250
PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI YA KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA KIKUU NA VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA MAGEREZA NCHINI TANZANIA KIJITABU CHA MWONGOZO KWA WAELIMISHA RIKA JULAI 2017

Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA

AJILI YA KUPUNGUZA HATARI ZA

KIFUA KIKUU NA VIRUSI VYA

UKIMWI KATIKA MAGEREZA

NCHINI TANZANIA

KIJITABU CHA MWONGOZO KWA

WAELIMISHA RIKA

JULAI 2017

Page 2: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015
Page 3: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Kitabu hiki kimeweza kutolewa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa

Kupunguza UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa Ushirika

namba AID-OAA-A-14-00046. Yaliyomo ni wajibu wa programu ya AIDSFree na si lazima kuwa yanawakilisha mawazo ya shirika

la USAID, PEPFAR au Serikali ya Marekani.

PROGRAMU YA ELIMU RIKA

KWA AJILI YA KUPUNGUZA

HATARI ZA KIFUA KIKUU NA

VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA

MAGEREZA NCHINI

TANZANIA

KIJITABU CHA MWONGOZO

KWA WAELIMISHA RIKA

JULAI 2017

Page 4: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

AIDSFree

Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI

(AIDSFree) ni mkataba wa miaka mitano unaofadhiliwa na Mpango wa

Dharura wa Ukimwi wa Rais wa Marekani (PEPFAR) na Shirika la Umoja

wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa

Ushirika -OAA-A-14-00046. AIDSFree inatekelezwa na Taasisi ya Utafiti na

Mafunzo ya JSI na washirika Abt Associates Inc., Elizabeth Glaser Pediatric

AIDS Foundation, EnCompass LLC, IMA World Health, Umoja wa

Kimataifa wa VVU / UKIMWI, Jhpiego Corporation, na PATH. AIDSFree

inasaidia na kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya PEPFAR kwa kujenda

na kuendeleza uwezo wa kitaalam na kutoa ushauri wa kitaalam kwa

USAID, serikali za nchi husika na watekelezaji wa miradi ya UKIMWI katika

ngazi ya wilaya, mkoa na kitaifa.

Recommended Citation

Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI

(AIDSFree). 2017. Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu

na virusi vya ukimwi katika magereza nchini Tanzania: Kijitabu cha

mwongozo kwa waelimisha Rika: Julai 2017. Arlington, VA: Programu ya

AIDSFree.

AIDSFree Tanzania Uniformed Services

JSI Research & Training Institute, Inc.

Plot No. 2 Mkwawa Road, Oyster Bay

P.O. Box 9263

Dar es Salaam, Tanzania

Page 5: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

SHUKRANI

Shukrani zetu za dhati kwanza ziwaendee watu

wa Marekani kupitia Msaada wa Shirika la USAID

la Serikali ya Marekani kwa kufadhili utolewaji wa

Kijitabu hiki

AIDSFree/JSI inatoa shukrani kwa Uongozi wa

Magereza Tanzania, hasa Dkt. Juma Malewa,

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania

kwa kuidhinisha na kupitisha utungaji na

uchapishaji wa Kijitabu hiki. Tunamshukuru

Bwana Ali Abdalla Ali, Kamishna wa Chuo cha

Mafunzo Zanzibar aliyefunga rasmi mafunzo ya

majaribio ya Kijitabu hiki.

Tunatambua ushiriki na mchango uliotolewa na

waakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo na

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi za

kiserikali na zisizo za kiserikali na maafisa 54 wa

magereza hususan Dkt. Wilson Rugamba,

Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt.

Richard Mwankina (Mrakibu Mwandamizi wa

Page 6: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Gereza la Ukonga ), Dkt. Juma A. Mwaibako

(Mrakibu, Gereza la Ruanda, Mbeya), Dkt. Hilda

Mmari (Mrakibu Msaidizi wa Magereza – Makao

Makuu), Dkt. Abdilatif Mkingule (Inspekta,

Ukonga Chuo), na Dkt. Dotto Pakacha (Inspekta,

Gereza la Segerea). Mapendekezo yao

yamesaidia kukiboresha Kijitabu hiki.

Shukrani za pekee ziwaendee Dkt. Beati Mboya,

Mkurugenzi Mkazi wa AIDSFree/Tanzania na Dkt.

Peter Maro, Mkurugenzi maswala ya kiufundi

kwa uongozi wao katika hatua mbali mbali

zilizochangia kuwepo kwa chapisho hili.

Tunatambua juhudi za Dkt. John Gulaka, Afisa wa

Uhusiano-Magereza wa AIDSFree/JSI katika

hatua mbali mbali za mchakato wa kukiandaa

Kijitabu hiki. Kwa wataalam wetu Bwana Ignatio

Chiyaka na Bi. Zuki Mihyo, Kijitabu hiki

hakingeweza kuwepo bila mchango wao kwenye

kuandaa yote yaliomo na kujumuisha maoni na

mapendekezo ya wadau husika wakiwemo

Uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania.

Page 7: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Msingi wa Kijitabu hiki umetokana na Kitabu cha

PharmAccess cha Waelimishaji Rika kwa Majeshi

ya Polisi, Magereza na Uhamiaji cha Mwaka

2013.

Page 8: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015
Page 9: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

vii

YALIYOMO

Vifupisho ........................................................... ix

Utangulizi .......................................................... 1

Jinsi ya kutumia kijitabu hiki ............................ 2

Namna ya kuanza ............................................ 2

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu

na VVU ............................................................... 5

Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na

UKIMWI ............................................................... 6

Somo 2: Viwango vya HATARI ya

maambukizi ya VVU kwenye magereza .... 63

Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi

ya VVU ................................................................ 64

Somo 3: Kifua kikuu na VVU: Matibabu,

huduma na msaada ........................................ 115

Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU ........... 117

Page 10: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

viii

Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu,

huduma, na msaada ........................................ 154

Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka

kwa mama kwenda kwa mtoto ...................... 170

Somo 4: Kuvunja ukimya kuhusu kifua kikuu

na VVU. .............................................................. 178

Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika

magereza ........................................................... 179

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU

na Kifua kikuu .................................................. 203

Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa

na VVU................................................................ 204

Orodha ya maneno ......................................... 222

Mirejeo ............................................................... 233

Page 11: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

ix

VIFUPISHO

UKIMWI upungufu wa kinga mwilini

WAVIU watu waishio na virusi vya ukimwi

SOSPA toleo maalumu la sheria ya makosa

ya kujamiiana 1998

VVU virusi vya ukimwi

Page 12: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

x

Page 13: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

1

UTANGULIZI

Malengo ya programu hii ni kusaidia kubadili

tabia miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi

wa magereza ili kupunguza hatari ya VVU na

kifua kikuu kwa kuwaelimisha juu ya mambo

yanayochangia na kuhamasisha matumizi ya

huduma za afya zipatikanazo. Waelimisha rika

kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza

watatoa mafunzo ili kuhakikisha wenzao

wanapata elimu, manufaa na ujuzi wa namna ya

kupambana na VVU na kifua kikuu mahali

popote iwe gerezani ama nje ya gereza. Kitabu

hiki kimetungwa kwa ajili ya matumizi ya

waelimisha rika kwa wafungwa na wafanyakazi

wa magereza na kimetengenezwa mahususi kwa

ajili ya kukidhi mazingira ya gerezani. Ingawa,

masomo yanaweza kupangwa kwa namna fulani

ili kutumiwa pia na wanufaikaji wengine ikiwemo

polisi.

Page 14: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

2

Jinsi ya kutumia kijitabu hiki

Kitabu hiki kinawapa waelimisha rika shughuli na

maelezo muhimu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya

VVU na kifua kikuu kwa wafungwa na

wafanyakazi wa magereza. Waelimisha rika

watatumia njia mbalimbali kuwashirikisha wenzao

kwenye majadiliano, michezo, michezo ya

kuigiza, pamoja na maswali na majibu. Mafunzo

haya yametengenezwa kwa ajili ya makundi

madogo madogo ya washiriki wasiozidi 20. Kila

kundi linapaswa kukamilisha masomo yote tano

yaliyo kwenye ratiba. Ratiba ya mafunzo inaweza

kupangwa kwa kuzingatia shughuli za kila siku za

magereza na uwepo wa wafanyakazi wa

magereza kwa ajili ya kusimamia nidhamu ya

wafungwa.

Mwongozo huu una masomo matano. Kila somo

lina utangulizi kwa ufupi sambamba na maelezo

ya kina na ya uhakika. Masomo yanahusisha

mada zifuatazo:

Page 15: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

3

1. Maelezo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI

2. Tabia hatarishi kwa maambukizi ya kifua

kikuu na VVU gerezani

3. Matibabu ya kifua kikuu na VVU, huduma, na

msaada

4. Kuvunja ukimya juu ya kifua kikuu na VVU

5. Kuishi kwa matumaini ukiwa na kifua kikuu

au VVU

Namna ya kuanza

Kabla ya kufundisha chochote au kuongoza

majadiliano ya kikundi, soma na pitia mwongozo

huu ili kutambua na kuelewa kwa kina mada na

maelezo yaliyomo. Maandalizi haya yatamsaidia

mwelimisha rika kuongoza majadiliano kwa

ufanisi na kujibu maswali yoyote ambayo

yanaweza kujitokeza.

Maelezo yaliyomo kwenye mwongozo huu

yanakwenda sambamba na malengo ya serikali

ya Tanzania kuzuia maambukizi ya VVU na kifua

Page 16: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

4

kikuu pamoja na kuzuia maambukizi nyemelezi

miongoni mwa wafungwa na watu waishio na

VVU, na hivyo kuboresha afya zao. Mwongozo

huu unatoa maelezo muhimu kwa wakati

muafaka.

Orodha ya maneno na maana zake imetolewa

mwishoni mwa mwongozo huu kwa ajili ya

kuwasaidia waelimishaji kuyatumia

wanapofafanua maneno magumu.

Page 17: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

5

SOMO 1: ELIMU YA MSINGI

KUHUSU KIFUA KIKUU NA

VVU

Lengo

Kukuza kiwango cha elimu ya msingi kuhusu

kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa na

wafanyakazi wa magereza.

Madhumuni ya Mafunzo

Mwisho wa somo hili, washiriki watakuwa na

uwezo wa:

Kueleza maana ya kifua kikuu, VVU na

UKIMWI.

Kuelezea dalili na ishara za kifua kikuu, VVU,

na UKIMWI.

Kueleza namna ambavyo kifua kikuu na VVU

vinaweza kuenezwa uraiani na gerezani.

Kueleza namna ugonjwa unavyoendelea.

Page 18: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

6

Kueleza mambo ya uhakika kuhusu kifua

kikuu, VVU, na UKIMWI nchini Tanzania kwa

ujumla na hasa kwenye magereza.

Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na

VVU gerezani.

Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na

UKIMWI

Dakika 60

Kipindi 1.1: Mazoezi:

Kuelewa VVU na UKIMWI

VVU na UKIMWI ukweli/uongo

Ueneaji wa VVU na magonjwa ya ngono

Uhusiano kati ya VVU na jinsia

Mwisho wa kipindi washiriki watakuwa na uwezo

wa:

Kueleza maana ya VVU na UKIMWI

Kutokomeza imani za upotoshaji kuhusu

UKIMWI

Page 19: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

7

Kueleza namna ambavyo VVU vinaenezwa

Kueleza hatua tano za dalili za UKIMWI.

Zoezi 1.Kuelewa VVU na ukimwi

Dakika 20

Hatua 1: Utambulisho

Jitambulishe kwa jina na uzoefu wako wa

shughuli za uwezeshaji wa kifua kikuu na

VVU (ukiwa nao). Eleza majukumu yako

kama mwelimishaji rika. Wakaribishe

washiriki kwenye majadilianao yao ya kwanza

juu ya kifua kikuu na VVU. Waombe

wajitambulishe. Kwa kifupi eleza mada kwa

ajili ya majadiliano.

Tambua kwamba kipindi hiki kinaweza kuwa

cha kibinafsi na chenye hisia kali. Ndani ya

kundi panaweza kuwepo na washiriki wenye

VVU au wenye rafiki wa karibu au

wanafamilia wanaoishi na VVU au UKIMWI.

Wakumbushe washiriki kwamba si vibaya

kuachana na swali na wahimize kutoa

Page 20: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

8

maelezo yale tu ambayo wanajisikia vizuri

kuyatoa. Kama hawajisikii vizuri kuzungumzia

mambo haya kwenye kundi

kubwa,wanaweza kuzungumzia kwenye

makundi madogo madogo ama wawili wawili

au kutochangia kabisa.

Hatua 2: Taratibu za mafunzo

Taja kanuni hizi muhimu

Usiri: Heshimu maelezo binafsi ya kila

mshiriki. Jaribu kujizuia kutoa maelezo nje ya

kikundi lakini ikiwa utafanya hivyo, toa

maelezo ya ujumla pasipo kutumia majina ya

washiriki.

Heshima: Mheshimu kila mtu kwenye kikundi.

Hii inamaanisha kutowashambulia wengine

(kwa maneno au matendo) na kuwa muwazi

na mwepesi wa kuhisi mitazamo ya wengine.

Kumbuka kutumia kauli ya “MIMI”. Inavutia

zaidi kusema “vizuri kwa mimi binafsi,

Page 21: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

9

ninahisi kwamba….” Badala ya kusema,

“Hapana, umekosea, ukweli ni kwamba…”.

Uangalifu: Sikiliza wanachokizungumza

wengine. Hutaishia kujifunza kitu fulani tu

bali utawafanya wengine wajisikie kuwa huru

zaidi.

Uwazi: Washawishi wengine kuzungumzia

uzoefu wao wenyewe, pasipo

kuwazungumzia wengine. Chukua tahadhari.

Usiwe mwoga wa kuzungumza kwa uwazi

bila ugomvi, kutukana ama kuwa mtu

asiyejali hisia za wenzake.

Hatua 3: Maswali na majibuvvu na UKIMWI

ni nini?

Swali: VVU ni nini?

Jibu: VVU maana yake ni virusi visababishavyo

upungufu wa kinga kwa binadamu. Virusi hivi

hushambulia mfumo wa kinga wa mwili ambao

huulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Page 22: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

10

Hatua 4: Utangulizi

VVU na UKIMWI nchini Tanzania kulingana na

“Ripoti ya Kuzuia VVU na UKIMWI 2016”(AVERT

2017)

Watu milioni 1.4

wanaishi naVVU

Asilimia 4.7 ya

watu wazima

wana maambukizi

ya VVU

Maambukizi

mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Vifo 36,000 vyenye uhusiano na UKIMWI

viliripotiwa mwaka 2015

Asilimia 53% ya watu wazima wenye VVU

wanapata tiba ya kupunguza makali

UKIMWI ni nini?

UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga

mwilini. Kuambukizwa virusi vya ukimwi

hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa kinga.

Page 23: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

11

Jambo hili humfanya mtu aliye na VVU

kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa ambapo

mtu asiye na maambukizi ya VVU huenda

asingepatwa au angepona kwa urahisi. VVU

hushambulia na kuharibu chembechembe za

mfumo wa kinga zijulikanazo kama CD4 ambazo

hupambana na maambukizi. Kupungua kwa

chembechembe za CD4 huufanya mwili

kushindwa kupambana na maambukizi na

baadhi ya saratani. Pasipo matibabu, VVU

vinaweza kuharibu taratibu mfumo wa kinga na

hatimaye kukua na kuwa ugonjwa unaoitwa

UKIMWI.

Hatua baada ya dalili za awali

Waambie washiriki kwamba mtazungumzia

hatua za ugonjwa zinazojitokeza baada ya

dalili za awali: maambukizi makali ya VVU,

kukua na kuongezeka kwa VVU bila

kuonesha dalili, na UKIMWI.

Page 24: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

12

Hatua 1: Dalili kali za VVU

Ndani ya wiki 1–4 baada ya maambukizi, virusi

vimeanza kusambaa, na mtu anaweza

kukumbana na mlolongo wa dalili zijulikanazo

kama dalili kali za VVU. Dalili katika hatua hii

zaweza kuwa pamoja na homa, kuumwa kichwa,

maumivu ya miguu, kuwashwa kooni, kukua kwa

fundo limfu, uchovu, ukurutu mwilini, maumivu

na kuuma kwa viungo , kuharisha, kubadilika kwa

tabia ya ulaji, na kichefu chefu. Hatua hii

hujulikana kitaalamu kama “acute retroviral

syndrome” au “acute primary HIV infection,” na

dalili hizi zinaweza kutokea kwa kuwa mwili wako

unakuwa ukipambana na virusi. Ni mwitikio wa

asili wa mwili dhidi ya VVU. Katika kipindi hiki

kiwango kikubwa cha virusi huzalishwa. Katika

hatua hii ya maambukizi makali ya VVU, mtu

anakuwa katika hatari kubwa ya kueneza VVU

kwa wapenzi ama watumiaji wenza wa madawa

ya kulevya kwa kutumia sindano kutokana na

kuwepo kwa kiwango kikubwa cha VVU kwenye

mishipa yao ya damu. Kwa hiyo ni muhimu

kuchukua hatua za kupunguza hatari za kueneza

virusi.

Page 25: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

13

Hatua 2VVU Kukua na kuishi mwilini bila

kuonekana:

Baada ya hatua ya maambukizi makali ya VVU,

ugonjwa huhamia kwenye hatua ijulikanayo

kama “kukua na kuishi kwa VVU mwilini bila

kuonekana.” Kipindi cha virusi kutoonekana

maana yake ni kipindi ambapo virusi vinaishi na

kukua ndani ya mwili wa mtu pasipo kuonesha

dalili zozote. Katika hatua ya ukuaji wa virusi

pasipo kuonekana, watu wenye VVU huwa

Chembechembe za CD4 ni chembechembe za damu

zinazofanya kazi kubwa ya kuulinda mwili dhidi ya

maambukizi. Virusi hutumia chembechembe hizi za

CD4 (mara nyingi huitwa chembechembe-T au

chembechembe –T saidizi) kuzaliana zaidi na kuenea

kote mwilini huku zikiharibu chembechembe hizo za

CD4. Baada ya hapo mwitikio wa kinga utaanza

kupunguza kiwango cha virusi mwilini hadi kufikia

kiwango fulani thabiti mwilini mwako. Wakati huu

chembechembe mpya za CD4 zitaanza kuongezeka,

lakini huenda zisifikie kiwango cha chembechembe za

CD4 zilizokwishaharibiwa.

Chembechembe za CD4 ni nini?

Page 26: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

14

hawaoni dalili zozote labda zile ndogo ndogo

sana. Hatua hii mara nyingine huitwa “dalili za

maambukizi ya VVU” au “maambukizi sugu ya

VVU.” Eleza kwamba katika hatua hii, VVU bado

vinazaliana na kuongezeka kwa kiwango kidogo

sana, lakini bado vipo hai. Ikiwa utakuwa kwenye

matibabu ya kupunguza makali, unaweza kuishi

kwenye hatua hii kwa miongo kadhaa, kwa kuwa

matibabu husaidia kuwepo kwa kiwango kidogo

cha virusi.

Hatua 3: Ukimwi

Hatua ya mwisho ya maambukizi ya VVU

hutokea pale ambapo mfumo wa kinga unakuwa

umeharibiwa vibaya na virusi na mtu huwa katika

hatari kubwa zaidi au huwa hatarini kupatwa na

maambukizi mazito na hatari zaidi au magonjwa

ya bacteria na ukungu magonjwa ambayo

vinginevyo angeweza kupambana nayo

(“maambukizi nyemelezi”). Idadi ya CD4

inaposhuka chini ya 200 kwa kiwango cha

Page 27: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

15

milimita za mchemraba za damu, yaani (200

chembechembe/mm3), unahesabiwa kuwa sasa

una UKIMWI. Kwa mtu mwenye mfumo wa kinga

imara, idadi ya CD4 huwa ni chembechembe

500–1,650 kwa milimita za mchemraba. Vile vile

utahesabiwa kuwa una UKIMWI ikiwa utapatwa

na ugonjwa nyemelezi mmoja ama zaidi, bila

kujali idadi ya CD4 zako.

Dalili za UKIMWI

Kupungua uzito ghafla

Homa za mara kwa mara au kutokwa na

jasho usiku

Uchovu wa kupindukia na usioelezeka

Kuendelea kuvimba kwa tezi za limfu kwenye

kwapa, kinena, au shingo

Kuharisha kwa zaidi ya wiki moja (uharo

usiosikia dawa)

Kuwashwa mdomoni, njia ya haja kubwa, na

sehemu za siri

Kukohoa pasipo kukoma

Page 28: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

16

Majibu yenye rangi nyekundu, kijivu, pinki,

ama zambarau juu ya au chini ya ngozi au

ndani ya mdomo, pua au kope za macho.

Kupoteza kumbukumbu, unyonge, na

maradhi mengine ya nyuroni.

Magonjwa makubwa makubwa

Tofauti ya VVU na UKIMWI ni ipi?

Mtu mwenye maambukizi ya VVU anaweza kuwa

na afya njema kwa miaka kadhaa bila ya kuwa na

ishara au dalili za maambukizi mwilini. Mtu

mwenye virusi bila ya dalili ni “mtu anayeishi na

VVU” au “mwenye maambukizi ya VVU”.UKIMWI

ni hatua ya mwisho ya maambukizi na si kila

mwenye VVU hufikia hatua hii. Baada ya mtu

kuambukizwa VVU kwa kipindi fulani (mara

nyingi kwa miaka mingi), dalili zinazosababishwa

na virusi huanza kujitokeza. Katika hatua hii, watu

wenye VVU huwa na uwezekano mkubwa wa

kupatwa na maambukizi nyemelezi. “UKIMWI” ni

ufafanuzi wa kidaktari unaowalenga watu wenye

VVU wanaosumbuliwa na ambukizi moja au

Page 29: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

17

maambukizi kadhaa mahususi, ikiwemo kifua

kikuu, saratani kwa kiasi kidogo, macho, ngozi,

na hali ya mfumo wa neva.

Zoezi 2. VVU zoezi la Kweli/Uongo

Dakika 20

Hatua 1: Zoezi

Eleza kwamba mtafanya zoezi la kutolea

ufafanuzi upotoshaji kuhusu VVU na

UKIMWI. Waambie washiriki kwamba

utasoma maelezo na kama wanaamini ya

kwamba maelezo ni ya“UKWELI” wasimame;

na kama wanaamini kuwa maelezo ni ya

“UONGO” wakae. Hakikisha maelekezo

yanaeleweka vizuri. Soma maelezo mara

moja au mbili. Waruhusu washiriki wajibu.

Waombe waelezee kwa nini wanaamini ya

kuwa maelezo ni ya KWELI/UONGO na

jadilianeni

Page 30: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

18

Muongozo wa majibu:

MAELEZO KWELI/UONGO

1. Unaweza

kuambukizwa VVU

kwa kung’atwa na

mbu

UONGO: Imethibitishwa

kwamba VVU haviwezi

kuenezwa kwa njia hii.

2. Kufanya mapenzi

kinyume na maumbile

ni moja kati ya njia

hatari zaidi kwa

ueneaji wa VVU.

KWELI: Kufanya mapenzi

kinyume na maumbile ni

hatari zaidi katika ueneaji

wa VVU kuliko namna

nyingine yoyote ya

kujamiiana. Wakati wa

kujamiiana kwa njia hii,

mboo inaweza kuchana

ngozi laini njia ya haja

kubwa, jambo ambalo

litaviwezesha virusi kuingia

kwenye mishipa ya damu.

3. Watu wanaweza

kuambukizwa VVU

ikiwa watafanya

mapenzi mdomoni na

KWELI: VVU vipo kwenye

shahawa za mtu mwenye

maambukizi. Hivyo, VVU

vinaweza kuenezwa ikiwa

Page 31: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

19

MAELEZO KWELI/UONGO

mtu mwenye

maambukizi ya VVU

shahawa zitaingia

mdomoni mwa mtu.

Hatari ya kuambukizwa

VVU unapofanya mapenzi

mdomoni huongezeka

ikiwa kuna vidonda

mdomoni. Hatari yaweza

kupunguzwa kwa kuvaa

kondomu na kuhakikisha

hakuna shahawa

zinazoingia mdomoni

mwa mwenza wako.

Kibaiolojia inawezekana

VVU kuenezwa kwa

kufanya mapenzi

mdomoni na mwanamke

mwenye VVU, lakini jambo

hili linadhaniwa kuwa ni

kwa kiasi kidogo. Kutumia

kinga kama kondomu au

kiwambo cha meno wakati

wa kufanya mapenzi

mdomoni kunaweza

Page 32: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

20

MAELEZO KWELI/UONGO

kuzuia kueneza zaidi kwa

VVU, magonjwa mengine

ya ngono, na homa ya ini.

Kiwambo cha meno ni

kipande mraba

chembamba cha mpira au

silikoni ambacho huwekwa

juu ya meno wakati wa

kufanya mapenzi

mdomoni.

4. Zinapotumiwa kwa

usahihi, kondomu

zinaweza kuwakinga

wanaume na

wanawake kutokana

na maambukizi ya

VVU.

KWELI: Kondomu hutoa

ulinzi dhidi ya VVU,

magonjwa mengine ya

ngono, na mimba

zisizotarajiwa. Zikitumiwa

mara kwa mara kwa

usahihi, kondomu ni moja

kati ya njia bora zaidi za

kujikinga na VVU.

5. Dawa maalumu

zinaweza kutibu

maambukizi ya VVU.

UONGO: Hadi sasa,

hakuna tiba wala chanjo

kwa maambukizi ya VVU.

Page 33: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

21

MAELEZO KWELI/UONGO

Ijapokuwa, kuna vidonge

vinavyoweza kupunguza

uzalianaji wa virusi ndani

ya mwili wa mtu aishiye na

VVU. Vile vile kuna dawa

zinazosaidia kukinga ama

kutibu maambukizi

nyemelezi

yaliyosababishwa na VVU.

6. VVU ni ugonjwa

unaowaathiri

makahaba na

wanaume

wanaofanya nao

mapenzi peke yake.

UONGO: Mtu yeyote

anaweza kuambukizwa

VVU.Hatari ya mtu kupata

VVU haina uhusiano na

jinsi mtu alivyo, bali tabia

aliyo nayo.

7. Ukiishi na mwenza

mmoja tu, huwezi

kuambukizwa VVU.

