIKA 3.0 L – 5.0 L 240 MLS – 400 MLS

Jina Aina Gramu kwa hekta

Kiasi cha chini kwa bomba la lita 16

Aina ya Nozo Ushauri/Maelekezo

CLASSIC UNGA 35 g 2.8 g BLUE FLAT FAN USITUMIE KWENYE MAHARAGE MATAMU (SUGAR BEANS). Changanya na Viua Magugu vilivyoko ukurasa wa 14 kudhibiti magugu jamii ya nyasi. Mara nyingi viauzwa kwenye ujazo unaotosha kwa bomba moja kama sivyo usinunue.

BEAN WEED KILLER UNGA 35 g 2.8 gRAZOR UNGA 35 g 2.8 gCHLORIMURON WDG UNGA 35 g 2.8 gLABEL UNGA 35 g 2.8 g

CHLORIMURON ETHYLUNGA 35 g 2.8 g

Page 20: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

20

ZINGATIA: Kijitabu/Kijarida hiki kimetayarishwa kama Mwongozo wa wakulima katika kuchagua na kutumia Viua Magugu. Pamoja na kuwa muda mwingi na umakini umetumika katika kuandaa Kijitabu/kijarida hiki, CFU haitawajibika kwa madhara yoyote yatakayotokea kwenye mazao kutokana na makosa ambayo yaweza kuwepo kwenye Kitabu/Kijarida hiki.

Kwa mawasilianoLusaka OfficePlot 279A/9/10Leopards Hill Road, New KasamaLusakaPhone: +260 965 238 058

Central Region Marshall Avenue, House # 27KabwePhone: +260 965 238 090

Chongwe: Plot No. 353/490 Great East RoadPhone: +260 965 238 055

Kafue: +260 965 238 072

Eastern Region Plot No. 3285 Lundazi RoadChipataPhone: +260 965 238 092

Southern Region Plot 983 Riverside Corner of Mpile and 3rd Street, ChomaPhone: +260965238 035

Lundaziplot No 0/0,149-149/A Chipata Road LundaziPhone: +260 965 238 140

Western RegionPlot 652 Kalenda StreetMumbwa Phone: +260 965 238 086

MonguZARI complexMongu Kalabo roadPhone: +260 965 238 039

Senanga: +260 965 238 053

Tuna ofisi sehemu zifuatazo:

ChongweKabweKafueKapiri MposhiMkushiMumbwaItezhi TezhiKaomaMonguSenangaChikankhataMazabukaMonzePembaChomaKalomoPetaukeKateteSindaChipataLundazi

Page 21: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

Utapata matokeo yale yale kwa kufanya palizi mapema na kila wakati kwa kutumia jembe la mkono

Muone Mratibu wa wakulima kwenye eneo lako kwa ushauri na hudhuria mafunzo mara kwa mara.

21

Page 22: Conservation Farming Unit · 2019-09-09 · ambacho sio sahihi ambacho kinaweza kuua mazao yako na kisiue magugu. Hatua ya 8: Ili usichanganyikiwe beba kipeperushi na rejea kwenye

©Conservation Farming UnitElianzishwa nchini Zambia mwaka, 1996

www.conservationagriculture.org