UONGO: Watu walio

waaminifu kwa wenza wao

bado wanaweza kuwa

katika hatari ya kupata

VVU ikiwa wenzi wao

wanashiriki kufanya

mapenzi ama kuchangia

Page 34: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

22

MAELEZO KWELI/UONGO

nyembe na watu wengine

wenye maambukizi.

8. Watu wenye

magonjwa ya ngono

(maambukizi

yaenezwayo kwa njia

ya kujamiiana) wapo

katika hatari kubwa ya

kuambukizwa VVU

kuliko wale wasio na

magonjwa ya ngono

ikiwa watafanya

mapenzi na mtu

mwenye maambukizi

ya VVU.

KWELI: Magonjwa ya

ngono sehemu za siri

huvipa VVU njia rahisi ya

kupenya kwenye mishipa

ya damu.

9. Mtu anaweza

kupona VVU kwa

kufanya mapenzi na

bikira.

UONGO: Bikira hawana

uwezo wowote wa

kuwaponya watu wenye

maambukizi ya VVU. Hadi

Page 35: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

23

MAELEZO KWELI/UONGO

sasa bado hakuna tiba

kwa VVU.

10. Huwezi kupata

VVU kwa sababu tu

unaishi kwenye

nyumba moja na mtu

mwenye ugonjwa.

KWELI: Kuishi kwenye

nyumba moja na mtu

mwenye VVU hakuwezi

kuwaweka hatarini wale

wanaoishi nae; VVU

havienezwi kwa migusano

ya kawaida ndani ya

familia.

11. Wakati wote

unaweza kutambua

kama mtu ana VVU

kwa mwonekano

wake.

UONGO: Watu wengi

wanaoambukizwa VVU

hawaoneshi dalili yoyote

ya ugonjwa kwa miaka

mingi. Ingawa, virusi

vinakuwepo mwilini mwao

na vinaweza kuenezwa

kwa watu wengine.

12. VVU vinaweza

kuenezwa kutoka kwa

mtu mmoja mwenye

KWELI: Kuchangia sindano

wakati wa utumiaji wa

madawa ya kulevya

Page 36: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

24

MAELEZO KWELI/UONGO

VVU kwenda kwa mtu

mwingine pale

wanapochangia

sindano wanapotumia

madawa ya kulevya.

kunabeba hatari kubwa

sana ya ueneaji wa VVU.

Damu yenye maambukizi

hupitishwa kwa urahisi

kutoka kwa mtu mmoja

kwenda kwa mtu

mwingine kupitia sindano

yenye maambukizi au

vifaa vingine vilivyotumika

kuandaa au kujidunga

madawa.

Hatari kwa wanaume

na wanawake

kuambukizwa VVU

huongezeka pale

ambapo pana

magonjwa ya ngono

mahali ambapo

kiwango cha VVU kiko

juu.

KWELI: Magonjwa ya

ngono kwa wanawake

hayatambuliwi kwa urahisi

na mara nyingi huisha

pasipo kuchunguzwa.

Magonjwa ya ngono

sehemu za siri huvipa VVU

njia rahisi kuingia kwenye

mishipa ya damu.

Unyanyapa kwa wanawake

pia ni kikwazo ambacho

Page 37: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

25

MAELEZO KWELI/UONGO

kinawavunja moyo

wanawake kutafuta

matibabu ya kutosheleza.

Zoezi 3: Jinsi VVU na magonjwa ya ngono

yanavyoenezwa

Dakika 10

Hatua 1: Maswali na majibi—uenezwaji wa

VVU

Swali: VVU vinaenezwaje?

Jibu: VVU haiambukizwi kwa urahisi kama surua

au homa ya mafua. Kwa mfano, virusi kama

surua na homa ya mafua huenezwa kwa njia ya

hewa kwenye maeneo yenye vizuizi palipo na

watu wenye maambukizi. VVU huishi kwenye

majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa kama

vile damu, shahawa, majimaji kabla ya shahawa,

uke, uteute kwenye njia ya haja kubwa, na

maziwa ya mama. VVU vinahitaji kuingia kwenye

Page 38: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

26

mwili wa mtu. Hivyo basi, VVU vinaweza

kuenezwa kwa njia zifuatazo:

Kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi

Kuongezewa damu au mazao ya damu na

mtu mwenye maambukizi ya VVU

Kuchangia matumizi ya sindano, mabomba

ya sindano, na vitu vyenye ncha kali vilivyo

na bacteria na mtu mwenye maambukizi ya

VVU

Kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda

kwa mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa ama

kunyonyesha.

Uwepo wa maambukizi yatokanayo na ngono

(kotokwa maji maji, vidonda, na miwasho )

huongeza hatari ya kupata na kueneza VVU. Hii ni

kwa sababu watu wenye VVU wenye maambukizi

ya magonjwa ya ngono wana kiwango kikubwa cha

VVU kwenye ute wa sehemu zao za siri na/au kwa

kuwa kuingia kwa virusi kumerahisihwa kutokana na

uwepo wa michubuko kwenye mucosa

Jinsi magonjwa ya ngono huongeza hatari ya kupata na

kueneza VVU

Page 39: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

27

Hatua 2: Eleza

Zungumzia magonjwa ya ngono

Hatua 3: Maswali na majibu

Swali: Jinsi gani VVU havienezwi?

Jibu:

Maji maji mengine mwilini kama, machozi,

mate, jasho, matapishi na mkojo

Migusano binafsi: busu kavu mdomoni

pasipo na vidonda, kukumbatiana, kushikana

mikono, kusalimiana kwa kushikana mikono.

Mikusanyiko kijamii: wakati wa kazi, shuleni,

kwenye sinema, mgahawani.

Hewa au maji: chafya, kukohoa, kuogelea

bwawani/madimbwi

Vifaa: kalamu, vyoo, taulo, mashuka, sabuni,

vifaa vya kulia chakula, mavazi.

Wadudu: kung’atwa na mbu ama wadudu

wengine

Page 40: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

28

Hatua 4: Maswali na majibu—upunguzaji wa

ueneaji wa vvu

Swali: Ueneaji wa VVU unawezaje kupunguzwa?

Jibu: “Mpango mkakati wa UNAIDS 2016–2021”

(ukurasa.58) eneo la matokeo 4, ili kupunguza

ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma

na bidhaa, umezitaka serikali za kitaifa kutoa

kipaumbele kwenye upatikanaji wa huduma za

kinga za VVU kwa makundi maalumu, ikiwemo

watu wanaotumia madawa ya kulevya na wakazi

wenza, ili kupunguza kwa haraka kwa kuwakinga

na kusimamia haki za watu wote kupata huduma

za kutosha zenye ubora wa juu bila ubaguzi.

Kupunguza hatari kwa vijana na makundi

maalumu kupata VVU na madhara yake kwenye

maeneo yote yenye maambukizi ni jambo

muhimu katika kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI

(2016).

Ikiwa wewe ni mfanyaji mapenzi, kuna mambo

kadhaa muhimu unayopaswa kuchukua ili

Page 41: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

29

kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU.

Kutojamiiana ni njia mojawapo ya kuzuia kupata

au kueneza VVU. Ikiwa huwezi kuacha

kujamiiana, tumia kondomu (ya kiume ama kike)

wakati wote ufanyapo mapenzi kwenye uke, njia

ya haja kubwa ama mdomoni. Inapotumiwa

wakati wote na kwa usahihi kondomu za kiume

na kike njia bora zaidi katika kuzuia kuzuia VVU.

Shughuli mbalimbali za kimapenzi vile vile

zinabeba viwango tofauti vya hatari ya VVU.

Ngono kinyume cha maumbile pasipo kutumia

kondomu au ngono ya kulazimisha ni njia hatari

zaidi kwa ueneaji wa VVU kwa kuwa hupelekea

kuchanika kwa kuta za uke na njia ya haja kubwa:

Usichangie sindano, bomba za sindano na

vifaa vingine vyenye ncha kali na mtu yeyote

ikiwa unatumia madawa ya kulevya.

Pata matibabu ya VVU ikiwa wewe ni mama

mjamzito unayeishi na VVU ili kupunguza

hatari ya kumwambukiza mtoto wako wakati

wa ujauzito, kuzaa na kunyonyesha.

Page 42: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

30

Hakikisha kwamba mazao ya damu

unayopokea yamefanyiwa uchunguzi wa

VVU.

Vaa vifaa vya kujikinga (Kama glavu na

miwani ya kuzuilia vumbi) na safisha mikono

baada ya kushika damu na maji maji

mengine (hasa kwa wataalamu wa huduma

za afya au watoa huduma).

Tumia dawa za kurefusha maisha au kinga ili

kujikinga na uwepo wa maambukizi (ikiwa

inapatikana) ikiwa upo katika hatari ya

kupata maambukizi ya VVU.

Jitolee mwenyewe, katahiriwe hospitalini

Punguza idadi ya watu unaofanya nao

mapenzi. Unapokuwa na idadi kubwa ya

wapenzi unajiongezea nafasi ya kupata

mpenzi mwenye VVU au ugonjwa mwingine

uenezwao kwa njia ya ngono.

Page 43: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

31

Hatua 5: Elezea

Elezea “mapenzi salama” kwenye magereza

Majadiliano kuhusu mapenzi salama

hayatawezekana kwa kuwa magereza ni

mahali wanapokaa wafungwa kulingana na

jinsia zao wenyewe. Kwa sababu hii

hawawezi kuzungumzia mapenzi salama

kwa watu wenye jinsia moja, lakini elimu hii

itawasaidia watakapomaliza kutumikia

vifungo vyao na kurudi majumbani mwao

au katika jamii.

Mapenzi salama katika magereza

Page 44: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

32

Zoezi 4: Uhusiano baina ya VVU na jinsi

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Kijamii jinsi imefafanuliwa, kwa kuzingatia zaidi

majukumu ambayo wanaume na wanawake

huyafanya katika jamii.Jinsi inaweza kufanya

jambo kubwa katika kupandikiza ufuasi. Kwa

pamoja jinsia na jinsi hutoa uzoefu wa kipekee

kwa wanaume na wanawake waishio na VVU.

Kwa hiyo kuelewa desturi za jinsi na ukosefu wa

usawa wa jinsi ni muhimu katika kupunguza

hatari ya VVU miongoni mwa wanaume na

wanawake, wavulana na wasichana. Ijapokuwa

kuwa mambo yanayofanana baina ya vihatarishi

vya VVU na tabia katika jinsi mbalimbali, tofauti

zipo na baadhi ya watu huambukizwa zaidi

kuliko wengine.

Page 45: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

33

Hatua 2: Maswali na majibu

Swali: Kuna mtu anayeweza kutupa mfano wa

namna ambavyo majukumu ya kijinsi

yanavyoweza kuathiri uwezo wa mwanamke

kutumia dawa.

Jibu: Wanawake wanaweza kukumbana na

changamoto nyingi na vikwazo inapokuja suala

la afya zao wenyewe na ustawi wao. Wengi

wanaishi kwenye mazingira ya uonevu,

wanakumbana na unyanyapaa na ubaguzi katika

jamii, ukosefu wa amana za kiuchumi na huduma

za kiafya na mara kwa mara wao ndio watoa

huduma wa kwanza katika familia. Changamoto

hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa uwezo wao

wa kumwona daktari, kufuata dawa, kunywa

dawa, kupumzika na kushusha kiwango cha

msongo wa mawazo.

Page 46: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

34

Hatua 3: Hitimisho

Swali: Hivyo, nini kifanyike kuhusu jambo hili?

Jibu: Tukumbuke kwamba jinsia zetu, umri,

hadhi katika jamii zetu, nakadhalika ni mambo

yanayobadilika ambayo yanaweza kumfanya kila

mmoja wetu kuwa na kiwango tofauti cha hatari,

uzoefu na uwezo wa kupata huduma na fursa.

Kipindi 1.2 Ufahamu juu ya Kifua Kikuu

Dakika 110

Kipindi 1.2: Mazoezi

Utangulizi juu ya kifua kikuu na ugonjwa

Ueneaji wa kifua kikuu

Kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa

wa kifua kikuu

Jinsi ya kuchunguza kifua kikuu

Mambo ya uhakika na upotoshaji kuhusu

kifua kikuu

Maambukizi ya kifua kikuu na

changamoto za ugonjwa magerezani.

Page 47: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

35

Madhumuni ya kipindi

Mwisho wa kipindi hiki, washiriki wataweza:

Kuelezea aina mbili za kifua kikuu

Kuainisha kifua kikuu kulingana na sehemu

ya mwili iliyoathiriwa

Kufuta dhana ya upotoshaji kuhusu kifua

kikuu

Kuelezea namna ambavyo kifua kikuu

kinaenezwa

Kuorodhesha viashiria na dalili za kifua kikuu

Kuelezea tofauti baina ya maambukizi ya

kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa

kifua kikuu.

Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na

maambukizi ya VVU.

Page 48: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

36

Zoezi 1. Utangulizi kuhusu maambukizi ya

kifua kikuu na ugonjwa

Dakika 10

Hatua 1: Eleza—kifua kikuu na vvu

VVU na kifua kikuu ni muunganiko hatari mno.

Kila ugonjwa huufanya ugonjwa mwingine uenee

haraka zaidi. VVU huufanya mfumo wa kinga wa

mwili kuwa dhaifu na mtu mwenye VVU halafu

akaambukizwa kifua kikuu huwa katika nafasi

kubwa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu kuliko

yule mwenye kifua kikuu asiye na VVU.

Hatua 2: Elezakifua kikuu nchini tanzania

Shirika la afya ulimwenguni limeitaja Tanzania

kama nchi yenye mzigo mkubwa wa kifua kikuu

(TB), na moja kati ya nchi zenye mzigo mzito wa

kifua kikuu na VVU. Mnamo mwaka 2013,

wagonjwa 64,000 wa kifua kikuu waliripotiwa na

asilimia 83 (53,120) ya wagonjwa hawa walikuwa

wamepatiwa ushauri nasaha na kupimwa VVU.

Page 49: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

37

Katika kundi hili, asilimia 39 (20,717) walikutwa

wakiwa na maambukizi ya VVU. Mwezi Aprili

2016 kulikuwa na takribani wagonjwa 295 wa

kifua kikuu mapafuni katika kila watu wazima

100,000 katika Tanzania (International

Organization for Migration in Tanzania 2016).

Serikali imeweka kipaumbele kutolewa kwa

pamoja kwa huduma za kifua kikuu na VVU ili

kupunguza mzigo wa magonjwa haya. Kwa hiyo,

watu waishio na VVU wanaotumia vidonge vya

kupunguza makali wana nafasi nzuri ya

kupambana na maambukizi ya kifua kikuu. Utoaji

wa huduma hizi pamoja utahakikisha pia

upatikanaji wa matibabu ya kifua kikuu na VVU

kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hatua 3: Jadili

Kifupisho “TB” kinamaanisha nini?

Unadhani ni jambo gani husababisha kifua

kikuu?

Page 50: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

38

Hatua 5: Elezavipi na kwa nini

Kifua kikuu kinasababishwa na bakiteria

wanaoitwa Mycobacterium tuberculosis. Kwa

kawaida bakiteria hawa hushambulia mapafu,

lakini bakiteria wa kifua kikuu wanaweza

kushambulia sehemu yoyote ya mwili ikiwemo

figo, uti wa mgongo na ubongo. Si kila

aliyeambukizwa na bakiteria wa kifua kikuu

huugua. Hivyo basi, kuna namna mbili zenye

uhusiano na kifua kikuu: maambukizi ya kifua

kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Ikiwa hautatibiwa vizuri, ugonjwa wa kifua kikuu

unaweza kuwa ugonjwa wa kifo. Wote wenye

hali fulani kiafya inayodhoofisha mfumo wa kinga

vile vile huwa hatarini kupata kifua kikuu.

Maziringira yanayowafanya watu kuwa katika

hatari kubwa ya kuathiriwa haraka na ugonjwa

wa kifua kikuu ni pamoja na:

Maambukizi ya VVU

Matumizi mabaya ya madawa

Page 51: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

39

Silikosisi/asbestosi: ugonjwa wa mapafu

unaosababishwa na kuvuta hewa iliyo na

madini ya silika ambayo ni sehemu ya

mchanga, miamba na mawe yenye madini

kama vile kwazi. Baada ya muda, kuwepo

katika mazingira yenye chembechembe za

silika husababisha makovu kwenye mapafu,

ambayo yanaweza kuathiri uwezo wa mtu

kupumua.

Ugonjwa wa kisukari (aina ya 2): ugonjwa

sugu wenye kiwango cha juu cha sukari

(glukosi) isivyo kawaida kwenye damu.

Ugonjwa mkali wa figo

Uzito mdogo wa mwili

Saratani

Matibabu kama vile corticosteroids au

upandikizaji wa viungo.

Page 52: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

40

Zoezi 2: Ueneaji wa kifua kikuu cha mapafu

Dakika 20

Hatua 1: Eleza: kifua kikuu cha mapafuni

nchini Tanzania

Idadi ya waathirika wa kifua kikuu cha mapafuni

katika Tanzania iliripotiwa kuwa watu 295 kati ya

watu 100,000, kulingana na hotuba ya bajeti ya

mwaka 2014/2015 ya waziri wa afya. Kifua kikuu

cha mapafuni ni moja kati ya maambukizi

nyemelezi kwa wengi miongoni mwa watu

waishio na VVU. Karibu asilimia 39 ya wagonjwa

wa kifua kikuu nchini Tanzania wameambukizwa

VVU (WHO 2012).

Hatua 2: Chemsha bongo

Wagawe washiriki katika makundi ya watu 3

au 4 na acha wajadili njia ambazo kifua kikuu

kinaenezwa kwa dakika 5. Yaombe makundi

yawasilishe majibu yao.

Page 53: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

41

Kuvuta hewa yenye

matone madogo sana ya

erosoli ambayo hutolewa

pale mtu mwenye PTB

ambukizi anapokohoa,

piga chafya, tema mate,

zungumza au imaba.

Namna kifua kikuu cha

mapafu kinavyoweza enezwa

Hatua 3: ElezaNamna kifua kikuu cha

mapafu kinavyoweza enezwa

Mtu anapovuta hewa

iliyou na bakiteria

wanaosababisha kifua

kikuu cha kwenye

mapafu, bakiteria

wanaweza kukaa

kwenye mapafu na

kuanza kuzaliana.

Kifua kikuu cha

mapafu

kinaambukizwa, maana yake bacteria wanaweza

kuenezwa kwa watu wengine. Kifua kikuu kwenye

sehemu nyingine za mwili, kama vile, figo au uti

wa mgongo hakiambukizi. Eleza zaidi kwamba

kuna aina mbili za kifua kikuu: (1) kifua kikuu

ndani ya mapafu, ambacho kinaambukiza, na (2)

kifua kikuu nje ya mapafu, ambacho

hakiambukizi.

Page 54: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

42

Hatua 4: Maswali na majibu: kwa nini kifua

kikuu cha mapafu ni ambukizi

Swali: Kwa nini wanadhani kifua kikuu cha

mapafu ni ambukizi?

Jibu: Kifua kikuu ndani ya mapafu kimo

mapafuni. Kinaenea pale mtu mwenye kifua

kikuu ambukizi anapotoa hewa nje iliyo na

bacteria wa kifua kikuu halafu mtu mwingine

anawavuta ndani bakiteria waliopo kwenye hewa

hiyo. Mtu mwenye maabukizi ya kifua kikuu cha

mapafu hutoa bakiteria zaidi pale anapofanya

vitendo kama kukohoa au kucheka. Kifua kikuu

nje ya mapafu hakiambukizwi kwa watu wengine

kwani kipo katika sehemu nyingine za mwili na

sio kwenye mapafu. Watu wenye ugonjwa wa

kifua kikuu cha mapafu wana uwezekano

mkubwa wa kuueneza kwa watu wanaokuwa nao

kwa karibu kila siku, ikiwemo wanafamilia, rafiki,

wafanya kazi wenzao na wafungwa.

Page 55: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

43

Hatua 5: Fuatilia

Angalia kama washiriki wana maswali

Hatua 6: Fafanua zaidi

Kuna aina nyingine ya kifua kikuu inayoitwa

bovine TB ambayo ipo zaidi Tanzania. Bovine TB,

au Kifua kikuu cha mifugo, kinaweza kuambukiza

zaidi kwa wanyama, wakiwemo binadamu.

Bovine TB husababishwa na bacteria wajulikanao

kitaalamu kama Mycobacterium bovis (M. bovis)

ambao ni sehemu ya aina ya wadudu

wanaoambukiza kifua kikuu wajulikanao kama

Mycobacterium tuberculosis complex.

Hatua 7: Uliza

Mnadhani zipi ni dalili na viashiria vya kifua

kikuu?

Pitia majibu yaliyoorodheshwa kwenye boksi.

Page 56: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

44

Viashiria na dalili za kifua kikuu

Kujisikia kuumwa au

dhaifu

Kupungua uzito

Homa za jioni na

kutoka jasho jingi usiku.

Kukohoa kwa zaidi ya

wiki mbili

Maumivu ya kifua na

kukohoa damu.

Zoezi 3: Maambukizi ya kifua kikuu

kisichoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Bakteria wa kifua kikuu wanaweza kuishi mwilini

bila ya wewe kuugua. Hii hujulikana kama

maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana. Kwa

watu wengi ambao wanawavuta bacteria wa

kifua kikuu na kuambukizwa, mwili huwa na

uwezo wa kupambana na bacteria ili kuwazuia

wasikue. Watu wenye maambukizi ya kifua kikuu

kisichoonekana:

Hawana dalili

Hawajisikii kuumwa

Page 57: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

45

Hawawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu

kwa wengine

Mara nyingi huonekana kuwa na

maambukizi ya kifua kikuu kwa kipimo cha

kuchunguza athari kwenye ngozi au kipimo

cha damu.

Wengi huugua ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa

hawatapatiwa matibabu kwa ajili ya

maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana.

Hatua 2: Taja

Watu wengi wenye maambukizi ya kifua kikuu

kisichoonekana hawataugua ugonjwa wa kifua

kikuu. Kwa watu hawa, bacteria wa kifua kikuu

hubaki mwilini bila kuwa na madhara kwa kipindi

chote cha maisha bila kusababisha ugonjwa.

Lakini kwa watu wengine, hasa wale wenye

mifumo dhaifu ya kinga kutokana na maambukizi

ya VVU, bakteria huweza kuleta athari, kuzaliana,

na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Page 58: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

46

Bakteria wa kifua kikuu huwa na athari ikiwa

mfumo wa kinga hautakuwa na uwezo wa

kuwazuia kukua. Bakteria wa kifua kikuu

wanapokuwa na athari (wanapoongezeka mwilini

mwako), hii huitwa ugonjwa wa kifua kikuu. Watu

wenye ugonjwa wa kifua kikuu ni wagonjwa.

Wanaweza vili vile kueneza bacteria kwa watu

wanaokuwa nao kila siku, hasa kwa kifua kikuu

cha kwenye mapafu. Baadhi ya watu hufikia

kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu mapema

mara baada ya kuambukizwa (ndani ya wiki

kadhaa) kabla hata ya mifumo yao ya kinga

kupambana na bakteria. Watu wengine

wanaweza kuanza kuugua baada ya miaka

kadhaa pale ambapo mifumo yao ya kinga

inapokuwa dhaifu kwa sababu nyingine.

Uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu

ni mkubwa kwa watu wenye VVU ukilinganisha

na wale ambao hawana maambukizi. Watu

wenye mifumo dhaifu ya kinga, hasa wale wenye

maambukizi ya VVU, wana hatari kubwa ya

Page 59: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

47

kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu kuliko watu

wenye mfumo wa kinga usio na maambukizi.

Zoezi 4: Tofauti kati ya kifua kikuu

kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye

mapafu

Dakika10

Hatua 1: Maswali na majibu

Swali: Ni nini tofauti kati ya kifua kikuu

kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye

mapafu?

Page 60: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

48

Jadili na pitia majibu yaliyopo kwenye

jedwali hapa chini.

MTU MWENYE

MAAMBUKIZI YA KIFUA

KIKUU KISICHOONEKANA

MTU MWENYE KIFUA

KIKUU NDANI YA

MAPAFU

Hana dalili Dalili zaweza kuwa:

Kikohozi kibaya

kinachochukua wiki

3 au zaidi

Maumivu kifuani

Kukohoa damu au

makohozi

Udhaifu au uchovu

Kupoteza uzito

Kukosa hamu ya kula

Homa za baridi

Homa

Kutoka jasho usiku

(kupita kiasi)

Hajisikii kuumwa Kwa kawaida hujisikia

kuumwa

Hawezi kueneza bacteria Anaweza kueneza kifua

Page 61: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

49

MTU MWENYE

MAAMBUKIZI YA KIFUA

KIKUU KISICHOONEKANA

MTU MWENYE KIFUA

KIKUU NDANI YA

MAPAFU

wa kifua kikuu kwa

wengine

kikuu kwa wengine

Kwa kawaida matokeo ya

kipimo cha TB kwenye

ngozi ama damu

huonesha kuwa ana

maambukizi ya TB

Kwa kawaida matokeo

ya kipimo cha ngozi

ama damu huonesha

kuwa ana maambukizi

ya kifua kikuu.

Kipimo cha x-ray ya kifua

hakina shida na makohozi

hayana maambukizi.

Anaweza kuwa na

kipimo cha x-ray ya

kifua kikionesha tatizo,

au makohozi

yakaonesha

maambukizi.

Anahitaji matibabu ili

kuzuia kifua kikuu ndani ya

mapafu

Anahitaji matibabu kwa

ajili ya kifua kikuu ndani

ya mapafu

Page 62: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

50

Zoezi 5: Uchunguzi wa kifua kikuu

Dakika 20

Hatua 1: Maswali na majibu

Swali: Nani anapaswa kupimwa kifua kikuu?

Jibu: Wale ambao wapo kwenye hatari kubwa

zaidi ya kuambukizwa na bakiteria wa kifua kikuu

ikiwemo:

Watu wanaoishi kwa karibu na mtu mwenye

ugonjwa wa kifua kikuu (kama, wanafamilia,

wafungwa)

Watu kutoka kwenye nchi ambazo zina

kiwango kikubwa cha kifua kikuu

Watu wanaoishi au kufanya kazi kwenye

mazingira hatarishi (kwa mfano: magerezani,

vituo vya kutolea matibabu ya kifua kikuu)

Watoa huduma za afya wanaowahudumia

wagonjwa walio katika hatari zaidi ya

ugonjwa wa kifua kikuu.

Watoto wachanga, watoto, vijana walio

pamoja na watu wa zima walio kwenye hatari

Page 63: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

51

zaidi ya maambukizi ya kifua kikuu

kisichoonekana au ugonjwa wa kifua kikuu.

Wenye VVU au wagonjwa wa UKIMWI.

Watu walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa

wa kifua kikuu

Wajawazito wenye

VVU

Watu wenye

maambukizi ya VVU

Watu waliopata

maambukizi ya

bakteria wa kifua

kikuu miaka miwili

iliyopita

Watu ambao

hawakupata

matibabu ya kifua

kikuu vizuri hapo

zamani

Watoto wachanga na

watoto wadogo

Watu wanaojidunga

madawa ya kulevya

Watu wanaoumwa

magonjwa mengine

yanayodhoofisha

mfumo wa kinga

Watu wenye umri

mkubwa

Page 64: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

52

Swali: Ni nani aliye katika hatari zaidi ya kupatwa

na ugonjwa wa kifua kikuu?

Jibu: Eleza kwamba vipimo ya kifua kikuu kwa

ujumla huwa havihitajiki kwa watu waliopo

kwenye hatari ndogo ya maambukizi ya bacteria

wa kifua kikuu.

Hatua 2: Maswali na majibuUpimaji wa

ugonjwa wa kifua kikuu

Swali: Je mnafahamu jinsi ugonjwa wa kifua

kikuu unavyopimwa?

Jibu: Elezea aina mbalimbali za vipimo kwa

maambukizi ya kifua kikuu:

Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya ngozi

(kipimo cha uchunguzi cha mantoux)

Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya damu

Makohozi (mchanganyiko wa mate na uteute

uliokoholewa kutoka kwenye njia ya

upumuaji, hasa kama matokeo ya

maambukizi au magonjwa mengine na mara

Page 65: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

53

nyingi huchunguzwa kwa kutumia darubini ili

kusaidia uchunguzi wa kitabibu.

Hatua 3: Eleza

Mtoa huduma za afya anapaswa kuchagua ni

kipimo gani cha kifua kikuu anapaswa kutumia.

Vigezo katika kuchagua kipimo gani kitumike ni

pamoja na sababu ya kufanya vipimo, uwepo wa

vipimo, na gharama. Kwa ujumla, haishauriwi

kumpima mtu kwa vipimo vyote viwili yaani

kipimo cha kifua kikuu kwenye ngozi na kile cha

damu.

Zoezi 6: Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua

kikuu cha kwenye mapafu

Dakika 15

Hatua 1: Eleza

Waambie washiriki kwamba utasoma

maelezo na kama wanadhani maelezo ni

UKWELI wahamie upande wa kulia, na kama

wanadhani ni UPOTOSHAJI wahamie

Page 66: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

54

kushoto. Kama hawajui, wasihame. Hakikisha

washiriki wameelewa maelekezo.Muulize

mshiriki mmoja ama wawili kutoa maelezo

kwa nini wanadhani maelezo ni ukweli au

uongo. Tumia ufunguo wa majibu (chini)

kwani una maelezo ya kina ambayo unaweza

kuhitaji kuwashirikisha washiriki ikibidi.

Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye

mapafu

MAELEZO MAJIBU

Kifua kikuu cha kwenye

mapafu hutokea

kwenye jamii masikini

tu.

UPOTOSHAJI Kifua kikuu

cha kwenye mapafu

unaweza kumpata mtu

yeyote. Ingawa, watu

fulani wapo katika hatari

kubwa Zaidi ya kupata

kifua kikuu cha mapafu

kushinda wengine. Kama

mtu anatambua

vihatarishi, inaweza

kupunguza uwezekano

wa mtu kupata kifua

kikuu cha mapafu.

Page 67: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

55

MAELEZO MAJIBU

Kwa kawaida matibabu

ya kifua kikuu cha

kwenye mapafu

huchukua miezi 6–8.

KWELI: Matibabu ya

kifua kikuu cha kwenye

mapafu kwa kawaida

huchukua miezi 6–8 na

yanaweza kufikia hadi

miezi 12 kwa kesi

maalumu.

Hakuna tofauti kati ya

ugonjwa wa kifua kikuu

cha mapafu na

maambukizi ya kifua

kikuu.

UPOTOSHAJI: Mtu

mwenye maambukizi ya

kifua kikuu haambukizi

kwa kuwa wadudu

hawana athari ama

hawaonekani. Mtu

hatambui kama

ameambukizwa kwa

kuwa hakuna viashiria

wala dalili

zinazoonekana. Mtu

mwenye kifua kikuu cha

mapafu ameathirika kwa

namna ya tofauti kabisa.

Mtu mwenye kifua kikuu

Page 68: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

56

MAELEZO MAJIBU

cha mapafu anaweza

kuambukiza na ana

viashiria na dalili.

Kama mtu anakohoa

naweza kupata kifua

kikuu cha mapafu.

UPOTOSHAJI: Kifua

kikuu cha mapafu

hakikoholeki kwa urahisi.

Unalazimika kuwa karibu

kabisa na mtu mwenye

kifua kikuu cha mapafu

kwa muda mrefu (kwa

kawaida masaa mengi

au siku nyingi, kama vile

gerezani). Unapaswa

kutambua dalili za

ugonjwa ili uweze

kutafuta matibabu

mapema iwezekanavyo.

Kifua kikuu cha kwenye

mapafu ni ugonjwa

unaoambukiza na

unaweza kuenezwa kwa

njia ya hewa.

KWELI: Kifua kikuu cha

kwenye mapafu ni

ugonjwa ambao

unaenezwa kutoka kwa

mtu mmoja kwenda kwa

mwingine kwa njia ya

hewa wakati wa

Page 69: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

57

MAELEZO MAJIBU

kukohoa, kupiga chafya,

kucheka, kuimba, kupiga

makelele na hata

kuzungumza. Ikiwa mtu

mwenye maambukizi

anakohoa ama kupiga

chafya, vijidudu

husambaa hewani

ambapo vinaweza

kuvutwa na wale

waliopo katika eneo hilo.

Kama mgonjwa

anakamilisha matibabu,

kwa kawaida huwa

amepona.

KWELI: Kama hakuna

usumbufu kwenye

matibabu na

yamefuatwa kama

ilivyoelekezwa kwa

kipindi husika, kwa

kawaida unakuwa

umepona kifua kikuu

cha mapafu.

Kumbuka: Kukamilisha

matibabu maana yake ni

kumaliza kozi ya

Page 70: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

58

MAELEZO MAJIBU

matibabu ya kifua kikuu

ndani ya mapafu na

kufanyiwa uchunguzi wa

kifua kikuu na madaktari

ili kuthibitisha uponyaji.

Zoezi 7: Kifua Kikuu Magerezani

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Kuzuia ueneaji wa kifua kikuu ni moja ya

changamoto kubwa kwenye maeneo ya

magereza hasa pale kunapokuwa na

msongomano wa watu.

Hatua 2: Jadili

Ni changamoto zipi zinazojitokeza wakati wa

kukabiliana na maambukizi ya kifua kikuu katika

magereza?

Page 71: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

59

Hatua 3: Eleza

Kuna changamoto nyingi: binafsi, kijamii na

kiutamaduni, sera, na mazingira, ikiwemo

zifuatazo:

Upungufu wa mbinu za kuthibiti maambukizi

na uwepo wa kiwango kidogo cha huduma

za afya kutokana na ufinyu wa rasilimali.

Wafungwa mara nyingi hutenganishwa

kwenye vizimba ama sehemu ya wagonjwa

bila ya kufanyiwa vipimo vya kiafya

(Wagonjwa wa kifua kikuu hutengwa).

Mlundikano, lishe hafifu, na ukosefu wa hewa

ya kutosha.

Idadi ndogo ya wafanyakazi wa afya.

Upungufu wa rasilimali kuendesha uchunguzi

wa kiafya na kununua madawa.

Kutofuata masharti ya matibabu miongoni

mwa wakazi wenza.

Hatari kubwa miongoni mwa wafungwa

kupata usugu wa kifua kikuu (kwa mfano,

Page 72: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

60

wadudu wa TB kupata usugu kutoka kwenye

dawa mbalimbali za TB) kutokana na

kutofuata masharti, ingawa utumiaji wa dawa

chini ya uangalizi wa mtoa huduma ukiwa

umezingatiwa kila siku.

Zoezi 8: Uhusiano kati ya VVU na kifua

kikuu

Dakika 15

Hatua 1: Mapitio

Waambie washiriki kuwa tumezungumzia

VVU, kifua kikuu, na madhara ya VVU

kwenye mfumo wa kinga wa mwili wa

binadamu.

Hatua 2: Jadili

Jinsi gani maambukizi ya VVU yanaweza

kumwathiri mtu mwenye maambukizi ya kifua

kikuu.

Pokea maoni machache.

Page 73: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

61

Hatua 3: Eleza

VVU huongeza kasi ya maambukizi ya kifua kikuu

kuwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa VVU

hudhoofisha mfumo wa kinga. Ukiwa una

maambukizi ya VVU una nafasi kubwa ya kupata

kifua kikuu kuliko mtu asiye na maambukizi ya

VVU. Bakteria wa kifua kikuu wana nafasi kubwa

ya kuwa na madhara na kushambulia mapafu na

sehemu nyingine za mwili.

Hatua 4: Maswali na majibu

Swali: Watu wafanyeje ikiwa wana VVU na kifua

kikuu ndani ya mapafu?

Jibu: Wanalazimika kupata matibabu moja kwa

moja pasipo kuchelewa ili kupunguza kuugua

zaidi. Kila mmoja anapaswa kutumia dawa zake

kwa usahihi kabisa kama daktari au mtoa

huduma za afya alivyowaelekeza.

Page 74: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

62

Hatua 5: Fafanua zaidi

Vidonge vya kifua kikuu ni vikali sana. Vinaweza

kutibu kifua kikuu, hata kwa watu wenye VVU

kwa baadhi ya watu. Kumbuka, Vidonge vya

kifua kikuu hufanya kazi vizuri pale tu ambapo

hutumiwa kulingana na maelekezo ya mtoa

huduma za afya.

Page 75: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

63

SOMO 2: VIWANGO VYA

HATARI YA MAAMBUKIZI YA

VVU KWENYE MAGEREZA

Lengo

Kukuza elimu juu ya vihatarishi vya VVU katika

maeneo ya magereza

Dhamira

Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

Kutambua na kuelezea viwango tofauti vya

vihatarishi vinavyochochea hatari ya

maambukizi ya VVU katika magereza.

Kuainisha jinsia na kuchunguza namna gani

desturi za kijinsia zinauhusiano na

maambukizi ya VVU.

Kueleza tofauti kati ya kuchukua tahadhari ya

VVU na kukabiliana na hatari za VVU

Page 76: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

64

Kutambua viwango vya hatari ya VVU

kutokana na tabia mbalimbali za kimapenzi

Kutambua majukumu ya kijinsia

yaliyopangwa na jamii kwa ajili ya wanaume

na wanawake.

Kulinganisha njia mbalimbali zilizopo za

kujikinga na VVU

Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya

maambukizi ya VVU

Masaa 2, dakika 15

Kipindi 2.1: Mazoezi

Utangulizi juu ya ngazi tatu za hatari za

VVU

Jinsi na jinsia

Jinsi, jinsia na VVU: Kuchukua tahadhari

na kukubaliana na hatari

Kiwango cha hatari

Page 77: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

65

Igiza kama mwanaume, igiza kama

mwanamke

Kufanya maamuzi kuhusu jambo

linalofaa na lisilofaa

Zoezi 1: Ngazi tatu za Viwango vya hatari

vya VVU

Dakika 10

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa za kuandikia, ubao wa chaki

Hatua 1: ElezaViwango vya hatari

Wafahamishe washiriki kwamba kuna ngazi

tatu za hatari za VVU:

Ngazi ya mtu binafsi

Ngazi ya familia

Ngazi ya jamii

Page 78: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

66

Elezea zaidi kuhusu vihatarishi vya VVU:

Viwango vina uhusiano na mambo ambayo

huwaweka watu kwenye hatari ya

maambukizi ya VVU.

Vihatarishi vya VVU katika viwango vya mtu

binafsi, familia, na jamii na mifano ifuatayo

kwenye jedwali hapa chini:

NGAZI YA MTU

BINAFSI

NGAZI YA

FAMILIA

NGAZI YA JAMII

Elimu (kwa

mfano,

Kutokuwa

kabisa au

kuwepo na

kiwango

kidogo cha

elimu)

Mtazamo

(kwa

mafano.,

Mila za

kitamadu

ni na

imani

Miiko.

Mila za

kijamii (kwa

mafano,

wajibu na

majukumu ya

wanaume na

wanawake)

Sera za

serikali

Siasa/uimara

wa kisiasa

Page 79: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

67

NGAZI YA MTU

BINAFSI

NGAZI YA

FAMILIA

NGAZI YA JAMII

dhana ya

uwanaume

miongoni

mwa

wanaume

ambayo

inapelekea

tabia

hatarishi,

dhana ya

uwanawake

miongoni

mwa

wanawake

inayozuia

majadiliano

kuhusu

mapenzi

salama)

Umri (kwa

Rasilimali

(kwa mfano;

ukosefu wa

vifaaa vya

kujifungulia

kwa

wafungwa

wajawazito).

Page 80: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

68

NGAZI YA MTU

BINAFSI

NGAZI YA

FAMILIA

NGAZI YA JAMII

mfano,

wakazi

wenza vijana

mara nyingi

huwa katika

hatari kubwa

kimwili,

kiakili, na

ukatili wa

kijinsia

kutoka kwa

wakazi

wenza

wakubwa)

Matendo ya

kimapenzi

yasiyo

salama

Kuchangia

vitu vyenye

Page 81: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

69

NGAZI YA MTU

BINAFSI

NGAZI YA

FAMILIA

NGAZI YA JAMII

ncha kali

(kama,

nyembe)

Ukosefu wa

elimu (kwa

mfano,

ukosefu wa

elimu

kuhusu

namna

ambavyo

VVU

huenezwa)

Matumizi

mabaya ya

madawa ya

kulevya na

pombe.

Page 82: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

70

Hatua 2: ElezaGerezani

Nchini Tanzania, tafiti zinaonesha uwepo wa

kiwango cha juu cha VVU (asilimia 6.7) ndani ya

magereza ukilinganisha na watu wazima

Mazingira ya kizuizi na msongamano ambayo

mara nyingi hupelekea msongo, wasiwasi,

fadhaa, na unyanyasaji, ikiwemo unyanyasaji

wa kimapenzi.

Baadhi ya wafungwa wa kiume wanaweza

kukumbana na unyanyasaji wa kimapenzi na

kushiriki shughuli za mapenzi yasiyo salama

na wanaume wengine kwa kubadilishana vitu

ama huduma, kitu kinachoongeza hatari kwao

kuambukizwa VVU.

Magonjwa ya ngono, kama herpes, chlamydia,

kaswende, au gono yapo miongoni mwa

wakazi wenza, huongeza hatari yao kwa VVU.

(Serekali ya Muungano ya Tanzania 2010)

Mazingira hatarishi kwa VVU ndani ya magereza

Page 83: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

71

kwingineko (asilimia 5.1)(Das and Horton, 2016)

kutokana na mazingira hatarishi ambayo ni

pamoja na: (tazama boksi la bluu).

Tanzania imetia sahihi na kuridhia hati zote rasmi

za haki za binadamu, sheria na sera za kimataifa

(umoja wa kimataifa) na kikanda kuhusu uzuiaji

wa VVU, zinazotoa idhini ya kuwapima watu VVU

kwa hiari, wakiwemo wafungwa walio katika

magereza.

Hatua 3

Kwa kina, jadili nini kifanyike ili kupunguza

mazingira haya hatarishi kwenye magereza.

Page 84: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

72

Zoezi 2: Jinsi na Jinsia

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa ya kuandikia na ubao

Maandalizi ya awali:

Andaa alama mbili moja iandikwe “jinsia” na

nyingine iandikwe “jinsi” kwa ajili ya zoezi hili.

Hatua 1: Eleza

Ingawa wafungwa hukaa kwenye vyumba

vidogo kulingana na jinsia zao, ni muhimu

kwao kuwa na taarifa kuhusu usawa wa

kijinsi, vurugu zenye misingi ya kijinsi, na

ukatili wa kijinsia. Elimu hiyo inaweza

kuwasaidia wafungwa baada ya kutumikia

vifungo vyao kuendeleza mila sahihi za kijinsi

na usawa wa kijinsi, ikiwa ni pamoja na

kupambana na ukatili wenye misingi ya

kijinsi.

Page 85: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

73

Hatua 2: Uliza na jadili maswali yafuatayo:

Jinsi maana yake ni nini?

Jinsi humaanisha sifa za kibaiolojia na

kimaumbile za wanaume na wanawake ambazo

hazibadiliki isipokuwa kwa upasuaji. Mifano ya

sifa za jinsia ni:

Viungo vya mwili: uume, uke, matiti,

korodani

Maumbile: mzunguko wa hedhi, uzalishaji

manii

Muundo wa kijenetiki: kromosomu XX na XY.

Jinsia maana yake ni nini?

Jinsia humaanisha kazi, haki, majukumu, fursa,

heshima, mipaka, matarajio na wajibu wa mtu

uliopangwa na jamii.

Page 86: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

74

Sifa za jinsi ni:

Hutofautiana miongoni na ndani ya

tamaduni

Hubadilika baada ya muda

Kazi na matarajio hupangwa kulingana na

jinsia, umri, ukabila, dini, na sababu nyingine

za kitamaduni

Huwahusu wanaume, wavulana, wanawake,

na wasichana; si wanawake pekee.

Hatua 3: Eleza

Baadhi ya mila za jinsi na ukosefu wa usawa wa

kijinsi huwaweka wanaume, wavulana,

wanawake, na wasichana katika hatari mbalimbali

za kupata maambukizi ya VVU:

Wanaume na wavulana wameathiriwa na

matarajio ya jinsi ambayo yanaweza

kuhamasisha tabia za kujihatarisha, kupinga

upatikanaji wa huduma za afya na kwa kiasi

kidogo kujipangia kazi zao kama wenza na

Page 87: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

75

wanafamilia. Kwa wasitani, kiwango cha

upimaji VVU na kupata matibabu ni mdogo

miongoni mwa wanaume ukilinganisha na

wanawake. Kote mashariki na kusini mwa

Afrika, kuna tofauti kubwa ya utumiaji na

unufaikaji wa huduma kati ya wanaume,

wavulana, wanawake, na wasichana.

Wanaume na wavulana hupata huduma za

afya kwa kiwango cha chini sana

ukilinganisha na wanawake na wasichana.

Asilimia 54 ya vifo vya watu wazima vyenye

uhusiano na UKIMWI vilitokea miongoni

mwa wanaume mashariki na kusini mwa

ukanda wa Afrika (makadirio ya UNAIDS

2016). Huduma za afya haziwafikii wanaume

wengi kusini mwa jangwa la Sahara, na hii

huchangia sana wanaume kuhitaji na

kutumia kwa kiasi kidogo huduma za VVU

katika kanda hizi. Matarajio ya wanaume

kuanza matibabu ni madogo sana, na mara

Page 88: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

76

nyingi hutegemewa kuwa na kiwango cha

chini cha CD4 wanapoanza na kukatiza

matibabu na kupoteza ufuatiliaji, hivyo

kufikiwa kwa kiasi kidogo kupungua kwa

virusi vya ukimwi ( Sonke Gender Justice

and Men Engage, 2017).

Ukosefu wa usawa wa kijinsi na usiri wa

ukatili wa wenza zinaweza kuwazuia

wanawake na wasichana, hasa wanawake

vijana kujikinga wenyewe dhidi ya VVU.

Nchini Tanzania, wanawake wameathirika

mno na VVU, Tanzania ina wanawake

690,000 wenye miaka 15 na zaidi waishio na

VVU. Kulingana na Utafiti wa Viashiria vya

VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania Mwaka

2011–12, (TACAIDS et al. 2011) maambukizi

ya VVU kwa wanawake yalikuwa asilimia 6.2,

ukilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

Wanawake wenye umri wa miaka 23–24

walikuwa na uwezekano wa kuishi na VVU

Page 89: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

77

mara mbili zaidi ya wanaume wa umri huo.

Wanawake huathiriwa mapema, kwa kuwa

wana wapenzi wakubwa na huolewa

mapema. Lakini pia wanakumbana na wakati

mgumu kujadiliana kuhusu mapenzi salama

kwa sababu ya ukosefu wa usawa wa kijinsi.

Nchini Tanzania asilimia 35 ya wanawake

inaaminika wamekumbana na ukatili wa siri

kwa wapenzi. Utafiti kutoka Tanzania

unaonesha kuwa huku wanawake

wakitegemewa kuwa watiifu kwa wapenzi

wao hata kama wapo kwenye mahusiano

mabaya, wanaume wanashawishiwa

kujihusisha na mapenzi ya ziada

yasiyosalama.

Hatua 3: Zoezi la jinsi na jinsia

Eleza kwamba sasa tutashiriki katika

shuughuli ya pamoja ili kujifunza zaidi

maneno jinsi na jinsia.

Page 90: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

78

Onesha alama mbili ambazo zimetengwa

kwa umbali wa fiti kadhaa. Moja ina

neno“jinsia” lililoandikwa juu yake, na

nyingine ina neno “jinsi.”

Soma sentensi moja moja na uwaombe

washiriki kuhamia kwenye alama ambapo

wanadhani sentensi inaegemea yaani jinsia

au jinsi. Baada ya kila mmoja kuhama,

endelea kwa kumwomba mtu mmoja

aliyesimama upande mmoja wa chumba

aeleze kwa nini waliamua kusimama upande

huo. Uliza ikiwa wengine wangependa

kuchangia sababu zao. Waulize kundi jingine

kwa nini wameamua kusimama chini ya

alama waliyopo. Baada ya kufanya hivyo kwa

muda soma sentensi inayofuata.

Page 91: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

79

MAELEZO YA JINSIA AU JINSI MAJIBU

Wanawake huzaa watoto Jinsi

Wasichana ni wapole na wakimya Jinsia

Wavulana ni werevu na thabiti Jinsia

Wanawake hunyonyesha watoto Jinsi

Wanaume ni vichwa vya familia

zao

Jinsia

Wanaume huanzisha mapenzi kwa

wenza wao

Jinsia

Wanaume wana akili kuliko

wanawake

Jinsia

Page 92: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

80

Zoezi 3: Jinsi, jinsia, na VVU: Kuchukua

tahadhari, kukabiliana na hatari

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa za kuandikia au ubao wa

chaki

Hatua 1. Utangulizi

Andika neno “hatari” kwenye karatasi ya

ubaoni au kwenye ubao wa chaki. Andika

maelezo yao ya ufafanuzi kwenye karatasi ya

ubaoni/ubao wa chaki. Fikieni muafaka

kuhusu maana ya neno hatari (tazama

kisanduku)

Maana ya hatari:

Hatari ni uwezekano au tishio la kupata

maambukizi (VVU, TB, n.k.), uharibifu, jeraha, deni,

upotevu, au matukio yoyote yanayoweza kuzuiwa

kwa kuchukua hatua stahiki.

Page 93: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

81

Hatua 2: Uliza

Waombe washiriki watoa mifano ya

mazingira ambayo wanaweza au mtu

wanayemjua, au watu wengine huchukua

tahadhari au hukabiliana na hatari za VVU

Hatua 3: Maswali ya kujadiliana:

Kuhusiana na VVU, ni nani anayechukua

tahadhari zaidi, mwanaume au mwanamke?

Kwa nini?

Kuhusiana na VVU, ni nani anayekabiliana na

hatari zaidi, mwanaume au mwanamke? Kwa

nini?

Nini faida na hasara za kuchukua tahadhari

na kukabiliana na hatari hizi kwa wanaume

na wanawake?

Ni mambo gani mengine yanayoathiri

tahadhari za VVU ambazo watu huchukua

na ambazo watu hukabiliana nazo?

Hatari hizi zinaweza kupunguzwa vipi?

Page 94: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

82

Hatua 4: Eleza

Wanawake hukumbana na hatari zaidi za

maambukizi ya VVU ukilinganisha na wanaume

kwa sababu ya mila za kijamii na kiutamaduni

(jinsi) na sababu za kibaiolojia (jinsia) (tazama

sanduku chini):

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

Wanawake mara

nyingi hawana nguvu

na maamuzi katika

maisha yao ya

kimapenzi.

Wanawake

hawatarajiwi kujadili

au kuamua kuhusu

mapenzi; jambo hili

huchukuliwa kama ni

kazi ya mwanaume.

Wanawake

wanaweza kuhisi

Wanawake wana

uwezekano

mkubwa wa kupata

VVU kutokana na

kitendo chochote

kimoja cha kufanya

mapenzi kwa

sababu shahawa

hubaki ndani ya

uke kwa muda

mrefu baada ya

kujamiiana, na

hivyo kuongeza

Page 95: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

83

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

kwamba hawawezi

kuuliza au kusisitiza

kutumia kondomu au

njia yoyote ya

kujikinga.

Wanawake

wanaweza kujisikia,

ingawa hawawezi

kukataa kufanya

mapenzi hata kama

wanajua wanajiweka

katika hatari ya

kupata mimba au

kuambukizwa

magonjwa ya ngono

au VVU.

Baadhi ya wanawake

hujihusisha kwenye

mahusiano ya

kimapenzi kupata,

uwezekano wa

kuambukizwa. Pia

kuna virusi vingi

kwenye shahawa

kuliko kwenye

majimaji ya ukeni.

Kuta za uke ni laini

sana na zinaruhusu

vitu kupenya, na

kuruhusu VVU

kupenya, na ngozi

ngozi laini ya ukeni

ni rahisi zaidi

kupata michubuko

au kuchanika kuliko

ngozi ya kawaida.

Wanawake wapo

katika hatari zaidi

ya kupata VVU

wakati wa

Page 96: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

84

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

pesa, simu, chakula,

au namna nyingine

za hadhi na ulinzi.

Wanawake

wanaweza

kukumbana na

namna nyingi za

mizozo kutokana na

unyonge wao katika

jamii, na kuongeza

hatari za maambukizi

ya VVU.

Wanawake ambao

huwaambia wenza

wao kwamba wana

ugonjwa wa

ngono/VVU

wanaweza

kukumbana na ukatili

wa kimwili, kiakili, au

kujamiiana kuliko

wanaume kwani

shahawa zinaweza

kusalia ndani ya

uke kwa siku

kadhaaa baada ya

kujamiiana, wakati

wanaume

hujihatarisha na

majimaji yenye

maambukizi ya

VVU tu wakati wa

kujamiiana.

Wanaume ambao

hawajatahiriwa

wana uwezekano

mkubwa wa

kuambukizwa VVU

ukilinganisha na

wale waliotahiriwa.

Page 97: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

85

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

hisia au kuachwa.

Wanawake

wanaweza kudai

matakwa ya

kimapenzi kwa

wenza wao kuzuia,

kuzomewa, kuachwa,

kupigwa, au kuuawa.

Wanawake pia

wanategemewa

kuwa na mahusiano

ya kimapenzi na au

kuolewa na wazee,

ambao wana

uwezekano mkubwa

kuwa na VVU.

Wanaume

wanahimizwa

kufanya mapenzi

kadri iwezekanavyo,

Uume haupo

kwenye hatari

kubwa ya

kusababisha

maambukizi kwa

sababu inakingwa

na ngozi ngumu

ukilinganisha na

uke ambao una

sehemu kubwa

inayoweza

kuruhusu

maambukizi ya

VVU toka kwenye

shahawa.

Unapokuwa na

magonjwa ya

ngono ambayo

hayajatibiwa

kunaongeza

Page 98: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

86

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

bila kufundishwa jinsi

ya kujilinda

wenyewe, na hivyo

kuongeza hatari

kwao kuambukizwa

VVU.

Kiashiria kikuu cha

uanaume na

mafanikio ni kuwa na

wapenzi wengi wa

kike kadri

iwezekanavyo. Kwa

wanaume waliooa na

wale ambao

hawajaoa, wapenzi

wengi ni jambo

linalokubalika

kiutamaduni.

Wanaume wanaweza

kudharauliwa na

uwezekano wa mtu

kupata VVU.

Page 99: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

87

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

kutaniwa kama

hawataonesha

kwamba

watachangamkia

fursa zozote ama

zote za kimapenzi.

Ushindani husisitizwa

kwa wanaume

kuonesha ni nani

aliye mkuu na bora.

Kiashiria kingine cha

uanaume ni kuwa na

uthubutu kwenye

mapenzi, ikiwemo

kutotumia kondomu

(matumizi ya

kondomu

huchukuliwa kama ni

ishara ya udhuru na

ni udhaifu).

Page 100: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

88

MILA ZA KIJAMII NA

KIUTAMADUNI (JINSIA)

SABABU ZA

KIBAIOLOJIA (JINSI)

Wanaume wengi

wanaamini kuwa

kondomu

hupunguza raha ya

mapenzi au ni

kiashiria cha ukafiri

na uzinzi.

Matumizi ya

kondomu vile vile

yanakinzana na kile

kinachoonekana

kama kiashiria

muhimu cha

uanaume—kuwa na

watoto wengi

iwezekanavyo.

Zoezi 4: Viwango vya hatari mchezo wa

kadi

Dakika 25

Page 101: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

89

Vifaa vinavyohitajika:

Kadi zilizoandikwa “vielelezo” Andika yafuatayo

kwenye kila kadi: Kuacha kabisa, kupiga

punyeto,mapenzi kwenye uke-bila kondomu,

kumkumbatia mtu mwenye VVU, Kupiga busu,

mapenzi makavu-bila kondomu, Kuchua,

Mwanaume aliyetahiriwa akijamiiana na

mwanamke, Kumnyonya mwanaume uume kwa

kutumia kondomu, Kumnyonya mwanamke

ukeni bila kondomu, watoto wachanga kunyonya

kwa mama mwenye maambukizi ya VVU,

Mapenzi kinyume na maumbile—bila kondomu

Kadi zilizoandikwa “kadi za hisa”: Andika

viwango kwenye kadi za hisa kwa mfano.

Hatari kubwa zaidi, Hatari kidogo, Hatari

kiasi, Hakuna hatari yenye uhusiano na

ueneaji wa VVU.

Page 102: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

90

Hatua 1: Fahamisha

Wafahamishe washiriki kuwa wanakwenda

kukamilisha zoezi linaloangazia tabia

zilizobeba hatari za kuambukiza VVU.

Weka kadi zenye tabia za kimapenzi

kuelekea chini kwenye kitita (tazama orodha

chini) halafu waombe washiriki kuchukua

kadi na kuiweka ukutani/sakafuni kwenye

kipengele sahihi, “Hatari kubwa” “Hatari

kidogo” “Hatari kiasi” na “ Hakuna hatari”

kuhusiana na ueneaji wa VVU

Kuachana na mapenzi kabisa

Kupiga punyeto

Mapenzi ukeni-bila kondomu

Kumkumbatia mtu mwenye VVU

Kupiga busu

Mapenzi makavu—bila kondomu

Kuchua

Mwanaume aliyetahiriwa akifanya mapenzi

na mwanamke

Page 103: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

91

Kumnyonya uume mwanaume kwa kutumia

kondomu

Kumnyonya mwanamke ukeni bila kutumia

kondomu

Watoto wachanga kunyonya kwa mama

mwenye maambukizi ya VVU.

Mapenzi kinyume cha maumbile-bila

kondomu.

Baada ya kadi zote kuwa ukutani/sakafuni,

waombe washiriki wapitie mahali ambapo

kadi zimewekwa. Halafu waombe wajitolee

kusema kama:

Hawakubaliani na mahali kadi zote

zilipowekwa

Hawaelewi uwepo wa kadi zote mahali zilipo

Walipata wakati mgumu kuweka kadi zote.

Hatua 2: Jadili

Jadili uwepo wa baadhi ya kadi, hasa zile

zenye utata kuhusu hatari, au kadi ambazo

Page 104: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

92

zimewekwa dhahiri mahali pasipo sahihi.

Anza kwa kuwauliza washiriki kwa nini

wanadhani kadi iliwekwa kwenye kipengele

fulani. Pitia vipengele hapa chini kama huna

uhakika mahali ambapo tabia fulani

inapaswa kuwapo.

Page 105: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

93

Hatari za ueneaji wa VVU kutokana na shughuli

za mapenzi

HAKUNA

HATARI

HATARI

KIDOGO

HATARI

KIASI

HATARI

KUBWA

Kuachan

a na

mapenzi

Kupiga

punyeto

Kumkum

batia

mtu

mwenye

VVU

Kupiga

busu

Kuwaza

tendo la

kimapen

zi

Kuchua

Kufanya

mapenzi

kwenye

uke kwa

kondomu

Kumnyony

a mboo

mwanaum

e mwenye

VVU- kwa

kutumia

kondomu

Kufanya

mapenzi

mdomoni

na

mwanamk

Wato

to

wach

anga

kuny

onya

kutok

a

kwa

Mwa

namk

e

mwe

nye

VVU

Map

enzi

Map

enzi

ukeni

bila

kond

omu

Map

enzi

kinyu

me

cha

mau

mbile

- bila

kond

omu

Page 106: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

94

e mwenye

VVU

Kutumia

vidole/mik

ono/vitu

vilivyosafis

hwa kabla

ya

kuchangia

kinyu

me

cha

mau

mbile

kwa

kutu

mia

kond

umu

na

vilaini

shi

Map

enzi

maka

vu-

bila

kond

omu

Hatua 3: Uliza

Waombe washiriki watazame tabia zilizopo

kwenye vipengele vya “Hatari kidogo” na

“Hakuna hatari”. Weka msisitizo kwenye

dhana ya kwamba baadhi ya tabia za

kimapenzi zenye kufurahisha zina hatari

kidogo au hazina hatari kabisa.

Page 107: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

95

Hatua 4: Hitimisha

Hitimisha na sisitiza kwamba hatari

hutegemea mazingira ya tabia au sababu

zingine. Hizi ni pamoja na mila za jinsio,

ikiwa kama mwenza ameambukizwa au la,

ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa

tabia za kimapenzi, na ugumu wa kufahamu

ikiwa kama mwenza wa mtu

ame/hajaambukizwa VVU.

Kiwango cha hatari kwa kiasi kikubwa kwa tabia

hizi kitatofautiana kulingana na sababu kadhaa.

Hizi ni pamoja na mila na ukosefu wa usawa wa

kijinsia, ikiwa kama mwenza ni/si mwathirika wa

VVU, ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa

tabia za kimapenzi, historia ya kimapenzi na hali

ya VVU kwa kila mwenza, na matumizi sahihi ya

kondomu. Kwa mapenzi ya mdomoni, uwepo wa

vidonda, au fizi zinazotoa damu kunaweza

kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU kwa

mtoaji.

Page 108: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

96

Zoezi 5: Igiza kama mwanaume, igiza kama

mwanamke

Dakika 40

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Hatua 1: Uliza

Waulize washiriki kama wamewahi kuambiwa

“kuigiza kama mwanaume” au “kuigiza kama

mwanamke.” Wape nafasi ya kuchangia

baadhi ya uzoefu ambao mmoja wao

ameusema au kitu kinachofanana kwao. Kwa

nini mtu kasema hili? Jambo hili linamfanya

mshiriki ajisikie vipi?

Hatua 2: Sema

Tutatazama kwa kina zaidi aya hizi mbili. Kwa

kuzichunguza, tunaweza kuanza kuona namna

ambavyo jamii inatambua maana ya kuwa

mwanaume au mwanamke.

Page 109: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

97

Hatua 3: Chunguza “kama mwanaume”

Kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande

cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza kama

mwanaume.”

Waombe washiriki kuchangia mawazo yao

kuhusu maana ya maneno haya. Andika

mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au

ubao wa chaki

“Igiza kama mwanaume”

Kuwa shupavu

Usilie

Wakoromee watu

Usioneshe hisia

Walinde watu

wengine

(wanawake na

watoto)

Pambana na

utakayokabiliana

nayo maishani ,

usionyeshe uwoga

Kuwa bosi

Ingiza kipato

Miliki wapenzi/wake

zaidi ya mmoja

Safiri kutafuta ajira

Page 110: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

98

Hatua 5: Jadili—“kama mwanaume”

Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya

washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya

matarajio ya kijamii?

Kunaweza kuwako na mipaka kwa

mwanaume kutazamiwa kutenda namna hii?

Kwa nini?

Ni hisia zipi wanaume hawapaswi

kuzionesha?

Ni kwa namna gani “kujifanya mwanaume”

kunaathiri mahusiano ya mwanaume na

mwenza na watoto wake?

Ni kwa namna gani mila za kijamii na

matarajio ya “kuigiza kama mwanaume”

yana matokeo hasi kwenye afya ya uzazi na

mapenzi kwa mwanaume?

Je inawezekana wanaume kutoa

changamoto na kubadili majukumu yaliyopo

kulingana na jinsi?

Page 111: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

99

Hatua 6: Chunguza “kama mwanamke”

Sasa kwa herufi kubwa, chapa kwenye

kipande cha karatasi ya ubaoni maneno,

“Igiza kama mwanamke.”

Waombe washiriki kuchangia mawazo yao

kuhusu maana ya maneno haya. Andika

mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au

ubao wa chaki.

“Igiza kama mwanamke”

Usioneshe hisia

Kuwa mwangalizi

Kuwa mrembo, ila

usiwe mrembo sana

Kuwa nadhifu, ila

usiwe nadhifu sana

Kuwa mkimya

Kuwa mke mwema

Kuwa mwaminifu

Kuwa mnyenyekevu

Page 112: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

100

Hatua 7: Jadili

Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya

washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya

matarajio ya kijamii?

Kunaweza kuwako na mipaka kwa wanawake

kutarajiwa kujimudu kwa namna hii? Kwa

nini?

Ni kwa namna gani “kuigiza kama

mwanamke” kunaathiri mahusiano ya

mwanamke na mwenza na watoto wake?

Ni kwa jinsi gani mila za kijamiii na matarajio

ya “kujifanya mwanamke” yana matokeo hasi

kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa

mwanamke?

Je wanawake wanaweza kuishi kinyume cha

mambo haya?

Je inawezekana wanawake kutoa

changamoto na kubadilisha majukumu

yaliyopo kulingana na jinsia?

Page 113: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

101

Hatua 8: Hitimisha

Hitimisha zoezi hili kwa kueleza kwa ufupi

baadhi ya majadiliano na kuchangia mawazo

yoyote ya mwisho. Swali la mwisho laweza

kuwa kama ifuatavyo:

Shughuli hii ni njia nzuri ya kuelewa maana ya

mila za jinsi. Lakini kumbuka kuwa hizi mila za

jinsi zinaweza pia kuathiriwa na matabaka,

utamaduni, kikundi fulani, na tofauti nyingine.

Page 114: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

102

Ujumbe ambao wanaume wanaupata kutokana

na “kuigiza kama mwanaume” ni pamoja na:

• Kuwa shupavu na usilie

• Kuwa mwingizaji wa kipato

• Jisimamie na usirudi nyuma

• Fanya mapenzi unapohitaji

• Wanawake ni vitu fulani kuwa navyo—mali

Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi

kufuatia “kuigiza kama mwanaume” zina

matokeo (madhara) yafuatayo kwenye

mitazamo ya wanaume na uume:

Wanaume wanathaminiwa zaidi kuliko

wanawake.

Wanaume wanaogopa kudhuriwa na

kuonesha hisia zao.

Wanaume wanahitaji uthibitisho mara zote

kwamba wao ni wanaume kweli.

Wanaume hutumia mapenzi kuthibitisha

kuwa wao ni wanaume kweli.

Page 115: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

103

Wanaume hutumia nguvu kuthibitisha kuwa

wao ni wanaume kweli.

Ujumbe ambao wanawake wanapata kutokana

na “kuigiza kama mwanamke” ni pamoja na:

Kutoonesha hisia na kukaa kimya

Kuwa waangalizi na wajenzi wa nyumba

Jifanye mrembo, ila usiwe mrembo sana

Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana

Fuata miongozo ya wanaume

Mtunze mmeo—mpe starehe ya mapenzi

Usilalamike

Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi

kufuatia “kuigiza kama mwanamke” vile vile

yana matokeo (madhara) yafuatayo kwenye

mitazamo ya wanawake na uke:

Mara nyingi wanawake hawajiamini

Wanawake huthaminiwa kwanza kama

mama na si kama watu

Wanawake huwategemea wenza wao

Page 116: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

104

Wanawake wana maamuzi kidogo kuliko

wanaume kuhusu maisha yao kimapenzi

Wanawake wameathirika zaidi na VVU na

UKIMWI na ukatili

Mila za jinsi zisizo na manufaa huongeza hatari

ya magonjwa ya ngono na VVU na mimba

zisizotarajiwa, na hutengeneza vikwazo

vikubwa kwa maendeleo ya wanawake kijamii,

kiuchumi, na kisiasa.

Page 117: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

105

Zoezi 6: Kufanya maamuzi kuhusu jambo

linalofaa na lisilofaa

Dakika 30

Hatua 1: Eleza

Tutatazama mchakato wa kufanya maamuzi

sahihi kwa kujitambua ili kujikinga na VVU.

Eleza kwamba watapewa orodha iliyo katika

namna tofauti na wanapaswa kuonesha kwa

matamshi au kwenye karatasi kama hatua

iliyochukuliwa ilikuwa “sahihi” au “si sahihi”

Hatua 2: Fafanua

Toa maana ya maneno haya: “kufaa” na

“kutofaa.”

Page 118: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

106

Kufaa Kutofaa

“Kufaa inamaanisha

kitendo au mwitikio

unaostahili, sahihi, au

unaoendana na

mazingira ya uzuiaji VVU

na mila za jinsia na

usawa kama

ilivyojadiliwa katika

shughuli zilizotangulia.

Kutofaa inamaanisha

kitendo au mwitikio

usiostahili, usio sahihi, na

usioendana na mazingira

ya uzuiaji wa VVU na

mila za jinsi na usawa

kama ilivyojadiliwa katika

shughuli zilizotangulia.

Hatua 3: Soma

Kariri hadithi ya kwanza (ukurasa unaofiuata)

halafu washiriki waseme wapi panafaa na

wapi hapafai na kwa nini.

Hatua 4: Jadili

Kufungua mjadala wa ukweli kuhusu

mapenzi inaweza kuwa jambo gumu lakini ni

mhimu.

Page 119: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

107

Watu wenye madaraka wasitumie vibaya

nafasi zao kuwalazimisha wengine kutenda

kinyume na matakwa yao.

Watu wanapaswa kuheshimu haki za

wengine kuchagua kama wanataka kufanya

mapenzi na kufanya mapenzi salama kwa

kutumia kondomu za kike au kiume.

Ili mradi tabia za kimapenzi ni jambo la

maridhiano pasipo kuumiza au kujeruhi,

wengine hawapaswi kuingilia.

Wapange washiriki wawili wawili halafu

wape eneo la kujadili na kuamua kama

linafaa au halifai. Wape dakika 10 kufanya

hivyo na elezea kwa kifupi kila eneo.

Page 120: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

108

Simulizi za Matukio

Tukio 1: Kumtembelea daktari

Afisa magereza ameambiwa na daktari kuwa ana

kifua kikuu, ambayo ni maambukizi nyemelezi ya

kawaida kwa wale waishio na VVU. Daktari

akashauri kwamba wote wawili afisa magaereza

na mwenzi wake wapate ushauri nasaha na

kupima VVU. Afisa magereza akamweleza

mpenzi wake kuwa kikohozi chake kisichoisha

kinasababishwa na hali mbaya ya ubaridi baada

ya muda kitaisha.

Haifai: Afisa magereza ana wajibu wa

kumfahamisha mwenza wake ukweli kuhusu

mkutano wake na daktari na kumpa nafasi

mwenza wake kujilinda na kushughulika na

uwezekano wa kuwa mwathirika wa VVU.

Page 121: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

109

Tukio 2 : Fadhaa za magonjwa ya ngono

Mfungwa ambaye hivi karibuni ameachiliwa

kutoka gerezani amekutana na binti/kijana

mtaani na kuanza mahusiano naye kimapenzi.

Siku moja

wakati

akioga,

binti/kijana

aliona

kidonda

chekundu kwenye sehemu zake za siri. Anaona

soni sana kuzungumza na mwenzi wake lakini

alimpeleka hospitali ili kupata vipimo na

kumweleza dakitari kuhusu kidonda.

Haifai: Ni muhimu kabisa kumfahamisha mpenzi

wako kuhusiana na ugonjwa wowote wa ngono

(VVU au vinginevyo) unaoutambua ili aweze

kuchunguzwa. Hii si kwa ajili ya afya zao tuu,

lakini pia kwa ajili ya afya ya jamii nzima kwa

Page 122: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

110

sababu ugonjwa ukitibiwa mapema, ndivyo

unavyoweza kudhibitiwa mapema na kupunguza

uwezekano wa kuwaambukiza wengine.

Tukio 3: Hakuna zawadi ya bure

Afisa magereza amekuwa akimchumbia

msichana anayeuza machungwa na mayai

sokoni. Alinunua vitafunwa vyake kila mara

alipomwona, pamoja na kumpa zawadi ndogo

ndogo. Alikuwa na usongo wa kufanya mapenzi

nae. Jioni moja walipigana busu na alimtomasa

matiti yake. Mzuka ulimpanda sana lakini binti

alisema hayuko tayari. Alimsukuma binti chini,

akamkandamiza mikono yake chini na

akajilazimisha hadi akazama ndani yake.

Haifai: Afisa magereza huwenda alifikiri binti

“alipaswa kumpa”mapenzi kwa kuchukua chakula

na zawadi lakini hakuwa na haki ya kumbaka.

Ubakaji huongeza hatari ya maambukizi ya VVU

kwa kuwa wabakaji mara chache sana hutumia

Page 123: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

111

kondomu na kitendo cha kutumia nguvu kufanya

ubakaji hupelekea kuchanika kwa kuta za uke au

njia ya haja kubwa.

Tukio 4: Matumizi mabaya ya cheo

Siku moja, mwalimu mkuu katika chuo cha

mafunzo katika gereza alimwomba mmoja wa

wanafunzi wake wa kike kubaki baada ya vipindi

kwisha na kumwambia kwamba alitaka

kujadiliana naye kuhusu maendeleo yake

kitaaluma. Baada ya vipindi msichana alibaki na

mkuu wa chuo alimsifia sana kuhusu uzuri wake.

Kitendo hicho cha kumsifia kilimchukiza sana

msichana, lakini hakusema chochote kwa kuwa

alikuwa mwalimu wake. Mwalimu alipoona

kwamba msichana hajafurahi, alimwambia awe

makini sana, kwani matokeo ya maendeleo yake

kitaaluma yalikuwa mikononi mwake, na

alimwomba msichana kwenda nyumbani kwake

Page 124: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

112

jioni ile, kitu ambacho msichana alitii kwani

aliogopeshwa kuwa hatafaulu mitihani yake.

Haifai: Mwalimu hakupaswa kutumia cheo chake

au nafasi yake kumtisha msichana mdogo.

Ingawa msichana alikwenda nyumbani kwa

mwalimu, ilikuwa ni kwa sababu ya vitisho

kwamba uhalali wa matokeo yake kitaaluma

ungeharibiwa kama asingefuata alichoambiwa na

mwalimu kufanya.

Tukio 5: Tabia za kutowajibika

Afisa magereza alihamishwa kwenda gereza la

wilaya ambapo alidhani angepaswa kwenda bila

ya mke wake na watoto ili kuepusha usumbufu

kwao kuhusiana na mambo ya shule na familia.

Afisa alikaa peke yake katika makazi yake mapya.

Siku moja, alipokuwa baa, alikutana na

mwanamke na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi

ulioendelea kwa kipindi fulani. Pamoja na kuwa

Afisa alikuwa ameoa na akijua kuwa mwanamke

Page 125: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

113

huyu alikuwa na mpenzi mwingine, hakuona hili

kama ni tatizo. Mwanamke alisisitiza kutumia

kondomu, lakini Afisa hakuona umuhimu wa

kondomu, na baadaye baaada ya mda

mwanamke aliacha kusisitizia.

Haifai: Pamoja na kwamba wote wawili

walikuwa wawazi kuwa wana wapenzi wengi

lakini hawakuwajibika kwa kufanya mapenzi

yasiyo salama, jambo ambalo haliwaweki wao tu

katika hatari lakini pia linawaweka wenzi wao

wengine katika hatari ya maambukizi ya VVU,

ambao huenda hawafahamu kuwa wenzi wao

walikuwa wakifanya mapenzi na watu wengine,

na mapenzi yasiyo salama.)

Tukio 6: Woga usiotakiwa

Mfungwa ajulikanaye kama Victor alihamishiwa

kwenye chumba kimoja kidogo kutokana na umri

wake mdogo ukilinganisha na wengine ambao

walionekana mabingwa na wenye kupenda

Page 126: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU

magerezani

114

kutaniana. Victor alikuwa mpole na mwenye aibu

na mara nyingi alipendelea kukaa peke yake.

Kwa tabia hiyo wenzake walimtania kwa kumwita

mwanamke nakadhalika. Siku moja wenzake

walimzunguka, wakamsukuma, na kumvua

suruali yake ili kuthibitisha kama kweli alikuwa

mwanaume au la. Mmoja wao alimshika kwa

nguvu na kumtisha.

Haifai: Ingawa walikuwa ni wakazi wenza wa

kiume, ukandamizaji na matendo mabaya

yanaweza kutokea kutokana na tofauti ya nguvu

za mamlaka. Waelimisha rika wanapaswa

kujadiliana na wafungwa nini kinapaswa

kufanyika kwenye tukio kama hili na taratibu

zinazopaswa kufuatwa katika kuripoti tukio kama

hili.)

Page 127: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

115

SOMO 3: KIFUA KIKUU NA

VVU: MATIBABU, HUDUMA

NA MSAADA

Lengo

Kupata maelezo ya msingi kuhusu kinga,

matibabu, huduma, na msaada wa Kifua

kikuu na VVU.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

Kueleza umuhimu wa kujua hali yako ya kifua

kikuu na VVU.

Kueleza maana ya upimaji VVU wa hiari na

ule unaoasisiwa na mtoa huduma.

Kuelezea umuhimu wa huduma za upimaji

VVU.

Kujadili dawa za kupunguza makali na

mahali pa kupata huduma na msaada.

Page 128: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

116

Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia

kondomu za kike na kiume.

Kueleza kwa kifupi upatikanaji wa matibabu

mengine kwa matatizo mtambuka ya kiafya

kama vile, maginjwa ya ngono, maambukizi

kwenye njia ya uzazi, na maambukizi

nyemelezi.

Kueleza maana ya maneno kinga ya

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto na kutokomeza

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto.

Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza

mama mwenye VVU na mtoto.

Page 129: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

117

Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU

Dakika 145

Kipindi 3.1: Mazoezi

Kuelezea maana ya maneno

Ufunguzi kuhusu upimaji wa VVU

Kweli/Uongo kuhusu upimaji VVU

Upimaji wa VVU kwa ujumla

Upimaji wa VVU gerezani

Matumizi ya kondomu za kike na kiume

Dhamira

Mwisho wa kipindi hiki washiriki wataweza:

Kufafanua upimaji wa hiari na ulioasisiwa na

mtoa huduma

Kueleza umuhimu wa kujua hali ya VVU

Kujadili umuhimu wa huduma za kupima

VVU

Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia

kondomu za kike na kiume

Page 130: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

118

Zoezi 1: Kueleza maana ya maneno

muhimu

Dakika 30

Shirika la afya duniani lilibadilisha maneno yao

mwezi wa saba 2015 kutoka “ Ushauri nasaha na

upimaji wa VVU” kuwa “Huduma za upimaji wa

VVU,” na nchi zinafuata inavyostahili zinapokuwa

zinahuisha miongozo yao. Maneno huduma za

upimaji wa VVU yanatumika kujumuisha huduma

zote zinazopaswa kutolewa pamoja na upimaji

wa VVU: ushauri nasaha (maelezo ya ushauri

nasaha kabla na baada ya kupima);

zilizounganishwa na huduma stahiki za kinga,

matibabu na usimamizi na huduma zingine za

kliniki na na msaadali; na kushirikiana na huduma

za maabara ili kusaidia uthibiti wa ubora na

utolewaji wa majibu sahihi.

Hatua 1

Waambie washiriki kuwa watatumia dakika

takribani 30 au chini yake wakitazama baadhi

Page 131: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

119

ya maneno muhimu ambayo watakuwa

wakiyatumia katika kipindi hiki na kwa muda

mrefu baada ya kozi.

Chaguo 1

Kwa kutumia karatasi ya ubaoni iliyoandaliwa

yenye vifupisho vyote, ligawe kundi katika

timu mbili. Waambie washiriki kwamba

watacheza mchezo wa vifupisho.

Wafahamishe kuwa vifupisho hivi

vimeandikwa kwenye karatasi ya ubaoni

ambayo mtaifungua mchezo utapoanza.

Taja kuwa kila kikundi kitachagua mwakilishi

ambaye atachagua kifupisho kimoja na

kuwaambia wanakikundi maana yake.

Atakapopatia kundi litapata alama 2 lakini

akikosea kundi litapoteza alama 2. Waambie

kuwa watapeana zamu mpaka vifupisho

vyote vitakapokwisha.

Page 132: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

120

Chaguo 2

Waalike washiriki kukaa wawili wawili na

kuchukua kipande cha karatasi. Wafahamishe

kwamba utatamka kifupisho ili wao waandike

kwa kirefu kama pea. Kwa ufafanuzi zaidi

ziunganishe pea mbili ili ziweze

kusahihishiana pale unapokuwa ukitoa

majibu sahihi kama yalivyotolewa kwenye

kisanduku cha maneno kulia kwako

Hatua 2: Pongezi

Pongeza kundi

zilizopata majibu

kwa usahihi zaidi.

Zoezi 2:

Utangulizi

kuhusu upimaji

wa VVU

Dakika 20

Page 133: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

121

Hatua 1: Eleza

Katika kipindi hiki tutatazama/zungumza mambo

kadhaa ya huduma za uchunguzi, uangalizi,

matibabu, na msaada, ikiwemo upimaji VVU wa

hiari, upimaji VVU ulioasisiwa na mtoa huduma

na kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama

kwenda kwa mtoto.

Hatua 2: Tamka

Shabaha mpya duniani 90–90–90 zinatoa wito

kwamba asilimia 90 ya watu waishio na VVU

kufanyiwa uchunguzi, asilimia 90 ya watu wenye

VVU waliofanyiwa vipimo kupatiwa dawa za

kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, na

asilimia 90 ya wale wanaotumia dawa za

kupunguza makali wanalazimika kuwa na

kiwango kidogo cha virusi ifikapo 2020. Asilimia

90 ya kwanza (upimaji wa VU), ni muhimu

kwenye asilimia 90 ya pili (kuanzishiwa dawa za

kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

miongoni mwa watu waishio na VVU), na

Page 134: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

122

matokeo ya msingi ya asilimia 90 ya tatu

(kupungua kwa virusi miongoni mwa watu

wanaotumia dawa za kupunguza makali virusi

vya ukimwi), ambayo huboresha matokeo ya

wateja na kuzuia ueneaji wa VVU. Huku ikiwa ni

jambo muhimu kupata watu wengi zaidi

kufanyiwa vipimo na kufanikiwa kuwafikisha

kwenye huduma za matibabu na uangalizi, ni

muhimu kwamba kiwango cha ongezeko

kisididimize ubora wa huduma.

Hatua 3: Zoezi la kikundi

Zoezi hili linazingatia faida na hasara kwa

mtu kujua hali yake ya VVU.

Kabla ya kuanza zoezi, waulize washiriki

kama wanafikiri ni lazima kujua hali zao za

VVU.

Wapange washiriki katika makundi ya watu 4

ili waweze kujadili na kuorodhesha faida na

hasara za mtu kujua hali yake ya VVU.

Wape washiriki dakika 10 kufanya hivyo.

Page 135: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

123

FAIDA MAELEZO

Ishi kwa mda

mrefu

Mpaka sasa dawa za kupunguza

makali zimeweza kuimarisha afya

za watu waishio na VVU, na kwa

kiasi kikubwa zimesaidia

kurefusha maisha kuanzia miaka

5–20. Inawezekana pia kuongeza

kipindi ambacho mfungwa

mwenye maambukizi anaweza

kuishi kwa kubadili mfumo wa

maisha na kupata matibabu ya

maambukizi nyemelezi. Kwa

mfano, kujiepusha na hatari

zaidi, kupunguza unywaji wa

pombe, na kula vizuri kunasaidia

kurefusha maisha.

Kunamaliza

wasiwasi

kuhusu hali

yako

Kupima VVU kunaondoa

wasiwasi kwamba

umeambukizwa au la. Wale

wenye wasiwasi kuhusu tabia zao

za zamani wanaweza kupata

nguvu mpya ya maisha kwa

kutambua hali zao.

Page 136: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

124

FAIDA MAELEZO

Kuanza

kujikinga upya

Kutambua kuwa hujaambukizwa

VVU kunakupa wewe mwanzo

mpya ulio safi ambao kwao

kunaweza kujengwa utamaduni

wa kufanya mapenzi salama.

Kumbuka kwamba robo tatu ya

watu waliopima

hawajaambukizwa.

Kuweka

mipango ya

maisha yako

yaliyobaki

Kwa wapenzi wachanga, kupima

pamoja kabla ya kuoana

kunawawezesha kutambua ya

kuwa wanaweza kupata watoto

ambao hawajaambukizwa ikiwa

wataendelea kujikinga na

maambukizi. Wale

watakaogundua kuwa

wameambukizwa VVU

wanaweza sasa kupanga maisha

yao yaliyobaki. Inaweza kuwa ni

miaka mingi ijayo kabla

hawajaanza kuugua na hatimaye

kufariki. Wakati huo huo,

wanaweza kuwakinga wenza

Page 137: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

125

FAIDA MAELEZO

wao na maambukizi na kuzuia

maambukizi ya VVU kutoka kwa

mama kwenda kwa mtoto.

Wanaweza pia kupanga

dhamana za hapo baadaye kwa

familia zao kwa kuandaa usia na

kuweka mipango ya kifedha.

Hatua 4: Wahakikishie

Washukuru washiriki kwa ushiriki wao na

eleza kuwa mara tutapoelewa ukweli kuhusu

VVU tutaweza kupunguza ueneaji wake na

kuishi kwa mda mrefu, maisha yenye afya.

Pia tunaweza kujilinda na kuwalinda wengine

kutokana na maambukizi ya VVU kwa kwa

kupunguza vihatarishi tunazokumbana nazo

gerezanni na mara baada ya kutoka. Kama

mwelimisha rika, unaweza kuwahakikishia kuwa

kama mwongozo wa kitaifa kuhusu VVU

utafuatwa na wafungwa na wafanyakazi wa

magereza tunaweza kupunguza hatari nyingi za

Page 138: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

126

maambukizi ya VVU magerezani na kusaidia

upimaji wa VVU.

Zoezi 3: Kueleza maana ya ushauri nasaha

na upimaji wa hiari na ushauri nasaha na

upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa

huduma

Dakika 20

Hatua 1: Dadisi

Waulize washiriki wanafikiri nini tofauti kati ya

upimaji VVU hiari na ulioasisiwa na mtoa

huduma?

Hatua 2: Elezea jedwali lifuatalo

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA HIARI

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA VVU

ULIOASISIWA NA MTOA

HUDUMA

Mtu huchagua

kutafuta vipimo.

Mtu anatafuta huduma za

matibabu, halafu upimaji

unapendekezwa na

kufanywa na daktari kama

Page 139: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

127

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA HIARI

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA VVU

ULIOASISIWA NA MTOA

HUDUMA

sehemu ya mashauriano.

Huduma

pasipokuweka jina au

huduma za siri

zinaweza kutolewa.

Huduma zitolewazo ni za

siri na hutunzwa kwenye

kumbukumbu za hospitali

ili kuhakikisha

mwendelezo wa huduma.

Lengo la msingi

limejikita katika kuzuia

ueneaji wa VVU kwa

kutathimini hatari,

kupunguza hatari, na

upimaji.

Lengo la msingi ni

kuwatambua watu

walioambukizwa VVU na

kuwaunganisha na

huduma za kinga,

uangalizi na matibabu.

Maridhiano kwenye

maandishi au alama

za vidole kwa

wasiojua kuandika na

kusoma huhitajika.

Maridhiano ya mdomo

huhitajika na yanapaswa

kutunzwa kwenye

kumbukumbu za

mgonjwa.

Mtumiaji wa kwanza Mtumiaji wa kwanza wa

Page 140: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

128

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA HIARI

USHAURI NASAHA NA

UPIMAJI WA VVU

ULIOASISIWA NA MTOA

HUDUMA

wa matokeo ya

vipimo ni mteja,

anayetumia taarifa

kufanya maamuzi

binafsi ya maisha

yake.

matokeo ya vipimo ni

mtoa huduma za afya

kufanya uchunguzi sahihi

na kutoa matibabu sahihi.

Hatua 3: Faida za upimaji wa vvu ulioasisiwa

na mtoa huduma

Waulize washiriki wanafikiri ni zipi faida za

upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa

huduma?

Elezea yafuatayo:

Hhuwasaidia wataalamu wa afya kuwatibu

wateja wao kwa usahihi kwa kuwatambua

wale wanaohitaji matibabu/au program za

uzima mapema.

Page 141: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

129

Huwasaidia watoa huduma za afya

kuboresha huduma za matibabu zitolewazo

kwa wateja wao na kupunguza ugonjwa na

vifo.

Inasaidia kupunguza unyanyapaa katika

jumuiya kama magerezani kwa kufanya

upimaji wa VVU kuwa ni jambo la kawaida.

Hatua 4: Sisitiza

Sisitiza kwamba bila kujali ni njia gani ya

upimaji imetumika, kanuni tano za upimaji

wa VVU zinapaswa kufuatwa. Waulize

washiriki “kanuni za upimaji wa VVU” ni nini.

Washiriki wanaweza kujibu au unaweza

kueleza kanuni hizi tano kama ifuatavyo:

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

Ushauri

nasaha

Ushauri nasaha ni majadiliano

baina ya mshauri wa VVU aliyepata

mafunzo na mteja anayetafuta

Page 142: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

130

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

kupunguza kupata na kueneza

VVU kupitia:

- Maelezo: Mteja hupokea

maelezo kuhusu ueneaji na

namna ya kujikinga na VVU na

maana ya matokeo ya vipimo

vya VVU. Watu ambao hupima

na kuonekana hawana

maambukizi ya VVU wanapaswa

kupata maelezo ya afya kwa

kifupi juu ya matokeo ya vipimo

vyao.

- Ushauri nasaha na kinga ya VVU:

Wateja hupokea msaada ili

kutambua tabia hatarishi

mahususi zinazopelekea kupata

au kueneza VVU na kupiga hatua

ya kupunguza hatari hii.

Mpaka leo tafiti hazijaonesha

kwamba kutoa ushauri nasaha kwa

Page 143: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

131

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

mda mrefu kunahitajika au

kunamanufaa zaidi. Isitoshe, utoaji

ushauri nasaha kwa mda mrefu

baada ya vipimo kwa watu ambao

hawakukutwa na maambukizi

unaweza kuelekezwa kwingine

rasilimali zilizotengwa kwa ushauri

nasaha ambazo zinahitajika na

wale waokutwa na VVU, wale

ambao majibu yao bado hayana

hitimisho, na wale waliokutwa

katika mahusiano ambayo mmoja

wao ana VVU na mwingine hana

VVU

Kuridhia Mtoa vipimo amekupatia maelezo

ya kina ili uweze kufanya maamuzi

sahihi kwa kujitambua kuhusu ikiwa

kama unataka kupima au la, ikiwa

ni pamoja na uhuru wa kukataa

kupima. Maelezo yanapaswa

kugusia, vipimo vinahusisha nini,

Page 144: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

132

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

majibu tarajiwa, na uwezekano wa

matokeo yatokanayo. Upimaji wa

lazima haufai.

Usiri Kile unachokijadili na mshauri

kitabaki kuwa siri yenu wawili.

Mshauri hataweza kumwambia mtu

mwingine yeyote mlichokijadili au

nini matokeo ya vipimo vyako.

Usahihi Watu wote ambao vipimo vyao

vinaonesha wana VVU wanapaswa

kupimwa tena ili kuthibitisha vipimo

vyao kabla ya kuanzisha huduma

na matibabu ya VVU.

Mshikamano Kutoa huduma za upimaji VVU

mahali ambapo hakuna upatikanaji

wa huduma, au uunganishwaji

dhaifu kwenye huduma, ikiwepo

dawa za kupunguza makali ya

virusi vya ukimwi, una manufaa

Page 145: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

133

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

kidogo kwa wale wenye VVU.

Zoezi 4: Upimaji VVU: Zoezi Kweli/Uongo

Dakika 15

Hatua 1: Zoezi

Waelezee washiriki kuwa utataja orodha ya

maelezo. Ungependa wao wasimame ikiwa

maelezo ni KWELI, au wakae ikiwa

wanadhani maelezo ni UONGO. Waambie

kuwa utawauliza waeleze sababu za majibu

yao.

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

Upimaji pasipo

kutumia jina

maana yake

unapewa namba

na hakuna

KWELI: Kutuliza hofu na

kupunguza unyanyapaa

baadhi ya huduma za upimaji

haziwahitaji wale walifanyiwa

vipimo kutoa majina yao.

Page 146: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

134

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

anayejua jina lako

unapopimwa.

Sampuli ya damu zao

hutambuliwa kwa kutumia

namba pekee. Huduma za

upimaji wa VVU zinapaswa

kuwa siri, maana yake kile

ambacho mtoa huduma na

mteja wanajadili hakitatolewa

kwa mtu yeyote bila ya

ridhaa ya mtu anayepimwa.

Usiri unapaswa kuheshimiwa,

lakini usiruhusiwe kutilia

mkazo siri, unyanyapaa, au

fedheha.

Mtu akigundulika

kuwa na VVU

baada ya kufanya

vipimo ya lazima

basi moja kwa

moja hufukuzwa

kazi.

UONGO: Upimaji wa hiari

unathaminiwa na watu wenye

VVU hawapaswi kufukuzwa

kazi. Ingawa, baadhi ya

waajiri huhitaji wafanyakazi

kupima kabla ya kwenda

kufanya kazi nje ya nchi. Mtu

anayekutwa na maambukizi

ya VVU kwa kawaida

huruhusiwa kuendelea

Page 147: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

135

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

kufanya kazi lakini haruhusiwi

kusafiri nje ya nchi.

“Kipindi cha

mficho” ni kipindi

ambacho kinga

dhidi ya VVU

huenda isionekane

kwenye damu ya

mtu

aliyeambukizwa.

KWELI: Huchukua hadi kati ya

miezi mitatu hadi sita kwa

kinga ya VVU kuonekana

kwenye damu. Ushauri siku

zote kwa kila anayepima VVU

na kujikuta hana maambukizi

ni kupima tena baada ya

“kipindi cha miezi mitatu” si

sahihi. Marudio ya upimaji

yanahitajika kwa wale tu

ambao matokeo ya vipimo

vyao yanaonesha

hawajaambukizwa ambao

wameripoti hivi karibuni

(miezi mitatu iliyopita) au

uwepo katika hatari

enderevu. Kwa watu wengi

ambao hawana maambukizi

ya VVU baada ya kupima,

upimaji kwa mara nyingine

kufanya uamuzi wakati wa

Page 148: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

136

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

kipindi cha mficho si lazima

na inaweza kupoteza

rasilimali.

Wale wanaokutwa

bila maambukizi ya

VVU baada ya

kupima hawapaswi

kujizuia na tabia

hatarishi hapo

baadaye

UONGO: Mtu anaweza

kujiingiza katika mahusiano

hatari ya kimapenzi pasipo

kuambukizwa. Lakini hii

haimaanishi kuwa

hawataambukizwa kwenye

shughuli zao za kufanya

mapenzi yasiyo salama

zinazofuata

Kila mmoja

anapaswa

kupimwa.

KWELI: Upimaji wa VVU ni

njia ya kujikinga, kupata

matibabu, uangalizi, na

huduma zingine za msaada

dhidi ya VVU. Uelewa wa

watu juu ya hali zao za VVU

kupitia huduma za upimaji ni

muhimu kwenye mafanikio ya

kupambana na VVU. Wigo

wa upimaji VVU miongoni

Page 149: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

137

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

mwa watoto ni mdogo.

Mbinu zinahitajika kuongeza

uchunguzi wa mapema kwa

watoto wachanga na

kuwaunganisha kwa wakati

watoto wachanga

watakaogundulika kuwa na

VVU kwenye matibabu na

huduma. Mbinu za ziada

zinahitajika kuongeza

utumiaji wa huduma za

upimaji VVU miongoni mwa

wanaume, ikiwemo utolewaji

wa huduma za upimaji VVU

katika maeneo ambayo

yanafaa zaid na kukubalika

na wanaume, na kubadili njia

za kuwahimiza upimaji wa

wenza wa wanaume katika

maeneo ambapo kuna

uwepo mkubwa na kwa

wapenzi na wenzi wa

wanaume na wanawake

Page 150: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

138

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

wenye VVU kwenye maeneo

yote. Kuyafikia makundi

maalumu ya watu, kama vile

wakazi wenza, ni jambo la

kupewa kipaumbele.

Kama mtu

atagundulika kuwa

na VVU mtu huyu

anapaswa

kuwaeleza wenzi

wake wote kuhusu

majibu ya vipimo.

KWELI: Ingawa kuweka wazi

kwa wapenzi, wanafamilia

wenye msaada, na

wafanyakazi wa afya, mara

nyingi kuna manufaa, hii

inapaswa kufanywa na au

kwa ridhaa ya mtu

aliyepimwa. Ushauri nasaha

kwa wateja wenye VVU

inapaswa kujadili majibu

yanayowezekana kuwekwa

wazi, na hatari na manufaa

ya kuweka wazi, hasa

miongoni mwa wanandoa na

wapenzi. Wape ushauri ili

kusaidia kuweka wazi kwa

pamoja. Wanandoa na wenzi

wanapaswa kupewa ushauri

Page 151: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

139

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

nasaha na upimaji wa hiari

pamoja na msaada wa

kuweka wazi kwa pamoja.

Mshauri anapaswa kutazama

hatari za vurugu za ndani za

wapenzi na kujadili hatua

zinazowezekana ili

kuhakikisha usalama wa

kimwili wa mteja hasa

wanawake ambao

wamegundulika kuwa na

VVU.

Mtu wa kwanza

kwa wanandoa

kugundulika na

VVU ndiye aliyeleta

virusi kwenye

familia.

UONGO: Wakati ambapo

mtu anajua kuwa ana

maambukizi ya VVU hauna

uhusiano na muda

alioambukizwa. Baada ya

kipimo kuonesha uwepo wa

VVU, unapaswa kuhimiza na

kuwapima wenzi, watoto, na

wanafamilia wengine wa

mteja. Jambo hili linaweza

kuwa mmoja mmoja, vipimo

Page 152: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

140

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

kwa wapenzi, kupima kwa

pamoja, au kumfahamisha

mwenza kwa ridhaa.

Zoezi 5: Upimaji wa VVU uraiani na

magerezani

Dakika 30

Hatua 1: ElezaUpimaji wa VVU

Kupima VVU ni njia pekee na muhimu kujua

kama una VVU. Ikiwa una VVU, ni jambo

muhimu kutambua ugonjwa. Jambo hili

litakupa nafasi nzuri ya kupata matibabu na

huduma unazohitaji ili kuishi kwa afya.

Unapokwenda kupima VVU, utakuwa na

nafasi kuzungumza na mtu aliyepata

mafunzo, hivyo unaweza kuuliza swali lolote

amabalo unaweza kuwa nalo. Mtu

anayekupima atakupatia maelezo jinsi

ambavyo vipimo vinafanyika na jinsi

utavyopata majibu.

Page 153: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

141

Kutegemeana na aina ya kipimo,

utachukuliwa sampuli ndogo ya damu

kutoka mkononi mwako, au tone la damu

kutoka kwenye kidole chako. Kuna baadhi ya

vipimo hufanyika kwa kutumia maji maji

yanayopatikana kuzunguka fizi.

Kuna aina mbalimbali za vipimo vya VVU.

Baadhi ya vipimo vya VVU huonesha uwepo

wa virusi halisi kwenye damu (kipimo cha

antijeni) na vipimo vingine huonesha kinga

za VVU zinzofanya kazi ya kupambana na

VVU. (kipimo cha kinga).

Ikiwa vipimo vitaonesha kuwa una VVU,

inamaanisha una maambukizi ya VVU. Ikiwa

vipimo vitaonesha kuwa huna VVU, maana

yake huna maambukizi ya VVU. Kwa baadhi

ya vipimo utahitaji kufanyiwa vipimo vya

ufuatiliaji ikiwa majibu ya yataonesha kuwa

una maambukizi ya VVU.

Page 154: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

142

Hatua 2: Maswali na majibu kipindi cha

mficho

Swali: Kipindi cha mficho maana yake nini?

Jibu: Kipindi kuanzia ulipoambukizwa VVU

mpaka pale ambapo mwili utatoa kinga ya

kutosha kwa VVU itakayoweza kuonekana kwa

kutumia kipimo cha kinga ya VVU hujulikana

kama kipindi cha mficho. Watu wengi huweza

kutengeneza kinga ya VVU ndani ya miezi mitatu

mara baada ya kupata maambukizi ya VVU.

Lakini kipindi cha mficho kinaweza kutofautiana

kulingana na kipimo cha VVU kilichotumika. Kwa

ujumla, mtu yeyote mwenye matokeo hasi

kupitia kipimo cha kinga ya VVU ndani ya miezi

mitatu ya uwezekano wa kuwa na VVU,

anapaswa kupima tena baada ya miezi mitatu.

Hatua 3: Maswali na majibuupimaji wa

VVU

Swali: Kipimo cha antijeni ni nini?

Page 155: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

143

Jibu: Kipimo cha antijeni hugundua antijeni za

VVU (sehemu ya virusi) kwenye damu. Kipimo

cha antijeni kinaweza kugundua maambukizi ya

VVU kabla ya kinga ya kutosha ya VVU

haijatolewa ili kuweza kugunduliwa kwa kipimo

cha kinga ya VVU.

Swali: Inachukua mda gani kupata majibu ya

vipimo vya VVU?

Jibu: Matokeo ya haraka ya kipimo cha kinga ya

VVU yanaweza kutolewa ndani ya dakika 15–30.

Ingawa, inaweza kuchukua siku kadhaa au wiki

kadhaa, kutegemeana na aina ya kipimo

kilichotumika. Katika Tanzania matokeo chanya

ya kipimo cha VVU ni lazima yathibitishwe kwa

kipimo cha uthibitishaji.

Swali: Watu waliopo nje ya gereza wanaweza

kwenda kupima wapi?

Jibu: Watoa huduma za afya wanaweza

kukufanyia vipimo vya VVU. Vipimo vya VVU vile

vile vinapatikana katika hospitali nyingi, kliniki za

Page 156: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

144

matibabu, vituo vya afya vya jamiii, vituo vya

ushauri nasaha na upimaji kwa hiari, na mashirika

ya huduma za UKIMWI.

Hatua 4: Maswali na majibu—vipimo vya

VVU gerezani

Swali: Ukiwa gerezani vipimo vya VVU hufanyika

vipi?

Jibu: Vipimo vya VVU hutolewa katika vituo vya

afya vya magereza ikiwemo huduma za kliniki za

ushauri nasaha na upimaji kwa hiari

zinazotembea ambazo hutembelea maeneo ya

magereza. Ingawa, upimaji wa lazima kwa

wafungwa ni kinyume cha maadili na hauna

ufanisi, upimaji unapaswa kuwa wa hiari

ukiambatana na ushauri nasaha kabla na baada

ya kupima. Matokeo yanapaswa kutolewa kwa

wafungwa na mfanyakazi wa afya ambaye

anapaswa kuhakikisha kutunza siri za kihospitali.

Page 157: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

145

Hatua 5: Maswali na majibu—bada ya

kugundua ugonjwa

Swali: Je unapaswa kufanya nini ikigundulika una

VVU au hauna maambukizi ya VVU?

Page 158: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

146

Ufanye nini ikiwa

huna VVU

Kuachana kabisa na

shuguli za mapenzi

ni njia bora zaidi

kuzuia kupata VVU.

Kuepuka maambukizi

huja pale unapokuwa

mwaminifu kabisa

kwa mpenzi mmoja,

inayohitaji wewe na

mpenzi wako

anagalau kupima

VVU kila mmoja, kwa

anagalau miezi

mitatu tofauti; na

mkiamua kufanya

mambo ya mapenzi

ya ndani ya(uke,

mdomo, na njia ya

haja kubwa)

kwamba mtumie kwa

usahihi kondomu ya

kike au kiume.

Ufanye nini ikiwa una VVU.

Kitu cha kwanza ambacho

kliniki itakifanya ni kupima

kiwango cha CD4.

Watachukua damu kutoka

kwako itakayopelekwa

maambara ili kupima idadi ya

seli za CD4 kwenye ujazo wa

mililita moja ya damu. Hii

itakusaidia kujua mfumo wako

wa kinga una afya kiasi gani.

Inapendekezwa kuwa watu

wenye VVU wapime viwango

vya CD4 zao kila baada ya

miezi sita. Pia unaweza

kuhitaji kipimo cha kutaza

wingi wa virusi utapoanza

kutumia ARVs na mara

nyingine baadaye kupima

upunguaji wa virusi kwa

kutumia dawa za ARVs

(ufanisi).Unapokuwa tayari na

salama kufanya hivyo, ni

muhimu kuweka wazi kwa

mwenzi wako kuwa una VVU

Page 159: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

147

Zoezi 6: Matumizi ya kondomu za kike na

kiume

Kuzuia ueneaji wa VVU

Dakika 30

Hatua 1: Eleza

Eleza kwamba hii ni fursa kwa ajili yao

kujifunza au kuchangia taarifa kuhusu jinsi ya

kutumia kondomu ya kiume na kike kwa

ufasaha kama njia ya kujikinga na VVU.

Kuzungungumzia kuhusu kondomu kwenye

maeneo ya gerezani inaweza kuwa ni jambo

gumu. Ingawa, ni muhimu kuweka wazi kuwa

kondumu hazitagawiwa magerezani.

Hairuhusiwa na sheria za Tanzania. Kwa hiyo ni

muhimu kupata taarifa hizi kuhusu kondomu

kwani zitawanufaisha mara baada ya kumaliza

kifungo au kuachiliwa kutoka gerezani kwa

mfano, mahabusu.

Page 160: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

148

Eleza kuwa kondomu hutoa kinga

madhubuti dhidi ya VVU ikiwa itatumika kwa

usahihi na wakati wote. Ingawa kondomu

zimezuiliwa gerezani, wafungwa wanaweza

kutumia kondomu mara baada ya kutoka

gerezani.

Hatua 2: Uliza

Kwa kunyosha mikono wangapi wamewahi

kutumia kondomu? Nani anaweza kueleza hatua

za namna ya kutumia kondomu ya kiume

kuanzia mwanzo hadi mwisho?

Page 161: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

149

Hatua 3: Hatua jinsi ya kutumia kondomu ya

kiume

Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kiume

Kata pakiti ya kondomu kwa

kufuata alama pembeni mwa

pakiti. Unapofungua pakiti ya

kondomu usitumie kucha wala

meno.

Iweke kondomu kwenye ncha ya

uboo halafu ikunjue kuelekea

chini ya urefu wa uboo kwa

kuisukuma chini kwenye mzingo

wa duara wa kondomu.Valisha

kondomu kwenye uboo ukiwa

bado umesimama. Minya chuchu

ya kondomu katikati ya kidole na

kidole gumba cha mkono mmjoja

(Ukiacha nafasi nchani ili

kukusanya shahawa au manii).

Page 162: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

150

Baada ya kufanya mapenzi na

kukojoa, shikilia mzingo wa

kondomu halafu toa uboo nje

kabla haujalala. Ifunge kondomu

katika kifundo kwenye manii au

shahawa.

Itupe kondomu iliyotumika mahali

salama. Kama vile kondomu ya

kike, kamwe usiidumbukize

chooni kondomu ya kiume.

Inaweza kuziba choo chako na

haiozi. Ifunike kwenye tishi halafu

itupe kwenye pipa la takataka au

kwenye choo cha shimo.

Hatua 4: Orodhesha

Jadili mambo magumu zaidi tunayokabiliana

nayo wakati wa kutumia kondomu. Waombe

washiriki kupendekeza ni namna gani

changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.

Page 163: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

151

Baadhi ya matatizo ya kawaida mara zote ni

pamoja na:

Kujaribu kuiviringisha kondomu kuelekea

chini wakati ikiwa “nje—ndani.”

Kondomu haikunjuki kuelekea kote chini.

Kondomu haijawekwa sawa kwenye kielelezo

Mtumiaji hana utulivu wakati akifungua pakiti

au hutumia meno kuifungua.

Hewa kwenye chuchu haijatolewa

Kamwe usitumie mafuta ya mgando kama

Vaseline®

au mafuta ya taa kama kilainishi

wanapotumia kondomu.

Page 164: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

152

Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kike

Fungua pakiti ya kondomu. Chana

moja ya mapengo mwishoni na

usitumie mkasi wala kisu. Kwani

hutaki kuiharibu kondomu. Shikilia

sehemu ya juu ya kondomu na

wakati huo huo sukumiza sehemu ya

ndani ya duara, huku sehemu ya

wazi ikining’inia.

Utagundua kwamba kuna duara

mbili kwenye kondomu ya kike,

tofauti na kondomu ya kiume. Duara

ya nje, ambayo ipo wazi, huenda nje

ya kondomu. Duara ya ndani

huenda ndani na husaidia kushikilia

kondomu juu wakati wa tendo la

ndoa. Sukumiza sehemu ya ndani,

duara iliyofungwa.Mara baada ya

duara kuonekana ndefu na

nyembamba, sasa ipo tayari

kuingizwa ndani ya uke.

Page 165: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

153

Tafuta sehemu ya faragha na iingize

sehemu ya ndani, sukumiza duara

ndani ya uke wako. Kama ni mara ya

kwanza kuingiza kisodo au kufanya

mapenzi, itakuchukua mda kabla

hujawa mzoefu wa kuisokomeza

hapo. Kiasi kidogo cha kilainishi

kinaweza kusaidia mambo kwenda

shwari. Unaweza kutumia kidole cha

kati kuisukuma ila hakikisha

haijageuzwa. Duara ya nje inapaswa

kubaki nje ya uke. Uko tayari

kwenda! Ukiwa tayari, hakikisha

unamwongoza mpenzi wako

kuingiza uboo kwenye kondomu.

Hakikisha haingizi pembeni au kwa

bahati mbaya kuikosa kabisa kwa

namna yoyote

Safisha. Ukishamaliza, geuza duara ya nje mara

kadhaa ili kuifunga halafu ivute nje taratibu. Kama

ilivyo kwa kondomu ya kiume, kamwe usitupe

kondomu ya kike kwenye choo cha maji. Inaweza

kuziba choo chako na haiozi. Ikunje kwenye tishu na

uitupe kwenye pipa la takataka au choo cha shimo.

Page 166: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

154

Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU:

matibabu, huduma, na msaada

Dakika 40

Kipindi 3.2: Mazoezi

Matibabu ya vvu na maambukizi

nyemelezi

Matibabu ya mgonjwa mwenye

maambukizi ya vvu

Dhamira

Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:

Kueleza kwa kifupi uwepo wa matibabu kwa

matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo,

magonjwa ya ngono, maambukizi ya njia ya

uzazi, na maambukizi nyemelezi.

Page 167: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

155

Zoezi 1: Matibabu ya VVU na maambukizi

nyemelezi

Dakika 40

Hatua 1: Eleza

Waambie washiriki kwamba sasa watajadili

matibabu ya maambukizi tuliyokwisha

kujadili kama VVU, kifua kikuu, magonjwa

mengine ya ngono, na maambukizi ya njia

ya uzazi.

Hatua 2: Maswali na majibu—maambukizi

Swali: Tunajikinga vipi na magonjwa ya ngono?

Chukua mawazo machache

Jibu: Njia bora ya kujikinga na magonjwa ya

ngono ni kuzuia kuupata. Katika hatua hii ya

kwanza ya kujikinga, uwezekano wa kupata

magonjwa ya ngono unaweza kupunguzwa kwa:

Usianze kufanya mapenzi mapema (kwa

vijana wadogo)

Page 168: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

156

Kupunguza idadi ya wapenzi

Kutumia kondomu kwa usahihi na wakati

wote

Utambuzi wa haraka na kupata matibabu

sahihi ya ugonjwa wa ngono

Swali: Maambukizi njia ya uzazi inamaanisha

nini?

Jibu: Maambukizi kwenye njia ya uzazi ni

maambukizi yaliyopo kwenye mkondo wa

sehemu za siri. Huwaathiri wanaume na

wanawake. Baadhi ya katika njia ya uzazi (kama

vile kaswende na gono) huambukizwa kwa njia

ya kujamiiana lakini mengi yao hayaambukizwi

kwa njia hiyo (kama maambukizi ya fangasi). Njia

bora ya kushughulikia ugonjwa wa ngono ni

kutafuta matibabu mara moja.

Hatua 3: Maswai na majibu—matibabu ya

VVU

Swali: VVU hutibiwa vipi?

Page 169: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

157

Unaweza usiwe na mda wa kupitia maswali

yote yafuatayo. Pitia maelezo kwa ufupi

kuhusu dawa za kupunguza makali ya virusi

vya UKIMWI kwenye ukurasa ufuatao.

Jibu: Maambukizi ya VVU hutibiwa kwa kutumia

dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

Swali: Nini maana ya dawa za kupunguza makali

ya virusi vya ukimwi?

Jibu: Ni dawa zinazotumika kutibu mambukizi ya

VVU. Watu wanaotumia dawa za kupunguza

makali hutumia muunganiko wa madawa

(yaitwayo HIV regimen) kila siku. Kuna

muunganiko mbalimbali wa madawa. Dawa za

kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

zinapendekezwa kwa kila mtu mwenye

maambukizi ya VVU. Dawa za kupunguza makali

ya ukimwi haziwezi kuponyesha kabisa VVU, bali

huwasaidia watu kuishi kwa mda mrefu, maisha

yenye afya. Dawa za kupunguza makali ya virusi

vya ukimwi pia hupunguza hatari ya kueneza

Page 170: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

158

VVU kwa mtu mwingine. Nchini Tanzania, kwa

watu wazima na vijana wadogo, hatua ya

mwanzo (ya kwanza) madawa ya regimen ni

miongoni mwa miunganiko ifuatayo ya dawa

tatu: (1) (tenofovir (TDF) + lamivudine (3TC) +

efavirenz (EFV); (2) zidovudine (AZT) +

lamivudine (3TC) + lopinavir/ritonavir (LPV/r); or

(3) abacavir (ABC) + lamivudine (3TC) +

nevirapine (NVP).

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya

UKIMWI kwa kifupi

Dawa za

kupunguza makali

ya virusi vya

UKIMWI ni utumiaji

wa dawa za VVU

kutibu maambukizi

ya VVU.

Inapendekezwa kwa

kila aliyeambukizwa

na VVU, na husaidia

Toleo jipya la

miongozo ya

kimataifa

linapendekeza

kutumia dawa mara

baada ya

kugundulika na VVU

(“Pima na Tibu”) kwa

kuanza matibabu

mapema

Page 171: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

159

watu wenye VVU

kuishi kwa muda

mrefu, maisha

yenye afya.

Watu wenye VVU

wanapaswa kuanza

kutumia dawa

kulingana na

mwongozo wa

kitaifa wa usimamizi

wa VVU/UKIMWI.

Kwa watu wenye

VVU wenye hali

zifuatazo. Ni

muhimu sana

kuanza matumizi ya

mara moja

mwanamke akiwa

na mimba

Magonjwa fulani

yenye uhusiano na

maambukizi ya VVU

kama vile utando

yatapunguza hatari

ya VVU na matatizo

ya kiafya yasiyo na

uhusiano na VVU

miongoni mwa watu

wenye VVU na

UKIMWI Na

itapunguza wingi wa

virusi kwa kiwango

kisichogundulika na

hivyo kupunguza

hatari ya kuenea

kwa VVU.

Ufanisi wa dawa

hutegemea ufuasi

mzuri wa dawa—

kutumia dawa kila

siku kama

ulivyoelekezwa na

mtoa huduma wa

afya. Kabla ya

kuanza kutumia

dawa, ni muhimu

Page 172: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

160

mdomoni, herpes

simplex, mkanda wa

jeshi, dalili kiunoni,

kansa ya mlango wa

kizazi, na kifua

kikuu.

kukabiliana na

maswala yoyote

yatakayoathiri makali

ya dawa.

Swali: Tiba ya virusi vya UKIMWI hufanya kazi

vipi?

Jibu: VVU hushambulia na kuharibu seli za CD4

kwenye mfumo wa kinga ambazo hupambana

na maambukizi. Seli zikiwa chache, ni vigumu

kwa mwili kupambana na maambukizi na aina

fulani za saratani. Dawa huzuia VVU kuongezeka

(kuzaliana wenyewe), kitu ambacho hupunguza

kiwango cha VVU mwilini ingawa haiondoi VVU

vyote mwilini. Uwepo wa VVU wachache mwilini

huupatia mfumo wa kinga nafasi ya kuponyesha

na kuzalisha seli za CD4 zaidi. Hata kama bado

mna kiasi fulani cha VVU mwilini, mfumo wa

kinga una nguvu za kutosha kupambana na

maambukizi na magonjwa yajulikanayo kama

Page 173: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

161

maambukizi nyemelezi kama vile kifua kikuu,

homa ya mapafu, na kansa ya mlango wa kizazi.

Maambukizi nyemelezi ni maambukizi ambayo

hutokea mara kwa mara na huwa makubwa zaidi

kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kinga, kama

vile watu waishio na VVU. Kwa kupunguza

kiwango cha VVU mwilini, dawa za VVU

zinaweza pia kupunguza hatari ya kueneza VVU

kwa mtu mwingine.

Swali: Ni wakati gani muafaka kuanza kutumia

dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi?

Jibu: Watu wenye maambukizi ya VVU

wanaostahili wanapaswa kuanza dawa mapema

iwezekanavyo. Watoa huduma za afya

watashirikiana na wagonjwa ili kuona nani

anastahili kulingana na mwongozo wa kitaifa.

Kwa watu wenye hali zifuatazo, ni muhimu sana

kuanza kutumia dawa mara moja: Ujauzito na

magonjwa fulani yenye uhisiano na maambukizi

Page 174: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

162

ya VVU kama utando mdomoni, mkanda wa

jeshi, au kansa ya malango wa kizazi.

Kulingana na Mwongozo Wa Kitaifa Wa

Kusimamia VVU Na UKIMWI Toleo 5 (Wizara ya

Afya na Maendeleo ya Jamii, Tanzania [MOHSW]

2015), dawa zinapaswa kuanzishwa kwa watu

wote wenye kifua kikuu na maambukizi ya

uhusiano na VVU, bila kujali hatua za kliniki za

WHO au kiwango cha seli za CD4. Matibabu ya

kifua kikuu yanapaswa kuanza kwanza,

yakifuatiwa na matibabu mapema iwezekanavyo,

ndani ya wiki mbili za awali baada ya kuanza

matibabu ya kifua kikuu.Watu wenye VVU wasio

na ishara wala dalili za uwepo wa kifua kikuu

wanastahili kupata dawa za kujikinga za

isoniazid. Jitihada zote zinapaswa kufanyika

kupambana na maambukizi nyemelezi. Msisitizo

unapaswa kuwekwa katika utambuzi wa

mapema, matibabu, na rufaa, pakiwa na ulazima.

Page 175: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

163

Kumbuka: Mwongozo mpya unapendekeza

kuanzisha dawa kwa wagonjwa wote mapema

mara maambukizi ya VVU yanapothibitishwa

kuwepo. (“Pima na Tibu”). Serikali inaweza

kutengeneza miongozo mipya kulingana na

kiwango cha utayari wao (usambazaji wa

madawa, uwezo wa maabara, rasilimali watu,

fedha, nakadhalika).

Swali: Nini faida za kutumia dawa za kupunguza

makali ya ukimwi?

Jibu: Baadhi ya faida za dawa za kupunguza

makali ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:

Watu wenye VVU wanaotumia dawa

wanaweza kuishi kwa mda mrefu

ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.

Watu wanaotumia dawa wana magonjwa

machache yenye uhusiano na VVU

ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.

Kwa kuwa watu wanaotumia dawa kama

ilivyoelekezwa wana afya bora, huenda

Page 176: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

164

hospitali mara chache na huepuka gharama

nyingine za kiafya.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia

dawa wana muda zaidi kukamilisha malengo

na dira za maisha yao.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia

dawa wanaweza kuzitunza familia zao vizuri

zaidi.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia

dawa wanaweza kuishi kama kawaida.

Kwa kuwa watu wanaotumia dawa wana kiasi

kidogo cha VVU ndani ya miili yao, wana

nafasi ndogo ya kueneza VVU kwa watu

wengine.

Hatua 4: Maswali na majibukuishi kwa

kutumia dawa za kupunguza makali

Swali: Sababu kubwa ya dawa kuota usugu na

matibabu kutofanya kazi ni nini?

Jibu: Ufuasi hafifu wa dawa huongeza hatari ya

dawa kuota usugu na matibabu kutofanya kazi.

Page 177: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

165

Kutumia dawa kila siku kama ilivyoelekezwa,

ijulikanavyo kama “ufuasi,” ni muhimu sana kwa

dawa kuweza kufanya kazi. Baadhi ya watu

huacha kutumia dawa kama ilivyoelekezwa kwa

kuwa hupatwa na madhara ya pembeni, au kwa

kuwa wanajisikia kuwa na nguvu na wenye afya

na kudhani hawahitaji dawa tena. Baada ya

muda, japo, bila ya dawa, VVU huongezeka tena

mwilini na watu huanza kuugua. Isitoshe, kuna

uwezekano kwamba dawa hizo hizo za

kupunguza makali zisimsaidie tena huyu mtu

mara atakapotaka kuanza matibabu tena kwa

kuwa VVU mwilini watakuwa wameshatengeneza

usugu kwa dawa hizo. Wanaweza wakaanza

kutumia aina nyingine ya dawa, lakini inaweza

kuwa ni vigumu sana kuzipata na /au kukumbwa

na madhara ya pembeni kuliko ulipokuwa

ukitumia dawa za mwanzo. Uenezaji wa kirusi

kinachopelekea usugu wa dawa za VVU kwa njia

ya mapenzi ni jambo linalowezekana pia. Usugu

Page 178: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

166

ni sababu ya msingi kwa nini matibabu yanaweza

yasifanye kazi.

Swali: Ni kwa muda gani dawa za kupunguza

makali ya virusi vya UKIMWI humwezesha mtu

mwenye maambukizi kuishi?

Jibu: Watu wengi wanaotumia dawa kama

ilivyoelekezwa huishi maisha ya kawaida na

huugua kwa vipindi sawa na watu wasio na

maambukizi ya VVU.

Swali: Changamoto za dawa za kupunguza

makali ya UKIMWI ni zipi?

Jibu: Uwezekano wa hatari za dawa ni pamoja

na madhara ya pembeni (madhara yoyote ya

dawa, kemikali, au dawa nyingine ambazo ni za

nyongeza kwa ajili ya madhara mahususi, hasa

madhara ambayo ni ya kudhuru au yenye

maudhi) yanayosababishwa na dawa za

kupunguza makali au dawa nyingine ambazo

mtu mwenye VVU anazitumia. Asili ya madhara

ya pembeni inategemeana na sehemu ya mwili

Page 179: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

167

ambako dawa imekusudiwa kutibu au namna

ambayo mwili unashughulika na dawa.

Dawa za kupunguza makali ni matibabu ya

muda mrefu—mtu analazimika kutumia

dawa kila siku kama ilivyoelekezwa na mtoa

huduma za afya. Ufuasi hafifu—kutotumia

dawa kila siku na kama ilivyoelekezwa—

huongeza hatari ya dawa kuota usugu na

matibabu kutofanya kazi.

Dawa nyingi za kupunguza makali humezwa

mara moja kwa siku, pamoja na au bila ya

chakula. Baadhi humezwa mara mbili kwa

siku au zinapaswa kumezwa pamoja na

chakula.

Baadhi ya aina za dawa za kupunguza

makali zinaweza kuwa na madhara ikiwa

zitamezwa pamoja na vidonge vingine au

wakati wa mimba. Ni muhimu kuzungumza

na mtoa huduma za afya kuhusu dawa

zingine unazotumia na mfahamishe kama

una mimba.

Page 180: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

168

Dawa za kupunguza makali zinaweza

kusababisha matatizo mengine. Baadhi ya

matatizo yanaweza kutatuliwa baada ya wiki

kadhaa za utumiaji, matatizo mengine

yanahitaji ushauri wa daktari au wataalamu

wa afya.

Ikiwa dawa hazimezwi kila siku kama

ilivyoelekezwa, dawa hazitafanya kazi vizuri

na mtu anaweza kuugua. Watu ambao dawa

hazifanyi kazi kabisa wanalazimika

kubadilisha na kupata aina nyingine ya dawa,

lakini machaguzi yao ya dawa hapo baadaye

yatakuwa yamepungua.

Ikiwa unapata matibabu kutibu matatizo

mengine ya kiafya au kinzamimba (uzazi wa

mpango), ni muhimu kumfahamisha daktari

wako. Baadhi ya dawa za kupunguza makali

(kama, efavirenz, nevirapine) huingiliana na

baadhi ya madawa ya uzazi wa mpango.

Kutumia madawa ya kulevya (kama bangi,

cocaine, ecstasy, na kadhalika) pia kunaweza

Page 181: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

169

kusababisha dawa kuacha kufanya kazi

vizuri.

Swali: Madhara ya pembeni ya kawaida ya dawa

za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ni

yapi?

Jibu: Madhara ya pembeni ya dawa yanaweza

kutofautiana kulingana na dawa na mtu

anayetumia dawa hizo. Watu wanaotumia aina

moja ya dawa wanaweza kuwa na madhara ya

pembeni tofauti kabisa. Madhara ya pembeni ya

kawaida ni pamoja na:

Maumivu ya kichwa, kizunguzungu cha mara

kwa mara, ambayo huenda yasiwe makubwa

sana.

Kuvimba kwa mdomo na ulimi au kuharibiwa

kwa ini, ambayo inaweza kutishia maisha

Ukurutu mwilini kote

Ganzi miguuni

Matatizo ya figo (hasa kwa matumizi ya

tenofovir)

Page 182: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

170

Ndoto za ajabu (hasa kwa matumizi ya

efavirenz)

Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya

VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto

Dakika 30

Kipindi 3.1: Mazoezi

Utangulizi kuhusu kuzuia na kukomesha

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:

Kueleza maana ya maneno kuzuia

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto na kukomesha

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

Page 183: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

171

Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza

mama mwenye VVU na mtoto

Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuzuia

maambukizi kwenda kwa mtoto

Dakika 30

Hatua 1: Anza

Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu kuzuia

na kukomesha maambukizi.

Hatua 2: Eleza

Eleza kuwa kuzuia inamaanisha kuzuia

maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda

kwa mtoto na kukomesha inamaanisha

kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa

mama kwenda kwa mtoto.

Hatua 3: Maswali na majibumaambukizi ya

VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Swali: Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto maana yake ni nini?

Page 184: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

172

Jibu: Maambukizi kutoka kwa mama kwenda

kwa mtoto ya VVU hutoka kwa mama aliye na

VVU kwenda kwa mtoto wake wakati wa ujauzito,

kuzaa, (hujulikana pia kama uchungu wa uzazi

na kujifungua), au wakati wa kunyonyesha (kwa

njia ya maziwa ya mama). Maambukizi ya VVU

kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto vile vile

huitwa maambukizi ya perinatal ya VVU.

Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto ni njia ambayo mara nyingi watoto

wachanga huambukizwa VVU.

Swali: Unadhani maambukizi ya VVU kutoka kwa

mama kwenda kwa mtoto yanaweza kukingwa?

Jibu: Ndiyo

Hatari za maambukizi ya VVU kutoka kwa

mama kwenda kwa mtoto ni ndogo pale

ambapo

Wanawake wenye

VVU wanapopata

dawa wakati wa

Watoto waliozaliwa

na wanawake

wenye VVU

Page 185: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

173

ujauzito na

kujifungua na katika

mazingira fulani,

kuzaa kwa upasuaji

uliopangwa (mara

nyingine hujulikana

kama C-section).

hupokea dawa za

VVU kwa kipindi

cha wiki sita baada

ya kuzaliwa na

kunyonya maziwa

ya mama kwa miezi

sita halafu

anaachishwa

Hatua 4: Eleza

Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeridhia njia

bora kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto

wachanga na watoto wadogo ili kufikia lengo la

kutokomeza maambukizi toka kwa mama

kwenda kwa mtoto. Mbinu ni pamoja na hizi

zifuatazo:

Kinga za awali za maambukizi ya VVU kwa

wanawake wenye umri wa kuzaa na wenza

wao.

Kuzuia mimba zisizotarajiwa kwa wanawake

wenye VVU

Page 186: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

174

Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa

wanawake waathirika kwenda kwa watoto

wachanga

Kutoa matibabu, huduma, na msada kwa

wanawake wenye maambukizi ya VVU,

watoto wao wachanga na familia zao.

Hatua 5: Maswali na majibu—wanaume na

nafasi yao katika kuzuia maambukizi ya vvu

toka kwa mama kwenda kwa mtoto

Swali: kuna faida gani

za kuwashirikisha

wanaume kwenye

kuzuia maambukizi

toka kwa mama

kwenda kwa mtoto?

Jibu: Ushahidi unaonesha kwamba wanaume

wanapounga mkono huduma za afya kwa

wanawake:

Page 187: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

175

Utumiaji wa huduma za kuzuia na kupata

matibabu ya VVU kwa wanawake na watoto

huongezeka.

Matokeo kiafya huboreka.

Kuna ongezeko na ufuasi wa matumizi ya

dawa.

Kuna ongezeko la upimaji na matibabu

miongoni mwa wanaume.

Unyanyapaa hupungua.

Hatua 6: Maswali na majibu—lengo

Swali: Nini lengo la kuzuia maambukizi ya VVU

toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini

Tanzania?

Jibu: Lengo ni kuzuia maambukizi ya VVU

kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa

matibabu kwa wajawazito wote wenye

maambukizi ya VVU na watoto wao wenye VVU

wanaohudhuria afya ya mtoto na uzazi na

huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa

mama kwenda kwa mtoto katika vituo vya afya

Page 188: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

176

gerezani. Hili linaweza kufikiwa kwa kutoa

huduma za upimaji wa VVU kwa wanawake

wajawazito ikifuatiwa na kuwapa mbinu kwa

wanawake wenye VVU kuzuia maambukizi wima

ya VVU kwa watoto wao wachanga.

Hatua 7: Fupisha

Kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa

mama kwenda kwa mtoto nchini Tanzania

kunahitajika:Jitihada endelevu ili kuzuia

maambukizi mapya miongoni mwa

wanawake, na kuboresha upatikanaji wa

huduma za uzazi wa mpango miongoni

mwa wanawake waishio na VVUKuboresha

upatikanaji wa huduma kabla ya kujifungua

na wahudumu wenye ujuzi wakati wa kuzaa

kwa wanawake wote, bila kujali mali, hali, na

makazi.

Uharakisha upanuzi wa huduma za kuzuia

maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda

kwa mtoto zenye ubora wa juu kwenye

Page 189: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

177

huduma zote kabla ya uzazi na vituo vya

kujifungulia na kuimarisha uwepo wa

huduma kwa kuzishirikisha jamii na vituo vya

afya.

Ubora na mwendelezo wa huduma kwa

wakati muafaka kwa mama na mtoto.

Ushirikishwaji wa wanaume kwenye jitihada

za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa

mama kwenda kwa mtoto ni hatua muhimu

ya kuweza kuwapima VVU wanaume.

Page 190: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

178

SOMO 4: KUVUNJA UKIMYA

KUHUSU KIFUA KIKUU NA

VVU

Lengo

Kukuza elimu na ujuzi wa mawasiliano kwa

mfungwa ili aweze kuripoti shutuma zenye

uhusiano na kifua kikuu na VVU miongoni mwa

wafungwa wenzake.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa mafunzo, wafungwa na wafanyakazi

wa magereza wataweza:

Kuelezea na kutambua aina za shutuma

kwenye magereza.

Kuzungumzia shutuma za kimwili au

kimapenzi kwa uwazi zaidi.

Kueleza maana na manufaa ya mawasiliano

kwa wenza.

Page 191: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

179

Kutambua njia za asili na zenye ufanisi za

mawasiliano kwa mwenza miongoni mwa

wakazi wenza na wafanyakazi wa magereza.

Kuelezea njia za kutoa taarifa na kutafuta

huduma miongoni mwa wakazi wenza.

Kutambua changamoto kuu na njia za

kuzitatua.

Kipindi 4.1: Kutambua aina za

shutuma katika magereza

Saa 2, Dakika 5.

Kipindi 4.1: Mazoezi

Aina za shutuma katika magereza

Kuzungumzia shutuma za kimwili na

kimapenzi

Jinsi ya kuvunja mazoea ya ukimya

Page 192: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

180

Zoezi 1: Aina za shutuma katika magereza

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika

Ubao wa chaki au karatasi za kuandikia

ubaoni

Maandalizi ya awali

Ikiwezekana washirikishe baraza la magereza

katika mjadala huu.

Hatua 1: Fafanua

Wafahamishe washiriki kuwa wafungwa

wanaweza kukumbana na uonevu wa kimwili au

kimapenzi na aina nyingine za vurugu na

kuonewa na wafungwa wenzao na wafanyakazi

wa magereza na kushindwa kutoa taarifa ya

uonevu kwa kuhofia ulipizaji kisasi.

Endelea kueleza kwamba wafungwa vile vile

wanaweza kukumbana na mambo ya kutendewa

vibaya, kudhihakiwa, lugha zisizi na adabu, na

Page 193: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

181

uongo wa kupindukia kutoka kwa wafungwa

wenzao. Wafanya kazi wa magereza wanaweza

kutumia kauli za vitisho kama njia ya

kuwaogopesha au kuwavunja moyo wafungwa

wenza ili kuwafanya watii kanuni na taratibu za

magereza

Hatua 2: Jadili

Eleza kwamba majadiliano haya yatatoa

mwanga juu ya haya mambo hivyo

wafungwa pamoja na wafanyakazi wa

magereza wanaweza kutatua mambo haya.

Matukio ya unyanyasaji kwa kiasi kikubwa

husababishwa na sababu za kimazingira na

mahali kama vile umati mkubwa/msongamano,

usimamizi hafifu, nguvu ya madaraka ambayo

inaweza kutengeneza fursa kwa aina mbalimbali

za unyanyasaji. Madhara ya unyanyasaji wa

kimwili na kimapenzi yanaweza kuwa pamoja na

majeraha, ugonjwa, kujiumiza mwenyewe,

Page 194: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

182

msongo wa mawazo, na ugonjwa wa akili.

Sababu hizi zinaweza kutatuliwa na kuzuiwa kwa

kuongeza usimamizi thabiti na kwa wafanyakazi

wa magereza kuzungukia vizimba na program

za elimu rika na uhamasishaji. Usimamizi usio

thabiti kutoka kwa maafisa wa magereza huleta

mianya kwa wafungwa kujiingiza kwenye vurugu

na kuwatendea vibaya wengine. Si rahisi

kufuatilia shutuma za unyanyasaji au uonevu

miongoni mwa wafungwa wenye maelezo

yasiyijitosheleza hasa kuhusu shutuma za

unyanyasaji wa kimapenzi miongoni mwa

wafungwa wenzao. Hali hii imekuzwa na mazoea

ya ukimya na ukosefu wa, au upungufu wa, njia

za ufuatiliaji na uwekaji kumbukumbu za

shutuma hizo katika vizimba vya magereza.

Uwekaji wa kamera na vibonyezo hisishi kwenye

vizimba kunaweza kusaidia kufuatilia unyanyasaji

na tabia za vurugu miongoni mwa wafungwa.

Page 195: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

183

Hatua 3: Chemsha Bongo

Wapange washiriki wawili wawili kwa ajili ya

chemsha bongo halafu waombe wajadili na

kuandika aina gani za unyanyasaji wa—

kimwili, hisia na kimapenzi—ambao hutokea

katika magereza. Wape takiribani dakika 10.

Hatua 4: Maoni

Waombe washiriki kuchangia aina za

unyanyasaji walizoziainisha.

Hatua 5: Mapitio

Eleza maneno kwenye jedwali hapa chini:

NENO MAANA

Ukatili: Shirika la afya duniani (WHO)

linaeleza ukatili kuwa ni “matumizi

ya nguvu za kimwili au madaraka

kwa kukusudia, kutishwa au kwa

uhalisia, dhidi ya mtu mwenyewe,

mtu mwingine, au dhidi ya kikundi

au jumuiya ambayo huenda

Page 196: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

184

NENO MAANA

yakasababisha au yakawa na

uwezekano mkubwa sana wa

kusababisha majeraha, kifo,

madhara ya kisaikolojia, maendeleo

mabaya au unyimaji” (Krug et al.

2002). maneno “Matumizi kwa

kukusudia” ni ya msingi mno

ambayo yanatofautisha vurugu na

madhara na majeraha ya

kutokukusudia.

Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani

pamoja na kusimamia na

kuwashawishi watu wengine na

matendo yao. Madaraka yanaweza

kutumiwa kwa njia chanya na hasi

pia. Unyanyasaji unaweza kutokea

iwapo madaraka yatatumika kwa nia

ya kudhulumu au kupata fadhila

kutoka kwa mtu asiye na nguvu kwa

kubadilishana faida au ahadi.

Ukosefu wa usawa wa madaraka

kati ya watu unaweza kufanywa kwa

Page 197: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

185

NENO MAANA

mabavu au kwa vitisho. Miundo ya

madaraka yaweza kuwa halisi au ya

kutambua. Miundo ya madaraka

yaweza kuwa; kuwa na madaraka,

uwezo wa kufanya maamuzi, au

umiliki wa chakula, pesa, au silaha.

Ridhaa: Maana yake ni kufanya uchaguzi

sahihi wa kufanya jambo fulani kwa

uhuru na kwa hiari. Hakuna ridhaa

pale ambapo makubaliano hufikiwa

kwa njia ya vitisho, nguvu, au njia

nyingine za lazima, utekaji nyara,

ulaghai, udanganyifu, uwakilishi

mbaya. Kutishia au kuzuilia au

kuahidi kutoa fadhila ili kupata

ridhaa ya mtu ni matumizi mabaya

ya madaraka. Matendo yote ya

ukatili na unyanyasaji wa kimapenzi

hutokea bila ya ridhaa stahiki. Hata

kama mtu atasema ndiyo wakati wa

moja ya matendo haya, si ridhaa

ikiwa alisema kwa kushinikizwa—

Page 198: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

186

NENO MAANA

yaani mkosaji alitumia nguvu fulani

au vishawishi ili kumshawishi

mhanga kusema ndiyo.

Ukatili wa

kimwili:

Inamaanisha matumizi ya nguvu

kwa kukusudia yenye nia ya

kusababisha kifo, ulemavu,

majeraha, au madhara mengine.

Matendo ya ukatili ni pamoja na

kukwaruza, kusukuma, kutupa,

kukwida, kung’ata, kukaba, kutikisa,

kupiga kofi, kupiga ngumi,

kuunguza, na matumizi ya silaha,

vizuizi, au ukubwa wa mwili wa mtu

au nguvu dhidi ya mtu mwingine.

Ukatili wa

kimapenzi:

Inamaanisha matumizi ya nguvu

kumlazimisha mtu kushiriki mapenzi

kinyume cha ridhaa yake, jaribio au

kukamilisha kitendo bila ya ruhusa

yake au kuelewa, au mwingiliano wa

ukatili wa kimapenzi. Vitendo vya

ukatili wa kimapenzi ni pamoja na,

Page 199: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

187

NENO MAANA

usumbufu wa kimapenzi, ubakaji,

jaribio la ubakaji, ubakaji kwenye

ndoa, unyonyaji, ukatili wa watoto

kimapenzi/uzinzi wa maharimu,

vitendo vya kimapenzi (bila-

kuingiliana kimapenzi), ukahaba a

kulazimishwa, ukahaba wa watoto,

na biashara za mapenzi.

Unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili

huambatana na tabia

hatarishi.Hatari ya ueneaji wa VVU

huongezeka wakati wa ukatili wa

kimapenzi kwa kuwa nguvu nyingi

hutumika, au kitendo cha

kulazimisha ambacho kinaweza

kusababisha kuchanika kwa ngozi

au ngozi nyembamba na hivyo

majimaji kuweza kupenya.

Page 200: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

188

Hatua 6: Uliza

Waombe washiriki wataje baadhi ya njia za

kuzungumzia ukatili wa kimapenzi kwa

ujumla.

Hatua 7: Tafakari

Jadili na washiriki kwa nini ni vigumu

kuzungumzia ukatili kwenye mazingira ya

magereza na uandike kwenye karatasi ya

kuandikia ubaoni au kwenye ubao wa chaki.

Mazoea ya kukaa kimya yaweza kuwa ni moja ya

sababu zinazopelekea ugumu wa kuzungumzia

ukatili katika magereza.

Page 201: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

189

Zoezi 2: Kuzungumzia ukatili wa kijinsia na

kimwili: Kuvunja mazoea ya ukimya

Dakika 45

Hatua 1: Eleza

Sema kwamba uongozi wa magereza nchini

Tanzania umejipanga kuhakikisha uwepo wa

usalama kwa wafungwa. Ingawa, kama ilivyo

kwenye magereza mengi ulimwenguni (Dennehy

na Nantel, 2006), Magereza ya Tanzania

yanakumbana na changamoto nyingi za uongozi

mbaya, matumizi mabaya ya madaraka, na ukatili

ambazo menejimenti ya magereza inajaribu

kuzishughulikia. Kama ilivyojadiliwa kwenye

shughuli zilizotangulia, eleza kwamba, wafungwa

wanaweza kukumbana na ukatili wa kimapenzi,

kimwili na namna nyinginezo za ukatili ndani ya

magereza kutoka kwenye mikono ya wafungwa

wengine ama wafanyakazi wa magereza wasio

waaminifu.

Page 202: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

190

Kwenye baadhi ya matukio wafungwa na

wafanyakazi wanaamini ya kwamba

kinachoendelea nyuma ya ukuta wa gereza,

hasa, ukatili wa kimapenzi, haupaswi kuwekwa

wazi kwa umma. Mitazamo kama hii hutambulika

kama “Mazoea ya ukimya,” ambayo,

isiposhughulikiwa, inaweza kupelekea

kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa

kimapenzi, kimwili, na ukatili mwingine ndani ya

magereza. Kutoshughulikia mazoea ya ukimya

kunadumisha na kuendeleza tabia za ukatili

ambazo zinaongeza hatari ya kifua kikuu,, VVU,

na magonjwa ya ngono, na hivyo kuwadhuru

wafungwa na maofisa wa magereza (Dannehy

na Nantel, 2006 uk. 177)

Hatua 2: Maswali na majibu—mazoea ya

kukaa kimya

Swali: Mazoea ya kukaa kimya maana yake

nini?”

Page 203: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

191

Wape nafasi washiriki wakupe maoni yao

wenyewe kabla hujawaelezea.

Jibu: ”Mazoea ya ukimya” (Martin 2002) maana

yake ni hali ya wafungwa, wafanyakazi, au

uongozi kutokuwa tayari kuzungumzia kwa

uwazi matukio ya uvunjifu wa sheria, ukiukaji wa

miiko, au yenye utata, kama vile ukatili wa

kimapenzi. Mazoea ya ukimya yamejengwa

katika kanuni zisizozungumzika.

Wafungwa wengi hushabihia mazoea ya ukimya

kwa sababu ya woga wa kulipiza kisasi na

kwamba wengine huenda wasiwalinde mara

baada ya kuvunja ukimya. Wangeweza

kuhatarisha nidhamu kuliko kukiuka mazoea ya

ukimya ndani ya gereza. Lakini ukimya huu si

sahihi kwani unawalinda wakosaji, hasa kwa kuwa

lengo la magereza ni kuhakikisha usalama na

mazingira salama kwa watu kupitia usimamizi

unaofaa na maofisa wanaowasimamia.

Page 204: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

192

Uwepo wa tabia zinazokiuka maadili, matumizi

mabaya ya madaraka, kufunika mambo

kunaweza kupelekea magereza kuwa mahali

hatari kuishi na kufanya kazi kwa kuruhusu

makundi ya watu kutumia kanuni wanavyopenda

wao pasipo kuwajibishwa. Jambo hili hupelekea

hasira, kuvunjika moyo, na mara nyingine huzuni

na ugonjwa wa akili

Hatua 3: Eleza

Ili kushughulikia mazingira yasiyo salama

yaliyosababishwa na ukatili wa kimapenzi na

namna nyingine za ukatili, mazoea ya ukimya

yanapaswa kushughulikiwa kwa kuhakikisha

wafungwa wanaelewa tofauti kati ya kuaminiana,

na kutii adhabu kwa ujumla. Kwa kutambua

kuwa, uaminifu ndani ya kikundi ni muhimu

katika kuimarisha umoja, kukuza usalama, na

kujenga uaminifu, kutii dhamira za magereza za

kuhakikisha usalama, ulinzi, na mazingira wezeshi

ni muhimu zaidi.

Page 205: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

193

Hatua 4: Ufupisho

Fupisha kwa kusema kwamba ni muhimu kwa

wafungwa kuvunja mazoea ya ukimya kwa

kuzungumzia ukatili gerezani, ikiwemo ukatili wa

kimapenzi. Serikali ya Tanzania ina vyombo,

program na miradi kadhaa, ambayo inadhibiti

unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili. Ikiwemo

“toleo maalumu la Sheria ya makosa ya

kimapenzi ya mwaka1998 ambayo inaweka wazi

aina mbalimbali za makosa ya jinai yenye

uhusiano wa ukatili wa kijinsi, ikiwemo ubakaji,

mashambulizi na maudhi kimapenzi, ukahaba,

ukeketaji, na biashara ya mapenzi.

Page 206: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

194

Hatua 5: Funga somo

Wape nakala (ikiwa zipo). Kama hakuna,

soma nakala zifuatazo kwa washiriki:

Toleo maalumu la Sheria ya makosa ya

kimapenzi Tanzania (SOSPA)

Mnamo mwaka 1998 bunge la Tanzania lilipitisha

Toleo Maalumu la Sheria ya Makosa ya

Kimapenzi (SOSPA)(Serikali ya Muungano wa

Tanzania 1998) ili kulinda “heshima na uadilifu

wa wanawake na watoto,” iliyotambulisha

makosa mapya kama vile maudhi kimapenzi,

unyanyasaji kimapenzi, na usafirishaji wa

binadamu.

SOSPA Ni chombo kikuuu cha kitaifa kinachotoa

idhini kupambana na ukatili wa kijinsi na namna

nyingine za unyanyasaji wa kimapenzi. Inatoa

adhabu kali na haki ya kupata fidia kwa wahanga

wa ukatili.

Page 207: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

195

SOSPA imerasimisha ubakaji kuwa ni kosa la jinai

na inatoa adhabu kali kwa mbakaji.

SOSPA imeingizwa kwenye sheria za adhabu za

Tanzania. Sheria za adhabu sura 16, Toleo jipya,

imeweka wazi yafuatayo:

Kifungu 130, sura 16, kinaeleza kuwa, ni kosa

kwa mwanaume kumbaka msichana au

mwanamke. Mwanaume atakuwa ametenda

kosa la ubakaji ikiwa atashirikiana mapenzi

na msichana au mwanamke ambaye si mke

wake, au kuwa mkewe ambaye ameachana

naye; au bila ya ridhaa yake kufanya jambo

hili wakati wa kufanya mapenzi; au kwa

ridhaa yake, pale ambapo ridhaa

imepatikana kwa mabavu, vitisho, au

kumweka katika hofu ya kifo au majeraha

Mtu yeyote anayejaribu kubaka anatenda

kosa la kujaribu kubaka na, isipokuwa kwa

mambo yaliyoainishwa kwenye kifungu

kidogo cha 3, anastahili kifungo cha maisha

Page 208: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

196

gerezani ikiwa kosa lake litathibitishwa, na

kwa namna yoyote ile anastahili kifungo jela

kwa si chini ya miaka 30 pamoja na au bila

ya adhabu ya viboko.

Mtu yeyote ambaye, anakusudia

kusababisha maudhi kimapenzi kwa mtu

yeyote kwa kutamka neno lolote au sauti,

kufanya ishara ya mwili, au kuonesha neno

lolote au kitu kwa nia kwamba neno hilo au

sauti isikike, au ishara ya mwili au kitendo

ionekane na mtu mwingine, mtu huyu

anatenda kosa la shambulizi kimapenzi.

Ikithibitika, anastahili adhabu ya kifungo

gerezani kwa kipindi kisichozidi miaka

mitano, faini isiyozidi shilingi 300, 000, au

vyote viwili faini na kifungo.

Mtu yeyote ambaye, kwa kujifurahisha

kimapenzi, anafanya kitendo chochote, kwa

kutumia sehemu zake za siri au kutumia

vibaya sehemu nyingine yeyote ya mwili wa

Page 209: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

197

binadamu au kitu chochote katika tundu

lolote au sehemu ya mwili ya mtu mwingine

yeyote, iwe kitendo ambacho hakijumuishi

ubakaji chini ya kifungu 130, ametenda kosa

kubwa la unyanyasaji wa kimapenzi.

Zoezi 3: Mazoezi ya jinsi ya kuvunja

ukimya

Dakika 60

Vifaa vinavyohitajika

Ubao wa chaki au karatasi ya kuandikia

ubaoni

Maandalizi ya awali

Soma na elewa kipengele hiki.

Page 210: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

198

Hatua 1: Jadili

Fungua kwa kusema kwamba kwa namna

nyingi gereza ni kama mji mdogo.

Katika mji huu wafungwa ndio raia. Na kama

ilivyo katika mji wako na mji wangu, raia wa

gerezani wanapaswa kuwekwa mahali salama na

pa uhakika. Hili hufanyika kwa kuwapa makazi

ambayo yanakidhi viwango vya afya ya jamii,

huduma za afya kitabibu na kiakili ambazo

zinakidhi viwango vya kitaifa, vyakula ambavyo

vina mahitaji ya msingi ya lishe, na misaada

mingine ili kusaidia urejeaji wenye mafanikio

kwenye jamii zao.

Ingawa, kama ilivyo kwa miji midogo, magereza

hayawezi kwa ufanisi huku kukiwa na mazoea ya

ukimya. Tunahitaji kuvunja mazoea ya ukimya

kwa sababu inadidimiza lengo la uwepo wa

magereza: “Kutoa huduma rekebishi kwa

kutengeneza maisha ya kirafiki na thabiti na

Page 211: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

199

mazingira ya kazi kwa ajili ya wafungwa na

wafanyakazi wasimamizi wa magereza.” (Smith

na Yarussi 2007)

Hatua 2: Eleza

Ukali wa aina yoyote ile, hasa ukatili wa kijinsia, ni

aina kubwa zaidi ya ukiukwaji wa haki za

binadamu katika mazingira rekebishi. Ukatili wa

kijinsia miongoni mwa wafungwa na au kati ya

wafanya kazi wa magereza pia ni jambo la

kiusalama na ulinzi kwa:

Kuhatarisha usalama, ulinzi na afya za

wafungwa na wafanya kazi

Kuongeza hatari ya kupata na kueneza VVU,

magonjwa ya ngono, na maambukizi

yanayohusiana.

Kupunguza uaminifu na motisha miongoni

mwa wafungwa na wafanyakazi gerezani.

Kupunguza heshima miongoni na baina ya

wafungwa na wafanya kazi.

Page 212: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

200

Kutishia usalama na ulinzi wa vituo vya

magereza.

Kudhuru mahusiano ya kifamilia

Kujenga mtazamo hasi kwa umma juu ya

magereza.

Kudumisha tabia za ukatili ndani na nje ya

magereza.

Hatua 3: Maswali na majibu—wakati

tunpovunja mazoea ya ukimya

Swali: Ni wakati gani tungeweza kusema

mazoea ya ukimya yamevunjwa?

Chukua maoni machache

Jibu: ”Wafungwa huhakikishiwa usiri mara baada

ya kuripoti matukio ya ukatili wa kimapenzi

kuwaepusha na maudhi au kisasi kutoka kwa

wakosaji. Pasipo na kamera zinazotazama,

walalamikaji wanapaswa kuruhusiwa kuonesha

ushahidi wa kimwili kuhusu kesi za unyanyasaji

wa kimwili na kimapenzi. Tekinolojia inaweza

Page 213: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

201

kusaidia kuvunja mazoea ya ukimya kwa kuwa

wafungwa na wafanyakazi wanajua kuwa kamera

zinatazama matendo na tabia zao.

Hatua 4: Maelezo

Mfumo wa mawasiliano unaathiri sana namna

ambavyo wafungwa wanavunja mazoea ya

ukimya. Kwa mfano wafungwa wa kiume na kike

wanaweza kutofautiana tabia zao na mfumo wa

mawasiliano, hata kama hawajawahi kukumbana

na ukatili katika mazingira ya magereza. Ingawa,

ni mhimu kwa wafungwa kujua kwamba

endapowamewahi kunyanyaswa kimapenzi,

kushambuliwa, au kuudhiwa na wafungwa

wenzao au wafanya kazi, wana haki ya kuripoti

kosa kwa usalama, kwa siri, na bila ya kutaja jina.

Mfungwa anaweza kutoa taarifa zote au kuminya

kiwango cha taarifa anazozitoa kadri anavyoona

yafaa. Ingawa, kadri taarifa nyingi zinapotolewa,

ndivyo itavyopelekea mfanyakazi wa magereza

Page 214: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU

Magerezani

202

kuchukua hatua dhidi ya mkosaji na kumweka

mhanga na wafungwa wengine salama.

Hatua 5: Shauri

Mfungwa yeyote akikumbana na

unyanyasaji wa kimapenzi, uonevu au

kupigwa bila sababu halali anatakiwa atoe

taarifa kwa uongozi wa gereza mara moja.

Page 215: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

203

SOMO 5: KUISHI KWA

MATUMAINI UKIWA NA VVU

NA KIFUA KIKUU

Lengo

Kuwajenga washiriki kiakili, kwa hisia, kiroho, na

kimwili jinsi ya kukubaliana na kuishi na kifua

kikuu na VVU.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa somo hili washiriki wataweza:

Kusema umuhimu wa ufuasi mzuri na kuishi

maisha yenye afya.

Kueleza madhara ya kifua kikuu na VVU,

kimwili, kisaikolojia, kijamii, kitabia, na

kiuchumi miongoni mwa wafungwa na

familia zao.

Kubainisha njia za kupunguza unyanyapaa,

na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU.

Page 216: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

204

Kueleza jinsi ya kuwasaidia watu waishio na

VVU na magonjwa nyemelezi.

Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya

kuwa na VVU

Dakika 60

Kipindi 5.1: Mazoezi

Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini

ukiwa na VVU na TB.

Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi

dhidi ya watu waishio na VVU

Page 217: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

205

Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuishi kwa

matumaini ukiwa na VVU na TB

Dakika 30

Vifaa vinavyohitajika

Jadili maswali yaliyopo kwenye karatasi ya

ubaoni au ubao wa chaki

Vipeperushi vinavyoelezea kuishi kwa

matumaini ukiwa na VVU gerezani

(ikiwezekana)

Maandalizi ya awali

Andika maswali ya kujadili (tazama hatua ya

3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao

wa chaki

Hatua 1: Eleza

Kutambua ya kuwa una maambukizi ya VVU

kutabadili maisha yako ghafla. Unaweza

kukumbana na wigo mpana wa hisia—wasiwasi,

Page 218: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

206

kupoteza, majonzi, huzuni, kukanwa, hasira,

mashaka. Haijalishi ni kwa kiasi gani daktari na

marafiki wanakuhakikishia, namna ambavyo

vidonge vina ufanisi mkubwa sasa na

zitakavyokuwa hapo baadaye, udogo wa

madhara kimwili yatokanayo na kiwango kidogo

cha maambukizi yaliyopo mwilini mwako kwa

sasa, au ni jinsi gani unapaswa kujiandaa kiakili

na kimawazo, uhitaji wako wa msaada itakuwa

jambo bora. Maswala kisaikolijia yanayowakumba

watu wengi wenye VVU hutofautiana. Matumaini

na matarajio ya maisha yako ya baadaye,

mahusiano yako, na mwenendo wa maisha yako

yote yatahitaji mabadiliko fulani ili kukufanya

uweze kukabiliana na hali ya kuwa na VVU na

kuishi maisha mazuri yenye afya.

Majadiliano haya yanalenga kujadili na kuibua

mbinu na njia za namna ambavyo mtu anaweza

kukabiliana na hali ya kuthibitika kuwa na

maambukizi ya Kifua Kikuuau VVU gerezani

Page 219: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

207

mahali ambapo rasilimali zinaweza kuwa chache

na kuna hatari ya ukatili, unyanyapaa na ubaguzi.

Hatua 2: Jadili

Yapatie makundi ya watu wanne wanne maswali

yafuatayo kwa ajili ya majadiliano:

Nini maana ya kuishi kwa matumaini ukiwa

na Kifua Kikuu na VVU gerezani?

Mfungwa au mfanyakazi wa magereza

anaweza kufanya nini ili kuishi kwa

matumaini akiwa na maambukizi?

Ni jinsi gani mafanyakazi wa magereza au

mfungwa anaweza kumjali mtu aishie na

VVU gerezani?

Wafanye au wasifanye nini ili kuonesha

kujali?

Hatua 3: Maelezo

Eleza kwa kifupi majibu kwa maswali haya

pamoja na washiriki.

Page 220: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

208

Gawa vipeperushi vifuatavyo (ikiwa vipo).

Kama havipo, soma baadhi ya njia muhimu

kuonesha kuwajali watu wenye VVU

magerezani.

Wafungwa waishio na VVU wanapaswa wajitahidi

kuiweka miili yao kuwa na nguvu, kwa kuhusisha

yafuatayo:

Kula mlo uliokamilika au kuongeza kiwango,

kila inapowezekana, ikiwemo vyakula vyenye

virutubisho ambavyo vina protini, vitamini,

na wanga. Ukosefu wa virutubisho

utachangia sana kuharibiwa kwa mfumo wa

kinga wa mwili. Mlo kamili huupatia mwili

nguvu za kuweza kupambana na magonjwa.

Vyakula vya asili vinafaa zaini kuliko vile vya

kwenye makopo na vyakula vilivyosindikwa.

Mboga mboga zina madini na vitamin

mahususi kwa ajili ya mwili kustawi .Chakula

kinapaswa kusafishwa na kupikwa vizuri

Page 221: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

209

kabla ya kuliwa ili kuulinda mwili kutokana na

magonjwa yatokanayo na vyakula.

Kuwa mkakamavu kwa kufanya mazoezi na

kupata muda wa kutosha kulala. Mazoezi ya

viungo yatapunguza msongo na uvunjikaji

moyo na kuchangia kupata afya njema na

uvumilivu.

Kujiunga au kuunda vikundi saidizi na

wafungwa wenzio ambao wana VVU

Kuzungumza na wafungwa wengine kuhusu

upimaji wa ugonjwa.

Kutafuta ushauri wa kidakitari pale mtu

anapojisikia kuumwa, au kuwa na msongo,

na kufuata ushauri, ikiwemo kutafuta ushauri

wa kidaktari, nasaha, na kijamii.

Ukiwa kwenye matumizi ya vidonge fuata

maelekezo ya dawa uliyoandikiwa. Kuwa na

rafiki wa matibabu ambaye utakumbushana

naye muda wa kunywa vidonge.

Page 222: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

210

Usivute sigara na usitumie dawa bila ya

maelekezo ya daktari.

Kuzungumza na mtu unayemwamini kuhusu

hisia zako.

Kumwambia mtu fulani unayemwamini

kwamba una VVU.

Njia za kuwahudumia watu waishio na VVU

gerezani

Usijitenge na wafungwa wenzio au

wafanyakazi wa magereza. Jenga urafiki. Ishi

kama ambavyo mmekuwa mkiishi kabla.

Usibadilike kwa sababu tu unajua mtu fulani

ana maambukizi ya VVU.

Tambua hisia zao. Usiwafanye wafadhaike

kutokana na hisia zao. Ni sawa kulia

wanapolia na kucheka wanapocheka. Ni

jambo zuri kiafya kutoa hisia kuliko kuziweka

moyoni. Kuweka hisia mbaya moyoni

husababisha msongo na msongo

Page 223: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

211

husababisha madhara kwenye mfumo wa

kinga.

Ikiwezekana waalike kwenye matembezi

unapopata nafasi ya kufanya mazoezi. Kuwa

mwangalifu na nguvu za miili yao.

Usiwaruhusu kufanya vitu ambavyo hawana

nguvu za kutosha kuvifanya.

Wasaidie kuweka mambo yao sawa. Watu

wengi waishio na VVU hawapendi kufanya

vitu vigumu kama kuandika wosia au

kuziambia familia zao kuhusu ugonjwa wao.

Washirikishe kwenye sikukuu za kidini au za

asili au sherehe ikiwa inawezekana.

Jitolee kuwahudumia watu wenye VVU ili

daktari wa magereza aweze kupumzika.

Ikiwa ni mfanya kazi wa magereza, wasaidie

baadhi ya majukumu ili kurahisisha maisha.

Ni sawa kuzungumzia ugonjwa wao, lakini

kuwa mwepesi wa kuhisi. Wafungwa

wenzako au wafanyakazi wa magereza

Page 224: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

212

wanaweza kuchagua siku ya kuzungumza.

Itategemea na namna ambavyo anajisikia

siku hiyo.

Kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote, watu

wenye VVU wana siku nzuri na mbaya. Katika

siku nzuri watendee kama ilivyo kawaida.

Katika siku mbaya watendee kwa kuwajali

zaidi na huruma.

Kujali kunaweza kuoneshwa pasipo maneno.

Huhitaji kuzungumza muda wote.

Wahimize kufanya maamuzi kwa muda

mrefu iwezekanavyo kwa ajili yao. Mtu

anapoumwa, maamuzi mengi hutolewa

kwao, hivyo basi waruhusu wafanye

maamuzi mengi iwezekanavyo.

Zingatia ahadi zako ikiwa utawaahidi watu

waishio na VVU. Usiwaambie utawaona

kesho huku ukijua kuwa kesho hutaweza

kuonana nao.

Page 225: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

213

Kuwa tayari kuona watu waishio na VVU

wakikasirika pasipo na sababu.

Hawajakukasirikia wewe. Wamekasirishwa na

kile kinachoendelea kwao na kutokuwa na

uwezo wa kukishughulikia.

Usiwafanyie kile ambacho bado wana uwezo

wa kukifanya.

Jaribu kuwa na mtazamo chanya.

Kwa kujenga urafiki unaleta mwanga kwenye

mazingira yenye giza nene.

Zoezi 2: Punguza unyanyapaa na ubaguzi

dhidi ya watu waishio na VVU

Dakika 30

Vifaa vinavyohitajika

Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Maandalizi ya awali:

Andika maswali(tazama hatua 3 chini)

kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.

Page 226: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

214

Hatua 1: Eleza

Uliza washiriki nini maana ya unyanyapaa na

ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU.

Chukua maoni machache.

Hatua 2: Eleza

Unyanyapaa Ubaguzi

Unyanyapaa maana yake

ni tabia isiyopendeza au

isiyoya heshima ambayo

mtu au kikundi kinakuwa

nayo ambayo hupelekea

kushuka kwa hadhi ya

mtu au kikundi hicho

katika macho ya jamii.

Unyanyapaa unaweza

kuletwa na mwonekano

mwilini, kama vile, dalili

za ugonjwa

zinazoonekana, au

mtazamo hasi kwa kundi

Ubaguzi unaweza

kuelezewa kwa

kujumuisha mtazamo

hasi au tabia fulani au

vitendo. Mara nyingi

huelezewa kama ni

utofauti unaojengwa

kuhusiana na mtu

unaopelekea

kutendewa bila haki na

bila kuthibitisha kwa

misingi ya uhusika wao,

au kuchukuliwa kama

wanahusika katika kundi

Page 227: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

215

fulani la watu au mtu fulani. Kwa mfano

unyanyapaa unaweza

kusababisha madhara

na ubaguzi

unaoelekezwa kwa

watu ambao kweli, au

wanahisiwa tu kuwa na

VVU, na vikundi vya

kijamii na watu

wanaoishi nao

Hatua 3: Zoezi

Wagawe washiriki kwenye makundi matano

na wape kila kundi hadithi moja. Waeleze

washiriki kuwa watajadili maswali yafuatayo:

Kwa maoni yako, unadhani kwa nini katika

hadithi hii watu wameonesha tabia hizo?

Unadhani nini kifanyike ili kupunguza

unyanyapaa na ubaguzi?

Unadhani ni nani anaweza kuwasaidia watu

wanaonyanyapaliwa au kubaguliwa?

Page 228: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

216

Hadithi 1

Siku moja afisa Mapendo

aliporudi nyumbani

kutoka kwenye

majukumu alikuta mke

wake akilia. Baada ya

kumwuliza kwa nini

analia, mkewe alisema ametoka kliniki ya uzazi

na ameambiwa kuwa ana VVU. Baada ya kusikia

haya, afisa Mapendo alighadhabika sana na

kuanza kumfokea mke wake, akisema kuwa

amepata maambukizi ya VVU kutoka kwa

mwanaume mwingine nje ya ndoa, na hivyo

hastahili kuendelea kuishi nae. Kwa hiyo,

alimtolea vitu vyake ndani ya nyumba na

kumfukuza nyumbani.

Page 229: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

217

Hadithi 2

Jane ni muuguzi

katika gereza

mkoani mwanza.

Amefanya kazi pale

kwa zaidi ya miaka

10. Anafanya kazi

kwa bidii anapotoa huduma kwa wagonjwa

wake. Mara zote anapogundua kuwa mgonjwa

ana maambukizi ya VVU, huhakikisha kuwa

anapomhudumia anavaa glavu na barakoa ili

kuikinga pua yake, hata kama mgonjwa hana

vidonda ambavyo vinaweza kusababisha

maambukizi.Mara nyingi mgonjwa anapogundua

jambo hili huchukizwa.

Page 230: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

218

Hadithi 3

Mariam ni mke wa

mfungwa

aliyefunguliwa

gerezani hivi

karibuni. Ana shiriki

katika vikundi vya ushirika wa kukopa na kuweka

katika mji wake. Anashirikiana vizuri na wenzake

kwenye shughuli zao za kila siku. Miezi miwili

iliyopita yeye na mmewe walikwenda kliniki

kupima VVU, na wote waligundulika kuwa na

maambukizi ya VVU. Tokea wakati huo

wanachama wenzake kwenye kikundi

wamemtenga na hawashirikiani naye tena

kwenye shughuli zao za kikundi kwa kuhofia

kuwa nao wangeweza kuambukizwa VVU. Hali hii

inamsikitisha Mariam na inatishia hali ya uchumi

wa familia yake.

Page 231: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

219

Hadithi 4

Salum ni mfungwa anayetumikia kifungo cha

miaka mitano gerezani. Anaishi na VVU na

amekuwa akitumia vidonge vya ARV kwa miaka

miwili. Kwa kipindi chote hicho amejitahidi

kuficha vidonge vyake ndani ya vitu vyake, lakini

siku moja mfungwa mwenzake alivikuta na

alianza kumzungumzia na kufikia hatua ya

kumtenga wakati wa chakula. Baada ya muda

Salum aligundua kuwa wenzake walikuwa

wakijiweka kando na yeye, hivyo aliamua kueleza

hali halisi lakini waliendelea kumcheka na

kumtenga.

Hadithi 5

Shida alifunguliwa kutoka gerezani. Alikuwa na

furaha kubwa kurudi nyumbani kuungana tena

na familia, mke, na watoto wake. Alipokuwa

gerezani Shida alipima VVU na aligundulika kuwa

navyo. Aliudhika sana kuhusu namna ambavyo

atakwenda kumweleza mke wake kwa kuwa

Page 232: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

220

hakutaka kuharibu siku yake ya furaha, hivyo

aliendelea kuficha na usiku huo alifanya mapenzi

na mkewe bila ya kutumia kondomu.

Hatua 4: Eleza kwa kifupi

Toa fursa kwa kila kundi kujadili hadithi yao

kwa kina.

Hatua 5: Jadili

Swali: Tunawezaje kupunguza unyanyapaa na

ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU?

Jibu: Kuendeleza mbinu/njia zinazoshughulikia

sababu kuu za unyanyapaa na makundi

maalumu ya waathirika, ikiwemo wafungwa.

Zifuatazo ni baadhi ya njia tunazoweza kujaribu

na kupunguza unyanyapaa katika ngazi ya kisera

na kijumuiya.

Kuzishirikisha jamii kuthibitisha kutoa msaada

kwa watu waishio na VVU (kwa mfano.

Page 233: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

221

biashara katika jamii, mashirika ya kijamii,

mashule, na viongozi wa jumuiya).

Kukuza uongozi katika jamii kwa watu

waishio na VVU.

Kukuza mbinu za kiafya kwa jamii kuhusu

kinga na huduma ya Kifua Kikuu na VVU.

Kuendelea kutoa elimu kuhusu mambo

yenye kuhusiana na Kifua Kikuu na VVU.

Page 234: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

222

ORODHA YA MANENO

CD4: Aina ya chembechembe –T ambazo

huukinga mwili dhidi ya maambukizi na kuutunza

mfumo wa kinga. VVU hushambulia

chembechembe za CD4 moja kwa moja, na

kuhatarisha mfumo wa kinga.

Daraja: Kikundi cha watu waliowekwa pamoja

kulingana na viwango vyao vya mali na/au kazi

wanazofanya katika uchumi.

Dhuluma: Kujenga maoni thabiti mara nyingi

maoni hasi kuhusu kitu fulani au mtu fulani

(kitengo cha kikundi cha watu) bila ya kuwa na

elimu ya kutosha au uchunguzi wa mambo kwa

kina.

Haki za binadamu: Haki za binadamu ni za watu

wote na hazitofautishwi. Kanuni ya kiulimwengu

ya haki za binadamu ndio msingi wa sheria za

kimataifa za haki za binadamu zilizotiliwa mkazo

katika azimio la kimataifa la haki za binadamu la

mwaka 1948, na zimeelezewa katika mikutano,

Page 235: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

223

maazimio na maamuzi mbalimbali ya haki za

binadamu za kimataifa. Haki za binadamu

zinarithiwa kwa wanadamu wote, bila kujali

utaifa, makazi, jinsia, taifa au asili ya kabila, dini,

lugha, au hali nyingine.

Imani: Maoni thabiti na mara nyingi hutokana na

misingi ya kidini na au kanuni za kiutamaduni.

Jinsia: Kazi, haki, majukumu, fursa, mipaka,

matarajio, stahili, na majukumu yanayotambuliwa

kijamii. Jinsi hutofautiana miongoni na ndani ya

tamaduni na inaweza kubadilika baada ya muda

fulani. Majukumu ya jinsia huzingatia, jinsia, umri,

kabila, dini, na sababu zingine za kiutamaduni.

Jinsi: Sifa za kibaiolojia na kimaumbile za

mwanaume na mwanamke ambazo hazibadiliki

bila ya kufanya upasuaji. Mfano wa viashiria vya

jinsi: viungo: uume, uke, matiti, korodani;

maumbile: mzunguko wa hedhi, utengenezwaji

wa shahawa; muundo wa kijenetiki: kromosomu

XX na XY.

Page 236: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

224

Kujamiiana: Tabia zote za maisha ya watu

kimapenzi, ikiwemo fikra, na hisia, shauku, tabia,

na sura.

Maambukizi yanayoenezwa kwa ngono: Kundi la

maambukizi ambalo mara nyingi huenezwa kwa

njia ya mwingiliano wa mapenzi yasiyo salama na

mtu mwenye maambukizi.

Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani

pamoja na kusimamia na kuwashawishi watu

wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza

kutumiwa kwa njia chanya na hasi pia.

Makundi maalumu: Watu wanaotumia madawa,

malaya, wasenge, watu wa jinsia mbili, madereva

wa masafa marefu, wachimbaji madini,

wafungwa, na watoto wa mitaani ni makundi

maalumu. Makundi maalumu yana uwezo

mdogo sana wa kupata huduma zinazostahili,

pia yana kiwango kikubwa cha hatari ya kupata

na kueneza VVU, na viwango vikubwa vya

kukumbwa na mauti na /au ugonjwa kwenye

Page 237: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

225

maeneo yenye magonjwa ya

mlipuko/kuambukiza ukilinganisha na makundi

mengine katika jamii.

Mapenzi kinyume na maumbile: Mapenzi katika

njia ya haja kubwa, bila kujali jinsi za washiriki.

Neno hili hutumiwa vibaya kwa kuchanganywa

na ubakaji, ambayo hushindwa kutofautisha

mapenzi ya lazima bila ya ridhaa. Mapenzi

kinyume na maumbile ni jinai pale tu inapokuwa

imelazimishwa.

Mapenzi salama: Hujulikana pia kama “mapenzi

yenye kinga,” humaanisha kupunguza hatari za

maabmbukizi au mimba, mara nyingi kwa

kufanya mapenzi kwa kutumia kondomu ya kike

au kiume au kwa kutafuta njia mbadala za

ushirikiano wa mapenzi.

Mateso: Adhabu kali za kimwili au mateso kiakili

yaliyofanywa chini ya mamlaka ya sheria.

Haijumuishi maumivu au mateso yanayotokana

na, asili, au matukio ya vizuizi kisheria.Ubakaji wa

Page 238: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

226

wafungwa umetambuliwa kama mfumo wa

mateso na kitengo maalumu cha umoja wa

mataifa kinachoshughulikia mateso. Hii ni kesi

bila kujali kitendo kimefanywa na mfungwa au

mfanyakazi wa magereza. Matendo mepesi ya

unyanyasaji wa kijinsi yanaweza kujumuisha,

ukatili, unyama, au kuwatendea vibaya. Kamati ya

umoja wa mataifa inayoshughulikia mateso

wakati wote imekuwa ikipambana na ukatili wa

kijinsi dhidi ya wafungwa na imetoa wito kwa

serikali kuchukua hatua thabiti kushughulikia

jambo hili.

Mila: Mfumo au mpangilio wa tabia

unaokubalika na kuchukuliwa kuwa ni “jambo la

kawaida” katika jamii au ndani ya kikundi kwenye

jamii.

Mitazamo: Maoni, mawazo na hisia za mtu

kuhusu kitu au jambo fulani.

Sera: Mpango, au mfumo wa utendaji wa serikali,

chama cha siasa, au biashara uliokusudiwa

Page 239: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

227

kushawishi na kufikia maamuzi, matendo, na

mambo mengine, kama vile sera za serikali

kwenye elimu, afya (ikiwemo VVU), au usawa wa

jinsi, sera ya kampuni kuhusu ajira na mafunzo

au rasilimali watu/wafanyakazi.

Ridhaa: Mmakubaliano ya hiari bila ya matumizi

ya nguvu. Hakuna ridha pale ambapo mkosaji

anatumia vibaya nafasi ya madaraka kumfanya

mhanga “kukubali” kitendo cha mapenzi. Hakuna

ridhaa huru ikiwa kulihusisha, ulaghai,

udanganyifu na ujanja. Sera zina malengo ya

jumla na malengo maalumu na taratibu

zinazoweka mfumo au njia za utendaji

zilizochaguliwa miongoni mwa njia nyingine kwa

kuzingatia mazingira fulani ili kutoa mwongozo

na kutambua maamuzi ya sasa na ya baadaye.

Sheria: Mifumo ya usimamizi, na mbinu za

kurekebisha maovu zinaweza kutungwa na

chombo chenye mamlaka; sheria hujenga

muundo wa siasa, uchumi na historia ya nchi kwa

ujumla kwa kufanya kazi kama msuluhishi wa

Page 240: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

228

mahusiano kati ya watu. Zinatungwa na

husimamiwa na katiba za nchi na zina mfumo au

seti ya kanuni zilizotungwa na serikali za miji,

taifa, au nchi ambazo husimamiwa na taasisi za

kijamii kuongoza mienendo. Sheria zilizotungwa

na serikali hutumika kutoa mwongozo wa namna

ambavyo jamii zinapaswa kuwa, kama vile, sheria

zinazokataza kuendesha huku ukiwa umelewa,

wizi, kuua, kutumia madawa, au kumiliki bunduki.

Ubaguzi: Huelezewa kuwa huenda ikajumuisha

yote mawili mtazamo hasi au tabia fulani au

kitendo. Mara nyingi huelezewa kama tofauti

inayotengenezwa kuhusu mtu inayosabaisha mtu

huyu kutendewa isivyofaa pasipo na haki kwa

misingi ya uhusika wake ama kuhisiwa kuhusika

katika kundi fulani. Kwa mfano, unyanyapaa

unaweza kusababisha madhara na ubaguzi moja

kwa moja kwa mtu ambaye kweli, au anahisiwa

tu kuwa na maambukizi ya VVU, na makundi

katika jamii na watu wanaoshirikiana nao katika

jamii.

Page 241: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

229

Ubakaji: Kitendo chochote cha upenyezaji bila ya

ridhaa kwenye uke, njia ya haja kubwa, au

mdomoni. Neno hili halibagui jinsi, wote

mwanamke na mwanaume wanaweza kubakwa.

Uenevu: Kwa kawaida hutolewa kama asilimia,

kama vile, uenevu wa VVU ni jamii yenye

maambukizi ya VVU katika kipindi fulani.

Ukatili: Shirika la afya duniani linaelezea ukatili

kama ni “matumizi ya nguvu au madaraka kwa

makusudi, kutishia au kufanya kweli, dhidi ya mtu

mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi ya kikundi

au jamii ambapo kunaweza kupelekea

uwezekano mkubwa wa majeraha, kifo, madhara

kisaikolojia, maendeleo mabaya, au unyimaji.”

Neno” matumizi ya kukusudia” ni kiungo

muhimu ambacho kinatofautisha ukatili na

majeraha au madhara ambayo hayakukusudiwa.

Ukatili kimwili: Matumizi ya nguvu kwa kukusudia

wenye nia ya kusababisha kifo, ulemavu,

mejeraha, au madhara mengine. Vitendo vya

Page 242: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

230

ukatili wa kimwili ni pamoja na kukwaruza,

kusukuma, kutupa, kukwida, kupiga, kukaba,

kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuchoma, na

matumizi ya silaha, vizuizi, au kutumia ukubwa

wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya mwingine.

Ukatili wa kijinsia: Kudhuru kimwili, kimapenzi, au

kisaikolojia kwa mwanaume au mwanamke

inayomlenga mtu kwa misingi ya jinsi yake.

Ukosefu wa usawa wa kimamlaka kati ya

wanaume na wanawake unachangia kwa kiasi

kikubwa ukatili wa kijinsia.Ukatili wa kijinsia

unalenga kudumisha ukosefu wa usawa wa

kijinsia na/au kusisitiza wajibu wa kimila wa jinsia

kwa wanaume na wanawake.

Ukatili wa kimapenzi: Matumizi ya nguvu

kumlazimisha mtu kushiriki tendo la kujamiiana

kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha

kitendo bila ya ridhaa au uelewa wake, au

mwingiliano mbaya wa kimapenzi. Vitendo vya

ukatili wa kimapenzi ni pamoja na usumbufu

kimapenzi, ubakaji, jaribio la ubakaji, ubakaji

Page 243: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

231

ndani ya ndoa, unyonyaji, unyanyasaji wa watoto

kimapenzi/ngono, vitendo vya mapenzi (bila

upenyezaji) umalaya wa kulazimishwa, umalaya

kwa watoto, na biashara ya mapenzi.

Unyanyapaa: Mtazamo wa kijamii kuwa mtu au

kikundi hakifai au ni cha hali ya chini.

Unyanyapaa unaweza kutokana na sifa za

kimwili, kama vile, dalili za ugonjwa

zinazoonekana, au kutokana na mtazamo hasi

unaoelekezwa kwenye kikundi fulani cha watu au

mtu.

Unyanyasaji: Matumizi ya kitu au kumtendea mtu

isivyostahili, kwa kumdhuru, au kinyume cha

sheria.

Unyanyasaji wa kijinsi: Aina yoyote ya

mwingiliano wa kimapenzi isiyotakiwa kama vile,

kulazimisha busu, kulazimisha, ulawiti, umalaya,

au upekuzi mbaya. Unyanyasaji wa kijinsia

huendekezwa na shauku ya kutumia mabavu,

Page 244: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

232

amri, na utawala-si mapenzi au tamaa. Mkosaji

anaweza kutumia nguvu au vitisho.

Usiri: Makubaliano au uwakilishi unaoweka wazi

kwamba taarifa hazitatolewa. Kuwa na uwezo wa

kuzungumza kwa usiri ni muhimu kwa wahanga

wengi wa unyanyasaji wa kijinsia, na mara nyingi

panakuwa hakuna usiri kwa waathirika.

Utamaduni: Imani, desturi, na mzoea ya jamii au

kikundi ndani ya jamii (kama vile utamaduni wa

vijana) na tabia za jamii zilizopatwa.

Wakala wa mabadiliko: Tukio, shirika, vifaa, au,

mara nyingi, mtu anayetenda kama kichocheo

cha mabadiliko.

Page 245: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

233

MIREJEO

AVERT. 2017. “HIV and AIDS in Tanzania.”

http://www.avert.org/professionals/hiv-around-

world/sub-saharan-africa/tanzania.

Das, Pamela, and Richard Horton. 2016. “On

Both Sides of the Prison Walls—Prisoners and

HIV.” The Lancet 388 (10049): 1032–33.

doi:10.1016/S0140-6736(16)30892-3.

Dennehy, Kathleen M., and Kelly A. Nantel. 2006.

“Improving Prison Safety: Breaking the Code of

Silence.” Washington University Journal of Law &

Policy 22: 175–185.

http://openscholarship.wustl.edu/law_journal_law

_policy/vol22/iss1/14.

International Organization for Migration (IOM).

2016. “Fighting Tuberculosis in Tanzania,” April

15, 2016, Tanzania: Migration for the Benefit of

All [website]. https://tanzania.iom.int/press-

releases/fighting-tuberculosis-tanzania.

Page 246: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

234

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS

(UNAIDS). 2014a. The Gap Report.

http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a

sset/UNAIDS_Gap_report_en.pdf

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS

(UNAIDS). 2014b. On the Fast Track to End AIDS:

UNAIDS 2016–2021. Geneva, Switzerland:

UNAIDS.

http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a

sset/20151027_UNAIDS_PCB37_15_18_EN_rev1.p

df.

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS

(UNAIDS). 2016. Global AIDS Update 2016.

Geneva, Switzerland: UNAIDS.

http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a

sset/global-AIDS-update-2016_en.pdf.

Krug, Etienne G., Linda L. Dahlberg, James A.

Mercy, Anthony B. Zwi, and Rafael Lozano.

World Report on Violence and Health. Geneva,

Switzerland: World Health Organization, 2002.

Page 247: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

235

http://www.who.int/violence_injury_prevention/vi

olence/world_report/en.

Martin, Keith L. “Cracking the Code of Silence.”

Prisonerlife.com. July 6, 2002.

https://www.prearesourcecenter.org/sites/default

/files/library/crackingthecodeofsilence7-6-

2002.pdf.

Mills Edward J., Nathan Ford, and Peter

Mugyenyi. 2009. “Expanding HIV Care in Africa:

Making Men Matter.” The Lancet 374 (9686):

275–276. doi:10.1016/S0140-6736(09)61348-9.

Office of the United Nations High Commissioner

for Human Rights (OHCHR). 2005. Human Rights

and Prisons: A Compilation of International

Human Rights Instruments Concerning the

Administration of Justice. Professional Training

Series No. 11 Add.1.

https://www.un.org/ruleoflaw/files/training11Add

1en.pdf.

Smith, Brenda V., and Jaime M. Yarussi. 2007.

Breaking the Code of Silence: Correction

Page 248: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

236

Officers' Handbook on Identifying and

Addressing Sexual Misconduct. Washington, DC:

NIC/WCL Project on Addressing Prison Rape and

National Institute of Corrections.

https://s3.amazonaws.com/static.nicic.gov/Librar

y/022473.pdf.

Sonke Gender Justice Network and MenEngage.

2012. Addressing HIV and Sexual Violence in

Correctional Services Facilities: A Guide for

Working with Members of the Correctional

Department of Correctional Services.

http://detentionjusticeforum.org.za/wp-

content/uploads/2013/09/Sonke-and-Just-

Detention-International-Addressing-HIV-and-

Sexual-Violence-in-Correctional-Facilities-Guide-

for-Correctional-Staff.pdf.

Sonke Gender Justice and MenEngage. 2017.

“Men and HIV in the ESA Region.” Sonke Gender

Justice. Accessed January 25.

http://www.genderjustice.org.za/publication/men

-hiv-esa-region/.

Page 249: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

237

Page 250: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · 2018-09-12 · Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya VVU Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015